Transcript
Page 1: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Tangazo la Serikali Na. 310 la Tarehe 20/07/2018

SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA MIJI)

(SURA YA 288)

KANUNI ZA KUDUMU

Zimetungwa chini ya kifungu cha 42 (1)

KANUNI ZA KUDUMU ZA HALMASHAURI YA MANISPAAKIGAMBONI

ZA MWAKA 2018

YALIYOMO

SEHEMU YA IMASHARTI YA MWANZO

1. Jina na tarehe ya kuanza kutumika2. Tafsiri ya misamiati iliyotumika

SEHEMU YA IIMIKUTANO YA HALMASHAURI

3. Mikutano ya Kawaida ya Halmashauri4. Utaratibu wa Uchaguzi5. Mkutano Maalum wa Halmashauri6. Mkutano wa Bajeti7. Mkutano wa Mwaka8. Taarifa za Mikutano9. Akidi katika mikutano ya Halmashauri.

SEHEMU YA IIITARATIBU ZA MIKUTANO

10.Uchaguzi wa Mstahiki Meya/ Naibu Meya 11.Uongozaji wa Mikutano ya Halmashauri12.Kumbukumbu ya mahudhurio13.Kuruhusu watu na Vyombo vya Habari kwenye Mikutano

ya Halmashauri

14.Utaratibu wa shughuli za Mikutano

1

Page 2: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

15.Kuthibitisha muhtasari16.Hoja za Meya/Mwenyekiti17.Taratibu za Majadiliano18.Fujo zinazosababishwa na Wajumbe.19.Fujo zinazosababishwa na Umma20.Hoja za Marekebisho ya Hoja21.Hoja zinazoweza kutolewa bila taarifa.22.Haki ya kujibu23.Maswali24.Maswali ya papo kwa papo25.Taarifa za Kamati26.Taarifa kutoka kwenye Kata27.Uhuru wa Kutoa mawazo wakati wa majadiliano28.Kauli zenye kashfa29.Maamuzi ya Mikutano ya Halmashauri30.Mwaliko kwa wasiokuwa Wajumbe kushiriki na

kuzungumza kwenye vikao vya Halmashauri

31.Mihtasari ya Kata na ya Vijiji/Mitaa32.Mihutasari kupelekwa kwa Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa

Mkoa33.Hoja kuhusu matumizi34.Kupokelewa kwa taarifa ya Kamati35.Kuidhinishwa kwa taarifa ya Kamati36.Uhalali wa majadiliano ya Halmashauri37.Uwezo wa Halmashauri kujigeuza kuwa Kamati ya

Halmashauri nzima.38.Hoja zinazohusu watumishi wa Halmashauri39.Kushiriki kwa Umma40.Uahirishaji wa Vikao

SEHEMU YA IVKAMATI

41.Kamati za Kudumu42.Meya/Mwenyekiti kuwa Mjumbe wa Kamati zote.

2

Page 3: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

43.Uwezo wa Kamati44.Kamati za Pamoja45.Kukasimu madaraka kwenye Kamati46.Kamati Ndogo47.Mikutano ya Kamati48.Mwenyekiti wa Kamati49.Mkutano maalum wa Kamati50.Ajenda za Kamati51.Mahudhurio katika Mikutano ya Kamati52.Mtoa hoja kualikwa kwenye Mkutano wa Kamati53.Waalikwa wasiokuwa Wajumbe kuhudhuria na kushiriki

katika Mikutano ya Kamati54.Mahudhurio ya Umma na Vyombo vya Habari kwenye

Mikutano ya Kamati na Kamati Ndogo55.Athari za nafasi wazi kwenye Kamati56.Akidi kwenye Mikutano ya Kamati57.Kanuni za kudumu kutumika katika Mikutano ya Kamati 58.Upigaji kura kwenye Mikutano ya Kamati59.Muhtasari wa Kamati60.Kufikiriwa upya maamuzi61.Kutunza siri za majadiliano ya Kamati na Kamati Ndogo62.Kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Kamati63.Kujiuzulu ujumbe wa Kamati na kujazwa kwa nafasi

iliyoachwa wazi.

SEHEMU YA VUNUNUZI WA VIFAA, UPATIKANAJI WA HUDUMA NA

UJENZI

64.Taratibu za uagizaji65.Kumbukumbu za majadiliano yanayohusu uagizaji66.Uzuiaji wa rushwa67.Usimamizi wa Mikataba68.Uvunjaji wa Mkataba69.Rejesta ya Mikataba70.Diwani au Afisa kutokuwa na maslahi kwenye Mikataba

SEHEMU YA VIMASUALA MENGINE

71.Kiapo cha kukubali wadhifa72. Majukumu ya Diwani

3

Page 4: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

73.Nafasi wazi74.Kutokuwepo kwa Wajumbe75.Taratibu za kutunga Sheria Ndogo76.Ukaguzi wa nyaraka77.Uanzishaji wa Bodi ya Huduma78.Diwani kutembelea maeneo, shughuli mbalimbali za

ujenzi 79.Uhifadhi wa lakiri ya Halmashauri80.Utiaji muhuri kwenye nyaraka81.Uandikishaji wa anwani82.Uteuzi wa Wajumbe kwenye Taasisi za nje83.Kumwondoa Meya/Mwenyekiti madarakani

SEHEMU YA VIIPOSHO KWA WAJUMBE

84.Aina za posho85.Posho endapo Mkutano utaahirishwa

SEHEMU YA VIIIMABADILIKO KWENYE KANUNI ZA KUDUMU

86.Kusitisha utumiaji wa Kanuni za kudumu87.Marekebisho na mabadiliko ya Kanuni za Kudumu88.Kanuni za Kudumu kutolewa kwa Wajumbe89.Kutafsiri Kanuni za kudumu90.Ziara za Wajumbe91.Wimbo wa Taifa,Dua na sala ya kuiombea Halmashauri92.Kufuta Kanuni zilizopo.

SEHEMU YA IMASHARTI YA MWANZO.

KWA KUWA kauli-mbiu ya Halmashauri nikuendesha shughuli kwa namnainayozingatia demokrasia, ufanisi, tija,ushirikishwaji, uwazi na uwajibikaji;

4

Page 5: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

NA KWA KUWA jukumu la Halmashauri nikuimarisha demokrasia katika ngazi zote nakutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatiaufanisi, usawa, haki na kwa namnainayochochea maendeleo ya maeneo yaliyochini ya mamlaka ya Halmashauri kwakuwashirikisha wananchi;

NA KWA KUWA madhumuni ya Kanuni hiziza kudumu ni kuweka utaratibu wa namnaHalmashauri itakavyoendesha Mikutano nashughuli zake kwa kuzingatia misingi yautawala bora;

SASA BASI, Kanuni hizi za kudumuzinaelekeza ifuatavyo;

Jina natarehe ya Kuanzakutumika

1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Kudumu zaHalmashauri ya Manispaa Kigamboni zaMwaka 2018 na zitaanza kutumika marabaada ya kutangazwa kwenye Gazeti laSerikali;

Tafsiri 2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama maelezohaya yatahitajika vinginevyo;

“Afisa wa Serikali za Mitaa” maana yakeni mtu ambaye ameajiriwa na au ambayeyumo katika Utumishi wa Mamlaka yaSerikali za Mitaa na ambaye anashika auanakaimu katika nafasi ya menejimenti;

“Akidi” ni idadi ya Madiwaniitakayokamilika baada ya kujiorodheshakatika rejesta ya Mahudhurio ya Mkutanoambayo itaruhusu kufanya maamuzi yaMkutano kwa mujibu wa Kanuni za 9, 49 na56;

“Chama” ni chama cha siasa chenyeuwakilishi katika Baraza la Madiwani;

5

Page 6: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

“Diwani” maana yake ni Mjumbe waHalmashauri aliyetajwa kwa mujibu wakifungu 24(2) cha Sheria ya Serikali za Mitaa(Mamlaka za Miji) Sura ya 288;

“Fujo” maana yake ni kitendo chochotekinachoweza kufanywa na Mjumbe auMshiriki wa Vikao vya Halmashauri auKamati ya Kudumu ambacho ni kinyume nataratibu za uendeshaji wa vikao,kinachoweza kuvuruga kikao. Mfanokuongea bila ruhusa ya Mwenyekiti, kutoalugha isiyofaa, kutoa kauli yenye maudhi,kuingia kwenye kikao akiwa umelewa,kuingia na silaha, kutoa lugha ya kashfa,kukaidi amri ya Mwenyekiti, kukaidi kutokanje pale anapoamriwa kutoka kutokana nafujo alizosababisha;

“Halmashauri” maana yake niHalmashauri ya Manispaa Kigamboni;

“Kamati”(a) Inapotumika

kuhusiana na Halmashauri yaManispaa Kigamboni ina maana yaKamati iliyoanzishwa au iliyoteuliwana Halmashauri ya ManispaaKigamboni chini ya Sheria;

(b) Inapotumikakuhusiana na Kamati ya Maendeleoya Kata ina maana ya Kamati hiyo;

(c) Inapotumikakuhusiana na Kamati Ndogo maanayake ni Kamati Ndogo hiyoiliyoteuliwa na Kamati;

(d) Inapotumikakuhusiana na Kamati nyingine inamaana ya Kamati hiyo;

(e) Kwa maana ya Bodiya Zabuni ni Katibu wa Bodi ya

6

Page 7: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Zabuni.

“Kura ya siri” Maana yake ni Kuraitakayopigwa katika eneo la faraghalililotengwa kwa madhumuni ya kupiga kura,eneo ambalo halitapungua umbali wa mitatano (5) kutoka kwa Msimamizi wa kura;“Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenziwa Manispaa Kigamboni pamoja na Afisayeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumuya Mkurugenzi;

“Mjumbe” maana yake ni Mjumbe waHalmashauri kama ilivyoainishwa na kifungucha 27 cha Sheria;

“Meya” kwa madhumuni ya Halmashaurimaana yake ni Meya wa Halmashauri yaManispaa Kigamboni na inajumuisha NaibuMeya wakati anapotekeleza majukumu yaMeya kwa mujibu wa kanuni hizi.

“Mwenyekiti” a) Kwa madhumuni ya Kamati, Bodi au

Kamati Ndogo maana yake niMwenyekiti wa Kamati, Bodi auKamati Ndogo.

b) Kwa maana ya Bodi ya Zabuni niMwenyekiti wa Bodi ya Zabuni

“Sheria” maana yake ni Sheria ya Serikaliza Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288;

“Waziri” maana yake ni Waziri mwenyedhamana ya Serikali za Mitaa;

7

Page 8: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

SEHEMU YA IIMIKUTANO YA HALMASHAURI

MikutanoyaKawaidayaHalmashauri

3 (1) Mikutano ya Kawaida ya Halmashauriitafanyika mara moja kila baada ya miezimitatu, na itafanyika mahali, tarehe nakatika muda kama utakavyokuaumepangwa katika kalenda ya Mikutano yaHalmashauri.

Mkutanowa KwanzawaHalmashauri.

(2) (a) Mkutano wa kwanza wa kawaida waHalmashauri utafanyika baada yaTume ya Uchaguzi kutangazamatokeo ya uchaguzi wa Madiwaniwa Kata na uteuzi wa Madiwani waViti maalumu, na utafanyika mahali,siku na katika muda utakaopangwana Mkurugenzi, ilimradi Mkurugenziatapaswa kuitisha Mkutano huo ndaniya siku thelathini kuanzia tarehe yamatokeo ya uchaguzi wa Madiwaniwa Kata na Uteuzi wa Madiwani VitiMaalum yanapotangazwa na Tume yaUchaguzi ambapo moja ya ajenda zaMkutano huo ni kumchaguaMeya/Mwenyekiti, NaibuMeya/Makamu Mwenyekiti naWajumbe wa Kamati za Kudumu zaHalmashauri.

(b) Katika Mkutano huo Mkurugenzi waHalmashauri atawasilisha Taarifa yakumbukumbu ya maamuzi yautekelezaji wa shughuli zaHalmashauri zilizofanyika katikakipindi ambacho Baraza la Madiwanililivunjwa. Wajumbe wa Barazawatapokea na kujadili bila kubatilishamaamuzi yaliyokwisha amuliwa.

Utaratibu 4 Uchaguzi wa Meya na Naibu Meya

8

Page 9: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

wauchaguzi

utafanyika kwa kupiga Kura za siri naupigaji wa kura utafanyikia sehemu yafaragha umbali usiopungua mita (5) kutokakwa Msimamizi wa Uchaguzi na mpiga kuraatachukua karatasi ya kupiga kura kutokakwa Msimamizi wa Uchaguzi.

MkutanomaalumwaHalmashauri

5 (1) Mkutano Maalum wa Halmashauri unawezakuitishwa na Meya ndani ya siku ishirini namoja baada ya kupokea maombi yamaandishi yaliyosainiwa na si pungufu yatheluthi moja ya Wajumbe wote kutakaMkutano huo ufanyike na maombi hayoyaeleze wazi madhumuni ya kuitishwa kwaMkutano Maalum huo.

(2) Endapo ajenda ya Mkutano huo itahusukumuondoa madarakani Mwenyekiti,Mkutano huo utaitishwa na Mkurugenzibaada ya kupokea maombi yaliyosainiwa naWajumbe wa Halmashauri wasiopunguatheluthi mbili ya Wajumbe wote.

(3) Baada ya Mkurugenzi kupokea maombikutaka kufanyika kwa Mkutano wa kujadiliajenda ya kumuondoa madarakani Meya,Mkurugenzi atamtaarifu Meya tuhuma nasababu za kutaka kuondolewa Umeya nakumtaka aandae majibu ya tuhuma ndaniya siku tano (5) baada ya kupokea tuhumahizo.

(4) Mkurugenzi katika muda wa siku Tatu (3)baada ya kupokea maelezo ya utetezikutoka kwa Meya, atawasilisha kwa Mkuuwa Mkoa tuhuma pamoja na maelezo yautetezi.

(5) Mkuu wa Mkoa baada ya kupokea taarifa yaMkurugenzi ndani ya muda wa siku tano (5)ataunda Timu ya Uchunguzi ambayoitakuwa na wajumbe wasiopungua watatu(3) na wasiozidi watano (5).

9

Page 10: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(6) Timu ya Uchunguzi itatakiwa kukamilishaUchunguzi katika muda wa siku kumi nanne (14) na kuwasilisha taarifa hiyo kwaMkuu wa Mkoa.

(7) Baada ya Mkuu wa Mkoa kupata taarifa yaTimu ya Uchunguzi atairudisha Taarifa hiyokwa Mkurugenzi ambaye naye katika mudawa siku kumi na Nne (14) ataiwasilishakwenye Kikao cha Baraza kwa uamuzi watuhuma hizo.

Kif.cha25(5) Sura288

(8) Endapo Meya hataridhika na uamuzi waBaraza, atakata rufaa kwa Waziri kuhusu tuutaratibu uliotumika kumuondoamadarakani na sio vinginevyo.

Utaratibuwakuwasilisha rufaa

(9) Utaratibu utakaotumika kuwasilisha nakushughulikia rufaa iliyowasilishwa na Meyani ule ulioelezwa kwenye Taratibu zakumuondoa madarakani Meya waHalmashauri.

(10)

Iwapo Meya anakataa kuitisha Mkutanomaalum wa Halmashauri baada ya kupokeamaombi ya kutakiwa kufanya hivyo,maombi yaliyosainiwa na Wajumbe waHalmashauri wasiopungua theluthi moja yaWajumbe wote wakionyesha sababu yakuitisha Mkutano huo maalum nakuwasilishwa kwake, au iwapo bila kukataa,Meya, ndani ya kipindi cha siku sabaataendelea kutoitisha Mkutano huo maalumbaada ya kupokea ombi la kuitisha Mkutanohuo maalum, basi theluthi mbili yaWajumbe waliotia saini na kuwasilisha kwaMkurugenzi wanaweza kuitisha Mkutanohuo maalum mara moja.

(11)

Taarifa ya Mkutano maalum itatolewaangalau saa ishirini na nne kabla yaMkutano.

10

Page 11: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(12)

Hakuna shughuli nyingine yoyoteitakayojadiliwa katika Mkutano maalum waHalmashauri isipokuwa ile tu iliyoelezwakwenye taarifa ya kuitishwa kwa Mkutanohuo.

Mkutanowa Bajeti

6 Kutakuwepo na Mkutano wa Halmashauriwa Bajeti utakaofanyika kwa muda wasiku mbili mfululizo na utafanyika miezimiwili kabla ya mwaka wa fedha kumalizikana utajadili mambo yafuatayo:-

(a) Utekelezaji wa Mipango na Bajeti yamwaka uliopita.

(b) Mipango na Bajeti ya mwakaunaofuata.

