Upload
others
View
1
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 1
كتاب اإلعتقادKitabu kuhusu ´Aqiydah
Mwandishi: Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-
Hanbaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 2
YALIYOMO
[1] Tunaanza kwa kutaja yale ambayo Allaah (Ta´ala) ameyafaradhisha kwa waja Wake, ............................ 4
[2] Imani inathibitishwa kwa kutamka kwa ulimi, kuamini na matendo ya viungo ...................................... 4
[3] Imani na Uislamu ni maneno mawili yenye maana mbili tofauti ........................................................... 4
[4] Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyoteremshwa na haikuumbwa ........................................................... 5
[5] Hakuacha na bado ni mwenye kuendelea kuzungumza ........................................................................ 5
[6] Allaah ni Mmoja asiyefanana na chochote ............................................................................................ 6
[7] Yule mwenye kuitakidi juu ya sifa hizi na mapokezi Swahiyh mfano wake kufanana ........................... 10
[8] Kuzikanusha sifa ni madhehebu ya Jahmiyyah ................................................................................... 10
[9] Yule mwenye kuzipitisha kama zilivyokuja ......................................................................................... 10
[10] Ni wajibu kuamini Qadar ................................................................................................................. 11
[11] Inatakiwa kuamini adhabu ya ndani ya kaburi na Munkar na Nakiyr ................................................. 12
[12] Inatakiwa kuamini ufufuliwaji na Njia .............................................................................................. 14
[13] Kuamini Mizani ............................................................................................................................... 14
[14] Inatakiwa kuamini Hodhi na Uombezi ............................................................................................. 14
[15] Mtu anatakiwa kuamini pia mahojiano ............................................................................................. 15
[16] Kuamini kwamba Allaah aliumba Pepo na Moto kabla ya kuumba viumbe ...................................... 16
[17] Kuhusiana na wapwekeshaji watenda madhambi .............................................................................. 16
[18] Inatakiwa kuamini vilevile kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Mtume wetu
............................................................................................................................................................... 17
[19] Miongoni mwa hayo ni kitabu chake ambacho kinavihukumu vitabu vyengine vyote ....................... 18
[20] Ana (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alama kubwa za ardhini na mbinguni ................................... 20
[21] Yule mwenye kunyanyua sauti yake mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) .................. 23
[22] Kiumbe bora baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) .................................... 28
[23] Ni wajibu kuwakata Ahl-ul-Bid´ah na wapotevu ............................................................................... 29
[24] Hii ndio ´Aqiydah yangu na yale ninayomwabudu kwayo Mola wangu ............................................. 29
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 3
Siku ya ijumaa tarehe 13 Shawwaal mwaka wa 573 alinikhabarisha
muheshimiwa Shaykh Abu Sa´iyd ´Abdul-Jabbaar bin Yahyaa bin ´Aliy bin
Hilaal al-A´rabiy kwa njia ya kunisomea na mimi nasikiliza. Amesema:
Muheshimiwa Abul-Husayn Muhammad bin Muhammad bin al-Farraa´
amsema:
Himdi zote anastahiki Allaah mpaka aridhie. Hapana mwabudiwa wa haki
isipokuwa Allaah, Aliyetukuka, Aliye juu kabisa. Himdi zote ni za Allaah
ambaye anastahiki kushukuriwa pasi na kikomo. Himdi zote anastahiki Allaah
ambaye ametuumba baada ya kutokuwepo, akatujaalia kuwa katika Ummah
bora na akatuteulia kiumbe Chake bora na Mtume Wake mtukufu zaidi
kutuongoza. Amemfanya kuwa mtu wa kwanza aliyetangulia inapokuja katika
manzilah na Mtume bora kabisa inapokuja katika ujumbe –Allaah amsifu na
familia yake wazuri swalah ambayo itawakusanya wote pamoja.
Allaah atukinge sisi na nyinyi juu ya kujikafilisha mambo tusiyoyaweza wala
kudai tusiyoyamairi. Allaah atulinde sisi na nyinyi kutokamana na Bid´ah na
uongo ambavyo ndio uovu na uchafu mkubwa zaidi ambavyo mtu anaweza
kuwa navyo.
Hakika umeniuliza kuhusu ´Aqiydah yangu na yale ninayomwabudu Mola
wangu (´Azza wa Jall) ili uweze kuyafuata na matokeo yake ufuzu kutokamana
na Bid´ah na matamanio yenye kupotosha na utunukiwe na Allaah (´Azza wa
Jall) ngazi za juu. Hivyo nakujibu yale uliyoniuliza hali ya kutaraji thawabu
kubwa kutoka kwa Allaah na kuogopa adhabu Yake kali na namtegemea juu
ya kuzungumza maneno yaliyo ya sawa.
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 4
[1] Tunaanza kwa kutaja yale ambayo Allaah (Ta´ala) ameyafaradhisha kwa waja Wake,
akamtumiliza Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akateremsha
vitabu Vyake; nako ni kule kumwamini Allaah (´Azza wa Jall). Maana yake ni
kusadikisha yale (Tabaarak wa Ta´ala) aliyosema, akayaamrisha,
akayafaradhisha na akayakataza kupitia yale yote yaliyofikishwa na Mitume
kutoka Kwake na yakateremshwa na vitabu. Mitume wametumwa kwa hayo.
