38
Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) Halmashauri ya Jiji la Mwanza Wilaya ya Nyamagana 2018 Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM Report 2018.pdfAfya ya Uzazi, Mama na Mtoto Halmashauri ya Jiji la Mwanza Wilaya ya Nyamagana Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji

  • Upload
    others

  • View
    25

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Jiji la Mwanza

Wilaya ya Nyamagana

2018

Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto

Kwa Ufadhili wa Shirika la Maendeleo:

(With core support by DANIDA)

Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto

Halmashauri ya Jiji la Mwanza

Wilaya ya Nyamagana

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii

Oktoba 2018

Zoezi la SAM limetekelezwa na Sikika kwa Hisani ya Mradi waIMPACT unaofadhiliwa na:

(SAM exercise was implemented by Sikika through specific support from IMPACT Project on behalf of)

1

Timu ya SAM Wilayani Nyamagana inatambua umuhimu wa wadau waliojitolea kwa lengo la kuijengea

jamii uwezo na maarifa ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii, yaani Social Accountability Monitoring

(SAM). Mradi huu ulifanikiwa kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika kusimamia rasilimali na

huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto zitolewazo kwa umma. Hili ni jambo kubwa lenye thamani

na linalostahili shukrani.

Kwa heshima tunapenda kuwatambua kwa nafasi ya pekee taasisi za Aga Khan Foundation na Sikika

kwa kuendesha miradi ya afya na hususanii ile inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya

ya uzazi, mama na mtoto. Pia, tunawashukuru sana kwa kuwajengea wananchi uwezo na maarifa ya

kuwa sehemu ya kupanga, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa mipango kuanzia ngazi ya jamii

mpaka Halmashauri.

Kipekee tunaushukuru uongozi wote wa Halmashauri ya Nyamagana kwa ushirikiano walio uonesha

kipindi chote cha utekelezaji wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Dk. Philis M. Nyimbi, Mstahiki Meya

wa Jiji Mh. James Marwa Bwire na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mwanza, Ndugu Kiomon Kibulwa

Kibamba. Pia, tunamshukuru Mganga Mkuu Dkt. Juma Mfanga na Timu ya Menejimenti ya Afya kwa Jiji

(CHMT), wakuu wote wa idara, waganga wafawidhi wa vituo, wananchi na wadau wote walioipa timu

ushirikiano wa dhati muda wote wa zoezi la SAM.

Mwisho naishukuru timu ya SAM kwa kuwa pamoja kipindi chote cha utekelezaji wa SAM mpaka

kukamilisha ripoti hii. Natumaini kuwa maarifa haya yatatumika kwa uendelevu ili kuboresha afya ya

uzazi, mama na mtoto wilayani.

Asanteni Sana

Mh. Germina Kabola (Diwani)

Mwenyekiti wa Timu ya SAM Nyamagana

Shukrani

2

Yaliyomo

Shukrani..........................................................................................................................................1

Yaliyomo...........................................................................................................................................3

Orodha ya Vifupisho.........................................................................................................................4

Muhtasari.........................................................................................................................................5

Sehemu ya Kwanza.........................................................................................................................6

1.0 Utangulizi...................................................................................................................................6

1.1 Mchakato wa Utekelezaji wa Zoezi la SAM..............................................................................6

1.2 Muundo wa Timu ya SAM Wilaya ya Nyamagana 2018............................................................7

1.3 Mafunzo ya Nadharia na Uchambuzi wa Nyaraka.....................................................................7

1.3.1 Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali........................................................................7

1.3.2 Usimamizi wa Matumizi.............................................................................................8

1.3.3 Usimamizi wa Utendaji..............................................................................................8

1.3.4 Usimamizi wa Uadilifu kwa Umma............................................................................8

1.3.5 Usimamizi wa Uwajibikaji..........................................................................................8

Sehemu ya Pili................................................................................................................................9

2.1 Mafanikio ya mipango ya afya - Nyamagana 2017/18..............................................................9

2.2 Uandaaji wa Nyaraka...............................................................................................................10

2.3 Utekelezaji wa Shughuli za Idara ya Afya 2017/18..................................................................11

2.3.1 Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana.......................................................................................14

2.3.2 Vituo vya Afya na Zahanati..................................................................................................17

Sehemu ya Tatu............................................................................................................................18

3.1 Utawala na Fedha..................................................................................................................18

3.1.1. Usimamizi Shirikishi................................................................................................18

3.1.2. Hali ya Mapato na Matumizi....................................................................................19

3.1.3. Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato.........................................................................19

3.1.4. Akaunti za Vituo.....................................................................................................19

3.1.5. Mafunzo kwa watumishi.........................................................................................20

3.1.6. Bodi na Kamati za Usimamizi wa Vituo vya Afya...................................................20

3.1.7. Mbao za Matangazo na Sanduku la Maoni..............................................................21

3

3.2 Rasilimali Watu katika Afya....................................................................................................22

3.2.1 Ikama ya Watumishi................................................................................................22

3.2.2 Malipo ya Stahiki za Watumishi..............................................................................22

3.2.3 Tathimini ya Utendaji kazi.......................................................................................23

3.3 Dawa na Vifaa Tibai................................................................................................. 23

3.3.1 Hali ya Upatikanaji wa Dawa Muhimu....................................................................23

3.3.2 Hali ya Upatikanaji wa Vifaa ..................................................................................23

3.3.3 Vyumba na Kabati za Kuhifadhia Dawa.................................................................23

3.4 Miundombinu ya Afya.............................................................................................................24

3.4.1 Vizimba vya Kuchomea Taka na Shimo la Kondo la Uzazi....................................25

3.4.2MfumowaMajiSafi................................................................................................25

3.4.3.HaliyaVyoonaUsafiwaMazingira......................................................................26

3.4.4 Ujenzi na Ukarabati wa Majengo na miundombinu ya barabara............................26

3.4.5 Nyumba za Watumishi............................................................................................27

3.4.6 Nishati ya Umeme...................................................................................................27

3.4.7 Usalama na Utulivu katika Vituo vya Kutolea Huduma...........................................28

Sehemu ya Nne............................................................................................................................29

4.0 Mapendekezo.........................................................................................................................29

4.1 Maazimio ya Pamoja...............................................................................................................31

4.2 Hitimisho.................................................................................................................................32

Kiambatanisho 1...........................................................................................................................33

Kiambatanisho 2...........................................................................................................................33

4

Orodha ya Vifupisho

SAM Social Accountability Monitoring (Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii)

CMT Council Management Team (Timu ya Menejimenti ya Jiji)

CHMT Council Health Management Team (Timu ya Menejimenti ya Afya kwa Jiji)

WDC Ward Development Committee (Kamati ya Maendeleo ya Kata)

CAG Controller Audit General (Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali)

WEO WardExecutiveOfficer(AfisaMtendajiwaKata)

HFGC Health Facility Govening Committee (Kamati ya Usimamizi wa Kituo)

DHSB District Health Service Board (Bodi ya Afya ya Wilaya)

CSO Civil Society Organizations (Asasi za Kiraia)

RBF Result Based Financing (Mpango wa Malipo kwa Ufanisi)

RCH Reproductive and Child Health (Afya ya Uzazi na Watoto)

IMPACT Improving Access to Maternal and Newborn Health in Mwanza,Tanzania (Mradi

wa Kuboresha Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto mkoa wa Mwanza)

5

Muhtasari

Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii - Social Accountability Monitoring (SAM) una

lengo la kuiwezesha jamii kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa mipango

kuanzia ngazi ya jamii mpaka Halmashauri. Lengo kuu la SAM ni kuimarisha mifumo kwa kuhimiza

Ushirikishwaji, Ufuatiliaji na Uwajibikaji Jamii kwa watoa huduma. Vilevile, kuwapa wananchi uelewa

kuhusu haki na wajibu wao kwenye jamii kama ilivyoainishwa katika sera, kanuni, taratibu na sheria za

nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Zoezi la SAM limeendeshwa wilayani Nyamagana kwa kuijengea uwezo jamii ambayo iliweza kufanya

uchambuzi wa taarifa mbalimbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali

inayotekelezwa katika vituo vya kutolea huduma za afya hususani huduma ya afya ya uzazi, mama na

mtoto.

Uchambuzi huo ullibainisha takribani jumla ya hoja 53 ambapo zimegawanyika katika makundi

yafuatayo:

• Hoja zilizofutwa baada ya ufafanuzi – 1

• Hoja zilizoibuliwa na zimeanza kushughulikiwa – 6

• Hoja zilizochukuliwa na menejimenti kwa ajili ya uchambuzi wa kina na uhakiki ili kujiri-

dhisha – 5

• Hoja zilizotolewa pongezi na ushauri – 10

• Hoja zilizopatiwa ufafanuzi wa kina na kukidhi haja kwa ajili ya maboresho – 31

Kwa ujumla wadau walikubaliana idara ishughulikie hoja hizo kwa kuboresha mifumo ya uandaaji wa

mipango na ripoti kwa kuzingatia miongozo ya serikali na kuimarisha uwepo na usimamizi wa kamati

za vituo. Vilevile, kuboresha huduma katika hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati hususani

huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ili kuimarisha uzazi salama. Kuimarisha miundombinu kama

vile, mifumo ya utupaji na uteketezaji taka na utambuzi wa mipaka ya vituo ili kudhibiti shughuli nyingine

zisizohusiana na huduma za afya kufanyika ndani ya maeneo ya vituo vya kutolea huduma.

