214
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Thelathini na Tano – Tarehe 23 Mei, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ABDALLAH ISSA – KATIBU MEZANI: TAARIFA YA SPIKA NAIBU SPIKA: Taarifa ya Mheshimiwa Spika ambayo inaletwa kwenu kwa mujibu wa Kanuni ya 33(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2016. Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka kwamba tarehe 10 na tarehe 14 Mei 2018, Mheshimiwa Spika alitoa taarifa hapa Bungeni kuhusu Wabunge wenzetu waliochaguliwa na kupata nafasi za uongozi katika Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) kama ifuatavyo:- Waheshimiwa Wabunge, utaratibu alioelekeza Mheshimiwa Spika wataingia Mheshimiwa mmoja mmoja kwa hivyo niwataje wote wawili halafu nitawaita. Moja Mheshimiwa Stephen Julius Masele Mbunge wa Shinyanga Mjini, alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika akiongoza kwa kura kati ya wagombea wanne wa nafasi hiyo. (Makofi) Mbunge Mwenzetu mwingine ni Mheshimiwa Mboni Mohamed Mhita ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Handeni

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA

MAJADILIANO YA BUNGE

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Thelathini na Tano – Tarehe 23 Mei, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu.

NDG. RAMADHAN ABDALLAH ISSA – KATIBU MEZANI:

TAARIFA YA SPIKA

NAIBU SPIKA: Taarifa ya Mheshimiwa Spika ambayoinaletwa kwenu kwa mujibu wa Kanuni ya 33(2) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la 2016. Waheshimiwa Wabungemtakumbuka kwamba tarehe 10 na tarehe 14 Mei 2018,Mheshimiwa Spika alitoa taarifa hapa Bungeni kuhusuWabunge wenzetu waliochaguliwa na kupata nafasi zauongozi katika Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP)kama ifuatavyo:-

Waheshimiwa Wabunge, utaratibu alioelekezaMheshimiwa Spika wataingia Mheshimiwa mmoja mmojakwa hivyo niwataje wote wawili halafu nitawaita. MojaMheshimiwa Stephen Julius Masele Mbunge wa ShinyangaMjini, alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kwanza waBunge la Afrika akiongoza kwa kura kati ya wagombeawanne wa nafasi hiyo. (Makofi)

Mbunge Mwenzetu mwingine ni Mheshimiwa MboniMohamed Mhita ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Handeni

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Vijijini alichaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Vijana wa Bungela Afrika akimshinda Mbunge kutoka nchi ya Chad ambayealikuwa anatetea nafasi yake. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nimearifiwa kwambaMheshimiwa Stephen Masele na Mheshimiwa Mboni Mhitawamesharejea nchini na wapo maeneo ya Bunge, kwahivyo muda si mrefu wataruhusiwa kuingia hapa ndanilakini baada ya kipindi chetu cha maswali na majibuwatapewa fursa ya kutusalimu Waheshimiwa Wabunge.(Makofi)

Kwa sasa naagiza waingie ndani ya Bunge nawataingia kwa utaratibu wa mmoja mmoja tutaanza naMheshimiwa Mboni Mohamed Mhita ambaye ni Mbunge waBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia niMbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, yeye ni Rais wa Umojawa Vijana wa Bunge la Afrika.

Mpambe wa Bunge sasa amlete Mheshimiwa MboniMhita. (Makofi)

(Hapa Mheshimiwa Mboni M. Mhita aliingia ukumbini)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabungesasa nimwite Mheshimiwa Stephen Julius Masele ambaye niMbunge wa Shinyanga Mjini ambaye alichaguliwa kuwaMakamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika.

Sasa Mpambe wa Bunge amlete Mheshimiwa StephenMasele. (Makofi)

(Hapa Mheshimiwa Stephen J. Masele aliingia ukumbini)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Waheshimiwa Wabungekwa salamu hizo, lakini pia nichukue fursa hii kwa niabaya Mheshimiwa Spika kuwapongeza sana wenzetuhawa wawili kwa heshima kubwa waliyoliletea Bungehili pia kwa heshima kubwa waliyoiletea nchi yetu.(Makofi)

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Waheshimiwa Wabunge, kwa namna ya kipekeekabisa nichukue fursa hii tena kwa niaba ya Mheshimiwa Spikakuwashukuru sana Wabunge wengine ambao walikuwapamoja na hawa wenzetu wakati wakifanya kampeniMheshimiwa Mheshimiwa Asha Abdullah Juma ‘Mshua’ naMheshimiwa David Ernest Silinde ahsanteni sana. Mmefanyakazi nzuri, mmeonesha umoja, kwa hivyo nasi kama Bungetunawashukuru sana kwa kazi nzuri. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tutaendelea, Katibu.

NDG. RAMADHAN ABDALLAH ISSA – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA NISHATI:

Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANOWA AFRIKA MASHARIKI:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikikwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.

Taarifa ya mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Kituocha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kwa Mwaka waFedha 2016/2017 (The Annual Report and Audited Acccountsof Arusha International Conference Center (AICC) for theFinancial Year 2016/2017.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS (K.n.y - MWENYEKITIWA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA:

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo zaNchi za Nje, Ulinzi na Usalama, kuhusu utekelezaji wa

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018;Pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa2018/2019.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu.

NDG. ABDALLAH RAMADHANI ISSA – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswalitutaanza na ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa David ErnestSilinde, Mbunge wa Momba, sasa aulize swali lake.

Na. 297

Mpango wa Kuongeza Ajira kwa Wahitimu wa Vyuo

MHE. DAVID E. SILINDE aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza ajira kwaWatanzania waliohitimu Vyuo bila kujali kada walizosomeaambao mpaka sasa wapo mitaani?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI,VIJANANA AJIRA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa DavidErnest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha wahitimuwa vyuo wanapata ajira za kuajiriwa na kujiajiri Serikaliimeendelea na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuongezafursa za ajira kama ifuatavyo:-

(i) Kusimamia utekelezaji wa sera ya uchumi waviwanda kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

viwanda nchini kupitia sekta binafsi kwa lengo lakutengeneza nafasi nyingi za ajira.

(ii) Utekelezaji wa miradi mikubwa nchini,ikiwemo mradi wa bomba la mafuta, ujenzi wa reli ya kisasana ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa nishati kupitiamiradi mbalimbali ambayo yote kwa ujumla itasaidiakupanua wigo wa nafasi za ajira.

(iii) Kutoa elimu kwa vijana kuhusiana namasuala ya ajira kwa lengo la kuongezea ufahamu mpanakatika masuala ya ajira na kuongeza uwezo wa kujiaminikatika kujiajiri kupitia sekta mbalimbali za kilimo, ufugaji,uvuvi na ujasiliamali.

(iv) Kuandaa na kusimamia utekelezaji waprogramu ya Taifa kukuza ujuzi nchini ambayo ina lengo yakutoa mafunzo kwa vitendo sehemu ya kazi kwa wahitimuwa vyuo. Mafunzo haya yatawapatia wahitimu wa vyuo ujuziunaohitajiwa na waajiri, hivyo kuwawezesha kuajirika.

(v) Kuendelea kuwezesha vijana kujiajiri kwakuwapatia mikopo yenye masharti nafuu kupitia MfukoMaendeleo ya Vijana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeleakusimamia utekelezaji programu ya Taifa kukuza ujuzi ambayoitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha vijana kuajirika nakupunguza tofauti ya ujuzi uliopo katika nguvu kazi namahitaji ya soko la ajira.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa David Ernest Silinde swalila nyongeza.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. majibu ya Serikali ni majibu ya siku zote ambayoyameshindwa kutatua tatizo la ajira nchini. Unawezakuonesha tu mifano midogo kwa mfano, sera ya uchumi naviwanda kwenye bajeti tu peke yake Serikali imeshindwakupeleka fedha ambayo ingeweza kuwezesha hivyo viwanda

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

kuanzishwa na wananchi kupata ajira, kipengele cha tanoutaona kabisa kwamba inasema kwamba Serikali moja yamkakati wake ni kuwapa mikopo nafuu kupitia Mfuko waMaendeleo ya Vijana, lakini kwenye bajeti tuliyoipitisha hapaunakuta Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni bilioni mojawakati vijana ambao wako mtaani ni wengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, ni kwa niniSerikali isikubali ama ikashauriana na taasisi za kifedha iliwanafunzi wa Vyuo Vikuu watumie vyeti vyao walivyomaliziaelimu ya juu, kama sehemu ya kukopea ili kuwasaidia wawezekujiajiri?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kwa nini sasaSerikali kupitia Wizara ya Ardhi wasigawe ardhi katika yalemaeneo muhimu kabisa bure kwa wanafunzi wotewanaomaliza Vyuo Vikuu ili waweze kujiajiri kwa kufanya hizokazi na baada ya hapo warejeshe hiyo mikopo yao, kwanini wasitumie hii mikakati ya muda mfupi ambayo inawezakuwawezesha hawa watu kupata hiyo ajira au kujiajiri?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya WaziriMkuu majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI, VIJANANA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza nikweli katika taasisi za kifedha moja ya masharti ya mtu yeyotekuweza kupata mkopo ni uwasil ishaji wa dhamana(collateral) ili aweze kufikia uwezo huo wa kupata mkopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana naMheshimiwa Silinde kwamba asilimia kubwa ya wahitimu wavyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu bado hawajawa nauwezo wa kuwa na hizo collateral ndiyo maana Serikali nakupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tumeonanjia pekee na bora ya kuweza kusaidia kundi hili la vijanakwa kuanzia, kwanza ni kuwahamasisha kukaa katikavikundi, pili ni kuwawezesha kupitia mifuko mbalimbali ya

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

uwezeshaji ambao chini ya Baraza la Uwezeshaji WananchiKiuchumi tuna mifuko takribani 19 ya uwezeshaji inayotoamikopo na inayotoa ruzuku ambayo ina ukwasi wa kiasi chashilingi trilioni 1.3 kwa maana ya liquidity.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa wahitimuwote wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Elimu ya Juu bado wanayofursa kutumia mifuko yetu hii ambayo ina riba nafuu sana,ambayo pia inaweza ikawasaidia wakabadilisha maisha yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mfano ukiendapale Sokoine University tuna vijana wana kampuni yaowanaitwa SUGECO ambao walihitimu pale wamekaapamoja ninavyozungumza hivi sasa SUGECO wanafanyamiradi mikubwa ya kilimo hapa nchini na wameanzakuwasaidia mpaka na vijana wenzao kwa sababu walipitiautaratibu huu, Serikali ikawawezesha na sasa hivi wamefikambali sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusiana namasuala ya ardhi, Novemba mwaka 2014, MheshimiwaWaziri Mkuu aliwaita Wakuu wa Mikoa wote hapa Dodomalikatengenezwa Azimio la Wakuu wa Mikoa wote kwendakutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za vijana,juzi Waziri Mkuu amesisitiza hilo jambo na mpakaninavyozungumza hivi sasa zimeshatengwa takribani hekari200,000 nchi nzima kwa ajili ya shughuli za vijana ambaomaeneo haya tumeyapa jina mahsusi kabisa kwamba niYouth Special Economic Zones (Ukanda Maalum Uchumi kwaajili ya vijana).

Mheshimiwa Naibu Spika, rai yangu ni kwambaniendelee kuwaomba Wakuu wa Mikoa na viongozi wotekatika Tawala za Mikoa kwa agizo la Waziri Mkuu watekelezekwa kutenga maeneo ili vijana wengi zaidi wapate nafasiya kwenda kufanya shughuli za ufugaji, kilimo na biashara.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Stanslaus Mabula swali lanyongeza.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa nafasi. Kwa kuwa ajira ambazo nirasmi zimekuwa na ukakasi mkubwa kulingana na idadikubwa ya vijana na Serikali i l ishaanzisha mfumo wakuwasaidia vijana kupitia ajira zisizo rasmi kwa vijana ambaotayari wana ujuzi, nini sasa mkakati wa Serikali kuwarasimishavijana hawa ili wapate mafunzo na vyeti wanavyoendeleavitakavyowasaidia, hasa wale ambao ni mafundi gereji,mafundi uwashi na mafundi seremala walioko Nyamaganana nchi nzima kwa ujumla?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya WaziriMkuu majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI, VIJANANA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue fursahii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwaanayoifanya kuwatetea vijana hasa vijana wa Jimbo lakela Nyamagana. Pia nimwondoe hofu kwamba chini ya Ofisiya Waziri Mkuu tuna mpango wa miaka mitano wa ukuzajiujuzi kwa vijana ambao lengo lake ni kuwafikia vijanatakribani milioni nne na laki nne ifikapo mwaka 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango huo mojaya component iliyopo tunaita ni RPL - Recognition of PriorLearning. Huu ni mfumo wa urasimishaji ujuzi kwa vijanaambao wana ujuzi lakini hawajapitia mfumo rasmi wamafunzo. Hivi sasa tunao takribani ya vijana 22,000 ambaowameomba kupitia ofisi ya Waziri Mkuu kufanya mafunzohaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyozungumza hivi sasavijana 3,448 nchi nzima wamenufaika na nimwondoe hofuMheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka huu wa fedhatunaendelea pia kuwachukua vijana hawa kwa ajili yakuwarasimisha katika ujuzi walionao na kuwapa cheti bilakupitia katika mafunzo maalum ya vyuo vya ufundi stadi.(Makofi)

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa James Mbatia swali lanyongeza.

MHE JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana. Tatizo kubwa la ajira ni mfumo wetu waelimu ambao hauwapi fursa vijana wetu kuwa creative nainnovative, yaani unakuwa na mfumo wa elimu ambaounaangalia miaka 50 unataka uwe na Taifa la namna ganibadala ya elimu yetu ya copy and paste. Je, Serikali haioniumuhimu wa kuhakikisha mitaala yake inaandaa Taifaambalo linakuwa innovative and creative badala ya copyand paste?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya WaziriMkuu majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI, VIJANANA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, alichokisemaMheshimiwa Mbunge pia kimeripotiwa na taarifambalimbali, moja kati ya changamoto iliyopo ni namnaambavyo tunaweza tukawa tuna vijana wahitimuwenye ujuzi ambao utawapa sifa za kuajiriwa katikasoko la ajira.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama ofisi ya Wazirikupitia mpango wa ukuzaji ujuzi, moja kati ya eneo ambalotumelipa kipaumbele ni hilo. Mwaka jana Mheshimiwa WaziriMkuu alizindua miongozo kwa ajili ya kuhakikisha vijana wetuwahitimu wa Vyuo Vikuu wanapata mafunzo ya vitendo iliwaongeze sifa ya ziada kwenda kuajiriwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikirudi katika msingi waswali lake ni kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizaraya Elimu tunafanya kazi hii kwa pamoja ili kuona namna borakuja na mitaala ambayo itamfanya kijana wa Kitanzaniaakihitimu elimu yake awe na sifa za kuajiriwa ili apate nafasiya kuajirika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyosema kwambakuna hoja ya kuhakikisha vijana wetu wanakuwa wabunifuili watakapomaliza vyuo kama hawajapata ajira rasmiwaweze kujiajiri. Kwa sasa Wizara ya Elimu ina mkakatimkubwa sana kuhakikisha kwamba tunakuza stadi za kaziili vijana wanapohitimu wasiwe wanaangalia kuajiriwa tuvilevile waweze kujiajiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kwa sasa inatekelezamradi unaitwa ESPJ - Education and Skills for Productive Jobs,mradi ambao unafadhiliwa na Wadau wa Maendeleo kwadola milioni 100. Moja kati ya malengo yake ambalo nikubwa, ni kuhakikisha kwamba kwenye shule zetu, vyuo vyetuvijana wanafundishwa stadi za kazi ili wakitoka hata kamahawajapata ajira rasmi waweze kujiajiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nitumie fursa hiikuendelea kusisitiza kwamba zamani tunapoenda kusomashuleni tunafikiria kwenda kuajiriwa, kwa sasa focus tokeamwanzo tunataka watu wajue kwamba ajira ni pamoja nakujiajiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa CatherineMagige, swali fupi.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi kwa kuuliza swali dogola nyongeza. Kwa kuwa waajiri wengi nawapotoa nafasiza ajira, wanahitaji waombaji ambao wanaomba wawena experience na wanachuo wengi wanaomaliza vyuowanakuwa hawana uzoefu. Je, Serikali ina mpango ganikuwasaidia wanavyuo wanapotoka vyuoni waajiriwe bilakuulizwa experience?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimuamesimama. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi naTeknolojia, majibu.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba, siyo kazi zotezinahitaji uwe umepata uzoefu. Kuna kazi ambazozinatangazwa ambazo wanachukuliwa wanafunzi waliotokavyuoni moja kwa moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kama nilivyosemalengo la kuanzisha mfumo wa elimu ambao vilevileunafundisha stadi za kazi ni kuhakikisha kwamba hatatunapokuwa mashuleni tayari kuna uzoefu ambaotumekuwa tumeupata. Ndiyo maana hata Serikali kwasasa inawekeza sana kwenye elimu ya ufundi iliwanafunzi wanapokuwa mashuleni na vyuoni wawetayari wameshaanza kufanya practicals ili wakiendakwenye ajira kwamba wawe tayari wanaweza kuajiriwa.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendasasa kwenye Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa NassorSuleiman Omar, Mbunge wa Ziwani, sasa aulize swali lake.

Na. 298

Athari za Uhakiki wa Vyeti Feki

MHE. NASSOR SULEIMAN OMARY aliuliza:-

Uhakiki wa vyeti feki umeathiri wafanyakazi wengi nawengine wamepoteza ajira zao:-

Je, ni wafanyakazi wangapi wamepoteza ajira zaosekta ya elimu pekee?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali laMheshimiwa Nassor Suleiman Omar, Mbunge wa Ziwani,kama ifuatavyo:-

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2016/2017 na 2017/2018, Serikali ilifanya uhakiki wa vyeti vyawatumishi wa umma ili kubaini waliokuwa na vyeti halali nawaliokuwa na vyeti vya kughushi. Katika uhakiki huo, jumlaya Walimu 3,655 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi,hivyo walipoteza sifa za kuendelea kuwa watumishi waumma.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nassor Omar, swali lanyongeza.

MHE. NASSOR SULEIMAN OMAR: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.Swali la kwanza, Serikali i l itoa kauli kwa wale wotewalioathirika na zoezi hil i kimakosa; Je Serikaliimeshawarejesha?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kuna waleambao walioathirika kimakosa na wako karibu na kustaafu;je Serikali ina kauli gani?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kwamba baada ya zoezi hili yalitokeamanung’uniko na vilevile zilitokea rufaa mbalimbali zawatumishi ambao walidhani kwamba wameonewa. Serikaliilifanya uchambuzi wa kina, wale ambao walionekanakwamba kulikuwa na makosa katika mchakato huowamesharejeshwa kazini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ameuliza swali linginekwamba wale ambao walikuwa wanakaribia kustaafuSerikali imewaangalia namna gani? Ukweli ni kwamba kwamakosa ambayo walikuwa wameyafanya walitakiwawapelekwe Mahakamani, lakini Serikali ilisema tuwasamehemambo ya kuwapeleka mahakamani kwa makosa yakughushi na wao wasilete madai mengine.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Madini.

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwaniaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napendakwanza kupongeza majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri lakini napenda tu kuongezea kuhusiana na idadiya waliokata rufaa na kurudishwa kazini, jumla ni watumishi1,907.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Halima Mdee, swali lanyongeza.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, zaliola vyeti feki ni Chama cha Mapinduzi na Serikali yake,Mheshimiwa Rais akiwa ni sehemu ya CCM kwa kipindi chotehicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kwambaWalimu ama Watumishi wengi walianza na cheti cha mtuwakaenda wakasomea taaluma, wakafaulu taaluma zao,wakaenda kulitumikia Taifa hili kwa miaka mingi sana. Serikaliya watu ni Serikali yenye ubinadamu. Sasa nauliza, hivi nikweli Serikali ya CCM inadhani ni sahihi kwa watu ambaowametumikia hili Taifa kwa miaka 20, wengine mpaka miaka40 wengine miaka 30, waondoke hivi hivi bila hata kupatakifuta jasho, wanadhani ni sahihi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge swali lakoumeshauliza na umeshaeleweka. Mheshimiwa Waziri waMadini majibu.

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, bahatinzuri dada yangu ama mdogo wangu naye ni Mwanasheria.You cannot benefit from your own wrong, suala hili lilikuwa nijinai, huwezi ukanufaika hata kama uliweza ku-penetratekatika mfumo ikafikia hapo na ndiyo maana MheshimiwaRais aliweza kutoa amnesty na amnesty hii haikuweza kutokabure.

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Halima awezekuelewa suala hili halijazalishwa tu hivi na Serikali ya CCM niCriminal Offence na ilikuwa ni lazima kufanya hivyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, msizipige sanahizo meza nawaona mkiwa mmesimama. Mheshimiwa JumaKombo, swali la nyongeza.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri katika jibu la msingiamesema kwamba jumla ya Walimu 3,655 walipoteza kazibaada ya uhakiki na kugundulika na vyeti feki. Nataka kujuatu katika mwaka 2016/2017 na 2017/2018 Serikali kamailipoteza Walimu hawa; je, hadi sasa imeajiri Walimuwangapi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): MheshimiwaNaibu Spika, baada ya zoezi hilo kukamilika Serikali katikamiaka hii miwili 2016/2017 na 2017/2018 imeajiri jumla yaWalimu 6,495. Kati ya hao Walimu wa shule za sekondari wamasomo ya sayansi na hisabati ni 3,728 na Walimu wa shuleza msingi ni 2,767. Idadi hiyo ni zaidi ya walioachishwa kazi nikwa sababu ya kuwa na vyeti vya kughushi.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na Wizaraya Maji na Umwagiliaji. Mheshimiwa Azza Hillal Hamad,Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake.

Na. 299

Huduma ya Maji Sekondari ya Masengwa

MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kupelekamaji katika Sekondari ya Masengwa?

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaji na Umwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa AzzaHillal Hamad, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza kutekelezaahadi yake ya kupeleka maji kwenye Shule ya SekondariMasengwa. Serikali imeandaa mradi wa kutoa maji Kijiji chaBugweto Manispaa ya Shinyanga kwenda katika Kijiji chaMasengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tararibu za kumpataMkandarasi atakayetekeleza mradi wa kupeleka maji katikaKijiji cha Masengwa zimekamilika. Utekelezaji wa mradi huoutaanza katika mwaka wa fedha 2018/2019. Matarajio nikwamba mradi huu utakapokamilika utawanufaisha wakaziwa Kijiji cha Masengwa ikiwemo na Shule ya SekondariMasengwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Azza Hillal Hamad, swali lanyongeza.

MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Naibu Spika,namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji kwa majibuyake mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Mradihuu wa maji ni ahadi ya toka mwaka 2006 ya MheshimiwaJakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu hivyo imekuwa ni ahadiya muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, Wizaraya Maji ipo tayari sasa kuondoa vikwazo vyote vilivyopoWizara ya Maji na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilikuhakikisha mradi huu unaanza mara moja?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa nahofu kubwa kwa wananchi wangu wa Mji Mdogo wa Tindekutokana na kwamba mradi wa maji wa Ziwa Victoriabomba kubwa linapita mbali sana na Mji Mdogo wa Tinde,hivyo kuwa na hofu kubwa kwamba mradi huu

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

hautawezekana kufika kwa wananchi wa Tinde. Je, Wizaraya Maji imefikia wapi kuwaondoa hofu wananchi wa Tindekuhakikisha kwamba wanapata maji safi na salama katikamradi huu wa mkubwa wa maji ya Ziwa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu kwa maswali hayo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nianze kumpongeza MheshimiwaMbunge Azza kwa jinsi ambavyo anawapenda wananchiwa Shinyanga na jinsi anavyowatetea katika Bunge hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza laMheshimiwa Mbunge, ni kweli kabisa kwamba miradi hiiilianza bajeti ya mwaka 2006/2007 na Mheshimiwa Mbungenaomba tu akumbuke ndipo tulioanza ile program yamaendeleo ya sekta ya maji, tukaweka kwamba tutajengamiradi 1,810. Tumeshakamilisha miradi 1,468, bado miradi366 na mradi wake ukiwa ni mmojawapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, umechelewa kwa sababuusanifu ulichelewa, lakini kwa sasa tunamhakikishia kwambahakuna vikwazo vya aina yoyote, tunatekeleza kwa mujibuwa sheria. Mradi wowote baada ya usanifu, baada yamanunuzi ili kuepuka upotevu wa fedha lazima tuupelekekwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaufanyie vetting, tusaini,ndiyo tuanze utekelezaji. Kwa hiyo, nimhakikishie kwambamradi utatekelezwa bila ya wasiwasi wowote.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kweli bombala KASHIWASA limepita mbali kidogo mbali na ule Mji waTinde, nimemwagiza Mhandisi Mshauri anayesimamia huumradi wa Tabora na tayari ameshabaini vij i j ivitakavyopelekewa maji ukiwemo Mji wote Tinde na vitongojivyake na amekamilisha utaratibu wa awali sasa hivi tunaingiakwenye usanifu wa kina.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba wakati tunaendelea na utekelezaji wa

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

mradi wa Tabora basi wakati unakamilika na Tinde yoteitakuwa imeshapata maji. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Oran Njeza, swali lanyongeza.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Naomba niiulize Serikali ni lini itapelekamaji kwenye Kata ya Mjele ambayo ni ahadi ya muda mrefuya Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nitumie nafasi hiinimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanyana nimeshafika hadi Mjele. Namwomba sana Mhandisi waMaji wa Jimbo la Mbeya Vijijini asilale ili kuhakikisha wananchiwale wanapata maji safi, salama na ya kuwatosheleza.Jambo la msingi sisi kama Wizara a-raise certificate tuko tayarikulipa kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri naombauwatazame hawa Wabunge, sitawaruhusu kuuliza maswaliwana mambo ya maji katika Majimbo yao.

Tutaendelea na Mheshimiwa Ignas Aloyce Malocha,Mbunge wa Kwela, sasa aulize swali lake.

Na. 300

Mradi wa Maji toka Mto Kalumbaleza

MHE. IGNAS A. MALOCHA aliuliza:-

Kutokana na tatizo kubwa la ukosefu wa maji katikaMji Mdogo wa Muze Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

ilipitisha mpango wake wa kuondokana na tatizo hilo kwakuanzisha mradi mkubwa wa kuchukua maji toka MtoKalumbaleza na kusambaza katika Vijiji vya Muze, Mlia, MnaziMmoja Asilia, Ilanga, Mbwilo Kalakala, Isangwa na Uzia:-

Je, ni lini Serikali itatoa fedha ili kutekeleza mradi huo?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaji na Umwagiliaji, naomba kujibu swali la MheshimiwaIgnas Aloyce Malocha, Mbunge wa Jimbo la Kwela, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutengafedha za utekelezaji wa miradi ya maji ili kuhakikisha wananchiwake wanapata huduma ya maji. Kwa sasa Mtaalam Mshaurianaendelea na kazi ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifuwa mradi wa maji wa Muze Group ili utekelezaji wake uwezekufanyika katika mwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika mwaka wafedha 2018/2019, Serikali imetenga kiasi cha Sh.500,000,000kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Muze Group.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ignas Malocha, swali lanyongeza.

MHE. IGNAS A. MALOCHA. Mheshimiwa Naibu Spikaahsante sana. Kwanza nimpongeze Naibu Waziri na Waziriwake kwa utendaji wa kazi, lakini ninayo maswali mawili yanyongeza. Swali la kwanza, mradi huu wa Muze Groupunategemewa kupeleka maji katika vijiji 10 vyenye wakazi40,000 ambavyo ni Kijiji cha Kalumbaleza A, B, Muze, Mbwilo,Mlia, Mnazi mmoja Asilia, Ilanga Kalakala, Izia na Isangwa.Maeneo haya hukumbwa na kipindupindu kila mwakakutokanana na shida ya maji, mwaka huu wananchiwapatao 605 waliugua kipindupindu, katika hao wananchi15 walikufa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuharakisha ujenziwa mradi huu ili kunusuru vifo kwa wananchi?

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Swali la pili, kwa vile Mtaalam Mshauri wa mradi huualishaanza kazi na amesha- raise certificate Wizara ya Maji;Je, ni lini watamlipa fedha zake haraka ili mradi huu uwezekuanza mapema? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu kwa maswali hayo.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kwanzakumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ya kipekeeanavyowatetea wananchi wake. Nataka niwahakikishiekwamba maji ni uhai, Wizara ya Maji hatutakuwa sehemuya kupoteza uhai wa wananchi wake. Nataka nimhakikishieMheshimiwa Mbunge tutakuwa sehemu ya kusimamia mradihuu ili uweze kutekelezeka kwa wakati wananchi wakewaweze kupata maji safi, salama na yenye kuwatosheleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili,nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, baada ya Bungecha saa saba tukutane ili twende kuhakikisha Mkandarasihuyu analipwa kwa wakati ili mradi usikwame na wananchiwaweze kupata maji. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri naaminiutaweza kuonana na hawa Wabunge wote, hebuwaangalie vizuri wamesimama. Wabunge hawa wanamiradi imekwama katika maeneo yao.

Mheshimiwa Deo Ngalawa, swali la nyongeza.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kuniona. Mji wa Makambako ni Mji mkubwana ni Mji ambao una tatizo kubwa sana la maji. Baadhi yawananchi wanashindwa kujenga viwanda kwa sababu yauhaba wa maji. Kuna miradi 17 ya fedha kutoka Serikali yaIndia. Serikali iniambie hapa je, ni lini sasa miradi hii ambayommojawapo ni ya Mji wa Makambako utaanza ili wananchiwa Makambako waweze kunufaika na wajipange kwa ajiliya kujenga viwanda?

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, kabla hujajibu hilo,nilikuwa nimemwita Mheshimiwa Deo Ngawala, kwa hiyoinabidi Mheshimiwa Deo Ngalawa aulize swali halafuutayajibu yote mawili kwa pamoja.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali. Tatizo lamaji katika Wilaya ya Ludewa limekuwa ni la kudumu naikizingatiwa kwamba Wilaya ya Ludewa ina vyanzo vya majivingi sana. Je, Serikali inajipangaje katika kuhakikishakwamba Ludewa inapata maji ya uhakika hususan LudewaMjini na Mavanga?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaNaibu Spika, naomba kujibu maswali mawili yaWaheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Mbunge waMakambako pamoja na Ludewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na MheshimiwaMbunge wa Makambako, kwanza kabisa tunaishukuruSerikali kwamba mkataba wa kifedha kati ya Serikali ya Indiana Tanzania umeshasainiwa tayari. Pili, kulingana na mashartiya mkataba huo, Serikali ya India imeshaleta WahandisiWashauri tayari, wengi ambao sasa hivi tutafanya manunuzikupitia kwenye hilo group.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba shughuli hii inakwenda kwakasi sana na matarajio yake ni kwamba kabla ya mwakahuu tulionao 2018 haujafika Desemba, tunataka tuhakikishekwamba Wakandarasi wako site na wanaanza utekelezajiwa miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la MheshimiwaMbunge wa Ludewa. Mheshimiwa Mbunge yeye mwenyeweni shahidi kwamba nilishaelekeza mamlaka yangu ya majiya Iringa na wanaendelea kutekeleza miradi katika Jimbo

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

lake na mwaka huu tumetenga fedha. Kwa hiyo,tutaendelea kutekeleza pamoja na pale Mjini ambapo mimimwenyewe nil ipatembelea, tutahakikisha kwambatunawapatia maji safi na salama wananchi wake. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Lameck OkamboAiro, Mbunge wa Rorya, swali lake litaulizwa kwa niaba naMheshimiwa Boniphace Mwita Getere.

Na. 301

Hitaji la Mahakama ya Mwanzo na WatumishiWilaya ya Rorya

MHE. BONIPHACE M. GETERE (K.n.y. LAMECK O. AIRO)aliuliza:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Rorya ilianzishwamwaka 2007 na ina ukubwa wa kilometa za mraba 9,345 naidadi ya watu wapatao 400,000, lakini inakabiliwa na tatizola uhaba wa watumishi katika Mahakama za Mwanzo zaKineri, Ryagoro, Obilinju na Shirati; hadi sasa Wilaya ya Roryainatumia Mahakama ya Wilaya ya Tarime hali inayosababishakesi kuchelewa kusikilizwa kwa wakati:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakamaya Wilaya kwenye Jimbo la Rorya?

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Lameck Okambo Airo, Mbunge wa Rorya, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango waMahakama wa kujenga na kukarabati majengo yaMahakama katika ngazi mbalimbali, Mahakama ya Wilayaya Rorya imepangiwa kujengwa katika Mwaka wa Fedha2019/2020.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere,swali la nyongeza.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.Nadhani sasa umefika wakati kwa Serikali kuamua kuangaliahaya mambo ya majengo ya Mahakama kwa sababuduniani kote haki ndiyo inajaaliwa, lakini kumekuwa tu namazoea ya kujibu kwa sababu nimemuona MheshimiwaLameck Airo akiwa na hoja hii miaka mitatu iliyopita na nimiaka 11 sasa toka Wilaya hii ianzishwe. Sasa uhakika ni upi?Kila mwaka anauliza wanasema mwaka unaofuata, kilamwaka anauliza anaambiwa mwaka unaofuata. Sasa Waziriatuthibitishie kwamba ni kweli bajeti inayokuja hiyoMahakama itajengwa kwa Wilaya ya Rorya.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Jimbo la Bundakuna Mahakama ya Nyamswa, imekuwepo muda mrefu sanahiyo Mahakama ilijengwa na Mtemi Makongoro miaka hiyompaka leo, ni lini sasa Serikali itaenda kukarabati ileMahakama na kuifanya iwe ya kisasa kwa ajili ya kusaidiawatu wa Jimbo la Bunda? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria,majibu kwa maswali hayo.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa NaibuSpika, napenda nimhakikishie Mbunge aliyeuliza swalikwamba Mahakama hiyo itajengwa katika mwaka huo wa2019/2020 na siyo Mahakama hiyo tu bali Mahakama zoteambazo zimepangwa kujengwa katika mwaka huo kwaMkoa wa Arusha ikiwa ni Arumeru na Ngorongoro; kwa Mkoawa Dodoma ikiwa Bahi; kwa Mkoa wa Geita ikiwa Geita;kwa Mkoa wa Kagera ikiwa ni Muleba, Bukoba, Ngara, kwaMkoa wa katavi ikiwa ni Mpanda na Tanganyika; na kwaMkoa wa Kigoma ikiwa ni Uvinza na Buhigwe.

Vile vile kwa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni Same; kwaMkoa wa Lindi ikiwa ni Nachingwea; kwa Mkoa wa Manyara,Babati, Hanang’, kwa Mkoa wa Mara ni Rorya na Butiama;

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

kwa Mkoa wa Mbeya itakuwa Rungwe; kwa Mkoa waMorogoro Gairo, Mvomero, Morogoro, Malinyi; kwa Mkoa waMtwara, Newala, Mtwara, Tandahimba; kwa Mkoa waMwanza, Kwimba; zote hizo ni Mahakama ambazozitajengwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na fedha yakeinatokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo vyanzo vya fedhavipo na bado zipo Wilaya nyingine nyingi ambazoMahakama zitajengwa mwaka huu wa 2019/2020. Kwa hiyoningependa nimhakikishie hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Mahakama yaNyamswa, kabla ya Bunge hili kuanza nilifanya ziara ya Mkoawa Mara na mahali ambapo nilipita pia ni Nyamswa. Hili nijengo la zamani ambalo linahitaji kukarabatiwa na hilolitatafutiwa fedha katika mpango wa dharura,itakapopatikana ili Mahakama hiyo ya Nyamswa iwezekukarabatiwa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso,swali la nyongeza.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza. Wilaya ya Tanganyika ni Wilaya ambayo hainaMahakama ya Wilaya, sambamba na Mahakama za Mwanzoni zile ambazo zimechakaa na hazina watumishi wakuzifanyia kazi hizo Mahakama. Je, ni lini Serikali itapelekawatumishi wa Mahakama za Mwanzo sambamba naMahakama ya Wilaya na ujenzi wa Mahakama ya Wilaya?Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kakoso, maswali mengikatika swali moja. Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheriamajibu.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa NaibuSpika, kwa upande wa Mahakama ya Wilaya, Mahakamaya Wilaya katika Wilaya ya Tanganyika itajengwa mwaka

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

2019/2020 na kama nilivyosema fedha imepatikana kwa hiyotuna uhakika kwamba Mahakama hiyo itajengwa kwakipindi hicho huko Tanganyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu watumishi waMahakama, ningependa kusema kwamba upo upungufu wawatumishi wa Mahakama ya Mwanzo 3,000 kwa sababu sasahivi wako watumishi 6,000 na wanahitajika watumishiwengine 3,000. Wizara inaendelea kuwasiliana na Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Borakupata vibali vya ajira. Mara vibali hivyo vitakapopatikanamiongoni mwa Mahakama ambazo zitapewa kipaumbeleni Mahakama za Mwanzo naamini pia zitagusa Wilaya yaTanganyika. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Mheshimiwa Stephen Hillary Ngonyani, Mbunge waKorogwe Vijijini, sasa aulize swali lake.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa NaibuSpika, kabla sijauliza swali, kwanza naomba nitoe neno lashukrani kwa Spika wa Bunge, Katibu wa Bunge pamoja naKamati ile yote ya Wahasibu na Wabunge wenzangu hasaWabunge wa Mkoa wa Tanga kwa mchango mkubwaambao wamenisaidia katika kuuguza familia yangu paleMuhimbii. Mungu awabariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya haya manenomachache, naomba swali langu sasa lipate majibu.

Na. 302

Kufungua Mahakama ya Mwanzo MagomaKorogwe Vijijini

MHE. STEPHEN H. NGONYANI aliuliza:-

Katika Kata ya Magoma, Korogwe Vij i j inikumejengwa Mahakama ya Mwanzo ya Kisasa, lakini tokaijengwe imefika miaka saba sasa haijafunguliwa:-

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Je, ni lini Serikali itafungua Mahakama hiyo iliwananchi waachane na usumbufu wa kufuata huduma zaMahakama Korogwe?

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Stephen Hillary Ngonyani, Mbunge wa KorogweVijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mahakama ya Mwanzo yaMagoma il i jengwa muda mrefu kama anavyosemaMheshimiwa Mbunge wa Korogwe, lakini jengo li lehalikukamilika. Mahakama il iyojengwa ni ya kisasa,iliyohusisha ujenzi wa jengo la Mahakama, nyumba ya Hakimuna kantini.

Mheshimiwa Naibu Spika, majengo haya yalisimamakwa muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbaliikiwemo ukosefu wa fedha. Mradi huu sasa umefufuliwa naunatekelezwa na SUMA JKT, chini ya usimamizi wa TBA Mkoawa Tanga na unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumikakabla ya Julai mwaka huu 2018.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Stephen Ngonyani, swalila nyongeza.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Profesamwenzangu. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.Swali la kwanza, kwa kuwa Tarafa ya Magoma ina KataNane na katika Kata hizi ina Mahakama moja tu yaMwanzo ambayo ni hiyo ya Mashewa na huu mradiumechukua muda mrefu bila kufunguliwa. Nataka Serikaliiniambie ni tarehe ngapi Mahakama hii itakuwaimefunguliwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, maneno anayoelezwahapo Mheshimiwa Waziri, naomba kama kutakuwa nauwezekano aende. Hayo anayoambiwa kwenye karatasi

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

yanalingana na jinsi Mahakama yenyewe inavyotengenezwakule nilipo? Nitaomba twende wote ili akahakikishe, aonekwamba imechukua muda mrefu, wanafanya kazi bilakudhibiti na tunapata usumbufu sana kwa walalamikajina washtakiwa kwenda zaidi ya kilometa 35. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria,majibu kwa maswali hayo.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa NaibuSpika, ni kweli Kata ile inahitaji Mahakama zaidi na naaminikatika mpango utakaofuata wa maendeleo wa miaka 10wa Mahakama baada ya huu unaoisha 2020 kukamilika,tutatazama tena maeneo ambayo Kata zao ni kubwa naMahakama ni chache ili katika mpango huo wa awamu yapili wa ujenzi wa Mahakama nchini maeneo hayo yawezekuangaliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la pili lakutembelea eneo la Mashewa ili kujionea jinsi Mahakamahiyo inavyojengwa, niko radhi kufika huko na sina wasiwasiProfesa kwa sababu na mimi mjomba wangu ni fundi kamawewe, kwa hiyo nitafika na kuondoka salama. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuumekwenda, kwa hiyo tutaendelea na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano. Swali la Mheshimiwa John JohnMnyika, Mbunge wa Kibamba, Mheshimiwa Julius Kalangaaulize kwa niaba yake.

Na. 303

Ujenzi wa Barabara za Pete na Mchepuo

MHE. JULIUS K. LAIZER (K.n.y. MHE. JOHN J. MNYIKA)aliuliza:-

Barabara za pete (ring roads) na barabara zamchepuo (feeder roads) ni muhimu katika kupunguzamsongamano na matatizo ya miundombinu kwa wananchi:-

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

(a) Je, Serikali itakamilisha lini ujenzi wa barabarahizo zilizoanza kujengwa katika Jimbo la Kibamba?

(b) Je, Serikali itaanza lini ujenzi wa barabaraambazo zimetajwa katika mipango ya Serikali lakinihazijaanza kujengwa mpaka sasa?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziriwa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibuswali la Mheshimiwa John John Mnyika, Mbunge waKibamba, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama mkakati wakupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar esSalaam, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano mnamo mwaka 2010 ilianza kutekeleza ujenziwa kiwango cha lami wa barabara za pete (ring roads) nabarabara za mchepuo (bypass).

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara zilizoingizwakwenye mpango huo ambazo ziko kwenye Jimbo la Kibambana hatua za utekelezaji wake uko katika hatua mbalimbalini kama ifuatavyo:-

Barabara ya Bunju B – Mpiji Magohe – Victoria – Kifuruhadi Pugu yenye urefu wa kilometa 33.7 (outer ring road);barabara ya Mbezi –Msigani –Malambamawili – Kifuru –Kinyerezi – Banana (sehemu ya Kinyerezi – Mbezi –Malambamawili – Kifuru) yenye urefu wa kilometa 10; nabarabara ya Tegeta – Kibaoni – Wazo Hill -Goba – Mbezi/Morogoro Road yenye urefu wa kilometa 20.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ambazo ujenzikwa kiwango cha lami umekamilika ni sehemu ya barabaraya Mbezi – Msigani – Malambamawili – Kifuru – Kinyerezi –Banana kuanzia Msigani – Kifuru yenye urefu wa kilometa nane

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

na barabara ya Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba Mbezi/Morogoro road sehemu ya Goba Mbezi/Morogoro Road yenyeurefu wa kilometa saba.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ambazo ujenziwa kiwango cha lami unaendelea ni barabara inayoanziaMsigani mpaka Mbezi yenye urefu wa kilometa mbili zikiwemobarabara za kutoka na kuingia kwenye kituo cha mabasi yaMbezi na barabara nyingine ni Goba – Madale yenye urefuwa kilometa tano. Barabara ambayo usanifu wake badounaendelea ni barabara ya pete (outer ring road) ya Bunju B– Mpiji Magohe – Victoria – Kifuru hadi Pugu yenye urefu wakilometa 33.7.

NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Halima Mdeekwa niaba ya Mheshimiwa Julius Kalanga Laizer ambaye piaameuliza kwa niaba ya Mheshimiwa Mnyika. (Makofi/Kicheko)

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Kwa niaba ya Mheshimiwa Kalanga naMheshimiwa John Mnyika, naomba kuuliza maswali mawilimadogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; moja kati yabarabara muhimu za ring road ama barabara za peteambazo zimeainishwa hapa ni barabara ya Goba kwendaMakongo – Chuo cha Ardhi, barabara hii kama ambavyomnafahamu kwa siku yanapita magari zaidi ya laki moja(100,000) lakini vilevile ni barabara yenye umuhimu mkubwasana pale ambapo tutakuwa tunajenga interchange yapale Ubungo kwa sababu magari mengi yatahitajibarabara za kuweza kuchopoka kwenda Mbezi na hatimayeMorogoro Road.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nataka nipate majibuya Serikali, kwa sasa zimejengwa kilometa nne tu halafuzinaonekana zime-stuck hakuna kitu kinachoendelea.Naomba majibu ya Serikali ni lini uendelezaji wa barabarakwa kilometa tano zilizobaki utafanyika kwa kiwango chalami? (Makofi)

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, maelezo amamajibu ya Mheshimiwa Waziri yanaainisha kama vilebarabara ya Goba – Madale – Tegeta Kibaoni imekamilika,lakini ukweli ni kwamba barabara iliyokamilika ni kipandecha Goba, kipande cha Goba – Madale ndiyo kinajengwasasa hivi kwa kilometa tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kazi nzuriambayo inaanza sasa kufanywa, swali langu ni dogo,kiwanda cha Twiga kimekuwa kinafanya matumizi mabovuya hii barabara kwa kupaki magari yake barabarani, haliambayo inahatarisha uhai wa barabara, lakini inahatarishauhai wa wananchi wetu. Kama Serikali ya mtaa imejaribukuingilia kati, Serikali ya Kata imeingilia kati, Mbungenimeingilia kati, lakini kiwanda kinaonekana ni kiburi. Natakacommitment ya Serikali kwamba itafuatilia kiwandani ilimatumizi ya barabara yaachwe kwa ajili ya barabara naisihatarishe uhai wa wananchi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaNaibu Spika, ahsante sana. Kwanza nashukuru kuonakuwa, Mheshimiwa Halima Mdee anatambua juhudikubwa ambazo Serikali hii inazifanya katika kujenga barabarana kuweza kupunguza msongamano katika Jiji la Dar esSalaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tulivyopitisha kwenyebajeti barabara zinazohusiana na kupunguza msongamanokatika Jiji la Dar es Salaam ziko kama kilometa 156, baadhiya barabara zimekamilika lakini baadhi ya barabara juhudizinaendelea kuweza kukamilisha. Kwa hiyo, niseme tukwamba Mheshimiwa Halima, hii barabara ambayounaizungumzia barabara ambayo inapita Madale kwambakuna kipande cha kilometa tano kinaendelea kukamilishwa,ni mpango wetu na hata ukiangalia kwenye bajeti ni kuwezakuikamilisha barabara hii nzima.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimwombe tu avutesubira na wananchi wavute subira, tunafahamu umuhimuna uharaka wa kutengeneza barabara katika Jiji la Dar esSalaam kupunguza msongamano.

Mheshimiwa Naibu Spika, ziko awamu nyingi zitakuja,kila awamu ikikamilika ni fursa ya kuanza awamu nyingine ilihatimaye tumalize kabisa msongamano katika Jiji la Dar esSalaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumza juu yabarabara kipande ambacho unasema kilometa tano kutokaMakongo Juu kwenda Chuo cha Ardhi, najua tunafanyajuhudi ya kumaliza tatizo la compensation eneo lile iliwananchi waweze kupisha barabara ikamilike. Niseme tukwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na watumiaji wabarabara kwamba, ni mkakati wa Serikali kwamba wakatiwa ujenzi wa interchange ya Ubungo barabara hiyoanayoitaja Mheshimiwa Mbunge ni muhimu sana. Nimuhimu sana kuhakikisha kwamba tunapunguzamsongamano kipindi chote cha ujenzi wa barabara paleUbungo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo Serikalitunaona uko umuhimu na kwa haraka sana kukamilishabarabara hii. Kwa hiyo avute tu subira, barabara hiitutaitengeneza pamoja na barabara zingine. Iko mipangomingi tu mizuri katika kupunguza msongamano katika Jiji laDar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwombe tu MheshimiwaHalima, akisoma pia kwenye hotuba ya bajeti ambayoMheshimiwa Waziri aliwasilisha hapa ukurasa wa 17 hadi wa18 na ukurasa wa 25 ataona mambo mazuri yaliyoko huku.Angepitia tu ili aone namna tulivyojipanga kuhakikishakwamba Dar es Salaam inabakia vizuri barabara zinakuwazinawasaidia wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kiwanda cha TwigaCement kupaki magari, naomba nilichukue hilo, lakini niseme

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

tu kwamba tunao mpango kabambe wa kuwashughulikiawanaotumia barabara vibaya katika Jiji la Dar es Salaam,pia tunafanya patrol na kwenda na mizani ile ya kuhama.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe tu watumiaji wamagari, siyo hao wa barabara hii lakini na maeneombalimbali ambao na wengine wanatumia wakati wa usiku.Tumeshaliona hilo tunalifanyia kazi ili kuhakikisha kwanzamagari yanaegeshwa vizuri kwa ajili ya usalama, lakini piakwa ajili ya kufanya barabara zetu zisiweze kuharibika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili nimelichukuanakushukuru tutaendelea kulifanyia kazi ili tuweze kuondoshahili tatizo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dunstan Kitandula, swalila nyongeza.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru. Hali ya ahadi kwa barabara za Dar esSalaam inafanana sana na ahadi ya barabara ya Tanga -Mabokweni - Maramba - Bombo Mtoni - Kitivo hadi Sameambapo barabara hii ilikuwa kwenye mpango wa kujengwakwa kiwango cha lami kupitia fedha za MCC II, lakini mradiule ukashindikana. Sasa ni lini Serikali itaanza usanifu wabarabara hii ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge,najua suala la barabara hii ya Tanga - Maramba Mawili-Bombo Mtoni kupanda mpaka kwenda upande mwinginetunakwenda Same na upande mwingine tunapita Lushoto,barabara hii nimeipita nimeiona.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile ilikuwa kwenyempango hauku-mature nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

na mara nyingi nampa feedback kwamba tunaitazama sasaili tuone namna bora ya kuweza kuitengeneza barabara hiimuhimu. Wananchi wa Maramba kwa kweli barabara hiinilipita niliiona wana shauku kubwa sana ya barabara hii.Mheshimiwa Mbunge naomba avute subira na nitaendeleakumpa mrejesho namna tunavyoweza kujipangakuitengeneza barabara hii.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, Mbunge waViti Maalum, sasa aulize swali lake.

Na. 304

Waendesha Bodaboda Kuwapa Wanafunzi Mimba

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza:-

Imebainika kuwa baadhi ya Madereva wabodaboda wamekuwa wakifanya ukatili kwa kufanyaubakaji, ulawiti na kuwapa baadhi ya wanafunzi mimba:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti halihii hasa kwa wale bodaboda wanaowahadaa baadhi yawanafunzi wa kike?

