Upload
nguyenkhanh
View
281
Download
5
Embed Size (px)
Citation preview
PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA AJILI YA
KUPUNGUZA HATARI ZA KIFUA KIKUU NA
VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA MAGEREZA
NCHINI TANZANIA
KIJITABU CHA MWONGOZO
KWA WAELIMISHA RIKA
JULAI 2017
Kitabu hiki kimeweza kutolewa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa
Kupunguza UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya Mkataba wa Ushirika
namba AID-OAA-A-14-00046. Yaliyomo ni wajibu wa programu ya AIDSFree na si lazima kuwa yanawakilisha mawazo ya shirika
la USAID, PEPFAR au Serikali ya Marekani.
PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA AJILI
YA KUPUNGUZA HATARI ZA KIFUA
KIKUU NA VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA
MAGEREZA NCHINI TANZANIA
KIJITABU CHA
MWONGOZO KWA
WAELIMISHA RIKA
JULAI 2017
AIDSFree
Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI (AIDSFree) ni mkataba wa
miaka mitano unaofadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Ukimwi wa Rais wa Marekani
(PEPFAR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya
Mkataba wa Ushirika AID-OAA-A-14-00046. AIDSFree inatekelezwa na Taasisi ya Utafiti na
Mafunzo ya JSI na washirika Abt Associates Inc., Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation,
EnCompass LLC, IMA World Health, Umoja wa Kimataifa wa VVU / UKIMWI, Jhpiego
Corporation, na PATH. AIDSFree inasaidia na kuendeleza utekelezaji wa mikakati ya PEPFAR
kwa kujenda na kuendeleza uwezo wa kitaalam na kutoa ushauri wa kitaalam kwa USAID,
serikali za nchi husika na watekelezaji wa miradi ya UKIMWI katika ngazi ya wilaya, mkoa na
kitaifa.
Recommended Citation
Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI (AIDSFree). 2017. Elimu rika
kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi vya ukimwi katika magereza nchini
Tanzania: Kijitabu cha mwongozo kwa waelimisha Rika: Julai 2017. Arlington, VA: Programu
ya AIDSFree.
AIDSFree Tanzania Uniformed Services
JSI Research & Training Institute, Inc.
Plot No. 2 Mkwawa Road, Oyster Bay
P.O. Box 9263
Dar es Salaam, Tanzania
SHUKRANI
Shukrani zetu za dhati kwanza ziwaendee watu wa Marekani kupitia Msaada wa Shirika la
USAID la Serikali ya Marekani kwa kufadhili utolewaji wa Kijitabu hiki
AIDSFree/JSI inatoa shukrani kwa Uongozi wa Magereza Tanzania, hasa Dkt. Juma Malewa,
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania kwa kuidhinisha na kupitisha utungaji na
uchapishaji wa Kijitabu hiki. Tunamshukuru Bwana Ali Abdalla Ali, Kamishna wa Chuo cha
Mafunzo Zanzibar aliyefunga rasmi mafunzo ya majaribio ya Kijitabu hiki.
Tunatambua ushiriki na mchango uliotolewa na waakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo
na Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali na maafisa 54 wa
magereza hususan Dkt. Wilson Rugamba, Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt. Richard
Mwankina (Mrakibu Mwandamizi wa Gereza la Ukonga ), Dkt. Juma A. Mwaibako (Mrakibu,
Gereza la Ruanda, Mbeya), Dkt. Hilda Mmari (Mrakibu Msaidizi wa Magereza – Makao
Makuu), Dkt. Abdilatif Mkingule (Inspekta, Ukonga Chuo), na Dkt. Dotto Pakacha (Inspekta,
Gereza la Segerea). Mapendekezo yao yamesaidia kukiboresha Kijitabu hiki.
Shukrani za pekee ziwaendee Dkt. Beati Mboya, Mkurugenzi Mkazi wa AIDSFree/Tanzania na
Dkt. Peter Maro, Mkurugenzi maswala ya kiufundi kwa uongozi wao katika hatua mbali mbali
zilizochangia kuwepo kwa chapisho hili. Tunatambua juhudi za Dkt. John Gulaka, Afisa wa
Uhusiano-Magereza wa AIDSFree/JSI katika hatua mbali mbali za mchakato wa kukiandaa
Kijitabu hiki. Kwa wataalam wetu Bwana Ignatio Chiyaka na Bi. Zuki Mihyo, Kijitabu hiki
hakingeweza kuwepo bila mchango wao kwenye kuandaa yote yaliomo na kujumuisha
maoni na mapendekezo ya wadau husika wakiwemo Uongozi wa Jeshi la Magereza Tanzania.
