25
VIDOKEZO MUHIMU KATIKA UNUNUZI NA USALAMA WA CHAKULA COUNSENUTH NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA, June, 2004 Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

ununuzi wa chakula - Counsenuthcounsenuth-tz.org/wp-content/uploads/2017/10/Lishe-na...VIDOKEZO MUHIMU KATIKA UNUNUZI NA USALAMA WA CHAKULA COUNSENUTH NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA

  • Upload
    others

  • View
    11

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

VIDOKEZO MUHIMUKATIKA UNUNUZI NA

USALAMA WA CHAKULA

COUNSENUTHNA

HALMASHAURI YA MANISPAAYA ILALA,

J u n e , 2 0 0 4

Lishe na Ulaji Bora kwaWatu Wanaoishi na Virusi vya

UKIMWI

ii

VIDOKEZO MUHIMU KATIKAUNUNUZI NA USALAMA WA

CHAKULA

ISBN 9987-8936-8-6

© COUNSENUTH, 2004

Kimetayarishwa na:The Centre for Counselling,Nutrition and Health Care(COUNSENUTH)P. O. Box 8218,Dar es Salaam.

Kwa kushirikiana na:Halmashauri ya Manispaaya IlalaS. L. P 20950,Dar es Salaam.

Kimefadhiliwa na:Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Sehemu yoyote ya kijitabu hiki inawezakunakiliwa kwa ajili ya matumizi yasiyo ya

kibiashara ilimradi ionyeshwe kwambataarifa hizo zimetoka kwenye kijitabu hiki.

COUNSENUTH Information Series No.7

iii

YALIYOMO

Shukrani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . iv

Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1

Mlo kamili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2

Vidokezo vya kuzingatia katika kununua nakuhifadhi chakula

• Mboga-mboga . . . . . . . . . . . . . . . . . 5

• Matunda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6

• Samaki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7

• Mayai . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8

• Nyama . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9

• Maziwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10

• Nafaka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11

Kula nje ya nyumbani . . . . . . . . . . . . . . 12

Tumia kwa kiasi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14

Ikiwezekana acha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

Usalama wa chakula . . . . . . . . . . . . . . . . 16

Hitimisho . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 18

Rejea . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19

Orodha ya vijitabu vingine . . . . . . . . . . . 20

iv

SHUKRANI

Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya(COUNSENUTH) kinatoa shukrani kwaHalmashauri ya Manispaa ya Ilala kwakufadhili utayarishaji na uchapishaji wakijitabu hiki. Shukrani za pekee kwa kamati yaUKIMWI ya Manispaa ya Ilala, Mwenyekiti -Diwani Mussa Azzan (Naibu Meya) naMganga mkuu wa Manispaa ya Ilala - Dr. Judith Kahama kwa mchango wao katikakuboresha kijitabu hiki. Shukrani pia kwaSHDEPHA+, TAHEA na watu binafsiwalioshiriki kwa njia mbalimbali katikakukamilisha kazi hii.

1

UTANGULIZI

Binadamu wote wanahitaji chakulamchanganyiko na cha kutosha ili kuwa na halibora ya afya na lishe. Hali bora ya lishe nimuhimu sana kwa watu wote hususan walewanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Hali bora ya lishe kwa watu wanaoishi na virusivya UKIMWI husaidia kuboresha kinga yamwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Vilevilehusaidia kurefusha kipindi mtu anachoishitangu kupata uambukizo wa virusi vyaUKIMWI hadi kuugua UKIMWI. Hali boraya lishe huweza pia kupunguza makali yamagonjwa nyemelezi, husaidia dawa kufanyakazi vizuri mwilini na huboresha hali ya maishakwa ujumla.

Kijitabu hiki kina maelezo kuhusu ulaji bora,vidokezo muhimu katika ununuzi wa vyakula,hifadhi, mambo ya kuzingatia inapobidi kulanje ya nyumbani, usalama wa chakula namengineyo.

Maelezo yaliyomo ndani ya kijitabu hikiyanaweza kutumiwa na watu wanaoishi navirusi vya UKIMWI, wale wanaowahudumiana jamii kwa ujumla. Kijitabu hikikimetayarishwa mahsusi kwa watu wanaoishiManispaa ya Ilala, vilevile kinaweza kutumiwana watu wengine wanaoishi kwenye mazingirayanayohitaji kununua chakula au kula nje yanyumbani. Jamii kwa ujumla pia inawezakufaidika na maelezo ya kijitabu hiki.

