26
ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua hivyo, umehakikishia mtoto wako maendeleo mema katika jamii ya wa Akadiani, nawazungumzaji wa lugha ya kifaransa ya Nouveau-Brunswick, na zaidi ya ufahamu wake wa lugha zote mbili rasmi nchini Kanada. Kwa kuhuzuria(kufwata) shule kwa lugha ya Kifaransa, mtoto wako upata elimu bora na utamaduni kwa kifaransa, ndani na inje ya masomo. Mwongozo huu ni kutoa taarifa kuhusu shule za lugha ya Kifaransa na kutoa mashauri mbalimbali ambayo, tunatumaini, itasaidia ushirikiano wako katika jamii yako mpya. Usomi njema. - Wafanya kazi wa wilaya ya shule ya 01 NENO LA MKURUGENZI MKUU WA WILAYA YA SHULE YA 1 Katika Wilaya ya shule ya1, tunao furaha kuwapa na kuwa fundisha wanafunzi wetu mazingira yawazi yenye nia na heshima ya utafauti. Sisi tunaamini kwamba utapata nafasi yako katika shule ya wilaya ya1, na wewe utashiriki vema katika elimu ya mtoto wako. Ahadi yako ni muhimu kwa mafanikio yake. Sisi pia tunawa- karibisha kushiriki katika maisha ya shule kwa kutoa muda wako; kwa kufanya hivyo, unaweza kuungana na familia nyingine na hivyo utazoea bora mazingira yako mapya. Nina uhakika, mutaona kwamba Akadiani ni wafurahivu sana na mutakuwa na hamu ya kushirikiyana nawo kwa mwenendo wao nzuri ya kukaribisha jamii. Karibu katika wilaya ya shule ya 1! Mkurugenzi Mkuu – Diane Albert-Ouellette NENO LA MKURUGENZI MKUU WA KITUO CHA MAPOKEZI NA KUSIN- DIKIZA WAHAMIAJI WAZUNGUMZA (AU WASEMA) KIFARANSA KUSINI MASHARIKI MWA NOUVEAU-BRUNSWICK. Hamujambo wazazi, Kituo cha mapokezi na KUSINDIKIZA wahamiaji wazungumza kifaransa kusini mashariki mwa Nouveau-Bruns- wick (CAFI) ina furahi kuwapa mfuko Karibuni shuleni ! Tunawakaribisha kwa kutumia mfuko huu ili kuwasaidia kuelewa zaidi mfumo wa shule ya Kanada ambayo mtoto wako anaingia ndani. Tunawasihi kusoma mfuko huu wote marakwamara ikiwezekanavyo. CAFI ni shirika isiyo na faida, ambao lengo ni kuhakikisha muungano kamili wa wahamiaji wasema Kifaransa katika kusini mashariki mwa Nouveau-Brunswick. Tupo tayari kuwasikia, kama muko na ma hulizo, na kuwasindikiza kwa makao yenu mapya ndani ya kusini mashariki mwa Nouveau-Brunswick. Usomi njema. - Wafanya kazi wa CAFI. Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

  • Upload
    others

  • View
    25

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE

KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua hivyo, umehakikishia mtoto wako maendeleo mema katika jamii ya wa Akadiani, nawazungumzaji wa lugha ya kifaransa ya Nouveau-Brunswick, na zaidi ya ufahamu wake wa lugha zote mbili rasmi nchini Kanada.

Kwa kuhuzuria(kufwata) shule kwa lugha ya Kifaransa, mtoto wako upata elimu bora na utamaduni kwa kifaransa, ndani na inje ya masomo.

Mwongozo huu ni kutoa taarifa kuhusu shule za lugha ya Kifaransa na kutoa mashauri mbalimbali ambayo, tunatumaini, itasaidia ushirikiano wako katika jamii yako mpya. Usomi njema.

- Wafanya kazi wa wilaya ya shule ya 01

NENO LA MKURUGENZI MKUU WA WILAYA YA SHULE YA 1 Katika Wilaya ya shule ya1, tunao furaha kuwapa na kuwa fundisha wanafunzi wetu mazingira yawazi yenye nia na heshima ya utafauti. Sisi tunaamini kwamba utapata nafasi yako katika shule ya wilaya ya1, na wewe utashiriki vema katika elimu ya mtoto wako. Ahadi yako ni muhimu kwa mafanikio yake. Sisi pia tunawa-karibisha kushiriki katika maisha ya shule kwa kutoa muda wako; kwa kufanya hivyo, unaweza kuungana na familia nyingine na hivyo utazoea bora mazingira yako mapya. Nina uhakika, mutaona kwamba Akadiani ni wafurahivu sana na mutakuwa na hamu ya kushirikiyana nawo kwa mwenendo wao nzuri ya kukaribisha jamii.

Karibu katika wilaya ya shule ya 1!

Mkurugenzi Mkuu – Diane Albert-Ouellette

NENO LA MKURUGENZI MKUU WA KITUO CHA MAPOKEZI NA KUSIN-DIKIZA WAHAMIAJI WAZUNGUMZA (AU WASEMA) KIFARANSA KUSINI MASHARIKI MWA NOUVEAU-BRUNSWICK. Hamujambo wazazi,

Kituo cha mapokezi na KUSINDIKIZA wahamiaji wazungumza kifaransa kusini mashariki mwa Nouveau-Bruns-wick (CAFI) ina furahi kuwapa mfuko Karibuni shuleni ! Tunawakaribisha kwa kutumia mfuko huu ili kuwasaidia kuelewa zaidi mfumo wa shule ya Kanada ambayo mtoto wako anaingia ndani. Tunawasihi kusoma mfuko huu wote marakwamara ikiwezekanavyo. CAFI ni shirika isiyo na faida, ambao lengo ni kuhakikisha muungano kamili wa wahamiaji wasema Kifaransa katika kusini mashariki mwa Nouveau-Brunswick. Tupo tayari kuwasikia, kama muko na ma hulizo, na kuwasindikiza kwa makao yenu mapya ndani ya kusini mashariki mwa Nouveau-Brunswick.

Usomi njema.

- Wafanya kazi wa CAFI.

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

Page 2: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE

SHUKURANI Mwongozo huu umewezekana kwa njia ya ushirikiano kati ya Wilaya ya Shule ya 01 na Kituo cha Mapokezi na Kusindikiza Wahamiaji wazun-gumza kifaransa kusini mashariki mwa Nouveau-Brunswick (CAFI).

Tunawashukuru wazazi wahamiaji, wafanyakazi wa shule na washirika kwa utaalamu wao katika mfululizo wa mashauriano kwa mwaka 2009-2010. Mchango wenu ni utajiri sana kwa mwongozo huu. Kamati ya ushauri imekutana mara kwa mara ili kuzibitisha yaliyomo. Wajumbe wa kamati hii ni wafwatao:

• LaurédahAllogho-Mbungu,mwanafunzi aliyemaliza kwa shule L’Odyssée

• AwaNiangBa,mzazi muhamiaji, shule L’Odyssée

• AichaBenimmas,Profesa na Mtafiti katika chuo kikuu cha Moncton

• JeanCodjo,Mwalimu wa mapokezi, shule L’Odyssée.