Amesema (Ta´ala):
و وا و ر و ر وا م قو ر م و م ر س ول م ر س وم م و ر م و ر س و م وقـ و م ر و و واعر س س وم
“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi Niabuduni.”1
[2] Imani inathibitishwa kwa kutamka kwa ulimi, kuamini na matendo ya
viungo. Inazidi kwa kufanya matendo [mema] mengi na kuzungumza na
inashuka kwa maasi.
Hakuna neno kwa mtu kufanya uvuaji katika imani yake. Kufanya uvuaji ni
jambo halina shaka yoyote kwani ni njia iliyotumiwa na wanachuoni. Mtu
akiulizwa kama ni muumini basi anatakiwa kusema:
”Mimi ni muumini Allaah akitaka.”
Vilevile anaweza kusema:
”Nataraji kuwa ni muumini.”
Pia anaweza kusema:
”Nimemwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Wake.”
[3] Imani na Uislamu ni maneno mawili yenye maana mbili tofauti. Uislamu
kwa upande wa Shari´ah ni zile shahaadah mbili pamoja na kusadikisha ndani
ya moyo ilihali imani ni ule utiifu wote.
1 21:25
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 5
[4] Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyoteremshwa na haikuumbwa pasi na
kujali namna itakavyosomwa na namna itakavyoandikwa na popote pale
itakaponakiliwa. Kitabu ni yale yaliyoandikwa, kisomo ni yale yanayosomwa.
Maneno ya Allaah ni ya kale [milele] na hayakuumbwa katika hali zote. Ni
maneno ya Allaah ambayo hayakuumbwa, hayakuzuliwa wala kutengenezwa
kwa hali yoyote ile. Wala sio mwili, kiungo, jauhari wala aradhi, Bali ni sifa
moja katika sifa za kidhati zinazotofautiana na viumbe vyote.
[5] Hakuacha na bado ni mwenye kuendelea kuzungumza. Maneno Yake
hayawezi kutengana na dhati Yake. Wakati fulani yanasikika kutoka Kwake
(´Azza wa Jall) na wakati mwingine yanasisika kutoka kwa msomaji. Yule
mwenye kuyasikia moja kwa moja kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)
ndiye aliyepokea uzungumzishwaji mwenyewe pasi na mkatikati wala
mkalimani. Kwa mfano Allaah alimzungumzisha Mtume wetu Muhammad
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa kupandishwa mbinguni. Kadhalika
aliongea na Muusa kwenye mlima wa Sinai. Vivyo hivyo Malaika
wanaozungumzishwa Naye. Vinginevyo, maneno ya Allaah ya kale yanasikika
kikweli kutoka kwa msomaji na yana herufi zenye kufahamika na sauti yenye
kusikika.
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 6
[6] Allaah ni Mmoja asiyefanana na chochote. Hatuzifananishi sifa Zake za
sifa za viumbe na wala hatuzifanyii namna sifa Zake. Allaah yuko kinyume
kabisa na vile ambavyo akili ya mtu inavofikiria.
Yuko hai kwa uhai, ni mjuzi kwa ujuzi, ni muweza kwa uwezo, ni misikivu
kwa usikizi, ni muoni kwa uoni, ni mwenye kuzungumza kwa maneno,
mwenye kutaka kwa utashi, mwenye kuamrisha kwa amri, mwenye kukataza
kwa makatazo.
Tunathibitisha kwamba amemuumba Aadam kwa mkono Wake kutokana na
maneno Yake (Ta´ala):
وا و قو و و وو و ر س و م وا و وقر س م و و ر
”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”2
ااس و ر س ووتواوم و ر و و
”Bali mikono Yake imefumbuliwa.”3
Kwamba ana mkono wa kuume, kutokana na maneno Yake (Subhaanah):
تت م و م م م وا ر وا واتس و ر م ر
”Mbingu zitakunjwa mkononi mwake mwa kuume.”4
Kwamba ana uso kutokana na maneno Yake:
كس ل و ر ل وا م ت م ر و ر و س
“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa uso Wake.”5
وم واإلرمكر واام و قو قرقو ـ و ر س و م و س اارو و
2 38:75 3 05:64 4 39:67 5 28:88
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 7
”Utabakia uso wa Mola Wako wenye utukufu na ukarimu.”6
Kwamba ana unyayo kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam):
”Mpaka pale Mola wako ataweka unyayo Wake juu yake ambapo utasema:
”Tosha, tosha.”7
Bi maana juu ya Moto. Ameipokea Ahmad, al-Bukhaariy, Muslim, Abu ´Iysaa
at-Tirmidhiy na wengineo.
Kila usiku Anashuka katika mbingu ya chini ya dunia kutokana na maneno ya
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mola wetu anashuka katika mbingu ya chini ya dunia pale kunapobaki
theluthi ya mwisho ya usiku.”
Tamko hili ni la al-Bukhaariy. Hadiyth hii imepokelewa na Ahmad, Maalik, al-
Bukhaariy, Muslim, Abu ´Iysaa at-Tirmidhiy, Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah,
ad-Daaraqutwniyna maimamu wengine wa Kiislamu.
Anamcheka mja Wake muumini kutokana na maneno ya Mtume wa Allaah
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Allaah (Ta´ala) anawacheka watu wawili. Mmoja amemuua mwengine na
wote wawili wanaingia Peponi.” Wakasema: “Vipi?” Akasema: “Mmoja
amepigana katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall) ambapo akauawa shahidi.