Ikumbukwe kuwa, kijitabu hiki kimetoasehemu tu ya maelezo yanayohusu lishe naulaji bora kwa watu wanaoishi na virusi vyaUKIMWI. Kwa maelezo zaidi ni vizuri piakusoma vijitabu vilivyoorodheshwa mwisho wakijitabu hiki.

MLO KAMILI

Mlo kamili huwa na chakula mchanganyiko nacha kutosha. Mlo huo unatakiwa kuwa nachakula angalau kimoja kutoka katikamakundi yafuatayo ya vyakula na viliwepamoja:-

1. Nafaka, mizizi na ndizi

Vyakula hivi huchukua sehemu kubwa ya mlona kwa kawaida ndivyo vyakula vikuu. Kundihili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele,ngano, mtama, uwele, viazi vikuu, viazivitamu, viazi mviringo, mihogo,magimbi, ndizi, n.k.

2. Vyakula vya mikunde navyenye asili ya wanyama

Vyakula vilivyoko kwenye kundi hili ni pamojana kunde, njegere, maharagwe, njugu mawe,fiwi, soya, karanga, dengu, choroko, aina zoteza nyama, mayai, maziwa, dagaa, samaki,jibini, na wadudu wanaoliwa kamakumbikumbi, senene, n.k.

3. Mboga-mboga

Kundi hili lina aina zote za mboga za majanikama matembele, mchicha, majani ya maboga,majani ya kunde, kisamvu, mgagani, figiri,spinachi, sukuma wiki, mnafu, mchunga, piamboga nyingine kama karoti, biringanyabamia, maboga, matango, pilipili hoho,mlonge, nyanya chungu, mlenda, bitiruti namboga mbalimbali za asili.

4. Matunda

Kundi hili lina matunda ainazote kama pera, chungwa,embe, papai, karakara(pesheni), limau, ndimu,

2

3

chenza, parachichi, ndizimbivu, zambarau, nanasi,fenesi, stafeli, pichesi,topetope, n.k. Pia yalematunda yanayoliwa ambayohayalimwi na wakati mwinginehuitwa “matunda pori”, ubora wake nisawa na matunda mengine. Matunda hayo nikama ukwaju, ubuyu, mabungo, embeng’ong’o, mavilu, mikoche n.k.

5. Mafuta na Sukari

Mafuta na sukari ni muhimu mwilini lakinivinahitajika vitumike kwa kiasi kidogo. Mafutayanaweza kutokana na mimea kama nazi,mawese, mbegu zitoazo mafuta kama karanga,korosho, alizeti, ufuta, mbegu za maboga,kweme, na pia yale mafuta yatokanayo nawanyama kama siagi na samli. Sukari nipamoja na miwa, asali, sukari, n.k.

Maji

Japo maji sio kundi la chakula lakini ni sehemumuhimu ya mlo. Maji ni muhimu kwakurekebisha joto la mwili na kusaidia mfumowa chakula. Ni muhimu kunywa maji angalaulita 1.5 (glasi 8) kwa siku. Maji huwezakutokana na kunywa maji safi na salama,madafu, maji ya matunda au majiyaliyochemshwa na viungo, n.k.

KUMBUKAMboga-mboga na matunda ni muhimu

sana kuwepo katika kila mlo. Mara nyingijamii zetu husahau mboga mboga na

matunda.

4

VIDOKEZO VYA KUZINGATIAKATIKA KUNUNUA NAKUHIFADHI CHAKULA

Mambo ya kuzingatia katika kununuachakula:

Kuishi na virusi vya UKIMWI kunahitajiuangalifu zaidi na kujali ubora wa chakula kilawakati chakula kinaponunuliwa. Ili kuepukaununuaji holela na usio wa muhimu au lazima,mnunuzi wa chakula anahitaji kuzingatiayafuatayo:

• Kufahamu kiasi cha pesa kilichopo kwamanunuzi ya vyakula;

• Kutayarisha orodha ya mahitaji muhimuya chakula, inayoendana na kiasi cha pesakilichopo;

• Kuorodhesha mahitaji muhimu ya familiahasa kwa watoto na wagonjwa;

• Uwezo na vifaa alivyonavyo kwa ajili yakuhifadhi vyakula kwa mfano jokofu;

• Vyakula vilivyoko kwenye msimu kwanimara nyingi huwa na bei nafuu;

• Vyakula vyenye thamani zaidi kilishemfano matunda halisi badala ya juisi auvinywaji bandia;

• Kununua zaidi vyakula freshi kulikovilivyosindikwa kwani mara nyingi ni borazaidi na ni bei nafuu;

• Kusoma maelezo (lebo) pale inapobidikununua vyakula vilivyosindikwa;

• Vyakula vinavyoharibika upesivisinunuliwe kwa wingi.