• LynnDoucet-Vautour,Mkurugenzi msaidizi, shule L’Odyssée

• PaulineGaudet,Mshauri kwa mafundisho ya rasilimali, katika Wilaya ya Shule ya 01

• FrancineGaumont,MfunzwawakaziyajamiikatikaCAFI

• ClaudetteLavigne,Mkuu wa elimu katika Wilaya ya Shule ya 01

• Marie-NoelRoss,Mkurugenzi msaidizi katika shule Saint-Henri

• ChristianeRunumyi, Mwalimu wa mapokezi, shule Saint-Henri

• LucileTaillieu, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha mapokezi na kusindikiza wahamiaji wazungumza kifaransa kusini mashariki mwa Nouveau-Brunswick (CAFI)

Shukurani vilevile kwa MÈlanie Boudreau, Mshauri wa wahamiaji katika Wilaya ya Shule ya 01, kwa Isabelle Lavoie, Mkuu waushirikiano jamii-shule katika CAFI na Uraia na Uhamiaji Kanada (Citoyenneté et Immigration Canada) kwa ajili ya ushiriki wao katika mradi huo

Page 3: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

JUKUMU LA WILAYA YA SHULE YA 1Kila Wilaya ya shule ina Baraza ya Elimu la Wilaya (CED) inayo usika na:

• Kuweka mwelekeo na vipaumbele(priorités) vya wilaya ya shule.

• kuamua jinsi ya matumikizi ya utawala ya wilaya ya shule zinazo usika.

Baraza ya Elimu la Wilaya (CED) inajumuika na watu walio chaguliwa.

Shule inasaidiwa katika kazi zake na Baraza ya wazazi (CPAÉ). Kamati ya wazazi inaweza pia kufanyika kwa kusaidia mipango ya shule.

MISHENI ( AU KAZI) YA WILAYA YA SHULE YA 01Wilaya ya shule 01 inayo misheni ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wake kuwa na ujuzi wa lugha, hesabu, sayansi, kijamii na utamaduni, kuwawezesha kufikia uwezo wao kamili kama watu binafsi wakizungumza kifaransa na kuchangia kwa ufanisi katika jamii ya Akadiani na wazungumuza Kifaransa, na katika jamii ya karne ya 21.

KALENDA YA SHULEWanafunzi wanasoma tangu mwezi wa tisa (Septemba) mpaka mwezi wa sita (Juni), na mwaka wa masomo ina siku 195. Kalenda ya mwakaujao wa shule utolewa kwa wazazi mwezi wa sita (juni) ya kila mwaka. Inaonyesha tarehe za mwanzo na mwisho wa masomo. Shule zina fungwa siku zifuatayo:

• Siku ya mapumuziko (konje)/ Mapumuziko ya Noheli/ Mapumuziko ya mwezi wa tatu;

• Siku ya mkutano ya wazazi na walimu na na mazoea ya walimu;

• Siku ya matayarisho/ ya mkutano/AEFNB (Chama cha walimu wasema kifaransa wa Nouveau-Brunswick).

ELIMU KATIKA NOUVEAU-BRUNSWICK

Page 4: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

ELIMU KATIKA NOUVEAU-BRUNSWICK

Nchini Canada, elimu ni wajibu chini ya utawala wa jimbo. Katika jimbo la Nouveau-Brunswick, Wizara ya Elimu na Maendeleo ya utotoni (MÉDPE) ni jukumu lautoaji wa programu ya masomo. Kwa kuona kama jimbo hii ni ya pekee inchini Kanada, ambao utumia lugha mbili rasmi, Wizara imegawanywa katika sekta ya lugha mbili sambamba, lakini tofauti: sekta ya Kifaransa na sekta ya Kiingereza. Elimu ni lazima kwa vijana tangu umri wa miaka mitano (desemba 31) mpaka miaka 18 au mpaka kumaliza shule ya sekondari (mbele ya miaka 21).

Shule zimegawa katika ngazi mbili:

• Ya msingi: tangu shule ya awali (kipushi) mpaka darasa la 8

• Ya sekondari: tangu darasa la 9 mpaka darasa la 12.

WILAYA YA SHULE YA 01 Wilaya ya shule ya 01 nimoja kati ya Wilaya tano za kifaransa kwa jimbo la Nouveau-Brunswick. Kulingana na taswira ( au ramani) ifatayo hapa chini, eneo la Wilaya ya shule 01 inapatikana kusini kwa jimbo la Nouveau-Brunswick.

TASWIRA (RAMANI) YA WILAYA ZA KIFARANSA ZA N.-B.

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

WILAYA YA 03EDMUNDSTON

WILAYA YA 05CAMPBELLTON WILAYA YA 09

TRACADIE-SHEILA

WILAYA YA 11RICHIBOUCTOU

WILAYA YA 01DIEPPE

Wilaya ya shule 01 hutumika na shule 15 katika kanda (Région) sita: Oromocto, Moncton, Saint-Jean, Fredericton, Dieppe na Memramcook.

Page 5: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

KUJIANDIKISHA SHULENI (MASOMONI)

Mzazi au mlezi ndiye anaohusika na kuandikisha watoto shuleni. Kanda moja moja zina mashirika, kama CAIIMM, zinazoweza kukusaidia katika kazi hii 1. Kama unataka kuandikisha mtoto wako katika shule lingine, mbali na eneo lako, lazima kupata kibali ( au ruhusa ) kutoka kwa wilaya ya shule. Kama maombi yako inakubaliwa, utahusika mwenyewe kwa kusafirisha mtoto wako shuleni hii. Kwa kuandikisha mtoto wako shuleni, utaalikwa kukutana na mkuu wa shule2. Wakati wa mkutano huwo, mzazi au mlezi, ni lazima kuongozana na mwanafunzi na kuleta yafuatayo: • Ushahidiwachanjoyamtoto(kadiyaafya);

• Nakala(kopiaufotokopi)yawarakarasmiinayoelezastatiyamtotonaikionyeshatarehe ya kuzaliwa kwake;

• Nakala(kopiaufotokopi)zahatiyoyoteyamuhimukwamwanafunzi(ripotiyakadiaukartasiya alamayamasomo,pasipoti,chetichakuzaliwa,nk).

MAELEZO ZAIDIUnawezakutazamasiteinternetyaWilayayashuleya01kutoataarifazamawasilianokwaajiliyashule.Anuanini:www.choisirlesucces.ca

KUTEMBELEA SHULEKwaKuelewahalihalisiyamtotowako,shuleuandaaziara(kutembelea)yasikuchachekablayakuanzashule katika darasa. Ziara hii ya kuongozwa shuleni ina fanyika na wewe, mtoto wako, mkuu wa shule nafamiliazinginempyaziliofika.Niwakatiwenuwakuulizamaswalimbalimbalinakujuawafanyakaziwa shule.

1 kwakujuakituoaushirikayamapokeziyawahimiajiyaeneolako,tazamaorodayamashirikakuNYONGEZO«ANNEXE» ya muongozo huu.2 InawezekanakamaswalifulanifulanizinawezapatajibukwaMkurugenziMkuuyaWilayayashule01.

