34
MAFUNDISHO YA UMISHENI MISIOLOJIA Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza kwa mada hiyo. I. Tafsiri ya Misiolojia II. Lengo la Kiuzi Hiki III. Viunganishi IV. Wamisheni ni Nani? V. Theologia ya Umisheni VI. Historia ya Umisheni VII. Tamaduni za umisheni VIII. Mkakati wa Umisheni IX. Kutazama Taswira ya Umisheni X. Kazi ya Kusoma Uliyopewa XI. Bibliografia Haki ya Kunakili © 2008 Shirika la Mafunzo ya Umisheni. Haki Imehifadhiwa.

MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

  • Upload
    vudiep

  • View
    380

  • Download
    5

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MAFUNDISHO YA UMISHENI

MISIOLOJIA

Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza kwa mada hiyo.

I. Tafsiri ya Misiolojia

II. Lengo la Kiuzi Hiki

III. Viunganishi

IV. Wamisheni ni Nani?

V. Theologia ya Umisheni

VI. Historia ya Umisheni

VII. Tamaduni za umisheni

VIII. Mkakati wa Umisheni

IX. Kutazama Taswira ya Umisheni

X. Kazi ya Kusoma Uliyopewa

XI. Bibliografia

Haki ya Kunakili © 2008 Shirika la Mafunzo ya Umisheni. Haki Imehifadhiwa.

Page 2: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

I. Tafsiri ya Misiolojia

Misiolojia ni masomo ya umisheni. Neno umisheni lina maana ya “kutumwa nje kwa mamlaka ya kufanya kazi maalum 1.” Wamisheni wa Kikristo huhusika hasa kwa kueneza Ukristo kutoka kwa tamaduni moja hadi nyingine. Kwa hivyo mishiolojia, kutokana na mtazamo wa Kikristo ni “Sayansi ya kueneza imani ya Kristo katika tamaduni tofauti 2."

1 Webster’s New World Dictionary, College Edition, s.v. “mission.” 2 http://mb-soft.com/believe/txo/missiolo.htm

RUDI KWA MUHTASARI

Page 3: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

II. Lengo la Kiuzi Hiki

Baada ya kusoma kiunzi hiki cha mafundisho,unafaa:

• Kujua kufafanua misiolojia na umisheniri

• Kujua baadhi ya wavuti muhimu kwa kazi ya umisheni

• Kujua lengo tatu za msingi za umisheni

• Kupitia mpango wa Mungu kwa umisheni katika Agano la Kale na Agano Jipya

• Kujua ni wapi Maandiko yanapatikana yanayo husika na umisheni katika Agano la Kale na Jipya

• Kutambua mpango wa Mungu wa kuleta haki

• Kuelewe mateso na tuzo la kuwa mmisheni

• Uelewe enzi tatu za umisheni tangu wakati wa Kristo

• Kujua wamisheni wa Kiprotestanti watano na mchango wao katika umisheni

• Kujua tafsiri ya tamaduni

• Kuelewa umuhimu wa kuweka injili katika mazingira yetu

• Tambua vizuizi vya kitamaduni kwa injili

• Kuelewa sehemu tatu za msingi za kutafsiri mwendo wa kuanzisha makanisa

• Kujua sehemu za hila zinazo ruhusu mwendo wa kuanzisha makanisa kufanyika

• Kuelewa vizuizi vya mwendo wa kuanzisha makanisa

• Kuwa na uwezo wa kupangia umisheni na kundi la watu wa kufanya uinjilisti

• Kuelewa umuhimu wa kuona taswira katika umisheni

RUDI KWA MUHTASARI

Page 4: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

III. Viunganishi

Kwa habari kwa jumla kuhusiana na misiolojia, tazama:

http://mb-soft.com/believe/txo/missiolo.htm

Kwa habari kuhusu theolojia ya umisheni, tazama :

http://www.imb.org/core/biblicalbasis/

http://www.mislinks.org/topics/theology.htm

Kwa kamusi ya misiolojia na habari zingine za umisheni, tazama:

http://missiology.org/Default.htm

Kwa Biblia na njia zingine za mawasiliano za Kikristo katika lugha tofauti, tazama:

http://www.ethnicharvest.org/bibles/

Kwa habari zaidi kuhusu makundi ya watu tofauti katika mataifa tofauti, tazama:

http://www.joshuaproject.net/index.php

Kwa habari zaidi kuhusu kueneza injili kwa njia ya kusimulia hadithi, tazama :

http://chronologicalbiblestorying.com/

Kwa ripoti za uhuru za kidini, tazama wavuti ilioko hapo chini. Elekeza mada kwa mwaka ulioko, na kama hakuna ripoti ya wakati huo kuhusu nchi ambayo unapenda , endelea kutazama kila mwaka uliotangulia mpaka upate ripoti.

http://www.state.gov/g/drl/irf/rpt/

RUDI KWA MUHTASARI

Page 5: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

IV. Wamisheni ni Nani

Kwa mapana, yeyote anaye eneza injili kwa tamaduni mbalimbali ni mmisheni. Wakristo wote wanafaa kutii Tume Kuu ili kuwafanya watu kuwa wanafunzi, na Wakristo wengine wana nafasi ya kufanya wanafunzi kutoka kwa watu wa tamaduni mbalimbali (tazama Mathayo 28:18-20). Wakristo wanapoendelea na shunghuli zao za kila siku, wanaweza kueneza injili kwa watu wa tamaduni mbalimbali. Kiunzi hiki cha mafunzo kina msingi wa kuwahutubia wamishenari ambao wameitwa na Bwana kuyakabidhi maisha yao kwa kazi za umisheni. Kabla ya kwenda nje kwa umisheni, mmisheni anafaa kuwa amepata mwito wa umisheni (tazama kiunzi cha mafunzo kiitwacho “Mwito kwa misheni”). Kama Bwana hajamuita mmisheni, mmisheni hatafaulu ama hataridhika. Tunahimiza wamisheni waende kwa makundi ya wawili ama zaidi. Ukiwa na mwenzio ama wenzio huleta usalama, kuhimizana, na kuzidisha nafasi ya misheni kufaulu. Mtume Paulo alienda na mtu au watu zaidi kwa kazi ya umisheni (tazama Matendo 13:2,3). Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili wawili kuinjili (tazama Luka 10:2). Ni muhimu kuwa mmisheni aliyekomaa kiroho akifanyia uanafunzi mmisheni mwanafunzi asiyekomaa kabisa kiroho. Yesu alizungukwa na wanafunzi kumi na wawili walio safiri naye, na kujifunza kutoka kwake. Kundi la wamisheni laweza kuwa na bwana na bibi. Kama jamii hii ya wamisheni wana watoto, watoto hao wataandamana na wazazi wao. Kundi la wamisheni laweza kuwa na wanaume wawili ama wanawake wawili. Sehemu zingine za umisheni huhitaji wanaume na zingine wanawake. Wamisheni wanahitaji mafunzo kabla ya kwenda kufanya umisheni. Wavuti huu unatoa mafunzo mengi yanayohitajika, na kukuunganisha na wavuti zingine muhimu. Kwa kuongezea, wamisheni wanafaa kupata mafunzo kutoka kwa Wakristo wenyewe. Uanafunzi huu unaweza kutoka kwa shirika la umisheni, kanisa la mahali, familia ya kikristo, ama kutoka kwa washauri wa Kikristo.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 6: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

V. Theolojia ya Umisheni

Kitabu cha Biblical Basis for Missions, kilichoandikwa na Avery Willis na kinachopatikana katika mtandao, kimetoa muhtasari wa Theolojia ya umisheni. Elekeza mada katika kiunganisho hiki ili uweze kusoma kitabu hicho:

http://www.imb.org/core/biblicalbasis/ A. Kusudi la Umisheni

Kusudi la kwanza la umisheni ni kumtukuza Mungu, la pili, kuwafanya watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi; na la tatu kushinda maovu ili kupanua ufalme wa Mungu.

1. Kumtukuza Mungu

Kusudi la kwanza la umisheni ni kuwaleta watu katika uhusiano mwema na Mungu ili Mungu atukuzwe. Kumtukuza Mungu kuna maana ya kumwabudu na kumtumikia. Injili inapoenezwa duniani kote, watu wa tamaduni tofauti katika kila nchi humpa Mungu utukufu. Kristo alimtukuza Mungu kwa kufa ili kuwaokoa waliopotea (Tazama Luka 19:10; Yohana 13:31). Yesu alimtuma Mtume Petro kuongoza kanisa na kufa kifo cha ushahidi. Katika kifo chake, Petro atamtukuza Mungu (Tazama Yohana 21:19). Kanisa ni mwili wa Kristo. Wayahudi na watu wa Kimataifa, wote pamoja wanaunda kanisa, na wote pamoja wanamtukuza Mungu (Tazama Warumi 15:5,6).

2. Kuwafanya Wote Kuwa Wanafunzi Kusudi la pili la umisheni ni kuwaleta watu katika wokovu. Ahadi kwa Ibrahimu inasema kuwa kupitia kwa uzao wake, jamaa zote za dunia watabarikiwa (tazama Mwanzo 12:2,3). Kristo, uzao wa Ibrahimu, kupitia kwa Mariamu, alibariki watu wote kwa kufa kwa ajili yao ili kuwaokoa kutoka kwa hukumu. Tume Kuu kwa kanisa ni kushiriki Habari Njema ya ukombozi mpaka mwisho wa dahari (tazama Mathayo 28:18-20; Matendo 1:8). Injili ikienezwa duniani kote, mwisho wa dunia utafika (tazama Mathayo 24:14). Kanisa hufanya wanafunzi, ambao hutukuza Mungu. Ni jambo la muhimu tueneze Habari Njema ya Kristo, kwa sababu Biblia inafundisha kuwa Yesu ndiye njia ya pekee ya wokovu (tazama Matendo 4:12). Maandiko yanakanusha wingi – wazo la kuwa kuna mungu wengi ambao wanaweza kuokoa; na pia inakanusha falsafa ya kiulimwengu – wazo kuwa watu wote wataokolewa kupitia kwa upatanisho wa Mungu na mwanadamu kupitia kwa maisha na kifo cha Kristo. Ni muhimu watu wajifunze ukweli wa Maandiko, na ni kazi ya kanisa kushiriki Habari Njema.

