View
7
Download
0
Category
Preview:
Citation preview
i
UTAYARI WA WAKENYA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERA
YA LUGHA YA KISWAHILI KAMA LUGHA RASMI NCHINI
KENYA
KAUNTI YA NAIROBI.
NA
KIIO MARY MUENI
TASNIFU HII IMETOLEWA KUTOSHELEZA BAADHI YA
MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA CHUO
KIKUU CHA KENYATTA
NOVEMBA, 2017
ii
iii
TABARUKU
Kazi hii ninaitabarukia baba yangu mzazi Joseph Musyimi, mama yangu Jennifer
Kiio. Nawashukuru kwa kunihimiza na kunitia moyo niendelee na shahada hii ya
uzamili. Kwa ndugu zangu Emanuel Mutiso na David Musyimi nawasihi msome
kwa bidii.
iv
SHUKRANI
Mwanzo kabisa, ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye
ameniwezesha na kunipa nguvu katika kufanikisha kazi hii yangu.
Shukrani nyingi ni kwa wasimamizi wangu Prof, Ireri Mbaabu na Dkt Onyango
kwa juhudi zao katika kunisimamia, kuisahihisha na kunielekeza kila nilipohitaji
kuelekezwa , hadi kazi hii ikafikia upeo wa juu, na kunipa moyo ulioniwezesha
kuifanya kazi hii kwa subira kubwa.
Ningependa kukishukuru Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa jumla na hasa Idara ya
Kiswahili na lugha za Kiafrika kwa ushirikiano mzuri ulioniwewzesha
kufanikisha kazi hii.
Shukrani zangu maalum ni kwa wahadhiri wangu walionifunza Kiswahili katika
Chuo Kikuu cha Kenyatta. Wote nawapa tahania kwa kunielekeza kwa njia
ambayo imeniwezesha kupiga hatua kubwa katika umilisi wa lugha ya Kiswahili
Mwisho ni kwa walionisaidia kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha kazi
hii kukamilika Mwendwa Stephen na Samuel Mbogo. Asanteni kwa usaidizi
wenu.
v
IKISIRI
Utafiti huu ulijikita katika kutathmini utayari wa Wakenya katika utekelezaji wa
sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya. Utafiti ulilenga
wakaazi wa mji wa Nairobi hasa katika ofisi za shughuli za kiutawala na vyombo
vya habari vinavyopatikana humo. Utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha ya
Kiswahili umeathiriwa na mambo mbalimbali. Baadhi ya mambo hayo ni kama
vile: hadhi ambayo lugha hii imepewa, manufaa ya lugha hii miongoni mwa
athari nyingine. Malengo ya utafiti huu yalikuwa; kubaini iwapo kuna utayari
katika kutekeleza sera ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi. Na namna utayari
huu utakavyosaidia katika kuimarisha sera hii mpya ya lugha ya Kiswahili hasa
katika urasmi wake, kuchunguza changamoto zinazokabiliwa katika shughuli za
kiutawala na vyombo vya habari kuhusu hadhi mpya ya lugha ya Kiswahili na
mwisho kutambua ni vipi utayari wa utekelezaji katika sera hii unavyoweza
kutekelezwa ili kuweza kufanikisha lengo lake la kuwa lugha rasmi. Utafiti huu
ulitumia mitazamo miwili ya upangaji wa lugha. Tulizingatia upangaji lugha
kihadhi ambao huzingatia juhudi zinazochukuliwa ili kubadilisha matumizi na
majukumu ya lugha katika jamii na mtazamo wa upangaji lugha kifahari
unaolenga kutoa mielekeo chanya ya kisaikolojia ambayo ni muhimu ikiwa
kutakuwepo na ufanisi wa muda mrefu katika upangaji lugha. Utafiti huu
uliongozwa na Nadharia ya Utekelezaji iliyoasisiwa na Spencer (1971). Utafiti
wa kina nyanjani ulifanywa ili kubaini ni changamoto zipi ambazo zinakumba
utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi. Mtafiti
alitumia sampuli finyu ili kupata matokeo bora zaidi. Data ilikusanywa nyanjani
kwa kutumia hojaji na mahojiano ili kubaini mambo yanayohusu utayari wa
utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili hasa baada ya lugha hii kufanywa
lugha rasmi. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia programu ya SPSS.
Kutokana na matokeo ya utafiti ilidhihirika kuwa hakuna usawa katika matumizi
ya lugha yaKiswahili na ile ya Kiingereza. Utafiti ulionyesha kuwa lugha ya
Kiswahili ilitumika sana katika idara ya polisi, Kiingereza kilitumika sana katika
vyombo vya habari. Hata hivyo, ni bora wabunge wapitishe miswada
inayohusiana na lugha ya Kiswahili ili iwe sheria. Utafiti huu utasaidia wadau
wanaohusika na maswala ya sera ya lugha na kuweka mikakati ya kuhakikisha
kuwa inatekelezwa. Mapendekezo yaliyofanywa na mtafiti yakizingatiwa na
kutekelezwa, hadhi ya lugha ya Kiswahili itaweza kuwa bora katika sekta
zilizofanyiwa utafiti kwa nchi nzima kwa ujumla.
vi
YALIYOMO
UNGAMO ......................................................................................................... ii
TABARUKU .................................................................................................... iii
SHUKRANI ..................................................................................................... iv
IKISIRI ............................................................................................................. v
YALIYOMO .................................................................................................... vi
MAJEDWALI ................................................................................................. ix
VIELELEZO .................................................................................................... x
UFAFANUZI WA ISTILAHI NA VIFUPISHO ............................................ xi
SURA YA KWANZA ....................................................................................... 1
UTANGULIZI .................................................................................................. 1
1.1 Usuli wa Mada .......................................................................................... 1
1.2 Suala la Utafiti .......................................................................................... 7
1.3 Maswali ya Utafiti .................................................................................... 8
1.4 Malengo ya Utafiti .................................................................................... 8
1.5 Upeo na Mipaka ....................................................................................... 9
1.6 Sababu za Kuchagua Mada ....................................................................... 9
1.7 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada ................................................................. 10
1.8 Misingi ya Nadharia ............................................................................... 17
1.9 Mbinu za Utafiti ..................................................................................... 21
1.9.1 Eneo la Utafiti .................................................................................. 22
1.9.2 Uteuzi wa Sampuli ........................................................................... 22
1.9.3 Ukusanyaji wa Data ya Utafiti.......................................................... 23
1.9.4 Uchanganuzi na Uwasilishaji wa Data .............................................. 24
1.9.5 Hitimisho ......................................................................................... 25
vii
SURA YA PILI ............................................................................................... 26
HISTORIA YA UTAYARI WA WAKENYA KUHUSU URASMI WA
LUGHA YA KISWAHILI NCHINI KENYA. .............................................. 26
2.1 Kipindi cha Ukoloni ............................................................................... 26
2.1.1 Kipindi cha Kabla ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ........................ 26
2.1.2 Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ........................................ 28
2.1.3 Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia .......................................... 29
2.2 Kipindi cha Baada ya Ukoloni ................................................................ 32
2.2.1 Shughuli za Kiutawala ..................................................................... 33
i) Sekta ya Umma ..................................................................................... 33
ii) Vyombo vya Habari ............................................................................. 37
2.3 Hitimisho ................................................................................................ 38
SURA YA TATU ............................................................................................ 39
UTAYARI WA WAKENYA KATIKA SERA MPYA YA KISWAHILI .... 39
3.0 Utangulizi ............................................................................................... 39
3.1 Uchanganuzi wa kauli za utayari wa Wakenya katika sera mpya ya
Kiswahili katika............................................................................................ 39
kuimarisha lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi. ........................................ 39
3.2: Kuimarika kwa Lugha ya Kiswahili ....................................................... 51
3.3 Muhtasari ............................................................................................... 59
SURA YA NNE ............................................................................................... 60
CHANGAMOTO NA MIKAKATI YA KUIMARISHA SERA HII MPYA
YA LUGHA YA KISWAHILI ....................................................................... 60
4.0 Utangulizi ............................................................................................... 60
4.1 Changamoto zinazowakabili wafanyikazi katika sekta zilizozingatiwa
katika utafiti ................................................................................................. 61
katika sera mpya ya Kiswahili kuwa lugha rasmi. ......................................... 61
4.2 Mikakati ya kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bora katika sekta
zilizotafitiwa ili ............................................................................................ 67
kukabiliana na changamoto zinazozuia kiwango kinachohitajika .................. 67
4.3 Muhtasari ............................................................................................... 73
viii
SURA YA TANO ............................................................................................ 74
HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ............................................................. 74
5.0 Utangulizi ............................................................................................... 74
5.1 Muhtasari wa Utafiti ............................................................................... 74
5.2 Matokeo ya utafiti ................................................................................... 75
5.2.1 Lengo la kwanza ............................................................................ ..75
5.2.2. Lengo la pili .................................................................................... 76
5.2.3 Lengo la tatu .................................................................................... 77
5.2.4. Lengo la nne ................................................................................... 78
5.3 Matatizo ................................................................................................. 80
5.4 Mapendekezo ya Utafiti .......................................................................... 80
5.5 HITIMISHO ........................................................................................... 82
MAREJELEO ................................................................................................ 83
KIAMBATISHO CHA A: Hojaji .................................................................. 88
KIAMBATISHO CHA B: Mwongozo wa Mahojiano................................... 93
ix
MAJEDWALI
Jedwali 3.1.1: Lugha ambayo wafanyikazi wanapenda kuitumia sana katika
mawasiliano ya kimaongezi ...................................................................... 40
Jedwali 3.1.2 : Sababu zinazowafanya kutumia Kiswahili ......................... 42
Jedwali 3.1.3: Sababu zinazowafanya kutumia lugha ya Kiingereza .......... 43
Jedwali 3.1.4: Matumizi ya lugha ya Kiswahili kabla ya kuidhinishwa kwa
katiba mwaka wa 2010 ............................................................................. 45
Jedwali 3.1.5: Mabadiliko ya utekelezaji wa sera hii baada ya kuidhinishwa
kwa katiba ................................................................................................ 47
Jedwali 3.1.6: Sababu za waliosema kuwa hakuna mabadiliko ya sera ya
lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ........................................................ 50
Jedwali 3. 2. 1: Sera mpya ya Kiswahili huimarisha hadhi yake ya kirasmi51
Jedwali 3.2.2: Sababu zinazofanya Kiswahili kuimarika kama lugha rasmi
................................................................................................................. 53
Jedwali 3.2.3: Sababu zinazofanya Kiswahili kutoimarika kama lugha rasmi
................................................................................................................. 55
Jedwali 3.2.4: Pendekezo la njia moja nzuri ambayo inaweza kufanya
Kiswahili kikubalike kama lugha rasmi ................................................... 57
Jedwali ya 4.1.1: Iwapo kuna sheria ambazo zimefanya Kiswahili kutofikia
kiwango kinachohitajika ........................................................................... 61
Jedwali ya 4.1.2: Changamoto zinazokumba lugha ya Kiswahili kuhusu
hadhi mpya ya Kiswahili katika sekta zilizotafiwa .................................... 64
Jedwali 4.1.3: Sababu zinazofanya Kiswahili bado kutofikia hadhi yake ya
kuwa rasmi na nini kilichochangia kutokuwepo na ukamilifu wa utayari wa
Wakenya .................................................................................................. 66
Jedwali 4.2.1: Njia ambazo zinawekwa katika kukipa Kiswahili nafasi yake
kwa mujibu wa katiba wa Katiba 2010 ..................................................... 68
Jedwali 4.2.2: Mapendekezo ya vile Kiswahili kinaweza kutekelezwa ili
kufanikisha lengo lake la kuwa lugha rasmi .............................................. 70
Kauli 4.2.3: Pendekezo moja muhimu kwa serikali kuhusiana na matumizi
ya lugha ya Kiswahili kufikia lengo linalohitajika. .................................... 72
x
VIELELEZO
Chati 3.1.1: Lugha inayotumiwa sana na wafanyikazi katika mawasiliano ya
kimaongezi ………………………………………………………….................. 40
Chati 3.1.2: Sababu za kutumia Kiswahili............................................................42
Chati 3.1.3: Sababu za kutumia lugha ya Kiingerez.............................................44
Chati 3.1.4: Matumizi ya Kiswahili kabla ya kuidhinishwa kwa katiba mwaka wa
2010 ……………………………………………………………………………..46
Chati 3.1.5: Mabadiliko ya sera hii baada ya kuidhinishwa kwa katiba mwaka wa
2010.......................................................................................................................48
Chati 3.2.1: Sera mpya ya Kiswahili huimarisha hadhi yake ya
Kiswahili………………………………………………………………………...52
Chati 3.2.2: Sababu za Kiswahili kuimarika kama lugha rasmi...........................53
Chati 3.2.3: Sababu za Kiswahili kutoimarika kama lugha rasmi........................55
Chati 3.2.4: Mapendekezo ya kukifanya Kiswahili kikubalike kama lugha rasmi
...............................................................................................................................57
Chati 4.1.1: Sheria zinazofanya Kiswahili kutofikia kiwango kinachohitajika....62
Chati 4.1.2: Changamoto zinazokumba lugha ya Kiswahili katika sekta
zilizotafitiwa..........................................................................................................64
Chati 4.2.1: Mikakati ya kukipa Kiswahili nafasi yake kwa mujibu wa Katiba..68
Chati 4.2.2: Mapendekezo ya vile Kiswahili kinaweza kufanikisha lengo la kuwa
lugha rasmi............................................................................................................71
xi
UFAFANUZI WA ISTILAHI NA VIFUPISHO
Lugha rasmi- Ni lugha ambayo hutumika katika miktadha rasmi ili kuwasiliana
kwa mfano katika shughuli za kiutawala kama vile bunge.
ITLC- Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki (Inter Territorial Language
Committee)
Sera ya lugha- mpango wa serikali kuhusu matumizi ya lugha nchini.
SPSS- Statistical Package for the Social Sciences. (Mtindo Changanuzi wa
Tarakimu Sayansi).
i
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.1 Usuli wa Mada
Sera ya lugha ni maamuzi katika maandishi kuhusu jinsi lugha zinavyopaswa
kutumika katika jamii ili kutekeleza majukumu mbalimbali. Kwa majibu wa
Mbaabu (1996) ni sera ya umma. Madhumuni ya utafiti huu ni kujadili utayari wa
Wakenya katika utekelezaji waKiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya: Kaunti
ya Nairobi. Mekacha (2011) anasema kuwa sera ya lugha huwa ni kipengele
kimojawapo cha mpango-lugha. Dhana hizi huingiliana sana na wakati mwingine
si rahisi kuzitofautisha. Ni jumla ya mawazo, matamko, sheria, kanuni na taratibu
zenye kuelezea taratibu za utekelezaji wa mabadiliko ya nafasi na matumizi ya
lugha katika jamii.
Aidha, katika mawasiliano na shughuli zote za jamii, sera ya lugha huelekeza
shughuli za kiutawala, elimu na vyombo vya habari. Nchini Kenya, lugha ya
Kiswahili imekuwa ikitumika kama lugha ya taifa kwa mujibu wa serikali, na
ilifanywa lugha rasmi mnamo mwaka wa 2010 (Katiba ya Kenya , 2010).
Kaplan na Balauf wakinukuliwa na Mekacha (2011) wanaziita sera
zilizotayarishwa kwa namna ya maandishi kuwa “ sera halisi” na zile ambazo ni
jumla tu ya matamko, kauli na nyaraka kuwa sera za “kiishara” kwa vile zipo tu
kama ishara ya kukidhi matakwa ya kisiasa. Naye Bamgbose (1991) anadai kuwa
‘sera za lugha’ katika nchi nyingi za Kiafrika ni za kiishara na zimebakia kuwa
matamko au maazimio ya nia ya kufanya mabadiliko lakini ambayo
hayatekelezwi. Mfano, nchini Kenya Kiswahili kimefanywa kuwa rasmi sawia na
2
Kiingereza lakini hakijapewa hadhi inayostahili katika maeneo mbalimbali: barua
rasmi na mihadhara rasmi,
Sera ya lugha ya Kiswahili nchini Kenya imekuwa ikipitia mabadiliko tangu
ukoloni. Baada ya uhuru, sera hiyo pia ilitiliwa mkazo na rais wa kwanza wa
Kenya. Kwa mujibu wa Mbaabu (1978) mnamo mwezi wa Agosti mwaka wa
1969, Rais wa Kenya Mhe. Jomo Kenyatta anaeleza kuwa Kiswahili kitakuwa
lugha rasmi ya Taifa la Kenya. Alisema kwamba Kiswahili kitatumika katika
Bunge la Kenya kwa sababu ndiyo lugha ya wananchi. Lugha hii ilianza
kutumika kama lugha rasmi katika majadiliano ya Bunge mwaka wa 1975. Jambo
hili lilipingwa na watu wengi kwa kudai kuwa Kiswahili hakina maneno ya
kutosha ya sayansi na ufundi na kuwa hakifai kuwa lugha rasmi ya Taifa la
kisasa. Hivyo, utayari wa utekelezaji wake haukufanywa kama ilivyotarajiwa
hivyo kutochukua nafasi iliyostahili. Ni dhahiri wapinzani hawa walikwepa
ukweli kuwa lugha ina uwezo wa kukua na kama ingeungwa mkono tangu wakati
huo ingetumika kihadhi sawa na lugha ya Kiingereza.
Sera ya lugha ya Kiswahili iliongozwa na mapendekezo ya Tume mbalimbali
zilizoteuliwa kuchunguza masuala yanayohusu Kiswahili. Tume ambayo
ilichangia pakubwa katika kuendeleza lugha ya Kiswahili ni tume ya Mackay ya
1981. Tume hii ilipendekeza kuanzishwa kwa chuo cha pili nchini na Kiswahili
kifundishwe chuoni kama somo la lazima. Somo hili pia lilipaswa kusomeshwa
katika shule za msingi na za upili, (Mbatiah, 2012). Haya yalitokana na
uchunguzi kuwa wanafunzi wengi hawakuweza kujieleza kwa ufasaha katika
3
lugha ya taifa. Pendekezo hili liliafikiwa pale ambapo, Chuo cha pili nchini cha
Moi kilianzishwa pamoja na idara ya Kiswahili mwaka wa 1987.
Katika mwaka wa 2010, tume ya mabadiliko ya katiba ilichangia pakubwa katika
kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi hasa baada ya kuidhinishwa kwa katiba
mpya. Shitemi (2011) anaeleza kuwa, tangazo la Kiswahili kuwa lugha ya
kwanza rasmi na lugha ya taifa, linahitaji kuwekwa katika vitendo vya kimitaala,
kiutendaji, kiuwezeshaji na pia katika asasi zote za kutumia lugha. Hii ni
kumaanisha kuwa bado Kiswahili hakijaweza kukita mizizi katika hadhi yake ya
kuwa lugha rasmi, hivyo, utayari miongoni mwa watu kutumia lugha hii
haudhihiriki.
Hata baada ya kuwepo kwa mabadiliko kadhaa katika sera ya lugha ya Kiswahili
bado watu wengi wanaipuuza na kuiona kama lugha ya kiwango cha chini.
Katika shule za msingi wanafunzi wasisitiziwa kutumia lugha ya Kiswahili katika
maongezi yao. Siku ya ijumaa ndiyo siku imetengwa kama siku ya kuzungumza
lugha ya Kiswahili. Lugha hii haitumiki katika hadhi sawa na lugha ya
Kiingereza. Katika baadhi ya shule kuna sheria kwamba wanafunzi hawapaswi
kuzungumza lugha ya Kiswahili hivyo wanazungumza lugha ya Kiingereza
pekee. Hali hii huwalazimu wanafunzi kuwa na mazoea ya kuongea lugha ya
Kiingereza na kuona lugha ya Kiswahili kwamba haina umuhimu wowote. Hali
hii inawanyima wanafunzi fursa ya kujifunza lugha ya Kiswahili. Hata hivyo,
kwa upande mwingine wanafunzi wengi wanaosomea katika vyuo vikuu hasa
katika somo la Kiswahili, hawapendi kuwasiliana kwa lugha hii.
