133
1 Simulizi katika mtiririko kama wa kitambaa kilichofumwa vizuri Kuwawezesha wanawake kuelezea simulizi za Mungu zinazosisimua juu ya upendo na tumaini

StoryTapestry Manual - Swahili

Embed Size (px)

DESCRIPTION

The StoryTapestry Manual in the Swahili language.

Citation preview

Page 1: StoryTapestry Manual - Swahili

1

Simulizi katika mtiririko kama wa kitambaa kilichofumwa vizuri

Kuwawezesha wanawake

kuelezea simulizi za Mungu zinazosisimua

juu ya

upendo na tumaini

Page 2: StoryTapestry Manual - Swahili

2

Shukurani

Tunapenda kuwashukuru watu wengi waliowezesha kukamilika kwa kitabu hiki cha mwongozo.

Carol Green

Jon Haahr

Sarah Haahr

Bob Mahone

Kevin Manous

Marcia Meyer

Beth Smith

Tricia Stringer

Sarai Torme

Page 3: StoryTapestry Manual - Swahili

3

YALIYOMO

1. Uumbaji hadi Kanisa*2. Ulimwengu wa Roho3. Uumbaji*4. Ukaidi/Uasi*5. Mwito wa Ibrahimu*6. Sara aahidiwa mtoto wa kiume7. Imani ya Ibrahimu yajaribiwa*8. Kupakwa Mafuta kwa Daudi 9. Daudi na Bethsheba10. Simulizi ya Nathani11. Ahadi*12. Malaika anawatembelea Mariamu na Yosefu**13. Kuzaliwa kwa Yesu**14. Ubatizo wa Yesu**15. Mwanamke Kisimani**16. Binti wa Yairo na Mwanamke aliyetokwa na Damu**17. Yesu awalisha 5000**18. Viongozi wa Dini wenye wivu**19. Mwanamke Mwenye Dhambi Asamehewa**20. Njama na karamu wa Mwisho**21. Yesu Asalitiwa**22. Mashtaka ya Yesu) Yesu ashtakiwa mbele ya hakimu**23. Yesu Achukua Msalaba Wake na Asulubiwa**24. Kufufuka kwa Yesu**25. Baada ya ufufuo26. Roho wa Mungu27. Mwafrika28. Paulo akutana na Yesu29. Petro aponya na kumfufua Tabitha kutoka kwa wafui30. Mwanamagereza Mfilipi31. Kurudi

*Simuliza za utangulizi kutoka Agano la Kale Magdalena: Afunguliwa toka katika Aibu

**Simulizi kutoka Magdalena: afunguliwa toka katika Aibu © 2006 Inspirational Films, Inc.

Zimetolewa na kusambazwa na Nardine Productions. Haki zote zimehifadhiwa

http://www.magdalenatoday.com Simulizi Inaanza

Page 4: StoryTapestry Manual - Swahili

4

Mwonekano

Uumbaji hadi Kanisa

Hapo mwanzo kabla wakati haujaanza, kulikuwa na Mungu wa Kweli mmoja tu. Alipoongea, aliuumba ulimwengu, mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo. Kisha Mungu akaamua kufanya uuambaji Wake maalumu, mwanaume na mwanamke. Mwanaume na mwanamke walikuwa na mahusiano mema/safi na Mungu. Walitembea na kuongea Naye.

Lakini siku moja, mwanamme na mwanamke hawakumtii Mungu, na ule uhusiano wao safi na Mungu ukaharibika. Ulimwengu wote ulilaaniwa kutokana na kutotii kwao. Mwanamume na mwanamke wakawa na na uzao mwingi, na matokeo yake ulimwengu wote ukajazwa. Watu waliendelea kutokumtii Mungu lakini Mungu hakuwasahau.

Siku moja, Mungu alisema/aliongea na mtu aliyeitwa Ibrahimu. Mungu alimwambia Ibrahimu, “Nitakwenda kukupa wazao wengi kuliko zilivyo nyota za angani. Nitawafanya kuwa taifa kubwa. Nao wataitwa watu wangu, nao watakuwa baraka kwa ulimwengu wote”. Ijapokuwa Ibrahimu alikuwa mzee, alimwamini Mungu. Mungu alitimiza ahadi yake na Ibrahimu akapata mtoto wa kiume. Kupitia mwanaye, Ibrahimu akawa na uzao mwingi. Wakawa taifa kubwa, kama Mungu alivyosema. Lakini watu waliendelea kutomtii Mungu na wakatengana naye.

Mungu alimtuma mjumbe kwa watu wake aliyeitwa Isaya. Isaya aliwaambia watu wale juu ya ‘mkombozi aliyeahidiwa’ ambaye siku moja angekuja. Isaya alisema, “Sisi wote tumetenda dhambi dhidi ya Mungu. Siku moja, mkombozi atakuja ambaye atateswa na kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Kisha Mungu atamrejezea uzima tena, naye ataishi milele. Watu wote watakaomwamini imani yao kwake watasamehewa dhambi zao na wataishi katika uhusiano safi/mwema/mkamilifu na Mungu milele”.

Hatimaye, kama Mungu alivyosema, mkombozi Yule aliyeadiwa alikuja. Alikuwa wa ukoo wa Ibrahamu. Jina lake aliitwa Yesu na alikuwa mkamilifu katika namna zote. Aliponya wagonjwa, alitoa pepo wachafu, na kutenda miujiza. Baadhi ya watu walimfuata Yesu, lakini wengine hawakumfuata. Yesu aliwaambia watu, “Natoa uzima wa milele kwa kila anayenifuata na hakuna atakayeweza atakayewanyang’anya toka kwangu kwa sababu Mungu na mimi tu wamoja/sawa.

Si kila mtu alipendezwa na kile ambacho Yesu alisema na kufanya. Wale ambao hawakumwamini Yesu walimfanya akamatwe, apigwe na kisha kuuawa. Yesu aliteseka na kufa, kama Mungu alivyosema atatendewa. Lakini pia, kama Mungu alivyosema Yesu alikuwa hai tena. Alitembea na kuongea, na kula pamoja na wafuasi wake ili kuthibitisha kuwa hai kwake. Na aliahidi kuwatumia Roho wa Mungu ili kuwafariji na kuwaongoza. Kisha Mungu alimtwaa Yesu kwenda mbinguni.

Page 5: StoryTapestry Manual - Swahili

5

Kama vile Yesu alivyoahidi, alimtuma Roho wa Mungu kukaa ndani yao wale waliomwamini Yeye. Watu walijionyesha kuwa wafuasi wake kwa ishara ya kuoshwa kwa maji ili kuonyesha kwamba wamebadilishwa mioyo na maisha yao. Walikusanyika pamoja. Waliomba na kuabudu pamoja. Walijifunza mafundisho yake na kusaidiana katika mahitaji yao. Waliyakumbuka maisha ya Yesu kwa kusikiliza simulizi na kufuata mafundisho Yake. Na waliwashikisha simulizi hizo na watu wote waliokutana nao. Leo hii, wafuasi wa Yesu wanaendelea kufanya mambo hayo yote na wanasubiri siku ile ambapo Yesu atakuja kuwachukua ili wakaishi pamoja Naye milele.

Page 6: StoryTapestry Manual - Swahili

6

Ulimwengu wa Roho

Maandiko ya Msingi

Ayubu 39:4-7; Zaburi 103:20-21; Zaburi 148:2, 5;

Mathayo 9:34; Mathayo 25:41; Yohana 1:1,2;

Waefeso 6:11, 12; 1Timotheo 1:17; 2Timotheo 3:16;

Yakobo 2:19; 2Petro 2:4; Yuda 6

Hii ni simulizi ya kweli inayoanzia mwanzo wa wakati. Tunajua juu ya mambo hayo, kwa sababu Mungu aliwaambia watu juu yake hapo zamani kupitia wasemaji wake.

Hapo mwanzo kabisa, kabla ya kitu cho chote kuwepo, Mungu alikuwepo. Amekuwepo siku zote tangu milele.

Aliumba viumbe visivyoonekana kwa macho kuwa watumishi wake. Wanaitwa malaika.

Viumbe hawa roho/wasioonekana walimsifu Mungu na walifuata amari zake.

Waliimba kwa furaha pale Mungu alipoumba ardhi na nchi, kuifanya kamilifu namna alivyotaka.

Kuna kipindi fulani viumbe hawa roho waligeuka kuwa waovu. Hawakuzifurahia nyadhifa walizopewa na Mungu. Walikosa utii dhidi ya Mungu na mambo yote mazuri aliyowapa Mungu.

Viumbe hawa wakaidi wakawa roho wachafu tunawajua kama mapepo au mashetani wabaya. Mmoja kati hao anaitwa Shetani, ni mtawala wa wengine wote.

Roho hawa wabaya wanaendelea kutenda kazi kinyume na yale Mungu anayofanya hapa duniani, na kinyume na wale wanaozifuata njia za Mungu.

Mungu alitamka hukumu juu ya hawa roho wabaya wote. Alisema, siku moja wataadhibiwa katika moto wa milele.

Page 7: StoryTapestry Manual - Swahili

7

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kuzingatia

Roho

Viumbe roho vilivyoumbwa na Mungu.

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Malaika

Ukaidi/kutokutii

Roho chafu

Shetani

Wasemaji

Mtazamo wa walimwengu

Wengi wa watazamaji wengi wa ulimwengu wataitazama simulizi hii kuwa ni ya kubuniwa (ya uongo). Hakikisha kuwa haieleweke (kutambulika) katika mtazamo huo.

Muundo na Simulizi

Simulizi hii imefupishwa kutoka vifungu mbalimbali vya maandiko katika Agano la Kale na Jipya.

Neno roho katika vifungu vilivyomo katika utangulizi huu halitakiwi kuchanganywa na Roho wa Mungu.

Simulizi hii inaelezea wapi Shetani alikotokea. Kama unafanya kazi katika jamii ya Kihindu, Kibudha, au ulimwengu wa kianimist, simulizi hii itakuwa ni nzuri kuifanyia kazi. Kama unafanya kazi katika lugha ambayo filamu haina tafsiri, itakuwa vema kuiacha kabisa filamu hii.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu ni Muumbaji wa kila kitu; Mungu ni mzuri katika kila jambo analolifanya.

Page 8: StoryTapestry Manual - Swahili

8

Uumbaji

Mwanzo 1:1-28; 31; 2:2, 3, 7-9, 15-18, 21-25

Imetumia tafsiri ya Biblia ya NLT

Mwanzo 1:1-27

Hapo mwanzo alikuwako Mungu. Alitamka, na alipofanya hivyo, aliumba ulimwengu wote na vyote vilivyomo/vilivyo ndani yake. Mungu alifanya nuru (mwanga) na maji. Alitengeneza nchi kavu na aina zote za mimea na miti. Mungu alitengeneza jua, mwezi na nyota. Aliumba aina zote za samaki, ndege na wanyama. Kisha Mungu aliwaumba watu, aliwafanya kwa mfano wake mwenyewe.

Mwanzo 2:7-9, 15

Mungu aliunda mwili wa mwanaume kutoka udongo wa ardhini na akampulizia pumzi na akaanza kuishi. Kisha Mungu akamweka mwanaume katika bustani ya miti ya matunda. Mungu alipanda aina zote za miti katika bustani. Ilikuwa miti mizuri ambayo ilizaa matunda matamu sana. Kati kati ya bustani aliweka miti miwili – mti ambao ulitoa uzima na mti ambao ulitoa ufahamu wa mema na mabaya.

Mwanzo 2: 16, 17

Mungu alimwambia mwanaume, Adamu, “Unaweza kula tunda lo lote katika bustani isipokuwa tunda kutoka mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Iwapo utakula matunda ya mti huo, utakufa.”

Mwanzo 2:18, 21-25

Mungu akasema si vema mtu awe peke yake. Kwa hiyo Mungu akamsababishia Adamu usingizi kulala mzito. Akachukua mmoja wa ubavu wa Adamu na akamfanya mwanamke kutoka kwenye ubavu huo na akamleta kwa Adamu. “Hatimaye!” Adamu kwa mshangao/furaha akatamka, “Anayo nyama na mifupa kama mimi!” Adamu na mkewe, Hawa, walikuwa uchi, lakini hakuna kati yao aliyeona haya. Walikuwa na uhusiano mzuri na Mungu.

Mwanzo 1:28, 31

Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke/jiongezeni na kuwa watawala juu ya samaki, ndege na wanyama wote”. Kisha Mungu akayaangalia yote aliyoyatengeneza, na akaona kwamba ni mema katika namna zote. Mungu aliuumba ulimwengu na vyote vilivyo ndani yake kwa siku sita.

Page 9: StoryTapestry Manual - Swahili

9

Mwanzo 2:2, 3

Siku iliyofuata, siku ya saba, Mungu aliacha kufanya kazi. Mungu aliitenga siku moja katika juma kwa ajili yake kwa sababu alikuwa amemaliza uumbaji wa ulimwengu.

Page 10: StoryTapestry Manual - Swahili

10

Maneno/Vifungu vya Maneno vya Kuzingatia

‘nyama na mifupa kama mimi’

Kifungu hiki kinarejea Adamu alipokuwa akitamka kwa furaha kwamba hatimaye amempata mtu kama yeye mwenyewe. Inaachana kidogo na wazo halisi la matamshi ya kiebrania ya, ‘nyama katika nyama yangu, mfupa katika mfupa wangu.’

‘Njema sana ( kwa kila hali)’

Mungu alipoona uumbaji wake kuwa ni ‘mzuri sana katika hali zote’, inaonyesha kwamba ilikuwa ni ya kuridhisha kwa Mungu – aliamua kuwa ni njema na iliyofaa kwa kusudi lake.

Angalia Faharasa kwa ajili ya;

Barikiwa

Uhusiano

(Mtazamo wa ulimwengu) Halisia

Uwe na hakika kuwa neno “Uchi” lililotumika hapa lipo sahihi. Kwa baadhi ya tamaduni; ni vizuri zaidi kusema, (‘walikuwa utupu)

Umahiri wa Simulizii

Waongeaji wengi wanaona kuwa ni vigumu kukumbuka ‘orodha’ ya siku saba za uumbaji katika kitabu cha Mwanzo 1.

Mwanzo 1 kwa hakika ilikuwa kama utenzi hata hivyo.

Mwanzo 2 inarejea kusimulia hadithi ya uumbaji katika namna (mtindo wa) ya simulizi. Mwanzo 1 imeandikwa kwa ufupisho. Hadithi imechukuliwa zaidi katika Mwanzo 2. Inaonekana ni rahisi watu kukumbuka hadithi inapokuwa imeelezewa namna hii.

Majina ya mito katika Mwanzo 2 yameachwa kwa ajili ya urahisi wa kurudia simulizi. Hata hivyo, iwapo kundi la watu wanaipenda mito kwa sababu fulani, basi ijumuishwe.

Mwanzo 2:3 maneno yaliwekwa mengine ili kufanya iwe rahisi kuyaelewa na kupunguza ugumu wakati wa kutafsiri. Kwa mfano, badala ya kusema Mungu alizifanya siku ya saba ‘takatifu’, imeieleza kama ni ya kujitenga.

“Mti wenye ujuzi wa mema na mabaya ni jina linaloonyeshs tendo, ili kwamba waliohudhuria (hadhara) waweze kuelewa zaidi kusudi kamili la mti.

Page 11: StoryTapestry Manual - Swahili

11

KanuniTabia na kawaida ya Mungu

Muumbaji; Anahusiana ana nguvu za kubariki

Kanisa

Kutenga siku ‘maalumu’, kuikabidhi kwa Mungu ambayo inaweka msingi wa Kanisa.

Page 12: StoryTapestry Manual - Swahili

12

Kukaidi

Mwanzo 3:1-19a, 21-24

Imetumia tafsiri ya: NLT

Mwanzo 3:1-5

Basa nyoka alikuwa mwerevu kupita wanyama wote Mungu aliowafanya. Shetani alimwingia nyoka na akamuuliza Hawa, “Hivi kweli Mungu alisema msile matunda yoyote katika bustani?” “Hakika tunaweza kula haswa,” Hawa alimwambia. “isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ndio haturuhusiwi kula. Mungu anasema tusiule wala tusiuguse au sivyo tutakufa” “Hamtakufa!” nyoka alifoka. “Mungu anajua kwamba mtakapokula tunda hili mtakuwa kama yeye, mkijua kila kitu, mema na mabaya.

Mwanzo 3:6, 7

Hawa alishawishika. Tunda lilionekana zuri na tamu, na lingemfanya kuwa na hekima! Kwa hiyo akala sehemu ya tunda. Akampa sehemu mme wake, ambaye alikuwa pamoja naye. Adamu akala pia. Wakati huo, kitu fulani ndani yao kilibadilika; ghafla walijisikia aibu kwa kuwa wako utupu Kwa hiyo wakashona majani na kuyavaa ili kuufunika uchi wao.

Mwanzo 3:8-18

Kuelekea nyakati za jioni, Adamu na Hawa walimsikia Mungu akitembea bustanini, kwa hiyo wakajificha kati ya miti. Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?” Adamu akajibu, “nilikusikia, kwa hivyo nikajificha. Niliogopa kwa sababu niko uchi.” “Ni nani aliyekuambia kwamba uko uchi?” Mungu aliuliza. “Je, umekula matunda niliyokuamuru usile”? “Ndio,” Adamu akakiri, “lakini ni mwanamke uliyenipa ndiye aliyeniletea tunda na nikalila. Kisha Mungu akamuuliza Hawa, “Umewezaje kufanya jambo kama hilo?” “Nyoka alinilaghai,”akajibu. Ndiyo maana nikalila.

Mwanzo 3:14, 15

Hivyo Mungu akamwambia nyoka, “Kwa sababu umefanya hivi, utaadhibiwa. Utatambaa katika mavumbi muda wote utakaoishi. Kuanzia sasa, uzao wako na uzao wa mwanamke watakuwa maadui. Utamuuma katika kisigono, lakini yeye atakuponda kichwa.”

Mwanzo 3:16 – 19a

Kisha Mungu akamwambia Hawa, “Utazaa watoto kwa maumivu makali na mateso.” Mungu akamwambia Adamu, “Kwa sababu umekula matunda niliyokuamru usiyale, nimeweka laana

Page 13: StoryTapestry Manual - Swahili

13

juu ya ardhi. Maisha yako yote utasumbuka/utaishi kwa taabu ili kuishi kutokana na hiyo. Nchi itazaa miiba na mbigili. Utazalisha chakula kwa kutoa jasho hadi kufa kwako.

Mwanzo 3:21-24

Kisha Mungu akasema, Sasa watu wanajua kila kitu, mema na mabaya. Itakuwaje kama watakula matunda kutoka katika mti wa uzima? Kisha wakaishi milele! Hiyo Mungu akawatoa Adamu na Hawa nje ya bustani na akawazuia wasirudi kwenye mti unaotoa uzima.

Page 14: StoryTapestry Manual - Swahili

14

Maneno/Vifungu vya maneno ya kuzingatia

Laana

Neno hili katika kifungu hiki, linamaanisha adhabu, hukumu, au kitu fulani kisichokizuri kinakwenda kumtokea mtu. Lugha nyingi zina namna ya kutamka laana kwa mtu au kitu, kwa hiyo uwe na hakika neno unalochagua halina pendekezo la namna yoyote ya mazingaombwe.

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Wazao

Uovu/Ubaya

Busara/Hekima

(Mtizamo wa kidunia – ki – ulimwengu)

Baadhi ya watu wanaweza kuabudu nyoka, kwa hiyo ni muhimu kwamba nyoka akaonekana kama ‘mtu mbaya’ katika simulizi hii.

Baadhi ya makundi ya watu wameisikia simulizi hii, lakini hawaamini kama kweli ilitokea kwa sababu mnyama anaongea. Wanadhani hii ni hadithi ya kubuni ya wanyama zaidi au ngano za kienyeji. Karibu wanazuoni wasomi wote wa Biblia wanakubali kwamba nyoka ni Shetani kwa kuzingatia nukuu kama vile Ufunuo 12:9; 20:2; 2Korintho 11:3. Ikiwa kutahitajika uelewa zaidi, mfano unaweza kuongezwa katika simulizi kwamba nyoka ni Shetani.

Mwambatano wa simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: mema na mabaya, utupu, Shetani, hekima na wazao yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia

Umahiri wa Simulizi

Simulizi inakuwa rahisi kuielezea iwapo maneno adhabu/laana yamerahisishwa.

Wazo la mwanamke kumtamani mwanamme na mwanamme kumtawala mwanamke limeachwa kwa sababu ni gumu kwa wasikilizaji wengi kulielewa. Kwa sababu hizo hizo, kufukuzwa kwa mwanamme na mwanamke kutoka bustanini kumerahisishwa.

KanuniTabia na kawaida ya Mungu

Anajua yote; amejitenga na uovu na dhambi; hupinga dhambi na uovu; ni wa haki; Anayeadhibu dhambi na ukaidi, hujenga mahusiano/anahusiana.

Hakika ya Wokovu

Msingi uliwekwa kwa kuweka uadui kati ya mwanadamu na Shetani kwa ‘mwanadamu’ kuwa mshindi.

Page 15: StoryTapestry Manual - Swahili

15

Maisha ya Uchaji

Msingi uliwekwa kwa mwanadamu kutembea na kuongea na Mungu na Mungu kutembea na kuongea na mwanadamu.

Maombi

Huonyesha Mungu na mwanadamu wakuwasiliana

Page 16: StoryTapestry Manual - Swahili

16

Mwito wa Ibrahimu

Mwanzo 12:1-7; 15:1-6

Imetumia tafsiri ya Biblia: NLT

Badiliko:

Kwa sababu ya ukaidi wa Adamu na Hawa, uhusiano wao na Mungu ulivunjika. Hata hivyo, Mungu hakuusahau uumbaji wake maalumu. Miaka mingi ilipita na Mungu akamchagua mmoja katika uzao wao, aliyeitwa Ibrahimu. Hii ni simulizi ya Abrahamu.

Mwanzo 12:1-3

Mungu akamwambia Ibrahamu, “Toka wewe katika nchi yako, na ukoo/ndugu zako, na nyumba ya baba yako, uende mpak nchi nitakayokuonyesha.” Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kukufanya maarufu ; nawe utakuwa baraka,jamaa zote zilizo duniani zitabarikiwa kupitia wewe.

Mwanzo 12:4-6

Hivyo Ibrahimu akaondoka kama alivyoelekezwa. Ibrahimu alikuwa mzee sana alipoondoka nyumbani kwao. Alimchukua mke wake Sara na mali zake zote- mifugo yake na watu wake wote aliokuwa akiishi nao katika nyumba yake na akaelekea kwenye nchi ambayo Mungu angemwonyesha. Walipofika huko, Ibrahimu alisafiri kupitia nchi ile. Hatimaye aliposimama; aliweka kambi kando ya mti mkubwa.

Mwanzo 12:7

Kisha Mungu akamtokea Ibrahimu na kusema, “Nitawapa kizazi chako nchi hii.” Ibrahimu akamwabudu Mungu aliyemtokea.