Page 7: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

3. Kupanua Ufalme wa Mungu – Kushinda Maovu

Kusudi la tatu la umisheni ni kupanua ufalme wa Mungu, kushinda giza na na maovu ya utawala wa Shetani.Ufalme wa Mungu ulianzishwa wakati Yesu alikuja mara ya kwanza. Kanisa inafanya umisheni wa kupanua ufalme wa Mungu duniani kote. Yesu alifundisha wanafunzi kuomba kuwa ufalme wake uje na mapenzi yake yatimizwe hapa (tazama Mathayo 6:10). Yesu anakuja tena kuondoa maovu duniani, na kuanzisha utawala wake mtimilifu (tazama “ufalme wa Mungu” katika kiuzi cha “Theolojia”). Kusudi la tatu la umisheni linafanana na kusudi la pili—kanisa linafanya watu kuwa wanafunzi ili kupanua ufalme wa Mungu. Lakini kusudi la tatu linasisitiza vita kati ya mema na mambaya. Ufalme wa Mungu unapoendelea kupanuka, wema unapanuka katika mataifa. Katika kipinga haya, maovu yanakua kama vile idadi ya watu inavyoongezeka. Kukiwa na silaha mpya, kupunguka kwa rasilimali za ulimwengu na shughuli za kigaidi, ulimwengu unaendelea kuwa mahali pa hatari kubwa. Wamisheni wakiendelea kukambiliana na maovu, Shetani na ufalme wake wataangushwa na kurudi kwa Kristo. Willis aliandika kuwa kanisa inapoendelea kueneza Injili ulimwenguni, hekima ya Mungu inaonyeshwa kwa viongozi wa kiroho:

“Ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo na namna nyingi ijulikane na falme ana mamlaka katika ulimwengu wa roho” (Waefeso 3:10 ).

Mungu hupokea utukufu kanisa linapomtii na kushinda maovu duniani kote. 3

B. Umisheni katika Agano la Kale

Mungu alitaka watu wake wateule – wana wa Israeli – watumike kama wamisheni kwa mataifa yale mengine. Kama waakilishi wa Mungu, walitakiwa kumtii. Mara nyingi, walikosa kumtii, kwa hivyo mara nyingi walikosa nafasi ya kushuhudia kwa niaba ya Mungu. Twaweza kujifunza kutoka kwa haya; ni lazima tumtii Mungu ili tushuhudie kwa niaba yake. Na tutasame baadhi ya mifano ya mpango wa Mungu kwa umisheni nyakati za Agano la Kale.

1. Makuhani wa Ufalme — Agano la Musa.

Mungu aliahidi wana wa Israeli kuwa wakimtii, atawafanya kuwa taifa la makuhani. Kwa maneno mengine, watatumika kama wapatanishi kati ya Mungu na mataifa mengine. Kama vile imeandikwa katika Agano la Musa, ulimwengu mzima (taifa zote) ni mali ya Mungu, lakini Wayahudi walikuwa na nafasi ya kutumika kama wamisheni katika mataifa mengine.

Page 8: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

5 sasa basi ikiwa mtatii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. ( Kutoka 19:5,6 union Version).

Wana wa Israeli hawakuweka ahadi ya Musa, kwa hivyo walipoteza nafasi ya kuwakilisha Mungu kwa mataifa mengine.

2. Yona Nabii Yona aliamrishwa kwenda na kuonya mji wa Ninawi juu ya hukumu ya Mungu iliyokaribia. Mungu alitukuzwa kwa sababu alimtuma Yona akalete watu wa Ninawi katika toba. Kwa huruma yake, Mungu hakuwahukumu wana wa Ninawi wakati huo (tazama Yona 1:1,2; 4:11). Lakini Yona hakutaka kutumika kama mmisheni. Mara ya kwanza alitoroka wito wa Mungu. Hata baada ya kutubu na kwenda Ninawi, hakufurahia kuwa wana wa Ninawi walikuwa wameacha njia zao mbaya na Mungu alikuwa amewaondolea hukumu. Watu wa Ninawi walikuwa maadui wa Yona. Kama wamisheni wa siku hizi, tumeitwa kushuhudia hata maadui zetu.

3. Sulemani Akiweka Wakfu Hekalu Wakati Sulemani aliweka wakfu hekalu kwa aliomba Mungu aweze kusikia maombi ya watu wa mataifa kutoka nchi mbali mbali, ili watu wote waweze kujua na kuogopa Mungu.

41 "Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wa Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako; - 42 maana watasikia habari za jina lako kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa – atakapokuja na kuomba kuielekea nyumba hii; 43 basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo, ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako wa Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako. (1 Wafalme 8:41-43).

Sulemani aliongea kulingana na mapenzi ya Mungu ya kuabudiwa na watu wa mataifa yote. Aliomba Mungu aweze kujibu maombi ya wageni ili watu wote waweze kujua na kuogopa Mungu.

Page 9: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

4. Mungu Anataka Kuokoa Watu Wote wa Dunia. Mkataba wake na Ibrahimu ulionyesha mapenzi ya Mungu ya kubariki watu wote wa dunia. 1 Bwana akawambaia Ibrahamu, “Toka wewe katika nchi yako, na

jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.

2 "Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe Baraka. 3 Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa." (Mwanzo 12:1-3). Mungu aliahidi kutuma masihi (kutoka ukoo wa Yuda) kuleta mataifa kwa utiifu. 10 Fimbo la enzi halitaondoka kutoka Yuda,

Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja yeye, mwenye milki ambaye mataifa watamtii. (Mwanzo 49:10).

Masihi ataleta wokovu si kwa wana wa Israeli pekee, hata kwa watu wa Mataifa. 1 Mungu na atufadhili na kutubariki,

Na kutuangazia uso wake.

2 Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. (Zaburi 67:1, 2 ).

6 naam, asema hivi:

"Ni neno dogo sana wewe kama mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia." (Isaya 49:6)

Masihi atatawala watu wote wa mataifa milele. 13 "Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa

mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake na mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. (Danieli 7:13,14 ).

Page 10: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

5. Mungu hutaka kuleta hukumu kwa mataifa. Watu wa Mungu wanatakiwa watafute haki siku hizi. 15 nanyi mkunjuapo mikono yenu,

nitajificha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia. Mikono yenu imejaa damu;

16 Jiosheni, jitakaseni.

Ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu! Acheni kutenda mabaya,

17 jifunzeni kutenda mema!

takeni hukumu na haki, wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake, mteteeni mjane. (Isaya 1:15-17).

Kama vile Isaya, nabii Amosi alitaka haki itendeke. 24 Lakini hukumu na itelemke kama maji,

na haki kama maji makuu! (Amosi 5:24 ). Ni kurudi tu kwa Masihi ambako kutaleta haki na amani kamili. 6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake. Naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.

7 Maongezi ya enzi yake na amani

hayatakuwa na mwisho kamwe. Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake, kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki, tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo. (Isaya 9:6,7)

C. Umisheni katika Agano Jipya

Kwa sababu wana wa Israeli walikosa kuwa makuhani wa ufalme, Kristo alitoa njia kwa watu wa mataifa kuwa makuhani. Kristo alikufa kama fidia ya dhambi zetu, na hutumika kama mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu. Kwa hivyo wale ambao hutubu na

Page 11: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

kumwamini Kristo husamehewa dhambi. Kwa sababu Wakristo wamesamehewa dhambi zao, waweza kutumika kama makuhani ambao wanawaambia wengine kuhusu Mungu

1. Yesu Haikuwa kusudi la Yesu kutumika kama mmisheni katika mataifa wakati alikuwa katika

mwili wa kibinadamu. Lengo la Yesu lilikuwa kuleta ujumbe wa wokovu kwa Wayahudi. Lakini kulikuwa na tukio za kipekee ambapo Yesu alishiriki Habari Njema nje ya tamaduni za Kiyahudi. Kwa mfano, Yesu aliongoza Wasamaria (Wayahudi ambao walikuwa wameolewa katika tamaduni zingine ) kwa imani (tazama Yohana 4:39-41). Badala ya kuinjilia watu wa mataifa, Yesu alifundisha wanafunzi kuwa wamisheni. Yesu alikuwa mfano bora kwa waanzilishi wa makanisa. Alionyesha mfano wa jinsi ya kuwafanya wanafunzi, kufanya uinjilisti, kuhubiri, kufundisha, kuchunga kondoo wake (kushughulikia wanafunzi wake). Alifundisha kwa mfano, kuwafundisha wanafunzi wake kufuata mwongozo wake. Alienda pamoja na wanafunzi wake, akiwapa nafasi ya kumtazama kila siku. Yesu alifunza wanafunzi wake kutumia yale waliyojifunza.

2. Mitume na Tume Kuu

Neno mtume linatoka kutoka kwa neno la Kigriki lenye maana “aliye tumwa”. 4 Katika Tume Kuu, Yesu aliamuru Watume kumi na mmoja waende na kuyafanya mataifa yote kuwa wanafunzi (Mathayo 28:19). Kwa kweli hao kumi na mmoja hawangeweza kufanya kazi yote, kwa hivyo ilimaanisha , Tume Kuu inatumika kwa wafuasi wote wa Yesu.

3. Mtume Paulo Yesu alimtokea Paulo wa Tarso (aliyekuwa Paulo) kama mwangaza, na kumwongoza kuwa mmisheni wa kwanza kwa watu wa mataifa. (Tazama Warumi 11:13). Kwa kipindi cha miaka mingi, Paulo alienda katika misheni tatu katika tamaduni za Greco-Roma ambazo zilizunguka Bahari ya Mediterania. Paulo alieneza ujumbe muhimu wa Injili bila kutaka watu wa Mataifa kuzingatia matendo ya kidini ya Kiyahudi. Paulo aliweka mfano kwa wamisheni kulenga makundi ya watu wasiofikiwa. 20 Kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la

Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.

21 Bali kama ilivyoandikwa:

"Wale wasiohubiriwa habari zake wataona, Na wale wasiojasikia watafahamu" (Warumi 15:20, 21 ).

Leo hii, wengi wa wamisheni wanafanya ka zi kati ya watu ambao wameshasikia kuhusu Kristo. Hitaji kubwa ni kwa wamishen i waweze kufuata mwongozo wa Paulo, waende kwa watu ambao hawajasikia Kristo akitajwa.

