16
1 TANZANIA PORTS AUTHORITY www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 22 9 - 15 Septemba, 2013 Wizara ya Uchukuzi yaibuka kidedea maonyesho ya Nane Nane Uk. 4 Kamilisheni miradi kwa waka - Mtutura Uk.6 Jiepushe na magonjwa ya figo Uk.11 Inaendelea Uk. 2 Na Janeth Ruzangi W afanyakazi wametakiwa kuhakikisha vigezo vilivyowekwa katika mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) vinatekelezwa ipasavyo ili kupata mabadiliko yanayokusudiwa katika sekta ya uchukuzi kwa lengo la kuinua uchumi wa Taifa. Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe amesema malengo yaliyoainishwa katika mpango huo yamefanyiwa utafiti wa kina na kwamba yanatekelezeka hivyo kumtaka kila mfanyakazi katika nafasi yake kuhakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo bila visingizio na kuonya kwamba mfanyakazi atakayeshindwa kwenda kwa kasi iliyopo atakuwa amejiondoa mwenyewe katika nafasi yake. Dk. Mwakyembe amesema yeye kama Waziri amewekeana saini na Mheshimiwa Rais kutimiza malengo yake yote katika mpango huo wa Mabadiliko Makubwa Sasa na hivyo kutaka utaratibu huo uendelee mpaka kwa mfanyakazi wa ngazi ya chini kabisa katika sekta ya uchukuzi. Waziri aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja iliyohusu Matokeo Makubwa Sasa ‘Big Results Now’ kwa ajili ya Maafisa wa Wizara, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wadau wa Sekta ya Uchukuzi. Wasioweza kasi ya mabadiliko wajiengue – Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe. Alisema malengo katika mpango huo kwa sekta ya Bandari ni kuona njia ya kati (Central Corridor) inafunguka na Bandari ya Dar es Salaam imewekewa lengo la kuhudumia tani milioni 18 mpaka ifikapo mwaka 2015 kutoka tani

Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es … · 2014. 11. 12. · kifungu cha 9 (2) na (b) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kuwa zipo kada fulani za watumishi wa umma ambazo haki

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • 1

    TANZANIA PORTS AUTHORITY

    www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 22 9 - 15 Septemba, 2013

    Wizara ya Uchukuzi yaibuka kidedea maonyesho ya Nane Nane

    Uk. 4 Kamilisheni miradikwa wakati - Mtutura

    Uk.6 Jiepushe na magonjwa ya figo

    Uk.11

    Inaendelea Uk. 2

    Na Janeth Ruzangi

    Wafanyakazi wametakiwa kuhakikisha vigezo vilivyowekwa katika mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) vinatekelezwa ipasavyo ili kupata mabadiliko yanayokusudiwa katika sekta ya uchukuzi kwa lengo la kuinua uchumi wa Taifa.

    Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe amesema malengo yaliyoainishwa katika mpango huo yamefanyiwa utafiti wa kina na kwamba yanatekelezeka hivyo kumtaka kila mfanyakazi katika nafasi yake kuhakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo bila visingizio na kuonya kwamba mfanyakazi atakayeshindwa kwenda kwa kasi iliyopo atakuwa amejiondoa mwenyewe katika nafasi yake.

    Dk. Mwakyembe amesema yeye kama Waziri amewekeana saini na Mheshimiwa Rais kutimiza malengo yake yote katika mpango huo wa Mabadiliko Makubwa Sasa na hivyo kutaka utaratibu huo uendelee mpaka kwa mfanyakazi wa ngazi ya chini kabisa katika sekta ya uchukuzi.

    Waziri aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja iliyohusu Matokeo Makubwa Sasa ‘Big Results Now’ kwa ajili ya Maafisa wa Wizara, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wadau wa Sekta ya Uchukuzi.

    Wasioweza kasi ya mabadiliko wajiengue

    – Mwakyembe

    Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.

    Alisema malengo katika mpango huo kwa sekta ya Bandari ni kuona njia ya kati (Central Corridor) inafunguka na Bandari ya Dar es Salaam imewekewa lengo la kuhudumia tani milioni 18 mpaka ifikapo mwaka 2015 kutoka tani

  • 2

    milioni 12.5 za sasa wakati reli ya Kati inatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi na kuhakikisha inaongeza kiwango cha mzigo unaobebwa sasa hivi kutoka tani 200,000 kwa mwaka na kufikia tani milioni 3 ifikapo 2015.

    Waziri wa Uchukuzi alionya juu ya tabia ya kufanya kazi kwa mazoea (business as usual) na kuwataka wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi kubadilika na kushirikiana ili kuleta mageuzi katika sekta hiyo

    ambayo alisema endapo hapatakuwa na mshikamano katika kazi dhamira ya kuwa na Mabadiliko Makubwa Sasa haitaweza kutekelezeka.

    Wakati huohuo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Prof. Joseph Msambichaka amemhakikishia Waziri kwamba, Bodi, Menejimenti pamoja na Wafanyakazi watahakikisha kwamba mpango huo unatekelezwa kama ulivyopangwa na kuongeza kwamba kama vile alivyojiwekea yeye Waziri

    malengo mbele ya Mheshimiwa Rais vivyo hivyo malengo hayo yatawekwa kuanzia ngazi ya Bodi hadi mfanyakazi wa chini ili kuhakikisha mabadiliko yanatokea.

