351
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 10 Mei, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wetu huu wa Kumi na Moja. Katibu. NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA - MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

  • Upload
    others

  • View
    16

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE

___________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 10 Mei, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendeleana Kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wetu huu wa Kumina Moja. Katibu.

NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NAUWEKEZAJI:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka waFedha 2018/2019.

MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA - MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA:

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka waFedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwakawa Fedha 2018/2019.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimwa MakamuMwenyekiti. Katibu.

NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE:

MASWALI KWA WAZIRI MKUU

SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa RichardMganga Ndassa, Mbunge wa Jimbo la Sumve, swali fupitafadhali.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kwa idhini yako, naomba uniruhusu niunganena Watanzania wenzangu kwa kuipongeza sana SerengetiBoys baada ya kushinda. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Ndassa, moja kwa moja kwenyeswali.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika,Tanzania imepewa heshima kubwa ya kuandaa mashindanoya vijana chini ya umri wa miaka 17, AFCON U17. Swali langukwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Serikali imejipangajekufanikisha mashindano hayo?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Ndassa, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Ndassa amezungumzia vijana ambao

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

wameshinda hivi karibuni Kombe la Afrika Mashariki lakinipia na hawa ambao tunawaandaa kwa mashindano yaAfrika. Kwanza, nitumie nafasi hii kuwapongeza sana vijanawetu wa umri chini ya miaka 17 kwa ushindi mzuri, mkubwawalioupata kule Burundi na ambao pia wataendelea mbele.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mbili, tunayo timu ya chini yamiaka 19 ambayo itatuwakilisha kwa kucheza Kombe laAFCON kama ambavyo ameeleza sambamba na heshimaambayo nchi yetu imepewa ya kuendesha mashindano yachini ya umri wa miaka 19 ambayo yatafanyika 2019. Kwaujumla wake, timu hizi zote ambazo tunazo kwa sasaambazo zinacheza kwenye ngazi ya Kimataifa ni jukumu letukama Serikali kuziandaa. Mimi nataka nitumie nafasi hiikulipongeza sana Shirikisho la Soka Tanzania kwa pamojana Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo kwamba wamefikia hatua nzuri baada ya kupataheshima hii kufanya maandalizi na maandalizi yanaendelea.Maandalizi haya, kwanza timu zenyewe tunaziandaa naninazo taarifa, moja kati ya maandalizi ambayo tunayafanyakwa timu hii ambayo itatuwakilisha tunaipeleka nchiniSweden kwa ajili ya kupata ufundi na maarifa zaidi ilikujihakikishia kwamba michezo yote itakayokuja mwakanitutaweza kushinda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sambamba na hayo, tunajiandaahuku ndani kupata viwanja ambavyo vitatumika kuchezeaKombe lile, lakini pili, maeneo ambayo yatafikiwa na wageniwetu kwa sababu tutakuwa na wageni wengi na mamboyote ambayo yanahusiana na afya, usafiri wao ndani ya nchi,haya yote yanaendelea kufanyiwa maandalizi. Kwa hiyo,nataka niwahakikishie Watanzania maandalizi juu yamichezo yetu ya Kimataifa ambayo pia tumepata heshimaya kucheza hapa nchi yote yanaendelea kama kawaida.

Mheshimiwa Spika, nitoe wito kwa Watanzania,pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Wizara na Shirikisho laSoka Tanzania, nawasihi Watanzania tuendelee kuziungamkono timu zetu zote zinazofikia ngazi za Kimataifa ili ziweze

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

kufanya vizuri na nchi yetu iendelee kupata heshima. Pia kwakufanya hilo, mashindano mengi mengine ambayo yatakuja,basi yaelekezwe nchini Tanzania ili tuweze kupata tija kwauwepo wa michezo hiyo hapa kwetu Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Ndassa, swali fupisana tafadhali.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, sawanitauliza swali fupi sana. Kupitia mashindano haya na kwasababu kutakuwa na wageni wengi kutoka nje na kwasababu tunazo fursa za utalii, je, TANAPA na Ngorogorowatashirikishwa namna gani? (Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swalila nyongeza la Mheshimiwa Ndassa, Mbunge wa Sumve,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeelezaheshima ambayo tumeipata ya kuendesha mashindano yadunia hapa kwetu mwakani nayo pia ni fursa kwetu na zikonyingi ikiwemo na hiyo ya kutangaza vivutio vyetu lakinikuwapeleka wageni wetu kwenye vivutio vile ili tuwezekujipatia fedha. Ni kweli tumeamua kutangaza na mipangoambayo Wizara ya Maliasili inayo sasa ni ya kuimarisha sektaya utalii kikamilifu kwa kutangaza mapori na vivutio vyotevilivyopo nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutatumia fursa kamahii, kwanza, kwenye viwanja vyake. Pili, kwenye matangazoya radio na television, lazima tuvionyeshe wakati wotewageni wakiwa hapa. Tatu, kutoa fursa kwao angalau timumoja, mbili, tatu kuwapeleka Kigoma huko wakaone sokwemtu; tuwapeleke Serengeti na Selou wakaone utalii wa hukona tuwapeleke Kilwa wakaone majengo ya zamaniyaliyokaliwa na Waarabu na maeneo mengine yote yenyevivutio vyetu. (Makofi)

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

Mheshimiwa Spika, ni matumaini yetu kwamba nafasihii tutaitumia vizuri na kimsingi niliposema tunafanyamaandalizi ni pamoja na kutangaza vivutio vya ndani. Kwahiyo, nawasihi Watanzania sasa tutumie fursa hii, kila mmojamwenye sekta ambayo anaona ujio wao utamletea farajabasi ajipange vizuri ili wakati ule wageni wanapoingia awezekuitumia. Kama unaimarisha sekta ya usafirishaji, kamaunaimarisha sekta ya vyakula, kama pia una sekta ambazounadhani wanahitaji mavazi na kila kitu, ni fursa kwetuWatanzania kutumia matukio kama haya ambayo pia Serikaliinaendelea kuyavutia nchini kwetu ili yafungue milango kwaWatanzania wote.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Twende CUF, MheshimiwaVedasto Edgar Ngombale.

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa maelekezo kwambakatika msimu huu wa mwaka 2018/2019 zao la ufutalitanunuliwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani. Mpakasasa navyozungumza, ufuta uko tayari, wakulimawameshavuna na wengine wameshauza. Pia maelekezo yaSerikali pia yalisisitiza mikoa yote inayolima zao la ufutaijiandae kwa mfumo wa stakabadhi ghalani. Je, ni nini tamkola Serikali maana iko kimya na mpaka sasa wafanyabiasharana wakulima hawajui nini kinachoendelea?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri Mkuutafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijubuswali la Mheshimiwa Vedasto Ngombale, Mbunge wa KilwaKaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tumewekautaratibu wa masoko ya mazao yetu yote nchini . Tumeanza

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

na mazao matano lakini pia tumeanza kuingia kwenyemazao haya ambayo yanaonekana yanazalishwa kwa wingiambayo pia yanatuletea tija kwa wakulima lakini hata kwaSerikali kwa ujumla wake ikiwemo na zao la ufuta. Tumetoamaelekezo kwa Wizara ya Kilimo iratibu vizuri mikoa yoteinayolima ufuta. Zao hili mwaka huu litauzwa kwa njia yamnada ili kuzuia mfanyabiashara mmoja mmoja kwendakuwarubuni wakulima na kusababisha kupata bei ndogo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapotoa maelekezo maanayake kila mmoja anayewajibika kwenye eneo hili lazimaafanye kazi yake. Tumetoa maelekezo maalum pia kwaWakuu wa Mikoa wote wakutane na Wizara na of courseWizara inawajibu wa kuwaita iandae utaratibu na utaratibuhuu uende sasa kwa wakulima waelimishwe, waeleweshwenamna nzuri ya kusimamia jambo hili na halmashaurizisimamie kwa karibu kuhakikisha kwamba wakulima ndaniya halmashauri zile hawadhulumiwi na hawauzi kwa beindogo ili iweze kuwapatia tija. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maelekezo haya na kwa swalilako sasa Wizara ya Kilimo wamesikia, Wakuu wa Mikoawamesikia na wilaya zinazolima ufuta kwa sababu siyo nchinzima wanalima ufuta, sasa wajipange wahakikishewanaratibu vizuri kupitia Maafisa Ushirika na Maafisa Kilimokuwatambua wakulima na maeneo watakayouza kamamnada il i wakusanye mazao, watangaze siku moja,wanunuzi waje, bei ipatikane wakulima wapate faida, ndiyomkakati wa Serikali. Wizara ipo na itasimamia jambo hili.(Makofi)

SPIKA: Tunaendelea. Mheshimiwa Saed Kubenea,CHADEMA.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Spika, sera ya Serikali ni kila mtu kuabududini anayoitaka na kutokuingilia dini ya mtu mwingine. Katiba

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

yetu, Ibara ya 3(1) inasema Serikali yetu haina dini isipokuwawatu wana dini.

Mheshimiwa Spika, Serikali imetoa kibali kwa BarazaKuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuratibu zoezi zima lahija kwa mwaka huu. Kwa msingi huo imeziacha taasisinyingine ambazo zilikuwa zinapeleka Mahujaji Makkahzisifanye kazi hiyo ikiwemo Kamisheni ya Wakfu na Mali yaAmana - Zanzibar ambayo nayo inatakiwa iratibiwe naBAKWATA.

Mheshimiwa Spika, swali langu kwa MheshimiwaWaziri Mkuu, nini msimamo wa Serikali sasa kwa kuwa sualahili limeleta sintofahamu na gharama za kupeleka MahujajiMakkah kupitia BAKWATA zimekuwa kubwa zaidi kulinganishana taasisi zingine, je, Serikali iko tayari kuziruhusu taasisi zinginezipeleke Mahujaji Makkah katika kipindi hiki kifupi kilichosalia?(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Kubenea, mbona kila ukisimamaunauliza maswali ya kidini? Yaani ukisimama una mamboya kidini, ukisimama una mambo ya kidini. (Makofi)

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Spika, kwanzanawakilisha Watanzania wakiwemo Waislam na mimimwenyewe ni Muislam na nina interest na jambo hili la Hijja.

SPIKA: Mheshimiwa Martha Mosses Mlata, swalilinalofuata.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, ahsante.Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na ubishani baina yaSUMATRA pamoja na TABOA kuhusu upitishwaji wa kanunibila kuwashirikisha wadau. Je, ni hatua gani Serikali inachukuaili kuweza kuinusuru sekta hii ya usafirishaji? Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu tafadhali.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Mlata, Mbunge wa Mkoa wa Singida,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, suala la SUMATRA na TABOA nisuala ambalo linaendelea kufanyiwa mazungumzo juu yauandaaji wa Kanuni za Usafirishaji kwa mujibu wakumbukumbu ambazo sasa ninazo. Suala hili nimelifanyia kazimimi mwenyewe hasa wakati ule TABOA walipokuwawanalalamikia SUMATRA, SUMATRA ilipokuwa inatengenezaKanuni za Usafirishaji na hasa zile kanuni ambazo zilikuwazinagusa sana juu ya adhabu na tozo mbalimbalizinazotozwa kwa wamiliki wakati mwingine kwa watumishiwa shughuli za usafirishaji na zikaanza kuleta migonganomiongoni mwao.

Mheshimiwa Spika, TABOA wamewahi kulalamikiauundaji wa Kanuni hizo na kwamba hawakushirikishwaKanuni hizo zilipokuwa zinatengenezwa na SUMATRA.Walipoleta malalamiko, tuliitaka SUMATRA sasa irudiemchakato wake kwa kukutanisha wadau wote wa sekta yausafirishaji. Tunajua kwenye sekta ya usafirishaji wako haoTABOA (wamiliki wa mabasi) lakini kuna TATOA (wasafirishajiwa malori) halafu wako pia hawa wenye mabasi yadaladala. Taasisi zote hizi zinashughulikia usafirishaji. Kanuniambazo zilikuwa zinalalamikiwa kwenye eneo hili kwamujibu wa kumbukumbu zangu ni pale ambapo maderevawaliopewa dhamana ya kuendesha mabasi yao au maloriyao wanapotenda kosa adhabu yake anatozwa mmiliki wabasi akiwa hayupo kwenye basi. Tozo hizi zimekuwazikilalamikiwa na wamiliki na kwamba lazima zifafanuliwevizuri ili kila mmoja atendewe haki yake pale ambapoanatenda kosa au la. Kama dereva anatenda kosa basiadhabu iende kwa dereva na siyo mmiliki na kama kosalitakuwa ni la basi lenyewe wataangalia vinginevyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mgongano uletulilazimika kuwataka wakae pamoja ili wazungumze,watengeneze Kanuni zinazoweza kutosheleza mahitaji yawote pamoja, SUMATRA pamoja na wamiliki wa vyombo

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

hivi vya usafirishaji. Kwa hiyo, jambo hilo limeendelea vizurina wajibu wa Serikali sasa ni kusimamia kuwa SUMATRAkama mwakilishi wa Serikali anashiirikisha wadau ambao niwamiliki wa vyombo vya usafirishaji ili kutengeneza Kanuniambazo zitawezesha hawa wamiliki pamoja na Serikalikufanya kazi bila ya kuwa na mgongano usiokuwa naumuhimu. Kwa hiyo, kazi hiyo tumeifanya na nimetoamaelekezo wakutane na taarifa ninazo kwambawanaendelea kukutana ili ku-harmonize zile Kanuni ilibaadaye zitakapokamilika ziendelee kutumika ili kila mmojaatendewe haki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge wa Busega, Dkt. RaphaelChegeni.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika,kwa kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakusanya fedhanyingi kutokana na tozo pamoja na kodi kutoka katikamasoko yaliyo rasmi na yasiyokuwa rasmi. Licha ya makusanyohayo, kumekuwepo na matatizo mengi ambayoyanasababisha kutokuwepo na uhalisia wa miundombinumizuri kutokana na uchafu na pengine kuwa na hali hatarishi.Je, ni nini kauli ya Serikali?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri Mkuu,tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Dkt. Chegeni, Mbunge wa Busega, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, upo ukweli kwamba halmashaurikaribu zote ndiyo zinamiliki masoko na ndiyo wanaohusikahasa na utozaji wa kodi kwenye masoko haya. Kodi hii kwakila halmashauri ni mapato ya ndani na mapato haya ni yaleambayo yanapangiwa matumizi yake na Baraza la Madiwanikatika kila halmashauri. Kwa hiyo, ni wajibu wa kilahalmashauri inapopata zile tozo kutenga mgao kwa ajili ya

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

usafi kwenye masoko yao. Siyo tu masoko bali maeneo yoteyanayohitaji kufanyiwa usafi ndani ya halmashauri yao, niwajibu wa kila halmashauri kupitia Baraza la Madiwanikutenga fedha kwa ajili ya shughuli za usafi kwenye maeneoyao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia usafihatuzungumzii kufagia na kuzoa taka tu, ni pamoja nakuimarisha miundombinu ambayo umeisema. Ni lazimamiundombinu iwe rafiki kwa ajili ya kuendesha shughuli zabiashara kwenye maeneo hayo au maeneo mengine.Tunajua kuna maeneo ni muhimu sana kwa halmashauripamoja na soko lakini pia kuna vituo vya mabasi, maeneoya hospitali na maeneo kadhaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, masoko mengi hayayanayomilikiwa na halmashauri lazima yaratibiwe vizuri.Tunajua yako masoko mengine kwenye mamlaka nyinginekama vile Soko la Kariakoo ambalo lina mamlaka yake, naopia wanawajibika, wakipata mapato yao watenge fedhakwa ajili ya usafi na kuimarisha ubora wa miundombinu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika hili Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli, alizindua kampeni ya usafi wa ujumla.Kwa hiyo, mambo yote haya tukiyachanganya pamojayanafanya Taifa hili kila eneo kuwa safi. Azimio lile limeelezakila Jumamosi itumike vizuri kuanzia asubuhi hadi saa tatu,saa nne kwa ajili ya usafi. Kwa hiyo, halmashauri na viongoziwote wanajibika kusimamia ili nchi iweze kuwa safi katikamaeneo yote yakiwemo ya kutolea huduma ikiwemo na eneola soko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kupitia Bunge lako, naombakutoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi naMaafisa Afya wa Halmashauri za Wilaya, ni jukumu laokusimamia suala hili. Nawasihi wahakikishe maeneo yote yakutolewa huduma ikiwemo masoko yanaimarishwa kwamiundombinu na usafi wake kwa ujumla . Nasi tutawapimakwa kuhakikisha kwamba halmashauri zao na maeneo yote

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

ya utoaji huduma huduma yanakuwa safi, vinginevyo hatuanyingine zinaweza kuchukuliwa pale ambapo tunaonahakuna uratibu mzuri wa usafi kwenye maeneo hayo, hakunauratibu mzuri wa uboreshaji wa miundombinu kwenyemaeneo ya kutolewa huduma kwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Hussein Bashe.

WABUNGE FULANI: Hayupo.

SPIKA: Mheshimiwa Abdallah Ally Mtolea, Mbunge waTemeke.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi nami nimuulize swaliMheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, Sera ya Elimu Bure imewarahisishiawazazi kuweza kuwapeleka watoto shule lakini haisaidiiwatoto kubaki shuleni kwa sababu kubaki shulenikunategemea na mazingira wezeshi kwa watoto kupendashule. Kwa sasa bado tunaona watoto wengi wanatorokashuleni tunakutana nao mitaani wakifanya kazi zaombaomba na wakisaidia watu kubeba mizigo sokoni iliwapate kitu cha kula. Je, ni lini Serikali itabadilisha sera hii ilisasa upatikanaji wa chakula shuleni uwe ni sehemu ya jambola lazima? (Makofi)

SPIKA: Majibu wa swali hilo, Mheshimiwa Waziri Mkuutafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swalila Mheshimiwa Mtolea, Mbunge wa Temeke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba hizi programuza elimu nchini tunaziratibu kwa kadri ya mahitaji na wakatikwa maana ya utoaji wa huduma ulio bora. Tumeanza naelimu bure kwa kuondoa michango ambayo haikuwa

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

muhimu iliyokuwa inawakwaza sana wazazi ili watoto hawasasa waweze kwenda shuleni.

Mheshimiwa Spika, nataka nimjulishe MheshimiwaMbunge kwamba Tanzania tuna shule zaidi ya 17,000 na kilashule ina watoto wasiopungua 300 na kuendelea, hasa shuleza msingi ambazo sasa tumeongeza hata usajili wa watotowetu. Nachoweza kusema ni kwamba programu ya chakulani muhimu sana kwa watoto wetu na Serikali hatuwezikulibeba jambo lote hili kwa kulisha shule zote 17,000, tukiwana sekondari zaidi ya 3,547 ambazo ni za boarding na day.Kwa hiyo, tumeanza na shule za bweni kwa upande wasekondari na sasa tunaendelea kuratibu vizuri tuone namnanzuri ya kutoa chakula kwenye shule za sekondari za kutwalakini pia na shule za misingi i l i vi jana wetu hawawanapokuwa shuleni waweze kupata huduma ya chakulaambayo inasaidia kimsingi kumfanya kila mtoto awezekupata masomo vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nini tumefanya? Tuliposema tutoeelimu bure kwa kuwapunguzia michango wazazi wetu, nafasihiyo pia inamfanya mzazi sasa kuchukua jukumu lingine lakumhudumia mtoto huyu ikiwemo na kuhakikisha mtotoanapata chakula cha kutosha, anapata sare na vifaamuhimu vya kwenda shule ili imuwezeshe mtoto huyukwenda shuleni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukiwa tunaendelea kuratibu hilindani ya Serikali na kwa kuwashirikisha wananchi, nitoe witopale ambapo wazazi wamevuna vizuri mwaka huo nawanaweza kupata chakula cha kutosha, iko haja naumuhimu wa kutekeleza dhana ya kupeleka chakula shulenina kuratibu. Tumeona baadhi ya halmashauri zilizokuwa naubunifu mzuri lakini zilikuwa na fursa nzuri ya uzalishaji, vijanawake wanapata chakula shuleni. Siyo lazima kiwe chakulakama ugali au wali lakini angalau uji kwa saa nnewanaendelea kupata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nitoe wito kwambapamoja na jitihada za Serikali za kuimarisha elimu, bado

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

tunahitaji kushirikiana pamoja na wazazi na wadaukuhakikisha kwamba tunatafuta njia nzuri ya kuboresha elimuikiwemo na utoaji wa huduma kwa vijana wetu ili wawezekusoma vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Abdallah Bulembo.

MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaSpika, ahsante sana. Serikali imechukua hatua kubwa na zakupongezwa katika usimamizi wa masoko ya mazao. Je, nilini itatoa mwongozo kwenye zao la kahawa kama ilivyotoakwenye pamba, chai na korosho? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Alhaj Bulembo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, zao la kahawa ni miongoni mwamazao yale ambayo tumeshaanza kuyasimamia na kutoleauratibu wake vizuri na sasa tunaenda kwenye msimu wake.Kwa bahati nzuri nimeshaita kikao cha viongozi wa Vyamavya Ushirika, Maafisa Ushirika, wakiongozwa na Mrajisi waUshirika ndani ya Wizara ya Kilimo, Wizara yenyewe ya Kilimokwa mikoa yote inayolima kahawa tukutane hapa Dodomatarehe 20, ili tuanze sasa kuzungumza kwa sababu bei dirakwa kila zao haitolewi tu na Serikali bali inatolewa kwakuwashirikisha wadau wakiwemo wakulima, wanunuzipamoja na Bodi ambayo inasimamia zao hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tunajua sasa zao lakahawa tunaenda sokoni na maelekezo ya ununuzi kwa njiaya ushirika ni pamoja na zao la kahawa, baada ya vikaohivi ambavyo pia vitaangalia gharama za uzalishaji. Pia beidira lazima iangalie na soko la dunia ili tuweze kutoamwelekeo na bei dira ni ile ambayo inamfanya mnunuziasinunue chini ya hapo. Kwa hiyo, bei dira hii tutaijadili kwapamoja kupitia vikao vyetu vya wadau baada ya kufanya

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

mapitio haya, gharama za uzalishaji na uendeshaji kwawanunuzi wetu lakini pia bei ya soko ya dunia ili baadayesasa tutaitangaza na kwa kuwa masoko yanaanzatutatangaza hivi karibu baada ya kikao chetu ili sasawakulima na wanunuzi wa kahawa waweze kujua bei dirahiyo ni kiasi gani na kila mmoja ajipange vizuri kununua kwamfumo ambao tumeuelekeza wa ununuzi wa njia ya ushirika.Jambo hili tutalisimamia kwa lengo la kumfanya mkulimaaweze kupata tija kwenye mazao yote haya ikiwemo na zaola kahawa.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Swali la mwisho kwa siku ya leo, MheshimiwaMbunge wa Kinondoni, Mbunge wa CCM, MheshimiwaMaulid Said Mtulia. (Makofi)

MHE. MAULID S. MTULIA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa fursa hii adhimu kabisa za kumuuliza swaliMheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga pesa nyingi sanakatika kuboresha mfumo wetu wa usafiri hasa mabasi yamwendo kasi katika Jiji la Dar es Salaam. Pamoja na fedhahizo nyingi bado suala la usafirishaji katika Jiji la Dar es Salaamkwa kutumia mradi huu lina changamoto nyingi ikiwepomgogoro kati ya mwendeshaji na MaxMalipo na hatamiundombinu. Je, Serikali ina mpango gani kuboresha usafirihuu? (Makofi)

SPIKA: Majibu Mheshimiwa Waziri Mkuu, tafadhali.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Mtolea, Mbunge wa Kinondoni, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna Mradi wa UsafirishajiJijini Dar es Salaam (UDART) ambao ni muunganisho wa UDApamoja na DART. Kwa sasa mradi huu kwa sasa unaendeleapamoja na changamoto ambazo Mheshimiwa Mbunge

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

amezisema. Niseme tu kwamba Serikali tunazijua kwambamiundombinu yetu na hasa makao makuu ya yale mabasisasa hivi yamekuwa ni mapito ya maji kutokana na mvuakuwa nyingi zaidi.

Mheshimiwa Spika, lakini mbili mgogoro anaousemaMheshimiwa Mbunge wa uendeshaji, popote panapokuwana taasisi mbili zimeunganishwa kuwa chombo kimoja ilikusimamia kunakuwa na migogoro ya ndani ambayotutaisimamia. Kwa kuwa DART ni sehemu ya Serikali na UDA-RT ni wawekezaji lakini pia Serikali ipo, jambo hili linaendeleakufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, lakini nataka niwaambie kwambamfumo huu wa usafirishaji Dar es Salaam UDART sasa hivitunaingia kwenye awamu ya pili ya uendeshaji ambapotutatafuta mbia mwingine aweze kuingiza mabasi yaketuweze kupata huduma bora na competitive kwa maanaya ushindani ili iweze kuwa na huduma bora zaidi. Sisitunaamini mwendeshaji mmoja anapoleta matatizo kamakuna mwingine inakuwa ni changamoto kwake, hivyoanaweza kuimarisha. Kwa hiyo, tunaendelea na hatua hiyoili kuondoa matatizo yote ya uendeshaji yaliyopo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pale ambapo itabainika kwambamwendeshaji wa sasa ana matatizo yaliyokithiri hatuna shidatutamuondoa kwa sababu waendeshaji wako wengi. WakoWatanzania wanaweza kuendesha, lakini yako mataifa yanje yanaweza kuendesha yakaleta mabasi lakini pia tunaumoja ule wa UWADA (Umoja wa Wasafirishaji wa Daladala)nao waliomba pia fursa ya kuweza kuendesha mabasi nausafirishaji Jijini Dar es Salaam nao pia tutawapa fursa yakuona kama wanaweza kufanya hilo.

Mheshimiwa Spika, muhimu zaidi, tunaendeleakuondoa changamoto za mwendeshaji aliyepo sasa. Piatumeshaanza utaratibu wa kupata mwendeshaji mwingineili tupate kampuni nyingine ambayo itaingiza mabasi yakekuimarisha usafiri wa Jijini Dar es Salaam.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Mheshimiwa Spika, suala la miundombinu, baada yamvua hizi kuisha tutaiimarisha. Naamini wote mmeonakwamba mvua hizi zimeharibu miundombinu mingi ikiwemona eneo la UDART. Kwa hiyo, tutaimarisha na tutajipangavizuri kuhakikisha huduma hii inaendelea na Watanzaniawananufaika na usafirishaji pale Jijini Dar es Salaam. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, ahsante sana. Mudawa maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu umeisha.Tunakushuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, at least orodha ya wotewalikuwa wameomba wamepata nafasi, wenginenimewanyima maswali ya nyongeza ili kuwapa na wenginenafasi. Kwa maana hiyo, wote mmepata nafasi angalau yakuuliza maswali ya msingi. Katibu.

NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

MASWALI NA MAJIBU

Na. 217

Bei ya Gesi Inayotumika Majumbani

MHE. ZAINABU M. AMIRI aliuliza:-

Je ni lini Serikali itapunguza bei ya gesi kwa matumiziya majumbani ili kuwawezesha wananchi wengi zaidikutumia gesi kwa matumizi yao ya nyumbani na kuondokanana matumizi ya kuni na mkaa?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Nishati, Mheshimiwa Subira Mgalu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwaniaba ya Waziri wa Nishati, napenda kujibu swali laMheshimiwa Zainabu Mndolwa Amiri, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Spika, gesi iliyogunduliwa nchini ni gesiasilia (natural gas) ambayo husafirishwa kutoka kwenyevisima vya gesi hadi kwa watumiaji kupitia mabomba.Mpaka sasa watumiaji wakubwa wa gesi hapa nchini niviwanda na mitambo ya kufua umeme. Mradi wa majaribiowa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ulianzakupitia mradi wa mfano (pilot project) ambapo nyumba 70zilizopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam zimeunganishwa nagesi kwa matumizi ya nyumbani.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa gesi inayotumiwa nawananchi kupikia majumbani ni Liquefied Petroleum Gas (LPG)ambayo huagizwa na wafanyabiashara kutoka nje kamailivyo katika mafuta ya petrol, diesel na mafuta ya taa aundege. Gesi hii hujazwa katika mitungi kwa ujazo tofautitofauti na gharama ya gesi hii inategemeana na soko ladunia.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuhamasishawawekezaji katika sekta ya gesi kwa ajili ya matumizi yamajumbani ili kuleta ushindani katika sekta hii. Mpaka sasamakampuni mengi yameanza kujenga miundombinu ya gesikatika sehemu mbalimbali za nchi na kuonesha nia yakushirikiana na Serikali katika kusambaza gesi asilia nchini.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC imeanzamatayarisho ya kutekeleza mradi wa kuunganisha gesimajumbani ambapo awamu ya kwanza ya mradi huoutapita katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaamna Mtwara na baadaye katika mikoa mingine ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Zainabu, swali la nyongeza.

MHE. ZAINABU M. AMIRI: Mheshimiwa Spika, ahsante.Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kutokana nakugundulika kwa gesi nchini mwetu, je, ni lini Serikali itasitisha

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

uingizaji wa gesi ili tuweze kutumia gesi yetu hapa nchini?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, pilot project iliyofanyikani Mikocheni Dar es Salaam, je, ni vigezo gani vimezingatiwakatika project hiyo na isiwe kule ilikotoka gesi Mtwara?(Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri Nishati, Mheshimiwa Subira Mgalu, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa ya kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Zainabu Mndolwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ameuliza nilini Serikali itasitisha uagizaji wa gesi kutoka nje ya nchi. Nikweli ugunduzi wa gesi asilia iliyogunduliwa hapa nchini nigesi zaidi ya mita za ujazo trilioni 55,000. Nataka nimwambieMheshimiwa Mbunge matumizi ya gesi yapo mengi kamanilivyoeleza kwenye swali la msingi ikiwemo kwenye uzalishajiwa umeme, matumizi ya viwanda na matumizi yamajumbani.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi kuna mipangombalimbali ambayo inafanywa na Serikali ikiwemo pia ujenziwa kiwanda cha kusindika gesi asilia Mkoani Lindi. Kwa hiyo,baada ya kiwanda hiki kukamilika na hizi fursa mbalimbaliza usambazaji gesi na miundombinu mbalimbali yakusambaza gesi kwa ajili ya matumizi ya majumbani naviwandani itakapokamilika, Serikali itatafakari kwa kinanamna ambavyo inaweza kusitisha uagizaji wa gesi hiyonchini. Kwa sasa bado tuna mahitaji na kwa kuwa mipangoinaendelea, naomba nimthibitishie Mheshimiwa Mbungekwamba Serikali itatafakari na kuchukua hatua paleambapo tutakuwa tumejiridhisha na soko na uhitaji wa gesiasilia ndani ya nchi na kwa matumizi ya nchi. (Makofi)

Mheshimwia Spika, swali lake la pili alikuwa anaulizakuhusu vigezo vilivyotumika kwa maeneo ya kusambaza gesi

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

kwa matumizi ya majumbani na ameuainisha Mkoa waMtwara. Nataka nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kunamiradi na tafiti zinazoendelea katika Mikoa ya Mtwara, Lindi,Pwani, Morogoro, Dodoma, Mwanza na Tanga chini ya Mradiwa JICA ili kuona mahitaji ya matumizi ya gesi ya kupikia ilikuanza mradi wa usambazaji wa gesi katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, nimthibitishie katika Mkoa waMtwara kwa mwaka huu wa fedha kiasi cha shilingi milioni140 zimetengwa kuendelea na study hiyo na kwamba mkoahuo utapatiwa usambazaji wa gesi kwa matumizi yanyumbani. Nakushukuru.

SPIKA: Mashekhe mnatumia gesi majumbani? Hili swalilina wenyewe hili. (Kicheko)

Mheshimiwa Halima Mdee, nimekuona, swali lanyongeza.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, kufuatiaugunduzi wa gesi, Serikali ya CCM iliwahakikishia Watanzaniana wananchi wa Mtwara kwamba maisha yetu kwa kiwangokikubwa yatabadilika. Ikumbukwe kwamba bomba la gesililijengwa kwa mkopo usiopungua shilingi trilioni 1.5 kwendashilingi trilioni 2. Hivi tunavyozungumza na kwa taarifa zaSerikali inaonesha kwamba tunatumia asilimia 5 tu ya gesikatika bomba husika. Nataka tu Serikali ituambie, Deni laTaifa linakua, tulikopa tukajenga bomba tukajua kwambatunapata suluhu lakini sasa hivi tunatumia bomba asilimia 5,ni nini kimetokea hapo katikati kilichopelekea kushindwakulitumia kwa asilimia 95 ? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaambiwa tena kuna mpangoStigler’s Gorge wa kuzalisha umeme. Sasa mtuambie bombala gesi limekwamia wapi katika uzalishaji wa umeme na hiiStiegler’s Gorge inaanzia wapi ili kama Taifa tuwe na taarifa,maana tunaona tunapelekwapelekwa tu. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Nishati, Mheshimiwa Subira Mgalu.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa ya kujibu swali la MheshimiwaHalima Mdee, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali ilitekeleza mradimkubwa huu wa ujenzi wa bomba la gesi la Mkoa waMtwara. Kama alivyoeleza kwenye swali lake, kwa sasamatumizi ya kusafirisha gesi kwa kupitia bomba hili kwamwaka huu unaoendelea imefika lita za ujazo milioni 175kutoka milioni 145 za mwaka 2016/2017, ni wazi ongezekolinatokana na mahitaji makubwa.

Mheshimiwa Spika, naomba nimthibitishie tulipokuwatunajenga bomba hili na ahadi tulizotoa kwa wana Mtwara,ahadi zile ni sahihi kwa sababu kuna miradi mbalimbaliambayo inayoendelea. Kwa mfano, Mtwara peke yaketunajega mradi wa kuzalisha umeme wa megawatts 300 kwakutumia gesi asilia ya Mkoa wa Mtwara. Sambamba na hilo,pia kuna mpango wa kujenga mradi wa kuzalisha umemekwa kutumia gesi asilia Somanga Fungu, kwa kuzalishamegawatts 330 kwa kutumia gesi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nchi yoyote lazima izalishe umemekwa vyanzo mbalimbali, huwezi kutumia gesi asilia peke yakeukatosheleza mahitaji ya nchi nzima. Ndiyo maanatunazalisha umeme kwa kutumia maji na gesi. Sasa hivi zaidiya asilimia ya 50 megawatts zinazozalishwa zinatumia gesi.Kwa hiyo, ni wazi kwamba gesi ambayo iligundulika Mtwaraimeleta tija katika uzalishaji wa umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kama tunavyofahamuumuhimu wa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vingine,Serikali imetafakari, kwa sababu lengo la Serikali ni kuzalishaumeme wa bei nafuu na kumfikia mtumiaji kwa bei nafuu.Ndiyo maana Serikali imekuja na mradi wa Stiegler’s Gorgeutakaozalisha megawatts 2,100. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimewahi kusema ndani ya Bunge

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

lako Tukufu kwamba uzalishaji wa umeme kwa kutumia majiuna unafuu zaidi, unatumia shilingi 36 ukilinganisha na gesiambayo ni shilingi 147. Kwa nchi inayotarajiwa kujengaviwanda nchi nzima na kazi inayoendelea lazima tuzalisheumeme kwa wingi. Kwa kuwa lengo la Serikali ya Awamu yaTano chini ya Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John PombeMagufuli ni kuzalisha megawatts 5,000 mradi wa Stiegler’sGorge ndiyo wakati wake muafaka.

Mheshimiwa Spika, nashukuru. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana kwa majibu ya uhakika. Hayandiyo majibu tunayoyataka kutoka Serikalini namna hii.Maana Mheshimiwa Halima amejibiwa mpaka mwenyewekakubali. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na swali la Mheshimiwa Dkt.Shukuru Kawambwa.

Na. 218

Fidia kwa Nyumba Zilizowekwa Alama ya “X”Kitongoji cha Sanzale-Bagamoyo

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA aliuliza:-

Upanuzi wa barabara kutoka mita 22.5 hadi 30 kutokakatikati ya barabara umesababisha baadhi ya wananchikatika Kitongoji cha Sanzale, Kata ya Magomeni kufuatwana barabara na nyumba zao kuwekwa X:-

Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi hao?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, tafadhali Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasil iano, Mheshimiwa EliasKwandikwa.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasil iano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, Mbunge waBagamoyo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Barabara ya mwaka 1932ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2007, ambapo eneo la hifadhiya barabara lilibadilika kutoka mita 22.5 kutoka katikati yabarabara kila upande wa barabara kuu na barabara zaMikoa kuwa mita 30 na hivyo kufanya eneo la hifadhi yabarabara kuwa mita 60 badala ya mita 45 za awali.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mabadiliko hayo,Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS)ilifanya zoezi la kuainisha maeneo yote yaliyoathirika na Sheriampya ya Barabara ya mwaka 2007 kwa nchi nzima. Aidha,wananchi wote wenye mali zao katika eneo la kuanzia mita22.5 hadi 30 kutoka katikati ya barabara kila upande ambaowamewekewa alama ya “X” ya kijani watalipwa fidia kwamujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa pindimaeneo yatakapohitajika kwa ajili ya ujenzi au upanuzi wabarabara na hivyo mali zao kuathirika.

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kawambwa, nilikuona.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaSpika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawiliya nyongeza, pamoja na shukrani kwa Mheshimiwa NaibuWaziri kwa majibu hayo ambayo amenipa.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, eneo lile laKitongoji cha Sanzale ni Bagamoyo Mjini na wananchi hawawamewekewa alama za “X” miaka nane imepita, hawawezikukarabati nyumba zao, hawawezi kujenga upya, hawawezi

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

kufanya chochote na majibu ni kwamba watafidiwa palemaeneo yatakapohitajika. Je, ni lini maeneo hayo yatahitajikakwa sababu wananchi hawa psychologically wameendeleakupata matatizo makubwa sana? Wafanye nini maanawanaishi na watoto wao katika nyumba ambazozimewekewa “X” lakini hawajui lini watalipwa fidia.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, katika barabara yaMakofia - Mlandizi ambayo imo katika Ilani ya Chama chaMapinduzi ya mwaka 2010 pia katika Ilani ya mwaka 2015kujengwa kwa kiwango cha lami. Wananchi hawawanapenda kujua fidia zao zitalipwa lini?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa EliasKwandikwa, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASLIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, napendakujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kawambwa,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, nampongeza sanaMheshimiwa Dkt. Kawambwa kwa kufuatilia sana maendeleoya Bagamoyo kwa ujumla wake. Natambua kwambakutakuwa na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na hivyo hizibarabara ambazo Mheshimiwa Mbunge anazitaja ni muhimukweli. Yeye mwenyewe anatambua kwamba zipo harakatiza awali ambazo zimefanyika ili kuhakikisha kwamba fidiakwa wananchi wake zinalipwa mapema.

Mheshimiwa Spika, swali lake anasema ni lini sasatutalipa fidia hiyo. Niseme kwamba harakati za ujenzi wabarabara ya lami kwa barabara ambazo zinaingiaBagamoyo zinaendelea na hatua za tathmini zimeshafanyikana kwa vile zina hatua mbalimbali, kwa upande waTANROADS tumeshafanya jukumu letu na tunaendelea

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

kuwasiliana ili kuweza kupata fedha ili wakati wowotetuweze kuwalipa wananchi hawa.

Mheshimiwa Spika, najua kwa eneo hili amelitajamahsusi Mheshimiwa Mbunge, wapo wakazi wasiozidi 20ambao wanahitaji kufanyiwa malipo ya compensation. Kwahiyo, nikuombe tu Mheshimiwa Mbunge na Ndugu zanguwananchi wa Bagamoyo eneo hili wavute subira wakatiwowote tutafanya zoezi la kuweza kuwalipa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, anauliza juu yacompesation kwenye barabara hii inayotoka maeneo yaMlandizi kuja Bagamoyo. Kama nilivyosema barabara hii nimuhimu sana kwa ajili ya kuja kutoa huduma katika Bandariya Bagamoyo itakapojengwa hii ikiwa ni pamoja na eneolingine kuja Bagamoyo ukitokea Kibaha, maeneo ya Vikawekuja Mapinga na kwenyewe harakati zinaendelea vizuri.

Mheshimiwa Spika, natambua Ilani ya mwaka 2010ya Chama cha Mapinduzi na Ilani ya mwaka 2015 imetajakupanua barabara hii. Kwa hatua ambazo tumefikiawananchi wameshapata valuation form wazijaze,wazirudishe halafu Serikali tutasimamia kwa haraka iliwananchi hawa pia waweze kulipwa kulingana na sheriainavyotaka.

SPIKA: Mheshimiwa James Mbatia, nilikuona, swali lanyongeza.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana.

Mheshimiwa Spika, majanga mengi sasa hiviyanasababishwa na binadamu zaidi ya asilimia 96 ikiwepokwenda kinyume na uumbaji wa dunia ya Mwenyezi Mungu.Sheria hii ya tangu mwaka 1932 mpaka 2007 kwa kiasikikubwa ni uharibifu mkubwa wa mazingira na hasa

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

barabara za vijijini. International Standard na vigezo vyakevya ujenzi wa barabara huwezi uka-upgrade barabarakutoka stage moja kwenda stage nyingine za vijijini ukafanyamita 60.

Mheshimiwa Spika, barabara hizi zinazoenda vijijini,kwa mfano barabara ya Kawawa - Pakula, Jimbo la Vunjona barabara ya Himo na Himo - Mwika, kwa nini mnaamuakuchukua mashamba bila fidia na siyo standard? Barabarazinajengwa kwenda juu na siyo kupanua tu kwa horizontally?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu WaziriUjenzi, Uchukuzi na Mawasil iano, Mheshimiwa EliasKwandikwa, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ELIASJ. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mbatia, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, nitumie nafasi hiikulipongeza Bunge kwa kutunga Sheria hii Na.13 ya mwaka2007 ambayo kwa kweli ilizingatia sana mabadiliko, ukiisomaSheria ya mwaka 1932 utaona namna ilivyokuwa. Kwanzailikuwa ni ndogo sana, ilikuwa na kama section saba tu nail ikuwa inatoa mamlaka makubwa sana kwa walewatekelezaji wa ujenzi wa barabara wanaweza wakafanyamaamuzi, sheria iliyowaruhusu. Mabadiliko haya yaliyokujamwaka 1969 na baadaye kuja hii Sheria Na.13 imetoa nafasikwa Mamlaka zetu za Barabara kuweza kuzingatia maeneomaalum na kuweza kufanya declaration ya ujenzi wabarabara. Hivyo, sheria ipo vizuri ni vema tu tuendeleekuitekeleza.

Mheshimiwa Spika, nimueleze Mheshimiwa Mbatianiseme kwamba Serikali inalipa fidia kulingana na sheriazilizopo pia lazima tuangalie na mamlaka zetu katikahalmashauri. Mamlaka za Barabara zipo kwenye Halmashauri

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

zetu, kwa mfano, sasa hivi tunayo TARURA na TANROADS kwaupande wa Serikali Kuu.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu tu tukatazama sheriazote, Sheria za Barabara pamoja na sheria za kusimamiamamlaka zetu ili wananchi waweze kupata haki. Kamajambo hili linaweza kuwa mahsusi Mheshimiwa Mbungealilete tulizungumze tuone namna nzuri ya kulishughulikialakini Serikali ina nia thabiti ya kuwalipa wananchi fidiakulingana na sheria zilizopo.

SPIKA: Ahsante sana Waheshimiwa. Tuendelee naWizara ya Kilimo tafadhali, swali linaulizwa na MheshimiwaInnocent Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa.

(Swali Na. 219 na Na.220 yalirukwa)

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika,samahani, swali langu Namba 219 umeliruka.

SPIKA: Tutalirudia.

Na. 221

Agizo la Kahawa Kuuzwa KwenyeVyama vya Msingi

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-

Serikali imezuia biashara ya BUTURA na wanunuzi wakahawa kwa watu binafsi (moja kwa moja kwa wakulima)na kuagiza yote iuzwe kwa Vyama vya Msingi wakati vyamakama KDCU vilishindwa kuwapa bei nzuri wakulima:-

(a) Je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha inakujana mbinu mpya ya kuwapa bei nzuri wakulima wa kahawa?

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

(b) Je, ni hatua zipi zimechukuliwa haraka ilikuhakikisha wale walioua Vyama vya Ushirika wanashtakiwa?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,napenda kujibu swali la Innocent Sebba Bilakwate, Mbungewa Kyerwa, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, katika msimu wa mwaka2018/2019, Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirikaimejipanga kuhakikisha kuwa biashara ya zao la kahawaitaendeshwa na kusimamiwa na Vyama vya Ushirika kwakushirikiana na wadau mbalimbali chini ya mfumo wastakabadhi za ghala. Aidha, kupitia mfumo huu, kahawa yamkulima itakusanywa na kukobolewa na kisha kuuzwamnadani chini ya usimamizi wa Vyama Vikuu vya Ushirika,Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Bodi ya Kahawa na Bodi yaStabadhi za Ghala ambapo kahawa itanunuliwa kwa beiya ushindani na yenye tija itakayowezesha mkulima kulipwamalipo ya pili na ziada.

(b) Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume yaMaendeleo ya Ushirika pamoja na Shirika la Ukaguzi naUsimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), imeendeleakufanya kaguzi za mara kwa mara na kaguzi za kiuchunguzikatika vyama vya ushirika na kuchukua hatua mbalimbaliza kisheria pindi inapobainika kuwepo kwa ubadhirifu. Aidha,wahusika wa ubadhirifu wamekuwa wakichukuliwa hatuambalimbali ikiwa ni pamoja na Bodi za Uongozi naMenejimenti zake kuondolewa madarakani na kuwafikishakwenye vyombo vya dola ambapo baada ya uchunguzikukamilika watuhumiwa hushtakiwa Mahakamani nakuwataka kurejesha fedha walizoiba.

SPIKA: Mheshimiwa Bilakwate, tafadhali.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili yanyongeza. Naipongeza Serikali kwa jitihada zake kuhakikishainaboresha zao la kahawa.

Mheshimiwa Spika, kwenye zao la kahawa kulikuwana kodi nyingi na Serikali imejitahidi kuondoa kodi 17, lakinihizi kodi hazimnufaishi mkulima moja kwa moja zinawalengawafanyabiasha. Je, Serikali imejipanga vipi kuondoa hizi kodiambazo zinamgusa moja kwa moja mkulima ili awezekupata bei nzuri ya kahawa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mara nyingi mkulimaanapoanza kulima, kupalilia mpaka kuvuna hasaidiwi kituchochote, mwisho anaanza kukatwa kodi na mambomengine. Je, Serikali imejipanga vipi kumsaidia huyu mkulimaili iweke miundombinu mizuri kuanzia anapolima akiwashambani mpaka kwenye mnada? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Kilimo, Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika,naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Bilakwate, Mbunge Kyerwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, naomba nimpongezeMheshimiwa Mbunge kwa jinsi ambavyo anafuatilia kwaukaribu sana zao hili la kahawa ambalo linalimwa pia kwawingi katika Jimbo lake lile la Kyerwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikija kwenye maswali yake mawiliya nyongeza, katika swali lake la kwanza, ni kweli kwambaSerikali tumeliona hili na ndiyo maana tumeanzisha uleutaratibu wa kuuza kahawa mnadani moja kwa moja kupitiaVyama vyetu vya Ushirika. Vilevile Serikali tumepunguza tozoya mauzo ya mazao kupitia cess au farm gate price kutokaasilimia 5 hadi asilimia 3.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Mheshimiwa Spika, swali lake lile la pili ni kwambazao la kahawa linategemea sana na muonjo ule wa kahawa.Kwa maana hiyo, katika kuweka ubora wa miundombinupia na ubora wa zao lenyewe, ni kwamba kulekule shambaniwakulima wanapaswa kutumia zile CPU kwa ajil i yakuchakata zile kahawa kwa sababu kahawa mbichihairuhusiwi, hivyo iweze kuanikwa na kusafishwa vizuri, kablahaijapelekwa kukobolewa kule kwenye curing.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na Wizara yaMifugo na Uvuvi, swali linaulizwa na Mheshimiwa SusanLimbweni Kiwanga, Mbunge wa Mlimba.

Na. 219

Hitaji la Malambo – Mlimba

MHE. SUSAN L. KIWANGA aliuliza:-

Jimbo la Mlimba lina mito mingi inayotiririka mwakamzima ambayo inaweza kutumika kujenga malambo kwaajili ya mifugo:-

Je, ni lini Serikali itajenga Malambo kwa ajili yakunyweshea mifugo katika Jimbo la Mlimba?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri,Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Ulega, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Mifugo na Uvuvi, napenda kujibu swali la MheshimiwaSusan Limbweni Kiwanga, Mbunge wa Mlimba, kamaifauatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Mbunge kwamba uwepo wa mito mingi katika Jimbo laMlimba ni fursa kwa ajili ya upatikanaji wa maji kwa matumizimbalimbali ikiwemo mifugo.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Wizara yanguimepokea ombi la Mheshimiwa Susan Kiwanga nalitazingatiwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019. Pia nitoewito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendeleakuhamasisha sekta binafsi, wafugaji pamoja na wadau wamaendeleo kuibua miradi ya ujenzi wa malambo, mabwawa,majosho na visima virefu kwa lengo la kuboresha shughuliza ufugaji ili kuleta tija.

SPIKA: Mheshimiwa Susan Kiwanga, swali lanyongeza.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante.Nimepokea majibu ya Naibu Waziri. Kwa kuwa ametoaahadi na bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi inakuja tarehe17 Mei,2018 na tarehe 18 Mei, 2018, nitajiridhisha kwenyevitabu vyao kama kweli wametenga na wameingiza kuhusuujenzi wa malambo ndani ya Jimbo la Mlimba.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, nampongezaMkurugenzi na Halmashauri ya Kilombelo angalau tumetengasisi kwa mapato ya ndani shilingi milioni 103 kwa ajili yakuboresha na kujenga malambo ndani ya Halmashauri naJimbo la Mlimba. Hizo ni jitihada tunafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu linakuja, kwa kuwa,Jimbo la Mlimba lina takribani vijjiji 18 na kuna kilometa 606eneo ambalo wafugaji wamekaa huko kwa wingi navinaenda kufutwa, je, Wizara hii au Naibu Waziri yupo tayarisasa kwenda Jimbo la Mlimba kuangalia taharuki hiiinayotokea kwa wafugaji hao na kuona umuhimu wakuweka malambo ili wananchi hao na wafugaji wasiendekuingia kwenye haya maeneo ambayo yanachukuliwa naSerikali kwa ajili ya kupeleka maji kwenye Stiegler’s Gorge?Kuna taharuki kubwa sana ndani ya Jimbo la Mlimba. Je,

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

yupo tayari sasa kwenda kuangalia na kupanga mipangosahihi? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Ulega, NaibuWaziri wa Mifugo na Uvuvi, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaSpika, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kujibu swali mojala nyongeza la Mheshimiwa Susan Kiwanga. Kwa ruhusa yako,naomba nimpongeze sana Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Mlimba kwa kutenga pesa hizo kwa ajili yakuhakikisha kwamba mifugo yetu inapata maji.

Mheshimiwa Spika, swali lake ni kutaka kujua kamaniko tayari kwenda naye Mlimba kuangalia juu ya adhawanayopata wafugaji. Nataka nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba sisi tunafahamu ufugaji ni maisha yetu namaisha yetu ni ufugaji. Hivyo, nipo tayari kwenda Mlimbakuungana naye kwa ajili ya kwenda kuwaona wafugaji hawa.

SPIKA: Swali la mwisho kwa siku ya leo ni la Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia na linaulizwa na MheshimiwaShaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, tafadhali.

Na. 220

Hitaji la Chuo cha Ufundi Lushoto

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:-

Wilaya ya Lushoto haina Chuo cha Ufundi (VETA) nakuna vijana wengi waliohitimu elimu ya msingi na sekondari:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga Chuo chaUfundi (VETA) ili vijana hao waweze kupata elimu ya ufundiya kuwasaidia katika kujiajiri?

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri,Elimu, Sayansi na Teknlojia, Mheshimiwa William Olenasha,tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la MheshimiwaShaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu waelimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwa ajili yakuandaa rasilimali watu watakaotumika katika viwanda ilikufikia lengo la Serikali kuwa na uchumi wa kati unaotegemeaviwanda ifikapo mwaka 2025. Vyuo hivi vitasaidiakuwaandaa vijana kwa kuwapatia ujuzi utakaowawezeshakujiajiri na kuajiriwa ikizingatiwa kuwa kundi kubwa la vijanawetu halipati fursa ya kuendelea na masomo ya elimu yajuu.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na mpangowake wa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya Mikoa na Wilayaikiwemo Lushoto kutegemeana na upatikanaji wa fedha.Lengo ni kila Mkoa na Wilaya kuwa na Chuo cha Ufundi Stadi.

Mheshimiwa Spika, aidha, pamoja na ujenzi wa vyuohivyo, Wizara itaendelea na utekelezaji wa Mradi wa KukuzaStadi za Kazi (Education and Skills for Productive Jobs – ESPJ)ambapo katika mradi huu Vyuo vya Maendeleo ya Wananchivitakarabatiwa ili kuongeza fursa za mafunzo ya ufundi stadisambamba na elimu ya wananchi. Hivyo, katika kipindi hikiambacho Serikali inaendelea na jitihada hizi, nashauriwananchi wa mikoa na wilaya zote ambazo hazijawa navyuo vya VETA kutumia vyuo vya ufundi vilivyopo nchinihususan kwenye mikoa na wilaya jirani ili vijana wetu wapate

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

ujuzi na stadi hizi muhimu kwa maendeleo yao na nchi kwaujumla.

SPIKA: Mheshimiwa Shekilindi, swali la nyongeza,tafadhali.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri. Naombaniulize maswali mawili madogo ya nyongeza, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Chuocha VETA kiko mbali sana na Wilaya ya Lushoto na hiiimesababisha vijana wengi wa Lushoto kukosa fursa yakujiajiri na kuajiriwa, je, Serikali haioni kwamba imefikia wakatisasa kuchukua hatua za haraka ili kuwajengea chuo hichovijana wa Lushoto waweze kupata elimu hiyo ya ufundi?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali pili, kwa kuwa kuna majengoya TBA na majengo yale yana karakana ya Halmashauri yaWilaya ya Lushoto. Je, Serikali haioni sasa kuwa kuna haja yakurudisha majengo hayo katika Wizara ya Elimu kwa nia yakufungua Chuo cha VETA katika majengo hayo ili vijana waLushoto waliokosa elimu hiyo ya ufundi kwa muda mrefuwaweze kuipata sasa? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Naibu Waziri, MheshimiwaWilliam Olenasha, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusu ni lini Serikali itajenga Chuocha Ufundi Stadi Lushoto, naomba nimhakikishie Mheshimiwa

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Mbunge kwamba kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi,Serikali itaendelea kujenga Vyuo vya Ufundi Stadi katika wilayana mikoa yote kadri fedha zitakavyopatikana. Kwa hiyo, kwasasa nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba fedhazikipatikana Serikali itajenga Chuo cha Ufundi Lushoto kamaitakavyofanya katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu majengoya TBA kama ni wakati sasa wa kurudishwa Wizara ya Elimuili yaweze kutumiwa kama Chuo cha VETA, naomba nimshauriMheshimiwa Mbunge kwamba hili linawezekana lakini waowaanzishe mchakato katika ngazi yao ya halmashauri,wawasiliane na TBA. Wakishapata yale majengo kwa maanaya wakiruhusiwa, sisi Wizara ya Elimu tuko tayari kujakuyakagua na kuangalia kama yanafaa kuwa VETA nahatimaye tukiona yanafaa hatuna kipingamizi, tutahakikishakwamba majengo yale yanageuzwa kuwa VETA.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mkiangalia mudamtaona muda wetu wa kipindi cha maswali unatakiwauishie hapo. Kwa hiyo, tuendelee na matangazo ya wageni.

Waheshimiwa Wabunge, kwanza katika Jukwaa laSpika, nina wageni maalum kabisa, wageni wa Spika ambaowamenitembelea nao ni mate wenzangu wanne ambaotulisoma nao Kibaha Sekondari enzi hizo. Karibuni sana.Naomba nimtambulishe kwenu ndugu Jackson Kalikumtima,karibu sana Jackson; Ndugu David Nchaina, karibu sanaDavid; Ndugu Hussein Mzara, karibu sana pamoja na NduguSadik Shekimweri. Karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, unajua ukipata nafasi yakukutana na wenzako mliosoma pamoja basi inatia moyopia kuona tumezeeka kiasi gani sasa toka enzi zile. Tulipokuwatukicheza ule mpira usiokuwa na refa wala usiokuwa na idadiya wachezaji, kule Kibaha Sekondari unaitwa Mbugi, hatawatu 100 mnacheza kwenye uwanja mmoja huo huo.(Makofi)

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Waheshimiwa Wabunge, pia, nimtambulishe NduguFrank Kanyusi, Afisa Mtendaji Mkuu BRELA, karibu sana. (Makofi)

Wageni wengine tulionao katika Jukwaa la Spika nipamoja na wageni wa Mheshimiwa Charles Mwijage, Waziriwa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambao wameongozanana Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Grabriel. Karibu sana KatibuMkuu. Naibu Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, NduguJoseph Buchweishaja, karibu. Naibu Katibu Mkuu Viwanda,Ndugu Ludovick James Nduhiye, karibu. (Makofi)

Pia, tunao Wenyeviti wa Bodi, Mwenyekiti wa Shirikala Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO), Prof.Patrick Makungu; Mwenyekiti wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS), Profesa Makenya Maboko na Mwenyekiti wa Mamlakaya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Eng.Christopher Chiza. (Makofi)

Mheshimiwa Chiza alikuwa ni Mbunge mwenzetu huyuna alipata kushika nafasi mbalimbali katika Serikali ikiwemoya kuwa Waziri wa Kilimo na masuala ya Umwagiliaji,Mbunge kutoka kule Kibondo, nadhani Jimbo la Muhambwekama sikosei, wakati huo. Karibu sana Mheshimiwa ChizaBungeni tena kwa mara nyingine. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaye Mwenyekiti wa Kituocha Uwekezaji Tanzania (TIC), Prof. Longinus Rutasitara, karibu;Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Dkt.Samuel Nyantahe; Mwenyekiti wa Shirika la Utafiti waMaendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Prof. Idris Mshoro;Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cha Zana za Kilimo na TeknolijiaVijijini (CARMATEC), Prof. Suleiman Chambo; Mwenyekiti waKampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Prof. Egid Mubofu.Karibuni sana. Pia, wameambatana na Wakurugenzi, Wakuuwa Taasisi mbalimbali, Idara, Vitengo vilivyo chini ya Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. (Makofi)

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Waheshimiwa Wabunge, mgeni mwingine waMheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara leo ambayeyuko kwenye Jukwaa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, MhandisiEvarist Ndikilo. Mhandisi Evarist Ndukilo ni Mkuu wa Mkoaambaye amejipambanua katika masuala ya uwekezaji waviwanda, mkoa wake ukiwa unaongoza kabisa katikakuvutia wawekezaji katika eneo la viwanda. Tunakushukurusana, tunakupongeza sana Mhandisi Ndikilo kwa kazi nzuriunayoifannya. (Makofi)

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge ni pamoja nawageni sita wa Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao ni Kamatiya Maudhui ya TCRA. Karibuni sana Kamati ya Maudhui.(Makofi)

Pia kuna wageni 74 wa Mheshimiwa EmmanuelPapian ambao ni wanafunzi na walimu kutoka Shule yaSekondari ya Engusero iliyopo Kiteto Mkoani Manyara. Karibunisana walimu na wanafunzi wa Engusero, majirani zetu waKongwa hawa. (Makofi)

Mgeni wa Bunge Sports Club kutoka Mkoani Morogoroambaye ni mgeni wa Mheshimiwa Ngeleja ni Ndugu FrancisCheka. Kwa hatua hii niwatambulishe, kama mnavyojuaNdugu Francis Cheka ni boxer, siku ya Jumamosi tarehe 12katika uwanja wa Jamhuri kutakuwa na pambani la mchezowa ngumi wa Kimataifa kati ya Ndugu Francis Chekaambaye atapambana na Ndugu Liben Masamba wa kutokaMalawi. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wotetunakaribishwa Jumamosi Uwanja wa Jamhuri, VIP mtaingiakwa Sh.50,000 na mzunguko Sh.10,000. Mnakaribishwa sana.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao pia wageni watatuwa Mheshimiwa Alex Gashaza ambao ni viongozi wa CCMkutoka Ngara, Mkoani Kagera. Karibuni sana wageni kutokaNgara. (Makofi)

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

Wageni 23 wa Mheshimiwa Silvestry Koka ambao niwafanyabiashara kutoka Kibaha Mkoani Pwani. Karibunisana wafanyabiashara kutoka Pwani. Mmekuja siku nzurisana maana leo ni siku ya mambo yenu ya biashara. Kwahiyo, kaeni hapa msikil ize mambo ya biasharayatakavyoteremka hapa. (Makofi)

Wapo pia wageni watatu wa Mheshimiwa YahayaMassare ambao ni viongozi wa CCM, Kata ya Sanjaranda -Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida. Karibuni sana palemlipo wageni wa kutoka kule Itigi. (Makofi)

Wageni 37 wa Mheshimiwa Elibariki Kingu ambao niWenyeviti na Makatibu wa CCM wa Kata za Jimbo la SingidaMagharibi wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilayana Katibu wa CCM wa Wilaya. Karibuni sana Wanyampaa.(Makofi)

Tunaye mgeni wa Mheshimiwa Seif Gulamali ambayeni mjomba wake Ndugu Hamdani Salum. (Makofi)

Wageni Sita wa Mheshimiwa Mahmoud Mgimwaambao ni familia yake na wapiga kura wake kutoka MufindiMkoa wa Iringa. Karibuni sana wageni kutoka kule Mufindi.Mheshimiwa Mgimwa ndiyo Mwenyekiti wa Kamati yaViwanda na Biashara na mtaona hapa akifanya mamboyake baadaye. Hapana, Mheshimiwa Mgimwa ni Mwenyekitiwa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji. Samahani sananimechanganya. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, wapo pia wageni wannewa Mheshimiwa Edward Mwalongo ambao ni kaka zakekutoka Jijini Dar es Salaam. Karibuni sana. (Makofi)

Mwisho ni wanafunzi 50 na walimu watano kutokaShule ya Sekondari ya John Merlini iliyopo Miyuji Jijini Dodoma.Ooh! Karibuni sana watoto wazuri. Karibuni sana Bungeni nabaadaye nina hakika mtapata maelezo yanayohusu Bungena mtapata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali. (Makofi)

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

Waheshimiwa Wabunge, ninalo tangazo kutoka kwaMheshimiwa Mendrad Kigola, anawatangazieniWaheshimiwa Wabunge ambao mnapenda kushiriki katikazoezi la kulenga shabaha ambalo huwa linafanyika JKTMakutupora, muda wa mazoezi mtatangaziwa ilaanachoomba ni kwamba mjiandikishe pale mapokezi. Kwawale wanaopenda mchezo wa range, kulenga shabaha kwasilaha mbalimbali, msiokuwa na mishtuko ya moyomjiandikishe Jengo la Utawala pale chini ili tukishapata idadiyenu basi ipangwe ratiba kwa ajili ya kwenda JKT Makutuporakwa ajili ya zoezi la kulenga shabaha.

Waheshimiwa Wabunge, mwisho wa matangazo.

MWONGOZO WA SPIKA

WABUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

SPIKA: Katibu, nisomee majina.

NDG. NENELWA MWIHAMBI - KATIBU MEZANI:Mheshimiwa Simba Chawene, Mheshimiwa Susan Lyimo,Mheshimiwa Esther Matiko, Mheshimiwa Gekul naMheshimiwa Maftaha.

SPIKA: Tunaanza na Mheshimiwa Maftaha.

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7), naomba nipateMwongozo wako kwa Kanuni yenyewe hiihii ya 68(7) nanaomba niisome, inasema kwamba:-

“Hali kadhalika, Mbunge anaweza kusimama wakatiwowote ambapo hakuna Mbunge mwingine anayesema nakuomba “Mwongozo wa Spika” kuhusu jambo ambalolimetokea Bungeni mapema...”.

Mheshimiwa Spika, naomba nipate ufafanuzi tafsiriya hili neno ‘Bungeni’, kwa maana ya kwamba Bungenitunamaanisha kwenye viti hivi ndani ya Bunge au Bungeni

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

hata ukiingia getini pale compound hii ya eneo lote niBungeni? Nilikuwa naomba mwongozo wako juu ya tafsirihii.

SPIKA: Eneo lote hili kama ulivyosema hilo la pili niBungeni.

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Ni eneo lote?

SPIKA: Haimaanishi chumba hiki peke yake.

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, jana nil iomba mwongozokutokana na mambo ambayo yalikuwa yanaendelea katikaeneo hili la Bunge. Kulikuwa na watu wa Serikali wa Wizaraya Ardhi lakini pia TAMISEMI wakiwa wanagawa viwanja kwaWaheshimiwa Wabunge na kwamba vile viwanjatumepewa muda maalum ndani ya siku 30. Kwa hiyo,niliomba mwongozo kwamba kwa nini Bunge lisiwekeutaratibu ili sisi Waheshimiwa Wabunge tuweze kuishi hapacomfortably tukiwa na viwanja na tumejenga nyumba kwasababu hali ya kiuchumi sasa hivi ni mbaya kwa WaheshimiwaWabunge, ukaongezwa muda hivi angalau miezi sita.

Mheshimiwa Spika, hivyo niliomba mwongozo...

SPIKA: Mheshimiwa Maftaha, nimekusikia nanimekuelewa. Utaratibu uliowekwa na Manispaa au sasa Jijila Dodoma ndiyo huo na ni kwa wananchi wote kwambaanayetaka kiwanja, viwanja vipo unachagua kiwanja,unalipia ndani ya mwezi mmoja, kwa wananchi wote. Sasaukisema Waheshimiwa Wabunge peke yao wachukuliwekama ni daraja la kipeke yake wao wapewe miezi sita,wakati mwananchi wa kawaida anapewa mwezi mmoja,sidhani kama jambo hilo linakubalika kwa kweli. Kwa hiyo,ukitaka kiwanja, kiwanja kipo ndani ya siku 30 uwe umemaliza

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

kulipa ili fedha zile zipime viwanja vingine. Kwa hiyo, Bungehatuwezi kubadilisha maamuzi ya Manispaa lakini ni ombiambalo Manispaa au Jiji sasa wamelisikia, tuwaachiewaangalie uzito wake kadri watakavyoona inafaa. (Makofi)

Tunaendelea na Mheshimiwa Gekul.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, naombamwongozo wako kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7) juu yajambo ambalo limetokea mapema Bungeni nalo ni swaliNa.218 la Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa kuhusu mitaza barabara ambazo zimeongezeka kwa sheria ya mwaka2007, mita nane kutoka zile 22.5 mpaka mita 30. Kila wakatiSerikali imekuwa ikijibu kwamba haya maeneo ya wananchiyatatumika pale Serikali itakapokuwa inahitaji na hata leoMheshimiwa Dkt. Shukuru amejibiwa hivyo hivyo.

Mheshimiwa Spika, sisi ni watu ambao tumeathirikasana na hizi mita, ni miaka 11 sasa wananchi wengi wa Jimbolangu wameathirika kwa sababu Babati Mjini tuna barabaratatu za lami tumeunganishwa Singida kilometa 163, Arushakutoka Babati kilometa 167, Babati – Dodoma kilometa 258,mita nane kila upande wananchi wana nyumba zao, Serikalihaijui ni lini itawafidia, inasema siku ikihitaji itawafidia.

Mheshimiwa Spika, wananchi hawa wamejenganyumba zao, hawaruhusiwi kukarabati wala hata kujengachoo kama kimebomoka. Naomba mwongozo wako, nikwa nini Serikali iendelee kutujibu hivi wakati sheria hii mwaka2007 wakati inatungwa, hii sheria iliwakuta na wana nyumbazao na wanategemea miaka 50 ijayo bado hatutapanuabarabara zetu na sitegemei kama upanuzi utafanyikamapema. Kwa nini wananchi hawa wasifidiwe na Serikaliinaendelea kutujibu hivyo wakati wananchi wanahangaikana nyumba zao zimedondoka?

Mheshimiwa Spika, naomba Mwongozo wako.(Makofi)

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

SPIKA: Sasa Mheshimiwa Gekul, si ni sheria ilipitishwana Bunge hili hili. Hebu tuendelee kwanza tuone, MheshimiwaEsther Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Naomba mwongozo ambao unaendakuzingatia majadiliano ambayo tunaendelea nayo ya bajetihasa wakati wa Kamati ya Matumizi.

Mheshimiwa Spika, nilitaka kujua na iweze kuelewekani Kanuni ipi hasa ambayo inatumika kipindi kile ambapounakuta umesimama ili kuweza kum-support Mbungeambaye amekuwa ameshika shilingi. Tumeona wakati waKamati ya Matumizi, Wenyeviti wamekuwa wakitumia Kanunimbili, kuna mwingine anatumia ya Kanuni ya 56 ambayoinataka watu 10 waunge mkono hoja ndiyo iweze kujadiliwalakini at a time unakuta kuna Mwenyekiti amekaa hapoanarejea Kanuni ya 103 ambayo mimi nahisi ndiyo right onekwa sababu inazungumzia hoja ya kuondoa shilingi kwenyemajadiliano wakati wa Kamati ya Matumizi na haiwekispecifically ni idadi ya watu wangapi ambao watasimamaili waweze kupewa nafasi kuweza kuunga mkono au ku-support kwa kuchangia hoja hiyo. Hii imeleta sintofahamuna inapoka haki ya kuweza kujadili kwa kina kuhusiana nahoja ambayo inakuwa Mezani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilitaka nijue, ni kwambainatumika Kanuni ya 56 ambapo unakuta kama Mbunge anahoja na imetaja kabisa kwamba Spika atamtaja Mbungeatoe hoja yake na baaaye ataendelea kuelezea kwa dakikatano na baadaye kuomba aungwe mkono kamaitakubaliwa au kukataliwa au tunatumia hii Kanuni ya 103ambayo imeweka bayana ni wakati wa Kamati ya Matumiziambapo kama mimi nimeshika shilingi nasema naendeleakushika shil ingi hata wakisimama wanne au watatu

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

wanachangia? Ningeomba ufafanuzi wa kina ili iwezekutusaidia.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Hili litatolewa ufafanuzi wakekesho baada ya Katibu wa Bunge kuchambua na kuona njiaipi bora zaidi. Japo la kuungwa mkono linakuwa na uzitolakini tutaona hiyo kesho kwa sababu watu wenginewanatuchelewesha na hoja ambayo haina hata uzito, yukonayo yeye peke yake, ndiyo maana ya kusema kwamba uwena hoja inayoungwa mkono lakini kesho tutapata maelekezoambayo ndiyo tutayafuata wote. Mheshimiwa Susan.

MHE. SUSAN A.J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, naminasimama kuomba mwongozo kwa Kanuni hiyohiyo ya 68(7).Tunaendelea na kipindi cha bajeti na najua kwamba bajetiinachukua mchakato mrefu kuanzia Serikali za Mitaa, wadau,kwenye Kamati zako za Bunge na baadaye inakuja hapaBungeni.

Mheshimiwa Spika, ni wiki iliyopita tu tumepitishabajeti ya Wizara ya Elimu na katika bajeti hiyo zilikuwazimetengwa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya upanuzi wa mabweniya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hata hivyo, ni juzi tuMheshimiwa Rais ameamua fedha hizo zihamishwekupelekwa Chuo Kikuu cha Sokoine.

Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako, nisahihi Bunge lako Tukufu liwe limepitisha mafungu haya halafuMheshimiwa Rais aweze kuhamisha? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Susan una uhakika na jambo hilo?Mheshimiwa Simbachawene.

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE: Mheshimiwa Spika,naomba mwongozo wako kwa kupitia Kanuni ya 68(7).Kimsingi mwongozo naouomba unahusu suala la utaratibuwa uendeshaji wa Bunge letu kupitia msingi wa Katiba, milana desturi za Taifa letu la Tanzania.

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Mheshimiwa Spika, kumetokea mazoea ya kukiukaKanuni ya 64 na naomba nisome eneo ambalo natakakupata mwongozo wako. Kanuni hii pamoja na kutambuahaki ya Wabunge ya mjadala, haki ya Wabunge kusemajambo lolote inayotajwa na Katiba katika Ibara ya 100 lakiniikatengenezwa Kanuni ya 64 ambayo inakataza mambofulani fulani katika Bunge hili. Inasema:-

“(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katibainayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadilianokatika Bunge, Mbunge:-

(d) hatatumia jina la Rais kwa dhihaka katika mjadala,au kwa madhumuni ya kutaka kulishawishi Bunge kuamuajambo lolote kwa namna fulani.

(e) hatazungumzia mwenendo wa Rais, Spika waBunge, Jaji, Hakimu au mtu mwingine yeyoteanayeshughulikia utoaji wa haki isipokuwa tu kamakumetolewa hoja mahususi kuhusu jambo husika”. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kanuni hii imekuwa ikivunjwamara kwa mara na Chief Whip wetu mara nyingi sanaamekuwa akisimama kwa ajili ya eneo hili na mara nyingisana Meza imekuwa ikikubaliana na Chief Whip. Je, utaratibuhuu unapozidi kuendelea kila siku wakati Katiba yetu katikaIbara ya 33(2) inamtaja Rais kama Mkuu wa Nchi, Kiongoziwa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. Katiba hii imewaweka watundani ya Bunge hili na Ibara ya 52 inamtaja Waziri Mkuuatakuwa na madaraka juu ya udhibiti na usimamiaji,utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikaliya Jamhuri ya Muungano yaani yuko humu ndani Bungeni napia kuna Mawaziri wako humu ndani Bungeni.

Mheshimiwa Spika, baadhi ya WaheshimiwaWabunge wanapochangia wanawaacha hawa wotehawa wanataka kuzungumza kuhusu Rais. Mazoea haya nikinyume kabisa na mila na desturi zetu za Kitanzania zakuheshimiana. Hivi katika nchi hii ni nani anayestahili

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

kuheshimiwa zaidi ya Rais? Ndiyo maana hata baadhi yaWaheshimiwa Wabunge kukutana na Rais uso kwa usowanazungumza hata yale ambayo hawakutakakuzungumza kwa sababu ndiye anayestahili kuheshimiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mazoea yaliyoko humu nikwamba utani wa baadhi ya Wabunge ni Rais, wanaachaWaziri Mkuu yuko hapa, Mawaziri wako hapa na ndiyomaana tumepewa katika Kanuni zetu siku ya kumuulizamaswali yoyote yale Mheshimiwa Waziri Mkuu maana ndiyeanaweza kuwajibishwa. Pia Bunge limewekewa utaratibuwa kuweza kumtoa Waziri Mkuu kama kuna jambo la Kiserikalikutokana na majukumu ya Waziri Mkuu halijaenda sawa. Hivihawa wote Waziri Mkuu na Mawaziri waliopo wanashindwajekuzungumza nao tukazungumza ndani ya Bunge lakinimpaka wamtaje mtu ambaye yuko nje ya Bunge na niKiongozi Mkuu wa Nchi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi naomba mwongozo wakokuhusu jambo hili. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene uliyoyasemasidhani kama nahitaji kuongeza hata sentensi moja kwasababu ndiyo ukweli wenyewe. (Makofi)

Ulichokifanya ni kutukumbusha tu wote kuzingatiaKanuni zetu na kuheshimu taratibu zetu na kama ulivyosemaKiti kimekuwa kikisisitiza mara kwa mara na Mheshimiwa ChiefWhip amesimamia jambo hili mara kwa mara. Kwa hiyo,umetusaidia kutukumbusha zaidi na zaidi katika jambo hilona sisi tunaendelea kusimamia kuona kwamba halijirudiirudiijambo hilo, nakushukuru sana sana.

Kwa wengine ambao sijatoa miongozo yaotutaifanyia kazi kadiri tunavyoenda, kama mezatumeichukua. Katibu.

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

NDG. STEPHEN N. KAGAIGAI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwaMwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Viwanda,

Biashara na Uwekezaji

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama alivyosomaKatibu, tunaingia katika kuangalia Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwaMwaka wa Fedha 2018/2019, siku mbili leo na kesho. Kwahiyo, sasa nimwite Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biasharana Uwekezaji kwa hotuba yake na baada ya hapo ajiandaeMwenyekiti wa Kamati. Bado hatuna hotuba ya Upinzani kwaupande huo, tunapata nusu saa ya nyongeza angalau,Mheshimiwa Waziri tafadhali, karibu sana. (Makofi)

(Hapa Waheshimiwa Wabunge waliongea bila mpangilio)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tusikilizane, nafikirimmeliona hilo buku. Kwa hiyo, tumpe nafasi MheshimiwaWaziri, tumuazime masikio yetu il i tuweze kumsikia.Mheshimiwa Waziri, karibu sana tafadhali. (Makofi)

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Spika, kabla ya kuwasilisha hotuba yangu,naomba nikuahidi muda si mrefu nitaleta addenduminayoonyesha marekebisho ya maandiko katika hotubayangu. Nitaomba mabadiliko hayo yaingizwe kwenyeKumbukumbu Rasmi za Bunge. Ukurasa wa 13 aya 33 kunamabadiliko ya takwimu katika sentensi ya kwanza, takwimuya jumla ya thamani ya miradi mipya ya viwanda iliyosajiliwakuanzia mwezi Julai 2017 hadi Machi 2018 isomeke Dola zaKimarekani milioni 3,667 badala ya Dola za Kimarekani milioni4,161. Vilevile jumla ya ajira 36,025 badala ya 44,798. Ukurasawa 29, aya ya 68, tarakimu 500 isomeke mita za luku 500,000.Ukurasa wa 349 iongezwe aya ya 350 itakayosemekaMheshimiwa Spika naomba kutoa hoja.

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Mheshimiwa Spika, kwa rususa yako, naombauniruhusu niwatambulishe wanaviwanda waliokujakushuhudia bajeti hii na wengi wao wakitoka Mkoa waPwani. Wanaviwanda wote naomba msimame juu hadharahii iwaone. Ahsanteni mnaweza kukaa, lakini kabla yakuendelea ningeomba utulivu.

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuendelea, naombaniombe samahani hiki kilichopo hapa mbele yenu nimekipatakwenye takwimu za Taifa ndivyo viwanda vilivyotengenezwakijiji kwa kijiji, vyote vimeandikwa hapa kurasa 900. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingirakuweka Mezani taarifa iliyochambua bajeti ya Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji, naomba kutoa hojakwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili nakupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha yaWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka 2018/2019.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sauti zenu ziko juusana, tafadhilini sana, hasa upande wangu wa kulia huku,endelea Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nimshukuruMwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezeshakukutana katika Bunge lako Tukufu kujadili utekelezaji waBajeti ya mwaka 2017/2018, vilevile kujadili Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji kwa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongezaMheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa SamiaSuluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania; na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuongoza kwa busara na hekima na hivyo kuendelea

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

kuifanya nchi yetu kuwa na amani, utulivu na maendeleo.Kwa namna ya pekee, nawapongeza kwa kusimamia kwavitendo agenda ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.Aidha, namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwa na imaninami na kuendelea kunipa dhamana ya kuiongoza nakuisimamia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, nawapongeza pia MheshimiwaDkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mheshimiwa BaloziSeif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya MapinduziZanzibar kwa kusimamia kwa umakini mkubwa masualamuhimu ya ushirikiano wa kisekta na ya Muungano kwaujumla.

Mheshimiwa Spika, pia nawapongeza WaheshimiwaMawaziri na Naibu Mawaziri wote walioteuliwa hivi karibunikuongoza Wizara mbalimbali. Kwa namna ya pekeenamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kumteua MheshimiwaMhandisi Stella Martin Manyanya kuwa Naibu Waziri Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Namshukuru kwaushirikiano anaonipa kama Naibu Waziri katika kusimamiautekelezaji wa majukumu ya Wizara yetu. Vilevile,nawapongeza Waheshimiwa Wabunge wapyawaliochaguliwa kupitia chaguzi ndogo.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napendakumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hotubayake ambayo imeweka msingi na mwelekeo wa utekelezajiwa majukumu ya Serikali kwa mwaka 2018/2019, ambayobaadhi yake yanahusu majukumu ya Wizara yangu. Pia,napenda kuungana na wenzangu kuwapongeza watoa hojawalionitangulia kuwasilisha bajeti zao na kupitishwa naBunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikumpongeza Mheshimiwa Ahmed Sadiq Suleiman, Mbungewa Mvomero kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Viwanda, Biashara na

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Mazingira. Pia, nampongeza Mheshimiwa Innocent LughaBashungwa, Mbunge wa Karagwe kwa kuchaguliwa kuwaMakamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. NawapongezaWaheshimiwa Wabunge wote waliochaguliwa kuwawajumbe wa Kamati hiyo. Ninaishukuru Kamati nzima kwaushauri, maoni na ushirikiano mkubwa inayoendelea kutupakatika kutekeleza majukumu yetu ikiwa ni pamoja namaandalizi ya Bajeti hii. Napenda kulihakikishia Bunge lakoTukufu kwamba Wizara itazingatia ushauri, mapendekezo namaoni yaliyotolewa na Kamati na yale yatakayotolewa naBunge lako Tukufu. Napenda pia kumpongeza MheshimiwaStanslaus Nyongo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwauongozi thabiti kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziriwa Wizara ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda pia kukupongeza wewebinafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuliongozaBunge letu Tukufu kwa umahiri mkubwa. Ni imani yangukuwa, mtaendeleza hekima na weledi mlionao kuisimamiana kuishauri Serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru kwa dhatifamilia yangu kwa kuniombea, kunivumilia na kunipa moyokutekeleza majukumu niliyopewa na Mheshimiwa Rais katikakujenga na kutetea maslahi ya Taifa letu ndani na nje yanchi. Pia nawapongeza na kuwashukuru wananchi wa Jimbolangu la Muleba Kaskazini kwa kuendelea kunipa ushirikianokatika kutekeleza majukumu ya kitaifa na ya Jimbo langu laMuleba Kaskazini.

Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru nakuwapongeza wafanyakazi wa Wizara na taasisi zilizo chiniya Wizara yangu wakiongozwa na Profesa Elisante OleGabriel Laizer, Katibu Mkuu; Profesa Joseph RwegasiraBuchweishaija, Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji)na Ndugu Ludovick James Nduhiye, Naibu Katibu Mkuu(Viwanda), kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikishakwamba dhana ya uchumi wa viwanda inafanikiwa.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kipekeekuwashukuru pia wahisani mbalimbali ambao wamekuwawakishirikiana nasi katika kutekeleza majukumu ya Wizarayangu. Naupongeza uongozi wa Sekta Binafsi na taasisi zakechini ya uongozi wa Dkt. Reginald Abraham Mengi, Mwenyekitiwa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) na Mkurugenzi Mtendajiwake Ndugu Godfrey Simbeye. Napongeza pia uongozi waBaraza la Biashara la Taifa (TNBC) chini ya Mhandisi RaymondMbilinyi na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo.

Mheshimiwa Spika, natoa pole kwako, WaheshimiwaWabunge na familia za wafiwa kwa kuondokewa naaliyekuwa Mbunge mwenzetu, Mheshimiwa Leonidas Gamawa Jimbo la Songea Mjini. Vilevile, napenda kutoa pole kwaWatanzania waliokumbwa na kadhia ya majangambalimbali kama mafuriko, ajali za moto viwandani, ajaliza barabarani na majanga mengine yanayofanana na hayo.

Mheshimiwa Spika, umuhimu wa viwanda katikauchumi wa Taifa. Kutokana na matakwa ya wakati, leo hiininapowasilisha bajeti yangu ya tatu nikiwa Waziri mwenyedhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, napenda tenakurejea tafsiri ya kiwanda. Kiwanda ni eneo ambalo malighafihuchakatwa kwa muktadha wa uongezaji wa thamani.Hivyo, shughuli yoyote, ndogo au kubwa, ya uongezajithamani kwenye malighafi kwa lengo la kuzalisha bidhaanyingine ni kiwanda.

Mheshimiwa Spika, vigezo vya kimataifa vya kugawaviwanda katika makundi ya viwanda vimeelezwa nanitaendelea kuvieleza zaidi. Napenda niwaeleze kuwa kwamujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), hadi kufikia mweziMachi 2018, nchi yetu ilikuwa na jumla ya viwanda 53,876.Kati ya hivyo, viwanda vikubwa ni 251, vya kati ni 173, vidogoni 6,957 na vidogo sana ni 46,495. Kwa kipindi ambacho Serikaliya Awamu ya Tano imeingia madarakani, chini ya uongozimahiri wa Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, hadiMachi 2018, viwanda vipya 3,306 vimejengwa.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia uchumi waviwanda tunamaanisha shughuli zinazolenga maendeleo yawatu na vitu wakati maendeleo ya watu yakipewakipaumbele na sekta ya viwanda ikiwa kiungo muhimu chakuhamasisha maendeleo ya sekta nyingine. Sekta hizo wezeshina tegemezi katika uchumi wa viwanda ni pamoja na kilimo,uvuvi, mifugo, misitu na madini kwa upande wa uzalishajimalighafi za viwanda. Kwa upande mwingine, ustawi waviwanda hutegemea miundombinu ya barabara, reli, usafiriwa anga, nishati, mawasiliano na maji. Aidha, uchumi waviwanda unahitaji rasilimali watu wenye afya thabiti ambaoni muhimu katika mnyororo mzima kuanzia uzalishajimalighafi, uzalishaji wa bidhaa viwandani na usambazajiwa bidhaa hadi mikononi mwa mlaji.

Mheshimiwa Spika, katika ujenzi wa uchumi waviwanda utakaoleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleoya watu, sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo nimuhimu sana. Umuhimu wa sekta hiyo unatokana na ukwelikwamba inahitaji ujuzi na mitaji ambayo Watanzania waliowengi wanaimudu. Sekta hiyo ni shule kwani kwa kupitiaviwanda vidogo na biashara ndogo, wajasiriamali hupataujuzi na uzoefu wa shughuli za uzalishaji na kuweza kuhitimukuwa wawekezaji na wafanyabiashara wa kati nawafanyabiashara wakubwa. Ili kuweza kuakisi vyemamchango wa sekta hiyo hatuna budi kuelekeza nguvu kubwakatika kubuni mikakati ya uanzishwaji na uendelezaji waviwanda vidogo.

Mheshimiwa Spika, ustawi wa shughuli za viwandaunategemea ushiriki wa wadau mbalimbali. Ujenzi waviwanda unaanza kwa kutambua eneo la kujenga kiwandaambalo hubainishwa na kuwekewa miundombinu wezeshina saidizi na mamlaka mbalimbali. Vilevile, ili kujenga sektaya viwanda iliyo endelevu, suala la mazingira ni muhimu.Ujenzi wa viwanda unaihitaji Serikali lakini unahitaji sektabinafsi pia.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mipango namaendeleo ya bajeti kwa mwaka 2017/2018. Kufikia mwezi

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Machi 2018, Wizara ilikusanya maduhuli ya Sh.9,728,635,810.84sawa na asilimia 48.64 ya malengo. Vilevile, hadi kufikiatarehe 9 April i 2018, Wizara il ikuwa imepokeaSh.47,267,949,999.91 kwa ajili ya Fungu 44 na Fungu 60, sawana asilimia 38.68 ya bajeti kwa ajili ya Wizara na taasisi zake.Kati ya fedha hizo, Sh.32,641,257,816.33 ni za Matumizi yaKawaida na Sh.14,626,688,183.58 ni za Matumizi yaMaendeleo.