Page 12: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

4. Wakristo Wengine

Baada ya kumpiga Stefano mawe, Wakristo waliteswa Yerusalemu, kwa hivyo wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, wakihubiri Injili mahali kote walipoenda (tazama Matendo 8:1-4). Wanafunzi wa kwanza walihubiri Injili walipokuwa wakitoka Israeli. Kwa mfano Prisila na mumewe Akila walikuwa mashahidi wa Kristo Korintho (Matendo 18:1, 2), Efeso (Matendo 18:24-26), na Rumi (Warumi 16:3).

5. Mungu Aliahidi Kuwa Umisheni Utafaulu.

Mungu aliumba nchi mpya.

Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. (2 Petro 3:13 ).

Kristo atarudi kutawala nchi uliyofanya upya.

19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako Bwana, 20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani. 21 Ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu. (Matendo 3:19-21).

Wamisheni watafaulu kueneza injili duniani kote.

Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. (Mathayo 24:14).

Watu wa makabila yote wataabudu Mungu.

9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao. 10 Wakilia kwa sauti kuu wakisema: "Wokovu una Mungu wetu, aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo." (Ufunuo 7:9, 10 ).

Tukiwa na hakikisho kuwa umisheni utafaulu, ni jukumu letu kutii mwito wa kufanya kazi ya umisheni. Mungu atatusaidia kutimiza yale anayotaka tutimize.

Page 13: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

6. Wamisheni Watateseka na Watazawadiwa.

Wamisheni watateseka na watapata zawadi kubwa. Mtu anapoitwa katika kazi ya umisheni, atateswa, lakini atapata furaha ya kumfuata Kristo. Atakosa kuwaona jamii zake, lakini atapata jamii ya kiroho kati ya wale atakaoongoza kwa Kristo. Anaweza kuwacha nyumba yake, lakini atakaribishwa katika nyumba za Wakristo walio katika umisheni. Anaweza kuwacha kazi yake ambayo ilimpa riziki, na kupata shughuli ambayo inamletea raha na inamtosheleza. Mtu anapoitwa katika umisheni, atatambua yale anayoweza kufanya na kupata amani kwa kuitikia wito wa umisheni.

29 Yesu akasema, “Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, 30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, (nyumba, ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba - pamoja na udhia) na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. (Marko 10:29, 30).

Dhiki za Mkristo huleta uthabiti wa moyo na kuleta Wakristo karibu na Mungu.

3 Wala si hivyo tu, ila namfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; 4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini. 5 Na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Matakatifu tuliyepewa sisi (Warumi 5:3-5).

7. Hakikisho ya Wamisheni Waaminifu. Kumbuka sisi ni nani: watu walioitwa kumwakilisha Kristo. Kwa hivyo tuwe wanyenyekevu na watiifu.

1 Kwa hivyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa. (Waefeso 4:1).

Tukiepuka dhambi—hasa uasherati na tabia ya kupenda pesa – Mungu atakuwa pamoja nasi wakati wote.

4 Ndoa na iheshimiwe na wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. 5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sitakupungukia kabisa; wala sitakuacha kabisa.” 6 hata twathubutu kusema, "Bwana ndiye anisaidiaye; sitaogopa. Mwanadamu atanitenda nini?" (Waebrania 13:4-6).

Page 14: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

Kristo huwa na wamisheni wakati wote. 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza

kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” (Mathayo 28:19, 20).

3 Tazama “ To Display the Wisdom of God to Evil Powers” katika wavuti

http://www.imb.org/core/biblicalbasis/chapter_1.htm4 Strongs

RUDI KWA MUHTASARI

Page 15: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

VI. Historia ya Umisheni 5

A. Kanisa la Kwanza

Wakristo wengi wa kwanza waliteswa chini ya utawala wa Kirumi. Lakini imani na ushahidi wa Wakristo hawa uliwaridhisha Warumi wa karne ya 325, Mfalme Constantino aliliita baraza la Nicaea na akaufanya Ukristo kuwa dini ya nchi6. Wamisheni wa leo wanaweza kujifunza kutokana na mfano wa Wakristo wa kwanza walioteswa. Uaminifu hata wakati wa mateso huleta kukua kwa kanisa.

B. Kanisa la Katoliki

Wakati mwingine kwa historia ya kwanza ya kanisa, kanisa lilishiriki kama Kanisa la Katoliki. Wakatoliki na Waprostetanti hawakubaliani tarehe ya kuanza kwa kanisa la Katoliki. Wakatoliki wanashikilia kwamba msafara wa maaskofu walioongoza kanisa la katoloki unaweza fuatwa nyuma mpaka kwa Mtume Petro unatokana na Mtume Petero. Waprostanti wanakataa wazo hilo na kudai kwamba kanisa liliwekwa chini ya mamlaka ya maaskofu wakuu wa katoliki wa kirumi muda mrefu baadaye. Mambo haya yanayotofautiana yamehutubiwa kwa kina katika wavuti ulio hapo chini. Katika wavuti tazama “Orodha Kamilifu ya Maaskofu Wakuu” na “Cheo chao: Historia yake, mfumo wa imani, mtu mwenye kipaji hicho, na matazamio.”

http://www.spurgeon.org/~phil/catholic.htm

Kanisa la Katoliki lilikuwa kanisa moja lenye nguvu mpaka wakati kanisa la Orthodox la mashariki lilipojitenga na kanisa la Katoliki mnamo mwaka wa A.D. 1054. Mvutano katika kanisa la Katoliki ulifikia kilele wakati wa ugomvi wa filioque (tazama “Imani Nicene ” katika kiunzi cha mafunzo cha “Thiolojia”), na kuleta mgawanyiko. Kulingana na Ralph Winter, Kanisa la Katoliki la Kirumi kwa utaratibu halikufanya mambo mengi kusaidia umisheni kutoka A. D. 400 hadi 1200. Walakini, jitihada za umisheni zisizo za rasmi, wanaojulikana sana ni wainjilisti wa Irish na wafuasi wao wa Anglo-Saxon , walioeneza injili Ulaya. Wasafili walianzisha uga la umisheni ambalo lifanya kazi ya kuweka imani ya Kikristo hai wakati wa vita. Makabila yaliyoshinda, kwanza Wabarbaria na baadaye waviking, walitambaa Ulaya kote na kugeuzwa kuwa Wakristo na halaiki yao mateka. Wakati wa vita hivi, Alfred Mkuu, Mfalme wa Wessex (Ufalme mdogo ulioko kusini na kusini magharibi ambao sasa ni Uingereza), alikubali kuabudu katika lugha ya kiasili ya Anglo-Saxon. Kubadilisha kuabudu kutoka kwa lugha ya kigeni (Latin) hadi kwa lugha ya tamaduni ya pale iliendeleza juhudi za umisheni. 7

Page 16: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

Winter aliandika kwamba kutoka mnamo mwaka wa A.D. 1200 hadi 1600, juhudi mbili za umisheni zilijitokeza. Kwanza, mikutano ya uinjilisti, uliongoza na ukoo wa Vikings, yalikuwa majaribio ya jeshi la askari kutoka kwa utawala wa Kiislamu kunyakua Nchi Takatifu ya Palestino. Huu ulikuwa msiba kwa Wakristo na pia Waislamu8. Kristo huwaalika watu kumfuata kwa hiari yao. Huwa hajaribu kuwalazimisha watu kumuamini. Na kama mtu anataka kubadili dini kutoka kwa Ukristo hadi kwa imani nyingine, huyo mtu ana uhuru wa kufanya hivyo. Kinyume na haya, watu wa imani zingine wanaweza kuwadhulumu, kuwakataa ama hata kuwauwa watu wanaobadili na kuwa Wakristo. Pili, Wafranciscans (Friars) walikuwa wamisheni waaminifu ambao waliendeleza Injili. La kuhuzunisha ni kuwa wengi wa Wafranciscan walikufa wakati thuluthi moja mpaka nusu ya halaiki ya Wazungu walikufa kwa ugonjwa wa Bubonic Plague mnamo karne ya kumi na nne. Kutoka A.D. 1600 hadi 2000, Wamisheni wa Katoliki walisafiri nje ya Ulaya na sehemu mbali mbali ulimwenguni9. Amri za wanawake Wakatoliki wa Kirumi zimesaidia katika kazi ya umisheni duniani.

C. Kanisa la Orthodox la Mashariki

Kanisa la Orthodox la Mashariki ni mkusanyiko wa makanisa katika nchi za mashariki. Makanisa ya Orthodox ya Mashariki ndio makanisa mengi ya Kikristo katika nchi za Belarus, Bulgaria, Georgia, Greece, Macedonia, Moldova, Romania, Russia, Ukraine, na Serbia. Ili kuona nambari ya wafuasi wa Kanisa la Orthodox la Mashariki, Kanisa la Katoliki, na Makanisa ya Kiprotestanti, enda kwa wavuti ufuatao:

http://www.adherents.com/adh_branches.html#Christianity

Kwa muhtasari wa mafikio ya misheni kwa makanisa ya Orthodox ya mashariki, tafuta “misheni, ” kisha angalia “Umisheni wa Orthodox ” katika wavuti ufuatao:

http://en.wikipedia.org

D. Makanisa ya Kiprotestanti

Ralph Winter anafafanua enzi tatu za wamisheni Waprostetanti. Enzi ya kwanza ilikuwa kutoka 1792-1910, ambapo umisheni ulifanyika sehemu za pwani za Afrika na Asia na visiwa vya Pacific. Enzi ya pili ilikuwa kutoka 1865-1980 ambapo umisheni ulifanyika katika sehemu za bara katika maelfu ya sehemu ulimwenguni. Enzi ya tatu ilianza 1934, na inatazamiwa kuwafikia watu wa ulimwengu wasiofikiwa. Kuna makundi ya watu10,000 ulimwenguni. Watu wasiofikiwa wanatofautiana sana katika tabia za kabila, lugha ama tabia za kutangamana kutokana na tamaduni zilizo makanisani ambamo maazimio ya misheni yanatakiwa kuwafikia.10 Makanisa mapya yaweza kuanzishwa nchini kote, na yakose kuwafikia watu fulani. Makanisa yaliyo mahali fulani yanaweza kuwa yanawafikia maskini, na yakose kuwafikia matajiri. Makanisa yaliyoko yanaweza kuwa na watu wa lugha moja, na kuwatenga watu