Msingi wa Kijitabu hiki umetokana na Kitabu cha PharmAccess cha Waelimishaji Rika kwa
Majeshi ya Polisi, Magereza na Uhamiaji cha Mwaka 2013.
iv
v
YALIYOMO
Vifupisho .......................................................................................................................................................... vii
Utangulizi ........................................................................................................................................................... 1
Jinsi ya kutumia kijitabu hiki ................................................................................................................................... 1
Namna ya kuanza ....................................................................................................................................................... 1
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU ............................................................................ 3
Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na UKIMWI .................................................................................................. 3
Somo 2: Viwango vya HATARI ya maambukizi ya VVU kwenye magereza ................................... 23
Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya maambukizi ya VVU ............................................................................ 23
Somo 3: Kifua kikuu na VVU: Matibabu, huduma na msaada ........................................................... 38
Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU ................................................................................................................. 38
Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU: matibabu, huduma, na msaada ................................................................ 50
Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ............................. 55
Somo 4: Kuvunja ukimya kuhusu kifua kikuu na VVU. ........................................................................ 58
Kipindi 4.1: Kutambua aina za shutuma katika magereza ......................................................................... 58
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu .......................................................... 67
Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya kuwa na VVU .......................................................................................... 67
Orodha ya maneno ....................................................................................................................................... 73
Mirejeo ............................................................................................................................................................. 77
vi
vii
VIFUPISHO
UKIMWI upungufu wa kinga mwilini
WAVIU watu waishio na virusi vya ukimwi
SOSPA toleo maalumu la sheria ya makosa ya
kujamiiana 1998
VVU virusi vya ukimwi
viii
1
UTANGULIZI
Malengo ya programu hii ni kusaidia kubadili tabia miongoni mwa wafungwa na wafanyakazi
wa magereza ili kupunguza hatari ya VVU na kifua kikuu kwa kuwaelimisha juu ya mambo
yanayochangia na kuhamasisha matumizi ya huduma za afya zipatikanazo. Waelimisha rika
kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza watatoa mafunzo ili kuhakikisha wenzao
wanapata elimu, manufaa na ujuzi wa namna ya kupambana na VVU na kifua kikuu mahali
popote iwe gerezani ama nje ya gereza. Kitabu hiki kimetungwa kwa ajili ya matumizi ya
waelimisha rika kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza na kimetengenezwa mahususi
kwa ajili ya kukidhi mazingira ya gerezani. Ingawa, masomo yanaweza kupangwa kwa namna
fulani ili kutumiwa pia na wanufaikaji wengine ikiwemo polisi.
Jinsi ya kutumia kijitabu hiki
Kitabu hiki kinawapa waelimisha rika shughuli na maelezo muhimu kwa ajili ya kutoa
mafunzo ya VVU na kifua kikuu kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza. Waelimisha rika
watatumia njia mbalimbali kuwashirikisha wenzao kwenye majadiliano, michezo, michezo ya
kuigiza, pamoja na maswali na majibu. Mafunzo haya yametengenezwa kwa ajili ya makundi
madogo madogo ya washiriki wasiozidi 20. Kila kundi linapaswa kukamilisha masomo yote
tano yaliyo kwenye ratiba. Ratiba ya mafunzo inaweza kupangwa kwa kuzingatia shughuli za
kila siku za magereza na uwepo wa wafanyakazi wa magereza kwa ajili ya kusimamia
nidhamu ya wafungwa.