Mheshimiwa Spika, sekta ya viwanda. Ukurasa wa 11mpaka wa 42 katika Kitabu cha Hotuba nimezungumzia sektahii.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kuhusu suala laubinafsishaji. Kufuatia zoezi la ubinafsishaji nchini, kati yataasisi za umma 341 zilizobinafsishwa, 156 zilikuwa na sifa yakuwa viwanda. Kufikia mwezi Mei 2017, kati ya viwandahivyo, 62 vilikuwa vinafanya kazi vizuri, 28 vilikuwa vinafanyakazi chini ya uwezo, 56 vilikuwa havifanyi kazi kabisa na 10vilikuwa vimeuzwa kwa mali moja moja (asset stripping).Kuanzia mwezi Agosti 2017 hadi Machi 2018, Wizara kwakushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wizara za Kisektailifanya tathmini ya viwanda vilivyobinafsishwa ili kubaini haliya viwanda hivyo baada ya kufanya zoezi la kuhamasishaufufuaji wa viwanda hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa muhtasari, hali ilivyo hadimwezi Machi, 2018. Kati ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa,61 vinafanya kazi vizuri, 22 vinafanya kazi chini ya kiwango,viwanda 18 vimefanyiwa maboresho na wamiliki wake,viwanda 35 viko chini ya uangalizi wa Serikali, viwanda 10visivyofanya kazi vinafanyiwa tathmini kabla ya kuchukuliwahatua za kisheria kulingana na mikataba ya ubinafsishwajina viwanda 10 vilivyouzwa mali moja moja na kupoteza sifaya kuendelea kuwa na shughuli za uzalishaji.

Mheshimiwa Spika, miradi mipya ya viwanda. KuanziaJulai 2017 mpaka Machi 2018, jumla ya miradi mipya 243 yenyethamani ya Dola za Kimarekani shilingi milioni 3,667 nainayotarajiwa kuajiri watu 36,025 ilikuwa imesajiliwa. Kati ya

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

hiyo, miradi 99 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni2,317 itakayoajiri watu 12,995 ilisajiliwa na TIC, miradi 22 yenyethamani ya Dola za Kimarekani milioni 368.92 iliyoajiri watu4,881 ilisajiliwa na EPZA na miradi 122 yenye thamani ya Dolaza Kimarekani milioni 981 na itakayoajiri watu 18,149 ilisajiliwana BRELA. Rejea kiambatanisho changu 4, 5 na 6.

Mheshimiwa Spika, viwanda mama na miradi yakielelezo. Mradi wa Mchuchuma na Liganga. Katikakufanikisha utekelezaji wa Mradi Unganishi wa Mchuchumana Liganga, Serikali iliunda Timu ya Wataalam wa Serikaliikiwa na jukumu la kutambua vivutio vilivyoombwa namwekezaji. Uchambuzi huu ulifanyika kwa kuzingatiamarekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 namabadiliko ya Sheria ya mwaka 2017 katika kusimamiarasilimali zetu. Timu hiyo imekamilisha taarifa ya awaliambayo inasubiri kutolewa maamuzi na mamlaka husika.

Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Matairi Arusha.Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha Kiwanda cha MatairiArusha kinafanya kazi. Jukumu la kuboresha na kuendeshakiwanda hicho litakuwa mikononi mwa sekta binafsi hukuSerikali ikibaki na hisa kulingana na rasilimali zilizopo bilakuwekeza mtaji zaidi. Mpaka sasa, Kamati Maalum ya Serikaliinaendelea kupitia mpango wa kiwanda hicho ili kuamuautaratibu utakaofaa katika kuwekeza na kwa kuzingatiamaslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kuzalisha MagadiEngaruka Soda. Wizara kupitia NDC na kwa kushirikiana naHalmashauri ya Wilaya ya Monduli imekamilisha zoezi laupimaji ardhi ya mradi pamoja na uthaminishaji wa mali yawananchi ili kubainisha kiasi cha fidia kitakacholipwa.Michoro na matumizi ya ardhi iko kwenye hatua yakukamilishwa. Aidha, NDC inaendelea kutangaza mradi huokwa wawekezaji mbalimbali i l i kumpata mbia wakushirikiana naye kuanzia hatua ya utafiti kwa kuzingatiateknolojia bora ya kuvuna magadi hayo.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Spika, Uendelezaji wa Maeneo yaUwekezaji. Maeneo Maalum ya Serikali ya Uwekezaji (EPZ).Wizara kupitia Mamlaka ya EPZ imeendelea kuhamasishawawekezaji ndani ya maeneo yote ya EPZ na SEZ. Hadi mweziMachi 2018, kuna jumla ya viwanda 111 katika maeneo yaEPZ na SEZ. Tathmini ya uwekezaji na matokeo ya viwandachini ya programu za EPZ na SEZ tangu kuanzishwa kwaMamlaka ya EPZ, imeonesha mafanikio. Hadi Machi 2018jumla ya mtaji wa Dola za Kimarekani bilioni 1.86 uliwekezwana mauzo ya bidhaa nje ya nchi yenye thamani ya Dola zaKimarekani milioni 1,359.94 yalifanyika na ajira 52,698zimeweza kupatikana.

Mheshimiwa Spika, viwanda vyenye hadhi ya EPZ njeya Maeneo Maalum ya Serikali. Hadi sasa, kuna viwanda 72ambavyo vinamilikiwa na kuendeshwa na sekta binafsi chiniya utaratibu wa EPZ nje ya maeneo maalum ya Serikali.Viwanda hivyo vimewekeza jumla ya Dola za Kimarekanimilioni 315 na kutoa ajira 13,930. Kwa mwaka 2017/2018pekee, viwanda hivyo vimeweza kuuza nje ya nchi bidhaazenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 115.12. RejeaKiambatisho Na. 8.

Mheshimiwa Spika, maendeleo katika sekta ndogona viwanda vidogo. Mradi wa kuunganisha matrekta ainaya URSUS unaendelea katika eneo la TAMCO Kibaha chini yausimamizi wa NDC. Hadi mwezi Disemba 2017, Semi KnockedDown (SKD) matrekta 727 yamewasili nchini ikiwa ni sehemuya matrekta 2,400 yaliyoanishwa katika mkataba nauunganishaji unaendelea. Kati ya SKD za matrektayaliyowasili, 148 yameunganishwa na yako tayari kwa mauzo.

Mheshimiwa Spika, uunganishaji wa magari. Kampuniya Jiefang Motors imeunganisha magari 803 yanayojumuishaSKD assembled 354, CBU 449. Aidha, Wizara kwa kushirikianana Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikiinaandaa sera ya kuunganisha magari, ili kuhamasishauendelezaji wa sekta hiyo nchini.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Mheshimiwa Spika, viwanda vya kuzalisha chuma nabidhaa za chuma. Hadi kufikia mwezi Machi 2018, kulikuwana viwanda 25 vya kuzalisha chuma na bidhaa za chumaikiwa ni ongezeko la viwanda vitatu kwa kipindi cha mwakammoja. Uwezo uliosimikwa ni wa kuzalisha tani 577,600 kwamwaka. Kwa sasa uwezo wa uzalishaji (capacity utilization)ni asilimia 42.

Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Kiluwa Steelkilichoko Mlandizi Mkoani Pwani kinaendelea na uzalishajiambapo mwaka 2017 kilizalisha tani 12,000 za vyuma.Kiwanda cha Lodhia Steel Industry kimeanza uzalishajiambapo wanazalisha takriban tani 3,700 za nondo namabomba mbalimbali. Kiwanda cha Lake Steel AlliedProducts kipo katika hatua za mwisho za kuweka mitambona Kampuni ya ALAF imetengeneza tawi lake hapa Dodoma.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya saruji. Mpaka sasakuna viwanda vya saruji 14 vyenye uwezo uliosimikwa wakuzalisha tani milioni 10.98 kwa mwaka na uwezounaotumika ni takriban tani milioni 7.4 kwa mwaka wakatimahitaji ya nchi ni takriban tani milioni 4.8. Aidha, uwekezajikatika kiwanda cha saruji unaendelea kukua ambapo katikakipindi cha mwaka 2017/2018, kiwanda kipya cha saruji chaKilimanjaro Cement kilichoko Mkoa wa Tanga kilianza kazi.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya vigae. Nchi yetu inaviwanda viwili vikubwa vya uzalishaji wa vigae vyenye uwezouliosimikwa wa kuzalisha mita za mraba 130,000 kwa siku.Kiwanda cha Vigae cha Goodwill Ceramic kimekamilika nakinaendelea na uzalishaji. Kiwanda hicho chenye uwezo wakuzalisha mita za mraba 80,000 kwa siku, kinaajiri watu 2,200kikihusisha ajira 700 za kudumu na vibarua 1,500. Asilimia 30 –40 ya vigae vinavyozalishwa na kiwanda hiki vinauzwa hapanchini, wakati asilimia 60 – 70 vinauzwa nje ya nchi. Vilevile,Kiwanda cha Twyford kilichoko Chalinze chenye uwezo wakuzalisha mita za mraba 50,000 za vigae kwa sikukimekamilika na kimeanza uzalishaji mwezi Novemba 2017.Kiwanda hiki kinasubiri mamlaka kuweza kukifungua.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mheshimiwa Spika, viwanda vya vioo. Tanzania inakiwanda kimoja cha vioo na juhudi zinafanyika na tumepatawawekezaji watatu kuja kuwekeza zaidi.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya kutengenezachokaa. Kiwanda cha Neelkanth Lime Ltd kilichopo katikaeneo la Amboni Mkoani Tanga kinazalisha tani 15,000 zachokaa kwa mwezi na kuajiri wafanyakazi 430. Kiwanda kipokatika hatua za awali za upanuzi ambapo Dola zaKimarekani milioni 18.4 zinatarajiwa kutumika. Upanuzi huounaotarajiwa kukamilika mwaka 2019 utaongeza uwezo wauzalishaji hadi tani 35,000 kwa mwezi na kuongeza ajira zamoja kwa moja mpaka 1,500 na zisizokuwa za moja kwamoja 2,500. Soko kuu la bidhaa hii ni Afrika Kusini, Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo, Malawi, Zambia pamoja na migodiya madini hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya dawa. Hivi sasa nchiina jumla ya viwanda 15 vya kuzalisha dawa na vifaa tiba.Viwanda hivyo vinazalisha asilimia 12 ya mahitaji ya dawanchini. Ili kutatua changamoto ya uwezo mdogo wa uzalishajinchini, juhudi za kuhamasisha uwekezaji zimeendeleakufanyika ambapo Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizaraya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilifanyamkutano na wadau tarehe 4 April i, 2018, ambapowawekezaji 38 walionesha nia ya kuwekeza katika sekta yadawa na vifaa tiba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha uwekezajikatika viwanda vya dawa na vifaa tiba, Bohari Kuu yaTanzania (MSD) imetoa kipaumbele na kuingia mikataba yakununua dawa kutoka viwanda vya ndani vinavyozalishadawa zinazokidhi viwango.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya nguo. Tanzania inaviwanda 11 vya nguo na mavazi vinavyofanya kaziambavyo kwa sasa hutumia asilimia 50 ya uwezo wakeuliosimikwa. Hali hiyo imetokana na ushindani wa nguokutoka nje ya nchi na baadhi ya viwanda kutumia teknolojiazilizopitwa na wakati na hivyo kutumia asilimia 30 tu ya

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

pamba inayozalishwa nchini. Serikali inaendelea kutekelezamkakati wa kundeleza sekta ya pamba mpaka mavazi ikiwani pamoja na kushirikisha Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi yaJamii kuwekeza katika sekta hiyo.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya kusindika nyama.Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani jumlaya viwanda 7 vyenye uwezo wa kuchakata ng’ombe 2,260na mbuzi na kondoo 9,200 kwa siku vinaendelea kujengwa.Kukamilika kwa viwanda hivyo kutaifanya Tanzania kuwana jumla ya viwanda 25 vyenye uwezo wa kuchakata jumlaya ng’ombe 3,800, mbuzi na kondoo 10,090, nguruwe 300 nakuku 44,000 kwa siku. Aidha, Serikali itaendelea na juhudi zakuhakikisha kiwanda cha Triple S kilichobinafsishwa naKiwanda cha Nyama cha Mbeya ambacho utaratibu waubinafsishaji wake haukukamilika vinafanya kazi. RejeaKiambatisho Na. 10.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya vinywaji. Tanzaniaina viwanda vingi vya kuchakata maji, juisi, maziwa, mvinyo,bia na vinywaji vikali na idadi ya viwanda hivyo inaongezeka.Moja ya viwanda vipya vya maji ni kiwanda cha Kampunicha Dodoma Innovation & Production Ltd kilichoko Ntyukakatika Jiji la Dodoma. Kiwanda hicho kiko katika hatua zamwisho za ujenzi na kitakuwa na uwezo mkubwa wakuzalisha maji na kuajiri watu 80 kwa siku wa moja kwa mojana 120 wasiokuwa wa moja kwa moja. Pamoja na kiwandahicho, viwanda vya vinywaji baridi vya Sayona na Lakairovya Jij ini Mwanza vil imezinduliwa mwaka 2017 navinaendelea na uzalishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Tanzania ina viwanda saba vyakusindika zabibu vilivyopo katika Mkoa wa Dodoma. Kati yahivyo, viwili hutengeneza mvinyo na vitano vinatengenezamichuzi ya zabibu na kuiuza kwa viwanda vya mvinyo.Kiwanda cha mvinyo cha CETAWICO kina uwezo wa kuzalishatani milioni 2 hadi 3 za mvinyo kwa mwaka. Kiwanda hichokinatoa ajira 35 za moja kwa moja na hupata malighafikutoka kwa wakulima zaidi ya 600. Kiwanda cha ALKO-VINTAGE Ltd cha Jijini Dodoma kina uwezo wa kuzalisha lita

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

milioni 1.5 za mvinyo na kutoa ajira 50 za moja kwa moja nahupata zabibu kutoka kwa wakulima zaidi ya 500.

Mheshimiwa Spika, pamoja na viwanda hivyo viwili,viwanda vitano vilivyosalia ni vidogo na vinatengenezamichuzi ya zabibu ambayo inauzwa kwa wenye viwandavikubwa vya mvinyo. Aidha, kiwanda cha DOWICOambacho kilibinafsishwa kinakarabatiwa ili kianze uzalishaji.Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ilikuhakikisha wakulima wa zabibu nchini wanapata soko lauhakika na kuongeza ajira.

Mheshimiwa Spika, Tanzania ina viwanda 82 vyamaziwa vyenye uwezo usiosimikwa wa kusindika jumla yalita 757,550 kwa siku. Kwa sasa usindikaji ni lita 154,100 kwasiku, sawa na asilimia 20.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya vifaa vya umeme.Kufuatia Serikali ya Awamu ya Tano kutoa kipaumbele kwaviwanda vya ndani, hatua hiyo imechochea kwa kiasikikubwa viwanda vya ndani kuongeza uwezo wa uzalishaji.Mfano, Kiwanda cha TANELEC Limited kina uwezo sasa watransformer 14,000 kwa mwaka na kitaongeza ajira kutoka120 hadi 300 ifikapo mwisho wa mwaka 2018. Kampuni yaEuro imewekeza Dola za Kimarekani 38 milioni kwa ajili yakutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme ikiwemotransformer. Kiwanda hicho kitakapokamilika kitaajiriwafanyakazi 800. Vilevile, Kuna viwanda viwili vya kutengezaLuku za umeme ambavyo ni INHEMETER kilichowekeza mtajiwa Dola za Kimarekani milioni 2 na kiwanda kingine BaobabEnergy Systems Tanzania kilichowekeza Dola milioni 1.7.Viwanda hivi vitakapokamilika tutaweza kuwa na mita zakutosha na kuuza nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kufuatia uhamasishaji mkubwakatika uwekezaji wa sekta ya sukari, Kampuni ya KigomaSugar imeonesha nia ya kuwekeza, Green Field Plantationsnayo inategemea kuwekeza Mkoani Kigoma, Nkusu TheoSugar Company itawekeza Mkoani Ruvuma. Napendanilieleze Bunge lako Tukufu kwamba hawa wawekezaji

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

ambao walipewa fursa hii watakapozembea Serikaliitachukua hatua mara moja, hasa Kampuni ya Kigoma Sugar.

Mheshimiwa Spika, ili kuhamasisha wenye viwandavya sukari kuongeza uzalishaji, utaratibu wa uagizaji waupungufu wa sukari (gap sugar) uliwekwa chini ya kampunizinazozalisha sukari kwa kupeana kiwango maalum (quota)na siyo wafanyabiashara wengine. Kupitia utaratibu huo,makampuni manne yanayozalisha sukari yamepewa jukumula kuagiza sukari kwa masharti kuwa hakutakuwepo naupungufu wa sukari nchini na lazima wapanue mashambaya miwa ili ifikapo mwaka 2020, Tanzania ijitosheleze kwasukari. Kwa kuzingatia masharti hayo, viwanda vya sukarivya Kilombero, TPC, Kagera Sugar, Mtibwa, vimeonesha niaya kupanua uwekezaji katika mashamba ya miwa na uwezowa usindikaji wa bidhaa hiyo.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya kusindika vyakula,mbogamboga na matunda. Jitihada zilizokwishaanza zakuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kusindika matundazinaendelea vizuri na hivyo kuwa suluhisho la uharibifu wamatunda. Kiwanda cha kusindika matunda cha Elven AgriCompany Limited kilianzisha uzalishaji mwezi Februari 2017,kinasindika tani 4 za matunda kwa siku. Kiwanda cha SayonaFruits kilichoko katika eneo la Mboga, Chalinze kimekamilishaujenzi wa majengo na uzalishaji unatarajiwa kuanza mweziJulai 2018. Ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyanya chaDABAGA kilichoko Mkoani Iringa eneo la Ikokoto, Ilulaumekamilika. Kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika tani1,200 kwa mwezi na kutoa ajira za moja kwa moja 100.

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya MahashreeAgroprocessing Tanzania Limited imewekeza katika kiwandacha kusindika mazao jamii ya kunde husasan mbaazi.Kiwanda hicho kinajengwa katika Kijiji cha Mtego wa Simba,Halmashauri ya Morogoro Vijijini ambapo Dola za Kimarekanimilioni 220 zitawekezwa. Ujenzi huo unategemea kukamilikana kuanza uzalishaji mapema mwaka 2019 nakitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 2,000mpaka 6,000 kwa mwezi.

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Spika, viwanda vya kusindika chai nakahawa. Ujenzi wa Kiwanda cha Kusindika Chai cha UNILEVERkilichoko Mkoani Njombe umekamilika. Kiwanda hichokil ichojengwa kwa gharama ya EURO milioni 7.5,kitakapokamilika kitaweza kusindika majani ya chai tani 50kwa siku na kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 150 kwasiku na kuajiri wafanyakazi 300 ikiwemo na kusaidiawakulima.

Mheshimiwa Spika, kuendeleza kanda na konganoza viwanda. Wizara iliingia Makubaliano ya Awali (Memorandof Understanding) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo yaViwanda tarehe 08 Machi, 2018 kwa ajili ya kutekelezaProgramu ijulikanayo kama Partnership for CountryProgramme. Programu hiyo inayosimamiwa na UNIDOinajielekeza katika ujenzi wa maendeleo endelevu na jumuishiya viwanda na inalenga kutekeleza mipango na programuza nchi na kuleta maendeleo ya viwanda kulingana naprogramu za kipaumbele tutakazojiwekea.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC imetengaeneo la ekari 95 kati ya ekari 230 za Eneo la Viwanda laTAMCO – Kibaha kwa ajili ya ujenzi wa Kongano maalum laviwanda vya nguo na mavazi. Mpango Kabambe (MasterPlan) kwa kuendeleza eneo hilo na michoro ya eneo hiloimetayarishwa na kuingizwa katika ramani ya Mji wa Kibaha.

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Ofisiya Taifa ya Takwimu inaendelea kukusanya takwimu zaviwanda vidogo, vya kati na vikubwa itakayowezeshakuandaa Taarifa ya Mwaka ya Utafiti wa Uzalishaji Viwandani(Annual Survey of Industrial Production) inayotarajiwakukamilika mwezi Juni 2018. Taarifa hizo zitatumika kufanyachambuzi mbalimbali zitakazosaidia Serikali kufanyamaamuzi ya kisera na kuweka mikakati ya kuendeleza sektaya viwanda.

Mheshimiwa Spika, mafanikio makuu ya sekta yaviwanda. Hivi sasa, nchi yetu inajitosheleza kwa mahitaji yasaruji tukiwa na viwanda 14. Kwa hivi sasa tunavyo viwanda

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

25 vya kuzalisha chuma. Hali hiyo imetuwezesha kujitoshelezakwa mahitaji ya mabati, nondo, angle bars, hollow section,kwa kutaja baadhi. Vilevile tuna viwanda 15 vya kuzalishabidhaa za plastiki ikiwemo mabomba ya maji. Hali hiyoimetufanya tuwe na uwezo wa kuzalisha mabomba yakutosha kwa mahitaji ya soko la ndani na ziada kuuza nje.Tunao uwezo wa kuzalisha vigae vyenye uwezo wa kuzalishamita za mraba 130,000 kwa siku na imekuwa kichocheo chakujenga nyumba nzuri na safi.

Mheshimiwa Spika, nchi yetu pia inajitosheleza kwamahitaji ya vinywaji mbalimbali hususan maji ya chupa, soda,vileo kwa kutaja baadhi. Maendeleo katika ujenzi waviwanda yanaonekana pia katika usindikaji wa vyakula kwakutumia mitambo ya kisasa na ujuzi katika ufungashaji. Halihiyo imesaidia kuongeza thamani ya mazao na kuwezeshawananchi mpaka ngazi ya vijiji kupata vyakula vyenyeviwango na ubora wa hali ya juu. Tumefanikiwa kuvutiaujenzi wa viwanda viwili vya kutengeneza mita za umeme,kama nilivyoeleza awali Europe pamoja na Africableswameongeza uwezo katika kutengeneza Transfoma.Tanzania hatupaswi kuagiza transfoma kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, sekta ya viwanda vidogo nabiashara ndogo, nimeieleza ukurasa wa 42 - 48 wa kitabuchangu cha hotuba.

Mheshimiwa Spika, viwanda vidogo ni muhimu katikaustawi wa Taifa letu kwani vinachochea ujenzi wa uchumijumuishi. Sekta hiyo inaajiri takribani Watanzania milioni 6 kwasasa na huchangia Pato la Taifa kwa takribani asilimia 35.Viwanda vidogo sana, vidogo na vya kati vimechukua zaidiya asilimia 98 ya idadi ya viwanda nchini na wawekezaji waviwanda katika kundi hilo ni Watanzania wenyewe.

Mheshimiwa Spika, nitaomba nirudie hapo, viwandavidogo sana, vidogo na vya kati vimechukua zaidi ya asilimia98 ya idadi ya viwanda nchini na wawekezaji wa viwandakatika kundi hilo ni Watanzania wenyewe. (Makofi)

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa viwanda vidogo nabiashara ndogo. Wizara imekamilisha Mwongozo waKusimamia Maendeleo na Ujenzi wa Viwanda nchiniutakaowezesha mikoa na wilaya kusimamia jukumu hilo kwaufanisi na tija. Mwongozo uko tayari.

Mheshimiwa Spika, ushirikiano na TAMISEMI. Katikamwaka 2017/2018, Wizara imetembelea baadhi ya mikoa ilikutathmini zoezi la utengaji wa maeneo ya uwekezaji waviwanda na biashara ndogo nchini. Maeneoyaliyotembelewa ni Mikoa ya Kigoma, Mbeya, Singida naTanga.

Mheshimiwa Spika, kuendelea kusimamia Mfuko waMaendeleo ya Ujasiriamali (NEDF). Hadi kufikia Machi 2018,mtaji wa NEDF umeweza kufikia shilingi bilioni 7.8. Ukuaji kwashilingi bilioni 2.7 umetokana na kuzungusha mtaji wa shilingibilioni 5.05 uliotolewa na Serikali tangu Mfuko ulipoanzishwamwaka 1994. Pamoja na ongezeko la pesa hizo, tumewezakutoa ajira 4,438 mwaka 2017/2018, kati yao wanawake ni2,308.

Mheshimiwa Spika, sekta ya uwekezaji, nimeielezeaukurasa wa 48 – 53. Ujenzi wa uchumi wa viwanda nchiniunahitaji ushiriki mpana na shirikishi wa sekta ya umma nabinafsi. Moja ya kazi muhimu katika kujenga uchumi waviwanda ni kuhamasisha na kuvutia mitaji na wawekezaji;kuweka mazingira wezeshi na rafiki; kutangaza fursa zilizopokatika miradi na maeneo mbalimbali; kuboresha nakutangaza vivutio katika maeneo mbalimbalii ya uchumi,kwa kutaja machache. Wizara kupitia TIC na kwa kushirikianana Taasisi za Sekta Binafsi imeendelea kuhamasishawawekezaji wa ndani na nje, napenda kuchomokeakwamba imefanya kazi hii vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuratibu uwepo wa mazingirabora ya uwekezaji. Wizara iliendelea kuandaa na kushirikivikao vya pamoja vya mashauriano kati ya Serikali na SektaBinafsi kwa lengo la kupata maoni ya kuboresha mazingiraya biashara na uwekezaji nchini. Katika mwaka 2017/2018,

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

mikutano miwili ya ngazi ya juu iliyohusisha Waziri wa Fedhana Mipango, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji naviongozi wakuu wa taasisi za Serikali na binafsi ilifanyikaOktoba na Januari 2018 Mjini Dodoma. Serikali na Sekta Binafsiwamekubaliana kuendelea kuwa na mikutano kama hiyoya majadiliano kwa kuwa ina umuhimu sana katika kupataufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuboresha mazingiraya uwekezaji nchini.

Mheshimiwa Spika, sekta ya biashara nimeielezeaukurasa wa 53 – 67 katika Kitabu changu. Wizara ina jukumula kujenga na kuendesha mfumo wa kibiasharaunaosimamiwa kisheria, unaotabirika na wenye uwazi ilikuwezesha ufanyaji biashara kwa urahisi na tija kubwa.Katika kutekeleza jukumu hilo, Wizara imeendelea kushirikikatika majadiliano ya kibiashara kati ya nchi na nchi, kikandana kimataifa kwa lengo la kufungua fursa mbalimbali zabiashara kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini.

Mheshimiwa Spika, kuendeleza majadiliano yabiashara il i kupanua fursa za masoko na uwekezaji,majadiliano baina ya nchi na nchi. Wizara iliratibu Mkutanowa Kamati ya Pamoja ya Biashara (JPC) kati ya Tanzania naIndia; Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano(JPC) kati ya Tanzania na Misri; na Mkutano wa Pamoja katiya Tanzania na Kenya. Aidha, Wizara ilipitia Mkataba waBiashara na Uchumi baina ya Tanzania na Urusi na Mkatabawa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Tanzania na Mauritius.

Mheshimiwa Spika, majadiliano ya Kikanda. Mwaka2017/2018, Tanzania iliendelea kushiriki katika Mikutano yaKikanda yenye lengo la kurahisisha ufanyaji biashara bainaya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika, kupitia Mkutano wa 19 wa Wakuuwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania imeendeleakuwa na msimamo wa kutokusaini Mkataba wa Ubia waKiuchumi baina ya nchi za Afrika Mashariki na Umoja waUlaya. Msimamo huo umezingatia Azimio la Bunge kuishauri

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Serikali kutosaini mkataba huo hadi hapo utakapokidhimaslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa 29 wa Kamatiya Mawaziri wa Biashara wa SADC, Tanzania ilifanikiwakutetea na kukubaliwa kuendelea kutoza ushuru sukari yaviwandani asilimia 10 na ya majumbani asilimia 25. Hivyo,sukari hiyo inayoingizwa nchini kutoka nchi za SADCitaendelea kutozwa ushuru kwa kipindi cha miaka mitatu(3) mpaka 2020 tutakapokuwa tunazalisha sukari ya kutoshakama nilivyoeleza awali.

Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki Mkutano wa Nnewa Mawaziri wa Biashara wa Umoja wa Afrika ambapoTanzania iliweza kutetea na kupendekeza maboresho kwenyevipengele vyenye kuleta unafuu kwa nchi katika Mkatabawa Africa Continental Free Trade Area (AfCFTA) hususan Itifakiya Masuala ya Biashara ya Bidhaa na Biashara ya Huduma.

Mheshimiwa Spika, sekta ya masoko nimeielezakwenye ukurasa wa 67 -77 katika Kitabu changu inahusu kutoatozo zenye kero, ada zinazojirudia na kurahisisha majukumuya taasisi mbalimbali. Vilevile, inahusu kuhamasisha Mamlakaza Serikali za Mitaa Kuanzisha Vituo Maalum vya KuuziaMazao. Katika sehemu hiyo tunahamasisha ushindani katikaununuzi na uuzaji wa mazao. Pia tunahamasisha kuimarishabiashara ya masoko mipakani.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa taasisi zilizoko chiniya Wizara nimeielezea ukurasa wa 85 – 135 katika kitabuchangu.

Mheshimiwa Spika, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).Majukumu yaliyotekelezwa na taasisi hii yameanishwa nautekelezaji wa miradi ya viwanda mama na miradi yakielelezo chini ya utekelezaji wa Sekta ya Viwanda, aya ya 34hadi 36 na aya ya 39 mpaka 92 ya kitabu changu cha hotuba.

Mheshimiwa Spika, kuna Mamlaka ya Maeneo Huruya Uzalishaji wa Bidhaa kwa ajili ya Mauzo Nje. Hapa

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

tunaelezea kuendeleza Eneo Maalum la Uwekezaji la Kurasini;uendelezaji wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone;na tunaelezea shughuli za Kitengo Maalum cha Teknolojia.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka imefikia hatua nzurikatika kutekeleza mpango wa maboresho ya Kituo chaHuduma kwa Wawekezaji (One Stop Service Centre) namifumo mbalimbali ya taasisi. Taasisi ya TradeMark East Africaimeidhinisha pendekezo kuhusu msaada wa kitaalam nafedha katika kuboresha mifumo mbalimbali ya taasisi kwakutumia TEHAMA. Pia, Mamlaka ya EPZ inashirikiana na Shirikala Maendeleo la Ujerumani (GIZ) katika kuandaa Programuya Usalama wa Maji (Water Security Program) ambayoitawahakikishia wawekezaji uwepo wa maji muda wote nakatika ubora unaokubalika.

Mheshimiwa Spika, Shirika la Utafiti wa Maendeleo yaViwanda Tanzania (TIRDO) litashughulika na kutoa hudumaza kitaalam viwandani; kuanzisha na kuhakiki Maabara yaMakaa ya Mawe na Mafuta na Gesi; na inashughulikia piashughuli za kushauri viwanda vyetu.

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Zana za Kilimo naTeknolojia Vijijini (CAMARTEC) inashughulikia kutafiti mahitajina kuendeleza na kutengeneza teknolojia mbalimbali,nimeielezea. Kwa kina nimeelezea kutafiti na kuendelezausambazaji wa teknolojia kwa matumizi bora ya nishati, hiyoni kazi ya CAMARTEC na kuhamasisha usambazaji wateknolojia zinazobuniwa nchini na hiyo ni kazi ya CAMARTEC.

Mheshimiwa Spika, Shirika la Uhandisi na Usanifu waMitambo Tanzania (TEMDO) wanaboresha, kuendeleza nakuhamasisha utengenezaji na utumiaji wa kibiashara wamitambo na wamebuni na kuendeleza teknolojia jadidifu.

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Mbolea Tanzania.Katika mwaka 2017/2018, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC),imesimamia uingizaji na usambazaji wa mbolea za ainambalimbali hapa nchini. Katika kipindi hicho, TFC imefanikiwakusambaza mbolea tani 5,720 katika mikoa yote ya Tanzania.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Spika, Shirika la kuhudumia ViwandaVidogo (SIDO) limejenga maeneo ya viwanda katika Mikoaya Dodoma, Geita, Kagera, Katavi, Manyara, Mtwara naSimiyu. Pia linaimarisha uwezo wa uhawilishaji wa teknolojiana uanzishwaji wa viwanda vidogo.

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),kinahamasisha kwa kuwalenga wawekezaji wa nje nauwekezaji wa ndani; kusajili miradi ya uwekezaji; kusimamiachangamoto za uwekezaji; kunaratibu miradi ya uwekezajimahiri kama nilivyoeleza hapo mwanzoni na wanaboreshautoaji wa huduma mahiri kwa kutumia One Stop Centre nakuwezesha usajili kwa njia ya mtandao kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu kuzungumza hili katikaTIC. Katika kipindi cha Julai, 2017/2018, taasisi imeendeleana maboresho katika kuhudumia wawekezaji ili kuwasaidiakupata vibali na leseni mbalimbali wanazozihitaji kuanzishamiradi yao. Katika juhudi hizo, Kituo kimeongeza idadi yataasisi zilizopo katika Huduma za Mahali Pamoja kwa kuwekapamoja Maafisa wa TANESCO, TFDA, TBS pamoja na OSHAwote wanapokutana TIC. TIC wanasaidia wajasiriamaliwadogo na wa kati kuibua fursa za uwekezaji nakuwaunganisha na wafanyabiashara wakubwa (BusinessLinkages).

Mheshimiwa Spika, Shirika la Viwango Tanzaniawanakagua ubora na bidhaa zitokazo nje kabla ya kuingianchini (Pre-Shipment Verification of Conformity to Standards-PVoC) ili kulinda bidhaa na viwanda vya Tanzania. Piawanatoa leseni ya ubora kwa bidhaa mbalimbali; wanatoamafunzo kuhusu viwango na udhibiti wa ubora (qualityassurance); wametayarisha viwango vya kitaifa katika sektandogo za uhandisi na usindikaji wa kufanya ugezi kwa vifaana mashine mbalimbali na wanapima sampuli na bidhaambalimbali.

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Usajili wa Biashara(BRELA) wanaboresha mifumo na taratibu za utoaji hudumakwa kutumia teknolojia mbalimbali.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Mheshimiwa Spika, Bodi ya Usimamizi wa StakabadhiGhalani wanaainisha na kufanya ukaguzi wa ghalazinazosajiliwa na zinazotarajiwa kusajiliwa nchini na wanatoaelimu ya mfumo wa stakabadhi ghalani.

Mheshimiwa Spika, Chama cha Hakimiliki (COSOTA)wanaongeza makusanyo ya mirabaha; wametoa elimu nawanaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau wasanaa kuhusiana na mambo ya haki miliki na haki shiriki;wanafanya ukaguzi wa kazi zinazolindwa na Sheria ya HakiMiliki na Haki Shiriki (Anti-Piracy Raids) na kushughulikiamigongano ya kikesi na wanaendelea kusajili wanachamawapya na wasanii katika kuratibu kazi zao.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maendeleo yaBiashara (TANTRADE) wanaboresha na wanaendeleakuboresha upatikanaji wa soko la bidhaa na hudumazinazozalishwa nchini; wanaratibu na kudhibiti uendeshaji wamaonyesho ya kimataifa nchini; wanaendelea kuandaamikutano ya wafanyabiashara; wanashiriki katika maonyeshoya kimataifa ndani na nje ya nchi; na kuboresha nakuimarisha mfumo wa Taifa wa Taarifa za kibiashara.

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Vipimo wanakaguana kusimamia matumizi sahihi ya vipimo na wanakaguabidhaa zilizofungashwa kwenye maeneo mbalimbali yamipakani bandarini na viwandani.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Ushindani (TFC) shughulizao, wanaendelea na kudhibiti na kupambana na uingizajiwa uzalishaji wa bidhaa bandia; wanachunguza mashauriyanayohusu migongano ya kimakampuni na wanamlindana kumuelimisha mlaji.

Mheshimiwa Spika, Baraza la Ushindani wanasikilizana kutoa maamuzi ya kesi za rufaa pale inapokuwa imetokaTFCC.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Elimu ya Biasharawanashughulika na ujenzi wa maktaba mpya; madarasa na

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

kumbi za mihadhara katika Kampasi ya Dar es Salaam nawanaimarisha uwezo wa watumishi (capacity building) ilichuo chetu kiweze kutoa elimu ya biashara.

Mheshimiwa Spika, mwelekeo wa sekta ya viwanda,biashara na uwekezaji kwa mwaka 2018/2019. Ujenzi wauchumi wa viwanda unatazamwa kuwa kiini cha mageuziyenye kuleta mafanikio na mwelekeo wa maisha bora nayenye furaha kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Mheshimiwa Spika, dhamira ya ujenzi wa uchumi waviwanda imefafanuliwa zaidi na kuwekewa mikakati katikaMpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017– 2020/2021. Msisitizo mkuu wa maendeleo ya viwandavinavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini hususanmazao ya kilimo (mafuta ya kula, sukari, vyakula na vinywaji),madini na chuma na kemikali. Aidha, Serikali imeahidikusimamia kutekeleza mipango hiyo kama ilivyoainishwakatika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 -2020.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naombasasa nieleze vipaumbele na malengo ya sekta kwa mwaka2018/2019. Vipaumbele kwa mwaka 2018/19 nirejee hotubayangu ukurasa wa 138 – 139 katika kitabu cha hotuba.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/2019,vipaumbele vya Wizara kwa kushirikiana na taasisi zake nikutunisha mtaji wa NEDF; kuendeleza miradi ya kielelezo:Mchuchuma na Liganga kwa kulipia fidia, Magadi SodaEngaruka na Kiwanda cha Matairi Arusha; uendelezaji waEneo la Viwanda TAMCO Kibaha; Mradi wa kuunganishaMatrekta ya URSUS; uendelezaji wa mitaa/maeneo yaviwanda vya SIDO; kuendeleza Kanda Kuu za Uchumi(Ruvuma, Tanga, Kigoma na Manyoni), Bagamoyo SpecialEconomic Zone, Kurasini Logistic Centre, Kigamboni IndustrialPark; kuendeleza utafiti kwa ajili ya TIRDO, CAMARTEC naTEMDO, Dodoma Leather and Dodoma Special EconomicZone na ujenzi wa industrial parks.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Spika, pamoja na vipaumbele hivyo,Wizara itaweka msukumo wa kipekee katika kuhamasishaujenzi wa sekta binafsi ya Kitanzania iliyo imara ili iweze kushirikina kuchangia ipasavyo katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako naomba nirudie,pamoja na vipaumbele hivyo, Wizara itaweka msukumo wakipekee katika kuhamasisha ujenzi wa sekta binafsi yaKitanzania iliyo imara ili iweze kushiriki na kuchangia ipasavyokatika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, malengo ya 2018/2019yameandikwa kwenye ukurasa wa 139 -159 katika kitabuchangu.

Mheshimiwa Spika, sekta ya viwanda. Katika mwaka2018/2019, sekta ya viwanda ina malengo yafuatayo: kufanyatathmini ya hali halisi ya uzalishaji viwandani pamoja namahitaji ya bidhaa za viwandani; kufanya mapitio ya Seraya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya mwaka 1996 – 2020(Sustainable Industrial Development Policy - SIDP) na kuandaamkakati wa utekelezaji; kujenga uwezo wa taasisi za utafitiza Wizara; kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi yaviwanda mama na Miradi ya Kimkakati; kuendelea nautekelezaji wa mikakati mikuu ya kuendeleza sekta za alizeti,ngozi na bidhaa za ngozi, pamba mpaka mavazi, viwandavya dawa; na kuendelea kuhamasisha ujenzi wa viwandanchini.

Mheshimiwa Spika, sekta ya viwanda vidogo. Katikamwaka 2018/2019, sekta ya viwanda vidogo na biasharandogo itatekeleza malengo yafuatayo: Kuendeleakuhamasisha ujenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogonchini; kuwezesha uanzishwaji wa kongano la karanga;kuendelea kufanya mapitio ya Sera ya Maendeleo yaViwanda Vidogo na Biashara Ndogo ya mwaka 2003;kuendelea kusimamia Mfuko wa NEDF na kutumia SIDO kamanyenzo ya kujenga viwanda vidogo na vya kati nchini.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Tutaitumia SIDO kama nyenzo ya kujenga viwanda vidogona vya kati nchini.

Mheshimiwa Spika, sekta ya uwekezaji. Katika mwaka2018/2019, Wizara kupitia sekta ya uwekezaji itatekelezamalengo yafuatayo: Kuendelea kuratibu utekelezaji wa Seraya Uwekezaji ya mwaka 1996; kukamilisha mapitio ya Sera,Mkakati na Sheria ya Uwekezaji; kufuatilia miradi ya uwekezajinchini na kuratibu kwa karibu uwekezaji katika sektamaalum.

Mheshimiwa Spika, sekta ya biashara. Katika mwaka2018/2019, Serikali kupitia Wizara yangu tutasimamia sektaya biashara na itatekeleza mambo yafuatayo: Kuendelezamajadiliano ya kibiashara kati ya nchi na nchi (Bilateral),Kikanda (Regional) na Kimataifa (Multilateral) kwa ajili yakupanua fursa za masoko na uwekezaji ili kuvutia uwekezajinchini; kuhamasisha jumuiya za wafanyabiashara kuhusu fursaza masoko ya upendeleo yatokanayo na majadiliano ya nchina nchi, kikanda na kikanda na kimataifa; na kukamilishamapitio ya Sheria ya Anti-dumping and CountervailingMeasures.

Mheshimiwa Spika, sekta ya masoko kwa mwaka2018/2019. Wizara kupitia sekta ya masoko itatekelezamalengo yafuatayo: Kuendelea kuboresha mazingira yabiashara na uwekezaji; kuwaunganisha wazalishaji namasoko; kuendelea kuhamasisha matumizi ya mfumo wastakabadhi za ghala; kutafiti na kutafuta masoko mapyandani na nje ya nchi hususan katika nchi za Afrika Mashariki,DRC Congo, China, Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, Ulayana nchi nyinginezo.

Mheshimiwa Spika, malengo ya taasisi chini ya Wizara.Malengo haya nimeyaeleza ukurasa wa 151 -152. Taasisi zakisekta zitajielekeza katika kuendeleza uwekezaji katikamiradi ya vielelezo na kimkakati; usimamizi wa viwango naubora; kuendeleza biashara ya ndani na nje; utafiti katika

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

teknolojia na viwanda; kumtetea na kumlinda mlaji; ulinzina kusimamia haki za wabunifu; usajili wa makampuni naleseni za biashara; kuendeleza maeneo ya uwekezaji waviwanda; kuendeleza na kuvilinda viwanda vidogo sanahadi vikubwa nchini; kutoa elimu ya biashara; kusimamiamfumo wa kumlinda mzalishaji na muuzaji; kusimamia hakiza biashara; kuhamasisha uwekezaji kutoka ndani na nje yanchi na kuendeleza teknolojia za kutumika vijijini. Malengoya kina taasisi za kisekta katika mwaka 2018/2019,yameanishwa vizuri ukurasa 151 mpaka 172 kama nilivyoeleza.

Mheshimiwa Spika, maombi ya fedha kwa mwaka2018 mpaka 2019 ambayo nimeyaandika vizuri katika hotubayangu ukurasa wa 175 - 177. Kwa mwaka 2018/2019, Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Taasisi zake inaombakutengewa jumla ya Sh.143,334,153,648, kati ya hizo,Sh.43,309,628,648 ni Matumizi ya Kawaida naSh.100,024,525,000/= ni za Matumizi ya Maendeleo. Katikafedha za matumizi ya kawaida, Sh.19,193,110,000 ni zamishahara na Sh.5,069,373,000 ni za matumizi mengineyo.Aidha, katika fedha za maendeleo Sh.90,500,000,000 ni fedhaza ndani na Sh.2,524,525,000 ni fedha za nje.

Mheshimiwa Spika, katika Fungu 44 (Viwanda) fedhazilizotengwa kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo, fedha zandani ni Shilingi bilioni 90.5 ambazo zimeelekezwa katikamiradi mikubwa ya kielelezo; miradi ya ujenzi wa msingi wauchumi wa viwanda; uanzishwaji wa kanda maalum zakiuchumi; uendelezaji wa eneo la viwanda la TAMCO Kibaha;kuendeleza Kongano za viwanda; kuendeleza tafiti zamaendeleo viwandani; kuendeleza viwanda vidogo,biashara ndogo, ujasiriamali na kuongeza Mfuko wa NEDF.

Mheshimiwa Spika, vilevile, katika Fungu 60 (Biasharana Uwekezaji) imetengwa Shilingi Bilioni 7 fedha za ndani kwaajili ya Matumizi ya Maendeleo katika miradi ya kuendelezaujenzi wa maabara ya kisasa; kuboresha mfumo wa usajiliwa kazi za wanachama wanaojishughulisha na kazi za

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

ubunifu kwa njia ya mtandao; Bodi ya Stakabadhi Maghala(WRRB); kuimarisha uhakiki wa vipimo na miradi mingine chiniya ASDP II. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hitimisho. Maamuzi ya ujenzi wauchumi wa viwanda ni msimamo makini wa Serikali yetuunaozingatia uzoefu kutoka nchi nyingine ulimwengunizilizopata mafanikio na maendeleo kupitia viwanda.Kuthubutu kutumia fursa, kufanya kazi kwa bidii na ushirikianokutumia rasilimali kwa nidhamu ni masuala muhimu yakuzingatiwa ili kufikia malengo. Wakati Serikali inaendeleana jitihada za kuweka mazingira rafiki na wezeshi, sektabinafsi ina jukumu la kutumia fursa zilizopo na zilizojitokezakuanzisha viwanda na kufanya biashara. Matokeo ya jitihadazilizofanyika yameanza kuzaa matunda.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, tunahitaji kuendeleakuunganisha nguvu kwa dhamira njema bila kuchoka katikavita ya kujenga uchumi wa viwanda ulimwengunikuhakikisha ushirikiano wa sekta binafsi na Serikaliunaendelezwa. Inawezekana endapo tukiweka nguvu yapamoja katika kuendeleza sekta hii muhimu.

Mheshimiwa Spika, kwa shabaha ya kumbukumbu yaHansard, naomba tena niombe kitabu changu chote chabajeti kwa mwaka 2018/2019 na marekebisho niliyotoa nanitakayoleta addendum yawekwe kwenye kumbukumbu.

Mheshimiwa Spika, hotuba hii inapatikana katikatovuti ya Wizara, www.mit.go.tz.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, naafiki.

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

HOTUBA YA WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NAUWEKEZAJI MHE. CHARLES J.P. MWIJAGE (MB.),

AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NAMATUMIZI YA FEDHA KWAMWAKA 2018/2019

KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara naMazingira kuweka mezani taarifa iliyochambua Bajeti yaWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, naomba kutoahoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadilina kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha yaWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka 2018/2019.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote naombanimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema nakutuwezesha kukutana katika Bunge lako Tukufu kujadiliutekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2017/2018, vilevile kujadiliMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2018/2019.

3. Mheshimiwa Spika, napenda kumpongezaMheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa SamiaSuluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania; na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa kuongoza kwa busara na hekima na hivyo kuendeleakuifanya nchi yetu kuwa na amani, utulivu na maendeleo.Kwa namna ya pekee, nawapongeza kwa kusimamia kwavitendo agenda ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.Aidha, namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwa na imaninami na kuendelea kunipa dhamana ya kuiongoza nakuisimamia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

4. Mheshimiwa Spika, nawapongeza piaMheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzina Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Raiswa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kusimamia kwaumakini mkubwa masuala muhimu ya ushirikiano wa kisektana ya Muungano kwa ujumla.

5. Mheshimiwa Spika, pia nawapongezawaheshimiwa mawaziri na naibu mawaziri wotewalioteuliwa hivi karibuni kuongoza wizara mbalimbali.Kwa namna ya pekee, namshukuru sana Mheshimiwa Raiskwa kumteua Mheshimiwa Mhandisi Stella Martin Manyanya(Mb.), kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji. Namshukuru kwa ushirikiano anaonipa kamaNaibu Waziri katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yaWizara. Vilevile, nawapongeza waheshimiwa wabungewapya waliochaguliwa kupitia chaguzi ndogo ambao niMheshimiwa Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.),Jimbo la Songea Mjini; Mheshimiwa Justin Joseph Monko (Mb.),Jimbo la Singida Kaskazini; Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollel(Mb.), Jimbo la Siha; Mheshimiwa Stephen Lemomo Kiruswa(Mb), Jimbo la Longido; na Mheshimiwa Maulid Said Mtulia(Mb.), Jimbo la Kinondoni. Pia, nampongeza MheshimiwaJaneth Maurice Massaburi (Mb.) kwa kuteuliwa kuwa Mbunge.

6. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napendakumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.),Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwahotuba yake ambayo imeweka msingi na mwelekeo wautekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa mwaka 2018/2019,ambayo baadhi yake yanahusu majukumu ya Wizara yangu.Pia, napenda kuungana na wenzangu kuwapongeza watoahoja walionitangulia kuwasilisha bajeti zao na kupitishwa naBunge lako Tukufu.

7. Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikumpongeza Mheshimiwa Ahmed Sadiq Suleiman, Mbungewa Mvomero kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Viwanda, Biashara naMazingira. Pia, nampongeza Mheshimiwa InnocentLugha Bashungwa, Mbunge wa Karagwe kwa kuchaguliwa

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Nawapongezawaheshimiwa wabunge wote waliochaguliwa kuwawajumbe wa Kamati hiyo. Ninaishukuru Kamati nzima kwaushauri, maoni na ushirikiano mkubwa inayoendelea kutupakatika kutekeleza majukumu yetu ikiwa ni pamoja namaandalizi ya Bajeti hii. Napenda kulihakikishia Bunge lakoTukufu kwamba Wizara itazingatia ushauri, mapendekezo namaoni yaliyotolewa na Kamati na yale yatakayotolewa naBunge lako Tukufu. Napenda pia kumpongeza MheshimiwaStanslaus Nyongo (Mb.), aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyokwa uongozi thabiti kabla ya kuteuliwa kwake kuwaNaibu Waziri wa Wizara ya Madini. Nampongeza kwakuaminiwa na Mheshimiwa Rais kushika wadhifa huo.

8. Mheshimiwa Spika, napenda pia kukupongezawewe binafsi, Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge kwakuliongoza Bunge letu Tukufu kwa umahiri mkubwa. Ni imaniyangu kuwa, mtaendeleza hekima na weledi mlionaokuisimamia na kuishauri Serikali katika kutekeleza majukumuyake.

9. Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru kwa dhatifamilia yangu kwa kuniombea, kunivumilia na kunipa moyokutekeleza majukumu niliyopewa na Mheshimiwa Rais katikakujenga na kutetea maslahi ya Taifa letu ndani na nje yanchi.

10. Mheshimiwa Spika, nawapongeza nakuwashukuru wananchi wa Jimbo langu la Muleba Kaskazinikwa kuendelea kunipa ushirikiano katika kutekelezamajukumu ya kitaifa na ya Jimbo. Nawapongeza kwa kazina juhudi wanazofanya katika kujiletea maendeleo. Aidha,ninawaahidi kwamba nitaendelea kutetea maslahi yao hapabungeni na hata nje ya Bunge il i kuhakikisha kuwamaendeleo yao yanazidi kushamiri.

11. Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuruna kuwapongeza wafanyakazi wa Wizara na taasisi zilizochini ya Wizara wakiongozwa na Prof. Elisante Ole GabrielLaizer, Katibu Mkuu; Prof. Joseph Rwegasira Buchweishaija,

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) na NduguLudovick James Nduhiye, Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) kwakazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha kwamba dhanaya uchumi wa viwanda inafanikiwa kwa vitendo.

12. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursahii kuwashukuru pia wahisani mbalimbali ambao wamekuwawakishirikiana nasi katika kutekeleza majukumu ya Wizarayangu. Baadhi yao ni: Benki ya Dunia, JICA, KOICA, GIZ, Serikaliya Uswisi na taasisi za Umoja wa Mataifa (UNIDO, UNDP,UNCTAD, UNWOMEN na ILO). Taasisi nyingine ni EIF, EU, TMEAna USAID. Naupongeza uongozi wa Sekta Binafsi na taasisizake chini ya uongozi mahiri wa Dkt. Reginald AbrahamMengi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) naMkurugenzi Mtendaji Ndugu Godfrey Simbeye. Napongezapia uongozi wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) nawatumishi wote wa TNBC chini ya uongozi wa MhandisiRaymond Mbilinyi, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwaushirikiano wanaoutoa katika juhudi za kuboresha mazingiraya biashara hapa nchini.

13. Mheshimiwa Spika, natoa pole kwako,waheshimiwa wabunge na familia za wafiwa kwakuondokewa na aliyekuwa Mbunge mwenzetu, MheshimiwaLeonidas Gama wa Jimbo la Songea Mjini. Vilevile, napendakutoa pole kwa Watanzania waliokumbwa na kadhia yamajanga mbalimbali kama mafuriko, ajali za motoviwandani, ajali za barabarani na majanga mengineyanayofanana na hayo.

14. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo,naomba sasa nieleze umuhimu wa viwanda katika uchumiwa nchi yetu.

2.0 UMUHIMU WA VIWANDA KATIKA UCHUMI WATAIFA

15. Mheshimiwa Spika, kutokana na matakwa yawakati, leo hii ninapowasilisha Bajeti yangu ya tatu nikiwa

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Waziri mwenye dhamana ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,napenda tena kurejea tafsiri ya kiwanda. Kiwanda ni eneoambalo malighafi huchakatwa kwa muktadha wa uongezajiwa thamani. Hivyo, shughuli yoyote, ndogo au kubwa, yauongezaji thamani kwenye malighafi kwa lengo la kutoabidhaa ni shughuli za kiwanda.

16. Mheshimiwa Spika, vigezo vya kimataifa vyakugawa makundi ya viwanda vinavyotumika mara nyingi niajira, mtaji na mapato. Vigezo vinavyotumika kwa Tanzaniani mtaji na ajira zinazotokana na shughuli husika za uongezajithamani. Hivyo, kiwanda kidogo sana, kinatakiwa kuwana mtaji wa hadi Shilingi 5,000,000 na ajira ya hadi watuwanne (4); kiwanda kidogo kinatakiwa kuwa na mtaji wakati ya Shilingi 5,000,000 hadi milioni 200 na ajira ya watuwatano (5) hadi 49; na kiwanda cha kati kinatakiwa kuwana mtaji wa kati ya Shilingi milioni 200 hadi 800 na ajira yawatu 50 hadi 99. Kiwanda kikubwa kinatakiwa kuwa na mtajiwa zaidi ya Shilingi milioni 800 na ajira ya kuanzia watu 100na kuendelea. Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, hadikufikia mwezi Machi 2018, nchi yetu ilikuwa na jumla yaviwanda 53,876. Kati ya hivyo, viwanda vikubwa ni 251 vyakati ni173, vidogo ni 6,957 na vidogo sana ni 46,495. Kwakipindi ambacho Serikali ya Awamu ya Tano imeingiamadarakani, chini ya uongozi mahiri wa Rais wetuMheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, hadi Machi2018, viwanda vipya 3,306 vimejengwa.

17. Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia uchumiwa viwanda tunamaanisha shughuli zinazolengamaendeleo ya watu na vitu wakati maendeleo ya watuyakipewa kipaumbele. Katika ujenzi wa uchumi waviwanda Sekta ya Viwanda inakuwa kiungo muhimu chakuhamasisha maendeleo ya sekta nyingine. Sekta hizo wezeshina tegemezi katika uchumi wa viwanda ni pamoja na kilimo;uvuvi na mifugo; misitu; na madini kwa upande wa uzalishajimalighafi za viwanda. Kwa upande mwingine, ustawi waviwanda hutegemea miundombinu ya barabara, reli, usafiri

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

wa anga, nishati, mawasiliano na maji. Aidha, uchumi waviwanda unahitaji rasilimali watu ambao ni muhimu katikamnyororo mzima kuanzia uzalishaji malighafi, uzalishaji wabidhaa viwandani na usambazaji wa bidhaa hadi mikononimwa mlaji.

18. Mheshimiwa Spika, katika kujenga uchumi waviwanda, ambao lengo lake kubwa ni kufanya mageuzi yakiuchumi na maendeleo ya watu, Sekta ya Viwanda Vidogona Biashara Ndogo ni muhimu sana. Umuhimu wa sekta hiyounatokana na ukweli kwamba inahitaji ujuzi na mitajiambayo Watanzania walio wengi wanaweza kuimudu. Sektahiyo ni shule kwani kupitia viwanda vidogo na biasharandogo, wajasiriamali hupata ujuzi na uzoefu wa shughuli zauzalishaji na kuweza kuhitimu kuwa wawekezaji nawafanyabiashara wa kati na wakubwa. Katika jitihada zakuhamasisha ujenzi wa viwanda kwa msambao wa nchinzima, ni viwanda vidogo sana, vidogo na vya kativinavyoweza kujengwa na kuendeshwa kwa tija nchi nzima.Ni dhahiri kuwa Sekta hiyo ni muhimu sana katika kushiriki nakuchochea ujenzi wa uchumi jumuishi kutokana nakutegemea malighafi inayozalishwa na wakulima waliowengi na hutumia teknolojia rahisi.

19. Mheshimiwa Spika, ili kuweza kuakisi vyemamchango wa Sekta hiyo ambao ni muhimu katika kufikiaazma ya uchumi wa kati, hatuna budi kuelekeza nguvukubwa katika kubuni mikakati ya uanzishwaji na uendelezajiwa viwanda vidogo. Wizara itaendelea kuweka mazingirawezeshi pamoja na kubuni mikakati mbalimbali i l ikuziwezesha shughuli za ujasiriamali mdogo na wa kati kukuana kuwa wenye tija.

20. Mheshimiwa Spika, pamoja na umuhimu huo waviwanda vidogo, viwanda vikubwa ni vya msingi katikakutoa chachu kwa ujenzi na uendelevu wa viwanda vidogo,vidogo sana na vya kati. Kwa upande mmoja, viwanda hivyohuzalisha bidhaa ambazo ndiyo msingi wa viwanda vinginena kuzalisha bidhaa za kati ambazo hutumiwa na viwanda

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

vya kati, vidogo na vidogo sana katika kuzalisha bidhaa.Kwa upande mwingine, viwanda hivyo hupokea bidhaakutoka viwanda vidogo au malighafi kutoka kwa wazalishajikuzalisha bidhaa nyingine. Hivyo, Wizara itafanya jitihada zakuunganisha nguvu na viwanda vikubwa kwa kuwa uwepowa viwanda vya aina hizo zote ni muhimu ili kukamilishamnyororo wa uzalishaji wa viwanda ambao ni endelevuna unganishi kwa sekta za uzalishaji malighafi hususanzitokanazo na kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini.

21. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa ustawi washughuli za viwanda unategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiwa wadau mbalimbali. Ujenzi wa viwanda unaanza kwakutambua eneo la kujenga viwanda ambalo ubainishwajiwake na uwekaji wa miundombinu wezeshi na saidiziunahusisha mamlaka mbalimbali. Vilevile, ili kujenga Sektaya Viwanda iliyo endelevu, suala la mazingira ni muhimusana. Kama ilivyoelezwa awali, uendeshaji wa viwanda nasekta wezeshi na saidizi zinahitaji nguvu kazi zenye ujuzi naweledi. Kwa misingi hiyo, mafanikio ya dhima ya ujenzi wauchumi wa viwanda ni matokeo ya ushirikiano na jitihadaza Wizara zote na Serikali kwa upande mmoja na Sekta Binafsikwa upande mwingine.

3.0 VIPAUMBELE NA UTEKELEZAJI WA MIPANGO NAMALENGO YA BAJETI KWA MWAKA 2017/2018

3.1 VIPAUMBELE KWA MWAKA 2017/2018

22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,vipaumbele vya Wizara vilikuwa ni kuvutia wawekezaji nakuhamasisha Sekta Binafsi kuanzisha na kuendeleza viwandavinavyotumia malighafi za hapa nchini; kufufua viwandavilivyobinafsishwa; kuendeleza viwanda mama na miradi yakimkakati (flagship projects) kwa kushirikisha Sekta Binafsi;kuendelea kubainisha maeneo ya viwanda katika mikoa yotena kuendeleza maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ & SEZ)pamoja na kongano za viwanda (industrial clusters) nchini;kujenga uwezo wa taasisi za utafiti zilizo chini ya Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji; kuhamasisha uanzishaji na

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

maendeleo ya viwanda vidogo sana, vidogo na vya kati;na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Utekelezajiwa mipango hiyo unalenga kuhakikisha kuwa Sekta yaViwanda nchini inakua na kuchangia zaidi katika Pato laTaifa, inazalisha bidhaa zinazotumiwa na Watanzania waliowengi na kuzalisha ajira kwa wingi.

23. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wavipaumbele hivyo umezingatia mipango iliyoainishwa katikaDira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mpango wa Pili waMaendeleo wa Miaka Mitano wa Mwaka 2016/2017 –2020/2021, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 naMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/2019.Mipango hiyo imefafanuliwa kisekta katika Mpango Mkakatiwa Wizara wa Miaka Mitano na Mpango Kazi wa mwaka2017/2018. Pia, Wizara imezingatia ahadi na maagizo yaviongozi wakuu wa Serikali, sera na mikakati mbalimbali yakisekta, kitaifa na kimataifa. Aidha, Wizara imeendeleakuzingatia ushauri mzuri ambao umekuwa ukitolewa naKamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia ViwandaBiashara na Mazingira na kamati nyingine za Bunge ambazozimehusika katika kuishauri Wizara yetu.

3.2 MWENENDO WA BAJETI3.2.1 Maduhuli

24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara ilitarajia kukusanya Shilingi 20,000,000,000 kutokanana ada za leseni za biashara, uuzaji wa nyaraka za zabunina faini kwa kukiuka Sheria ya Leseni ya Biashara. Hadi kufikiamwezi Machi 2018, Shil ingi 9,728,635,810.84 zil ikuwazimekusanywa, sawa na asilimia 48.64 ya malengo. Mwelekeowa makusanyo hadi mwezi Juni 2018, inategemewa kufikiaasilimia 65 ya lengo.

3.2.2 Bajeti Iliyoidhinishwa na Kupokelewa

25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara ilitengewa Shilingi 122,215,109,750. Kati ya fedha hizo,Fungu 44 (Viwanda) lilitengewa Shilingi 98,012,870,000

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

zinazojumuisha fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi24,172,493,000 na fedha za Maendeleo Shilingi 73,840,377,000.Aidha, Fungu 60 (Biashara na Uwekezaji) lilitengewa Shilingi24,202,239,750 zinazojumuisha Shilingi 17,852,239,750 fedha zaMatumizi ya Kawaida na Shilingi 6,350,000,000 fedha zaMaendeleo.

26. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 9 Aprili 2018,Wizara ilikuwa imepokea Shilingi 47,267,945,999.91 kwa ajiliya Fungu 44 na Fungu 60, sawa na asilimia 38.68 ya Bajetikwa ajili ya Wizara na Taasisi zake. Kati ya fedha hizo, Shilingi32,641,257,816.33 ni za Matumizi ya Kawaida na Shilingi14,626,688,183.58 ni za Matumizi ya Maendeleo. Kati ya fedhazilizopokelewa, Wizara ilipokea fedha za Matumizi yaKawaida Shilingi 8,066,718,730.33 na Taasisi zilipokea Shilingi24,503,739,886. Aidha, kwa upande wa fedha za Maendeleo,Wizara ilipokea Shilingi 3,026,341,089.58 na Taasisi zilipokeaShilingi 11,600,347,094.

3.3 UTEKELEZAJI WA MIPANGO NA MALENGO

3.3.1 Sekta ya Viwanda27. Mheshimiwa Spika, mchango wa Sekta ya

Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2017 ulikuwaasilimia 5.5, ikilinganishwa na asilimia 4.9 mwaka 2016, sawana ongezeko la asilimia 0.6 (Kiambatisho Na.1). Kasi ya ukuajiwa Sekta ya Viwanda ilikuwa asilimia 7.1 mwaka 2017ikilinganishwa na asilimia 7.8 mwaka 2016 (Kiambatisho Na.2).Aidha, ajira katika Sekta ya Viwanda imeongezeka kwaasilimia 5 kutoka ajira 267,524 mwaka 2016 hadi 280,899mwaka 2017 (Kiambatisho Na. 3).

a) Uendelezaji wa Viwanda Vilivyobinafsishwa

28. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maelekezoya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala - CCM (2015- 2020),Wizara yangu, pamoja na mambo mengine, inatakiwakuhakikisha utekelezaji wa mambo makubwa matatuyafuatayo: Kwanza, ni kuhakikisha kwamba viwandavilivyopo bila kujali umiliki wake vinazalisha kwa uwezo wa

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

juu uliosimikwa (maximum installed capacity); Pili, kuhakikishakuwa viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazivinafanya kazi; na Tatu, kuhamasisha uanzishaji wa viwandavipya.

29. Mheshimiwa Spika, kufuatia zoezi la ubinafsishajinchini, kati ya taasisi za umma 341 zilizobinafsishwa, ni taasisi156 zilizokuwa na sifa ya kuwa viwanda. Kufikia mwezi Mei2017, kati ya viwanda hivyo, viwanda 62 vilikuwa vinafanyakazi vizuri; 28 vilikuwa vinafanya kazi chini ya kiwango; 56vilikuwa havifanyi kazi kabisa na 10 vilikuwa vimeuzwa kwamali moja moja (Asset Stripping). Kuanzia mwezi Agosti2017 hadi Machi 2018, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi yaMsajili wa Hazina na wizara za kisekta ilifanya tena tathminiya viwanda vilivyobinafsishwa, ili kubaini hali ya viwandahivyo baada ya kufanya zoezi la kuhamasisha ufufuaji wake.

30. Mheshimiwa Spika, kutokana na uhamasishaji huo,baadhi ya wamiliki ambao viwanda vyao vilikuwa havifanyikazi walioonesha utayari wa kuvifufua na hivyo walipewamuda maalum wa kutekeleza mipango ya ufufuaji. MpakaMachi 2018, viwanda 18 vilikuwa vimefikia hatua mbalimbaliza ufufuaji. Vipo viwanda ambavyo vimekamilisha ukarabatina kuanza uzalishaji wa majaribio; vipo viwanda ambavyowamiliki wamewekeza mitaji mikubwa kukarabati mitamboiliyokuwepo na hata kununua mitambo mipya. Pia, vipoviwanda ambavyo wamiliki wamewekeza katika kupanuamajengo yaliyopo na kujenga majengo mapya.

31. Mheshimiwa Spika, kati ya viwanda 56 ambavyovilikuwa havifanyi kazi kabisa, viwanda 35 vimewekwa chiniya uangalizi wa Serikali. Katika kundi hilo, kuna viwandaambavyo uboreshaji wake umekwama kutokana na kuwana mashauri mahakamani. Vipo viwanda ambavyokutokana na hali yake, havina sifa ya kuendelea kuitwaviwanda. Taratibu zinafanywa ili kuviondoa katika orodhaya viwanda. Pia, kuna viwanda ambavyo ni mali ya Serikaliau taasisi zake ambavyo mamlaka husika ziko katika hatuambalimbali za kuviendeleza. Viwanda vitatu (3) katika kundila viwanda 56, pamoja na viwanda vingine saba (7)

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

vimeunganishwa katika kundi la viwanda 10 ambavyo hatuambalimbali za kiutawala zinachukuliwa ikiwemo kutafutawawekezaji wengine.

32. Mheshimiwa Spika, kwa muhtasari, baada ya zoezila uhamasishaji, hadi mwezi Machi 2018, kati ya viwanda156 vilivyobinafsishwa, 61 vinafanya kazi vizuri; 22 vinafanyakazi chini ya kiwango; viwanda 18 vinafanyiwa maboreshona wamiliki; viwanda 35 viko chini ya uangalizi wa Serikali;viwanda 10 visivyofanya kazi vinafanyiwa tathmini kablaya kuchukuliwa hatua za kisheria kulingana na mikataba yaubinafsishwaji; na 10 ni vilivyouzwa mali moja moja nakupoteza sifa ya kuendelea na shughuli za uzalishaji.

b) Miradi Mipya ya Viwanda

33. Mheshimiwa Spika, kuanzia Julai 2017 mpakaMachi 2018, jumla ya miradi 243 yenye thamani ya Dolaza Kimarekani milioni 3,667 na inayotarajiwa kuajiri watu36,025 ilikuwa imesajiliwa. Kati ya hiyo, miradi 99 yenyethamani ya Dola za Kimarekani milioni 2,317 na itakayoajiriwatu 12,995 ilisajiliwa na TIC (Kiambatisho Na. 4); miradi 22yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 368.92 naitakayoajiri watu 4,881 ilisajiliwa na EPZA (KiambatishoNa. 5); na miradi 122 yenye thamani ya Dola za Kimarekanimilioni 981 na itakayoajiri watu 18,149 ilisajiliwa na BRELA(Kiambatisho Na. 6).

c) Viwanda Mama na Miradi ya Kielelezo

i) Mradi wa Mchuchuma na Liganga

34. Mheshimiwa Spika, katika kufanikishautekelezaji wa Mradi Unganishi wa Mchuchuma na Liganga,Serikali iliunda timu ya wataalam wa Serikali ikiwa na jukumula kuchambua vivutio vilivyoombwa na mwekezaji. Vilevile,uchambuzi ulikuwa ufanyike kwa kuzingatia marekebisho yaSheria ya Madini, 2010; Sheria ya Natural Wealth and Resources

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

Permanent Sovereignity Act, 2017; na The Natural Wealth andResources Contracts (Review and Renegotiation ofUnconscionable Terms), 2017 na kutoa mapendekezo ya hatuaza kuchukuliwa na Serikali. Timu hiyo imekamilisha taarifa yaawali ambayo inasubiri kutolewa maamuzi na mamlakahusika.

ii) Kiwanda cha Matairi Arusha

35. Mheshimiwa Spika, msimamo wa Serikali nikuhakikisha Kiwanda cha Matairi Arusha kinafanya kazi.Jukumu la kuboresha na kuendesha kiwanda hicho litakuwamikononi mwa Sekta Binafsi huku Serikali ikibaki na hisakulingana na rasilimali zilizopo bila kuwekeza mtaji zaidi.Mpaka sasa, Kamati Maalum ya Serikali inaendelea kupitiampango wa kiwanda hicho ili kuamua utaratibu utakaofaakatika uwekezaji kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

iii) Mradi wa Kuzalisha Magadi wa Engaruka

36. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC nakwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Monduliimekamilisha zoezi la upimaji ardhi ya mradi pamoja nauthaminishaji wa mali za wananchi, ili kubainisha kiasi chafidia kitakachohitajika. Michoro ya matumizi ya ardhi hiyoiko kwenye hatua ya mwisho ya kukamilishwa. Aidha, NDCinaendelea kutangaza mradi huo kwa wawekezajimbalimbali ili kumpata mwekezaji wa kushirikiana nayekuanzia hatua ya utafiti kwa kuzingatia teknolojia bora yakuvuna magadi hayo.

d) Uendelezaji wa Maeneo ya Uwekezaji

i) Maeneo Maalum ya Serikali ya Uwekezaji(Government EPZ/SEZ)

37. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka ya EPZimeendelea kuhamasisha uwekezaji ndani ya maeneo yoteya EPZ na SEZ. Hadi mwezi Machi 2018, kuna jumla ya viwanda111 katika maeneo ya EPZ na SEZ (Kiambatisho Na.7). Tathmini

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

ya uwekezaji na matokeo yake kwa viwanda chini yaprogramu za EPZ na SEZ tangu Mamlaka ya EPZ kuanzishwa,imeonesha mafanikio. Hadi mwezi Machi 2018, jumla yamtaji (cummulative) wa Dola za Kimarekani bilioni 1.86uliwekezwa na mauzo ya bidhaa nje ya nchi yenye thamaniya Dola za Kimarekani milioni 1,359.94 (cummulative)yalifanyika na ajira 52,698 za moja kwa moja zimepatikana.Aidha, kwa mwaka 2017/2018 pekee, jumla ya mtajiuliowekezwa ni Dola za Kimarekani milioni 368.92, ajirazilizopatikana ni 4,881 na mauzo ya nje ni Dola za Kimarekanimilioni 159.89.

ii) Viwanda vyenye hadhi ya EPZ/SEZ nje ya MaeneoMaalum ya SEZ/EPZ (Stand Alone EPZ/SEZ)

38. Mheshimiwa Spika, pamoja na maeneo ya EPZyaliyoko chini ya umiliki na usimamizi wa Serikali, yako maeneoyenye hadhi hiyo ya EPZ yanayomilikiwa na kuendeshwa naSekta Binafsi. Hadi sasa, kuna viwanda 72 ambavyovinamilikiwa na kuendeshwa na Sekta Binafsi chini yautaratibu wa EPZ (Kiambatisho Na.8). Viwanda hivyovimewekeza jumla ya Dola za Kimarekani milioni 315.01 nakutoa ajira 13,930. Kwa mwaka 2017/2018 pekee, viwandahivyo vimeweza kuuza nje bidhaa zenye thamani ya Dolaza Kimarekani milioni 115.12.

e) Maendeleo katika Sekta Ndogo zaViwanda (Industrial Sub-Sectors)

i) Viwanda vya Kuunganisha Magari na Matreka -SKD

39. Mheshimiwa Spika, mradi wa kuunganishamatrekta aina ya URSUS unaendelea katika eneo la TAMCOKibaha chini ya usimamizi wa NDC. Hadi mwezi Desemba2017 Semi Knocked Down (SKD) za matrekta 727 yamewasilinchini ikiwa ni sehemu ya matrekta 2,400 yaliyoanishwa katikamkataba na uunganishaji unaendelea. Kati ya SKD zamatrekta yaliyowasili, 148 yameunganishwa na yapo tayarikwa mauzo. Uunganishaji wa matrekta katika Kituo cha

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

TAMCO ni hatua ya muda ikisubiri shughuli hizo kuhamishiwakatika kiwanda kipya kinachojengwa katika eneo hilo laKibaha. Pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuunganishamatreka, vituo nane (8) vya kuhudumia wateja vitajengwakatika mikoa nane (8) nchi nzima. Kufuatia maelekezo yaWaziri Mkuu, matrekta hayo ni kwa ajili ya matumizi ya kilimovijijini.

40. Mheshimiwa Spika, pamoja na viwanda vyakuunganisha matrekta, hivi sasa kuna kampunizinazojishughulisha na kuunganisha magari na kutengenezamatrela hapa nchini. Kampuni ya Superdoll Co.Ltd ni kati yakampuni ya muda mrefu nchini katika utengenezaji wamatrela ya magari makubwa. Vilevile, kumejitokeza kampuninyingine za kuunganisha magari kwa kuagiza SKD na CBU(Complete Build Up) kutoka nje. Kwa mfano, kati ya mwaka2015 hadi 2017, Kampuni ya Jiefang Motors (T) Ltdimeunganisha magari 803 yanayojumuisha SKD assembled(tipper, light cargo truck rigid trailers) 354 na CBU (tractorhead truck) 449. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaandaaSera ya Kuunganisha Magari, ili kuhamasisha uendelezaji wasekta hiyo nchini.

ii) Viwanda vya Kuzalisha Chuma na Bidhaa zaChuma

41. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2018,kulikuwa na viwanda 25 vya kuzalisha chuma na bidhaa zachuma ikiwa ni ongezeko la viwanda vitatu (3) kwa kipindicha mwaka mmoja. Uwezo uliosimikwa ni wa kuzalisha tani577,600 kwa mwaka. Baadhi ya bidhaa za chuma kama vilemabati kwa sasa viwanda vyetu vinatosheleza mahitaji yandani. Kwa sasa, uwezo wa uzalishaji (capacity utilization)ni wastani wa asilimia 42. Hali hiyo ya uzalishaji chini ya uwezoimesababishwa na kupanda kwa bei ya malighafi kutokanje (billets) na kuadimika kwa vyuma chakavu nchini.

42. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Kiluwa Steel Ltdkilichopo Mlandizi Mkoa wa Pwani kinaendelea na uzalishaji

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

ambapo mwaka 2017 kilizalisha tani 12,000. Kiwanda chaLodhia Steel Industry Ltd kimeanza uzalishaji ambapowanazalisha tani takriban 3,700 za nondo na mabombakwa mwezi na kinaajiri wafanyakazi 231. Aidha, Kiwanda chaLake Steel and Allied Products Ltd kipo katika hatua yakumalizia usimikaji wa mashine na kinatarajia kuanzauzalishaji katikati ya mwezi Juni, 2018. Katika kuleta hudumakaribu na wajenzi wa makao makuu ya nchi, Kiwanda chaALAF kimefungua tawi lake mjini Dodoma na kilizinduliwana Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

iii) Viwanda vya Saruji

43. Mheshimiwa Spika, mpaka sasa kuna viwanda14 vya saruji ambavyo ni Tanzania Portland Cement Co. Ltd(TPCC), Mbeya Cement Co. Ltd (MCC), Tanga Cement Co.Ltd. (TCCL), Dangote Industry (T) Ltd (DIL), Lake Cement Co.Ltd (LCC), Maweni Limestone Ltd (ARM), Kilimanjaro CementCo. Ltd (KCC), Kisarawe Cement Co. Ltd (KCCL), CamelCement Co. Ltd Ltd (CCC), Fortune Cement Co. Ltd (FCC),Lee Building Material Ltd (LBM), Changjiang Cement Co. Ltd,Arusha Cement Co. Ltd na Moshi Cement Co. Ltd. Viwandavyote kwa ujumla vina uwezo uliosimikwa (InstalledCapacity) wa kuzalisha takriban tani milioni 10.98 kwamwaka na uwezo unaotumika (Utilized Capacity) ni takribantani milioni 7.4 kwa mwaka wakati mahitaji ya nchi nitakriban tani milioni 4.8.

44. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka 2017/2018, kiwanda kipya cha saruji cha KilimanjaroCement Co. Ltd kilichopo mkoani Tanga kilianza uzalishaji.Pamoja na hayo kuna miradi mipya ya viwanda vya sarujivyenye uwezo wa kuzalisha saruji takribani tani milioni 8 kwamwaka vitakapokamilika. Viwanda hivyo ni Mamba CementCo. Ltd (tani milioni 1.0) kitakachojengwa Mkoa waPwani na Mradi wa Kiwanda cha Hengya Cement Co. Ltdkitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni saba(7,000,000) za saruji. Mradi wa Kiwanda cha Hengya Cement

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Co. Ltd umehamishiwa katika eneo jipya la Mtimbwani katikaWilaya ya Mkinga kutokana na eneo la Amboni kutofaa kwauwekezaji mkubwa kama huo.

iv) Viwanda vya Vigae (Tiles)

45. Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina viwandaviwili (2) vikubwa vya uzalishaji wa vigae (tiles) vyenye uwezouliosimikwa wa kuzalisha mita za mraba 130,000 kwa siku.Kiwanda cha Vigae cha Goodwill Ceramic Ltd kilichopo Kijijicha Mkiu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kimekamilikana kinaendelea na uzalishaji. Kiwanda hicho kinachozalishamita za mraba 80,000 kwa siku, kimeajiri watu 2,200 kikihusishaajira 700 za kudumu na vibarua 1,500. Asilimia 30 hadi 40 yavigae vinavyozalishwa vinauzwa hapa nchini, wakati asilimia60 hadi 70 vinauzwa nje ya nchi. Vilevile, Kiwanda cha TwyfordLtd kilichopo Chalinze chenye uwezo wa kuzalisha mita zamraba 50,000 za vigae kwa siku kimekamilika na kimeanzauzalishaji mwezi Novemba 2017. Kiwanda hicho kimeajiriwafanyakazi 860. Bidhaa hizo huuzwa katika soko la ndanina nje ya nchi hususan Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo , Rwanda na Zambia.

v) Viwanda vya Vioo

46. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina kiwanda kimoja(1) cha Kioo Ltd ambacho kinazalisha chupa kwa ajili yaufungashaji wa bidhaa hususan vinywaji na dawa. Wizaraimeendelea kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vyakutengeneza vioo ambapo jumla ya miradi mitatu (3) yaviwanda imesajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC). Miradi hiyo ni Java Glass Limited kuwekeza Dola zaKimarekani milioni 2 na kuajiri watu 38; Zion Glass (T) Ltdutakaowekeza mtaji wa Dola za Kimarekani milioni 3 na kuajiriwatu 12; na EA Glass Investment Limited utakaowekeza Dolaza Kimarekani milioni 1.2 na kuajiri watu 163. Miradi hiyo ikokatika hatua za awali za uanzishaji wa viwanda husika.

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

vi) Viwanda vya Kutengeneza Chokaa

47. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Neelkanth LimeLtd kilichopo katika eneo la Amboni Mkoa wa Tangakinazalisha tani 15,000 za chokaa kwa mwezi na kuajiriwafanyakazi 430. Kiwanda kipo katika hatua za awali zaupanuzi ambapo Dola za Kimarekani milioni 18.4 zinatarajiwakutumika. Upanuzi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka2019, utaongeza uwezo wa uzalishaji hadi tani 35,000 kwamwezi na kuongeza ajira za moja kwa moja 1,500 na zisizoza moja kwa moja 2,500. Soko kuu la bidhaa zinazozalishwana kiwanda hicho ni nchi za Afrika Kusini, Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo, Malawi, Zambia pamoja na migodiya Barrick Gold Mines Ltd ya hapa nchini.

vii) Viwanda vya Dawa za Binadamu na Vifaa Tiba

48. Mheshimiwa Spika, hivi sasa nchi ina jumla yaviwanda 15 vya kuzalisha dawa na vifaa tiba. Katikakuendeleza viwanda vya dawa na vifaa tiba, Bohari Kuu yaDawa (MSD) imetoa kipaumbele na kuingia mikataba yakununua dawa kutoka viwanda vya ndani vinavyozalishadawa zinazokidhi viwango. Viwanda hivyo vinazalishaasilimia 12 tu ya mahitaji ya dawa nchini. Ili kutatuachangamoto hiyo, juhudi za kuhamasisha uwekezajizimeendelea kufanyika ambapo Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotoilifanya mkutano na wadau tarehe 4 Aprili 2018, ambapowawekezaji 38 walionesha nia ya kuwekeza katika Sekta yaDawa na Vifaa Tiba. Baadhi ya wawekezaji hao ni KairukiPharmaceutical Industry Ltd, SUMA JKT watakaozalishaIntravenous Infusion, Biotech Ltd na Novabi Ltdwatakaozalisha dawa na chanjo za mifugo (vaccines, oralsolid and liquids). Wizara inaendelea kufuatilia wawekezajiwaliojitokeza.

49. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto inaendelea kuandaa Mkakati wa Taifa wa Sekta yaViwanda vya Dawa za Binadamu na Vifaa Tiba. Mkakati huo

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

unafadhiliwa na Shirika la UNDP kupitia Mradi wa Access ofMedicine and Delivery. Aidha, Serikali kwa kushirikiana nawadau mbalimbali imeshiriki kuandaa Taratibu za UzalishajiBora wa Dawa katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(East Africa Community Good Manufacturing Practice-EACGMP Roadmap), ili kuhakikisha kuwa viwango stahikivinazingatiwa.

50. Mheshimiwa Spika, mradi wa kutengeneza vifaatiba vitokanavyo na pamba (medical textile) katika Mkoawa Simiyu unaojengwa na NHIF, upo katika hatua yakufungua kampuni itakayoendesha mradi huo. Aidha,hatua za awali za kuanzisha kiwanda cha kuzalisha dawacha Zinga Pharmaceutical Ltd, Bagamoyo zimefanyikaikiwemo kufanya upembuzi yakinifu, kuandaa michoropamoja na kuainisha teknolojia itakayotumika. Aidha, katikauendelezaji wa viwanda vya kemikali nchini, kiwandakikubwa cha kuzalisha kemikali aina ya Chlorine kwa ajili yakusafisha maji kiliwekewa jiwe la msingi tarehe 24 Aprili 2018.Mradi huo utakaojengwa Mlandizi Mkoa wa Pwaniutagharimu Shilingi bilioni 246 na utatoa ajira 700 za mojakwa moja kitakapoanza uzalishaji na wakati wa ujenzi utaajiriwatu 300. Malighafi ya Kiwanda hicho ni chumvi ghafi kiasicha tani 2,500 kwa mwezi.

viii) Viwanda vya Nguo na Mavazi

51. Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina viwanda 11 vyanguo na mavazi vinavyofanya kazi. Viwanda hivyovinatumia wastani wa asilimia 50 ya uwezo uliosimikwa. Halihiyo imetokana na ushindani usio wa haki kutokana na nguozinazoagizwa kutoka nje ya nchi na baadhi ya viwandakuendelea kutumia teknolojia zilizopitwa na wakati. Aidha,kuzalisha chini ya kiwango kumesababisha matumizimadogo ya pamba inayozalishwa nchini ambayo ni asilimia30 tu na hivyo asilimia 70 inayobaki huuzwa nje ya nchi ikiwaghafi. Serikali inaendelea kuhamasisha uendelezaji wa Sektaya Pamba mpaka mavazi ikiwa ni pamoja na kuhakikishasekta inaendeshwa kwa haki na kuweka mazingira wezeshiya uwekezaji.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

52. Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha uwekezajinchini, Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Tanzania SocialSecurity Association-TSSA) linashiriki katika juhudi za kuwekezakatika viwanda vya kuchambua pamba na kuzalisha nguo.Shirikisho hilo lina mpango wa kuwekeza katika vinu 10 vyakuchambulia pamba ambapo uchambuzi kwa vinu vitatu(3) vya awali umekamilika. Uchambuzi unaonesha kuwa vinuvya Ngasamo, Nyambiti na Kasamwa ni miradi itakayoanzakutekelezwa. Aidha, Shirikisho hilo limekamilisha maandaliziyote muhimu kwa ajili ya kuwekeza katika Kiwanda chaMorogoro Canvas Mill Ltd ambapo ukarabati unatarajiwakuanza mwezi Mei 2018, na uzalishaji kuanza mwezi Juni2018. Vilevile, Shirikisho limepokea maandiko ya miradi yaviwanda vya MWATEX na URAFIKI kwa ajili ya kuipitia kwalengo la kuwekeza.

ix) Viwanda vya Ngozi na Bidhaa za Ngozi

53. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina jumla yaviwanda sita (6) vya kusindika ngozi vinavyofanya kazi.Viwanda hivyo vina uwezo uliosimikwa wa kusindika futi zamraba 71,520,000 za ngozi kwa mwaka. Viwanda hivyo niLake Trading Co. Ltd kilichopo Kibaha, Himo Tanners andPlanters Ltd na Moshi Leather Industries Ltd (Moshi), SAKInternational Ltd na Meru Tannery Ltd. (Salex) (Arusha) na ACELeather (T) Ltd (Morogoro) (Kiambatisho Na. 9).

54. Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Hifadhi ya Jamiiwa PPF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza wapo katikahatua za uboreshaji wa majengo ya kiwanda na ukarabatina mfumo wa umeme kwa lengo la kuboresha Kiwanda chaKutengeneza Viatu cha Karanga (Karanga Leather IndustriesCo. Limited). Upanuzi wa kiwanda hicho utaongeza uwezowa uzalishaji kutoka jozi 150 hadi 400 za viatu kwa siku. Aidha,taratibu za kumpata mzabuni atakayekiuzia kiwandamitambo mipya kwa ajili ya upanuzi amepatikana nataratibu za manunuzi zinaendelea.

55. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kiwanda chaViatu cha Karanga unahusisha pia ujenzi wa kiwanda kipya

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha jozi 4,000 za viatukwa siku pamoja bidhaa nyingine zinazotokana na ngozi.Mradi huo mpya umetengewa ekari 20 na kupewa Hati Milikitofauti na kiwanda cha zamani. Tafiti mbalimbali zikiwemoGeotechnical & Topographical Sur veys, EnvironmentalImpact and Social Assessment - EIA zimefanyika na michoroya majengo imeandaliwa. Aidha, taratibu za ununuzi wamitambo zimeanza na ujenzi wa majengo unategemeakuanza katika robo ya kwanza ya mwaka 2018/2019.

56. Mheshimiwa Spika, juhudi za kuendeleza viwandavya ngozi zimewezesha kiwanda cha viatu cha Borakil ichoanza uzalishaji mwanzoni mwa mwaka 2017kuendelea kuzalisha viatu vya ngozi, ambapo kwa sasakinazalisha jozi 1,000 za viatu kwa siku. Vilevile, Kiwanda chaWoiso Shoes Company Ltd kimeagiza mashine zakutengeneza soli za viatu zenye uwezo wa kuzalisha jozi100 hadi 300 kwa siku. Juhudi hizo za kufufua na kupanuawigo wa bidhaa zinategemewa kuongeza uzalishaji waviatu na bidhaa za ngozi. Mkakati huo wa kuzalisha zaidikutumia viwanda vya ndani utaongeza makusanyo ya kodi,kuokoa matumizi ya fedha za kigeni na kupunguza uagizajiwa bidhaa hizo kutoka nje. Kiwanda cha Mwanza TennariesLtd kilichokuwa kimebinafsishwa kimewekwa chini yauangalizi wa Serikali na Mthamini wa Serikali amekamilishatathmini kama hatua ya kuelekea kutangazwa, ili kupatamwekezaji mwingine.

57. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mradi waKuimarisha Biashara na Uwekezaji kati ya Afrika na India(Supporting Indian Trade and Investment for Africa - SITA)iliwezesha wadau wa ngozi kukutana na wawekezaji kutokaIndia na Italia mwezi Desemba 2017, Jijini Dar es Salaam.Matokeo ya mkutano huo ni kwamba Kiwanda cha Viatucha Bora kilipata ushauri wa kitaalam wa namna ya kuzalishabidhaa za ngozi zenye ubora wa kimataifa. Pia, baadhi yawataalam wao wamewezeshwa kupata mafunzo nchiniEthiopia.

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

58. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Maoneshoya DTIF, Wizara ilitenga siku na banda maalum la maoneshoya viatu na bidhaa za ngozi. Lengo lilikuwa kuzitangazabidhaa hizo kwa umma na kuhamasisha matumizi yabidhaa za Tanzania. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Taasisiza TANTRADE, TBS, DIT, VETA, SIDO, BRELA na OSHA walitoamafunzo kwa watengenezaji 20 wa viatu na bidhaa za ngozikuhusu elimu ya urasimishaji wa biashara, misingi yaujasiriamali na utunzaji wa kumbukumbu; mbinu mbalimbaliza kuingia kwenye masoko na uzalishaji kwa kulengamasoko.

x) Viwanda vya Kusindika Nyama

59. Mheshimiwa Spika, viwanda vya kuongezathamani mazao ya mifugo vimeendelea kuongezekaambapo tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani,jumla ya viwanda 7 vimejengwa katika mikoa ya Dodoma,Iringa, Pwani na Shinyanga. Viwanda hivyo vina uwezo wakuchakata ng’ombe 2,260 na mbuzi na kondoo 9,200 kwasiku. Viwanda hivyo vitakapokamilika na kuanza uzalishajivitaifanya Tanzania kuwa na jumla ya viwanda 25 vyenyeuwezo wa kuchakata ng’ombe 3,800, mbuzi na kondoo10,090, nguruwe 300 na kuku 44,000 kwa siku (KiambatishoNa. 10).

60. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Nyama chaNguru Hills Ranch Ltd kilichopo Wilaya ya Mvomero Mkoa waMorogoro ambacho nilitoa taarifa zake katika Hotuba yanguya mwaka 2017/2018, kipo katika hatua za awali za ujenzi.Kazi ya kusimika mitambo imeanza kwa ushirikiano na LAPFambao wameingia ubia na kukubali kuwekeza Shilingi bilioni3.89. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchakatang’ombe 300 na mbuzi 2,000 kwa siku na kutoa ajirazisizopungua 500. Aidha, Kiwanda kitajihusisha na mnyororowa thamani kwa kushirikiana na wafugaji wadogo wadogo,kurutubisha mifugo na kusindika nyama.

61. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Triple S kilichopokatika mkoa wa Shinyanga ambacho kil ikuwa

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

kimebinafsishwa na sasa kimewekwa chini ya uangalizi waSerikali. Mthamini wa Serikali amekamilisha tathmini yakeikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kukitangaza kwamwekezaji mwingine. Aidha, Kiwanda cha Nyama cha Mbeyaambacho utaratibu wa ubinafsishaji wake haukukamilikahapo awali, kinafanyiwa tathmini upya ili nacho kitangazwekwa lengo la kutafuta mwekezaji mahiri.

i) Viwanda vya Vinywaji

62. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Maji katikaeneo la Ntyuka kil ichopo katika Jij i la Dodomakinachomilikiwa na Kampuni ya Dodoma Innovation &Production Ltd kipo katika hatua za mwisho za ujenzi.Kiwanda hicho kitakachokuwa na uwezo wa kuzalishachupa za maji 150,000 kwa siku, kinategemea kutoa ajira 80za moja kwa moja na 120 zisizo za moja kwa moja nakinategemea kuanza uzalishaji mwezi Mei 2018. Pamoja nakiwanda hicho, viwanda vya vinywaji baridi vya Sayona naLakairo vya jijini Mwanza vilizinduliwa mwaka 2017 navinaendelea na uzalishaji.

63. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina viwanda saba(7) vya kusindika zabibu vilivyopo katika Mkoa wa Dodoma.Kati ya hivyo, viwili (2) hutengeneza mvinyo na vitano (5)vinatengeneza michuzi ya zabibu na kuiuza kwa viwandavya mvinyo. Kiwanda cha Mvinyo cha CETAWICO Ltd kinauwezo wa kuzalisha lita milioni 2 hadi 3 za mvinyo kwamwaka. Kiwanda hicho kinatoa ajira 35 za moja kwa mojana hupata malighafi kutoka kwa wakulima zaidi ya 600.Kiwanda cha ALKO-VINTAGE Ltd cha jijini Dodoma kinauwezo wa kuzalisha lita milioni 1.5 za mvinyo na kutoa ajira50 za moja kwa moja na hupata zabibu kutoka kwawakulima zaidi ya 500. Pamoja na viwanda hivyo viwili (2),viwanda vitano (5) vilivyosalia ni vidogo na vinatengenezamichuzi ya zabibu ambayo inauzwa kwa wenye viwandavikubwa vya mvinyo. Viwanda hivyo ni muhimu katikakukamilisha mnyororo wa thamani wa zao la zabibu ambaloni dhahabu ya Mkoa wa Dodoma. Serikali inaendelea kuwekamazingira mazuri ya uwekezaji, ili kuhakikisha wakulima wa

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

zabibu nchini wanapata soko la uhakika na hivyokuwaongezea kipato.

64. Mheshimiwa Spika, mmiliki wa Kiwandacha kutengeneza mvinyo cha DOWICO cha mkoani Dodomakilichobinafsishwa ameanza kukifanyia ukarabati. Ukarabatihuo unategemea kukamilika mwezi Desemba, 2018 nakukiwezesha kuanza uzalishaji. Kukamilika kwa ukarabati huoutaongeza fursa kwa wakulima kupata soko la zabibu zao.Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ilikuhakikisha wakulima wa zabibu nchini wanapata soko lauhakika na kuongeza kipato.

65. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina viwanda 82vya maziwa vyenye uwezo uliosimikwa wa kusindika jumlaya lita 757,550 kwa siku. Kati ya hivyo, viwanda sita (6)havifanyi kazi. Viwanda vinavyofanya kazi vinasindika jumlaya lita 154,100 kwa siku, sawa na asilimia 20 ya uwezouliosimikwa (Kiambatisho Na.11). Uzalishaji wa chini ya uwezouliosimikwa unatokana na kiasi kidogo cha maziwakinachozalishwa na wafugaji. Kampuni ya Watercom Ltdyenye Kiwanda cha Kusindika Maziwa kwa teknolojia ya Ultra-Heat Treatment (UHT) kilichopo Kigamboni, Mkoa wa Dar-es-Salaam kimeanza uzalishaji mwezi Novemba 2017.Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 67.5 zamaziwa kwa mwaka ambapo kwa sasa kinazalisha litamilioni 3 kwa mwaka na kuajiri wafanyakazi 500. Aidha,mitambo ya kuzalisha juisi na soda imesimikwa na kiwandakimeanza uzalishaji.

66. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Maziwa chaTanga (Tanga Fresh Ltd) chenye uwezo wa kusindika lita 50,000kwa siku na kutoa ajira za moja kwa moja 150 kinafanyaupanuzi ili kuongeza uzalishaji. Upanuzi huo utakaogharimuShilingi bilioni 12 unategemea kuongeza uwezo uliosimikwakutoka lita 50,000 za sasa hadi lita 120,000 kwa siku. Upanuzihuo ambao uko katika hatua ya majaribio ya mashineutawezesha kuongezeka kwa ajira za moja kwa moja kutoka150 za sasa hadi 200 wakati ikitegemewa kuongezeka mara

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

mbili kwa wafugaji wanaokiuzia maziwa kutoka 6,000 kwasasa.

ii) Viwanda vya Vifaa vya Umeme

67. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha TANELECLimited kinachozalisha transfoma za umeme kimeongezauwezo wa kuzalisha kutoka transfoma 10,000 hadi 14,000 kwamwaka. Upanuzi huo umegharimu Dola za Kimarekani milioni1.4 na kimeweza kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 120 hadi180 na inatarajia kuongeza ajira hadi kufikia 300 ifikapomwisho wa mwaka 2018. Viwanda hivyo ni muhimu kwauchumi wa nchi yetu kwani vinatekeleza azma ya Serikali yakufikisha umeme nchi nzima na hivyo kuchochea ujenzi waviwanda nchi nzima. Kampuni ya Europe Inc Industries Ltdiliyoko Dar es Salaam nayo imewekeza Dola za Kimarekanimilioni 38 kwa ajili ya kutengeneza vifaa mbalimbali vyaumeme vikiwemo transfoma. Kiwanda hichokitakapokamilika kitaajiri wafanyakazi takriban 800.

68. Mheshimiwa Spika, kama inavyojulikana,Tanzania imekuwa ikitumia fedha nyingi za kigeni kwa ajiliya kuagiza mita za LUKU kwa ajili ya matumizi ya majumbani,maofisini na viwandani. Changamoto hiyo imepataufumbuzi baada ya wawekezaji INHEMETER (T) Ltd kuwekezanchini. Kiwanda hicho kimewekeza mtaji wa Dola zaKimarekani 2,000,000 na kinatarajiwa kuzalisha mita 1,000,000kwa mwaka. Kiwanda cha Baobab Energy SystemsTanzania Ltd (BEST) kimewekeza Dola za Kimarekani 1,700,000kinachotarajiwa kuzalisha mita za LUKU 500,000 kwa mwakana inatarajiwa kuuzwa katika soko la ndani na nje ya nchi.Jumla ya ajira 200 zinatarajiwa kupatikana katika viwandahivyo viwili (2). Viwanda hivyo ni muhimu kwa uchumi wanchi yetu kwani vitawezesha upatikanaji wa mita za kutoshaambazo zilikuwa zinaagizwa na TANESCO kutoka nje. Aidha,uzalishaji huo utatosheleza mahitaji ambayo ni wastani wamita 483,000 kwa ajili ya uunganishaji mpya unaofanywa naTANESCO na Wakala wa Nishati Vijiji. Upatikanaji wa mita zaumeme nchini utawezesha utekelezaji wa azma ya Serikali

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

ya kufikisha umeme nchi nzima na hivyo kuchochea ujenziwa viwanda nchini.

iii) Viwanda vya Mafuta ya Kula

69. Mheshimiwa Spika, mafuta ya kula ni moja yabidhaa zinazoagizwa kwa wingi kutoka nje ya nchi ambapohuigharimu nchi fedha nyingi za kigeni. Takwimu za mwaka2013 zinaonesha kuwa uagizaji mafuta ya kula uligharimuDola za Kimarekani bilioni 44.83, ikiwa ni namba mbili baadaya mafuta ya petroli. Kwa sasa kuna viwanda 21 vya kati navikubwa na vidogo vipatavyo 750 vyenye uwezo wauzalishaji wa tani 210,000, kati ya hizo alizeti ni tani 180,000.Mahitaji ya mafuta ya kula ni tani 700,000, hivyo uzalishaji wandani wa mafuta ya kula unatosheleza kwa asilimia 30 tuwakati asilimia 70 ikiagizwa kutoka nje. Kwa umuhimu huo,nchi haina chaguo jingine zaidi ya kutoa msukumo wakipekee wa kuongeza uzalishaji wa mbegu za mafuta nakufanya usindikaji kwa kutumia viwanda vya ndani nakutumia kwa teknolojia ya kisasa. Jitihada mbalimbalizinaendelea kufanyika, ili kupata suluhu ya kudumu kuhusuuzalishaji wa mafuta ya kula nchini. Mkakati wa KuendelezaMafuta ya Alizeti umeandaliwa ili kuelekeza hatua zakuendeleza zao la alizeti nchini.

70. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naasasi ya Global Community Tanzania imewezeshakukutanisha wadau wa Sekta ya Mafuta ya Kula wapatao300 na wanunuzi wakubwa wa hapa nchini. Mikutano hiyoya ana kwa ana ya biashara (Business to Business –B2B)iliyofanyika sambamba na Maonesho ya 41 ya DTIF. Wadauwalipata fursa ya kupata maelezo kuhusu Mkakati waKuendeleza Sekta ya Alizeti pamoja na matarajio ya Serikalikuona Sekta ya Alizeti inakua na kulinufaisha Taifa.

71. Mheshimiwa Spika, kutokana na jitihadaza kuhamasisha ujenzi na upanuzi wa viwanda, usindikajiwa mbegu za mafuta umeendelea kuongezeka. MheshimiwaDkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania alizindua Kiwanda cha Kusindika

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Mafuta cha Mount Meru Millers Ltd kilichopo mkoani Singida.Kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika mbegu za alizetitani 300,000 kwa mwaka na kuzalisha mafuta tani 90,000 hadi150,000 kwa mwaka kitakapofikia uwezo wake wa juu wauzalishaji na kuongeza ajira za moja kwa moja kufikia 300na zisizo moja kwa moja 900.

iv) Viwanda vya Sukari

72. Mheshimiwa Spika, mahitaji ya sukari nchini nitakriban tani 630,000 kwa mwaka. Kati ya hizo, tani 485,000ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na tani 145,000 ni kwaajili ya matumizi ya viwandani. Sukari kwa matumizi yaviwandani haizalishwi hapa nchini. Uwezo wa uzalishajiwa ndani kwa sasa ni wastani wa tani 320,000 kwa mwaka.Pengo la mahitaji ya takriban tani 165,000 za sukari yakawaida na tani 145,000 za viwandani huzibwa kwakuagizwa kutoka nje.

73. Mheshimiwa Spika, katika msimu wa 2017/2018, hadi kufikia tarehe 20 Aprili, 2018 tani 303,899 za sukarizilikuwa zimezalishwa, wakati matarajio yalikuwa kuzalishatani 314,000. Lengo halikufikiwa kutokana hali ya ukamemkubwa uliozikumba nchi za ukanda wa Mashariki, Katina Kusini mwa Afrika. Kwa kutambua ongezeko la mahitajiya sukari lisiloendana na uzalishaji sukari nchini, Serikaliinahamasisha uwekezaji katika miradi mipya na upanuzi yauzalishaji miwa na sukari kwa viwanda vikubwa na vidogovilivyopo nchini, ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza ziadanje ya nchi.

74. Mheshimiwa Spika, kufuatia uhamasishaji huomiradi mipya mikubwa mitatu (3) ya kilimo cha miwa nauzalishaji sukari imeanza. Miradi hiyo ni:- Mradi wa Kilimo chaMiwa na Uzalishaji wa Sukari Mbigiri uliopo Dakawa katikaMkoa wa Morogoro; Mradi wa Kilimo cha Miwa na UzalishajiSukari Mkulazi ulio katika Wilaya ya Morogoro Vijijini; na Mradiwa Kilimo cha Miwa na Uzalishaji wa Sukari Bagamoyo, Mkoawa Pwani. Miradi hiyo iko katika hatua mbalimbali zautekelezaji. Kampuni ya Morogoro Sugar Co. Ltd inaendelea

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

na taratibu za uhaulishaji wa ardhi ngazi ya wilaya. Kiwandacha Sukari cha Mbigiri kinatarajia kuzalisha tani 48,000 za sukarikwa mwaka. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapomwaka 2022. Mradi wa Sukari wa Mkulazi unategemeakuzalisha tani 200,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025; naMradi wa Sukari Bagamoyo unatarajiwa kuzalisha tani 50,000kwa mwaka ifikapo 2020.

75. Mheshimiwa Spika, katika Mradi wa BagamoyoSugar Co. Ltd, kampuni imekamilisha upembuzi wa kinamwezi Desemba 2017. Tayari Kampuni hiyo imeanzisha kitalucha mbegu za miwa (seedcane nursery) chenye ukubwawa ekari 20 katika Kijiji cha Nambari Nne wilayani Bagamoyo.Hii ni sehemu ya matayarisho ya kuanzisha shamba kuu lamradi huo linalotegemewa kuanza mwezi Juni 2019. Ujenziwa Kiwanda umeanza na unatarajia kukamilika na kuanzauzalishaji katika msimu wa 2019/2020. Vilevile, makampunimengine yanayojishughulisha na uzalishaji wa sukari nipamoja na Kigoma Sugar Co. Ltd na Green Field PlantationsCo. Ltd ya Kigoma na Nkusu Theo Sugar Company Ltd yaRuvuma. Katika Mkoa wa Ruvuma, kampuni ya Nkusu TheoSugar Company Ltd imetengewa hekta 40,000 na inaendeleana mchakato wa kuhaulisha ardhi katika vijiji husika kwaajili ya kilimo cha miwa. Kwa miradi iliyopo katika Mkoa waKigoma, Serikali inapitia upya miradi hiyo, ili kuona namnabora ya uwekezaji.

76. Mheshimiwa Spika, ili kuhamasisha wenyeviwanda vya sukari kuongeza uzalishaji, utaratibu wa uagizajiwa pengo la mahitaji ya sukari (gap sugar) uliwekwa chiniya kampuni zinazozalisha sukari kwa kupeana kiwangomaalum (quota) na siyo wafanyabiashara wengine. Kupitiautaratibu huo, makampuni manne (4) yanayozalisha sukariyamepewa jukumu la kuagiza sukari kwa masharti kuwahakutakuwepo na upungufu wa sukari nchini na lazimawapanue mashamba ya miwa, ili ifikapo mwaka 2020,Tanzania ijitosheleze kwa sukari.

77. Mheshimiwa Spika, kutokana na uamuzi huo waSerikali, Kampuni ya Kilombero Sugar Ltd imeonesha nia ya

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

kuwekeza kiasi cha Shilingi bilioni 500 kupanua uzalishaji.Kampuni hiyo itaboresha mifumo ya kilimo cha umwagiliajikwenye hekta 1,500 na kupanua mashamba ya miwa ilikuongeza mavuno kwa hekta. Pia, itatoa mbegu bora nahuduma za ugani kwa wakulima wa miwa wapatao 8,000,ili waongeze uzalishaji wa miwa. Ongezeko la uzalishaji wamiwa litaendana na upanuaji wa usindikaji miwa kutoka tani270 za miwa kwa saa (Tons Cane per Hour -TCH) kwa sasahadi tani 380 ifikapo Juni 2021.

78. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Sukari cha TPCnacho kinafanya upanuzi wa uwezo wa usindikaji wa miwakutoka tani 190 za miwa kwa saa hadi kufikia tani 220. Vilevile,Kiwanda kitaboresha miundombinu ya umwagiliaji, ilikuongeza mavuno ya miwa na uzalishaji wa sukari. KatikaKiwanda hicho, ongezeko la uzalishaji wa sukari umejikitazaidi kwenye mavuno ya miwa na usindikaji miwa (verticalexpansion).

79. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Sukari cha Kagerakinaendelea kufanya upanuzi wa kiwanda na kilimo chamiwa. Ufungaji wa miundombinu ya umwagiliaji ya kisasaya center pivot unaendelea sambamba na kuongezwa hekta3,800 za miwa kwa awamu hii na hekta 4,000 kuanzia mwaka2020. Pia, Kiwanda kinafunga mitambo ambayo itaongezauwezo wa usindikaji wa sukari kutoka tani 180 za miwa kwasaa awamu ya sasa hadi tani 220 mwaka 2022.

80. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Sukaricha Mtibwa kinafanya upanuzi wa kilimo cha miwa na piakuweka miundombinu mikubwa ya kisasa ya umwagiliaji.Vimejengwa vituo vikubwa vya kusukuma maji (pumpstations) kwa ajili ya umwagiliaji mashambani na usambazajimabomba makubwa chini ya ardhi umefanywa. Uwekezajikatika mitambo ya kisasa ya umwagiliaji maji mashambani(Center Pivot Irrigation System) unaohusisha hekta 5,000 kwaawamu ya kwanza unaendelea. Ujenzi wa miundombinu yaumeme kwa kuvuta umeme wa 33KV kutoka Morogoro hadiMtibwa na kuusambaza eneo lote la mradi, ili kuwezeshaumwagiliaji umefanyika.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

81. Mheshimiwa Spika, uwekezaji katika upanuzi wamashamba, miundombinu ya umwagiliaji na mitambo yausindikaji miwa unaoendelea utawezesha kuongezekakwa uzalishaji wa sukari ya matumizi ya kawaida kutoka tani320,000 hadi kufikia tani 482,000 kwa mwaka katika msimuwa 2021/2022. Serikali inaendelea kujadiliana na nchiwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuwekamazingira wezeshi, hususan ushuru wa forodha stahikiutakaochochea uzalishaji sukari kwa matumizi ya viwandanihapa nchini.

v) Viwanda vya Kusindika Vyakula, Mbogambogana Matunda

82. Mheshimiwa Spika, jitihada zilizokwishaanza zakuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kusindika matundazinaendelea vizuri na hivyo kuwa suluhisho la uharibifu wamatunda. Kiwanda cha kusindika matunda cha Elven AgriCo.Limited kilichoanza uzalishaji mwezi Februari 2017, kinasindikatani 4 za matunda aina ya maembe, papai, ndizi namananasi kwa siku. Aidha, asil imia 80 ya bidhaainazozalishwa na kiwanda hicho huuzwa katika nchi zaBotswana, Italia, Ufaransa, Uingereza na Zambia na asilimia20 huuzwa katika soko la ndani. Aidha, Kiwanda kimefanyajuhudi ya kutumia mabaki yanayotokana na uzalishajikutengeneza nishati ya umeme na mbolea hivyo asilimia 50ya nishati hutokana na mabaki matunda. Kiwanda chaSayona Fruits Limited kilichopo katika eneo la Mboga,Chalinze kimekamilisha ujenzi wa majengo na uzalishaji wamajaribio unaendelea na uzalishaji wa kibiashara unatarajiwakuanza Julai 2018.

83. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa kiwanda chakusindika nyanya cha DABAGA kilichopo mkoani Iringa eneola Ikokoto Ilula umekamilika. Kiwanda hicho kimewekezamtaji wa Shilingi bilioni 5 na kina uwezo wa kusindika tani1,200 kwa mwezi na kutoa ajira za moja kwa moja zipatazo100. Kukamilika kwa kiwanda hicho kutatoa fursa kwawakulima kupata soko la uhakika la mazao ya nyanya, pilipili,

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

tangawizi, vitunguu saumu, karoti, maembe, nanasi namazao mengine ya mbogamboga. Uzalishajiunategemewa kuanza mwezi Mei 2018.

84. Mheshimiwa Spika, Serikali imehamasishauwekezaji katika usindikaji wa nafaka na kufanikiwakumpata mwekezaji Mahashree Agroprocessing TanzaniaLimited anayewekeza katika kiwanda cha kufungashamazao jamii ya kunde husasan mbaazi. Kiwanda hichokinajengwa katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Halmashauriya Morogoro Vijijini ambapo Dola za Kimarekani milioni220 zitawekezwa. Ujenzi huo unategemea kukamilika nakuanza uzalishaji mapema mwaka 2019. Kiwandakitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 2000hadi 6,000 kwa mwezi. Kiwanda hicho kitakuwa mkombozikwa mkulima kwani mbali na kununua mazaoyanayozalishwa na wakulima kitapunguza upotevu wamazao baada ya mavuno na hivyo kuwaongezea kipato.Aidha, mwekezaji Murzah Wilmar Rice Millers ameanza ujenziwa kiwanda cha kisasa kitakacho sindika mpunga katikaeneo la viwanda la Kihonda mkoani Morogoro.

vi) Viwanda vya Kusindika Chai

85. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Kiwanda chaKusindika Chai cha UNILEVER Ltd kilichopo katika Mkoawa Njombe kilichojengwa kwa gharama ya EURO milioni 7.5umekamilika ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu yabarabara na umeme. Hatua inayoendelea ni usimikaji wamitambo. Wakulima wa chai karibu na eneo hilowameendelea kuhamasishwa kuendeleza na kilimo cha chaiil i kurahisisha upatikanaji wa malighafi. Kiwandakitakapoanza uzalishaji kitakuwa na uwezo wa kusindikamajani ya chai tani 50 kwa siku na kuongeza uzalishaji hadikufikia tani 150 kwa siku na kuajiri wafanyakazi wapatao 300.

vii) Viwanda vya Kusindika Kahawa

86. Mheshimiwa Spika, zao la kahawa ni moja yachanzo kikuu cha fedha za kigeni hapa nchini. Ili kuhakikisha

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

kuwa nchi inaendelea kupata fedha za kigeni, Serikaliimeendelea kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vyakusindika kahawa. Kiwanda cha GDM Co. Ltd kilichopo eneola Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe, kilianzakujengwa mwanzoni mwa mwaka 2017 kwa mtaji wa Shilingibilioni 5.2. Kiwanda hicho kitakacho jishughulisha naukoboaji na usindikaji wa kahawa kipo katika hatua zamwisho za usimikaji wa mitambo na kinatarajiwa kutoa ajira450.

viii) Viwanda vya Sabuni

87. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha KEDS TanzaniaLtd chenye uwezo wa kuzalisha sabuni za unga kiasi cha tani50,000 kwa mwaka, ujenzi wake umekamilika na kimeanzauzalishaji. Vilevile, Kiwanda cha Sabuni Industries Ltd chaTanga kilichobinafsishwa ambacho sasa kinaitwa MurzahWilmar Soap Industry, kimefanyiwa ukarabati na kuanzauzalishaji mwezi Machi 2018.

ix) Viwanda vya Kutengeneza Sigara

88. Mheshimiwa Spika, viwanda vya sigara nikichocheo kikubwa cha uongezaji thamani wa zao latumbaku nchini. Hadi kufikia mwaka 2017, Tanzania ilikuwana viwanda viwili (2) vya kutengeneza sigara vya TanzaniaCigarette Company (TCC) na kiwanda cha TobaccoMastermind vilivyopo mkoani Dar es Salaam. Viwanda hivyovina uwezo wa kuzalisha sigara milioni 7,412 kwa mwaka.Kutokana na mchango wake katika uchumi, Serikaliimeendelea kuhamasisha uwekezaji katika uongezajithamani zao la tumbaku ambapo mwekezaji wa Kampuniya Philip Morris Tanzania Ltd alipatikana na kuwekeza kwaajili ya kuzalisha sigara katika eneo la Kingolwira mkoaniMorogoro. Uzinduzi wa kiwanda umefanyika mwezi Machi2018. Kiwanda hicho kina uwezo wa kutengeneza sigaramilioni 400 kwa mwaka na kuajiri wafanyakazi 224.

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

f) Viwanda Vinginevyo

89. Mheshimiwa Spika, uwekezaji wa viwandaumeendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchinikwa kulenga makundi manne ya viwanda:- (i) ujenzi waviwanda vya vifungashio maalum kwa ajili ya kutunzia nakuhifadhi mazao; (ii) viwanda vya kusindika mazao ikiwemousindikaji wa nafaka; (iii) viwanda vya vinywaji vikali; na (iv)viwanda vya vipodozi.

g) Kuendeleza Kanda na Kongano za Viwanda

90. Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimuwa kuharakisha kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda,Wizara iliingia Makubaliano ya Awali (Memorandum ofUnderstanding) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo yaViwanda (UNIDO) tarehe 8 Machi, 2018. Makubalianohayo yataiwezesha Tanzania kutekeleza Programu ya Nchiya Ushirikiano (Partnership Country Programme-PCP)inayosimamiwa na UNIDO na inayojielekeza katika ujenzi wamaendeleo endelevu na jumuishi ya viwanda. Utekelezaji waPCP unatarajiwa kuanza baada ya Bodi ya UNIDO kuridhiaTanzania kuitekeleza mwezi Juni 2018. Mfumo wa utekelezajiwa PCP hushirikisha wadau mbalimbali chini ya udhaminiwa UNIDO wakiwepo wadau wa maendeleo, taasisi za fedhaza kimataifa na UNIDO kama mtaalam na Mshauri Mkuu waProgram ya PCP. Aidha, Programu huwezesha vijana kupatamafunzo maalum ya taaluma muhimu za viwanda nahuwahamasisha wawekezaji wakubwa wanaoaminikakuwekeza katika uendelezaji wa viwanda vinavyotekelezwana Programu hiyo.

91. Mheshimiwa Spika, Programu ya PCP italengakutekeleza mipango na programu za nchi yetu za kuletamaendeleo ya viwanda kulingana na vipaumbeletulivyojiwekea. Maeneo makubwa ambayo Programu ya PCPitajihusisha ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya uzalishajikama vile kanda na kongano za uzalishaji ili kuiwezesha SektaBinafsi ya ndani na nje kuwekeza na kuzalisha bidhaa boraza viwandani kwa maendeleo ya nchi yetu. Programu hii

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

itaiwezesha nchi yetu kutekeleza Mpango wa Pili waMaendeleo kwa kasi zaidi.

92. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Shirika laMaendeleo la Taifa (NDC) imetenga eneo la ekari 95 kati yaekari 230 za eneo la viwanda la TAMCO - Kibaha kwa ajili yaujenzi wa kongano maalum la viwanda vya nguo namavazi. Mpango Kabambe (Master Plan) wa kuendelezaeneo hilo umeandaliwa kwa msaada wa Shirika la GatsbyAfrica na michoro ya eneo hilo imetayarishwa na kuingizwakatika ramani ya Mji wa Kibaha. Aidha, Serikaliimekubaliana na SUMA JKT kutekeleza kazi ya kusawazishaeneo hilo ili kurahisisha ujenzi wa miundombinu.

h) Kujenga na Kuimarisha Mifumo ya Taarifaza Viwanda

93. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naOfisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inaendelea kukusanyatakwimu za viwanda vidogo, vya kati na vikubwaitakayowezesha kuandaa Taarifa ya Mwaka ya Utafiti waUzalishaji Viwandani (Annual Survey of Industrial Production -ASIP) inayotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2018. Taarifa hizozitatumika kufanya chambuzi mbalimbali zitakazosaidiaSerikali kufanya maamuzi ya kisera na kuweka mikakati yakuendeleza Sekta ya Viwanda.

i) Tathmini na Uendelezaji wa Mahitaji ya UjuziMaalum wa Viwanda katika Sekta ya Nguo na Mavazi

94. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mradi waSupporting Indian Trade and Investment for Africa (SITA),imetafiti hali ya ujuzi katika Sekta ya Nguo na Mavazi.Utafiti huo ulibaini upungufu mkubwa wa ujuzi (technical andsoft skills) hasa kwa waendesha mitambo. Juhudi zakupunguza tatizo la ujuzi (technical skills) zimefanyika kwakutoa mafunzo maalum yaliyofanyika nchini Ethiopia nakufadhiliwa na mradi wa SITA. Mafunzo hayo yalihusishabaadhi ya wafanyakazi kutoka viwanda vya 21st Centuary,A-Z na MWATEX. Aidha, Ofisi ya Waziri Mkuu ilidhamini mafunzo

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

kwa kushirikiana na Mamlaka ya EPZ, viwanda vya MazavaFabrics Ltd na TOUKU. Mafunzo hayo yalihusisha kutoa stadiza uzalishaji viwandani kwenye Sekta ya Nguo na Mavazikwa vijana wa kitanzania hususan katika maeneo ya usanifu,ukataji na ushonaji wa mavazi. Lengo la mafunzo hayo nikufanya uzalishaji wa nguo na mavazi nchini kufikia viwangovinavyokidhi mahitaji ya masoko ya nje ya nchi kupitia fursambalimbali zikiwemo za AGOA na EBA (Everything But Arms)na pia soko la ndani .

j) Mafanikio Makuu ya Sekta ya Viwanda

95. Mheshimiwa Spika, katika Mpango wa Pili waMaendeleo wa Miaka Mitano, Serikali imejielekeza katikaujenzi wa viwanda ambavyo vinatumia kwa wingi malighafizinazozalishwa nchini hususan kutoka sekta za kilimo, mifugo,madini na misitu. Vilevile, tunalenga kuendeleza viwandavinavyozalisha bidhaa zinazotumika na wananchi waliowengi ili kuboresha ustawi wa jamii na kuokoa matumizi yafedha za kigeni ambazo zingetumika kuagiza bidhaa hizokutoka nje ya nchi. Aidha, eneo jingine linalopewa msukumoni viwanda vinavyoajiri watu wengi.

96. Mheshimiwa Spika, hivi sasa, nchi yetuinajitosheleza kwa mahitaji ya saruji tukiwa na viwanda 14vyenye uwezo uliosimikwa wa tani milioni 10.98. Uzalishajiuliowahi kufikiwa ni tani milioni 7.4 kwa mwaka wakatimahitaji ya soko la ndani kwa sasa ni tani milioni 4.8. Hivyo,nchi yetu ina ziada ya uwezo wa kuzalisha wa tani milioni2.6 kwa kuzingatia uzalishaji halisi inayoweza kuuzwa nje yanchi (Kiambatisho Na.12).

97. Mheshimiwa Spika, kwa hivi sasa tunavyoviwanda 25 vya kuzalisha bidhaa za chuma. Hali hiyoimetuwezesha kujitosheleza kwa mahitaji ya mabati, nondo,angle bars, hollow section, kwa kutaja baadhi. Vilevile,tunavyo viwanda 15 vya kuzalisha bidhaa za plastikizikiwemo mabomba ya maji. Hali hiyo imetufanya tuwe nauwezo wa kuzalisha mabomba ya kutosha kwa mahitaji yasoko la ndani na ziada kuuza nje ya nchi. Pia, ujenzi wa

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

viwanda viwili vya vigae vyenye uwezo wa kuzalisha mitaza mraba 130,000 kwa siku imetufanya tujitosheleze kwamahitaji ya vigae nchini. Hivyo, ongezeko hilo limekuwakichocheo cha kujenga nyumba imara na za kisasa mpakamaeneo ya vijijini.

98. Mheshimiwa Spika, nchi yetu pia inajitoshelezakwa mahitaji ya vinywaji mbalimbali hususan maji ya chupa,soda, vileo kwa kutaja baadhi. Maendeleo katika ujenzi waviwanda yanaonekana pia katika usindikaji wa vyakula kwakutumia mitambo ya kisasa na ujuzi katika ufungashaji. Halihiyo imesaidia kuongeza thamani ya mazao na kuwezeshawananchi mpaka ngazi ya vijiji kupata vyakula vyenyeviwango na ubora wa hali ya juu.

99. Mheshimiwa Spika, tumefanikiwa kuvutiaujenzi wa viwanda viwili vya kutengeneza mita za umeme,hali itakayotuwezesha kupunguza gharama za kuagizamita hizo kutoka nje ya nchi. Vilevile, Tanzania sasa tunauwezo mkubwa wa kutengeneza transfoma kufuatiaupanuzi wa Kiwanda cha TANELEC, ujenzi wa kiwanda kipyacha Europe Inc Industries Ltd, na uanzishaji wa kitengo chakutengeneza transfoma katika Kiwanda cha Africables Ltd.Pamoja na viwanda hivyo, miradi mingi iko katika hatua zaawali ikilenga sekta ya kutengeneza vifaa vya umemeikiwemo nguzo za zege.

3.3.2 Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

100. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapoawali, viwanda vidogo ni muhimu katika ustawi wa Taifaletu kwani vinachochea ujenzi wa uchumi jumuishi. Sektahiyo inaajiri takribani Watanzania milioni 6 kwa sasa. Viwandahivyo huchangia Pato la Taifa takriban asilimia 35. Viwandavidogo sana, vidogo na vya kati vimechukua zaidi ya asilimia98 ya idadi ya viwanda nchini na wawekezaji wa viwandakatika kundi hilo ni Watanzania wenyewe.

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

(a) Kuendelea Kuhamasisha Ujenzi wa ViwandaVidogo na Biashara Ndogo

(i) Kutoa Mwongozo wa Usimamizi wa Ujenziwa Viwanda kwa Mamlaka za Wilaya na Mikoa

101. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kuwa ujenziwa viwanda hufanyika chini ya mikoa na mamlaka za serikaliza mitaa, Wizara imeandaa na kukamilisha Mwongozowa Kusimamia Maendeleo na Ujenzi wa Viwanda Nchiniutakaowezesha mikoa na wilaya kusimamia ujenzi waviwanda kwa ufanisi na tija. Lengo kuu la Mwongozo huo nikujenga uelewa wa pamoja kwa watendaji wa mikoana mamlaka za serikali za mitaa. Mwongozo pia utatoamaelekezo kwa watendaji, ili kurahisha usimamizi, utekelezajina uendelezaji wa ujenzi wa viwanda. Hatua hiyo itasaidiana kuharakisha mafanikio ya ujenzi wa viwanda ambaoni endelevu na jumuishi. Mwongozo huo pia umeainishawadau muhimu katika ujenzi wa viwanda ambao mikoa namamlaka za serikali za mitaa zitapaswa kushirikiana nao ilikuharakisha maendeleo ya viwanda nchini.

(ii) Kushirikiana na TAMISEMI katika KuhamasishaUtengaji wa Maeneo ya Ujenzi wa Viwanda na Biashara Ndogo

102. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara ilitembelea baadhi ya mikoa ili kutathmini zoezi lautengaji wa maeneo ya uwekezaji wa viwanda na biasharandogo nchini. Maeneo yaliyotembelewa ni mikoa ya Kigoma,Mbeya, Singida na Tanga. Katika ufuatiliaji huo, imebainikakuwa mikoa inaendelea vyema katika kutenga maeneo.Mkoa wa Tanga umetenga maeneo yafuatayo: Halmashauriya Jiji la Tanga, hekta 27.8 (Kange); hekta 68 (Pongwe); nahekta 3.9 (Masiwani). Vilevile, viwanja 101 (Pongwe) naviwanja 324 (Amboni) vimetengwa. Pia, jumla ya mita zamraba 23,671 zimetengwa katika maeneo ya Tangasisi,Mnyanjari na Mzingani. Halmashauri ya Muheza imetengaekari 2,829 katika eneo la Chaturi; ekari 5,730(Shambamombwera); ekari 12,255 (Azimio Kilapua); ekari2,148 (Shamba Kibaranga); na ekari 2,829 (Sigimiembeni).Halmashauri ya Mji wa Korogwe imetenga mita za mraba

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

21,600 katika eneo la Makorakanga na hekta 114.68 katikaeneo la Kalalani. Aidha, hekta 2,043 zimetengwa kwa ajili yaEPZ.

103. Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Mbeyaumetenga maeneo yafuatayo: Halmashauri ya Kyela ekari39.5 katika eneo la Ipyana; ekari 50 katika eneo la Kajujumle;na ekari 60 katika eneo la Busele. Halmashauri ya Jiji la Mbeyaimetenga ekari 54 kwa ajili ya viwanda vya kati na ekari 36kwa ajili ya viwanda vidogo katika eneo la Inyala na ekari 7katika eneo la Iwindi. Halmashauri ya Rungwe imetenga ekari17 kwa ajili ya viwanda vidogo na ekari 10.67 kwa ajili yabiashara ndogo katika eneo la Ilenge.

104. Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Singida umetengamaeneo katika Halmashuri zake kama ifuatavyo: Iramba(ekari 20); Mkalama (ekari 10); Itigi (ekari 10); Manyoni (ekari11); na Ikungi (ekari 4). Aidha, Mkoa wa Kigoma umetengamaeneo katika Halmashauri za Kasulu Vijijini (ekari 25); KasuluMji (ekari 20); Uvinza (ekari 20); Kakonko (ekari 20); Buhigwe(ekari 20); na Kibondo (ekari 20). Wizara itaendeleakushirikiana na mikoa na mamlaka za serikali za mitaakuhakikisha kuwa kila Halmashauri inatenga na kulindamaeneo kwa ajili ya viwanda na biashara na kuwekamikakati ya kuyaendeleza.

(iii) Kitabu cha Taarifa Muhimu kwa Wajasiriamali105. Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha

uendelezaji wa biashara kwa wajasiriamali, Wizaraimeandaa Kitabu cha Taarifa Muhimu kwa Wajasiriamalikilichoweka pamoja taarifa zilizo chini ya usimamizi wamamlaka mbalimbali zinazohusika katika kuanzisha nakuendesha biashara. Taarifa hizo zitawarahisishia wananchikufahamu aina ya vibali au leseni zinazotakiwa wakatiwa kuanzisha aina tofauti za biashara. Kitabu hichokinaainisha taasisi na mahali huduma zinapopatikana tofautina hali ya sasa ambapo mjasiriamali analazimika kufuatiliamwenyewe na wakati mwingine anakuwa hafahamumahali na aina ya huduma husika zilipo. Hatua inayofuata

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

ni kuchapisha, kufanya uzinduzi, kusambaza na kutoa elimukwa umma.

(iv) Kuwezesha Uanzishwaji wa Kongano za Samani

106. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naChuo Kikuu cha Mzumbe chini ya ufadhili wa taasisi yaInternational Growth Centre ya Uingereza imekamilisha utafitiulioangalia namna ya kuendeleza Sekta ya Samani nchini.Lengo la utafiti huo ni kubaini fursa katika sekta hiyo nakupanga mikakati ya kuendeleza na namna nzuri yakushirikisha wadau. Utafiti huo umekamilika na unamapendekezo mbalimbali ya kuboresha sekta ikiwemokuanzisha kongano kwa aji l i ya kuwaweka pamojawajasiriamali wa Sekta ya Samani. Mapendekezo mengineni kuboresha teknolojia na nyenzo zinazotumikakutengenezea samani na kuwapa wajasiriamali mafunzomuafaka ya kutengeneza samani bora na shindani katikasoko. Aidha, utafiti huo utawezesha kujua stadi zinazohitajika,vifaa na mashine zinazohitajika. Maeneo lengwayatakayotumika kuanzisha kongano hizo ni yale yaliyotengwana Halmashauri kwa ajili ya shughuli za viwanda.

(v) Mapitio ya Sera ya Maendeleo ya ViwandaVidogo na Biashara Ndogo ya Mwaka 2003

107. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea na mapitioya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogoya Mwaka 2003. Tathmini ya utekelezaji wa sera imekamilikana hivi sasa Wizara inaendelea na tafiti katika maeneoyaliyobainishwa kuhitaji utafiti wa kina. Maeneo hayo ni sanaaza mikono; sekta zinazoibuka hasa mafuta, gesi na madini;na ukuaji wa jasiriamali. Maeneo mengine ni mfumo washeria na usimamizi wa biashara; upatikanaji wa masoko;uratibu wa sekta; na upatikanaji wa fedha. Aidha, maandaliziya kufanya utafiti katika maeneo ya ubunifu na teknolojia;maswala mtambuka; huduma za kuendeleza biashara; namiundombinu ya msingi na uendelezaji viwanda vijijiniyanaendelea.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

(vi) Kuendelea Kusimamia Mfuko wa Maendeleoya Ujasiriamali (NEDF)

108. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi2018, mtaji wa NEDF umekua na kufikia Shilingi 7,819,422,990.Ukuaji huo umetokana na kuzungusha mtaji wa Shilingi5,051,000,000 uliotolewa na Serikali tangu Mfuko uanzishwemwaka 1994. Ongezeko la Shilingi 2,768,422,990 katika mtajihuo limetokana na juhudi za Wizara na SIDO kufuatilia kwaumakini maendeleo ya shughuli za wajasiriamali wanufaikana kuimarisha mifumo ya marejesho ya mikopo inayotolewa.

109. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mfukowa NEDF katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Singida naTabora. Ufuatiliaji huo ulibaini kuwepo kwa maombimengi ya mikopo ikilinganishwa na uwezo wa Mfuko.Maombi yaliyowasilishwa yalikuwa Shilingi bilioni 6.398ikilinganishwa na uwezo wa Mfuko wa kutoa mikopo yaShilingi bilioni 3.344. Licha ya kuwepo kwa changamoto hizo,Mfuko huo umefanikisha kupatikana ajira 4,438 mwaka 2017/2018, kati yao wanawake ni 2,308. Mafanikio mengine nikuimarika kwa biashara na viwanda vidogo vilivyopatamikopo ya NEDF, wajasiriamali kumudu kusomesha watoto,kujenga nyumba za kisasa, kununua vyombo vya usafiri nakukuza vipato vya familia.

(b) Kutumia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) kama Nyenzo ya Kujenga Viwanda

(i)Kulifanyia Mageuzi Shirika la SIDO

110. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuliwezesha Shirika la SIDO ili liweze kushiriki kikamilifu katikaujenzi wa viwanda. Kwa mwaka 2017/2018, SIDO imepokeaShilingi 5,000,000,000 kwa ajili ya kuongeza maeneo yakufanyia kazi wajasiriamali na kuendelea kujenga ofisi katikamikoa mipya ya Geita, Katavi na Simiyu ili kufikisha hudumaza SIDO katika mikoa hiyo. Aidha, Wizara imeendeleakuongeza miundombinu ya majengo ili kuongeza idadi ya

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

wajasiriamali wa viwanda katika mitaa ya viwanda ya SIDO.Kwa kuanzia, majengo ya kufanyia shughuli za viwanda kwawajasiriamali wadogo (industrial sheds) yanajengwa katikamikoa ya Dodoma, Geita, Kagera, Manyara, Mtwara naNjombe.

(ii) Kuhamasisha Wananchi Kushiriki katika Ujenziwa Viwanda

111. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara kupitia SIDO iliandaa maonesho ya kanda katikamikoa ya Iringa, Kigoma, Kilimanjaro na Lindi. Maonesho hayoyalishirikisha wajasiriamali 520 kati ya hao wanawake ni 390.Wizara ilitumia fursa ya maonesho hayo kuhamasishawajasiriamali kuwekeza katika viwanda; kutoa ushauri wakuboresha bidhaa; na kuelezea sera na mikakati ya kisektainayolenga kuendeleza viwanda kupitia vipeperushi. Vilevile,wananchi walihamasishwa kutumia bidhaa zinazozalishwana viwanda vya ndani ili kutanua soko la ndani na hivyokuchochea viwanda hivyo kuzalisha zaidi.

(c) Ushirikiano na Wadau112. Mheshimiwa Spika, Wizara inashirikiana na

Serikali ya Canada kutekeleza mradi wa Strengthern SmallBussiness Value Chain. Taasisi isiyo ya Kiserikali ya MEDAinatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na SIDO, TCCIA naTanzania Women Chamber of Commerce. Mradi huounaohusisha ujenzi wa uwezo wa kuziwezesha jasiriamalikukua kupitia huduma za mafunzo, mitaji na teknolojia.Jasiriamali hizo ni zile zinazojihusisha na sekta za uongezajithamani mazao, ujenzi, usambazaji (logistics), uchimbajimadini na uzalishaji viwandani. Mradi huo unatekelezwakatika mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro,Manyara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Singida,Songwe na Tanga. Aidha, Mradi huo unaotekelezwa kuanziamwaka 2015 hadi 2021, una thamani ya Dola za Canadamilioni 30 na utanufaisha jasiriamali 10,000 katika mikoahusika. Hadi kufikia Machi 2018, Mradi huo umetoa hudumaza kuendesha na kukuza biashara kwa jasiriamali 6,213;jasiriamali 1,428 zimewezeshwa kupata mitaji midogo

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

midogo na teknolojia na jasiriamali 500 zimepata ruzuku yambegu bora kwa zao la vanilla ili kuboresha uzalishaji.

3.3.3 Sekta ya Uwekezaji113. Mheshimiwa Spika, jitihada za ujenzi wa

uchumi wa viwanda nchini, pamoja na mambo mengine,zinahitaji ushiriki mpana na shirikishi wa sekta ya umma nabinafsi. Jitihada hizo zinajumuisha uhamasishaji na uvutiajimitaji na wawekezaji, kuweka mazingira wezeshi na rafiki,kutangaza fursa zil izopo katika miradi na maeneombalimbali, kuboresha na kutangaza vivutio katika maeneombalimbalii ya uchumi kwa kutaja machache. Wizara kupitiaTIC na kwa kushirikiana na Taasisi za Sekta Binafsizinajishughulisha na uhamasishaji wawekezaji wa ndani nanje ya nchi.

a) Kuhamasisha Wawekezaji wa Ndani na Nje

114. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara ilihamasisha wawekezaji kupitia makongamanoyaliyofanyika katika mikoa ya Tanga (Agosti 2017) na Kagera(Desemba 2017). Vilevile, Wizara ilishiriki katika Kongamanola uwekezaji kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Dares Salaam mwezi Novemba 2017; Tanzania na Jordan mweziDesemba, 2017; Tanzania na Ufaransa, tarehe 18 Aprili2018, Dar es Salaam; na Tanzania na Israel lililofanyikajijini Dar es Salaam tarehe 23 hadi 24 Aprili 2018. Vilevile, kupitiaprogramu ya kuimarisha uwekezaji na biashara kati ya Indiana Tanzania (SITA) iliwakutanisha wawekezaji wa ngozi nabidhaa zake mwezi Desemba, 2017. Makongamanoyalihusisha wafanyabiashara wa ndani na nje zaidi ya 1,000na fursa mbalimbali zilizopo Tanzania ziliainishwa. Aidha,Wizara ilishiriki Mkutano wa Pili wa Afrika Mashariki wa Biasharana Wajasiriamali ulioenda sambamba na maonesho yabiashara za wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaamkuanzia tarehe 14 hadi 16 Novemba, 2017.

115. Mheshimiwa Spika, kufuatia makongamano namikutano hiyo pamoja na ushirikiano wa karibu wa Ofisi zetuza Ubalozi, ujumbe wa wawekezaji mbalimbali wameweza

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

kufika nchini na kutembelea Kituo cha TIC, Wizara na taasisinyingine za umma na Sekta Binafsi. Baadhi ya kampunizilizotembelea nchini ni: Ujumbe wa taasisi ya CRG Group ofInstitutions ya India inayotaka kuwekeza katika ujenzi nauendeshaji wa chuo cha ufundi stadi; Ujumbe wa kampuniya Artech Fze Group kutoka Misri wameonesha nia yakuwekeza kwa ubia na taasisi au shirika la Serikali kwa ubiakatika mradi wa uchimbaji makaa ya mawe na uzalishajiwa saruji kwa ajili ya kuuza nje ya nchi; na ujumbe wakampuni ya A & T Agricultural Ltd ya Vietnam kwa ajili yakufanya biashara ya korosho ghafi na kuwekeza katikaviwanda vya kubangua korosho.

116. Mheshimiwa Spika, wengine ni makampuni tisa(9) ya China yakiongozwa na taasisi ya Kongamano naViwanda Kati ya China na Afrika yaani China Africa IndustrialForum (CAIF) wakilenga Sekta ya Nishati, viwanda namiundombinu; ujumbe wa kampuni ya TVS GlobalAutomotive kutoka India ukiwa na nia ya kuwekeza katikauzalishaji wa pikipiki hapa nchini; na ujumbe wawafanyabiashara na wawekezaji kutoka Chinawakiongozwa na wawakilishi wa China WTO Africa AffairsCommittee on Trade Promotion Centre (CWTO) uliooneshania ya kuwekeza kwenye Sekta ya Kilimo na Biashara.

117. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha jitihadaza kuvutia wawekezaji kutoka nje, Wizara imeandaa rasimuya mwongozo kwa balozi za Tanzania nje ya nchi. Mwongozohuo unaelekeza ofisi hizo kutumika kuvutia mitaji nauwekezaji nchini. Pia, unasisitiza jukumu la kutafuta masokoya bidhaa za Tanzania zikiwemo zinazozalishwa na viwandavidogo na vya kati; na kutangaza fursa za uwekezaji zilizokonchini. Mwongozo huo unaelekeza kuanzishwa kwamadawati maalum ya kushughulikia masuala ya biasharana uwekezaji. Rasimu hiyo itawasilishwa kwa wadau naWizara za kisekta ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki ambayo ndiyo mtekelezajimkuu. Aidha, ili kuimarisha diplomasia ya uchumi, Wizara kwakushirikiana na Wizara na taasisi nyingine ilifanya maonesho

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

ya bidhaa za Tanzania katika nchi za Kenya na Dubai tarehe26 Aprili, 2018.

118. Mheshimiwa Spika, maamuzi ya Serikali yakuhamia makao makuu Dodoma yameambatana nakuhamasika kwa sekta binafsi kujenga viwanda Dodoma.Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd (TBL) imeazimiakuwekeza katika ujenzi wa kiwanda kipya cha kuzalisha biamkoani Dodoma kama mkakati wake wa kuongeza uzalishajinchini. Kampuni hiyo inatarajia kuwekeza Shilingi bilioni225. Kiwanda hicho kipya kinatarajia kuzalisha lita milioni100 za bia kwa mwaka na kutoa ajira kwa watu 600.Kiwanda hicho kitahitaji malighafi kiasi cha tani milioni 5.6na hivyo kutoa fursa nzuri ya soko kwa wakulima wa mtama,mahindi, shayiri na mihogo.

b) Kuratibu Uwepo wa Mazingira Bora yaUwekezaji

119. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kuandaana kushiriki vikao vya pamoja vya mashauriano kati ya Serikalina Sekta Binafsi kwa lengo la kupata maoni ya kuboreshamazingira ya biashara na uwekezaji nchini. Katika mwaka2017/2018, mikutano miwili (2) ya ngazi ya juu iliyohusishaWaziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Viwanda, Biasharana Uwekezaji, na viongozi wakuu wa taasisi ya Sekta Binafsiilifanyika mwezi Oktoba 2017 jijini Dar es Salaam na Januari2018 mjini Dodoma. Serikali na Sekta Binafsi wamekubalianakuendelea kuwa na mikutano kama hiyo ya majadilianokwa kuwa ina umuhimu sana katika kupata ufumbuzi wachangamoto zilizopo na kuboresha mazingira ya biasharana uwekezaji.

120. Mheshimiwa Spika, katika kutekelezamaazimio ya mikutano hiyo iliyopendekeza kuitishwa kwamikutano midogo ya sekta maalum, Wizara za Serikali kwakushirikiana na vyama vya kisekta zimefanikisha kuitishwamikutano ya mashauriano ya kisekta kati ya Wizara husikana wadau. Mikutano hiyo ni pamoja na mikutano kati ya

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Sekta Binafsi na Wizara ya Fedha na Mipango kujadili masualaya kikodi; Wizara ya Nishati kujadili masuala ya nishati; naWizara ya Maliasili na Utalii kujadili masuala ya utalii. Vilevileyalifanyika majadiliano na Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Kilimona TAMISEMI kujadili changamoto za uongezaji thamanikwenye mnyororo wa uzalishaji wa pamba. Pia, Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji ilijadiliana na Sekta Binafsikuhusu changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Chumana Mabati ikiwemo kupanda kwa bei ya chuma. Kimsingi,mikutano hiyo imeendelea kuimarisha ushirikiano kati yaSerikali na Sekta Binafsi, na Serikali imeahidi kuendeleakushauriana na wafanyabiashara na wawekezaji ili kuimarishamazingira ya biashara na uwekezaji na hivyo kukuza uchumi.

c) Kukamilisha Mapitio ya Sera ya Uwekezajiya Mwaka 1996

121. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018,Wizara imefanya mapitio na kukamilisha rasimu ya Sera yaUwekezaji ili iendane na matakwa ya mipango ya kitaifa.Rasimu hiyo itapelekwa kwa wadau wa Sekta ya Umma naSekta Binafsi ili kupata maoni yao kabla ya kuandaa mkakatiwa utekelezaji. Vilevile, Wizara inaendelea kuratibumaandalizi ya Sera ya Uwekezaji ya Jumuiya ya AfrikaMashariki (EAC Investment Policy) ambayo inalengakuhamasisha matumizi ya fursa za uwekezaji kwa nchiwanachama kwa pamoja.

d) Kukamilisha Mapitio ya Sheria ya Uwekezaji ya1997

122. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipangoimefanya uchambuzi wa Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997na Sheria nyingine za kodi na kupendekeza maboresho ilikubadili sifa na vigezo vya aina ya uwekezaji unaotambulikana Sheria ya Uwekezaji. Aidha, hatua hiyo inalenga kuzifanyasheria za kodi kuitambua misamaha ya kodi inayotolewa chiniya Sheria ya Uwekezaji ili kuwezesha utekelezaji wa

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

maamuzi ya Kamati ya Taifa ya Uwekezaji (NationalInvestment Steering Committee-NISC). Hatua hiyo ni muhimukatika kukabiliana na changamoto zilizopo hususan katikautekelezaji wa sheria za kodi katika kutoa misamaha kwawawekezaji mahiri (Strategic Investors) ambayoimeidhinishwa na NISC. Mapendekezo hayo yamewasilishwakatika hatua za mwisho za majadiliano na maamuzi.

3.3.4 Sekta ya Biashara123. Mheshimiwa Spika, Wizara ina jukumu la

kujenga na kuendesha mfumo wa kibiashara unaosimamiwakisheria, unaotabirika na wenye uwazi ili kuwezesha ufanyajibiashara kwa urahisi na tija. Katika kutekeleza jukumu hilo,Wizara imeendelea kushiriki katika majadiliano ya kibiasharakati ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa kwa lengo lakufungua fursa mbalimbali za biashara kwa bidhaa nahuduma zinazozalishwa nchini. Jitihada hizo zimeshirikishakwa ukaribu wadau wa Sekta ya Umma na Binafsi kwaTanzania Bara na Zanzibar. Matokeo ya jitihada hizoyamechochea katika kukuza mchango wa Sekta ya Biasharakatika Pato la Taifa ambapo kwa mwaka 2017 ulikuwaasilimia 11.0 ikilinganishwa na asilimia 10.8 mwaka 2016.

a) Mwenendo wa Biashara ya Kimataifa

124. Mheshimiwa Spika, mauzo ya bidhaa kwenyemasoko ya upendeleo yalikuwa kama ifuatavyo: soko laChina yalipungua kutoka Dola za Kimarekani milioni 355.9mwaka 2016 hadi Dola za Kimarekani milioni 142.3 mwaka2017. Upungufu huo ulitokana kwa kiasi kikubwa na kupunguakwa mauzo ya vito vya thamani. Manunuzi ya Tanzaniakutoka China yalikuwa Dola za Kimarekani milioni 1,630.2mwaka 2016 ikilinganishwa na Dola za Kimarekani milioni1,408.1 mwaka 2017 (Kiambatisho Na. 13). Mauzo katika Sokola India yaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani milioni 706.4mwaka 2016 hadi Dola za Kimarekani milioni 977.6 mwaka2017. Ongezeko hilo l i l itokana na uuzaji wa bidhaambalimbali kama karafuu, korosho, ngozi za wanyama, nazi,mazao ya jamii ya kunde, samaki, pamba na nyuzi za katani.Manunuzi ya Tanzania kutoka India yalipungua kutoka

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Dola za Kimarekani milioni 1,421.6 mwaka 2016 hadi Dola zaKimarekani milioni 1,077.6 mwaka 2017 (Kiambatisho Na. 14).Hali hiyo ilisababishwa na kupungua kwa kiwango chauingizaji wa bidhaa kama vile chuma, chai, tumbaku(Tobacco, partly or wholly stemmed/stripped), nafaka, bidhaaza plastiki na kemikali.

125. Mheshimiwa Spika, mauzo katika soko laJapan yalipungua kutoka Dola za Kimarekani milioni 139.2mwaka 2016 hadi Dola za Kimarekani milioni 75.7 mwaka2017. Upungufu huo unatokana na kupungua kwa mauzo yavito vya thamani (precious metal ores), chai, kahawa napamba. Mwaka 2016, manunuzi ya bidhaa kutoka Japanyalikuwa na thamani ya Dola za Kimarekani milioni 369.2ikilinganishwa na Dola za Kimarekani milioni 365.2 mwaka2017, sawa na upungufu wa asilimia 1.2 (Kiambatisho Na.15). Upungufu huo unatokana na kupungua kwa uagizaji wabidhaa za chuma (Flat rolled products of iron), magarikuanzia cc 1500 hadi 2000 (of cylinder capacity exceeding1500cc but not exceeding 2000cc), magari yasiyozidi cc 1500(of a cylinder capacity not exceeding 1500cc)

126. Mheshimiwa Spika, bidhaa zilizonunuliwana Tanzania kutoka Jumuiya ya Ulaya zilikuwa na thamaniya Dola za Kimarekani milioni 557.7 mwaka 2016ikilinganishwa na Dola za Kimarekani milioni 936.1 kwamwaka 2017, ikiwa ni ongezeko la asilimia 67.9. Pia mauzoya bidhaa za Tanzania kwenda Jumuiya ya Ulayayaliongezeka kutoka Dola za Kimarekani milioni 236.5 kwamwaka 2016 hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni 441.4mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 86.7. Kutokanana hali hiyo urari wa biashara umeonesha nakisi ya Dola zaKimarekani milioni 494.7 (Kiambatisho Na. 16), ikimaanishathamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ni kubwaikilinganishwa na thamani ya mauzo ya bidhaa za Tanzaniakatika soko hilo. Hii inatokana na Tanzania kuuza zaidimalighafi katika soko la Jumuiya ya Ulaya wakati Tanzaniainaagiza bidhaa za viwandani (finished products).

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

127. Mheshimiwa Spika, mauzo ya bidhaa zaTanzania kwenda Marekani kupitia Mpango wa AGOAkwa mwaka 2017 yaliongezeka na kufikia Dola za Kimarekanimilioni 40.545 ikilinganishwa na Dola za Kimarekani milioni37.476 kwa mwaka 2016 (Kiambatisho Na. 17). Mauzo hayokwa kiasi kikubwa yalichangiwa na Sekta ya Nguo naMavazi kwa asilimia 99.2. Aidha, ili kuongeza mauzo zaidikatika soko hilo, Wizara imeanza kutekeleza Mkakati waKitaifa wa Kukuza Mauzo ya Tanzania katika soko la Marekanikupitia Mpango wa AGOA.

128. Mheshimiwa Spika, katika kutumia fursa zamasoko ya kikanda, mauzo ya Tanzania katika nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2017 yalikuwa Dola zaKimarekani milioni 349.6 ikilinganishwa na Dola za Kimarekanimilioni 437.7 mwaka 2016. Upungufu huo umetokana nauzalishaji wa bidhaa zinazofanana kwenye nchi za Jumuiyaya Afrika Mashariki. Aidha, bidhaa za Tanzania zilizouzwa kwawingi katika soko hilo ni pamoja na mbogamboga, chai,matunda, magunia, mifuko ya plastiki, wanyama hai, viazi,samaki, udongo asilia, kahawa, mahindi, mchele, unga wanafaka, karanga, mawese, ufuta, pamba na makaa yamawe. Kwa upande mwingine, ununuzi wa Tanzania kutokanchi za Jumuiya hiyo ulipungua kutoka Dola za Kimarekanimilioni 220.4 mwaka 2017 ikil inganishwa na Dola zaKimarekani milioni 298.9 mwaka 2016 (Kiambatisho Na. 18).Hali hiyo imechangiwa na kuimarika kwa uzalishaji bidhaandani hivyo kupunguza kasi ya uagizaji wa bidhaa kama vilemadawa (medicaments), Chewing gum, whether or notsugar-coated, chumvi, sabuni, vifaa vya plastiki, mafuta yakupikia, sukari, nyama, wanyama hai, vinywaji na bidhaa zamifugo.

129. Mheshimiwa Spika, mauzo ya Tanzania kwendakatika soko la nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusinimwa Afrika (SADC), mwaka 2017 yalikuwa Dola za Kimarekanimilioni 877.8 ikilinganishwa na Dola za Kimarekani milioni1,017.9 mwaka 2016. Upungufu huo umetokana kwa kiasikikubwa na kushuka kwa uuzaji wa dhahabu katika soko laAfrika ya Kusini. Aidha, bidhaa zilizouzwa katika soko la SADC

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

ni pamoja na dhahabu, chai, mazao jamii ya kunde,tumbaku, ngano, ngozi, pamba, matunda ya kutengenezajuisi, mawese, mbolea, vipuri vya magari na samaki. Ununuziwa Tanzania kutoka katika soko hilo uliongezeka kutoka Dolaza Kimarekani milioni 612.4 mwaka 2016 hadi Dola zaKimarekani milioni 1,7781.4 mwaka 2017 (Kiambatisho Na.19).Ongezeko hilo limetokana na uagizaji kwa wingi bidhaa zachuma, petroli [Motor Spirit (gasoline) premium], dawa zabinadamu (medicaments), gas oil, mafuta ghafi (crude oil),mafuta ya taa (Kerosene type Jet Fuel), Turbojets, turbo-propellers

b) Kuendeleza Majadiliano ya Kibiashara iliKupanua Fursa za Masoko na Uwekezaji

i) Majadiliano Baina ya Nchi na Nchi

130. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka 2017/2018, Wizara iliratibu mikutano mbalimbalikati ya Tanzania na nchi nyingine ili kuendelea kutafuta fursanafuu za biashara na uwekezaji. Mikutano hiyo ni pamojana Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati yaTanzania na India uliofanyika New Delhi, India tarehe 28 –29 Agosti, 2017. Mkutano huo ulifikia makubaliano yakukamilisha Mkataba wa Kuhamasisha na Kulinda Uwekezaji;Mkataba wa Ushirikiano kwenye Usimamizi wa Forodha; namkopo wa kutekeleza mradi wa maji kwa ajili ya miji 17 nchini.

131. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki katikaMkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC)kati ya Tanzania na Misri uliofanyika Cairo, tarehe 10Januari, 2018. Makubaliano yaliyofikiwa kwenye Sekta yaViwanda na Biashara ni pamoja na kukamilisha Makubalianoya Ushirikiano wa Kibiashara ambapo kwa upande waTanzania rasimu ya makubaliano hayo imekamilika naimepitia taratibu zote za ndani na kuwasilishwa upande waMisri kwa ajili ya kuridhiwa na kusainiwa. Pia, makubalianoya kushirikiana katika maonesho ya kibiashara; kuanzishakiwanda cha uzalishaji wa nyama nchini; kituo kwa ajili ya

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

maonesho ya bidhaa za Misri; na kiwanda cha bidhaa zangozi yalifikiwa.

132. Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilishamapitio ya Mkataba wa Biashara na Uchumi baina yaTanzania na Urusi ambao umewasilishwa Urusi mwezi Januari2018 kwa ajili ya kuridhiwa na kusainiwa. Aidha, Wizarainaendelea kukamilisha Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumina Biashara baina ya Tanzania na Mauritius na taratibu zoteza ndani zimekamilika na utasainiwa baada ya upande waMauritius kukamilisha taratibu zao.

133. Mheshimiwa Spika, Wizara iliandaa mkutanowa pamoja kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika Namangatarehe 3 Agosti, 2017 na jijini Dar es Salaam tarehe 6 hadi 8Septemba, 2017. Mikutano hiyo ililenga kuondoa Vikwazo vyaKibiashara Visivyo vya Kiushuru (NTBs) baina ya nchi hizo mbili.Katika mikutano hiyo, Kenya iliridhia uingizaji wa gesi yakupikia majumbani (LPG) na unga wa ngano kutoka kwawafanyabiashara na wazalishaji wa Tanzania ambapo hapoawali zilizuiliwa kuingia nchini Kenya.Vilevile, Wizara ilishirikikatika mkutano wa pamoja baina ya Tanzania na Kenyauliofanyika Mombasa, Kenya tarehe 24-31 Januari, 2018.Mkutano huo ulilenga kuondoa Vikwazo vya NTBs baina yapande hizo mbili ambapo Kenya imeruhusu unga wamahindi, mafuta ya kupikia na bidhaa za Azam (Azam icecream, juice na soda) kuingia nchini humo bila vikwazovyovyote.

ii) Majadiliano ya Kikanda

134. Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kurahisishabiashara baina ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki, Wizarakupitia mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri waBiashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliofanyika jijiniArusha tarehe 9 Februari 2018, Tanzania iliridhia kuondoa tozoya Dola za Kimarekani 40 kwa ajili ya stika za kubandikakwenye magari yanayobeba bidhaa kutoka Bandari yaDar es Salaaam kupeleka nchi za Burundi, Rwanda naUganda. Tanzania iliondoa tozo hiyo kwa kuwa imekuwa

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

ikilalamikiwa na wadau wa usafirishaji na hata kusababishabaadhi ya waagizaji wa mizigo kutoka nchi hizo kuanzakutumia bandari za nchi jirani.

135. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa Dharurawa 35 wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki uliofanyikamjini Kampala, Uganda tarehe 15 hadi 20 Februari 2018, Wizarailifanikiwa kuomba na kukubaliwa kutoza ushuru wa forodhawa asilimia 35 ya thamani ya bidhaa za mitumba ya nguona ngozi inayotoka nje ya Afrika Mashariki. Hii inatokana nakusudio la Marekani la kutaka kuziondoa nchi za Tanzania,Rwanda na Uganda kwenye Mpango wa AGOA. Uamuzi waMarekani ulitokana na nchi za Afrika Mashariki kuongeza kodikwa bidhaa za mitumba ikiwemo nguo na viatu kutoka Dolasenti 20 hadi Dola senti 40 kwa kilo na kutoza kodi ya asilimia35 ya thamani ya bidhaa. Hatua hiyo itawezesha Tanzaniakuendelea kunufaika na fursa za soko la AGOA.

136. Mheshimiwa Spika, kupitia Mkutano wa 19wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyikamjini Kampala, Uganda tarehe 23 Februari, 2018 Tanzaniaimeendelea kuwa na msimamo wa kutokusaini Mkatabawa Ubia wa Kiuchumi baina ya nchi za Afrika Mashariki naUmoja wa Ulaya (EAC-EU EPA). Msimamo huo umezingatiaAzimio la Bunge kuishauri Serikali kutosaini Mkataba huo hadihapo utakapokidhi maslahi ya Taifa.

137. Mheshimiwa Spika, katika kuhamasishajumuiya za wafanyabiashara kuhusu fursa nafuu zaupendeleo za biashara zinazotokana na majadilianoya nchi na nchi, kikanda na kimataifa, Wizara kwakushirikiana na Sekretarieti ya EAC iliandaa mafunzo ya kutoataarifa kwa mfumo wa kielekroniki kwa Sekta Binafsi nawataalam wa taasisi za udhibiti jijini Dar es Salaam tarehe13 Desemba,2017. Mafunzo hayo yalilenga kuwezeshawalengwa kutumia vyema fursa za miradi mbalimbali zilizopokwenye mikataba ya urahisishaji biashara; ulinzi wa afya zabinadamu, wanyama na mimea (SPS); na vikwazo vyakiufundi vya kibiashara (TBT). Pia, mafunzo yalilengakuwajengea uwezo na uelewa zaidi wadau kutoka Sekta

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Binafsi na Umma kuhusu utekelezaji wa Mkataba waUshirikiano baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Marekani,hususan kwenye eneo la urahisishaji biashara na utatuzi wavikwazo vya biashara vinavyohusiana na masuala yaviwango na ubora wa bidhaa.

138. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki katikamkutano wa tatu wa wataalam wa EAC kwa ajili ya kupitiaMpango Kazi wa Vikwazo vya TBT wa mwaka 2016/2017 nakuandaa Mpango Kazi wa mwaka 2017/2018. Mkutano huoulifanyika Kampala, Uganda tarehe 4 hadi 6 Oktoba, 2017.Pia, Wizara ilishiriki katika mkutano wa uwezeshaji Jukwaala Kikanda la Vikwazo vya Kiufundi vya Kibiashara (EAC TBTForum) uliofanyika Dar es Salaam tarehe 12 hadi 14Desemba, 2017. Washiriki waliweza kupata taarifa mbalimbalikuhusu masuala ya TBT na kubadilishana uzoefu, haliinayotarajiwa kusaidia uboreshaji wa matumizi ya TBT kamasehemu ya kurahisisha ufanyaji wa biashara.

139. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa29 wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara wa SADC uliofanyikaPretoria, Afrika Kusini tarehe 14 Agosti, 2017 Tanzania ilifanikiwakutetea na kukubaliwa kuendelea kutoza ushuru sukari yaviwandani asilimia 10 na ya majumbani asilimia 25. Hivyo,sukari hiyo inayoingizwa nchini kutoka nchi za SADCitaendelea kutozwa ushuru kwa kipindi cha miaka mitatu(3) kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2019/2020. Vilevile,Mkutano huo uliridhia, maombi ya Tanzania ya kutoza ushuruwa asilimia 25 kwa bidhaa za karatasi za vifungashio (Pulpand Paper) zinazoingizwa nchini kutoka nchi za SADC kwakipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia mwaka 2017/2018 hadi2019/2020. Hatua hizo zinalenga kulinda na kutoa fursa kwaviwanda vyetu vya sukari na karatasi kuweza kujipangavyema kuhimili ushindani katika bidhaa hizo kutoka kwawazalishaji wa soko la SADC.

140. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikishatunatekeleza ipasavyo Itifaki ya Biashara ya SADC, Wizaraimefanikiwa kupata ufadhili wa EUR 1,400,000 kupitia mradiwa SADC Trade Related Facility (SADC-TRF) unaofadhiliwa na

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Umoja wa Ulaya. Hadi kufikia mwezi Machi 2018, Wizaraimepokea EUR 420,000 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu yakwanza ya mradi. Mradi huo unalenga kusaidia uendelezajiwa mnyororo wa uongezaji thamani hususan katikamazao ya kilimo; kuboresha usimamizi wa viwango;uwezeshaji biashara, na ukuzaji wa masoko. Aidha, ulilengakurejea Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka1996 – 2020.

141. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki Mkutano waNne wa Mawaziri wa Biashara wa Umoja wa Afrika uliofanyikaNiamey, Niger tarehe 1-2 Desemba, 2017 kwa lengo lakukamilisha majadiliano ya uanzishwaji wa Eneo Huru laBiashara Barani Afrika (African Continental Free Trade Area-AfCFTA). Kupitia Mkutano huo, Wizara iliweza kutetea nakupendekeza maboresho kwenye vipengele vyenye kuletaunafuu kwa nchi katika Mkataba wa AfCFTA hususan Itifakiya Masuala ya Biashara ya Bidhaa na Biashara ya Huduma.Rasimu ya Mkataba na itafiki hizo ziliwasilishwa katika ngaziya Wakuu wa Nchi na Serikali kwa uamuzi.

142. Mheshimiwa Spika, Wizara imeshiriki katikaMkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali kwa ajiliya kuanzisha Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) uliofanyikamjini Kigali, Rwanda tarehe 21 Machi, 2018. Mkutano huoulitanguliwa na mikutano iliyofanyika mjini Kigali kuanziatarehe 26 Februari, 2018 katika ngazi za wataalam,mabalozi, makatibu wakuu na mawaziri wanaohusika namasuala ya biashara, sheria na mambo ya nje. Mkutano huoulikamilika kwa Wakuu wa nchi na Serikali kutia sainimakubaliano ya uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika.Kupitia Mkutano huo, Tanzania imetia saini Azimio la KuungaMkono Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (The KigaliDeclaration on the Establishment of the African ContinentalFree Trade Area). Azimio hilo linaunga mkono na kubainishania na dhamira ya Tanzania na nchi nyingine wanachamakatika kukamilisha baadhi ya maeneo ya majadilianoyaliyobaki katika hatua ya kwanza ya majadiliano kuwezeshanchi zote za Umoja huo kutia saini na kisha kuridhia Mkatabawa uanzishwaji wa AfCFTA. Maeneo yatakayojadiliwa katika

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

hatua ya pili yanahusu Uwekezaji, Sera ya Ushindani, Haki Milikina Ubunifu (Intellectual Property Rights-IPR). Kwa ujumla,Mkataba huo utatoa fursa za upendeleo kupitia ushirikianowa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi nyinginewanachama wa Umoja wa Afrika. Makubaliano hayoyanatoa fursa kwa Tanzania kuuza na kununua bidhaa kwaupendeleo kutoka nchi 55 za Afrika zenye soko lenye watubilioni 1.2.

143. Mheshimiwa Spika, Wizara imeshirikikatika mkutano wa majadiliano ya biashara ya hudumakatika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya MaendeleoKusini mwa Afrika. Lengo la ushiriki huo ni nchi wanachamakufunguliana masoko ya biashara ya sekta za kipaumbeleza huduma kwa kuondoa vikwazo vya kisera, kisheria, kanunina taratibu mbalimbali. Kwa upande wa Jumuiya ya AfrikaMashariki, nchi wanachama zinatumia mfumo maalumkwa ajili ya kuhimiza mashirikiano ya kuondoa vikwazovinavyoathiri biashara ya huduma miongoni mwao. Aidha,kwa upande wa SADC, nchi wanachama wamekubalianakuendelea kukamilisha majadiliano ya kufungulianamilango katika baadhi ya sekta zikiwemo usafirishaji, utalii,fedha, mawasiliano, ujenzi na nishati. Majadiliano hayoyatakapokamilika yatasaidia wazalishaji, wafanyabiasharana watoa huduma wa Tanzania kushiriki kikamilifu katikakutumia fursa za utoaji huduma zinazopatikana katikaJumuiya hizo.

144. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki Mkutano wakikosi kazi cha kikanda cha mapitio ya ushuru wa forodhawa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Common External Tariff-CET review) uliofanyika mjini Kampala, Uganda kuanziatarehe 20 hadi 23 Machi, 2018. Lengo la mkutano huo lilikuwani kujadili na kukubaliana makundi ya viwango vipya vyapamoja vya kodi (tariff bands) vitakavyotumika katikaJumuiya ya Afrika Mashariki. Hata hivyo, Mkutano huohaukuweza kukubaliana kuhusu makundi mapya ya viwangovya pamoja vya kodi. Imekubalika kuwa suala hilo lisogezwembele ili kutoa muda zaidi kwa kila nchi mwanachamakujitathmini.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

iii) Majadiliano ya Biashara za Kimataifa

145. Mheshimiwa Spika, katika kuendelezamajadiliano ya biashara ya kimataifa (Multi lateralnegotiations) kwa ajili ya kupanua fursa za masoko nabiashara, Wizara ilishiriki katika Mkutano wa Kumi na Mojawa Mawaziri wa Biashara wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO11th Ministerial Conference-MC11) uliofanyika mjini BuenosAires, Argentina tarehe 10 hadi 13 Desemba, 2017. Baadhi yamafanikio ya mkutano huo ni kukubaliana kuendelea na kaziya kuandaa mkataba (legal text) wa uondoaji wa ruzukukwenye Sekta ya Uvuvi; kuongeza muda (moratorium) wamiaka miwili kwa ajili ya kukamilisha mkataba wa kusimamiabiashara kwa njia ya mtandao (e-commerce) hususankwenye utozaji kodi kwenye miamala ya kibiasharainayofanyika kwa njia ya mtandao; kuongeza muda wamiaka miwili (2) kwa ajili ya kukamilisha makubaliano yakimkataba yanayozifunga nchi changa ikiwemo Tanzaniakwenye suala la Haki Miliki na Ubunifu (Trade RelatedIntellectual Property Rights-TRIPS); na Sudani ya Kusinikukubaliwa fursa ya observer status wakati mchakato wakuwa mwanachama kamili ukiendelea.

146. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudiza usimamizi na ujenzi wa uwezo katika masuala ya viwangovya bidhaa, na kwa kuzingatia matakwa ya mkatabawa WTO wa masuala ya SPS, Wizara imeunda Kamati yaKitaifa ya Kuratibu Masuala ya Afya ya Binadamu, Wanyamana Mimea. Kamati hiyo inayojumuisha wajumbe wapatao36 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ina jukumu la kusimamiana kushauri Serikali kuhusu masuala ya SPS. Aidha, Wizara kwakushirikiana na wataalam kutoka Umoja wa Afrika (AfricanUnion Inter-Bureau for Animal Resources AU-IBAR) iliendeshamafunzo ya siku tatu jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 23hadi 25 Oktoba, 2017. Mafunzo hayo yalilenga kujenga uwezona uelewa wa Kamati ili kusimamia ipasavyo masuala yaSPS nchini.

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

147. Mheshimiwa Spika, Wizara ina wajibu, kamanchi mwanachama wa WTO, kuweka wazi sera, sheria,mikakati na kanuni zinazolenga kusimamia biashara ilikufanya soko letu kuwa lenye kutabirika. Katika kipindi chamwaka 2017/2018, Wizara imewasilisha taarifa za viwangovipya 28 vya ubora (notifications of technical standards)kwenye Shirika la Biashara la Dunia (WTO) kwa bidhaa zamayai, nyama, nafaka, vileo, karatasi, vifaa vya huduma yakwanza, nyaya za umeme, vifaa vya usafi na matairi yamagari kwa ajili ya maoni ya wajumbe wa WTO kabla yakuanza kwa matumizi.

148. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu kikao chatatu cha Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Biasharakilichofanyika tarehe 16-19 Januari, 2018 Jijini Dar es Salaamkwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake. Kamati hiyo yenyewajumbe 53 kutoka sekta za umma na binafsi za TanzaniaBara na Zanzibar. Kikao kilipitia na kupitisha maeneo muhimuya utekelezaji wa Mkataba wa Uwezeshaji Biashara (TradeFacilitation Agreement - TFA). Maeneo hayo yaliwasilishwakatika Shirika la WTO mwezi Machi 2018. Pia, kikao kilijadilimapendekezo ya miradi inayotarajiwa kutekelezwa nchini ilikukidhi matakwa ya TFA. Wadau mbalimbali wa maendeleowamejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kusaidia Tanzaniakatika kutekeleza mkataba huo.

c) Kuratibu zoezi la kuridhiwa kwa Mkataba waShirika la Biashara la Dunia (WTO) wa Uwezeshaji waBiashara (Trade Facilitation Agreement-TF)

149. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuboreshamazingira ya ufanyaji biashara nchini, Wizara imekamilishakuandaa na kuwasilisha Serikalini rasimu ya Waraka kwa ajiliya kuishauri Serikali kuridhia Mkataba wa WTO wa Uwezeshajiwa Biashara. Ni matarajio yetu kuwa mara baada ya Serikalikujiridhisha, mapendekezo kuhusu uridhiwaji wa Mkataba huowa uwezeshaji biashara utawasilishwa katika Bunge lakoTukufu kwa ajili ya kufanya maamuzi. Licha ya kwambaTanzania haijaridhia, Mkataba huo umeanza kufanya kazi

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

rasmi tarehe 22 Februari, 2017 baada ya theluthi mbili ya nchiwanachama wa WTO kuridhia mkataba huo.

d) Kufanya Mapitio ya Sera za Biashara kwa Nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki chini ya Shirika la Biashara laDunia

150. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki kwenye kikaocha Jumuiya ya Afrika Mashariki kama sehemu ya maandaliziya mapitio ya sera za biashara kwa nchi za Jumuiya hiyo.Warsha ya kikanda ilifanyika tarehe 30 Oktoba hadi 3Novemba, 2017 mjini Arusha na iliandaliwa kwa ushirikianowa Sekretariati ya WTO na Sekretariati ya EAC. Kikao hichokililenga kufanya majumuisho ya taarifa zilizokusanywa nakila nchi mwanachama kwa ajili ya kukamilisha zoezi lamapitio ya sera za biashara kwa nchi husika. Taarifa hizozinatarajiwa kutumika katika mapitio ya sera za biashara zanchi wanachama wa EAC chini ya WTO ambayoyamepangwa kufanyika Novemba, 2018. Aidha, Wizara kwakushirikiana na wadau wa Sekta za Umma na Binafsi kutokaTanzania Bara na Zanzibar waliweza kukusanya majibukwenye masuala yaliyoulizwa na WTO kwa kutegemea halina mazingira ya nchi wanachama. Hatua inayofuata ni WTOkufanyia kazi taarifa hizo na kufanya vikao vingine na wadaukuanzia mwezi Mei 2018. Zoezi hilo la mapitio ya sera zabiashara linalenga kujenga uelewa zaidi kwa nchi nyinginewanachama wa WTO kuhusu soko na namna ya ufanyaji wabiashara nchini Tanzania. Kwa upande wa Tanzania, zoezihilo linalofanywa na WTO kila baada ya miaka minne (4)linatusaidia kujitathmini na kujipanga vema zaidi katikakuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na namnatunavyokidhi matakwa ya uanachama wetu katika Shirikala Biashara la Dunia.

3.3.5 Sekta ya Masokoa) Mwenendo wa Biashara ya Ndani

151. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakukusanya na kusambaza taarifa za mwenendo wa bei yamazao na ule wa mifugo pamoja na bidhaa za mifugo

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

(Livestock Information Network and Knowledge System -LINKS) kwa lengo la kuongeza uwazi na ushindani wa hakikatika biashara nchini. Aidha, taarifa za baadhi ya bidhaaza viwandani hususan vifaa vya ujenzi (nondo, mabati nasaruji) na sukari zimeendelea kukusanywa.

152. Mheshimiwa Spika, taarifa hizo zamasoko husambazwa kwa wadau kwa njia ya radio zakijamii, ujumbe wa simu za kiganjani, barua pepe, tovuti namagazeti. Taarifa zinazokusanywa ni bei za jumla za mazaomakuu ya chakula kutoka katika masoko 26 ya miji ya mikoa.Pia bei za rejareja kwa bidhaa zote muhimu kutoka masoko114 yaliyo katika Halmashauri zote nchini hukusanywa. Aidha,Wizara imeendelea kukusanya taarifa za mwenendo wa beiza mifugo (ng’ombe, mbuzi na kondoo) kutoka katikaminada 58 nchini. Taarifa zinazokusanywa zinahusu idadi yamifugo iliyouzwa kwa kila mnada, bei za wastani kwamadaraja kwa dume, na wastani kwa madaraja kwa jike.Taarifa hizo zimeongeza uwazi katika biashara na hivyokuwasaidia wafugaji kupata bei nzuri ya mifugo yaowanapopeleka katika minada.

153. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,bei ya mazao makuu ya chakula hususan mahindi, maharagena mchele zimeshuka na baadhi yake kupanda kwaviwango tofauti ikilinganishwa na msimu wa 2016/2017. Kwamfano, wastani wa bei ya jumla ya mahindi kwa gunia lakilo 100 ilipungua kutoka Shilingi 98,077 msimu wa 2016/2017 hadi kufikia Shilingi 49,386 msimu wa 2017/2018, sawana upungufu wa asilimia 49.65. Bei ya jumla ya maharagekwa gunia la kilo 100 ilishuka kutoka Shilingi 178,070 mwaka2016/2017 hadi kufikia Shilingi 169,771 mwaka 2017/2018,sawa na upungufu wa asilimia 4.66. Kushuka kwa bei zamahindi na maharage kumechangiwa na kuongezeka kwaugavi kulikotokana na hali ya hewa nzuri iliyosababishauzalishaji mzuri wa mazao hayo msimu wa 2017/2018. Aidha,bei ya jumla ya mchele kwa gunia la kilo 100 iliongezekakutoka wastani wa Shilingi 174,316 msimu wa 2016/2017 hadiShilingi 195,201 msimu wa 2017/2018 sawa na ongezeko laasilimia 11.98 (Kiambatisho Na.20). Ongezeko hilo la bei ya

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

mchele linatokana na ongezeko la mahitaji kwa zao hiloikilinganishwa na uzalishaji wake.

154. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,bei ya jumla ya ng’ombe wa daraja la pili iliongezeka kutokawastani wa Shilingi 1,074,431 mwaka 2017 hadi Shilingi1,080,975 mwezi Februari 2018, sawa na ongezeko la asilimia0.6. Bei ya ng’ombe wa daraja la tatu (3) iliongezeka kutokaShilingi 806,490 mwaka 2017 hadi Shilingi 823,978 mweziFebruari 2018, sawa na ongezeko la asilimia 2.2 (KiambatishoNa. 21). Katika mwaka 2018, ugavi wa mifugo iliyopelekwakatika minada umepungua ukilinganishwa na mwaka 2017.Hali hiyo imesababisha bei ya ng’ombe karibu kwamadaraja yote (isipokuwa madume daraja la II) kupanda.Kupungua kwa ugavi kumesababishwa na hali nzuri yamalisho ambayo imefanya wafugaji wengi kubaki na mifugoyao badala ya kuiuza. Aidha, malisho mazuri yamechangiakatika kuongeza ubora na bei ya ng’ombe katika minada.

b) Kuondoa Tozo zenye Kero, Ada Zinazojirudiana Kurazinisha Majukumu ya Taasisi za Udhibiti

155. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaaandiko maalum la Mpango wa Kuboresha Mfumo waUdhibiti wa Biashara Nchini linaloitwa Blue Print for RegulatoryReforms to Improve the Business Enviroment for Tanzania.Andiko hilo limeainisha sheria, kanuni na taratibu mbalimbalizinazojirudia au kukinzana na hivyo kuongeza gharama zakufanya biashara nchini. Andiko hilo liko katika hatua yamaamuzi Serikalini na mapendekezo yake yataanzakutekelezwa mwaka 2018/2019.

156. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini kupitia taasisihusika chini ya Wizara ambazo ni BRELA, FCC, TBS, TIC naWMA kwa kuongeza muda wa kufanya kazi hadi saa 24, siku7 kwa wiki. Vilevile, taasisi hizo zimeendelea kutoa elimu kwaumma na kufanya vikao vya mara kwa mara na wadau ilikujadili utekelezaji wa majukumu yao.

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

c) Kuhamasisha Mamlaka za Serikali za MitaaKuanzisha Vituo Maalum vya Kuuzia Mazao

157. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Bodi yaUsimamizi Stakabadhi za Ghala na Halmashauri zamaeneo yanayotekeleza Mfumo stakabadhi katika mwaka2017/2018, imefikia makubaliano ya kuanzisha matumizi yavituo maalum vya kuuzia mazao. Vituo hivyo vina lengo lakuwasaidia wakulima kudhibiti ubora wa mazao yao, kupatataarifa za masoko na kuimarisha ushindani wa bei.

d) Kuhamasisha Ushindani Katika Ununuzi naUuzaji wa Mazao

158. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuhamasisha ushindani kwa kutumia Mfumo wa Stakabadhiza Ghala ambao umefanikisha uuzaji wa mazao kwauwazi na hivyo kumpatia mkulima bei shindani. Kwa mfano,Mfumo umewezesha bei ya korosho kupanda na kufikiawastani wa Shilingi 3,880 kwa kilo msimu wa 2017/2018ikilinganishwa na Shilingi 3,346 kwa kilo msimu wa 2016/2017.Aidha, mauzo ya korosho kupitia Mfumo huo yameongezekakutoka tani 249,912 msimu wa 2016/2017 hadi tani 291,614msimu wa 2017/2018 sawa na ongezeko la asilimia 16.7.

e) Kusimamia na Kuhimiza Matumizi ya VipimoRasmi

159. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuhimiza matumizi ya vipimo rasmi katika biashara ikiwemokwenye vituo vya kuuzia mazao vilivyopo katika Halmashaurimbalimbali nchini. Aidha, Wizara inaendelea kushirikiana naOfisi ya Rais – TAMISEMI kuanzisha na kusimamia vituo vyakuuzia na kununulia mazao katika kila Mamlaka ya Serikaliza Mitaa. Vile vile, Wizara kwa kushirikiana na OR- TAMISEMIipo katika hatua za maandalizi ya Sheria Ndogo yakusimamia matumizi ya vipimo rasmi katika biasharakwa lengo la kumlinda mlaji.

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

f ) Kuimarisha Biashara na Masoko ya Mipakani

160. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango katikakuboresha utendaji wa Vituo vya Pamoja Mipakani (OSBP).Hadi sasa, vituo vimejengwa katika mipaka ya Holili/Taveta,Sirari/Isebania, Namanga/Namanga, Kabanga/Kobero,Rusumo/Rusumo, Mutukula/Mutukula na Horohoro/Lungalunga. Aidha, ujenzi wa Kituo cha Pamoja Mpakanicha Tunduma/Nakonde upande wa Tanzania ulioanza mweziNovemba 2016, unatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2018. Hadikufikia mwezi Februari 2018 ujenzi wa kituo hicho umefikiaasilimia 75.

g) Kutoa Elimu kwa Jamii ya WafanyabiasharaKuhusu Fursa na Taratibu za Kufanya Biashara ya Mipakani(Cross Border Trade)

161. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naTanTrade, BRELA, WMA, SIDO, na OR - TAMISEMI imetoamafunzo katika mikoa ya Kagera, Mara na Mbeya yaliyolengakuhamasisha uanzishwaji wa vikundi na kuvisajili kwa ajili yakurasimisha biashara mipakani. Mafunzo yaliyotolewa yalihusuujasiriamali na vipimo, urasimishaji wa biashara na umuhimuwa wafanyabiashara kuungana katika vikundi. Mafunzohayo yalifanyika kati ya mwezi Septemba na Disemba 2017.Jumla ya vikundi 44 vilianzishwa na kusajiliwa rasmi katikamikoa hiyo. Kazi hiyo itaendelezwa katika mikoa mingine yamipakani.

h) Kuhamasisha na Kuwezesha WananchiKutangaza Bidhaa na Huduma za Tanzania

162. Mheshimiwa Spika, Wizara na Taasisi zake 14zilishiriki Maonesho ya Wakulima (Nane Nane) mweziAgosti 2017 mkoani Lindi kwa lengo la kuelimisha ummakuhusu kazi na huduma mbalimbali zinazotolewa naWizara na Taasisi zake. Aidha, kwa kutambua umuhimuwa wajasiriamali katika kutoa ajira, kuhamasisha viwandavidogo vidogo na kuongeza kipato, Wizara katika Maonesho

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

hayo ilidhamini vikundi 15 vya wajasiriamali. Wajasiliamalihao walikuwa ni wasindikaji wa mazao ya kilimo kutokamikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani ambaowalipata fursa ya kutangaza bidhaa zao na kujifunza kutokakwa washiriki wengine.

163. Mheshimiwa Spika, katika maonesho hayo,Wizara kupitia Bodi ya WRRB iliendesha mafunzo kuhusuMfumo wa Stakabadhi kwa wakulima wapatao 198 na kwaviongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Masoko(AMCOS) zipatazo 85 kutoka katika Mikoa mbalimbali nchini.Mafunzo hayo yalilenga kuhakikisha kuwa wakulimawanapata bei nzuri ya mazao kwa kuuza katika mfumorasmi; kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno;na kuwa na biashara ya mazao inayozingatia ubora navipimo sahihi.

i) Ushirikiano katika Masuala ya Biasharakati ya SMT na SMZ

164. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka 2017/2018, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji(SMT) na Wizara ya Viwanda na Biashara (SMZ) zimefanya vikaovya ushirikiano kujadili masuala ya kisekta ili kutafuta suluhuya changamoto mbalimbali za ushirikiano. Vikao hivyovil iwezesha kupatikana kwa ufumbuzi wa masualambalimbali. Hivi sasa taasisi za TBS na ZBS zinatekelezaMkataba wa Makubaliano ya kufanya kazi kwa pamojakatika kusimamia ubora wa bidhaa zinazozalishwa nakuuzwa katika pande zote mbili. Aidha, TFDA na ZFDAzinafanya kazi kwa pamoja katika uthibiti wa bidhaa zachakula na dawa ili kulinda afya ya mlaji.

j) Kuandaa na Kupitia Sera, Mikakati, Sheriana Kanuni Mbalimbali

i) Sera ya Taifa ya Kumlinda Mlaji

165. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Taifalinakuwa na mfumo mahiri wa kumtetea na kumlinda mlaji,

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Wizara imeanza maandalizi ya kuandaa Sera ya Taifa yaKumlinda Mlaji. Mwezi Septemba 2017, wataalam walikutanana kuandaa mpango kazi wa kutekeleza kazi hiyo. Aidha,katika hatua za kutekeleza mpango kazi huo mwezi Februari2018, timu imeanza kukusanya taarifa mbalimbalizitakazosaidia katika kuandika Sera ya Taifa ya Kumlinda Mlajina Mkakati wake.

ii) Sera ya Taifa ya Viwango

166. Mheshimiwa Spika, bidhaa za wazalishaji wenginchini zimekuwa zikikutana na vikwazo na hivyo kushindwakukidhi matakwa ya soko la ndani na nje ya nchi. Katikajitihada za kukabiliana na changamoto hizo, Wizara kupitiaTBS kwa kushirikiana na wadau wengine, imeanza maandaliziya Sera ya Taifa ya Ubora na Mkakati wake. Kukamilika kwaSera hiyo itasaidia kutoa mwongozo wa usimamizi wa uborana viwango vya bidhaa na huduma zinazotolewa kwawalaji. Vivyo hivyo, Sera hiyo itasaidia kuandaa mkakati namipango mbalimbali ya mafunzo juu ya ubora kwawazalishaji wadogo na wa kati. Katika kufanikisha jukumuhilo, Wizara imeunda kikosi kazi cha kuandaa rasimu ya Seraya Taifa ya Ubora ambacho kimekusanya maoniyatakatotumika katika kuandaa Rasimu ya Sera hiyo.

iii) Sera na Mkakati wa Miliki Bunifu

167. Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisharasimu ya Sera na Mkakati wa Miliki Bunifu na hivi sasa ikokatika hatua za kujumuisha maboresho zaidi kufuatia maoniyaliyowasilishwa kutoka kwa wadau.

iv) Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009

168. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekusanyamaoni ya wadau kuwezesha marekebisho ya Sheria yaViwango Na. 2 ya mwaka 2009. Hivi sasa, Wizara inafanyauchambuzi wa maoni hayo ili kukamilisha mapendekezo yaSheria hiyo kwa kushirikisha taasisi husika.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

v) Sheria ya Haki Miliki na Haki Shiriki ya Mwaka1999

169. Mheshimiwa Spika, katika kuiwezesha COSOTAkutekeleza majukumu yake wakati ikisubiri marekebisho yaSheria mama, Wizara imeandaa MiscellaneousAmmendments katika baadhi ya vifungu vitakavyorahisishautendaji wa Taasisi hiyo katika kipindi cha mpito. Aidha,Wizara kupitia COSOTA na kwa kushirikiana na Rulu ArtsPromoters kwa ufadhili wa Best AC ilikusanya maoni kutokakwa wadau mbalimbali na kuandaa mapendekezo yamarekebisho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na. 7/1999.Mapendekezo hayo yapo katika hatua ya maamuzi.

vi) Kanuni za Sheria ya Vipimo ya Mwaka 2016

170. Mheshimiwa Spika katika mwaka 2017/2018,Wizara iliunda timu ya wataalam kutoka Wizarani, Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakala wa Vipimo ilikupitia Kanuni za jumla za Vipimo (Weight & Measure GeneralRegulation) za mwaka 2016. Lengo ni kuhakikisha kuwaKanuni za Vipimo zinazingatia marekebisho ya Sheriambalimbali yaliyofanyika na kugusa Sheria ya Vipimo.Marekebisho hayo yanalenga kuipa uzito Sheria hiyo kwakuongeza adhabu ili iweze kuendana na wakati na uzito wamakosa husika. Pia iliangalia dosari nyingine za kisheria ilikuongeza ufanisi wa Wakala wa Vipimo.

vii)Kuandaa Sheria Ndogo ya Kusimamia Matumizi yaVipimo Rasmi katika Biashara Ngazi ya Vijiji, Vitongoji naWilaya

171. Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa kikao chawataalam kutoka Wizarani, Wakala wa Vipimo, TAMISEMI naOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kitakachofanyikamwezi Mei 2018, ili kuandaa rasimu ya sheria ndogo kufuatiamarekebisho yaliyofanywa katika Sheria ya Vipimo ya mwaka2016. Lengo la sheria hizo ndogo ni kuimarisha usimamizi wavipimo sahihi ili kumlinda mlaji. Aidha, baada ya kukamilisha

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

rasimu na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza,vitafanyika vikao vya wadau kujadili rasimu ya Sheria hizondogo.

k) Kuelimisha Umma kuhusu Masuala yaKibiashara

172. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya mikutano yakazi kwa njia ya mtandao (Video Conference) na Sekretarietiza Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa tarehe 18 hadi 20Desemba, 2017. Mikutano hiyo iliandaliwa ili kuwafikia kwapamoja na kwa gharama nafuu wadau muhimu wa ujenziwa uchumi wa viwanda nchini wakiwemo Makatibu Tawalawa Mikoa na Wilaya na Maafisa Biashara. Nia ya mikutanohiyo ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa serana mikakati ya Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.Mikoa 19 ya Tanzania Bara kati ya Mikoa 25 ilifikiwa. Jumla yawadau 530 walishiriki kwa mchanganuo ufuatao: Arusha (19),Dar es Salaam (19), Dodoma (18), Geita (6), Iringa (14), Kagera(31), Katavi (30), Kigoma(42), Kilimanjaro (64), Lindi (31),Manyara (29), Mbeya na Songwe (46), Morogoro (20), Mtwara(33), Mwanza (5), Pwani (15), Singida (58), Tabora (34) na Tanga(16).

3.3.6 Huduma za Sheria

173. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Wizara imesimamia na kufuatilia mashauri ambayo Wizarana Taasisi zake zimeshitaki au kushitakiwa kwa kushirikianana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia imesimamiamarekebisho ya Sheria na Kanuni za Wizara na Taasisizake ikiwemo; marekebisho ya Sheria ya Leseni Tanzania ilikuhamisha jukumu la utoaji leseni Daraja “A” kutoka Wizaranikwenda BRELA; na Kanuni za Wakala wa Vipimo kuhusu gesiasilia na umeme. Aidha, imesimamia Mikataba na Hati zaMaelewano (MoU) mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwakushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamojana Wizara na Taasisi husika.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

3.3.7 Teknolojia ya Habari na Mawasiliano174. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/

2018, Wizara imeendelea kusimamia matumizi bora na sahihiya miundombinu ya TEHAMA katika kutoa huduma kwawateja wa ndani na nje. Miundombinu ya TEHAMAimeboreshwa na mafunzo mbalimbali yametolewa kwawatumishi kuhusu matumizi bora na sahihi ya miundombinuna rasilimali za TEHAMA. Aidha, Tovuti ya Wizara imehuishwaili kuwapatia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati nakuwawezesha kutoa na kupata mrejesho wa maoni aumalalamiko juu ya huduma zinazotolewa na Wizara.Maboresho hayo yamehusisha uzinduzi wa barua pepemahususi kwa ajili ya kuwapatia msaada wananchi/wawekezaji juu ya masuala yote yanayohusiana na Wizara,ambayo ni: dawatilamsaaada@ mit.go.tz [email protected] .

3.3.8 Mawasiliano Serikalini

175. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018,Wizara iliendelea kuelimisha umma kuhusu majukumu na kazizinazofanywa na Wizara. Aidha, Wizara iliweza kutoa taarifambalimbali za kisekta kwa wadau ikiwemo fursa mbalimbalizinazojitokeza ili wananchi waweze kuzichangamkia.

3.3.9 Udhibiti wa Matumizi176. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,

Wizara imeendelea kutekeleza majukumu yake kulinganana sheria, miongozo na kanuni zilizowekwa na kuwezeshakupata hati safi ya hesabu za mwaka 2016/2017. Pia, Wizarail iendesha mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi (riskmanagement) kwa watumishi wake pamoja na kuanzishadaftari la kusajili vihatarishi (risk Register) na hivyo kuwezakupanga mipango yake kwa kuzingatia maeneo yenyevihatarishi. Aidha, Wizara imefanikisha kuhakiki na kutoaushauri katika taasisi zilizoko chini yake zikiwemo SIDO, FCTna WRRB na kuziwezesha kutekeleza majukumu yaokulingana na taratibu, kanuni na miongozo waliyojiwekeana hivyo kuweza kupata hati safi za ukaguzi.

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

3.3.10 Usimamizi wa Ununuzi177. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea

kusimamia shughuli mbalimbali za ununuzi kwa kuzingatiaSheria ya Ununuzi Na.7 ya mwaka 2011(il iyofanyiwamarekebisho mwaka 2016) na kanuni zake za mwaka 2013,GN 446. Katika mwaka 2017/2018, Wizara iliandaa Mpangowa Ununuzi na kusimamia utekelezaji wake. Pia iliandaataarifa za ununuzi za kila mwezi na kila robo ya mwaka nakuwasilishwa kwa Taasisi ya kudhibiti Ununuzi wa Umma(PPRA). Aidha, Wizara ilihakiki mali zake na kufanikishauhuishaji wa daftari la Mali za Wizara kwa mujibu wa Sheriaya Fedha Na. 6 ya Mwaka 2001 na Kanuni zake, GN.132iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004.

3.3.11 Maendeleo ya Rasilimali Watu na Utoaji waHuduma

a) Ajira za Watumishi

18. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ikamailiyoidhinishwa mwaka 2017/2018, Wizara inapaswa kuwa nawatumishi 249. Hadi kufikia Machi 2018, Wizara ina Watumishi233, kati ya hao Viongozi ni 5, Wachumi 49, Watakwimu 14,Wahandisi 4, Maafisa Tawala 6, Maafisa Utumishi 3, MaafisaSheria 4, Maafisa TEHAMA 6, Maafisa Ugavi 6, Maafisa Biashara67, Maafisa Habari 2, Wakaguzi wa Ndani 5, Wahasibu 15,Wasaidizi wa Maktaba 2, Wasaidizi wa Kumbukumbu 11,Fundi Sanifu 2, Makatibu Mahsusi 17, Wasaidizi wa Ofisi 5,Opereta wa Kompyuta 1 pamoja na Madereva 9.

179. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018,Wizara imeajiri madereva 2, Katibu Mahsusi 2, Afisa TEHAMA 1na Opereta wa Kompyuta 1 na kuwapandisha vyeowatumishi 16 ambao tayari walikuwa wamekasimiwa kwamwaka 2016/2017. Aidha, zoezi la upandishaji vyeolimefanyika baada ya Serikali kuruhusu utekelezaji wa utoajiajira mpya, ajira mbadala pamoja na masuala yoteyanayohusisha marekebisho ya mishahara yanayotokana naupandishwaji vyeo kwa watumishi.

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

b) Mafunzo

180. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018,Wizara iliandaa Mpango wa Mafunzo wa muda wa mwakammoja ili kuwajengea watumishi uwezo na kuongezaufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Mpango huoulilenga kuwapeleka watumishi 15 katika mafunzo ya mudamrefu na watumishi 50 katika mafunzo ya muda mfupi. Hadikufikia Aprili 2018, Wizara imepeleka watumishi 14 katikamafunzo ya muda mrefu na watumishi 16 katika mafunzo yamuda mfupi, ndani na nje ya nchi.

c) Upimaji wa Utendaji Kazi wa Watumishi

181. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,watumishi 222 kati ya 241 wamesaini mikataba yao yakazi kwa wakati na kufanya mapitio ya nusu mwaka mweziDesemba 2017. Watumishi 14 hawakuweza kusaini mikatabayao kwa kuwa wapo masomoni. Aidha, kufikia mwisho wamwezi Juni 2018 kila mtumishi wizarani atafanyiwa tathminiya utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha mwaka mzimakwa kutumia utaratibu wa MWAMTUKA.

d) Michezo na Afya za Watumishi182. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018

katika kutekeleza dhana ya michezo kwa afya, furaha naufanisi kazini, Wizara imeshiriki katika bonanza lililohusishawashiriki kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi. Lengola kushiriki michezo hiyo ilikuwa ni kujenga afya za watumishikupitia mazoezi na michezo na kujenga uhusiano mzurimiongoni mwa watumishi na wadau wa sekta binafsi. Aidha,Wizara imeendelea kuwahimiza watumishi kujenga tabia yakufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kujikinga naMagonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) yanayowezakuepukika kama vile, uzito uliopitiliza, shinikizo la damu nakisukari.

e) Baraza la Wafanyakazi183. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018,

Wizara imeendelea kuwashirikisha watumishi katika vikao

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

vya maamuzi kupitia Baraza la Wafanyakazi ili wawezekutetea maslahi yao na kuwasilisha mawazo yao. Wizaraimefanya kikao kimoja cha Baraza la Wafanyakazi tarehe 6April i, 2018 ambapo li l ipitia, kushauri na kuridhiamapendekezo ya Mipango na Bajeti ya Wizara kwamwaka 2018/2019 na kupokea hoja za watumishi nakuzifanyia maazimio ya utekelezaji.

f) Kuhamia Makao Makuu Dodoma

184. Mheshimiwa Spika, kufuatia agizo la Serikali lakuhamishia shughuli zake Makao Makuu ya Nchi Dodoma,Wizara ilipanga kuhamisha watumishi katika awamu tatu.Awamu ya kwanza ilipanga kuhamisha Watumishi 94, awamuya pili 69, na awamu ya tatu 70. Aidha, kila awamu inahusishakuhamisha vifaa na mifumo ya utendaji ikiwemo Mifumo yaMitandao ya Kompyuta. Hadi kufikia mwezi Aprili 2017,Wizara imewahamisha watumishi 163. Wizara inatarajiakuwahamisha watumishi 70 waliosalia ifikapo mwezi Agosti2018.

3.3.12 Masuala Mtambuka

a) Kupambana na Rushwa185. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018,

Wizara imeendeleza jitihada za mapambano na udhibiti warushwa kwa kuwaelimisha na kutoa maelekezo kwawatumishi wake kutoa huduma bora kwa wateja wa ndanina nje bila kupokea rushwa. Aidha, wizara imeongezamsisitizo kwa watumishi kuunga mkono jit ihada zaMheshimiwa Rais za kupinga vitendo vya rushwa kwakutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibuza utumishi wa umma.

186. Mheshimiwa Spika, Wizara iliitisha kikao chawadau wa ndani tarehe 28 Septemba, 2017 kwa ajili yakupokea maoni na maandalizi ya Mpango Mkakati waWizara katika kupambana na kuzuia rushwa. Aidha, Wizarailifanya kikao tarehe 28 na 29 Novemba, 2017 ili kuandaampango kazi wa kutekeleza Mkakati wa Taifa Awamu ya

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

Tatu wa Kupambana na Kuzuia Rushwa. Mpango kazi huoumekamilika.

b) Usimamizi wa Mazingira

187. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka 2017/2018, Wizara imeshiriki katika shughulimbalimbali za utunzaji mazingira na kuzuia uchafuzi wamazingira kutokana na shughuli za viwanda hasa viwandavya saruji na chuma. Aidha, Wizara imeshiriki katika tathminiya athari za mazingira kwa viwanda vipya vinavyoanzishwanchini kwa kushirikiana na NEMC.

c) Mapambano ya UKIMWI

188. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka 2017/2018, Wizara imeendelea kuwahudumiawatumishi watatu (3) wenye maambukizi ya VVU nawaliojitokeza kwa kuwapa posho ya lishe, usafiri navirutubisho ili kuwaweka katika hali ya afya bora na kudumuzaidi kwenye utumishi wa umma. Aidha, kupitia michezoWizara imetoa fursa kwa watumishi wake wote kuimarishaafya zao kwa njia ya kufanya mazoezi na pia kutoa ujumbewa umuhimu wa mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) na magonjwa sugu yasiyoambukiza.

d) Masuala ya Jinsia

189. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/2018,Wizara ilishiriki warsha ya mapitio ya utekelezaji wa sheria yauondoaji wa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushurupamoja na kutoa maoni katika sheria hiyo ambayo ipokatika rasimu ya awali. Warsha hiyo iliandaliwa na TGNPmtandao kupitia Mfuko wa AWDF kwa kushirikiana na Kamatiya Kitaifa ya Usimamiaji na Uondoaji Vikwazo vya BiasharaVisivyokuwa vya Kiushuru tarehe 8-9 Februari, 2018 Dar esSalaam. Lengo la warsha li l ikuwa kuhakikisha sheriazinazoandaliwa zinajumuisha masuala ya jinsia na urahisishajibiashara ndani na nje ya nchi.

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

190. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki mkutanowa kikanda uliofanyika nchini Uganda tarehe 24 Januari,2018. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni ushirikishwaji wawanawake wafanyabiashara mipakani katika uandaaji wasera mbalimbali za masuala ya biashara. Aidha, Wizara ilishirikikwenye kikao tarehe 23 Februari, 2018 cha uandaaji wataarifa ya utekelezaji wa Itifaki ya Maendeleo ya Jinsia yamwaka 2008 na kutoa mchango wake katika kipengele cha17 (Economic Empowerment) na 18 (Access to property andresources) cha Itifaki hiyo.

191. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki mafunzoya kuzingatia masuala ya kijinsia katika biashara za mipakanikuanzia tarehe 6-7 Februari, 2018. Mafunzo hayo yalilengakuwajengea uwezo washiriki namna ya kuwasaidiawanawake wafanyabiashara mipakani kufanya biashara zaokwa ufanisi na kufuata utaratibu wa biashara. Mafunzo hayoyaliandaliwa na TGNP Mtandao kupitia Mfuko wa Maendeleowa Wanawake wa Afrika (AWDF).

192. Mheshimiwa Spika, Wizara imeshiriki katikakuandaa Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mpango Kaziwa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake naWatoto (NPA- VAWC 2017/2018 – 2021/2022) uliofanyikatarehe 16-17 Februari, 2018. Mpango huo utasaidia ufuatiliajiwa matokeo ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake nawatoto kwa kupata taarifa za kimkakati zitakazotumikakatika kufanya uamuzi kuanzia ngazi ya Taifa. Aidha, viashiriavimeandaliwa katika kila eneo la utekelezaji na baselinesurvey inatarajiwa kufanyika ili kukusanya takwimu ambazozinakosekana kwenye baadhi ya viashiria.

3.4 UTEKELEZAJI WA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA

3.4.1 Shirika la Maendeleo la Taifa

a) Kuanzisha Mgodi wa Mawe wa Kuzalisha Kokoto193. Mheshimiwa Spika, Shirika la Maendeleo la Taifa

(NDC) kwa kushirikiana na TRC inafanya juhudi za kumpatamwekezaji katika mradi wa mgodi wa mawe katika Kijiji cha

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

Muhamba, Wilaya ya Muheza ambapo kampuni kadhaazimeonesha nia ya kuwekeza. Aidha, NDC na TRCzimeendelea kuhakikisha kwamba leseni za kumiliki eneo laMgodi wa Mawe lililoko katika Halmashauri ya Wilaya yaMuheza zinalipiwa wakati taratibu za kupata Hati ya Umilikizinaendelea. Vilevile, NDC na TRC kwa kushirikiana nauongozi wa kijiji cha Muhamba zinaendelea kuhifadhi eneola mgodi ili lisivamiwe.

194. Mheshimiwa Spika, Majukumu mengineyaliyotekelezwa na taasisi hii yameanishwa katika utekelezajiwa miradi mama na ya kielelezo chini ya utekelezaji wa Sektaya Viwanda.

3.4.2 Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji waBidhaa kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi

a) Kuendeleza Eneo Maalum la Uwekezaji laKurasini

195. Mheshimiwa Spika, katika eneo la Kurasini TradeLogistic Centre hatua iliyofikiwa ni kuwa, Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekamilisha uthamini wanyumba tatu ambazo hazikuthaminiwa awali ambapoShilingi 441,295,000 zitahitajika kwa fidia hiyo. Malipo hayoyatafanyika mara baada ya kupokea fedha kutoka Serikalini.Kazi za upimaji wa maeneo imefanyika na ukamilishajiwa ramani ya mipango miji sambamba na taratibu zaupatikanaji wa hati ya eneo hilo uko hatua za mwisho. Aidha,timu ya wataalam ya kushauri njia bora za kutekeleza mradiimekamilisha kazi yake na imeshauri uendelezaji wa eneohilo kwa kuhusisha ujenzi wa viwanda (light industries)utakaoambatana na maghala ya kutunzia mizigo.

b) Uendelezaji wa Mradi wa Bagamoyo SEZ

196. Mheshimiwa Spika, majadiliano kuhusuuendelezaji wa Eneo la Uwekezaji la Bagamoyo (BagamoyoSEZ) linalohusu ujenzi wa bandari na eneo la viwanda(Portside Industrial Zone) yanaendelea. Majadiliano hayo

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

yanatumia andiko lililoandaliwa na wawekezaji (CMPort naSGRF) na kuridhiwa na Serikali mwezi Oktoba 2017 kama msingiwa majadiliano. Lengo la majadiliano hayo ni kupata namnanzuri zaidi ya kushirikiana katika kutekeleza mradi huo kwamanufaa ya pande zote (Serikali ya Tanzania na Wawekezaji).Makubaliano ya awali yamefikiwa na hatua inayofuatani majadiliano ya kina ya mikataba yanayotegemewakukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2018. Mbali nawawekezaji waliotajwa hapo juu, makampuni mengine12 yamepewa leseni kwa ajili ya kujenga viwanda katikaeneo la Bagamoyo SEZ lililokwisha lipiwa fidia nje ya eneolililotolewa kwa CMport na SGRF.

197. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya EPZ inashirikianana Serikali ya Korea Kusini kupitia programu ya KnowledgeSharing Program (KSP) na Korea Exim Bank kuendeleza kituocha teknolojia ya juu kitakachojengwa katika eneo la mradiwa Bagamoyo SEZ. Mshauri mwelekezi kutoka chuo chaScience and Technology Policy Institute (STEPI) amefanyasehemu ya kwanza ya Stadi ya mradi kwa lengo la kupatauelewa mpana wa mradi na kuishauri Mamlaka ya EPZkuhusu Masterplan ya Mradi iliyoandaliwa na Kampuni yaVoyant Solutions Pvt kutoka India. Aidha, STEPI kitaishauri KoreaExim Bank kuhusu gharama za ujenzi wa miundombinuwezeshi katika eneo la mradi. Benki hiyo imeonesha nia yakusaidia kiasi cha Shillingi Bilioni 40.

198. Mheshimiwa Spika; Mamlaka ya EPZinaendelea na maandalizi ya kutekeleza Makubaliano yaAwali (MoU) yaliyofikiwa baina yake na SNTL GROUP (SNTL) yaMorocco kuhusu uendelezaji wa maeneo ya maalum yauwekezaji. Makubaliano hayo yalifikiwa mwezi Oktoba,2016 wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Tanzania.Mamlaka ya EPZ inakamilisha Project Portfolio itakayokuwamsingi wa mazungumzo yatakayofikia hatua ya kuingiamkataba wa kushirikiana kuendeleza maeneo kadhaa yaSEZ kama Industrial Parks na Trade and Logistics Centre.

199. Mheshimiwa Spika, Mamlaka imefikia hatuanzuri katika kutekeleza Mpango wa Maboresho ya Kituo cha

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Huduma kwa Wawekezaji, One Stop Services Centre namifumo mbalimbali ya taasisi. Taasisi ya TradeMark East Afica(TMEA) imeidhinisha pendekezo la taasisi kuhusu msaada wakitaalam na fedha katika kuboresha mifumo mbalimbali yataasisi kwa kutumia TEHAMA. Pia, Mamlaka ya EPZinashirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) katikakuandaa Programu ya Usalama wa Maji (Water SecurityProgram) ambayo itawahakikishia wawekezaji uwepo wamaji muda wote na katika ubora unaokubalika kimataifa.Utekelezaji wa Programu hiyo unatarajiwa kuwavutiawawekezaji wengi katika maeneo ya EPZ na SEZ.

200. Mheshimiwa Spika; Mamlaka ya EPZimeendelea kuwashirikisha waandishi wa habari wa TV namagazeti katika kutembelea viwanda na maeneo maalumya uwekezaji ili kutangaza kwa usahihi shughuli za uwekezajizilizopo chini yake. Kupitia utaratibu huo, habari, vipindi namakala maalum zipatazo 42 zilitolewa kwa umma kupitiavyombo vya habari vya TBC1, ITV, Azam TV, Clouds TV, ChannelTen, Mwananchi, Citizen, The Guardian, Daily News na kwenyetovuti ya Idara ya Habari Maelezo. Vile vile, maafisawaandamizi wa EPZA wamekuwa wakishiriki mijadala katikavipindi vya televisheni na radio ili kuelezea dhana ya viwandana maeneo maalum ya uwekezaji. Juhudi hizo zitaendeleakadri miradi mipya itakapokuwa inaanzishwa ili kufikishaelimu na taarifa kwa umma kuhusu miradi hiyo na fursaambazo watanzania na wawekezaji kutoka nje ya nchiwataweza kunufaika nazo.

201. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha utoaji wataarifa sahihi kuhusu miradi, EPZA imekuwa ikifuatilia habariza kisekta na kitaasisi zinazotolewa na vyombo mbalimbali.Lengo ni kuitumia vizuri fursa ya uwepo wa waandishi ambaokwa juhudi zao wenyewe wamekuwa wakiandika habarimbalimbali kuhusu viwanda ama miradi iliyo chini yaMamlaka ya EPZ. Mbinu hiyo imewezesha kuchapishwa kwamakala maalum saba (7) kuhusu bidhaa na viwanda vilivyochini ya maeneo maalum ya uwekezaji. Pia, juhudi zakutangaza shughuli zote zilizo chini ya Mamlaka zimeendeleakutangazwa kupitia tovuti yake www.epza.go.tz ambayo

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

imekuwa msaada mkubwa kwa wawekezaji wa ndani nanje ya nchi

3.4.3 Shirika la Utafiti na Maendeleo ya ViwandaTanzania

a) Kutoa Huduma za Kitaalam Viwandani

202. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO)limeendelea kushirikiana na TIB Development Bank katika kazimbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa kiwanda cha bidhaaza pamba za mahospitali (Cotton based medical products)na kiwanda cha kuzalisha maji ya dripu za mahospitali(IV fluid Industry) katika Mkoa wa Simiyu. Miradi hiyo iko chiniya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwaWafanyakazi (WCF). Vilevile, Shirika limefanya kazi na Benkiya CRDB katika kutoa ushauri wa kitaalam na kiufundiinayohusu mikopo ya wanaoanzisha na kuendeleza viwandaikiwemo Kiwanda cha Mabomba kilichopo Vingunguti Dares Salaam, Kiwanda cha Nyama Sumbawanga, Kiwanda chaCeramics kilichopo Same na Kiwanda cha Kahama Oil Millskilichopo Shinyanga. Pia TIRDO ni mshauri kiongozi (leadconsultant) katika Mradi wa Kuboresha Kiwanda cha Viatucha Gereza la Karanga lililoko mjini Moshi Kilimanjaro.

203. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kufufuaviwanda vilivyoacha uzalishaji, Shirika limefanya ukaguziwa kitaalam (technical audit) katika Kiwanda cha SAAFI,Kiwanda cha Magunia cha Canvas Morogoro, na Kiwandacha Nguo Ibadakuli – Shinyanga na kushauri namna bora yaufufuaji wa viwanda hivyo. Pamoja na shughuli hizo, Shirikalimeendelea kutoa huduma za upimaji wa uharibifu wamazingira unaotokana na shughuli za uzalishaji viwandanina kutoa ushauri. Viwanda vilivyopatiwa huduma nipamoja na Tanzania Cigarette Company-Dar es salaam,Tanzania Tobacco Processors Ltd -Morogoro, Premium ActiveTanzania Ltd- Mbeya, na Tanga Cement Company - Tanga.Pia maabara imeendelea kutoa huduma za mazingira kwataasisi mbalimbali zikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya NdegeTanzania na Shirika la Viwango Tanzania.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

b) Kuanzisha na Kuhakiki Maabara ya Makaaya Mawe, Mafuta na Gesi

204. Mheshimiwa Spika, Shirika limeendeleakuimarisha maabara zake kwa kuhakiki maabara za makaaya mawe na uanzishwaji na uhakiki wa maabara ya mafutana gesi ili kufikia viwango vya kimataifa. Maabara ya makaaya mawe imekwishaanza kufanya kazi mbalimbali za upimajiwa ubora wa makaa ya mawe kwa wateja mbalimbalikama vile STAMICO, Magamba Coal Ltd, na Tancoal EnergyLtd. Hata hivyo, jitihada zinaendelea kufanyika ili maabarahiyo ipate vifaa vya kutosha ili kuweza kuhakiki na kukidhivigezo vya kimataifa. Aidha, jitihada zinaendelea kufanyikaza kuanzisha maabara ya mafuta na gesi.

c) Kuanzisha na Kuboresha Maabara205. Mheshimiwa Spika, katika maabara ya

mazingira, Shirika limewasilisha maombi ya usajili kwaMamlaka ya Uhakiki (SADCAS). Shirika linaendelea kutafutafedha kwa ajili ya upimaji stadi (proficiency testing). Kwaupande wa maabara ya vifaa vya kihandisi (NDT), Shirikalimeendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kununua vifaana kuendelea na uhakiki wa maabara hiyo. Aidha, Shirikalimeandaa na kuwasilisha kwa wafadhili mbalimbali andikokwa ajili ya kutafuta fedha za kuanzishia Maabara ya Vipimovya Chuma Kigumu (Iron and Steel).

3.4.4 Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijinia) Kujenga Uelewa na Kuhamasisha Jamii kuhusu

Umuhimu wa Kununua Zana za Kilimo zilizofanyiwa MajaribioNchini

206. Mheshimiwa Spika, Kituo cha Zana za Kilimo naTeknolojia Vijijini (CAMARTEC) kimeandaa Kanuni za Majaribioya Zana za Kilimo ambazo zimechapishwa kwenye Gazeti laSerikali Tarehe 23 Februari 2018. Kupitia vyombo mbalimbalivya habari vya Televisheni, Radio, Magazeti na Mikutano,Kituo kimewaelimisha wadau kuhusu umuhimu wa vifaa vyaokufanyiwa majaribio kabla ya kuviuza kwa wateja. Aidha,Kituo kimetenga bajeti kwa ajili ya kuanzisha vituo vyaukaguzi na majaribio katika maeneo muhimu na pia

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

kuwasaidia wazalishaji wa ndani kuzifanyia majaribio nakukagua zana za kilimo wanazozizalisha. Hatua hiyo nisehemu ya kufanikisha mpango wa kujenga uelewa nakuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kufanyia majaribiozana za kilimo.

b) Kutafiti Mahitaji, Kuendeleza na KutengenezaTeknolojia mbalimbali za Kilimo

207. Mheshimiwa Spika, CAMARTEC kwa kushirikianana Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), kimefanya utafitiwa mahitaji na hali ya matumizi ya teknolojia za kilimo katikamikoa 12 ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Dodoma,Iringa, Kil imanjaro, Lindi, Manyara, Mbeya, Njombe,Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora. Matokeo yanaoneshakuwa, asilimia kubwa ya wakulima katika mikoa hiyowanahitaji teknolojia za kupandia mazao mbalimbaliikifuatiwa na teknolojia za kupalilia, kupura na kupepetamazao ya nafaka. Vile vile imebainika kuwa, wakulima wengikatika maeneo yaliyofanyiwa utafiti bado wanatumiateknolojia duni kufanya shughuli za kilimo. Hali hiyo inatokanana ukosefu wa taarifa za uwepo wa teknolojia zinazowezakuwasaidia kurahisisha shughuli za kilimo, ugumu waupatikanaji wa teknolojia za kilimo katika maeneo yao napia uwezo mdogo wa kifedha wa kumudu kununuateknolojia hizo.

208. Mheshimiwa Spika, Kituo kimeendeleana ukamilishaji wa trekta 5 na uboreshaji wa trekta 4aina ya CFT 221 (CAMARTEFastrucktor-221). Maboreshoyanafanyika kwenye mfumo wa kuinua jembe, mfumo wakuongoza na kushikilia jembe lisiyumbe wakati wa kulima.Trekta tatu (3) kati ya nne (4) zimeboreshwa na kutumikakulima mashamba ya wakulima kwa majaribio katika eneola Lake Tatu, USARIVER katika Wilaya ya Arumeru. Katikamsimu huu wa kilimo, trekta hizo zimelima jumla ya ekari120, ambapo ufanisi wake ni wastani wa ekari 3-4 kwa siku,kutegemea aina ya udongo.

209. Mheshimiwa Spika, ili kurahisisha upandaji wazao la pamba kwa mstari na kwa nafasi sawa, CAMARTEC

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

imefanya utafiti wa kipandio cha mbegu za pambakinachokokotwa na ng’ombe na kufanikiwa kuundavipandio 50 kwa ajili ya wakulima wa Wilaya ya Meatu,Mkoa wa Simiyu ambao wanafadhiliwa na Kampuni ya bioRETanzania Ltd. Vile vile, kwa kushirikiana na mjasiriamalianayemiliki Kampuni ya Elmi Farm Implement Manufactureriliyoko mjini Kateshi, CAMARTEC imeweza kufanya majaribiona kuboresha Kipandio kinachovutwa na trektakilichobuniwa na kutengenezwa na mjasiriamali huyo baadaya kubaini mapungufu katika mfumo wake wa kudondoshambegu (Seed metering system). Seed metering systems 100ziliagizwa kutoka China kwa ajili ya kuzifunga kwenyekipandio hicho na nyingine kuendelea kutumika kufanyautafiti wa vipandio vingine. Kituo kwa kushirikiana na ChuoKikuu cha Kilimo cha Sokoine, kimeendelea kufanya utafitiwa Solar Dryer isiyoathiri virutubisho na rangi ya vituvinavyokaushwa. Vilevile, CAMARTEC inaendelea kufanyautafiti wa teknolojia mbalimbali ikiwa ni pamoja nazinazohusiana na matumizi ya nishati ya biogas, kupaliliampunga, kuandaa malisho ya wanyama, kupura nakupepeta mazao ya nafaka.

c) Kutafiti na Kuendeleza Usambazajiwa Teknolojia za Matumizi Bora ya Nishati

210. Mheshimiwa Spika, CAMARTEC imeshirikiana naTanzania Breweries Ltd-Arusha (TBL) kufanya utafiti wamatumizi ya chachu (yeast extract) katika uzalishaji wabiogas. Matokeo ya awali yameonesha kuwa, kiwango chabiogas kinachozalishwa kimeongezeka na pia kiwango chajoto kwenye biogas inayowaka kimeongezeka kutokanana kupungua kwa kiwango cha gesi zisizohitajika. Hivyo,wastani wa tani 2 za chachu ambazo huzalishwa kwasiku zitaweza kutumika moja kwa moja kulisha mitambomidogo (6m3) kati ya 32 hadi 48 na kuwanufaisha wananchiwanaozunguka maeneo hayo kuzalisha biogas au zitatumikana wafugaji kwa kuchanganya chachu hiyo na kinyesi chang’ombe ili kuharakisha na kuongeza uzalishaji wa biogas.Vilevile, Kituo kwa kushirikiana na University of Nottingham(UoN), ECHO (Arusha) na Creative Energy kutoka Uingerezakimeendelea kufanya utafiti unaohusisha matumizi ya kifaa

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

maalum (sensor) katika kutambua utendaji wa mtambo wabiogas hata bila kufika kwenye mtambo husika. Aidha, taarifazitakazopatikana kupitia kifaa hicho zitatumika kuwashauriwakulima njia bora ya kurekebisha mtambo bila kufikahuko na hivyo kupunguza gharama ambazo zingetumikakuitembelea mitambo hiyo ili kukagua utendaji wake.

211. Mheshimiwa Spika, CAMARTEC kwa miaka zaidiya 35, imekuwa mstari wa mbele kwenye utafiti nausambazaji wa teknolojia ya nishati mbadala ya kupikia namajiko banifu. Katika mwaka 2017, CAMARTEC kupitiamafundi iliyowafundisha sehemu mbalimbali hapa Tanzania,imefanikisha ujenzi wa mitambo ya biogas (biogas plants)ngazi ya kaya 198 yenye thamani ya Shilingi milioni 336. Kwawastani, asilimia 14 ya fedha hizo ni ruzuku kutoka Serikali yaTanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na asilimia86 ni fedha zilizowekezwa na wananchi wenyewe na wadauwengine wa maendeleo. Kwa mfano, HEIFER Internationalimejenga jumla ya mitambo ya biogas 32 ya ngazi ya kaya.Kati ya hiyo, mitambo 22 imejengwa kupitia miradi yake yaIgunga Eco Village iliyoko katika Kata za Mbutu na Igunga,Wilayani Igunga, Mkoa wa Tabora na mitambo 10 imejengwakupitia mradi wake wa Mbozi Farmers LivelihoodImprovement ulioko katika Kata za Igamba na Isansa,wilayani Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

212. Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa mitambo yabiogas kwa mikoa ni kama ifuatavyo: Arusha (21), Dar-es-Salaam (5), Geita (1), Kilimanjaro (45), Manyara (7), Mara (5),Mbeya (20), Njombe (3), Pwani (3), Shinyanga (1), Simiyu (9),Singida (1), Songwe (10), Tabora (56) na Tanga (10). Ujenzi wamitambo hiyo umetoa ajira za moja kwa moja za kudumuna za muda kwa Kampuni za biogas 22, mafundi 44 navibarua zaidi ya 200.

213. Mheshimiwa Spika, CAMARTEC kupitiaMradi wake wa Tanzania Domestic Biogas Programme(TDBP) unaofadhiliwa na Africa Biogas Partnership Programme(ABPP) imeshirikiana na Shirika la SNV kupitia Mradi wake waSNV Sustain ulioko Sumbawanga kutoa mafunzo ya ujenzi

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

wa mitambo ya biogas kwa vijana 32. Kwa upande wamajiko banifu, Kampuni zilizozalisha kutokana na teknolojiaya CAMARTEC zimeendelea kusambaza majiko na sufuriakatika sehemu mbalimbali za Tanzania. Kwa mwaka 2017,majiko na sufuria takriban 700 yenye thamani inayokadiriwakufikia Shilingi bilioni 1 yalitengenezwa na kusambazwa.Majiko na sufuria hayo yanatumika zaidi kwenye shule zasekondari, vyuo, magereza na hospitali na yamesaidiakupunguza matumizi ya kuni kutoka malori 1,300 mpaka 450kwa mwaka. Biashara hiyo kwa mwaka 2017 imeweza kutoaajira za moja kwa moja za muda na za kudumu kwa zaidiya wajasiriamali na wafanyabiashara 42 na vibarua zaidi ya150. Hii ina maana kwamba, biashara ya majiko banifu nikubwa zaidi kwani kuna wajasiriamali wengine walioko njeya eneo la Kanda ya Kaskazini wanaofanya biashara kamahiyo, ingawa kwa asil imia kubwa majiko hayoyanatengenezwa na kusambazwa kutokea Arusha.

d) Kuhamasisha Usambazaji wa TeknolojiaZinazobuniwa na Taasisi

214. Mheshimiwa Spika, CAMARTEC imeendeleakutafiti na kusambaza teknolojia za matumizi bora ya nishatiya kuni, mkaa na biogas kwa kushirikiana na wajasiriamali,makampuni binafsi, mafundi, Wizara ya Nishati, Wizara yaMadini, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na wadau wetu wamaendeleo ambao ni Africa Biogas Partnership Programme(ABPP). Kuhusu ujenzi wa mitambo ya biogas, Kituo kilijengamitambo 52 midogo ngazi ya kaya na mitambo 3 ya ngaziya jumuiya katika maeneo ya Shule ya Msingi Emboreti katikaMkoa wa Manyara na Shamba la Nyabirezi katika Mkoa waGeita. Ukarabati wa mitambo miwili ulifanyika katika Shuleya Sekondari Inyonga, Masasi na Shule ya Sekondari yaWasichana, Tabora. Aidha, mafunzo ya utumiaji na utunzajiwa mitambo ya biogas yalifanyika maeneo ya Arusha,Shule ya Sekondari Inyonga, Masasi na Shule ya Sekondari yaWasichana, Tabora ambapo zaidi ya watu 51 walipatamafunzo hayo.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

3.4.5 Shirika la Uhandisi na Usanifu wa MitamboTanzania

a) Kujenga Uwezo wa Taasisi katika Kubuni,Kuendeleza na Kusambaza Teknolojia

215. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO)limefanikiwa kutoa mafunzo ili kuongeza ujuzi katika utendajikazi kwa wafanyakazi zaidi ya kumi katika nyanja za uborawa bidhaa, uzalishaji, CAD/CAM, usimamizi wa biashara yakimataifa na ubunifu. Mafunzo hayo yalienda sambamba namaboresho ya karakana ya Taasisi kwa kupata na kusimikamashine mpya tano kwa ufadhili wa Shirika la Umoja waMataifa la Uendelezaji wa Viwanda (UNIDO). Mashine hizoni: computerized plasma cutting machine; computerizedtensile testing machine; computerized hardness tester;computerized material analyzer na semi-automatic spotwelding machine.

b) Kuboresha, Kuendeleza na KuhamasishaUtengenezaji na Utumiaji Kibiashara wa Mitambo

216. Mheshimiwa Spika, usanifu, uendelezaji nautengenezaji wa mashine tatu za kuchakata bidhaa zamarumaru umekamilika. Mashine hizo ni za kufyatua matofaliya kuhifadhi joto (refractory bricks), mashine ya kusagaudongo na mashine ya kuchekecha. Majaribio ya mashinehizo yanaendelea kwa kutumia malighafi za udongounaopatikana nchini. Baada ya majaribio hayo na uhakikiwa ubora wake Shirika litaitangaza kupitia SIDO au kampunibinafsi zitakazojitokeza ili zizalishwe kibiashara. Kuhusu mafutayatokanayo na mbegu za alizeti, wataalam wa TEMDOwametembelea na kushauriana na wadau mbalimbali kwalengo la kuwahamasisha kutumia teknolojia zilizobuniwa.Mwitikio ni mzuri na kwa sasa mipango inafanyika ili kufungamitambo hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa namtaa wa viwanda, SIDO mkoani Singida.

c) Kubuni na Kuendeleza Teknolojia Jadidifu217. Mheshimiwa Spika, uendelezaji na utengenezaji

wa chasili cha mtambo wa kuzalisha umeme kutokana na

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

nguvu za maji uitwao Crossflow Turbine na usanifu wamtambo wa kuzalisha umeme unaotokana na nguvu za majiuitwao Reverse Pump Turbine umekamilika. Aidha, taarifamuhimu kuhusu aina ya makaa ya mawe yapatikanayo nchinina teknolojia zitakazotumika kutengeneza brikwiti za makaaya mawe (Coal dust briquettes) zitakazotumika kupikiazimekusanywa. Taarifa muhimu za usanifu na utengenezajiwa mtambo huo zimekusanywa na usanifu umeanza.Inategemewa kuwa tafiti hizo zikikamilika na kutumikavizuri zitasaidia zaidi kupata nishati mbadala itakayosaidiakupunguza matumizi ya kuni na hivyo kutunza mazingira.

3.4.6 Kampuni ya Mbolea Tanzania218. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), imesimamia uingizaji nausambazaji wa mbolea za aina mbalimbali hapa nchini.Katika kipindi hicho, TFC imefanikiwa kusambaza mboleatani 5,720 katika mikoa yote ya Tanzania Bara inayojumuishaaina ya DAP tani 1,800, UREA tani 3,000, SA tani 670 na CANtani 250. Katika mtandao wa usambazaji wa mbolea nchini,Kampuni ya TFC ina maghala katika mikoa saba na imekodimaghala mengine saba katika mikoa mingine na hivyo kuwana maghala katika mikoa 14 yenye uwezo wa kuhifadhi tani95,500 za mbolea kwa wakati mmoja.

3.4.7 Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogoa) Kujenga Maeneo ya Viwanda katika Mikoa ya

Dodoma, Geita, Kagera, Katavi, Manyara, Mtwara na Simiyu219. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) limeendeleana ujenzi wa miundombinu ya ofisi na majengo (industrialsheds) ya kuendeshea miradi ya ujasiriamali. Ujenzi umeanzakatika mikoa ya Geita, Kagera na Simiyu chini ya Mkandarasi- SUMA JKT. Aidha, mikataba ya ujenzi katika mikoa yaDodoma, Katavi, Manyara na Mtwara imekwisha sainiwa nakazi ya ujenzi itaanza wakati wowote.

b) Kusajili Viwanda Vidogo Nchini220. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,

Shirika limehamasisha na kufanikisha kusajiliwa viwanda

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

vidogo 429 katika mikoa yote nchini kupitia BRELA na kupewaleseni na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneovilikoanzishwa.

c) Kuimarisha Uwezo wa Uhawilishaji waTeknolojia

221. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,teknolojia mpya 59 zilitambuliwa na kusambazwa. Mashinena zana za teknolojia hizo ziliwezesha kuanzishwa nakuimarisha shughuli za miradi 260 ya uzalishaji kote nchini.Teknolojia hizo zinahusu ubanguaji wa korosho; usindikaji wamihogo; ukamuaji wa mafuta ya mawese; usindikaji wavyakula; upunguzaji wa matumizi ya miti na mazao yakekama nishati; ufungashaji wa vyakula vilivyosindikwa;utengenezaji wa vifaa vya ujenzi hasa matofali; utengenezajiwa chokaa na chaki; utengenezaji wa sabuni; na usindikajingozi kwa njia za asil i. Aidha, Shirika limewezeshautengenezaji wa mashine na zana 174 kwa ajili ya matumiziya wajasiriamali wadogo mijini na vijijini. Teknolojia hizozimesaidia kuimarisha na kuongeza ubora wa bidhaa zawajasiriamali.

d) Kuwezesha Uanzishwaji wa Viwanda Vidogo222. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,

Shirika limefanikisha uanzishwaji wa viwanda vipya vidogovya aina mbalimbali 429 na kuzalisha ajira 1,287. Mafanikiohayo yametokana na huduma za kiufundi, ushauri, mafunzo,masoko na mikopo ilizozitoa kwa wajasiriamali. Aidha,maandiko 15 yaliandaliwa kwa ajili ya kuandaa miradi yakuanzisha viwanda vidogo na vya kati chini ya Mkakati waODOP.

e) Upatikanaji wa Mitaji kwa Wajasiriamalikupitia NEDF

223. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,mikopo 1,948 yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.344 ilitolewakupitia Mfuko wa NEDF ambapo asilimia 51 ya mikopo hiyoilitolewa kwa wajasiriamali wanawake. Aidha, asilimia 42ya mikopo ilitolewa kwa miradi ya vijijini. Mikopo hiyo

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

iliwezesha kupatikana ajira 4,438 zinazojumuisha wanaume2,130 na wanawake 2,308.

3.4.8 Kituo cha Uwekezaji Tanzaniaa) Uhamasishaji kwa Kuwalenga Wawekezaji

wa Nje na Ndani

224. Mheshimiwa Spika, Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kilishiriki katika makongamano manne ya biasharana uwekezaji na kunadi fursa za uwekezaji zilizopo nchini.Pia Kituo kiliwaalika wafanyabiashara mbalimbali nakushirikisha taasisi za umma katika makongamanombalimbali yakiwemo yaliyofanyika katika nchi za Vietnam,India, China na Korea ya Kusini. Kutokana na mikutano hiyo,Kituo kimepokea Kampuni mbili (2) ambazo zimeoneshania ya kuwekeza nchini. Kampuni hizo ni MECEN IPC Limitedambayo inatafuta mbia wa kuwekeza katika mradi wakuzalisha chupa za plastiki na Kampuni ya Hyundai ambayoimemtuma mwakilishi wake kuja Tanzania kuangalia fursana kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa miundombinu kupitiaMfumo wa PPP.

225. Mheshimiwa Spika, Kituo kiliratibu ziara zawawekezaji toka China, Czechoslovakia, Japan, Marekani,Mauritius, Misri na Thailand kuja nchini. Matokeo ya ziara hizoni ujio wa Kampuni ya Gullin Pharmaceuticals (Tanzania) Ltdambayo inaendelea na majadiliano ya ubia na kampuni yadawa kutoka China ili kuwekeza katika kiwanda cha dawaDar es Salaam. Pia majadiliano yanaendelea kati ya Kampuniya Argenta Capital Partners Ltd ya Mauritius na SUMA JKTkuhusu mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Dawa za Binadamueneo la Ruvu. Vilevile, Kampuni ya Saisan Co. Ltd kutokaJapan ilikuja na kuonesha nia ya kuwekeza katika usambazajiwa nishati ya gesi (LPG Bulk Distribution) kwenye taasisi zaumma kama vile shule, jeshi, na vyuo. Kampuni hiyo imenuiakushirikiana na Commercial Petroleum Company of Tanzania(COPEC) ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleoya Mafuta ya Petroli Tanzania (TPDC). Taratibu za kujakuwekeza zinaendelea.

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

b) Kupeleka Taarifa kwenye Balozi za Tanzania Njeya Nchi

226. Mheshimiwa Spika, TIC imeshiriki katika kutoana kusambaza taarifa kwenye Balozi za Tanzania nje ya nchizinazosaidia kuvutia uwekezaji nchini. Katika kutekelezajukumu hilo, Kituo kimepeleka machapisho ya uhamasishajiuwekezaji katika Balozi hizo na kutoa mafunzo ya namna yakuhamasisha wawekezaji wa nje ili waje kuwekeza nchini.

c) Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani227. Mheshimiwa Spika, TIC ilishiriki kwenye Maonesho

ya DITF yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Dar es Salaam mwezi Julai hadi Agosti, 2017. Maonesho hayoyalitoa fursa kwa Kituo kutoa elimu kwa wananchi juu yahuduma mbalimbali zinazotolewa na TIC kwa wawekezajiwa ndani na wa nje. Vilevile TIC ilishiriki kwenye Maoneshoya Nane Nane yaliyofanyika katika Kanda za Kusini (Lindi),Kaskazini (Arusha) na Nyanda za Juu Kusini (Mbeya) mweziJulai na Agosti, 2017. Katika Maonesho hayo, TIC ilifanikiwakupata Cheti cha Ushindi wa pili kwenye Kanda ya Nyandaza Juu Kusini na Cheti cha Ushindi wa tatu kwenye Kanda yaKaskazini katika kundi la taasisi. Vile vile, TIC ilishiriki katikaMaonesho ya Mwanza East Africa Trade Fair ambapoilitunukiwa kikombe cha ushindi kwa kushika nafasi ya kwanzakwa kundi la Taasisi na Idara za Serikali. Ushiriki katikamaonesho hayo ulitoa fursa kwa Kituo kujitangaza nakuufahamisha umma juu ya kazi na majukumu yake katikakuhamasisha na kuvutia uwekezaji nchini.

d) Kusajili Miradi ya Uwekezaji228. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwezi

Julai 2017 hadi Februari 2018, TIC imefanikiwa kuandikishamiradi 169 ambayo inatarajia kuwekeza mtaji wa Dola zaKimarekani 107,855,688 na kuajiri wafanyakazi wapatao19,799 ikiwa ni ajira mpya. Miradi yote iliyosajiliwa katikakipindi hicho ilikuwa ni miradi mipya.

e) Kutatua Changamoto za Uwekezaji Nchini229. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwezi

Julai 2017 hadi Februari 2018, Kituo cha Uwekezaji kimeanzisha

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Kamati ya Wakuu wa Taasisi zinazohusika katika KutoaHuduma zinazofanikisha Uwekezaji (National InvestmentFacilitation Committee-NIFC). Kamati hiyo ipo chini yauenyekiti wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezajina hukutana mara moja kila mwezi na kujadili namna taasisihusika zinavyoweza kuondoa changamoto wanazokutananazo wawekezaji wakati wa kuomba vibali na lesenimbalimbali.

f) Kuanzisha Mkutano wa Wawekezaji na Wakuuwa Taasisi

230. Mheshimiwa Spika, Kituo cha Uwekezajikimefanikisha mkutano unaowakutanisha wawekezaji nawakuu wa taasisi zinazohusika katika kutoa leseni na vibalimbalimbali (Investors Dialogue Meeting). Lengo la mkutanohuo ni kuwawezesha wakuu wa taasisi kusikiliza changamotowanazokutana nazo wawekezaji wakati wanapoombaleseni na vibali mbalimbali kwenye taasisi zao ili wawezekuzifanyia kazi. Mkutano huo hufanyika mara moja kwamwaka na mkutano wa kwanza ulifanyika tarehe 31 Oktoba,2017 ambapo masuala yaliyoibuliwa na wawekezajiyanafanyiwa kazi kupitia NIFC.

g) Kuwasaidia Wawekezaji Kupata Vibali na Hatimbalimbali za Kisheria

231. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mweziJulai 2017 mpaka Februari 2018, maombi ya vibali mbalimbaliyaliyoshughulikwa katika taasisi yalikuwa 9,127.

h) Kuratibu Miradi ya Uwekezaji Mahiri

232. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018, TIC iliratibu mkutano mmoja wa Kamati ya Wataalamwa NISC ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana nawawekezaji mahiri. Katika mkutano huo, NISC ilichambuana kutoa ushauri kuhusu namna ya kutatua changamoto zawawekezaji mahiri. Kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha naMipango, Ofisi ya Waziri Mkuu, na Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA), Kituo kilitembelea miradi sita (6) iliyoomba

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

hadhi ya uwekezaji mahiri ili kujionea hatua ya utekelezajiwa miradi hiyo ilipofikia. Katika kikao chake cha mwisho,NISC ilifanikisha kupitisha miradi mikubwa sita na kuipatiahadhi ya miradi mahiri yaani strategic investment status.

i) Kufanya Tafiti zitakazotumika KuishauriSerikali kuhusu Sera ya Uwekezaji

233. Mheshimiwa Spika, Kituo kimeweza kushiriki nakuendesha tafiti mbalimbali kwa kushirikiana na wadauzikihusisha tafiti za kisera na za masoko (Policy and MarketResearch). Kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania na Ofisiya Takwimu ya Taifa, Kituo kimeweza kukamilisha utafiti wamitaji kutoka nje (FDI) kwa mwaka 2016 na taarifa hiyoinasubiri maoni ili kuwasilishwa katika Kamati ya Utendaji.Pia utafiti kama huo kwa mwaka 2017 unaendelea ambapotaarifa za makampuni kwa mwaka 2016/17 kwa Mkoa waDar es Salaam zimeshakusanywa. Kwa kushirikiana naInternational Growth Centre (IGC), Kituo kimekamilisha utafitiya muundo wa kisheria wa Sekta ya Vipodozi na kushirikishawadau wa sekta hiyo kwa ajili ya uhakiki na kikao cha wadaukujadili taarifa ya utafiti huo kinatarajia kufanyika nusu yamwaka ya pili ya 2017/2018. Utafiti huo utawezesha kuonachangamoto zinazoikabili sekta hiyo katika kuanzisha nakuendesha miradi yao. Vilevile, Kituo kimeweza kushirikianana Mradi wa Supporting India Investment and Trade withAfrica (SITA) kwa udhamini wa International Trade Centre (ITC)kukamilisha utafiti wa fursa za uwekezaji katika Sekta ya Ngozina utafiti katika fursa ya alizeti upo katika hatua za awali.

j) Kuboresha Utoaji Huduma Mahali Pamoja (OneStop Shop) na Kuwezesha Usajili kwa Njia ya Mtandao kwaWawekezaji

234. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwezi Julai 2017 mpaka Februari 2018, Taasisi imeendeleana maboresho katika kuhudumia wawekezaji ili kuwasaidiakupata vibali na leseni mbalimbali wanazohitaji ili kuwezakuanzisha miradi yao. Katika juhudi hizo Kituo kimeongezaidadi ya taasisi zilizopo katika Huduma za Mahali Pamojakwa kuweka pamoja maafisa wa TANESCO, TFDA, TBS pamojana OSHA.

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

k) Kuwasaidia Wajasiriamali Wadogo na wa KatiKuibua Fursa za Uwekezaji na Kuwaunganisha nawafanyabiashara Wakubwa (Business Linkages)

235. Mheshimiwa Spika, Kituo cha UwekezajiTanzania kimeendelea kuwaunganisha wawekezajiwakubwa na wadogo, ili wawekezaji wadogo wawezekuwauzia (kuwasambazia) bidhaa wale wawekezajiwakubwa kulingana na ubora na mahitaji ya wawekezajiwakubwa. Kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2017 hadiDisemba 2018, wawekezaji wadogo wapatao 63 wameshirikimafunzo hayo. Kazi hiyo hufanyika kupitia mafunzo maalumambayo wawekezaji wadogo wadogo wa ndaniwanapewa ili waweze kuendana na mahitaji ya wawekezajiwakubwa.

l) Kutangaza Kazi za Kituo na Vivutio vya Uwekezaji

236. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,TIC ilishiriki katika vipindi maalum vya televisheni na radioikiwamo Radio One, Clouds FM, City Radio, na TBC ili kutoaelimu kwa umma kuhusiana na majukumu yake. TIC ilitumiafursa hizo kutoa taarifa za uwekezaji na kuelezea malengomakuu ya Kituo katika shughuli za kuhamasisha uwekezaji,kuhudumia wawekezaji na kutoa huduma za mahalapamoja yaani One Stop Facilitation Centre. TIC iliweza kushirikivipindi mbalimbali ikiwemo vipindi vya ‘tunatekeleza’ kupitiaTBC, ‘kumekucha na kipima joto’ kupitia ITV. Vile vile, Taasisiimefanya mahojiano maalum na waandishi wa TBC, ChannelTen na ITV.

3.4.9 Shirika la Viwango Tanzania

a) Kukagua Ubora wa Bidhaa zitokazo Nchi zaNje kabla ya Kuingia Nchini (Pre-Shipment Verification ofConformity to Standards- PVoC ) ili Kulinda Viwanda vyaNdani

237. Mheshimiwa Spika, Shirika la ViwangoTanzania (TBS) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Zanzibar

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

(ZBS), SIDO, TRA, GCLA, EWURA, SUMATRA, TFDA, FCC,NEMC, NIT, TPA na Jeshi la Polisi imeendelea kusimamia uborawa bidhaa zikiwemo zinazotoka nje kwa kufanya ukaguziwa mara kwa mara. Lengo ni kuhakiki na kuthibitisha uboraili kuwalinda walaji na viwanda vya ndani. Hadi kufikiaMachi 2018, vyeti vya ubora wa bidhaa zitokazo nje ya nchi(Certificate of Conformity - CoCs) 25,055 vimetolewa, sawana asilimia 73.7 ya lengo ya kutoa vyeti 34,000 vya uboramwaka 2017/2018.

238. Mheshimiwa Spika, Shirika limeendelea kudhibitiubora wa bidhaa, ambapo bidhaa ambazo hazikukidhiviwango ziliteketezwa au kurudishwa nchi zilikotoka.Baadhi ya bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na nondo tani126, vilainishi vya mitambo (engine oil) lita 1,000, betri za solarvipande 91 na nyaya za umeme (flat twin cables) rola 208.Bidhaa zilizoteketezwa zilikuwa na thamani ya Shilingi217,301,000. Vilevile, bidhaa zilizorejeshwa nchi zilikotoka nipamoja na shehena za mafuta ya petroli ya tani 74,968.95,nyaya za kuzuia radi (earth rod) vipande 4,950, mafuta yabreki za magari (brake fluid DOT 3) lita 9,880, malighafiya kutengenezea bati tani 60.3 na nyaya za umeme (PVCinsulated cables) katoni 53. Bidhaa zilizorejeshwa zilikuwa nathamani ya Shilingi 9,464,967,232.

b) Kutoa Leseni ya Ubora kwa Bidhaa Mbalimbali239. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi

2018, leseni 225 za ubora za TBS zimetolewa sawa na asilimia93.8 ya lengo la kutoa leseni 240. Miongoni mwa lesenihizo, 41 zilitolewa kwa wajasiriamali wadogo kwa bidhaaza mvinyo, iliki, unga wa soya, unga wa mahindi, mafuta yakujipaka, pilipili manga, maji ya chupa, chumvi, jemu, karafuu,tangawizi ya kusaga, chaki, sabuni za maji, mikate, sabuniza kuogea, maziwa, mtindi, mafuta ya alizeti, asali, vigae,grisi, chokaa, sharubati ya nanasi na mchele. Shirikalimeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali (SMEs) nawadau mbalimbali katika dhana nzima za kuzingatia mifumobora ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

c) Kutoa Mafunzo kuhusu Viwango na Udhibitiwa Ubora (Quality Assurance Training)

240. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi2018, semina 37 za mafunzo zilitolewa, sawa na asilimia123.3 ya lengo la kutoa semina 30. Mafunzo na semina hizozilitolewa kwa wajasiriamali wadogo pamoja na wadaumbalimbali wapatao 3,201 katika mikoa ya Arusha, Dar esSalaam, Iringa, Katavi, Kigoma, Mara, Mbeya, Morogoro,Mwanza, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Songwe na Tabora.

d) Kufanya Ugezi kwa Vifaa na Mashine mbalimbali241. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi

2018 mitambo 4,211 ilifanyiwa ugezi, sawa na asilimia 52.9ya lengo la kufanya ugezi wa mitambo 8,000.

e) Kutayarisha Viwango vya Kitaifa katika SektaNdogo za Uhandisi na Usindikaji

242. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi2018, Shirika limekamilisha viwango muhimu 267 katikasekta za uhandisi na usindikaji sawa na asilimia 76.3 ya lengola kutayarisha viwango 350 kwa mwaka. Shirika pialiliendelea kusimamia viwango vya kitaifa kwa kutumiamifumo iliyopo ya kuhakiki ubora (Certification Schemes).

f) Kupima Sampuli za Bidhaa Mbalimbali243. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi 2018,

sampuli 15,120 zilikuwa zimepimwa katika maabarambalimbali za Shirika kwa lengo la kuhakiki ubora wake. Hiyoni sawa na asilimia 122.9 ya lengo la kupima sampuli 12,300kwa mwaka. Ongezeko hilo limetokana na kuimarikakwa ukaguzi wa bidhaa zinazoingizwa nchini haliiliyosababisha kuongezeka kwa sampuli zinazohakikiwaubora hapa nchini (Destination Inspection).

g) Kufanya Ukaguzi na kutoa Leseni za Ubora waMagari Yaliyotumika yanayoingizwa Nchini

244. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi2018, vyeti 26,706 vya ukaguzi wa magari vimetolewa, sawana asilimia 63.6 ya malengo ya vyeti 42,000. Kati ya magari

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

hayo yaliyokaguliwa, magari 31 yalikataliwa baada yakushindwa kukidhi viwango vya ubora. Aidha, Shirikalinatekeleza mradi unaofadhiliwa na Trade Mark East Africa(TMEA) wenye lengo la kuboresha miundombinu ya ubora yaShirika. Kwa kupitia mradi huo, miundombinu ya TEHAMA yaTBS imeboreshwa hivyo imerahisisha utoaji wa huduma nakufupisha muda wa kuwahudumia wateja wa Shirika (TurnAround Time).

h) Kuanzisha Ofisi Mpya za Mipakani na KufunguaOfisi Mpya za Kanda

245. Mheshimiwa Spika; katika kupanua wigo wautoaji huduma na kudhibiti mianya ya uingizwaji wabidhaa zisizokidhi ubora, Shirika limeomba ofisi kwaMamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na majadilianoyanaendelea ili kupata ofisi katika mipaka ya Itungi, Bukobana Mtwara. Vilevile, Shirika linaendelea na jitihada za kutafutaofisi katika mipaka ya Mtambaswala na Tarakea sambambana kufuatilia vibali vya ajira ili kuwezesha ukaguzi wa bidhaakatika mipaka hiyo. Shirika limefungua ofisi za kanda zilizopoArusha (Kanda ya Kaskazini)Mbeya (Kanda ya Nyanda za JuuKusini), Mwanza (Kanda ya Ziwa)Dodoma (Kanda ya Kati)naMtwara (Kanda ya Kusini).

3.4.10 Wakala wa Usajili wa Biashara na Lesenia) Kuboresha Mifumo na Taratibu za

Utoaji Huduma kwa Kutumia Njia za Kiteknolojia246. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Usajili wa

Biashara na Leseni imejenga Mfumo Mpana wa Usajili kwaNjia ya Mtandao (Online Registration System - ORS) ambapohuduma zote zitolewazo na BRELA ambazo ni usajili wamakampuni, majina ya biashara, alama za biashara nahuduma, hataza, leseni za biashara na viwanda zinatolewakwa njia ya mtandao. Mfumo wa ORS umeunganishwa naMamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya nambaya uraia na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili yaNamba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) wa Kampuniambayo pia huwa ni namba ya usajili wa Kampuni. Aidha,mfumo huo umekwishaunganishwa na Mfumo wa Serikali wa

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

Ukusanyaji wa Maduhuli (Government Electronic PaymentGateway - GePG), pamoja na Mamlaka ya MawasilianoTanzania (TCRA) kwa ajili ya utambuzi wa maeneo na anuaniza makazi. Mfumo huo wa ORS unaweza kuunganishwa nataasisi nyingine za Serikali kwa lengo la kutoa huduma kwapamoja (Electronic One Stop Shop).

247. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanza kutoahuduma kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 4 Januari, 2018,BRELA il itoa mafunzo kwa wanasheria, wahasibu nawakaguzi, wawakilishi wa Sekta Binafsi na benki. Aidha, katikakuhakikisha kuwa wananchi wanaelewa kutumia mifumoya TEHAMA na kufanya usajili, Wakala imeanzisha dawati lakuelimisha na kusaidia wadau kusajili kwa njia ya mtandaokatika jengo jipya la Ushirika. Mfumo huo unategemewakufungwa katika Ofisi za Maafisa Biashara nchini ili kurahisishautoaji wa huduma na elimu kwa wananchi katikaHalmashauri zote nchini. Aidha, Wakala imetoa mafunzo kwaMaafisa Biashara wote wa Halmashauri za mikoa ya Dar esSalaam na Pwani yaliyofanyika tarehe 5 na 6 Machi, 2018.

b) Kuboresha Mifumo ya Uwajibikaji, Weledi naUadilifu kwa Watumishi

248. Mheshimiwa Spika, Wakala imeendeleakuboresha mifumo ya uwajibikaji kwa watumishi kwakusimamia ujazaji wa fomu za MWAMTUKA (OPRAS). Wakalaimekuwa na utamaduni kwa watumishi wake kutoataarifa za utendaji za siku na wiki. Pia, katika kuhakikishasuala la maadili na uadilifu linafanyiwa kazi, Wakala inakamati ya maadili ambayo pamoja na majukumu mengineinaratibu malalamiko ya wateja na kushughulikia masualaya maadili ya wafanyakazi. Utaratibu huo umeweza kubainimaeneo yenye viashiria vya rushwa na pia kudhibiti na hatakuongeza usimamizi zaidi.

c) Kutoa Elimu na Uhamasishaji wa Usajili naUrasimishaji wa Biashara kwa Wananchi

249. Mheshimiwa Spika, Wakala imeendeleakutoa elimu kuhusu taratibu za usajili kwa njia ya mtandao

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

kwa kutumia vyombo vya habari, semina na warshambalimbali kwenye maeneo ya wafanyabishara wadogowadogo mikoani na wilayani kwa kuanzia na ofisi zakanda za Mbeya, Mtwara na Mwanza. Aidha, Wakalaunahamasisha urasimishaji wa biashara kupitia njiambalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa vipeperushivilivyoandaliwa kwa Kiswahili vikielezea taratibu za usajilina ada. Hadi kufikia Januari 2018, vipeperushi 22,480vimetolewa kwa wajasiriamali mbalimbali mikoani nawilayani. Vilevile, Wakala inalenga kuwaelimisha na kuwapahuduma za usajili popote walipo kwa njia ya mtandao.Aidha, wafanyakazi wameelimishwa kuhusu mbinu nakuwahudumia wateja na kutekeleza mkataba kwa wateja.

3.4.11 Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghalaa) Kuainisha na Kufanya Ukaguzi wa Ghala

zilizosajiliwa na zinazotarajiwa Kusajiliwa chini ya Mfumo

250. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Usimamizi waStakabadhi za Ghala (WRRB) imetoa leseni 23 kwawaendeshaji wa ghala kwenye mazao ya korosho, kahawa(1), mpunga (2), na mahindi (1) na kufikia jumla ya leseni 27.Aidha, Bodi imefanya kaguzi zote zinazotakiwa kisheriaambazo ni ukaguzi kabla ya mfumo kuanza (Pre-Inspection),na ukaguzi wakati Mfumo unaendelea (Survil l ianceInspections). Leseni za kuendesha ghala hutolewa baada yaBodi kutangaza kwenye tovuti yake na waombaji wenye sifakukidhi matakwa ya kisheria ya uendeshaji wa ghala.

b) Kutoa Elimu ya Mfumo wa Stakabadhi kwaWadau

251. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Usimamizi waStakabadhi za Ghala imeendelea kutoa elimu ya Mfumo kwawadau wote ili kuongeza uelewa. Katika kipindi cha Julaihadi Oktoba 2017, wafanyakazi wa makampuniyanayoendesha ghala wapatao 52 walipewa mafunzo yajinsi ya kupokea na kutoa mazao ghalani, Sheria ya Mfumowa Stakabadhi za Ghala, Kanuni na Miongozo ya mazaoyanayotumia Mfumo wa Stakabadhi. Bodi kwa kushirikianana Benki Kuu ya Tanzania, NMB PLC, CRDB PLC, NHIF, TIGO

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

Tanzania, Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja naMashirika ya Hifadhi ya Jamii walitoa mafunzo kwa wakulimawa Mtwara na Lindi mwezi Agosti 2017.

252. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,Bodi kwa kushirikiana na FSDT ilihamasisha wakulima wakorosho kutumia huduma za kibenki ikiwa ni pamoja nakufungua akaunti kwa ajili ya malipo wanapouza korosho.Zaidi ya wakulima 420,000 walifungua akaunti na kutumiahuduma za kibenki kama ifuatavyo: NMB 224,000, CRDB196,000, na POSTAL BANK 2,033. Aidha, wakulimawanaelimishwa na kuhamasishwa kutumia mitandao ya simukupata taarifa za kila siku za masoko ya bidhaa na mazao.

253. Mheshimiwa Spika, Bodi imeendelea kufuatiliautendaji wa ghala zilizosajiliwa kuhifadhi mazao na kutoaelimu kuhusu uingizaji wa taarifa kwenye kanzidata nakurekebisha makosa mapema. Bodi kwa kushirikiana na Sokola Bidhaa Tanzania imetoa mafunzo kwa wakulima wapatao200 wa mahindi katika Mkoa wa Rukwa katika wilaya zaSumbawanga, Kalambo na Nkasi kuhusu matumizi ya Mfumowa Stakabadhi za Ghala na jinsi ya kuuza mazao kupitia Sokola Bidhaa Tanzania.

3.4.12 Chama cha Hakimiliki Tanzania

a) Kuongeza Makusanyo ya Mirabaha254. Mheshimiwa Spika, Chama cha Hakimiliki

Tanzania (COSOTA) imeendeelea kuboresha ukusanyaji wamirabaha, kwa kuongeza maafisa leseni wawili (2) namatumizi ya mfumo wa kielektroniki. Kwa sasa kuna jumlaya maafisa leseni watano (5) na maafisa ugani watatu (3)ambao wanafanya kazi ya ukusanyaji mirabaha kwausimamizi wa COSOTA. Hadi Februari 2018, Shilingi 90,164,820zilikusanywa na zoezi la kugawa mirabaha kwa wasaniilitaendelea baada ya kukamilika kwa maboresho ya mfumoyanayofanywa na wataalam kutoka WIPO. Maboreshohayo yanayotarajiwa kukamilika tarehe 17 Mei, 2018yatawezesha mirabaha kugawanywa kutokana na matumiziya kazi za wasanii. Aidha, COSOTA imejiunga na Mfumo wa

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Kielektroniki wa Government e-Payment Gateway ili kuongezamapato.

b) Kutoa Elimu kwa Wananchi na Wadau waSanaa Kuhusiana na Mambo ya Hakimiliki na Hakishiriki

255. Mheshimiwa Spika, COSOTA kwa kushirikianana wadau wengine imetoa elimu katika mikoa ya Arusha(195), Dar es Salaam (54), Dodoma (190), Mbeya (220), Mwanza(188), Morogoro na Tanga kuhusu masuala ya Hakimiliki naHakishiriki kwa watunzi na wabunifu wa kazi za sanaazinazolindwa na Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na. 7 yamwaka 1999 na umuhimu wa kusajili na kulinda kazi zao namasuala ya uharamia.

c) Kufanya Ukaguzi wa Kazi Zinazolindwa naSheria ya Hakimiliki na Hakishiriki (Anti-Piracy Raids)

256. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai2017 hadi Februari 2018, COSOTA ilifanya ukaguzi wa matumiziya kazi za wasanii kupitia mfumo wa televisheni wa cablekatika mikoa ya Arusha, Dodoma, Manyara, Mara, Morogoro,Mtwara, Singida na maeneo ya Namanga na Karatu.Kufuatia ukaguzi huo, kesi mbili zimefunguliwa kwa kukiukaSheria moja ikiwa mkoani Singida na kesi nyingine katikamkoa wa Arusha wilayani Karatu. Aidha, kesi mojail iyofunguliwa mkoani Dodoma mwaka 2017 badoinaelendea kusikilizwa.

d) Kushughulikia Migogoro na Kesi za Hakimiliki naHakishiriki

257. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Februari 2018,COSOTA imepokea jumla ya migogoro 27. Kati ya hiyo, miwili(2) imeshughulikiwa na kumalizika, iliyobaki inaendelea nausuluhishi.

e) Kuendelea Kusajili Wanachama Wasanii na KaziZao

258. Mheshimiwa Spika, COSOTA imeendelea kusajiliwasanii na kazi zao. Katika kipindi cha 2017/2018, jumla yawanachama 348 walisajiliwa. Kati ya hao, 77 walikuwa wafani ya muziki, 125 fani ya filamu na 146 wa kazi za maandishi.

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

Kazi zilizosajiliwa ni 1,432 inayojumuisha kazi 908 za muziki,276 za filamu na 248 za maandishi.

3.4.13 Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

a) Kuboresha Upatikanaji wa Soko la Bidhaa naHuduma Zinazozalishwa Nchini

259. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Maendeleo yaBiashara Tanzania (TanTrade) ilifanya tathmini ya mahitaji yamalighafi ya viwanda 70 vya matunda, viungo na nafaka ilikuunganisha wazalishaji wa mazao na viwanda. Hatua hiyoililenga kusaidia upatikanaji wa masoko ya uhakika. Jitihadahizo zinajumuisha kutafuta soko kwa bidhaa zitokanazo nashughuli za kilimo, ufugaji, uvuvi, ubunifu, utamaduni nahuduma mbalimbali zitolewazo nchini.

b) Kuratibu na Kudhibiti Uendeshaji wa Maoneshoya Kimataifa Nchini

260. Mheshimiwa Spika, TanTrade iliandaaMaonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) yaliyofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2017.Kupitia Maonesho hayo, Watanzania walipata muda wakutembelea, kujifunza teknolojia, ujuzi na mbinu mbalimbaliza kibiashara. Makampuni ya ndani 1,999 yalishirikiikilinganishwa na makampuni 1,811 yaliyoshiriki maoneshoya 40 ya DITF ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.4. Aidha, kampuni501 kutoka nje ya nchi yalishiriki ikilinganisha na kampuni491 katika Maonesho ya 40 ya DTIF, sawa na ongezeko laasilimia 2.03. Vilevile, nchi 31, Wizara 6 na taasisi 37 za Serikalizilishiriki.

261. Mheshimiwa Spika, kupitia Maonesho hayo,wafanyabiashara waliingia mikataba mbalimbali yenyethamani ya Shilingi bilioni 15 na mauzo ya papo kwapapo ya Shilingi bilioni 10. Maonesho hayo yameendeleakuboreshwa ikiwa ni pamoja na kuwa na siku maalum zakutangaza bidhaa za Tanzania. Aidha, mabanda maalum

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

kama vile Banda la Tanzania mahsusi kwa ajili ya kutangazabidhaa zinazozalishwa nchini na Banda la Asali kwa ajili yakutangaza bidhaa za asali yalitengwa. Mabanda hayoyameendelea kuwavutia watembeleaji wengi wakati wamaonesho.

c) Kuandaa Mikutano ya Wafanyabiashara

262. Mheshimiwa Spika, TanTrade kwakushirikiana na shirika binafsi la Global Community iliratibumikutano ya ana kwa ana ya biashara ili kuwaunganishawazalishaji na masoko. Katika mikutano hiyo, mikatabambalimbali isiyofungamana yenye thamani ya Shilingi bilioni7, ikiwahusisha wanunuzi na wazalishaji wa alizeti, matundana choroko kutoka mikoa ya Mtwara, Njombe na Singidailisainiwa. Kadhalika, viwanda vya usindikaji wa maziwavilionesha uhitaji mkubwa ikilinganishwa na uzalishaji wamaziwa unaofanywa kwa sasa. Mathalan, viwanda vyaTanga Fresh na Milk Com vilionesha utayari wa kutuma garila kukusanya maziwa popote wafugaji watakapowezakuzalisha zaidi ya lita 10,000 kwa siku. Vilevile, wakulima waviungo na matunda waliunganishwa na viwanda vya ElvenAgri na Vegeta vilivyopo wilayani Bagamoyo.

d) Kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa Nje yaNchi

263. Mheshimiwa Spika, ili kutangaza na kukuzamahusiano ya kibiashara na nchi za nje, TanTrade iliratibuushiriki wa kampuni za kitanzania katika maoneshombalimbali nje ya nchi. Kampuni 72 zilishiriki katikamaonesho ya nje ya nchi ikijumuisha Rwanda (18), Swaziland(11), Uganda (10) na Kenya (23). Mafanikio yaliyopatikanakatika ushiriki huo ni pamoja na; mauzo ya papo kwa papoya takribani Shilingi milioni 197; Kampuni tatu (3) ikijumuishaKiwanda cha Mvinyo (Alko Vintage Co. Ltd), Urafiki, 21stCentury na Kampuni ya Waasili Asilia ziliingia makubalianoya kuuza bidhaa za mvinyo, khanga, vitambaa na bidhaaza ngozi nchini Swaziland. Makubaliano ya kufanya biashara

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

ikiwa ni pamoja na oda ya kuuza tani 50 za kahawa, jozi 300za viatu vya ngozi vya wazi (Sandals), tani 200 za mchele,tani 10 asali mbichi na tani 40 za nafaka.

e) Kushiriki katika Mikutano na Makongamano

264. Mheshimiwa Spika, TanTrade ilishiriki katikaKongamano la Tatu (3) la Watanzania Waishio Nje ya Nchi(Diaspora) lililofanyika Zanzibar kwa lengo la kutangaza fursaza biashara nchini. Kongamano hilo pia lililenga kuhamasishauwekezaji katika Sekta ya Utalii nchini kupitia Diaspora,kutambua mchango wa Diaspora katika kuleta muonekanompya wa uchumi wa kati na kuweka mazingira ya kuandaamakongamano ya biashara na uwekezaji nje ya nchi kwakushirikiana na Diaspora.

f) Kuimarisha na Kuijengea Uwezo Sekta Ndogo naya Kati ya Biashara (SMEs)

265. Mheshimiwa Spika, TanTrade inatambuamchango mkubwa wa kukuza uchumi, ajira na maendeleokwa ujumla unaotolewa na Sekta Katiti, Ndogo na ya Katiya Biashara (MSMEs). Kwa kutambua jukumu hilo, Mamlakaimeendelea kuwajengea wafanyabiashara uwezo kwa njiaya mafunzo na kuwapatia taarifa za biashara na masoko.Vilevile, Tantrade kwa kushirikiana na wadau wengineimesaidia kutatua changamoto na vikwazo vya kiutendajina kushiriki kuweka mazingira rafiki ya kibiashara il iwafanyabiashara hao waweze kufikia vigezo vya ushindanina kuongeza tija na ufanisi katika biashara.

g) Kuboresha na Kuimarisha Mfumo wa Taarifaza Biashara

266. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha nakuimarisha upatikanaji wa taarifa za kibiashara zilizo sahihina kwa muda muafaka kutoka vyanzo vya kuaminika,TanTrade inatumia Mfumo wa Serikali wa Taarifa kwa Njia ya

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Ujumbe Mfupi kwa Simu ya Mkononi (E-Government MobilePlatfom) kwa lengo la kukusanya na kusambaza taarifa zamasoko ya bidhaa na huduma mbalimbali kwa umma. Halikadhalika, katika kipindi cha 2017/2018, TanTrade ilifanikiwakuziingiza kampuni 1,046 kwenye kanzidata ya mfumo huoambao utawezesha kampuni hizo kupata wateja wa bidhaazao na kuongeza mauzo hususan kwenye sekta za chai,kahawa, pamba, nguo, katani na korosho.

h) Kutoa Ushauri wa Kibiashara kwa WajasiriamaliWadogo

267. Mheshimiwa Spika, TanTrade ilitoa ushauri kwakampuni ndogo 20,036 na kuziwezesha kubuni, kuanzisha nakuendesha biashara kwa njia ya vikundi; kuandaa maandikoya miradi; kutengeneza rajamu za bidhaa; kutoa ushauri wakitaalam wa masuala ya kibiashara; kutengeneza nemboza kampuni; machapisho mbalimbali yanayotumikakutangaza bidhaa pamoja na huduma nyingine za kibiasharakupitia Kitengo cha BSB. Lengo la ushauri huo lilikuwa nikuimarisha uwezo wa kampuni hizo kufanya biashara yenyetija. Vilevile, kampuni hizo ziliweza kuunganishwa na Taasisiza SIDO, TBS na TFDA kwa ajili ya kupata huduma nyingine zakibiashara. Huduma hiyo imekuwa kiunganishi muhimu katiya taasisi na wadau mbalimbali kwenye masuala ya biasharanchini.

i) Kuwaunganisha Wazalishaji wa Ndanina Masoko

268. Mheshimiwa Spika, TanTrade ilifanikiwakuwaunganisha wazalishaji 529 wa bidhaa za viungo,asali, maharage, mbaazi, soya, samaki, mboga na matunda,mikundekunde, chai, kahawa, miwa, chakula cha mifugo,ufugaji wa samaki, bidhaa za ngozi na usindikaji wa samakina vyakula na bidhaa nyingine katika soko la ndani na lanje.