Page 17: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

wa lugha nyingine. Makanisa yaliyomo yanaweza kuhusisha kabila moja, na kuitenga kabila yenye historia ya uhasama kwa kabila hili la kwanza. Winter anaandika kwamba kabla ya mwaka wa 1792, wamisheni Waprostanti walikuwa wadogo sana. Tangu wakati huo, wanaume wanne walichukua jukumu la kuendeleza kazi ya umisheni ya Waprotestanti. Kwanza, William Carey, mwanamume wa Kiingereza katika miaka yake ya ishirini, aliandika “Akiuliza Wajibu wa Wakristo Kutumia Mbinu za Kuwabadili Kafiri.” Uchambuzi huu uliochapishwa mwaka wa 1792, uliwahimiza baadhi ya marafiki za Carey kujiunga naye na kuunda shirika dogo la umisheni ambayo baadaye lilikuja kujulikana kama Shirika la Umisheni ya Kibatisti. Carey alikuwa na uwezo wa kifedha kwa hivyo alitumika kama mmisheni karibu na Calcutta, India. Kijitabu chake kidogo kiliwatia moyo wengine kuanzisha mashirika ya kimisheni huko London, Scotland, Holland, England, na United States. Waprostanti walijifunza kutoka kwa Carey kwamba mashirika ya kimisheni yanahitajika ili kufanikisha Tume Kuu. Kama vile Umisheni wa Katoliki wakati wa enzi za katikati haukufanikishwa hasa na parokia za mtaa bali kwa amri za watawa, kwa hivyo makundi ya wamisheni wa Kiprotestanti, mbali na makanisa ya mtaa, yalitumika kufanya umisheni ya kimataifa. Makanisa ya mtaa na Shirika za Umisheni za Kimataifa ni muhimu katika kutimiza kazi ya kanisa la Kikristo.11 Pili, Hudson Taylor, mwanamume mwingine Mwiingereza katika miaka yake ya ishirini, alianzisha China Inland Mission mnamo mwaka wa 1865. Alifanya kazi kama mmisheni huko China na kuwahimiza wengine kuunda mashirika ya umisheni. Matokeo ya ushawishi wake, ni kuwa zaidi ya mashirika ya umisheni ya imani 40 mapya yalianzishwa. Taylor alianzisha enzi ya pili ya umisheni ya Waprotestanti—inland missions.12 Tatu, Cameron Townsend, mmisheni wa Guatemala, aligandamizwa na hitaji la Biblia katika lugha za dunia. Alitoa Biblia ya Wycliffe Bible Translators mnamo mwaka wa 1942, Townsend, aliweza kutoa Biblia katika lugha za makabila mengi ya mpakani.13 Nne, Donald McGavran, mmisheni kwa nchi ya India kuanzia mnamo mwaka wa 1923, aliandika kuhusu kushinda vizuizi vya ushirikiano katika kueneza injili. McGavran aligundua “vitu vya jinsi moja” vya watu, ambavyo siku hizi vinajulikana kama “makundi ya watu14.” McGavran alianzisha shule iitwayo Shule ya Fuller ya Umisheni wa Dunia mahali paitwapo Seminari ya Theologia ya Fuller.15 Wanafunzi walitumika katika misheni za karne ya kumi na tisa na ya ishirini. Kwa kuvutiwa na maandishi ya William Carey’s, wanafunzi wa chuo watano wa Amerika walikusanyika mnamo 1806 kwa kile ambacho kilikuja kujulikana kama “Mkutano wa Maombi wa Haystack.” Kutokana na mkutano huyo, Shirika la Umisheni la—the American Board of Commissioners of Foreign Missions lilipatikana. Katika miaka ya 1880 na 1890, shirika la Student Volunteer Movement For Foreign Missions lilitoa wamisheni 20,000 wa kimataifa, na watu wakujitolea 80,000 kwa umisheni wa nyumbani.16 Mara nyingi, Wanawake wameongoza sana katika mashirika ya umisheni. Mnamo mwaka wa 1865, wanawake wa Amerika ambao hawajaolewa walipanga kuwatuma wanawake ambao hawajaolewa kama Wamisheni wa Kiprotestanti.17

Page 18: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

Shirika kubwa la umisheni la wanawake duniani lilianzishwa mnamo 1888 kama Umoja wa Wanawake Wamisheni, kutoka kwa Jumuiya ya Kibatisti ya Kusini.18 Umoja wa Wanawake Wamisheni uliwatia moyo wanaume na wanawake kufanya kazi kama umisheni. Lottie Moon alikuwa mmisheni mashuhuri wa Wabatisti wa Kusini, ambaye alitoa maisha yake kufanya kazi ya umisheni huko Uchina. Moon alianza kazi yake Uchina mnamo mwaka wa 1873, na kutumika kwa miaka 41. Alishiriki chakula chake na watu wa China, baadaye akafa kwa sababu ya kukosa chakula.

5 Vitabu vya historia ya kanisa vya marejeo kutoka kwa mtazamo wa tawi tofauti za kanisa na kutoka kwa mtazamo usio sahihi wa madhehebu vimetolewa katika wavuti: http://www.spurgeon.org/~phil/hall.htm 6 The American People’s Encyclopedia, s.v. “Constantine I or Constantine The Great.” 7 Ralph D. Winter, “The Kingdom Strikes Back: Ten Epochs of Redemptive History,” in Ralph D. Winter and Steven C. Hawthorne, eds., Perspectives on the World Christian Movement, The Notebook, (Pasadena, California: William Carey Library, 1999) 154-158. 8 Winter, “The Kingdom Strikes Back,” 158-162. 9 Winter, “The Kingdom Strikes Back,” 158-162. 10 Ralph D. Winter, “Four Men, Three Eras, Two Transitions: Modern Missions,” in Ralph D. Winter and Steven C. Hawthorne, eds., Perspectives on the World Christian Movement, The Notebook, (Pasadena, California: William Carey Library, 1999) 180-186. 11 Ralph D. Winter, “Four Men,” 180-186. See also Ralph D. Winter, “The Two Structures of God’s Redemptive Mission, in Ralph D. Winter and Steven C. Hawthorne, eds., Perspectives on the World Christian Movement, The Notebook, (Pasadena, California: William Carey Library, 1999) 170-176. 12 Ralph D. Winter, “Four Men,” 182-183. 13 Ralph D. Winter, “Four Men,” 184. 14 Ralph D. Winter, “Four Men,” 184. 15 Donald A. McGavran, “The Bridges of God,” , in Ralph D. Winter and Steven C. Hawthorne, eds., Perspectives on the World Christian Movement, The Notebook, (Pasadena, California: William Carey Library, 1999) 365. 16 Ralph D. Winter, “Four Men,” 181,183. 17 Ralph D. Winter, “Four Men,” 181. 18 See the link: http://en.wikipedia.org/wiki/Women%27s_Missionary_Union

RUDI KWA MUHTASARI

Page 19: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

VII. Tamaduni na Umisheni

Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Uinjilisti wa Dunia uliwaleta pamoja viongozi wainjilisti huko Lausanne, Switzerland mnamo mwaka wa 1974 ili kujadiliana mambo yanayohusika na Uinjilisti. Kutokana na mkutano huu kulitokea Maagano ya Lausanne, tangazo la kuwa na nia ya kufanya uinjilisti duniani kote. Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Uinjilisti wa Dunia (pia unaojulikana kama Lausanne II) ulifanyika Manila mnamo mwaka wa 1989. Makaratasi ya mara kwa mara yameandikwa na viongozi wainjilisti wanaofanya kazi pamoja na Maagano ya Lausanne. Ripoti ya Willowbank ni moja wapo ya karatasi za mara kwa mara zilizoandikwa na Mkutano wa Lausanne. Ripoti hii, iliyotayarishwa na viongozi wanaojulikana katika uinjilisti wa dunia, inatahini Injili na Tamaduni. Soma ripoti hii kuhusu Injili na Tamaduni katika:

http://community.gospelcom.net/Brix?pageID=14322

http://www.gospel.com/ Baadhi ya ncha za kimsingi katika ripoti ya Injili na Tamaduni zimepeanwa hapo chini, p amoja na mawazo zaidi ya kiini hiki. A. Ufafanuzi ya Utamaduni

Ripoti ya Willowbank inasema ufafanuzi wa utamaduni kwa mapana ni “mtindo wa watu ambao hufanya vitu pamoja19.” Utamaduni unahusisha imani, thamani, desturi, na vyama vinavyoshikilia jamii pamoja20

.

B. Tamaduni Katika Bibilia

Injili inapotangazwa, inatolewa kwa watu fulani katika mahali fulani na kwa wakati fulani. Ili Injili iwe na matokeo ya hali ya juu, lazima iwekwe katika mazingira yetu—itolewe kwa njia ambayo itakubalika na tamaduni fulani. Biblia ni Injili—Habari Njema kwa wale ambao wanataka kujua kuwa Mungu anafanya kazi kwa juhudi katika historia yote ili kuleta ukombozi kwa mwanadamu. Kwa hivyo waandishi wa Biblia na manabii walieneza Neno la Mungu kwa lugha ya wasikilizaji: Kiebrania, Aramaic, na Kigiriki. Pia walizingatia kuelewa kwa tamaduni za wasikilizaji. Kwa mfano, kitabu cha Waebrania kiliandikwa kwa ajili Wakristo Waebrania, kwa hivyo kina kumbukumbu nyingi za maandishi ya Kihebrania ya Agano la Kale. Kwa sababu ya Wayahudi kutekwa nyara na kupelekwa Babeli, lugha iliyojulikana kwa Waebrania ikawa Aramaic. Kwa hivyo Maandiko mengine yameandikwa katika Aramaic. Mtume Paulo aliwaandikia Wagiriki, kwa hivyo alieleza mambo yaliyo katika barua zake kwa njia ambayo Wagiriki wangeweza kuelewa. Ripoti ya Willowbank ina kumbukumbu za elimumwendo yenye usawa. Hiyo ni, unapoeneza injili, wamisheni wanafaa kutafuta jinsi ya kuweka ukweli wa maandiko wanapotumia lugha na mawazo yanayojulikana na msikilizaji.

Page 20: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

Unapoanzisha kanisa na kuanzisha ibada, amri muhimu za Maandiko lazima zidumishwe. Lakini kwa mambo ambayo maandiko hayataji, makanisa ya mtaa ni lazima yapewe uhuru wa kuanzisha shirika lao na mtindo wa kuabudu.

