74
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 111 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Sita – Tarehe 13 Novemba, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu. NDG. LINA KITOSI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Goodluck Asaph Mlinga, Mbunge wa Ulanga sasa aulize swali lake. Na. 71 Wananchi wa Kata ya Iragua kujenga Shule za Msingi MHE. GOODLUCK A. MLINGA aliuliza:- Wakazi wa Kata ya Iragua, Vijiji vya Mafinji, Mbenja, Mikochi na Kipingo wamejenga shule za msingi kwa nguvu zao wenyewe na zina muda mrefu sasa. Je, kwa nini Serikali imeweka vikwazo vya kuzisajili shule hizo?

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA KUMI NA TATU

Kikao cha Sita – Tarehe 13 Novemba, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu.

NDG. LINA KITOSI – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisiya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Goodluck Asaph Mlinga,Mbunge wa Ulanga sasa aulize swali lake.

Na. 71

Wananchi wa Kata ya Iragua kujenga Shule za Msingi

MHE. GOODLUCK A. MLINGA aliuliza:-

Wakazi wa Kata ya Iragua, Vijiji vya Mafinji, Mbenja,Mikochi na Kipingo wamejenga shule za msingi kwa nguvuzao wenyewe na zina muda mrefu sasa.

Je, kwa nini Serikali imeweka vikwazo vya kuzisajili shulehizo?

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, napenda kujibu swali laMheshimiwa Goodluck Asaph Mlinga, Mbunge wa Ulangakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Shule za Mafinji, Mbenja,Mikochini na Kipingo zilizotajwa na Mheshimiwa Mbunge nivituo vilivyoanzishwa chini ya Mpango wa Elimu ya Msingikwa Waliokosa (MEMKWA) ambavyo hutoa elimu kupitiaMpango wa Elimu Nje ya Mfumo Rasmi. Vituo hivyo,vilifanyiwa ukaguzi mwaka 2013 na Mdhibiti Ubora wa Shuleakisaidiwa na Mhandisi wa Wilaya na Afisa Ardhi wa Wilayaili kuona kama vituo hivyo vinaweza kukidhi vigezo vyakusajiliwa kuwa shule za msingi na kuanza kupokea wanafunzikatika mfumo rasmi wa elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vitu hivyo havikupata usajilikutokana na upungufu wa miundombinu inayohitajika ilikusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamojana uwepo wa chumba cha darala la elimu ya awali, vyumbavya darasa la kwanza hadi la saba, vyoo vya walimu, vyoovya wanafunzi (kwa wavulana uwiano wa tundu moja kwawanafunzi 25 na wasichana kwa uwiano wa tundu moja kwawanafunzi 20), eneo lisilopungua ekari saba na nusu kwa vijijinina ekari tatu na nusu kwa maeneo ya mijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile baadhi ya maeneovilipojengwa vituo hivyo yako ndani ya hifadhi chini ya PoriTengefu la Kilomero. Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Rais,TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo yaMakazi kupitia mradi wa KILORWEMP zimepanga kupitia upyampaka wa Pori Tengefu la Kilombero ili kubaini maeneoyatakayokidhi mahitaji ya kisheria kwa ajili ya maendeleo yawananchi ikiwemo ujenzi wa shule.

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

333

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, MheshimiwaGoodluck Mlinga swali la nyongeza.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA:- Asante MheshimiwaNaibu Spika, kwanza naomba nichuke nafasi hii kuipongezaWizara ya TAMISEMI kwa kupata timu mpya mchezaji mpya,Mwita Waitara Mwikabe. Naomba kuuliza swali langu lanyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi ninavyoongeatayari Wizara zimeshapitia mipaka na kubaini shule ya msingiMikochi ipo nje ya eneo oevu, na sasa hivi ninavyoongeashule ina madarasa manne, walimu wa tano na vyoomatundu saba na mimi Mbunge naenda kutia nguvu zangukufikisha madarasa yawe saba. Je, Serikali ipotayari kukaguatena shule hizi na kuzifanyia usajili? Hilo la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuna mpango waEP4R. Je, Serikali ipo tayari kusaidia shule hili kuboreshamiundombinu yake?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, Kwanza naomba kwa niaba ya Wizara yaTAMISEMI nipokee pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Mlinga,tunazipokea na tunaahidi tutashirikiana na yeye.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanzaanasema sasa hivi tayari imeshabainika eneo lile haliko katikaeneo oevu na hivyo kwa mujibu wa maelezo yake ni kwambaitakuwa inafaa kuanzisha shule ya msingi. Naomba kwanzani mhakikishie ni azma ya Serikali kuhakikisha kwambahuduma zinasogezwa jirani na Wananchi na kama ambavyoameahidi yeye mwenyewe naomba nimpongeze kwambana yeye ataweka nguvu zake ili kuhakikisha kwamba ile hajaya kuhakikisha kwamba yanakuwepo madarasa kuanziamadarasa mpaka la saba yanakamilika, hakika akikamilisha

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

kama sisi Serikali tutakuwa tayari kuhakikisha shule inasajiliwakwa sababu itakuwa imekidhi vigezo ambavyo awaliilisababisha isiweze kusajiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili,anaomba kwamba katika Mpango wa EP4R ni vizuri na waowakawa considered, naomba nimwambie MheshimiwaMbunge kwanza takwa la kwanza ni kuhakikisha shuleinasaji l iwa na shule hil i isaji l iwe lazima kwanza iweimekamilisha vyumba vya madarasa saba na ye ameahidikwamba ataakikisha kwamba ina kamilika, sasaikishakamilika itakuwa ni raisi sasa hata kuelekeza pesa zaEP4R kwa sababu tunapeleka sehemu ambayo tayari shuleimekwisha kusajiliwa.

NAIBU SPIKA: Niwakumbushe Waheshimiwamliosimama maswali yanahusu vikwazo vya usajili wa shule,ndiyo maswali ya nyongeza. Mheshimwa Cecilia Paresso.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, vikwazo hivyo vya usajilihaviko tu katika shule za msingi lakini yapo pia viporo katikavyumba vyetu madarasa katika sekondari zetu nchini,maabara, nyumba za walimu, zahanati zetu kwa maanaimetumiaka nguvu za wananchi lakini miradi hiyohaijakamilika, Serikali iko tayari sasa kufanya tathmini kwaupya kuziangalia na kuzikamilisha na zile ambazo zinakidhiusajili ziweze kupatiwa usajili?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, kwanza sio vizuri tukaita kwamba ni vikwazo kwasababu kimsingi kuna standard ambazo lazima zifikiwe ili usajiliwa shule uweze kufanyika. Naomba nimwambie Mheshimiwa

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

555

Paresso na Wabunge wengine ni azma ya Serikali kuhakikishakwamba changamoto zinatatuliwa ili huduma ya elimuziweze kuwafikia watoto wetu kupunguza umbali mrefu wakufuata elimu na hivi sasa hivi haitazidi mwezi Disemba, tayariSerikali imeshatenga bilioni 54 ambayo tunaenda kufanyaukarabati pamoja na ujenzi ikiwepo vyumba vya madarasa,kumalizia maabara, pamoja na vyoo. Ni azma ya Serikaliinaongozwa na CCM kuhakikisha kwamba itatatua kero zawananchi.

NAIBU SPIKA, Mheshimiwa Lubeleje swali kuhusuvikwazo vya usajili.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali moja lanyongeza.

Kwa kuwa walimu wanaishi katika mazingira magumusana, hawana nyumba tulikuwa na mradi wa MMEMhatukujenga nyumba za walimu tulijenga madarasa, sasaMheshimiwa Waziri Serikali ina mikakati gani ya kutenga fedhaza kutosha ili kuwajengea walimu wa shule za msingi nyumba?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu usajilimaana hapa umetaja vigezo kwamba madarasa yawemangapi na vitu kama hivyo. Lakini shule za msingi kwasababu zinaanza darasa la kwanza ama na zile za awali,nadhani wananchi wakishajenga madarasa kadhaawanayoweza kuanza nayo, ni vizuri Serikali iangalie walewananchi kama wanaweza kuendelea kujenga basi,wapewe kama ni usajili wa muda ili wakati unajitazamia.lakini awezi kujenga madarasa yote saba wakati wanafunziwatakaokuwepo ni wadarasa la kwanza. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Wizara yaFedha na Mipango, Mheshimiwa Zainab Mussa Bakar,Mbunge, wa Viti Maalum sasa aulize swali lake.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Na. 72

Asilimia ya Mapato kwenda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

MHE. ZAINAB MUSSA BAKAR aliuliza:-

Kwa mujibu wa Katiba kuna asilimia ya mapatoyanatakiwa yaende Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Je, utekelezaji wa suala hili umefikia wapi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha naMipango, majibu.

NAIBU WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha naMipango, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zainab MussaBakar, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 133 inazungumziauwepo wa Akaunti ya Fedha ya Pamoja kwa ajili ya miamalaya shughuli za Muungano. Chanzo cha mapato kwa ajili yashughuli za muungano, yatakayoingizwa kwenye Akaunti yaPamoja ni mchango kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.Aidha, Ibara ya 134 ya Katiba inatamka kwamba Tume yaPamoja ya Fedha itakuwa na jukumu la kupendekezautaratibu wa kuchangia na kugawana mapato yatokanayona shughuli za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa uendeshaji waAkaunti ya Pamoja ya Fedha umependekezwa kwenye Ripotiya Mapendekezo ya Vigezo vya Kugawana Mapato nakuchangia gharama za Muungano iliyoandaliwa na Tumeya Pamoja ya Fedha ya mwaka 2006. Hata hivyo, Akauntiya Pamoja ya Fedha haijafunguliwa na kuanza kufanya kazikwa kuwa majadiliano kati ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakuhusu mapendekezo ya Tume hayajakamilika.

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

777

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zainab Bakar swali lanyongeza.

MHE. ZAINAB MUSSA BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante na maswali mawili madogo ya nyongeza.

Kwa kuwa akaunti ya pamoja haijafunguliwa hadi leo,ni takribani ni miaka 34. Je, ni lini sasa hiyo akauntiitafunguliwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, majadilianotunaambiwa hayajakamilika ndiyo maana ikawa akauntihiyo haijafunguliwa, sasa nataka kujua je, Tanzania Bara naTanzania Zanzibar inachangia kiasi gani mpaka leomajadiliano hayo hayajakamilika?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha naMipango.

NAIBU WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa NaibuSpika, kuhusu swali lake la kwanza ni lini akaunti itafunguliwakama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwambamajadiliano yanaendelea kati ya Serikali mbili ya Mapinduziya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa hiyo,tutakapomaliza majadiliano na kukubaliana kamailivyoelekezwa na Katiba Ibara ya 34 lazima kuwe namakubaliano Akaunti ya Pamoja itafunguliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili nikiasi gani kinachangiwa; kwa mfumo uliopo sasa mapatoyate yanayotokana na shughuli za Muungano zinazofanyikaZanzibar huwa yanatakiwa kubaki Zanzibar na kutumika kwaajili ya shughuli za kiuchumi na maendeleo katika Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar na mapato yote yanayotokana nashughuli za Muungano ambazo zinafanyika Tanzania Barabasi nayo yote ni makubaliano na mfumo ambao uliopondiyo ambayo hutumika Tanzania Bara kwa shughuli zile zaMuungano.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Suleiman, swali lanyongeza.

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu haki yaZanzibar katika vyanzo vyote vya mapato vya Muungano niasilimia 4.6 ikiwemo misaada pamoja na mikopo, natakakujua ni mara ngapi ambapo Zanzibar imepata haki yakekamili ya asilimia 4.6?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha naMipango, majibu.

NAIBU WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza naomba afahamu ni asilimia 4.5 ndiyo ambayomgao ulivyo na ni mara zote na miaka yote Zanzibar imekuwamgao huu wa asilimia 4.5 wa yale mapato yanayotakiwakupelekwa Zanzibar ikiwa ni pamoja ni misaada na mikopokama alivyosema.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Mheshimiwa Janet Zebedayo Mbene, Mbungewa Ileje.

Na. 73

Hitaji la Kituo cha Ushuru wa Forodha na Ukaguzi – Ileje

MHE. JANET Z. MBENE aliuliza:-

Wilaya ya Ileje ipo mpakani mwa nchi za Zambia naMalawi na kuna biashara na mwingiliano mkubwa wa jamiikatika eneo hilo. Lakini hayo yote yanafanyika bila utaratibumzuri wakati mwingine kuhatarisha usalama kwa sababuhapana kituo cha ushuru wa forodha wala soko la kimataifa,hakuna kituo cha uhamiaji, hakuna kituo cha kudhibiti mazaona mifugo na pia hakuna kituo cha ukaguzi wa silaha.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

999

Je, ni lini Serikali itajenga miundombinu hiyo muhimukwa ufanisi na maendeleo ya Ileje?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha naMipango, majibu.

NAIBU WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba Waziri wa Fedhana Mipango napenda kujibu swali la Mheshimiwa JanetZebedayo Mbene, Mbunge wa Ileje kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambuachangamoto iliyopo ya mwingiliano wa kibiashara baina yawananchi wa Wilaya ya Ileje, Mkoani Songwe na wananchiwa nchi za Malawi na Zambia. Ili kukabiliana na changamotohiyo, Serikali imeanza mchakato wa kuanzisha Kituo chaForodha Isongole mpakani mwa Tanzania na Malawi.

Aidha, mchakato wa kufungua kituo kipya chaforodha unatakiwa kuzingatia Sheria ya Forodha ya Jumuiyaya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 ambayo inaitka nchimwanachama kuwasilisha kwenye Sekretarieti ya Jumuiyaya Afrika Mashariki maombi ya idhini ya kuanzisha kituo kipyacha forodha na hatimaye kutangazwa kwenye Gazeti laJumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Corporation LegalNotice) ili kupata nguvu ya kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bungelako tukufu kuwa Serikali imewasilisha maombi ya kufunguaKituo cha Forodha Isongole kwenye Sekretarieti ya Jumuiyaya Afrika Mashariki mwezi Julai, 2018. Pia eneo la kujengamiundombinu ya Ofisi ya Forodha Isongole limepatikana nataratibu za kupata hatimiliki zinaendelea. Aidha, ujenzi wamiundombinu utaaanza mara idhini ya kuanzisha kituo hichoitakapotolewa na kutangazwa kwenye Gazeti la Jumuiya yaAfrika Mashariki na hatimiliki ya eneo husika kupatikana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Janet Mbene swali lanyongeza.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana, kwanza kabla sijauliza swali la nyongezaniipongeze sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwasikivu, tumeomba hiki kituo muda mrefu lakini hatimayetunaona kinaenda kufanyiwa kazi. Nakushukuru sanaMheshimiwa Naibu Waziri nashukuru sana Serikali. (Makofi)

Naomba sasa niulizwe swali moja tu la nyongeza kuwaIsongole ni kata ambayo ni ya kibishara sana kutokana naposition yake katika mpaka huu na tumekuwa tukiombaSerikali itujengee soko la kimataifa pale kwa sababu hizohizoza kibiashara pamoja, siyo na Malawi na Zambia tu hata naDRC.

Je, Serikali ipo tayari sasa kutokana na maendeleoya barabara inayojengwa pale na hiki Kituo cha Forodhakinachokuja kujitokeza kutuwekea soko la kimataifa?Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha naMipango, majibu.

