16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1038 Dhuul-Qaad 1434, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Moyo awabomoa wahafidhina Asema Jamhuri na Dola ya Zanzibar inakuja Uamsho, wasomi, wanasiasa sasa lao moja Salim, Prof. Shariff: hakuna sulhu ni mkataba tu MZEE Hassan Nassor Moyo. Habari Uk. 4 “MIMI sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba. Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na AFISA Elimu Mkoa wa Mtwara, Bw. Kipenya, Afisa Elimu Mtwara amfuta Mwalimu kwa kuvaa kofia Awagawa wasimamizi wa mtihani kidato 4 Waislam kwao, Wakristo upande ule wakizoza Na Bakari Mwakangwale amedaiwa kumuengua Mwalimu Fadhili M. Mgwigwi, kuwa mmoja wa wasimamizi wa mtihani wa kidato cha nne, kwa kukataa kuvua kofia yake. Tukio hilo limetokea Inaendelea Uk. 2 Naibu Waziri wa Bara VS Waziri Kamili Zanzibar Kielelezo cha kudharauliwa Zanzibar Hatutaki Bendera inayoishia Chumbe Hizi ni njama kuuwa uchumi Zanzibar muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Inaendelea Uk. 3 BAADHI ya mahujaji nchini wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya kuelekea Hija, Makka Saudi Arabia. Safari ya Hijja Hijiria 1433 Tanzania Muslim Hajj Trust inawaalika wote kwenye HAFLA ya kuwaaga Mahujaji. Tarehe: 14/10/2012 Jumapili Ukumbi: Starlight Hall Wakati: Saa 8 - 11 jioni KARIBUNI WOTE

ANNUUR 1038

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ANNUUR 1038

ISSN 0856 - 3861 Na. 1038 Dhuul-Qaad 1434, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

Moyo awabomoa wahafidhina Asema Jamhuri na Dola ya Zanzibar inakujaUamsho, wasomi, wanasiasa sasa lao mojaSalim, Prof. Shariff: hakuna sulhu ni mkataba tu

MZEE Hassan Nassor Moyo. Habari Uk. 4

“MIMI sitafuni maneno kwamba ni muumini w a Z a n z i b a r y e n y e mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba.

Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na

AFISA Elimu Mkoa wa Mtwara, Bw. Kipenya,

Afisa Elimu Mtwara amfuta Mwalimu kwa kuvaa kofia

Awagawa wasimamizi wa mtihani kidato 4Waislam kwao, Wakristo upande ule wakizoza

Na Bakari Mwakangwale amedaiwa kumuengua M w a l i m u F a d h i l i M . Mgwigwi, kuwa mmoja wa wasimamizi wa mtihani wa

kidato cha nne, kwa kukataa kuvua kofia yake.

Tukio hi lo l imetokea Inaendelea Uk. 2

Naibu Waziri wa BaraVS

Waziri Kamili ZanzibarKielelezo cha kudharauliwa ZanzibarHatutaki Bendera inayoishia ChumbeHizi ni njama kuuwa uchumi Zanzibar

muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha.

H i v i h u y u a n a j u a anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma?

Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe?

Mimi nataka niione b e n d e r a y a D o l a y a

Inaendelea Uk. 3

BAADHI ya mahujaji nchini wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya kuelekea Hija, Makka Saudi Arabia.

Safari ya Hijja Hijiria 1433Tanzania Muslim Hajj Trust inawaalika wote kwenye HAFLA ya kuwaaga Mahujaji.Tarehe: 14/10/2012 JumapiliUkumbi: Starlight HallWakati: Saa 8 - 11 jioni

KARIBUNI WOTE

Page 2: ANNUUR 1038

2 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Habari

Afisa Elimu Mtwara amfuta Mwalimu kwa kuvaa kofia

Inatoka Uk. 1Octoba 6, mwaka huu katika ukumbi wa Sekondari ya Newala, Mkoani Mtwara, wakat i wa semina ya k u w a f u n d a w a l i m u kwa kazi ya kusimamia mtihani wa kidato cha nne, unaoendelea hivi sasa nchi nzima.

Chanzo chetu cha habari kutoka Newala, kilieleza kuwa kulitokea mvutano baina ya Afisa Elimu wa Mkoa wa Mtwara aliyemtaja kwa jina moja la Bw.Kipenya na mwalimu Fadhil i Mussa, baada ya bosi huyo wa Elimu Mkoani humo kumuamuru Mwalimu Fadhili kuvua kofia ili aweze kuapishwa.

Chanzo hicho kilisema, Mwalimu Fadhili alitoa hoja kwamba haoni sababu ya kuvua kofia yake kwa sababu hakuna sharia ya nchi wala ya Baraza la Mitihani inayosema kuwa mtu aliyevaa kofia hawezi kuwa ms imamiz i wa mitihani.

Taarifa kutoka katika kikao hicho zi l ie leza k w a m b a , h a l i h i y o ilisababisha zogo na kutoa sura ya mgawanyiko wa kiitikadi kwani kwa walimu Wais lamu wal imtetea mwalimu Mussa huku wale Wakristo, walishupalia msimamo wa Afisa Elimu.

An nuur ilimtafuta Afisa Elimu huyo Bw. Kipenya, ili kutoa ufafanuzi ambapo al isema kuwa hawezi kukanusha wala kukubali kama lilitokea kupitia chombo cha habari, kwa sababu kama mtumishi wa Serikali, kuna taratibi zake za kufuata.

“Sikanushi wala sikubali kama tukio hilo lilitokea.” Alisema Afisa Elimu huyo wa mkoa wa Mtwara.

Hata hivyo Mwandishi alipomdadisi zaidi juu ya tukio hilo, ambalo lilielezwa kuwa liliegemea zaidi chuki za kidini badala ya kusimamia kanuni za utumishi wa umma, alisema yeye hakumuambia atoe kofia aliyokuwa ameivaa Mwalimu Fadhili.

Alisema, yeye na huyo ni watumishi wa Serikali, na kama mwalimu huyo hakuridhika, alipaswa afuate ngazi za kufikisha malalamiko yake ambapo alisema hatua ya kwanza ni kwa Mkurugenzi na si katika magazeti.

“Kama hakuridhika, a l i p a s w a k u p e l e k a malalamiko yake kwa M k u r u g e n z i , k u w a nimetendewa hivi na hivi, na kama hapo hakuridhikia pia, aende kwa Mkuu wa Mkoa, si kwenda katika vyombo vya habar i .” Alisema Bw. Kipenya.

Akielezea mkasa mzima Mwalimu Fadhili, alisema yeye ni mwal imu wa Sekondari ya Makukwe, N e w a l a , n a k w a m b a a l i sh i r i k i k ikami r i fu semina ya kusimamia mitihani ya kidato cha nne, iliyoendeshwa chini ya Afisa Elimu Mkoa (Kipenya) mpaka kufikia hatua ya kula kiapo.

Alisema, ilipofika hatua ya kuanza utaratibu wa kuapa, ndipo bosi wake (Afisa Elimu) alipomuamuru avue kofia.

“Afisa Elimu alisema, m w a l i m u v u a k o f i a , sikuvua. Ndipo aliposimama Mwalimu Lihipuka, alisema, unamuamuru avue kofia kwa sheria ipi ya utumishi wa Serikali, inayomkataza a s i v a e b a l a g h a s h i a ” A l i s e m a M w a l i m u Fadhili, akimnukuu, mwl. Mwenzake.

Alisema, Afisa Elimu hakujibu wala hakufafanua swali hili la Mwl. Lihipuka, badala yake liliibuka zogo na minog’ono kutoka k w a w a n a s e m i n a n a kugawanyika, ambapo Wakristo walitaka nivue na Waislamu wakisema nisivue, kwa kuwa hakuna sheria inayo kataza kuvaa kofia hiyo.

“Amri yako nimeipokea, ila ili nafsi yangu isije ikajuta naomba naomba nisivue kofia hii. Ndipo Af i sa E l imu a l i sema ‘utawezaje kuapa wakati wakati unakofia hebu toka nje’ na mimi nikawa

natoka, huku akiniuliza ni mwalimu wa shule gani nami nikamjibu Makukwe.” Alisema, huku akinukuu maelezo ya afisa elimu.

Alisema, baada ya hapo, aliondoka kwenda kwa Afisa Elimu wa Wilaya, aliye mtaja kwa jina la Karitasi Munyongwa, kwa lengo la kufuata barua yake ya kwenda kusimamia mitihani, ambapo aliambiwa kuwa amendolewa katika zoezi hilo.

An nuur ilipotaka kujua kama malalamiko hayo kayapeleka katika ngazi za juu, kama alivyodai Afisa Elimu Bw. Kipenya, alisema anashindwa kwa kuwa bosi wake huyo amemuengua kienyezi pasi ya kumpa barua yoyote, inayo ainisha kosa lake.

Alisema, anachoelewa yeye ni kuwa si kosa kuvaa balaghashia kazini au kuwa kikwazo cha kuapa akiwa ameivaa, kwani katika muongozo wa kazi hakuna sehemu inayozuia kuvaa kofia ya Kiislamu.

A l i s e m a , k a t i k a muongozo wa kazi kwa watumishi wa umma, bali zinakatazwa nguo zinazo bana, kaptula, Sketi fupi, nguo yoyote inayoonyesha ishara ya chama fulani cha siasa, na kwamba katazo la kuvaa balaghashia halimo katika orodha ya mavazi yasiyo takiwa.

DKT. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

HIVI sasa Chama cha Mapinduzi CCM kipo katika mchakato wa uchaguzi ili kuwapata v iongoz i wa kutumikia chama katika nafasi mbalimbali.

Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama-NEC kuanzia ngazi za wilaya na mikoa, viongozi wa chama mikoa, viongozi wa Jumuia mbalimbali za chama n.k wameshapatikana.

Walioshinda wanaendelea kufurahi na kujivunia ushindi wao. Walioshindwa wameumia moyoni huku wakisononeka na kutoa shutuma mbalimbali dhidi ya walioshinda au dhidi ya wapambe wa walioshinda.

M i o n g o n i m w a waliolalamikia vitendo vibovu katika uchaguzi huo wa chama ni Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, ambaye alishindwa na Waziri wa Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu katika nafasi ya ujumbe wa NEC kupitia wilaya ya Hanang.

Wapo ambao wameamua kuachana na CCM kabisa baada ya kuangushwa au baada ya majina yao kuondoshwa katika nafasi ya kugombea n.k.

A i d h a w a m e k u w e p o w a n a o l a l a m i k i a u t i t i r i wa watoto wa vigogo na maveterani wa CCM kugombea katika uchaguzi huo, ambao wanaonekana kuwa na nguvu au kuwa na nafasi kubwa ya kushinda, si kwa sababu wana sifa tu, bali kutokana na hisia kwamba wa kutumia umaarufu wa wazazi wao ambao aidha ni vigogo au walikuwa vingunge na makada mashuhuria ndani ya chama, basi wanakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa.

Kwa jinsi mazingira yalivyo, tunaona kuwa sasa maumivu yanayotokana na athari za rushwa yamewagusa hata wagombea maveterani, ambao enzi zao hawakuhisi kuguswa na kadhia hii.

K u a n g u s h w a v i g o g o waliokuwa wameshika dola ziku za nyuma, iwe ni kwa rushwa au mizengwe mingine ya k iuchaguz i , ha ikuwa tatizo enzi zile ambazo wao walikuwa wameshika mpini japo ilikuwepo kama ilivyo sasa.

Itoshe tu kuwa somo kwamba hiyo ndio hali ilivyo katika chaguzi za chama hicho na imekuwepo kwa kipindi kirefu, japo ilikuwa haiwashughulishi waliokuwa wameshika mpini kwa wakati wao.

Mapungufu haya katika

Komesheni mazoea ya kugombea nafasi za chama kusaka nyadhifa na umaarufu

kuwachagua viongozi na wajumbe ndani ya CCM na jumuia zake, yametokana na mazoea mabaya kwamba mwanachama hawezi kuwa kiongozi wa serikali au kupata nafasi ya kuteuliwa na Rais kushika wadhifa fulani, au kuchaguliwa kushika madaraka zaidi ndani ya chama bila kwanza kushika wadhifa fulani kwenye chama ili kujijengea umaarufu na kufahamika.

Kwamba kuwa mwanachama t u w a C C M h a k u w e z i kumhakikishia mtu kupata fursa ya kufahamika na kupimwa ili kupata fursa ya kuteuliwa au kuchaguliwa kushika wadhifa wa juu serikalini au ndani ya chama kutokana sifa na uwezo wake.

Kwa j ins i hal i i l ivyo, mwanachama bila kuwa na wadhifa wowote wa kichama, hata kama ana uwezo na sifa, inakuwa vigumu kwake kuwania iwe Ubunge au udiwani kwa kuwa sio maarufu na hafahamiki vyema kwa makada wa chama.

N d i o m a a n a t u n a o n a kwamba pamoja na kuwa nafasi nyingi zinazogombewa hazina kipato cha maana, lakini watu wapo tayari kuparurana na kuchafuana, kutembeza rushwa, kuwekeana mizengwe n.k lakini mtu ashinde.

Baada ya kushinda basi hapo mtu ana uhakika kwamba kwa nafasi yake ndani ya chama, siku moja ataweza kuteuliwa au kuchagul iwa kushika wadhifa fulani kwa kuwa tayari ameshafahamika na kuzoeleka katika mboni za vigogo.

Aidha tunaona kwamba baadhi wanagombea nafasi hizi zisizo na vipato ili tu kulinda umaarufu na nydhifa zao serikali.

Mtu tayari ni Waziri, ni mwanachama hai wa chama tawala, lakini hayo yote hayakidhi kiu, bado anaona kuna haja ya kuweka mizizi zaidi ndani ya chama kwa kuwania wadhifa wa kichama kama ujumbe NEC, uenyekiti wa Jumuia, uenyekiti wa chama mkoa, Wilaya n.k!

Katika hali hii tunaona kuna haja CCM kutizama zaidi nia na dhamira za wagombea wake katika chaguzi za chama na asasi zake.

Mtu achaguliwe kwa sifa na uwezo wake, sio umaarufu na uwezo wa wazazi wao kiuchumi.

Vinginevyo chama kinaweza kuwa taasisi ya watu kusaka maslahi yao na familia zao serikalini badala ya maslahi ya umma wa Watanzania.

Page 3: ANNUUR 1038

3 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Habari

Yule tapeli aliyeandikwa kwenye gazeti hili la An nuur la wiki iliyopita, amenaswa tena Mbeya akisilimu kwa mara nyingine.

Alinaswa katika Msikiti wa Uyole, Njia Panda siku ya Jumanne ya tarehe 09/10/2012.

Kijana huyu alifika katika msikiti wa Uyole, Njia Panda, muda wa saa 12:00 jioni, Jumanne na akaomba kuonana na Imamu.

Mbele ya Imamu Hamisi Yusuph, kijana alijitambulisha kuwa kiasili yeye ni Mmasai, jina lake kabla ya kusilimu aliitwa Peter John.

Akij i tambulisha zaidi akasema kuwa, yeye kwa sasa anaitwa Ismail John na kwamba amesilimu siku hiyo hiyo.

Alidai kuwa, awali alikuwa Mwinjilist wa Kanisa la KKKT la Uyole, Mbeya mjini.

Habari zaidi zinafahamisha k u w a I m a m u H a m i s i alimpeleka Msikitini na kumpa nafasi ya kuzungumza na Waislamu baada ya swala ya Magharibi.

Akiwa mwenye kipaji cha kusema, alijieleza vizuri huku akitoa mistari ya Biblia inayoonyesha upotofu wa dini ya Kikristo, hali iliyoleta Takbiira nyingi zisizo na mipaka.

Kijana ‘Peter’ aliwavuta na kuwaokota Waislamu kiasi cha kawafanya wawe wepesi kufumua mifuko yao kwani baada ya kuanza mchango z i l i pa t ikana 130 ,000 /= kinyume na zile shilingi mia

Yule tapeli wa kusilimu anaswa tena jijini Mbeya

Adai anasilimu baada ya kumsoma Doctor Sule Abanwa, akiri ni Muislamu wa kuzaliwa ila njaa

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

mia wanazotoa wakitakiwa kuwachangia vitu vingine vya kimaendeleo ya Waislamu.

‘Peter’ alidai kuwa tarehe 04/07/2012, Mhadhiri Doctor Sule na wenzake walifanya mhadhara katika mji mdogo wa Tunduma na kusilimisha watu saba.

Akasema, yeye hakusilimu japo alishauona ukweli ila badala yake alimwomba Doctor Sule amwazime vitabu alivyokuwa navyo ili akasome na kuchambua zaidi.

A k a s e m a , b a a d a y a kuvisoma vitabu hivyo, haki ilimdhihirikia zaidi na ndipo tarehe 09/10/2012 aliamua kusilimu.

Akaongeza kuwa, baada ya viongozi wa Kanisa na baba yake anayeishi Mererani kupata taarifa ya kusilimu, walimfuata na kumnyang’anya kila kitu na sasa anataka aende kwao Mererani akasome Uislamu zaidi.

Hiyo ikawa ndiyo gia ya kuwafanya Waislamu kutia mikono mfukoni, kwa kila aliye na chochote akatoa.

P a m o j a n a m a e l e z o hayo mazuri, alikuwepo

msomaji mzuri wa An nuur, aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani Yusuph ambaye a l imsh tuk ia na kuanza kunong’ona na mwenzake kuwa huyu bwana ndiye aliyeko kwenye gazeti la an nuur.

Hapo ukafunguka ukurasa mpya kwani baada ya gazeti la An nuur kuletwa alikiri kuwa picha ile ni yake na alipigwa Ifakara, Mororgoro.