C. Vizuizi vya Kitamaduni kwa Injili

Mmisheni anapoeneza Injili, msikilizaji anaweza kutambua vitisho viwili kwa utamaduni wake:

1. Ujumbe wa Biblia, na 2. Utamaduni wa mmishenari. Asili ya Ujumbe wa Biblia ni wa namna mbali mbali. Wanaoufuata ukweli wamegawanyika kutoka kwa wale hawafuati. Yesu alisema, “Sikuja kuleta amani, bali upanga” (Mathayo 10:34). Lakini wasikilizaji wengi wako tayari kuufuata ukweli, kama utatolewa kwa njia ambayo wataelewa na kukubali. Mungu ameweka hamu ya uzima wa milele katika roho za watu wa kila tamaduni, na kama watu wataweza kuelewa ya kwamba Yesu ndiye njia ya uzima wa milele, wataikubali Injili. Kama watu wataona kuwa Injili inahitaji wabadilishe utamaduni wao, wanaweza kuikataa. Don Richardson anasema kuwa katika tamaduni, kuna maelewano ya kiroho yasiyotumika ambayo yanaweza kuamshwa na analojia ya kuokoa. Ulimwenguni, wahubiri wanatumia analogia wanapoeneza ukweli wa Kibiblia wa wokovu. Mhubiri mzuri, anapoongea na wakulima atatumia analojia za kilimo, kama anaongea na madaktari, atatumia analojia za idara ya kiafya na madawa. Yesu aliongea kwa jinsi ambayo wasikilizaji wake walielewa: Aliongea kuhusu mabwana na watumishi, kondoo na wachungaji, wapanzi na wavunaji. Jinsi hiyo hiyo, alipotumika kama mmisheni kwa kabila la Sawia la Irian Jaya, Richardson alitumia analojia ya tabia kuwaongoza wengi kumpokea Kristo. Kulingana na utamaduni wa Sawi, ili kuwe na amani kati ya kabila mbili, baba lazima amkubalie mwanawe mmoja kulewa na mtu wa kabila adui. Mtoto huyu alikuwa “mtoto wa amani.” Richardson alipoonyesha Yesu kama yule mtoto wa amani aliyepeanwa na Mungu kuleta amani kati ya Mungu na mwanadamu, Wasawi waliamini. Hivi sasa asilimia sabini ya Wasawi ni Wakristo. Richardson aliandika kuhusu mashuhudio haya katika kitabu chake cha mtoto wa amani (Peace Child). Ameandika kuhusu analojia za ukombozi zinazotumiwa kuwaleta watu kwa Kristo katika tamaduni zenginezo. 21

Watu humwamini Kristo mara nyingi wanapoona Injili ikiendeleza utamaduni wao sio kuuharibu.Taharuki ya pili ni kwamba wasikilizaji wanaweza kudhania wamisheni wanajaribu kulazimisha tamaduni zao kwa walio amini. Ikiwa mmisheni atachukulia utamaduni wao kuwa bora kuliko ule wa wasikilizaji, huenda akawasilisha haya kwa kufahamu au kutofahamu. Kwa kawaida msikilizaji huwa hapendi kubadili utamaduni wake na kuiga wa mmisheni. Paulo na Barnabas walielewa ya kuwa ili kufikia tamaduni za Wagiriki na injili, Habari Njema isizuiliwe kwa kuongeza tamaduni za Kiebrania kama hitaji la kidini

Page 21: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

(tazama Matendo 15:1-31). Ili kufaulu, lazima mmisheni ajitambulishe na tamaduni. Utamaduni wake hauwezi kufanana na wa wale waliozaliwa katika tamaduni za mahali pale, lakini anaweza kujaribu kuwaelewa watu, kuwasikiliza, kujifunza kutoka kwao, kucheka nao, kulia nao. Mmisheni wa kufana ni mnyenyekevu. Kristo ni mfano wa unyenyekevu—kuacha utukufu wake ili awe katika kiwango cha mwanadamu (tazama Wafilipi 2:5-11). Vitisho kwa muumini anayetazamiwa ni amri za kidini na za watu wa mji wake. Mbadili dini kwa Ukristo anaweza kufukuzwa, kudhulumiwa, hata kuuawa. Wamisheni katika mahali kama hapo wanafaa kuwa na subira. Wabadili dini lazima wawe na uhakika kuwa Yesu ndiye njia ya uzima wa milele kabla wawe tayari kufanya dhabihu kwa Kristo.

D. Mwitikio wa Wabadili Dini

Mmisheni anapenyeza Injili kwa njia bora, anafaa kumwachia Mungu matokeo. Ni Roho Mtakatifu pekee anayeweza kubadili mtu kutoka kwa dhambi na kumpa uzima wa milele. Mtu anapompokea Kristo, anaweza kuukataa utamaduni wake. Anapotafuta mtindo mpya wa kuishi, anaweza kujaribu kuiga utamaduni wa mmisheni. Mmisheni hafai kuwahimiza wabadili dini kuiga tamaduni zake. Ni vyema wabadili dini wakikaa katika tamaduni zao na kuwa mashahidi kwa wale walio karibu nao. Walakini, Wakristo wapya wanafaa kuonywa juu ya kupatia nafasi Ukristo kwa utamaduni, kubadilisha mafunzo ya Kibiblia ili yasigongane na tamaduni. Wakristo wanafaa kubadilishwa na amri za Ki biblia.

E. Shirika na Ibada

Wamisheni wanafaa kuwapa Wakristo uhuru, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu na Maandiko, kukuza kanisa la kiasili na jinsi ya kuabudu. Washauri wa wamisheni kama vile Henry Vann, Rufus Anderson, na Roland Allen waliendeleza mpango wa makanisa ya kiasili ambayo yangekuwa ya: - Kujitawala - Kutoongozwa na wamisheni au dini ya kigeni, - Kujitegemea- Kutotegemea pesa za msaada kutoka nje, na - Kujizalisha – Kuzaa na kuzidisha kwa namba. Ni nini chaweza kuzuia makanisa kama haya kutokuwa syncretistic—kuchanganya Ukristo na imani za uongo? Makanisa mengine yataepukana na ukweli, lakini kama makanisa ya kiasili yatajizidisha, lazima yapewe uhuru.

Page 22: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

Kuna kinga za kuweka makanisa katika njia za kweli. Mtume Paulo aliweka mfano alipoanzisha makanisa mahali mbalimbali.

• Kwanza, alikaa nao kwa muda mrefu ili kuwaelekeza kwa mambo muhimu ya imani.

• Pili, aliwaacha chini ya uongozi wa wazee—wanaume waliokomaa kiroho zaidi kanisani.

• Tatu, baada ya kuwaacha, aliwasiliana nao kwa barua au kuwatembelea, kuona jinsi walivyokuwa wanaendelea. Aliwashawishi kubakia katika njia iliyofaa. Waraka za Paulo zinaonyesha maagizo ya Paulo kwa makanisa.

• Nne, aliyategemea Maandiko. Paulo alikuwa amefundishwa vizuri katika Maandiko ya Agano la Kale, na aliwatia wengine moyo kuyafuata Maandiko (tazama 2 Timotheo 3:14-17).

• Tano, alimtegemea Roho Mtakatifu (tazama Matendo 16:6). Roho alimwongoza Paulo, na Roho anawaongoza waumini makanisani duniani kote.

F. Hatua ya Kubadilika

Mmisheni anafaa katika maombi kutambua ni sehemu gani ya mtu ya kitamaduni inayofaa kubadilika, mtu anapokuwa Mkristo. Vitu vingine ni lazima vibadilike mara moja (kwa mfano, imani ya kuabudu miungu wengi). Mambo mengine yaweza kuchukua muda kabla ya kubadilika (kama tabaka katika jamii). Mambo mengine yanaweza kukosa kubadilika (kama vile mavazi).

19 Tazama “Fasili ya Tamaduni” katika kiunganisho: http://community.gospelcom.net/Brix?pageID=14322 20 Tazama “Fasili ya Tamaduni” katika kiunganisho: http://community.gospelcom.net/Brix?pageID=14322 21 Don Richardson, “Redemptive Analogy,” in Ralph D. Winter and Steven C. Hawthorne, eds., Perspectives on the World Christian Movement, The Notebook, (Pasadena, California: William Carey Library, 1999) 285-289.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 23: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

VIII. Mkakati wa Umisheni

ILI UFANIKIWE KATIKA KUWAFIKIA WATU WENGI KWA AJILI YA KRISTO, MMISHENI ANAHITAJI MKAKATI WA KIBIBLIA. Mahali pengi umisheni umekosa kufaulu au umekua pole pole kwa sababu ya kutumia mikakati isiyofaa. Kwa hivyo karne zimeendelea kupita na kanisa halipanuki katika sehemu zingine. David Garrison, katika kijitabu chake, Church Planting Movements, anatambua mambo ambayo inaendeleza vitu vinavyo zuia kukua kwa kanisa katika maeno ya umisheni. Tafadhali soma kijitabu katika wavuti ufuatao. Tafakari faharasa zilizo hapo mwisho kabla ya kusoma kijitabu.