    Semina hiyo ya siku moja, ambayo ilikuwa na lengo la kuwapa uelewa washiriki hao juu ya Mpango huo wa Serikali, iliandaliwa na Wizara kwa kushirikiana na Kampuni ya Trade Mark East Africa ambayo inajihusisha na kusaidia maendeleo ya uchukuzi na usafirishaji katika nchi mbalimbali za Afrika.

    BRN/Waraka

    Inatoka Uk. 1

    Maafisa Waandamizi wasijihusishe na uongozi

    wa vyama vya wafanyakaziNa Focus Mauki

    Imebainika kwamba wapo Viongozi au Watumishi Waandamizi katika Utumishi wa Umma ambao wamekuwa wakijihusisha na uongozi katika Vyama vya Wafanyakazi ambapo wanafanya hivyo ama kwa kutofahamu wajibu wao kama Viongozi au kwa kutofahamu vizuri Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.Angalizo limetolewa kukumbusha wafanyakazi kuzingatia waraka namba 2 wa mwaka 2013 ambao umetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Balozi Ombeni Sefue.

    Waraka huo unabainisha masharti ya wafanyakazi kujiunga na chama cha wafanyakazi ambapo unanukuu kifungu cha 9 (2) na (b) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kuwa zipo kada fulani za watumishi wa umma ambazo haki na uhuru wa jumla

    wa kujiunga na Chama cha Wafanyakazi umezuiliwa.

    Waraka huo umeendelea kufafanua kwamba miongoni mwa watumishi ambao haki na uhuru huo umewekewa mipaka ni watumishi waandamizi walio katika ngazi ya uongozi wa taasisi husika ‘Senior Management Employees.’

    Kwa mujibu wa kifungu cha 9(2)(c) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kinaeleza kuwa “Mwajiriwa wa ngazi ya juu ya uongozi hatakiwi kuwa katika Chama cha Wafanyakazi Katibu Mkuu Kiongozi

    Balozi Ombeni Sefue

  • 3

    ambacho kinawakilisha Wafanyakazi wasio katika ngazi ya waandamizi.”

    Kifungu cha 9 (6) (b) kinafafanua zaidi kwamba mwajiriwa wa ngazi ya juu ya uongozi ni mwajiriwa ambaye kutokana na cheo chake anatengeneza sera kwa niaba ya mwajiri na amepewa mamlaka ya kufanya makubaliano ya pamoja kwa niaba ya mwajiri na kwamba haiwezekani kiongozi

    mwenye mamlaka ya nidhamu mahali pa kazi awe ni kiongozi wa chama cha wafanyakazi.

    Kwa mujibu wa waraka huo ni kwamba kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa waraka huo wa Aprili 1, 2013 watumishi wa umma wenye nafasi za juu za uongozi katika maeneo mbalimbali ya kazi na wakati huohuo wanashika nafasi za uongozi katika vyama vya wafanyakazi wanapaswa

    kuachia nafasi mojawapo.

    Waraka huo umefafanua kwamba wale watakaopenda kuendelea na nafasi za uongozi wa vyama vya wafanyakazi itabidi waachie ngazi za uongozi wa juu katika utumishi wa umma na kwamba haitaruhusiwa mwajiriwa mwenye ngazi ya juu ya uongozi wakati huohuo kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi.

    Mafunzo/Waraka

    Dk. Mwakyembe: Wapatieni Wafanyakazi mafunzo

    ya mizigo hatarishiNa Levina Msia

    Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ameziasa Taasisi zinazoshughulikia Sekta ya Uchukuzi kuwapatia mafunzo ya kuhudumia mizigo hatarishi wafanyakazi wake.Waziri ametoa wito huo wakati wa hafla ya kukabidhi idhibati ya mafunzo ya kuhudumia shehena hatarishi kwa uongozi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) iliyofanyika chuoni hapo hivi karibuni.

    Ili kuhakikisha chuo hicho kinatoa mchango katika Sekta ya Uchukuzi na kufikia malengo yake, Dk. Mwakyembe amesema Serikali kupitia Wizara yake itakisaidia chuo hicho kifedha.

    “Nimefarijika sana na mabadiliko makubwa yanayofanywa na chuo hiki, naahidi kuwa Wizara itakisaidia chuo hiki kifedha kutokana na umuhimu wake katika Sekta ya usafirishaji hususani

    Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akikabidhi Ithibati ya kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo hatarishi kwa Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT), Bw. Juma Fimbo wakati wa sherehe maalum za kukabidhi ithibati hiyo ziliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Dk. Zacharia Mganilwa(wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo cha NIT, Bi. Priscilla J. Chilipweli (wa pili kushoto).Inaendelea Uk. 4

  • 4

    kinaandaa mitaala ili kutoa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko,” amefafanua zaidi Dk. Nganilwa.

    Waziri alikabidhi Idhibati ya mafunzo ya kuhudumia shehena hatarishi katika sekta ya anga kwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la NIT Mhandisi Priscilla Chilipweri na kutunuku vyeti kwa wahitimu watatu wa Shirika la Posta kati ya wanafunzi 15 wa kwanza kuhudhuria mafunzo hayo.

    mafunzo hayo ni sehemu ya Mpango Mkakati wa chuo kuboresha Sekta ya Uchukuzi.

    Dk. Nganilwa alisema kuwa Sekta inakabiliwa na upungufu wa raslimali watu hususani katika sekta ya anga ambapo lengo la chuo hicho ni kuzalisha wataalamu wazalendo kama marubani, wahandisi na wafanyakazi wa kuhudumia mizigo hatarishi.