Kisha Allaah akamsamehe yule muuaji ambaye aliingia katika Uislamu. Halafu
akapigana katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall) ambapo akauawa shahidi.”8
Ameipokea al-Bukhaariy na wengineo.
Tunathibitisha kuwa Allaah ana nafsi isiyofanana na nafsi zengine. Amesema:
و سو م سكس س ا رق س قو ر و س
“Allaah anakutahadharisheni na nafsi Yake.”9
6 55:27 7 al-Bukhaariy (4848) na Muslim (2846) 8al-Bukhaariy (2826) na Muslim (1890). 9 03:28
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 8
واصر و قو رتس و م قو ر م
“Nimekuchagua kwa ajili Yangu.”10
Abu Hurayrah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) amesema:
“Allaah (´Azza wa Jall) anasema: “Mimi ni vile anavyonidhania mja Wangu na
mimi niko pamoja naye pindi anaponitaja. Akinitaja ndani ya nafsi yake, basi
Namtaja ndani ya nafsi Yangu.”11
Tunathibitisha kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake amelingana. Hivi
ndivyo ilivyokuja katika Qur-aan katika Suurah saba: al-A´raaf, Yuunus, ar-
Ra´d, Twaa Haa, al-Furqaan, as-Sajdah na al-Hadiyd.
Tunathibitisha kuwa:
“Mwingi wa huruma amemuumba Aadam kwa sura Yake.”
Ameipokea Ahmad bin Hanbal, Ibn Khuzaymah na wengineo. Vilevile
imepokelewa:
“… kwa sura ya Mwingi wa huruma.”
Ameipokea ad-Daaraqutwniy, Abu Bakr an-Najjaad, Abu ´Abdillaah bin
Battwah na wengineo.
Tunathibitisha kuwa Allaah ana vidole. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh)
amesema:
“Kuna mwanachuoni mmoja wa kiyahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) na akamwambia: “Ee Muhammad! Sisi tunakuta kuwa
Allaah ataziweka mbingu juu ya kidole, ardhi juu ya kidole, miti juu ya kidole,
maji juu ya kidole na viumbe vyengine vilivyobaki juu ya kidole. Halafu
atasema: “Mimi ndiye Mfalme.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
akacheka mpaka magego yake yakaonekana kwa kusadikisha maneno ya
mwanachuoni huyu wa kiyahudi. Kisha akasoma maneno ya Allaah (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam):
10 20:41 11 al-Bukhaariy (7405) na Muslim (2675).
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 9
تت م و م م م و ر س وم عا قو ر وتس س قو راو ا رقم وا و م وا ر ا واتس و ر م ر و وا و و س ا اارو وو ر و ر مام واار”Hawakumkadiria Allaah inavyostahiki kukadiriwa! Ardhi yote itakamatwa
mkononi Mwake wa kuume siku ya Qiyaamah.”1213
Ameipokea Hibatullaah at-Twabariy, al-Bukhaariy, Muslim na Abu ´Iysaa at-
Tirmidhiy ambaye tamko yeye limekuja ifuatavyo: Amenikhabarisha al-
Mubaarak bin ´Abdil-Jabbaar as-Sayrafiy kwenye kikao cha baba yangu
(Rahimahu Allaah) kwenye msikiti wa Mansuur kwa cheni ya wapokezi wake
kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:
”Kuna myahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na
kusema: ”Ee Muhammad! Allaah ataziweka mbingu juu ya kidole, ardhi juu ya
kidole na viumbe wengine juu ya kidole. Kisha atasema: ”Mimi ndiye
Mfalme.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza
kucheka mpaka magego yake yakaonekana. Kisha akasoma:
تت م و م م م و ر س وم عا قو ر وتس س قو راو ا رقم وا و م وا ر ا واتس و ر م ر و وا و و س ا اارو وو ر و ر مام واار”Hawakumkadiria Allaah inavyostahiki kukadiriwa! Ardhi yote itakamatwa
mkononi Mwake wa kuume siku ya Qiyaamah.”
Abu ´Iysaa amesema:
”Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh.”
Katika upokezi mwingine imekuja:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka kwa
kupendekezwa na kumsadikisha.”
Abu Sa´iyd amesimulia kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) akisema:
”Mola wetu atafunua muundi Wake ambapo atamsujudia kila muumini
mwanaume na muumini mwanamke na watabaki [hali ya kusimama] wale
ambao walikuwa wakisujudu duniani kwa kujionyesha na kutaka kusikika. Pale
12 39:67 13 al-Bukhaariy (4811) na Muslim (2786).
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 10
atapoenda ili kusujudu, tahamaki mgongo wake utarudi na kuwa talaka
moja.”14
Anas ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
amesema:
”Allaah hufurahishwa na tawbah ya mja wake zaidi kuliko vile anavyofurahi
mmoja wenu pale anapomkosa ngamia wake ambaye yuko na chakula na
kinywaji chake juu yake. Kisha akamtafuta na asimpate. Baada ya hapo akalala
chini ya mti na huku akisubiria kifo. Tahamaki ngamia yule amesimama juu
yake. Akamshika khatamu na kwa furaha nyingi akasema: ”Ee Allaah! Wewe
ni mja wangu na mimi ndiye Mola Wako.”15
´Abdullaah amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
alimtaja ad-Dajjaal kisha akasema:
”Hakika ana chongo, lakini Mola wenu (´Azza wa Jall) hana chongo.”16
[7] Yule mwenye kuitakidi juu ya sifa hizi na mapokezi Swahiyh mfano wake
kufanana inapokuja katika miili, aina, shakili na urefu, ni kafiri.