http://www.imb.org/CPM/default.htm

Ufuatao ni muhtasari wa wazo muhimu kutoka kwa kijitabu cha Garrison, pamoja na habari za ziada. Lengo la mmisheni latakiwa kuwa kusaidia kuanzisha mwendo wa kuanzisha makanisa katika makundi ya watu. Garrison anafafanua Mwendo wa Kuanzisha Makanisa kama “namba kipeo cha kuongezeka kwa haraka kwa makanisa ya kiasili yakianzisha makanisa kati ya watu fulani au makundi ya watu.”22 Mwendo wa Kuanzisha Makanisa ni wa haraka – matokeo yake yaweza kuwa kuanzishwa kwa makanisa mengi mapya kwa muda wa miaka michache. Mwendo wa Kuanzisha Makanisa ni namba kipeo – makanisa mawili yanakuwa manne, manne yanakuwa manane, makanisa nane yanakuwa kumi na sita, n.k. Mwendo wa Kuanzisha Makanisa inahusisha makanisa ya kiasili—watu wa tamaduni hiyo wanaanza na kuendeleza makanisa. Mwendo wa Kuanzisha Makanisa unakaribisha watu wa kundi lolote, lakini kwanza ni lazima kila kanisa liwe na lengo la kuwafikia watu katika kundi fulani au watu wa sehemu fulani. Watu huvutika kwa watu wa lugha yao au walio na tamaduni zinazo fanana. Mwendo wa Kuanzisha Makanisa unafanyika huko Amerika Kaskazini, China, Latin America, Western Europe, na Ethiopia. Mbinu zinazoelezwa katika kitabu cha Garrison zinasaidia kuanzisha Mwendo wa Kuanzisha Makanisa katika tamaduni kadhaa. Msingi wa baadhi ya mbinu hizi ni mafundisho ya Biblia. Kwa mfano, Garrison akuza kuwa makanisa yaanzishwe na makanisa ya kiasili. Paulo Mtume alianzisha makanisa karibu na Mediterania, baadaye akatia moyo washiriki kufanya kazi yote ya kanisa. Kati ya kazi hiyo ilikuwa kufanya uinjilisti ili watu wa kiasili waweze kuanzisha makanisa mengine. Paulo alifundisha kuwa kila mmoja ya washiriki wa kanisa alikuwa na kipawa kimoja au zaidi ambacho kingetumika. Wengine walikuwa na kipawa cha unabii, na tunaona kuwa manabii hao walinena si tu kwa makanisa yaliokuwapo lakini pia kwa makanisa mapya (tazama Warumi 12: 6). Baadhi yao walikuwa na kipawa cha uinjilisti, kwa hivyo makanisa mapya yalianzishwa Injili ilipokuwa ikienezwa (tazama Waefeso 4:11). Garrison anasema kuwa makanisa ya kiasili yasichukue tamaduni za wamisheni. Mtume Paulo alitia moyo makanisa ya kiasili ya Giriki bila kuwataka wasichukue tamaduni zote za Kiebrania na taratibu za tambiko, na Petro na Yakobo walikubaliana na Paulo (tazama Matendo 15:1,2,6-21).

Page 24: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

Garrison anaeleza jinsi makanisa ya siku hizi hukutana kama kundi za seli manyumbani. Mtume Luka anaeleza jinsi Wakristo wa kwanza walimega mkate nyumba kwa nyumba (wakisherehekea Chakula cha Bwana) na jinsi kanisa lilizidishwa kila siku (tazama Matendo 2:46,47). Lengo la msingi la Mwendo wa Kuanzisha Makanisa si kuzidisha makanisa, lakini ni kuleta watu wa makanisa mengi kuabudu Mungu. Lengo la umisheni ni kumtukuza Mungu, na huwa tunampa Mungu utukufu watu wanapoletwa katika imani ndani Yake. Mkakati wa Mwendo wa Kuanzisha Makanisa si kuwafunza wamisheni wa kiasili jinsi ya kuanzisha makanisa kwa ajili ya makanisa. Bali ni kusaidia makanisa ya kiasili kujizidisha. Mmisheni mmoja ana upeo ya idadi ya makanisa anayoweza kuanzisha. Lakini makanisa yaweza kujizidisha mpaka yatawanyike duniani kote. Hata hivyo, ni muhimu kila kanisa likikuza kundi la wamisheni au linaungane na shirika la umisheni kwa lengo la kuanzisha makanisa mapya. Historia imeonyesha kuwa makanisa huwa hayafanyi umisheni isipokuwa kama kuwa kundi la umisheni linalofanya kazi hiyo ya uinjilisti. Garrison anaeleza jinsi Mwendo wa Kuanzisha Makanisa ulivyofanyika kati ya kundi la watu wa Latin American kutoka mwaka wa 1989 hadi 1998. Wamisheni wa kigeni walikuwa wameweka msingi wa kiroho kwa makanisa kwa kuwafundisha washiriki jinsi ya kutegemea Maandiko na kujiona kama makuhani (wazo la ukuhani wa waumini). Selikali iliwafukuza wamisheni wa kigeni. Hii ililazimisha kanisa kuwa ya kiasili. Washiriki walisisitiza maombi. Waliimba nyimbo kwa lugha zao wenyewe, si kwa lugha za wageni. Kwa sababu ya shida ya kifedha, washiriki hawakuweza kusafiri kwenda kwa makanisa yao, kwa hivyo walilazimika kukutana katika makundi madogo nyumbani. Wamisheni ambao walikuwa wamerudi kusaidia, lakini si kutawala, kanisa walitoa habari juu ya mtindo wa kundi dogo kama ulivyotumika katika sehemu tofauti ulimwenguni. Kukutana kwa kundi ndogo kuliharakisha kukua kwa kanisa. Shule ya kutayarisha wamisheni ilianzishwa na wamisheni walitumwa nchi nzima. Kusini, idadi ya makanisa iliongezeka kutoka 129 mwaka wa 1989 hadi 1,918 mwaka wa 1998. Kaskazini, idadi ya makanisa iliongezeka kutoka 95 mwaka wa 1989 hadi 1,340 mwaka wa 1998. Kanisa la kiasili lilikua haraka mara kumi katika muda wa miaka kumi kama vile ilivyokuwa imekua kwa miaka mia moja iliyopita! Ni nini kilicholeta mabadiliko? Mwendo wa Kuanzisha Makanisa ulikuwa umefanyika kwa maombi ma mkakati. Mwendo wa Kuanzisha Makanisa kwa haraka kama huu umefanyika katika mataifa mengine. Na tuchunguze madokezo kumi ambayo ilikuwa katika Miendo ya Kuanzisha Makanisa ulioelezwa na Garrison.

1. Maombi. Mmisheni huonyesha mtindo wa maombi na kuyafunza makanisa nguvu za maombi.

2. Kutoa Injili kwa Wingi. Kupitia kwa uinjilisti katika vyombo vya habari na uinjilisti wa kibinafsi, Injili inatolewa kwa watu wengi.

3. Kuanzisha Makanisa Ulimwenguni. Hata kabla ya mwendo wa kuanzisha makanisa kuanza, mtu anaanza kanisa moja au zaidi.

Page 25: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

9. isa husema kuwa kukua kwa haraka hutia moyo

na kuendeleza kukua zaidi.

10. M a ni:

Kanisa”). Garrison ameorodhesha shughuli tano ambazo ni sawa na hizi.

ambayo yanapatikana kwa waida katika Miendo ya Kuanzisha Makanisa.

1. . Wamisheni wajifunze si tu lugha ya biashara lakini pia lugha ya mahali hapo.

2. wa

ti uaji wa

wa kushuhudia, na kutafuta mwongozo wa Mungu kuhusu jinsi ya kushuhudia.

4. Mamlaka ya Maandiko. Kanisa inaelewa kuwa Biblia ndiyo yenye mamlaka. Ni vyema kuwa na Maandiko katika lugha ya kiasili ya watu. Watu hufunzwa Biblia kwa maneno na kwa maandishi.

5. Viongozi wa Mahali Pale Pale. Mmisheni huonyesha wajibu wa mchungaji na wajibu wa kiongozi wa kundi la kujifunza Biblia. Mmisheni hajichukulii wajibu huu; badala yake huwafunza watu wa mahali hapo kuchukua wajibu huo.

6. Uongozi wa mtu wa kawaida. Mwanzo, viongozi wanatoka kwa watu wa kawaida, badala ya kuwa wamefunzwa katika chuo cha Biblia.

7. Seli au Ushirika wa Nyumbani. Kanisa limepangwa katika seli au mashirika ya nyumbani – kila seli ikiwa na washiriki 10 hadi 30. Nia ya seli inatoka kwa wazo la seli katika mwili wa mwanadamu, ambazo hujizidisha mwili unapoendelea kukua. Seli moja linakuwa seli mbili, seli mbili zinakuwa seli nne n.k. katika kanisa, makundi ya seli yameunganishwa na uongozi moja.Kiunganisho hiki kina faida ya kuongoza makundi ya seli katika kanuni zinazofaa. Makanisa ya nyumbani yanajitawala, kwa hivyo hayawezi kudhulumiwa na upelelezi na kukandamizwa na selikali zenye uhasama.

8. Makanisa Kuanzisha Makanisa. Makanisa ya kiasili huanzisha makanisa zaidi ya kiasili. Washiriki wanaelewa kuwa wanaweza na wanatakiwa kuzidisha makanisa.

Kuzaa kwa Haraka. Waanzilishaji wengi wa makanisa ambao wamehusika na Mwendo wa Kuanzisha Makan

akanisa Yenye Afya. Makanisa yenye afya hushikilia shughuli tano za kaniskama vile zilivyoorodheshwa katika Matendo 2:41-47. Shughuli hizi tano kuabudu, Kueneza Injili, kutumika, ushirika na uinjilisti (tazama kiuzi cha mafunzo cha “Uongozi wa

Kuongezea madokezo kumi ambayo inatumika na kila Mwendo wa Kuanzisha Makanisa, Garrison ameorodhesha madokezo kumi ka

Kuabudu katika lugha za Asili. Hatimaye, watu huabudu katika lugha za asili

Uinjilisti Unahusisha watu wengi. Kama inafaa, waumini wapya wanahimizkushuhudia jamii zao wenyewe. Kuna hali zingine ambazo muumini aweza kuteswa anaposhuhudia jamaa zake, kwa hivyo ni lazima busara itumiwe wakawa kushuhudia. Lakini, mbinu hii huwa na matokeo mema zaidi kwa ukkanisa. (tazama Matendo 16:31-32). Mpangilio ni muhimu wakati wa kushuhudia. Kwa maombi, waumini watafute mpangilio wa Mungu kuhusu wakati

Page 26: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

3. Kushirikisha Waumini Wapya kwa Haraka Katika Maisha na Huduma ya Kanisa. Waumini wapya wanatiwa moyo kushuhudia wengine mara moja na kusaidia kuanzisha makanisa mapya.

4. Kuwa na Shauku na Ujasiri. Kuna uthabiti na umuhimu kwa upande wa waumini walio katika Miendo wa Kuanzisha Makanisa.

5. Bei ya Kulipa Kuwa Mkristo. Katika sehemu ambazo Injili hairuhusiwi na jamii au selikali, washiriki wasio na uthabiti hutolewa na wale waliosalia huwekwa wakfu. Yesu aliwafunza wanafunzi wake washuhudie hata wakati wa mateso, na wanapoteswa mahali pamoja, wakimbilie mahali pengine kushuhudia (tazama Mathayo 10:16-23).

6. Shida ya Viongozi Wanaofahamika au Utupu wa Kiroho Katika Jamii. Nchi au kundi la watu wanapokosa usalama kwa sababu ya shida, watu hutaka sana kuelekea Mungu kwa majibu.