4
Hali hii si tofauti hasa tukiangazia katika shughuli za kiserikali na vyombo vya
habari. Katika shughuli za kiserikali hasa ofisini za umma, lugha ya Kiingereza
ndio imetumika kwa kina. Wakati unapoenda katika ofisi hizi na kujieleza katika
lugha ya Kiswahili, huenda usishughulikiwe ikilinganishwa na mtu ambaye
anatumia lugha ya Kiingereza. Ni ofisi chache mno ambazo unaweza
ukazungumza lugha ya Kiswahili na kuhudumiwa, mfano ni katika idara ya
polisi, pale ambapo lugha ya Kiswahili inatumika zaidi kuliko lugha ya
Kiingereza. Katika sikukuu ya taifa ya Madaraka, tarehe 1/06/2015 Rais wa
Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta alitoa hotuba yake kwa muda mrefu sana
katika lugha ya Kiingereza na ilibidi wananchi kumwambia azungumze lugha ya
Kiswahili. Hili ni dhihirisho kuwa ingawa kikatiba lugha ya Kiswahili ni lugha
rasmi, haizingatiwi kuwa hivyo sawa na lugha ya Kiingereza.
Katika vyombo vya habari, ni dhahiri kwamba taarifa ya habari na baadhi ya
mijadala huendelezwa katika lugha ya Kiingereza kwa wakati mwingi. Kwa
mfano ukiangalia muda unaotumika katika kusoma taarifa ya habari katika
runinga ‘Citizen Nipashe’ kwa lugha ya Kiswahili si mwingi ukilinganishwa na
taarifa ya lugha ya Kiingereza. Kisha katika magazeti, magazeti mengi yanatumia
sana lugha ya Kiingereza. Ni gazeti la “Taifa Leo” pekee ambalo ni la Kiswahili.
Hivyo, ni dhahiri kuwa bado lugha ya Kiswahili haipo katika hadhi sawa na
lugha ya Kiingereza.
Maoni ya wataalamu kama vile King’ei (2010) na Mukhwana (2008) ni kwamba
sera ya lugha nchini Kenya imekuwa na utata tangu nyakati za ukoloni (1895-
1963). Wanaeleza kwamba, kukwezwa kwa Kiingereza juu ya lugha zote nchini
5
Kenya ni hali inayoendelea kutinga maendeleo ya Kiswahili na lugha nyingine
asilia hasa kupitia sera ya lugha katika sekta ya elimu, vyombo vya habari na
shughuli za Kiserikali. Wanajamii basi wamekuwa wakikionea fahari Kiingereza
kama lugha inayoweza kuwaletea ufanisi wa kikazi katika jamii. Kulingana na
Mukhwana (2008) hii ni kwa sababu kutoka nyakati za ukoloni, lugha ya
Kiingereza imenasibishwa na elimu bora ambapo elimu bora kwa wengi ni daraja
ya kupata ajira nzuri.
Maoni ya Mirianga (2014) yanabainika kuwa, Wakenya wengi hasa waliosoma
hupendelea na kuonea fahari matumizi ya lugha ya Kiingereza hasa katika
miktadha rasmi, huku wakipuuza lugha ya Kiswahili. Ili matumizi ya lugha ya
Kiswahili kutekelezwa , ni muhimu kuipa nafasi nzuri katika mfumo wa elimu na
shughuli za kiutawala. Ni muhimu pia kuondoa dhana kuwa, lugha ya Kiswahili
ni lugha ya kiwango cha chini, dhana iliyoenezwa na sera ya lugha ya wakoloni
nchini Kenya na kuangamiza matumizi ya lugha ya Kiswahili.
Kulingana na Mbatiah (2012), baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya
Mzee Jomo Kenyatta kutoa agizo Kiswahili kiwe lugha ya taifa nchini na iwe
lugha ya bungeni, jambo hili lilinuia kukipa Kiswahili hadhi ya kuwa lugha ya
taifa kikatiba. Hata hivyo, hili halikutekelezwa ipasavyo. Ngigge (2014)
akimnukuu Mohochi (2011) anaeleza kuwa tume ya marekebisho ya katiba
nchini Kenya ilipendekeza Kiswahili kuwa lugha rasmi na pia kuwa lugha ya
taifa. Kuidhinishwa kwa katiba mwaka wa 2010 kulikifanya Kiswahili kuwa
lugha rasmi na pia kuwa lugha ya Taifa. Baada ya mabadiliko hayo mtafiti alitaka
kubaini, iwapo kuna utayari wa kutekeleza mabadiliko haya ipasavyo kwa
6
kuangazia vyombo vya habari na shughuli za kiutawala ambavyo ni viungo
muhimu katika kuangazia sera ya lugha.
Kwa mujibu wa Mirianga (2014) kuteuliwa kwa lugha ya Kiswahili kama lugha
ya taifa na kuongezewa jukumu la kuwa lugha rasmi sambamba na Kiingereza
kutasaidia lugha hii kutumika katika nyanja tofauti tofauti nchini Kenya. Jambo
hili pia litasaidia katika ukuaji na ustawi wa lugha hii, ili kuwezesha haya
yatekelezwe, sharti kuwepo utayari miongoni mwa watu ili kutekeleza sera hii
ipasavyo.
Hivyo, kutokana na maelezo ya wataalamu hawa, ni wazi kuwa utayari wa
kuitekeleza sera hii sharti uzingatiwe kwa kuwa bado sera hii haijakita mizizi
ipasavyo ikilinganishwa na lugha ya Kiingereza ambapo lugha hizi zapaswa
kuwa katika hadhi moja. Imebainika wazi kuwa katika miktadha mingi ya shule,
shughuli za kiutawala na hata katika vyombo vya habari bado lugha ya Kiswahili
haitekelezwi ipasavyo na hivyo bado Kiingereza kinaenziwa zaidi.
Ufahamu na ukubalifu kuhusu majukumu yaliyopewa lugha ya Kiswahili kuwa
lugha rasmi, nchini Kenya kama inavyojitokeza katika Katiba ya Kenya ni swala
muhimu. Ni kutokana na majukumu haya mapya na hadhi yake mpya, ambapo
mtafiti alichunguza ili kubaini kama kuna utayari wa kutekeleza sera hii au la, na
kuchunguza ni matatizo yepi yanayokumba utayari wa Wakenya katika
utekelezaji huo na kisha changamoto zinazokumba shughuli za kiutawala na
vyombo vya habari katika kutekeleza Kiswahili kama lugha rasmi kama
ilivyoidhinishwa kikatiba.
7
1.2 Suala la Utafiti
Utafiti huu ulichunguza sera ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya na
utayari wa Wakenya katika utekelezaji unavyodhihirika, iwapo inapewa hadhi
yake ya urasmi kama inavyobainika katika katiba iliyopitishwa mwaka wa 2010
au la. Mtafiti alifanya utafiti wa kina ili kubaini iwapo sera hii ya Kiswahili kuwa
lugha rasmi inafuatwa ipasavyo na iwapo watu wapo tayari kuimudu hali hii.
Alichunguza jinsi utekelezaji wake unavyoathiriwa katika shughuli za kiutawala
na vyombo vya habari. Pia alichunguza changamoto zinazokabili utayari wa watu
katika utekelezaji wa sera hii katika nyanja hizi.
Nchini Kenya lugha ya Kiswahili imekuwa ikitumika kama lugha ya Taifa kwa
miaka mingi sasa. Baada ya kuidhinishwa kwa katiba mwaka wa 2010, lugha ya
Kiswahili ilipata hadhi mpya ya kuwa lugha rasmi. Kwa kuzingatia hali ilivyo
sasa lugha ya Kiswahili ni maarufu katika miktadha isiyo kuwa rasmi miongoni
mwa wanasiasa kwani wao hutumia lugha hii kwa mikutano yao lakini lugha hii
bado haijapokelewa vyema kama lugha rasmi na hivyo utafiti huu ulinuia kubaini
utayari wa Wakenya katika matumizi ya Kiswahili kama lugha rasmi. Hii ni kwa
kuwa lugha ya Kiswahili imekuwa ikipuuzwa nchini Kenya na hadhi yake ya
kuwa lugha rasmi kama ilivyo katika katiba haizingatiwi kwa kina. Utayari huu
una umuhimu upi hasa katika urasmi wake kisha ni vipi utayari katika sera hii
mpya ya lugha ya Kiswahili unavyoweza kutekelezwa ili kuweza kufanikisha
lengo lake la kuwa lugha rasmi. Utafiti huu ulichunguza jinsi utayari wa
Wakenya hasa wakaazi wa Nairobi ulivyo katika matumizi ya Kiswahili katika
shughuli za kiutawala na vyombo vya habari.
8
1.3 Maswali ya Utafiti
i) Je, kuna utayari katika kutekeleza sera ya Kiswahili kuwa lugha rasmi?
ii) Utayari huu utasaidiaje katika kuimarisha lugha ya Kiswahili hasa katika
urasmi wake?
iii) Je, ni changamoto zipi zinazokabiliwa katika shughuli za kiutawala na
vyombo vya habari
kuhusu hadhi mpya ya Kiswahili?
iv) Je, ni vipi utayari huu katika sera hii mpya ya lugha ya Kiswahili unavyoweza
kutekelezwa ili kuweza kufanikisha lengo lake na kuwa lugha rasmi?
1.4 Malengo ya Utafiti
i) Kubaini iwapo kuna utayari katika kutekeleza sera ya lugha ya Kiswahili kuwa
lugha rasmi.
ii) Kubaini namna utayari huu utakavyosaidia katika kuimarisha sera hii mpya ya
lugha ya Kiswahili hasa
katika urasmi wake.
iii) Kuchunguza changamoto zinazokabiliwa katika shughuli za kiutawala na
vyombo vya
habari kuhusu hadhi mpya ya lugha ya Kiswahili.
iv) Kutambua ni vipi utayari wa utekelezaji katika sera hii unavyoweza
kutekelezwa ili
kuweza kufanikisha lengo lake la kuwa lugha rasmi.
9
1.5 Upeo na Mipaka
Sera ya lugha kimsingi huelezwa kwa kushughulikia shughuli za kiutawala, elimu
na vyombo vya habari. Sera ya lugha ya Kiswahili inapaswa kutumika katika
mawanda yaliyotajwa hapo juu lakini utafiti huu ulijikita katika shughuli za
kiutawala na vyombo vya habari ili kuonyesha kama kuna utayari katika
utekelezaji wa sera hii.
1.6 Sababu za Kuchagua Mada
Kama ilivyoelezwa hapo awali, utafiti huu ulilenga kudhihirisha utayari katika
utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya, na
iwapo kuna changamoto zinazokabiliwa katika sera hii hasa katika utekelezaji
wake, katika shughuli za kiutawala na vyombo vya habari. Kwa mujibu wa katiba
mpya ambayo ilipitishwa mwaka wa 2010, sera ya lugha ya Kiswahili ilipata
hadhi mpya na kuwa lugha rasmi. Ilipotambulika kuwa lugha rasmi, lugha hii
ilitarajiwa kutumika katika kiwango sawa na ile ya Kiingereza.
Sababu nyingine ni kuwa hakuna utafiti uliofanywa ambao ni sawa na huu.
Ingawa kuna tafiti nyingi ambazo zimefanywa kuhusu sera ya lugha kwa mfano
ni ‘Mielekeo na changamoto za maafisa wa kaunti katika utekelezaji wa katiba
kuhusu sera ya lugha Kaunti ya Nakuru (Nggige, 2014)’, ‘Mielekeo ya
wafanyakazi kuhusu Kiswahili kama lugha rasmi katika wizara za serikali nchini
Kenya’ Kaunti ya Kisii (Nyandwaro, 2015). Kuna tafiti chache ambazo
zimefanywa kuhusiana na utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha kama lugha
rasmi. Utafiti uliofanywa unaokaribiana na huu uliangazia mielekeo na
changamoto za maafisa wa kaunti katika utekelezaji wa katiba kuhusu sera ya
lugha katika kaunti ya Nakuru, (Ngigge, 2014) kisha wa Nyandwaro (2015)
10
ambaye alitafiti mielekeo ya wafanyakazi kuhusu Kiswahili kama lugha rasmi
katika wizara za serikali nchini Kenya.
Sababu nyingine ni kwamba lugha ya Kiswahili haipewi nafasi mwafaka katika
uimarishaji wake; baadhi ya watafitiwa wanakiona Kiswahili kama lugha duni na
wanaipuuza (Mirianga, 2014). Pia kutokana na swala la utayari katika utekelezaji
wake sharti kuwe na changamoto zinazoifanya sera ya lugha ya Kiswahili kuwa
lugha rasmi kuafikiwa kama ilivyo katika katiba. Utafiti huu ulisaidia kuonyesha
utayari katika utekelezaji na changamoto hizo ili kupata jinsi tunavyoweza
kuimarisha sera hii ili itumike ipasavyo.
Mwisho, utafiti huu uliweza kutoa mwanga kuhusu utayari wa utekelezaji wa
sera ya lugha ya Kiswahili. Iwapo matokeo ni chanya tutaangazia mbinu ambazo
zinaweza kuifanya sera hii iwe bora zaidi. Iwapo hakuna athari yoyote, itakuwa
bora ikiwa mikakati mingine ya kufanya sera hii ya lugha ya Kiswahili kubuniwa
ili umaarufu wake upatikane hasa katika urasmi wake miongoni mwa watumizi
wake.
1.7 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada
Katika utafiti huu, mtafiti alieleza baadhi ya watafiti walioshughulikia sera ya
lugha na wale walioangazia utekelezaji wa sera hii ya lugha kwa kuangazia
changamoto na hali ya utekelezaji wake. Waandishi ambao wameshughulikia
swala la sera ya lugha nchini Kenya ni pamoja na Mbaabu (1996), Harries
(1968) kisha utekelezaji wa sera hii ya lugha ni Shitemi (2011). Waandishi
mbalimbali walitumiwa kuelezea chngamoto zinazokumba utekelezaji wa sera ya
11
lugha, jinsi tunavyoweza kuimarisha sera mpya ya Kiswahili kuwa bora ili
kukidhi hadhi yake ya kuwa lugha rasmi na kuonyesha kiwango cha utayari wa
Wakenya katika utekelezaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi.
Kuna tafiti nyingi ambazo zimejihusisha na maswala haya lakini hakuna utafiti
ambao umejihusisha moja kwa moja na Utekelezaji wa sera ya lugha ya
Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya. Hata hivyo, utafiti huu
ulijishughulisha na wataalamu wengi iwezekanavyo ambao wamechangia kwa
njia moja au nyingine kuhusu suala la sera ya lugha au utekelezaji wa sera ya
lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi.
Kwa mujibu wa Sikma (1990), hadhi ya lugha hutegemea majukumu ambayo
lugha hiyo huyatekeleza katika jamii. Lugha inayowawezesha watu kuboresha
maisha yao hushikilia nafasi ya juu katika ngazi ya umuhimu wa lugha na ile
isiyotoa mchango wowote hudharauliwa. Lugha tofauti huwa na hadhi tofauti.
Anaendelea kwa kusema kuwa lugha ya wanajamii wengi hutazamwa kama
lugha bora. Hivyo, watu wana imani kuwa ina hadhi ya juu kijamii na kwa
kuitumia mzungumzaji hupata hadhi ya juu. Utafiti wa Sikma una uhusiano
mkubwa na utafiti huu kwa kuwa lugha ya Kiswahili ilifanywa kuwa lugha rasmi.
Mtafiti alitaka kubaini iwapo baada ya lugha ya Kiswahili kufanywa lugha rasmi
hadhi yake iliongezeka na hivyo kutekelezwa kwa kuongezewa majukumu zaidi.
Wasomi maarufu kama vile Charles Njonjo, aliyekuwa wakati mmoja mkuu wa
sheria, alitoa madai kuhusu lugha ya Kiswahili. Katika tafsiri ya Onyango
(1990), madai hayo ni ‘Kiswahili ni lugha ya mwananchi wa kawaida, si lugha ya
mtu kama mimi’. Onyango (1990) pia alishughulikia mielekeo ya wasomi
12
kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili. Matokeo yake yanabainika kuwa, wengi
wa wasomi hao nchini Kenya hawapendelei kutumia lugha ya Kiswahili,
wanapenda zaidi kutumia Kiingereza hasa katika miktadha rasmi. Hali hii
inafanya watu wengi kutotumia lugha hii ya Kiswahili. Akimnukuu Harries
(1968), anaendelea kwa kusema kuwa lugha ya mawasiliano kati ya watu wa
tabaka la chini na tabaka la juu ni Kiingereza. Hili linamaanisha kuwa hata baada
ya Kiswahili kutangazwa kuwa lugha ya taifa nchini Kenya, bado kinaendelea
kudunishwa na kupewa hadhi ya chini. Utafiti huu ulimsaidia mtafiti kwani
alifahamu ni kwa nini watu wengi hupuuza lugha ya Kiswahili na ni nini haswa
kinachoweza kufanywa ili utekelezaji wa lugha hii uwe katika kiwango
kinachohitajika.
Mbaabu (1996) ameshughulikia sera ya lugha katika Afrika Mashariki. Kulikuwa
na Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki – the Inter Territorial Language
(Swahili) Committee (ITLC) ambayo ilitilia mkazo sana lugha ya Kiswahili na
lugha hii iliinuliwa sana hasa katika miaka ya mwanzo mwanzo ya kamati hii.
Hata hivyo, mabadiliko kuhusu sera ya lugha yaliendelea hasa wakati wa
wakoloni pale ambapo lugha ya Kiswahili ilidunishwa na pahali pake
pakachukuliwa na Kiingereza. Baada ya vita vya pili vya dunia ufadhili
uliokuwepo na misaada iliyotolewa ilipungua; hili lilifanya umaarufu wa
Kiswahili kupungua. Wakoloni nao walihakikisha kwamba waliibua sera ambayo
iliifanya lugha ya Kiswahili kuwa na majukumu machache sana. Anaendelea kwa
kutoa mfano, Kiingereza kilikuzwa shuleni kwa kuadhibu wanafunzi
waliozungumza Kiswahili na lugha za kiasili. Akimnukuu Fasold, 1984 anaeleza
kuwa, ingawa sera ya lugha huundwa na kutekelezwa na serikali, hatua za
13
kiserikali hufanikiwa zaidi iwapo zinaungwa mkono na mashirika yasiyo ya
kiserikali kama waandishi wa vitabu vya shule, waandishi binafsi na magazeti.
Kutokana na maoni ya Mbaabu, ni dhahiri kuwa mawazo haya yalisaidia katika
utafiti huu kwa kuwa serikali inaweza kuwa katika mstari wa mbele katika
utekelezaji na kuinua lugha fulani. Hivyo, kuna uwezekano kuwa iwapo serikali
itaungana na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali utekelezaji wa sera hii mpya
utatekelezwa ipasavyo.
Mohochi (2002) amezungumzia kuhusu mchango wa vyombo vya habari katika
kuendeleza lugha ya Kiswahili kama vile radio, televisheni na magazeti.
Anaeleza kuwa kwa muda mrefu sana vyombo vya habari vya Afrika Mashariki
na vingine vya kigeni vimekuwa katika mstari wa mbele kukitumia Kiswahili.
Hata hivyo, vingi bado vinapendeleza lugha ya Kiingereza. Matangazo yake
hufanywa kwa lugha ya Kiingereza kwa wakati mwingi. Katika upande wa
magazeti nchini Kenya, magazeti mengi sana yamechapishwa kwa lugha ya
Kiingereza kwa mfano ni gazeti la ‘Daily Nation’, ‘The Standard’, ‘Peoples
Daily’ na moja tu ndilo la Kiswahili ambalo ni la “Taifa Leo”. Utafiti huu
ulimfaa mtafiti kwa kuwa aliweza kujua iwapo vyombo hivi vya habari
vinapendelea lugha ya Kiingereza hata baada ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha
rasmi. Je, mapendeleo haya yanaathiri vipi utayari katika utekelezaji wa sera ya
lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi. Hata hivyo, hakushughulikia utekelezaji
wa sera ya lugha ya Kiswahili jambo ambalo ni tofauti kati ya utafiti huu na
wake.
14
Ali (2011) alifanya utafiti uliohusu Kiswahili kama Lugha rasmi. Aliangazia
changamoto zinazowakumba watu wanapowasiliana ofisini wakitumia Kiswahili
kama lugha rasmi. Alifanya utafiti wake katika ofisi mbili; moja ya kibinafsi na
nyingine ya umma katika eneo la Nairobi. Utafiti wake ulionyesha kuwa
matumizi ya lugha ya Kiswahili ni ya kiwango cha chini na waliohojiwa
walisema kuwa ni lugha iliyozungumzwa na watu wa tabaka la chini. Utafiti huu
ulitupa mwanga ya hali ya Kiswahili ilivyo katika shughuli za kiutawala. Hivyo
kubaini utayari wa Wakenya katika kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha
rasmi.