Farida Mzambili, mjumbe wa timu ya SAM akiwasilisha ripoti ya SAM kwa wadau wa afya, Nyamagana

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akitoa maelekezo ya namna bora ya utekelezaji

wa maazimio ya SAM kwa wadau wa afya

6

Sehemu ya Kwanza 1.0 UtanguliziDhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) ni dhana shirikishi inayohimiza uwajibikaji wa

pamoja kati ya wananchi (wenye wajibu na haki) na watoa huduma (wenye wajibu na dhamana)

ilikuhakikisha upatikanaji endelevu wa mahitaji muhimu ya jamii.

Utekelezaji wa SAM katika Wilaya ya Nyamagana ulilenga kuiwezesha jamii kufahamu haki na wajibu

wao katika upatikanaji wa huduma ya afya ya uzazi, mama, baba na mtoto. Lengo ni kuwezesha

wananchi kushiriki katika kusimamia rasilimali zilizopo na kuwa na mipango ya pamoja kwa kuzingatia

miongozo, sera, sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Miongoni mwa nyenzo zilizotumika kuandaa ripoti hiini:

a) Toleo la IV la Mwongozo wa Uandaaji wa Mpango Kabambe wa Afya (CCHP) la Mwaka

2011.

b) Muongozo wa uandaaji wa mipango ya vituo vya afya na zahanati.

c) Mpango kabambe wa afya 2017/2018 na ripoti za utekelezaji kwa kila robo mwaka.

d) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

e) Mkataba wa Kimataifa wa ICESCR wa 1966.

1.1 Mchakato wa Utekelezaji wa Zoezi la SAMUshirikiano wa pamoja kati ya Sikika na Aga Khan Foundation ulifanikisha kukamilisha maandalizi ya

awali ikiwemo mikutano na viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali. Hatua hiyo ilihusisha viongozi

na wasimamizi wa Jiji la Mwanza na wilaya ya Nyamagana kwa utambulisho wa mradi na dhana ya

ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utekelezaji wake hivyo kutoa fursa ya kufanya mikutano ya jamii

ngazi ya kata ili kupata wawakilishi wa jamii na kuunda timu ya SAM yenye wajumbe 15.

Utekelezaji wa zoezi la SAM umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni mafunzo kwa

timu kuhusu dhana na mchakato wa utekelezaji zoezi la SAM. Sehemu ya pili ilihusisha uchambuzi wa

nyaraka mbalimbali kama zilivyotajwa hapo juu na kufanya uhakiki vituoni ili kupata uthibitisho wa hoja

zilizojitokeza katika uchambuzi. Katika sehemu hii pia timu ya SAM ilikutana na CHMT na CMT kwa

pamoja ili kupata ufafanuzi wa hoja zilizojitokeza kwenye uchambuzi na uhakiki vituoni. Sehemu ya

tatu, timu iliandaa ripoti ya hoja zinazohitaji kujadiliwa na kuwekewa mikakati na muda wa maboresho

(action plan) katika mkutano wa wadau wa afya kwa halmashauri.

1.2 Muundo wa Timu ya SAM Wilaya ya Nyamagana 2018Timu ya SAM kwa wilaya ya Nyamagana ina wajumbe 15 wanaowakilisha makundi mbalimbali;

uwakilishi pia ulizingatia jinsia na umri. Kundi la kwanza ni wananchi hususani vijana ambao sio tu

kwamba wana haki ya kupata huduma bora na wana wajibu wa kushiriki katika kuboresha huduma hizi

7

lakini pia wao ndio walengwa na wanufaika watarajiwa wa huduma ya afya ya uzazi. Kundi la pili ni

watendaji kutoka ngazi mbalimbali ambao kimsingi wana wajibu wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kundi la tatu ni wasimamizi walioko kisheria wenye wajibu wa kuhakikisha utawala bora na uwajibikaji

unakuwepo katika kutoa huduma kwa wananchi. Jedwali No. 1 linaonesha idadi ya uwakilishi kutoka

kila kundi.

Jedwali 1: Timu ya SAM Wilaya ya NyamaganaUwakilishi kutoka kwenye Jamii Watendaji Wasimamizi

Wananchi (ME&KE)

WananchiMahitaji Maalum

WAVIU Mashirika ya Kijamii

Watend-aji wa Kata

Timu ya Afya ya

Hal-mashauri

Timu ya Utawala ya Hamashau-

ri

Madiwani(ME & KE)

Bodi ya Afya ya Wilaya

Kamati ya Afya ya Kituo

5 1 1 1 1 1 1 2 1 18 3 4

1.3 Mafunzo ya Nadharia na Uchambuzi wa NyarakaTimu ilipatiwa mafunzo ya uchambuzi wa nyaraka muhimu za afya za wilaya za mwaka 2017/18.

Taarifa zilizochambuliwa zilijumuisha mpango mkakati wa halmashauri, mpango kabambe wa afya wa

halmashauri (CCHP), ripoti za utekelezaji wa mpango wa afya kwa kila robo mwaka na mihtasari ya

vikao vya baraza la madiwani. Mafunzo yalihusisha hatua 5 zilizoakisi mfumo wa uwajibikaji katika

uandaaji wa mipango na utekelezaji wa bajeti. Hatua hizo ni kama ifuatavyo;

1.3.1 Mipango na Mgawanyo wa RasilimaliTimu ya SAM ilipata fursa ya kujifunza uandaaji wa mpango mkakati wa wilaya na mpango kabambe

wa afya; hususani dhana, muundo na umuhimu wa ushiriki wa wananchi na wadau wengine katika

uandaaji wa mipango. Vilevile, timu ilijifunza namna ya kutathmini mahitaji na mgawanyo wa rasilimali

kwa kuzingatia vipaumbele vya upatikanaji wa huduma za afya hususani katika kipengele cha mama,

baba, mtoto na uzazi salama.

Bw. Fredrick Ngao kutoka Sikika akiendesha mafunzo kwa wajumbe wa timu ya SAM

Wajumbe wa timu ya SAM wakifanya uchambuzi wa taarifa za Halmashauri

8

1.3.2 Usimamizi wa MatumiziTimu iliweza kufanya ulinganifu wa vipaumbele, mipango, mapato na matumizi katika kutekeleza

mipango ya afya. Kwa kutumia ripoti za utekelezaji wa mipango na fedha, timu iliangalia matumizi ya

fedha katika kila robo mwaka. Pia timu ilitathmini njia za usimamizi wa mifumo na vyombo mahususi

vilivyoko katika halmashauri katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali fedha kwa kuzingatia miongozo,

kanuni na sheria za matumizi ya fedha za umma.

1.3.3 Usimamizi wa UtendajiTimu ya SAM ilifanikiwa kufanya ulinganifu wa mipango na ufanisi wa huduma zitolewazo na watoa

huduma vituoni. Maazimio katika nyaraka mbalimbali na hali halisi ya utekelezaji wake vilitoa mwanga

na uelewa namna ambavyo usimamizi katika utekelezaji wa mipango unavyofanyika.

1.3.4 Usimamizi wa Uadilifu kwa UmmaMifumo na mamlaka zenye dhamana ya kuchukua hatua za kinidhamu kwa watoa huduma zilitathiminiwa

na timu kwa kuwa ni nguzo muhimu katika kuimarisha uadilifu. Timu iliangalia namna ambavyo sheria

na miongozo iliyopo inawawezesha watoa huduma kutekeleza majukumu yao na jinsi ambavyo sheria

namiongozohuziwezeshamamlakazanidhamukufuatilianakudhibitimatumizimabayayaofisina

uzingatiaji wa miongozo ya matumizi ya fedha za umma. Mamlaka hizi ni pamoja na baraza la madiwani,

bodi na kamati za afya, mkaguzi wa fedha wa ndani, mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

1.3.5 Usimamizi wa UwajibikajiTimu ilichambua nyaraka kwa kuangalia namna ambavyo vyombo vya usimamizi vinavyowajibika

katika kila hatua. Kuanzia jamii kuibua vipaumbele vyake, ushirikishwaji katika kamati za afya za vituo,

kamati ya maendeleo ya kata (WDC), bodi ya afya ya wilaya na Baraza la Madiwani. Timu ilijifunza ni

maeneo na fursa zipi ambazo jamii inaweza kushiriki na kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama

na mtoto.

1.4 Maeneo yaliyotembelewa kwa UhakikiBaada ya mafunzo na uchambuzi, timu ilipata fursa ya kutembelea baadhi ya vituo ili kuona uhalisia

wa utekelezaji wa huduma za afya hususani huduma za mama, baba na mtoto. Vilevile, timu ilitumia

fursa hii kufanya uhakiki wa hoja zilizojitokeza kwenye uchambuzi kwa kufanya majadiliano na watoa

huduma au kuangalia (observations). Vituo tisa vya kutolea huduma za afya vilivyotembelewa ni

vile ambavyo viko kwenye mradi unaofadhiliwa na AgaKhan Foundation ujulikanao kama Mradi wa

Kuboresha Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto (IMPACT). Kiambatanisho Na. 1 kinaonyesha

vituo vilivyotembelewa na timu ya SAM.