Mkutanowa Mwaka

7. (1) (i) Mkutano wa Mwaka wa Halmashauriutafanyika tarehe, mahali na mudautakaopangwa na Halmashauri katikakalenda ya Mikutano na utaitishwa naMkurugenzi baada ya kuwasiliana na Meyawa Halmashauri.

(ii) Mikutano yote ya Baraza itapangwa naBaraza la Madiwani kwa kuzingatia ratiba yaVikao vya Bunge ili kuwezesha Wabungekuhudhuria Mikutano ya Baraza laMadiwani. Endapo italazimika kuitishwakwa Mkutano wa Baraza wakati wa Vikaovya Bunge, Mkurugenzi atamjulisha aukuwajulisha Wabunge husika kuhusu kikaohicho ili wahudhurie.

(2) Mkutano wa Kwanza wa Uchaguzi wa Meya,Naibu Meya na Wajumbe wa Kamatiutaongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya naMkurugenzi wa Halmashauri atakuwaKatibu.

(3) Katika Mkutano wa kawaida wa mwaka,

11

Page 12: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Halmashauri itajadili mambo yafuatayo:-(a) Kumchagua Naibu Meya,(b) Kuteua Wajumbe wa Kamati za

Kudumu;(c) Kujadili taarifa ya utendaji na

uwajibikaji wa Halmashauri kwamwaka uliopita.

(d) Kupitisha ratiba ya vikao vyaHalmashauri na Kamati zaHalmashauri.

Taarifa zaMkutano

8 (1) Mkurugenzi atatoa taarifa ya Mkutano kwamaandishi kwa kila Mjumbe katika mudausiopungua siku saba akieleza mahali, sikuna saa ya Mkutano unaokusudiwa namambo yatakayojadiliwa katika Mkutanohuo.

(2) Taarifa ya Mkutano itaambatana na nyarakaau kumbukumbu muhimu zitakazotumikakatika Mkutano huo.

(3) Isipokuwa kwa idhini ya Meya na au ya idadiya Wajumbe isiyopungua robo tatu yaWajumbe waliohudhuria Mkutano, hakunashughuli yoyote itakayofanywa katikaMkutano wa Halmashauri mbali na shughulizilizotajwa katika mwaliko wa Mkutano huo.

AkidikatikaMikutanoyaHalmashauri

9 (1) Hakuna Mkutano wa kawaida waHalmashauri utakaofanyika isipokuwa kamakutakuwepo idadi ya Wajumbe isiyopunguanusu ya Wajumbe wote waliohudhuria nakujiandikisha kwenye daftari la mahudhurio.

(2) Akidi katika Mikutano maalum yaHalmashauri itakuwa ni theluthi mbili yaWajumbe wote wa Halmashauri naitahesabiwa wakati wa ufunguzi waMkutano.

12

Page 13: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(3) Akidi katika Mkutano wa kawaida wa mwakana Mkutano wa kwanza wa Halmashauriitakuwa theluthi mbili ya Wajumbe wote waHalmashauri.

(4) Endapo Wajumbe waliohudhuria Mkutanohawatafikia akidi ya Mkutano, Mkurugenziatauahirisha Mkutano huo na kuitisha tenandani ya siku saba (7) na endapo akidihaitatimia tena, idadi yoyote ya Wajumbewaliohudhuria itatengeneza akidi yaMkutano na Mkurugenzi atamjulisha Wazirikuwepo kwa hali hiyo.

(3) Akidi katika Mikutano maalum yaHalmashauri itakuwa ni theluthi mbili yaWajumbe wote wa Halmashauri naitahesabiwa wakati wa ufunguzi waMkutano.

(4) Akidi katika Mkutano wa kawaida wa mwakana Mkutano wa kwanza wa Halmashauriitakuwa theluthi mbili ya Wajumbe wote waHalmashauri.

SEHEMU YA IIITARATIBU ZA MIKUTANO

Uchaguziwa Meya/Mwenyekiti naNaibuMeya/MakamuMwenye-iti waHalmashauri

10

(1) Meya na Naibu Meya watachaguliwa naWajumbe, kutokana na Wajumbe waHalmashauri kwa kura ya siri itakayopigwana Mjumbe mmoja mmoja kwenye eneo lafaragha litakalotengwa umbali usiopunguamita 5 kutoka mahali alipoketi Msimamiziwa Uchagu

(2) Mjumbe kabla ya kwenda sehemu yafaragha kwa ajili ya kupiga kura, atapatiwana Msimamizi wa Uchaguzi karatasi yakupigia kura kutoka kwenye chombomaalum kitakachowekwa mbele ya

13

Page 14: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Msimamizi wa Uchaguzi, na atakwendamoja kwa moja kupiga kura yake kwenyesehemu ya faragha.

(3) Mtu atatangazwa kuchaguliwa kuwa Meyaau Naibu Meya iwapo atapata zaidi ya nusuya kura zilizopigwa.

(4) Iwapo wakati wa kumchagua Meya au NaibuMeya, jina moja tu limependekezwa,Wajumbe watapiga kura za siri za “ndiyo”au “hapana”na endapo kura za “ndiyo”zitazidi asilimia hamsini ya kura zotezilizopigwa basi mgombea atatangazwakuwa Meya au Naibu Meya.

(5) Iwapo kura za “Hapana” zitazidi asilimiahamsini ya kura zote zilizopigwa, jina lamgombea mwingine litapendekezwa kwanjia na utaratibu uliotumika hapo awali.

(6) Iwapo kura zitafanana, uchaguzi utarudiwakwa mara ya pili na endapo hata baada yakurudia uchaguzi kura zimefanana, Barazalitaamua kugawana muda wa kuwamadarakani kwa wagombea hao ambaokura zao zimefanana.

(7) Kama itatokea nafasi wazi ya Meya auNaibu Meya, Halmashauri itamchagua Meyaau Naibu Meya katika muda wa sikuzisizozidi sitini tangu nafasi hiyo ilipotokea.

Uongozaji wa Mikutano ya Halmashauri

11

(1) Mkutano wa Halmashauri utaongozwa na:-(a) Meya; au(b) Kama Meya hayupo, Naibu Meya; au(c) Kama Meya na Naibu Meya wote

hawapo, au kama Meya na NaibuMeya wote hawawezi kuongozaMkutano, Mjumbe yeyoteatachaguliwa na Wajumbe kutokamiongoni mwa Wajumbewaliohudhuria kwa ajili ya kuongoza

14

Page 15: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Mkutano huo,(d) Wajumbe wawapo ndani ya ukumbi

wa Mikutano wa Halmashauriwatavaa mavazi maalumyaliyochaguliwa na kushonwamaalum kwa ajili hiyo,

(e) Endapo vazi maalum lililochaguliwana Halmashauri ni joho basi litavaliwajuu ya vazi la Mjumbe, na EndapoHalmashauri haina joho basi Mjumbeatavaa vazi la heshima, na mavazikama jeans, kofia zinazohusiana nadini na sare za Chamahazitaruhusiwa kuvaliwa wakati waMikutano ya Halmashauri na vikaovya Kamati za Kudumu zaHalmashauri.

(f) Vazi rasmi la Meya, Mkurugenzi naNaibu Meya litakuwa lenyekuonyesha rangi za Bendera ya Taifana mazao yanayolimwa kwa wingikatika eneo la Halmashauri kadriHalmashauri itakavyoona inafaa.Hata hivyo, Kanuni hii haitaathirimajoho ambayo yanatumika kabla yaKanuni hii,

(g) Endapo katika Mkutano huoHalmashauri itajigeuza kuwa Kamati,Wajumbe watavua majoho.

(h) Endapo Baraza litajigeuza kuwaKamati taratibu za kuendesha Vikaovya Kamati zitatumika na kikao hichokitakua cha siri.

(2) Madaraka au jukumu lolote la Meyakuhusiana na uendeshaji wa Mikutanoyanaweza kutekelezwa na mtuanayeongoza Mkutano huo.

(3) Halmashauri itatenga siku mbili kila wikikwa ajili ya Meya kufika ofisini na

15

Page 16: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

kutekeleza majukumu yafuatayo;

(a) Kusikiliza matatizo ya Wananchi;(b) Kupata maelezo toka kwa

Mkurugenzi kuhusu uendeshaji washughuli za Halmashauri ikiwa nipamoja na masuala ya manunuzi;

(c) Kusaini mikataba mbalimbali yaHalmashauri;

(d) Kushughulikia jambo ambaloMkurugenzi ataona linahitajikushughulikiwa au kutekelezwa naMeya.

Kumbukumbu yamahudhurio

12

(1) Kila Mjumbe anayehudhuria Mkutano waHalmashauri au Kamati yoyote yaHalmashauri ambamo yeye ni Mjumbehatahudhuria Mkutano huo mpaka aweameweka saini yake kwenye Rejesta yamahudhurio inayotunzwa na Mkurugenzikwa ajili hiyo.

(2) Isipokuwa siku ya kufanyika kwa Mikutanoya Baraza au Kamati ambayo Diwani niMjumbe au pale atakapoitwa kutekelezamajukumu ya Serikali, si ruhusa kwa Diwanikuwa katika Ofisi za Halmashauri nakufanya shughuli ambazo hazihusiani naHalmashauri au Serikali.

Kuruhusuwatu navyombovya habarikwenyeMikutanoyaHalmashauri

13

(1) Mikutano ya Halmashauri itakuwa wazi kwawatu wote pamoja na vyombo vya habari.

(2) Halmashauri itapaswa kuutangazia Ummakuhusu muda, wakati na mahali pa Mkutanona italiweka tangazo hilo mahalipanapoonekana kwa urahisi katika eneo laHalmashauri siku zisizopungua tatu kabla ya

16

Page 17: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Mkutano, na kama Mkutano umeitishwakatika muda mfupi zaidi basi wakati wakuitisha Mkutano huo.

UtaratibuwashughulizaMikutano

14

(1) Isipokuwa kama Halmashauri, kutokana nasababu za dharura, itaamua kubadiliutaratibu wa shughuli za Mikutano,utaratibu wa shughuli katika kila Mkutanowa kawaida wa Halmashauri utakuwa kamaifuatavyo:-

(a) Meya akiongozwa na Katibu ataingiaukumbini baada ya Mratibu wa vikaokutoa ishara maalum kuashiria Meyakuingia ukumbini na Wajumbewatasimama na kukaa kimya mpakapale Meya atakaporuhusu Wajumbekukaa

(b) Mkutano utaanza kwa Sala au Duaitakayosomwa na Meya,

(c) Endapo Meya au Naibu Meyahawatakuwepo, Wajumbewatachagua mtu wa kuongoza kikao,

(d) Baada ya Sala/Dua kusomwaMkurugenzi na Meya/watajibumaswali ya papo kwa papo kutokakwa Wajumbe wa Baraza lamadiwani kwa utaratibu nampangilio kama ilivyooneshwakwenye Kanuni hizi,

(e) Kupokea na kujadili taarifa zakwenye Kata kutoka kwa Madiwaniwa Kata husika,

(f) Kujadili jambo lolote linalotakiwa kwamujibu wa Sheria kushughulikiwakabla ya shughuli nyingine yoyote,

(g) Kupokea taarifa yoyote inayopaswakupokelewa kisheria kabla ya

17

Page 18: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

shughuli nyingine yoyote,

(h) Kusoma au kuthibitisha muhtasariwa Mkutano wa kawaida waHalmashauri uliopita na Mikutanoyoyote maalum ya Halmashauriiliyofanyika baada ya Mkutano huowa kawaida. Hata hivyo iwaponakala za mihtasari zimesambazwakwa kila Mjumbe kabla au wakati wakupeleka taarifa ya kuhudhuriaMkutano, mihtasari hiyo itachukuliwakuwa imesomwa,

(i) kupokea taarifa yoyote ambayoMeya atapenda itolewe kwaHalmashauri,

(j) Kujibu maswali kufuatana na Kanuniya 23 ya Kanuni hizi,

(k) Kumalizia shughuli yoyote iliyobakikatika Mkutano wa kawaida uliopita,

(l) Kupokea na kufikiria taarifa zaKamati za Halmashauri, kutoka kwaWenyeviti wa Kamati ambaowatahusika kujibu maswali yaWajumbe kuhusiana na kazi zaKamati husika,

(m) Kupokea na kujadili taarifa kutokakwa Mkurugenzi wa Halmashauri,

(n) Kuidhinisha utiaji lakiri katika hati,

(o) Kufikiria hoja binafsi kufuatana najinsi zilivyopokelewa, na,

(p) Kushughulikia mambo mengineyaliyoonyeshwa katika taarifa yaMkutano.

(2) Halmashauri inaweza, katika Mkutanowowote wa kawaida, kubadili utaratibu wahoja za mazungumzo ili kutoa kipaumbele

18

Page 19: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

kwa shughuli yoyote ambayo kwa maoni yaMeya na uharaka wa pekee, lakinimabadiliko hayo hayatabadilisha mpangiliowa shughuli zilizotajwa katika aya (c), (f) na(g) za Kanuni ya 14(1) ya Kanuni hii.

Kuthibiti-shamuhtasari

15

(1) Katibu ataandika muhtasari wamazungumzo ya kikao unaozingatia majinaya Wajumbe waliohudhuria nawasiohudhuria, jina la mtoa hoja, aliyeungamkono hoja, mabadiliko ya hoja kwa ufupi,ushauri uliotolewa na azimio lililofikiwa.Muhtasari huo utasomwa, kurekebishwa,kuthibitishwa na kusainiwa na Mwenyekitiwa Mkutano na kutunzwa katika rejestamaalum ya mihtasari.

(2) Mara baada ya kusoma Muhtasari, au kamaitachukuliwa kama umesomwa Mwenyekitiatauliza swali “Je Muhtasari wa Mkutano waHalmashauri wa tarehe…………… yamwezi…………. Mwaka……..utiwe sainikama kumbukumbu sahihi?.”

(3) Hakuna hoja au majadilianoyatakayofanywa kuhusiana na muhtasariisipokuwa kuhusiana na usahihi wamuhtasari, kama hakuna swali lililoulizwa,basi mara baada ya kuthibitishwa Meyaatatia saini katika muhtasari huo.

(4) Muhtasari ambao utakuwa umesainiwavilivyo na kama hakuna ushahidi wa kuwepokwa makosa utakuwa kumbukumbu sahihina Mkutano utahesabika kuwa umeitishwana kufanyika vilivyo na Wajumbewaliohudhuria watahesabika halali.

(5) Mihtasari ya Halmashauri itakuwa wazi kwaukaguzi na Wajumbe na kwa umma kwawakati unaofaa na kwa utaratibuutakaokubaliwa na Halmashauri na kwambamtu yeyote anaweza kupewa sehemu yamuhtasari huo kama akiomba na baada yakulipa ada kama itakavyoidhinishwa na

19

Page 20: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Halmashauri.

Hoja zaMeya/Mwenyekiti

16

Hoja zinazowasilishwa na Meya hazitazidihoja tatu, bila kuathiri haki yake, kamaMjumbe ya kuwasilisha hoja katika taratibuza kawaida.