NAIBU WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa NaibuSpika, Serikali yetu ipo tayari kufanya shughuli za maendeleopopote pale ambapo wananchi wetu wanashughulika nashughuli za kiuchumi, naomba nimuahidi Mheshimiwa Janetkwamba sisi kama Serikali na hasa Wizara ya Fedha naMipango tutakwenda kufanya tathimini na tutakapojiridhishakwamba sasa tuko tayari kufanya hayo maendeleo hayoanayoyasema ya Kituo cha Kimataifa tupo tayari kamaSerikali kwenda kujenga lakini tuingiza kwenye mipango yetuya Serikali kama taratibu zinavyotuelekeza.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Victor KilasileMwambalaswa swali la nyongeza.

MHE. VICTOR K.MWAMBALASWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushuru sana nami kuongeza swali dogo la nyongezakama ifuatavyo:-

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111111

Serikali imefanya nzuri sana kwenye mpaka wa WilayaMomba mpaka wa Zambia na Tanzania kwa kulasimishamatumizi ya sarafu ya Zambia na ya Tanzania ili kukomeshamagendo na ulanguzi, Serikali inasemaje kuhusu mpaka katiya Malawi na Tanzania na Kituo cha Isongole na kufanyakazi kama hiyo hiyo? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimwia Naibu Waziri wa Fedha naMipango, majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nimepokea pongezi za kurasimisha sarafu palempakani na huku mpaka anaoutaja upande huu alioutajakama Serikali tunaenda kulifanyia kazi na naamini kamatuliweza kurasimisha upande mmoja tutaweza pia na upandeuliobaki.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Deo Ngalawa swali lanyongeza.

MHE. DEO F. NGALAWA: Mheshimwa Naibu Spika,ahsante sana, kama ilivyo Wilaya ya Ileje kuwa imepakanana nchi za Malawi na Zambia pia Wilaya ya Ludewaimepakana na nchi ya Malawi; na ikumbukwe Wilaya yaLudewa ni mzalishaji mkubwa sana wa mahindi penginekuliko hata maeneo maengine yoyote.

Je, ni lini sasa Serikali itaona kuna haja ya kuweka vituovya forodha katika vijiji vya Manda na Lupingu ili kurasimishana biashara zingine ziweze kwenda katika namna ambayoinafaa?

NAIBU SPIKA: Mheshimwia Naibu Waziri wa Fedha naMipango, majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Deo Ngalawaamekuwa akilifuatilia jambo hili sana na nimeshakaa nayemara kujadiliana kuhusu kujenga kituo hiki cha forodha katikavijiji vya Manda na Lupingu, na tayari tangu tulilvyo fanya

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

majadilianao Mheshimwa Ngalawa nilishawapa maelekezomamlaka ya mapato Tanzania waende wakafanye tathiminina sasa wako tayari kuingiza kwenye mipango yaokuhakikisha kituo hiki cha forodha kina jengwa kulinga nasheria za zinavyotuelekeza.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Mheshimiwa Neema William MgayaMbunge waviti Maalum sasa aulize swali lake.

Na. 74

Azimio Kuhusu Masuala ya Demokrasia, Chaguzi naUtawala Bora

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:-

Miaka sita iliyopita Serikali ya Tanzania ilishiriki nakupitisha Azimio kuhusu Masuala ya Demokrasia, Chaguzi naUtawala Bora lililopitishwa na Umoja wa Afrika.

(a) Je, Serikali inaweza kueleza ni kwa nini hadi sasaAzimio hilo halijaridhiwa na kusainiwa rasmi?

(b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Azimiohilo linaridhiwa na kusainiwa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI alijibu:-

Mheshimwa Naibu Spika, awali ya yote nichukue fursahii kumshukuru Mheshimwa Dkt. John Joseph Pombe Magufulikwa kuniteua kuwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya NjeUshirikiano wa Kimataifa ili niweze kumsaidia Mheshimiwa Dkt.Balozi Augustine Philip Maiga. (Makofi)

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131313

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako na kwanaiba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki - Dkt. Balozi Augustine Philip Maiga ambaye yupondani hapa Bungeni leo hii, napenda kujibu swali laMheshimwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalumlenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkataba wa Afrika kuhusuDemokrasia. Chaguzi na Utawala Bora yaani African Charteron Democracy, Elections and Governance ulipotishwa naUmoja wa Afrika wakati wa Mkutano wa Wakuu wananchina Serikali wa Umoja wa Afrika tarehe 30 Januari, 2007. Lengola mkataba huu ni kuzitaka nchi wanachama kuzingatia nakutekeleza utawala bora, utawala wa sheria na haki zabindamu kama ilivyoelezwa katika ibara ya 3 na 4 yamkataba huo. Hadi hivi sasa ni jumla ya nchi wanachama 35tu ndizo zimeridhia mkataba huo ilihali nchi 19 badohazijaridha ikiwemo Tanzania.

Mheshimwa Naibu Spika, naomba kulieleza Bungelako tukufu kuwa sababu zinazoifanya Tanzania isitie auichelewe kuweka saini na kuridhia mkataba huo ni kutokanana kuwepo ibara ambazo zipo kinyume na Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania pamoja na sheria zetu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Neema Mgaya swali lanyongeza.

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza maswaliya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikari itafanyamabadiliko ya mkataba ili uweze kuendana na Katiba yanchi yetu? Swali la kwanza hilo.

Swali la pili nilitaka kujua kwa kutosaini mkataba huuvipi kuhusu usimamizi wa masuala ya uchaguzi, demokrasiyanakwendaje? Nashukuru.

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimwa Naibu Spika, ahsante sanaawali ya yote Neema Mgaya kwa swali lake zuri na lenyetija.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuridhia mikatabambalimbali ya kimataifa, nchi inaangalia vigezo vingimbalimbali ikiwepo ukinzani wa mikataba hiyo na sheria zetuza ndani, Katiba pamoja na tamaduni nyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kama zilivyokuwanchi zingine 19 tunafanya mchakato wa ndani wa kuangaliani kwa jinsi gani tunaweza tukarekebisha ama sheria zetu zandani ama kurudi kwenye AU na kuomba vifungu kadhaakwenye mkataba huo virekebishwa ili viendane na sheria naKatiba yetu na hilo likikamilika kama ambavyo tumeridhamikataba mingine mbalimbali na mkataba huu piautaridhiwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Abdallah Mtolea swali lanyongeza.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, majibu ya Serikali yanasemavipo baadhi ya vipengele haviendi sawa na Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio maana Serikaliinachele kuridhia mkataba huu, na mkataba huu unahusudemokrasia, changuzi...

NAIBU SPIKA: Uliza swali Mheshimiwa, uliza swali.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: ...kwa majibu haya sasaSerikali inakiri kwamba namna ambavyo tunaendeshademokrasia, chaguzi na utawala bora hapa nchini ni kinyumena mataifa mengine ya Afrika? (Makofi)

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151515

NAIBU SPIKA: Mheshimwa Naibu Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimwa Naibu Spika, ahsante,masuala ya uchaguzi, demokrasia na utawala borayanaratibiwa vilivyo na ipasavyo kwa kuzingatia Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwakuzingatia Sheria ya Uchaguzi pamoja na kanuni zakembalimbali, pia kwa kuangalia sheria mbalimbali ambazozinaratibu suala nzima la utawala bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ni mhakikishieMheshimwa Mbunge kwamba masuala hayoyanaendeshwa vizuri na ndio maana tuna Katiba, tuna Sheriaya Uchaguzi ambayo imemuweka leo yeye Bungeni hapandani. Nimhakikishie kwamba Tanzania itaendelea kuheshimusuala la utawala bora, suala la demokrasia na lakini piaitaendesha uchanguzi wake kwa uhuru kwa haki na amani.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan Lyimo swali lanyongeza.

MHE. SUSAN A. J. LYMO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli ulio wazi kwambaTanzania tumekuwa tukiridhia maazimio mabalimbali namengi sana, lakini domestication imekuta tatizo kubwa sana.Nilitaka kujua nafasi ya Wizara hii katika kuhakikisha kwambamaazimio yote ambayo tumeyaazimia yanakuwadomesticated, mfano CEDAW, Africa Union kwa lile suala laasilimia 50 kwa 50 kuwa katika maamuzi ni kwa jinsi ganiWizara yenu inatekeleza hayo maazimio ambayo tumeridhia?

NAIBU SPIKA: Mheshimwa Naibu Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki majibu

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimwa Naibu Spika, ahsante sana,naomba nimhakikishie Mheshimiwa Susan Lyimo kwambaTanzania inatekeleza vizuri sana mikataba ya mbalimbali yakimataifa ambayo tumeshairidhi, lakini sio mikataba yotetunaweza kukairidhia kwa sababu mikataba mingine inakinzana na misingi ambayo tumejiwekea, misingi ya kikatiba,mila, desturi na utamaduni.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni kumekuwepona mijadala mingi sana hapa kuhusu masuala ya ushoga namasuala mengine, hiyo masuala ushoga yanatokana namikataba ya kimataifa sio kila mkataba tunawezatukauridhia, lakini kuhusu swali lake la haki sawa kwa jinsiazote hasa 50 kwa 50. Tanzania moja kati ya nchi ambayoimetekeleza sualahilo kuhakikisha kwamba tuna Viti Maalumkuongeza uwakilishi wa wanawake katika Bunge hili na katikanafasi nyingine za uongozi Serikalini. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwamoto swali lanyongeza.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi wa tano Marais waAfrika walikutana na walikubaliana waweze kuridhia protocolya Malabo ili kufanya Bunge la Afrika kuwa huru.

Je, nini msimamo wa nchi yetu?

NAIBU SPIKA: Mheshimwa Naibu Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimwa Naibu Spika, ahsante sana,Bunge la Afrika limeanzishwa kwa mujibu wa taratibu naKanuni za AU na kwa mujibu wa taratibu hilo Bunge ni hurukama chombo cha AU inatekeleza majukumu yake kwa

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171717

uhuru kabisa na hata sisi katika Bunge hili tuna wawakilishikatika Bunge la Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkataba wa Malabounaongelea mambo mengi sio tu kuhusiana Bunge la Afrika.Mambo ambayo yanahusu masuala mengi ya haki zabindamu na uwekezaji na Utawala Bora kwa Afrika kwa hiyonimuhakikishie Mheshimiwa Mwamoto kwamba Bunge laAfrika lipo huru na litendelea kuwa huru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimwa Saada Mkuya swali lanyongeza.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana.

Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amezungumza kunabaadhi ya vipengele vya hii charter ya demokrasia, uchaguzina utawala bora vinakinzana sana na Katiba yetu pamojana sheria zingine, labda specifically ni vifungu gani katika hiyocharter vinakinzana ili tuone kwa utaratibu gani tunawezatukavirekebisha ama tukaomba AU wakarekebisha kulingana mazingira yetu?

NAIBU SPIKA: Mheshimwa Naibu Waziri hilo swalilitahitaji majibu ya baadae kwa sababu hivyo vifunguhautakuwa na mkataba hapo sasa hivi.

Waheshimwa Wabunge, tunaendelea MheshimiwaMartha Moses Mlata sasa aulize swali lake.

Na. 75

Wimbo Maalum wa Afrika Mashariki

MHE. MARTHA M. MLATA aliuza:-

Je, Tanzania ilishiriki kwa namna gani katika mchakatowa kuupata Wimbo Maalum wa Afrika Mashariki?

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako na kwaniaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Mheshimiwa Dkt. Balozi Augustine Philip Maiga,kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Martha Moses Mlata,Mbunge wa Viti Maalum naomba kutoa ufafanuzi kuwa huusi wimbo maalum ni wimbo wa Jumuiya ya Afrika Masharikikama zilivyo nyimbo nyingine za Taifa katika nchi mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya ufafanuzi huo,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martha Moses Mlata,Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mchakato wa kuupatawimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanywa na nchi tatuwaanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kenya na Jamhuri yaUganda ambapo lilitolewa tangazo la kuwapata watunzikutoka katika nchi hizi tatu ambazo kwa wakati huo ndiyozilikuwa nchi wanachama. Baada ya tangazo kutolewa kilanchi iliwasilisha wimbo mmoja katika Mkutano wa Nane waWakuu wa Nchi uliofanyika mjini Arusha tarehe 30 Novemba,2006. Kwa hiyo, katika hatua hii tulikuwa na nyimbo tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nyimbo zote tatu ziliimbwakatika Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Kampala,Uganda mwezi Novemba, 2017. Wakuu wa Nchi wakaagizanchi za Rwanda na Burundi ambazo ndiyo kwanza zilikuwazimejiunga na Jumuiya kutoa maoni yao katika nyimbo hizotatu zilizoimbwa.

Aidha, Wakuu wa Nchi hao waliagiza ziandaliwenyimbo mbili kutokana na nyimbo tatu zilizoimbwa. Uamuzihuu ulifikiwa ili kuondoa changamoto ya kuwa na wimbo wajumuiya ulioandaliwa na nchi moja.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191919

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa Wakuu waNchi uliofanyika Kigali, Rwanda mwezi Aprili, 2009 nyimbo mbilizil i imbwa ukiwemo wimbo wenye maneno mengi yamtaalam wa Kiswahili kutoka Tanzania, Profesa HermasMwansoko, ambaye wakati huo alikuwa Mkurugenzi waUtamaduni, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Mheshimiwa Spika, Mchakato huu haukuishia hapokwani katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliofanyikaNgurdoto, Arusha mwezi Disemba, 2010 aliamuliwa kwambaziunganishwe sintaksi za nyimbo hizo mbili ili kupata wimbommoja. Sintaksi yaani msuko wa sentensi za lugha ya kiswahilikatika wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ziliandaliwa naJamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ilishiriki kikamilifu katika mchakatowote wa kuandaa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Martha Mlata, swali lanyongeza.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwanza nimpondeze Mheshimiwa Naibu wawaziri kwa majibu Mazuri ambayo ameyatoa na kwelialichoeleza hapa ni sahihi na huo wimbo wa Jumuiya yaAfrika Mashariki alivyosema sio maalum ni wimbo na miminasema ni wimbo rasmi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa maswali yangu mawili,kwanza kabisa mchakato aliuleza katika kuwapata watunzini kweli walitoka nchi hizo tano kama alivyosema nawalivyofika kule kulikuwa na makubaliano rasmi au maalumvyovyote, lakini kwa makubaliano yale ninaomba aniambieni staiki gani mtunzi kutoka Tanzania ambaye anaitwa JohnJoseph Mgango kutoka Bukoba alizipata kutokana namakubaliano yale?

Je, yale makubaliano yote yaliyofanywa na Jumuiyaya Afrika Mashariki kwa watunzi wa nchi zote tano ili kuweka

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

kumbukumbu sahihi kwamba kila nchi imeshiriki katikakutunga wimbo huo, ni yapi ambayo yametekelezwa, yapiambayo yanatekelezwa, ni lini yatatekelezwa yote nakuwapa stahiki zote watunzi wa nyimbo hizi? Ahsante.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri nitakupa uhurukama hayo maswali utayajibu baadae kwa sababuyanahitaji taarifa rasmi lakini kama unayo unaweza kujibu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, mchakato huuuliendeshwa Jumuiya ya Afrika na Sekretarieti ya AfrikaMashariki ndio ilikuwa inaendesha mchakato mzima. Tarehe12 Oktoba, 2018 Wizara ilipokea barua kutoka Wizara yaHabari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo kwamba kunaMtanzania huyo kwamba anadai stahiki zake.