9

Sehemu hii inazungumzia masuala mbalimbali yaliyobainishwa na timu wakati wa utekelezaji wa zoezi

la SAM. Maeneo makuu matatu yameripotiwa: mafanikio ya mipango ya afya, uandaaji wa nyaraka na

utekelezaji wa shughuli za mpango kabambe wa afya na uhakiki vituoni.

Sehemu hii pia inabainisha masuala yaliyohitaji ufafanuzi kutoka Timu ya Menejimenti ya Jiji (CMT)

na Timu ya Menejimenti ya Afya kwa Jiji (CHMT), vilevile inatoa mchanganuo wa namna kila suala

lilivyopatiwa ufafanuzi na kuingizwa katika mpango wa pamoja wa wadau unaobainisha namna ya

kuboresha huduma za Afya hususanii huduma ya afya ya uzazi, mama na mtoto.

2.1 Mafanikio ya mipango ya afya - Nyamagana 2017/18Tathmini ya timu ya SAM ilibaini kuwa katika kipindi cha mwaka 2017 – 2018, Idara ya Afya ilifanikiwa

kutekeleza mambo mbali mbali katika kuinua ufanisi wa huduma zitolewazo na idara na vituo vyake

vya huduma katika halmashauri ya manispaa ya Nyamagana:

(i) Kuongeza vituo viwili vya huduma: Zahanati za Isebanda na Bulale.

(ii) Watumishi wapya 11 ambao wamepangwa kwenye vituo mbalimbali kulingana na uhitaji wa

watumishi.

(iii) Ukarabati wa zahanati 9 kwa kutumia fedha za mfuko wa fedha kwa matokeo (Result Based

Financing – RBF) ili kuweka majengo katika ubora wa huduma na pia kuweka mazingira

bora kwa watoa huduma na watumiaji.

(iv) Kufunga mfumo wa umeme wa jua katika Hospitali ya Nyamagana ambao uimeimarisha

huduma za dharura na kuimarisha huduma zitumiazo nishati ya umeme.

(v) Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vituoni umeimarika toka 80% (2016/2017) mpaka 95%

(2017/2018).

(vi) Kuboresha miundombinu ya msingi katika kituo cha Igoma ikiwa ni pamoja na vyoo,

vichomea taka, mashimo ya kutupia kondo la nyuma baada ya akina mama kujifungua,

umeme,majisafinasalamanapiamifumoyamajitakanavifaavyauhifadhiwatakangumu

na hatarishi.

(vii) Halmashauri kwa kutumia fedha za vyanzo vyake vya ndani inajenga zahanati 4

ambazo zipo kwenye hatua mbalimbali jambo ambalo ukamilikaji wake utapunguza adha ya

watumia huduma kutembea umbali mrefu kufuata huduma hususani akina mama wajawazito

na wale wenye watoto wachanga.

Sehemu ya Pili

10

(viii) Kwa mwaka wa fedha 2018/19 idara ilianza kufanya upanuzi mkubwa wa kituo cha Afya Igo

ma ili kupunguza msongamano katika baadhi ya vituo, uimarishaji wa huduma kwa vifaa na

wataalam hivyo kutoa huduma bora zaidi hasa huduma za uzazi.

(ix) Mpango kabambe wa afya wa wilaya umezingatia vipaumbele vyote 13 vya afya.

Kipaumbele cha huduma ya uzazi, mama na mtoto kilibainishwa bayana katika Uk. XVI,

Jedwali Na. 2.2. Uchambuzi umeonesha uwepo wa mchanganuo wa bajeti na mahitaji yote muhimu ya

kuokoa vifo vya mama na mtoto.

2.2 Uandaaji wa Nyaraka2.2.1 Uandishi wa Nyaraka

Timu inapongeza Halmashauri ya Jiji na idara ya afya kwa kuzingatia miongozo ya uandaaji wa

Mpango Mkakati wa Jiji, Mpango Kabambe (2017/18) na Ripoti za Utekelezaji (2017/18). Mipango na

ripoti hizi zimezingatia kwa kiasi kukubwa miongozo kwa kuainisha taarifa muhimu hususani malengo,

viashiria, vipaumbele na taarifa za bajeti.

Hoja ya Timu

Timu inashauri menejimenti kuongeza umakini wa uhakiki wa taarifa ili ziwe bora na kuakisi uhalisia

na kuondokana na dosari kama kunakili taarifa zilizopita “copy and paste” kama ilivyoonekana wakati

wa uchambuzi wa taarifa. Kwa mfano, katika ripoti ya robo ya 1 ukurasa (uk) wa 8 na ripoti ya robo ya

2 uk. wa 9 taarifa ni moja; kukarabati vifaa tiba na jokofu la mnyororo baridi vituo vya Afya Igoma na

Makongoro. Pia timu haikuona uidhinishwaji wa Mpango Kabambe 2017/2018, hivyo inashauri ni vema

idara ihakikishe mipango inaidhinishwa na mamlaka husika.

Chanzo, SAM 2018: Mjumbe wa CMT akifafanua jambo wakati wa kikao cha ndani baina ya timu ya SAM na menejimenti

11

Majibu ya Menejimenti

Baada ya majadiliano ya timu, menejimenti iliahidi kufanyia kazi ushauri ili kuboresha mipango ya Jiji,

idara ya afya na ya vituo vya huduma kwa mwaka ujao wa fedha kwani kwa sasa mipango yote ime-

shaanza kutekelezwa vituoni.

2.3 Utekelezaji wa Shughuli za Idara ya Afya 2017/18Kipengele hiki kinaonyesha maoni ya timu yaliyotokana na hoja mbalimbali zilizotokana na uhakiki

katika ngazi ya hospitali, vituo vya afya na zahanati.

2.3.1 Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana

i) Kuzalisha zana za kukusanya taarifa na kuchapa kadi za mama wajawazito na watoto ifikapo Juni 2018.Hoja ya timu

Uchambuzi wa timu ulibaini kuwa shughuli ilipangwa kufanyika katika robo zote nne za mwaka, lakini

fedha zilipokelewa na utekelezaji ulifanyika katika robo ya tatu pekee. Vilevile, uhakiki katika vituo

ulibaini kuwa baadhi ya kina mama hudurufu (hutoa nakala ngumu) kadi za mama wajawazito na

watoto kutokana na upungufu wa kadi hizo vituoni. Timu ilipenda kufahamu kwanini katika robo ya

kwanza na pili kadi hizi hakikuchapwa na je, idara iliweka mkakati upi kukabiliana na changamoto hiyo?

Majibu ya Menejimenti

Suala hili lilisababishwa na kuchelewa kutolewa kwa fedha za mfuko wa afya wa pamoja (Health

Basket Fund - HBF) ambazo ziliingia mwishoni mwa robo ya pili na utekelezaji ukafanyika robo ya tatu.

Aidha, baadhi ya vituo vilivyodurufu kadi hizo vilitumia fedha za mpango wa malipo kwa Ufanisi (Result

based Financing – RBF).

Maoni ya timu

Timu ilipendekeza kuwa ni vema serikali ikazingatia muda wa utoaji wa fedha kwa Idara ili kutoathiri

utoaji wa huduma za afya ya uzazi, wajawazito na watoto unaosababishwa na ucheleweshwaji wa

fedha.

ii) Ukusanyaji wa damu salama kwa kiwango cha uniti 1,200 ifikapo juni 2018Hoja ya timu

Uchambuzi wa timu ulionyesha kuwa idara ilipokea na kutumia jumla ya shilingi 9,561,517/= kati ya

shilingi 17,300,000/= zilizopangwa kwa ajili ya ukusanyaji wa damu salama. Kwa kuzingatia umuhimu

wa damu salama kwa huduma za mama na mtoto, timu ingependa kufahamu kama kuna athari zozote

zilizotokana na kutopata fedha zote za kufanyia shughuli hii (kukusanya damu salama).

Majibu ya Menejimenti

Lengolilikuwakukusanyaunit1200zadamunahalikufikiwa.Aidha,hospitaliililazimikakutafutadamu

12

kwenye Taasisi nyingine kama Hospitali ya Bugando na SekouToure ili kuweza kuokoa maisha. Hata

hivyo, jamii inajengewa uelewa wa umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari ili kuweza kuwa na hifadhi

ya damu salama ya kutosha.

(iii) Kufanya mafunzo elekezi ya usimamizi wa lishe kwa wahudumu wa afya 71Hoja ya timu

Uchambuzi ulibaini shilingi 6,400,000/=zilitengwa kwa ajili ya mafunzo na kupangwa kufanyika kila

robo ya mwaka lakini haikufanyika na ripoti hazikutoa ufafanuzi wowote. Hivyo, timu iliomba kujua idara

ilikabilianajenachangamotoyausimamizihafifuwalishenaupimkakatiuliopokwasasa?

