144
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _______ MAJADILIANO YA BUNGE _______ MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao cha Nane - Tarehe 14 Novemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Saba, leo ni Kikao cha Nane. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Maelezo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvikuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramu kupitia Bandari za Nchi Wanachama. MHE. RITTA E. KABATI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramu kupitia Bandari za Nchi Wanachama.

MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA_______

MAJADILIANO YA BUNGE_______

MKUTANO WA KUMI NA SABA

Kikao cha Nane - Tarehe 14 Novemba, 2019

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Job Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutanowetu wa Kumi na Saba, leo ni Kikao cha Nane. Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI:

Maelezo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvikuhusu Azimiola Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa FAO waKuzuia Uvuvi Haramu kupitia Bandari za Nchi Wanachama.

MHE. RITTA E. KABATI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI):

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji kuhusu Azimio la Bunge la KuridhiaMkataba wa Kimataifa wa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramukupitia Bandari za Nchi Wanachama.

Page 2: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MHE. TUNZA I. MALAPO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA MIFUGONA UVUVI):

Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Azimiola Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa FAO waKuzuia Uvuvi Haramu kupitia Bandari za Nchi Wanachama.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI:Maelezo ya Waziri wa Nishati kuhusu Azimio la

Bunge la Kuridhia kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kimataifawa Nishati ya Jua.

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI):

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia kuanzishwa kwaUshirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua.

MHE. TUNZA I. MALAPO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA NISHATI:

Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Azimiola Bunge la Kuridhia Kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kimataifawa Nishati ya Jua.

SPIKA: Ahsante sana. Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

MASWALI KWA WAZIRI MKUU

SPIKA: Maswali kwa Waziri Mkuu, tunakuomba sasaMheshimiwa Waziri Mkuu usogee. Ahsante sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nawakumbusha kuhusuufupi wa swali lako na kwamba lijielekeze kwenye sera nalisiwe linalohitaji takwimu za papo kwa papo, vinginevyoutakuwa umelifuta swali lako wewe mwenyewe.

Page 3: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Muuliza swali wetu wa kwanza kwa kifupi niMheshimiwa Allan Kiula. (Makofi)

MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi ya kumuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swalila kwanza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kumekuwa namalalamiko katika maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali zaMitaa ambao karibu unafanyika, wapo watu ambao wanahofu ya kukosa haki zao za msingi za kupiga kura au kupigiwakupigiwa kura. Je, nini kauli ya Serikali?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu ya swali hilo,tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Kiula, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo tunafahamukwamba tarehe 24 mwezi huu wa Novemba kutakuwa nauchaguzi kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa. Uchaguzi huuulisharatibiwa na uratibu wake ulianza kutoka kwenyekutengeneza kanuni za uchaguzi wenyewe lakini pia kulikuwana maandalizi ya kujiandikisha, kuchukua fomu na kurudishana muda umeshapita. Kinachofuata sasa ni tarehe 17 kuanzakampeni za wale wagombea ili kila mmoja akaeleze nia nanamna akavyoweza kushirikiana na wananchi katikakuongoza kwenye nafasi aliyoiomba. Baada ya hapo sasatarehe 24 Novemba Watanzania wote watatumia fursa nademokrasia yao kwenda kumchagua kiongoziwanayemtaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa utaratibu huu ambao piaunaongozwa na sheria, kanuni na taratibu, tunaamini kilammoja atapata haki yake ya msingi, muhimu ni kuzingatiahizo kanuni, sheria na taratibu ili uweze kukamilisha azma yakoya kuchagua kiongozi ambaye unamtaka mahali ulipo kamani kitongoji au kijiji. Nitoe wito kwa Watanzania kutumia fursahii kwanza kipindi ambacho kinakuja watu waende kusikiliza

Page 4: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

sera za wagombea hao na nia thabiti ya kuwaleteamaendeleo kwenye maeneo yao na kila Mtanzania apatenafasi ya kumchagua kiongozi ambaye anamtaka.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa utaratibu huu nakwa namna ambavyo Mheshimiwa Mbunge amekuwa nahofu hiyo, kila mmoja atapata haki yake kwa sababumaelekezo yote yapo sahihi na kila mmoja sasa ni fursa yakeyeye mwenyewe kwenda kufanya maamuzi ya kumchaguakiongozi. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Juma SelemaniNkamia.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kumuulizaMheshimiwa Waziri Mkuu swali kwa mara ya kwanza katikahistoria ya maisha yangu hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, kiapo chetu kinatutaka tuwewakweli na tutasema ukweli daima. Baadhi ya Mikoa hapanchini ikiwemo ya Dodoma na Wilaya zake zote, Manyara,Singida inakabiliwa na tatizo kubwa la chakula. Baadhi yaWenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama kwenye Wilaya naMikoa inawezekana hawatoi taarifa sahihi kwa wogakutokana na pengine kutoelewa vizuri kauli ya MheshimiwaRais. Je, Serikali iko tayari sasa pengine kuunda Tume auKamati Maalum ifanye utafiti ije na data zinazoonesha kunaupungufu gani wa chakula katika maeneo haya ili wananchihawa wapelekewe chakula walau cha bei nafuu kwasababu hali si shwari? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimwia Waziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Juma Nkamia, Mbunge wa Chemba, kamaifuatavyo:-

Mheshmiwa Spika, jambo hili limekuwa likizungumzwahapa mara kadhaa na Waheshimiwa Wabunge wakieleza

Page 5: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

hali ya chakula kwenye maeneo yao. Upungufu wa chakulaupo kwa baadhi ya Wilaya na maeneo kadhaa na hiiilitokana na tatizo la hali ya hewa kwamba yapo maeneomsimu uliopita hayakupata mvua za kutosha. Jambo hililinapotokea kule kwenye ngazi hiyo tunao viongozi natumeweka utaratibu kama Serikali wa viongozi waliopokwenye maeneo hayo kuratibu shughuli zote ikiwemo nahayo yanayotokea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewana kusababisha kuwa na upungufu wa chakula.

Mheshimiwa Spika, Serikali tunacho chombokinachonunua vyakula na vinahifadhiwa ambacho ni NFRA.NFRA inaponunua chakula ni kwa ajili ya maeneo ambayohayana chakula na hukipeleka na kuwauzia na kurudishazile fedha ili ziendelee kununua chakula kingine ili ile benkiiendelee kuwepo. Kwa hiyo, tunachosubiri sasa ni viongoziwa maeneo hayo wakiwemo Wakuu wa Wilaya kuandikawao wenyewe kuonesha kwamba eneo lao lina upungufuwa chakula na mahitaji ni kiasi fulani ili sasa Wizara ya Kilimoinapoandikiwa taarifa hiyo itaratibu vizuri utaratibu wanamna ya kuwafikishia chakula lakini kwa kwenda kuwauziaili tupate fedha za kununua chakula kingine ili benki yetu yachakula iendelee kuwepo.

Mheshmiwa Spika, jambo hili limeshafafanuliwa sanana Waziri wa Kilimo. Hata hivyo, hofu ambayo MheshimiwaMbunge anayo kwamba labda Mheshimiwa Rais aliagiza nipale ambapo hali ya hewa ni nzuri, kila mmoja ana nafasi yakwenda kulima au kufanya kazi halafu kunakuwa hakunachakula. Hapo sasa maelekezo yale ndiyo yanachukua nafasiyake kwamba viongozi waliopo kwenye maeneo hayowanao wajibu wa kusimamia kuhakikisha kila mmojaanafanya kazi pamoja na kulima mazao ya chakula nabiashara ili waweze kujipatia tija inapofikia kipindi kama hikikila mmoja anakuwa na akiba yake. Sasa inapotokea haliya hewa ni mbaya, Mkuu wa Wilaya akieleza atakuwaanaeleweka kwa sababu pia baada ya kutoa taarifa hiyotimu ya Wizara ya Kilimo itakwenda kuona hali halisi nakuweza kuzungumza na mamlaka ile ili iweze kupelekewachakula cha bei nafuu. (Makofi)

Page 6: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mheshimiwa Spika, lakini pia nitoe wito kwawafanyabiashara wetu nchini, Tanzania maeneo yote hayayana hali ya hewa tofauti; yapo maeneo yamepata mvuanyingi na wamezalisha chakula cha kutosha na yapomaeneo hakuna mvua na hakuna chakula cha kutosha.

Kwa hiyo, ni jukumu la wafanyabiashara wetu kutumiafursa hiyo kufanya biashara; kuhamisha chakula kutoka eneoambalo lina chakula cha kutosha na kupeleka mahaliambapo hakuna chakula ili waweze kujipatia pia uchumi.Kwa hiyo, ni muhimu hata pia Wakuu Wilaya, Wakuu waMikoa kwenye maeneo yao wanapoona jambo hili wakutanena wafanyabiashara wawashawishi kwenda kuchukuachakula eneo ambalo hakuna uhaba wa chakulawalete hapo ili ku-stabilize soko na kuwa na chakula chakutosha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, bado ni muhimu kwaMkuu wa Wilaya kwenye Wilaya ya Mheshimiwa Mbungekuiandikia Wizara ya Kilimo kueleza mazingira hayo yaliyopokatika Wilaya yake. Kwa utaratibu wa Wizara Kilimo unawezakwenda kwenye Wilaya hiyo kujionea na kujiridhisha hiyotakwimu iliyotolewa halafu waruhusu sasa chombo chetukupeleka mahindi kwa kuuza ili wananchi waweze kununua.Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante.

Waheshimiwa Wabunge, kabla hatujaendelea,niwakumbushe tu kwamba utaratibu wetu wa kipindi chamaswali kwa Waziri Mkuu, swali la kwanza kabisa huwalinakuwa reserved kwa Kiongozi wa Kambi ya UpinzaniBungeni. Ndiyo utaratibu wetu kwenye Commonwealth huwani fursa pekee ambayo Upinzani wanapata nafasi ya kuulizamaswali. Kwa hiyo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungenianaweza asiwepo Bungeni siku yoyote lakini siku ya Alhamisiya Maswali kwa Waziri Mkuu anakuwepo.

Kwa hiyo, hatujapata swali lile kwa sababu Kiongoziwa Upinzani Bungeni hayupo, uwe wapi na wapi kama Spika

Page 7: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

hana taarifa zako wewe ni mtoro tu. Kwa hiyo, ni mtoro nandiyo maana leo mnaona kwamba hiyo fursa ambayoimewekwa kwenye Kanuni haijaweza kutumia. Ndiyo maanamnaona mara nyingi fursa hiyo inapotea kwa sababu yautoro. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na maswali,Mheshimiwa Jasson Rweikiza. (Makofi)

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi kumuuliza Mheshimiwa WaziriMkuu swali la papo kwa papo.

Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali yetu nikwamba ifikapo mwaka 2021 vijiji vyote viwe na umemeTanzania na ndivyo hata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka2015 inavyosema lakini hadi leo 2019 inaisha vijiji vingihavijapata umeme na 2021 ni kesho kutwa tu bado mwakammoja tunafika 2021. Ni nini mpango wa Serikali kuhakikishakwamba ifikapo mwaka 2021 vijiji vyote Tanzania vitakuwana umeme? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu ya swali hilo,tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imedhamiria kupelekaumeme kwa wananchi mpaka ngazi ya vijiji na Serikali kupitiaWizara ya Nishati kupitia Shirika letu la TANESCO na taasisiyetu ya REA kazi hiyo inaendelea kutekelezwa kwa awamukama ambavyo wamejipangia. Mamlaka hii inayo taarifa nainayo maelekezo sahihi kutoka Serikalini kwamba tunatakakuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme. Hata Raiswetu wa nchi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakatiwote anapozungumza anaendelea kusisitiza kwambaanataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme.(Makofi)

Page 8: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba kilanyumba ya Mtanzania inawaka umeme amepunguza na beiili Watanzania wote mpaka wale wa vijijini wamudu kuvutaumeme kupeleka majumbani kwao kwa thamani ya shilingi27,000 tu. Ameenda mbali zaidi kwamba Watanzania hawaambao hawana uwezo wa kununua gharama za bidhaanyingine za kupeleka umeme kwenye maeneo yao ikiwemonguzo na nyaya bado Mtanzania akilipa shilingi 27,000 kulekijijini nguzo za kufika nyumbani kwake ni bure hakuna kulipa.Hata nyaya zenyewe ni bure mpaka nyumbani kwake. Kwahiyo, Mtanzania anapaswa kulipa shilingi 27,000 tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, azma ya Serikali hiiambayo tumejipangia mpaka mwaka 2021 kwamba kilanyumba ya Mtanzania iweze kupata umeme tumejipangavizuri na kazi hiyo inaendelea vizuri na taasisi yetu ya REA.Kila Wilaya tumepeleka wakandarasi na wanaendelea nakazi yao. Tulikuwa na tatizo la nguzo, tatizo hilo sasalimekwisha kwani tuna nguzo za kutosha kule Mufindi. Mimimwenyewe nimeenda kushuhudia uwepo wa nguzo kwenyemakampuni yanayozalisha nguzo.

Kwa hiyo, kazi zinaendelea vizuri na malengo yetuyatafikiwa. Kama itatokea kutakuwa na tatizo lolote hapakatikati tusiweze kumudu kufikia vijiji vyote ambavyotumejipangia kufikia mwaka 2021, nataka niwahakikishieWatanzania kuwa zoezi la uwekaji umeme vijijini litaendeleakwa awamu nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niwahakikishieWatanzania mpaka ngazi ya vijiji kwamba malengo ya Serikaliya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijinibado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazihiyo inasimamiwa vizuri sana na Wizara ya Nishati na ninyiwenyewe mnajua Waziri wa Nishati, Naibu Waziri wa Nishatiwametoa maelezo hayo mara kadhaa kuwahakikishiaWatanzania kwamba umeme utapatikana. Jambo lamuhimu zaidi tupeane ushirikiano, tuwape fursa wakandarasiwafanye kazi yao vizuri, tuwape nafasi Watanzania washirikikwenye ajira hizo ili wafanye kazi kwa bidii ili malengo haya

Page 9: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

ya kufikisha umeme kwenye nyumba mpaka ngazi ya kijijiyaweze kufikiwa. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa tunahamia upande waCHADEMA, Mheshimiwa Devotha Mathew Minja, uliza swalilako tafadhali.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni kumekuwa namatamko mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,TAMISEMI na Naibu wake wakisisitiza kwamba Uchaguzi waSerikali ya Mtaa upo pale pale tarehe 24 Novemba, 2019 lichaya Vyama vya Upinzani kujitoa. Aidha, Mawaziri haowamekuwa wakisisitiza kwamba kujitoa…

SPIKA: Mheshimiwa Devotha, Kanuni zetu zinakataaMbunge kuandikiwa swali huko, akaja hapa akaanzakutusomea. Kwa kuwa swali hilo linaonekana rasmi kwambasiyo la kwako. (Makofi)

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,hapana

SPIKA: …bali umeandikiwa na watu hukowaliokutuma…

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika,sijaandikiwa…

SPIKA: …kwahiyo namuita Mheshimiwa Mussa BakariMbarouk…

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika, aahh!!

SPIKA:…uliza swali lako.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsante.Mimi kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu lakini

Page 10: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

pia nikushukuru wewe kwa kunipa nafasi. Swali languMheshimiwa Waziri Mkuu ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika tumekuwa na taratibu za kupewabei za mafuta kila mwezi na hii Taasisi ya EWURA, lakini sasakwa Mkoa wetu wa Tanga watu wamekuwa na malalamikokidogo, kwamba mafuta ya Petrol na Diesel yamekuwa beikubwa ilhali yanashushwa pale pale. kwa mfano, Tanga Petrolsasa hivi lita ni shilingi 2,300 na Diesel ni kama kwenye shilingi2,200 ilhali hapa Dodoma, Petrol ilikuwa ni shilingi 2,153 navilevile Diesel ikawa ni kama kwenye shilingi 2,100.

Mheshimiwa Spika, sasa nilikuwa nataka kujua, nivigezo gani vinavyotumika kwa hii bei ya mafuta kwa baadhiya Mikoa kama Tanga, ambako mafuta yanashushwa palepale lakini bei iko kubwa kuliko Dodoma, kuliko Iringa, kulikoSingira na Mikoa mingine? Ahsante.

SPIKA: Najaribu kupima kama vigezo gani ni swali laWaziri Mkuu au ni swali linalotakiwa liende kwa Waziri wasekta. Mheshimiwa Waziri Mkuu kama una jambo labdakidogo tu; limenipa tabu kidogo lakini karibu MheshimiwaWaziri Mkuu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ahsante, ahsante.

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Mbunge wa Tanga Manispaa kama ifuatavyo:-

Ni kweli kwamba swali hili linahusisha takwimu maanalazima nieleze kanuni iliyotumika kufanya calculation hiyo.Hata hivyo kimsingi mafuta haya yanaangizwa kutoka njeya Tanzania na kufika nchini; na yanapofika nchinihawaangalii yametua kwenye bandari gani lakini gharamaza kutoka huko yanakotoka mpaka Tanzania kuanzia haposasa kupitia kanuni hiyo ndiyo yanatoa mgao wa mikoa hiikupata hizo bei. Sina uhakika Tanga wananunua shilingi ngapina huko Mwanza wananunua shilingi ngapi ili kukidhimatakwa yako; lakini muhimu zaidi Waziri wa Nishati yukohapa, ameisikia na kama kweli Tanga wananunua gharama

Page 11: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

hiyo, na kama mafuta yanafika Tanga bei ni hiyo atakuwaamesikia basi nimpe fursa Mheshimiwa Waziri baada yakipindi hiki ukutane naye ili aweze kukuelewesha kwamanufaa ya wananchi wa Tanga ili tuweze kuondoa hilojambo ambalo unaona kama vile haliwezekani na kwamaelezo utakayopata naamini pia utaridhika na wanunuzipia nao wataridhika. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi ulizaswali lako Mheshimiwa.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa nafasi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu sekta yaelimu na afya zina upungufu mkubwa sana wa watumishi;na hii imechangiwa hasa katika sekta ya afya kutokana naujenzi wa hospitali za Wilaya 69 lakini pia ujenzi wa vituo vyaafya 350 na zahanati karibia kila Kijiji Nchi nzima. Sasa ni upimkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunapata watumishiwa kutosha kwenda kuwahudumia Watanzania ili ile dhananzima ya kupeleka huduma kwa Wananchi iweze kutimia?Ahsante.

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuutafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Shangazi, Mbunge wa Mlalo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba sekta hizi mbili,ya elimu na afya zina mahitaji makubwa ya watumishikwasababu pia tumepeleka maeneo ya utoaji huduma zakempaka ngazi ya vitongoji. Vilevile ukweli mwingine ni kwambawote ni mashahidi namna ambavyo tumefanya maboreshokama sera yetu inavyohitaji; kwamba kwenye sekta ya afyasera yetu inasema kila kijiji kiwe na zahanati na angalau kilakata kuwe na kituo cha afya na kila wilaya kuwe na hospitaliya wilaya. Kazi ambayo sasa inafanywa ni ya ujenzi wazahanati kupitia wanakijiji wenyewe na halmashauri zao, vituo

Page 12: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

vya afya kwa mpango wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI wa ujenzimzuri, mkubwa unaonedelea sasa wa vituo vya afya vyenyemahitaji makubwa ya madaktari; vivyo hivyo, kwenye sektaya elimu.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sera yetu kwenyesekta ya elimu tunapeleka huduma ya elimu mpaka kwenyevijiji kwa kujenga shule za msingi; na kwenye vitongoji vikubwatuna zile shule zinazoitwa shule bebeshi (satellite schools)ambazo pia zinatakiwa zijengwe ili kuwarahisishia watotokusafiri kwa umbali mfupi.

Mheshimiwa Spika, maeneo yote haya yanahitajiwataalam, walimu na waganga upanda wa afya. Nini Serikaliinafanya; ni kuongeza watumishi kadri tunavyoongezamiundombinu; na watumishi hawa ni pamoja na vifaa vyake.

Mheshimiwa Spika, upande wa watumishi, Serikaliimeanza kutoa vibali vya ajira kwa sekta hizi mbili za afya naelimu; na sasa tumeenda hata pia kwenye kilimo kwa kupatamaafisa ugani kwenda vijijini kusaidia wakulima kulima vizurikwa vigezo.

Mheshimiwa Spika, upande wa elimu tumeshaajirikuanzia mwaka 2016, na mwaka jana tumeajiri kwa mara yamwisho walimu 6,000 na sasa tuna kibali ambacho kitatokahivi karibuni cha walimu 16,000 kwa upande wa sekondarina msingi. Kwahiyo, tunaamini kwenye sekta ya elimu baadaya ajira hii tutakuwa tumepunguza kwa kiasi kikubwa uhabawa walimu kwenye shule za msingi.

Mheshimiwa Spika, hivyo hivyo kwenye sekta ya afya,huko ambako tunajenga vituo vya afya vingi, hospitali zawilaya lakini pia na hospitali za rufaa za mikoa na za kanda;kote huko lazima tuhakikishe tunapeleka watalam ili wawezekuhudumia Watanzania maeneo hayo. Kwahiyo mkakatiwetu ni kutoa vibali kadri Wizara zinavyotoa taarifa namahitaji yake na kadri ambavyo tuna uwezo wa kifedhatunatoa ajira hizo, na tunaendelea nazo. Kwahiyo natakaniwasihi Watanzania, mkakati wetu wa kujenga miundmbinu

Page 13: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

hautaishia hapo, tutakwenda pia na kuleta wataalam kwakuajiri. Kwahiyo wasomi wetu walioko vyuoni na wale ambaowako nje wanasubiri ajira tunayo matumaini tukitoa vibaliwatapata matangazo wajitokeze na kila mmoja akubalikupelekwa kwenye kituo anakopelekwa il i awezekufanyakazi. Kwahiyo Mheshimiwa Mbunge utoaji wa vibaliutaendelea, na tutapeleka watumishi wa afya mpakaWilayani Lushoto na tutahakikisha tunapeleka mpka Mlalokwenye vijiji vyako na kwenye kata zako ili kuwe na Watumishiwatakaoweza kusaidiana na Wananchi katika kutoa hudumahii. Ahsante sana.

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Sikudhani YassiniChikambo, uliza swali lako.

MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Spika,ahsante Mheshimiwa Waziri Mkuu miongoni mwa mazao yabiashara ambayo yamekuwa yakilipatia Pato Taifa letu nipamoja na zao la korosho. Katika msimu wa mwaka 2018/2019 wakulima walitimiza wajibu wao, walilima koroshowakazipeleka ghalani lakini hawakupata pesa kwa wakati,na hii imepelekea kuwa na mashaka makubwa. Je, Serikaliimejipangaje katika msimu huu ambao umeshaanzakuhakikisha wakulima wale wanapeleka korosho ghalani nawanapata pesa kwa wakati kulingana na Sheria ya minadainavyosema? Ahsante.

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuutafadhali la wakulima wa korosho.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Chikambo, Mbunge wa Mkoa wa Ruvumakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba msimu wamwaka 2018/2019 mfumo uliotumika kununua zao la koroshgohaukuwa mfumo rasmi bali ilikuwa ni kuokoa mazingirayaliyojitokeza kutokana na tabia iliyoonyeshwa na baadhiya wafanyabiashara ya kutaka kuhujumu zao hili na hasakuwapunja wakulima. Kwahiyo Serikali kupitia Mheshimiwa

Page 14: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Rais alifanya maamuzi ya kununua kwa gharama ya shilingi3,300 korosho zote; na msimu ule tulizalisha vizuri sana kwatani zaidi ya 230,000, na koroshgo zote zimeendelea kulipiwakwa wakulima.

Mheshimiwa Spika, kiwango cha mwiho kilichokuwakimebaki ni bilioni 40 ambayo baada ya kukutana na Wakuuwa Mikoa wanaotoka kwneye Mikoa inayozalisha koroshowalimpa taarifa Mheshimiwa Rais ya madai hayo yawakulima kila mkoa. Yalipojumlishwa yalikuwa ni bilioni 40 naMhehsimiwa Rais alitoa kibali kwa hazina kutoa bilioni 40 maramoja na bilioni 40 zote zimetoka na sasa kazi ya ulioajiinaendelea. Ninaamini mikoa mingine tilishamaliza kamailikuwa na wakulima wachache ukiondoa Mkoa wa Mtwaraambao una wakulima wengi wa korosho kwahiyo tunaaminimalipo haya yanaendelea.

Mheshimiwa Spika, sasa msimu wa mwaka huu 2019/2020 umeshaanza mwezi Oktoba na kazi ya manunu ziimeanza na tumeamua mfumo ule ule uliuokuwa unatumikakuuzia zao la korosho ambao ulikuwana tafrani hiyounaendelea; na mfumo wetu ni wa Ushirika na ni kwa njia yaminada. Tangu tumeanza minada yetu mpaka leo hakunatatizo lolote lile minada inaendelea. Naamini kuna idadikubwaya minada imeshafanywa Mtwara, Mkoa wa Ruvumana Mkoa wa Lindi ambako korosho zimeshaanza nahatujapata kelele.

Mheshimiwa Spika, kwahiyo, niseme tu kwambaseriakli imejipanga vizuri kusimamia minada hiyo kamaambavyo tumesimamia hii iliyoko tayari na wakulimawatapata fedha zao. Tumeweka masharti, mnunuzi yoyoteatakayepata offer ya ule mnada kwamba yeye ndiyoanapaswa kununua kama alivyoomba, tumempa siku nnetu za kisheria. Tumesimamia ndani ya siku nne aweameshalipa fedha hiyo kwa chama kikuu cha ushirika; nachama kikuu cha ushirika kupeleka chama cha msingi chaushirika na kumfikishia mkulima. Angalau tumetenga siku sabampaka 10 mkulima awe ameshalipwa malipo yake yote.

Page 15: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Kwahiyo ni imani yangu hata minada iliyotanguliawakulima watakuwa wameshalipwa kutokana na usimamizina Sheria hiiz ambazo tumejiwekea ambazo pia wanunuziwenyewe walikubali walipokuwa wanasaini kukubali kununuamazao haya. Kwahiyo nataka niwaondolee mashakaWaheshimiwa Wabunge mnaotoka kwenye maeneoyanayolima korosho, niwaondolee mashaka pia wakulimaambao pia sasa korosho zenu mnapeleka kwenye masokokwamba Serikali itasimamia kikamilifu kuhakikisha kwambawakulima mnalipwa kwa wakati kama ambavyotumekubaliana na wanunuzi na biashara itakwenda bila yakuwa na mgogoro wowote ukiondoa ule utaratibu uliotumikamwaka jana ambao haukuwa wa kawaida. Ahsante sana.(Makofi)

SPIKA: Ahsante. Swali la mwisho kwa siku ya leolitaulizwa na Kamishina, Mary Pius Chatanda. MheshimiwaChatanda uliza swali lako tafadhali.

MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Spika,nashukuru.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, mvuaambazo zimeendelea kunyesha hapa nchini hususani Mikoaya Pwani zimeathiri sana miundombinu ya barabara pamojana vifo ambavyo vimetokea katika mikoa hiyo. Sasa basi,Serikali imejipangaje kuwasaidia TARURA na TANROADSkuwapa fedha za kutosha ili waweze kukamilisha barabarazile ambazo zimeharibiwa kabla ya mvua za masika?

Mheshimiwa Waziri Mkuu nashukuru sana.

SPIKA: Mvua zimekuwa kubwa sana Korogwe naHandeni mwaka huu. Mheshimiwa Waziri Mkuu majibu yaswali hilo tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Kamishina Chatanda, Mbunge wa KorogweMjini kama ifuatavyo:-

Page 16: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Kwanza nianze kwa kutoa pole nyingi sana kwaWaheshimiwa Wabunge na wakazi wa Mkoa wa Tangaambao wamepata athari kubwa ya kuondokewa nawenzetu kufutia mvua kubwa zilizonyesha wiki moja, mbilizilizopita. Tuwaombee Mwenyezi Mungu azilaze roho zaomahali pema peponi, Amina.

Mheshimiwa Spika, kufuatia mvua hizi ambazozinanyesha kwa wingi na kuharibu miundombinu yetu, Serikalitumejipanga; na mpango wetu kupitia TARURA na TANROADSkwenye maeneo yote nchini pamoja na kamati za maafaambazo pia zinasimamiwa na Wakuu wa Wilaya, Wakuu waMikoa kwenye ngazi zao wanaendelea kufuatilia mwenendowa mvua hizi na madhara yake. Pale ambapo kuna madharahatua za haraka zitachukuliwa na Kamati zile za maafa nawatashirikiana na taasisi zinazohusika na maafa hayo;ikiwemo na kuondolewa kwa miundombinu ya barabara kwaTANROADS na TARURA. Tayari maeneo ya Mkoa wa Tangaambayo yamepata athari, TARURA na TANROADSwamefanyakazi yao.

Mheshimiwa Spika, utakumbuka lilipotokea suala lakuvunjika daraja linalounganisha kati ya Tanga na Pangani,Mheshimiwa Rais alir idhia Jeshi la Wananchi l iendelikafanyekazi hiyo kwa haraka sana ili kusaidia TARURA naTANROADS kurudisha miundombinu angalau kuwezeshawananchi kupita na kuendelea na huduma zao, huo ndiyomkakati ambapo tunauweka.

Mheshimiwa Spika, pale ambapo inatokeatunapeleka huduma ya dharura halafu tunawaongezeabajeti watu wa TARURA na TANROADS kuendelea kuimarishamiundmbinu hiyo na kuirudisha katika hali yake ya kwaida.Kwahiyo Serikali imejipanga vizuri kwenye hili kwasababu inaoutaratibu mzuri tu kuanzia huko mwanzo.

Mheshimiwa Spika, kufuatia bajeti inategemea mradihuo utagharimu kiasi gani, mwaka huu wa fedha walipangakiasi gani, kama kuna mapungufu kwa umhimu huotutawaongezea fedha ili waweze kukamilisha ujenzi wa

Page 17: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

miundmbinu hiyo. Kwa hiyo, Serikali itaendelea kushirikianana vyombo vyetu kwenye maeneo yote Nchini kusimamiautoaji huduma kwa Wananchi iwe ni kwa hali ya kwaida aupanapotokea dharura na tutalichukua jambo hilo kwadharura hiyo hiyo kuhakikisha kwamba tunaokoamiundombinu hiyo kwa haraka sana.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa maswali hayo.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mudawa nusu saa wa maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuuumekamilika. Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuukwa heshima uliyotupatia ya kuwepo na kuweza kujibumaswali ya Waheshimiwa Wabunge, naamini nchi nzimailikuwa ikifuatilia na wananchi wamefaidika sana kwamaelezo yako ambayo pia ni maelezo ya Serikali.

Katibu!

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

MASWALI NA MAJIBU

Na. 100

Mji wa Mombo Kuwa Halmashauri ya Mji

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:-

Mji wa Mombo umekidhi vigezo vyote vya kuwaHalmashauri ya Mji na maombi yalishawasilishwa Serikalini.

Je, ni lini Serikali itaipa Mji wa Mombo hadhi yaHalmashauri ya Mji?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MITAA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante.

Page 18: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisiya Rais, TAMISEMI,naomba kujibu swali la MheshimiwaTimetheo Paul Mnzava, Mbunge wa Korogwe Vijijini kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwambamaombi yakupandisha hadhi mamlaka ya Mji mdogo wa Mombo kuwaHalmashauri ya Mji yaliwasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMIAgosti, 2016. Timu ya kuhakiki kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMIilifika Mombo kufanya uhakiki wa vigezo vinavyotakiwa ilikuupandisha mji huo hadhi.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya uhakiki inaonesha kuwakulingana na Mwongozo wa Kuanzisha Maeneo ya Utawalawa Mwaka 2014, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mombohaukukidhi vigezo vya kupanda hadhi na kuwa Halmashauriya Mji, na walijulishwa kwa barua yenye Kumb. Na. CCB.132/394/01/16. Baadhi ya vigezo ilivyoshindwa kukidhi ni pamojana idadi ya watu wasiopungua 150,000, eneo lenye ukubwausiopungua kilomita za mraba 300 na kata zisizopungua 12.Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Mnzava umesima, tafadhali.

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri,masharti ambayo tulipewa tukishayafanyiakazi na yalishakaavizuri. Hata hivyo naomba niulize maswali madogo mawili yanyongeza:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa majibuhaya hayaoneshi matumaini ya Mji Mdogo wa Mombo kuwaHalmashauri ya Mji. Mheshimiwa Waziri unajua kwamba eneolikishatangazwa kuwa mamlaka ya Mji Mdogo, vijiji vinafutwa;jambo linalosababisha kubadilika kwa taratibu za uendeshajiikiwemo ukusanyaji wa mapato na utumiaji wake; nainasimamiwa moja kwa moja na Halmashauri ya Wilaya.

Mheshimiwa Spika, nataka kujua Serikali haionikwamba iko haja sasa ya kupitia upya taratibu za uendeshaji

Page 19: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

wa mamlaka za miji midogo ili kuweze kuboresha na kusaidiamamlaka ili ziweze kufanyakazi zake vizuri?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Jiografia na ukubwawa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe imekuwa nichangamoto, jambo linalosababisha migogoro kwneye eneola kujenga hospitali ya wilaya lakini pia hata sasa kwenyeeneo la kujenga Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya.Pamoja na kwamba Baraza la Madiwani limeshafanyamaamuzi, ni lini Serikali itakuwa tayari kupitia upya mipakaya maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe naHalmashauri ya Mji wa Korogwe ili kuondoa changamoto hizikwa wananchi wetu?

SPIKA: Majibu ya swali hilo tafadhali MheshimiwaNaibu Waziri, TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MITAA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisiya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Timetheo Mnzava, Mbunge waKorogwe Vijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tumepokea hoja za MheshimiwaMbunge. Hata hivyo, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi,ni kwamba tulipotuma timu kutoka TAMISEMI ikaenda kuleKorogwe baadhi ya vigezo vilikuwa havijakamilika. Kwamaelezo yake ni kwamba vigezo vimekamilika naanazungumza habari ya ukubwa wa eneo na mipaka yaeneo hilo. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbungetutachukua mawazo yake, tutayafanyiakazi, tushirikiane paleitakapowezekana Serikali iweze kuchukua hatua. Lengo laSerikali ni kwamba maeneo haya yasimamiwe vizuriwananchi wetu waweze kupata huduma kirahisi nakupunguza migogoro katika maeneo yetu ya kiutawala.Ahsante.

Page 20: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Hasna Mwilimanimekuona, swali la nyongeza tafadhali.

MHE. HASNA S. MWILIMA: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza. Kwa ruhusa yako, naomba kabla sijauliza swali lanyongeza, tarehe 7 Novemba, 2019 nikiwa hapa Bungeniwakati nachangia Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitanonilichangia jambo ambalo kwa namna moja au nyingineinaweza ikawa limewagusa sana Watanzania lakini piabaadhi ya Waheshimiwa Wabunge humu ndani ya Bunge.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nil ifanya vile kwa kutakakuboresha Shirika letu la ATCL, lakini kwa kuwa inawezekanakwa namna moja au nyingine nikawa nimewakwazaWatanzania hasa wanawake wenzangu, naomba nichukuenafasi hii kuomba radhi kwa kauli yangu ile ambayo niliitoahapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwaomba radhiWatanzania hasa wanawake wenzangu, naomba sasaniulize…

SPIKA: Mheshimiwa Hasna kabla hujaendelea natakakuwaambia Waheshimiwa Wabunge, huo ndiyo uungwana!(Makofi)

Tumeipokea radhi hiyo. Mheshimiwa, endelea kuulizaswali.