Mwongozo huu una masomo matano. Kila somo lina utangulizi kwa ufupi sambamba na
maelezo ya kina na ya uhakika. Masomo yanahusisha mada zifuatazo:
1. Maelezo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI
2. Tabia hatarishi kwa maambukizi ya kifua kikuu na VVU gerezani
3. Matibabu ya kifua kikuu na VVU, huduma, na msaada
4. Kuvunja ukimya juu ya kifua kikuu na VVU
5. Kuishi kwa matumaini ukiwa na kifua kikuu au VVU
Namna ya kuanza
Kabla ya kufundisha chochote au kuongoza majadiliano ya kikundi, soma na pitia mwongozo
huu ili kutambua na kuelewa kwa kina mada na maelezo yaliyomo. Maandalizi haya
yatamsaidia mwelimisha rika kuongoza majadiliano kwa ufanisi na kujibu maswali yoyote
ambayo yanaweza kujitokeza.
Maelezo yaliyomo kwenye mwongozo huu yanakwenda sambamba na malengo ya serikali ya
Tanzania kuzuia maambukizi ya VVU na kifua kikuu pamoja na kuzuia maambukizi nyemelezi
miongoni mwa wafungwa na watu waishio na VVU, na hivyo kuboresha afya zao. Mwongozo
huu unatoa maelezo muhimu kwa wakati muafaka.
2
Orodha ya maneno na maana zake imetolewa mwishoni mwa mwongozo huu kwa ajili ya
kuwasaidia waelimishaji kuyatumia wanapofafanua maneno magumu.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
3
SOMO 1: ELIMU YA MSINGI KUHUSU
KIFUA KIKUU NA VVU
Lengo
Kukuza kiwango cha elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU miongoni mwa wafungwa
na wafanyakazi wa magereza.
Madhumuni ya Mafunzo
Mwisho wa somo hili, washiriki watakuwa na uwezo wa:
Kueleza maana ya kifua kikuu, VVU na UKIMWI.
Kuelezea dalili na ishara za kifua kikuu, VVU, na UKIMWI.
Kueleza namna ambavyo kifua kikuu na VVU vinaweza kuenezwa uraiani na gerezani.
Kueleza namna ugonjwa unavyoendelea.
Kueleza mambo ya uhakika kuhusu kifua kikuu, VVU, na UKIMWI nchini Tanzania kwa
ujumla na hasa kwenye magereza.
Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na VVU gerezani.
Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na UKIMWI
Dakika 60
Kipindi 1.1: Mazoezi:
Kuelewa VVU na UKIMWI
VVU na UKIMWI ukweli/uongo
Ueneaji wa VVU na magonjwa ya ngono
Uhusiano kati ya VVU na jinsia
Mwisho wa kipindi washiriki watakuwa na uwezo wa:
Kueleza maana ya VVU na UKIMWI
Kutokomeza imani za upotoshaji kuhusu UKIMWI
Kueleza namna ambavyo VVU vinaenezwa
Kueleza hatua tano za dalili za UKIMWI.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
4
Zoezi 1.Kuelewa VVU na ukimwi
Dakika 20
Hatua 1: Utambulisho
Jitambulishe kwa jina na uzoefu wako wa shughuli za uwezeshaji wa kifua kikuu na VVU
(ukiwa nao). Eleza majukumu yako kama mwelimishaji rika. Wakaribishe washiriki kwenye
majadilianao yao ya kwanza juu ya kifua kikuu na VVU. Waombe wajitambulishe. Kwa
kifupi eleza mada kwa ajili ya majadiliano.
Tambua kwamba kipindi hiki kinaweza kuwa cha kibinafsi na chenye hisia kali. Ndani ya
kundi panaweza kuwepo na washiriki wenye VVU au wenye rafiki wa karibu au
wanafamilia wanaoishi na VVU au UKIMWI. Wakumbushe washiriki kwamba si vibaya
kuachana na swali na wahimize kutoa maelezo yale tu ambayo wanajisikia vizuri kuyatoa.
Kama hawajisikii vizuri kuzungumzia mambo haya kwenye kundi kubwa,wanaweza
kuzungumzia kwenye makundi madogo madogo ama wawili wawili au kutochangia
kabisa.
Hatua 2: Taratibu za mafunzo
Taja kanuni hizi muhimu
Usiri: Heshimu maelezo binafsi ya kila mshiriki. Jaribu kujizuia kutoa maelezo nje ya
kikundi lakini ikiwa utafanya hivyo, toa maelezo ya ujumla pasipo kutumia majina ya
washiriki.