Majibu ya Menejimenti

Shughuli hii haikutekelezwa kutokana na kutopokelewa kwa fedha za utekelezaji. Aidha, elimu ya lishe

inaendelea kutolewa kwa mama wajawazito wanapohudhuria kliniki kwenye vituo vya kutolea huduma.

Utekelezajizaidiutafanyikafedhazitakapopatikanailikufikialengokuu.

Maoni ya Timu

Timu inashauri wizara ya afya iweke asilimia mahususi ya bajeti kwa ajili ya huduma ya lishe ili kutatua

tatizo litokanalo na athari za lishe kwa mama wajawazito na watoto wachanga.

iv) Ununuzi wa virutubisho kwa watoto 280 wenye dalili za utapiamlo chini ya miaka mitanoHoja ya timu

Uchambuzi wa timu ulibaini jumla ya shilingi 21,000,000/= zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa virutubisho

hivyo hata hivyo ununuzi haukufanyika na hakukuwa na maelezo katika ripoti ya utekelezaji. Hivyo

timu ilipenda kufahamu ni kwa nini shughuli hii haikutekelezwa? Je, kuna mkakati gani kukabiliana na

changamoto hiyo ya utapiamlo.

Majibu ya Menejimenti

Shughuli hii haikutekelezwa kutokana na kutokuwepo kwa fedha za utekelezaji. Aidha, idara imejielekeza

kuhakikisha inasimamia uandaaji wa mipango ya vituo ili kuhakikisha shughuli zinapangwa kulingana

na vipaumbele na rasilimali zilizopo.

Maoni ya Timu

Timu inashauri idara kuongeza usimamizi wa uandaaji, utekelezaji na utoaji wa taarifa katika ngazi za

vituo ili kukuza ufanisi.

(v) Upanuzi wa jengo la mionzi katika Hospital ya Nyamagana Hoja ya timu

Uchambuzi wa timu ulibaini kuwa jumla ya kiasi cha shilingi 19,588,006/= ilipangwa katika robo ya

kwanza kutoka chanzo cha mfuko wa pamoja wa afya kwa ajili ya upanuzi wa jengo. Aidha, katika

taarifa za utekelezaji timu ilibaini kuwa upanuzi wa jengo la mionzi haukufanyika hata hivyo vyoo katika

13

hospitali vilibainika kujengwa. Timu ilipenda kufahamu kwa nini ujenzi ulibadilika na mpango wa

upanuzi wa jengo la mionzi uliishia wapi?

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti inaendelea kufuatilia usahihi wa taarifa hii ili kuweza kujiridhisha na kutoa ufafanuzi zaidi.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa majibu na itaendelea kufuatilia na kupata majibu sahihi ili kuboresha uandaaji na

utoaji wa taarifa na huduma.

(vi) Ujenzi wa jengo la utawala Hoja ya timu

Uchambuzi ulibaini kuwa jengo la utawala lilipangwa kujengwa kwa gharama ya shilingi 481,069,341/=

kutoka chanzo cha mapato ya ndani na kupangwa kufanyika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha

2017/18 lakini halikutekelezwa. Timu iliomba ufafanuzi kwanini ujenzi haukufanyika, na ni lini

utatekelezwa? Pia CHMT inavyokabiliana na jengo la utawala.

Majibu ya Menejimenti

Utekelezaji wa shughuli hii ulikwama kutokana na baadhi ya vyanzo vya mapato vya halmashauri

kuhamishiwa serikali kuu, hivyo kupelekea kuwa na makusanyo kidogo. Aidha menejimenti inapata

adhakwakukosekanakwa jengo lautawalahivyokumelazimikakuwanaofisimaeneo tofautihali

inayopelekea utendaji kuwa mgumu.

Maoni ya Timu

Timu inashauri menejimenti ya halmashauri kulipa kipaumbele suala hili kwa kuliweka katika mipango

ijayo ili kuondoa kadhia ili kuleta ufanisi wa kiutendaji na huduma za afya.

(vii) Ununua wa mashine ya mionziHoja ya timu

Uchambuzi ulibaini kuwa mashine ya mionzi haikununuliwa japo iliwekwa kwenye mpango na bajeti.

Hivyo, timu ilipenda kujua mashine ya mionzi itanunuliwa lini na je, hospitali kwa sasa ina utaratibu gani

kwa huduma za mionzi?

Majibu ya Menejimenti

Hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ili kuweza kununua dawa, na vifaa

tiba hususani mashine ya mionzi ili kuboresha huduma za afya. Aidha katika kipindi hiki wagonjwa

wamekuwa wakipata huduma hii kwenye hospitali za Bugando na SekouToure.

Maoni ya Timu

Timu ilipendekeza idara itekeleze mikakati iliyoweka angalau katika kipindi cha robo ya tatu (Januari –

14

Machi 2019) ili kuboresha huduma hii muhimu ya vipimo kwa mama wajawazito.

(viii) Kununua seti (kit) za dawa, maabara na meno Hoja ya timu

Uchambuzi ulibaini kuwa manunuzi haya yalitengewa kiasi cha shilingi 85,686,199/=. Robo ya kwanza

imeonesha ununuzi wa seti mbili kwa shilingi 16,684,158/= na robo ya pili zilinunuliwa setimbili kwa

3,435,021/=. Timu ilipenda kujua gharama ya kila seti na kwa nini bakaa ya shilingi 6,565,795/= haiku-

tumika wakati uhitaji wa vifaa ulikuwepo? Na, kwa nini seti saba badala ya nne kama ilivyokusudiwa?

Majibu ya Menejimenti

Kutokana na mfumo wa vituo kununua dawa na vifaa tiba vyenyewe kumekuwa na baadhi ya vituo

kutokuwasilisha maombi yao hali inayopelekea vituo kubaki na fedha mwisho wa robo au mwaka.

Aidha vituo vinaendelea kujengewa uwezo namna ya uagizaji wa dawa na vifaa tiba. Pia kumekuwa na

ongezeko la seti za dawa toka 4 hadi 7 hali hii imesababishwa na aina ya dawa zilizoagizwa pamoja

na mabadiliko ya gharama za dawa wakati wa ununuzi.

2.3.2 Vituo vya Afya na Zahanati(i) Ukarabati vifaa tiba na friji katika vituo vya Makongoro na IgomaHoja ya timu

Uchambuzi ulibaini ukarabati ulipangwa kufanyika kwa jumla ya shilingi 1,500,000/= kwa robo zote nne.

Hata hivyo uchambuzi ulionesha kuwa robo 1 na 2 zilinunuliwa seti za vifaa tiba badala ya ukarabati wa

vifaa vya Hospitali na Friji kama ilivyopangwa ila robo ya nne ndo ukarabati ukafanyika. Timu iliomba

ufafanuzi juu ya mkanganyiko huu na zipi zilikuwa sababu za mabadiliko hayo?

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti inaendelea kufuatilia kwenye vituo husika ili kuweza kubaini ni kwa namna gani mfumo

uliweza kufanya malipo nje ya utaratibu.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa majibu na itaendelea kufuatilia ili kupata uhalisia wa suala hili.

(ii) Kununua dawa na vifaa tiba - seti 8 kila mojaHoja ya timu

Uchambuzi ulionesha bajeti iliyotengwa kwa shughuli hii ilikuwa shilingi 95,522,203/= lakini kiasi

kilichopokelewa ni shilingi 10,902,428/=. Na, kati ya hizo, fedha zilizotumika ni shilingi 6,301,384/=

hivyo kuacha bakaa ya shilingi 4,601,044/= ambayo haikuonekana na wala hakukuwa na maelezo

yoyote. Timu iliomba kupata ufafanuzi wa fedha hizo ambazo hazijaonekana katika bakaa ya robo ya

nne.

15

Majibu ya Menejimenti

Kwa utaratibu wa mfumo wa kuandalia bajeti na kutolea taarifa, kiasi cha fedha kilichopokelewa na

kilichotumika kikiingizwa kwenye mfumo bakaa hutokea. Aidha, ufuatiliaji unaendelea kuona ni kwa nini

mfumo ulishindwa kuonesha salio wakati kuna fedha zilipokelewa.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa majibu na itaendelea kufuatilia ili kuthibitisha kama ni suala la mfumo ama ni

sababu nyinginezo.

(iii) Ununuzi wa kadi za wajawazito na watoto kwa vituo vya Makongoro na Igoma Hoja ya timu

Uchambuzi ulibaini jumla ya shilingi 4,810,000/= zilitengwa kutumika katika kila robo ya mwaka. Kazi

hii ilifanyika robo ya nne hivyo timu iliomba kupata ufafanuzi juu ya namna vituo vilivyojiendesha kwa

robo ya kwanza, pili na tatu bila kadi hizo muhimu.

Majibu ya Menejimenti

Katika kipindi cha robo ya 1 hadi 3 vituo vilitumia fedha za RBF kuhakikisha vinakuwa na kadi za

wajawazito. Aidha, fedha zilipopokelewa robo ya 4 manunuzi yalifanyika kwa kutumia mfuko wa pamoja.