Wakati mzozo ukipamba m o t o , a l i j i t o k e z a m t u aliyesema alimwona Ifakara Msikitini akitoa maelezo na kusilimishwa.

‘Mmasai Peter’ alipoulizwa amesilimu mara ngapi, alidai ni mara nyingi tu na kwamba anafanya hivyo kwa nja tu.

Akijieleza upya akasema kuwa yeye ni Muislamu wa kuzaliwa na jina lake ni Ismail Athumani Hassani wa Mererani na kabila lake ni Mnyiramba.

Aliwaomba Waislamu wamwadhibu humo humo Msiki t ini kwani Allah amemuumbua.

Hata hivyo, baada ya kushaurina, Waislamu waliona TAPELI Peter John.

ni bora wampeleke kituo cha polisi na wawasiliane na wenzao wa Ifakara waone hatua watakazo mchukulia.

Baada ya kumpeleka kituoni walishauriwa kuwa wanaweza kumfungul ia mashitaka au watumie RB ile ile iliyotumiwa na wenzao wa Ifakara kwani Jeshi la Polisi ni lilelile.

Imamu wa Msikiti, Uyole, amewanas ih i wa is lamu kuchukua tahadhar i na watu kama hawa kwani ni majambazi kupitia anuwani ya kusilimu na kwamba wasifikiri majambazi yako uchochoroni tu bali hata misikitini wanafika.

K u h u s u f e d h a zi l izochangwa alishauri ziende kwenye ujenzi wa fensi ya msikiti na Waislamu wakaridhia.

Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuwa kijana mmoja ‘amesilimu’ mara nyingi na kujizolea fedha kutoka kwa Waislamu.

Kwa mara ya kwanza kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Peter John, akidai ni Mmasai kutoka Simanjiro, alifika Ifakara na kudai kwamba yeye ni Muinjilisti lakini ameona ukweli na kwamba anataka kusilimu.

Hiyo ilikuwa ni Alhamisi ya tarehe 27 Septemba, 2012 saa 12 jioni katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa ambapo alisilimishwa na Amiri wa kundi la Tabligh Sheikh Nassor lililo kuwa Msikiti Mkubwa wa Ifakara Wilaya ya Kilombero.

Aliendelea na utaratibu wake huo wa kusilimu na kuchangiwa fedha katika Misikiti mbalimbali hadi alipokamatwa ila akaachiwa baada ya kuomba msamaha.

Naibu Waziri wa Bara VS Waziri Kamili ZanzibarInatoka Uk. 1

Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale.

Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu.

Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje.

L e o h a t a m a m l a k a ya k iuchumi ha tuna . Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika w a m e k w a m i s h a , wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu.

Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru

tena. Lengo ni kuua uchumi

wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao.

Yaguju! Wasahau hilo. Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu.

Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi.

Tutarejesha mamlaka yetu kamili. Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa maslahi ya watu wetu.

Tu n a t a k a t u w e n a uanachama katika jumuiya na mashir ika yote ya

kimataifa. Tuwe na Waziri wa

M a m b o y a N j e w a Zanzibar.

Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni.

Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana!

Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya.

Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili.” (Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad, Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF) Maalim Seif Shariff Hamad

Page 4: ANNUUR 1038

4 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Habari

Moyo awabomoa wahafidhina ZILE porojo za wahafidhina wasiotaka kuona Jamhuri y a w a t u w a Z a n z i b a r, z i m e b o m o l e w a h u k u wakikatishwa tamaa kwa kuambiwa kuwa wamechelewa, Dola inakuka.

Porojo na hoja za wahafidhina hao zimefukiwa na Mzee Nassoro Moyo pale aliposema kuwa ni kufilisika kisiasa na kutapatapa kwa wanaokuja na madai ya kurudi kwa Sultan na Hizbu.

Kwa upande mwingine, msimamo na maoni ya kutaka muungano wa mkataba kati ya Zanzibar na ‘Tanganyika’ umezidi kupata nguvu baada ya kupatikana umoja na kuungana katika msimamo huo kwa viongozi wa kidini, wasomi na wanasiasa.

H a y o y a m e j i r i k a t i k a kongamano la kuadhimisha miaka mitatu toka kuundwa kwa Kamati ya Maridhiano ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ambapo mada kuu ilikuwa ni kujadili nafasi ya Zanzibar katika Katiba Mpya lililofanyika hivi karibuni.

Katika kongamano hilo, Wazanzibari kutoka taasisi mbali mbali waliendelea kuonesha msimamo wao wa kuwepo Muungano wa Mashirikiano ya Kimkataba kati ya Zanzibar na Tanganyika na kwamba wale wote ambao wanaoshurutisha watu kubaki na msimamo wa Serikali mbili zilizopo wamepitwa na wakati.

A k i t o a m a d a k a t i k a Kongamano hilo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hassan Nassor Moyo aliendelea na Msimamo wake wa kudai Zanzibar huru chini ya Mashirikiano ya Kimkataba na kwamba wale wote wanaolazimisha wananchi kufuata matakwa wanayotaka wao Serikali inajukumu la kuwachukulia hatua.

Moyo amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuwaelezea wananchi ni mfumo wa aina gani ambao Zanzibar inafaa kuufuata na kuongeza kuwa Muungano wa Kimkataba ndio suluhisho la matatizo na Kero zilizodumu kwa muda wote wa miaka 48.

Amesema, Kamati yake ya Maridhiano ilifanya kazi kubwa bila hata malipo hadi kuweza kupatikana k wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nakufahamisha kuwa chemchem ya Kamati hiyo ni Rais Mstaafu wa awamu ya sita Zanzibar Dk. Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim seif Sharif Hamad ambao walisaidiwa na Isamil Jussa, Eddy Riyamy, Mansour Himid, Aboubakar, Binaamir chini ya Mzee Moyo.

Alifahamisha kuwa Serikali ya Umoja wa kitaifa haikuja kirahisi, bali ni juhudi zilizojaa uzalendo na kubainisha kuwa hapo awali Zanzibar ilishapitia Miafaka 3 chini ya Wazungu na washiriki kulipwa fedha nyingi lakini hakukusaidia lolote

A l i e n d e l e a k u w a k w a vile walijali maslahi ya nchi wallisahau tofauti zao za kiasili,kivyama na kuweka utaifa

Na Mwandishi Wetu

mbele jambo ambalo limesaidia uwepo wa Serikali hiyo

“Niliwauliza wajumbe wa kamati yangu, nani kati yenu anaweza kunishinda mimi kuwa Hizbu? Nani atanishinda kuwa ASP, ZPP au CCM? Kama kweli mnataka kuikomboa nchi yenu, basi sahauni vyama vyenu..kadi yangu ya CCM ni no. 7 na kina Jussa nao CUF lakini walikubali shauri langu na kusahau vyama vyao na kuweka utaifa mbele”. Alisema Moyo

Moyo aliwataka washiriki wa Kongamano hilo kuendelea kutunza amani na mshikamano uliopo na kwamba wasikubali kugawanywa na baadhi ya watu ambao alidai ni viongozi wal iopi twa na wakat i na wababaishaji.

“ Wa l e Wa j i n g a w a l e wanaozungumza mambo ya kijinga kuwa sisi tunaotaka Muungano wa Mkataba ati tunataka kumrudisha Sultani..wewe na baba yako ndio mnafikiria hivyo” Alifoka Moyo.

Amesisitiza kuwa mawazo ya kisultani yaliondoka toka yalipofanyika Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 na kwamba Sultani hatokuja kwa watu kudai haki zao.

Alisema kiongozi wa aina hiyo ambaye hupandikiza mbegu za uoga ili wananchi wasahau kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ndio ajenda kuu amefilisika kisiasa

“Kwanza tunakwambia umefil isika kisiasa, hujui unalolifanya, unatumia madaraka vibaya, unataka kuwatisha watu, lakini hakuna wa kuogopa tena katika kupigania maslahi ya Zanzibar chini ya Mkataba wa Muungano”. Alisisitiza Mzee Moyo

Moyo alisisitiza kuwa kwa vile waliweza kupigania haki zao na kuweza kumtoa Sultani katika himaya ya Zanzibar pia hawatoweza kusimama na kumuogopa mtu yeyote katika kudai Haki ya Zanzibar.

Ameongeza kuwa Kamati ya Maridhiano inamtambua Dk. Shein kuwa Rais halali wa Zanzibar na Makamo wake wa kwanza Maalim Seif Shariff na kwamba viongozi w a l i o b a k i w a n a w a j u w a wenyewe waliowachagua wao hawawatambui.

“Ni l iwah i kumwambia Maalim Seif na leo nasema tena hadharani kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa tulimkabidhi Dk. Shein na Maalim Seif ili tuondekane na chuki na uhasama, wengine ambao wapo katika Serikali hii wanawajua wao..nasema tena leo Sisi tunawajuwa wao baasi wengine hatuwajui”. Alisisitiza kwa hasira.

A k i o n e k a n a m w e n y e kukerwa na baadhi ya watu ambao anaamini hawakuridhika na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Moyo alisema, “baadhi ya viongozi hili jambo la maelewano hawalitaki kabisa wale 33 % ambao walipinga uwepo wa GNU ndio hao pia wanaoendelea na uhafidhina huo na kutupa shida leo”.

Al i sema, wamej ipanga na mapambano yoyote dhidi ya wahafidhina na kwamba tayari Kamati yake imepeleka mapendekezo yao Serikalini

kupitia kwa Dk. Shein na Maalim Seif ambapo pia mapendekezo hayo walimpelekea Dk Aman Karume kwamba ili kuwepo usawa na maelewano mazuri kati yetu na Tanganyika, Suluhu ni Muungano wa Mkataba.

Kwa upande wake Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi Salum Said Rashid alipokuwa akielezea historia ya Muungano alifurahishwa na umoja wa Wazanzibari waliouonesha katika kujadil i ajenda na kuunga Mkono hoja ya kuwa na Muungano wa Mkataba

Alisema, toka mwanzo M a t a i f a y a M a g a h r i b i hawakuyaridhia Mapinduzi ya Januari 12 na kuhisi yataifanya Afrika kuwa Cuba ndio maana kwa kushirikiana na Nyerere walifanya Muungano huo ili kuyadhibiti Mapinduzi hayo.

“ U k w e l i n i k w a m b a Muungano u l i f anywa i l i kuidhibiti Zanzibar na ndio maana hakuna natija yoyote ambayo imepatikana, sasa fursa imekuja Wazanzibari tuitumieni ya kutoa maoni kuwa maendeleo yatapatikana kwa kuwepo Muungano wa Kimkataba”. Alitanabahisha Rashid.

Alisema kuwa Muungano wa Mkataba ndio Suluhisho na muafaka kwa nchi mbili huru na kuongeza kuwa Muungano wa Katiba unafaa kwa Taifa moja na Nchi moja lakini kwa Nchi mbili kama Zanzibar na Tanganyika Mkataba wa mashirikiano ndio suluhu.

“Idadi ya Serikali siyo kitu muhimu tunachokitaka sisi, kwetu Uhuru wetu wa na mamlaka kamili ya kuweza k u j i a m u l i a m a m b o y e t u wenyewe na kuwa na urafiki na mashirikiano na mataifa mengine ikiwemo taifa la Tanganyika ndio jambo la msingi kwetu”, alisisitiza Rashid.

Aliwaasa Wazanzibari kuwa macho na watu wanaoendelea kutoa picha kwa nchi za nje kuwa ambayo haina ukweli kuwa Zanzibar kuna chama chenye msimamo mkali wa kidini.

N a y e M w e n y e k i t i w a K o n g a m a n o h i l o P r o f . Shariff alisema Wazanzibar walikuwa wamegawanywa na kugawanyika bila kujifahamu kuwa wao wanaunganishwa na Uzanzibari wao na kwamba hata vyama vya siasa vilikuja ikiwa wao wameshakuwa Wazanzibari na kuwataka Wazanzibari kutokurudia tena.

Alisema wako watu ndani ya nchi hii na nje ya nchi hii ambao hawakuridhika na mafanikio ya maridhiano yaliyopo na kwamba wanaendelea kufanya kila mbinu mpaka watimize azma yao ya kuigawa Zanzibar ili waimeze kabisa lakini hawatofainkiwa.

“Wakati wa kudangwanywa na kubabaishwa ushapitwa na wakati na sasa zama za kuweka mbele Maslahi ya Zanzibar, si lazima maslahi ya Chama kuwekwa mbele kama baadhi wanavyodai”, aliongezea Proff Shariff.

Kwa upande wake Amir wa Jumuiya ya Uamsho na M i h a d h a r a y a K i i s l a m u Sheikh Mselem Ally alisema Miaka yote 48 ya muungano kamati mbalimbali ziliundwa na kushindwa kuondoa Kero hivyo kizazi cha sasa kimeona

Suluhisho ambalo ni Mamalaka kamili kwa kila Nchi chini ya Mkataba wa Muungano.

Al iwa taka Wazanz iba r kutokubali kutumiwa na baadhi wasioitakia mema Zanzibar na kuwakumbusha Washiriki wa Kongamano hilo kuwa wao wana lengo moja tu kama walivyo watu wengine la kupatikana Mamalaka huru ya Zanzibar.

Naye Father Immanuel Masoud wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Mjini Zanzibar ambaye alikuwa akitoa maoni yake alisema amefurahishwa na hali ya maridhiano iliyopo na kusema kuwa Suala la Zanzibar kusimama katika uhuru wake halizuiliki.

“Zanzibar ni watu na kwa vile watu wenyewe ndio tunasema tunataka mamlaka kamili ya Zanzibar, basi hakuna njia ya kulizuia hilo, ninaungana na waliotangulia kuwa kwa vile Muungano tumeunza muda mrefu si vyema tukauondoa moja kwa moja lakini njia pekee ya kufanikisha hilo ni Mkataba wa Muungano” Alisema Father huyo na kujinata na Uzanizbari wake.

Amir Far id i Hadi kwa upande wake alisema kushiriki Kongamano hilo kwa taasisi mbali mbali na watu wenye dini tofauti na kusimamia kauli mbiu ya kutaka Mamlaka Kamili ya Zanzibar kumeonesha njia ya mafanikio ya jambo hilo.

Al is is i t iza pia haja ya Wazanzibari kushiriki kwa wingi katika kutoa maoni yao juu ya Katiba mpya na kwamba haihitaji kutoa maneno mengi zaidi ya kusimamia kauli mbiu ya Mamlaka Kamili ya Zanzibar

A l i s e m a k u t o k a n a n a mwelekeo wa utoaji wa Maoni unavyoenda Tume ya kerekebisha Katiba ijiandae kutayarisha Katiba ya Tanganyika na Mkataba wa maridhiano baina ya Jamhuri ya Watu wa Zaznibar na Tanganyika.

Mansour Himid Wazir i asiyekuwa na Wizara Maalum alisema katika kipindi hiki kitu cha pekee ni busara na kustahamiliana huku Washiriki h a o w a k i f a h a m u k u w a watakaposema wajue kuwa nao watajibiwa.

Alisema haoni haja ya kutishana na na wale alioadai ni Vitimbakwiri wanaojaribu kuwatisha wanamapinduzi halali wa Zanzibar bila ya hoja ya msingi na kwamba hata kama hawapendezi kwa wengine lazima ukweli wauseme.

“Huwa najiuliza kulikoni Vitimbakwiri kulazimishana? Viongozi ambao wanaendelea kuwashurutisha wenzao juu ya Mfumo wa Muungano ni Waovu, Wapumbavu na wamekosa mwelekeo”. Alishangazwa Mansour.

Kiongozi hawezi kushurutisha watu labda kuwe na jambo ambalo linahatarisha amani kama ambavyo Dk. Shein amekuwa ak i fanya p ind i amani inapotetereka lakini si kushurutishana juu ya Mfumo wa Muungano.

Alikemea baadhi ya Waroho wa madaraka ambao huwabagua

na kuwaponda Wapemba ili waonekane wema na kupendeza kwa lengo la kupatiwa vyeo katika Chama au Serikali.

Aliongeza kuwa hakuna haja ya kuwabagua Wakristo katika mapambano ya kupigania Mamlaka huru ya Zanzibar na kwamba kila Mzanzibari kwa nafasi yake awe Mkristo, Mbudha au Shia anahitajika kuunga gurudumu hilo kwa uzalendo mkubwa.

Alizitaja Kamati ambazo ziliwahi kuundwa bila mafanikio kwa kipindi chote cha miaka 48 ya Muungano na kusema kuwa hazikupata mafanikio yoyote kutokana na kukosekana Mfumo sahihi wa kuondoa kero za Muungano ambao kwa sasa ni Mfumo wa Mkataba.

Ismail Jussa kwa upande wake alianza kwa kuwatoa wasiwasi Wananchi juu ya kujiuzulu nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar kwa kile alichodai kuwa kutoa nafasi zaidi katika kufanya shughuli za Jimbo lake na kujipanga zaidi katika kupigania Maslahi na Jamhui ya Watu wa Zanzibar .

Alisema kama kuna watu wanakaa katika vilinge na kupanga njama za kuharibu maridhiano wamechelewa kwani Wazanzibari wamelijua hilo la asilani hawako tayari kugawanywa.

Alisema kumpandisha cheo mtu cha Balozi Mkaazi wa Tanganyika nchini Zanzibr hakumaanishi kukejeli asili yako hata na kwamba hata yeye anaweza pia kuwa Balozi wa Tanganyika iwapo atakuwa anasimamia maslahi ya Tanganyika katika nchi ya Zanzibar

“ I k i w a k a m a h u t a k i kuitwa Balozi wa Tanganyika nchini Zanzibar basi simama na Wazanzibar i wenzako katika kusimamia maslahi ya Wazanzibar i ndani ya Muungano”. Alisisitiza Jusa

Aidha Jussa alitahadharisha k u w a k a m a Tu m e h i y o haitoyaheshimu maoni hayo na kuamua kuyachakachua maoni ya Wazanzibar walio wengi juu Zanzibar hapatokalika kwani watatumia njia za kidemokrasia kufanya maamuzi magumu.