7. Kufunzwa Ukiwa Bado Kiongozi wa Kanisa. Badala ya kuchelewesha Mwendo wa Kuanzisha Makanisa kwa kuondoa viongozi kutoka kwa makanisa yao, mafunzo ya theolojia yaweza kutolewa mahali hapo. Kiuzi cha muda mfupi, kama zile zinazotolewa katika wavuti wetu (www.missionstraining.org) ni njia inayofaa ya kukuza wamisheni na viongozi wa kanisa.

8. Mamlaka ya Uongozi Yagawanywe. Kila seli na kila kanisa la nyumbani lahitaji mamlaka ya kutumika na kuanzisha makanisa bila kupata kibali kutoka kwa utawala msonge.

9. Watu wa Nje Huwa Hawaonekani. Wamisheni hushauri viongozi wa kanisa kisiri siri.

10. Wamisheni Huteseka. Mara nyingi wamisheni wanaohusika na Mwendo wa Kuanzisha Makanisa huteseka. Baadhi yake ni kwa sababu ya tabia zao wenyewe za kujiharibu na zingine ni kwa sababu ya maadui. Kwa hivyo wamisheni wanahitaji kuomba.

Ni jukumu la Mungu kuwaokoa watu kutokana na hukumu na kuwavuta kwa kanisa lake. Lakini amewatuma washiriki wa kanisa kufanya kazi yake. Garrison anaorodhesha njia kumi za kiutendaji ambazo wamisheni wanaweza kutumia kuendeleza Mwendo wa Kuanzisha Makanisa. Baadhi ya mbinu hizi zaweza kutumika katika hali zingine na kutotumika katika hali tofauti.

1. Shikilia mwelekeo wa Mwendo wa Kuanzisha Makanisa kuanzia mwanzo. Kuanzia mwanzo, washiriki katika seli wanafunzwa kushikilia malengo ya Mwendo wa Kuanzisha Makanisa.

2. Kuza na Utekeleze Mikakati Unaofahamu. Mkakati uwe na mambo manne: Maombi, Maandiko, Uinjilisti na Kuanzisha makanisa. Mambo mengine yatategemea hali.

Page 27: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

3. Tathmini Kila Kitu ili Upate Maono ya Mwisho. Viongozi waondoe mambo yale ambayo hayaleti matokeo ambayo tunatarajia.

4. Tumia Usahihi katika Mavuno. Katika sehemu ambazo uinjilisti unafanyika kwa watu wengi, mwanzilishi wa kanisa anaweza kupata majina na anwani za watu ambao wameitikia uinjilisti. Ni vyema kufanya kazi pamoja na wale wanaohusika katika huduma kama hizo. Katika tukio lingine mtangazaji nje ya nchi anaweza kuendeleza uinjilisti. Mtangazaji huyo aweza kutoa habari muhimu kwa mmisheni anayeingia katika nchi fulani.

5. Tayarisha Waumini Wapya kwa Mateso. Waumini wapya wawe tayari kwa mateso, si kushangazwa na mateso (tazama Marko 8:34).

6. Walete Pamoja, Baadaye Wavute. Wakati mwingine, wenye dhambi huletwa pamoja ili wajifunze kuhusu Mungu na wakati huo huo wanapewa maono ya Mwendo wa Kuanzisha Makanisa.

7. Anzisha Makanisa Yenye Tabia zifuatazo:

- Masomo ya Bablia ya kushiriki - Kutii Biblia kama kipimo cha pekee cha kufaulu. - Uongozi usio na malipo na mfumo wa madaraka - Kundi la seli (njia moja ya kukutana) - Kanisa za nyumbani (njia nyingine ya kukutana)

8. Kuza Viongozi Wengi Katika Kila Kundi la Seli. Kutoka mwanzo tayarisha viongozi wengi ili wasimamie mahitaji ya kanisa inayokua.

9. Wafunze Wanapohudumu. Jambo hili limezungumziwa chini ya madokezo kumi ambayo yanapatikana kwa kawaida katika Miendo ya Kuanzisha makanisa. Viongozi wa kanisa waweza kuondolewa kwa kazi yao ili wapate mafundisho ya theolojia kwa muda wa majuma machache kila baada ya muda fulani, badala ya mafunzo ya muda mrefu yote kwa wakati mmoja.

10. Onyesha, Saidia, Tazama na Uondoke . Wamisheni wanatakiwa waonyeshe mtindo wa kufanya jambo, wasaidie viongozi kufanya kazi, watazame waone kama kazi imefanywa vyema, na waondoke kama kiongozi amejifunza. Kuonyesha huja pamoja na kufanya jambo mbele ya watu wengine. Hii inaitwa “kanuni ya 222,” inayopatikana katika 2 Timotheo 2:2. Mmisheni haonyeshi tu, bali anafundisha wanafunzi wake jinsi ya kuonyesha wengine.

Garrison anajishughulisha na baadhi ya maswali yanayoulizwa kwa wingi.

1. Jengo ya kanisa ni muhimu? Kwa kuanzia, jengo la kanisa halihitajiki kwa jumla, na laweza kuleta msigo wa kulitunza ambao waweza kuzuia kukua kwa kanisa.

Page 28: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

2. Je, Mwendo ya Kuanzisha Makanisa huendeleza Uasi? Njia bora ya kuzuia uasi ni kuwafundisha wanafunzi, “kuyashika yote niliyowaamuru ninyi” (Mathayo 28:20). Weka maanani kuwa wanafunzi wamefunzwa kuyashika - “kushika kwa nguvu” mambo ambayo Kristo aliamuru. Wanafunzi hawafunzwi kuona tu Maandiko, wamefunzwa kutii Maandiko.

3. Utafanyaje na watoto wakati kundi la seli linakutana? Wanaweza kuletwa kwa mkutano wa kundi hilo la seli au kuwekwa katika kundi tofauti chini ya viongozi tofauti kutoka kwa seli hiyo.

Garrison anaorodhesha vikwazo tisa vya Mwendo wa Kuanzisha Makanisa.

1. Kuweka Masharti ya ziada ya Kibiblia kabla ya kuwa Kanisa. Kutaka kundi liwe na vitu kama jengo au mchungaji anayelipwa kabla ya kuwa kanisa ni kupinga matokeo.

2. Kuacha mila zao wanazo thamani. Makanisa ambayo yanatakiwa kufuata mila za wageni si rahizi zijizalishe haraka.

3. Kukabiliana na Mifano Mimbaya ya Ukristo. Kanisa ambalo lina washiriki ambao hawaonyeshi maadili ya Kikristo waweza kufanya watu katika desturi fulani kujihadhari na Wakristo wengine.

4. Mtindo wa kanisa ambao hauwezi kutengenezeka upya. Kama watu wa kiasili hawawezi kuiga sehemu za kanisa, sehemu hizo zisitambulishwe. Kwa mfano, kama mti ya cinder au viti vya kukunja havipatikani katika sehemu hiyo, visitambulishwe katika kanisa la kwanza.

5. Ruzuku Inayoleta Utegemeaji. Pesa kutoka nje zaweza kutumiwa kununua vifaa vya uinjilisti, lakini si kuruzuku mishahara au jengo.

6. Masharti ya ziada ya Kibiblia kuhusu uongozi. Unapochagua wanafunzi, Biblia inasisitiza kuchaguliwe watu walio na tabia nzuri ambao wanataka kufuata, badala ya kutafuta watu ambao wana elimu nyingi ya Kitheolojia. Tazama kifungu kinachoeleza jinsi Yesu alivyochagua wanafunzi wake kumi na wawili (Mathayo 4:18-22) na pendekezo la Paulo kuhusu askofu na mashemasi (1 Timotheo 3).

7. Kufuatana. Badala ya kufuata hatua fulani kabla ya kuanzisha kanisa (kwanza kujifunza lugha, baadaye kufanya urafiki, arafu kushuhudia, arafu kufanya uanafunzi, arafu kuwa na washiriki, arafu kuwafunza viongozi, arafu kuanza kanisa lingine.), ni vyema kushuhudia na kushiriki maono ya Mwendo wa Kuanzisha Makanisa.

8. Kuanzisha makanisa ya “vyura” badala ya “mijusi”. “Vyura” hukaa wakinona na kuridhika, wakingonjea wasioamini wawakujie. “Mijusi” huwaendea wasio amini kutoka kwa ufa na kwenye mwamba. Mijusi yaweza “kujibadilisha rangi” au kuchukua hali ya mazingira.

Page 29: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

9. Mikakati yenye kuelekeza. Badala ya kufuata mbinu iliyowekwa ya kuanzisha kanisa, ni vyema kufuata Roho Mtakatifu. Mikakati iliyodokezwa katika kiuzi hiki ni pendekezo tu. Ni vyema wamisheni waweze kuona jinsi Mungu anavyofanya kazi, na kujiunga naye kwa kazi hiyo (tazama kiuzi cha mafundisha - Mwito wa Umisheni).

Kwa kuongezea mawazo yaliyotolewa na Garrison, fikiria sehemu ambazo ni muhimu kwa mafanikio ya umisheni.

1. Penda. Wamisheni ni lazima wapende watu. Kama hakuna upendo, mambo mengine yote ambayo yanafanywa haifaidi kitu (tazama 1 Wakarintho 13).

2. Nendeni wawili wawili mkatafute mwana wa amani. Kama ilivyoelezwa kwa muhtasari hapo juu, wamisheni wanatiwa moyo kwenda wawili wawili. Yesu aliwatuma wainjilisti wake wawili wawili, na akawaambia watafute na kukaa na “mwana wa amani.”

1 Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, [a] akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. 3 Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. 4 Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. 5 "Na nyumba yo yote mtakayoingia. Semeni kwanza, `Amani iwemo nyumbani humu.' 6 Na akiwemo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la hayumo, amani yenu itarudi kwenu. 7Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba. (Luka 10:1-7) a. Luke 10:1 mswada mwingine sabini; pia katika kifungu cha 17. Pia tazama Luka 10:8-24. Wamisheni wengine wanapoingia nchi fulani huwa wanamjua mtu ambaye wataishi naye. Wanaweza kukaa katika mahali pa kukodi wakitafuta “mwana wa amani.” Mwanamume (au mwanamke) wa amani aweza kuwa mtu wa kuwasiliana naye na kupitia kwake wamisheni wanapata ufahamu wa tamaduni hiyo.