(iv) Ununuzi wa “Valve” 25 za gesiHoja ya timu

Uchambuzi umebaini kuwa ununuzi ulipangwa kufanyika kwa gharama ya shilingi 625,000/= kwa robo

ya kwanza. Hata hivyo ununuzi wa valve 60 badala ya 25 ulifanyika katika robo ya nne kwa shilingi

625,000/= wakati fedha iliyopokelewa ni Tshs 563, 770/=. Timu iliomba ufafanuzi juu ya ongezeko la

idadi ya “valve” na fedha zilizotumika zilitoka wapi wakati fedha zilizopokelewa zilikuwa pungufu.

Majibu ya Menejimenti

Manunuzi ya ‘valve’ yalifanyika kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwa ni pamoja na fedha za

papo kwa papo, RBF na HBF. Vyanzo hivyo vilipelekea idadi kuongezeka kutoka ‘valve’ 25 hadi 60, hii

ilitokana na umuhimu wa vifaa hivyo vinavyotumika kwenye majokofu ya kuhifadhia chanjo.

Maoni ya Timu

Timu ilishukuru kwa majibu, pia ilishauri maelezo ya aina hii yawekwe katika kipengele cha maoni ili

kupunguza maswali kwa watumia taarifa.

(v) Uchapishaji wa miongozo 300 ya usimamizi wa ustawi wa mtoto kwa zahanati 50 Hoja ya timu

Uchapishaji ulipangwa kufanyika kwa bajeti ya shilingi 5,400,000/= kwa robo ya pili pekee. Hatahivyo

miongozo 150 tu ndio ilichapishwa na sio 300 kama ilivyopangwa. Timu ilipenda kujua kwa uchapishaji

ulikuwa pungufu na huku fedha ikiwa imetumika karibu yote kwa nusu ya kazi?

16

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti imeona changamoto hii ya makisio, hali hii kwa sehemu kubwa inachangiwa na uelewa

mdogo wa waandaaji wa mipango ngazi ya vituo. Aidha Menejimenti inaendelea kuwajengea uwezo

watumishi ili waweze kuandaa mipango inayoakisi mahitaji na vipaumbele.

(vi) Ukarabati wa majengo ya zahanati Hoja ya timu

Uchambuzi ulionesha kuwa ukarabati ulipangwa kufanyika robo zote kwa shilingi 175,540,200/= kwa

chanzo cha matumizi mengineyo (Other Charges-OC). Kiasi chote kilichotengwa kilipokelewa na

matumizi yameonesha fedha zilitumika zaidi ya kiasi iliyopokelewa ambapo kuna ongezeko la shilingi

6,706,734 ambalo halionekani chanzo. Timu ilipenda kupata ufafanuzi wa mkanganyiko huo wa chanzo

kutojulikana.

Majibu ya Menejimenti

Ukarabati ulifanyika kwa fedha za RBF zilizopokelewa awamu ya kwanza baada ya bajeti kuwasilishwa.

Maoni ya Timu

Timu ilishukuru kwa majibu lakini inashauri maelezo ya aina hii yawekwe katika kipengele cha maoni ili

kupunguza maswali kwa watumia taarifa.

(vii) Ununuzi wa seti (kit) 4 za dawa kwa zahanati 12 Hoja ya timu

Kiasi cha shilingi 114,396,678/= kilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa seti 4 za dawa na ununuzi ulipangwa

kufanyika robo zote za mwaka. Ripotii ya utekelezaji ununuzi wa seti hizo za dawa zikiwemo dawa za

msingi za matibabu ya awali kwa afya ya kinywa na meno (dental supplies) ngazi ya zahanati. Timu

ilipenda kupata ufafanuzi juu ya ununuzi wa dawa hizi katika ngazi ya zahanati wakati huduma za

kinywa na meno hazipo kwenye zahanati?

Majibu ya Menejimenti

Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya hususani wilaya zilizopo mjini, vituo

vilielekezwa kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa za msingi za matibabu ya awali kwa

afya ya kinywa na meno kwenye ngazi ya zahanati kabla ya matibabu ya kina katika ngazi za juu kama

vituo vya afya na hospitali.

(viii) Ununuzi wa seti (kit) 12 za dawa kwa zahanati Hoja ya timu

Ununuzi wa seti za dawa ulipangwa kufanyika kwa kutumia fedha kutoka NHIF kiasi cha shilingi

17,451,197/= kwa kila robo. Utekelezaji umeonesha manunuzi ya shilingi 68,000/= pekee yalifanyika

kutokana na changamoto ya upungufu wa fedha japo katika robo ya tatu kulikuwa na bakaa ya shilingi

454,590/=. Aidha, katika robo ya nne imeonekana bakaa ya shilingi 1,284,590/= tofauti na shilingi

17

454,590 zilizotoka robo ya tatu. Timu iliomba ufafanuzi ni kit zipi ziligharimu fedha ndogo kiasi hicho

tofauti na mpango na kwa nini kumekuwa na bakaa tofauti tofauti?

Majibu ya Menejimenti

Utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kwa vyanzo vya fedha vya makusanyo ya kituo unategemea na

makusanyo halisi. Aidha maboresho yanaendelea kufanyika kwenye vituo ili kuimarisha vyanzo vya

mapato ya ndani pamoja na uhakiki wa fomu za Bima zinazojazwa kabla ya kuwasilishwa NHIF. Lengo

likiwa kupunguza dosari zinazoweza kusababisha fomu kurejeshwa na kituo kukosa mapato.

Maoni ya Timu

Timu ilishukuru kwa majibu japo suala la bakaa halijipatiwa ufafanuzi, hivyo timu inasisitiza idara

kuendelea kuchambua na kutoa ufafanuzi kuhusu bakaa ya shilingi 1,284,590/=

Mwenyekiti wa wa timu ya SAM, Bi. Germina Kabola akichangia mada wakati wa mafunzo ya zoezi la SAM wilaya ya Nyamagana

18

Sehemu ya Tatu

Masuala yatokanayo na uhakiki vituoni

3.1 Utawala na Fedha3.1.1. Usimamizi Shirikishi

Katika vituo vya huduma vilivyotembelewa timu ilitaka kujua maswala mbalimbali yanayohusu

usimamizi shirikishi na jinsi yanavyolenga kuboresha huduma ya Mama, Baba na Mtoto.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kujua katika kipindi cha mwaka 2017/2018 na robo ya kwanza 2018/2019 idara ilifanikiwa

kwa kiasi gani kufanya usimamizi shirikishi katika robo zote? Na je ni changamoto zipi ambazo timu ya

usimamizi /CHMT inazokumbana nazo katika kutekeleza usimamizi shirikishi?

Majibu ya Menejimenti

Ziara za usimamizi shirikishi zilifanyika kwenye vituo vya huduma za afya japo kulikuwa na changamoto

mbalimbali zikiwa ni pamoja na:-

• Uhabawamagariyakufanyiaziara(Idarainagarimojatuzimakwashughulizautawala).

• Uhabawamafutauliosababishwanakiasikidogochapesakilichopangwawakatiwabajeti.

• KucheleweshwakwafedhazaMfukowaPamojaambapokunashughulizausimamizi

3.1.2. Hali ya Mapato na MatumiziUhakiki wa timu vituoni ulibaini uwepo wa hali duni ya mapato ya ndani ukilinganisha na makadirio ya

makusanyo. Hata hivyo taarifa za mapato na matumizi ya vituo ziliwekwa katika mbao za matangazo

kwa ajili ya matumizi ya umma.

Hoja ya Timu

Timu imeipongeza idara na vituo kwa kusimamia na kuhakikisha uwepo wa taarifa za mapato na

matumizi katika mbao za matangazo. Hata hivyo, ingependa kufahamu mkakati uliopo wa kuongeza

mapato katika vituo.

Wajumbe wa timu ya SAM wakifanya zoezi la uhakiki vituoni

19

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti imepokea pongezi hizi na inaendelea kuboresha masuala ya uwazi na uwajibikaji

hususani kwenye fedha na bajeti katika ngazi za vituo vya huduma kwa ujumla.

3.1.3. Mfumo wa Ukusanyaji wa MapatoUhakiki wa timu katika vituo vyote ulionesha kuwa sehemu kubwa ya mapato yanatokana na malipo

ya ‘papo kwa papo’ huku mfumo wa ukusanyaji kwa TIKA ukionesha kutokuwa hai jambo linaloweza

kuathiri uendelevu wa huduma vituoni.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kufahamu mkakati uliopo kuimarisha TIKA ama CHF iliyoboreshwa ili kuongeza mapato

na kumpunguzia mwananchi wakawaida mzigo wa malipo ya papo kwa papo.

Majibu ya Menejimenti

Idara inaendelea na mikakati mbalimbali inayoelekezwa kwa ajili ya kuboresha Bima za Afya za Jamiii

ikiwemo CHF ya sasa kuwa CHF iliyoboreshwa. Aidha, katika kufanikisha hilo idara imenunua jumla

ya simu za kiganjani 36 kwa lengo la kuimarisha uandikishaji wa wanachama wa CHF kwenye mfumo

mpya na taratibu za kuwapata waratibu na kuwapa mafunzo zinaendelea.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa ufafanuzi na mikakati na itaendelea kufuatilia utekelezaji hususani uandikishaji

wa wanachama na hali ya utoaji wa huduma.