Page 6: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

KUJIANDIKISHA SHULENI (MASOMONI)

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

MCHANGO WA SHULEKwa kulipa gharama inazohusiana na kazi za utamaduni ao za elimu zinayotolewa wakati wa Mwaka,utaombwakulipakiasichafeza(pesa)wakati wakumuandikisha mtoto wako. Kiasi hiki wanawezakuombakatiya$30na$50kwamtoto,kulingana na kazi zilizopangwa. Kama hali yako ya kifeza siyo nzuri, unaweza kuongea na usimamizi wa shule yako.

UPANGAJI WA DARASA SHULENISikuchachekiishakumwandikishamtotoshuleni, mtotohuyuupimwaauuchunguzwakatika masomo moja moja. Mapimo haya yana lengo ya kuamua vema darasa (somo) gani mtoto wako anastahili kusoma ndani. Shule ufanya iwezekanavyo kwa kuweka mtoto wako kwa somolakekamili;nakuongeanamzazinamtoto, ili kuhakikisha ushirikiano bora kwa mwanafunzi. Nimuhimu,kwakiasiiwezekanavyo,kuleta kartasi ya alama ya masomo yashule ya zamani ya mtoto wako, hili shule ipate kuelewa maendeleo ya kielimu ya mtoto wako.

Page 7: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

PROGRAMU YA SHULE

ELIMU YA MSINGIKatika ngazi ya msingi, shule ya msingi inajumuisha na masomo upashwa kutolewa kwa wanafunzi kwa kukutana na mahitaji ya Wizara ya Elimu na ya Maendeleo ya utotoni ya N.-B. Elimu hizi za masomo ni: kifaransa, sayansi ya kibinaadamu, elimu sanaa (ni pamoja na sanaa macho na muziki), elimu ya binafsi na ya kijamii na elimu ya kimwili, hesabu, sayansi na teknolojia, na ESL au lugha ya kingereza kama lugha ya pili. Kumbuka kuwa katika eneo la Fredericton, Dieppe, na Memramcook, wanafunzi wanachukua masomo ya Kiingereza kama lugha ya pili tangu mwaka wa tano, wakati katika eneo la Oromocto, wanafunzi wanachukua kiingereza kutoka mwaka wa tatu, na katika eneo la Saint-Jean, bila shaka zinatolewa mwaka wa nne. Kama una maswali (maulizo) kuhusu mitaala au programu ya masomo, tazama site Internet ya Wizara ya Elimu na Maendeleo ya awali utotoni katika: www.gnb.ca/0000 au wasiliana(ongea) na shule ya mtoto wako.

Page 8: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

PROGRAMU YA SHULE

ELIMU YA SEKONDARI Shule ya sekondari ina jumla ya mikopo ya 30, tangu darasa la 10 mpaka darasa la 12, isipokuwa tu ni darasa la 9 lilipo mwaka wampito kati ya elimu ya msingi na sekondari. Kila somo ya masaa 93.5 mfululizo, tangu darasa la 10 mpaka darasa la 12, ni sawa kipindi cha mkopo moja ya kufundisha.

Mafunzo nyingi zinazotolewa kwa semestri moja ( masaa 93.5 = mkopo 1), zingine katika mwaka wa shule (masaa 187= mikopo 2).

Kupita bila shaka, mtoto wako lazima apate 55%.

Kwa kumaliza elimu ya sekondari ya jimbo, ni lazima kabisa mwanafunzi kupata mikopo isiyo chini ya 24, ikiwa ni pamoja na 17 kutoka Mafunzo zinazohitajika na serkali, na 7 kutoka Mafunzo mbalimbali ya mahitajizake pekee. Mafunzo zinazo hitajika na serkali ni:

KIFARANSA•Mikopo5zinazohitajikanaserkali •Kifaransa10231au10232(Somolamwaka=mikopo2) •Kifaransa10331*au10332(Somolamwaka=mikopo2) • Kifaransa10411au10412(Somolasemestri1=mkopo1)

*Mwanafunziambayeatapataalama85%auzaidikwamtihaniwajimboyakifaransa10331anaweza kubadirisha kifaransa 10411 na ingine somo la kifaransa ya mahitaji yake pekee.

LUGHA LA PILI NA LUGHA ZA KIGENI•Mikopo2zinazohitajikanaserkali•Kiingereza21211*au22211*(Somolasemestri1=mkopo1)•Kiingereza21311au22311(Somolasemestri1=mkopo1)

*Mwanafunziambayeamefikiangaziyajuuwakatiwamahojiano(maongezi)yalughayakiingereza21211 na ya Kiingereza 22211, anaweza kubadirisha kiingereza 21311 au 22311 na Kiingereza au na lugha ya kigeni fulani ya maitaji yake peke.

Page 9: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

HESABU•Mikopo3zinazohitajikanaserkali

•Hesabu30231*au30232*(Somolamwaka=mikopo2)•Hesabu30311au30312(Somolasemestri1=mkopo1)

SAYANSI NA TEKINOLOJIA•Mikopo3zinazohitajikanaserkali•Sayansiyaasili50211au50212(Somolasemestri1=mkopo1)•Somomojayatekinolojia(Somolasemestri1=mkopo1)•Mkopo1kwamahitajiyamutubinafsikatikamafunzozifwatayo:biolojia53411/53412, fiziki51311/51312,kemistri52311/52312,sayansiyamazingira5441,astronomi55411 na sayansi ya asili 50312 (Somo la semestri 1= mkopo 1)

SAYANSI YA KIBINAADAMU• Mikopo2zinazohitajikanaserkali

•Hadisiyadunia42211au42212(Somolasemestri1=mkopo1)•HadisiyaKanada42311au42312(Somolasemestri1=mkopo1)

MALEZI YA MTU BINAFSI• Mikopo2zinazohitajikanaserkali

•Elimuyabinafsinayakijamii74211(Somolasemestri1=mkopo1)•Elimuyakimwili71211(Somolasemestri1=mkopo1)

Mtoto wako pia ana ruhusa ya kujiandikisha katika Mafunzo zingine za mahitaji zake binafsi .

Kama una maswali yoyote kuhusiana na uteuzi Mafunzo kwa mtoto wako, unaweza kuwasiliana na Mkuu au na mshauri wa uongozi katika shule yako.

Page 10: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

KULINGANISHA (AU ULINGANIFU WA) MIFUMO MBALIMBALI YA SHULEIli kuelewa zaidi mfumo wa shule ya Kanada, tazama kulinganisha na nchi mbalimbali.

1. Kwa N.-B., mtoto ukubaliwa kwanza masomo ya awali (kipushi) na miaka 5.2. ÉP - Shule baada ya sekondari (yunivasti, chuo kikuu au koleji, au taasisi au shule nyingine za baada ya sekondari).

