16
Mbiu Ya Banana TOLEO LA 32 umuhimu wa MAJi mwilini

Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

  • Upload
    others

  • View
    12

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Mbiu Ya BananaTOLEO LA 32

umuhimu wa MAJi mwilini

Page 2: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Beatha Anthon

Mhariri Mkuu, Gerald Lyimo

Mwenyekiti,

BODI YA WAHARIRI

David Damian

Mjumbe,

JobMjumbeAdrian Anthon

Mjumbe,

Natumaini kwamba wasomaji wa jarida hili mu wazima na afya tele tayari kwa kusoma yale yote mapya yaliyojiri katika Kampuni ya Banana Investments Ltd.Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuomba radhi kwa kuchukua muda mrefu kutoa jarida hili kinyume na utaratibu wetu wa kawaida, ila natumaini hamna lililoharibika kwani jarida limeboreshwa na kuongezewa Makala nyingi nzuri za kuelimisha na kuburudisha.Vilevile nampongeza Mr. Job Costantine kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe mpya wa bodi hii ya uhariri. Natumaini tutajifunza mengi kutoka kwake na atasaidia kunyanyua uhariri wa jarida hili kutoka hatua moja hadi nyingine.Baada ya kusema hayo niwakumbushe kuwa bado tunapokea Makala kwa ajili ya kuchapishwa kwenye Majarida yetu na kila Makala itakayochapishwa mwandishi atalipwa sh 15,000/= . Karibuni sana. Pia nachukua nafasi hii kuwatangazia wadau wa Banana Investments Ltd kwamba BadoKuna fursa nyingi za kufanya biashara ya bidhaa zetu, kwani ubora wake umeongezeka maradufu na bidhaa zinazokubalika, au kwenye depot zetu

Beatha AnthonyMhariri Mkuu

YA L I Y O M O MBIU YA BANANA

2 Bodi ya wahariri

3 Mwaka Mmoja wa mtambo wa etp 3 kampuni yajiimarisha kusaidia jamii 4 Mzalendo industries ltd yadhamini michezo

4 ziara ya timu ya masoko dar

5 waajiriwa wapya

6 habari picha

7 shule ya adili iko juu

7 MAMBO 7 MUHIMU KUYAJUA ILI KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA.

8 asili ya migomba

10 kazi ya chakula mwilini

10 mkurugenzi mpya wa mauzo na masoko

10 utawezaje kumudu ushindani wa kibiashara

11 NDIZI ZA KUUNGA KWA NAZI

12 UMUHIMU WA MAJI MWILINI

14 FAHAMU UMUHIMU WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KATIKA BIASHARA

A. R. OlomiMkurugenzi Mtendaji.

KUTOKA KWA MHARIRI

Salaam kwa wasomaji wote wa Mbiu ya Banana. Natumai wote ni wazima na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku vizuri. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wateja na wadau wote wa Banana Investments Ltd kwa ushirikiano mliotupatia mwaka 2015 jambo ambalo limefanya kampuni yetuk uendelea kukua na kuimarika.Mwaka 2015 ulikuani mwaka mzuri kwa kampuni kwani tulifanikiwa mambo mbali mbali ikiwepo uzinduzi wa mtambo mpya kabisa wakusafisha maji taka, tukio ambalo lilifanywa na aliyekua waziri wa sayansi na teknolojia Mh Mbarawa Manake. Pia kampuni iliteuliwa kwenye Top 100 mid-sized company kutokana na ukuaji wake.Mwaka 2016 kampuni imepanga kuimarisha bidhaa zetu na usambazaji ili kuhakikisha wateja wanapata huduma iliyo bora na kwa wakatiNawatakia mafanikio mema.

HOJA YA MKURUGENZI

Page 3: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Mwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa ya Arusha. Mtambo huu umekuwa msaada mkubwa katika ufanisi wa kampuni wa kushughulikia maji machafu kutoka utaratibu wa zamani wa kutumia mabwawa, na hivyo umeboresha sana uhifadhi wa mazingira Mtambo huu umejengwa kwa ushirikiano kwa msaada mkubwa wa ushauri kutoka chuo kikauu cha Dar es salaam na Chuo kikuu cha Nelson Mandela ulizunduliwa rasmi na waziri wa Sayansi na Teknologia wakati huo Mbarawa mnamo tarehe …………. Mradi huu wa aina yake hapa nchini umevuta watu wengi kutembelea na kujionea namna mtambo huu unavyofanya kazi. Wageni wengi wamekua ni wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi na hata wataalamu kutoka makapuni mengine yanayozalisha maji machafu ambao wanadhamiria kujenga mitambo ya namna hiyo kwenye viwanda vyao.Maji yaliyosafishwa kutoka kwenye mtambo huu yanatumika kunyeshea

bustani za kampuni na pia za majirani. Manufaa mengine yatokanayo na mtambo huu wakati wa kusafisha maji ni pamoja na mbolea na gesi asilia, ambayo inatumika kuendesha mitambo ya mvuke (boiler) ya kampuni., na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya boiler hivyo kupunguza garama za uendeshaji kwa ujumla.Kampuni inajivunia kwa kuwa na mtambo huu wa kisasa ambaoni mfano wa kuigwa na viwanda vingine kwa utunzaji wa mazingira