3.1.4 Akaunti za Vituo Uhakiki wa timu umejiridhisha na uwepo wa akaunti za vituo na zimeonekana kubandikwa katika mbao

za matangazo

Pongezi

Timu inapongeza idara na vituo kuhakikisha uwepo wa akaunti za vituo na kuwa na uwazi wa taarifa

za fedha.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti inaendelea kuhakikisha akaunti za vituo vya huduma zinatumika kulingana na taratibu na

miongozo iliyopo pamoja na kutoa taarifa za fedha zilizo sahihi kwa umma.

3.1.5 Mafunzo kwa watumishiUhakiki wa timu umebaini kuwa mafunzo kazini hutolewa mara kwa mara hatahivyo kuna uhitaji

mkubwa wa mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi wengi.

Hoja ya Timu

Timu ingependa kujua mkakati ulipo kuhakikisha kuna uwiano wa watumishi kupata mafunzo

20

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti imekuwa ikiandaa mpango wa mafunzo kila mwaka kulingana na mahitaji, pia watumishi

wamekuwa wakishiriki mafunzo ya muda mfupi na mrefu yanayokuwa yanatolewa na wadau mbalimbali

kulingana na uhitaji na huduma zinazotolewa kwenye vituo.

Maoni ya Timu

Timu inashauri utaratibu wa mafunzo uwe endelevu na uzingatie uwiano wa watumishi vituoni.

3.1.6. Bodi na Kamati za Usimamizi wa Vituo vya AfyaUhakiki wa timu katika vituo vyote vilivyotembelewa ulionesha uwepo wa kamati za usimamizi wa vituo

hata hivyo baadhi ya kamati zilikuwa na changamoto za kimuundo na kiutendaji.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kujua kama bodi ya afya imeanza kutekeleza majukumu yake hususani kupitia na

kuidhinisha mipango na ripoti za utekelezaji.

Pia, ni muongozo na utaratibu upi unaotumika kupata wajumbe na wenyeviti wa kamati za usimamizi

wa vituo kwani baadhi ya kamati zimeonesha kuwa wenyeviti wake ni wenyeviti wa mitaa? Kwa

mfano Zahanati za Sahwa na Buhongwa. Pia timu ilipenda kujua taratibu za mafunzo na miongozo ya

uendeshaji wa kamati.

Majibu ya Menejimenti

Wajumbe wa Bodi ya Afya ya Wilaya walishapatikana/chaguliwa na taratibu za uzinduzi wa Bodi

utafanyika kabla ya 15, Oktoba 2018. Aidha, utaratibu wa uundaji wa kamati za vituo unaendelea

kuelekezwa kwenye vituo ili kuweza kupata wajumbe wanao stahili kusimamia kituo na tija kuonekana,

lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya.

Maoni ya Timu

Timu inashauri menejimenti ishirikiane na uongozi wa kata na mitaa kurekebisha dosari zilizopo

kwenye kamati za vituo. Kwa mfano katika zahanati za Buhongwa na Sahwa kumeonekana wenyeviti

wa mitaa kuhodhi vyeo vya uenyekiti wa kamati ya afya ya vituo kinyume na miongozo jambo linaloleta

mgongano wa maslahi na uwajibikaji.

3.1.7. Mbao za Matangazo na Sanduku la MaoniUhakiki wa timu umeonesha uwepo wa mbao za matangazo na sanduku la maoni japo katika Hospitali

yaWilaya sanduku lamaoni limedondoka hivyo kuwekwa sehemuambayo si rafiki kwa wapokea

huduma.Masandukumengi hayakuwa na kufuli mbili na pia hayako sehemu rafiki hivyo kufifisha

uwajibikaji na usiri.

21

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kuipongeza idara na vituo kwa kuhakikisha uwepo wa mbao zenye taarifa na sanduku la

maoni. Aidha, timu ilishauri idara kusimamia kamati za vituo kupanga na kuhakikisha masanduku yana

kufuli mbili na funguo zinakaa kwa M/Kiti wa kamati na katibu.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti inaendelea kufanya maboresho kwenye suala la wateja/wagonjwa kutambua haki zao

pamoja na wajibu wa watoa huduma ili waweze kutoa maoni yao. Aidha, maboresho yanafanyika

kwenye vituo kuhakikisha kunakuwa na masanduku ya kutolea maoni yaliyopo kwenye sehemu za

wazi ambapo mteja anapoweza kuweka maoni bila kuwa na kipingamizi.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa ufafanuzi na itaendelea kufuatilia maboresha yaliyobainishwa na utawala.

Bi. Edna Selestine kutoka Aga Khan akitoa utangulizi juu ya Mradi wa Kuboresha Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kwa madiwani, wilayani Nyamagana

22

3.2 Rasilimali Watu katika afya3.2.1 Ikama ya WatumishiUhakiki wa timu katika vituo tisa vilivyotembelewa umebaini uhaba wa watumishi vituoni ukilinganisha

na ikama inayopelekea uwiano wa wingi wa kazi na mtumishi kutokuwa sawa. Kwa mfano katika vituo

vya Nyamagana, Buhongwa na Igoma vilionyesha kuzidiwa na wagonjwa huku baadhi ya vituo vengine

vikionekana kuwa na wagonjwa wachache.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kupata ufafanuzi kuhusu mgawanyo wa watumishi na sababu zinazopelekea baadhi ya

vituo kuwa na wagonjwa wengi huku vingine vikibaki na idadi ndogo.

Majibu ya Menejimenti

Mgawanyo wa watoa huduma unazingatia Ikama ya (2014-2019) pamoja na wingi wa wagonjwa

kwenye baadhi ya vituo. Japokuwa kwa sasa kuna upungufu wa 24% ya watumishi wa kada mbalimbali,

idara inahakikisha watumishi waliopo wanagawanywa kwa usahihi na wale wanaoajiriwa na kuhamia

wanapangwa kulingana na mahitaji na uwiano.

3.2.2 Malipo ya Stahiki za WatumishiKatika vituo vyote tisa vilivyotembelewa, kulikuwapo na madai ya stahiki za watumishi hususani

zinazotokana na kutoa huduma za mkoba.

Hoja ya Timu

Timu ingependa kupata ufafanuzi kuhusu madai ya stahiki hizo kwa kuwa kutokulipwa stahiki kwa

wakati kunaweza kuathiri ari ya utendaji kazi.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti imekiri kuwepo kwa madai mbalimbali ya stahiki za watumishi kama likizo, wito wa

dharura(on-call), na matibabu. Aidha, idara imejipanga kuhakikisha inapunguza madai haya kwa

kulipa pindi fedha zinapokuwepo. Kwa mfano, katika kipindi cha mwezi Agosti zaidi ya watumishi 25

wametengewa fedha za kulipwa posho za likizo na taratibu za malipo zimeanza. Pindi fedha za mfuko

wapamojazitakapofikawatumishiwanaodaiposhozahudumayamkobawatalipwakwanizilikuwa

zimetengwa kwenye bajeti.

Maoni ya Timu

Timu inapongeza kwa jitihada hizo na itaendelea kufuatilia hali ya utekelezaji wa mkakati huo ngazi ya

menejimenti na ngazi ya vituo.

3.2.3 Tathimini ya Utendaji kaziSuala la maadili ya watumishi lilijitokeza kwa baadhi ya vituo hususani zahanati ya Fumagila na

kituo cha Afya Igoma. Utendaji umeonekana kutoridhisha kwani wagonjwa walilalamika lugha chafu,

23

kutokuthaminiwa na watoa huduma kutokuwepo kazini kwa wakati. Kwa mfano, katika zahanati ya

Fumagilawatumishiwannetukatiyatisawalikuwepokituoniwakatitimuilipofikasaa5asubuhi.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kufahamu kama idara ya afya inatambua changamoto hizo na upi mkakati uliopo

kurekebisha changamato hizo.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti imeendelea kuwaelekeza watumishi taratibu na maadili ya utumishi wa umma pamoja na

kuwakemea wale wanaobainika kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa au kwa wahudumu wenzao. Aidha,

Ofisihaitositakumchukuliahatuazakinidhamumtumishiatakayebainikakwaushahidiwakukiuka

taratibu za Utumishi wa Umma.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru na kupongeza idara dhamira hiyo kwani hatua hizo ni za kiuwajibikaji.

3.3. Dawa na Vifaa Tiba3.3.1 Hali ya Upatikanaji wa Dawa MuhimuUhakiki wa timu umebaini uwepo wa dawa katika vituo vyote. Timu inapenda kuipongeza idara kwa

kuhakikisha upatikanaji wa dawa katika vituo. Pamoja na pongezi hizo, timu inashauri idara kuhakikisha

upungufu wa dawa vituoni unakuwa historia kwa kuweka mikakati endelevu.