5

Si vyema kwenda kununua chakula wakatiuna njaa kwani mara nyingi utajikutaunanunua vyakula ambavyo sio muhimu

Ununuzi na uhifadhi wa baadhi yavyakula:

Mboga-mboga

Ni muhimu kuwa waangalifu wakati wakununua mboga-mboga kwa kuzingatiayafuatayo:

u Kuepuka mboga-mboga zote zenyemichubuko, zilizonyauka, kupukutishabaadhi ya majani au zilizoharibika.

u Kuhakikisha mboga za majani ni kavu(hazina unyevu mwingi) na zina rangi yaasili.

u Kuepuka mboga-mboga zilizoliwana wadudu, zilizoota ukungu auzilizoanza kuoza.

u Kwa mboga za mizizi kamakaroti, kuhakikisha hakunamikato, mikwaruzo yoyote audalili ya kuanza kuota au kuoza.

u Kununua mboga-mboga kiasi cha kutoshamatumizi ya muda mfupi.

Mboga-mboga zote zihifadhiwe vizuri ilizisipoteze ubora. Mboga za majani hupotezabaadhi ya virutubishi na maji kwa urahisiwakati wa kuhifadhiwa, hivyo inapowezekanani vyema kununua mboga-mboga kiasi kwaajili ya matumizi ya muda mfupi.

Yafuatayo ni muhimu:

v Ikibidi kuhifadhi kwa muda mfupi (kamasiku moja), baada ya kuoshwa na majikukauka, mboga-mboga (kama za majani,hoho, biringanya, bamia, matango)

6

ziwekwe kwenye mfuko laini, safi waplastiki, kwenye sehemu yenye ubaridi,iliyo kavu na isiyo na mwanga.

v Mboga aina ya mizizi kama karoti, bitirutin.k. zihifadhiwe sehemu ya wazi, iliyokavu na inayoruhusu mzunguko wa hewa.

v Katika jokofu mboga-mboga zihifadhiwesehemu isiyo na baridi kali. (Majokofumengi huelekeza sehemu inayofaa kwamboga-mboga).

MUHIMU KWA KUDUMISHAUBORA WA MBOGA-MBOGA

• Osha kabla ya kukata;

• Katakata na kupika mara moja;

• Mboga-mboga zitayarishwe wakati ulewa kupika na zipikwe na maji kidogo.Kufanya hivyo kunapunguza upotevuwa baadhi ya virutubishi;

• Tumia mafuta kidogo katika mapishi;

• Pika kwa muda mfupi (ipua marazinapoiva);

• Ziliwe mara tu baada ya kupikwa.

Matunda

Ununuzi wa matunda unapofanyika, nimuhimu kuzingatia yafuatayo:

• Kuhakikisha tunda limeiva vizuri, halinamichubuko yoyote na halina dalili zakuoza.

• Kununua matunda yaliyokatika msimu kwani huwa nabei nafuu.

Matunda pia yanahitaji uangalifukatika kuhifadhi. Hakikisha

7

kwamba:

• Matunda hayapati michubuko wakati wakuhifadhi;

• Matunda yahifadhiwe mahali penyeubaridi na panaporuhusu mzunguko wahewa;

• Matunda laini yatumike mapema auyahifadhiwe ndani ya jokofu kwanihuweza kuharibika kwa urahisi zaidi.

• Iwapo hakuna jokofu ni vyema kununuamatunda ya kutumia kwa muda mfupi.

