Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris...

Preview:

Citation preview

Wimbo wa SakimaWimbo wa Sakima

Ursula Nafula Peris Wachuka Ursula Nafula swahili nivå 3

Sakima aliishi na wazazi wake na dada yake wamiaka minne. Waliishi katika shamba la mtu tajiri.Nyumba yao ya nyasi ilikuwa mwisho wa safu yamiti iliyopendeza.

2

Sakima alipokuwa na umri wa miaka mitatu,aliugua na kupoteza uwezo wa kuona. Hata hivyo,Sakima alikuwa mvulana mwenye kipaji.

3

Sakima alitenda mambo mengi ambayo wavulanawengine wa umri wake hawakufanya. Kwa mfano,aliketi na watu wazima na kujadili mambomuhimu.

4

Wazazi wa Sakima walifanya kazi katika nyumbaya yule tajiri. Walitoka nyumbani asubuhi namapema na kurudi jioni. Sakima aliachwa nadada yake.

5

Sakima alipenda kuimba nyimbo. Siku mojamama yake alimuuliza, “Sakima, unajifunzanyimbo hizi kutoka wapi?”

6

Sakima alimjibu, “Nazisikia akilini mwangu kishanaziimba.”

7

Sakima alipenda kumwimbia mdogo wake hasaakihisi njaa. Dada yake alimsikiliza na kucheza.

8

“Naomba uimbe tena na tena, Sakima,” mdogowake alimsihi. Sakima alikubali na kuimba maranyingine.

9

Jioni moja, wazazi wake waliporudi nyumbani,walikuwa kimya sana. Sakima alijua kwambalazima kulikuwa na jambo baya.

10

“Kuna shida gani, mama, baba?” Sakima aliuliza.Sakima aligundua kwamba mwana wa tajiri waoalikuwa amepotea. Tajiri alihuzunika na kuwa naupweke mkubwa.

11

“Labda atafurahi tena nikimwimbia,” Sakimaaliwaambia wazazi wake. Wazazi wake walidharauwazo lake. “Yeye ni tajiri sana. Wewe ni mvulanaasiyeona. Unadhani wimbo wako utamsaidia?”

12

Hata hivyo, Sakima hakukata tamaa. Mdogo wakealimpa moyo. Alisema, “Nyimbo za Sakimahunituliza mimi nikiwa na njaa. Zitamtuliza tajirivile vile.”

13

Siku iliyofuata, Sakima alimwomba mdogo wakeamwongoze hadi kwenye nyumba ya tajiri.

14

Alisimama chini ya dirisha moja kubwa na kuanzakuimba wimbo wake alioupenda. Pole pole,kichwa cha tajiri kilionekana dirishani.

15

Wafanyakazi waliacha kazi zao. Wakasikilizawimbo mzuri wa Sakima. Hata hivyo,mwanamume mmoja alisema, “Hakuna aliyefaulukumtuliza bwana. Je, huyu mvulana asiyeonaanafikiri atamtuliza?”

16

Sakima alipomaliza kuimba wimbo wake alianzakuondoka. Tajiri alitoka nje kwa haraka nakusema, “Tafadhali, imba tena.”

17

Wakati huo huo, watu wawili walikuja wakiwawamembeba mtu kwenye machela. Walimkutamwana wa tajiri akiwa amechapwa na kuachwakando ya barabara.

18

Tajiri alifurahi sana kumwona mwana wake tena.Alimzawadia Sakima kwa kumliwaza. Aliwapelekamwanawe na Sakima hosipitali ili Sakima awezekusaidiwa kuona tena.

19

Barnebøker for NorgeBarnebøker for Norgebarneboker.no

Wimbo wa SakimaWimbo wa SakimaSkrevet av: Ursula Nafula

Illustret av: Peris WachukaOversatt av: Ursula Nafula

Denne fortellingen kommer fra African Storybook (africanstorybook.org) og ervidereformidlet av Barnebøker for Norge (barneboker.no), som tilbyr barnebøkerpå mange språk som snakkes i Norge.

Dette verket er lisensiert under en Creative Commons Navngivelse 4.0 Internasjonal Lisens.

20

Recommended