Kwa upande wa Washiriki wengine walisisitiza haja ya kuendelea kushikama na kutoa elimu juu ya Muungano wa Mkataba kwa watu ambao bado hawajelewa maana na faida za Muungano huo

Aidha Walidai kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuondoshwa katika Wadhifa wake Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye alilalamikiwa katika Kongamano hilo kutokana na kauli zake za kushurutisha watu katika kutoa maoni.

Kongamano hilo ambalo limevuta hisia za watu na kuonesha mshikamano wa kudai Mamlaka huru ya Zanzibar lilihudhuriwa na Wawakilishi wa Mabalozi nchini, Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar, Umoja wa Kiislamu, Uchumi na Maendeleo UKUEM na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo WAHAMAZA.

Page 5: ANNUUR 1038

5 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Habari za Kimataifa

LONDONU t a f i t i w a k i e l i m u umeonyesha kwamba raia 5200 wa Uingereza walisilimu mwaka uliopita wa 2011.

Kwa mujibu wa tovuti ya aps, utafiti huo uliofanywa n a C h u o K i k u u c h a Swansea nchini Uingereza, unaonyesha kwamba mwaka 2011 karibu Waingereza 5200 walisilimu ambapo asilimia 75 ya Waislamu hao wapya ni wanawake.

U c h u n g u z i h u o p i a unathibitisha kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita karibu Waingereza laki moja wameukubali Uislamu na kusilimu ambapo robo tatu ya hao ni wanawake.

Utafiti huo pia umeashiria m a t a t i z o m b a l i m b a l i yanayowakabili Waislamu wa Uingereza na kusema kuwa, chanzo cha matatizo hayo kinatokana na familia zao ambazo huwa na mtazamo mbaya na usiozingatia ukweli kuhusiana na dini hii tukufu.

Tatizo jingine la Waislamu h a o w a p y a n i k u k o s a chombo kimoja maalumu kinachoweza kushughulikia matatizo yao na kuwaongoza kwenye njia nyoofu.

AMSTERDAMZIKIWA ni harakati za kuhamasisha utoaji mimba katika dola zinazokaliwa na Waislamu wengi, boti moja ya Waholanzi imepinga kusafiri kwenda Morocco, hatua ambayo bila shaka itazua tafrani katika nchi hiyo ya Kiarabu.

“Meli ipo njiani,” Rebecca Gomperts, mwasisi wa shirika lisilo la kiserikali la Women on Waves, wakati akizungumza na Agence F r a n c e - P r e s s e ( A F P ) Jumatatu hii.

“Bado hatuwezi kuweka wazi sehemu na muda wa kuwasili…tunataraji kuwa huko kwa wiki moja.”

Shirika hilo la Kiholanzi limesema kuwa wamealikwa kwenda Morocco na kundi la vijana ambao ndio wenyeji wao lililotambulishwa kama

Meli ya watoa mimba kutua MoroccoNi mkakati kuharibu maadili ya Kiislamu

Alternative Movement for Individual Liberties (MALI), ili kusaidia katika kuunga mkono kuhalalishwa utoaji mimba nchini humo.

Likiwa limefanya safari katika nchi mbalimbali kwa zaidi ya miaka kumi na moja, ziara ya shirika hilo nchini Morocco ni ya kwanza kwa nchi za Kiislamu ambako utoaji mimba ni marufuku na ni kosa la jinai.

Likinukukuu takwimu za serikali, Shirika hilo la Kiholanzi limedai kuwa nchini Morocco zinatolewa mimba kati ya 600 na 800 kila siku.

“Tatizo ni kwamba ni mimba 200 zinazotolewa kwa usahihi, na hizo ni kwa wanawake wenye fedha,” alisema Gomperts.

Aliongeza kuwa kiwango cha watoa mimba walio salia

wanakuwa hatarini kwa kuwa wanatumia njia za hatari kwa sababu hawana uwezo wa kugharamia matibabu ya ghali.

Akadai Gomperts kuwa hili limesababisha vifo vya wanawake 78 wa Morocco kila mwaka kwa wastani huku akitoa mifano ya takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani -World Health Organization.

Hata hivyo, takwimu na madai kama hayo mara nyingi yamekuwa yakibuniwa kama propaganda ya kushawishi watu waone kuwa kuna tatizo.

Mfano wale walioleta sera za utoaji mimba Marekani katika karne ya 19 na 20, walikuwa wakitoa madai kama hayo lakini utafiti wa kweli baadae ukabaini kuwa zilikuwa takwimu za urongo zinazobuniwa na watu wanaotaka kuchafua maadili ya watu.

Meli hiyo ya watoa mimba tayari imezuru katika nchi za Ireland, Poland, Ureno na Hispania, ambako nako huko kulizuka maandamano kutoka

makundi ya kutetea uhai pro-life groups.

Pamoja na hayo, kwa upande wake Gomperts ambaye ni daktari, amedai kuwa ziara ya meli hiyo haina mahusiano kwa yoyote na imani za kidini.

“Lakini hili ni kwa ajili ya afya ya wanawake. Haihusiani kwa chochote na dini.” Alinukuliwa akitetea ziara yake.

Uislamu hauruhusu na ni haram kutoa mimba, isipokuwa tu iwapo itathibitika kitabibu na kiafya kwamba mimba hiyo itaangamiza maisha ya mzazi.

Jumatatu, gazeti la kila siku la Al-Tajdid, ambalo ndio chombo kinachoaminiwa na chama tawala cha Morocco cha Islamist Party, kilihoji iwapo serikali itaruhusu meli hiyo kuingia katika maji ya Morocco.

Hata hivyo alidai kuwa jaribio lolote la kuwazuia kuzuru Morocco litakuwa kinyume na kuvunja sheria ya uhuru wa kusafiri na uhuru wa kujieleza.

SAO PAOLO.Wanawake Waislamu nchini Brazil wataruhusiwa kuvaa vazi la hijabu katika picha za vitambulisho vya kitaifa, pasipoti, leseni ya kuendesha gari n.k.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hatua hiyo imechukuliwa kitaifa baada ya kupitishwa kwanza katika jimbo la mpakani Foz do Iguaçu, magharibi mwa nchi hiyo.

M o h s i n A l h a s s a n i , Mkurugenzi wa Msikiti wa Omar ibn al Kattab huko Foz do Iguaçu amesema hijabu si nadharia bali ni sehemu ya mavazi ya wajibu ya wanawake Waislamu.

Hijabu iligeuka suala la kitaifa hivi karibuni Brazil baada ya mkazi mmoja Muislamu Ahlam Abdul El-Saifi, kukataa kutoa vazi hilo la stara wakati akipigwa picha ya leseni ya kuendesha gari

Brazil yaruhusu hijabu katika vitambulisho

katika mji wa Sao Bernardo do Campo, uliopo katika jimbo la Sao Paulo.

Tukio sawa na hilo pia liliripotiwa katika mji wa Foz do Iguaçu.

Baraza la mji huo lilisikiliza malalamiko ya Waislamu na kutuma mapendekezo kwa serikali ya kitaifa likitaka wanawake Waislamu waruhusiwe kuvaa hijabu wakati wakipigwa picha za vitambulisho rasmi.

Uamuzi wa kuidhinisha hijabu katika vitambulisho unatazamiwa kuidhinishwa rasmi katika kipindi cha mwezi moja ujao.

Inakadiriwa kuwa Waislamu katika mji wa Foz do Iguaçu ni karibu elfu 20 kati ya wakazi laki mbili na nusu.

Idadi ya Waislamu Brazil inakadiriwa kuwa milioni moja na nusu.

Matukio 400 ya mauaji yajiri Chicago Duru za habari zimeripoti kuwa matukio ya mauaji yaliyofanywa katika mji wa Chicago nchini Marekani tangu ulipoanza mwaka huu, hadi sasa yamefikia 400.

Idadi ya matukio hayo ya mauaji katika mji huo yamefikia 400 baada ya tukio la siku ya Jumapili la mauaji ya Jose Escobar, kijana mwenye umri wa miaka 25.

Idadi hiyo imeelezewa kuwa ni ongezeko la asilimia 25 ikilinganishwa na mwaka uliopita katika kipindi kama

hicho. Miaka 20 iliyopita, yaani

mwaka 1992 ulitajwa kuwa ndio mwaka wa vitendo vingi zaidi vya utumiaji nguvu katika mji wa Chicago ambapo watu 943 waliuawa.

Licha ya kuongezeka mauaji na vitendo vya utumiaji nguvu nchini Marekani, msemaji wa Ikulu ya White House Jay Carney, amesema Rais wa nchi hiyo Barack Obama anaheshimu haki ya kisheria ya raia kutumia silaha kama ilivyoelezwa na katiba.

Waingereza 5000 walisilimu 2011

BAADHI ya Maimamu wakiwa katika semina mkoani Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. Semina hiyo iliandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Markaz Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.

Page 6: ANNUUR 1038

6 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Makala

“LABBAIKA Allahumma Labbaik”. Mola wangu mlezi! Nimeitikia wito wako. Hizo ni sauti murua zinazotolewa na Mahujaji, ambazo hivi sasa zinachukua nafasi katika anga la mji mtakat i fu wa Makka. Mahujaji wanaonyesha unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kwa kumudu kuitikia kwa vitendo agizo la nguzo ya tano ya Hija kutoka kwa Allah (sw).

H i j a n i i b a d a inayokusanya mambo mengi yanayomkurubisha mja kwa Mola wake Karima. Ni shule ya kutoa malezi na maarifa kwa waja kwa msingi wa tawhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Safari ya Hija huanza kwa kuwekwa nia safi na ikhlasi na kukamilika kwa ibada na amali makhsusi.

H i v i s a s a Wa i s l a m u wanasafiri kuelekea katika ardhi tukufu ya Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada tukufu ya Hija. Ni safari ya muda kidogo lakini yenye matunda na manufaa makubwa kwa Mahujaji na Waislamu kwa ujumla.

Ni safari ambayo wenye uwezo wa kifedha na afya njema, wametenga muda wao ili kuitekeleza Hija baada ya kupata tawfiqi ya Mwenyezi Mungu. Mahujaji wakiwa

Timizeni Hija kwa utimilifu wake

Na Shaaban Rajab Makka, wanakuwa na fursa ya kujionea athari muhimu za Uislamu. Hufaidika kihistoria na kimantiki na athari za Uislamu katika mji wa Makka na Madina.

Safari hii ya kiroho huleta mabadiliko makubwa kwa Mahujaji pindi wanaporejea makwao baada ya kutekeleza ibada ya Hija. Al-Kaaba ni nyumba ya Mwenyezi Mungu i l iyobar ik iwa na yenye uongofu. Mwenyezi Mungu anasema katika Surat al-Imran aya ya 96: “Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ajili ya ibada ni ile iliyoko Makka, iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote.”

Tunafahamishwa kwamba al-Kaaba ilijengwa katika zama za Nabii Adam (AS). Kitabu cha Taarikh al-Yaaqubi kinaeleza kuwa baada ya Nabii Adam, kumaliza kujenga al-Kaaba alifanya tawafu. Kwa kipindi chote cha historia, Kaaba ikawa ni mahala pa kufanya ibada kwa Manabii wengi wa Mwenyezi Mungu.

Nabii Ibrahim aliamrishwa n a M w e n y e z i M u n g u kuikarabati al-Kaaba. Allah (sw) anasema katika Surat al-Haj aya za 26 na 27 kwamba, “Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu na

wanaokaa hapo kwa ibada, na wanaorukuu, na wanaosujudu. Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.”

Awali al-Kaaba haikuwa kibla cha Waislamu. Mtume (SAW) na wafuasi wake walikuwa wakiswali ibada zao wakielekea Baytul Muqaddas.

Watu wa Makka walikuwa wameigeuza Kaaba kuwa nyumba ya waabudu sanamu.

Al-Kaaba ina nafasi muhimu sana katika ibada za Waislamu. Waislamu kwa siku huelekea upande wa al-Kaaba mara tano wakati wa kusali. Hii ina maana kwamba, kwa siku moja mamilioni kwa mamilioni ya Waislmu usiku na mchana, huswali na kufanya ibada nyingine kwa kuelekea upande wa al-Kaaba.

Hil i ni jambo ambalo h u z i f a n y a n y o y o z a Wais lamu kuwa pamoja n a k u z i f u n g a m a n i s h a zaidi . Mwenyezi Mungu amewataka Waislamu popote watakapokuwa kuelekea upande wa Makka wakati wa kufanya ibada zao hususan swala, kwani al-Kaaba daima ni mhimili na kitovu cha kukusanyika Waislamu wote.

Mahujaji wanapokiwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, hufanya tawafu katika mahali ambapo malaika wanatufu na Mitume wa Mwenyezi Mungu

na maswahaba wake walikuwa kando ya eneo hilo kumhimidi Mwenyezi Mungu.

Mtume (SAW) anasema: M w e n y e z i M u n g u anaj ifakharisha na watu wanaofanya tawafu, na laiti inge l ikuwa imeamul iwa kwamba malaika wapeane m i k o n o n a m t u , b a s i wangepeana mikono na wenye kufanya tawafu katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Kaaba ni mahali pa amani na usalama kwa wanadamu wote. Mwenyezi Mungu anasema katika Suratul Baqara aya ya 125 kwamba, “Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Al-kaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani.” Hivyo basi, kila mtu atakayekuwa kando ya Kaaba, anakuwa yuko katika amani kimwili na kiroho na huwa na utulivu.

Usalama na amani ya nyumba hii ya Mwenyezi Mungu unatokana na dua aliyoiomba Nabii Ibrahimn (AS) kama inavyosema aya ya 126 ya Suratul Baqarah:

“Na aliposema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.”

Mwenyezi Mungu aliijibu dua ya Ibrahim (AS). Ni

kutokana na sababu hiyo ndio maana kwa karne nyingi, al-Kaaba imesalimika na shari za wanaoitakia mabaya.

Safari kuelekea katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na kutekeleza amali za Hija, ni miongoni mwa njia za kumbadilisha mwanadamu katika hali ya kutojali ibada na kumpeleka katika njia ya kupupia ibada. Hija ni semina inayomfanya Muislamu ajitambue na kujifahamu.

Akiwa katika Hija, Hujaji hupata wasaa wa kushuhudia kujitathmini na kufanya yaliyo mema na wakati huo kujipanga kuendeleza matendo ya amali njema.

Kimantiki Hija ni funzo bora kabisa kwa mwanadamu na huongeza imani yake. Ibada ya Hija ni fursa muhimu ya Hujaji kujitakasa. Humfanya Hujaji ahisi kuwa ana deni kwa Mwenyezi Mungu, hivyo kuongeza juhudi za kumuabudu na kuhakikisha hafanyi makosa ya kijinga na kibri kama alivyokuwa kabla ya Hija.

K i p i n d i h i k i H u j a j i h u o n g e z a j u h u d u z a kumuabudu Allah, na kwa mtindo huo, hujengeka jamii ya waumini wa Kiislamu. Wakiwa Makka, Mahujaji husahau hadhi na daraja zao za fahari za kidunia, yaani tofauti za hali na mali kama vile utajiri, elimu, vyeo, rangi, utaifa, kazi n.k. Wote huwa kitu kimoja na umoja huo hudhihirika katika kila hatua ya kutekeleza ibada.

Hija hakuna mwenye hadhi zaidi ya mwingine. Huko Hujaji huweka kando nguo na mapambo mengine yote na kuvaa Ihram, vazi ambalo huvaliwa na mahuji wote. Hatua hii ya ibada inathibitisha dhahiri kwamba katika Uislamu hakuna mbora kuliko mwenzake ila yule tu anayemwabudu Allah (sw). Hili limekuwa likiwashangaza wengi katika binadamu. Kwamba Makka hakuna ‘nyota’ wala mtu wa daraja la chini. Wote huwa katika hali moja hadi Hija inapokwisha.

M w e n y e z i M u n g u awajaalie mahujaji wetu watekeleze kwa amani na salama hatua zote za ibada ya Hija. Apokee ibada zao na watakaporejea, wawe wamefaidika vya kutosha na yale yalipatikana katika Hija.

Aidha Mwenyezi Mungu awajaalie nia, uwezo na afya wale wanaokusudia kwenda Hija safari ijayo.

Page 7: ANNUUR 1038

7 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Makala/Habari

OKTOBA 14 ya kila mwaka, taifa huadhimisha kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa nchi hii, baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wiki nzima kabla ya siku hiyo, tumeshuhudia kupitia vyombo vya habari, hotuba mbalimbali za hayati baba wa taifa, makongamano na midahalo ya kumtukuza.

Vyombo vya habari hapa nchini vimekuwa vikijaribu kuchora picha isiyo halisi ya Mwalimu Nyerere, kama vile alikuwa ni mtu mtukufu sana, asiye na makosa wala dosari. Na watu wasiomfahamu vizuri Nyerere wamekuwa mateka wa kampeni hii bila wenyewe kujua. Makala hii inajaribu, japo kwa uchache, kumuanika Nyerere kama alivyo, hususan katika nukta ya udini na vita vyake dhidi ya Waislamu.

Kwa Watanzania wengi wasio na taarifa sahihi , Mwalimu Nyerere alikuwa ni mlinzi imara wa Usekula ndani ya chama tawala na Serikali. Lakini mikutano yake ya siri na viongozi wa Kanisa, inathibitisha wazi kwamba Mwalimu alikuwa tofauti kabisa na vile alivyodhaniwa n a w e n g i . D h u l m a wanayofanyiwa Waislamu nchini katika Elimu, kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kama ilivyobainika hivi juzi ni matokeo ya Mfumo-Kristo aliouasisi.