NCHI

KANADA N.-B.1

(Wilaya ya shule)

MFUMO WA UFARANSA (Akademia)

UJERUMANI

UBELJIJI(Wilaya ya shule)

USWISI(Kanto)

UMRI WA CHINI

6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 ÉP2 ÉP

MSINGI SEKONDARI ÉP

CP CE1 CE2 CM1 CM2 6e 5e 4e 3e 2e 1ère T ÉP ÉP

MSINGI CHUO CHA SHULE LA SEKONDARI ÉP

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 ÉP2 ÉP

MSINGI ( Wakati mwingine SEKONDARI ÉP hadi darasa la 6) (Kuna njia nyingine)

1ère 2e 3e 4e 5e 6e 1ère 2e 3e 4e 5e 6e ÉP ÉP

MSINGI SEKONDARI ÉP

1ère 2e 3e 4e 5e 6e 1ère 2e 3e 1ère 2e 3e ÉP ÉP

MSINGI MPITO SHAHADA YA SHAHADA YA ÉP (AU KIANGO) (AU KIANGO) CHA PILI 1 CHA PILI 2

Page 11: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

SHULENI AU MASOMONI

VIFAA VYA SHULEKila mwaka, katika shule ya msingi, mtapewa orodha ya vifaa vya shule vyenyi mtoto wako atahitaji. Kuhusu shule za sekondari, walimu wanaarifu wanafunzi kuhusu vifaa muhimu, siku ya kwanza ya darasa. Maduka nyingi kubwa zinauuza vifaa hivyo. Ni muhimu kutambua jina la mtoto wako ku vifaa yake ya shule, sababu kama vinapotea, lazima virudishwe kwepesi. Unaweza kutambua vifaa hivyo, ukiandika na kalamu ya wino usiyozimika. Mwanzo wa kila mwaka wa masomo, mtoto wako atapokea vitabu vya shule. Kwa kua vitabu ni mali ya shule, wanafunzi wana vikopesha tu kwa mda wa masomo. Vitabu vinapashwa kurudi mwisho wa mwaka ku shule ya msingi, na mwisho wa somo fulani ku sekondari, bila kuharibika.

KAZI YA WAKATI WA MCHANA SHULENI NA KAZI YA BAADA YA SHULE, NJE YA SHULE.Wafanyakazi wa shule wanapanga kazi mbalimbali (michezo, ukumbi wa michezo, improvisation, nk) ya wakati wa mchana shuleni na ya baada ya shule, nje. Kazi hizi zina saidia mtoto wako kujenga ujuzi wake kwa furaha na kupata rafiki zake na za jamaa. Mtoto wako analazimishwa kueshimu kawaida ya shule yake. Shule inaweza kuomba pesa fulani ya kusaidia ku kazi hizo. Kama uko na magumu ya pesa, ni vema kuongea na wakubwa wa shule ya mtoto wako.

Kwa shule ya msingi, watakuomba kuhakikisha na barua kama una kubali mtoto wako kushiriki ku kazi moja kati ya yote shule inapanga. Kazi hii ikawa wakati wa masomo, shule ita safirisha watoto wanao shiriki. Kama kazi hii ifanyika baada ya ma saa ya shule, wewe mwenyewe uta safirisha mtoto wako.

Page 12: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

NGUO AU MAVAZI KANUNIMtoto wako anapashwa kufika shuleni akivaa nguo inayostahili, ya heshima, safi, kulingana na kanuni ya shule. Kuna wakati, watoto wa natoka nje ya darasa lao asubui, mchana kati na baada ya mchana kati. Kwa faida ya mtoto wako, ni vema avae mavazi inayostahili kwa wakati ule na sawa sawa na hali ya hewa.

• Mavazi ya majira ya baridi:Koti ya baridi, suruhali ya baridi, kofia ya baridi, «gants», kitambaa ya shingo, viatu ya baridi.

• Mavazi ya siku ya mvula:Koti ya kukinga mvua, mwavuli na viatu ya mvua.

• Mavazi ya siku ya jua kali:Nguo nyepesi ya kukinga mianga ya jua, kofia nyepesi na mafuta ya kujipakaa wakati wa jua. Kama mtoto wako hawezi kujipakaa mafuta mwenyewe, ni vema wazazi wam-pagae mbele ya kwenda shuleni.

• Mavazi ya siku ya elimu ya mwili:Mupira, kapitula, suruhali ya mchezo, viatu ya mchezo, na kwa vijana, kiondoa arufu.

Wanafunzi wote wanao nafasi ya kupanga mavazi yao. Wanafunzi wa shule la msingi, ni vema wawe na nguo ya ndani ya kubadirisha ya kuacha shuleni kila siku. Shule zimoja zina kabati ya wanafunzi kupanga nguo zao.

MAZINGIRA BILA ARUFU

Kuna watu hawataki arufu. Kanada haitaki arufu ya nama yote. Kwakufikia kwa lengo hiyo, ni vema kila mtoto awe msafi, hasitumie manukato, na atumikishe kiondoa arufu bila arufu kali.

MASHAURI Nivema kila mzazi kufuata hali ya hewa asubui kwenye redio ya mahali au kwenye tivi«Météomédia», kwa kumuvalisha mtoto wake vema. Environnement Canada inaweza pia kukupa hali ya hewa kwa njia ya simu.

•FrederictonnaOromocto: 451-6001

•Moncton,DieppenaMemramcook: 851-6610

•KandayaSaint-Jean: 636-4991

Ukawa na Internet, tazama site www.meteomedia.com au www.ec.gc.ca kwa fujua hali ya hewa.

SHULENI AU MASOMONI

Page 13: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

KAZI YA MASOMO NYUMBANI NA MAWASILIHANO KATI YA WAZAZI NASHULE

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

KAZI YA MASOMO NYUMBANIMtoto wako akitoka shuleni, inafaa ujiakikishe kama ameleta kazi ya masomo. Ni mapashwa yako mzazi au mlezi kujua kama mtoto anatimiza vema kazi ya masomo nyumbani.

MASHAURI KUHUSU KAZI YA MASOMO NYUMBANIIfwatayo ni mashauri kwa wakati ya kufanya kazi yamasomo nyumbani:

Matayarisho:Wakati wakufanya kazi ya masomo nyumbani, ni lazima mtoto wako kutia akili yake yote ku kazi hiyo. Inafaa akae kwenye chumba kimia na mwangaza. Kila siku, inafaa mtoto awe na zoezi ya kufanya kazi hiyo kwa wakati fulani. Vile vile, umupatiye vifaa vyote anayolazima (kalamu, kartasi, kamusi, nk).

MASHAURIServisi ya Internet na simu «SOS DEVOIRS» ina saidia wanafunzi wa shule za kifaransa, tangu darasa la 1 mpaka darasa la 12, kwa kazi zao za masomo nyumbani. Mtoto akipata magumu fulani kwa kazi yake, wewe ao yeye munaweza kupata msadaa ya mwalimu.Namaba za simu bila malipo: 1-800-627-0609Saa ya kazi: saa kumi na nusu mpaka saa ine ya usiku.website: www.sosdevoirs.org kujiandikisha ku Internet ni kwa lazimaCAIIMM inapana vile vile servisi ya usaidizi kwa kazi ya masomo nyumbani. Mashirika ingine ya mapokezi ya wahamiaji inaweza kupana servisi kama hiyo. Uwasilihane na shirika ya mahali unaishi kwa mafasiriyo mengi.

Page 14: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

Wakati ya kazi ya masomo nyumbaniWakati ya kufanya kazi ya masomo nyumbani, mtoto wako anaweza kuwa mwenyewe. Ni lazima kumfwata vizuri na kumusaidia kama anayo magumu.

