Transcript
Page 1: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA! NI MAHALA PATAKATIFU; IKULU NI MZIGO; MSITEMEE MATE KABURI

LANGU- Mwal J.K NYERERE (AHERA) Rai ya Mtanzania

Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga

Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]

Usiku nalala ghafla usingizi mzito unanipata; Mara namuona Muasisi wa Taifa

hili baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ananipa barua

niwaletee watanzania na kuniagiza wasilitemee mate kaburi langu kwa kivuli

cha Katiba na Madaraka ya Urais. Anaeleza jinsi ambavyo alinusurika kupata

kifo kwa kile alichoita Adha ya Uhaini ya Mwaka 1964 na 1982 kama

ifuatavyo.

Mnamo tarehe 20 Januari, 1964, nilikoswa kupinduliwa na Jeshi la Tanganyika

Rifles ambalo liliasi na Maasi hayo yalizimwa tarehe 25 Januari, 1964. Maasi

yalihusisha Vikosi vya Dar-es-salaam na Tabora Brigedi ya Kwanza na ya Pili.

Kipindi hiki ndicho kipindi cha Majeshi ya Ukombozi ya Msumbiji pia

yalipambana katika nchi yao.

Ilipofika Saa 7.50 alfajiri, ya tarehe 21 Januari, 1964, Mkuu wa Kikosi cha

Kwanza cha TR Brigedia Patrick Sholto Douglas, aliamshwa nyumbani kwake

na Sauti ya Baruji na Ving’ora, karibu na Kambi ya Jeshi la Colito ambayo sasa

inaitwa Lugalo Barracks. Alipotoka nje, aliona askari wake 12 wameshikiliwa

na wenzao wenye silaha na hatimaye kutiwa Mahabusu. Ndipo alipofahamu

kwamba, baadhi ya Askari wa Kikosi hicho walikuwa wameasi. Aliweza

kutoroka yeye na familia yake hadi katikati ya Jiji, akaiacha familia kwa Balozi

wa Australia nchini, kisha akakimbilia kwa Afisa mwenzake eneo ya Oysterbay

Dar-Es-Salaam.

Page 2: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

Akiwa huko, akampigia simu Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akimuomba

kupeleka ndege tatu Kikosi cha pili cha huko Tabora, kuleta askari waliokuwa

bado waaminifu kwa Serikali. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa wamefunga

barabara iendayo Uwanja wa ndege huko Ukonga; hii ikawalazimu Marubani

warudi mbio inasemekana Brigedia Patrick Sholto Douglas akakimbilia kwenye

Ubalozi wa Uingereza, akajificha kwa siku tano hadi tarehe 25 Januari, 1964.

Brigedia Patrick Sholto Douglas alimpigia simu Mkuu wa Polisi, ambaye

alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Makamu wa Rais wakati huo Mzee

Rashid Mfaume Kawawa, na kumwamsha, kisha hao wawili wakaja kunipa

habari.

Nilihamaki na kukasirika sana; nikataka kwenda mimi mwenyewe kukutana na

Waasi hao ili wanieleze sababu za kitendo hicho cha aibu; lakini Honey wangu

Mama Maria kwa machozi na kwa kupiga magoti, alinisihi nisitoke kwenda

kukutana na watu wenye silaha. Nilimkaidi mpenzi wangu lakini Juhudi za

ziada zilifanywa baadaye nilikubali. Radhid Kawawa na Mama Maria Nyerere,

wakatorokea mahali nisikokujua. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa kwenye

lango kuu la Ikulu wakinitafuta.

Kufikia saa 9.00 alfajiri siku hiyo hiyo, Waasi walikuwa wamekamata Kambi

ya Colito (Lugalo), kisha wakajigawa Vikundi vitatu na kuingia mjini. Kikundi

kimoja kilibakia kulinda Kambi hiyo, Kikundi cha Pili, kikiongozwa na Sajini

Francis Higo Ilogi, ndicho kilichokuja Ikulu kunitafuta, wakati Kikundi cha tatu

kililinda barabara kuu zote mjini.