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

j) Kuratibu Programu za Mafunzo

269. Mheshimiwa Spika, TanTrade iliratibuprogramu mbili (2) za mafunzo ya kujenga uwezo kwawazalishaji na wafanyabiashara wapatao 307 ili wawezekufanya biashara kiushindani, kwa kuzingatia ubora katikamnyororo wa thamani ya bidhaa na namna ya kutafutamasoko. Mafunzo hayo yalitolewa kwa kada mbalimbali zawazalishaji na wafanyabiashara nchini katika mikoa yaKagera, Kigoma, Lindi, Mtwara na Shinyanga Programu hiyoiliratibiwa kwa ushirikiano na wadau kutoka taasisi za ummana binafsi zikiwemo TBS, TFDA na Agha Khan Foundation.Walengwa wa mafunzo hayo walikuwa ni vikundi vyawasindikaji wa mafuta ya alizeti, wafugaji nyuki na wasindikajiasali na bidhaa zake ili waweze kuongeza uzalishaji nakufahamu mbinu za kutafuta masoko.

k) Kuongeza Ushindani katika Sekta ya Biashara

270. Mheshimiwa Spika, TanTrade imeendeleakufanya tafiti za kibiashara ili kuimarisha na kukuza biasharakatika mikoa na nchi zinazoizunguka Tanzania; kufanyatathmini na upembuzi yakinifu wa bidhaa na mazaombalimbali ili kubaini mifumo ya masoko; kuhamasishauwekezaji na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo ilikuendeleza fursa za viwanda nchini.

3.4.14 Wakala wa Vipimo

a) Kukagua na Kusimamia Matumizi SahihiyaVipimo

271. Mheshimiwa Spika, vipimo 455,962vimekaguliwa na kuhakikiwa, sawa na asilimia 95.6 yavipimo 477,159 vilivyopangwa kukaguliwa kuanzia Julai, 2017hadi Januari, 2018. Wakala imeendelea kufanya zoezi lakuzuia ufungashaji batili maarufu kwa jina la LUMBESAambapo mikoa yote imeanzisha vituo maalum vya ukaguzi(Barriers). Katika kipindi cha Julai 2017 hadi Januari 2018,

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

wafanyabiashara 2,501 walikaguliwa na 768 ambao niasilimia 31 kati ya hao walipatikana na makosa na hatuambalimbali za kisheria zilichukuliwa ikiwemo kufilisiwa nakupelekwa mahakamani.

272. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi,2018, Wakala iliendesha zoezi la ukaguzi wa mizani katikazao la korosho, sambamba na utoaji wa elimu katika mikoaya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Katika zoezi hilo, mizani 2,023ilikaguliwa ambapo mizani 2,005 sawa na asilimia 99.1 ilikuwasahihi kwa matumizi na mizani 18 (asilimia 0.9) ilihitajimarekebisho kabla ya kutumika. Aidha, Wakala ilifanyauhakiki wa mizani mikubwa (weigh bridges) katikamaghala makuu matano (5) mkoani Lindi (Mtama,Nachingwea na Buko) na Mtwara (MCC na OLAM) ambakovyama vya msingi (AMCOS) hupeleka na kuuza korosho zao.

273. Mheshimiwa Spika, Wakala imeendeleakufanya uhakiki wa mizani inayotumika kununulia ufutamkoani Lindi katika wilaya za Lindi Vijijini, Kilwa, na Ruangwaambako vijiji 30 na vyama vya msingi sita (6) vilipitiwa. Katikaukaguzi huo mizani 65 ilihakikiwa na mizani 47 ilipitishwa,wakati mizani 18 ilifanyiwa marekebisho kabla ya kutumika.Wakati ukaguzi wa mizani ukiendelea, elimu ilitolewa kwawakulima na wanaushirika kuhusu matumizi sahihi ya vipimowakati wa uuzaji wa ufuta.

274. Mheshimiwa Spika, Wakala ilikagua mizaniishirini na tano (25) iliyotumika kwa ununuzi wa zao latumbaku na kuhakikisha usahihi wake. Aidha, zoezi hilo lauhakiki wa mizani hiyo kwa msimu wa 2017/2018 lilifanyikakatika vituo vya mauzo ili kuondokana na wasiwasi uliopomiongoni mwa wadau kuwa mizani huharibiwa wakati wakusafirishwa inapohakikiwa nje ya vituo. Wakulima waliuzatumbaku yao kupitia mizani iliyohakikiwa na kupata stahikikulingana na uzito sahihi na kuwaongezea hamasa yakuzalisha zaidi.

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

275. Mheshimiwa Spika, Wakala iliendelea kufanyauhakiki wa mizani ya kupimia madini na vito katika maeneombalimbali hapa nchini, ambapo hadi kufikia robo ya tatuya mwaka 2017/2018, ukaguzi ulifanyika katika vituo vyamikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Geita, Kilimanjaro, Manyara,Mara, Ruvuma na Shinyanga ambapo mizani 89 ilikaguliwa.Kati ya hizo, mizani 64 ilipitishwa kuwa ni sahihi na mizani 25ilielekezwa ifanyiwe marekebisho.

276. Mheshimiwa Spika, kutokana na uhakikihuo wa mizani za madini na vito, Serikali imeweza kubainiudanganyifu uliokuwa ukifanywa na wauzaji na wasafirishajiwa madini ndani na nje ya nchi na kusaidia kudhibiti upotevuwa mapato ya Serikali. Aidha, Serikali imetoa fedha zamaendeleo kwa ajili ya kununulia vifaa vya kitaalam(Precision weighing scales and standard weights)vitakavyosaidia kuongeza kasi na ufanisi wa ukaguzi huo.Ununuzi wa vifaa hivyo uko katika hatua mbalimbali zamanunuzi.

277. Mheshimiwa Spika, Wakala iliendelea kuhakikiflow meter zinazopokea mafuta, hususan mafuta mazito(diesel) yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salam.Hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka 2017/2018, mita hiyoiliweza kupitisha kwa usahihi lita za ujazo 4,326,179,690 zamafuta ya dizeli. Aidha, Wakala iliendelea kuhakiki mitazilizopo kwenye pampu za kuuzia mafuta na pia matenkiyanayobeba mafuta ili kumlinda mtumiaji na kuhakikishaSerikali inapata mapato stahiki. Katika kuhakikisha magarina matenki yanayobeba mafuta yana ujazo sahihi, Wakalainakamilisha ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Kupimia Matenkiya Mafuta (Calibration Bay) katika eneo la Misugusugu,Kibaha – Mkoani Pwani. Kituo hicho kitakuwa na uwezo wakuhakiki matenki nane (8) kwa wakati mmoja badala ya kituocha sasa kilichopo Ilala chenye uwezo wa kuhakiki matenkimawili (2) kwa wakati mmoja. Kituo hicho kipya kinatarajiwakuanza kazi mapema mwezi Juni 2018 ambapo kasi na ufanisikatika ukaguzi wa magari yabebayo mafuta itaongezeka.

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

278. Mheshimiwa Spika, Wakala iliendelea kufanyaukaguzi wa vituo vya kuuzia gesi itumikayo majumbani(LPG). Ukaguzi umefanyika katika vituo vinavyopokea nakufungasha gesi (Gas Plants) na pia katika vituo vya kuuziagesi vya jumla na reja reja ili kuwalinda watumiaji. Pamojana ukaguzi huo, Wakala wa Vipimo imeendelea kutoa elimuhususan kwa watumiaji kupitia luninga, radio, vipeperushina kwenye maonesho mbalimbali namna ya kutambuamitungi ya gesi iliyo na kipimo sahihi. Aidha, Wakala imefanyakaguzi za kushitukiza katika vituo vya kuuzia gesi ili kuhakikishakuwa kila muuzaji wa gesi anayo mizani iliyohakikiwa namitungi imewekwa alama stahiki za kuonesha uzito sahihiwa mtungi na gesi. Hadi kufikia robo ya tatu ya 2017/2018,Wakala imefanya ukaguzi kwa wauzaji wa jumla na reja rejakwa vituo 1,358 ambapo vituo 1,158 (asilimia 85.3) vilikuwana mizani na vituo 200 (asilimia 14.7) havikuwa na mizani.

279. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha dira zamaji (water meters) zinahakikiwa, Wakala imeanza kuhakikidira za maji zinazoingia nchini kabla ya kufungwa kwa ajiliya matumizi, pamoja na zile zilizoko kwenye matumizi. Katikakipindi cha mwezi Julai 2017 hadi Januari 2018, Wakalaimehakiki dira za maji 682 ambapo dira za maji 670zilipitishwa na dira za maji 12 zilikataliwa. Uhakiki umefanyikakatika mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga na Tanga.Jedwali Na. 1: Uhakiki wa Dira za Maji (Julai 2017 hadiMachi 2018)

Mkoa

Mita zilizohaki-

kiwa

M

ita zilizopit- ishw

a kwa m

a- tum

izi (Passed)

Mita zilizokata-

liwa (Rejected)

Dar es Salaam 61 5 1Shinyanga 6 6 - Tanga 3 3 - Jumla 68 6 1

 

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

b) Kutoa Elimu Kwa Umma280. Mheshimiwa Spika, taarifa na maandiko 38

yalitolewa kwenye magazeti mbalimbali katika kipindi chamwezi Julai 2017 hadi Januari 2018. Vipindi 22 vya redio, vipindi20 vya luninga, matangazo mawili (2) ya redio na matatu(3) ya luninga yalitolewa. Mikutano mitatu ya waandishi wahabari (3) na semina nne (4) kwa wajasirimali (TASWE, TWCC,MOWE na Lindi) zimefanyika. Aidha, Wakala imeshiriki katikamaonesho mbalimbali (DITF, NaneNane, SIDO-Kigoma naIringa; MOWE na wadau wa maji -Tanga).

281. Mheshmiwa Spika, hadi kufikia robo yatatu ya mwaka 2017/2018, Wakala wa Vipimo imewezakutoa elimu na mafunzo maalum kwa wajasiriamali waliokatika vikundi vipatavyo tisa (9) katika mikoa ya Kilimanjaro(Nandra Scales Enginnering, Moshi Common Facility, HangScales, Hagu Scales, IJM Scales na Paramount Scales); Arusha(Urito Weighing Scales); Dar es Salaam (Hasat InspirationCo. Ltd); na Mwanza (Msunga Bench Products) ambapo tayariwameanza kuunda mizani na kuingiza kwenye soko hapanchini. Mizani inayoundwa na wajasiriamali wazalendo,imeonesha ubora mkubwa ambao umethibitishwa naWakala ikilinganishwa na mizani zinazoagizwa kutoka njeya nchi. Viwanda hivyo vidogo vya uundaji wa mizanivimetoa ajira kwa vijana takriban 150 na kuwaongezeakipato.

c) Kuiboresha Kanzidata ya Vipimo282. Mheshimiwa Spika, Wakala imeendelea na

ukusanyaji wa takwimu za vipimo katika mikoa ili kupataidadi sahihi (Kanzidata) ya vipimo kwa nchi nzima. Kwamujibu wa kanzidata iliyofanyika hadi mwezi Januari 2018imeonesha kuwa kuna vipimo 830,000 kwa nchi nzima nakazi hiyo ni endelevu.

d) Kununua Vitendea Kazi

283. Mheshimiwa Spika, magari sita (6) kati ya magari10 yaliyopangwa kununuliwa mwaka 2017/2018 yamelipiwaGPSA. Aidha, vifaa vya kitaalam vya kuhakiki dira za maji

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

(Water Meter Test Bench) na mizani ya kupimia uzito wamadini na vito (Weighing instrument) viko katika hatuambalimbali za manunuzi.

e) Kuanzisha na Kutekeleza Mfumo wa Ufuatiliaji naTathmini (M&E)

284. Mheshimiwa Spika, Wakala imeendeleakuimarisha mfumo wake wa ufuatiliaji na tathmini kwakuhuisha mifumo ya ICT ili kuharakisha ufuatiliaji katika mikoayote ya Tanzania ambako Wakala ina ofisi.

f) Kuongeza Idadi ya Watumishi na KuwaongezeaUwezo wa Kitaalam

285. Mheshimiwa Spika, Watumishi 21 katikaajira mbadala wameajiriwa, kati yao 10 ni Maafisa Vipimona 11 ni Madereva. Aidha, watumishi 24 wamepata mafunzombalimbali ya kitaalam ndani na nje ya nchi kwa ajili yakuwajengea uwezo.

g) Kufanya Maboresho ya Ofisi za Wakala naKukamilisha Ujenzi wa Kituo cha Upimaji Matenki ya MafutaMisugusugu Kibaha

286. Mheshimiwa Spika, Ofisi nne (4) za Wakala katikaMikoa ya Mwanza, Mtwara, Temeke na Kitengo cha Bandari(Dar es Salaam) zimefanyiwa maboresho. Aidha, Kituo chaupimaji wa manteki ya mafuta cha Misugusugu kinatarajiwakukamilika mwezi Mei, 2018.

h) Kuhamasisha Matumizi ya TEHAMA katikaKutekeleza Majukumu ya Wakala

287. Mheshimiwa Spika, Wakala imendelea namatumizi ya TEHAMA ili kuboresha utendaji kazi. Aidha,mifumo mbalimbali inatumika ikiwemo; Shakira, EPICOR,Asset Management System, pamoja na mfumo wa ukaguziwa bidhaa zilizofungashwa (pre-packed goods).

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

i) Ukaguzi wa Bidhaa Zilizofungashwa kwenyeMaeneo Mbalimbali ya Mipakani, Bandarini na Viwandani

288. Mheshimiwa Spika, Wakala imeendeleakuongeza nguvu katika kukagua bidhaa zilizofungashwakwenye maeneo ya viwanda; vituo vya Bandari za Dar esSalaam, Tanga na Mwanza pamoja na mipaka ya Horohoro,Holili, Mtukula, Namanga, Kasumulu, Tunduma na Sirari. Kwakipindi cha mwezi Julai 2017- Januari 2018, aina zabidhaa 2,272 zilikaguliwa ikilinganishwa na aina 1,985zilizokaguliwa kwa kipindi hicho kwa mwaka uliopita.

3.4.15 Tume ya Ushindani

a) Kudhibiti na Kupambana na Uingizajina Uzalishaji wa Bidhaa Bandia

289. Mheshimiwa Spika, Tume ya Ushindani (FCC)ilifanya kaguzi katika Bandari ya Dar es Salaam na bandarikavu (ICDs) ambako jumla ya makasha (makontena) 4,004yalikaguliwa na kati ya hayo makasha 415 yalibainikakuwa na bidhaa mbalimbali zilizokiuka Sheria ya Alama zaBidhaa ya mwaka 1963 kama ilivyorekebishwa. Tume piailifanya kaguzi za kushtukiza zipatazo 13 kwenye maduka namaghala jijini Dar es Salaam. Katika kaguzi hizo, watuhumiwawapatao 56 walikamatwa na bidhaa bandia zikiwemovilainishi vya magari, vifaa vya mabomba na kofia ngumuza pikipiki. Pia, Tume ilifanya operesheni saba (7) nakukamata bidhaa zilizokiuka Sheria ya Alama za Bidhaa katikamikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Iringa, Morogoro,Mtwara, Shinyanga, Songwe na Tanga. Katika opereshenihizo, watuhumiwa wapatao 94 walikamatwa na bidhaabandia zikiwemo dawa za meno na miswaki, wino (toner),mvinyo, vifaa vya ujenzi, vifaa vya mabomba, mabati yakuezekea, viatu na sabuni. Bidhaa zingine zilizokamatwa nimafuta ya maji ya kupaka, pampu za kumwagilia maji, majiya tindikali, na pikipiki. Vilevile, Tume iliendesha opereshenitano (5) za uteketezaji na kugawa bidhaa bandia zilizothibitika kukiuka Sheria ya Alama ya Bidhaa.

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

290. Mheshimiwa Spika, Tume imeendeleana mapambano dhidi ya bidhaa bandia kwa kushirikianana vyombo vingine vya Serikali vikiwemo TBS, TFDA na Jeshila Polisi nchini na Mtandao wa Polisi wa Kimataifa INTERPOL.Kupitia ushirikiano huo, Tume imefanikiwa kutekelezaoperesheni nne (4).

b) Uchunguzi na Usikilizaji wa Mashauri Ushindani;

291. Mheshimiwa Spika , Tume imeendeleakuchunguza makubaliano ya siri ambayo yanakiuka Sheriaya Ushindani katika maeneo mbalimbali yakiwemo; SektaNdogo ya Mafuta, Uuzaji na Ununuzi wa Vifaa Tiba na Hakiza Utangazaji wa Michuano ya Mpira wa Miguu.

c) Kuchunguza Mashauri yanayohusu Miunganoya Makampuni

292. Mheshimiwa Spika , Tume imeendeleakuchunguza miunganiko ya siri ambayo inakiuka Sheria yaUshindani (Un-notified mergers) katika maeneo mbalimbaliyakiwemo; Sekta ya Nishati na Madini, Sekta Ndogo ya Saruji,Mabenki, Utalii na Vinywaji baridi. Pia, Tume imepitishamaombi 28 ya muungano wa makampuni yaliyowasilishwambele ya Tume. Katika maombi hayo yaliyopitishwa, 17yalipitishwa bila masharti na 11 yalipitishwa kwa masharti.

d) Utekelezaji wa Sheria juu ya Mashauri yahusuyoMatumizi Mabaya ya Nguvu katika Soko (Abuse of MarketPower)

293. Mheshimiwa Spika , Tume imeendeleakuchunguza mashauri yanayohusisha matumizi mabayaya nguvu ya soko yanayofanywa na baadhi ya washindani.Mashauri hayo yalijitokeza katika maeneo mbalimbaliyakiwemo; sekta ndogo za tumbaku, filamu, benki navinywaji.

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

e) Utafiti wa Masoko il i KubainiMienendo Inayofifisha Ushindani katika Masoko

294. Mheshimiwa Spika, Tume imeendeleakukamilisha tafiti mbili (2) katika miradi mikubwa yaujenzi wa barabara nchini na sekta ndogo ya uzalishaji nausambazaji wa mbolea. Tafiti katika miradi ya ujenzi wabarabara inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha robo yatatu ya mwaka 2017/2018 wakati tafiti katika soko la mboleanchini upo katika hatua za awali za uandaaji wa conceptpaper na unategemewa kukamilishwa ifikapo robo yakwanza ya mwaka ujao wa fedha. Aidha, Tume itaendeleana mpango wake wa kufanya utafiti katika Sekta ya Afyakwa lengo la kubaini matatizo ya kiushindani katika sokohilo.

f) Kumlinda na Kumuelimisha Mlaji

295. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018malalamiko 39 ya walaji yaliwasilishwa ambapo malalamiko21 yalipatiwa ufumbuzi, malalamiko mawili (2) yanafanyiwauchunguzi, malalamiko tisa (9) yapo katika hatua yausuluhishi na malalamiko 7 yanaendelea kufuatiliwa. Aidha,asilimia 80 ya malalamiko yalihusiana na bidhaa zakielektroniki na asilimia 20 yalihusiana na vitendo hadaifu nadanganyifu sokoni. Tume ilitoa elimu kwa umma katikamaonesho ya wakulima ya Nane Nane yaliyofanyika kitaifamkoani Lindi na DITF yaliyofanyika Jijini Dar-es Salaam.Maonesho hayo ni fursa nzuri ya kuwaeleza wadau nawananchi kwa ujumla kuhusu shughuli za Tume, kugawa vitinina kufanya vipindi mubashara vya radio. Aidha, Tumeimeendesha vipindi 11 vya radio na kwenye luninga kwamadhumuni ya kuelimisha umma kuhusu haki na wajibu wamlaji na jinsi ya kuzitambua bidhaa bandia nchini.

296. Mheshimiwa Spika, pia, Tume iliendeshasemina kwa ajili ya wahariri wa vyombo vya habari kwalengo la kuhakikisha wadau hao wanapata uelewa wakuweza kuelimisha jamii kuhusu masuala ya utetezi wa mlajina udhibiti wa bidhaa bandia nchini. Makala tisa (9)zimetolewa katika magazeti mbalimbali yanayosomwa sana

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

zikielimisha umma kuhusu masuala ya utetezi wa mlaji,madhara ya bidhaa bandia na udhibiti wa bidhaa hizo.Tume imeandaa utaratibu wa kuanzisha vilabu (clubs) katikashule za msingi Mkoani Dodoma ili kujenga uelewa wamasuala ya utetezi wa mlaji kwa watoto ili kuwa na kizazikinachoelewa haki na wajibu wao wangali wadogo iliwaweze kujisimamia vizuri katika uchumi wa soko.

g) Kufanya Mapitio na Usajili wa Mikataba yaWalaji

297. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mweziJulai 2017 hadi Machi 2018, mikataba 196 ya walaji ilipokelewakwa ajili ya kupitiwa na kusajiliwa. Aidha, mikataba 24 yawalaji ilipitiwa na kusajiliwa na Tume baada ya kukidhi vigezokulingana na kanuni zinazo simamia mikataba ya walaji.

3.4.16 Baraza la Ushindania) Kusikiliza na Kutoa Maamuzi ya Kesi za Rufaa

298. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka 2017/2018, Baraza lilipokea kesi 46, kati ya hizo, rufaani 24 na maombi ni 22. Vilevile, kulikuwa na kesi 33 zilizokuwahazijaamuliwa katika kipindi cha 2016/2017 na hivyo kufanyakesi zinazopaswa kusikilizwa na kuamuliwa kwa mwaka2017/2018 kuwa 79. Hadi kufikia mwezi Machi, 2018, Barazaliliweza kusikiliza na kuamua kesi 25 na kesi 54 zilizobaki zipokatika hatua mbalimbali za usikilizwaji.

b) Kuongeza Uwezo wa Baraza Kushughulikia Kesizinazohusu Masuala ya Ushindani wa Kibiashara.

299. Mheshimiwa Spika, Baraza limewezeshawajumbe na watumishi wa Baraza kushiriki mafunzombalimbali kwa lengo la kuwaongezea ujuzi na taalumakatika kutekeleza majukumu yao. Aidha, mafunzo hayoyamejumuisha induction course kwa Wajumbe wa Baraza,mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi wawili (2) namafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 13. Mafunzo hayoyamejikita katika nyanja za utawala, uhasibu, manunuzi,huduma kwa wateja, sheria na kazi za Baraza.

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

c) Kuelimisha Umma kuhusu Kazi za Baraza300. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,

Baraza limetoa elimu katika masuala yanayohusu ushindaniwa kibiashara kupitia maonesho mbalimbali yakiwemoMaonesho ya DITF yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl. JuliusK. Nyerere vilivyopo katika Jiji la Dar es Salaam, Maoneshoya Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongomkoani Lindi, Maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katikaViwaja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam na Maadhimishoya Siku ya Haki za Mlaji Duniani yaliyofanyika Mkoani Kagera.

301. Mheshimiwa Spika, Baraza pia limetoa elimuya uelewa juu ya utendaji kazi wa Baraza na masualayanayohusu ushindani wa kibiashara kwa wadau waBaraza katika Mkoa wa Morogoro ambapo wadau waBaraza wakiwemo mahakimu, mawakili, waandishi wahabari pamoja na wawakilishi kutoka asasi za kidini na zisizoza kiserikali.

3.4.17 Chuo cha Elimu ya Biashara

a) Ujenzi ya Maktaba Mpya, Madarasa, Kumbiza Mihadhara katika Kampasi ya Dar es Salaam

302. Mheshimiwa Spika, uboreshaji wamiundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika Kampasiya Dar es Salaam umeanza na unatarajiwa kukamilika katikamwaka 2018/2019. Kazi zinazofanywa ni kuongeza ghorofanne katika jengo la zamani la Kafeteria ili kuweza kuongezakumbi za mihadhara, ofisi za walimu pamoja na maktabakubwa na ya kisasa. Gharama ya utekelezaji wa mradi huoni Shilingi 3,180,000,000 na tayari Chuo kimefanya upembuziyakinifu (Feasibility study) ya mradi huo.

b) Ujenzi na Ukarabati wa Majengo Kampasiya Mwanza

303. Mheshimiwa Spika, Chuo kimenunua eneo lenyeukubwa wa ekari 10.9 huko Nyasaka Mwanza ambaloawali lilikuwa ni Shule ya Sekondari Crest Hill. Eneo hilo linamajengo ambayo yalikuwa yakitumika kama ofisi na

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

madarasa. Chuo kimekarabati majengo ya madarasa, ofisiza walimu, hosteli pamoja na kafeteria. Kazi zinazofanywani kuweka vigae sakafuni, kupaka rangi, kuweka madirishana milango mipya kutandaza mfumo mpya wa mabombaya maji safi na maji taka, ukarabati wa vyoo na kubadilishamasinki. Gharama iliyotumika kufanya ukarabati huo ni ShilingiMilioni 800.

c) Kuboresha Mifumo ya TEHAMA

304. Mheshimiwa Spika, Chuo kimeboreshamifumo yake ya TEHAMA katika kampasi zote nne. Mifumohiyo inajumuisha kufunga mifumo ya kihasibu (PASTEL), nausajili wa wanafunzi uliounganishwa na wa kihasibu (SARIS).

d) Kuimarisha Uwezo wa Watumishi(Capacity Building)

305. Mheshimiwa Spika, watumishi 78 wapo katikamafunzo ya muda mrefu katika ngazi za shahada ya uzamivu(PhD), shahada ya uzamili (Masters degree), shahada yakwanza (bachelor degree) na stashahada (Diploma). Katiya wafanyakazi 40 wanaochukua shahada ya uzamivu,29 ni wanaume na 11 wanawake; 28 wanasoma ndani yanchi (21 wanaume, na 7 wanawake) na 12 wanasoma njeya nje (8 wanaume, na 4 wanawake). Kati ya watumishi32 wanaochukua shahada ya uzamili, 28 ni wanaume nawanne (4) wanawake; kati yao 22 wanasoma ndani ya nchi(18 wanaume, 4 wanawake) na 6 wanasoma nje ya nchi(wote wanaume). Kati ya watumishi wane (4) wanaochukuashahada ya awali, wawili (2) ni wanaume na wawili (2) niwanawake. Kwa upande wa stashahaha, watumishi ni wawili(2) ambao wote ni wanaume.

4.0 MWELEKEO WA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARANA UWEKEZAJI

306. Mheshimiwa Spika, tafsiri ya viwanda iliyotolewani taswira kuwa ujenzi wa uchumi wa viwanda unatazamwakuwa kiini cha mageuzi yenye kuleta mafanikio na mwelekeowa maisha bora na yenye furaha kwa kizazi cha sasa na

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

kijacho. Kwa maneno mengine, ujenzi wa uchumi waviwanda ni suala jumuishi, unganishi na shirikishi. Muunganiko(forward and backward linkage) wa uzalishaji katika Sektaya Viwanda na sekta nyingine ni muhimu katika uchumiwa nchi (economic complementarity). Tanzania inatambuaumuhimu huo na msingi mkuu wa ujenzi wa uchumi waviwanda umewekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo yamwaka 2025 ambayo imelenga kufikia uchumi wa kati waviwanda wenye muunganiko ifikapo mwaka 2025.

307. Mheshimiwa Spika, dhamira ya ujenzi wauchumi wa viwanda imefafanuliwa zaidi na kuwekewamikakati katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa MiakaMitano 2016/2017– 2020/2021. Msisitizo mkuu ni maendeleoya viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa nchinihususan mazao ya kilimo (mafuta ya kula, sukari, vyakula navinywaji), madini (chuma) na kemikali. Aidha, Serikaliimeahidi kusimamia na kutekeleza mipango hiyo kamailivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka2015. Vilevile, viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali wametoamsisitizo juu ya dhamira ya ujenzi wa uchumi wa viwandakupitia hotuba katika Bunge na mikutano mbalimbali.Miongozo hiyo ndiyo nguzo ya Sheria, Sera, Mikakati naMipango yote ya kisketa katika uwekezaji na ujenzi wa uchumiwa viwanda na kufanya biashara nchini.

308. Mheshimiwa Spika, Mpango wa MwakaMmoja wa Maendeleo wa Mwaka 2018/2019 unawekamsisitizo katika kushirikisha zaidi Sekta Binafsi kutumia fursazilizopo na vivutio vinavyotolewa na Serikali kujenga viwandavidogo sana, vidogo na vya kati ili kuchochea ujenzi waviwanda vipya na kuendeleza vilivyopo. Aidha, miradimikubwa ya viwanda vya kimkakati na vya kielelezoitaendelea kutiliwa mkazo.

309. Mheshimiwa Spika, kwa misingi hiyo,mwelekeo wa kisketa ni kuhakikisha kuwa, nyaraka zote zakisekta zinazoongoza uwekezaji, uzalishaji na ufanyajibiashara nchini zinaboreshwa kwa kuzingatia mazingira namatakwa ya nyakati hususan ushindani wenye haki na

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

kuwezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika kuzalishana kutumia mali, huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini.Lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa, mchango wa sekta katikaPato la Taifa unakua, ajira kwa Watanzania zinazalishwana kulindwa, bidhaa zinazalishwa kwa wingi hususan zilezinazotumika na wananchi walio wengi, uzalishaji wenyetija unahimizwa, kipaumbele kikiwa kutumia rasilimali zilizoponchini, viwanda vya ndani vinapata ulinzi wenye tija nashindani, viwanda vipya vinajengwa na kuendelezwa,viwanda vilivyopo vinaendelea kuzalisha kwa malengoyaliyokusudiwa na vile vyenye changamoto kupata tibastahiki.

310. Mheshimiwa Spika, katika ujenzi waviwanda, uendelezaji na ulinzi wa viwanda vidogo sana,vidogo na vya kati litakuwa jukumu letu la kipaumbele nakuhakikisha kuwa Taasisi zinazohusika kuendeleza viwandahivyo zinajengewa uwezo unaotakiwa kumudu majukumuna matakwa ya wadau katika maeneo yote nchini. Kuwekamifumo muhimu ikiwemo miundombinu ya msingi na saidizipamoja na ujenzi wa soko la ndani vitapewa msukumo wakipekee ili kuleta tija kwa gharama nafuu kwa wawekezajiwa ndani ya nchi yetu. Mipango ya kuboresha na kurahisishamazingira ya uwekezaji na biashara itaendelea kuwa ajendaya kudumu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenyemvuto kwa uwekezaji na kufanya biashara.

311. Mheshimiwa Spika, msukumo mkubwa kwasasa ni kuendeleza viwanda vidogo sana, vidogo na vyakati kutokana na mchango wake katika uchumi ulio shirikishi.Msingi wa msukumo huo ni kuwa viwanda vidogovinasambaa kirahisi katika kila kona ya nchi na pia viwandahivyo humilikiwa na wananchi wenyewe na hivyo inakuwarahisi kuviendeleza na kupanua wigo wa makusanyo ya kodi.Ndio maana hata sasa nchi zilizoendelea kiviwanda dunianikwa kiasi kikubwa uchumi wao unachangiwa na sekta hiyo.Mathalani, katika nchi ya Ujerumani sekta hiyo inachukuaasilimia 99 ya Sekta ya Viwanda, Marekani asilimia 99.7,Ufaransa asilimia 98, Australia asilimia 97 na Italia asilimia 98.

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

Kwa Bara la Afrika, nchi zilizopiga hatua kama vile AfrikaKusini, sekta hiyo inachukua asilimia 91 na Ghana asilimia 92ya viwanda vyote. Hivyo, ili kufikia azma ya uchumi waviwanda, hatuna budi kuelekeza nguvu kubwa katikakubuni mikakati ya uanzishwaji na uendelezaji wa viwandavidogo sana, vidogo na vya kati. Wizara itaendelea kuwekamazingira wezeshi pamoja na kubuni mikakati mbalimbaliili kuziwezesha shughuli za ujasiriamali mdogo na wa katikukua na kuongeza tija.

312. Mheshimiwa Spika, maelezo hayo yanalenga kukumbusha dhamira ya Taifa ya kujenga uchumi waviwanda na nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tanokutekeleza ajenda ya viwanda ili kuleta maendeleo endelevukwa kasi na maisha bora kwa Watanzania. Hivyo, vipaumbelena mipango kwa mwaka 2018/2019 inatokana na mipangoya kitaifa ambayo imeanishwa hapo juu.

313. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo,naomba sasa nielezee vipaumbele na malengo ya sekta kwamwaka 2018/2019.

5.0 VIPAUMBELE NA MALENGO YA MWAKA 2018/2019

5.1 VIPAUMBELE KWA MWAKA 2018/2019314. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/2019,

vipaumbele vya Wizara kwa kushirikiana na Taasisi zake nikutunisha mtaji wa NEDF; kuendeleza miradi ya kielelezo ya:Mchuchuma na Liganga, Magadi Soda Engaruka, na Kiwandacha Matairi Arusha; Uendelezaji wa Eneo la Viwanda TAMCOKibaha, Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS, uendelezajiwa Mitaa/maeneo ya viwanda vya SIDO; Kuendeleza KandaKuu za Uchumi (Ruvuma, Tanga, Kigoma na Manyoni);Bagamoyo SEZ & BMSEZ ; Kurasini Logistic Centre andKigamboni Industrial Park; Kuendeleza utafiti katika taasisiza TIRDO, CAMARTEC na TEMDO; Dodoma Leather andDodoma SEZ; na ujenzi wa industrial parks.

315. Mheshimiwa Spika, pamoja na vipaumbelehivyo, Wizara itaweka msukumo wa pekee katika

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

kuhamasisha ujenzi wa Sekta Binafsi ya Kitanzania iliyo imaraili iweze kushiriki na kuchangia ipasavyo katika ujenzi wauchumi wa viwanda.

5.2 MALENGO5.2.1 Sekta ya Viwanda316. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Sekta ya Viwanda ina malengo yafuatayo:-

(a) Kufanya tathmini ya hali halisi ya uzalishajiviwandani pamoja na mahitaji ya bidhaa za viwanda kwa:-

i) Kufanya tathmini ya sekta ya sukari;

ii) Kufanya tathmini ya sekta ya mafuta ya kula;iii) Kufanya tathmini ya sekta ya vifaa vya ujenzi; iv) Kufanyatathmini ya sekta ya chuma;

v) Kufanya tathmini ya sekta ya mbao na bidhaaza mbao;

vi) Kufanya tathmini ya sekta ya ngozi na bidhaa zangozi;

vii) Kufanya tathmini ya sekta ya nguo na mavazi;

viii) Kufanya tathmini ya sekta ya usindikaji vyakula(mchele, unga, mbaazi na vyakula vingine);

ix) Kufanya tathmini ya usindikaji wa vyakula vyabinadamu na wanyama; na

x) Kufanya tathmini ya dawa za binadamu navifaa tiba na vifungashio.

(b) Kufanya mapitio ya Sera ya MaendeleoEndelevu ya Viwanda ya mwaka 1996 – 2020 (SustainableIndustrial Development Policy - SIDP) na kuandaa Mkakatiwa Utekelezaji;

(c) Kujenga uwezo wa taasisi za utafiti za wizara kwa:-

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

i) kuimarisha uwezo wa maabara za utafiti;

ii) kuhamasisha usambazaji wa teknolojiazinazobuniwa na taasisi; na

iii) kuhamasisha Sekta Binafsi kutumia teknolojiahusika.

(d) Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi yaviwanda mama na Miradi ya Kimkakati kwa:-

i) Kukamilisha uchambuzi wa mikataba ya Mradikwa kuzingatia marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka2017;

ii) Kutafuta wawekezaji wa mradi magadi sodawa Engaruka na mradi wa kiwanda cha matairi cha Arusha;na

iii) Kukamilisha taratibu za kumpata mwekezaji nakuanza utekelezaji wa mradi wa Kurasini SEZ.

(e) Kuendelea na utekelezaji wa mikakati mikuuya kuendeleza sekta za alizeti, ngozi na bidhaa za ngozi,pamba mpaka mavazi, na viwanda vya dawa;

(f) Kuendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchinikwa:-

i) kuendelea kutenga maeneo ya uwekezajikwa kuzingatia msambao wa viwanda nchi nzima;

ii) kuendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kuwekezakatika sekta za kipaumbele na kuendeleza maeneo yauwekezaji; na

iii) kushiriki makongamano ya uwekezajiyatakayofanyika mikoa mbalimbali nchini.

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

5.2.2 Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo317. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo itatekelezamalengo yafuatayo:-

(a) Kuendelea kuhamasisha ujenzi wa viwandavidogo na biashara ndogo nchini kwa:-

i) Kushirikiana na Serikali ngazi ya Wilaya naMkoa kutenga maeneo ya ujenzi wa viwanda na biasharakwa kulenga mahitaji ya sasa na baadae;

ii) Kutengeneza kanzidata ya maeneo yaliyotengwakwa ajili ya viwanda vidogo na vya kati;

iii) Kuhamasisha wajasiriamali kuchangamkiamasoko ya ndani na nje ya nchi;

iv) Kuhamasisha ujenzi wa viwanda kupitiamwongozo wa ujenzi wa viwanda kwa Mamlaka za Tawalaza Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na

v) Kuhamasisha na kuelimisha wajasiriamali namnaya kuanzisha na kuendeleza biashara. Kitabu chenye taarifamuhimu za namna ya kuanzisha biashara nchini hasa kwawajasiriamali wadogo kitatumika.

(b)Kuwezesha uanzishwaji wa kongano la karangakwa:-

i) Kuhamasisha wajasiriamali kulima zaola karanga kwa lengo la kutumia nafasi ya konganolitakaloanzishwa la kuongeza thamani zao hilo; na

ii) Kutafuta rasilimali za kuendeleza kongano lakaranga.

(c) Kuendelea kufanya mapitio ya Sera yaMaendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo yamwaka 2003:

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

i) Kufanya tafiti za kina katikamaeneoyaliyoanishwa;

ii) Kukamilisha mfumo wa uratibu wa sekta; na

iii) Kukamilisha mfumo wa kuwezesha sektakifedha.

(d) Kuendelea kusimamia Mfuko wa NEDF kwa:-

i) Kuongeza mtaji wa Mfuko; na

ii) Kufuatilia maendeleo ya mfuko huo;

(e) Kutumia SIDO kama nyezo ya kujenga viwandavidogo na vya kati kwa:-

i) Kuendelea kulifanyia maboresho Shirika laSIDO; na

ii) Kuhamasisha ubunifu na matumizi ya teknolojiana viatamizi.

5.2.3 Sekta ya Uwekezaji

318. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,Wizara kupitia Sekta ya Uwekezaji itatekeleza malengoyafuatayo:

(a) Kuendelea kuratibu utekelezaji wa Sera yaUwekezaji ya mwaka 1996 kwa:-

i) Kuratibu uwepo wa mazingira bora yauwekezaji;na

ii) Kuendelea kuchochea uwekezaji nchini kupitiaushiriki kwenye mikutano, makongamano na warsha zauwekezaji zinazofanyika ndani na nje ya nchi;

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

(b) Kukamilisha mapitio ya Sera, Mkakati na Sheria yaUwekezaji kwa:-

i) Kukamilisha mapitio ya Sera ya Uwekezaji yamwaka 1996;

ii) Kukamilisha mapitio ya Sheria ya Uwekezaji ya1997;na

iii) Kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Sera yaUwekezaji.

(c) Kufuatilia miradi ya uwekezaji nchini kwa:-

i) Kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na tathminiya uwekezaji nchini; na

ii) Kufuatilia utekelezaji wa mikataba ya miradiiliyosajiliwa na TIC.

(d) Kuratibu kwa karibu uwekezaji katika sektamaalum kwa:-

i) Kuhamasisha uwekezaji katika kilimo cha miwana uzalishaji wa sukari;

ii) Kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya Uvuviwa Bahari Kuu (deep sea fishing) na viwanda vya samaki; na

iii) Kuboresha vivutio vya uwekezaji katika viwandavinavyozalisha ajira kwa wingi.

5.2.4 Sekta ya Biashara319. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/

2019, Wizara kupitia Sekta ya Biashara itatekeleza yafuatayo:-

(a) Kuendeleza majadiliano ya kibiashara kati ya Nchina Nchi (Bilateral), Kikanda (Regional) na Kimataifa(Multilateral) kwa ajili ya kupanua fursa za masoko nauwekezaji ili kuvutia uwekezaji nchini kwa:-

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

i) Kuendeleza majadiliano ya biashara kwenyenchi za China, Urusi, Mauritus, Uturuki, Misri, Israel, DRC Congo,Sudani ya Kusini, Vietnam na Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE) na kuingia nazo makubaliano ya biashara kwakushirikiana na sekta binafsi;

ii) Kuendelea na majadiliano ya kuanzishwa kwaEneo Huru la Biashara kwa Nchi za Afrika (Continental FreeTrade Area – CFTA);

iii) Kukamilisha majadiliano ya kuanzisha Eneo Hurula Biashara la Utatu linalojumuisha Kanda za COMESA, EACna SADC;

iv) Kukamilisha majadiliano ya biashara ya hudumakwa sekta sita za kipaumbele katika nchi wanachama waSADC;

v) Kutekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiyaya Afrika Mashariki kwenye masuala ya biashara ya bidhaana huduma; na

vi) Kuratibu na kushiriki kwenye majadiliano yabiashara ya kimataifa katika mashirika yaliyo chini yaUmoja wa Mataifa na mengineyo ikiwemo (WTO, UNCTAD,CFC na ITC).

(b) Kuhamasisha jumuiya ya wafanyabiashara kuhusufursa za masoko ya upendeleo yatakonayo na majadilianoya Nchi na Nchi, Kikanda na Kimataifa;

(c) Kukamilisha mapitio ya Sheria ya Anti-dumpingand Countervailing Measures;

() Kutekeleza Mkataba wa Shirika la BiasharaDuniani (WTO) unaohusu uwezeshaji wa Biashara;

(e) Kuendelea na mapitio ya Sera ya Taifa yaBiashara 2003;

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

(f) Kuimarisha kamati za kitaifa za kusimamiaurahisishaji wa biashara nchini ambazo ni; Kamati yakusimamia Uondoaji wa Vikwazo vya Kibishara visivyokuavya kiushuru (NTBs); Kamati ya Urahisishaji Biashara (NationalTrade Facilitation Committee); Kamati ya usimamizi wamasuala ya Afya za Binadamu, Wanyama na Mimea (NationalSPS Committee); na Kamati ya Vikwazo vya Biashara vyaKiufundi (National TBT Committee); na

(g) Kuandaa miradi na program mbalimbali kwaajili ya kujenga uwezo kwa wataalamu na sekta binafsi katikamajadiliano ya kikanda na kimataifa.

5.2.5 Sekta ya Masoko320. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Wizara kupitia Sekta ya Masoko itatekeleza malengoyafuatayo:-

(a) Kuendelea kuboresha mazingira yabiashara na uwekezaji kwa:-

i) Kuondoa tozo kero, ada zinazojirudiana kurazinisha majukumu ya taasisi za udhibiti;

ii) Kuondoa mwingiliano wa majukumu ya taasisi zaumma ili kupunguza gharama za uanzishaji na uendeshajiwa biashara;

ii i) Kuhakikisha huduma za usajil i wa biasharazinafanyika kupitia mitandao ya kompyuta (onlineregistration) na usajili wa makampuni ufanyike kwa mudamfupi kadiri iwezekanavyo; na

iv) Kuhamisha jukumu la utoaji wa leseni za biasharatoka Wizarani (Daraja A) kwenda BRELA na kutolewa katikakanda za Arusha, Dar, Dodoma, Mbeya, Mtwara na Mwanza.

(b) Kuwaunganisha wazalishaji na masoko kwa:-

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

i) Kuwahamasisha wakulima kuzalishana kuwaunganisha na viwanda vya usindikaji; na

ii) Kushirikiana na viwanda kutafuta masoko ndanina nje kwa bidhaa zinazozalishwa nchini;

(c) Kuendelea kuhamasisha matumizi ya mfumowa stakabadhi za ghala kwa:-

i) Kuhamasisha sekta binafsi kujenga maghala;

ii) Kuanzisha matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi zaGhala kwa maeneo yote yanayozalisha zao la korosho;

iii) Kuanzisha matumizi ya Mfumo kwa mazao yaufuta, mbaazi, mahindi na nafaka; na

iv) Kuunganisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala nasoko la mazao na bidhaa (commodity exchange).

(d) Kutafiti na kutafuta masoko mapya ndani na njeya nchi hususan katika nchi za Afrika Mashariki, DRC, China,Mashariki ya Kati, Mashariki ya mbali, Ulaya, na nchi nyinginekwa:-

i) Kuanisha mahitaji ya soko kwa kila zao nakuwaunganisha wazalishaji wa mazao husika na wanunuziwa ndani na nje ya nchi;

ii) Kuimarisha na kuboresha taarifa za uzalishaji,masoko na kusambaza taarifa kwa wadau katika mnyororowa thamani kupitia tovuti na aina nyingine za mawasiliano;

iii) Kuhamasisha na kutoa elimu kwa umma kuhusuumuhimu wa kutumia bidhaa na mazao yanayozalishwandani ya nchi; na

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

iv) Kuimarisha matumizi ya fursa za masoko nje yanchi kupitia mikataba ya ushirikiano kati ya nchi na nchi,Kanda na Kimataifa.

(e) Kuhamasisha matumizi ya Vituo maalum vyakuuzia mazao kwa:-

i) Kuhamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzishavituo maalum vya kuuzia mazao;

ii) Kusimamia matumizi ya vituo hivyo ili vitumike kwauuzaji na ununuzi wa mazao;

iii) Kuhamasisha ushindani katika ununuzi na uuzajiwa mazao ili mkulima apate bei nzuri; na

iv) Kusimamia na kuhimiza matumizi ya vipimo rasmikwa nia ya kumlinda mlaji.

(f ) Kuimarisha biashara na masoko ya mipakanikwa:-

i) Kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipangokujenga Vituo vya Pamoja Mipakani-OSBP;

ii) Kutoa elimu kwa jamii ya wafanyabiashara kuhusufursa na taratibu za kufanya biashara ya mipakani (crossborder trade); na

ii i) Kuwezesha wafanyabiashara hususanwafanyabiashara wadogo kufanya biashara ya mipakanikwa urahisi kwa kuboresha mazingira ya biashara kwakushirikiana na mamlaka nyingine mpakani.

(g) Kuhamasisha na kuwezesha wananchikutangaza bidhaa na huduma za Tanzania kwa:-

i) Kuwapatia mabanda wakulima, wajasiriamalina wafanyabiashara wadogo na makundi maalumkutangaza bidhaa kupitia maonesho;

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

ii) Kuratibu ushiriki wa wajasiriamali nawafanyabiashara wa Tanzania katika maonesho ya ndanina nje ya nchi; na

iii) Kuratibu ushiriki wa sekta binafsi na wataalam waSerikali katika safari maalum za kutafuta fursa za masoko njeya nchi.

(h) Kuimarisha na kuboresha Mfumo wa Ukusanyajiwa Taarifa za Masoko kwa:-

i) Kupanua wigo wa vyanzo na aina ya taarifaza masoko; na

ii) Kutoa vitendea kazi vya kisasa kwa vyanzovya taarifa na kukuza matumizi ya TEHAMA kukusanya nakusambaza taarifa muhimu za masoko.

(i) Kuandaa na kupitia Sera, Sheria na Kanunimbalimbali kwa:-

i) Kuandaa Sera ya Taifa ya Kumlinda Mlaji(National Consumer Protection Policy);

ii) Kuandaa Sera ya Ubora ya Taifa (National QualityPolicy);

iii) Kukamilisha Sera na Mkakati wa Miliki Bunifu;

iv) Kukamilisha marekebisho ya Sheria ya ViwangoNa. 2 ya mwaka 2009 na Kanuni zake;

v) Kukamilisha Marekebisho ya Sheria ya Haki Milikina Haki Shiriki ya Mwaka 1999;

vi) Kuandaa kanuni za utekelezaji wa marekebishoya Sheria ya Vipimo ya 2016;

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

vii) Kushirikiana na OR-TAMISEMI kuandaa sheria ndogoya kusimamia matumizi ya vipimo rasmi katika biashara ngaziya vitongoji, vijiji na wilaya; na

viii) Kuandaa Mkakati wa Kukuza Mauzo Nje.

(j) Kukamiliasha taratibu za kuridhia itifakiya Marakhesh kwa:-

i) Kukusanya maoni ya wadau kuhusu mkatabahuo,

ii) Kuchambua maoni ya wadau, na

iii) Kuandaa andiko kuhusu umuhimu wa kuridhiaitifaki hiyo

5.3 MALENGO YA TAASISI CHINI YA WIZARA

5.3.1 Shirika la Maendeleo la Taifa321. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) litatekeleza malengoyafuatayo,

(a) Kuendeleza mradi unganishi wa makaa yamawe Mchuchuma na Chuma cha Liganga kwa:-

i) kurejea tathmini ya mali zawananchi watakaopisha eneo la mradi na kulipa fidia;

ii) Kupitia upya vivutio kwa ajili ya uwekezaji,

iii) Kutangaza mradi kwa wawekezaji,

iv) kuelimisha wananchi kuhusu faida za mradi katikaMkoa wa Njombe; na

v) kuratibu na kufuatilia kazi za miradi

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

(b) Kuendeleza mradi wa kuzalisha Magadi waEngaruka kwa:-

i) Kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha eneo lamradi;

ii) kusimamia ujenzi wa miundombinu wezeshi;

iii) kulipa tozo ya ardhi;

iv) kufanya utafiti wa faida za kiuchumi za mradi; na

v) Kutangaza mradi kwa wawekezaji

(c) Kuendeleza mradi wa ufufuaji wa Kiwandacha Matairi Arusha kwa:-

i) kuandaa taarifa ya kina ya upembuzi yakinifuambayo inaweza kuvutia taasisi za fedha;

ii) kuratibu ununuzi wa mitambo na mashine zakiwanda;

iii) Kutangaza mradi kwa ajili ya kupata wawekezajina kulipa tozo ya ardhi.

(d) Kuendeleza mradi wa mashamba ya mpiraMorogoro na Tanga;

(e) Kuendeleza mradi wa kujenga miundombinukatika eneo la viwanda la TAMCO Kibaha kwa:-

i) kuratibu ujenzi wa mtandao wa barabaraza ndani ya eneo la mradi;

ii) Kujenga uzio kuzunguka eneo la mradi;

i i i) kusanifu na kujenga bwawa la maji taka(oxidation pond) na kusimamia shughuli za ujenzi.

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

(f) Kuendelea kutekeleza Mradi wa KuunganishaMatrekta aina ya URSUS katika eneo la TAMCO Kibaha kwa:-

i) Kugharamia uingizaji wa vifaa bandarinina kuvipeleka kwenye eneo la mradi;

ii) Kuratibu uunganishaji wa matrekta mapya,

iii) Kuratibu ujenzi wa kiwanda kipya,

iv) Kuratibu mauzo,

v) kusimamia uanzishwaji wa maeneo menginenane ya kufanya matengenezo ya matrekta yaliyounganishanchini; na

vi) kulipa tozo ya ardhi;

5.3.2 Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji waBidhaa Kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi

322. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji wa Bidhaa kwa ajiliya Mauzo Nje ya Nchi (EPZA) itatekeleza yafuatayo:-

a) Kukamilisha majadiliano na kuendelea kutekelezamiradi ya maeneo huru ya Bagamoyo SEZ na Benjamin MkapaSEZ kwa:-

i) Kufanya usanifu wa kina na ujenzi wamiundombinu ya ndani (Detail design of onsite infrastructure-Roads) katika eneo la kituo cha Teknolojia Bagamoyo(Bagamoyo Technological Park);

ii) Kuandaa nyaraka za kisheria kwa ajili ya mradiwa Bagamoyo SEZ;

iii) Kukamilisha hatua zote za utwaaji wa Ardhina kufanya upimaji wa eneo ili kupata hati miliki ya eneolililokwishalipiwa fidia katika eneo la Bagamoyo SEZ;

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

iv) Kuratibu uendelezaji wa mradi wa BagamoyoSEZ; na

v) Kukarabati miundombinu ya ndani ya eneo laBenjamin William Mkapa SEZ ikiwa ni pamoja na kukarabatimifumo ya uhifadhi na upitishaji wa maji na kujenga upyaukuta ulioanguka na kuweka kamera za ulinzi katika eneola Benjamini Mkapa SEZ.

b) Kutekeleza mradi wa Kurasini Trade and LogisticCentre (Kurasini SEZ) kwa:-

i) Kukamilisha malipo ya fidia kwa wakazi watatu(3) ambao nyumba zao hazikuthaminiwa awali baada yakurukwa na Mthamini Mkuu wa Serikali wakati wa zoezi laUthamini; na

ii) Kuwezesha kuanza utelekezaji wa mradi. c)Kuendeleza Maeneo ya SEZ kwa:-

i) Kumaliza malipo ya fidia katika maeneo ya SEZyaliyokwishafanyiwa uthamini ya Tanga; Kigoma, Ruvuma naManyoni;

ii) Kufanya utafiti wa faida za kiuchumi za mradikatika eneo maalum la uwekezaji Dodoma;

iii) Kufanya usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wamiundombinu ya ndani (Detail design of on siteinfrastructure (Roads, Water, Power and Telecommunication)katika eneo la Kigamboni Industrial Pack; na

iv) Kuratibu ulipaji wa fidia kwawananchi watakaopisha maeneo ya miradi.

5.3.3 Shirika la Utafiti na Maendeleo ya ViwandaTanzania

323. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO)limepanga kutekeleza yafuatayo:-

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

a) Kuendelea kutoa huduma za kitaalamuviwandani zenye lengo la kuongeza uzalishaji wa bidhaabora bila kuchafua mazingira na zinazolenga matumizi boraya nishati;

b) Kuanzisha na kuhakiki maabara ya makaaya mawe, na maabara ya mafuta na gesi itakayokuwa naviwango vya kimataifa na kuweza kutoa huduma bora kwawazalishaji viwandani;

c) Kuendelea na mchakato wa kufanyautafiti na kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa sektaya ngozi jinsi ya kupunguza uharibifu wa mazingira kwakuhifadhi na kurejesha taka za ngozi ili kutengeneza bidhaakama ‘Leather boards’;

d) Kuendelea na kukamilisha mchakatowa kuhakiki (Accreditation) na kuboresha maabara yachakula, mazingira, kemia, na maabara ya vifaa vya kihandisiili ziweze kufikia viwango vya kimataifa na kuweza kutoahuduma bora kwa wazalishaji viwandani;

e) Kuanzisha na kuhakiki (Accreditation) maabaraya vipimo vya chuma kigumu (Iron and Steel metallurgylaboratory);

f) Kufanya matengenezo ya vifaa vya maabara yamazingira, chakula na kemia;

g) Kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenyelengo la kuleta teknolojia mpya za uzalishaji, na

h) Kuhuhisha teknolojia ya kutumia sensorkufuatilia uzalishaji viwandani kwa wajasiriamali (sensorindustrial process monitoring).

5.3.4 Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini324. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/

2019, Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC)kitatekeleza yafuatayo:-

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

a) Kuendelea kufanya utafiti na kuunda teknolojiazinazolenga kuongeza tija na kupunguza kazi za sulubu nazenye kuchosha katika shughuli za kilimo vijijini;

b) Kuendelea kuhamasisha utengenezajiwa mashine za kilimo, zana za kilimo na teknolojia nyingineza ufundi vijijini;

c) Kusimamia utekelezaji wa kanuni za majaribiona ukaguzi wa zana za kilimo na teknolojia za ufundi vijijini;na

d) Kuendelea kuimarisha miundombinu yautafiti ya Kituo.

5.3.5 Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo325. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO)kitatekeleza yafuatayo:-

a) Kujenga miundombinu ya kiatamizi chateknolojia na biashara pamoja na kuwajengea uwezowajasiriamali wa kati na wadogo kuanzisha viwanda vyakuunda na kutengeneza mashine na mitambo;

b) Kuendelea na uboreshaji wa karakana na ofisiya usanifu pamoja na miundombinu ya Taasisi kwa ujumla;

c) Kupitia upya sheria iliyoanzisha Taasisi yaTEMDO, kutengeneza kanuni zake, na kujenga uwezo wawafanyakazi wa Taasisi kwa kuwapatia mafunzo ya mudamfupi na mrefu;

d) Kubuni na kuendeleza chasili cha mtambo wakukausha mazao ya kilimo ili kuongeza thamani;

e) Kubuni na kuendeleza chasili cha mtambomdogo wa kusindika chai;

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

f) Kubuni na kuendeleza utengenezaji wa mtambowa kuweka baridi (cold room) il i kuhifadhi bidhaambalimbali kama vile mboga mboga, mazao ya mifugo,bidhaa za hotelini, machinjio;

g) Kuendeleza chasili cha mtambo mdogowa kutengeneza brikwiti kutokana na vumbi la makaa yamawe;

h) Kuhamasisha utengenezaji kibiashara wateknolojia za kuzalisha bidhaa za marumaru kama vile vigaevya marumaru (ceramic tiles) kwa kutumia malighafizinazopatikana nchini;

i) Kufanya utafiti ili kubainisha mahitaji ya sokokatika teknolojia na huduma za kitaalamu pamoja nakutangaza shughuli za Taasisi kupitia vyombo vya habarina kushiriki kwenye maonesho ya kibiashara (DITF, Nane Nane,Maonesho ya kanda ya SIDO) ili kutangaza teknolojiazinazobuniwa na Taasisi; na

j) Kuanzisha na kuwezesha mpango wakusambaza viwanda nchini kwa utaratibu wa kiwandakimoja kila wilaya (One District One Factory - ODOF).

5.3.6 Kampuni ya Mbolea Tanzania326. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) itatekeleza yafuatayo:-

a) Kusambaza mbolea tani 95,000 za aina ya DAP(tani 30,000), UREA (tani 30,000), SA (tani 5,000), CAN (tani5,000), NPK (tani 10,000), SULPHUR (tani 15,000) nchi nzima;

b) Kukamilisha majadiliano na kusaini mkataba waushirikiano baina ya Kampuni ya TFC kwa upande wa Serikaliya Tanzania na: OCP-SA kwa upande wa Serikali ya Moroccokuhusu mbolea aina ya DAP; na Kampuni ya Sirius PLC yaUingereza utakaohusu mbolea za aina ya NPKs; na

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

c) Kufanikisha uagizaji wa tani 15,000 za Sulphur yaunga.

5.3.7 Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo327. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) litatekelezamalengo yafuatayo:-

a) Kuendeleza Mitaa ya Viwanda ya SIDO nakutengeneza Mfumo Unganishi wa shughuli za TEHAMA zaShirika kwa:-

i) Kujenga miundombinu ya viwanda(barabara mifumo ya maji, umeme, mitaro, ya maji taka nauzio) katika mikoa ya Morogoro, Mara, Shinyanga, Lindi,Songea, Sumbawanga na Singida;

ii) Kujenga majengo (industrial sheds) ya viwandakatika mikoa ya Morogoro, Katavi, Simiyu na Njombe;

iii) Kujenga ofisi tatu (3) za kutolea huduma katikaMikoa ya Morogoro, Songwe na Katavi;

iv) Kuhamasisha matumizi ya majengo ya shughuli zaviwanda industrial sheds; na

v) Kutengeneza mfumo unganishi wa shughuli zaTEHAMA za Shirika.

b) Kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vidogo nakati chini ya Mkakati wa Bidhaa Moja Wilaya Moja (ODOP)kwa:-

i) Kuboresha karakana za kutengenezea mashinena mitambo mbalimbali katika mikoa ya Arusha, Mbeya naShinyanga; na

ii) Kuwezesha upatikanaji teknolojia zakutengeneza vifungashio.

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

c) Kuwezesha uhawilishaji wa teknolojia kwa:-

i) Kuimarisha Vituo vya Uendelezaji Teknolojia(TDCs) vilivyopo Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya naShinyanga; na

ii) Kuanzisha vituo vya kiatamizi kwa ajili ya kuendelezateknolojia na ubunifu katika Mikoa ya Singida, Arusha, Lindina Mwanza.

d) Kuendesha Mfuko wa WafanyabiasharaWananchi (NEDF) kwa:-

i) Kutoa mikopo kwa wajasiriamali;

ii) Kutoa elimu ya uendeshaji miradi inayohusika namikopo; na

iii) Kufuatilia urejeshwaji wa mikopo.

5.3.8 Kituo cha Uwekezaji Tanzania328. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kitatekeleza yafuatayo:-

a) Kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusushughuli za TIC;

b) Kuhamasisha, kuvutia na kuwezesha uwekezajikwa kushiriki na kuandaa makongamano ya biashara nauwekezaji ndani na nje ya nchi;

c) Kuendelea kusajili miradi ya uwekezaji nchini;

d) Kuendelea kuboresha huduma za mahalapamoja kwa wawekezaji kwa kuongeza taasisi zinazohusikakutoa huduma kwa wawekezaji na kuongeza maofisa katikataasisi zilizopo;

e) Kuweka taarifa zote zinazohusiana na utaratibuwa usajili miradi na utoaji wa vibali na leseni za taasisi

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

mbalimbali kwa mfumo wa huduma za mahala pamoja(One Stop Shop) kwenye jarida moja;

f) Kupitia mkataba wa huduma kwa wawekezaji ilikuuboresha na kusimamia utekelezaji wake;

g) Kushirikiana na mamlaka za Serikali kutafutamaeneo yanye ardhi inayofaa kuwekeza kwa ajili yawawekezaji na pia kushirikisha Sekta Binafsi kujengamiundombinu ya uwekezaji wa viwanda (Industrial Parks);

h) Kutoa huduma ya haraka kwa wawekezajiwaliosajiliwa ili kutatua changamoto zinazokwamishakuanza utekelezaji wa miradi;

i) Kutekeleza mkakati wa kuperemba miradiiliyosajiliwa kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaaili kujua faida halisi kiuchumi zinazotokana na miradi hiyokama kiasi cha ajira, mitaji na matumizi ya vivutiovinavyotolewa na Serikali; na

j) Kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kuishauriSerikali jinsi ya kuboresha sera ya uwekezaji nchini.

5.3.9 Shirika la Viwango Tanzania329. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha

mwaka 2018/2019, Shirika la Viwango Tanzania (TBS)litatekeleza yafuatayo:-

a) Kutayarisha viwango 400 vya kitaifa katika sektandogo ndogo, ambavyo kati ya hivyo 180 ni vya uhandisi(Engineering) na 220 ni vya usindikaji (Process Technology);

b) Kutoa leseni za ubora kwa bidhaa 300 kutoka katikasekta mbalimbali zikiwemo bidhaa za wajasiriamali wadogo(SMEs);

c) Kukagua ubora wa bidhaa 36,000 zitokazo nchiza nje kabla ya kuingia nchini [Pre-Shipment Verification ofConformity to Standards - PVoC (CoCs)];

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

d) Kufanya ukaguzi wa ubora na kutoa leseni zaukaguzi 40,000 za magari yaliyotumika (used motor vehicles)yanayoingizwa nchini;

e) Kutoa hati 40 chini ya mpango wa msaada wakiufundi kwa wauzaji wa bidhaa za nje (Technical Assistanceto Expoters - TAE);

f ) Kutoa mafunzo na semina 32 kuhusu viwango naudhibiti wa ubora (Quality Assurance Training) kwa wadaumbalimbali;

g) Kupima sampuli 21,000 za bidhaa mbalimbali;

h) Kufanya ugezi kwa vifaa/mashine mbalimbalivipatavyo 9 ,000;

i) Kuanzisha ofisi mpya 3 za mipakani;

j) Kuendelea na ujenzi wa maabara mpya ya Kisasa(New TBS Test House); na

k) Kuendelea kusimamia ubora wa bidhaa hasazinazotoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani kwakushirikiana na taasisi nyingine za umma.

5.3.10 Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni330. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) itatekelezayafuatayo:-

a) Kuendelea kuboresha mifumo na taratibu za utoajihuduma kwa kutumia njia za kiteknolojia ili kutoa hudumabora na kwa wakati kwa:-

i) Kuendeleza mfumo wa kutoa huduma kwanjia ya Mtandao (ORS) ;

ii) Kuunganisha mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao(ORS) na mifumo ya taasisi nyingine za Serikali; na

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

iii) Kuingiza taarifa za Makampuni na Majina yaBiashara yaliyosajiliwa nje ya Mfumo wa ORS katika kanzidataya mfumo mpya.

b) Kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchikwa kushirikiana na ofisi za maafisa biashara katika ngazi zamikoa na wilaya kwa kuanzisha vituo elimishi na saidizi katikaofisi za maafisa Biashara katika ngazi za Mkoa na Wilaya.

c) Kupitia sheria zote zinazosimamiwa na Wakala iliziweze kwenda na wakati na kuwezesha utoaji wa hudumazetu kwa njia ya mtandao;

d) Kutoa elimu na kuendeleza uhamasishaji wa usajilina urasimishaji wa biashara kwa,

i) Kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji wausajili na urasimishaji wa biashara kwa wananchi katika ngaziza Mikoa na Wilaya kwa kushirikiana na maafisa biasharakote nchini; na

ii) Kuendesha mafunzo na warsha mbalimbali kwamaafisa biashara mikoani na wilayani ili waweze kujuamajukumu ya wakala na namna ya kutumia mifumo yakekwa lengo la kuwasaidia wananchi katika utoaji hudumaza wakala mikoani na wilayani.

5.3.11 Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala331. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB)itatekeleza yafuatayo:-

a) Kuainisha na kufanya ukaguzi wa ghalazinazotumika chini ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala;

b) Kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mfumowa Stakabadhi za Ghala katika maeneo husika;

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

c) Kutoa elimu ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghalakwa wadau wote il i wapate uelewa wa jinsi mfumounavyofanya kazi;

d) Kupanua wigo wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghalakatika mazao ya nafaka na mbegu za mafuta; na

e) Kuanzisha mfumo wa mawasiliano wa wadaukutoa maoni kwa njia ya mtandao kuhusu utekelezaji wamfumo;

5.3.12 Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania

332. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA)kitatekeleza yafuatayo:-

a) Kuhakikisha wabunifu wa kazi zasanaa wananufaika kwa kupata mirabaha stahiki ili:-

i) Kuongeza makusanyo ya mirabaha kutokakwa watumiaji wa kazi za hakimiliki na kugawa kwa wabunifuhusika;

ii) Kuendelea kusajili wanachama wabunifu nakazi zao;

b) Kutoa elimu kwa Umma na wabunifu kuhusianana masuala ya Hakimiliki na Hakishiriki;

c) Kufanya ukaguzi wa kazi zinazolindwa na Sheriaya Hakimiliki na Hakishiriki (anti piracy raids);

d) Kusimamia na kuhamasisha mashirika yaUtangazaji kulipa mirabaha ya kazi za wasanii; na

e) Kushughulikia migogoro na kesi za Hakimiliki naHakishiriki.

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

5.3.13 Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania333. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)itatekeleza yafuatayo:-

a) Kutafuta masoko ya bidhaa za viwandani, mazaona bidhaa za mazao ndani na nje ya nchi;

b) Kutangaza bidhaa na huduma zinazozalishwanchini katika masoko ya ndani na nje ya nchi kupitiamaonesho ya kimataifa ya biashara;

c) Kuratibu na kudhibiti uendeshaji wa maoneshoya kimataifa nchini;

d) Kuimarisha Sekta Ndogo ya Biashara (SMEs) kwakutoa mafunzo na taarifa za biashara na masoko; na

e) Kuendeleza Fursa za Biashara na Masoko yaNdani;

5.3.14 Wakala wa Vipimo334. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Wakala wa Vipimo (WMA) itatekeleza yafuatayo:-

a) Kusimamia, kuhakiki na kukagua vipimo vyotevitumikavyo na viingiavyo nchini kwa lengo la kumlindamlaji;

b) Kuendelea na ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwakwenye maeneo ya mipakani, bandarini, na viwandani kwalengo la kuhakiki usahihi wa kiasi/ Idadi iliyotamkwa (decraledquantity);

c) Kununua vitendea kazi yakiwemo magari 10 navitendea kazi vya kitaalam (Gas Mobile Prover, ElectricityMeter Test Bench na Optical Scanner for Verification of fuelTanks);

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

d) Kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihiya vipimo;

e) Kuongeza idadi ya watumishi (Maafisa Vipimo 100na Maafisa vipimo wasaidizi 50); na

f ) Kujenga ofisi ya Makao Makuu ya Wakala waVipimo Mkoani Dodoma na Kuboresha ofisi za Wakala zaMikoa.

5.3.15 Tume ya Ushindani335. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Tume ya Ushindani (FCC) itatekeleza yafuatayo:-

a) Kuboresha hali ya ushindani katika soko(Competition Protection and Promotion improved) kwa:-

i) Kuharakisha uchunguzi na kufanya maamuzi kwenyemashauri 15 yaliyoko mbele ya Tume;

ii) Kufanya tafiti tatu (3) katika sekta mbalimbali zenyelengo la kubaini mienendo inayokinzana na Sheria yaUshindani; na

iii) Kutoa elimu na ushawishi juu ya uelewa waSheria ya Ushindani katika soko.

b) Kumlinda mlaji dhidi ya mienendohadaifu (Consumer Protection Enhanced) kwa:-

i) Kufanya uchunguzi wa malalamiko ya walajijuu ya vitendo hadaifu vya wafanyabiashara nchi nzima nakuyatatua;

ii) Kuelimisha umma juu ya haki na wajibu wa mlajikupitia semina na vipindi vya vyombo vya habari kwa nchinzima; na

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

iii) Kuongeza mapambano dhidi ya bidhaa bandiana pia kuhakikisha kiwango cha bidhaa hizo kinapunguakatika soko.

c) Kuongeza ufanisi katika kutoa huduma (Servicedelivery capacity improved) kwa:-

i) Kuboresha vitendea kazi kwa kununua magari 13mapya na kuyaondoa magari chakavu na kuweka mifumoya kielektronikia ndani ya Tume;

ii) Kuongeza wafanyakazi mpaka kufikia 85ukilinganisha na idadi ya sasa ya wafanyakazi ambao ni 53;na

iii) Kuanzisha ofisi Dodoma na ofisi za kanda katikamikoa ya Mwanza, Tanga na Mbeya.

5.3.16 Baraza la Ushindani336. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/

2019, Baraza la Ushindani (FCT) litatekeleza yafuatayo:-

a) Kupokea, kusikiliza na kutoa maamuzi ya kesi 35za rufaa zinazotokana na mchakato wa udhibiti wa ushindaniwa kibiashara nchini;

b) Kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwaWatumishi wa Baraza na Wajumbe wa Baraza kwa lengola kuwaongezea uwezo; na

c) Kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusumajukumu ya Baraza na namna ya kuwasilisha rufaa katikaBaraza.

5.3.17 Chuo Cha Elimu ya Biashara337. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,

Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) itatekeleza yafuatayo:-

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

a) Kuendeleza na kumalizia ujenzi wa ghorofa nne(4) katika jengo la ‘Cafeteria’ (Vertical Extension of CafeteriaBuilding) Kampasi ya Dar es Salaam;

b) Ununuzi wa shule na majengo katika eneo laNyasaka kwa ajili ya upanuzi na matumizi ya Kampasi yaMwanza;

c) Ujenzi wa Kampasi ya Mbeya katika eneo la Iganzo;

d) Kuandaa Mpango Kamambe (Master Plan) katikaKampasi ya Zanzibar;

e) Kuboresha Maktaba pamoja na mifumo yaTEHAMA ikiwa ni pamoja na kuboresha Computer Labs 2 ilikuongeza ufanisi wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia;

f) Kuendeleza rasilimali watu kupitia mafunzo yamuda mrefu (Human Resources Development);

g) Kufanya upembuzi yakinifu wa kuanzisha kampasikatika ukanda wa Kaskazini wa nchi;

h) Kufanya upembuzi yakinifu katika ujenzi wamiundombinu kupitia ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi(Public Private Partnership – PPP); na

i) Kuimarisha miundombinu na kufanya ukarabatiwa majengo wa kuimarisha uzio wa makazi ya watumishiwake Oysterbay, kuezeka upya hema la mihadhara Kampasiya Dar es Salaam na ukarabati wa madarasa na ofisi.

5.4 MAENDELEO YA RASILIMALI WATU NA UTOAJIHUDUMA

338. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara itatekeleza yafuatayo:-

a) Kuhamisha watumishi 70 waliobaki katika awamuya tatu kuja Dodoma;

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

b) Kuajiri watumishi wapya 25 wa kada mbalimbaliili kukidhi mahitaji ya Wizara;

c) Kupandisha vyeo watumishi 183 wa kadambalimbali;

d) Kujenga uwezo kwa rasilimali watu kwakuwapeleka watumishi kumi na wanane (18) mafunzo yamuda mrefu na watumishi arobaini (40) katika mafunzo yamuda mfupi ndani na nje ya nchi;

e) Kutathmini utendaji kazi watumishi (236) kwa kipindicha mwaka mzima 2018/2019 kwa kutumia Mfumo waWazi wa Mapitio ya Tathmini ya Utendaji Kazi (MWAMTUKAau OPRAS);

f ) Kujenga na kulinda afya za watumishi kwakuandaa programu mbalimbali za michezo yakiwemobonanza;

g) Kuendelea kuratibu shughuli za utoaji hudumastahiki kwa viongozi na watumishi wa Wizara kwa kuzingatiaTaratibu, Miongozo, Kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma;na

h) Kuhakikisha watumishi watakaohitimisha ajirazao wanalipwa mafao kwa wakati.

5.5 MASUALA MTAMBUKAa) Kupambana na Rushwa

339. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara itaongeza jitihada za kupambana na kudhibitirushwa kwa kuweka na kutekeleza mikakati mbalimbalipamoja na kutoa mafunzo ya sheria, miongozo, kanuni namaadili ya utumishi wa Umma. Wizara itahakikisha, watumishiwanazingatia kanuni na taratibu zinazotoa miongozo katikakutoa huduma bora na uwajibikaji katika utumishi waumma. Aidha, Wizara haitasita kuwachukulia hatua zakinidhamu watumishi wote ambao itabainika kuwa

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

wanajihusisha na vitendo vya rushwa. Pia, Wizara itaendeleakutoa mafunzo kwa watumishi na kusimamia utekelezaji waMkataba wa Huduma kwa Mteja katika utoaji huduma borakwa wateja wa ndani na nje ya Wizara.

b) UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza

340. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/2019,Wizara itaendelea na jitihada za kupambana namaambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) mahala pa kazipamoja na kutoa huduma bora kwa watumishi wanaoishina Virusi vya UKIMWI waliojiweka wazi kwa mujibu waMwongozo wa Serikali. Aidha, Wizara itaendelea kuandaasemina za kuelimisha na kuwahamasisha watumishikujikinga na VVU pamoja na Magonjwa SuguYasiyoambukiza (MSY) na kuzingatia upimaji wa afya kwahiari ili kuendeleza kampeni ya ujenzi wa afya bora kwawatumishi jambo ambalo ni muhimu kwa uchumi waviwanda.

c) Mazingira341. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha

mwaka 2018/2019, Wizara itaendelea kuhamasisha uelewawa athari za mazingira kwa wenye viwanda nawafanyabiashara sambamba na kuwashauri kutumiateknolojia rafiki (cleaner production technologies) kwamazingira.

d) Masuala ya Jinsia342. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/2019,

Wizara itaendelea kuhamasisha na kuhuisha masuala ya jinsiakatika sera, mipango na mikakati ya kisekta; kushirikikatika mikutano ya kitaifa na kimataifa katika masuala yakijinsia; na kuwajengea uwezo waratibu wa masuala ya jinsiaWizarani na katika taasisi zilizo chini ya Wizara juu ya uratibuwa masuala ya jinsia, ufuatiliaji na tathmini.

5.6 UDHIBITI WA MATUMIZI343. Mheshimiwa Spika, Wizara itahakikisha matumizi

yanafanyika kwa kuzingatia Kanuni, Taratibu na Sheria za

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

fedha za Serikali. Wizara itaendelea kuimarisha Kitengocha Ukaguzi wa Ndani ili waweze kuhakikisha taratibu zoteza fedha zinafuatwa na malipo yanafanyika kulingana navipaumbele vilivyowekwa kwenye bajeti ya Wizara.

6.0 MAOMBI YA FEDHA MWAKA 2018/2019

6.1 MAPATO YA SERIKALI

344. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,Wizara inatarajia kukusanya Shilingi 20,006,300,000 kutokanana uuzaji wa nyaraka za zabuni, ada za leseni na marejeshoya mshahara endapo mtumishi ataacha kazi.

Jedwali Na. 2: Mchanganuo wa Maduhuli na Makusanyokwa Mwaka 2018/2019

(a) Fungu 44

Maelezo Kiasi (Shs).

Uuzaji wa Nyaraka za Zabuni na Marejesho ya Mishahara.

5,300,000

JUMLA FUNGU 44 5,300,000  

(b) Fungu 60

Uuzaji wa Leseni za Biashara, Faini kutokana na kukiuka Mashariti ya Leseni na Marejesho ya Mishahara.

20,001,000,000

JUMLA FUNGU 60 20,001,000,000

JUMLA KUU (FUNGU 44 NA FUNGU 60)

20,006,300,000  

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

6.2 MAOMBI YA FEDHA345. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/

2019, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inaombakutengewa Shilingi 143,334,153,648, kati ya hizo, Shilingi43,309,628,648 ni za Matumizi ya Kawaida na Shilingi100,024,525,000 ni za Matumizi ya Maendeleo.

Jedwali Na. 3: Mchanganuo wa Fedha kwaMwaka 2018/2019 Fedha zilizotengwa 2018/2019

(Tshs.) (a) Fungu 44

Matumizi ya Kawaida

Mishahara 19,193,110,000

Matumizi Mengineyo

5,069,373,000

Jumla Ndogo 24,262,483,000

Matumizi ya Maendeleo

Fedha za Ndani 90,500,000,000

Fedha za Nje 2,524,525,000

Jumla Ndogo 93,024,525,000

Jumla Fungu 44: 117,287,008,000

(b) Fungu 60  

Matumizi ya Kawaida

Mishahara 17,077,055,000

Matumizi Mengineyo

1,970,090,648

Jumla Ndogo 19,047,145,648

Matumizi ya Maendeleo

Fedha za Ndani 7,000,000,000

Fedha za Nje 0

Jumla Ndogo 7,000,000,000

Jumla Fungu 60 26,047,145,648

Jumla Kuu (Fungu 44 na 60)

143,334,153,648

 

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

Jedwali Na. 4: Mgawanyo wa Fedha za OC (Mishahara naMatumizi Mengineyo) kwa Mwaka 2018/2019

Jedwali Na. 5: Mchanganuo wa Matumizi ya Fedha zaMaendeleo katika Fungu 44 na Fungu 60 kwa Mwaka 2018/2019

FUNGU

Jina la Fungu

Mishahara

Matumizi Mengineyo

Jumla

44 Viwanda 2,940,928,000 5,069,373,000 8,010,301,000

44

Mashirika chini ya Fungu 44

16,252,182,000

0

16,252,182,000

60

Biashara na Uwekezaji

1,164,224,000

1,887,909,000

3,052,133,000

60

Mashirika chini ya Fungu 60

15,912,831,000

82,181,648

15,995,012,648

JUMLA KUU 36,270,165,000 7,039,463,648 43,309,628,648

 

FUNGU

AINA YA MATUMIZI

KIASI (Tshs)

44 Fedha za Maendeleo za ndani

90,500,000,000

44 Fedha za Maendeleo za nje.

2,524,525,000

Jumla Fungu 44 93,024,522,000

60 Fedha za Maendeleo za ndani

7,000,000,000

Jumla Kuu Fungu 60 7,000,000,000

Jumla Kuu fungu 44 na 60 100,024,525,000

 

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

6.3 MATUMIZI YA FEDHA ZA MAENDELEO

6.3.1 Fungu 44346. Mheshimiwa Spika, katika fedha

zilizotengwa kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo, fedha zandani, zimeelekezwa katika Miradi Mikubwa ya Kielelezo;Miradi ya Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda;Uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi; Uendelezaji waEneo la Viwanda TAMCO Kibaha; Kuendeleza Kongano zaViwanda; Kuendeleza Tafiti za Maendeleo ya Viwanda;Kuendeleza Viwanda Vidogo, Biashara Ndogo, Ujasiriamalina Kuongeza mtaji kwenye mfuko wa NEDF. Miradi hiyo niifuatayo:-

a) Miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na ChumaLiganga imetengewa Shilingi 10,000,000,000.00 ili kurejeatathmini ya mali za wananchi watakaopisha eneo la mradi,kuratibu na kufuatilia kazi za miradi ya Makaa ya MaweMchuchuma na Chuma Liganga, na kuelimisha wananchikuhusu faida za mradi katika Mkoa wa Njombe;

b) Mradi wa Magadi Soda katika Bonde la Engarukaumetengewa Shilingi 2,000,000,000.00 kwa ajili ya kufanyautafiti wa faida za kiuchumi, mazingira na kujengamiundombinu ya maji safi;

c) Kiwanda cha Matairi Arusha kimetengewa Shilingi200,000,000.00 kwa ajili ya kutafuta wawekezaji na kuratibumradi huo;

d) Uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumiumetengewa Shilingi 22,715,918,000 inajumuisha kanda zaBagamoyo (Technological Park), Tanga, Kigoma, Ruvuma,Dodoma na Manyoni ikiwa ni pamoja na Uanzishwaji waKituo cha Biashara cha Kurasini; na Kigamboni Industrial Pack.

e) Uendelezaji wa Eneo la ViwandaTAMCO umetengewa Shilingi 13,000,000,000.00, kati ya hizoShilingi 11,000,000,000.00 ni kwa ajili ya uendelezaji wamiundombinu ya Eneo la Viwanda TAMCO na Shilingi

Page 218: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

2,000,000,000 ni za kuendeleza viwanda vya nguo na Mradiwa kuunganisha matrekta ya URSUS;

f) Uendelezaji wa Kongano za Viwanda umetengewaShilingi 1,000,000,000.00 kwa ajili ya Kongano la Ngozi nabidhaa za ngozi Dodoma;

g) Uendelezaji wa Tafiti za Maendeleo ya Viwandaumetengewa Shilingi 10,000,000,000.00 kwa ajili ya kuendelezatafiti za maendeleo ya viwanda katika Taasisi za TIRDO,TEMDO na CAMARTEC;

h) Uendelezaji wa Viwanda Vidogo, Biashara Ndogona Ujasiriamali umetengewa Shilingi26,834,082,000.00,ambapo Shilingi 11,834,082,000 ni kwa ajili ya kujenga maeneoya viwanda katika mikoa ya Manyara, Mtwara, Dodoma,Kagera, Njombe, Katavi, Geita na Simiyu; Shil ingi5,000,000,000.00 kwa ajilli ya kutekeleza Mkakati wa BidhaaMoja kwa kila Wilaya – ODOP; na Shilingi 10,000,000,000.00 nikwa ajili ya kuongeza mtaji Mfuko wa NEDF;

i) Chuo cha Elimu ya Biashara –CBEkimetengewa Shilingi 700,000,000 ikiwa ni mchango waSerikali katika kuboresha miundombinu inayojumuisha ujenziwa kumbi za mihadhara, ofisi za walimu pamoja na maktabakatika kampasi ya Mwanza;

j) Mradi wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II)umetengewa Shilingi 2,500,000,000.00 ni kwa ajil i yakuchochea uongezaji thamani wa bidhaa za ngozi (Shilingi620,000,000); kuboresha na kuanzisha viwanda vinavyosindikamazao ya kilimo ikiwemo mihogo, alizeti na pamba (Shilingi380,000,000,00); kubainisha miundombinu ya uchakataji wamazao ya kilimo kwenye mnyororo wa thamani uliopo(Shilingi.220,000,000); kufanya upembuzi yakinifu katikakuanzisha kongano la karanga Mpwapwa (Shil ingi.240,000,000); kujenga miundombinu muhimu kwenyekongano la karanga mpwapwa (Shilingi 540,000,000); nakuratibu, Kufuatilia na Kutathmini utekelezaji wa Mradi waASDP (Shilingi 500,000,000); na

Page 219: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

k) Mchango wa Serikali katika Miradiinayofadhiliwa na Washirika wa Maendeleo (CounterPartFund) umetengewa Shilingi1,550,000,000 inayojumuisha miradiya UNIDO, (Programme for Coutry Partneship- CPC) Shilingi1,000,000,0000; miradi ya KAIZEN Shilingi 200,000,0000; TradeMainstreaming Shilingi 250,000,0000 na Gender Shilingi100,000,0000.

6.3.2 Fungu 60347. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018,

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Fungu la 60(Biashara na Uwekezaji) imetenga Shilingi 2,000,000,000 nikwa ajili ya TBS kuendeleza ujenzi wa maabara ya kisasaikiwemo maabara ya kisasa ya kemia; Shilingi 900,000,000 nikwa jili ya COSOTA kuboresha mfumo wa usajili wa kazi nawanachama wanaojishughulisha na kazi za ubunifu kwa njiaya mtandao; na Shilingi 1,400,000,000 ni kwa ajili ya Bodi yaStakabadhi ya Maghala (WRRB) kugharamia ujenzi wa ghalala kimkakati mkoani Dodoma lenye uwezo wa kutunza tani30,000 kwa wakati mmoja, pamoja na miundombinu yaukaushaji kwa ajili ya kuhifadhia mahindi, Karanga na Alizeti.Pia Shilingi 1,300,000,000 ni kwa Wakala wa Vipimo, kati yakeShilingi 500,000,000 ni kwa ajili ya kununua optical scanner yauhakiki wa matenki makubwa ya mafuta, Shilingi450,000,000ni kwa ajil i ya ununuzi wa gari la uhakiki wa vipimo(Verification Truck with Crane) kwa ajili ya kupima mizanimikubwa inayotumika kwenye udhibiti wa matumizi yaBarabara na Biashara ikiwemo ya mazao ya Korosho, Pambana Shilingi 100,000,000 za ununuzi wa vipimo vya uhakiki wavifaa vya kupima kasi ya Magari (Speed Detectors Standards)na Shilingi 250,000,000 kwa ajili ya kununua mizani na maweya upimaji wa madini (weighing instrument class II capacity1200 g na inspection kit).