MHE. HASNA S. MWILIMA: Mheshimiwa Spika, naombasasa niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Mji wanguwa Nguruka ambao una vijiji viwili tumeshaomba sanaTAMISEMI Mji ule uweze kukuzwa na uwe Mamlaka ya MjiMdogo, lakini kwa mujibu wa vigezo lazima Kata ya Nguruka,Kata ya Itebula zipewe mamlaka ya kuongeza vijiji nakuongeza vitongoji ili waweze kukidhi haja. Kwa kuwa Mjiule una watu zaidi ya 100,000 niombe sasa Serikali yaTAMISEMI.

Page 21: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Je, iko tayari kutupa ruhusa ya kufanya mchakato wakuongeza vijiji na vitongoji ili tuweze kukidhi haja ya kuwa naMji Mdogo wa Mamlaka ya Nguruka. Nakushukuru.

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Naibu WaziriTAMISEMI, Mheshimiwa Mwita Waitara, majibu kuhusu Mji waNguruka.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Hasna Mwilima,Mbunge wa Uvinza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyosemaMheshimiwa Mbunge mwenyewe kwamba tayari eneo lakehalikidhi vigezo vya eneo hili kuwa mji mdogo kwa maanaya Mamlaka, lakini tunaomba tupokee maoni yaketutayafanyia kazi na pale ambapo itakuwa imekidhi vigezo,basi tutaona namna ya kuboresha eneo hili. Ni kweli kwambaMji wa Nguruka ni Mji mkubwa, ukipata hadhi unawezaukawa wa kwanza kiuchumi, lakini pia kupeleka karibuhuduma za wananchi. Ahsante.

SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na swali 101 naMheshimiwa Upendo Furaha Peneza, Mbunge wa VitiMaalum. Nimekuona Mheshimiwa Susan Lyimo.

Na. 101

Kuwahamisha Wananchi Walio Karibu na Mgodi wa GGM

MHE. SUSAN A. J. LYIMO (K.n.y. MHE. UPENDO F.PENEZA) aliuliza:-

Wananchi wa maeneo ya Katoma Kompaundi,Nyakabale wameathirika sana na shughuli za mgodi wa GGMna Serikali ilikwishatoa maelekezo kwamba wananchi wamaeneo hayo wahamishwe:-

Je, ni lini sasa wananchi hao watahamishwa?

Page 22: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Upendo Furaha Peneza, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kifungu cha 95(b)cha Sheria ya Madini, mgodi unapaswa kulipa fidia kwawananchi wanaomiliki maeneo yanayozunguka eneo lauchimbaji lenye umbali wa mita 200. Hata hivyo, mwaka 2013,Mgodi wa GGM ulilipa fidia kwa wananchi walioko katikaeneo lenye kipenyo cha mita 500 katika Mitaa ya KatomaKompaundi na Nyamalembo ambapo wananchi 155walilipwa kiasi cha shilingi bilioni 6.83. Aidha, kwa upandewa Nyakabale, Mgodi haukuwalipa wananchi fidia kwa kuwamaeneo yao yapo zaidi ya umbali wa mita 200 kutoka eneola mgodi.

Mheshimiwa Spika, wananchi wote 155 waliolipwafidia mwaka 2013 wanapaswa kuachia maeneo hayoyaliyofidiwa ili kupisha shughuli za uchimbaji. Naielekeza Ofisiya Mkuu wa Mkoa wa Geita kusimamia zoezi la kuwahamishawananchi hao. Ahsante.

SPIKA: Ahsante. Endelea Mheshimiwa Suzan Lyimo.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogoya nyongeza. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri,katika viwango vya Kimataifa huwa wanapima maeneoambayo hayatapata athari hizo. Swali la kwanza, je, Serikaliiko tayari sasa kuunda Tume au Kamati yoyote kupimamaeneo hayo ili wannachi wasije wakajenga nyumba karibuna maeneo hayo ambayo yanaweza kupata mitetemo paleambapo migodi hiyo inapasua miamba?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa kauli mbiuya Awamu ya Tano ni Hapa Kazi Tu na kwa kuwa wananchi

Page 23: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

wengi katika maeneo haya wanapokuwa wanahamishwamaana yake wanapata madhara ya kisaikolojia na kwamaana hiyo wanashindwa hata kufanya kazi. Je, Serikalihaioni kutokuwahamisha kwa wakati kutapoteza dhana hiyoya Hapa Kazi Tu?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, MheshimiwaMwita Waitara, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaSpika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Susan Lyimo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ametoaushauri tunaomba tuupokee. Tutaangalia kiutaalam sheriazinasemaje kwa sababu tuna sheria za uchimbaji hapa nchini.Kama zitaonekana zinafaa basi zitafanyiwa kazi. Hilo lakupima maeneo ya mitetemo ili kutoathiri nyumba za watu.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili kama nilivyoelekezakwenye jibu langu la msingi na kimsingi hii imekuwa ni maeneomengi kwamba kunakuwa na fidia zinaandaliwa watuwanalipwa halafu wanahama au wakati mwinginewanachukua muda mwingi sana. Sasa hivi tumeshaelekezakwamba Mkuu wa Mkoa wa eneo hili aweze kuchukua hatuakuwahamisha wananchi ambao kimsingi wameshalipwa fidiana hawadai ili wapishe eneo hilo wale wenye shughuli zaoza uchimbaji waende kufanya kazi zao bila vikwazo nakuondoa migogoro.

Mheshimiwa Spika, pia nitoe wito kwa wananchi wetuwa Tanzania wenyewe kwamba kama kuna eneo linachukuashughuli ya kiuchumi kama ya machimbo na tayari mtualishalipwa fidia ni muhimu ahame katika eneo hilo kwasababu anaendelea kukaa pale kwa muda mrefu, halafuukienda kuwaondoa wanaanza malalamiko na migogoro,utakuta gharama ya vitu inapanda bei. Kwa hiyo wenyewewachukue hatua, tumeshakulipa fedha upishe eneo lile

Page 24: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

ukaanzishe maisha mengine ili kuepuka migogoro mbalimbalikatika maeneo haya. Ahsante.

SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Devotha Minja, ulizaswali lako tafadhali.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Mheshimiwa Naibu Waziri amesikika akisisitizakwamba hata kama Vyama Vya Upinzani vimejitoa kwenyeuchaguzi wa Serikali za Mitaa haviwezi kuzuia uchaguzi kwakuwa Serikali ina-deal moja kwa moja na wagombea na sioVyama vya Upinzani.

Mheshimiwa Spika, naomba kumuuliza MheshimiwaWaziri, hivi…

SPIKA: Mheshimiwa Devotha, leo umeamka kushotokabisa. (Kicheko)

Swali la nyongeza lazima liendane na swali la msingi.Swali la msingi linahusu wananchi wa Katoma, Nyakabalena wengine ambao wamethirika na shughuli za mgodi waGGM, sasa swali lako la nyongeza liko nje kabisa. Ni bahatimbaya sana. Tunaendelea, Mheshimiwa Naibu Waziri…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila kufuatautaratibu)

SPIKA: Hapana, swali nimeli-disqualify…

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, nilikuwanataka niboreshe katika lile swali la nyongeza aliloulizaMheshimiwa Lyimo.

SPIKA: Ok, haya hilo nakuruhusu.

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Katika swali la kwanza la Mheshimiwa Lyimo nikwamba kwa mujibu wa Sheria ya Uchimbaji sehemu yoyoteambayo ni active mining area yaani sehemu ambapo kuna

Page 25: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

shughuli za uchimbaji zinafanyika, Mwekezaji anatakiwa a-compensate mita 200 zaidi ya lile eneo ambalo ni active areakwa maana ya buffer area ili kuwaondoa hawa watu wasiwekaribu na maeneo ambayo wanaweza wakapata mitetemona nyumba zikapata nyufa.

Kwa hiyo wanatakiwa wakishalipwa compensationmita 200 watoke lile eneo kwa maana ya kuzuia hiyomitetemo na hii imepimwa kitaalam na ni sheria na ndiyoutaratibu wa uchimbaji. Ahsante sana.

SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na swali laMheshimiwa Joram Ismail Hongoli, Mbunge wa Lupembe.Bado tupo TAMISEMI. Mheshimiwa Hongoli uliza swali lako

Na. 102

Fedha kwa Ajili ya Ukarabati wa Vituo vya Afya

MHE. JORAM I. HONGOLI aliuliza:-

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ndiyo Halmashauripekee iliyokosa fedha kwa ajili ya ukarabati wa Vituo vyaAfya:-

Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ukarabatiwa Vituo vya Afya katika Jimbo la Lupembe ikiwemo Kichiwa,Lupembe, Sovi na Kituo cha Afya Ikina ambacho wananchiwamejenga OPD bado majengo mengine ili kukamilika?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, MheshimiwaJosephat Sinkamba Kandege, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa JoramIsmael Hongoli, Mbunge wa Lupembe, kama ifuatavyo:-

Page 26: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020, Serikali imeidhinisha kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajiliya ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya Kichiwa kilichopokatika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Aidha, Kituo chaAfya Lupembe kimeidhinishiwa shilingi milioni 25 kupitia Mfukowa Pamoja wa Afya kwa ajili ya ukarabati ili kukiwezeshakutoa huduma za dharura na upasuaji.

SPIKA: Mheshimiwa Hongoli, swali la nyongeza.

MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Spika, ahsante.Kwanza nianze kuishukuru Serikali kwa kutenga hizi fedhamilioni 200 na milioni 25, lakini pia nishukuru kwa kutupatiabilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.

Mheshimiwa Spika, nina swali moja tu la nyongeza;kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kupitia mapatoyake ya ndani na nguvu za wananchi imeweza kujenga Kituocha Afya cha Ikuna lakini hatujafanikiwa kujenga wodi kwaajili ya wagonjwa. Pia halmashauri na kupitia nguvu zawananchi imeweza kujenga jengo la mama na mtoto paleLupembe, imeweza pia kukarabati chumba kwa ajili yaupasuaji na upasuaji ulishaanza toka mwaka 2017. Tatizotulilonalo pale hatuna mawodi ya kutosha, je, Serikali ipotayari kusaidia kuhakikisha kwamba kunakuwa na wodi zakutosha ili wananchi wakipata operation waweze kupatahuduma nzuri zaidi kwa ajili ya kupumzika na kupata huduma?Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Majibu kwa maswali hayo mawili, MheshimiwaNaibu Waziri TAMISEMI, Mheshimiwa Kandege, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, naomba nijibu swali la nyongeza la MheshimiwaHongoli kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, niruhusu kipekee nimpongezeMheshimiwa Hongoli na wananchi wake. Kama kunamaeneo ambayo wananchi wanajitolea kwa kufanya kazi

Page 27: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

ni pamoja na jimbo lake, lakini pia yeye mwenyeweamekuwa mfuatiliaji mkubwa sana kuhakikisha kwambawananchi wake wanapata zahanati, vituo vya afya pamojana hospitali za halmashauri. Naomba nimhakikishie ni azmaya Serikali kuwaunga mkono wananchi popote pale ambapowanaonesha nguvu yao na sisi kama TAMISEMI tutahakikishakwamba tunaunga mkono il i wodi ziweze kujengwawananchi waweze kupumzika baada ya kupata matibabu.

SPIKA: Ahsante sana. Nataka tu kusema kwambaSerikali inafanya kazi nzuri sana ya kujenga zahanati, vituovya afya na kadhalika nzuri sana, lakini katika matumizi yadawa kwenye zahanati na vituo vya afya, makusanyo yalekupitia user fee yamekuwa ni madogo sana ambayoyanakuwa realized. Makusanyo yale ni muhimu katikakuviboresha vituo vya afya kiuendeshaji. Yamekuwa nimadogo sana kwa sababu ya mfumo unaotumika, unaitwasijui GoT-HoMIS, sijui unaitwaje, lakini huo mfumo kuununua kwakituo cha afya ni milioni 14.

Sasa fikiria vituo vya afya Tanzania milioni 14, 14zahanati milioni 14, 14 ni kwa nini vituo vya afya, huduma zaafya zitumie mfumo huo ambao ni ghali sana badala yakutumia mfumo mwingine wowote ambao ni rahisi tenamfumo wenyewe hauingiliani na mifumo ya halmashauri. Kwahiyo vituo vingi viko havina mfumo wowote, wanajikusanyiahela wanajilia. Naomba Serikali ikaangalie habari ya huomfumo unaotumika kwenye huduma za afya, huo unaoitwaGoT-HoMIS huo yaani mapato mengi mno yanapotea kupitiaeneo hilo. (Makofi)

Tunaendelea na Ofisi ya Rais, Utumishi na UtawalaBora, swali la Amina Saleh Mollel, Mbunge wa Viti Maalum.

Na. 103

Mipango ya Usafiri kwa Watumishi wa UmmaWenye Ulemavu

MHE. AMINA S. MOLLEL aliuliza:-

Page 28: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

Mwongozo wa huduma kwa Watumishi wa UmmaWenye Ulemavu unawaelekeza waajiri kuweka mipango yausafiri wa kuwawezesha Watumishi Wenye Ulemavu kwendana kurudi kazini:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatiamafuta ya gari kwa Mtumishi ambaye ana chombo chakecha usafiri?

(b) Je, Serikali imeweka mkakati gani wakuwakopesha vyombo vya usafiri?

SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu sana MheshimiwaDkt. Mary Mwanjelwa, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Amina Saleh Mollel, lenyesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamotoza usafiri wanazokumbana nazo watumishi wenye ulemavuwakati wa kwenda na kurudi kazini au wanapohitaji usafirikwa shughuli nyingine za kikazi. Ili kuhakikisha kuwa watumishihao wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi, Taasisi zote zaUmma zimeelekezwa kupitia Mwongozo wa Huduma kwaWatumishi wa Umma Wenye Ulemavu (2008), Sura ya tatukifungu 3.15(a) kuhakikisha pale hali inaporuhusu, wawapatiewatumishi hao usafiri au walipie gharama za mafuta kwendana kurudi kazini kwa watumishi ambao wana vyombo binafsivya usafiri. Waajiri kupitia Mwongozo huo wamekuwa wakitoahuduma kulingana na mahitaji ya watumishi wa kundi hili.

(b) Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Waraka waWatumishi wa Serikali Na.3 Kumb.Na. C/AC.7/228/01/16 watarehe 30 Juni, 2011, kuhusu utaratibu wa kukopehsa fedhataslimu watumishi wa Serikali kwa ajili ya kununulia magari/

Page 29: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

pikipiki, samani na matengenezo ya magari na pikipiki iliwekamkakati wa kuwapatia watumishi wake wote wakiwemowatumishi wenye ulemavu mikopo kwa ajili ya kujinunuliavyombo vya usafiri yakiwemo magari na pikipiki. Utekelezajiwa waraka huo umekuwa ukifanyika kwa usawa kwawatumishi wote bila kujali jinsi, hali ya kimaumbile kwawatumishi wanaokidhi vigezo vya ukopaji. Waajiri wotewanakumbushwa kutoa kipaumbele kwa Watumishi wenyeulemavu ambao wanakidhi vigezo vya kukopa wakati wautekelezaji wa waraka huu. Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Amina Mollel, swali la nyongezatafadhali.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Awali ya yote kwanza niruhusu nikupongeze wewemwenyewe kwa kuwa Taasisi yako unayoiongoza imekuwamstari wa mbele kujali haki za watu wenye ulemavu tukiwemosisi Wabunge wenye ulemavu. Naomba ifahamike kwambasisi wote ni walemavu watarajiwa. Pia nimpongeze Iron LadyDkt. Mwanjelwa kwa kuwa nimekuwa msumbufu mkubwakwake kufuatilia haki za watu wenye ulemavu hasa watumishikutokana na changamoto wanazokutana nazo.

Mheshimiwa Spika, sasa nina maswali mawili yanyongeza. La kwanza, ni kweli kuwa taasisi nyingi hazitumiimwongozo huu na miongozo hii inatokana na haki za watuwenye ulemavu ambazo nchi imeridhia mikataba mbalimbaliya Kimataifa. Mimi nilikuwa muajiriwa na sikuwahi kuona hililikifanyika na maeneo mengi nimepata malalamiko haya yawatumishi. Sasa naomba kufahamu kutoka kwa Serikali ni ninitamko lao hasa kwa zile Taasisi za Serikali ambazo hazitimizikabisa sheria hii? Naomba kujua tamko la Serikali.

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, ningependakufahamu kwamba ni kweli kwamba Waraka huo Na.3ambao unaruhusu watumishi wa Serikali kupewa mikopokupitia HAZINA. Ningependa kufahamu kipaumbele kwawatu wenye ulemavu kutokana na changamoto na kamanilivyosema sisi wote ni walemavu watarajiwa na hasa ajali

Page 30: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

siku hizi zimekuwa ni changamoto kubwa. Sasa, je, ni mkakatigani mahsusi unaandaliwa ili basi watu wenye ulemavuwakapewa kipaumbele kwa sababu inasemwa tu ila ukiendakwenye maandishi hamna?

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mollel.Umeeleweka. Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa, majibu yaswali hilo tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, naombakujibu maswali madogo mawili ya nyongeza yote kwapamoja ya Mheshimiwa mdogo wangu Amina Mollel, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza kipekee naombanimpongeze sana yeye kama mwakilishi wa walemavu hapaBungeni kwa jinsi amnbavyo anafuatilia sana kwa karibumasuala yote yanayohusu walemavu nchini, lakini vile vilenaomba niliambie Bunge lako tukufu kwamba kila binadamuana ulemavu unaoonekana na usionekana na kila binadamupia ni mlemavu mtarajiwa.

Mheshimiwa Spika, nikianza kujibu hayo maswali yakemawili madogo ya nyongeza kwa pamoja, amezungumziaSerikali tuna mikakati gani. Naomba niliambie Bunge lakoTukufu kwamba Miongozo yote inayotolewa na Serikali ikokisheria, kisera, kikanuni mbalimbali katika kuboresha ufanisiwa kazi Serikalini. Kwa maana hiyo, kama tamko la Serikaliniwaagize waajiri wote nchini kuhakikisha kwambawanazingatia hii miongozo yote ambayo inatolewa na Serikalikwa maana ya kwamba iko kikanuni, kisheria na serambalimbali na wasipozingatia hivyo watachukuliwa hatuakali za kisheria. Nasema hivyo, kwa sababu sisi kama Serikalisasa hivi tumejipanga kuhakikisha kwamba tunatumiaMonitoring and Evaluation (M&E) kuhakikisha wale ambaohawafuatil i i hii miongozo wanajitafsir ia wenyewewanavyotaka au labda hii miongozo hawafuati basiwatachukuliwa hatua kali za kisheria.

Page 31: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Mheshimiwa Spika, vile vile naomba niseme kabisakwamba, kama Serikali katika ile Kanuni ya Sekretarieti yaAjira Kanuni ile ya mwaka 2019 tumezingatia sana walemavukwamba hata kama ni kwenye ajira, endapo huyu mlemavuamegongana katika usaili na mtu ambaye hana ulemavubasi huyu mwenye ulemavu atapewa kipaumbele.

Vilevile hata kama kuna ajira yoyote, huyu mlemavuanatakiwa anapo-apply on line anatakiwa kuzungumza niniulemavu wake ili mazingira rafiki yaweze kufanywa. Taasisiyoyote ambayo ina watumishi zaidi ya 20, basi tumewaagizakutokana na Mwongozo kwamba watenge asilia tatu kwaajili ya walemavu na haya yote pia yanafanyika hata katikaule mkopo ambao ni wa Mfuko Maalum kwa watumishi waSerikali. Ahsante.

Mheshimiwa Spika, vilevile hata kama kuna ajirayoyote huyu mlemavu anatakiwa anapo apply on lineanatakiwa kuzungumza nini ulemavu wake ili mazingira rafikiyaweze kufanywa. Na Taasisi yoyote ambayo ina watumishizaidi ya 20 basi tumewaagiza kutokana na Mwongozokwamba watenge asilia tatu kwa ajili ya walemavu na hayayote pia yanafanyika hata katika ule mkopo ambao ni wamfuko maalum kwa watumishi wa Serikali, ahsante.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri,Mheshimiwa Naibu Waziri an Serikali kwa ujumla, ulemavuupo katika makundi mengi, na kuna ulemavu ambao sasahivi ni tatizo ni janga na hasa kwa mfano vijana wa kiumematatizo mengi, sasa hizi sera ziwaguse pia na hilo kundimaalum, nafikiri mmenielewa Waheshimiwa Wabunge. Sasatunaye Balozi wa walemavu hapa nchini MheshimiwaMwamoto uliza swali lako.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi, Serikali inapoajiri hasa watuwasioona inajua kabisa wanahitaji wasaidizi, lakini wakati wakulipawa mishahara huwa hawalipwi na Serikali baliwanalipwa na wale watu wenye ulemavu.

Page 32: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Sasa haioni sasa imefikia wakati aidha, kutunga seraau kuwaweka hao wasaidizi wa watu wenye wasioona iliwalipwe nao mshahara?

SPIKA: Swali hilo hilo ni muhimu na ni zuri sana sisi Bungetukiwa na Mbunge katika wasiyoona tunampa msaidizi,kwanini Serikali haifanyi hivyo, majibu Mheshimiwa NaibuWaziri.

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTIYA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwakaka yangu Venance Mwamoto, Balozi wa walemavu nchinikama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli swali lake ni la muhimusana kwa walemavu wote wenye wasaidizi ambao huwawanatoa pesa yao wenyewe kuwalipa hao wasaidizi nawalemavu wenyewe unakuta kwamba wengine hawaoni.Lakini naomba niseme kama nilivyojibu kwenye maswaliyangu mawili ya nyongeza kwamba tunaandaa miongozomingine katika kuboresha na tayari tumekutana na wadaumbalimbali na Wizara mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu), Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya na sisiwenyewe Utumishi kuona na kuangalia ni j insi ganitunavyoweza kuboresha kanuni, Sheria mbalimbali ili tuwezekuangalia hata hilo ambalo Mheshimiwa Mwamotoamesema kwa sababu na lenyewe ni la muhimu natunalipokea kwamba tutaliweka katika ajenda ambazo vikaovinaendelea, ahsante.

SPIKA: tunaenda Viwanda na Biashara WaheshimiwaWabunge swali linauliza na Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmedupande wa CUF, Mheshimiwa Rukia uliza swali lako tafadhali.

Na.104

40% Kuajiriwa Sekta ya Viwanda Ifikapo 2020

MHE. RUKIA AHMED KASSIM aliuliza:-

Page 33: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania alisema kwamba ifikapo 2020 asilimia 40 ya Watuwawe wameajiriwa katika sekta ya Viwanda na sasa hivi nimwaka 2018.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza kauli hiyokwa wakati?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri waViwanda na Biashara majibu tafadhali.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Rukia Kassim Ahmed, Mbunge wa Viti Maalumkama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kutokana na takwimu zilizotolewana Ofisi ya Taifa ya Takwimu yaani NBS kwenye Kitabu chaHali ya Uchumi cha mwaka 2018 zinaonyesha kuwa ajirakatika Sekta ya Viwanda imeongezeka kutoka watu 254,786mwaka 2015 hadi kufikia watu 306,180 mwaka 2018, ikiwa niongezeko la watu 51,395 sawa na asilimia 20.17. Hata hivyo,ajira hizo ni za moja kwa moja mbali na zile zinazotokana namnyororo mzima wa thamani kama vile; usafirishaji, hudumaza vyakula na malazi. Ni imani yangu kuwa ajira zitaendeleakuongezeka kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, ili kuweza kuongeza kasi ya Ajirakutokana na mchango wa Sekta ya Viwanda, Wizara yanguimeelekeza nguvu kubwa katika uhamasishaji wa uanzishwajina uendelezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwakatika mnyororo wa thamani. Aidha, Serikali itaendeleakuweka mazingira wezeshi pamoja na kubuni mikakatimbalimbali ili kuwezesha wajasiliamali wa ngazi zote na hivyokuchangia ipasavyo katika kuongeza ajira.

SPIKA: Mheshimiwa Bashungwa siku hizi tunaenda nateknolojia na wewe ni Waziri kijana tunatumaini itakuwa mara

Page 34: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

ya mwisho kuja na hard copies, Mheshimiwa Rukia swali lanyongeza.

MHE. RUKIA AHMED KASSIM: Mheshimiwa Spika,ahsante pamoja na majibu mazuri ya Mheshimwia NaibuWaziri, lakini bado nina maswali mawili ya nyongeza. Sektaya Viwanda ni sekta ambayo ina ajiri watu wengi nainategemewa sana, lakini kuna baadhi ya viwandavinafungwa kutokana na ongezeko la kodi pamoja nasababu nyingine.

Je, Serikali ina mkakati gani ya kuhakikisha viwandavyote ambavyo vinatoa ajira kubwa kwa watu wetuvinaendelea kufanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili watanzania waliowengi wajasiliamali wana nia ya dhati ya kuanzisha viwandavidogo vidogo mbalimbali, lakini wanashindwa kufanya hivyokutokana na changamoto ambazo zinawakabili kama vilekukosa mitaji, pamoja na mikopo ambayo inakuwa namasharti magumu.

Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha watanzaniahawa wajasiliamali wanatimiza ndoto zao?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri tafadhali.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaSpika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Rukia Kassim Ahmed kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza la MheshimiwaRukia ni kwamba zipo changamoto za utitili wa kodi katikakufungua viwanda, na nipende kumwambia MheshimiwaRukia pamoja na Waheshimiwa Wabunge kwamba Serikaliimelitambua hilo na ukiangalia blue print mkakati wa blueprint action plan yake utitili wa kodi na kodi kero zotezimeorodheshwa katika mpango huo na Serikali tayariimeshaondoa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020

Page 35: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

kodi 54 zimeshaondolewa na tunaendelea na jitihada yakuhakikisha maeneo ambayo yameainishwa ambayo ni kerokwa viwanda na wafanyabiashara nchini kwenye blue printtutawaletea bill, Muswada wa Sheria hapa Bungeni ambaounajulikana kwa business facilitation bill ili kuweza kuchukuayale maeneo ambayo yako kwenye blue print yaingiekwenye Sheria ili tuzidi kuweka mazingira mazuri ya kujengaviwanda na kufanya biashara nchini.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ni kuhusu changamotoza wajasiliamali hasa hasa kwenye mitaji na mikopo, pamojana Waheshimiwa Wabunge jambo hili Serikali inalifanyia kazikupitia Taasisi mbalimbali Benki ya Kilimo, Baraza la UwezeshajiWananchi Kiuchumi Ofisi ya Waziri Mkuu na zile asilimia kumikwenye halmashauri zetu ambapo kuna asilimia mbili za watuwenye ulemavu, asilimia nne ya wakinamama na asilimia nneya vijana.

Pia ndani ya Serikali tunaangalia namna bora yascronize mifuko hii ili iweze kuwasaidia vijana na akinamamakatika kuwapatia mikopo yenye riba nafuu, nashukuru.

SPIKA: Ahsante sana tunaendelea na Wizara ya UjenziUchukuzi na Mawasiliano, swali linauliza na Mheshimiwa AlexRaphael Gashaza Mbunge wa Ngara.

Na. 105

Barabara Inayounganisha Rwanda na Tanzania

MHE. ALEX R. GASHAZA aliuliza:-

Barabara ya Rusumo mpakani – Murukulazo – Ngaramjini yenye urefu wa km. 24 ni barabara inayounganisha nchijirani ya Rwanda na Tanzania hususani Makao makuu yaWilaya ya Ngara kwa upande wa Tanzania.

Je, ni lini Serikali itajenga barabara hii muhimu kwakiwango ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja eneo la mtoRuvuvu unaokatiza katika barabara hiyo eneo la Rusumo feri.

Page 36: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri,Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elias JohnKwandikwa tafadhali.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali la MheshimiwaAlex Raphael Gashaza, Mbunge wa Ngara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Rusumo mpakani–Murukulazo hadi Ngara mjini ni barabara ya mkoainayosimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala waBarabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kagera. Barabarahii ina urefu wa kilometa 22.65 ambapo kilometa 21.62 ni zakiwango cha changarawe na kilometa 1.03 katika eneo laNgara mjini ni za kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wabarabara hii kiuchumi na kijamii. Kwa kutambua umuhimuhuo, Serikali imekuwa ikitoa fedha kila mwaka kuhakikishakuwa barabara hiyo inafanyiwa matengenezo ili iwe inapitikawakati wote. Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikaliimetenga jumla ya Shilingi milioni 127.966 ili kufanyamatengenezo mbalimbali katika barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Wizara yangu hainampango wa karibuni wa kujenga Daraja la Mto Ruvuvu nabarabara hiyo kwa kiwango cha lami. Aidha, Wizara yangukupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) itaendeleakukihudumia kivuko kilichopo cha Mv Ruvuvu ili kiendeleekutoa huduma kwa wananchi.

SPIKA: Mheshimiwa Gashaza Serikali haina mpangowa kujenga daraja swali la nyongeza.

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Spika, pamojana majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza, nikweli kwamba barabara hii kipande cha kilometa 22.65 kiko

Page 37: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

chini ya wakala wa barabara TANROAD. Lakini barabara hiiinaweza kuwa barabara ya kimataifa kwa sababuinaunganisha nchi tatu, nchi ya Rwanda, Nchi ya Tanzaniakupitia Makao Makao Makuu ya Wilaya Ngara na Nchi yaBurundi kupitia border ya Rwanda ni shortcut kilometa 50 tu,ukilinganisha na mzunguko uliopo wa kutoka Rusumo, Benako,Ngara Mjini kwenda Kabanga kilometa 84, Serikali haionikwamba upo umuhimu kutokana na sera ya kuunganishabarabara zinazounganisha nchi na nchi kwa kiwango chalami kwamba kipande hiki kilichobaki cha kilometa 21kijengwe kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa kipo kivukohiki cha MV Ruvuvu ambacho sasa kinatoa huduma mpakasaa moja za jioni, Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) hawaoni kwamba upo umuhimu wa kuongeza sasamasaa ya kivuko hiki kitoe huduma mpaka saa tanoukizingatia kwamba upo mradi mkubwa unaoendelea waumeme Rusumo na movement za watu ni kubwa wanapatashida hasa kivuko kinapofunga huduma mapema?

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Gashaza, majibu yamaswali hayo Mheshimiwa Elias Kwandika.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, kwanzanimpongeze sana Mheshimiwa Gashaza kwa juhudi kubwaanazozifanya. Nikianza na swali lake la kwanza la kuhusukivuko, tumeweka kivuko kipya pale Ruvuvu kama nilivyosemakatika jibu langu la msingi na kuna kivuko kilikuwepo zamaniambacho kimsingi Mheshimiwa Gashaza pamoja nawananchi wa Ngara wamefanya juhudi ya kutengenezabarabara ili kivuko cha zamani tukipeleke maeneo yaMayenzi Kanyenye. Kwa hiyo nakupongeza sana kwa juhudihizo na sisi kama Serikali tuna kuunga mkono kwa kiasikikubwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kuongeza safari palekwenye kivuko cha Ruvuvu tulishatoa maelekezo kwambatuongeze safari pale ili huduma ziwe nyingi zaidi na hasa

Page 38: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

wakati usiku na pia tulitoa maelekezo kwamba tufunge taapale ili sasa huduma za usiku zikifanyike pia pawe salamazaidi. Kwa hiyo, tutaendelea kulisimamia hili kwa harakatuweze kufanya hivyo ili huduma ziongezeke katika hilo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara hii utakubalianana mimi kwamba barabara iko kwenye kiwango kikubwasana ni kizuri hata wewe mweyewe wakati nimekujakutembea maeneo haya ulitumia dakika kumi tu Ngara Mjinikuja kule kwenye kivuko, kwa maana ya kwambatunaendelea kukifanyia matengenezo makubwa.

Mheshimiwa Spika, niseme kuhusu kuboresha nakufanya barabara hii itumike kama barabara ya kuunganishakati ya Burundi na Rwanda na kwa sababu pia kuna maeneokumekuwa na changamoto ya kupitisha magari makubwasehemu za Mjini, na naomba ukubaliane na mimi kwambabarabara ya kutoka Ngara kwenda Benako iendeleekutumika na magari makubwa yale ambayo yanatokaBurundi na kwa maana hiyo tukiboresha barabara hii hatakwa kiwango cha lami siku za usoni lakini magari magodoyapite kwenye eneo hili ili tusiwe na usumbufu eneo la Mjiniya kupitia magari makubwa na imejitokeza changamotonyingi kama magari makubwa yatapita pale Mjini kunawezakuwa na hatari kubwa.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo tutaendeleakusimamia barabara kutoka Ngara kwenda Benako iwe nzuriwenzetu wanaotoka Burundi wapiti vizuri na magari menginemadogo yanaweza kupita kwenye kivuko hiko, ahsante sana.

SPIKA: Nil ikuwa Mheshimiwa Sesil i Pareso naMheshimiwa Nchambi utafuata.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa spika, ahsantekwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza, kunabarabara ya muda mrefu ambayo inaunganisha Mkoa waManyara na Mkoa wa Arusha ambayo inatokea Karatu,Kilimakunda mpaka Mbulu haijajengwa kwa kiwango chalami.

Page 39: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Je, ni lini barabara hii itajengwa kwa kiwango chalami?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Karatu, Mbulu haina lamitafadhali Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, ni kweli mudamrefu barabara jitihada ya kuitengeneza kiwango cha lamiipo, na ukweli kwamba barabara hii imefanyiwa usanifu nakuna kazi ilikuwa inaendelea kukamilishwa ili kutoka Karatu,Kilimapunda, Mbulu, Dongobeshi, Haydom ipite Sibiti iendempaka Mwanza. Na niseme katika Bunge lako tumepishafedha kuanza ujenzi sehemu ile ya Mbulu kuja Haydom, kujaDongobeshi itaanza kujengwa; kwa maana hiyo sasatunatambua umuhimu kadri tunavyopata pesa tutaendeleakuijenga barabara hii yote ili iweze kuwa kwa kiwango chalami.

SPIKA: Nilikutaka Mheshimiwa Nchambi swali fupi.

MHE. SULEIMAN M. NCHAMBI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa niaba ya wananchi Shapu wa Jimbo laKishapu kwa kuwa Serikali imekuwa na ahadi ya muda mrefuya ujenzi wa barabara ya kutoka Kolandoto kwenda Kishapu.

Je, Mheshimiwa Waziri uko tayari sasa kunipatiamajibu yenye matumaini kwa wananchi Shapu wa Kishapujuu ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kolandoto kwendaKishapu?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Kolandoto Kishapu,Mheshimiwa Naibu Waziri Ujenzi.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, kwanzanimpongeze sana Mheshimiwa Nchambi kwa juhudi kubwasana anazozifanya katika kusimamia mambo mbalimbali naeneo hili la Kishapu linazalisha sana mazao pamba, pialinazalisha almasi, lakini juhudi za Mheshimiwa Mbunge

Page 40: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

zinaonekana. Niseme tu barabara hii anayoitaja MheshimiwaMbunge kutoka Mwangongo, Kaulandoto itakuwa ni sehemuya barabara hii ambayo inayopita Sibiti kwa maana tunakipande cha kuja Kolandoto kwenda mpaka Sibiti lakini kikokipande kingine kutoka Mwananuzi kuja Maswa. Kwa hiyo nisehemu ya barabara hii ambayo ni muda mfupi nimejibu swalila nyongeza la Mheshimiwa Paresso.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, MheshimiwaNchambi nikuhakikishie tu kwamba hizi kilometa 50 na kidogokutoka Mwangongo kuja Kolandoto tutaanza kufanya ujenzikidogo kidogo kadri tunapopata pesa, na tumejipanga napia kufanya maboresho makubwa kwenye Mji wa Kishapukwa sababu ni Makao Makuu haina barabara ya lami paletumejipanga tutaanza na kilometa kadhaa pale nafikirituonane baadaye kwa sababu ni Mbunge wa Shinyangamwezangu ili saa nyingine uone pia kwa ukubwa waketumejipangaje kuboresha Mji wa Kishapu pamoja nabarabara hii uliyoitaja, ahsante sana.