MWAKA MMOJA BAADA YA UFUNGUZI WA MTAMBO WA KUSAFISHA MAJI MACHAFU KATIKA KAMPUNI

Kampuni ya Banana Investments inatekeleza shughuli mbalimbali za kutegemeza jamii kama sehemu ya wajibu wake katika jamii (Corporate Social responsibility CRS. ) Kupitia utaratibu huu kampuni inashirikiana na shirika la Themisimba Old Age Trust (TOAT) kwa uratibu wa ofisi ya kata ya Oloirien, jirani na ilipo kampuni ya Banana Investments Ltd,ambapo hutoa shs 10,000 kila mwezi kwa kila mzee kwa wazee 10. Malipo haya huwasaidia wazee hawa kupunguza kidogo ukali wa maisha . Wazee walengwa ni wale wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na kipato wala wategemezi.Kama sehemu ya mpango huu tunatarajiakusajili watu wa kujitolea kuwasadia wazee kwa ushauri, kufuatilia matibabu ya bure katika hosipitali za

serikali, na kuwapatia mahitaji mbalimbali kama vile nguo na chakula kutoka kwa wahisani, kadiri ya upatikanaji wa misaada.

Kupitia mpango huu tunatarajia kuona jamii na serikali katika ngazi mbalimbali inajitokeza kuanzisha na kukuza huduma kwa wazee, tukianza kidogo kidogo kujenga uzoefu na uwezo.Tunakaribisha wadau mbalimbali kushirikiana na sisi katika kukuza huduma hii iwafikie wahitaji wengi zaidi kuliko hawa 10 wanaonufaika kwa sasa. Mtendaji wa kata ya Oloirien atatoa maelekezo stahiki kwa wale wanaohitaji kuuelewa zaidi mpango huu na hata kuwa wadau.

K A M P U N I YA I M A R I S H A MPANGO WA KUSAIDIA JAMII.

BEATHA ANTHONYIMEANDALIWA NA:

IMEANDALIWA NA: BEATHA ANTHONY

Page 4: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Timu ya mauzo na masoko kutoka Arusha (Makao Makuu), ilienda Dar es salaam kwaajili ya kuwatembelea wateja Mbalimbali wa kinywajicha Raha. Wateja wa Dar es salaam waliwapokea vizuri timu ya masoko kutoka Arusha. Timu ya Masoko kutoka Arusha ilifurahia mapokezi mazuri kutoka kwa wateja wa Dar es Salaam kwani uliwatia moyo sana hasa kwa jinsi walivyokipokea kinywaji cha Raha.Timu ya Masoko kutoka makao makuu iliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kama Mbagala, Ubungo, Ilala, Mwenge, Sinza, Kijichi, Tandika n.k, ila pia timu ya masoko ilifanikiwa kwenda maeneo ya nje ya mji kama vile Vikindu, Yombo, Mji mwema, Kawe nk

Timu ya wanamasoko ilifanikiwa kwenda mikoa pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam kama Pwani (Msata, Kibaha etc), Lindi na Mtwara, ambapo wanamasoko wa Arusha walifanikiwa kwenda kuangalia fursambalimbali za biashara zilizopo katika mikoa ya kusini ya Tanzania. Ziara hiyo ya kimasoko iliwapa fursa ya kujua mahitaji ya wateja ili kupatia ufumbuzi changamoto zao. Tunawaahidi wote huduma iliyotukuka kwa maana ya kuwapatia huduma ya bidhaa zetu za Raha, Raha Poa na pombe kali ya Fiesta.

ZIARA YA TIMU YA MAUZO DAR

Mzalendo Industries Company Ltd (MZACO) ni kampuni inayotengeneza maji ya kunywa ya Mzalendo na kusambaza kinywaji cha kutia nguvu cha Atomic Energy. Kampuni inazalisha maji kwa ujazo wa nusu lita, lita moja na nusu, lita 5, lita 10, na lita 20 .Kampuni hii inathamini michezo kwa kujua kuwa inajenga, afya, urafiki na pia ni ajira. Katika mbio za Kilimanjaro marathon zilizofanyika mjini Moshi tarehe 28 Februari wafanayakazi 29 wa kampuni walishiriki mbio hizo.Ili kuenzi na kuendeleza michezo kampuni imedhamini mchezo wa squash uliofanyika tarehe 31 Januari katika viwanja vya AICC Kijenge jijini Arusha. Wachezaji 16 kutoka timu hiyo walishiriki ambapo washindi wa kwanza hadi wa nne walipewa tuzo mbalimbali.Mshindi wa kwanza alikuwa Musa Juma, , wa pili alikuwaNoah Marijani, wa tatu alikuwa Agaeli Lucas, na wanne Linderman Lekei. Captain Mushi alipewa tuzo ya kuwa mshiriki mwenye umri mkubwa kuliko wachezaji wengine.Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mzalendo Industries Co ,Bwana Adolf Olomi alikuwa mmoja wa wachezaji katika mashindano hayo.Mchezo wa squash unachezwa kwa kasi inayosababisha mchezaji kutokwa na jasho sana, hivyowashiriki walipata fursa ya kuburudika na maji ya kunywa ya Mzalendo.Kampuni pia imedhamini maandalizi ya uanzishwaji wa timu ya Arusha City Sports Club inayoratibiwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha

MZALENDO INDUSTRIES LTD YADHAMINI MICHEZO

Afisa Masoko wa Mzalendo Industries JobConstantine akiwakabidhi vifaa vya michezo wawakilishi wa Arusha City Sports Club (ACSC)

Imeandaliwa na: Job Constantine

Imeandaliwa na: Job Constantine

Page 5: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

WAAJIRIWA WAPYAKELVIN MARANDUMKAGUZI MSAIDIZI Ana Shahada ya Uhasibu kutoka chuo kikuu cha IFM cha Dar - es - salaam

HASHIMU SHABANI AFISA MASOKO MSAIDIZI

Ana astashahada ya Masoko na mauzo kutoka chuo cha Keyfield

ROGASIAN MOSHIAFISA STOO MSAIDIZI

Ana Stashahada ya Procurement & Supplies kutoka chuo cha TIA

LESSION LUKUMAYSUPPLIES MANAGERAna masters ya Ugavi na manunuzi kutoka chuo cha IAA cha Arusha na ana uzoefu wa miaka mitano

ERNEST MKANIAFISA STOOAna Stashahada ya Uhasibu kutoka chuo cha St. Stephano Moshi Memorial University na uzoefu wa mwaka 1

STANLEY MASSAWEAFISA MASOKO

Mhitimu wa kidato cha nne pia ana cheti cha udereva

PETER I. KIMAROMKAGUZI MSAIDIZIAna Shahada ya Uhasibu kutoka chuo kikuu cha IAA cha Arusha na uzoefuwa mwaka mmoja

GREGORY VENANCEDEREVA FOLK WA LIFT

Ana Astashahada ya folk lift operators ya chuo cha Bandari na ana uzoefu wa mwaka mmoja

DIDAS MAKYAODEREVA MAUZOAna cheti cha udereva kutoka Morden Driving na pia cheti cha ufundi magari cha Veta

FRANCIS GODFREYMWAKILISHI WA MAUZO

Ana Stashahada ya Usimamizi wa biashara kutoka chuo St. John

DEI AMANDIMDHIBITI UBORA

Ana Shahada ya Sayansi ya Chakula na ana uzoefu wa mwaka mmoja

Page 6: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Waziri wa sayansi na teknolojia Mh. Makame M. Mbarawa wa pili kulia wakati akikagua mradi wa kuzalisha gesi (ETP) uliojengwa kwenye kampuni ya Banana Investment Ltd. Wakwanza toka kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Banana Investments Mh. Adolf R. Olomi.

Mh. Waziri akipata maelezo kuhusu mradi wa gesi ETP alipotembelea kwa ajili ya kuuzindua rasmi.

Kikundi cha sarakasi wakitumbuiza wageni waalikwa wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa gesi.

Hiki ni kibao kinachoonyehsa maelezo mbalimbali kuhusu mradi wa gesi kinavyoonekana baada ya uzinduzi kufanywa na Mh. Makame M. Mbarawa waziri wa sayansi na teknolojia.

Mh. Waziri wa pili kulia na Mkurugenzi mtendaji wa Banana Investment wa tatu kulia katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali baada ya kukamilisha zoezi la kuzindua rasmi mradi wa gesi wa ETP.

HABARI PICHA

Page 7: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Shule ya sekondari ya Adili ipo katika Mtaa wa Laizer,kata ya Moshono,wilaya ya Arusha kusini Mashariki mwa jiji la Arusha. Shule ya sekondari ya Adili ni matokeo ya uthubutu baina ya wanataaluma wa hali ya juu,viongozi wa dini na wakereketwa wa elimu wenye lengo moja la kujenga na kuendesha sekondari ya wavulana yenye viwango. Shule ya sekondari Adili imeinuka kidedea katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015, ambapo wanafunzi 27 walifanya mtihani wa kidato cha nne. Katika mtihani huo, wanafunzi 5 walipata daraja la kwanza(Div 1), wanafunzi 13 daraja la pili(Div 2), wanafunzi 8 daraja la tatu(Div 3) na mwanafunzi 1 daraja la nne(Div 4).Matokeo hayoyameweza kuifanya shule ya Adili kushika nafasi ya 8 katika mkoa wa Arusha kwa shule zenye wanafunzi chini ya 25 na kushika nafasi ya 59 kitaifa ambapo imeweza kuwashangaza watu wengi katika matokeo hayo. Mkuu wa shule hiyo bwana Andrew Shayo amesema mafanikio hayo yametokana na walimu wajuzi na wenye uzoefu wa kutosha, mazingira rafiki kwa wanafunzi (mazingira tulivu)na chakula kizuri, maadili na nidhamu ya walimu

na wafanyakazi. Maadili na kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi ni moja ya malengo ya shule juu ya malengo ya kawaida ya kuongoza katika taaluma. Maadili ni moja ya masomo yanayofundishwa shuleni. Pia Shule ya Adili inazana nzuri za kufundishia kama Maktaba nzuri, Maabara na madarasa ya kisasa. Kwa mwaka wa 2016 shule ya Adili inanafasi chache za kidato cha kwanza, cha pili na cha tatu kwa wanafunzi wanaohamia. Pia inakaribisha wanaotaka kujiunga kidato cha tano michepuo ya PCM, PCB, CBG, PGM, ECA na EGM kwa wanaotafuta shule nzuri kwaajili ya kidato cha tano.