Kikundi cha Sajini Ilogi kilipofika Ikulu, kiliruhusiwa na Mmoja wa Maafisa

Usalama wa Taifa, wamuone kwanza Waziri Mheshimiwa Oscar Kambona; nao

wakakubali kufanya hivyo. Wakaenda hadi kwa Kambona na kumleta Ikulu, na

kumweleza kwamba walikuwa wamewakamata na kuwaweka Mahabusu baadhi

ya Wanajeshi ambao wanasemekana walikuwa 16; na kwamba, kama

Mheshimiwa Oscar Kambona alikuwa tayari kusikiliza Malalamiko yao,

afuatane nao hadi Colito (Lugalo). Kamabona alikubali, aliondoka akiwa

amepanda gari la Mkuu wa Polisi na aliweza kukubali kuandamana na askari

wenye silaha, na wenye hasira kali kwenda Colito Barracks.

Walipofika Colito Barracks, walimtaka Oscar Kambona aaamue papo hapo,

pamoja na mambo mengine kuondolewa mara moja kwa Maafisa wa Kiingereza

Jeshini, na nafasi zao zishikwe na Wazalendo. Walitaka pia mishahara

iongezwe, kutoa Shilingi za Tanzania 105/= hadi kufikia Shilingi za Tanzania

Page 3: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

260/= kwa mwezi. Hata hivyo, Mheshimiwa Oscar Kambona aliomba wateue

wawakilishi wachache ili wafuatane naye hadi Ikulu kwa Mashauriano nami

(Nyerere). Ndipo Kiongozi wa Waasi hao Sajini Francis Higo Ilogi, alipokataa

na kusema “Tunataka kila kitu leo hii” Yowe zikasikika “Apigwe risasi,

apigwe Kambona huyo”. Kwa kuogopa kuuawa, Kambona akauliza, “Mnataka

nani awaongoze?” Lilitajwa jina la Alex Nyirenda; lakini likakataliwa kwamba

alikuwa na majivuno. Akatajwa Luteni Elisha Kavana, akapitishwa kwa kauli

moja na kuvishwa kofia ya Brigedia Douglas.

Walipofika huko, askari hao walijipanga barabara iingiayo Ikulu, ingawa Sajini

Ilogi aliwakataza wasiingie ndani; Baada ya mashauriano kwa muda na

wasaidizi wa Rais pamoja na Mama mzazi wa Mwalimu Nyerere, Kambona

alitoka nje na kuwatangazia Waasi hao kuwa Rais ameyakubali madai yao;

Lakini askari hao wakapiga kelele “Muongo huyo Rais hayumo ndani; mpige

risasi, muongo huyo” Hata hivyo, waliondoka wameridhika, wakarejea

Kambini siku hiyo. Hima, Kambona aliwaondoa Maafisa wa Uingereza na

kuwasafirisha kwao kupitia Nairobi Kenya.

Akiwatangazia Wananchi kupitia Kituo cha Redio wakati huo “Tanganyika

Broadcasting Corporation (TBC), Mzee Oscar Kambona alisema;

“Huyu ni Waziri wenu wa Mambo ya Nje na Ulinzi; Serikali

ingalipo……kumekuwa na kutoelewana baina ya askari Waafrika na Maafisa

wa Uingereza katika Jeshi. Baada ya kuingilia kati Shauri hili, sasa askari

wamerudi kambini”

Kuna uwezekano mkubwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi

Mheshimiwa Oscar Kamabona ndiye aliyewashawishi Wanajeshi walioasi

Januari, 21, 1964 kurejea Kambini, kwa ahadi ya kushughulikia malalamiko

yao; siku ya pili baada ya kurejea Kambini, askari Waasi walionekana kufurahi

baada ya Maafisa wa Uingereza kuanza kuondoka, kama walivyoahidiwa na

Oscar Kambona. Ingawa, Sajini Francis Higo Ilogi hakuwa na furaha kama

wengine.

Nakumbuka, wakati wa Uasi Mwarabu mmoja alifanikiwa kuwaua Askari

wawili mtaani ambao walizikwa Dar-Es-Salaam. Wakati wa maziko ya askari

hao, ilipokelewa taarifa kwamba, Kikosi cha pili cha Jeshi kilichokuwa Tabora

nacho kilikuwa kimeasi, baada ya kupata habari kwamba wenzao wa Colito

{Lugalo} walikuwa wameasi.