Mheshimwa Naibu Spika, Wizara tumewasiliana tayarina Jumuiya ya Afrika Mashariki na tunasubiri majibu kuonamakubaliano hayo kati ya mtunzi huyu na Jumuiya yalikuwajena yalitekelezwa kiasi gani na nini tufanye ili kumsaidia kuonakama haki yake bado ipo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Moshi Kakoso, swali lanyongeza.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza,Shirika la Kenya Airways ni Shirika la Ndege ambalo linatumianembo ya jina Mlima Kilimanjaro kwenye baadhi ya ndegezake na kufanya mataifa ya nje yaamini kwamba MlimaKilimanjaro unatoka nchi ya Kenya.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali imechukua hatuagani kudhibiti kitendo kama hiki ambacho kinaipotezeamapato ya nchi yetu?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Salma Kikwete swali lanyongeza.

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212121

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kuniona. Kutokana na swali la msingi, na miminaomba niulize swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi zote duniani zinawimbo wake wa Taifa, na wimbo wa Taifa una taratibu rasmiwakati unaimbwa, sisi kama Tanzania, tuna wimbo wetuvilevile wa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu ni upi wakati wakuimba Wimbo wa Taifa kwa sababu wengine ukiimbwaWimbo wa Taifa wanasimama kikakamavu, wengineukiimbwa wimbo wa Taifa wanashika hapa (kifua) sasa katiya hayo ni lipi kwa wimbo wetu wa Taifa wa Tanzania?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu zawakati wa kuimba wimbo wa Taifa ni kwamba tunafuataukakamavu wa kijeshi, tunaweka mikono yote miwili chini,unasimama kama vile uko katika gwaride la Jeshi ukiwamkakamavu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, MheshimiwaJustin Joseph Monko, Mbunge wa Singida Kaskazini sasaaulize swali lake.

Na. 76

Zao la Alizeti Kukosa Soko

MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:-

Wenye viwanda, vya kukamulia alizeti wamekuwawakilalamika kukosa alizeti na wakati huo huo wakulimawamekuwa wakibaki na alizeti kwa kukosa wanunuzi.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

(a) Je, ni nini kauli ya Serikali juu ya hali hiyo yawakulima kukosa soko la alizeti?

(b) Je, Serikali ipo tayari kununua alizeti kwa wakulimaili wapate fedha za kuendesha maisha yao na kujiandaa kwamsimu mwingine wa kilimo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa niaba ya Waziri, waViwanda, Biashara na Uwekezaji, naomba kujibu swali laMheshimiwa Justin Joseph Monko, Mbunge wa SingidaKaskazini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitiamaonesho mbali mbali ikiwemo maonesho ya Sabasaba naSIDO na kwa kupitia Kongano za Alizeti imekuwaikiwakutanisha wakulima wa alizeti, watafiti na wazalishaji wamafuta wa ndani na nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya soko laalizeti na mafuta kwa ujumla.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha wakulimawanapata soko, Serikali imeendelea na juhudi za kuwekamazingira bora ya uwekezaji ili kuvutia ujenzi wa viwandavya kusindika mbegu za mafuta ikiwemo zao la alizeti. Mpakasasa kuna zaidi ya viwanda 20 vya kusindika mbegu zamafuta vyenye crushing capacity tani 1,445,000 na refiningcapacity tani 295,000. Aidha, Chama cha Wasindikaji waAlizeti Tanzania (Tanzania Sunflower Processors Association –TASUPA) kimeendelea kushirikiana na wakulima kwa kwakununua na kusindika alizeti inayozalishwa hapa nchini, ikiwani pamoja na kulipia gharama za usindikaji wa mafutayanayopatikana na kutafuta soko lenye tija. Vilevile katikakulinda na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vya mafutaya kula yanayozalishwa nchini Serikali imeweka kiwango cha

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232323

asilimia 35 kwa uingizwaji wa mafuta safi na asilimia 25 kwamafuta ghafi kutoka nje ya nchi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Justin Monko swali lanyongeza.

MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Naibu Spika,nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswalimadogo mawili ya nyongeza.

Awali ya yote ningependa uniwie radhi nisemekwamba naona majibu yangu maswali niliyouliza ni kamayamepata majibu ya kisanii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu spika, nilitaka kujua kauli ya Serikalikuhusiana na sakata hili kwamba wakulima wa SingidaKaskazini wamebaki na alizeti majumbani wakati viwandavyetu havina malighafi za kutosha kwa sababuwameendelea kuwatumia madalali kuchukua kwa beindogo. Sasa kauli ya Serikali hapa naambiwa habari ya SIDOMaonesho ya SIDO, Maonesho ya Sabasaba, kiukweli hililinasikitisha sana.

Sasa kama hii ndio kauli ya Serikali nilitaka niulize je,Mheshimiwa Naibu Waziri sasa yuko tayari kuwasafirishawakulima wa Mkoa wa Singida ili waende wote kwenyeMaonesho ya Sabasaba na Nanenane ili waende sasawakajifunze na kukutanishwa na hao wasindikaji?

Swali la pili, nilitaka kujua kama Serikali iko tayari sasakununua alizeti hiyo ili Wananchi waweze kupata fedha?Lakini sasa hapa nimepewa...

NAIBU SPIKA: Umeshauliza mawili Mheshimiwa,maswali mawili. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, akutukanaye hakuchagulii tusi.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kama yeye kwenyeswali alijua kwamba tatizo ni madalali pengine swalilingesema moja kwa moja ni madalali.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusu kuwasafirishawananchi wote kuwapeleka kwenye SIDO, sio utaratibuunaotumika, lakini matangazo yamekuwa yakitolewa nayeye mwenyewe ni shahidi pia hata kupitia katika clusterambayo ipo Ntinku tumeendelea kuwakutanisha pamoja nawatafiti mbalimbali kwa hiyo mimi nilitegemea kwamba jibuambalo tumemjibu atahusisha na hata cluster ambayo niKongani ipo katika eneo lake la Ntiku.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sware Semesi, swali lanyongeza.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na sintofahamukwa soko ya mazao ya biashara si tu kwa alizeti hususani piakwenye mazao ya mbaazi na mtama mweupe. Sasa ni ninimkakati wa Serikali kuweza kutoa huduma kwa wananchihao wanaoteseka na mazao yao na kuwaongezea umaskini?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutafutamasoko na hata jana tu kupitia hotuba ya Mheshimiwa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John PombeMagufuli amezidi kutuagiza kwamba tufanye kasi katikakuhakikisha kwamba mazao mengi yanapata soko kupitiataasisi zetu ikiwemo TANTRADE. Kwa hiyo. tutaendeleakufanya hivyo, lakini vilevile kuendelea kuhamasishawananchi kutumia fursa ya mazao yanayopatikana nchini.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fatma Toufiq swali lanyongeza.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252525

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana, kwa kunipa fursa na mimi kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mikoa yaDodoma na Singida ni miongoni mwa mikoa katika nchi hiiambayo inazalisha zao la alizeti kwa wingi sana.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga soko maalumla alizeti katika Mkoa wa Singida ili wenye viwanda, nawawekezaji wawe na eneo maalum la kununua alizeti iliwenye viwanda na wakulima waweze kupata tija? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali imeona umuhimuwa kufanya hivyo na tayari imeshatenga eneo kwa ajili yakuwezesha wakulima waweze kupata eneo la kupata sokopamoja na kuongeza thamani ambalo lipo katika eneo laZuzu, kwa hiyo, naamini fedha zikipatikana soko hilo litawezakuendelezwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mariam Ditopile swali lanyongeza.

MHE. MARIAM D. MZUZURI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kuwa Wakulima wa Mkoa wa Dodoma piawamekuwa wanalima alizeti kwa wingi, na pia tumeonajuhudi za Serikali katika kuwekeza kwenye viwanda vyakukamua mafuta haya lakini, kumekuwa na malalamikomakubwa sana ya mizani ambayo inapimia alizeti hizi kulekiwandani na inawezekana hiyo ndiyo sababu kubwawakulima hawa, wanavunjika moyo kwenda kuuza alizeti zaoviwandani huko.

Je, Serikali imejipanga vipi na inatumia aina gani yavipimo kuhakikisha hizi mizani hazichezewi na zinatoa kilohalisi? Nashukuru.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ziko changamotombalimbali kuhusiana na zao hili la alizeti, mojawapo ikiwani hivyo vipimo, kama alivyosema, lakini vilevile ni pamoja nauhafifu wa mbegu zinazotumika katika uzalishaji wa mafutahaya ya alizeti, Serikali imeliona hilo, kupitia taasisi yetu yaVipimo, tunaendelea kukagua mizani na kuhakikishakwamba mizani inafuata taratibu na Viwango vilivyowekalakini vilevile, kuhamasisha wakulima kutumia mbegu bora ilializeti hizo ziweze kuwa na uzito unaokidhi na kuweza kutoamafuta yanayostahili.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tunaendelea na Wizaraya Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Seleman Said Bungara,Mbunge wa Kilwa Kusini swali lake litaulizwa kwa niaba naMheshimiwa Ally Saleh.

Na. 77

Hitaji la Elimu ya Uvuvi wa Kisasa - Ukanda wa Pwani

MHE. ALLY SALEH ALLY (K.n.y. MHE. SELEMAN S.BUNGARA) aliuliza:-

Wavuvi wengi wanakabiliwa na tatizo la kutokuwana elimu ya uvuvi wa kisasa ambapo wengi wao hutumiazana duni za uvuvi hali ambayo haiwaletei tija wavuvi haona uvuvi ni sekta mojawapo inayochukua vijana wengihususan kwenye Ukanda wa Pwani.

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia wavuvihao elimu ya uvuvi bora ili uvuvi wao uwe wenye tija?

(b) Je, Waziri atakuwa tayari kuwatembelea nakukutana na wavuvi kwa nia ya kujua changamotozinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi?

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272727

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, wa Mifugo naUvuvi majibu.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali laMheshimiwa Seleman Said Bungara, lenye vipengele (a) na(b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imeandaampango mkakati wa kuboresha sekta ya uvuvi ambaounalenga kuboresha uvuvi nchini ikiwemo kutoa elimu yauvuvi wa kisasa kwa wavuvi; kusambaza teknolojia za uvuvina kuboresha zana za uvuvi. Pia mpango unazingatia wavuvikupatiwa elimu ya uvuvi endelevu ili kuhakikisha uvuvi nchiniunaleta tija kwa wavuvi na Taifa kwa ujumla.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Mifugo naUvuvi amekuwa na utaratibu wa kutembelea wavuvi nawafugaji ili kujua matatizo na changamoto zinazowakabili.Aidha, kwa mwaka huu 2018 Naibu Waziri alitembelea katikaWilaya ya Kilwa katika Vijiji vya Kilwa Kivinje na Somanga nakusikia changamoto zinazowakabili wavuvi pamoja nawafugaji ambapo alitoa maagizo kwa Halmashauri ya Wilayaya Kilwa kushughulikia matatizo yao na matatizo mengineyanaendelea kutatuliwa na Wizara. Kwa mfano tatizo lakuharibika kwa dagaa wakati wa mvua za masika ambapoWizara kupitia Taasisi ya Utafiti ya TAFIRI na kwa kushirikianana VETA inawatafutia majiko banifu yanayotumia teknolojiarahisi itakayowasaidia wavuvi kuondokana na upotevu wadagaa yaani post harvest loss katika kipindi hicho.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh swali la nyongeza.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kuniruhusu niulize swali la nyongeza, kwa kwelisekta ya uvuvi inaweza kuitoa Tanzania kiuchumi kwa sababubado hatujatumia fursa ya ukanda wa bahari wa mile 1400na pia eneo la economic zone.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

Sasa je, ni lini sasa Mkakati huo wanaosema Waziriutawafikia kwa vitendo ili kuwatoa wavuvi wa Kilwa naWatanzania katika umaskini ambao si wa lazima?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, moja ya njiabora kabisa ya kuwa na uvuvi wa kisasa ni kuwa na sera yauvuvi wa bahari wa kuu na wa mwambao yaani blueeconomy.

Je, Serikali sasa, itakuwa imejitayarisha kiasi ganikutengeneza Sera hiyo ili io-compas suala zima la Uvuvi iliTanzania iweze kufaidika na Uvuvi ambao hadi hivi sasahatujautumia kiasi cha kutosha.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mifugo naUvuvi majibu.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaNaibu Spika, ni lini tutaanza kutekeleza mkakati huu, hivi sasatumeshaanza kutekeleza mkakati huu, wa kuhakikisha sektaya uvuvi inaleta tija katika Taifa letu na kwa kuanzia tumefufuaShirika letu la Taifa la Uvuvi yaani TAFICO tayari tunamanagement na katika kuhakikisha kwamba tunakwendambele na kuitumia vizuri rasilimali hii TAFICO inakwendakushirikiana na hata sekta binafsi kununua meli za uvuvi ilituhakikishe kuwa tunapata manufaa na bahari yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile ameulizatumejitayarishaje ili kunufaika na bahari yetu. Tumejitayarishavyema sana na ndio maana hivi sana tunakwenda katikaujenzi wa bandari ya uvuvi ambapo mshauri mwelekezi yukokazini toka mwezi wa saba mwaka huu na ifikapo mweziFebruari 2019 atakuwa amekamilisha kazi ya kutuelekezawapi tujenge bandari ya uvuvi na namna gani tujengebandari ya uvuvi ambapo hii itatusaidia katika kufanyamavuvi yetu ya kisasa na kupata tija kwa ajili ya maendeleaya Taifa yetu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Aida Khenani swali lanyongeza.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

292929

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru, kuna operation ambayo inaendelea hivi sanakatika ziwa Tanganyika, ambayo imegubikwa na unyanyasajimkubwa kwa Wavuvi pamoja na rushwa.

Je, Serikali iko tayari, kusitisha kwanza zoezi hilo badalayake ikajikita kutoa elimu ili kutoa matokeo chanya?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wakati ukijahapa mbele, Waheshimiwa Wabunge niwakumbushe tenakabla hujasimama soma swali la msingi linauliza kuhusu nini.Niwakumbushe tena, soma swali la msingi linahusu kitu ganikabla hujaomba swali la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Wazirimajibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli Wizara yetu inaendesha oparesheni, natunaita Operation Sangara. Operation hii inafanyika kwamujibu wa sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 naKanuni zake za mwaka 2009 tuhuma hizi anazozitoaMheshimiwa Aida, naomba kama ana specific issueinayohusiana na haya anayoyasema ya unyanyaswaji waWavuvi na Rushwa atuletee Wizarani kwetu nasitutashughulikia mara moja.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vedastus Manyinyi swali lanyongeza.

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kunipatia nafasi niweze kuuliza swali swali dogola nyongeza.

Pamoja na mikakati mizuri ambayo watu wa Idara yaUvuvi wanayo ya kuzuia Uvuvi haramu lakini kumekuwa nachangamoto kubwa mfano, katika zile adhabu wanazozitoakatika kukomesha tatizo hili, leo akishikwa muendeshabodaboda akiwa amepakia samaki ambao ni haramu,anapigwa faini kati shilingi milioni mbili mpaka shilingi milionitatu, ambapo bei ya kununua bodaboda ni kati ya shilingimilioni moja na nusu mpaka milioni mbili, na kutokana na hali

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

hiyo yule muendesha bodaboda analazimika ku-surrenderile...

NAIBU SPIKA: Uliza swali Mheshimiwa.