348. Mheshimiwa Spika, Mradi wa ASDP umetengewaShilingi 1,400,000,000. Kati ya hizo Shilingi 63,700,000 zitatumikakuimarisha mnyororo wa thamani na kuwezesha wakulimakuunganishwa na masoko; Shilingi 184,000,000 kuendelezampango wa kukuza masoko ya bidhaa za kil imozinazozalishwa nchini; Shilingi 162,750,000 za kuimarisha

Page 220: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

mifumo ya taarifa za masoko ya mifugo, mazao na bidhaanyingine; Shilingi 380,531,173 za kufanya sensa ya mazao yakilimo na mifugo na kufanya tafiti za mwenendo wa masokoya mazao makuu ya biashara na mifugo; shilingi 58,000,000kupitia na kukamilisha Mkakati wa Sera ya Masoko;Shilingi123,368,827 kuendeleza na kukuza matumizi yamifumo ya kuzuia majanga ya masoko kwa mazao nabidhaa zinazo zalishwa nchini, kuperemba na kufuatiliautekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa zao lakorosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani na katikamaeneo mapya yatakayo anza kutekeleza Mfumo huo;Shilingi 68,950,000 kuimarisha na kukuza soko la bidhaa(operationalize of Agricultural Commodity Exchange); Shilingi70,875,000 kuimarisha na kukuza biashara na masoko yamipakani kwa bidhaa za kilimo na zinazozalishwa nchini;shilingi 90,250,000 kuendeleza na kuunganisha Mfumo waSoko la Bidhaa (Commodity Exchange ) na Mfumo waStakabadhi Gghalani kwa mazao ya alizeti, mahindi, mchele,na ufuta pamoja na maeneo mapya ambayo hayajawahikutumia Mfumo wa stakabadhi ghalani pamojakupanua wigo wa matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi zaGhala; shilingi 84,950,000 kuendeleza miundombinu yamasoko katika mkakati kwa kuimarisha na kukamilisha ujenziwa vituo vya biashara mipakani Sirari, Murongo, Nkendwa,Kabanga na Kahama; na Shilingi 112,625,000 kuwezeshaujenzi wa maghala matano (5) ya kimkakati kwa mazaoyaliyopo kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani.

7.0 HITIMISHO349. Mheshimiwa Spika, maamuzi ya ujenzi wa

uchumi wa viwanda nchini ni msimamo makini wa Serikaliyetu unaozingatia uzoefu uliopo ambao umeinua uchumiwa nchi nyingi ulimwenguni na kuleta mafanikio namaendeleo katika nchi hizo. Kuthubutu, kutambua ushindani,kutumia fursa, kufanya kazi kwa ushirikiano na kutumiarasilimali kwa nidhamu ni masuala muhimu ya kuzingatiwaili kufikia malengo. Ni dhahiri kuwa changamoto za uwekezajihuambatana na fursa ambazo hatuna budi kufungamananazo. Wakati Serikali inaendelea na jitihada za kuwekamazingira rafiki na wezeshi, sekta binafsi ina jukumu la

Page 221: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

kuzitumia fursa zilizopo na zinazojitokeza ndani na nje ya nchikwa kuwekeza na kufanya biashara. Matokeo ya jitihada hizoyameanza kuzaa matunda. Hata hivyo, tunahitaji kuendeleakuunganisha nguvu kwa dhamira njema bila kuchokakukabili vita dhidi ya uchumi wa viwanda ulimwenguni kwakuhakikisha kuwa ushirikiano wa sekta binafsi na Serikaliunaendelezwa. Inawezekana, tukiweka nguvu ya pamojakatika kuendeleza sekta hii muhimu.

349. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono.Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biasharana Uwekezaji, ahsante sana kwa hotuba yako ambayoimetupatia mwanga mkubwa. Mheshimiwa Waziri kunabidhaa zipo mezani kwako hujasema chochote sasa sijui,lakini basi haina neno labda baadaye kidogo.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Spika, samahani nilipitiwa, nilijiandaa siku nyingikusoma hotuba hii. Naibu Waziri wangu niliyepewa naMheshimiwa Rais, nguo aliyovaa imeshonwa na mwanamama mjasiriamali aliyepo Mbeya kwa kutumia nyuzi. NaibuWaziri viatu alivyoshika vimetengenezwa na Kiwanda chaKaranga Prison Arusha na mimi suti niliyovaa imeshonwa naKhimji wa Dar es Salaam. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Huo ndio umaliziaji wa hotuba niliokuwanautazamia. Pia kwa wale ambao hawakusikia lile bookalilolibeba lile ndiyo lina orodha ya viwanda, maana wengimlikuwa mnasema ooh viwanda, orodha iko wapi, lile booklile ndiyo orodha yote, hajaweka mezani bado msidai,ahsante sana. (Kicheko)

Sasa nitamuita Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji baada ya hapo tutakuwa nauchangiaji, mchangiaji wa kwanza atakuwa ni MheshimiwaZitto Kabwe (ACT), wa pili atakuwa CCM, MheshimiwaSilvestry Koka mjiandae, mara baada ya Mwenyekiti kumalizahotuba yake. (Makofi)

Page 222: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

Mheshimiwa Mweyekiti, Mheshimiwa Suleiman Sadiq,karibu sana. Ni mara chache Mheshimiwa Suleiman Sadiqamewahi kupiga suti. (Makofi/Kicheko)

MHE. SULEIMAN A. SADIQ – MWENYEKITI KAMATI YABIASHARA, VIWANDA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi hiiasubuhi ya leo lakini naomba nimshukuru sana MwenyeziMungu kwa kunijalia salama siku ya leo na kunipa afya njema.Pia namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Kamatikufanya kazi hii hadi kuikamilisha siku ya leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niwashukuru sanawananchi wa Mvomero kwa kuendelea kuwa na imani namimi na hatimaye Bunge nalo limenipa kazi kubwa na nzitona kunijenga imani kubwa. Nami naahidi kuifanya kazi hiikwa uaminifu na uadilifu mkubwa. Sitakuangusha wewe naBunge lako.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira, inaomba sasa itoe rasmitaarifa ya Kamati kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Fungu 44 na Fungu 60kwa mwaka wa fedha 2017/2018 pamoja na maoni ya Kamatikuhusu makadirio ya mapato na matumizi Fungu 44 na 60kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9)na 117(11) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari,2016, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wamajukumu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Fungu 44-Viwanda na Fungu 60-Biashara na Uwekezaji kwaMwaka wa Fedha 2017/2018 na 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi yakipato cha kati na kupitia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.Kamati imeona na kupongeza jitihada za Serikali katikakutekeleza hili.

Page 223: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

Mheshimiwa Spika, naomba kutumia nafasi hiikumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kusimamia nakuipeleka nchi hii katika Tanzania ya Viwanda. Kamatiinampongeza na inamuunga mkono katika juhudi zake zotehizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilizingatia masharti yaKanuni ya 98(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge katikakutekeleza majukumu yake ambapo Kamati ilipata fursa yakutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini yaWizara kwa lengo la kujionea hali halisi ya utekelezaji wamiradi hiyo na hatimaye wajumbe kuishauri Serikali ipasavyo.Kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za kudumu zaBunge, Kamati ilipokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji waBajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Fungu44 na Fungu 60) kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 nakuchambua Mpango wa Bajeti hiyo kwa Mwaka wa Fedhawa 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)kikisomwa pamoja na Kifungu cha 7(1)(a) ya Nyongeza yaNane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016,bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ilipitiwana kuchambuliwa na Kamati ya Viwanda, Biashara naMazingira na hatimaye kutoa maoni yake.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha taarifa hiimbele ya Bunge lako Tukufu kwa lengo la kuliomba Bungekuidhinisha maombi ya Fedha kwa ajili ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji. Aidha, taarifa hii itaainishamapendekezo kuhusu masuala kadhaa ambayo Kamatiinaamini ni muhimu yakafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa majukumu yaWizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Kamati ilipokeana kujadili taarifa ya Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji kuhusu utekelezaji wa malengo/majukumuyaliyopangwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 ambayo ni pamoja na kutenga maeneo ya maalumuya uwekezaji kwa kuzingatia msambao wa viwanda nchini.

Page 224: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

Kamati ilipokea taarifa kuwa hadi kufikia Machi, 2018 jumlaya ekari 622,030.65 zilikuwa zimeainishwa na kutengwa kwaajili ya maeneo maalum ya uwekezaji. Kamati inapongezajitihada hizi za Serikali katika kutekeleza lengo hili. Kamatiina maoni kwamba ili zoezi hili liwe na ufanisi, Serikali itengefedha za kutosha kwa ajili ya kulipa fidia na kuendelezamaeneo haya kwa kuweka miundombinu stahiki ili kuyafanyamaeneo haya kuwa tayari kwa ajili ya uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara inahimizauanzishwaji wa viwanda nchi nzima katika mikoa nahalmashauri zote. Kamati inaona ni jambo jema lakiniinaishauri Serikali kuzingatia faida za kijiografia katika kutengamaeneo hayo. Katika kufanya hivyo itasaidia kupunguzagharama kwa wawekezaji wetu hasa usafirishaji wamalighafi au bidhaa na hatimaye kupunguza mzigo wa beikwa walaji.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati kuhusuutekelezaji wa mpango na bajeti wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2017/2018,ulizingatia makusanyo ya maduhuli na upatikanaji wa fedhakutoka Hazina. Chanzo cha taarifa hizi ni zilizowasilishwa naWizara mbele ya Kamati na majadiliano yalifanyika nahatimaye kupata taarifa hizi muhimu.

Mheshimiwa Spika, makusanyo ya maduhuli kwamwaka wa fedha 2017/2018. Wizara ya Viwanda, Biasharana Uwekezaji pamoja na taasisi zilizopo chini yake ilipangakukusanya jumla ya Sh.28,000,000,000. Makadirio hayayalipangwa kukusanywa kutoka katika ada za leseni, mauzoya nyaraka za zabuni na faini za kukiuka Sheria ya Leseni yaBiashara.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea taarifa kuwa hadikufikia Desemba, 2017, Wizara ilikuwa imekusanya jumla yaSh.8.6 kiasi hiki ni sawa na asilimia 30.7 ya lengo lililokusudiwa.Kamati inaona fedha hizi ni ndogo sana, juhudi kubwazinatakiwa ziendelee katika eneo hili.

Page 225: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati ulibainishakuwa, Desemba, 2017, ilikuwa ni takribani miezi sita ya mudautekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/2018 na kiasikilichokusanywa ni kidogo ukilinganisha na makisio/malengoya Sh.28,000,000,000, hivyo kuwepo uwezekano mdogo wakufikia lengo lilowekwa mpaka kufikia mwisho wa mwakawa fedha. Kamati inaendelea kusisitiza kwa Serikali kupangamakusanyo ya maduhuli kwa kuzingatia uhalisia wa vyanzovya mapato ili kuwa na uhakika wa kufikia malengo. Kamatiinashauri Wizara iwe makini zaidi katika eneo hili.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mpango na bajetikatika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa Fungu 44 na 60.Fedha zilizotengwa na kuidhinishwa kwa ajili Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji katika mwaka wa fedha2017/2018 ni jumla ya shilingi bilioni 122, kati ya fedha hizoshilingi bilioni 80 ikiwa ni kwa ajili ya kutekeleza miradi yamaendeleo na shilingi bilioni 42 kwa ajili ya matumizi yakawaida kwa mafungu yake yote mawili Fungu 44 (Viwanda)na Fungu 60 (Biashara na Uwekezaji).

Mheshimiwa Spika, Fungu 44 (Viwanda) lilitengewashilingi bilioni 98 Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 73.8 zilikuwakwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shilingibilioni 24 zilitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Fungu60 (Biashara na Uwekezaji) lilitengewa shilingi bilioni 24.2 katiya hizo shilingi 17.8 ni bajeti ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 6.3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa fedha kutokaHazina. Kamati ilipokea taarifa kuwa, hadi kufikia Machi,2018, Wizara ilikuwa imepokea jumla ya shillingi bilioni 37.4kutoka Hazina kwa ajili ya matumizi ya Wizara na taasisizilizopo chini yake. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 30.64 tu yafedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mafungu yote 44 na 60.Kamati ina maoni kwamba, kuchelewa kutolewa kwawakati fedha kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Wizaraimekuwa ni kikwanzo pia katika utekelezaji wa miradi yamaendeleo na huku tukizingatia kwamba hii ni Tanzania yaviwanda.

Page 226: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

Mheshimiwa Spika, kati ya fedha zilizopokelewakutoka Hazina shilingi bilioni 29.4 ni kwa ajili ya matumizi yakawaida sawa na asilimia 70 ya bajeti yote ya matumizi yakawaida. Mgawanyo wa fedha zilizopokelewa kutoka Hazinakatika mafungu (44 na 60) ni kama ifuatavyo: Shilingi bilioni17.3 kwa Fungu 44, kiasi hiki kinajumuisha mishahara, Shilingibilioni 13.2 na shilingi bilioni 4.1 ni kwa ajili ya matumizimengineyo (OC). Fungu 60 limepokea shilingi bilioni 12 katiya hizi shilingi bilioni 10 ni kwa ajili ya mishahara na shilingibilioni 1.12 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC).

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa fedha kutokaHazina kwa kiwango kikubwa unaonyesha kuwa Serikaliinapanga matumizi makubwa yasiyoakisi uhalisia wa vyanzovya mapato vya ndani. Hali hii imeathiri kwa kiasi kikubwautekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2018, kati yashilingi shilingi 80 fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo nishilingi bilioni 8 tu ndizo zilikuwa zimepokelewa kwa mafunguyote mawili 44 na 60 kutoka bajeti ya fedha za ndani, kiasihiki ni sawa na asilimia 9.97 ya fedha zote za miradi yamaendeleo. Kiasi hiki ni kidogo sana kwa uhalisia waviwanda nchini.

Mheshimiwa Spika, baada ya uchambuzi wa kina wataarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa mwaka fedha 2017/2018, Kamatiilibaini kwamba:-

(i) Kumekuwa na ucheleweshaji wa fedha zamaendeleo jambo linalokwamisha utekelezaji wa miradi hiyokwa wakati na hatimaye kupanda kwa gharama hizomwaka hadi mwaka. (Makofi)

(ii) Hakuna uwiano wa upatikanaji wa fedha zamatumizi ya kawaida na fedha za miradi ya maendeleo.

(iii) Upatikanaji wa fedha kutoka Hazinaumekuwa mdogo ukilinganishwa na fedha zilizoidhinishwana Bunge lako Tukufu. Maelezo hayo yanaonyeshwa kwenyeJedwali lifuatalo ambalo linaonyesha fedha zilizoidhinishwa

Page 227: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

na Bunge pamoja na kiasi kilichopokelewa. Jedwali lipokatika kitabu changu cha hotuba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa uchambuzi huuupatikanaji wa fedha kutoka Hazina umekuwa siyo wakuridhisha. Kamati inaendelea kuishauri Serikali kuhakikishainapeleka fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa wakati ilikuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, Kamati yetu i l ifanikiwakutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo. Kamatiilifanya ziara katika maeneo ya SIDO na taarifa yangu ya ziarahiyo ipo katika ukurasa wa 8, 9 na 10 wa hotuba yangu.

Mheshimiwa Spika, mapitio ya utekelezaji wa maagizoya Kamati kuhusu bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018.Wakati wa kupitia na kuchambua taarifa ya utekelezaji waWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wafedha 2017/2018, Kamati ilitoa ushauri kwenye maeneombalimbali. Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Serikaliimejitahidi kuzingatia ushauri wa Kamati. Hata hivyo, kunamaeneo ambayo Serikali haikuyatekeleza ipasavyo kamainavyoainishwa kwenye taarifa hii. Tunashauri Serikali iwekekipaumbele zaidi kwenye maoni na ushauri wa Kamati.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali ipeleke fedha zilizosaliakwa ajili ya mradi wa TAMCO ili uweze kukamilika kwa wakatikama ilivyopangwa. Pia miradi ya aina hii itekelezwe katikamaeneo mengine ya uwekezaji yaliyotengwa katika sehemumbalimbali nchini. Mara ya mwisho wakati Kamatiinautembelea mradi huu ilipokea taarifa kuwa mradi ulikuwaunahitaji shilingi bilioni 16.9 kwa ajili ya kukamilisha utekelezajiwake. Maelezo yaliyotolewa na Wizara ni kuwa imetekelezaagizo hili.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018, mradi huu ulitengewa shilingi bilioni 12.9 ambazo hadikufikia Machi, 2018 ni shilingi bilioni 2 tu ndizo ambazo zilikuwazimepokelewa na kutumika katika ujenzi kiwanda cha

Page 228: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

kuunganisha matrekta. Kamati bado inaendelea kusisitizaSerikali kupeleka fedha zilizosalia katika eneo hilo kwamwaka huu wa fedha unaoishia wa 2017/2018. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali iangalie mazingira yakufanya biashara hapa nchini ili kuwavutia wawekezajiwengi. Maelezo ya Serikali ni kuwa yapo majadilianoyanayoendelea katika hatua mbalimbali za kutafutaufumbuzi wa kudumu jambo hili. Kamati hairidhishwi jinsiSerikali inavyolishughulika suala hili kwani bado wawekezajiwengi wanalalamika kuhusu ugumu wa mazingira ya kufanyabiashara Tanzania. Ni maoni ya Kamati kuwa Serikali iongezekasi katika mchakato wake wa kutafuta utatuzi wa kudumuna kupunguza urasimu katika taasisi zake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa mpango namakadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha2018/2019. Kamati ilipokea taarifa kuwa katika mwaka wafedha 2018/2019, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezajiimepanga kukusanya shilingi bilioni 20 kwa Fungu 44 na Fungu60. Kiasi hiki ni pungufu kwa asililimia 28.5 ya shilingi bilioni 28kiasi kilichokadiriwa katika ya mwaka wa fedha unaoishia.

Mheshimiwa Spika, Fungu 44 (Viwanda) linatarajiakukushanya jumla ya shilingi milioni 5.3 kutokana na uuzajiwa nyaraka za zabuni na marejesho ya mishahara endapomtumishi ataacha kazi. Fungu 60 (Biashara na Uwekezaji)linatarajia kukushanya jumla ya shilingi bilioni 20 kutokanana uuzaji wa leseni za biashara, faini kutokana na kukiukamasharti ya leseni na marejesho ya mishahara endapomtumishi ataacha kazi.

Mheshimiwa Spika, Kamati iliipongeza Wizara kwakuzingatia ushauri wa Kamati uliokuwa ukitolewa kwa mudamrefu sasa wa kujikadiria kwa kuzingatia uwezo wao halisiwa makusanyo. Aidha, Kamati inaendeela kuisisitiza Serikalikuangalia changamoto zilizopelekea kutofikia malengo hayona kufanya jitihada za kukabiliana nazo ili kuhakikishawanafikia malengo wanayojiwekea.

Page 229: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

Mheshimiwa Spika, Makadirio ya Matumizi kwaMwaka wa Fedha 2017/2018. Maombi ya fedha kwa Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mafungu yote mawili; 44na 60, ni jumla ya shilingi bilioni 143.3. Kiasi hiki ni zaidi yaasilimia 17.28 ya shilingi bilioni 122.2 zilizoidhinishwa kwa bajetiinayotekelezwa sasa. Kati ya fedha zilizoombwa, kiasi chashilingi bilioni 43.3 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi bilioni 100 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Fungu 44 - Viwanda. Katika Mwakawa Fedha 2018/2019, Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji, Fungu 44, limetengewa jumla ya shilingi bilioni 117.2kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Wizara. Kiasi hiki ni sawana asilimia 81.8 ya shilingi bilioni 143.3. Fedha zote hizizinaombwa na Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni93, sawa na asilimia 79.3 ya bajeti ya Fungu lote la 44 ni kwaajili ya matumizi ya maendeleo; shilingi bilioni 24.2, sawa naasilimia 20.69 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambaposhilingi bilioni 19.1 ni mishahara ya watumishi na shilingi bilioni5.1 ni matumizi mengineyo (OC).

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati umebainimambo yafuatayo. Katika bajeti iliyoombwa kuna ongezekola asilimia 17.28 ukilinganisha na bajeti inayotekelezwa kwasasa. Kamati inapata mashaka kama kweli bajeti hii itawezakutekelezwa kwa kuwa upatikanaji wa fedha kutoka Hazinasi wa kuridhisha, hasa ikizingatiwa kwamba hadi kufikiaMachi, 2018, ni asilimia 30 tu ya bajeti ya 2017/2018 ndiyoiliyopokelewa. Eneo hili kuna tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, fedha zinazotengwa kwa ajili yamiradi ya maendeleo zimekuwa zikiongezeka kila mwaka.Ongezeko la mwaka huu ni asilimia 24.7, changamoto niupatikanaji wa fedha hizi kutoka Hazina, jambolinalosababisha kukwamishwa utekelezaji wa miradi hiyo.Kamati inaendelea kuisisitiza Serikali kutoa fedha zote zamiradi ya maendeleo kabla ya tarehe 30, Juni, 2018. (Makofi)

Page 230: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

Mheshimiwa Spika, maoni, ushauri na mapendekezoya Kamati. Baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi nauchambuzi wa taarifa mbalimbali ikiwemo taarifa yautekelezaji wa Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 naMakadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara kwa Mwaka2018/2019, Kamati inatoa maoni na ushauri ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Viwanda. Ni matarajioya Watanzania walio wengi kuona uanzishwaji wa viwandaunazingatia pia uanzishaji wa viwanda vikubwa na vya katiambavyo vitachakata mazao ya kilimo, kwa mfano pamba,tumbaku, kahawa, alizeti, korosho na miwa. Kamatiinaishauri Serikali kuwa na malengo maalum ya viwandavikubwa na vya kati kwa lengo la kuongeza mapato yaSerikali na ajira. Kamati inakubaliana na utaratibu waviwanda vidogo, viwanda vya vyerehani, lakini Kamatiinasisitiza kuongeza malengo maalum kwa viwandavikubwa na vya kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakulima wengi nchini badowanalima kwa kutumia zana duni, hasa jembe la mkono.Kwa kuwa SIDO, CAMARTEC, TEMDO na TIRDO wana uwezowa kutengeneza na kusambaza zana mbalimbali za kilimokwa teknolojia rahisi na kuuza kwa bei nafuu kwa wakulima,Kamati inaishauri Serikali kuziwezesha taasisi hizi ili ziwekichocheo kwa uanzishaji wa viwanda vikubwa, vya kati navidogo, lakini pia vitakavyotumia teknolojia rahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, viwanda vinavyochakatamatunda na mbogamboga nchini vinalazimika kufanyauzalishaji kwa msimu kutokana na wakulima wengikutegemea kilimo cha mvua. Hali hii imesababisha wenyeviwanda vingi kuzalisha chini ya kiwango kwa kuwa na ajiraza msimu, matokeo yake Serikali kukosa mapato. Kamatiinaishauri Serikali kuwahamasisha na kuwawezesha wakulimanchini kulima kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na mavunomsimu wote. Kamati inaishauri Wizara inayohusika kuongezafedha katika eneo hili la umwagiliaji. (Makofi)

Page 231: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea malalamiko yawenye viwanda vya bidhaa ya karatasi wakilalamikakutopata kwa wakati malighafi za karatasi kutoka Kiwandacha Mgololo, Iringa. Kamati inaishauri Serikali kuangalianamna ya kupunguza kodi kwa malighafi ya karatasi kutokanje ya nchi ili kuleta ushindani wa haki ndani ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, liko tatizo kubwa sana ambaloSerikali inakosa mapato. Tofauti ya bei katika soko la bidhaaaina ya pombe na vinywaji vikali kumezua hofu. Piakumekuwepo na stika bandia za TRA katika bidhaa za pombena vinywaji vikali. Suala hili TRA wanalifahamu lakini hadi leolinaendelea na liko ndani ya nchi yetu. Aidha, kumekuwepona viwanda vinavyotoa taarifa zisizo sahihi za uzalishaji, halihii huisababishia Serikali kupoteza mapato mengi katika eneohili. Kamati inashauri Serikali kutoza kodi katika spirit ambayondiyo malighafi inayoingia nchini wakati ambapo inaingiakatika boda na bandari zetu ili kuondokana na udanganyifuunaofanywa na wenye viwanda. Eneo hili Serikali iwe makinisana, inapoteza mabilioni ya fedha katika stika bandia zaTRA katika vinywaji vya pombe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati Serikali inaendeleakuhimiza uanzishaji wa viwanda nchini, wamiliki wengi waviwanda nchini bado wanalalamikia nishati ya umeme kuwasiyo ya kutosheleza, wakati mwingine kusababisha hasara.Kamati inaunga mkono dhamira ya Serikali kujenga mradimkubwa wa Stiegler’s Gorge ili kupata ufumbuzi wa kudumu.Kamati inaendelea kusisitiza Serikali kuharakisha kupatasuluhu ya kudumu kwa tatizo la umeme ili kufikia Tanzaniaya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Biashara. Serikali katikakuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini, hasavinavyochakata mazao ya kilimo, inalenga kuwainuawakulima wadogo lakini hili litafanikiwa kama yatawekwamazingira ya haki katika biashara kati ya wakulima na wenyeviwanda. Eneo hili wakulima na wenye viwanda halijakaavizuri, tunaomba Serikali iwatendee haki. Wakulima wengiwanalalamika kuwa viwanda hununua mazao yao kwa bei

Page 232: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

ya chini, hasa kwa kuwa mengi yanazalishwa kwa msimummoja. Kamati inashauri Serikali kuandaa utaratibu mzuriwa soko ambao utakuwa ni kwa manufaa ya pande zotembili; wakulima na wenye viwanda.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua kazi yaTanTrade katika kusogeza mbele gurudumu la uzalishaji namasoko kwa kuandaa maonesho makubwa ya biashara.TanTrade ina wajibu wa kuhakikisha bidhaa za Tanzaniazinaingia katika masoko ya kimataifa. Kamati inashauriSerikali kuiwezesha TanTrade kuwekeza katika miundombinuya masoko, maghala na viwanja vya maonesho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mapinduzi ya teknolojia yametoamianya kwa wafanyabiashara ambao si waaminifu kuzalishabidhaa bandia zinazoshabihiana kabisa na bidhaa halisi kwakuzalisha na kuwafanya walaji kushindwa kutofautishabidhaa hizo. Njia inayotumika sasa na Tume ya Ushindanikutambua bidhaa hizo kwa kuangalia usanifu, maandishi narangi haiwezi kupata majibu sahihi. Kamati inashauri FCCitumie njia za kisasa zaidi, teknolojia bora ya kutofautishakati ya bidhaa bandia na bidhaa halisi na Sheria ya FCCifanyiwe marekebisho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tofauti kubwa yabei za bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinazotoka nje yanchi. Bidhaa nyingine za ndani ya nchi bei zake zimekuwakubwa na bidhaa kutoka nje ya nchi bei zimekuwa ndogo,mfano bidhaa za sukari, mabomba ya maji, nguo na vifaavya ujenzi. Kwa sababu hiyo, bidhaa za ndani zinakosaushindani wa soko. Kamati inashauri Serikali kukaa nawazalishaji wa ndani kupitia gharama za uzalishaji nakuondoa mizigo mikubwa ambayo mwisho wake mtumiajiwa mwisho ndiyo anabeba mzigo wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Watanzania wengi wameitikiawito wa Serikali kwa kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili yakuzalisha bidhaa mbalimbali, mfano usindikaji wa asali,matunda na mbogamboga. Katika kutafuta masokowamekuwa wanakumbana na vikwazo mbalimbali ikiwemo

Page 233: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

kupata alama ya ubora kutoka TBS. Kamati inaishauri Serikalikuhakikisha kwamba TBS inawafikiwa wajasiriamali wotenchini ili waweze kujenga uwezo na bidhaa zao kuingiakatika soko.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaitambua nia njema yaSerikali katika kudhibiti uingizaji wa sukari ya viwandani. Badokuna malalamiko kutoka kwa wenye viwanda wanaotumiamalighafi hiyo kuwa kuna urasimu wa upatikanaji wa vibalikuingiza sukari hiyo ya viwandani kwa sababu viwanda hivyovinazalisha chini ya kiwango, baadhi ya viwanda wameanzakupunguza wafanyakazi wao na kubwa zaidi ni kuikoseshaSerikali mapato. Kamati inaendelea kusisistiza inaunganamkono na juhudi za Serikali lakini utaratibu mzuri zaidiuandaliwe ili viwanda viendelee kuzalisha kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, wazalishaji wa ndani wa maziwawanalalamikia Ongezeko la Kodi ya Thamani (VAT)inayotozwa kwenye maziwa yanayozalishwa na viwanda vyandani. Hatua hii inapunguza ushindani ukilinganisha namaziwa yanayoingizwa kutoka nchi jirani ambayo hayatozwikodi hiyo katika nchi yao. Kamati inaendelea kuisisitiza Serikalikuangalia uwezekano wa kuondoa kodi hiyo ili kuvilindaviwanda vya ndani na pia kuongeza soko la maziwa.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Uwekezaji. Kumekuwana uwekezaji katika Sekta ya Viwanda usiozingatiaupatikanaji wa malighafi na faida za jiografia katika eneohusika. Kwa sababu hiyo kunakuwa na gharama kubwa yausafirishaji wa malighafi kutoka eneo moja kwenda eneolingine, lakini pia linawakosesha fursa nyingine za kiuchumizinazotokana na uwekezaji. Kamati inaishauri Serikali kablaya kuanzisha viwanda ufanyike utafiti wa kutosha ilikutambua aina ya kiwanda kutokana na faida ya jiografiaya eneo husika.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizi nzurizinazochukuliwa na Serikali, bado kuna malalamiko kwawawekezaji wengi kwamba mazingira ya uwekezaji nchinisi rafiki. Baadhi ya wawekezaji wanalalamikia uwepo wa

Page 234: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

changamoto kama mamlaka nyingi za udhibiti, urasimukatika upatikanaji wa vibali vya uhamiaji na mlolongo wakupata vibali vya uwekezaji. Kamati inaishauri Serikali iendeleekuboresha mazingira haya chini ya TIC ili uwekezaji wa kuvutiaufanyike nchini kwetu.

Mheshimiwa Spika, ni takribani miaka 20 sasa tanguwawekezaji wengi waliponunua viwanda vilivyokuwavinamilikiwa na Serikali kwa njia ya ubinafsishaji. Kati ya mweziSeptemba na Desemba, 2017, Serikali ilifanya sensa yaviwanda hivyo katika mikoa 13 ikiwemo Mikoa ya Dar esSalaam, Pwani, Tanga, Morogoro, Mtwara, Arusha,Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Shinyanga naDodoma.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya sensa yameoneshakati ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa ni viwanda 62 tuambavyo ndivyo vinafanya kazi, sawa na asilimia 39.7. Kwatakwimu hiyo inamaanisha kwamba asilimia 61.3 ya viwandavyote havifanyi kazi. Kamati inaishauri Serikali kuendeleakuchukua hatua kwa wawekezaji wote ambao hawajafufuaviwanda hivyo kwa lengo lililokusudiwa. Sambamba na hilo,ipo haja ya Serikali kuunda Tume Maalum ili kufuatilia kwakaribu eneo hilo. (Makofi)

SPIKA: Nakupa dakika mbili ku-wind up MheshimiwaSaddiq, soma mafungu tu yale.

MHE. SULEIMAN A. SADDIQ – MWENYEKITI WA KAMATIYA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika,hitimisho. Naomba nikushukuru wewe sana na MheshimiwaNaibu Spika kwa uongozi wenu mahiri. Nawashukuru piaWenyeviti wote wa Bunge kwa kuratibu vyema shughuli zaBunge. Kwa namna ya pekee, napenda kuwashukuruWajumbe wangu wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biasharana Mazingira kwa kushiriki kikamilifu katika kupitia bajeti hiina kuchambua na hatimaye kuwasilisha maoni yao leombele ya Bunge lako Tukufu. Naomba orodha ya majina yoteyaingie kwenye Hansard. (Makofi)

Page 235: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya sasanaomba Bunge lako Tukufu likubwali kuidhinisha Makadirioya Mapato na Matumizi ya Fungu 60 na Fungu 44 kwa Mwakawa Fedha 2018/2019, kiasi cha shilingi bilioni 143.3 ambaposhilingi bilioni 43.3 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi bilioni 100 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha, naungamkono hoja. (Makofi)

TAARIFA KAMATI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAWIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI, FUNGU 44NA FUNGU 60 KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 PAMOJANA MAONI YA KAMATI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATONA MATUMIZI FUNGU 44 NA FUNGU 60 KWA MWAKA WA

FEDHA 2018/2019 KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI____________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9)na 117 (11) ya Kanuni za Kudumu Kanuni za Bunge, Toleo laJanuari, 2016, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wamajukumu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Fungu 44-Viwanda na Fungu 60-Biashara na Uwekezaji kwaMwaka wa Fedha 2017/2018 na maoni ya Kamati kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Fungu 44-Viwanda na Fungu 60-Biashara na Uwekezaji kwa Mwakawa Fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi yakipato cha kati na kupitia Uchumi wa Viwanda ifikapo 2025.Kamati imeona na kupongeza jitihada za Serikali katikakutekeleza hili.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilizingatia masharti yaKanuni ya 98(1), ya Kanuni za Kudumu za Bunge katika

Page 236: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

kutekeleza majukumu yake ambapo Kamati ilipata fursa yakutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezezwa chini yaWizara kwa lengo la kujionea hali halisi ya utekelezaji wamiradi hiyo na hatimaye wajumbe kuishauri Serikali ipasavyo.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za kudumuza Bunge Kamati ilipokea na kujadiri Taarifa ya Utekelezajiwa Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji(Fungu 44-Viwanda na Fungu 60-Biashara na Uwekezaji) kwaMwaka wa Fedha 2017/2018 na kuchambua Mpango waBajeti hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)kikisomwa pamoja na Kifungu cha 7(1) (a) ya Nyongeza yaNane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016,Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ilipitiwana kuchambuliwa na Kamati ya Viwanda, Biashara naMazingira na hatimaye kutoa maoni yake.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha Taarifa hiimbele ya Bunge lako tukufu kwa lengo la kuliombakuidhinisha maombi ya Fedha kwa ajili ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji. Aidha, taarifa hii itaainishamapendekezo kuhusu masuala kadhaa ambayo Kamatiinaamini ni muhimu yakafanyiwa kazi.

2.0 UCHAMBUZI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WAMAJUKUMU NA MPANGO WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA2017/2018 NA MATOKEO YA UKAGUZI WA MIRADI YAMAENDELEO ILIYOTENGEWA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA2017/2018.

2.1 Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Mwakawa Fedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kujadili taarifaya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhusuutekelezaji wa malengo/majukumu yaliyopangwa

Page 237: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

kutekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2017/2018 ambayo nipamoja na:-· Kutenga maeneo ya maalumu ya uwekezajikwa kuzingatia msambao wa viwanda nchini. Kamati ilipokeataarifa kuwa hadi kufikia Machi, 2018 jumla ya Ekari 622,030.65zilikuwa zimeainishwa na kutengwa kwa ajili ya maeneomaalum ya uwekezaji. Kamati inapongeza jitihada hizi zaSerikali katika kutekeleza lengo hili. Kamati ina maonikwamba ili zoezi hili liwe na ufanisi, Serikali itenge fedha zakutosha kwa ajili ya kulipa fidia na kuendeleza maeneohaya kwa kuweka miundombinu stahiki ili kuyafanya maeneohaya kuwa tayari kwa ajili ya uwekezaji.

· Serikali(Wizara) kuhimiza uanzishwaji wa viwanda nchinzima katika Mikoa na Halmashauri zote. Kamati inaona nijambo jema lakini inaishauri Serikali, kuzingatia faida zakijiografia katika kutenga maeneo hayo. Katika kufanyahivyo itasaidia kupunguza gharama kwa wawekezaji wetuhasa usafirishaji wa malighafi au bidhaa na hatimayekupunguza bei kwa walaji.

2.2 Uchambuzi wa Utekelezaji wa Mpango na Bajetikwa mwaka wa fedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati kuhusu utekezajiwa Mpango wa Bajeti wa Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 ulizingatiamakusanyo ya maduhuli na upatikanaji wa fedha kutokaHazina. Chanzo cha taarifa hizi ni taarifa zilizowasilishwa naWizara mbele ya Kamati na majadiliano yaliyofanyika nahatimaye kupata taarifa hizi muhimu.

2.2.1 Makusanyo ya Maduhuli

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018,Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na taasisizilizopo chini yake ilipanga kukusanya jumla ya Shilingi28,000,000,000. Makadirio haya yalipangwa kukusanywakutoka katika ada za leseni, mauzo ya nyaraka za zabuni na

Page 238: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

faini ya kukiuka Sheria ya Leseni ya Biashara. Kamati ilipokeataarifa kuwa hadi kufikia Desemba, 2017 Wizara ilikuwaimekusanya jumla ya Shilingi 8,598,083,500.07 kiasi hiki ni sawana asilimia 30.7 tu ya lengo lililo kusudiwa.

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi wa Kamati ulibainishakuwa, Desemba, 2017, ilikuwa ni takribani miezi sita (6), yamuda utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2017/2018, na kiasikilichokusanywa ni kidogo ikilinganishwa na makisio/lengola Shilingi bilioni 28, hivyo kuwepo uwezekano mdogo wakufikia lengo lilowekwa mpaka kufikia mwisho wa mwakawa fedha. Kamati inaendelea kusisitiza kwa Serikali kupangabajeti makusanyo maduhuli kwa kuzingatia uhalisia wavyanzo vya mapato ilikuwa na uhakika wa kufikia malengo.

2.2.2 Utekelezaji wa Mpango na Bajeti katika Mwakawa Fedha 2017/2018 kwa Fungu 44 na 60

i) Fedha zilizotengwa na kuidhinishwa kwa ajili Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwatika mwaka wafedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2017/2018,Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ilitengewa nakuidhinishiwa jumla ya shilingi 122,215,109,750.00 kati ya fedhahizo Shilingi 80,190,377,000.00 ikiwa kwa ajili ya kutekelezaMiradi ya Maendeleo na Shilingi 42,024,732,750.00 kwa ajili yamatumizi ya kawaida kwa mafungu yake yote mawili Fungu44 Viwanda na Fungu 60 Biashara na Uwekezaji.

a) Fungu 44 Viwanda

Mheshimiwa Spika, Fungu 44 Viwanda lilitengewa shilingi98,012,870,000.00 Kati ya fedha hizo Shilingi 73,840,377,000.00zilikuwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo naShilingi 24,172,493,000.00 zilitengwa kwa ajili ya matumizi yakawaida.

Page 239: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

b) Fungu 60 - Biashara na UwekezajiMheshimiwa Spika, Fungu 60 Biashara na Uwekezajililitengewa Shilingi 24,202,239,750.00, kati ya hizo Shilingi17,852,239,750.00 ni Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi6,350,000,000.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

ii) Upatikanaji wa Fedha kutoka Hazina

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea taarifa kuwa,hadi kufikia Machi, 2018, Wizara ilikuwa imepokea jumla yaShillingi 37,447,911,373.33 kutoka Hazina kwa ajili ya Matumiziya Wizara na taasisi zilizopo chini yake. Kiasi hiki ni sawa naasilimia 30.64 tu ya fedha zote zilizotengwa kwa ajili yamafungu yote 44 na 60. Kamati ina maoni kwamba,kuchelewa kutolewa kwa wakati fedha kwa aji l i yautekelezaji wa majukumu ya Wizara kumekuwa kikwanzo piakatika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kati ya fedha zilizopokelewakutoka Hazina Shilingi 29,447,911,373.33 ni kwa ajili yamatumizi ya kawaida sawa na asilimia 70.07 ya bajeti yoteya matumizi ya kawaida. Mgawanyo wa fedhazilizopokelewa kutoka Hazina katika mafungu (44 na 60) nikama ifuatavyo; Shilingi 17,389,887,635.33 kwa fungu 44. Kiasihiki kinajumuisha Mishahara (PE) Shilingi 13,255,892,435.33 naShilingi 4,133,995,200.00 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo(OC).Fungu 60 limepokea Shilingi 12,058,023,738.00 kati ya hizi Shilingi10,929,162,438.00 kwa ajili ya Mishahara(PE) na Shilingi1,128,861,300.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC).

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa fedha kutokaHazina kwa kiwango kikubwa unaonyesha kuwa Serikaliinapanga matumizi makubwa yasiyoakisi uhalisia wa vyanzovya mapato. Hali hii imeathiri kwa kiasi kikubwa utekelezajiwa miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2018,kati ya Shilingi 80,190,377,000.00 fedha kwa ajili ya miradi yamaendeleo ni Shilingi bilioni 8 tu ndizo zilikuwa zimepokelewa

Page 240: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

kwa mafungu yote mawili 44 na 60 kutoka bajeti ya Fedhaza Ndani, kiasi hiki ni sawa na asilimia 9.97 ya fedha zote zaMiradi ya Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, baada ya uchambuzi wa kina waTaarifa ya Utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa mwaka fedha 2017/2018, Kamatiilibaini kwamba:-

i) Kumekuwa na ucheleweshaji wa fedha za maendeleojambo linalokwamisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakatina hatimaye kupanda kwa gharama hizo mwaka hadimwaka;ii) Hakuna uwiano wa upatikanaji wa fedha za matumiziya kawaida na fedha za Miradi ya Maendeleo.iii) Upatikanaji wa fedha kutoka Hazina umekuwamdogo ukilinganishwa na fedha zilizoidhinishwa na Bunge.Maelezo hayo yanaonyeshwa kwenye Jeduali lifuataloambalo linaonyesha fedha zilizoidhinishwa na Bunge pamojana kiasi kilichopokelewa kutoka Hazina kuanzia mwaka 2016/17 na 2017/18 hadi kufikia mwezi Aprili.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa uchambuzi huuupatikanaji wa fedha kutoka Hazina umekuwa siyowakuridhisha, Kamati inaendelea kuishauri Serikali kuhakikishainapeleka fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa wakati ilikuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Page 241: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

2.3 MATOKEO YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEOILIYOTENGEWA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu kanuni ya 98 (1) yaKanuni za Kudumu za Bunge toleo la Februari, 2016, katikakutekeleza majukumu yake Kamati i l ifanya ziara yakutembelea baadhi ya miradi iliyotengewa fedha nainatekelezwa na Wizara hii. Lengo la kufanya ziara yakutembelea miradi ya maendeleo ni kujionea hali halisi nahatua zilizofikiwa katika utekelezaji wake.

i) Ziara ya Kamati katika Mradi wa Institutional Support-SIDO Iringa

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipata fursa ya kutembelaMradi Na. 6260 unaojulikana kama Institutional Support kwaupande wa Taasisi ya SIDO. Mradi huu unatekelezwa nchinzima lakini Kamati ilipata fursa ya kutembelea karakana yaSIDO-Iringa (kituo cha uendelezaji wa Teknolojia Iringa) ilikujionea jinsi wanavyoendesha shughuli zao lakini pia kutoamaoni na ushauri.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mradi huuWizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo nipamoja na; Matumizi ya mitambo ya zamani (tangu miakaya 1970) ambayo inasababisha

· Kuwepo matumizi makubwa ya umeme nakusababisha bidhaa wanazozalisha kuuzwa bei kubwaikilinganishwa na washindani wao.· Uchakavu wa mitambo unaosababisha kazi nyingikufanywa kwa mikono hivyo kutumia muda mwingi kwauzalishaji wa bidhaa chache.

Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine niupungufu mkubwa wa watumishi ambapo Karakana hiiinawafanyakazi watatu (3) tu hivyo kusababisha fundi mmojakufanya kazi zaidi ya moja kuliko uwezo wake.

Page 242: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto tajwahapo juu bado karakana ya SIDO-Iringa imepata mafanikioikiwa ni pamoja na kubuni na kutengeneza mitambombalimbali ikiwepo Mtambo wa kusafisha mafuta ya alizeti-Double refinery, Mtambo wa wa upepo na mvuke wakukausha chai, Mtambo wa kusindika zao la Kakao.

Aidha, karakana inatoa mafunzo kwa vitendo kwawanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi, mafunzo naushauri kwa wajasiriamali.

ii) Maoni ya Kamati kuhusu utekelezaji wa Mradi waInstitutional Support-SIDO Iringa

Mheshimiwa Spika, Kamati inaitazama SIDO kamataasisi muhimu sana katika kutekeleza azma ya Tanzaniakuwa nchi ya uchumi wa viwanda kwa kutengeneza vipurikwa ajili ya viwanda vingine. Kamati inaishauri Serikali kuwa,ni kwa kuzingatia umuhimu huu taasisi hii inapaswakuwezeshwa kikamilifu ili kufufua karakana zake zote nchinipamoja kununua mitambo ya kisasa inayoendena nateknolojia ya sasa.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, iliidhinishiwashilingi 14,146,800,000 kwa ajili ya SIDO nchi nzima. Kiasi hikikinajumuisha shilingi 7,146,800,000.00 kwa ajili ya Mfuko NEDFili kusaidia kukuza mitaji ya wajasiriamali. Kamati hairidhishwina jinsi Serikali inavyotoa fedha kwa ajili ya Mfuko huu muhimukwakuwa hadi kufikia Machi, 2018 hakuna fedha zilizokuwazimetolewa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaona niwakati muafakasasa kwa Serikali kutoa nyenzo zote muhimu ili SIDO iwezekujiendesha kikamilifu. Aidha, Kamati ina maoni kwambaSIDO ikiwezeshwa vizuri inaweza kusaidia pia katika kubuniteknolojia rahisi ya kutengeneza majiko ya kupikia hatuaambayo itaisadia Serikali katika kupambana na uharibifu wamazingira nchini.

Page 243: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

3.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA KAMATIKUHUSU BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Mheshimiwa Spika, wakati wa kupitia na kuchambuataarifa ya utekelezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Kamati ilitoaushauri kwenye maeneo mbalimbali. Naomba kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa Serikali imejitahidi kuzingatia ushauri waKamati, hata hivyo kuna maeneo ambayo serikalihaikuyatekeleza ipasavyo kama inavyoainishwa kwenyetaarifa hii.

i) Serikali ipeleke fedha zilizosalia kwa ajili ya mradi waTAMCO ili uweze kukamilika kwa wakati kama ilivyopangwa.Pia miradi ya aina hii itekelezwe katika maeneo mengine yauwekezaji yaliyotengwa katika sehemu mbalimbali nchi. Maraya mwishaio wakati kamati inautembelea mradi huu ilipokeataarifa kuwa Mradi ulikuwa unahitaji shilingi bilioni 16.9 kwaajili ya kukamilisha utekelezaji wake. Maelezo yaliyotolewana Wizara ni kuwa imetekeleza agizo hili. Katika mwaka wafedha 2017/2018 mradi ulitengewa sh.12.9 ambazo hadikufikia machi, 2018 ni shilingi bilioni 2 tu ambazo zilikuwazimepokelewa na kutumika katika ujenzi kiwanda chakuunganisha matrekta. Kamati bado inaendelea kusisitizaSerikali kupeleka fedha zilizosalia katika bajeti ya Mwaka waFedha 2017/2018 ili kazi zilizopangwa ziwezekufanyika. Aidha,suala la kutekeleza mradi huu katika maeneo mengine badolinasisitizwa na Kamati.

ii) Serikali iangalie mazingira ya kufanya biashara hapanchini ili kuwavutia wawekezaji wengi. Maelezo ya Serikali nikuwa yapo majadiliano yanayoendelea katika hatuambalimbali za kulitafutia ufumbuzi wa kudumu jambo hili.Kamati hairidhishwi jinsi Serikali inavyolishughulika suala hilikwani bado wawekezaji wengi wanalalamika kuhusu ugumuwa mazingira ya kufanya biashara hapa nchini. Ni maoni yaKamati kuwa Serikali iongeze kasi katika mchakato wakewa kutafuta utatuzi wa kudumu na kupunguza urasimukupitia taasisi zake.

Page 244: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

4.0 UCHAMBUZI WA MPANGO NA MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019

4.1 Makisio ya Maduhuli

Mheshimiwa Spika, kamati ilipokea taarifa kuwa katikamwaka wa fedha 2018/2019 Wizara ya Viwanda, Biasharana Uwekezaji imepanga kukusanya Shilingi 20,006,300,000.00kwa Fungu 44 na 60. Kiasi hiki ni pungufu kwa asililimia 28.5ya Shilingi 28,000,000,000.00 kiasi kilichokadiriwa katika yaMwaka wa Fedha unaoishia.

Mheshimiwa Spika, Fungu 44 - Viwanda linatarajiakukushanya jumla ya shilingi 5,300,000.00 kutokana na uuzajiwa nyaraka za zabuni na marejesho ya mishahara endapomtumishi ataacha kazi. Fungu 60 – Biashara na Uwekezajilinatarajia kukushanya jumla ya shilingi 20,001,000,000.00kutokana na uuzaji wa leseni za biashara, faini kutokana nakukiuka masharti ya leseni na marejesho mishahara endapomtumishi ataacha kazi.

Mheshimiwa Spika, Kamati iliipongeza Wizara kwakuzingatia ushauri wa Kamati uliokuwa ukitolewa kwa mudamrefu sasa wa kujikadiria kwa kuzingatia uwezo wao halisiwa Makusanyo. Aidha, Kamati inaendeela kuisisitiza Serikalikuangalia changamoto zilizopelekea kutofikia malengo hayona kufanya jitihada za kukabiliana nazo ili kuhakikishawanafikia malengo wanayojiwekea.

4.2 Makadirio ya Matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, maombi ya fedha kwa Wizara ya Viwanda, Biasharana Uwekezaji katika Mafungu yote Mawili (Fungu 44 na 60) niShilingi 143,334,153,648.00. Kiasi hiki ni zaidi kwa asilimia 17.28ya shilingi 122,215,109,750.00 zilizoidhinishwa kwa bajetiinayotekelezwa sasa. Kati ya fedha zinazoombwa Shilingi43,309,628,648.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi100,024,525,000.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Page 245: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

a) FUNGU 44 – Viwanda

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Fungu 44-Viwanda limetengewa jumla ya shilingi 117,287,008,000.00 kwaajili ya kutekeleza majukumu ya Wizara. Kiasi hiki ni sawa naasilimia 81.8 ya shilingi 143,334,153,648.00 fedha zotezinazoombwa na Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, kati ya fedha hizo shil ingi93,024,525,000.00 sawa na asilimia 79.31 ya bajeti yote yaFungu 44 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo, shilingi24,262,483,000.00 sawa na asilimia 20.69 kwa ajili ya Matumiziya Kawaida, ambapo Shilingi 19,193,110,000.00 ni mishaharaya watumishi na Shilingi 5,069,373,000.00 ni MatumiziMengineyo (OC).

b) FUNGU 60- Biashara na Uwekezaji

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Wizara Sehemu ya Biashara na Uwekezaji imetengewaShilingi 26,047,145,648.00 kwa ajili ya kutekeleza majukumuyake. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 18.17 ya bajeti yote yaWizara, Shil ingi 143,334,153,648.00. Kati ya fedhazinazoombwa Shilingi 19,047,145,648.00 ni kwa ajili ya Matumiziya Kawaida na kati ya hizo Shilingi 17,077,055,000.00 sawa naasilimia 65.56 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi, kiasikinachosalia Shilingi 1,979,090,648.00 sawa na asilimia 7.56 nikwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC). Bajeti ya Maendeleoni shillingi 7,000,000,000.00 sawa na asilimia 26.87 ya fedhazote zinazoomba kwa ajili ya Fungu hili.

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi wa Kamati umebainimambo yafuayo:-· Katika bajeti inayoombwa kunaongezeko la asilimia17.28 ukilinganisha na bajeti inayotekelezwa kwa sasa.Kamati inapata mashaka kama kweli bajeti hii itatekelezeka,kwakuwa upatikanaji wa fedha kutoka hazina si wakuridhisha hasa ikizingatiwa kwamba, hadi kufikia Machi, 2018

Page 246: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

ni asilimia 30.64 tu ya bajeti ya 2017/2018 ndiyo ilikuwaimepokelewa.

· Fedha zinazotengwa kwa ajili za Miradi ya Maendeleozimekuwa zikiongezeka kila mwaka (ongezeko la mwakahuu ni asilimia 24.7) changamoto ni upatikanaji wa fedhahizo kutoka Hazina jambo linalopelekea kukwamishautekelezaji wa miradi hiyo. Kamati inaendelea kusisitizaSerikali kutoa fedha zote za miradi ya maendeleo kabla yatarehe 30 Juni,2018.

5.0 MAONI, USHAURI NA MAPENDEKEZO YA KAMATI

Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya ziara zaukaguzi wa miradi, uchambuzi wa taarifa mbalimbaliikiwemo taarifa ya Utekelezaji wa Wizara kwa Mwaka wafedha 2017/2018 makadirio ya mapato na matumizi ya Wizarakwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 kamati inatoa maoni naushauri ufuatao:-

5.1 Sekta ya Viwanda

Mheshimiwa Spika, ni matarajio ya watanzania waliowengi kuona uanzishwaji wa viwanda unazingatia piauanzishaji wa viwanda vikubwa na vyakati ambavyovitachakata mazao ya kilimo mfano pamba, tumbaku,kahawa, alizeti na korosho. Kamati inaishauri Serikali kuwana malengo maalumu ya viwanda vikubwa na vya kati kwalengo la kuongeza mapato ya Serikali na ajira.

Mheshimiwa Spika, wakulima wengi nchini badowanalima kwa kutumia zana duni sana hasa jembe lamkono, kwakuwa SIDO, CARMATEC, TEMDO na TIRDOwanaouwezo wa kutengeneza na kusambaza Zanambalimbali za kilimo kwa teknolojia rahisi na kuuza kwa beinafuu kwa wakulima. Kamati inaishauri Serikali, kuziwezeshataasisi hizi ili ziwe kuchocheo katika uanzishwaji wa viwandavidogo lakini pia vitakavyotumia teknolojia rahisi.

Page 247: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

Mheshimiwa Spika, viwanda vinavyochakatamatunda na mbogamboga nchini vinalazimika kufanyauzalishajii kwa msimu kutokana na wakulima walio wengikutegemea kilimo cha mvua. Hali hii imesababisha wenyeviwanda kuzalisha chini ya kiwango na kuwa na ajira zamsimu matokeo yake ni Serikali kukosa mapato. Kamatiinaishauri Serikali kuwahamasisha na kuwawezesha wakulimanchini kulima kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na mavunomisimu yote.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea malalamiko yawenye viwanda vya bidhaa za karatasi zikilalamikiwakutopata kwa wakati malighafi za karatasi kutoka kiwandacha Mgololo. Kamati inaishauri Serikali kuangalia namna yakupunguza kodi kwa malingafi ya karatasi kutoka nje ya nchiili kuleta ushindani wa haki.

Mheshimiwa Spika, tofauti ya bei katika soko labidhaa za aina ya pombe na vinywaji vikali kumezua hofu,pia kumekuwepo na stika bandia za TRA katika bidhaa zapombe na vinywaji vikali. Aidha, kumekuwepo na viwandavinavyotoa taarifa zisizo sahihi za uzalishaji. Hali hiihuisababishia Serikali kupoteza mapato mengi katika eneohili. Kamati inaishauri Serikali kuitoza kodi spirit ambayo ndiyomalighafi ya kutengeneza pombe ili kuondokana naudanganyifu wa sasa.

Mheshimiwa Spika, wakati Serikali inaendeleakuhimiza uanzishwaji wa viwanda nchini, wamiliki wengi waviwanda nchini bado wanalalamikia Nishati ya Umeme kuwasiyo ya kutosheleza na wakati mwingine kuwasababishiahasara. Kamati inaunga mkono dhamira ya Serikali kujengemradi mkubwa wa Stiegler’s Gorge ili kupata ufumbuzi wakudumu. Kamati inaendelea kusisitiza kwa Serikalikuharakisha kupata suluhu ya kudumu ya tatizo hili.

5.2 Sekta ya Biashara

Mheshimiwa Spika, Serikali katika kuhamasisha ujenziwa viwanda nchini hasa vinavyochakata mazao ya kilimo

Page 248: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

inalenga kuwainua wakulima wadogo, lakini hili litafanikiwakama yatawekwa mazingira ya haki katika biashara kati yawakulima na wenyeviwanda. Wakulima wengiwanawalalamikia wenye viwanda kwa kununua mazao yaokwa bei za chini sana hasa kwakuwa mengi yanazalishwakwa msimu mmoja. Kamati inaishauri Serikali kuandaautaratibu mzuri wa soko ambao utakuwa na manufaa kwapande zote mbili.

Mheshimiwa Spika, Kamati za inatambua kazi yaTANTRADE katika kusogeza mbele gurudumu la uzalishaji namasoko kwa kuandaa maonyesho makubwa ya biashara.TANTRADE ina wajibu wa kuhakikisha bidhaa za Tanzaniazinaingia katika masoko ya kimataifa. Kamati inashauriSerikali kuiwezesha TANTRADE kuwekeza katika miundombinuya masoko, maghala na viwanja vya maonyesho.

Mheshimiwa Spika, mapinduzi ya Teknolojia yametoamianya kwa wafanyabiashara ambao siyo waaminifu nakuzalisha bidhaa bandia zinazo shabihiana kabisa na bidhaahalisi hivyo kuwafanya walaji kushindwa kutofautisha bidhaahizo. Njia inayotumika sasa na Tume ya Ushindani kutambuabidhaa ni kwa kuangalia usanifu, maandishi, kufifia kwa rangiambazo haziwezi kupata majibu sahihi. Aidha, sheria ya FCCimeonekana kukizana na mazingira halisi ya kufanyabiashara. Kamati inaishauri Serikali kuwa na teknolojia boraya kutofautisha kati ya bidhaa bandia na bidhaa halisi nasheria ya FCC ifanyiwe marekesho.

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na tofauti kubwaya bei za bidhaa zinazozalisha nchini na zile zinazoingiakutoka nje, mfano bidhaa za sukari, mabomba ya maji, nguona vifaa vya ujenzi n.k. Kwasababu hiyo bidhaa za ndanizinanakosa ushindani katika soko. Kamati inaishauri Serikalikukaa na wazalishaji wa ndani na kupitia gharama zauzalishaji ili kuondoa mizigo mikubwa kwa watumiaji wabidhaa za ndani.

Mheshimiwa Spika, watanzania wengi wameitikiawito wa Serikali kwa kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili ya

Page 249: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

kuzalisha bidhaa mbalimbali mfano usindikaji wa asali,matunda na mbogamboga. Katika kutafuta masokowamekuwa wanakumbana na vikwazo mbalimbali ikiwemokupata alama ya ubora inayotolewa na Shirika la ViwangoTanzania (TBS). Kamati inaishauri Serikali, kuhakikisha TBSinawafikia wajasiriamali wengi nchini ili iwe rahisi kwa bidhaahizo kuuzwa katika bei za ushindani.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaitambua nia njema yaSerikali katika kudhibiti uingizaji holela wa sukari yaviwandani. Bado kuna malalamiko kutoka kwa wenyeviwanda vinavyotumia malighafi hiyo kuhusu urasimu katikaupatikanaji wa vibali vya kuingiza sukari hiyo. Kwa sababuhiyo viwanda hivyo vinazalisha chini ya kiwango, baadhi yaviwanda kupunguza watumishi na kubwa zaidi ni kuikoseshamapato Serikali kwa njia ya kodi. Kamati inaendelea kusisitizakwa Serikali kuwa utaratibu utakaowekwa uzingatie maslahimapana ya pande zote wawekezaji na Serikali.

Mheshimiwa Spika, wazalishaji wa ndani wa maziwawanalalamikia kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)inayotozwa kwenye maziwa yanayozalishwa hapa nchini.Hatua hii inayapunguzia ushindani ikilinganishwa na maziwayanayoingizwa kutoka nchi jirani ambazo hazitozi kodi hiyo.Kamati inaendelea kuisisitizia Serikali kuangalia uwezekanowa kuondoa kodi hiyo ili kuvilinda viwanda vya ndani.

5.3 Sekta ya Uwekezaji

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na uwekezaji katikaSekta ya viwanda usiozingatia upatikanaji wa malighafi nafaida za kijiografia za eneo husika. Kwa sababu hiyokunakuwa na gharama kubwa za usafirishaji wa malighafikutoka eneo moja kwenda jingine, lakini pia inawakoseshafursa nyingine za kiuchumi zinazotokana na uwekezaji.Kamati inaishauri Serikali kabla ya kuanzisha viwanda ufanyikeutafiti wa kutosha ili kutambua aina ya kiwanda chakuanzisha kutokana na faida za kijiografia za eneo husika.

Page 250: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua nzurizinazochukuliwa na Serikali, bado kuna malalamiko kutokakwa wawekezaji kuhusu Mazingira ya Uwekezaji nchini kuwasiyo rafiki. Baadhi ya wawekezaji wanalaamikia uwepo wachangamoto kama, mamlaka nyingi za udhibiti; urasimukatika upatikanaji wa vibali vya uhamiaji; na mlolongo wakupata vibali vya uwekezaji. Kamati inaishauri Serikali iendeleekuboresha mazingira ya uwekezaji nchini i l i kuvutiawawekezaji wengi.

Mheshimiwa Spika, ni takribani miaka Ishirini (20) sasatangu wawekezaji wengi waliponunua viwanda vilivyokuwavinamilikiwa na Serikali kwa njia ya ubinafishaji. Kati ya mweziSeptemba na Desemba, 2017, Serikali ilifanya sense yaviwanda hivyo katika mikoa kumi na tatu (13) (Mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Tanga, Morogoro, Mtwara, Arusha,Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Shinyanga naDodoma). Matokeo ya sense hiyo ni kwamba kati ya viwanda156 vilivyobinafishwa ni viwanda 62 tu sawa na asilimia 39.7vinavyofanya kazi vizuri. Kwa takwimu hizo inamaanisha niasilimia 61.3 ya viwanda hivyo havifanyi kazi. Kamati inaishauriSerikali kuendelea kuchukua hatua kwa wawekezaji ambaobado hawajafufua viwanda hivyo ili lengo lilokusudiwalifikiwe. Sambamba na hili ipo haja ya Serikali kuunda tumemaalumu itakayofuatilia kwa karibu eneo hili ili kujua ukweliwake.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua uwepo wajitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katikakuhamasisha uwekezaji kwenye Sekta ya mafuta ya Kulanchini. Hata hivyo bado wapo baadhi wafanyabiasharaambao siyo waadirifu kwa nia ya kulitawala Soko kwamaslahi binafsi. Kamati inaishauri Serikali kuendeleakuhamasisha uwekezaji mkubwa katika Sekta ya hii ili kulindamaslahi ya mlaji.

6.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sanawewe na Mhe. Naibu Spika kwa uongozi wenu mahiri.

Page 251: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

Niwashukuru pia Wenyeviti wote Bunge kwa kuratibu nakusimamia vema shughuli za Bunge.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kumshukuruWaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. CharlesMwijage (Mb), Naibu Waziri wake Mhe. Stella Manyanya (Mb)Makatibu Wakuu, pamoja na wataalamu wote wa Wizarakwa jinsi walivyoshiriki katika kujibu hoja za Wajumbe waKamati kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo kwaMwaka wa Fedha 2017/2018, na kufafanua kwa kina kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha2018/2019.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa,napenda kuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa kushiriki kikamilifuwakati wa kupitia, kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni kuhusu Bajeti hii mbele ya Bunge lako tukufu. Orodhayao ni kama inavyosomeka hapa chini na kwa rukhusa yakonaomba majina yao yaingie kwenye kumbukumbu Rasmi zaBunge (Hansard).

i) Mhe. Suleiman Ahmed Sadiq, Mb Mwenyekitiii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, MbM/Mwenyekitiiii) Mhe. David Cecil Mwambe, Mb Mjumbeiv) Mhe. Balozi Dkt. Diodorus B. Kamala, Mb Mjumbev) Mhe. Salim Hassan Turky, Mb Mjumbevi) Mhe. Gimbi Dotto Masaba, Mb Mjumbevii) Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mb Mjumbeviii) Mhe. Lucy Thomas Mayenga, Mb Mjumbeix) Mhe. Kiteto Zawadi Koshuma, Mb Mjumbex) Mhe. Munde Tabwe Abdalah, Mb Mjumbexi) Mhe. Hawa Subira Mwaifunga, Mb Mjumbexii) Mhe. Munira Mustafa Khaibu, Mb Mjumbexiii) Mhe. Mussa Rashid Ntimizi, Mb Mjumbexiv) Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb Mjumbexv) Mhe. Omary Ahmad Badwel, Mb Mjumbexvi) Mhe. Kmamis Ali Vuai, Mb Mjumbe

Page 252: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

xvii) Mhe. Zainab Mdolwa Amiri, Mb Mjumbexviii) Mhe. Kanal (Mst.) Masoud Ali Khamis, Mb Mjumbexix) Mhe. Ahmed Ally Salum, Mb Mjumbexx) Mhe. Josephine Johnson Genzabuke, Mb Mjumbexxi) Mhe. Mansoor Hirani Sharif, Mb Mjumbexxii) Mhe. Sylvestry F. Koka, Mb Mjumbexxiii) Mhe. Abdulaziz Mohamed Abood, Mb Mjumbexxiv) Mhe. Gibson Blasius Meiseyeki, Mb Mjumbexxv) Mhe. Shamsia Azizi Mtamba, Mb Mjumbexxvi) Mhe. Ahmed Juma Ngwali, Mb Mjumbe

Mheshimiwa Spika, naomba pia kumshukuru Katibuwa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai, pamoja na yeyenamshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Kamati Bw. AthumaniHussein; Mkurugenzi msaidizi Sehemu ya Fedha na Uchumi Bw.Michael Chikokoto; Makatibu wa Kamati Bw. Wilfred Magovana Bi. Zainab Mkamba na Msaidizi wa Kamati Bi. PaulinaMavunde kwa kuratibu vema shughuli za Kamati hadi taarifahii kukamilika.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, sasanaliomba Bunge lako tukufu likubali kuidhinisha Makadirioya Mapato na Matumizi ya fungu 44 na 60, kwa mwaka wafedha 2018/2019 kiasi cha shilingi 143,334,153,648.00 ambaposhilingi 43,309,628,648.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaidana shilingi 100,024,525,000.00 ni kwa ajili matumizi yamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naungamkono hoja.

Suleiman Ahmad Sadiq, (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA

10 Mei, 2018

Page 253: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwenyekiti waKamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, MheshimiwaSuleiman Saddiq, kwa maoni hayo mazuri sana ya Kamatiyanayotusaidia wachangiaji wote katika kuchangia hoja yaMheshimiwa Waziri iliyo mbele yetu. (Makofi)

Kwa hiyo, tunaanza sasa zoezi la uchangiaji, kamanilivyosema, ataanza Mheshimiwa Zitto Kabwe, atafuatiwana Mheshimiwa Silvestry Koka na Mheshimiwa AndrewChenge ajiandae. Mheshimiwa Zitto Kabwe, tafadhali.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi ya kuchangia Wizara hii kwa mara ya tatusasa, toka mwaka 2016, ni Wizara ambayo sijaachakuichangia.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016 mchango wanguulijikita kwenye kufungamanisha sekta ya kilimo na sekta yaviwanda. Moja ya jambo kubwa ambalo tulikuwa nalowakati ule ilikuwa ni mgogoro wa sukari ambao sasaunazungumzwa na tulikuwa pia na mgogoro wa kuhusumafuta ya kula ambao bado tunauzungumza.

Mheshimiwa Spika, Wabunge wa Mikoa ya Dodoma,Manyara na Kigoma ni Wabunge ambao tukipambanavilivyo tunaweza kabisa kuiondoa nchi yetu na aibu yakuagiza mawese kutoa nje. Migogoro ambayotunaizungumza kila siku hapa na mijadala ambayo tunayona wewe mwenyewe juzi ulikuwa mkali sana ni kwa sababuya mawese kutoka nje. Tuna uwezo wa kuzalisha maweselakini Serikali haijaweka mkakati wowote ule wa kuhakikishakwamba tunajitosheleza na tunaweza tukauza nje.Haijaweka mkakati wowote ule wa kuhakikisha kwambatunaongeza uzalishaji wa alizeti, tuweze kuchakata hapana tuondokane kabisa na hii aibu ya kuagiza mawese kutokaMalaysia, watu ambao walikuja kuchukua mbegu Kigoma.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, huu ni mwaka wa tatu sijaonakatika mpango wowote wa Serikali kuhusiana na jambo hili

Page 254: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

na bado tunabishana na kulumbana na kushutumiana kwauagizaji wa mawese. Hili ni jambo ambalo linapaswa liwe niaibu hata kulizungumza katika Bunge hili kwa sababu tunaalizeti, tuna mawese Kigoma na maeneo mengine kamaKyela yangeweza kabisa kumaliza matatizo kama haya.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana nil izungumzafungamanisho kuhusu miradi mikubwa inayoendelea nchinina viwanda na hasa hasa niliangalia suala la ujenzi wa relina jinsi ambavyo tunaagiza malighafi za ujenzi wa reli kutokanje. Leo umemsikia Waziri hapa anazungumza, bado tunalipafidia Mchuchuma na Liganga. Leo umemsikia Wazirianazungumza kwamba wamekwenda wamefunguakiwanda cha nondo wapi, kiwanda cha nondo sehemunyingine, nondo zote hizi malighafi zake ni kutoka nje na sisituna chuma Mchuchuma na Liganga miaka yotetunazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mbunge tangu mwaka2000 unakumbuka, tangu mwaka 2000 tunazungumzaMchuchuma na Liganga, leo Waziri anazungumza kulipa fidiaMchuchuma na Liganga. Sisi ni watu wa namna gani? Kunatakwimu moja inaonesha kwamba 40 percent yaWatanzania ni stunted, inawezekana humu 40 percent of usni stunted, kwa sababu tunaongea vitu vilevile, miaka yotetunakumbushana, nothing happens. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii kweli inaingia akilini, tunachuma na makaa ya mawe yamejaa pale Ludewa tunampamkandarasi kazi ya kujenga reli, vyuma vinatoka Uturuki,India, China, kweli? Wenzetu Kenya wanajenga reli nawenyewe wanaagiza hukohuko wakati tungewezakuwauzia. Zambia wanajenga reli kuunganisha Angola naZambia, tungeweza kuwauzia chuma, kwa kweli mimi sioniwhat we are doing. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016 Serikali ilikuja hapana mpango unaitwa C2C, Cotton-to-Clothing, nimeangaliahotuba ya Waziri hapa, hata kulizungumza neno hiloameona aibu. Unaondoaje umaskini bila viwanda vya nguo?

Page 255: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

Niambie nchi gani? Uingereza ambayo ni moja ya nchi kubwaumasikini wake umeondolewa na viwanda vya nguo nahawakuwa na pamba walikuwa wanaagiza pamba kutokakwenye makoloni yao. Hata kuzungumza MheshimiwaMwijage Cotton-to-Clothing, agenda yenu wenyewe naulikuja hapa ukatamba na vitabu kama ulivyovileta leo,where is it? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo kubwa ambalo napendakuliongelea, nimalizie dakika zangu za mwisho ni biasharaya nje. Tunazungumza viwanda lakini kwa miezi 24 iliyopitaSerikali hii ya Awamu ya Tano imesababisha hasara ya nchiyetu ya mauzo nje ya thamani ya dola bilioni moja na siyotakwimu zangu, ni takwimu zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, angalia ukurasa unaozungumziaChina, ukurasa wa 51, mauzo yetu nje Chinayameporomoka. Nasoma takwimu, China mauzo njeyameporomoka kutoka dola milioni 356 mwaka 2016 mpakadola milioni 217 mwaka 2017, kutoka takwimu za Serikali.Japan, mauzo yetu nje yameporomoka toka dola milioni 140mpaka dola milioni 75.

Mheshimiwa Spika, lakini zaidi tumeshindwa hatakuuza mbaazi India. Waziri alikwenda India amesemaamezungumza, mimi sina hakika kama Waziri kwelialikwenda kuzungumza na Waziri mwenzake lakini biasharani diplomasia. Mwigaje huwezi wewe unazunguka kunaviwanda, Naibu wako anazunguka na viwanda, internationaltrade ni Foreign Affairs. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, juzi Vice President alikuwa London,Modi alikuwa London, mmeshindwa kuseti appointment yaVice President na Modi wakazungumza tukatatua tatizo lambaazi? Mbaazi bei imeporomoka kutoka Sh.3,000 mpakaSh.150 kwa kilo. Mwezi Machi nimezunguka kwenye kata 16nchi hii nimekuta watu wanalia mbaazi zimo ndani. WaziriMstaafu Nape alizungumza hapa, alimuuliza Naibu Waziri,Naibu Waziri akasema kwamba tutakula, no it is foreign trade!It is about forex! (Makofi)

Page 256: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

Mheshimiwa Spika, nchi hii tunaagiza nje vitutunahitaji fedha za kigeni, mbaazi, choroko, giligilani, zilikuwazinatupa dola milioni 224 kuuza India mwaka 2016, mwaka2017 ikaporomoka dola milioni 131, mwaka 2018 sasa hividola milioni 75, what are you doing? Unapopoteza hizi forexutanunua mafuta na nini kwa sababu inabidi uagize. Whatwill you buy mafuta with?

Mheshimiwa Spika, mimi nashindwa kuelewa whatare we doing. Wizara ya Viwanda na Biashara that part yabiashara especially foreign trade hamna, tumepoteza onebillion dollars in the span of 24 months, ni sawasawa nakupoteza kila siku shilingi za Kitanzania bilioni tatu in the last24 months, you are still here Mwigaje, why don’t you just quit?Umeshindwa kazi. You can’t run Wizara ya Viwanda naBiashara as if you are running TAMISEMI, it is diplomacy, it isabout going out getting markets. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo Malaysia kule a friend ofTanzania has been elected as a new Prime Minister, MzeeMahathir, a very close friend of Mwalimu Nyerere, go thereimmediately, get the markets. Hamuwezi mkajidanganya naviwanda vya cherehani mkadhani kwamba you save thiscountry! Foreign trade is power.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, haiwezekani sisi tukakosa sokoIndia. The majority ya Wahindi ambao unawaona hapaTanzania they are from Gujarat, Modi is from Gujarat, use that,talk to them! Hebu tuwaokoe hawa wakulima wa mbaazi,wakulima wa giligilani, giligilani imeshuka bei, mbaaziimeshuka bei, choroko imeshuka bei na dengu imeshuka bei,what are you doing?

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Zitto Kabwe kwamchango wako uliotuanzishia. Baadhi ya mambotunakubaliana na wewe kwa kweli, Mawaziri inabidi msafirikweli. Waziri wa Biashara hawezi kukaa na sisi hapa, lazimaaende. Tumuombee popote pale kwenye mamlaka lazima

Page 257: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

aondoke, asafiri. Maana bidhaa zetu sasa tutauza wapi?Tutauza Kongwa, kuna soko? Waziri wa Maliasili lazimaaondoke, lazima asafiri, Waziri wa Utalii lazima apigemawingu huko na Mawaziri wengine, kabisa ndiyo ukweliwenyewe jamani, sisi Wabunge ndiyo tuwasemee. (Makofi)

Tunaendelea na Mhishimwa Silvestry Koka, halafuatafuatia Mheshimiwa Komu.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia. Nichukuenafasi hii kwanza kuishukuru sana Serikali yetu ya Chama chaMapinduzI kwa kazi nzuri inayofanya. Wizara ya Viwandaimekuwa ikijitahidi kwa hali mali ili kuhakikisha Sera yetu yaViwanda inakua. Nichukue kweli nafasi hii kumshukuru sanaMheshimiwa Rais kwa kujitoa na kujitolea kwa ajili yawananchi wa Tanzania kuhakikisha Watanzania wenyewetunajenga viwanda na tunakwenda kushika hatamu zauchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile nitoe pongezi kwa kazikubwa ya kujenga miundombinu mbalimbali kwa sababukupitia miundombinu hii ndiyo tunaweza kujenga uchumi wakati na hata uchumi mkubwa. Mifano iko wazi, ujenzi wareli, ujenzi wa miundombinu ya umeme kama Stiegler’s Gorgeni jambo ambalo tunahitaji tumuunge Mheshimiwa Raismkono kwa nguvu zetu zote.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu mojawapo yachangamoto tuliyonayo katika uanzishaji wa viwanda nipamoja na nguvu za kusukuma au kuendesha viwanda kwamaana ya umeme. Ndugu zangu wote tunafahamu kwambaumeme unaozalishwa kwa maji ni rahisi kuliko umememwingine wote. Kwa hiyo, tutakapopata umeme mkubwaunaozalishwa na maji kutoka Stiegler’s Gorge maana yakeni kwamba hata gharama za uzalishaji zitapungua, tutawezakuzalisha kwa gharama nafuu na hatimaye kufikisha bidhaakwa wananchi kwa gharama iliyo nafuu.

Page 258: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndugu zanguwafanyabiashara wa Tanzania na Watanzania wotetumuunge mkono Rais, tujitokeze tujenge viwanda, tuungemkono miradi ambayo ipo mbele yetu ili siku ya mwishojihitada za kwenda kwenye uchumi wa kati ziweze kukamilikabila tatizo lolote.

Mheshimiwa Spika, Serikali yetu ina sababu hasa yakutazama sasa balance ya biashara ya ndani nje. Tuangaliena tuweze kuona ni namna gani tunapoanza sasa kuleaviwanda vyetu tuna balance pamoja importation ya bidhaamuhimu kwa ajili wananchi. Kwa sababu lengo la biasharapamoja na kupata faida na kulipa kodi lakini ni kuwafikishiawananchi bidhaa kwa bei iliyo nzuri, nafuu na ubora. Sasakama hatutarudi tukaangalia bado kuna watu wachachewata-take advantage na wananchi wataendelea kununuabidhaa kwa gharama kubwa na wao kujilimbikizia faidakubwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kuwepo nabalance kati ya bidhaa zinazoletwa kutoka nje nazinazozalishwa ili yale mabadiliko ya bei ya uzalishaji namalighafi yaweze kumnufaisha vilevile mwananchi ambayendiye mtuamiaji. Nina imani kwa kufanya hivi tutatimizaazma ya Serikali ya kumhudumia na kumsaidia mwananchiwa kipato cha chini.

Mheshimiwa Spika, kujenga viwanda ni jambo mojalakini kuviendesha ni jambo lingine ambalo ni gumu zaidi.Nitoe mfano wa kiwanda kinachozalisha viuadudu paleKibaha. Kiwanda hiki kilianza kujengwa mwaka 2010kikakamilika 2015 na kikaanza uzalishaji 2016. Kiwanda hikini cha pekee Afrika na kina uwezo wa kuzalisha viuaduduau viatilifu vinavyoua viluilui vya mbu kiasi cha tani milionisita kwa mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini navyoongea na wewekuanzia kilipoanza kufanya kazi mwaka 2016 hadi leokimezalisha tani laki nne tu na hakuna wanunuzi. MheshimiwaWaziri atakubaliana na mimi kwamba tarehe 22 Juni, 2017

Page 259: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

Mheshimiwa Rais alipotembelea viwanda Kibahaalikitembelea kiwanda hiki na alifurahishwa sana na kiwandahiki kwa sababu ndiyo njia pekee ya kumaliza malaria nchini.Alitoa maagizo kwamba kila halmashauri inunue dawa hiiiweze kutumika kuuwa viluilui vya mbu na tuangamizemalaria hapa nchini. Tangu kipindi kile katika ya halmashauri81 ambazo walichukua dawa hii ni halmashauri 25 tu ndizoambazo zimelipa, nyingine hawajalipa kiwanda kinaendeleakudorora. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, dawa hii ndugu zanguWaheshimiwa Wabunge kama hamuifahamu kazi yakeinashambulia viluilui vya mbu katika maeneo mbalimbaliikiwa ni pamoja na maeneo ambayo maji yamesimama nakuhakikisha kwamba mbu hawawezi kuzaliwa. Nafikiri hiindiyo njia pekee ya kumaliza malaria badala ya kutumiafedha nyingi kununua dawa kwa ajili ya malaria. Dawa hii ninzuri sana, kwanza kabisa ni environmental friendly, yaani siyokama dawa nyingine mfano DDT na nyingine tunazotumiakiasi kwamba unaweza hata ukainywa. Watengenezaji wali-demonstrate mbele ya Mheshimiwa Rais kwa kunywa iledawa, haina hata madhara hata ukiinywa lakini ni sumu kwaviluilui vya mbu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa makusudi kabisaimetenga fedha nyingi kwa ajili ya huduma ya dawa na afyaza Watanzania kutoka bajeti ya shilingi bilioni 30 mpakashilingi bilioni 200 kwa ajili ya dawa ikiwa ni pamoja nakuhakikisha kwamba malaria inapigwa vita nchini. Sasatunachoangalia ni watu tumeangukia, ndiyo tunahangaikakutibu malaria hatutaki kuangalia ni wapi tumejikwaa natutapojikwaa ni kung’atwa na mbu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namwomba sana MheshimiwaWaziri, kama kweli tunataka kusaidia viwanda vyetu vyandani kiwanda ambacho kimejengwa kwa ushirikiano aukwa msaada kati ya Cuba na Tanzania ambacho hadi sasatayari wenzetu wa Angola, Nigeria wameshaanza kupatahamu na kuleta order kwa ajili ya dawa hii, tusaidie kiwandahiki kizalishe dawa na bajeti ya Wizara ya Afya itengwe kwa

Page 260: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

260

ajii ya kulipia dawa hizi kwa sababu lengo letu ni kuangamizambu si kuendelea kila siku Watanzania wanauguatunahangaika kuwatibu kwa gharama kubwa. Niombe sanaWizara ya Viwanda na Biashara ishirikiane na Wizara ya Afyaili waweze kununua dawa hizi, Watanzania wapewe elimuya kuzitumia na hatimaye tuangamize mbu na Tanzania iwefree from malaria. Inawezekana, kiwanda tunacho,tutachekwa kama tutaendelea kuugua malaria na wakatitulishajipanga hadi kuweza kujenga hiki kwa gharamakubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kiwanda hiki hakijasimamiwavizuri, kiko chini ya NDC, lakini hadi sasa hakina hata Bodi yaWakurugenzi sasa kinajiendeshaje? Kina wafanyakazi,uzalishaji ni duni na hakuna anayekiangalia ipasavyomatokeo yake tunakwenda kwenye hasara na tunatoka sasanje ya azma na sababu ya Tanzania ya viwanda. Ni wazikama kitasimamiwa kina uwezo mkubwa sana wa kuuzabidhaa hii ndani na hata nje ya nchi yetu na kikailetea Serikalimapato makubwa ya kigeni kwa sababu kiko pekee Afrikana dawa inayotengeneza ni pekee ambayo inakwendakulenga mbu na kumwangamiza na kuhakiksha kwambamalaria haitaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Spika, niiombe sana Wizara ya Viwandana Biashara pamoja na kuhimiza ujenzi wa viwanda vileviletushiriki katika kuhakisha viwanda hivi tunavisimamia,tunavisaidia ili viweze kuleta tija na hatimaye tuweze kufikiamalengo makubwa ya Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kuwaasawafanyabiashara wenzangu Tanzania, kama nilivyosemalengo kubwa la biashara mbali ya kulipa kodi na kupatafaida ni kumhudumia Mtanzania. Tuna wajibu wa kuhakikishatunapopeleka bidhaa katika masoko ya Mtanzaniatunamlenga Mtanzania apate nafuu katika bidhaa hiyo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameshanyooshamkono kwa wafanyabiashara, ameamua kutuunga mkono

Page 261: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

261

na kutusaidia na hata amekuwa akitoa maamuzi ya papokwa papo kusaidia wafanyabiashara wa Tanzania. Ametakawafanyabiashara wa Tanzania tufanye biashara, tuzalishe,tujenge viwanda na tutumie soko la ndani na fedha za ndanikuboresha viwanda vyetu. Sasa kutokupeleka azma hiyokwa wananchi na kuwafanya wananchi wakawawanatapatapa wapate wapi mahitaji ni sawasawa nakuiudhi Serikali.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge wa Kibaha.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Spika, kwa hiyo,nimalizie kwa kuomba tujitahidi twende sambamba na azmaya Mheshimiwa Rais na Serikali yetu. Naunga mkono hojatuendelee kujenga nchi yetu ya viwanda. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mhehimiwa Silvestry Koka.Nilishakutaja Mheshimiwa Antony Komu, atafuatiwa naupande wa CUF Mheshimiwa Zainabu Mndolwa.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Spika, naminikushukuru kwa kunipa nafasi kuchangia bajeti hii yaViwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ambayo kimsingindiyo inayobeba kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais wa Awamuya Tano, Dkt. Joseph Pombe Magufuli.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hiyo kaulimbiu yaMheshimiwa Rais lakini uhalisia kwa maana ya bajeti haupo.Kwa sababu 2015/2016 bajeti ya kwanza ya Mheshimiwa Rais,utekelezaji kwenye bajeti ya maendeleo kwenye Wizara hiiilikuwa ni asilimia 5 tu, 2017/2018 ikawa asilimia 9.47. Katikahali ya namna hii ukiunganisha hiyo kaulimbiu na majigamboyote yaliyokuwepo na dhamira ya kutaka kuona kwambatunakwenda kwenye uchumi wa viwanda haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye ripoti ya CAGambayo inaangalia ufanisi kwenye viwanda vidogo vidogo

Page 262: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

262

na vya kati ambavyo mahali popote duniani ndiyo moyowa mapinduzi ya uchumi wa viwanda, anasema hali si nzuri,bajeti kwenye sekta hiyo imeendelea kushuka katika ngazizote maana yake mpaka kule kwenye halmashauri zetu, sizaidi ya asilimia 16, kwa hiyo, bado uhalisia unaendeleakuonekana kwamba haupo. Mafunzo kwenye viwanda hivividogo vidogo kwenye sekta hii bado yameendelea kushuka,CAG anasema yako kwenye wastani wa asilimia 7 tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye Vituo vya Maendeleo yaTeknolojia ambavyo vilianzishwa na Mwalimu Nyereremashine ambazo zinatumika mpaka leo zina umri wa miaka40, amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,siyo sisi tunaosema. Sasa seriousness iko wapi? UkiangaliaCAG anasema, sekta ya viwanda vidogo vidogo na katiinaporomoka kwa asilimia 30 ikilinganishwa na kukua kwakekwa asilimia 5.6. Kwa hiyo, kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais yakujenga Tanzania ya Magufuli ya Viwanda haina uhalisiawowote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mwenyekiti wa Kamati alivyokuwaanazunguza hapa amezungumzia mazingira ya kufanyabiashara Tanzania. Mpaka tunavyoongea hapa sasa hivi sisini wa 137 duniani kati ya mataifa 190 kwa mazingira rahisi yakufanya biashara. Kinachokwenda kupeleka huo ugumu ninini? Ni matamko ya viongozi wetu wa siasa wa upandehuu wa CCM ambayo yanafanya mazingira yetu yawe si yakutabirika na kwa sababu hiyo uwekezaji unakuwa ni mgumukatika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukitaka kupata kupata kibali chakuanzisha kiwanda hapa pamoja na mbwembwe zoteanazosema Mheshimiwa Waziri hapa unaweza ukatumiamiezi kadhaa. Kuna marufuku zinatolewa tu kila siku na hatawafanyabiashara waliomo humu ndani wamekuwawakilalamika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni-declare interest nilikuwa kwenyeKamati ya Viwanda na Biashara, tulikutana na tatizo hiliambalo Mwenyekiti amelizungumza hapa vilevile la vibali

Page 263: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

263

vya sukari ya viwandani. Vipo viwanda ambavyotunapozungumza sasa hivi vimefungwa kama Kiwanda chaSAYONA kule Dar es Salaam kutokana na sukari yao kuzuiliwabandarini tangu mwezi wa nane eti uhakiki unafanyika naukimuuliza Mheshimiwa Waziri anasema hili liko kwa tajirimwenyewe. Kwa hiyo, masuala kama haya yanaleta shida.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kuna masuala ya hizi mamlakazetu za udhibiti, TRA, ubabe mtupu na urasimu ambaohausaidiaa nchi hii. Nimeona kwenye magazeti ya leo TRAsasa wanawaomba wafanyabiashara walifunga biasharazao warudi. Hizi kauli za kukinzanakinzana zinatupa shida.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, jana Waziri wa Fedha alikirikwamba hali ni mbaya na ndiyo maana bajeti hazitekelezeki.Hawawezi kukusanya mapato kwa sababu ya hiimikanganyiko ambayo ipo kwenye uendeshaji wa Serikaliyetu. Kwa hiyo, tunawataka waache hayo mambo ambayowanafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni kushikashika vitu vingibila ya kuwa na jambo moja ambalo tumeamua kulifanyakwa sababu ya tafiti ambazo tumefanya na tukalikamilisha.Mheshimiwa Zitto hapa amezungumzia Mchuchuma naLiganga. Hivi kweli kama tuna akili sawasawa, tumefanyatafiti zetu na tumedhamiria kweli kuleta mapinduzi nakukomboa watu wetu ni kwa nini hatuutekelezi mradi huu?Tuna mradi wa Bwawa la Kidunda pale Morogoro ambalolinahitaji Dola za Marekani milioni 251 ili tupate umeme, ajira,kusaidia kilimo chetu, ku-stabilize Mto Ruvu na maji kwa ajiliya viwanda lakini jambo hili linaendelea kuwa ni hadithi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati huo huo nilisema hapa juzi,nchi hii inaagiza chakula kwa mwaka kulingana na takwimuza Benki Kuu ya kwetu sisi bilioni 888.5. Hivi jamani hii Serikalihaina uchungu na nchi hii? Hivi hawaoni kwambatungechukua hizo Dola bilioni 251 tukawekeza pale Kidunda

Page 264: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

264

tungeweza tukaokoa hizo bilioni 888.5 na baada ya hapotukaenda sasa kuwekeza katika mambo mengine ambayokwa kweli mimi naita ni mambo ya kishamba tu, yakujionyesha. Eti na sisi tuwe na ndege kwa kuwekeza trilionimoja tena sisi kwa sera ya nchi yetu tumeshakubalianakwamba twende kwenye Private Public Partnership (PPP)hatufanyi. Tungeweza tukaweka hayo masuala ya ndegekwenye hiyo PPP, sasa hivi tunajenga reli ya standard gaugeambayo ni kitu cha maana na muhimu sana lakini tukaendakwenye utaratibu huo. Tunachukua pesa za Watanzania,badala ya kuwekeza kwenye mambo ya msingi ambayoyatawapa matokeo ya haraka na yatakayosaidia kupigahatua kwa haraka…

TAARIFA

MHE. RICHARD P. MBOGO: Taarifa.

