30
chapta 13 inspiring kenyan youth not for sale check out our new website www.shujaaz.fm web fm sms comix

13 - Shujaaz.FM - Chapta 13

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Chapta 13 - Full Comic

Citation preview

chapta 13

inspiring kenyan youth

not for sale

check out our

new website

www.shujaaz.fm

web fm sms comix

Anarudi bana! Niunganishie kuku tumpikie, at least ka-welcome hivi!

...ksskss...

Unakumbuka O.G.? Yule boy alituingiza kwa

gang?

...ksskss...

oe!

tosh!!!

kumbe ni wewe, slim? mbona unajificha?

Ni kutuliza kiasi, si unajua tunasakwa na

makarao mtaani.

Hizo risto za gang nilichoka nazo. Ndio job ni hard lakini najitegemea.

heh.

uko down.

Napenda sana ma-electronics na radio. So nimeamua kujenga pirate radio station- Shujaaz.fm! DJ B mwenyewe, ndani ya nyumba!

Lifeya Gangsta

3

Ala! Nani huyo

anakuja na hiyo kelele

yote?

Skia vile ndai yake inachuna ngoma!!

Chunga wasichana

wako wasiharibiwe

na huyu!

ati o.g. amehepa

jela mara 10!

wacha?!

ana garikama 20!

Walalala!

sasa amerudi

huku kufanya nini???

aki nataka kuwa kama

o.g. ...

4

Eh, Mwas alidedi.

Oh?! Lakini hiyo ndio life ya magangsta

kama sisi.

mwas yuko wapi?

Na Blackie mnamskia?

alishikwa.

Chekini, Godpapa ameni-organiz-ia nitulize huku kiasi.

Nasakwa.

Ni tuff, lakini sisi ni ma-thug.

Hatu-represent-iwi kwa gava, so

wana-expect nini?

Mabuda hawatujali. Lazima sisi mayuts tujitetee kwa hizi gang zetu, ausio?

No mercy!

Msi-mind, elections zina-come, Godpapa ataangusha dooh

ile mbaya.

Sasa acheni niende nicheki mtoi wangu.

Sijamwona kwa miaka kama 15 hivi.

Si sasa mtoi amekusahau?

Sasa ni-do? Lazima aelewe hali ya

u-gangsta! Twende Slim.

baadaye kwa gangheadquarters...

5

6

LiPA!!!

Hii ni youth group ya aina gani?!

AAAAAAH,Slim!

Hizi mbio zinanikumbusha

operations zetu za tene!

Hehehehe! Ah! Kama hii ndio life

ya u-gangsta wacha

nirudi kwa shamba!

oe! Slim bana, si unionyeshe

kwenye nitajificha kwanza?!

Sema, Slim! Kuna youth group flani nime-join. Si uicheki?

7

Unaweza ni-save na job? Nimechoka na story za gang,

jo! Si uli-help Tosh?

Wazi Slim. Kuwa gangsta ni kuji-waste. Unaskianga DJ B? Ana show flani ina ideas mob za ku-make

dooh.

slim?Sema.

niaje boyie?

Yule wa Shujaaz.FM? Hata wacha nimtumie

sms nimwambie a-show mayuts

vile gangs hazibambi!

ala! kumbe Hii ndio

maisha ya gangsta?!

Ah, shhhh! Makarao

watanipata!

SKIA KUTOKA MSEE WA NGUVU,

JOHN KIRIAMITI.

Ina dooh sana.

Utajibamba, utaweza ku-buy

nguo noma, ndula, kama

wasee wa majuu wa music video.

Uki-get dooh kwa njia illegal, ni rahisi

kupatikana na makarao, hizo dooh

hazi�chiki easily!

Music videos

zime-act-iwa, si real!

Uki-join gang, utafanya

vitu mob dangerous

kabla upate dooh, na

hauta-enjoy hizo dooh

juu utabambwa uishie

jela. Usiamini kila kitu

unaona kwa TV!

“Kuwa kwa gang ndio mwanzo wa kuwa criminal.”