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: Serikali haioni kamakuna haja ya kuwapa viwango wanavyoweza kuvilipa kulikokuendelea kupoteza ile bodaboda?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaNaibu Spika, tozo na faini zote zinazotolewa na Wizara yetuwakati oparesheni zipo kwa mujibu wa sheria yetu, lakininaomba nimtoe hofu Mheshimiwa Manyinyi na WaheshimiwaWabunge wengine wote ya kwamba hatumkamati mtu nakumtoza kwa sababu amesafirisha samaki katika bodaboda.Naomba niwaeleze ya kwamba tumetoa mwongozo wanamna ambavyo mtu anatakiwa apigwe faini, kwa hivyonaomba niwatoe hofu na kama liko tatizo la namna hiyo mtuamekamatwa kisa amebeba katika bodaboda, bodabodani chombo kinachoruhusiwa kubeba samaki, isipokuwaabebe katika cooler, lile lenye kuhifadhi samaki wabichi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tunajua mazingira yavijijini na sisi tunataka Watanzania wanufaike na rasilimali zao.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hasna Mwilima swali lanyongeza.

MHE. HASNA S. K. MWILIMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na majibu ya swalila nyongeza sasa hivi aliyoyatoa Mheshimiwa Naibu Wazirikamba wao kama Wizara wametoa mwongozo wa namnagani faini zipigwe kwa vyombo vinavyobeba samaki. Mimininao ushahidi na nilimpigia simu Naibu Waziri, gari la abirialimebeba mama aliyekuwa anakwenda kwenye msiba nasamaki 20, mwenye gari katozwa faini shilingi milioni 15.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

313131

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ni kweli sheria yaondiyo inavyowalinda kwamba mwenye gari atozwe faini yashilingi milioni 15 kwa ajili ya kubeba abiria aliyebeba samakiwatano, 10 au samaki 20. Je, kwa nini sasa Wizara isitoe tamkoni kiasi gani wanatakiwa kutozwa kama faini ili nchi nzimatufahamu? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kama unazohizo takwimu za ni kiasi gani unaweza kujibu, kama hunatakwimu ya ni kiasi gani unaweza ukalijibu baadae, nakupauhuru huo.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaNaibu Spika, nashukuru sana kwa swali la nyongeza laMheshimiwa Hasna Mwilima na umenipa option ya kwambaje, ni kiasi gani kinachotakiwa. Mheshimiwa Hasna Mwilimana Waheshimiwa Wabunge wote narudia kusema kwambafaini zetu zipo kwa mujibu wa sheria yetu wenyewe ya Bungela Jamhuri ya Muungano la Tanzania, hilo la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, sheria ipo wazi inaelezaviwango vya faini ambazo zinapaswa kupigwa katika makosambalimbali yanayofanywa katika tasnia hiyo ya uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa jamboambalo ni mahususi alilolisema Mheshimiwa Hasna Mwilimakama anahisi lipo tatizo tunnamkaribisha na milango yetuiko wazi, tuweze kujadiliana na kama kweli kipo kosalililofanyika katika eneo hilo tutarekebisha.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge waTunduma sasa aulize swali lake.

Na. 78

Huduma kwa Wagonjwa Wenye Magojwa Sugu

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:-

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Je, ni l ini Serikali itawahudumia watu wenyemagonjwa sugu kwa asilimia mia moja mfano wagonjwa wamoyo na magonjwa mengine ili kuondokana na adha yakuombaomba michango na kusababisha vifo kwa wagonjwawanaokosa michango hiyo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge waTunduma kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na ongezekokubwa la magonjwa sugu ikiwa ni pamoja na magonjwa yamoyo, mishipa ya fahamu, saratani, kisukari, magonjwa suguya figo na magonjwa na mengineyo ambayo kitaalamuhujulikana kama magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Utafiti waviashiria vya magonjwa haya uliofanywa na STEP hapa nchinimwaka 2012 na ulioshirikisha Wizara ya Afya, Taasisi ya Utafitiwa Magonjwa ya Binadamu na Shirika la Afya Dunianiulionyesha kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari hadi kufikia9% ukilinganisha na utafiti uliofanywa mwaka 1980 ambapokulikuwa na Watanzania chini ya asilimia moja tu wenyekisukari.

Aidha, utafiti huo ulionesha kuwa asilimia 25.9 yaWatanzania wana shinikizo la juu la damu ukilinganisha naule wa mwaka 1980 ambapo ilikuwa ni asilimia 2.7 tu wenyeshinikizo la juu la damu. Kwa kutambua ongezeko lamagonjwa yasiyo ya kuambukiza, Wizara yangu ilianzishasehemu ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza nakutengeneza mkakati wa kupambana na magonjwa hayowa mwaka 2009 – 2015 na hivi sasa tuna mkakati wa pili wa2016-2020.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

333333

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Afya ya mwaka2007 inatoa mwongozo kwa wananchi kuchangia hudumaza afya. Aidha, imeainisha makundi yanayostahili kupatamsamaha wa kulipia huduma za afya katika vituo vyote vyakutolea huduma vya umma. Makundi yanayopewakipaumbele ni pamoja na watoto wa umri wa chini ya miakamitano, wanawake wajawazito na wazee wenye miaka 60na kuendelea wasio na uwezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwaikigharamia baadhi ya huduma za matibabu kwa watuwenye magonjwa sugu katika hospitali za ndani na nje yanchi. Hata hivyo, hali halisi imeonyesha kuwa siyo rahisikuwahudumia wagonjwa hawa kwa asilimia mia moja kwanigharama zake ni kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, rai yangu kwa wananchi nikujitahidi kwa nguvu zote kujikinga na magonjwa haya kwakufanya mazoezi mara kwa mara, kutokutumia tumbaku nakuacha matumizi ya pombe kupita kiasi na kula mlo wenyeafya hususan mbogamboga, matunda, kuepuka kula vyakulavingi vya nafaka iliyokobolewa, sukari nyingi pia mafutayatokanayo na wanyama.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ninatoa rai kwawananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ili kuwa nauhakika wa matibabu kabla ya kuugua. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Frank George Mwakajokaswali la nyongeza.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa NaibuSpika, pamoja na majibu marefu ya Mheshimiwa Waziri lakiniswali langu halijajibiwa. Mimi nilichokuwa nauliza ni kuhusianana huduma ya matibabu kwa wagonjwa mahususi wamagonjwa sugu bila kujali jinsia wala umri, lakini kilichotokeaMheshimiwa Waziri ameeleza zaidi utafiti na mambo mengineambayo yamekuwa yakitokea.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukweli tu ni kwambaninayo mifano michache ambayo ningeomba niitoe, mfanokuna mtoto mmoja anaitwa Hyasinta Zaya anatokea Matai,Mkoa wa Rukwa ameanza matibabu akiwa na miaka tisamwaka 2013 na mpaka leo hajapata matibabu na alitakiwakufanyiwa upasuaji kipindi chote hicho. Wazazi wake walikosafedha shilingi milioni 10 za matibabu.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwambainawatibu wananchi bure ambao wanakosa fedha zamatibabu ili kuokoa maisha ya watanzania walio wengi?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajua wazee wengi katikaTaifa hili wametumia nguvu zao nyingi sana kulijenga Taifahili, lakini wazee hawa sasa hivi hawana uwezo wa kuhimiligharama za matibabu hasa matibabu sugu kama figopamoja na magonjwa mengine ya moyo. Serikali ina mpangogani wa kuwapa bima ya afya ili wazee hawa wawezekutibiwa bure kuliko usumbufu unaojitokeza sasa hivi ambapowazee hawa wanakosa matibabu? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sanaMheshimiwa Mwakajoka kwa maswali yake mazuri mawili.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza umeulizakwa nini Serikali isigharamie kwa asilimia 100 matibabu yamagonjwa sugu. Sasa siwezi kusema tu lazima utoe angalauka-preamble kuonesha hali halisi ya ongezeko la magonjwahaya na njia kubwa ya kupambana na magonjwa sugu nikinga. Kwa hiyo, nilikuwa nataka kuwaonesha hali halisiWatanzania, wapi tumetoka na wapi tunaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mtoto Hyasintaambaye umetoa taarifa hapa kwamba ana tatizo laugonjwa wa moyo na amekosa matibabu, zipo taratibu za

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

353535

kufuata. Juzi Jakaya Kikwete Cardiac Institute imetoamatibabu bure kwa watoto zaidi ya 50 wamefanyiwaupasuaji kwa kushirikiana na madaktari kutoka Israel. Kwahiyo, utaratibu upo na nikuombe mtoto yule apelekweHospitali ya Rufaa ya Mkoa watampa rufaa kwenda Kandana Kanda watampeleka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwetena mimi mwenyewe nitahakikisha anapata matibabu burekwa sababu sera inataka mtoto mwenye umri wa chini yamiaka mitano kupata matibabu bure. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye hili tunamshukurusana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli,amewekeza sana kuhakikisha huduma za matibabu yakibingwa zinapatikana ndani ya nchi. Mwaka jana wagonjwazaidi ya 167 tulikuwa tunawapeleka nje ya nchi mwaka 2015,mwaka 2017 ni wagonjwa wawili tu, wagonjwa wotewanafanyiwa upasuaji ndani ya nchi. Kwa hiyo, hii ni kazi nzuriya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu bima ya afya kwawazee; tumetoa maelekezo kwa Halmashauri zote kuwapatiawazee vitambulisho vya matibabu ikiwa ni hatua ya awalikuelekea bima ya afya kwa kila mtu. Tunategemea ndaniya Bunge lijalo tunakuja kwenye Bunge lako tukufu kuletamuswada wa sheria ambao itafanya bima ya afya kuwa nilazima na wazee wote wenye stahili tutawapa bima za afyabure ili waweze kupata huduma za matibabu bila kikwazo.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Shaabani Shekilindi swalila nyongeza.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI:Mheshimiwa NaibuSpika, asante kwa kuniona. Katika Wilaya ya Lushotokumekuwa na watu wengi wenye magonjwa sugu hasa kwawale waishio vijijini.

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuwapatia dawawagonjwa sugu hasa wale wenye magonjwa sugu pamoja

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

na wale wenye mahitaji maalum hasa kwa wale waishiovijijini?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEENA WATOTO:Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumjibuMheshimiwa Shekilindi, Mbunge wa Lushoto al-maarufuBosnia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tunao wagonjwawa magonjwa sugu katika Halmashauri zetu mbalimbali lakininataka kurudia kwamba gharama za magonjwa sugu hayani kubwa sana kwa sababu mtu anatakiwa kutumia kila sikuakianza kutumia. Kwa hiyo, rai yangu ni kwamba tutajitahidikadri inavyowezekana kuhakikisha dawa hizi zinapatikanaikiwemo dawa za kisukari.

Mheshimiwa Naibu Spika, suluhisho la kudumu nikuwahimiza wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya.Tumeanzisha bima ya afya tunaita ya Kikoa shilingi 76,400unapata matibabu mwaka mzima mpaka Hospitali ya Rufaaya Taifa na Hospitali za Kanda. Kwa hiyo, nitoe rai kwaWatanzania kuwa na utamaduni wa kulipia matibabu kablaya kuugua kwa sababu wananchi wengi wanakuwa maskinikwa sababu wakiumwa inabidi wauze ardhi ama baiskeli,bima ya afya ndiyo suluhisho. Tutajitahidi kuongeza bajeti yadawa, lakini pia kwa mujibu wa sera lazima wananchiwachangie huduma za afya. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri mtusaidie kwasababu ile bima ya afya ya mtu mmoja ya shilingi 76,000 hiviinataka yule mtu alipe fedha zile kwa mkupuo ili awezekupata matibabu. Sasa ile fedha ni kubwa kwa mtu wa kijijinikuweza kulipa yote kwa pamoja, mtusaidie utaratibu ambaoataweza yeye kuchangia kama wengine wanavyochangiakila mwezi ili mchango wake uwe ni kidogo kidogo, lakiniaweze kupata matibabu. (Makofi)

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

373737

Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Wizara yaKilimo, Mheshimiwa Dkt. Dalaly Peter Kafumu, Mbunge waIgunga sasa aulize swali lake.

Na. 79

Changamoto Zinazowakabili Wakulima wa Pamba Nchini

MHE.DKT. DALALY P. KAFUMU aliuliza:-

Mwaka 2017 Serikali iliamua kulifufua zao la pambalililokuwa limekufa lakini licha ya wakulima wa pamba kuitikiawito wa kulima pamba kuanzia msimu wa mwaka 2018, badowanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kuchelewakupelekewa pembejeo kama viuatilifu, kupelekewa viuatilifuvisivyoua wadudu, bei ndogo ya pamba, kuuziwa mbegukwa mikopo yenye riba kubwa.

(a) Je, ni lini Serikali itazishughulikia changamoto hizoili kukuza ari ya wakulima kulima pamba kwa wingi?

(b) Je, ni kwa nini wakulima wasipewe mbegu burekama il ivyokuwa zamani i l i kuondoa usumbufu wakukopeshwa na wanaposhindwa kulipa wanakamatwa nakuteswa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwa niaba yaWaziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Dalaly Peter Kafumu, Mbunge wa Jimbo la Igunga lenyesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, mojawapo yachangamoto za wakulima wa pamba katika kuongeza tijana uzalishaji ni upatikanaji wa pembejeo kwa wakati,wakulima kutotumia kikamilifu pembejeo na uzingatiaji wa

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

kanuni za kilimo bora cha zao la pamba. Aidha, Serikaliimeendelea kudhibiti ubora wa pembejeo kupitia mamlakambalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi ya TPRI na Mamlakaya Udhibiti wa Ubora Mbegu (TOSCI) kwa kufanya majaribio(germination tests) ya mbegu za pamba kabla ya kupelekakwa wakulima kwa ajili ya kupanda pamoja na kuainishamaeneo ya Meatu na Igunga kama maeneo ya kuzalishambegu za pamba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeelekezawakulima wote kuanzia msimu wa mwaka 2018/2019 kutumiambegu aina ya UKM08 na iliyoondolewa manyoya (delintedseeds). Aidha, kutokana na mikakati hiyo, uzalishaji wapamba umeongezeka kwa asilimia 67 kutoka tani 133,000msimu wa ununuzi wa 2017/2018 hadi tani 221,600 msimu wa2018/2019.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali nikuweka mazingira wezeshi ili wakulima waweze kufanyashughuli zao kwa ufanisi na kupata faida ikiwa ni pamoja naupatikanaji wa mitaji kwa ajili ya kuendeleza kilimo ikiwemoununuzi wa pambejeo. Katika kuhakikisha wakulimawanapata pembejeo, Halmashauri ya Wilaya ya Igungailidhamini mkopo kwa wakulima kwa kutumia ushuru wakeunaotokana na pamba ambapo wakulima walipata fursaya kukopa mbegu msimu uliopita na hadi mwezi Oktoba, 2018wamerejesha shilingi 1,293,997,400 kati ya shilingi 1,567,698,000zilizokopeshwa sawa na asilimia 82.5. Aidha, utaratibu wazamani haukuwa kuwapatia wakulima mbegu bure baliwakulima wa pamba waliwekewa utaratibu wa kukopeshwakupitia Vyama Vikuu vya Ushirika na vya Msingi na kukatwawakati wa kuuza pamba yao. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Dalaly Peter Kafumuswali la nyongeza.

MHE. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa NaibuSpika,asante sana. Nashukuru sana kwa majibu yaMheshimiwa Naibu Waziri, naomba sasa niulize maswalimawili ya nyongeza.

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

393939

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, wakulimakwenye msimu wa mwaka 2017/2018 hawakupata mavunotarajiwa kwa sababu walipata viuatilifu ambavyo havikuuawadudu, lakini pia mvua ilikuwa kubwa sana, kwa hiyo,pamba ikarefuka sana. Kwa nini sasa Serikali isiamuekuhamisha deni la mbegu kwenda msimu unaokuja kwa waleambao wameshindwa kulipa kwa sababu ya kushindwakupata mazao ya kutosha?