(b) Je, ni wanafunzi wangapi walioripotiwakupewa mimba na waendesha bodaboda katika kipindicha miaka mitatu (3) iliyopita?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali laMheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum,lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua kuwakuna wanaume wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji,

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

ulawiti na kuwapa mimba baadhi ya wanafunzi. Baadhi yaMadereva wa bodaboda wameripotiwa kujihusisha navitendo hivyo viovu, vitendo hivyo hutokana na tabiambaya, vishawishi na changamoto za mazingira kamavile umbali kutoka nyumbani kwenda mashuleni kwawanafunzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kukabiliana navitendo hivyo mwaka 2016 Serikali ilifanya Marekebisho yaSheria ya Elimu Na. 25 ya Mwaka 1978 ambapo mtuatakayepatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunziakihukumiwa hufungwa miaka 30. Aidha, Sheria ya Kanuniza Adhabu, Sura 16 inabainisha Hukumu ya kifungo chamaisha kwa mtu atakayetenda kosa la kubaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na sheria hizoSerikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibitivitendo hivyo kwa kutoa huduma za ushauri na unasihiambapo shule zimeelekezwa kuwa na Walimu washauri wakike na kiume. Hivyo, mwongozo wa ushauri na unasihi shulenina vyuoni umeandaliwa. Vilevile Serikali kwa kushirikiana nawadau inaendelea na ujenzi wa mabweni, hostel na shulekatika maeneo ambayo wanafunzi wanalazimika kutembeaumbali mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, wanafunzi hupewa mimbana wanaume mbalimbali, wanaweza kuwa ni wakulima,wafugaji, wafanyakazi au wafanyabiashara wakiwemoMadereva bodaboda. Hata hivyo takwimu za wanafunziwaliyopata mimba hazikokotolewi kwa kuanisha makundiya wanaume waliowapa ujauzito. Hivyo ni vigumu kupataidadi ya wanafunzi waliyopewa mimba na madereva wabodaboda.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fatma Toufiq, swali lanyongeza.

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri nina maswali

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa suala laubakaji na ulawiti linazidi kuongezeka; je Serikali haioniimefika wakati wa kuwa na hotline maalum ya kutoa taarifaza ukatili kwa wale ambao wanapata tatizo hilo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwaSerikali imeweka mpango mzuri wa kuwa na dawati la jinsia.Kwa nini Serikali isiweke utaratibu wataalam hawawakaenda kutoa elimu katika shule zetu mbalimbali hapanchini?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi maswali yake yote mawilini kutoa ushauri na mapendekezo, nimhakikishe tuMheshimiwa Mbunge kwamba mapendekezo ambayoanayotoa, nitayafikisha Serikalini tuone namna ya kuyafanyiakazi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge,tumalizie maswali yaliyobaki, Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa Mheshimiwa Desderius John Mipata Mbungewa Nkasi Kusini, sasa aulize swali lake.

Na. 305

Shule Iliyojengwa na Wananchi KuhamishwaKupisha Jeshi

MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:-

Wananchi wa Kata ya Nkandasi wamejitahidi kujengaShule ya Sekondari ya Kata ya Milundikwa hadi kufikia Kidatocha Sita, lakini Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa imeamua shule hiyo kuhamishwa mara mojakuanzia tarehe 1 Januari, 2017 ili kuliachia Jeshi:-

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

(a) Je, Serikali inatoa mchango gani katikauhamishaji na ujenzi mpya wa shule hiyo?

(b) Je, Serikali iko tayari kufanya tathmini yamiundombinu yote ya shule na majengo yaliyojengwa nawananchi na thamani hiyo kuitoa katika fedha taslimu kwaujenzi mpya wa shule?

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Desderius John Mipata, Mbuge wa Nkasi Kusini,lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la Milundikwa lilikuwani Kambi ya JKT iliyokuwa ikiendesha shughuli za malezi yavijana na uzalishaji mali kabla ya Serikali kusitisha mpangowa kuchukua vijana mwaka 1994. Wakati JKT linasitishashughuli zake katika Kambi hiyo liliacha majengo ya ofisi nanyumba za makazi, baadaye Halmashauri ya Wilaya ilianzishashule ya Sekondari ya Milundikwa na kuongeza miundombinumichache katika shule hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hatua ya kuliongezeaJeshi la Kujenga Taifa uwezo wa kuchukua vijana wengi zaidimwezi Novemba mwaka 2016 Serikali ilitoa maelekezo kwaJKT kufufua makambi yaliyokuwa yameachwa mwaka 1994likiwemo la Milundikwa. Kufuatia maagizo hayo ofisi ya Mkuuwa Wilaya ya Nkasi na Halmashauri ya Wilaya hiyo waliratibuna kusimamia utaratibu wa kuhamisha Walimu na wanafunziwaliyokuwa katika shule Milundikwa kwenda katika shulejirani. Baadhi ya wanafunzi walihamishiwa katika shule yaSekondari ya Kasu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangiamaendeleo ya wanafunzi waliokuwa wakisoma katika Shuleya Sekondari ya Milundikwa mnamo tarehe 9 Februari, 2017Wizara ya Ulinzi na JKT kupitia Makao Makuu ya JKT ilitoamabati idadi 2,014 il i kuhakikisha kuwa vyumba vyamadarasa vilivyokuwa vinaendelea kujengwa vinakamilika

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

na kuanza kutumika. Wizara yangu itakuwa tayari kuendeleakushirikiana na Halmashauri ya Wilaya katika kutoa vifaa vyaujenzi kadri uwezo utakavyoruhusu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Desderius Mipata, swali lanyongeza.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili yanyongeza. Nakiri kwamba ni kweli Jeshi la Kujenta Taifawametusaidia na wanaendelea kutusaidia hata katika kazinyingine, lakini wakati shule hii inatwaaliwa ilikuwa namiundombinu mingi sana na sasa miundombinu badohaijarejeshwa yote.

Mheshimiwa Naibu Spika,Shule hii sasa haina nyumbahata moja ya Mwalimu na ukizingatia kwamba ina Kidatocha Tano na Sita ambayo ni boarding ni wasichanawanakaa peke yako. Je, Serikali haioni umuhimu wakuendelea kutupatia pesa zaidi na hasa pesa za kujenganyumba za Walimu ambapo sasa hivi hakuna hata nyumbamoja?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili wakati Serikaliinatwaa eneo hili na kuipatia Jeshi limezuka suala lingineambalo ni gumu zaidi. Wanajeshi walipokuja palewamechukua eneo sasa la mashamba wanayolimawananchi na kufanya wananchi zaidi ya elfu tano wa Vijijivya Kasu, Milundikwa, Kisula na Malongwe zaidi ya elfu nnekukosa mahali kabisa pa kulima. Naiomba Serikali je, iko tayarikufikiria upya na wakati mwingine ione uwezekano wakuwagawia wananchi sehemu ya eneo ili waendeleekuendeleza maisha yao? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa, majibu.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu langula msingi ni kwamba Wizara yangu iko tayari kuendelea

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

kusaidiana, kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya katikakutoa vifaa vya ujenzi ili waweze kukidhi mahitaji yao yakuifanya shule hii ipate miundombinu inayotakiwa. Bila shakakutakuwa kuna bajeti za kawaida za kupitia Halmashaurinazo hizo wakizielekeza huko na sisi tutakuwa tayari kutoamchango wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Serikali kutwaa eneohili na kufanya watu wengi karibu elfu nne kukosa sehemuya kulima nataka nimfahamishe tu Mheshimiwa Mbungekwamba Serikali haijalitwaa eneo hili bali eneo hili lilikuwa nimali ya Serikali mali ya JKT toka mwanzoni. Kama wakatiwa JKT kurudi pale imetokea kwamba eneo lililochukuliwani zaidi ya lile la awali hilo naweza nikalingalia, lakiniukweli ni kwamba taarifa tulizokuwa nazo ni kwamba JKTwamekwenda kuchukua eneo lao la awali walilokuwa nalokabla ya mwaka 1994 kusitisha shughuli za JKT.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitamwomba MheshimiwaMbunge tukae ili tulijadili suala hili na ikiwezekana tufanyeziara pale tuone tunaweza kusaidia vipi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tumalizie swali la mwishoWizara ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mattar Ali Salum,Mbunge wa Shaurimoyo sasa aulize swali lake.

Na. 306

Ununuzi wa Meli za Uvuvi

MHE. MATTAR ALI SALUM aliuliza:-

Uvuvi wa Bahari Kuu unaingiza kipato kikubwa sanana unaweza ukachangia katika bajeti ya nchi yetu:-

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kununua meliza uvuvi?

(b) Je, Serikali imefikia wapi katika ujenzi waBandari ya Uvuvi nchini?

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali laMheshimiwa Mattar Ali Salum, Mbunge wa Shaurimoyo, lenyevipengele (a) na (b) kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Ilani ya Uchaguzi ya Chamacha Mapinduzi ya mwaka 2015 - 2020 inaelekeza Serikaliumuhimu wa nchi kuvuna rasilimali za uvuvi zilizopo katikaukanda wa Bahari Kuu kwa kuwa na meli za Kitanzania.Lengo la kununua meli hizo ni kuwa na meli za Kitaifakuwezesha uvunaji wa rasilimali za uvuvi katika ukanda waBahari Kuu kwa lengo la kupata chakula na lishe, kuongezaPato la Taifa na kutoa ajira kwa Watanzania watakaofanyakazi katika meli hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kufanikisha azmahiyo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza utaratibu wa kufufuali l i lokuwa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) hatuaitakayowezesha meli zitakazonunuliwa kuwa chini yausimamizi wa TAFICO. Makadirio ya kufufua Shirika laUvuvi Tanzania (TAFICO) ni jumla ya shilingi za Kitanzaniabilioni 45 ikiwemo maandalizi ya ununuzi wa meli za uvuvi.Aidha, Wizara inahamasisha Mifuko ya Kijamii, Taasisi,Mashirika ya Umma na Watanzania kuwekeza katika uvuviwa Bahari Kuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara tayari imempatamtaalam mwelekezi atayefanya upembuzi yakinifu waujenzi wa Bandari ya Uvuvi ambapo kukamilika kwakazi hii kutawezesha kujua gharama halisi za ujenzi naaina na ukubwa wa bandari itakayojengwa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mattar Salum, swali lanyongeza.

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Wazirianafanya kazi vizuri, lakini nimfahamishe Mheshimiwa

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Waziri eneo hili la uvuvi na ununuaji wa meli za uvuvi naujengaji wa Bandari ya uvuvi ni suala very importantlazima tulifanyie kazi kwa kina. Sasa swali la kwanza,Shirika la TAFICO ni lini litakamilika ili hizi meli ziwezekununuliwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kila sikutunasema tuna wataalam ambao wanafanya upembuziyakinifu, lakini nimwambie Mheshimiwa Waziri hebu atuelezeni lini hawa wataalam watakamilisha huu upembuzi waoyakinifu ili hii bandari ya uvuvi iweze kujengwa kwa maslahiya Watanzania. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvimajibu.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa NaibuSpika, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba, kama ambavyo Mheshimiwa Naibu Waziriameeleza hapa kwamba tumeshampata mshauri elekezi natayari ataingia mkataba mwezi huu huu na kulipwamalipo ya awali na atafanya kazi ndani ya miezi nane. Baadaya miezi nane tayari tutakuwa tumeingia hatua sasa yaujenzi wenyewe. Kwa hiyo, atuvumile katika hiyo hatua,Mshauri Elekezi ameshapatikana na tayari zoezi litaanza.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge mtakumbukawakati nikisoma taarifa ya Mheshimiwa Spika kwambatutawasikia wenzetu waliyotuletea heshima wakitusalimu,tutaanza na Mheshimiwa Mboni Mohamed Mhita atusalimukwa dakika tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Stephen Masele. (Makofi)

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Naibu Spika,awali ya yote napenda nichukue nafasi hii kukushukuru wewebinafsi na kulishukuru Bunge letu Tufuku, niwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa mapokezi mazuriambayo mmetuandalia pia nimshukuru Mheshimiwa Spika

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

na Watumishi wote wa Bunge kwa namna ya pekeeambavyo wametusaidia, wametuombea kuhakikishakwamba tunailetea heshima nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii piakumshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli na Serikalikwa ujumla kwa msaada mkubwa waliotupatia, bilakusahau kwamba leo ni siku muhimu ambayo Wizara yaMambo Nje inawasilisha bajeti yake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwasilisheniwasilishe pongezi na shukrani za dhati kabisa kwa Waziriwa Mambo ya Nje Mheshimiwa Dkt. Mahiga, Naibu Waziri,Katibu Mkuu, Waheshimiwa Watendaji wote, Naibu KatibuMkuu, Waheshimiwa Mabalozi walioko Afrika na waliyokonje ya Afrika. Nitawataja wachache wakiwemo Balozi wetualiyepo Addis Ababa; Balozi wetu Mama Asha Rose Migiroaliyepo London, yuko mbali yuko Ulaya lakini aliweza kufanyakubwa ya kutusaidia. Balozi wetu aliyepo Nairobi, BaloziEmmanuel Nchimbi aliyepo Brazil pamoja na Balozi wa Afrikaya Kusini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimshukuru Balozi Graceambaye yupo Mkuu wa Idara ya Afrika wapo Grace wawilipale, Grace Mujuma na Grace Martin ambaye ni Mkuuwa Itifaki kwa kweli wamekuwa msaada mkubwa sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee niwashukuruwajumbe wote wa Bunge la Afrika wanaotoka Tanzania,tukiongozwa na Mheshimiwa mama Asha Abdullah Jumamaarufu kama Bi. Macron na ndugu yangu MheshimiwaDavid Ernest Silinde, Mheshimiwa Mboni Mhita kwa ushirikianomkubwa sana ambao wameutoa katika kampeni ambazotulikuwa tukifanya kule Afrika Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimechaguliwa kuwaMakamu wa Rais wa Bunge la Afrika ambayo ni organmuhimu ya Umoja wa Afrika. Moja ya majukumu kama First

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Vice President ni kusimamia shughuli za Utawala, za Fedha,Human Resources na Operation zote za Bunge la Afrika.Jukumu kubwa la haraka ambalo ninalo sasa hivi nikusimamia timu inayofanya reform ya African Union. Timu hiiipo chini ya Rais Paul Kagame, kwa hiyo kwa nafasi yanguautomatic naingia kusimamia timu hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, naomba Bunge lakoTufuku liweze kunipa ushirikiano ili niweze kutimiza majukumuyangu vizuri. Kwa nafasi hii nawashukuru sana, Munguawabariki sana, sina maneno mazuri ya kuwashukuru zaidiya hayo. Ahsanteni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bila kusahau naombaniwashukuru wananchi wa Shinyanga na naombaniwashukuru kwa kunivumilia, kwa sababu haikuwa kazirahisi, nil ihitaji muda wa kutosha kufanya kampeni.Nawashukuru sana na Jumamosi nitakwenda Shinyangakuwasalimia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Makamu waRais wa Bunge la Afrika. Mheshimiwa Mboni Mhita. (Makofi)

MHE. MBONI M. MHITA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Mawaziri,Waheshimiwa Naibu Mawaziri, Waheshimiwa Wabunge,timu nzima ya Staff wa Ofisi ya Bunge, naomba kutumiafursa hii kwanza kuwashukuru sana kwa ushirikianomkubwa ambao mmekuwa mnatupa. Ushirikianomkubwa ambao pia mmetupa kwa kipindi hikiambacho tulikuwa kwenye uchaguzi, lakini kikubwa zaidinaomba nitumie fursa hii kuwashukuru sana kwa kutuamini.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama mjuavyo sisi niWabunge ambao ni Bunge hili mlituchagua kuweza kwenda

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

kuwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mliwezakutuchagua pia kuweza kuwakilisha Bunge letu hili la Jamhuriya Muungano wa Tanzania kuweza kwenda kuwakilishakatika Bunge la Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nafasi ambayo Tanzania,nasema Tanzania kwa sababu sikugombea kamaMheshimiwa Mboni, bali nimegombea kama Tanzania, nafasiambayo tumeipata ni ya Urais wa Caucus. Ni mara yakwanza kabisa kwamba, tumeweza kupata Binti kushikanafasi hii toka Caucus hiyo ya Vijana ya Bunge la Afrikaambayo ndiyo jukwaa kubwa kabisa ambalo linazungumziakutatua na kusikiliza changamoto na kero za Vijana Afrikalianzishwe katika Bunge la Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwahakikishiekwamba, nitafanya kazi kwa uadilifu mkubwa nikiwekamaslahi ya nchi yangu mbele, nikiweka maslahi ya Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele. Nawaomba tuBunge letu pamoja na Caucus yetu ya vijana ambayo sisituko hatua ya mbele kabisa, nchi nyingi bado hawanacaucus, lakini nilijivunia sana pale ambapo nilisema kwamba,Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuko hatua zambele na tuna Caucus ya Vijana katika Bunge letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitawaomba sana wadogozangu na uongozi mzima, niko hapa kwa lolote lile ambalolitahitaji intervention yangu kwenye platform ya Bunge laAfrika na Afrika kwa ujumla niko tayari kuwatumikia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie fursa hiipia kumshukuru sana Mama yangu ambaye ameongozananami leo, ndugu Zabein Muhaji Mhita.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Rais waCaucus ya Vijana Bunge la Afrika. Waheshimiwa Wabungenitaleta kwenu matangazo tuliyonayo, tutaanza namatangazo ya wageni:-

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Kwanza ni wageni walioko jukwaa la MheshimiwaSpika. Tutaanza na wageni 133 wa Mheshimiwa Balozi Dkt.Augustine Mahiga ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki ambao ni Ndugu ElizabethMahiga ambaye ni Mke wa Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahiga.Tunaye pia, Profesa Adolf Mkenda ambaye ni Katibu Mkuu.Tunaye pia, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye ni NaibuKatibu Mkuu na Dkt. Stergomena Tax ambaye ni KatibuMkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).(Makofi)

Vile vile tunaye pia, Balozi Dkt. Ladislaus Kombaambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa chaMikutano cha Afrika (AICC). Tunaye pia, Ndugu Ali SaidMatano ambaye ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bondela Ziwa Viktoria. Tunaye pia Ndugu Alishilia Kaaya ambaye niMkurugenzi Mtendaji wa AICC. Tunaye pia, Dkt. BenardAchiula ambaye ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, hawa viongozi wetuwameambatana na Mabalozi wa nchi mbalimbali namashirika ya Kimataifa ambao ni Mheshimiwa Eugen Kayihuraambaye ni Balozi wa Rwanda. Mheshimiwa Lucas Domingoambaye ni Balozi wa Cuba. Tunaye pia, sasa sijui kama hili nijina la mtu mmoja ama vipi, lakini Balozi HernandesPolledo, pengine ni huyohuyo mmoja, many thanks, sawa.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaye pia MheshimiwaBenson Keith Chali ambaye ni Balozi wa Zambia;Mheshimiwa Sahabi Isa Gada ambaye ni Balozi wa Nigeria;Mheshimiwa Gervais Abayeho ambaye ni Balozi wa Burundi;na Ndugu Joel Cumbo ambaye ni Kaimu Balozi wa Angola.(Makofi)

Tunaye pia, Ndugu Joerg Herrera ambaye ni NaibuBalozi wa Ujerumani; Ndugu Alexandre Peaudeau ambayeni Naibu Balozi wa Ufaransa; Balozi William Ruben ambaye niNaibu Balozi wa Sudan Kusini; Ndugu Peter Sang ambaye ni

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mwakilishi wa Balozi wa Kenya; Ndugu Zhu Jianzheng ambayeni Mwakilishi wa Balozi wa China; Ndugu Vassily Chitaezambaye ni Mwakilishi wa Balozi wa Urusi. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaye pia, Ndugu AndreaHeath ambaye ni Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu (RedCross Tanzania); Ndugu Amin Kurji ambaye ni Mwakilishi Mkaziwa mtandao wa Agha Khan Tanzania; Ndugu Nima Sittaambaye ni Mkuu wa Ofisi Ndogo ya Shirika la Chakula Duniani(World Food Program); tunaye pia, Ndugu Justine Kajereroambaye ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Diplomasia ya UchumiTanzania (TEDEF). (Makofi)

Vile vile tunaye Ndugu Lunda Asmani ambaye niMwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Baraza la Diaspora laWatanzania Wanaoishi Marekani (DICOTA); pia NduguEmmanuel Kasoga, ambaye ni Mkurugenzi wa Asasi yaKidiplomasia ya Vijana (YDI); na Ndugu Renatus Muabhiambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii Taifa. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, pia wapo Mabalozi ndaniya Wizara, Mkuu wa Itifaki, Wakurugenzi na Wakuu wa Idarana Vitengo vilivyopo chini ya Wizara hii. Mabalozi na wageniwetu wote tunawakaribisha sana Bungeni. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tunao pia wageni wawiliwa kwangu ambao ni marafiki zangu kutoka Dar-es-Salaamna hawa ni mtoto wa Mheshimiwa Richard Ndassa,anayeitwa Ndugu Annie Ndassa na Ndugu Kauye Magelejaambaye ni dada wa Mheshimiwa Ndassa. Karibuni sana.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao pia wageni waWaheshimiwa Wabunge na tutaanza na mgeni waMheshimiwa Mboni Mohamed Mhita, ambaye ni mama yakemzazi, Ndugu Zabein Mhita, ambaye ni Mbunge Mstaafu.Karibu sana mama. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tunao pia, wageni wawiliwa Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde Naibu Waziri, Ofisi

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), ambao ni Wakurugenziwa kampuni ya Ecosol Design & Consultant inayojishughulishana utengenezaji wa mashine za kutengeneza mkaa kupitiapumba na taka ngumu, ambao ni Ndugu Kareem Hassanna Ndugu Jamal Mohamed. Karibuni sana. (Makofi)

Tunaye pia Mgeni wa Dkt. Rashid Chuachua, ambayeni rafiki yake na huyu ni Ndugu Faya Almasi kutoka MasasiMkoani Mtwara. Karibu sana. (Makofi)

Pia tunaye mgeni wa Mheshimiwa Flatei Massay,ambaye ni Mke wake, Ndugu Zamzam Abdi kutoka Mbulu,Mkoani Manyara. Karibu sana. (Makofi)

Kuna mgeni wa Mheshimiwa Vedastus Manyinyi,Mwenyekiti wa CCM Kongoto, Mkoani Mara. Naye huyu niNdugu Nestory Matiku. Karibu sana. (Makofi)

Tunao pia, wageni wawili wa Mheshimiwa PaulineGekul, ambao ni wadogo zake kutoka Babati, MkoaniManyara. Karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao pia, wageniwaliotembelea Bunge kwa ajili ya mafunzo. Kundi la kwanzani wanafunzi 58 na Walimu sita kutoka Shule ya Msingi yaMarangu Hills iliyopo Marangu, Mkoani Kilimanjaro. Karibunisana. (Makofi)

Tunao pia, wanafunzi 10 na Wahadhiri wawili kutokaChuo Cha Biblia, ETBC cha Dodoma. Karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia, wanafunzi 48 na Walimu Watano kutokashule ya Sekondari ya Wasichana – Huruma ya Dodoma.Karibuni sana. (Makofi)

Tunao pia, wanafunzi 80 kutoka Chuo Kikuu chaDodoma wanaosomea Uhusiano wa Kimataifa naDiplomasia. Karibuni sana na Mheshimiwa Waziri naona kwelihawa wanasomea Diplomasia, kwa suti walizopiga leo hapohatari kabisa. Karibuni sana. (Makofi)

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Waheshimiwa Wabunge ninalo pia, tangazo kutokakwa Mheshimiwa Joseph Mhagama ambaye ameleta kwaniaba ya uongozi wa volleyball na Basketball, anawatangaziaWaheshimiwa Wabunge kuwa mazoezi kwa wachezaji watimu za Bunge za mpira wa wavu (volleyball) na mpira wakikapu (basketball) kwamba, mazoezi yameshaanza katikaviwanja vya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kila sikukuanzia saa 12.00 mpaka saa 1.00 asubuhi, mnaombwakuhudhuria bila kukosa. Pia, Wabunge wapya ambaowangependa kujiunga na michezo hiyo wanakaribishwakujiunga.

Waheshimiwa Wabunge, tumefika mwisho wamatangazo na tutaendelea na ratiba iliyo mbele yetu.Katibu.

NDG. RAMADHAN ABDALLAH ISSA – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Nje na

Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mwongozo wa Spika.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nitamwitaMheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa AfrikaMashariki.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwaruhusa yako nitoe pongezi za pekee kwa Mheshimiwa StephenMasele kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais waBunge la Afrika, ni fahari kwa Tanzania, ni fahari kwaBunge, ni fahari kwa mgombea mwenyewe, hongera sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia, kutoa pongezikwa Mheshimiwa Mboni Mhita, Rais wa Kikosi cha Vijana –

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Bunge katika Afrika. Sisi kama Wizara tumepata heshima yakuwasaidia hawa Wabunge wetu kugombea na kushindanafasi hizo walizowania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia taarifailiyowasilishwa leo Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamanaomba sasa kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likubalikupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango wabajeti ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na UshirikianoAfrika Mashariki Mwaka 2017/2018. Aidha, naomba Bunge lakoTukufu lijadili na kupitisha mpango wa bajeti ya Wizara kwamwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, napendakumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa fadhila narehema kwa kutujalia afya njema na kutuwezeshakukutana tena katika Bunge lako Tukufu, kujadilimpango wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizarayangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naungana na wenzanguwalionitangulia kuwashukuru na kuwapongeza watoa hojawaliozungumza kabla yangu, hususan, Mheshimiwa KassimMajaliwa Majaliwa Mbunge, Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, kwa hotuba yake ambayo imetoamwelekeo wa utekelezaji na wa majukumu ya Serikalikwa Mwaka wa fedha 2018/2019 ambayo pia imetoa dirana kuainisha masuala muhimu ya Kitaifa, Kikanda naKimataifa ambayo baadhi yake yanagusa majukumu yaWizara yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi yetu imekuwa nyepesizaidi kutokana na ushirikiano mzuri na ushauri tunaoupatamara kwa mara kutoka kwenye Kamati ya Kudumu ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hivyo naomba pianitumie fursa hii kutoa shukrani zangu kwa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamachini ya uongozi wa Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu,Mbunge. (Makofi)

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati hii imetoa mchangomkubwa na imekuwa mhimili muhimu katika kuiwezeshaWizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa kutoa ushaurikuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaposimama mbele yenukusoma hotuba hii, nyuma yangu kuna kundi kubwa laWatendaji na Watumishi walioniwezesha kutekelezamajukumu yangu kwa ufanisi mkubwa. Sina budi kutoashukrani zangu za dhati kwa kuwa, kwa kiasi kikubwa ndiyowanaowezesha nisimame mbele yenu leo kuwasilisha hotubahii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekeenaomba nitumie nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Dkt.Susan Alphonce Kolimba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki; Profesa Adolf Faustine Mkenda,Katibu Mkuu; Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, NaibuKatibu Mkuu; Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi, Wakuu waIdara na Vitengo, Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chiniya Wizara yangu kwa kujituma na kutekeleza majukumu yaokwa weledi na kufanikisha kwa kiwango cha juu utekelezajiwa Bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018, pamoja nakuandaa bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2018/2019.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwa,naungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa polekwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wa Jimbola Songea Mjini kwa kifo cha Mheshimiwa Leonidas Gamaaliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kilichotokea mweziNovemba 2017. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemumahali pema peponi. Amina.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza Wabungewote waliochaguliwa na kuteuliwa kisha kupitishwakatika kipindi cha mwaka huu wa fedha. Kuchaguliwana kuteuliwa kwao ni kielelezo cha kuaminiwa nawananchi ili kuwawakilisha ipasavyo katika Bunge hiliTukufu.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekeenaomba nichukue fursa hii kumpongeza Dkt. Stergormena L.Tax kwa kuchaguliwa tena kuendelea kushika nafasi yaKatibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.Aidha, napenda kumpongeza Bi. Sabina Seja kwakuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Umoja waAfrika kuhusu Masuala ya Rushwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile, napendakuwapongeza tena Mheshimiwa Stephen Masele kwakuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika; naMheshimiwa Mboni Mhita kwa kuchaguliwa kuwa Rais waKamati ya Vijana ya Bunge la Afrika. Kuchaguliwa kwao tenani kielelezo cha kuaminiwa kwa Taifa letu katika medani zakimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa mchoyo wafadhila kama sitamshukuru kwa dhati mke wangumpendwa Elizabeth Mahiga pamoja na watoto wetu kwakunivumilia, kuniunga mkono na kuniombea kwa MwenyeziMungu ili niweze kutekeleza majukumu niliyopewa naMheshimiwa Rais katika kujenga na kutetea maslahi ya Taifaletu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba yangu hii kamainavyoonekana katika kitabu cha hotuba kilichowasilishwakwako naomba iingizwe kwenye kumbukumbu za Bunge hiliTukufu; hivyo basi nitasoma muhtasari wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hali ya Mahusiano yaTanzania na Nchi Nyingine. Mahusiano ya Tanzania na nchina mashirika mbalimbali ya kikanda na kimataifayameendelea kushamiri kwa manufaa ya pande zotezinazohusika. Kutokana na mahusiano hayo, tunazo ofisi zaubalozi katika nchi zote ambazo ni majirani zetu kwenye nchikavu na pia visiwa vya Comoro.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa Tanzania ina jumlaya balozi 41 zinazotuwakilisha nje ya nchi. Pamoja na balozihizo nchi yetu ina ofisi tatu za Konseli (Consular) Kuu katika

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Miji ya Mombasa, Jeddah na Dubai. Kadhalika, Tanzania inajumla ya Makonseli (Consulars) wa heshima 35wanaotuwakilisha katika miji mbalimbali duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeendelea kuwa namahusiano mazuri ya kidiplomasia na nchi mbalimbaliduniani. Hadi sasa jumla ya nchi 62 zina Mabalozi Wakaazina Makonseli (Consulars) wa heshima 24 wanaoiwakilisha nchizao hapa nchini Tanzania. Aidha, nchi 39 zinawakilishwanchini na mabalozi wasio wa makaazi ambao ofisi zao ziponje ya Tanzania. Katika kuonesha kuimarika kwa mahusiano,nchi za Ethiopia na Belarus zipo katika hatua za kufunguabalozi zao hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo ya kina kuhusu haliya mahusiano kati ya Tanzania na nchi nyingineyanapatikana kuanzia aya ya tisa hadi aya ya 14 katikakitabu cha hotuba yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Misingi ya Nchi katikaMahusiano Kimataifa; Tanzania inaheshimu misingi yamahusiano na mataifa mengine duniani ambayo tunamahusiano ya kidiplomasia na yale ambayo bado hatunamahusiano ya kidiplomasia. Ni kwa misingi hiyo mataifamengine nayo yanawajibika kuheshimu misingi ya Tanzaniaambayo ni pamoja na kulinda uhuru wetu, umoja wetu,kujiamulia mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa, kulindamipaka ya nchi yetu, kulinda haki, kuimarisha ujirani mwemana kuunga mkono Sera ya Kutofungamana na Upandewowote.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kulihakikishia Bungelako Tukufu kuwa Tanzania italinda misingi hiyo daima.Aidha, napenda tueleweke wazi kuwa Tanzaniainaendelea kushirikiana na mataifa yote duniani na kushirikikikamilifu katika mijadala ya majukwaa ya kimataifakatika kutetea uhuru, haki za binadamu na usawa kwakuzingatia mahusiano yaliyopo kwa kila nchi kwa ajili yamaslahi mapana ya uchumi, jamii na maendeleo ya nchiyetu.

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa mantiki hiyo,Tanzania itaendelea kutekeleza Sera ya Kutofungamana naUpande wowote kama ambavyo imekuwa ikifanya miakayote na siku zote. Tanzania haitarajii nchi nyingine yoyotekuiamulia mambo yake, kushinikizwa, kutishwa au kuingiliwana nchi yoyote katika mambo yetu ya ndani. Marafiki wetuni lazima waheshimu msimamo wetu kwambahatutachaguliwa nani awe rafiki yetu na nani awe adui wetu.Maslahi ya nchi yetu ni imani yetu ya haki na usawa waubinadamu ndio dira ya msimamo wetu kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo ya kina kuhusumisingi ya nchi yetu katika mahusiano ya kimataifayanapatikana kuanzia aya ya 15 hadi 17 katika kitabu chahotuba yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Msimamo wa Tanzaniakatika Masuala Mbalimbali ya Kimataifa; napenda kutumiafursa hii kulieleza Bunge lako Tukufu kuwa msimamo waTanzania kuhusu suala la Palestina na Israel haujabadilika.Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifawa suluhu ya kuwa na mataifa mawili yaani Palestina huruna Israel salama. Tunaendelea kuunga mkono kufanyika kwamajadiliano yatakayosaidia kumalizika kwa mgogoro huowa Mashariki ya Kati uliodumu muda mrefu kati ya nchi hizimbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwambamahusiano yetu na Israel yanaongezeka na tutahakikishayanaimarika kwa manufaa na maendeleo ya Taifa letu.Tanzania inatambua kuwa Israel ina haki ya kuishi kama Taifahuru na salama; na hivyo ndivyo iwe kwa Wapalestinaambao ni majirani zao. Tutashiriki katika mijadala yotekimataifa katika kutafuta suluhu ya Mashariki ya Kati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania pia inaendeleakuunga mkono juhudi za usuluhishi wa mgogoro waSahara Magharibi katika mchakato wa maelewanounaosimamiwa na Umoja wa Mataifa na kuungwa mkonona Umoja wa Afrika. Tuna imani kuwa kurejea kwa

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Morocco katika Umoja wa Afrika kutatoa fursa kwa umojahuo kutoa mchango wake katika kutafuta suluhu yamgogoro huo ambao kwa muda mrefu umekuwaukishughulikiwa na Umoja wa Mataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mfalme Mohamed VI waMorocco alitembelea hapa nchini mwishoni mwa mwaka2016 na kutiliana saini mikataba 21 ya ushirikiano katika sektambalimbali. Tanzania iliunga mkono Morocco kurudi katikaUmoja wa Afrika na kuingia katika Baraza la Usalama naAmani la Umoja wa Afrika. Tanzania itaendelea kushirikianakatika vikao mbalimbali vya kutafuta suluhu ya mgogorohuo. Tunatarajia uhusiano wetu na nchi ya Moroccoutaendelea kukua katika sekta mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, POLISARIO ni chama chaukombozi wa Western Sahara ambacho kilipewa hadhi yanchi yenye Serikali na uanachama wa Umoja wa Afrika tangumwaka 1982. Suala hili limeanza kuleta utata kisheriakatika Umoja wa Afrika na katika duru za kimataifa. KihistoriaMorocco inadai kuwa eneo hilo lilikuwa ni sehemu yaufalme wa Morocco kabla ya ukoloni wa Hispania. Kwakuzingatia maamuzi ya OAU Tanzania imekuwa nauhusiano wa Kibalozi na Western Sahara kupitia chama chaPOLISARIO.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ushiriki wa Tanzania katikaMasuala ya Kulinda Amani na Kulinda Amani; Tanzaniaimeendelea kuunga mkono jitihada za kikanda na za Umojawa Mataifa za kuimarisha amani na usalama duniani.Maelezo ya kina kuhusu jitihada hizo yanapatikana katikaaya ya 20 hadi 24 katika kitabu cha hotuba yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mapitio ya Utekelezaji waMajukumu ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018; katikakutekeleza majukumu ya Wizara kwa mwaka 2017/2018,Wizara yangu ilitengewa kiasi cha Sh. 157,980,248,704/=. Katiya fedha hizo, Sh.149,980,248,704/= ilikuwa kwa ajili yamatumizi ya kawaida na Sh.8,000,000,000/= ilikuwa kwa ajiliya bajeti ya maendeleo. Katika fedha zilizotengwa kwa

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

matumizi ya kawaida; Sh.140,496,296,704/= ilikuwa kwa ajiliya matumizi mengineyo; na Sh.9,483,952,000/= ilikuwa kwaajili ya mishahara.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018, Wizara ilitarajia kukusanya maduhuli kiasi chaSh.25,773,882,820/=. Hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2018, Wizaraimefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. 22,198,966,840/=, sawana asilimia 86 ya makisio ya makusanyo yote ya maduhuli.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia tarehe 30 Aprili2018, balozi zetu nje zimerejesha katika Mfuko Mkuu wa Serikalikiasi cha Sh.13,025,539,324/=. Wizara yangu inaendeleakusimamia na kutekeleza na kuhakikisha kuwa kiasi chotecha maduhuli kitakachokusanywa kwa mwaka wa fedha2017/2018, kinarejeshwa katika Mfuko Mkuu kamailivyoagizwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia tarehe 30 Aprili,2018, Wizara ilipokea jumla ya Sh.114,185,986,274/=, sawa naasilimia 72 ya bajeti iliyopitishwa na Bunge. Kati ya fedha hizo,Sh.104,534,835,394/=, ilikuwa kwa ajili ya bajeti ya matumizimengineyo; Sh.6,226,955,225/= ilikuwa kwa ajili ya mishahara;na Sh. 3,420,195,655/= ilikuwa kwa ajili ya kutekeleza miradiya maendeleo ya Wizara.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018, Wizara ilipangiwa bajeti ya maendeleo kiasi chaSh.8,000,000,000/=. Hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka huumwezi Mei 2018, Wizara ilipokea kutoka Hazina mgao wafedha wa bajeti ya maendeleo kiasi cha Sh.3,420,195,655/=,sawa na asilimia 42.7 ya fedha za bajeti ya maendeleoiliyokadiriwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya fedha hizo, Sh.1,815,527,215/= zimepangiwa kutumika kufanya ukarabati wajengo la ofisi ya makazi ya watumishi kwenye Ubalozi waTanzania Kampala; Sh. 315,425,000/= ni kwa ajili ya ukarabatiwa makazi ya Balozi Kinshasa; Sh.593,300,000/= kutumikakukarabati nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Lilongwe;

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Sh.195,943,440/= kukarabati makazi ya Balozi wa TanzaniaBrussels; na Sh.500,000,000/= kwa ajil i ya kukarabatimiundombinu ya Chuo cha Diplomasia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendelea kufuatiliaWizara ya Fedha na Mipango upatikanaji wa fedha zamaendeleo kiasi cha Sh.4,579,804,343/=, sawa na asilimia 57.3ambazo hazijatolewa ili kutekeleza miradi ya maendeleoiliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imeendeleakuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya fedha zaumma kama inavyothibitika mapato na matumizi ya Serikali.Kwa kudhihirisha hilo, Wizara pamoja na Balozi zake 39zimepata hati safi isipokuwa Balozi mbili tu zimepata hatizenye shaka katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2016/2017.Nachukua fursa hii kuwashukuru watendaji wa Wizarana kuwahimiza kwamba waendelee kuzingatia sheria,kanuni, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha zaumma na ununuzi wakati wote wanapotekelezamajukumu yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kutoa taarifa yamapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha wa2017/2018, naomba sasa nitumie fursa hii kueleza kwa kifupibaadhi ya mafanikio ya Wizara katika kipindi hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika malengo ya Sera yaMambo ya Nje kuna malengo ambayo ni ya kudumuyanayoiwezesha nchi kuwa katika nafasi yake ndani yajumuiya ya mataifa, kama taifa huru lenye umoja, usalamana lenye hadhi na sifa inazostahili. Hii hasa ni diplomasia yasiasa. Pia kuna malengo ambayo yanaendana na wakatihuo na uongozi uliopo na vipaumbele vya Serikali kwa wakatihuo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika miaka ya sitini hadithemanini malengo ya ziada katika Serikali na Sera yaTanzania yalikuwa ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwaukoloni na ubaguzi wa rangi. Baada ya kukamilisha hayo

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Tanzania iliona umuhimu wa kuwa na Sera ya Mambo yaNje yenye msisitizo wa diplomasia ya uchumi ili kusukumamaendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, diplomasia ya uchumi nimsisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje yenye mikakati, malengo,mbinu na maarifa yanayoelekeza Taifa kupata na kuvunarasilimali na utaalam kutoka Jumuiya ya Mataifa ili kuleta nakuchochea maendeleo ya Taifa letu. Katika Awamu hii yaTano, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alitangazamapema kuwa Tanzania iwe ni nchi ya viwanda ili kusukumazaidi maendeleo ya uchumi na ajira katika uchumi wetu iliifikapo mwaka 2025 tufikie uchumi wa kati.

Mheshimiwa Naibu Spika, azma hii inamaanisha kuwadiplomasia ya uchumi lazima iongeze mkakati wa Diplomasiaya Uchumi wa Viwanda ili kutekeleza maono na mawazo yaMheshimiwa Rais ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwandavilivyojikita kwenye sekta ya kilimo. Kwa hiyo, Diplomasia yaUchumi wa Viwanda lazima itoe vipaumbele katikauwekezaji, miundombinu, nishati, biashara na masoko yabidhaa kutoka kwenye viwanda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Diplomasia ya Uchumi waViwanda ni nyongeza iliyokuja katika Awamu hii ya Tano.Sambamba na mkakati huo, dhana ya Diplomasia ya Uchumiwa Viwanda lazima ilenge sekta nyingine kama kilimo, utaliina madini ambavyo kwa namna moja au nyinginezinawiana na viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kushirikiana na wadaumbalimbali, Wizara yangu imeendelea kutekeleza Diplomasiaya Uchumi wa Viwanda kupitia ziara za viongozi, mikutanoya Tume za Pamoja za Kudumu na ushirikiano wa balozi zetuna nchi nyingine na kwa makongamano ya biashara nauwekezaji yaliyofanyika ndani na nje ya nchi. Kupitia juhudihizo tumeweza kufanikisha kuleta ujumbe wa wawekezajina wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali duniani;kuwezesha wafanyabiashara wa Tanzania kutafuta masokoya bidhaa nje ya nchi na kuvutia utalii.

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kurahisishamazingira ya biashara kati ya Tanzania na nchi nyingine;kupata misaada na mikopo yenye masharti nafuu; na kupataufadhili wa miradi ya maendeleo katika maeneo ya kimkakati.Kwa ujumla nchi imenufaika kupitia sekta za viwanda,biashara, uwekezaji, kilimo, ufugaji, uvuvi, umwagiliaji, ujenziwa miundombinu, afya, nishati, madini, elimu pia mafunzoya ufundi.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya hatua inayofanywana Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara nyingine nikushawishi nchi marafiki kutufutia madeni, kuyapunguza aukuweka masharti nafuu ya kulipa.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa nilipofanya ziara nchini Iran mwezi Oktoba2017, Serikali ya nchi hiyo iliridhia na kutangaza kusameheriba ya deni lililokuwa tangu mwaka 1984 ambayo kwa sasaimefikia kiasi cha Dola za Marekani milioni mia moja hamsini.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, mwezi Septemba2017, Serikali ya Brazil pia ilitoa msamaha wa thamani yaDola za Marekani milioni 203.6 ambayo ni asilimia 86 ya denilote tunalodaiwa na nchi hiyo. Misamaha hiyo ni wazi itaipanafuu nchi yetu katika kulipa madeni. Naomba kutumianafasi hii kuzishukuru Serikali za Iran na Brazil kwa kutusamehemadeni hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo ya kina kuhusuutekelezaji wa diplomasia ya uchumi na hasa uchumi waviwanda yanapatikana kuanzia aya ya 32 hadi 54 katikakitabu cha hotuba yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ushiriki wa Tanzania KatikaJumuiya za Kikanda na Kimataifa. Katika kipindi hiki, Wizarailiendelea kuratibu na kushiriki katika masuala ya ushirikianowa kikanda ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiyaya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Nchizinazopakana na Bahari ya Hindi na Umoja wa Afrika kamaifuatavyo:-

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Mheshimiwa Naibu Spika, Jumuiya ya Afrika Mashariki.Wizara inaendelea kuratibu ushiriki wa Tanzania katikaJumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutekeleza kikamilifumajukumu mbalimbali kwa lengo la kuendeleza maslahimapana ya Taifa letu katika Mtangamano wa AfrikaMashariki. Aidha, Wizara inaendelea kuratibu utekelezaji nauondoaji wa vikwazo visivyo vya forodha, wigo wa pamojawa ushuru wa forodha, itifaki ya soko la pamoja, Itifaki yaUmoja wa Fedha ya Afrika Mashariki, na Ushirikiano baina yaJumuiya ya Afrika Mashariki na Kanda nyingine. Vile vile,Wizara inaendelea kuratibu sekta za uzalishaji, uendelezajiwa miundombinu na uchumi na huduma za jamii namasuala ya siasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo ya kina kuhusuhatua hizo ndani ya Afrika Mashariki yanapatikana kuanziaaya ya 55 hadi 77 ya kitabu cha hotuba yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jumuiya ya MaendeleoKusini mwa Afrika. Katika kuimarisha ushirikiano na Jumuiyaya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Tanzania imeendeleakushiriki kikamilifu katika mikutano na majukwaa mbalimbaliya Jumuiya hiyo. Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Wizarailiratibu ushiriki wa nchi yetu katika masuala ya siasa, ulinzi,usalama na ushirikiano katika SADC na Umoja wa Ulaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na ushiriki wetukatika Jumuiya hiyo, Tanzania imenufaika kwa kupata ufadhiliwa Euro milioni 1.4 kati ya Euro milioni 31.6 zilitolewa na Umojawa Ulaya. Fedha hizo zitatumika kufanya mapitio ya sera zaviwanda ndani ya Tanzania, kuhamisha biashara na kuondoavikwazo vya biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo ya kina kuhusuushirikiano wetu na SADC yanapatikana katika aya ya 78 hadi82 ya kitabu changu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jumuiya ya NchiZinazopakana na Bahari ya Hindi. Wizara inaendelea kushirikikatika masuala yote yanayohusu Jumuiya ya Nchi

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

zinazopakana na Bahari ya Hindi. Katika kipindi cha mweziOktoba, 2017 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikianana Indian Ocean Rim Association (IORA) ilifanya warsha yakuandaa Mkakati wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu waRasilimali ya Uvuvi katika Ukanda wa Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Tanzania imeanzakunufaika na mtandao wa kupeana taarifa za biashara(trade repository) ikiwemo mfumo wa kodi, uajiri na bidhaa,taratibu za forodha na upatikanaji wa leseni za kuingiza nakutoa bidhaa kwa kila nchi iliyo ndani ya Jumuiya ya Bahariya Hindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Umoja wa Afrika; katikakuimarisha ushirikiano na sera na Bara la Afrika, Wizara iliratibuna kushiriki katika mikutano ya 29 na 30 ya Umoja wa Afrikailiyofanyika Addis Ababa Julai, 2017 na Januari, 2018, ambayoilipitisha maazimio mbalimbali. Maelezo ya kina kuhusuushiriki wa Tanzania katika Umoja wa Afrika, maazimioyaliyofikiwa pamoja na mikataba iliyosainiwa yanapatikanakuanzia ukurasa wa 85 hadi 90.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ushirikiano wa Kimataifa;katika kutekeleza jukumu lake la kuratibu masuala yakimataifa, Wizara yangu iliratibu na kushiriki mikutanombalimbali. Baadhi ya Mikutano hiyo ni pamoja na:-

Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa;UN-HABITAT; UNIDO; Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusuHali ya Wanawake; Mikutano ya Kimataifa inayohusuwakimbizi na uhamiaji; Baraza la Haki za Binadamu; Shirikala Chakula Duniani (FAO); na Mkutano wa 25 wa Wakuu waSerikali wa Jumuiya za Madola. Maelezo ya kina kuhusumasuala haya na mikutano hiyo yanapatikana kutokaukurasa wa 91 hadi 94 wa kitabu cha hotuba yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kuratibu na KusimamiaMasuala ya Watanzania Waishio Ughaibuni. Wizarainaendelea kutekeleza azma ya Serikali ya kuwahamasishana kuwashirikisha Watanzania waishio ughaibuni katika

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

kuchangia maendeleo ndani ya nchi yetu. Katikakutekeleza azma hiyo, Wizara kwa kushirikiana na Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar iliandaa Kongamano la Nnela Diaspora lililowakutanisha Watanzania zaidi ya 200kutoka nchi mbalimbali za wadau wa maendeleo hapanchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati ambapokipaumbele cha Taifa ni viwanda, tunahitaji kufikiria na kuletaujuzi maalum walionao Watanzania wanaoishi katikadiaspora au ughaibuni; na vile vile mchango wa kifedhaambao wanaweza kuchangia kutoka kwenye vyanzo vyaobinafsi au kwa kushirikiana na raia wa nchi za nje, mabenkina taasisi nyingine za nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwezesha viwandavyetu kukua na kuwa na masoko huko nje tunahitajikutambua, kupima na kupenya katika masoko mbalimbaliya kigeni. Watanzania walioishi nchi za kigeni na watoto waowanaweza kuchangia zaidi kutokana na ujuzi wao kwakupata masoko kwa kutumia ujuzi wao na lugha ya nchiwaliko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania wengi waliodiaspora wanachangia sana maendeleo ya kijamii, uchumina familia zao za Tanzania na wako tayari kushiriki katikajukumu kubwa la kujenga uchumi wa Taifa hili. Penginetunahitaji kuwa na mfumo rasmi wa kisheria na kisera ilikuwapa nafasi na fursa Watanzania walio nje kuchangiakikamilifu katika maendeleo ya nchi yetu. Inakisiwa kuwaWatanzania walio nje wanatuma Tanzania trilioni shilingimoja kila mwaka. Maelezo ya kina kuhusu mchango wadiaspora katika maendeleo ya nchi yanapatikana kuanziaaya ya 106 mpaka 110.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tathmini ya Hali ya Dunia.Hali ya usalama duniani imeendelea kuimarika pamoja nakwamba changamoto kadhaa zinaendelea kuwepo katikabaadhi ya nchi zetu. Changamoto hizo ni pamoja namigogoro ya kisiasa katika baadhi ya nchi, matukio ya kigaidi

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

na kuongezeka kwa makundi yenye itikadi kali na dhati zakiuchumi na kiusalama zinazosababishwa na mabadiliko yatabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kukabiliana nachangamoto hizo, Tanzania imeendelea kuunga mkonojitihada za kikanda na za Umoja wa Mataifa za kuimarishaamani na usalama duniani. Maelezo ya kina kuhusu tathminiya hali ya usalama duniani yanapatikana kuanzia aya ya 112hadi 131 ya kitabu cha hotuba yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchumi wa duniaumeendelea kuimarika ambapo kwa sasa unakadiriwakukua kwa asilimia tatu ikilinganishwa na asilimia 2.4 mwaka2016. Ukuaji huo umechangiwa zaidi na kuimarika kwauchumi wa mataifa yaliyoendelea, uwekezaji na mitajikwenye nchi zinazoibukia kiuchumi, pamoja na kupandakwa bei za bidhaa. Hali hii inatoa matumaini yakuimarika kwa biashara ya bidhaa hususan kutoka nchizinazoendelea. Maelezo ya kina yanapatikana kuanzia ayaya 132 hadi 137.