Heshima: Mheshimu kila mtu kwenye kikundi. Hii inamaanisha kutowashambulia
wengine (kwa maneno au matendo) na kuwa muwazi na mwepesi wa kuhisi mitazamo ya
wengine. Kumbuka kutumia kauli ya “MIMI”. Inavutia zaidi kusema “vizuri kwa mimi
binafsi, ninahisi kwamba….” Badala ya kusema, “Hapana, umekosea, ukweli ni kwamba…”.
Uangalifu: Sikiliza wanachokizungumza wengine. Hutaishia kujifunza kitu fulani tu bali
utawafanya wengine wajisikie kuwa huru zaidi.
Uwazi: Washawishi wengine kuzungumzia uzoefu wao wenyewe, pasipo kuwazungumzia
wengine. Chukua tahadhari. Usiwe mwoga wa kuzungumza kwa uwazi bila ugomvi,
kutukana ama kuwa mtu asiyejali hisia za wenzake.
Hatua 3: Maswali na majibuvvu na UKIMWI ni nini?
Swali: VVU ni nini?
Jibu: VVU maana yake ni virusi visababishavyo upungufu wa kinga kwa binadamu. Virusi hivi
hushambulia mfumo wa kinga wa mwili ambao huulinda mwili dhidi ya magonjwa.
Hatua 4: Utangulizi
VVU na UKIMWI nchini Tanzania kulingana na “Ripoti ya Kuzuia VVU na UKIMWI
2016”(AVERT 2017)
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
5
Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU
Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya
VVU
Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015
Vifo 36,000 vyenye uhusiano na UKIMWI
viliripotiwa mwaka 2015
Asilimia 53% ya watu wazima wenye VVU
wanapata tiba ya kupunguza makali
UKIMWI ni nini?
UKIMWI maana yake ni upungufu wa kinga mwilini. Kuambukizwa virusi vya ukimwi
hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa kinga. Jambo hili humfanya mtu aliye na VVU
kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa ambapo mtu asiye na maambukizi ya VVU huenda
asingepatwa au angepona kwa urahisi. VVU hushambulia na kuharibu chembechembe za
mfumo wa kinga zijulikanazo kama CD4 ambazo hupambana na maambukizi. Kupungua kwa
chembechembe za CD4 huufanya mwili kushindwa kupambana na maambukizi na baadhi ya
saratani. Pasipo matibabu, VVU vinaweza kuharibu taratibu mfumo wa kinga na hatimaye
kukua na kuwa ugonjwa unaoitwa UKIMWI.
Hatua baada ya dalili za awali
Waambie washiriki kwamba mtazungumzia hatua za ugonjwa zinazojitokeza baada ya
dalili za awali: maambukizi makali ya VVU, kukua na kuongezeka kwa VVU bila kuonesha
dalili, na UKIMWI.
Hatua 1: Dalili kali za VVU
Ndani ya wiki 1–4 baada ya maambukizi, virusi vimeanza kusambaa, na mtu anaweza
kukumbana na mlolongo wa dalili zijulikanazo kama dalili kali za VVU. Dalili katika hatua hii
zaweza kuwa pamoja na homa, kuumwa kichwa, maumivu ya miguu, kuwashwa kooni, kukua
kwa fundo limfu, uchovu, ukurutu mwilini, maumivu na kuuma kwa viungo , kuharisha,
kubadilika kwa tabia ya ulaji, na kichefu chefu. Hatua hii hujulikana kitaalamu kama “acute
retroviral syndrome” au “acute primary HIV infection,” na dalili hizi zinaweza kutokea kwa
kuwa mwili wako unakuwa ukipambana na virusi. Ni mwitikio wa asili wa mwili dhidi ya VVU.