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka nikiwa kijanamiaka ya 1960 mpaka 1980 nilikuwa nalima pamba kwa ajiliya kujilipia ada na tulikuwa tunaenda kwenye godown lapamba la ushirika tunachukua mbegu na tunalima, hatukuwana mikataba yoyote. Kwa nini sasa Serikali isirudishe utaratibuhuo tuweze kupata mbegu wakulima tukalima bilakusumbuliwa kama tunavyofanyiwa sasa kiasi kwambatunapelekwa jela na tunatishwa? Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Niabu Waziri wa Kilimomajibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye jibulangu la msingi lakini kama alivyoeleza kwenye swali lake lanyongeza kwamba uzalishaji uliathirika kwa wakulima wengikutokana na viuatilifu anasema hafifu, lakini pamoja namabadiliko ya tabianchi kutokana na mvua kubwailiyonyesha na ombi lake la kusema kwamba tuhamishe denihili mpaka msimu ujao, kwanza ushauri wake tunaupokealakini kwamba jambo hili linahitaji tufanye tathmini ya kinana kufanya uhakiki ili tubaini ni wakulima gani ambaowalipata na wakulima gani ambao hawajapata. Baada yauhakiki huo ndio tutaweza kutoa maamuzi kama Serikali naniambaye asamehewe mpaka mwakani na nani anastahilikulipa kwa sababu dawa ya deni ni kulipa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, utaratibu wakuwapatia mikopo au mbegu kama utaratibu wa zamani.Huo ushauri wake tunauchukua lakini kama anavyofahamu,hivi Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) pamoja na

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

unions, zile Ushirika Mkuu vilikufa, kama Serikali ndiyo tukokwenye mkakati mkubwa wa kuweza kuvifufua nchi nzima ilibaadae vikishakuwa vimeshahimili na kupata uzoefututaweza kurudisha majukumu hayo kwao, lakini kwa sasalazima kama Serikali tuweze kusimamia kwa sababu badovyama hivi ni vichanga, twende kwa utaratibu uliokuwepompaka hapo vyama hivi vitakapoimarika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hadji Mponda swali lanyongeza.

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogola nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Malinyi, Mkoa waMorogoro ni mojawapo ya Wilaya zinazolima zao la pamba.Sasa hivi karibu miaka mitatu zao hilo linaathirika na panyawaharibifu wanaokula mbegu za pamba mashambani,msimu wa kilimo karibu unakaribia (Desemba), maana yakemwezi ujao.

Swali langu je, Serikali ni lini wataleta viuatilifu (sumuya kuua panya hao) vya kutosha na kwa wakati muafaka?Nakushukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli, hasa Kanda yaMashariki iliathirika sana na athari ya wanyama hawa panya,wadudu panya, kuharibu mazao wakati wa kupanda. Lakininimwambie kwamba kama Serikali, mimi binafsi au kwa niabaya Serikali, tulishatembelea katika kituo chetu cha kudhibitipanya na kwa bahati nzuri kipo palepale Morogoro, Mkoanikwake na tulishawapa maelekezo kwa sababu mfumo waSerikali pesa tulikuwa tunawapelekea kwa bajeti, lakini kwakuzingatia msimu wa kilimo mwaka huu tumejipangakwamba pesa zote kwa mujibu zinahitajika kwenye sekta ya

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

414141

kilimo ziende kabla ya msimu ili zisipishane na msimu wa kilimo,ziende kutekeleza lengo lililokusudiwa.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba mwaka huu Serikali imejipanga na pesa hizi zaviuatilifu kuhusu wadudu wa panya zitaenda kwa wakati.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Pascal Haonga swali lanyongeza.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto zinazolikabilizao la pamba zinafanana kabisa na changamoto za zao lakahawa. Katika Kijiji cha Mbimba, Wilaya ya Mbozi kuna Kituocha Utafiti cha TaCRI ambacho kinafanya utafiti wamagonjwa ya zao la kahawa pamoja na mbegu za zao lakahawa. Lakini kituo hiki cha TaCRI hakijapelekewa fedhakwa muda mrefu sana ili kiendelee kufanya utafiti wa mbegubora ya kahawa.

Je, ni lini sasa Serikali itapeleka fedha kwenye kituohiki cha TaCRI kilichopo Mbozi ili kiendelee kufanya kazi vizurikabisa, kufanya utafiti pamoja na kupeleka mbegu kwawakulima wa zao la kahawa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimomajibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika Wilaya ya Mbozi tunaKituo chetu cha TaCRI ambacho ni Kituo cha Utafiti cha Zaola Kahawa, na kituo hiki kinapata bajeti yake kupitia sehemumbili ambao ni kupitia Serikalini na sehemu kupitia wadauwengine wa maendeleo, sisi kama upande wa Serikali, kamaunakumbuka mwaka jana tulileta sheria hapa na ikapitishwana Bunge lako, Sheria Na. 10 ya TARI kwa vituo vyote vyautafiti kuwa katika mwavuli mmoja na baada ya hapo kilakimoja kitapelekewa pesa kutokana na bajeti yake.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka huu, kamanilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba baada yakujua mahitaji hayo ya Sekta ya Kilimo kama Serikali pamojana Kituo hiki cha TaCRI tutakipelekea fedha kwa mujibu wabajeti yao na kwa wakati.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Richard Mganga Ndassaswali la nyongeza.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye swali la msingilinazungumzia kuhusu changamoto za zao la pamba, lakinikuhusu viuatilifu ni kwamba vinaletwa ambavyo havinaviwango na ndiyo maana inasababisha wadudu kutokufa.

Swali langu, je, ni lini sasa uchakachuaji huu wamadawa ya kuua wadudu wa pamba utaisha?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimomajibu kwa swali hilo.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli hayo malalamiko yapo, siyoMwanza tu au Kanda ya Ziwa, ni sehemu kubwa yawanaolima pamba, kwamba kuna viuatilifu ambavyovimeonekana kwamba haviui hao wadudu wa pamba, lakinisisi kama Serikali baada ya kupata tatizo hili tuliwatumawataalam wetu kwenda kufanya uhakiki na tathmini kamayale yanayosemwa ni kweli. Wataalam hawa walivyokwendahuko wamethibitisha mbele ya wakulima sehemu zinginekwamba imegundulika kwamba ni matumizi hafifu au uelewamdogo wa baadhi ya wakulima walionao wa jinsi ya kutumiayale madawa kwa sababu wale wataalam waliwathibitishiambele yao yalionekana kwamba yale madawa yanaua.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, nitoe wito kwawakulima; kwa sababu tuna Taasisi yetu ya Udhibiti waViuatilifu na Madawa yote kwa maana ya TOSCI, kwa yeyote

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

434343

ambaye anaona kwamba ile dawa haijaua waweke countersample ili dawa ile kama imeonekana na imethibitishwa haiuituirudishe kwa wataalam na ikithibitishwa basi wale wakulimawatafidiwa na hiyo kampuni ambayo imesambaza mbeguhizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ila nimhakikishie mwaka huuTaasisi yetu ya TPRA iko vizuri na zingine kwa ajili ya udhibitiwa viuatilifu hivyo, hili tatizo halitatokea tena.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni swalila nyongeza.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kuweza kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la msingi hapalinalozungumziwa ni tatizo la pamba. Zao la pambalimewakumba matatizo makubwa sana kwa wakulima,viuatilifu vimekuwa ni moja ya matatizo, lakini kuna pambawananchi walipanda ikakua kama miti badala ya kuwapamba ya kawaida. Sijui ni kwa nini sasa Serikali na hasakupitia Wizara hii ya Kilimo, mnafikiri mtafanya nini kuwapastahili wakulima hawa ambao wamepata hasara sana katikamsimu huu ambao umekwisha?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimomajibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la msingi anataka kujuakwamba Serikali tutafanya nini kuwalipa fidia wakulimaambao wamepata madhara ama ya mbolea feki aukutokana na pamba kukua bila kutoa matunda. Kamanilivyosema kwenye jibu la awali, jambo hili hatuwezikuchukua kwa ujumla wake, ni vizuri kwanza timu ikaendaikafanya tathmini na ikafanya uhakiki ili tupate walewalioathirika zaidi, tukibaini hao walioathirika then Serikalitutajua nini cha kufanya.

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, MheshimiwaDeogratias Francis Ngalawa, Mbunge wa Ludewa sasa aulizeswali lake.

Na. 80

Tatizo la Mawasiliano ya Simu

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA aliuliza:-

Kumekuwa na tatizo kubwa la mawasiliano ya simukwenye Tarafa ya Mwambao, Wilaya ya Ludewa, Mkoa waNjombe, eneo hili lina urefu wa kilometa 150 na lina vijijivisivyopungua 22.

Je, Serikali ina mpango gani wa kupelekamawasiliano kwenye maeneo hayo ambayo pia ni ya kiulinzina nchi jirani na ni tarafa pekee ambayo haina mawasilianoya simu kabisa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naombanitoe shukrani za dhati kwa Mwenyezi Mungu, mwingi warehema kwa kuniokoa na ajali mbaya kabisa iliyotokea juzijioni, saa kumi baada ya gari niliyokuwa nikitumia kupindukakama mara tano, lakini Mungu ametusaidia tumetokasalama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru WaheshimiwaWabunge wote waliopata nafasi ya kunitumia message, hatakunipigia simu kwa ajili ya kunipa pole, ninawashukuru hatawananchi wa jimboni kwangu ambao walipata nafasi yakunipigia simu au kunitumia salamu, namshukuru Mungunaendelea vizuri, afya yangu iko salama kabisa. (Makofi)

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

454545

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho nimshukuru sanaMheshimiwa Ndassa ambaye baada ya dakika tano tu alifikaeneo la ajali akiwa njiani naye kuelekea huku Dodomaambaye vilevile aliweza kunipa lifti mpaka kufika Dodomasalama na kunipeleka hospitali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya shukrani hizo, kwaniaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Deogratias FrancisNgalawa, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimuwa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya mipakanimwa nchi yetu hususan katika kuimarisha ulinzi na usalama.Hivyo Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Woteiliziainisha kata nne za Tarafa ya Mwambao na kuziingizakatika zabuni iliyotangazwa mwezi Februari, 2017 na Kata hizoni Lumbila, Kilondo, Makonde na Lupingu. Kazi ya ujenziilitolewa kwa Kampuni ya Simu ya Viettel (Halotel) ambayoilishinda zabuni na huduma ya mawasiliano inategemewakupatikana kuanzia mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Deogratias Ngalawa swalila nyongeza.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawiliya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nipende kuishukuruSerikali kwamba hizo kata ambazo Mheshimiwa Naibu Waziriamezitaja, kwa maana ya Kata za Lupingu, Makonde,Lumbila na Kilondo, tayari mkandarasi yupo kazini. Sasaninachopenda kuuliza ni kuwa je, ni lini minara hiyoitawashwa; kwa sababu baadhi ya minara tayariimeshajengwa lakini kuwashwa bado, ni lini itawashwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kuna baadhi yamaeneo ambayo tayari tuliomba mfano Kata ya Ludende,

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Kata ya Lupanga na Kata ya Iwela, ni lini Serikali itatufikiriakwenda kujenga tena mawasiliano mengine?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Deogratius Ngalawakwa sababu bahati nzuri nimekwishafanya naye ziara kwenyeJimbo lake la Ludewa, hasa Kata ya Mwambao ambakotulitembelea maeneo ya Lupingu, Vijiji vya Nindi, Mtumbatu;lakini tulitembelea Kata ya Makonde kwenye Vijiji vyaManyanya na Liunji; vilevile tulitembelea Kata ya Kilondokwenye Vij i j i vya Kilondo Kij inini na Nsele na kuonachangamoto za mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini na yeye mwenyeweamekiri kwamba tayari kuna baadhi ya minaraimeshawekwa, tulikuwa bado tuna changamoto ya batterykwa sababu maeneo yale Mheshimiwa Mbunge anaendeleakufanya jitihada ya kuhakikisha kwamba umeme wa REAunafika na sisi kwa sababu tunahitaji watu wawasilianetuliweka system ya solar ambayo betri zake zilikuwa zinachangamoto kidogo na sasa nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba battery zimekwishafika na ndiyo maananimezungumza kwa uhakika kwamba inapofika mwishonimwa mwezi huu basi tutakwenda kuwasha hiyo minara.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu Kataza Iwela, Lupanga na Ludende, kuna orodha ambayotunaendelea kuiandaa ambayo mwisho wa mwezi huutunategemea tutakuwa na kata zaidi ya 206 ambazotutakwenda kuziweka kwenye programu ya kuwapatiamawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo MheshimiwaMbunge nakushauri itakapofika kipindi hicho uje tuwasilianeofisini ili uangalie kama vijiji vyako kwenye kata hizo vitakuwavimewekwa. Ahsante. (Makofi)

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

474747

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zuberi Kuchauka swali lanyongeza.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kuniona na kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya yaLiwale yenye kata 20 ni kata tano tu zinafikika kwamawasiliano ya simu. Nini kauli ya Serikali ili kuwapatiawananchi wa Kata za Mirui, Mkutano, Mtungunyu, Lilombe,Ngongowele, Mpigamiti pamoja na Mlemwe ili wawezekupata mawasiliano ya simu?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika,ni kweli kuna changamoto kubwa sana ya mawasiliano katikaJimbo la Liwale na hivi karibuni nilituma timu yangu yawataalam kutoka TCRA na UCSAF kwenda kukagua maeneohayo ambapo tayari nasubiri taarifa hivi karibuni, zitakapokujatunategemea kwenye hizi kata 203 tunazotegemeakuzitangaza na wao watakuwepo. Tuna nia ya kuhakikishakwamba wananchi wanapata mawasiliano nchi nzimakuhakikisha kwamba usalama na uchumi wao unalindwaipasavyo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rashid Shangazi swali lanyongeza.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kumuulizaMheshimiwa Waziri, ni lini sasa mawasiliano katika Kata yaMalindi, Kijiji cha Makose na katika Kijiji cha Chagoka Kataya Rangwi, lakini pia katika Kijiji Longoi eneo la Bustani

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

yatakamilika kwa sababu ndiyo maeneo pekee ambayoyamebaki katika Jimbo la Mlalo, Halmashauri ya Lushoto?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika,ni kweli Vijiji vya Makose, Kata za Langoi, Bustani na Kinkopamoja na Goka mawasiliano ni hafifu sana. Serikali kupitiaMfuko wa Mawasiliano kwa Wote imeendelea kufanyauchambuzi kuhakikisha kwamba minara iliyopo jiani kwanzainaongezewa nguvu kuweza ku-cover eneo kubwa sana lamawasiliano; lakini pili, tumeendelea kuyaainisha maeneoambayo hayataweza kufikiwa na improvement ya minarahiyo kuanza kuweka minara mipya.

Namshauri Mheshimiwa Mbunge tuendeleekuwasiliana kwa sababu mara nyingi kwa kweli nampongezakwa jinsi anavyofuatilia suala la mawasiliano kwa wananchiwake. Tuendelee kuwasiliana naye ili kuona vijiji ambavyohavitafikiwa baada ya kupata ripoti ya watu wa TCRA naUCSAF tuweze kuviingiza kwenye mpango ambao mwishowa mwezi huu tutatangaza hizo orodha za kata na vijijivitakavyowekewa mawasiliano.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwita Getere swali lanyongeza.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Nimpe pole ndugu yangu, MheshimiwaEngineer Nditiye na kwa sababu humu ndani kuna bibi, kunamke wa Chifu Makongoro ana miaka 100 na amekuonaatakuombea ndugu yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuuliza swali,Serikali imekuwa ikiahidi kujenga minara katika Vijiji vyaNyangere, Nyaburundu, Tiling’ati na Jabuzunde kwa mudamrefu sasa. Sasa ni lini ahadi ya Serikali itatekelezwa?