SPIKA: Taarifa, Mheshimiwa Mbogo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika,naomba nimpe taarifa Kaka yangu Mheshimiwa Komu,namna ya uwekezaji kwenye ndege ni moja ya eneo labiashara ambapo litaingiza mapato. Mapato yako ya ainanyingi, mojawapo ni corporate tax, Pay As You Earn, SDL,tutaimarisha utalii, kwa hiyo, itaendelea kusaidia sekta zingineambazo zinaingiza pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, nashukuru. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Antony Komu hamna haja, mudaumekwisha, huu ubishi wa mambo ya ndege sitakikuuendeleza tena, imeshasemwa vya kutosha.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Naona upande wa CUF hamjajiandaa.Tuendelee na Mheshimiwa Joseph Mhagama.

Page 265: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

265

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi asubuhi ya leo yakuchangia sekta muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa.Kwanza kabisa, niwapongeze Wizara na nimpongeze sanaMheshimiwa Rais kwa kusimamia vizuri sana sekta hii yaviwanda na biashara kiasi kwamba wadau tunapatamatumaini kwamba tunaweza kuifikia Tanzania ya viwandandani ya kipindi chake cha miaka 10 ya uongozi wake mahiri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, huwezi kupata Tanzania yaviwanda kama tutaendelea kupuuza mradi wa Liganga naMchuchuma. Mradi huu wa Liganga na Mchuchuma, natakanitumie nafasi hii nieleze vizuri, ulianza kuzungumziwa naMbunge mtangulizi wa Mheshimiwa Jenista Mhagama,Mheshimiwa Prof. Simon Mbilinyi, lakini imekuja kuongelewakwa zaidi ya miaka 10 na Mheshimiwa Jenista Mhagama(Waziri) na mimi ni Mbunge wa tatu kulizungumza hili lakinimpaka leo commitment ya Serikali imekuwa ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Liganga kuna chuma, tathminiinaonesha chuma iliyopo Liganga inaweza kuchimbwa kwakiwango cha tani milioni moja kwa mwaka, hiyo ni tani yachuma. Chuma hii pamoja na kuzalisha chuma, inazalishamazao mengine yanayoambatana na chuma. Kuna madiniya vanadium pentoxide na kuna titanium dioxide, haya nayoni madini yanayoambatana na chuma. Watanzania wotetunajua chuma ni malighafi ya msingi ya viwanda. Ujenzi waviwanda unatumia sehemu kubwa chuma, mashine zote zaviwandani kwa asilimia kubwa zinahitaji chuma, unaipatajeTanzania ya viwanda bila kuchimba chuma ya Liganga?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda jikoni utakuta kijiko, kisu,na uma, hivi vyote vinatengenezwa na chuma. Ukiendashambani utakuta jembe, panga, nyundo, vinatengenezwana chuma. Ukipanda gari, asilimia 80 ya gari ni chuma, niutajiri mkubwa sana Watanzania tumeauacha pale Liganga.Ipo mifano mingi, tukienda kwenye nyumba zetu

Page 266: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

266

tunazozijenga, bati ni product ya chuma, madirisha yetu,nondo na grill zote hizi ni product ya chuma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni viwanda vingapi vinawezakuanzishwa kutokana na chuma ya Liganga? Tunawezakutengeneza viwanda vya bati, viwanda vya nondo,viwanda vya magari na kila aina ya kiwanda tunachokitakatutatengeneza na sisi wenyewe tutakuwa wateja nambamoja wa hivyo viwanda. Hatuwezi kuipata Tanzania yaviwanda kama hatuweki makusudi kwenda kuchimbachuma ya Liganga.

Mheshimiwa Spika, mwaka 1864, nchi ya Marekaniiliahirisha ujenzi wa reli kwa sababu walitaka watumie chumayao kujenga reli kwa sababu waliamini kiwango cha chumaambacho kitahitajika kujenga reli iwapo kitachimbwa ndaniya nchi husika, kwanza kitaokoa pesa kubwa ya Serikali lakinikitachangia sana kwenye pato la Taifa. Mwaka ule 1864wakati Marekani wanajenga reli chuma cha ndani kilikuwana bei mara mbili ya chuma kilichokuwa kinatoka nje ya nchiya Marekani, hata hivi kwa sababu ya uzalendo waliamuakutumia chuma iliyozalishwa ndani. Kwenye hili niombe sanaWizara iamue sasa kwenda kuchimba chuma cha Liganga.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, chuma cha Liganga pamoja nakutoa malighafi ya tani milioni moja ya chuma kwa mwakaitatoa ajira takriban 4,000. Ajira 4,000 ni mchango mkubwasana kwenye idadi ya ajira. Tumesikil iza hotuba yaMheshimiwa Waziri, ni nzuri. Hata hivyo, ukifanya uchambuzi,ajira zilizozalishwa kati ya mwaka 2015 mpaka 2017 ni 26,113,ajira 4,000 zina mchango gani katika hiyo maana yake nizaidi ya robo ya ajira zilizozalishwa katika kipindi hicho.

TAARIFA

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa Spika,taarifa.

Page 267: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

267

SPIKA: Hizi taarifa tungeomba ziwe za maana. NdiyoMheshimiwa.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa Spika,naomba nimpe taarifa mjumbe anayezungumza kwambaajira zitakazotolewa na Mradi wa Makaa ya Mawe yaMchuchuma na Liganga ni ajira zaidi ya 32,000 na siyo 4,000.(Makofi)

SPIKA: Nakubaliana na wewe, ajira 4,000 zinawezazikawa za moja kwa moja lakini baada ya hapo ajira ni nyingisana. Pokea taarifa hiyo Mheshimiwa Mhagama. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika,naipokea kwa mikono miwili taarifa hii. Nikibaki hapo, ajirazitakazozalishwa kwenye mgodi huu wa chuma pamoja naspillover effect, maana yake ni zaidi ya ajira zilizozalishwakatika kipindi hiki chote cha utawala huu, kwa hiyo, si jambola kulifanyia dhihaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nabaki hapo hapo kwenyeLiganga na Mchuchuma, mradi wa Mchuchumautakaozalisha kuzalisha umeme kwa kutumia makaa yamawe, umeme ambao utazalishia chuma cha Liganga,mtambo huu utakuwa na uwezo wa kuzalisha umememegawatts 600, hiyo ni faida nyingine. Sasa megawatts 600ni sawasawa na nusu ya umeme wote tuliokuwa nao mwaka2015. Mheshimiwa Rais amekabidhiwa nchi hii ilikuwa naumeme wa megawatts 1,308 sasa Mchuchuma peke yakeitazalisha umeme megawatts 600, si kitu kidogo wala siyocha kukidharau. Umeme huu sawa na robo ya umeme woteutakaozalishwa kwenye Stiegler’s Gorge. Stiegler’s Gorgewatazalisha umeme megawatts 2,100 na megawatts 600 nirobo ya huo umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nisisitize kwa kusema umeme huuwa megawatts 600 utakaozalishwa Mchuchuma ni asilimia12.2 ya malengo tuliyojiwekea ya umeme tunaohitaji mpakaifikapo mwaka 2020. Sasa unajua huwezi kuipata Tanzaniaya viwanda bila umeme. Katika michango yangu

Page 268: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

268

iliyotangulia nilisema, umeme tulionao Tanzania hauwezikutupa Tanzania ya viwanda. Afrika Kusini mwaka 1970walikuwa na megawatts 14,000, sisi leo tuna megawatts 1,500mpaka 2,500, tunahitaji uzalishaji mkubwa wa umeme. Mradiwa Stiegler’s Gorge ni mradi muhimu sana kwa Taifa letu,lazima tuupe nguvu, lazima tuunge mkono lakini lazimatuongeze vyanzo, chanzo kingine ni huu wa Mchuchuma,megawatts 600, kwa kutumia makaa ya mawe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeongea kwa msisitizo mkubwakwa sababu ninaamini hatuwezi kuipata Tanzania yaviwanda bila umeme wa kutosha na hatuwezi kuipataTanzania ya viwanda bila kwenda Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Spika, niongezee tu hapo, kwenye hilisuala la umeme. Wenzetu nchi nyingine wanaongeamegawatts 84,000 sisi tunaitafuta Tanzania ya viwanda bilakwenda kuchimba chuma, bila kwenda kushughulika naLiganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine nichangie tukwamba, Tanzania tuna bahati, tumeendelea kuvutiawawekezaji na nimpongeze sana Mheshimiwa Waziriamefanya sana kazi tumeona wawekezaji toka nchimbalimbali wanakuja kutoka Ujerumani, Ufaransa, ni initiativekubwa sana hii, watu wamebeza lakini wanabeza kwasababu hawajui misingi ya uchumi. Hawa wanapokujawatatuongezea teknolojia na mtaji, tutahakikisha kwakuwatumia hao tunavuka, tunafikia haya malengo yetu lakinieneo muhimu ni kulinda viwanda vyetu vya ndani.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu mudahaujanitosha, nichukue nafasi hii kukushukuru sana na naungamkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Joseph Mhagamakwa mchango wako. Ni kweli haya mambo ya Mchuchumana Liganga kwa kweli yamesemwa kwa miaka, ni vizuriwakati fulani Mheshimiwa Waziri utakapokuwa kesho una-wind up ukatupa kidogo picha na Mwenyekiti wa Bodi ya

Page 269: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

269

NDC, Dkt. Samuel Nyantahe yuko hapa, tulimtambulisha.Ninyi NDC mnatuangusha sana, kuna siku tutawaita hapa,inaelekea ndiyo mnaomwangusha Mheshimiwa Waziri ninyiNDC. Hiki kitu kimeongelewa sana kwa nini kiwe kinakwendaslow-slow. (Kicheko/Makofi)

Twende CUF, Mheshimiwa Shamsia Azizi Mtambaatafuatiwa na Mheshimiwa Jitu Soni.

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipatia nafasi ili na mimi niweze kuchangiakatika Wizara hii ya Viwanda na Biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napendakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya nzuri naleo hii kuweza kusimama katika Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi za dhatikabisa kwa Mwenyekiti wangu wa Chama-Taifa, full bright,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kazi kubwa ambayo anaifanyaya ujenzi wa Chama changu. Pia napenda kutoa pongeziza dhati kabisa kwa Naibu Katibu Mkuu, MheshimiwaMagdalena Sakaya kwa kazi kubwa ambayo anaifanya yaujenzi wa Chama changu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niingie katika mada.Wakati Tanzania tunaelekea katika uchumi wa viwanda, nilazima tuwe na umeme wa uhakika na hakuna mwekezajiatakayekubali kujenga kiwanda ili apate hasara kwa sababuumeme unapokosekana kwa saa nne tu ni hasara kubwakwa mwekezaji. Kwa mfano, itabidi apunguze wafanyakazilakini pia wafanyakazi wataliobaki wanahitaji mishahara. Piauzalishaji utakuwa chini ya kiwango, kwa mfano, kiwandakilichopo kule kwetu Mtwara, Kiwanda cha Saruji chaDangote kama kilikuwa kinazalisha kwa siku tani 100,umeme unapokatika uzalishaji utapungua, kiwandakitazalisha tani 60 badala ya tani 100. Hii ni hasara kubwakwa Taifa na mwekezaji. (Makofi)

Page 270: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

270

Mheshimiwa Spika, nije katika masuala ya ajira.Umeme unapokuwa wa mgao au unapokatika mwekezajiitabidi apunguze wafanyakazi. Akifanya hivyo atakuwaamepunguza ajira na familia nyingi zitaishi maisha ya dhikikwa kuwa kipato cha familia kitakuwa kimepungua.

Mheshimiwa Spika, vijana wengi sasa wameamuakujiajiri kwenye viwanda vidogo vidogo kama viwanda vyakuchomelea (welding), viwanda vya kuwekea samaki,viwanda vya kutengeneza barafu, viwanda vya salon za kikena za kiume, vyote vitakuwa hazifanyikazi kwa kukosaumeme wa uhakika. Hii ni hasara kubwa kwa Taifa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nije upande wa kodi za Serikali.Uzalishaji wa viwandani ukipungua hata kodi za Serikali nazozitapungua. Serikali itashindwa kutimiza majukumu yake yakupeleka miradi ya maendeleo kwa wananchi wake. Ushauriwangu kwa Serikali iwekeze nguvu kubwa katika uzalishajiwa gesi iliyoko kule Msimbati, gesi ya Mnazi Bay ili iwezekutimiza majukumu yake ya kusambaza umeme wamajumbani na viwandani.

Mheshimiwa Spika, niongelee masuala ya kibiashara.Akina mama wengi tumepata mwamko wa kufanyabiashara lakini kikwazo kikubwa tunachokumbana nachoni kodi kubwa tunazotozwa na Maafisa wa TRA, tunafanyiwamakadirio makubwa mno. Naiomba Serikali yetu Tukufu yaMheshimiwa Rais John Pombe Magufuli itupunguzie kodi hizikwa sisi wajasiriamali, kama maduka ya nguo, vifaa vya ujenzi,mahoteli, biashara ya magari ya abiria yaendayo mikoanina daladala. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi.(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Jitu Soni na atafuatiwa naMheshimiwa Kiteto Koshuma.

Page 271: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

271

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwakupata nafasi siku ya leo kuchangia. Awali ya yote, naombakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya na kunijaliakufika hapa leo.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kwanzakumshukuru Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Rais wetukwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya pamoja na watendajiwake wote. Muhimu ni kuelewa dhana nzima na mahaliambapo wanataka nchi yetu ielekee. Mimi nashukuru kwahii dhana nzima ya kuwa na Sera ya Viwanda ambaponaamini kabisa tukienda vizuri na wote tukachangia vizurina kila mmoja akaweka mawazo yake pale na tukaangaliachangamoto zilizopo na namna ya kukabiliana nazo,mafanikio yapo na uchumi wetu utaendelea kukua.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi uchumi wetu ni mzuri naunaendelea kukua, kuna changamoto ndogo ndogoambazo naamini Wizara ya Viwanda na Biashara chini yaMheshimiwa Mwijage na Naibu Waziri pamoja na timu nzimaikiongozwa na Katibu Mkuu na wote wanafanya kazi nzurina kubwa. Changamoto bado zipo na tunahitaji kuwapamsaada, kuwapa mawazo mbadala na maeneo ambayowanafanya vizuri tuwapongeze lakini maeneo ambayowanatakiwa kuyafanyia kazi wafanyie kazi.

Mheshimiwa Spika, jambo la muhimu ni kuangalianamna ya kuunganisha Serikali yaani coordination badohaipo. Waziri unafanya kazi peke yako na kila Wizarainajitegemea. Mngefanya kazi kwa kuunganisha Wizara zoteili tupate mafanikio makubwa. Tanzania bado easy of doingbusiness haipo. Bado kuna ukiritimba mkubwa na ukiangaliakila mmoja anajitahidi kuhakikisha kwamba anafanikiwa.

Mheshimiwa Spika, muhimu ni kuangalia namna yakulinda viwanda vya ndani. Namna ya kulinda viwanda vyandani ni lazima muwekeze kufanya utafiti wa uhakika

Page 272: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272

kuhakikisha kwamba bei ya uzalishaji wa viwanda vyetu vyandani inakuwa ndogo ili isishindane na bidhaa zinazotokanje, hilo ndilo jambo kubwa kuliko yote. Leo hii wotewanaowekeza kwenye viwanda gharama yao ikiwa nikubwa kuliko zile bidhaa zinazotoka nje watashindwakufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi watu binafsi tukifanya utafititunakuta bado tuna changamoto kwenye regulatory bodieszetu. Tunaendelea kushauri mziunganishe, ziwe moja na watuwasiwe analipa kwenye hizi regulatory bodies, ingekuwaukishalipa kwenye leseni ya biashara basi huko huko kila kitukiwe kimelipiwa ili tusipate usumbufu. Wanapokuja kukaguawakague wakati wowote lakini wasisumbuliwe kwa maanakwamba kila mmoja anataka alipwe tozo yake.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine muhimu nikuwekeza kwenye utafiti. Kwa sababu bila kufanya utafitiwa uhakika, kwenye TIRDO, SIDO na COSTECH ipatiwe fedhabado suala hili la namna ya sisi kuendelea itakuwa ni ngumu.Kwa mfano, ukiangalia viwanda vya ndani bei ya kuzalishasukari, mafuta lakini pia bidhaa zote zinazoweza kuzalishwandani ya nchi, leo tuangalie kwenye pamba (Cotton toClothing) ni ngumu. Kamati yetu ilitembelea kule MWATEXna viwanda vingine, bado unakuta gharama zao ni kubwasana ukilinganisha na bidhaa inayotoka nje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa usiangalie tu pale kwenyekiwanda anaajiri watu wangapi na analipa nini, angaliaspillover effect kwamba kuanzia mkulima mpaka hapoinapofika kwenye kiwanda na bado ile nguo itakayozalishwawale washonaji na wengine ni kiasi gani itaweza kuzalisha.Bei ya bidhaa inayotoka nje Serikali ilituahidi kwamba nchiambazo tunaagiza kutoka kwao kwa wingi mtaangalia beizao, wengi wana-under declare. Wakisha-under declare kwamfano kwenye hii Cotton to Clothing mtu wa ndani hawezikushindana na huyu wa nje.

Page 273: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

273

Mheshimiwa Spika, ni vizuri tukapata uhakika wa beiya uzalishaji na ni vizuri mkakaa na wafanyabiasharawakawaeleza bei ya uzalishaji wa viwanda vya ndani.Sehemu nyingine, kwa mfano, kwenye pombe kali, ni mahaliambapo Serikali inapoteza pesa nyingi sana kwa sababugharama yake ya uzalishaji haijulikani. Wengine wanauzakwa bei ya kodi tu, sasa ile pombe anauzaje? Ina maanakuna mahali ambapo tunapoteza mapato mengi ni vizurikuangalia. Pia tukiangalia viwanda vyetu kwa mfano vyambolea, yeye kwa upande wa kodi anatozwa kodi zotehawezi ku-claim kwa sababu end product yake bado hainaVAT lakini ile inayotoka nje haitozwi, unakuta gharama yakeya uzalishaji inakuwa kubwa hawezi kushindana na ilembolea ambayo imetoka nje.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ni viwanda nabiashara mngeangalia pia kwa nini informal sector inazidikukua? Leo hii asilimia 80 ya watu wako kwenye informalsector (sekta isiyokuwa rasmi), ni kutokana na hizi tozo, kodina ushuru mbalimbali ambapo mtu anaona ni kero anaonani bora aendelee kuwa informal na maisha yanaenda. Kamatuki-formalize na tukiangalia namna ya kwenda harakaSerikali itapata mapato mengi zaidi kwa sababu tax baseyetu tukiitanua nina uhakika kabisa kwamba unawezaukapunguza hizo kodi nyingine ili wengi walipe kodi ziteremkena compliance itakuwa ni kubwa. Kwa hiyo, hilo ni jambomuhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama mngekuwa mnafanya kazina viwanda vingine, niwape mfano, Manyara tuna Kiwandacha Kuchambua Pamba, ambapo kwenye sekta nzima yakilimo wanatumia umeme kwa muda mdogo, ni viwandakabisa vikubwa vinatumia kwa muda wa mwezi au miezimiwili halafu wanafunga mpaka msimu ujao. Unakutawanalipishwa capacity charges ya miezi mitatu asilimia 70ya ile gharama, cost of production lazima iwe juu. Kwamwendo huo viwanda vingi vitaendelea kufungwa.

Page 274: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

274

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukija kwenye maziwana viwanda karibu vyote msipoangalia, msipokaa na Wizaranyingine ambazo zote ziko kwenye sekta hiyo ya viwanda,kuanzia production mpaka wakati wa kuuza, badohamtakuwa mmevilinda viwanda vya ndani. Ni muhimukuangalia namna ya kupata cost of production, faida nakodi. Ni muhimu Serikali iendelee kupata kodi yake sahihimaana isipopata kodi yake sahihi hizi ndoto zetu za kuwekezakwenye huduma nyingine hatutafanikiwa.

Mheshimiwa Spika, pia tuangalie viwanda ambavyovitalenga wakulima, wafugaji, wavuvi, vitu wanavyozalishavinawezekana kupatikana ndani ya nchi. Kwa ninitunaendelea kuagiza vitu vyote kutoka nje? Bahati nzuriMheshimiwa Rais pia amelizungumzia mara nyingi,tunaomba sasa muendelee kushirikiana kama Serikali moja,kuwe na uratibu baina ya Wizara zote ili ndoto yetu iwezekutimia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kuna jambo lingine ambaloni muhimu tujue kwamba viwanda haviwezi kujitegemeabila kujua raw material yatakuwa yanatoka wapi. Kwa nchiyetu raw material kwa sehemu kubwa ni sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi. Tukiwekeza kwenye hizo sehemu tatu namkaweka mkakati kwamba mwaka huu tunafanya kwenyeproduct mbili au tatu, tukawekeza value chain nzima, yaanimnyororo wa thamani kutokea kwenye uzalishaji, viwandanimpaka kwenye kuuza, nina uhakika kabisa kwamba ndaniya miaka miwili, mitatu, tutaona mabadiliko makubwa.

Mheshimiwa Spika, ni aibu kwa nchi yetu kuagizabidhaa ambazo tungeweza kuzalisha ndani ya nchi hii.Mifano ipo mingi, kwanza tuangalie kwenye matunda nambogamboga, samaki, vitu vyote hivi tunaweza kuzalishandani ya nchi. Ni vizuri kama Serikali kwa pamoja tuwekezekwa aji l i ya upatikanaji wa bidhaa hizo. Juice zotetunazokunywa hakuna hata tone moja linalozalishwa hapanchini zote ni concentrates kutoka nje.

Page 275: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

275

Mheshimiwa Spika, hata kwenye biashara, kwa mfanokwenye pombe kali, bei ya kodi baina ya pombeinayozalishwa ndani ya nchi na nje ya nchi ni ndogo, hivyohivyo kwenye juice. Sasa tuangalie, inayozalishwa ndani yanchi ama tufute kabisa au ipungue kabisa lakini ile inayotokanje tuipandishe ili watu wawe na incentive ya kuwekeza hapanchini, waone kwamba ni bora kuwekeza hapa nchini kulikokuagiza kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, nchi nyingine bado zina mamlakaya kusamehe kodi kwenye bidhaa zao za export lakini sisihatuna. Kama Kenya au Zambia wanazalisha waowanapewa kuingiza nchini bila kodi unakuta bidhaa zao ndioziko kwenye soko letu badala ya sisi bidhaa zetu kuingiasokoni, kwa sababu sisi hatuna msahama wa aina yoyote.Nchi za SADC tayari tuna ile SADC Protocol ambapo bidhaazao zinapouzwa kwenye nchi hizi kodi yake ni ndogo, kwahiyo, ushindani unakuwa mdogo.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri kama Serikali muangaliemambo haya na Wizara hii ya Viwanda na Biashara ndiyomnatakiwa kufanya utafiti wa uhakika, mshauri Wizaranyingine zote kwa pamoja mfanye nini. Pia tuhakikishe kunamiundombinu muhimu kama barabara na umeme kwa walewanaohitaji kuwekeza kwenye viwanda. Vileviletuwaondolee changamoto nyingine, kwa mfano, watuwanaanzisha viwanda halafu unasema barabara hii mwishotani kumi hatuwezi kufika. Ni muhimu Wizara hii iendeleekushauriana na wengine.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA : Ahsante sana Mheshimiwa Jitu Soni.Tunaendelea na Mheshimiwa Kiteto Zawadi Koshuma.

Page 276: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

276

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kutoamchango wangu katika Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji.

Mheshimiwa Spika, naomba leo nianze kwa kutoatafsiri fupi ya nini maana ya viwanda. Kiwanda ni mahaliambapo malighafi inachakatwa kuwa bidhaa iliyokamilikakwa ajili ya mtuamiaji au bidhaa kwa ajili ya viwanda vingineviweze kufanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa tafsiri hiyo fupi yaviwanda, sasa tutaona Tanzania tutaweza kuelekea katikanchi ya viwanda. Historia ya viwanda duniani kote ukiangaliakwa mfano Britain, America, India, France, China walianzakwa kuwa na viwanda vya nguo na ndipo wakawezakuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto ameeleza kwakifupi mimi nitaenda kwa undani zaidi. Inasikitisha sana nikwa namna gani sisi kama Tanzania tunaweza kuwa ni nchiya viwanda kama hatutaongelea viwanda vya nguo. Leokatika kitabu hiki cha Mheshimiwa Waziri sijaona ni namnagani ameongelea viwanda vya nguo nchini Tanzania. Hiiinasikitisha sana kwa sababu inaonesha ni kwa namna ganihatuwezi kuwa na nchi ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la kuwa na nchi ya viwandanchini Tanzania halijaanza leo, lilianzishwa na MheshimiwaRais wetu Mtukufu, Hayati Julius Kambarage Nyerere mwaka1970 hadi mwaka 1992 viwanda vikabinafsishwa. InasikitishaSerikali haijaweza kuvichukulia hatua yoyote viwanda 156vilivyobinafsishwa na havifanyi kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niko katika Kamati yaViwanda na biashara. Kamati ilitisha list ya viwanda 156ambavyo vilibinafsishwa mwaka 1992. Taarifa ambayoililetwa mbele ya Kamati na ninayo hapa, Serikali inajaribukueleza ni kwa namna gani inachukua hatua lakini ukiangaliamaelezo yanayotolewa ni kwamba ushauri wa Mwanasheria

Page 277: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

277

Mkuu wa Serikali unachukuliwa na wanasema mashaurimengi yako mahakamani.

Mheshimiwa Spika, taarifa hii kusema ukweli hataKamati ilisoma na ikaona na haikuweza kuridhika na majibuya Serikali. Nilitegemea leo hii katika kitabu hiki ambacho nicha Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Waziri angewezakuelezea na kufafanua ni kwa namna gani Serikali imejipangakuwachukulia hatua watu ambao walibinafishiwa viwanda156. Watu hawa ni wezi, ingekuwa ni nchi nyingine kamaChina wangenyongwa kwa sababu ndiyo wametufikishahapa sisi Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, umasikini tulio nao Tanzania leoni kwa sababu ya viwanda vilivyobinafishwa. Viwanda hivyo156 vingi ambavyo ni vikubwa vilikuwa ni vya nguo. Sasaukiangalia kama nilivyoanza kusema viwanda vya nguovilisababisha nchi za Marekani, Britain, France na Chinakuweza kufanikiwa kuwa nchi za viwanda lakini leo hii sasasisi Tanzania tuko wapi, tunaenda wapi? Naitaka Serikalikuchukua hatua kwa hivi viwanda ambavyo vilibinafsishwa.(Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge huyo anaitwaMheshimiwa Kiteto Koshuma. (Kicheko/Makofi)

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Spika, baadaya kutangulia kusema hayo, naomba sasa tuangalie katikaMkoa wa Mwanza. Mwanza tuna Kiwanda cha MWATEX.Kiwanda cha MWATEX kilikuwa kina wafanyakazi zaidi ya3,500 miaka ya nyuma kikashusha wafanyakazi hadi kufikia1,500. Leo hii tunaongelea wafanyakazi si zaidi ya 150 katikaKiwanda cha MWATEX. Suala hili linasikitisha sana. Siku mojanilisikia Mheshimiwa Rais akisifia kwamba Kiwanda chaMWATEX kinafanya vizuri, yawezekana Mheshimiwa Raishajapata ukweli kutoka kwa watendaji juu ya Kiwanda chaMWATEX. (Makofi)

Page 278: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

278

Mheshimiwa Spika, naomba sana sana, watendaji waWizara hii ya Viwanda wamsaidie Mheshimiwa Rais, kwakumueleza ukweli na si kwa kuja hapa kwa kujitambakwamba tuna viwanda vingi, viwanda vingi wakati impactkwa Watanzania haionekani? Mtu anakuja hapa anaongeleasuala la viwanda vya cherehani, hivi unataka kusema leo hiimimi nikimuita Waziri wa Viwanda na Biashara kwambatwende naye Mwanza tukazindue viwanda watu wanavyerehani vinne, atakuja kweli? Je, inaleta impact? Mimihainiingii akilini, sahamahi sana kwa kusema hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna Kiwanda chaMUTEX ambacho kiko Musoma kimekufa. Pamoja na viwandavingine ambavyo vimekufa Kiwanda hiki cha MUTEXkinanisikitisha kwani kilikuwa kinatoa vitenge na kanga nzuri,vitenge vilikuwa vinauzwa mpaka nje ya nchi Swaziland. Leohii kiwanda kimekufa lakini katika kitabu kiwanda hikihakionekani kuongelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naitaka Serikali kuangalia ni kwanamna gani inachukua hatua madhubuti za mikakati kuwezakuviinua viwanda ambavyo vilikuwa vimekufa ambavyo niviwanda vya nguo ili nasi tuweze kuitumia pamba yetu.Katika Mkoa wa Mwanza na mikoa mingine kama Simiyu naShinyanga wanalima pamba kwa wingi lakini unapoangaliakwenye taarifa ya Waziri ni asilimia 30 tu ya pamba ndiyoambayo inatumika, pamba nyingine yote inaenda nje.

TAARIFA

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Kiteto, jamani hizi taarifa kamanilivyosema ziwe za maana.

MHE. SAED A. KUBENEA: Ndiyo Mheshimiwa.

SPIKA: Ndiyo Mheshimiwa.

Page 279: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

279

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Spika, nampataarifa mchangiaji kwamba aliyeua viwanda katika nchi hiisi Mheshimiwa Mwaijage aliyekuja jana, viwanda vimeuawana Sera ya Ubinafsishaji ya Chama cha Mapinduzi. (Kicheko)

SPIKA: Kweli ni usumbufu tu, ungemuachaMheshimiwa aendelee kusema. Hizo blame gamemnazofanya ndizo zinaleta migawanyiko ambayo hainamaana. Hapa tunataka tujenge direction ya viwanda katikanchi yetu, mwacheni Mheshimiwa aendelee. (Makofi)

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kuweza kunisaidia kujibu taarifa ileisiyokuwa na maana yoyote. Kwa sababu mimi sijasemaviwanda ameviua Mheshimiwa Mwaijage ndiyo maananaona kwamba taarifa ya kaka yangu pale haijakaa vizurisana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini naomba niendelee kwakusema kwamba viwanda hivi vinapaswa kufufuliwa kwaari kubwa sana ili pamba iweze kutumika kwa asilimia walau70 ndani ya nchi hii.

Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Urafiki kinasikitisha.Leo hii ukienda kwenye kiwanda kile kuna show room yamagari ya Wachina iko pale. Ni kwa sababu gani Kiwandahiki cha Urafiki hakifanyi kazi? Tunakuomba MheshimiwaMwaijage pamoja na watendaji wote katika Wizara hiimuangalie viwanda hivi ambavyo ndivyo vinawezakutusaidia Watanzania kujivunia na kuwa nchi ya viwanda.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii ukiangalia Kiwanda chaKiltex, Mbeya Textile, Sungura Textile, Tabora Textile vyotehavipo. Katika taarifa tunaambiwa kuna viwanda 11 vyanguo, sijui ni viwanda gani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na yote hayoniliyoyaongea, naomba nitumie dakika mbili kutoa ushaurikwa Serikali. Hatuwezi kuwa na viwanda vya uhakika kama

Page 280: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

280

hatuwezi kusaidia upatikanaji wa uhakika wa umeme katikaviwanda vyetu. Mashine nyingi zinakufa katika viwanda kwasababu umeme upatikanaji wake siyo effective. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sana Serikali iwezekujitahidi kuangalia viwanda vyetu vinapata umeme wauhakika lakini pia vinapata maji ya uhakika na pia barabaraza kutoa malighafi sehemu moja kupeleka katika viwandana kutoa bidhaa viwandani kwenda sehemu za masoko ilikuweza kusaidia viwanda vyetu kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia naomba kutoa ushauri, kamainawezekana Serikali ichukue ushauri huu, kwamba viwandavya nguo vitolewe ile asilimia 18 ya kodi ili kuweza kuvi-motivate kuweza kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombaniunge mkono hoja lakini yale niliyoyasema yawezekuzingatiwa na Serikali na hatimaye yaweze kufanyiwa kazi.Nashukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Huyo ni Mheshimiwa Kiteto Koshuma, nilikuwasimfahamu. Amechangia vizuri sana, huo ndiyo ukweli, sanakabisa na hii ndiyo michango ya Wabunge inayotarajiwa.(Makofi)

Maana Mheshimiwa Rais ameshaweka directionkwamba safari hii ni viwanda. Sasa tunakwendaje kwenyeviwanda lazima tumsaidie Waziri hapa na timu yake. Leoametuletea bodi zote, wataalam wamejaa hapa, watu waviwanda wako hapa wanaangalia Bunge linasemaje kuhusuviwanda? Kwa hiyo, nia ni njema, sisi wote tusaidie kujenganyumba hii inayoitwa viwanda. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, jioni tutaendelea nauchangiaji, wale wote ambao majina yenu yamo humu,mtaendelea kupata nafasi kadri tunavyoendelea.Nawashukuru sana, mjadala wetu unaendelea jioni. Kwa jinsihiyo, nasitisha shughuli za Bunge hadi saa 11.00 jioni.

(Saa 7.00 Mchana Bunge Lilisitishwa Mpaka Saa 11.00 Jioni)

Page 281: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

281

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alikalia Kiti

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae.Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na majadiliano.Tutaanza na Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu baadayeMheshimiwa Elibariki Kingu.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nichukue fursa hii kukushukuru sana kwa kunipa fursaya kuchangia kwenye sekta hii ambayo ni kipaumbele chaTaifa na vilevile ni Dira ya Taifa kupitia Mpango wa II wa MiakaMitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda vilevile niipongezesana Wizara kupita kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri naKatibu Mkuu na Watendaji wote kwa sababu kwa kweliutaona wanafanya kazi na kama walivyoeleza kwambaviwanda vinaongezeka, niwapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hiikumshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwakuonyesha dhamira yake ya dhati ya kujenga Sekta yaViwanda katika Taifa letu. Ukikuta Rais ameonyesha dhamirayake nina hakika Watanzania wote watajielekeza huko nanaomba tufanye hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais katikahotuba yake ndani ya Bunge hili, alisisitiza kuwa sekta yaviwanda ina jukumu kubwa la kuipeleka Tanzania kwenyeuchumi wa kati ifikapo 2025. Toka alipozindua Bunge hili,dhamira ya Rais inatupa uhakika wa kufikia azma hiyo.

Mheshimiwa Spika, vilevile nilimuona Mhesimiwa Waziriwa Fedha, akizindua kitabu kilichoandikwa na WatendajiWakuu wa Serikali kilichoelezea changamoto ambazozinaikabili azma yetu hii, kama ifuatavyo:-

(i) Ukosefu wa vipaumbele madhubuti;

Page 282: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

282

(ii) Sera thabiti;

(iii) Ukosefu wa umeme wa uhakika;

(iv) Ukosefu wa mitaji;

(v) Ukosefu wa uzalendo wa kiuchumi; na

(vi) Ukosefu wa mfumo mzuri wa elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuwe na viwanda hayoyote ni muhimu. Nimefurahi sana katika ukurasa wa 140, Waziriwa Viwanda mwenyewe amesema kwamba watajaribukuangalia Sera ya Viwanda endelevu na ndiyo ilikuwachangamoto ya pili kwamba sera zikipitwa na wakati azmayetu inaweza isifikiwe. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri fanyeniharaka ili tusishindwe kufika kwenye azma yetu ifikapo 2025.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napendanizungumzie mradi wa Liganga na Mchuchuma wa chumana mkaa. Kama Waheshimiwa Wabunge wenginewalivyosema, kwanza niipongeze sanasana Serikali kwakuuweka mradi huu kuwa mradi wa kielelezo. Wamefanyahivyo, umeanzia Awamu ya Nne na awamu hii imewekaumuhimu mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwa uhakikauchimbaji wa chuma ni nguzo muhimu na ni sekta mamakwa kweli, ni viwanda mama au ni viwanda vya msingi.Liangalieni jengo hili thamani yake robo tatu ni chuma uonechuma inavyohitajika nchi hii. Kwa hiyo, tutakavyoharakishautekelezaji wa mradi huu utasaidia sana nchi hii. Angalienihata maendeleo ya nchi za Ulaya yametokana na chumawakati wa Oliver Twist. Angalieni maendeleo ya India,Mahalanaumis alifungwa lakini chimbuko la uchumi wa Indialeo ni mradi wa chuma kule India. (Makofi)

Page 283: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

283

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tuonehilo, fikirieni kama reli hii ya kati inayojengwa sasa hivi chumachake kingekuwa kinatoka Liganga ni kiasi gani cha ajirakingebaki Tanzania? Ni kiasi gani cha manufaa makubwaya uchumi yangebaki Tanzania? Kwa hiyo, naomba sanatuangalie mradi huu ambao unaelezwa toka nikiwa shulenihata kabla, naomba utekelezaji wake uende kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana miradi kamahiyo incentive zinazoombwa mziangalie, tunaweza tusipatefaida lakini baadaye maendeleo ya kiuchumi na ya viwandayatakuwa ni ya upesi zaidi, iron and steel industry ni chimbukola maendeleo yote duniani. Angalieni chuma tutakachoagizanje na kitakavyojenga ajira na uchumi wa nchi ambazozinatuletea, hayo tunawanyima Watanzania. NikimwangaliaWaziri na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano, sina wasiwasina nina hakika tunataka bati na misumari itoke hapa, kilakitu ambacho kinataka chuma kitoke hapa, tuna uwezo.Chuma kina multiplier effect, sina neno la Kiswahili,kinanufaisha sana sekta zingine kwa haraka. Naomba Serikaliiharakishe utekelezaji wa mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda vilevile kuongeleamasuala ya biashara, naomba Serikali ijitahidi sana kuwekamazingira bora ya kufanya biashara nchini. Tumejitahidi tokamiaka iliyopita lakini sasa tuendelee na jitihada hizo. Jambokubwa ambalo linafanya sasa biashara iwe ya shida, Waziriwa Fedha yupo hapa ni mzunguko mdogo wa fedha.Mzunguko wa fedha uongezeke lakini ziwe fedha ambazozinakubalika zisiwe ni fedha chafu. Kama cash haipo biasharahaitakuwepo. Kwa hiyo, Serikali iangalie ni namna ganimzunguko wa fedha utaongezeka ili biashara iende na nchiyetu iendelee kupata faida kutokana na biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni mazingira yauwekezaji, nami ni-declare interest hapa nilikuwa Waziri waUwekezaji. Mazingira ya uwekezaji yakiwekwa sawa ujenziwa viwanda hivi utaenda kwa kasi kubwa.

Page 284: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

284

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo nitalishaurihapa na ambalo limeanza na najua Wizara nayo na Serikalikwa ujumla inafanyia kazi, ni kuwa na One Stop Center.Hatuwezi kuwa na taasisi mbalimbali zinazohusika na ambazozimetawanyika tukafikiri kwamba mwekezaji atakuwa nauvumilivu awaze kuona kwamba atabaki hapo na hela zakezinabaki benki halafu hazimletei faida hatakubali . Kwa hivyo,naomba tuharakishe hii One Stop Center ianze kufanya kazi.Ukimkamua ng‘ombe kama humlishi hutapata maziwa. Kwahiyo, wawekezaji tuwawezeshe ili waweze kuwekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niongelee juuya viwanda Hanang. Hanang ni eneo la kilimo, kwa hiyo,viwanda ambavyo vinatakiwa pale ni vya kilimo. Sisi tunalimestone nyingi sana kwenye ukuta wa bonde la ufa nahakuna mahali patakuwa na bei na gharama nafuukutengeneza cement kama Hanang. Kuna mwekezajiamekuwa anaomba kuwekeza pale mpaka anakata tamaakwenda Singida lakini hatapata mazingira mazuri kama yaHanang, ukuta ule wote una limestone. Itigi kuna gypsumambayo inatakiwa umbali wake ni chini ya kilomita 100. FikiriaDar es Salaam na Mtwara wanapata gypsum wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sanakiwanda hiki kiweze kuanzishwa na tumfanye yule mwekezajiawe na matumaini na kwa hivyo tusimzungushe. Napendakusema kwamba bureaucracy au urasimu unapaswautumike kuwezesha viwanda vianzishwe na kurahishauwekezaji. Naomba tusitumie urasimu kuzuia wawekezajikuwekeza vinginevyo nchi yetu haitapiga hatua. Natakaniseme kwamba Tanzania ni ya pili Afrika katika ukuaji wauchumi na naipongeza Serikali kwa hili. Ili maendeleo ya nchiyawe sustainable lazima yapitie kwenye uwekezaji.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

Page 285: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

285

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naishukuru sana Wizara, naunga mkono hotuba ya Waziri natukizingatia ushauri huu, kazi yangu ni ushauri siyo kupinga.Ahsanteni sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mary.Tunaendelea na Mheshimiwa Elibariki Kingu, ajiandaeMheshimiwa Mariam Kisangi.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Kingu hayupo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mariam.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kunipa nafasi ya kuchangia katika Wizara hiiya Viwanda na Biashara. Kwanza nimshukuru MwenyeziMungu kwa kuniwezesha siku hii ya leo kusimama hapa mbelena kuweza kuchangia katika Wizara hii. Pia niipongeze Serikaliyangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwawanayoifanya ya kuhakikisha kwamba tunapata Tanzaniaya Viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahia kuona hotubaya Mheshimiwa Waziri inaeleza wazi kwamba nchi yetuimekuwa na jumla ya viwanda 53,876 lakini katika hivyoviwanda vikubwa ni 251, viwanda vya kati ni 173, viwandavidogo 6,957 na vile viwanda vidogovidogo sana ni 46,495,sio kazi ndogo. Mara nyingi huwa tunatoa mfano kujenganyumba ni kazi ngumu lakini kusema nyumba hii mbaya nikazi rahisi sana, unatumia maneno sita tu. Leo hii Serikali hiiya Chama cha Mapinduzi imefanya kazi kubwa sana yakuielekeza Tanzania yetu katika uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema peke yake hata kulekupiga debe ni kazi. Wananchi wa Tanzania sasawameelekea katika kuileta Tanzania ya viwanda. Wawekezajiwote sasa wamebadilika na kutaka kuwekeza kwenye

Page 286: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

286

viwanda. Si jambo dogo lililofanywa na Serikali ya Chamacha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimshukuru nanimpongeze Mheshimiwa Rais wetu, John Magufuli kwa kazikubwa anayoifanya ya kuelezea na kutia nia yake ya dhatikabisa katika moyo wake kwamba anataka kuileta Tanzaniakatika uchumi wa viwanda. Lengo la viwanda si kwambaanavileta viwanda vile anataka kukuza ajira kwa vijana.Tumekuwa na vijana wetu wengi hawana ajira viwanda hivivitakavyojengwa vijana wengi watapata ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mazuri yapo lakinichangamoto kwa kila binadamu ipo na kwa jambo loloteutakalolifanya utakutana na vikwazo. Vikwazo hivyovinaweza vikatatuliwa polepole lakini azma ya nchi yetu nikuipata Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuipongezaSerikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwainayoifanya sasa naomba nirudi katika mchango wangu nanitachangia kuhusu leseni za biashara. Nimeona wazi kunaeneo wamesema wameweza kutoza faini za kukiuka sheriaza biashara takribani shilingi bilioni 9.7. Kitendo hiki cha watukukiuka kukata leseni na kuingiza pesa kiasi hiki tunawezakuona ni kizuri lakini ndani yake kuna ubaya, lazima tujiulizekwa nini wananchi wanakiuka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya leseni na hasakatika Jiji langu la Dar es Salaam imekuwa mtihani. Mamalishe akikaa barabarani hana leseni, mama lishe akijiongezaakasema nikachukue tu kakibanda kadogo niweke hapasufuria yangu ya wali, vikombe vyangu na meza yangu mojaimekuwa shida katika Mkoa wa Dar es Salaam. Mama lishehuyo ataambiwa aende kwanza Manispaa kuomba leseni,ataambiwa nenda TRA ukapate clearance, ukifika TRAhakuachi hivihivi akakupa ile clearance tax clearance yahivihivi kwamba unakwenda kwanza biashara lazima uanze

Page 287: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

287

kulipia si chini ya Sh.300,000. Unawenda halmashauriwanakwambia ulipe leseni hiyohiyo Sh.100,000, unarudiSh.500,000 imeshaondoka mama lishe huyu biasharahajaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, akija kuanza biashara miezimitatu anaambiwa ulipe kodi. Hivi huyu anayejitahidikuboresha mazingira yake ndiyo sisi tunamuumiza kuliko yulealiyekaa pale anauza bila ya kitu chochote wala usafi.Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri uliangalie hili akinamama wa Dar es Salaam kweli wanaendesha kwa kutumiabiashara ndogondogo. Sisi katika Mkoa wetu wa Dar esSalaam hatuna mashamba ya kulima kwamba tunawezakupitisha mazao yetu kwenye ki-carry kidogokidogo kukwepakodi, sisi tunayo biashara. Biashara zetu ndiyo hizi akina mamakukaanga mihogo, kuuza ice cream lakini yule anayepatamtaji kidogo anahamisha mtaji wake, anauboresha,anaangalia ananunua viti vyake vya plastic sita, anaweka,anafanya biashara. Niiombe Serikali iangalie biashara zanamna hii, waangalie jinsi gani watawaelekeza akina mamahawa waweze kulipa leseni vizuri si kwa uonevu, walakukandamizwa na kodi lakini pia waweze na wao wenyewekujiendesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nije TBS. TBS si rafiki wamfanyabiashara mdogo ni rafiki wa mfanyabiasharamkubwa. Nasema hivyo kwa sababu akina mama wa mkoawangu wanatengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo sabuni,mafuta ya nazi, majani, mdalasini, wanajitahidi kwa kadri yauwezo wao lakini wanavyokwenda TBS hawapati ushirikianowa kuangalia ule ubora wa zile biashara zao hali ambayoinawafanya akina mama hao wakate tamaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimefuatwa namabinti, nina deni la kulipa hapa Kinondoni, vijana wa filamubadala ya kuonyesha filamu wamejiongeza wakasema waowawe wajasiriamali, wanatengeneza vitu vyao lakini TBShaiwapi ushirikiano kabisa. Nawaona wanatenga fedha za

Page 288: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

288

semina, semina hizo mnawapa akina nani wakati akinamama bado wanahangaika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nichangieeneo la TANTRADE ambayo sisi tunaita Sabasaba.Niwapongeze sana hawa TANTRADE wanawezeshakuonyesha maonesho mazuri, watu wanajaa, wanapatafedha, lakini sisi kama akina mama wa Dar es Salaamtunafaidika na nini wakati hatuna hata banda?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sikatai kabisa naniwapongeze wanachukua akina mama Tanzania nzima. SisiDar es Salaam hatuna mgodi, ardhi ile ndiyo rasilimali iliyokokwetu na uwanja ule ndiyo tunautegemea angalau na sisiSerikali ituwezeshe kupitia Uwanja ule wa Sabasaba. Leo hiiakina mama wa Dar es Salaam wanahenyahenya tu mitaaniinafika Sabasaba anaingia kwa tiketi anaenda kuangalia kaziza wenzie yeye kazi yake haipo. Niiombe Serikali, nikuombeMheshimiwa Waziri utakaposimama unieleze kwamba Mkoawa Dar es Salaam mwaka huu TANTRADE wako tayarikuwatengea banda angalau tent tu pembezoni na waowaweze kuonyesha bidhaa zao ili na sisi tuweze kufaidika?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna suala linginekuhusu watoto. Watoto wa Temeke hawana sehemu yakuchezea. Inapofika Sikukuu ya Iddi na Christmaswanazagaazagaa maeneo yale ya Uwanja wa Sabasaba,hawana pa kuchezea. Hivi Serikali inashindwa ninikuwafungulia watoto wale kucheza mle ndani ya uwanja sikuya Sikukuu ya Iddi na Christmas angalau na wao wafaidikena mradi ule wa Serikali yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyeki, lakini pia katika kuingizawatoto wale wakiletwa wajasiriamali wakaleta bembea namichezo mbalimbali ya kitoto, itaisaidia Serikali pia kuingizamapato. Kwa hiyo, niiombe Serikali yangu wafanye jitihadaili watoto wetu nao wakafurahie uwanja ule. (Makofi)

Page 289: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

289

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nichangiekuhusu masoko. Ni ukweli kabisa kuna tatizo kubwa la masoko.Pamoja na kuhangaika kote na viwanda, bado bidhaa zetuzinakosa masoko. Mimi nashindwa kuelewa, bidhaa zaWatanzania tunafika sehemu tunahamasisha lakini baadaya kutengeneza kile kitu unakuta gharama yake imekuwakubwa.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mariam.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja kwa kumpongeza Waziri na Watendajiwote wa Wizara hii. Kazeni mwendo, mwendo huo huo,Mwenyezi Mungu atawasaidia. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa MariamKisangi. Tunaendelea na Mheshimiwa Andrew Chenge,baadaye Mheshimiwa Jaku Hashim na Mheshimiwa JumanneKishimba wajiandae.

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Naibu wake,Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu na Watendaji wote waWizara hii pamoja na wataalam wa taasisi ambazo ziko chiniya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba hii ni pana, ni nzurina inatoa mwelekeo. Sote tumekubaliana kwamba Wizarahii ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni mojawapo ya sektaza kipaumbele katika Mpango wetu wa Maendeleo katikakuipeleka nchi yetu kufikia uchumi wa kati na nguzo kubwani viwanda. Tunaliona hili, wamelisemea vizuri, changamotozilizopo na jinsi wanavyokabiliana nazo, nawapongeza sana,endeleeni. (Makofi)

Page 290: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

290

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado nasumbuliwa sana nasuala zima la gharama za uwekezaji nchini, bado ziko juusana. Hili limesemwa vizuri tu kwenye hotuba unaona hali yaupatikanaji wa umeme, maji na miundombinu mingine yoteya kiuchumi ambayo inaendana na kufanikisha uwekezajigharama gharama ziko juu. Sasa, kuanzia leo mniite BwanaReli, kwa sababu nitakuwa naizungumzia katika kila Wizarahata kama haihusiki nayo. Nimshukuru sana Mheshimiwa Raiskwa uamuzi wake huo na tutakapokamilisha reli hii tutaonauchumi wa Tanzania utaibuka kama uyoga, ikumbukenitarehe ya leo, Bwana Reli anasema. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali,narudia kama nilivyosema juzi wakati nachangia kwenyeWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Pamoja na jitihadanzuri za sasa, napenda Serikali iendelee kutafuta mikopo yamasharti nafuu ili tuweze kushambulia ujenzi wa reli hiituikamilishe. Hii ni kwa maana ya reli ya kati pamoja namatawi yake yote ya msingi, tufanye kazi hiyo na tutaonauchumi wa nchi utakavyokua kwa kasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishuke kwenye upande wamradi huu wa siku nyingi sana wa Liganga kwa chuma naMchuchuma kwa upande wa makaa ya mawe. Kusemaukweli kwa nchi hii kama mpaka leo tunaendelea kuongeakwa lugha hiyo ni tatizo. Hata kwenye hotuba ya MheshimiwaWaziri nadhani ukurasa wa 13, hiyo Kamati ya wataalam,kinachosemwa pale ni kwamba timu hiyo imekamilishataarifa ya awali wala hatuambiwi ni nini. MaanaWaheshimiwa Wabunge, hizi sheria mbili tulizopitisha mwakajana, mimi nasema Bunge lipo, kama kuna vifungu ambavyotunaamini kwamba vinakwamisha kwenda mbele, Serikalindiyo ileile iliyoleta Miswada hiyo Bungeni sasa Serikalihiyohiyo haiwezi ikaogopa kurejea Bungeni na kueleza kwanini hatuendi mbele. Bunge lipo ndiyo kazi hiyo, watajengahoja, tutawasikiliza na tutafanya marekebisho twende mbele.Haiwezekani tunaenda mbele tunarudi. Tangu mwaka 2011Septemba waliposaini mkataba, NDC pamoja na ile kampuniya China, what is wrong with us Tanzanians? (Makofi)

Page 291: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

291

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani tuna vivutiolakini hatuendi mble, jenga hoja, unamwambia mwekezajibwana, haya hatuyakubali, mwambie ili afunge viragoaende lakini hatuwezi kila mwaka tunaenda mbele na kurudinyuma. Mimi nasema tuufikishe mradi huu mwisho.Mheshimiwa Waziri, tueleze exactly changamoto ni nini kwasababu navyokumbuka mimi mkataba ule unatoa 20% yafree carried interest kwa Serikali bila kulipa kwa sababumadini hayo ni National patrimony yetu. Pia inaiwezeshaSerikali kupitia NDC kupata an additional 49%. Tuliweka wazikabisa kwamba mikopo yote ya uwekezaji itakayochukuliwaambayo wana-estimate kuwa three billion US dollars, ni lazimaikubalike na pande zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi huwa nasema tufikemahali mradi huu utekelezwe. Tulikuwa tumepanga by now,mwaka huu wa fedha, kwa upande wa umeme tungekuwatumefikia hizo megawatt 600 na chuma kingekuwa kimeanzakuzalishwa mwaka 2015. Kwa hiyo, reli hii tungekuwatunaanza kutumia vyuma vyetu lakini what is wrong with us?Tusimuangushe Rais Magufuli kwa nia yake njema ya kuletamaendeleo ya haraka kwa nchi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma ukurasa wa 69 wahotuba kuhusu hili suala la tozo na ada zenye kerozinazojirudiarudia, tumelisema, bado tunaelezwa ooh,tunakaribia kumaliza. Mheshimiwa Waziri nadhaniunapohitimisha, hebu mtueleze exactly, najua kuna vestedinterest za Mawaziri, wanataka kuendelea taasisi ambazo zikochini ya Wizara zao, wanategemea sana mapatoyanayotokana na tozo na ada hizi lakini sisi tunataka kujengamazingira mazuri ya kuwekeza na kufanyia biashara Tanzania.Kama tozo basi ziwe na mtiririko mmoja, tunasema One StopCentre. Tumeona Benjamin Mkapa wameweka wote pale,tungependa hata Export Processing Zones za maeneo yamikoani utaratibu huohuo utumike maana humkwazimwekezaji. Nadhani tuyafanyie kazi haraka haya maanatumeyasema sana mpaka unafika mahali unachoka.(Makofi)

Page 292: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

292

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa jambo la jumlatu. Kusema kweli tunafanya kazi nzuri, amelisema vizuri sanaMheshimiwa Dkt. Mary Nagu na nilimsikiliza Mheshimiwa Raiskwenye National Business Council siku ile lakini hayo ambayoyameamuliwa pale napenda visiwe vikao hivi ambavyohavina record, havina yatokanayo ili kikao kinachokuja hayamengi haya yawe yameshatanzuliwa, siyo tenawanakumbushana kulikuwa na kikwazo gani, tumalizetunaenda mbele. Mheshimiwa Waziri, wewe ndiyo sekta yakohii, hayo ambayo unadhani yanakukwamisha lazima uwemwepesi kuyasema na ndiyo maana taasisi ambazo ziko chiniya Wizara hiyo zina wataalam wengi tu. Angalia hayoambayo wameyafanya, nadhani tukifanya kwa harakatutayafanikisha lakini sio ya watu wazima tunaongea kilamwaka yale yale hatuendi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nimeona projectza kielelezo ni hii reli yetu ya kutoka Tanga – Arusha - Engaruka.Sasa najiuliza, nimesoma speech ya Waziri wa Ujenzi juzi, ninyimnachotuambia ni nini hapa maana inaonekanahamuongei pamoja. Mnachosema kwenda kutekeleza,mtatekeleza nini maana kule kwenye ujenzi hatukuonachochote ambacho kinaongelewa kuhusu ujenzi wa relimpya ya kutoka Arusha - Lake Natron na mwaka keshomtakuja na lugha hizi hizi, kwa hiyo tunabaki hapo hapo. Let’swalk the talk tumalize, yale ambayo hatuwezi kuyafanyatuseme haya hatuwezi kuyafanya sekta binafsi itakuja tukama tutaijengea mazingira wezeshi na rafiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana,nikupongeze sana Waziri na timu yako, endeleeni. Mazingirandiyo hayo lakini tusibebe mambo mengi kwa wakati mmoja.Tuchukue vipaumbele vichache tuweze kuvisimamia ilitwende mbele. Ahsanteni sana, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa AndrewChenge. Tunaendelea na Mheshimiwa Jaku Hashim,baadaye Mheshimiwa Jumanne Kishimba na MheshimiwaIbrahim Raza. (Makofi)

Page 293: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

293

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nami nikushukuru kwa kunipa fursa hii, jioni hiikuchangia Wizara hii ya Viwanda na Biashara. HataMheshimiwa Rais wetu amekuwa akihimiza sana viwanda nakasi yake. Tumpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe sanaMheshimiwa Waziri, maneno mazuri sisi Waislam tunasema nisadaka au maneno mazuri humtoa nyoka pangoni.Nimuombe Mheshimiwa Waziri, uongozi ni dhamana, ni jambola kupita, leo lipo kesho halipo na baada ya siasa kuna maishanje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, biasharani nini? Biashara haifanywi na mtu mmoja, biashara lazimaiwe na monopoly. Biashara haiwezi kufanywa na mtu mmojahata kidogo. Uzuri wa Wizara ya Biashara haiwezi kwendabila ya fedha. Fedha ndiyo biashara, biashara ndiyo fedha,kwa hiyo, hivi vitu kidogo vinaoana. Hapa kidogo MheshimiwaWaziri nataka unisikilize kwa makini, hasa Waziri wa Fedha,Mheshimiwa Dkt. Mpango, nikuombe sana, kuomba siyo kosa,kuiba ndiyo kosa, kama kuna watu wanateseka, Benki yaFBMEwatu wanateseka, nimepiga kelele, nitaendelea kupigakelele mpaka pumzi yangu ya mwisho. Watu wanaweka hakizao kule, wananyanyasika, wengine wameshaanzakutangulia mbele ya haki, hakuna harufu yoyote na BenkiKuu ndiyo dhamana na kama nilivyosema cheo ni dhamanana tutaenda kuulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu au mbeleya haki, tumetumia vipi dhamana zetu hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wanatakakusomesha, fedha zao zimekwama benki. Mnawaambia nini?Benki Kuu iko chini ya Wizara ya Fedha, Bureau de Changezote mna-control ninyi. Tumeona Greenland Bank imefungwana wakati huohuo mnasema fedha za wateja ziko salama,salama iko wapi? Au Salama jina la mtu? Maana kuna jinala mtu Salama. Kuna wawekezaji Zanzibar pesa zaozimekwama, wafanyakazi wa benki pesa zao zimekwama,mishahara yao haipatikani.

Page 294: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

294

Mheshimiwa Spika, nimwombe sana MheshimiwaWaziri kwa huruma na unyenyekevu, sijawahi kukuambia hiviMheshimiwa Dkt. Mpango. Wewe binadamu na mimibinadamu, tuwe na jicho la huruma. Je, ungefanyiwa weweau mimi tungekubali? Tuwaonee huruma wananchi.Wananchi ndiyo walioweka Serikali hii madarakani. Mtu anashilingi milioni 200, unampa milioni moja na laki tano nisawasawa na kumpa peremende baadayeukamnyang’anya, haifai hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije katika kero zaMuungano, biashara ndogondogo bandarini. Hii tuliambiwamoja kati ya kero ya Muungano. Msijali mtu wa mbali, jiraniyako ndiyo mtu wa karibu. Tumetimiza miaka 54 ya Muunganohuu na tuombe uendelee kudumu. Wafanyabiasharabandarini Mheshimiwa Mwijage wanateseka na hesabuinaanza moja ndipo ije mbili na tatu. Hawa wotewafanyabiashara wameanzia biashara ndogondogowakafika kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwananchi wa Zanzibaramechukua TV moja, amechukua mashati yake matatu,amechukua kilo zake sita za sukari akafika paleananyanyaswa. Imefika wakati watu wakathubutu kuvunjaTV zao, huu siyo ubinadamu wala siyo uungwana. NikuombeMheshimiwa Dkt. Mpango, Waziri wa Fedha na Waziri waBiashara mliangalie hili suala. Leo imekuwa mali inayotokaZambia, Uganda, Burundi na Kenya inaingia hapa iko salama,inayotoka kwa ndugu zetu upande wa pili utafikiri umeletabangi au unga, kwa nini tunafanya hivi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema na nitaendeleakusema, baada ya siasa kuna maisha nje, haya mambo niya kupita na cheo ni dhamana lakini hatuwatendei haki.Zanzibar inategemea zao la karafuu, uchumi wake wa pili nibiashara. Leo bandari imezuiwa usajili wa meli, kuna matatizohatujui kinachoendelea, lakini tusiwanyanyasewafanyabiashara. Mtu ana TV moja, mbili, atakula nini?Anakuja na boti yake asubuhi, jioni apate kuuza aondokelakini anakuja mzigo unaoza ndani mle, ndiyo lengo hilo?

Page 295: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

295

Katika moja ya kero kubwa ya Muungano hili ni moja, tuwewakweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie Kiwanda chaSukari cha Mahonda, hapa nisikilizeni vizuri. Kiwanda hiki kipoTanzania, Tanzania hii imeitwa na Zanzibar ikiwemo. Tunalindaviwanda vya Tanzania, je, Zanzibar haipo Tanzania? That ismy question. Tunalinda viwanda vya Tanzania, Zanzibar haikoTanzania? This is my question au hailindwi Zanzibar?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunalinda viwanda vyaTanzania Bara kwa hiyo Zanzibar haipo? Pombe, nondo, saruji,unga wa ngano unaingia Zanzibar lakini bidhaa kutoka kulekuleta huku imekuwa mtihani, tuwe wakweli. Ndiyo yalenimemwambia Mheshimiwa Keissy, moja iwe moja, mbili iwembili, mbichi iwe mbichi, kavu iwe kavu. Kama tunalindatuseme tunalinda viwanda vya Tanzania Bara siyo Tanzania,tuwe na vigezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. au Prof.Mwijage maana cheo chao kikubwa, juzi ulijibu swali la 205.Mheshimiwa Spika aliona udhaifu wa swali hili, ningesemamimi ingekuwa mtihani, huku unakataa Tanzania hakunauhaba wa sukari, huku unasema baada ya miaka mitanosukari itakuwa ya kutosha, tukamate wapi? Huku unakataa,uhaba wa sukari haupo, baada ya miaka mitano unasemauhaba wa sukari utakuwa umekwisha. Sasa tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu Waziri toka kaangaliebandarini, hiyo sukari imeshafika usije ukauziwa mbuzi kwenyegunia. Uende ukapate ushahidi, usije ukapata ushahidi waKinyamwezi. Nenda kaangalie hii sukari uliyowapa vibaliimefika? Isije kufika Ramadhan hapa tukawasumbua aukuwatesa wananchi. Narudia tena, Serikali hii isingekuwamadarakani bila wananchi. Hata Uwaziri wakohuu,Mheshimiwa Waziri ungekuwa mtihani tungetawala nini,miti au barabara? Wananchi ni kitu muhimu. HataMheshimiwa Rais mwenyewe anawajali wananchi,tumpongeze kwa dhati kabisa hasa wananchi wa chini,credit yake kubwa iko hapa. (Makofi)

Page 296: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

296

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali isiogope kula hasarakwa mambo madogo madogo kama haya na wewe mshauriMheshimiwa Rais usiogope kuwa hiki kiko hivi, hiki kiko hivi,mueleze tuna upungufu huu. Tuliwapa vibali vya sukari, mimina ninyi, twende mguu kwa mguu kama sukari mliyotumbiaimeshaingia tani 135,000, twende tukaiangalie.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Jaku.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,sijamaliza lakini itabidi nishukuru hivyo hivyo kwa mudaulionipa. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Jumanne Kishimba, baadaye MheshimiwaIbrahim Raza na Mheshimiwa Zainabu Mndolwa.

MHE. JUMANNE K. KISHIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi kuchangia Wizara hii yaViwanda na Biashara. Nitaanza upande wa viwanda nauwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hili suala ambalolinaendelea sasa hivi kwa Kiswahili linasema kuongezathamani au kwa Kingereza ku-add value. Suala hili kamahatukulifanyia utafiti wa dhati litatuletea mtafaruku mkubwa.Maana yangu kusema hivyo ni kwamba, kila mwenyekiwanda sasa hivi anapigania kuzuia wananchi wasiuze malizao akiwa anasema yeye yupo tayari kununua mali yote nakui-add value. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano. Hapatunakatazwa kuuza mahindi nchi za nje tunaambiwa tuuze

Page 297: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

297

sembe lakini watu wa Kongo sembe wanachanganya namuhogo, sasa utawauziaje sembe na wenyewewakachanganye muhogo, wanakwambia wanatakamahindi ili wakasage waweke muhogo. Kwa kuwa Waziri yukohapa aliangalie kwa makini sana suala hili, kama mtuanasema anataka ku-add value ni lazima aoneshe uwezowa kiwanda chake ataweza kweli kununua mali zaWatanzania ili watu wasikae na mali zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano kwenyengozi. Sasa hivi karibu ngozi zote zinatupwa, zimezuiwa nazimewekewa export levy ya 80% na indication priceiliyowekwa na TRA ni senti 58 ya Dola ambayo ni Sh.1,300lakini bei ya ngozi leo duniani ni senti 35 ambayo ni Sh.800.Itawezekana vipi sasa mtu alipie Sh.1,300 auze Sh.800?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumesaini mkataba naUganda na Kenya kwenye hilo suala la ngozi. WenzetuWaganda na Wakenya wana-under value invoice, wanalipiakwa bei chini na kununua mali zetu, ni kwa nini na sisiwananchi wetu wasiruhusiwa kuuza mali zao ili kuondoa huumtafaruku ambao unaendelea? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaungana na Wabungewenzangu kwenye suala hili la Liganga na Mchuchumaingawaje mimi mtizamo wangu uko tofauti kidogo. Mtizamowangu mimi ni kwamba, madini haya kwa utafiti wawataalam wetu wanavyosema yako mengi kiasi cha kutoshamiaka 100 lakini miaka 100 kwa dunia inavyokwenda harakani kweli teknolojia hiyo au chuma hicho kitakuwa kinatakiwaduniani. Kwa nini tusiwe na option mbili, tukawa na optionya kuuza udongo wa chuma kama ulivyo na tukawa naoption ya kuyeyusha? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kufanya analysis yamadini yaliyomo mle ndani nchi nyingi duniani wakati bei yachuma au madini fulani yanapanda wanauza kwa ajili ya

Page 298: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

298

kupata pesa muda ule na kujikimu. Sasa hivi hapa kwetutunalia kwamba, hatuna pesa ya maji lakini tuna mlima zaidiya miaka 50, kuna ubaya gani kufanya analysis na baadhiya mawe yale yakaendelea kuuzwa ili tupate pesa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kwenye Jimbo letu laKahama au Wilaya yetu ya Kahama na Mkoa wa Shinyangamwaka huu tuna mavuno mazuri sana ya mpunga.Tunamwomba Mheshimiwa Waziri hili neno la add valuealiangalie. Sisi tunataka kuuza mpunga au mchele kwaWaganda lakini tunabanwa na sheria inayosema huwezikuuza mpunga lazima ukoboe mchele, lakini wakati unasubirikukoboa mchele hilo soko litakuwa linakusubiri kweli kuleUganda? Haiwezekani. Ni lazima Mawaziri wafikirie sana sualahilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakwenda kwenye suala labiashara. Kwenye mkutano wa Mheshimiwa Rais ni kwelimambo mengi sana yalijitokeza pale. Ukiangalia maswalimengi ya wafanyabiashara ilikuwa ni kwenye tatizo la Sheriaya Importation na Sheria ya Kodi ya Mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Importationinatusumbua, sisi tunatumia tarrif ambayo haisumbui sanaukienda kwenye vitu kama mafuta ta dizeli, sukari, simentina vinywaji kwa kuwa hawa wanatumia ujazo au kilo lakiniunapokwenda kwenye item ndogondogo, nitatoa mfano waitem moja, kwa mfano wewe ume-import glass, glass kwenyetarrif inaitwa glassware, lakini kuna glass ya Sh.10,000 na yaSh.1,000 lakini TRA ata-pick glass ya Sh.10,000 kuku-chargewewe wa glass ya Sh.1,000/=. Kwa hiyo, tunamwombaMheshimiwa Waziri wa Fedha kwa kuwa yuko hapa nimiongoni mwa kero nyingi sana ambazo wafanyabiasharawamezionesha wakati wa kufanya importation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna tatizo kubwa sisitunaotoka mikoa ya mpakani. Kuna hii sheria mpya ya ku-declare pesa. Wananchi walioko Kongo, Burundi, Ugandawanataka kuja kununua mali kwetu Mikoa ya Mwanza,

Page 299: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

299

Shinyanga na Geita. Haiwezekani mtu atoke Uganda auatoke Kongo afike Mutukula aoneshe Dola zake 50,000apande basi, ni kitu ambacho hakiwezekani hata iweje.Tumeshuhudia wote hapa mtu anatoka kuchukua pesa paleMlimani City anavamiwa anauawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Waziri waFedha kwa kuwa yuko hapa alifikirie, hili neno tume-copy kwaWazungu, kwao ni sawa, London uki-declare hakuna mtuatakuvamia lakini ku-declare kilometa 300 upite poriniambako mpaka mabasi yanafanyiwa escort na weweulionesha dola, tumekwama kabisa watu wa nje wamekataakuja kununua mali kwetu kwa sababu hiyo, hawawezi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia nchi hizo ni zileambazo hazina mfumo wa kibenki, Kongo hakuna benki,Burundi kuna vita, watu hao wote wanatembea na cash.Nafikiri Waziri wa Fedha kwa kuwa yuko hapa ajaribu sanakulifikiria suala hili ambalo linatusumbua sana. Sisi Mwanzatunauza samaki, mchele na vitu vingi lakini mpaka sasatumekwama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia kwa kuwa naWaziri wa Nishati yuko hapa tungeomba sana wenzetu waTANESCO waruhusu, kama walivyoruhusu kwenye transformer,kwa wafanyabiashara hasa wanaotaka kuanzisha viwandakama wanaweza kuvuta umeme kwa gharama yao halafuwakawarudishia wakati wa bili inapoanza. Kwa kuwa, yeyesasa hivi analalamika kwamba hana pesa ya kununua nguzoau vifaa vya umeme itasaidia watu wanaotaka kuanzishaviwanda waweze kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya mchango huo,naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Ibrahimu Raza, baadaye Mheshimiwa ZainabuMndolwa na Mheshimiwa Frank Mwakajoka.

Page 300: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

300

MHE. IBRAHIM HASSANALI MOHAMMEDALI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii.Namshukuru Mwenyezi Mungu vilevile kwa kunipa uzima waafya nikiwa nimesimama hapa kwa nguvu zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze kakayangu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Mwijage.Kwa kweli, hiki kitabu nimekipitia leo mchana vizuri kabisa,nakiona kipo vizuri sana. Nimpongeze yeye na timu yakenzima kwa jinsi walivyoandaa bajeti hii na ripoti ya Wizara yaBiashara na Viwanda, Mheshimiwa Mwijage na timu yakohongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nichukue nafasi hiinimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa mamboaliyoyaweka jana vizuri sana. Amewatoa wananchi wasiwasi,maneno yalikuwa mengi kwamba katika Mwezi huu Mtukufuwa Ramadhan kutakuwa hakuna mafuta na sukari.Tunamshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja naMheshimiwa Mwijage kwa kutuhakikishia kwamba,hakutakuwa na suala hilo wala matatizo hayo ya mafutawala sukari. Nawashukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu naMheshimiwa Mwijage. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa mwizi wa fadhilakama sijampongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. John PombeMagufuli kwa jinsi anavyohangaika kufufua viwandaambavyo vilikuwa vimekufa. Naweze kusema kwambajitihada ya Mheshimiwa Rais imetuletea faraja kubwa sanana naamini kwa Waziri aliyekuwa naye ni Waziri jembe kabisa,Mheshimiwa Mwijage. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwijagenimefanya naye kazi wakati nilipokuwa kwenye Kamati yaBiashara na Viwanda miaka miwili iliyopita. Namjua kazi yake,ni mtu ambaye yuko straight kabisa na makini kabisa, hongerasana Mheshimiwa Waziri kwa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilikuwa na ushauri kwaWizara ya Biashara na Viwanda. Mheshimiwa Mwijage

Page 301: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

301

nataka utusaidie au uwasaidie wafanyabiashara ambaowanapakia mizigo yao Dubai kuja Dar-es-Salaam wanalipiaSGS kule Dubai na kila item wanatozwa kwa Dola 20 mpakaDola 30. Baada ya ku-register SGS Dubai wanatakiwa baadaya mali kufika hapa TBS inawa-charge tena katikakuchunguza vile vitu walivyoleta. Kwa hiyo, wanakuwawanalipa SGS kule Dubai wakija huku wanachajiwa tena naTBS. Sasa utakuta mfanyabiashara analipa mara mbili ya kilekitu ambacho amekinunua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wa SGS kule Dubaiwamekuwa very slow yaani ukiwapelekea sampuli, huchukuamore than four or five weeks, sasa utakuta mfanyabiasharaanaumia na kule ameweka mzigo kwenye godown za watuanalipa zile gharama kwa sababu Dubai hakuna mtuambaye atakuwezesha kukuwekea mali kwa mwezi mmoja,mwezi mmoja na nusu. Kwa hiyo, nashauri Mheshimiwa Wazirilabda ukae na hawa wenzetu wa SGS Dubai na TBS, kwa niniwanakuwa wana-charge mara mbili mzigo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine kwa sababu,tukiwasaidia wafanyabiashara naamini watapata nguvu yakutuletea mali kwa wingi na Wizara ya Fedha itapata kodi.Kwa hiyo, hapa tunampa motisha mfanyabiashara at thesame time Wizara ya Fedha na TRA wanapata pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuna tatizo mojakubwa la wenzetu hawa wa TFDA. Naweza kusema kwambaTFDA sio wote, sitaki kuwakaanga wote, baadhi yaohupelekewa sampuli ikiwa ya maziwa, juice au kitu chochotewanakwambia kwamba utapata ripoti after 60 or 70 days.Mheshimiwa Mwijage wenzetu hawa TFDA hivi kweliwanatutakia mema Tanzania hii? Wakati wewe unapiganiawafanyabiashara walete mali wauze nchi ipate pesa tupatekodi, wanaambiwa warudi after 70 days?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi navyozungumza hayahuwa nina ushahidi, sizungumzi tu kwa kuwaelemea TFDA.Kwa hiyo, naomba TFDA kama kuna upungufu wa watu basiwaajiriwe watu wengine lakini huwezi kumuweka mtu 60 or

Page 302: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

302

70 days ndiyo unampa report, inarejesha nyuma maendeleoyetu na sisi tunataka kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu hata hizo adaambazo wana-charge TFDA ni kubwa sana MheshimiwaWaziri. Ningeomba kidogo hizo ada ziteremshwe ili watuwawe na hamu ya kuleta mali nchini. Kiwango kinachotozwasasa hivi ni kubwa sana. Hata hivyo vitu ambavyo SGS wana-charge kule Dubai kwa kila item ni Dola 30 nyingi MheshimiwaMwijage. Wewe ni msikivu naamini utachukua hatua. Hayandio yalikuwa ni kero na nilikuwa natoa ushauri kupitia Wizarayako ifuatilie kwa karibu sana hili suala ili tufike hapotunapotaka kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa sana watuwanapoiponda Serikali hii, mimi siwafahamu. Kwa sababu,hiki kitabu kimeeleza kuna wawekezaji 99 wamesajilikuanzisha viwanda Tanzania hii. Ina maana hao wawekezajiambao wanakuja kuwekeza hapa si wendawazimu,wameshajua Tanzania ni nchi ya amani, Tanzania kuna kunamoja, mbili, tatu. Sasa wanapoponda kwamba hakunaviwanda au hakuna chochote wasome hiki kitabu ambachokimeandikwa kwenye ukurasa wa 186, miradi mipya yaviwanda vilivyosajiliwa na TIC mwaka 2017/2018. Hii ni ushahiditosha kwamba watu wana imani na Serikali ya MheshimiwaMagufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna wenginewanakuwa na choyo na binadamu sisi tunakuwa na choyo.Mheshimiwa Mwijage ukivaa suti nzuri kama mtu hakupendiatakwambia unaringa lakini kwa sababu umevaa suti nzuri.Kwa hiyo, nasema tupunguze uchoyo, tumpe haki yakeMheshimiwa Rais Magufuli anavyofanya hii kazi kwa sababu,kuileta Tanzania katika amani ni kitu kikubwa sana ndiomaana hawa wawekezaji 99 wamekuja kuwekeza Tanzaniabillions of Dollars, it is billions of Dollars. Leo kwa nini tunakaatunaiponda hii Serikali? Why? Badala ya kuipa nguvu?(Makofi)

Page 303: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

303

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini katika miakamichache ijayo tutakwenda kwenye uchumi wa kati, hapatulipo tutasonga mbele. Ni juhudi zetu sisi Watanzania,Wabunge waliokuwa humu ndani tumpe nguvu na ushirikianoMheshimiwa Rais pamoja na Mawaziri wake wote walikuwahumu ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanaposemakwamba labda kiwanda kiwe na ekari tano, ekari sita, kuleChina unaweza kukuta kichumba kidogo sana wanazalishamambo ambayo huwezi kuyaamini Mheshimiwa Mwijage.Wana vyerehani 10, 15 lakini the production ambayo wana-make ni kubwa sana. Kwa hiyo, kiwanda si lazima kiwe naekari 10 ndiyo ukaita kiwanda. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Ibrahim Raza.

MHE. IBRAHIM HASSANALI MOHAMMEDALI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana na naipongezasana Wizara hii na naiunga mkono asilimia 100 Wizara yaBiashara na Viwanda. Inshallah Mwenyezi Mungu atatusaidiana tumuombee Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli, ahsanteni sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMhesimiwa Zainabu Mndolwa baadaye Mheshimiwa FrankMwakajoka na Mheshimiwa Gimbi Masaba.

MHE. ZAINABU M. AMIR: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Awali ya yote, napenda kumshukuru MwenyeziMungu ambaye ametuumba sisi kuwa wanadamu kishaakatupa akili na ufahamu ili kuweza kujadili mambombalimbali kuhusu Taifa letu. Pili, nikushukuru wewe kwakunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia katika Wizara hiiya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. (Makofi)

Page 304: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

304

Mheshimiwa Mwenyekiti, Dar es Salaam ni kitovu chabiashara katika nchi yetu na wafanyabiashara wa Dar esSalaam huchangia pato kubwa katika Taifa hili lakiniwanakabiliwa na changamoto nyingi sana. Ili uanzishebiashara kuna taratibu za kufuata hadi biashara yakoifunguliwe, kwanza lazima upate leseni, lakini kinachotokeakwa wafanyabiashara hao wanaanza kulipa mapato kablaya kufanya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inawaumiza sanawafanyabiashara. TRA wanakadiria watu mapato kulinganana eneo analilopo na siyo biashara wanayoifanya.Wanapoenda kudai leseni wanaambiwa kwanza waendeTRA wakakadiriwe mapato, nauliza inawezekanaje mtuhajaanza kufanya biashara anakadiriwa mapato, kauza ninihuyu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali Taasisi yaMamlaka ya TRA itoe grace period kwa wafanyabiashara.Wakati wanataka kuanzisha biashara zao kwanza wapeweleseni, pia wapewe muda wa kufanya biashara hiyo angalaumiezi mitatu wakati wanatumia mashine za EFD kisha ndiyowakadiriwe. Kitendo kinachofanywa na TRA kuwakadiriawatu mapato kabla ya biashara kwa kweli, kinawaumizasana wafanyabiashara, hususan wa Jiji hili la Dar-es-Salaam.Naomba sana Serikali ilichukue hili na ilifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, naishauri Serikali walendugu zetu wafanyabiashara ndogondogo Wamachinga niwafanyabiashara pia lakini watengewe maeneo maalum.Sasa hivi ukifika katikati ya Kariakoo maeneo yaNarung’ombe, Kongo, Mchikichi, wafanyabiasharandogondogo wameweka bidhaa zao mbele ya maduka yawafanyabiashara ambao wanalipa kodi kihalali. Kutokanana buyer behavior ya watu wetu wa Tanzania wenye kipatocha chini kuona kwamba biashara zilizokuwa barabarani nirahisi kuliko za ndani hupelekea watu wenye madukakushindwa kufanya biashara zao vizuri na Taifa kukosamapato kutokana na kwamba wafanyabiashara walewanaosambaza barabarani kutolipa mapato ya aina yoyote.