SPIKA: Nilikuwa Mheshimiwa Dkt. Stephen Kiruswa swalila mwisho la nyongeza kwenye eneo hili.

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali lanyongeza na pamoja na swali naomba nitumie fursa hiikuishukuru Serikali kwa sababu ya ujenzi wa barabara ya lamiinayotoka Sanya Juu Wilaya ya Siha kuelekea Rombo kupitiaVijiji sita vya Wilaya ya Longido ikiwepo Eleray ambayoimeshafikiwa na lami hilo Olomoloko, Nyalan’gwa, Kitenten,likwaswa na Kamwanga swali langu ni kwamba.

Je, barabara yenye kilometa 56 inayounganishaWilaya ya Longido na Wilaya ya Siha ambayo sasa inapitiwana hiyo barabara West Kilimanjaro ambayo ni moja yabarabara iliyohaidiwa katika ilani ya chama cha Mapinduziya mwaka 2015/2020 itaanza kujengwa lini?

Page 41: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

SPIKA: Majibu ya swali hilo kwa kifupi itaanza kujengwalini barabara hiyo sijui kama umeshafika huko MheshimiwaNaibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, ni kwelinimeshafika maeneo haya na nimekagua barabara hiikutoka Aleray Kamwanga, tumebakiza kilometa 44 tufikeKamwanga na Mheshimiwa Mbunge utakubaliana na mimi.Lakini na kile kipande cha kutoka maeneo hayo kwendaLongido kiko kwenye mpango, nafikiri hata kwenye bajetikitabu chetu ninacho hapa Mheshimiwa Mbunge tuonanetu ili tupitie. Lakini tunajipanga tulikuwa tunakwenda hatuakwa hatua baada ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiimpaka Aleray tunakuja sasa kwenda hatua nyingine kujengabarabara hii Mheshimiwa Mbunge unayoitaja.

SPIKA: Tunaenda Wizara ya Maji swali linaulizwa naMheshimiwa Fratei Gregory Massay Mbunge wa Mbulu Vijijiniuliza swali lako Mheshimiwa.

Na. 106

Utekelezaji wa Ahadi ya Kuchimba Kisima Hydom

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:-

Serikali iliahidi kuchimba kisima katika Mji mdogo waHydom na kumalizia miradi ya Visima Jimbo la Mbulu Vijijini.Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi hiyo ili kumtua Mama ndookichwani.

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriMaji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Haweso.

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory MassayMbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini kama ifuatavyo:-

Page 42: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Mheshimiwa Spika, mji wa Hydom unapata majikutoka vyanzo vya visima virefu vitatu (kimoja kinaendeshwakwa jenereta na visima viwili kwa umeme wa TANESCO).Kupitia vyanzo hivyo yamejengwa matenki ya kuhifadhia majimatatu yenye jumla ya ujazo wa lita 555,000, vituo vyakuchotea maji 36, vinywesheo vya mifugo vitatu (3), namtandao wa mabomba wenye urefu kilomita 34.12. Mradihuu unanufaisha watu binafsi 399 na Taasisi 14.

Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika harakati zakuongeza upatikanaji wa maji katika mji mdogo wa Hydom.Hivi sasa, Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa MazingiraVijijini (RUWASA) ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilishauchimbaji wa visima virefu sita vya maji katika vijiji vyaNg’orati, Genda, Maretadu Juu, Labay, Garbabi naEndahagichan ambapo kazi ya uchimbaji imefanyika na kaziiliyobaki ni kusafisha kisima cha Garbabi pamoja na kufanyapump test na kupima ubora wa maji katika visima hivyo. Mradihuu unategemea kukamilika mwezi Januari, 2020.

Mheshimiwa Spika, mipango iliyopo ni kuendeleakutafuta vyanzo zaidi vya maji ili kuongeza kiwango chaupatikanaji wa maji kufikia asilimia 85% ifikapo 2020. Wizarakupitia Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa MazingiraVijijini (RUWASA) itatuma wataalam wa kufanya utafiti wa majichini ya ardhi, ikifuatiwa na kufanya usanifu wa mradi ilikufahamu gharama za ujenzi. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Massay, nimekuona. Swali lanyongeza tafadhali.

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. DDCA walikuja wakachimba visima sita na badohawajaweka pump na sasa pia DDCA wamepata visimanane na je, lini watafanya au kumaliza kazi hiyo ya kumaliziavisima hivi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili Jimbo la Mbulu Vijijiniliko juu ya Bonde la Ufa na vijiji vingi vina shida sana ya maji:Je, Serikali itakuja na mpango gani ili kuhakikisha ya kwamba

Page 43: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

tunatimiza ile slogan ya kumtoa au kumtua mama ndookichwani? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Maji, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa niabaya Waziri wa Maji, nampongeza Mheshimiwa Mbunge,amekuwa mfuatiliaji mkubwa sana katika suala la maji kanakwamba ni Mhandisi wa Maji. Kikubwa ambacho natakakusema, utekelezaji wa miradi ya maji unategemeana nafedha.

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba tumepata fedha zaidi ya shilingi bilioni 20kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika mikoa 17 naMkoa wa Manyara ni moja ya Mkoa wa wanufaika. KatikaJimbo lake, zaidi ya shilingi bilioni 1.3 tumeshazipeleka kwaajili ya kutatua tatizo la maji katika maeneo matatu.

Moja, katika Kijiji cha Maganga Juu na Kijiji chaDongobeshi. Yote ni katika kuhakikisha tunapeleka hudumahii ya maji. Pia tumewapa fedha zaidi ya shilingi milioni 135kwa ajili ya kukarabati vituo ambavyo havitoi maji ili wananchiwapate maji.

Mheshimiwa Spika, kubwa, namsisitiza Mhandisi waMaji wa Mbulu afanye kazi kwa sababu fedha ipo, kamaakishindwa, basi tutamtafutia kazi ya kufanya. Ahsante sana.(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu nimekuona.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Moja ya Wilaya yenyematatizo makubwa ya maji ni Wilaya ya Hanang na kunawakati Serikali ilikuwa imetenga shilingi bilioni 1.2 kwa ajili yamaji ya Maskta, Maskaroda na Malama, lakini mpaka leosidhani hata kama shilingi milioni moja imepelekwa.

Page 44: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Spika, naomba sana Mheshimiwa Wazirianieleze, badala ya kwenda kwenye Bonde ambalo ni karibuna ule mradi uliotengwa: Je, ni lini sasa zile hela zilizotengwana Serikali katika bajeti iliyopita italetwa ili watu wa Malamawaweze kupata maji?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri,sijui kama umeshafika huko Maskata, Maskaroda.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanzanikiri nimeshafika katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge naanafanya kazi kubwa na nzuri katika Jimbo lake. Kamanilivyozungumza awali, utekelezaji wa miradi ya majiinategemeana na fedha na tumepata fedha kutoka Benkiya Dunia zaidi ya shilingi bilioni 120 na mmoja wa mkoa wawanufaika ni Mkoa wa Manyara.

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba fedha tumeshashazipeleka na ninaombatuonane baada ya hapa ili tufanye mawasiliano katikakuhakikisha anazifuatilia na kwenda kutekeleza kazi kamailivyopangwa.

SPIKA: Bado tuko Wizara ya Maji, Swali la MheshimiwaOmari Kigua. Waheshimiwa kwa sababu ya muda ndiyomaana tuwiane radhi.

Na. 107

Kutatua Changamoto ya Maji - Kilindi

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:-

Wilaya ya Kilindi yenye Vitongoji 613 na Vijiji 613 hainamto wala ziwa:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuipatia Wilaya hiyomradi mkubwa wa maji kutoka Mto Pangani ili kutatuachangamoto ya maji?

Page 45: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

SPIKA: Majibu ya swali hilo la wana Kilindi MheshimiwaNaibu Waziri Maji, nakukumbusha pia masuala ya e-parliament Waziri kijana.

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua tatizo kubwala huduma ya maji linaloikabili Wilaya ya Kilindi kutokana nakutokuwa na mito wala maziwa yanayotumika kwa ajili yashughuli za binadamu na wanyama kwa kipindi cha mwakamzima na vyanzo vikuu vya maji katika Halmashauri hiyo nimaji yaliyopo chini ya ardhi.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto hiyo, Serikali ilichimba visima vinne katika Mijiya Songe na Bokwa ambapo katika Mji wa Bokwa tayarihuduma ya maji inapatikana kwa wananchi waishio maeneohayo na katika Mji wa Songe tayari usanifu umekamilika ilikujenga miundombinu ya usambazaji maji. Aidha, kwaupande wa huduma ya maji vijijini kuna visima vifupi 67 navisima virefu 13 vinavyotoa huduma ya maji kwa maeneombalimbali ya vijiji pamoja na malambo 12 ya maji.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inakarabati mradimkubwa wa Kitaifa wa HTM unaotoa maji Mto Pangani ilikuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwawakazi wa Wilaya ya Handeni na baadhi ya Vijiji vya Wilayaya Korogwe. Serikali itafanya tathmini ya kina kuangaliauwezekano wa ukarabati wa mradi huo endapo baadayeutaweza kuwanufaisha wananchi wanaoishi Wilaya ya Kilindi.

SPIKA: Mheshimiwa Omari Kigua, swali la nyongezatafadhali.

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, ahsante.Namshukuru Naibu Waziri kwa majibu ambayo kwa kweli

Page 46: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

kimsingi hayajaniridhisha hata kidogo. Kwa sababu swali lamsingi ilikuwa ni kuomba mradi mkubwa wa maji, lakini majibuya Mheshimiwa Naibu Waziri hayaoneshi wala hayatoimatumaini kabisa kwamba Serikali inaweza kutoa maji kutokaMto Pangani hadi Kilindi kwa sababu idadi ya visimaambavyo vimeainishwa hapa, hili ni suala la muda tu:-

Je, Serikali haionai kwamba kuna ulazima wakuchukua maji kutoka Mto Pangani hadi Kilindi?

Mheshimiwa Spika, swali la pil i, namwombaMheshimiwa Naibu Waziri aangalie namna ya kufanyaverification ya hivi vijiji 67 kwamba vinatoa maji. Ni kwambamajibu haya siyo sahihi hata kidogo. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. Umeambiwamajibu ya mwanzo siyo sahihi Mheshimiwa.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanzanampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzurianayoifanya, lakini nami pia ni miongoni mwa kijana waMkoa wa Tanga, sipo tayari katika kuhakikisha kwambatunawaumiza wananchi wa Mkoa wa Tanga.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Wizara ya Maji,tunatekeleza mradi wa kuyatoa maji Pangani na kuyapelekaHandeni. Ninachotaka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge,hii ni safari moja na safari moja huanzisha nyingine. Majiyatakapofika Handeni, lazima tuyapeleke Kilindi na mpangowa Wizara yetu ya Maji ni kuhakikisha tunatumia vyanzovikubwa katika kuhakikisha tunatatua tatizo maji kabisa.

Mheshimiwa Spika, namwagiza Katibu Mkuukuhakikisha wanafanya tathmini ya Mradi wa Mto Pangani iliwananchi wa Kilindi waweze kupata maji safi, salama nayenye kutosheleza. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa, muda uliobaki nimdogo sana na tuna maswali mawili ya kumalizia, naombatusameheane. Tunaelekea Wizara ya Afya, Maendeleo ya

Page 47: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo ina maswali mawiliya kujibu. Kwanza swali la Mheshimiwa Ritta Enespher Kabati,Mbunge wa Viti Maalum Iringa, uliza swali lako Mheshimiwa.

Na. 108

Kuwapatia Watu Wenye Ulemavu Matibabu Bure

MHE. RITTA E. KABATI aliuliza:-

Kundi kubwa la Watu Wenye Ulemavu wana vipatoduni:-

Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka kuwatambuana kuwapatia vitambulisho ili waweze kutibiwa bure kamawazee?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Ndugulile tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya mapitio ya Seraya Afya ya mwaka 2007 na kuandaa mapendekezo ya SeraMpya ya Afya ya Mwaka 2019. Katika mapitio ya Sera yaAfya ya Mwaka 2007, changamoto mbalimbali za matitabukwa makundi ya misamaha ziliibuliwa na watoa hudumapamoja na watumiaji wa huduma hizo.

Mheshimiwa Spika, moja ya changamoto iliyojitokezani hospitali zetu kuwa na wagonjwa wengi wa msamaha nahivyo kushindwa kuboresha huduma za afya. Kutokana nachangamoto hiyo ya kuwa na makundi mengi ya msamaha,Wizara yangu iliona ni vyema ikaboresha utaratibu wa

Page 48: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

misamaha kwa kuhakikisha kuwa wananchi wasio na uwezotu ndio wanaopatiwa msamaha.

Mheshimiwa Spika, katika mapendekezo ya SeraMpya ya 2019 kila mwananchi mwenye uwezo atapaswakugharamia huduma za afya. Sera pendekezwa inaainishanjia mahususi zitakazowezesha Serikali kubaini wananchi wotewenye uwezo ili waweze kuchangia gharama kabla yakupokea huduma. Kwani ni wazi kuwa siyo kila mlemavu anakipato duni. Hivyo, wananchi watakaothibitika katikamaeneo yao kuwa hawana uwezo wa kuchangia ikiwemowalemavu, wataendelea kupata matibabu pasipo waokuchangia.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa, Serikali inaendelea namaandalizi ya Bima ya Afya kwa wananchi wote. Pinditaratibu zikikamilika, Muswada utawasilishwa Bungeni.

SPIKA: Mheshimiwa, swali linahusu kuwatambua nakuwapatia vitambulisho walemavu. Swali la nyongezaMheshimiwa Ritta Kabati.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sanakwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo yanyongeza. Kwanza kabisa nina imani na Serikali hii ya Awamuya Tano kwamba yote yanawezekana siku moja watu wenyeulemavu basi wataweza kupatiwa hivyo vitambulisho. Pianawapongeza Waheshimiwa Mawaziri kwa kazi nzuri.Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mahitaji makubwa sanakwa watu wenye ulemavu hasa wale wa ngozi ni mafutamaalum ambayo yamekuwa yakiuzwa bei ghali sana katikamaduka na kushindwa kumudu gharama ya hayo mafuta;na kwa kuwa Serikali i l itoa agizo kuwa Halmashaurizinapoagiza dawa MSD ziagize na hayo mafuta:-

Je, nini kauli ya Serikali kwa Halmashauri ambazozimekuwa hazitii agizo hilo? Kwa sababu watu wenye

Page 49: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

ulemavu wamekuwa wakipata mpaka cancer kutokana nakukosekana kwa hayo mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwavitanda vya kujifungulia wajawazito siyo rafiki kabisa na watuwenye ulemavu na walemavu wanapokwenda kujifunguawamekuwa wakipata mateso makubwa sana na wenginekupoteza maisha:-

Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwambainaweka vitanda rafiki vya kujifungulia watu wenye ulemavukuanzia ngazi ya Zahanati mpaka Hospitali ya Rufaa ilikuwatendea haki watu wenye ulemavu? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo muhimu, MheshimiwaNaibu Waziri wa Afya.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, ni kweli walemavuwa ngozi wapo katika hatari zaidi ya kupata saratani ya ngozikutokana na kutokuwa na ile kinga nzuri ya mionzi ya jua.Kama Serikali katika Hospitali ya KCMC pale kuna kiwandakizuri nami nimepata fursa ya kukitembelea ambapo mafutahaya yanatengenezwa kwa ajili ya walemavu. Siku za nyumakatika Bunge lako Tukufu tulishawahi kutoa maelekezo kwaHalmashauri kwamba waweke utaratibu wa kuagiza mafutahaya kupitia katika bajeti zao za dawa na vifaa tiba ambazowanazipata.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie tena fursa hiikupitia Bunge lako Tukufu kuzikumbusha Halmashauri kubainimahitji ya walemavu wa ngozi katika maeneo yao nakuhakikisha kwamba mafuta haya ambayo yanawakingawalemavu wa ngozi, basi yanakuwa ni moja ya sehemu yavitu ambavyo wanaagiza kupitia bohari ya dawa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ameulizakuhusiana na vitanda ambavyo siyo rafiki sana kwawajawazito walemavu. Kwanza, napenda sana kumpongezaMheshimiwa Ritta Kabati, amekuwa ni Balozi mzuri sana na

Page 50: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

amekuwa anawasemea watu wenye ulemavu. Hil itumelipokea kama Serikali na tulishatoa maelekezo kwa MSDkuhakikisha kwamba vitanda vya kujifungulia ambavyotunavinunua viweze kukidhi mahitaji ya watu wote, walewenye uemavu na wale wasiokuwa na ulemavu. Hili tunalona tunaendelea kulisisitiza kupitia bohari ya madawa.

SPIKA: Ahsante Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Waziri hii ya kuwapatiavitambulisho walemavu wote, Mheshimiwa Almasi Maigealiwahi kunipa taarifa wakati fulani kwamba liko tatizo kubwasana la ulemavu wa upungufu wa nguvu za kiume miongonimwa Wanyamwezi. Sasa mwandae vitambulisho kwaWanyamwezi kule wote wenye matatizo hayo wapatevitambulisho. Mheshimiwa Maige hiyo huwezi kujibu tena,nimekuwahi leo. (Kicheko)

Mheshimiwa Catherine Nyakao Ruge, uliza swali lakotafadhali na ndiyo swali la mwisho leo.

Na. 109

Kupungua Vifo vya Akina Mama

MHE. CATHERINE N. RUGE aliuliza:-

Kwa mujibu wa Ripoti ya TGHS-MIS ya 2015/2016 yamasuala ya afya, vifo vya akina mama wakati wa kujifungua(Maternal Mortality Rate) vimeongezeka kufikia akina mama556 kati ya kina watoto 100,000 waliozaliwa hai.

Je, ni nini mkakati mahususi wa Serikali katikakupunguza vifo hivi ikizingatia kuwa bajeti ya Serikali kwaWizara ya Afya kwa mwaka 2018/2019 imepungua kwa zaidiya asilimia 19.6?

SPIKA: Majibu ya swali hilo tafadhali, MheshimiwaNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, tafadhali.

Page 51: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Naomba kujibu swali laMheshimiwa Catherine Nyakao Ruge, Mbunge Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendeleana juhudi mbalimbali za kuboresha huduma za Afya ya Uzazina Mtoto. Kupunguza vifo vitokanavo na uzazi na watotowachanga ni suala linalopewa kipaumbele katika Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, dhamira hii inaonekana nakuthibitishwa katika miongozo mbalimbali ya Serikali kamavile, Sera ya Taifa ya Afya ya Mwaka 2007, Dira ya Maendeleoya Taifa ya Mwaka 2025, Mkakati wa Kukuza Uchumi naKupunguza Umaskini (MKUKUTA), Mpango Mkakati wa Nnewa Afya (Health Sector Strategic Plan IV), Mkakati waKupunguza na Kuimarisha Afya ya Uzazi, Watoto na Vijana(National Road Map to Improve Reproductive, Maternal,Newborn, Child & Adolescent Health in Tanzania (One planII) na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka2015.

Mheshimiwa Spika, lengo la Wizara ni kupunguza vifovya akina mama na watoto vitokanavyo na uzazi kutoka 556kwa kila vizazi hai 100,000 hadi 292 kwa kila vizazi hai 100,000na kupunguza vifo vya watoto kutoka 21 kwa kila vizazi hai1,000 hadi 16 kwa kila vizazi hai 1,000 ifikapo mwaka 2020.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mikakati hii,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotokwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeboresha Vituovya Afya zaidi ya 352 na vingine kujengwa upya ili viwezekutoa huduma za afya ya uzazi kabla, wakati wa ujauzito nawakati wa kujifungua ikiwepo kumtoa mtoto tumboni kwanjia ya operesheni na kuzijengea uwezo wa kuweza kutoahuduma za damu salama kwa watakaohitaji. Aidha, Hospitalimpya 67 za Halmashauri zinajengwa ili huduma ziweze

Page 52: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

kuwafikia wananchi wote wa vijijini na mjini kwa usawa naurahisi.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwambaupatikanaji wa dawa na vifaa tiba vinakuwepo muda wote,Serikali imeongeza zaidi ya mara tisa bajeti ya dawa na vifaatiba, kutoka shillingi bilioni 31 mwaka 2015/2016 hadi shilingibilioni 270 mwaka 2018/2019. Ongezeko hili la kibajeti nausimamizi imara wa rasilimali vimeongeza upatikanaji wadawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma kutokaasilimia 53% (2015/2016) hadi kufikia asilimia 94% (2018/2019).

Aidha, juhudi hizi zimewezesha wajawazito kuendeleakupata huduma za afya ya uzazi na mtoto ikiwemo kingatiba dhidi ya Malaria (SP), Fefol ambayo ni kinga tiba dhidiya upungufu wa damu, vipimo vya shinikizo la damu,kaswende, wingi wa damu, sukari na kadhalika. Huduma hizihupatikana kila siku wajawazito wanapohudhuria Kliniki.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2019kuelekea 2020 Serikali ina mpango wa kuendelea kuboreshahuduma za afya ya uzazi na mtoto kwa kutoa mafunzo kazinikwa watoa huduma ya afya juu ya namna bora ya kutibumatatizo yatokanayo na uzazi na watoto wachanga,kuanzisha benki ya damu salama katika mikoa ambayo vituovipya vya upasuaji vya kumtoa mtoto tumboni vimejengwana kuimarisha mpango wa kutoa huduma kamili ya afya yauzazi na mtoto katika zahanati zote nchini.

Mheshimiwa Spika, tarehe 6 Novemba, 2018 JijiniDodoma Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alizinduakampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama ambayo ni kampeniya Kitaifa inayolenga kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifovya watoto wachanga nchini.

Mheshimiwa Spika, madhumuni ya kampeni hii nikuhamasisha viongozi wa Serikali, dini, Mashirika yasiyo yakiserikali, wadau wa maendeleo watoa huduma za afya,familia na jamii kwa ujumla ili kuchangia katika juhudi za Taifa

Page 53: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watotowachanga. Wakuu wote wa Mikoa walisainishwa mikatabaya utekelezaji na ufuatiliaji katika Mikoa yao.

SPIKA: Wizara ya Afya, majibu yanakuwa marefu sana.Mheshimiwa Ruge uliza swali.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.Mwaka 2017 Serikali kupitia Wizara ya Afya ilipata pesa kutokaBenki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha vituo 100 nchini ilikupunguza vifo vya akina mama na watoto. Kituo cha AfyaIramba kilichopo Wilaya ya Serengeti kilitengewa shilingimilioni 400 lakini mpaka sasa pesa hizo hazijapelekwa.

Mheshimiwa Spika, napenda kupata majibu, ni linisasa Serikali itapeleka pesa hizo ili kuweza kukarabati chumbacha kujifungulia pamoja na maabara ya damu ili kupunguzavifo vya akina mama na watoto wa vijiji vya Kinyamonta,Nyagasense, Iramba, Misaga pamoja na Heki?

Mheshimiwa Spika, swali la pili Wizara ya Afyaimekuwa ikiwatumia watoa huduma ngazi ya jamii kwamaana ya WAJA Community Health Workers katika harakatiza kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifunguapamoja na watoto; kwa kutambua hilo, Serikali iliamuakurasimisha kada hii kwa kuanzisha kozi ya mwaka mmojakwa ajili ya (Community Health Workers) ili kuajiri…

SPIKA: Mheshimiwa na wewe tena unaanza tenamaswali marefu!

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Spika, ilikuwaajiri WAJA Community Health Workers lakini program hiiimesitishwa:-

Je, Serikali haioni haya ni matumizi mabaya ya fedhaza walipakodi kwa kuanzisha program na kuisitisha kabla yakutimiza malengo yake?

Page 54: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

SPIKA: Ahsante sana. Majibu ya swali hilo MheshimiwaNaibu Waziri, tafadhali

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswalimawili ya Mheshimiwa Catherine Ruge, Mbunge Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli hapo awali Kituo hiki chaAfya cha Iramba katika Jimbo/Wilaya ya Serengetikiliainishwa katika moja ya vituo ambavyo vilitakiwa kupatafedha kwa ajili ya maboresho ili kuweza kutoa huduma zaafya ya uzazi. Hata hivyo, baada ya kufanya mapitio nakiwango cha fedha tulichokuwa nacho kituo hiki kilitolewakatika orodha hii. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbungekwamba bado tunaendelea na uboreshaji wa vituo hivi vyaafya na katika awamu ya tano basi kituo hiki nachokitafikiriwa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ameulizia suala lamatumizi ya Community Health Workers. Community HealthWorkers (watu wa afya wa jamii) kwetu ni watu muhimu sana,hususan katika mipango yetu ya Serikali. Leo tunafanyauzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa MagonjwaYasiyoambukiza lakini tuna mipango ya ugonjwa wa UKIMWI,Malaria na Kifua Kikuu na magonjwa mengi. Sisi kama Serikalisasa hivi tuko katika hatua za mwisho kabisa za kukamilishamuundo, taratibu wa jinsi gani ya kuweza kuwatumia hawaCommunity Health Workers. Utaratibu utakapokamilikatutatoa taarifa kwa umma.

SPIKA: Ahsante sana.

Waheshimiwa Wabunge, mkiangalia muda wetumtaona tunapaswa kuendelea na shughuli inayofuata.Naomba niwatambue wageni lakini kabla sijawatambuawageni naomba niwakumbushe Waheshimiwa Mawaziri naManaibu Waziri naomba mtuunge mkono sana katikamatumizi ya mfumo wetu wa e-parliament. Kwa hiyo,unapokuja kujibu maswali karatasi mnakuja nazo kama

Page 55: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

backup incase mtandao wako umeleta shida vinginevyohatu-encourage kuja na makaratasi hapa, hapana. (Makofi)

Kwa hiyo, tunaenda kwenye matangazo yetu.Kwanza naomba kuwatambulisha wageni 24 wa MheshimiwaLuhaga Mpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambao niWatendaji Wakuu wa Wizara hiyo ambao wamekujakushuhudia kuwasilishwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa FAOwa Kuzuia Uvuvi Haramu kupitia bandari za nchi wanachama.Wageni hao ni Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dkt. RashidTamatamah; Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. NazaelMadalla; Mkurugenzi wa TAFIRI, Dkt. Semvua Mzighani;Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA), Dkt. Islam Nchenga; Mkurugenzi wa Sera na Mipango(Uvuvi) Ndugu Sayi Magessa na Mkurugenzi wa Uvuvi, NduguMagese Bulayi, naona yeye hajaja, ahsanteni sana nakaribuni sana Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri, huyu Magese Bulayi kule ChuoKikuu cha Dar-es-Salaam tukiwa mwaka wa kwanza tulikuwatunalala wote chini, tulipewa magodoro ya kulala chini.Aliyetupatia magodoro ni Mheshimiwa Susan Lyimo, alikuwakule janitor kwenye mabweni ya chuo. Kwa hiyo, ka-SusanLyimo kazamani nako haka. (Kicheko)

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge ni wageniwatatu wa Mheshimiwa Doto Biteko, Waziri wa Madini ambaoni wapiga kura wake kutoka Jimbo la Bukombe, NduguBenjamin Ngaiwa, Ndugu Mbula Charles na NduguMerikizedeck Ndabagoye. Karibuni sana pale mlipo. (Makofi)

Wageni wawili wa Mheshimiwa Musukuma Kashekuambao ni Waheshimiwa Madiwani wa Jimbo la Geita; DiwaniKata ya Kakubilo Mheshimiwa Nyanda Igayo na Diwani waKata ya Isurwa, Mheshimiwa Maweda Gwesandilyi. Karibunisana Waheshimiwa Madiwani. (Makofi)

Wageni 20 wa Mheshimiwa Hassan Masala ambao nimarafiki zake na walimu kutoka mikoa mbalimbali Tanzania

Page 56: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

wakiongozwa na Ndugu Zawadi Sanga. Ooh, karibuni sanawageni wetu. (Makofi)

Wageni watano wa Mheshimiwa George Lubelejeambao ni walimu na viongozi wa Chama cha Mapinduzikutoka Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma wakiongozwa naMwenyekiti wa CCM wa Kata ya Chunyu, Ndugu PeterChilagane. Wale wa kutoka Chunyu karibuni sana na mkirudiChunyu basi msalimieni Diwani, Mheshimiwa Kongowa Dodona Mheshimiwa Mbunge wenu Lubeleje yuko amejaa hapatele. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Zubeir Kuchauka ambaye nimpiga kura wake mkulima kutoka Liwale Mkoa wa Lindi,Ndugu Juma Lipenga. Karibu sana Juma kutoka Liwale,tusalimie Liwale. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Wilfred Lwakatare ambaye nimtoto wake kutoka Jijini Dar-es-Salaam Ndugu LoveletLwakatare. Ahsante sana Lovelet. (Makofi)

Wageni watatu wa Mheshimiwa Zainab Mwamwindiambao ni viongozi wa CCM kutoka Iringa Mjini wakiongozwana Ndugu Joseph Nzala, Ndugu Salvatory Ngerera naNdugu Shadrack Masanika. Karibuni sana wageni kutokaIringa. (Makofi)

Wageni wawili wa Mheshimiwa Flatei Massay ambaoni madaktari wa Hospitali ya Haydom iliyoko Mbulu, NduguYeconia Zacharia na Ndugu Leokadia Fissoo. Karibuni sana,wale kule wageni wetu toka Hospitali Maarufu ya Haydom.(Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Hamida Abdallah ambaye nimume wake kutoka Mkoa wa Lindi, Ndugu Hitesh Mehta. Leotarehe 14 Novemba, 2019 wanatimiza miaka 30 ya ndoa.Karibu sana Ndugu Hitesh Meta na Mheshimiwa Hamidaamekaa upande gani, karibu sana Ndugu Hitesh kutoka kuleLindi. (Makofi/Vigelegele)

Page 57: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Wageni waliopo Bungeni kwa ajili ya mafunzo nimadaktari watano kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbiliambao wameletwa na Ofisi ya Bunge kwa ajili ya kutoahuduma ya afya kwa Waheshimiwa Wabunge na Watumishiwa Bunge katika kipindi hiki cha Bunge wakiongozwa na Dkt.Kennedy Nchimbi. Madaktari karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, madaktari hawawamekuwepo kwenye kituo chetu cha afya hapa wanatoahuduma za vipimo mbalimbali. Ukiwa unajisikia kuna mahalikidogo panaleta shida tafadhali fika tu pale na wapo hadikesho. Kwa hiyo, nawaomba tuonane na madaktari wetuhawa wapendwa. (Makofi)

Ahsante sana, sasa tuendelee.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mwongozo wa Spika.

SPIKA: Mwongozo, nimekuona Mheshimiwa GoodluckMlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Naomba Mwongozo kwa busara zako, jananiliomba Mwongozo kuhusiana na gharama halisi zauunganishwaji wa umeme wa REA, umeme jazilizi na umememwingineo. Kwa kuwa, kumekuwa na kauli za viongozi wetuwakuu akiwemo Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu,hata Mheshimiwa Waziri wa Nishati kuwa gharama ambayomwananchi anatakiwa alipe ni shilingi 27,000 tu, lakiniwananchi wetu wanapoenda katika Ofisi za TANESCOwanapotaka kuunganishiwa umeme wanaambiwa gharamatofauti kuanzia shilingi 200,000 hadi shilingi 1,000,000. Waziribado anasisitiza gharama halisi ni shilingi 27,000 sasa kunagharama inaitwa service charge, hiyo service chargewanapima umbali tangu umeme unapotokea mpakakwenye nyumba yako, yaani wanahesabu zile nguzo lakiniwanakwambia nguzo hailipiwi, mita hailipiwi, wala wayahaulipiwi. Tunataka kujua kwa maandishi yaani hiyo shilingi

Page 58: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

27,000 anayosema Mheshimiwa Waziri iandikwe namwananchi apewe barua kuwa pesa halisi anayotakiwakulipa ili apate umeme iwe hiyo, hii service line iondoke tupatemaandiko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba mwongozowako kwa mamlaka yako, Waziri atoe maandishi hapatuondoke nayo. Mimi nitawasaidia hata kuzisambaza hizobarua. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Waziri wa Nishati, natumaini umemsikiaMheshimiwa Mbunge, yeye anachosema tu kwamba hebutupatieni Wabunge wote andiko halisi ili tunapoendamajimboni, kwa sababu ni kweli kuna usumbufu, mnasemakila mahali lakini unapoenda huko utekelezaji tofauti. Tupenimaandishi kama Wabunge ukishalipa shilingi 27,000 hakunacha nguzo, waya wala vikombe Wabunge ile ndiyo iwe silahayetu sasa, ndio hoja ya Mheshimiwa.

Mheshimiwa Waziri, kama kuna maelezo tafadhali?

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwa maranyingine tena niendelee kumpongeza Mheshimiwa Mbungekwa hoja hii mahsusi sana yenye manufaa makubwa kwawananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, kwanza circular na nyarakazimeshasambazwa kwa Mameneja wote wa Kanda, Mikoana Wilaya. Kwa kuwa Wabunge wote wako katika Wilaya nimatumaini yetu kwamba watapata nyaraka hizo. Napendakutoa maelekezo sasa kwamba Mameneja wote wa Wilaya,Mikoa na Kanda katika maeneo yao wawasilishe nyarakahizo kwa kila Mheshimiwa Mbunge na WaheshimiwaMadiwani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakubaliana pia na hoja yakuwapa maandishi Waheshimiwa Wabunge. Hayomaelekezo uliyotoa Mheshimiwa Spika tutayatoa kila Mbungeatatoka na barua hiyo ili anakokwenda aweze kulisimamiavizuri. Ahsante. (Makofi)

Page 59: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri. Miminitalifuatilia jambo hilo kabla ya kesho kuahirisha hapanitawauliza Wabunge kama kila mmoja tayari ameshapatabarua yake kwa sababu jambo hili ni muhimu kweli kwawananchi na ukifanya mkutano wowote lazima siku hiziutaulizwa maswali yanayohusu umeme.

Sasa Wabunge ni kujikanyaga tu maana huna hakikaukisema hiki huenda labda ni kinyume na mwelekeo waSerikali sasa ni vizuri wawe na kitu fulani ambachokinawaongoza waweze kusema with authority. Kwa hiyo,mjitahidi by kesho tunapoahirisha Bunge kila Mbunge awena barua yake kabisa inayofafanua ni kitu gani exactly.

Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Nishati,tunakushukuru mno kwa hilo. Mheshimiwa Waziri Mkuu piaamejibu swali hapa asubuhi ameeleza kwa ufafanuzi mambohayohayo, ahsante sana.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea, Katibu.

NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI:

MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI

Muswada wa Sheria kwa ajili ya Kufanya Marekebishokatika Sheria Mbalimbali zipatazo Kumi na Nne (14) kwa lengola kuondoa upungufu ambao umejitokeza katika Sheria hizowakati wa utekelezaji wa baadhi ya masharti katika Sheriahizo [A bill for An Act to Ammend Certain Written Laws]

(Kusomwa Mara ya Kwanza)

SPIKA: Ahsante sana. Baada ya Muswada huoKusomwa kwa Mara ya Kwanza, sasa natangaza moja kwamoja kwamba Katibu utaupeleka kwenye Kamati ya Katibana Sheria kwa hatua zinazofuata ili uweze kufanyiwa kazi.