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

494949

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika,ni kweli kuna changamoto katika Vijiji vya Nyandetere naTimati na maeneo kadhaa ambayo ameyaruka kidogo, lakininimuahidi tu Mheshimiwa Getere kwamba mwezi ujaotutakuwa wote jimboni kwake kwa ajili ya kuchunguzamaeneo mengi zaidi tuhakikishe kwamba wananchi wa jimbolake wanapata mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwanza nichukuenafasi hii kuwapongeza Watanzania wote kwa ujumla,kwamba tunapoelekea uchumi wa kati ambao ni waviwanda mwaka 2025, tumeona jinsi ambavyo wananchiwanahitaji mawasiliano kiuchumi na kiusalama na ndiyomaana sasa hivi huwezi kusikia tu changamoto za maji,barabara, umeme bila kusikia changamoto za mawasiliano,ni kwa sababu kila mwananchi sasa hivi (asilimia 94) anamilikisimu za mkononi na anahitaji mawasiliano na sisi kama Serikalituendelee kuwahakikishia wananchi kwamba tumejipangakuhakikisha kwamba kabla ya mwezi Machi mwakanitutakuwa na asil imia 99 ya wananchi wote ambaowanawasiliana ili kufanya kwamba shughuli zao za kiuchumiziwe imara na usalama wao uimarike zaidi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vedasto Ngombale swalila nyongeza.

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itajenga minaraya mawasiliano katika Viji j i vya Mtumbei, Mpopera,Kandawale, Kibata, Nandete na Kinjumbi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano majibu.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika,Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imeendeleakuorodhesha maeneo mbalimbali ya nchi yetu ambayohayana mawasiliano na vijiji ulivyovitaja Mheshimiwa ninahakika vimo, lakini kwa uhakika zaidi, kama hutajali, upatenafasi uje ofisini ili ujiridhishe mwenyewe kwenye databaseyetu kwamba vijiji ulivyovitaja vimo na vitatangazwa kablaya mwezi huu kuisha kuhakikisha kwamba tunapelekamawasiliano maeneo hayo. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana Mheshimiwa Mbaraka Kitwana Dau, Mbunge wa Mafia.

Na. 81

Hitaji la Kivuko Maalum Kilindoni na Nyamisati

MHE. MBARAKA K. DAU aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga kivuko maalum (landingcraft) kwa usafiri wa Kilindoni (Mafia) na Nyamisati (Kibiti)?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwaniaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianoninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbaraka Kitwana DauMbunge wa Mafia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala waUfundi na Umeme (TEMESA) katika mpango wa bajeti wamwaka 2018/2019 imepanga kunua Kivuko kwa ajili ya usafiriwa majini katika bahari ya Hindi kati ya Nyamisati na kilindoniMafia Mkoani Pwani ili kutoa huduma salama ya kuvushaabiria na mizigo na hivyo, kukuza uchumi wa wananchi wamaeneo haya.

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

515151

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala wa Ufundi naUmeme umeanza taratibu za ununuzi wa kivuko hiki ambakozabuni kwa aji l i ya ununuzi wa nkivuko hicho kipyakitakachokuwa na uwezo wa kubeba uzito wa tani 100 sawana abiria 200 na magari madogo sita imetangazwa tarehe24 Oktoba, 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo Wizarakupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandara (TPA) mwaka 2013ilikamilisha ujenzi wa gati katika eneo la Kilindoni, KisiwaniMafia. Kwa sasa Wizara inaendelea na ujenzi wa gati upandewa Nyamisati Wilayani Kibiti pamoja na miundombinumingine yaani nyumba na ofisi ya Mhandisi, jengo la mizigona abiria na maliwato. Mradi huu ambao utatekelezwanaMkandarasi Alpha Logistics and Southern EngineeringCompany JV kwa gharama ya shilingi 14,434,673,467 ulianzatarehe 16 March, 2018 na umepangwa kukamilika ndani yamuda wa miezi 12.

Mheshimiwa Naibu Spika, maendeleo ya ujenzi waGati ya Nyamisati pamoja na ujenzi wa miundombinu minginekatika eneo hilo hadi sasa umefikia kiasi cha 35% namkandarasi ameshalipwa kiasi cha shilingi 1,373,073,256.71.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbaraka Kitwana Dau swalila nyongeza.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Naibu Spika,ninakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali inakiri botihii itakuwa tayari baada ya mwaka mmoja; na kwa kuwakatika kipindi chote hicho wananchi wa Mafia wataendeleakutumia vyombo hatarishi vya baharini vilivyojengwa kwamagogo; na kwa kuwa Serikali imeshasema kwamba boti hiiitakamilika ifikapo mwaka 2019; na kwa kuwamfanyabiashara maarufu Bakharesa ametoa boti bure kwaSerikali ambayo hivi sasa inamaliziwa matengenezo; na kwakuwa wataalam wa DMI ambao wamekabidhiwa boti hiyowameshakuja Mafia na wamejiridhisha na miundombinu na

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

kupanga nauli kinachosubilika sasa ni Mheshimiwa sana Wazirimwenye dhamana kuridhia tu boti ile ije Mafia na kuanzakutoa huduma.

Je, ni lini sasa Mheshimiwa Waziri ataridhia boti ileiliyotolewa na mfanyabiashara Bakharesa ije Mafia na ianzekutoa huduma? Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili MheshimiwaNaibu Waziri Gati la Kilindoni lipo katika hali mbaya sana,mbao zimechakaa, ngazi imechakaa na pepo za Kaskazizinatarajia kuanza wakati wowote hivi sasa.

Je, ni lini sasa Wizara itaiagiza Mamlaka ya Usimamiziwa Bandari (TPA) kufanya ukarabati mkubwa wa Gati laKilindoni ili likidhi hadhi ya kuchukua abiria? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu, Mheshimiwa Nditiye.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Waziri,ahsante sana kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano napenda kwanza kumpongeza Naibu Wazirimwenzangu kwa majibu yake mazuri lakini naomba nijibuswali la Mheshimiwa Mbaraka Dau maswali yake mawili kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikiri kwambatulikuwa na kikao kirefu sana kati ya Mheshimiwa MbarakaDau ambaye anafuatilia sana changamoto za usafiri wamajini kwa wananchi wake, lakini tulikuwa na watu wa DMIna pia tukawa na watu wa bandari katika kuhakikishakwamba hiyo meli ambayo DMI walipewa na Bakharesainaweza kuanza kufanya kazi na process zote ambazotulikuwa nazo mimi na Mheshimiwa Mbaraka Dau anazijua,tulifanya kikao na tukakubaliana sasa ile boti ianze kufanyasea test. Siku ambayo tulikuwa tumekubaliana ifanye sea testkukawa na hali mbaya ya hewa ambako boti nyingi sana

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

535353

hata Zanzibar hazikuweza kwenda, tukaahirisha kwa ajili yakufanya siku nyingie.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuhakikishie tuMheshimiwa Mbunge kwamba Serikali bado ina nia yakuwasaidia wananchi wa Mafia kwa dharura hiyo kwasababu mpango endelevu ni wa kutengeneza kivukokikubwa, lakini hivi karibuni tutaanya tena sea test halafututapanga namna ya kuanza safari za kutoka Mafia mpakaDar es Salaam Mjini katikati.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kunawataalam ambao tumeshawatuma kutoka bandariMamlaka ya bandari kwa ajili ya kwenda kufanya tathiminina ripoti imekwishakuwa tayari tunaangalia namna sasa yakuanza kutafuta mkandarasi wa kurekebisha hiyo Gati yaKilindoni ambayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Mafia.Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Dkt. Charles Tizeba Mbunge wa Buchosa.(Makofi)

MHE. DKT. CHARLES J. TIZEBA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza, lakini kabla sijauliza swali hilo niruhusu nisememaneno mawili tu, la kwanza ni kumshukuru Mheshimiwa Rais,namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa fursa aliyokuwaamenipa ya kulitumikia Taifa. Pia nikushukuru wewe naMheshimiwa Spika kwa ushirikiano nilioupata wakatinikitumika Serikalini ndani ya Bunge lako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naswali dogo lanyongeza, kwamba Jimbo langu la Buchosa linavyo visiwazaidi ya 28 na katika Visiwa hivi 28 kuna vivuko viwili kivukokimoja kimepitwa na wakati kinakuwa overloaded na watuwakati mwingine wnaogopa hata kukipanda, hili jamboMheshimiwa Naibu Waziri Kwandikwa analifahamu vizuri,ninachoomba kujua, je, commitment ya kujenga kivuko kipyakati ya Nyakalilo na Kome bado iko palepale au la? (Makofi)

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kwandikwainavyoonekana majibu ya swali hili yanasubiriwa na Bungezima kwa namna ya Mheshimiwa alivyopokelewa humundani.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza na mimi nimshukuru Mungu kupata nafasi ya kujibuswali la Mheshimiwa Tizeba ambalo limepigiwa makofi mengisana. Lakini maalum nimshukuru Mheshimiwa Tizeba kwasababu tulitembelea Jimboni kwake, tulitembelea Kivuko chaNyakalilo na nilijionea shida wananchi wanayopata kuvukakwenda kule Kisiwani. Lakini pia nil ishuhudia juhudiMheshimiwa Mbunge alifanya ili kuhakikisha kunakuwa nauchumi, kuna shughuli za uvuvi, kuna kilimo cha misitu kule,fursa ziko nyingi lakini kikwazo pia ni usafiri wa kuvuka kwendakule visiwani.

Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na wananchiwa Buchosa kwamba tumeunda timu maalum ambayoinatembelea maenewo yote ya vivuko na itawasilisha taarifakwa ajili kuboresha kuangalia namna nzuri ya kuendeleavivuko vyetu. Na katika eneo hilo la Nyakalilo tuliona namnajinsi ambavyo watu kupanda tu kwwenye kivuko mpakawanagombana wanapigana hadi ngumi kwa sababu yauwezo mdogo wa kivuko ulichokuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo MheshimiwaTizeba nikuhakikishie ni kwamba tutabadilisha kile kivukoutaratibu unaendelea vizuri na nitaendelea kukupa mrejeshohatua ya haraka ambayo tunaifanya ilituweze kuboreshausafiri wa kwenda Buchosa, lakini il i tuweze kwendasambamba na mahitaji ya ongezeko la watu na huduma zakijamii ambazo ziko katika eneo lako Mheshimiwa Tizeba.Nashukuru.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tunaendelea na swali laMheshimiwa Philipo Augustino Mulugo, Mbunge wa Songweswali lake litaulizwa kwa niaba na Mheshimiwa Victor KilasileMwambalaswa, Mbunge wa Lupa.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

555555

Na. 82

Barabara ya Mbalizi - Makongolosi

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. PHILLIPOA. MULUGO) aliuliza:-

Serikali kupitia TANROADS walishafanya upembuziyakinifu kwenye barabara ya Mbalizi - Makongolosi tokamwaka 2013 lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.

Je, ni lini Serikali itaanza kuweka lami barabara hiyo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI, UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA)alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika,kwa niaba ya Waziri waUjenzi Uchukuzi na Mawasiliano napenda kujibu swali laMheshimiwa Philipo Augustine Mulugo Mbunge wa Songwekama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Mbalizi hadiMakongolosi ni barabara ya Mkoa yenye urefu wa kilometa116.98 ambayo inahudumiwa na Wakala wa BarabaraTanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe na Mkoa wa Mbeya.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ni muhimu sanakwa wananchi wa Mkoa wa Songwe na Mkoa wa Mbeyakwa kuwa inapita Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe kwakupitia Mbalizi Mkoa wa Mbeya na inapita katika machimboya madini ya Shanta eneo la Saza lililoko Wilayani Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa kwakutambua umuhimu wa barabara hii Serikali imefanya kaziya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuijengakwa kiwango cha lami sehemu ya Mbalizi hadi Galula yenyeurefu wa kilometa 56 na Serikali imekuwa ikitenga fedha kila

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

mwaka kupitia TANROADS Mkoa wa Songwe na Mkoa waMbeya kwa ajil i ya kuifanyia matengenezo ya ainambalimbali ili iweze kupitika majira yote ya mwaka ambapokatika mwaka wa fedha 2017/2018 ilitenga kiasi cha shilingimilioni 553.920 kupitia TANROADS Mkoa wa Songwe na kiasicha shilingi milioni 441.885 kupitia TANROADS Mkoa wa Mbeyana katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali imetenga kiasicha shilingi milioni 633.920 kupitia TANROADS Mkoa waSongwe na kiasi cha shilingi milioni 730.778 kupitia TANROADSMkoa wa Mbeya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutafutafedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami sehemuya barabara iliyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wakina kuanzia Mbalizi hadi Galula kilometa 56.0 na kwa ajili yakuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina sehemu yabarabara iliyobaki ya kuanzia Galula - Mkwajuni hadiMakongolosi kilometa 61.

NAIBU SPIKA:Mheshimiwa Victor Mwambalaswa swalila nyongeza.

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili madogo yanyongeza.

La kwanza sasa hivi Bunge lako linakaa kama Kamatiya Mipango tunapanga mpango wa mwaka kesho bajeti2019/2020 na hii barabara ya Mbalizi - Makongolosi nibarabara ambayo inaunganisha mikoa miwili Mkoa waSongwe na Mkoa wa Mbeya na Serikai imesema imefanyaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara hi kutokaMbalizi mpaka Galula.

Je, kwenye bajeti ijayo Serikali itatenga fedha kidogoili barabara hii ianze kujengwa kwa lami kidogo kidogo? Lakwanza. (Makofi)

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

575757

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili hii barabara ikifikapale Makongolosi inakuta na barabara inayotoka Mbeya -Chunya - Makongolosi kwenda Rungwa. Hasa barabara hiyokutoka Chunya kwenda Makongolosi inajengwa kwa lamisasa hivi na imepata mkandarasi ambaye yuko kazini.Mheshimiwa Waziri alipita mwezi wa nane akamkuta huyumkandarasi kwanza ana vifaa vichache, pili kasi yake nindogo.

Je, Serikali inachukua hatua gani kurekebisha huyumkandarasi ili ajenge katika mkataba ambao tulikuwatumesainiana naye? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) Mheshimiwa Naibu Spika, kamanilivyosema kwamba tuna fedha zikipatikana mara mojatutaaanza kujenga hii barabara kama nilivyosema katika jibulangu la msingi. Kwa hiyo tukipata fedha tuaanza ujenzi wabarabara hii. Lakini pia niseme tu kwamba mimi wkelinilitembelea barabara hii na maeneo yote ambayo yalikuwakorofi tayari yalikuwa yameshawekewa klipande cha lamimuda mrefu na kipande hichi kimechoka kwa hiyo umuhimuwa kujenga barabara hii upo tutajenga.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuhusu barabara hiiya Makongolosi hadi Chunya kweli ni kilometa chachekutoka upande wa Songwe zitaunganika na hii barabaraambayo tunajenga kiwango cha lami upande huu waChunya. Lakini kasi kweli ilikuwa ndogo na mimi nilifika eneola mkandarasi huyu lakini tu nimfahamishe MheshimiwaMbunge kwamba Mheshimiwa Waziri alishachukua hatuatayari za kuhakikisha kwamba ujenzi huu unachukua kasi yakekama Serikali tunavyotegemea, na mkandarasi kamaunavyojua Mheshimiwa Mbunge wale wataalamwaliokuwepo tuliona kwamba wana mapungufu naMheshimiwa Waziri alielekeza wale waondolewe ili tupatewataalam ambao mkandarasi atawatumia kuhakikisha

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

kwamba ile kasi ambayo tunaitegemea kama Serikalikwamba tunaipata lakini pia tunapata ubora lakini wananchiwanahitaji kwa muda mfupi waweze kutumia barabara hii,kwa hiyo hatua tayari imeshachukuliwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Innocent Bilakwate swalila nyongeza.