[8] Kuzikanusha sifa ni madhehebu ya Jahmiyyah. Yule mwenye kuzifasiri
kutokana na lugha na majazi ni Jahmiy.
[9] Yule mwenye kuzipitisha kama zilivyokuja bila kuzipindisha maana,
kuzifasiri, kuzifanya mwili wala kuzifananisha, kama walivyofanya
Maswahabah na Taabi´uun, amefanya jambo la wajibu kwake.
14 al-Bukhârî (4919) na Muslim (183). 15 al-Bukhaariy (6308) na Muslim (2747). 16 al-Bukhaariy (7131) na Muslim (2933).
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 11
[10] Ni wajibu kuamini Qadar, kheri na shari yake, matamu yake na machungu
yake, makubwa yake na machache yake, yenye kuonekana na yenye kujificha,
yale yenye kupendwa na yale yenye kuchukiwa na mazuri yake na yasiyokuwa
mazuri.
Mwanzo na mwisho wake ni kutoka kwa Allaah. Amepanga mipango Yake
juu ya waja Wake na akakadiria makadirio juu yao. Hakuna yeyote awezaye
kushinda matakwa ya Allaah (´Azza wa Jall) na wala hakuna yeyote awezaye
kushinda mipango Yake, bali wote hawana ujanja ni wenye kupita chini ya yale
aliyowaumba kwayo. Huu ni uadilifu kutoka kwa Mola wetu (´Azza wa Jall).
Anataka utiifu utendeka, yuko radhi nao, anaupenda na ameuamrisha. Hata
hivyo hakuamrisha maasi na wala hayapendi na kuyaridhia. Upande mwingine
ameyahukumu, akayakadiria na akataka yatendeke. Muuliwaji anauawa pindi
muda wake unapofika.
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 12
[11] Inatakiwa kuamini adhabu ya ndani ya kaburi na Munkar na Nakiyr.
Allaah (Ta´ala) amesema:
وإمور و س و م شو ع ضو كعا
“Basi hakika atapata maisha ya dhiki kabisa.”17
Wafasiri wa Qur-aan wamesema:
”Bi maana adhabu ya ndani ya kaburi.”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Umar bin al-
Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh):
”Ee ´Umar! Hali ingelikuwa vipi endapo ungeliona fitina za Malaika wawili wa
kaburi? Ni weusi na wana macho ya bluu na kama umeme na sauti yao ni
kama radi. Wanaingia kwenye nywele zao na wanachimba kwa meno yao ya
kuchimba. Mikononi mwao wana nyundo za vyuma. Lau wangeliwapiga watu
na majini, basi wangelikufa.” ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) akasema: ”Siku
hiyo nitakuwa na hali gani?” Akasema: ”Katika hali yako hiyohiyo ulionayo.”
Akasema: ”Basi nitakutosheleza nao, ee Mtume wa Allaah!”18
Umm Khaalid (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:
”Nilimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiomba kinga dhidi ya
adhabu ya kaburi.”19
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Lau angelikuweko yoyote atakayeokoka na mbano wa kaburi, basi
angeliokoka Sa´d bin Mu´aadh ambaye ´Arshi ya Mwingi wa rehema ilitikisika
kwa ajili yake.”20
Halafu baada ya hapo mtu anatakiwa kuamini sauti ya parapanda kutoka kwa
Israafiyl kwa ajili ya kufufuka kutoka ndani ya makaburi. Ulazimishe moyo
kwamba utakufa na utabanwa ndani ya kaburi. Ni wajibu pia kuamini kuwa
mtu atahojiwa ndani ya kaburi na atafufuliwa baada ya kufa. Mwenye
kuyakanusha haya ni kafiri.
17 20:124 18 al-Bayhaqiy katika ”Ithbaat ´Adhaab-il-Qabr” (116–117) na Ibn Abiy Daawuud katika ”al-Ba´th” (7). 19 al-Bukhaariy (6364) na Muslim (584). 20 Ahmad (6/55).
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 13
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 14
[12] Inatakiwa kuamini ufufuliwaji na Njia. Nembo ya waumini siku hiyo
itakuwa:
”Salimisha, salimisha.”
Imekuja katika Hadiyth kwamba Njia itakuwa yenye makali zaidi kuliko
upanga na nyembamba zaidi kuliko unywele21.