Katika kipindi hiki kiwango kikubwa cha virusi huzalishwa. Katika hatua hii ya maambukizi
makali ya VVU, mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kueneza VVU kwa wapenzi ama
watumiaji wenza wa madawa ya kulevya kwa kutumia sindano kutokana na kuwepo kwa
kiwango kikubwa cha VVU kwenye mishipa yao ya damu. Kwa hiyo ni muhimu kuchukua
hatua za kupunguza hatari za kueneza virusi.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
6
Hatua 2VVU Kukua na kuishi mwilini bila kuonekana:
Baada ya hatua ya maambukizi makali ya VVU, ugonjwa huhamia kwenye hatua ijulikanayo
kama “kukua na kuishi kwa VVU mwilini bila kuonekana.” Kipindi cha virusi kutoonekana
maana yake ni kipindi ambapo virusi vinaishi na kukua ndani ya mwili wa mtu pasipo
kuonesha dalili zozote. Katika hatua ya ukuaji wa virusi pasipo kuonekana, watu wenye VVU
huwa hawaoni dalili zozote labda zile ndogo ndogo sana. Hatua hii mara nyingine huitwa
“dalili za maambukizi ya VVU” au “maambukizi sugu ya VVU.” Eleza kwamba katika hatua hii,
VVU bado vinazaliana na kuongezeka kwa kiwango kidogo sana, lakini bado vipo hai. Ikiwa
utakuwa kwenye matibabu ya kupunguza makali, unaweza kuishi kwenye hatua hii kwa
miongo kadhaa, kwa kuwa matibabu husaidia kuwepo kwa kiwango kidogo cha virusi.
Hatua 3: Ukimwi
Hatua ya mwisho ya maambukizi ya VVU hutokea pale ambapo mfumo wa kinga unakuwa
umeharibiwa vibaya na virusi na mtu huwa katika hatari kubwa zaidi au huwa hatarini
kupatwa na maambukizi mazito na hatari zaidi au magonjwa ya bacteria na ukungu
magonjwa ambayo vinginevyo angeweza kupambana nayo (“maambukizi nyemelezi”). Idadi
ya CD4 inaposhuka chini ya 200 kwa kiwango cha milimita za mchemraba za damu, yaani
(200 chembechembe/mm3), unahesabiwa kuwa sasa una UKIMWI. Kwa mtu mwenye mfumo
wa kinga imara, idadi ya CD4 huwa ni chembechembe 500–1,650 kwa milimita za
mchemraba. Vile vile utahesabiwa kuwa una UKIMWI ikiwa utapatwa na ugonjwa nyemelezi
mmoja ama zaidi, bila kujali idadi ya CD4 zako.
Dalili za UKIMWI
Kupungua uzito ghafla
Homa za mara kwa mara au kutokwa na jasho usiku
Uchovu wa kupindukia na usioelezeka
Kuendelea kuvimba kwa tezi za limfu kwenye kwapa, kinena, au shingo
Kuharisha kwa zaidi ya wiki moja (uharo usiosikia dawa)
Kuwashwa mdomoni, njia ya haja kubwa, na sehemu za siri
Kukohoa pasipo kukoma
Majibu yenye rangi nyekundu, kijivu, pinki, ama zambarau juu ya au chini ya ngozi au
ndani ya mdomo, pua au kope za macho.
Kupoteza kumbukumbu, unyonge, na maradhi mengine ya nyuroni.
Chembechembe za CD4 ni chembechembe za damu zinazofanya kazi kubwa ya kuulinda mwili
dhidi ya maambukizi. Virusi hutumia chembechembe hizi za CD4 (mara nyingi huitwa
chembechembe-T au chembechembe –T saidizi) kuzaliana zaidi na kuenea kote mwilini huku
zikiharibu chembechembe hizo za CD4. Baada ya hapo mwitikio wa kinga utaanza kupunguza
kiwango cha virusi mwilini hadi kufikia kiwango fulani thabiti mwilini mwako. Wakati huu
chembechembe mpya za CD4 zitaanza kuongezeka, lakini huenda zisifikie kiwango cha
chembechembe za CD4 zilizokwishaharibiwa.
Chembechembe za CD4 ni nini?
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
7
Magonjwa makubwa makubwa
Tofauti ya VVU na UKIMWI ni ipi?
Mtu mwenye maambukizi ya VVU anaweza kuwa na afya njema kwa miaka kadhaa bila ya
kuwa na ishara au dalili za maambukizi mwilini. Mtu mwenye virusi bila ya dalili ni “mtu
anayeishi na VVU” au “mwenye maambukizi ya VVU”.UKIMWI ni hatua ya mwisho ya
maambukizi na si kila mwenye VVU hufikia hatua hii. Baada ya mtu kuambukizwa VVU kwa
kipindi fulani (mara nyingi kwa miaka mingi), dalili zinazosababishwa na virusi huanza
kujitokeza. Katika hatua hii, watu wenye VVU huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na
maambukizi nyemelezi. “UKIMWI” ni ufafanuzi wa kidaktari unaowalenga watu wenye VVU
wanaosumbuliwa na ambukizi moja au maambukizi kadhaa mahususi, ikiwemo kifua kikuu,
saratani kwa kiasi kidogo, macho, ngozi, na hali ya mfumo wa neva.