Mwanzo 15:1-3

Baada ya muda fulani, Mungu aliongea na Ibrahimu katika maono na akamwambia, “Usiogope, nitakulinda, na utapata zawadi kubwa.” Lakini Ibrahimu alijibu, “Ee Mungu, kuna raha gani kupata baraka zote hizo ikiwa mimi sina mwana wa kiume ? Kwa vile hujanipa watoto, mtumishi wa nyumbani mwangu atarithi utajiri wangu wote. Hujanipa uzao wangu mwenyewe, kwa hiyo mmoja wa watumishi wangu atakuwa mrithi”

Mwanzo 15: 4, 5

Kisha Mungu akamwambia Ibrahimu, Hapana, mtumishi wako hatakuwa mrithi wako, kwa kuwa utapata mwana wa kiume wa kwako mwenyewe ambaye atakuwa mrithi wako.” Mungu akamchukua Ibrahimu nje na akamwambia, “Tazama angani na uhesabu nyota kama utaweza. Hivi ndivyo wingi wa uzao wako utakavyokuwa.

Mwanzo 15:6

Ibrahimu akamwamini Mungu, na kwa sababu ya hiyo, Mungu akamhesabia kuwa na uhusiano mzuri naye.

Page 17: StoryTapestry Manual - Swahili

17

Maneno/Vifungu vya Kuzingatia

Uadilifu/Uhusiano sahihi

Katika Agano la Kale wazo la uadilifu limetokana na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, au kati ya mwanadamu na mwanadamu. ‘Uadilifu’ unaelekeza kwenye utakatifu. Katika Toleo la kingereza cha kisasa (CEV) dhana hiii inatafsiri katika Isaya 53:11katika namna ifuatayo: Ataadhibiwa kwa ajili ya dhambi za wengine, ili kwamba wengi wao wasiwe na hatia tena. Kwa maneno mengine, ‘uadilifu’ huondoa hatia.

Angalia Faharasi kwa ajili ya:

Kusadiki /kuamini Imani/ Bariki/Barikiwa/Kubariki; Ukaidi/uasi; na Kuabudu

Mtazamo wa kidunia

Ibrahimu ni mtu wa muhimu katika pande zote mbili, mtazamo wa maisha ya Kibiblia na Kiislamu. Ikiwa unafanya kazi kati kati ya Waislamu, kumjumulisha Ibrahamu katika simulizi itaweka daraja kati ya utamaduni wa Kibiblia na utamaduni wao.

Kwa kuwa miti inaabudiwa katika baadhi ya tamaduni, hakikisha haitafsiriwi kuwa Ibrahimu aliabudu mti katika simulizi hii.

(Mtiririko uhalisia katika simulizi)

Hakikisha unatumia neno lile lile kwa ajili ya, wazawa, uhusiano, na kubarikiwa yalivyotumika katika simulizi zilizopita.

Umahiri wa Simulizi

Mungu hakuwa amebadilisha jina la Abramu kuwa Ibrahimu bado, bali kwa ajili ya kurahisisha ‘Ibrahimu ‘ limetumika. Iwapo baadaye itaonekana kwamba kubalishwa kwa jina la Abrahamu kuna umuhimu katika mpangilio wa simulizi, jumuisha simulizi na badilisha jina lake tena kuwa Abramu katika simulizi hii.

Kanaani na maeneo mengine yaliyotajwa yameachwa kwa makusudi ili hadithi iwe rahisi kukumbukwa na kurejea

Malengo katika hadithi hii ni kuandaa ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu. Ahadi ni kuwa Mungu atamfanya Ibarahimu kuwa taifa kubwa na kupitia taifa hilo, watu wote watabarikiwa. Ahadi hii ilitunzwa na Mungu. Ibrahimu alivyoishi katika uhusiano mzuri na Mungu, amepewa umuhimu.

KanuniTabia na kawaida ya Mungu

Anayetoa ahadi; anayebariki, anayehusiana, ndiye atakayemuumba mtu kwa ajili yake mwenyewe, ndiye anayeongoza na kuelekeza, ndiye anayejifunua na kulifunua mapenzi yake, anayestahili kuabudiwa, aliye na nguvu za kubariki, anayelinda na kutupa thawabu, anayezungumza na watu, anayejali watu wake, anayewaita watu wake kwa ajili ya kusudi lake.

Kanisa

Mungu atawainua/atawajenga watu wake – akiweka msingi kwa ajili ya kanisa; Ibada

Maisha ya Uchaji

Katika msingi wa uhusiano na kuamini, kutembea na kuongea na Mungu

Maombi Mfano mzuri wa mawasiliano kati ya Mungu na mwanadamu – iliyo sahihi na binafsi, huweka msingi kwa ajili ya maombi.

Page 18: StoryTapestry Manual - Swahili

18

Sara aahidiwa mtoto wa kiume

Mwanzo 18:1-5, 6-9, 10-15; 21:1, 2

Imetumia tafsiri ya: NLT

Badiliko:

Miaka mingi ilipita. Ibrahimu na Sara walikuwa wazee sana na bado hawakuwa na wamepata watoto. Wakati huu sasa Sara alikuwa amekwishapita umri wa kuwa na watoto.

Mwanzo 19:1-5

Mungu alimtokea Ibrahimu alipokuwa ameketi mlangoni pa hema lake. Ibrahimu aliangalia kwa mbali na aliwaona wageni watatu wamesimama. Alipowaona alikimbia mbio kukutana nao na kuwakaribisha, akainama mpaka nchi kuwasalimu. Ibrahimu akasema karibu, Pumzikeni kwenye kivuli cha mti huu wakati maji yanaletwa muoshe miguu yenu. Na kwa kuwa mmemheshimu mtumwa wenu na kunitembelea, naomba niandae chakula ili kuwaburudisha kabla hamjaendelea na safari yenu”. “Sawa” Walijibu. “Fanya kama ulivyosema.”

Mwanzo 18:6-9

Kwa hiyo Ibrahimu akarudi mbio kwenye hema na akamwambia Sara, “Harakisha! Tengeneza mkate.” Kisha Ibrahimu akaandaa chakula kizuri kwa ajili ya wageni wake. “Yuko wapi Sara mkeo?” Wageni waliuliza. “Yupo ndani ya hema,” Ibrahimu alijibu.

Mwanzo 18:10-15

Kisha Mungu akasema, “Nitakurudia wakati huu mwakani, na tazama mkeo Sara atapata mwana wa kiume!” Sara alikuwa akiyasikiliza mazungumzo haya na akacheka moyoni mwake na akashangaa itakuwaje mwanamke mzee kama yeye aweza kupata mtoto. Kisha Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kwa nini Sara amecheka? Kwa nini amesema, ‘inawezekanaje mwanamke mzee kama mimi kupata mtoto? Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Mungu? Nnitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. Sara akaogopa, na akasema “Sikucheka” Bali Mungu akasema, “ umecheka.”

Mwanzo 21: 1, 2

Mungu alitunza neno lake na akafanya vile vile kama alivyoahidi. Akapata mimba, na akamzaa mtoto wa kiume katika umri wake mkongwe. Hii ilitokea katika wakati ule ule Mungu alivyosema itakuwa/itatokea.

Page 19: StoryTapestry Manual - Swahili

19

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kuzingatia

‘Osheni miguu yenu’

Kuosha miguu ya mtu mwingine ilikuwa ni ishara ya heshima kwa mgeni.

Mtazamo wa kiulimwengu

Wageni wale watatu wanaweza kuelezewa kuwa ni Mungu na malaika wawili. Inasaidia kufafanua wageni hawa walikuwa akina nani. Mwanzo 18:17-33 na Mwanzo 10:1-26 ni mistari inayotoa msaada kwa kueleza kwamba alikuwa Mungu na malaika wawili.

Umahiri katika Simulizi

Sara alitambulishwa katika simulizi iliyotangulia. Hakikisha unatumia jina lake hapa.

Simulizi hii ni utimilifu wa ahadi iliyofanywa kwa Ibrahimu na Sara miaka 25 kabla iliyotangulia (katika simulizi za mwito wa Ibrahimu)

Katika baadhi ya tamaduni, desturi ya kuinama mbele ya mtu mwingine inaweza isiwepo au inaweza kuwa na maana tofauti. Katika simulizi hii, Ibrahimu alikuwa anaonyesha heshima kwa wageni wake. Iwapo maana hii haieleweki kwa hadhira, basi hii inaweza kurahisishwa kwa kusema tu kwamba Ibrahimu aliwasalimia wageni wake kwa heshima.

KanuniTabia na kawaida ya Mungu

Mungu anatiminza ahadi zake; Mungu huwatembelea watu wake binafsi; Mungu anajua hata mawazo yetu; Mungu hutenda kazi katika kila jambo kwa ajili ya kukamilisha mpango wake.

Page 20: StoryTapestry Manual - Swahili

20

Imani ya Abrahamu yajaribiwa

Mwanzo 22:1-4; 6-8; 9-13; 15-18

Imetumia tafsiri ya : NLT

Mwanzo 22:1-4

Siku moja Mungu aliijaribu imani na utii wa Ibrahimu. “Ibrahimu!” Mungu aliita, “Ndio,” aliitika, “Mimi hapa”. Mchukue mwanao, mwanao wa pekee Isaka, ambaye unampenda sana na uende kwenye nchi nyingine. Mtoe sadaka huko katika moja ya milima nitakayokuonyesha.” Asubuhi iliyofuata Ibrahimu aliamka mapema akawachukua watumishi wake wawili pamoja na mwanaye Isaka. Siku ya tatu ya safari, Ibrahimu aliunua macho na akapaona mahali kwa mbali.

Mwanzo 22:6-8

Ibrahimu alimvisha Isaka kuni mabegani mwake, wakati, yeye akiwa amechukua kisu na moto. Hao wawili walipokuwa wakienda pamoja, Isaka akamgeukia Ibrahimu na akasema, “Baba?” “Ndio, mwanangu,” Ibrahimu alijibu.. “Tunazo kuni na moto”, alisema kijana, “lakini mwanakondoo kwa ajili ya sadaka yuko wapi?” “Mungu atatupatia huyo mwanakondoo, mwanangu.” Ibrahimu alijibu. Na wakaendelea mbele pamoja.

Mwanzo 22:9-13

Walipofika mahali ambapo Mungu alimwambia, Ibrahimu aende akaandaa mahali pa kufanyia ibada na akapanga kuni juu yake. Kisha akamfunga mwanaye Isaka na akamweka juu ya kuni. Na Ibrahimu akatoa kisu chake ili kumchinja mwanaye kama sadaka kwa Mungu. Wakati huo, Malaika wa Mungu alimwita kwa sauti kubwa, “Ibrahimu! Ibrahimu!” “Ndio,” akajibu, “Ninasikiliza.” “Usimnyoshee kijana mkono!” Malaika alisema. “Usimdhuru kijana kwa namna yoyote, kwa kuwa sasa nimejua kwamba hakika unamwogopa Mungu. Hukumzuilia hata mwanao, mwanao wa pekee.”

Kisha Ibrahimu akatazama juu na akamwona mwana kondoo dume kichakani. Kwa hiyo akamchukua mwanakondoo na akamtoa sadaka mahali pa mwanaye.

Mwanzo 22:15-18

Kisha malaika wa Bwana akamwita tena Ibrahimu, “Hivi ndivyo Mungu anavyosema, Kwa sababu umenitii na hukunizuilia hata mwanao, nimekuahidi kuwa nitakubariki nitauzidisha uzao wako kuwa mamilioni yasiyohesabika, kama nyota za angani na mchanga wa pwani. Watawashinda/watawateka maadui zao kupitia uzao wako, mataifa yote yatabarikiwa – yote ni sababu umenitii mimi.”

Page 21: StoryTapestry Manual - Swahili

21

Maneno/Vifungu vya kuzingatia

Kujaribiwa

Hii inamaanisha kuangalia iwapo Ibrahimu kweli alimwamini Mungu au alikuwa na imani katika Mungu.

Utii. Hii inamaanisha kutekeleza au kufanya kile unachotakiwa au umeamriwa kufanya.

Malaika/Malaika wa Mungu

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Imani

Kafara/sadaka

Mtiririko halisi ndani ya simulizi)

Hakikisha kuwa unatumia maneno yale yale kwa: uzao, imani, bariki, Mungu, kuabudu na kuamini yaliyotumika katika simulizi zilizopita.

Umahiri wa Simulizi

Ili kuifanya ivutie zaidi, mazungumzo mengi yamejumuishwa katika simulizi hii.

Simulizi hii imemtambulisha Isaka kama mwana wa kiume wa Ibrahimu. Katika baadhi ya tamaduni inaweza kuwa bora kusema alimtoa mwanaye wa kiume bila kutaja jina la Isaka.

Hakikisha unaonyesha hii si kafara ya mtoto bali ni namna tu ambayo Mungu aliujaribu utayari wa Ibrahimu katika kumtii yeye.

KanuniTabia na kawaida ya Mungu

Mungu anatarajia utiifu kutoka kwa watu wake hata kama hatuelewi; Mungu hutoa kila kitu kinachohitajika; Mungu ni mwaminifu siku zote katika ahadi zake; Mungu hutuma malaika wake kuongea na watu; Wakati mwingine Mungu atatutaka tumpe au tumtolee yeye kitu ambacho ni maalumu sana au cha thamani sana kwetu.

Page 22: StoryTapestry Manual - Swahili

22

Daudi apakwa mafuta

1Samweli 16:1-13

Imechukuliwa toka tafsiri ya: NLT

Pitio:

Mungu aliitunza ahadi yake kwa Ibrahimu na wazao wake wakawa taifa kubwa mno. Siku moja walidai kwamba Mungu awape mfalme wa kidunia ili wawe kama mataifa mengine. Hili halikumpendeza Mungu lakini akawaruhusu. Mungu alianza kusema na taifa hili kupitia watu walioitwa wasemaji. Miaka mingi baadaye, Mungu alimchagua mtu kuwa mfalme juu ya taifa hili. Hivi ndivyo alivyofanyika kuwa mfalme…

1Samweli 16:1-3

Mungu alisema kwa mmoja wa wasemaji wake, Samweli, “Ijaze chupa yako mafuta na uende hadi Bethlehemu. Mtafute mtu aitwaye Yese ambaye anaishi huko, maana nimemchagua mmoja wa watoto wake kuwa mfalme Wangu.” Lakini Samweli aliuliza, “Nawezaje kufanya hilo? Ikiwa mfalme atalisikia, ataniua.” “Chukua ndama pamoja nawe,” Mungu alijibu, “na useme kwamba umekuja kuniabudu mimi. Mwalike Yese na wanaye na mimi nitakuonyesha yupi utamtia mafuta kwa ajili yangu.

1Samweli 16:4-10

Samweli alifanya kama alivyoagizwa na Mungu. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji walikuja kumlaki wakitetemeka. “Kuna tatizo gani?” Waliuliza. “Je, umekuja kwa amani?” “Ndiyo,” Samweli alijibu. Nimekuja kumwabudu Mungu. Jitakaseni na njooni pamoja nami.” Kisha Samweli alimwalika Yese na wanawe pia. Walipofika Samweli alimwangalia mtoto wa kwanza na akafikiri, “Hakika huyu ndiye mpakwa mafuta wa Mungu!” Lakini Mungu alimwambia Samweli, “Usimchague kwa mwonekano au kimo chake,kwa maana mimi nimemkataa. Mimi siangalii kama ninyi muangaliavyo. Maana wanadamu huangalia sura ya nje, bali mimi huutazama moyo.” Kisha waliobakia kila mtoto akapita mbele ya Samweli lakini Mungu hakumchagua yeyote kati yao. Hivyo, Samweli akamwambia Yese, “Mungu hakumchagua yeyote kati ya hawa.”

1Samweli 16:11-13

Kisha Samweli akauliza, “Je hawa ndio watoto ulionao wote?” “Bado yupo mdogo,” Yese alijibu. “Lakini yuko nje uwandani akichunga kondoo na mbuzi.” “Tuma aletwe haraka,” Samweli akamwambia, “Hatutaketi kula hadi afike.” Kwa hiyo Yese akatuma aletwe. Alikuwa mweusi na mzuri, mwenye macho mazuri. Na Mungu akasema, “Huyu huyu ndiye, mtie mafuta.” Kwa hiyo Daudi alipokuwa amesimama kati ya ndugu zake, Samweli akachukua pembe ya mafuta ya mzeituni aliyokuja nayo na akampaka kwa yale mafuta Daudi. Na Roho wa Mungu akaja juu ya Daudi kwa nguvu sana kuanzia siku ile.

Page 23: StoryTapestry Manual - Swahili

23

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kuzingatia

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Kupaka mafuta

Roho wa Mungu

Wasemaji

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha kutumia maneno yale yale kwa ajili ya kuabudu na uzao yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

Baadhi ya majina yameachwa ili kurahisisha kuikumbuka na kuisimulia tena.

Sababu ya Samweli kuja Bethlehemu limerahisishwa kama, ‘kuabudu’ ili kwamba simulizi iwe rahisi kukumbuka na kuisimulia tena, na kuondoa uwezekano wa kutoka kwenye mpango mkuu uliowekwa.

Sehemu ya simulizi ambayo watoto wote saba walipitishwa kwa Samweli imerahisishwa. Kama itakuwa na msaada kipande hiki ikijumuishwa kama sehemu kifaa cha simulizi, i.e. hadhira yako kweli inataka kurudia na kusika kwamba kila mtoto, kwa zamu, alikataliwa, basi unaweza kukijumuisha katika sehemu hii ya simulizi.

Kanuni

Tabia na kawaida ya Mungu

Hutunza ahadi zake; anastahili kuabudiwa; hujifunua yeye mwenyewe na kusudi lake; anaongea na watu; anajua mawazo na nia za watu; hufanya maamuzi tofauti na wanadamu; Roho wake huja juu ya watu; anawaita watu kwa ajili ya kusudi lake; upendo wake haushindwi.

Kanisa

Nyumba ya ibada; wazo Mungu wa Milele

Hakika ya Wokovu

Ufalme wa Mungu ni wa Milele

Maisha ya Uchaji

Kutembea na kuongea na Mungu; ibada nyumbani

Page 24: StoryTapestry Manual - Swahili

24

Daudi na Batsheba

2Samweli 11:1-18, 22-25, 26, 27

Kigezo katika: NLT

2Samweili 11:1-5

Muda fulani, wakati wa majira ya mwaka ya majani kuchipuka wakati wafalme waendapo vitani, Daudi alituma jeshi lake kupigana bali yeye alibaki nyumbani. Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme. Na alipotazama mjini, alimwona mwanamke mzuri akioga. Alimtuma mtu kuangalia alikuwa ni nani, na aliambiwa, “Ni Betsheba, mke wa mmoja wa askari wako waaminifu na waliojitoa kikamilifu.” Kisha Daudi akamchukua. Alipokuja katika jumba la kifalme (ikulu), Daudi akalala naye na kisha akarudi nyumbani. Baadaye, Betsheba alipogundua amekuwa mjamzito, alituma ujumbe kwa Daudi ili kumjulisha, na hakukuwa na shaka kwamba mtoto alikuwa wake kwani hakuwa na mimba mme wake alipokuwa nyumbani.

2Samweli 11:6-13

Kwa hiyo Daudi akamtumia ujumbe kamanda wa jeshi lake kumrudisha mme wake nyumbani. Alipofika, Daudi alimuuliza mme wake jinsi gani vita inaendelea. Kisha Daudi akamwambia, “Nenda zako nyumbani na ukapumzike,” lakini yeye hakwenda nyumbani. Usiku ule alibakia kwenye lango la nyumba ya mfalme pamoja na watumishi wa mfalme. Daudi aliposikia hakwenda nyumbani, alimuuliza, “Kwa nini hukwenda nyumbani kwako jana usiku baada ya kuwa mbali kwa muda mrefu?” Alijibu, jeshi linalala viwanjani. Ningewezaje kwenda nyumbani na kupumzika?” Kisha Daudi akamwalika kwa chakula cha usiku siku iliyofuata na akamlevya. Bali hata hivo, hakumfanya askari kwenda nyumbani kwa mke wake. Kwa mara nyingine tena akalala langoni pa jumba la mfalme.

2Samweli 11:14-17

Siku iliyofuata asubuhi Daudi aliandika barua kwenda kwa kamanda wa jeshi lake na akampa mmewe Betsheba aupeleke. Barua ilitoa maelekezo kwa kamanda, “Mweke askari huyu mstari wa mbele ambako vita ni kali. Kisha ondokeni ili kwamba auawe.” Kwa hiyo kamanda akafanya kama alivyoambiwa. Mme wa Batsheba akauawa pamoja na askari kadhaa wengine.

2Samweli 11:18, 22-25

Kisha kamanda wa jeshi akamtuma mjumbe kwa Daudi kumpa taarifa za vita. Mjumbe alisema kwamba, mme wa Betsheba ameuawa pamoja na wengine. “Vema. Mwambie kamanda asivunjike moyo”, Daudi alisema. “Watu wameuawa katika vita! Wakati mwingine piganeni kwa bidii!”

2Samweli 11:26, 27

Page 25: StoryTapestry Manual - Swahili

25

Na Betsheba aliposikia kwamba mme wake amekufa, akamwombolezea mmewe. Na kipindi cha maombolezo kilipokwisha, Daudi alimchukua katika jumba la mfalme, na akawa mmoja wa wake zake. Baadaye akamzaa mtoto wa kiume. Lakini Mungu alichukizwa sana na kile Daudi alichokifanya.

Falsafa za Maisha

‘akalala naye’

Lugha nyingi zina namna mbalimbali za kuelezea uhusiano wa mapenzi. Tumia misemo sahihi ambayo haitaidhalilisha hadhira (walengwa).

Umahiri wa Simulizi

‘na hapakuwa na shaka kwamba mtoto alikuwa wake’

Kifungu hiki cha maneno kimeongezewa katika simulizi, kwa kuzingatia maelezo yaliyopo kwenye maandiko. ‘Mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake baada ya kumaliza siku zake za mwezi’ Maandiko yanajumuisha taarifa hii kuonyesha kwamba mtoto lazima alikuwa wa Daudi…. Hakuwa mtoto wa mmewe.

Baadhi ya majina yameachwa kwa ajili ya kurahisha ukumbukaji na kuisimulia tena.

KanuniTabia na Asili ya Mungu

Hapendezwi na dhambi

Page 26: StoryTapestry Manual - Swahili

26

Simulizi ya Nathani

2Samweli 12:1-18, 24, 25

Kigezo NLT

Mpito:

Kwa sababu Mungu aliksirishwa na kile ambacho Daudi alifanya,

2Samweli 12:1-4

Mungu alimpeleka msemaji wake Nathani kumwambia Daudi hadithi hii: “Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini. Yule tajiri alikuwa na kondoo na ng’ombe wengi. Yule maskini hakuwa na kitu, ila mwana kondoo mmoja, mdogo. Alimkuza na kumlea kama vile alikuwa mmoja wa watoto wake. Siku moja mgeni alifika katika nyumba ya Yule tajiri. Badala ya kuchinja mnyama kutoka katika kundi la mifugo yake, alimchukua kondoo wa yule msikini, akamchinja na kumwandalia mgeni wake.”

2Samweli 12:5, 6

Daudi akakasirika. Akasema, Mtu yeyote anayeweza kufanya kitu kama hicho anastahili kufa! Ni lazima amrudishe mwanakondoo mara nne kwa yule maskini kwa yule mmoja aliyemwiba.