Baada ya kazi ya masomo nyumbaniMtoto akiisha maliza kazi yake, mzazi au mlezi anamapashwa ya kuchungua kama yote imefanyika vema. Unaweza pia kumuuliza maswali fulani kwa kuhakikisha kama ameelewa somo lake. Hasipotimiza kazi yake, inafaa ujue sababu. Unaweza kuwasihiliana na mwalimu wake kutambua magumu ya mtoto.

CYUMBA YA KUSOMEA VITABU.Kila shule inayo cyumba ya kusomea vitabu. Mtoto anapashwa kuheshimu kanuni ya mahali hapo, sawa kimia na heshima kwa wengine. Anaweza vile vile kusoma vitabu vya lazima au kuazima vitabu kuhusu kazi ya masomo.

MAWASILIHANO KATIKA AJENDA YA MWANAFUNZIKila mwaka mtoto wako atapokea ajenda kwa kuandika matukio muhimu au kazi ya masomo. Ndani ya ajenda hii, kunapatikana vile vile mipango ya masaa yake ya siku na mashauri mengi kuhusu majifunzo yake.

MKUTANO YA MAFASIRIYOKila mwanzo ya mwaka ya masomo, shule zina alika wazazi kwa mkutano ya mafasiriyo. Niwakati kwa wazazi kukutana na walimu wote, kuelewa matumikio ya shule na programu ya elimu kwa mwaka.

INFORMATIONNi vema kufahamu kwamba kila siku ya tatu (jumatano), Masomo inamalizika, saa moja, mbele ya wakati nyumbani au mahali ya kuchunga watoto. Desturi hii inasaidia saana waongozi wa Wilaya ya shule pamoja na walimu na wakubwa ya masomo (watahalamu) kuweza kukutana na kupana mawazo au kuongozana, kwa matukio na mafanikio mema ya wanafunzi wote.

KAZI YA MASOMO NYUMBANI NA MAWASILIHANO KATI YA WAZAZI NASHULE

Page 15: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

MIKUTANO KATI YA WAZAZI NA WALIMUMara mbili kwa mwaka, utahalikwa kwa mukutano ya walimu na wazazi (Tarehe ziko ndani ya kalenda ya shule) kwa kuzungumzia maendeleo ya mtoto wako. Unaweza pia kuomba kukutana na mwalimu wakati yoyote, ikiwezekana. Mikutano hii itakusaidia kuelewa maendeleo ya mtoto wako. Nifaida kwako kukutana mara kwa mara na walimu na wakubwa ya shule kuhusu majifunzo ya mtoto wako.

KARTASI YA ALAMA YA MASOMOKwa shule ya msingi (kipushi mpaka darasa la 7), mtoto wako anapokea kartasi ya alama ya masomo mara tatu kwa mwaka. Kartasi hii inaeleza maendeleo ya mtoto, na kuonyesha magumu na nguvu zake. Alama inapewa wakitumia A, B, C au D.

Kwa shule la msingi ni kama ifwatayo:

A - YA JUU Mtoto amesikia vizuri saana vyote amefundishwa.

B - ILIVYOTARAJIWA AU Mtoto amesikia kyango ya kutosha ya vyote amefundishwa. ILIVYONGOJEWA

C - HAKI AU INAWEZA Mtoto amesikia vimoja kati ya mafundisho, lakini angali na KUBALIWA magumu fulani fulani hapa na hapa.

D - HAITOSHI Mtoto aelewe kitu na hawezi programu hii.

Shule itakupatia «Kartasi ya alama ya masomo kwa shule ya msingi» mwanzo wa mwaka yenyi kweleza mashauri mengi kuhusu namna ya kujikamata wakati mtoto analeta kartasi yake ya alama ya masomo.

Tangu darasa la 8, mtoto anapokea kartasi ya alama ya masomo yenyi kuwa na hesabu, mara inne kwa mwaka. Kartasi hiyo ina kuonesha alama zake kwa asilimia (%) kwa kila somo lake.

KAZI YA MASOMO NYUMBANI NA MAWASILIHANO KATI YA WAZAZI NASHULE

Page 16: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

USHIRIKI WA WAZAZINchini Kanada, shule zina unga mkono wazazi kwa kushiriki saana kwa maisha ya masomo ya watoto wao. Kwa njia hiyo, utapata marafiki, utasikia vizuri maisha ya mtoto wako shuleni, na unaweza pana mawazo yako kwa maendeleo ya shule. Kuna namna nyingi ya kushiriki kwa maisha ya masomo ya mtoto wako:

Unaweza kuijitolea(kutumika bila malipo) ukisaidia kukazi ya chumba ya vitabu, kuchunga watoto wakati wa burudani au michezo ya mapumuziko kidogo, kuwafundisha kusoma, nk. Wakubwa wa shule au mwalimu wa darasa la mtoto wako wanaweza kukupa mafasiriyo mingi kuhusu namna ya kujitolea shuleni.

Shule nyingi zina programu fulani fulani nje ya shule. Wazazi au walezi wana weza pia leta msaada wao kwa zile programu wakisindikiza watoto na walimu nje ya shule. Ukishiriki kwa kazi zote za shule ya mtoto wako, utapata faida nyingi kwa kupata marafiki, na kusaidia kwa maisha ya shule.

Wakati mzazi au mlezi anaunga mtoto mkono katika maisha yake ya shule, inamsaidia kutumika kazi za masomo na bidii na kupata alama nzuri shuleni. Kwa hiyo, masikilizano na ushirikiano kati ya wazazi, walezi, watoto, walimu, wakubwa wa shule na jamii lote la shule, ni njia ya maendeleo mema.

MASHAURI Tangu utoto, mtoto anapashua fahamu kwamba:• Siyovizurikuongeanawatuhasiyefahamu, bila mtu mzima wakuaminika kua karibu;

• Hasingiyendaniyagariyamtuasiyefahamu;

• Hasikulechakula(mkate,kitumbula,pipiau «bonbon», biskuti, nk. ) au kupokea zawadi kutoka kwa mtu hasiye fahamu.

Zaidi, ni lazima:• Kutembeakwakikundi,ikiwezekana;

• Kujuamajinayakeyote;

• Kujuanambayasimuyake;

• Kujuamajinayawazaziwake,babanamama au ya walezi wake;

• Kufahamunafasiyakwendawakatiwa shida za araka;

• Kujuanamba911wakatiwashidazaaraka.

Page 17: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

MWENENDO WA MWANAFUNZI Kila mwaka, mwalimu na wanafunzi wake wanaunda kanuni za darasa lao. Kutoheshimu hiyo kanuni inaweza kuleta matokeo fulani fulani kwa mtoto. Nchini Kanada na shuleni, heshima na kusitisha vurugu (ghasia au unyanyasaji) ni ya muhimu. Walimu wanakataza shuleni vitisho, ubaguzi, ukatili au unyama au vurugu yote ya mwili au ya akili. Mtoto wako akipata tatizo kamahii, ni vema azungumze na mwalimu wake au na wakubwa wa shule. .