Page 4: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

Wakati Kikosi cha Tabora kikiendelea na Maasi, ilipokelewa hapo Tabora simu

ya maandishi (Telegraph) kutoka kwa Mhehimiwa Oscar Kambona kuwa

Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha

Tabora. Wakati huo Sarakikya na Maafisa wengine walikuwa wamekamatwa na

kuwekwa Mahabusu na askari walioasi hapo Tabora.

Ndugu yangu Sarakikya akatolewa Mahabusu na akaomba simu hiyo isomwe

kwa sauti; kisha akatoa amri wasimame “Mguu Sawa”, wafunge beneti na kutoa

risasi. Nao wakamtii. Usiku huo, Sarakikya alifanya Mipango ya kuwasafirisha

maafisa wa Uingereza kutoka Tabora kwenda Dar-Es-Salaam na hatimaye

Makwao.

Tukio la Januari, 21 1964 na lile la Tabora pamoja ilienda sambamba na hali ya

Hatari huko Kenya, Uganda na Zanzibar, ambapo Serikali ya Uingereza ilibidi

ichukue tahadhari ya ziada kwa kupeleka askari wanaokisiwa kuwa 2,000 ndani

ya Ukanda wa Afrika ya Mashariki. Kwa hiyo, Manowari iliyoitwa Rhy, ikwa

imetia nanga hima Pwani ya Dar-es-salaam, na nyingine iitwayo Centaur,

iliyobeba ndege iliwasili na askari wapatao kama 600.

Nilifanya mazungumzo na Waasi; lakini ilipofika Ijumaa ya tarehe 25

Mazungumzo hayo hayakufikiwa vyema kwani Viongozi wa Vyama vya

Wafanyakazi, kupitia Chama Kikuu (Shirikisho) cha Wafanyakazi

(TFL),walikuwa wakikutana kwa siri na askari walioasi kwenye Kambi ya

Colito (Bienne P43); na Vyma hivyo vilikuwa vimeandaa Mgomo nchi nzima

kuungana na askari hao. Ilipofika saa 11.30 jioni siku hiyo, nilimuita Ikulu

Naibu Balozi wa Uingereza Bwana F. Stephen Mills; kumuomba Msaada wa

Kijeshi wa nchi yake na Mills bila kuchelewa, akapeleka taarifa London na

maombi kukubaliwa bila masharti yoyote.

Wakati huohuo, Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akaenda mbio kwenye

Ubalozi wa Uingereza kumtafuta Brigedia Douglas ambaye alikuwa amejificha

humo kwa wiki nzima, kumuomba msaada wa kuratibu Mipango. Usiku wa

siku hiyo, Douglas na Ofisa mwingine, walinyatia hadi kwenye Manowari

Centaur iliyokuwa imefichwa.

Jumamosi ya Januari tarehe 26, 1964 saa 12.20 asubuhi, helikopta sita kutoka

Manowari Centaur zilichukua askari wanaokisiwa kuwa 60 akiwamo Brigedia

Douglas hadi eneo la Karibu na Kambi ya Colito. Dakika kumi baadaye saa

12.30 Manowari hiyo, na meli nyingine ya Vita Cambrian iliyokuwa ikisubiri

zilianza Mashambulizi kwa kupiga Mizinga kuwatisha Waasi. Wakati huo

Page 5: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

mpango wa kuwalevya kwa ushindi wao bandia ulifanywa kwa kuchukuwa

pombe kwenye kiwanda cha Bia cha Ilala na Waasi hao wakanywa ipasavyo na

ndiyo msingi wa Colito kuitwa Lugalo ikiwa na maana ya pahali pa kulewea

pombe au tafrija ya pombe kwa lugha ya Kihehe au Kinyakyusa na baadhi ya

makabila yenye asili ya Kibantu. Kutoka umbari upatao kama mita 20 hivi, na

kwa ujasiri mkubwa, Douglas akatangaza kwa kipaza sauti, kwamba alikuwa

ameshika madaraka yake tena; akatoa amri askari wote watoke nje Kambini

“Mikono juu” na kukaa chini barabarani.