Wa i s l a m u w a n a j u a , Wakristo waadilifu wanajua, Maaskofu wanajua, Wasomi waadilifu wanajua na vyombo vya habari vinajua, kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa adui mkubwa wa Uislamu katika eneo zima la Afrika Mashariki, ingawa baadhi ya hao niliowataja, wanaficha ukweli huu kwa kutumia propaganda za ulaghai na kuhamisha ajenda.

Katika mazungumzo yake ya siri, August 2 mwaka 1970 na Rev.Robert Rweyemamu, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) wakati ule, Nyerere amenukuliwa katika Kitabu ‘Development and Religion in Tanzania’, kilichoandikwa na J.P Van Bergen akisema ameanzisha Idara ya Elimu ya Siasa katika TANU, na kwa makusudi amemteua Mkristo kuiongoza, si kwa sababu ni mwanasiasa mahiri, isipokuwa kwa sababu ya imani yake thabiti ya Kikatoliki.

Ki tabu h ik i ambacho kimechapishwa na Kanisa

Tuseme ukweli kuhusu NyerereNa Said Rajab

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

Katoliki, kimebainisha wazi kwamba hiyo ndiyo sababu Padri Mushendwa, Mkatoliki Mkereketwa, akafanywa kuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Siasa ya TANU. Kwa kifupi, Nyerere aliendeleza tu ule ubaguzi dhidi ya Waislamu kat ika e l imu ul ioachwa na Waingereza. Alikuwa anafahamu hasira za Waislamu katika eneo la elimu. Aliandika katika kitabu chake ‘Freedom and Unity’ kwamba upogo (disparity) katika elimu, unaweza kutumiwa kama jambo la kisiasa:

“ U a d u i u n a o w e z a kuchochewa na fikra mbaya kati ya Waislamu na Wakristo kama wote tunavyofahamu, S e r i k a l i y a K i k o l o n i haikujihusisha zaidi na Elimu, kwa hiyo wengi waliobahatika kupata elimu walipata katika Shule za Kanisa, wengi wao ni Wakristo. Kwa hiyo hapa tuna mgawanyiko ambao kuwepo kwake unaleta tishio la kisiasa kwa umoja” `(P.179)

Waislamu wa Tanganyika ambao waliongoza harakati za mapambano ya kudai Uhuru kutokana na ukandamizaji wa Wakoloni, bado hawajavuna matunda ya kazi yao tangu Uhuru upatikane mwaka 1961.

Waislamu wengi wa sasa wanajiuliza kuhusu hatima ya fumbo hili kubwa. Upogo wa Kielimu kati ya Waislamu na Wakristo hapa nchini unaendelea kama kawaida.

Waislamu wamebaguliwa na kuhujumiwa kielimu ndani ya nchi yao wenyewe, kabla na baada ya Uhuru. Uzoefu waliopata kutokana na hujuma walizofanyiwa na Nyerere, umewafunza kwamba ni makosa kumtarajia Mkristo, hata akionekana muadilifu kiasi gani mbele ya umma, kulinda maslahi ya Waislamu. Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya kitabu chake:

“ E n y i M l i o a m i n i ! Msiwafanye wasiri wenu watu wasiokuwa katika ninyi, hao hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yale yanayokudhuruni. Bughudha (yao juu yenu) inadhihirika kat ika midomo yao. Na yanayof i chwa na v i fua vyao ni makubwa zaidi . Tumekubainishieni dalili (zote) ikiwa ninyi ni watu wa kufahamu” Qur(3:118).

N y e r e r e a l i h a k i k i s h a kwamba pengo la kielimu kati ya Wakristo na Waislamu, Tanzania Bara na Visiwani,

kamwe halipungui na badala yake linaongezeka zaidi, ingawa katika kitabu chake, au majukwaa ya siasa alijifanya kulipunguza.

Utafiti uliofanywa na G.A Malekela, Profesa Mkristo katika Kitivo cha Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, umefichua kwamba katika Sekondari za Serikali Tanzania Bara mwaka 1983, Wakristo walikuwa asilimia 78 na wasio Wakristo asilimia 22. Bila ubishi Wakristo wamezidi mno, licha ya ukweli kwamba Waislamu wanakadir iwa kuwa zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania wote.

Uta f i t i mwingine p ia uliofanywa na ‘Udhamini wa Waislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ‘(DUMT) na kuchapishwa na Jarida la ‘Al - Haqq International’ umeonyesha kwamba idadi ya wanafunzi Waislamu imekuwa ikipungua katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vya umma hapa nchini.

Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam peke yake, utafiti umeripoti kwamba idadi ya wanafunzi waliodahiliwa katika kipindi cha mwaka 1986-1990 ilikuwa 4,191. Katika idadi hii, wanafunzi Waislamu walikuwa 586 tu au asilimia 13, wakati Wakristo walikuwa 3,609 au asilimia 87.

Kwa hiyo kutokana na ushahidi kama huu wa kiutafiti, si bahati mbaya katika kipindi chake chote cha miaka 24 bila kuingiliwa, kama Rais wa Tanzania (1961 -1995), Nyerere akiwa Mkatoliki, m a r a z o t e a m e m t e u a Mkristo kuongoza Wizara ya Elimu. Mara zote Waislamu wamekuwa wakilalamika kwamba upendeleo huu wa Wakristo katika shule za sekondari na Elimu ya Juu, umewafanya wadhibiti nafasi zote muhimu katika utawala na taasisi za umma.

H a l i h i i i m e w a f a n y a Waislamu nchini wabaki na fursa chache mno na wafanye kazi za kawaida kabisa zisizohitaji elimu au taaluma yoyote kama udereva na uhudumu wa ofisi. Waislamu wanadai mgao wa haki katika keki ya taifa. Tangu tupate uhuru, idadi ya wanafunzi Waislamu katika vyuo vikuu vya umma inazidi kushuka. Hali hii si matokeo ya makosa ya kibinadamu, bali ni mkakati maalumu wa mawakala wa kanisa Serikalini.

Marehemu Prof. Kighoma M a l i m a , M u i s l a m u w a kwanza kuongoza Wizara ya

Elimu na Utamaduni mwaka 1987, al igundua dhulma hii kubwa wanayofanyiwa wanafunzi Waislamu. Prof. Malima alichukua hatua ya kubadili utaratibu huo mbovu na kuanzisha utaratibu wa kuchagua wanafunzi kwa kutumia namba badala ya majina, ili wanafunzi wote wawe na haki sawa. Utaratibu huu mpya ulipotekelezwa kwa mwaka mmoja, idadi ya wanafunzi Wais lamu waliofaulu na kujiunga na sekondari za umma iliongezeka kwa asilimia 40.

Lakini kama kawaida yao, mawakala wa Kanisa ndani ya Serikali wakaanza kumuandama Prof. Kighoma Malima na kumchafua kwa propaganda zenye sumu. Mfumo-Kristo ukahakikisha Prof. Malima anaoondoka Wizara ya Elimu na Utamaduni, na ule utaratibu wa kuchagua wanafunzi kwa kutumia namba ukaondolewa pia.

Kadinali Pengo alitangaza kupitia vyombo vya habari kwamba “Malima ni mtu Hatari” na vyombo vya habari vikaendesha kampeni maalumu ya kumuandama Prof. Malima kila alipokwenda, na hata baada ya kujiondoa Serikalini na CCM. Hatimaye Malima akafa ghafla jijini London Uingereza katika mazingira ya utatanishi. Kosa lake kubwa Prof. Malima lilikuwa ni kuhoji Mfumo-Kristo unaohujumu Waislamu, ambao umeasisiwa na Nyerere.

Kama i l ivyo Tanzania Bara, Waislamu wa Zanzibar pia wamebaguliwa kielimu na nafasi zao za kusoma nje zimehujumiwa kwa sababu ya Muungano wa kulazimisha kati ya Tanganyika na Zanzibar u l iobuniwa na Nyerere . Mohammed Mwinyi Mzale, aliyepata kuwa Waziri wa El imu Zanzibar a l iwahi kutamka kwamba wajumbe 12 wa Kamati ya pamoja ya kuchagua wanafunzi kwa ajili ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya juu ndani na nje ya Tanzania ‘Joint Selection Commi t t ee ’ ( JOSECO) , hakuna hata mmoja aliyetoka Zanzibar. Alibainisha wazi kwamba Wanafunzi waliopata ‘Scholarships’ za Zanzibar, wanapokwenda kwenye balozi za Tanzania nchi za ng’ambo walikuwa wakifukuzwa kwa kisingizio kwamba hawamo kwenye ‘Scholarships’ za Jamhuri ya Muungano, licha ya ukweli kwamba Zanzibar ilikuwa ikichangia kiasi chake kwenye bajeti ya Elimu ya Juu ya Muungano.

Inaendelea Uk. 14

Page 8: ANNUUR 1038

8 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Makala

SASA kuna kila aina ya sababu iliyo wazi kusema kwamba maridhiano ya Wazanzibari yalikuwa ni ya Maalim Seif Sharif Hamad na CUF yake kwa upande mmoja. Kwa upande wa pili wa CCM, maridhiano hayo yalikuwa na bado yamebaki kuwa ni ya watu wachache nao ni waasisi wa maridhiano hayo Mzee Hassan Nassoro Moyo, Rais mstaafu Mhe. Amani Abeid Karume, Waziri Mansoor Yussuf Himid, pamoja na wafuasi wao wachache walioweza kuwafahamu na kuikubali kwa dhati agenda hii ya maridhiano

Kundi kubwa lililoanzia serikalini halikuyapenda wala kuyakubali maridhiano hayo. Viongozi wengi wa serikali hawakuyataka maridhiano hayo tokea yanaasisiwa. Viongozi hao walilazimika tu kutii mawazo na maamuzi ya Rais Karume na si ridhaa na hiari yao. Agenda ya maridhiaano haikuwa ya CCM, viongozi wa CCM wala ya wana CCM. CCM walilazimika kuheshimu mawazo ya Rais Amani Karume kwa kuwa alikuwa na msimamo mkali juu ya kuifanikisha agenda hiyo ili kunusuru amani na utulivu wa nchi kabla ya kuondoka madarakani. Halikadhalika nafasi yake kubwa ya kisiasa na kiserikali aliyokua nayo kwa Zanzibar iliipelekea NEC kulazimika kuheshimu uwamuzi wake.

Pia kuna tetesi zilizotoka ndani ya vikao vya CCM kwamba agenda ya Amani K a r u m e i t a l a z i m i k a kuheshimiwa shingo upande na sio kukubaliwa ili kunusuru “kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar kwa mara nyengine”. Machafuko ya hali ya hewa Zanzibar yaliwahi kutokea katika miaka ya 1980 pale Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Aboud Jumbe alipojidhatiti kutaka kuleta mabadiliko makubwa ya mfumo wa Muungano kutoka serikali mbili kwenda serikali tatu. Jambo hilo lililoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar lilipelekea kufukuzwa kiongozi huyo katika madaraka ya urais na katika madaraka makubwa ya chama cha CCM aliyokuwa nayo. Kwa kuwa agenda ya maridhiano Zanzibar ilikubaliwa na kiongozi huyu mkuu wa seriakali ya Zanzibar ambae ni Rais na ni kiongozi mwenye madaraka makubwa ndani ya CCM (Makamo Mwenyekiti), haikuwa rahisi hata kidogo kwa NEC kuipiga ngwara agenda hiyo baada ya kufikiria na kujifunza kwa makini somo la kuchafuka kwa hali ya hewa la miaka

Jee maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa ni ndoa ya kulazimisha?

KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) na Rais Mstaafu wa Zanazibar, Amani Abeid Karume.

MZEE Hassan Moyo

ya 1980.CCM imekuwa ikipinga

wazi wazi na kwa vitendo maazimio yote ya miafaka iliyowahi kufanywa huko nyuma. CCM pia ilipinga maazimio ya muafaka wa mwisho ambao ulipendekeza pamoja na mambo mengine kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Hii ni hatua ya mapema, muhimu na ya wazi wazi iliyobainisha kuwa chama hicho kamwe hakikuwa tayari kuingia katika maridhiano na serikali ya Umoja wa kitaifa wala jambo hilo hal ikukubal ika kamwe. Viongozi kadhaa wa CCM walitamka bayana mara baada ya maridhiano hayo kwamba maridhiano hayakuwa halali kwani yalifanywa kwa siri na hayakuvishirikisha vikao vya CCM katika kufikiwa kwake. Mmoja wa viongozi wa CCM aliyetamka maneno kama hayo ni Nape Nnauye, ambae ni msemaji mkuu wa CCM wakati vyombo vya habari vilipotaka kauli ya CCM kuhusu maridhiano ya Rais Amani Karume na Maalim Seif.

Mawaziri, Wawakilishi, Wabunge wengi kutoka CCM na viongozi wa CCM wal ionyesha ku ikuba l i agenda hiyo mbele ya uso wa Rais Amani Karume na kufanya unafiki wa hali ya juu katika kuipotosha na kuipinga agenda hiyo. Viongozi hao wa kisiasa wanaokubalika katika maeneo yao walitumia nafasi zao kwa siri kufanya kampeni chafu ya kinafiki ya kupinga kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa. Kiongozi mkuu wa serikali aliyedhihirisha mapema kuwa yeye hakuyakubali maridhiano hayo ni Waziri Ali Juma Shamhuna, Mwakilishi wa Jimbo la Donge. Pamoja na maridhiano na kukubaliana kusameheana yaliyopita, waziri huyo alitayarisha jeshi la polisi na vikosi vya SMZ kuhakikisha chama cha CUF hakifanyi kampeni zake katika jimbo lake kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.

Wakuu wa wilaya na masheha nao walifanya kila wawezalo kuhakikisha agenda ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa haifanikiwi katika kura ya maoni. Mkuu wa Wilaya ya Kati kwa wakati huo aliitisha kikao kisicho rasmi na masheha wa wilaya yake na kuwapa maagizo masheha hao wawahamasishe watu wao wapige kura ya HAPANA jambo ambalo lilimlazimisha Rais Karume kumpokonya cheo Mkuu huyo wa Wilaya. Vita hivyo vya kuipinga serikali ya

Inaendelea Uk. 10

Page 9: ANNUUR 1038

9 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Makala

Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike:

Changamoto kwa Wananchi kukuza fursa nchini Tanzania

Kwa niaba ya watu wa Marekani, nina fahari kubwa kuadhimisha siku ya kwanza kabisa ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike pamoja na Watanzania.

Siku hii ilianzishwa ili kutambua haki za watoto wa kike na kuimarisha jitihada za kimataifa za kutokomeza unyanyasaji, ubaguzi na ukatili wa kijinsia na tofauti ya fursa za kiuchumi zinaowaathiri zaidi watoto wa kike.

Siku hii inatupa sote - wasichana, wavulana, wanaume na wanawake fursa adhimu ya kutafakari ni kwa namna gani tunaweza kushirikiana ili kuhakikisha kuwa vijana wetu wote wanapata fursa sawa ya kuchangia katika jamii na kujijengea wao wenyewe, familia zao na taifa lao maisha bora ya siku zijazo.

Kama ambavyo nimekuwa nikieleza kwa hadhira mbalimbali pande zote za Tanzania nilizopata heshima ya kuzitembelea katika kipindi cha miaka mitatu nikiwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania, mojawapo ya mambo yanayopewa kipaumbele na Marekani ni kuinua maendeleo na ustawi kwa wanawake na wasichana wa Tanzania.

Na Alfonso E. Lenhardt Ukweli ni kuwa usawa wa kijinsia na uwekezaji wa wanawake na wasichana ni msingi muhimu wa sera ya mambo ya nje ya Marekani ya kuinua ustawi, amani na usalama.

Ushahidi unaonyesha kuwa nchi zinaweza tu kufikia kiwango cha juu kabisa cha uwezo wao wa kujiletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa pale ambapo wanawake na watoto wa kike wanashiriki kikamilifu na kwa usawa katika nyanja zote za jamii, katika elimu na huduma za afya na pale ambapo wanawake na watoto wa kike wanalindwa dhidi ya ubaguzi na vitendo vingine vyote vya kikatili, mathalan, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia.

Ni kwa sababu hii Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bibi Clinton na utawala mzima wa Rais Obama wamebainisha wazi kuwa kuinua hali za wanawake na watoto wa kike ni kipaumbele muhimu cha kidiplomasia cha Marekani.

Katika jamii nyingi duniani, ikiwemo Marekani, watoto wa kike hawana fursa sawa ya kuweza kufikia upeo wa uwezo wao.

Theluthi mbili ya watu wote duniani wasiojua kusoma na kuandika ni wanawake. Watoto wa kike wapatao milioni 38 duniani kote hawaendi shule.

Watoto wengi wa kike na wanawake wanapata huduma duni sana za afya na huku wakikabiliwa na lishe duni.

Katika maeneo mengine, wasichana huwa wa mwisho kupewa chakula na hunyimwa huduma za afya kwa sababu tu wao ni wasichana.

Inakadiriwa kuwa wasichana wapatao milioni 10 walio chini ya miaka 18 huolewa na takriban wasichana milioni 16 wenye umri wa kati ya miaka 15 na 19 hujifungua kila mwaka jambo ambalo husababisha vifo vinavyotokana na uzazi, kukatishwa masomo na kupungua kwa kiwango kikubwa kwa fursa za kiuchumi.

Hakuna tamaduni au mila inayoweza kuhalalisha hali hii ya kusikitisha inayokwamisha na kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.

Kuwekewa kwa watoto wa kike kuna manufaa makubwa kwa familia nzima, jamii na taifa kwa ujumla.

Takwimu zinaonyesha kuwa nchi zinazowaelimisha watoto wa kike kwa usawa huwa na ustawi na maendeleo makubwa zaidi.