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza,barabara ya kutoka Mgakolongo kwenda Kigalama,Ugomola mpaka Mlongo ni ahadi ambayo imehaidiwa mudamfrefu na barabara hii bado haijatengenezwa kwa kiwangocha lami.

Mheshimiwa Naibu Waziri naomba kujua ni linibarabara itajengwa kwa kiwango cha lami ili kuondoa keroambayo iko kwa wananchi wetu?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweliharakati za ujenzi wa barabara hii kutoka Mgakolongo -Kigalama hadi Mulongo tulishaanza usanifu na tulikuwa tupokwenye hatua za mwisho. Mara ya baada ya usanifu wabarabara hii Mheshimiwa Bilakwate na wananchi wa Kyelwana maeneo ya Jimbo la Karagwe niwahakikishie tu kwambatutaanza kujenga kwa sababu utaona kwamba liko hitajieneo hili la Mulongo ni eneo ambalo lina miteremko mikalisana, ni hatari, lakini utaona ule upande wa wenzetu upandewa Uganda wameshatengeza barabara tayari kwa sababuya mkakati ule wa kuunganisha nchi yetu na nchi jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, upo umuhimu wa kufanyaujenzi wa barabara hii pia tutaanza hivi karibuni kupanuadaraja hili la Mulongo, kwa sababu daraja lile lina muda mrefuna lilitengenezwa kwa teknolojia ya zamani, kwa hiyo uleutaratibu wa kutengeneza daraja hili katika eneo hili la

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

595959

Mulongo Mheshimiwa Mbunge nikufahamishe pamoja nawananchi kwamba tunaanza kulipanua daraja hili, lakinitutakapokamilisha usanifu wetu ujenzi wa barabara hiimuhimu kilometa utaanza kujengwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Oran Njeza swali lanyongeza.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kunipa fursa na mimi ya kuuliza swali lanyongeza. Kama ilivyokuwa umuhimu wa barabara ya Mbalizi- Makongolosi vilevile kuna barabara ya kutoka Mbalizi -Shigamba mpaka Isongole ambayo ni muhimu sana kiuchumina vilevile ni ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nnena pia na ahadi ya Mheshimiwa Rais wetu.

Je ni lini hii barabara itajengwa kwa kiwango chalami? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) Mheshimiwa Naibu Spika,Mheshimiwa Mbunge anatambua kwamba miminilitembelea eneo hili na nafahamu kwamba yako maeneoambayo ni korofi lakini pia kuna sehemu kubwa ya uzalishajikatika eneo hili. Pia kwa sababu tumeshaanza kujengabarabara ile inayokwenda Ileje ni muunganiko mzuri wawananchi wa maeneo haya, kwa hiyo tunaendelea naharakati za kufanya maandalizi ya awali ili kuhakikishabarabara hii muhimu tunaijenga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo MheshimiwaMbunge hii ni ahadi ya viongozi wakuu, awamu ya nne ilikuwani ahadi pia kwenye mpango mkakati wa ujenzi wa barabarahii tumeionyesha kwa hiyo nikuombe tu uvute subira yakomaboresho ya barabara kwenye eneo lako MheshimiwaMbunge ambayo tunayazingatia kwa sababu hukoumuhimuwa wakuwaunganisha wananchi wa Ileje wakipita

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

kwenye maeneo ya kwako kwenda upende ule wa Kyela.Kwa hiyo, tunaitazama kwa macho mawili pia itakuwamsaada mkubwa wa kupunguza misongamano ambayo siyoya lazima katika Jiji la Mbeya. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ester Bulaya swali lanyongeza.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua Serikali ina mkakatiwa kujenga hizi barabara za pete kwa kiwango cha lamikwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Pwani na Dar es Salaamkwa mfano barabara ya kutoka pale stand ya Kibahaunatokea Baobao kabla ya mpakani mwa Dar es Salaamna Bagamoyo lakini na barabara hii ya Makongo - Goba -Kimara.

Sasa nilitaka kujua ni lini hizi barabara zitajengwa kwakiwango cha lami kwasababu ni kweli zinapunguza foleni nakusaidia watu wengi ambao wanasafiri kutoka mikoambalimbali kuja Dar es Salaam au kutoka Dar es salaamkwenda Dodoma? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi naUchukuzi majibu.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Naibu Spika,ingefaa Mheshimiwa Bulaya labda baadae tunawezatukakaa kwa sababu ile mikakati ilyopo ni mingi ili niwezekuipata sawasawa nikushauri tu ukipata nafasi tuwezekuzungumza.

Lakini kwa ufupi kabisa niseme kwamba tunaendeleakuhuisha mipango mbalimbali ambayo ipo. Tulikuwa na uleuratibu wa kutengeneza barabara ya njia sita kutoka Mbezikwenda ule upande wa Pugu, lakini kutoka Mbezi kwendaupande wa Bunju, lakini tumeona kwamba tuitazamesambamba na kuona ule ukuaji ukija huku upande wa

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

616161

Kibaha, sasa tunatazama hii barabara ya njia sita ili tujekutoka Kibamba kwenda Bunju na kutoka Kibamba kutafutauelekeo ule wa kwenda Pugu. Kwa hiyo tunaendelea nausanifu ili kuona the best way tunaweza tukaziona hizibarabara zinakaa vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hizi barabara sasakama tutafanya marekebisho ina maana barabara za kutokaMbezi zinaweza zisiwe na njia sita zikabakia njia mbili ilikuruhusu sasa ujenzi uje Kibamba wkahiyo bado tunafanyamapitio, ndiyo maana nikushauri tu upate nafasi ili tuwezekuangalia network nzima ya Jiji na Dar es Salaam kwa sababunjia sita zitakavyokuwa zinakuja Kibaha bado kutakuwa namvuto mkubwa sana wa kuyachochea magari mengiyanayotoka katikati ya mji kwamba inaweza ikasababishatena foleni kwa upande huu. Kwa hiyo tunaitazama kwamacho mawili.

Kwa hiyo nikushauri tuonane ili angalau uipate sawasawa ili wananchi wanayo nafasi ya kuwajulisha namna nzuriSerikali inafanya ili kuboresha usafiri wa Jiji la Dar es Salaam.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kiruswa swali lanyongeza.

MHE. DKT. STEPHEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuruna mimi naomba niulize swali dogo lanyongeza.

Kwa kuwa kuna umhimu mkubwa wa kutengenezahizi barabara za bypasses (za pete), kuna barabara nzuri hiya kutoka Lingido kwenda Kilimanjaro kupitia Siha na ni mojaya barabara ambazo zimebainishwa katika ilani ya Chamacha Mapinduzi 2015/2020 na ninaomba kuuliza, je, ni lini sasamchakato wa kujenga barabara hii kwa kiwango cha lamiutaanza? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mwasiliano majibu.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweliupo umuhimu wa kujenga hizi barabara za bypass nanimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge tumezungumza maranyingi, lakini na mimi pia nilitembelea eneo hili kuona logisticza kuunganisha barabara hii ya kwenda Longido.Nilivyotembelea hii barabara, ukitoka Bomang’ombe kunahuu mradi ambao unatoka Lelai kwenda Kamwanga ambaopia utakuwa kiungo kizuri cha hii bypass ambayo inakwendaLongido.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie tukwamba tunaitazama kwa makini barabara hii. Iko ile hajaya kuiunganisha barabara hiyo na kwenye mradi huo wabarabara ambao tutakwenda Kamwanga kwenda kuungaupande ule wa Rombo tutaitaza kwa macho mawili kipandehiki ili kiweze kuunganika na barabara hii muhimu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Amina Makilagi swali lanyongeza

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali moja lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Musoma -Busekela - Makojo mpaka Bukumi ilifanyiwa upembuzi yakinifutangu miaka mitatu iliyopita na Mheshimiwa Rais alivyofanyaziara Mkoa wa Mara mwezi mmoja uliopita aliagiza barabarahii ijengwe kwa kiwango cha lami na tender itangazwe maramoja. Ningepanda kujua tangu Rais ametoa maelekezo hayampaka sasa hatua imefikia wapi ili barabara ya Majita -Busekela - Makojo iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

636363

kabisa Mheshimiwa Rais alivyofanya ziara katika mkoa alitoamaelekezo na mimi nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge nawananchi wa Mara kwa ujumla wake kwamba tayari hatuaza kutangaza ujenzi wa barabara Mheshimiwa Rais alitoamaelekezo kwa barabara inayotoka Bunda MheshimiwaMbunge umeitaja, kwa hiyo, hii barabara inatangazwa kwaajili ya ujenzi lakini iko barabara nyingine kwa upande huowa Mara kutoka kule Nata, Sanzate na yenyewe iko katikahatua ya kutangazwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilihakikishie tuBunge lako na Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kutekelezamaelekezo ya Mheshimiwa Rais na nimushukuru sanaMheshimiwa Rais anatupa support kubwa ili na sisi kamaWizara tuendelee kutekeleza majukumu ya Wizara kwaumahiri mkubwa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Wizata yaElimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Susan Anselm Lyimo,Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swali lake.

Na. 83

Wizi wa Kuvuja kwa Mitihani

MHE. SUSAN A. J. LYIMO aliuliza:-

Wizi wa kuvuja kwa mitihani hapa nchini umekuwaukijirudia mara kwa mara na kwa ngazi zote.

Je, Serikali ina maelezo gani?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Elimu, Sayansina Teknolojia majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Mheshimiwa Susan Anslem Lyimo, Mbunge wa Viti Maalumkama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha kuwaelimu yetu ni bora, Serikali imeendelea kuchukua hatuambalimbali ikiwemo kuhakikisha kuwa usimamizi nauendeshaji wa mitihani unafuata sheria, kanuni na taratibuzilizopo katika ngazo zote za elimu. Matukio ya udanganyifukatika mitihani au wizi wa maswali ya mitihani yamekuwayakitokea kenye baadhi ya shule au Halmashauri katika ngaziya elimu ya sekondari na msingi na wahusika huchukuliwahatua kwa mujibu wa sheria na taratibu. Aidha, katika ngaziya vyuo hakuna wizi wa mitihani ulioripotiwa isipokuwa yapomatukio ya udanganyifu na inapotokea hatua huchukuliwakwa mujibu wa kanuni za mitihani za chuo husika.

Mjheshimiwa Naibu Spika, Serikali imesikitishwa sanana tukio la hivi karibuni la baadhi ya viongozi wa elimu nawakuu wa shule kujihusisha na kusambaza maswali ya mitihaniya kuhitimu darasa la saba katika Halmashauri ya Wilaya yaChemba kwa lengo la kufanya udanganyifu. Tatizo hilo pialilitokea katika baadhi ya shule za msingi kwenye Halmashauriza Kondoa, Kinondoni, Ubungo, Temeke na Mwanza Jiji.Kufuatia tukio hilo, Serikali imechukua hatua zifuatazo:-

Kwanza kufuta matokeo ya mtihani na kurudiwa kwamtihani huo kwa shule zilizohusika na pili kuwachukulia hatuawaliohusika na usambazaji wa maswali ikiwa ni pamoja nakuwasimamisha kazi, kuwavua madaraka na kuwafikishakwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukua mkondo wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeleakuimarisha ulinzi na usalama wa mitihani katika ngazo zoteza elimu. Aidha, Serikali itaendelea kuchukua hatua kali zakisheria kwa mtu yoyote atakayebainika kujihusisha navitendo vya wizi na udanganyifu katika mitihani nchini.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan Lyimo swali lanyongeza.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

656565

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitegemea kwambaMheshimiwa Naibu Waziri au Wizara kwa ujumla ingeongeleazaidi suala la kuboresha maslahi ya walimu kwa sababu elimubila walimu haiwezekani. Maswali yangu mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni hasa kwenyeAwamu hii ya Tano kumekuwa na utaratibu wa viongozi waSerikali hususani Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa nakadhalika kuwavua madaraka walimu wakuu wa shule auwalimu pale inapobainika kwamba shule zao zimefanyavibaya bila kuangalia mazingira ya kufundishia na yakujifunzia.

Swali langu, Serikali haioni kwamba hatua kama hizoni kuwadhalilisha walimu na ni kinyume cha utaratibu wautumishi na kwa maana hiyo walimu hao wanawezakuhakikisha kwamba wanafanya njia mbadala za kuibamitihani ili watito hao wafaulu na ili kuhakikisha kwamba kazizao zinaendelea, hilo swali la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika Mpangowa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kuna kipengele chakuzawadia wanafunzi au walimu pale wanapofaulisha bilakuangalia mazingira ya shule kwa sababu tunajua shulenyingi zingine zina mwalimu mmoja, nyingine wawili nanyingine 50.

Je, Serikali haioni kwa kufanya hivyo kunapelekea zileshule ambazo labda zina matatizo makubwa ya walimukuweza nao kufanya mbinu za kuiba kama ambavyoimetokea Chemba ambapo Chemba mwaka jana ilikuwaya mwisho lakini mwaka huu walitaka kuwa wa kwanza?

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kwamba alitegemea nitoejibu kuhusiana na namna ya kuboresha maslahi ya elimu, siyoswali ambalo Mheshimiwa Mbunge ameuliza kwahiyo ilikuwani vigumu mimi kwenda kujitayarisha kujibu swali ambalohalijaulizwa.

Lakini kihusiana na hilo alilosema kwamba kumetokeautaratibu wa Wakuu wa Wilaya kuwavua madaka walimuna kwamba ndiyo anahisi kwamba inahusika na wizi wamitihani au udanganyifu naomba nimhakikishie kwamba,kwa taarifa ambazo tumezipata, udanganyifu au wizi ambaoumetokea hauna uhusiano wowote na hilo ambaloamesema, tumeangalia, tuna ushahidi tunajua kwamba wiziule umafanyika lakini hauna uhusiano na kuvuliwa madaraka.