Samaki

Unaponunua samaki wabichi zingatiayafuatayo:

• Samaki awe na harufu halisi ya samaki nasi harufu tofauti auinayoashiria kuharibika;

• Awe na macho angavu nayaliyochomoza aukujitokeza kwa nje;

• Awe na mashavu au matamvua safiyaani rangi ya damu na si weusi;

• Awe na mkia uliokakamaa na awe mgumuau mkakamavu (stiff );

• Unapombonyeza kwa kidole au mkono nakuondoa pasibaki bonde;

• Awe na ngozi yenye unyevu;

• Kwa samaki wenye magamba hakikishamagamba yameshikana na ngozi;

• Inapowezekana samaki wabichiwanunuliwe na kupikwa kwa matumizi yamuda mfupi.

Inapobidi kuhifadhi samaki wabichi yafuatayoni muhimu:

8

• Waondolewe uchafu wote, wasafishwevizuri na wawekwe kwenye mfuko waplastiki na kuhifadhiwa kwenye jokofu,sehemu yenye baridi kali au barafu(freezer);

• Samaki wabichi wasigusishwe na vyakulavingine hasa vile vinavyoliwa bilakupikwa, kwani wanaweza kuwa navimelea vya magonjwa;

• Ndani ya jokofu samaki wawekwe mbalina vyakula vinavyofyonza harufu kwaurahisi, kama maziwa, juisi n.k.

Mayai

Ni muhimu kuzingatia yafuatayo wakati wakununua mayai:

• Yai liwe na uzito fulani kwahisia linaposhikwa (lisiwejepesi kuliko umbilelinavyoonekana);

• Hakikisha yai linapotazamwakwa angani kwenye mwangahalionyeshi weusi wowote;

• Ikibidi yai linaweza kujaribiwa kama nizima kwa kuliweka ndani ya chombochenye maji yenye chumvi kidogo. Yaibovu huelea kwenye maji;

• Usinunue yai lililo na ufa.

Hifadhi bora ya mayai ni muhimu kwanimayai yanaweza kuwa zalio zuri la vimelea vyamaradhi. Yafuatayo ni muhimu:

• Inashauriwa kuhifadhi mayai mahali safi;

• Hakikisha sehemu ya yai iliyo bapainaangalia juu ili kuepuka yai kuharibikamapema;

• Inashauriwa kutoosha mayai wakati wakuhifadhi, inapobidi yafutwe kwakitambaa kikavu ili kuondoa vumbi. Yailikioshwa hupoteza ngozi fulani ya asiliambayo hulinda yai.

• Epuka kutumia yai lililo na ufa.

• Kwa wale wenye jokofu, mayaiyahifadhiwe mahali penye ubaridi mdogo(majokofu mengi huonyesha sehemu yakuweka mayai).

Nyama

Wakati wa kununua nyama mbichi zingatiayafuatayo:

• Nyama iwe na rangi halisi ya nyama freshi,mfano; nyama ya ng’ombe iwe na ranginyekundu;

• Hakikisha nyama ina harufu halisi yanyama mbichi sio harufu inayoashiriakuharibika;

• Nyama iwe angavu na isidondoshemajimaji wala damu;

• Nyama isiwe na mifupa mingi;

• Epuka nyama yenye mafutayanayoonekana kwa macho;

• Katika mazingira yetu ni bora kununuanyama mapema asubuhi kuliko mchanaambapo nyama huwa imeshinda dukanibila kuwekwa katika jokofu;

• Hakikisha nyama za ndani kwa mfanomaini, figo, moyo, utumbo n.k. ni freshina hazijaanza kuoza, nyama hizo zipikwemapema baada ya kununuliwa.

9

10

KUMBUKA• Kuosha nyama kabla ya kuikatakata;• Kukatakata nyama kabla ya kupika

husaidia nyama kuiva haraka;• Kupika nyama pamoja na kiasi kidogo cha

papai bichi lililopondwa, ndimu au limauhusaidia nyama kulainika na kubaki naunyevu wake;

• Nyama iliyotolewa kwenye barafu na kuyeyushwa, isigandishwe tena.

Uhifadhi bora wa nyama mbichi ni muhimusana kwani nyama mbichi huweza kuwa zaliozuri la vimelea vya magonjwa. Ni vyemanyama mbichi ikanunuliwa kadiri ya mahitajiya muda mfupi au ikahifadhiwa kwakuzingatia yafuatayo:

• Nyama isafishwe kabla ya kuikata;

• Inapohifadhiwa iwekwe kwenye chombocha plastiki chenye mfuniko au mfuko wanailoni, kifurushi cha kutumia mara moja;

• Ihifadhiwe kwenye jokofu sehemu yenyebaridi kali au barafu (freezer);

• Nyama iliyoganda ikiyeyushwaisigandishwe tena.