Kwa kuwapa watoto wa kike mwaka mmoja wa ziada wa masomo baada ya muda wa wastani katika elimu ya msingi utawaongezea kati ya asilimia 15 na 20 ya kipato chao.

Mwaka mmoja wa ziada katika elimu ya sekondari utaweza kumuongezea mtoto wa kike kipato chake kwa kati ya asilimia 15 na 25.

Aidha, watoto wa kike walio shuleni hukawia zaidi kuolewa na kupata watoto, huwa na kiwango kidogo zaidi cha maambukizi ya VVU/UKIMWI na maradhi mengine ya zinaa na huchukuliwa kwa usawa zaidi wawapo nyumbani na katika jamii. Hali kadhalika, kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa wasichana waliopata elimu hapo baadaye kuwa na watoto wenye afya njema na ambao pia watapata elimu nzuri.

Wale ambao wanashughulika na suala la maendeleo ni lazima wazingatie ukweli kuwa pale watoto wa kike wanapostawi ndipo taifa hustawi.

Wataa lamu kadhaa wa uchumi duniani wamebaini kuwa nchi zenye ushindani na ustawi mkubwa ni zile ambazo zimepunguza kwa kiwango kikubwa tofauti za kijinsia katika upatikanaji wa fursa za elimu, afya, ushiriki katika uchumi na ushiriki katika siasa.

Kwa kupit ia Shirika la Marekani la Ushirikiano wa Kimataifa (USAID) na taasisi nyingine , watu wa Marekani wamekuwa wakijihusisha na jitihada za kuhakikisha kuwa watoto wa kike katika nchi zinazoendelea wanapata fursa ya kuendeleza maisha yao kwa kadri ya upeo wa uwezo wao na kuchangia katika maendeleo yao. Kati ya mwaka 2009 na 2011 Marekani iliwasaidia wasichana milioni 84 duniani kote kwenda shule.

Tunasaidia kujenga uwezo w a w a n a f u n z i k u s o m a , t u n a w a f u n d i s h a w a l i m u kuzingatia masuala ya jinsia wawapo darasani, tunasaidia kuandaliwa kwa vitabu vya ziada na kiada vinavyozingatia na kuonyesha usawa wa kijinsia na kutoa mafunzo yatakayowapa wanafunzi ujuzi kwa ajili ya kazi za karne ya 21.

Kutoka Malawi hadi Yemen na Tajikistan programu yetu ya Shule Salama inashirikiana na walimu, watawala wa shule, wananfunzi na wazazi i l i kuyafanya mazingira ya shule yawe salama kwa watoto wa kike na yasiyo na ukatili wa kijinsia wa aina yoyote. Tunafanya kazi na vikundi na mashirika ya kijamii ili kuzishawishi familia kutowalazimisha binti zao kuolewa katika umri mdogo. Aidha tunaunga mkono jitihada mbalimbali duniani za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

Ninafahari kueleza kuwa kwa hapa Tanzania, sehemu ya msaada wetu wa Dola za Kimarekani 750 (sawa na Shilingi za Kitanzania trilioni 1) kwa mwaka huelekezwa katika kuongeza fursa za kiuchumi za wanawake wa Kitanzania kwa kukuza sekta ya kilimo na ujasiriamali.

Programu ya kuendeleza kilimo na usalama wa chakula ya Feed the Future, iliyozinduliwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani Bibi Clinton

alipokuwa katika ziara yake nchini Tanzania hapo mwezi Juni 2011 ni mfano wa dhamira yetu ya dhati katika kutekeleza azma hii.

H a l i k a d h a l i k a k w a kupitia programu mbalimbali zinazoendeshwa na USAID na Kituo cha Udhibiti wa Maradhi (CDC) kwa ushirikiano na Watanzania tunaimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wanawake ikiwa ni pamoja na huduma za uzazi na kupunguza vifo vya watoto, kudhibiti malaria na VVU/UKIMWI kwa kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na VVU/UKIMWI (PEPFAR).

Hata hivyo jitihada zaidi zinahitajika, hususan katika ngazi ngazi ya jamii. Mara kwa mara nimekuwa nikisisitiza kuwa programu mbalimbali zitakuwa na maana na manufaa za id i pa le z inapobuniwa na Watanzania kwa ajili ya Watanzania wenyewe.

Hii inaoana na ushauri wa Rais Obama kwa Waafrika kutafuta majibu ya matatizo yao na kuongoza jitihada za kukabiliana na changamoto zinazolikabili bara la Afrika.

Kwa msingi huo, ninatoa wito kwa kila Mtanzania, hususan wanaume, kushiriki kikamilifu katika jitihada za kuinua haki za wanawake na watoto wa kike katika jamii zao.

Kila mwanajamii akishiriki katika jitihada hizi, basi tutaweza kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kike wa Kitanzania anapata fursa ya kutumia uwezo na vipawa vyake kwa kadri ya upeo ambao Mungu amemjaalia.

S iku ya K ima ta i f a ya Mtoto wa Kike inatupa fursa ya kutafakari na kujadil i masuala haya muhimu na jinsi tunavyoweza kushirikiana ili kukabiliana na vikwazo vinavyoweza kuwakwamisha vijana na watoto wetu wa kike na wa kiume kufikia ndoto zao na maendeleo kwa kadri ya uwezo wao.

N i k i w a b a b a m w e n y e fahari wa wanawake watatu waliofanikiwa - Wanasheria wawili na daktari mmoja, n ingependa kuona ki la mtoto wa kike wa Kitanzania anapata fursa sawa na zile walizopata binti zangu hao.

Wao ndio wanaobeba maisha yetu ya baadaye hivyo yatupasa sisi sote tuyajenge matarajio yao na kuwawezesha kuwa na ndoto kubwa na kisha kuwawezesha kwa jitihada zao kufikia ndoto hizo kwa mafanikio.

Sote tuj i toe kwa moyo kutimiza ahadi hii tunayowapa. Hili ni mojawapo ya mambo m e m a s a n a t u n a y o w e z a kuyafanya katika zama zetu.

(Alfonso E. Lenhardt ni Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.)

Page 10: ANNUUR 1038

10 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Makala

Jee maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa ni ndoa ya kulazimisha?

MHE. Juma Shamhuna

Inatoka Uk. 8

umoja wa kitaifa ndani ya CCM ilipelekea takriban asilimia 90 ya wana CCM kuipigia kura ya HAPANA agenda hiyo katika kura ya maoni. Mambo pekee yaliyosaidia ushindi wa kura ya NDIO katika kura ile ya maoni kwa asilimia 66 ni haya yafuatayo:

(1) wingi wa wana CUF ambao wote waliikubali agenda hiyo, (2) wana CCM wachache sana waliomfahamu na kuamua kumtii kwa moyo wote rais Karume waliweza kuongeza j apo k idogo asilimia ya kura ya NDIO na (3) agizo la Rais Karume kwa tume ya uchaguzi kutothubutu kutumiwa na mtu yeyote kufanya hila na kuyachakachua matokeo ya kura hiyo ya maoni.

Pamoja na seriakali ya umoja wa kitaifa kuundwa kwa mafanikio makubwa na kuanza kufanya kazi zake vizuri, haikuwemo katika miyo ya viongozi wengi wa CCM na wafuasi wao wengi kama ambavyo haikuwa wakati wa kuasisiwa kwake. Bila shaka viongozi hawa wanafanya kazi kubwa mpaka sasa katika maeneo yao kuendelea kuwatia chuki wafuasi wao wasiipende serikali hiyo ya umoja wa kitaifa na waione ndio adui na kikwazo kwa chama chao. Dalili za wazi wazi za haya ni

tabia ya kudumu ya maskani maarufu na muhimu za CCM hapa Zanzibar (KISONGE, KACHORORA na maskani ya Wazee J ang ’ombe) kuchapisha mabango ya matusi dhidi ya chama cha CUF, viongozi wa CUF na watu wenye asili ya kisiwa cha Pemba huku viongozi wa chama chao na serikali inayoongozwa na chama chao ikitazama kama haioni bila ya kuchukua hatua yeyote dhidi ya vitendo hivyo.

Mikutano kadhaa ya hadhara imewahi kufanywa na viongozi na makada maarufu wa CCM ambayo inaashiria wazi CCM haiyaheshimu maridhiano wala serikali ya umoja wa kitaifa. Viongozi na makada hao wamekua wakipanda katika majukwaa na kutamka matusi ya wazi dhidi ya chama cha CUF na viongozi wa seriakali ya umoja wa kitaifa kutoka CUF akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Katiba na Sheria Abuu Bakar Khamis Bakari, wote wawili wakituhumiwa et i ndio wanaowalinda UAMSHO.

Makada hao wamekuwa wakitangaza wazi kuwa majanjawiri wao bado wapo na silaha zao zikiwemo nondo bado zipo na hwenda zikatumika wakati wowote

kama zilivyokuwa zikitumika kabla ya kuja kwa maridhiano na serikali ya umoja wa k i t a i f a . H a l k a d h a l i k a h a k u n a y o t e h a y o yakitendwa hakuna mhusika aliyeonywa, aliyekemewa au aliyechukuliwa hatua kwa kumtukana kiongozi wa juu serikali, kuhatarisha amani ya nchi au kufanya uchochezi.

Katika muundo wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa Zanzibar, CCM ilihakikisha nafasi nyeti za utendaji wa shughuli kuu muhimu na ndogo ndogo za serikali sio tu zote zishikwe na CCM lakini pia wapewe viongozi wa CCM ambao hawakuyakubali maridhiano. Kufanya hivyo kutasaidia kwa kiwango kikubwa na hivyo kulinda maslahi ya chama chao dhidi ya nguvu yoyote ya kisiasa ambayo itajaribu kuhamisha nguvu za CCM na kuzipeleka katika serikali ya Umoja wa kitaifa. Viongozi hao wahakikishe pamoja na uwepo wa CUF katika serikali, serikali hiyo inabaki kama vile ni ya chama kimoja tu cha CCM kwa kulinda misimamo na maslahi yote ya CCM ikiwemo ile inayopingana na uwepo wa serikali yenyewe ya umoja wa kitaifa. Viongozi hao ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Mwinyihaji Makame na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Mwinyiha j i Makame ameshawahi kufanya vitimbi vingi tokea kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa akionyesha yupo katika nafasi hiyo kulinda maslahi ya chama chake na kuendeleza yale ya zamani ya uonevu na unyanyasaji hasa kwa wafuasi wa CUF. Mfano mzuri ni maamuzi yake ya kuyahamisha makontena ya Darajani yaliyopo hapo k i sher ia na kupingana uwamuzi wa mahakama na kukusudia kuanzisha ujenzi wa bustani katika eneo hilo. Kilichomo katika mawazo ya Mwinyihaji ni chuki dhidi ya wafanya biashara wale ambao takriban wengi na wafuasi wa CUF na watu wenye asili

ya kisiwa cha Pemba. Lakini pia Mwinyihaji ana ajenda ya kuwatia chuki na hasira wafanyabiashara wale dhidi ya chama chao cha CUF ili waione na CUF kwa kuemo kwake katika serikali itakua imeshiriki uovu huo.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu umeanika hadharani ukweli kwamba chama cha CCM hakiyataki w a l a h a k i y a h e s h i m u maridhiano ya November 9, 2009 na serikali ya umoja wa kitaifa. Inavyoonekana ni sawa na mtu aliyepewa mke au mume kwa lazima na wazazi wake lakini hana mapenzi hata kidogo bali anaishi nae kwa kukosa maamuzi ya kumuacha. Katika serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar, R a i s M s t a a f u A m a n i Karume amewalazimisha CCM kuingia katika ndoa ambayo hawana mapenzi nayo hata kidogo, jambo ambalo linaonekana wazi baada ya CCM kutumia ubabe kulazimisha maslahi yake katika ndoa hiyo.

Uchaguzi wa Bububu umekuja kufichua siri hii nzito ambapo viongozi wa CCM wamejitia wenyewe mtegoni baada ya muda mrefu kukataa hoja kwamba wao si waumini wa dhati wa maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar. Kabla ya siku ya upigaji kura yalikuwepo matukio kadhaa ambayo yailtoa kila aina ya dalili ya kuwepo kwa harufu ya kuharibiwa kwa uchguzi na bila shaka kuzuka kwa vurugu ambapo bila shaka ni kukejeliwa kwa maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa. Hapa lazima ifahamike kwamba tatizo la msingi la Zanzibar ni chaguzi zisizoheshimiwa, chaguzi zinazokorogwa kwa kuvunjwa kwa makusudi sheria zinazosimamia chaguzi hizo ili kukipatia ushindi wa lazima chama cha CCM tokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa 1995 baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Akifunga kampeni CCM za uchaguzi huo wa Bububu Balozi Sefu Iddi alisema hadharani kwamba CUF

wajue kabisa karamu ya Bububu ambayo italiwa siku ya kupiga kura si yao ni ya wenyewe CCM. Hakuishia hapo ila aliwapa maagizo wana CCM kutumia kila njia kuhakikisha CUF hawasogei na ndizi zao kutaka kula karamu ambayo sio yao. Balozi alikwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba mseto wa CCM na CUF umebak i shwa juu kwa makusudi, utaendelea kubaki juu na kamwe hautaruhusiwa kufika chini mpaka ngazi ya jimbo na shehia. Akimaanisha kwa kuwa jimbo hilo lina mbunge kutoka CCM hakuna ni lazima na mwakilishi atoke CCM. Aliwauliza wana CCM kama wako tayari kuruhusu mseto ka t ika j imbo la Bububu nao wakamuahidi Balozi kwamba kamwe hawatauruhusu. Serikali ya umoja wa kitaifa imewekwa katika ngazi ya uwaziri pekee ili kuepusha kupunguza nguvu za kiutendaji za CCM katika ngazi zote. Pindipo CUF ikiachiwa kushinda katika jimbo la Bububu ni kuweka mchanganyiko wa CUF na CCM katika uongozi wa jimbo jambo ambalo Balozi Seif aliwaagiza wana CCM walizuie kwa nguvu zao zote.

Halkadhalika Balozi Seif ni muumini wa Mfumo wa sasa kandamizi wa Muungano na anaitumikia Tanganyika wazi wazi kuimaliza Zanzibar. I n a v y o s e m e k a n a h a n a mizizi mirefu na nasaba ya Kizanzibari bali mizizi yake mirefu ni ya Tanganyika. Balozi anafahamu wazi kuwa ushindi wa CUF katika jimbo hilo ni kuongezeka kwa sauti ya chama hicho ambacho ndio championi wa muungano wa MKATABA katika bunge la katiba ambalo litazaa mabadiliko ya mfumo na muundo wa muungano hapo baadae. Balozi akifahamu tayari CCM imeshapoteza nguvu kubwa katika kuulinda muungano wa serikali 2 baada ya baadhi ya wawakilishi wa CCM kuapa kuunga mkono M K ATA B A a m e a m u a kutumia nguvu za ziada kulirejesha jimbo la Bububu katika CCM kwa lazima.

(Makala haya yametolewa kwa hisani ya Ahmed Omar Khamis)

Page 11: ANNUUR 1038

11 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Tangazo

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo:• Mkuzo Islamic High School - (Songea) - BWENI TU.• Kirinjiko Islamic Sec. School – (Same) - BWENI TU• Nyasaka Islamic Sec.School – (Mwanza) - BWENI TU.• Ubungo Islamic High School –(Dar es Salaam) - KUTWA NA BWENI

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi ya Kiislamu.2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Qur’an na mafunzo yake, Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics,

Chemistry, Biology, Geography, History, Civics, Book – keeping na Commerce.3. Patakuwa na mtihani tarehe 01/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoorodheshwa kwenye fomu ya maombi. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote.4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11 /20125. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani.

• Arusha - Ofisi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni -0763 282 371/ 0784 406 610• Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha – 0654 723 418 - Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075• Tanga - Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533• Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 - Ofisi ya Islamic Education Panel - Mwanza -Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin – 0785 086 770• Musoma - Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni-0714587193• Kagera - Bukoba: Alhuda Café Kwa mzee Kinobe karibu na ofisi za TRA.-0688 479 667

• Shinyanga - Msiikiti wa Majengo-0718866869 - Kahama ofisi ya AN –NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 • Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 - Ofisi ya Islamic Ed.Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin-0655144474• Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380• Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086• Singida - Ofisis ya Islamic Ed. Panel –karibu Nuru snack Hotel-0714285465• Manyara - Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575• Kigoma - Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 - Kibondo – Islamic Nursery School: 0784 442860 - Kasulu: Murubona Isl.ss 0714710802• Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663• Mtwara - Amana Islamic S.S 0786 729 973• Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU—0715 68 1 701/0716791113 - Mkuzo Islamic High School. 0716 791113• Mbeya - Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole-0713 200209 - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209

• Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073

• Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566

• Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122

• Pemba - Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331

• Unguja - Madrasatul –Fallah: 0777125074- • Mafia - Ofisi ya ust.Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu – 0653705627

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

MKURUGENZI

WABILLAH TAWFIIQ

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA – 2013

Page 12: ANNUUR 1038

12 AN-NUURBarua/Tangazo Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie:Mhariri AN-NUUR,

S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe

E-mail: [email protected]

MNAMO tarehe 28-07-2011 niliwafikiwa kuandika kitabu kilichobeba jina “FUNGA YA ARAFA NA SIKU TISA ZA DHUL-HIJJA” na mpaka hii leo kitabu hicho kinapatikana katika Duka la vitabu la Ibnu Hazmi jirani ya msikiti wa Mtoro, hapa Dar Es Salaam. Makusudio yakiwa ni kusisitiza funga ya siku hizi (tisa) zinazo tukabili na Arafa ikiwa ni mojawapo ya siku tisa hizo.