[13] Kuamini Mizani. Amesema (Ta´ala):
ئعا ثقرقواوو وو ر ل م ر و ردوول و و وعس ا ر و وازم و ا رقم رطو م قو رام ا رقم وا و م و و سظر و س قو رست و قر و مو كواوو م وكو و ـ م وا ووا م م و و قو قر وا بموا
“Tutaweka mizani ya uadilifu siku ya Qiyaamah, basi hakuna nafsi itakayodhulumiwa chochote japo ikiwa uzito wa mbegu ya haradali Tutaileta. Inatosheleza Kwetu kuwa wenye kuhesabu.”22
´Abdullaah bin Mas´uud amesema:
”Siku ya Qiyaamah watu wataletwa kwenye Mizani na hapo watabishana
ubishi mkubwa kabisa.”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mkono wa kuume wa Allaah (´Azza wa Jall) umejaa. Haupungui kwa kutoa
mchana na usiku. Kwenye mkono Wake mwingine kuna mizani ambayo
hushusha na hupandisha.”23
[14] Inatakiwa kuamini Hodhi na Uombezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) amesema:
21 Muslim (195). 22 21:47 23 al-Bukhaariy (4684), Muslim (993), Ahmad (2/242) na at-Tirmidhiy (3045) ambaye amesema: “Hdiyth hii ni nuri na Swahiyh na akaifasiri Aayah:
ااس و ر س ووتواوم س م س كو ر و وشوا س غس ر ر و ر م م ر و س م س ا بموا وا س ا و وا و م ا ر قو س دس و س اارم وغر س و ت و ر و و
“Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale
waliyoyasema. Bali mikono Yake imefumbuliwa hutoa atakavyo.” (05:64)
Hadiyth imepolewa na maimamu. Tunaiamini kwa udhahiri wake pasi na kuifasiri wala kuifanyia namna. Hivyo ndivo
walivosema maimamu akiwemo Sufyaan ath-Thawriy, Maalik bin Anas, Ibn ´Uyaynah na Ibn-ul-Mubaarak;
zinatakiwa kupitishwa na kuziamini pasi na kuzifanyia namna.”
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 15
”Mimi nina Hodhi inayoanzia Ayla kwenda mpaka Adeni na vikombe vyake
ni sawa na idadi ya nyota mbinguni.”24
Bi maana ni kubwa sana.
Anas bin Maalik amesema:
”Mwenye kukadhibisha Hodhi basi hatokunywa humo.”
[15] Mtu anatakiwa kuamini pia mahojiano. Allaah (Ta´ala) atamuhoji mja kwa
yale yote aliyoyafanya, madogo na makubwa.
24al-Bukhaariy (6591) na Muslim (2298).
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 16
[16] Kuamini kwamba Allaah aliumba Pepo na Moto kabla ya kuumba
viumbe. Neema za Peponi zitaendelea kuwepo milele na kamwe wanawake wa
Peponi hawakutokufa.
Adhabu ya Motoni ni yenye kudumu na watu wake ambao walitengana na
dunia hii hali ya kuwa si wenye kumwabudu Allaah pekee na si wenye kufuata
Sunnah, watadumishwa humo.
[17] Kuhusiana na wapwekeshaji watenda madhambi, watatolewa humo ndani
kwa uombezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Uombezi wangu ni kwa ajili ya watenda madhambi makubwa kutoka katika
Ummah wangu.”25
Watoto wa washirikina watakuwa Motoni.
25 Ahmad (3/213), Abu Daawuud (4739) na at-Tirmidhiy (2345).
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 17
[18] Inatakiwa kuamini vilevile kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) ndiye Mtume wetu, Nabii wa mwisho, bwana wa Mitume, kiongozi
wa wachaji na mjumbe wa Mola wa walimwengu.
Amemtumiliza kwetu na kwa viumbe wengine wote. Yeye ndiye bwana wa
wana wa Aadam na ndiye wa kwanza atakayefufuliwa na ardhi. Aadam na
walioko chini yake watakuwa chini ya bendera yake. Yeye ndiye shahidi wa
kila Mtume na ndiye shahidi wa kila Ummah. Allaah (Ta´ala) amechukua
mkataba kwa Mitume kumwamini, kutoa bishara njema juu yake, kumwelezea
na kumbainisha katika vitabu vyao pamoja na zile alama na miujiza yenye
kugonga ambayo Allaah alimtunuku kabla na baada ya kupewa utume.
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 18
[19] Miongoni mwa hayo ni kitabu chake ambacho kinavihukumu vitabu
vyengine vyote na kinachovitolea khabari, kinachovitolea ushahidi na
kuvisadikisha. Hakifanani na mashairi wala barua. Kimetakasika na maneno
mengine yote. Kimefazaisha usikizi na uelewa. Hakiingiliwi na batili mbele
yake wala nyuma yake. Ni Uteremsho kutoka kwa Mwingi wa hekima,
Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Watu na majini wameshindwa kuleta mfano
wake, japokuwa watakuwa ni wenye kusaidizana wao kwa wao. Ni kitabu
kilichokusanya mifumo, miujiza, ufafanuzi, ufaswaha, balagha,
matahadharisho, mawaidha, maamrisho kuhusu kila utiifu, karama, adabu,
makatazo kuhusu kila uovu na aina zote kubwa za ´ibaadah kama twahara,
swalah, swawm, zakaah, hajj, jihaad, kuunga udugu, kujitolea, zawadi,
swadaqah, utimizaji, kuogopa, kutaraji na aina nyenginezo zisizohesabika.