Maziwa

Maziwa yanayonunuliwa kwa wafugaji au yakupima, yachemshwe vizuri pia yaleyanayotumika kutengeneza mtindi. Kwakawaida maziwa ya paketi (ya kiwandani)huwa yamechemshwa ili kuua vijidudu(Pasteuralized). Maziwa haya ni salama kwakutumia. Unaponunua maziwa yaliyo kwenyepaketi ni muhimu kuhakikisha kwamba paketihaijatoboka na muda wa kutumiahaujamalizika. Inashauriwa:

• Maziwa freshi au mtindi yahifadhiwekwenye jokofu, au yanunuliwe kiasi cha

11

kutumia kwa muda mfupi.

• Maziwa yaliyo kwenye paketi zinazoelezakwamba yanaishi muda mrefu (UHT)yanaweza kuhifadhiwa katika joto lakawaida kama paketi haijafunguliwa.Ikishafunguliwa, yatumiwe mara moja auyawekwe kwenye jokofu, na tarehe zamatumizi zilizoshauriwa zifuatwe.

Nafaka

Ni muhimu wakati wa kununua nafaka kamamahindi, mchele, ngano, ulezi, mtama na ungaunaotokana na nafaka hizo kuhakikishakwamba hazikuota ukungu, hazijawa nawadudu na hazina harufu ambayo sio yakawaida. Kwa zile nafaka zilizofungwa kwenyepaketi, hakikisha tarehe ya kutumiahaijamalizika. Nafaka zihifadhiwe mahalipakavu.

Vyakula vingine

Hakikisha unga, mihogo, karanga havinaukungu vinaponunuliwa na vihifadhiwemahali pakavu.

VIDOKEZO KUHUSUMATUMIZI YA JOKOFU

v Chakula kiwekwe kwenye chombo aukifurushi kwa matumizi ya mara moja;

v Chakula kilichotolewa kwenye jokofukichemshwe kabisa kabla ya kuliwa;

v Nyama mbichi au samaki wabichiwawekwe sehemu yenye baridi kali(freezer), katika vifurushi vya matumiziya mara moja;

v Nyama au samaki iliyotolewa katikabarafu ikiyeyushwa ipikwe yote,isigandishwe tena;

v Hakikisha nyama mbichi au samakiwabichi havigusishwi na vyakula vingine.

12

Hii huepusha uambukizo unaowezakutokana na vyakula hivi;

v Matunda yaliyokatwakatwa yawekwekwenye chombo chenye mfuniko, nayahifadhiwe kwa muda mfupi;

v Vyakula ndani ya jokofu vifunikwe aukufungwa kwenye mfuko safi wa plastikiili kudumisha ubora wake na kuepukamuingiliano wa harufu;

v Maji ya kunywa yafunikwe;v Mlango wa jokofu usiachwe wazi kwa

muda mrefu. Funga mara unapotoa aukuweka kitu.

KULA NJE YA NYUMBANI

Zipo sababu nyingi zinazomfanya mtu kula njeya nyumbani au katika mazingira ambayomara nyingi mlaji hana uwezo wa kudhibitinamna chakula kinavyopikwa au vituvilivyochanganywa ndani yake. Ni muhimukwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIkuwa mwangalifu zaidi kwani chakulakinaweza kuwa chanzo cha maambukizi yamagonjwa iwapo hakitatayarishwa katika haliya usafi na usalama.

Sehemu ambazo mara nyingi mtu anakula njeya nyumbani ni pamoja na:-

• Hotelini au katika migahawa;

• Kafeteria;

• Katika sherehe au misiba;

• Vyakula vinavyouzwa kando ya barabara;

• Wauzaji wanaotembeza chakula n.k.