3.3.2 Hali ya Upatikanaji wa Vifaa TibaUhakiki wa timu umeonesha vifaa tiba havitoshelezi katika vituo vya kutolea huduma. Kwa mfano

ukosefu wa kifaa cha kupimia wingi wa damu kituo cha Sahwa, uhaba wa vifaa vya kutolea huduma za

dawa ya usingizi katika hospitali ya Nyamagana (kipo kimoja na uhitaji ni mkubwa kwa wastani kila saa

moja mtoto mmoja huzaliwa hospitali hapo na baadhi huhitaji upasuaji).

Hoja ya Timu

Timu ingependa kufahamu mkakati uliopo kurejesha huduma za dawa za usingizi na kifaa cha

kumsaidia mtoto mchanga kupumua ili kuokoa maisha ya wakina mama na watoto wachanga.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti inapenda kukiri kuwa hospitali ya wilaya ilikuwa na changamoto ya huduma ya usingizi

kwa kipindi cha wiki 3 lakini kwa sasa vifaa na dawa zimenunuliwa na huduma za upasuaji wa dharura

zinaendelea kutolewa kama kawaida.Aidha, kutokana na ufinyu wa jengo la wazazi kuna baadhi

ya vifaa vinalazimika kuwepo kimoja ama viwili na pindi upanuzi wa jengo utakapokamilika huduma

zitaboreka zaidi.

24

3.3.3 Vyumba na Kabati za Kuhifadhia DawaUhakikiwatimukatikavituovilivyotembelewaumeoneshauwepowavyumbafinyuvisivyokidhimahitaji

ya uhifadhi wa dawa na kabati za kutunzia dawa zisizoridhisha.

Hoja ya Timu

Timu ingependa kufahamu mkakati uliopo wa kutatua changamoto hiyo vituoni.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti imeendelea kuwaelekeza watumishi taratibu na maadili ya utumishi wa umma pamoja na

kuwakemea wale wanaobainika kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa au kwa wahudumu wenzao. Aidha,

Ofisihaitositakumchukuliahatuazakinidhamumtumishiatakayebainikakwaushahidiwakukiuka

taratibu za Utumishi wa Umma.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti inakiri kuwepo na changamoto ya miundombinu katika vituo vya huduma suala ambalo

linafanyiwa kazi na idara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mathalani shirika kisilo la kiserikali

AGPAHI wanaokarabati majengo ya kuhifadhia dawa kwenye baadhi ya zahanati.

3.4 Miundombinu ya Afya3.4.1 Vizimba vya kuchomea Taka na Shimo la Kondo la UzaziUhakiki wa timu katika vituo vilivyotembelewa umeonesha uwepo wa vichomea taka na shimo la kondo

la uzazi vyenye ubora katika vituo vya Nyamagana, Igoma, Bugarika, Shadi na Sahwa.

Hata hivyo, vituo vya Fumagila na Buhongwa havikuwa kabisa na vichomea taka wala shimo la kondo

la uzazi. Aidha kwa vituo vya Makongoro na Mkolani kuna vichomea taka na shimo la kondo visivyo na

ubora.KwaupandewaMakongorohusafirishatakakatikaHospitaliyaNyamaganakwauteketezaji.

Karibu vituo vyote, mashimo ya kondo la uzazi hayana kufuli na imeonekana kondo kuchanganywa na

mifuko ya nailoni kitu kinachoweza kupelekea kuchelewa kuoza na kuwahi kujaa shimo.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kujua idara ina mkakati upi kuondoa changamoto hizo zilizoainishwa?

Majibu ya Menejimenti

Ujenzi wa mashimo ya kuchomea taka pamoja na utupaji wa kondo la nyuma la mama anapomaliza

kujifungua unaendelea kwenye vituo mbalimbali visivyokuwa na huduma hiyo kwa kutumia fedha za

uchangiaji na RBF. Aidha suala la utupaji wa kondo pamoja na mifuko ya nailoni si sahihi, menejimenti

itaendelea kutoa maelekezo ya utupaji sahihi.

25

3.4.2 Mfumo wa Maji SafiUhakiki wa timu umeonesha kuwa vituo vya Fumagila, Igoma, Makongoro, Bugarika vina mifumo

thabitiyamajisafina taka.Aidha,pamojanahospitaliyaNyamaganakuwanamfumowamajiya

MWAUWASA, kuna ukosefu wa mifumo ya kuhifadhi maji. Pia zahanati ya Shadi ilionekana kukatiwa

maji tangu mwezi wa tano ambapo ankara ya maji waliyopewa ya laki mbili haikuwa inaakisi matumizi.

Aidha katika vituo vingine mifumo ya kuhifadhi maji haikuwa na maji kabisa jambo linaloweza kuathiri

usalama na afya wa watoa na watumia huduma.

Hoja ya Timu

Timu ilingependa kujua mkakati uliopo kufunga mfumo wa uhifadhi maji Hospitali ya Nyamagana na

kurejesha maji katika kituo cha Shadi ambacho kimekatiwa maji.

Majibu ya Menejimenti

Maji ni muhimu sana hususani kwenye taasisi zinazohusika na kutoa huduma za kijamii, Idara

inahakikishavituovyakevyotevinafikiwanahudumayamajikwakushirikishaofisiyaMhandisiwa

Maji wa Jiji. Aidha hospitali inarekebisha mifumo yake ya maji na kwa na tanki za kuhifadhi.

Kushoto: Mifuko ya nailoni ikiwa imetupwa katika shimo la kutupia kondo la uzazi kinyume na utaratibu, zahanati ya SahwaKulia: Wajumbe wa timu ya SAM pamoja na mtoa huduma katika kituo cha Igoma wakihakiki ubora wa kichomea taka

26

3.4.3. Hali ya Vyoo na Usafi wa MazingiraUhakiki wa timu katika vituo vilivyotemebelewa umeonesha uwepo wa vyoo na hali ya usafi kwa

sehemu kubwa inaridhisha isipokuwa miundombinu inahitaji maboresho. Mfano; Milango ya vyoo vya

zahanati ya Fumagila. Timu inaipongeza idara na vituo kwa kuboresha mazingira ya vyoo.

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti inapokea pongezi hizo na kuahidi kuboresha huduma za vyoo sio kwa vituo vya kutolea

huduma tu bali hata ngazi ya kaya ili kuhakikisha wilaya haipati magonjwa ya mlipuko yakiwemo

kipindupindu na kuhara.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa ufafanuzi na inapongeza kwa mkakati wa kufika ngazi ya kaya. Itaendelea

kufuatilia utekelezaji wa mkakati huo.

3.4.4 Ujenzi na Ukarabati wa Majengo na miundombinu ya barabaraUhakiki wa timu vituoni umeonesha kuwa hospitali ya Nyamagana inahitaji mkakati maalumu ili

kuboresha wa miundombinu pamoja na majengo kwa kuwa majengo mengi hayakidhi hadhi ya hospitali.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kujua mkakati uliopo ili kuboresha hospitali ya wilaya.

Majibu ya Menejimenti

Hospitali ya wilaya haikidhi vigezo, hii inatokana na kuhuishwa kutoka kituo cha afya kuwa Hospitali

mwaka 2007. Hali hii inapelekea kukosekana kwa miundombinu ya msingi ikiwemo jengo la utawala,

wodi ya wanaume, jengo la kuhifadhia maiti na mengineyo. Aidha, Idara inaendelea kuboresha

miundombinu hiyo kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali, shukrani ziwaendee AGPAHI wanaojenga

jengo la kinamama na jengo la huduma za upasuaji.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa ufafanuzi na itaendelea kufuatilia utekelezaji wa mikakati hiyo.

Wajumbe wa timu ya SAM wakifanya

uhakiki wa wa hali ya vyoo katika

zahanati ya Fumagila wilayani

Nyamagana

27

3.4.5 Nyumba za WatumishiUhakiki wa timu katika vituo vilivyotembelewa umebaini kuwa baadhi ya zahanati hazina nyumba

za watumishi, na zilizopo zinahitaji ukarabati. Katika zahanati ya Mkolani, timu iligundua kuwa kuna

nyumba moja ya watumishi japo anayeishi si mtumishi wa kituo hicho kwani alihamishiwa hospitali ya

Nyamagana. Vilevile, nyumba hiyo inahitaji ukarabati.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kupata ufafanuzi ikiwa mtumishi wa kituo kingine anaweza kuishi katika nyumba za vituo

vingine. Pia, usimamizi wa nyumba na mtumishi huyo uko chini ya mfawidhi wa kituo kipi?

Majibu ya Menejimenti

Wilaya ina uhaba wa nyumba za watumishi kwa zaidi ya 80%, hali inayopelekea watumishi kupanga

aukutumiagharamakubwakufikakwenyevituovyaovyakutoleahuduma.Aidha,wilayainaendelea

na mkakati wa kujenga nyumba za watumishi. Suala la mtumishi wa hospitali anayeishi katika nyumba

yazahanatiyamkolani;ofisiinalifanyiakazi.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa ufafanuzi na inashauri halmashauri iendelee kuhakikisha ujenzi wa nyumba

unatekelezwa ili kuboresha mazingira ya kazi vituoni.

3.4.6 Nishati ya UmemeUhakiki wa timu umeonesha uwepo wa nishati ya umeme na unafanya kazi katika vituo vingi

vilivyotembelewa isipokuwa zahanati ya Shadi.