Wakati watu wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipomwambia:
ا و ر و م ر س قـ و اار م مقس ر ول غو رم و
“Lete Qur-aan nyingine badala ya hii au ibadilishe.”
akasema:
مور و ر معس م ر وا س وو ـ ملور وا وكس وس لم وور س و م و س م م رقوا م قو ر م
“Hainipasii mimi kuibadilisha kwa khiyari ya nafsi yangu. Mimi sifuati isipokuwa tu yale nilofunuliwa Wahy.”26
Bi maana kutoka kwa Mola wangu. Halafu akawaambia:
و و و قوقو ر و مثر س م كس ر عس س عا م قو ر م م ر ر وا و ا رق س وا قو و ر س س عو و ركس ر و و ودر واكس م م قو رقم س وو
“Kama angetaka Allaah nisingelikusomeeni na wala asingelikujulisheni nayo. Kwani nimekwishaishi nanyi umri wote kabla yake. Je, basi hamfahamu?”27
26 10:15 27 10:16
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 19
Bi maana kwa miaka arubaini mimi ni yatima, fakiri, si mwenye kujua kusoma
wala kuandika, sikuwa naenda kwa mwalimu wowote, mchawi, kuhani wala
mshairi. Je, hivi si mzingatie hayo? Mnajua fika ya kwamba Aayah mfano wa
hizi hakuna aziwezaye isipokuwa Allaah – hamkuweza kufanya hivo na wala
hamtoweza kufanya hivo.
Akafanya Aayah hizi ni zenye kushinda katika uhai wake na baada ya kufa
kwake pasi na yeyote kuja na mfano wake. Hakuna yeyote aliyefanikiwa kuja
na mfano wa Qur-aan kwa upande wa Aayah zake, mpangilio wake, ukweli
wake, usahihi wa maana yake na elimu zake kubwa. Kadhalika viumbe
hawakuweza kuzunguka uelewa wake wala kufikia kilele cha elimu yake.
Isitoshe yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekhabarisha kuhusu watu
wa kale na wataokuja nyuma:
و ر م و س م قو ر م غو و م م ر و قوغر م س وو م م رعم م م و غس م و م ا ل اس م ودر و اار
“Warumi wameshindwa. Katika nchi iliyo karibu, nao baada ya kushindwa kwao watashinda hivi karibuni. Katika miaka michache.”28
عس و قس و ل وو ا ل قس و و قس ر واس اارو ر
“Utashindwa mjumuiko wao na watageuza migongo.”29
Ameelezea hayo kabla ya kutokea kwake. Amesema (Ta´ala):
ا م و ر و ا م ر و م ر و وا م ا رغو ر م س وم و قـ و ا و و و و قو ر س و م قو ر م و وا كس و قو ر و س و
“Hizo ni katika khabari zilizofichikana Tunazokufunulia Wahy. Hukuwa unazijua wewe na wala watu wako kabla ya hii [Qur-aan].”30
28 30:02-04 29 54:45 30 11:49
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 20
[20] Ana (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alama kubwa za ardhini na
mbinguni. Hakuna mtu mwingine anayeshirikiana naye kwazo wala kuzifikia.
Mtu mwenye busara na mwenye uoni wa mbali akizizingatia, basi atatambua
kuwa Allaah amemtunuku nafasi na ngazi tukufu na akamfadhilisha kwazo juu
ya walimwengu wengine wote. Alama hiyo ni kwamba usiku mmoja
alimpanda mnyama al-Buraq kumpeleka Yerusalemu. Halafu akanyanyuliwa
juu mbinguni ambapo akawasalimia Malaika na Mitume ambao pia
aliwaswalisha. Aliingia Peponi na akauona Moto. Katika usiku huo
akafaradhishiwa swalah na akamuona Mola Wake. Akasogea karibu Naye na
akazungumza Naye na akamtukuza. Akaona karama na alama. Akamsogelea
Mola Wake na akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.
Allaah aliuweka mkono Wake juu ya mabega yake na akahisi ubaridi kati ya
matiti yake na akapata elimu za wale wa mwanzo na wa mwisho. Amesema
(´Azza wa Jall):
و وا و و ر وا ا ل ر و ا ر م و و قر وااو م ر متقر و ع م راام
“Hatukuijaalia ndoto ambayo tulikuonyesha isipokuwa ni [kutaka kuwatia] mtihani kwa watu.”31
Uonaji huu ulitokea katika hali ya umacho na haikuwa ndoto. Usiku huohuo
akarudi kwa mwili wake kwenda Makkah. Akaeleza kwamba yeye (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) huko Aakhirah atapewa fadhilah na utukufu zaidi
kuliko alivyopewa hapa duniani na akasema:
و و و ر و قس ر م و و ل و قوتقو رضو ـ
“Bila shaka Mola wako atakupa na utaridhika.”32
Miongoni mwa yale atakayopewa huko Aakhirah ni kile Cheo chenye kusifiwa
ambacho hakuna yeyote ambaye atakisogelea. Abu Bakr Ahmad bin Abiy
Khaythamah amesimulia kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Mujaahid
ambaye amesema kuhusu maneno Yake:
31 17:60 32 93:05
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 21
عو و ـ وو قو قر وثو و و ل و وقوا عا مرر س دعا
“Hakika Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.”33
”Atamkaza juu ya ´Arshi.”34
Abu Bakr bin Abiy Shaybah na ´Uthmaan bin Abiy Shaybah wamepokea kwa
cheni za wapokezi wao kutoka kwa Mujaahid ambaye amesema kuhusiana na
Aayah hiyohiyo:
”Atamkaza juu ya ´Arshi.”