Nilifanya hivyo kwa lengo la kutaka kudhoofisha hoja za wale ambao waliokuwa wakijaribu kutaka kudunisha fadhila ya funga katika kumi hili la mwanzo la mwezi wa Dhul-Hijja na badala yake ikawa ni kuwahamasisha watu wafunge siku moja tu ya Arafa. Au pengine siku hiyo moja (ya Arafa) ikaachwa pale inapo sadifu kukutana na siku ya Jumamosi.

Siku kumi za mwanzo za mwezi wa Dhul-Hijja utukufu

Funga ya arafa imo katika siku tisa za Dhul-Hijja

wake umo ndani ya Qur-ani na Hadithi za Bwana Mtume (S.A.W.), na kufunga siku tisa katika kumi hilo la mwanzo ni katika mafunzo ya Bwana Mtume (S.A.W.). Katika kitabu “Sunan Abu Daawoud” imo hadithi na Sheikh Al-Baaniy ameisahihisha (ameipa daraja ya sahihi). Kwamba Bwana Mtume (S.A.W.) alikuwa akifunga siku tisa za (mwezi wa) Dhul-Hijja. Aidha funga hii ipo katika madhehebu yote manne (Hanafiy, Maalikiy, Hambaliy na Shaafiy) na hata katika madhehebu ya Ibadhi. Almarhumu Sheikh Abdul Aziz bin Baaz alipoulizwa kuhusu mtu anayeikataa funga hii, alijibu kwa kusema: “Mtu huyo hana elimu, anahitaji kufunzwa”.

Ndani ya siku hizi (kumi), imo siku bora zaidi kwa kufunga na hiyo ndio siku ya Arafa. Bwana Mtume (S.A.W.) anasema kwamba funga ya Arafa inafuta madhambi ya mwaka uliopita na huu ulio baki (uliopo).

Hapa nchini kwetu mara tu mwezi wa Dhul-Hijja unapoandama, utawaona watu (khususan Masheikh) wakibishana na kuvutana kuhusu siku hii moja ya Arafa. Wengine wanasema kwamba siku ya kufunga ni ile siku ambayo watu wamesimama katika Uwanja wa Arafa. Na wengine wanasema kwamba

siku ya kufunga ni ile siku ya mwezi tisa kwa muandamo wa hapa kwetu. Siyo lazima siku hiyo iwe ndio siku ile ile ya kisimamo cha Arafa. Ukweli ni kwamba mjadala huu ni tasa hauna maana yoyote, hauna matunda/natija wala mwisho, kwa sababu makundi mawili yote haya hayana dalili kutoka kwa Bwana Mtume (S.A.W.).

Kwanza kabisa hakuna dalili (Hadithi) inayosema kuwa katika mwezi wa Mfunguo Tatu (Dhul-Hijja) Bwana Mtume (S.A.W.) alikuwa akifunga siku moja pekee katika mwezi wa Dhul-Hijja na kwamba siku hiyo ndio Arafa. Aidha siku hiyo Bwana Mtume (S.A.W.) na maswahaba wake walikuwa wakifunga v ip i? Hasa maswahaba waliokuwa wakiishi mbali na Makka (Iraq, Shaam au Misri) walikuwa wakifunga siku gani? Ni kweli kwamba walikuwa wakifunga sawa na

siku ile ya kisimamo cha Arafa au walikuwa wakifunga kwa mujibu wa “Matwaalii” yao huko waliko? Mjadala kama huu katika wakati wetu wa leo umewalemaza baadhi ya watu hadi wakawa ni wavivu kufunga siku tisa za mwezi huu na badala yake wanabaki kubishana na ha t imaye wanaipoteza Sunna ya Bwana Mtume (S.A.W.) kwa sababu ya ushabiki tu. Kubwa zaidi na baya mno, ni lile lililo tokea kwa baadhi ya wasomi hapa Tanzania miaka minne/mitano nyuma, hao walisusia na pia walihamasisha baadhi ya Waislamu kususia funga ya

siku ya Arafa. Eti kwa sababu siku ile ilikuwa ni sawa na siku ya Jumamosi. Wamefanya hivyo na hali wanajua kwamba katika Sunna ya Bwana Mtume (S.A.W.) inafaa (inaswihi) kwa Muislamu kufunga siku ya Ijumaa na Jumamosi. Na zipo Hadithi za Bwana Mtume (S.A.W.) zinazolithibitisha hilo. Kwa kosa hilo watu hao, bila shaka wamepingana na Bwana Mtume (S.A.W.) m a r a m b i l i . K w a n z a wameikataa kauli ya Bwana Mtume (S.A.W.) ya kuruhusu kufunga siku ya Ijumaa na Jumamosi. Kadhaalika wamekataa kufunga siku ya Arafa pamoja na utukufu wake wote. Mjadala kama huu na ushabiki kama huu, una hatari ya kutuweka mbali sisi Waislamu na Sunna sahihi ya Bwana Mtume (S.A.W.).

Mzozo na ushabiki wetu katika mas-ala khilafiya (yenye kukhi ta laf ianwa rai), ni mambo mawili ya f i t ina ya l iyo tushawish i hadi kukubaliana sote kwa pamoja kuvunja Umoja wa Waislamu nchini. Tumekuwa tukiswali nchini mwetu Idi moja ya Al-Hajji mara mbili: hawa wanaswali leo, wengine ndio wamefunga Arafa na waliofunga leo kesho ndio wanaswali . Hi l i n i j ambo ambalo tangu Uislamu ulipoanza hadi hii leo, halikuwahi kutokea isipokuwa katika karne yetu hii. Masheikh/viongozi wetu wa Dini ya Kiislamu wanao shabikia mzozo huu, ni lazima wajue kwamba hilo wanalolifanya ni kupinga aya ya Qur-ani tukufu inayotuamrisha Umoja na mshikamano. Na hatimaye ni kwenda kuwajibika mbele ya Allah (S.W.T.) kwa kwenda kinyume na amri yake.

Wabillah taufiq.Abdallah Ahmad Bawazir.

NDUGU Mhariri, naomba unipe nafasi tena kwa mara nyingine niweze kuelezea yangu ya Moyoni katika gazeti lako Tukufu, sauti ya Waislamu Gazeti la An-nuur.

Katika mambo ambayo yametugharimu pakubwa sana Waislamu wa nchi hii na ambayo Mwalimu Nyerere hakuwa na “Compromise” (Msal ie Mtume) dhidi ya Waislamu ni elimu na muungano. Ndiyo maana, jaribio lolote la kutaka kuondoa au kurekebisha taasisi kama NECTA au muungano lazima likutane na upinzani mkubwa kutoka kwa wale wanaonufaika na mifumo hiyo. Hawa si wengine bali ni wale wale mawakala wa ubeberu na mabeberu wenyewe. Wal ipanga mbengu ya ubaguzi na kuviza moyo wa uzalendo.

Sakata la NECTA kama linavyoendelea kurindima l ina toa mwanya za id i jinsi elimu ya Tanzania inavyoendelea kutolewa kwa ubaguzi dhindi ya Waislamu kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Pia inaonyesha “Brain washing” ya Wazungu inavyofanya kazi mpaka leo.

Hakuna utulivu katika elimu na mitihani yake, mara utasikia somo la Maarifa ya Kiislamu hivi, halitambuliwi n.k matokeo ya ubaguzi huu, ndio leo miaka 51 ya uhuru tunaona ofisi zote za umma zimejaa Wakristo asilimia kubwa sana ingawa tulianza darasa la kwanza pampja na Waislamu tulikuwa wengi sana!

S i y o s i r i k w a m b a k u a n g u k a k i u c h u m i , kijamii na kiutamaduni kwa nchi yetu kumetokana na Wakristo kuhodhi nafasi zote muhimu za utumishi wa umma na utendaji. Vyeti nq mitihani ni mashaka matupu, inashangaza sana kutokuona katika Utumishi wa Umma Wahindi, Waarabu n.k wao si Watanzania au wataalamu? Hii bila shaka ndiyo Mfumokristo katika utendaji.

Hapa ndipo tofauti kubwa sana ya maendeleo kati ya nchi za “Tigers Economy” – Singapore, Malaysia, Indonesia, Taiwani…….. Na hizi zetu za Afrika, Tanzania ikiwa moja wapo, kule kwa wenzetu, elimu ni elimu kweli, wameithibiti na kuiendesha kwa maslahi yao, huku kwetu, elimu imeendelea kudhibitiwa na mawakala wa ubeberu:

NECTA, ngome ya mabeberu?Roman Catholic Church, Lutheran, Anglicana nk. Wameandaa vijana watiifu kweli kweli kwa makanisa yao, tangu kwa Nyerere, wao wanaona fahari kwamba wana wakomoa Waislamu lakini wanasahau kuwa wanafanya k a z i y a k u k w a m i s h a maendeleo ya nchi kwa faida ya mabeberu. Wasomaji wakumbuke misamaha ya kodi, kadinali Pengo na mh. Membe kuhusu OIC huyu Askofu Tutu kawa mkweli na madhubuti kwa sababu kanisa lake halina makao makuu Ulaya au Marekani. Ni la Afrika kusini Afrika haiwezi kuendelea kwa kasi itakiwayo bila kuvunja mtandao huu wa mawakala wa ubeberu. Afrika ndiyo bara tajiri kuliko yote.

Hivi nchi hii itakuwa wapi kimaendeleo miaka 10 ijayo endapo itaongozwa na Prof. Ibrahimu Lipumba, Dr. Ramadhani Dau, Dr. Harison Mwakyembe, Dr. John Magufuli na Kijana Zito Kabwe? Hawa ni kwa uchache tu.

Kilio cha Waislamu na wapenda haki wote kuhusu k u f u m u l i w a N E C TA lazima kipokelewe kwa moyo mkunjufu. Serikali iwashirikishe wale Waislamu wanaolipigia kelele na hata mengineyo. Siyo kuchukua Waislamu ili muradi tu, iwashirikishe ma-genius, we led i , wa taa luma na wenye msimamo. Kasumba z a N y e r e r e z i a c h w e , kumjua zaidi alivyokuwa wasomaji wa some pia kitabu KWAHERI UKOLONI KWA HERI UHURU.

Kwa sasa NECTA ni kero kubwa sana kwa maslahi ya nchi yetu. Waislamu na wengineo waendelee kupambana na zimwi hili. Umoja ndiyo nguvu na ushindi, uwezo upo tena mkubwa na utazidi kuonekana siku baada ya siku.

Wasikilizwe viongozi wetu wanaokubalika na yamewafika mengi kwa k u t u s e m e a Wa i s l a m u . Bahati nzuri viongozi wetu wanatekeleza Sunnah ya Shura katika kuyaendea mambo yetu: katiba, Sensa, NECTA n.k.

Sasa tunataka Diplomasia inayotoa majibu stahiki kwa wakati na siyo ile ya kuomba. Hii yumeitumia kwa miaka 50 na imefeli vibaya. Kweli NECTA ni janga la kitaifa.

Mohamed MohamedDar es Salaam

Jina: Rajabu Eliamini Msofe, Aina ya Mtihani ni CSEE, Mwaka wa Mtihani ni 2007Namba ya mtihani S.2431-0023Anwani 42 Utete / RufijiNamba ya Simu: 0759 677734, 0765 404370, 0714546064, 0767 546064nimepotelewa na vyeti vya shule tarehe 22/08/2012 maeneo ya Stendi ya Mbagala Rangi tatu katika kituo cha Daladala majira ya saa tisa Alasiri vyeti hivyo vilikuwa katika

Tangazo la kupotelewa na vyeti vya Shule

begi la rangi nyeusi katika bengi hilo kulikuwa na Leving Certificate ya Sekondari ya Mabogino, Cheti cha kuzaliwa, Living ya Chuo cha Ualimu Krinjiko na Result Slep ya Ualimu Grade IIIA pamoja na Nguo.

Page 13: ANNUUR 1038

13 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Makala

DUNIA ni uwanja wa fujo, kila mwenye ngoma yake aingie acheze. Maneno haya yametamkwa karne nyingi zilizopita. Katika safu hii nimeyatumia kulinganisha na mabadiliko ya mifumo ya kisiasa hapa duniani.

Mwishoni mwa miaka ya tisini tulishuhudua namna ujamaa ukianguka kwa kasi kubwa na ile kambi ya Mashariki ikilazimika kubadil i mwelekeo wa chombo chake.

Pamoja na mabadiliko hayo, wapo wanasiasa wasiokubali mabadiliko ya jambo katika jamii. M a r a n y i n g i h u i t w a “Muhafidhina”. Na hapa Zanzibar Muhafidhina wapo, lakini sio wengi sana.

Muhafidhina wamekuwa wakijaribu kupotosha ukweli kwa maslahi binafsi ya kisiasa na ya kujaza matumbo yao. Utawasikia wakitamka kwamba Zanzibar itarejea kwa Waarabu!!

Tishio hilo wanadhani kuwa lina nguvu na linaweza k u w a t i a w o g a v i j a n a kutopaza sauti zao kutoa maoni kwa mambo muhimu ya nchi kama mabadiliko ya katiba ya Tanzania na mfumo wa Muungano wanaoutaka.

I t a k u m b u k w a k u w a J a m h u r i y a w a t u w a Zanzibar ilianzishwa baada ya Mapinduzi ya 1964 iliyomaliza Utawala wa Usultani wa Zanzibar ambapo mwezi mmoja baadaye Taifa huru la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar likajiunga na Jamhuri ya Tanganyika. Sultan wa mwisho kutawala Zanzibar ni Jamshid bin Abdullah Al Said ambaye kwa sasa anaishi Portsmouth, Uingereza akiwa na umri wa miaka 82.

Kabla ya Mapinduzi, Zanzibar haikuwa Jamhuri, ilikuwa chini ya Sultan, lakini Mapinduzi ya umma ndio yaliyoifanya Zanzibar kuwa Jamhuri. Umoja wa Mataifa uliyatambua Mapinduzi hayo kuwa ni halali na uliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika(OAU) ulitambua pia Mapinduzi hayo.

Masharti ya uanachama wa Umoja wa Mataifa yapo wazi na pia mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika upo Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na ni mkataba wa Kimataifa ambao kuvunjika kwake kumeelezwa wazi katika sheria za Kimataifa.

Hakuna mtu wa kuzuwia mabadiliko ZanzibarSasa i k iwa omb i l a

vijana na wananchi walio wengi kutaka muundo wa Muungano kama wa EU kila nchi itarejea kukaa kwenye kiti chake sio Sultan maana Ban-Kimoon hamtambui Jamshid anaitambua Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndio iliyoungana mwaka 1964.

Kwa hivyo, hakuna njia wala upenyo kwa Sultan kurejea kuitawala Zanzibar wala Umoja wa Mataifa kumpa kiti kule New York akikalie. Atakaa kwa misingi ipi na kwa hoja gani?

Visiwa vya Zanzibar s io pekee vi l ivyofanya M a p i n d u z i . U f a r a n s a imefanya Mapinduzi, sasa nayo UN watarejesha kiti kwa mfalme Louis XVII? Mapinduzi ya Ufaransa ni jina linalojumlisha matukio muhimu ya siasa kwa kipindi cha miaka 10, tangu 1789 hadi 1799, yaliyobadilisha uso wa Ufaransa na utamaduni wa Ulaya kwa jumla.

Athari zake zilienea kote duniani kama fikra za haki za binadamu, uhuru na maendeleo ambapo dhana ya kuwa mamlaka ya dola ni haki ya raia, si ya wafalme wala watawala wengine, ilienea polepole pande zote za dunia na ilipofika Januari 12,1964 Wazalendo wa Zanzibar chini ya Afro Shiraz Party walirejesha heshima na utu kwa wakulima na wakwezi.

Vugu vugu la mabadiliko lilianza baada ya Wafaransa kuchoshwa na ugumu wa maisha huku watu wachache wakinufaika. Kama ilivyo kwa nchi yetu wahafidhina wanaonekana kuneemeka na migogoro ya kisiasa kwa kuwatumilia vijana kwa kupandikiza chuki na hasama miongoni mwao.

M a d e n i m a k u b w a yal iyokuwa yaki ikabi l i U f a r a n s a k w a w a k a t i huo ilisababisha Mwaka 1789 mfalme Louis XVII kuitisha Bunge kwa mara ya kwanza baada ya miaka 170. Wananchi walilalamika kwamba matumizi makubwa ya mfa lme pamoja na gharama za vita vya uhuru vya Marekani vilivyosaidiwa na Ufaransa dhidi ya Uingereza kumewabebesha mzigo Wafaransa.

Tangu Louis XIV (1643–1715) wafalme waliotawala Ufaransa bila Bunge, lakini kisheria mfalme hakuwa na madaraka ya kuongeza kodi bila idhini ya bunge, na Louis XVII hakuwa tena na nguvu ya kutosha kupuuza utaratibu huo.

Kutokana na vurugu za kisiasa na mfumuko wa bei za chakula, wananchi wa Paris waliasi wakashambulia gereza la Bastille na kuibomoa. Mfa lme a l i yedhoof ika hakutaka kukandamiza uasi huo na Bunge la taifa liliendelea kubadilisha sheria kwa kufuta haki za pekee za waungwana. Mashambani wakulima walianza kuasi na kukataa ulipaji kodi katika mikoa mbalimbali.

Mfalme alipoona kwamba madaraka yake yanapungua zaidi na zaidi ali jaribu kuondoka lakini alikamatwa na kurudishwa kama mfungwa mwaka 1791.

Mwelekeo mkali kati ya wabunge ulipata ushindi na 1792 Ufaransa ulitangazwa kuwa jamhuri . Mfalme alishtakiwa kuwa msaliti wa Taifa akapewa hukumu ya kifo na kukatwa kichwa pamoja na mke wake Januari 21, 1793 .