Mheshimiwa Spika, Taasisi Zilizo Chini ya Wizara; Wizarayangu inasimamia taasisi tatu ambazo ni Chuo chaDiplomasia, Taasisi ya Mpango wa Kujitathmini KiutawalaBora Barani katika Afrika na Kituo cha Kimataifa cha Mikutanowa Arusha, ambacho pia kinasimamia Kituo cha Mikutanocha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Dar es Salaam.Maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisihizo yanapatikana katika ukurasa wa 138 hadi 146.

Mheshimiwa Spika, Kusimamia Utawala naMaendeleo ya Rasilimali Watu. Wizara yangu ina jumla yawatumishi 456 wa kanda mbalimbali. Kati ya hao 347 wapoMakao Makuu ya Wizara na 109 wapo katika Balozi zetunje ya nchi. Aidha, katika kipindi cha mwaka 2017/2018,Wizara ilipata kibali cha kuajiri watumishi 10 wa kandambalimbali ambapo hadi sasa watumishi watano tayariwameripoti kazini na watumishi watano tayari ajira zaozinakamilishwa.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2017/2018,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania alifanya uteuzi wa mabalozi watanoambapo kati yao watatu wamepangiwa vituo na wawilitaratibu za kuwapangia vituo zinaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara iliandaa SeminaElekezi kwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la AfrikaMashariki iliyofanyika mwaka huu, Januari, 2018, Jijini Dar esSalaam. Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kuwajengea uelewaWaheshimiwa Wabunge hao katika masualayatakayowawezesha kutekeleza kazi zao kikamilifu. Nisemehapa pia kwamba Wizara na Chuo chetu cha Diplomasiatunaandaa mkakati wa kutoa semina kama hizo kwaWaheshimiwa Wabunge wa Bunge hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha mwakawa fedha 2017/2018 Wizara yangu inakabiliana nachangamoto mbalimbali za kimfumo wa dunia, pamoja nazile za kiutendaji. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizoWizara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledina ufanisi mkubwa kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano nawadau wote wa ndani na wa nje, kuhakikisha kwambamalengo ya Serikali yetu na ushirikiano wa kimataifayanaendelea na kuimarika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Shukrani. Kwa namna yapekee naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru Mabalozi,Wawakilishi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Mataifana mashirika mengine ya kimataifa kwa ushirikiano mkubwawanaoutoa kupitia nchi na mashirika yaowanayoyawakilisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Tanoimeendelea kupata mafanikio makubwa kutokana namchango wa wadau na washirika wa maendeleo kutokanchi na asasi mbalimbali za kitaifa, kikanda, kimataifapamoja na sekta binafsi. Naomba nitumie fursa hii kuzishukurunchi za Afrika Kusini, Algeria, Australia, Austria, Brazil, Canada,China, Cuba, Denmark, Finland, Hungary, India, Italia, Ireland,

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Israel, Iran, Japan, Korea Kusini, Kuwait, Malaysia, Marekani,Malta, Misri, Morocco, New Zealand, Norway, Oman, Pakistan,Palestina, Poland, Qatar, Saudi Arabia, Sweden, Singapore,Sri-Lanka, Thailand, Ubelgiji, Ufaransa, Uhispania, Uholanzi,Uingereza, Ujerumani, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ureno,Urusi, Uswisi, Uturuki na Vietnam. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, shukrani ziwaendee piaUmoja wa Ulaya, Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfricanCapacity Building Facility, Benki ya Dunia, Shirika la FedhaDuniani (IMF), Investment Climate Facility for Africa, UNDP naMashirika mengine yote ya Umoja wa Mataifa. Pia TradeMarkEast Africa, Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi yaAfrika, The Association of European Parliamentarians withAfrica, WWF, The Belinda and Bill Gates Foundation, GlobalFund, International Committee of the Red Cross, InternationalFederation of the Red Cross and Red Crescent Societies,Medecins Sans Frontieres pamoja na Mifuko na Mashirikambalimbali ya Misaada. Ni dhahiri kuwa mafanikiotuliyoyapata yamechangiwa kwa misaada wa pekee kabisana mashirika na nchi hizo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo pamoja nachangamoto hizo, wizara imeendelea kutekeleza majukumuyake kwa weledi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Malengo ya Wizara kwaMwaka wa Fedha 2018/2019. Katika mwaka wa fedha huu,pamoja na mambo mengine, Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki imepanga kutekelezamalengo muhimu kulingana na majukumu yake kamayalivyobainishwa katika aya ya 157 ya kitabu changu chahotuba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha wa2018/2019, Wizara yangu imetengewa bajeti ya kiasi chaSh.177, 006,232,000/=. Kati ya fedha hizo Sh.154,410,812,000/=ni kwa ajili ya matumizi mengineyo; Sh.11,795,420,000/= ni kwaajili ya mishahara na Sh.10,400,000,000/= ni kwa ajili ya bajetiya maendeleo.

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti ya matumizimengineyo, Sh.116,010,729,689/= ni kwa ajili ya matumizi yavifungu vya Balozini. Sh.35,324,806,566/= ni kwa ajili yavifungu vya Makao Makuu ya Wizara; Sh.1,077,362,234/=ni kwa ajili ya Mpango wa Kujitathmini Kiutawala boraTanzania; Sh.1,000,000,000/= ni kwa ajili ya fedha zamatumizi mengineyo ya Chuo cha Diplomasia;Sh.1,239,633,751/= ni kwa ajili ya Mahakama ya Afrika ya Hakiza Binadamu na Watu na Sh.158,279,760/= ni kwa ajili ya Bodiya Utekelezaji na Ushauri wa Masuala ya Rushwa ya Umojawa Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika fedha za bajeti yamaendeleo, kiasi cha Sh.10,400,000,000/= zilizopangwa kwamwaka wa fedha 2018/2019, kiasi cha Sh.6,180,676,000/=zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Ubalozi waTanzania Muscat, Oman; Sh.1,819,324,000/= ni kwa ajili yaukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo Ubaloziwa Tanzania Khartoum, Sudan.

Mheshimiwa Naibu Spika, samahani lazima sasanimalizie; nadhani kumekuwa na mchanganyiko hapa.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Omba hela tu.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwezakutekeleza kikamilifu majukumu ya Wizara, kwa mwaka wafedha 2018/2019, naomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumlaya Sh.177,006,232,000/=. Kati ya fedha hizo Sh.166,606,232,000/= ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh.10,400,000,000/=ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchukua nafasihii kukushukuru wewe binafsi na Waheshimiwa Wabunge kwakunisikiliza.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge hojaimeungwa mkono.

HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. AUGUSTINE PHILIPMAHIGA (MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANOWA AFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO

YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWAMWAKA WA FEDHA 2018/2019

UTANGULIZI1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamakuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti yaWizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufulikubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpangona bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki kwa mwaka wa fedha 2017/18. Aidha, naombaBunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti yaWizara kwa mwaka wa fedha 2018/19.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuruMwenyezi Mungu, mwingi wa fadhila na rehema, kwakutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana tena katikaBunge lako Tukufu, kujadili Mpango na Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara yangu.

3. Mheshimiwa Spika, naungana na wenzanguwalionitangulia kuwashukuru na kuwapongeza watoa hojawaliozungumza kabla yangu, hususan Mheshimiwa KassimMajaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Dkt. Philip IsdoryMpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango ambao kwahakika hotuba zao sio tu zimezungumzia mafanikio ya Serikaliya Awamu ya Tano, bali pia zimetoa dira katika mustakabaliwa taifa letu kwa kuainisha masuala muhimu ya kitaifa,

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

kikanda na kimataifa ambayo baadhi yake yanagusamajukumu ya Wizara yangu.

4. Mheshimiwa Spika, naomba pia nitumie fursa hii kutoashukrani zangu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mamboya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya uongozi wa Mhe. Mussa AzanZungu (Mb) na Makamu wake Mhe. Salum Mwinyi Rehani (Mb).Kamati hii imetoa mchango mkubwa na imekuwa muhimilimuhimu katika kuiwezesha Wizara yangu kutekelezamajukumu yake kwa kutoa ushauri kuhusu masualambalimbali ya kiutendaji.

5. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naombanitumie nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. SusanAlphonce Kolimba (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki; Prof. Adolf Faustine Mkenda,Katibu Mkuu; Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, NaibuKatibu Mkuu; mabalozi wa Tanzania nje ya nchi; Wakuu waIdara na Vitengo; watumishi wa Wizara; na taasisi zilizo chiniya Wizara yangu kwa kujituma na kutekeleza majukumu yaokwa weledi na kufanikisha kwa kiwango cha juu utekelezajiwa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18, pamoja na kuandaaBajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2018/19.

6. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa, naunganana Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole kwa familia,ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wa Jimbo la SongeaMjini kwa kifo cha Mhe. Leonidas Gama aliyekuwa Mbungewa Jimbo hilo kilichotokea mwezi Novemba 2017. MwenyeziMungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Amina.

7. Mheshimiwa Spika, nawapongeza wabunge wotewaliochaguliwa na kuteuliwa kisha kuapishwa katika kipindicha mwaka huu wa fedha. Kuchaguliwa na kuteuliwa kwaoni kielelezo cha kuaminiwa na wananchi ili kuwawakilishaipasavyo katika Bunge hili.

8. Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila kamasitamshukuru kwa dhati mke wangu mpendwa Elizabeth

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Mahiga pamoja na watoto kwa kunivumilia, kuniunga mkonona kuniombea kwa Mwenyezi Mungu ili niweze kutekelezamajukumu niliyopewa na Mheshimiwa Rais katika kujenga nakutetea maslahi ya taifa letu.

HALI YA MAHUSIANO NA NCHI NYINGINE

9. Mheshimiwa Spika, mahusiano ya Tanzania na nchi namashirika mbalimbali ya kikanda na kimataifa yameendeleakushamiri kwa manufaa ya pande zote zinazohusika. Tanzaniatuna mahusiano mazuri na majirani zetu wote. Kupitia Jumuiyaya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika, Tanzania ina makubaliano ya kuondoa vikwazo vyabiashara na nchi zote jirani, yaani Msumbiji, Malawi, Zambia,Kongo DRC, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya. Kwakuzingatia misingi ya Sera yetu ya Mambo ya Nje,tumeendelea kuchukua kila hatua kudumisha ujirani mwemana nchi jirani. Tunazo ofisi za ubalozi katika nchi zote ambazoni majirani zetu kwenye nchi kavu na pia katika visiwa vyaKomoros. Tumeendelea na jitihada za kujenga ujirani mwemakwa jamii zinazoishi mipakani na jamii za nchi jirani.

Katika kuimarisha mahusiano hayo, viongozi wa nchi namashirika mbalimbali wameendelea kufanya ziara hapanchini. Mathalan, kwa mwaka wa fedha 2017/18, Tanzaniailipokea Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Uganda, Misri,Burundi, Msumbiji na Rwanda. Aidha, Mawaziri na NaibuMawaziri kutoka nchi za Ujerumani, Israel, Uingereza, Norway,Oman, Burundi, Misri, Poland, Shelisheli, Maldves, China naBrazil walitembelea Tanzania katika kipindi hicho. Pia, Tanzaniailipokea wajumbe maalum wa wakuu wa nchi na serikalikutoka nchi za Uganda, Rwanda, Misri, Poland, Burundi,Morocco, Mjumbe Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni yaUmoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Palestina. Aidha,Ethiopia ipo katika hatua za mwisho za kufungua ubalozi hapanchini na Belarus nao wametuma timu ya uangalizi mweziDesemba 2017 na kuahidi kufungua ubalozi wao mwezi Juni2018.

10. Mheshimiwa Spika, nchi yetu.ilitembelewa.pia na

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yakiwemo Shirika laMaendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO); Benkiya Maendeleo ya Afrika (AfDB); Shirika la Umoja wa Mataifalinaloshughulikia Chakula na Kilimo (FAO); Shirika la Umojawa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS); naJumuiya ya Madola. Aidha, viongozi wengine na wataalamkutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za kimataifaikiwemo Shirika la Maendeleo la Japan (JICA); Shirika laMaendeleo la Korea (KOICA) na Aga Khan walitembeleaTanzania.

11. Mheshimiwa Spika, Viongozi wetu Wakuu wa Kitaifayaani Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamu wa Rais,Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Waziri Mkuu naMheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar naowalifanya ziara za kiserikali na kushiriki mikutano katika nchimbalimbali.

12. Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendelea kuwa namahusiano mazuri ya kidiplomasia na nchi mbalimbaliduniani. Hadi sasa jumla ya nchi 62 zina mabalozi wakaazi hapanchini. Kati ya hizo, nchi za China, Oman, Msumbiji na Indiazinaendesha pia ofisi ndogo za ubalozi (konseli kuu) Zanzibar.Kadhalika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja nakuwa na ubalozi Dar es Salaam, ina Konseli Kuu mjini Kigoma.Aidha, nchi 39 zinawakilishwa nchini na mabalozi wasiowakaazi ambao ofisi zao zipo nje ya Tanzania. Vilevile, wapomakonseli wa heshima 24 wanaowakilisha nchi zao hapanchini na yapo mashirika 23 ya kimataifa yenye hadhi yakidiplomasia yanayofanya kazi nchini.

13. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina jumla ya balozi 41zinazotuwakilisha nje ya nchi. Pamoja na balozi hizo nchi yetuina ofisi 3 za Konseli Kuu katika miji ya Mombasa, Jeddah naDubai. Kadhalika Tanzania ina jumla ya makonseli wa heshima35 wanaotuwakilisha katika miji mbalimbali duniani.

14. Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu ya bajetimwaka jana nilieleza kuhusu Serikali kufungua balozi mpya sitakatika nchi za Algeria, Israel, Uturuki, Sudan, Qatar na Korea

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Kusini. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba tayaritumepeleka mabalozi kwenye vituo hivyo.

MISINGI YA NCHI KATIKA MAHUSIANO YA KIMATAIFA

15. Mheshimiwa Spika, taifa lolote duniani huongozwana misingi ambayo lengo lake kuu ni kudumisha amani, ulinzi,usalama na mshikamano wa wananchi wake na taifa kwaujumla. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa namisingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa letu mara baada yauhuru. Misingi hiyo ni pamoja na kulinda uhuru wetu; kujiamuliamambo yetu wenyewe bila kuingiliwa; kulinda mipaka ya nchiyetu; kulinda haki; kuimarisha ujirani mwema; na kuungamkono Sera ya Kutofungamana na Upande wowote kamadira na msimamo wetu katika mahusiano na nchi nyinginekatika Jumuiya ya Kimataifa.

16. Mheshimiwa Spika, misingi hiyo ndiyo inayotufanya leotujivunie Taifa lenye amani, ulinzi imara na usalama duniani;taifa ambalo limekuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge,haki na uhuru; kutafuta amani na kutatua migogoro ya nchimbalimbali kwa gharama kubwa ya rasilimali watu na fedha;Taifa linalojitolea wanajeshi wake kwenye ulinzi wa amani,na kuwa tegemeo la mataifa katika misheni za kulinda amani;Taifa ambalo limekuwa kimbilio kubwa kwa wananchi wamataifa mengine yenye migogoro na ambao wanalazimikakukimbilia nchi nyingine kuokoa maisha yao na kupewa hifadhinchini mwetu.

17. Mheshimiwa Spika, Tanzania inaheshimu misingi yamahusiano na mataifa mengine duniani ambayo tunamahusiano ya kidiplomasia na yale ambayo bado hatunamahusiano ya kidiplomasia. Ni kwa misingi hiyo, mataifamengine nayo yanawajibika kuheshimu misingi ya Tanzaniakama ilivyoainishwa hapo juu. Nataka kulihakikishia Bungelako Tukufu kuwa Tanzania italinda misingi hiyo daima. Aidha,napenda ieleweke wazi kuwa Tanzania itaendelea kushirikianana mataifa yote duniani na kushiriki kikamilifu katika mijadalana majukwaa ya kimataifa katika kutetea uhuru, haki zabinadamu na usawa kwa kuzingatia mahusiano yaliyopo kwa

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

kila nchi kwa ajili ya maslahi mapana ya uchumi, jamii namaendeleo ya nchi yetu.

Ni kwa mantiki hiyo, Tanzania itaendelea kutekeleza Sera yaKutofungamana na Upande wowote kama ambavyoimekuwa ikifanya siku zote. Tanzania haitarajii nchi nyingineyoyote kuiamulia mambo yake, kushinikizwa, kutishwa aukuingiliwa na nchi yoyote katika mambo yetu ya ndani. Marafikiwetu ni lazima waheshimu msimamo wetu kwambahatutachaguliwa nani awe rafiki yetu na nani awe adui wetu.Maslahi ya nchi yetu na imani yetu ya haki na usawa wabinadamu ndio dira ya msimamo wetu kimataifa.

MSIMAMO WA TANZANIA KATIKA MASUALA MBALIMBALI YAKIMATAIFA

18. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikulieleza Bunge lako Tukufu kuwa msimamo wa Tanzaniakuhusu suala la Palestina na Israel haujabadilika. Tanzaniainaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhuya kuwa na mataifa mawili yaani Palestina huru na Israelsalama. Tunaendelea kuunga mkono kufanyika kwamajadiliano yatakayosaidia kumalizika kwa mgogoro huouliodumu muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Ni kweli kwambamahusiano yetu na Israel yanaongezeka na tutahakikishayanashamiri kwa manufaa na maendeleo ya Taifa letu.Tanzania inatambua kuwa Israel ina haki ya kuishi kama Taifahuru na salama na hivyo ndivyo iwe kwa Wapalestina ambaoni majirani zao. Tutashiriki katika mijadala yote kimataifa katikakutafuta suluhu ya mashariki ya kati.

19. Mheshimiwa Spika, Tanzania pia inaendelea kuungamkono juhudi za usuluhishi wa mgogoro wa Sahara Magharibi,katika mchakato wa maelewano unaosimamiwa na Umojawa Mataifa na kuungwa mkono na Umoja wa Afrika. Tunaimani kuwa kurejea kwa Morocco katika Umoja wa Afrikakutatoa fursa kwa Umoja huo kutoa mchango wake katikakutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao kwa muda mrefuumekuwa ukishughulikiwa na Umoja wa Mataifa. POLISARIOni chama cha ukombozi ambacho kilipewa hadhi ya Serikali

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

na uanachama waUmoja wa Afrika tangu mwaka 1982. Sualahili limeanza kuleta utata wa kisheria katika Umoja wa Afrikana katika duru za kimataifa. Morocco imeanzisha Ubalozi hapanchini. Mfalme Mohamed VI alitembelea hapa nchini mwishonimwa mwaka 2016 na kutiliana saini mikataba 21 ya ushirikianokatika sekta mbalimbali. Tanzania iliunga mkono Moroccokurudi katika Umoja wa Afrika na kuingia katika Baraza laUsalama na Amani la Umoja wa Afrika. Tanzania itaendeleakushiriki katika vikao mbalimbali vya kutafuta suluhu yamgogoro huo. Tunatarajia uhusiano wetu na nchi ya Moroccoutaendelea kukua hasa katika sekta mbalimbali.

UTEKELEZAJI WA SERA YA MAMBO YA NJE

Kulinda Amani

20. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama dunianiimeendelea kuimarika pamoja na kwamba changamotokadhaa zimeendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo.Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya kisiasainayoendelea katika nchi mbalimbali duniani, matukio yakigaidi na kuongezeka makundi yenye itikadi kali pamoja naathari za kiusalama zinazosababishwa na mabadiliko yatabianchi. Tishio jingine kimataifa ni biashara haramu kamavile za madawa ya kulevya, usafirishaji wa binadamu nautakatishaji wa fedha ambayo haina mipaka. Katikakukabiliana na changamoto hizo, Tanzania imeendeleakuunga mkono jitihada za kikanda na za Umoja wa Mataifaza kuimarisha amani na usalama duniani.

21. Mheshimiwa Spika, katika kuunga mkono jitihadaza Umoja wa Mataifa zinazolenga kuimarisha amani nausalama duniani, nchi yetu imeendelea kutoa mchango waaskari wake kwenye misheni za kulinda amani za Umoja waMataifa. Mchango huu ni muhimu na umeiletea nchi yetu sifakubwa kimataifa kwa askari kuwa na nidhamu na kujitoakatika kuifanya dunia kuwa salama. Ushiriki wa askari wetukatika misheni hizo umewaongezea weledi na ujuzi katikamasuala ya medani za kijeshi na usalama wa kimataifa.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

22. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikioyaliyopatikana, tumekuwa tukipata changamoto zakupoteza baadhi ya askari wetu katika misheni hizo. Kwamfano, shambulio la tarehe 8 Desemba 2017 lililosababishaaskari wetu 15 kupoteza maisha na wengine 43 kujeruhiwanchini DRC, linabaki kuwa moja ya shambulizi baya zaidikuwahi kutokea kwenye misheni za kulinda amani duniani kwatakribani miaka 25 iliyopita.

23. Mheshimiwa Spika, tunaushukuru Umoja wa Mataifakwa kuunda timu ya kuchunguza chanzo cha tukio hiloiliyojumuisha maafisa wawili wa ngazi ya juu kutoka Jeshi laWananchi wa Tanzania. Timu hiyo imeshakamilisha uchunguziwake kuhusu chanzo cha tukio hilo na kutoa mapendekezoya hatua za kuchukua ili kuzuia matukio kama hayo yasitokeetena. Serikali inaendelea kuwasiliana na Umoja wa Mataifakwa ajili ya utekelezaji wa taarifa hiyo ambayo itasaidia piaUmoja wa Mataifa kuboresha utendaji wake na ulinzi wa askarikwenye misheni za kulinda amani.

24. Mheshimiwa Spika, naomba ifahamike kwamba,pamoja na shambulio hilo kubwa na la kusikitisha, kamwehatutarudi nyuma wala kukatishwa tamaa. Tunaamini kwenyemisingi yetu ya kusimamia haki na kulinda amani kwa ajili yakuokoa maisha ya watu na kuweka mazingira mazuri yaustawi wa jamii. Tanzania itaendelea kusimamia misingi hiyona kuimarisha ushiriki wetu katika misheni za kulinda amaniduniani.

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA KWAMWAKA WA FEDHA 2017/18

25. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yaWizara kwa mwaka 2017/18, Wizara yangu ilitengewa kiasicha Shilingi 157,980,248,704. Kati ya fedha hizo, Shilingi149,980,248,704 ilikuwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida naShilingi 8,000,000,000 ilikuwa kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.Katika fedha zilizotengwa kwa Matumizi ya Kawaida, Shilingi140,496,296,704 ilikuwa kwa ajili ya Matumizi Mengineyo naShilingi 9,483,952,000 ilikuwa kwa ajili ya mishahara.

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18, Wizara ilitarajia kukusanya maduhuli kiasi cha Shilingi25,773,882,820. Hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2018, Wizaraimefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi 22,198,966,840, sawana asilimia 86 ya makisio ya makusanyo yote ya maduhuli.Hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2018, balozi zetu nje zimerejeshakatika Mfuko Mkuu wa Serikali kiasi cha Shilingi 13,025,539,374.Wizara yangu itaendelea kusimamia na kuhakikisha kuwakiasi chote cha maduhuli kitakachokusanywa kwa mwakawa fedha 2017/18 kinarejeshwa katika Mfuko Mkuu kamailivyoelekezwa na Serikali.

27. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2018,Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 114,185,986,274, sawa naasilimia 72 ya bajeti iliyopitishwa na Bunge. Kati ya fedha hizo,Shilingi 104,538,835,394 ilikuwa kwa ajili ya bajeti ya MatumiziMengineyo; Shilingi 6,226,955,225 ilikuwa kwa ajili ya mishahara;na Shilingi 3,420,195,655 ilikuwa kwa ajili ya kutekeleza miradiya maendeleo.

Miradi ya Maendeleo ya Wizara

28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18, Wizara ilipangiwa bajeti ya maendeleo kiasi cha Shilingi8,000,000,000. Hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi Mei 2018,Wizara ilipokea kutoka Hazina mgao wa fedha za bajeti yamaendeleo kiasi cha Shilingi 3,420,195,655, sawa na asilimia42.7 ya fedha za bajeti ya maendeleo iliyoidhinishwa. Kati yafedha hizo, Shilingi 1,815,527,215 zimepangwa kutumikakufanya ukarabati wa jengo la ofisi na makazi ya watumishikwenye ubalozi wa Tanzania Kampala; Shilingi 315,425,000 nikwa ajili ya ukarabati wa makazi ya balozi Kinshasa; Shilingi593,300,000 kutumika kukarabati nyumba.za.ubalozi waTanzania Lilongwe; Shilingi 195,943,440 kukarabati makazi yabalozi wa Tanzania Brussels; na shilingi 500,000,000 kwa ajiliya kukarabati miundombinu ya Chuo cha Diplomasia.

29. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kufuatiliaWizara ya Fedha na Mipango upatikanaji wa fedha zamaendeleo kiasi cha Shilingi 4,579,804,345 sawa na asilimia

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

57.3 ambazo hazijatolewa ili kutekeleza miradi ya maendeleoiliyopangwa kwa mwaka wa fedha 2017/18.

30. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuzingatiasheria, kanuni, taratibu na miongozo ya fedha za ummakatika kudhibiti mapato na matumizi ya Serikali. Kwakudhihirisha hilo, Wizara pamoja na balozi zake 39 zimepatahati safi isipokuwa balozi mbili zimepata hati zenye shakakatika ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2016/17. Nachukua fursahii kuwashukuru watendaji wa Wizara na kuwahimizawaendelee kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozoya matumizi ya fedha za umma na ununuzi wakati wotewanapotekeleza majukumu yao.

31. Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa taarifa yamapato na.matumizi ya.Wizara.kwa mwaka.wa.fedha 2017/18, naomba sasa nitumie fursa hii kueleza kwa kifupi baadhi yamafanikio ya Wizara katika kipindi hicho.

DIPLOMASIA YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAWIZARA

32. Mheshimiwa Spika, katika malengo ya Sera yaMambo ya Nje kuna malengo ambayo ni ya kudumuyanayoiwezesha nchi kuwa katika nafasi ya jumuiya yamataifa kama Taifa huru lenye umoja, usalama na lenyehadhi na siha nzuri. Hii hasa ni diplomasia ya siasa. Pia kunamalengo ambayo yanaendana na wakati huo wa uongozina vipaumbele vya Serikali na Taifa kwa ujumla. Katika miakaya sitini hadi themanini malengo ya ziada katika Sera yaTanzania yalikuwa ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwaukoloni na ubaguzi wa rangi. Baada ya kukamilisha hayoTanzania iliona umuhimu wa kuwa na Sera ya Mambo yaNje yenye msisitizo wa diplomasia ya uchumi ili kusukumamaendeleo ya Taifa letu.

33. Mheshimiwa Spika, Diplomasia ya uchumi nimsisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje yenye mikakati, malengo,mbinu na maarifa yanayoelekeza taifa kupata na kuvunarasilimali na utaalam kutoka jumuiya ya mataifa ili kuleta na

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

kuchochea maendeleo ya taifa husika. Mwaka 2001 Tanzaniailipitisha sera inayosisitiza diplomasia ya uchumi ili kuendelezamaendeleo hasa katika sekta ya uchumi. Katika Awamu hiiya tano, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alitangazamapema kuwa Tanzania iwe ni nchi ya viwanda ili kusukumazaidi maendeleo ya uchumi na ajira kufikia uchumi wa katiifikapo mwaka 2025. Azma hii inamaanisha kuwa diplomasiaya uchumi lazima iongeze mkakati wa Diplomasia waViwanda ili kutekeleza maono na mawazo ya MheshimiwaRais kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vilivyojikitakwenye kilimo. Diplomasia ya uchumi wa viwanda lazima itoevipaumbele katika uwekezaji, miundombinu ikiwa ni pamojana nishati, biashara na masoko ya bidhaa kutoka viwandani.Sambamba na mkakati huo, dhana ya diplomasia ya uchumilazima iendelee kulenga sekta nyingine kama kilimo, utalii namadini ambayo kwa namna moja au nyingine zinashabihianana viwanda.

Viwanda, Biashara na Uwekezaji

34. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza diplomasia yauchumi, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau wenginendani ya Serikali na kutoka sekta binafsi inaratibu upatikanajiwa masoko, mitaji, na teknolojia kwa ajili ya kukuza biasharana uwekezaji nchini. Miongoni mwa juhudi zilizofanywa naWizara yangu ni kushawishi wawekezaji kupitia ziara zaviongozi, balozi zetu nje ya nchi, na makongamano yabiashara na uwekezaji yaliyofanyika ndani na nje ya nchi.Kupitia juhudi hizo, tumeweza kufanikisha kuleta ujumbe wawawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchi kadhaazikiwemo Ujerumani, Ufaransa, Hispania, Misri, China, India,Falme za Kiarabu, Oman na Israel. Baadhi ya wawekezaji haotayari wameingia ubia na kampuni za Tanzania na wenginewameanza hatua mbalimbali za uwekezaji nchini. Moja yahatua hizo ni uamuzi uliofanywa na jumuiya yawafanyabiashara wa Ujerumani mwezi Aprili 2018 wakufungua ofisi maalum ya biashara ya nchi hiyo inayoitwaAHK kwa lengo la kuratibu kwa ukaribu zaidi uwekezaji nabiashara zinazofanywa na zitakazofanywa na Ujerumani hapanchini. Aidha, Ufaransa imefungua ofisi ya biashara kupitia

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

kampuni ya BASF kwa lengo la kuratibu shughuli za kibiasharazitakazokuwa zikifanywa na kampuni hiyo na wabia wakehususan katika masuala ya uzalishaji wa kemikali zaviwandani.

35. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu pia iliratibu ushirikiwa Tanzania kwenye makongamano mbalimbali ya biasharana uwekezaji yaliyoandaliwa nje ya nchi. Makongamano hayoni pamoja na yale yaliyofanyika nchini Kenya, Hispania, Uturuki,Uholanzi, Indonesia, Korea Kusini, China, Vietnam, Ujerumanina Umoja wa Falme za Kiarabu. Aidha, viongozi wetuwanapopata fursa ya kufanya ziara mbalimbali nje ya nchiwamekuwa wakitumia fursa hiyo kuzungumza nakuwashawishi wawekezaji kuwekeza nchini, binafsi nimekuwanikifanya hivyo na viongozi wenzangu pia wamekuwawakifanya hivyo. Kwa mfano, mwezi Aprili 2018 Rais waZanzibar, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein alitembeleaFalme za Kiarabu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masokowa Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipofanya ziara yakikazi nchini China walitumia fursa hiyo kushawishi wawekezajikatika sekta za uvuvi, viwanda, kilimo na utalii na hatimayekuingia nao makubaliano ya kuanza hatua za uwekezajikwenye sekta hizo.

36. Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2018, Wizaraikishirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji;Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania; na Taasisi yaSekta Binafsi Tanzania kupitia ubalozi wetu nchini Kenyailiandaa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwandavya Tanzania, yaliyofanyika Nairobi. Haya yalikuwa nimaonesho ya kipekee kuwahi kufanywa na nchi yetu. Jumla yakampuni 27 zinazozalisha bidhaa za viwandani kutokaTanzania zilishiriki ili kutangaza bidhaa zao na kuvutia utalii.Maonesho hayo yalitoa fursa kwa wafanyabiashara waTanzania kutafuta masoko ya bidhaa zetu nchini Kenya.

37. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa maonesho hayo yamefungua soko.zaidi kwabidhaa za Tanzania nchini Kenya na kuimarisha mahusiano

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

kati ya nchi zetu mbili na wafanyabiashara. Natoa wito kwawafanyabiashara kuchangamkia fursa ya masoko ya bidhaaza Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi zetunyingine pia zimekuwa zikiendesha makongamano na shughulinyingine mbalimbali za kukuza utalii, kuvutia wawekezaji nakutafuta masoko.

38. Mheshimiwa Spika, juhudi hizi zinazofanywa naWizara yangu pamoja na wadau wengine ndani na nje yaSerikali zinatoa nafasi kwa wafanyabiashara na wawekezajikujionea fursa mbalimbali za uwekezaji, biashara, masoko,teknolojia na upatikanaji wa mitaji. Hivyo, ninatoa rai kwawadau wote wanaosimamia masuala ya biashara nauwekezaji kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwawawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza nchini. Nitumiefursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara wetu kutumia fursahizo kikamilifu.

39. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha biashara kati yaTanzania na Misri, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadauhusika iliratibu majadiliano ya kuondoleana ushuru waforodha na Misri. Majadiliano hayo yamekamilika mwezi Machi2018 kwa pande zote kukubaliana kuwa, Misri iondoe ushurukwa kiwango cha asilimia 100, na Tanzania iondoe kwakiwango cha asilimia 96.89. Kiwango kilichosalia kwa Tanzaniakitaondolewa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

40. Mheshimiwa Spika, mwezi Febuari, 2018 nilifanya ziaraya kikazi nchini Korea Kusini ambapo nilifungua kongamanola biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi hiyo. Kufuatiakongamano hilo viongozi wa kampuni ya Hyundai walifikanchini kufanya mazungumzo na Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC) kwa lengo kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vipulivya magari. Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji itaendelea kufuatiliamazungumzo hayo. Halikadhalika, nilipotembelea Chinamwishoni mwa mwaka jana nilikutana na wawekezaji katikaviwanda vya magari ambao wameahidi kuja kuonauwezekano wa kuwekeza hapa nchini.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Umwagiliaji

41. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliratibu upatikanajiwa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 55 kutokaSerikali ya Poland ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wamradi wa maghala na vihenge vya kuhifadhia nafaka katikamikoa ya Ruvuma, Njombe, Rukwa, Songwe, Dodoma,Shinyanga, Manyara, na Katavi. Kukamilika kwa mradi huokutapunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno (post-harvest loss). Wizara yangu pia imeratibu upatikanaji waufadhili wa mradi wa kituo kikubwa cha ujenzi wa kuzalishasamaki cha Zanzibar unaodhaminiwa kwa ushirika kati ya KoreaKusini kupitia Shirika lake la maendeleo la KOICA pamoja naShirika la Chakula Duniani (FAO) wenye thamani ya Dola zaMarekani milioni 3.2.

42. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana nawadau wengine imefanikisha kupatikana ufadhili wa miradiya umwagiliaji ya Muhongo-Kagera na bonde la Luiche-Kigoma kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait. Baada yakukamilika kwa tathmini ya miradi hiyo mwezi Machi 2018,rasimu ya mkataba wa kuipatia Tanzania mkopo wamasharti nafuu wenye thamani ya Dola za Marekani milioni15.3 ilisainiwa. Aidha, ushirikiano wa Tanzania na China kupitiajukwaa la FOCAC umeendelea kuchangia sekta ya majiambapo katika kipindi hiki, Zanzibar imefadhiliwa mradi wakujenga kituo kipya cha kutibu maji katika eneo la DongeMbiji, wilaya ya Kaskazini Unguja wenye thamani ya Dola zaMarekani milioni 5.5.

Ujenzi na Miundombinu

43. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakujenga mahusiano mazuri na nchi marafiki na mashirika yakimataifa ambao ni washirika wetu wa maendeleo. Uhusianohuo mzuri umewezesha Serikali kupata ufadhili wa miradimbalimbali ya maendeleo. Miongoni mwa ufadhili huo ni uleuliotoka Umoja wa Ulaya, Serikali ya Marekani kupitia shirikalake la maendeleo la USAID, Serikali ya Uingereza kupitiashirika lake la maendeleo la DFID, Serikali ya Japan kupitia

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

shirika lake la maendeleo la JICA, Serikali ya Korea Kusini kupitiashirika lake la maendeleo la KOICA, Serikali ya Ujerumanikupitia GIZ, Serikali ya Denmark kupitia DANIDA, Serikali yaCanada kupitia CIDA, Serikali ya Ufaransa kupitia shirika lakela AFD, Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia Mfuko waMaendeleo wa Abudhabi, Serikali ya Saudi Arabia kupitia Mfukowake wa Maendeleo wa Saudia, pamoja na Serikali yaKuwait kupitia Mfuko wake wa maendeleo wa Kuwait.Serikali ya Oman pia imekubali kusaidia kufadhili uboreshajiwa baadhi ya miundombinu katika mikoa mbalimbali ikiwani pamoja na Jiji la Dodoma.

44. Mheshimiwa Spika, halikadhalika, Chinaimezikaribisha nchi za Afrika kujiunga na mpango wake waOne Belt One Road Initiative ambao unatoa manufaamapana katika uwekezaji wa miundombinu ya nishati, reli,barabara, bandari na viwanja vya ndege. Kutokana na hatuahiyo, nilipofanya ziara yangu nchini China, niliwasilishamaombi ya Tanzania kujiunga na mpango huo. Napendakulifahamisha Bunge lako kuwa, mwezi Aprili 2018 Serikali yaChina ilikubali ombi hilo na taratibu za kujiunga na mpangohuo zinaendelea.

Afya na Ustawi wa Jamii

45. Mheshimiwa Spika, sekta ya afya ni miongoni mwasekta zinazonufaika na ufadhili wa miradi ya maendeleokutoka nchi wahisani pamoja na washirika wetu wamaendeleo. Serikali ya Marekani mwezi Mei 2018 iliahidi kutoaDola za Marekani milioni 512 kufadhili Mpango wa Kupambanana Virusi vya Ukimwi nchini chini ya program yake ijulikanayokama President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR).Serikali ya Kuwait pia imezindua mpango maalum wakusaidia sekta ya afya hapa nchini wenye thamani ya Dola zaMarekani 500,000. Mpango huo ujulikanao kama Half-MillionDollar Program umewezesha upatikanaji wa vifaatiba kwawatu wenye mahitaji maalum katika Taasisi ya Moyo yaJakaya Kikwete, Taasisi ya Mifupa ya MOI, pamoja na Hospitaliya Benjamin Mkapa ya Dodoma. Aidha, Kuwait imetoa Dolaza Marekani milioni 13.6 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Zanzibar; na Serikaliya China pia imesaidia ukarabati wa Hospitali ya AbdullaMzee, Pemba kama moja ya miradi yake ya afya hapa nchini.Serikali ya Israel itaongeza misaada yake ya wataalam,mafunzo na vifaa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya MrishoKikwete.

46. Mheshimiwa Spika, Tanzania pia imenufaika naMfuko wa Afya duniani ujulikanao kama Global Fund unaotoaufadhili wa programu mbalimbali za kukabiliana na maradhiya Malaria, Kifua Kikuu na Ukimwi. Tangu mfuko huouanzishwe hapa nchini mwaka 2013, tayari Tanzaniaimenufaika na Dola za Marekani takriban bilioni 2 na hivyokuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazonufaikazaidi na ufadhili wa mfuko huo barani Afrika. Aidha, mwezi Aprili2018 Serikali ilisaini makubaliano na mfuko huo ya kiasi kinginecha Dola za Marekani milioni 700 kwa ajili ya ufadhili wa miradiya afya katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Wadau wenginewanaosaidia sekta ya afya ni mashirika ya maendeleo yakimataifa pamoja na nchi marafiki kama vile Uingereza,Denmark, Canada, Ireland, Palestina, Umoja wa Falme zaKiarabu, Cuba, Misri, Israel, Ujerumani, na Brazil.

Nishati na Madini47. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kutambuaumuhimu wa sekta hii katika maendeleo ya uchumi wa nchiimeendelea kuitafutia washirika kutoka nchi marafiki namashirika ya kimataifa katika miradi yake mbalimbali.Miongoni mwa wafadhili wakubwa ni Benki ya Maendeleo yaAfrika na Benki ya Dunia. Aidha, kupitia ziara iliyofanywa naWaziri wa Mambo ya Nje wa Norway hapa nchini mwezi Juni2017, Serikali ya nchi hiyo imezindua awamu ya pili ya programitakayodumu hadi mwaka 2020, kwa ajili ya kuendeleza sektaya mafuta nchini. Kupitia programu hiyo, Norway itatoa kiasicha Dola za Marekani millioni 5.9 kwa ajili ya kuendeleza sektaya mafuta hapa nchini, na kiasi kingine cha Dola za Marekanimilioni 10.5 kwa ajili ya kuendeleza mfumo wa ukusanyaji kodi.Nchi nyingine zinazofadhili miradi kwenye sekta hii kwa kupitiaWizara yangu ni pamoja na Ujerumani, Sweden, Finland naIndia.

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Elimu na Mafunzo ya Ufundi

48. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakuratibu upatikanaji wa fursa za masomo na mafunzo yaufundi kutoka nchi marafiki. Ufadhili huo ni katika mafunzo yamuda mfupi, shahada ya kwanza, uzamili, uzamivu,uboreshaji mafunzo ya ualimu, uboreshaji mitaala namiundombinu ya kufundishia katika vyuo vyetu vya ufundi nateknolojia; vitabu; pamoja na ujenzi wa maktaba ya kisasakatika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nachukua fursa hiikuzishukuru nchi zote zinazofadhili miradi katika sekta ya elimuna mafunzo ikiwa ni pamoja na China, Italia, Hungary,Poland, Uholanzi, Australia, India, Malta, Misri, Korea, Malaysia,Indonesia, Vietnam, Japan, New Zealand, Algeria, Uingereza,Ujerumani, Uswisi, Brunei, Oman, Cuba, Israel, Palestina naSaudi Arabia. Natoa wito kwa Watanzania watumie fursa hiziipasavyo.

Utalii

49. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Balozi zetunje imeendelea kushirikiana na wadau wengine wa Serikalikutangaza vivutio vya utalii na kuratibu ujio wa watalii nchini.Nafurahi kutambua ripoti iliyotolewa mwezi Mei 2018 na Wizaraya Maliasili na Utalii pamoja na ripoti za balozi zetu zikiainishakwamba idadi ya watalii nchini sio tu imeongezeka lakinipia pato litokanalo na sekta hiyo limeongezeka. Aidha, ripotihizo zimebainisha kwamba tofauti na ilivyozoeleka hukonyuma kwa watalii wengi walikuwa wakitoka nchi zaMarekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Hispania,hivi sasa kuna ongezeko kubwa pia la watalii kutoka nchi zaChina, Australia, Uholanzi, Uswisi, India na Israel. Ongezeko hilola idadi ya watalii ni matokeo ya kasi ya kuvitangaza vivutiovya utalii vilivyopo nchini inayofanywa na mamlaka za ndanipamoja na balozi zetu nje ya nchi. Wizara yangu kupitia balozizetu itaendeleza juhudi hizi kwa kasi zaidi hasa katika Balozizetu mpya za Korea Kusini, Uturuki, Qatar na Israel.

50. Mheshimiwa Spika, katika kutangaza vivutio vyautalii vya Tanzania katika nchi zenye watalii wengi, ubalozi

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

wa Tanzania Beijing umeendelea kutumia nafasi yake yakimkakati kwa kutangaza utalii wetu kupitia mitandao yakijamii ya China kama QQ na WeChat kwa kuwekamatangazo ya vivutio kwa lugha za kichina. Aidha, ubalozikwa kushirikiana na mamlaka za utalii nchini ziliandaa ziaraza waigizaji mashuhuri kutoka China ambapo waliandaamakala za kutangaza utalii wa Kisiwapanza-Pemba, Hifadhiya Taifa ya Serengeti, Mbuga ya Selou na Ziwa Eyasi. Makalahizo zilizoandaliwa zimelenga kutangazwa katika runingazinazoangaliwa na watu wengi zaidi nchini China. Soko lawatalii kutoka China ni kubwa kuliko yote kama tukijitangazavizuri.

51. Mheshimiwa Spika, kufuatia ziara ya meli ya Sultan waOman mwezi Oktoba 2017, Serikali ya Oman imeahidikukarabati na kuhifadhi Jumba la Maajabu (Beit el Ajab)Zanzibar. Aidha, mwezi Aprili 2018 Tanzania na Oman zilisainimakubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya kumbukumbuna nyaraka ili kukuza utalii unaotokana na historia kati ya Omanna Zanzibar.

Msamaha wa madeni ya nje

52. Mheshimiwa Spika, moja ya hatua inayofanywa naWizara yangu kwa kushirikiana na wizara nyingine nikushawishi nchi marafiki kutufutia madeni, kuyapunguza aukuweka masharti nafuu ya kuyalipa. Napenda kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa nilipofanya ziara nchini Iran mwezi Oktoba2017, Serikali ya nchi hiyo iliridhia na kutangaza kusamehe ribaya deni lililokopwa mwaka 1984 ambayo kwa sasa imefikiakiasi cha Dola za Marekani milioni 150. Aidha, mwezi Septemba2017, Serikali ya Brazil pia ilitoa msamaha wa thamani ya Dolaza Marekani milioni 203.6 ambayo ni asilimia 86 ya deni lotetunalodaiwa na nchi hiyo. Misamaha hiyo ni wazi itaipa nafuunchi yetu katika kulipa madeni. Naomba kutumia nafasi hiikuzishukuru Serikali za Iran na Brazil kwa misamaha hiyo.

53. Mheshimiwa Spika, pamoja na wajibu wa Serikalikulipa madeni yake nje, Wizara yangu kwa kushirikiana nawadau wengine ndani ya Serikali itaendelea na juhudi za

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

kuomba kusamehewa au kupata nafuu ya aina yoyote katikakulipa madeni ya Serikali.

MIKUTANOYA TUME ZA PAMOJA ZA KUDUMU ZA USHIRIKIANO54. Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha,Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliratibu nakushiriki katika mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu yaUshirikiano kati ya Tanzania na Misri uliofanyika Cairo, mweziJanuari 2018. Mimi binafsi niliongoza ujumbe wa Tanzaniakatika mkutano huo ambapo nchi zetu mbili zilikubalianakushirikiana katika sekta za viwanda, biashara na uwekezaji;maji; kilimo, mifugo na uvuvi; ujenzi, uchukuzi na mawasiliano;afya, nishati, maliasili na utalii; elimu, mambo ya ndani yanchi na habari. Majadiliano ya utekelezaji wa maazimiombalimbali yameshaanza na tayari uongozi wa Shirika landege la Misri umeshatembelea nchini na kukutana nawataalam wa Idara na Taasisi za Serikali.

USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA JUMUIYA ZA KIKANDA NAKIMATAIFA

Jumuiya za Kikanda

Jumuiya ya Afrika Mashariki

Uondoaji wa Vikwazo Visivyo vya Forodha

55. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibukamati ya kitaifa ya kufuatilia uondoaji wa vikwazo vyakibiashara visivyo vya forodha pamoja na mikutano yakikanda kwa ajili ya kujadili vikwazo mbalimbalivinavyojitokeza. Kwa kipindi cha mwezi Julai 2017 hadi Machi2018, jumla ya vikwazo sita vilivyodumu kwa muda mrefuvimeondolewa na hivyo kufikia jumla ya vikwazo 122vilivyoondolewa tangu mwaka 2009. Majadiliano yakuviondoa vikwazo vingine 33 bado yanaendelea. Miongonimwa vikwazo vilivyoondolewa vinavyoihusu Tanzania nikupunguzwa kwa vizuizi barabarani katika njia kuu ya kati nakaskazini; kuwianisha muda wa kufanya kazi baina yamamlaka za mapato za Tanzania na Kenya kwenye ukaguzi

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

wa mizigo katika bandari kavu mjini Nairobi; kuondoa kodiya ongezeko la thamani katika huduma za bandari kwamizigo inayosafirishwa kwenda nje ya nchi; tozo ya Dola zaMarekani 152 kwa mabasi yanayotoka Rwanda na zuio lakuuza bidhaa za chakula kwenda Uganda, pamoja nakurekebisha sheria na kuainisha ubora wa bidhaa mbalimbalitunazouziana.

Mapitio ya Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha

56. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana nawadau wengine imeendelea kuratibu na kusimamia mapitioya Wigo wa Pamoja wa Ushuru wa Forodha. Kwa sasa nchi zaJumuiya zimeendelea kufanya tafiti katika ngazi ya nchi nakanda kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi ya namna yakupanga viwango vya ushuru wa forodha katika Wigo waPamoja wa Ushuru wa Forodha wa Jumuiya. Majumuisho yaawali ya matokeo ya tafiti kutoka kila nchi mwanachamawa Jumuiya yanapendekeza mabadiliko ya viwango vyaushuru wa forodha yazingatie ukuzaji wa viwanda kwa nchiwanachama; kupunguza gharama za uzalishaji; kuongezabiashara miongoni mwa nchi wanachama; na kuwalindawalaji.

Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki

57. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18, Wizara iliratibu majadiliano ya mapitio yaJedwali la Biashara ya Huduma katika Itifaki ya Soko laPamoja. Lengo la kufanya mapitio hayo ni kuondoachangamoto zilizokuwa zikikwaza utekelezaji wa Itifaki hiyokatika eneo la huduma. Tayari nchi zote wanachamazimewasilisha maboresho ya jedwali la huduma katika Itifakiya Soko la Pamoja ambapo changamoto zilizoainishwazimepatiwa ufumbuzi.

58. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibuutoaji wa elimu kwa umma mijini na vijijini ili kuwawezeshawananchi na hasa vijana kushiriki katika kuchangamkia fursazilizoko kwenye soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wizara kwa

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

kushirikiana na asasi za kiraia pamoja na vyombo vya habarikupitia makongamano mbalimbali iliendesha programumaalum ya kuhamasisha vijana wa Kitanzania kuzitambuana kuzitumia ipasavyo fursa zitokanazo na Mtangamano waAfrika Mashariki. Programu hiyo ilipewa jina la Kampeni yaMsafara wa Vijana ya Biashara ya Kuvuka Mpaka. Kampenihiyo ilifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma,Mwanza, Manyara na Arusha. Wizara pia kwa kushirikiana naBenki ya Dunia ilitoa elimu kwa umma kwa vijana wa vyuovikuu juu ya kuchangamkia fursa katika mtangamano.

Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedha ya AfrikaMashariki

59. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18Wizara yangu imeendelea kuratibu na kushiriki katika uandaajiwa sera, sheria, kanuni na taratibu za kuendeleza sekta yafedha katika eneo la usimamizi wa bima, huduma ndogoza kifedha (microfinance), pensheni na benki. Aidha, Wizarayangu kwa mwaka wa fedha 2018/19 itaendelea kuratibuna kushiriki majadiliano ya maeneo tajwa hapo juu hadiyatakapokamilika.