Baada ya dakika kumi bila kuona kitu, Brigedia Douglas akaanza kuhesabu

“Moja ; Mbili; …………Kumi”, askari wa Uingereza wakafyatua roketi hadi

Kambini. Waasi wakaanza kujisalimisha. Dakika kumi zingine zilizofuata

askari 150 walijisalimisha na wengine 150 baada ya saa moja. Kufikia saa 1.30

asubuhi, wote walikuwa wamesalimu amri; Maasi yakawa yamezimwa katika

zoezi ambalo askari walioasi, baadhi waliuawa na wengine walijeruhiwa.

Nakubaliana, na maoni ya Balozi Abbas Kleist Sykes akinukuliwa kuwa, “Maasi

ya Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) Mwaka 1964 yalitokana na sehemu kubwa

kwa kuchelewa kuwaondoa Makamanda wa Kizungu na kuwapandisha vyeo

Waafrika”. Kama ilivyofanyika kwa Jeshi la Polisi na Watumishi wengine

Serikalini. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Maasi ya Kenya na Uganda.

Kutokana na Maasi hayo, nilikifuta Kikosi chote cha Kwanza (Colito Barracks)

na kuwafukuza kazi askari 100 wa Kikosi cha Pili cha Tabora. Nilifukuza pia

asilimia 10 ya askari wa Polisi na Usalama 5,000 waliokuwapo, kwa kushindwa

kutekeleza Wajibu wao wa Kudhibiti Maasi. Watu zaidi ya 400 walikamatwa na

kuhojiwa, wakiwamo viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi; na wengine 500

walitiwa nguvuni chini ya Sheria ya “The Preventive and Detention Act” lakini

wengi waliachiwa.

Nalo lililokuwa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TFL), lilifutwa, badala yake

kikaundwa Chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kama

Jumuiya ya Chama tawaa –TANU. Nilimteua Mirisho Sam Hagai Sarakikya

kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi na kumpandisha cheo kuwa Brigedia.

Mwanzoni mwa Aprili, 1964, Majeshi ya Uingereza yaliondoka na nafasi yake

kuchukuliwa na Kikosi cha Tatu cha Jeshi la Nigeria, chini ya Luteni Kanali

James Pam. Sajini Francis Higo Ilogi alipatikana na Hatia ya Uasi wa Jeshi na

kufungwa miaka 15, ambapo washirika wake 13 wakafungwa kifungo cha kati

ya miaka mitano hadi kumi.

Page 6: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) liliundwa baada ya Tanganyika kupata Uhuru

tarehe 9 Desemba, 1961 likibadilishwa kutoka Jeshi la Kings African Rifles

(KAR) lililokuwa chini ya Waingereza. Pamoja na kubadilika Jina Tanganyika

Rifles ilikuwa na Muundo sawa na KAR. Jeshi hilo liliongozwa na Jenerali

Morisho Sarakikya kuanzia tarehe 8 Januari, 1964 hadi tarehe 12 Februari, 1974

lilipoongozwa na Jenerali Abdalah Twalipo hadi tarehe 8 Novemba, 1980.

Kipindi Jeshi linaasi, Sheria ya Kuwekwa Kizuizini ilikuwa tayari

imekwishaundwa yaani Tangayika Preventive and Detention Act, Cap 490 ya

Mwaka, 1962 kwa sasa ni Cap 361 [R.E 2002]. Hata hivyo, sikuipenda sana

Sheria hiyo ingawa niliweka saini. Kwa sababu niliamini niSheria

inayomuweka mtu hatiani bila Mashitaka hali anapaswa kuwa na Haki ya

kusikilizwa.