Vijana wa Zanzibar na pengine Tanzania nzima sasa wanataka mabadiliko. Hawatafanya kama wale wa Ufaransa isipokuwa watatumia haki ya kutoa maoni kukataa ukandamizaji wa hoja na maoni sahihi katika mwelekeo wa Muundo wa Muungano wanaoutaka ambao kwa mtazamo wa wengi wanatamani kama ule Umoja wa Ulaya.

Saa ya mabadiliko imefika, vijana wasiokuwa na ajira, uhakika wa chakula na mahali pa kulala, wamefikia pahala wanataka kuona mabadiliko ya kweli yanatokea, sio tu katika siasa, bali hata katika uchumi na ndio maana wanataka Muungano wa Kiuchumi zaidi kuliko mfumo ulipo wa Serikali mbili tena katika mkataba wa kikatiba.

Ni lazima Wahafidhina wafahamu kuwa ulimwengu wa vijana haukubali tena kuburuzwa na mara nyingi vijana wa kileo, waliozaliwa katika Tenknohama wanaunga mkono siasa yenye uchumi na Wanazuoni wanaipima hoja hiyo katika mizania miwili: mosi msukumo binafs i wa kijana wa Zanzibar wa uhitaji wa mabadiliko. Pili ni mhemko wa majira (seasonal e m o t i o n s / e x c i t e m e n t ) . Mhemko huu ni kama kilevi ambapo kama ukweli ulivyo, idadi kubwa ya vijana ndio wanjwaji ambao hawatapenda kunywa kilevi kisichokuwa na stim yoyote kwao kama kile cha Kihafidhina.

Demokrasia ya kisasa inalazimisha kuheshimu

maoni ya mwengine hata kama huyataki. Ndio maana watu makini wanaamini kuwa uvumilivu mzuri ni ule unaojiepusha na chuki zisizo na msingi (prejudice).

Hata kama anaye toa maoni au kueleza ni yule msiyeafikiana, au kimaumbile si mzungumzaji mzuri, jaribu kuuweka sawa ujumbe huo. Zingatia “alichokizungumza siyo namna alivyozungumza”. Mara zote chuki isiyo na msingi huviza mabadiliko.

Ikiwa dhana ya ujana ndio nguvu ya mabadiliko katika jamii, Wahafidhina waliozeeka kifikra na kimwili hawawezi tena kutumia mbinu chafu tena za kizamani kuwapotosha vi jana au kuwatumia kwa kuendeleza chuki.

Kwa kutambua dhana hiyo, Chama cha Mapinduzi kiliwahi kuelezea siku za nyuma dhamira yake ya mabadiliko katika Idara zake na Maofisa huku viongozi w a k e w a k i j i t a y a r i s h a kukikabidhi Chama hicho kwa umma wa Vijana kuongoza na wao kubaki kama washauri.

Katika operesheni hiyo, CCM imetenga bilioni 7 kuwaondoa wa tumish i

w a s i o k u w a n a u w e z o wasiofundishika na viongozi mzigo. Bila shaka fagio la chuma litafagia uozo uliosheheni CCM na katika hili Wahafidhina siku zao zinahesabika.

Tumeshuhudia vyama vya Upinzani viongozi wao vijana, CUF yupo Ismail Jussa, CHADEMA Zitto Kabwe, CCM Bara yupo Januari Makamba na Nape Nnauye ambao utawapata kwa anuani za barua pepe na kwenye mitandao ya kijamii.

I w a p o m a o n i y a v i j ana ya t apuuzwa au kunyamazishwa kwa aina yoyote ile, CCM itambue kuwa inapaswa kujiandaa kuishi maisha mapya ya kambi ya upinzani mwaka 2015 na Vuai ndio atakuwa Naibu Katibu Mkuu wa kwanza akiwa Chama pinzani.

Kama nilivyoeleza awali kwamba mara nyingi sifa kuu ya ujana kama rika ni kuwa na mapenzi katika mabadiliko. Kufanya mambo au kuwa na vitu tofauti na mazoea. Huo ndio ujana daima ambapo Wahafidhina w a m e k u w a w a k i t a k a

MWANASHERIA Mkuu mstaafu wa Zanzibar Dorado

Inaendelea Uk. 14

Page 14: ANNUUR 1038

14 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012Makala

Hakuna mtu wa kuzuwia mabadiliko Zanzibar

Inatoka Uk. 13kuendeleza mwenendo

wao kwa mazoea.Hali ilivyo hivi sasa ni ya

upepo mkali wa mabadiliko ya kisiasa ambapo tumeshuhudia Mataifa kadhaa ya Afrika y a k i s h i n d w a k u h i m i l i vishindo vya mabadiliko hususan kwa wanasiasa v ing ’ang’an iz i . H ivyo anayedhani kuwa amesimama, ajitazame asianguke kama alivyoanguka Hosni Mubarak, Gadaff na wengineo.

Kwa kuthibitisha hilo, tumeona namna kura ya maoni iliyofanyika mwezi Julai mwaka 2010 iliamua kuzika kabisa siasa za chuki Zanzibar huku Wahafidhina wakibaki vinywa wazi; wengine ukiwatazama hata kwenda mbio hawawezi pale panapotokezea balaa! Mungu aepushe mbali nchi yetu iendelee kubaki na amani na utulivu daima.

Bado tunakumbuka namna Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye kwa wakati huo akiwa Rais wa Zanzibar alipata ukinzani mkali uliosababishwa na kuko lezwa chumvi na Wahafidhina waliorusha mitaani vipeperushi vya kumkejeli.

V i o n g o z i w e n g i n e w a l i o k u w a w a k i u n g a mkono umoja na mapatano walihesabiwa kuwa ni vibaraka

wa Hizbu huku wengine wakiambiwa walikuwa Hizbu tangu zamani. Lakini jambo la kushangaza Wahafidhina hao hao ndio waliokwenda kuomba vyeo kwa chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Pamoja na Wahafidhina wa siasa za chuki kuanza kuhaha kila kona, Mheshimiwa Karume hakutishwa wala kukatishwa tamaa na hali hiyo na hatimaye kaburi la siasa za chuki, uhasama wa kulipiza kisasi Zanzibar likachimbwa na marehemu siasa za mti kwa macho kuzikwa humo na hivi sasa hakuna hata anayemuombea dua.

Matokeo ya kura ya maoni iliyoamua mfumo wa muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yanathibitisha kuchoshwa kwa wananchi na siasa za chuki kwani waliosema ndio walikuwa 175,476 sawa na asilimia 66.0 na waliosema hapana ni 90,588 sawa na asilimia 34.0 .

Vijana wengi walipiga kura ya ndio kutaka mabadiliko huku Wahafidhina wakipinga bila mafanikio na ndivyo utabiri wangu kuhusu anguko lao katika mabadiliko mapya ya muundo wa Muungano kuwa kama ule wa Umoja wa Ulaya.

(Makala hii imetolewa kwa hisani ya Vuai A.)

Tuseme ukweli kuhusu NyerereInatoka Uk. 7Bwana Mohamed Mwinyi

Mzale alibainisha wazi kwamba vyombo vinavyosimamia Elimu ya juu Tanzania ni vya ‘Muungano’ kwa maneno tu, lakini kwa vitendo na miundo yake ni vya Tanganyika. Bunge la Jamhuri ya Muungano linatunga sheria kwa maslahi ya Tanganyika, ambayo ni pacha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Wakati wa uongozi wa Nyerere (1961- mpaka sasa), Wakristo wamekuwa na uhuru mkubwa wa dini yao, ambao umelindwa vizuri na Katiba ya nchi. Uhuru wao ni pamoja na kuwabatiza Waislamu na kuwahubiria Injili. Lakini Waislamu, walio wahanga wa kubatizwa, hawakuwa na ruhusa wala uhuru wa kupanga na kuendesha mambo yao wenyewe, bila ya kuingiliwa na mamlaka kuu ya nchi.

Masuala yote yanayowahusu Wais lamu wa Tanzania , yakawekwa mikononi mwa Bakwata, baraza lililoundwa kwa minajili ya kuwahujumu Waislamu wa Tanzania, baada

ya Nyerere kuvunja chombo kilichoundwa na Waislamu wenyewe, kwa lengo la kusimamia maendeleo yao eneo zima la Afrika Mashariki. Bakwata linafanyakazi chini ya ulinzi na maelekezo ya serikali inayoendeshwa kwa misingi ya Mfumo Kristo.

Kukosekana kwa chombo huru cha kuwasemea Waislamu wa Tanzania, kuliunda ombwe la kiitikadi hapa nchini. Kwa kipindi cha miongo mitatu (1961 -1990) , Wa i s l amu wa Tanzania hawakuweza kufanya mambo ya maana kimaendeleo katika jamii yao, kama mafundisho ya dini yao yanavyoelekeza. Katika jitihada za kuziba ombwe hilo, Waislamu walijaribu kuunda taasisi mbalimbali, zikiwemo zile za mlingano wa dini kama ‘Umoja wa Wahubiri wa Mlingano wa Dini (UWAMDI).

Hata hivyo, wataalamu

n a w a s o m i Wa i s l a m u , wakipingwa vikali na Bakwata, walifanikiwa kuunda chombo chao huru, Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, mwezi Novemba mwaka 1992. Lakini pamoja na j i t ihada zote hizi za Waislamu kujinasua kutoka kwenye makucha ya Bakwata, Baraza lililoundwa na Nyerere, adui mkubwa wa Waislamu Afrika Mashariki nzima, kwa lengo la kuwadumaza na kuwakandamiza Waislamu, kuna baadhi ya wenzetu, bila ya hofu wala kuona haya, wanatuhadaa kushirikiana na Bakwata kwa kisingizio cha umoja! Umoja gani na Bakwata? Juzi tu hapa, katika suala la kumtafuta kadhi wa Tanzania, Bakwata imewageuka Waislamu! Katika ajenda ya kugomea sensa imewageuka Waislamu! Vipi tunashirikiana na maadui, hali ya kuwa tunafahamu?

Kuna baadhi ya wenzetu wameamua kutumikia mfumo unaokandamiza Waislamu na hili wala si jambo la ajabu. Historia imerikodi vizuri tu kwamba maadui wa Waislamu kama Nyerere, wamefanikiwa sana kwa sababu ya kuwatumia wanafiki miongoni mwa Waislamu. Hili Waislamu wanalijua na hawataumwa na nyoka mara mbili kwenye shimo moja. Baada ya juhudi za miaka mingi kujikomboa, leo tujiingize tena kwenye kibano cha Bakwata!? Kuna maana gani ya kuitwa Waislamu! Si bora tuwe masharobaro tu! Tuvae mregezo halafu tucheze ‘pool’ misikitini, kwa sababu hatuna maana yoyote ya kuwepo!

Kama tunavyofahamu, w a k a t i w a u t a w a l a w a Nyerere, Wamissionari wa Kikr is to wal ikuwa huru kuendesha shughuli zao namna walivyopenda, ikiwa ni pamoja na kuwabatiza Waislamu wanaokandamizwa. Mwaka 1982, kundi linalojiita “Crusaders” lilizuru mikoa yote ya Tanzania kuhubiri Ukristo katika mikutano ya hadhara, lakini Abubakar Mwilima, Othman Matata, Ngariba Fundi Mussa na Mohammed Ali Kawemba walizuiwa mwaka 1987.

Vy o m b o v y a h a b a r i vinavyodhibitiwa na dola, ambavyo vimejaa Wakristo katika nafasi za uongozi, viliwatuhumu akina Ngariba kwa “kupanda mbegu ya chuki na vurugu” nchini Tanzania. Rais Ali Hassan Mwinyi, ambaye ni Muislamu alishambuliwa w a z i w a z i n a k a m b i z a Wakristo. Mtu aliyeendesha kampeni ya kuwahamasisha Wakristo kupinga uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi, ili kukabiliana na “kitisho cha

Waislamu” alikuwa Mchungaji Christopher Mtikila, Mkristo mwenye itikadi kali.

Akiwa kiongozi mkuu wa ‘Full Salvation Church’, Mchungaji Mtikila pia ni kiongozi wa batalioni ya kanisa hilo ya kupambana na Uislamu, ambapo alishawahi kutangaza wazi kwamba ‘Crusade’ yake ni kulinda Ukristo dhidi ya Uislamu.

Mchungaji Christopher Mtikila alipata umaarufu zaidi mwaka 1988 katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika Kizota mjini Dodoma, wakati alipomuandikia barua Nyerere, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM kwa niaba ya Wakristo, akipinga Urais wa Ali Hassan Mwinyi kwa kosa la kujaribu kuimarisha Uislamu kwa gharama ya Ukristo. Barua yake hiyo ya uchochezi ilisambazwa kwa wajumbe wote wa mkutano huo uliofunguliwa na Joseph Warioba, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati ule.

Barua ilitaka ufanyike uchunguzi wa haraka na kurekebisha kile alichoita “Dangerous Government Stand” (msimamo hatari wa Serikali) chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi. Katika hatua ya kushangaza, Mchungaji Mtikila alisisitiza katika barua yake kwamba, eti TANU ilipokuwa chini ya Nyerere, kiongozi huyo alipigania uhuru, umoja na usawa miongoni mwa raia kwa kuondoa ubaguzi wa kidini!

Huo ni uongo ulio wazi na unaweza kuaminiwa na watu wenye akili za Mtikila tu! Anajua ukweli ulivyo, lakini anajaribu kuuficha kwa maneno ya uongo. Nyerere alimteua Rev.Mushendwa kuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Elimu ya siasa ya TANU kwa sababu tu ya imani yake madhubuti ya Kikristo, kama inavyonukuliwa katika kitabu cha Jan P. Van Bergen, ‘Development and Religion in Tanzania’ kilichochapishwa na kanisa Katoliki.

Kwa kipindi cha miongo mitatu ya uongozi wake, Nyerere hakuwahi kumteua Muislamu hata mmoja kuwa Waziri wa Elimu, lakini Waislamu hawakulalamika w i z a r a h i y o k u g e u z w a himaya ya Wakristo. Tuhuma za Mtikila na Wanadhimu wengine wa Mfumo Kristo zilikuwa, eti Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa na lengo la kuisilimisha Tanzania nzima. Kosa lake Mwinyi lilikuwa kuteua wakurugenzi wanne Waislamu katika Wizara ya Elimu. Bila ya kutambua, Mwinyi alikuwa amegusa mshipa wa fahamu wa Mfumo Kristo!

Makamanda wa Mfumo

Kristo wanaeneza propaganda za sumu kwamba Waislamu wanahatarisha amani na umoja wa Watanzania, licha ya ukweli kwamba amani na umoja huo imekuwa ikitunzwa na Waislamu, tangu kipindi cha harakati za kupigania uhuru na baada ya uhuru kupatikana. Inajulikana vizuri kwamba, u k i w a o n d o a m a r e h e m u Hassan bin Amir na Sheikh Zubeir Mtemvu, Waislamu wa Tanganyika walikataa kukiunga mkono chama chao wenyewe cha ‘All-Muslim National Union of Tanganyika’ (AMNUT), ili kulinda umoja wa kitaifa chini ya TANU, ambacho Rais wake alikuwa Nyerere.

Waislamu hawa walijaribu kuwanasihi ndugu zao katika imani kwamba Wakristo, ingawa ni Watanganyika wenzao, lakini wana chuki ya ndani na uadui mkubwa dhidi ya Waislamu. Kamwe h a w a t a w a t e n d e a h a k i Waislamu watakapodhibiti nguvu za kisiasa.Walijaribu kuwaelewesha Waislamu w e n z a o k w a m b a b a a d a ya Uhuru, upogo kat ika elimu hautarekebishwa na nafasi za Waislamu katika maeneo mengine ya kijamii hazitaboreshwa pia. Waislamu hawakuelewa kabisa, ingawa nasaha za akina Sheikh Suleiman Takadir na Hassan bin Amir zilitoka ndani ya Qur’an Tukufu! Bangi ya Nyerere ilipofua kabisa akili zao.

Kutokana na msimamo wao, Sheikh Suleiman Takadir alifukuzwa kutoka kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Sheikh Hassan bin Ameir alifukuzwa Tanganyika na kurejeshwa Zanzibar na Zubeir Mtemvu alianzisha chama kingine ‘African National Union’(ANC), aki ipinga TANU chini ya uongozi wa Mkristo, Julius Nyerere.

Ukweli ambao wapiganaji wa Mfumo Kristo Tanzania, iwe waandishi wa habari, w a n a s i a s a , w a s o m i , wakurugenzi , maaskofu, B a k w a t a n a w e n g i n e o hawathubutu kuusema ni huu hapa. Makanisa nchini Tanganyika yaliikataa TANU; mara mbili mwaka 1958 mjini Sumbawanga na mwaka 1965 mjini Mbulu. Makanisa ya l ikuwa yaki fanyakazi kwa karibu sana na Serikali ya kikoloni, ambayo ndiyo iliyomlea Nyerere ili aje kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika b a a d a y a Wa i n g e r e z a kuondoka.

Baada ya uhuru kupatikana, nchi ikiwa chini ya uongozi wa Nyerere, Wakristo wa Tanzania sasa wanavuna kile ambacho hawakupanda. Wanafurahia matunda ya uhuru kila sekta kutokana na Mfumo Kristo ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere, akiungwa mkono na mataifa ya Magharibi.

Page 15: ANNUUR 1038

15 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012HABARI

NECTA wakataa vyeti vya Waarabu

Inatoka Uk. 16kidato cha nne katika shule ya serikali ya Mareya Al-Qebteya Girls School Dubai mwaka 2012.

Kwa mujibu wa cheti hicho, alifaulu masomo ya Islamic Education, Arabic Language, English Language, Mathemat ics , Phys ics , Chemistry, Biology, Geology na kupata alama ‘A’ kwa masomo yote.