Lakini vilevile kuhusiana na kwamba utaratibu wakuwazawadia wanafunzi waliofaulu kwamba ndiyounahusika na walimu kujaribu kuiba mitihani, naombanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisitunachofanya kama Wizara ni kuhakikisha kwamba hakunaupenyo wowote wa kuiba mitihani kwa sababu ni kinyumena sheria, haijalishi kwamba mtu anaiba mtihani kwa sababugani, sisi tunachoisema kwamba ni kosa kuiba mitihani nayeyote yule atakepatikana na kosa atachukuliwa hatua kwamujibu wa sheria zilizopo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, walimu wetuwanafanyakazi nzuri sana na wanafanyakazi ngumu sanakwahiyo tukumbuke kutumia maneno “baadhi” tunapotakakusema maneno kama hayo kwamba kuna uwezekano wawalimu kuhusika kwenye kuiba mitihani, tukumbuke kutumiamaneno “baadhi” kwa sababu walimu wanafanyakazi nzurisana katika mazingira magumu. (Makofi)

Mheshimiwa Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa VitiMaalum sasa aulize swali lake.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

676767

Na. 84

Ongezeko la Vitendo vya Kikatili Shuleni

MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza:-

Kumekuwa na ongezeko la vitendo vya kikatili kwenyeshule zetu nchini kama vile kuchapa viboko hadi kusababishavifo.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kudhibiti aukukomesha adhabu hizi za kutweza (corporal punishement)?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu swali laMheshimiwa Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa viti maalumkama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, vitendo vya kikatili auunyanyasaji kwa watoto vina madhara makubwa katikamakuzi ya kimwili na kiakili. Serikali imeweka mikakatimablimbali kuhakikisha ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili na auunyanyasaji. Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009,kifungu cha 13 inakataza mtu kumsababishia mtoto matesoau aina nyingine ya ukatili, kumpa adhabu zisizo zakibinadamu au kumdhalilisha. Aidha, kwa mujibu wa Kanuniza Adhabu Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyorejewamwaka 2002 ni kosa la jinai kumdhuru, kumjeruhi aukusababisha kifo kwa mtu yeyote na ikithibitika muhusikaatachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Elimu, Sura ya 353kama ilivyorejewa mwaka 2002, imetoa utaratibu wa namnaya kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi. Wizara kupitia

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Waraka wa Elimu Namba 24 ya mwaka 2002 ilitoa maelekezona utaratibu wa utekelezaji wa Sheria hii ambapo adhabuya viboko inaweza kutolewa kwa utovu wa nidhamu uliokitihiriau kwa makosa ya jinai yaliyotendeka shuleni au nje ya shule.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeleakuchukua hatua kwa wanaobainika kujihusisha na vitendovya kikatili au unyanyasaji dhidi ya watoto kwa mujibu wataratibu za kiutumishi na sheria za nchi, kwa mfano; walimuwaliohusika kumpiga mwanafunzi wa shule ya msingi Kibetailiyopo Manispaa ya Bukoba na kusababisha kifo chakewalisimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani ambapo kesiinaendelea.

Aidha, Afisa Elimu Kata, Mwalimu Mkuu na Msaidiziwake wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, hivyonitumie fursa hii kuwataka wasimamizi wa elimu kusimamiakikamilifu utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo yaSerikali. Aidha, napenda pia kuwaasa walimu wote nchinikuepuka vitendo vya kikatili au unyanyasaji kwa watoto.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rose Tweve swali lanyongeza.

MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana na mimi nakubaliana kabisa na maelezoyako ya awali kuwa walimu wetu wana mchango mkubwasana katika malezi na makuzi ya vijana na watoto wetu hapanchini na sisi wengine tumeweza kufika hapa ni misingi mizuriambayo tumepewa na walimu wetu.

Mheshimiwa Waziri ameeleza vizuri kabisa sheria zetuziko vizuri, kanuni zetu zipo vizuri lakini kumekuwa nachangamoto kubwa katika utekelezaji juu ya utaoji waadhabu mashuleni. Kwa mfano, sheria inamtaka kabla yamwalimu hajatoa adhabu lazima apate kibali kwa Mkuu waShule na kiasi cha viboko ni viboko vinne, kwa hiyo kamaulivyoonesha Mheshimiwa Waziri kuna baadhi ya walimuwachache ambao wamekuwa na changamoto kubwa yakufuata taratibu na sheria zilizowekwa.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

696969

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nilikuwa nakuombakupitia Bunge lako tukufu, Mheshimiwa Waziti utoe tamkorasmi kwa walimu wetu wote nchini juu ya umuhimu wa waokufuata Sheria na taratibu za utoaji wa hizi adhabu kwawatoto wetu. Nashukuru sana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Naibu Waziriwa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya tamko mahususilililoombwa na Mheshimiwa Mbunge.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa tamko mahususikama alivyoomba Mheshimiwa Mbunge kwa sababu nafikirini muhimu sana na kwanza niseme kwamba utaratibuuliowekwa na sheria wa kuchapa viboko umeainishwa vizurikatika Waraka wa Elimu Namba 24 wa mwaka 2002uliotengenezwa chini ya kifungu cha 66 cha Sheria ya Elimu.Mwongozo huo pamoja na mambo mengine, umeelezadhahiri kwamba kuna makosa ambayo ndiyo yataruhusiwaviboko vitumike na siyo kila kosa, kwa hiyo siyo kila kosamwalimu anaweza akatumia kiboko. Ni makosa makubwaya kinidhamu na yale yenye sura ya kijinai.

Lakini vilevile kuhusu idadi ya viboko ambayomwanafunzi anaweza akachapwa, kwa wakati mmojahaitakiwi izidi viboko vinne, lakini vilevile anayeruhusiwakuchapa ni Mkuu wa Shule au Makamu wake au mwingineyeyote ambae amepewa ruhusa hiyo kwa maandishi.

Lakini kitu kingine cha nne ni kwamba kuchapaviboko ni lazima iombwe na kutolewa kwa maandishi, lakiniwaraka ule vilevile unasema waziwazi kwamba ni marufukumwalimu yeyote kutembea na kiboko kwa ajili ya kuchapawanafunzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hiyo, naombanitoe tamko kwamba ni marufuku mwalimu yeyotekumchapa mwanafunzi kinyume na utaratibu ulioko na sheria,lakini vilevile ni marufuku mwalimu yeyote kuonekana

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

akitembea na kiboko kwa lengo la kumchapa mwanafunzina kufanya hivyo ni kuvunja sheria na hatua zitachukuliwa.

Lakini vilevile naomba nitumie nafasi hii kuwaagizaMaafisa Elimu wote wahakikishe kwamba wanagawaWaraka Namba 24 wa Elimu wa mwaka 2002 kwa walimuwote ili waweze kujua taratibu ambazo ainatakiwa zifuatwekama wanataka kuwachapa wanafunzi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumefikamwisho wa kipindi chetu cha maswali na majibu, lakinikwenye hili swali la mwisho Mheshimiwa Naibu Wazirimmesema mmewasimamisha kazi hawa watu na kwa sheriazilivyo ni kwamba mtu akisimamishwa kazi hulipwa sehemuya mshahara pamoja na kwamba anakuwa hajahukumiwapengine ni vizuri kuangalia utaratibu vizuri ili akiwa kule Serikaliisiwe inaingia hasara kwa mtu ambaye ameua mtoto.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nitaleta matangazotuliyonayo mezani siku ya leo. Kwanza ni wageni waliopoJukwaa la Mheshimiwa Spika; tutaanza na wageni watatuwa Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Job Yustino Ndugaiambao ni Maaskofu wa hapa Jijini Dodoma watakaofanyaibada na Waheshimiwa Wabunge kwa ajili ya maombi yakufunga mwaka 2018 na hawa ni Mchungaji Gonda, tunayepia Askofu Amon Kinyunyu, tunaye pia Askofu YohanaMasinga. Karibuni sana viongozi wetu wa dini na tunaaminiibada hii itatusaidia katika mwaka unaokuja pia. (Makofi)

Tunao pia wageni wa Waheshimiwa Wabunge nakundi la kwanza ni mgeni wa Mheshimiwa Dkt. AdeladusKilangi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambae ni mdogowake kutoka VETA, Mkoani Mwanza na huyu ni MwalimuMartin Shigongo Lubangu, karibu sana, karibu sana. (Makofi)

Tunao pia wageni 55 wa Mheshimiwa ZainabMwamwindi ambao ni kwaya ya Ruaha, Kanisa la Anglikanakutoka Ruaha, Mkoa wa Iringa wakiongozwa na NduguJohnson Mgimba. Karibuni sana wanakwaya, mmependeza

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

717171

sana sijui kama mtatuimbia kidogo hapo nje! Karibuni sana.(Makofi)

Tunao pia wageni 43 wa Mheshimiwa LolesiaBukwimba ambao ni wana kwaya wa Kanisa la AnglikanaUvuke, Jijini Dodoma wakiongozwa na Mwenyekiti waoNdugu Nicolaus Ndaro. Karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia wageni 44 wa Mheshimiwa Anna Lupembeambao ni wanamaombi kutoka Jijini Dodoma wakiongozwana Ndugu Said Suleiman Said. Karibuni sana wanamaombinaamini wataungana na Maaskofu wetu kutuombea humundani, lakini na Taifa zima kwa ujumla. (Makofi)

Tunao pia wageni wawili wa Mheshimiwa VenanceMwamoto ambao ni wapigakura wake kutoa Jimboni kwakeKilolo, Mkoani Iringa na hawa ni Ndugu Peter Kisambwe naNdugu Juma Kandenyela. Karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia wageni watano wa MheshimiwaBoniphace Mwita Getere ambao ni watoto na wake waMarehemu Chifu Makongoro kutoka Bunda, Mkoani Marawakiongozwa na mtoto wa Chifu Haruna Makongoro.Karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kabla hamjakaa kwanza namama hapo, maelezo ya Mheshimiwa Getere kuhusu wagenihawa anasema chifu huyu, Chifu Makongoro alifariki mwaka1958 na aliacha wajane 47 na watoto 80 kwa hiyo hawawageni ni sehemu ya hiyo familia ya marehemu, kwa hiyoChifu wetu alifanyakazi nzuri kwanza ya kujaza dunia, lakiniya kututengenezea nguvukazi. Ahsante sana Mama naMheshimiwa Getere anasema yule Mama pale mnamuonapale ama kwa wengine humu ndani ni bibi ana miaka 100.Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Afya alivyokuwa anasisitizahapa kuhusu mazoezi jamani mmemuona mama pale? Hanawasiwasi hata kidogo. (Makofi/Kicheko)

Sawa, tuna pia wageni wawili wa Mheshimiwa FatmaHassan Toufiq ambao ni Makatibu wa Umoja wa Wanawake

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

- Tanzania kutoka Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma,Ndugu Diana Madukwa na Ndugu Victoria Komba. Karibunisana viongozi wetu kutoka Chamwino. (Makofi)

Tunao pia wageni wanne wa Mheshimiwa MaulidMtulia ambao ni wadau wa maendeleo ya Jimbo laKinondoni kutoka Belerics Limited Jijijini Dar es Salaamwakiongozwa na Mkurugenzi wa Mahusiano Ndugu AzizRashid Chonya. Karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia wageni wawili wa Mheshimiwa RashidShangazi ambao ni rafiki zake kutoka Ilala, Mkoa wa Dar esSalaam na huyu ni Ndugu Warda Obathani ambaye niMkurugenzi wa Arabic Chocolate Cake. Karibu sana. Na huyuameambatana na Ndugu Nasra Shaban ambaye ni nduguyake. (Makofi)

Lakini pia tuna wageni wanne wa Mheshimiwa AbbasAli Mwinyi ambao ni Makatibu wa Matawi ya CCM kutokaZanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi wakiongozwa na KatibuTawi la Michenzani, Ndugu Ibrahim Mwinyi. Karibuni sanaviongozi wetu. (Makofi)

Tunao pia wageni waliotembelea Bunge kwa ajili yamafunzo, nao ni watumishi watatu kutoka Divisheni ya TaarifaRasmi (Hansard) ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaowamekuja kubadilishana uzoefu na watumishi wa Bunge nahawa ni Ndugu Fatma Msabaha ambaye ni Mkuu waDivisheni, sijui wamekaa upande gani hawa! Karibu sana.Tunaye pia Ndugu Mohamed Gharib ambaye ni Mhariri waTaarifa Rasmi, karibu sana. Tunaye pia Ndugu Mariam Jumaambaye ni Mwandishi wa Taarifa Rasmi. Karibuni sana katikakubadilishana uzoefu na wenzetu wa Hansard wa hapaBunge. (Makofi)

Tunao pia wageni 17 ambao ni wanafunzi 14 nawalimu watatu kutoka Chuo cha Evangelistic Central BibleCollege cha Ilazo Jijini Dodoma ambao wamekuja kujifunzanamna Bunge linavyoendesha shughuli zake. Karibuni sana.(Makofi)

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

737373

Tunaye pia mgeni kutoka SHIKANA Law Group ya JijiniDar es salaam ambae ni Mkuu wa Shirika hilo ndugu AmneSued Kagasheki, amekuja kwa ajili ya mafunzo ya kikaziBungeni. Sijui amekaa upande gani huyu!! Karibu sana sijuikama ni ndugu na Balozi Kagaesheki lakini mpe salama zetu,tunamsalimia sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, ninayo pia matangazomengine. Tangazo la kwanza linatoka kwa Katibu wa Bunge,anawatangazia Waheshimiwa Wabunge kuwa TanzaniaEducational Publishers Limited wanafanya maonesho yavitabu mbalimbali katika maeneo ya Bunge. Maonesho hayoyanafanyika kati ya Jengo la Utawala na Jengo la Habari.Mnaombwa kutembelea maeneo hayo na kujipatia vitabuna kuona ni vitu gani wanaonesha hapo.

Tangazo lingine Waheshimiwa Wabunge linatoka kwaMheshimiwa Dkt. Harrison George Mwakyembe ambae niWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja naMwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa WilliamNgeleja wanawatangazia Waheshimiwa Wabunge kuwa sikuya Jumamosi tarehe 10 Novemba, 2018 yalifanyikamashindano ya riadha ndefu, lakini kilometa tano katika hiyoDodoma Marathon, Waheshimiwa Wabunge mbalimbaliwalishiriki lakini Wabunge wetu ambao walikuwa ni vinara nikama ifuatavyo:-

Kwa upande wa wanaume aliongoza MheshimiwaVenance Mwamoto, alifuatiwa na Mheshimiwa Daniel Mtukana Mheshimiwa Desderius Mipata alikuwa ni wa tatu. (Makofi)

Kwa upande wa wanawake aliongoza MheshimiwaKunti Majala, alifuatiwa na Mheshimiwa Ritta Kabati na watatu alikuwa ni Mheshimiwa Susan Kiwanga. MheshimiwaSusan Kiwanga, Mbunge wa Mlimba kwenye neema yachakula. (Makofi)

Bunge Sports Club pamoja na Mheshimiwa Waziriwanawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge kwanza kwakushiriki, lakini pia kwa kuonesha ushindani ambao ulikuwa ni

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1543929957-13...kusajili shule ya msingi. Miundombinu inayohitajika ni pamoja na uwepo wa chumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

mkali sana hawa ndiyo wametuongozea. Ahsanteni sana.(Makofi)

Tangazo lingine linatoka kwa Mheshimiwa AnnaLupembe ambaye ni Mwenyekiti wa ibada, chapel yaDodoma. Anawatangazi Waheshimiwa Wabunge wotekwamba leo kutakuwa na ibada katika eneo la wazi labasement mara baada ya kusitisha Bunge sasa hapaameandika saa 7:00 mchana, naamini ni baada ya kusitishaBunge sasa.

Aidha, katika ibada hiyo tutakuwa na watumishi waMungu, Askofu Kinyunyu kutoka Kanisa la Lutheran, Dayosisiya Dodoma na viongozi wetu wote tuliowataja waliokoJukwaa la Spika pia watakuwepo. Kwa hiyo, WaheshimiwaWabunge wote mnakaribishwa kwenye hiyo ibada.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayonaahirisha shughuli za Bunge mpaka siku ya kesho saa tatuasubuhi.

(Saa 5:26 Asubuhi Bunge Lilihirishwa hadi Siku ya Jumatano,Tarehe 14 Novemba, 2018 Saa Tatu Asubuhi)