    “Kutokana na mahitaji makubwa ya wataalamu katika sekta ya uchukuzi, chuo

    Sekta ya anga inayokabiliwa na changamoto nyingi,” amesema Dk. Mwakyembe na kuongeza kuwa, “pia naamini kuanzishwa kwa mafunzo ya kuhudumia mizigo hatarishi katika sekta ya anga kutasaidia kuondokana na changamoto katika Sekta ya usafirishaji hususani madawa hatarishi kwa binadamu, wanyama, mimea na viumbe wa majini.”

    Awali Rekta ‘Rector’ wa NIT Dk. Zacharia Nganilwa alisema kuanzishwa kwa

    Wizara ya Uchukuzi yaibuka kidedea

    maonyesho ya Nane NaneNa Beatrice Jairo na Lydia Mallya

    Wizara ya Uchukuzi imeibuka mshindi katika kundi la Wizara Uchumi zinazotoa huduma na kujinyakulia Hati ya Ushindi katika maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni.Akifunga maonyesho hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Idd aliitangaza Wizara hiyo kuwa mshindi wa tatu na kujinyakulia Hati ya Ushindi katika kundi la Wizara za Sekta ya Uchumi , upande wa huduma.

    Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) zilishiriki maonyesho hayo ya mwaka huu yaliyokuwa na kaulimbiu isemayo, “Zalisha mazao ya Kilimo na Mifugo kwa kulenga mahitaji ya soko’’.

    Kutokana na TPA kuwa mdau muhimu katika kampeni ya kitaifa ya KILIMO KWANZA, ilishiriki maonyesho hayo ili kuelezea na kufafanua uwezo wake katika kuhudumia shehena mbalimbali za pembejeo zinazoingizwa nchini kwenda kwa wakulima, wavuvi na wafugaji.

    Inatoka Uk. 3

    Afisa Masoko Mkuu, Bi. Lidya Mallya (kulia) akifafanua jambo kwa wakazi wa Mji wa Dodoma waliotembelea Banda la TPA.

    Mafunzo/Nane Nane

  • 5

    Pembejeo zinazopita katika Bandari ni kama vile mbolea, zana za kilimo na uvuvi pamoja na madawa ya kuulia wadudu waharibifu. Bandari vile vile inahudumia shehena za vifaa vya kilimo kama vile matrekta, mitambo na mashine mbalimbali zinazotumika katika kilimo, na pia kusafirisha mazao kama vile zabibu, kahawa, chai, korosho, mkonge, pamba, karafuu na mazao ya misitu kwenda nchi za nje ambazo ni Asia, Amerika ya Kaskazini na Kusini, Ulaya na Australia.

    Watu mbalimbali wakiwemo viongozi, wakulima, wafanyabiashara na wanafunzi walipata fursa ya kutembelea banda la TPA ambapo walipata fursa ya kufahamu shughuli za Bandari na umuhimu wake kwa Taifa na nchi jirani inazozihudimia kama vile Zambia, Malawi, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na Sudan Kusini.

    Wageni waliotembelea Banda la TPA, walielezwa kuwa Mamlaka imejidhatiti kuwahudumia wakulima wafugaji na wafanyabiashara kupitia Bandari zake ili kuwaunganisha na soko la Kimataifa.

    Maonyesho ya wakulima maarufu kama Nane Nane hufanyika kila mwaka ifikapo Agosti 1 hadi 8 ambapo taasisi mbalimbali za Serikali vikundi mbalimbali vya wajasiriamali, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara hupata fursa ya kuzitangaza bidhaa na huduma wanazotoa katika jamii.

    Mwaka huu maonyesho yalifanyika katika viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma na kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopher Chiza ambaye aliwaasa walishiriki kutumia fursa hiyo kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu kilimo bora.

    Waziri amemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima nchini (TASO) kuangalia uwezekano wa kufuta au kupunguza viingilio vya wakulima au kutafuta namna ya kuwatambua, ili wapate fursa ya kushiriki kikamilifu maonyesho hayo kwani wakulima ndio walengwa wakuu wa Nanenane.

    Dhana ya kaulimbiu mwaka huu ni muendelezo wa Kampeni ya Kilimo Kwanza ikiwa na lengo la kuwafanya wakulima,wavuvi na wafugaji kuwa na njia bora zaidi za kilimo, uvuvi na ufugaji ili waweze kuwa na maisha bora zaidi.

    Afisa Masoko Mkuu, Bi. Lydia Mallya (kulia) na Afisa Mawasiliano Bi. Beatrice Jairo wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa cheti na kikombe cha ushindi.

    Nane Nane

  • 6

    Ziara

    Na Janeth Ruzangi

    Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Alhaj Mtutura Abdalah Mtutura amesema Kamati hiyo imeridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka katika kuboresha miundombinu ya Bandari zake na kuitaka Mamlaka kukamilisha miradi yake kwa wakati ili kuleta manufaa yaliyokusudiwa.Mtutura aliyasema hayo hivi karibuni Wilayani Kyela wakati wa kuhitimisha ziara ya Kamati hiyo kutembelea Bandari za Mamlaka ambapo

    walipata fursa ya kutembelea Bandari za Dar es Salaam, Bagamoyo, Tanga, Lindi, Musoma, Bukoba, Mwanza na Kyela.