Naye Maryam alisoma katika shule ya binafsi (private) ya Al Adhwa Private School iliyopo katika mji wa Al Ain na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2012 na cheti chake kinaonyesha kuwa alisoma masomo ya Arabic Language Islamic Studies, English Language, Mathematics, Physics, Chemistry, Biology na Computer na kufaulu kwa wastani wa asilimia 78.

Hata hivyo baada ya majibu ya Baraza kutoka, afisa mmoja wa Baraza aliwaeleza kuwa vyeti walivyowasilisha ni maelezo ya matokeo, yaani (statement of results) na sio vyeti halisi vinavyohitajika.

Majibu hayo yamepingwa vikali na mabinti hao na wazazi wao na kueleza kuwa vyeti walivyoviwasilisha ndio vyeti halisi na kwamba hakuna aina nyingine ya cheti inayotolewa na serikali ya

Dubai.“Sijui wao wamejirishisha

je kwamba vyeti vya wenetu sio halisi bali ni maelezo tu ya matokeo. Walipaswa kuvihafamu vyeti vya shule za Dubai kwanza kabla ya kuja na kauli za haraka haraka za kutukatalia”. Alisema Bw. Mohamed Ali, mzazi wa Aisha ambaye naye ni Mtanzania anayeishi Dubai.

Hata hivyo Bw. Mohamed Ali, amesema kuwa bado hajakata tamaa na elimu ya wanawe na kwamba sasa anakwenda Wizara ya Mambo ya Nje kuonana na wahusika ili kusaidia kupata uhakikia juu ya vyeti vya UAE na kuwathibitishia NECTA uhalali vyeti vya wanawe.

“Nakwenda Wizara ya Mambo ya Nje, hata ikibidi Ubalozi wa UAE nchini uhusishwe ili kubaini haki na wanangu wapate chuo. Sihitaji mkopo wa bodi wala udhamini wa mtu, hawa nawasomesha mwenyewe na kusoma UAE haiwezi kuwa sababu ya wanangu kukataliwa kusoma hapa nchini”. Alisema Bw. Mohamed Ali.

Juhudi za mwandishi kumpata Afisa wa NECTA aliyekataa kutambua vyeti hivyo kutoka nchi ya Kiarabu hadi tunakwena mitamboni hazikuweza kufanikiwa.

WA K AT I h a r a k a t i z a Mchakato wa Marekebisho ya Katiba ya Nchi, kuanzia Zoezi la Utoaji wa Maoni, utakaoamua mustakabali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiendelea, Viongozi, Wananchi, Wanasiasa na Wasomi wa Visiwa vya Unguja na Pemba, wamemtumia salamu maalumu Raisi wa Zanzibar , Dokta Ali Mohamed Shein.

Salamu hizo ni juu ya kutekeleza ahadi ya kuitumikia na kulinda maslahi kamili ya Zanzibar , kama Nchi yenye M a m l a k a y a k u s i m a m i a maendeleo, uchumi, na ustawi wa wananchi wake.

Katika sehemu ya ahadi ya Raisi Dokta Shein, ambayo pia Wananchi wameikumbusha, ni pale Tarehe 1, Novemba, 2010, katika Hoteli ya Bwawani, mara tu baada ya kutangazwa kushinda Wadhifa huo, ambapo Kiongozi huyo a l iu tangaz ia umma kwamba, angelirekebisha hitilafu na kasoro zote za utekelezaji wa demokrasia zikiwamo za Uchaguzi ndani ya Zanzibar

Ahadi hiyo pia usoni mwa Jamii ya Kimataifa iligusia haja

Shein akumbushwa ahadi yake ya kuitetea ZanzibarAtakiwa kuwa mbali na ‘vitimbakwiri’Mabalozi wakaazi ndani ya Zanzibar

Na Waandishi wetu, Zanzibar

ya marekebisho makubwa ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar , ZEC, ambayo kwa mujibu wa uchunguzi wa wafuatiliaji wa mwenendo wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Saba , inayoongozwa na Raisi Dokta Shein, bado haijatekelezwa.

“Tunamkumbusha Raisi Dokta Shein atekeleze ahadi yake mwenyewe ambayo hajaitekeleza kwani kufanya hivyo ndiyo uungwana”, alisema aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Zanzibar , Bw. Ismail Jussa Ladhu, akihutubia maelfu ya Wananchi wa Kisiwa cha Pemba waliohudhuria Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kambini, Jimbo la Ole, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, mwanzoni kabisa mwa wiki hii, maneno ambayo pia waliyakariri Wana-CUF, katika Risala yao Maalumu waliyoiwasilisha hapo.

Bw. Jussa, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Unguja, alisema kushindwa kutekeleza ahadi hizo kunadhoofisha hima na azma ya Wazanzibari kutetea Mamlaka kamili ya Nchi yao ya Zanzibar , Kitaifa na Kimataifa.

Mbali na Jussa, ahadi hiyo

ya Umma wa Wazanzibari, Viongozi wa Ser ika l i na Wanasiasa pamoja na Wananchi, pia wamekuwa wakiikumbusha katika mikusanyiko na mikutano iliyofanyika katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba, na Mkoa wa Arusha, hivi karibuni.

Waliotuma salamu hizo kwa Dokta Shein ni pamoja na Katibu Mkuu wa CUF, ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Raisi wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, alipohutubia Mikutano ya Hadhara ya Jimbo la Bububu, Magogoni, Ole, na pia alipoongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari, Mjini Unguja, hivi karibuni.

Waliowahi kupaza sauti hiyo kwa Raisi Dokta Shein, ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha Wakulima, Bw. Said Soud Said, ambaye alisisitiza hatua ya kuwawajibisha watu wote waliochafua Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu, wa Tarehe 16, Septemba, 2012, ambao ni pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Serikali, Wakuu wa Vikosi vya Serikali ya Zanzibar, Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na Watendaji wote wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, ZEC.

Pamoja na hao, Wasomi,

Wa n a n c h i , Vi o n g o z i w a Taasisi za Dini, na Wanasiasa, walimtumia Waraka Maalumu, Raisi Dokta Shein, kumtaka pia yeye na Serikali anayoiongoza, k u t a m b u a m s i m a m o w a Umma wa Wazanzibari, juu ya Mapambano yao ya Kuitetea mamlaka Kamili ya Zanzibar , Kitaifa na Kimataifa.

Hatua hiyo il i tangazwa kufanikishwa rasmi na Kamati Maalumu ya Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar , chini ya Mwenyekiti wake, Muasisi wa Mapinduzi ya Mwaka 1964, Mzee Hassan Nassor Moyo, katika Kongamano la Kujadili Mmarekebisho ya Katiba na Hali ya Siasa, lililoandaliwa na kamati hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Hoteli ya Bwawani, Mjini hapa.

“Nakwambieni waheshimiwa t u m e s h a t u m a s a l a m u n a msimamo wetu kwa Wakuu wa Serikali hii kwamba wananchi wanachotaka ni ahadi ya kuitetea Zanzibar na hiyo itawezekana kupitia Muungano wa Mkataba

wala si vingenevyo hivyo ndivyo tutakavyo”, alisema Mzee Moyo.

Pamoja na misitizo huo takriban wachangiaji wote wa kongamano hilo huku wakisikika kuhamasisha ile kauli isemayo “Zanzibar Kwanza”, walikarir iwa wakimtumia salamu Raisi Dokta Shein kumtaka awachukulie hatua na kuwadhibiti Watendaji na Wasaidizi wake wote walioitwa ‘vitimbakwiri’ wasio unga mkono Maridhiano ya Kisiasa ya Zanziba, na pia waliodaiwa kutishia juhudi za Wazanzibari kupigania Utaifa wao.

“ T u n a s e m a h a w a n i v i t imbakwir i ha tar i sana wasioitakia mema Zanzibar ”, alisema Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalumu wa Serikali ya Zanzibar , Bw. Mansour Yussuf Himid, katika kauli ambayo mara kadhaa baadhi ya Viongozi akiwemo Mhe. Jussa wakiikariri na kukoleza hamasa za wananchi pale aliposema “hawa ni wale vitimbakwiri mabalozi wakaazi ndani ya Zanzibar ”.

WA I S L A M U n c h i n i , wametakiwa kujifunza na kuifahamu kikamilifu ibada ya Hijja kabla ya kuiende ili waweze kufikia lengo lililokusudiwa na Mwenyezi Mungu kupitia nguzo hiyo.

Hayo yamebainishwa na Sheikh Hashimu A. Rusaganya, akiongea na An nuur, mapema wiki hii, katika Ofisi za Taasisi ya Hidmat Islamiya Charitable Society, inayoshughulika na kusaf i r isha Wais lamu wanaokwenda Kuhiji Makka.

Hashim amesema, Waislamu walio wengi hawapati fursa ya kuisoma na kujifunza nguzo hiyo mpaka pale wanapo amua kwenda Hijja, na kwamba mafunzo/semina wanazopata kwa muda mchache zinakuwa hazikidhi haja kwa wengi.

Sheikh Rusaganya, aliye kiongozi mwandamizi wa Taasisi hiyo, alikuwa akifafanua sababu mbalimbali zinazosababisha Waislamu wengi kutofikia lengo la Hijja pamoja na kuitekeleza ibada hiyo, ambayo hufanywa

Someni Hijja kabla ya kuhijiNa Bakari Mwakangwale kwa yule tu aliyejaaliwa uwezo

wa kifedha.Aidha, alisema kutokana na

uzofu wake, amebaini kuwa tatizo lingine ni kuwa Waislamu wengi hivi sasa wanapewa ghafla ya kwenda Hijja, jambo ambalo haliwezi kumjenga Muislamu kuiendea ibada hiyo kikamilifu.

“ Wa i s l a m u w e n g i w a Kitanzania wanapewa ghafla ya Hijja, kuna watu wanawapa pesa Waislamu dakika za mwisho, huyu Muislamu atawezaje kujiandaa, mwenendo huo sio mzuri, kwani wanakuwa wanahij ishwa kwa ghafla maandalizi yake ya kuiendea ibada hiyo yanakuwa duni au anayakosa kabisa.” Alisema.

Akifafanua zaidi alisema, Muislamu huyo aliyepata ghfla ya Hijja, akili yake kisaikolojia inakuwa haiko sawa, hivyo hatoweza kukamata mafundisho ya ibada ya Hijja kwa muda mchache.

Alisema, hana maana ya kuwa wanaowazesha Waislamu kwenda Hijja, wanakosea, ila aliwataka waendelee na mwenendo huo lakini wazingatie muda wa kutoa ili kuwapa fursa watu wao kujiandaa kwa ibada

hiyo.Awali, Sheikh Rusaganya,

alisema ibada ya Hija ni moja ya nguzo tano za Uislamu, hivyo ni vyema Waislamu wakaipa uzito kama ilivyo katika nguzo nyingine, pindi wanapopata uwezo wa kuitekeleza nguzo hiyo.

Alisema, unapokwenda kuhiji unakuwa umemtii Mwenyezi Mungu, kwa sababu hiyo ni amri yake.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo Sheikh Muhsin Mohammed Hussein, alisema jumla ya Waislamu 164, wamejiandikisha kwa ajili ya kwenda kuhiji Hijja ya mwaka huu.

Hivi sasa waislamu wake kwa waume duniani kote wanaelekea nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya Uislamu, ambayo ni Ibada ya Hijja.

J i j i n i Da r e s Sa l aam, Mahujaji waliaza kuondoka kuelekea Saudi Arabia, siku ya Jumanne wiki hii ambapo taasisi mbalimbali zimekuwa zikifuatilia ratiba ya mahujaji wao kwa ajili ya kuwasafirisha kwenda kutelekeleza ibada hiyo tukufu.

Page 16: ANNUUR 1038

16 AN-NUURDhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 12-18, 2012

Usikose nakala yako ya

AN-NUUR kila Ijumaa

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa linalotarajiwa kuanza hivi karibuni hapa Zanzibar.

Maalim Seif amesema kuwa suala la vitambulisho limekuwa na umuhimu wa kipekee duniani katika kutunza kumbukumbu na mipango ya kitaifa, hivyo wananchi wasipuuze kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho hivyo.

“Wananchi tafadhal ini m u s i p u u z e , n e n d e n i mukajiandikishe ili mupate vitambulisho vya Taifa, na nakwambieni mukija mukipuuza mutakuja juta baadae”.

Alitahadharisha Maalim Seif na kuongeza akisema, “hivi sasa tunasikia kuna baadhi ya maeneo wananchi waliokataa kuhesabiwa katika sensa ya watu na makaazi

Seif ahimiza wananchi kuchukua vitambulisho

iliyomalizika hivi karibuni nchini kote, hawapatiwi huduma katika maeneo yao, kwa hivyo nakunasihini sana wananchi musipuuze kabisa”.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa CUF na wananchi baada ya kufungua tawi la Chama hicho katika jimbo la Magogoni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Aidha Maalim Seif aliwaonya watenda j i wanaoende lea kuwahangaisha wananchi wakati wanapoomba kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi kuwa, kuwa wanakwenda kinyume na maagizo ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohd Shein, na kwamba watachukuliwa na hatua za kisheria kwa kukaidi amri hiyo.

Amesema, katika baadhi ya maeneo yakiwemo mikoa ya Pemba pamoja na Mkoa wa Kaskazini Unguja, hali ya

upatikanaji wa vitambulisho hivyo imekuwa ikienda vizuri lakini tat izo kubwa zaidi limekuwa likijitokeza katika Mkoa wa Mjini Magharibi, jambo ambalo halitofumbiwa macho.

“Vitambulisho hivi ni haki ya kikatiba ya kila Mzanzibari a l i y e t i m i z a m a s h a r t i y a ukaazi, leo anajitokeza sheha anawaambia wananchi kuwa hatoi barua hadi mtu atimize umri wa miaka 50”, alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF huku akitaka kupatiwa jina la sheha huyo.

Amewataka watendaji wa ofisi ya vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kufanya kazi kwa uadilifu na kuepuka kutumiwa vibaya na viongozi kwa maslahi ya kisiasa.

“Unapomkosesha mwananchi kitambulisho unakusudia nini, huu ni ukiukwaji wa katiba na l az ima tuukomeshe” , aliongeza.

Akizungumzia kuhusu nia ya kujiuzulu kwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Ismail Jussa Ladhu, Maalim Seif amewathibitishia wanachama juu ya ukweli wa jambo hilo, na kuwataka wasifadhaike kwani anafanya hivyo kwa nia njema.

“Jussa bado ni mwanachama kindakindaki wa CUF na ni mjumbe wa Baraza Kuu la

Uongozi ndani ya Chama chetu, lakini baada ya kutuletea maoni yake nikiwa mimi, Profesa Lipumba na Makamu Mwenyekiti Mhe. Machano Khamis, tuliona sababu zake ni za msingi na hakuna haja ya kumzuia kutimiza maamuzi yake”, alisema.

Amesema, ifikapo tarehe 10 mwezi huu, Jussa atakuwa si Naibu Katibu Mkuu tena wa Chama hicho, na kwamba viongozi wanatafakari juu ya kumpata mwanachama atakae kaimu nafasi hiyo.

Ametaja sababu za msingi zilizotolewa na Jussa kutaka kujiuzulu kuwa ni pamoja na kumuwezesha kupata muda wa kutosha kushugulikia maendeleo ya jimbo lake la Mji Mkongwe pamoja na kufanya utafiti kabla ya kuibana serikali katika vikao vya Baraza la Wawakilishi.

Kat ika Mkutano huo, Maalim Seif alikabidhi baiskeli tisa kwa ajili ya makatibu wa matawi ya CUF katika Jimbo la Magogoni, kigari kwa ajili ya bwana Ali Khamis Ali (mwenye ulemavu), pamoja na shilingi laki tatu kwa ajili ya kikundi cha ushirika cha Jimbo hilo.

(Habari kwa hisani ya Hassan Hamad (OMKR).

BARAZA la Mit ihani nchini NECTA limekataa k u t a m b u a v y e t i v y a w a n a f u n z i w a w i l i waliomaliza kidato cha nne katika nchi ya Falme za Kiarabu- UAE.

Aisha Mohamed Ali Al-Falahi na mwenzake Maryam Abdul Seif, mabinti wa Kitanzania ambao walikuwa wakisoma UAE, walirejea nchini baada ya kuhitimu kidato cha nne na kutaka kujiunga na vyuo vya elimu ya juu katika vyuo vya hapa nchini.

Hata hivyo kabla ya kujiunga na vyuo vya hapa nyumbani, waliandika barua kuliomba Baraza la Mitihani nchini NECTA kuhakiki vyeti vyao na kukadiria uwiano wa vyeti vyao vilivyotolewa UAE kulingana na hadhi ya vyeti vya hapa nchini ili waweze kujiunge na vyuo vya elimu ya juu nchini.

Akizungumza na An-nuur jijini Dar hivi karibuni, M z a z i w a A i s h a B w. Mohammed Ali, alisema kuwa awali Baraza lilitoa fomu za kujaza (application form) na kuwapatia wanawe ili wazijaze na kuzirejesha ofisi za Baraza pamoja na kulipia gharama za uhakiki ambazo ni shilingi 20,000 na vyeti vyao vya matokeo ya kitaaluma yaani- Academic Certificates, zoezi ambalo walilikamilisha na kusubiri majibu ya Baraza.

Alisema Aisha Mohamed na Maryam Abdulla, wote waliomba huduma hiyo ya Baraza kupitia barua zao za Septemba 11, 2012.

Kulingana na taarifa za vyeti vyao, Aisha alimaliza

NECTA wakataa vyeti vya Waarabu

Na Shaaban Rajab

Inaendelea Uk. 15

KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa CUF na wananchi baada ya kufungua tawi la Chama hicho katika jimbo la Magogoni Wilaya ya

Magharibi Unguja.