SHULE YA ADILI IKO JUU

ADILI HIGH SCHOOL (MOSHONO)

Page 8: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

PREMIUM QUALITY BRANDY

Uza kile wateja wako wanataka: Usiangazie tu kile unachotaka. Usipotafakari kuhusu wa-teja wako,kuna uwezo wa kutonunua bidhaa yako. Hakiki-sha unatafiti soko ili kujua kama huduma au bidhaa yako ni ya maana na nafuu kwa uwezo wa wateja.

Andika mpango wa biashara: Hii ni njia moja ya kuwavutia wawekezaji na watoa hudu-ma za kifedha kwa biashara yako. Mpango mzuri wa bi-ashara pia hukusaidia kuweka rekodi zilizo na maelezo zaidi kuhusu ruwaza na malengo yako. Andika mpango wa biashara.

Ujue uwezo wako: Angazia sana sana yale unayoyafanya vizuri na uache mengine. Hustahili kujua majibu yote wala kukusan-ya maswali yote .Kuwa mwaminifu kwa yale unayoweza kutekeleza na yale usiyomudu kutekeleza. Kumbuka, ni vizuri kuomba msaada iwapo hujui kitu fulani.

Fanya utafiti wako: Tumia madarasa, hafla au semina, vitabu na kanda ili kuji-funza yale unayoweza kabla hujaanza biashara.Kama hu-jui chochote kuhusu uendeshaji wa biashiara, kuna ma-funzo mengine ya malipo ya chini, vitabu na kanda.Jaribu maktaba ya mahali pale unapoishi ama hifadhi ya vitabu,

na uulize yale yote usiyoyafahamu kuhusu soko, nguvu na uwezo wako, mahali halisi na yale watu wanataka.

Tegemea juhudi zako: Unahitaji kuwa macho katika bajeti yako, la sivyo, utaishia katika madeni makubwa ama utoweke kutoka biasharani haraka sana. Kama huwezi kupata kila kitu unachokihitaji sasa hivi, achana nacho na ufikirie zaidi kuhusu mpango wako.

Unda mpango wa mauzo: Hili ndilo swala nyeti la kuwavutia wateja wako. Toa rama-ni ya jinsi ya kupata wateja wa kutumia bidhaa au hudu-ma yako na namna utakavyowashawishi warejee. Unasta-hili kujiuza ili watu wakujue.

Huwezi kushughulikia biashara peke yako: Unapokuwa na watu wengi wa kukusaidia na vitu “vi-dogovidogo”,ndivyo utakavyochukua muda mwingi kun-awiri biashara yako. Usiogope kuomba usaidizi na ushau-ri kutoka kwa rafiki zako na hata watu wa familia.

MAMBO 7 MUHIMU KUYAJUA ILI KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA.

IMEANDALIWA NA: STEVEN MVUNGI

Page 9: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kwa jina la kisayansi kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano. Zao la migomba ni ndizi amabazo ndiyo malighafi kuu katika uzalishaji wa kinywaji cha Raha.

Hapa Tanzania mikoa inayoshughulika na kilimo cha migomba na kuzalisha zao la

ndizi kwa wingi ni pamoja na Kilimanjaro, Kagera, Mbeya, Arusha, Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Kigoma, na Pwani. Hata hivyo zao hili linaendelea kuenea katika mikoa mingine nchini ikiwa ni pamoja na Dar es salaam,, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga ,Lindi, Dodoma na Singida.Kilimo cha migomba kinaweza kufanyika katika kipindi chote cha mwaka kulingana na kiasi na mtawanyiko wa mvua hasa mabondeni au kwa umwagiliaji.Pia zao la ndizi hutumika kuzalishia kinywaji cha Raha ambacho kimekuwa maarufu hapa nchini kwa sasa. Kutokana na matumizi haya zao la ndizi

limeongezewa thamani na kumnufaisha mkulima. Pia matumizi haya yamesaidia kuongeza pato la taifa na hivyo kuharakisha maendelea ya nchi.

ASILI YA MIGOMBA

PREMIUM QUALITY BRANDY

IMEANDALIWA NA: DAVID DAMIAN

Page 10: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Kampuni imemuajiri mkurugenzi wa mauzo na masoko Bw. Reginald Mosha, Ili kuhakikisha wateja wanapata huduma za haraka na uhakika.Bw Reginald Mosha ana shahada (degree) ya biashara na masoko kutoka chuo kikuu cha Mzumbe na shahada ya uzamili (Masters’ Degree) kutoka chuo cha ESAMI pamoja na uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika kazi hii. Uongozi wa kampuni unamkaribisha sana kwenye familia ya wafanyakazi wa Banana Investment Ltd.

MKURUGENZI MPYA W A M A U Z O N A M A S O K O

KAZI YA CHAKULA MWILINI

Mwili wa binadamu unahitaji nishati-lishe na virutubisho mbalimbali ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi. Nishati-lishe (nguvu) na virutubisho hivyo vinatokana na

chakula tunachokula.Chakula kinapoliwa hupitia hatua mbalimbali katika mfumo wa chakula ikiwa ni pamoja na kuyeyushwa na hatimaye virutubisho kufyonzwa na kupelekwa sehemu mbalimbali za mwili. Katika hatua zote vichocheo na vimengenyo mbalimbali huhitajikaBAADHI YA KAZI MUHIMU ZA CHAKULA MWILINI1. Kutumika katika kutengeneza seli za mwili na kukarabati seli zilizoharibika au kuchakaa.2. Kusaidia katika ukuaji wa mwili au ustawisho wa akili.3. Kuupa mwili nguvu, joto, na uwezo wa kufanya kazi.4. Kuupa kinga dhidi ya maradhi mbalimbali.5. Kutengeneza vichocheo na vimeng’enyo mwilini .6. Kusaidia katika utengenezaji wa maziwa ya mama.