Shitemi (2011) alieleza kuwa faida ya kutokana na uwepo wa tamko kuhusu
swala la lugha katika katiba mpya ya Kenya (2010). Hii ni kufuatia mapendekezo
ya tume ya marekebisho ya katiba, yanahitaji kudumishwa na kutekelezwa
ipasavyo. Tangazo la Kiswahili kuwa lugha ya kwanza rasmi na lugha ya taifa
linahitaji kuwekwa katika vitendo kimitaala, kiutendaji, kiuwezeshaji, na pia
katika asasi zote za kutumia lugha. Tangazo hilo linakabiliwa na changamoto za
kiutekelezaji katika usambazaji wa mbinu za utekelezaji na majukumu ya
Kiswahili katika sekta mbalimbali. Kuna uhusiano kati ya haya na utafiti huu kwa
kuwa mtafiti alitaka kubaini ni changamoto zipi ambazo zinakumba utayari
katika utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya.
Mbatiah (2012) anaeleza kuwa katika baada ya ukoloni kulikuwa na mikabala
hasi kuhusiana na Kiswahili. Hivi ni kusema kwamba walikuwa na kasumba ya
kiukoloni kiasi kwamba walikidharau Kiswahili na kupendelea Kiingereza.
Hawakuamini kuwa lugha ya Kiafrika kama Kiswahili ingeweza kutumika
15
kutekeleza shughuli rasmi za kitaifa. Hali hii ni ya kutamausha sana kwa kuwa
inatajiriwa viongozi kama hawa ndio wanapaswa kuwa katika mstari wa mbele
katika kukikuza Kiswahili. Hii ni kuonyesha kuwa licha ya kuwepo kwa
mabadiliko ya sera ya lugha hii bado kuna Wakenya ambao wanaidunisha lugha
hii na kuinasibisha na wale walio katika kiwango cha chini. Utafiti huu ulilenga
kubaini iwapo hii ni mojawapo ya changamoto ambayo inakumba utekelezaji wa
sera ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi.
Kulingana na Hudon (2013) bunge lilihakikisha kuwa limeteua waziri na mkuu
wa fedha ambao wangewajibikia mambo mbalimbali kuhusiana na lugha hizi
rasmi. Mifumo hii ilihakikisha kuwa kuna haki ya wafanyikazi katika vituo
mbalimbali kutumia lugha yoyote waipendao kwa watu wanaowahudumia.
Serikali pia ilitoa nafasi sawa kwa watu wanaozungumza Kiingereza na
Kifaransa katika nchi hiyo.
Lugha hizi rasmi zilitekelezwa kwa njia zifuatazo; kwanza serikali ya Canada
ilijitolea katika kuhakikisha kuwa lugha hizi rasmi zimetekelezwa ipasavyo. Pia
ilitoa fedha katika vituo mbalimbali kuendeleza lugha hizi. Pili serikali imetoa
mwongozo jinsi utekelezaji wa lugha hizi unavyoweza kutumika katika sekta za
umma katika kuwahudumia watu. Tatu, waziri anayehusika na maswala ya lugha
aliweka mikakati ya lugha hizi ambayo inahusu masomo, maendeleo ya kijamii
na umma. Kupitia juhudi za waziri huyo, katika mwaka wa 2012 fedha zaidi
zilipangiwa kutolewa katika masomo ya lugha, viwanda vya lugha, maendeleo ya
kiuchumi, usaidizi katika jamii na kuimarisha uwililugha katika umma.
16
Katika makala ya Osore na Midika (2016) nchi ya Kenya, Canada na Afrika
kusini yamejaribu kutekeleza sera ya lugha katika kufanya lugha mbalimbali
kuwa lugha rasmi. Kwa mfano nchini Canada sawa na Kenya kuna ukwasi wa
tamaduni tofauti ambapo kuna lugha nyingi ambazo hutumika. Nchini Canada
kuna lugha mbili rasmi Kifaransa na Kiingereza ambazo hutumika katika Quebec
na maeneo mengine ya Canada mtawalia. Hata hivyo, kuna lugha nyingine
ambazo pia hutumika ingawa lugha hizi si rasmi.Hali hii si tofauti sana na ile ya
humu nchini kwa kuwa lugha ya Kiiingereza na ile ya Kiswahili ni lugha rasmi
kwa mujibu wa Katiba ya mwaka wa 2010.
Nchini Canada sera ya lugha huongozwa na mifumo maalum ambayo husaidia
kuendeleza lugha hizi rasmi. Mifumo hii imechangia pakubwa katika kuhakikisha
kuwa lugha hizi zinazungumzwa. Changamoto ambayo ilidhihirika katika nchi
hii ni pale ambapo hakukuwa na mwelekeo wazi katika matumizi ya lugha ya
Kifaransa kule Quebec.
Tukiangazia sera ya lugha nchini Afrika Kusini utekelezaji wake pia
umetekelezwa na bunge kupitia njia zifuatazo; Kwanza mikoa mbalimbali
imechukua jukumu kuhusiana na lugha rasmi ambayo ina makala yanayoonyesha
lugha ambazo zinatambulikana kama lugha rasmi, pili, kuna makala kuhusu sera
ya lugha ambayo idara ya wizara ya utamaduni, sayansi na teknolojia huangazia
mambo halisi ya tafsiri na lugha ya teknolojia. Tatu, kuna asasi kumi na nne za
kitaifa kuhusiana na lugha ambazo zina majukumu ya kuangazia maendeleo ya
lugha. Kazi hii ni muhimu katika utafiti wetu kwa kuwa ilisaidia katika
17
kuonyesha mambo mbalimbali tunayoweza kufanya ili kuimarisha lugha ya
Kiswahili na kuweza kutumika nchini Kenya.
Kutokana na wasomi mbalimbali kama vile Mbaabu, Shitemi, Mohochi, Osore
na Midika kuhusiana na swala hili la utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili, ni
dhahiri kuwa tafiti hizo zinahusiana kwa njia moja au nyingine na utafiti huu.
Hivyo basi, zina umuhimu katika kufanikisha utafiti huu wa utayari wa Wakenya
katika utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya.
Iwapo Kiswahili kitatumika katika kutekeleza majukumu ya kirasmi na katika
maeneo yote katika sera ya lugha, hali hii itaendelea kuipa lugha ya Kiswahili
nafasi na hadhi zaidi katika jamii na hili litarahisisha utekelezaji wa sera hii kwa
mujibu wa katiba iliyoidhinishwa katika mwaka wa 2010. Utafiti huu ulilenga
kutambua iwapo kuna utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili
katika shughuli za kiutawala na vyombo vya habari kama lugha rasmi.
1.8 Misingi ya Nadharia
Ni muhimu kuelewa kwamba ili kutekeleza sera yoyote ya lugha sharti kuwe na
upangaji lugha. Mwanaisimu wa Kijerumani Heinz Kloss (1967, 1969) kama
anavyonukuliwa na Mesthrie (2000) anaeleza aina mbili za upangaji lugha
ambazo ni upangaji lugha wa kikongoo na upangaji wa kihadhi. Aina hizi mbili
ndizo zinazungumziwa pia na Ngugi na Chacha (2004). Upangaji wa kikongoo
ndio unahusu muundo wa lugha katika vipengele vya othografia, msamiati, hijai
na maendelezo ya sarufi. Upangaji wa kihadhi unahusishwa na uamuzi
unaozingatia majukumu ya kila lugha kulingana na maeneo : jimbo, mkoa au
18
taifa. Huzingatia juhudi zinazochukuliwa ili kubadilisha matumizi na majukumu
ya lugha katika jamii, (Mesthrie, 2000).
Van Els (2005) anasema kuwa upangaji kikongoo unahusu uasili wa lugha ya
kufundisha. Shughuli hii inategemea mbinu na miktadha ya kiisimu lakini
ikizingatia mipaka yake katika upangaji kihadhi. Mafanikio na matokeo yake
huwa yanachangia sana kwa ufunzaji na ufundishaji wa lugha na huchangia
vilevile kuhusu umaarufu wa lugha katika jamii.
Mtazamo wa upangaji wa kihadhi ulifaa katika utafiti huu kwa kuwa unahusu
lugha kupewa majukumu mapya. Katika muktadha huu, lugha ya Kiswahili
imepewa hadhi mpya ya kuwa lugha rasmi nchini Kenya. Hii ni kumaanisha
kuwa lugha ya Kiswahili sawa na Kiingereza zinatambulikana kihalali katika
matumizi ya kisiasa na kitamaduni katika nchi ya Kenya.
Kutwika kwa jukumu mpya katika lugha ya Kiswahili kunahitaji mabadiliko ya
mfumo wa kiisimu kama vile kuzindua mitindo mipya na leksimu za maeneo
tofauti. Uzinduzi wa leksimu mpya katika lugha ni muhimu kwa kuwa
unaiwezesha lugha hiyo kufanikisha jukumu lake jipya. Mesthrie (2000)
anaeleza mtazamo wa upangaji lugha kifahari ni ule unaolenga kutoa mielekeo
chanya ya kisaikolojia ambayo ni muhimu ikiwa kutakuwepo na ufanisi wa muda
mrefu katika upangaji lugha. Upangaji kifahari huwa muhimu pale ambapo lugha
ambayo imeteuliwa huwa ya hadhi ya chini. Ili watu wakubali hadhi ya lugha
hiyo, kuna haja ya kuboresha na kuendeleza ufahari wa lugha hiyo na ndiyo
sababu upangaji kifahari hutangulia upangaji wa kihadhi. Naye Van Els (2005)
alitoa maoni yake akisema kuwa upangaji kifahari unahusu mambo matatu ya
19
kuzingatiwa: kwanza kuna taswira ambayo inahusu ukabila au utambulisho wa
uraia na uendelezaji wa lugha kama ilivyokuwa katika jimbo la Quebec; pili
kuna taswira inayoelekea kueleza mbinu ya utekelezaji na urekebishaji wa sera ya
lugha na mwisho kuna taswira inahusiana na msukumo na shughuli za
watekelezaji wenyewe hasa hasa na jamii inayohusika.
Nadharia ya Utekelezaji ilishughulikia malengo tuliyojiwekea. Imeasisiwa na
watu mbalimbali wakiwemo Spencer (1971) na Durkheim. Spencer (1971)
anaeleza kuwa katika matumizi ya kawaida, kugawa vipande vinavyotokana na
kitu kimoja ni hatari. Kauli hii ya kweli kwa kuwa hatuwezi tenganisha lugha na
jami.. Hii ni kwa kuwa Kiswahili hakiwezi kutenganishwa na jamii yake ya
Kiafrika na badala yake kuingizwa kwa lugha za kigeni kama vile Kiingereza.
Nadharia ya utekelezaji hujumuisha weledi wa mfumo na viasilia vyake. Kila
kiasilia kina mchango unaoupa uhai mfumo ili uendelee kufanya kazi ama
kuukwamisha iwapo viasilia vitatenganishwa. Kila mfumo ni muungano wa
viasilia ambavyo huunda umbo fulani lionekalo. Kila jamii ni muundo wenye
viasilia vinavyohusiana na kufungamana kwa kipekee. Viasilia katika jamii ni
watu katika jamii na lugha wanayoitumia.
Kutokana na maelezo haya nchini Kenya lugha ya Kiswahili ingeweza kutumika
katika shughuli zote za kirasmi bila kupuuzwa lakini hakitumiwi katika shughuli
zote. Ingawa tunajua ukweli kwamba lugha hii inapaswa kutumiwa kama lugha
rasmi, hatutekelezi wajibu huu. Mbona ukweli hautumiki kwa mambo ambayo
yanafaa? Ili kuweza kuakisi matumizi ya lugha inavyohitajika ndipo tunahitaji
20
kutafuta ukweli. Mjadala kuhusiana na nadharia hii ya utekelezaji unaungwa
mkono na wasomi wa leo kama Mbaabu (1996) na Mazrui (1995).
Hivyo ili mfumo fulani kuweza kuendelea kufanya kazi, kuna mambo ya
kimsingi ambayo yanaupa mfumo huo matokeo yanayofaa kama yafuatayo
i) Mawasiliano.
ii) Utambuzi wa pamoja juu ya umuhimu wa kila kipengele kinachounda
umbo fulani linalojadiliwa.
iii) Uzoefu wa ufungamano wa viasilia katika muundo au mfumo wa
jamii.
iv) Kuwepo kwa uhusiano kati ya mahitaji, uwezo na mazingira
yanayoshabihi mkabala (Ngigge, 2014)
Kupitia mitazamo na nadharia tulizozijadili hapo juu ni dhahiri kuwa nadharia hii
ilifaa katika utafiti huu. Ni muhimu hasa kwa kuzingatia shughuli za kutumia
lugha ambazo zinapaswa kutumiwa kwa minajili ya mawasiliano. Mitazamo ya
upangaji lugha ilitusaida katika utafiti huu kwa kutufahamisha jukumu jipya ya
kihadhi katika lugha ya Kswahili kisha katika ile ya utekelezaji ilifaa kwa
kushughulikia malengo yetu. Katika mapitio ya vitabu mbalimbali, kuhusiana na
matumizi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili katika nchi za Afrika Mashariki
hususan Kenya, lugha hii imepewa majukumu ya lugha rasmi kwa mujibu wa
katiba iliyoidhinishwa 2010.
21
1.9 Mbinu za Utafiti
Katika sehemu hii mtafiti alijadili njia za utafiti. Njia hizi za utafiti ziligawanywa
katika makundi manne: eneo la utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data na
uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Kwa kuwa lugha ya Kiswahili inatumika
katika nchi nzima ya Kenya, utafiti huu ulifanywa katika kaunti ya Nairobi kwa
kuwa katika kaunti hii ndiko kuna ofisi nyingi za kiutawala na pia vyombo vingi
vya habari vinapatikana huko. Pili, kuna mtagusano wa watu wa jamii
mbalimbali zinazopatikana nchini Kenya na pia kuna wataalamu wa kila aina
wanaopatikana katika kaunti ya Nairobi. Sampuli iliyotumiwa ilikuwa kiwakilishi
mwafaka cha jumuiya katika kaunti ya Nairobi na Kenya kwa ujumla.
Waliohojiwa ni washikadau kama vile Kamati ya Nyachae ya ‘Commission on
the Implementation of the Constitution’ (Kamati ya Utekelezaji wa Katiba) katika
utekelezaji wa sera mpya ya lugha ya Kiswahili. Kamati zingine za bunge na
wizara ya utamaduni Utafiti huu ulifanywa katika Wizara ya Utamaduni, watu
waliohusika katika kamati ya Nyachae ambayo iliundwa ili kuhakikishwa
utekelezaji wa Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 unatekelezwa ipasavyo; baadhi
ya majukumu yalikuwa ni, kufanya kazi na kamati ya Katiba kuhakikisha kuwa
Katiba inaheshimiwa; kutoa ripoti kila mara kwa kamati ya Utekelezaji wa
Katiba kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa katiba, idara ya Polisi, vyombo vya
habari ambavyo ni ‘KBC’, ‘KTN’, ‘NTV’ na ‘Citizen’. Maeneo haya yataonyesha
vile ambavyo utayari wa Wakenya katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kama
lugha rasmi yalivyo nchini Kenya, na kama kuna juhudi zozote katika kuimarisha
lugha hii kuwa bora zaidi.
22
1.9.1 Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanywa katika kaunti ya Nairobi ambao ni mji mkuu wa nchi ya
Kenya. Kaunti hii ina ofisi za kiutawala na kuna mashirika mbalimbali ya
vyombo vya habari. Utafiti huu ulimulika kaunti hii kwa kuwa huku ndiko kuna
ofisi nyingi za kiutawala na pia vyombo vya habari vimeenea huku. Jambo
lingine ni kuwa kuna wataalamu wa kila aina. Hili lilimwezesha mtafiti kuzuru
maeneo yaliyohitajika ili kupata habari msingi zilizosaidia katika utafiti huu.
1.9.2 Uteuzi wa Sampuli
Ili kuweza kupata kundi wakilishi katika jamii pana, utafiti huu ulitumia uteuzi
wa sampuli ya kimakusudi. Hatua hii ilimwezesha mtafiti kupata walengwa
binafsi ili kupata data hiyo. Mtafiti alitumia vibadala vine ambavyo ni elimu,
jinsia, umri na lugha ya mzungumzaji. Kitengo cha lugha kiligawanywa katika
vikundi viwili: Kiswahili na Kiingereza.
Mtafiti aliwahoji washiriki arobaini na wawili. Idadi hii ilizingatiwa kwa kuwa
iliwezesha mtafiti kupata data ya kina. Kila jinsia ilikuwa na watafitiwa ishirini
na mmoja. Mtafiti alichagua watafitiwa ishirini na mmoja katika kila idara
mbalimbali. Watafitiwa tano walifanyiwa mahojiano.
23
Jedwali la 1.9.2.1: Mgao wa watafitiwa kutegemea vibadala vine: jinsia, elimu,
jinsia na lugha ya mzungumzaji katika sehemu zilizotafitiwa.
kiwango Idadi kiwango idadi kiwango idadi jumla
Jinsia kiume 21 Kike 21 42
Elimu stashahada 20 Shahada
ya kwanza
17 Shahada
ya
uzamili
5 42
Umri 25-35 15 35 na zaidi 27 42
Lugha ya
mzungumzaji
Kiswahili 27 Kiingereza 11 Lugha
mseto
4 42
Kutokana na jedwali la 1.9.2.1 , ni wazi kuwa uteuzi huu ulimsaidia mtafiti
kupata data isiyoegemea upande mmoja.
1.9.3 Ukusanyaji wa Data ya Utafiti
Hojaji na mahojiano ndizo njia mbili kuu zilizotumiwa katika utafiti huu. Mtafiti
alikusanya habari kuhusu taaluma ya mtafitiwa pamoja na matumizi yake ya
lugha. Hojaji ililenga maswali juu ya utayari wa Wakenya kuhusu utekelezaji wa
matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi na changamoto zinazokabiliwa
katika utayari huo. Hojaji hiyo ilikuwa na maswali funge na maswali wazi.
Katika hojaji funge mtafitiwa alihitajika kuchagua jibu kati ya majibu aliyopewa.
Hii ilimsaidia mtafiti katika kumwelekeza mtafitiwa kwenye jibu mahususi. Njia
hii ilimwezesha mtafitiwa kujaza hojaji haraka bila kuchoka
24
Hojaji wazi ilimwezesha mtafitiwa kutoa maoni yake kuhusiana na kile
alichoulizwa hivyo mtafiti alipata maoni tofauti kuhusiana na jambo hilo.
Kutokana na hojaji kuwa na sehemu hizi mbili, mtafiti aliweza kupata data nzuri
ambayo aliweza kujua vyema jambo aliloliangazia.
Maswali na majibu yalitungwa kwa njia ambayo ilidhihirisha jinsi lugha ya
Kiswahili inavyoendelezwa kama lugha rasmi katika utekelezaji wake na pia
iliangazia changamoto za utaayari wa Wakenya kuhusiana na lugha ya
Kiswahili.. Maswali na majibu yalitungwa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
nia, matendo na athari kwa nyanja mbalimbali. Maswali pia yalijikita katika
vigezo vya mitazamo ya upangaji lugha, ambavyo vilimwongoza mtafitiwa
kutambua utayari wa utekelezaji wa sera hii mpya ya lugha ya Kiswahili kama
lugha rasmi.
Mahojiano yasiyo ya moja kwa moja yaliyofanyiwa watafitiwa yalilenga
kumwelekeza mtafiti kuhusu sera mpya ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi
hasa kuhusiana na jinsi sera hii inavyotekelezwa. Jambo hili lilimfaidi sana kwa
kuwa wahojiwa walitoa maelezo mengi na hivyo kupata habari muhimu.
Wengine walihojiwa moja kwa moja. Mwisho, mtafiti alisoma vitabu
vilivyohusiana na mada hii ili kuweza kuendeleza mada ipasavyo.
1.9.4 Uchanganuzi na Uwasilishaji wa Data
Baada ya data kukusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia program ya SPSS
(Mtindo Changanuzi wa Tarakimu Sayansi) ili kuweza kupata matokeo mwafaka
na ya kuaminika. Mtindo changanuzi wa tarakimu sayansi ni program ya
kompyuta ambayo hutumiwa kuingiza data za utafiti na huchanganua data hizo za
25
utafiti. Uchanganuzi huu pia ulifanywa kwa kuzingatia kipengee cha mitazamo
ya upangaji lugha. Vielelezo vya chati mraba na michoro pia vilitumika katika
uwasilishaji ili data iweze kueleweka kwa njia rahisi. Data iliyochanganuliwa,
ilikuwa imetokana na maswali ambayo watafitiwa walijibu.