    Katika ziara hiyo Kamati ilipata fursa ya kupokea taarifa za utendaji kazi katika Bandari hizo ambapo mbali na kupata ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali pia ilitoa maagizo na mapendekezo ya uboreshaji unaotakiwa kufanyika katika sehemu mbalimbali za kazi.

    Kamati hiyo pia ilipata fursa ya kutembelea maeneo yanayotegemewa kuanzishwa Bandari mpya za Mbegani, Mwambani, Rushungi na Mwigobelo na kutaka mipango ya ujenzi huo kufanyika katika muda uliopangwa ili kuhakikisha Bandari zinakuwa na uwezo wa kutoa huduma inayokusudiwa.

    Ziara ya Kamati ya Bunge

    Kamilisheni miradi kwa wakati - Mtutura

    Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu wakisikiliza maelezo juu ya Bandari ya Bagamoyo kutoka kwa mwakilishi wa Mamlaka (hayupo pichani).

  • 7

    Wafanyakazi watakiwa kuzingatia taratibu za usalama,

    afya na mazingira Bandarini

    Usalama

    Na Peter Millanzi

    Wafanyakazi, wateja na wote wanaoingia katika Bandari ya Dar es Salaam wametakiwa kuzingatia taratibu za usalama, afya na mazingira ya Bandari, kwani baadhi ya watu wamekuwa wanakiuka taratibu mbalimbali wanapokuwa ndani ya Bandari.

    Wito huo umetolewa na Afisa Mkuu Zimamoto na Usalama Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mazaba Ndege, alipokuwa anaongea na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni.

    Ndege ameainisha mambo mbalimbali ambayo ni kosa kwa mfanyakazi au mtumiaji mwingine wa Bandari kufanya anapokuwa Bandarini kuwa ni pamoja na kufanya kazi au kuingia katika maeneo ya Bandari bila kuvaa vifaa vya kinga (PPE) kama vile ‘reflector, helmet, boots, mask, overoll’.

    Mambo mengine ambayo Ndege ameyataja kuwa ni kosa ni pamoja na kuendesha gari au chombo chochote cha moto kwa mwendo kasi unaozidi kilomita 20 kwa saa, kuegesha magari au vyombo katika maeneo yasiyoruhusiwa, kuendesha gari au chombo cha moto bila kuwa na leseni husika, kuingiza Bandarini magari mabovu au machakavu, kujisaidia ovyo, kuoga katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuvuta sigara Bandarini.

    Ndege amesema ni kosa kuosha magari katika maeneo yasiyo rasmi, kutupa takataka

    ovyo, mfanyakazi kuingia kazini akiwa amelewa, kutupa takataka au mafuta baharini na mfanyakazi kuvaa ‘earphones’ anapokuwa Bandarini.

    “Mtu yeyote atakayefanya kosa lolote kati makosa aliyoyataja hapo juu atakuwa amekiuka kanuni na anaweza kuadhibiwa

    kwa mujibu wa Kanuni na Masharti ya Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari za mwaka 2012 au Kanuni za OSHE za mwaka 2010,” amefafanua Ndege.

    Kuhusu suala la usalama Bandarini Ndege anasema ni la kila mfanyakazi hivyo basi kila mtu anapaswa kuzingatia taratibu za usalama, afya na mazingira katika eneo lake la kazi bila shuruti ili kupunguza ajali na magonjwa yanayozuilika. Ndege amewataka wawakilishi wa OSHE kutoka kila idara kutoa elimu ya usalama, afya na mazingira katika sehemu zao za kazi.

    Picha kwa hisani ya mtandao

  • 8

    Ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu katika pichaBandari ya Bagamoyo

    Bandari ya Bukoba

    Bandari ya Musoma Bandari ya Mwambani

    Bandari ya Lindi

    Bandari ya Dar es Salaam

    Soma habari kamili ya ziara hii uk. 4.

  • 9

    Ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu katika pichaBandari ya Lindi

    Bandari ya Dar es Salaam

    Bandari ya Itungi - Kiwira

    Bandari ya Kemondo

    Bandari ya Kilwa Masoko - Rushungi

    Bandari ya Mwanza South - North

  • 10

    Afya

    Dr. Mwinyi: Wafanyakazi pimeni afya zenu mara kwa mara

    Na Peter Millanzi

    Mganga Mkuu Bandari ya Dar es Salaam, Dkt. Abdallah Mwinyi amewashauri wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam kupima afya zao mara kwa mara ili kupata fursa ya kuanza matibabu mapema pale wanapogundulika kuwa wana matatizo ya kiafya.

    Dkt. Mwinyi ametoa ushauri huo wakati akiwasilisha mada ya ugonjwa wa kisukari kwenye semina ya Baraza la Wafanyakazi iliyofanyika hivi karibuni. Mwinyi amewaasa wafanyakazi kuchukua taadhari mbalimbali kwenye vyakula na kufanya mazoezi mara kwa mara.

    Akielezea dalili za ugonjwa wa kisukari, Mwinyi amesema dalili za ugonjwa huu ni kusikia kiu mara kwa mara, kuchoka sana, kupungua uzito ilhali unakula, majeraha kutopona haraka, kutokuona vizuri na kushindwa kufanya tendo la ndoa.

    Watu walio katika hatari za kupata ugonjwa wa kisukari ni pamoja na mtu aliyezaliwa na mzazi mwenye kisukari, mtu yoyote hasa mwenye umri kuanzia miaka 40, mwenye uzito mkubwa ambaye hafanyi mazoezi na mwenye familia ya wanaoumwa kisukari.