2Samwili 12:7-12

Kisha Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe mtu huyo! Mungu anasema, “Nilikutia mafuta kuwa mfalme. Nilikupa ufalme wote. Na kama hayo yangalikuwa machache, ningelikuongezea zaidi, mambo kadhaa wa kadhaa. Kwa nini umeniasi na kufanya mambo haya mabaya? Umeua mtu na kuiba mke wake. Kwa sababu umemtendea Mungu dharau, kuanzia sasa na kuendelea, vurugu zitakuwa kwenye familia yako. Ulilolifanya kwa siri litatokea kwako wazi wazi”.

2Samweli 13, 14

Kisha Daudi akakiri kwa Nathani, Nimemtenda Mungu Dhambi.” Nathani akamjibu, “Ndiyo, lakini Mungu amekusamehe na hutakufa kwa ajili ya dhambi. Lakini kwa sababu ya kile ulichokifanya mtoto wako atakufa.

2Samweli 12:15 – 18

Baada ya Nathani kurudi nyumbani kwake, mtoto wa Betsheba akaugua sana. ? Daudi akamsihi Mungu kumponya mtoto. Lakini siku saba baadaye mtoto alikufa.

2Samweli 12: 24, 25

Daudi akamfariji Betsheba na kisha akalala naye. Akapata mimba na akamzaa mtoto wa kiume. Wakampa jina la Sulemani, ambaye Mungu alimpenda.

Page 27: StoryTapestry Manual - Swahili

27

Page 28: StoryTapestry Manual - Swahili

28

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kujadili

Ufalme

Ni milki au eneo ambalo mfalme anatawala au kumiliki.

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Kusamehe

Dhambi

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa upako, ukaidi/uasi na msemaji yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

‘Kwa sababu umemtenda Mungu kwa dharau’

Kuweka wazi matendo ya ukaidi/uasi dhidi ya Mungu ni yapi; Fanya kwa uwazi kwa kusema, kitu kama, ‘kwa sababu umenikaidi kwa kumuua na kufanya uzinzi.’

KanuniTabia na asili ya Mungu

Hapendezwi na dhambi; Hutumia wasemaji kukabiliana na dhambi; hutumia hadithi; hutoa; hapendi ukaidi, aliadhibu dhambi; husamehe dhambi; hutunza ahadi.

Page 29: StoryTapestry Manual - Swahili

29

Ahadi

Isaya 53

Kigezo katika: NLT

Simulizi hii ni ngumu kuielezea. Tunao mfano hapa chini wa simulizi yenye umahiri

Mfano wa Simulizi yenye umahiri

Kama mfalme Daudi, watu wa Mungu waliendelea kumtenda dhambi na kumkadi Mungu. Lakini Mungu hakuwasahau watu wake. Kwa sababu ya uasi wao, aliruhusu nchi zilizowazunguka kuingia na kuwateka na watu walitawanywa ulimwengu kote. Kabla hili halijatokea, Mungu alimtuma msemaji, Isaya, ili kuwapa ujumbe wake wa tumaini. Aliwaambia:

Mungu atatupelekea Mkombozi. Kuna watu watamchukia na kumtenda vibaya. Atateswa kwa niaba yetu. Atachukua mizigo yetu na huzuni zetu. Atachapwa kwa mijeledi na kupigwa ili kutuletea amani.

Sisi ni kama kondoo. Unajua jinsi kondoo walivyo. Wanazunguka zungaka nje ya njia na kupotea, tunazunguka nje ya njia ya Mungu. Tunamtenda dhambi, tunamkaidi Mungu. Bali, Mungu anaziweka dhambi zetu zote juu ya Mkombozi.

Kwa hakika, Yeye ni kama kondoo apelekwaye machinjoni. Hawezi kusema lolote. Ataadhibiwa na kuawa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini kitu cha kushangangaza ni kwamba atauona uzima tena.

Na kwa sababu ya hilo, watu wengi watarejesha uhusiano na Mungu.

Huu ni ujumbe ambao Isaya aliupeleka kwa watu, na kuanzia wakati huo na kuendelea watu walisubiri kwa matarajio kwa ajili ya Mkombozi Aliyeahiwa kuja.

Page 30: StoryTapestry Manual - Swahili

30

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kujadili

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Mkombozi/Mkombozi aliyeahidiwa

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha umatumia maneno yale yale kwenye ukaidi, uhusiano, dhambi na msemaji yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Chagua misemo ile ile kuielezea kwa watu wa Mungu katika mpangilio wote wa simulizi.

Umahiri wa Simulizi

Maelezo (commentaries) yanayokubaliana na kifungi hiki kuhusisha na matukio yajayo. ‘Unabii katika muda uliopita’ yametumika mara nying katika mipito, lakini yanahusishwa na matukio ya baadaye. Vitenzi vimebadilika kwenda kwenye muda ujao ili kuonyesha usahihi zaidi, maana na kurahisisha simulizi kwenye hadhira.

‘Mkombozi Aliyeahidiwa’ limetumika hapa badala ya ‘mtumishi’ kuweka muda na wajibu wa ukombozi wa Yesu kwa uthabiti katika mpangilio wote wa simulizi. (Angalia hotuba ya Simeoni katika hadithi ya kuzaliwa). Maelezo yanakubaliana ‘mtumishi’ huyu, yanamzungumzia Masihi atakayekuja’ Tumia msemo wowote unaozungumzia wazi zaidi kwenye makundi ya watu. Ni viuzri kutunza misemo hii kwa udhabiti katika mfululizo wote wa simulizi.

‘aliongozwa kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni’

Kama inaonekana inachanganya, uondoe mstari huu na kusema, ‘Yeye ataongozwa kwenda kufa’

‘Sisi ni kama kondoo’

Kama maelezo ya watu kuwa kama kondoo aliyetoka nje ya njia ya Mungu yanawachanganya, maneno kama ‘Tumetangatanga nje ya njia ya Mungu, tumetenda dhambi’, yanaweza kutumika.

KanuniTabia na asili ya Mungu

Huadhibu uasi/ukaidi, hujifunua, hutumia wasemaji wake; anaahidi Mkombozi, anarejesha uhusiano, na anasamehe; analeta tumaini; analeta njia ya wokovu; analeta amani, anazichukua dhambi; anateka kifo.

Hakika ya Wakovu

Mungu ana mpango kwa ajili yetu ili tuokolewa kutoka dhambi zetu na kuwa na uhusiano na yeye kupitia Mkombozi Aliyeahidiwa.

Page 31: StoryTapestry Manual - Swahili

31

Page 32: StoryTapestry Manual - Swahili

32

Malaika awatembelea Mariamu na

Yusufu

Mathayo 1:19-21, 24, 25;

Luka 1:26-30, 34-39, 46-50, 56

Kigezo NLT

Mpito:

Baada ya miaka mingi, hatimaye Mungu alimpeleka Mkombozi Aliyeahidiwa. Hii ni simulizi yake.

Luka 1:26-30

Mungu alimtuma malaika kwa bikira aliyeitwa Mariamu. Alikuwa amechumbiwa ili aoelewe na mwanamme aliyeitwa Yusufu. Malaika akamtokea na Mariamu na kumwambia, “Salaam, mwanamke uliyepata neema! Mungu yuko pamoja nawe!” Akiwa amechanganyikiwa na kusumbuka, Mariamu alijaribu kufikiri malaika anaweza kumaanisha nini. “Usiogope, Mariamu,” malaika akamwambia, “kwa kuwa Mungu ameamua kukubariki! Utachukua mimba na utapata mtoto wa kiume, na utamwita jina lake Yesu. Atakuwa mtu mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu.”

Luka 1:34-39

Mariamu akamuuliza malaika, “Lakini nitawezaje kupata mtoto? Mimi ni bikira.” Yule malaika akajibu, “Roho wa Mungu atakujilia juu yako. Mtoto atakayezaliwa kwako atakuwa mtakatifu, na ataitwa Mwana wa Mungu. Kwa kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu.” Mariamu akaiitikia, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, na niko tayari kukubali chochote Anachokitaka. Yote uliyoyanena na yawe dhahiri.” Na kisha malaika akaondoka. Mariamu akaenda kumtembelea ndugu yake Elizabeti aliyeishi kaktika mji mwingine.

Luka 1:41 – 50, 56

Elizabeti na Mariamu walipoonana, walifurahi pamoja. Kisha Mariamu akasema “Oo ni kwa jinsi gani ninamsifu Bwana. Ninafurahi katika Mungu mkombozi wangu! Kwa kuwa amemtazama mtumishi mdogo wa kike, na sasa vizazi na vizazi vitamwita mbarikiwa. Kwa kuwa aliye Mkuu ni Mtakatifu, na amefanya mambo makuu kwa ajili yangu. Rehema zake zinakwenda kizazi hadi kizazi, kwa wote wanaomhofu yeye.” Mariamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu na kisha alirudi nyumbani kwao.

Page 33: StoryTapestry Manual - Swahili

33

Mathayo 1:19-21

Yusufu, mchumba wake hakutaka kumwaibisha mchumba wake, kwa hiyo akaamua kuvunja uchumba kimya kimya. Alipokuwa akifikiri hayo, alilala usingizi, na malaika kutoka kwa Mungu akamotkea katika ndoto. “Yusufu, mwana wa Daudi,” malaika alisema, “Usiogope, kuendelea na mipango yako ya harusi kumuoa Mariamu. Mtoto aliye ndani yake ametungwa kwa uwezo wa Roho wa Mungu. Atapata mtoto wa kiume, na utamwita jina lake Yesu, kwa sababu ndiye atakayewakomboa watu kutoka kwenye dhambi zao.

Mathayo 1:24, 25

Yusufu alipoamka, alifanya kile alichoaamriwa na malaika na akamchukua Mariamu kama mke wake. Bali hakuwa na uhusiano naye wa kimapenzi mpaka baada ya mtoto wake kuzaliwa.

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kujadili

Utakatifu

Kuwa na uhusiano na Mungu, kuwekwa wakfu Kwake au kama Yeye.

Tumia neno au kifungu cha maneno ambayo ni sahihi kuulezea utakatifu kama umetoka kwa Mungu

Rehema

Hii ni pale Mungu anapoonyesha ukarimu usio na sababu au huruma kwa mtu.

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Bwana

Okoa

Mwana wa Mungu

Falsafa za Maisha

Matumizi ya neno ‘bikira’ linamaanisha, ‘kabla hawajaishi pamoja kama mme na mke.” Inaweza pia kumaanisha. ‘kabla hawajawa na uhusiano wa kimapenzi.’ Tumia maelezo yoyote katika lugha itakayoonyesha wazi kwamba Mariamu hakuwa na mwanamme. Hakikisha kwamba linafaa kwa ajili ya kusanyiko la watu mchanganyiko kusikia na kusema. Ili kuuelewa mkangonyo aliokuwa nao Yusufu, ni muhimu kujua kwa namna gani utamaduni unautazza uchumba. Ikiwa unaandaa kwa ajili ya kusanyiko la wa Wamarekani, ongeza baadhi ya taarifa za kitamaduni ili kuonyesha ni kwa namna gani kufunga uchumba kunavyokuwa.

Mwambatano ndani ya simulizi

Page 34: StoryTapestry Manual - Swahili

34

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa: Roho wa Mungu, malaika, Mkombozi Aliyeahidiwa, bariki, mkombozi, dhambi, wazao yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

Jina la malaika limeondolewa ili kurahisha simulizi.

‘Roho wa Mungu atakuja juu yako.”

Namna ya kusema hili inaweza kuwa ‘Roho wa Mungu alisababisha Mariamu kuwa mjamzito’ au ‘nguvu ya Roho wa Mungu iliwezesha hili kutokea’ Hata hivyo, unaweza kusema hivi, hakikisha kwamba tendo la ndoa kati ya Roho wa Mungu na Mariamu HALITAFSIRIWI VIBAYA.

Mwana wa ALiye Juu

‘Aliye juu mara nyingi hutumika katika nafasi ya jina la Mungu kama ishara ya ukuu. Iwakiwa hadhira ina cheo (jina) sawa na hilo kwa ajili ya Mungu, hii inaweza kwenda vizuri. Kama sivyo, hakikisha kuwa linamaanisha Mungu. Kama sivyo sema tu, ‘Mwana wa Mungu.’ Tumia kanuni hiyo hiyo, kwa ‘Aliye Mkuu’ kama jina au cheo cha Mungu.

Kwa kuwa yeye, Aliye Mkuu, ni Mtakatifu

‘Utakatifu’ huu unamaanisha kuwa kitu fulani kujitenga kutoka dhambini au kisafi.

KanuniTabia na asili ya Mungu

Hutunza ahadi zake; Roho wake yuko hai; Huongea na hulifunua kusudi lake; Anawahikikisha watoto wake; Huongea katika ndoto; hutumia wasemaji; humtuma mkombozi.

Page 35: StoryTapestry Manual - Swahili

35

Kuzaliwa kwa Yesu

Luka 2:21, 22, 25, 28, 30-40

Kigezo kwenye NLT

Mpito:

Miezi michache baadaye, mtoto wa kiume alizaliwa na Mariamu katika Bethlehemu.

Luka 2:21, 22, 25, 28

Siku nane baada ya kuzaliwa kwake. Aliitwa Yesu, jina alilopewa na malaika. Wazazi wake walimchukua kwenda Yerusalemu, mji maalumu kwa ajili ya Ibada ili kumweka wakfu mtoto kwa Mungu mahali pao pa kuabudia. Walipokwenda huko, walikutana na mzee mmoja ambaye alikuwa akimsubiri mkombozi aliyeahidiwa kuja na kuokoa watu wake. Alipomwona Yesu alimchukua mtoto mikononi mwake na akamtukuza Mungu, kwa kusema:

Luka 2:30-32

“Nimemwona mwokozi uliyemtoa kwa watu wote. Yeye ni nuru ya kumfunua Mungu kwa mataifa.”

Luka 2:33, 34

Yusufu na Mariamu walikuwa wakiyastaajabia yale yaliyonenwa kuhusu Yesu. Kisha yule mzee aliwabariki, na akamwambia Mariamu, “Mtoto huyu atakataliwa na wengi na itakuwa kwa kuanguka kwa wengi. Lakini atakuwa ni mtu mkuu kwa wengine wengi. Na upanga utaingia moyoni mwako.”

Luka 2: 39, 40

Wazazi wa Yesu walirejea nyumbani. Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu. Akijaa hekima na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Page 36: StoryTapestry Manual - Swahili

36

Maneno/Vifungu vya maneno ya Kujadili

Angalia faharasa

Yerusalemu

Hekima

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya mkombozi aliyeahidiwa, malaika, mkombozi/mwokozi, kuokoa, kuabudu na kubarikiwa yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizii

‘mji ambapo walimwabudu Mungu’

Mji huo uliitwa Yerusalemu na utatokea mara kwa mara katika mpangilio wa simulizi.

‘mahali pa ibada/kuabudu’

Mahali pa ibada/kuabudu limetumika badala ya ‘Hekalu’

Kuwekwa wakfu kwa Yesu, katika Hekalu kumewekwa kuonyesha kwamba Yesu ni utimilifu wa unabii wa Isaya kutoka kwenye simulizi ya Ahadi.

Kifungu cha kuwekwa wakfu katika simulizi kimetumiwa ili mfumo wa kafara katika hekalu usiweze kuelezewa katika mpangilio wa simulizi.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Hutunza ahadi yake; Roho wake yu hai; Anazungumza na kulifunua kusudi lake; anawakilisha watoto wake; anamtuma mkombozi.

Kanisa

Kwenda mahali pa kuabudia, kuabudu, kuweka wakfu watoto

Uchaji

Kuabudu/ibada.

Page 37: StoryTapestry Manual - Swahili

37

Ubatizo wa Yesu

Luka 3:1-3, 10-16, 21-22; Mathayo 3:7-9, 13-15

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Yesu akakua na kuwa kijana. Mungu alimtuma mjumbe mbele yake kuandaa njia kwa ajili ya watu kumpokea mkombozi aliyeahidiwa, Yesu.

Luka 3:1, 2

Baada ya muda, ujumbe kutoka kwa Mungu ulimjia mtu aliyeitwa Yohana ambaye alikuwa akiishi nje nyikani.

Luka 3:3

Yohana alikwenda sehemu mbalimbali akiwaambia watu wabatizwe kuonyeshwa kwamba wamegeuka kutoka dhambini na kumgeukia Mungu ili wasamehe.

Mathayo 3:7-9

Baadhi ya viongozi wa dini walikuja kumsikiliza Yohana, na akawaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira ya Mungu inayokuja? Maisha yenu yadhihirishe kwamba mmemgeukia Mungu. Msismezane nini kwa ninyi kwamba, “sisi tu salama, kwa kuwa tu wa uzao wa Ibrahimu.” Hiyo haina maana yo yote. Mungu anaweza kuyabadili mawe haya kuwa uzao Ibrahimu.

Luka 3:10-14

Makutano wakamuuliza, “Tufanye nini basi?” Yohana akajibu, “Ikiwa una kanzu mbili, mpe maskini, ikiwa una chakula wape wale walio na njaa. Hata watoza ushuru mafisadi wakamjia ili kubatizwa na wakauliza, “Mwalimu, tufanyeje sisi nasi?” “Onyesheni uaminifu wenu”, akajibu. Hakikisheni hammtozi mtu zaidi ya kodi ambayo serikali inawataka ninyi kukusanya. “Tufanyeje sisi nasi?” Wakamjia baadhi ya askari. Yohana akajibu, “msimdhulumu mtu, wala msimshitaki mtu kwa mambo manayojua hawakufanya. Mtoshewe na mshahara wenu.”

Luka 3:15, 16

Kila mtu alikuwa akimtarajia Mkombozi Aliyeahdiwa kuja haraka, na walikuwa na shauku kujua ikiwa Yohana ndiye. Yohana aliwajibu maswali yao kwa kusema, “Mimi nabatiza kwa maji, bali yupo mtu anakuja karibuni, huyo ni mkuu kuliko mimi – mkubwa sana kiasi ambacho mimi sistahili hata kuwa mtumwa wake. Yeye atawabatiza ninyi kwa Roho wa Mungu na kwa moto.

Page 38: StoryTapestry Manual - Swahili

38

Luka 3:21a

Siku moja makutano walipokuwa wakibatizwa,

Mathayo 3:13 – 15

Yesu mwenyewe akaja ili abatizwe na Yohana japokuwa Yesu hakutenda dhambi. Lakini Yohana alijaribu kusema naye juu ya hilo. “Mimi ndiye ninayestahili kubatizwa na wewe,” akasema, “hivyo kwa nini unakuja kwangu?” Lakini Yesu alisema, “Hivi ndivyo itupasavyo kufanya, kwa kuwa tunavyopaswa kuyatimiza yote tuliyoamuriwa na Mungu: Kwa hiyo Yohana akakubali kumbatiza.

Luka 3:21b-22

Baadaye, Yesu alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka, na Roho wa Mungu akashuka juu yake katika mfano wa hua. Na sauti kutoka mbinguni ilisema, “Wewe ni mwanangu, ninakupenda na ninapendezwa nawe.”

Page 39: StoryTapestry Manual - Swahili

39

Maneno/Vifungu vya maneno ya Kujadili

Sauti kutoka mbinguni

‘Sauti kutoka mbinguni’ tayari imekubalika kuwa ni sauti ya Mungu mwenyewe. Inakubalika kutumiwa ‘sauti ya Mungu’

‘waligeuka kutoka dhambini na kumgeukia Mungu ili wasamehewe. Hivi ndivyo NLT inavyosema.

‘majuto makubwa’. Hii ni picha nzuri ya nini hasa kinatokea pale tunapotubu au kujuta, na limependekezwa badala yake litumike neno moja ‘tubu’.

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Ubatizo

Viongozi wa Dini

Falsafa za Maisha

Kumbuka kwamba katika tamaduni na dini nyingi watu wana taratibu za kunawa/kujiosha mara kwa mara kuondoa dhambi. Fafanua kwamba, huu ni utaratibu unaofanyika mara moja tu. Ikiwa ni lazima ishara ya kuoshwa inaweza kutumika.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: msemaji, dhambi, Mkombozi Aliyeahidiwa, kusamehe, wazao wa Ibrahimu na Roho wa Mungu kama yalivyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

‘Wazao wa Ibrahimu’

Tafadhali zingatia kwamba ‘uzao wa Ibrahimu’ katika maandiko ya NLT inamaanisha ‘watoto wa Ibrahimu. Kifungu hiki cha maneno pia kinakazia mwambatano ndani ya simulizi kwa kutumia ‘wazao wa Ibrahimu’ mahali pa ‘watu wa Mungu katika mfululizo wote wa simulizi.

‘kwa moto’

Kifungu hiki cha maneno kimujumuishwa kwenye masimulizi ya Mathayo na Luka, lakini si katika masimulizi ya Marko.

Watoa maelezo wana maoni tofauti kuhusiana na kinachoitwa ‘kwa moto’. Ikiwa kutumia kifungu ‘kwa moto’ linaichanganya zaidi hadhira, yanaweza kuachwa.

‘hata kama Yesu hakutenda dhambi’

Kwa sababu Yesu hakutenda dhambi; kifungu hiki kilijumuishwa ili kuzuia rabsha (kuchanganyikiwa). Imetiliwa mkazo katika 1Korintho 5:21.

Page 40: StoryTapestry Manual - Swahili

40

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu hutuma Roho wake, Hutumia wasemaji, anamkubali Yesu kama mwanaye, anatunza ahadi zake, anasamehe dhambi, anahukumu dhambi, huzungumza na kulifunua kusudi na utashi wake.

Kanisa

Ubatizo: Watu wa Mungu inajumuisha watu wengi zaidi ya wazao wa Ibrahimu.

Maisha ya Uchaji

Mfano wa Yesu akiomba

Kushirikisha Injili

Yesu aliwaambia watu wabatizwe, wageuke kutoka dhambi zao na kumgeukia Mungu

Maombi

Yesu alipokuwa akiomba, Roho wa Mungu alishuka juu yake katika mfano wa hua.

Page 41: StoryTapestry Manual - Swahili

41

Mwanamke Kisimani

Yohana 4:5-19, 25-30, 42

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Baada ya hayo, Yesu aliwachangua wanaume kumi na mbili kuwa wafuasi wake wa karibu. Walisafiri maeneo mbalimbali wakihubiri ujumbe wa Ufalme wa Mungu kila walipokwenda. Wanaume na wanawake wengi walianza kumfuata.

Yohana 4:5-8

Yesu alikwenda katika kijiji cha Samaria karibu na kisima. Alikuwa amechoka kutokana na safari ndefu na akaketi chini kando ya kisima. Mara mwanamke msamaria alikuja kuchota maji. Yesu akamwambia, “Nipe maji ninywe.” Naye alikuwa pekee yake wakati huo kwa sababu wafuasi wake wa karibu walikwenda kijijini kununua chakula.