IMEANDALIWA NA: E.M. MASSAWE

Kama unaendesha biashara ndogo, au unaendesha biashara mpya ambayo tayari kuna watu wengine ambao wanaifanya biashara hii kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe, basi una njia nyembamba sana ya kuweza kufanikiwa.Ukweli ni kwamba hawa waliopo kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe wana nafasi kubwa sana kiushindani kuliko wewe. Wanaweza kutumia fedha nyingi kwenye matangazo wewe huwezi. Wanaweza kutoa zawadi nyingi kwa wateja wewe huwezi.

unamjua mteja wako kama rafiki yako. Tengeneza urafiki mzuri kati yako na wateja wako na itakusaidia sana kufanikiwa.Kumbuka unafanya haya yote sio kwa ajili ya kushindana na biashara kubwa, ila kwa ajili ya kuwa bora sana kuliko mtu mwingine yeyote anayefanya biashara hiyo.Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kwa vyovyote vile kuingia kwenye biashara ambayo kuna watu wachache wameitawala inaweza kuonekana ni kama kujiingiza kwenye shimo la simba. Lakini leo nataka nikupe siri moja ambayo itakuwezesha kufanikiwa kwenye biashara hata kama mshindani wako ni mkubwa kiasi gani.Kwanza kabisa ni lazima ukubali kwamba huwezi kumzidi mshindani wako huyo kwa matumizi ya fedha, huwezi na sahau kuhusu hilo. Ila unaweza kumzidi kwa vitu muhimu sana. Unaweza kumzidi kwa kazi, unaweza kumzidi kwa ubunifu na unaweza kumzidi kwa huduma bora sana kwa wateja wako.Fanya kazi mara mbili ya wanavyofanya watu wengine waliopo kwenye biashara hiyo. Ndiyo nimesema mara mbili. Kama wenzako wanaanza kazi saa mbili na kufunga saa kumi, wewe anza saa kumi na mbili na funga saa mbili usiku. Hakikisha unakuwa mbele sana kwenye kazi unayofanya kwenye biashara yako.Kuwa mbunifu sana, tatizo la biashara kubwa ni kwamba hawapo tayari kubadili vitu haraka. Ila wewe mwenye biashara ndogo unaweza kubadili kitu chochote kwa haraka sana. Tumia nafasi hii kujaribu kila aina ya ubunifu ili kutoa kilicho bora kwa wateja wako.Toa huduma bora sana kwa wateja wako. Kadiri biashara inavyokua ndivyo huduma kwa wateja inazidi kuwa mbovu. Sasa wewe wa biashara ndogo hakikisha

Utawezaje kumudu Ushindani…

IMEANDALIWA NA: PETER MAPUNDA

Page 11: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Mapishi ya ndizi ni marahisi sana kwa kupika, hasa kwenye maandalizi yake, ambayo ina-chukua kama ifuatavyo;Kuan-daa: dakika 10, Mapishi: dakika 20, Ujuzi: Rahisi, Gharama: Nafuu.Kuna aina tofauti za ndizi – malindi, mkono wa tembo, bukoba, na nyingine kibao. Haya mapishi unaweza kupika aina yeyote ya hizo ndizi, ili mradi tu ziwe hazijaiva. Uwepo wa nazi kwenye hiki chakula unahakikisha uhalisia wa ladha na utamu wa kipekee. Unaweza kula hizi ndizi kama kitafun-wa cha chai, chakula kamili au chakula kiambato ukiwa na chakula kingine mfano wali, tambi au ugali.

Mahitaji ya Walaji: 2 • Ndizi mbichi 6• Nazi 1• Vitunguu 2• Pilipili hoho 1• Karoti 2

• Nyanya 3• Chumvi kijiko 1 kikub-waMaelekezo• Menya ndizi kisha zi-weke kwenye maji. Hii inasaidia kutopata weusi na utomvu un-aotokana na kutokuwa kwenye maji. Kisha osha ndizi zako na uweke tena kwenye chombo chenye maji mengi.• Menya vitunguu na ki-sha katakata vipande vidogo.• Kata pilipili hoho, menya nyanya uzikate vipande.• Kata karoti na nyingine kwangua maganda.• Andaa nazi kwa kuiku-na na kukamua tui 2 – moja tui zito weka kwenye chombo pembeni na tui jepesi kwenye chombo tofauti.• Bandika chungu au su-furia ya kupikia jikoni. Ongeza tui zito kidogo, acha lichemke mpaka litoe mafuta.• Tui likishatoa mafuta, weka vitunguu vyako mpaka

vikaribie kuiva halafu ongeza pilipili hoho, Koroga kiasi hala-fu weka karoti. Endelea kukoro-ga mchanganyiko kwa dakika 2 halafu ongeza nyanya kwenye sufuria. Ongeza chumvi na ki-sha funika sufuria na mfuniko hadi nyanya ziive (takribani dakika 5 hadi 8).• Nyanya zikiiva, ongeza ndizi kwenye sufuria yenye viungo. Endelea kukoroga.• Ongeza tui jepesi kwenye sufuria yenye ndizi huku unaendelea koroga ili tui lisikatike.• Ikishachemka, ongeza na kupunguza tui, ongeza tui zito huku ukiendelea koroga mpaka lichemke.• Acha mchanganyiko uchemke kwa takribani dakika 10 ili tui liive.• Ndizi zako zitakua zi-meiva.Furahia chakula chako