Kisheria sehemu zote zinazouza chakulazinatakiwa kuzingatia usafi na usalama, lakiniinawezekana sio sehemu zote zinatimizamasharti ya usafi. Hivyo ni muhimu sana kuwa

13

waangalifu hasa kwa watu wanaoishi na virusivya UKIMWI kwani kinga yao ya mwiliimepungua.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kula nje yanyumbani:

• Kuepuka mboga-mboga mbichi kamakachumbari na saladi, kwani zina hatarikubwa zaidi ya kuwa na vimelea vyamagonjwa, iwapo hazikutayarishwa katikahali ya usafi;

• Kama ni hoteli uliza kama inawezekanakutengenezewa chakula namnaunavyotaka;

• Kuhakikisha nyama, samaki, mayai ni vyamoto na vimeiva vizuri;

• Vyakula vinavyopikwa kwa wingi nakuachwa kusubiri wateja kwa muda mrefuvinaweza kuwa sio salama, ni borakuviepuka;

• Vyakula vinavyouzwa kando ya barabaramara nyingi uhifadhi wake sio salama,hivyo ni bora kuviepuka kwani hatari yasibiko (contamination) ni kubwa;

• Mara nyingi vyakula vinavyopikwa katikamikusanyiko kama misiba au sherehehuwa ni vingi. Inawezekana kukatokeaupungufu wa vifaa au mahitaji mengine,na hivyo kusababisha sibiko(contamination) katika chakula. Ni vizurimtu anayeishi na virusi vya UKIMWIkuwa mwangalifu hasa inapobidi kulakatika mikusanyiko ya watu. Ni vyemakuepuka pale inapowezekana.

14

Baadhi ya vyakula huhitajika mwilini kwa kiasikidogo. Ni muhimu kutumia vyakula hivi kwakiasi. Vyakula hivyo ni kama; mafuta, sukari nachumvi.

Mafuta

Mafuta huhitajika mwilini kwa kiasi. Mtuanayeishi na virusi vya UKIMWI anatakiwakutumia mafuta, ila atumie kwa kiasi.Ikumbukwe kwamba vyakula vinavyopikwakwa kukaangwa au kutumbukizwa kwenyemafuta na vile vinavyokandwa kwa mafuta autui la nazi huwa na mafuta mengi. Vyakula hivivitumike kwa kiasi. Mfano wa vyakula hivyo nikama maandazi, chapati, chipsi, vitumbua,sambusa, kababu, kaukau, “crisps”, n.k.Vyakula vingine vinavyoweza kuwa na mafutamengi ni pamoja na soseji, aiskrimu za maziwa,baadhi ya biskuti na mbegu zitoazo mafuta.Badala ya kupikwa kwa kutumbukiza kwenyemafuta njia nyingine za kupika zinawezakutumika ili kupunguza mafuta kwa mfano;kuoka, kuchoma, kupika kwa mvuke aukuchemsha. Pia ni vizuri kuondoa mafutayanayoonekana kwa macho kwenye nyamakabla ya kupika.

Ni bora zaidi kutumia mafuta yanayotokana namimea lakini pale yanapokosekana, mafutayanayotokana na wanyama yanawezakutumika. Usiache kabisa kutumia mafuta.

Sukari

Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIanahitaji sukari kwa sababu inampatia nguvu.Hata hivyo vipo vyakula vingine ambavyo

TUMIA KWA KIASI…!!!

15

humpatia mtu nguvu, hivyo vyakula vyenyesukari kwa wingi vitumike kwa kiasi. Vyakulahivyo ni pamoja na sukari, sukari guru, keki,chokoleti, jamu, soda na vinywaji vinginevyenye sukari kwa wingi. Ni vyema vyakulahivi vitumike mara chache au kwa kiasi.

Chumvi

Chumvi huongeza ladha kwenye chakula nahuupatia mwili baadhi ya madini. Wakatimwingine chumvi hutumika katika kuhifadhivyakula. Chumvi nyingi sio nzuri kwa afya.Vyakula vyenye chumvi nyingi ni pamoja navyakula vilivyosindikwa kwa chumvi kamanguru aliyekaushwa, soseji, achari, baadhi yavyakula vilivyosindikwa kama samaki nanyama za makopo, supu za paketi, baadhi yavyakula vingine vya makopo, “bacon” n.k.Vyakula hivi vinapotumika vitumike kwa kiasi.Ili kupunguza matumizi ya chumvi nyingi,kiasi kidogo cha chumvi kitumike katikakupikia chakula na ni vizuri kuepuka kuongezachumvi mezani.

IKIWEZEKANA ACHA…!!!

Baadhi ya vyakula havina umuhimu mwilinikwa mfano pombe au vinywaji vyenye kafeinikwa wingi. Ni vizuri kupunguza matumizi yavyakula hivi au kuviacha kabisa.