“Ukitaka kutoka kwa gang, toka na usi-communicate na wasee wenye wamebaki huko!

“Kuwa na friends positive.”

“Gang si ‘brotherhood’. Kila mtu atashikwa peke yake, na utaenda jela peke yako!”

SI WORTH KUWA GANGSTA!Kuna njia mob za ku-make

dooh, kaa rada, cheki www.shujaaz.fm.”

BIG UP JOHN KIRIAMITI KWA ADVICE!

REALITY!

REALITY!

CHEKI MAVACO NA REALITY JUU YA GANG LIFE…

8

9

10

Nili-discuss na buda juu ya

interest yangu...Nilipenda sana fish tangu

nikuwe mtoi. Kuna time hata nilijaribu ku-plant bones za fish

kwa shamba!

Er, um, er, Erico. Kwa nini uli-decide

kufuga fish?

He, he, alitaka kukuuliza

swali kidogo

11

So, unalisha fish nini?

Cheki, hata wewe unaweza try kwa ka-pond

kadogo ausio? Shika hizi

fingerlings.

Mdogomdogo, tulianza.

Tunatumia vitu cheap kuzilisha,

kama mbolea ya kuku.

After form 4, alinigawia kaploti kwa

shamba yake nitumie kufuga fish. Then,nika-share idea yangu na mabeste

ndio tu-work pamoja.

As a group, tuli-manage ku-apply

for youth fund na tuka-get

dooh.

Thanks sana Erico. Er, em, nikupe number yangu ndio tubonge

hii story more baadaye?

12

Ha, ha. Nitamwuliza.

Amekuwa akinipe tips mob na nili-share na DJB ndio mayuts

wengi wapate hii idea. Erico ni guy mpoa sana.

, ulienda ocha ku-do?

Hata sidhani huyo chali alikuwa

m-hot…

Malkia, alikupe number ya

beste yake yeyote

uniunganishie?

13

14

» Naskia una kichwa bigi, ukienda kinyozi ina-bidi ukuwe admitted.

» Ati umechapa hadi shadow yako hukuambia “endaga, na-come”.

» Nyanya yako ni toothless hadi hawezi uma vaco.

» Comp yako ni mzee hadi inatumia miti shamba kama anti-virus.

» Una kisogo refu, ukivaa marvin kichwa inakaa windsock.

» Ma-siz wako ni ma-ugly hadi buda wenyu ameandika kaw gate: “Marry

1, get 2 free”.

» Umefanya dhambi mob hadi sheito akikuona, ye huwika: “Oh my God!”

» Wewe ni fala, ulienda bloodtest na mwakenya.

» Ati wewe ni mjinga, mwalimu wa Kiswahili alikuuliza udogo was mawe

ukasema kokoto.

» Kwenyu kuna insecurity hadi ukipigwa ngeta unapewa receipt.

» Ati wewe ni mnono, uliingia Facebook kama group.

» Sanifu (v) - Tafuta

» Mrengo (n) - Food

» Kisisa / Mawinch (n) - Dooh /Money

» Kabambe (n) - Job / Kazi

» Chwara / Maurero (n) - Dem / Girl

» Buju (n) - Gari

» Usoro (v) - Kuchunguza

» Gouko (n) - Vita / Fight

» Gwangi (adj) - Mwanaume ugly

» Duanzi (adj) - Fala

» *Maru (n) - Works / Job *by Gadisa Gashu

[ UME-WIN TISHO! ]

Shuj

aaz(

TM) i

s pu

blis

hed

by W

ell T

old

Stor

y Lt

d. ,

P. O

. Box

170

0 00

502

Nairo

bi, K

enya

. Tel

: 02

0260

3214

ww

w.w

ts.c

o.ke

. Prin

ted

by C

olou

rprin

t Lim

ited,

P. O

. Box

444

66 -

0010

0 Na

irobi

GPO

. Pro

duce

d in

col

labo

ratio

n w

ith: S

afar

icom

, Tw

awez

a, R

IU.

Dist

ribut

ed b

y Sa

turd

ay N

atio

n an

d Sa

faric

om.