1.9.5 Hitimisho
Katika sura hii ya kwanza, vipengele vya utafiti vilivyojadil;iwa ni: usuli wa
mada, suala la utafiti, maswali na malengo ya utafiti yaliyoongoza utafiti huu,
sababu za kuchagua mada, misingi na mihimili ya Nadharia ya Utekelezaji,
mbinu za utafiti kwa jumla zilizotumiwa katika utafiti huu na jinsi matokeo ya
utafiti huu yalivyokusanywa, kuchanganuliwa na kuwasilishwa.
26
SURA YA PILI
HISTORIA YA UTAYARI WA WAKENYA KUHUSU URASMI
WA LUGHA YA KISWAHILI NCHINI KENYA.
2.0 Utangulizi
Utayari wa Wakenya kuhusu matumizi ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini
Kenya ni muhimu sana katika utafiti huu. Hii ni kwa kuwa kutokana na utayari
wao, lugha hii inaweza kutumika katika nyanja mbalimbali hasa katika shughuli
za kiutawala miongoni mwa wafanyakazi wa wizara za kiserikali na pia kutumika
katika vyombo vya habari. Katika kujadili historia ya utayari wa Wakenya
kuhusu Kiswahili, mtafiti aligawa historia hii katika vipindi viwili. Kipindi cha
kwanza ni kipindi cha ukoloni na kipindi cha pili ni kipindi cha baada ya ukoloni.
Lengo kuu la sura hii ni kubaini ni vipi utayari wa lugha ya Kiswahili kama lugha
rasmi umekuwa ukipokelewa kupitia vipindi tofauti kihistoria.
2.1 Kipindi cha Ukoloni
Kipindi hiki kimegawanywa katika sehemu tatu; Sehemu ya kwanza ni kipindi
kabla ya vita vikuu vya pili vya dunia, sehemu ya pili ni wakati wa vita vikuu vya
pili vya dunia na mwisho ni baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.
2.1.1 Kipindi cha Kabla ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
Katika kipindi hiki kulikuwa na wadau wengi waliochangia katika kuunda sera ya
lugha nchini Kenya. Miongoni mwa wadau hao walikuwa Wamishenari. Baadhi
yao walifikiria kuwa injili ingeenezwa vizuri kupitia lugha za kienyeji huku
wakisema Kiswahili kilikuwa kimefungamana sana na dini ya Kiislamu (Nabea,
2009). Kuna wale ambao waliona ni muhimu kutumia lugha ya Kiswahili kwani
ni lugha iliyokuwa imeenea sana miongoni mwa Wakenya.
27
Kongamano la Umoja wa Wamishenari nchini Kenya (United Missionary
Conference) mwaka wa 1909 liliidhinisha matumizi ya lugha mama katika
madarasa matatu ya kwanza katika shule za msingi, Kiswahili katika madarasa
mawili ya kati katika shule za msingi na Kiingereza kilikuwa kitumike katika
madarasa yaliyosalia hadi chuo kikuu (Gorman, 1974).
Kwa upande wa wakoloni, wakoloni walipenda kuwafunza Waafrika Kiingereza
ili wapate wafanyakazi ambao wangewasaidia katika utawala wao. Waafrika
kufahamu Kiingereza ilikuwa hatua muhimu kwani mawasiliano kati ya Waafrika
na wakoloni yangekuwa na hitilafu. Kwa upande mwingine, walowezi walipinga
hoja ya kuwafunza Waafrika Kiingereza kwani waliona hali hiyo ingewafanya
Waafrika kuwa kama wao na wangetaka wafanye kazi za mapato ya chini.
Kutokana na maoni haya ni dhahiri kuwa lugha ya Kiswahili imekuwa na
changamoto tangu enzi za ukoloni. Utayari wa matumizi ya lugha ya Kiswahili
umepitia changamoto na hivyo hali ya wamishenari na wakoloni kuwafunza
Waafrika Kiingereza inaashiria kuwa lugha ya Kiswahili haikutambuliwa kuwa
yenye umuhimu. Ingekuwa bora iwapo wangesisitiza matumizi ya lugha
Kiswahili sawa na Kiingereza.
Kufikia mwaka wa 1924, kamati ya Phelps-Stoke ilizuru Kenya na walilalamikia
mzozo uliokuwa kati ya wamishenari, wakoloni na walowezi kuhusa sera ya
lugha (Mbaabu, 2007). Tume hiyo ilipendekeza kuwa lugha za kienyeji zitumiwe
kuwafunza wanafunzi shuleni na lugha ya Kiswahili itumike tu katika maeneo
ambayo ilikuwa lugha ya kwanza kama vile Pwani.
28
Kupitia maoni haya, sera hii inaonyesha kuwa katika kipindi hiki kabla ya vita
vikuu vya pili, wakoloni, wamishenari na walowezi walikuwa na mwelekeo hasi
kuhusu lugha ya kiswahili ikilinganishwa na lugha za kienyeji na lugha ya
Kiingereza licha ya Kiswahili kuenea.
Walipendekeza kuwa lugha ya Kiingereza ifunzwe kuanzia madarasa ya juu
katika shule za upili hadi Chuo Kikuu. Tume hii iligundua kwamba ili wazazi
Waafrika wawapeleke watoto wao shuleni, shule hizo zilipaswa kufunza
Kiswahili kama kichocheo. Hii inadhihirisha kwamba Waafrika walikuwa tayari
kutumia lugha ya Kiswahili kama tu ingetumika katika shule hizo.
Hivyo, katika kipindi hiki inadhihirika kuwa utayari wa matumizi ya lugha ya
Kiswahili yalikuwa na changamoto sana.
2.1.2 Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
Ni kipindi ambacho kilikuwa hatari kwa kuwa hakukuwa na usalama na hivyo
basi machache yalitekelezwa katika kipindi hiki kuhusu masuala ya lugha. Hata
hivyo, kuna baadhi ya sera za lugha zilizopendekezwa katika kipindi hiki kuhusu
lugha nchini Kenya ambazo zilikuwa ni kubalifu katika matumizi ya lugha ya
Kiswahili. Sera hizi ziliathiri utayari wa Wakenya kwa ujumla kuhusu Kiswahili.
Katika mwaka wa 1941, Kamati ya Mashauri kwa Mkoloni iliundwa ili
kuchunguza njia bora zaidi ya kuwafunza watu wote kusoma na kuandika.
Kamati hii ilipendekeza kusomeshwa kwa lugha za Kienyeji na Kiingereza
(Mbaabu, 2007). Hali hii ilikuza lugha ya Kiingereza na zile za Kienyeji na
hivyo lugha ya Kiswahili haikutiliwa mkazo.
29
Mwaka wa 1942, tume ya Beecher iliundwa ili kushughulikia ufunzaji wa lugha
katika shule za Afrika. Waliandaa ripoti ambayo walipendekeza itumiwe baada
ya vita vikuu vya pili. Tume hiyo ilipendekeza kuwa kusomeshwa kwa lugha za
kienyeji kutiliwe mkazo na lugha ya Kiingereza ichukue nafasi ya Kiswahili
kama lugha ya mawasiliano nchini Kenya. Ripoti hii ilipinga matumizi ya
Kiswahili katika elimu na hivyo matumizi yake katika elimu yakakatizwa
(Mbaabu, 2007:102). Katika mwaka wa 1943, kumbukumbu ya ofisi ya mkoloni
kuhusu lugha katika shule za Waafrika ilitilia mkazo kusomeshwa kwa lugha ya
Kiingereza na lugha za Kienyeji.
Kupitia maoni haya inadhihirika kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yalikuwa
katika kiwango cha chini. Utayari wa matumizi ya lugha hii haukutumika katika
hali zozote rasmi. Hivyo Kiswahili ilitumika kama lugha ya maongezi ya
kawaida. Msisitizo wa lugha ya Kiingereza kama lugha ya ufundishaji ulifanya
lugha ya Kiswahili kupuuzwa. Hivyo, Wakenya na wakoloni hawakuwa tayari na
hawakudhihirisha ukubalifu katika kutumia lugha ya Kiswahili.
2.1.3 Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
Baada ya vita vya pili vya dunia, kulikuwa na mabadiliko kuhusu sera ya lugha
mwaka wa 1948. Wakati wakoloni walipobaini wazi kuwa nchi ya Kenya ilikuwa
inaelekea kujinyakulia uhuru wake, wakoloni walianzisha harakati za kuwa na
kikundi cha wasomi nchini ambacho kingelinda maslahi yao baada ya uhuru.
Hatua hii kwa kiasi kikubwa iliimarisha lugha ya Kiingereza.
30
Mbaabu (2007) anaeleza kwamba tume ya Beecher ilitoa ripoti ya pili ambayo
pia ilijulikana kwa jina la Ripoti ya Elimu ya Waafrika nchini Kenya mwaka 1949
ikifafanua mapendekezo ya mwaka wa 1942. Walipendekeza kuwa lugha ishirini
za kienyeji zitumike katika shule za msingi. Lugha hizo zilikuwa Kikamba,
Kikuyu, Kimeru, Kimaasai, Kitaveta, Kikisii, Kitende, Kiborana, Kipokomo,
Kijaluo, Kigiriama, Kigala, Kisagala, Kisuk, Kinandi, Kidabida, Kiteso,
Kiturkana, Kiluhya na Kisomali. Kufikia mwaka wa 1950, shirika la uchapishaji
la East Africa Literature Bureau liliagizwa lichapishe vitabu katika lugha hizo
ishirini zilizopendekezwa. Shirika hili halikuweza kuchapisha vitabu vingi vya
lugha hizo kwa sababu zilikuwa nyingi na kulikuwa na uhaba wa rasilimali.
Licha ya Kiswahili kupingwa, vitabu vya Kiswahili viliweza kuchapishwa na
kampuni hiyo. Hii inadhihirisha kuwa ingawa Kiswahili kilikumbwa na matatizo
hapa na pale bado kuna washika dau ambao walizingatia lugha hii kuenea.
Katika miaka ya 1950, wanafunzi wote nchini Kenya katika shule za msingi
walifunzwa kwa lugha zao za mama katika miaka minne ya kwanza nacho
Kiingereza kikafunzwa kama somo kwa miaka miwili kisha kikawa somo la
kufundishia kuanzia darasa la tano hadi la nane (Chimera 2000). Mwaka wa
1953- 1955, ripoti ya East Africa Royal Commission ilitaka lugha ya Kiingereza
ifunzwe kama somo na pia itumiwe kama lugha ya kufundishia kuanzia madarasa
ya chini. Ripoti hii iliendelea kusema kuwa ufunzaji wa lugha ya Kiswahili
ulikuwa ni upotezaji wa wakati na nguvu (Ngigge, 2014). Kufikia mwaka wa
1957, mabadiliko ya lugha ya kufundishia kutoka kwa lugha mama hadi lugha ya
31
Kiingereza katika aina zote za shule yalikuwa na nguvu sana hivi kwamba
yalikuwa na athari ya kudumu katika sera ya lugha hata baada ya Kenya kupata
uhuru (Mbaabu, 1996). Kulikuwepo na Idara ya Ukaguzi iliyoanzishwa na
Wizara ya Elimu katika mwaka wa 1957 ili kuja na mbinu mpya ya kufundishia
lugha ya Kiingereza. Shule za Aga Khan zilikuwa zikitumia Kiingereza kama
lugha ya kusomeshea kuanzia darasa la kwanza. Ni mfumo ulioanzishwa mwaka
wa 1961 na kufikia mwaka wa 1962, shule zote za Nairobi zilikuwa zikitumia
Kiingereza kama lugha ya kusomeshea kuanzia darasa la kwanza.
Katika maoni haya, ripoti ya East Africa Royal Commission kusema kuwa
ufunzaji wa lugha ya Kiswahili ulikuwa ni kupoteza wakati na nguvu yalikuwa
potovu kwa kuwa hii ilikuwa lugha ya Waafrika hivyo ingesisitizwa miongoni
mwa Waafrika kama lugha moja kuu zikiwepo lugha zingine. Kupuuzwa kwa
lugha ya Kiswahili katika nyakati hizi zimechangia katika lugha ya Kiswahili
kutozingatiwa katika hadhi sawa na lugha ya Kiingereza katika hali ya sasa.
Nyandwaro (2015) anaeleza katika mwaka huo huo wa 1961, mitihani ya Kenya
African Preliminary Examination ya kuingilia shule za sekondari iliondolewa na
nafasi yake ikachukuliwa na Kenya Preliminary Examination. Lugha ya
Kiswahili iliondolewa kabisa na haikutahiniwa katika mtihani huo.
Lugha ya Kiingereza ilipata umaarufu sana. Waliopatikana shuleni wakiongea
lugha mama au Kiswahili ambayo ilikuwa lingua franca, waliadhibiwa (Mbaabu,
1996). Hali hii iliifanya lugha hii kustahimili kuwa lugha rasmi nchini Kenya
baada ya uhuru. Kiswahili kilitengwa na wakoloni ili kudhoofisha uwezo wake
32
kama lugha ya kuwazindua Waafrika dhidi ya utawala wao (Mazrui & Mazrui
1995).
Katika kipindi hiki lugha ya Kiingereza ilienezwa katika shule hizo kama somo
na sio lugha ya kufundishia. Kulikuwa na shule chache sana za Waafrika. Katika
shule za upili za wakoloni, lugha ya Kiingereza ilitumika kama lugha ya kufunzia
na Waafrika ambao walifuzu kutoka shule hizo, walikuwa na misingi dhabiti ya
lugha hiyo. Hali hii ilileta utabaka wa kielimu kwa kuwa waliofuzu kutoka shule
za wakoloni walichukuliwa kuwa wasomi katika jamii. Hii inaonyesha kuwa
wakati huu athari ya wakoloni iliwafanya Waafrika kutozingatia lugha ya
Kiswahili na hivyo hawakuwa tayari kujifunza lugha hii. Kifuatacho ni kipindi
cha baada ya ukoloni.
2.2 Kipindi cha Baada ya Ukoloni
Katika kipindi hiki, hali ya lugha nchini Kenya inajadiliwa katika shughuli za
kiutawala hasa katika sekta ya umma na pia kibinafsi na vyombo vya habari huku
swala la utayari wa Wakenya kuhusu matumizi ya Kiswahili likizingatiwa.
Baada ya Kenya kupata uhuru mwaka wa 1963, lugha ya Kiingereza ilitangazwa
kuwa lugha rasmi. Ilikuwa itumike katika sekta zote za serikali ikiwemo elimu.
Lugha hii ilichukuliwa kama lugha ya wasomi na ilipewa hadhi ya juu kuliko
lugha ya Kiswahili katika mashirika mbalimbali. Chimerah (1998) anaeleza kuwa
nchini Kenya, makabila ambayo hayakuwa ya Kibantu yalipinga matumizi ya
Kiswahili kwa sababu waliona Kiswahili kimewabagua kimaendeleo hasa kabila
la Wajaluo. Viongozi wengi na wasomi wakati huo hawakutaka kujifunza
Kiswahili kikamilifu. Kiswahili kilitumika tu katika masuala yasiyo rasmi na
33
wakati walitaka kuleta hali ya kusikizana miongoni mwa wananchi. Hali hii
ilionyesha kuwa kulikuwa na utayari wat matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa
kiwango cha chini.
2.2.1 Shughuli za Kiutawala
i) Sekta ya Umma
Kufikia mwaka wa 1963 wakati Wakenya walipata uhuru, viongozi wengi
walikuwa wamejifunza na kuzungumza lugha ya Kiswahili vizuri. Walifanya
hivyo ili kuweza kuwasiliana na wanajamii wote. Kuna mswada uliopitishwa
bungeni kuwa lugha ya Kiswahili iweze kuwa lugha rasmi nchini Kenya katika
mwaka wa 1969, hatua hii haikupokelewa vyema kwa kuwa kuna baadhi ya watu
waliopinga na wale waliounga mkono. Walipinga lugha ya Kiswahili kwa
kusema kuwa kujifunza Kiswahili kulikuwa ni kupoteza wakati. Waliona kuwa
Kiswahili kingewatenganisha Wakenya ambao lugha yao ya kwanza haikuwa
Kiswahili na ujuzi wa lugha hii ulihitajika katika kazi duni.
Mbaabu (2007) anaeleza kuwa baadhi ya wale waliopinga ni G.G Kariuki
aliyesema kuwa Kiswahili ni lugha ya Kiarabu inayotumiwa na Waislamu katika
dini yao, naye Charles Njonjo ambaye alikuwa mwanasheria alipinga kwa
kusema kuwa ni lugha ya Kiarabu na ni lugha geni kama vile Kiingereza.
Maongezi haya yanadhihirisha kuwa baadhi ya watu hawakuwa tayari kutumia
lugha ya Kiswahili kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Hakukuwepo na utayari
wa kutumia lugha ya Kiswahili na hali hii iliendelezwa na viongozi wa serikali.
Hata hivyo, kuna baadhi ya wabunge ambao waliunga mkono mswada kuwa
lugha ya Kiswahili iwe lugha rasmi, waliona kuwa ndio lugha pekee ambayo
34
inawaleta pamoja Wakenya wanaotumia lugha tofauti tofauti. Walisema ni lugha
ya Kiafrika kinyume na Kiingereza ambayo ilikuwa lugha geni (Mbaabu, 1978)
Rais Jomo Kenyatta alikipenda Kiswahili na alitumia lugha hiyo katika
kuwahutubia wananchi. Kutokana na hali hii aliweza kupitisha miswada
mbalimbali bungeni ambayo ilikuza lugha ya Kiswahili. Katibu mkuu mtendaji
Robert Matano alitangaza mpango wa kuinua hadhi ya Kiswahili mwaka wa 1974
na serikali ilipanga kutekeleza mpango huo katika awamu mbili. Awamu ya
kwanza ilipaswa kutekelezwa mwaka wa 1971, ambapo ilihitajika Wakenya wote
wazungumze Kiswahili miongoni mwao na pia kwa wale ambao si Wakenya
katika shughuli rasmi na shughuli zisizo rasmi. Katika awamu ya pili walisema
kuwa lugha ya Kiswahili ndio lugha ambayo ingetekeleza shughuli zote rasmi
isipokuwa katika vyuo vikuu na korti (Mbaabu,1996). Anaendelea kwa kuelezea
kuwa, wafanyakazi wote wa serikali walipaswa kufanya mtihani wa Kiswahili na
kupita ili waweze kupandishwa cheo kazini. Wabunge walihitajika kujua
Kiswahili ili waweze kuwasiliana na wananchi. Vituo mbalimbali vya kufunza
Kiswahili vilijengwa katika kila mkoa ili Wakenya waweze kujifunza Kiswahili
kama ilivyopendekezwa na serikali.
Nyandwaro (2015) akimnukuu Mbaabu (1996) anaeleza kuwa, kuna mabadiliko
yaliyofanywa kwenye katiba ya awali kuhusu lugha. Kifungu cha 53 kilifanyiwa
mabadiliko pale ambapo lugha ya Kiswahili ilipewa hadhi mpya ya kuwa lugha
rasmi bungeni badala ya Kiingereza. Hali hii iliwakanganya wabunge kwani
walihitajika kufanya mitihani ya Kiingereza na wala sio Kiswahili. Kutokana na
35
haya, mwaka wa 1975 Julai, marekebisho yalifanywa katika kifungu hicho hivyo
basi lugha ya Kiswahili na Kiingereza zikachaguliwa kuwa lugha rasmi za bunge.
Katika miaka ya 1990, viongozi walitoa hotuba zao katika lugha ya Kiswahili.
Jambo hili lilifanya Kiswahili kupata hadhi mpya pale ambapo kiliweza kutumika
katika siasa. Wanasiasa walitumia Kiswahili katika kuwasiliana na wananchi
hasa wakati wa uchaguzi. Hali hii si tofauti na sasa kwa kuwa wanasiasa
wanafanya hivi hadi sasa. Pia mijadala bungeni inafanywa kwa lugha ya
Kiswahili na Kiingereza.
Lugha ya Kiswahili kwa sasa inatumika hadi mashinani (Ryanga, 2001). Hii
inatokana na mfumo wa elimu kuwa kila mtu kutoka jamii yoyote anaweza
kutumia lugha ya Kiswahili.
Ni wazi kuwa nchini Kenya hivi leo kuna lugha mbili rasmi, Kiingereza na
Kiswahili. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya Kenya ya sasa (2010) sura ya pili
kifungu cha 7 ibara (ii). Jambo hili linadhihirisha kuwa lugha ya Kiswahili
imepewa hadhi ya juu na serikali. Hivi sasa, Kiswahili chaweza kuwekwa katika
lugha pana za mawasiliano au lugha ya kimataifa kwa kuwa inatumika na
wazungumzaji wengi katika mataifa kumi na manne ya Afrika Mashariki na kati.