Pombe

Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIanashauriwa kupunguza sana matumizi yapombe na ikiwezekana kuacha kabisa.Matumizi ya pombe yameonyesha madharambalimbali katika mwili kwa kuingilia ulaji wachakula, uyeyushwaji wa chakula, ufyonzwaji

16

wa virutubishi mwilini pamoja na uwekajiakiba wa baadhi ya virutubishi. Piaimeonekana kwamba pombe huongeza hatariya kupata magonjwa sugu kama saratani hasaza kinywa, koromeo, zoroto (larynx) na ini.Vilevile huongeza hatari ya kupata vidonda vyatumbo na magonjwa ya moyo. Vinywajivyenye kileo ni pamoja na bia, mvinyo, pombezote kali, pombe za kienyeji n.k. Ni vyemakujaribu kutumia vinywaji visivyo na kileokama juisi ya matunda halisi, madafu, togwan.k.

Kafeini

Kafeini hupatikana kwenye baadhi ya vinywajina vyakula. Kafeini ni kichangamsha mwili,lakini huzuia usharabu wa madini ya chumayatokanayo na vyakula vya mimea. Vyakulavyenye kafeini kwa wingi ni pamoja na chai,kahawa, baadhi ya soda, chokoleti na kokoa.Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIanashauriwa kupunguza matumizi ya vinywajihivi. Inapobidi kutumia vinywaji hivi,vitumike kwa kiasi kidogo, na vitumikeangalau saa moja kabla au baada ya kula.

Ni vizuri kujaribu vinywaji vya aina nyingine,kwa mfano vile vinavyotengenezwa kutokanana viungo, majani ya mchaichai, majani yamlimau, choya (rozela), nanaa, tangawizi navinginevyo, au juisi itokanayo na matundahalisi.

USALAMA WA CHAKULA

Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI yukokwenye hatari ya kupata maambukizi yamagonjwa mbalimbali kwa urahisi zaidi. Hivyobasi ni muhimu kwa mtu huyo au mtayarishajiwa chakula kuzingatia yafuatayo ili kufanya

17

chakula na maji viwe safi na salama kwamtumiaji:

• Vyombo vinavyotumika kutayarishia nakupakulia chakula viwe safi.

• Vyombo na vifaa vilivyotumikakutayarisha nyama mbichi, samakiwabichi na mayai mabichi vioshwe vizurikwa maji na sabuni kabla ya kuvitumiakwa matumizi mengine. Majivu yanawezakutumika pale ambapo hakuna sabuni.

• Kuhakikisha chakula kimepikwa na kuivavyema, na pia kiliwe kingali cha moto.

• Kuosha matunda na mboga-mboga kwamaji ya kutosha. Mboga zinazoliwa bilakupikwa mfano kachumbari na matundayanayoliwa na maganda yasafishwe kwamaji salama.

• Sehemu zenye michubuko katika mbogana matunda zikatwe na kutupwa.

• Kuepuka nafaka au vyakula vilivyootaukungu.

• Kuhakikisha kuwa nyama, samaki namayai vinapikwa na kuiva vizuri ilikuepuka maambukizo ya magonjwa.Vyakula hivi kamwe visiliwe vikiwavibichi.

• Kuepuka vyakula vilivyokaa zaidi ya saambili baada ya kupikwa au viporo, ikibidikuliwa vichemshwe vizuri kabla ya kuliwahata kama bado vina uvuguvugu. Ni borakuepuka viporo.

• Kuepuka mgusano wa vyakula vibichi navile vilivyopikwa, hasa nyama mbichi,samaki wabichi na mayai mabichi.

• Kuchemsha maji ya kunywa na kuyaachayaendelee kuchemka kwa muda wa dakika

18

5 hadi 10. Maji hayo yatunzwe katikachombo safi chenye mfuniko. Iwapounahitaji kutumia barafu, hakikisha majiyaliyotumika kutengenezea barafuyalichemshwa.

• Kuosha mikono kwa sabuni namaji ya kutosha kabla yakutayarisha chakula. Majivuyanaweza kutumika pale ambapohakuna sabuni.

• Kunawa mikono mara baada ya kutumiachoo au kujisaidia, kupiga chafya, kufutakamasi au kushika taka.