Cont

ent p

rodu

cers

: Aud

rey

Wab

wire

Co

nten

t: Pa

ul P

eter

Kad

es, C

harle

s O

uda,

Dav

id O

uma

Ar

t Pro

duce

r: Fa

tima

Aly

Jaffe

r L

ayou

t Des

ign:

Sal

im B

usur

u

Art:

Dani

el M

uli,

Eric

Mut

hoga

, Nad

dya

Olu

och-

Olu

nya,

Jo

e Ba

rasa

Ra

dio:

Eun

ice

Mai

na

Spe

cial

than

ks to

Jus

t A B

and

for t

heir

fant

astic

mus

ic o

n Sh

ujaa

zFM

radi

o

Wel

l Tol

d St

ory

© 2

011

All r

ight

s re

serv

ed. N

o pa

rt of

this

pub

licat

ion

may

be

repr

oduc

ed, s

tore

d in

any

retri

eval

sys

tem

or b

e tra

nsm

itted

in a

ny fo

rm o

r by

any

mea

ns, e

lect

roni

c or

mec

hani

cal w

ithou

t prio

r per

mis

sion

of t

he

publ

ishe

rs. A

lthou

gh e

very

effo

rt ha

s be

en ta

ken

to e

nsur

e th

e ac

cura

cy o

f inf

orm

atio

n co

ntai

ned

in th

is p

ublic

atio

n, in

no

even

t sha

ll th

e pu

blis

hers

be

liabl

e fo

r any

inci

dent

al, i

ndire

ct, c

onse

quen

tial l

osse

s or

dam

ages

of a

ny

kind

with

out l

imita

tion

aris

ing

out o

f or i

n co

nnec

tion

with

the

use

of th

e in

form

atio

n in

this

pub

licat

ion.

15

Hi DJ B, just did my KCPE but Shujaaz imeni-keep home. Huwa c zururi. Instead, mi hupanda skuma home na 2me save dooh mob. Ian, KTL, 14 yrs from Kitale.

Sema Boyie, mi na like comix yenu, ime tu-encourage sisi ma-youth. Kama hiyo story ya skuma ita help many youths. Nilikuwa nataka ku advise vijana waanze entertainment group zao na wata get pesa. Eva Maina from Nyeri district, Munyu location.

Rabbit noma; moja hu bear upto 10 kids, zina grow faster, na kuzaana faster pia. Urine yake na manure pia ni dooh, ukiuza ama utumie kupanda healthy crops. Meat yake ni super na ni white meat. Gatimu L.

Mi ni Richard, kutoka mtaani Kibera. Hiyo idea ya kuanza TV station ni poa sana. Ita-help ma-yuth na pia itawa-encourage. Asante sana DJ B!

Hi DJ B! Imagine my poultry project imeni-inua tu sana kidooh. Nimeji-cloth na ku-achieve vitu mob. Mayouth wai-try. Ken Mukonyi, 18. Kakamega.

Niaje DJ B. Idea ni wasee wenye wame-mada chuo waache kukaa home idle so sakanya works yeyote uanze ku-earn. Si works ni works bora unaearn doo yako? Betty K.

Manze DJ B wewe hunibamba mbaya sana nimekuwa addicted 2 ur show. Tresia ELDY aka DJ T

Niaje DJ B. Mko yuu maze. Na-like zile ma advise mnagive. Pia da dicmusi iko swadakta.

Asante DJ B. Yaani items zako ziko poa mpaka sina hamu ya food na uzingizi. Tena hakuna homework roundi hii. Ryan Paul Kipkorir from Sotik

Hi DJ B! It's Mavo 4rm Juja. Hapa mtaani wajamaa walikuwa na shida ya maji lakini mimi na mabeshte wangu tuli-talk na chief na sisi mayouth tuli-represent shida zetu kisha tukaungana na ma-villagers ku-help in the job of tapping water and within 2 days it was finished. You can build a better nation! Mayouth, don't be afraid to express your grievances. Mavo Premier from Juja.