Lugha hii inatumika sambamba na Kiingereza katika shughuli za makanisa na pia
machifu na wasaidizi wa machifu hutumia Kiswahili wanapowahudumia
mashinani ambapo wengi hukifahamu Kiswahili kuliko Kiingereza.
Hutumika kutolea mafunzo katika taasisi za ualimu, taasisi za kutolea stashahada
na pia katika vyuo vyote vya umma na vingine vya kibinafsi. Chimerah (2000)
anaeleza kwamba Kiswahili hufunzwa kama lugha ya kigeni katika takriban vyuo
36
mia moja kule Marekani na mataifa mengine ulimwenguni. Hatua zingine
ambazo lugha ya Kiswahili imepiga ni pamoja na toleo la kamusi ya Kiswahili –
Kiswahili.
Hutumika katika kutolea huduma za stakabadhi za serikali kwa kuwa
zimetafsiriwa kwa Kiswahili kwa mfano katika wizara ya uhamiaji na usajili wa
watu zimetafsiriwa kwa Kiswahili. Wizara ya afya ina maelezo ya Kiswahili
kama ya kuhusu magonjwa ya zinaa, Ukimwi na matibabu. Hutumika pia katika
ujazaji wa fomu za usafiri na pia kitambulisho cha kitaifa. Stakabadhi zingine ni
za vifo, ndoa pasipoti na vyeti vya kuzaliwa. Hali hii inaonyesha kuwa Kiswahili
kimekubalika miongoni mwa Wakenya kwa wakati huu ikilinganishwa na hapo
awali. Katika idara ya polisi na vikosi vyake, Kiswahili hutumika wakati wa
mawasiliano ya mdomo hasa wanapowahudumia wananchi. Hata hivyo,
wananchi wengi hukifahamu Kiswahili kutokana na hafla mbalimbali ambazo
huangazia matumizi ya Kiswahili.
Wananchi wengi wamekifahamu Kiswahili kutokana na hafla mbalimbali
ambazo huangazia matumizi ya Kiswahili katika ngazi za kitaifa na pia kimataifa.
Mfano mzuri ni ule wa Wakfu wa Jomo Kenyatta wa kutunza waandishi wa
vitabu vya Kiswahili (Ngigge, 2014). Hali hii ilichangia kuandikwa kwa vitabu
vingi na tuzo nyingi zikapatikana.
Katika makongamano yanayoandaliwa na chama cha Kiswahili, lugha ya
Kiswahili imekuwa ikitumika na hii imechangia kuimarika kwake. Kumekuwepo
na tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanywa, hasa baada ya Kiswahili kufanywa
lugha rasmi ili kutafuta njia za kuifanya ikidhi mahitaji ya lugha rasmi. Hata
37
hivyo, wasomi wameweza kuonyesha mtazamo kubalifu kuhusu Kiswahili. Hatua
kama hizi bila shaka zitaendelea kuendeleza hadhi zote mbili za Kiswahili na pia
kujenga utayari wake kimatumizi miongoni mwa wakenya.
ii) Vyombo vya Habari
Vyombo vya habari vimesaidia kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili katika
viwango mbalimbali nchini Kenya. Kwa sasa Kiswahili kinatumika katika
mashirika ya utangazaji ndani na nje ya Kenya (Ngigge, 2014). Katika
televisheni tuna vipindi ambavyo hutumia Kiswahili. Taarifa za habari za
Kiswahili husomwa saa moja jioni katika kila kituo cha runinga na saa kumi
alasiri katika runinga ya KBC, Citizen, NTV, na KTN. Kuna vipindi mbalimbali
ambavyo hupeperushwa kwa lugha ya Kiswahili, vipindi kama ‘Inspekta Mwala’
na Machachari katika kituo cha Citizen. Hii ni kuonyesha kuwa lugha hii
inakubalika ingawa si kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ile ya Kiingereza.
Katika redio kuna idhaa mbalimbali za redio ambazo hupeperusha vipindi,
matangazo na habari kwa lugha ya Kiswahili. Idhaa hizi za Kiswahili husikilizwa
na watu wengi hasa watu wa mashambani na hupeperusha vipindi
vinavyowaelimisha wananchi na pia kuwaburudisha. Idhaa hizi ni kama vile
idhaa ya Taifa, Redio Citizen, Redio Milele, Redio Maisha, Redio Jambo na Q-
fm. Katika Redio Citizen kuna kipindi ambacho watangazaji hutoa mijadala na
michango ya lugha ya Kiswahili. Kipindi hicho hutoa mafunzo mengi kwa
wasikilizaji wake hasa wanafunzi na wasomi wa Kiswahili.
Kuna gazeti la ‘Taifa Leo’ ambalo ndilo gazeti pekee linalochapishwa katika
lugha ya Kiswahili. Gazeti hili huwa limegawanywa katika sehemu mbalimbali
38
kama vile taarifa za spoti, taarifa ya nchi na kimataifa, dondoo za hapa na pale,
shindano la uandishi wa insha, sehemu ya fasihi ambapo waandishi mbalimbali
huandika makala yao wakitoa michango mbalimbali kuhusiana na mambo tofauti
na kisha sehemu ya sokomoko ambapo mashairi huchapishwa.
Hata ingawa vyombo hivi vya habari vinaendeleza lugha ya Kiswahili na
kuonyesha ukubalifu miongoni mwa wananchi, bado si watu wote ambao
wanadhihirisha ukubalifu huu. Hii ni kwa kuwa kuna baadhi ya vipindi ambavyo
vinadhihirisha utabaka pale ambapo maonyesho katika vipindi hutumia lugha ya
Kiingereza hasa kule ofisini katika sehemu ya wafanyakazi ambao wanafanya
kazi za hadhi ya chini kama mayaya; waajiriwa wao huwasiliana nao kwa lugha
ya Kiswahili.
2.3 Hitimisho
Kutokana na maelezo ya sura hii, ni wazi kwamba lugha ya Kiswahili imeweza
kuwa na ukubalifu tofauti kulingana na hali tofauti tofauti. Katika kipindi cha
ukoloni, Kiswahili hakikukubalika na wakoloni na Wakenya waliona ni lugha
ambayo haingewafaa kimaendeleo. Baada ya ukoloni, lugha hii ilianza
kukubalika kutokana na sera mbalimbali zilizowekwa na serikali na sasa ni lugha
rasmi. Hii ilikuwa hatua muhimu kwa kuwa sasa watu wamekubali kutumia
lugha hii katika sehemu mbalimbali ijapokuwa bado haitumiki kila mahali.
39
SURA YA TATU
UTAYARI WA WAKENYA KATIKA SERA MPYA YA
KISWAHILI
3.0 Utangulizi
Katika sura ya pili, tumejadili Historia ya utayari wa Wakenya hasa kuhusiana na
sera ya urasmi wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya. Sura hiyo ilionyesha utayari
wa Wakenya wanavyotumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi na pia
matumizi yao kimaongezi. Katika sura hii ya tatu, lengo lililojadiliwa lilionyesha
utayari wa Wakenya katika kutumia Kiswahili ili kuimarisha lugha ya Kiswahili
kama lugha rasmi. Katika utafiti huu, kuna vigezo mbalimbali ambavyo
vilitumiwa ili kusaidia katika uchanganuzi wa data hili kuonyesha jinsi ambavyo
utayari wa Wakenya katika matumizi ya Kiswahili ulivyo, kwa mujibu wa
mtazamo wa upangaji wa lugha kihadhi. Upangaji lugha ni swala muhimu hasa
tukizingatia katika sera ya Kiswahili, ambapo tunahitaji Kiswahili kitumike kama
lugha rasmi.
3.1 Uchanganuzi wa kauli za utayari wa Wakenya katika sera mpya ya
Kiswahili katika
kuimarisha lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi.
Changanuzi hizi zilionyesha jinsi washiriki walivyotoa majibu yao kuhusiana na
utayari wao katika matumizi ya lugha ya kiswahili. Matokeo ni kama ifuatavyo
40
Jedwali 3.1.1: Lugha ambayo wafanyikazi wanapenda kuitumia sana katika
mawasiliano ya kimaongezi
Maelezo Idadi ya Watafitiwa Asilimia
Kiswahili 27 64.3
Kiingereza 11 26.2
Lugha mseto 4 9.5
Jumla 42 100
Chati 3.1.1: Lugha inayotumiwa sana na wafanyikazi katika mawasiliano ya
kimaongezi
Watafitiwa arobaini na wawili (42) walijibu swali hili. Watafitiwa ishirini na saba
ambao ni asilimia 64.3 walisema wanapenda kutumia lugha ya Kiswahili,
watafitiwa kumi na mmoja ambao ni asilimia 26.2 walisema wanapenda kutumia
lugha ya Kiingereza, watafitiwa wanne ambao ni asilimia 10 walisema
wanapenda kutumia lugha mseto. Katika uchanganuzi huo, ilidhihirika kuwa
64%
26%
10%
0%
Kiswahili
Kiingereza
41
asilimia kubwa ya watafitiwa ambao walipenda kutumia lugha ya Kiswahili
katika maongezi yao ya kila siku walikuwa na miaka thelathini na tano (35) na
zaidi, wengi wao walitoka katika idara ya polisi. Waliopenda kutumia
Kiingereza walitoka katika sekta ya utamaduni na vyombo vya habari.
Ilidhihirika wazi kuwa Kiswahili kilitumika tu katika vitengo vichache katika
sekta ya utangazaji. Aidha, jinsia ya kike ilionekana sana kupendelea kutumia
lugha ya Kiingereza sana kuliko lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, lugha mseto
ambayo ni mchanganyiko wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza vilevile ilitumika.
Matumizi ya Kiswahili katika idara ya Polisi yalionekana kutumika sana,
walisema kuwa Wananchi wengi walijieleza kwa lugha hii na hivyo kwa wakati
mwingi lugha hiyo ndiyo iliyotumika. Lugha hii imeonekana kutumika kwa
wingi katika maongezi lakini bado haijakita mizizi kama lugha rasmi kama
ilivyoidhinishwa kikatiba. Sababu ni kuwa, watu wengi bado wanaichukulia
kuwa ni ya hadhi ya chini. Hii ni kuonyesha kuwa lugha hii bado haijafikia
kiwango cha urasmi. Kwa mujibu wa mtazamo wa upangaji lugha kihadhi,
huzingatia juhudi zinazochukuliwa ili kubadilisha matumizi na majukumu ya
lugha katika jamii. Hali ndiyo hii nchini Kenya ambapo lugha ya Kiswahili
inatumika lakini si kwa misingi ya kama lugha rasmi kwa wingi katika
mawasiliano.
Swali lililofuata lililenga kuelezea ni kwa nini wao hutumia lugha hiyo ya
mawasiliano. Jibu hilo limeonyeshwa katika jedwali na chati
42
Jedwali 3.1.2 : Sababu zinazowafanya kutumia Kiswahili
Maelezo Idadi ya Watafitiwa Asilimia
Ni lugha ya taifa 6 22.2
Hutumiwa na matabaka
mbalimbali kurahisisha
mawasiliano
3 11.1
Ni rahisi kueleweka 18 66.7
Jumla 27 100
Chati 3.1.2: Sababu za kutumia Kiswahili
Watafitiwa waliosema kuwa huzungumza lugha ya Kiswahili walikuwa 27. Kati
ya hao 27, asilimia 66.7 walisema kuwa lugha ya Kiswahili ni rahisi kueleweka
na kuzungumza. Watafitiwa 6, ambao ni asilimia 22.1 walisema lugha ya
Kiswahili ni lugha ya taifa. Watafitiwa 3 wakiwakilisha asilimia 11.1 walisema
kuwa wao hutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa hutumiwa na matabaka
mbalimbali kurahisisha mawasiliano.
22%
11%
67%
0%
Ni lugha ya Taifa
Hutumiwa na matabaka mbalimbali
Ni rahisi kueleweka
43
Kutokana na maelezo haya, lugha ya Kiswahili inatumika sana kutokana na
kueleweka kwake kwa urahisi.
Jambo hili huenda limetokana na mazoea ya watu kutumia lugha hii katika
mawasiliano yao ya kila siku na pia lugha hii ina asili ya Afrika hasa Afrika
Mashariki. Kwa kuwa Kiswahili ni lugha yenye asili ya Kibantu, watu wengi
hujihusisha nayo.
Kutokana na historia fupi tuliyoitoa katika sura ya pili, kumedhihirika ukubalifu
wa sera hii miongoni mwa Wakenya pale ambapo wameweza kuitumia katika
shughuli zao. Ukubalifu huu unadhihirisha kuwa lugha hii wanaiona rahisi na
inaeleweka. Hata hivyo, lugha ya Kiingereza hutumika katika miktadha rasmi
ilhali katika kimaongezi lugha ya Kiswahili ndio inayotumika kwa wingi zaidi.
Jedwali 3.1.3: Sababu zinazowafanya kutumia lugha ya Kiingereza
Maelezo Idadi ya Watafitiwa Asilimia
Ina hadhi ya juu 3 27.3
Ni rahisi kujieleza 7 63.6
Ni lugha rasmi 1 9.1
Jumla 11 100
44
Chati 3.1.3: Sababu za kutumia lugha ya Kiingereza
Waliosema kuwa hutumia lugha ya Kiingereza, asilimia 63.6 walisema kuwa ni
lugha rahisi katika mazungumzo yao wanapojieleza. Asilimia 27.3 walisema
kwamba lugha ya Kiingereza ni lugha ya hadhi ya juu. Asilimia 9.1 walisema
wao hutumia lugha ya Kiingereza kwa kuwa ni lugha rasmi na kwa njia hiyo
kunadhihirika kuwa lugha hii bado inaonekana kuwa na umaarufu.
Maelezo haya yanaonyesha kuwa lugha hii ni rahisi katika mazungumzo ya
watumiaji wake wakati wanapojieleza katika miktadha mbalimbali. Hali hii
inadhihirisha kuwa lugha ya Kiswahili bado haijafaulu katika hadhi yake ya kuwa
lugha rasmi, na hivyo bado Wakenya hawajaweza kuitumia lugha hii kikamilifu.
Hii ni kwa kuwa lugha ya Kiingereza imetiliwa mkazo na kutumika sana katika
sekta nyingi sana hapa nchini, ikilinganishwa na lugha ya Kiswahili ambayo
27%
64%
9%
0%
Ina hadhi ya juu
Ni rahisi kujieleza
Nilugha rasmi
45
hutumika kama lugha ya mawasiliano pekee. Lugha hii ilionekana kukita mizizi
katika matumizi yake hasa katika vyombo vya habari pale ambapo katika vitengo
vya utangazaji. Watu wengi waliotumia lugha ya Kiingereza walieleza kuwa
katika vitengo vyao hakukuwepo na istilahi mwafaka zilizowawezesha kutumia
Kiswahili hivyo wao walipendelea kutumia lugha ya Kiingereza. Kwa kurejelea
nadharia ya Utekelezaji mambo ya kimsingi ambayo nadharia hii huzingatia ni
mawasiliano. Ijapokuwa tunatambua kuwa lugha ya Kiswahili inaweza kutumiwa
katika miktadha rasmi, Wakenya wengi hawafuati kauli hii. Ili kuweza kuwa na
matokeo yananyofaa sharti tuzingatie mifumo inayofaa.
Swali lingine lililenga kutathmini matumizi ya lugha ya Kiswahili kabla ya
kuidhinishwa kwa katiba mpya. Majibu ya swali hili yameonyeshwa katika
jedwali lifuatalo
Jedwali 3.1.4: Matumizi ya lugha ya Kiswahili kabla ya kuidhinishwa kwa
katiba
mwaka wa 2010
Maelezo Idadi ta Watafitiwa Asilimia
Mazuri 13 31
Mazuri kiasi 21 50
Mabaya 8 19
Jumla 42 100
46
Chati 3.1.4: Matumizi ya Kiswahili kabla ya kuidhinishwa kwa katiba
mwaka wa 2010
Swali hili lilijibiwa na watafitiwa wote 42. Watafitiwa ishirini na mmoja ambao
ni asilimia 50 walisema kuwa matumizi ya lugha hii yalikuwa mazuri kiasi. Hii ni
nusu ya watafitiwa waliohojiwa. Watafitiwa 13 ambao ni asilimia 31 walisema
kuwa matumizi ya sera hii ya lugha kabla ya katiba kuidhinishwa yalikuwa
mazuri, ilhali watafitiwa 8 ambao ni asilimia 19 wakasema yalikuwa mabaya.
Kutokana na waliotafitiwa, matokeo yao yanaonyesha kuwa, matumizi ya
Kiswahili kabla ya katiba ya 2010 yalikuwa mazuri kiasi. Hii ni kuonyesha kuwa
Kiswahili kilitumika kama lugha rasmi ingawa kwa kiwango kidogo sana. Hivyo,
hungeweza kujieleza kwa lugha hii katika miktadha rasmi na hivyo lugha hii
kihadhi ilikuwa lugha ya taifa pekee. Asilimia 19 ambayo ilisema kuwa matumizi
ya Kiswahili yalikuwa mabaya kabla kuidhinishwa kwa katiba 2010, inaweza
kuelezwa kwa misingi kuwa iwapo mtu angejieleza kwa lugha hii katika ofisi za
31%
50%
19%
0%
Mazuri
Mazuri kiasi
Mabaya
47
umma hangepuuzwa hivyo, hali hii inaonyesha hali ya matumizi ya lugha hii
yalivyokuwa. Hata hivyo, kuna wale walioona kuwa matumizi ya lugha ya
Kiswahili yalikuwa yakitumika vizuri.
Swali lililofuatia lilinuia kutathmini mabadiliko ya utekelezaji wa sera hii baada
ya kuidhinishwa kwa katiba mwaka wa 2010. Majibu ya swali hilo
yameonyeshwa katika jedwali lifuatalo
Jedwali 3.1.5: Mabadiliko ya utekelezaji wa sera hii baada ya kuidhinishwa
kwa katiba
mwaka wa 2010
Maelezo Idadi ya watafitiwa Asilimia
Mazuri Sana 11 26.2
Mazuri 19 45.2
Mazuri kiasi 4 9.5
Hayajabadilika 8 19.1
Jumla 42 100
48
Chati 3.1.5: Mabadiliko ya sera hii baada ya kuidhinishwa kwa katiba
mwaka wa 2010
Watafitiwa wote 42 walijibu swali hili, hii ikiwa ni asilimia 100 ya watafitiwa.
Asilimia kubwa ya waliotafitiwa walibaini kuwa mabadiliko ya utekelezaji wa
sera ya Kiswahili yalikuwa mazuri. Hii ilikuwa ni watafitiwa kumi na tisa ambao
ni asilimia 45.2 ya waliohojiwa. Watafitiwa kumi na mmoja ambao ni asilimia
26.2 walisema kuwa mabadiliko hayo yalikuwa mazuri sana, watafitiwa wanane
ambao ni asilimia 19.1 wakasema kuwa hakukuwa na mabadiliko yoyote ilhali
asilimia 9.5 wakasema kuwa mabadiliko hayo yalikuwa mazuri kiasi.
Kwa mujibu wa mtazamo wa upangaji lugha kihadhi, ili lugha kubadilisha
matumizi na majukumu yake katika jamii, sharti kuwe na juhudi fulani
zinazowekwa ili mabadiliko hayo kufikiwa. Haya ndiyo yanayojitokeza.
Kiswahili kilipata mabadiliko ya kihadhi baada ya katiba ya 2010 kuidhinishwa.
Lugha huweza kuimarika kwa watumiaji wake iwapo; majukumu yake
26%
45%
10%
19%
Mazuri sana
Mazuri
Mazuri kiasi
Hayajabadilika
49
yanaongezeka kwa kuwa huwa kuna manufaa kwa watumiaji hao hasa ikiwa
lugha hiyo inapewa hadhi ya juu. Kufanywa kwa Kiswahili kuwa lugha rasmi,
kuliwafanya watafitiwa wengi kukubali kutumia lugha hii na kuitumia kwa wingi
huku wakiwa na matarajio kuwa lugha hii ingewafaa zaidi na kujipatia umaarufu.
Kutokana na majibu hayo, ni wazi kuwa kuna kundi la waliotafitiwa ambao
hawakuona mabadiliko yoyote katika sera ya Kiswahili baada ya kuidhinishwa
kwa katiba mpya ya 2010. Kikundi hiki kilitoa maoni haya kwa misingi kuwa,
Kiswahili bado hakikupata ukubalifu miongoni mwao na hivyo bado walisita
kutumia lugha hiyo, aidha baadhi yao walisema kuwa hakukuwa na mikakati
kabambe ya kutekeleza Kiswahili kuchukua mahali pake pa kuwa lugha rasmi.