Taratibuzamajadiliano

17

(1) Isipokuwa kwa idhini ya Halmashauri mtoahoja atahutubia Mkutano wa Halmashaurikwa dakika zisizozidi kumi. Wajumbewengine ikiwa ni pamoja na mtoa hojawatazungumza kwa muda usiozidi dakikatano kila mmoja;

(2) Mjumbe anaruhusiwa kuzungumza maramoja katika hoja yoyote ile isipokuwa hojainayowasilishwa bila mjadala;

(3) Mtoa hoja atakuwa na haki ya kuzungumzakwa muda usiozidi dakika tano katika kujibumajadiliano na muda huo utaanzakuhesabika mara atakapoanza kuchangiaau kujibu. Mratibu wa vikao atatoa isharamaalum kumjulisha mtoa hoja kuwa mudawake umeisha na mjadala juu ya hoja hiyoutafungwa. Utaratibu huu wa kuhesabumuda utatumika pia kwa Mjumbe yeyoteatakayepewa muda wa kuchangia hoja namara tu baada ya kujibu, mjadala juu yahoja utafungwa;

(4) Mjumbe yeyote aliyekwishachangia kwenyehoja hawezi kutoa au kuunga mkonomarekebisho, ila marekebisho yakitolewa nakuungwa mkono, Mjumbealiyekwishazungumza katika hoja ya awalianaweza kuzungumza kwenye hojailiyorekebishwa kwa muda usiozidi dakikatatu;

(5) Iwapo Wajumbe wawili au zaidi watasimamawakati mmoja kuzungumza, Mjumbe

20

Page 21: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

atakayetamkwa na Meya ndiyeatakayepewa nafasi kwanza;

(6) Bila kuathiri masharti ya Kanuni Ndogo ya(5) ya Kanuni hii, Meya atahakikisha kuwa,nafasi ya kuchangia inatolewa kwa uwianounaofaa miongoni mwa aina zote zauwakilishi wa Madiwani walioombakuchangia hoja hiyo;

(7) Mjumbe anapozungumza ataelekezamazungumzo yake kwa Meya tu naatapaswa kusimama;

(8) Mjumbe anapozungumza hatakatizwa,isipokuwa kwa suala la utaratibu, lakinianaweza kutoa nafasi kwa Mjumbeanayetaka kujieleza;

(9) Mjumbe anaposimama kutoa taarifa kuhusuutaratibu, Mjumbe anayezungumza ataketina atabaki ameketi hadi hoja ya utaratibuitakapokuwa imeamuliwa na Meya,isipokuwa kama anasimama kumwelezaMeya kuhusu suala la utaratibu;

(10)

Meya ndiye pekee mwenye uamuzi kuhusuutaratibu katika Mikutano ya Halmashauri,na anayo madaraka ya kuzuia fujo nakuhakikisha kuwa maamuzi yake katikakusimamia usalama yanatekelezwa maramoja. Wakati wa majadiliano Meyaakisimama, Mjumbe anayezungumza aualiyesimama ataketi na hakuna Mjumbeatakayesimama hadi Meya aketi;

(11)

Hakuna Mjumbe atakayebaki amesimamawakati Mjumbe mwingine anaelekezamazungumzo yake kwa Meya;

(12)

Mkurugenzi wa Halmashauri atajibu swalilolote atakaloulizwa na Meya kutokana nashughuli zinazoendelea kwenye Mkutanoisipokuwa kama atadai haki ya kukataa

21

Page 22: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

kujibu swali kwa msingi ya kwamba jibulinaweza kumweka hatiani au kuvunjauaminifu wake au linamhusisha yeye kamamtetezi mahakamani;

(13)

Hakuna mtu kwa niaba yake mwenyewe, aukwa niaba ya watu wengine walio kwenyeujumbe wa watu, atakayeruhusiwakuzungumza katika Mkutano waHalmashauri isipokuwa kwa idhini yaHalmashauri iliyotolewa kwa njia ya azimio.Idhini ya namna hiyo haitatolewa isipokuwakama mtu huyo au watu hao wanaotakakuihutubia Halmashauri watakuwawamempatia Mkurugenzi au Afisaaliyeruhusiwa naye, taarifa ya mudausiopungua siku tisa kabla ya Mkutano waHalmashauri ambamo wangetaka maombiyao yafikiriwe kupewa idhini, maombi yakimaandishi ikieleza jambo linalotarajiwakujadiliwa, na mpaka taarifa ya kupokelewakwa maoni hayo itakapokuwa imebandikwakwenye mbao za matangazo zaHalmashauri;

(14)

Hakuna zaidi ya watu wawili watakaokuwana haki ya kuhutubia Halmashauri kwaniaba ya uwakilishi; na wala hakuna ujumbeutakaozidi idadi ya watu watanowatakaoruhusiwa;

(15)

Kiwango cha juu cha muda wa kuzungumzana Halmashauri ikiwa ni pamoja na mudawa kusoma risala hakitazidi dakika kumi;

FujozinazosababishwanaWajumbe

18

(1) Katika Mkutano wowote wa Halmashaurikama Mjumbe wa Halmashauri ataonyeshakukosa heshima kwa madaraka aliyonayoMeya au kudharau Kanuni za Kudumu zaHalmashauri kwa kuzuia kwa makusudishughuli za Halmashauri zisiendelee auvinginevyo, Meya ataelekeza Mkutano kwatukio hilo kwa kumtaja jina mtuanayehusika.

22

Page 23: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(2) Endapo baada ya kutajwa jina mjumbeataendelea kudharau madaraka ya Meya,basi Meya ataliomba Baraza kuahirishashughuli za Mkutano na Meya atatafakarijambo hilo na kuagiza yafuatayo;

(a) Mjumbe atolewe nje ya Mkutano,(b) Mjumbe asihudhurie vikao vitatu

mfululizo.(c) Bila kuathiri masharti ya kanuni ya 18

(2) (a) na (b) Mjumbe huyoataendelea kupokea posho ya mweziya udiwani.

(3) Iwapo kutatokea fujo kubwa katika Mkutano

wowote wa Halmashauri, Meya anawezakama ataona ni muhimu kufanya hivyo,kuahirisha Mkutano bila majadiliano auswali, au kusimamisha Mkutano kwa mudaatakaoona unafaa.

Fujozinazosababishwana umma

19

(1) Iwapo mtu yeyote kati ya ummaunaohudhuria Mkutano waHalmashauri atavuruga Mkutano waHalmashauri, Meya atamuonya mtuhuyo aache kufanya hivyo. Endapomtu huyo ataendelea kuvurugaMkutano, Meya ataamuru mtu huyoatolewe kwenye chumba chaMkutano.

(2) Endapo kutakuwa na vurugu katikasehemu yoyote ya chumba chaMkutano kinachotumika na umma,Meya ataamuru kuondolewa kwa watuwote walio katika eneo hilo.

Hoja namarekebisho ya hoja

20

(1) Taarifa ya kila hoja, isipokuwa hojailiyowasilishwa chini ya Kanuni ya 21,itawasilishwa kwa maandishi yaliyowekwasaini na Diwani au Madiwani waliotoa

23

Page 24: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

taarifa, na itapelekwa kwa Mkurugenziangalau siku nne kabla ya Mkutano waHalmashauri unaofuata na akishaipokea,Mkurugenzi atagonga tarehe na kuipanamba na kuiingiza kwenye daftari kadrihoja zilivyowasilishwa, na daftari hiyoitakuwa wazi kukaguliwa na Mjumbe yeyotewa Halmashauri.

(2) Mkurugenzi ataonyesha katika taarifa yakila Mkutano wa Halmashauri hojazilizowasilishwa na kwa kadrizilivyopokelewa isipokuwa kama Diwanialiyetoa hoja hiyo ameeleza kwa maandishiwakati alipoleta hoja hiyo, kwamba anatakakuitoa katika Mkutano utakaofanyikabaadaye, au baada ya kuwasilisha ameifutahoja hiyo kwa maandishi.

(3) Iwapo hoja ambayo imeonyeshwa katikataarifa ya Mkutano haiwezi kutolewa naMjumbe aliyewasilisha taarifa; au naMjumbe mwingine yeyote kwa niaba yake,basi hoja hiyo, isipokuwa kamaimeahirishwa kwa idhini ya Halmashauri,itachukuliwa kama imeondolewa nahaitawasilishwa tena bila ya kutoa taarifaupya.

(4) Iwapo hoja itahusu jambo linalohusu Kamatiau Kamati mbalimbali baada yakupendekezwa na kuungwa mkono, hojahiyo itapelekwa bila majadiliano kwenyeKamati ambayo Halmashauri itaelekeza iliiweze kufikiriwa na kutayarishiwa taarifa.

(5) Ni lazima kila hoja ihusu jambo ambaloHalmashauri ina uwezo na wajibu nalo, auiwe inahusu Halmashauri ya husika.

(6) Marekebisho ya hoja yaliyopendekezwa nakuungwa mkono yanaweza kuondolewa tu

24

Page 25: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

kwa ridhaa ya Wajumbe wa Halmashauriwalio wengi waliopo katika Mkutano.

(7) Marekebisho ya hoja yanapokuwayamethibitishwa, hoja ya msingi kamailivyorekebishwa itatolewa na Meya kamandiyo hoja ya msingi ambayo nayo inawezakufanyiwa marekebisho. Kama marekebishoya hoja hayakukubaliwa, rekebisho linginelinaweza kupendekezwa.

(8) Kwa idhini ya Meya, zaidi ya rekebisho mojalinaweza kutolewa kwa wakati mmoja mbeleya Mkutano wa Halmashauri, lakini kilarekebisho la namna hii litatolewa mojabaada ya jingine kufuatana na jinsimapendekezo hayo yalivyotolewa.

(9) Rekebisho halitachukuliwa kuwa sahihikama litakuwa sawa na kuikataa hoja mojakwa moja au kama si rekebisho la hoja yamsingi linalokusudiwa kurekebisha.

(10)

Rekebisho ambalo halikutolewa taarifa,halitapendekezwa baada ya mjadala wahoja inayozungumzwa kuendelea kwa nususaa, ila kwa mujibu wa sharti hili, taarifa yaidadi yoyote ya marekebisho inawezakutolewa.

(11)

Hoja ya kufuta azimio itapitishwa naWajumbe wasiopungua theluthi mbili yaWajumbe wote.

(12)

Hoja ya kuzingatia taarifa ya Kamati aukuidhinisha majadiliano au mapendekezo yaKamati inaweza kutolewa na Mwenyekiti waKamati husika, au na Mjumbe yeyote waKamati husika kwa niaba yake.

(13)

Mjumbe yeyote ambaye hajachangia katikamjadala wa hoja, au hajaitolea

25

Page 26: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

marekebisho, anaweza kupendekeza“kwamba Halmashauri iendelee na shughuliinayofuata”. Hoja ya aina hiyo inaweza tukuzingatiwa baada ya hoja kupendekezwana kuungwa mkono. Hoja inapotolewa,itaamuliwa bila marekebisho au mjadala, nakama ikikubaliwa, shughuli iliyokatizwa naazimio hilo haitaendelea kujadiliwa katikakikao hicho. Hoja ya kupendekezakuendelea na shughuli inayofuatahaitatolewa zaidi ya mara moja katikamjadala wa jambo lolote.

(14)

Baada ya mjadala kuhusu hoja kuendeleakwa muda usiopungua nusu saa, Mjumbeambaye hajachangia katika majadilianoanaweza kuomba idhini ya kutoa hoja“kwamba suala lililo mbele yetu sasaliamuliwe” na kama idhini hiyo itatolewakwa kukubaliwa na si chini ya Wajumbewatano, hoja “kwamba suala lililo mbeleyetu sasa liamuliwe” itawasilishwa maramoja, na kama ikiafikiwa, mtoa hoja yamsingi anaweza kuzungumza kwa dakikazisizozidi tano, na baada ya hapo swali aumaswali yaliyo mbele ya Halmashauriyatafanyiwa uamuzi.

(15)

Hoja “kwamba suala lililo mbele yetu sasaliamuliwe” haitatolewa zaidi ya mara mojakatika mjadala unaoendelea kuhusu jambololote mpaka hapo mjadala utakapokuwaumeendelea kwa angalau nusu saa tangukuwekwa mbele ya Mkutano hoja ya ainahiyo ilipopendekezwa awali.

Hojazinazowezakutolewabilataarifa

21

Hoja zifuatazo zinaweza kutolewa bilataarifa.

(a) Kumchagua Mwenyekiti wa Mkutanoambamo hoja imetolewa.

(b) Hoja kuhusu usahihi wa muhtasari,kufunga Mkutano, kuahirisha

26

Page 27: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Mkutano, utaratibu wa Mkutano, ausuala linalofuata.

(c) Kuteua Kamati au Wajumbe waKamati, au wawakilishi katika taasisiza nje, unaotokana na jambolililotaarifiwa katika wito wa Mkutano.

(d) Kukubali taarifa na mapendekezo yaKamati na maazimio yoteyanayotokana na taarifa aumapendekezo hayo;

(e) Kwamba idhini itatolewa kuiondoahoja.

(f) Kusahihisha hoja.(g) Kuongeza muda wa hotuba.(h) Kuwa, jambo lililotajwa katika taarifa

ya kuitisha Mkutano litangulie.(i) Kusimamisha Kanuni za kudumu;(j) Kwamba Mjumbe asisikilizwe tena au

aondoke katika Mkutano.(k) Kumwomba Mjumbe abakie

Mkutanoni, na(l) Kutoa idhini ya Halmashauri pale

ambapo idhini inatakiwa kwa mujibuwa Kanuni za kudumu hizi.

Haki yakujibu

22

(1) Mtoa hoja atakuwa na haki ya kujibumaswali wakati wa kufunga mjadala juu yahoja; kabla ya hoja kupigiwa kura au kablaya hoja kutolewa “kwamba kikaokiahirishwe,

(2) Mjumbe anayetumia haki yake ya kujibuhataanzisha hoja nyingine mpya,

(3) Baada ya kutolewa kwa jibu ambalolinahusiana na Kanuni hizi, uamuzi utafikiwabila majadiliano zaidi.

Maswali 23

(1) Mjumbe anaweza kumuuliza Mwenyekiti waKamati swali lolote kuhusu muhtasari waKamati uliofikishwa mbele ya Halmashauri,

(2) Kila swali litaulizwa na kujibiwa bila

27

Page 28: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

majadiliano,

(3) Swali au maswali yatajibiwa na Mwenyekitiwa Kamati mara moja, na Mjumbeanayeuliza maswali hayo hatanyimwa hakiyake ya kujadili hoja ambayo maswali hayoyanarejewa au kutoa hoja ya marekebisho,

(4) Pale ambapo swali la maandishilimeelekezwa kwa Mwenyekiti wa Kamati,au Mkutano na taarifa inayotakiwa imokatika mojawapo ya mihtasari yaHalmashauri, kuonyesha sehemu yamuhtasari ambapo habari hiyoimeonyeshwa, kutachukuliwa ni jibu lakutosha.

Maswaliya papokwa papo’

24

(1) Halmashauri itatenga muda wa angalaudakika thelathini katika kila Mkutano waKawaida wa Halmashauri ambapo Meya naMkurugenzi wa Halmashauri watajibumaswali ya papo kwa papo kutoka kwaWajumbe kabla ya kuanza kwa shughuli yakawaida za Mkutano wa Halmashauri.

(2) Wajumbe ambao watataka kuuliza maswaliya papo kwa papo kwa Meya na Mkurugenziwatatakiwa kujiorodhesha kwanza kwaMeya angalau masaa ishirini na nne (24)kabla ya Mkutano wa Halmashauri kuanza.

(3) Mjumbe yoyote ambaye hatajiorodheshakwa Meya ndani ya masaa ishirini na nneatahesabika kuwa amechelewa nahataruhusiwa kumuuliza Mkurugenzi auMwenyekiti swali la papo kwa papo.

(4) Kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali yapapo kwa papo Mwenyekiti au Meya atatajamajina ya Wajumbe waliojiorodheshakuuliza maswali ya papo kwa papo na idadiya maswali,

28

Page 29: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(5) Meya ataweka utaratibu ambao ataonaunafaa na kuridhiwa na Wajumbe wa namnabora ya kuendesha kipindi cha swali la papokwa papo.

(6) Mjumbe hataruhusiwa kuuliza zaidi ya swalimoja la papo kwa papo.

(7) Maeneo ya muhimu ambayo Wajumbewatatakiwa kuuliza maswali ya papo kwapapo:-

(a) Uendeshaji wa jumla wa Halmashauri;(b) Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo;(c) Mipango ya kimkakati ya Halmashauri

kuwaondolea wananchi umaskini;(d) Mipango ya baadaye ya maendeleo

ya Halmashauri;(e) Usimamizi na utekelezaji wa Mipango

na Bajeti kwa mwaka husika;(f) Utoaji wa huduma za jamii kama vile

elimu, afya, maji, barabara namadaraja;

(g) Hifadhi ya mazingira na utunzaji wavyanzo vya maji;

(h) Usalama wa Chakula, Raia na Malizao;

(i) Utawala Bora na utatuzi wa kero zawananchi.

(8) Baada ya kujibiwa kwa swali, Mjumbealiyeuliza swali atapewa fursa ya kuulizaswali moja tu la ufafanuzi na maswaliyatajibiwa bila mjadala.

(9) Meya atakuwa na uwezo wa kuruhusu aukukataa swali lolote la papo kwa papoambalo litaonekana linahitaji takwimu auutafiti zaidi au swali ambalo linalengakumdhalilisha Meya au mjumbe yeyote waBaraza na uamuzi wake utakuwa wamwisho.

29

Page 30: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(10)

Mara baada ya muda wa nusu saakumalizika, kipindi cha maswali ya papokwa papo kitamalizika na kuruhusu shughulizingine za kikao kuendelea.

Taarifa zaKamati

25

(1) Kila Kamati au Kamati ya pamojailiyoteuliwa chini ya Kanuni hizi itatoa,katika mojawapo ya vikao viwili vyaHalmashauri iliyoteua Kamati, Kamati yapamoja au Kamati Ndogo, taarifa yamajadiliano yanayohusiana na utekelezajimajukumu iliyokasimiwa, kwa ujulisho waHalmashauri.

(2) Muhtasari wa Kamati unaohitaji idhini yaHalmashauri, na taarifa zozotezinazohusiana na muhtasari huo, na ambazozinaonekana kwa Kamati kuwa zinastahili,zitapelekwa kwa kila Mjumbe waHalmashauri angalau siku saba kabla yaMkutano wa Halmashauri ambamoutafikiriwa.