Pongezi

Timu inaipongeza idara na vituo kwa kuhakikisha uwepo wa nishati ya umeme na inafanya kazi katika

maeneo mengi.

Majibu ya Menejimenti

Idara imepokea pongezi hizo na inaendelea kuhakikisha vituo visivyo na umeme mfano zahanati ya

Shadi vinafungiwa umeme na taratibu zinaendelea kwa sasa.

28

3.4.7 Usalama na Utulivu katika Vituo vya kutolea HudumaKatika zahanati ya Buhongwa imeonekana jamii kuingilia eneo la zahanati kwa kukata wigo na kuhifadhi

matenga ya nyanya na vifaa vya biashara. Hali hii inaweza kuondoa utulivu na kuhatarisha usalama

katika zahanati.

Hoja ya Timu

Timu ilipenda kufahamu mkakati uliopo usalama na utulivu katika vituo vya kutolea huduma unakuwepo

Majibu ya Menejimenti

Menejimenti itawasiliana na uongozi wa serikali za mitaa na kamati za vituo kuhakikisha vituo vinakuwa

kwenye hali ya usalama muda wote na maeneo ya vituo yanalindwa na kuheshimiwa.

Maoni ya Timu

Timu inashukuru kwa dhamira iliyooneshwa ila inapenda kushauri suala la wafanyabiashara wa nyanya

katika kituo cha Buhongwa linashughulikiwa kwa haraka.

Diwani kutoka kata ya Mhandu wilayani Nyamagana Mh. Sima Constantine akichangia jambo katika mkutano wa Madiwani wakati wa utekelezaji wa zoezi la SAM

29

4.0 Mapendekezo

Timu ya SAM imetoa mapendekezo yafuatayo;

1. Kuimarisha Mifumo ya Uwajibikaji: Kwa kuwa mfumo wa SAM unaakisi vizuri namna ya kusimamia

mzunguko wa mipango na bajeti wa serikali, timu ya SAM inapendekeza mamlaka na vyombo vya

usimamizi vya Jiji kuanza mchakato wa kutumia mfumo huu ili kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi

wa rasilimali za umma na huduma zitolewazo kwa umma.

2. Kuboresha Uandaaji wa Mipango na Ripoti za afya kama vile mpango kabambe wa afya wa wilaya

na vituo, ripoti za utekelezaji na fedha n.k.

3. Kuimarisha usimamizi katika vituo ili kuweza kugundua changamoto zilizoko na kuzipatia ufumbuzi

kwa wakati.

4. Kuboresha majengo na miundombinu mingine ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za uzazi

kwa jamii.

Sehemu ya Nne

30

4.1 Maazimio ya PamojaMaazimioyaliyofikiwakwapamojanawadauyalilengakuboreshamaeneoyaliyobainishwana timu

kwa idara na halmashauri kuyafanyia kazi ikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuboresha upatikanaji

wa huduma ya afya kwa Mama, Baba na Mtoto.

Jedwali 2: Maazimio ya UtekelezajiNa Azimio Utekelezaji Muhusika1 Kuboresha Uandaaji na

Uandishi wa NyarakaKuongeza umakini wakati wa uandaaji wa nyaraka mbalimbali kwa kuzingatia miongozo na kanuni ili kuondoa kasoro zilizobainishwa na timu ya SAM katika mipango ijayo.

CHMT

CMT

2 Kuboresha Mifumo ya Uwajibikaji, Usimamizi na Uangalizi

Kuweka kufuli mbili kwenye masanduku ya maoni, Kubandika wa taarifa kwenye mbao za matangazo kwa ajili ya umma (bajeti za vituo, majina ya wajumbe wa kamati, majina na namba za simu za waganga wafawidhi) ili kukuza utawala bora katika ngazi zote.

CHMT

HGGC

DHSB

Kamati ya huduma za Jamii na Baraza la Madiwani

3 Mwingiliano wa shughuli za jamii na vituoni

Kumaliza Changamoto ya muingiliano wa jamii/wafanyabiashara katika zahanati ya Buhongwa kwa kushirikisha uongozi wa mtaa, kata na jamii.

WEO Buhongwa

4 Kuimarisha Usimamizi Shirikishi

Kutoa taarifa juu ya mwenendo wa huduma na maadili ya watoa huduma na watumia huduma kwa kuzingatia miongozo inayobainisha wazi haki na wajibu wa watoa na wapokea huduma kwa ngazi zote.

CHMT

HGGC

DHSB

5 Kufuatilia na kufanyia kazi madai na stahili mbalimbali za watumishi

Kufuatilia, kufanyia kazi na kulipa stahiki mbalilimbali za watumishi ili kuimarisha ufanyaji kazi bila kuathiri ari ya watumishi.

CHMT

31

6 Kuboresha mafunzo kazini kulingana na mahitaji

Kutoa mafunzo kazini kulingana na mahitaji pamoja na upatikanaji wa fedha au wadau mbalimbali wanaofanya kazi na Jiji.

CHMT

7 Kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba

Kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vituoni.

CHMT

Hospitali

Vituo vya afya

Zahanati

8 Uboreshaji wa miundombinu ya kuhifadhia dawa

Vituo kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji kuweka mikakati na mipango kwa mwaka 2019/20 kuboresha miundombinu ya kuhifadhia dawa ikiwa ni pamoja na vyumba na makabati ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba katika vituo.

CHMT

Hospitali

Vituo vya afya

Zahanati

9 Mkakati wa kupata magari kwa ajili ya huduma za afya

Idara kushirikiana na Jiji kuweka kwenye mipango ya 2019/20 kupata magari hasa sehemu ya utawala na vituo vya afya ili kuimarisha utaratibu wa huduma haswa wagonjwa/kina mama wajawazito na hata kuwapeleka rufaa.

CMT

CHMT

Hospitali

Vituo vya afya

Zahanati

10 Kuwashirikisha viongozi wa mitaa

Kuwaandikia barua yenye kuwataka viongozi wa mitaa/vijiji, kuimarisha ushiriki na ushirikishwaji wa jamii katika maswala ya afya ya uzazi.

CHMT

WEOs

32

4.2 HitimishoUtekelezwaji wa zoezi la SAM kwa Jijila Mwanza ulianza kwa kupitia hatua mbalimbali na umekamilika

katika sehemu yake ya kwanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana na ushirikiano uliotolewa na

viongozi wa wilaya, jiji, Aga Khan Faundation na wadau wote wa afya. Ni jambo linalotia faraja kwa

wadau wote kuonyesha mwamko wa kuboresha huduma za afya ya Mama, Baba na Mtoto. Hivyo ni

matumaini makubwa kwamba changamoto na mapendekezo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi kwa wakati

naIdarayaAfyanawadauwenginekamailivyoafikiwakatikakikaochandaninakilechamrejesho

kwa wadau wa afya. Utekelezaji wa maazimio kwa wakati utachangia katika kuboresha upatikanaji wa

huduma za afya hasa huduma za afya ya mama, baba na mtoto. Vilevile, utekelezaji utaipa nguvu timu

ya SAM na jamii nzima ya Nyamagana kushiriki kikamilifu katika kuboresha huduma za afya katika

maeneo yao.

33

Kiambatanisho 1Vituo vilivyotembelewa na timu ya SAM

1. Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana

2. Kituo cha Afya Igoma3. Kituo cha Afya Makongoro4. Zahanati ya Bugarika5. Zahanati ya Buhongwa6. Zahanati ya Fumagila7. Zahanati ya Mkolani8. Zahanati ya Sahwa9. Zahanati ya Shadi

Kiambatanisho 2

Wajumbe wa Timu ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UJJ) /SAM-2018Na JINA JINSIA UWAKILISHI1 ADAM H. MALUZUKU ME WEO - BUHONGWA2 ADELFINA E MWENURA KE MWAKILISHI JAMII3 EDITH JOHN KE CHMT

4 EDWARD MISALABA ME MWAKILISHI JAMII5 FARIDA MZIMBIRI KE TAHEA MWANZA6 FORTUNATA SWAI KE CMT7 GERMINA P. KABOLA KE DIWANI8 IBRAHIM N. ENOCK ME CHAWATA9 NATUS MAGORI ME M/KITI BODI YA AFYA10 NYEMBE ROBERT NYEMBE ME M/KITI ZAHANATI SAHWA11 PENDO PASCHAL KE VIKUNDI WANAWAKE12 SAPHIA RAMADHAN KE MWAKILISHI JAMII13 VICENT L.TEGGE ME MADIWANI14 WINFRIDA PETER KE MWAKILISHI JAMII15 YUSTO A. KEMBO ME KAMATI YA AFYA KATA

Sikika inafanya kazi ya kuhimiza uboreshaji wa mifumo ya afya na

usimamizi wa fedha kupitia uwajibikaji jamii na uraghibishi

katika ngazi zote za serikali

Nyumba Na.69Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 26 663 55/57

Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania. Simu: 0262321307 Nukushi: 0262321316

Ujumbe mfupi: 0688 493 882 Nukushi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.sikika.or.tzTwitter: @sikika1Facebook: Sikika1Instagram: Sikika1