• Kuzingatia usafi wa mwili na nguo.

• Kufunga vidonda vya mkononi ili kuzuiasibiko (contamination) wakati wakutayarisha chakula.

• Sehemu zote za kutayarishia chakula ziwesafi. Funika vyakula na maji kwa vyombosafi kuzuia wadudu hasa inzi.

KUMBUKAv Inapobidi kula nje ya nyumbani, ni

muhimu kuhakikisha unakula chakulacha moto.

v Chakula ambacho hakikupikwanyumbani kwako inaweza kuwa vigumukujua usafi na usalama wake.Inapowezekana, jaribu kula mahaliambapo unaweza kudhibiti usafi nausalama wa chakula na maji.

HITIMISHO

Hali bora ya lishe ni muhimu katika kuboreshaafya ya mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI.Ikumbukwe kwamba ulaji bora ni pamoja nakuzingatia ununuzi bora wa vyakula

19

mbalimbali, uhifadhi bora, usafi na usalama.Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIanashauriwa kutumia vizuri kiasi cha pesakilichopo katika kununua vyakula ambavyovina thamani kubwa kilishe na vinavyoupatiamwili virutubishi muhimu. Sio lazima kwambavyakula vyenye bei kubwa ndio bora zaidi.Vyakula vingi vya asili ambavyo sio vya beikubwa sana ni bora pia kilishe. Ikumbukwekuwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWIinabidi awe mwangalifu zaidi katika usafi nausalama wa chakula, kwani kinga ya mwiliimepungua hivyo anaweza kupata maambukiziya magonjwa mbalimbali kwa urahisi zaidi.

REJEA

1. Burgess, A. and others, CommunityNutrition for Eastern Africa, AfricanMedical and Research Foundation,Nairobi, Kenya, (1994).

2. FAO - Living well with HIV/AIDS, Amanual on nutritional care and supportfor people living with HIV, (2002).

3. FAO - Get the best from your food (1997)

4. Ndungi, H.K., Food and Nutrition forSchools and Colleges, Nairobi, (1992).

5. NFTRC, Healthy eating, shopping forfood and food safety guidelines,(Botswana).

6. Tull, A., Food and Nutrition, GCSEEdition, Oxford University Press, (1991).

20

Orodha ya vijitabu vinginekuhusu Lishe na Ulaji Bora kwaWatu Wanaoishi na Virusi vya

UKIMWI vilivyotolewa naCOUNSENUTH

1. Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusivya UKIMWI: “Vidokezo Muhimu”(COUNSENUTH, Information seriesNo. 2), Toleo la Pili, January, 2004.

2. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishina Virusi vya UKIMWI: “Majibu yaMaswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara”(COUNSENUTH, Information seriesNo. 3) Toleo la Pili, January, 2004.

3. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishina Virusi vya UKIMWI: “VyakulaVinavyoboresha Uyeyushwaji wa Chakulana Ufyonzwaji wa Virutubishi Mwilini”(COUNSENUTH Information seriesNo. 4), March, 2003.

4. Ulishaji wa Mtoto Mchanga kwa MamaMwenye Virusi vya UKIMWI: “VidokezoMuhimu kwa Washauri Nasaha”(COUNSENUTH Information seriesNo. 1), Toleo la Pili, January, 2004.

5. Matumizi ya Viungo vya Vyakula katikaKuboresha Lishe na Afya(COUNSENUTH, Information seriesNo. 6), Toleo la Kwanza, March, 2004.

25

Kwa kushirikiana na:

Halmashauri ya Manispaa ya IlalaS.L.P 20950

Dar es Salaam

Kimefadhiliwa na : Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:Mkurugenzi

The Centre for Counselling, Nutrition and Health Care (COUNSENUTH)

Kijarida hiki kimetayarishwa na: The Centre for Counselling, Nutrition and

Health Care (COUNSENUTH)United Nations Rd./Kilombero Str.

Plot No. 432, Flat No. 3P. O. Box 8218, Dar es Salaam, Tanzania

Tel/Fax: +255 22 2152705, Cell: 0744 279145

Designed & printed by:Desktop Productions Limited

P.O. Box 20936, Dar es Salaam, TanzaniaContact: 0748 387899, Email: [email protected]

Reprinted January 2005

Reprinting facilitated by COUNSENUTHand MUCHS, in partnership with the

Government of Tanzania.