Katibu usome shughuli inayofuata.

Page 60: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

MAAZIMIO

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifawa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramu kupitia Bandari

za Nchi Wanachama

SPIKA: Moja kwa moja, naomba nikuite Waziri waMifugo na Uvuvi ili uwasilishe Azimio lako. Waziri wa Mifugona Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Mpina, karibu tafadhali.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Azimio laBunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa FAO wa KuzuiaUvuvi Haramu Kupitia Bandari za Nchi Wanachama (TheAgreement on Port State Measures to Prevent, Deter andEliminate Illegal, Unreported and Unregulated Fishing-PSMA).

KWA KUWA Tanzania ni mwanachama wa Shirika laChakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (Food and AgriculturalOrganisation of The United Nations – FAO) tangu mwaka 1962ambalo linaongoza juhudi za kuongeza usalama wa chakulana lishe duniani.

KWA KUWA katika kutekeleza majukumu yake, mwaka2001 liliandaa mpango mahsusi (International Plan of Action)wa kuzuia, kudhoofisha na kuondoa uvuvi haramu katikaukanda wa uchumi wa bahari kuu ambao umetokana naongezeko la matukio ya uvuvi haramu unaosababishauharibifu wa ikolojia, upotevu wa rasilimali za uvuvi na kuathirimaisha ya wavuvi na usalama wa chakula na lishe duniani.

NA KWA KUWA kwa kutambua umuhimu wa bandariza nchi wanachama wa FAO na kwa kuzingatia uhitaji wanchi zinazoendelea katika kukabiliana na uvuvi haramu katikaukanda wa uchumi wa bahari kuu, nchi wanachamazil iafikiana kuchukua hatua madhubuti za pamoja

Page 61: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

kukabiliana na uvuvi haramu usiotolewa taarifa nausiodhibitiwa kwa kutumia bandari.

NA KWA KUWA yapo baadhi ya mataifa ya kigeni nakampuni zinazokiuka masharti ya kujihusisha na uvuvi haramukwa kificho kwa kufanya uvuvi usiotolewa taarifa nausiodhibitiwa.

NA KWA KUWA Mkataba wa Kimataifa wa KuzuiaUvuvi Haramu Usiotolewa Taarifa na Usiodhibitiwa kwaKutumia Bandari (The Agreement on Port State Measures toPrevent, Deter and Eliminate Illegal, Unreported andUnregulated Fishing-PSMA) uliandaliwa na kukubaliwa na nchiwanachama kwa ajili ya kuzuia uvuvi haramu duniani.

NA KWA KUWA lengo la kuzuia uvuvi haramu ni kulindarasilimali za uvuvi ili kuwa na uendelevu na kuleta faida kwaTaifa husika na kuhakikisha usalama wa chakula na lishekupitia mkataba wa PSMA uliopitishwa katika kikao cha 137cha Baraza la FAO mwezi Oktoba, 2009 na kuridhiwa na nchiwanachama katika Kongamano Na.36 la FAO lililofanyikatarehe 18 mpaka 23 Novemba, 2009 Roma, Italia.

NA KWA KUWA Mkataba wa PSMA ni muhimu kwaajili ya kulinda rasilimali za uvuvi zilizopo nchini katika maeneoya maji ya bahari eneo ambalo linajumuisha maji ya Kitaifa(Territory Sea) lenye kilometa za mraba zipatazo 64,000 naUkanda wa Uchumi wa Bahari Kuu (Exclussive Economic Zone– EEZ) lenye kilometa za mraba zipatazo 223,000.

NA KWA KUWA kwa kuridhia mkataba huu nchiitapata manufaa ya kupunguza upotevu wa rasilimali zauvuvi, uharibifu wa mazingira ya bahari kutokana nakuimarika kwa udhibiti wa uvuvi haramu na usimamizi wamatumizi endelevu wa raslimali za uvuvi, kuongeza mchangokwa sekta ya uvuvi katika pato la Taifa, upatikanaji wamasoko ya uhakika ya kimataifa kwa mazao ya uvuviyanayotoka baharini, kuimarika kwa ushirikiano wa kikandana kimataifa katika uendelezaji wa rasilimali za uvuvi,kuongezeka kwa fursa za uwekezaji katika sekta za uvuvi na

Page 62: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

hivyo kutoa fursa za ajira, kuimarika kwa ukusanyaji naupatikanaji wa takwimu na taarifa mbalimbali zinazohusuuvuvi katika bahari kuu, kuwezesha udhibiti wa uvuvi haramukati ya nchi wanachama na kuijengea nchi uwezo wa kulindarasilimali za uvuvi.

NA KWA KUWA nchi zaidi ya 60 duniani zimesharidhiaMkataba huu na Nchi wa Ukanda wa Kusini Magharibi mwaBahari ya Hindi zinazojumuisha Nchi ya Reunion, Kenya,Madagascar, Maldives, Mauritius, Msumbiji, Seychelles,Somalia na Afrika Kusini zimesharidhia mkataba huu.

NA KWA KUWA mkataba unaopendekezwa kuridhiwaunaendana na sheria na miongozo ya kimataifa inayohusuusimamizi wa rasil imali za uvuvi ambazo Tanzaniainazitekeleza ikiwemo United Nations Convention on the Lawof the Sea – UNCLOS ya mwaka 1982, FAO Code of Conductfor Responsible Fisheries, Indian Ocean Tuna Commission –IOTC na Malengo Endelevu – Sustainable DevelopmentGoals, Lengo Na.14, Itifaki ya SADC kuhusu Uvuvi, Tamko laJakarta kuhusu Uchumi wa Bahari Kuu, Mkataba wa PSMAna miongozo hiyo inalenga kulinda, kuendeleza, kuhakikishakuwa rasilimali za uvuvi zinakuwa endelevu kwa ajili yauhakika wa chakula, lishe pamoja na manufaa ya kiuchumikwa nchi wanachama.

NA KWA KUWA mkataba huu unaendana na Sera yaTaifa ya Uvuvi ya Mwaka 2015 na Sheria ya Uvuvi, Sura 279 naSheria ya Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu, Sura388.

HIVYO BASI kwa kuzingatia manufaa yatokanayo naMkataba huu kwa Tanzania na kwa nchi wanachama, Bungehili katika Mkutano wa Kumi na Saba na kwa mujibu wa Ibaraya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaya Mwaka 1977, sasa linaazimia kuridhia Mkataba waKimataifa wa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramu Kupitia Bandariza Nchi Wanachama (The Agreement on Port State Measuresto Prevent, Deter and Eliminate Illegal, Unreported andUnregulated Fishing-PSMA).

Page 63: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono;tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na UvuviMheshimiwa Luhaga Mpina kwa wasilisho zuri kuhusiana naazimio tajwa la masuala ya uvuvi. Sasa naomba nimuiteMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Majiili awasilishe taarifa ya Kamati kuhusu azimio hilo. MheshimiwaDkt Christine Ishengoma, Makamu Mwenyekiti.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA - MAKAMUMWENYEKITI KAMATI YA KUDUMU YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI:Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa mujibu wa Kanuni ya53 (6) (e) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari,2016 kwa niaba ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Kilimo, Mifugo na Maji, naomba kuwasilisha Maoni naUshauri wa Kamati kuhusu Mapendekezo ya Serikali KuridhiaMkataba wa Kimataifa wa Shirika la Chakula na Kilimo laUmoja wa Mataifa (FAO) wa Kuzuia Uvuvi Haramu KupitiaBandari za Nchi Wanachama (Agreement on Port StateMeasures to Prevent, Deter and Eliminate Illegal, Unreportedand Unregulated Fishing – PSMA).

Mheshimiwa Spika, baada ya kuipatia Kamati kazi yakushughulikia mkataba huu kama ilivyo ada, Kamati ilianzakuchambua mkataba husika kwa kushirikiana na wadaumbalimbali waliofika mbele ya Kamati na wale waliotumamaoni yao kwa njia ya maandishi ili kuweza kufahamuchimbuko la mkataba, vipengele muhimu vilivyoko kwenyemkataba na manufaa yatakayopatikana kwa taifa na kwanchi wanachama kuridhia mkataba husika.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania ni miongonimwa nchi wanachama wa Shirika la Chakula na Kilimo laUmoja wa Mataifa (Food and Agriculture Organization of theUnited Nation- FAO), na kwa kuwa Tanzania ni moja ya nchizinazopakana na bahari, mwaka 1985 iliridhia Mkataba waKimataifa wa Sheria ya Bahari ya Mwaka 1982 (The United

Page 64: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Nation Convention on the Law of the Sea – UNCLOS 1982),ambao unatoa fursa kwa nchi zinazopakana na baharikutangaza mipaka ya maeneo ya bahari. Fursa hii inatoahaki kwa nchi hizo kutafuta, kutumia, kuhifadhi na kusimamiarasilimali hai na zisizo hai hadi maili za bahari (Nautical Mile)200 kutoka ufukweni.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 1989 Bunge lakoTukufu lilitunga Sheria ya Bahari ya Kitaifa ya Ukanda Maalumuwa Uchumi (Territorial Sea and Exclusive Economic Zone Actof 1989; ambayo ilitambua kuwepo kwa maeneo matatu yaBahari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maeneo hayoni Bahari ya Ndani (Inner Sea), Bahari ya Kitaifa (Territorial Sea)na Ukanda Maalum wa Uchumi wa Bahari (ExclusiveEconomic Zone EEZ).

Mheshimiwa Spika, Eneo Maalum la Uchumi wa BahariKuu (Exclusive Economic Zone EEZ) ambapo hufanyikashughuli za uvuvi wa Bahari Kuu na samaki wa asil iwanaopatikana katika eneo hili ni wa aina ya Jodari na jamiizake husifika kwa tabia ya kuhama kwa kasi kubwa tenakatika makundi kutoka eneo moja la maji ya bahari hadi eneolingine.

Mheshimiwa Spika, hali hii imepelekea baadhi ya nchizinazoendelea, kushindwa kunufaika ipasavyo na Uvuvi waBahari Kuu kutokana na uwekezaji mkubwa unaohitajikakwenye Uvuvi wa Bahari Kuu. Changamoto nyinginezinazokabili Uvuvi wa Bahari Kuu ni gharama kubwa katikakuendeleza, kusimamia na kudhibiti shughuli za uvuvi ikiwemoUvuvi Haramu Usiotolewa Taarifa na Kuratibiwa (Illegal,Unreported and Unregulated – IUU – fishing).

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua changamoto hiina kwa kuzingatia uhitaji wa nchi zinazoendelea katikakukabiliana na Uvuvi Haramu sehemu za Ukanda wa Uchumina Bahari Kuu, Nchi Wanachama zikiongozwa na Shirika laChakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (Food and AgricultureOrganization of the United Nation – FAO) ziliafikiana kuchukua

Page 65: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

hatua madhubuti za pamoja za kukabiliana na uvuvi haramu,usiotolewa taarifa na usiodhibitiwa kwa kutumia bandari.

Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza adhima hiyo,Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Uvuvi Haramu, UsiotolewaTaarifa na Usiodhibitiwa kwa Kutumia Bandari (The Agreementon Port State Measures to Prevent, Deter and Eliminate Illegal,Unregulated Fishing- PSMA) uliandaliwa na kukubaliwa.Mwaka 2009 mwezi Oktoba uliridhiwa na nchi wanachamakwa ajili ya uzuiaji wa uvuvi haramu.

Mheshimiwa Spika, Madhumuni na Faida za Mkatabawa Kimataifa wa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramu KupitiaBandari za Nchi Wanachama. Lengo kuu la kuzuia uvuviharamu ni kulinda rasilimali za uvuvi ili kuwa na uvuvi endelevuna kuleta faida kwa taifa husika, na kuhakikisha usalama wachakula na lishe kupitia Mkataba wa FAO-PSMA. Aidha,Mkataba huu ni muhimu kwa ajili ya kulinda rasilimali za uvuvizilizopo nchini katika maeneo ya maji ya bahari.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Tanzania, Bungelikiridhia Mkataba huu, manufaa yatakayopatikana nipamoja na:-

(a) Kupungua kwa upotevu wa rasilimali za uvuvi nauharibifu wa mazingira ya bahari kutokana na kuimarika kwaudhibiti wa uvuvi haramu na usimamizi wa matumizi endelevuya rasilimali za uvuvi.

(b) Kuongezeka kwa mchango wa Pato la Taifa.

(c) Upatikanaji wa masoko ya uhakika ya kimataifakatika uendelezaji wa rasilimali za uvuvi.

(d) Kuongezeka kwa fursa za uwekezaji katika Sektaya Uvuvi na hivyo kutoa fursa za ajira, kuimarika kwaukusanyaji na upatikanaji wa takwimu na taarifa mbalimbalizinazohusu uvuvi katika Bahari Kuu.

Page 66: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

(e) Kuwezesha udhibiti wa uvuvi haramu kati ya NchiWanachama.

(f) Kuijengea Nchi uwezo wa kulinda rasilimali za uvuvizilizoko ndani ya mipaka ya bahari katika eneo letu.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa itifaki Mkataba waKimataifa wa FAO wa kuzuia Uvuvi Haramu kupitia Bandariumegawanyika katika sehemu kuu kumi (10) zenye jumla yaIbara 37; naomba ziorodheshwe kwenye hansard kamazilivyoandikwa.

Maelezo yafuatayo yatafafanua kwa ufupi vipengelemuhimu vilivyochambuliwa na Kamati.

Ibara ya Pili; Ibara hii inaelezea madhumuni yaMkataba wa FAO-PSMA kuwa ni kuzuia, kudhoofisha nakutokomeza uvuvi haramu usiotolewa taarifa na usiodhibitiwaili kuhakikisha uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali zabaharini na kulinda ikolojia.

Ibara ya Nne; Ibara hii inaelezea uhusiano waMkataba wa FAO-PSMA na Sheria za Kimataifa pasipo kuathirisheria za nchi husika. Hivyo Mkataba huu hautazuia nchikujiamulia mambo yake.

Ibara ya Tano; Inaelezea ushirikiano na uratibu katikangazi ya Kitaifa katika utekelezaji wa Mkataba wa FAO-PSMA.

Ibara ya Sita; Inaelezea ushirikiano katikakubadilishana taarifa zinazohusu usimamizi wa rasilimali zauvuvi baharini kati ya nchi wanachama, FAO na mashirikaya Kikanda na Kimataifa.

Ibara ya Saba; Inaeleza wajibu wa nchi wanachamakubainisha bandari zenye sifa stahiki ambazo zitatambulikakwa ajili ya shughuli za ukaguzi katika utekelezaji wa Mkatabawa FAO-PSMA.

Page 67: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Ibara ya Nane na Tisa; Zinaelezea utaratibuunaopaswa kuzingatiwa na meli za uvuvi za kigeni kupatakibali cha kuingia bandarini na kukaguliwa. Iwapo itathibitikakuwa meli inayoomba kibali cha kuingia bandarini imehusikana uvuvi haramu haitaruhusiwa kuingia wala kupata hudumayoyote.

Ibara ya Kumi; Inaeleza mazingira ambayo meliinayohusika na uvuvi haramu itaruhusiwa kuingia bandarinina kupata huduma za dharura hususan zile zinazohusu afya/uhai wa binadamu.

Ibara ya Kumi na Moja; Inaeleza huduma ambazohazitapaswa kutolewa bandarini kwa kuzingatia sheria nakanuni za nchi husika na sheria za kimataifa kwa meli ambayotaarifa zake za ukaguzi zitathibitishwa kuwa inajihusisha nauvuvi haramu.

Ibara ya Kumi na Mbili, Kumi na Tatu, Kumi na Nne,Kumi na Tano na Kumi na Sita; Ibara hizi zinaeleza taratibu zakuzingatia katika kufanya ukaguzi wa meli kwa mujibu waMkataba wa FAO-PSMA, taratibu za uandaaji wa ripoti nanamna ya kubadilishana taarifa za ukaguzi baina ya nchiwanachama.

Ibara ya 17 na Ishirini na Moja; Zinaeleza kuhusukujengewa uwezo kwa wakaguzi wa meli, kubadilishanauzoefu baina ya nchi wanachama, kupata misaada yakitaalam na kuwezesha utekelezaji wa Mkataba wa FAO-PSMA.

Ibara ya Ishirini; Inaeleza wajibu wa meliinayopeperusha bendera ya nchi mwanachama kutoaushirikiano, kufuatilia na kuhakikisha vyombo vyao vinafuatamasharti kwa mujibu wa sheria za nchi na za Kimataifa.

Ibara ya Ishirini na Mbili; Inaeleza kuhusu upatikanajiwa suluhu pindi nchi wanachama zinapoingia katikamigogoro.

Page 68: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Aidha, Mkataba umeruhusu migogoro inapojitokezakutatuliwa kwa njia ya majadiliano kabla ya kufikia ngazi zamahakama za Kimataifa.

Ibara ya Thelathini na Tatu; Ibara hii inatoa fursa kwanchi mwanachama kupendekeza mkataba kufanyiwamarekebisho endapo kuna haja ya kufanya hivyo.

Ibara ya Thelathini na Tano; Inaeleza kuhusu nchimwanachama kujitoa katika Mkataba wa FAO-PSMA.Mktaba huu unatoa fursa kwa nchi mwanachama kujitoamuda wowote baada ya mwaka mmoja tangu tarehe yakuridhiwa kwa mkataba husika.

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakokuwa, hoja zilizoibuliwa na Wabunge zilipata maelezo yakuridhisha kutoka kwa Serikali na wadau kama ifuatavyo: -

(i) Tanzania haina sababu ya kutoridhia kwa kuwakipindi cha Ratification kimeshapita baada ya idadi yawanachama wa FAO wa kuridhia ilipotimia. Hivyo Tanzaniaby Default haiwezi kukwepa kutekeleza makubaliano hayokwani kwa kutofanya hivyo kunaiondolea sifa Tanzania nakuonyesha ni nchi inayosaidia kuendelea kuwepo kwa uvuviharamu na uharamia mwingine baharini.

(ii) Pamoja na kwamba nchi yetu bado haijaridhiamakubaliano hayo, hata hivyo imeendelea kutekelezamakubaliano hayo kwa vitendo kwa kufuatilia na kufanyaukaguzi wa meli za nje zinazokuja kwenye bandari zetu ilikuhakikisha kuwa ni meli halali na mizigo iliyobeba ni ileiliyoruhusiwa kimataifa.

(iii) Kwa muda mrefu hatua za kuridhia zilikwamakutokana na ukweli na ugumu wa kutopata maoni ya wadaukutoka pande zote mbili za muungano.

Kwa sasa pande zote mbili za Muunganozimejiridhisha faida zinazoambatana na Mkataba huu nahivyo zimekubaliana nchi yetu iridhie Mkataba wa FAO-PSMA.

Page 69: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Mheshimiwa Spika, mbali na ufafanuzi huo uliotolewa,faida zingine zinazoambatana na kuridhiwa kwa Mkatabawa FAO-PSMA ni pamoja na:-

(i) Nchi yetu itanufaika kwa kutolipa kwa gharamazozote zinazoambatana na uanachama (Accession nicostless);

(ii) Wataalamu wetu watapatiwa mafunzo burekwenye Idara mbalimbali zinazojihusisha na shughuli za uvuvina mazao ya uvuvi kama Bandari, Askari wa Majini kupitiaJeshi la Wanamaji, Idara ya Uvuvi, Shirika la ViwangoTanzania, Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu;

(iii) Nchi yetu kupitia mwamvuli wa FAO itapatamisaada mingine mingi inayopitia Umoja wa Mataifa, hususanmisaada inayoendana na udhibiti wa uharamia kwenye majiyote yaliyoko eneo la Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Maoni na Ushauri wa Kamati.Baada ya kufanya uchambuzi wa Mkataba wa Kimataifawa FAO - PSMA wa kuzuia uvuvi haramu kupitia bandari zanchi wanachama, Kamati inakubaliana na mapendekezoya Serikali kulingana na dhamira njema ya Mkataba huu kwaTaifa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikioyatakayopatikana, Kamati ina maoni na ushauriufuatao:-

Ili nchi iweze kunufaika ipasavyo na Mkataba waKimataifa wa FAO – PSMA na kuwezesha utekelezaji wamapendekezo yaliyomo kwenye mkataba ni vyemaSerikali:-

(i) Ikaziwezesha ipasavyo Wizara za Uvuvi na Mifugoza Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa kutenga bajetizinazowezesha Wizara hizi zitekeleze majukumu yakeipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kifedha na kuipatiarasilimali watu ya kutosha Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu;

Page 70: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

(ii) Kuimarisha Shirika la Uvuvi Tanzania Bara (TAFICO)na Shirika la Uvuvi Zanzibar (ZAFICO);

(iii) Kujengwa kwa Bandari za Uvuvi;

(iv) Kuanzishwa kwa viwanda vya kuchakata samakikatika ukanda wa bahari na;

(v) Ununuzi wa meli za kitaifa kubwa zenye uwezo wakuvua eneo la Ukanda wa Bahari na hivyo kuwezesha uvuviwa kibiashara.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaamini kuridhiwa kwaMkataba wa FAO - PSMA pamoja na kuimarisha uwekezajikwenye Ukanda wa Bahari Kuu kutawezesha nchi yetukuzifikia, na kuzimiliki rasilimali za uvuvi katika Ukanda waUchumi wa Bahari Kuu kutokana na ushirikiano wa nchiwanachama kudhibiti uvuvi haramu na hivyo kunufaika narasilimali hizo zilizopo eneo la Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Hitimisho. Napenda kukushukurukwa kunipa nafasi ya kuwasilisha Maoni, Ushauri naMapendekezo ya Kamati kwa niaba ya Wajumbe wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumpongeza nakumshukuru Waziri wa Mifugo Mhe. Luhaga J. Mpina, (Mb)na Naibu Waziri Mhe. Abdalla Ulega (Mb), Katibu Mkuu UvuviDkt. Rashid Tamatama pamoja na Wataalamu wote waWizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano walioipa Kamatiwakati ikichambua na kujadili Mkataba wa FAO - PSMA.

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru wadauwote waliotoa michango yao kwa maandishi na kwa kufikambele ya Kamati. Michango yao ilisaidia kuijengea uwezoKamati na hivyo kuwawezesha Wajumbe kuwa na uelewakuhusiana na Mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa napendakuwashukuru Wajumbe wa Kamati kwa ushirikiano na

Page 71: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

michango yao waliyoitoa wakati wa kupitia na kuchambuamkataba huu pamoja na kuandaa taarifa hii hadi kukamilikakwake. Naomba majina yao yote yaweze kuingia kwenyehansard.

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kumshukuruKatibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai, Ndg. MichaelChikokoto Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bungekwa kuisaidia na kuiwezesha Kamati hii kutekeleza majukumuyake kwa weledi mkubwa.

Mheshimiwa Spika , kwa namna ya kipekeenawashukuru Watumishi wote wa Ofisi ya Bungewakiongozwa na Sekreterieti ya Kamati ambao ni Ndg. VirgilMtui na Ndg. Rachel Nyega pamoja na msaidizi wa KamatiNdg. Mwimbe John kwa kuihudumia Kamati ikiwa ni pamojana kukamilisha taarifa hii kwa wakati.

Mheshimiwa Spika , baada ya maelezo hayo,naliomba sasa Bunge lako lipokee, lijadili na liridhie Mkatabawa Kimataifa wa FAO - PSMA wa kuzuia uvuvi haramu kupitiabandari za nchi wanachama.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naombakuwasilisha, ahsante sana.

MAONI YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA KURIDHIA

MKATABA WA KIMATAIFA WA FAO WA KUZUIA UVUVIHARAMU KUPITIA BANDARI ZA NCHI WANACHAMA – KAMA

YALIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53(6)(b) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016. Kwa niabaya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, naomba kuwasilisha Maoni na Ushauri waKamati kuhusu Mapendekezo ya Serikali Kuridhia Mkatabawa Kimataifa wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa

Page 72: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Mataifa (FAO) wa Kuzuia Uvuvi Haramu Kupitia Bandari zaNchi Wanachama (Agreement on Port State Measures toPrevent, Deter and Eliminate Illegal, Unreported andUnregulated Fishing – PSMA).

Mheshimiwa Spika, Nyongeza ya Nane Kifungu cha 7(1) (b)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, inazipaKamati za Kisekta ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge yaKilimo, Mifugo na Maji jukumu la kushughulikia Miswada yaSheria, Maazimio na Mikataba inayopendekezwa kuridhiwana Bunge iliyo chini ya Wizara inazozisimamia. Aidha, jukumuhili pia ni jukumu la Kikatiba chini ya Ibara ya 63(3)(e) ya Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuipatia Kamati kazi yakushughulikia mkataba huu kama ilivyo ada, Kamati ilianzakuchambua Mkataba husika kwa kushirikiana na Wadaumbalimbali waliofika mbele ya Kamati na wale waliotumamaoni yao kwa njia ya maandishi ili kuweza kufahamuChimbuko la Mkataba, Vipengele muhimu vilivyoko kwenyeMkataba na manufaa yatakayopatikana kwa Taifa na kwanchi Wanachama kuridhia Mkataba husika.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchiwanachama wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja waMataifa (Food and Agriculture Organization of the UnitedNation- FAO) na kwa kuwa Tanzania ni moja ya nchizinazopakana na bahari, mwaka 1985 iliridhia Mkataba waKimataifa wa Sheria ya Bahari ya Mwaka 1982 (United NationConvention on the Law of the Sea – UNCLOS 1982) ambaounatoa fursa kwa nchi zinazopakana na bahari kutangazamipaka ya maeneo ya bahari. Fursa hii inatoa haki kwa nchihizo kutafuta, kutumia, kuhifadhi na kusimamia rasilimali haina zisizo hai hadi maili za bahari (Nautical Mile) 200 kutokaufukweni.

Mheshimiwa Spika, mwaka 1989 Bunge lako Tukufu lilitungaSheria ya Bahari ya Kitaifa ya Ukanda Maalumu wa Uchumi(Territorial Sea and Exclusive Economic Zone Act of 1989;ambayo ilitambua kuwepo kwa maeneo matatu ya Bahari

Page 73: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maeneo hayo ni:Bahari ya Ndani (Inner Sea), Bahari ya Kitaifa (Territorial Sea)na Ukanda Maalum wa Uchumi wa Bahari (ExclusiveEconomic Zone EEZ).

Mheshimiwa Spika, eneo Maalum la Uchumi wa Bahari(Exclusive Economic Zone EEZ) ambapo hufanyika shughuliza uvuvi wa Bahari Kuu na samaki wa asili wanaopatikanakatika eneo hili ni wa aina ya Jodari na jamii zake husifikakwa tabia ya kuhama kwa kasi kubwa tena katika makundikutoka eneo moja la maji ya bahari hadi eneo lingine.

Mheshimiwa Spika, hali hii imepelekea baadhi ya nchizinazoendelea, kushindwa kunufaika ipasavyo na Uvuvi waBahari Kuu kutokana na uwekezaji mkubwa unaohitajikakwenye Uvuvi wa Bahari Kuu. Changamoto nyinginezinazokabili Uvuvi wa Bahari Kuu ni gharama kubwa katikakuendeleza, kusimamia na kudhibiti shughuli za uvuvi ikiwemoUvuvi Haramu, Usiotolewa Taarifa na Kuratibiwa (Illegal,Unreported and Unregulated – IUU- fishing).

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua changamoto hii na kwakuzingatia uhitaji wa nchi zinazoendelea katika kukabilianana Uvuvi Haramu sehemu za Ukanda wa Uchumi na BahariKuu, Nchi Wanachama zikiongozwa na Shirika la Chakula naKilimo la Umoja wa Mataifa (Food and AgricultureOrganization of the United Nation – FAO) ziliafikiana kuchukuahatua madhubuti za pamoja za kukabiliana na uvuvi haramu,usiotolewa taarifa na usiodhibitiwa kwa kutumia bandari.

Mheshimiwa Spika, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja waMataifa (Food and Agriculture Organization of the UnitedNation – FAO) pamoja na mambo mengine linaongoza juhudiza kuongeza usalama wa chakula na lishe duniani. Katikakutekeleza majukumu yake, mwaka 2001 FAO iliandaaMpango Mahsusi (International Plan of Action) wa kuzuia,kudhoofisha na kuondoa uvuvi haramu katika Ukanda waUchumi na Bahari Kuu ambao umetokana na ongezeko lamatukio ya uvuvi haramu unaosababisha uharibifu wa

Page 74: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

ikolojia, upotevu wa rasilimali za uvuvi na kuathiri maisha yawavuvi na usalama wa chakula na lishe duniani.

Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza adhima hiyo, Mkataba waKimataifa wa Kuzuia Uvuvi Haramu, Usiotolewa Taarifa naUsiodhibitiwa kwa Kutumia Bandari (The Agreement on PortState Measures to Prevent, Deter and Eliminate Illegal,Unregulated Fishing- PSMA) uliandaliwa na kukubaliwa.Mwaka 2009 mwezi Oktoba uriridhiwa na nchi Wanachamakwa ajili ya kuzui uvuvi haramu duniani.

2.0 MADHUMUNI NA FAIDA ZA MKATABA WA KIMATAIFA WAFAO WA KUZUIA UVUVI HARAMU KUPITIA BANDARI ZA NCHIWANACHAMA

Mheshimiwa Spika, lengo kuu la kuzuia uvuvi haramu nikulinda rasilimali za uvuvi ili kuwa na uvuvi endelevu na kuletafaida kwa taifa husika na kuhakikisha usalama wa chakulana lishe kupitia Mkataba wa FAO - PSMA. Aidha, Mkatabahuu ni muhimu kwa ajili ya kulinda rasilimali za uvuvi zilizoponchini katika maeneo ya maji ya bahari.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Tanzania, Bunge likiridhiaMkataba huu, manufaa yatakayopatikana ni pamoja na: -

(i) Kupungua kwa upotevu wa rasilimali za uvuvi na uharibifuwa mazingira ya bahari kutokana na kuimarika kwa udhibitiwa uvuvi haramu na usimamizi wa matumizi endelevu yarasilimali za uvuvi.

(ii) Kuongezeka kwa mchango wa Pato la Taifa.

(iii) Upatikanaji wa masoko ya uhakika ya kimataifa katikauendelezaji wa rasilimali za uvuvi.

(iv) Kuongezeka kwa fursa za uwekezaji katika Sekta ya Uvuvina hivyo kutoa fursa za ajira, kuimarika kwa ukusanyaji naupatikanaji wa takwimu na taarifa mbalimbali zinazohusuuvuvi katika Bahari Kuu.

Page 75: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

(v) Kuwezesha udhibiti wa uvuvi haramu kati ya NchiWanachama.

(vi) Kuijengea Nchi uwezo wa kulinda rasilimali za uvuvi zilizokondani ya mipaka ya bahari katika eneo letu.

3.0 UCHAMBUZI WA ITIFAKI

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Kimataifa wa FAO wa kuzuiaUvuvi Haramu kupitia Bandari umegawanyika katika sehemukuu kumi (10) zenye jumla ya Ibara 37. Maelezo yafuatayoyatafafanua kwa ufupi vipengele muhimu vilivyochambuliwana Kamati.

Ibara ya PiliIbara hii inaelezea madhumuni ya Mkataba wa FAO - PSMAkuwa ni kuzuia, kudhoofisha na kutokomeza uvuvi haramuusiotolewa taarifa na usiodhibitiwa ili kuhakikisha uhifadhi namatumizi endelevu ya rasilimali za baharini na kulinda ikolojia.

Ibara ya NneIbara hii inaelezea uhusiano wa Mkataba wa FAO - PSMA naSheria za Kimataifa pasipo kuathiri sheria za nchi husika. HivyoMkataba huu hautazuia nchi kujiamulia mambo yake.

Ibara ya TanoInaelezea ushirikiano na uratibu katika ngazi ya Kitaifa katikautekelezaji wa Mkataba wa FAO - PSMA.

Ibara ya SitaInaelezea ushirikiano katika kubadilishana taarifa zinazohusuusimamizi wa rasilimali za uvuvi baharini kati ya nchiwanachama, FAO na mashirika ya Kikanda na Kimataifa.

Ibara ya SabaInaeleza wajibu wa nchi wanachama kubainisha bandarizenye sifa stahiki ambazo zitatambulika kwa ajili ya shughuliza ukaguzi katika utekelezaji wa Mkataba wa FAO - PSMA.

Page 76: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Ibara ya Nane na TisaZinaelezea utaratibu unaopaswa kuzingatiwa na meli za uvuviza kigeni kupata kibali cha kuingia bandarini na kukaguliwa.Iwapo itathibitika kuwa meli inayoomba kibali cha kuingiabandarini imehusika na uvuvi haramu haitaruhusiwa kuingiawala kupata huduma yoyote.

Ibara ya KumiInaeleza mazingira ambayo meli inayohusika na uvuviharamu itaruhusiwa kuingia bandarini na kupata huduma zadharura hususan zile zinazohusu afya/ uhai wa binadamu.

Ibara ya Kumi na MojaInaeleza huduma ambazo hazitapaswa kutolewa bandarinikwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi husika na sheria zakimataifa kwa meli ambayo taarifa zake za ukaguzizitathibitishwa kuwa inajihusisha na uvuvi haramu.

Ibara ya Kumi na Mbili, Kumi na Tatu, Kumi na Nne, Kumi naTano na Kumi na SitaIbara hizi zinaeleza taratibu za kuzingatia katika kufanyaukaguzi wa meli kwa mujibu wa Mkataba wa FAO - PSMA,taratibu za uandaaji wa ripoti na namna ya kubadilishanataarifa za ukaguzi baina ya nchi wanachama.

Ibara ya 17 na Ishirini na MojaZinaeleza kuhusu kujengewa uwezo kwa wakaguzi wa meli,kubadilishana uzoefu baina ya nchi wanachama, kupatamisaada ya kitaalam na kuwezesha utekelezaji wa Mkatabawa FAO - PSMA.

Ibara ya IshiriniInaeleza wajibu wa meli inayopeperusha bendera ya nchimwanachama kutoa ushirikiano, kufuatilia na kuhakikishavyombo vyao vinafuata masharti kwa mujibu wa sheria zanchi na za Kimataifa.

Ibara ya Ishirini na MbiliInaeleza kuhusu upatikanaji wa suluhu pindi nchi wanachamazinapoingia katika migogoro.

Page 77: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Aidha, Mkataba umeruhusu migogoro inapojitokezakutatuliwa kwa njia ya majadiliano kabla ya kufikia ngazi zamahakama za Kimataifa.

Ibara ya Thelathini na TatuIbara hii inatoa fursa kwa nchi mwanachama kupendekezamkataba kufanyiwa marekebisho endapo kuna haja yakufanya hivyo.

Ibara ya Thelathini na TanoInaeleza kuhusu nchi mwanachama kujitoa katika Mkatabawa FAO - PSMA. Mktaba huu unatoa fursa kwa nchimwanachama kujitoa muda wowote baada ya mwakammoja tangu tarehe ya kuridhiwa kwa mkataba husika.

Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kufanya uchambuzikwenye Ibara hizo za msingi, Kamati ilitaka kujiridhisha kwenyemaeneo yafuatayo: -

(i) Idadi ya nchi wanachama wa FAO waliokwisha ridhiaMkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Uvuvi Haramu.