    Aidha Dkt. Mwinyi ameyataja mambo ya kufanya kwa wagonjwa wa kisukari kuwa ni pamoja na kula mlo kamili, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kutumia dawa kwa kuzingatia ushauri wa daktari.

    Dkt. Mwinyi amewataka wagonjwa wenye kisukari kutunza miili yao vizuri ili wasipatwe na vidonda, kutunza vizuri miguu, kutunza vizuri macho yao na kinywa.

    Mganga Mkuu Bandari ya Dar es Salaam, Dkt. Abdallah Mwinyi.

    Wafanyakazi wa Mamlaka wakicheza mpira wa miguu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya zao. (Picha na Maktaba)

  • 11

    wa figo ni kubwa hasa kwa mtu wa kipato cha kawaida, ni vyema wafanyakazi na umma wakafahamu namna ya kujikinga na magonjwa yanayoweza kusababisha matatizo ya figo,” anafafanua Dkt. Mlay.

    Dkt. Mlay anasema ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu mara nyingi unasababisha magonjwa ya figo kwa asilimia sabini. Anafafanua kwamba, “Ikiwa tutadhibiti magonjwa haya mawili basi tutakuwa tumefanikiwa kuzuia uwezekano wa kuugua magonjwa ya figo kwa asilimia sabini.”

    Afya

    Jiepushe na magonjwa ya figo

    Na Focus Mauki

    Ukweli ni kwamba gharama za matibabu ya figo ni kubwa kuliko gharama za kutibu ugonjwa wa ukimwi. Hii inatokana na ukweli kwamba wakati mwingine kubadili figo lililoharibika inabidi kupata figo kutoka kwa mtu mwingine.Katika hali ya kawaida kumpata mtu wa kuchangia figo sio kazi rahisi kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu katika jamii hata ndugu wa karibu wanahofu ya kuchangia figo kwa mgonjwa.

    Jambo jingine linaloleta changamoto ya kubadili figo ni kwamba ni lazima figo la mchangiaji lifanane na figo la mgonjwa, hata kama utapata mchangiaji bado unaweza kukumbana na changamoto hii.

    Lakini si hivyo tu endapo Madaktari watafanikiwa kubadili figo la mgonjwa lililoharibika bado itampasa mgonjwa kutumia dawa zinazogharimu takribani milioni moja au saba kwa mwezi katika kipindi cha maisha yake yote.

    Ili kupata ukweli na kufahamu kinga ya kuzuia magonjwa yanayoweza kusababisha figo kuharibika na kushindwa kufanya kazi nimefanya mahojiano na Mganga Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Dkt. Mkunde Mlay ambaye anaanza kwa kusema, “gharama za kumtibu mgonjwa

    Kazi ya figoKabla ya kuendelea kuelezea zaidi kuhusu ugonjwa huu wa figo, Dkt. Mlay anaanza kwa kuelezea kazi ya figo ambapo anasema, katika mwili wa binadamu figo zipo sehemu ya chini ya tumbo juu kidogo ya kiuno upande wa nyuma karibu na mgongo. Kazi kubwa ya figo ni kuchuja uchafu na sumu mbalimbali katika mwili. Kiungo hiki pia kina kazi ya kudhibiti sukari, chumvi na madini mbalimbali mwilini ikiwa ni pamoja na kurekebisha au kuimarisha mzunguko wa damu katika mwili.

    Hayo yote yasipofanyika mwili wa binadamu utakumbana na matatizo mbalimbali ambayo sasa yatakuwa yamesababishwa na figo kushindwa kufanya. Namuuliza Dkt. Mlay ni zipi dalili za figo kushindwa kufanya kazi ambapo anajibu kuwa baadhi ya dalili za figo kushindwa kufanya kazi ni pamoja na maji kujaa mwilini, mwili kuvimba, kutapika, kupata uchovu na kushindwa kupumua vizuri.

    • Gharama za tiba ni kubwa kuliko HIV• Kujikinga epuka sukari na shinikizo la damu

    Inaendelea Uk. 12

    Mganga Mkuu wa Mamlaka,Dkt. Mkunde Mlay.

  • 12

    Pamoja na uzito wa kazi ya figo katika mwili wa binadamu na hatari zake za kushindwa kufanya kazi vizuri, habari njema ni kwamba mwili wa binadamu unahitaji moja ya nne au asilimilia 25 tu ya figo zake mbili kufanya kazi.

    Jambo hili linadhihirishwa na ukweli wa kitabibu kuwa binadamu anaweza kuishi vizuri hata kama atakuwa ana figo moja pekee. Lakini pamoja na habari hii njema bado inatupasa kubadili aina ya maisha yetu kwa kujijali na kujitunza ili kuepukana na magonja nyemelezi yanayoweza kuharibu figo zetu.

    Bado jamii inachukulia kwa wepesi matatizo yanayoweza kusababishwa na magonjwa ya figo ambapo takwimu zinaonesha yanaendelea kushika kasi ulimwenguni hasa kutokana na kukukua kwa kasi kwa magonjwa nyemelezi yanayosababisha ugonjwa huu ambayo ni kisukari na shinikizo la damu.

    Takwimu za Taasisi ya Figo Tanzania zinaonesha kwamba kati ya wagonjwa 1,000 wanaohudhuria hospitali kwa ajili ya matibabu mbalimbali, asilimia 3 hadi 9 wanasumbuliwa na magonjwa ya figo.