NDIZI ZA KUUNGA NA NAZI

Page 12: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza watu kunywa maji mara kwa mara, lakini wengi wamekuwa wakichanganyikiwa juu ya kiwango wanachopaswa kunywa na ni kwa namna gani.Maji huunda zaidi ya theluthi mbili ya miili yetu, lakini wengi wetu huacha kunywa maji na kunywa vinywaji vingine tukisahau kunywa maji ya kutosha.Takwimu zinaonyesha kuwa mwili wa mwanadamu umejengwa kwa asilimia kati ya 55 na 75 za maji na watu wembamba wana kiasi kikubwa cha maji mwilini kuliko wanene.Asilimia 60 ya uzito wako ni maji na mifumo ya mwili wako hutegemea maji ili kufanya kazi zake kwa ufanisi. Unapoanza kuhisi kiu, mwili unakuwa umepungukiwa na maji. Hata katika upungufu mdogo wa maji mwilini, wakati na asilimia moja hadi mbili ya uzito wa mwili inapungua, suala hilo humfanya mtu akose nguvu na ajisikie amechoka.Mwili unahitaji kwa kiasi kikubwa maji ili kufanya kazi zake vema. Kwa mfano, mapafu yako yanahitaji vikombe viwili vya maji hadi vinne kila siku ili kufanikisha kazi yake ya upumuaji kwa ufanisi. Na kiasi hicho huhitajika zaidi wakati wa baridi. Kunywa glasi nane za maji zenye ujazo wa mililita 237 au robo lita kila siku ndio kiwango ambacho kipo akilini

mwa wengi, wote wakiwa na imani kwamba ndicho kiwango kinachokubalika kiafya.‘’Ukweli ni kwamba kiwango cha maji ambacho unachopaswa kunywa kinategemeana na mtu na mtu,” anasema Dk Robert Huggins wa Chuo Kikuu cha Connecticut na kuongeza:“Mahitaji ya maji yanatofautiana kati ya mtu na mtu. Mambo kama jinsia, hali ya hewa, kiwango cha joto la mwili, ushiriki wa mazoezi, aina ya kazi, umri na aina ya mlo unaokula ni mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa”. Faida ya maji mwiliniMaji yana faida nyingi katika mwili ikiwa ni pamoja na kusaidia umeng’enyaji wa chakula, huboresha hali ya viungo na misuli, maji yanaweka ubongo katika hali nzuri zaidi ya ufanisi zaidi hivyo kunywa maji ya kutosha kunamuwezesha mtu kufikiria vyema zaidi, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa kama mafua na kusaidia kupona haraka ugonjwa huo, mawe ya figo, matatizo ya ini, baadhi ya saratani na magonjwa mengine.Ikiwa unataka kupunguza unene na uzito, maji yanaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki na kufanya mwili kutumia nishati nyingi zaidi, hivyo kupunguza kiasi cha

nishati kitakachohifadhiwa mwilini katika hali ya mafuta hivyo kupunguza unene na uzito kiujumla. Dalili za kupungukiwa maji mwiliniUnapopungukiwa maji mwilini, mwili huwa katika kiwango cha chini kuliko kinachotakiwa kwa mwili kufanya kazi vizuri. Ishara kuu nne zinazoonyesha mwili wako umepungukiwa maji ni: UchovuKuna vitu vingi vinavyosababisha uchovu, lakini ukihisi uchovu wakati wa mchana inaweza kuwa kwa sababu unakunywa vinywaji vyenye kafeini kama kahawa bila kunywa maji ya kutosha. Kitu cha kwanza unapoamka asubuhi kunywa maji ya uvuguvugu kwa kuwa husaidia kukuchangamsha vizuri kuliko kahawa, yatachangamsha ini na mfumo wa umeng’enyaji wa chakula. Kuvimbiwa na kukosa choo au kupata choo kigumuMaji husaidia kulainisha njia ya utumbo, husaidia kuweka unyevunyevu ndani ya utumbo. Usipotumia maji ya kutosha, unajiweka katika hatari ya utendaji mbaya wa mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kusababisha kuvimbiwa, kukosa choo au kupata choo kigumu.