60. Mheshimiwa Spika, ninapenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa, Bunge la Afrika Mashariki lililokaa Dodomamwezi Aprili 2018, lilipokea na kujadili miswada miwiliinayohusiana na utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedhawa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Miswada hiyo ni ya kuanzishaTaasisi ya Fedha na Taasisi ya Takwimu ya Jumuiya ya AfrikaMashariki. Muswada wa Kuanzisha Taasisi ya Fedha ya Jumuiyaya Afrika Mashariki ulipitishwa na Bunge hilo na hatuainayofuata ni kuidhinishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama.

Ushirikiano Baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki naKanda Nyingine

61. Mheshimiwa Spika, Viongozi Wakuu wa Nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutano wao wa 18uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2017 pamoja na mambomengine, walikubaliana kuwa Mheshimiwa Yoweri Kaguta

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Museveni, Rais wa Uganda na mwenyekiti wa Jumuiya,akutane na Rais wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Jean- ClaudeJuncker ili kujadili changamoto za Mkataba wa Ubia waKiuchumi (EPA) baina ya Jumuiya hizo. Kufuatia maamuzi hayo,Wizara iliratibu ushiriki wa Tanzania katika ziara hiyo iliyofanyikaBrussels, Ubelgiji mwezi Septemba 2017. Mwenyekiti aliwasilisharasmi hoja za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu changamotoza EPA na mwezi Desemba 2017, Rais wa Umoja wa Ulaya,Mhe. Jean- Claude Juncker aliwasilisha majibu ya hoja hizo.

62. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa 19 waViongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Masharikiuliofanyika Kampala mwezi Februari 2018 Rais wa Uganda naMwenyekiti wa Jumuiya aliwasilisha majibu ya Umoja waUlaya kwa Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya. ViongoziWakuu hao hawakuridhishwa na majibu yaliyotolewa naUmoja wa Ulaya hivyo, walimpa mamlaka Mwenyekiti waJumuiya kuendelea kuwasiliana na Umoja wa Ulaya kwa lengola kupata majibu yanayoendana na hoja zilizowasilishwa naJumuiya ya Afrika Mashariki.

63. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2017/18, Wizara iliendelea kuratibu majadiliano ya maeneoyaliyosalia katika kuanzisha Eneo Huru la Biashara la Utatu waCOMESA-EAC-SADC pamoja na kuweka katika lugha yakiuandishi viambatisho vya Mkataba huo. Majadilianoyamekamilika katika Kiambatisho Na. II kinachohusuUsuluhishi wa Migogoro ya Biashara, Kiambatisho Na. IVkinachohusu Sheria ya Utambuzi wa Uasilia wa Bidhaa naKiambatisho Na. X kinachohusu Utatuzi wa Migogoro.Majadiliano yanaendelea baina ya nchi wanachama kwenyekanuni za utambuzi wa uasilia wa bidhaa pamoja na uondoajiwa ushuru wa forodha.

Sekta za Uzalishaji

64. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeratibumaandalizi na ushiriki wa Tanzania katika mikutano yakuandaa sera na mikakati ya kukuza viwanda katika Jumuiya

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

ya Afrika Mashariki hususan katika maeneo yaliyoainishwa naWakuu wa Nchi kuwa ya vipaumbele hasa utengenezaji wamagari, uzalishaji wa dawa na bidhaa za nguo na ngozi. Wizarailihakikisha vipaumbele vya nchi vinajumuishwa katika serana mikakati iliyoandaliwa ikiwemo Mkakati wa Tano waMaendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2016/17-2020/21.Ni mategemeo yetu kuwa sera hizi za mtangamanozitasaidia kukuza viwanda na hivyo kuchangia kuifikishaTanzania katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Uendelezaji wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma zaJamii

65. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibuutekelezaji wa programu na miradi ya kikanda ya uendelezajiwa miundombinu ya uchumi na huduma za jamii kamaifuatavyo:

Maendeleo ya Miundombinu ya Uchukuzi, Nishati naUwekezaji katika Sekta ya Afya

66. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na kushiriki katikaMkutano wa Kazi wa Wakuu wa Nchi Wanachama waJumuiya ya Afrika Mashariki uliojadili maendeleo ya sekta yamiundombinu ya uchukuzi, nishati, na uwekezaji katika sektaya afya uliofanyika Kampala mwezi Februari 2018. Lengo lamkutano huo li l ikuwa ni kubaini kiasi cha fedhakinachohitajika kutekeleza miradi hiyo ambapo imeelezwakuwa katika miaka 10 ijayo kiasi cha Dola za Marekani bilioni78 zitahitajika kutekeleza miradi ya miundombinu ya uchukuzina nishati. Hivyo, miradi 17 ya kipaumbele cha juu ilipitishwaambapo miradi 10 kati ya hiyo itatekelezwa Tanzania.

67. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha sekta ya afya,Wakuu wa Nchi walipitisha vipaumbele tisa. Miongoni mwavipaumbele hivyo ni kupanua wigo wa huduma za tiba zaubingwa kwa kuimarisha miundombinu, vifaatiba nawataalam; na kupambana na magonjwa ya mlipuko nadharura za kiafya zinazotokana na mwingil iano wakimataifa. Vilevile, vipaumbele hivyo vimeelekezwa katika

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

kujenga uwezo wa taasisi na vyuo vinavyotoa mafunzo yaafya kwa kuwianisha mitaala ya mafunzo, viwango namiongozo katika sekta ya afya ili kuwa na wataalam wakutosha na wenye weledi; kupanua wigo wa matumizi nahuduma za bima ya afya na hifadhi ya afya ya jamii; nakuendeleza utafiti katika sekta ya afya.

68. Mheshimiwa Spika, ni matumaini yangu kuwa Wizaraza kisekta kwa kadri hali ya bajeti itakavyoruhusu, zitaendeleakutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kipaumbele.

Usimamizi wa Mazingira Bonde la Ziwa Victoria

69. Mheshimiwa Spika, wakati wa kikao kilichopita chabajeti cha 2017/18, nililiarifu Bunge lako Tukufu kuhusu Awamuya Pili ya Mradi wa Usimamizi wa Mazingira katika ZiwaVictoria. Naomba kuliarifu Bunge lako kuwa mradi huoumekamilika mwezi Desemba 2017 ambapo faidazilizopatikana ni pamoja na kupunguza magugu maji nakuwapatia maji safi na salama wananchi wanaoishimaeneo ya mradi. Wizara yangu kwa kushirikiana na wadauwengine inaratibu majadiliano ya Awamu ya Tatu ya Mradihuo.

70. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu upatikanaji wakiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kikanda cha Uratibuwa Usalama na Uokozi (Maritime Rescue Coordination Centre- MRCC) katika Ziwa Victoria j i j ini Mwanza. Tanzaniaimewasilisha Hati ya Umiliki wa Kiwanja chenye ukubwa wamita za mraba 13,287 kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ujenziwa kituo hicho utakuwa na manufaa ya kurahisishausafirishaji katika Ziwa Victoria na udhibiti, uokozi na usalama.

Masuala ya Siasa

71. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarishademokrasia, utawala bora, na kulinda haki za binadamu kwakushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki. Kwa kuzingatia hilo, Wizara iliratibu na kushirikikwenye kongamano la Utawala Bora la Jumuiya ya Afrika

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Mashariki lililofanyika Arusha mwezi Oktoba 2017. Pamoja namambo mengine, kongamano hilo liliazimia kwamba Tumeza Haki za Binadamu za nchi wanachama zitoe mafunzokwa vyombo vya usalama. Aidha, nchi wanachama zilitakiwakuimarisha uwezo wa Tume za Uchaguzi ili ziweze kutekelezamajukumu yake kwa usawa na kwa kuzingatia maadili.

Uchaguzi Mkuu Nchini Kenya na Rwanda

72. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza demokrasia nakulinda amani katika Jumuiya, Tanzania ilikuwa sehemu ya timuya waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Masharikikatika chaguzi zilizofanyika nchini Rwanda na Kenya mwaka2017. Katika chaguzi hizo, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kutokamuungano wa Jubilee alichaguliwa kuwa Rais Kenya naMheshimiwa Paul Kagame kutoka chama cha RPFalichaguliwa kuwa Rais Rwanda. Ripoti za usimamizi katikachaguzi hizo zimeeleza kuwa chaguzi zilikuwa huru na haki.Nachukua nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa wananchiwa Kenya na Rwanda kwa kufanya chaguzi kwa amani.

Fungamano la Kisiasa la Afrika Mashariki

73. Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 35 wa dharura waBaraza la Mawaziri wa Jumuiya uliofanyika Kampala, mweziFebruari 2018 ulipitisha Rasimu ya Andiko, Hadidu za Rejea,na Mpangokazi wa kuanzisha Fungamano la Kisiasa la AfrikaMashariki. Aidha, maandalizi ya rasimu ya Katiba yaFungamano yanaendelea kwa mujibu wa mpangokaziulioidhinishwa na zoezi hili linatarajiwa kukamilika mwaka 2022.

Hati Mpya ya Kusafiria ya Kielektroniki ya AfrikaMashariki

74. Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Nchi Wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mkutano wao wa 17uliofanyika Arusha mwezi Februari 2016 walizindua rasmi hatiya kusafiria ya kielektroniki ya Jumuiya ya Afrika Masharikina kukubaliana kuwa kila nchi mwanachama ianzekuzitumia ifikapo mwezi Januari 2018.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

75. Mheshimiwa Spika, napenda kulieleza Bunge lakoTukufu kuwa mwezi Januari 2018, Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Mugufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaalizindua rasmi hati hiyo kwa wananchi wa Tanzania.Wananchi wa Tanzania wataruhusiwa kuendelea kutumia hatiwalizonazo kwa kipindi cha miaka miwili hadi ifikapo mweziDesemba 2019. Utoaji wa hati hizi unasimamiwa na mamlakahusika katika kila nchi mwanachama kulingana na sheria zanchi yake.

Mapambano Dhidi ya Ugaidi na Uharamia

76. Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Afrika Masharikiinaandaa mpango wa utekelezaji wa mkakati wa kupambanana ugaidi. Mkutano wa wadau uliofanyika Mwanza, mweziOktoba 2017 uliandaa mfumo utakaowezesha vyombovinavyohusika na mapambano dhidi ya ugaidi kufanya kazikwa pamoja katika kutekeleza mkakati huo.

77. Mheshimiwa Spika, katika kupambana na uharamiakwenye Bahari ya Hindi, Wizara kwa kushirikiana na wadauwengine imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mkakati waKikanda wa kupambana na uharamia kwa kuratibumakubaliano maalum ya namna ya kubadilishana taarifa zawahalifu. Kufikiwa kwa makubaliano hayo kutasaidia nchiwanachama kubadilishana uzoefu na kubaini mbinuzinazotumiwa na maharamia ili kuimarisha mapambanodhidi ya uharamia katika Bahari ya Hindi. Vilevile, Wizara kwakushirikiana na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliratibuzoezi la pamoja la kijeshi la kamandi za kijeshi ya nchiwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lijulikanalo kama‘EAC CPX USHIRIKIANO IMARA 2017’ lililofanyika Dar es Salaammwezi Desemba 2017. Lengo la zoezi hilo lilikuwa ni kujengauwezo wa majeshi ya nchi wanachama katika kuendeshaoperesheni za kulinda amani; kupambana na ugaidi;kupambana na uharamia; na kukabiliana na majanga.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

78. Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 37 wa Wakuu wa

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrikaulifanyika Pretoria mwezi Agosti 2017. Ujumbe wa Tanzaniakatika Mkutano huo uliongozwa na Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania akimwakilisha Mheshimiwa Rais.

79. Mheshimiwa Spika,.naomba.kuliarifu.Bunge lakoTukufu kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, kama Mwenyekitiwa Asasi hiyo, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumuya Asasi ya SADC ya ushirikiano katika siasa, ulinzi na usalamakwa kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017. Taarifa hiyo ilielezakwa kina tathmini ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katikakanda hususan katika Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo, Jamhuri ya Madagascar na Falme ya Lesotho.Tanzania ilipongezwa kwa kusimamia vizuri majukumu ya Asasihiyo.

80. Mheshimiwa Spika, Mkutano huo, pamoja namambo mengine, ulimteua Dkt Stergomena L. Tax, kuendeleana wadhifa wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa kipindi chapili na cha mwisho; uliazimia kuisaidia Serikali ya Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo kufanya uchaguzi tarehe 23 Desemba2018; na kuridhia ombi la Serikali ya Visiwa vya Comoro kuwamwanachama wa 16 wa Jumuiya hiyo.

81. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa Tanzania ilikabidhi rasmi uenyekiti wa Asasi yaSADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama kwaJamhuri ya Angola.

Ushirikiano kati ya SADC na Umoja wa Ulaya

82. Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Maendeleo Kusinimwa Afrika na Umoja wa Ulaya ziliingia makubaliano yampango wa ushirikiano wa miaka mitano kuanzia mwaka2015 hadi 2020. Katika Mpango huo, Umoja wa Ulaya, pamojana mambo mengine, uliridhia kutoa kiasi cha Euro milioni 31.6kupitia Awamu ya 11 ya Mfuko wa Maendeleo wa Umoja waUlaya, kuzisaidia nchi wanachama wa SADC kutekeleza Itifaki

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

ya Biashara. Tayari Tanzania imenufaika na mpango huo kwakupokea kiasi cha Euro 420,000 kati ya Euro milioni 1.4zilizoahidiwa. Kiasi hicho cha fedha kitatumika kufanyamapitio ya Sera ya viwanda ya Tanzania, kuhamasishabiashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vyakiushuru.

Jumuiya ya Nchi Zinazopakana na Bahari ya Hindi

83. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwakushirikiana na IORA ilifanya warsha ya kuandaa Mkakati waKikanda wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Uvuvi katikaUkanda wa Bahari ya Hindi mwezi Oktoba 2017.

84. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Tanzania imeanzakunufaika na mtandao wa kupeana taarifa za biashara (IORATrade Repository) ikiwemo mfumo wa kodi, uasili wa bidhaa,taratibu za forodha na upatikanaji wa leseni za uingizaji wabidhaa kwa kila nchi iliyo ndani ya Jumuiya uliozinduliwa rasmimwezi Agosti 2017.

Umoja wa Afrika

85. Mheshimiwa Spika, Wizara il iratibu ushiriki waTanzania kwenye Mkutano wa 30 wa Wakuu wa Nchi naSerikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mweziJanuari 2018. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa KassimMajaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, alimuwakilisha Mheshimiwa Raisambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo ulijadilitaarifa ya Mheshimiwa Paul Kagame, Rais wa Jamhuri yaRwanda na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuhuisha Mifumo yaKitaasisi ya Umoja wa Afrika. Mkutano huo uliazimia nchiwanachama ziendelee na majadiliano ya namna bora yakutekeleza mapendekezo ya mabadiliko ya kuhuisha Mifumoya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika ili kufikia muafaka kwa nchizote. Aidha, mkutano huo ulizindua soko moja la usafiri waanga Afrika. Hadi sasa nchi wanachama 21 zimesainiMkataba wa soko hilo unaotarajiwa kuchochea utalii nakuongeza ajira.

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

86. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa 29 wa Wakuuwa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika AddisAbaba mwezi Julai 2017, Tanzania ilipata nafasi ya kuchaguliwakuwa miongoni mwa wajumbe wanne wa Bodi ya Ushauri yaUmoja wa Afrika kuhusu Masuala ya Rushwa ambapo Bi. SabinaSeja anaiwakilisha Tanzania. Wajumbe wengine kwenye Bodihiyo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Algeria na Misri.

87. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji iliratibu na kushirikikatika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikaliwa Umoja wa Afrika uliofanyika Kigali mwezi Machi 2018.Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa kupitia mkataba naitifaki tatu za uanzishwaji wa eneo Huru la Biashara Afrika(AfCFTA). Hatua hiyo ni utekelezaji wa maazimio ya Wakuuwa Nchi na Serikali yaliyofikiwa mwaka 2012 kutaka kuanzishaEneo Huru la Biashara Afrika ambapo majadiliano yakeyalizinduliwa rasmi mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2017.Katika mkutano huo nchi wanachama 44 zilitia saini mkatabahuo na hatua inayofuata ni nchi kuridhia ili utekelezaji wakeuanze rasmi.

88. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba huoutazisaidia nchi za Afrika kukua kiuchumi kwa kushiriki kwenyesoko la pamoja ambalo lina watu zaidi ya bilioni moja napato ghafi linalokadiriwa kuwa na jumla ya zaidi ya Dola zaMarekani trilioni 3.4. Ni muhimu kwa Tanzania kuongeza uzalishajina kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji wa mitajiili kutumia vyema fursa ya soko hilo.

Mkutano wa Masuala ya Mipaka ya Nchi za Umoja waAfrika89. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maazimio yaUmoja wa Afrika yaliyofikiwa Addis Ababa mwezi Juni 2007,Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuhakiki na kuimarishamipaka yake na nchi tunazopakana nazo na tayaritumeanza kuhakiki mipaka kati ya Tanzania na nchi za Kenyana Uganda.

90. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Tukufu kuwa mbali na utekelezaji wa azimio hilo, zoezi lauhakiki wa mipaka ya nchi yetu ni endelevu, na linalengakuweka usimamizi mzuri wa maeneo ya mipaka; kuimarishaulinzi na usalama wa nchi yetu; kurahisisha ukusanyaji wamapato mipakani; kudhibiti uhalifu katika maeneo yamipaka; kuweka mipango ya maendeleo na utoaji wahuduma za msingi za jamii; na kuimarisha mahusiano mazuriyaliyopo baina ya jamii za mipakani.

Ushirikiano wa Kimataifa Umoja wa Mataifa

91. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu lake lakuratibu masuala ya kimataifa, Wizara yangu iliratibu na kushirikimikutano mbalimbali. Baadhi ya Mikutano hiyo ni pamojana: Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa; UN-HABITAT; UNIDO; Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifakuhusu Hali ya Wanawake; Mikutano ya Kimataifa inayohusuwakimbizi na uhamiaji; Baraza la Haki za Binadamu; Shirikala Chakula Duniani (FAO); na Mkutano wa 25 wa Wakuu waSerikali wa Jumuiya ya Madola.

92. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliratibu na kushirikikatika Mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifauliofanyika New York, Marekani kuanzia mwezi Septemba hadiDesemba 2017. Nilipata fursa ya kumwakilisha MheshimiwaDkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania katika vikao vya ngazi ya juuvil ivyokutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali za nchiwanachama wa Umoja wa Mataifa. Masuala muhimuyaliyojadiliwa wakati wa vikao hivyo yalihusu uhusiano wakidiplomasia, ajenda ya uendelezaji wa viwanda, biashara,uwekezaji, hali ya usalama na amani duniani na mapambanodhidi ya ugaidi.

93. Mheshimiwa Spika, pamoja na masuala mengine,Tanzania ilitumia fursa hiyo kuelezea jitihada za Serikali yaAwamu ya Tano ya kuendelea kuimarisha ushirikiano naUmoja wa Mataifa na Mashirika yake. Vilevile, Tanzania ilielezahali ya utekelezaji wa ajenda ya Umoja wa Mataifa ya mwaka2030 (Malengo ya Maendeleo Endelevu) na hatua

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaletea maendeleowatu wake ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa; dawaza kulevya; uwindaji haramu; kuimarisha ukusanyaji wamapato ya ndani na kuziba mianya ya ukwepaji kodi; nakusimamia uwajibikaji na nidhamu ya utumishi wa umma. Aidha,Tanzania ilitumia fursa hiyo kuomba mashirika ya kimataifana wadau wengine wa maendeleo kuendelea kutoamisaada ya fedha, teknolojia na utaalam ili kuunga mkonojuhudi za Serikali za kuleta maendeleo endelevu na kuondoaumaskini nchini.

94. Mheshimiwa Spika, Tanzania kama zilivyo nchiwanachama wengine wa Shirika la Umoja wa Mataifalinaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ilishirikikatika Mkutano Mkuu wa 39 wa Shirika hilo uliofanyika Parismwezi Oktoba 2017. Ajenda kuu ya Tanzania katika Mkutanohuo ilikuwa kuwasilisha uamuzi wake wa kutekeleza mradimkubwa wa umeme wa Stigler’s Gorge. Katika kutekelezaazma hii, ujumbe wa Tanzania uliungana na wajumbewengine wa nchi zinazoendelea kusisitiza umuhimu wa Shirikahilo kuweka uwiano kati ya uhifadhi wa maeneo ya urithiwa dunia na kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo kwenyemaeneo husika. Aidha, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzaniazilitumia mkutano huo kuomba msaada wa kuimarishamiundombinu katika maeneo hayo.

95. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inaendeleakushirikiana na wadau wengine kusukuma ajenda ya kitaifa yakufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. Katikakutekeleza azma ya kukuza viwanda, Wizara iliratibu ujio waDkt. Li Yong, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifalinaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO)mwezi Machi 2018. Moja ya manufaa ya ziara hiyo ilikuwa nikusainiwa kwa tamko la kusudio la kuiingiza Tanzania katikampango maalum wa ushirikiano wa kuendeleza viwandaunaojulikana kama Program for Country Partnership. Kwakuwa mpango huu umefanyika kwa mafanikio katika nchiza Ethiopia, Senegal na Peru, Tanzania inaendelea namajadiliano ya karibu na UNIDO ili nayo iingizwe katikampango huo wenye fursa kubwa katika kusukuma

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

maendeleo ya viwanda ikiwemo ujenzi wa miundombinuya viwanda.

96. Mheshimiwa Spika, katika ziara hiyo Shirika la UNIDOlilitoa msaada wa vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Dolaza Marekani 80,000 kwa wakulima wa zao la mwani Zanzibar.Vifaa hivyo vitatumika kwa ajili ya shughuli za kilimo, usafirishajina usindikaji wa mwani jambo ambalo litasaidia kuongezathamani ya zao hilo katika soko la dunia.

97. Mheshimiwa Spika, mwaka jana nililijulisha Bunge lakoTukufu kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuridhiaMkataba wa Paris chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifakuhusu Mabadiliko ya Tabianchi ambao Bunge lako Tukufuliliridhia mwezi Aprili 2018. Napenda kulishukuru Bunge lakoTukufu kwa hatua hiyo na tayari Mheshimiwa Rais alisaini hatiya kuridhia na hivyo kuwezesha nchi yetu kutambuliwa rasmikama mwanachama wa makubaliano hayo. Naombakutumia fursa hii kukushukuru wewe Mheshimiwa Spika,kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge na wadau wenginewote ndani na nje ya Serikali kwa ushirikiano mkubwawaliotoa kuwezesha suala hili kufanikiwa. Ni dhahiri kwambamakubaliano haya yana manufaa kwa nchi yetu na dunianzima.

Kushughulikia Masuala ya Wakimbizi

98. Mheshimiwa Spika, moja ya nguzo za Sera ya Mamboya Nje ya Tanzania ni kulinda utaifa wetu, mipaka ya nchi nauhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katikakusimamia nguzo hii muhimu, mwezi Januari 2018, Serikali ilifanyauamuzi wa kujitoa kwenye mpango maalum wa majaribiowa kuhudumia Wakimbizi ujulikanao kama ComprehensiveRefugees Response Framework (CRRF). Mpango huo unalengakuwanufaisha wakimbizi kwa kupanua wigo wa hifadhi yaona kuwawezesha kujitegemea kwa Serikali kuwapatia ardhi,uhuru wa kutembea mahali popote na vibali vya kufanya kazipopote nchini.

99. Mheshimiwa Spika, uamuzi wa Serikali kujitoa kwenye

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Mpango huo umezingatia maslahi mapana ya Taifa letuhususan masuala ya usalama. Nitumie fursa hii kulihakikishiaBunge lako Tukufu kuwa pamoja na nia yetu nzuri yakuwasaidia wakimbizi; usalama, amani na ulinzi wa Taifa letundivyo vipaumbele namba moja vya Taifa letu.

100. Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali kutokuafikimpango huo bado Tanzania itaendelea kupokea na kuhifadhiwakimbizi pale inapolazimika kwa kuzingatia sheria za nchina mikataba ya kikanda na kimataifa. Aidha, tunaendeleakutoa wito kwa wakimbizi kurudi makwao kwa hiari paleambapo hali ya usalama kwenye nchi zao inapotengemaa.

Jumuiya ya Madola

101. Mheshimiwa Spika, Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,alimwakilisha Rais kwenye mkutano wa 25 wa Wakuu waSerikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika London mwezi Aprili2018. Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, ulipitishamaazimio matano yanayosisitiza kuifanya dunia kuwa mahalipenye ustawi na.salama zaidi ili kuchochea maendeleo, kuletausawa, utunzaji wa mazingira, amani, haki za binadamu nademokrasia. Maazimio hayo pia yameweka msisitizo kwenyemapambano dhidi ya ugaidi, usafirishaji haramu wabinadamu, utumwa, makundi yenye misimamo mikali nauhalifu mwingine wa kimataifa.

102. Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Serikali kwa kauli mojawalikubaliana kufanya kila liwezekanalo kuongeza biasharana uwekezaji miongoni mwa nchi wanachama. Tanzaniailifanikiwa kuingiza ajenda ya viwanda, nishati ya uhakika nakukuza uchumi kuwa sehemu ya majadiliano na hatimayekuingia kwenye tamko la mwisho la mkutano huo.

103. Mheshimiwa Spika, wakati wa mkutano huo,Mheshimiwa Makamu wa Rais alifanya mazungumzo naviongozi wa nchi mbalimbali wakiwemo Rais wa Uganda,Waziri Mkuu wa Australia, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifawa Uingereza na Mjukuu wa Malkia, Prince William. Katika

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

mikutano hiyo, viongozi hao waliahidi kuendelea kushirikianana Tanzania katika masuala mbalimbali yakiwemo ya elimu,biashara na uwekezaji na mapambano dhidi ya ujangili nabiashara haramu ya wanyamapori. Prince William ni mmojakati ya viongozi wanaounga mkono jitihada za Tanzaniakatika mapambano dhidi ya ujangili na uwindaji haramu.

104. Mheshimiwa Spika, akiwa London, MheshimiwaMakamu wa Rais alikutana na viongozi wa makampuni sitayanayowekeza na yenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.Kwenye mikutano hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Raisaliwathibitishia na kuwahakikishia kuimarika kwa mazingiraya uwekezaji nchini na kukaribisha wawekezaji wengine.

KUSIMAMIA MIKATABA NA MAKUBALIANO YA KIMATAIFA

105. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18 Wizara iliratibu na kusimamia kusainiwa kwamikataba, hati.za.makubaliano.na.kumbukumbu zamazungumzo baina ya Tanzania na nchi mbalimbali.Mikataba na makubaliano hayo ni kiashiria kikubwa katikakuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi yetu nanchi nyingine, mashirika ya Kikanda na Kimataifa katikakuongeza kasi ya kuvutia uwekezaji, kukuza biashara nakutangaza utalii. Wizara inaendelea kufuatilia utekelezaji wamikataba hiyo kwa kuzingatia maslahi mapana.ya nchi yetu.Orodha ya mikataba na hati za makubaliano zilizosainiwakatika kipindi hicho ni kama inavyooneshwa kwenyeKiambatisho.

KURATIBU NA KUSIMAMIA MASUALA YA WATANZANIAWAISHIO UGHAIBUNI

106. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua Watanzaniawanaoishi ughaibuni kama wadau muhimu wa maendeleo,Wizara yangu imeendelea kubuni mbinu mbalimbali zakuwashirikisha katika kuchangia maendeleo ya nchi. Moja yambinu hizo ni kuandaa makongamano ndani na nje ya nchiambapo mwezi Agosti 2017, Wizara yangu kwa kushirikianana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliandaa Kongamano la Nne

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

la Diaspora lililowakutanisha Watanzania zaidi ya 200 kutokanchi mbalimbali na wadau wa maendeleo hapa nchini.Kupitia kongamano hilo, Diaspora walihimizwa kushirikikikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu kwa kuhamasishauwekezaji wa mitaji kutoka nje.

107. Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili 2018 lilifanyikakongamano lingine lililoandaliwa na Diaspora jijini DallasMarekani, ambalo pamoja na masuala mengine, lililengakutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na kuhamasishawawekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo utalii.

108. Mheshimiwa Spika, mchango wa Diaspora katikamaendeleo ya nchi unajidhihirisha katika maeneo mbalimbaliya kiuchumi na kijamii. Yafuatayo ni baadhi ya maeneo hayo:

i. Diaspora imenunua nyumba zenye thamani ya Shilingibilioni 29.7 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwaajili ya nyumba za makazi, ofisi, maeneo ya biasharana viwanja mbalimbali kati ya mwaka 2011 hadi 2017.

ii. Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kuwakwa kipindi cha miaka mitano iliyopita 2013-2017,Diaspora kwa ujumla wao walituma nchini kiasikisichopungua Dola za Marekani bilioni 2.3.

iii. Timu ya madaktari wa kitanzania waishio Marekanikupitia taasisi.ya afya, elimu na maendeleo (Head Inc.)ilitoa huduma ya afya bila malipo na vifaatiba katikahospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, vyenye thamaniya zaidi ya shilingi bilioni moja;

iv. Jumuiya ya Watanzania nchini Marekani (DICOTA)iliandaa jukwaa la afya mwezi Novemba 2017ambalo lilihudhuriwa na wataalam wa afya zaidi ya130 kutoka Tanzania na Marekani ili kubadilishana ujuzi,uzoefu na kutathmini njia madhubuti za kuendelezasekta ya afya nchini Tanzania. Juhudi hizi ziliwezeshakupatikana kwa ufadhili wa masomo kwa wanafunzina wafanyakazi zaidi ya 60 kutoka vyuo vikuu na

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

hospitali nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Tiba KCMC,Hubert Kairuki, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ShirikishiMuhimbili na hospitali ya Bugando.

v. Aidha, Dkt. Frank Minja mtanzania mtaalam waRadiolojia wa Chuo Kikuu cha Yale Marekani amesaidiakuimarisha mfumo wa teknolojia ya kisasa yaradiolojia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

109. Mheshimiwa Spika, wakati ambapo kipaumbele chakitaifa ni viwanda, tunahitaji kufikiria ujuzi maalum walionaoWatanzania wanaoishi katika Diaspora, na vile vile mchangowa kifedha ambao wanaweza kuchangia kutoka kwenyevyanzo vyao binafsi au kwa kushirikiana na raia wa nje,mabenki na taasisi nyingine za nje. Ili kuwezesha viwanda vyetukuuza nje, tunahitaji kutambua, kupima na kupenya katikamasoko mbalimbali ya kigeni. Watanzania walioishi nchi zakigeni na watoto wao wanaweza kuchangia zaidi kutokanana ujuzi wao kwa kupata masoko kwa kutumia ujuzi waowa lugha za kigeni.

110. Mheshimiwa Spika, watanzania wengi walioDiaspora wanachangia sana maendeleo ya kijamii nauchumi wa familia zao na Tanzania kwa ujumla, na wakotayari kushiriki katika jukumu kubwa la kujenga uchumi waTaifa hili. Pengine tunahitaji kuwa na mfumo wa kisheria nasera ya kutoa huduma hiyo kwa uhalali na uhakika.

TATHMINI YA HALI YA DUNIA

Hali ya usalama

111. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama dunianiimeendelea kuimarika pamoja na kwamba changamotokadhaa zimeendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo.Changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya kisiasa katikabaadhi ya nchi, matukio ya kigaidi na kuongezeka makundiyenye itikadi kali na athari za kiusalama zinazosababishwana mabadiliko ya tabianchi. Katika kukabiliana nachangamoto hizo, Tanzania imeendelea kuunga mkono

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

jitihada za kikanda na za Umoja wa Mataifa za kuimarishaamani na usalama duniani.

112. Mheshimiwa Spika, kuhusu migogoro ya kisiasa katikabaadhi ya nchi, naomba nitumie fursa hii kuizungumzia kamaifuatavyo:

Lesotho

113. Mheshimiwa Spika, hali ya siasa, ulinzi na usalamanchini Lesotho bado hairidhishi. SADC ilituma misheni maalumya ulinzi wa amani ili kusaidia nchi hiyo kutekeleza maazimioya kurejesha amani. Naomba niliarifu Bunge lako Tukufu kuwamisheni hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 2 Desemba 2017 na inajumla ya maafisa 269. Serikali ya Lesotho imetakiwakutekeleza maazimio yanayohusu maboresho ya mifumo yaSerikali kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

114. Mheshimiwa Spika, hali ya ulinzi na usalama nchiniDRC hairidhishi. Hivi sasa Serikali ya nchi hiyo inaendelea namaandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambao umepangwa kufanyikatarehe 23 Desemba 2018. Maandalizi ya uchaguzi huuyanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa zoezila kuandikisha wapiga kura na kupitisha sheria mpya yauchaguzi. Natoa rai kwa wadau wa ndani na nje kuhakikishauchaguzi unafanyika kwa utulivu kama ulivyopangwa. Hatahivyo, DRC inahitaji kusaidiwa kwa hali na mali katika kuandaauchaguzi huo hususan ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ni kubwakuliko nchi yoyote Barani Afrika.

Madagascar

115. Mheshimiwa Spika, hali ya siasa nchini Madagascarhairidhishi na SADC imetuma ujumbe wa Baraza la ushauri lamasuala ya uchaguzi nchini humo ili kufanya tathmini ya utayariwa nchi hiyo kufanya uchaguzi mkuu Novemba 2018. Aidha,SADC ilimtuma Mheshimiwa Joaquim Chissano, Rais Mstaafuwa Msumbiji na mjumbe maalum wa SADC tarehe 8 hadi 13

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Mei 2018 kwa lengo la kusaidia kuweka mazingira ya amanikabla ya uchaguzi mkuu.

Sudan Kusini

116. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama nchini SudanKusini imeendelea kuwa ya wasiwasi kutokana na uhasamakati ya Serikali na upinzani. Aidha, hatua ya waliokuwaviongozi wa juu wa jeshi la nchi hiyo kuamua kuunda vikundivya uasi imezidi kuchochea mgogoro huo. Hadi sasamgogoro huo umesababisha zaidi ya watu milioni mbilikukimbilia nchi jirani na wengine zaidi ya 230,000 kulazimikakuyakimbia makazi yao na kuhifadhiwa kwenye makambi yaUmoja wa Mataifa nchini humo.

117. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba wamwezi Agosti 2015 wa kugawana madaraka umeendeleakusuasua licha ya jitihada za Jumuiya ya Maendeleo ya IGADza mwaka 2017 za kufufua utekelezaji wa makubaliano hayo.Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Mataifa na Umoja waUlaya zinaendelea kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogorohuo. Tanzania inaunga mkono jitihada zote zinazofanywakutafuta suluhu ya kudumu nchini humo.

Somalia

118. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama na siasa nchiniSomalia inaendelea kuimarika baada ya kuwa na Katibampya na uchaguzi wa Bunge kufanyika. Kwa kupitia jitihadakubwa za Jeshi la Serikali ya Somalia kwa kushirikiana naAMISOM, Serikali imerejesha zaidi ya asilimia 80 ya maeneoyaliyokuwa yanashikiliwa na kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab. Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo kikundihicho kimeendelea kuwa ni kikwazo cha kuleta amani nchinihumo.

119. Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine majeshiya AMISOM yameanza kuondoa askari wake na kuhamasishaJeshi la Somalia kuanza kuchukua jukumu la kulinda usalamawa nchi yake. Katika kipindi cha mwezi Oktoba na Desemba

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

2017, jumla ya askari 1,000 wa AMISOM waliondolewa nakurudishwa katika nchi zao. Tanzania inaitakia Serikali yaSomalia na watu wake mafanikio katika mipango yakurejesha na kuimarisha amani na usalama nchini humo.

Libya

120. Mheshimiwa Spika, hali ya amani na usalama nchiniLibya ni tete. Hali hiyo imechangiwa na Dola kukosa udhibitiwa nchi, kuongezeka kwa makundi yanayokinzana nakukwama kwa mazungumzo ya amani. Tanzania inaungamkono juhudi za kimataifa zinazoendelea kupitia Umoja waAfrika za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

121. Mheshimiwa Spika, siku za hivi karibuni, imeripotiwakuibuka kwa biashara haramu ya binadamu na utumwa katikabaadhi ya maeneo nchini Libya. Tanzania inalaani kwa nguvuzote kuwepo kwa biashara hiyo na kuitaka jumuiya yakimataifa kuchukua hatua stahiki kwa wale waliohusika.

Burundi

122. Mheshimiwa Spika, kuhusu mgogoro wa kisiasanchini Burundi napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwambajitihada kubwa zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki,chini ya usuluhishi wa Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni,Rais wa Uganda akisaidiwa na Mwezeshaji MheshimiwaBenjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania zimesaidia kurejesha hali ya amanina utulivu nchini Burundi tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015mgogoro huo ulipoibuka.

123. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na kushiriki katikamazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundiuliofanyika Arusha, mwezi Novemba 2017. Mazungumzo hayoyalijumuisha.Serikali.ya.Jamhuri ya Burundi na makundiyanayohusika na mgogoro huo wakiwemo wanasiasa,Marais wastaafu, viongozi wa dini, vyama vya siasa na vyamavya kiraia.

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Syria

124. Mheshimiwa Spika, mgogoro wa Syria badounaendelea kuwa moja kati ya ajenda muhimu kwenyejumuiya ya kimataifa. Mgogoro huo unazidi kuwa mgumukutokana na mvutano wa mataifa makubwa. Tunayasihimataifa yanayohusika na mgogoro huo kushirikiana ilikurejesha amani nchini humo kwa njia ya mazungumzo. Hiiinatokana na ukweli kwamba vita vinavyoendelea bainaya makundi mbalimbali yanayoungwa mkono na nchi zakigeni huzidisha uhasama na kusababisha hasara kubwa kwamaisha ya binadamu wasio na hatia pamoja na uharibifu wamiundombinu ya nchi hiyo.

Yemen

125. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina imani kwambawananchi wa Yemen wana haki ya kujiamulia mustakabaliwa nchi yao. Kutokana na mgogoro huo idadi ya vifo, raiawanaokimbia nchi yao na wanaopoteza makazi inazidikuongezeka. Tanzania inaamini kuwa mgogoro huu unawezakupatiwa suluhu kwa pande zinazohasimiana kukaa pamojana inaunga mkono juhudi za usuluhisho wa mgogoro huo,kupitia jumuiya za kimataifa.

Iran

126. Mheshimiwa Spika, mwaka 2015 nchi wanachamawa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa naUjerumani ziliingia makubaliano na Iran kuhusu mpangowake wa nyuklia ili kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.Mkataba huo ulitoa matumaini ya ushirikiano wa kimataifakatika juhudi za kuondokana na silaha za nyuklia. Hata hivyomwanzoni mwa mwezi Mei 2018, mmojawapo wa wadauwakuu ametangaza kujitoa katika mkataba huo. Tanzaniainazisihi pande zote zinazohusika kuendelea kuheshimumkataba huo na kama kuna dosari katika mkataba huozitatuliwe kwa njia ya mazungumzo.

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Rasi ya Korea

127. Mheshimiwa Spika, Rasi ya Korea ni miongoni mwamaeneo yenye historia ya mgogoro wa muda mrefu nakutishia hali ya amani na usalama duniani. Hata hivyo, hali hiyoimeanza kubadilika kufuatia tukio la kihistoria lililoshuhudiwamwezi Aprili 2018 wakati Marais wa Korea Kaskazini na KoreaKusini walipokutana katika eneo la mpaka wa nchi hizo(Demilitarized Zone) baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhasama.Marais hao walikutana kujadili namna ya kumaliza tofauti zaona kushirikiana. Aidha, mkutano huo umefanyika baada yamiaka 10 tangu viongozi watangulizi wa nchi hizo mbili, RaisKim Jong Il na Rais Roh Moo-hyun kukutana mwaka 2007.

128. Mheshimiwa Spika, baada ya Rais wa Jamhuri yaKorea Moon Jae-in kuingia madarakani mwaka 2017, mojaya agenda za serikali yake ilikuwa ni kukaa katika meza yamajadiliano na Korea ya Kaskazini ili kutafuta suhuhu. Nia hiyonjema ya kiongozi huyo iliimarishwa na hotuba ya Rais waKorea Kaskazini ya mwaka mpya 2018, ambapo alimtakiaheri na mafanikio Rais wa Korea Kusini katika kuwa mwenyejiwa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi ya Februari2018. Baada ya salamu hizo Rais wa Korea Kusini alimwalikamwenzake kushiriki ufunguzi pamoja na kutuma timu kushirikikatika mashindano hayo. Mwanzo huo mzuri ulizaa matundana dunia iliendelea kushuhudia mazungumzo mbalimbalikatika ngazi za juu za Maofisa wa usalama wa nchi hizo mbilina hatimaye mkutano huu wa kihistoria.

129. Mheshimiwa Spika, Tanzania kama nchimwanachama wa Umoja wa Mataifa, ambayo imekuwaikichangia sana katika harakati za kuimarisha amani nausalama duniani, na kusimamia suluhu ya migogoro kupitiamazungumzo inapongeza kwa dhati hatua hii ambayoimeonesha umuhimu wa diplomasia katika kutatua migogorokwa njia ya mazungumzo. Dunia inasubiri kwa hamu matokeoya mazungumzo kati ya Rais Donald Trump wa Marekani narais Kim Jong-un wa Korea ya Kaskazini yatakayofanyikabaadae mwaka huu.

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Bahari ya Kusini ya China (South China Sea)

130. Mheshimiwa Spika, Tanzania imekuwa ikifuatilia kwamakini hali ya usalama katika Bahari ya Kusini ya China navisiwa vyake. Tunaunga mkono msimamo wa Chinaunaotaka pawe na mazungumzo baina ya nchi zinazohusikakatika kutatua mgogoro na kuondoa tofauti zilizopo kati yanchi hizo kwa mazungumzo ili.kufikia suluhu kwa njia ya amani.

Nchi za Ghuba

131. Mheshimiwa Spika, Tanzania inafuatilia kwa makinimwelekeo wa siasa na tofauti zilizopo katika nchi za ghuba,hususan Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri kwaupande moja na Qatar kwa upande mwingine, nchi zote hizizina uhusiano mzuri na Tanzania. Nchi hizi zina rasilimali kubwaya mafuta na gesi ambayo ni muhimu kwa uchumi wao nadunia kwa ujumla. Tanzania inazisihi nchi hizi ambazo nimuhimu kwa amani na uchumi wa dunia kuzungumza nakufikia muafaka wa tofauti zao kwa amani.

Hali ya Uchumi

132. Mheshimiwa Spika, uchumi wa dunia umeendeleakuimarika ambapo kwa sasa unakadiriwa kukua kwa asilimia3 ikilinganishwa na asilimia 2.4 mwaka 2016. Ukuaji huoumechangiwa zaidi na kuimarika kwa uchumi wa mataifayaliyoendelea, uwekezaji wa mitaji kwenye nchi zinazoibukiakiuchumi, pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa. Hali hiiinatoa matumaini ya kuimarika kwa biashara ya bidhaahususan kutoka nchi zinazoendelea.

133. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Afrika, shughuliza kiuchumi zimeendelea kuimarika zikisaidiwa kwa kiasikikubwa na kuimarika kwa uchumi wa mataifa yaliyoendeleapamoja na masoko yanayoibukia. Uchumi wa Afrikaunakadiriwa kukua kwa asilimia 3.1 mwaka 2018 kutoka asilimia1.5 mwaka 2016. Ukuaji huu unatarajiwa kuendelea kutokanana kuimarika kwa hali ya soko la fedha la nje (external

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

financial market conditions). Hali hii itasaidia kuongezeka kwauwekezaji katika miundombinu ya kimkakati kama vile reli,bandari na barabara. Hata hivyo, ukuaji wa uchumi katikaAfrika unatarajiwa kuwa na viwango tofauti ambapo nchiza Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatarajiwa kuendeleakuimarika zaidi. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuendelea kuwakinara katika ukuaji wa uchumi ndani ya Jumuiya ya AfrikaMashariki na hata katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika.

134. Mheshimiwa Spika, hali hii nzuri ya ukuaji kiuchumikwa ujumla wake, unaweza kuathiriwa na baadhi ya matatizoya kimfumo hususan kwenye sekta ya fedha na kodi. Jumuiyaya kimataifa inapaswa kuweka mfumo mahsusi wa ushirikianowa masuala ya kodi kwa ajili ya kuondoa ushindani wakukusanya kodi na kuyalazimisha makampuni ya kimataifakulipa kodi stahiki kwenye nchi yanapowekeza. Aidha, Tanzaniainahamasisha ushirikiano madhubuti wa kimataifa kwa ajiliya kukabiliana na uhamishwaji haramu wa fedha i l ikupambana na vitendo vya rushwa vya kimataifa. Kwa sasathamani ya fedha zinazohamishwa kutoka nchizinazoendelea kwenda nchi tajiri ni kubwa kuliko thamaniya misaada ya maendeleo inayotolewa kwa nchizinazoendelea hivyo ni muhimu kuwa na mkakati wa pamojakudhibiti uhalifu huu unaokwamisha jitihada za maendeleoAfrika na kwingineko. Changamoto hizi zinahitaji ushirikianowa kimataifa kuzitatua na kuimarisha mifumo ya kisiasa nakiusalama ili kuweka mazingira mazuri ya kujenga uchumiimara kwa watu wote.

135. Mheshimiwa Spika, tangu kuanzishwa kwake Shirikala Biashara Duniani (WTO), limekuwa muhimili mkubwa katikakuhakikisha biashara duniani zinaendeshwa kwa kuzingatiasheria, kanuni na taratibu zilizojadiliwa na kukubalika na nchizote wanachama. Kama leo hii pasingekuwepo na WTO ilikusimamia uendeshaji wa biashara na hasa kulinda maslahiya nchi zinazoendelea kama Tanzania, dunia ingekuwa siyomahali salama pakufanya biashara. Migogoro na mivutanoya kibiashara ingekuwa mingi na ingezorotesha maendeleo.

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

136. Mheshimiwa Spika, hivi sasa Shirika hili linapitiachangamoto zinazotishia uwepo wake na ustawi wabiashara duniani tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 20iliyopita. Hali hii inasababishwa na kuongezeka kwa maamuziya nchi moja moja (unilateralism) badala ya kuzingatia misingiya kuamua kwa pamoja (multilateralism) iliyojengwa na WTO.Nchi zinazoendelea zikiruhusu hili, zitakuwa za kwanzakuangamia. Natoa wito kwa nchi zote hususan zilizoendeleakuheshimu na kulinda misingi ya ushirikiano wa kimataifakatika kufanya maamuzi ya biashara duniani. Palepanapotokea sintofahamu, ni vizuri kufuata taratibu zausuluhishi za kimataifa zinazokubalika.

137. Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa Tanzania itaendelea kusimamia na kuteteamisingi ya ushirikiano wa kimataifa katika kufikia maamuziyanayohusu mustakabali wa dunia kwenye nyanja zote.

TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA

138. Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia taasisi tatuambazo ni Chuo cha Diplomasia, Taasisi ya Mpango waKujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika na Kituo chaKimataifa cha Mikutano cha Arusha, ambacho piakinasimamia Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha JuliusNyerere kilichopo Dar es Salaam. Naomba nichukue fursa hiikutoa taarifa juu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizokama ifuatavyo:

Chuo cha Diplomasia

139. Mheshimiwa Spika, Chuo kimeendelea kutekelezamajukumu ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kushauriWizara katika masuala ya diplomasia na uhusiano wakimataifa. Mafunzo yanayotolewa chuoni hapo yamejikitazaidi katika programu ya diplomasia ya uchumi ili kwendasambamba na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano yakufanya mageuzi ya uchumi wa Tanzania kuwa wa viwanda.

140. Mheshimiwa Spika, katika kujiimarisha, Chuo

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

kinatekeleza mradi wa upanuzi na uboreshaji wamiundombinu yake ili kuongeza udahili wa wanafunzi.Madhumuni ya hatua hizi ni kutoa nafasi zaidi ya elimu kwaumma na kukiongezea chuo mapato na hatimayekupunguza utegemezi wa fedha za uendeshaji kutoka Serikalini.Katika kufanikisha hilo, Wizara inaendelea kutenga fedha zaidikwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho.

Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha

141. Mheshimiwa Spika, Kituo cha Kimataifa cha MikutanoArusha (AICC) kimeendelea kuwa kitovu cha diplomasia yamikutano hapa nchini na kuchangia katika kukuza uchumi.Hadi kufikia mwezi Machi 2018 Kituo kilikuwa mwenyeji wamikutano 257 ambapo kati ya hiyo, mikutano 57 ni yakimataifa na 200 ya kitaifa ambayo imeingiza jumla ya Shilingi2,036,218,423.

142. Mheshimiwa Spika, katika kipindi.cha.mwaka wafedha 2018/19, Kituo.kimepanga.kuingiza.mapato ya Shilingi16,743,620,893. Kati ya fedha hizo, Shilingi 15,587,877,637 ni kutokavyanzo mbalimbali vya ndani; na Shilingi 1,155,743,256zitatokana na mkopo. Aidha, Kituo cha Mikutano chaKimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kinategemewa kuingizakiasi cha Shilingi 3,338,800,000.

143. Mheshimiwa Spika, Kituo cha AICC kinategemeakukopa Shilingi 1,155,000,000 kwa ajili ya mradi wa upanuziwa Hospitali ya AICC. Aidha, kituo kinaendelea kufanyataratibu za kuwezesha ujenzi wa kituo mahsusi cha mikutanokitakachoitwa Mt. Kilimanjaro International Convention Centre(MK-ICC). Kituo hicho ndicho kitakachokuwa suluhisho lautekelezaji wa diplomasia ya mikutano ya kimataifa namaonesho hapa nchini. Vilevile, Kituo kimeiomba Wizara yaArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupatiwa eneo kwaajili ya ujenzi wa kituo cha mikutano jijini Dodoma.

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika(APRM)

144. Mheshimiwa Spika, APRM ni mpango wa nchi zaAfrika wa kujitathmini katika masuala ya utawala bora.Tanzania ilijiunga na Mpango huo mwaka 2004, na uliridhiwana Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005.Lengo la APRM ni kuziwezesha nchi za Afrika kuimarisha utawalabora kwa kushirikisha wananchi wake kubainishachangamoto na kuzigeuza kuwa fursa za maendeleo ilikubaini mambo mazuri ya kuendelezwa kwa faida ya nchiyenyewe na hata kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

145. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18, kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, APRM Tanzania iliendeleakutekeleza shughuli zilizopangwa kwenye mpangokazi kamaifuatavyo:

(i) Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi waAPRM kwa ufadhili wa jumla ya Dola za Marekani100,000 kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja waMataifa (UNDP) Tanzania;

(ii) Kusimamia uzinduzi wa Ripoti ya nchi uliofanywa tarehe19 Julai 2017 na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania;

(iii) Kufanya warsha ya kuwajengea uwezo watendaji waSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuunganishamipango ya maendeleo ya nchi pamoja nampangokazi wa APRM;

(iv) Kushiriki mikutano ya APRM kulingana na Mkataba waMakubaliano wa kujiunga na APRM; na

(v) Kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi kuhusuutekelezaji wa shughuli za APRM.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

146. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua.umuhimu wamisingi ya utawala bora, Wizara yangu itaendelea kuiwezeshaAPRM kutekeleza majukumu yake.