Zoezi 2. VVU zoezi la Kweli/Uongo
Dakika 20
Hatua 1: Zoezi
Eleza kwamba mtafanya zoezi la kutolea ufafanuzi upotoshaji kuhusu VVU na UKIMWI.
Waambie washiriki kwamba utasoma maelezo na kama wanaamini ya kwamba maelezo
ni ya“UKWELI” wasimame; na kama wanaamini kuwa maelezo ni ya “UONGO” wakae.
Hakikisha maelekezo yanaeleweka vizuri. Soma maelezo mara moja au mbili. Waruhusu
washiriki wajibu. Waombe waelezee kwa nini wanaamini ya kuwa maelezo ni ya
KWELI/UONGO na jadilianeni
Muongozo wa majibu:
MAELEZO KWELI/UONGO
1. Unaweza kuambukizwa VVU kwa
kung’atwa na mbu
UONGO: Imethibitishwa kwamba VVU haviwezi
kuenezwa kwa njia hii.
2. Kufanya mapenzi kinyume na
maumbile ni moja kati ya njia hatari
zaidi kwa ueneaji wa VVU.
KWELI: Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
ni hatari zaidi katika ueneaji wa VVU kuliko namna
nyingine yoyote ya kujamiiana. Wakati wa
kujamiiana kwa njia hii, mboo inaweza kuchana
ngozi laini njia ya haja kubwa, jambo ambalo
litaviwezesha virusi kuingia kwenye mishipa ya
damu.
3. Watu wanaweza kuambukizwa VVU
ikiwa watafanya mapenzi mdomoni na
mtu mwenye maambukizi ya VVU
KWELI: VVU vipo kwenye shahawa za mtu
mwenye maambukizi. Hivyo, VVU vinaweza
kuenezwa ikiwa shahawa zitaingia mdomoni mwa
mtu. Hatari ya kuambukizwa VVU unapofanya
mapenzi mdomoni huongezeka ikiwa kuna
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
8
MAELEZO KWELI/UONGO
vidonda mdomoni. Hatari yaweza kupunguzwa
kwa kuvaa kondomu na kuhakikisha hakuna
shahawa zinazoingia mdomoni mwa mwenza
wako.
Kibaiolojia inawezekana VVU kuenezwa kwa
kufanya mapenzi mdomoni na mwanamke
mwenye VVU, lakini jambo hili linadhaniwa kuwa
ni kwa kiasi kidogo. Kutumia kinga kama
kondomu au kiwambo cha meno wakati wa
kufanya mapenzi mdomoni kunaweza kuzuia
kueneza zaidi kwa VVU, magonjwa mengine ya
ngono, na homa ya ini. Kiwambo cha meno ni
kipande mraba chembamba cha mpira au silikoni
ambacho huwekwa juu ya meno wakati wa
kufanya mapenzi mdomoni.
4. Zinapotumiwa kwa usahihi, kondomu
zinaweza kuwakinga wanaume na
wanawake kutokana na maambukizi ya
VVU.
KWELI: Kondomu hutoa ulinzi dhidi ya VVU, magonjwa
mengine ya ngono, na mimba zisizotarajiwa.
Zikitumiwa mara kwa mara kwa usahihi, kondomu ni
moja kati ya njia bora zaidi za kujikinga na VVU.
5. Dawa maalumu zinaweza kutibu
maambukizi ya VVU.
UONGO: Hadi sasa, hakuna tiba wala chanjo kwa
maambukizi ya VVU. Ijapokuwa, kuna vidonge
vinavyoweza kupunguza uzalianaji wa virusi ndani ya
mwili wa mtu aishiye na VVU. Vile vile kuna dawa
zinazosaidia kukinga ama kutibu maambukizi
nyemelezi yaliyosababishwa na VVU.
6. VVU ni ugonjwa unaowaathiri
makahaba na wanaume wanaofanya
nao mapenzi peke yake.