IDEA ZA

KU-MAKE DOOH

Cheki chapta 14, ina-come na info ya

rabbit farming!

Cheki Chapta 9 na 10 www.shujaaz.fm!

Cheki Chapta 8 www.shujaaz.fm

IDEA YA CAREER

MI NA-LIKE SHUJAAZ!

KU-APPROACH

LEADERZ

NI POA KUFUGA WANYAMA..

T-SHO WINNERS

16

Sup DJ B! Mi natoa advice ya myn kwa ma youths, na especially mateeniez, wa join groups za maana ili ku-avoid kuwa idle na wa discover talents zao. Groups kama karate ime-nisaidia 2 sana. Kwanza kwa ma-dem ina-help na self-defence against rape.

Vijana tu-form youth groups ili tujiinue kiuchumi. Kwani ni rahisi ku access loans tukiwa wengi kuliko individually.

Hi DJ B! Manze when I cleared 4th I was idle bt idea ya ku-dry fruits ime-nisave 2 sana. Nilishow matha akaanza hiyo projo na sasa amenifungulia base ya pudding. - Edu.

Niaje DJ B. Thanks kwa ku-help mayouths. Why can't u tackle the issue of drug abuse? Manze zina-kill na ku-waste time mob ya may-ouths. Wa-show drugs ni gwan. Thanks. Ann M.

Niaje DJ B, walahi risto zako za alcoholism ni true. Kip it up. What I wld tel u iz that advice ma-youth much more about drug abuse pliz. Oliver from Dandora.

“Congrats wote kwa kupata cert za KCSE!! Hii ni step kubwa na I

hope mna-plan kitu mta-do next. Hata kama hauta-make kuenda cole, kuna ideas mob hapa

Shujaaz.FM zenye unaeza try uanze kujitegemea!”

Eunice MwangiBase: DandoraDream: Kuwa Bank Manager

Eunice example poa kwa mayuts wengine, coz hapendi story za traibo.

“Shujaaz imenifundisha vitu mob. Uki-scream kama kuna shida, ni neighbour wako ndio atakuja kuku-saidia. Sio necessarily mtu wa tribe yako.”

Asanteni kwa tips zenu wasee. Nitaangalia

story ya drug abuse vipoa hivi karibuni.

Hi DJ B! Hiyo risto ya new variety sweet potato vines imeni-jaz sana nimei-try na nina sale vine moja 5bob. Dooh nilipata nimenunua mbegu za kales. Kudos

NEW SWEET POTATO VARIETY

IMPORTANCE YA KUWA

KWA YOUTH GROUP

KUKAUSHA MA-FRUITS

SHUJAAOF THE MONTH

NOMA YAALCOHOLISM

facebook 3008sms

17

18

Laana ilioje?!

Walalala!

Si yule ni Tina?! Woshe pole,

nini ime-happen?

Rubo amenipiga!

Ni kama Rubo ameumia,

tumpeleke hosi.

Asante Afande. Tujaribu

kuongeza security hapa…

Eeeeesh! Ondokeni

hapa!

uuuuwi!!

uuuuuww w wiii ! !uuuuuww w wiii ! !

19

CLINIC

Manze karibu bizna yangu i-die, juu ya

hizi risto za gej!

Pombe ina dangers nyingi sana, lakini watu hawajui.

Kulewalewa inaweza kukupa risks kadhaa na HIV.

Usi-suffer peke yako.

Unaweza kupata usaidizi.

Rubo alikuwanga mpoa, lakini gej inam-spoil!

20

Asante sana. Naskia ubao, unaweza

ni-save na finje…?

leta keg ingine!

Karibuni chai. Naona gej

inaturudisha nyuma sana.

We wacha! Si nimezika kijana yangu juzi tu!

Alitafuta kazi sana after Form 4,

mwishowe alichoka na akamalizwa na ulevi.

Na-like Rubo sana, lakini pombe zake

hum-show anipige! Sasa hata kiosk

yake anashindwa ku-manage.

Bwana yangu amefukuzwa kazi juu ya ulevi. Nyumbani

hakuna chakula, watoto hawaendi shule!