UTAWALA NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU

147. Mheshimiwa Spika, Wizara ina jumla ya watumishi456 wa kada mbalimbali. Kati ya hao, 347 wapo MakaoMakuu ya Wizara na 109 wapo katika Balozi zetu nje ya nchi.

Ajira Mpya

148. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2017/18, Wizara ilipata kibali cha kuajiri watumishi 10 wa kadambalimbali ambapo hadi sasa watumishi 5 tayari wameripotikazini na watumishi 5 taratibu za ajira zao zinaendelea.

Upandishaji vyeo watumishi

149. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2017/18, Wizara imepata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti yaUtumishi wa Umma na Utawala Bora cha kuwapandisha vyeowatumishi 97. Taratibu za kuwapandisha vyeo watumishi haozinaendelea kukamilishwa.Uteuzi

150. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya uteuzi wamabalozi watano ambapo kati yao watatu wamepangiwavituo na wawili taratibu za kuwapangia vituo zinaendelea.

Mafunzo

151. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwajengeauwezo Watumishi kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu namuda mfupi ndani na nje ya nchi. Watumishi 31 walihudhuriamafunzo ya muda mfupi na watumishi 9 wanaendelea namafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya Shahada ya Uzamili.Aidha, Wizara ilipokea nafasi 5,220 za mafunzo kutoka nchi 27

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

wahisani na marafiki. Kati ya nafasi hizo mafunzo ya mudamfupi ni 4,650 na ya muda mrefu ni 570. Wizara iliratibu fursahizo kwa kuzitangaza kwa umma wa watanzania kupitiavyombo vya habari, tovuti ya wizara, mitandao ya kijamii nanyingine ziliwasilishwa moja kwa moja kwenye Wizara na Idaraza kisekta ili watanzania wenye sifa waweze kuomba nafasihizo.

152. Mheshimiwa Spika, Wizara iliandaa Semina Elekezikwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Masharikiiliyofanyika mwezi Januari, 2018, Jijini Dar es Salaam. Lengola Semina hiyo lilikuwa ni kuwajengea uelewa WaheshimiwaWabunge hao katika masuala yatakayowawezeshakutekeleza majukumu yao, wakihakikisha kuwawanawasilisha na kutetea hoja zenye manufaa na maslahimapana kwa ustawi wa nchi yetu wakati wa mijadala ndaniya Bunge hilo.

153. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2017/18 Wizara yangu imekabiliana na changamotombalimbali za kimfumo wa dunia, pamoja na zile zakiutendaji. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo Wizaraimeendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisimkubwa kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na wadauwote wa ndani na nje kuhakikisha kwamba malengo ya Serikalikwenye ushirikiano wa kimataifa yanatimia bila kujali uwepowa changamoto hizo. Napenda kutumia fursa hii kuhimizawadau kuendelea kushirikiana na Wizara yangu ili kwa pamojatuweze kutimiza azma ya Serikali ya kukuza uchumi nakuboresha maisha ya wananchi wote.

SHUKRANI

154. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naombakuchukua fursa hii kuwashukuru Mabalozi, Wawakilishi waTaasisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine yaKimataifa kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kupitia nchina mashirika yao kufanikisha mipango mbalimbali yamaendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

155. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tanoimeendelea kupata mafanikio makubwa kutokana namchango wa wadau na washirika wa maendeleo kutoka nchina asasi mbalimbali za kitaifa, kikanda, kimataifa pamoja nasekta binafsi. Naomba nitumie fursa hii kuzishukuru nchi za AfrikaKusini, Algeria, Australia, Austria, Brazil, Canada, China, Cuba,Denmark, Finland, Hungary, India, Italia, Ireland, Israel, Iran,Japan, Korea Kusini, Kuwait, Malaysia, Marekani, Malta, Misri,Morocco, New Zealand, Norway, Oman, Pakistan, Palestina,Poland, Qatar, Saudi Arabia, Sweden, Singapore, Sri-Lanka,Thailand, Ubelgiji, Ufaransa, Uhispania, Uholanzi, Uingereza,Ujerumani, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ureno, Urusi, Uswisi,Uturuki na Vietnam kwa kuchangia mafanikio hayo muhimukwa Taifa.

156. Mheshimiwa Spika, shukrani ziwaendee pia Umojawa Ulaya, Benki ya Maendeleo ya Afrika, African CapacityBuilding Facility, Benki ya Dunia, IAEA, Shirika la Fedha Duniani(IMF), Investment Climate Facility for Africa, UNDP na Mashirikamengine yote ya Umoja wa Mataifa, TradeMark East Africa,Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Afrika (BADEA),The Association of European Parliamentarians with Africa, WWF,The Belinda and Bill gates Foundation, Global Fund,International Committee of the Red Cross, InternationalFederation of the Red Cross and Red Crescent Societies,Medecins Sans Frontieres pamoja na Mifuko na Mashirikambalimbali ya Misaada. Ni dhahiri kuwa mafanikiotuliyoyapata yamechangiwa kwa misaada na ushirikianowenu.

MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19

157. Mheshimiwa Spika, kwa muhtasari miongoni mwamalengo yaliyopangwa kutekelezwa na Wizara yangu katikamwaka wa Fedha 2018/19 ni pamoja na:

i. Kuendelea kulinda na kutetea misingi ya Taifa;

ii. Kuendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Seraya Mambo ya Nje ikiweka msisitizo kwenye diplomasiaya uchumi kuelekea Tanzania ya viwanda;

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

iii. Kuendelea kuvutia fursa za uwekezaji katika sektambalimbali, biashara pamoja na kutangaza vivutiovya utalii;

iv. Kuratibu Tume za Pamoja za Kudumu za Ushirikiano(JPC);

v. Kufuatilia mwelekeo wa siasa na uchumi duniani nakutathmini matokeo yake kwa siasa ya mambo ya njeya Tanzania;

vi. Kuendelea kuratibu utekelezaji wa makubaliano yakikanda na kimataifa ikiwemo agenda ya Umoja waAfrika ya 2063; na agenda ya Umoja wa Mataifa ya2030;

vii. Kufuatilia fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiwa Tanzania katika mtangamano wa kikanda namashirika ya kimataifa;

viii. Kuendelea kuongeza uwakilishi wa Tanzania nje kwakufungua Balozi mpya, Konseli Kuu, kutumia Konseli zaHeshima sambamba na kuongeza umiliki wa nyumbaza makazi ya watumishi na ofisi balozini;

ix. Kuendelea kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yaViongozi Wakuu wa Kitaifa;

x. Kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mikatabambalimbali iliyosainiwa kati ya nchi yetu na nchinyingine na kufuatilia ahadi mbalimbali zilizotolewakwa nchi yetu na nchi wahisani na mashirika yakimataifa;

xi. Kuongeza mshikamano na jumuiya za watanzaniawanaoishi ughaibuni na kuweka utaratibu madhubutiutakaowawezesha kuchangia kwenye maendeleo yaTaifa;

xii. Kuendelea kushirikiana na Wizara, Taasisi za Serikali,Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia na vyombo vya habarikatika kuelimisha umma juu ya fursa mbalimbali

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

zitokanazo na ushiriki wa Tanzania katika Jumuiya zakikanda na kimataifa;

xiii. Kuendelea kutafuta nafasi za masomo, misaada nakushawishi nchi na mashirika kutufutia madeni; na

xiv. Kuendelea kujenga uwezo wa watumishi Wizarani.

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWAMWAKA WA FEDHA 2018/19

158. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2018/19,Wizara yangu imetengewa bajeti ya kiasi cha Shilingi177,006,232,000. Kati ya fedha hizo Shilingi 154,810,812,000 nikwa ajili ya matumizi mengineyo, Shilingi 11,795,420,000 nikwa ajili ya mishahara na Shilingi 10,400,000,000 ni kwa ajili yabajeti ya maendeleo.

159. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya matumizimengineyo, Shilingi 116,010,729,689 ni kwa ajili ya matumizi yavifungu vya Balozini, Shilingi 35,324,806,566 ni kwa ajili ya vifunguvya makao makuu ya Wizara, Shilingi 1,077,362,234 ni kwa ajiliya Mpango wa Kujitathmini Kiutawala bora Tanzania, Shilingi1,000,000,000 ni kwa ajili ya fedha za matumizi mengineyo yaChuo cha Diplomasia, Shilingi 1,239,633,751 ni kwa ajili yaMahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu naShilingi 158,279,760 ni kwa ajili ya Bodi ya Ushauri waMasuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika.

160. Mheshimiwa.Spika,.katika. fedha. za. bajeti yamaendeleo, kiasi cha Shillingi 10,400,000,000 zilizopangwakwa mwaka wa fedha 2018/19, kiasi cha Shilingi 6,180,676,000zitatumika kwa ajili.ya.ujenzi wa jengo la ofisi ya ubalozi waTanzania Muscat, Oman; Shilingi 1,819,324,000 ni kwa ajili yaukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo ubaloziwa Tanzania Khartoum, Sudan; na Shilingi 2,400,000,000 ni kwaajili ya upanuzi na uboreshaji wa miundombinu ya chuo chadiplomasia.

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

161. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/19, Wizara kupitia balozi zake, inatarajia kukusanya kiasi chaShilingi 28,564,158,100 ikiwa ni maduhuli ya Serikali.

HITIMISHO

162. Mheshimiwa Spika, ili kuweza kutekeleza kikamilifumajukumu ya Wizara, kwa mwaka wa fedha 2018/2019,naomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi177,006,232,000. Kati ya fedha hizo Shilingi 166,606,232,000 nikwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 10,400,000,000 nikwa ajili ya bajeti ya maendeleo.

163. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua nafasi hiikukushukuru wewe binafsi na waheshimiwa wabunge kwakunisikiliza.

164. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sasa namwitaMwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo yaNje, Ulinzi na Usalama, kwa niaba yake Mheshimiwa MboniMohamed Mhita. (Makofi)

MHE. MBONI M. MHITA (K.n.y. MHE. MUSSA A. ZUNGU- MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NAUSALAMA): Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, naombataarifa hii iingie katika Hansard kama ilivyowasilishwa mezani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumshukuru sanaMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamchango wake wa dhati, kutupigania vijana wake nakuweza kushinda uchaguzi huu. Namshukuru vilevileMheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Spika, Katibu waBunge, staff wa Bunge na Wabunge wote kwa ujumla.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia kumshukurusana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na timu nzima yaWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Mabalozi, timu nzima ya Wabunge wenzangu ambao niwawakilishi wa Bunge la Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016,naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wamajukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2017/2018; pamojana maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019; na kuliombaBunge lako Tukufu liipokee taarifa hii na kuikubali, kishakuidhinisha bajeti ya Wizara hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kifungu cha6(3) cha Nyongeza ya Nane, ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Wizara hii ni mojawapo ya Wizara inayosimamiwa na Kamatiya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Aidha,Kifungu cha 7(1)(a) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni zaKudumu za Bunge kimezipa jukumu Kamati za Kisektaikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama kushughulikia Bajeti za Wizarainazozisimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kulijulisha Bungelako Tukufu kuwa katika kutekeleza jukumu hilo, Kamatiilikutana na Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa AfrikaMashariki tarehe 23 na 26 Machi, 2018. Katika kikao hicho,Kamati ilipokea Taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa Bajetikwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 kama inavyoelekeza Kanuniya 98(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kwa lengo lakulinganisha na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizarahii, kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kulisaidia Bunge lakoTukufu kufuatilia ipasavyo utekelezaji wa bajeti kwa mwakawa fedha 2017/2018, pamoja na kuishauri vema Serikali kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hii kwa mwakawa fedha 2018/2019, taarifa ninayoiwasilisha inatoa maelezokuhusu:-

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, mapitio ya taarifaya Wizara kuhusu uzingatiaji wa maoni yaliyotolewa naKamati Bungeni wakati wa kujadili Bajeti ya Wizara hii kwaMwaka wa Fedha 2017/2018;

Mheshimiwa Naibu Spika, mbili, uchambuzi waukusanyaji wa maduhuli ikilinganishwa na lengo lililowekwakwa mwaka wa fedha 2017/2018;

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, mapitio ya taarifa yaWizara kuhusu upatikanaji wa fedha zilizoidhinishwa na Bungepamoja na utekelezaji wa majukumu na malengo ya bajetikwa mwaka wa fedha 2017/2018;

Mheshimiwa Naibu Spika, nne, uchambuzi wamajukumu na malengo yanayowekwa kwa mwaka wafedha 2018/2019;

Mheshimiwa Naibu Spika, tano, uchambuzi wamakadirio ya mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019; na

Mheshimiwa Naibu Spika, sita, mapitio ya malengoya bajeti na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha2018/2019.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo ni kuliwezesha Bungekupata taswira ya hali ya utekelezaji wa Bajeti kwa mwakawa fedha 2017/2018 na kulinganisha na makadirio ya fedhaza matumizi yaliyowasilishwa na mtoa hoja mapema leoBungeni ili liweze kujadili na kuamua kuhusu maombi yaWizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa ya Utekelezaji waMajukumu ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, ilihusumaeneo makuu mawili. Maeneo hayo ni uzingatiaji waMaoni na Ushauri wa Kamati na mapitio ya bajetiiliyoidhinishwa na Bunge. Naomba kulijulisha Bunge lako hilikuwa, Kamati ilipitia na kuchambua kwa kina mambo yotemawili kama ifuatavyo:-

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

Mheshimiwa Naibu Spika, tutakumbuka kuwa Bungehili lilipokuwa linajadili hoja ya Serikali kuhusu Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hii kwa mwaka wa fedha2017/2018, Kamati ilitoa ushauri katika jumla ya mambomakuu kumi na tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kufuatilia uzingatiajiwa ushauri huo, tarehe 23 Machi, 2018 Waziri wa Mambo yaNje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki aliijulisha Kamati kuhusuutekelezaji wa ushauri huo. Naomba kulijulisha Bunge lakokwamba upo ushauri uliozingatiwa, upo unaoendeleakuzingatiwa na upo ushauri uliopewa uzito kidogo katikautekelezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, miongoni mwa ushauriuliozingatiwa ni kuhusu ufunguzi wa ofisi za Ubalozi au Baloziza Heshima katika nchi zenye uhusiano mkubwa wakibiashara na Tanzania kama vile Lubumbashi DRC, Cubana Guangzhou – China. Maelezo ya Waziri yalionesha kuwakwa mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali imetengaSh.9,329,800,000 kwa ajili ya kufungua ubalozi mpya Cubana Konseli (Consular) Kuu katika miji ya Lubumbashi – Jamhuriya Kidemokrasia ya Kongo na Guangzhou nchini China.Kamati inaipongeza Serikali kwa hatua hiyo inayowezakuinufaisha nchi yetu kutokana na fursa mpya za kiuchumina kibiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri unaoendeleakufanyiwa kazi na ambao utekelezaji wake haujaanza nipamoja na ujenzi wa ofisi ya Wizara kwa upande wa Zanzibar.Naomba kulikumbusha Bunge lako Tukufu kuwa, tarehe 31Mei, 2017 wakati wa kujadili bajeti ya Wizara hii, Kamatiilishauri kwamba Serikali ifanye matengenezo makubwa aukujenga jengo jipya la ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki huko Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia tarehe 23 Machi,2018, Kamati ilipochambua taarifa ya Wizara hii, hakunaukarabati wa jengo hilo au ujenzi wa jengo jipya kwamadhumuni hayo, uliokuwa umepangwa. (Makofi)

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ya Waziri ilioneshakuwa bado mazungumzo yanaendelea baina ya Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kuhusu umiliki wa jengo linalotumiwa hivi sasana Idara ya Mambo ya Nje ya Zanzibar. Ahadi iliyotolewa nikwamba, mazungumzo yatakapokamilika na Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ikipatiwa umiliki wajengo husika, ukarabati utaanza mara moja. Ni maoni yaKamati kuwa kasi ya kufanikisha mazungumzo hayoinapaswa kuongezwa na njia ya kujenga jengo lingineinaweza kutumika iwapo mazungumzo hayo hayatafanikishaazma ya Wizara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla ushauri waKamati umefanyiwa kazi na uzingatiaji upo katika hatuambalimbali. Hata hivyo, Kamati inasisitiza kuwa, kwa mamboambayo uzingatiaji wake haujafikia hatua kubwa, ushauriwa Kamati unapaswa kupewa uzito stahiki. Kwa mfano,suala la kukamilisha Sera mpya ya Mambo ya Nje, inayopaswakutoa dira na mwelekeo unaoendana na hali ya kisasa yadiplomasia ya uchumi duniani linapaswa kupewa uzitomkubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kulijulisha Bungelako Tukufu kuwa taarifa il iyotolewa kwenye Kamatiinaonesha kuwa hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa Rasimuya Sera. Aidha, hatua inayofuata na ambayo haijaanza nikuandaa mkakati wa utekelezaji wa sera iwapo itapitishwandani ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, imepita takribani miaka 17sasa tangu sera iliyopo ilipotungwa. Wakati huo Wizarahaikuwa na jukumu la kushughulikia au kuratibu masuala yamtangamano wa Afrika Mashariki. Kamati ina maoni kuwakuna umuhimu mkubwa wa kuongeza kasi ya kukamilishamchakato wa sera hii na mkakati wake ili kuikamilisha kablaya mwaka wa fedha 2019/2020. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilipitia taarifa yautekelezaji wa bajeti kwa kuchambua hali ya ukusanyaji wa

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

mapato hadi mwezi Februari 2018 pamoja na upatikanajiwa fedha kutoka Hazina kwa kipindi cha Julai, 2018 haditarehe 20 Machi, 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018, Wizara hii ilikuwa na lengo la kukusanya maduhuliya Serikali kiasi cha shilingi bilioni ishirini na tano milioni miasaba sabini na tatu. Hata hivyo, Kamati ilijulishwa kuwa hadikufikia mwezi Februari, 2018, Wizara ilikusanya jumla yaSh.18,665,000,000/=, sawa na asilimia 72 ya lengo la ukusanyaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilifanya ulinganishowa hali ya ukusanyaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 hadikufikia Februari, 2017. Naomba kulijulisha Bunge lako Tukufukuwa katika kipindi cha Julai, 2016 hadi Februari, 2017makusanyo yalifikia asilimia 60.7 tofauti na asilimia 72.4 yalengo kwa kipindi cha Julai, 2017 hadi Februari, 2018. Kamatiina maoni kwamba mwenendo huu wa ukusanyaji wamaduhuli ulikuwa wa kuridhisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilipochambuataarifa ya upatikanaji wa fedha kwa mwaka wa 2017/2018ilibaini kuwa hadi kufikia tarehe 20 Machi, 2018 Wizara ilipokeaSh.98,617,000,000/=, sawa na asilimia 65.38 ya bajetiiliyoidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Hali hiyo ni tofauti naMwaka wa Fedha 2016/2017 ambapo hadi kufikia mweziMachi, 2017, Wizara ilipokea Sh.87,201,000,000/=, sawa naasilimia 56 ya bajeti iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya fedha zilizopokelewakatika mwaka wa fedha 2017/2018, Sh.88,228,000,000/=zilikuwa za matumizi mengineyo, sawa na asilimia 66 yaSh.133,424,000,000/= zilizotengwa. Sh.7,468,000,000/= kwa ajiliya mishahara, sawa na asilimia 79 ya Sh.9,421,000,000/=zilizotengwa na Sh.2,920,000,000/= zilikuwa za miradi yamaendeleo, sawa na asilimia 36.5 ya Sh.8,000,000,000/=zilizotengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilijulishwa kuwaasilimia kubwa ya fedha zilizopatikana kutoka Hazina

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

zilitumika kugharamia uendeshaji wa ofisi za balozi zetu njeya nchi; safari za viongozi wa kitaifa nje ya nchi, ukarabatiwa majengo ya Balozi zetu zilizopo Kampala, Kinshasa,Lilongwe na Brussels pamoja na utekelezaji wa majukumumengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwelekeo huu wa matumizihautofautiani sana na mwelekeo ulivyokuwa kwa kipindi chaJulai, 2016 hadi Machi, 2017. Hata hivyo, bado kuna umuhimumkubwa kwa Wizara kupitia vipaumbele vyake kabla yakuanza matumizi ya fedha zinazopokelewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kueleza uchambuziwa Makadirio ya Matumizi ya Wizara hii kwa Mwaka waFedha 2018/2019, napenda kutoa taarifa kwa Bunge lakoTukufu kuwa, Kamati ilielezwa miongozo 12 iliyozingatiwawakati wa maandalizi ya bajeti ya Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, miongoni mwa miongozohiyo, ni Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, ambayo inaumri wa takribani miaka 17. Miongozo mingine ni pamojana Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano(2016/2017 – 2020/2021) na Mkataba wa Uanzishwaji waJumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilielezwa zaidi kuwaWizara imepanga malengo makuu 12 ya kibajeti kwa Mwakawa Fedha 2018/2019. Mfano wa malengo hayo ni kuandaaSera ya Taifa ya Diaspora itakayotoa mwongozo wa namnaya kuwashirikisha Diaspora wa Tanzania katika kuchangiamaendeleo ya nchi yao. Lengo lingine ni kuratibu nakusimamia majadiliano ya Rasimu ya Andiko la Katiba yaFungamano la Kisiasa la Afrika Mashariki (East Africa PoliticalFederation).

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi wa Kamatiumebaini kwamba hakuna lengo mahsusi la ukamilishaji wamapitio ya Sera ya Taifa ya Mambo ya Nje kwa wakati huu,ambapo Wizara itaratibu majadiliano kuhusu Andiko laKatiba ya Fungamano la Kisiasa la Afrika Mashariki. Ni maoni

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

ya Kamati kuwa jambo hili linapaswa kupewa umuhimu kwakiwango stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika uchambuzi wa bajetiya Wizara hii, Kamati ilichambua makadirio ya ukusanyajiwa mapato yanayopendekezwa kwa mwaka wa fedha wa2018/2019 na kubaini kuwa makadirio hayo yanatofautianakidogo na lengo lililowekwa kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018. Katika mwaka wa fedha unaoisha, Wizara ilikuwa nalengo la kukusanya Sh.25,773,000,000/=, wakati kwa mwakawa fedha 2018/2019, Wizara inalenga kukusanya kiasi chaSh.28,564,000,000/=. Lengo hili la makusanyo limeongezekakwa kiasi cha Sh.2,790,000,000/= sawa na asilimia 10.8.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi zaidi ulioneshakuwa ongezeko hilo lipo katika lengo la makusanyo ya balozizetu za nje ya nchi ambapo zilikuwa na lengo la kukusanyajumla ya Sh.25,672,000,000/= kwa mwaka wa fedha 2017/2018;lakini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 zinapewa lengo lakukusanya jumla ya Sh.28,448,000,000/=.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ililinganisha lengola kukusanya mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019 namwenendo halisi wa ukusanyaji wa mapato kwa mwakawa fedha 2017/2018, ili kutathmini lengo la maduhulilinalopangwa kwa mwaka wa fedha unaofuata. Tathminiimeonesha kuwa hadi kufikia mwezi Februari, 2018, ni kiasicha Sh.18,665,000,000/=, sawa na asilimia 72.7 kilikuwakimekusanywa. Kwa mwenendo huo, kiasi cha lengokilichobaki ni Sh.7,113,000,000/= sawa na asilimia 27.3ambacho kinaweza kukusanywa kwa kipindi cha mweziMachi hadi Juni, 2018. Kwa mwenendo huu, Kamati inaridhikakuwa lengo la mapato linalowekwa linaendana na hali halisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilijulishwa kuwaWizara hii inaomba kuidhinishiwa kiasi cha Sh.177,000,000,000/= ambapo Sh.154,000,000,000/= ni kwa ajili ya matumizimengineyo (OC) Sh. 11,795,000,000/= ni kwa ajili ya mishaharana Sh.10,400,000,000 ni kwa ajili ya kugharamia miradi yamaendeleo.

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilifanya uchambuziwa maombi hayo na kuona kuwa asilimia 87.5 ya makadiriohayo ni kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli, asilimia 6.7 nikwa ajili ya mishahara na asilimia 5.1 ni kwa ajili yakugharamia miradi ya maendeleo kama inavyoonekanakatika jedwali Na. 01 na graph Na. 01 na Na. 02 katika taarifahii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilifanya ulinganishokati ya Bajeti ya Mwaka 2017/2018 na Mwaka 2018/2019 kamainavyoelekeza Kanuni ya 98(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.Katika ulinganisho huo, Kamati i l ibaini kuwa fedhazinazoombwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019zimeongezeka kwa asilimia 17.3 kutoka shilingi bilioni 150.8zilizoidhinishwa mwaka 2017/2018 hadi shilingi bilioni 177zinazoombwa kuidhinishwa na Bunge leo kamailivyobainishwa katika Jedwali Namba 01.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilipochambua zaidiilibaini kuwa bajeti ya mishahara, bajeti ya matumizimengineyo na bajeti ya miradi ya maendeleo imeongezekaikilinganishwa na mwaka 2017/2018. Bajeti ya mishaharaimeongezeka kwa asil imia 25.2, bajeti ya matumizimengineyo imeongezeka kwa asilimia 16 na bajeti yamaendeleo kwa asilimia 30. Pamoja na hivyo, sura ya uwianowa bajeti iliyotengwa kwa vipengele hivyo vitatu kwamwaka wa fedha 2017/2018 na 2018/2019 haitofautiani sanakama inavyoonekana katika Jedwali Na. 01 na Graph Na.01 pamoja na Graph Na. 02.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inatambua kuwamwenendo huu wa uwiano wa bajeti utaendelezwa na hatakuboreshwa zaidi. Ni imani ya Kamati kuwa hata baada yakuidhinisha makadirio haya, upatikanaji wa fedha utakuwamzuri na unaozingatia namna Bunge linavyoidhinishamakadirio haya ya mapato na matumizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia dhamira yaWizara ya kusimamia na kutekeleza diplomasia ambayoitachangia katika shughuli za kiuchumi na kuwezesha

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

mageuzi ya haraka na maendeleo endelevu ya Tanzania,Kamati inatoa maoni na ushauri ufuatao:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ihakikishe fedha zotekiasi cha Sh.9,329,000,000/= ambazo zimetengwa kwa ajiliya kufungua ubalozi mpya huko Cuba na Konseli (consular)Kuu katika Miji ya Lubumbashi – Jamhuri ya Kidemokrasi yaKongo na Guangzhou ambayo ipo Nchini China, zinatolewakwa wakati na kutumika kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inaamini pesa hizozikitolewa kwa ukamilifu zitawezesha ufunguzi wa ubalozihuo na Konseli kuu hizo na hatimaye nchi yetu kunufaika nafursa za kiuchumi na kibiashara. Aidha, Serikali iweke mikakatizaidi ya kufungua Balozi au Balozi za Heshima katika nchinyingine zinazoendelea kukua kwa kasi kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kiwango chafedha za bajeti zinazotolewa kwa Wizara kimekuwahakiendani na mtiririko wa fedha uliopangwa, jamboambalo linasababisha Wizara na balozi zake kutotekelezaipasavyo majukumu yake ya msingi hususana Sera ya Mamboya Nje inayoweka msisitizo wa diplomasia ya uchumi, Serikaliihakikishe kuwa fedha zinazotengwa zinatolewa kwakuzingatia mtiririko uliopangwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kiwanjakilichotolewa na Serikali ya Oman kwa ajili ya kujenga Ubaloziwa Tanzania Jij ini Muscat hakijaendelezwa tangukilipowekewa jiwe la msingi na Rais Mstaafu wa Awamu yaNne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2012,na kwa kuwa upo uwezekano wa kiwanja hicho kutwaliwana Serikali ya nchi hiyo endapo kitaendelea kukaa bilakuendelezwa, Serikali itoe shilingi bilioni moja milioni mia nanetisini na nne zilizokuwa zimetengwa katika mwaka wa fedha2017/2018 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ubalozi kabla yamwaka huu wa fedha kwisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na ushauriuliotolewa hapo juu, Serikali itoe fedha za maendeleo

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

zilizotengwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili yaukarabati wa majengo ya Ubalozi wetu wa Cairo, ukarabatiwa miundombinu ya Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaamna ujenzi wa makazi ya Balozi, Addis Ababa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwamba Serikaliilijiwekea mkakati wa miaka 15 (2001 - 2003 – 2016/2017)wa kuendeleza viwanja, kukarabati na kununua majengoya ofisi na makazi ya watumishi balozini, mkakati huohaujatekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha. Kamatiinaendelea kuishauri Serikali kutoa kipaumbele katikakuendeleza viwanja 12 ambavyo baadhi yake ni vyamuda mrefu (kama vile viwanja vilivyopo huko Maputo,London, Addis Ababa, Nairobi na Muscat); na kuboreshamajengo ya ofisi na makazi ya watumishi katika Balozi zetuikibidi kwa kutumia mikopo ya muda mrefu lakini yenye ribanafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii itasaidia Serikali kuokoafedha nyingi za walipa kodi zinazotumika kwa ajili ya kukodimajengo ya ofisi na makazi katika Balozi zetu nje ya nchi;ambapo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Sh. 21,667,000,000/= zimetengwa kwa ajil i hiyo. Sambamba na hilo, hiiitawezesha Serikali kujenga majengo ya kisasa ya balozi zetuambayo yakikamilika yataingiza fedha nyingi za kuendeshaBalozi hizo na kusitisha utaratibu wa kupanga ofisi na nyumbaza watumishi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Kamati imebainikuwa utaratibu huo ni wenye tija na mafanikio makubwakama vile inavyoonekana katika Ubalozi wa Maputo –Msumbiji ambako kwa mwaka ujao wa fedha wa 2018/2019hawatahitaji na hawakupangiwa fedha za pango.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Wizaraimekubaliana na ushauri wa Kamati wa kupanga miradimichache itakayoweza kutekelezwa kwa mwaka nahatimaye kuweka miradi mitatu tu ya maendeleo kwamwaka ujao wa fedha 2018/2019, Serikali ihakikishe kuwainaipatia fedha miradi hiyo, hususan ule wa ujenzi wa Ofisi

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

ya Ubalozi wa Muscat, Oman ambako Serikali inawezakukusanya fedha nyingi za maduhuli kwa miaka ijayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho; napendakukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha taarifa hii.Napenda kuwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Mambo yaNje, Ulinzi na Usalama ambao maoni, ushauri na ushirikianowao umewezesha kukamilika kwa taarifa hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Wajumbe waKamati napenda kutumia fursa hii kumshukuru Waziri waMambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, MheshimiwaBalozi Dkt. Augustine Philip Mahiga; Mheshimiwa Naibu Waziri,Dkt. Susan Alphonce Kolimba; Katibu Mkuu, Profesa Mkenda;Naibu Katibu Mkuu, Balozi Ramadhan Muombwa; pamojana watendaji wote wa Wizara kwa ushirikiano na mchangowao katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yaKikanuni ya Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, lakini si kwaumuhimu, napenda kumshukuru Katibu wa Bunge, NduguStephen Kagaigai kwa kuratibu vema shughuli za Kamatina Bunge. Aidha, nawashukuru sana Mkurugenzi wa Idaraya Kamati za Bunge, Ndugu Athumani Hussein; MkurugenziMsaidizi bi. Angelina Sanga; na Makatibu wa Kamati hiiNdugu Ramadhan Abdallah na bi. Grace Bidyawakisaidiwa na bi. Rehema Kimbe, kwa kuratibu vemashughuli za Kamati na kuhakikisha taarifa hii inakamilika kwawakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo,sasa naliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha2018/2019 kama yalivyowasilishwa na mtoa hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja nanaomba kuwasilisha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YANJE, ULINZI NA USALAMA KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI

YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI (FUNGU 34) KWA MWAKA WA FEDHA

2017/2018; PAMOJA NA MAONI YA KAMATI KUHUSUMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA

HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019 KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI

SEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, [Kanuniza Bunge], naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumuya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusuutekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje, naUshirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018; pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha2018/2019, na kuliomba Bunge lako tukufu liipokee taarifa hiina kuikubali, kisha kuidhinisha Bajeti ya Wizara hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (3)cha Nyongeza ya Nane, ya Kanuni za Bunge, Wizara hii nimojawapo ya Wizara inayosimamiwa na Kamati ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Aidha, Kifungu cha 7 (1)(a) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge kimezipajukumu Kamati za Kisekta ikiwemo Kamati ya Kudumu yaBunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kushughulikiaBajeti za Wizara inazozisimamia. Naomba kulijulisha Bungelako tukufu kuwa katika kutekeleza jukumu hilo, Kamatiilikutana na Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa AfrikaMashariki tarehe 23 na 26 Machi, 2018.

Mheshimiwa Spika, katika kikao hicho, Kamatiilipokea Taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa Bajeti kwa

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Mwaka wa Fedha 2017/2018 kama inavyoelekeza Kanuni ya98 (2) ya Kanuni za Bunge kwa lengo la kulinganisha naMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hii, kwa Mwakawa Fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, ili kulisaidia Bunge lako Tukufukufuatilia ipasavyo utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka waFedha 2017/2018, pamoja na kuishauri vema Serikali kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hii kwa Mwakawa Fedha 2018/2019, Taarifa ninayoiwasilisha inatoa maelezokuhusu:-

i) Mapitio ya Taarifa ya Wizara kuhusu uzingatiajiwa maoni yaliyotolewa na Kamati Bungeni wakati wa kujadiliBajeti ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018;

ii) Uchambuzi wa ukusanyaji wa maduhuliikilinganishwa na lengo lililowekwa kwa Mwaka wa Fedha2017/2018;

iii) Mapitio ya Taarifa ya Wizara kuhusuupatikanaji wa fedha zilizoidhinishwa na Bunge pamoja nautekelezaji wa majukumu na malengo ya bajeti kwa Mwakawa Fedha 2017/2018;

iv) Uchambuzi wa majukumu na malengoyanayowekwa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019;

v) Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato kwaMwaka wa Fedha 2018/2019; na

vi) Mapitio ya Malengo ya bajeti na Makadirio yaMatumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Mheshimiwa Spika, lengo ni kuliwezesha Bungekupata taswira ya hali ya utekelezaji wa Bajeti kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 na kulinganisha na Makadirio ya fedhaza matumizi yaliyowasilishwa na mtoa hoja mapema leo iliBunge liweze kujadili na kuamua kuhusu Maombi ya Wizarahii.

SEHEMU YA PILI

MAPITIO YA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWAMWAKA WA FEDHA 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Utekelezaji wamajukumu ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 ilihusumaeneo makuu mawili. Maeneo hayo ni Uzingatiaji waMaoni na Ushauri wa Kamati na Mapitio ya bajetiiliyoidhinishwa na Bunge. Naomba kulijulisha Bunge hili kuwa,Kamati ilipitia na kuchambua kwa kina mambo yote mawilikama ifuatavyo:-

Uzingatiaji wa Maoni na Ushauri wa Kamati

Mheshimiwa Spika, tutakumbuka kuwa Bunge hilililipokuwa linajadili hoja ya Serikali kuhusu Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha2017/2018, Kamati ilitoa ushauri katika jumla ya mambomakuu kumi na tano katika kufuatilia uzingatiaji wa ushaurihuo, tarehe 23 Machi, 2018 Waziri wa Mambo ya Nje, naUshirikiano wa Afrika Mashariki aliijulisha Kamati kuhusuutekelezaji wa ushauri huo. Naomba kulijulisha Bungekwamba upo ushauri uliozingatiwa, upo unaoendeleakuzingatiwa na upo ushauri uliopewa uzito kidogo katikautekelezaji.

Mheshimiwa Spika , miongoni mwa ushauriuliozingatiwa ni kuhusu ufunguzi wa Ofisi za ubalozi au Baloziza heshima katika nchi zenye uhusiano mkubwa wakibiashara na Tanzania kama vile Lubumbashi DRC, Cuba

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

na Guangzhou – China. Maelezo ya Waziri yalionesha kuwakwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Serikali imetenga shilingi9,329,800,000/= kwa ajili ya kufungua ubalozi mpya Cuba naKonseli kuu katika miji ya Lubumbashi – Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo na Guangzhou – China. Kamatiinaipongeza Serikali kwa hatua hiyo inayoweza kuinufaishanchi yetu kutokana na fursa mpya za kiuchumi na kibiashara.

Mheshimiwa Spika, ushauri unaoendelea kufanyiwakazi na ambao utekelezaji wake haujaanza ni pamoja naujenzi wa Ofisi ya Wizara kwa upande wa Zanzibar. Naombakulikumbusha Bunge lako tukufu kuwa, tarehe 31 Mei, 2017wakati wa kujadili Bajeti ya Wizara hii, Kamati ilishaurikwamba Serikali ifanye matengenezo makubwa au kujengajengo jipya la Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki huko Zanzibar. Hadi kufikia tarehe 23Machi, 2018 wakati Kamati ilipochambua Taarifa ya Wizarahii, hakuna ukarabati wa jengo hilo au ujenzi wa jengo jipyakwa madhumuni hayo, uliokuwa umepangwa.

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Waziri ilionesha kuwabado mazungumzo yanaendelea baina ya Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kuhusu umiliki wa jengo linalotumiwa hivi sasana Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar. Ahadi iliyotolewa nikwamba, mazungumzo yatakapokamilika na Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ikipatiwa umiliki wajengo husika, ukarabati utaanza mara moja. Ni maoni yaKamati kuwa kasi ya kufanikisha mazungumzo hayoinapaswa kuongezwa na njia ya kujenga jengo lingineinaweza kutumika iwapo mazungumzo hayo hayatafanikishaazma ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla ushauri wa Kamatiumefanyiwa kazi na uzingatiaji upo katika hatua mbalimbali.Hata hivyo, Kamati inasisitiza kuwa, kwa mambo ambayouzingatiaji wake haujafikia hatua kubwa, ushauri wa Kamatiunapaswa kupewa uzito stahiki. Kwa mfano, suala lakukamilisha Sera mpya ya Mambo ya Nje, inayopaswa kutoa

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

dira na mwelekeo unaoendana na hali ya kisasa yaDiplomasia ya Uchumi duniani, linapaswa kupewa uzitomkubwa zaidi kuliko ilivyo sasa.

Mheshimiwa Spika, Naomba kulijulisha Bunge lakotukufu kuwa Taarifa iliyotolewa kwenye Kamati inaoneshakuwa hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa Rasimu ya Sera.Aidha, hatua inayofuata na ambayo haijaanza ni kuandaamkakati wa utekelezaji wa Sera iwapo itapitishwa ndani yaSerikali.

Mheshimiwa Spika, imepita takribani miaka kumi nasaba sasa tangu Sera iliyopo ilipotungwa. Wakati huo Wizarahaikuwa na jukumu la kushughulikia au kuratibu masuala yamtangamano wa Afrika Mashariki. Kamati ina maoni kuwakuna umuhimu mkubwa wa kuongeza kasi ya kukamilishamchakato wa Sera hii na mkakati wake ili kuikamilisha kablaya Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Uchambuzi wa Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwaMwaka wa Fedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Kamati i l ipitia Taarifa yautekelezaji wa Bajeti kwa kuchambua hali ya ukusanyaji wamapato hadi mwezi Februari 2018 pamoja na upatikanajiwa fedha kutoka Hazina kwa kipindi cha Julai, 2018 haditarehe 20 Machi, 2018.

Ukusanyaji wa maduhuli

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2017/2018 Wizara hii ilikuwa na lengo la kukusanya maduhuli yaSerikali kiasi cha shilingi 25,773,820,000/=. Hata hivyo, Kamatiilijulishwa kuwa hadi kufikia mwezi Februari, 2018, Wizarailikusanya Jumla ya shilingi 18,665,002,685.57/= sawa naasilimia 72.4 ya lengo la ukusanyaji.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya ulinganisho wahali ya ukusanyaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 hadi

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

kufikia Februari, 2017. Naomba kulijulisha Bunge lako tukufukuwa katika kipindi cha Julai 2016 hadi Februari, 2017makusanyo yalifikia asilimia 60.7 tofauti na asilimia 72.4 yalengo kwa kipindi cha Julai, 2017 hadi Februari, 2018. Kamatiina maoni kwamba mwenendo huu wa ukusanyaji wamaduhuli ulikuwa wa kuridhisha.

Upatikanaji wa fedha kutoka Hazina

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipochambua Taarifa yaupatikanaji wa fedha kwa mwaka 2017/2018 ilibaini kuwahadi kufikia tarehe 20 Machi, 2018 Wizara ilipokea Shilingi98,617,704,687.20 sawa na asilimia 65.38 ya Bajetiiliyoidhinishwa na Bunge lako tukufu. Hali hiyo ni tofauti naMwaka wa Fedha 2016/2017 ambapo hadi kufikia mweziMachi, 2017, Wizara ilipokea Shilingi 87,201,012,183.00 sawana asilimia 56 ya Bajeti iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, kati ya fedha zilizopokelewakatika Mwaka wa Fedha 2017/2018, Shilingi 88,228,634,384.20zilikuwa za Matumizi Mengineyo sawa na asilimia 66 ya Shilingi133,424,290,000.00 zilizotengwa, Shilingi 7,468,874,648.00 kwaajil i ya Mishahara sawa na asilimia 79 ya Shil ingi9,421,129,000.00 zilizotengwa, na Shilingi 2,920,195,655.00zilikuwa za Miradi ya Maendeleo sawa na asilimia 36.5 yaShilingi 8,000,000.00 zilizotengwa.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilijulishwa kuwa asilimiakubwa ya fedha zilizopatikana kutoka Hazina ilitumikakugharamia uendeshaji wa Ofisi za Balozi zetu nje ya nchi;safari za Viongozi wa Kitaifa nje ya nchi; ukarabati wamajengo ya Balozi zetu zilizopo Kampala, Kinshasa, Lilongwena Brussels; pamoja na utekelezaji wa majukumu mengine.

Mheshimiwa Spika, Mwelekeo huu wa matumizihautofautiani sana na mwelekeo ulivyokuwa kwa kipindi chaJulai 2016 hadi Machi, 2017. Hata hivyo, bado kuna umuhimumkubwa kwa Wizara kupitia vipaumbele vyake kabla yakuanza matumizi ya fedha zinazopokelewa.

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

SURA YA TATU

UCHAMBUZI WA MPANGO NA BAJETI YA MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019

Uchambuzi wa Malengo ya Bajeti

Mheshimiwa Spika, kabla ya kueleza uchambuzi waMakadirio ya Matumizi ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha2018/2019, napenda kutoa Taarifa kwa Bunge lako tukufukuwa, Kamati ilielezwa Miongozo Kumi na Mbili iliyozingatiwawakati wa maandalizi ya Bajeti ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, Miongoni mwa miongozo hiyo,ni Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001, ambayo ina umriwa takribani miaka kumi na saba. Miongozo mingine nipamoja na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo waMiaka Mitano (2016/2017 – 2020/21) na Mkataba waUanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilielezwa zaidi kuwaWizara imepanga Malengo Makuu Kumi na Mbili ya Kibajetikwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Mfano wa Malengo hayoni kuandaa Sera ya Taifa ya Diaspora itakayotoa mwongozowa namna ya kuwashirikisha Diaspora wa Tanzania katikakuchangia maendeleo ya nchi yao. Lengo lingine ni kuratibuna kusimamia majadiliano ya Rasimu ya Andiko la Katiba yaFungamano la Kisiasa la Afrika Mashariki (East Africa PoliticalFederation).

Mheshimiwa Spika , Uchambuzi wa Kamatiumebaini kwamba hakuna lengo mahsusi la ukamilishaji waMapitio ya Sera ya Taifa ya Mambo ya Nje kwa wakati huu,ambapo Wizara itaratibu majadiliano kuhusu Andiko laKatiba ya Fungamano la Kisiasa la Afrika Mashariki. Ni maoniya Kamati kuwa jambo hili linapaswa kupewa umuhimu kwakiwango stahiki.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

Uchambuzi wa Makadirio ya MapatoMheshimiwa Spika, katika uchambuzi wa bajeti ya

Wizara hii, Kamati ilichambua Makadirio ya ukusanyaji waMapato yanayopendekezwa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na kubaini kuwa Makadirio hayo yanatofautiana kidogona lengo lililowekwa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. KatikaMwaka wa Fedha unaoisha, Wizara ilikuwa na lengo lakukusanya shilingi 25,773,882,820/- wakati kwa Mwaka waFedha 2018/2019, Wizara inalenga kukusanya kiasi cha Shilingi28,564,154,100/-. Lengo hili la Makusanyo limeongezeka kwakiasi cha shilingi 2,790,271,280/- sawa na asilimia 10.8.

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi zaidi ulionesha kuwaongezeko hilo lipo katika lengo la Makusanyo ya Balozi zetunje ya nchi ambapo zilikuwa na lengo la kukusanya jumla yashilingi 25,672,638,700/- kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 lakinikwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 zinapewa lengo lakukusanya jumla ya shilingi 28,448,635,288/-.

Mheshimiwa Spika, Kamati ililinganisha lengo lakukusanya Mapato kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 namwenendo halisi wa ukusanyaji wa Mapato kwa Mwaka waFedha 2017/2018 il i kutathmini lengo la maduhulilinalopangwa kwa Mwaka wa Fedha unaofuata.

Tathmini imeonesha kuwa hadi kufikia Mwezi Februari,2018 ni kiasi cha Shilingi 18,665,002,685.57 sawa na asilimia72.70 kilikuwa kimekusanywa. Kwa mwenendo huo, kiasi chalengo kilichobaki ni shilingi 7,113,591,658.32 sawa na asilimia27.30 ambacho kinaweza kukusanywa kwa kipindi cha mweziMachi hadi Juni, 2018. Kwa mwenendo huu, Kamati inaridhikakuwa lengo la Mapato linalowekwa linaendana na hali halisi.

Uchambuzi wa Makadirio ya MatumiziMheshimiwa Spika, Kamati ilijulishwa kuwa Wizara

hii inaomba kuidhinishiwa kiasi cha shilingi 177,006,232,000/=ambapo shilingi 154,810,812,000/= ni kwa ajili ya matumizimengineyo (OC), shilingi 11,795,420,000/= ni kwa ajili yaMishahara na shilingi 10,400,000,000/= ni kwa ajili yakugharamia Miradi ya Maendeleo.

 

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya Uchambuzi wamaombi hayo na kuona kuwa 87.5% ya Makadirio hayo nikwa ajili ya uendeshaji wa shughuli, 6.7% ni kwa ajili yaMishahara na 5.1% ni kwa ajili ya kugharamia Miradi yaMaendeleo kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 1 naGrafu Na 1 na Na. 2 katika Taarifa hii.

Jedwali Na. 01: Uwiano wa aina za Bajeti ya Matumizi na ulinganisho wake kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019

MWAKA 2017/2018 2018/2019

% O

NG

EZEK

O

AINA YA MATUMIZI KIASI

ASI

LIM

IA

KIASI

ASI

LIM

IA

MISHAHARA (PE)

9,421,129,000.00 6.2 11,795,400,000.00 6.7 25.2

MATUMIZI MENGINEYO (OC)

133,424,290,000.00 88.5 154,810,812,000.00 87.5 16.

MIRADI YA MAENDELEO

8,000,000,000.00 5.3 10,400,000,000.00 5.9 30

JUMLA 150,845,419,000.00 100 177,006,212,000.00 100 17.3

Chanzo: Randama ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Uk. 10 na Uk. 74, Mwezi, Machi, 2018  

MISHAHARA (PE)6%

MATUMIZI MENGINEYO

(OC) 89%

MIRADI YA MAENDELEO

5%

Grafu Na. 1: Ulinganisho kwa mwaka 2017/2018

Chanzo: Takwim u katika Jedwali Na. 1.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya ulinganisho katiya Bajeti ya mwaka 2017/2018 na mwaka 2018/2019 kamainavyoelekeza Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za Bunge. Katikaulinganisho huo, Kamati ilibaini kuwa fedha zinazoombwakwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 zimeongezeka kwa asilimia17.3 kutoka shilingi 150,845,419,000/= zilizoidhinishwa Mwaka2017/2018 hadi shilingi 177,006,212,000/= zinazoombwakuidhinishwa na Bunge leo kama ilivyobainishwa katikaJedwali Namba 1.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipochambua zaidi ilibainikuwa Bajeti ya Mishahara, Bajeti ya Matumizi Mengineyo naBajeti ya Miradi ya Maendeleo imeongezeka ikilinganishwana mwaka 2017/2018. Bajeti ya Mishahara imeongezeka kwaasilimia 25.2, Bajeti ya Matumizi Mengineyo imeongezeka kwaasilimia 16 na Bajeti ya Maendeleo kwa asilimia 30. Pamojana hivyo, sura ya uwiano wa Bajeti il iyotengwa kwavipengele hivyo vitatu kwa Mwaka 2017/2018 na Mwaka2018/2019 haitofautiani sana kama inavyoonekana katikaJedwali Na. 1 na Grafu Na. 1 pamoja na Grafu Na. 2.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua kuwamwenendo huu wa uwiano wa Bajeti utaendelezwa na hata

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

kuboreshwa zaidi. Ni imani ya Kamati kuwa hata baada yakuidhinisha Makadirio haya, upatikanaji wa fedha utakuwamzuri na unaozingatia namna Bunge linavyoidhinishaMakadirio haya ya Mapato na Matumizi.