UONGO: Mtu yeyote anaweza kuambukizwa
VVU.Hatari ya mtu kupata VVU haina uhusiano na
jinsi mtu alivyo, bali tabia aliyo nayo.
7. Ukiishi na mwenza mmoja tu, huwezi
kuambukizwa VVU.
UONGO: Watu walio waaminifu kwa wenza wao
bado wanaweza kuwa katika hatari ya kupata VVU
ikiwa wenzi wao wanashiriki kufanya mapenzi ama
kuchangia nyembe na watu wengine wenye
maambukizi.
8. Watu wenye magonjwa ya ngono
(maambukizi yaenezwayo kwa njia ya
kujamiiana) wapo katika hatari kubwa
ya kuambukizwa VVU kuliko wale wasio
na magonjwa ya ngono ikiwa watafanya
mapenzi na mtu mwenye maambukizi
KWELI: Magonjwa ya ngono sehemu za siri
huvipa VVU njia rahisi ya kupenya kwenye mishipa
ya damu.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
9
MAELEZO KWELI/UONGO
ya VVU.
9. Mtu anaweza kupona VVU kwa
kufanya mapenzi na bikira.
UONGO: Bikira hawana uwezo wowote wa kuwaponya
watu wenye maambukizi ya VVU. Hadi sasa bado
hakuna tiba kwa VVU.
10. Huwezi kupata VVU kwa sababu tu
unaishi kwenye nyumba moja na mtu
mwenye ugonjwa.
KWELI: Kuishi kwenye nyumba moja na mtu mwenye
VVU hakuwezi kuwaweka hatarini wale wanaoishi nae;
VVU havienezwi kwa migusano ya kawaida ndani ya
familia.
11. Wakati wote unaweza kutambua
kama mtu ana VVU kwa mwonekano
wake.
UONGO: Watu wengi wanaoambukizwa VVU
hawaoneshi dalili yoyote ya ugonjwa kwa miaka mingi.
Ingawa, virusi vinakuwepo mwilini mwao na vinaweza
kuenezwa kwa watu wengine.
12. VVU vinaweza kuenezwa kutoka kwa
mtu mmoja mwenye VVU kwenda kwa
mtu mwingine pale wanapochangia
sindano wanapotumia madawa ya
kulevya.
KWELI: Kuchangia sindano wakati wa utumiaji wa
madawa ya kulevya kunabeba hatari kubwa sana
ya ueneaji wa VVU. Damu yenye maambukizi
hupitishwa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja
kwenda kwa mtu mwingine kupitia sindano yenye
maambukizi au vifaa vingine vilivyotumika
kuandaa au kujidunga madawa.
Hatari kwa wanaume na wanawake
kuambukizwa VVU huongezeka pale
ambapo pana magonjwa ya ngono
mahali ambapo kiwango cha VVU kiko
juu.
KWELI: Magonjwa ya ngono kwa wanawake
hayatambuliwi kwa urahisi na mara nyingi huisha
pasipo kuchunguzwa. Magonjwa ya ngono
sehemu za siri huvipa VVU njia rahisi kuingia
kwenye mishipa ya damu. Unyanyapa kwa
wanawake pia ni kikwazo ambacho kinawavunja
moyo wanawake kutafuta matibabu ya
kutosheleza.
Zoezi 3: Jinsi VVU na magonjwa ya ngono yanavyoenezwa
Dakika 10
Hatua 1: Maswali na majibi—uenezwaji wa VVU
Swali: VVU vinaenezwaje?
Jibu: VVU haiambukizwi kwa urahisi kama surua au homa ya mafua. Kwa mfano, virusi kama
surua na homa ya mafua huenezwa kwa njia ya hewa kwenye maeneo yenye vizuizi palipo na
watu wenye maambukizi. VVU huishi kwenye majimaji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa kama
vile damu, shahawa, majimaji kabla ya shahawa, uke, uteute kwenye njia ya haja kubwa, na
maziwa ya mama. VVU vinahitaji kuingia kwenye mwili wa mtu. Hivyo basi, VVU vinaweza
kuenezwa kwa njia zifuatazo:
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
10
Majadiliano kuhusu mapenzi salama
hayatawezekana kwa kuwa
magereza ni mahali wanapokaa
wafungwa kulingana na jinsia zao
wenyewe. Kwa sababu hii hawawezi
kuzungumzia mapenzi salama kwa
watu wenye jinsia moja, lakini elimu
hii itawasaidia watakapomaliza
kutumikia vifungo vyao na kurudi
majumbani mwao au katika jamii.