Yohana 4:9-15

Mwanamke alishangazwa, kwa sababu wazao wa Ibrahimu walikataa kuwa na uhusiano wowote na Wasamaria. Mwanamke akamwambia Yesu, “Wewe ni wa uzao wa Ibrahimu, na mimi ni mwanamke Msamaria. Kwa nini unaniomba maji ya kunywa?” Yesu akamjibu, “……. Watu hupata kiu tena baada ya kunywa maji haya. Lakini maji nikupayo huondoa kiu kabisa. Maji hayo yatakuwa chemichemi ibubujikayo ndani yao, ikiwapa uzima wa milele au maisha halisi ambayo hayatakuwa na mwisho. “Tafadhali Bwana,” Mwanamke akasema, “Unipe maji hayo kisha sitakuwa nafuata maji hapa tena.”

Yohana 4:16-19

“Nenda umlete mmeo,” Yesu akamwambia. “Sina mume,” mwanamke akajibu. Yesu akasema, “Sawa, umesema vema! Huna mume – kwa kuwa umekuwa na waume watano na hata sasa huyo unayeishi naye hujaolewa naye. Kwa hakika umesema kweli. “Bwana,” mwanamke akasema, “Wewe lazima utakuwa msemaji wa Mungu.” (**)

Yohana 4:25-30

Mwanamke akasema, “Mimi najua Mkombozi Aliyeahidiwa anakuja – yule aitwaye Kristo. Huyo atakapokuja, atatueleza mambo yote.” Kisha Yesu akamwambia, “Mimi ndiye mkombozi aliyeahidiwa!” Mara kitambo wafuasi wake wakarudi. Walistaajabu kumkuta akiongea na mwanamke. Mwanamke aliacha mtungi wake karibu na kisima na alikimbia kwenda kijijini,

Page 42: StoryTapestry Manual - Swahili

42

akimwambia kila mtu, “Njooni na mmuone mtu aliyeniambia mambo yote niliyofanya. Yawezekana kuwa ndiye Mkombozi Aliyeadiwa?” Kwa hiyo watu wakaja kwa wingi kutoka kijijini kumwona Yeye (Yesu).

Yohana 4:42

Kisha watu wakamwambi mwanamke, “Sasa tunaamini, siyo tu kwa sababu ya yale uliyotuambia, bali kwa sababu tumekwisha msikia wenye. Sasa tunajua hakika huyu ndiye mwokozi wa ulimwengu.

Page 43: StoryTapestry Manual - Swahili

43

Maneno/Vufungu vya Maneno ya Kujadili

Msamaria

Wasamaria si wa uzao wa Ibrahimu. Wazao wa Ibrahimu waliwachukia Wasamaria. Ikiwa tamaduni za watu unaofanya nao kazi zina kitu hicho hicho, tumia majina hayo. Vinginevyo itazalisha chuki kwa kutumia majina hayo ya ….

Angalia Faharasa kwa ajili ya:

Wafuasi wa Karibu

Uzima wa milele

Wafuasi

Ufalme wa Mungu

Falsafa za Maisha

Yesu alichukua hatua kuvuka mipaka ya uhusiano kati ya wazao wa Ibrahimu/Msamaria wa kiume/kike kwa kuongea na mwanamke huyo. Hakikisha walengwa wanaelewa kwamba Yesu alifanya kwa namna inayofaa na heshima kwa mwanamke huyo; na kwamba hakukuwa na tabia isiyofaa iliyojitokeza, kiasi kwamba yule mwanamke alimwita Yesu “Bwana.” Tumia neno katika lugha ambayo ni ya heshima na itatoa mtazamo mzuri (chanya) wa Yesu. Ikiwa kutamka kwamba Yesu alikuwa pekee yake na mwanamke, pale mwanzo wa simulizi, kunaweza kusababisha wasikilizaji kwa haraka kumfikiria vibaya Yesu, itoe sentensi hiyo. Itazuia kuleta picha mbaya ya Yesu kabla hadhira haijapata fursa ya kusikia mazungumzo kati ya Yesu na mwanamke.

Inaweza kuwa muhimu kusema Wasamaria pia walikuwa wakiutarajia ujio wa Mkombozi Aliyeahidiwa.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: Wazao wa Ibrahimu, Kuabudu, Roho wa Mungu, Msemaji, Mkombozi, na Mkombozi aliyeahidiwa yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia

Umahiri wa Simulizi

Neno ‘Uzima wa milele’ katika simulizi limejuishwa ili kufafanua kwamba maji anayoyatoa Yesu yanakuwa kama chemichemi. Baadhi ya lugha zinazaweza kuhitaji ufafanuzi ili sentensi zilete maana au zieleweke.

Page 44: StoryTapestry Manual - Swahili

44

Mazungumzo kati ya Yesu na mwanamke ni vigumu kuyarudia na kuyakumbuka. Baadhi ya mambo yaliyojirudia yamerahishwa na sehemu ya mazungumzo ambayo hayahusiani moja kwa moja na sababu za kuwa na simulizi hii katika mpangilio wa hadithi yameondoelewa. (**) Yohana 4:20-24; Yaliyopigiwa mstari hapa chini, yanaweza kuingizwa isipokuwa kama hayatailetea rabsha hadhira. “Niambie, ni mahal gani sahihi pa kumwabudu Mungu? Aliuliza mwanamke. Yesu alijibu, “Haijalishi wapi unaabudu. Kwa nguvu za Roho wa Mungu watu watamwabudu Mungu katika uhalisia wake, wakimfanyia ibada kamili anayoitaka”

Kanuni

Tabia na Asili ya Mungu

Hutaka vitu maalumu kwa watu; anataka watu kumjua Yeye; Huwaambia watu ukweli hata kama hawauelewi; Hukabiliana na watu katika hali ya upendo; Huwapa mwaliko kupokea kile alicho nacho kwa ajili yao; Huwasaidia watu kuondokana na udini na kuingia katika uhusiano halisi na Mungu; Hukabiliana na dhambi zetu; Husaidia watu kutafuta kumjua Yeye.

Kushirikisha Injili

Mwanamke alipoifahamu kweli, alitaka kushirikiana na watu wa mji wote.

Ushuhudiaji

Ni vizuri kwa waamini wapya kuwaeleza watu wote katika jamii juu ya imani yao. Hawahitaji kusubiri mpaka wawe wamefundishwa.

Page 45: StoryTapestry Manual - Swahili

45

Binti wa Yairo na

Mwanamke aliyetokwa na Damu

Luka 8:40-56

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Yesu aliendelea kusafiri maeneo mbalimbali akifundisha watu na kufanya miujiza mingi.

Luka 8:40-42

Makutano walimkaribisha Yesu, kwa sababu walikuwa wakimsubiri Yeye. Mwanamme aliyeitwa Yairo, kiongozi katika kusanyiko la kuabudia la mahali pamoja, alikuja na kuanguka miguuni pa Yesu, akamsihi kwenda naye nyumbani kwake. Binti yake wa pekee, ambaye alikaribia miaka kumi na miwili alikuwa kufani. Yesu alipokuwa akienda na Yairo, alikuwa amezungukwa na makutano.

Luka 8:43-46

Mwanamke katikati ya makutano alikuwa ameteswa kwa miaka kumi na mbili kwa kutokwa na damu, na hakuweza kupata tiba. Akija nyuma ya Yesu, aligusa pindo la nguo Yake. Ghafla damu ilikoma. “Ni nani aliyenigusa?” Yesu aliuliza. Kila mtu alikataa, na mmoja kati ya wafuasi wa karibu wa Yesu alisema, “Bwana, makutano hawa wote wanakusonga wewe.” Lakini Yesu akasema, “Kuna mtu kwa hakika amenigusa, kwa kuwa nimehisi nguvu ya kuponya ikinitoka.”

Luka 8:47, 48

Mwanamke alipogundua kwamba hawezi kuendelea kujificha, alianza kutetemeka na akaanguka magotini mbele Yake. Mkutano wote walisikia mwanamke akieleza kwa nini alikuwa amemgusa Yesu na kwamba aliponywa saa ile ile. “Mwanamke,” Alimwambia mwanamke, “imani yako imekufanya uwe mzima. Nenda kwa amani.”

Luka 8:49-56

Alipokuwa akiendelea kuongea na mwanamke, mjumbe alifika kutoka nyumbani kwa Yairo, kiongozi wa mahali pa kuabudia. Akamwambia, Binti yako amekufa. Hakuna haja ya kumsumbua Mwalimu sasa.” Lakini Yesu aliposikia kile kilichotokea, akamwambia Yairo, “Usiogope. Uwe na imani tu, na ataponywa.” Walipofika katika nyumba, Yesu hakuruhusu mtu yeyote kuingia ndani pamoja naye isipokuwa watatu kati ya wafuasi wake wa karibu, Petro, Yohana, Yakobo, na baba na mama wa binti mdogo. Nyumba ilikuwa imejaa watu wakilia na kumboleza, lakini aliwaambia, “Nyamazeni! Hakufa; Amelala tu.” Bali makutano walimcheka kwa sababu walijua alikuwa amekufa. Kisha Yesu akamshika binti mkono na akasema kwa sauti, “Mwanangu, inuka!” Na wakati ule uhai wake ukarejea, na ghafla

Page 46: StoryTapestry Manual - Swahili

46

akasimama! Kisha Yesu akawaambia mpeni chakula ale. Wazazi wake wakastaajabu sana, bali Yesu akasisitiza kwamba wasimwambie mtu kile kilichotokea.

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kujadili

Angalia Faharasi kwa ajili ya:

Imani

Bwana

Muujiza

Falsafa za Maisha

Kutokwa damu kwa mwanamke kutakuwa kulimfanya awe najisi katika mfumo dini yao. Hili linaweza kumwelezea kwa nini alikuwa na tabia isiyo ya kawaida. Tumia maneno kulielezea tatizo lake la kutoka damu kwamba si la kuchikiza katika mkusanyiko wa watu.

Watu walikuwa wanalia na kuomboleza. Hii inaonyesha uzito wa maombelezo kwa ajili ya mtu aliyekufa.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha kutumia maneno yale yale kwa ajili ya: mahali pa kuabudia na wafuasi wa karibu yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

Hakikisha tafsiri ya kifungu cha maneno ‘Nilihisi nguvu za kuponya zikinitoka’ haimaanishi kwamba Yesu alipoteza cho chote katika nguvu yake ya kuponya kwa sababu ya mama kumgusa. ‘Mwanangu’ haimaanishi msichna ni binti wa Yesu kibaolojia.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu anamjua kila mtu – hata kama ni maskini na mgonjwa; anajali juu ya masuala ya watu wanayoyapitia; anajali juu ya wanawake, anatuhamasisha kumwamini na kumtumaini Yeye; Anahuruma kubwa kwa ajili ya watu wake, Ana nguvu dhidi ya kifo.

Imani

Mungu anatutegemea sisi kumwendea yeye kwa imani, tukiamini atatuponya na kutusaidia wakati wa uhitaji.

Page 47: StoryTapestry Manual - Swahili

47

Yesu Awalisha 5,000

Luka 9:10-17

Kigezo kwenye NLT

Mpito:

Yesu aliwapa nguvu na mamlaka wafuasi wake wa karibu. Siku moja aliwatuma waende vijijini ambako waliwafundisha watu na kufanya miujiza mingi.

Luka 9:10-12

Wakati wafuasi wa Yesu wa karibu waliporudi, walimweleza Yesu kila kitu walichofanya. Kisha akaondoka nao kimya kimya kwenda kwenye mji wa karibu. Lakini makutano walijua wapi alikuwa akienda, na wakamfuata. Aliwakaribisha na akawafundisha juu ya Ufalme wa Mungu, na akawaponya wale waliokuwa wagonjwa. Baadaye jioni wafuasi wake wa karibu walimwendea na kusema, “Waruhusu makutano waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, ili waweze kutafuta chakula na mahali pa kulala kwa ajili ya usiku. Hakuna chakula cho chote katika eneo hili la porini.

Luka 9:13-14

Lakini Yesu akasema, “Wapeni ninyi chakula.” “Lakini tunayo mikate mitano tu na samaki wawili,” walijimjibu. Au unatutegema sisi tuende nje na kununua chakula cha kwa kuwatosha hawa makutano wote?” Kulikuwa na zaidi ya watu 5,000 wanaume ukijumulisha wanawake na watoto. Yesu akajibu, “Waketisheni chini katika makundi ya kama watu hamsini.”

Luka 9:15-17

Kwa hiyo watu wakakaa chini. Yesu akaichukua mikate mitano na samaki wawili, akaangalia kuelekea mbinguni, na akavibarikia. Kisha, akaikata mikate katika vipande vipande, Aliendelea kuwagawa mikate na samaki kwa wafuasi wake wa karibu ili waweze kuigawa kwa watu. Wote walikula kwa kadri walivyotaka, na baadaye, wafuasi wa karibu walikusanya makapu kumi na mbili yaliyojaa mabaki!

Page 48: StoryTapestry Manual - Swahili

48

Mwambatano Ndani ya Simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: wafuasi wa karibu, miujiza, Ufalme wa Mungu, mbinguni, na kubarikiwa yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

‘Mkate na Samaki’

Kuongezeka kulikuwa kwa tendo la kimuujiza au muujiza. Hakikisha kulihusisha katika namna ambayo ni rahisi kueleweka.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Anazo nguvu za kufanya miujiza; Mungu anajali juu ya mahitaji ya watu; Mungu anaweza kuchukua kidogo mtu alicho nacho na kukiongeza; Mungu anawaamini wafuasi wake.

Page 49: StoryTapestry Manual - Swahili

49

Viongozi wa Dini wenye Wivu

Luka 19:47, 48; 20:1-8

Kigezo kwenye NLT

Mpito:

Watu wengi waliomfuata Yesu walipenda kile alichokifanya, lakini siyo Viongozi wa Dini. Walikuwa na wivu juu ya Yesu.

Luka 19:47, 48

Baada ya hayo, Alifundisha kila siku mahali pa kuabudia, lakini viongozi wa dini wa watu walijaribu namna wakatakavyomuua. Lakini kwa sababu watu walimsikiliza Yeye kwa karibu, hawakufikiria kwa njia gani.

Luka 20:1, 2

Siku moja wakati Yesu akiwafundisha watu na kuhubiri ujumbe wa Mungu katika mahali pa kuabudia, viongozi wa dini walimjia. Walimtaka, “Kwa mamlaka ya nani unafanya haya yote? Nani aliyekupa wewe haki?”

Luka 20:3-8

“Ngojeni niwaulize swali kwanza,” Yesu aliwajibu. “Je, mamlaka ya Yohana kubatiza ilitoka mbinguni, au ilitoka tu kwa wanadamu?” Wakasemezana wao kwa wao. “Kama tukisema ulitoka mbinguni, Atatuuliza kwa nini hatukumwamini Yohana. Lakini tukisema ulitoka tu kwa wanadamu, watu watatupiga mawe sisi kwa sababu kwa sababu wamemkubali Yohana kuwa alikuwa mmoja wa wajumbe wa Mungu.” Kwa hiyo mwishowe walijibu kwamba hawakujua. Na Yesu akajibu, “Basi sitawaambia kwa mamlaka ya nani nafanya mambo haya yote.”

Page 50: StoryTapestry Manual - Swahili

50

Falsafa za Maisha

Viongozi wa dini hawakuwa na haki ya kisheria kumuua mtu au kumfanya mtu auwe.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha kutumia maneno yaleyale kwa ajili ya: viongozi wa dini, mahali pa kuabudia, Ujumbe wa Mungu, Batiza, mbinguni, na Msemaji wa Mungu (mjumbe) yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

‘Tupige sisi kwa mawe’

Njia ya kifo (adhabu ya kifo).

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Yesu hakuwaogopa watu au viongozi; Yesu alikabiliana na kutokuamini.

Page 51: StoryTapestry Manual - Swahili

51

Mwanamke Mwenye Dhambi Asamehewa

Yohana 8:1-11

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Yesu alisafiri kwenda Yerusalemu, mji ambapo wazao wa Ibrahimu walimwabudu Mungu. Wakati wa mchana, alikuwa akifundisha katika mahali pa kuabudia.

Yohana 8:2 – 6

Siku moja, alipokuwa akifundisha makutano ghafla walikusanyika, na alikaa chini na kuwafundisha. Alikuwa akiongea, viongozi wa dini walimleta mwanamke waliyemkamata katika tendo la uzinzi. Walimweka mbele ya makutano. “Mwalimu,” walimwambia Yesu, “mwanamke huyu amekamatwa katika tendo la uzinzi. Sheria ya dini yetu inasema auwe kwa kupigwa mawe. Je wewe unasemaje?” Walikuwa wakijaribu kumkamata katika kusema kitu watakachokitumia dhidi yake, lakini Yesu hakujibu mara moja.

Yohana 8:7, 8

Waliendelea kudai jibu, kwa hiyo akasimama tena na kusema, “Sawa, mpigeni mawe. Lakini wale ambao hawajawahi kutenda dhambi warushe jiwe la kwanza!”

Yohana 8:9-11

Wale washitaki waliposikia hili, waliondoka taratibu mmoja mmoja, kuanzia ya yule mkubwa, hadi Yesu alipoachwa katikati ya kundi na mwanamke. Yesu alisimama tena na kumwambia mwanamke, “Wako wapi washitaki wako? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?” “Hapana, Bwana”, mwanamke alisema. Na Yesu alisema, “Na mimi sikuhumu. Nenda na usitende dhambi tena.”

Page 52: StoryTapestry Manual - Swahili

52

Mwambatano ndani za Simulizi

Hakikisha unatumia maneno yaleyale kwa ajili ya: wazao wa Ibrahimu, mahali pa kuabudia, Yerusalemu, Kuabudu, viongozi wa dini, dhambi, na Bwana yaliyotumika katika simulizi zilizopita.

Umahiri wa Simulizi

Viongozi wa dini walikuwa wakijaribu kuthibitisha kwamba Yesu alikuwa akiwafundisha watu kuikaidi sheria.

Viongozi wa dini wanarejea kwenye ‘Sheria ya Musa,’ lakini kwa sababu hatumtaji Musa katika mpangilio wa simulizi, tumekirahisisha kifungu cha maneno kuwa, ‘sheria za dini yetu.’

Zingatia kwamba hawakumleta mwanamme aliyeshirikiana naye katika tendo. Sheria inataka kwamba wote wawili wanatakiwa kupigwa mawe.

Kifungu cha maneno ‘auawe kwa kupigwa mawe’ kimejumuishwa ili walengwa ambao hawana uzoefu wa kupigwa mawe wataweza kuelewa kwamba inamaanisha ni namna ya adhabu ya kifo.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Wakati dini inalaumu watu, Mungu anataka kuwaokoa; Mungu huwatendea sawa sawa, wanawake na wanaume.

Page 53: StoryTapestry Manual - Swahili

53

Njama na Mlo wa Mwisho wa Jioni.

Luka 22:1-6, 14, 15, 19-23; Yohana 13:3-5, 12-17;

Mathayo 26:30

Imetumia tafsiri ya Biblia ya: NLT

Badiliko:

Viongozi wa dini wa wakati ule walianza kukosa amani kwa sababu Yesu alitoa madai, kama“Mimi na Baba tu umoja; Yeye anaionaye mimi amemwona Baba/Mungu.” Walikuwa na wivu kwa sababu watu wengi walimwamini na walikuwa wakimsifu Yeye. wakajikusanya pamoja kupanga namna ya kumuua.

Luka 22:1-6

Sikukuu kubwa ya kidini ilikuwa inakaribia. Wakuu wa viongozi wa dini walichangamkia mpangowa mauaji ya Yesu. Lakini walitaka kumuua bila kuanzisha machafuko, uwezekano ambao waliuhofia sana. Kisha Shetani akamuingia Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wafuasi kumi na wawili wa karibu, na alikwenda kwa viongozi wa dini kujadilana nao ana njia nzuri ya kumsaliti Yesu kwao. Walifurahishwa kwamba alikuwa tayari kuwasaidia, na wakamuahidi zawadi. Kwa hiyo akaanza kutafuta fursa ya kumsaliti Yesu ili waweze kumkamata kimya kimya wakati makutano hawatakuwapo.

Luka 22:14, 15

Yesu na wafuasi wake kumi na mbili wa karibu, walikaa pamoja mezani kusherehekea mlo kwa ajili ya sikukuu ya kidini. Yesu akasema, “Nimekuwa nikitazamia kula mlo huu pamoja nanyi kabla yakuanza kwa mateso yangu.”

Yohana 13:3-5, 12-17

Yesu alijua Mungu amempa mamlaka juu ya kila kitu. Aliondoka kutoka mezani, akavua vazi lake, akajifunga taulo kiunoni mwake, na akamiminamaji kwenye beseni. Kisha akaanza kuwanawisha wafuasi wake wa karibu miguu na kuwafuta kwa taulo alilojifunga kiunoni. Baada ya kuwatawadha miguu yao, alivaa vazi lake tena na kukaa chini na akawauliza, “Mnaelewa kile nilichokuwa nafanya? Mnaniita ‘Mwalimu’ na ‘Bwana,’ Na mko sahihi, kwa sababu ni kweli. Kwa kuwa Mimi, Bwana na Mwalimu wenu, nimewaosha miguu yenu, imewapasa kuoshana miguu ninyi kwa ninyi. Nimewapeni mfano wa kufuata. Fanyeni hivyo ninyi kwa ninyi kama nilivyowatendea. Ni kweli mtumishi si mkuu kuliko Bwana.Mnayajua mambo haya yote-sasa ya fanyeni!”

Luka 22:19-23

Yesu pia alichukua sehemu ya mkate, akamshukuru Mungu na akawagawia wafuasi wake wa karibu wapate kula. Akasema, Mkate huu unawakilisha Mwili wangu, umetolewa kwenu. Fanyeni hivi ili kunikumbuka mimi.” Baada ya chakula cha jioni alichukua kikombe cha mvinyo na kusema, Mvinyo ni ishara ya ahadi mpya ya Mungu kuwaokoa ninyi – makubaliano yaliyofungwa kwa damu nitakayoimwaga kwa ajili yenu.”

Mathayo 26:30

Page 54: StoryTapestry Manual - Swahili

54

Kisha wakaimba wimbo wa sifa, na wakaenda mahali palipoachwa ukiwa katika mlima wa Mizeituni nje ya mji.

Page 55: StoryTapestry Manual - Swahili

55

Maneno/Vifungu vya Maneno vya kujadili

‘mtumishi si mkuu kuliko Bwana’

Maana yake ni kwamba Wafuasi wa Yesu hawawezi kujihesabia kuwa wa muhimu sana kutenda kama watumishi, kwa sababu Yesu mwenyewe alijifanya mtumishi. Wao pia wasitegemee kutendewa vizuri zaidi kutoka kwenye ulimwengu kuliko Yesu alivyopewa.

‘Mkate’

Hadhira inaweza isilielewe neno ‘mkate.’ Neno lingine la mkate kama vile ‘mikate kwa lugha nyingine inaweza kutumika’ kutumika.