    Kutokana na kukua kwa matatizo ya figo, Dunia imeamua kuadhimisha siku ya Figo mwezi Machi kila mwaka kwa lengo la kuelimisha umma juu ya tatizo hili.

    Lengo la makala hii ya afya sio kueleza kazi ya figo pekee bali pia kufahamu namna ya kutunza figo zako. Dkt. Mlay anasema figo linapopoteza uwezo wake wa kutenda kazi, kusanyiko na limbikizo la maji, uchafu na sumu hutokea mwilini mwa

    mgonjwa, kushindwa kufanya kazi kwa figo husababisha pia kutokea kwa maradhi mengine kama vile upungufu wa damu mwilini (anemia), shinikizo la damu (hypertension), ongezeko la tindikali kwenye damu (acidosis), ongezeko la lehemu na mafuta kwenye damu, na magonjwa ya mifupa.

    Sababu za Ugonjwa wa figoKwa mujibu wa Dkt. Mlay, zipo sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha ugonjwa wa figo lakini zipo sababu kubwa mbili. “Ugonjwa wa figo hutokana na vyanzo mbalimbali vya magonjwa ambayo yanapelekea kuharibika kwa figo lenyewe, sababu kubwa mbili ni pamoja na kisukari na shinikizo la damu,” anasema Dkt. Mlay.

    “Hapa naomba nisisitize kwamba magonjwa haya mawili ambayo yanazuilika yanaweza kuwa ni sababu kubwa ya mtu kuugua ugonjwa wa figo, kama tulivyosema katika makala iliyopita kwamba mtu akila, kunywa kwa afya na kufanya mazoezi anaweza kuepuka sukari na shinikizo la damu na wakati huo huo ataepuka magonjwa ya figo,” anasema Dkt. Mlay.

    Kauli hii ya Dkt. Mlay inabainisha kwamba sukari na shinikizo la damu ndio sababu kubwa za magonjwa ya figo, hivyo basi endapo mfanyakazi atabadili ulaji na unywaji wake na kuzingatia mazoezi atakuwa na fursa nzuri ya kudhibiti uwezekano wa figo kushindwa kufanya kazi.

    Sababu nyingine za ugonjwa wa figo ni pamoja na maambukizi ya bakteria ambao husababisha madhara na kuathiri mfumo wa uchujaji uchafu katika figo. Bahati mbaya ni kwamba

    matatizo ya figo pia yanaweza kusababishwa kwa njia ya kurithi.

    Kwa mujibu wa Dkt. Mlay matumizi ya kila siku au ya muda mrefu ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu pia yanaweza kusababisha ugonjwa wa figo. Magonjwa kama vijiwe figo (kidney stones), kuvimba kwa tezi dume (BPH), kuziba kwa njia ya mkojo (urethra stricture) pamoja na saratani, vyote vinaweza pia kusababisha madhara katika figo.

    Vyanzo vingine vya ugonjwa sugu wa figo ni pamoja na maambukizi ya VVU, ugonjwa wa ‘sickle cell’, matumizi ya dawa za kulevya, maambukizi sugu katika figo pamoja na saratani za figo.

    Kinga ni bora kuliko tibaSiku zote kinga ni bora kuliko tiba, kutokana na uhalisia huu Kitengo cha Tiba cha Mamlaka kimeona ni vyema kikaelimisha wafanyakazi wake kupitia gazeti hili ili kudhibiti magonjwa ya figo. Lazima watu wabadili namna ya maisha kwa kula mlo uliokamilika na kupunguza ulaji wa vyakula vya mafuta na vyenye sukari nyingi.

    “Lazima watu wapunguze ulaji wa vyakula vya mafuta na vinywaji vyenye sukari nyingi mfano unywaji wa soda ambayo haina faida yoyote katika mwili wa binadamu, kupunguza ulaji wa vyakula na vinywaji vya namna hii utaepuka unene wa kupindukia unaoweza kukuletea madhara ya sukari au shinikizo la damu linaloweza kusababisha magonjwa ya figo,” anafafanua Dkt. Mlay.

    Kuna njia mbili za kupata ugonjwa wa kisukari ukiachilia mbali sababu ya ulaji wa vyakula

    Afya

    Inatoka Uk. 7

  • 13

    vyenye mafuta na sukari nyingi, njia nyingine inayowamaliza watu taratibu ni ile ya mfumo wetu wa maisha tunayoishi ‘life style.’ Endapo tutakula vizuri hasa vyakula vya mbogamboga ambavyo havina mafuta mengi na kufanya mazoezi tutaepuka magonjwa ya figo.

    “Ufanyaji wa mazoezi niliuzungumzia katika toleo lililopita naomba nikumbushe tena kwamba zipo faida kama saba ambazo mtu atazipata kwa kufanya mazoezi ambayo kwa siku unapaswa kufanya mazoezi kwa dakika thelathini mpaka arobaini na tano,” anasema Dkt. Mlay.

    Faida mojawapo ya mazoezi ni kwamba ukifanya mazoezi unapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, kutokana na ukweli kwamba

    mazoezi yanaimarisha misuli ya moyo na kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu na rihemu ‘cholesterols’ kubwa katika mwili na pia kudhibiti shinikizo la damu.