Ngozi kavuIkiwa wewe ni mkavu kwa nje kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mkavu ndani ya mwili pia. Usitumie losheni na krimu kufunika tatizo, badala yake jitahidi kunywa maji ya kutosha. Kuumwa kichwaKichwa kuuma ni kiashiria kwamba unahitaji maji, hivyo unapoumwa kichwa jitahidi kunywa maji.Dalili zingine ni kuhisi kiu, mdomo kukauka, kukosa mkojo au kiasi cha mkojo kuwa kidogo na wakati mwingine kuwa na rangi iliyokolea sana na harufu kali, udhaifu wa misuli na kuhisi kizunguzungu. Kunywa kiwango sahihi cha majiNjia bora ya kuupa mwili maji ya kutosha ni kutii kiu yako kila unaposikia kiu inabidi unywe maji ya kutosha. Njia nyingine ni kuchunguza mkojo wako kwa makini kuanzia rangi na harufu yake, ikiwa una rangi nzito na harufu kali hii ina maana mwili hauna maji ya kutosha.Kwa wale wanaofanya mazoezi, Dk Huggins anasema; “Watu wengi hupoteza kati ya lita moja na mbili za jasho kila saa moja la mazoezi ya kawaida. Hivyo mtu anapaswa kurudishia maji yaliyopotea kupitia jasho ingawa kuhisi kiu bado ndiyo mwongozo wa kunywa maji.

UMUHIMU WA MAJI MWILINI

IMEANDALIWA NA: DAVID DAMIAN

Page 13: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa
Page 14: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Mawasiliano yana mchango mkubwa sana katika ukuaji na uendelezaji wa biashara. Hii inatokana na kwamba mawasiliano hutumika katika maeneo mengi hususani kwenye shughuli za kibiashara za kila siku. Kutokana na ukuaji wa teknolojia matumizi ya simu za mkononi na mtandao wa intaneti vimekuwa ni msaada mkubwa katika kuwafikia wateja wengi na wadau mbalimbali wa biashara kwa muda mfupi. Matumizi sahihi ya teknolojia ya mawasiliano yanasaidia ufanisi wa biashara. Makala hii inaeleza kwa undani maeneo muhimu na ni namna gani unaweza kutumia fursa hii kabambe na ya pekee ili kuongeza tija kwenye biashara yako.

Masoko. Huu ni moyo wa biashara yoyote kwasababu ukuaji wa biashara unategemea soko kwa kiasi kikubwa. Kutokana na ukuaji wa teknolojia wafanyabiashara wengi wanatafuta masoko kupitia teknolojia ya mawasiliano kama vile mitandao ya kijamii mfano whatsapp, facebook , linkedin na instagram ambapo kufanya matangazo ya bishara ni bure au ni kwa bei nafuu. Pia kama mfanyabiashara unaweza kuuza bidhaa au huduma mtandaoni ambapo unaweka bidhaa yako mtandaoni pamoja na taarifa zote muhimu kama bei, mawasiliano na namna gani mteja anaweza kuipata bidhaa au huduma yako. Hivyo kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano sio lazima wateja waje sehemu yako ya biashara ili waweze kupata bidhaa au huduma kutoka kwako, mfano mzuri wa biashara za mtandaoni ni kama vile kupitia maduka ya mtandaoni kama kaymuu, ebay na alibaba ambapo mteja anaweza kuagiza kitu kutokea popote pale duniani na akapata hiyo bidhaa.

Njia hii inasaidia kupata wateja wengi hivyo kuongeza mauzo na hatimaye kukuza biashara yako.

Utunzaji wa kumbukumbu. Wahenga wanasema, ’’mali bila daftari hupotea bila habari’’. Msemo huu unaonesha umuhimu wa kutunza kumbukumbu ndani ya biashara kwa kuwa utunzaji wa kumbumbuku unakusaidia kuona mwenendo wa bishara yako na kulipia malipo mbalimbali ikiwemo kodi ya mapato ya serikali. Kutokana na ukuaji wa teknolojia utunzaji wa kumbukumbu za biashara umerahisishwa kwani unaweza kufanyika kupitia mfumo maalumu wa kidigitali (Record Keeping software) ambao unamsaidia mjasiriamali kutunza kumbukumbu za biashara yake kwa haraka na kiurahisi. Mfumo huu unaotumia kompyuta ni rahisi na salama kabisa. Pia mfanyabiashara anaweza kutunza kumbukumbu kwa kutumia mashine za utoaji stakabadhi za kielektroniki (Electronic Fiscal Device) ambapo mjasiriamali anapaswa kuitumia kuwapatia risiti wateja wake na kwa kufanya hivyo kumbukumbu zinajitunza kwenye mashine na inakua ni rahisi kulipa kodi ya serikali kwasababu taarifa zitakazopatikana ndani ya mashine zinatumika kukadiria mapato kwa ajili ya kulipia kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa. Hii pia inasaidia kuepuka gharama zisizo za msingi zinazoweza kusababishwa na makosa ya kihesabu.

Manunuzi. Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano una mchango mkubwa sana katika kufanya manunuzi ya malighafi kwa mjasiriamali na hata manunuzi ya bidhaa kwa wateja. Mfano mzuri wa manununzi kupitia mitandaoni ni uwepo wa maduka ya mitandaoni kama vile kivuko , ebay na alibaba haya yote ni mfano wa maduka