Hata hivyo, kuna wale waliosema kuwa kulikuwa na mabadiliko ya sera ya
Kiswahilli na yalichangia lugha hii kukubalika na kupokelewa vyema kama
lugha rasmi. Ni wazi kuwa mabadiliko haya yalikubaliwa kwani hakuna
aliyesema kuwa alikichukia Kiswahili zaidi baada ya kuidhinishwa kwa katiba ya
mwaka wa 2010. Hii inaonyesha kuwa majukumu mapya yaliyopewa lugha ya
Kiswahili yalipokelewa vyema.
Swali lililofuatia lililenga kuonyesha sababu zilizowafanya wale waliosema kuwa
hakuna mabadiliko ya sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi
50
Jedwali 3.1.6: Sababu za waliosema kuwa hakuna mabadiliko ya sera ya
lugha ya
Kiswahili kama lugha rasmi
Maelezo Idadi ya watafitiwa Asilimia
Ukosefu wa mikakati
mwafaka katika sekta zao
5 58.1
Uhaba wa istilahi katika
Nyanja mbalimbali
2 27.50
Ukosefu wa vifaa
muhimu vya kuinua
lugha ya Kiswahili
1 14.4
Jumla 8 100
Watafitiwa 5 ambao ni asilimia 58.1 ya waliotafitiwa walisema kuwa hakuna
mabadiliko katika sera ya Kiswahili kama lugha rasmi walieleza kuwa hakuna
mikakati yoyote katika sekta wanazofanya kazi. Hata hivyo, ilibainika wazi kuwa
katika sekta ya utangazaji baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa hawakujua
kuwa lugha ya Kiswahili ilipata hadhi mpya ya kuwa lugha rasmi. Watafitiwa 2
ambao ni asilimia 27.50 yao walisema kuwa hakuna istilahi za kutosha ili kukidhi
mabadiliko na ukuaji wa teknolojia ilhali mtafitiwa mmoja ambaye ni asilimia
14.4 alieleza kuwa Kiswahili kina ukosefu wa vifaa muhimu kama vile vitabu na
majarida ya kutosha ili kuiinua lugha ya Kiswahili.
Swali hilo lililenga wale ambao hawakuona mabadiliko yoyote katika mabadiliko
ya sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi baada ya kuidhinishwa kwa
katiba ya 2010. Matokeo ya swali hilo yanadhihirisha kuwa hakukuwa na
mikakati yoyote ya kukifanya Kiswahili kuwa bora. Hali hii inawafanya wao
51
kuona lugha hii kama haina manufaa na kwa misingi hii, lugha hii haijapokelewa
vyema kwa kuwa iwapo hakuna utekelezaji au ukiwa wa hali ya chini
hakutakuwa na mabadiliko yanayofaa.
3.2: Kuimarika kwa Lugha ya Kiswahili
Sehemu hii ya utafiti ililenga kuchunguza iwapo mabadiliko ya Kikatiba kuhusu
hadhi mpya ya lugha ya Kiswahili nchini Kenya imeimarika. Mabadiliko
yaliyolengwa ni yale yaliyofanywa mnamo mwaka wa 2010. Maswali
yaliyoulizwa yalilenga kumwelekeza mtafitiwa kutoa majibu ambayo
yangemsaidia mtafiti kufikia lengo hilo.
Swali la kwanza katika sehemu hii lililenga kutambua kuimarika au kutoimarika
kwa hadhi mpya ya lugha ya Kiswahili baada ya kuidhinishwa kwa katiba ya
2010. Majibu ya swali hilo yameonyeshwa kama ifuatavyo
Jedwali 3. 2. 1: Sera mpya ya Kiswahili huimarisha hadhi yake ya kirasmi
Maelezo Idadi ya watafitiwa Asilimia
Ndio 23 54.8
La 19 45.2
Jumla 42 100
52
Chati 3.2.1: Sera mpya ya Kiswahili huimarisha hadhi yake ya Kiswahili
Watafitiwa ishirini na watatu ambao ni asilimia 54.8 walikubali kuwa Kiswahili
kwa hakika kilikuwa kimeimarika zaidi tangu kuidhinishwa kwa katiba mpya ya
2010 kuwa lugha rasmi. Watafitiwa kumi na tisa ambao ni asilimia 45.2 ya
walieleza kuwa Kiswahili hakikuwa kimeimarika hata baada ya kuidhinishwa
kwa katiba ya 2010 kuhusiana na hadhi yake ya kuwa lugha rasmi.
Kwa mujibu wa washiriki wanaonyesha wazi kuwa Kiswahili kimeimarika na
kuwa lugha rasmi zaidi tangu kuidhinishwa kwake. Uimarikaji huu unatokana na
matarajio makuu ambayo watafitiwa wanayo. Lugha inapoinuka kihadhi watu
wengi hutaka kufaidika kutokana nayo na pia wanaionea fahari
wanapoizungumza. Hali hii mpya ya Kiswahili iliwafanya watafitiwa kuhisi
kwamba Kiswahili kitawafaa watu wengi kwa njia mbalimbali.
Swali lilofuatia lililenga watafitiwa kuelezea sababu moja kuu ya jibu
walilolichagua katika swali la (3.2.1). Majibu yake ni kama ifuatavyo
55%
45%
0% 0%
Ndio
La
53
Jedwali 3.2.2: Sababu zinazofanya Kiswahili kuimarika kama lugha rasmi
Maelezo Idadi ya watafitiwa Asilimia
Kutumiwa katika ofisi
mbalimbali za serikali
3 13.0
Kutumiwa katika
shughuli za kitaifa
3 13.0
Watu wengi hutumia
lugha hii
15 65.2
Kutumika katika sekta ya
utangazaji
2 8.7
Jumla 23 100
Chati 3.2.2: Sababu za Kiswahili kuimarika kama lugha rasmi
13%
13%
65%
9%
kutumiwa katika ofisi mbalimbali za serikali
kutumiwa katika shughuli za kitaifa
watu wengi kutumia lugha hii
kutumika katika sekta ya utangazaji
54
Waliosema kuwa lugha ya Kiswahili imeimarika kama lugha rasmi walitoa
sababu zao huku watafitiwa 15 ambao ni asilimia 65.2 ya wakisema kuwa watu
wengi katika sekta zilizotafitiwa walitumia lugha hii ikilinganishwa na hapo
awali ambapo lugha hii haingetumika katika miktadha rasmi hasa katika ofisi
zao. Watafitiwa 3 ambao ni asilimia 13 walidai kuwa lugha hii ilitumika katika
shughuli za kitaifa mfano ni pale ambapo lugha ya Kiswahili sasa inatumika
katika sherehe za Kitaifa na halfa mbalimbali kukiwepo na makongamano
ambayo yanaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili hivyo lugha hii imeimarika kama
lugha rasmi.
Watafitiwa 3 ambao ni asilimia 13 walieleza kuwa lugha hii imetumiwa katika
ofisi mbalimbali za Kiserikali. Hii ni kuonyesha kuwa kuna ukubalifu ingawa
matarajio ni kwamba asilimia hiyo ingekuwa bora iwapo ingekuwa ya juu zaidi.
Mtafiti mmoja ambaye ni asilimia 8.7 ya waliotafitiwa alieleza kuwa Kiswahili
kiliweza kutumika katika sekta ya utangazaji kwa kuwa idadi ya vipindi
vilivyotumia lugha ya Kiswahili vilikuwa vimeongezeka ikilinganishwa na hapo
awali.
Mtafiti pia alinuia kujua sababu za watafitiwa kusema kuwa Kiswahili
hakijaimarika kirasmi. Baadhi ya sababu zilizotolewa na watafitiwa
zimefafanuliwa katika kauli la (3.2.3)
55
Jedwali 3.2.3: Sababu zinazofanya Kiswahili kutoimarika kama lugha rasmi
Maelezo Idadi ya Watafitiwa Asilimia
Matumizi ya lugha ya
sheng
3 15.8
Ukosefu wa serikali
kuendeleza shughuli za
kukuza Kiswahili kama
lugha rasmi
8 42.1
Lugha ya Kiingereza
bado kutumika sana
katika nyanja mbalimbali
3 15.8
Stakabadhi nyingi
zinapatikana katika lugha
ya Kiingereza
5 26.3
Jumla 19 100
Chati 3.2.3: Sababu za Kiswahili kutoimarika kama lugha rasmi
16%
42% 16%
26%
Matumizi ya lugha ya Sheng
Ukosefu wa sera za kiserikali kuendeleza shughuli za kukuza kama lugha rasmi
Lugha ya Kiingereza bado kutumika sana katika nyanja mbalimbali
Stakabadhi nyingi zinapatikana katika lugha ya Kiingereza
56
Waliosema kuwa Kiswahili hakikuwa kimeimarika katika hadhi yake ya kuwa
lugha rasmi, walitoa sababu zao ili kuunga madai yao. Asilimia 42.1 walisema
kuwa ukosefu wa sera za kiserikali kuendeleza Kiswahili kama lugha rasmi
ndiyo ilikuwa sababu kuu ya lugha hii kutoimarika. Asilimia 26.3 walieleza
kuwa stakabadhi nyingi rasmi zilipatikana katika lugha ya Kiingereza hivyo
jambo hili lilizuia kuimarika kwa lugha hii kuwa rasmi. Asilimia 15.8 ya
waliohojiwa walisema kuwa lugha ya Kiingereza bado ilitumika sana katika
nyanja mbalimbali, ilhali asilimia nyingine sawa na hiyo ya 15.8 ya waliohojiwa
walisema kuwa matumizi ya sheng yalizuia hali ya Kiswahili kutoimarika na
kuwa lugha rasmi. Swala la sheng limekuwa changamoto katika lugha ya
Kiswahili kwa kuwa watu wana dhana kuwa lugha ya Kiswahili ni ngumu na
hivyo wanapendelea kutumia ‘Sheng’ katika mazungumzo yao.
Watafitiwa pia walihitajika kupendekeza njia moja nzuri ambayo walifikiria
ingeweza kukifanya Kiswahili kiimarike nchini Kenya, kama lugha rasmi. Jibu
la swali hilo limeelezwa na kauli (3.2.4)
57
Jedwali 3.2.4: Pendekezo la njia moja nzuri ambayo inaweza kufanya
Kiswahili
kikubalike kama lugha rasmi
Maelezo Idadi ya watafitiwa Asilimia
Kiswahili kupewa hadhi
sawa na Kiingereza
9 21.4
Kuwepo na magazeti zaidi
ambayo yanachapishwa
kwa lugha ya Kiswahili
3 7.1
Kiswahili kutumika katika
shughuli zote za Kiserikali
rasmi
30 71.4
Jumla 42 100
Chati 3.2.4: Mapendekezo ya kukifanya Kiswahili kikubalike kama lugha
rasmi
21%
7%
72%
0%
Kupewa hadhi sawa na Kiingereza
Kuwepo kwa magazeti zaidi ambayo yanachappishwa kwa lugha ya Kiswahili
Kiswahili kutumika katika shughuli zote za Kiserikali rasmi
58
Asilimia 71.4 ya watafitwa walipendekeza Kiswahili kitumike katika shughuli
zote za Kiserikali rasmi, jambo hili litawezesha lugha hii kuafikia lengo lake la
kuwa lugha rasmi kwa kuwa itawalazimu kutumika katika maeneo mengi
Serikalini. Hata hivyo, hadhi yake mpya iliyopewa kikatiba 2010 itaweza
kuafikiwa na kukomesha hali yake ya kuchukuliwa kuwa ni lugha yenye hadhi ya
chini. Asilimia 21.4 ya watafitiwa walipendekeza kuwa Kiswahili kupewa hadhi
sawa na Kiingereza kwa sasa jinsi hali ilivyo ni kuwa bado watu katika sekta
zilizofanyiwa utafiti wanaona kuwa lugha ya Kiingereza ina hadhi ya juu kuliko
Kiswahili ingawa Kikatiba lugha hizi zina hadhi sawa. Asilimia 7.1 ya
watafitiwa walipendekeza kuwepo na ongezeko la magazeti zaidi ya lugha ya
Kiswahili, kwa sasa tuna gazeti la ‘Taifa Leo’ pekee ambalo huchapisha habari
kwa lugha ya Kiswahili.
Kutokana na mapendekezo haya, ni wazi kuwa watafitiwa wengi walihisi kuwa
ukosefu wa Serikali kutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli zote za kiserikali
ndio hasa sababu kuu ya lugha ya Kiswahili kutoimarika na kuwa lugha rasmi.
Kwa hivyo, ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa kwanza, waifanye hadhi hii
mpya ya lugha kisheria kisha wahakikishe kuwa inatumika katika shughuli za
kiserikali kwa wingi. Pia jibu la Kiswahili kutopewa hadhi sawa na lugha ya
Kiingereza lilionekana kuwa pingamizi la kutoimarika kwa Kiswahili na hali hii
inatambulikana kikatiba. Lugha ya Kiswahili ni lugha muhimu na hivyo ni
jukumu la serikali kuhakikisha kuwa kisheria, hadhi hiyo imewekwa na
kuzingatiwa ili matumizi yake yadhihirike katika nyanja zake mbalimbali.
59
3.3 Muhtasari
Katika sura hii, mtafiti ameshughulikia uchanganuzi wa data kuhusu utayari wa
Wakenya kuhusiana na sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini
Kenya kulingana na walioshiriki kwenye utafiti. Kutokana na matokeo ya utafiti
imedhihirika kuwa Wakenya wapo tayari kuitumia lugha ya Kiswahili kama
lugha rasmi baada ya kuidhinishwa kwa katiba ya 2010. Pia, matokeo ya
kuimarika kwa lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia hadhi yake ya kuwa lugha
rasmi katika katiba bado yanaonyesha kuwa kuna chngamoto zinazokumba
uimarikaji wake.
.
60
SURA YA NNE
CHANGAMOTO NA MIKAKATI YA KUIMARISHA SERA
HII MPYA YA LUGHA YA KISWAHILI
4.0 Utangulizi
Katika sura ya tatu tumejadili suala la utayari wa Wakenya kuhusiana na sera
mpya ya lugha ya Kiswahili na pia uimarikaji wa Kiswahili kama lugha rasmi
baada ya mabadiliko ya katiba ya 2010 nchini. Katika sehemu hiyo, imebainika
kuwa asilimia kubwa ya watafitiwa wapo tayari kutumia lugha ya Kiswahili
katika hadhi yake ya kuwa lugha rasmi. Imedhihirika pia, lugha ya Kiswahili
haijapokelewa ipasavyo na Wakenya wote huku pia swala la kuimarika likiwa
halijatimizika inavyotakikana kwa kuwa serikali haijaweza kuendeleza sera hii
mpya kadri ya uwezo wao.
Katika sura hii, mtafiti ametumia nadharia ya Utekelezaji kuchanganua data.
Nadharia hii inafaa katika sehemu hii kwa kuwa imejaribu kutathmini jinsi sera
ya lugha inavyopaswa kutekelezwa ili kuafikia madhumuni yake na wakati huo
huo kuangazia changamoto ambazo zaweza kujitokeza katika kuwezesha sera
hiyo mpya kutumika.
Watafitiwa waliulizwa maswali yaliyolenga kumpa mtafiti majibu ambayo
yangemwezesha kufahamu changamoto na pia mbinu wanazotumia wafanyikazi
wa sekta ya Idara ya Polisi, vyombo vya habari na wizara ya utamaduni ili
kuimarisha na kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo katika
kuimarisha lugha ya Kiswahili. Waliweza kutoa maoni yao jinsi wanavyoona ni
61
bora sera hii mpya kuendelezwa ili kuafikia malengo yake ya kuwa lugha rasmi
katika sekta zao mbalimbali.
Sura hii imegawika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza inazungumzia
changamoto zinazokumba wafanyikazi katika sekta zilizohusika katika utafiti
kisha sehemu ya pili inazungumzia mikakati inayowekwa au inayozingatiwa na
watu katika sekta hizi ili kuimarisha na kufanya Kiswahili kuwa na hadhi ya
urasmi na kuonyesha ukubalifu kamili miongoni mwa Wakenya nchini.
4.1 Changamoto zinazowakabili wafanyikazi katika sekta zilizozingatiwa
katika utafiti
katika sera mpya ya Kiswahili kuwa lugha rasmi.
Katika kushughulikia sehemu ya changamoto kulikuwa na maswali kadhaa
yaliyoulizwa watafitiwa kuhusiana na Kiswahili kuwa lugha rasmi. Swali la
kwanza lililenga kubaini iwapo kuna vikwazo katika kufanya Kiswahili kutofikia
malengo yake yanayohitajika. Majibu ya swali hilo yameonyeshwa kama
ifuatavyo katika kauli ya (4.1)
Jedwali ya 4.1.1: Iwapo kuna sheria ambazo zimefanya Kiswahili kutofikia
kiwango
kinachohitajika
Maelezo Idadi ya Watafitiwa Asilimia
Ndio 16 38.1
La 26 61.9
Jumla 42 100
62
Chati 4.1.1: Sheria zinazofanya Kiswahili kutofikia kiwango kinachohitajika
Watafitiwa wote (42) walijibu swali hilo. Asilimia 61.9 ya watafitiwa walisema
kuwa hakuna sheria ambazo zimewekwa ili kuzuia Kiswahili kisifikie kiwango
cha juu cha ufanisi ilhali asilimia 38.1 ya watafitiwa walidai walieleza kuwa
kuna sheria ambazo zimewekwa kukandamiza ukuaji wa lugha ya Kiswahili.
Waliosema kuwa zipo sheria ambazo zimewekwa kufanya Kiswahili
kutoimarika, baadhi yao walisema kuwa, katika ofisi nyingi sharti mtu kujieleza
kwa lugha ya Kiingereza na uandishi wa ripoti au maombi ya chochote
huandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo inayotambulikana kuwa
lugha rasmi. Wengine walisema kuwa vipindi vingi huwa katika lugha ya
Kiingereza. Ingawa tunasema idadi ya vipindi vya Kiswahili vimeongezeka
bado idadi hii haifikii idadi ya vipindi vya Kiingereza. Taarifa kwa mara nyingi
pia ilisemekana kusomwa kwa lugha ya Kiingereza na kwa mara chache
kusomwa kwa lugha ya Kiswahili; wengine walieleza kuwa mawasiliano ya
kimaongezi rasmi baina ya wakubwa kwa wadogo wao hutumia lugha ya
Kiingereza.
38%
62%
0% 0%
Ndio
La
63
Kutokana na matokeo ya swali hili la kuwepo kwa sheria zinazozuia kufikia
malengo katika lugha ya Kiswahili, Asilimia 38.1 walisema kuwa kuna sheria
kuonyesha kuwa bado kuna vikwazo ambavyo vinaifanya lugha ya Kiswahili
kutofikia kiwango chake kinachohitajika. Matumizi ya kukuzwa kwa lugha ya
Kiingereza yanafanya Kiswahili kukandamizwa pale ambapo lugha ya
Kiswahili huonekana ikiwa lugha duni. Lugha zote hizi zapaswa kupewa nafasi
sawa kwa kuwa zote zina hadhi sawa kikatiba. Hivyo ni muhimu iwapo wakuu
katika sekta za utangazaji wanaweza kukipa Kiswahili nafasi sawa
ikilinganishwa na lugha ya Kiingereza hivyo basi kutakuwa na mabadiliko
katika sekta hii.
Swali lingine lililenga kuonyesha changamoto ambazo wafanyikazi wa sekta
zilizotafitiwa hukumbana nazo kuhusu hadhi ya Kiswahili kuwa lugha rasmi.