Ukweli ni kuwa nilipata kusema maneno yafuatayo “Take the question of

detention without trial. This is a desperately serious matter. It means that you

are imprisoning a man when he has not broken any written law, or when you

cannot be sure of proving beyong reasonable doubt that he has done. You are

restricting his liberty, and making him suffer materially and spiritually, for

what you belive he has done. Few things are more dangerous to the freedom of

a society than that. For freedom is indivisible, and with such an opportunity

open to the Government of the day, the freedom of every citizen is reduced; to

suspend Rule of Law under any circumtances is to leave open the possibility of

the grossest injustices being perpetrated. Yes knowing these things. I have still

supported the introduction of a law which gives the Government power to

detain people without trial. I have myself signed Detention Orders. I have done

these things as an inevitable part of my responsibilities as President of the

Republic…………………”

Pamoja na Sheria hiyo kuwepo, Mheshimiwa Kasanga Tumbo aliyekuwa

Kiongozi wa Chama cha People’s Democratic Party ndani ya Bunge ambaye pia

aliwahi kuwekwa Kizuizini kuanzia Januari, 1964 hadi Julai, 1966 aliipinga

vikali Sheria hiyo, iliyotangaza pamoja na mambo mengine “Hali ya Hatari kwa

Watu wa Tanganyika” Hata hivyo, niliamini kuwa Sheria hiyo iliwalenga

wahaini.

Ilipofika Mwezi Aprili, 1965 raia 14 wa Tanzania mbali ya Wajumbe wa awali

wa Baraza huko Zanzibar na Wanajeshi wapatao 20 wa Jeshi la Tanganyika

Rifles waliwekwa Kizuizini. Hata hivyo, ilipofika tarehe 25 Julai, 1966

Page 7: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

ilitangazwa kuwa Watanzania waliokamatwa kwa ajili ya Uhaini walikuwa

wameachiwa huru; Hayo yalisemwa na Mheshimiwa Job Lusinde wakati huo

akiwa Waziri wangu wa Mambo ya Ndani ambaye alisisitiza kuwa kwa mujibu

wa Sera ya Jumla iliyofikiwa waliotuhumiwa wote wako huru na kuwa kamwe

haiashirii kuhatarisha Amani nchini.

Mnamo Mwezi Agosti, 1967, Ndugu Abdalah Khasim Hanga aliyekuwa

Makamu wa Rais wa Zanzibar, na Mlinzi wake Ndugu Eli Anangisye Mbunge

wa Tanzania Bara, ndugu zake Oscar Kambona na Maafisa watatu wa Wizara

ya Mambo ya Nchi za Nje waliohisiwa kuwa mahasimu wa karibu wa Kambona

waliwekwa ndani kwa kuhusishwa na kufanya njama za Mapinduzi; Hii

ilijumuisha pia kuwaweka ndani baadhi ya viongozi, marafiki na ndugu.

Baadaye, ikatangazwa kuwa viongozi wa tuhuma za Mapinduzi hayo

watafungwa kwa kosa la Uhaini.

Mbali ya Uhaini huo, pia Nusra nipoteze nafasi ya Urais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, mnamo Mwaka 1982. Jaribio hilo la Mapinduzi

lilifanywa na baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania wakisaidiana

na Bwana mmoja aliyeitwa Thomas Pius Mtakubwa Rugangira huyu alijulikana

pia kwa majina ya “Father Tom” au “Unle Tom”.

Kipindi hicho idara yangu ya Usalama ilitumia sana usafiri wa Teksi na hata

bendi maarufu ya DDC Mlimani park msingi wake mkubwa ni chama cha

Tanzania Transport, Tax and Services (TTTS) kilikuwa na watu wenye weledi

huo. Hivyo, Watuhumiwa hao walifichuliwa njama zao na dereva teksi mmoja

waliyekuwa wakimtumia mara kwa mara ambapo njama zao zilikuwa kuniua na

kuniondoa Madarakani na Kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania. Hivyo walikabiliwa pia na Shitaka mbadala la kuficha kosa la Uhaini

kwa kushindwa kutoa taarifa kwa Mamlaka iliyohusika huku wakielewa juu ya

Mpango wa Kuipindua Serikali.