(ii) Sababu zilizopelekea nchi yetu kuchelewa kuridhiaMkataba huu.

(iii) Kwa nchi yetu kutoridhia Mkataba huu, Je hakuna namnayoyote nchi yetu inatekeleza makubaliano yaliomo kwenyeMkataba huu? Ikiwa ni pamoja na kuzifuatilia na kuzikaguameli za kigeni zinazokuja kwenye bandari zetu? Kama ndiokuna madhara gani?

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako kuwa, hojazilizoibuliwa na Wabunge zilipata maelezo ya kuridhishakutoka kwa Serikali na Wadau kama ifuatavyo: -

(i) Tanzania haina sababu ya kutoridhia kwa kuwa kipindi chaRatification kimeshapita baada ya idadi ya Wanachama waFAO wa kuridhia ilipotimia. Hivyo Tanzania by Default haiwezikukwepa kutekeleza Makubaliano hayo kwani kwa kutofanyahivyo kunaiondolea sifa Tanzania na kuonyesha ni nchi

Page 78: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

inayosaidia kuendelea kuwepo kwa uvuvi haramu nauharamia mwingine baharini.

(i i) Pamoja na kwamba nchi yetu bado haijaridhiamakubaliano hayo, hata hivyo imeendelea kutekelezamakubaliano hayo kwa vitendo kwa kufuatilia na kufanyaukaguzi wa meli za nje zinazokuja kwenye bandari zetu ilikuhakikisha kuwa ni meli halali na mizigo iliyobeba ni ileiliyoruhusiwa kimataifa.

(iii) Kwa muda mrefu hatua za kuridhia zilikwama kutokanana ukweli na ugumu wa kupata maoni ya wadau kutokapande zote mbili za muungano.

Kwa sasa pande zote mbili za Muungano zimejiridhisha faidazinazoambatana na Mkataba huu na hivyo zimekubaliananchi yetu iridhie Mkataba wa FAO - PSMA.

Mheshimiwa Spika, mbali na ufafanuzi huo uliotolewa, faidazingine zinazoambatana na kuridhiwa kwa Mkataba wa FAO-PSMA ni pamoja na:-

• Nchi yetu itanufaika kwa kutolipa kwa gharama zozotezinazoambatana na uanachama ~ (Accession ni costless);

• Wataalamu wetu watapatiwa mafunzo bure kwenye Idarambalimbali zinazojihusisha na shughuli za uvuvi na mazao yauvuvi kama Bandari, Askari wa Majini kupitia Jeshi laWanamaji, Idara ya Uvuvi, Shirika la Viwango Tanzania,Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu;

• Nchi yetu kupitia mwamvuli wa FAO itapata misaadamingine mingi inayopitia Umoja wa Mataifa hususan misaadainayoendana na udhibiti wa uharamia kwenye maji yoteyaliyoko eneo la Tanzania.

4.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATIMheshimiwa Spika, baada ya kufanya uchambuzi waMkataba wa Kimataifa wa FAO - PSMA wa kuzuia uvuviharamu kupitia bandari za nchi Wanachama, Kamati

Page 79: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

inakubaliana na mapendekezo ya Serikali kulingana nadhamira njema ya Mkataba huu kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio yatakayopatikana,Kamati ina maoni na ushauri ufuatao: -Ili nchi iweze kunufaika ipasavyo na Mkataba wa Kimataifawa FAO – PSMA na kuwezesha utekelezaji wa mapendekezoyaliyomo kwenye mkataba ni vyema Serikali: -• Ikaziwezesha ipasavyo Wizara za Uvuvi na Mifugo zaTanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa kutenga bajetizinazowezesha Wizara hizi zitekeleze majukumu yakeipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kifedha na kuipatiarasilimali watu ya kutosha Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu;

• Kuimarisha Shirika la Uvuvi Tanzania Bara (TAFICO) na Shirikala Uvuvi Zanzibar (ZAFICO);• Kujengwa kwa Bandari za Uvuvi;

• Kuanzishwa kwa viwanda vya kuchakata samaki katikaukanda wa bahari na

• Ununuzi wa meli za kitaifa kubwa zenye uwezo wa kuvuaeneo la Ukanda wa Bahari na hivyo kuwezesha uvuvi wakibiashara.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaamini kuridhiwa kwa Mkatabawa FAO - PSMA pamoja na kuimarisha uwekezaji kwenyeUkanda wa Bahari Kuu kutawezesha nchi yetu kuzifikia, nakuzimiliki rasilimali za uvuvi katika Ukanda wa Uchumi waBahari Kuu kutokana na ushirikiano wa nchi wanachamakudhibiti uvuvi haramu na hivyo kunufaika na rasilimali hizozilizopo eneo la Tanzania.

Mheshimiwa Spika, vile vile Pato la Taifa litaongezekakutokana na upatikanaji wa fedha za kigeni na hivyo kukuzauchumi wa Taifa, kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wamalighafi kwa ajili ya viwanda vya samaki, kuongezeka kwafursa za uwekezaji katika sekta ya uvuvi na hivyo kutoa fursaza ajira na kuongeza upatikanaji wa chakula na lishe nahatimae kuijengea nchi uwezo wa kulinda rasilimali za uvuvi.

Page 80: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

5.0 HITIMISHOMheshimiwa Spika, napenda kukushukuru kwa kunipa nafasiya kuwasilisha Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya Kamatikwa niaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaKilimo, Mifugo na Maji.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumpongeza nakumshukuru Waziri wa Mifugo Mhe. Luhaga J. Mpina, (Mb)na Naibu Waziri Mhe. Abdalla Ulega (Mb), Katibu Mkuu UvuviDkt. Rashid Tamatama pamoja na Wataalamu wote waWizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano walioipa Kamatiwakati ikichambua na kujadili Mkataba wa FAO - PSMA.

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru wadau wotewaliotoa michango yao kwa maandishi na kwa kufika mbeleya Kamati. Michango yao ilisaidia kuijengea uwezo Kamatina hivyo kuwawezesha Wajumbe kuwa na uelewa kuhusianana Mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa napenda kuwashukuruWajumbe wa Kamati kwa ushirikiano na michango yaowaliyoitoa wakati wa kupitia na kuchambua Mkataba huupamoja na kuandaa taarifa hii hadi kukamilika kwake.Naomba kuwatambua kwa kuwataja majina kamaifuatavyo: -1. Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa, Mb - Mwenyekiti2. Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma, Mb - M/Mwenyekiti3. Mhe. Dkt. Mary Michael Nagu, Mb- Mjumbe4. Mhe. Prof. Sospeter M. Muhongo, Mb - Mjumbe5. Mhe. Eng. Edwin A. Ngonyani, Mb - Mjumbe6. Mhe. Katani Ahmad Katani Mb - Mjumbe7. Mhe. Khadija Hassan Aboud, Mb - Mjumbe8. Mhe. Haroon Mulla Pirmohamed, Mb - Mjumbe9. Mhe. Ritta Enespher Kabati, Mb - Mjumbe10. Mhe. Mattar Ali Salum, Mb - Mjumbe11.Mhe. Lucy Simon Magereli, Mb - Mjumbe12. Mhe. Justine Joseph Monko, Mb - Mjumbe13. Mhe. Omar Abdallah Kigoda, Mb - Mjumbe14. Mhe. Anna Richard Lupembe, Mb - Mjumbe

Page 81: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

15. Mhe. Pascal Yohana Haonga - Mjumbe16. Mhe. Salim Mbaraku Bawazir Mb - Mjumbe17. Mhe. Deo Kasenyenda Sanga, Mb - Mjumbe18. Mhe. Devotha Methew Minja, Mb - Mjumbe19. Mhe. Haji Ameir Haji, Mb - Mjumbe20. Mhe. Haji Khatib Kai, Mb - Mjumbe21. Mhe. Sikudhani Yasini Chikambo, Mb - Mjumbe22. Mhe. Juma Ali Juma, Mb - Mjumbe23. Mhe. Emmanuel Papian John, Mb - Mjumbe24. Mhe. Kunti Yusuph Majala, Mb - Mjumbe25. Mhe. Anthony Calist Komu, Mb - Mjumbe26. Mhe. Jitu V. Soni, Mb - Mjumbe

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kumshukuru Katibu waBunge, Ndg. Stephen Kagaigai, Ndg. Michael ChikokotoKaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge kwa kuisaidiana kuiwezesha Kamati hii kutekeleza majukumu yake kwaweledi mkubwa.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee nawashukuruWatumishi wote wa Ofisi ya Bunge wakiongozwa naSekreterieti ya Kamati ambao ni Ndg. Virgil Mtui na Ndg.Rachel Nyega pamoja na msaidizi wa Kamati Ndg. MwimbeJohn kwa kuihudumia Kamati ikiwa ni pamoja na kukamilishataarifa hii kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naliomba sasaBunge lako lipokee, lijadili na liridhie Mkataba wa Kimataifawa FAO-PSMA wa kuzuia uvuvi haramu kupitia bandari zanchi wanachama.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naombakuwasilisha.

Mahmoud Hassan Mgimwa, (Mb)MWENYEKITI,

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI

14 NOVEMBA, 2019

Page 82: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt Ishengoma kwakupitia taarifa ya Kamati vizuri sana na kuweza kutusomeahapa mbele sasa nimuite Msemaji Rasmi wa Kambi yaUpinzani kuhusu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa DktSware Semesi karibu tafadhali

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI – MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA MIFUGONA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Naombakutoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusuazimio la kuridhia mkataba wa Kimataifa wa FAO wa kuzuiauvuvi haramu kupitia bandari za nchi wanachama(Agreement on Port State Measures Prevent, Deter andEliminate Illegal, Unreported and Unregulated Fishing – PSMA).

Mheshimiwa Spika, kwasababu ya muda naombanianzie Aya ya 5, lakini vyote naomba viingie kwenye hansard.Mkataba huu unatoa suluhisho kwa nchi wahusikakukomesha na kutokomeza uvuvi haramu, usiotolewa taarifana usiodhibitiwa ili kuhakikisha uhifadhi na matumizi endelevuya rasilimali za baharini.

Mheshimiwa Spika, mkataba huu una maana panainayohusisha na kuangalia maeneo yafuatayo:-

(i) Meli na shughuli za uvuvi zinazokinzana na sheria ya kitaifa,kikanda na kimataifa,

(ii) Meli zisizotoa au kutoa taarifa pungufu na zisizosahihi,

(iii) Meli zisizo na usajili wa taifa zinazotokea (status versols),

(iv) Uvuvi wa meli za nchi zisizowanachama katika maeneoyaliyondani ya mikataba ya usimamizi wa uvuvi ya taasisi zakikanda, na

(v) Shughuli za uvuvi usioratibiwa kisheria na nchi husikaambao ni vigumu kuufuatilia na kuudhibiti.

Page 83: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatambua kuhusika kikamilifu kwa nchi yetu kupitiawataalamu wetu wa pande zote mbili za Muungano kamawanachama wa FAO katika maandalizi ya makubaliano yaKitaifa ya udhibiti uvuvi haramu na biashara haramu yasamaki na mazao yake kupitia bandari na za nchiwanachama (PSMA).

Mheshimiwa Spika, Pia naomba kuwatambua Shirikala WWF wamekuwa wakiweka kipaumbele katika masualahaya.

Mheshimiwa Spika, sasa naenda kugusia umuhimu wakuridhia PSMA. Pamoja na kuwepo Ukanda wa uchumi waBahari Kuu (EEZ) ambamo nchi wanachama wanalazimikakulinda kwa gharama zote rasilimali zilizomo na kuzitumiakiuendelevu bado kuna eneo la Bahari Kuu (High Seas)ambao ni kubwa zaidi ya ukanda wa uchumi wa bahari kuu(EEZ) za nchi zote na ambalo nchi zote ikiwemo Tanzaniainaruhusiwa kutumia rasilimali zake zilizo hai na zisizo hai. Hatahivyo, bado imekuwa vigumu nchi zote wanachama wa FAOna zile ambazo si wanachama kuweza kuungana kwapamoja kuzilinda na kuhakikisha uendelevu wake hususanrasilimali zilizo hai ambazo ni renewable lakini zisizo vuliwakiuendelevu zitapotea na mazingira yake kuharibika.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hii imekuwa nichangamoto kubwa kusimamia rasilimali zetu katika ukandahuu wa bahari. Ndiyo maana kama nchi mwanachama waFAO njia rahisi ya kuweza kupigana vita dhidi ya uvuvi haramumaharamia na wafanyabiashara haramu ni kupitia bandariza nchi husika. Hii ni njia rahisi sana kwani pamoja na ukwelikuwa meli zinaweza kukaa baharini zikivua kwa muda mrefu,hata miaka miwili, bado zitalazimika kurudi kwenye moja yabandari kwa ajili ya ukarabati mkubwa na hata mdogo nahivyo kuwa rahisi kudhibitiwa.

Mheshimiwa Spika, njia nyingine rahisi na ya muhimuni kukagua na kufuatil ia mizigo ya mazao ya uvuviyanayotolewa bandarini na meli za uvuvi, ili kubaini meli

Page 84: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

zilizohusika na mzigo unaotolewa bandarini. Njia hii imekuwani bora zaidi na imesaidia sana kupunguza uvuvi haramu napia uharamia kwani PSMA, inazo protocol zinazoelekeza nchiwanachama kuchukua hatua kabla meli haijaruhusiwakuingia bandarini; na pia zipo orodha hakiki za ukaguzi wameli husika .

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa Tanzania badohaijaridhia makubaliano ya PSMA, bado imeendeleakuyatekeleza kwa vitendo makubaliano hayo kwa kufuatiliana kuzikagua meli za ndani na za kigeni zinazokuja kwenyebandari zetu ili kujihakikishia kuwa ni meli halali na mizigo yakeni ile inayoruhusiwa Kimataifa. Meli hizo huja bandarini kwetukwasababu mbalimbali; kwa mfano kushusha mabahariawagonjwa au waliomaliza mikataba yao, meli mbovu amakuja kwa ukaguzi wa awali kabla ya kupatiwa leseniUtekelezaji na makubaliano hayo ya PSMA kwa vitendo nimoja ya sababu ya msingi ya kuridhia makubaliano hayo.

Mheshimiwa Spika, kimsingi Tanzania haina sababuya kutoridhia makubaliano haya kwani kipindi cha uridhiwajikilishapita baada ya idadi ya wanachama wa FAO kuridhiailipotimia. Hivyo Tanzania haiwezi kukwepa utekelezaji wamakubaliano hayo kwani kutofanya hivyo kunaiondolea sifana kuonesha ni nchi inayosimamia uvuvi haramu na uharamiamwingine baharini

Mheshimiwa Spika, Tanzania ikiwa mwanachama waIndian Oncean Tuna Commission (IOTC), wanachama wakewaliamua kukubali FAO-PSMA kama IOTC binding resolutionna hivyo na Tanzania italazimika kuutekeleza mkataba huuwa PSMA kwa upande wa uvuvi wa samaki aina ya Jodari(tuna) na aina zinazofanana au kuhusiana na Jodari kwaupande wa Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu kwa Tanzania kuridhiamakubaliano haya kwa kuwa haitawajibika kwa malipo,gharama au mchango wowote kwa FAO au popote katikautekelezaji wake.

Page 85: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Mheshimiwa Spika, Tanzania kwa pande zote mbili zaMuungano imekuwa ikikosa misaada mbalimbali kwa mfanofursa za mafunzo yanayofadhiliwa na FAO na pia UN kwawataalam wake wa idara na taasisi mfano bandari, navy,polisi, idara za uvuvi, mamlaka za udhibiti wa viwango vyachakula, dawa na vifaa tiba, mamlaka ya kusimamia uvuviwa bahari kuu na mamlaka za usajili wa meli ili kuwawezeshakupata mafunzo mbalimbali ya kufanya udhibiti halisi kwenyebandari zetu kama timu moja. FAO inatoa fursa za mafunzonchi zilizoridhia makubaliano hayo tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuridhia azimio hili nchi chiniya mwamvuli wa FAO Tanzania itapata misaada minginemingi inayopitia Umoja wa Mataifa katika kudhibiti uharamiakwenye maji yetu yote na sio bahari peke yake. Tanzaniakwa miaka yote imekosa misaada ya fedha, mali na utaalamkutokana na kutoridhia mkataba huu. Pia tumeshindwakushirikishwa kikamilifu katika mipango ya hali ya juu na yakiteknolojia za hali ya juu katika udhibiti wa uvuvi haramu namapambano ya uharamia baharini. Tukiridhia maana yakeTanzania itanufaika na yale yanayopangwa kwenye nyanjambalimbali kimataifa chini ya mwamvuli wa Umoja waMataifa na FAO. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nchi nyingine zote za ukanda wamagharibi wa Bahari ya Hindi na nchi za South West IndianOcean Commission zimeridhia isipokuwa Tanzania naComoro tu. Hali hii haipendezi kwa nchi yetu ambayo nikubwa na yenye sifa kubwa ukilinga na Comoro. Aidha,inaonesha kwa kiwango fulani udhaifu wa kutokwendapamoja na wenzetu katika masuala nyeti na hususan vitavya kimataifa dhidi ya mambo mabaya kama uvuvi nabiashara haramu, uharamia, usafirishaji haramu wa silaha,madawa ya kulevya, binadamu na maliasili mbalimbalikupitia meli.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kuwa Tanzania niMwenyekiti wa SADC ambayo ina protocol maalum yakuongoza sekta ya uvuvi kwa pamoja na kutambua kuwanchi zote za SADC zenye bahari zimeridhia makubaliano

Page 86: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

haya, ni vema tusirudi nyuma na kuacha maswali mengi sanakwa nchi wenzetu wa SADC bila sababu yoyote ile.

Mheshimiwa Spika, mapitio ya baadhi ya ibara katikamkataba. Mkataba wa PSMA una sehemu 10 na ibara 37 naviambatanisho vitano. Ibara ya 6 inaelekeza ushirikiano katikakubadilishana taarifa zinazohusu usimamizi wa rasilimali zauvuvi bandarini kati ya Nchi Wanachama na FAO namashirika ya kikanda na kimataifa. Kambi inaishauri Serikalikuizingatia hii na kuwezesha Wizara husika kutekeleza jukumuhili.

Mheshimiwa Spika, licha ya kuwa Kambi Rasmi yaUpinzani kwa mara kadhaa imekuwa ikisistiza kwa Bunge lakoumuhimu wa kuwa na bandari ya uvuvi katika mwambaowa nchi yetu, lakini mapendekezo na mipango hiyo imebakiakwenye makabrasha ya Serikali. Bado kambi inasisitizaumuhimu wa kuwekeza katika sekta ya uvuvi wa bahari kuukwa kuwa na bandari ya uvuvi kwani Serikali imekuwa ikikosamapato yake halali inayostahili kutoka uvuvi wa bahari kuu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkataba wa PSMAunahusika na meli zote za kigeni za uvuvi zinazotaka kuingiakatika bandari zilizochaguliwa na nchi husika na kwakuzingatia Ibara ya 7 ya mkataba ambayo inahusu wajibuwa Nchi Wanachama kubainisha bandari zenye sifa stahikiambazo zitatambuliwa kwa ajili ya shughuli za ukaguzi katikautekelezaji wa mkataba wa PSMA, ni muhimu sasaMheshimiwa Waziri akawaeleza Watanzania ni bandari zipiambazo kwa sasa zimekwishatambuliwa katika kuhakikishazinatekeleza jukumu hilo.

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Taifa wa Pili waMaendeleo ya Miaka Mitano ukurasa wa 251 unaelezeakuhusu kujengwa kwa bandari ya uvuvi katika Mikoa yaTanga, Dar es Salaam au Mtwara na bahati nzuri bajeti yaujenzi kuanzia mwaka wa fedha 2016 – 2021 imeanishwa. Hojaya msingi ambayo pia Waziri anatakiwa kuliezea Bunge nikiasi gani sasa kimeshatolewa kati ya shilingi trilioni 2.5

Page 87: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

zilizopangwa kwenye Mpango kwa ajili ya kukamilisha ujenziwa bandari ya uvuvi.

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 8 inaongelea utaratibuunaopaswa kuzingatiwa na meli za uvuvi za kigeni kupatakibali cha kuingia bandarini na kukaguliwa. Sharti hili linawezakuwa jepesi na gumu kwa kuwa nchi zetu nyingi hasa zaukanda wa pwani wa Afrika Mashariki na Kusini hazinavyombo vya kufanya doria hivyo si rahisi kufahamu meli husikana mizigo iliyonayo imeipata kutoka ukanda wa nchi gani.Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza kuwaSerikali kuimarisha doria katika maeneo ambayo tunayamilikiili tuweze kuwa na uhakika kwamba rasilimali zinazotoka zinamanufaa kwa watu wetu na nchi yetu kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, naomba niende kwenye maoniaya ya 25. Ufanisi wa utekelezaji wa PSMA utapelekeamchango wa muda mrefu wa uhifadhi wa matumizi endelevuwa viumbe hai na rasilimali za bahari na mifumo ya kiikolojia.Tunaporidhia mkataba huu nchini kwetu basi hatuna budikutekeleza majukumu yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, moja; kuandaa sheria, kanuni nataratibu zake za utawala kitaifa; Mbili, kushiriki katika mijadalaya kuandaa makubaliano, maazimio na miongozoyanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa; Tatu, nchi zinahitajikufuata taratibu za kusaini na kuridhia mwongozo aumkataba husika ili kuwezesha kujumuisha mwongozo huokatika sheria za kitaifa; Nne, kuanzisha utaratibu wa mashartiya bandari ambapo meli za uvuvi zitalazimika kufuatautaratibu uliowekwa ili ziweze kutumia bandari husika; Tano;chini ya Mkataba wa PSMA Nchi Wanachama zitalazimikakutekeleza hatua na miongozo yote kama ilivyoainishwakatika mkataba huo; na Sita, kwenye rasimu ya warakatunashauri suala hili lipanuliwe zaidi isiwe kwa ajili ya ukandawa uchumi wa bahari kuu (EEZ) yetu pekee, bali udhibiti uwepia hadi kwenye bahari kuu (high seas) ambapo Watanzaniawanapaswa kuwezeshwa ili wakavue EEZ na zaidi ya hapo.Hivyo, pale ambapo kumeorodheshwa maeneo ya bahariyaani inner sea, territorial sea na ukanda wa uchumi wa

Page 88: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

bahari yaani EEZ, tuongezee na bahari kuu kwani naWatanzania pia wanaruhusiwa kuvua kwenye ukanda wauchumi wa bahari kuu za nchi nyingine na pia bahari kuukatika maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, naomba nihitimishe; Kambi Rasmiya Upinzani haioni sababu yeyote ya kupinga uridhiwaji wamkataba huu kulingana na maudhui ya mkataba huu. Aidha,ili faida zinazoongelewa katika mkataba huu zikainufaishenchi yetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitizakuzingatia ushauri ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, moja; kuhakikisha bandari ya uvuviinajengwa kwa haraka kama ilivyoelezwa kwenye Mpangowa Maendeleo wa Awamu ya Pili; Mbili, kuweka utaratibumzuri wa kupata wakaguzi kulingana na matakwa yamkataba; Tatu; kuwekeza katika vyombo vya kufanya doriakwenye ukanda wa uchumi na bahari kuu; na Nne na mwishokuimarisha masoko yetu ya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakuwasilisha. (Makofi)

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSUAZIMIO LA KURIDHIA MKATABA WA KIMATAIFA WA FAO WA

KUZUIA UVUVI HARAMU KUPITIA BANDARI ZA NCHIWANACHAMA (AGREEMENT ON PORT STATE MEASURES TO

PREVENT, DETER AND ELIMINATE ILLEGAL, UNREPORTEDAND UNREGULATED FISHING-PSMA) KAMA

YALIVYOWASILISHWA MEZANI

“Yanatolewa kwa Mujibu wa Kanuni ya 53(6)(c) ya Kanuniya Bunge, Toleo la Mwaka 2016)”

I. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni mwanachama waShirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) tangumwaka 1962 na mwaka 2001 FAO kutokana na ongezeko lauvuvi haramu il iandaa mpango mahsusi wa kuzuia,

Page 89: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

kudhoofisha na kuondoa uvuvi haramu usiotolewa taarifa nakudhibitiwa (Illegal, Unreported and Unregulated) ambaohufanyika kwa kiasi kikubwa katika ukanda wa uchumi wabahari kuu (Exclusive Economic Zone - EEZ) za nchi za pwani.Hali hii hutishia uhakika wa upatikanaji wa chakula kutokamazao ya baharini kwa watu trakribani milioni 45 kwa Barala Afrika, na kupelekea pia kupata hasara ya takribani dolaza kimarekani bilioni 1.5 katika Bara letu kwa mwaka.

2. Mheshimiwa Spika, mkataba huu ni matokeo ya uvuviharamu uliokithiri katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari Kuu(EEZ) na baadae meli hizo haramu za uvuvi kupata hudumawanazohitaji kwenye bandari zingine tofauti na walipokuwawanafanya uvuvi haramu. Jambo hili limeota mizizi hasa kwamataifa ya dunia ya tatu ambayo hayana uwezo wa kufanyadoria katika eneo lake la Ukanda wa Bahari Kuu kwa ujumlawake.

3. Mheshimiwa Spika, kama azimio hili linavyosema,mchakato mzima wa uvuvi haramu unasababisha uharibifumkubwa wa ikolojia, upotevu wa rasilimali za uvuvi na hivyokuathiri maisha ya wavuvi wadogo ambao ikolojia ya baharini muhimu katika kazi zao za kila siku, sambamba nakuhatarisha usalama wa chakula na lishe kwa nchi husika naduniani kwa ujumla.

4. Mheshimiwa Spika, lengo mahususi pia la mkatabahuu ni kuongeza mtandao wa ushirikiano baina ya mataifaya kikanda na kimataifa katika kutokomeza uvuvi haramu.Katika kufikia utekelezaji huo, bandari za nchi mwanachamandizo zitakuwa na jukumu la ziada katika kupambana nauharamia huo.

5. Mheshimiwa Spika, mkataba huu unatoa suluhishokwa nchi wahusika kukomesha na kutokomeza uvuvi haramuusiotolewa taarifa na usiodhibitiwa ili kuhakikisha uhifadhi namatumizi endelevu ya rasilimali za baharini.

6. Mheshimiwa Spika, mkataba huu una maana panainayohusisha na kuangalia maeneo yafuatayo:-

Page 90: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

i. Meli na shughuli za uvuvi zinazokinzana na sheria za kitaifa,kikanda na kimataifa;

ii. Meli zisizotoa au kutoa taarifa pungufu na zisizo sahihi;

iii. Meli zisizo na usajili wa Taifa zinakotokea (status vessel);

iv. Uvuvi wa meli za nchi zisizo wanachama katika maeneoyaliyo ndani ya mikataba ya usimamizi wa uvuvi ya taasisi zakikanda; na

v. Shughuli za uvuvi usioratibiwa kisheria na nchi husika ambaoni vigumu kufuuatilia na kuudhibiti.

7. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatambua kuhusika kikamilifu kwa nchi yetu kupitiawataalamu wetu wa pande zote mbili za Muungano kamamwanachama wa FAO katika maandalizi ya makubalianoya kitaifa ya kudhibiti uvuvi haramu na biashara haramu yasamaki na mazao yake kupitia bandari za nchi wanachama(PSMA)

II. UMUHIMU WA KURIDHIA PSMA

8. Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwepo Ukanda waUchumi wa Bahari Kuu (EEZ) ambamo nchi wanachamawanalazimika kulinda kwa gharama zote rasilimali zilizomona kuzitumia kiuendelevu bado kuna eneo la BAHARI KUU(high seas)ambalo ni kubwa zaidi ya Ukanda wa Uchumi waBahari Kuu (EEZ) za nchi zote na ambalo nchi zote ikiwemoTanzania inaruhusiwa kutumia rasilimali zake zilizo hai na zisizohai. Hata hivyo, bado imekuwa vigumu nchi zotewanachama wa FAO na zile ambazo si wanachama kuwezakuungana kwa pamoja kuzilinda na kuhakikisha uendelevuwake hususani rasilimali zilizo hai ambazo ni ‘renewable’ lakinizisipovuliwa kiuendelevu zitapotea na mazingira yakekuharibika.

9. Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hii, imekuwa nichangamoto kubwa kusimamia rasilimiali zetu katika ukanda

Page 91: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

huu wa bahari, na ndiyo maana kama nchi mwanachamawa FAO njia rahisi ya kuweza kupigana vita dhidi ya uvuviharamu, maharamia na wafanyabiashara haramu ni kupitiaBandari za nchi husika. Hii ni njia rahisi sana kwani pamoja naukweli kuwa meli zinaweza kukaa baharini zikivua kwa mudamrefu hata miaka miwili (2) bado zitalazimika kurudi kwenyemoja ya bandari kwa ajili ya ukarabati mkubwa na hatamdogo na hivyo kuwa rahisi kudhibitiwa.

10. Mheshimiwa Spika, njia nyingine rahisi na ya muhimuni kukagua na kufuatil ia mizigo ya mazao ya uvuviyanayoletwa bandarini na meli za uvuvi (at Sea Trans-shipment) ili kubaini meli zilizohusika na uvuvi na mzigounaoletwa bandarini. Njia hii imekuwa ni bora zaidi naimesaidia sana kupunguza uvuvi haramu na pia uharamiakwani PSMA inazo protokali zinazoelekeza nchi wanachamakuchukua hatua kabla meli haijaruhusiwa kuingia bandarinina pia zipo orodha hakiki (checklists) za ukaguzi wa melihusika.

11. Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa Tanzania badohaijaridhia makubaliano ya PSMA, bado imeendeleakuyatekeleza kwa vitendo makubaliano hayo kwa kuzifuatiliana kuzikagua meli za ndani na za kigeni zinazokuja kwenyebandari zetu ili kujihakikishia kuwa ni meli halali na mizigo yakeni ile inayoruhusiwa kimataifa. Meli hizo huja bandarini kwetukwa sababu mbalimbali mfano; kushusha mabahariawagonjwa au waliomaliza mikataba yao, meli mbovu (forcemajoure) ama kuja kwa ukaguzi wa awali kabla ya kupatiwaleseni (Pre License Inspections). Utekelezaji wa makubalianohayo ya PSMA kwa vitendo ni moja ya sababu ya msingi yakuridhia makubaliano haya.

12. Mheshimiwa Spika, kimsingi, Tanzania haina sababuya kutoridhia makubaliano haya kwani kipindi cha uridhiwajikilishapita baada ya idadi ya wanachama wa FAO wakuridhia (ratification) ilipotimia. Hivyo, Tanzania haiwezikukwepa kutekeleza makubaliano hayo kwani kutofanyahivyo kunaiondolea sifa na kuonesha ni nchi inayosimamiauvuvi haramu na uharamia mwingine baharini.

Page 92: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

13. Mheshimiwa Spika, Tanzania ikiwa mwanachama wathe Indian Ocean Tuna Commission (IOTC), wanachamawake waliamua kukubali FAO PSMA kama ‘IOTC bindingresolution’ na hivyo Tanzania italazimika kuutekelezamkataba huu wa PSMA kwa upande wa uvuvi wa samakiaina ya jodari (tuna)na aina zinazofanana au kuhusiana najodari kwa upande wa bahari ya Hindi.

14. Mheshimiwa Spika, ni muhimu kwa Tanzania kuridhiamakubaliano haya kwa kuwa haitawajibika kwa malipoyoyote au gharama yoyote au mchango wowote kwa FAOau popote katika utekelezaji wake.

15. Mheshimiwa Spika, Tanzania (kwa pande zote mbiliza Muungano) imekuwa ikikosa misaada mbalimbali kwamfano fursa za mafunzo yanayofadhiliwa na FAO na pia UNkwa wataalam wake wa Idara na Taasisi mbalimbali mfano:Bandari, Navy, Polisi, Idara za Uvuvi, Mamlaka za Udhibiti waViwango vya Chakula, Dawa na Vifaa Tiba, Mamlaka yaKusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu na Mamlaka za Usajili waMeli ili kuwawezesha kupata mafunzo mbalimbali ya kufanyaudhibiti halisi kwenye bandari zetu kama timu moja. FAOinatoa fursa za mafunzo nchi zilizoridhia makubaliano hayatu.

16. Mheshimiwa Spika, kwa kuridhia azimio hili, chini yamwamvuli wa FAO Tanzania itapata misaada mingine mingiinayopitia Umoja wa Mataifa (UN) katika kudhibiti uharamiakwenye maji yetu yote na siyo Bahari pekee. Tanzania kwamiaka yote imekosa misaada ya fedha, mali na utaalamkutokana na kutoridhia mkataba huu. Pia tumeshindwakushirikishwa kikamilifu katika mipango ya hali ya juu na yakiteknolojia za hali ya juu katika udhibiti wa uvuvi haramu namapambano ya uharamia Baharini. Tukiridhia maana yakeTanzania itanufaika na yale yanayopangwa kwenye nyanjambalimbali kimataifa chini ya mwamvuli wa Umoja waMataifa (UN) na FAO.

17. Mheshimiwa Spika, nchi nyingine zote za ukanda waMagharibi wa Bahari ya Hindi na chini za South West Indian

Page 93: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Ocean Commission zimeridhia isipokuwa Tanzania na Komorotu. Hii ni haipendezi kwa nchi yetu ambayo ni kubwa na yenyesifa kubwa kulinganisha na Komoro. Aidha, inaonesha kwakiwango fulani udhaifu wa kutokwenda pamoja na wenzetukatika masuala nyeti na hususani vita za kimataifa dhidi yamambo mabaya kama uvuvi na biashara haramu, uharamia,usafirishaji haramu wa silaha, madawa ya kulevya, binadamuna maliasili mbalimbali kupitia meli.

18. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kuwa Tanzania niMwenyekiti wa SADC ambayo ina protokali maalum yakuongoza sekta ya uvuvi kwa pamoja; na kwa kutambuakuwa nchi zote za SADC zenye Bahari zimeridhia makubalianohaya; ni vyema tusirudi nyuma na kuacha maswali mengisana kwa nchi wenzetu za SADC bila sababu yoyote ile.

III. MAPITIO YA BAADHI YA IBARA KATIKA MKATABA

19. Mheshimiwa Spika, Mkataba wa PSMA una sehemu10 na Ibara 37 na viambatisho 5. Ibara ya 6 inaelezeaushirikiano katika kubadilishana taarifa zinazohusu usimamiziwa rasilimali za uvuvi bandarini kati ya nchi wanachama waFAO na mashirika ya kikanda na kimataifa.

20. Mheshimiwa Spika, licha ya kuwa Kambi Rasmi yaUpinzani kwa mara kadhaa imekuwa ikisisitiza kwa Bunge lakoumuhimu wa kuwa na bandari ya uvuvi katika mwambaowa nchi yetu, lakini mapendekezo na mipango hiyo imebakiakwenye makabrasha ya Serikali. Bado Kambi inasisitiziaumuhimu wa kuwekeza katika sekta ya uvuvi wa bahari kuukwa kuwa na bandari ya uvuvi kwani Serikali imekuwa ikikosamapato yake halali inayostahili kutoka uvuvi wa bahari kuu.

21. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkataba PSMAunahusika na meli zote za kigeni za uvuvi zinazotaka kuingiakatika bandari zilizochaguliwa na nchi husika, na kwakuzingatia Ibara ya 7 ya Mkataba ambayo inahusu wajibuwa nchi mwanachama kubainisha bandari zenye sifa stahikiambazo zitatambuliwa kwa ajili ya shughuli za ukaguzi katikautekelezaji wa Mkataba wa PSMA; ni muhimu sasa

Page 94: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Mheshimiwa Waziri akawaeleza watanzania ni bandari zipiambazo kwa sasa zimekwisha tambuliwa katika kuhakikishazinatekeleza jukumu hilo.

