View
22
Download
0
Category
Preview:
Citation preview
BULLETIN
ambapo mkoa wa Kagera umeweza kuleta Skauti wapatao 186 na mkoa wa
Kilimanjaro 125 hii ni kwa mujibu wa Kamishna wa Skauti wa Mkoa huo.
Akielezea sababu zilizopelekea wao kuweza kuleta Skauti wengi zaidi Padri
Prochesus Mtungi ambaye pia ni Kamishna wa Skauti mkoa wa Kagera
alisema kuwa na ushirikiano mzuri na umoja walionao kati ya viongozi wa
Skauti wa Skauti mkoani Kagera kwa usimamizi mzuri wa watoto na vijana
mashuleni.
Hongera Mama Afrika katika kum-
bukumbu ya siku ya kuzaliwa
kwako.
Rashidi (kushoto) na Helena (kulia)
(kibaha- Pwani) wakiwa Skauti Pr-
Lab studio kwa mahojiano.
Picha na: Sassi Salim na Fransco
Nyoni
Je…
Wajua siri ya Skauti
Kutoka Mbeya na Pikipiki hadi
Dodoma..?
Skauti PR Lab wakiweka
mabango mjini Dodoma.
Samina Rajab na Devina Adosi
SKAUTI WAMIMINIKA DODOMA
Skauti Morogoro na Mbeya
waweka historia
Kagera watiafora
Katika hali ya kufurahisha na ku-
washangaza wengi Skauti wameamua
kuweka historia ya aina yake hapa Tan-
zania ambayo haijawahi kutokea. Skauti
hao ambao wamedhaminiwa na Mkuu
wa Morogoro pamoja na SAT
(SUSTAINABLE AGRICULTURE TANZANIA)
hawakusita kuonyesha furaha yao na
shahuku waliyonayo ya kutaka kuanza
na kumaliza safari yao ili lengo lao la
Ujasiri liweze kutimia na kuweka historia
ya kipekee ambayo haijawahi kutokea
katika Skauti hapa nchini.
Akizungumza na Pr Lab Tanzania
kiongozi wa watembea kwa miguu
kutoka Morogoro hadi Dodoma Rova
Aloyce Zengwe ambaye pia ni askari
wa jeshi la ukoaji na zimamoto Tanza-
nia alisema kuwa ujumbe ambao wal-
ikabidhiwa na Dkt. Steven Kabwe
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kupitia
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania ni kupiga vita mimba za
utotoni,kupambana na kuzuia rush-
wa,kupambana na madawa ya
kulevya,kutoa elimu ya kilimo endele-
vu kilimo ambacho hakitumii dawa
wala mbolea zenye kemikali na kutoa
elimu juu ya kuwafichua wahalifu.
Naye Rova Allen J. Mpande alisema
kuwa” Kila kitu kinahitaji uthubu-
tu,huwezi kufanya jambo bila kuthubu-
tu,hii sherehe ya Skauti wote,hivyo
tunapaswakufanya yale yanayoweze-
kana kufanywa kwa wakati huu ili jamii
na Tanzania nzima ijue kuwa
tunaazimisha miaka 100 ya Skauti”
Skauti hawa wamefika Dodoma
tarehe 21 mwezi Julai 2017 na
wametembea umbali wa kilomita
264.4.
Wakati huo huo ndugu Nsubili Solo-
mon Kibopile kiongozi wa Skauti St.
Mary International Mbeya na Kaimu
naibu kamishna wa Skauti Mkoa wa
Mbeya. Aliamua kutumia usafiri wa
pikipiki kutoka wilaya ya Kyela Mkoa
wa Mbeya hadi Dodoma iwe moja ya
historia na kuweka kumbukumbu hasa
wakati huu wa kuadhimisha miaka 100
ya Skauti Tanzania. Changamoto am-
bazo amekutana nazo njiani ni pamoja
na kuwa baadhi ya madereva wengine
hawapo makini barabarani, wakati wa
usiku kulikuwa na tatizo kidogo hasa
kwenye maeneo ambayo yana
mashimo, ama madereva wengine
kuwasha taa na kuweka mwanga
mkali wakati wa usiku ama mwanga
mdogo sana. Umbali aliotumia kutoka
Kyela hadi Mbeya ni kilomita 124,
Mbeya hadi Iringa kilomita 340 na
Iringa hadi Dodoma ni kilomita 260
jumla ametumia kilomita 724.
Tusiwe waoga tuwe wajasiri kama
alivyotembea yeye mchana na usiku
na kuweza kutoa huduma mbali mbali
njiani, pia wasiokuwa Skauti wajiunge
na Skauti kwani ndugu Kibopile ana
amini Skauti imemjengea ujasiri na
uthubutu huu. Aliondoka Kyela tarehe
20 Julai 2017 na kufika Dodoma
tarehe 21 Julai 2017 saa kumi nambili
jioni. Katika safari hiyo aliongozana na
Skauti mwingine anayejulikana kwa
jina la Ayubu. Skauti wengine wakuto-
ka Mbeya wanakuja kwa basi na wa-
tawasili siku ya tarehe 22 julai 2017
(mapema leo).
Wakati huo huo Skauti kutoka Mkoa
wa Kagera na Kilimanjaro wametiafora
kwa kuleta Skauti wengi Zaidi ukilin-
ganisha na Skauti wa mikoa mingine,
PR LAB
UKIWA NA HABARI ZA
SKAUTI, TAFADHARI WASILI-
ANA NA KITENGO CHA MA-
HUSIANO NA UMMA (PR
LAB) SKAUTI TANZANIA
+255-789-012-364
TUMA HABARI NA PICHA ZA
MATUKIO YA SKAUTI PO-
POTE TANZANIA.
tanzaniascout.org
Recommended