(3) Mwenyekiti wa Kamati, au Mjumbemwingine wa Kamati kwa niaba yake,wakati wa kupendekeza kuidhinishwa kwamuhtasari wa Kamati, anaweza kusemakuwa hakusudii kuwasilisha kipengele auvipengele fulani vya muhtasari huo kwalengo la kupata idhini ya Halmashauri.Katika hali hiyo Mjumbe yeyote hatawezakukizungumzia kipengele au vipengelehivyo na muhtasari utawasilishwa bilavipengele hivyo. Kuondolewa kwa kipengelecha aina hiyo kutatolewa taarifa kwenyeMkutano unaofuata.

(4) Taarifa ya Kamati inapokuwa imepokelewana Halmashauri itamaanisha kuwa hatuazilizochukuliwa na Kamati husikazimekubaliwa na mapendekezo yaliyokwenye taarifa hiyo yatatekelezwa nakwamba Mkurugenzi atakuwa ameelekezwa

30

Page 31: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

ipasavyo.Taarifa zakutokakwenyeKata

26

(1) Kila Kata itatakiwa kuwasilisha taarifa zautekelezaji katika Mkutano wa Halmashauriulioitishwa chini ya Kanuni ya 3(1) yaKanuni hizi;

(2) Taarifa za utekelezaji kutoka katika Katazitawasilishwa na Diwani wa Kata husika, aukama diwani hayupo, taarifa hiyoitawasilishwa na Diwani wa Viti Maalumanayeishi katika Kata hiyo na kama DiwaniViti Maalum hayupo, Meya atamtaarifumapema Diwani yeyote ili ajiandaekuwasilisha taarifa hiyo;

(3) Kutakuwa na aina tatu za taarifazitakazowasilishwa:-(a) Taarifa ya utekelezaji wa miradi ya

maendeleo katika Kata ambayoitajumuisha ujenzi wa Madarasa,Nyumba za Walimu, Matundu ya Vyoo,Maabara, Viwanja vya Michezo, Vituovya Afya, Zahanati, Madaraja,Barabara, Mashamba darasa, Ofisi zaVijiji, Mitaa, Kata na Tarafa; Idadi yawatu na vizazi

(b)Taarifa zinazohusu hali ya Kata ambazozitajumuisha-

(i) Maendeleo ya Elimu katika Katakuhusiana na uandikishaji wawatoto wenye umri wa kwendashule, ufundishaji, utoro, hali yamahudhurio, mimba mashuleni,ukaguzi na uratibu wa shule.

(ii) Hali ya majanga kama vilemagonjwa ya mlipuko, mafuriko,njaa, na hali ya uhalifu na vifo.

(iii) Maendeleo ya Kilimo, mifugo

31

Page 32: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

na uvuvi ambayo itajumuishaupatikanaji wa wataalamu, zanaza kisasa na pembejeo zakilimo, mifugo na uvuvi.

(iv) Uimarishaji wa dhana yauzalendo na utaifa kwakuhamasisha vijana kuanzishana kujiunga na vikundi vyaVijana Wagani kazi na mafunzoya Jeshi la Mgambo, Ulinzishirikishi na Polisi jamii.

(c) Taarifa ya utekelezaji wa miradi yaMaendeleo na taarifa ya hali ya Katasharti ijumuishe pia taarifa zashughuli za kiuchumi, taarifa yamavuno ya mazao ya chakula nabiashara pamoja na taarifa yautunzaji wa mazingira na vyanzo vyamaji.

(4) Mkurugenzi wa Halmashauri atahakikishataarifa kutoka kwenye Kata, zinaandaliwana kuwasilishwa na Diwani wa Kata hiyokwenye Baraza la Madiwani ili ipitiwe nakuchambuliwa kwa nia ya kupata hojazitakazowasilishwa katika Vikao vya Kamatihusika na kutoa mrejesho.

Mafanikionachangamo-to

(5) Mwasilishaji wa taarifa atatakiwa kuelezeamafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza na mbinu za kukabiliana nazo.

(6) Mbinu za kukabiliana na changamoto shartiziwekewe malengo na muda maalum wakuzitatua.

(7) Taarifa za mapokeo ya fedha na matumiziyake zitakazokuwa zimeandaliwa na AfisaMtendaji wa Kata, zitawasilishwa sanjari namiradi iliyotekelezwa na gharama zake.

32

Page 33: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(8) Baada ya taarifa kutoka kwenye Katakupokelewa na Halmashauri, itamaanishakuwa taarifa hizo zimeidhinishwa namapendekezo yaliyomo kwenye taarifayatatekelezwa na Halmashauri, na Katakupewa taarifa ya utekelezaji wa majukumuhayo.

Uhuru wakutoamawazowakatiwamajadiliano

27

Kutakuwepo na uhuru wa kutoa mawazowakati wa majadiliano katika Mikutano yaHalmashauri na uhuru huo hautawezakuhojiwa katika mahakama yoyote aumahali popote nje ya Mkutano waHalmashauri.

Kaulizenyekashfa

28

(1) Inapotokea, kulingana na maoni yaMwenyekiti au mtu yeyote anayeongozaMkutano, kuwa kauli iliyotolewa na Mjumbeinamkashifu mtu yeyote, Mwenyekitiatamtaka Mjumbe aliyetoa kauli hiyo kufutakauli yake na kumwomba msamaha mtualiyekashifiwa kwa maandishi ndani yamuda wa siku saba tangu kauli hiyo yakashfa ilipotamkwa.

(2) Endapo Mjumbe aliyetoa kauli za kashfaatakataa kufuta kauli yake na kuombamsamaha kwa maandishi kamainavyoelekezwa katika Kanuni Ndogo (1) yaKanuni hii. Meya wa Mkutano,atamsimamisha Mjumbe huyo kuhudhuriavikao vitatu mfululizo vya Halmashauri.

(3) Mjumbe aliyesimamishwa kwa mujibu wakanuni Ndogo(2) ya Kanuni hii atapotezahaki zake zote ikiwa ni pamoja naposho,nauli na upendeleo na kinga kwamuda wote wa kusimamishwa kwake;

Maamuziya

29

(1) Masuala yote yaliyojadiliwa na kupendekezakatika Mkutano wowote wa Halmashauri

33

Page 34: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

MikutanoyaHalmashauri

yataamuliwa kulingana na wingi wa kura zaWajumbe waliohudhuria Mkutano huo, naikitokea kura za Wajumbe zikalingana, basiMeya au Mjumbe yeyote mwingineanayeongoza Mkutano, atapiga kura yaturufu mbali ya kura ya kawaida.

(2) Iwapo suala linalopigiwa kura linahusukutokuwa na imani au kumwondoa Meyamadarakani, au jambo lolote lingine kamaitakavyoamuliwa na Halmashauri, kurazitapigwa kwa siri.

MwalikokwawasiokuwaWajumbekushirikinakuzungumzakwenyevikao vyaHalmashauri

30

(1) Meya, baada yakushauriana na Wajumbe,anaweza kumwalika mtu yeyote kuhudhuriana kuzungumzia jambo lolote, au kushirikikwa njia yoyote, katika Mkutano wowote waHalmashauri lakini mwalikwa huyohatakuwa na haki ya kupiga kura katikaMkutanohuo.

(2) Wakuu wa Idara za Halmashauri na MaafisaTarafa wanapaswa kuhudhuria Mikutanoyote ya Halmashauri lakini hawatakuwa nahaki ya kupiga kura katika Mikutano hiyo.

Mihtasariya KamatiyaMaendeleo yaKata,Mitaa/Vijiji

31

Mkurugenzi wa Halmashauri atahakikishamihtasari yote ya Kamati za Maendeleo zaKata, na Mikutano Mikuu ya Mitaa inapitiwana kuchambuliwa kwa nia ya kupata hojazitakazowasilishwa katika vikao vya Kamatihusika na kutoa mrejesho inavyopaswa.

MihtasariyaHalmashaurikupelekwa kwaMkuu waWilaya naMkuu wa

32

(1) Mihtasari ya Halmashauri itatolewa nakupelekwa kwa taarifa, kwa Mkuu wa Wilayana Mkuu wa Mkoa ambamo Halmashauriimo katika muda wa siku 7 baada yakuthibitishwa kwa mihutasari hiyo.

34

Page 35: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Mkoa(2) Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa

wanaweza kupewa, wakiomba, nakala yamihutasari au sehemu ya mihtasari yaKamati za Kudumu na Kamati nyingine.

(3) Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoahawatabadilisha au kubatilisha au kuagizakubadilisha au kubatilisha uamuzi waHalmashauri.

Hojakuhusumatumizi

33

Hoja yoyote isiyotokana na mapendekezoau taarifa ya Kamati ya Fedha na Utawala,na ambayo, kama ikikubaliwa, itaongezamatumizi au kupunguza mapato yaliyo chiniya usimamizi wa Kamati yoyote, auitasababisha matumizi ya Kamati yaKudumu, baada ya kupendekezwa aukuungwa mkono, itaahirishwa bilamajadiliano mpaka Mkutano wa kawaida waHalmashauri unaofuata, na Kamati yoyoteinayohusika na hoja hiyo itafikiria iwapoingependa kutoa taarifa kuhusu athari zakifedha za pendekezo hilo.

Kupokelewa kwataarifa zaKamati

34

(1) Taarifa ya Kamati inapowasilishwa kwenyeHalmashauri, hoja itakuwa “kwamba taarifaipokelewe”na baada ya kukubaliwa naWajumbe taarifa itaanza kujadiliwakipengele kimoja baada ya kingine.

(2) Mapendekezo yoyote yaliyomo katikataarifa hiyo yatapigiwa kura iwapo Mjumbeyeyote atapenda iwe hivyo. Baada ya hapotaarifa nzima itawasilishwa mbele yaMkutano kwa kupokelewa ikiwa na au bilamarekebisho.

Kuidhinishwa kwataarifa yaKamati

35

Taarifa ya Kamati inapokuwa imepokelewana Halmashauri itamaanisha kuwa hatuazilizochukuliwa na Kamati iliyowasilishataarifa hiyo zimeidhinisha na mapendekezo

35

Page 36: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

yaliyo kwenye taarifa yatatekelezwa nakwamba Mkurugenzi wa Halmashauriatakuwa ameelekezwa kama inavyotakiwa.

Uhalali wamajadiliano yaHalmashauri

36

Uhalali wa majadiliano kwenye Halmashaurihautaathiriwa na nafasi yoyote wazi yaMjumbe, dosari zozote zilizo katika uchaguziau uteuzi wa Wajumbe wa Kamati au zile zamaafisa wake.

Uwezo waHalmashaurikujigeuzakuwaKamati yaHalmashauri nzima

37

Halmashauri inaweza kujigeuza kuwaKamati ya Halmashauri, na mara baada yakujigeuza, taratibu za kuendesha vikao vyaKamati za Kudumu zitatumika.

HojazinazohusuWatumishi waHalmashauri

38

Kama litajitokeza jambo lolote katika kikaocha Halmashauri linalomhusu Mtumishiyeyote wa Halmashauri kuhusu Uteuzi,kupandishwa cheo, kufukuzwa kazi,mishahara, mazingira ya kazi au utendajikazi kwa jumla wake, jambo hilo litajadiliwakatika Kamati ya Halmashauri nzima.

KushirikikwaUmma

39

(1) Mtu yeyote ambaye ni mkazi katika eneo laHalmashauri anaweza kuhudhuria kikao chaHalmashauri kwa nia ya kuwasilisha hojambele ya Halmashauri, baada ya kutoataarifa kwa maandishi kwa Mkurugenzi, naMkurugenzi akamkubali kufanya hivyo.

(2) Mtu yeyote ambaye ni mkazi katika eneo laHalmashauri anaweza kualikwa kuhudhuriakikao cha Kamati au Kamati Ndogo kablauamuzi haujafanyika kuhusu masualaambayo ana maoni mahsusi.

Uahirishajiwa vikao

40

(1) Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni Ndogoya (2) ya Kanuni 18 na Kanuni Ndogo ya 2ya Kanuni hii, Halmashauri haitaahirisha

36

Page 37: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Mkutano wake hadi dondoo zote za agendaya Mkutano huo zitakapojadiliwa nakutolewa uamuzi.

(2) Pale ambapo katika Mkutano wowote waHalmashauri akidi haikutimia, Wajumbewaliopo wataahirisha Mkutano na utaratibuwa kuitisha Mkutano mwingine utafanyikakwa kuzingatia maelekezo ya Kanuni hizi.

37

Page 38: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

SEHEMU YA IVKAMATI

Kamati zaKudumu

41 (1)

Halmashauri katika Mkutano wake wa mwakaitateua Wajumbe wa Kamati za Kudumuzifuatazo ambazo zitakuwa na idadi yaWajumbe (ukimwondoa Meya au Mwenyekitiwa Halmashauri isipokuwa katika Kamati yaFedha na Utawala) kama inavyoonyesha hapachini au kama itakavyorekebishwa naHalmashauri mara kwa mara. Isipokuwa katikakuteua Wajumbe wa Kamati ya Fedha naUtawala, Meya na Mkurugenzi watazingatiauwiano wa uwakilishi wa vyama katikaHalmashauri.

Kamati Idadi ya Wajumbe

Akidi

(a) Kamati ya Fedha na Utawala

7 4

(b)Kamati yaUchumi, Afyana Elimu.

7 4

(c)Kamati yaMipango Mijina Mazingira.

8 4

(d)Kamati yaMaadili yaMadiwani

4 2

(e) Kamati yaUKIMWI

8 4

(2)

Kila Mjumbe wa Halmashauri atakuwa Mjumbewa angalau Kamati moja ya Kudumu. Kamatiya Fedha na Utawala itakuwa na Wajumbewafuatao;

(a) Meya ambaye atakuwa Mwenyekiti.(b) Naibu Meya.(c) Mbunge au Wabunge wa Majimbo

38

Page 39: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

wanaowakilisha Majimbo katika eneo laHalmashauri.

(d) Wenyeviti wa Kamati za Kudumu zaHalmashauri.

(e) Wajumbe wengine wasiozidi wawili (2)watakaopendekezwa na Mwenyekiti auMeya na kupigiwa kura na Baraza laHalmashauri mmoja kati yao awemwanamke.

(3)

Halmashauri yenye Madiwani wasiozidi ishirini(20), idadi ya wajumbe wa Kamati wa Fedhaitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye Kanuniya 41(2) ya Kanuni hizi.

(4)

Bila kuathiri masharti ya Kanuni Ndogo ya (2)ya Kanuni hii, Halmashauri yenye idadi yaMadiwani wanaozidi ishirini (20) na wasiozidithelathini na tano (35) Wajumbe wa Kamati yaFedha watakuwa kama ilivyoonyeshwakwenye Kanuni ya 41(2) pamoja na wajumbewengine wawili (2) watakaotokana na orodhaitakayopendekezwa na Mwenyekiti au Meyana kupigiwa kura na Baraza la Halmashaurimmoja kati yao awe wanawake.

(5)

Bila kuathiri masharti ya Kanuni Ndogo ya (2)(3) na (4) ya Kanuni hii, Halmashauri yenyeidadi ya Madiwani wanaozidi thelathini natano(35) na zaidi Wajumbe wa Kamati yaFedha watakuwa kama ilivyoonyeshwakwenye Kanuni ya 41(2) pamoja na wajumbewengine wanne(4) watakaotokana na orodhaitakayopendekezwa na Mwenyekiti au Meyana kupigiwa kura na Baraza la Halmashauriwawili kati yao wawe wanawake.

(5)

Wajumbe wa Kamati za Kudumu watashikanyadhifa zao kwa muda wa mwaka mmoja nawataendelea kushika nyadhifa hizo mpakaMkutano wa mwaka wa Halmashauriunaofuata. Isipokuwa Wajumbe

39

Page 40: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

waliochaguliwa kwenye Mkutano wa kwanzabaada Uchaguzi Mkuu watashika nyadhifa zaokwa muda uliobaki kumaliza Mwaka wa Fedhaambapo Uchaguzi utafanyika tena.

(6)

Halmashauri inaweza wakati wowote kuvunjana kuunda upya Kamati ya Kudumuiliyoteuliwa kwa mujibu wa Kanuni hii yakudumu, endapo kufanya hivyo kutakuwa nikwa manufaa ya Halmashauri.

(7)

Hakuna Halmashauri itakayounda Kamati yaKudumu mpya zaidi ya Kamati zilizotajwakwenye Kanuni ya 41(1) hapo juu, isipokuwabaada ya kuomba na kupata idhini yamaandishi kutoka kwa Waziri.