Kadhalika ´Abdullaah bin Ahmad amepokea kwa cheni ya wapokezi wake
kutoka kwa Mujaahid. Vivyo hivyo amepokea Ishaaq bin Raahuuyah kutoka
kwa Ibn Fudhwayl kutoka kwa Layth kutoka kwa Mujaahid ambaye amesema
kuhusiana na Aayah hiyohiyo:
”Atakaa pamoja naye juu ya ´Arshi.”
Ibn ´Umayr amesema:
”Nimemsikia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal akiulizwa kuhusu Hadiyth
ya Mujaahid ambapo akasema: ”Wanachuoni wameinukuu kwa kuikubali na
hivyo tunaipitisha kama ilivyokuja.”
Ibn-ul-Haarith amesema:
”Ndio, Muhammad atakazwa juu ya ´Arshi.”
´Abdullaah bin Ahmad amesema:
”Mimi namkemea kila yule ambaye anairudisha Hadiyth hii.”
Ibn ´Abbaas amesema kuhusiana na Aayah hiyohiyo:
”Atamkaza juu ya ´Arshi.”
Mapokezi haya yamepokelewa na Shaykh wetu Abu Bakr al-Marwaziy na
akatunga kitabu kikubwa juu ya maudhui hayo. Kadhalika ameeleza baba
yangu kutoka kwake kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Ibn ´Umar
kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na Aayah
hiyohiyo:
33 17:79 34Taariykh Ibn Abiy Khaythamah.
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 22
”Atakaa pamoja naye juu ya kiti.”
Kadhalika kwa cheni ya wapokezi kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu
´anhaa) ambaye amesema:
”Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu
Cheo chenye kusifiwa. Akasema: ”Mola wangu ameniahidi kukaa juu ya
´Arshi.”
Vivyo hivyo kwa cheni ya wapokezi kutoka kwa Ibn ´Umar ambaye amesema:
”´Umar bin al-Khattwaab alisema kunambia: ”Nilimuuliza Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) kile alichomuahidi Mola wake Akasema:
”Ameniahidi Cheo chenye kusifiwa ambacho ni kukaa juu ya ´Arshi.”
Vilevile ana Hodhi hiyo siku ya Qiyaamah.
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 23
[21] Yule mwenye kunyanyua sauti yake mbele ya Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) kunachelea juu yake kuporomoka matendo yake. Amesema
(´Azza wa Jall):
م و و تور و س ا و س بم رقو روم كو و ر م و و قل وا ا ر م و و س ا و قو ر قو س ا وصر وا وكس ر قو رقو صو رتم ا ربم قو ر مكس ر م قو ر ل وو ور وطو وعر وا سكس ر و و تس ر و وشر س س وو
“Enyi walioamini! Msizinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Mtume na wala msiseme naye kwa sauti ya juu kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu, yasije yakaporomoka matendo yenu nanyi hamhisi.”35
Akawafunza adabu namna wanavyotakiwa kuwa pindi wanapomzungumzisha
na kuzungumza na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema:
ر تور و س ا دسعوا و ا ر س وم قو قر وكس ر كو سعوا م قو ر مكس قو ر عا
“Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi.”36
Msisemi: ”Ee Ahmad! Ee Muhammad! Ee Abul-Qaasim!” Badala yake
semeni: “Ee Mtume wa Allaah! Ee Nabii wa Allaah!” Allaah (´Azza wa Jall)
amesema:
م تقس ر م س ا بم رق م و و س م م و قس و م س اس و قس و م س اس و س و م س اس سكر وةع و وصم ع
“Ili mumwamini Allaah na Mtume Wake na mumtukuze na mumheshimu na mumsabihi asubuhi na jioni.”37
Amewaamrisha kumuadhimisha yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama
ambavyo Yeye kamuadhimisha na kumtukuza mbele ya Mitume wengine wote
kwa vile anamsemesha:
و و قل وا ا ر س وس و م ر وا س موو م و ر و م ر م و
35 49:02 36 24:63 37 48:09
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 24
“Ee Mtume! Fikisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako.”38
Sambamba na hilo amewasemesha Mitume kwa majina yao: “Ee Aadam!”,
“Ee Nuuh!”, “Ee Ibraahiym!”, “Ee Muusa!” na “Ee ´Iysaa!” Amesema:
كس س ا ر س وس وخس س اس و وا قو واكس ر عو ر س وا تقو س ا و وا تو
“Kile anachokupeni Mtume basi kichukueni na anachokukatazeni basi kiacheni.”39
Amefanya maamrisho na makatazo yake kuwa na nafasi kama ya Qur-aan.