64
Jedwali ya 4.1.2: Changamoto zinazokumba lugha ya Kiswahili kuhusu
hadhi mpya ya
Kiswahili katika sekta zilizotafiwa
Maelezo Idadi ya watafitiwa Asilimia
Sera za utangazaji
kupendelea matumizi ya
Kiingereza zaidi
9 21.4
Ukosefu wa nafasi sawa
baina ya Kiswahili na
Kiingereza
13 31
Matumizi ya lugha ya
mama
12 28.6
Serikali bado kusisitiza
matumizi ya Kiingereza
katika shughuli zake
8 19
Jumla 42 100
Chati 4.1.2: Changamoto zinazokumba lugha ya Kiswahili katika sekta
zilizotafitiwa
21%
31%
29%
19% Sera za utangazaji kupendelea matumizi ya kiingereza zaidi
Ukosefu wa nafasi sawa baina ya Kiingereza na Kiswahili
Matumizi ya lugha ya mama
Serikali bado kusisitiza matumizi ya Kiingereza katika shughuli zake
65
Watafitiwa wote arobaini na wawili (42) walijibu swali hili. Watafitiwa kumi na
tatu ambao ni asilimia 31 ya watafitiwa walisema kuwa changamoto kuu
wanayokumbana nayo ni kuwa kuna ukosefu wa nafasi sawa baina ya
Kiingereza na Kiswahili. Watafitiwa kumi na wawili ambao ni asilimia 28.6 ya
watafitiwa walieleza kuwa changamoto wanayokumbana nayo ni matumizi ya
lugha ya mama katika maeneo yao ya kazi. Asilimia 21.4 ya watafitiwa ambao
walikuwa tisa walisema kuwa changamoto waliyokumbana nayo ni sera za
utangazaji kupendelea lugha ya Kiingereza kisha watafitiwa wanane
waliowakilishwa na asilimia 19 walisema kuwa changamoto waliokumbana
nayo ni jinsi serikali bado imesisitiza matumizi ya Kiingereza katika shughuli
zake.
Kutokana na majibu haya ni dhahiri kuwa idadi kubwa ya watafitiwa walidai
kuwa lugha ya Kiingereza inakuzwa zaidi kuliko lugha ya Kiswahili kama lugha
iliyo bora zaidi. Tokeo hilo linaafikiwa pale ambapo kunadhihirika kuwa
asilimia 21.4 ilisema kuwa katika sera za utangazaji lugha ya Kiingereza
hupendelewa zaidi. Kulikuwa pia na matumizi ya lugha ya mama kama
changamoto. Ni jambo la kushangaza kuwa bado watu wanatumia lugha mama
katika miktadha rasmi, wakati tuna lugha mbili ambazo zinaweza kutumika
katika miktadha hiyo. Hata hivyo, sharti kubuniwe mipango maalum ya kuweza
kufanya lugha hizo kuwa na usawa.
Swali lililofuatia lilieleza kwa nini bado Kiswahili hakijakita mizizi kama lugha
rasmi kikatiba aidha pia mtafiti alitaka kubaini ni nini kilichochangia
66
kutokuwepo ukamilifu katika utayari wa wakenya katika matumizi ya lugha ya
Kiswahili.
Jedwali 4.1.3: Sababu zinazofanya Kiswahili bado kutofikia hadhi yake ya
kuwa rasmi na nini kilichochangia kutokuwepo na ukamilifu wa utayari wa
Wakenya
Mahojiano yaliyofanyika miongoni mwa watu walioko serikalini yalibaini
kuwa, kuna mswada ambao upo bungeni ambao haujapitishwa rasmi. Mswada
huo ni ‘Sera ya lugha za Kenya’. Kupitishwa kwa mswada huu hakuzui nafasi
ya lugha ya Kiingereza ya hali yoyote ile. Mswada huu hapo awali ulikuwa
umejadiliwa katika wizara ya michezo na utamaduni kisha ukapelekwa katika
wizara ya mawasiliano na teknolijia. Katika hatua za mwanzo washika dau
waliamini kuwa mswada huu ungepitishwa kwa haraka lakini mambo haya
yalikwenda kinyume na matarajio yao. Kamati ya Afrika Mashariki tayari
inatekeleza majukumu yake lakini nchi ya Kenya bado haijaweza kuwa na
baraza la kitaifa la Kiswahili. Katika kuendeleza lugha ya Kiswahili inatoa
nafasi ya uhakika wa kitaifa kupitia kusherekea kwa lugha na tamaduni
mbalimbali.
Wabunge wamekuwa wakipitisha baadhi ya miswada ambayo inawafaidi wao
na hivyo hali hii imechelewesha kupitishwa kwa mswada wa Kiswahili kuwa
lugha rasmi kuwa mswada huu ukipitishwa itakuwa sheria maalum na hivyo
itaweza kutumika ipasavyo katika ofisi zote za Kiserikali.
Ilibainika kuwa serikali haijawajibika kwa ambavyo mikakati iliyowekwa
haijatekelezwa kikamilifu hivyo hiyo ni sababu nyingine ya kuifanya Kiswahili
kutofikia hadhi yake ya kuwa lugha rasmi.
67
Pia ilibainika kuwa kufungwa kwa kituo cha ‘QTV’ kulisababishwa na
kutozalisha kwa fedha. Kituo hiki ni moja ya vituo ambavyo vinaendeleza lugha
ya Kiswahili. Kituo hiki kilitumia lugha ya Kiswahili kwa kiwango kikubwa
sana na hivyo kwa kuwa hakikuzalisha fedha hali hii ilifanya kituo hiki
kufungwa. Hoja kuwa kituo hiki kilikuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili
haikuzingatiwa. Hii ni kudhihirisha kuwa biashara ndio ilikuwa ya maana sana.
Hivyo hayo ndiyo baadhi ya maoni ambayo yalitolewa na wahojiwa.
4.2 Mikakati ya kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bora katika sekta
zilizotafitiwa ili
kukabiliana na changamoto zinazozuia kiwango kinachohitajika
Sehemu inayofuata imeshughulikia mikakati ambayo viongozi katika sekta
zilizofanyiwa utafiti wameweka na mapendekezo yao kwa serikali kuu nchini ili
kuweza kukabiliana na changamoto zinazofanya Kiswahili kutofikia hadhi yake
ya urasmi.
Ili kupata data iliyokamilika na ambayo ilimwezesha mtafiti kufikia malengo
yake, mtafiti aliwahoji watafitiwa wachache na kuuliza maswali aliyonuia
kupata majibu ambayo yalimwezesha mtafiti kupata matokeo aliyonuia.
Swali la kwanza katika sehemu hii lililenga mtafitiwa aeleze iwapo kuna njia
ambazo anafikiri serikali inaweza kubuni ili kukabiliana na changamoto ya hadhi
yake ya kuwa lugha rasmi.
Matokeo ya swali hilo yamefafanuliwa katika kauli ifuatayo
68
Jedwali 4.2.1: Njia ambazo zinawekwa katika kukipa Kiswahili nafasi yake
kwa mujibu
wa Katiba 2010
Maelezo Idadi ya Watafitiwa Asilimia
Sekta ya utangazaji kuzingatia
matumizi ya Kiswahili
17 40.5
Kuwepo kwa hati nyingi zaidi
kwa lugha ya Kiswahili
16 38.1
Kuhimizwa kwa watu kutumia
lugha ya Kiswahili kwa wingi
9 21.4
Jumla 42 100
Chati 4.2.1: Mikakati ya kukipa Kiswahili nafasi yake kwa mujibu wa
Katiba
41%
38%
21%
0%
Sekta ya utangazaji kuzingatia matumizi ya Kiswahili
Kuwepo kwa hati nyingi zaidi kwa lugha ya Kiswahili
Kuhimizwa kwa watu kutumia lugha ya Kiswahili kwa Wingi
69
Kutokana na kauli hii watafitiwa wote arobaini na wawili (42) walijibu swali hili
ambao ni asilimia 100 ya watahiniwa waliojibu swali hilo. Wote walikubali kuwa
kuna njia ambazo zinaweza kutumiwa ili kufanya Kiswahili kichukue mahali
pake kwa mujibu wa katiba ya 2010. Kati ya njia zilizopendekezwa ni; sekta ya
utangazaji kuzingatia matumizi ya Kiswahili kwa wingi zaidi ili kuinua hadhi
yake kwa kuwa bado lugha hii huchukuliwa kuzungumzwa na watu ambao
hawajasoma. Hali hii ikizingatiwa kutakuwa na mabadiliko katika hadhi ya lugha
hii. Njia hii ilipendekezwa na watafitiwa kumi na saba ambao ni asilimia 41.
Watafitiwa kumi na sita ambao ni asilimia 38.1 walipendekeza kuwa kuwepo
kwa hati nyingi za lugha ya Kiswahili mfano Magazeti na vitabu. Lugha sharti
iwe na ukwasi mwingi wa vitabu ili wazungumzaji wake wafaidike nayo. Lugha
ya Kiingereza ina vitabu vingi na matumizi yake ni mapana zaidi hivyo tunaweza
kutafsiri baadhi ya vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza hadi lugha ya
Kiswahili kuongezea ukwasi wa lugha hii. Watafitiwa tisa ambao ni asilimia 21.4
walieleza kuwa itakuwa bora iwapo watu wengi wataweza kutumia lugha ya
Kiswahili katika miktadha rasmi. Maeneo mengi yale ya kiserikali na yasiyo ya
kiserikali yaweze kutumia lugha ya Kiswahili kama moja wapo ya lugha ya
mawasiliano, kwa njia hii Kiswahili kitapata idadi nyingi ya wazungumzaji wa
lugha hii.
Kutokana na kauli hii ya (4.2.1) mapendekezo kuhusu mikakati ambayo yaweza
kutumika katika kufanya Kiswahili kuwa lugha rasimi yamebainika. Hata hivyo,
ni wazi kuwa watafitiwa kumi na saba ambao ni asilimia 41 walitaka sekta zote
za utangazaji kutumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano yao ya kirasmi.
70
Matokeo haya yanaoana vizuri na mtazamo wa upangaji lugha kihadhi
unaoelezea kuwa ili sharti kuwe na juhudi zinazochukuliwa ili kuhakikisha kuwa
jukumu la lugha limeafikiwa katika jamii. Hivyo, ni wajibu wa viongozi katika
baadhi ya sekta za utangazaji kuhakikisha Kiswahili kinapewa hadhi kwa
kukitumia ipasavyo.
Swali linalofuatia linaeleza maoni yao kuhusiana na matumizi ya lugha ya
Kiswahili kama lugha rasmi. Matokeo ya swali hilo yameelezwa kwa mhutasari
katika jedwali lifuatalo la kauli (4.2.2)
Kauli 4.2.2: Mapendekezo ya vile Kiswahili kinaweza kutekelezwa ili
kufanikisha lengo
lake la kuwa lugha rasmi
Maelezo Idadi ya Watafitiwa Asilimia
Matumizi ya Lugha ya
Kiswahili na Kiingereza yawe
sawa
22 52.4
Kuzingatiwa kwa lugha ya
Kiswahili kimasomo katika
madarasa ya chini
4 9.5
Kiswahili kizingatiwe kama
lugha ya Taifa na rasmi ofisini
8 19.0
Kuhimiza watu kutumia
Kiswahili sanifu
8 19.0
Jumla 42 100
71
Chati 4.2.2: Mapendekezo ya vile Kiswahili kinaweza kufanikisha lengo la
kuwa lugha rasmi
Kwa mujibu wa kauli (4.2.2) watafitiwa wote arobaini na wawili (42) walijibu
swali hili wakiwakilisha asilimia 100 ya watafitiwa. Watafitiwa 22 ambao ni
asilimia 52.4 walipendekeza matumizi ya Kiswahili kuwa sawa na ya lugha ya
Kiingereza ili kufikia lengo linalohitajika. Watafitiwa 8 ambao ni asilimia 19
walipendekeza kuwa lugha ya Kiswahili itumike kama lugha rasmi huku
watafitiwa wengine 8 ambao ni asilimia 19 wakapendekeza kuwa watu
wahimizwe kutumia Kiswahili sanifu. Watafitiwa 4 ambao ni asilimia 9.5
walipendekeza kuwa Kiswahili kizingatiwe kimasomo kuanzia madarasa ya
chini.Walimu waweze kufunza watoto kwa kudumisha kuwa lugha ya Kiswahili
na Kiingereza zina hadhi sawa hivyo ni muhimu kuzingatia lugha hizo.
Kutokana na mapendekezo ambayo watafitiwa walitoa ni dhahiri kuwa wengi
wanaonelea kuwa lugha ya Kiingereza inatumika kwa hadhi ya juu zaidi
ikilinganishwa na lugha ya Kiswahili hivyo viongozi katika sekta mbalimbali
52%
10%
19%
19%
Matumizi ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza yawe sawa
Kuzingatiwa kwa lugha ya Kiswahili kimasomo katika madarasa ya chini
Kiswahili kizingatiwe kama lugha ya taifa na rasmi ofisini
Kuhimiza watu kutumia Kiswahili sanifu
72
wanapaswa kuhakikisha kuwa lugha hizi zinatumika katika kiwango sawa.
Tamko la Kiswahili kusisitizwa kimasomo kama somo na lugha muhimu kama
lugha ya Kiingereza na kuwa ni lugha rasmi ni muhimu sana. Kudumisha usanifu
wa Kiswahili ni jambo muhimu kwa kuwa humwezesha mzungumzaji
kuzungumza kwa ufasaha.
Swali lililofuatia lililenga watafitiwa kutoa pendekezo moja muhimu kwa serikali
kuhusiana na matumizi ya lugha ya Kiswahili kufikia lengo linalohitajika
Kauli 4.2.3: Pendekezo moja muhimu kwa serikali kuhusiana na matumizi
ya lugha ya
Kiswahili kufikia lengo linalohitajika.
Maelezo Idadi ya watafitiwa Asilimia
Uundwaji wa sheria zinazofanya
Kiswahili kutumika ipasavyo
20 48.23
Kuhimiza watu kutumia Kiswahili
kuwahoji wanaotafuta kazi
13 32.5
Kubuniwa kwa kamati ya
kutekeleza sera ya lugha
9 19.27
Jumla 42 100
Watafitiwa wote 42 walihusika katika utafiti. Watafitiwa ishirini ambao ni
asilimia 48.23 walipendekeza kuwa serikali iunde sheria zinazofanya Kiswahili
kutumika ipasavyo. Hali hii itawezesha lugha hii kutumika kama lugha rasmi
kama inavyotakikana na kuondoa dhana kuwa Kiswahili ni lugha duni
inayozungumzwa na watu ambao si wastaarabu. Watafitwa 13 ambao ni asilimia
32.5 walipendekeza watu kuhimizwa kutumia Kiswahili kuwahoji wanaotafuta
kazi na pia kuwataka wajieleze kwa lugha ya Kiswahili. Watafitiwa 9 ambao ni
73
asilimia 19.27 walipendekeza kubuniwa kwa kamati ya kutekeleza sera ya lugha
ya Kiswahili.
Kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na watafitiwa, ni dhahiri kuwa wengi
wao wanaamini kuwa sheria ni muhimu na kuwepo kwa sheria kandamizi kama
vile kuwepo na lugha ambayo inapaswa kutumika wakati fulani kunainyima
Kiswahili kuwa na nafasi katika jamii kwa hivyo sheria hizo ziondolewe. Ni
vyema iwapo sheria ambazo zinakuzwa katika sekta zilizotafitiwa, zinaruhusu
lugha ya Kiswahili kutumiwa kwa wingi katika sekta hizo. Hali hii itaifanya
lugha ya Kiswahili kuimarika zaidi na kutumika katika miktadha mbalimbali
iliyo rasmi. Waliopendekeza kubuniwa kwa kamati kutekeleza sera ya lugha
walielewa kuwa serikali ina uwezo mkubwa wa kuwezesha lugha hii kutumika
bora zaidi. Nadharia ya Utekelezaji yaonyesha kuwa, ili utekelezaji ufaulu, ni
lazima serikali ijitolee na kutoa tamko rasmi kuhusu matumizi ya lugha.
4.3 Muhtasari
Katika sura hii, mtafiti ameshughulikia uchanganuzi na upangaji wa data kuhusu
changamoto na mikakati ya kufanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi
kikatiba. Kutokana na matokeo ya utafiti, ni wazi kuwa kuna changamoto nyingi
ambazo zinazikumba sekta zilizotafitiwa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili
kama lugha rasmi kwa mujibu wa katiba ya 2010. Matokeo ya utafiti huu
yamedhihirisha kuwa mikakati inafaa kuwekwa ili kuinua hadhi mpya ya lugha
ya Kiswahili. Katika sura inayofuata mtafiti ameshughulikia hitimisho na
mapendekezo ya utafiti kwa ujumla.
74
SURA YA TANO
HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.0 Utangulizi
Utafiti huu ulinua kubaini utayari wa Wakenya katika utekelezaji wa sera ya
lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi. Malengo ya utafiti huu yalikuwa, kubaini
iwapo kuna utayari katika kutekeleza sera ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha
rasmi, kubaini utayari huu utasaidiaje katika kuimarisha sera hii mpya ya lugha
ya Kiswahili hasa katika urasmi wake kuchunguza changamoto zinazokabiliwa
katika shughuli za kiutawala na vyombo vya habari kuhusu hadhi mpya ya lugha
ya Kiswahili. kutambua ni vipi utayari wa utekelezaji katika sera hii unavyoweza
kutekelezwa ili kuweza kufanikisha lengo la Kiswahili la kuwa lugha rasmi.
Malengo haya yaliongozwa na Nadharia ya Utekelezaji na mtazamo wa upangaji
lugha kihadhi.
Katika sura hii ya tano, matokeo ya utafiti, changamoto za utafiti, mapendekezo
na hitimisho zimejadiliwa kama ifuatavyo.
5.1 Muhtasari wa Utafiti
Utafiti huu ulichukua sura tano. Katika sura ya kwanza vipengele vilivyojadiliwa
ni pamoja na usuli wa mada, suala la utafiti, malengo na maswali ya utafiti, upeo
na mipaka, sababu za kuchagua mada, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa
kuhusu mada na mbinu za utafiti.
75
Sura ya pili, historia na utayari wa wakenya kuhusu urasmi wa lugha ya
Kiswahili nchini Kenya iliweza kujadiliwa ili kuweza kudhihirisha miktadha
mbalimbali ya Wakenya kuhusu Kiswahili hadi sasa.
Katika sura ya tatu, mtafiti ameonyesha upangaji na uchanganuzi wa data kwa
kujadili utayari wa Wakenya katika sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi
katika idara ya polisi, wizara ya utamaduni na katika vyombo vya habari.
Sura ya nne imeangazia changamoto zinazokumba utayari wa Wakenya katika
sera ya Kiswahili kama lugha rasmi na pia mikakati inayowekwa ili kukabiliana
na changamoto hizo ili kuona iwapo zitaweza kuimarisha lengo la utendakazi wa
lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi. Sura ya tano muhtasari, matokeo ya utafiti
na mapendekezo zilijadiliwa
5.2 Matokeo ya utafiti
Katika sehemu hii tumejadili malengo manne na kurejelea matokeo ya utafiti.
Kila lengo limejadiliwa kwa mujibu wa matokeo ya utafiti
5.2.1 Lengo la kwanza
Utafiti huu ulikuwa na malengo manne. Lengo la kwanza lilikuwa kubaini iwapo
kuna utayari katika kutekeleza sera ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi.
Kutokana na data iliyokusanywa, mtafiti aliweza kubaini kuwa kulikuwa na
ukubalifu wa kuitekeleza lugha ya Kiswahili miongoni mwa Wakenya kama
lugha rasmi. Kwa kuzingatia mtazamo wa upangaji lugha kihadhi, baada ya lugha
hii kupewa jukumu mpya ilionekana kuzingatiwa huku ikidhihirika kuwa watu
wengi walijaribu kuitumia lugha hii katika miktadha rasmi. Hii imejitokeza pale
ambapo baadhi yao waliona mabadiliko ya utekelezaji wa lugha ya Kiswahili
76
baada ya katiba ya 2010. Kuna wale ambao waliona utekelezaji wa Kiswahili
ulikuwa mzuri baada ya kupata katiba mpya ya 2010 ikilinganishwa na hapo
awali ambapo utekelezaji wake ulikuwa mzuri kiasi. Hakuna aliyeona kuwa hali
ya Kiswahili kuwa mbaya baada ya hadhi yake mpya ya kuwa lugha rasmi. Hii ni
kubainisha kuwa wengi wa watafitiwa wanaona kuwa lugha ya Kiswahili ina
matumaini na itaweza kuafikia malengo na majukumu yake ambayo yalipewa
lugha hii na hili litakuwa na manufaa zaidi kwa wazungumzaji wake.
5.2.2. Lengo la pili
Lengo la pili la utafiti lilikuwa kubaini utayari huu utasaidiaje katika kuimarisha
sera hii mpya ya lugha ya Kiswahili hasa katika urasmi wake. Kwa kuzingatia
mtazamo wa upangaji lugha kihadhi, lugha ya Kiswahili ilipewa hadhi ya kuwa
lugha rasmi na lugha ya taifa. Kutokana na maelezo yaliyotolewa ni kuwa hadhi
ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi imeimarika. Hii ni kwa kuwa watu
wengi wameweza kuitumia lugha hii katika miktadha rasmi na pia katika maeneo
mengine. Kutokana na matokeo ya uchanganuzi wa data tuliyopata kutoka kwa
watafitiwa, ni wazi kuwa Kiswahili kimeimarika kwa kuwa hadhi mpya ya
Kiswahili kama lugha rasmi imefanya lugha hii kupata hadhi ya juu. Baada ya
katiba ya 2010 kuidhinisha lugha hii kuwa rasmi, hali hii ilifanya Kiswahili kuwa
na hadhi mbili tofauti; hadhi ya kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi.