(8) Maombi ya Halmashauri ya kuanzisha Kamatimpya ya Kudumu lazima yakidhi na yawe namaelezo yafuatayo;

(a) Upekee wa majukumu yanayoombewakuundwa kwa Kamati ya Kudumu mp yana majukumu hayo yawe ambayohayawezi kutekelezwa na Kamati zaKudumu zilizopo na zilizotajwa kwenyeKanuni ya 41(1) hapo juu,

(b) Gharama za uendeshaji wa Kamati hiyokwa mwaka,

(c) Kuundwa kwa Kamati ya Kudumu hiyompya ni hitaji la lazima na nikipaumbele cha Halmashauri na jamiikwa ujumla.

(9)

Kamati yoyote itakayoundwa na Halmashauribila idhini ya Waziri itakuwa batili na maamuziyake yote yatakua batili.

MeyakuwaMjumbewa Kamatimoja

42 Meya atakuwa Mjumbe wa Kamati zote zakudumu za Halmashauri.

40

Page 41: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Uwezo waKamati

43 Kamati zote za Halmashauri zitawasilishataarifa zao kwa Halmashauri, na hakuna hatuaitakayochukuliwa kutekeleza uamuzi wowotewa Kamati yoyote mpaka hapo taarifa yaKamati husika itakapokuwa imekubaliwa naHalmashauri, isipokuwa pale ambapo idhini yakuchukua hatua imekasimiwa kwa Kamati.

Kamati zapamoja

44 (1)

Halmashauri inaweza kukubaliana naHalmashauri nyingine kuteua Kamati yapamoja kutokana na Wajumbe wao kwamadhumuni yoyote yale ambayo wanamaslahi ya pamoja, na Halmashauri hizozinaweza kukasimu kwa Kamati hiyo yapamoja, kutegemea na masharti na mipakazitakazoweka kama watakavyoona inafaa,madaraka au kazi ya Halmashaurizinazohusiana na madhumuni yaliyozifanyaziunde Kamati hiyo, isipokuwa shughuli zileambazo Halmashauri haziruhusiwi kukasimu.

(2)

Muundo na muda wa kazi wa Wajumbe wakena mipaka ya eneo ambamo Kamati hiyo yapamoja itafanya kazi, itapangwa naHalmashauri zinazoiteua.

(3)

Kamati ya pamoja haitaingia katika gharamazozote zaidi ya zile ambazo zimeidhishwa namamlaka iliyoteua Kamati hiyo.

KukasimumadarakakwenyeKamati

45 (1)

Kufuatana na Kanuni Ndogo ya (2) ya Kanunihii pamoja na masharti mengine ambayoHalmashauri itaona inafaa, Halmashauriinaweza kukasimu kwa Kamati uwezo wakutekeleza kazi yoyote kwa niaba yake.

(2)

Halmashauri haitakasimu kwa Kamati yoyoteuwezo wa:-

(a) Kutunga Sheria Ndogo;(b) Kuweka na kutoza kodi;(c) Kuidhinisha makadirio ya mapato na

matumizi ya Halmashauri;

41

Page 42: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(d) Kutoza ada na ushuru;(e) Kuidhinisha mpango na Bajeti ya

Halmashauri;(f) Kuingia mikataba mbalimbali ikiwa ni

pamoja na mikataba ya kukopa,(g) Kupitisha mpango wa utoaji huduma.

(3)

Kazi za kila Kamati ya Kudumu yaHalmashauri ni kama zilivyoonyeshwa katikajedwali la kwanza la Kanuni za kudumu hizi.

(4)

Halmashauri inaweza kusitisha au kurekebishauamuzi wa kukasimu madaraka yoyote kwaKamati, lakini usitishaji au urekebishaji huohautaathiri jambo lolote lililofanywa kutokanana uamuzi wowote uliochukuliwa kihalali naKamati.

(5)

Shughuli yoyote iliyotekelezwa na Kamatikutokana na kukasimiwa kwa mujibu waKanuni hii itatambuliwa kuwa imefanywa aukutekelezwa na Halmashauri.

KamatiNdogo

46 (1)

Kamati yoyote au Kamati ya pamoja inawezakuteua Kamati Ndogo kutokana na Wajumbewake kadri itakavyoona inafaa kwa ajili yakuchunguza na kutoa taarifa kuhusu jambololote, lakini Kamati haitakasimu madarakayake ya kiutendaji kwa Kamati Ndogo yoyote.

(2)

Idadi ya Wajumbe wa Kamati Ndogo pamojana muda watakaotumikia vitaamuliwa naKamati iliyoteua Kamati Ndogo hiyo.

(3)

Mwenyekiti wa Kamati atakuwa Mjumbe waKamati Ndogo yoyote kwa mujibu wa wadhifawake isipokuwa kama atamfahamishaMkurugenzi kwa maandishi kuwa hatakuwaMjumbe wa Kamati hiyo.

(4)

Kila Kamati Ndogo inaweza kumteua mmojawa Wajumbe wake kuwa Mwenyekiti wa

42

Page 43: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Kamati Ndogo husika.

Mikutanoya Kamati

47 (1)

Mkutano wa kwanza wa Kamati utaitishwa naMkurugenzi ndani ya mwezi mmoja baada yaKamati kuteuliwa na baada ya hapo kulinganana ratiba ya Mikutano kamaitakavyoidhinishwa na Halmashauri.

(2)

Taarifa ya angalau saa ishirini na nne yenyeajenda za kikao itabidi kutolewa kwa Wajumbekabla ya Mkutano wa Kamati.

(3)

Idadi ya Kamati haitazidi idadi ambayoitawekwa na Waziri kutokana na uwezoaliopewa chini ya kifungu cha 75(3) chaSheria.

Mwenyekiti waKamati

48 (1)

Katika kikao chake cha kwanza baada yaMkutano wa mwaka wa Halmashauri na kablaya kuendelea na shughuli yoyote nyingine,kila Kamati itamchagua Mwenyekiti wa Kamatikwa mwaka unaohusika.

(2)

Mwenyekiti wa Kamati, isipokuwa Kamati yaFedha na Utawala, atachaguliwa kwa kura yasiri ya Wajumbe walio wengi kwa kupiga kuraya siri kwenye eneo la faragha litakalotengwana Mkurugenzi kwa ajili hiyo.

(3)

Meya atakuwa pia Mwenyekiti wa Kamati yaFedha na Utawala.

(4)

Endapo nafasi ya Mwenyekiti wa Kamatiitakuwa wazi katika kipindi cha mwaka husika,Mkurugenzi atatoa taarifa kwa Wajumbe wotewa Kamati kuwa katika kikao kijacho chakawaida cha Kamati husika dondoo yakumchagua Mwenyekiti wa Kamati kwa kipindicha mwaka kilichosalia itakuwa ya kwanzakatika agenda.

Mkutano 49 (1 Mkutano Maalum wa Kamati utaitishwa baada

43

Page 44: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

maalumwa Kamati

) ya theluthi mbili ya Wajumbe wa Kamatikuomba kwa maandishi kuwa Mkutano huoufanyike na kueleza sababu.

(2)

Taarifa ya Mkutano Maalum wa Kamatiitaonyesha shughuli itakayofanyika katikaMkutano huo Maalum huo na hakuna jambojingine lolote litakalojadiliwa katika Mkutanohuo.

Ajenda zaKamati

50 Mjumbe wa Kamati atakuwa na haki ya hojazake kuwekwa katika ajenda ya Kamati kamaatatoa taarifa ya angalau siku nne kabla yatarehe ya kikao.

Mahudhurio katikaMikutanoya Kamati

51 (1)

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu au KamatiNdogo, ambaye ameshindwa kuhudhuriaMkutano wa Kamati Ndogo, hataruhusiwakutuma mtu mwingine kumwakilisha kwenyeMkutano wa Kamati au Kamati Ndogo.

(2)

Mjumbe wa Halmashauri hatakuwa na haki yakuhudhuria kikao chochote cha Kamati auKamati Ndogo ambamo yeye si Mjumbe,isipokuwa kama Kamati au Kamati Ndogoinayohusika imemwalika kuhudhuria, na hatahivyo hatakuwa na haki ya kupiga kura aukudai posho kwa kuhudhuria Mkutano huo waKamati au Kamati Ndogo.

MjengahojakualikwakwenyeMkutanowa Kamati

52 Mjumbe wa Halmashauri anayewasilisha hojaambayo imepelekwa kwenye Kamati atapewataarifa ya Mkutano wa Kamati ambamo hojayake imepagwa kuzungumzwa na kamaatahudhuria atapewa nafasi ya kuizungumzia.

WaalikwawasiokuwaWajumbekuhudhuria nakushirikikatikaMikutanoya Kamati

53 Mwenyekiti wa Kamati, Kamati ya pamoja auKamati Ndogo baada ya kushauriana naWajumbe wa Kamati, Kamati ya pamoja naKamati Ndogo, anaweza kumwalika mtuyeyote kuhudhuria na kuzungumza kwenyeMkutano kuhusu suala lolote au kushiriki kwanamna yoyote kwenye kikao cha Kamati,lakini mtu huyo atakayealikwa hatakuwa nahaki ya kupiga kura kwenye Mkutano huo.

44

Page 45: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Mahudhurio yaumma navyombovya habarikwenyeMikutanoya Kamatina KamatiNdogo

54 Majadiliano katika Kamati, Kamati ya pamojaau Kamati Ndogo hayatakuwa wazi kwa ummana vyombo vya habari, isipokuwa kwakutokana na azimio la Halmashaurilinaloruhusu kuwa umma na vyombo vyahabari vihudhurie.

Athari zanafasiwazikwenyeKamati

55 (1)

Kunapotokea nafasi wazi kwenye Kamati,Kamati ya pamoja au Kamati Ndogo, Kamatiitaendelea kutekeleza shughuli zake licha yakuwepo kwa nafasi wazi hiyo au hizo aumpaka nafasi hiyo au hizo zitakapojazwa kwanjia ya uchaguzi au uteuzi. Mjumbeatakayejaza nafasi hiyo atashika nafasi wazihiyo kwa kipindi kilichosalia cha Mjumbeambaye nafasi yake imekuwa wazi.

(2)

Uhalali wa tendo lolote au maamuzi yaMkutano wowote wa Kamati hautaathiriwakutokana na hitilafu katika uteuzi wa Mjumbealiyeshika nafasi hiyo au nafasi hizo kuachwawazi na Mjumbe, au Wajumbe au Mjumbe auWajumbe kuamua kutoka kwenye kikao kwalengo la kukwamisha jambo linalotakakutolewa maamuzi na Kamati hiyo.

AkidikwenyeMikutanoya Kamati

56 Endapo Wajumbe waliohudhuria Mkutanohawatafikia akidi ya Mkutano, Mkurugenziataahirisha Mkutano huo na kuuitisha tenandani ya siku saba (7) na endapo akidihaitatimia tena, idadi yoyote ya Wajumbewaliohudhuria itatengeneza akidi ya Mkutanoambapo mkutano huo utaendelea na utakuwahalali na Mkurugenzi atamjulisha Wazirikuwepo kwa hali hiyo.

Kanuni zakudumukatikaMikutano

57 (1)

Kanuni ya 17 ya Kanuni hizi za Kudumuitatumika,baada ya kufanya marekebishoyanayostahili, kwenye Mikutano ya Kamati za

45

Page 46: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

ya Kamati Halmashauri.(2)

Mjumbe anapozungumza katika Mkutano waKamati atakuwa ameketi na anawezakuzungumza zaidi ya mara mbili juu ya jambolinalojadiliwa.

UpigajikurakwenyeMikutanoya Kamati

58 Masuala yote yanayoletwa mbele ya Kamatiyataamuliwa kwa wingi wa kura za Wajumbewaliohudhuria na kupiga kura kwenyeMkutano husika. Endapo kunatokea kuramlingano mtu anayeongoza kikao hichoatakuwa na kura ya turufu.

Mihtasariya Kamati

59 (1)

Muhtasari wa kila Kamati, Kamati ya pamojana Kamati Ndogo, utajumuisha majina yaWajumbe waliohudhuria na wasiohudhuria,na utasainiwa kwenye Mkutano unaofuata namtu aliyeongoza Mkutano na muhtasariuliosainiwa hivyo, kama hakuna ushahidi wakuwa una makosa, utapokelewa kwa ushahidibila uthibitisho zaidi.

(2)

Hakuna hoja au mjadala utakaoendeshwakuhusiana na muhtasari wa Kamati isipokuwakuhusu usahihi wa suala lolote linalohusuusahihi litatolewa kwa hoja.

Kufikiriwaupyamaamuzi

60 Pale ambapo suala lililowasilishwalimeamuliwa kwa mujibu wa Kanuni ya 58,suala hilo halitaanza kujadiliwa upya katikaMkutano huo wa Kamati isipokuwa kama hojahiyo inaungwa mkono na theluthi mbili yaWajumbe waliohudhuria na kupiga kura.

Kutunzasiri zamajadiliano yaKamati naKamatiNdogo

61 Mjumbe wa Kamati au Kamati Ndogo hatatoanje jambo lolote lililoletwa au kuzungumzwakwenye Kamati au Kamati Ndogo bila ruhusaya Kamati hiyo, au kuzungumza kwenyeKamati Ndogo mpaka hapo Kamati hiyo auKamati Ndogo hiyo itakapokuwa imetoataarifa kwenye Halmashauri au itakapokuwaimekamilisha utekelezaji wa jambo hilo.

Kujiuzulu 62 Mwenyekiti wa Kamati anaweza kujiuzulu

46

Page 47: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

wadhifawaMwenyekiti waKamati

wadhifa wake kwa kutoa taarifa ya maandishialiyoisaini na kutuma kwa Mkurugenzi.

Kujiuzuluujumbe waKamati nakujazwakwa nafasiiliyowazi

63 (1)

Mjumbe yeyote wa Kamati anaweza kujiuzuluwadhifa wake kwa kutoa taarifa ya maandishialiyoisaini na kuituma kwa Mkurugenzi.

(2)

Nafasi inayotokana na kujiuzulu kwa Mjumbeitajazwa na Halmashauri katika kikao chakecha kawaida baada ya tarehe ya kujiuzulu kwaMjumbe.

SEHEMU YA VUNUNUZI WA VIFAA, UPATIKANAJI WA

HUDUMA NA UJENZI

Taratibuza uagizajiSura ya290

64 (1)

Uagizaji wa mali, huduma na ujenzi katikaHalmashauri utazingatia Kanuni za Manunuzizilizotungwa chini ya kifungu cha 68 chaSheria za Fedha za Serikali za Mitaa,Sura ya290 na Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2011.

(2)

Kutakuwepo na Bodi ya Zabuni ambayoimeanzishwa kwa mujibu wa Kanuni za Bodiya Zabuni (Uanzishwaji na Mwenendo) zaSerikali za Mitaa na ambayo itasimamiashughuli zote za uagizaji katika Halmashauri.

(3)

Muhtasari wa Bodi ya Zabuni utapaswakuwasilishwa kwenye kikao kifuatacho chaHalmashauri baada ya muhtasari huokujadiliwa na kupitishwa kwanza na Kamati yaFedha na Utawala.

Kumbukumbu zamajadilianoyanayohusu uagizaji

65 Bodi ya Zabuni ya Halmashauri itawekakumbukumbu ya majadiliano yanayohusutaratibu za ununuzi zikiwa na angalau taarifazifuatazo:-

(a) Maelezo mafupi kuhusu vitu, ujenzi auhuduma zinazotarajiwa kutolewa na

47

Page 48: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

haja iliyosababisha Bodi kuitishazabuni.

(b) Majina na anuani ya Wazabuniwaliowasilisha zabuni, maelezo kuhususifa au ukosefu wa sifa za wazabuniwaliowasilisha zabuhi zao.

(c) Bei au msingi wa upangaji wa bei namuhtasari wa masharti menginemuhimu ya kila zabuni na ya kilamkataba wa uagizaji wa mali, hudumana ujenzi.

(d) Muhtasari wa tathmini na mlinganishowa zabuni pamoja na upendeleouliokuwepo katika tathmini hiyo.

(e) Kama zabuni zilikataliwa tamko kuhusuuamuzi huo na sababu za uamuzi huo.

(f) Kama utaratibu mwingine wa kupatavitu au huduma mbalimbali ya utaratibuwa zabuni ndio uliotumika, basi tamkokuhusu sababu zilizoifanya Bodi iamuekutumia utaratibu huo mwingine.

(g) Kama zabuni ilikataliwa kwa kuwamzabuni alitoa, alikubali kutoa mojakwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwamoja, kwa mtumishi wa sasa au wazamani wa Halmashauri, bakshishi yaaina yoyote, ahadi ya kumwajiri au kituchochote kinachohusiana na ajira auchenye thamani, kama hamasisho kwautendaji au uamuzi au utaratibu wakutumia, tamko kuhusu jambo hilo.