Sikupenda sana iwepo kesi dhidi yao kwani nikiwa Mkatoliki niliyekuwa

kwenye Jumuiya Parokia ya Msasani na hata Kanisa la Mtakatifu Petro la

Oysterbay nilijifunza kusamehe mara saba sabini. Lakini Dola iliamua Kesi ya

Uhaini iungurume hapa nchini Tanzania chini ya Mheshimiwa Jaji Nassor

Mnzavas. Washitakiwa kwenye kesi hiyo walikuwa 19; miongoni mwao

alikuwepo Thomas Rugangira au “Uncle TOM”au “Father Uncle Chek Bob”,

wenzake walikuwa ni Khatibu Ghandhi au “Hatty MacGhee”, Kapteni

Mohammed Tamimu, Kapteni Ditrick Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege,

Page 8: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Vitalis Mapunda. Wengine

walikuwa ni Banyikwa na Mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Has Pope,

Kapteni Rodrick Rosham Robert na wengine ambao jumla yao walikuwa 19.

Kundi hilo lilikuwa na vijana watundu waliojiita Makomandoo sikumbuki

walijifunza wapi? Ambao ni Rugangira na Hatty MacGhee ambao wakati Kesi

inaendelea walipanga njama na kufanikiwa kutoroka katika Gereza la Keko,

Mjini Dar-Es-Salaam.

Vijana wale walitorokea nchini Kenya na baada ya kufika Kenya, Rugangira

akatorokea nchini Uingereza. Wakati huo viwanja vyetu vya ndege havikuwa na

ulinzi sana na hata mipakani hapakuwa na ulinzi mkali kubaini utorokaji wao.

Kwa bahati nzuri, Yule kijana Hatty MacGhee tukafanikiwa kumkamata na

kumrudisha hapa Tanzania; kukawa na Makubaliano na Kenya ya

kubadilishana wahalifu na ndipo tukabadilishana na mtu mmoja aliyekuwa

akitakiwa Kenya aliyetajwa kwa jina la Private Hezekiah Ochuka ambaye

ilidaiwa kuwa alifanya madudu huko Kenya.

Kijana Hatty MacGhee aliporejeshwa nchini aliunganishwa na wenzake na kesi

ikapamba moto. Nakumbuka, Katika Jaribio hilo, Komandoo Tamimu aliuawa

wakati wa purukushani za kumkamata pale Kinondoni Mkwajuni Dar-Es-

Salaam wakati wakimkimbiza Komandoo Tamimu alidandia gari moja Pick Up

iliyokuwa imebeba masanduku ya bia na kuanza kuwarushia wanaUsalama

waliokuwa wakimkimbiza, hivyo akapigwa risasi na kufa.

Ingawa nakumbuka, Mahakamani wakati wa kutoa ushahidi juu ya Komandoo

huyo mwanaUsalama mmoja aliyekuwa akiitwa MrX alisema walijaribu

kumkamata lakini akawatoroka kwa kuruka ukuta wa nyumba aliyokuwa

akiishi.

Kesi hiyo ya Uhaini ilikuwa imesimamiwa na Wakili machachari wa Utetezi

aliyejulikana kwa jina la Murtaza Lakha mwenye asili ya Asia. Mawakili

wengine wa Utetezi alikuwepo Mucadam, Jadeja na Tarimo. Upande wa

Serikali ulikuwa unaongozwa na Wakili William Sekule, pia alikuwepo Johnson

Mwanyika.

Watuhumiwa wengine sita wa Uhaini waliachiwa huru siku mbili baadaye

kutoka kwenye Gereza la Ukonga Dar-Es-Salaam. Wakati wakiachiwa huru,

Maganga alikuwa amehamishwa kwenye Magereza mengi ndani ya Dar-Es-

Page 9: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

Salaam na Gereza lake la mwisho lilikuwa Butimba Mwanza. Pamoja na tabu

walizozipata Gerezani Eugen Maganga anadaiwa kusema;

“Hatujutii kujaribu kuangusha Serikali bali tunajutia tu kwa kushindwa kwa

Mipango ya kupindua.”

Kabla hawajafikia kuwa na wazo la kuangusha Serikali, Maganga aliyekuwa na

miaka 26 na Kadego walifika Jeshini na Tank Battalion. Maganga alikuwa

Luteni wakati Kadego alikuwa Kapteni.

Maganga alikuwa ndiyo anarudi kutoka Mjini London Uingereza ambapo

alikuwa akipata mafunzo ya kujinoa Kijeshi ya kupigana vita ya Uganda

Mwaka 1978. Akiwa mmoja wapo ya askari wa mstari wa mbele, Maganga

anaamini Tanzania ilishinda vita dhidi ya Uganda kwa vile Uganda ilikuwa na

Jeshi dhaifu.