machache ambayo yapo kwenye mtandao. Uwepo wa huduma hii unarahisisha ufanyikaji wa manunuzi kupitia mtandao. Hivyo unaweza kuwasiliana na wagavi na hatimaye kupata malighafi bila wewe kusafiri. Aina hii ya manunuzi imeshamiri sana katika biashara ya kisasa. Inasaidia kuokoa gharama za kifedha na muda pia. Huduma kwa wateja. Utoaji wa huduma bora kwa wateja umeboreshwa kwa kiasi kikubwa. Hii imetokana na urahisishwaji wa mawasiliano baina ya mfanyabiashara na mteja ambapo imekuwa ni rahisi kufuatilia kama bidhaa imemfikia mteja na kupata mrejesho kutoka kwa mteja baada ya matumizi ya bidhaa na kujua kama kuna maboresho yoyote yanayohitajika. Vilevile matumizi ya teknolojia ya mawasiliano na habari imefanya kuwepo kwa mahusiano ya karibu kati ya mfanyabiashara na mteja kwani imekuwa ni rahisi kufanya mawasiliano. Hata kama mteja akiwa mbali na biashara ilipo uwezekano wa kufanya mawasiliano umekuwa ni mkubwa sana na kwa gharama nafuu zaidi.

Pamoja na hayo imeonekana kuwa wajasiriamali wengi wanashindwa kutumia fursa hizi kwa sababu mbalimbali. Baadhi wanakumbana na changamoto ya matumizi ya vifaa vya Teknolojia ya mawasiliano kama vile simu za kisasa na kompyuta, huku wengine wanaofahamu matumizi yake wanachukulia kama gharama na upotevu wa muda hivyo kutupilia mbali fursa hii. Hata hivyo ukweli utabaki kuwa ukweli kwamba teknolojia ya habari ni mkombozi na wale wanaotumia teknolojia hii wanaendelea kuonyesha utofauti na kuwa mfano bora katika soko. Hivyo basi ni vizuri kila mjasiriamali anayetaka kufanikiwa aweze kuchukua hatua inayostahili ili kuboresha huduma kwa wateja, kudhibiti gharama na kuleta mabadiliko katika biashara na soko kwa ujumla.

Fahamu Umuhimu wa Teknolojia Ya Mawasiliano Katika Biashara.

IMEANDALIWA NA: DAVID DAMIAN

Page 15: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa
Page 16: Mbiu Ya BananaMwaka 2015 kampuni ya Banana Investments Ltd ilikamilisha ujenzi wa kusafisha maji taka kutoka katika kiwanda chakekilichopo kata ya Olorien, Manispaa

Adili High School (AHS) ni shule ya kisasa iliyopo Moshono 8km Mashariki mwa Mnara wa saa jijini Arusha.Ni shule iliyojengwa katika ukubwa wa heka 22 maalumu kwa elimu ya sekondari kwa wavulana.

Kuna nafasi nzuri za kusomea na malazi. Maombi yanakaribishwa wahi nafasi ni chache.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:- Mr. Andrew E Shayo Mkuu wa Shule

Adili High School / P.O. Box 15449 Arusha / Tel. 0754 285769E-mail:[email protected] / Website: www.adilischool.ac.tz

KWA MAWASILIANO ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NASIBANANA INVESTMENTS LTD

MAKAO MAKUUKiwanja Na 311 Kitalu JJ Olorien Village,P. O. Box 10123, ArushaTANZANIAsimu: +255754224440,+255272506475E-mail: [email protected]

UBUNGO KIBANGU,S. L. P. 79407, Dar es SalaamTANZANIASimu: +255 222 774 276, +255 756 707 983Email: [email protected]

MOROGORO DEPOTKihonda AreaSimu +255763 992844Email: [email protected]

TANGA DEPOTBarabara ya nne, S. L. P. 5150, Tanga, TANZANIASimu: +255 272 646 134Email: [email protected]. tz

IDARA YA MASOKO ARUSHA KUPITIAE-mail [email protected],Meneja mauzo 0755423026,Meneja masoko 0753 619977.

BANANA INVESTMENTS LTDOfisi ya MwanzaS. L. P. 2350 MwanzaSimu: 0769 960276/ 0763 840978 /0687 475548Barua pepe: [email protected]

MBEYA DEPOTUyoleSimu: 0755 853623ROMBO DEPOT

Rombo MkuuSimu +255758383657Email: [email protected]

ADILI HIGH SCHOOLAdili Boys High School ni shule ya wavulana iliyopo katika Kata ya Moshono jijini Arusha.

Shule hii ni kwa ajili ya wavulana pekee, na inatoa nafasi za Bweni kwa wanafunzi wake wote.

Mkuu wa shule Mwalimu Andrew Shayo anao uzoefu mkubwa kama kiongozi wa shule za sekondari, na kuwa mkuu wa shule za Karatu, Umbwe, Old Moshi, Arusha Day na Arusha Sekondari

-.

Ili kujipambanisha na shule nyingine za sekondari shule imepan-ia kuwajengea maadili na kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wanaosoma hapo.

Kama ilivyohitaji la kila shule na mzazi, shule impania kufanya vizuri katika mitihani ya Kikanda na Kitaifa.

Katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha PILI mwaka 2013 shule ya Adili ilishika nafasi ya 19 kati ya shule 355 zilizoko kwenye Kanda ya Kaskazini.

Kwa sasa nafasi ni chache kwa wanaotoka kuhamia kidato cha kwanza, pili na tatu.

ADILI IMEKUWA SHULE YA KWANZA WILAYA YA ARUSHA, KWENYE MTIHANI WA KIDATO CHA PILIPIA WANAFUNZI WOTE WA KIDATO CHA PILI WAMEFAULU.