Viwakilishi/Ishara

Baadhi ya wasomi wa Biblia wanakubaliana kwamba Yesu alikuwa akitumia mkate na mvinyo kama ishara au viwakilishi ya mwili na damu yake. Yesu alitumia,viwakilishi vinavyoshabihiana katika hotuba alipotoa matamshi kama vile; “Mimi ni mlango” na Mimi ni mkate wa uzima”

‘Wimbo wa Sifa’

Huu unawezakana kabisa ulikuwa wimbo ulioimbwa kama sehemu ya Mlo wa Pasaka uliojulikana kama Hallel, wimbo wa sifa kwa Mungu.Kwa kawaida ya tafsiri msemo huu ni ‘wimbo wa shukrani’ au ‘wimbo wa sifa’ kwa Mungu

Angalia faharasa kwa ajili ya:

Baba

Falsafa za Maisha

Katika tamaduni ambapo kutaja neno mvinyo ni machukizo ya hali juu au kutasababisha watu kutomheshimu Yesu, sema ‘kikombe’ au ‘kikombe cha kinywaji.’

Mwambatano ndani ya Simulizi

Hakikisha kutumia maneno yale yale kwa ajili; Wafuasi wa karibu, Shetani, Bwana, viongozi wa dini na Okoa, yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahili wa simulizi

‘Kuokoa’

Hadhira haielewi Mungu anatuokoa kutoka wapi, tengeneza ahadi mpya iliyo wazi kwa kusema kitu kama, ‘kuwaokoa ninyi kutoka dhambi zenu’ ‘kuwasamehe ninyi kutoka dhambi zenu’ n.k.

‘Agano lililofungwa kwa damu nitakayoimwaga kwa ajili yenu’

Page 56: StoryTapestry Manual - Swahili

56

Hadhira inaweza kuifahamu au kutoifahamu ahadi/agano lililofungwa katika damu. Ikiwa sivyo, badilisha kifungu hiki cha maneno kuwa kitu kama, ‘makubaliano yaliyowezeshwa na kifo change kwa kuwaruhusu watu waniue mimi.’ Tukio la Yesu kuwatawadha miguu wafuasi wake limejumuishwa kwa sababu limeonekana kuwa la muhimu sana katika utamaduni wa Asia kuonyesha wazo la uongozi wa kitumishi. Hii imedhihirishwa wazi katika tamaduni nyingi kwa neno picha kutawadha miguu. Simulizi hii ilipokuwa ikijaribiwa, watu wengi walisema hii ndio ilikuwa sehemu ya muhimu sana katika simulizi.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu amelitoa agano au ahadi mpya; anao mpango.

Kanisa

Utumishi/huduma; Mlo wa Mwisho uliasisiwa; Kuabudu

Maombi

Yesu alimshukuru Mungu kwa ajili ya elementi za Mlo wa Mwisho

Page 57: StoryTapestry Manual - Swahili

57

Yesu Asalitiwa

Luka 22:47-54, 63-71

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Yesu na wafuasi wake wa karibu, waliondoka mahali pa kuabudia na kwenda mahali penye utulivu kuongea na kuomba. Yuda alikubali kwa siri kumsaliti Yesu kwa viongozi wa dini kwa hiyo aliondoka kwenda kukutana nao.

Luka 22:47-54

Wakati Yesu alipokuwa akiongea na wafuasi wake wa karibu, kundi la watu lilimkaribia likiongozwa na Yuda aliyekuwa akimsaliti Yesu. Yuda alikwenda moja kwa moja kwa Yesu kumsalimia kwa busu. Lakini Yesu akamwambia, “Yuda, unaweza kunisaliti mimi kwa busu?” Wafuasi wengine wa karibu waliposogea waliona nini kilikuwa kinakwenda kutokea, wakatamka ghafla, “Je tunaweza kupigana nao? Tumekuja na mapanga yetu!” Mmoja wao akamshambulia kichwani mmoja wa watumishi wa viongozi wa dini, akamkata na kuliondoa sikio lake la kuume. Lakini Yesu akasema, “hakuna tena haya” Akaligusa sikio la mtu huyu na kumponya. Kisha Yesu akazungumza na viongozi wa dini waliokuja kumkamata. “Je mimi ni mhalifu hatari,” aliuliza, “kwamba mnanijia kwa mapanga na marungu kunikamata? Kwa nini hamkunikamata katika mahali pa kuabudia? Nilikuwa pale kila siku. Lakini huu ni wakati wenu, wakati ambao mamlaka za giza hutawala.” Kwa hiyo wakamkamata na kumpekeka nyumbani kwa kiongozi wa dini. Petro alimfuata kwa mbali.

Luka 22: 63-71

Walinzi waliomlinda Yesu walianza kumdhihaki na kumpiga. Walimfunga macho yake na kusema, “Tuambie ni nani aliyekupiga wakati ule?” wakamtolea maneno mengi mengi ya kumtukana. Kulipokucha viongozi wote wa dini walikusanyika. Yesu aliongozwa mbele ya mkutano wa dini, na walisema, “Tuambie, wewe ni Mkombozi Aliyeahidiwa?” Akajibu, “Ikiwa nitawaambia hamtaniamini. Na kama nikiwauliza swali, hamwezi kunijibu. Lakini tangu sasa, Nitakuwa nimeketi mahali penye nguvu, mkono wa kuume wa Mungu.” Wakapaza sauti, “Kwa hiyo unadai kuwa Mwana wa Mungu? Na akajibu, Ninyi mnasema mimi ndiye.” “Kwa nini tunahitaji mashahidi wengine?” walisema, “Sisi wenyewe tumesikia alichokisema.”

Page 58: StoryTapestry Manual - Swahili

58

Falsafa za Maisha

‘Mwana wa Mungu’

Kama unafanya kazi katikati ya makundi ya watu wa Kiislamu ambao wanaweza kukasirishwa kwa neno ‘Mwana’, au ikiwa inamaanisha ‘mtoto wa kuzaliwa kibaiolojia’ tu katika lugha yao, jaribu kutafuta neno kwa ajili ya ‘mwana’ ambalo halitamaanisha ‘mtoto aliyezaliwa kibaiolojia’.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: wafuasi wa karibu, viongozi wa dini, Mkombozi Aliyeahidiwa, mahali pa kuabudia, mkutano wa dini, Kuhani mkuu, kusaliti, uovu, na Mwana wa Mungu yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Neno/ahadi za Mungu zilitimizwa; Yesu anasema Yeye ni Mwana wa Mungu.

Page 59: StoryTapestry Manual - Swahili

59

Hukumu ya Yesu

Luka 23:1-5, 13-16, 21-24

Kigezo katika: NLT

Luka 23:1-5

Kisha wale walikuwepo kwenye mkutano wa dini walimchukua Yesu kwenda kwa Pilato, gavana. Walianza kueleza mashitaka yao. “Mtu huyu amekuwa akiwapotosha watu wetu na kuwazuia watu kulipa kodi zao Serikalini kwa kudai kuwa ni Mkombozi Aliyeahiwa, mfalme.” Kwa hiyo Pilato akamuuliza, “Je wewe ni mfalme wa watu hawa?” Yesu akajibu, “Wewe wasema.” Pilato akawageukia viongozi wa dini na makutano na kusema, “Sioni kosa lo lote kwa mtu huyu!” Kisha wakaweka msisitizo. “Lakini anasababisha machafuko kwa mafundisho yake kila anakokwenda!”

Luka 23:13-16

Kisha Pilato akawakutanisha pamoja viongozi wa dini, pamoja na watu na akatangaza hukumu yake. “Ninyi mmleta mtu huyu kwangu, mkimshitaki kwa mba anapotosha watu. Mimi nimemchunguza kwa makini mbele yenu na kumkuta hana hatia. Hakuna neno lolote alilolitenda mtu huyu limpasalo adhabu ya kifo. “Atachapwa mijeledi, na kisha nitamfungua.”

Luka 23:21, 22

Bali waliendelea kupiga kelele, “Auawe! Auawe!”. Kwa mara ya tatu akawauliza, “Kwanini? Huyu ametenda uovu gani?

Luka 23:23, 24

Lakini sauti za watu zikawa na nguvu zaidi, wakimtaka kwamba Yesu auawe, na sauti zao zikashinda. Pilato akamhukumu Yesu kuawa kama walivyotaka.

Page 60: StoryTapestry Manual - Swahili

60

Falsafa za Maisha

Katika baadhi tamaduni, swali la kiongozi wa wakuu dini juu ya Yesu kuwa Mwana wa Mungu na majibu yake ya nguvu ya uthibitisho wa Yesu kwamba Alikuwa ni Masihi, Mwana wa Mungu’ ni sahihi kabisa. Jina hili linaweza kutoeleweka kumaanisha uzao wa kibaiolojia wa Mungu. Simulizi hii haijitoshelezi kujenga hoja ya Yesu kama Mwana wa Mungu. Itakuwa vema kutumia maelezo ya Luka ya hukumu ambapo kiongozi wa wakuu wa dini ambaye aliuliza tu ikiwa Yesu ni Masihi (‘Mkombozi Aliyeahidiwa’) (Luka 22:67).

Viongozi wa dini hawakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu ya hukumu ya kifo, kwa hiyo walitakiwa kumshawishi gavana wa Kirumi kufanya hivyo. Kama inachanganya kwa hadhira kwa nini walikwenda kwa gavana, fanya hili kuwa uwazi katika simulizi.

Mwambatano wa ndani wa simulizi

Hakikisha kutumia maneno yale yale kwa ajili: viongozi wa dini na Mkombozi Aliyeahidiwa, yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahili wa Simulizi

Yesu ‘kuchapwa mijeledi,’ na kupewa hukumu isiyo ya haki yote ni kutimizwa kwa unabii kutoka Isaya 53.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Neno la Mungu/Kutimizwa kwa ahadi; Yesu hana dhambi; Yesu hakufanya kosa lo lote; Yesu kwa hiyari yake alijitoa kukidhi matakwa ya watu.

Kushirikishana Injili

Yesu hakuhukumiwa kifo kwa ajili ya dhambi zake, bali dhambi zetu.

Page 61: StoryTapestry Manual - Swahili

61

Yesu aliubeba Msalaba Wake

na Alisulubiwa

Luka 23:26-28, 31-35, 39-46, 50-56

Kigezo kwenye NLT

Luka 23:26-27

Na walipokuwa wakimtoa Yesu, mtu aitwaye Simon, aliyekuwa anatokea mji mwingine, ilitokea alikuwa akiingia kutokea mashambani. Askari walimchukua na kuweka msalaba juu yake na wakamtaka auchukue nyuma ya Yesu. Kundi kubwa la watu lilitembea nyuma, ikiwa ni pamoja na wanawake waliokuwa wameshikwa na majonzi.

Luka 23:28, 31

Yesu akawaambia wanawake, “Enyi wanawake, msinililie mimi, bali lieni kwa ajili yenu na watoto wenu. Ikiwa Mungu amenitoa mimi katika mateso haya kwa sababu nimejitoa kuwa kafara/sadaka kwa ajili ya dhambi, je atafanya nini kwa watenda dhambi wenyewe?”

Luka 23: 32-35

Wahalifu wawili walitolewa ili wauawe pamoja na Yesu. Wakachukuliwa kwenda mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa. Huko walimpiga misumari kwenye viganja na miguu yake na wakampigilia misumari juu ya mbao za mti. Akainuliwa juu – mhalifu mmoja mkono wake wa kuume, mwingine mkono wa kushoto kwake. Yesu alisema, “Baba Mungu, uwasamehe hao wanaoniua mimi, kwa kuwa hawajui walitendalo.” Askari walipiga kura kuona ni nani atakayepata mavazi yake. Makutano waliangalia na viongozi walifanya dhihaka. “Aliokoa wengine,” walisema, “na ajiokoe mwenyewe ikiwa ndiye Mkombozi Aliyeahidiwa na Mungu.”

Luka 23:39-43

Mmoja wa wale wahalifu aliyekuwa akining’inia alimdhihaki, “kwa hiyo wewe ndiye Mkombozi Aliyeahidiwa, Ni wewe? Dhihirisha hili kwa kujiokoa mwenyewe na sisi pia wakati huu!” Lakini mhalifu mwingine alipinga, “Humwogopi Mungu hata wakati huu ambao umehukumiwa kufa? Tunastahili kufa kwa ajili ya uhalifu wetu, lakini mtu huyu hakufanya lo lote baya.” Kisha akasema, “Yesu, nikumbuke mimi utakaporudi tena kwa nguvu kutawala.” Yesu akajibu, Ninakuhakikishia, siku ya leo ikiisha, utakuwa nami mbinguni.”

Luka 23:44-46

Muda wa saa sita mchana, na giza likatanda katika nchi yote hadi saa tisa . Kisha Yesu akapaza sauti, “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu!” Kwa maneno hayo akafa.

Page 62: StoryTapestry Manual - Swahili

62

Luka 23:50-53

Kulikuwa na kiongozi wa dini mzuri ambaye hakukubaliana na yale ambayo wengine waliyafanya. Alikwenda kwa gavana na akauomb mwili wa Yesu. Aliuchukua mwili kutoka kwenye mbao za mti, akaufunga katika sanda na akaulaza kwenye kaburi ambalo lilikuwa limechongwa mwambani. Jiwe kubwa likawekwa mbele ya mlango wa kaburi. Kisha wakaenda nyumbani na kuandaa manukato ya kuweka kwenye mwili wake kwa ajili ya maziko. Siku yao ya dini ya kupumzika ilikuwa imeanza, kwa hiyo walitakiwa na sheria zao za dini kusubiri hadi ipite ndipo wangeweza kwenda tena kwenye kaburi.

Page 63: StoryTapestry Manual - Swahili

63

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kujadili

Angalia Faharasi kwa ajili ya:

Roho

Kaburi

Falsafa za Maisha

Ikiwa hadhira hailielewi ‘msalaba’, uelezee kama ni kitu fulani kama ‘mbao za mti’ au msalaba ulitengenezwa kwa mbao mbili za mti’

Baadhi ya tamaduni hawaamini mwanamke anaweza kuona maiti. Wanaweza kuhisi matendo ya wanawake hapa kuwa si sahihi au ya kigeni. Kwa hiyo, chagua kusema ‘baadhi ya wafuasi wa Yesu’

Mwambatano wa ndani wa Simulizi

Hakikisha kutumia maneno yale yale kwa ajili ya: Baba, kafara/sadaka, dhambi, kusamehe, kuokoa, wafuasi, viongozi wa dini, Mkombozi Aliyeahidiwa, mbinguni, na kuuawa yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahili wa Simulizi

Simulizi hii inaonyesha mwitikio wa mhalifu kwa Yesu alipomkubali Yesu kama Mkombozi Aliyeahidiwa na Mungu/Masihi.

‘utakaporudi na nguvu kutawala’

Hii ni kukubalika kunakotafsiriwa kuwa ‘kuja kwa ufalme wako’

Maelezo ya Luka juu ya Yesu Kubeba Msalaba Wake na simulizi ya kusulubiwa imetumika kwa sababu inaonyesha kutimizwa kwa unabii katika mpangilio wa simulizi hii.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu ni Baba

Hakika ya Wokovu

Yesu alisema, ‘Ninakuhakikishia kuwa, utakuwa naimi.’

Maombi

Yesu aliongea na Baba wakati wa adhabu yake.

Page 64: StoryTapestry Manual - Swahili

64

Kufufuka kwa Yesu

Luka 24:1-7; Yohana 20:11-18

Kigezo katika: NLT

Luka 24:1-4

Mapema sana asubuhi baada ya kifo cha Yesu wanawake walikwenda kaburini kuuandaa mwili wa Yesu sawa sawa na mila zao. Walikuta kwamba jiwe limeondolewa kutoka mlangoni. Waliingia ndani, lakini hawakuuona mwili Wake. Wanaume wawili waliovaa mavazi ya kumeta meta waliwatokea.

Luka 24:5-7

Wanawake waliogopa na kuinama kifudifudi hata nchi. Wanaume wakauliza, “Kwa nini mnaangalia ndani ya kaburi kwa ajili ya mtu ambaye yuko hai? Hayupo hapa! Amefufuka kutoka kwa wafu! Kumbukeni alipowaambia kwamba, ni lazima asalitiwe na kuhukumiwa, na kwamba atafufuka tena siku ya tatu.

Luka 24:8-12

Kisha walikumbuka kwamba Yesu alisema hayo. Walikimbia kutoka kaburini kwenda kuwaambia wafuasi wake wa karibu na kila mtu kile kilichootokea. Alikuwa ni Mariamu Magdalena na wanawake wengine wengi waliowaambia wafuasi wake wa karibu nini kilichotokea lakini hawakuwaamini. Moja wao alikimbia kwenda kaburini kuangalia. Alitazama na kuona vile vitambaa vya sanda tu. Kisha alirudi nyumbani tena, wakistaajabu nini kilikuwa kimetokea.

Yohana 20:11-18

Mariamu alikuwa akisimama nje ya kaburi akilia, na alipokuwa akilia, alitulia na kutazama ndani ya kaburi. Aliwaona malaika wawili wenye mavazi meupe. “Ee mwanamke, kwa nini unalia?” Malaika walimuuliza. “Kwa sababu wamemchukua Bwana wangu,” alijibu, “na sijui wamemweka wapi?” Mwanamke aligeuka na alipokuwa akiondoaka alimwona mtu amesimama pale. Alikuwa Yesu, lakini hakuweza kumtambua. “Ee mwanamke, kwa nini unalia?” Yesu alimuuliza mwanamke. “ni nani unamtafuta?” Mwanamke alifikiri kuwa alikuwa ni mtunza bustani na kusema, “ Bwana, ikiwa umemuondoa, niambie wapi umemweka, na nitakwenda na kumchukua.” “Mariamu!” Yesu akasema. Alimgeukia na kulia kwa sauti, “Mwalimu!” “Usiniguse,” Yesu alisema, “Kwa kuwa bado sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda watafute ndugu zangu na uwaambie kwamba huko ndiko ninakokwenda.” Mariamu Magdalena aliwakuta wafuasi wake wa karibu na kuwaambia kwamba, “Nimemwona Bwana” Kisha akawapa ujumbe Wake.

Page 65: StoryTapestry Manual - Swahili

65

Falsafa za Maisha

‘kwa kadri ya desturi/mila zao’

Kifungu hiki cha maneno kimejumuishwa katika maelezo ya wanawake kwenda kaburini kwa sababu tamaduni nyingi haziandai maiti kwa maziko.

Mwambatano ndani ya Simulizi

Hakikisha kutumia maneno yale yale kwa ajili ya: kaburi, Bwana, wafuasi wa karibu, kuamini, malaika, na Baba yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahili wa Simulizi

Hakikisha kwamba hadhira inaelewa kwamba Yesu alikuwa amekufa lakini yu hai sasa.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Kila kitu ambacho Yesu aliwaambia wafuasi wake wa Karibu kimetimia; Yesu alikuwa mwema/upendo katika utendaji wake kwa wanawake; Yesu anawaagiza wafuasi wake kuwaambia wengine ujumbe Wake; Yesu hayuko tenda kifoni bali yu hai.

Page 66: StoryTapestry Manual - Swahili

66

Baada ya Kufufuka

Mathayo 28:18-20; Matendo 1:3-5, 8-14

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu, Aliwatokea wafuasi wake mara kadhaa. Aliwapa maagizo muhimu kuhusu nini cha kufanya.

Mathayo 28:18-20

Yesu alikuja kwa wanafunzi wake na kusema, “Mamlaka yote mbinguni na duniani nimepewa. Nendeni mkawafanye kuwa wafuasi wote mtakaokutana nao, mkiwabatiza na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Kumbukeni, niko pamoja nanyi siku zote.

Matendo 1:3-5

Kipindi cha siku arobaini baada ya kuuawa na kufufuka kwake, Yesu alijitokeza kwa wafuasi wake wa karibu na kuwathibitishia kwa namna mbalimbali kwamba kwa hakika alikuwa hai. Wakati fulani alipokuwa akila nao chakula, Aliwaambia, “Msitoke katika mji mnaoabudia mpaka Baba (Mungu) anapowapa ninyi kile alichoahidi. Katika siku chache tu mtapokea Roho wa Mungu.

Matendo 1:8

“Roho wa Mungu atakapowajilia, mtapokea nguvu na mtawaambia watu habari zangukila mahali - hapa, maeneo yote yanayozunguka vijiji, katika miji iliyo karibu na hata mwisho wa nch.”

Matendo 1:9-11

Haikuchukua muda mrefu tangu Yesu aliposema haya Alichukuliwa juu kwenda mbinguni. Wafuasi wake walipokuwa wakimtazama, alipotelea katika mawingu. Walipokuwa wakikaza macho kumtazama, wanaume wawili waliovalia kanzu nyeupe ghafla walisimama karibu nao. Wakasema, “Kwa nini mmesimama hapa mkiangalia mbinguni? Yesu amekwisha twaliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni. Siku moja, kama mlivyomwona akienda, Atarudi tena!”

Matendo 1:12-14

Wafuasi wa Yesu walitembea kurudi mjini mahali walipoabudu na kwenda kwenye nyumba ambayo walikuwa wakikaa. Hapo, walikutanika kwa pamoja wakiendelea na maombi, pamoja na mama yake Yesu, wanawake wengine wengi na ndugu zake Yesu.

Page 67: StoryTapestry Manual - Swahili

67

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha kutumia maneno yale yale kwa ajili ya: wafuasi wa karibu, Baba, Roho wa Mungu, mbinguni, batiza, utii, wafuasi, mji ambao wanaabudu, na kuabudu yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu alikuwa mwaminifu kwenye Neno Lake na alimpeleka Roho Mtakatifu kwao; Nguvu huja kutoka kwa Mungu; Yesu aliishinda nguvu ya uvutano.

Kushirikisha Injili

Chukua ujumbe huu kwa watu wote; pata nguvu kutoka kwa Mungu.

Page 68: StoryTapestry Manual - Swahili

68

Roho wa Mungu

Mdo 1:15, 16, 18, 20-26; 2:1-12

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Wafuasi wa Yesu walikaa mjini wakisubiri Roho wa Mungu kama walivyoagizwa.

Mdo 1:15, 16

Walipokuwa wakisubiri, siku ambayo karibu wafuasi mia na ishirini walikuwepo, Petro alisimama na kusema, “Ndugu zangu, ilikuwa lazima kwamba Neno la Mungu limtizwe katika habari ya Yuda aliyewaongoza viongozi wa dini waliomkata Yesu. Hili lilitabiriwa zamani za kale na Roho wa Mungu.

Mdo 1:18

“Tunajua kwamba alikufa mara tu baada kumsaliti Yesu”

Mdo 1:20-22

Petro aliendelea, “Imeandikwa katika ujumbe wa Mungu kwamba mtu mwingine atachukua nafasi yake ya uongozi. Sasa ni lazima tuchague mtu mwingine. Ni lazima awe mtu ambaye amekuwa pamoja nasi wakati wote tulipokuwa pamoja na Yesu – kutoka wakati alipobatizwa, mpaka siku aliyochukuliwa kutoka kwetu kwenda kuwa na Mungu.”

Mdo 1:23-26

Kisha wote wakaomba kwa ajili ya kumchagua mtu sahihi. Mathiya alichaguliwa na akawa mmoja wa wale kumi na wawili, kundi la wafuasi wa karibu wa Yesu ambao walikuwa sasa viongozi wa wale waliomfuata Yesu.

Mdo 2:1

Baadaye, katika siku ya sikukuu muhimu ya kidini, baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu, wafuasi wake walikuwa wakikutana mahali pamoja.