SURA YA NNEMAONI NA USHAURI

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Dhamira yaWizara ya kusimamia na kutekeleza diplomasia ambayoitachangia katika shughuli za kiuchumi na kuwezeshamageuzi ya haraka na maendeleo endelevu ya Tanzania,Kamati inatoa maoni na ushauri ufuatao:-

i) Serikali ihakikishe fedha zote kiasi cha Shilingi9,329,800,000.00 ambazo zimetengwa kwa ajili ya kufunguaBalozi mpya huko Cuba na Konseli Kuu katika miji yaLubumbashi- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo naGuangzhou- China zinatolewa kwa wakati na kutumikakama ilivyokusudiwa. Kamati inaamini pesa hizo zikitolewakwa ukamilifu zitawezesha ufunguzi wa Ubalozi huo na Konselikuu hizo na hatimaye nchi yetu kunufaika na fursa za kiuchumina kibiashara. Aidha, Serikali iweke mikakati zaidi ya kufunguaBalozi au Balozi za Heshima katika nchi nyinginezinazoendelea kukua kwa kasi kiuchumi.

ii) Kwa kuwa kiwango cha fedha za bajetizinazotolewa kwa Wizara kimekuwa hakiendani na mtiririkowa Fedha uliopangwa jambo ambalo linasababisha Wizarana Balozi zake kutotekeleza ipasavyo majukumu yake yamsingi hususana Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizowa Diplomasia ya Uchumi, Serikali ihakikishe kuwa fedhazinazotengwa zinatolewa kwa kuzingatia mtirir ikouliopangwa.

iii) Kwa kuwa Kiwanja kilichotolewa na Serikaliya Oman kwa ajili ya kujenga Ubalozi wa Tanzania jijini Muscathakijaendelezwa tangu kilipowekewa jiwe la Msingi na RaisMstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya MrishoKikwete Mwaka 2012, na kwa kuwa upo uwezekano wa

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

Kiwanja hicho kutwaliwa na Serikali ya Nchi hiyo endapokitaendelea kukaa bila kuendelezwa, Serikali itoe Shilingi1,894,056,560.00 zilizokuwa zimetengwa katika Mwaka waFedha 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ubalozi kablaya Mwaka huu wa Fedha kuisha.

Sambamba na ushauri uliotolewa hapo juu, Serikaliitoe fedha za Maendeleo zilizotengwa katika Mwaka waFedha 2017/2018 kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya Ubaloziwetu wa Cairo, Ukarabati wa miundombinu ya Chuo chaDiplomasia, Dar es Salaam na Ujenzi wa Makazi ya Balozi,Addis Ababa.

iv) Pamoja na kwamba Serikali ilijiwekeaMkakati wa miaka kumi na tano (2001/2003-2016/2017) wakuendeleza viwanja, kukarabati na kununua majengo ya Ofisina Makazi ya Watumishi Balozini, Mkakati huohaujatekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha. Kamatiinaendelea kuishauri Serikali kutoa kipaumbele katikakuendeleza viwanja 12 ambavyo baadhi yake ni vya mudamrefu (Kama vile Viwanja vilivyopo Maputo, London, AdisAbaba, Nairob, Muscat) na kuboresha majengo ya Ofisi naMakazi ya Watumishi katika Balozi zetu ikibidi kwa kutumiamikopo ya muda mrefu lakini yenye riba nafuu.

Hii itasaidia Serikali kuokoa fedha nyingi za walipakodi zinazotumika kwa ajili ya kukodi majengo ya Ofisi naMakazi katika Balozi zetu nje ya Nchi ambapo kwa Mwakawa Fedha 2018/2019 Shilingi 21,667,174,191.00 zimetengwakwa ajili hiyo. Sambamba na hilo, hii itawezesha Serikalikujenga majengo ya kisasa ya Balozi zetu ambayoyakimalizika yataingiza fedha nyingi za kuendesha Balozi hizona kusitisha utaratibu wa kupanga Ofisi na nyumba zawatumishi.

Aidha, Kamati imebaini utaratibu huo ni wenye tijana mafanikio makubwa kama vile inavyoonekana katikaUbalozi wa Maputo – Msumbiji ambako kwa Mwaka ujaowa Fedha wa 2018/2019 hawatahitaji na hawakupangiwafedha za pango;

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

v) Kwa kuwa Wizara imekubaliana na ushauri waKamati wa kupanga Miradi michache itakayowezakutekelezwa kwa mwaka na hatimae kuweka Miradi mitatutu ya Maendeleo kwa Mwaka ujao wa Fedha 2018/2019,Serikali ihakikishe kuwa inaipatia fedha Miradi hiyo hususanule wa ujenzi wa Ofisi ya Ubalozi wa Muscat – Oman ambakoSerikali inaweza kukusanya fedha nyingi za maduhuli kwamiaka ijayo;

vi) Kamati inatambua nia njema ya Serikalikatika kuondoa suala la retention kwa Wizara zake zote. Hatahivyo, Kamati inaishauri Serikali kuweka utaratibu maalumutakaoruhusu Balozi zetu nje ya Nchi kubaki na angalauasilimia 40 ya makusanyo yao ili yawawezeshe katikakutekeleza majukumu yao hususan kukarabati majengoambayo mengi yao yamekaa muda mrefu bila kufanyiwaukarabati. Aidha, Serikali ione umuhimu wa kuweka utaratibumaalum wa kuziwesha baadhi ya Balozi kutuma fedha zamakusanyo moja kwa moja Serikalini badala ya kupitia katikaUbalozi mwingine ili kuepukana na changamoto ya exchangelosses ambayo inaathiri kiwango cha mapatoyanayokusanywa.

vii) Kwa kuwa baadhi ya Balozi zetuzinakabiliwa na changamoto ya kuwa na watumishiwachache kutokana na baadhi ya watumishi kustaafu nawengine kurejea nyumbani baada ya kumaliza muda wakufanya kazi Balozini, Serikali ione umuhimu wa kupelekawatumishi zaidi katika Balozi zenye uhitaji ili kuziwezeshakutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Aidha, kwa kuwabaadhi ya wataalam katika Balozi zetu hawana weledi waDiplomasia ya Uchumi, Serikali ihakikishe watumishiwanaopelekwa katika Ofisi zetu za Ubalozi wana utaalam,ujuzi na uzoefu “Professionals” kuhusu masuala yanayohusuDiplomasia ya Uchumi, i l i kuondoa changamoto zauwajibikaji na utekelezaji wa kazi za Kibalozi zilizojitokezahuko nyuma.

viii) Kwa kuwa ni dhahiri Utalii wa Mikutano namatukio (business tourism) ni muhimu katika kuchangia na

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

kukuza pato la Taifa kupitia Sekta ya Utalii, na kwa kuwaVituo vyetu Vya Mikutano ya Kimataifa hususan kituo chaArusha (AICC) havina Chombo Mahsusi (National ConventionBureau) cha kuitangaza Nchi na kuvutia Mikutano namaonesho ya Kitaifa kufanyika nchini, Serikali ione umuhimuwa kuanzisha Chombo hicho ili kuvutia Mikutano naMaonesho mengi ya Kimataifa kufanyika nchini na hatimayekuongeza Pato la Taifa.

ix) Sambamba na ushauri uliotolewa hapo juu,ili kuimarisha Sekta ya Utalii nchini na kukuza pato la Taifa,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikikwa kupitia Balozi zake, iendelee kushirikiana na Wizara yaMaliasili na Utalii kutangaza utalii nje ya nchi ili watalii wengizaidi watembelee Tanzania.

x) Kwa kuwa Serikali imekuwa na kasi ndogoya ubadilishaji wa Sheria za Nchi ili kuendana na matakwaya Itifaki ya Soko la pamoja la Afrika Mashariki, Serikali pamojana Idara na Taasisi zake iongeze kasi ya ubadilishaji wa Sheriaza Nchi zilizoainishwa ili ziendane na matakwa ya Itifaki yaSoko la Pamoja. Hii itawezesha Watanzania kunufaikaipasavyo na fursa za Soko la Pamoja la Afrika Mashariki naJumuiya nyingine za Kikanda.

xi) Kwa kuwa ni dhahiri kuwa kuna uelewamdogo miongoni mwa wananchi kuhusu masuala yaMtangamano na faida zake, Serikali iendelee kutoa elimukwa Umma kuhusu fursa zitokanazo na Jumuiya za Kikandana Kimataifa ambazo Tanzania ni Mwanachama.

xii) Kamati inaendelea kuishauri Serikalikuongeza kasi ya kuandaa Sera maalum kuhusumtangamano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Serikali kuwana mwongozo wa kisera inapotekeleza masuala mbalimbaliya kijumuiya. Ushauri huu umekuwa ukitolewa mara kwamara lakini haujazingatiwa kikamilifu.

xiii) Kwa mara nyingine tena, Kamati inaendeleakuisisitiza Serikali kukamilisha haraka upatikanaji wa Sera

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

Mpya ya Mambo ya Nje. Kamati imekuwa ikishauri mara kwamara kuhusu upatikanaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Njeitakayoendana na hali ya sasa ya Diplomasia ya Uchumi lakiniutekelezaji wake umeendelea kuchukua muda mrefu.

xiv) Serikali kwa kushirikiana na wadau wengineijenge Chuo kipya cha Diplomasia cha kisasa Jijini Dodomakitakachohamasisha nchi nyingine za Afrika na Duniani kwaujumla kuleta wanafunzi wao na hatimaye kuongeza patola Taifa kutokana na mapato yatokanayo na udahili wawanafunzi hao. Aidha, ili kuvutia wanafunzi wengi zaidi, Chuohiki kwa sasa kianze kufundisha lugha ya Kiswahili.

xv) Kamati inaendelea kuishauri Serikali kulipamichango yote ya Kimataifa na Mashirika yake ambayo nchiyetu inadaiwa hadi muda huu hususan ya “InternationalConference on the Great Lakes Region – ICGLR” ili kuendeleakujenga heshima ya muda mrefu ya nchi yetu mbele yaJumuiya ya Kimataifa. Ushauri huu umekuwa ukitolewa marakwa mara lakini haujazingatiwa kikamilifu;

xvi) Kamati inaendelea kuishauri Serikali kuonaumuhimu wa kuharakisha mchakato wa kupatikana kwajengo la kisasa la Kurugenzi ya Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar;

xvii) Kamati imebaini kuwa bado vitendo vyaunyanyasaji wa wafanyakazi wa majumbani kwa baadhi yanchi za nje vinaendelea, hivyo Serikali iweke utaratibuutakaohakikisha kuwa panakuwepo na usalama waWatanzania wanaofanya kazi mbalimbali nje ya nchi kablana baada ya kuondoka nchini Tanzania;

xviii) Serikali iweke utaratibu mahsusi wa kufuatiliautekelezaji wa mikataba yenye tija kwa Taifa ambayotumeingia na Serikali nyingine za Nchi za Nje. Hii itawezeshaTanzania kunufaika na faida zitokanazo na mikataba hiyoambayo baadhi yake imekuwa haitekelezwi kwa kasiinayostahili;

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

SURA YA TANOHITIMISHO

Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru kwa kunipanafasi ya kuwasilisha Taarifa hii. Napenda kuwashukuruWajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamaambao maoni, ushauri na ushirikiano wao umewezeshakukamilika kwa taarifa hii. Naomba niwatambue kwa majinakama ifuatavyo:-

1Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mb, Mwenyekiti2.Mhe. Salum Mwinyi Rehani, Mb, M/Mwenyekiti3.Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Mb4.Mhe. Mussa Hassan Mussa, Mb5.Mhe. Prosper J. Mbena, Mb6.Mhe. Victor Kilasile Mwambalasa, Mb7.Mhe. Fakharia Shomari Khamis, Mb8.Mhe. Cosato David Chumi, Mb9.Mhe. Bonnah Mosses Kaluwa, Mb10.Mhe. Masoud Abdallah Salim, Mb11.Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda, Mb12.Mhe. Gerson Hosea Lwenge, Mb13.Mhe. Shally Josepha Raymond, Mb14.Mhe. Dkt. Suleiman Ally Yussuf, Mb15.Mhe. Joram Ismael Hongoli, Mb16.Mhe. Zacharia Paulo Issaay, Mb17.Mhe. Joseph Michael Mkundi, Mb18.Mhe. Mboni Mohamed Mhita, Mb19.Mhe. Fatma Hassan Toufiq, Mb20.Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Mb21.Mhe. Silafu Jumbe Maufi, Mb22.Mhe. Ruth Hiyob Mollel, Mb23.Mhe. Janeth Maurice Masaburi, Mb24.Mhe. Augostino Manyanda Masele, Mb25.Mhe. Almasi Athuman Maige, Mb

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Wajumbe waKamati napenda kutumia fursa hii kumshukuru Waziri waMambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. BaloziDkt. Augustine Philip Mahiga, (Mb), Naibu Waziri, Mhe. Dkt.

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Susan Alphonce Kolimba (Mb), Katibu Mkuu Prof. Adolf F.Mkenda, Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan Muombwapamoja na Watendaji wote wa Wizara kwa ushirikiano namchango wao katika kipindi chote cha utekelezaji wamajukumu ya Kikanuni ya Kamati.

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini si kwa umuhimu,napenda kumshukuru Katibu wa Bunge Ndg. StephenKagaigai kwa kuratibu vema shughuli za Kamati na Bunge.Aidha, nawashukuru Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za BungeNdg. Athumani Hussein, Mkurugenzi Msaidizi Bi. AngelinaSanga na Makatibu wa Kamati hii Ndg. Ramadhan Abdallahna Bi. Grace Bidya wakisaidiwa na Bi. Rehema Kimbe, kwakuratibu vema shughuli za Kamati na kuhakikisha Taarifa hiiinakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasanaliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirioya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 kama yalivyowasilishwa na mtoa hoja.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naombakuwasilisha.

Mussa Azzan Zungu, MbMWENYEKITI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE,ULINZI NA USALAMA

23 Mei, 2018

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumemsikiaMheshimiwa Waziri, pia ushauri wa Kamati. Tutaendelea nautaratibu wetu; nimeletewa majina ya kuchangia hapa, lakinikabla sijaanza kuita wachangiaji, wako wageni ambaohawakutangazwa asubuhi, nitawatangaza sasa kablahatujaendelea.

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Nianze na Mheshimiwa Roberto Mengoni ambaye niBalozi wa Italia; tunaye pia Mheshimiwa Theresia Samariaambaye ni Balozi wa Namibia; vile vile yupo MheshimiwaMonica Patricio Clemente Mussa ambaye ni Balozi waMsumbiji; karibuni sana wageni wetu. (Makofi)

Tunao pia wanafunzi 49 wa Chuo cha Diplomasia,pengine wameshatoka lakini majina haya yamekujabaadaye. Karibuni sana wageni wetu Bungeni.

Waheshimiwa Wabunge, sasa tunaanza na ninayomajina hapa kwa mujibu wa uwiano wetu tulionao;tutaanza na Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, atafuatiwa naMheshimiwa Cosato David Chumi na Mheshimiwa MasoudAbdallah Salim ajiandae.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwanza naomba niwashukuru sana Wanambeyawenzangu kwa kusimama na mimi nilipofungwa kisiasakwenye Gereza Kuu la Luanda, Mbeya, pia nawapa pole kwawao kufungwa kisaikolojia. Nawashukuru pia Watanzaniawote ndani na nje ya Tanzania kwa kulaani kufungwakwangu kiholela. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sana Wabungewote hasa wa Upinzani, kwa support kubwa waliyotoa, lakinipia hata upande wa CCM, japo kuwa mliogopa kujakuniangalia lakini salamu zenu nilizipata; na source ya hofuyenu wote tunaelewa, lakini nimshukuru mzee, Profesa MarkMwandosya, aliwawakilisha upande wa CCM kwa kujakunitembelea jela. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba naminiwapongeze Mheshimiwa Stephen Masele na MheshimiwaMboni Mhita kwa nafasi walizochaguliwa kwenye Bungela Afrika. Bunge letu limejiunga kwenye Vyama vyaKibunge vya kimataifa kama CPA, PAP, ACPEU, IPU nakadhalika, lakini wote tunafahamu ni kwamba hatushirikivyema na tatizo sijajua ni nini. Hata hivyo, kama hatujuiumuhimu mbona tunafurahia matunda ya ushindi wa

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Mheshimiwa Masele na Mheshimiwa Mboni Mhita wakatiwote tunajua hata kwenda huko walijigharamia wenyewe?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye hoja, nanitaanza na masuala ya sera za mambo ya nje (foreign policy).Mheshimiwa Waziri wakati anaanza kuchangia alisisitiza sanakwamba mwelekeo wetu wa foreign policy hatutakubalikuingil iwa wala kuchaguliwa marafiki. Naombanimhakikishie na kumkumbusha Mheshimiwa Waziri, najuaana weledi katika nyanja za kimataifa, kwamba sisi kamaTanzania hatujawahi kuburuzwa wala kuchaguliwa marafikitangu enzi ya Mwalimu Nyerere na ndiyo maana tulikuwamember wa nchi zisizofungamana na upande wowote.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ile Non-AlignedOrganization (movement) sisi tulikuwa ni member muhimusana na tulitambulika kimataifa. Tanzania il ikuwainaheshimika kimataifa kwa mambo kadhaa. Kwanza namuhimu tulikuwa na sera ya kutetea wanaokandamizwaduniani; mfano South Africa, Mozambique, tuliwasaidiasana mpaka kufikia kujiondoa katika makucha ya apartheidna wale Mozambique kupata uhuru wao kutoka kwaWareno.

Mheshimiwa Naibu Spika, sera hizo hizo tulizokuwanazo dhidi ya South Afrika na Mozambique ndizo tulisimamiaSera yetu ya Mambo ya Nje kwa Palestina na Sahara yaMagharibi. Mwalimu Nyerere alifuta uhusiano wa kibalozi naIsrael kwa ku-support struggle ya Wapalestina kudai uhuru.Sasa tujiulize leo hii tunaenda kufungua Ubalozi Israel, je, ilecourse ya Mwalimu ku-support uhuru wa Palestina imefikiawapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababuukiangalia ni kwamba hali imezidi kuwa mbaya Wapalestinandani ya Gaza na maeneo mengine yanayokaliwa kimabavuwanazidi kuuawa kila siku kadri Israel inavyoongeza uwezowake wa kijeshi.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Naibu Spika, halikadhalika MwalimuNyerere na sisi kama Taifa tulifuta uhusiano na Morocco kwaku-support kudai haki kwa Sahara ya Magharibi chini yaPOLISARIO. Sasa leo tumeacha sera zetu dhidi ya Moroccokwa ahadi ya kujengewa uwanja wa mpira stadium,tunajivunjia heshima kwa ahadi ya kujengewa uwanja wampira ambao Mheshimiwa Mkapa amejenga pale Dar esSalam uwanja wa mpira kwa support ya Wachina bila kuuzanchi wala bila kukiuka misimamo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina uhakika MheshimiwaWaziri na Bunge hili Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa hukoalikolala kaburini Mwitongo anageuka geuka kwa jinsi Taifahili linavyokwenda sasa hivi katika sera ya mambo ya nchiza nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, diaspora; naomba sanaMheshimiwa Waziri tuache siasa kwenye maisha yaWatanzania wenzetu. Ni lini Serikali itatambua Watanzaniawanaoishi nje ya nchi (diaspora)? tuache kutoa ahadi kilatena nasikia mwakilishi yuko hapa, I hope amekuja ile straighthakuja kisiasa kwa sababu wenzake anaowawakilishawanalia sana kule, sisi tumekaa kule, tuna mawasiliano kule,tunajua kilio chao, hata hapa kwenye simu nina mawasilianoya kutoka diaspora baada ya wao kujua kwamba leokinaenda kuzungumzwa nini, wametoa nao changamotozao wanataka tuzizungumze humu.

Mheshimiwa Naibu Spika, wanachotaka watu wadiaspora ni kuruhusiwa uraia pacha, kama ambavyo uraiapacha uko katika nchi nyingine. Wapewe uraia pacha iliwaweze kushiriki kujenga uchumi na si tu makongamanomara kuwaalika Zanzibar, mara kuwaalika wapi. Wakatiumefika turuhusu sasa uraia pacha ili watu hawawaweze kushiriki katika uchumi wa nchi. Hawa watu wadiaspora sasa wanaanzisha kitu kinachoitwa TanzaniaGlobal Diaspora Council (TGDC). Sasa tusije sisi namawazo yetu tunataka kuwasaidia vipi sijui kuwashirikishavipi, wale wana exposure wamefunguka, wanajuawanachokitaka.

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa itakiwa tutambue naSerikali iniambie imejipangaje kufanya kazi hiki chombo chadiaspora cha Tanzania Global Diaspora Council ambachokinaenda kuanzishwa na hawa Watanzania wenzetu katikakusaidia kuji-integrate kwenye masuala ya nchi yao ambayowanaipenda. Kwa sababu, otherwise mtu kama ameshapatauraia wa wapi anaweza akaamua kuendelea na maisha nakusaidia kuleta maendeleo kwenye yale maeneo wakatitungewapa fursa wangeweza kafanya hivyo katika nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuna ajenda ya pamojakwa diaspora. Mheshimiwa Mzee Kikwete alipokuwaanaenda nje aliwashawishi experts wa Tanzania huko njewarudi kujenga nchi yao; lakini utawala huu uliofuataukawageuka na kuanza kuwanyanyasa mfano ni yule mamaJulieth Kairuki wa TIC. Mheshimiwa Dkt. Kikwete alikwendakumshawishi South Afrika ameacha kazi yake nzuri, ameachakila kitu kilicho kizuri kinachoendana na weledi wake amekujanyumbani kusaidia kujenga nchi, lakini leo unamwambiakwamba hatuwezi kukulipa huo mshahara mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi alikuja kwamakubaliano gani kutoka South Afrika anakuja hapatunakuja tunawageuka? Wengine waliambiwa warudikujenga nyumbani na kuwekeza wakaanza kurudi kwa wingiwakajenga majumba, wakafungua biashara. Leo hii Waziriwa Ardhi hawa si raia halali, kwa hiyo mali zao zitataifishwatunawatia woga Watanzania wezetu hawa wakatiwalikuwa wangeweza kushiriki vizuri sana katika masualayetu ya uchumi na kujenga nchi.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbilinyi kengele ya kwanzaimegonga, lakini kuna taarifa kule nyuma, naomba ukaeMheshimiwa upokee taarifa.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: (Aliongea bila kutumiakipaza sauti)

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbilinyi naomba ukae kunataarifa.

(Hapa Mheshimiwa Joseph Mbilinyi aliendelea kuongeabila utaratibu)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbilinyi kama ni hayoyaliyokuleta humu ndani unajua kitakachokupata,Mheshimiwa Mollel kule nyuma.

MHE. DKT. GODWIN O MOLLEL: Mheshimiwa NaibuSpika, nataka nimpe rafiki yangu taarifa kwamba kwa sisikufungua Ubalozi Israel hatujapingana na Mheshimiwa Raisaliyekuwa Baba yetu wa Taifa; kwa sababu moja; ni kwambakama ni watu wa kwanza kupingana na Mheshimiwa Rais niwao kwa sababu tuliwaona sehemu wakifanya kikao nawale watu ambao Rais alienda kuwashtaki Umoja waMataifa lakini wao sasa ndio watetezi wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tunajua kwambawamezunguka sehemu nyingi dunia kuhakikisha kwambataifa hili linasusiwa na mataifa. Jinsi Rais Dkt. Magufuli alivyomzuri wao wakizunguka kwa viranja, Rais ameenda kwaMwalimu Mkuu amefungua na nyumba ya kuishi kule, kwahiyo wamechanganyikiwa hawawezi kutimiza azma yao,kwa hiyo tunacho…

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, MheshimiwaMbilinyi unaipokea taarifa hiyo?

MHE. JOSEPH. O MBILINYI: Mheshimiwa Naibu Spika,siipokei taarifa ya Dkt. Shika. Nimpe tu utaalam mdogo;tulikuwa na Ubalozi wetu Egypt ambao ulikuwa ni ubalozineutral...

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa kuangaliamuda tuliobaki nao sitaruhusu taarifa tena sasa hivi,Mheshimiwa Mbilinyi.

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

MHE. JOSEPH. O MBILINYI: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa hiyo ilifaa kabisa kubakisha ubalozi wetu pale Cairo,Egypt, kwa sababu ule ubalozi ulikuwa neutral na ulikuwaunaweza ku-harmonize pande zote yaani Palestina na Israelmpaka mambo yao yatakapokaa sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais ni topdiplomat wa nchi, suala la kusafiri bado ni muhimu, labdakama ana tatizo la kiafya. Tena anapokwenda nje anawezakutumia lugha ya Kiswahili kwa sababu Rais wa Xi Jinpingwa China kila anakokwenda anaongea Kichina japokuwani msomi aliyesomea Marekani. Yeye amesomea chuo kikuuna elimu zake za juu Marekani anazungumza Kiingereza vizuri,lakini kila anapokwenda anazungumza lugha ya Kichina; kwahiyo tena tutakuwa tunaitangaza na lugha yetu ya Kiswahili.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na kama tatizo ni gharamambona anatuma delegations? Mara Makamu wa Rais, maraWaziri Mkuu nao wanatumia gharama kwa sababuhawaendi kule kwa miguu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hatuendi UN, hatuendiDavos, hatuendi Common Wealth. Common Wealth niMkutano wa Wakuu wa Nchi (Head of States), lakini sisitunatuma wawakilishi wakati kule kuna fursa za kiuchumina biashara. Rais Uhuru Kenyatta ametumia vizuri sanafursa za kiuchumi na kibiashara kwa nchi alipokwendaCommon Wealth, hali kadhalika Rais Ramaphosa waSouth Afrika pia alitumia huo kukutana na investors wakutosha aka-archive miradi ya takribani Rand trilioni 1.2kwa ajili ya nchi yake; ndizo faida ya majukwaa haya.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo Rais kusafirihaiepukiki, ni muhimu na kama alivyonukuliwa mzee KikweteRais aliyepita kwamba kusafiri kulimsaidia sana, mkaa buresi sawasawa na mtembea bure; hii alisema wazi. Kwa hiyokusafiri ni muhimu sana, kwa sababu Mabalozitunaowachagua huko hawatusaidii kwa sababu

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

tunachagua Mabalozi wetu kisiasa bila kuangalia weledi.Aidha, tunawapa ubalozi watu kama zawadi au kuwa-control.

Mheshimiwa Naibu Spika, Dkt. Slaa tumempa zawadikwa kazi aliyoifanya 2015 katika uchaguzi, tumempa ubalozi,lakini Dkt. Emmanuel Nchimbi tumempa ubalozi Brazil kum-control ili awe mbali kudhibiti ushawishi wake ndani yaChama cha Mapinduzi. Haya ni mambo ambayo yako wazina yanaeleweka kabisa. Sasa hawa ni shida sana kusimamiadiplomasia ya uchumi, watakuwa wanaleta siasa pekeyakena iko hivi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Sekunde 30 maliza muda wako kengeleimeshagonga.

MHE. JOSEPH. O MBILINYI: Mheshimiwa Naibu Spika,nilisimamishwa kidogo. Diplomasia ya uchumi bila stabilityni shida. Tunawatisha wawekezaji, tunapiga risasi Wabunge,tunafunga ovyo Wabunge. Wawekezaji wa nje walifuatiliahaya mambo. Wakifuatilia haya mambo inakuwa wanasitasasa kuja kuwekeza kwa sababu hakuna mwekezajianayetaka kuweka kwenye nchi ambayo haiko stable, hainaamani na usalama. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

Waheshimiwa Wabunge nilimtaja MheshimiwaCosato David Chumi atafuatiwa na Mheshimiwa MasuodAbdalla Salim, Mheshimiwa Fakharia Shomar ajiandae.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa na mimi kuchangia Wizara hii na kwaharaka kabisa napenda kuipongeza Wizara kuanziaMheshimiwa Waziri, Naibu, Makatibu Wakuu pamoja naMabalozi ambao ni Wakurugenzi wanaoongoza idarambalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi hizi haziwezikwenda tu hivi hivi zitaendana na ukurasa wa 25 ambaounaelezea misamaha ya madeni ya nje. Hii yote nijitihada za kazi nzuri ambao Wizara pamoja na Wakurugenzina Mabalozi kote waliko wanaifanya na ndiyo maanatumeweza kusamehewa baadhi ya madeni katika Taifa letu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia na mimi nichukuenafasi hii kuwapongeza wenzangu Mheshimiwa Masele naMheshimiwa Mboni Mhita kwa nafasi walizochaguliwa. Hiiinaendelea kuthibitisha kwamba Taifa bado linaendelea ku-maintain heshima yake katika nyanja za kidiplomasia Afrikana dunia kwa ujumla. Kwa hiyo tuendelee kusonga mbelena kuchapa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwa sababu si habaniseme kidogo, sina nia ya kumjibu ndugu yangu MheshimiwaMbilinyi lakini niseme tu kwamba, katika nyanja zakidiplomasia nchi kama Algeria nitawapa mfano ndiyesupporter mkubwa wa POLISARIO Chama cha Ukombozi waSahara. Hata hivyo, Algeria hii ambao POLISALIO Makao yakeMakuu yako Algeria ina mahusiano (bilateral) na Morocco.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kum-support mtufulani haikuzuii wewe kufanya mahusiano na yule mtumwingine as far as you have interest in that particularmahusiano. Kwa hiyo si jambo geni, hata South Afrika nisupporter mkubwa wa POLISARIO, ndio wanao financePOLISARIO, lakini wana mahusiano bilateraly na Morocco.Kwa hiyo, unaangalia wewe una interest gani namisimamo yako inabaki vile vile; niliona ni muhimu kulisemahilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo nipendepia kupongeza kwa kufunguliwa hizi balozi zetu nyingine,sita na Mheshimiwa Waziri amesema mabalozi wameshakwenda. Pia kama ambavyo Kamati ilikuwa imeshauri kuwa

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

na umuhimu wa kufungua zile tunaita General Consulatekatika Miji ya Lubumbashi na Guangzhou. Nimeonakwamba Serikali imezingatia ushauri wa Kamati naWabunge kwa ujumla na kwamba sasa tunakwendakufungua General Consulate katika hiyo miji ambayo ikostrategically kibiashara kwa Taifa letu, kama hiyo Lubumbashina Guangzhou.

Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni mambo ambayoya kupongeza na yanaonesha kwamba Serikali inachukuamawazo yetu Wabunge na kuyafanyia kazi. Kwa hiyo niwasihitu kama Serikali twende kwa haraka katika kulitekeleza kwavitendo jambo hili ambalo mmelichukua kutokana na ushauriwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nizungumzie;Mheshimiwa Waziri amekuwa kwenye nyanja hii yadiplomasia, atakuwa anafahamu kwamba sasa hivi kunareform inaendelea UN Security Council, kwamba na sisi kamaAfrika tungependa tupate nafasi katika sehemu ile ya zilekura tano za veto.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama Taifa nimwombeMheshimiwa Waziri tujipange vizuri na hatua mojawapo yakujipanga ni pamoja na kuhakikisha kwamba tunapelekamaafisa katika vituo vyetu vya ubalozi. Tukiwa na maafisawa kutosha maana yake ni kwamba ushiriki wetu utakuwani madhubuti. Kuna vituo ambavyo ni multilateral stations,Mheshimiwa Waziri anafahamu, kama New York, anafahamupale kuna Kamati sita ambazo kila Kamati inapaswa iwe naafisa kwa ajili ya kutetea maslahi mbalimbali ya Taifa letu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mfano wa Kamatiya tano, Mheshimiwa Waziri anafahamu kabisa kwambabaada ya kufunga ICTR tuko kwenye transition kupitia ileMechanism For International Criminal Tribunala. Katika bajetiya 2018/2019 mapendekezo yalikuwa kwamba tupatenadhani dola milioni mia mbili kumi na tano. Hata hivyo,

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

kutokana na kukosa ushawishi wa kutosha, Wazirianafahamu mataifa makubwa yamepunguza tumepatadola milioni 88.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jitihada za baadhi yamataifa kuhakikisha kwamba hata ikiwezekana ile iliyokuwaICTR ifungwe ihamie The Hague. Sasa jambo hili likifanyika nihasara kwa Taifa letu kwa sababu, imagine kamamahakama ile inapangiwa dola milioni 215 maana yake nikwamba hata kiuchumi zitaongoza mzunguko katika Taifaletu, siyo tu pale Arusha. (Makofi)

Mheshimiwa Nanibu Spika, pia jitihada hizi inabiditujipange kikamilifu kuweka kukabiliana nazo; kwa nini; kwasababu wa uwepo wa ICTR pale Arusha ni legacy kubwakwa Taifa letu katika dunia. Sasa jitihada hizi kamahatutahakikisha tunapeleka watumishi wa kutosha katikabalozi zetu, maana yake ni kwamba hata ushiriki wetu katikavyombo mbalimbali especial hizi Kamati utakuwa niminimum. Kwa hiyo nimuombe Mheshimiwa Waziri tu speedup hii process ya kupeleka maafisa kwani umuhimu wakeuko wazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kama vile haitoshi, kwanini mimi nasema nasema masuala haya, watu wengitunapozungumza masuala ya peace keepingwanazungumzia chapter six na chapter seven; lakiniukweli UN imeendelea kupunguza fedha za kulindaamani katika maeneo ya migogoro Afrika. Hii ni kwa sababuama tunapunguziwa ushawishi kutoka labda naunderstaffing.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimwmbe MheshimiwaWaziri kwa sababu yeye ni nguli katika nyanja hii, katika hiireform inayoendelea ya UN Security Council hebu sisi kamawatu ambao tunaaminika kiplomasia na kimataifa, kwambatuna ushawishi mkubwa Kusini mwa Afrika, tuna ushawishimkubwa katika bara la Afrika, tuna ushawishi mpaka katikaSouth East Asia, hebu tu-play role yetu ili kusudi ushawishikama Taifa katika Umoja wa Mataifa uendelee kuwa

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

mkubwa ili kusudi hata yanapokuja masuala ya bajeti kwamfano za peace keeping tuweze kushawishi pesa itengweya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu madhara yakeni nini, tumeona tumepoteza wanajeshi pale Congo.Ingekuwa UN inapeleka bajeti ya kutosha ya peacekeeping; maana tumeambiwa mapigano yalidumu masaa14, maana kama vingekuwa vifaa vya kisasa, tuna ndegeza rescure maana yake tungeweza kuokoa wanajeshiwetu wale. Haya yote hayafanyiki kwa sababu ndani yamfumo wa UN wakubwa wa dunia wanajitahidikuhakikisha ile keki inapelekwa katika mambo ambayowao wanaona yatakuwa yanawasaidia lakini sisihayatusaidii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niishauri Serikalikwamba tuendelee kuthibitisha kwa vitendo kwambasisi ni taifa kubwa katika ushawishi wa diplomasiakimataifa Afrika na duniani kwa ujumla; na ushiriki huuutathibishwa kwa sisi kuendelea kuwa na staff wa kutosha.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia sitakuwanimetenda haki kama sitawashukuru Wizara katika ujumlawake. Nimeona hapa wametuletea kijitabu kinasema findabout us; ndani yake kina anuani za Balozi zetu. Maana yakeni kwamba sisi hapa ama tuna ndugu zetu ama tuna watuwanaenda katika matibabu au watu wanaenda kutafutafursa za kibiashara au kuna wanafunzi. Sasa kijitabu hikikitarahisisha yale mawasiliano ya kidiplomasia kujua nchi ganibalozi ni nani na anuani yake ni ipi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama haitoshi wametupapia kijitabu ambacho kinaonesha anuani za Balozi za njeambazo ziko hapa nchini. Vile vile wametupa kijitabu hikikinachoonesha diplomasia ya Tanzania ambapo ndani yakewametuonesha picha, wameandika na caption yautekelezaji mbalimbali wa Diplomasia Tanzania kuelekeauchumi wa viwanda.

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli niwashukuru sanana naamini Mheshimiwa Masoud, Mzee wangu wa Matambilepale atakuwa leo amefurahi na atacheka mpaka jino lamwisho kwa sababu ni kitu ambacho tumekuwa piatukizungumza katika Kamati na Serikali imeweza kuthibitisha.Niongeze tu wakati ujao wanaweza kutuboreshea pia kwakutuletea kijitabu ambacho kinaeleza kila nchi ina fursa ganina watu wanaweza kuzipata fursa zile kwa namna gani.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maneno haya,napende kushukuru na naunga mkono hoja. Mungu ibarikiTanzania, Mungu ibariki Afrika. Ahsante sana (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Masoud kwamaneno hayo bado unachangia? Nilifikiri umeahirisha!Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim atafuatiwa naMheshimiwa Fakharia Shomari Khamis na Mheshimiwa ZittoZuberi Kabwe ajiandae kwa dakika tano.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi MunguSubhanahu Wataala aliyetujalia uzima na afya njema katikamwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, tuwatakie sotetunaofunga Mwenyezi Mungu a-taqabbal funga zetu, atulipeujira mwema, na Insha Allah bi-idhinillah malipo ya kheri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwombe MhehimiwaWaziri muhusika, tatizo la mahujaji waliosota, waliokaa mudamrefu wakati wanakwenda Hija mwaka uliopita tatizo hililisirejee tena. Ilikuwa ni aibu kubwa, tatizo kubwa, lililetataswira mbaya miongoni mwa watu mbalimbali. Wizarahusika ni Wizara hii hii. Kwa watu wote wanaoshughulika nakwenda nje kwa vyovyote iwavyo bado Wizara ya Mamboya Nje inahusika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu wazi wazi;tumekuwa tukipiga kelele kwamba wameiandikia BAKWATAtena kuwapa Mamlaka na madaraka ya kuwapeleka watuMahujaji hawa kwenda kuhijji, tafadhali sana BAKWATA kama

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Taasisi nyingine kwa hiyo msiwape mamlaka, yakitokeamambo mengine hasa tutasema kwamba BAKWATA nisehemu ya Serikali na ndivyo inavyonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunachosema nikwamba waacheni taasisi nyingine za kidini ziandaeutaratibu wake wa kupeleka mahujaji Makka, ndiyonikasema sasa ni vyema tujitathmini na hili. Upungufu huuwa kupeleka Mahujaji Makka dosari hii isitokee tena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, APRM (African Pear ReviewMechanism), mpango wa kujitathmini wenyewe kiutawalabora, kisiasa, kiuchumi na mambo mengine. Nashukurukwamba wameongeza fedha. Hata hivyo, natakaMheshimiwa Waziri aniambie kisiasa wamejitathmini kiasigani kwa wakati huu pale ambapo mwendelezo auwanakaa mahabusu muda mrefu Mahakamani, unaambiwaupelelezi haujakamilika. Masheikh wa Uamsho wamekaamuda mrefu, juzi tu Mheshimiwa Waziri alisema kwambaushahidi umepatikana, wanasubiri e-mail kutoka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi watu wanakaamahabusu miaka minne, miaka mitano hili hawalioni,wanataka tafsiri nyingine zije tafsiri za aina gani? Masheikhwa Uamisho wamekaa muda mrefu sana. Kwa hiyowanajitathmini kiasi gani? Amesema Mheshimiwa Bwegempaka akatoka machozi. Watu wamepigwa risasi Msikitinikule Chumo, damu imemwagwa msikitini Chumo. Tafadhalisana, hakuna kitu kibaya katika mambo haya ya hisia zadini. Waliopigwa risasi kule Chumo msikitini liwe jambo lamwisho tafadhalini sana. Mheshimiwa Mahiga anifahamu nawalionifahamu wanifahamu, wale Taasisi za Serikali za kiulinziwanifahamu, risasi msikitini isilie tena maisha, tafadhalini sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina suala lingine ambaloni juu ya mahusiano yetu ya mambo ya nje na Mataifambalimbali uko vizuri. Nafahamu uhusiano mzuri tulionaosisi na Msumbiji, nafahamu jinsi Tanzania ilivyoshiriki katikaukombozi ule wa Msumbiji, nafahamu mambo mengi mazuri

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

yetu sisi na Msumbiji na mimi naunga mkono. KunaWatanzania ambao wako gerezani kule Msumbiji katikaGereza la Beyo kule eneo la Pemba ambao wako gerezanihasa kwa muda wa miezi sita. Hawa ni wapiga kura na kwamahusiano mazuri sisi na Msumbiji na nadhani nampongezasana Balozi wetu Monica hapa leo yupo hongera, sananampongeza sana Balozi Monica. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu hawa naomba sananiwataje kwa majina wapo Beyo hapo Msumbiji kwenyeGereza hilo. Kwanza kutoka Jimbo la Kiwani na MtambileJimboni kwangu na hawa wamefanya makosa madogomadogo tu, hawana yale makosa makubwa ukasemamakosa yale labda ya madawa ya kulevya; nao ni

Shahali Makame Omary wa Chole-Kiwani; FadhiliKhamisi Makame, Chole-Kiwani; Khamisi Fadhili Khamisi,Chole-Kiwani; Mussa Rare Mussa, Chole-Kiwani; Ally ZidiniNgali, Chole-Kiwani; Zahoro Ngwali Ally, Chole-Kiwani;Zaharani Fadhili Khamisi, Chole-Kiwani; Silima Yakoub Ally,Chole-Kiwani; Ally Shahali Makame, Chole-Kiwani; MbaroukHijja Silima, Chole-Kiwani; na Juma Tabu Mussa, Chole-Kiwani.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Jimbo la Ziwanikuna Abdallah Khalfani, wa Wesha; na Hamza Fikira Sharif,wa Wesha. Kuna Jimbo la Mkoani nako kuna MakameBurhani Kombo, wa Chokocho; na Faki Shahali, waChokocho. Donge-Unguja yuko Mselem Khalfani Mohamedna Chumu Mshenga, hawa wako kwenye gereza la Beyohuko Pemba-Msumbiji. Tafadhali sana, kwa ujirani tulionaona ubora wa Balozi wetu Monica ninavyomwona yuko vizurisana, hongera sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hili jambowalichukue, utaratibu wa nchi nyingine wanakuwawanafahamiana, utaratibu wa kuwarudisha mahabusu auwafungwa kutoka nchi hizo sembuse hapo jirani tu. Naombenisana hawa watu waandae mazingira mazuri wawezekuwarejesha. Nina imani kwa ujumbe huo Mheshimiwa

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

ataweza kufanya jambo lolote la msingi la kuweza kufanyashughuli zinazohitajika.

Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye jambolingine la tatu ambalo ni miradi ya maendeleo. Mara nyingitunasema kwamba baadhi ya miradi ya maendeleo inatakaitekelezwe kwa wakati wake. Kuna miradi inayopaswakutekelezwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba yaaniZanzibar. Mpiga duru yupo katika mikakati, naomba sanaMheshimiwa Waziri aliangalie suala la mpiga duru.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni miaka kadhaawamekuwa wakisema kwamba wana mpango mkakati wakuboresha uwanja wa ndege Pemba, lakini kila marawanataja, wanataja katika mipango yao hii ya kiujumlakatika bajeti hii ya Afrika mashariki. Ni kwa nini na ni sababuzipi za msingi zilizopelekea uwanja wa Ndege, Pembahaupewi kipaumbele ukapewa nafasi yake ili ile dhana yauchumi unaohitajika ukaendelea, tatizo ni nini? Pemba ipoTanzania nataka wafahamu haiko sehemu nyingine yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bandari ya Mkoani walisemamuda mrefu kwamba nayo wataiboresha, watakwendavizuri lakini hadi leo inaonekana bado ni danganya toto.Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa aniambiehabari ya mpiga duru, aniambie habari ya uwanja wa Ndegewa Pemba, anipe habari rasmi ya Bandari ya Mkoani naBandari ya Wete. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, atumishi ambao wakokatika Balozi inafika wakati Maafisa huwa hawapeleki kwawakati na ile dhana ya diplomasia ya kiuchumi inakuwainasuasua. Naomba waniambie sasa kwamba kwa niniwanakuwa na kigugumizi cha kupeleka Maafisa kwenyeBalozi kwa haraka haraka pale ambapo wenginewameshamaliza muda wao. Anipe habari, nataka kujua kuleAnkara, Uturuki, anipe habari ya Korea, Doha-Qatar, Brusselsambapo kuna vikao vingi ya European Union nako sasahawapo au ni kidogo sana. Addis Ababa napo ni tatizo,New York nako vilevile.

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hili tatizo ni liniwataweza kulisawazisha kwamba tunasema tuna economicdiplomacy (diplomasia ya kiuchumi) lakini Maafisa wale waUbalozi ambao wanahitajika kwenda kule hawako, sasa hilinalo ni tatizo. Sasa Mheshimiwa Waziri aniambie jambo hilini lini litakaa vizuri.

Mheshimiwa naibu Spika, la mwisho, tuepukane naaibu kubwa ambayo tunaipata kwenye vile viwanjaambavyo haviendelezwi. Majengo ambayo wanatakakuyakarabati hapa yapo, lakini kila wakati tunaweka bajetitu lakini fedha zile hazipelekwi. Kwa hiyo atuambie sasamkakati wa kuepukana na aibu ni upi. Leo tunaambiwakwamba Tanzaia itashtakiwa katika nchi husika kwambamajengo yale ni machakavu, mabovu na viwanjahaviendelezwi. Nimwambie Mheshimiwa Waziri, hii ni aibukwa Taifa kama letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema sasa tujifunze,tuepukane na aibu kwa nchi za nje, tunajitia aibu sisiwenyewe kwa sababu hatupeleki zile fedha. Kama ingekuwatunaona kwamba kuepuka aibu Mataifa ya wenzetuwasiweze kututafsiri vinginevyo, basi majengo hayotungeyakarabati, tungepeleka fedha na vile viwanjaambavyo vilitaka kuchukuliwa ambavyo vimekuwa ni porina tunataka kushtakiwa ile aibu sisi tungekuwa hatunayo.Naomba sana Mheshimiwa Waziri, kwa sababu Serikali nimoja waandae mazingira kuona kwamba majengo yetuyanakarabatiwa, fedha zinapelekwa na vile viwanjaambavyo vinatia aibu, aibu hiyo inaondoka.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie la mwisho, ni hatiza utambulisho (Present Credential), wamepanga marakadhaa Mheshimiwa Naibu Waziri, hizi hati za utambulishokatika maeneo ambayo tumepanga basi tufanye kweli.Ukiangalia…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Namalizia sekunde30.

NAIBU SPIKA: Ameshasikia hati za utambulisho,ahsante sana Mheshimiwa. Mheshimiwa Fakharia ShomariKhamis atafuatiwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe dakikatano na Mheshimiwa Machano Othman Said dakika tano.

MHE. FAKHARIA SHOMARI KHAMIS: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Kwanza, sina budi kuipongeza Wizara kwahatua nzuri wanayofikia katika majukumu yao Waziri, NaibuWaziri, Katibu Mkuu na Kurugenzi yake yote kwa utendajiwao mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pil i, sina budikumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa kuwasamehe wafungwa na kuwa huru kwa mujibu waKatiba na ndani yake ndiyo Mheshimiwa Mbilinyi na yeyekapata msamaha leo tunaye hapa Bungeni na tunawezakuwa naye na kuchangia naye katika Bunge letu hili Tukufu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nazungumzia diplomasiaya uchumi; diplomasia ya uchumi inasaidia kwa Wizara nanchi nzima kuweza kujua jinsi Mabalozi wetuwanavyokwenda nje nini majukumu yao ya kufanya. Hatahivyo, ilivyo Wizara bado haijajipanga kuweza kupatikanasera mpya yao ya Wizara ikaungana na hii ya diplomasia yauchumi ikaenda pamoja, vikawa vitu viwili sambambatukaweza kufanikiwa katika majukumu ya utendaji wetu wakazi na Wizara mpaka leo sijui inasubiri nini na kushindwakutoa sera mpya ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje.Mheshimiwa Waziri naomba atakapokuja atuambiewanakwama nini hata wanashindwa kutoa sera mpyaitakayoendana na sera ya uchumi ya diplomasia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sera hiyo ya diplomasia yauchumi itasaidia kutupatia masoko, kutuletea watalii tenasiyo wale wa makundi tunataka waliokuwa na hadhi za juu,itaweza kutuletea wawekezaji maana tuna sera ya viwanda,

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

tunataka kuanzisha viwanda Tanzania ili tuweze kutanuauchumi wa Watanzania. Zanzibar kuna fukwe nzuri za watalii,Bara kuna Kilimanjaro nzuri kwa watalii, tuna mbuga zawanyama, kuna bahari au bustani ndani ya bahari ambavyohivyo vyote ni vivutio kwa utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwa MheshimiwaWaziri, kama inavyozungumzwa, anavyopeleka watendajikatika Balozi zetu, apeleke watendaji ambao wanaendanana diplomasia ya uchumi ili waweze kutusaidia katikamajukumu yetu tunayotaka kuyaanzisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukija kwa upande waZanzibar, Zanzibar tunataka au tungependa tuwe na jengoletu kama Ofisi ya Wizara ya Muungano, kama walivyoMambo ya Ndani, kama walivyo Wizara nyingi za Muunganozina Ofisi zao wenyewe wamejenga. Sasa tunashangaaMambo ya Nje mpaka leo kuanzia 1964 hadi leo hamnajengo, wana jengo lile ambapo wanasema wapo kwenyemazungumzo na mazungumzo hayo haijulikani yatamalizikalini.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawaomba viwanjaZanzibar kwa kujenga Ofisi vipo. Waache mazungumzo,waombe viwanja waweze kujenga lakini wakisubiriwanazungumza hii kama inabidi wanavuta muda na wakati,wakati muda wa kujenga hawajakuwa nao na walahawajakuwa na tamaa ya kujenga. Mheshimiwa Wazirinaona Kamati imemwambia kwamba tunataka Kurugenziza Zanzibar na wao wafanye kazi katika jengo linaloridhishana linaloitwa kwamba ni jengo la Ofisi siyo nyumbaimegeuzwa jengo wanasema ni Ofisi, hiyo haitowezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, makazi ya Ofisi za Ubaloziwetu wa nje pamoja na Ofisi zao hayaridhishi na kwa ninihayaridhishi? Kwa sababu kuanzia sasa pesa nyingitunapoteza kulipa katika majengo. Ikifika mwaka lazimatutenge bajeti ili tulipe pesa za Ofisi. Kwa mwaka huu tayariWizara imeshatenga bilioni 21.6. Pesa hizi ni za kodi zawalalahoi tunazokwenda kulipa, kwa nini tunashindwa

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

kujenga? Tungejenga ili kunusuru pesa za walipa kodi wetutena maskini wa Tanzania walalahoi.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri, hili wazidi kuliangalia maana hizi pesa zitatoka nyingina pesa hizi kama wangekuwa wanatoa kidogo kidogohuku wanaanza kujenga Ofisi zetu za Ubalozi tungekuwatayari tuko mbali na tungeweza kupata mafanikio.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine, Ubalozi waOman umetoa kiwanja Muscat. Tayari Mheshimiwa RaisMstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amekwenda kuweka jiwe lamsingi. Hata hivyo, toka mwaka 2012 hadi hii leo hakunakinachoendelea na wako tayari wenyewe kuchukua sehemuyao kwa sababu wameshatuona hatuna maendeleo yakuyafanya. Ingawa aliomba 1.8 billion lakini mpaka leohajapewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naiomba Wizara yaFedha wangefanya kila mbinu, hizi pesa zikatoka angalautukaonekana na sisi tunajihangaisha kuleta maendeleo. Ikiwawatu wamesema ukibebwa na wewe jikaze, wametupakiwanja, wako tayari kutusaidia ina maana sisi kujiendelezatunashindwa? Mheshimiwa Waziri akishirikiana na Wizara yaFedha, naomba hili waliangalie na liweze kufanikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, unyanyasaji wa wafanyakaziwa majumbani nje. Unyanyasaji huu umekuwa mkubwa navijana wetu wengi wanaondoka kinyemela, Wizara au Serikaliinakuwa haijuii, Balozi kule za nje hawajui kama vijana wetuwapo. Sasa hili walitilie mkazo na waweze kujua mbinuwanazopita na waweze kujua Ma-agent wanaosimamia ilihili jukumu liweze kumalizika.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtoto yeyote anauma,lakini akiwa wa mwenziwe, mtu anajifanya punguanianamwuona haumi, lakini mtoto anauma na hasa akiwakatika nchi yako akaondoka, akaenda nchi nyingine na nchiyenyewe ina ubalozi na akafika akateseka bila Wizara kujuaau ubalozi kujua na hiyo yote inaelekea kwamba

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

wanaondoka hawajui, watafute mbinu wanapita vipi,inakuwaje mpaka wanafika waweze kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba bado Wizara yaFedha kwa bajeti hii ingawa safari hii imepanda kidogo kwa17 percent basi waweze kusimamia hii bajeti itoke kwaniikitoka ndiyo manufaa kwa Tanzania. TunamwonaMheshimwia Waziri anavyohangaika, anavyokwenda safarizote ndani na nje ili kuisaidia Tanzania na hali tunaionaTanzania tunavyopiga hatua. Naomba Mheshimiwa Wazirihizi pesa zitoke, Balozi zetu zipate pesa, waweze kufanyakazi na tufaidike. Haitofaidika Balozi itafaidika Tanzania nzima.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa haya machache,naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Zitto ZuberiKabwe Ruyagwa dakika tano atafuatiwa na MheshimiwaMachano Othman Said dakika tano, Mheshimiwa SalumRehani ajiandae dakika tano.