Page 305: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

305

Kwa hiyo, naishauri Serikali itenge maeneo maalum kwa ajiliya Wamachinga ili nao waweze kufanya biashara pia walipekodi kwa Taifa letu. Najua kwamba Machinga ni wapiga kurapia wafanyabiashara wa madukani ni wapiga kura wa Taifahili, kwa hiyo, naiomba Serikali izingatie hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine sasa hivi kumetokeamtindo kwa Kikosi cha Zimamoto kupita katika maduka yawafanyabiashara Kariakoo kuwalazimisha waweke fireextinguisher ndani ya maduka. Fire extinguisher ina kilo 5 nakila mtungi mmoja ni Sh.200,000 na kila mwisho wa mwakaulipe Sh.40,000 unaweka ndani ya duka, je, moto ukitokeasaa 8.00 za usiku wakati mfanyabiashara huyo yuko nyumbanikwake ile fire extinguisher itamsaidia nini kuokoa mali zake?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni dhahiri kwamba Kikosicha Zimamoto kimeanzisha mradi mwingine kwawafanyabiashara ili kuwakandamiza. Naishauri Serikaliikutane na Kikosi cha Zimamoto, iwashauri wale wamiliki wamajengo waweke fire extinguisher kwenye corridors zanyumba na siyo ndani ya maduka ya wafanyabiashara, kwasababu huwezi kujua moto utatokea wakati gani. Ni borafire extinguisher ziwekwe kwenye corridor kuliko ndani yamaduka ya wafanyabiashara, hii itasaidia moto ukitokeawakati wowote aidha, asubuhi, mchana hata usiku kuwezakutumia fire extinguisher kuzima moto ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuelekea Tanzania yaViwanda kuna viwanda vingi ambavyo vimepewawawekezaji. Nitatolea mfano Kiwanda cha Nguo cha KaribuTextiles Mills ambacho kiko Wilaya ya Temeke. Kwa sasa hivikiwanda kile kimefungwa na kimegeuzwa kuwa ghala lakuhifadhia soda. Nimetembelea mwezi uliopita palewameweka soda na kiwanda kile kilikuwa kinazalisha nguo,vitenge, khanga pia mashuka na kilikuwa kinaleta ajira kwazaidi ya watu 1,000. Kwa sasa hivi Mheshimiwa Wazirikimegeuka kuwa ghala la kuhifadhia soda na hakunakiwanda tena pale. (Makofi)

Page 306: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

306

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naishauri Serikali,wakati tunaelekea Tanzania ya Viwanda badala ya kutafutamaeneo ya kuanzisha viwanda vingine ni bora kwanzatuvifufue vile viwanda ambavyo vimepewa wawekezaji.Maeneo mengi yalikuwa na viwanda, nitakutolea mfanoMkoa wa Morogoro, mwaka wa 1980 ulikuwa ukifikaMorogoro unaweza kupata ajira mapema kuliko kupatachumba cha kuishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kuna Kiwanda chaCanvas Mill, Ceramics, Polyester, Moro Shoe, Tanneries,Magunia, Kiwanda cha Tumbaku, Kiwanda cha SukariMtibwa, Kiwanda cha Sukari Kilombero, vyote hivi vilikuwaMkoa wa Morogoro, lakini kwa sasa hivi viwanda vilewamepewa wawekezaji na haviendelezwi. Morogoro nikatikati ya Dar es Salaam na Dodoma, viwanda vile vifufuliwena kupewa wawekezaji na kusimamiwa vizuri, iwe ni samplingarea. Sasa hivi tunajenga treni ya mwendokasi ambayoitarahisisha watu kufika kwa urahisi Morogoro, italeta ajira kwawatu wa Morogoro, Mkoa wa Pwani pia wa Dodomawanaweza kupata ajira katika Mkoa wa Morogoro. Badalaya kutafuta maeneo ya kwenda kuanzisha viwanda vingineni bora tuvifufue viwanda vile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona viwanda vingi piaMkoa wa Tanga. Kilikuwepo Kiwanda cha Mbolea, Kiwandacha Chuma, Kiwanda cha Amboni, Kiwanda cha Gardeniana Mbuni, viwanda vile vyote vifufuliwe kuliko kwendakuanzisha maeneo mengine mapya, ili viweze kutoa ajira kwawatu wetu. Mkoa wa Tanga unazalisha matunda mbalimbalilakini katika hotuba ya Mheshimiwa tunashauri, kuanzishweKiwanda cha Juice ambapo itasaidia wakulima kwendakuuza matunda yao katika kiwanda kile, kuliko sasa hivimatunda ikifika msimu yanaharibika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushauri Mheshimiwasana wakati unaelekea kuanzisha viwanda vipya vile vyazamani visimamiwe kwa uhakika ili kuleta ajira na pato laTaifa letu. Naomba haya yazingatiwe kwani yatasaidia sanakuliendeleza Taifa letu kuliko kuanza kukata misitu huko na

Page 307: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

307

kutafuta mashine za kufunga, tuboreshe mashine katikaviwanda vya zamani ambavyo vitasaidia kuleta ajira kwakwa wananchi wetu na pia kuchangia katika pato la Taifaletu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana, naomba maoni ya Kamati yazingatiwe ilikuelekea Tanzania ya Viwanda. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa ZainabMndolwa. Tunaendelea na Mheshimiwa Frank Mwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kupata nafasi hii. Kwanza nitumiefursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbilinyi (MheshimiwaSugu) kwa kutoka siku ya leo. Namshukuru sana Mungualiyemwezesha kukaa gerezani kwa muda wote bilakutetereka na sasa ametoka anakuja kutekeleza majukumuyake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuchangia hotubahii na nataka kumaanisha ili ushauri wetu ambao tumekuwatukiutoa kila wakati katika Bunge Serikali iweze kuufanyia kaziSerikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namkumbuka sanaMheshimiwa Mbilinyi alijaribu kuzungumzia sana kuhusianana jambo ambalo li l ikuwa linafanywa na Serikali yakuikusanyia nchi ya Kongo mapato. Baada ya ushauri ulenafikiri Serikali ilikubali na sasa ilishaondoa na sasa hivi naonaWakongo wanatumia Bandari ya Dar es Salaam vizuri namambo yanakwenda sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema tu kwambasiasa safi ni uchumi. Tusije tukajidanganya hata siku mojatukafikiri siasa za kibabe, siasa za kutenganatenganazinaweza zikasababisha nchi ikawa na uchumi bora. Siasa niuchumi lakini pia uchumi ni sayansi. Kwa hiyo, sisi ni lazima

Page 308: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

308

tujue kabisa kwamba umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu,bila kujua hili tukaendeleza ubabe tunakoelekea siko kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonataka kulizungumza ni kuhusiana na wafanyabiasharawengi Tanzania wanaohama nchi. Liko kundi kubwa sana lawafanyabiashara ambao wanahama katika nchi yetu nawanakwenda kufanya biashara kwenye nchi zingine.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo liko wazi naMheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara wajibu wakemkubwa ni kuhakikisha kwamba ustawi wa wafanyabiasharana biashara zao katika nchi hii ya Tanzania ni kipaumbelekikubwa kabisa. Huwezi kuamini wafanyabiashara wengisasa hivi, ukienda Malawi wengi wamehamia kule. UkiendaZambia maeneo yote kuna wafanyabiashara wametokaTanzania wamehamia Zambia. Pia ukienda Kongo ambakohali kwa kweli ya usalama si nzuri lakini wafanyabiasharawako tayari kuondoka Tanzania waende wakafanyebiashara Kongo, kwa sababu ya mazingira mabaya ambayoyapo kwa wafanyabiashara wetu ambao wanajitahidikuwekeza kwenye nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema tu jambomoja kwamba leo Mtanzania akitoka na mzigo wake Dubai,akifika kwenye Bandari ya Dar es Salaam amekuja na invoiceyake ya kiwandani kabisa alikonunua mzigo kinachotokeawatu wa TRA wanamwambia kwamba hii wamekukadiriavibaya umetengeneza invoice, anaanza kukadiriwa upyaakiwa bandarini Dar es Salaam. Amenunua mzigo wa Dolamilioni 10 anaambiwa huu mzigo bwana ni milioni 20,mfanyabiashara anakimbia, anaacha mzigo, mizigo inakaapale kwa muda mrefu na biashara baadaye zinakufa na huyomfanyabiashara anapoteza fedha zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nakumbuka wakatitunajadili hapa, juzi nil ikuwa nasikil iza Radio Cloudswanasema tumeshangaa sana Wabunge wetu, wanasemawakati Mbunge anaomba mwongozo watu walishangilia

Page 309: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

309

sana, wakati Mwijage anajibu watu wakashangilia sana lakiniwakati Mheshimiwa Spika anatoa ufafanuzi na kutoamaelekezo kwa Serikali watu wakashangilia tena. Sasawanasema Wabunge wetu hawa tatizo ni nini hapa yaanikipi ambacho walikuwa wakikishangilia, ni ule mwongozouliotolewa na yale majibu ya Waziri au kil ichokuwakinashangiliwa ni yale maamuzi ambayo Mheshimiwa Spikaaliiagiza Serikali? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana tumesikia hapa wakatiMheshimiwa Waziri Mkuu akitoa maelekezo kuhusiana natatizo la mafuta ambayo yako bandarini. Ametoa maelezohapa na akasema kwamba anatoa siku tatu. Tunaombasana uchumi hauhitaji nguvu, unahitaji kukaa na kuzungumza.Hawa wafanyabiashara ambao wamekaa kule na mizigoyao nia yao kubwa ni kuja kuuza na kuhakikisha kwambawanalipa kodi kwenye Taifa hili lakini kitendo cha kuendeleakutumia nguvu kwa kuwalazimisha haitaweza kutusaidiasana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Serikali ikubalikukaa na wafanyabiashara. Hata mwanzo tuliwaambiakukaa na wafanyabiashara na kuzungumza nao ni jambokubwa katika nchi hii. Hawa ndiyo watu wanaoweza kulipakodi na ndiyo ambao wanaweza wakaendesha Taifa hili,lakini bila wafanyabiashara kukubali kufanya biashara katikanchi hii na kuwekewa mazingira mazuri nchi hii haitakusanyakodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Waziri waFedha amekiri hapa ndani, amesema tatizo kubwa kwa ninimnasema fedha hazijaenda huku, kwa sababu makusanyoyamekuwa madogo, fedha hakuna. Tafsiri yake ni kwambawafanyabiashara hawalipi kodi kwa sababu biashara zaozimeshadhoofi lakini wengine wamefunga biashara, wenginewamehama na biashara zao, sasa anataka kodi kutoka kwanani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni jukumu la Serikalikuangalia ni namna gani wanaweza wakatengeneza

Page 310: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

310

mazingira mazuri kwa ajili ya wafanyabiashara wetu iliwaweze kufanya biashara vizuri. Ukienda Tunduma palempakani tumepakana na eneo la Nakonde Zambia. Sasahivi nyumba ambazo walikuwa wanaishi Wazambiazimeshafumuliwa Watanzania wameingia mikatabawameamua kuhamisha biashara zao na sasa wamefunguamaduka makubwa upande wa Zambia kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezungumza sana,nimesema ndani ya Bunge lakini pia nimewashauri Mkuu waMkoa, Mkuu wa Wilaya hawawezi kusikiliza wanaendeleakukomaa wanasema hapana tunataka tufunge barabara.Wamefunga njia ambazo watu walikuwa wanapita,wafanyabiashara wa Zambia na Kongo wakitokawamenunua mizigo wanapita katika njia ambazo walikuwawanazipita siku zote. Wamefunga wameweka matarumawafanyabiashara wa Kongo na wa Zambia wamesema hatujitena Tanzania tunakwenda kununua maeneo mengine. Kwahiyo, walichokifanya wafanyabiashara wameamua kutumiaakili zao za haraka haraka na kwenda kuhamia upande waZambia na leo Zambia maduka ni mengi. Wafanyabiasharawalioko pale sasa hivi ni karibuni wafanyabiashara 3,000waliohama kutoka Tunduma wanafanya biashara Zambialakini wanalala Tanzania. Kwa hiyo, tunachokizungumza hapatunakuwa tunamaanisha katika Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri waFedha ni lazima pia afike mahali aangalie kodi kwenye Taifahili limekuwa ni tatizo. Kila mwaka wanaleta taarifa hapakwamba wanakwenda kuzifanyia kazi hizi kero za kodi iliwafanyabiashara wetu waweze kwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuamini,wafanyabiashara wengi sasa hivi wanakadiriwa kodi, mtuanakadiriwa shilingi milioni 300, shilingi milioni 400, mwingineanakadiriwa shilingi bilioni 1, shilingi bilioni 2 bila sababu zamsingi na kuelezwa kwa nini anatakiwa kulipa kodi hiyo.Wafanyabiashara sasa hivi wamekuwa kama wakimbizi,Serikali haiwaamini wafanyabiashara wa Tanzania. Serikaliinawaona ni wezi wafanyabiashara wa Tanzania na Serikali

Page 311: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

311

inawaona wafanyabiashara wa Tanzania ni watu ambaowanakwepa kodi wakati si kweli. Kazi ya Serikali ni kuwekamazingira bora na safi ya kufanyia biashara na siyokuwayumbisha wafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema ni lazimatukubaliane ukienda TRA sasa hivi wanakukadiria fedhawanayotaka na ukiwaambia sina fedha wanakwambianenda halafu baadaye wanakwambia bwana ili tukufanyievizuri tunaomba utupe labda shilingi milioni 10 au shilingi milioni5 au shilingi milioni 6 na kwa sababu Serikali imewatia wogawafanyabiashara wanakwenda kutoa rushwa badala yakuingizia mapato Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi wanatumia msemommoja wanasema wewe hujui kama ni Serikali ya Awamuya Tano ya Magufuli hii, ni hapa kazi tu, hakuna namna yoyoteutatoa na usipotoa tunakufilisi. Ndicho wanachowaambiawafanyabiashara, imefika mahala wafanyabiasharawameamua kusema sasa ngoja na sisi tuache. Wenginewanafunga biashara wanaona afadhali waende maeneomengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nirudi kwenye vitabu vyabajeti vya Waziri. Nakumbuka kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 fedha iliyokuwa imetengwa kwenye viwanda ilikuwashilingi bilioni 45 lakini fedha iliyokwenda kwenye viwandakutekeleza majukumu ya maendeleo ni shilingi bilioni 6.7ambayo ni sawa na asilimia 8 ya bajeti yote. Hii inaonyeshani jinsi gani Serikali ya Chama cha Mapinduzi inazungumzandani ya Bunge lakini haijajiandaa kutengeneza viwanda nakuleta viwanda katika Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona ni jinsi ganiambavyo utekelezaji wa bajeti umeendelea kuwa chinimwaka hadi mwaka na hatujui tatizo ni nini. Leo mnasemaviwanda, viwanda haviji kwa maneno, viwanda haviji kamaalivyokuja Mwijage na Kitabu kikubwa hapa. Viwandavinakuja kwa kutenga fedha na fedha hizo kuzipeleka katika

Page 312: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

312

maeneo husika ili zikafanye kazi. Kwa hiyo, yote haya ni lazimayaeleweke vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye bajeti ya 2017/2018walikuwa wamepangilia kukusanya shilingi bilioni 28 kwenyeWizara lakini wamekusanya shilingi bilioni 6.6 peke yake. Hiiinaonyesha hata uwezo wa kukusanya mapato kwenyeWizara yenyewe imekuwa ni chini kabisa. Yote hayayanafanyika kwa sababu ya kutokuwa na maandaliziambayo yako sawasawa.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mwakajoka.Tunaendelea na Mheshimiwa Gimbi Masaba na MheshimiwaSabreena Sungura kwa dakika tano tano.

MHE. GIMBI D. MASABA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Wizara hiiya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, napendanimpongeze Mheshimiwa Joseph Mbilinyi na nimpe hongerakwa kuongeza CV ya siasa katika Taifa hili. Tunamwambiakaribu tuendelee na kulijenga Taifa hili, mapambanoyanaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo mengi yakuzungumza kutokana na kwamba mimi ni Mjumbe waKamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, yapo menginayofahamu na Waziri wa Viwanda anafahamu niniambacho nimekuwa nikikidai katika Kamati hiyo. Kwa leo

Page 313: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

313

nataka nibebe angalau hoja moja au mbili kutokana namuda na naomba nizungumzie kuhusu uhaba wa sukarinchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitaji la sukari kwa mwakani tani 440,000, uwezo wa viwanda vyetu ni kuzalisha tani 3,000pekee. Hivi navyozungumza bei ya sukari kwa mfuko wa kilo50 ni Sh.110,000 lakini kila mwaka tunakuwa na upungufu wasukari karibia tani 140,000 sawa na asilimia 32.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilitoa vibali kwa ajiliya kuagiza sukari kwa wafanyabiashara kwa lengo la kukidhimahitaji ya Taifa letu au kwa maana nyingine kwa walaji.Nikizungumzia suala la bei ya Brazil, sukari kwa bei ya Brazil nisawa na dola 3,090 sawa na Sh.860,000 na hiyo ni pamoja nakodi asilimia 25 na VAT asilimia 18. Kwa bei hii sukari ilipaswakuuzwa Sh.65,000 na siyo Sh.110,000 au ingeweza kuuzwaSh.80,000 maana wao kule wananunua kilo 50 Sh.65,000maana yake wangeweza kuuza hapa Sh.80,000 na isiweSh.110,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumza haya kwamasikitiko kwa sababu kila kukicha tunaisikia Serikali inasemani Serikali ya wanyonge. Kama Serikali ni ya wanyonge ni kwanini Serikali inawauzia wananchi sukari kwa bei ya juu kiasihiki? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ina maana ukigawanyahapa ni kama wanauza kwa kilo Sh.3,000. Kama Serikali ni yawanyonge, kwa nini basi Watanzania wasipate sukari kwaSh.1,500 kwa kilo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilitoa vibali watuwaagize sukari kwa lengo la kuleta ushindani wa soko. Chakushangaza ni kwamba sukari ile ile ya ndani na nje inauzwabei moja. Sukari kwa bei ya ndani inauzwa Sh.110,000 na sukariya nje inauzwa bei ileile. Sasa najiuliza, ni kwa nini Serikali ilitoavibali kwa walewale wenye viwanda badala yawafanyabiashara wengine ili kuleta ushindani wa soko nakuleta tija kwa walaji? (Makofi)

Page 314: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

314

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja anipe majibu, kwa nini Serikali haikutoa vibalikwa wafanyabiashara wengine na ni kwa nini imetoa kwawafanyabiashara walewale ambao sisi tunasema sukariambayo wanazalisha wao haikidhi na ndiyo maana Serikaliiliamua kutoa vibali ili tukidhi hitaji la Watanzania? Kwa hiyo,naomba majibu atakapokuja Mheshimiwa Waziri waViwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya pil i, natakanizungumzie suala la uhaba wa…

(Hapa kengele ililila kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Gimbi, muda wakowa dakika tano umemalizika. Tunaendelea na MheshimiwaSabreena Sungura, dakika tano na baadaye MheshimiwaEng. Gerson Lwenge.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Nimewahi kuhoji kwenye Bunge hili kwamba ninani kati yetu atapewa mtaji wa shilingi milioni 250 a-raisempaka shilingi bilioni 2 ndani ya miaka mitano? Hoja yanguni kwamba mabenki mengi yamefungiwa baada ya kukosavigezo vya kutimiza mtaji wa shilingi bilioni 2. Athari yake ninini kwa uchumi wa nchi yetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wengi walikuwawamewekeza pesa kwenye mabenki hayo na wakatiwakisubiri process za insolvency maana yake watachukuamuda mrefu sana il i waweze kuletewa fedha zao.Waliahidiwa kwamba kwa awali watalipwa Sh.1,500,000 kilammoja halafu watasubiri process ya mfilisi mpaka itakapofikiamwishoni ndiyo waweze kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati muafaka sasa kwaSerikali ya Chama cha Mapinduzi iweze kuhakikisha kwambainashusha riba ili watu wetu waweze kuwa na uwezo wakurudisha mikopo katika mabenki yetu. Ukiangalia ripoti ya

Page 315: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

315

CAG inaonesha mikopo isiyolipika ilipanda kutoka shilingibilioni 9.1 mpaka shilingi bilioni 2.5. Watu wengi kushindwakulipa mikopo kwa sababu mbalimbali. Wapo ambaowanashindwa kulipa mikopo kwa sababu kodi za TRA zimezidilakini wapo ambao wanashindwa kulipa mikopo kwasababu sekta ya biashara na uchumi imezidi kudorora katikanchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraka harakanapenda nizungumzie Special Economic Zone. Kuna sualazima la fidia ambalo limezungumziwa katika Ibara ya 24 yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia hatakwenye sheria zetu, mfano Sheria ya Land Acquisition Act,section 15 inaelezea kwamba maeneo ambayoyamefanyiwa tathmini kwa ajili ya kulipwa fidia ya SpecialEconomic Zone (SEZ) na Export Processing Zone (EPZ) yawezekulipwa takriban shilingi bilioni 60 kwa mwaka 2015/2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa hivi fidia zilezimefikia shilingi bilioni 190. Hiyo ni kwa sababu kila mwakakwa mtu ambaye alithaminiwa na alitakiwa alipwe fidiaukipita mwaka mmoja kuna 6% kama nyongeza ambayoanatakiwa aongezewe. Kwa hiyo, kwa wananchi wote wamaeneo ya Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Kigamboni kwamaana ya Kurasini (Tanzania-China Logistic Center), Mara,Ruvuma na maeneo mengine yote, fidia imeongezeka kwakiwango kikubwa kwa sababu Serikali imeshindwa kulipafidia kwa wakati na hivyo kuliingizia Taifa hasara na mzigomkubwa kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraka napendakuitaka Wizara iwasaidie wawekezaji wetu kutoka nje. KunaTanzania Diaspora, tumeona hapa wenzetu Wachina naIndia, juzi hapa waliitishwa Wahindi wote waliopo dunianiwarudi India kwa ajili ya kwenda kufanya uwekezaji ambaoutakaokuwa na tija. Wahindi waliopo Tanzania na wenginewalitoka kwenye Bunge letu hili walienda India kuwekeza.Kwa nini Diaspora wetu ambao wapo nje ya nchi wenyeuwezo mzuri, ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi

Page 316: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

316

hii, hawawi included katika kuendeleza uchumi wa nchi hii?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Nneiliweka Desk la Diaspora pale na walikuwa wameshaanzaprocess hizi lakini mpaka sasa bado kimya. Ukiangalia katikaKatiba pendekezwa ya Ndugu Warioba, Ibara ya 72, iliwekakipengele kwamba Watanzania ambao walibadili uraia kwaajili ya kutafuta maisha wapewe special priority au hadhimaalum ili waweze kutambulika katika uchumi wa nchi yetu,waweze kumiliki ardhi, kuwekeza katika hisa na wawezekumiliki mali katika nchi yetu. Kwa hiyo, tunaomba tuwekedesk maalum kwa ajili ya Diaspora ili waweze kujiungavikundi kwa vikundi, waweze kuwekeza kwenye sekta zamaji, kilimo, viwanda na kadhalika kwa sababu kunaWatanzania wenye fedha na wenye uwezo mzuri katika nchiza Arabuni, America na Ulaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwishoni kabisa napendanimalizie kwa kuzungumzia hali ya uchumi katika Mkoa waKigoma. Ukitaka kuhakikisha kwamba hali ya uchumiimekuwa mbaya, mwaka uliopita Mkoa wa Kigoma takribanmiezi sita au mpaka saba wafanyakazi na wafanyabiasharawa maduka mbalimbali katika Mji wa Kigoma waligomakufungua maduka kwa sababu walipandikiziwa tozo kutokaSh.15,000 mpaka Sh.50,000 na Chama cha ACT Wazalendo.Hiyo inaonesha kabisa kwamba uchumi unayumba ndiyomaana watu waliamua kufunga maduka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Chama cha ACTWazalendo walilikoroga akaja Ndugu Polepole akalinywa,alipoingia pale aliambia wananchi wanatakiwa wafunguemaduka na kodi ile inashushwa. Kupandisha kodi nimchakato wa sheria na ulifanywa kwa mujibu wa sheria naBaraza la Madiwani ndiyo lililopandisha na ikaenda Mkoani,TAMISEMI, Mheshimiwa Waziri akaweka saini ikashuka,inakuwaje anakuja Mwenezi na kukataza kodi ile isilipwe?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti…

Page 317: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

317

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Sabreena.Tunaendelea na Mheshimiwa Eng. Gerson Lwenge nabaadaye Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa ajiandae.

MHE. ENG. GERSON H. LWENGE: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi.Kabla sijachangia, naomba nimtangulize Mungu mbele kwakumshukuru sana kwa kunipa afya na hekima. Kwa kuwanatambua kwamba maandiko yanasema katika mamboyote tutangulize dua na sala na Bunge lako huwa tunaanzana dua na sala na mahali popote unapomtaja Mungutunasema lazima umtaje katika roho na kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mbunge unapotoamchango wako ni lazima umtangulize Mungu ili akupehekima uweze kuchangia vitu ambavyo vitatupeleka mbele.Kwa hiyo, naomba sana nimpongeze Mheshimiwa Waziri,Naibu Waziri na Watendaji wake kwa namna walivyoleta hojahii. Hoja imeandikwa vizuri sana, inatoa matumaini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sanaMheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwakuamua kwamba ili tuweze kufikia uchumi wa kati lazimatuweke nguvu yote kwenye uchumi wa viwanda. Kwa hiyo,ni jambo moja zuri, lazima tumuunge sana mkono Rais wetuili tufikie azma hiyo ya uchumi wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka niseme tu kwambakatika viwanda ambavyo tunavizungumza, kweli vipo vingi;nimejaribu kuangalia karibu nusu ya kitabu ina orodha yaviwanda lakini unaweza ukaona uhalisia wa uchumi waviwanda na uchumi wa kipato cha mtu mmoja mmoja.Tanzania wananchi walio wengi ni wakulima na tunawezatukawasogeza mbele kama tutawekeza viwanda ambavyovitasaidia sana wao kuuza mazao yao il i wawezekuwaongeza kipato walichonacho. Kwa hiyo, naomba sanaMheshimiwa Mwijage katika orodha kubwa aliyokuwa nayo

Page 318: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

318

hapa, ajaribu kuangalia na kuweza kulea viwanda vileambavyo vinasaidia sana wakulima wetu kuuza mazao yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo langu laWanging’ombe asilimia 90 ni wakulima wa mahindi na viazimviringo. Wakulima hawa hawana soko la kuuza mazaohaya ya viazi. Katika viazi kuna tatizo sana la vipimo. KunaWakala wa Vipimo, nimesoma kwenye hotuba yaMheshimiwa Waziri, wanasema wanashughulikia namna yakusimamia vifungashio. Wakati wa mwanzo walikuwa navifungashio vikubwa ambavyo wanajaza vile viroba vikubwavya lumbesa ambapo ukipima kwenye kilo ni zaidi ya kilo100 ambayo ipo kwenye sheria. Hata hivyo, usimamizi wakeni mgumu sana kwa sababu wafanyabiasharawanatanguliza mawakala ambao wanakwenda kuwarubuniwakulima kule mashambani. Naomba hii Wakala itafutembinu za kusimamia jambo hili, kusiwepo na kurubuniwakulima katika kuuza mazao yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchezo mwingine ambaowanafanya wanasema wewe Wanging’ombe usipouza viaziwanakwenda kununua Mporoto au Arusha ambapowanaweza kuuza kwa vipimo hivi vya lumbesa. Nafikiri kwasababu huu Wakala upo basi uwajibike ili wakulima wetuwauze viazi kwa kilo siyo kwa vipimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi wameleta virobavidogo ambavyo vinaweza kujaza debe tano. Sasa ili gunialitimie unajaza viroba viwili na lumbesa yake. Kwa hiyo,unakuta kwa wastani kunakuwa na debe kumi ambazowanasema hizi sasa ndiyo kilo 100 kwa vipimo. Kwa hiyo,tukiweza kwenda kwa kipimo cha kilo, tutafika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vingine ambavyonafikiri navyo tungevifanyia kazi ni viwanda vya mazao yapamba, korosho, chai, kahawa, pareto, mahindi, mpungana alizeti. Kwenye Jimbo langu tuna viwanda viwili; kimojakinazalisha sembe, kinaitwa Mbomole Investment Company.Kile kiwanda hakizalishi kwa kiwango kikubwa kwa sababu

Page 319: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

319

tu TANESCO wameshindwa kutoa transformer ya KVA 200 kwazaidi ya mwaka mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kiwanda kinginekimewekezwa pale cha kukamua mafuta ya alizeti kinaitwaWende Investment Company. Hiki nacho kimeisha mwakamzima lakini TANESCO wameshindwa kutoa transformer yaKVA 200. Sasa inawezekana mifano ya namna hii iko maeneomengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Wazirikama anavyokimbia hivi, nilifikiri ni vizuri viwanda hiviambavyo vimeshaanzishwa visaidiwe. Wananchi wetutumewahasisha wananchi wetu walime sana alizeti kwasababu kiwanda kipo, najua watapata mahali pa kuuzalakini kama kinakuwa white elephant kwa sababu yatransformer tu, basi Serikali ni moja, uweze kuona namna yakuwasil iana na Mheshimiwa Dkt. Kalemani tupatetransformer, wananchi wangu wapate mahali pa kuuza hiyoalizeti na transformer nyingine kwa ajili ya wananchi wangukuuza mahindi ili waweze kuinua kipato chao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uuzaji wa mahindi imeonekani ngumu sana kwa sababu kipindi fulani Serikali ilikuwaimefunga mipaka lakini nashukuru sasa mmefungua. Hatahivyo, kuna urasimu sana katika kuuza mahindi nje ya nchiau maeneo mengine. Tuwasaidie kwa viwanda hivi ambavyovinaanza kuibuka kwa kuwezesha mambo kama ya umemena vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka nichangie pia sualala kuinua uchumi. Nchi nyingi ambazo zimeendelea zilianzana viwanda vinavyohusiana na chuma. Tanzaniatumezungumza habari ya Liganga na Mchuchuma kwakarne, kuanzia awamu ya kwanza ya Serikali zetu hizi lakinihakuna kinachoendelea. Unajua ukisema umtegemeeMchina, naye anataka kuinua uchumi wa nchi yakehataweza. (Makofi)

Page 320: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

320

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nataka uamuzi wa Raisuje kama wa Stiegler’s Gorge kwamba sasa tunaamuakujenga Stiegler’s Gorge, basi tuamue na kujengaMchuchuma kwa namna yoyote inavyowezekana. Ninauhakika tutakuwa hatulii umaskini kwamba hatuna maji navitu vingine, tunaweza kujitegemea wenyewe kamatulivyoanza kujenga reli. Nilifikiri kwamba nishauri na ndiyomaana naunga mkono hoja hii ili unisikie vizuri na ukalifanyiekazi kusudi Tanzania kweli ifike azma ya kuwa na uchumi wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambalo lingine ambalonataka kulizungumzia ni kwamba hapa Dodoma kunamwekezaji mmoja alianzisha kiwanda cha kutengeneza hiziceiling boards kwa kutumia gypsum na malighafi yakeinatoka Dodoma hapa hapa, kipo hapo Kizota naMheshimiwa Waziri nilishawahi kumwambia. Mwekezaji yuleameshindwa kukiendeleza kile kiwanda kwa sababu yaushindani wa soko. Tatizo lipo kwa wafanyabiashara ambaowanaleta semi-finished goods, wanasema hii ni gypsum ghafilakini kumbe ni finished goods ambazo sasa wao hawalipiikodi. Sasa hiki kiwanda kimefungwa na huyu mtu ameamuakuondoka. Aliwekeza fedha na wananchi wa Dodomawalikuwa wamepata ajira na Serikali inakosa kipato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Wazirialifuatilie suala hili ili kusudi mwekezaji yule akifungue hikikiwanda cha Dodoma na kama kuna kodi ambazo zipo kwamujibu sheria, basi yeye anasema hana tatizo kulipa kodi,lakini kwa nini watu wengine wanasamehewa kodi kwafinished products, wanadanganya kwamba wanaletamalighafi ya gypsum? Tutakuwa tumeendeleza sana Mkoawetu wa Dodoma ambao sasa ni makao mapya ya Serikali.Kwa hiyo, naomba kumshauri Mheshimiwa Waziri walifanyiekazi jambo hili kiwanda kile kifufuliwe ili kiweze kuleta ajirakwa wananchi wetu na Serikali pia itapata kodi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme, nashukurusana kwa nafasi na naunga mkono hoja. (Makofi)

Page 321: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

321

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Eng. Lwenge.Tunaendelea na Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa baadayeMheshimiwa Deogratias Ngalawa.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, naomba nichukuefursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja naMheshimiwa Naibu Waziri, dada yangu Mheshimiwa Eng.Stella Manyanya. Naendelea kumpongeza sana kwa sababumwaka 2011/2012 na 2012/2013 Mheshimiwa Eng. StellaManyanya alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati yaViwanda. Kwa hiyo, yupo kwenye nafasi sahihi kabisa.Miongoni mwa hoja nyingi ambazo zimezungumziwa hapa,Engineer anazifahamu. Kwa hiyo, atakuwa kwenye nafasinzuri sana kumwelekeza Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwanza niMchuchuma na Liganga. Mwaka 2012 pale Mlimani City, Dkt.Cyril Chami akiwa Waziri, Tanzania kupitia NDC tulisainimkataba wa Liganga na Mchuchuma, mimi nikiwepo naNaibu Waziri alikuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ninapozungumza nitakriban miaka sita. Mambo yote ya msingi kwenye mkatabaule tulikubaliana na naamini kwa kiasi kikubwayametekelezwa. Inasikitisha sana miaka sita imeshapita tokasasa hakuna kitu chochote kil ichofanyika kwenyeMchuchuma na Liganga. Kama kweli tunataka kwendakwenye uchumi wa viwanda, miongoni mwa maeneoambayo tutatakiwa tuyaenzi kwa nguvu zetu kubwa ni eneola Mchuchuma na Liganga ambapo malighafi za uhakikaza umeme na chuma zinapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, makaa ya mawe yaMchuchuma na makaa ya mawe ya Ngaka yanawezakuzalisha umeme wa megawatt 120. Tulikuwa tuna tatizokubwa la transmission line, lakini kwa bahati nzuri tumepatahela kwa wafadhili na transmission line ile inajengwa. Kwa

Page 322: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

322

hiyo, umeme umeshapatikana, sasa kigugumizi kinatokawapi cha kutoanzisha mradi wa Mchuchuma? Naaminikabisa Mheshimiwa Waziri akija hapa atatuambia ni sababuzipi zinapelekea leo mpaka miaka sita imefika hatujafanyachochote kwenye mradi mkubwa huu wa Liganga? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Awamu ya Tano,tumejielekeza kwenye uchumi wa viwanda. Tunapotakakuzungumzia habari ya viwanda kuna baadhi ya mambotunatakiwa tuyaangalie kwa karibu zaidi. Malighafi kubwaambayo inatakiwa ipatikane kwenye eneo hili inatakiwa itokekwenye kilimo. Tumejipanga vipi ku-invest kwenye kilimokusudi tuwe na uhakika wa kupata raw materials za kutosha?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa viwandaunakwenda simultaneously na uchumi wa kilimo. Tunawezatukajenga viwanda vikubwa hapa nchini lakini kamamalighafi hakuna, tutakuwa tuna hadithi, tutakuwa naviwanda ambavyo haviwezi kufanya uzalishaji. Kwa hiyo,tujiangalie, tunapotaka kujenga viwanda, tujiulize, hiyomalighafi inatoka wapi? Kwa hiyo, nashauri, tunapojiangaliakwenye uchumi wa viwanda, tujiangalie na namna yakuandaa malighafi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilitakakulichangia na kumwomba Mheshimiwa Waziri aje kuniambiani suala la Kurasini Logistic Center. Tumelipa fidia zaidi yashilingi bilioni 90 kwenye Kurasini Logistic Center na tulisainimkataba wa mwaka 2013 na Wachina kwa ajili ya kujengalogistic ile lakini leo ni miaka mitano hatujafanya chochotena shilingi bilioni 90 imeshakwenda pale. Kwa hiyo, tusije kuwatuna matumizi ambayo siyo sahihi. Mheshimiwa Waziriatakapokuwa anakuja, aje atueleze kwa nini mpaka leologistic center haijaanza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sanaMheshimiwa Waziri wa Viwanda kwa kazi na juhudi kubwaanayoifanya katika eneo lake, lakini pamoja na kazi kubwaanayoifanya, tunatakiwa sisi kama Tanzania tujipange namna

Page 323: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

323

ya kuvi-protect viwanda vyetu vya ndani. Kwa mfano, tunaviwanda vikubwa tu vya maziwa hapa nchini na maziwamengi tunayotumia hapa nchini yanakuwa-imported kutokanje, matokeo yake tunashindwa kuvisaidia viwanda vyandani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye taasisinyingi za Serikali utakuta maziwa yanayotumika ni ya nchi zanje. Ukiuliza sababu zipi zimesababisha kutumia hizo Lactogenna maziwa mengine kutoka nchi za nje, hupati majibu. Kwahiyo, kama tulivyofanya kuzuia importation ya furniture zanje, ifike wakati na Serikali izuie importation ya maziwakutoka nchi za nje. Sisi kama Watanzania ni nchi ya pili kwakuwa na ng’ombe wengi katika Afrika. Kwa hiyo, tutumieutamaduni huo na rasilimali tuliyonayo kuhakikisha tunafanyavizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pamba huwalinaajiri watu wengi sana. Ukienda Cambodia pamoja nakwamba hawalimi pamba lakini watu wengi wameajiriwakatika industry ya textile. Kwa hiyo, ifike wakati sasa tuanzisheviwanda vingi hapa nchini vya nguo, naamini vitaajiri watuwengi kuliko kujielekeza kwenye kuuza rasilimali yetu yapamba tutakuwa hatuitendei haki. Tuko tayari kumuungamkono Mheshimiwa Waziri kwa kuhakikisha raw materialzinazopatikana kwenye maeneo ya pamba, nyingi zinatumikandani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo wenzetu waviwanda wamefanya vizuri sana. Kwa mfano, eneo la BRELA(Msajili wa Makampuni), siku za nyuma palikuwa na shidasana, lakini sasa hivi wamefanya vizuri sana. Usajili unafanyikiaonline na unafanyika kwa kipindi kifupi. Kwa namna yakipekee, tumpongeze Mheshimiwa Waziri na Mtendaji Mkuuwa BRELA kwa kazi nzuri anayoifanya katika maeneo yake.Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni, kama anafanyavizuri, naomba tumpongeze sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayomachache, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

Page 324: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

324

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa MahmoudMgimwa. Tunaendelea na Mheshimiwa Deogratias Ngalawana Mheshimiwa Riziki Lulida ajiandae.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nakupongeza kwa kunipa fursa yakuweza kujadili hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kiasi kikubwa napendatu kuzungumzia suala la Mchuchuma na Liganga. Suala hililimekuwa likizungumzwa muda mrefu sana. Huu mfupaumekuwa mkubwa na mgumu. Liganga na Mchuchumaimeanza kuzungumzwa toka mwaka 1929 kipindi chaMkoloni. Mkoloni alishindwa na hizi Serikali nyingine zotezimekuwa zinaweka mipango lakini ni mipango ambayo kwakweli haitekelezeki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia kitukinachoitwa mradi ni lazima uwe na mwanzo na mwisho.Lazima kuwepo na activities au programs za kuhakikishakwamba tunaanza hivi, tunapita hapa mpaka mwisho wasafari inakuwaje. Kitu kinachoshangaza katika Mradi waLiganga na Mchuchuma ni kwamba hatuoni ile mipangoambayo inawekwa, kwamba sasa Liganga na Mchuchumaimewekwa kwenye Programu ya Miaka Mitano ya Serikali;Liganga na Mchuchuma imezungumzwa kwenye Ilani yaChama cha Mapinduzi; Liganga na Mchuchuma inawekwakwenye kila bajeti ya mwaka ambazo tunazipitisha hapa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ule Mpango wa MiakaMitano sasa tunaingia mwaka wa tatu lakini badohatujaona Liganga na Mchuchuma hasa ina tatizo gani.Tuliambiwa kwamba tatizo ni incentives, tunajaribu kujiulizahizi incentives Serikali inashindwa kuchukua hatua ili tuwezekuona namna gani tunazi-accommodate na baada ya hapohii miradi iweze kuanza? (Makofi)

Page 325: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

325

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejaribu kupitia kitabu chabajeti, nimeona Liganga imewekewa shilingi bilioni 5 naMchuchuma imewekewa shilingi bilioni 5, lakini sasahaifafanui activity ya hizi shilingi bilioni 5 zilizowekwa kwenyeLiganga na Mchuchuma ni kwa ajili ya nini hasa? Kwa hiyo,naamini kwamba Mheshimiwa Waziri atakapokujakuhitimisha hotuba yake basi atatueleza hizi shilingi bilioni 5ni kwa ajili ya nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo ya fidia pale,mpaka leo imekuwa ni kizungumkuti. Alipita MheshimiwaWaziri Mkuu tarehe 26 Januari, 2017, tulilizungumzia kwa kiasikikubwa suala la fidia na ikaonekana kama fidia imekuwaexaggerated na ikasemekana kwamba itaweza kuundwaTume au tukafanya review ya ile fidia ili wale watu waliopishaile miradi iweze kufanyika pale walipwe kwa sababu sasahivi wala hawajui nini cha kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye incentives kuletunaona kuna suala la Power Purchase Agreement. Mara yakwanza ilikuwa ungetumia ule mfumo wa Build, Own andTransfer lakini baadaye kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziriya mwaka 2017, wakaja tena na mfumo ule mwingine kwamaana ya kubadilisha kwamba itakuwa ni Build, Own andTransfer. Sasa hatujajua ni incentives zipi ambazozinasababisha ule mradi usianze? Kwa hiyo, naaminiMheshimiwa Waziri atakapokuja basi atatuambia wamefikiawapi. Hizo incentives ambazo zinasemwa kwambazinashindikana kufanya ule mradi uanze ni zipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza kwamba kunamiundombinu wezeshi ambayo inafanya sasa ule mradiunaweza ukaanza, lakini pia inahitaji maamuzi magumu.Naona upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabaraambazo zinakwenda kwenye ile miradi, kwa maana kunabarabara inayotoka Mchuchuma kwenda Liganga na piakuna barabara ambayo inatoka Mkiu kupitia Ligangakwenda Madaba. Naona zoezi lile linakwenda vizuri naupembuzi yakinifu na usanifu wa kina safari hii utaisha mweziOktoba. (Makofi)

Page 326: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

326

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaona umeme wa Gridiya Taifa ambao vilevile utashushwa pale eneo la Ligangana pia moja kwa moja utaelekea kule Mchuchuma. Jitihadahizi za Serikali tunaziona, miundombinu wezeshi hii ya Serikalitunaiona. Napenda kuiomba Serikali, suala la fidia basimwaka huu iwe mwisho. Wale watu wamesubiri kwa mudamrefu, tuondokane nalo hilo. Kama itashindikana mwekezajikulipa basi Serikali ichukue jukumu hilo na kuhakikishakwamba hii adha ya fidia kwa wananchi wetu waMkomang’ombe na kule Mundindi inaisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mchuchuma na Ligangatumekuwa tukiiongelea muda mrefu sana. Mimi nawatangulizi wangu wote nane wamekuwa wakiongeleaMchuchuma na Liganga katika Bunge lako hili. Mwaka 2017zaidi ya asilimia 80 ya Waheshimiwa Wabunge wamekuwawakiiongelea Mchuchuma na Liganga. Tukijaribu kuangaliakwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri, Mchuchuma naLiganga haijapewa ile weight yake yaani ni maneno ya mistari11 tu, basi Liganga na Mchuchuma imeisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe tunasemakwamba Liganga na Mchuchuma ni miradi kielelezo. Miradikielelezo ya nchi sikutegemea kwamba ingeweza kupewaweight ndogo kiasi hiki. Tungeweka weight kubwa na tujuetatizo ni nini? Angedadavua kiasi cha kutosha il iWaheshimiwa Wabunge tujengewe uelewa ili mwisho wasiku tuweze kuishauri Serikali vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nanukuu maelezo yaMheshimiwa Waziri ya masuala ya viwanda mama na miradikielelezo ya nchi, Mradi wa Mchuchuma na Liganga.Anasema, katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi Unganishiwa Mchuchuma na Liganga, Serikali il iunda Timu yaWataalam wa Serikali ikiwa na jukumu la kuchambua vivutiovilivyoombwa na wawekezaji. Vilevile uchambuzi ulifanyikakwa kuzingatia marekebisho ya Sheria ya Madini, 2010; Sheriaya The Natural Wealth and Resources Permanent SovereignityAct, 2017; na The Natural Wealth and Resources Contracts(Review and Renegotiation of Unconscionable Terms), 2017

Page 327: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

327

na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa na Serikali.Timu hiyo imekamilisha taarifa ya awali ambayo inasubirikutolewa maamuzi na mamlaka husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelezo haya ni ya kila sikuna kwenye kila bajeti huwa yanakuja haya haya, kwambatunaendelea na mchakato. Sasa ifike wakati Serikali ije namaamuzi magumu kuhusu mradi huu. Kwa hiyo, bado Taifalinasimama na naamini kwamba unapozungumzia viwandandani ya nchi hii, unazungumzia Liganga na Mchuchuma kwasababu multiplier effect yake inaenda mbali. Kwa hiyo, ifikemahali sasa tuchukue maamuzi magumu. Nami naaminikwamba Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli ina uwezo wa kuchukua maamuzi magumu nakuhakikisha kwamba miradi hii ina-take-off. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye upande wabiashara, mimi huwa najiuliza, tunawajua wafanyabiasharawetu? Tunayo database ya wafanyabiashara wetu? Kwasababu tunaweza tukawa tunazungumza biashara nainaweza ikaleta impact gani wakati hatuwafahamuwafanyabiashara wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mlivyo-categorize,kuna wafanyabiashara wa kati, wadogo na wakubwa. Je,tunayo hiyo database ya hao watu kiasi ambacho tunawezatukawa na uhakika kabisa kwamba tunapozungumzia sualala biashara impact yake ni hii na revenue tutakayoipata kwawafanyabiashara ni hii hapa ili mwisho wa siku sasatutengeneze platform kwenye kila maeneo, tunawezatukaweka semina kwa wafanyabiashara wa kati, wadogona wakubwa. Otherwise tutatakuwa tunatwanga majikwenye kinu kama hatuwajui wafanyabiashara wetu ni nanina tunatarajia nini kutoka kwao na impact kwa wananchiwetu kiuchumi kuanzia mtu mmojammoja, vikundi na mpakaTaifa inakuaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ifike mahali sasahawa Maafisa Biashara wetu kwenye Halmashauri, kwenyemikoa, ni lazima watengeneze database za wafanyabiashara

Page 328: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

328

wetu. Kwa sababu database hiyo inaweza ikatumika kamarole model kwa watu ambao wanataka kuingia kwenyebiashara ili waweze kujua kwenye biashara playground yaoikoje? Sometimes tukiwa na role models wana uwezo wakushawishi watu wengine kuja kuingia kwenye mfumo wakibiashara. Tusipotengeneza semina hizi wezeshihatutaweza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa DeoNgalawa.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Naunga mkono hoja.

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa Riziki Lulidana baadaye Mheshimiwa Salome Makamba.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalianami kuchangia katika hoja iliyopo mezani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiona mahali WaheshimiwaWabunge wanaliongelea eneo hilo basi Serikali ilifanyie kazi.Waheshimiwa Wabunge wengi wanaongelea TRA. Sasa hiviTRA ni eneo ambalo haliko rafiki na wafanyabiasharawadogo wadogo. Wameweka urasimu wa makusudi, siwezinikasema ni wote, lakini maeneo mengi ya TRA sasa hivi nieneo ambalo linawakwamisha wafanyabiashara wadogowadogo, hivyo, siyo eneo rafiki kwao. Hili eneo litawakatishatamaa wafanyabiashara hawa ili wasiweze kuendelea.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ulivyosikia, unatakiwakwanza wakutoze ushuru hata kazi hujafanya. Mama Ntilieanapika wali, hajajua kama anaweza akauza wali wake,umeshamwekea tayari, lipa shilingi milioni moja, anaipata

Page 329: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

329

wapi? Huu ni unyanyasaji wa kibiashara kwa wazawa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka kwenda katikaTanzania ya viwanda. Tanzania ya viwanda inahitajimazingira wezeshi kwa viwanda. Enzi za Mwalimu Nyererealianzisha maeneo ya viwanda na maeneo yale aliwekamazingira mazuri ya maji, umeme na barabara. Kwa mfano,alianzisha viwanda 14 vya korosho, hili nalirudia tena karibumara ya tatu, viwanda vile vilikuwa na umeme, maji na ajiraya kutosha. Vilevile walikuwa wana uwezo wa kupatamalighafi ya korosho palepale katika mikoa inayozalishakorosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nimeona katika hotubaya Mheshimiwa Waziri ametaja mikoa yote ambayo imepewakipaumbele cha viwanda; Lindi, Mtwara na Ruvuma sijaionahapa. Kwa maana moja, hata hivi viwanda vya koroshovilivyopo, mategemeo ya kuvifufua hayapo. Ni aibu kiasi ganikorosho inalimwa Tanzania inanunuliwa inapelekwa India,wanakwenda ku-process tunaletewa korosho ileiliyobanguliwa kuja kula tena Tanzania. Huu siyo mfumo mzuriwa kibiashara. Tunavyo viwanda vya korosho Tanzania lakiniunavikuta vinapeleka korosho nje ya nchi as a raw material.Huu ni uharibifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekwenda katika seminaya korosho, tunaambiwa Tanzania haionekani kabisa kamani mzalishaji wa korosho, kwa vile tunaipeleka nje wale ndiowanaonekana wanazalisha na kusafirisha korosho. Je,tutapata lini ajira kama korosho yote tunaipeleka nje?Viwanda vyote vimefungwa. Cha kusikitisha zaidi, Mkoa waLindi hatuna kiwanda hata kimoja. Hivyo viwanda vyakorosho vil ivyokuwepo; vya Mtama na Lindi, vyotevimefungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kama MheshimiwaWaziri ameikutia tu hii issue, ni makosa makubwa yalifanyikaya ubinafsishwaji na uwezeshaji. Uwekezaji wa nchi hiihaukuweka mazingira mazuri katika mikataba, haukuweka

Page 330: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

330

mazingira mazuri kwa kujua nini tufanye katika kubinafsisha.Tumewabinafsishia watu, wamevifunga viwanda, watuwalewale ndiyo wanapeleka korosho nje. Haiwezekanikabisa. Nataka utupe taarifa, ni nani wamechukuaviwanda? Bado walewale waliochukua viwandawanapeleka korosho nje, huu ni uhujumu wa uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na viwandaTanzania ambavyo vinakamua mafuta. Mwanza tulikuwatunapata Mafuta ya OKI, SUPA-GHEE, TanBond ya Tanzaniaambayo hata Kenya walikuwa wanaipeleka, viwanda vilevyote vimefungwa, kwa nini vimefungwa na naniamevifunga? Kama ni mkataba, mkataba wake ulikuwa wamuda gani? Palikuwa na mikataba mibovu ambayohaikuwa na timeframe. Hivyo mtu amechukua kiwanda,amekifunga, anaagizia mafuta machafu kutoka nje wakatitunaweza kutengeneza mafuta masafi Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki ni nini? Nafika mahalisielewi kama najielewa au pengine mimi niko nyuma yawakati. Viwanda vya mafuta tunavyo. Nachingwea tulikuwana viwanda vya mafuta, Mafuta Ilulu, ufuta wetu woteulikuwa unakamuliwa Nachingwea. Leo ufuta wote waTanzania tunaupeleka nje, halafu hapa tunalalamika tunauhaba wa mafuta wakati mafuta yetu mnapeleka mbegunje, mnapeleka ajira nje na raw material inabakia kule namakapi yanatengeneza feed cake za wanyama. Huu ni uhuniwa kibiashara ambao umechezwa kwa muda mrefu,tunafanya biashara kwa mazoea, matokeo yake tunaiwekanchi katika crisis. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila inapofika karibu naRamadhani wafanyabiashara wanaanza uhuni wao; marahakuna mafuta, sukari, hii ni crisis ya makusudi wanatakakupandisha bei i l i wananchi wapate ghadhabu naRamadhani. Mfanyabiashara kupata pepo ni ngumu sana.Wanaangalia ni eneo gani nitafanya fujo yangu halafu watuwatahamasika ili angalau hili litakuwa ni chachu kwawananchi kulalamika hakuna sukari na mafuta. Nina imanisukari ipo, mafuta yapo, yatafutwe na wananchi wapate

Page 331: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

331

sukari na mafuta. Tumechoka kusikiliza uhuni wa kibiasharawa muda mrefu. Nchi haiendeshwi kwa uhuni wa kibiashara,nchi inaendeshwa kwa taratibu zilizopangwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii alizeti inapelekwa nje,magazi kutoka Kigoma yanapelekwa nje, wanachujawanatuletea tena, ooh, tuna mafuta yako njeyamenasanasa. Kwa nini mmefunga viwanda vyetu vyamafuta na mmevizuia hamkamui mafuta, mnatuleteamatatizo kibiashara? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasikitika sana kusemaubinafsishaji ndiyo donda ndugu la nchi hii. Tumefungaviwanda vyote. Tulikuwa na viwanda vya kusokota nyuzi.Kamati ya PIC tulikwenda Ubungo, eti hata nyuzi tunaagizakutoka China. Tulikuwa na viwanda vya kusokota nyuziTanzania, pamba inatoka Mwanza na Shinyanga. Wenzetu,ndugu zetu, watani zangu Wasukuma wanalima pamba, ilepamba inabidi ipelekwe nje ikatengenezwe nyuzi tuleteweTanzania wakati tulikuwa na viwanda vya nyuzi, tulikuwana Kiwanda cha Mwatex na Kiwanda cha Kilitex. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, yeye nimbuzi wa kafara, haya mambo ameyakuta. Naomba timunzima ya Mawaziri irudi ikakae ituambie viwanda hivi vikowapi, vinafanya nini? Tupate database, nani wamechukuana kwa nini wanatuletea crisis ya mambo ya viwanda?Haiwezekani kila siku tunachukua khanga mbovu kutoka nje,madira mabovu kutoka nje, wakati Tanzania tulikuwatunatoa khanga nzuri; Kenya na Uganda soko kubwa lilikuwaTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitaki kusema sana lakininajiuliza, kulikoni Tanzania? Tumekuwa katika zigizaga, nendambele rudi nyuma, nenda mbele rudi nyuma. Viwanda hivikwanza vingefanya kazi, basi hivyo vingine vingekuwa vyaziada kwa vile tayari ajira na uchumi ungekuwa mkubwa,lakini vile viwanda vikubwa vyote vimefungwa, kwa nini?Nani amevifunga, ni hao hao wafanyabiashara. Natakautakapokuja kesho, uniorodheshee majina yote ya

Page 332: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

332

waliochukua viwanda na mpaka leo wamevifungia. Kwanini wamevifungia na kwa nini nguo hazitengenezwiTanzania? Kwa nini nyuzi hatusokoti Tanzania? Kwa ninikorosho tunapeleka nje, tunaletewa tena zile zile hapaTanzania? Kwa nini ufuta mnapeleka nje na tunakosa mafutaTanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina mengine ya kusema,nataka jibu hilo kesho. Ahsanteni sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Riziki.Tunaendelea na Mheshimiwa Salome Makamba baadayeMheshimiwa Munira Mustafa.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi nichangie hotuba yaMheshimiwa Waziri wa Viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekaa najiuliza swalimoja, hivi hii Serikali ya Awamu ya Tano ndiyo Tanzania yaViwanda au ilikuwa ni Serikali ya Awamu ya Nne? Kwasababu kinachofanyika sasa hivi, mwaka 2014/2015 katikabajeti ambayo Waheshimiwa Wabunge wenzetu walikuwepohumu waliipitisha, asilimia 82 ya bajeti ilipelekwa kwenyeviwanda na vikaboreshwa. Leo 2015/2016 bajeti ya shilingibilioni 35.3 tumepeleka shilingi bilioni 1.6 sawa na asilimia 5.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiacha hiyo, mwaka 2016/2017 tumepeleka 8% ya bajeti nzima. Mwaka 2018 mpakaMachi, taarifa tuliyopewa kwenye Kamati tumepelekaasilimia 9.4 tu yaani hakuna mwaka ambao tumepelekaangalau asilimia 50 ya bajeti ya viwanda halafu tunajinasibukwamba tunaenda kwenye Serikali ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala linanipa wasiwasina ndiyo maana ukiona mtu anajitetea sana, ujue kunamaovu nyuma yake. Ndiyo maana ukiangalia viongozimbalimbali wa Serikali wana matamko tofauti tofauti juu yani viwanda vingapi vimeanzishwa Tanzania mpaka leo hii?

Page 333: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

333

Mkuu wa nchi anasema tumeanzisha viwanda zaidi ya 3,060,Waziri kwenye hotuba yake anasema kwamba ameanzishaviwanda 1,287, kitabu cha Mapendekezo ya Mpangowanasema viwanda viko 50. Kila mtu anaongea statementyake, Serikali moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima ujichanganye kwasababu Watanzania tumewaaminisha tunakwenda kwenyeuchumi wa viwanda. Laiti kama Watanzania wangegunduakwamba viwanda wanavyoahidiwa kwenye kampeni ni vyakutengeza juisi, zile blender, ni viwanda vya cherehani, sijuikama leo tungekuwa tunaongea haya maneno. Leotumebadilishiliwa story tunaambia kwamba viwanda ni ainayoyote, vya kati na vidogo. Sawa, basi hivyo viwanda vidogo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kwenye ripoti yaCAG, SIDO wanaweza kutoa mikopo kwa asilimia 40 tu yapesa ambazo walikuwa wame-propose kwamba wanatoamikopo. Watu wanaoahidiwa watapewa mikopo kwa SIDOndio hao wenye viwanda vya kati na viwanda vidogo lakinipesa hawapelekewi. Mheshimiwa Waziri anajitapa hapaameanzisha viwanda vipya. Jamani, wengi hapa sisi ni wazazi.Hivi kweli mtoto wako hata kama una watoto wengi kiasi gani,mtoto wako mmoja akifa kwa kifo ambacho umesababishawewe mwenyewe mzazi utajisikiaje? Viwanda vinakufavidogo na vya kati, pesa hatupeleki halafu tunajinasibukwamba tunatengeneza Serikali ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika bajeti yamwaka 2018, hiyo 8% ninayosema imepelekwa siyo fedha zandani, ni fedha za wafadhili, fedha ambazo tunapewa nawatu wengine. Uangalie seriousness ya Serikali katika kukuzauchumi wa viwanda, wewe mwenyewe utaona kunachangamoto kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme, ili viwandaviweze kukua, Mheshimiwa Waziri atakubaliana namikwamba lazima tukuze malighafi, lazima tuhakikishetunaboresha pamba, tumbaku na barabara. Shinyanga ni

Page 334: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

334

wakulima wakubwa wa pamba. Sisi mpaka sasa hivi tuna-export pamba tani 700,000. Yes, tunauza marobota 700,000lakini tuna-import marobota ya nguo 2,000,000 kuletaTanzania. Mbona tunafanya biashara kichaa? Kwa nini Serikaliisiwekeze kwenye malighafi ili kukuza viwanda?

Mheshimiwa Mwenyekiti, namweleza MheshimiwaWaziri, hivyo viwanda anavyovitaja kwenye kitabu chakewanampigia makofi, anapiga nao picha, anatuma kwenyemitandao, hao watu wanamwangalia waone yeye anacommitment gani kukuza viwanda? Wale watuwamewekeza Tanzania lakini Waziri unathubutu kukaa naWizara ya Uchukuzi, Wizara ya Miundombinu na Wizara yaKilimo kuangalia utarahisisha vipi uzalishaji kwenye hiviviwanda? Au tunafanya majaribio ya kusema tumeletaviwanda na baada ya miaka mitano viwanda vimeshindwakufanya kazi au viwanda vyote vimefungwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi viwandaanavyotuaminisha leo Mheshimiwa Waziri, hebu jiulize swali,vinaajiri Watanzania wangapi? Juzi nimesikia MheshimiwaWaziri anasema kwamba cherehani tano ni kiwanda.Mheshimiwa Waziri tusifanye mchezo na Watanzania,wanatutegemea sisi Wabunge na Serikali kuamua hatimaya maisha yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda kwanguKahama, Shinyanga na Mikoa ambayo kimsingi ilikuwaimekaa strategic kibiashara, nikikueleza tangu Serikali yenuimeingia madarakani, zaidi ya asilimia 70 ya wafanyabiasharawaliokuwa wanamiliki maduka na biasharawameshapokonywa mali zao na Serikali. Watu wana mikopoMheshimiwa Waziri. Wewe unachekelea kuleta viwandavipya, una mkakati gani kuhakikisha viwanda ambavyovilikuwepo ambavyo kimsingi vilikuwa vinalipa kodi navinaendesha Serikali unavi-maintain? Una mkakati gani wakuhakikisha hawa watu pamoja na kutusaidia kuendeshaSerikali, wanaendelea kuwepo kwenye circular ya uchumi?(Makofi)

Page 335: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

335

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwa nakaa namfikiriaMheshimiwa Waziri, sijui anaposema kwamba tuna viwanda3,000 anakuwa ana-project nini? Kwa sababu kama mwishowa siku Shinyanga pale kuna Kiwanda cha Nyama hakinauwezo wa kuajiri hata watu 2,000. Shinyanga leo maji nabarabara ni changamoto, ng’ombe ndiyo kwanzammekazana kupiga chapa mnakusanya ushuru wa Sh.5,000,umeme ndiyo kabisa, labda wanunue na power bank palekwenye kile kiwanda, hali ni mbaya, lakini Mheshimiwa Wazirianajinasibu anasema viwanda vinaendelea, tunafanya vizuri,tunafanya vizuri wapi? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka commitment yaSerikali, tutafanyaje kuhakikisha wawekezaji wa kati nawadogo ambao ni wafanyabiashara kwa Tanzania hii nandiyo walezi wa Tanzania hii, wanarudi kwenye hali yao yakiuchumi kuweza kuendesha nchi hii? Nataka commitmentya Serikali juu ya huu utaratibu wenu, mtu akiamka asubuhi,TRA inapanga leo tunatoza kodi kiasi hiki, kesho asubuhiwanasema kiasi hiki, nini commitment ya Serikali? Watuwanafunga biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoaleo, huyo huyo ambaye ni sehemu ya Serikali, anasemamnaofunga maduka, fungueni, njooni mezani tuzungumze,tunaweza tuka-negotiate bei ya kulipa kodi TRA.

TAARIFA

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimpe taarifa Mheshimiwa SalomeMakamba, kwa bahati njema amegusa sekta ya mifugo naamekitaja Kiwanda cha Nyama cha Shinyanga.

Page 336: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

336

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilitaarifu Bungetu kwamba Kiwanda cha Shinyanga Serikali imeshachukuahatua, tena hatua nzuri sana. Kiwanda hicho kilikuwakinamilikiwa na Triple S tumesharudisha na hivi sasamchakato wa kuhakikisha kwamba kiwanda kinatangazwaili kiweze kupata mbia wa kuhakikisha kwamba kinafanyakazi na kuleta tija katika sekta ya mifugo unaendelea.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nalotaka kumwambiani kwamba hakuna ng’ombe aliyepigwa chapa kwa bei yaSh.5,000 katika nchi hii. Mwongozo ni Sh.500 na almost nchinzima ng’ombe wote wamepigwa chapa kwa Sh.500 kwaajili ya kuleta tija katika sekta hii ya mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Salome, taarifa hiyo.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimshauri Mheshimiwa Waziri, halafu naomba kitukimoja, tukiwa tunawashauri muwe mnatusikiliza kwasababu Tanzania nzima haiwezi kuja hapa kuongea, sisi niWawakilishi wa wananchi. Tena kwa taarifa yako, kule kijijininjoo kwangu watu wanapiga chapa ng’ombe mpakaSh.7,000 siyo Sh.5,000, ninyi mmekaa hapa sisi tunatoka kwawananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuhusu suala la kiwanda,mimi kwa uelewa wangu, kwa mujibu wa Sheria ya UwekezajiTanzania, anapokuja kuwekeza Tanzania anapewa kitu kinatax incentive. Akipewa incentive, maana yake kwa kipindicha muda fulani yule mwekezaji hatalipa kodi mpakaambapo ule muda wa incentive uwe umeisha. Kama hiyohaitoshi, kuna kitu kinaitwa operational cost, yule mwekezajiyuko pale hana miaka miwili, amekuwa anafanya operationpale na halipi kodi kwa sababu anasema costs zake zauzalishaji hazijalipwa. (Makofi)

Page 337: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

337

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Serikali wanatujia hapana mazingaombwe eti wanatafuta mbia mpya, what aboutthe incentive? Vipi kuhusu ile tax holiday mliowapa walewawekezaji? Jamani nyie si mnajisema kwamba ninyi niWataalam, ni wataalam wa nini basi? Tusifanye siasa kwenyemaisha ya Watanzania. Siasa hizi zitakuja kutuadhibu,makaburi yetu yatapigwa fimbo na wajukuu zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusijifiche nyuma kwakusema kwamba Serikali inatafuta mbia. Mheshimiwa Wazirihata standard gauge miujiza hii hii ilifanyika. Tumeachamkopo wenye riba ya asilimia 1.2 tumeenda kuchukuamkopo wenye asilimia 4. Unakaa unasema umekaa nawataalam wanakokotoa mimi sijui mahesabu au biashara,lakini kwa uelewa wangu tu wa kawaida, siwezi kufanyabiashara ya namna hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali iwasaidieWatanzania, itengeneze miradi. Wakae pamoja, naaminiBalaza la Mawaziri ni moja, wamsaidie Mheshimiwa Waziriwa Viwanda na Biashara tutengeneze miundombinu kwa ajilikusafirisha malighafi na tuboreshe zao la pamba. Zaidi yaWatanzania milioni 16 wa Lake Zone wanalima pamba.Mheshimiwa Rais anasema hao ndiyo wapiga kura wake.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ki l imo chetutunategemea pamba. Hebu tuboreshe zao la pamba ilituweze kufungua viwanda vya nguo na kufungua viwandavya mafuta. Leo kelele za mafuta zisingekuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nikitembea tukidogo kilometa moja kutoka nyumbani, naona maua yapamba yametanda kila mahali, leo tuko busy tunanunuandege, tunajenga flyover, Tanzania siyo Dar es Salaam,Tanzania ina Mikoa zaidi ya ishirini na kitu. Tanzania siyo Dares Salaam. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

Page 338: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

338

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa. Tunaendeleana Mheshimiwa Munira Mustafa na Mheshimiwa JosephMusukuma ajiandae. (Makofi)

MHE. MUNIRA M. KHATIB: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami nashukuru kwa kupata nafasi kuchangia jioni hii ya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongezaMheshimiwa Waziri, Naibu Waziri wake na timu yake yote,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu kwa hotuba nzuri yaViwanda, Biashara na Uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali kwakauli yake ya kusema sasa suala la mafuta ndani ya nchiyetu siyo tatizo. Naipongeza sana Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais alipokuwakatika ufunguzi wa Kiwanda cha Singida alisema kuwaviwanda vya kuzalisha mafuta anaondoa VAT kwa asilimia18. Naomba Serikali iniambie, imetekeleza vipi agizo hili laMheshimiwa Rais kwa kuondoa VAT katika mafuta ya alizeti?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli tunataka tufikiekatika uchumi wa viwanda basi la kwanza ni kuvilindaviwanda vyetu vya ndani. Siyo viwanda vya mafuta tu, hataviwanda vyetu vya maziwa, tunaiomba Serikali iwezekuangalia suala hili ya VAT ya asilimia 18. Tutapoondoa asilimiahii 18, kwanza tutaweza kuongeza uzalishaji ndani ya nchiyetu, tutaweza kupunguza kuagiza mafuta ndani ya nchi yetu,tutaweza kuwasaidia wakulima wetu kimaisha ndani ya nchiyetu, hata pia tutaweza kuondoa tatizo la wafugaji kwenyenchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusuSIDO. Katika taarifa ya CAG, SIDO inaonekana iko katika halimbaya. SIDO inafanya vibaya ndani ya mikoa yetu naTanzania kwa ujumla. Mwaka 2017/2018 imepangiwa shilingibilioni 6 lakini ndani ya pesa hii haijapatikana hata asilimia1. (Makofi)

Page 339: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

339

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira nyingi za vijanazinapatikana katika viwanda vidogo vidogo. Kamatungeisaidia vizuri SIDO basi tungeweza kuzalisha ajira nyingikwa vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetembelea SIDO ya Iringaina wafanyakazi watatu tu ambao wameajiriwa na Serikali.Hivi tutafikiaje uchumi wa viwanda na tunawasaidiajevijana? Naiomba Serikali iangalie namna ya kuajiri watumishiwa SIDO ndani ya mikoa yetu na wazisaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SIDO ina wafanyakaziwatatu, waliobakia wote wanajitolea mpaka Mnunuzi Mkuuna Mhasibu ndani ya SIDO wanajitolea, hizi kazizinaendeshwaje? Naiomba Serikali na Mheshimiwa Waziri ukohapo, uisaidie SIDO ili kuweza kufikia katika uchumi waviwanda. Kama hatuwezi kuzisaidia SIDO zetu, basihatutaweza kusaidia uchumi wa viwanda. Ndani ya SIDOkuna mashine za miaka 70 kabla mimi sijazaliwa ndizozinatumika mpaka leo. Naomba hizi pesa ambazozimetengwa kwa ajili ya SIDO, zifike na zitolewe kwa wakati.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hii FCC imekuwa tatizosana kwa wafanyabiashara. Wamekaa kwa ajili kupigapenalty tu. Naiomba Serikali wangekaa na hizi taasisiwakawapa wafanyabiashara elimu. Wakienda sehemu zakuchukua bidhaa wajue ni bidhaa gani ambazo zinatakiwaziingie ndani ya nchi yetu ili wasiwe wanachukua mzigoambapo kisa tu haukuandikwa Sumsung au haukuandikwaiPhone ukifika ndani ya Tanzania mzigo ule ikawa nikuharibiana biashara kwa kuchomeana moto. Tungekaatukafikiria, kuna wafanyabiashara mpaka wanaumwa,wengine wanakufa kwa sababu ya hii FCC. Namwombasana Mheshimiwa Waziri akae basi aangalie Watendaji wakeaweze kuwasaidia wafanyabiashara wengi. Juzi kontenanzima ya chupi imechomwa moto na FCC. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna viwandavimebinafsishwa ambavyo vilikuwa haviwezi kufanya kazi.

Page 340: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

340

Naiomba basi Serikali viwanda vile virudi katika mikono yaSerikali. Viko ambavyo havijabinafsishwa lakini vinamilikiwana sekta binafsi na zipo share za Serikali. Naiomba basi Serikaliikaangalie viwanda hivi ili viweze kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi niliuliza swali hapakuhusu Kiwanda cha Nguo cha Urafiki lakini sikupata majibuya kutosha na ndani ya kitabu cha Mheshimiwa Waziri sikuonamaelezo yoyote kuhusu kiwanda hiki. Naomba basi wakatianahitimisha aniambie suala hili la Kiwanda cha Urafikilimefikia wapi kuhusu zile shares ambazo tunazo na wenzetuwa China? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Kiwanda cha NyamaDar es Salaam, naomba Mheshimiwa Waziri akiwaanahitimisha pia aje aniambie. Pia kuna Kiwanda cha ZZKMbeya, kilikuwa kinatengeneza vifaa vya kilimo. NaombaMheshimiwa Waziri akija aniambie, kwa sababu mpaka sasahivi wakulima wetu kutumia majembe ya mkono wakati sisiwenyewe tulikuwa tuna kiwanda kikubwa tu na hakifanyikazi, itakuwa ni aibu. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja hapa aniambie kuhusu viwanda hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala hili la vinywajivikali ambapo Serikali inapoteza kodi nyingi. Vinywaji hivivikali vinakosa kodi kwa kubandika sticker bandia na hili sualakuna baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wameliongea naushahidi upo. Naomba basi Serikali iangalie inapotezamapato kiasi gani katika suala hili la kubandika hizi stickerbandia katika vinywaji vikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vinywaji vikali Serikaliingekuwa ina-charge ile spirit wakati inaingia hapa nchinibadala ya spirit ikiwa imeshatumika ndani ya vinywaji vikalindiyo inakuja kuchajiwa. Hizi spirit zinapoingia tu nchinizichajiwe. Kwa sababu hizi spirit zinachajiwa kwa kiwangokidogo tu zinazokwenda kwenye hospitalini na sehemunyingine lakini kiwango kikubwa kinatumika katika vinywajivikali. Kwa hiyo, Serikali ingekaa ikaangalia vizuri kwaupande wa spirit inapoingia nchini. Tusi-charge ndani ya

Page 341: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

341

vinywaji, bali tu-charge inapoingia tu ndani ya nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naungamkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Munira.Tunaendelea na Mheshimiwa Dkt. Chegeni baadayeMheshimiwa Oran Njeza.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niwezekuchangia katika hotuba hii ya bajeti ya Wizara ya Viwandana Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnyonge mnyongeni lakinihaki yake mpeni. Mheshimiwa Mwijage na Naibu wakewanafanya kazi nzuri sana. Naomba tukiri hilo kwambawanafanya kazi nzuri isipokuwa tu ni kwamba uwezeshwajiwa kufanya kazi ndiyo kuna matatizo. Hii nadhani sisi kamaBunge tufikie mahali tutafute namna ya kuweza kuwasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni mtambuka, inamambo mengi sana. Bila kusaidiwa na kuwezeshwa kufanyakazi, itakuwa ni hadithi. Ndiyo maana anajiita ni Mzee waSound, ni kweli anapiga sound tu, anazunguka huku na huku,anapiga sound. Nadhani tafsiri halisi ya Mheshimiwa Mwijagemimi ninavyofikiri ilikuwa ni kwamba kauli ya Watanzaniakatika uchumi wa viwanda iweze kushamiri. MheshimiwaMwijage, umefanya kazi nzuri, lakini bado kuna wingu kubwasana la tafsiri ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tufike mahali kama nchituweze kuwa na tafsiri pana na iliyo sahihi. Unaposemaviwanda, cherehani tano ni kiwanda, kwa baadhi ya watutunashindwa kukuelewa vizuri zaidi, kuna vitu vinaitwa factoryna industry, sasa ni lazima kuwe na utofauti wa namna hiyo.Tukitofautisha hivyo, tukisema kwamba tumekuwa naviwanda 3,000 na kitu Watanzania wataelewa ni kitu gani.Nadhani tamaa kubwa ya Watanzania ni kuona kwamba

Page 342: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

342

mnapozungumzia viwanda ni vya kati na vile vikubwa zaidiili viweze kuchochea zaidi katika kuleta uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii pamoja na yoteinayofanya, kuna vitu ambavyo ni lazima mvisimamie kwauhakika zaidi. Ni namna gani ya kumsaidia mwananchi huyuna hasa mkulima maana zaidi ya asilimia 75 ya Watanzaniani wakulima kuongeza thamani ya mazao yao, tukishafaulupale hiyo ndiyo Tanzania ya viwanda tunayoitaka. Bila hivyo,itakuwa tunaongea kama ngonjera tu. Haiwezekani leo hiitunazidi ku-import vitu kutoka nje ambavyo tunawezakuzalisha hapa nchini na tukapunguza kutumia fedha zetuza kigeni kununua bidhaa kutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusumkulima wa pamba. Mkulima wa Pamba ana matesomakubwa sana. Mwaka 2017 alilima pamba na akapata beinzuri ya Sh.1,200 ikamhamasisha kulima zaidi mwaka huu,lakini utaratibu uliopo mwaka huu unamvunja moyo mkulimawa pamba. Ni vema kuangalia namna ya kuwezakumsaidia, vivyo hivyo hata kwa wakulima wa mazaomengine, tuangalie namna ya kuweza kufufua vinu vyakuchambua pamba ambavyo vitaongeza thamani yamazao ya mkulima. Namna ya kuanza kuwa na viwandavya kuweza ku-process bidhaa ya mkulima kama ni pamba,tuweze kupata nguo hapa nchini. Bila ya kufanya hivyo,haiwezekani na lazima tuwe na sera ya kulinda viwandavyetu. Bila kulinda viwanda haitawezekana. Haiwezekanitunaacha soko letu, tunaingiza tu bidhaa kutoka nje bilakuangalia viwanda vya ndani. Bila ya kuwa na hiyo sera,hatutafanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba sanaMheshimiwa Mwijage pamoja na Wizara yako, hili jambomliangalie kwa makini, linamgusa Waziri wa Fedha. Lazimatuwe na sera za fedha na za kodi za makusudi kabisa zakulinda viwanda vya ndani. Kama ni kodi, basi tutoze kodikubwa kwa bidhaa kutoka nje na tufanye zero rating kwabidhaa za ndani. Tukifanya hivyo itasaidia kuchocheamkulima huyu aweze kunufaika.

Page 343: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

343

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii mkulima wa koroshoamepata bei nzuri, wamehamasika zaidi na koroshoinaendelea vizuri lakini mazao mengine yanaanguka. Mazaokama chai, kahawa, mbaazi na kadhalika, sina haja yakuyarudia sana, lakini leo hii Tanzania miaka 57 ya uhuru badotuna-import mafuta ya kula kutoka nje, hii ni aibu. Tufikemahali tuangalie namna gani nzuri zaidi ya kuwezeshakuzalisha bidhaa hapa hapa nchini ambazo zitasaidia kwakiwango kikubwa kuweza kupata uzalishaji wa kutosha.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, Wizarahii, Mheshimiwa Waziri acha tu kutembea mikoani, toka njekaone, fanya economic diplomacy. Zunguka, tembea,unganisha nchi hii na mataifa mengine ili biashara ziwezekwenda. Haiwezekani kuna maonyesho mbalimbali yakidunia, sijaona Waziri wa Viwanda na Biashara au Naibuwake nao wanafunga safari kwenda kuiunganisha Tanzaniana dunia nyingine. Bila kufanya hivyo hatutakwendatunapotaka. Mheshimiwa Waziri, wewe sio Waziri wa kwendakijijini kwangu, kwenye kata, wewe Wizara yako ni muhimusana. Tumwache Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI azungukena kata na vijiji lakini wewe zunguka nje, tafutia Tanzaniamasoko na namna ya kuiunganisha kibiashara. Kama huwezikushona suti, tukusaidie kutafuta suti nzuri uweze kuzunguka.(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namheshimu sanaMheshimiwa Mwijage kwa sababu anafahamu na upeowake ni mkubwa sana na toka amekuwa Waziri waViwanda na Biashara, tunaona anavyohangaika, sasa hiyosound ipige mpaka nje, isiishie hapa peke yake. MsaidieMheshimiwa Rais, kila siku anazungumza, ninyi wasaidizi wakemsipomsaidia itakuwa ni mbio ya mtu mmoja. Hawezi kupigangoma mwenyewe akacheza mwenyewe, lazima Mawazirimumsaidie Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani ifike mahaliWatanzania sasa tumsaidie Mheshimiwa Rais zaidi. Kila wakatiunaona anavyolia, anavyohangaika, ninyi mnasema kama

Page 344: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

344

mlivyoagizwa, sasa mjiongeze zaidi ya hapo. Nami naombasana kupitia hotuba hii ya bajeti, kwa kweli ningependa sanafungu la bajeti ya Wizara hii tuliongeze. Tufanye kila namnana Mheshimiwa Mpango najua wewe ndiyo unajaribukumgawa huyu sungura mdogo, lakini tuwe na prioritysectors na ministries kwamba tukiweka hela hapa itazaa nakusaidia Watanzania zaidi. Tufike mahali tufikirie zaidi, let’sthink big, tusifikirie kidogo kidogo, tufikirie zaidi kwamustakabali wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Wizara yaFedha, najua kuna changamoto kubwa sana za kimapato,lakini tujaribu kugawa resources kulingana na mahitaji halisiya kila Wizara. Wizara hii inatakiwa ipate fedha za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli ya Cotton to Clothlazima ndiyo iwe wimbo wa Mheshimiwa Mwijage wa sikuzote. Naomba katika sounds zake tutamuelewa tu kamakweli atatimiza azma hii. Hii inakuwa record yake kama Waziriambaye ameanzisha mbio za Cotton to Cloth. Naombasana viwanda vyetu hapa ndani tuzidi kuvil inda nawanaowekeza hapa ndani tuwasaidie, tuondoe urasimu wauwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TIC iwasaidie. Siku hizi hakunatax holiday, kuna tax incentives, lakini kuna conflicts. Mtuanakuwa na cheti cha TIC lakini watu wa TRA baadhi ya vituhawavikubali, tufike mahali tu-harmonize. Haiwezekanimwekezaji anakuja hapa anazungushwa. Tunapatawawekezaji wanakuja hapa Tanzania kupata kibali tu hapacha kujenga kiwanda au kufanya shughuli hapa,anazungushwa, wengine wanahama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona kuna watuwalikuja hapa tukawazungusha wakaenda nchi jirani,wameanzisha viwanda vikubwa vya magari na vingine.Naomba tuache urasimu. Kama tunataka tuisaidie nchi hiiMheshimiwa Mwijage, Mheshimiwa Waziri wa Fedha naMipango na wadau wengine wanaohusika tuondoe urasimukwa watu wanaokuja kuwekeza hapa Tanzania. Tukifanya

Page 345: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

345

hivyo, tutakuwa tumeisaidia nchi yetu kuweza kukuzauchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, Mikoa ya Kandaya Ziwa inategemea sana kilimo, uvuvi na mifugo. Sasawakulima wanalia, wavuvi wanalia na wafugaji wanalia. Sasanaomba tutoke kule, mtusaidie namna ya kufanyacoordination na hasa viwanda hivi viweze kufanikiwa zaidi.Tukifufua viwanda itasaidia kuweka ajira hata kwa vijana.Vijana wengi wako mtaani hawana kazi, tuwasaidie kupitiaviwanda. Naomba kuwe na sera mahsusi ya kuwawezeshaWatanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu South Africawalikuwa wana sera inayosema ‘Black EconomicEmpowerment’ na sisi Watanzania tuwe na TanzaniaEconomic Empowerment, tuwawezeshe Watanzania. Leo hiiMtanzania ukienda hata kukopa hela unaonekana kamanyanya chungu au pilipili hoho, unaonekana kama mtu waajabu tu. Naomba Watanzania wapewe nafasi. Kama mtuanawekeza, apewe nafasi kadri anavyoweza kuwekeza.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Watanzaniatuachane na mawazo ambayo ni ya kizamani, tuangaliedunia inavyokwenda sasa hivi. Wawekezajiwanabembelezwa, akishaondoka kuja kumpata inakuwa nitatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwakusema kwamba Mheshimiwa Mwijage kaza buti. Punguzamaneno kidogo tuone kazi zaidi na vitendo. Maana yaketukikutana mtaani hapo, unauliza unataka kiwanda? Kamaunacho mfukoni, Mheshimiwa Mwijage acha style za namnahiyo, hebu kuwa serious kidogo. Maneno yako yaakisi kileunakifanya, nina imani una wasaidizi wazuri kwenye Wizarayako, fanyeni kazi kama Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, naungamkono hoja. (Makofi)

Page 346: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

346

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. Chegeni.Tunaendelea nna Mheshimiwa Oran Njeza.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hotubaya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo ni Wizaramuhimu sana hasa kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwasababu ni Serikali ya viwanda na kwa ajili ya kukuza uchumiwa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwakumpongeza Waziri, Naibu Waziri na timu yake yote yawataalam pamoja na watu wote wanaomsaidia,wanafanya kazi vizuri sana. Ni kweli pamoja na kwambawatu wanasema labda Mheshimiwa Mwijage anaongea kwautani lakini kwa jinsi navyomwangalia nafikiri yupo seriousndiyo sababu hata Mheshimiwa Rais amemwamini kwakipindi chote hicho amebaki kuwa Waziri wa Viwanda naBiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa ambacho natakanichangie kwenye Wizara hii, naona tumejikita mno kwenyeviwanda, hatujaangalia biashara. Leo hii ukiniuliza hatamimi, masoko yako kwa nani? Yako kwa Wizara ya Viwandaau yako Kilimo au Mifugo au yako kwa nani, sijui. Wakulimawanahangaika na sehemu ya kuuza mazao yao. Ni nanimwenye jukumu hilo, hatuelewi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye kil imo,tumehangaika kuhusu mahindi hapa, aliyesulubiwa ni Waziriwa Kilimo. Nimezungumza kwa muda mrefu kuhusu paretohapa. Nilikuwa naongelea kupitia kwa Waziri wa Kilimo lakinileo hii nilipoangalia hotuba hii, nikakuta kuna chombo chiniya Wizara ya Viwanda na Biashara kinaitwa TANTRADE, kaziyake ni kutafuta masoko ya viwandani na mazao. Jiulizehumu ndani kama kweli hawa watu hizo kazi wanazifanyazaidi ya Maonyesho ya Sabasaba. Inabidi tusifumbianemacho, tunapata shida. (Makofi)

Page 347: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

347

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule kwangu nalima pareto.Nimeongelea kuhusu pareto mpaka Wizara imeamua iifutepareto kwenye mazao manne ya kimkakati Tanzania wakatipareto tunayolima Tanzania tunaongoza Afrika na ni ya piliduniani. Sasa uangalie ni kwa kiasi gani wakati mwinginetunafanya vitu vya ajabu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pareto tunayozalisha leo hiihaizidi tani 1,000 ndiyo tumejitahidi sana, lakini potential nikaribu tani zaidi ya 10,000, ndiyo inatakiwa duniani. Kwa ninihatufiki huko? Kwa sababu mnunuzi ni mmoja. Ni nanialitakiwa atutafutie wanunuzi? Ni huyu mtu anaitwaTANTRADE au Wizara ya Viwanda ba Biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachomwombaMheshimiwa Waziri aje na mkakati ni namna gani atusaidieTanzania kwa sababu potential tuliyonayo Tanzania ni kuwawazalishaji wakubwa wa pareto duniani. Leo hii paretotunaiuza mkulima anapata kwa bei kati ya Sh.2,300 mpakaSh.2,700 lakini ukipeleka sokoni moja kwa moja, walewanaonunua wanapata kati ya Sh.8,000 mpaka Sh.10,000na hiyo ni kwa vile ni biashara wanaotuchezea. Anayenunuana anayezalisha Tanzania ndiyo huyo huyo anayenunuaMarekani. Anapeleka Marekani kama crude, anakwendakuichakata kule na sisi Tanzania hatuonyeshwi kama ndiyotumeizalisha hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kiwanda kilianzishwaInyala kikajaribu kupeleka pareto nje, wale waliponunua nakuingia mkataba, wakatishiwa kwamba kwa sababumnanunua pareto kwa huyu mzalishaji mwingine kutokaTanzania, nasi ndiyo tumekamata zao la pareto duniani, basihatutawaletea tena pareto, kwa hiyo, wale watuwakaogopa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona kuna chombo chiniya Wizara hapa kinaitwa FCC kama sikosei na kazi zake, sijuikama haya wanayaona ya kwamba zao ambalotunaongoza Afrika, hata FCC sijui kama wanajua ni kiasi ganiwakulima wananyonywa? Mnunuzi ni mmoja, ame-dominate

Page 348: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

348

soko la pareto ndiyo giant duniani. Tukiendelea namna hiitutakuwa tunamsaidia vipi mkulima wa Tanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho nilitakanichangie kidogo ni kuhusu kufufua viwanda. Watuwameongelea kuhusu kufufua viwanda na MheshimiwaWaziri ametamka kuwa ana nia ya kufufua Kiwanda chaNyama kwa kutafuta mnunuzi wa Kiwanda cha Nyama chaTanganyika Packers kule Mbeya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu nimfahamisheMheshimiwa Waziri, tuna kiwanda ambacho kimejengwa naHalmashauri. Ni kiwanda cha thamani ya shilingi bilioni 2,kimejengwa kwa asilimia 90. Vifaa ya UNIDO vimeshawekwamle ndani na sasa hivi Halmashauri inaomba pesa kidogo tukama shilingi milioni 900 ili waweze kumalizia. Kiwanda hikini cha kisasa na ni kizuri kuliko hicho ambacho wanatakakufufua sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanganyika Packers ilijengwakabla ya mwaka 1970, yale mashamba sasa hiviyamezungukwa na jiji, yako mjini. Kuna ekari pale karibu 5,000ziko mjini na mjini huruhusiwi kufuga wala kulima zaidi yaekari tatu. Sasa unakuta Mheshimiwa Waziri naye anasimamaanasema tunatafuta mwekezaji kwa ajili ya TanganyikaPackers. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba muwe mna-coordinate. Halmashauri imeomba lile eneo wapewe nawao wametoa ekari 7,000 kwenye sehemu ambayo ndiyokuna ng’ombe wengi iwe kama holding ground, lakinitubakize kiwanda, kutoka pale ni kilomita 30. Wizara ya Ardhiwalishauja, Naibu Waziri wa Ardhi alikuja, Katibu Mkuu waArdhi alikuja, wote waka-recommend nami mwenyewenimeongea na Treasury Registrar akaona hilo ni wazo zuri ililile eneo sasa ambalo lilikuwa ni la Tanganyika Packerslibadilishane na hili eneo, Halmashauri iliendeleze hili eneokwa ajili ya kuupanga mji.

Page 349: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

349

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo hilo ni karibu kabisana Songwe International Airport. Sasa badala ya kutengamaeneo kwa ajili ya EPZ unataka wewe ukachungieng’ombe, nafikiri hivyo ni vitu ambavyo katika dunia ya leohavikubaliki. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nalisema hilo kwa makusudikwa vile hiki kiwanda ni kwa ajili ya soko la ndani na nje.Kiwanja cha ndege sasa hivi kimetengenezwa ili kiwezeshendege kubwa kutua Mbeya ziende moja kwa moja Ulaya,tuweze kupeleka nyama kutoka Mbeya kwenda Ulaya natupeleke maparachichi na kadhalika. Kwa hiyo, hatukataiKiwanda cha Nyama ila tunachosema ni mfumo ganituuchukue ambao unaendana na leo? Ile spirit ya 1970 huweziukaitumia hiyo hiyo mpaka leo ukawa unaimba humoBungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho napendakuchangia kidogo ni hii taasisi mpya ya inaitwa TanzaniaCommodity Exchange Market, ni nzuri mno na inaweza kuwamkombozi. Sasa ndiyo hivyo ambavyo nachanganyikiwakwamba, je, itakuwa chini ya nani; Wizara ya Viwanda,Wizara ya Fedha au labda Wizara ya Kilimo? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nalisema hilo kwa makusudi.Kilimo sasa hivi walikuwa wanahangaika jinsi ya kuuzakahawa. Unajaribu kuangalia, je, kuuza kahawa ni Wizaraya Kilimo, au ni Wizara ya Viwanda au ni TANTRADE? SasaWizara ya Kilimo badala ya kuboresha kilimo wanaanzakuhangaika na kutafuta masoko. Nafikiri tutapotezamwelekeo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hivi vitu tuvifanyekwa makini. Imarisha Tanzania Commodity Exchange, tuigeEthiopia, Nairobi wana soko la kuuza kahawa. Tanzaniatunauza kahawa kwa kilo 50 dola 150 wakati Nairobi ni katiya dola 350 mpaka 400 na Ethiopia ni zaidi hapo. Sasa angaliani kiasi gani uchumi wa nchi hii tunavyoupoteza kwakutokuwa na mipango mizuri? (Makofi)

Page 350: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

350

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba hiliwenzetu nao wakajipange vizuri. Zao la kahawa liingie mojakwa moja kwenye Tanzania Commodity Market Exchange.Kwa sababu gani TCB wao ni regulator, huwezi ukamfanyaregulator vilevile akawa ni muuzaji. Sisi wengine ni wakulimawa kahawa, unaona kabisa kuna watu pale wanajifanyawana mnada lakini wanaangalia kahawa ya leo ya Tanzaniatununue kwa shilingi ngapi? Tumenyonywa kiasi cha kutosha,naomba tubadilike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa Wakala waVipimo. Amezungumza Mheshimiwa Lwenge akafikiria labdaviazi vya kutoka Mporoto ambako ndiyo Jimboni kwangulabda kuna nafuu, sisi ndiyo kuna usumbufu mkubwa, hatulali.Magari yanakuwa yamebeba viazi, wakulima maskiniamekodi gari tani saba siyo ya mtu mmoja, hana hela,akiuza Dar es Salaam ndiyo apate nauli ya kumrudishiamwenye gari lakini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Njeza mudawetu umemalizika.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Waheshimiwa Wabunge,muda wetu kwa siku ya leo na shughuli zetu zimefikia mwisho.Nawashukuru wote ambao mmeweza kutoa michango yenukwa siku ya leo, Mwenyezi Mungu awabariki sana.

Kabla sijaahirisha shughuli za Bunge, nina tangazo laNaibu Waziri wa Elimu, Mheshimiwa Olenasha, jana jionialiacha simu yake aina ya Samsung Note 4 nyeupe. Kwa hiyo,

Page 351: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … M… · HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Hotuba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

351

anaomba yeyote ambaye ameiokota aweze kumrudishia.Pia anaomba watu wa camera waweze kumsaidia ku-trace.

Baada ya tangazo hilo, naahirisha shughuli za Bungehadi kesho tarehe 11 Mei, 2018 saa tatu kamili asubuhi.

(Saa 1.45 Usiku Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Ijumaa,tarehe11 Mei, 2018 Saa Tatu Asubuhi)