Moja ya sababu walizozibainisha ni pamoja na 1) kutokuwa na furaha jinsi

Watanzania walivyokuwa Maskini na kulazimishwa kwenye Vijiji vya Ujamaa ;

2) Vita dhidi ya Uganda na Tanzania havikuwa na umuhimu na hivyo kuishia

kutumia fedha vibaya-vita havikuwa vya nchi hizi mbili bali vita vya Mwalimu

Julius Nyerere na Idd Amin na pia 3) Hali iliyokuwepo Jeshini ilikuwa siyo

nzuri ukilinganisha na hali iliyokuwepo wakati wa Meja Jenerali Mrisho

Sarakikya, Kiongozi wa Kwanza wa Jeshi la Ulinzi toka Mwaka 1964 hadi

1974 4) Waliopanga njama za kuangusha Serikali walihisi kuwa mimi

(Nyerere) sina imani na watu wa Kaskazini kwa sababu wamesoma nje ya nchi

na hivyo nawahofia kuwa wanaweza kuangusha Serikali 5) Watu waliokuwa

hawajasoma sana ndiyo waliopewa Madaraka na kuwa mambo hayakwenda

sawa; na 6) Wanajeshi hawakupewa vyeo na kuwa mimi nilipenda kujenga

Jeshi lenye watu ambao hawawezi kunipa Changamoto zozote.

Wahaini hao walidhani wangefanya mabadiliko bali inaonekana watu ambao

walijipanga nao hawakuwa tayari kujitoa Mhanga. Hata hivyo, hawakukata

tamaa, wakiwa baadhi yao wanapanga njama hizo wakakutana na Marehemu

Thoma Pius Rugangira ambaye alikuwa Mfanyabiashara wa Tanzania huko

nchini Kenya, na alikuwa akiishi pia Uganda na kwa vile baba yake Mzazi

alikuwa Uganda alikuwa akidhaniwa kuwa ni Afisa Usalama wa Serikali ya

Uganda.

Wahaini hao hawakuwashirikisha kabisa viongozi wa juu wa Jeshi waliweza

kujipanga wenyewe wakiwa vijana wadogo. Thomas Pius Rugangira ndiye

Page 10: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

alikuwa mfadhiri wao na kamwe hawakupata fedha zozote nyingi toka nje ya

nchi. Wahaini hao walidhani wangeweza kuleta mfumo wa Demokrasia ya

Vyama Vingi ambako watu huwa huru kutoa mawazo yao na kuchagua Rais wa

nchi wanayemtaka. Waliahidiwa kuwa Thomas Pius Rugangira ndiye ambaye

angechukua nafasi ya Uwaziri Mkuu badala ya kuwa na mimi (Nyerere) kwa

masharti kuwa asingepaswa kugombea nafasi ya Urais kwa muda wa Miaka

iliyokuwa inafuata.

Siku tatu kabla ya Uhaini kufanyika Thoms Pius Rugangira aliwauliza ni nafasi

gani wangehitaji kama wakiunda Serikali mpya; lakini walijibu kuwa

wasingehitaji chochote.

Wakati Mipango yote imekuwa tayari, walisubiri nirudi toka nje ya nchi kwani

nilisafiri; Nilirudi Mnamo Mwezi Januari, 1982 baada ya kukaa nje kwa muda

wa miezi miwili na kwenda nyumbani kwetu Butiama. Lengo lao la kunisubiri

ilikuwa kuniuwa na mipango hiyo ilipendekezwa na Thomas Pius Rugangira.

Bila matarajio, nilikaa muda kidogo pale Butiama na sikurudi Dar-Es-Salaam

katika kipindi cha siku mbili ambazo Mapinduzi yalipangwa ambapo

yalipangwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 9 Januari, 1982. Siku ya Ijumaa

Mnamo tarehe 6 Januari, 1982 wakapanga kukutana kwa mara ya mwisho kabla

ya kutekeleza Uhaini wao; hata hivyo, baadhi ya wenzao hawakuonekana.