PROGRAMU Le MaiLLon Wanafunzi wa darasa la 6 mpaka darasa la 12, ndiyo wanasaidiwa na programu Le Maillon. Mtoto mwenyi kuwa na magumu ya kipekee anasaidiwa na watu wa shule lake wakimpa mashauri. Kwa hiyo, kila mtoto anapokea kadi kidogo ya njano mwanzo wa mwaka. Akipata shida, mtoto anampatia mtu wa masiliano kadi hiyo. Mtoto wako akiwa na shida shuleni, ni vema, mbele ya yote, wewe na mtoto muzungumze kuhusu shida hiyo. Shida ika dumu, unaweza kuzungumza na mwalimu wa mtoto wako au mwalimu anaweza kukutuma ku servisi inayostahili.

HEWA BORA YA MAJIFUNZO

Kila shule iko na kanuni zake kwa lengo la kutia mazingira ya usalama na ya kujifunza vizuri. Unaweza kupata kanuni hizi katika ajenda ya mtoto wako.

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

MASHAURIMbele ya masomo kuanza, unaweza ongea na mtoto wako kuhusu mwenendo ya shuleni ukimfasiria, tabia inayostahili na hisiyostahili. Kwa mfano, unaweza kumweleza kama inakatazwa kukimbia ndani ya koridoro, kuonyesha mkono kwa kuomba ruhusa ya kwenda chooni, kusema na sauti kubwa shuleni, kusukuma na vurugu watoto wengine shuleni, nk.

Page 18: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

VITU HARAMU, MARUFUKU AU INAKATAZWA SHULENISimu ya mkono au vifaa vya umeme au elektronik ( kama vile: MP3, michezo ya video, nk.) inakatazwa shuleni.

Inakatazwa wanafunzi kunywa pombe au madawa ya kulevya shuleni, yahani shule ni mahali ya mazingira bila moshi. Mtu asivute ndani au nje ya kiwanja ya masomo. Mtoto hasiye heshimu hii kanuni anaweza fukuzwa kwa mda shuleni.

MAHUZURIO AU JUHUDI YA KUFIKA SHULENIKwa lengo la majifunzo mema ya mtoto wako, ni vema ashiriki kila siku kumasomo na kazi zote za darasa lake na ya shule. Mtoto hasipoenda shuleni, tuma simu shuleni kuwakumbusha ukipitia sekretariati.

Wilaya ya shule 01 inatia mkazo juu ya juhudi ya kufika shuleni, sababu ni moja kati ya njia bora ya maendeleo mema ya wanafunzi.

MTOTO WAKO AKIGONJWA SHULENIMtoto wako akigonjwa au akipata ajali au bahati mbaya shuleni, watakuita shuleni kwa namba yako ya simu yenyi kuwa nadani ya ajenda ya mtoto. Wewe au mtu anaeusika, muta ombwa kufika shuleni kuchukua mtoto wako. Ajali au hali ya mtoto ikawa mbaya saana, shule itapeleka araka mtoto hospitalini na gari ya wagonjwa, na mtuwakazi moja wa shule atakupasha habari. Pesa ya kulipa gari ya wagonjwa itatolewa na wazazi. Kwa hiyo, ukabadirisha namba ya simu au anuani yako, kumbusha sekretariati ya shule kwa araka.

HEWA BORA YA MAJIFUNZO

MASHAURIHii ni mfano ya ujumbe mfupi ya kutuma shuleni:

«Mimi (jina lako), mtoto wangu (jina la mtoto) ni mgonjwa na hakuna namna afike shuleni leo. Mwalimu wake (jina la mwalimu). Mumpashe habari hii. Asante.».

Shule moja moja inahitaji mtoto alete, siku yake ya kurudi shuleni, kartasi ya mafasiriyo kamili kuhusu kutofika kwake.

Kama mtoto atarudi nyumbani mbele ya masomo kumalizika, ni vema umupe kartasi kidogo ya mafasiryo kwa mwalimu wake. Kwa usalama ya wanafunzi wote, shule inapashwa kujua kama mtoto fulani hatafika shuleni siku fulani, sababu fulani. Kwa sababu hiyo, wanafunzi hawawezi kutoka shuleni bila ruhusa ya wazazi.

Page 19: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

CHAKULA

Mbele ya kwenda shuleni, ni lazima mtoto wako akule chakula kizuri cha asubui au kifungua kinywa, sawa mkate, sereali, matunda, maziwa au yuguru (Tazama maelezo ya ziada kuhusu Muongozo ya chakula ya Kanada). Unaweza pia kutia ndani ya sakoshi yake ya masomo chakula kidogo kidogo au «collation santé», ya kukula wakati ya mapumziko kidogo asubui ao nyuma ya saa sita.

CHAKULA YA SAA SITA AU YA MCHANA KATISaa sita, mtoto wako ataenda kwenyi Kafeteria ya shule kwa kukula. Kuna namna mbili ya kufanya:

• Anaweza kula chakula ya Kafeteria akilipa pesa kidogo kwani wana chakula mbalimabli;

• Anaweza pia kuleta chakula kilichotayarishwa nyumbani (Kibweta ya chakula).

KIBWETA YA CHAKULA YA MCHANA KATINi vizuri chakula ya mtoto wako iwekwe ndani ya kibweta ya chakula ya jyenyi kuwa safi, ya kufungwa vema na yenyi kusafishwa kila siku.

Kulingana na Muongozo ya chakula ya Kanada, ni lazima chakula ya mtoto wako iwe na aina inne ya chakula. Kwa mfano, sandwichi na matunda au «dessert» na kinywaji kama maziwa, maji ya matunda au maji. Unaweza tazama Muongozo ya chakula ya Kanada kwa lugha 12 ku site ya hafia ya Kanada www.hc-sc.gc.ca.

Shule zimoja ziko na jiko la mikrowave yenye itasaidia mtoto wako kuchamusha chakula yake. Wakubwa wa shule wanaweza kukueleza kama kunapo jiko hii.

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

Page 20: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

CHAKULA

KIBWETA YA CHAKULA YA SAA SITA, INAENDELEA Tazama mifano ya aina ya kibweta ya chakula ya saa sita:

Tazama mifano vile vile ya vyombo ya kubeba vizuri chakula:

MAPUMZIKO KIDOGO NA YA AFIAWanafunzi wapo uhuru wakati wa mapumziko kidogo na ya afia shuleni, kwa muda mufupi. Niwakati wake wa kuimarisha urafiki na kufurahi shuleni. Kila siku, wanachungwa wakati huu na mwalimu mmoja au mzazi wakujitolea bila malipo.

Baada ya wakati huu, kengele au filimbi ya sauti kubwa inapigwa, mtoto anapashwa kujielekeza ndani ya darasa lake. Mbele ya kuingia darasani, anapashwa kuvua viatu au mavazi yake ya inje.

MASHAURI Ifwatayo ni mashauri wakati wa kutayarisha chakula ya mtoto wako:

- Kwa kuweka hakiba, tengeneza orodha ya chakula ya kununua ukiangalia bei ya chini ku makatrasi unapokea kwa njia ya barua au posta toka wachuuzi;

- Usisahahu kutia vyombo ya kula (kanya, kijiko, kisu) ndani ya kibweta ya chakula ya mtoto wako;

- Pendelea zaidi matunda na mboga;

- Pendelea zaidi vilevile sereali: mkate ya ngano, mchele isiyo nyeupe, nk.