(h) Katika upataji wa huduma, sababu nahali iliyoifanya Bodi kuchagua utaratibuwa kutumia katika upataji huo wahuduma.

(i) Katika upataji wa vitu au hudumaambao Bodi imeamua kudhibiti ushirikikwa misingi ya Taifa, Mkoa au Wilaya,tamko kuhusu sababu na hali iliyofanyaBodi kudhibiti ushiriki huo.

(j) Katika upataji wa vifaa na huduma kwa

48

Page 49: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

kuwaomba watoaji kutoa mapendekezoyao moja kwa moja tamko la sababu nahali iliyofanya Bodi kuamua kutumiautaratibu huo, na

(k) Muhtasari wa maombi yoyote yaufafanuzi kuhusu mchujo wa zabuni aunyaraka za zabuni na majibuyaliyotolewa pamoja na muhtasari wamarekebisho yoyote yaliyofanywakatika nyaraka hizo.

(2)

Sehemu ya kumbukumbu zilizotajwa kwenyeKanuni Ndogo ya (1) (a) na (b) ya Kanuni hiizitatolewa, kama zikiombwa, kwa mtu yeyotebaada ya zabuni kutangazwa, kufunguliwa nakukubaliwa, au baada ya kusimamishwa kwataratibu za uagizaji bila ya kuingia katikamkataba wa uagizaji.

(3)

Sehemu ya kumbukumbu zilizoelekezwakatika Kanuni Ndogo ya (1) (c) hadi (g) yaKanuni hii kama itaombwa, itatolewa kwawazabuni waliowasilisha zabuni baada yazabuni kukubaliwa au baada ya kusitishwabila ya kuingia kwenye mkataba wa utoaji wavitu au huduma.

(4)

Isipokuwa kama itaelekezwa hivyo namahakama yenye mamlaka na kutegemeanana masharti ya maelekezo hayo, Bodi haitatoahabari-

(a) kama utoaji huo wa habari utakuwakinyume cha Sheria; utazuia utekelezajiwa Sheria; hautakuwa na maslahi kwaumma; utahatarisha maslahi halali yakibiashara ya wahusika au utazuiaushindani halali; na;

(b) habari zinazohusu uchambuzi, tathminina ulinganisho wa zabuni pamoja na beimbali ya muhtasari ulioelezwa kwenyeKanuni Ndogo ya (1) (e) ya Kanuni hizi.

49

Page 50: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(5)

Mara baada ya Zabuni kujadiliwa na Bodi,Katibu atamjulisha Mzabuni aliyefanikiwa ilimakubaliano ya nyaraka za mkataba yawezekufikiwa.

(6)

Nakala za muhtasari zitapelekwa kwa siri kwakila Mjumbe wa Bodi, Mkurugenzi, MwekaHazina, Mkaguzi wa Ndani na Mkuu wa Idarahusika kwa taarifa na kumbukumbu.

(7)

Kila Mzabuni ambaye hakufanikiwaatajulishwa na akiomba sababu zakutokubaliwa kwa zabuni yake atapaswakupewa sababu.

(8)

Bodi ya Zabuni kwa kuzingatia masharti yaKanuni za uagizaji itaandaa taarifa yamwenendo na maamuzi ya zabunizilizoitishwa na kuwasilishwa kwenye Mkutanowa kawaida wa Halmashauri kupitia Kamati yaKudumu husika.

Uzuiaji warushwa

66 Katika mkataba wowote wa kimaandishi,yatawekwa maneno ambayo yataonyeshakuwa Halmashauri itakuwa na haki kusitishamkataba na kumdai Mkandarasi malipo yafidia kutokana na kusimamishwa kwamkataba huo endapo Mkandarasi atabainikakuwa ameahidi kutoa au ametoa, auamekubali kutoa kwa mtu yeyote zawadiyoyote au upendeleo wa aina yoyote kamakishawishi au zawadi kwa kufanya aukumpendelea au kutomkubali mtu yeyotekuhusiana na mkataba na Halmashauri aukama vitendo hivyo vitakuwa vimefanywa namtumishi yeyote aliyeajiriwa naye au kwaniaba yake iwe Mkandarasi anafahamu auhafahamu atakuwa ametenda kosa chini yaSheria ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa yamwaka 2007.

50

Page 51: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Usimamiaji wamikataba

67 (1)

Mkurugenzi wa Halmashauri atawajibikakatika usimamiaji na ufuatiliaji mzuri waMikataba.

(2)

Mkataba wa upataji vitu hautabadilishwa kwanamna yoyote ile baada ya kutiwa saini napande zonazohusika isipokuwa kamamabadiliko hayo ni-

(a) kwa faida ya Halmashauri na hayaileteihasara Halmashauri;

(b) yamethibitishwa na Bodi ya zabuni yaHalmashauri; na

(c) Upande mwingine unaafiki.

(3)

Malipo ya mwisho hayatafanywa mpakamkataba mzima utakapokuwa umekamilikakutokana na kuridhika kwa Halmashauri nakulingana na vipengele vya mkatabaunaohusika.

(4)

Malipo ya fedha za salio hayatalipwa mpakaupite muda wa miezi sita na kazi iwe hainakasoro.

Uvunjajiwamkataba

68 Pale ambapo mkataba uliotiwa lakiri/muhurina Halmashauri haukufuatwa na mkandarasi,ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji usiokuwawa kimsingi, Mkurugenzi atashaurianamapema iwezekanavyo na Kamati ya Fedhana Utawala kwa kuzingatia taratibuzilizowekwa kwenye mkataba, itaamua hatuamuafaka za kuchukua na kumfahamishaMkandarasi juu ya uamuzi.

Rejesta yamikataba

69 (1)

Mkurugenzi atatunza maelezo yote yamikataba kwenye rejesta ya mikataba naatafanya ulinganifu wa malipo halisi na yaleyaliyoidhinishwa.

(2)

Taarifa ya matumizi yote ya ziada lazimayapelekwe kwenye Bodi ya Zabuniyakiambatana na maelezo kutoka kwa

51

Page 52: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Mkurugenzi.

Diwani/Afisakutokuwana maslahikatikamikataba

70 (1)

Endapo Diwani au Afisa wa Halmashauri anamaslahi ya kifedha ya moja kwa moja auvinginevyo katika mkataba wowote, mkatabaunaopendekezwa au jambo lolote, na yupokwenye Mkutano wa Halmashauri au Kamatiambapo mkataba huo, au mkatabaunaopendekezwa au jambo lingine lolotelinajadiliwa, atatangaza jambo hilo maraMkutano utakapokuwa umeanza na hatashirikiwala kuwepo katika majadiliano au kupigakura kuhusu jambo linalohusu mkataba aumkataba unaopendekezwa au jambo linginelolote ambalo ana maslahi nalo.

(2)

Kanuni hii haitatumika kuhusiana na maslahikatika mkataba au suala lingine ambaloMjumbe au Afisa wa Halmashauri ana maslahinalo kama mlipa kodi au mkazi katika eneolililo katika himaya ya Halmashauri.

(3)

Diwani atahesabika kuwa na maslahi ya mojakwa moja katika mkataba au jambo jingineendapo-

(a) yeye au mtu aliyemchagua ni Mjumbewa kampuni au chombo kingine auanayo hati ya hisa katika kampuniambayo itaingia, au imependekezwaiingie katika mkataba, au anaouhusiano wa kifedha katika jambolinalojadiliwa; au

(b) yeye ni mbia au ameajiriwa na mtuambaye mkataba unafanywa naye, auutakuwa chini yake, au anao uhusianowa kifedha wa moja kwa moja katikasuala linalojadiliwa au kuzungumzwa.

(4 Katika Kanuni hii maslahi ya moja kwa moja

52

Page 53: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

) na yasiyo ya moja kwa moja ya mwanandoaau ndugu wa familia kama inafahamika kwaMjumbe wa Halmashauri itachukuliwa kuwa nimaslahi ya moja kwa moja au yasiyo ya mojakwa moja.

(5)

Taarifa ya jumla itakayotolewa kwaMkurugenzi na Diwani au Afisa waHalmashauri kuhusiana na yeye, mkewe,mumewe au ndugu yake kwamba ana maslahiya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwamoja katika mkataba unaokusudiwa au jambolingine na akieleza aina ya maslahiitachukuliwa, isipokuwa pale atakapoondoataarifa hiyo, kuwa ametoa taarifa ya kutoshaya maslahi yake kuhusiana na suala ambalolimo katika mjadala.

(6)

Mkurugenzi ataandika taarifa za watu wenyemaslahi waliotoa taarifa chini ya KanuniNdogo ya (1) na taarifa yoyote iliyomo katikaKanuni Ndogo ya (5) itakuwa wazi kwaukaguzi wakati wa saa za kazi.

(7)

Halmashauri inaweza baada ya kupata kibalicha Waziri, kuondoa kizuizi chini ya Kanuni hiikinachoifanya ishindwe wakati wowotekufanya Mkutano pale ambapo idadi yaWajumbe wenye maslahi ni kubwa mno kiasicha kukwamisha shughuli za Halmashauri auitakuwa ni kwa maslahi ya wakazi waHalmashauri kuondoa kikwazo hicho.

(8)

Katika Kanuni za Kudumu hizi ,ndugu wafamilia itachukuliwa kuwa ni pamoja na baba,mama, mtoto, kaka, au dada na wanandoawao.

SEHEMU YA VIMASUALA MENGINE

Kiapo nakukubali

71 Kila Diwani kabla ya kushika wadhifa wakekama Diwani na kabla ya Mkutano wa kwanza

53

Page 54: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

wadhifa wa Halmashauri:-

(a) atakula kiapo kama kilivyoonyeshwakwenye jedwali la pili la Kanuni hizi zakudumu kitakachosimamiwa na HakimuMkazi au Hakimu wa Wilaya; na

(b) atatoa tamko la kimaandishilililoandikwa kwa Mkurugenzi akiahidikutekeleza jambo linalohusiana natamko la maslahi katika shughuli zakibiashara, mali, na kadhalika nakuzifuata Kanuni za Maadili yaMadiwani.

Majukumuya Diwani

72 (1)

Diwani atakuwa na majukumu yafuatayo:-(a) kuwa karibu na wapiga kura na kupata

ushauri wa Wananchi katika mamboyanayotarajiwa kujadiliwa kwenyeHalmashauri.

(b) kutoa maoni na mapendekezo yawananchi kwa Halmashauri.

(c) kuhudhuria Mikutano ya Halmashaurina ya Kamati au Kamati Ndogoambamo yeye ni Mjumbe.

(d) kutenga angalau siku moja kila mwezikukutana na wananchi katika eneo lakela uchaguzi.

(e) kutoa taarifa kwa wapiga kura kuhusumaamuzi ya jumla ya Halmashauri nahatua zilizochukuliwa na Halmashaurikuondoa matatizo yaliyowahi kuelezwana wakazi wa eneo lake la uchaguzi.

(f) kuchangia ujuzi na uzoefu wake katikamajadiliano yanayofanyika katikaMikutano ya Halmashauri na Kamati zaHalmashauri, na

(g) kushiriki katika shughuli za pamoja zamaendeleo katika eneo lake la uchaguzina katika eneo zima la Halmashauri.

(2 Katika kutekeleza wajibu wake diwani

54

Page 55: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

) atazingatia-

(a) Maslahi ya Taifa na maslahi yaWananchi katika eneo la Halmashauri;

(b) Katiba, Sheria na Kanuni;

(c) Kanuni za Maadili ya Madiwani,Mwongozo juu ya mahusiano yaMadiwani na Watumishi na miikomingine.

Nafasiwazi

73 (1)

Kiti cha Mjumbe wa Halmashauri kitakuwawazi endapo Mjumbe-

(a) amefariki;(b) anakubali ajira kama mtumishi wa

Halmashauri;(c) kwa mujibu wa Sheria yoyote

anatangazwa kuwa hana akili timamu;(d) yuko chini ya hukumu ya kifo au

kifungo kinachozidi miezi sitakilichotolewa kwake na mahakama;

(e) kwa mujibu wa Sheria yoyoteanatamkwa kuwa anapoteza sifa zakuendelea kuwa Mjumbe;

(f) atakoma kuwa mwanachama wa chamacha siasa kilichompendekeza kuwamgombea wa kiti cha udiwani;

(g) anapokuwa amepatikana na kosakutokana na Kanuni za Maadili yaMadiwani na adhabu ya kosa alilotendani pamoja na kumwondoa Mjumbemadarakani; na

(h) anapoteza ujumbe kwa mujibu waKanuni ya 71 (2) ya Kanuni hizi zakudumu;

(i) anahukumiwa kwa kosa la kutotajamaslahi yake.

(j) amejiuzulu kutoka kiti chake;

55

Page 56: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(k) Halmashauri imevunjwa na kuathirimipaka ya majimbo ya uchaguzi;

(l) uchaguzi wa Mjumbe umetangazwakuwa batili;au

(m) bila sababu ya kuridhisha au bila idhiniau kibali cha maandishi chaMwenyekiti, Mjumbe anakosakuhudhuria Mikutano mitatu ya kawaidainayofuatana ya Halmashauri au Kamatiambamo yeye ni Mjumbe.

(2)

Waziri atatangaza kiti kuwa wazi paleatakapojulishwa na Meya kwa maandishikwamba kiti kiko wazi kwa kuzingatiamasharti ya kifungu cha 42 (1) cha Sheria yaSerikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya288.

Kutokuwepo kwa Wajumbe

74 (1)

Halmashauri yaweza kutoa idhini yakutokuwepo katika Mikutano yake kwa mudausiozidi miezi kumi kwa Mjumbe yeyoteanayetaka kwenda nje ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

(2)

Pale ambapo Mjumbe kwa sababu yoyote ileamekuwa nje ya nchi kwa muda unaozidimiezi kumi kiti chake cha udiwanikitachukuliwa kuwa kipo wazi.

TaratibuzakutungaSheriaNdogo

75 (1)

Pale ambapo Halmashauri inakusudia kutungaSheria Ndogo itatoa tangazo kwa wakazi waeneo husika kuhusu kusudio hilo katika namnaambayo itahakikisha kuwa watakaoathirika naSheria Ndogo inayokusudiwa kutungwawanafahamu vilivyo na kuwaombawanaopenda kutoa pingamizi lolote aumapendekezo yao kwa maandishi katikamuda uliowekwa.

(2 Pale ambapo baada ya muda wa taarifa

56

Page 57: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

) kumalizika hakuna pingamizi au malalamikoyaliyowasilishwa, au hakuna mtu yeyotealiyetoa kipingamizi kinachokubalika mbele yaHalmashauri, Halmashauri itaendelea kutungaSheria Ndogo ikizingatia malalamiko napingamizi zilizotolewa.

(3)

Sheria Ndogo zikishatungwa na Halmashaurizitapelekwa kwa Waziri ili awezekuziidhinisha.

(4)

Waziri anaweza kuidhinisha, kukubali aukukataa kuidhinisha Sheria Ndogo au kutoa aukusimamisha kibali chake kwa kutoa mashartiatakayoyaeleza na anaweza baada ya kutoaidhini yake, kupanga tarehe ya kuanzakutumika kwa Sheria Ndogo hizo.

(5)

Waziri anaweza, kabla ya kuidhinisha SheriaNdogo zenye athari kwenye maeneoyaliyotengwa au maeneo maalum au kwaSheria nyingine yoyote, kushauriana na Wazirianayehusika na Sheria husika au na jambolililotungiwa Sheria Ndogo kadri itakavyokuwa.

(6)

Sheria Ndogo yoyote iliyotungwa naHalmashauri lazima itangazwe katika Gazeti laSerikali kabla ya kuanza kutumika.

Ukaguziwanyaraka

76 (1)

Mjumbe ataweza, kwa madhumuni yakutekeleza wajibu wake kama Mjumbe, na sivinginevyo, kukagua waraka wowote ambaoumejadiliwa na Kamati ya Halmashauri nakama nakala zinapatikana, anaweza kupewa,akiomba, nakala kwa madhumuni hayo hayo.

(2)

Mjumbe hatakagua kwa makusudi au kutakaapewe nakala ya waraka wowote unaohusujambo ambalo yeye ana maslahi nalo kwamujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa(Mamlaka za Miji), Sura ya 288. Hata hivyo

57

Page 58: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Kanuni hii haitamzuia Mkurugenzi kuzuiakukaguliwa kwa waraka wowote ambaoumezuiliwa kutolewa kwa mujibu wa Sheriayoyote au Kanuni zilizotungwa chini ya Sheriahizo.

Uanzishajiwa Bodi zaHuduma

77 (1)

Halmashauri inaweza, kwa mujibu wa kifungu88 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlakaza Miji), Sura ya 288 kwa madhumuni yakutekeleza kazi zake katika eneo lililo chini yamamlaka yake, kuunda Bodi za Huduma kwahati rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti laSerikali, kama itakavyoona inafaa kufanyahivyo.