Keshoye…

21

Cheki JK ana-come na Chief.

Nimeitwa na huyu kijana kwa sababu,

nimesikia complaints mengi juu ya pombe

hapa mtaani.

Ni vizuri sasa tusimame tukatae hii

maneno. Tuite wanaume wetu kwa baraza ndio

tujadiliane zaidi. Ama mnaonaje?

22

Ulevi ukizidi unaweza kusababisha hasara nyingi sana: » Ku-fight ovyo ovyo, » Ku-lose relationship na family na mabeste, »Na kwa ma-stude, hopes za chuo zote zitaishia hapo pap!

Kama una-feel concerned kwa msee alcoholic, get help kwa AA [Alcoholics Anonymous] helpline: 0726 530137

Wacha ni SMS DJ B kwa 3008, nim-show vile pombe ime-mess wasee mtaani.

I believe excessive drinking, lyk Cruiz’s bro is as a result of an underlying issue lyk emotional problem flani. He is hiding behind alcohol. Pliz make him open up and deal with what he’s running away from. - Judith K.

My younger bro, i don’t know what 2 do. Akipata job, hui-lose

after 1 week. Weekends ye hulewa sana na ikifika Monday hajijui, Amefutwa

kazi mara mob! Then my neighbour, imagine ye alikuwa msee gej mbaya. He

died eti gej ilimchoma maini. atazikwa this week. Advice them pliz. - Cruiz B.

23

Discussion ya alcoholism imekuwa hot kwa Fan page ya DJ Boyie

Facebook. Cheki vile wasee wanadai:

eish, charlie! unangara

sunday-best tuesday?

kwani unaenda

wapi?

naenda kwa

funeral.

nyanya wa rosie ameaga

dunia...

24

N i !

Field ya ball ndio base yangu sanasana, lakini

budangu ni mkabila vinoma, I hope kuna siku ata-change….

25

26

27

nimewaacha. naweza

ku-respect maagizo yenyu.

poleni kwa kifo...

sawa.

ahem!

aaaah, mimi siwezi kuenda kabla nisikike!

watu wangu, najua mnataka kupata ujumbe wangu

wa leo!

election ziko around the

corner! ni lazima

tuungane...

hatuwezi kubali kunyanyaswa

hivi!

serikali imetusahau! mkinipa kura

zenyu, nitawa-

represent vipoa...

nitaleta development

funds hapa hata sisi tuji-enjoy

kidogo...

28

kuna nyoka

nguoni! mmenirogaaaa!!!!

dere, tuhepe! Hawa

watu ni wachawi!

Viongozi wengine hawana tabia!

Leo, ni siku yetu ya kuomboleza, sio mahali pa

campaign! Tukatae haya mambo

kabisa!

ndio!

kuna nyoka

nguoni! mmenirogaaaa!!!!

dere, tuhepe! Hawa

watu ni wachawi!

Viongozi wengine hawana tabia!

Leo, ni siku yetu ya kuomboleza, sio mahali pa

campaign! Tukatae haya mambo

kabisa!

ndio!

29

MPS NA

MASOURC

E

WENGINE

WANAHAK

I YA

KUONGE

A:

• Kwa mikutano yenye wame-organise

wenyewe.

• Kama amekuwa invited kuongea.

• Kwa rally na mikutano ya chama yake.

Mnaonaje hii noma? Ni poa ku-use

functions kama harusi, mazishi ama

family meeting kwa campaign? Tu-

debate hii noma kwa Facebook [DJ

Boyie Fanpage], sms views zako kwa

3008!

wacha ni sms dj b kwa 3008 nimwambie hii risto. leaders lazima wajifunze

kuheshimu wananchi.

naomi kariuki

i

joni

joni

silas wabwile

ARTKONAartkona

Asanteni sana kwa wale wote walinitumia artwork.

Mko Juu tu sana! Wote nawapatia T-sho

30

polsa tsuma

nancy chela

polsa tsuma

nancy chela

nan

brian nyawade

31