MHE. ZITTO R. Z. KABWE: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi na kutokana na mudanimewasilisha kwa Mheshimiwa Waziri maelezo ya mchangowangu katika maeneo mbalimbali ambayo nachangia ilituweze kupata majibu ya Serikali. Kwa hiyo, nitachangiamaeneo machache tu kutokana na muda ambaoumepatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, nchi yetu ilijengaheshima kubwa duniani siyo kwa sababu ya utajiri, siyo kwasababu ya idadi ya watalii ambao tunao bali ni kwa sababuya kupigania utu mahali popote pale duniani. Mwaka 1961wakati tunapata uhuru, usiku wa kuamkia siku ya uhurutuliweka Mwenge juu ya Mlima Kilimanjaro na MwalimuNyerere alitamka maneno yafuatayo:- (Makofi)

‘Tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu yaMlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

matumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo palepalipo na chuki, heshima pale palipojaa dharau.’ (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huu ndio umekuwa msingiwa sera yetu ya mambo ya nje miaka nenda miaka rudi.Ndio mambo ambayo Waziri Mahiga, amekuwa akifundisha,ametumikia nchi yetu, amekuwa Balozi wa Umoja wa Mataifalakini leo mambo ambayo yanatekelezwa tunashindwakuelewa kabisa kama ni Mheshimiwa Dkt. Mahiga huyutunayemjua au kuna Mheshimiwa Dkt. Mahiga mpya baadaya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimetazama kura zote UNSecurity Council, wakati Waziri Dkt. Mahiga anaiwakilisha nchiyetu. Kura zote zilizokuja kupigania wanyonge tulikuwapamoja na wanyonge, lakini toka mwaka 2016 kura zotetunazopiga kwenye majukwaa ya kimataifa uanzie UNESCOParish, mwezi Oktoba, 2017 na mpaka hivi majuzi ama tunaabstain tunaona aibu kusimama na wanyonge au tunapigana watu ambao wanawakandamiza watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna mtu anayekatazanchi yetu kuwa na mahusiano ya kibalozi na Israel. HataMwalimu Nyerere hakukataza kuwa na mahusiano na Israellakini Mwalimu Nyerere alisema kwamba mahusiano hayoyasitufanye tuache kusimamia wanyonge. Mheshimiwa Wazirialikuwa Israel juzi, amekwenda Israel at the time, ambayondio inawaumiza Wapalestina kuliko wakati mwinginewowote miaka 70 ya Taifa la Israel. Amekwenda kutembeleamiji ambayo inapakana na Gaza, kulikuwa na massacre. Nchiyetu leo inaona aibu kulaani mauaji ya watu wanyongewanaokandamizwa, walionyang’anya ardhi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma maelezo yaWizara ukurasa wa nane mpaka wa tisa, propaganda kutakakuridhisha watu ambao bado wanaamini misimamo yaMwalimu Nyerere kwamba bado tuna misimamo hiyo, lakiniukitaka kujua hasa nini misimamo ya Serikali kwenye mamboya kimataifa nenda angalia ukurasa wa 51 mpaka 60 yahotuba ya Mheshimiwa Waziri. No mention of Palestina, no

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

mention of POLISARIO, Ame-mention kwenye preamble hukuili kuturidhisha kwamba misimamo yetu haijabadilika, lakinihuku amekuja kuzungumzia mpaka mambo ya North Koreahuko, nothing about watu ambao tumekuwa tukiwapigania.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi watu ambaotumewakomboa South Africa, baada ya massacre ya Gaza,wamemwondoa balozi wao, Waziri wetu anakunywa mvinyona Netanyahu, the butchery ya Wapalestina. Anaendakwenye television za Israel, television za Taifa anapongezaIsrael, anashindwa kutoa neno moja la kulia na watu ambao,sasa mambo yote aliyokuwa anafundisha Mheshimiwa Dkt.Mahiga siku zote ya foreign yanaenda wapi? At this ageanavunja heshima yake yote ya huku nyuma. Kwa sababuya nini misaada ya Israel? POLISARIO, its true, amezungumzarafiki yangu Mheshimiwa Cosato kwamba Algeria wanaubalozi wana… mwisho. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Machano OthmanSaid dakika tano, atafuatiliwa na Mheshimiwa Salum Rehandakika tano na Mheshimiwa Asha Abdallah Juma ajiandaedakika kumi.

MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa NaibuSpika, awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungukwa kupata nafasi hii ya kuchangia mchana huu wa leo. Pianimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwakutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weledi mkubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze piaMheshimiwa Masele na Mheshimiwa Mboni kwa nafasiambazo wamezipata katika Bunge la Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa haraka harakanizungumzie baadhi ya majukumu ya Wizara hii na umuhimuwake. Wakati wa bajeti ya Wizara ya Maji Mheshimiwa Waziriwa Maji alizungumzia pia kuhusu mradi wa maji ambao

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

tunatarajia kutoka India. Sasa mradi huu karibu ni mwakawa tatu naomba Wizara hii nayo itusaidie kutupa maelezoya ziada kuhusu hatima ya mradi huu wa maji ambao piana Zanzibar ipo katika mpango huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni kuhusu Wizara yaMambo ya Nje katika ofisi za Zanzibar. Baadhi yaWaheshimiwa Wabunge na Kamati naipongeza sanawamezungumzia umuhimu wa kufanywa matengenezo yajengo la Zanzibar au kujenga jengo jipya. Kwanza nikirikwamba lile eneo ni nzuri na liko katika sehemu nzuri naniiombe Wizara ijenge au ifanye matengenezo makubwakwa jengo lile lakini pia na vitendea kazi kwa ofisi ya Zanzibar.Pamoja na watenda kazi wenyewe bado ni tatizo kwaupande wa Zanzibar. Kwa hiyo, natarajia Mheshimiwa Wazirihili nalo atalitilia mkazo na kutuletea majibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipongeze uamuzi waWizara wa Serikali wa kufungua ofisi ndogo au Council katikaMji wa Guangzhuo na Lubumbashi. Vile vile pia niipongezesana Serikali kwa kuamua kufungua ubalozi mjini Havana,Cuba kwa masilahi ya Tanzania. Cuba ndio nchi ya kwanzakutambua Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 64, kwa hivyo kwaCuba, Tanzania ni rafiki wao wa kudumu kwa hivyonimefurahi nawashukuru na kuwapongeza Wizara kwambamwaka huu pengine tunaweza tukafungua Ubalozi nchiniCuba.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine suala la Mahujaji,Mheshimiwa Masoud alizungumza lakini mimi kidogo natofautiana naye. Ni kweli tunazo fursa na uhuru wa makundikupeleka mahujaji Makka, lakini mwaka jana kupitiamakundi haya haya mahujaji wa Tanzania walipata tabusana nchini Saudi Arabia. Wengine walitapeliwa na imefikiahatua Serikali ya Saudia kuagiza mahujaji wa Tanzaniamwaka huu walipiwe mwanzo kabla ya wakati wa Hija ilikuepusha tatizo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo ambalolimewasababisha baadhi ya mahujaji kuwa katika wakati

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

mgumu kwa sababu kwa utaratibu Mahujaji wanachangafedha kidogo kidogo ili wawahi nao kutekeleza ibada. Sasakwa uamuzi huu imekuwa kazi kubwa sana na ngumu.Nimwombe Waziri pia kwa sababu masuala haya ya dinipamoja na kwamba ni Tanzania lakini yanashughulikiwasehemu mbalimbali, kulikuwa na wazo kwa mahujaji waZanzibar kufunguliwa akaunti yao peke yao na mahujajikutoka Bara wawe na akaunti yao. Sasa sijui Serikali yaJamhuri ya Muungano imefikia wapi katika suala hili lakuweka sawa ili kupunguza hili suala la utapeli kwa mahujajiwetu na kuweza kupata huduma nzuri katika mji wa Maka.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu Ubaloziwetu Msumbiji. Msumbiji ukiacha lile jengo kubwa ambalotumejenga la ghorofa tisa liko kwenye sehemu nzuri lakinipia tunayo majengo mengine yasiyopungua mawili mpakamatatu. Maeneo ambayo tumepewa Msumbiji ni mazuri nawenyewe Msumbiji wanaona wametuheshimu sana kutupamaeneo yale, lakini kwa bahati mbaya tumeshindwakuyaendeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Wizara kamaingewezekana wangebadilisha matumizi ya lile jengo jipyabadala ya kulitumia kwa Ofisi ya Ubalozi, tungelitumiakwa kituo cha biashara na yale majengo menginetukayajenga na tukatumia kwa shughuli za kibalozi ambayoyanatosha sana. Yaani pale fedha nyingi tumetumialakini tuna maeneo mazuri tunaweza tukawa vizuri zaidi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hata wao MsumbijiTanzania yapo maeneo bado wanadai kwamba walipewana wamenyang’anywa katika utaratibu ambao hauko wazi.Ukiacha chuo cha…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wao umekwisha Mheshimiwa.

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

MHE. KHAMIS YAHAYA MACHANO: Mheshimiwa NaibuSpika, naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Salum Rehani dakika tanoatafuatiwa na Mheshimiwa Asha Abdallah Juma dakika kumi.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana. Vilevile niungane na wenzanguwale ambao walimpongeza ndugu yetu Sugu kwa kuwezakurudi hapa Bungeni, baada ya kutoka kifungoni kule Mbeya.Pia tumshukuru Rais kwa kuliona hilo na kuweza kuleta tafifuya kumrudisha hapa na leo tunaye. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo natakakusema kwa haraka haraka kulingana na muda suala lakwanza, Tanzania ndani ya tasinia ya Afrika mashariki. Kilatunapokwenda bado hakujawa na mikakati chanya yakuweza kukabiliana na ushindani iwe wa uchumi, elimu, hatautamaduni. Tunahitaji Wizara ieleze kwa undani ni mikakatigani ambayo itaweze kutufanya sisi kama nchi kuwezakukabiliana na tasinia ya ushindani ndani ya East Africa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaona wenzetu kila sikuwanafungua fursa nyingi za kiuchumi katika maeneo yao,lakini bado pamoja na harakati ya miradi ambayo iliyokondani ya nchi ya Tanzania haionyeshi competitive advantageya kuweza kushindana na wenzetu ambao wako katikamaeneo yetu wakati sisi tuna rasilimali nyingi ambazozinaweza kutupaisha haraka zaidi kuliko wao. Kwa hiyo,nimwombe Waziri aje atupe maelezo hapa mkakati ganitunao ndani ya utengamano huu wa East Africa, kukabilianana ushindani wa kibiashara, ushindani wa kielimu lakinivilevile na kiutamaduni baina ya nchi zetu hizi sita zilizo katikamtengamano huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo natakakulizungumza ni suala zima la Balozi zetu zilizo nchi za nje.Bado uwezo wa Mabalozi kuona output katika nchi hii nimdogo. Tegemeo la kupewa post hizi hawa Mabalozitunategemea waitangaze hii nchi kwa vivutio mbalimbali

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

vya kiuchumi, kiutamaduni na teknolojia vilivyoko ndani yanchi hii. Hata hivyo, tumeona tu wenzetu Wafaransa juzibalozi amechangamka na kuweza kuleta delegation hapaya Wafaransa kuja kuangalia fursa za uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, na sisi Tanzania tunahitajikuona tunatoa delegation mbalimbali zinakwenda katikanchi mbalimbali kuangalia fursa. Siyo hao tuwafanyabiashara hata nao Wabunge pia wapewe fursa zakwenda nje kuangalia fursa mbalimbali za kiuchumi,kiutamaduni na teknolojia ili waweze kuisemea nchi hii nakuleta matunda ambayo yataweza kuisaidia hii nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna vitu vingi ambavyotunaweza kufanya uwekezaji, lakini tuna miradi mingi yakimkakati ambayo inaweza kuitoa nchi hii, lakini tunasemamiradi hii tumeifungasha sisi wenyewe tu. Wazo langu tuitoe,tuitangaze kama tunaanzisha mradi mkubwa wa Stiegler’sGorge, tuutangaze duniani utapata support, watu wanahitajikuuona na kuujua, ziletwe ripoti za hii miradi ili tuweze kuonamiradi hii inapata ufadhili, lakini vilevile inapata…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa muda wakoumekwisha. Mheshimiwa Asha Abdullah Juma atachangiakwa huo muda uliobaki.

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuwezakuchangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nchi zaNje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima kubwa kupitiaBunge hili Tukufu naomba nitoe shukurani za dhati kwaMheshimiwa David Silinde, Mbunge wa Momba mwanatimuya mapambano kwa mashirikiano na juhudi zake amefanyakazi kwa moyo wa kijasiri na kwa kujitolea mpaka kuhakikishaushindi wa Mheshimiwa Mboni Mhita, Rais wa Caucus ya

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

vijana, Mheshimiwa Stephen Masele, Makamu wa Rais waBunge la Afrika wamepata ushindi na kuIletea nchi yetuheshima kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa taarifa yakokamanda wa jeshi hilo la ushindi si mwingine isipokuwa nimimi mwenyewe Asha Mshuwa na nampelekea salamuMheshimiwa Dkt. Magufuli japokuwa mimi hakunialika mimina Mheshimiwa Silinde lakini sisi ndio tuliofanya mapambanoya infantry na ya air wing.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine la heshimakwa viongozi hawa wawili tulioweza kupata ni vilewameahidi kwamba watatumia lugha ya Kiswahili katikakuendesha shughuli katika Bunge la Afrika. Hii ni turufu kubwana heshima kwa Tanzania yetu. Tanzania hoyee.

WABUNGE FULANI: Hoyeeee!

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, jambo ambalo linakuwa na uzito sana…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mshua inabidi tulifutemaana wewe umewafanya Wabunge wazungumze bilakuruhusiwa na mimi. Endelea Mheshimiwa Mshuwa.

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante nakubali. Katika hotuba Waziri amezungumzasana kuhusu diaspora na vile wanavyoweza kuchangia. Nikweli wana-diaspora wameongezeka na uchumi wao hukowaliko ni mzuri, hivyo wana nafasi kubwa kuchangia hapakwetu. Sasa Serikali irahisishe mazingira ya wao kuwezakuwekeza hapa nchini Tanzania, kwa hili bado halijawa vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, iko mifano kadhaa ya nchiambazo zimeweza kuwatumia diaspora na kuendeleza nakunyanyua uchumi wa nchi hizo na kipato cha familia zao.Hasa kwa kuzingatia kama watu hawa wana uchumimzuri na wanapata experience na exposure za kutoka katikanchi zile.

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalolinanikereketa na naomba Serikali inisaidie na tuwezekupata ufumbuzi ni hili suala la uraia pacha (dualcitizenship). Suala hili tuiombe Serikali ilifanyie tafakariupya na kulipatia utekelezaji japo kwa masharti.Ikiwezekana basi kama wasiwasi wa kiusalama basituweke vipengele ambavyo vitazuia watu hawa wasiingiekatika mistari ya kupiga kura au kuhatarisha usalama wanchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nafikir ia nanapendekeza kwamba, basi tutazame uwezekano wakufanya kama ule mfano ambao wanatumia India. Indiawao hawana duals citizenship lakini wanao utaratibuunaotiwa Person of India Origin, Wahindi hao wanapewautambuzi ambao unawapa haki sawa isipokuwa hawawezikupata uraia.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa jambo kama hili kwakutumia watalaam wao watafute namna kama kuwa natimu kabambe kama zile za makinikia ili tuwezekuwasaidia hawa vijana wetu ambao wako nje huko nawanapoteza nguvu kazi nyingi sana, ambao wana niahasa ya kuendeleza rasilimali katika Tanzania yetu nahasa hivi tunavyotaka Tanzania ya viwanda hawa watunaamini wanao uwezo sana wa kutengeneza viwandahata vidogo vidogo. Mbona hamnipigii makofi, hamtaki?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya ombi hilo lakuiomba Serikali, sasa naomba tena suala la pass yadiplomatic. Diplomatic Pass imetoka agizo kwambawasipewe wenza. Sasa naomba Serikali ifikirie jambohilo kwa sababu inakuwa haipendezi unasafiri na mkeoau na mumeo japo mimi sina mume l akini nawasemeawenzangu wenye waume. Wewe mke unakwenda huku,mume anakwenda kwingine inakuwa haipendezi nahaijengi heshima ya nchi. Hata hivyo, tutazame kwawale watu ambao wanaongeza wake wengi waliozidi,waliozidi wanne au ishirini, basi waambiwe awekewe wake

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

zake wawili tu. Kwa sababu tukisema apewe mke mmojahapa nitaingilia utaratibu hata Mzee Ally Hassan nitakuwanimemwingilia kwa hivyo atakuwa haweze kuwachukuliawake zake wote wawili.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Asha naomba ukae kidogo.

Waheshimiwa Wabunge kwa Mujibu wa Kanuni ya28(2) nakusudia kuongeza nusu saa ili tuweze kumalizashughuli iliyoko mbele yetu, lakini fasili hii inataka niwahoji,hivyo nitawahoji Waheshimiwa Wabunge wanaokubalianana hoja ya kuongeza nusu saa ili tumalize shughuli iliyokombele yetu.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

NAIBU SPIKA: Walioafiki wameshinda. MheshimiwaAsha Abdallah, endelea. (Makofi)

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante. Sasa nasema kwa sababu ukisema apewemke mmoja tu au mume mmoja inaweza kuleta tatizo kwasababu mzee wetu wa heshima baba yetu Rais wetu AliHassan anao wake wawili. Sasa utakuwa upendeleo ukisemammoja aende. Kwa hivyo wakae watazame namna ganiwata-sort out jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalonataka kuzungumzia ni kuhusu viwanja vya ubalozi. Nchiyetu tulipata heshima kubwa na viwanja vingi tulipata kwaheshima ya mwenyewe hayati Baba wa Taifa MwalimuNyerere, lakini viwanja vingi mpaka hivi sasa hivi badohavijaendelezwa. Sasa tubadilike tutafute namna hatakushirikiana na investors wengine sio tu haya majengo yawekwa ajili ya ubalozi lakini tuweze kufanya shughuli nyinginekwenye majumba yale kujenga ofisi, kupangisha na kufanyaubalozi. Maana yake hiyo tunu tuliyopewa mwisho itapotea,nyota ile tuliondoka nayo itapotea, majengo yetu mengihayako katika hali nzuri.

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

Mheshimiwa Naibu Spika, tutumie hii nafasi yakidemokrasia ya kiuchumi kushawishi ili tuweze kuviendelezaviwanja hivyo, lazima kuwe na uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwafedha zilitengwa kwa mfano wa kujenga jengo la Omanlakini hazikuweza kupatikana. Sasa nataka nishauri kwa vileOman ni rafiki zetu sana na nimeona hapa kwenye hiliripoti wanasaidia kukarabati Bete la Jaibu basi tutafutenamna kwa kushirikiana kwa mazungumzo kama vilewafalme wengine wanaweza kuja kutujengea uwanja aukama marehemu Gadafi alivyojijengea misikiti na haowatusaidie kujenga hili jengo la ubalozi pale Omanitatusaidia sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia kumuulizaMheshimiwa Waziri...

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili tayari Mheshimiwa.

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Muda wangu umeisha?Astaghfiru-Allah! Naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nampongeza Waziri, Mheshimiwa Dkt. AugustineMahiga na Naibu wake Mheshimiwa Dkt. Suzan Kolimba naWatendaji wote wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya yakuendelea kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia kwamasuala ya uhusiano wa Kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, napenda kuendeleakuipongeza Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini yauongozi wa Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. JohnJoseph Pombe Magufuli, kwa kazi nzuri na kubwa yakuijenga Tanzania ya viwanda na maendeleo ya uchumiwa kati.

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya pongezi hizinaomba sasa nichangie hoja ya Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali ipatiekipaumbele haja ya kurekebisha Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ili kuruhusu raia wake kuweza kuwana uraia pacha (Dual Citizenship). Nionavyo kuna faidakubwa kuliko hasara kama Watanzania wanaopenda kuwana uraia wa nchi mbili watahalalishwa kufanya hivyo, kwanikwa kufanya hivyo, tunajiongezea fursa za kiuchumi na kijamii,hasa kwa Watanzania wenzetu wanaoishi na kufanya kazinchi za nje (The Diaspora Community).

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la Itifaki yaSoko la Pamoja la Afrika ya Mashariki. Ingawa hotuba yaWaziri inatamka bayana katika ukurasa wa 28, aya ya mwishokuwa, wananchi na hasa vijana washiriki katikakuchangamkia fursa zilizoko kwenye soko la Jumuiya ya AfrikaMashariki, hali ilivyo sasa kwa wasafiri wanaotumia Hati zaDharura za kusafiria siyo rafiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, zamani Hati za Dharura zaKusafiria zilikuwa zinatolewa kwa kuruhusu kutumika kwamultiple entries kwa muda wa mwaka mmoja, lakini kwasasa na kwa sababu ambazo wananchi wanaosafiri marakwa mara kwenda na kurudi katika nchi jirani zetu AfrikaMashariki hupewa hati za dharura ambazo zinaruhusu singleentry visa tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni kumaanisha kuwa,mara msafiri anapopita kwenda nchi ya jirani, mfano Kenya,kwa wajasiriamali wa mpaka wa Kenya na Tanzania,Namanga, ambao hufanya biashara katika masoko ya nchijirani kila wiki hulazimika kukata hati mpya ya dharura yakusafiria kila trip hata kama atasafiri kwenda na kurudi kilasiku.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili siyo rafiki kwauchumi wa wananchi na vijana wanyonge ambao Itifaki ya

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Soko la Pamoja ililenga kuwasaidia. Gharama ya hati kwakila safari ni wastani wa Sh.20,000/= na kama msafiri atahitajikwenda Kenya mara tano kwa mwezi, kwa mfano,atalazimika kutumia hadi Sh.100,000/= kwa hati ya kusafiria.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nishauri nakuiomba Serikali watengeneze mazingira rafiki ya amakurejesha Hati za Dharura ambazo ni valid for multiple entriesfor one year au utoaji wa Pasi za Afrika Mashariki urahisishwena kuwezekana kutolewa mpakani tofauti na sasa ambaponi mpaka maombi yapelekwe Dar-es-Salaam na kuchukuazaidi ya miezi sita mpaka msafiri apate pasi hiyo, au ikubalikesasa kuwa, Watanzania waruhusiwe kusafiri nchi za Jumuiyayetu kwa kutumia vitambulisho vyao vya Kitaifa tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kumpongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu naWatendaji wote walioko katika Wizara hii. Pamoja napongezi nina machache yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itenge fedha zakutosha kwa Balozi ambazo zinatumika nchi tatu mpakatano ili Balozi aweze kuzitembelea na kutafuta fursa zakiuchumi kama utalii, viwanda na usalama na uwakilishi uwewenye manufaa katika nchi hizo. Ofisi za Ubalozi zitengewefedha za ukarabati wa ofisi za ubalozi na nyumba zawatumishi katika Balozi husika ili ziendane na hadhi ya nchiyetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanja vya Ubaloziambavyo havijajengwa vitengewe fedha kwa ajili ya ujenziwa ofisi za Ubalozi na makazi ya Balozi zetu na watumishiwake. Kwa mfano, kiwanja cha Ubalozi Jijini Londonkimetelekezwa na kimejaa magugu na mbwa mwitu. Kilaofisi za Ubalozi wetu nje ya nchi ziwe na wataalam wa faniambazo zitasaidia kuiuza nchi yetu kiutalii, kiutamaduni,lugha ya Kiswahili, kuvutia wawekezaji kuja Tanzania kujengaviwanda, Kujenga hospitali za kitalii kwenye website ya kila

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Ubalozi kuwe na vivutio vyote vilivyoko katika nchi yetu ilikila mtalii aamue ni eneo gani anapenda kwenda kutalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano, kuna mazoea yakuona vivutio vichache tu Serengeti National Park, MlimaKilimanjaro, Ngorongoro Crater, Zanzibar lakini ukiangalianchi yetu ina vivutio vingi sana kama, Kitulo National Park,Ruaha National Park, Manyara National Park, Mahale NationalPark, Maporomoko ya Kalambo (Rukwa), Gombe NationalPark, Saa Nane Island, Arusha National Park, TarangireNational Park, Udzungwa National Park, Kilimanjaro NationalPark, Serengeti National Park, Selou National Park, Majengoya Kale Kilwa, Mafia, Bagamoyo, Olduvai George, NyagozaMtu wa Kale, Mapango ya Amboni Tanga, Kaburi la Babawa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere – Butiama, Fukwe za Bahari,Utalii wa Water Sports (Bahari na Maziwa Victoria, Tanganyikana Nyasa - Matema Beach). Maeneo ya kale MtwaraMikindani na Utamaduni wa Ngoma za asili na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vivutio hivyo vyotena vingine ambavyo sikuvitaja viwekwe kwenye matangazombalimbali duniani na hasa ziwekwe kwenye website za kilaBalozi zetu nje ya nchi. Balozi ziandae maonesho kwa lengola kuitangaza nchi yetu ya Tanzania, katika sekta za utalii,kiutamaduni na kutumia fursa ya kijiografia ya nchi yetukupakana na nchi zaidi ya tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kupata fursa ya kuchangia kwa maandishi. Aidha,nawapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuuna Watendaji wote walioandaa hotuba hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu kuwa ofisi zaUbalozi zimepewa jukumu la kutoa Visa kwa wagenimbalimbali wanaotaka kufika nchini kwa shughulimbalimbali, suala la Visa rejea. Katika utoaji wa Visa rejeakumekuwa na ucheleweshaji sana kuwapata waombaji

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

wanaotoka katika zile nchi ambazo nchi yetu inawapatiaVisa hizo. Kuna nyakati Visa rejea hutolewa baada yamiezi mitatu na wakati mwingine waombaji hawapatimajibu kabisa. Hii inaleta adha kwa wale wageniwanaotaka kuja pamoja na Maafisa Balozi. Hali yakuchelewa au kutopata Visa rejea, husababisha Serikalikukosa mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali kulipitiaupya sharti la Visa rejea ili kwenda na wakati kwa kufunguamilango il i wageni waweze kuingia. Mfano watali i,wawekezaji, wafanyabiashara na wageni wengine ambaohuja kwa shughuli za mikutano na ziara za utafiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, malipo ya ada ya Visa kuwajuu na kwa dola. Kuna baadhi ya mawakala wamekuwawakitoa pesa juu sana kwa ajili ya Visa mfano baadhi yamawakala wa Saudi Arabia wamekuwa wakitoza ada sichini ya dola 600, sambamba na hilo kuna baadhi yamawakala hawana ofisi maalum, ni budi Wizara kufanyauhakiki wa mawakala wote il i kuwaondolea adhaWatanzania kulanguliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 66 ajira mpya,pamoja na kupata kibali cha kuajiri watumishi 10 bado ofisinyingi za Ubalozi zina upungufu wa wafanyakaziwanadiplomasia. Hebu Serikali ifanyie kazi ili wapatikane nakutosheleza ili kuleta ufanisi katika utendaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafasi za kazi nje ya nchi.Tanzania imekuwa ikisisitiza umuhimu wa Watanzania wanadiaspora waishio nje kuchangia uchumi wa Taifa letu kwakuleta mapato wapatayo huko ughaibuni. Je, Serikaliimejipangaje kuhakikisha jambo hili linaenda sawa na kuletatija kwa nchi? Mkakati upoje ili Watanzania wote waishioughaibuni wafahamike wapo nchi zipi na wanafanya kaziau shughuli zipi?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata fursaya kuchangia kwa maandishi na naunga mkono hoja.

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, sisisi Tanzania ya Nyerere, ni Tanzania mpya, Tanzania mbayainayokalia kimya mauaji ya kinyama ya Wapalestina nakuunga mkono waonevu.

(i) Msimamo wa Tanzania kuhusu Palestine (aya 18ya Hotuba ya Waziri), maelezo ya Serikali hayaendani namatendo. Tanzania imewatupa mkono wanyonge waPalestine.

(ii) Msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi(aya 19 ya Hotuba ya Waziri), kuna dalili zote kuwa Serikaliinataka kuwafukuza POLISARIO baada ya kuikumbatiaMorocco.

(iii) Unafanyaje diplomasia bila wanadiplomasia?Vituo vingi nje havina FSOs.

Mheshimiwa Naibu Spika, msimamo wa Tanzaniakuhusu mgogoro wa Israel na Palestina unaelezwa vizuri sanana nukuu hii ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa mwaka 1967 nandiyo umekuwa msingi wa Sera yetu ya Mambo ya Nje kwamiaka mingi kabla ya utawala wa sasa wa CCM mpya.

“….Tanzania’s position. We recognize Israel and wishto be friendly with her as well as with the Arab Nations. Butwe cannot condone aggression on any pretext, nor acceptvictory in war as a justification for the exploitation of otherlands, or Government over other peoples.”

Mheshimiwa Naibu Spika, kwamba Tanzaniainaitambua Israel na inapenda kuwa na urafiki nayo pamojana urafiki na mataifa mengine ya kiarabu, lakini hatuwezikukalia kimya uvamizi kwa namna yoyote ile, pia ushindi vitanihauhalalishi unyonyaji dhidi ya ardhi ya wengine au dhidi yaSerikali za watu wengine. Msingi huu unaendana kabisa nadhamira ya sasa ya Sera ya Mambo ya Nje. Hata hivyo, halini tofauti kabisa. Mambo tunayoyayafanya kwenye Sera yetuya Mambo ya Nje yanamfanya Mwalimu Nyerere ageuke hukokaburini kwake.

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaeleza kwa mifano, 26Oktoba, 2016 kulikuwa na kikao cha Wajumbe wa Nchi 21zinazounda ‘Kamati ya Urithi wa Dunia’ ya UNESCO-Shirikala Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni kupigakura ya kupitisha makubaliano ya kuridhia kuupa hadhi yaurithi wa Dunia Mji wa Jerusalemu pamoja na moja yamajengo ya Mji huo (Temple Mount) na kufungamanishwana uasili wake na si hali ya sasa inayotokana na uvamizi waIsrael juu ya eneo hilo lililoko Jerusalemu Mashariki (lililovamiwamwaka 1967 na mpaka leo kutambuliwa na UN kama eneola Palestina, ambao wanauona ndiyo Mji Mkuu wa nchi yaPalestina iwapo makubaliano ya ‘Two States Solution’yatafikiwa).

Mheshimiwa Naibu Spika, ACT Wazalendo tulihoji juuya jambo hili linalokwenda kinyume na Sera ya Nje ya nchiyetu. Msimamo wa Tanzania ni kukubaliana na UN kupingauvamizi wa eneo hilo uliofanywa na Israel. Serikali ilitoamajibu mepesi tu, tena pembeni kuwa upigaji wa kura ulehaukuwa msimamo rasmi wa nchi yetu ni ukiukwaji wa serayetu ya Mambo ya Nje na kuwa ni jambo ambalo Afisa wetukwenye mkutano ule wa UNESCO alilifanya kwa makosa nahivyo hatua zingechukuliwa dhidi yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri hayo yalikuwa nighiliba tu, matukio ya karibuni yameonesha kwa uwazi surampya ya Taifa letu pamoja na msimamo mpya wa Sera yetuya Mambo ya Nje. Kwenye diplomasia matendo ya nchi huwana maana zaidi kuliko maneno ya wanadiplomasia wake,matendo yetu yafuatayo ya karibuni yameonesha kuwaTanzania hatuiungi mkono tena Palestina.

(1) Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuwaangushaWapalestina kule Paris kwenye Mkutano wa UNESCO, Serikaliiliahidi kuwa ingemchukulia hatua Afisa yule wa Wizara yaMambo ya Nje aliyekwenda kinyume na Sera yetu ya Mamboya Nje, hatujafanya hilo zaidi tumempandisha cheo nakumteua kuwa Balozi Elizabeth Kiondo apige kura namnaile kule UNESCO na sasa tumempa cheo zaidi kwa kazi njemaaliyoifanya. Jambo hil i l inaonesha kuwa kwa sasa

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

tunawaunga mkono Waisrael na hatuko tena naWapalestina.

(2) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa tumeamuakufungua Ubalozi wetu Israel, Tel Aviv, kuongeza uchungukwenye kidonda, tukachagua wakati huu wa maadhimishoya miaka 70 ya uvamizi wa Israel ardhi ya Taifa la Palestinakuzindua ubalozi wetu huo. Jambo hili linafanyika kukiwana tuhuma kuwa hata huo ubalozi unagharamiwa na Israelyenyewe, ndiyo maana tumepangiwa hata kipindi chakuufungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kidiplomasia kuufunguaubalozi wetu katika wakati huu ni kuadhimisha uvamizi waIsrael katika ardhi ya Palestina. Maana tulikuwa na uwezowa kuchagua wakati mwingine wowote kufanya uzinduziwa ubalozi wetu, lakini kwa kuwa aliyegharamia uwepo waUbalozi huo (Israel) alitaka tuufungue wakati huu wamaadhimisho ya miaka 70 ya uvamizi wa Israel kwa Palestina,ilitubidi tufanye hivyo. Jambo hili limeonesha kuwa kwa sasahatuungi mkono tena utu (Palestina) bali tunamtumikia kilamwenye kitu (Israel).

(3) Mheshimiwa Naibu Spika, wakati akiwa ziaraniIsrael, Balozi Dkt. Mahinga alifika sehemu ya miji inayokaliwakimabavu na Israel ambayo inapakana na ukanda wa Gaza,na baadaye alihojiwa na Televisheni ya Taifa ya Israel ambakoalionesha tu masikitiko yake kwa Waisrael wanaokaamaeneo hayo kwa kusumbuliwa na mashambulizi ya Hamas,lakini hakulaani kabisa uendelezaji wa Israel kujenga makazikwenye maeneo hayo ya uvamizi kama wanadiplomasiawengine wa nchi zenye msimamo wa ‘Two States Solution’kama sisi wanavyofanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Balozi Dkt. Mahingamwanadiplomasia mzoefu na mbobezi, kutokulaani kwakemakazi yale haramu ni jambo la makusudi kabisa, si bahatimbaya. Ni kitendo cha kutuma salamu kwa Wapalestinakuwa tunaunga mkono uendelezaji makazi wa Israel katikamaeneo hayo iliyoyavamia.

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

(4) Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania imetajwa navituo mbalimbali vya habari vya Kimataifa kuwa ni katikanchi 33 ambazo zilihudhuria ufunguzi wa Ubalozi wa MarekaniMjini Jerusalemu, Mei 14 kilele cha maadhimisho ya miaka 70tangu uvamizi wa Israel katika maeneo ya Wapalestina.Chanzo cha taarifa ya Tanzania kuhudhuria ni Serikali ya Israel,ikitaja nchi ilizozialika na zilizohudhuria.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu inasemainapinga uwepo wa Ubalozi wa Marekani Mjini Jerusalem,lakini hapo hapo inatajwa kuhudhuria uzinduzi huo. Pichatunayoitoa hapa kwa Wapalestina ni kuwa tunaunga mkonojambo hili la ufunguzi wa Ubalozi wa Marekani Mjini Jerusalem.

(5) Mheshimiwa Naibu Spika, siku ya uzinduzi huo waubalozi wa nchi ya Marekani Mjini Jerusalemu, Jeshi la Israelliliwaua kwa risasi zaidi ya watu 54 wa Palestina, wakiwemowanawake, watoto, walemavu na hata wanahabari. Nchimbalimbali duniani zimelaani mauaji hayo. Nchi ya Afrika yaKusini imekwenda mbali zaidi kwa kumrudisha nyumbaniBalozi wake aliyeko Israel. Tanzania tuliyoikomboa Afrika yaKusini tumekaa kimya, tumeshindwa hata kutoa kauli yakulaani mauaji hayo. Kuhudhuria kwetu ufunguzi wa ubalozina kukaa kimya juu ya mauaji hayo kunaonesha tumewaacharasmi Wapalestina.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo hayo matanoyanaonesha kuwa sisi si tena ile Tanzania ya Mwalimu JuliusNyerere, sisi kwa sasa ni Tanzania mpya (kama yasemavyomatangazo ya Ikulu yetu) – Tanzania mpya inayosimama nawaonevu wa dunia, wauaji na wavunja haki za wanyonge.Sisi si tena Tanzania ya kusimama na wanyonge, bali niTanzania ya kusimama na wanyongaji kwa sababu ya maslahiya kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, si ile Tanzania iliyongozaukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwenye makucha yaukoloni, bali ni Tanzania mpya inayounga mkono nakushabikia ukoloni na uvamizi. Sisi si ile Tanzania yenyemsimamo mkali tuliopinga Taifa kubwa la Marekani dhidi ya

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

uvamizi wake kwa wanyonge wa Taifa la Vietnam, bali sasani Tanzania mpya ya kuunga mkono uvamizi wa Taifa onevula Israel kule Palestina.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi si Tanzania ile iliyoiteteaChina ipate nafasi na Kiti chake stahili kule UN, bali sasa sisini Tanzania mpya inayowaacha watu wa Palestina bilautetezi wa hadhi, kiti na nafasi yake stahili kule UNESCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi si ile Tanzania huru tenaya Mwalimu Nyerere, iliyowaheshimu watu na Mataifakwa sababu ya utu wao na kuamini kwamba binadamuwote ni sawa. Sasa sisi ni Tanzania mpya, inayowapaheshima watu kwa sababu ya kitu inachotuhonga, tukiuzausuli wa Utaifa wetu kwa maslahi machache ya kifedha aukiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuwashi tena Mwengena kuuweka Mlimani Kilimanjaro, hatumuliki tena nje yamipaka yetu, hatuleti tena matumaini pale pasipo namatumaini, hatupeleki tena upendo kule kuliko na chuki nahatuleti heshima pale palipojaa dharau. Sisi si Tanzania yaMwalimu Nyerere, sisi sasa ni Tanzania mpya, Tanzania mbaya,Taifa lililokiuka misingi yake, Taifa linalowaacha Wapalestinawakiuawa kinyama na sasa linalosapoti waonevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kujengewa uwanja wa mpirana msikiti visiifanye Tanzania likumbatie Morocco na kuachakuiunga mkono Sahara Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado niko kwenye Sera yaMambo ya Nje ya Nchi yetu, si hii ya Tanzania mpya bali ileTanzania ya tangu wakati wa Baba wa Taifa MwalimuNyerere ya kusimama na wanyonge. Wakati tulipoamuakufuata ‘Diplomasia ya Uchumi’ bado msingi wetu huu wakusimama na wanyonge ulibaki palepale. Ndiyo maanawakati wa Rais Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete badotulibaki kuwa ni sauti ya Mataifa yanayoonewa kama Cuba(tukipinga vikwazo vya Marekani dhidi yao), Palestina naSahara Magharibi.

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

Mheshimiwa Naibu Spika, msingi huo wa kusimama nawanyonge ni muhimu zaidi kwa Chama chetu cha ACTWazalendo, ndiyo maana tulipinga ujio wa Mfalme waMorocco hapa nchini tarehe 23 - 25 Oktoba, 2016. Kwa kuwaTaifa hilo bado linaikalia kimabavu ardhi ya wanyonge waSahara Magharibi, ndiyo msingi pia wa kutangaza wazimahusiano yetu rasmi na Chama cha Siasa na Ukombozi waTaifa hilo cha POLISARIO kinachopigania uhuru wa nchi yaSahara Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Umoja wa Afrika (AU) uliamuakukubali ombi la Morocco kurudi bila masharti kwenyeJumuiya hiyo. Ikumbukwe kuwa kwa zaidi ya miaka 33Morocco haikuwa na mahusiano na Jumuiya hiyo (tanguOAU mpaka sasa AU) baada ya kujitoa kwa kupingaOAU kuitambua Sahara Magharibi kama Taifa huru nakupewa Kiti rasmi ndani ya OA mwaka 1984.

Mheshimiwa Naibu Spika, uamuzi wa OAU wa kuiruhusuSahara Magharibi kuwa mwanachama wa umoja huoulitokana na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa yaHaki (International Court of Justice-ICJ) ya mwaka 1975iliyopinga madai ya Morocco kuwa ina mahusiano yakihistoria na kisheria na Sahara Magharibi (na hivyokuitawala kinguvu) na kutoa haki ya kujitawala kwa Taifahilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaheshimu maamuzi yaleya mkutano wa AU uliofanyika Januari, 2017 ulioirudishaMorocco kwenye AU, lakini tabia za Taifa hilo onevubado hazijabadilika, hivyo ni muhimu tulieleze Bunge hiliTukufu masuala yafuatayo ili liweke msimamo wakekwa Serikali juu ya kuminywa kwa watu wa SaharaMagharibi:-

(1) Kikao cha AU cha tarehe 28 - 29Januari, 2018kiliazimia kuwa Morocco iruhusu Kamati Maalum ya Uangaliziya AU iende kwenye maeneo ya Sahara Magharibiambayo inayakalia kimabavu ili kuja kuijulisha AU hali yamambo ilivyo.

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

(2) Tarehe 29 Machi, 2018 Morocco iliwajulisha UN juu yakutoruhusu waangalizi wowote wa AU kwenda kwenyemaeneo yote ya Sahara Magharibi inayokalia.

(3) Tangu mwaka 1991 Morocco imetumia mbinu, hilana uzandiki ili kuzuia Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili yakura ya maoni ya uhuru wa Sahara Magharibi (MINURSO)kufanya kazi yake kwenye maeneo inayoyakalia kimabavuya Sahara Magharibi. Siku za karibuni Umoja wa Mataifa(UN) ulipitisha Azimio Na. 2414 (2018) la kuongeza mudawa mamlaka, uhai na madaraka ya MINURSO kwamiezi sita, Morocco imepinga jambo hilo na kutishiakufanya mashambulizi ya kijeshi kwenye maeneo yaSahara Magharibi ambayo yameshakombolewa (LiberatedZones).

(4) Bado Morocco inaendeleza uvunjaji mkubwa wahaki za binadamu kwa watu wote wa Sahara Magharibiwanaodai uhuru wao.

(5) Kurudishwa kwa Morocco kwenye AU kuliendapamoja na Taifa hilo kuridhia ‘AU Constitutive Act’ inayotakaMataifa ya Afrika kuheshimu Maazimio ya AU na hata yaleya UN yanatolewa kwa ushirikiano na AU. Hata hivyo,kwa matendo yake tuliyoyaainisha hapo juu ni dhahirikuwa Morocco haitaki usuluhishi na Sahara Magharibi,bado inataka kuitawala na kuikalia kimabavu, ndiyomaana imekataa hata kumpa ushirikiano msuluhishi wamgogoro huu, Ndugu Horst Kohler Rais wa zamani waUjerumani.

(6) Matendo ya Serikali yetu kwa sasa yanaoneshahatuna msimamo kwenye mambo ya msingi ya kidiplomasia,namna tulivyoenenda kwenye mahusiano yetu na wanyongewa Palestina ni mfano hai, sasa tukijali vitu kuliko utu kamailivyo zamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, nataka kulishawishiBunge lako litoe mwongozo kwa Serikali juu ya kuenendakwenye hili jambo la Morocco na Sahara Magharibi ili kuzuia

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

ahadi ya kujengewa uwanja na msikiti na Serikali ya Morocco.Vitu visitufanye tuwaache ndugu zetu wanyonge wa SaharaMagharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu ni kimbilio la nchiya Sahara, Serikali yetu chini ya Mwalimu Nyerere ililitambuaTaifa la Sahara Magharibi tangu siku za mwanzo kabisa zaharakati zao, ndiyo maana wanao Ubalozi hapa nchini.Kumuenzi Baba wa Taifa na kulinda misingi ya Taifa letu nilazima tusimame na watu wa Sahara Magharibi natusiwatupe kama tulivyofanya kwa watu wa Palestina.

Mheshimiwa Naibu Spika, naliomba Bunge liibaneSerikali ili itoe ahadi hiyo hapa Bungeni, pamoja na kuitakaSerikali kutumia ushawishi wake kule AU na UN kuibanaMorocco iruhusu kura ya maoni ya kuamua mustakabali wawatu wa Sahara Magharibi kama ilivyoridhiwa kwenye Azimiola UN. Viva Sahara Magharibi, Viva POLISARIO, Mungu IbarikiAfrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna Diplomasia bilawanadiplomasia, tuna uhaba mkubwa wa Watumishikwenye Balozi zetu. Msingi wa tano wa Sera ya Mambo yaNje ya Tanzania unatutaka tushirikiane kikamilifu na nchi,Mashirika pamoja na Taasisi mbalimbali katika nyanja zaDiplomasia, siasa, uchumi, utaalam na teknolojia. Wizara hiiina jukumu la kubuni na kusimamia utekelezaji wa misingiyote ya sera yetu ya mambo ya nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Wizara hii pia ina jukumula kusimamia na kuratibu mahusiano kati ya Tanzania na nchipamoja na mashirika mbalimbali. Utimizaji wa jambo hilounafanyika kupitia Balozi zetu zilizotapakaa kwenye nchimbalimbali ulimwenguni. Kwa sasa ufanisi wetu si mkubwakwa sababu ya uhaba wa Watumishi kwenye Balozi zetumbalimbali duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wastani ukimwondoaBalozi, kila kituo cha Ubalozi wetu nje ya nchi kinapaswakuwa na Mhasibu, mtu wa TISS pamoja na mwanadiplomasia

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

(FSO). Vituo vingi vya Balozi zetu havina kabisa Maafisa waDiplomasia (FSO’s), wale wachache waliokuwepo awaliwalirudishwa nchini kwa sababu mbalimbali (ikiwemokumaliza muda wao wa Utumishi Nje ya Nchi). Tumerudishawatu bila kupeleka mbadala wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Balozi zetumbalimbali Watendaji hasa wa kazi za Kibalozi naKidiplomasia ni hawa Maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Sasakwa uhaba huu tunawezaje kufanya diplomasia ya nchi yetu?Hiyo Diplomasia ya Uchumi tunafanyaje bila kuwa na haowanadiplomasia?

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa tu mfano wa Balozizetu chache ulimwenguni, China nchi ambayo ni mshirikawetu mkubwa kidiplomasia na kiuchumi, hatuna kabisa FSOhuko, labda ndiyo sababu mauzo yetu kwenda Chinayameshuka mno, maana biashara ya nje ni diplomasia. Sasawakati unamtaka ndugu yangu Charles Mwijage asafiri ninani atakayemuandalia hiyo mikutano ya kupata wawekezajihuko China kama hatuna FSO hata mmoja? WenzetuUganda wana FSO’s nane huko China, Kenya na Sudani waowanao tisa kila mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi nyingine ambayo hatunaFSO ni Ethiopia-Makao Makuu ya AU, utaona tunavyodharaunafasi yetu katika Afrika. Pia hatuna FSO Afrika Kusini, nchirafiki na moja ya zenye uchumi mkubwa Afrika, hatuna kabisaFSO Ujerumani, nchi kubwa zaidi kiuchumi katika Umoja waUlaya (EU). Hata India ambako tangu Bunge lianze Wabungetunalalamikia kukosa soko la mbaazi kutoka huko nakohatuna FSO hata mmoja. Tumeufanya kuwa ubalozi wakupokea wagonjwa tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi za BRICS (ukiondoaChina, India na Afrika Kusini ambazo hatuna kabisa FSO’s)zilizobaki, Brazili na Urusi tuna FSO mmoja mmoja tu. HataDRC Congo nchi ambayo zaidi ya theluthi moja ya mizigoya transit inapita kwenye bandari ya Dar es Salaam inatoka,nayo tuna FSO mmoja tu tofauti na watatu ilivyozoeleka.

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Kenya nchi ya Afrika Mashariki tunayofanya nayo biasharazaidi nayo ina FSO mmoja tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali iko hivyo karibu katikaBalozi zetu nyingi ulimwenguni, FSO’s ndiyo Maafisa hasawaliyofundwa na kupikwa kutekeleza sera yetu ya Mamboya Nje. Foreign Service Officers (FSO’s) ndiyo diplomats(wanadiploma wetu). Kama hawapo vituoni nahatuwatumii maana yake hatufanyi diplomasia na kwakuangalia mbali tunaua diplomasia yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sitapitisha bajeti hii mpakaWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki itakaponihakikishia kuwa itapeleka Maafisa waDiplomasia (FSO’s) katika vituo ambavyo hatuna kabisana pia kuwaongeza katika vile vituo ambavyo wakowachache.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kupata nafasi hii ya kutoa mchangowangu kwa njia ya maandishi katika Wizara hii. Naombanianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri na NaibuWaziri kwa kazi nzuri sana wanayoifanya. NampongezaKatibu Mkuu na Naibu wake na watendaji wote na Wakuumbalimbali wa Idara zote zilizoko Wizarani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongeze sanana kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John PombeMagufuli kwa dhamira yake ya dhati ya kutaka kuinua Taifaletu katika Diplomasia ya Uchumi na uhusiano mzuri naMataifa mengine duniani kwa kuwapa nafasi wataalamwake kufanya kazi hiyo bila yeye kukanyaga katika nchi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakika uamuzi wake wakuwaamini na kuwapa nafasi wataalam wote wakiwepoMabalozi wetu wote walioko nje ya nchi na waliopo ndaniya nchi. Uwezo wao wa uzalendo wao, tumeuona kwanimahusiano ya Taifa letu yamezidi kuwa mazuri na kuimarika,kiuchumi, kiusalama na kisiasa, ahsante sana MheshimiwaRais na hongera sana watendaji na Mabalozi wote.