Mdo 2:2-4

Ghafla, kulikuwa na sauti kama ya upepo mkuu uvumao., na ukaijaza nyumba mahali walipokuwa wakikutana. Kisha kile kilichoonekana kama ndimi za moto zilitokea na kuwakalia juu yao kila mmoja aliyekuwepo alijazwa kwa Roho wa Mungu na wakaanza kunena kwa lugha nyingine kadri Roho wa Mungu alivyowapa uwezo huo.

Mdo 2:5-12

Wazao wa Ibrahimu kutoka pande zote za dunia walikuwa mjini ajili ya sikukuu. Walikuja na wakawasikia wafuasi wa karibu wa Yesu wakinena. Walisema, “Watu hawa ni wenyeji wa

Page 69: StoryTapestry Manual - Swahili

69

mahali hapa, na bado tunawasikia wakiongea lugha za nchi tulikozaliwa juu ya mambo makuu aliyoyafanya Mungu! “Walisimama pale wakishangaa na kuchanganyikiwa. “Maana yake nini mambo haya?” Waliulizana wao kwa wao.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: wafuasi, Roho/Roho wa Mungu, wafuasi wa karibu, viongozi wa dini na wazao wa Ibrahimu yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu ni Roho; Mungu anao mpango; Mungu anamwadhimisha Yesu ambaye ni Bwana na Mkombozi Aliyeahidiwa

Kanisa

Waamini wanakusanyika pamoja katika eneo moja; wamejazwa Roho.

Maisha ya uchaji

Kujazwa Roho.

Page 70: StoryTapestry Manual - Swahili

70

Mwafrika

Mdo 8:26 – 32, 34-39

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Wafuasi wa Yesu walikwenda kila mahali wakiwaambia watu habari za ajabu juu ya Yesu. Roho wa Mungu aliwapa baadhi yao maelekezo juu ya wapi pa kwenda. Mmoja wa wafuasi hawa aliitwa Filipo.

Mdo 8:26, 27

Malaika kutoka kwa Mungu alimwambia Filipo, “Nenda pande za chini kusini kwenye barabara ya jangwa inayoetelemkia Yerusalemu.

Mdo 8:27, 28

Kwa hiyo akaenda, na akakutana na mtunza hazina wa taifa la Afrika ambaye sasa alikuwa akirudi nyumbani kwao baada ya kuabudu huko Yerusalemu. Akiwa ameketi katika gari lake, alikuwa akisoma kwa sauti kutoka kitabu cha Nabii Isaya.

Mdo 8:29-32

Roho wa Mungu akamwambia Filipo, “Nenda karibu, na ukatembee kando ya gari.” Filipo akaenda mbio na akamsikia yule mtu akisoma, kwa hiyo akamuuliza, “Je, umeyaelewa hayo unayoyasoma?” Yule mtu akajibu, “Nitawezaje kuyaelewa, wakati hakuna mtu wa kunielekeza? Na akamsihi Filipo apande garini na kukaa naye. Haya ndiyo aliyokuwa akiyasoma: ‘Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni. Na kama vile mwana kondoo alivyo kimya mbele ya amkataye manyoya, hakufumbua kinywa chake.’

Mdo 8:34, 35

Mwafrika alimuuliza Filipo, “Je msemaji alikuwa akiongea habari zake mwenyewe au mtu mwingine? Filipo alianza na ujumbe huo huo wa msemaji wa Mungu na akamweleza kitu gani Mungu alikuwa akisema juu ya Yesu.

Mdo 8:36-39

Walipokuwa wakiendela pamoja, wakafika mahali penye maji na yule mtu wa Afrika akasema, “Tazama, maji haya! Kwa nini nisibatizwe?” “Unaweza,” Filipo akajibu, kama kweli unaamini.” Na yule Mwafrika akajibu, “Ninamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.” Yule Mwafrika akamuru gari lisimame, wakatelemka chini majini na Filipo akambatiza. Kisha yule Mwafrika akaenda njiani akifurahi.

Page 71: StoryTapestry Manual - Swahili

71

Maneno/Vifungu vya maneno ya kujali

“Garini”

Garini linaweza kumaanisha pia ‘mkokoteni’ au gari fulani linalovutwa na farasi au ng’ombe.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha kutumia maneno yaleyele kwa ajili ya: wafuasi, Yerusalemu, kuabudu, malaika, msemaji, Roho wa Mungu, kubatiza na Mwana wa Mungu kama yalivyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahili wa Simulizi

Simulizi hii ilichaguliwa kwa sababu ya uwiano wake na simulizi ya Isaya 53 na inaweka mfano wa mwitikio wa Yesu unaofuatiwa na utii wa kubatizwa mara moja.

Kanuni

Kanisa

Ubatizo, kazi ya maandiko

Kushirikisha Injili

Wale walioamini walikwenda kila mahali wakishikisha ujumbe wa Mungu wakiongozwa na Roho.

Page 72: StoryTapestry Manual - Swahili

72

Paulo Akutana na Yesu

Mdo 8: 1, 3, 9:1-13, 15, 17-21

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Wafuasi wa Yesu walikuwa wakienda kila mahali wakizungumza juu yake. Paulo, kiongozi wa dini, alikuwa pia akisafiri kila mahali akijaribu kuliharibu kanisa.

Mdo 8:1, 3; 9:1-2

Paulo alikuwa akitamka vitisho na alidhamiria kuwaharibu waamini. Alielekea kwenye mji mwingine ili kuwakamata waamini na kuwaleta Yerusalemu katika vifungo.

Mdo 9:3-6

Alipokuwa akiukaribia mji, mwanga mkali kutoka mbinguni ukamwangazia juu yake. Akaanguka chini hata nchi na akasikia sauti ikimwambia, “Paulo, Paulo! Kwa nini unaniudhi?” “Ni nani wewe Bwana?” Paulo akauliza. Sauti ikajibu, “Yesu, unayeniudhi! Sasa inuka na uingie mjini na utaambiwa yakupasayo kufanya.”

Mdo 9:7-12

Watu waliokuwa na Paulo walisimama kimya wakiwa na mshangao, kwa kuwa waliisikia sauti ya mtu lakini hawakuona mtu! Paulo alipoinuka katika nchi alijikuta amekuwa kipofu. Watu aliokuwa nao walimwongoza kwa kumshika mkono kwenda mjini. Alibakia pale akiwa kipofu kwa siku tatu. Basi palikuwa na mwamini aliyeitwa Anania katika mji. Yesu alisema naye katika maono, akamwita! “Ndiyo Bwana!” alijibu. Yesu akasema, “Nenda kwenye nyumba moja. Utakapofika umuulizie Paulo. Anaomba kwangu saa hii. Nimemwonyesha kuwa utakuja na kuweka mikono juu yake ili kwamba aweze kuona tena.”

Mdo 9:13, 15

“Lakini Bwana,” akajibu Anania. “Nimesikia juu ya mambo ya kutisha mtu huyu aliyoyafanya kwa waamini katika Yerusalemu!” Lakini Yesu akasema, “Nenda na ufanye kile ninachosema. Nimemchagua Paulo kuuchukua ujumbe wangu kwa mataifa, wafalme na kwa wazao wa Ibrahimu pia.”

Mdo 9:17, 18

Kama Mungu alivyomwambia, Anania alikwenda na kumkuta Paulo. Aliweka mikono yake juu yake na kusema, “Paulo, Yesu aliyekutokea Yerusalemu amenituma mimi ili kwamba uweze kuona tena na ujazwe kwa Roho wa Mungu.” Ghafla vitu kama magamba vilianguka machoni kwa Paulo, na akapata kuona tena. Kisha akainuka na akabatizwa.

Page 73: StoryTapestry Manual - Swahili

73

Mdo 9:19-21

Paulo alikaa na waamini katika mji ule kwa siku kadhaa, mara akaanza kusema juu ya Yesu akisema, “Yeye ni Mwana wa Mungu hakika!” Wote waliomsikia walikuwa wakishangaa. Je huyu si mtu yule yule ambaye aliwatesa wafuasi wa Yesu katika Yerusalemu?”

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kujadili

‘kanisa’

Ikiwa neno ‘kanisa’ linatoa kitu fulani kutoka kwenye tafsiri ya Agano Jipya, jaribu kulielezea neno katika kifungu cha maneno badala ya kutumia neno ‘kanisa.’ Katika Agano Jipya, neno kamwe halikumaanisha jengo, bali kundi la watu waliomwamini Yesu. Katika Agano Jipya, ‘kanisa’linaweza kumaanisha kundi la waamini wanaoishi mahali pamoja, au jamii pana ya kanisa lote la Yesu.

‘Maono’

Yanaweza kutafsiriwa kama mafunuo ya kimiujiza, wakati mwingine yanakuja kama sehemu ya ndoto kama yalivyokuwa kwa Yusufu kabla ya kuzaliwa kwa Yesu.

‘’Udhi/Tesa’

Kuudhi/kutesa ni kumtendea mtu kikatili au vibaya kwa sababu ya uhusiano alionao na Yesu. Baadhi ya maudhi ni ya kimwili, mengine akili na mengine hisia.

‘Weka mikono juu yake’

Hii ni moja ya njia za msingi ambazo Mungu alitumia watu kuachilia nguvu za Roho Mtakatifu kwa mtu mwingine. Si nguvu za mtu bali ni nguvu za Roho zilizoachiliwa kupitia mtu huyo kwenda kwa mwingine ili kusudi la Mungu liweze kutimizwa.

Angalia faharasa kwa ajili ya:

Waamini

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yaleyale kwa ajili ya: mbingu au mbinguni, Bwana, Wazao wa Ibrahimu, wafuasi, viongozi wa dini, Mji ambapo tunabudu, Roho wa Mungu; Batiza, Yerusalemu, na Mwana wa Mungu yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu: Nguvu ya Mungu humbadilisha mtu; Mungu ana nguvu; Mungu anafanya kazi kupitia watu wanaomfuata Yesu; Mungu hujifunua hata kwa watu wasio wafuasi wake; Roho wake anatenda kazi.

Maombi: Mungu huzungumza na watu na watu huzungumza na Mungu.

Page 74: StoryTapestry Manual - Swahili

74

Uchaji: Watu wanawadhuru wafuasi wa Yesu, ni sawa na kumfanyia Yesu; wafuasi wa Yesu humtii Yeye; wafuasi wa Yesu huwaambia wengine juu Yake; Watu wasiomjua Yesu hutambua wengine wanapobadilishwa na Mungu.

Page 75: StoryTapestry Manual - Swahili

75

Petro Anaponya na Kumfufua

Tabitha kutoka kwa wafu

Mdo 9:32-43

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Petro, mmoja wa wafuasi wa karibu wa Yesu, aliendelea kuwaeleza watu juu ya Yesu.

Mdo 9:32-36

Petro alisafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Alikuja kwenye kijiji kimoja kuwatembelea wamini na akakutana na mtu ambaye hakuweza kutembea na amekuwa kitandani kwa miaka minane. Petro akamwambia, “Yesu mwana wa Mungu akuponya! Simama juu na uchukue godoro lako!” Na mtu yule aliponywa mara moja. Watu wote wa vijiji vile waliomuona mtu huyu akitembea, wakamwamini Yesu.

Mdo 9:36-38

Alikuwapo mfuasi wa Yesu aliyeitwa Tabitha. Sikua zote alifanya mambo mema na kuwasaidia maskini. Tabitha akawa mgonjwa na akafa. Mwili wake uliandaliwa kwa ajili ya maziko na ulilazwa juu orofani. Wafuasi wa Yesu wakasikia kwamba Petro alikuwa karibu, kwa hiyo waliwatuma watu wawili kumsihi aje haraka iwezekanavyo.

Mdo 9:39-43

Petro alirudi pamoja nao. Mara alipofika, walimchukua kwenda chumba cha orofani. Chumba kilikuwa kimejaa wajane ambao walikuwa wakilia na kumwonyesha kanzu na nguo nyingine alizoshona kwa ajili yao. Petro akawataka wote kuondoka chumbani, Kisha, akapiga magoti na kuomba. Akiugekia mwili akasema, “Inuka Tabitha.” Alifungua macho yake! Alipomwona Petro aliketi. Akampa mkono wake akamsaidia kuinuka. Kisha akawaita kuingia wale wajane na waamini wote, na akamweka Tabitha kwao akiwa hai. Habari zilienea katika mji wote, na wengi walimwamini Yesu! Petro alikaa hapo kwa muda zaidi kwa mtu aliyeitwa Simon.

Page 76: StoryTapestry Manual - Swahili

76

Falsafa za Maisha

Ikiwa kufuatia utamadanu si sahihi kubaki pekee yake na mwanamke, isaidie hadhira kuelewa kwamba Petro alikuwa akifuata mpango wa Mungu kwa ajili ya Tabitha.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: wafuasi, wafuasi wa karibu, waamini, Mwana wa Mungu, waliamini na waliomba yaliyotumika katika simulizi iliyotangulia.

Umahili wa Simulizi

Baadhi ya tamaduni zina shida kwa mtu kuongea na mwili uliokufa. Angalia kuona ikiwa hili ni tatizo kwa watu kuambiwa simulizi hii.

Kanuni

Tabia na asili ya Mungu

Mungu hutoa nguvu kwa wale wanaomwani Yeye; Yesu anazo nguvu dhidi ya magonjwa na kifo

Maombi

Mungu hujibu maombi ya wafuasi wa Yesu.

Kanisa

Yesu anao wafuasi katika maeneo mengi.

Kushirikisha Injili

Yesu alipofanya miujiza kupitia wafuasi wake, wengine wengi walifanyika wafuasi wa Yesu.

Page 77: StoryTapestry Manual - Swahili

77

Mlinzi wa Gereza wa Filipi

Mdo 16:12 – 17, 21- 30, 34, 35, 40; 17:1

Kigezo katika: NLT

Mpito:

Kabla Yesu hajaenda mbinguni, aliwaahidi wafuasi wake kuwa watapata nguvu za kushirikisha juu Yake ulimwengu wote. Na hivyo ndivyo walivyofanya. Hii ni simulizi ya safari ya watu wawili waliowaongoza wengine wengi kumfuata Yesu.

Mdo 16:12 – 15

Paulo na Sila walikwenda kwenye mji wa Filipi. Walipokuwa wakienda kuabudu, walikwenda mbali kidogo nje ya mji kando ya mto, ambapo walidhani watu walikuwa wanakutana kwa ajili ya maombi. Walikaa chini na kuongea na baadhi ya wanawake waliokusanyika huko. Mmoja wao alikuwa Lidia, mfanyabiashara wa nguo za gharama,ambaye alimwabudu Mungu. Walipowasikiliza Mungu aliufungua moyo wake na akakubalina na yale aliyokuwa akiyasema Paulo. Alibatizwa pamoja na watu wengine wa nyumbani mwake na akawaomba Paulo na Sila wawe wageni wake. “Kama mmeona kuwa mwaminifu wa kweli kwa Yesu,” alisema, “Njooni na mkae nyumbani kwangu.” Wakakubali.

Mdo 16:16 – 21

Siku moja Paulo na Sila walikuwa wakishuka kwenda mahali pa kusali, walikutana na kijakazi aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu. Alikuwa mwaguzi ambaye aliwapatia bwana zake fedha nyingi. Alimfuata Paulo na kupiga kelele, “Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye Juu, na wamekuja kuwaambia ninyi jinsi ya kuokoka.” Hii iliendelea siku kadhaa wa kadhaa, Paulo akachoshwa na hilo kwamba aligeuka na kusema kwa yule pepo mchafu aliye ndani yake, “Ninakuamuru kwa Jina la Yesu toka.” Mara akaondoka.

Tumaini na mabwana zake la utajiri zikakoma. Wakawakamata Paulo na Sila na waliwakokota mpaka sokoni mbele ya wenye mamlaka. “Mji wote umechafuka kwa sababu ya watu hawa!” waliwapigia kelele wakuu wa mji. “wanawafundisha watu kufanya mambo ambayo yanapingana na mila zetu.

Mdo 16:22 – 28

Ghafla kundi kubwa likakusanyika. Paulo na Sila wakapigwa sana na kisha wakatupwa katika gereza. Mlinzi wa gereza akaagizwa kuhakikisha hawatoroki kwa hiyo akawaweka katika chumba cha ndani na wakafungwa kwa minyororo. Panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kumwimbia Mungu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasilikza. Ghafla, kukawa na tetemeko kubwa na gereza na hata misingi yake ikatikiswa. Milango yote ikafunguka, na vifungo vya wafungwa wote vikaanguka chini! Mlinzi wa gereza akaamka na kuona milango ya gereza imefunguliwa. Alidhani wafungwa wametoroka, kwa hiyo, akavuta upanga wake ili kujiua mwenyewe. Lakini Paulo akampazia sauti, “Acha. Usijiue mwenyewe! Wote tupo hapa!”

Page 78: StoryTapestry Manual - Swahili

78

Mdo 16:29 – 34

Mlinzi wa gereza alitaka taa ziletwe na kukimbilia ndani mbele ya Paulo na Sila. Kisha akawatoa nje na kuwauliza “Bwana zangu yanipasa nifanye nini ili kuokoka?” Walijibu, “Mwamini Yesu nawe utaokoka na wote katika nyumba yako. Wakamwambia ujumbe wa Mungu juu ya Yesu na wote walioishi katika nyumba yake. Kisha yeye na wote wa nyumbani mwake walibatizwa. Mara mlinzi wa gereza akawapa chakula nyumbani kwake na wote wakafurahi kwa sababu wamemwani Mungu.

Mdo 16:35, 40; 17:1

Kesho yake asubuhi wakuu wa mji waliwafungua Paulo na Sila. Paulo na Sila walipoondoka gerezani, walirudi nyumbani kwa Lidia. Hapa walikutana na waamini na wakawatia moyo tena. Kisha wakaondoka kwenda mji mwingine.

Page 79: StoryTapestry Manual - Swahili

79

Maneno/Vifungu vya Maneno ya Kujadili

‘Alifungua moyo wake’

Huu ni msamiati ambao unaweza usieleweke katika lugha zote. Kifungu hiki cha maneno kinamaanisha kwamba Mungu alimfanya awe na uhiyari/uwezo wa kuelewa na kukubali/kuamini kile kilichokuwa kikisemwa na Paulo kuhusu Yesu.

‘Katika Jina la Yesu’

Kifungu hiki cha maneno kimetafsiriwa katika uhalisia wake, kinaweza kisibebe uzito kamili uliokusudiwa. Kama siyo, tumia mojawapo ya mistari hapa chini.

1. Kwa Jina/Mamlaka ya Yesu

2. Kwa mamlaka niliyopewa na Yesu

3. Kwa mamlaka iliyo katika Jina la Yesu.

‘Mwamini Yesu’

Ili kukifanya kifungu hiki kiwe wazi, tumia maelezo kama vile ‘Amini kwamba Yesu atakuokoa’

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya: wafuasi, waamini, kanisa, batiza, roho mchafu, Mungu aliye Juu sana, kuabudu, kusali/kuomba, amini, mbingu au mbinguni na kuokoka.

Kanuni

Kanisa

Walikutana katika nyumba, ubatizo, waliwatia moyo na kuwaimarisha waamini.

Maisha ya Uchaji

Maombi na kuimba

Kushirikisha Injili

Angali maeneo ambayo Mungu yuko kazini; Roho hutoa nguvu ya kushirikisha.

Hakika ya Wokovu

Amini nawe utaokolewa.

Page 80: StoryTapestry Manual - Swahili

80

Kurudi

Mdo 17:1-10; 1Thesalonike 1:1, 2, 6, 7, 9, 10;

2:17, 18, 3:2, 6-8; 4:16-18, 5:25

Kiegezo katika: NLT

Mdo 17:1-5

Kisha Paulo na Sila wakaendelea kusafiri kote kote katika eneo karibu na Filipi. Siku moja walikuja kwenye mji wa Thesalonika. Huko, Paulo aliwaambia watu wengi waliokuwa wa uzao wa Ibrahimu juu ya Yesu. Aliwaambia, “Huyu Yesu ninayewaambia habari zake ni Mkombozi Aliyeahidiwa.” Watu wengi waliamini neno lake. Lakini baadhi ya watu wa uzao wa Ibrahimu waliona wivu, kwa hiyo wakawakusanya baadhi ya watu wasiofaa kutoka mitaani na kuanza ghasia. Walivamia nyumba za wafuasi wa Yesu wakiwatafuta Paulo na Sila ili waweze kuwatoa nje kwenye makundi ya watu.

Mdo 17:6, 7

Walipowakosa Paulo na Sila waliwatoa baadhi ya waamini badala yake na wakawachukua mbele ya wakuu wa mji. Wakapaza sauti, “Mmoja kati ya watu hawa amewaruhusu Paulo na Sila kukaa katika nyumba yake. Paulo na Sila walishitakiwa kwa vurugu kote ulimwenguni na sasa wako hapa wakisumbua mji wetu.”

Mdo 17:8-10

Japokuwa mji ulikumbwa na ghasia kwa taarifa zile, hatimaye mamlaka ya mji iliwaachia Paulo na Sila. Usiku ule ule, waamini waliwatoa nje Paulo na Sila kwa ajili ya usalama wao.

1Thesalonike 2:17, 18; 3:2, 6-8; 1:1

Paulo hakuwasahau waamini wa Thesalonike, kwa hakika, alijaribu mara kwa mara kuwatembelea lakini hakuweza. Kwa hiyo baadaye, Paulo alimtuma rafiki yake aliyeitwa Timotheo. Timotheo aliporudi kwa Paulo na kumpa taarifa, Paulo alifurahi kujua kwamba waamini wale walikuwa wakiendelea kumfuata Yesu pamoja na mateso waliyoyapata. Aliamua kuandika barua yeye mwenyewe, Sila na Timotheo. Alisema,

1Thesalonike 1:2

Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi mara kwa mara.

1Thesalonike 1:6, 7, 9, 10

“Mlipokea ujumbe juu ya Yesu kwa furaha kutoka kwa Roho wa Mungu pamoja na mateso mliyoyapata. Matokeo yake, mmekuwa mfano kwa waamini wote wa eneo hili. Waamini hawa wanazungumza namna mlivyogeuka kutoka katika kuabudu sanamu na kumgeukia Mungu wa kweli anayeishi. Na wanazungumza mnavyokutarajia kurudi kwa Mwana wa Mungu, Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu.

Page 81: StoryTapestry Manual - Swahili

81

1Thesalonike 4:16-18; 5:27

Na Yesu atakaporudi, Yeye mwenyewe atashuka chini kutoka mbinguni kwa sauti kuu. Kwanza waamini wote waliokwisha kufa watafufuliwa, kisha, pamoja nao, sisi tulio hai na waliosalia hapa duniani tutanyakuliwa mawinguni kumlaki Yesu hewani. Tutakuwa pamoja naye milele. Kwa hiyo farijianeni ninyi kwa ninyi na waraka huu usomwe kwa waamini wengine wote.

Mwambatano ndani ya simulizi

Hakikisha unatumia maneno yale yale kwa ajili ya wazao wa Ibrahimu, Mkombozi Aliyeahidiwa; wafuasi, waamini, Roho wa Mungu, amini, mateso, Mwana wa Mungu, na mbingu au mbinguni yaliyotumika katika simulizi zilizotangulia.