22. Mheshimiwa Spika, Mpango wa Taifa wa II waMaendeleo wa Miaka Mitano ukurasa wa 251 unaelezeakuhusu kujengwa kwa Bandari ya Uvuvi katika Mikoa ya Tangaama Dar es Salaam au Mtwara na bahati nzuri bajeti ya ujenzikuanzia mwaka wa fedha 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021imeainishwa. Hoja ya msingi ambayo pia Waziri anatakiwakulieleza Bunge ni kiasi gani hadi sasa kimeishatolewa kati yashilingi trilioni 2.53878 zilizopangwa kwenye mpango kwa ajiliya kukamilisha ujenzi wa bandari ya uvuvi.

23. Mheshimiwa Spika, Ibara ya 8 inaongelea utaratibuunaopaswa kuzingatiwa na meli za uvuvi za kigeni kupatakibali cha kuingia bandarini na kukaguliwa. Sharti hili linawezakuwa jepesi na gumu kwa kuwa nchi zetu nyingi hasa zaukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na Kusini hazina vyombovya kufanya doria hivyo si rahisi kufahamu meli husika namizigo iliyonayo imeipata kutoka Ukanda wa nchi gani. Hivyo,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza kwa Serikalikuimarisha doria katika maeneo ambayo tunayamiliki ilituweze kuwa na uhakika kwamba rasilimali zinazotoka zinamanufaa kwa watu wetu na nchi yetu kwa ujumla.

24. Mheshimiwa Spika, ni ukweli kwamba kwa kila ukaguziwa meli husika, mkataba haukuweka wazi pale meliitakapokuwa imejaza shehena ya samaki, zipimwe nakuilazimisha meli husika kulipa mrahaba kulingana na sheria,kanuni na taratibu za nchi husika. Kama hili lingezingatiwa,tunaamini ingekuwa ni fundisho, kwani hata wakifanya uvuviharamu na kukimbia bado wangelazimika kulipa kulinganana mavuno waliyopata. Hii ni kutokana na ukweli kwambamkataba huu unalenga kukomesha na kutokomeza uvuviharamu unaofanywa katika ukanda wa kiuchumi kwenyebahari kuu na hilo lingekuwa ni fundisho stahiki kwa vyombovyote vitakavyo kamatwa katika kadhia hiyo.

Page 95: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

IV. MAONI

25. Mheshimiwa Spika, ufanisi wa utekelezaji wa PSMAutapelekea mchango wa muda mrefu wa uhifadhi namatumizi endelevu wa viumbe hai na rasilimali za bahari namifumo ya kiikolojia.

26. Mheshimiwa Spika, tunaporidhia mkataba huu nchinikwetu, basi hatuna budi kutekeleza majukumu yafuatayo:-

i. kuandaa sheria, kanuni na taratibu zake za utawala kitaifa;

ii. kushiriki katika mijadala ya kuandaa makubaliano,maazimio, miongozo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa;

iii. nchi zinahitaji kufuata taratibu za kusaini na kuridhiamwongozo au mkataba husika ili kuwezesha kujumuishamwongozo huo katika sheria za kitaifa;

iv. kuanzisha taratibu na masharti ya bandari ambapo meliza uvuvi zitalazimika kufuata utaratibu uliowekwa ili ziwezekutumia bandari husika;

v. chini ya mkataba wa PSMA, nchi wanachama zitalazimikakutekeleza hatua na miongozo yote kama ilivyoainishwakatika mkataba huo; na

vi. Kwenye rasimu ya waraka tunashauri suala hili lipanuliwezaidi isiwe kwa ajili ya ukanda wa uchumi wa bahari kuu (EEZ)yetu pekee bali udhibiti uwe pia hadi kwenye Bahari Kuu (highseas) ambako Watanzania wanapaswa kuwezeshwa iliwakavue EEZ na zaidi ya hapo. Hivyo, pale ambapokumeorodheshwa maeneo ya bahari yaani Inner Sea,Territorial Sea na Ukanda wa Uchumi wa Bahari Kuu (EEZ)tuongezee na Bahari Kuu kwani Watanzania piawanaruhusiwa kuvua kwenye Ukanda wa Uchumi wa BahariKuu (EEZ) za nchi nyingine na pia Bahari Kuu.

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inaisisitizia Serikalikuwawezesha Watanzania katika kuhamasishwa kwenye

Page 96: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

uwekezaji na pia kuwezeshwa kwenda Ukanda wa Uchumiwa Bahari Kuu (EEZ) na Bahari Kuu kama vile ambavyowenzetu wa nchi nyingine wanavyovua kwenye EEZs zao, EEZsza nchi nyingine na pia Bahari Kuu.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina maoni kuwa uanzishwajiwa Shirika la Uvuvi - TAFICO na kuendeshwa na Serikali is anon starter project bali tunaamini kuwa njia yenye tija nikuiwezesha sekta binafsi kuingia kwenye uvuvi wa Bahari Kuuama kwa Watanzania wenyewe kuwezeshwa au kuingia ubiaau vyote viwili.

V. HITIMISHO27. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haionisababu yoyote ya kupinga uridhiwaji wa mkataba huukulingana na maudhui ya mkataba huu. Aidha, ili faidazinazoongelewa katika mkataba huu zikainufaisha nchi yetu,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza kuzingatia ushauriufuatao:-

i. Kuhakikisha bandari ya uvuvi inajengwa kwa haraka kamailivyoelezwa kwenye Mpango wa maelendeleo awamu yapili;

ii. Kuweka utaratibu mzuri wa kupata wakaguzi kulingana namatakwa ya mkataba;

iii. Kuwekeza katika vyombo vya kufanya doria kwenyeukanda wa uchumi na bahari kuu; na

iv. Kuimarisha masoko yetu ya ndani.

28. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naombakuwasilisha.

……………………..Dr. Sware I. Semesi (Mb)

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani-Wizara yaMifugo na Uvuvi

14/11/2019

Page 97: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

SPIKA: Ahsante sana Dkt. Sware Semesi, Msemaji Mkuuwa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Mifugo naUvuvi. Sasa naomba nimuite Mheshimiwa Waziri wa Nishati iliawasilishe Azimio la Bunge la Kuridhia Kuanzishwa kwaUshirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua, Mheshimiwa Dkt.Kalemani, karibu tafadhali.

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kuanzishwa kwaUshirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (The Framework

Agreement on the Establishment of International SolarAlliance)

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, naombakuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Azimio la Bunge laKuridhia Mkataba wa Kuanzishwa kwa Ushirikiano waKimataifa wa Nishati ya Jua (The Framework Agreement onthe Establishment of International Solar Alliance).

Mheshimiwa Spika, KWA KUWA Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ni Nchi Mwanachama wa Jumuiya ya Umojawa Mataifa (UN) na kwa kuwa Mkataba wa kuanzishwa kwaJumuiya ya Umoja wa Mataifa ina hamasisha NchiWanachama kushirikiana katika utafiti, uendelezaji nautumiaji wa rasilimali mbalimbali za nishati ikiwemo nishati yajua katika kuzalisha umeme,

NA KWA KUWA Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaimeamua kushirikiana na nchi nyingine duniani hususanzilizopo katika ukanda wa tropiki ya kansa na kaprikoniambazo zinapata nishati ya jua kwa wingi kuendeleza tafitipamoja na matumizi ya nishati yakiwemo umeme.

NA KWA KUWA Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniailishiriki katika Mkutano wa 21 wa Conference of Partiesuliofanyika Jijini Paris, Ufaransa mwezi Novemba mwaka 2015sambamba na kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusumabadiliko ya tabianchi (The United Nations FrameConvention of Climate Change) ambapo pamoja namambo mengine, kulikuwa na makubaliano kuwa kiundwechombo cha pamoja (alliance) kitakachowezesha nchi

Page 98: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

mbalimbali duniani hususan zilizopo katika ukanda wa kitropikikukuza tafiti katika kuzalisha nishati ya safi ambapo ni cleanenergy inayotokana na nguvu ya jua.

NA KWA KUWA, katika utekelezaji wa maamuziyaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 21 wa Conference ofParties mwezi Novemba, 2016, Jamhuri ya Muungano waTanzania ilisaini Mkataba wa ISA Mjini Marrakesh, Moroccona KWA KUWA Mkataba huo umetambua na kuzingatiaMkataba wa Umoja wa Mataifa wa Paris kuhusu mabadilikoya tabianchi (Paris Agreement on Climate Change);

NA KWA KUWA Ibara ya 13 ya Mkataba inaeleza kuwaMkataba wa ISA utaanza kufanya kazi siku 30 baada yatarehe ambayo hati ya kuridhia mwanachama 15 itakuwaimekubalika na utaanza kutumika katika nchi husika baadaya kuridhiwa na sheria kupitia taratibu za wanachama;

NA KWA KUWA kutokana na mkataba huu Jamhuriya Muungano wa Tanzania itapata faida na manufaayafuatayo:-

(a) Kuimarika kwa upatikanaji wa nishati ya umemenchini hususan katika maeneo ya vijijini utakaochochea ukuajiwa shughuli za kiuchumi na hatimaye kukuza mapato yawananchi;

(b) Kuongezeka kwa matumizi ya nishati safi na boranchini na hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokanana uwepo wa hewa ya ukaa;

(c) Kukua kwa teknolojia hasa ya umeme jua nchinina hivyo kuboresha upatikanaji wa nishati hapa nchini;

(d) Kuongezeka kwa utaalam na ujuzi waWatanzania kutokana na fursa za mafunzo;

(e) Kuimarika kwa uwekezaji katika miradi ya nishatiya jua hususan kutoka sekta binafsi; na

Page 99: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

(f) Kuimarika kwa mahusiano ya kiplomasia nakibiashara kati ya Tanzania na nchi nyingine zinazotekelezampango wa ISA.

HIVYO BASI kwa kuzingatia manufaa yatokanayo namkataba huu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakwa mujibu wa Ibara ya 63(e) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Kumi na Sabalinaazimia kuridhia Mkataba wa Kuanzishwa kwa Ushirikianowa Kimataifa wa Nishati ya Jua (The Framework Agreementon the Establishment of International Solar Alliance - ISA).

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono,tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Nishati,Mheshimiwa Dkt. Kalemani kwa uwasilishaji mzuri sana waAzimio hili la Bunge la Kuridhia Kuanzishwa kwa Ushirikianowa Kimataifa wa kuhusiana na Nishati ya Jua.

Sasa naomba nimwite Mwenyekiti wa Kamati yaNishati na Madini, karibu sana Mheshimiwa Mwenyekitimwenyewe, Mheshimiwa Dunstan Kitandula.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA – MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaSpika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuwasilisha taarifahii kwa niaba ya Kamati.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa 53(6)(b) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, naombakuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishatina Madini kuhusu Azimio la Kuridhia Mkataba wa Kuanzishwakwa Ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (Framework

Page 100: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Agreement on The Establishment of the International SolarAlliance - ISA).

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipata fursa ya kujadilimkataba huu na kufanya mapitio mbalimbali baada yakupokea hoja hiyo kutoka Serikalini. Aidha, Kamati ilipata fursaya kuwaalika wadau mbalimbali ili waweze kutoa maoni yaojuu ya mkataba huu, vikao hivi vilifanyika hapahapa Dodoma.Niseme tu tunawashukuru sana wadau ambao walishirikikutoa mawazo yao kwa Kamati kwa sababu maoni yaoyameisaidia sana Kamati kuweza kufanya uchambuzi kuhusumakubaliano ya Mkataba wa ISA.

Mheshimiwa Spika, Jamhuri ya Muungano waTanzania ilishiriki katika Mkutano wa 21 uliofanyika Parisambao ulijadili mambo haya.

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa kuanzishwa Jumuiyaya Umoja wa Mataifa unaohamasisha Nchi Wanachamakushirikiana katika utafiti na uendelezaji wa utumiaji warasilimali mbalimbali za nishati ikiwemo nishati ya jua unalengakatika kuziwezesha nchi hizi kuweza kupata manufaa yamatumizi ya nishati ya jua, kupunguza gharama za nishatihiyo na mambo mengine kadhaa.

Mheshimiwa Spika, katika kuuchambua mkataba huuKamati ilitumia nyaraka mbalimbali ikiwemo Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini vilevile tafitimbalimbali zilizofanywa na shirika letu la umeme TANESCOkuhusu rasilimali jua katika nchi yetu. Kamati ilitafakari nakujiridhisha juu ya faida zinazoweza kupatikana kutokana nakuridhia mkubaliano ya mkataba kama ulivyo. Faida hizo nipamoja na hizi zinazofuata:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, ni kuimarika kwaupatikanaji wa nishati ya umeme nchini hususan katikamaeneo ya vijijini utakaochochea ukuaji wa shughuli zakiuchumi na hatimaye kukuza vipato vya wananchi. Vilevilekuongezeka kwa matumizi ya nishati safi na bora nchini nahivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira na kutoa uwepo wahewa ya ukaa. Vilevile, mkataba huu utawezesha kukua kwa

Page 101: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

teknolojia hasa ya umeme wa jua nchini hivyo kuboreshaupatikanaji wa nishati hiyo hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, vilevile nchi itafaidika nakuongezeka kwa utaalam na ujuzi wa Watanzania kutokanana fursa za mafunzo. Kubwa ni kuimarika kwa uwekezaji katikamiradi ya nishati ya jua hususan katika sekta binafsi na vilevilekuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara katiya Tanzania na nchi nyingine zinazotekeleza mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa umeme wa jua kwateknolojia ya solar PV hapa nchini upo katika kiwango chachini sana, inakadiriwa kuwa ipo katika megawatt chini yatano. Changamoto zinazochangia hali hiyo ni pamoja nakuwepo kwa utaalam mdogo, gharama kubwa za uwekezajina ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbaliya umeme.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ushirikiano wa ISAunajielekeza katika kupunguza gharama za uzalishaji wanishati na kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati safi, borana endelevu ili Tanzania iweze kunufaika ipasavyo, kwa hiyoni maoni ya Kamati kwamba ni bora nchi yetu ikaridhiamkataba huu.

Mheshimiwa Spika, aidha, katika upande wa hasaraKamati ilijielekeza kuona kama zipo hasara zozote ambazonchi inaweza kupata kwa kuingia kwenye ushirikiano huu.Baada ya Kamati kupitia vipengele vyote 14 ilijiridhisha bilawasiwasi wowote kwamba mkataba huu ni mzuri na haunachagamoto/hasara kwa upande wa nchi yetu. Aidha, Ibaraya 11 ya Mkataba inatoa fursa vilevile kwa nchi itakapoonahainufaiki kuweza kujitoa katika mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, maoni na ushauri wa Kamati;Mkataba wa ISA unalenga kuhamasisha Nchi Wanachamakushirikiana katika utafiti, uendelezaji na utumiaji wa rasilimalimbalimbali za nishati ikiwemo nishati ya jua katika kuzalishaumeme. Kwa kuzingatia sera na azma ya Serikali yetu yaAwamu ya Tano ya kuelekea katika uchumi wa viwanda,

Page 102: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

kama nchi tunahitaji kuwepo kwa nishati ya uhakika katikauzalishaji wa umeme. Baada ya Kamati kumaliza uchambuziwa Azimio hili, inatoa maoni na ushauri ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Nchi Wanachamazinaelimishwa na kuhamasishwa kuanzisha mtandao waushirikiano kama sehemu ya hatua ya kitaifa ya kukaziamaendeleo, basi mchakato huu kwa hapa nchini unapaswakujumuisha viongozi wa Serikali kuanzia ngazi za chini,mawakala wanaoshughulika na sekta ya nishati, asasi zakiraia, asasi zisizo za Kiserikali, sekta binafsi na wadau wenginewenye nia na malengo ya kuendeleza mifumo ya umemehapa nchini.

Mheshimiwa Spika, uanzishwaji wa mtandao waushirika wa ISA unapaswa kuzingatia taswira ya hali yaupatikanaji wa umeme wa Gridi ya Taifa hapa nchini iliuendelezaji wa uzalishaji wa umeme huu uweze kupelekwazaidi katika maeneo ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa,Gridi ndogo na maeneo ya Visiwa na maeneo ya nje ya Gridikwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mifumo ya Serikaliya sasa katika Sekta Ndogo ya Nishati mbadala Serikaliiangalie uwezekano wa Mamlaka hiyo kuunda miongozokadhaa ambayo inaweza kujumuisha Sera, Mikakati naMipango ya nchi hii kuendana na matakwa ya makubalianoya mashirikiano ya Mkataba tunaouzungumzia. Aidhatunashauri Serikali kutumia Wataalam wa ndani zaidi kulikokutumia wataalam wa nje ya Mifumo ya Serikali na siyowashauri wa nje ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, hii itaimarisha umiliki wa teknolojiana kujifunza kiufundi kwa wataalam wa ndani na hivyokurahisisha kukubalika na kupenya kwa teknolojia ya Nishatiya jua katika pembe tofauti za nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa fedha ambazozitapatikana kutokana na makubaliano ya Mkataba huuSerikali inapaswa kuhusisha Mashirika yake pamoja na Wadau

Page 103: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

wa sekta binafsi katika sekta ya Nishati kama vile AZAKI ZAKIRAIA na Makampuni binafsi kwa kuzingatia uwezo wao, ilikuchochea zaidi uendelezaji wa maendeleo ya uzalishaji waumeme hususan katika maeneo ya Vijijini.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali tunapendekezaSerikali kuangalia faida ya malengo ya baadaye ya nchikatika kutekeleza makubaliano ya Mkataba huu il imakubaliano haya yawe chachu ya kuendeleza maendeleoya miaka ijayo katika uzalishaji wa umeme.

Mheshimiwa Spika, Kamati katika uchambuzi wakeimebaini kuwa katika uanzishwaji wa Hisa nchi kumi na Tanoza kwanza, zilizokamilisha taratibu za kusaini na kuridhiaMkataba husika zilipewa hadhi ya kuwa wanachamawaanzilishi, na kwa kufanya hivyo zilinufaika na fedhazilizotengwa na Serikali ya India takribani dola bilioni kumi kwaajili ya miradi ya uendelezaji wa miradi mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, katika kiasi hicho dola bilioni mbilizilitengwa kwa ajili ya Afrika, kwa ajili ya Miradi ya NishatiJadidifu. Kamati imebaini kuwa kutokana na nchi yetukuchelewa kukamilisha taratibu za kuridhia Mkataba huuilishindwa kunufaika na fursa hii.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali kuwa sikuzijazo ni vyema kuharakisha tathmini ya mapitio ya Mikatabaya aina hii hususan pale inapoonekana kuwa na faida zawazi na kutokidhana na matakwa ya Katiba ya nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewebinafsi kwa uongozi wako mahiri na kwa kunipa nafasi yakuwasilisha maoni haya ya Kamati, nimshukuru MheshimiwaNaibu Spika pamoja na Wenyeviti wote wa Bunge kwakuratibu na kusimamia shughuli za Bunge lako Tukufu kwaumakini na umahiri mkubwa, aidha naomba nitumie fursa hiikuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Nishati na Madinikwa umahiri wao waliouonyesha katika kujadili Azimio hili, na

Page 104: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

katika hil i naomba majina yao yote yaingie katikakumbukumbu rasmi za Bunge letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitoe pia shukrani zangu za dhatikwa niaba ya Wajumbe wa Kamati kwa Mheshimiwa Dkt.Medard Kalemani Mbunge Waziri wa Nishati, Naibu Waziriwa Nishati Mheshimiwa Subira Mgalu pamoja na Watendajiwote wa Wizara ya Nishati wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt.Khamis Mwinyimvua kwa ushirikiano wao mkubwa kwaKamati yetu wakati wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda vilevile kumshukuruKatibu wa Bunge ndg. Stephen Kagaigai, Kaimu Mkurugenziwa Idara ya Kamati za Bunge Ndugu Michael Chikokoto,Makatibu wa Kamati Bi. Felister Mgonja na Bi. Angelina Sangapamoja na Msaidizi wa Kamati yetu Bi. Grace Mwenye kwakuratibu vyema shughuli za Kamati yetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombaTaarifa yetu yote iingie kama ilivyo, tulivyoiwasilisha naombakuwasilisha na naunga mkono Azimio. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mwenyekiti wa Kamati hii yaNishati na Madini, Mheshimiwa Dunstan Kitandulatunakushukuru sana kwa kutusomea Taarifa ya Kamati yakovizuri kabisa na kwa umakini mkubwa.

Sasa, nimuite Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzanikuhusu Wizara ya Nishati, karibu sana. (Makofi)

MHE. TUNZA I. MALAPO - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA NISHATI:Mheshimiwa Spika, Maoni ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni katika Azimio la kuridhia kuanzishwa kwa ushirikianowa Kimataifa wa Nishati ya Jua yaani Protocol FrameworkAgreement on The Establishment of The International SolarAlliance (ISA) yanatolewa kwa Mujibu wa Kanuni ya 53(6)(c)ya Kanuni za Bunge, Toleo la mwaka 2016.

Page 105: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Mheshimiwa Spika, The International Solar Alliance(ISA) ni ushirikiano unaotarajiwa kuwa na nchi wanachama121 ambao ulianza na India ikiwa ndio mwanzilishi wake.Nyingi ya nchi hizo ni zile zinazojulikana kama sunshinecountries, ambazo zimelalia au katikati ya tropiki ya Cancerna zingine kwenye Tropiki ya Capricon. Hadi sasa Mataifa 74tayari yameshasaini ushirikiano huo na kati ya hayo mataifa52 yamekwisha ridhia ushirikiano huo.

Mheshimiwa Spika, lengo la ushirikiano huu ilikuwa nikunufaika na nishati jua na hivyo kupunguza utegemezi wamatumizi ya nishati itokanayo na mafuta yaani (fossil energy)na hivyo kuwa nyenzo mojawapo ya kupambana namabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Spika, mbali ya lengo hilo, pia ushirikianohuu unatarajia kupunguza mahitaji makubwa ya nishati hasakwa nchi wanachama ambazo nyingi zake ni zi lezinazoendelea. Nishati ya jua ni ya uhakika kwa kuwainapatikana popote ambapo jua linaangaza kwa muktadhawa nchi zilizopo katika ukanda wa tropiki ya Cancer naCapricon.

Mheshimiwa Spika, ushirikiano huu ni mkatabaunaohusisha Mashirika ya Kimataifa ambayo wanachamawake ni Mataifa huru. Mataifa ambayo hayapo kwenyeukanda wa Tropiki ya Cancer au Capricon nayoyanaruhusiwa kujiunga na kunufaika na yale yote yatokanayona mkataba huo ila tu hayataruhusiwa kupiga kura kwa ajiliya maamuzi yoyote yatakayotolewa kwenye vikao halali vyaushirikano huo.

Mheshimiwa Spika, mpango huu ulizinduliwa na WaziriMkuu wa India kwenye kikao cha India Africa ambachokilihudhuriwa na wakuu wa nchi toka Afrika, kikitangulia nakikao cha mwaka cha Umoja wa Mataifa kuhusu mabadilikoya tabianchi kilichofanyika Paris Novemba 2015.

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni mojawapo ya nchiambazo zilishasaini makubaliano ya ushirikiano wa nchi

Page 106: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

mwanachama wa matumizi ya Nishati Jua ambapo mkatabaulianza kuwa wazi kwa ajili ya Mataifa kusaini hapo Novemba2016. Hili ni jambo zuri na kubwa japokuwa utekelezaji wakekwa vitendo ndio jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linahitajiutashi wa kisiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, India kwa kushirikiana na Ufaransawanatoa usaidizi kwa nchi mwanachama katika kujengamiundombinu ya utekelezaji wa miradi ya nishati itokanayona jua. Ushirikiano huu umetenga kiasi cha dola za Kimarekanitril ioni moja kama fedha za uwekezaji kwa lengo lakupunguza gharama za nishati jua hasa kwa maeneoambayo jamii zake za vijijini haziwezi kumudu gharama.Ushirikiano uliidhinisha India ili kutimiza au kufanikisha malengoya kuzalisha nishati ya jua ya GIGA WATT 100 sambamba naGIGA WATT 175 ya nishati jadidifu yaani Renewable energyifikapo mwaka 2020/2022.

Mheshimiwa Spika, taarifa zinaonesha kuwa Juni 302016 ushirikiano uliingia makubaliano na Benki ya Dunia ilikuweza kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza au kutekelezamiradi ya nishati jua SOLAR ENERGY. Benki ilitakiwa kuwa najukumu la kutafuta zaidi ya US Dollar trilioni moja kwauwekezaji utakaohitajika hadi mwaka 2020/2030 ili kutimizamalengo ya ISA katika kuhakikisha uzalishaji wa nishati juakwa gharama nafuu.

Mheshimiwa Spika, mkataba huu wa ushirikianoambao unatakiwa kuridhiwa na Bunge hili umegawanyikakatika Ibara 14 ambapo kila Ibara imejieleza kwa kifupi nakwa ufasaha.

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 1 inaelezea kwa kifupilengo la ushirikiano huu kwamba ni kutafuta suluhisho lapamoja katika kutatua changamoto zilizopo za matumizi yanishati jua katika mataifa wanachama kwa matumizi namahitaji yao.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaifanyiatafakari Ibara hii na kuja na muafaka kwamba ni kweli kuwa

Page 107: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

katika kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda nahivyo kupelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati, uwekezajikatika nishati ni jambo ambalo haliepukiki.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa fursa ya sisi kuwawashirika wa ISA ilikuwa tangu mwaka 2016, ina maanakwamba fursa pia ya kupata usaidizi wa fedha, elimu nateknolojia katika uzalishaji umeme kwa kutumia nishati ya juakama wenzetu wa India ambao wameweza kuzalishaumeme wa jua wa GIGA WATT 20 ndani ya kipindi kisichozidimiaka mitano na sasa wanatarajia kuzalisha umeme wa juawa GIGA WATT 100 pamoja na GIGA WATT 175 kwa nishatijadidifu ifikapo mwaka 2020/2022 na sisi tulikuwa na fursa hiyolakini tukashindwa kuitumia.

Mheshimiwa Spika, tunapofanya mambo yetu ni vizuritukachungulia na kwa wenzetu ambao wako kwenyemazingira kama sisi ili tuweze kubadilishana uzoefu, sasa waondani ya miaka mitano wamezalisha umeme wa jua wa GIGAWATT 20 sisi tunatarajia kuzalisha umeme wa MEGA WATT 2100za umeme wa maji ndani ya miaka mingapi? Hapa ndipoule usemi unaosema kuwa ukitaka kwenda haraka tembeapeke yako, lakini ukitaka kufika mbali basi tembea na wenzio.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa muktadha huo ni dhahiri ileharaka yetu ya kufua umeme wa maji kwenye maporomokoya Mto Rufiji itatuletea matatizo makubwa kiuchumi kwa sikuzijazo, kwani ISA inatoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradihiyo ya umeme wa jua, rejea Ibara ya 6 ya Mkatabainayohusu, budget and financial resources. Aidha, kamatulivyoainisha hapo awali kuwa Benki ya Dunia imeshatoaahadi ya kutafuta fedha kiasi cha dola za Kimarekani trilionimoja kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi ya nishati juakwa mwanachama wa International Solar Alliance.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayomachache kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,naomba kuwasilisha. (Makofi)

Page 108: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza MalapoMsemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Nishatinakushukuru sana kwa mchango wako pia. SasaWaheshimiwa Wabunge tunaingia kwenye eneo lauchangiaji na tutaanza na Mbunge wa Mafia. MheshimiwaMbaraka Dau, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Saada SalumMkuya.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru kwa fursa hii, ili niweze kuchangia kwenyeAzimio hili, awali ya yote ninaunga mkono Bunge letu kuridhiaItifaki hii ya kuzuia Uvuvi haramu.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiokuwa na shaka katikaeneo letu la exclusive economic zone (EEZ).

SPIKA: Waheshimiwa katika kuchangia mnaruhusiwakuchangia ama mojawapo ya Azimio hili ama Maazimio yotekatika uchangiaji wako. Lakini pia niwakumbushe Kamati yaUongozi tukitoka saa saba by saa saba na nusu tuwe palekwenye Ukumbi wa Spika, Kamati ya Uongozi tukutaneUkumbi wa Spika kuna kikao kidogo, Mheshimiwa MbarakaDau endelea.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa ufafanuzi huo, nitachangia kwenye Azimiola Itifaki ya Uvuvi haramu, ni ukweli usiokuwa na shaka katikaeneo letu la exclusive economic zone EEZ kumekuwa navurugu nyingi sana ya meli za kigeni zinazoingia kwendakuvua kule bila ya na vibali na ruhusa ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa haina uwezo,ilikuwa haina uwezo wa aina mbili, haina uwezo wa Vyombovya kwenda kuwazuia kule kwa sababu ni mbali na bahari nikali sana, lakini la pili tulikuwa hatuna uwezo kwa sababuMikataba kama hii ya Kimataifa haikuwepo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Itifaki hii inakwendakujibu swali hilo gumu kwamba sasa tunao uwezo, wale

Page 109: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

ambao wataingia katika eneo letu la EEZ na tukawezakuwaona kwenye ile VMS Versa Monitoring System yetu paleDSFA. Tunao uwezo sasa wa kwenda kuwafatil iawatakapokwenda kuweka nanga meli zao katika nchiWanachama hizi sitini, tunaweza kwenda kufatilia kule nakujua kwamba meli kadhaa iliingia katika EEZ ya Tanzaniabila ya kibali ikavua na sasa Serikali inachukua hatua.

Mheshimiwa Spika, sasa faida kubwa inayopatikanani hiyo, na mimi katika faida hiyo nilikuwa na maombi aunyongeza au ushauri kwa Waziri mwenye dhamana wa ainatatu, ushauri wa kwanza, twende tukafanye overall yaregulation zetu, Kanuni zetu za ile Taasisi yetu ya Uvuvi waBahari Kuu.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu gani? Kwa sababusasa tunayo nyenzo ya kujua kwamba kuna meli iliingiakwenye EEZ yetu haina kibali ikaenda kutia nanga labdaSeychelles tunatumia Mikataba ya Kimataifa kuikamata kule,Je, tumeshaikamata sasa tunafanya nini? Kwa sababu Sheriainataka ile meli au meli zile zije zihukumiwe kwa mujibu waSheria za Tanzania. Sasa ipo haja sasa ya kwenda kufanyiaoverall zile Kanuni zetu kwamba sasa je, meli ya aina hiiinayokamatwa itaingia kwenye kosa lipi? Tunaitaifisha,tunapiga faini, tunafanyaje?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa naombawenzetu wa, na nimemsikia Mkurugenzi Mkuu hapa waMamlaka ya Bahari Kuu yupo wenzetu wa Wizara kwakushirikiana na Mamlaka ile waende wakaanze kufanyia kazihizo regulation sasa ili tuweze kunufaika na hii Itifaki.

Mheshimiwa Spika, ombi au ushauri wa pili, Bandariya Uvuvi limesemwa hapa na Kamati, limesemwa na Taarifaya Kambi Rasmi ya Upinzani, bila ya kuwa na Bandari ya Uvuvina nilizungumza hapa nadhani wiki iliyopita, bila ya kuwa naBandari ya Uvuvi faida hizi zinatutoka kwa sababu hii EEZ yetukwa wakati mmoja inaweza ika-accommodate meli zaidi yamia moja, zinavua wakishavua wanakwenda kwa wenye

Page 110: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Bandari za Uvuvi Seychelles, Mauritius, Mordait na maeneomengine huko.

Mheshimiwa Spika, sasa sisi tunakosa haya manufaatukiwa na Bandari yetu ya Uvuvi zile zile meli zile tutazishawishizije huku kwenye Bandari yetu zianze kushusha ule mzigowafanye processing halafu baadaye na biashara yenyeweitaanza ku-boom kama vile ambavyo tulishuhudia biasharaya minofu ya samaki kule Mwanza kipindi kile Ndege zinakujakuchukua mzigo na kuondoka.

Mheshimiwa Spika, nafasi ile bado tunayo kwa kupitiaItifaki hii na kuweza kufufua au kujenga Bandari yetu ya Uvuviambayo itasaidia sana katika kuwavutia sasa hawa wenyemeli, tunaweka regulations kwa mfano sasa hivi tunaregulation zinazowataka wale wanaovua katika Bahari Kuuwaje katika Bandari zetu, lakini wanashindwa kuja kwenyeBandari zetu kwa sababu hatuna Bandari za Uvuvi, tunaBandari za Mizigo na Sheria za Kimataifa zinakataa kushushamzigo wa chakula kwenye Bandari ya Mizigo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naendelea kusisitiza nakumuomba Mheshimiwa Waziri ule mchakato wa kujengaBandari ya Uvuvi hata hii ya kununua meli inaweza ikasubirituanze na Bandari ya Uvuvi, ikijengwa Bandari ya Uvuvimultiply effect yake ni kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kutakuwa na ajira kwa vijana wetukwa sababu inakuja na logistics centers zile, kutakuwa naajira, biashara ita-boom kwa maana ya kwamba sasa mizigoitakuwa inakwenda ama kupitia Uwanja wa Ndege au kupitiakwenye Bandari zetu kwenda sokoni na maeneo mengineya nchi.

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia, pia nina ombijingine dogo kwa Mheshimiwa Waziri, tumeona kwamba mojaya faida tutakazozipata hapa ni kunufaika na misaadambalimbali inayotolewa na FAO kwa Tanzania. Kule Mafiaeneo la Kitutia ndiyo nursery, ndiyo labour ya samaki zaidi yaasilimia 70 wanaozaliwa katika Bahari ya Hindi, lakini eneo

Page 111: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

lenyewe la Mafia limechoka, eneo lenyewe halitunzwi, eneolenyewe wananchi wale ambao wanaitunza ile rasirimalihawanufaiki na chochote.

Mheshimiwa Spika, ningeomba kupitia Itifaki hii naMheshimiwa Waziri tumeambiwa kwamba kutakuwa na ainahiyo ya misaada mbalimbali, basi tuangalie namna gani lileeneo litakavyoweza kutunzwa vizuri na kuweza kuletamanufaa makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa fursa hii, naninaridhia Bunge letu liliridhie Itifaki hii ya Uvuvi haramu katikaBahari Kuu, nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, nakushukuru sana MheshimiwaMbaraka Kitwana Dau kwa mchango wako. Sasanilishamtaja Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum naatafuatiwa na Mheshimiwa Ruth Mollel. Mheshimiwa Saada,hayupo ehhe? Mheshimiwa Ruth na atafuatiwa naMheshimiwa Jitu Soni.

MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, ahsante kwakunipa nafasi hii, nami niweze kuchangia katika itifaki hizi mbili.Moja, nitachangia ya solar energy na pia nitagusia kidogokwenye hii ya PSMA ya FAO.

Mheshimiwa Spika, hii itifaki ya International SolarAlliances, tuliisaini mwaka 2015, tukiwa na ule Mkutano waClimate Change, Paris, mwaka 2015 na sasa imeletwaturidhie. Tumeona kwamba baadhi ya nchi, kwa mfano Indiaambao pia waliridhia mkataba huu, wao wamefika mbalisana katika kutekeleza huu mkataba na kuanza kutumiaenergy hii ya solar ambayo ni muhimu sana; kwa sababukwanza inafika vijijini, ambako energy nyingine ya umemehaifiki na vilevile ni energy ambayo ni safi kuliko tunavyoonakwenye energy nyingine ambazo zinaleta carbon monoxidekatika mazingira.