- Chakula cha kujenga (protéines) ni ya lazima kwa kukomaza watoto. Inapatikana mu nyama, na pia mbegu sawa maharagi;

- Usizoee chakula ya sukari nyingi sawa shokola, siyo nzuri kwa afia;

- Mtoto hasipelek kalanga (noix) na vyakula vya baharini (crustacés) shuleni, sababu watoto wamoja wako na «allergies». Kuna wakati inaweza waletea magumu saana. Shule ina orodha ya vifaa vya kuepuka.

Page 21: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

USAFIRI KWA SHULE

Mu N.-B., wizara ya elimu na ya maendeleo ya utoto (MÉDPE) inasafirisha wanafunzi shuleni, bila malipo, wakitumia otobisi au basi, kwa shurti zifwatayo: wanafunzi wanapashwa:

• Kuhishindaniyaeneoyashulelao,karibuna:

- km 1 na shule, kwa wale wa masomo ya kipushi na ya musingi mpaka darasa la 2;

- km 1 na nusu, kwa wale wa darasa la 3 mpaka darasa la 12;

• KuhishindaniyaeneoambayoWilayayashule imetambua kama haina usalama;

• Kuwanamaitajiyakipekee(Mfano:kitiyagurudumu aukitiyakutembea).KartasiyaMganganiyalazma.

UMBALI YA KUTEMBEAMtoto wako anapashwa kutembea na miguu kama umbali wakutembea tangu nyumbani na mahali ya kukamata otobisi au basi haipite:

• Mita300,kwawanafunziwadarasalakipushimpakadarasala5;• Mita500,kwawanafunziwadarasala6mpakadarasala12.

UENDESHAJI YA BASI YA SHULEKamamtotowakoanastahilikukamatabasiyashule,unalazimayakutambuavizurihabarihizi:mahaliaufasi ya basi kusimama, namba ya basi, na saa kamili ya kufika. Una weza kupata habari hizi ku site Internet yaWilayayashule01(www.district1.nbed.nb.ca)aukwanjiayasimuyashuleyamtotowako.Kilasiku,mtotowakoanapashwakufikakwafasiyakukamatabasidakika5mbeleyabasikufika.Mtotoakikosabasi yake, mzazi au mlezi anapashwa kumleta shuleni.

YA LAZMA AU YA MUHIMUDereva wa basi haruhusiwe kuacha mtoto mahali ingine isipokuwa tu nafasi ya ku kamata basi. Kwa usalama, mtu mzima anapashwa kuwa mahali ya mtoto kukamata basi, kila siku, kwa wanafunzi wa kipushi mpaka darasa la 2 la msingi, wakati ya kupanda na kushuka ndani ya basi.

Wakatiwakufikashuleniasubui,mtotoanapashwakuelekeakukiwanjayamapumzikokidogo(cour derécréation)yamasomo.Nihapoatasubirikengeleaufilimbiyakuruhusukuingiadarasani.Anaweza kufurahihapo,nawenginewatoto.Kwamtotowasekondari,anawezakuingiapalepaledarasanimwake.

Baada ya masomo, mtoto analazimishwa kwenda palepale ku basi yake, kwa kimia kwa usalama wake na wengine.

SHAURIKwakufahamu mahali ya kukamata basi na namba ya basi ya mtoto wako, tazama «Info-bus» mu site www.district1.nbed.nb.ca au tuma simu ku sekretariati ya shule ya mtoto wako.

Page 22: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

USAFIRI KWA SHULE

YA LAZMA AU YA MUHIMUKama unahama mahali ingine au kukawa mabadiriko ku ratiba(horaire) yako, ni vema ujulishe shule ya mtoto wako.

KANUNI ZA KUHESHIMU KWA USAFIRI KWA SHULEWakatiyausafirikwashuleyamtotowako,anapashwaheshimukanunizifwatayo:

• Kuheshimudereva.

• Kutosemanaderevawakatianatembezabasi,isipokuwakunakoshidayaharaka.

• Kuheshimuderevanawanafunziwengine.

• Kufikakwawakati,nakubakinjeyabarabaraakigonjeabasikufika.

• Kungojaruhusayaderevakwakutambukanjianakutambukaakitembeakumeta3mbeleyabasi. Hasitambuke nyuma ya basi.

• Kuachaumbaliyakutembeayausalamapembeniyabasi.

• Ndaniyabasi,kujielekezapalepalekukitichakenakukubalikushirikiaukugawakitinawengine. Yafaa kukaa ku kiti.

• Kukaanakuangaliambeleyabasi,nakutiasakoshiyakejuuyamagotiyakeauchiniyakitichake. Kuachanjiawazikatiyaviti.

• Kuombaruhusakwaderevambeleyakufunguadirishayabasiaumlangoyakutokakwaaraka.Kuto tupakitufulaniaukuachakitukinayembeleakudirishayabasi.

• Kusemakwasautikubwainakatazwa.Kamamukokaribuyanjiayagariyamoshi,kunyamazakabisa.

• Kutokulaaukunywandaniyabasi.

• Kuletavyombovikubwandaniyabasinimakosa.

• Kuvaanguosawanahaliyahewa.

• Nguonasakoshiisiwenamikabanyingi.

• Inakatazwakuvutasigarayeyote.

Kwa usalama ya mtoto wako , kuna vitu fulani vinakatazwa ndani ya basi, sawa vile:

1. «Plancheàroulettes»na«Plancheàneige»;

2. «Patinsàglace»au«Patinsàroulettes»wazi,bilakuwekwandaniyasakoshiyake;

3. Mpirayakuchezaisiyofunikwandaniyasakoshiyake;

4. Vifaayamchezo(FimboyaHockey,nk.);

5. Vifaavikubwayamuziki(gitari,tuba,nk.);

6. Michezoyakutupavituauinayowezakuachanaaukuungwa;

7. Vituyafujoyakuletamahuzikwadereva;

8. Kituchotekikubwasaanakinachowezafunganjiandaniyabasiauyakukamatafasikubwa;

9. Kitukiahatarikwausalamawawatoto.

Nyamazotezinakatazwandaniyabasi.Derevaanaruhusiwakukataakituchochotekisipostahilindaniyabasi.Kamanikitukinaombwashuleni,wazaziwanapashwakukipelekashuleniwenyewe.

Page 23: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

SHAURIKwa kuhangalia dokimenti kuhusu usafiri kwa shule, tazama site internet: http://www.gnb.ca/0000/transport-f.asp

ZARUBA YA MAJIRA YA BARIDINchiniKanada,majirayabaridinikalisaanamarakwamara.Kwahiyo,wanawezafunga shule,nabasiinawezakufikanyumayasaa.Funguaredioyakokwakupatahabarikuhusu mamboyote.Shuleikafungwa,mzaziaumlezianapashwakuchungamtotowakenyumbani siku hiyo.