Umahiri wa Simulizi

Mwisho wa simulizi umetoa muhtasari wa kuifanya iwe rahisi kwa ajili ya hadhira kukumbuka na kuiweka katika muktadha wa simulizi. Simulizi hii ni mfano wa namna ‘mafundisho’ kutoka kwenye nyaraka yanavyoweza kuwasilishwa. Smulizi hii inaoanisha mafundisho kutoka 1Thesalonike na simulizi zinazoshabihiana kutoka kitabu cha Matendo

Kanuni

Maisha ya Uchaji

Kutazamia mbele kuja kwa Yesu mara ya pili.

Kanisa

Mateso na maumivu kwa waamini; neno la faraja kwa waamini.

Kushirikisha Injili

Wafuasi wa Yesu wanawaeleza watu wengi

Page 82: StoryTapestry Manual - Swahili

82

Faharasa

Manenoufunguo ya Kujadili katika simulizi za Biblia

Manenoufunguo haya yanafungua utambuzi na uelewa katika maandiko. Ikiwa yanaleta picha mbaya katika akili ya wasikilizaji, yanaweza kuuharibu uelewa wote wa mtu wa Habari Njema. Faharasa hii inajaribu kufafanua maana ya ‘manenoufunguo’ katika uelewa wa kibiblia, na namna nzuri ya kuyatafsiri inayofikiriwa. Mara nyingi yamejumuisha mapendekezo juu ya namna ya kutafsiri maneno au kuyaelezea katika maana nzuri kwenye hadhira. Baada ya kila ingizo kuna orodha ya simulizi ambako nenoufunguo linapatikana.

Malaika

Ikiwa tafsiri ya Biblia inapatikana, njia nzuri itakuwa kutumia neno katika tafsiri, isipokuwa hakuna mtu nje ya kanisa halielewi. Kama sivyo, changamoto ni kupata neno ambalo linawasilisha kwa usahihi maana yake ya asili (mwanzo). ‘Malaika’ ni kiumbe wa kimiujiza wa kiroho ambaye ni mjumbe kutoka kwa Mungu. Malaika wanaweza kuwatokea wanadamu katika umbile la binadamu. Wana kiwango cha chini kuliko Yesu, na mara nyingi wanakuja na ujumbe maalumu au kufanya kazi maalumu. Kama hakuna neno katika lugha badala ya malaika ambalo wasioamini watalielewa, tafsiri neno hili kama ‘tarishi wa/kutoka kwa Mungu’; ‘mjumbe wa Mungu’ au labda ‘balozi wa/kutoka kwa Mungu’. Hata hivyo, kumbuka kwamba ‘nabii’ inawakilisha maana hizo. ‘Roho’ (Mjumbe kutoka kwa Mungu) linaweza kuongezwa katika maelezo hayo.

Linatikana katika: Ulimwengu wa Roho; Imani ya Ibrahimu Yajaribiwa; Malaika awatembelea Mariamu na Yusufu; Kuzaliwa kwa Yesu; Kufufuka kwa Yesu na Mwafrika.

Upako/Kupakwa

Kupakwa mafuta katika Agano la Kale kulimaanisha tendo la Mungu ambalo mtu alipokea neema au kuchaugaliwa kwenye eneo, huduma, au kazi maalumu katika kusudi la Mungu (hasa kuwa Mfalme). Kupakwa mafuta, mara nyingi kulihusishwa na kupokea Roho wa Mungu. Katika simulizi ya “Kupakwa Mafuta kwa Daudi”, tendo hili lilifanywa na mtu aliyechaguliwa na Mungu kulifanya. Alijaza pembe yake (Pembe ya Beberu) kwa mafuta na kuyamiminia mafuta kichwani kwa Daudi. Ikiwa watu katika eneo hilo wana shughuli/sherehe zinazofanana na hii (tafuta neno sahihi litalotumika) kumchagua mtu katika kazi maalumu. Kifungu cha meneno “Alipakwa (mafuta) kichwani vinaweza kutumika. Ikiwa haiwezekani, unaweza kusema kwa namna nyingine kama, ‘alimimina mafuta juu ya kichwa ili kumchagua/kumdhihirisha kuwa ndiye mfalme ajaye.

Linapatikana katika: Kupakwa Mafuta kwa Daudi na Simulizi ya Nathani.

Ubatizo/Kubatiza

Neno hili ni neno lenye umuhimu katika Biblia na linahitaji kutafakariwa kwa umakini kabla ya kujaribu kulitafsiri. Ikiwa tafsiri ya Biblia ipo itumike. Ikiwa tafsiri inatumia neno la kuazima (kama tunavyoazima neno kutoka Kigiriki ‘baptizo’) lakini hakuna mtu anayelielewa hilo, fikiria kulielezea neno hilo. Ikiwa unafanya kazi pamoja na waamini, angalia ni neno gani watajisikia

Page 83: StoryTapestry Manual - Swahili

83

vizuri kulitumia. Kama ni lazima kutafuta neno kwa sababu yoyote ile, utafiti wa kina juu ya dhana zima ya ‘ubatizo’ unahitajika. Neno la Kigiriki linamaanisha ‘kuwenda ndani, au chini ya maji, au kuosha katika maana ya kiroho’. Yohana Mbatizaji alikuwa akifanya pale mtu alipotaka kuacha kutenda dhambi na kumtii Mungu ili asamehewe dhambi zake. Inawezekana kusema kwamba, ‘Ishara ya kuoshwa kunaonyesha kwamba mioyo yao imebadilika. Kumbuka kwamba katika tamaduni na dini nyingi, watu wana desturi ya kujiosha mara kwa mara ili kuandoa dhambi. Ikiwezekana fafanua kwamba hii ni shughuli/sherehe inayofanyika mara moja tu.

Linapatikana katika: Ubatizo wa Yesu; Viongozi wa Dini wenye Wivu; Roho wa Mungu, Mwafrika; Paulo Akutana na Yesu; na Mlinzi wa Gereza wa Filipi.

Imani/Kuamini

Ni neno linaloelezea mwitikio wa mwanadamu kwenye ahadi ya Mungu. Inaelekea kumaanisha zaidi ya makubaliano ya kiakili, kwa kuweka imani/tumaini la mtu katika Mungu.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mwito wa Ibrahimu; Imani ya Ibrahimu Ilijaribiwa; Mwanamke Kisimani; Viongozi wa Dini wenye Wivu; Njama na Mlo wa Mwisho; Kufufuka kwa Yesu; Mwafrika; Paulo akutana na Yesu; Petro aponya na Kumfufua Tabitha kutoka kwa Wafu; Mlinzi wa Gereza wa Filipi na Kurudi.

Waamini

Baada ya Pentekoste, watu waliomfuata Yesu waliitwa pia ‘waamini.’ Neno hili limetumika katika mpangilio wa simulizi kumaanisha wafuasi wa Yesu baada ya Pentekoste na kutilia mkazo ukweli kwamba watu walifanyika wafuasi wa Yesu kupitia imani katika Yeye.

Lipatikana katika: Paulo akutana na Yesu; Petro aponya na kummfufua Tabitha kutoka kwa wafu; Mlinzi wa Gereza wa Filipi; na Kurudi.

Bariki/Barikiwa/Baraka

Neno hili humaanisha pale Mungu anaposaidia, anamfanyia mazuri au kumpendelea mtu au kitu. Katika simulizi za Uumbaji na Ibrahimu, baraka maalumu zimejumuisha Mungu kuwapa uwezo wa kuzaliana na kuongezeka. Jaribu kuzuia utumiaji wa neno linalohusiana na bahati au mchezo wa bahati nasibu.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mwito wa Ibrahimu; Imani ya Ibrahimu Ilijaribiwa; Malaika Awatembelea Mariamu na Yusufu; Kuzaliwa kwa Yesu na Yesu awalisha 5,000.

Wafuasi wa Karibu (Angalia pia Wafuasi)

Wanafunzi kumi na wawili walijulikana kama wafuasi wa karibu na wanafunzi wengine wafuasi tu. Tofautisha kati ya makundi hayo mawili katika namna moja pia.

Linapatikana katika: Mwanamke Kisimani; Binti Yairo na Mwanamke Aliyetokwa na Damu; Yesu Awalisha 5,000; Njama na Mlo wa Mwisho; Yesu Alisalitiwa; Kufufuka kwa Yesu; Baada ya Kufufuka; Roho wa Mungu; na Petro Aponya na Kumfufua Tabitha kutoka kwa Wafu.

Page 84: StoryTapestry Manual - Swahili

84

Wazao

Lugha mbalimbali zina maneno mbalimbali kwa ajili ya neno ‘wazao’. Wengine wanasema ‘watoto’, ‘vizazi’, au ‘wanafamilia’. Hakikisha kwamba neno lolote linalotumika litamaanisha wazao wakati wote na siyo tu watoto au wajukuu wa karibu. Neno hili katika maandiko ni nomino mkusanyiko ikamaanisha uwingi.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mwito wa Ibrahimu; Imani ya Ibrahimu Ilijaribiwa; Malaika awatembelea Mariamu na Yusufu; Ubatizo wa Yesu; Mwanamke Kisimani; Mwanamke mwenye dhambi asamehewa; Roho wa Mungu; Paulo akutana na Yesu; na Kurudi.

Uasi/Ukaidi

Ni tendo la hiari la ukaidi kwa Mungu. Hakikisha kwamba neno lililotumika hapa halimaanishi kwamba mtu fulani ameshindwa kufanya tendo la kidini (mf. Sadaka kwa maskini, tambiko, maombi, kufuata taratibu za kidini katika mlo, n.k.). ikilazimu unaweza kutumia neno ‘dhambi’.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Ulimwengu wa Roho; Mwito wa Ibrahimu; Simulizi ya Nathani na Ahadi.

Uzima wa Milele

‘Uzima wa Milele’ katika Agano Jipya lina vipengele viwili.

1. Uzima ambao hauna mwisho

2. Ubora wa maisha yanayoanza pale mtu anapomruhusu Mungu kutawala maisha yake.

Namna nyingine ya kuwasilisha maana hizo mbili za kifungu hiki cha maneno ni pamoja na:

a) Maisha halisi yasiyo na mwisho.

b) Maisha mapya ambayo hayana mwisho.

Au Ikiwa lugha haina nomino ya ‘uzima’

c) Maisha halisi yasiyo na mwisho kwa ajili Yake.

d) Atasababisha watu kama hao kutofika mwisho wa kuishi kihalisi

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mwanamke Kisimani.

Uovu (Ubaya)

Uovu ni uasi au upinzani dhidi ya Mungu na kusudi lake.

Page 85: StoryTapestry Manual - Swahili

85

Linapatikana katika: Ulimwengu wa Roho; Uumbaji hadi Kanisa; Ukaidi na Mlo wa Mwisho na Yesu Alisalitiwa

Pepo Wabaya

‘Pepo Wabaya’ linamaanisha viumbe vya kiroho chini ya mamlaka ya Shetani. Viumbe hivi vya kiroho vina nguvu ya kumtesa mwanadamu na hata kumtawala. Biblia inasema kwamba, roho hawa waliumbwa na Mungu na baadhi yao wakawa wabaya pale walipochagua kumuasi Yeye. Inaelekea lugha nyingi za Asia ya Kusini hazina neno ambalo linaweza kutosheleza kulielezea neno hili. (Pepo wabaya kwao inaweza kumaanisha roho ya mtu aliyekufa ambaye huwaingia watu). Jaribu kuchagua neno ambalo litamaanisha roho inayojitegemea (iliyo huru) ambayo ni mbaya na inayopingana na Mungu. Kama lipo, tumia neno lisilopendelea upande wowote kwa ajili ya roho inayojitegemea na ongeza sifa kama ‘roho kutoka kwa Shetani’ au ‘roho wabaya/waovu.’ Kumbuka kwamba maelezo ya ziada yanaweza kuwa muhimu wakati wa majadiliano.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Ulimwengu wa Roho; na Mlinzi wa Gereza wa Filipi.

Imani

Kuamini kile Mungu amesema hata kama hakijaonekana bado au huna uzoefu nacho.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; na Binti Yairo na Mwanamke Aliyetokwa Damu.

Baba

Ikiwa hadhira haitaelewa kwamba ‘Baba’ inamaanisha Mungu, sema ‘Mungu’ au ‘Mungu, Baba’.

Linapatikana katika: Imani ya Ibrahimu Ilijaribiwa; Njama na Mlo wa Mwisho; Yesu Auchukua Msalaba Wake na Alisulubiwa; Kufufuka wa Yesu na Baada ya Kufufuka.

Wafuasi (Wafuasi wa Karibu pia)

Ikiwa lugha ina neno linaloeleweka kwa ajili ya wafuasi waaminifu wa guru (walimu wa dini ya Kihindu), unaweza kutumia neno hilo hapa. Wanafunzi kumi na wawili waliitwa ‘wafuasi wa karibu na wengine wafuasi tu. Hakikisha unatofautisha kati ya makundi hayo mawili.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mwanamke Kisimani; Yesu Auchukua Msalaba Wake na Akasulubiwa; Baada ya Kufufuka; Roho wa Mungu; Mwafrika; Paulo Akutana na Yesu; Petro Aponya na Kumfufua kutoka kwa Wafu; na Mlinzi wa Gereza wa Filipi.

Kusamahe/Msamaha

Page 86: StoryTapestry Manual - Swahili

86

Baadhi ya lugha hazina neno linalotosheleza badala ya neno ‘kusamehe.’ Katika hali hiyo, kuelewa nini msamaha unamaanisha ni muhimu katika kutafsiri kwa usahihi. Msamaha unahusisha watu wawili, mmoja wa hao amemfanyia kosa mwingine na amemuudhi. Yule aliyeudhika hamwadhibu yule mwingine kama anavyostahili. Ikiwa huyo mwingine anaukubali msamaha, uhusiano kati ya wawili hao unarejeshwa na hatia inaondoka.

Linapatika katika: Uumbaji hadi Kanisa; Simulizi ya Nathani; Ubatizo wa Yesu; na Yesu Auchukua Msalaba wake na Alisulubiwa.

Roho wa Mungu

Kiebrania ‘ruach’ (Roho) linaweza kuwa na maana ya kimwili ‘upepo’ au ‘pumzi’. Linaweza pia kumaanisha ‘nguvu’ au mamlaka ambayo Mungu anampa mtu kufanya mambo yasiyo ya kawaida. Dhana ya ‘utakatifu’ inamaanisha kuwa watu au vitu vinavyohusiana na Mungu. Hata hivyo, mara nyingi tafsiri ya maandiko inatumia ‘Roho wa Mungu’ kwa sababu lugha nyingi hazina neno kwa ajili ya ‘utakatifu’ ambalo linatosheleza kuielezea dhana. Kwa kuwa ‘utakatifu’ katika lugha nyingi za Asia ya Kusini ni neno ambalo wasioamini hawatalielewa, au ni neno lenye tafsiri isiyotakiwa, tumia ‘Roho wa Mungu’.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Kupakwa Mafuta kwa Daudi; Malaika awatembelea Mariamu na Yusufu; Ubatizo wa Yesu; Mwanamke Kisimani; Baada ya Kufufuka; Roho wa Mungu; Mwafrika; Paulo Akutana na Yesu na Kurudi.

Mbingu(ni)

Mbingu au mbinguni linaweza kumaanisha angani, au mahali ambapo Mungu na Malaika zake wanakaa, kutegemea na muktadha. Inapomaanisha mahali ambapo Mungu anaishi, ni hatima ya mwisho ya safari ya mwanadamu pia. Kwa sababu imehusishwa kwa karibu sana na mahali alipo Mungu, mwingine anaweza kutumia ‘Ufalme wa Mbinguni’ na ‘Ufalme wa Mungu’. Ikiwa lugha haina neno linalotosheleza kwa ajili ya neno Mbingu(ni) au wasikiaji hawaelewi vya kutosha dhana ya mbingu(ni) katika hatua hii, libadilishe neno kuwa ‘mahali ambapo Mungu anakaa’

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Ubatizo wa Yesu; Yesu awalisha 5,000, Viongozi wa Dini wenye Wivu; Yesu Auchukua Msalaba wake na Alisulubiwa; Baada ya Kufufuka; Paulo akutana na Yesu; Mlinzi wa Gereza wa Filipi; na Kurudi.

Yerusalem

Mji ambao sehemu ya kuabudia ilikuwepo kwa ajili ya Waebrani au Wayahudi. Huu ulikuwa ni mji ambao Mungu aliuchagua kwa ajili yao kujenga Hekalu au mahali pa kuabudia ili kumheshimu/kumwadhimisha Yeye.

Linapatikana katika: Kuzaliwa kwa Yesu; Mwanamke mwenye Dhambi Asamehewa; Mwafrika, na Paulo Akutana na Yesu.

Ufalme wa Mungu au Ufalme wa Mbinguni

Page 87: StoryTapestry Manual - Swahili

87

Miliki ambayo Mungu anamiliki au kutawala. Hii inaweza kumaanisha eneo linaonekana kwa macho au moyo wa mtu kwa kuwa vyote vinamilikiwa na Mungu.

Linapatikana katika: Mwanamke Kisimani; na Yesu Awalisha 5,000.

Bwana

‘Bwana’ ni jina lingine kwa ajili ya Mungu mwenye Mamlaka, ambaye ni Yehova. Neno ‘Bwana’ linamaanisha kuwa mmiliki halali wa kitu fulani. Mwenye nyumba ni mmiliki halali au kisheria wa ardhi. Neno ‘Bwana’ linamaanisha Mungu au Yesu ambaye ndiye mmiliki halali wa vitu vyote, ikiwa ni pamoja na watu kwa sababu Yeye ni muumbaji wa vitu vyote.

Linapatikana katika: Malaika Awatembelea Mariamu na Yusufu; Yesu Asalitiwa; na Kufufuka kwa Yesu.

Bwana Mkuu

Asili ya neno ‘bwana’ hapa lina tafsiri ya Bwana Mkuu; mwenye mamlaka ya juu au mmiliki. Katika ngazi ya chini hiki ni cheo cha mtu anayeheshimiwa kama vile, ‘Bwana’. Neno lolote kati ya hayo linakubalika kutumika.

Linapatikana katika: Binti Yairo na Mwanamke Aliyetokwa na Damu; Mwanamke Aliyetenda Dhambi Asamehewa; Njama na Mko wa Mwisho; na Paulo Akutana na Yesu.

Muujiza

Ni tendo au jambo linalofanywa kwa nguvu za Roho Mtakatifu ambazo haziwezi kutimizwa kwa nguvu za asili za mtu. Roho Mtakatifu wakati mwingine alifanya kazi kupita mtu kama Yesu alipoishi hapa duniani wakati alipolisha watu 5000 au kupitia wafuasi wake kama wakati Petro alipoponya na kumfufua Tabitha kutoka kwa wafu. Wakati mwingine Roho Mtakatifu anatekeleza tendo au jambo pasipo mtu wa mwilini.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Binti Yairo na Mwanamke Aliyetokwa Damu; na Yesu Awalisha 5,000.

Ahadi

Ni nadhiri au kiapo, kwa maandishi au kwa mdomo kinachotolewa na mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mtoto Aliyeahidiwa kwa Sara; Imani ya Ibrahimu Ilijaribiwa; Kupakwa Mafuta kwa Daudi; Njama na Mlo wa Mwisho; Baada ya Kufufuka na Mlinzi wa Gereza la Filipi.

Uhusiano

Baadhi ya lugha zinaweza zisiwe na neno moja kwa ajili ya neno ‘uhusiano’, au neno kuwa matamshi yasiyotakiwa. Baadhi ya lugha zinalielezea wazo kwa njia ya vitendo. Uhusiano unatokea pale watu, mataifa au vitu viwili vinapokubaliana kuwa na shughuli kati yao. Katika

Page 88: StoryTapestry Manual - Swahili

88

mwito wa Ibrahimu, Bwana alipendezwa pale Ibrahimu alipoweka imani yake katika Yeye na Bwana alimkubali kwa ajili hiyo.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mwito wa Ibrahimu; na Kurudi.

Viongozi wa Dini

Wote, Mafarisayo na Masadukayo walikuwa viongozi wa dini ya Kiyahudi wakati ule. Waandishi na Makuhani wengi walikuwa washirika katika moja ya madhehebu hayo. Ikiwezekana, ni vizuri kutunza majina ya madhehebu haya ‘as generic’ kadri inavyowezekana – ‘viongozi wa dini’. Kama neno kwa ajili ya ‘viongozi wa dini’ linatumika katika dini kubwa, hakikisha kwamba majina HAYAMAANISHI dini hizo maalumu tu. Viongozi wa dini wa nyakati hizi wanaweza kuwa wafuasi waaminifu kwa Neno la Mungu au wasiwe wafuasi/waaminifu.

Linapatikana katika: Ubatizo wa Yesu; Viongozi wa Dini wenye Wivu; Mwanamke Mwenye Dhambi Asamehewa; Njama na Mlo wa Mwisho; Yesu Alisalitiwa; Hukumu ya Yesu Yesu Auchukua Msalaba wake na Alisulubiwa; Roho wa Mungu na Paulo Akutana na Yesu.

Kafara/Sadaka

Ni kitu ambacho kimewekwa wakfu na kutolewa kabisa kwa Mungu au kitu kinachotolewa kwa ajili ya wengine.

Linapatikana katika: Imani ya Ibrahimu Ilijaribiwa; na Yesu Auchukua Msalaba Wake na Alisulubiwa.

Shetani

Roho ambaye aliumbwa akiwa mzuri sana, mwenye nguvu na busara kuliko roho nyingine, lakini akawa na wivu kwa Mungu na kutaka kuwa Mungu. Tafuta neno au kifungu cha maneno katika utamaduni wa watu ambalo litawasaidia kulielewa hili.

Linapatikana katika: Ulimwengu wa Roho; Uasi/Ukaidi; na Njama na Mlo wa Mwisho

Kuokoa

Ni kumuokoa mtu au kitu kutokana na madhara au hatari. Yesu anatuokoa kutoka kwenye kifo cha milele kwa kuchukua dhambi zetu Yeye mwenyewe juu ya msalaba.

Linapatikana katika: Malaika Awatembelea Mariamu na Yusufu; Kuzaliwa kwa Yesu; Njama na Mlo wa Mwisho; Yesu Auchukua Msalaba Wake na Alisulubishwa na Mlinzi wa Gereza la Filipi.