(2)

Bodi ya Huduma iliyotajwa katika KanuniNdogo ya (1) ya Kanuni hizi itawajibika mojakwa moja kwenye Halmashauri kupitia Kamatiya Kudumu husika na itatekeleza kazi zakekama ilivyofafanuliwa katika hatiinayoianzisha.

Diwanikutembeleamaeneo,shughulimbalimbali za ujenzin.k

78 (1)

Mjumbe wa Halmashauri anaweza kutembeleaeneo, jengo au shughuli za ujenzizinazotekelezwa na au kwa niaba yaHalmashauri na anaweza kutuma taarifa kwaMkurugenzi akieleza sababu za matembeziyake ili aweze kupangiwa Wataalam wa mradiau shughuli husika kwa ajili kupata maelekezoya kitaalam.

(2)

Mjumbe wa Halmashauri anapotembeleashughuli au miradi ya maendeleoinayotekelezwa na au kwa niaba yaHalmashauri hataruhusiwa kutoa maelekezoau maagizo ya kitaalam awapo kwenye eneola mradi.

(3)

Baada ya diwani kutembelea maeneo aumajengo kama ilivyoainishwa kwenye KanuniNdogo ya (1) ya Kanuni hii anaona kunaumuhimu wa kutoa maoni au mang’amuzi

58

Page 59: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(4)

yake juu ya matembezi hayo atafanya hivyokwa kuwasilisha maoni au mang’amuzi yakekwa Mkurugenzi ambaye atafanyia kazi aukuyapeleka kwa afisa anayesimamia kazihusika kwa utekelezaji;

Endapo maoni au mang’amuzi ya Diwanihayawezi kufanyiwa kazi na Mkurugenzi auAfisa mhusika, basi atamshauri diwanikupeleka maoni na mang’amuzi yake kwaKamati inayohusika ili yachunguzwe zaidi nakuamuliwa.

(5)

Kamati za Kudumu za Halmashauri zinawezakutembelea miradi ya maendeleo au shughuliyoyote inayotekelezwa na au kwa niaba yaHalmashauri ili mradi katika kutembeleamiradi hiyo Kamati itaongozana na Wataalamwa mradi au shughuli husika ili kupatamaelekezo ya kitaalam.

(6)

Kamati ya Kudumu itatembelea miradi aushughuli za maendeleo kabla ya Kikao chaKamati ambacho kitajadili mradi au shughulihiyo.

Uhifadhiwa LakiriyaHalmashauri

79 Lakiri ya Halmashauri itatunzwa kwa usalamana kufungiwa katika Kasiki kwenye Ofisi yaMkurugenzi mwenyewe.

Utiajimuhurikwenyenyaraka

80 (1)

Lakiri ya Halmashauri haitabandikwa katikaHati yoyote mpaka ubandikaji huoumeidhinishwa na azimio la Halmashaurilikiidhinisha kukubaliwa kwa zabuni, ununuzi,uuzaji au upangishaji au kuchukua maliyoyote, utoaji wa Hati yoyote ya ukopeshajifedha, uwasilishaji wa madai yoyote, uwekajiwa viwango vya kodi, uingiaji kwenyemkataba, kutunga Sheria Ndogo, au hatiyotote iliyo rasmi ambayo kwa mujibu waSheria au Kanuni yoyote inahitaji kuwekwalakiri ya Halmashauri.

59

Page 60: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(2)

Lakiri itashuhudiwa au kuthibitishwa na Meyaau Naibu Meya na Mkurugenzi, na hatizilizowekwa lakiri zitasainiwa na Meya auNaibu Meya, kama hali itakavyokuwa.

Uandikishaji waanuani

81 (1)

Itakuwa wajibu wa kila Mjumbe katika kikaocha kwanza cha Halmashauri, baada yauchaguzi kutoa taarifa ya maandishi kwaMkurugenzi juu ya anuani yake ya kudumu yakupokelea taarifa. Taarifa zilizopelekwa kwakutumia anuani iliyoandikishwa itachukuliwakama ndiyo sahihi na inatosheleza kwamatumizi yote.

(2)

Iwapo Mjumbe atatoa taarifa ya maandishikwa Mkurugenzi kuwa angependa taarifa yaMikutano ya Halmashauri iwe inatumwakwake kwa kutumia anuani atakayoitajakwenye taarifa hiyo ambayo ni tofauti na ilekatika Kanuni Ndogo ya (1), taarifa yoyoteitakayoachwa au itakayotumwa kwa njia yaposta kwa kutumia anwani hiyo itachukuliwakuwa inatosha kwa ajili ya kutoa taarifainayotakiwa kwa mujibu wa Kanuni zaKudumu hizi.

Uteuzi waWajumbekwenyetaasisi zanje

82 (1)

Katika Mkutano wake wa kwanza,Halmashauri itateua wawakilishi wake kwenyeBodi na Taasisi za nje ambazo Halmashauriinastahili kuwakilishwa.

(2)

Mjumbe au Wajumbe, wanaoiwakilishaHalmashauri kwenye Bodi na Taasisi za nje,watatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzitaarifa kuhusu shughuli za Bodi au Taasisizinazogusa Sera na maslahi ya Halmashaurina wakazi wake kijumla na Mkurugenziatachukua hatua zifaazo.

Kumwondoa Meyamadarakani

83 (1)

Halmashauri inaweza kumwondoa Meyamadarakani kwa azimio linaloungwa mkonona theluthi mbili ya Wajumbe kutokana na

60

Page 61: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

hoja au sababu yoyote kati ya sababuzifuatazo:-

(a) Kutumia nafasi yake vibaya;(b) Kushiriki katika vitendo vya rushwa;(c) Kushindwa kutekeleza majukumu yake(d) Mwenendo mbaya au ukosefu wa

adabu; au(e) Ulemavu wa kimwili au kiakili kwa kiasi

cha kumfanya kushindwa kutekelezamajukumu yake kama Meya.

(2)

Hoja au sababu zitakazotolewa lazima iweimetimiza masharti yafuatayo:

(i) Iwe na tuhuma mahsusi yenye ushahidiwa kutosha

(ii) Iwe imetolewa maelezo kamili na yenyekueleweka kuhusu tuhumazinazohusika.

(3)

Kwa madhumuni ya kumwondoa Meyamadarakani, kwa sababu zozote zilizotamkwachini ya Kanuni Ndogo ya (1) ya Kanuni hii,Halmashauri itatumia taratibu zilizotolewakatika Taratibu za Kumwondoa Meyazilizotangazwa kwenye gazeti la Serikali naWaziri kwa mujibu wa Sheria.

SEHEMU YA VIIPOSHO KWA WAJUMBE

Aina zaposho

84 (1)

Wajumbe wa Halmashauri watalipwa poshombalimbali kama itakavyopendekezwa naHalmashauri na kuidhinishwa na Waziri.

(2)

Posho zitakazolipwa kwa Wajumbe waHalmashauri zitakuwa za aina zifuatazo-(a) Posho ya usafiri;(b) Posho ya kuhudhuria kikao;(c) Posho ya madaraka;(d) Posho ya kujikimu;

61

Page 62: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(e) Posho ya mwezi.(f)Kiinua mgongo

(3)

Endapo Mjumbe wa Halmashauri ataugua auataumia wakati akifanya kazi aliyotumwa naHalmashauri, gharama za matibabu yakezitalipwa na Halmashauri.

PoshoendapoMkutanoutaahirishwa

85 Endapo Mkutano wa Halmashauri au Kamatiutaahirishwa kwa sababu ya kukosekana kwaakidi, Mjumbe au Wajumbe waliofika kwa ajiliya kuhudhuria Mkutano huo ulioahirishwawatastahili malipo yaliyotajwa katika Kanuniya 84 (2) (a) na (d) iwapo wamelazimika, bilakukusudia, kulala njiani au kwenye Makaomakuu ya Halmashauri. Hakuna malipo yaposho ya kuhudhuria kikao yatakayofanywakatika hali ya namna hiyo.

SEHEMU YA VIIIMABADILIKO KWENYE KANUNI ZA

KUDUMU

Kusitishautumiajiwa KanunizaKudumu

86 (1)

Kanuni yoyote inaweza kusitishwa kwa azimiolililoungwa mkono na theluthi mbili zaWajumbe waliohudhuria Mkutano waHalmashauri kwa hoja iliyopendekezwa bilataarifa kwa madhumuni ya kuwezeshashughuli yoyote iliyofafanuliwa iliishughulikiwe na Halmashauri kama jambo ladharura au lenye manufaa.

(2)

Halmashauri haitasitisha matumizi ya Kanuniyoyote kama kusitisha huko kutasababishakufanya jambo ambalo limezuiliwa na Sheriaau kutofanya jambo linalotakiwa kufanywachini ya Sheria yoyote.

Marekebisho namabadilikoya Kanuniza Kudumu

87 Halmashauri inaweza kubadilisha, kuongeza,kurekebisha au kutengua Kanuni hizi zakudumu kwa azimio lililoungwa mkono kwawingi usiopungua theluthi mbili ya kura na

62

Page 63: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

baada ya kupata idhini ya Waziri.

Kanuni zaKudumukutolewakwaWajumbe

88.

Nakala iliyochapishwa ya Kanuni za Kudumuhizi zitatolewa na Mkurugenzi kwa kilaMjumbe.

KutafsiriKanuni zaKudumu

89.

Uamuzi wa Meya kuhusu maana ya matumiziya Kanuni hizi au mwenendo wa Mkutano waHalmashauri hautapingwa wakati wa Mkutanowowote wa Halmashauri.

SEHEMU YA IXZIARA ZA WAJUMBE

Ziara zaWajumbe

90.

(1)

Wajumbe wa Halmashauri wanaweza kwendaziara mbalimbali za mafunzo ili mradi ziarahizo ziwe zimeainishwa kwenye mpango naBajeti ya Halmashauri. Isipokuwa kwa ziaraambazo gharama zake hazihusiani na Bajetiya Halmashauri, Wajumbe watafanya ziarahizo kwa mujibu wa ratiba ya mpango huo.

(2)

Bila kuathiri masharti ya Kanuni Ndogo ya (1)ya kanuni hii Halmashauri kabla ya kuruhusukufanyika kwa ziara itahaikikisha kwamba-

(a) shughuli ya ziara hiyo inafanana nashughuli zinazofanywa na Halmashauri;

(b) ziara hiyo inapata kwanza kibali chaMkuu wa Mkoa;

(c) Wajumbe wanakitu cha kwendakuonyesha kule wanakokwendakujifunza;

(d) ziara zinazofanyika nje ya Mkoazihusishe wadau mbalimbali waHalmashauri kutegemeana na ziarahusika.

(e) ziara iwe na matunda yanayoonekana;(f) Wajumbe walioshiriki kwenye ziara

warejeapo wanatakiwa kuandaa na

63

Page 64: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

kuwasilisha ripoti ya maandishi kwaHalmashauri kuhusu mambo mapya naya msingi waliyojifunza na kuwekautaratibu mzuri wa kuyatekelezakwenye Kata zao na kwenyeHalmashauri;

(g) Ziara zinafanywa kwa vikundi vyaWajumbe wachache kadriitakavyokubalika na Halmashauri.

Wimbo waTaifa,Dua/Sala yakuiombeaHalmashauri

91.

Kabla ya kuanza kwa Mkutano waHalmashauri,utaimbwa wimbo wa Taifa nakufuatiwa na Dua au Sala ya kuiombeaHalmashauri ifuatayo; “Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu,Muumba wa Mbingu na Dunia umewekakatika Dunia Serikali za Wanadamu ilihaki yako itendeke. Twakuomba, uibarikiManispaa yetu ya Kigamboni idumisheuhuru, umoja, haki na amani. Uwajalieviongozi wetu wa Manispaa hekima, afyanjema na maisha marefu ili pamoja nawanaowashauri wadumishe utawalabora. Utuongezee hekima na busara sisiMadiwani wa Halmashauri ya ManispaaKigamboni na utupe uwezo wa kujadilikwa dhati, mambo yatakayoletwa mbeleyetu leo, ili tufanye maamuzi sahihiyenye manufaa kwa watu wote na ustawiwaManispaa yetu. Amina”.

64

Page 65: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

JEDWALI LA KWANZA

Chini ya Kanuni ya 45(3)

HADIDU ZA REJEA ZA KAMATI ZA KUDUMUZA HALMASHAURI ZA MIJI.

Madhumuni ya jumla:

1. Kuishauri Halmashauri kutengeneza malengoyanayozingatia matakwa ya Miji na kuchukua hatuaambazo zitaonekana zinafaa ili kufikia malengoyaliyokusudiwa.

2. Kuishauri Halmashauri kufanya maamuzi juu ya Seramuhimu.

3. Kuishauri Halmashauri kufanya maamuzi juu ya utoaji wahuduma kulingana na rasilimali walizo nazo.

4. Kuiwezesha Halmashauri kutengeneza taratibuzitakazoongoza utendaji wa Kamati, Kamati Ndogo, na ulewa watumishi ili watimize wajibu wao.

5. Kufanya mapitio yatakayowezesha Halmashauri kuamuajuu ya kuongeza, kupunguza, kubinafsisha aukuwashirikisha wadau katika utoaji wa huduma.

6. Kuhakikisha kuwa miundo na taratibu za utendaji waHalmashauri zinazingatia ufanisi, uthabiti na tija katikakufikia malengo ya Halmashauri.

7. Kuiwezesha Halmashauri kujenga mahusiano imara katiyake na Serikali kuu, Serikali zingine za Mitaa na Ummakwa ujumla.

A. Kamati ya Fedha na Utawala:

Majukumu ya jumla:Kamati hii inawashirikisha Wenyeviti wa Kamati zote zakudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja.Aidha, madaraka ya Kamati hii ni kama ya Kamati zingineza kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanyakazi/majukumu ya Kamati zingine za kudumu. Kwa ujumla,majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibitiukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali yaHalmashauri kwa kupitia vikao vyake.Majukumu Maalum ya Kamati:

(i) Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wamapato

(ii) Kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti na mpangowa Maendeleo kwenye Halmashauri ilikuidhinishwa na Halmashauri.

(iii) Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwani pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri,ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na

65

Page 66: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

kuomba vibali maalum kwa matumiziyanayohitaji kibali cha Waziri mwenyedhamana ya Serikali za Mitaa.

(iv) Kufikiria na, pale inapowezekana, kupendekezakwenye Halmashauri masuala yanayohusuSheria Ndogo na utendaji katika ngazi za chiniza Halmashauri.

(v) Kupokea na kuzingatia mapendekezo yakubadili matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisioyaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwaHalmashauri.

(vi) Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamatizingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradina kuyawasilisha kwenye Halmashauri.

(vii) Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashaurimikopo yote ya Halmashauri.

(viii) Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwamadhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibuwa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Suraya 290.

(ix) Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wafedha na mali ya Halmashauri na kupendekezahatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezona maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa Sheria zaSerikali za Mitaa, Sura ya 290.

(x) Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha zaHalmashauri, kwa kuzingatia taratibuzilizowekwa na Waziri na taratibu nyinginezitakazowekwa na Halmashauri;

(xi) Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwahususan kuhusu taratibu za fedha, ikiwa nipamoja na mapitio ya mara kwa marayanayohusu thamani ya fedha ambapo Kanunimbalimbali za manunuzi ya mali na vifaahutumika;

(xii) Kufikiria na kupendekeza mabadiliko yaviwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali,vinavyotolewa na Halmashauri;

(xiii) Kufikiria mapendekezo ya Bajeti na Mipango yaMaendeleo ya kila Kamati ya Kudumu nakuiwasilisha kwenye Halmashauri ili kupataidhini;

(xiv) Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizikatika bajeti yote na kupendekeza hatuastahiki ya kuchukua kuondoa mapungufukatika mapato au ziada matumizi;

(xv) Kufikiria mapendekezo yote yanayohusumatumizi makubwa ya fedha kablahayajawasilishwa kwenye Halmashauri ilikupata idhini;

66

Page 67: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(xvi) Kupokea mahesabu ya mwaka ya Halmashaurina kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya mwakainawasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;

(xvii) Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuziwa Halmashauri kwa kuzingatia mpango waBajeti uliopitishwa na Halmashauri;

(xviii) Kupitia taarifa ya kila robo mwaka kuhusuManunuzi iliyowasilishwa na Afisa Masuuli;

(xix) Kusimamia utekelezaji wa mikataba yaHalmashauri kwa kukagua miradiinayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa;

(xx) Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuziau ukaguzi wa huduma au vifaavilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi,itafanyika hivyo endapo itadhihirika kwamba,maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi yavifaa au huduma hayaridhishi;

(xxi) Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi yazabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu waSheria husika;

(xxii) Kushughulikia orodha ya wadaiwa woteitakayokayowasilishwa kwenye Kamati nakutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;

(xxiii) Kupendekeza njia na taratibu za kuondoshavifaa chakavu. Uondoshaji wa vifaa unawezakufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu;

(xxiv) Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kilamwezi na kila robo mwaka;

(xxv) Kupendekeza kwa Halmashauri hatua zakuchukua kuhusu kufuta madeni yaHalmashauri;

(xxvi) Kushughulikia Sera kuhusu kukopa nauwekezaji,

(xxvii) Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzishana kuendeleza uhusiano na Halmashaurinyingine.