Matokeo ya utafiti yameonyesha kuwa hali hii imefanya Kiswahili kuimarika
zaidi. Kutokana na majibu yaliyopatikana, ni bayana kuwa lugha hii imeanza
kutumika katika shughuli za kitaifa na katika ofisi za kiserikali hivyo hali hii
imeimarika ikilinganishwa na hapo awali. Pia imebainika kuwa lugha hii imeanza
77
kutumiwa katika utangazaji pale ambapo idadi ya vipindi ambavyo vinatumia
lugha ya Kiswahili vinaendelea kuongezeka. Ijapokuwa hali hii mpya ya
Kiswahili haijaafikiwa kikamilifu kuna matumaini kuwa lugha hii itafikia lengo
lake la kuwa lugha rasmi, kwa kuwa matokeo haya yanaonyesha kuwa lugha hii
inaendelea kukubalika kutumika katika miktadha rasmi.
5.2.3 Lengo la tatu
Lengo la tatu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza changamoto zinazokabiliwa
katika shughuli za kiutawala na vyombo vya habari kuhusu hadhi mpya ya lugha
ya Kiswahili. Kutokana na matokeo ya utafiti, ilibainika kuwa kuna changamoto
nyingi zinazokabili shughuli za kiutawala na vyombo vya habari katika
kufanikisha hadhi mpya ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi.
Baadhi ya changamoto ambazo zilijitokeza ni kwamba katika sekta ya utangazaji
kuna kupendelea matumizi ya Kiingereza sana katika mawasiliano, usomaji wa
habari na hata uandishi wa magazeti. Hii inaendeleza ukosefu wa nafasi sawa
baina ya Kiingereza na Kiswahili. Hiki ni kikwazo katika kuimarisha lugha ya
Kiswahili. Hivi karibuni pia runinga ya ‘QTV’ ilifungwa ambayo kiwango
kikubwa iliendeleza lugha ya Kiswahili. Sababu za kufungwa kwake ni kuwa
haikuleta faida kifedha hivyo ni dhahiri kuwa lengo la kuendeleza Kiswahili
kutumika kwa ufasaha na kama lugha rasmi halikuwa la umuhimu sana.
Changamoto nyingine iliyobainika ni kuwa watu walitumia lugha ya mama
katika maeneo yao ya kazi. Hali hii ilibainika wazi katika ofisi za kiutawala. Ni
jambo la kutamausha hasa kwa kuwa kuna lugha mbili rasmi ambazo zaweza
kutumika katika ofisi za kiutawala badala ya kutumia lugha ya mama. Pia,
78
ilisemekana kuwa serikali bado inasisitiza matumizi ya Kiingereza katika
shughuli zake. Hii inadhihirika katika Bunge pale ambapo wabunge huzungumza
lugha ya Kiingereza sana kuliko lugha ya Kiswahili.
Ukosefu wa maandishi ya lugha ya Kiswahili ili kuimarisha lugha hii pia ni
changamoto nyingine. Kunahitajika vitabu, magazeti na majarida ya kutosha ili
kuendeleza kuimarisha hali ya Kiswahili nchini na pia ili watu wengi waweze
kutumia lugha hii. Changamoto nyingine ilikuwa ni kukawia kwa sera ya
Kiswahili kutumika kama lugha rasmi. Ilibainika kuwa mswada wa sera ya lugha
ya Kiswahili kama lugha rasmi bado haujapitishwa bungeni na hivyo hii ni
sababu lugha hii haijapata hadhi yake kikamilifu. Changamoto hizi ndizo
zinazoikabili lugha ya Kiswahili kutoafikia lengo lake la kutekeleza kazi yake
kama lugha rasmi kwa mujibu wa watafitiwa.
5.2.4. Lengo la nne
Lengo la nne lilitaka kutambua ni vipi utayari wa utekelezaji katika sera hii
unavyoweza kutekelezwa ili kuweza kufanikisha lengo la Kiswahili la kuwa
lugha rasmi. Mtafiti aliazimia kutambua njia ambazo zinaweza kutumika ili lengo
la Kiswahili katika kutekeleza kazi yake kama lugha rasmi kuafikiwa katika
maeneo yaliyohusika katika utafiti huu.
Kutokana na maswali yaliyoulizwa, ilibainika kuwa sekta zote za utangazaji
ziweze kutumia lugha ya Kiswahili ili kuweza kuimarisha lugha hii zaidi na
kuweza kufanikisha hadhi yake mpya ya kuwa lugha rasmi. Hata hivyo, idadi ya
vipindi vinavyotumia lugha ya Kiswahili iongezwe katika vituo vya runinga.
Pana haja ya kuwa na hati nyingi zaidi kwa lugha ya Kiswahili kama vile vitabu,
79
magazeti na hata majarida. Ilibainika pia matumizi ya lugha ya Kiswahili yawe
sawa na ya Kiingereza. Wale ambao walipendelea matumizi ya Kiingereza katika
mawasiliano yao, walihimizwa kutumia lugha ya Kiswahili katika nyanja zote
rasmi. Hata hivyo lugha ya Kiswahili itumike kuwahoji wanaotafuta kazi. Kupitia
kufanyika kwa mambo haya, lugha zote mbili zitaweza kutumika kulingana na
majukumu yaliyowekewa lugha hizi kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ya 2010.
Pendekezo lililotolewa kutokana na kuwepo kwa sheria kandamizi ni kuwa,
sheria hizo ziondolewe kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili na lugha hiyo
izingatiwe kama lugha rasmi. Ili lugha hii iendelee kuenziwa ilipendekezwa
kutumiwa katika shughuli zote za umma na pia za kibinafsi. Baadhi ya majibu
yaliyopatikana yalionyesha kwamba wahojiwa walitaka wabunge kutumia lugha
ya Kiswahili katika mijadala yao na katika hotuba zao. Kwa kufanya hivi
wataonyesha umuhimu wa kutumia Kiswahili kwa kuwa wana ushawishi
mkubwa.
Kuna wale waliopendekeza kuwa lugha ya Kiswahili izingatiwe katika madarasa
ya chini kimasomo. Watafitiwa walieleza kuwa wanafunzi huhimizwa kuongea
lugha ya Kiingereza na walimu wao na kutokana na haya mtoto hukua akijua
kuwa lugha ya Kiingereza ni bora kuliko ya Kiswahili ndio maana hadi sasa
lugha hii inapuuzwa kwa kuhusishwa na hadhi ya chini. Hivi sasa Kiswahili
kimepewa hadhi mpya ya kuwa rasmi hivyo, kinastahili kuwa na hadhi ya juu
kuliko Kiingereza kwani ni lugha rasmi na pia ni lugha ya taifa nchini Kenya.
80
5.3 Matatizo
Mtafiti alikumbana na matatizo katika ukusanyaji wa data. Katika ukusanyaji wa
data, kuna baadhi ya wafanyakazi ambao walikataa kujaza hojaji na pia waliojaza
walichukua muda mwingi kujaza hojaji hizo. Haikuwa kazi rahisi kuwapata
waliohojiwa kwa kuwa walikuwa na shughuli nyingi ingawa wengine walikataa
kuhojiwa. Baadhi ya waliojaza hojaji walisema kuwa Kiswahili ni lugha ngumu
hivyo ilibidi watoe maelezo yao kwa lugha ya Kiingereza. Hata hivyo baadhi ya
waliohojiwa walitumia lugha ya Kiswahili. Maelezo yaliyotolewa kwa lugha ya
Kiingereza yalimlazimu mtafiti kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili.
5.4 Mapendekezo ya Utafiti
Kutokana na majibu yaliyotolewa, ni wazi kuwa kuna changamoto zinazokumba
utayari wa Wakenya katika sera ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya.
Ingawa baada ya kuidhinishwa kwa katiba ya 2010 hali ya Kiswahili ilibadilika
na kuwa bora zaidi, bado Kiswahili hakijafikia lengo lake la utendakazi wake wa
kuwa lugha rasmi haujafikiwa kikamilifu. Kutokana na maelezo haya ni jukumu
la serikali kuwezesha lugha ya Kiswahili kuwa na hadhi yake kama lugha rasmi.
Hata hivyo, mtafiti anapendekeza mapendekezo yafuatayo kwa kuzingatia majibu
yaliyopatikana.
Kwa watafitiwa wajao wanaweza kuangazia changamoto zinazokabili ukosefu
wa nafasi sawa baina ya Kiswahili na Kiingereza. Baadhi ya wafanyikazi katika
vituo vya habari hupendelea kutumia lugha ya Kiingereza ambayo ina hadhi
sawa na lugha ya Kiswahili. Ukosefu wa nafasi sawa kwa lugha ya kiswahili
umesababisha lugha hii kutotumika ipasavyo. Mtafiti katika suala hili azingatie
81
kuwa wazungumzaji wengi wanapendelea kutumia lugha ya Kiingereza na hivyo
ajiami katika kutafsiri data atakazokusanya kwenye hojaji.
Pendekezo lingine ni kuwa, Bunge lihakikishe kuwa linapitisha mswada wa sera
ya lugha ya Kiswahili kufanya kazi kama lugha rasmi ili mswada huu uweze
kuwa sheria. Wabunge wakifanya hivyo watawezesha lugha hii kutumika katika
maeneo mengi zaidi yakiwa yale ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali. Jambo hili
litaimarisha lugha hii zaidi.
Kuwe na matumizi sawa ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza katika vyombo vya
habari. Idadi ya vipindi vinavyopeperushwa kwa lugha ya Kiswahili viweze
kuzingatiwa katika vituo vya runinga. Mawasiliano katika sekta hii pia
yazingatiwe na dhana kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha duni kuondolewa kwa
wanaopendelea kutumia lugha ya Kiingereza. Hali hii ikizingatiwa lugha ya
Kiswahili itapata hadhi yake.
Kuwe na hati nyingi zaidi kwa lugha ya Kiswahili. Pale ambapo waandishi wa
Magazeti na vitabu waweze kuandika vitabu vingi zaidi kwa lugha ya Kiswahili.
Hali hii itaweza kukuza lugha ya Kiswahili kwa wasomaji wake.
Kuhimizwa kwa watu kutumia lugha ya Kiswahili kwa wingi kama moja wapo
ya lugha ya mawasiliano. Hivyo basi, lugha hii itapata wazungumzaji wengi zaidi
na kutumika katika maeneo pana zaidi.
Kuhimizwa kwa usawazishaji wa vipindi vya lugha ya kiswahili kuwa sawa na
vya Kiingereza kwa kufanya hivi walimu watakuwa na muda wa kutosha katika
kufafanua mada wanazozishughulika nazo kikamilifu. Serikali kuajiri wasomi wa
82
Kiswahili ili waweze kutoa mafunzo ya ziada kwa wafanyakazi kuhusu
Kiswahili. Hili liwe jambo la lazima kwa wafanyakazi wote.
5.5 HITIMISHO
Kijumla katika uchanganuzi wa utafiti huu tumeona changamoto ambayo
inakumba sera ya lugha ya Kiswahili ni kwamba lugha hii haijafiki lengo
lakekatika utendakazi wake wa kuwa lugha rasmi. Hata hivyo, mapendekezo
kadhaa yametolewa ili kuonyesha jinsi ambavyo athari hii inavyoweza
kukabiliwa.
83
MAREJELEO
Ali, J N, (2011) ‘Changamoto zinazokumba Mawasilianoya Kiofisi kwa Kutumia
Kiswahili kama Lugha Rasmi’. Mradi wa Shahada ya Kwanza.
Chuo Kikuu cha katoliki cha Afrika Mashariki (Haijachapishwa
Bamgbose, A. (1991). Language and Nation. The Language Question in Sub-
Sahara Africa. England: Eanglewood University Press.
Chimerah, R. (1998) Kiswahili Past, Present and Future Horizons. Nairobi:
Nairobi University Press
Gorman, T. P. (1974) “The Development of Language Policy in Kenya with
Particular reference to Education System”. In Whiteley,
W.H. (ed.) Language in Kenya. Nairobi: Oxford
University Press, 397-446
Harries, L, (1968 ) “ Nationalisation of Swahili in kenya” Katika Kennedy,
C.(ed). Language and planning and Language and
Education. London: George Allen and Unwin
84
Hudon, M. (2013) Official Languages in Canada, Federal Policy (Background
Paper), Library of Parliament, Ottawa, Canada
King’ei, K. (2010). Misingi ya Isimujamii. Dar es Salaam: TUKI
Masinde, E. (2012). Kiswahili katika Ujenzi na Utangamano. K. Njogu, C.
Momanyi & M. Mukuthuria (Wahar.) Kiswahili na Utaifa
Nchini Kenya Kenya waweza Communications. Uk 17-25
Mazrui, A. A. and Mazrui. A.M (1995) Swahili State and Society. Nairobi: East
African
Mbaabu, I. (2007) Historia ya Usanifishaji wa Kiswahili. Dar-es- Salaam: Taasisi
ya Uchunguzi wa Kiswahili
Mbaabu, I. (1996). Language Policy in East Africa. Educational Resesarch and
Publication. (ERAP)
(1978a). Kiswahili Lugha ya Taifa. Nairobi: Kenya Literature Bureau
Mbatiah, M. (2012). Suala la Utaifa wa Kenya: Nafasi ya Kiswahili. K. njogu, C.
Momanyi & M. Mukuthuria (Wahar.) Kiswahili na Utaifa
Nchini Kenya Kenya Twaweza Communications. Uk 3-10
Mekacha, R. D. K. (2011). Isimujamii: Nadharia na Muktadha wa Kiswahili. Dar
es Salaam: TUKI.
85
Mesthrie, R. S. (2000) Introducing Sociolinguistics. Edinburgh: University Press
Mirianga, R .K. (2014). Mielekeo ya Walimu wa Shule za Msingi Kuhusu Suala
La Lugha kama Linavyoelezwa Katika Katiba ya Kenya.
Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya
Mohochi, E.S. (2002). Kiswahili na Vyombo vya Habari Nchini Kenya: Matatizo
katika Matumizi ya Lugha. K Njogu & C. Momanyi
(Wahar.) Kiswahili Katika Karne ya Ishirini na Moja.
Cape town: CASA. Uk 147-157
Mukhwana, A. (2008). Language Attitudes in Urban Kenya: The Case Study of
Kisumu, Nairobi and Mombasa.Tasnifu ya Uzamifu
ambayo haijachapishwa, Chuo Kikuu cha Nairobi
Nabea, W. (2009) Language Policy in Kenya: Negociation with Hegemony
katika The Journal of Pan Arican Studies. Vol.3 No 1
September 2009 uk. 121-138
Ngigge, B. N. (2014). Mielekeo na Changamoto za Maafisa wa Kaunti katika
Utekelezaji wa Katiba Kuhusu Sera ya Lugha: Mfano wa
Kaunti ya Nakuru. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha
Kenyatta, Kenya
86
Ngugi, P. na Chacha, L. (2004). Sociolinguistics. Nairobi: KUIOL
Nyandwaro, L.K.( 2015) Mielekeo ya Wafanyakazi Kuhusu Kiswahili kama
Lugha Rasmi katika Wizara za Serikali Nchini Kenya.
Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta
Onyango, J. O. (1990). Mielekeo ya Wasomi Kuhusu Matumizi ya Kiswahili
Nchini Kenya. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha
Kenyatta, Kenya
Osore, K. M na Midika, B. (2016) Operationalizing Kiswahili as a Second
Official Language Examples from Canadian
and South African Language Policy
Frameworks. (Makala) Hayajachapishwa
Ryanga, S. (2001) Reaching out for Linguistic Identity: The State of Kiswahili in
Kenya. In: Naomi Shitemi na Mwanakombo Noordin (eds.).
Kiswahili: A Tool for Development. Moi University Press.
24-35
Shitemi, L. N. (2011). Kubidhaaisha na Kuwezesha Lugha kama Sarafu ya
Kiuchumi na Kijamii: Kielezo cha Taaluma za Kiswahili
87
na Tafsiri.Kenya: Moi University Press
Sikma, J. (1990). The Education of Minority Languages and Conflicting
Attitudes. In PNelde (ed.). Language Attitudes and Language
Conflict. (pp 86-92). Bonn: Duemmler
Spencer, J. (1971). Colonial Language Policies and their Legacies. In Sebeok,
Thomas (ed.). Current Trends in Linguistics, Vol, 537- 547.
The Hague: Mouton de Gruyter
Van Els, T. (2005). Status planning for learning and teaching. In E. Hinkel (Ed.)
Handbook of Research in Second Language Teaching and
Learning (Chapt 53). Mahwah, NJ: Erlbaum. (in press).
http://www.kenyaembassy.com/pdfs/Constitution of Kenya.pdf. Accessed on
Monday 7th
NOV,2016 7:28PM
88
KIAMBATISHO CHA A: Hojaji
Sehemu ya A: Maelezo ya Kibinafsi.
Weka alama ya (×) mahali panapofaa.
1. Umri: (25-35) [ ] (36 na zaidi) [ ]
2. Jinsia Kiume [ ] (kike) [ ]
3. Kiwango cha elimu: Cheti [ ]
Stashahada [ ]
Shahada ya kwanza [ ]
Shahada ya Uzamili [ ]
Sehemu ya B: Maswali ya hojaji
Tafadhali jibu maswali uliyoulizwa kama ulivyooagizwa
1 a) Wewe kama mfanyikazi katika sekta hii, ni lugha gani unapenda kuitumia
sana katika mawasiliano ya maongezi
A) Kiswahili [ ] B) Kiingereza [ ] C) Lugha mama [ ] D) Lugha mseto [ ]
b) Ni sababu zipi hukufanya kutumia lugha hiyo ya mawasiliano? Toa hoja moja
muhimu
89
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
………………………………………………….
2 a) Kabla ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, utekelezaji wa lugha ya
Kiswahili katika sekta hii ulikuwa vipi?
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………
b) Baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, mabadiliko katika sera hii ya
Kiswahili yanatekelezwa vipi?
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………
3a) Kwa maoni yako, sera hii mpya ya Kiswahili imesaidia katika kuimarisha
hadhi yake ya kirasmi?
90
Ndio [ ] La [ ]
b) Toa maelezo ikiwa jibu lako ni ndio
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………
c) Ikiwa jibu lako ni la, eleza njia moja nzuri ambayo unafikiria inaweza kufanya
Kiswahili kikubalike kama lugha rasmi
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………
4. Je, kunazo sheria katika sekta hii ambazo unafikiri zimefanya Kiswahili
kutofikia kiwango kinachohitajika? Kama zipo taja mojawapo
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………
91
5. Ni lugha ipi ya mawasiliano ya kimaongezi ambayo watu hupendelea kuitumia
katika sekta hii. Toa sababu kuu za uteuzi huo
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
…………………………………………………
6. Ni mikakati ipi ambayo inawekwa katika sekta hii ili kukipa Kiswahili nafasi
yake kwa mujibu wa Katiba ya 2010? Taja miwili
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………
7. Je, kunazo changamoto mnazokumbana nazo katika utekelezaji wa katiba
kuhusu hadhi mpya ya Kiswahili? Kama zipo, taja mbili kuu
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………
92
8. Kwa maoni yako Kiswahili kinaweza kutekelezwa vipi katika sekta hii ili
kuweza kufanikisha lengo lake la kuwa lugha rasmi
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
…………………………………………………….
93
KIAMBATISHO CHA B: Mwongozo wa Mahojiano
1. Wewe kama mmoja mwanakamati wa tume iliyoshughulikia maswala ya sera
ya lugha ya Kiswahili katika hadhi ya urasmi kikatiba, unafikiria mabadiliko
yanayotokea kuhusu sera ya lugha husaidia kuimarisha kiwango cha lugha ya
Kiswahili?
2. Je, watu wanapokea vipi mabadiliko hayo?
3. Ni mambo yepi unafikiria serikali inafaa kufanya ili kuhakikisha ndoto yake ya
kufanya Kiswahili kuwa lugha ya rasmi inaafikiwa?
4. Imebainika kuwa utekelezaji wa Katiba ni jambo ambalo huwa ngumu mno. Ni
njia zipi mtachukua kuhakikisha kuwa Kiswahili kimepata mahali pake kwa
mujibu wa katiba mpya?
Recommended