Mkombozi/Mkombozi Aliyeahidiwa

Ukamilifu wa mtu unajumuisha vipengele viwili, mwili na roho, na wakati mwingine ni vigumu kuvitofautisha. Mkombozi au mwokozi kwenye Agano Jipya limetumika tu kwa ajili ya Yesu kama Mkombozi wa Kiroho. ‘Mkombozi Aliyeahidiwa’ ni kifungu cha maneno kilichochaguliwa kutumika katika tafsiri ya Kiswahili ya mada ya simulizi ya ukombozi kama ni neno la kumwelezea huyu Yesu ni nani – Masihi, Kristo, Mkombozi Aliyeahidiwa, Mpakwa

Page 89: StoryTapestry Manual - Swahili

89

Mafuta, n.k. Vipengele vingi vya wajibu na tabia ya Yesu vimetafsiriwa katika neno “Mpakwa Mafuta”, ikijumuisha ufalme wake juu ya mataifa yote, mwakilishi wa Mungu, njia ya kuleta ushindi wa Mungu dhidi ya adui zake na aliyechaguliwa kukamilisha ukombozi kwa watu wa Mungu. Rasilimali za tafsiri zinataka kutafiti kwa ajili ya neno ambalo linajumuisha dhana ya mmoja ambaye ni maalumu aliyechaguliwa na Mungu na mmoja aliye mkombozi na mfalme. Neno ‘Mkombozi Aliyeahidiwa’ linaelekea kuwa ni cheo ambacho kinamfaa Yesu Kuingia katika ulimwengu. Ufalme na upako wake umetambulishwa (umeanzishwa) kupitia simulizi kuliko kumpa cheo cha ‘mfalme’ au ‘mpakwa mafuta’. Ikiwa lugha haina nomino ambayo inalieleza wazo la mkombozi/mwokozi, tumia neno ‘Yule anayeokoa’ au ‘mtu anayeokoa’.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Ahadi; Malaika Awatembelea Mariamu na Yusufu; Kuzaliwa kwa Yesu; Ubatizo wa Yesu; Mwanamke Kisimani; Yesu Asalitiwa; Hukumu ya Yesu; Yesu Auchukua Msalaba Wake na Alisulubiwa; na Kurudi.

Dhambi

Dhambi ni tendo la ukaidi au uasi kwa Mungu. Hakikisha neno lilitomika halimaanisha mtu fulani ameshindwa kutekeleza tendo la kidini (mfano, sadaka kwa maskini, tambiko, maombi, kufuata sheria za kidini za mlo n.k.) kama kuna lazima tumia neno “ukaidi’

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Simulizi ya Nathani; Ahadi; Malaika Awatemblea Mariamu na Yusufu; Ubatizo wa Yesu; Mwanamke mwenye dhambi Asamehewa; na Yesu Auchukua Msalaba wake na Alisulubiwa.

Mwana wa Mungu

Dokezo kwa Yesu kuwa Mwana wa Mungu inamtambulisha kwamba alikuja kutoka kwa Mungu. Hii HAIMAANISHI kwamba Yesu ni mtoto wa Mungu Kibailojia au ni mtoto, lakini ni kwamba alikuja kutoka kwa Mungu na ni mmoja na Mungu.

Linapatikana katika: Malaika Awatembelea Mariamu na Yusufu; Yesu Asalitiwa; Mwafrika; Paulo Akutana na Yesu; na Petro Aponya na Kumfufua Tabitha kutoka kwa Wafu.

Roho

Roho linamaanisha ‘nafsi’ au ‘uzima’ na ndicho chanzo (kiini) cha utu wa ndani wa mtu – hisia na mihemuko yake.

Linapatikana katika: Ulimwengu wa Roho; na Yesu Auchukua Msalaba Wake na Alisulubiwa.

Msemaji/Wasemaji

Chagua neno kwa ajili ya ‘nabii’ ambalo kiusahihi linaelezea kazi za nabii. Nabii 1) Anapokea mwito kutoka kwa Mungu; 2) Hutoa ujumbe anaupokea kutoka kwa Mungu kwenda kwa watu; 3) Kipaumbele chake cha pekee ni kuleta Neno la Mungu kwa wanadamu. ‘Msemaji’ lilichaguliwa kwa sababu katika kiingereza, linaweza kuwasilisha maana hizi tatu, lakini halichukui maana zisizotakiwa za wabashiri. Ikiwa neno la kidini limetumika hakikisha lina maana ambayo msikilizaji wa kawaida atalielewa. Kama si gumu sema kwa kulirudia rudia, ‘msemaji wa Mungu’ katika simulizi yote, tumia jina la nabii.

Page 90: StoryTapestry Manual - Swahili

90

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa, Ulimwengu wa Roho, Kupakwa Mafuta kwa Daudi; Simulizi ya Nathani; Ahadi, Ubatizo wa Yesu; Mwanamke Kisimani, Viongozi wa Dini wenye Wivu; na Mwafrika.

Kaburi

Mahali ambapo mwili wa mtu aliyekufa unawekwa.

Linapatikana katika: Yesu Auchukua Msalaba wake na Akasulubiwa; na Kufufuka kwa Yesu.

Busara/Hekima

Dhana ya Biblia juu ya hekima inajumuisha wazo la ‘kufikiri’ mambo ambayo ni kweli na kufanya mambo ambayo ni mazuri! Ni Mungu pekee yake anayeweza kumfanya mtu awe na busara/hekima. Kiukweli, katika Agano Jipya inamaanisha kwamba pale mtu anapokuwa na hekima, anao ufahamu katika kusudi la Mungu.

Linapatikana katika: Ukaidi/Uasi; na Kuzaliwa kwa Yesu.

Kuabudu

Msingi wa kuabudu ni wazo la ‘huduma’ inayoonyeshwa kupitia kuonyesha heshima na maajabu kwa Mungu (IVP New Bible Dictionary). Mababa walidhani kuabudu kungefanyika mahali popote ambapo Mungu angejifunua mwenyewe. Agano la Kale lilianzisha mfumo mgumu wa utoaji wa kafara katika Hekalu. Yesu aliuweka wazi mfumo wa Ibada wa utoaji wa kafara kwamba haukuwa wa muhimu tena na kwamba ibada zijengwe katika upendo wetu kwa Mungu. Tamaduni na lugha mbalimbali zina maneno tofauti kwa ajili ya kuabudu/ibada, baadhi yao yanamaanisha sherehe au matambiko fulani tu ambayo mtu lazima ayafanye kile ambacho hadithi katika mpangilio wa simulizi hii ambapo kuabudu/ibada limetumika likimaanisha ni zaidi ya kufanya matambiko tu. Inajumuisha moyo wa upendo, heshima na maajabu ya wafanya ibada kwa Mungu. Hakikisha neno au vifungu vya maneno yaliyochaguliwa kwa ajili ya kuabudu/ibada yamejumuisha wazo hili.

Linapatikana katika: Uumbaji hadi Kanisa; Mwito wa Ibrahimu; Imani ya Ibrahimu Ilijaribiwa; Kupakwa Mafuta kwa Daudi; Kuzaliwa kwa Yesu; Mwanamke Kisimani; Binti Yairo na Mwanamke Aliyetokwa na Damu; Viongozi wa Dini wenye Wivu; Mwanamke mwenye Dhambi Asamehewa; Yesu Asalitiwa; Baada ya Kufufuka; Mwafrika; na Mlinzi wa Gereza wa Filipi.

Page 91: StoryTapestry Manual - Swahili

91

Viambatanisho

1. Wanawake Katika Biblia Ukurasa 75 – 79

2. Sampuli ya Mafunzo ya Simulizi ya

Kitambaa Kilichofumwa Vizuri Ukurasa 81 – 82

Page 92: StoryTapestry Manual - Swahili

92

Wanawake Katika Biblia

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Mke kwa ajili ya Adamu

2. Ukaidi/Uasi

3. Sara na Hagai

4. Sara, na Mtoto Aliyeahidiwa

5. Mtoto wa Sara – Utoaji wa Mungu

6. Bibi Harusi kwa ajili ya Isaka

7. Raheli na Lea

8. Tamari Mjane

9. Mke wa Potifa na Yusufu

10. Mama yeke Musa na dada yake Miriamu

11. Rahabu

12. Simulizi ya Debora

13. Ruthu na Naomi

14. Hana

15. Abigaili

16. Sauli na mwanamke wa Endori

17. Batsheba

18. Wanawake wawili na mtoto

19. Malkia wa Sheba

20. Mjane wa Serapta

21. Malkia Yezebeli

22. Mafuta ya mjane

23. Mjane Mshunami (*?)

24. Hekima ya Mtumwa wa kike

Mwanzo 2

Mwanzo 3

Mwanzo 16 na 17:20

Mwanzo 17 na 21:1-7

Mwanzo 18

Mwanzo 24

Mwanzo 29:1-35; 30:1-24

Mwanzo 38

Mwanzo 39

Kutoka 2:1-10

Yoshua 2:1-24

Waamuzi 4 na 5

Ruthu

1Samweli 1:2:1-10

1Samweli 25

1Samweli 28

2Samweli 11

1Wafalme 3

1Wafalme 10:1-13

1Wafalme 17:7-24

1Wafalme 21:1-28

2Wafalme 4:1-7

2Wafalme 4:8-37; 8:1-6

2Wafalme 5

Page 93: StoryTapestry Manual - Swahili

93

25. Malkia Atalia

26. Esta

27. Elizabeti na Zakaria

28. Mariamu na Kuzaliwa kwa Yesu

29. Mariamu na Yusufu wamtafuta Yesu Hekaluni

30. Harusi ya Kana

31. Mwanamke Kisimani

32. Mwana wa Pekee wa Mjane

33. Mwanamke nyumbani kwa Simoni

34. Binti Yairo na Mwanamke aliyetokwa Damu

35. Imani ya Mwanamke

36. Mariamu, Martha na Lazaro

37. Ombi la mama

38. Sadaka ya mjane

39. Wanawali kumi

40. Wanawake wakati wa Kifo cha Yesu

41. Wanawake watembelea kaburi lililo wazi

2Wafalme 11

Esta 1:8-23; 4

Luka 1:5-23

Luka 1:26-45; 2:1-7

Luka 2:41-51

Yohana 2:1-11

Yohana 4:1-42

Luka 7:11-17

Luka 7:36-50

Luka 8:40-56

Marko 7:24-37

Yohana 11:1-44

Mathayo 20:20-28

Marko 12:41-44

Mathayo 25:1-13

Marko 15:33-47

Luka 24:1-11

Page 94: StoryTapestry Manual - Swahili

94

Akina Mama katika Biblia

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Wana wa Hawa

2. Hagai na Mtoto, Ishmaeli

3. Sara na Mtoto, Isaka

4. Watoto Mapacha wa Rebeka

5. Raheli na Kuzaliwa kwa Benyamini

6. Binti Farao anampata mtoto Musa

7. Naomi, watoto wake na wakwe zake

8. Hana, mama wa Nabii

9. Wanawake wawili na mtoto

10. Mjane wa Serapta na mtoto wake

11. Mwanamke Mshunami

12. Elizabeti, Mama wa Yohana

13. Mariamu, Mama wa Yesu

14. Kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji

15. Kuzaliwa kwa Yesu

16. Yesu akiwa kijana ndani ya Hekalu

17. Mwana pekee wa mjane

18. Ombi la Mama

Mwanzo 4:1-26

Mwanzo 16:1-16

Mwanzo 21:1-7

Mwanzo 25:19-34

Mwanzo 35:16-20

Kutoka 1:15-22; 2:1-10

Ruthu 1:1-22

1Samweli 1:1-24

1Wafalme 3:16-28

1Wafalme 17:17-24

2Wafalme 4:8-37

Luka 1:5-25

Luka 1:26-45

Luka 2:57-66

Luka 2:1-7

Luka 2:41-52

Luka 7:11-17

Mathayo 20:20-28

Page 95: StoryTapestry Manual - Swahili

95

Wanawake Walioteseka

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Uasi wa Adamu na Hawa

2. Sara ni Tasa

3. Raheli na Lea

4. Kunajisiwa kwa Dina

5. Miriamu aliteswa kutokana na Ukoma

6. Binti wa Yefta katika Mizpa

7. Huzuni ya Naomi

8. Wake wa Wabenjamini

9. Daudi na Betsheba

10. Amnoni na Tamari

11. Mke wa Mfalme Yeroboamu huko Shilo

12. Yusufu anamtilia mashaka Mariamu na mimba ya kimuujiza

13. Mwanamke mwenye Dhambi

14. Mwanamke Mjane Aliyeng’ang’ania

15. Sadaka ya Mjane

16. Wanawili Kumi

17. Mke wa Pilato alipata ndoto

18. Mariamu ampoteza mtoto wake.

Mwanzo 3:1-19

Mwanzo 18:1-15

Mwanzo 30:1-24

Mwanzo 34:1-31

Hesabu 12:1-16

Waamuzi 11:29-40

Ruthu 1:1-22

Waamuzi 21:1-25

2Samweli 11:1-26 na 12:1-20

2Samweli 13:1-22 na 23-29

1Wafalme 14:1-20

Mathayo 1:18-25

Yohana 8:1-11

Luka 18:1-8

Marko 12:41-44

Mathayo 25:1-13

Mathayo 27:11-19

Yohana 19:17-37

Page 96: StoryTapestry Manual - Swahili

96

Simulizi za Mungu za Kutia Moyo (Kufariji)

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Wimbo wa Miriamu

2. Ruthu anakutana na Boazi

3. Hana, Mke wa Elkana

4. Mjane wa Serapta

5. Mafuta ya Mjane

6. Mwanamke Mshunami

7. Ardhi ya Mshunami Yarejeshwa

8. Nehemia asaidia maskini

9. Elizabeti na Zakaria

10. Mwanamke kutoka Naini

11. Mwanamke mlemavu na Yesu

12. Mwanamke aliyeteseka kwa miaka 12.

13. Petro, Ainea na Tabitha

Kutoka 15:19-29

Ruthu 2:1-12

1Samweli 1:1-20

1Wafalme 17:7-16

2Wafalme 4:1-7

2Wafalme 4:8-17

2Wafalme 8:1-6

Nehemia 5:1-19

Luka 1:5-25

Luka 7:11-17

Luka 13:10-17

Marko 5:21-34

Matendo 9:32-43

Page 97: StoryTapestry Manual - Swahili

97

Simulizi za Mungu za Hekima kupitia Wanawake

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Wazalishaji wa Misri

2. Rahabu na Wapelelezi

3. Debora

4. Yaili, Mwanamke Aliyekaa-Hemani

5. Ruthu na Naomi

6. Hana, Mama wa Samweli

7. Abigaili

8. Yoabu na Mwanamke mwenye Busara/akili

9. Binti Mtumwa na Naamani

10. Yehosheba Amwokoa Yoashi

11. Malkia wa Sheba

12. Hulda, Nabii Mke

13. Esta – Aomba kwa Mfalme

14. Esta na njama za kumuabisha Hamani

15. Anna, alidumu katika Maombi na Kufunga

16. Mariamu, Mama wa Yesu huko Kana

17. Mariamu wa Bathania

18. Mwanamke Aliyempaka Mafuta Yesu

19. Lidia, Muuza wa Nguo za rangi ya zambarau

20. Prisila sambamba na Mmewe

Kutoka 1:8-21

Yoshua 2:1-24

Waamuzi 4:1-16

Waamuzi 4:17-24

Ruthu 1

1Samweli 1:1-20

1Samweli 25:1-44

2Samweli 14:1-33

2Wafalme 5:1-44

2Wafalme 11:1-14

2Nyakati 9:1-28

2Nyakati 34:14-33

Esta 5:1-14

Esta 5:1-13; 7:1-10

Luka 2:25-40

Yohana 2:1-11

Luka 10:38-42

Mathayo 26:6-11

Matendo 16:6-15

Matendo 18:18-26

Page 98: StoryTapestry Manual - Swahili

98

Wanawake Waliopenda

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Mke wa Adamu

2. Rebeka na Isaka

3. Yakobo na Raheli

4. Mke kwa ajili ya Musa

5. Ruthu na Boazi

6. Malkia Esta na Mfalme

7. Mariamu na Yusufu

8. Yesu anafundisha dhidi ya talaka

Mwanzo 2:1-25

Mwanzo 24:34-67

Mwanzo 39:1-30

Kutoka 2:11-25

Ruthu 3:1-18

Esta 2:1-18

Mathayo 1:18-25

Mathayo 19:1-9

Wanawake Wagumba/Tasa

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Sara ni Mgumba/Tasa

2. Isaka anaomba kwa ajili ya Rebeka

3. Raheli ni Mgumba/Tasa

4. Mama wa Samsoni

5. Hana, Mke wa Elkana

6. Mwanamke Mshunami

7. Elizabeti na Zakaria

Mwano 18:1-15

Mwanzo 25:19-34

Mwanzo 29:3-35; 30:1-24

Waamuzi 13:1-25

1Samweli 1:1-20

2Wafalme 4:8-17 (au mst. mbadala 8-37)

Luka 1:5-25

Page 99: StoryTapestry Manual - Swahili

99

Simulizi za Uongo/Ulaghai

(Mifano Mibaya ya Maadili)

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Hawa anamshawishi Adamu

2. Sara na Hagai

3. Mabinti wa Lutu wafanya njama za uovu

4. Rebeka anamtawala Yakobo

5. Mke wa Potifa

6. Bibi Harusi wa Samson

7. Delila

8. Mwanamke wa Endoni

9. Wake wa Sulemani Waugeuza moyo wake

10. Malkia Mama wa Yuda

11. Usaliti wa Yazebeli (Shamba la mizabibu la Nabothi)

12. Malkia Atalia amwongoza mwanaye katika uovu

13. Yezebeli na Mfalme Yehu

14. Kifo cha Yezebeli

15. Njama za wana wa Shimeathi na Shimrithi dhidi ya Mfalme

16. Mke wa Ayubu anamtia moyo mmewe kumsaliti Bwana

(tumia utangulizi kutoka Ayubu 1:6-20)

17. Mke wa Mfalme Herode na Bintiye

18. Safira wala njama na Anania

Mwanzo 3

Mwanzo 16 na 17:20

Mwanzo 19:30-38

Mwanzo 27:1-24

Mwanzo 39

Waamuzi 14

Waamuzi 16:4-22

1Samweli 28

1Wafalme 11:1-13

2Nyakati 15:10-19

1Wafalme 21:1-29

2Nyakati 22:1-12

2Wafalme 9:1-29

2Wafalme 9:29-37; 10:36

2Nyakati 24:17-27

Ayubu 2:1-10

Marko 6:14-29

Matendo 5:1-11

Page 100: StoryTapestry Manual - Swahili

100

Wanawake Wafuasi

Rejea za Maandiko katika Mpangilio

1. Mwanamke Kisimani

2. Mwanamke Aliyesamehewa Dhambi zake

3. Mwanamke Mkanaani

4. Mariamu na Martha

5. Mariamu, Martha na Lazaro

6. Wanawake Wampaka Yesu Manukato

7. Wanawake wakati wa kifo cha Yesu

8. Yesu anamtokea Mariamu Magdalena

9. Baada ya Kupaa

10. Ushirika wa Waamini

11. Tabitha wa Jopa

12. Petro kutoka gerezani kwenda kwenye nyumba ya Mariamu

13. Kugeuka kwa Lidia na Kubatizwa huko Filipo

14. Damaris wa Athene

15. Walio nyumbani mwa Krispo

16. Prisila na Akila katika Efeso

Yohana 4:1-39

Luka 7:36-50

Mathayo 15:21-28

Luka 10:38-42

Yohana 11:1-44

Mathayo 26:6-13

Marko 15:33-47

Yohana 20:1-18

Matendo 1:1-14

Matendo 2:42-47

Matendo 9:32-43

Matendo 12:1-19

Matendo 16:11-15

Matendo 17:22-34

Matendo 18:5-8

Matendo 18:24-28

Page 101: StoryTapestry Manual - Swahili

101

Sampuli ya Mafunzo ya Simulizi ya Kitambaa Kilichofumwa Vizuri

Kipindi cha 1 – Utangulizi

Kutambulishana

Utangulizi katika Kusumulia – namna ya kuwasilisha Injili

Kipindi cha 2 – Uwasilishaji wa Simulizi

Mndhari Yote – Uumbaji hadi Kanisa

Ulimwengu wa Roho

Kipindi cha 3 – Uwasilishaji wa Simulizi

Uumbaji

Uasi/Ukaidi

Mwito wa Abrahamu

Kipindi cha 4 – Masuala ya Falsafa za Ulimwengu

Imani za Wenyeji (Watu wanaokaa mahali pamoja)

Wanaamini nini juu ya Mungu

Wanaamini nini juu ya familia, marafiki, n.k.

Sherehe muhimu

Maadili Muhimu ya Kitamaduni

Kipindi cha 5 – Ufundi wa Simulizi

Mwana Aliahidiwa kwa Sara

Imani ya Abrahamu ilijaribiwa

Kipindi cha 6 – Kuhakiki Simulizi

Hakiki simulizi zote ambazo zimefanywa

Maswali na Majibu kuhusiana na chochote ambacho kimeshafundishwa

Kipindi cha 7 – Ufundi na Kusimulia

Kupakwa Mafuta kwa Daudi

Daudi na Betsheba

Page 102: StoryTapestry Manual - Swahili

102

Simulizi ya Nathani

Kipindi cha 8 – Kufanya ufundi katika hadithi ambayo siyo hadithi

Ahadi

Malaika awatembelea Mariamu na Yusufu

Rudi nyuma – Ulimwengu wa Roho

Kipindi cha 9 – Utambulisho wa Simulizi za Agano Jipya

Kuzaliwa kwa Yesu

Ubatizo wa Yesu

Mwanamke Kisimani

Kipindi cha 10 – Yesu Anakutana na Wewe

Kanuni za kusimulia hadiy yako (Tumia karatasi katika mwongozo)

Fanyia kazi ushuhuda wa simulizi ya Mungu (unaweza kuchukua simulizi kutoka kwenye orodha)

Linganisha hadithi zao na simulizi ya Mungu

Kipindi cha 11 – Ufundi na Usimuliaji

Binti Yairo na Mwanamke Aliyetokwa Damu

Yesu Awalisha 5,000

Viongozi wa Dini wenye wivu

Kipindi cha 12 – Ufundi na Usimuliaji

Mwanamke mwenye dhambi asamehewa

Njama na Mlo wa Mwisho

Yesu Asalitiwa

Hukumu ya Yesu

Kipindi cha 13 – Ufundi na Usimuliaji

Yesu alichukua msalaba wake na alisulubiwa

Kufufuka kwa Yesu

Baada ya Kufufuka

Kipindi cha 14 – Ufundi na Usimuliaji

Roho wa Mungu

Page 103: StoryTapestry Manual - Swahili

103

Mwafrika

Paulo akutana na Yesu

Kipindi cha 15 – Ufundi na Usimuliaji

Petro aponya na alimfufua Tabitha kutoka kwa wafu

Mlinzi wa Gereza

Kurudi

Kipindi cha 16 – Ufundi na Usimuliaji

Maswali

Kusimulia tena simulizi zote kuanzia mwisho hadi mwanzo

Kipindi cha 17 – Toa maagizo

Ushirika (shirikisha simulizi ya Njama na Mlo wa Mwisho)

Kuosha Miguu (ikiwezekana) (Shirikisha kipengele cha Kuosha Miguu cha Njama na Mlo wa Mwisho)

Kupakwa Mafuta (ikiwezekana) (shirikisha simulizi ya kupakwa mafuta kwa Daudi)

Maombi

Zingatia: Ufundi wa simulizi – hakikisha umahiri katika simulizi kufanya kazi katika vikundi vidogo. Mpe nafasi kila mmoja kueleza hadi katika kikundi.

Page 104: StoryTapestry Manual - Swahili

104

Bibliografia

Allen, Gerald. Translator’s Notes on Luke: Inatusaidia kuelewa na kuitafsiri Injili ya Luka. Dallas,