    Lakini pia kubwa zaidi mazoezi yanasaidia kwa mtu kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi ambapo tafiti zilizofanyika zinaonesha kwamba watu wanaofanya mazoezi wanapunguza kwa asilimia thelathini uwezekano wa kuugua kiharusi.

    Ukiwa na unene wa kupindukia ‘obesity’ unakuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya figo na tiba pekee na salama ni kwa mtu kufanya mazoezi na kuzingatia ulaji wa vyakula visivyo na mafuta na sukari nyingi.

    Dkt. Mlay anakumbusha kwamba ni vyema wagonjwa wa sukari au shinikizo la damu kuendelea na dawa bila kuacha kwani mgonjwa atakapoacha ataongeza uwezekano wa kupata matatizo katika figo zake, hivyo ni vyema kwa wagonjwa wa aina hii kuzingatia matumizi ya dawa wanazopewa katika maisha yao yote.

    Mamlaka sasa hivi ina kituo cha afya cha kufanyia upimaji wa shinikizo la damu na sukari na kama mfanyakazi atakuwa nayo atapewa ushauri nasaha au kuanzishia dawa mapema. Mamlaka pia inawafatilia wagonjwa wa sukari na shinikizo la damu ili kuwasadia kudhibiti uwezekano wa kuugua magonjwa yanayoweza kusababishwa na figo kushindwa kufanya kazi.

    Afya/Tangazo

    Namba za Dawatila Huduma

    Ext: 1002530 Makao Makuu 1002550 Bandari Dar es SalaamHotline: 0222137286Mobile: 0713 720006Email: [email protected]

    Kaimu Mkurugenzi wa UtumishiBw. Peter Gawile

    inafanya kazi siku saba (7) za wiki na saa ishirini na nne kila siku, hivyo basi mfanyakazi yoyote atakayepangwa kufanya kazi siku hiyo atalazimika kufika na kufanya kazi na atafidiwa ipasavyo.

    Na Mwandishi Wetu

    Kifungu cha 4 (c) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 pamoja na makubaliano yaliyofikiwa katika Kikao cha 27 cha CJIC kilichokaa tarehe 31 Mei, 2013 katika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Livingstone, yamebainisha kwamba siku ya Jumapili ni siku za mapumziko hivyo basi mfanyakazi atakayepangwa na kuidhinishwa kufanya kazi siku ya Jumapili atastahili kufidiwa kwa kiwango cha mara mbili ya stahili ya malipo ya mashahara wake wa saa moja.

    Hata hivyo Uongozi umetoa angalizo kwamba, Mamlaka

    Watakaofanya kazi siku yaJumapili kufidiwa mara mbili

    Una tatizo la Kompyuta yako au

    Mtandao?

  • 14

    Tangazo

    Usalama Kwanza!Ewe ndugu mfanyakazi wa Bandari:EPUKA AJALI, ZUIA MOTO, JIKINGE NA MAGONJWA.

    AJALI/MAGONJWA/MAJANGA HUSABABISHA:

    • VIFO

    • ULEMAVU WA KUDUMU/MAGONJWA KAMA KANSA,TB, N.K

    • MAUMIVU MAKALI MWILINI

    • TAIFA KUPOTEZA NGUVU KAZI

    • GHARAMA KUBWA ZA MATIBABU

    • KUPOTEA KWA KIPATO BAADA YA KUPOTEZA AJIRA

    • MAHANGAIKO KATIKA FAMILIA BAADA YA TEGEMEO LA FAMILIA KUUMIA/KUFARIKI

    • KUHARIBIKA KWA VITENDEA KAZI

    ZINGATIA YAFUATAYO:

    • TARATIBU ZA USALAMA KAZINI

    • PATA MAFUNZO/MAELEZO YA NAMNA YA KUENDESHA CHOMBO/MASHINE KABLA YA KUFANYA KAZI

    • VAA VIFAA VYA KINGA KWA USAHIHI MUDA WOTE UNAPOKUWA KAZINI (Reflector, Helmet, Boots, Mask, Overoll)

    • ENDESHA GARI/CHOMBO POLEPOLE (20KM/Hr.)

    • USIVUTE SIGARA

    • USICHAFUE MAZINGIRA

    • USIVAE EARPHONES UNAPOKUWA BANDARINI

    • INAPOTOKEA DHARURA TOA TAARIFA MARA MOJA ZIMAMOTO HALAFU NENDA KWENYE ENEO LA KUKUSANYIKIA (Emergency Assembly area)

    FANYA KAZI SALAMA URUDI NYUMBANI SALAMA KILA SIKU.

    USALAMA KWANZA/SAFETY FIRST.

    WAKATI WA DHARURA PIGA SIMU CHUMBA CHA HABARI

    +255 22-2116287, +255 755-195896, +255-658-195986 AU 1005955

    Imetolewa na Idara ya Zimamoto, Usalama na Uokoaji.

  • 15

    Tanzia

    Marehemu Rashidi Said

    Tangazo

    Na Mhariri

    Nenda kwa amani Kagera nyuma yako tupo, tunakuombea raha ya milele na upumzike kwa amani, tupo njia moja kwani tumeumbwa kwa mavumbi na mavumbini tutarudi.Ama kwa hakika TPA Gazeti imempoteza mmoja wa malenga mahiri ambaye Mwenyezi Mungu ameamua kumuita katika pumziko la milele.

    Pigo hili sio tu kwa Safu ya Malenga bali ni pigo na huzuni kubwa kwa Wafanyakazi wote wa Mamlaka kumpoteza mfanyakazi mwenye busara na upendo kwa wafanyakazi wenzake.