Mheshimiwa Spika, sasa napendekeza kwamba, huumkataba tumeusaini na ingekuwa ni vizuri vilevile kuhakikisha

Page 112: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

kwamba tunakuwa na mpango mkakati. Tumepitisha itifakinyingi hapa na sijui Bunge lako Tukufu ni kwa jinsi ganilinafuatilia hizi itifaki ambazo tunazipitisha hapa kuonakwamba zinatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, vilevile mradi huu utaongeza tijakwa wanavijiji na kuboresha maisha yao na kuwa na umemewa kuwasaidia kuzalisha na kuongeza pato lao la nchi. Kwahiyo, napendekeza kwamba, kuwepo na mpango mkakatina Waziri atueleze utakuwa vipi, ni kwa jinsi gani sasa, tunasolar energy na tuna REA? Tuone ni jinsi gani atajipanga,aweze kutekeleza hizi energy zote kwa pamoja; ya REA naSolar.

Mheshimiwa Spika, nitafurahi sana kama atakapokujaatatupa tu taarifa ni kwa jinsi gani hizi energy zote zitakwendakwa pamoja? Kwa sababu tunajua REA nayo inakwendavijijini na hii solar pia inakwenda vijijini; na solar ni rahisi zaidikwa sababu haihitaji miundombinu mikubwa other than hizisolar panels na miundombinu mingine midogo midogo najua tunalo kila siku. Kwa hiyo, nilikuwa nafikiri kwa mawazoyangu, itakuwa ni gharama nafuu zaidi kutekeleza hili la solarenergy, sambamba na REA vilevile.

Mheshimiwa Spika, nikienda kwenye suala ya ile itifakinyingine ya kuzuia uvuvi haramu kwenye deep seas; ni vizuritukaridhia huu mkataba, kwa sababu, kwanza kutakuwa namsaada, kwa sababu, bajeti yetu kama tunavyojua haikidhimahitaji. Tutakuwa na bajeti ya msaada ambayo tutaitumiakwa ajili ya kujenga uwezo wa watu wetu na vilevile kulindarasilimali yetu ambayo ni muhimu kama Wabunge wenginewengi walivyochangia. Siyo hivyo, kulinda rasilimali pia. Hatameli zinazokuja, zita-generate income ambayo itaingia katikamzunguko wa fedha.

Mheshimiwa Spika, tunajua jinsi ambavyo uvuviharamu umekithiri. Kwa hiyo, kwa kuridhia huu mkataba,tutasaidia kulinda rasilimali zetu zisiweze kupotea na badalayake tuweze kupata fedha zika-generate revenue ambayo

Page 113: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

tutaweza kuendelea katika maisha yetu na kujenga uchumiwetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache,ninaipongeza Serikali kwa kuleta hizi itifaki hapa mbili tuziridhiena tuwe na monitoring system; hiyo ndiyo concern yangukubwa. Tuna-monitor vipi sisi Bunge, kwamba hizi itifakitunazopitisha hapa kila siku, zinafuatiliwa na zinafikia wapi?Maana yake, tunapimaje utekelezaji wa hizi itifaki? Ahsante.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Ruth Hiyob Mollel.Kwa wasiomfahamu Mheshimiwa Ruth Mollel, alikuwa KatibuMkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na alihudhuria hizicoup kadhaa zilizopitisha baadhi ya maazimio makubwamakubwa ambayo baadhi yake ndiyo haya tunayoyapitishahapa. Hongera sana Mheshimiwa Ruth Mollel. (Makofi)

Sasa namwita Mheshimiwa Salum Rehani naatafuatiwa na Mheshimiwa Anastazia Wambura naMheshimiwa Mussa Mbarouk, ajiandae.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru nami kupata nafasi hii ya kuchangia kwenyeitifaki hii. Kwanza niseme kwamba naunga mkono naninaomba Wajumbe mbalimbali tuweze kuiridhia itifaki hii yaFAO ambayo sasa inatupeleka na sisi kutuunga miongonimwa nchi ambazo zinanufaika katika itifaki hii kwa walewaliokuwa wameanza kuridhia. Sisi tumechelewa.

Mheshimiwa Spika, hasara ya mwanzo ambayoinatokana na kutokuridhia kwetu, Tanzania imekosa siyo chiniya dola za Marekani 184,000 ambazo zilikuwa ni fedhamaalum za nchi ambazo zinapitiwa na bahari upande wamashariki na hasa zile ambazo zinatumika kupitishia melikubwa zinazomwaga dawa na sumu mbalimbali katika eneoletu. Kwa hiyo, eneo letu limekuwa linaathirika sana na watuambao wanafanya biashara ya kutupa uchafu mbalimbalihasa wa sumu katika eneo letu, lakini sisi kwa kutokuridhia

Page 114: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

mkataba huu, tumeshindwa kutetewa au kulindwa kwapamoja na wale waliokuwa wameridhia mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, la pili, tunaingia miongoni mwanchi ambazo zitakuwa zina ule mpango, routine research namonitoring ya meli zile ambazo zinaingia katika mkumbo wameli ambazo zinaitwa za eneo la Indian Ocean and Pacific,ambapo tutakuwa tunapata takwimu sasa za fish stock karibukila baada ya miaka mitatu katika eneo letu hili la baharikuu.

Mheshimiwa Spika, lingine mabalo linanufaisha;Tanzania pamoja na kuwa na ukubwa wa eneo la mita zamraba laki mbili, tulizoziongeza hizo la uvuvi wa uvuvi wabahari kuu, lakini tumeomba tena eneo lingine tuongezewela zaidi ya nautical miles 150,000. Kwa hiyo, tunakwenda kuwana eneo kubwa zaidi la uvuvi wa bahari kuu au eneo la baharikuu ambalo tunatakiwa sisi wenyewe tuweze kulilinda, tuwezekulitumia na litunufaishe kama ni sehemu ya rasilimali.

Mheshimiwa Spika, sasa huwezi kuwa na eneokubwa kama hili halafu ukasema kwamba wewe huungimkono wenzako ambao wanatumia vyombo mbalimbalikuweza kulilinda eneo hilo. Kwa hiyo, tukiridhia, hizo ni mojakati ya faida ambazo tutazipata.

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo linakwendakutupeleka sasa hivi, ni kwamba Serikali na mtazamo wa watumbalimbali, tumeomba hapa kwamba, nchi hii iwekezekwenye uvuvi wa bahari kuu. Tukiwekeza kwenye uvuvi wabahari kuu na sisi sasa tunakuwa miongoni mwa nchi ambazozinaingia kwenye ile wanaita Tuna World Market; Soko lile laJapani, kuna Soko la China na Soko lile la Norway, ambaponasi tutapata fursa ya kuweza kuuza samaki wetu katikamasoko ya nje.

Mheshimiwa Spika, faida nyingine ambayoimejitokeza hapa, ni kwamba zile meli ambazo tutazikamatazikichafua mazingira katika eneo letu la bahari kuu, tutawezakupiga faini au kuweza kuzilipisha faini za uchafuzi wa

Page 115: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

mazingira pale kisheria, kuliko kusema kwamba tunatumiasheria zetu za ndani, kitu ambacho wale wanaotumia sheriaza nje, hatuwezi kuwabana na baada ya kufanya huouchafuzi wanakwenda zao, kwa sababu hakuna kitu auhakuna mkono wa sheria unaowakamata na kuwezakuwaadhibu kwa vitendo ambavyo wanatufanyia.

Mheshimiwa Spika, la mwisho katika faida ambazozinapatikana, ni kulindwa katika ile wanaita Ocean BiologicalWeapons, ambapo katika eneo letu la bahari kuu huwezakutumika kwa uhalifu wa kibiolojia. Katika njia mbalimbaliambazo wenzetu nchi za nje zinatumia uharamia huo, eneoletu litakuwa linalindwa na vifaa maalum, zile VMS, maalumza Kimataifa kupita satellites na chochote kitakachopitakatika eneo hilo kwa nia ya kufanya uhalifu wa kibiolojia,kisheria zitaweza kuchukua mkondo wake.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nawambaWaheshimiwa Wabunge wa Bunge hili la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, turidhie, kwa sababu tukiridhia nasisi tutapata faida ya kuwemo miongoni mwa hao watuambao ni wanufaika wa mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, nawaombaSerikali kwa upande mwingine, tuweze kushiriki baadhi yamikutano na makongamano ambayo yanakwendakutunufaisha na miradi mbalimbali ya kimazingira katika eneoletu. Bado tu tuendelee kuwakumbusha Watanzaniakwamba, asilimia 67 ya tuna ambao wanaliwa duniani auwanaoingia katika Soko la Dunia, wanatoka katika belt hiiya Tanzania ambapo ni eneo lile la Kizimkazi mpaka Kitutiokule Mafya.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, fursa hii iliyokuwekoduniani mwote, tunaweza kusambaza samaki duniani,tuweze kuilinda na kuitunza. Ni kitu ambacho kwa kwelihakiwezi kupatikana, yaani faida yake haiwezi kupatikanakwa miradi mingine yoyote. Bado tuikumbushe Serikalikwamba eneo hili tukiwekeza, hakuna cha dhahabu, hakunacha bidhaa nyingine yoyote itakayoweza kuishinda hii blue

Page 116: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

sea kwa kipato. Kwa hiyo, nawataka wadau mbaimbali,wawekezaji mbalimbali, waje tukae na Serikali, tuangalieuwezekano wa kuwekeza katika eneo hili la uvuvi wa baharikuu.

Mheshimiwa Spika, siyo hilo tu, fursa nyingine ambayotunaipata sasa Tanzania, baada ya kuondoa ile 0.4,nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa hatua kubwaaliyoifanya na kuridhiana na wenzie wa Zanzibar na kuwezakumaliza tatizo lile la 0.4, sasa tunakwenda kurudisha leseniza uvuvi wa bahari kuu, na kuifanya Mamlaka ile ya Uvuviwa Bahari Kuu kuwa na kipato cha ajabu sasa hivi. Kwasababu, pending ya meli ambazo zinakaa zinagoja kufanyauvuvi wa bahari kuu ni zaidi ya 200 zinangoja leseni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, issue ilikuwa ni 0.4, Serikali imesikiakilio cha wadau, imekiondoa kwa muda hivi. Nami nasemakwamba, tukiweke pembeni, ili tuweze kupata faida ya melizile ku-land katika maeneo yetu au kubaki katika maeneoyetu, ambapo kila meli itaweza kuacha zaidi ya shilingi milioni40, ikija kutua katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, vilevile tusisahau; tujiandae sasana kufaidika na by-catch ambazo zitakuja katika maeneoyetu, ambazo zitaziba gap lile la upungufu wa samaki, ambaowanahitajika kwa kupunguza lishe na utapia mlo uliokuwekohapa nchini. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Rehani,Mheshimiwa Anastazia Wambura, atafuatiwa na MheshimiwaMbarouk.

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia katikahoja zetu za maazimio mawili. Kwanza, niseme naungamkono hoja za maazimio yote mawili ambayo ni Azimio laNishati ya Jua na Azimio la Mkataba wa Kimataifa wa FAO.

Mheshimiwa Spika, nitazungumzia zaidi Azimio hili laMkataba wa Kimataifa wa FAO. Nianze tu kwa kusema

Page 117: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

kwamba, Azimio hili linahusu sana vipengele vitatu, ambapokimojawapo kinahusu illegal, ambayo ni uvuvi usiozingatiasheria na cha pili ni unreported na cha tatu ni unregulated.Sasa katika hiki cha tatu cha unregulated fishing, niseme tukwamba, katika suala zima la udhibiti hatuwezi tukaepukakufanya resource assessment, kama nchi.

Mheshimiwa Spika, huwezi ukadhibiti kama hujui unakiasi gani cha rasilimali au aina gani ya rasilimali ya mazaoya bahari. Kwa hiyo, naomba sana Serikali, katika kutekelezasuala zima la udhibiti, iweke nguvu zake katika utafiti ili kusudituweze kujua ni kiasi gani ambacho tunacho katika bahariyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zipo hoja na dhana tofauti tofautikatika suala hili. Kwa sababu kuna wengine ambaowanasema kwamba, aina kubwa ya samaki bahari yetu kuuni jodari; na hawa jodari wana-move sana, wana-movefaster, hawakai katika eneo moja la nchi yetu. kwa hiyo siyowetu. Pia, wanasema kwamba ufanyaji wa resourceassessment ni kitu kigumu sana, lakini mimi niseme tu kwambahii siyo hoja kubwa sana kwa sababu hata kama tutakuwatumemsikia vizuri mchangiaji aliyetangulia, ametueleza wazikwamba asilimia 70 ya jodari inatokea Mafia, katika eneo laKitutia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni kwamba hawa samakini wetu na tuna kila sababu ya kufanya resource assessment.Hata ukiangalia katika mbuga yetu ya Serengeti, utaonakwamba wale nyumbu, pundamilia na wanyama mbalimbalihuwa wana-move kutoka eneo letu la Tanzania nawanaenda Kenya, lakini resource assessment huwainafanyika. Tunajua tuna kiasi gani cha nyumbu, tunajua tunakiasi gani cha pundamilia na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hili suala naomba Wizaraisilikwepe, itilie maanani, iwezeshe vituo vyetu vya utafiti(TAFIRI) na hata Chuo chetu cha Mbegani ili wawezekushirikiana kufanya resource assessment, ndipotutakapoweza kudhibiti vizuri.

Page 118: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

SPIKA: Mheshimiwa Anastazia, nilitaka kukwambia tu,hawa nyumbu ambao wanazunguka Kenya, Masai Marakurudi Tanzania na kurudi Kenya tena, zaidi ya 90%wanazaliwa Tanzania. Endelea tu namchango wako.(Makofi)

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa taarifa.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naependanizungumzie ni kuhusiana hasa na faida kubwa ambayotunapewa na huu mkataba. Tunapewa fursa kubwa sanana hasa kupitia ile United Nations Conversions on the Law ofthe Sea, ambapo kuna kifungu kimoja ambacho kinazitakahizi nchi wanachama wahakikishe kwamba wanatumiarasilimali hizi za bahari wao wenyewe na ile ziada ndiyowanawapa nchi nyingine na hasa kipaumbele kiwe kwa zilenchi ambazo hazina bahari.

Mheshimiwa Spika, hapa napenda tu kusisitizakwamba Serikali yetu sasa inatakiwa iangalie suala zima laustawi wa wananchi na hasa kwa kuzingatia upatikanaji wasamaki kama lishe kwa wananchi. Kwa kweli hili ni muhimusana na hasa ukiangalia kwamba katika nchi yetu matumiziya samaki ni madogo sana, lakini ni muhimu sana kuliko hatanyama na vyakula vingine. Samaki ni muhimu sana kwa afya,lakini tunatumia kilo karibu saba hadi kumi kwa mwaka nawakati mahitaji hasa yanatakiwa tupate takribani kilo 20 kwamwaka. Kwa hiyo, tunachotakiwa sasa kufanya nikuwawezesha wavuvi wetu wadogo waweze kupata hawasamaki kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wapate lishebora.

Mheshimiwa Spika, kuna suala zima la Sheria ya DSFApamoja na kanuni zake. Kumekuwepo na malalamikoambayo tumeyashuhudia hasa kutoka Zanzibar, kwamba,kulikuwa na kanuni ambayo inawataka wale wavuvi wawezekuleta by-catch katika nchi husika. Wanapokuwa wamevuana kupata wale samaki ambao hawakuwa wamepewaruhusa yake kuwavua, basi wawalete katika nchi husika. Sasa

Page 119: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

kilichokuwa kinatokea ni kwamba, wanawaleta wale samaki,halafu wanauza. Kwa hiyo, kilio kwa wavuvi ni kwamba beiya samaki inashuka na wakati wao wametumia gharamakubwa katika kuvua.

Mheshimiwa Spika, ninachotaka kupendekeza hapani kwamba, hii Sheria ya DSFA pamoja na kanuni zake, irejeweili kusudi suala zima la by-catch pale ambapo tutakuwatumeziruhusu sasa meli nyingine za nchi za nje kuja kuvuasamaki, suala la by-catch liwekewe utaratibu maalum ilikusudi wale wavuvi ambao wanavua karibu karibu wawezekuwapata hawa by-catch angalau waweze kushusha beiya samaki kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba, sheria au uleMkataba wa UNCLOS unasema kwamba hawa by-catch nimali ya nchi husika, siyo mali ya wale wavuvi wakubwa. Kwahiyo, ni makosa makubwa sana wanapokuwa wakiletasamaki halafu wanawauza wao wenyewe kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo ningependanisemee, unapofanya regulation au udhibiti, huwezi kuepukasuala zima la kuwa na bandari. Bandari ya Uvuvi ni lazima,lakini vilevile dry-dock, sijui inaitwaje kwa Kiswahili. Dry-dockni muhimu sana ili kusudi kuweza kuzihudumia zile meliambazo zinakuja pale. Badala ya kusema kwambawanaenda nchi jirani, waende Mauritius au waende Kenya,basi wafanyie pale pale matengenezo ambapo inawezaikahakikisha nchi yetu inapata kipato kikubwa ukichanganyapamoja na tozo za leseni na mambo mengine basi hata dry-dock inaweza ikachangia kukuza uchumi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipafursa hii ya kuchangia, ahsante sana.

SPIKA: Ahsante sana, nakushukuru sana. MheshimiwaAnastazia Wambura alikuwa ndio Mwenyekiti wa Kamati yetuMaalum kwa ajili ya masuala yanayohusiana na uvuvi wabahari kuu.

Page 120: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

Nilishakutaja Mheshimiwa Mussa Mbarouk, naweukichangia kwa kifupi nitafurahi. Atafuatiwa na MheshimiwaAlly Saleh.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsante;na mimi niungane na wenzangu kwanza kuunga mkonokuridhia nchi yetu kujiunga na itifaki hizi ambazo zilizotajwahapa ambazo ni FAO na masuala ya umeme wa jua yaanisolar power. Mimi nianze kuzungumzia kwenye suala hili lamkataba wa FAO.

Mheshimiwa Spika, wazungumzaji waliopitawamezungumza lakini ni ukweli usiofichika; ni kweli kwambameli nyingi za nje zinavua katika bahari yetu bila sisi wenyewekufaidika, na hili tuliligundua tulipokuwa kwenye ile KamatiMaaluma. Tukaona kwamba kuna meli zinakuja zinatumiabendera yetu lakini wanavua halafu mapato sisi hatupati kodiwala hatupati hao bycatch wanaotajwa.

Mheshimiwa Spika, labda Mheshimiwa Mwenyekitiwangu wa Kamati hakuifafanua vizuri hiyo bycatch. Ni samakiwale ambao wanaovuliwa hasa kuna Kanuni za kiuvuvikwamba lazima katika ile nchi ambayo mmevua mpelekesamaki kwa ajili ya lishe kwa matumizi mbalimbali, labda kwamfano kama kwenye watoto au shule au magereza ni Kanuniinatakiwa samaki wale washushwe hapo, na wasiuzwe.

Mheshimiwa Spika, lakini sasa kama alivyosealiyekuwa Mwenyekiti wetu; wamekuwa wakishushwa hapa;kwanza hatuna bandari ya uvuvi, kwa hiyo wanaposhushwawajanja wachache wananufaika wanawachukua walesamaki halafu wanawuza; sasa hili Wizara nalo iliangalie. Mimi,si kwa kujipendelea, lakini niseme hii bandari ya uvuvi ni vizuriikajengwa haraka na nilikuwa napendekeza basi kama kunasehemu ya kujengwa basi ingejengwa Tanga kwa sababuhakuna msongamano mwingi kwa masuala ya uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hilo mimi niseme tukwamba tu kwamba tumeona kwamba katika masualamazima ya uvuvi…

Page 121: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

SPIKA: Mheshimiwa Mbarouk ijengwe Tanga sioKongwa? (Kicheko)

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, Kongwahakuna bandari, kwa hiyo hili jambo ni vyema tukalifanya.

Mheshimiwa Spika, pia tumeona faida zinazopatikanakutokana na kuridhia hii mikataba tumeona kumbwatunapata fedha za mafunzo za kujenga uwezo lakinitunapata pia misaada ya vifaa vya doria. Kwenye nchi zetutumejifunza kwamba nchi kama Seychelles, Mauritius nakwingineko wanazo meli za doria, sisi hapa hatuna. SasaSerikali nao baada ya kuridhia hili jambo la uvuvi lakini iangalienamna ya kupata hizi meli za doria ambazo tukijiungatutapata misaada lakini na sisi wenyewe pia tujipange kuwanayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine hata meli za uvuvizitatusaidia tutapata ajira kwa vijana wetu lakini na Serikaliitapata fedha za mapato mengi kutokana na uvuvi wa baharikuu. Kama alivyosema msemaji mmoja, kwamba kamatukisimamia uvuvi wa bahari Kuu vizuri tunaweza tukapatafedha nyingi kuliko kwenye dhahabu na almasi; hili sasatulifanyie bidii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo napenda kulishauriBunge letu na Serikali kwa ujumla; kwa wale wenzetu ambaowamefanikiwa katika masuala haya, Serikali isione tabu katikakutumia fedha, kwa mfano ama kupeleka WaheshimiwaWabunge kwenda kujifunza ama kupeleka wataalam wetuwakajifunze. Wanafarsafa wanasema, ukitaka kula lazimauliwe, kwa hiyo na sisi tuhakikishe kwamba tunapeleka watuwetu kwa kutumia fedha zetu ili tuweze kukusanya mapatovizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nikija kwenye suala hili laumeme, nimeona hapa kwenye huu mkataba wa Solar kunamambo mengi ambayo sisi Tanzania tunaweza kusema siokisiwa. Wenzetu wengi wamefanikiwa kutokana na umemewa solar kwa sababu kwanza ni umeme wa bei rahisi, lakini

Page 122: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

hata bidhaa za viwandani zinashuka bei kwasababugharama za uzalishaji zinakuwa ni ndogo na umeme wa solarndio umeme wa bei rahisi zaidi duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, niseme tu kwambaSerikali isisite kutoa elimu hii ya manufaa ya umeme wa solarkwa sababu wengine wanatia dosari, wanasema umemewa solar kama ni fridge la futi tano haligandishi vizuri, umemewa solar kwenye nyumba hauna nguvu vizuri, sijui kwenyewelding haufanyi vizuri; kumbe tumeona baadhi ya nchiwanautumia huu umeme katika kila jambo.

Mheshimiwa Spika, nilibahatika kwenda Denmark,tukakuta wenzetu wanautumia umeme wa solar, wametegakila maeneo wameweka panel zinachukua umemeunakwenda magerezani, viwandani, shule, na kwenye vyuo.Wenzetu wananufaika, sasa sisi sasa kwa hili naomba na sisitusibaki nyuma, tutumie umeme wa solar kuendeleza maslahiya wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine, kuna mwekezaji mmojakule Kigoma, yeye huyu anazalisha umeme wa megawatttano; kuna sehemu inaitwa Kisenzi. Sasa TANESCO watu kamahawa iwasogeze karibu, iwe inasaidia, kwa sababu TANESCOhaiwezi ikasambaza umeme nchi nzima bila kuwa nawashirika. Sasa watu kama hawa nao watumike kuwasaidiamaeneo ya vijijini kuwasambazia wananchi wetu umeme.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho niseme tu, napo hatahapa katika masuala ya umeme wa solar tujitahidi sasa katikavyuo vyetu kama VETA, katika mafundi wetu hawawanaotumia umeme huu wa TANESCO, nao wapewe elimukwa ajili ya kujifunza kutumia umeme wa solar ili kuepushagharama za umeme, na ili kuyafanya maisha ya wananchiwetu yawe rahisi zaidi. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbarouk,Mheshimiwa Ally Saleh atafuatiwa na Mheshimiwa ProfesaAnna Kajumulo Tibaijuka.

Page 123: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Mimi nitabaki katika hili suala la solar power agreementambayo imesainiwa miaka michache tuliyopita, lakininimefurahi kwamba nchi yangu ilikuwa katika nchi zamwanzo na leo hata muda haujapita sana linaletwa Bungenituridhie. Kwa kweli tumekuwa tukipitwa na maazimio mengiya kimataifa lakini hili limekuja haraka sana. Nitafurahi spirithii ya kukipitisha maazimio haraka inavyowezekanaikiendelea.

Mheshimiwa Spika, la pili ni kwamba jana na juzinilisema kwamba Mungu ameiweka Tanzania kwa makusudiyake. Katika mfano huu wa solar ni kwamba ametuwekakatika maeneo kati ya tropical of cancer na tropical ofCapricorn ambayo inatajwa katika mkataba huo na katikatiinapita IKweta. Kwa maana tumewekwa kwenye sunshinestate kama inavyotajwa, na kama anavyosema NarendraModi wa India. Kwamba tuko katika eneo ambalo jua ni 12seven, lakini tunalitumiaje? Jua liko wakati wote na likotakriban nchi nzima; sasa tunalitumiaje ndiyo muhimu; kwahivyo tumekuwa katika pahala ambapo sasa hivi tuna fursanzuri sana. Nchi ambazo jua si wakati wote kama Ujerumanibado ni katika nchi 10 duniani ambazo zinaongoza kwa solar.

Mheshimiwa Spika, nchi kama ya Norway jua ambalosi siku zote lakini bado inaongoza kwa solar, sembuse sisiambapo asubuhi mpaka jioni jua.

Mheshimiwa Spika, kikundi hiki cha International SolarPower Agreement sasa hivi ni kundi kubwa la pili la nchi zaKimataifa zinazokutana baada ya Umoja wa Mataifa. Kwahivyo ni eneo ambalo linakua haraka sana na nafikiri takwimuza mwisho labda kama signatories kama 121 tayari mpakahivi sasa, kwa hivyo ni kundi kubwa. Hata hivyo si kundi kubwakwa jina tu, ni kundi kubwa kwa dhamira; kwa sababu kunamipango mingi ya kufanya ili kuiokoa dunia, linalofanywahapa ni kujaribu kuiokoa dunia. Ndiyo maana wanatakatufanye kila njia ili tuache kutumia fossil energy badala yaketutumie energy ambayo ni renewable, kwa hivyo sisi tusiiachefursa hii.

Page 124: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Mheshimiwa Spika, nasema tusiiache kwa sababunina experience, kwamba labda pengine kwa hii sasakutakuwa na mabadiliko; na ningependa Mheshimiwa Waziriwa Uwekezaji anisikilize katika hili.

Mheshimiwa Spika, na narudia tena hapa Bungeniniwahi kupata ofa ya wawekezaji ambao wako tayarikuwekeza three billion dollar’s kwa ajili ya three thousandsmegawati za umeme nikataabishwa, nikasumbuliwa mpakayule muwekezaji akakata tamaa. Hivi sasa nasema, pengineMheshimiwa Waziri ananisikia, kwamba nina offer nyingineya mtu ambaye yuko tayari kuwekeza vituo zaidi ya 50 vyasolar kwa ajili ya magari, kwa ajili ya vyombo vya umeme,kwa pesa zake; I mean ni self financing. Kwa hiyo kama Serikaliwatakuwa tayari huu ndio mwanzo mzuri, tunaanza kidogokidogo ku-phase kwenye petroleum tunaingia katika vituvingine. Kwa hiyo ningependa baadaye nikae nizungumzena Mheshimiwa Waziri tuone tatafanya kitu gani.

Mheshimiwa Spika, lakini pia ni njia nzuri ya energymix tunalalamika kila siku juu ya energy mix. Wengine tulisemasana hapa juu ya umeme wa Julius Nyerere; lakini kusemakweli tulikuwa na ushindani. Wengine tunasema kwambaumeme wa solar ni rahisi zaidi, wengine wanasema umemewa maji rahisi zaidi, lakini namna ya uwekezaji wenyewe. Sasahivi kumepatakana solution, hawa walioko mbele, kwamfano India, wao wametenga three fifty billion dollar’s kwaajili ya kuzisaidia nchi kufanya kazi hii. Pia World Bank waowanatarajia kuhamasisha uwekezaji wa takriban bilioni 1000mpaka kufikia 2030 ili nchi zote ambazo zina fursa zipo katikasunshine area ziweze kunufaika. Kwa hiyo sisi tusikae nyumasasa maadam tulishaingia katika uwanachama huu na tunafursa.

Mheshimiwa Spika, Dodoma peke yake hapaikitumika, maeneo ambayo hayafai kwa kilimo, maeneoambayo hayaoti miti basi tunaweza tukatoa megawati kwamamia kabisa sembuse nchi nzima, kwa hiyo tutumie fursahiyo kwa vizuri.

Page 125: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mheshimiwa Spika, lakini pia sasa hivi kuna nchi; kwamgano Venezuela, ambazo tayari zinaweza kufikia 100percent sasa ya mahitaji yao. Kwa hivyo sisi tusiona kwambaJulius Nyerere kama tumefika kwa zile megawati 2000 naushehe. Bado nchi hii kama tunataka kweli kwenda kwenyeviwanda tuondokane na dhana, kama alivyosemaMheshimiwa Mbarouk, ya kuona umeme wa jua si umemekitu. Umeme wa jua ni umeme kama umeme mwingine naunaweza kuuzalisha viwandani na unaweza ukatumikasehemu nyingine nyingi hata hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, imagine hapa jua linalopiga kutwanzima katika paa la nyumba hii na namna paa yaliyopo humundani kiasi ambacho pengine tukiweka solar tu humu ndaniya Bunge tunaweza tukakoa mamilioni ya fedha. Kama vileambavyo tumeokoa karatasi kwa kwenda kwenye tabletsna huku tunaweza tukaokoa pesa tukatumia renewableenergy lakini pia tukaokoa fedha nyingi kwa kuitandika solarpower eneo lote la Bunge au eneo lolote lingine ambaloumeme wake utakuja mpaka Bungeni. Kwa hiyo miminasema katika hili Tanzania tusikae nyuma…

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh nilitaka kukubaliana nawewe katika eneo la Bunge kutumia solar power. Niliwahaikutembelea Bunge la Israel wanatumia 1005 umeme waokwenye Bunge la Israel solar power. Endelea tu Mheshimiwa.(Makofi)

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, faharikubwa kukubaliwa wazo langu. Kwa hivyo mimi nafikiri Bungelioneshe mfano kwamba hiki kinawezekana na taasisi zaKiserikalia kwa mfano Mji wetu wa Mtumba utandikwe solar,inawezekana kufanya, ili Serikali iwe mfano na ili tuwetunaweza kujiendesha wenyewe kidogo mpaka hapoambapo wakubwa wa dunia watakapotuona na kuwekezakatika maeneo haya; kwa sababu umeme utaendeleakuhitajika kwa sababu tunasema tunataka Tanzania yaviwanda ahsante sana. (Makofi)

Page 126: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

SPIKA: Ahsante sana nilishakutaja Mheshimiwa AnnaTibaijuka karibu nisikie mchango wako.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi. Mimi pia naomba niunganena waliotangulia kuwapongezeni Waheshimiwa Mawaziriwote wawili waliotuletea mikataba hii ya Kimataifa kusudina sisi tuweze kuiridhia. Katika uchangiaji wangu, ni jambozuri na wote kama ilivyosema, hasa ule mkataba wa FAO,nataka kusema kwamba ni mkataba umekuwepo kwa mudamrefu mimi nimeushuhudia wakifanyiwa kazi bado niko hukoUmoja wa Mataifa. Sasa niseme kwamba labda ni muhimusana kusema, kwamba kwa kuwa tumechelewa kidogokuridhia mikataba hii mimi nimefarijika sana kuona kwambakatika Bunge hil i Tukufu inaonekana pande zotetunakubaliana kwamba turidhie, kwa hiyo naunga mkonohoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa katika kuridhia hilo na Serikalikatika kutupa taarifa nina mambo mawili ya kusema. Kwanzanaomba Mheshimiwa Waziri wetu wa Mifugo na Uvuvi ajaribukuangalia kwa wenzake hali tuliyo nayo huko katika baharikuu. Maana ninachofahamu mimi ni kwamba sisi Tanzaniatuna haki ya kupewa eneo zaidi katika bahari kuu ambayobado tunalidai. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kazi hiyo imekwama kule Umojawa Mataifa na nadhani sasa Mheshimiwa Waziri Mpina wewendiwe mhamasishaji, wewe ndiwe mwenye samaki, wewendiwe mwenye viumbe kule baharini. Nadhani ni muhimukuangalia mchakato wa kudai extended continental shelfya Tanzania umefikia wapi. Kazi naifahamu kwa sababumwaka 2012 nikiwa Waziri wa Ardhi niliwakilisha Umoja waMataifa New York kwenye kamati husika ya InternationalConvention on the Taw of The Sea, kudai eneo letu. Sasatusipoangalia tunaweza tukaridhia mikataba hii lakini kunasheria zinazotawala utawala wa maji duniani, InternationalLaw of the Sea. Labda ingekuwa ni vizuri kulijulisha Bunge hilimchakato huo umefikia wapi.

Page 127: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Mheshimiwa Spika, labda kwa kufafanua zaidi; nikwamba tumesikia hapa, na kamati imezungumza vizuri,kwamba exclusive economic zone ni nautical mile 200unapewa baada ya maji yako (territorial waters). LakiniTanzania kwa sababu ya mito yetu, hususan Mito ya Rufiji,Pangani, Wami; ndiyo inalisha viumbe baharibini. Kwa sababuhiyo tunastahili kupewa nautical mile 150 zaidi ndani yabahari.

Mheshimiwa Spika, sasa hiyo ni hazina kubwa ya Taifa,na ninadhani kwamba Mheshimiwa Waziri wa Uvuvi aangaliena wenzake wanaohusika hususani Waziri wa Mambo ya Nchiza Nje na Waziri wa Ardhi kwamba hatupotezi hazina hiyo,kwa sababu unapopeleka maombi Umoja wa Mataifa kunamuda usipofatilia unaweza ukaondolewa kwenye orodha.Kwa hiy ni jambo ambalo nimeona kwamba niliseme na huuni wakati wake.

Mheshimiwa Spika, tunaporidhia mkataba huu piatujue utawala wa bahari duniani na tutaweza kudhibiti huouvuvi haramu katika bahari zetu. Suala la uvuvi haramunadhani ni suala ambalo wote tunakubaliana kwamba nisuala hatari lakini pia ni suala la teknolojia na sisi kama nchiinayoendelea wakati mwingine tufaidike kwa kuombamisaada pale tunapohitaji. Kwa sababu uwezo pia wakudhibiti hizi meli kubwa, gharama inayohitajika na teknolojiainayohitajika unaweza kukuta kwamba hatuna. Tukisharidhiamkataba kama huu na sisi basi; na imesemwa na wengine;tunaweza pia kuomba msaada wa wataalamu, vifaa nafedha za kutusaidia kuhakikisha kwamba hapa kwenyebahari yetu kuu si inakuwa shamba la bibi, kwamba kila mtuanafanya anachotaka na hasa uchafuzi wa sumuzinazotupwa katika bahari yetu.

Mheshimiwa Spika, ilifikia kuna mahali pale wala siendimbali pale Kawe Beach waliwahi kutupa magunia ya sumuhatari kwa hiyo unakuta vitu kama hivi wanaendelea kwasababu hatujajua...

MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Spika, taarifa

Page 128: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

T A A R I F A

SPIKA: Ndio taarifa tafadhali Mheshimiwa Zungu

MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Spika, naombakumpa taarifa Mheshimiwa Profesa. Kwanza nimpongezekwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuhakikisha extended yacontinental shelf ya Tanzania na kupata hizo km 150. Juzi miminilikuwa umoja wa mataifa tumelifatilia hili suala tuko katikanamba 59 ya shauri la Umoja wa Mataifa na limekaa vizuri.Tatizo vikao vya Umoja wa Mataifa havikai kutokana nchiwanachama ambao wako kwenye commission i lewanatakiwa walipiwe gharama zao za kuhudhuria vikao nanchi zao kwa vile nchi zao hazilipi gharama ile commissionhaikai. Kwa kutokukaa justice delayed justice deniedtunakosa haki yetu.

Mheshimiwa Spika, vilevile Kenya nao wana shauri naSomalia na shauri lile linaweza likatuathiri kama Somaliawakishinda kutokana na mpaka kati ya Kenya na Pemba.Kwa hiyo nilitaka nimpe taarifa tu kwamba suala liko vizuriSerikali wanalifuatilia na kamati tuko karibu nao kuhakikishahaki ya Tanzania inapatikana. (Makofi)

SPIKA: Asante sana ni kweli Mheshimiwa Mwenyekitiwa Kamati ya Mambo ya Nje alikuwa UN kwenye GeneralAssembly akifatana na Waziri wa Mambo ya Nje hivi juzi tu.Mheshimiwa Profesa Tibaijuka endelea na mchango wako.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Mheshimiwa Spika,ninashukuru sana kwa Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamatiya Mambo ya Nchi za Nje na nimefarijika kusikia kwambasuala hilo linafatiliwa ni muhimu sana. Sasa nikirudi kwenyeuwezo wetu wa kutekeleza hii mikataba tukishasaini. Sisi ninchi inayoendelea, bado tuna haki ya kupata msaada wahao wenzetu waliotangulia. Kwa kweli wenyewe kwa sababuya teknolojia zao ndio wana uwezo wa kuchafua na kutumiahizi mbinu haramu ambazo zinakuwa na athari kubwa. Kwahiyo tusibaki nyuma, Mheshimiwa Waziri usibaki nyuma katikakuweka sasa ufatiliaji ambao ni chanya. Kuna ufatiliaji

Page 129: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

mwingine ni urasimu tu mtu hana vifaa atakaa anasumbuameli anaweza akaleta kero.

Mheshimiwa Spika, mimi nafikiria kwamba tufanye kazikwa weledi kwa sababu tunaposema tuweke watu wakudhibiti, je, wana uwezo wa kudhibiti? Wanakuja kufanyajuhudi au kama Mwalimu Nyerere alivyosema, kwamba nijuhudi bila maarifa. Suala hili ni muhimu sana hasa katikavyombo tunavyojiwekea kudhibiti.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili nirudi sasa kwaharaka kwenye suala la mkataba wa umeme wa jua. Umemewa solar huu na umeme wa jua ni kitu kizuri sana. Naombakusema kwamba sisi kitu kimoja kinachotukwaza kama taifalinaloendelea na kama taifa lenye vijana na vijana ambaohawana ajira ni kushindwa kuweka utaratibu kwa vijanakuunda kampuni za solar zitakazoweza kuleta teknolojiakatika nyumba na kutoa huduma.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, nirudi sasa kwaharaka kwenye suala la mkataba wa umeme wa jua. Umemewa solar huu na umeme wa jua ni kitu kizuri sana. Naombakusema kwamba lakini sisi kitu kimoja kinachotukwaza kamaTaifa linaloendelea na kama Taifa lenye vijana na vijanaambao hawana ajira ni kule kushindwa kuweka utaratibu kwavijana kuunda makampuni ya solar yatakayoweza kuletateknolojia katika majumba na kutoa huduma. KutegemeaTANESCO bila kutumia solar ni kutwanga maji kwenye kinukwa sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, nafikiri ingekuwa ni boraMheshimiwa Waziri akatueleza sasa anavyojaribu kusaidiavijana wetu hawa ambao tunawaambia wajiajiri wakati sisitumeajiriwa, lakini hatuwawekei utaratibu wa kwa mfanokuunda kampuni mahususi ambazo zitaweza kuenezaumeme wa solar; vijana wanamaliza Engineering wapo kulemijini hawana kazi.

Mheshimiwa Spika, nadhani tunaposaini mkatabakama huu ni fursa muafaka pia kuwapatia teknolojia, lakini

Page 130: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

na huduma inayotakiwa maana yake unaposambaza kitukipya kina ukakasi, ukiwaambia watu tukufungie solar yeyeanaona nyaya za TANESCO zinapita juu anaonaunamsumbua kama unamfanyia shamba la majaribio, kwahiyo mtu anataka kitu ambacho ana uzoefu nacho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukiwa na vijanaambao wanaweka makampuni ya kuhakikisha kwambayanapata soko, sasa kazi yetu nini? Kazi yetu ni halmashauri,kuweka sehemu il i ziwape masoko inaitwa publicprocurement ambayo ni lazima iwezeshe dissemination yateknolojia, teknolojia mpya haiwezi kusambaa kama hainaPublic Procurement Policy inayoi-support yaani kwamba kulekununua kwa upendeleo kabisa kampuni za vijana, ndiyotutaweza kuondokana na hii ngonjera ya umeme wa solarumeme wa solar, lakini watu hawapo tayari kuwa kwenyemajaribio, tuwawekee uwezeshaji.

Mheshimiwa Spika, huo ndiyo mchango wangu,naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa Profesa. SasaWaheshimiwa Wabunge ili twende vizuri tuwaruhusu sasaWaheshimiwa Mawaziri waweze kupitia michango yetumbalimbali na tumekubaliana kila mmoja atasoma robo saaili tuweze kumaliza asubuhi mambo yote ili jioni WaheshimiwaWabunge muweze kufanya mambo mengine muhimu zaidi.

Sasa kama tulivyowasilisha mwanzoni naombanimwite Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, MheshimiwaLuhaga Mpina ili aweze kupitia michango mbalimbali yaWaheshimiwa Wabunge na uzuri wa mambo haya mawilikwa kweli Wabunge wameunga mkono sana na wametoaushauri wa namna gani Serikali itekeleze. Mheshimiwa WaziriKaribu sana.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,nikushukuru sana kwa nafasi uliyonipa tena, lakini pianimshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge waKilimo Mifugo na Maji, lakini na Msemaji wa Kambi ya Upinzani

Page 131: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

anayesimamia masuala ya Mifugo na Uvuvi wa hotuba zaonzuri sana walizozihutubia hapa Bungeni na vile vile michangoya Waheshimiwa Wabunge wote. Nichukue nafasi hiikuwashukuru sana kwa mchango ambayo mliyoitoa na sisitumenufaika sana na michango yenu mliyoitoa.

Mheshimiwa Spika, Azimio letu hii la PSMA, bahati nzurisana Wabunge wote waliopata nafasi wameunga mkonona wametoa ushauri. Kwa ujumla kwa masaa na dakikaulizonipa, ni ngumu sana kupitia maswali ya WaheshimiwaWabunge, lakini pia na ushauri walioutoa, lakini itoshe kusemakwamba ushauri wote ambao Waheshimiwa Wabungewametupatia tumeuzingatia na utatusaidia sana katikautekelezaji wa majukumu yetu ya maeneo haya ya uvuvi wabahari kuu.

Mheshimiwa Spika, la kwanza, labda ambaloWabunge wameliongelea sana na limezungumzwa miakamingi suala la Bandari ya Uvuvi, nataka niwaambie Wabungekwamba hii Serikali ya Awamu ya Tano inaenda kutanzuahuu mtego wa miaka mingi ambao umekuwa kilio kikubwakwa Taifa. Bandari hatua ambayo tumefikia mpaka sasahivi tuliliambia Bunge lako wakati wa Bajeti kwamba,tunafanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kujenga bandari yauvuvi hapa nchini. Nataka nilitaarifu Bunge lako Tukufu kuwaMshauri Mtaalam Mwelekezi wa kampuni ya Italyamekamilisha report yake ya upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa hivi maeneoyaliyopendekezwa kwa ajili ya kuijenga hiyo bandari niBagamoyo, Kilwa Masoko na Lindi. Kwa hiyo, kati ya hayomaeneo hayo tutachagua sasa eneo imebaki sasa kwenyemaamuzi ya ku-decide kama Serikali kwamba tutajengabandari ya uvuvi kati ya maeneo haya mawili. Kama hiyohaitoshi Serikali tayari iko kwenye hatua za mwisho kabisa naSerikali ya Jamhuri ya Korea Kusini kwa ajili ya kuanza ujenziwa bandari ya uvuvi hapa nchini. Kwa hiyo ninachotakakusema kwa sasa ni kwamba kilichobaki kwa sasa hivi nimaamuzi ya bandari ijengwe wapi na baada ya hapo katikamwezi huu jambo hili litaamuliwa na mwezi unaofuata wa

Page 132: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

Desemba ni matarajio kwamba Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Koreazitasaini makubaliano tayari kwa kuanza bandari ya uvuviwa bahari kuu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili lililoulizwa, ni bandarizinazotambuliwa ni bandari zipi zinazotambuliwa sasaambazo zitahusika huu Mkataba wa PSMA. Bandarizinazotambuliwa na ambazo zimeingia na ambazo zitahusikana PSMA ni Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa, Bandari yaZanzibar, Bandari ya Mtwara na Bandari ya Tanga, hizi ndizozitakazohusika katika utekelezaji wa makubaliano yetu naMkataba wetu huu wa PSMA.

Mheshimiwa Spika, suala lingine lililozungumzwa hapana Waheshimiwa Wabunge ni suala la udhibiti wa uvuviharamu kwenye eneo la high seas kwamba hivi sasa hakunaudhibiti na hata hii PSMA tunayoazimia haifiki katika eneohilo la high seas. Nataka nitoe taarifa kwamba tayari UNwameanza kuandaa legal instruments za usimamizi zaresource katika high seas, yaani biodiversity beyond nationaljurisdiction, tayari inaandaliwa na mara hii instrumentitakapokuwa imekamilika, sasa mfumo huu wa PSMAutaenda mpaka high seas. Kwa hiyo, huu ulinzi wa rasilimaliwale waliokuwa wanafanya uvuvi haramu kwenye maeneohayo hawatapata excuse tena.

Mheshimiwa Spika, suala la marekebisho ya Sheria yaMamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1968 pamojana kanuni zake za mwaka 2007 ambazo zil ifanyiwamarekebisho mwaka 2016, hivi sasa tuko kwenye marekebishoya Sheria yenyewe pamoja na kanuni zenyewe. Katikamarekebisho hayo eneo hili la PSMA ambalo tunalozungumzalitaingizwa, lakini pia tutazingatia maombi mbalimbaliambayo yatawezesha ruhusa ya uvuvi yaani authorizationto fish kwa meli zenye bendera ya Tanzania kuweza kuvuakatika maeneo ya high seas na EEZ za nchi nyingine. Kwahiyo katika hizi kanuni ambazo kanuni na sheria ambazotunazifanyia mapitio kwa sasa na zingine zitaingia Januarikwenye Bunge lako Tukufu, tunawaahidi Waheshimiwa

Page 133: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Wabunge kwamba maboresho mengi yatakayohusika naKanuni ya uvuvi wa bahari kuu yatazingatiwa katika hayamarekebisho ambayo tunafanya kwa sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambao WaheshimiwaWabunge wamelizungumza ni suala la eneo la kitutia Mafiakwamba ni muhimu sana kwa mazalia ya samaki, lakinihalilindwi ipasavyo, nataka nitoe taarifa kwamba hili eneolinalindwa ipasavyo na liko chini la MPRU, linalindwa uvuvihauruhusiwi eneo hilo kwa sababu ni eneo ambalo linamazalia ya samaki, kwa hiyo eneo letu hili tunalilinda natunatambua umuhimu wake kwamba ni eneo mahususi sanakwa ajili ya mazalia ya samaki.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge hapawalizungumza sana na wakaomba sana kwamba hiikuondolewa kwa tozo ya dola za Kimarekani 0.4 kwa kilo yasamaki inayovuliwa na kusafirishwa nje ya nchi hasa na melihizi za foreign vehicles kutoka nje ya nchi zinazofanya uvuvikatika ukanda wetu wa uchumi wa uvuvi wa bahari kuu.Waheshimiwa Wabunge walisema na waliomba sana Serikalikwa muda iondoe tozo hii ili kuwezesha uvuvi uweze kufanyikakwa sababu meli zilizokuwa zinakuja kuvua zilishindwa kabisakuvua baada ya kuweka hii tozo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kusema kwambana kama wewenyewe walivyosema ni kweli kabisa sisi Serikalitumeridhia kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja wakatitunatafakari njia bora ya kunufaika na rasilimali zetu zilizokokatika ukanda wa bahari kuu ili tuweze kunufaika kwa hiyo,hii tozo tumeiondoa na Waheshimiwa Wabunge tayaritumeshasaini nadhani GN itatoka muda wowote, lakiniwavuvi wetu wako ni rurksa sasa hivi kuvua na kwamba 0.4haitatozwa ila watatozwa zile gharama zingine ikiwemokulipia leseni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ilikuwa ni suala lakuwekeza kikamilifu katika utafiti; ni kweli kabisa kwambahakuna mtu anayeweza kukubali ku-risk investment yakekatika eneo ambalo halina utafiti. Hakuna Taifa ambalo

Page 134: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

linaweza kuwa na mipango mizuri kama hakuna taarifa zakiutafiti za kutosha kwenye eneo husika na sisi kama Serikalitunakubaliana na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge nawamekuwa wakitushauri mara kwa mara na kwa sasatumeanza. Kwa mfano sasa hivi hii Mamlaka ya Uvuvi waBahari Kuu (DSFA), tumeshaipatia fedha kupitia Mradi waSWIOFISH. Jumla ya shilingi milioni 457.7 ambazo hizi tunaanzasasa kufanya utafiti wa kujua rasilimali zetu zilizoko katika eneola uvuvi wa bahari kuu.

Mheshimiwa Spika, tutafanya hivyo kuhakikishakwamba zipatikane taarifa zote za uhakika ambazowananchi wetu wanazitaka, wawekezaji wetu wanazitaka ilisasa tuweze kuhakikisha tunaweka mipango madhubutiyenye taarifa za uhakika za kiutafiti juu yake na sisi tunaaminikwamba tunazo resources katika eneo letu la EEZ ambazohaziko maeneo mengine yote na kwamba pia sisi katikausimamizi wa rasilimali na katika mapambano juu ya uchafuziwa bahari, pamoja na usimamizi wa uvuvi haramu tunafanyavizuri Waheshimiwa Wabunge, sisi kimataifa eneo letulinatambulika kuwa eneo ambalo bado ni clean, maeneomengi katika sehemu nyingi duniani watu wameshachafuasana mazingira, lakini maendeleo haya …

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naongeza nusu saaili tuweze kumaliza mambo yetu. Haya Mheshimiwa Wazirimalizia.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,nataka kusema kwamba nchi yetu inazidi kupata sifa kubwakimataifa katika usimamizi wa rasilimali hizi na tulivunja rekodikubwa sana tulipokamata ile meli maarufu inaitwa meli yaMagufuli, lakini baadaye majuzi, tukaja kukakamata meli yaBuhanaga One, sisemi ya Mpina, lakini hiyo ni ya BuhanagaOne. Ile meli tulipoikamata tumepata sifa kubwa sanaduniani katika kuhakikisha kutuma message kubwa sana yaulinzi wa rasilimali hizi za Taifa.

Mheshimiwa Spika, nataka niwaambie Waheshimiwatuko vizuri sana tunapongezwa kila kona kwa jinsi ambavyo

Page 135: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

tumesimama kidedea katika kuhakikisha kwamba hizirasilimali zinalindwa sana. Hivi majuzi kuna baadhi ya viongozituliwaambia wanaotaka kutumia rasilimali hizi za Taifa kujipasifa za ziada katika kuchaguliwa, kiongozi anashindwa kutajasifa zake za kuchaguliwa anaanza kuwaambia wananchiwakafanye uvuvi haramu au anaanza kusitisha zoezi la dorialinalolinda rasilimali kwamba kwa sababu hiki ni kipindi chauchaguzi. Tunazidi kusisitiza Watanzania wasimamie sheriarasilimali hizi za uvuvi zitalindwa muda wote, bila kuzingatiamajira ya mvua au ya jua, uchaguzi hauwezi kuwa namahusiano na ulinzi wa rasilimali hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kusema kwamba viongoziwote wanaohusika wahakikishe kwamba na leo tunaungamkono hili Azimio hii kubwa la dunia ambalo litaleta mchangomkubwa katika kusimamia kwa dhati hizi rasilimali tulizonazoili tuendelee kuzivua kwa uendelevu kwa leo na siku zijazo.

Mheshimiwa Spika, sitaki niende nje sana ya mudahuu ulionipa, lakini nizungumzie suala la by-catch, suala hilitunaangalia changamoto zake katika haya marekebisho yakanuni ambayo tunayazungumza ili kuweka utulivu nakuondoa malalamiko yaliyoko hivi sasa ya by-catch.

Mheshimiwa Spika, mwisho suala la ku-extend ilecontinental shelf ambayo imezungumzwa hapa, nimshukurusana Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Njeametoa ufafanuzi mzuri, lakini na Mheshimiwa aliyezungumziahoja hii naye alizungumza vizuri. Sisi kama Serikali tunaendeleakufuatilia kwa karibu kuhakikisha kwamba tunafikia hayamalengo yetu.

Mheshimiwa Spika, nalishukuru sana tena Bunge lakokatika kuunga mkono hii hoja iliyoko mbele yetu kwa sasabaada ya kusema hayo, naomba kutoa hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Mifugona Uvuvi, hoja imetolewa na imeungwa mkono.Tunakushukuru sana kwa uhitimishaji kuwa hoja hiyo.

Page 136: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Sasa Waheshimiwa Wabunge naomba niwahojikuusiana na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba waKimataifa wa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramu Kupitia Bandariza Nchi Wanachama.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na kuafikiwa)

SPIKA: Wote wameafiki. Nawashukuruni sanaWaheshimiwa Wabunge, tunakushukuru sana MheshimiwaWaziri, tunaishukuru sana Serikali kwa ujumla wake pamojana wataalam wetu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwakazi nzuri ambayo mmekuwa mkifanya. Tunawaunga mkonotuendelee na doria, habari ya kufuata sheria haina chauchaguzi wala nini na wananchi wetu wajue kabisa ili rasilimalihizi ziendelee kuwepo, lazima tufuate taratibu na sharia.Bahati mbaya ni rasilimali ambazo zikitoweka, zimetowekajumla zilizo nyingi kwa hiyo, ni lazima tuzilinde na tuungemkono taratibu tulizojiwekea, kwa sababu sheria zinapitakwenye Bunge hili hili, sasa ikionekana Mbunge unapingasheria huko mtaani kwenye jimbo lako na kadhalika ni kitucha ajabu sana. Siasa isiwe mahali pa kutia moyo wananchikatika kuharibu rasilimali zetu.

Tunawashukuruni sana, tunaamini utekelezaji waAzimio hili utakwenda vizuri na lile suala ambalo umetuambiala kwamba huenda bandari ya uvuvi ikaanza kujengwaharaka sana hivi karibuni, kati ya kule Kilwa au Bagamoyonadhani Bagamoyo labda ni Mbegani au somewhere, nijambo jema sana sana na litatusaidia sana katika kuongezamapato yetu yanayotokana na uvuvi wa bahari kuu,ahsanteni sana.

Sasa nimwite Waziri wa Nishati ili na yeye awezekuhitimisha hoja yake kwa muda usiozidi robo saa. Waziri waNishati, Mheshimiwa Dkt. Kalemani karibu sana.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nami napendanitoe shukrani kwako mwenyewe pamoja na Makatibuwanaokusaidia katika meza wakati wa kuliongoza Bunge hili

Page 137: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

Tukufu wakati wa mawasilisho Azimio hili muhimu. Niendeleekuwapongeza Waheshimiwa Wabunge na kwa kuanziaMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati ya Madini kwawasilisho lake nzuri ambalo kimsingi limeunga mkono karibukwa asilimia mia moja. Pia niwapongeze sana WaheshimiwaWabunge wote ambao wamechangia na kwa kiasi kikubwawametoa mapendekezo lakini kimsingi wameridhia kwambaAzimio hili liungwe mkono.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayomachache, yako mambo mahususi ambayo yamejitokezaambayo Waheshimiwa Wabunge wangependa kupatauhakika wa ufafanuzi wa kina. Baadhi ya mambo ambayoni ya msingi sana ambayo wananchi wangependa kusikiakutoka kwenye Bunge letu Tukufu ni utashi wa Serikali.Napenda niliambie Bunge lako Tukufu kwamba utashi waSerikali wa kutekeleza Azimio hili ni mkubwa sana na ndiyomaana mmeridhia katika kikao chako hivi leo na sisi kamaSerikali baada ya Azimio kuridhiwa na Bunge sisi ni kwendakutekeleza mara moja. Kwa hiyo utashi wa kiserikali upo,niwaondoe wasiwasi Waheshimiwa Wabunge na Watanzaniawanaotusikiliza.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na matumizi ya solar,baadhi ya vyanzo vya nishati hapa nchini ni pamoja narasilimali ya solar. Tunavyo vyanzo vingi sana vya kuzalishaumeme, kama ambavyo mnafahamu tuna vyanzo vyarasilimali gesi, tuna vyanzo vya rasilimali maji, makaa yamawe, upepo na kadhalika, lakini pia solar.

Mheshimiwa Spika, kulingana na tafiti ambazozimeshafanywa, na nimeshukuru sana baadhi yaWaheshimiwa Wabunge kutaka kujua mikakati. Mkakati wakwanza uliokwishafanyika ni kufanya utafiti wa kina na kubainiuwezo uliopo wa kuzalisha nishati ya solar. Tafiti zilizofanywampaka kuishia mwaka 2015 zinaonesha Tanzania tunawezatukazalisha umeme wa solar kufikia mpaka megawati 1,000.

Mheshimiwa Spika, na bahati nzuri sana, Tanzaniatuna potential kubwa ya mionzi ya jua. Potential tuliyonayo

Page 138: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

sisi ni kilowatt-hours 4 mpaka 7 kwa mita za mraba kwa sikuambapo kipimo cha kimataifa ni kilowatt-hours 3.97, kwa hiyotuko juu sana kwa maana ya rasilimali ya jua tuliyonayo. Lakinikatika mwaka pia Tanzania tunaweza tukapata mionzi yajua mpaka takribani ya saa 2800 mpaka saa 3500 kwa mwakakwa hiyo vyanzo vya kuzalisha umeme wa solar ni vingi.

Mheshimiwa Spika, nilitaka kutoa taarifa hiyo ilikuwapa uhakika kwamba baada ya azimio hili kupita namatarajio tuliyonayo ni kwamba Serikali tunakwendakufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwepo na umeme wa solarhapa nchini.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine limeelezwa kwambapengine ni muhimu kutekeleza mradi huu kuliko Bwawa laJulius Nyerere. Nataka niseme mkakati wa Serikali ni kuzalishaumeme mchanganyiko kwa kutumia rasilimali zote tulizonazo.Ni kweli zipo tofauti kutoka chanzo kimoja kwenda kinginelakini nataka niseme, chanzo cha kwanza kabisa kwa unafuukatika kuzalisha umeme ni umeme wa maji ambao unatumiashilingi 36 kuzalisha uniti moja ya umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na umeme wa pili unaofuata kwaunafuu ni huu umeme wa solar ambao wenyewe utazalishauniti moja kwa Shilingi ya Tanzania 103.28, kwa hiyo badonao ni wa nafuu. Lakini pamoja na hayo bado tunaona nijambo la busara kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzomchanganyiko ndiyo maana tunaendelea kuzalisha piavyanzo vingine.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunasema, pamoja namambo mengine, unapotumia umeme wa solar unakabilianakwa hatua ya juu sana na uharibifu wa mazingira, lakini piausimamizi wake nao ni mwepesi na kwa sababu vyanzotunavyo, rasilimali ya kutosha, na tumejipanga kwa ajili yakutekeleza jambo hilo tunadhani azimio hili likipitia itachangiakwa kiwango kikubwa sana kuzalisha umeme wa solar nakuingiza kwenye Gridi ya Taifa.

Page 139: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, ni kwelikwa sasa katika Gridi ya Taifa hatujaweza kuunganishaumeme wa solar ingawa tunao umeme wa off-grid katikamaeneo mtambuka nje na Gridi ya Taifa chini ya megawatttano. Kwa hiyo mkakati wetu ni kuzalisha walau megawatt1,000 za umeme wa solar nazo ziingie kwenye Gridi ya Taifa,na ni kupitia azimio hili likipitishwa na Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, na ndugu zangu WaheshimiwaWabunge, kwa hiyo ni muda mwafaka sana sasa kukubaliazimio hili ili tuingize umeme wa solar katika Gridi ya Taifa nakuchangia ipasavyo katika kujenga uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge Ruth alisematulisaini mwaka 2015, ninapenda niweke sahisho dogo tu; sisitulisaini mwezi Novemba, 2016. Hata hivyo, mikakati ambayoMheshimiwa Mbunge alipenda kuona tumechukua ni kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mkakati wa kwanza ni kuwekampango wa kuzalisha umeme wa solar kwa miaka 30 ijayoambao tumeweka walau zaidi ya megawati 1,000. Lakinimkakati wa pili ni kuendelea kutafuta fedha; napendakuishukuru sana Serikali, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020kupitia Mpango wa Umeme Vijijini, Serikali ilitenga shilingibil ioni 38 kwa aji l i ya kuwawezesha wazalishajiwadogowadogo kuzalisha umeme wa solar kwa ajili yakusambaza umeme vijijini. Hii ni hatua kubwa sana kwa Serikaliilichofanya katika hatua za kwanza za mipango mikakati yakuhakikisha kwamba rasilimali ya jua nayo inatumika kwenyekuunganishia umeme wananchi.

Mheshimiwa Spika, hatua ya pili ni kwamba badotunaendelea kupata fedha kwenye makampuni na mashirikaya kimataifa. Benki ya Dunia katika mwaka huu wa fedhapia imetoa dola milioni moja kwa ajili ya kusambaza umemevijijini. Na hii ni hatua kwa ajili ya kuwawezesha Watanzaniawadogowadogo kuweza kuzalisha umeme huu wa solar ilinao uweze kutumika katika maeneo ambako Gridi ya Taifa

Page 140: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

haijafanikiwa kupita; hii ni mikakati ambayo Serikaliinaendelea kuifanya.

Mheshimiwa Spika, mikakati mingine ambayo Serikaliinafanya katika eneo hili ni kuhakikisha kwamba wazalishajiwadogowadogo wa Tanzania, hasa binafsi nao wanashirikikatika kuzalisha umeme wa aina hii. Mwaka jana mweziOktoba tulitangaza kwa wazalishaji wadogowadogo, nahasa Watanzania, ili waanze nao kuzalisha umeme huu wasolar walau kuanzia megawati 50 mpaka megawati 250.Taratibu zinazofanyika sasa ni kukamilisha uchambuzi ilikuwapata wakandarasi wa ndani ili nao waweze kuzalishaumeme huu. Huu ni mkakati muhimu sana shirikishi ambaoWatanzania pia tunawashirikisha.

Mheshimiwa Spika, mkakati mwingine mahususi katikaeneo hil i, kama ambavyo nimeeleza, ni kuhakikishamakampuni ya Kitanzania yanashiriki. Hivi sasa – kwa kujibuswali la Mheshimiwa Profesa Tibaijuka – yako makampuni zaidiya saba ya Watanzania; yupo Lex Energy, yupo Enzora, yupoBaraka, yupo ITOZ, yupo ZOTI, yote hayo ni makampuni yaWatanzania wadogowadogo na wanashiriki katika kuzalishaumeme mdogomdogo na kusambaza kwa Watanzania. Kwahiyo, ushirikishwaji wa Watanzania uko palepale.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, bado kama Serikalitunawahamasisha Watanzania waendelee kushiriki kwakiwango kikubwa sana katika kuzalisha umeme huu wa solarili kuweka mchango mkubwa kwa ajili ya matumizi, lakinikujenga sustainability kwa Watanzania hata kwa miaka mingiijayo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo niliyosemakatika eneo hili, lakini ningependa tu kusema kwambamkakati mwingine tumetenga maeneo. Yapo maeneomahususi sana ambayo ni muhimu na yanaweza kuzalishaumeme wa jua. Baadhi ya maeneo tunayo hata hapaDodoma, eneo la Zuzu linaweza kuzalisha megawati 50mpaka 100; eneo la Kishapu kule Shinyanga, megawati 150mpaka 250; eneo la Mkwese kule Manyoni, Singida megawati

Page 141: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

100 mpaka 250 na eneo la Same kule Kilimanjaro nayoyanaweza kuzalisha umeme. Haya maeneo tumeyaainishana kuyatenga kwa ajili ya kuzalisha umeme wa solar.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, hii nibaadhi ya mikakati tu tuliyochukua kuhakikisha kwambaumeme huu unanufaisha hasa rasilimali ya ujenzi wa uchumiwa viwanda.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa manufaa;pamoja na kwamba kwa sasa tunaomba kuridhiwa, lakinikwa vile tulishasaini mkataba huu yapo manufaa ambayoSerikali ilishaanza kuyapata. Hivi sasa ninapongea wapoWatanzania ambao wameshaenda kupata ufadhili wa ISAambao wanakwenda kusoma kwa level ya PhD kwa ajili yamasuala hayahaya ya solar ili waweze kutoa mafunzo kwaWatanzania wengine. Na bado kuna nafasi ambazotutaendelea kuzipata kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa levelsza chini, kati na juu ili Watanzania wengi waweze kupataelimu hii na kuweza kuwafundisha Watanzania wengi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunaposema tutakuwana umeme mwingi hapa nchini, umeme mwingine unatakiwautokanae na huu utaratibu wa solar. Na tuna mpango huokwa sababu unapokuwa na umeme wa kutosha namchanganyiko, hata inapotokea dharura katika vyanzovingine bado unaweza kuendesha nchi bila kuwa namashaka yoyote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo utaratibu huu wa ISA hadisasa mwaka jana tulishiriki kwenye mkutano na ISA ime-commit kwa mwaka wa fedha ujao kutoa takribani Dola zaMarekani milioni 385 kwa nchi yetu, na nchi yetu imekuwa-committed pesa nyingi kuliko nchi zote duniani ambazozimeshiriki kwenye hii ISA, kwa hiyo ni mafanikio makubwaendapo Serikali yetu itaridhia.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu yaliyosemwa nimengi, itoshe tu nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwakweli kwa michango yenu mizuri, lakini Serikali imedhamiria

Page 142: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

kujenga uchumi wa viwanda kwa kutumia umememchanganyiko. Na mikakati na malengo yetu ni kufikishamegawatt 10,000 mwaka 2025 na kuwapelekea Watanzaniaumeme pote wanapokaa mijini na vijijini kwa zaidi ya asilimia85 na kupeleka Gridi ya Taifa maeneo yote ya pembe nneza nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,naafiki.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Nishati,Mheshimiwa Dkt. Kalemani. Hoja imetolewa na imeungwamkono, tunakushukuru sana kwa namna ulivyohitimisha hojayako na jinsi Wabunge walivyokuunga mkono.

Sasa Waheshimiwa Wabunge, kama ilivyo ada inabiditulifanyie uamuzi azimio hili linalohusu kuridhia kuanzishwa kwaushirikiano wa kimataifa wa Nishati ya Jua.

(Hoja Ilitolewa Iamuliwe)(Hoja Iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Azimio la Bunge la Kuridhia kuanzishwa kwa Ushirikiano waKimataifa wa Nishati ya Jua lilipitishwa na Bunge)

SPIKA: Nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge,pia nitoe shukrani kwa niaba ya Waheshimiwa Wabungewote kwa Wizara, Mheshimiwa Waziri, wasaidizi wako wotekwa jinsi mnavyohangaika na kutupatia mibadala ya vyanzovya umeme katika nchi yetu. Na leo hapa umetuletea azimiohili linalolenga zaidi katika nishati ya jua. Nishati ya jua ni nishatiya uhakika, ni nishati ambayo ni cheaper kamaalivyotuambia, ya nafuu zaidi.

Ninapenda kuwatia moyo WaheshimiwaWabungewakati kwa wakati na kuwakumbushatunapoweka majengo yetu basi ni vizuri tukawa na solar

Page 143: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

panels hata mbili tatu kwa ajili ya matumizi fulani, labdakuchemsha maji ya moto, labda ku-run television na vitukama hivyo, au kule jikoni ikatumika solar na vitu vya namnahiyo. Kwa hiyo inapunguza gharama za huu umememwingine, na kupunguza gharama ni sehemu muhimu sanaya maisha.

Pia ni aibu kwamba umeme tunaoutegemea wa Gridiya Taifa ukikatika tu basi nyumbani kwako inakuwa gizatotoro, wakati hata ukiwa na panel moja basi utapata vibalbuviwili vitatu vya kuweza kufanyia mambo mengine. Kwa hiyotuelekee huko na tuzidi kuiomba Serikali izidi kupunguza kamani kodi, kama ni nini kwenye vifaa vya umeme jua ili umemehuu uzidi kusambaa kwa Watanzania walio wengi hasa vijijini,mashambani na mahali pengine ili maisha ya watu wetuyazidi kuwa bora zaidi.

Zahanati za vijijini ambako umeme huu haujafikakwingine ziweze kutumia umeme jua, mafriji yetu yawezekutumia umeme jua. Kwa sababu unaweza ukawa umejazavitu vyako katika friji, nyama labda za wiki nzima, nyanya navitu vingine, umeme huu ukakatika tunaoutegemea kwa sikunzima kwa mfano, saa 24, maana yake ni kwamba ndani yafriji humo vitakavyolika baada ya pale ni vichache sana. Lakiniukiwa na umeme jua maana yake ni kwamba huna wasiwasiwa friji hiyo 24 hours, 24/7.

Kwa hiyo mtaona umeme jua kwa kweli una faidanyingi; ni ghali lakini Serikali izidi kuangalia na kusaidia kuonani maeneo gani ya kupunguza kidogo gharama ili tuwezekwenda pamoja.

Waheshimiwa Wabunge, nawashukuru mno kwaushirikiano kwa kuwa shughuli za leo zote zilizopangwatumeshazikamilisha kwa wakati unaotakiwa. Kwa jinsi hiyobasi kabla sijaahirisha Bunge niwakumbushe Kamati yaUongozi tukutane saa saba na nusu pale Ukumbi wa Mikutanowa Spika; saa nane kamili Kamati ya Kanuni tukutanepalepale mpaka saa kumi na mbili jioni na baada ya hapoTume ya Huduma za Bunge kwenye ukumbi huohuo. Kwa

Page 144: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA …...ya kusambaza umeme mpaka kwenye nyumba zilizopo vijijini bado litafikiwa na kazi hiyo inaendelea. Kwa bahati nzuri kazi hiyo inasimamiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

hiyo, wakati ninyi mnakwenda kidogo kubarizi sisi wenginetunaendelea na mikutano na mambo mengine mpaka saambili na nusu au zaidi kidogo usiku wa leo; kwa hiyo, shughuliza hapa sio rahisi jamani, ni ngumu kidogo zinataka uvumilivu.

Kwa jinsi hiyo, naahirisha shughuli za Bunge hadi kesho,saa tatu kamili asubuhi.

(Saa 7.08 Mchana Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Ijumaa,Tarehe 15 Novemba, 2019, Saa Tatu Asubuhi)