(xxviii) Kurekebisha na kusimamia makusanyo namatumizi ya mapato ya vijiji na miji midogokwa mujibu wa Sheria,

(xxix) Kuteua wakaguzi wa fedha/mali za Serikali zaVijiji kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 290).

(xxx) Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua zakuchukuliwa kuhusu mambo yote yayanayohusu masuala ya ajira na kinidhamu yawafanyakazi na watumishi.

(xxxi) Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusumasuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.

(xxxii) Kupokea na kutoa uamuzi juu ya mapendekezoya watumishi wanaokwenda masomoni.

67

Page 68: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(xxxiii) Kujadili na kupendekeza masuala yoteyanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi,ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri,matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.

(xxxiv) Kupitisha mapendekezo ya kuthibitishawatumishi kazini baada ya kumaliza kipindi chamajaribio kulingana na miundo husika yautumishi.

B: Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya:

Majukumu ya Jumla

Kushughulikia mambo yote yanayohusu afya ya jamii, elimu nahuduma za maji. Kamati hii pia itashughulikia mamboyanayohusiana na jitihada za wanannchi Vijijini kujileteamaendeleo yao kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamojana kushauri, kushawishi, kuzindua, kuelimisha na kushirikishawananchi hao hasa katika kutayarisha, kutekeleza, kusimamiana kutathmini mipango yao ya maendeleo.

Majukumu maalum ya Kamati:

(i) Kuandaa mipango madhubuti ya maendeleo yaupanuzi na ujenzi wa hospitali, vituo vya afya nazahanati

(ii) Kuandaa mipago ya maendeleo ya upanuzi naujenzi wa shule za awali na msingi na elimu yawatu wazima kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya1978 kama ilivyorekebishwa mwaka 1995.

(iii) Kupendekeza mipango ya ujenzi au upanuzi wavituo, viwanja, majengo na mazingira ya burudani,starehe, mapumziko na michezo.

(iv) Kuamua juu ya mambo yanayohusu uhifadhi wamambo ya kale na mandhari mbalimbali yenyesura nzuri.

(v) Kuandaa na kuratibu njia bora juu ya uhifadhi wanyaraka muhimu kwa ajili ya kumbukumbu hizozitahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali zaMitaa Sura ya 288

(vi) Kupendekeza njia bora juu ya uhifadhi wa sanaambalimbali za ufundi na za maonyesho kwamujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 288

(vii) Kupendekeza matumizi mazuri ya lugha ya taifa.

68

Page 69: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(viii) Kupendekeza namna ya malezi ya vijana iliwaweze kuwa wazalishaji katika Taifa.

(ix) Kusimamia uanzishaji wa uendelezaji wa vikundivya jamii na vya hiari vya wananchi katikaHalmashauri kwa mujibu wa Sera wa maendelo yajamii.

(x) Kusimamia na kuhakiki maeneo ya misitu, mapori,na mbuga zilizotengwa kama hifadhi ya mamlakaya Serikali za Mitaa.

(xi) Kupendekeza na kufanya tathmini ya uendelezajiwa mabonde, mito na mabwawa.

(xii) Kubuni na kupendekeza namna ya kudhibiti moto

(xiii) Kubuni na kupendekeza mikakati ya utumiaji wanishati mbadala, kuzuia ukataji miti ovyo, nakuhimiza upandaji miti kwa wingi.

(xiv) Kuhakikisha kwamba ukaguzi wa majengounafanyika mara kwa mara.

(xv) Kupendekeza mipango madhubuti ya ujenzi wabarabara vijijini na wilayani kwa ujumla.

(xvi) Kupendekeza Sheria Ndogo zinazohusu Kamatihizi.

D: Kamati ya Kudumu ya Kudhibiti Ukimwi

Majukumu ya Kamati:

1. Kushirikisha wadau tofauti katika maeneo husika ilikuongeza uchangiaji wa mawazo na/au nyenzo,usimamizi, uratibu na utekelezaji wa kazi za Tume zakudhibiti UKIMWI;

2. Kusimamia uundaji wa Kamati zote za kudhibitiUKIMWI;

3. Kupendekeza na kuchambua hali ya UKIMWI/Mipangona utekelezaji wake na kufikisha katika ngazi husukakwa hatua zaidi;

4. Kutathmini hali ya UKIMWI katika eneo lake;(i) Idadi ya waathirika: wagonjwa, yatima,

wajane,

(ii) Kasi ya maambukizo.

69

Page 70: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(iii) Mazingira maalum yanayochangiamaambukizo.

(iv) Uelewa wa wananchi juu ya janga hili.

(v) Serikali haitatoa fedha kwa Halmashauriisiyokuwa na mipango madhubuti yakudhibiti UKIMWI.

(vi) Kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikishakila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shuleanafanya hivyo.

(vii) Kuweka mikakati ya makusudi juu ya njiabora za kuchangia baadhi ya huduma zaElimu na Afya.

(viii) Kubuni na kupendekeza njia bora za kuzuiana kudhibiti magonjwa ya milipuko.

(ix) Kupendekeza Sheria Ndogo za Kamati hii.

C: Kamati ya Mipango Miji na Mazingira:

Majukumu ya jumla

Kamati hii itashughulikia masuala ya uzalishaji mali ikiwemokilimo, mifugo, viwanda, madini, Biashara n.k. Aidhaitashughulikia pia miundombinu na suala zima la mendeleo yaArdhi na hifadhi ya mazingira.

Majukumu maalum ya Kamati;

(i) Kupendekeza kwa Halmashauri mipango yakupanua biashara na jinsi ya kukusanyamapato yatokanayo na upanuzi huo.

(ii) Kupendekeza mipango ya matumizi ya ardhikatika eneo la Halmashauri.

(iii) Kusimamia matumizi ya Sheria ya nguvu kazi.

(iv) Kuandaa mipango madhubuti ya maendeleo yaupanuzi wa kilimo katika Halmashauri

(v) Kusimamia na kuhakiki miradi ya ujenzi wamasoko, minada, majosho na vituo vya mifugo.

70

Page 71: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

(vi) Kushughulikia uanzishaji na uendelezaji wavyama vya ushirika kwa mujibu wa Sheria yaVyama vya Ushirika.

FAHARASA – HALMASHAURI ZA MIJI.

KanuniNa.

Kifungu cha Sheria

AAjenda za KamatiAkidi katika Mikutano yaHalmashauriAkidi kwenye Mikutano ya KamatiAthari za nafasi wazi kwenyeKamati

BCDDiwani au Afisa kutokuwa namaslahi katika mikatabaDiwani kutembelea maeneo,shughuli mbalimbali za ujenzi nk.Wimbo wa Taifa/Dua ya kuiombeaHalmashauriEFFujo zinazosababishwa na ummaFujo zinazosababishwa naWajumbe

509

5655

70

78

91

1918

Sura ya 288 kif.36Sura ya 288 kif.51(2) na(3)Sura ya 288kif.51(1);51(3)

Sura ya 288 kif.43

71

Page 72: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

GHHaki ya kujibuHoja kuhusu matumiziHoja na marekebisho ya hojaHoja za Mwenyekiti/MeyaHoja zinazohusu watumishi waHalmashauriHoja zinazoweza kutolewa bilataarifaIJKKamati za KudumuKamati za pamojaKanuni za kudumu kutumikakatika Mikutano ya KamatiKanuni za kudumu kutolewa kwaWajumbeKauli zenye kashfaKiapo na kukubali wadhifaKuidhinishwa kwa Taarifa yaKamatiKufikiriwa upya maamuziKufutwa kwa Kanuni zilizopo

Kujiuzulu ujumbe wa Kamati nakujazwa kwa nafasi iliyoachwawazi.

Kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekitiwa KamatiKumbukumbu ya mahudhurio.

Kumwondoa Meya/MwenyekitimadarakaniKupokelewa kwa taarifa za KamatiKuruhusu watu na vyombo vyaHabari kwenye Mikutano yaHalmashauri.

2233201638

21

4144

57

88287135

6092

63

62

12

83

3413

Sura ya 288 kif.40 (2)

Sura ya 288 kif.25(5) ; GN263/95

Sura 288 kif.39(1)

Kushiriki kwa UmmaKusitisha utumiaji wa Kanuni zakudumu.Kutafsiri Kanuni za kudumuKuthibitisha muhtasariKutokuwepo kwa WajumbeKutunza siri za Majadiliano yaKamati na Kamati Ndogo.LM

3986

89157461

72

Page 73: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Maamuzi ya Mikutano yaHalmashauriMahudhurio katika Mikutano yaKamatiMajukumu ya DiwaniMarekebisho na mabadiliko yaKanuni za kudumuMaswaliMaswali ya papo kwa papoMihtasari ya Kamati zamaendeleo za Kata na Vijiji/Mitaa.Mihtasari kupelekwa kwa Mkuuwa Wilaya na Mkuu wa Mkoa.Mihtasari ya KamatiMikutano ya KamatiMikutano ya kawaida yaHalmashauriMtoa hoja kualikwa kwenyeMkutano wa Kamati.Mkutano wa BajetiMkutano wa MwakaMkutano maalum wa HalmashauriMkutano maalum wa KamatiMwaliko wa wasiokuwa WajumbeNNafasi wazi

29

51

7287

232431

32

59473

52

6754930

73

Taz.pia Sura ya 290 kif.47Sura ya 288 kif.40(1)

Sura ya 288 kif.34(1)Sura ya 288 kif.34(3)

Sura ya 288 kif.45, 50

PAina za poshoPosho endapo MkutanoutaahirishwaQ

8485

Sura ya 288 kif. 42(2)

RRejesta ya mikatabaSTTaarifa za KamatiTaarifa kutoka kwenye kataTaarifa za MikutanoTafsiriTaratibu za kutunga Sheria NdogoTaratibu za MajadilianoTaratibu za UagizajiUUahirishaji wa vikaoUandikishaji wa AnwaniUandishaji wa Bodi za Huduma Uchaguzi wa Meya/ Mwenyekiti naNaibu Meya/Makamu Mwenyekitiwa HalmashauriUhalali wa majadiliano yaHalmashauri

69

252682751764

40817710

36

Sura ya 288 kif.35

73

Page 74: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

Uhuru wa kutoa mawazo wakatiwa majadilianoUkaguzi wa nyarakaAkidi kwenye Mikutano ya KamatiUpigaji kura kwenye Mikutano yaKamatiUsimamiaji wa mikatabaUtaratibu wa shughuli zaMikutanoUteuzi wa Wajumbe kwenyeTaasisi za njeUtiaji mhuri kwenye NyarakaUvunjaji wa mkatabaUwezo wa Halmashauri kujigeuzakuwa Kamati ya Halmashaurinzima.Uwezo wa KamatiUzuiaji wa Rushwa

27

7656

58

6714

82

806837

4366

Sura ya 288 kif.38

VWWaalikwa wasiokuwa Wajumbekuhudhuria na kushiriki katikaMikutano ya Kamati.XYZZiara za Wajumbe

53

90

Sura ya 288 kif.45(1)

JEDWALI LA PILILimetungwa Chini ya kanuni ya 71 (a

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KIAPO CHA DIWANI

Mimi ………………………………...... naapa/natamka kwa dhati kwamba

nitaitumikia Halmashauri ya Manispaa Kigamboni kwa wadhifa wangu wa

Udiwani na kwamba nitahifadhi, nitalinda na kutetea, Katiba ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, Sheria za Tanzania, Maadili ya Madiwani na Kanuni za

Kudumu za Halmashauri kama zilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na kwamba

74

Page 75: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

nitaitumikia Halmashauri ya Manispaa Kigamboni kwa uaminifu, kwa uwezo na

moyo wangu wote.

(Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie)

Kiapo/Tamko hili limetolewa hapa; ………………………………………

Na……………………………………………………………………………..

Leo tarehe…………………… Mwezi wa…………………..20……….

Mbele ya:………………………………………..

Jina:………………………………………………

Cheo:…………………………………………….

Saini:……………………………………………

Anuani………………………………………….…………………………………..

JEDWALI LA TATULimetungwa Chini ya kanuni ya 71(b)

HAKIMU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU

RASILIMALI NA MADENI

(Kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi waUmma)

Mimi……………………………………………………………….………………Anuani; …………………… baada ya kuchaguliwa/kuteuliwa na kuapishwa katikawadhifa wa…….……...tarehe……………………….mwaka 20……. Ninatamkarasmi na kwa moyo mnyofu kwamba hadi sasa nina rasilimali na madeniyafuatayo:-

(1) Fedha taslimu, Amana katika benki au taasisi ya fedha; taja namba yaakaunti, benki au taasisi ya fedha na kiasi:……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….…………2) Hawala za Hazina (Treasury Bills) na dhamana nyingine maalum:-

75

Page 76: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..…………………….........................................................................

3) Faida ya akiba, mafungu ya mgawanyo wa faida zinazotokana na hisa n.k.…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………..

4) Nyumba au majengo ya kupangisha, taja mahali yalipo na ukubwa au eneo:……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………….

* Rasilimali zinazotakiwa ni pamoja na zifuatazo, ambazo ni zako binafsi, zamume/mke au watoto wadogo wasiooa au kuolewa wa Kiongozi wa Umma.

(a) Fedha taslimu na amana katika Benki au Taasisi nyingine ya fedha.

(b) Hawala za Hazina Treasury Bills) na nyinginezo za dhamana maalumzinazotolewa au kudhaminiwa na Serikali au vyombo vya Serikali.

(c) Faida itokanayo na fedha iliyowekwa akiba Benki, Chini ya Ujenzi au Taasisinyingine ya fedha.

(d) Mgao wa fedha kutokana na fungu la rasilimali ya Kampuni (Stocks) au hisaza Kiongozi wa Umma katika Kampuni au Shirika lolote.

(e) Maslahi katika chombo cha biashara kisichokuwa na mkataba na Serikali,na kisichokuwa na au kisichotawala amana zinazouzwa bayana na vyombo vyaumma.

(f) Mashamba ya kibiashara.

(g) Mali halisi zisizohamishika ambazo si rasilimali zisizotakiwa kutajwa; na

(h) Rasilimali zinazoleta faida, ambazo si rasilimali zisizotakiwa kutajwa naambazo zinamilikiwa kwa mbali.

(5) Mashamba ya kibiashara, mifugo, madini n.k.…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….......................................................................(6) Magari na aina nyingine za usafiri wa kibiashara;…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….......................................................................(7) Mashine za kusaga nafaka, viwanda na shughuli nyingine za kibiashara aumitambo:

76

Page 77: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….........................................................................................(8) Rasilimali nyinginezo au maslahi ambayo kiongozi wa umma anapendakutaja:…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….......................................................................(9)Madeni;……………………………………………………………………………………………………………………………………………………….......................................................................Tamko hili linatolewa na kusainiwa mbele yangu………………………………………………………….........................................na (mtoa tamko)……………………………………….......................................ninayemfahamu binafsi, au aliyetambulishwa kwangu na………………………………………………………………….............................….…………........................................................................................................ambaye ninamfahamu leo tarehe ………………………….........Mtoa tamko Mwezi wa …………………………………………………….............................saini……………………………………………………………Wadhifa:………………………………………………………Anuani:……………………………………………………….………………………………………………………………….(Tamko hili lazima litolewe mbele ya Kamishna wa Viapo)

KWA: KAMISHINA WA MAADILI, SEKRETARIETI YA MAADILI,S.L.P 13341,DAR ES SALAAM.

Nembo ya Halmashauri ya Manispaa Kigamboni imebandikwa kwenye hiziKanuni za Kudumu kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano waHalmashauri uliofanyika mnamo tarehe 31 Januari, 2018 mbele ya:-

STEPHEN E. KATEMBA

Mkurugenzi,Halmashauri ya Manispaa Kigamboni.

MAABAD SULEIMAN HOJA

Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa Kigamboni.

77

L.S

Page 78: KANUNI ZA KUDUMU - HALMASHAURI YA MANISPAA YA …

Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa KigamboniTangazo la Serikali Na. 310 (linaendelea)

NAKUBALI

DODOMA, MHE. SELEMANI S. JAFO (MB) 07 Juni, 2018 Waziri Wa Nchi/OR Tamisemi.

78


Recommended