    Hakika taa imezimika ghafla lakini yote ni kwa kudra zake Mwenyezi Mungu mwenye Mamlaka ya kupanga tutaishi kwa muda gani juu ya uso wa Dunia hii.

    Kwa wanaomfahamu Kagera watakuambia alikuwa ni mtu mkimya anayezungumza kwa upole na umakini na asiyetaka makuu, gazeti hili litamkumbuka kwa mchango wake muhimu wa kuandika mashahiri yenye ujumbe mzito.

    Kagera hakuwa analizimishwa kuleta shahiri alikuwa anajituma anahakikisha limechapwa katika kompyuta na limefikia kwa mhariri kwa wakati. Kagera alifahamu kuwa kupitia sanaa hii ya mashahiri analo jukumu la kukumbusha utendaji kazi wetu ndani ya Mamlaka .

    Kwa upande mwingine mashahiri yake yameleta umoja

    na mshikamano katika kazi.

    Kabla mauti hayajamkumba Kagera alitimiza wajibu wake kwa kuandika shahiri lake la

    mwisho hapa duniani ambalo tumelichapa katika ukurusa wa mashahiri kama ilivyo ada.

    Pumzika kwa Amani. ‘RIP’

    Pumzika kwa Amani ‘Kagera’

  • 16

    TUNAOMBA DAKTARI (Shairi hili aliandika Marehemu Rashid Said ‘Kagera’ kabla ya mauti kumfika)

    Mhariri wa Bandari, nipokee muhisaniNaja na langu shairi, usiliweke kapuniKurasini lishhamiri, walisome gazetiniDaktari ni muhimu, kwenda naye Ngorongoro

    Ni ngiri amenishika, sehemu ya kiunoniDume zima napindika, chozi latoka machoniHuku kule nahangaika, kifo kiko mkononiDaktari ni muhimu, kwenda naye Ngorongoro

    Chala kanipa mizizi, nitafune mdomoniSikufanyia ajizi, nikaiweka kinywaniSikupata usingizi, niko macho kitandaniDaktari ni muhimu, kwenda naye Ngorongoro

    Dawa kanipa Umande, tiba yake ni “Waini”Kunywa kwake ni kwa mbinde, kurudia hutamaniNi chonde chonde Kipande, uone yangu maoniDaktari ni muhimu, kwenda naye Ngorongoro

    SALAMU KWENU MALENGAMhariri tafadhali, zangu salamu pokeaNijue na yako hali, ndiyo yetu mazoeaPole kwa nyingi shughuli, wengi twakutegemeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Nawatumia wa mbali, malenga walopoteaWale magwiji wakali, wa tungo walobobeaMteke ninawajali, japo mwanipotezeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Salamu kwa jitu kali, wendako unapoteaKutunga bado ungali, mdogo wachechemeaNi bora uwe dalali, njuruku kuongezeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Kyomile nakupa hali, hakika utapokeaSiko karibu ni mbali, roli ninalingojeaNyanya nazo pilipili, ndimu nitakubebeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Kinunda wa bomba mbili, ujumbe nakuleteaNaja kwako na kandili, kwa mwanga kuongeeaHaya mambo tujadili, malenga kuwateteaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Malenga wengi mahili, gazeti kulisemea Twahamasisha makuli, kwa kazi kutozembeaNi yetu mbiu kauli, uzembe kuukemeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Kikore uwe wakili, hili nakusogezeaNi yupi wa kuijali, fani tuwe kidedeaJapo iwe siku mbili, mikumi kutembeleaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Michezo yote Bandari, dokta yupo kundiniWafanyakazi hodari, dokta haonekani?Ombi langu ufikiri, Kipande kwa umakiniDaktari ni muhimu, kwenda naye Ngorongoro

    Mwenyekiti na katibu, utaratibu fanyeniNa mtimize wajibu, mukaseme vikaoniOmbi langu matibabu, tunapokuwa poriniDaktari ni muhimu, kwenda naye Ngorongoro

    Kagera namaliza, kalamu naweka chiniNimeshindwa kunyamaza, nikikumbuka mbuganiKweli mungu muweza, bado nipo dunianiDaktari ni muhimu, kwenda naye Ngorongoro

    Rashidi Said (Kagera) Hq(Kanogaikilo)

    Kagera mwana lugali, ni vipi unamezeaUko karibu na goli, kufunga unazembeaLau kama uko chali, machela takuleleaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Nawe mgosi wa mbuli, Nambole jata ekeaMwendo wako si mkali, magongo watembeleaTunazo tungo za hali, nyingi zinatuadodeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Hamsa nusu kamili, Alawi nakungojeaUkubwa kustamili, mengi yata kutokeaHalina mmoja hili, silo la kulichekeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Mkuu wa maadili, lukuni untegeaAcha wako ubahili, zako tunazingojeaKama mbaya yako hali, zangu nitakumegeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Makavu nakujadili, kutunga umecheleaUsilete uswahili, kwa tungo za kuhemeaRuhusa zangu nakili, nasema sitakuzomeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    Ewe mjumbe kivuli, Mbumo wachekeleaSije azan a sifuli, umri umesogeaHiyo karata kamali, usende kuichezeaMgosi nipo sijambo, salamu kwenu malenga

    USTAADHI TAIMURU S. MWALIKO (MGOSI MTEKE)ULINZI DSM – 0784 - 479460

    Malenga