Mohammed Tamimu ni mmoja ya Wahaini ambao hawakuonekana siku hiyo.

Wajumbe wengine walihofu sana kitendo cha Mohammed Tamimu

kutoonekana. Wakaamua kumtuma mmoja wao Kinondoni Mkwajuni ambako

alikuwa anakaa, lakini wakashangaa kuona Polisi wamezingira nyumba yake na

wamemuuwa. Hapo wakagundua kuwa suala lao siyo siri tena. Mohammed

Tamimu alikuwa na kawaida ya kutunza rekodi za mikutano yao na majina ya

wahusika.

Ikawa Polisi na Wanausalama wameanza kuwasaka; Kadego na Maganga

wakaamua kutorokea Kenya kupitia Tanga na Mombasa ambapo walikaa

Nairobi miezi kumi kama Wakimbizi wa kisiasa. Hawakujilaumu sana kuvuja

kwa Suala lao kwani waliamini pengine Hatty MacGhee ametoa siri kwa vile

alikuwa raia na alikuwa hajui kutunza siri. Walihisi pia kuwa Mohammed

Tamimu alijua kuwa Hatty MacGhee hakuwa Askari Mstaafu wa Jeshi la

Marekani kama alivyojitapa na wakagundua baadaye kuwa jina lake halisi

alikuwa Khatibu Hassan Ghandhi na alikuwa rubani Mtanzania.

Page 11: IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

Kuna wakati siku chache baadaye, Maganga na Kadego wakiwa wanazurura

mitaa ya Nairobi ghafla wakawaona Wahaini wenzao Uncle Thom na Hatty

MacGhee waliokuwa wamewaacha Dar-Es-Salaam. Hawa watuhumiwa wawili

walikuwa wametoroka katika Gereza la Keko lililopo mjini Dar-Es-Salaam.

Ingawa walifurahia maisha pale Nairobi, Rugangira aliamua kusafiri kwenda

London Uingereza kujaribu kutafuta njia ya kuwahamishia Malawi. Alihofu

kuwa Serikali ya Kenya ingeshirikiana na Serikali ya Tanzania kuwakamata.

Watuhumiwa wa Uhaini wote nane, walifanikiwa kutorokea Nairobi. Kabla ya

Pius Rugangira hajarudi kutoka London kundi lao likakamatwa Nairobi na

wakabadilishana na Koplo Ochuka na Sajini Pancras Oteyo ambao nao

walikuwa na Mpango kama huo wa kuagusha Serikali ya Rais Daniel Arap Moi

wa Kenya Mwaka huo huo wa 1982 na wakakimbilia Tanzania. Walifungwa

pingu mikononi na kufungwa vitambaa usoni na kupelekwa kwenye Gereza la

Isaka lenye ulinzi Mkali lililopo Mjini Dodoma ambako walikaa kuanzia Mwezi

Novenber, 1983 hadi Oktoba, 1084.

Watu waliokuwa wanawalinda hawakuwa wakali sana, kitu kilichowafanya

waweze kuandika barua Ubalozi wa Marekani wakitaka Dunia ielewe kuwa

walifungwa kwa sababu hakuna mtu alikuwa anajua chochote wakati huo. Hii

ilifanya Kamishana wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa kutembelea Tanzania

na kulazimisha kupeleka Kesi Mahakamani.

Kesi ilianza kuunguruma rasmi Januari, 1985 na Mnamo tarehe 28 Desemba,

1985 Mheshimiwa Jaji Nassoro Mnzavas alitoa Hukumu ambapo washitakiwa

wengine aliwafunga kifungo cha maisha na wengine walifungwa miaka kadhaa

lakini Banyikwa na Ngaiza waliachiwa huru.

Kwenye Gereza la Butimba, ndipo alipokuwepo Eugene Maganga ambapo

Mnamo tarehe 22 Oktoba, 1995, Rais Ali Hassan Mwinyi alitoa Msamaha na

wenzaka kadhaa.

[HAKIKA IKULU SI PA KUKIMBILIA “MUNGU IBARIKI AFRIKA

IBARIKI TANZANIA”]


Recommended