SHAURI Tazama namba za simu na stasyo za redio zenyi unaweza kusikiliza wakati wa zaruba ya majira ya baridi, au wakati basi inachelewa. Taharifa utolewa tangu saa 12 ya asubui kwa stasyo za redio zifwatayo:

DIEppE, MEMRAMcooK NA MoNcToN

Wasema kifaransa

Radio-Canada(CBAF-FM)-88.5 Country89(CJSE-FM)-89.5 BOFM(CFBO-FM)-90.7 Choix99(CHOY-FM)-99.9

FREDERIcToN NA oRoMocTo

Wasema kifaransa

CJPN-FM-90.5 Radio-Canada(CBAF-FM)-102.3

SAINT-JEAN Wasema kifaransa

CHQC-FM-105.7

Taharifa imesalijiwa (enregistré) ina kujulisha hali ya shule kwa namba ifwatayo:

Dieppe, Memramcook na Moncton: 869-6751

Fredericton: 453-4239

oromocto: 357-4298

Saint-Jean: 643-2003

Wasema kiingereza K945(CKCW-FM)-94.5 XL96(CJXL-FM)-96.9 C103(CJMO-FM)-103.1MAXFM(CFQM-FM)-103.9

Wasema kiingereza KHJ(CKHJ)-1260AMFredericton, 95.1FMNewMarylandna 103.5FMOromocto Fox105FM(CFXY-FM)-105.3 CapitalFM(CIBX-FM)-106.9

Wasema kiingereza 98.9BIGJOHNFM(CJYC-FM)-98.9 K100(CIOK-FM)-100.5

Page 24: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

SERVISI YA HUDUMA AU YA KUcHUNGA MToToKufwatananasheriayaKanada,watotowaumriyamyaka 12 na zaidi wanaweza kubaki peke yao nyumbani, kiisha masomo.Kuachamtotowamyaka11nachinipekeyake nyumbani,inakatazwakabisa.Kiishamasomo,nivemakumuachamtotowakowamyaka11aochini,kuulinziyamtumzimaaukijanawamyaka12nazaidi.

Kunaservisiyahuduma,kiishamasomo,mahalimengindani yajiji.Kwakutiamtotowakokwaservisihii,watakuombapesa.ServisihiiniyakipekeenahainauhusianowotenaWilayayashule01,lakiniinaruhusiwanaserkali.

Page 25: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

Centre d’accueil et d’accompagnement francophone des immigrants du Sud-Est du Nouveau-Brunswick

NYONGEZO

KAMUSI NDOGO YA KANADA

MANENO MAANA NCHINI KANADA

Kibweta ya chakula ya mchana Ni kibweta ya chakula. Ni chakula ya baridi, ina fungwa vizuri, inaweza chamushwa au hapana, ya mtu moja. Kama mtoto wako hawezi kununua chakula shuleni, ni vema mzazi au mlezi amutayarishiy chakula hiki nyumbani.

Vyatu ya majira ya baridi Ni vyatu ya mrefu inayo funga miguu vizuri wakati wa baridi. Ni ya lazima kama mtu yeyote anatoka nje ya nyumba wakati huo.

Chuma ya kukamatisha makartasi Ni «agrafeuse» au chuma ya kukamatisha makartasi pamoja, yakipangwa vizuri.

Kartasi ya alama ya masomo Ni kartasi ianyofasiria vizuri maendeleo ya mtoto wako shuleni.

(Covoiturage) Wazazi wamoja wanafanya «covoiturage», wakati wa kazi fulani fulani ndani au nje ya shule. Covoiturage ni wakati watu wengi wa naenda ndani ya gari moja pamoja kwa kwenda mahali moja. Kuna weza kuwa mzuguuko wa kwanza, wa pili, nk. Na vile vile, ma dereva wawili au zaidi.

Suruali Nchini Kanada, «Culotte» ni «Pantalon» au suruali.

Kifungua kinywa au Nchini Kanada, «Déjeuner» ni «Petit déjeuner» au chakula cha asubui. chakula cha asubui.

Chakula cha mchana kati. Nchini Kanada, «Diner» ni «Déjeuner» au chakula cha saa sita au mchana kati.

Chakula cha moto. Ni chakula mtoto wako anaweza kula ku kafeteriati ya shule kwa bei kidogo, saa sita, na inatayarishwa na watumishi wa shule.

Nguo au Mavazi ya «gym» Ni nguo mtoto wako atavaa wakati ya elimu ya mwili. Mavazi hii inapashwa kuwa nyepesi na hisiwe na kivukutu nyingi. (Mfano: T-shirt na kapitula, nk.).

au chakula cha saa sita. (Lunch) Kwa masemi ya kawaida, neno hii ya kiingereza ni chakula ya saa sita.

UJUMBE Ni ujumbe uliyo andikwa na mtuwakazi moja wa shule kwa kukupa habari fulani kuhusu mtoto au masomo. Na wewe pia unaweza kuandikia mwalimu wa mtoto wako ujumbe fulani wakati yeyote unapenda.

(Mitaines) Nchini Kanada, «Mitaines» ni «Gants» ya kufunika mikono wakati wa majira ya baridi.

Mkutano wazazi na walimu. Mkutano ya wazazi na walimu inafanyika mara mbili kwa mwaka. Ni wakati mzazi atafasiriwa vizuri maendeleo ya mtoto wake shuleni.

(Souper) Ni chakula ya «Diner». Ni chakula ya mangaribi sawa saa 12 ya mangaribi.

Kofia ndogo «Tuque» ni «Bonnet», ni kofia ndogo ya wakati wa majira ya baridi, ya pamba safi na yenyi kuwa na sanamu.

Eneo ya shule Ni eneo yenyi kupatikana shule fulani.

Page 26: ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE · ELIMU KWA KIFARANSA : UCHAGUZI WA BAADAYE KARIBU! Umemwandikisha mtoto wako katika moja ya masomo ya wilaya ya shule ya 1. Kwa kuamua

MASHIRIKA YA KUPOKEA WAHAMIAJI

FREDERICTON• JamiiyautamadunimbalimabliyaFredericton 123 York Street, Suite 201 Fredericton(N.-B.)E3B3N6 Téléphone:(506)454-8292 [email protected]

• JamiiyautamaduniyamuhunganoyawasemakifransayaFredericton 715, rue Priestman Fredericton(N.-B.)E3B5W7 [email protected]

GRAND MONCTON• Kituochamapokezi na ushirikiano ya wa hamiaji katika Moncton kubwa 319,rueSaint-George Moncton, N.-B. E1C1W8 Téléphone:(506)382-7494 www.caiimm.org

• JamiiyautamadunimbalimbalikatikaMonctonkubwa 150, rue Queen Moncton, N.-B. E1C1K8 Téléphone:(506)858-9659 [email protected]

SAINT-JEAN• KituochamapokeziyautamadunimbalimbalinayawahamiajiyaSaint-Jean Case postale 20100 30, rue King Saint-Jean,N.-B. E2L5B2 Téléphone:(506)642-4242 www.sjmnr.ca

INGINE VYUNGO YA LAZIMATazama site Internet yenyi mafaa kwako:

Wilaya ya shule 01www.district1.nbed.nb.ca

Msaada kwa kazi ya masomo nyumbaniwww.sosdevoirs.org

Wizara ya elimu na maendeleo ya utotowww.gnb.ca/0000

Muhungano ya inchi ya ushauri ya shule ya wasema kifaransa Oroda ya nafasi ya kuchunga mtoto www.fncsf.ca/annuaire

Jamii ya wazazi wasema kifaransa ya N.-B. www.afpnb.ca

ANNExES