3. Kwa kufuata Roho Mtakatifu, tambua na ujue kuhusu kundi unalo. Ili kupata usaidizi kwa mambo haya, kuna habari inayopatikana kupitia kwa wavuti inayoeleza makundi ya watu:

http://www.joshuaproject.net/index.php

Page 30: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

Wamisheni wanatakiwa kujua mambo mengi iwezekanavyo kuhusu watu ambao wanafanyia uinjilisti.

4. Jifunze Kufanya Uinjilisti na Uanafunzi kwa watu wa Kundi Fulani. Inasaidia sana kuelewa mbinu kadhaa za uinjilisti na uanafunzi. Ni muhimu kutumia mbinu hizo kutimiza utamaduni fulani. Mbinu ambayo inatumika katika tamaduni moja yaweza ikakosa kutumika katika tamaduni nyingine.

5. Pata vifaa vya kazi. Chukua ujuzi unaotumika na vifaa vya kueneza Injili katika kundi la watu. Amua kama Biblia zinapatikana katika lugha ya watu hao. Pata au tayarisha hadithi za Biblia ambazo zinafanya muhtasari wa kweli muhimu wa Biblia. Wamisheni wengi hutoa hadithi ili kupata usikivu wa wasikilizaji na kueleza Injili. Yesu alitoa mfano kwa kutumia mithali. Watu wanapenda kusikiza hadithi, wanaweza kukumbuka hadithi. Wavuti ufuatao unatoa mifano ya hadithi, na maelezo ya kutayarisha hadithi zingine:

http://chronologicalbiblestorying.com/

Ikiwa selikali itaruhusu vifaa vya Kikristo kuletwa katika eneo la umisheni, pata video na vifaa ya kusikiza vinavyofaa. Filamu ya Yesu inapatikana katika lugha nyingi, na inafaa sana kwa kutoa Habari Njema. Chukua vitabu vya msingi za kukusaidia kufundisha na kutayarisha hotuba. Chukua Biblia au Biblia ambazo zinaambatana na muswada wa kiasili wa Hebrew, Greek, na Aramaic. Biblia njema ya Kiswahili ni kama vile Toleo la Union. Kuna Biblia nyingi na miongozo ya kusoma Biblia ambazo zinapatikana kwa mtandao, kama unaweza kufikia wavuti kama hizo ukiwa katika eneo la umisheni. Wavuti kama hiyo ni:

http://www.bibles.net/

Vitabu vingine ambavyo utahitaji ni pamoja na Biblia iliyo na Mada, Mpangilio wa kialfabeti wa maneno muhimu katika Biblia, Fasiri ya Biblia.

6. Enenda mahali Mungu anataka uende. Omba ili Mungu akuongoze katika eneo la umisheni. Uliza kanisa lako au Uajenti wa misheni ambao unakutuma wapate kuomba kwa ajili ya mwongozo. Tafuta mwongozo wa Mungu ili akuongoze kwa kundi la watu. Fuata Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu aliongoza Mtume Paulo na wenzake kuepuka mahali pengine na kuelekea Makedonia kufanya umisheni (tazama Matendo 16:6-10). Roho Mtakatifu alimwonya Paulo kuhusu hatari, lakini alimlazimisha kwenda kushuhudia Yerusalemu (tazama Matendo 20:22-24). Nenda mahali watu walipo. Wakati mmoja watu wengine waliuliza mwizi wa benki sababu ya kuiba katika benki. Naye alijibu, “Hapo ndipo pesa zilipo.” Mtu akiuliza, “Kwa nini unaanza umisheni mijini?” Huwa tunajibu, Hapo ndipo watu walipo.” Mtume Paulo aliweka mfano wa kwenda mahali kufuatao:

Page 31: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

• Kwanza, mijini. Watu wa mashambani uhama kutoka na kwelekea mjini. Kwa hivyo Injili huenea kutoka mjini hadi mashambani. (tazama Matendo 17:16-21).

• Pili, katika mahali ambapo watu wanamfahamu Mungu. Paulo kwanza alienda katika Sinagogue – mahali pa Ibada kwa Wayahudi. Wayahudi walikuwa na ufahamu wa Yehova Mungu. Hawakuwa wamemwamini Yesu. Kwa hivyo Paulo alijenga juu ya msingi wa yale Wayahudi walijua, na kutambulisha Habari Njema ya Kristo. Paulo alikuwa Myahudi, na alikuwa na mwito wa kutambulisha Injili kwa Wayahudi kwanza.

• Tatu, Watu wa Mataifa Wanao ogopa Mungu. Wakati Wayahudu walikataa Injili, Paulo alishuhudia kwa watu wa mataifa ambao waliogopa Mungu. “Watu wanaoogopa Mungu” walikuwa wamebadilishwa kutoka kwa Uyahudi.

• Nne, mahali ambapo watu wanaweza kuitikia Injili kwa urahisi. Katika Filipi, mji wa Makedonia, Paulo alienda kwanza mtoni mahali alijua atapata mahali pa kuomba (tazama Matendo 16:12,13). Huko Athens, Paulo alienda sokoni. Alialikwa kuongea katika Aeropagus, mahali pa mijadala ya falsafa.

• Tano, kwa watu wengi nafasi ilipojitokeza. Katika Tyrannus ( Efeso), Paulo alihubiri kila siku katika ukumbi wa mhadhara ili Wayahudi wote na Wagriki katika Mkoa wa Asia walisikia Injili (tazama Matendo 19:9,10). Paulo alitetea Injili kwa watu waliokuwa na fujo huko Yerusalemu (tazama Matendo 21:30,40; 22:1-22).

• Sita, ofisa wa juu selikalini ambao waliuliza Paulo maswali. Paulo hakuepuka maofisa kama hawa, lakini wakati aliitwa kujaribiwa, aliwashuhudia. Katika kesi zingine, ni vyema kunyamaza kimya. Na kwa kesi zingine ni vyema kuongea. Katika hali yake, Paulo hakuona haja ya kunyamaza, lakini kwa uwazi alitangazia Mtukufu Feliki Injili (Matendo 24:2), na kwa Mfalme Agripa na Mtukufu Festo (Matendo 26).

Tambua kwamba Paulo alifuata utaratibu kuwatafuta watu ambao alidhania ni rahisi kupokea Injili. Alitaka kuwafikia watu wengi haraka iwezekanavyo. 22 Tazama ukurasa wa 1, “Mwendo wa Kuanzisha Makanisa ni nini” katika http://www.imb.org/CPM/default.htm

RUDI KWA MUHTASARI

Page 32: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

IX. Kutazama Taswira ya Umisheni

Ili kuendeleza umisheni, shirika moja kubwa la umisheni lilitambua maswali mawili ambayo kila mmisheni anafaa kujiuliza. Kwanza, kila mmisheni ajiulize swali hili: “Bwana, unawezaje kunitumia ili kuufikia ulimwengu uliopotea kwa niaba ya Yesu Kristo?”23 Swali hili linakuongoza kujikabidhi kumfuata Kristo kwa kazi ya umisheni. Swali la pili linakuongoza kutazama taswira ya umisheni: “Bwana itanigharimu nini ili kazi ifanyike?”24 Kwa kuuliza swali hili la pili, mmisheni anatazama kazi yote, bali sio yeye mwenyewe. Hii inamruhusu mmisheni kufanya kazi na wengine kwa njia ya mpangilio. Mmisheni anaona kuwa watu wengine na raslimali kadhaa zinahitajika ili kukamilisha kazi aliyopanga Mungu. Anaona hawezi kukamilisha Tume Kuu peke yake, na kuwa anahitaji Mungu kutoa mawasiliano na raslimali kwa ajili ya kazi hiyo. Mmishenari anapofungua macho kutazama taswira ya umisheni, huwa anawatafuta watu wanaoweza kuendeleza juhudi za umisheni. Wakati mwingine anaweza kutaka kufanya kazi kijuujuu na wasio wakristo ili kufungua nafasi za umisheni. Kwa mfano, anaweza kuomba usaidizi kutoka kwa serikali ili kuja mahali penye watu wengi, ama kujua mahitaji ya kimwili ya watu (mahitaji ya chakula, mavazi, madawa, nk.). Mbali na hayo, mmisheni anaweza kufanya kazi pamoja na wamisheni wainjilisti kutoka madhehebu mengine kutoka maeneo iliyo karibu. Kuna makanisa ya Kiinjilisti yaliyo na dini zaidi ya 20,000 na shirika za kigeni zaidi ya 1,000 ulimwenguni.25 Mwinjilisti ni yule ambaye anaamini juu ya wokovu wa kuzaliwa tena, mamlaka ya Bibilia, na kujitoa kwa Kristo kama Bwana.26 Mmisheni—akitambua kundi lingine la umisheni ambalo linashiriki katika kanuni zake - akishikilia Biblia kama neno la Mungu lenye uhakika —anaweza kutamani kushirikiana na kundi hilo lingine la umisheni.

23 Something New Under the Sun , January 1999, (Office of Overseas Operations, International Mission Board of the Southern Baptist Convention, P. O. Box 6767, Richmond, VA 23230-0767) 25. 24 Something New Under the Sun , January 1999, p. 25. 25 Something New Under the Sun , January 1999, p. 30. 26 Something New Under the Sun, January 1999, p. 51.

RUDI KWA MUHTASARI

Page 33: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

X. Kazi Ya Kusoma Uliyopewa

Soma kitabu hiki kwenye mtandao , The Biblical Basis for Missions, by Avery Willis. Kitabu hiki kinapatikana katika:

http://www.imb.org/core/biblicalbasis

Soma kitabu hiki kwenye mtandao, Church Planting Movements, by David Garrison.

http://www.imb.org/CPM/default.htm

RUDI KWA MUHTASARI

Page 34: MAFUNDISHO YA UMISHENI - Missions Training Free …missionstraining.org/Kiswahili/Courses/Misiolojia.pdfMISIOLOJIA V. Theolojia ya Umisheni Kitabu cha Biblical Basis for Missions,

MISIOLOJIA

XI. Bibliografia

Ralph D. Winter and Steven C. Hawthorne, eds. Perspectives on the World Christian Movement, The Notebook. Pasadena, California: William Carey Library, 1999. Something New Under the Sun. January 1999. Office of Overseas Operations, International Mission Board of the Southern Baptist Convention, P. O. Box 6767, Richmond, VA 23230-0767.

RUDI KWA MUHTASARI