Kadhalika akamkusanyia sifa mbili miongoni mwa sifa Zake na akasema:
كس ر عو م ت عو و ر م وا عو متل ر وو م يت عو و ركس بم ر س ر م م و و س ت روم ت وقو ر وا وكس ر و س وت م ر و س م
“Hakika amekujieni Mtume anayetokana na jinsia yenu nyinyi wenyewe. Yanamuhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni na kwa waliomuamini ni mpole na mwenye huruma.”40
Hakuwahi kuapa kwamba yeyote ni Mtume isipokuwa yeye. Amesema:
توقم ل وا رقس ر وم ااروكم م م ر و و م و ا ر س ر و م و عو و ـ صم واال ل ر
“Naapa kwa Qur-aan yenye hekima. Hakika wewe ni miongoni mwa Mitume. Uko juu ya njia iliyonyooka.”41
Vilevile amesema:
م ر قو ر و س وو و و ر ساو م قر س ر و م وكر و م
“Naapa kwa umri wako hakika wao walikuwa katika ulevi wao wanatangatanga kwa upofu.”42
Ameeleza kwamba Ibraahiym amesema: 38 05:67 39 59:07 40 09:128 41 36:02-04 42 15:72
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 25
و و سر م م قو راو قس قر وثس وو
“Usinihizi siku watakayofufuliwa.”43
Halafu akamjibu juu ya hilo. Hata hivyo ameyasema haya juu ya Mtume wetu
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na yeye kuanza kumuomba:
ر وا ر م و و س ا و و س قو راو و سر م ا رق س ا ربم
“Siku ambayo Allaah hatomfedhehesha Nabii na wale walioamini pamoja naye.”44
Muusa amesema:
واوو وبم ا ر وحر لم صو ر م
“Akasema: “Mola wangu nikunjulie kifua changu.”45
Allaah akamjibu juu ya hilo na akasema:
و ر س م و س ر و و و س و ـ
“Umekwishapewa ombi lako, ee Muusa.”46
Hata hivyo alisema kumwambia Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam):
و ور وشر وحر و و صو ر واو
“Je, kwani hatukukupanulia kifua chako kukubainishia?”47
Amemsamehe madhambi yake pamoja na kuyaficha na wakati huohuo
amesamehe madhambi ya wengine pamoja na kuyaweka wazi. Amesema:
43 26:87 44 66:08 45 20:25 46 20:36 47 94:01
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 26
تقو وااس و ل س قوتوابو عو و ر م و و و ـ وعو و ـ دواس و ر س قوغو و ـ سر ا ر
“Aadam akamuasi Mola wake akapotoka kisha Mola wake akamteua akapokea tawbah yake na akamwongoza.”48
Amesema kumwambia Daawuud:
تقوغر و و و ر س و و ر واكم عا و و وبو قوغو و ر و و س وـ م و و مور و س عم و و و س ر و ـ و و ر دوا س دس و روا قوتقو رااس وا ر ووس ر و و بل
“Daawuud akahisi kwamba Tulimpa mtihani, basi akamuomba Mola wake msamaha na akaanguka chini kusujudu na akatubia. Hivyo tukamsamehe hayo na hakika yeye bila shaka ana Kwetu makurubisho na marejeo mazuri.”49
Vilevile amesema:
ا سر و وبو و وقو ر قوتقو را س و ر واوو و و رقو قر وا عو و ـ كس ر م م م و و ع
“Hakika Tulimpa mtihani Sulaymaan na tukamtupia juu ya kiti chake mwili kisha akarejea.”50
Pia amesema:
و وا ا ل وم م ر و و سغواضم عا وظو ر وو ر قرقر م و عو و ر م قو وادو ـ م ا ظل س واتم وو ر م وقـ و م ر و و س ر وا و و م م كس س م و ا ظرا م م و
“Dhan-Nuun alipoondoka hali ya kuwa ameghadhibika akadhani kwamba hatutamdhikisha, akaita katika kiza kwamba: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako! Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”51
Amesema kumwambia Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
48 20:121-122 49 38:24-25 50 38:34 51 21:87
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 27
م قوغر م و و و ا رق س وا قوقو راو م و م و و وا وو ر و
“Ili Allaah akusamehe yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia.”52
Hakuyataja madhambi hayo. Kadhalika amesema:
و ور وشر وحر و و صو ر واو و وضو ر وا عو و مزر واو ا ر م و قو و و ر واو
“Je, kwani hatukukupanulia kifua chako kukubainishia na Tukakuondolea mzigo [madhambi] wako ambao ulithakilisha mgongo wako?”53
Hata hivyo hakutaja mzigo huo.
52 48:02 53 94:01-03
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 28
[22] Kiumbe bora baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) na ambaye ana manzilah ya juu kabisa baada ya Manabii na Mitume na
ambaye ana haki zaidi ya ukhaliyfah baada ya Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh).
Baada ya hapo anafuatia ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh).
Halafu anafuatia Dhun-Nuurayn ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu
´anh). Kisha anafuatia Abul-Hasan ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu
´anh).
Tunawashuhudilia wale kumi Pepo ambao ni Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan,
´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, Sa´d, Sa´iyd, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Abu
´Ubaydah bin al-Jarraah. Mtu anatakiwa kumuomba Allaah awarehemu
Maswahabah wote wa Mtume wa Allaah, kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa
mwisho wao, na pia kuyataja mazuri yao.
Mu´aawiyah ndiye mjomba wa Waumini na alikuwa ni mwandishi wa Wahy
wa Mola wa walimwengu.
Kitabu kuhusu ´Aqiydah Imaam na Haafidhw Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
www.firqatunnajia.com 29
[23] Ni wajibu kuwakata Ahl-ul-Bid´ah na wapotevu. Kama mfano wa
Mushabbihah, Mujassimah, Ash´ariyyah, Mu´tazilah, Raafidhwah, Murji-ah,
Qadariyyah, Jahmiyyah, Khawaarij, Saalimiyyah, Karraamiyyah na mapote
mengine yaliyobaki yenye kusemwa vibaya.
[24] Hii ndio ´Aqiydah yangu na yale ninayomwabudu kwayo Mola wangu na
ndio ambayo baba yangu amekufa juu yake – Allaah amrehemu.