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Mheshimiwa Naibu Spika, natambua kazi kubwa sanainayofanywa na Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, KatibuMkuu na Naibu Katibu Mkuu ya kumwakilisha MheshimiwaRais kwenye mikutano mbalimbali na majukumu mbalimbaliya Kimataifa, huko nako hatujapungukiwa. Pia pongezi kwaMabalozi ambao wao wako hapa Tanzania, lakini nchinyingine ya kuibua mazuri yote kwenye Kandawanazozisimamia mfano, Mabalozi wanaosimamia Idarambalimbali kama; Mashirika ya Kimataifa, Kanda ya Afrika,Kanda ya Asia, Kanda ya Ulaya na Kanda ya Amerika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza sana hawabalozi wanaosimamia Kanda hizi. Kwani mambo yanaendavizuri sana tumeona viongozi mbalimbali wakija nchini nawafanya biashara wengi wakija nchini kwetu, pongezi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba nipongezeutaratibu nzuri sana ambao Wizara imefanya wa kuletavitabu ambavyo vina anwani za Balozi zote zilizoko nje yanchi na ndani ya nchi yetu, pongezi sana. Pia kitabu kizuricha utekelezaji wa diplomasia ya Tanzania kuelekea uchumiwa viwanda 2020. Utaratibu huu ni mzuri sana, naombauendelee na ikiwezekana, angalau kuonyeshwe na moja yafursa iliyoko katika nchi husika. Pongezi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa ushaurikuhusu nyumba na majengo ya baadhi ya Balozi zetu nje.Majengo haya yanatia doa nchi yetu kwa uchakavu.Naomba Waziri alipeleke shauri hili kwenye Baraza la Mawaziriili jambo la bajeti ya kukarabati nyumba hizi lichukuliwe naHazina, Wizara haitaweza bajeti yake ni ndogo. Mfano,nyumba za London niliwahi kwenda, haziridhishi. Naombasana u-smart wa mtu humpa heshima kwa wanaomtazama.Hivyo, tunaweza tukadharaulika na Mataifa menginekutokana tu na uchakavu wa majengo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na utaratibu wakubadilishana wafungwa, Je. Serikali inasemaje juu yakuwarejesha Watanzania ambao wamehukumiwa kwamakosa mbalimbali duniani?

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika,usalama wa Watanzania wanaoishi nchi za nje, suala hililimekuwa na changamoto kubwa sana kwa Watanzaniawenzetu wanaojishughulisha na mambo mbalimbali ikiwemokutafuta kazi za ndani na masuala mbalimbali yanayohusianana biashara. Wanapopata matatizo wanaobeba jukumu nindugu zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutumia diplomasia kwawafungwa kwenye magereza zilizopo nje ya nchi kuwaombawaje watumikie kifungo kwenye nchi yao kwa maana yaTanzania ili kuendelea kujenga ushirikiano mzuri. Kutumiabalozi zetu kunufaisha Taifa letu. Serikali ifuatilie kwa karibuutendaji wa Mabalozi na kuwapa semina elekezi kwakutazama uhitaji wa Taifa letu kwa wakati huo nakuwakumbusha wajibu wao ili Taifa letu liweze kunufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la diplomasia yauchumi; jambo hili ni vyema likapewa kipaumbele kwa kuwaTaifa letu bado linakua na kujenga ukaribu kwa mataifaambayo ni marafiki zetu ili kukuza uchumi wa Taifa letu.Kutumia diplomasia Serikali itumie fursa hiyo kutafuta masokoya mazao ya biashara. Suala hili halijatunufaisha kama Taifakuwa na manufaa ni pale ambapo tutatumia nafasi hiyoinapotokea na ziada ya kutosha na tukawa na ziada.

Mheshimiwa Naibu Spika, lugha ya Kiswahili, suala hilitumelizungumza sana, nashauri Serikali kupitia diplomasiakushawishi nchi marafiki kutumia lugha ya Kiswahili ambayoitasaidia kwa Taifa letu kwa wakufunzi ambao watakuwaWatanzania na kama Taifa tutanufaika kwa kupata ajira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutumia Ziwa Tanganyika,Victoria na Ziwa Nyasa kwa kuwa mazingira haya kushirikianakatika uvuvi ni vyema kama Taifa tukawa na uvuvi wa kisasautakaoleta tija kwa Taifa letu badala ya kuchoma nyavuzetu za wavuvi. Kutumia Watanzania wanaoishi nje ya nchi

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

kunufaisha Taifa letu. Tukiwatumia vizuri Watanzania hawakatika biashara na katika elimu tutapata manufaa makubwahasa pale ambapo na wao watatambua kuwa Taifalinatambua uwepo wao kule waliko.

Mheshimiwa Naibu Spika, waliopelekwa kusoma njeya nchi, Serikali kupitia ubalozi watumie nafasi zao kushawishina kuomba wanafunzi hawa kupunguziwa ada au kufutiwakabisa ili kuwatia moyo wazazi na walezi ambao wamejitoleakuwapeleka watoto au ndugu kusoma nje ya nchi kwani nikwa manufaa ya nchi nzima.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afyanjema. Pia nawatakia Waislam wote Tanzania na dunianikwa ujumla Heri na Baraka ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mahusiano ya Kimataifa;Tanzania bado ni nchi inayotambulika kuwa bado amanina utulivu unapatikana, lakini kadri siku zinavyokwendambele Tanzania inapoteza heshima na umuhimu tunaopewana dunia. Mfano, moja, demokrasia inaminywa kwakutoruhusiwa mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mbili, maiti zinazookotwakatika mito na fukwe za bahari na mito na Serikali kupitiaWizara ya Mambo ya Ndani, Waziri Mwigulu Nchembaanajibu bila shaka hao maiti ni wahamiaji haramu. Napatashaka dunia itatuelewaje Watanzania? Je, wahamiajihawatakiwi au tumepitisha sheria ya kuwaua hao wahamiajiharamu?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Waziri MheshimiwaDkt. Mahiga alijibu Bunge na kutoa tafsiri sahihi kwa kuwabadala yake Watanzania waishio nje ya nchi (Diasporas)wanaweza kudhuriwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania waliofungwanje; katika nchi nyingi duniani, Watanzania katika kutafutamaisha, wanapatikana na hatia mbalimbali kama vile:-

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

(a) Kuishi bila ya “Permit” au “overstay” baada ya VISAkuisha na kufungwa magerezani.

(b) Wanaotuhumiwa kujihusisha/kushirikiana nawafanyabiashara wa dawa za kulevya. Mfano, familia yaTanga iliyokamatwa China na mtoto wao wa miaka mitatukurudishwa nchini kutokana na tuhuma za dawa za kulevya.

(c) Wanaokwenda kutafuta ajira za viwandani,mashambani na majumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali, je, Serikali ina mpangogani wa Kidiplomasia wa kubadilishana wafungwa iliwarejeshwe Tanzania kuhukumiwa kwa Sheria zetu?

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanja vya Ubalozitunavyovitelekeza; kwa masikitiko makubwa, natoa hojahii nikiwa bado nashangaa kuwa Serikali ya Kifalme yaOman imetupa Kiwanja “Low Density” huko Muscat, lakinimpaka leo tumeshindwa kukijenga. Nashauri Serikaliitafute fedha na kujenga na kuondoa aibu hii inayochafuaTaifa letu.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa NaibuSpika, Serikali imefikia wapi juu ya suala la mpaka eneo laZiwa Nyasa baina ya nchi yetu na Jamhuri ya Malawi. Sualahili limekuwa ni la muda mrefu sana na hakuna ufumbuziuliofikiwa juu ya suala hili la mpaka. Naomba kufahamu sualahili limefikia wapi? Naomba Mheshimiwa Waziri wakatianahitimisha mjadala tupate ufafanuzi wa kina juu ya mahaliwalipofikia katika maamuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Ludewaambayo imepakana kwa eneo kubwa na nchi ya Malawikuliko Wilaya za Kyela na Nyasa lakini hatuna customsambazo zingerahisisha kwa watu wanaosafiri kwendaMalawi badala ya kupitia Kyela ambako ni mbali na kunaletausumbufu mkubwa kwa wananchi wanaotaka kusafirikibiashara na kushindwa kulitumia soko la nchi jirani. Wilayaya Ludewa ni eneo zuri kwa uzalishaji wa mazao ya biashara

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

kama mahindi, maharage, chai, pareto, alizeti na kadhalika.Kuna umuhimu wa kuwa na bandari na TRA kurahisishamienendo ya watu na bidhaa.

MHE. KHADIJA HASSAN ABOUD: Mheshimiwa NaibuSpika, naipongeza Wizara, Mheshimiwa Waziri, Naibu Wazirina watendaji wote wa Wizara, Mabalozi wetu wotewanaowakilisha Tanzania kwa jitihada kubwa ya kuitangazanchi yetu pamoja na kuitafutia misaada mbalimbali kwamaendeleo ya nchi yetu na wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, michango na ushauri:-

Mheshimiwa Naibu Spika,Wizara hii ipelekewe fedhakwa wakati ili kutekeleza majukumu yake kwa mudamuafaka. Pia fedha za maendeleo ziongezwe ili kutekelezamiradi mingi ambayo inahitajika kwa muda huu na baadayekwa maslahi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema Serikali yaMuungano ijenge jengo jipya la Ofisi ya Mambo ya Nje hukoZanzibar. Serikali iombe kiwanja kwa SMZ na ijenge jengojipya na la kisasa kulingana na kazi na mahitaji husika.

Mheshimiwa Naibu Spika,Wizara iendelee na juhudiza kuwatafutia ajira vijana wa Tanzania nchi za nje na Taasisinyingine za Kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania waishio nchiza nje ambao wamepata mafanikio na maendeleomakubwa, wahamasishwe zaidi kuja kuwekeza nchini kwaoTanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Balozi zetu ziongezewefedha il i kukabiliana na changamoto mbalimbalizinazojitokeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itenge fedha kwamadhumuni ya kufanyia matengenezo Balozi zetu nchi zanje.

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na naunga Mkonohoja. Nawatakia utekelezaji mwema wa majukumu ya kazina kulitumikia Taifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba Wizara hii muhimu niwatakie masuala yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Israel, sera yetu yamambo ya nje siku na katika Awamu zote Nne zilizotangulia,zilikuwa rafiki wa kweli wa Israel na Palestine. Awamu yaTano imefungua Ubalozi kwa mbwembwe zote Israel. Je,wanajua mlivyoikwaza the Arab World!

Mheshimiwa Naibu Spika,Morocco/Western Sahara,awamu hii imefungua Ubalozi Algeria. Hii ni sawa, lakiniwakati huo huo wanafunga ndoa ya rafiki na unafiki naMorocco. Algeria ndiyo mtetezi wa Sahara Magharibi. Mbinuzetu za ukombozi zimeishia wapi? Morocco ilikuja mwakajana na kuweka mikataba 21, iko wapi sasa? Waziri atuelezemikataba yote imefika wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua hamna kitu, Mfalmewa Morocco alikuja kwa nia ya kuishawishi Serikali iungemkono azimio la ombi la Morocco kurejea AU na siyovinginevyo. Mengine yote yalikuwa danganya toto. Mbayazaidi ukikutana na watu wa Morocco utasikia Dkt. Mahigamtu wetu, Dkt. Mahiga mtu wetu. Sasa hapa ni Dkt. Mahigaau ni Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, ushiriki hafifu wa nchi katikamikutano ya kimataifa na kimkakati. Safari za nje kwaMheshimiwa Rais kuzikatisha amechemsha, Watanzania sasalazima tumlazimishe Mheshimiwa Rais kuhudhuria mikutanomuhimu. Mwaka huu tumlazamishe aende UN akahutubieUmoja wa Mataifa tufurahi kwa kuwakilisha nchi yetu nakupata fursa mbalimbali. Haiwezekani Mheshimiwa Rais aweametembelea Rwanda na Uganda tu miaka yote hii, tukiulizatunaambiwa ni kubana matumizi, hapana! Siyo kweli. Ikuluna Wizara ituambie tu ukweli, kuna tatizo gani? Je ni lugha?Kama ni lugha si atumie Kiswahili tu kwanza atakuwa

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

anakuza na kuitangaza lugha yetu. Je, ni afya? Je, niusalama wake anahofia au ni majukumu? Katika haya yotesioni sababu labda kama ni ya kiafya.

Mheshimiwa Naibu Spika, msiba wa Winnie Mandela,kwenye msiba huu katika nchi yenye mahusiano mazuri ni sisitangu enzi hizo hatukuweza kupeleka mwakilishi. Ajabu nchizote za SADC zilituma wawakilishi, sisi Tanzania hatukwenda!Hii ni aibu sana!

Mheshimiwa Naibu Spika, je, kuna economicdiplomacy tena nchini? Ipi! Hakuna economic diplomacy,sasa kuna diplomasia ya miundombinu tu, ambayo nidiplomasia ya barabara na Bombadier!

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi amesikikaakisema kuwa kwenye vikao mbalimbali inapofika zamu yaTanzania kuongea basi watu wote walikuwa wanaachakwenda hata chooni, walikuwa na shauku ya kusikiliza. Sasani kinyume chake, sasa hawana shauku na kwa kweli hakunacha kusikiliza. Tumefika hapo? We are a laughing stock! Goneare the good days. Inachosha sana leo Bungeni tumeshangilianafasi walizopata wenzetu kwenye Bunge la Africa (PAP).Tumeshuhudia si Mheshimiwa Rais tu haudhurii bali hataMawaziri na mbaya zaidi Wabunge katika mikutano ya jimboambayo ni calendar meeting, hii sio sawa.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Ofisi za Balozi zetu,nashauri Serikali kujenga Ofisi zake katika Balozi zetu kwanifedha nyingi zinatumika kugharamia Ofisi hizi wakati kunaviwanja. Mfano, Msumbiji kuna eneo la kujenga natunashindwa kujenga. Tukope hata mikopo ya mashartinafuu ili ije ilipwe kwa fedha zile ambazo tungelipa kodi yamajengo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, uteuzi wa Mabalozi; nashauriSerikali kuangalia uteuzi unaofanyika kama unaendana na

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

faida tunazopata kutokana na uwekezaji huo katika Balozihizo. Ni kwa kiasi gani upimaji wa utendaji wa Balozi zetuukichukulia kuwa kuna malengo mahususi ya uanzishaji Balozihizo ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vya Tanzania ilikuwezesha Tanzania kupata wawekezaji.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nichangie katika hoja hii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kurejesha Wafungwa Nchini;naomba Wizara ishughulikie kurudisha Watanzaniawaliofungwa huko nje, kama vile Msumbiji, warejeshwenchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wanajeshi WanaofarikiKwenye Mapambano; kuna Wanajeshi wanaokwendakusaidia nchi nyingine kwa ajili ya ulinzi kama vile Congo nasehemu nyingine, wanapofariki kwenye mapambano hayofamilia zao zinasahaulika. Naiomba Serikali ihakikishe familiaza Wanajeshi hao zinapata huduma stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, Unyanyasaji wa MabintiWanaokwenda Kufanya Kazi za Majumbani Nje; naiombaSerikali ifuatilie wale wote wanaowasafirisha mabinti kwendanje kufanya kazi za ndani, wachukuliwe hatua kwa sababumabinti hao wanateseka sana na wengine wanakufa nahawapati masaada wowote.

Mheshimiwa Naibu Spika, Upungufu wa MaafisaKwenye Balozi; Maafisa kwenye Balozi zetu hawatoshi.Naiomba Serikali ijitahidi kupeleka maafisa katika balozi zetuzote.

Mheshimiwa Naibu Spika, Viwanja Visivyoendelezwa.Kuna viwanja ambavyo havijaendelezwa basi viendelezwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. HAMOUD A. JUMAA: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kunifikishamahali hapa salama ili nami nichangie hotuba hii muhimu

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikiya Mwaka wa Fedha 2018/2019. Naipongeza Wizara pamojana wataalam wake kwa kuandaa bajeti nzuri. Bajeti hiiitatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikishanchi yetu inaimarisha ushirikiano na mahusiano mazuri namataifa mengine duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali kwajuhudi mbalimbali inazochukua katika kuimarisha mahusianoyetu na mataifa mbalimbali duniani, ni hatua nzuri na yakupongezwa, hatua hiyo italiwezesha Taifa kufaidika namasuala mbalimbali ya kimaendeleo na mataifa hayo.Juhudi hizo zitasaidia pia kulitangaza Taifa letu nakuvitangaza vivutio vyetu na kuvutia watalii, wawekezajikuja nchini kuangalia fursa mbalimbali tulizokuwa nazo zakiuwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ya kufungua ubalozimpya nchini Israel ni ya kupongezwa. Taifa hilo limepigahatua kubwa kimaendeleo, uchumi, viwanda na teknolojia.Ubalozi huo utatuweka karibu, kushirikiana katika masualambalimbali ya kimaendeleo. Naishauri Serikali kupitia Wizarahii kuwakumbusha Mabalozi wetu wote wanaotuwakilishakatika nchi mbalimbali, kutumia fursa hiyo kuvitangazavivutio vya kitalii tulivyo navyo na fursa mbalimbali zakiuwekezaji zilizopo nchini, hatua hiyo itasaidia sana kunufaikakama nchi kwa sekta husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Umoja wetu wa AfrikaMashariki unazidi kuimarika na kuleta taswira nzuri yakimaendeleo. Watu wetu wanaendelea kufaidika naushirikiano huo kwa kiasi kikubwa, wafanyabiashara wetuwanavuka mipaka na kushirikiana na wenzao katika biasharambalimbali. Hii ndiyo dhana ya ushirikiano huu ambao unatija kwa kila Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto hazikosekani,hivyo naishauri Serikali kuziangalia kwa jicho la pekeechangamoto zote na kuzipatia ufumbuzi ambao utaletamalengo chanya kwa mataifa yote wanachama.

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangukatika Wizara hii muhimu ambayo ni kioo cha nchi yetu katikauso wa kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na ukarimu kwakuendelea kutupa ruhusa ya kupumua pamoja na maudhitunayomfanyia kama binadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya utangulizi huonaanza na mchango wangu kwa kujielekeza hasa katikaukurasa wa 14; kuhusu Diplomasia ya Uchumi. Tanzaniatunategemea kilimo kwa chakula, ajira, biashara namalighafi, lakini tatizo kubwa ni masoko ya uhakika na yenyebei nzuri na tija kwa wakulima wetu. Kwa mfano, zao lambaazi kukosa soko mwaka jana 2017/2018 na bei yakekuanguka kutoka 2,000 ya mwaka 2016/2017 na kufikia 150kwa kilo moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii imeathiri uchumi wa Taifana kipato cha wakulima wetu na kusababisha hasarakubwa. Pia imeleta madeni katika taasisi za fedha zikiwemobenki na SACCOS ambako waliwalichukua mikopo kwa ajiliya kuongeza uzalishaji wa mbaazi kuzingatia bei nzuri naushindani wa soko kwa msimu wa mwaka uliopita.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu ina ardhi kubwana faida ya kijiografia katika mikoa mingi katika uzalishajiwa mbaazi ikiwemo Morogoro, hasa Morogoro Vijijini, Kilosa,Turiani na Ifakara na mikoa mingine kama Arusha, Manyara,Shinyanga, Pwani, Lindi na Mtwara ambayo ilikuwa inatoaajira, chakula na kuongeza vipato vya watu wetu; ukizingatiakwamba zao hili la mbaazi kilimo chake hakina gharamakubwa na usumbufu mkubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, zao hili si la kupuuza nakuliacha kwa sababu lina fursa nyingi za kiuchumi, lakini tatizo

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

kubwa ni soko lake, kwamba linategemea jamii moja tu nasehemu moja ambayo ni India. Kutokana na kutegemea sokomoja wakulima wetu wanaathirika zaidi kwa sababumabadiliko yoyote ya sera ya soko hilo au uzalishaji mzuri wambaazi wa India kunaathiri soko la mbaazi la wakulima wetunchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina ushauri katika Wizarahii katika Diplomasia ya Uchumi kutafuta soko la mbaazikabla ya msimu kuanza katika nchi ya India na hasa mnunuzimkuu ambaye ni Serikai ya India ili kuwa na uhakika wa sokona bei nzuri kwa wakulima wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuishauri Serikalikuingia mkataba wa ununuzi na Serikali ya India kutoka kwetukwa bei ya kiasi ili kutumia vizuri Diplomasia ya Uchumi nakuongeza fedha za kigeni na kipato kwa wakulima nakuepuka hasara kama mwaka jana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika,nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasiya kutoa mchango wangu katika hotuba ya Waziri waMambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Aidha,napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri na watendajiwake wote kwa kutayarisha na kuwasilisha kwa umakinimkubwa hotuba hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotubahii napenda kutoa mchango wangu katika maeneoyafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Uwakilishi wa Tanzaniakatika Mabunge ya Nje. Napenda kuchukua nafasi hii kutoapongezi zangu za dhati kwa Waheshimiwa Wabunge wetuwaliopata nafasi ya kuteuliwa katika nafasi kwenye Bungela Afrika. Wabunge hawa wameonesha uwezo mkubwakatika nyanja za kimataifa na kuonesha kuwa Tanzania tunaowatu ambao wanaweza katika maeneo ya kimataifa.

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na matokeo hayoya kihistoria yaliyopatikana bado juhudi za uwakilishi wanchi yetu katika Mabunge hayaridhishi kidogo. Badokunakosekana uwakilishi katika Mabunge kadhaakwenye mikutano ya Mabunge. Najua kuwa hali yauchumi wa nchi yetu bado haijatengemaa vizuri, lakininaiomba Serikali kulipa umuhimu wa kipekee jambo hili lauwakilishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Utafutaji wa Misaada kwaAjili ya Miradi ya Maendeleo. Napenda kuipongeza Serikaliyetu kupitia Wizara hii kwa namna wanavyochukua juhudiza kutafuta misaada kwa wafadhili kwa ajili ya miradi yamaendeleo. Jambo la kutafuta misaada ni jambo la kawaidakwa nchi nyingi ulimwenguni.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu katikajambo hil i ni kwamba, ni vyema Wizara ikawa nawafanyakazi wenye ujuzi wa aina zote hasa za mikataba yamiradi hiyo pamoja na biashara. Hii itatuepusha na ujanjawa mitego ya kisheria za mikataba ambayo mara nyingibaadhi ya wafadhili huwa wanaitumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. OTHMAN OMAR HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,Maendeleo ya Utumishi Wizarani. Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Wizara ya Muunganowa pande mbili za Tanganyika na Zanzibar. Wizara imekuwaikilalamikiwa kwa kutotenda haki kwenye masuala yautumishi ndani ya Wizara. Watumishi walio wengi ni waupande mmoja wa Muungano. Wakati Wazanzibariwanapohoji Mawaziri wenye dhamana huwa wanatoa hojaya kuwa utumishi huhitaji weledi na vigezo. Je, Wazanzibariwamekosa sifa hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Mikutano chaKimataifa (AICC). Wakati AICC inatimiza karibu miaka 40tangu kuanzishwa kwake, kimekuwa kikifanya uwekezajimkubwa upande wa Tanzania Bara pekee. Pamoja na

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

miradi hiyo iliyopo sasa hivi AICC bado ina malengo yakujenga kituo kikubwa cha mikutano cha Mt. KilimanjaroInternational Convention Center nyingine katika eneo la Jijila Dodoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu mazingira yauwekezaji kwa shughuli za AICC yaliyoko yanaruhusu, nisababu zipi zilizofanya Wizara isifanye uwekezaji katika Visiwavya Zanzibar? AICC kutowekeza Zanzibar ni kuwanyimaWazanzibari fursa za kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kutafuta Wawekezaji Njeya Nchi. Miongoni mwa kazi ya Wizara ni kusimamia balozizetu katika kutafuta wawekezaji, fursa za ajira, nafasi zamasomo kwa bidhaa zetu. Wawekezaji wengi kutokanje ya nchi wamekuwa wakija kuwekeza hapa nchinilakini kwa bahati mbaya wanaishia Tanzania Bara pekee.Ni kwa nini Wizara hii haiwaongozi wawekezaji kutokanje kuwekeza katika visiwa vya Zanzibar kwa ajili yakuimarisha uchumi wa visiwa hivyo ambao unadorora?Niombe Wizara isifanye upendeleo katika kufanya kazizake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Changamoto za UtawalaBora Zilizobainishwa na APRM. APRM inaamini kwambaTanzania ina tatizo la kutozingatia utawala bora naunaokubalika kwa wananchi wake. Hii imetokana hasa paleTanzania inapominya uhuru wa Wazanzibari wa kuiwekamadarakani Serikali wanayoitaka wenyewe. Serikali yaZanzibar iliyopo madarakani sasa hivi si chaguo la wananchiwa Zanzibar, ni Serikali iliyowekwa kwa nguvu za dola, hivyobasi Serikali hii si halali.

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe tu Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania itoe ripoti kwa APRM kwambaTanzania haiwezi Mfumo wa Vyama Vingi kwa sababuChama cha Mapinduzi hakiko tayari kukabidhi madarakapale wanaposhindwa kwenye uchaguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaingiaupande wa Serikali na tunaanza na Mheshimiwa Dkt. SusanKolimba dakika tano, Mheshimiwa Balozi ajiandae.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANOWA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusayako naomba nimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipaafya na uzima na kuweza kusimama mbele yako nakuchangia katika hoja hii ambayo Waziri wanguameiwasilisha leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchukua nafasihii ya kipekee kama wenzangu walionitangulia kumshukuruna kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uongozi wakemadhubuti. Vilevile nimpongeze pia Waziri wangu ambayenafanya naye kazi kwa karibu kwa kazi nzuri anayoifanyakuitetea Tanzania kuisemea, kujenga mahusiano kati ya nchimbalimbali na kuhakikisha kwamba diplomasia ya kiuchumiinatekelezwa ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kwa sababu yamuda nimshukuru kwa namna ya kipekee mume wangumpendwa Dkt. George Ayese Mrikalia kwa uvumilivu waokwangu pamoja na familia yangu watoto wawili wanajuakwamba nimepewa kazi na mimi nimekubali, tutapambanampaka kieleweke. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya mudanaomba niende moja kwa moja kwenye hoja ambazozimetolewa na Waheshimiwa Wabunge najua kwambahatutaweza kuzijibu hoja zote, lakini tunaahidi kwamba kwaniaba ya Wizara tutaweza kuzijibu kwa maandishi nakuzikabidhi kwao. Nikienda kwenye hoja ambazo zilikuwazimetolewa na Waheshimiwa Wabunge hasa kwenye Kamatinitajibu tu baadhi ya hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa kuna suala laKamati kutushauri kuhusu kuandaa sera ya Taifa ya diaspora.Nasema kwamba Wizara imeunda timu mahususi i l ikufanikisha uandaaji wa sera hii ya Taifa ya diaspora

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

itakayoainisha mikakati na kutoa mwongozo kuhusu ushirikiwa diaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi. Timu hiyotayari imekwishaanza hatua za awali za maandalizi ya serahiyo. Pia Wizara imetenga fedha kwa mwaka huu kwenyebajeti ya mwaka 2018/2019 kwa ajili ya zoezi hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuhusu kuongezakasi ya kukamilisha mchakato wa sera mpya yaani ReviseForeign Policy, niseme tu kwamba Wizara imekamilishakuandaa rasimu ya Sera hiyo Mpya ya Mambo ya Nje yaTanzania, lakini hatua inayofuata sasa ni kuandaa mkakatiwa utekelezaji ambao pamoja na rasimu ya sera hiyovitawasilishwa kwa wadau kwa maana ya Serikali na sektabinafsi ili kupata maoni yao na Wizara imetenga fedha kwaajili ya zoezi hili ya bajeti ya 2018/2019 kwa ajili ya kukamilishasera hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, niruke kidogo niende kwaMheshimiwa Masoud ambaye alizungumzia kuhusu walewafungwa 11 ambao wako kwenye gereza lile la BEO kuleMsumbiji niseme tu nimeshakwisha wasiliana na Mbungewao ambaye alikuwa anafuatilia hilo na tumewasiliana naBalozi wetu kule Msumbiji. Alimtuma Afisa kwendakuangalia wiki mbili zi l izopita, pia juzi alienda yeyemwenyewe na anasema tu kwamba anasubiria taratibu zakimahakama watakavyomaliza process za kuandaa kila kitututakuwa tunaendelea kumtaarifu Mbunge husika nakuhakikisha kwamba maslahi ya wale Watanzaniayanalindwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, nimpongezesana Mheshimiwa Masoud kwa kuhakikisha kwambaanafuatilia masuala ya Watanzania wakiwemo Watanzaniaambao yeye ni Mbunge wao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nikienda kwenye sualalingine ambalo pia limetolewa na Kamati kwa kushauriWizara ambalo linahusu kuhusu upatikanaji wa fedha zaujenzi wa majengo ya ubalozi na makazi katika Balozi zetu.Suala hili limekwishaongelewa sana kwenye hotuba ya

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

Mheshimiwa Waziri na mikakati tuliyokuwa nayo mkakati wakwanza wa miaka 15 ambao ulikuwa ulioanza mwaka wafedha 2002/2003 mpaka mwaka wa fedha 2016/2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia sasa hivitumetengeneza mkakati mpya ambapo tumejaribukuangalia kuhakikisha kwamba suala la kutengenezamkakati wa upatikanaji wa fedha na ujenzi pamoja naukarabati wa Balozi zetu zilizoko nje unafanyika kwa harakaiwezekanavyo. Tutaendelea kulisimamia hilo na kufuatiliakwenye Wizara ya Fedha na kwa vile Wizara ya Fedhapamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ni Serikali basi nadhaniMungu atatusaidia na tutaweza kufikia mahali pazuri.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iangalie uwezekanowa kuziruhusu Balozi kubakiza angalau asilimia 40 yamakusanyo kwa maana ya maduhuli ili ziwezeshe kutekelezamajukumu yao kwenye Balozi husika; hili suala ni la kanunina sheria. Tutajaribu kuangalia kukaa pamoja na Wizara yaFedha na kupata ushauri wao wa kitaalam na kama sheriazitakuwa zinaruhusu basi sisi tuko tayari kupokea ushauri waKamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi ni wasikivu kamamnavyoona, tumetekeleza yale ambayo tumefanya,mmesema tufungue Counsel tumefungua, mmesematufungue Balozi Cuba, tumefungua; lakini mmesema kwambatuhakikishe jengo letu la Maputo linajengwa nakukarabatiwa na watu wanahamia, tumefanya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa sekunde 30, muda wakoumekwisha.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANOWA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, naombaniunge mkono hoja ya Waziri wangu. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Balozi Dkt.Augustine Mahiga, mtoa hoja.

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, naombanitumie muda uliobakia kujibu baadhi ya maswali ambayonimeyasikia kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, ni lile linalohusuhaki za Wapalestina na watu wa Western Sahara. Katikahotuba yangu nimesema misingi ya Tanzania katika Jumuiyaya Kimatifa ni kuheshimika, kuthamini utu na kulinda uhuru.Kama hilo ndio letu inafuata kwamba wale ambaowamenyimwa uhuru, wamenyimwa utu, lazimawashughulikiwe na wapate haki zao. Sasa sisi kama Tanzanialazima tufanye mambo matatu; la kwanza, tutambuekutokuwepo kwa haki hizo kwa watu huku duniani maanayake kama tunalitaka sisi na tunataka wenzetu wapate nahilo hatuwezi kuliacha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sisi wenyewe Tanzaniatumesema ili hilo lipatikane lazima iwe ni diplomasia ya siasana diplomasia ya siasa kusaidia nchi moja au nyingineinapatikana kwenye majukwaa ya kimataifa. Utazungumziauhuru na haki na heshima ya Wapalestina au ya WesternSahara kwenye majukwaa muda umepita. Wakati ambapokutetea haki za Afrika Kusini au Msumbiji au Namibia tulisematutatumia silaha hatutumii silaha tena, tunasema tutaongeana moja ya silaha zetu ni kwamba tutashiriki kikamilifu katikamijadala ya kimataifa katika majukwaa mbalimbali kuhususuala la Palestina na suala la POLISARIO. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini wakati huo huo tunadiplomasia ya uchumi; wagomvi wa Palestina ni wa Israeli.Sasa hawa wa Israeli katika diplomasia ya uchumi kuna vitupale tunaweza kuvipata na sisi tumesema hayoyanayozungumza kuhusu haki za wa Palestina tuyapelekekwenye vikao, majukwaa ya kimataifa, Tanzania ni pekeyake ilikuwa nchi ya kwanza kuipa Palestina diplomaticstatus hakuna nchi nyingine. Hiyo baada ya Mwalimu Arafationdoa majeshi yako Uganda alipoondoa majeshi Ugandawakati wa vita akasema tutawapa diplomatic status.(Makofi)

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi ni watu wa kwanza nanilifanya makusudi kwamba Trump anapokwenda kufunguaJerusalem mimi nafungua Tel Aviv kwa sababu hilo nikutambua kwamba Jerusalem ni mji wa utata. Nilipokwendakule kwa makusudi nilisema nipelekeni Gaza Strip pale kwenyekivuko nikaona pale na nimewaambia Waisrael kimachomacho nikasema this is a time bomb lazima muishughulikiesuala hili tulizungumze. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika resolutions 12 zaUmoja wa Mataifa kuhusu Palestina na kuhusu Israelinimewaambia pande zote mbili na umoja wa Mataifawanakubali kwamba tukae tutazame kwamba kunaresolution nyingine zimepitwa na wakati na tufanye zoezi hilotutazame lakini hatutaweza kuacha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Kabwe leokatika hotuba yangu nimeanza na aya inayosema POLISARIOna imeishia maneno ya POLISARIO sijawasahau. Ni kwelikwamba suala hili linazungumzwa mbele ya Umoja waMataifa, lakini maadam tumewaambia Morocco warudindani ya Afrika suala hili litaongezewa tija zaidi kama piaAfrika itachangia. Nadhani suala hili sio rahisi kihivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, wakati huo huoMorocco ni nchi yenye uchumi mkubwa ya tano ndani yaAfrika, sio uwanja tu wa ndege au uwanja wa mpira austadium, lakini kuna maeneo hasa katika diplomasia yakutengeneza mbolea na utalaam na mafunzo ambavyotunaweza kupata. Hiyo haitatuzuia katika majukwaa yoteAfrika and non-aligned countries au Umoja wa Mataifakuwaambia jamani hili suala tulishughulikie kwa pamoja.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la diplomasia yauchumi uliojikita kwenye viwanda ili uwe na viwanda navinavyofanya kazi kuna mambo manne muhimu. La kwanza,ni mtaji lazima kupata investors tupate pesa, kama zinatokahapa au zinatoka nje. La pili, huwezi kuwa na viwanda kamahuna energy, nishati ya kutosha, huwezi kuwa na viwanda

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

kama huna miundombinu mizuri na huwezi kuwa na viwandakama huna wataalam wanaoshika ule umeme na kufungana kufungua wale watalii wataalam na hatimaye lazimauwe na soko. Sisi katika kuandaa vijana wetu tumesema hayounapokwenda kule, hayo ndio uyafuate matano utafutepesa, mtafute wawekezaji, kwenye miundombinu, mtafutewatakaoshiriki katika nishati, watakaoweza kutoa mafunzona masoko ambayo lazima tuwe nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hili linaingia katikakutayarisha vijana wetu wanaokwenda nje kwa miaka miwilitumekuwa tunarudisha watu kuna wengine walikuwawanakaa miezi na miezi, miaka na miaka hawarudi,tumehakikisha kwamba Balozi zote zinatazamwa natunarudisha watu. Kurudisha watu ni fedha nyingi sana,tumerudisha 109 katika miaka miwili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaandaa kupelekavijana ambao wanafanana na haya matano niliyoyasema.Tayari tumeshawatambua na sasa hivi tuko katika ngazi yaupekuzi, lazima wapekuliwe na vyombo vinavyohusika kablahatujawapeleka. Natumaini hela nitakayopata kutoka bajetihii ndio itakayotumika kuwapeleka vijana katika vituo vyote.Wote majina yao tumeshayaandaa na tunasubiri wapatekibali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Umoja wa Mataifa ulizaliwamwaka 1945, leo una wanachama 193. Katika 193 chombochenye nguvu kupita vyote ni Baraza la Usalama na Barazala Usalama lina watu wa kudumu Mataifa matano Marekani,Uingereza, Ufaransa, Urusi na China. China isingeingia SecurityCouncil bila Tanzania, kabla ya mwaka 70 China ilikuwainawakilishwa na Taiwan au Formosa au Sheing Tang Sheinglakini sisi Mwalimu akasema haiwezi kuwa Umoja wa Mataifabila China. Hivyo ikarudi na ndio tuliiweka kule kwenyeSecurity Council.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya mageuzi yamwisho yalifanyika mwaka 1963 kuongeza Baraza la Usalamakutoka tisa kufika 15, tangu mwaka 1963 hakujawa na

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

mabadiliko. Sasa kuna aina nyingine ya mabadilko, kunawale wanaosema tuingie na tupewe turufu na hao niwakubwa Japan, Brazil, German...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri dakika mojaumalizie.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, sawa basi nikwamba hayo mageuzi Afrika nayo inadai ipewe haki kamahizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge kwa mchango wao. Maswali menginimeyapata na mengi tutayajibu kwa maandishi na hayayataleta tija sana katika kuboresha, kuna mengine ambayolazima niseme wazi hatuwezi kuyafanya bila nyinyi kutusaidiakupitisha bajeti hii ili tuweze kuendeleza vizuri zaidi kwapamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipanafasi hii. Baada ya kusema hayo, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, naafiki.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabungehoja imeungwa mkono. Katibu.

NDG. YONA KIRUMBI - KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 34 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki

Kif.1001- Administration and HRM……..…Sh.23,914,247,000/=

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa mujibu wakanuni ya 104(1) naongeza nusu saa. Sasa nitawahoji, kuhusukifungu kilichotajwa hapo juu.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

kif. 1002 - Finance and accounts ……………Sh.993,726,000/=Kif. 1003 – Foreign affairs office Zanzibar…..…Sh.840,334,000/=Kif. 1004 – Policy and Planning ……………Sh.1,332,414,000/=Kif. 1005 – International Cooperation…..…Sh.1,000,950,000/=Kif. 1006 – Europe and America ……….……Sh.667,956,000/=Kif. 1007 – Asia and Australia ..………………Sh.703,969,000/=Kif.1008 – Africa ..………………………….Sh.1,889,751,000/=Kif. 1009 – Regional cooperation ……………Sh.766,223,000/=Kif. 1010 – Protocol …………………………Sh.8,557,024,000/=Kif. 1011 – Legal service..…………………...Sh.2,175,611,000/=Kif. 1012 – Government communication unitSh.464,403,000/=Kif. 1013 – Middle East Division ………………Sh.567,591,000/=Kif. 1014 – International audit unit...………...Sh.403,640,000/=Kif. 1015 – Procurement management Unit…Sh.649,580,000/=Kif. 1016 - Information and Com. TechnologySh.418,139,000/=Kif.1017 - Diaspora Engagement

and Opportunity.............................Sh.618,397,000/=Kif. 1018 – Economic Infrastructure and

Social Support Service…................Sh.759,689,000/=Kif. 1019 – Political defense and Sec. Affairs....Sh.687,626,000/=Kif. 1020 – Trade investment and productive

sector division.............................….Sh.707,658,000/=Kif.1021 – Embassy of Tanzania –

Addis Ababa.................................Sh.2,632,428,000/=Kif 2002 - Embassy of Tanzania Berlin…..….Sh.3,414,752,000/=Kif. 2003 – Embassy of Tanzania – Cairo..….Sh.1,648,331,000/=Kif. 2004 – Embassy of Tanzania- Kinshasa ..Sh.1,955,480,000/=Kif. 2005 – High Commission of

Tanzania – Abuja Sh........................2,698,660,000/=Kif. 2006 – High comm. of TZ – London..……Sh.3,792,141,000/=Kif. 2007 – High Comm. of TZ – Lusaka..........Sh.1,420,114,000/=Kif. 2008 – High Comm. of TZ – Maputo.…..Sh.1,625,383,000/=Kif. 2009 – Embassy of Tanzania–Moscow....Sh.3,359,266,000/=

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

Kif. 2010 – High Commission of TZ– New Delh...............................…Sh.2,999,406,000/=

Kif. 2011 – Permanent Mission to the UN – New York............................ Sh.5,399,267,000/=

Kif. 2012 – High Comm. of TZ –Ottawa…….Sh.2,652,964,000/=Kif. 2013 – Embassy of Tanzania –Paris .……Sh.3,027,266,000/=Kif. 2014 – Embassy of Tanzania Beijing .…...Sh.3,428,158,000/=Kif. 2015 – Embassy of Tanzania –Rome.…..Sh.4,175,232,000/=Kif. 2016 – Embassy of Tanzania –

Stockholm..................................Sh.3,596,012,000/=Kif. 2017 – Embassy of Tanzania – Tokyo..…. Sh.3,133,070,000/=Kif. 2018 – Embassy of Tanzania –

Washington............................. Sh.4,414,961,000/=Kif. 2019 – Embassy of Tanzania – Brussels.....Sh.2,999,051,000/=Kif. 2020 – Permanent Mission to the

UN-GENEVA...................................Sh.6,146,258,000/=Kif. 2021 – High Commission of Tanzania –

Kampala.......................................Sh.2,309,551,000/=Kif. 2022 - High Commission of Tanzania –

Harare..........................................Sh.1,673,975,000/=Kif. 2023 – High Commission of Tanzania –

Nairobi.........................................Sh.4,486,684,000/=Kif. 2024 - Embassy of Tanzania Riyadh …… Sh.3,099,463,000/=Kif. 2025 - High Commission of Tanzania –

Pretoria.......................................Sh.3,215,352,000/=Kif. 2026 - Embassy of Tanzania- Kigali .....…Sh.2,047,230,000/=Kif. 2027 - Embassy of Tanzania- Abudhabi..Sh.3,450,132,000/=Kif. 2028 - Embassy of Tanz.- Bujumbura.......Sh.1,718,702,000/=Kif. 2029 - Embassy of Tanzania- Muscat..... Sh.2,627,554,000/=Kif. 2030 - High Commission of Tanzania –

Lilongwe........................................Sh.1,549,824,000/=Kif. 2031- Embassy of Tanzania- Brasilia ……Sh.3,404,104,000/=Kif. 2032- High Commission of Tanzania –

Kualalumpa..............…………… Sh.2,179,889,000/=Kif. 2033 - Embassy of Tanzania- The Hague Sh.2,963,353,000/=Kif. 2034 - Embassy of Tanzania- Morocco…Sh.1,893,979,000/=Kif. 2035 - Embassy of Tanzania- Kuwait……Sh.1,567,422,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, aliyewashamic, azime.

Kif. 2036 - Embassy of Tanzania- Algiers….Sh.2,402,105,000/=Kif. 2037 - Embassy of Tanzania- Ankara…...Sh.2,531,037,000/=Kif. 2038 - Embassy of Tanz. - Khartoum........Sh.2,114,141,000/=Kif. 2039 - Embassy of Tanzania- Seoul.……. Sh.4,092,976,000/=Kif. 2040 - Embassy of Tanzania- Tel-Aviv......Sh.2,620,398,000/=Kif. 2041 - Embassy of Tanzania- Doha……..Sh.2,100,178,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 34 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki

Kif. 1004- Policy and Planning……………… Tsh.10,400,000,000Kif. 2010- High Commission of Tanzania – NewDelhi ……….. 0

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

NDG. YONA KIRUMBI – KATIBU MEZANI: MheshimiwaNaibu Spika, naomba kutoa taarifa kwamba Kamati yaMatumizi imekamilisha kazi yake.

MWENYEKITI: Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae, mtoahoja, taarifa.

T A A R I F A

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lakoTukufu limekaa kama Kamati ya Matumizi na kupitia

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

mapendekezo ya bajeti ya Wizara na kuyapitisha. Sasanaomba taarifa ya Kamati ya Matumizi ikubaliwe na Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, naafiki.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge hojaimeungwa mkono sasa kwa mujibu wa utaratibu wetu sasanitawahoji. (Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mamboya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2018/

2019 yalipitishwa na Bunge)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge nichukue fursahii kwanza kuwapongeza sana Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuweza kutuleteakama Bunge makadirio ya mapato na matumizi kwamwaka wa fedha 2018/2019 lakini pia wataalam ambaommefanya nao kazi. Tuipongeze pia Kamati yetu yaBunge ambayo imefanya kazi nzuri imetuletea,mapendelekezo mazuri na pia imeonesha namna ganiWizara inashirikiana na Kamati hii katika kusikiliza ushauriambao Bunge linatoa.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hivyo, nichukue fursahii kuwashukuru sana Kamati kwa niaba ya Bunge kwa kazinzuri mlioifanya. Pia Waheshimiwa Wabunge walipopatafursa ya kuchangia kwa maandishi na kwa kuzungumzahumu ndani, Waziri na Naibu wake wameahidi hoja hizozitajibiwa. Kwa hiyo, naamini kwamba itatuweka mahalipazuri kwa kuweza kuisimamia vizuri hii Wizara hii ili iwezekufanya vizuri katika Nyanja za kimataifa, lakini hata hapanchini kwenye suala la diplomasia.

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

Waheshimiwa Wabunge, badala ya kuyasema hayo,ninayo taarifa ya Mheshimiwa Selasini anataka kuombamwongozo halafu nitaleta matangazo kabla hatujamaliza.Mheshimiwa Selasini.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru Bunge hili lilifanya uchaguzi wa wawakilishiwetu katika Bunge la Afrika na kama tulivyosikia ni kwambawenzetu wawili wamechaguliwa kuongoza katika nafasimbili tofauti na kubwa katika Bunge hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wako,Bunge hili tumewashangilia kwa nguvu wenzetu kwasababu wameliletea sifa Bunge na nchi. Hata hivyo,Wabunge wote wanne wamekuwa wakijitegemea katikakufanya shughuli zao, wamekuwa hawapatiwi tiketi,hawapatiwi fedha kwa namna yoyote. Kazi hiiwaliyoifanya wameifanya kwa nguvu zao. Naombamwongozo wako kama kweli hawa tunawahitajikutuwakilisha kama Bunge la Taifa, ni kwa nini Bungelinashindwa kuwahudumia il i waweze kufanya kazikikamilifu?

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mtakumbukaMheshimiwa Spika alipata kueleza kwa kirefu jambo hili hapaBungeni na sina lengo la kurudia maelezo aliyokuwaameyatoa kuhusu jambo hili. Mheshimiwa Selasini ameombamwongozo huo kuhusu wenzetu Wabunge wa Bunge la Afrikana yale ambayo Waheshimiwa Wabunge tumepata fursa leoya kushangilia ushindi wao kwamba wanajihudumiawakienda kutuwakilisha sisi kama Bunge, lakini pia kama nchikwenye Bunge la Afrika.

Sasa kwa sababu maelezo mahususi kuhusu jambohili si kwa Bunge tu la Afrika, lakini jambo hili la ujumla kwauwakilishi wa wa Wabunge kwenye vyombo vya huko nje,ambavyo huwa vinaenda kutuwakilisisha sisi kama Bunge,lakini pia kama nchi alishalitolea ufafanuzi. Huo ndiomwongozo wangu ufafanuzi aliotoa Mheshimiwa Spikaunaendelea kuwa hivyo.

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

Waheshimiwa Wabunge, nilete kwenu matangazoniliyonayo mezani sasa, Waheshimiwa Wabunge Mwenyekitiwa TWPG Mheshimiwa Magreth Sita anawatangaziaWaheshimiwa Wabunge wote, kwamba TWPG imeandaahafla ya uchangishaji fedha itakayofanyika hapa Dodomamwishoni mwa mwezi Juni, 2018 kwa ajili ya ujenzi wa vyoovya mfano katika Majimbo 264 ya uchaguzi nchini.

Waheshimiwa Wabunge, kwa kuwa shughuli hiiitawahusisha Waheshimiwa Wabunge wenyewe na MgeniRasmi anatarajiwa kuwa mmoja kati ya Viongozi Wakuu waNchi hivyo kumeandaliwa burudani mbalimbali ikiwepomaonesho ya mitindo, yaani fashion show, vichekesho,kuimba na kucheza mziki katika kunakshi siku hiyo, ikiwa nisehemu ya kuchangisha fedha.

Pia mwanamitindo maarufu hapa nchini HadijaMwanamboka atatoa mafunzo hapa Bungeni kwa ajili yakuwafundisha Waheshimiwa Wabunge miondoko yajukwaani kimitindo yaani catwalk. Hivyo basi, WaheshimiwaWabunge wote wanawake na wanaume, mnaombwakushiriki katika burudani hizo, kwa kujiorodhesha katika fomumaalum iliyopo katika meza ya mapokezi lango kuu lakuingilia Bungeni, leo tarehe 23 Mei, 2018 hadi tarehe 24 Mei,2018 hadi saa nne asubuhi.

Kwa hiyo mnaombwa mpitie hizo fomu WaheshimiwaWabunge ili mjiorodheshe, kila mtu atashiriki kwenye lipi katiya hayo. Pengine baadhi yetu tutakuwa tumeshashaurianatutashiriki kwenye lipi kuna wengine ni wazuri katikauchekeshaji, basi nadhani tutashauriana.

Waheshimiwa Wabunge, ninalo tangazo linginekutoka kwa Mheshimiwa Shally Raymond ambaye niMwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Thomas Moore, Bunge,anawatangazia Waheshimiwa Wabunge ambao ni WakristoWakatoliki kwamba mara baada ya kuahirisha shughuli zaBunge kutakuwa na ibada katika ukumbi wa Pius Msekwaghorofa ya pili. Aidha, Waheshimiwa Wabunge wengine wotemnakaribishwa kuhudhuria ibada hiyo.

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536903365... · Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema haya,naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho asubuhi saa tatutarehe 24 Mei, 2018.

(Saa 7.40 Mchana Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaAlhamis, Tarehe 24 Mei, 2018, Saa Tatu Asubuhi)