Upload
others
View
18
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
TAHARIRI
YALIYOMO
Gazeti hili la Habari Ilala, ni gazeti la kila Mwezi linalotolewa na
Manispaa ya Ilala, Ambapo ndani yake utaweza kusoma Habari mbalimbali na
matukio yaliyojiri Ndani ya Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha mwezi mmoja
ikiwa ni pamoja na Utekelezaji wa Miradi ya kimaendeleo
Ulipaji wa kodi ni chachu ya maendeleo ………………Uk 4
Ilala yatoa shilingi 1.7 billion kwa wanawake, vijana na watu
Wenye ulemavu ……………………………………… Uk 6
Koica yaendeelea kuwezesha hospitali ya mama na mtoto
Chanika ……………………………………………… Uk 8
Toleo la mwezi aprili 2019 Sema Ilala
Afisa Uhusiano Manispaa ya Ilala Bibi Tabu Shaibu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hivi
karibuni wakati wa kutoa elimu kuhusiana na tozo ya kodi ya huduma( Service Levy) pamoja
na kuhamasisha wafanyabiashara wakalipe kwa wakati kabla ya operesheni ya kuwabaini
wasiolipa tozo hiyo, katikati ni Afisa mapato Manispaa ya ilala James Bangu kulia, ni Afisa Biashara Manispaa
ya Ilala Bw.Nickas Msemwa )Picha na Heri Shaabani
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA YATOA ELIMU KWA MLIPA KODI
NA KUHAMASISHA ULIPAJI WA KODI YA HUDUMA (SERVICE LEVY).
Akizungumza na waandishi wa Habari, Afisa Uhusiano wa Halmashauri Bibi Tabu Shaibu
alieleza kuwa kodi ya Huduma inatozwa kwa mujibu wa sheria ya Serikali,
ambayo inaruhusu Halmashauri Kutoza kodi ya huduma kutoka kwa kila Taasisi ya
Kibiashara katika kila mwaka wa Fedha ambayo ni sawa na Asilimia (0.3%) ya hesabu ya
shughuli zote zikiwemo za uzalishaji wa Biashara na Huduma kutoka nje ya nchi
zinazofanyika katika eneo la Halmashauri ukiondoa kodi ya Ongezeko la Thamani na kodi
ya Mlaji
4
Toleo la mwezi aprili 2019 Sema Ilala
Aidha Mhasibu wa Mapato Bwana James Bangu katika Mkutano huo alieleza kuwa
kodi ya Huduma hulipwa kila baada ya miezi mitatu(3), aliendelea kueleza kuwa kodi
hii ni muhimu kwa ajili ya kugharamia huduma zinazotolewa na Halmashauri ikiwa ni
pamoja na mazingira salama ya uendeshaji wa shughuli za kiuchumi ndani ya Manispaa
ya Ilala. ya biashara kama, Uwashaji wa Taa za Barabarani, Ujenzi wa Barabara
Mhasibu wa Mapato Bwana James Bangu
5
ILALA YATOA SHILINGI 1.7 BILIONI KWA WANAWAKE,
VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU
Na Neema Njau
Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waaswa kutumia kwa uadilifu fursa ya mikopo
waliyopewa ili iweze kuwanufaisha na kuwawezesha kukua kiuchumi na baadaye kurejesha mikopo hiyo
ili wananchi wengine waweze kunufaika
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Sophia Mjema wakati wa hafla fupi yakukabidhi
mikopo kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu yenye thamani ya shilingi 1.7
Bilioni iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala katika viwanja vya Mnazi Mmoja
sehemu ya Mashujaa
Mikopo hiyo ni azma ya utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya Awamu yaTano ya Halmashauri
kutenga Asilimia kumi ya Mapato yanayotokana na makusanyo ya vyanzo vya ndani kwa
kuwawezesha Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.
Toleo la mwezi aprili 2019 Sema Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwapungia mkono wananchi wa Wilaya ya Ilala
baada ya kukabidhi bodaboda na Bajaji, kulia ni Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Ubaya Chuma
6
Akiwasilisha taarifa ya Utoaji wa Mikopo hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Ndg Jumanne K. Shauri .ameeleza kuwa Manispaa ya Ilala leo inatoa mikopo kwa awamu ya pili yenye
Jumla ya shilingi 1.7 bilioni kwa vikundi 295, ikiwa kati ya hivyo vikundi vya wanawake ni 243,
vijana 43 na watu wenyeu lemavu9
Ndugu Shauri ameeleza kuwa Kati ya vikundi hivyo, vipo vikundi ambavyo vimekopeshwa fedha
Na tayari vimenunua bajaj 30 na pikipiki 26 zenye thamani ya shilingi 353 Milioni kwa ajili yautoaji
Wa huduma yau safari ambapo katika hafla hiyo zimekebidhiwa bajaj 22 na pikipiki 10.
Aidha katika awamu ya kwanza Manispaaya Ilala ilitoa jumla ya shilingi 153 Milioni, kwa vikundi 44
Vya wajasiriamali ambapo kati ya hivyo 32 ni vikundi vya wanawake, vikundi 7 vya Vijana naVikundi
5 vya watu wenye ulemavu.
Toleo la mwezi aprili 2019 Sema Ilala
Ndugu Jumanne k. Shauri Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala katikati akiwasilisha Taarifa ya utoaji wa mikopo
7
Mkurugenzi mkazi wa KOICA nchini Tanzania, Bw. Kyucheol Eo, akikabidhi gari aina
ya RAV 4 kwa ajili ya Hospital ya mama na mtoto iliyopo
Chanika. Vifaa hivyo na gari vimepokelewa na Afisa uhusiano Manispaa ya Ilala,
Bi Tabu shaibu aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
Sema Ilala Toleo la mwezi aprili 2019
KOICA YAENDELEA KUWEZESHA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO CHANIKA
“Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya mama na mtoto iliyopo Chanika,Dkt. Kansansia Shoo
akimuonyesha Mkurugenzi mkazi wa koica nchini Tanzania,bw. Kyucheol EO, vifaa vilivyopo
Hospitalini hapo.
8