Mapenzi salama katika magereza
Uwepo wa maambukizi yatokanayo na
ngono (kotokwa maji maji, vidonda, na
miwasho ) huongeza hatari ya kupata na
kueneza VVU. Hii ni kwa sababu watu wenye
VVU wenye maambukizi ya magonjwa ya
ngono wana kiwango kikubwa cha VVU
kwenye ute wa sehemu zao za siri na/au kwa
kuwa kuingia kwa virusi kumerahisihwa
kutokana na uwepo wa michubuko kwenye
mucosa
Jinsi magonjwa ya ngono huongeza hatari ya
kupata na kueneza VVU
Kufanya ngono na mtu mwenye maambukizi
Kuongezewa damu au mazao ya damu na mtu mwenye maambukizi ya VVU
Kuchangia matumizi ya sindano, mabomba ya sindano, na vitu vyenye ncha kali vilivyo na
bacteria na mtu mwenye maambukizi ya VVU
Kutoka kwa mama mwenye VVU kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, kuzaa ama
kunyonyesha.
Hatua 2: Eleza
Zungumzia magonjwa ya ngono
Hatua 3: Maswali na majibu
Swali: Jinsi gani VVU havienezwi?
Jibu:
Maji maji mengine mwilini kama, machozi,
mate, jasho, matapishi na mkojo
Migusano binafsi: busu kavu mdomoni
pasipo na vidonda, kukumbatiana,
kushikana mikono, kusalimiana kwa
kushikana mikono.
Mikusanyiko kijamii: wakati wa kazi, shuleni, kwenye sinema, mgahawani.
Hewa au maji: chafya, kukohoa, kuogelea bwawani/madimbwi
Vifaa: kalamu, vyoo, taulo, mashuka, sabuni, vifaa vya kulia chakula, mavazi.
Wadudu: kung’atwa na mbu ama wadudu wengine
Hatua 4: Maswali na majibu—upunguzaji wa ueneaji wa vvu
Swali: Ueneaji wa VVU unawezaje kupunguzwa?
Jibu: “Mpango mkakati wa UNAIDS 2016–2021” (ukurasa.58) eneo la matokeo 4, ili
kupunguza ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma na bidhaa, umezitaka serikali za
kitaifa kutoa kipaumbele kwenye upatikanaji wa huduma za kinga za VVU kwa makundi
maalumu, ikiwemo watu wanaotumia madawa ya kulevya na wakazi wenza, ili kupunguza
kwa haraka kwa kuwakinga na kusimamia haki za watu wote kupata huduma za kutosha
zenye ubora wa juu bila ubaguzi. Kupunguza hatari kwa vijana na makundi maalumu kupata
VVU na madhara yake kwenye maeneo yote yenye
maambukizi ni jambo muhimu katika kutokomeza
ugonjwa wa UKIMWI (2016).
Ikiwa wewe ni mfanyaji mapenzi, kuna mambo
kadhaa muhimu unayopaswa kuchukua ili
kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU.
Kutojamiiana ni njia mojawapo ya kuzuia kupata
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
11
au kueneza VVU. Ikiwa huwezi kuacha kujamiiana, tumia kondomu (ya kiume ama kike)
wakati wote ufanyapo mapenzi kwenye uke, njia ya haja kubwa ama mdomoni. Inapotumiwa
wakati wote na kwa usahihi kondomu za kiume na kike njia bora zaidi katika kuzuia kuzuia
VVU. Shughuli mbalimbali za kimapenzi vile vile zinabeba viwango tofauti vya hatari ya VVU.
Ngono kinyume cha maumbile pasipo kutumia kondomu au ngono ya kulazimisha ni njia
hatari zaidi kwa ueneaji wa VVU kwa kuwa hupelekea kuchanika kwa kuta za uke na njia ya
haja kubwa:
Usichangie sindano, bomba za sindano na vifaa vingine vyenye ncha kali na mtu yeyote
ikiwa unatumia madawa ya kulevya.
Pata matibabu ya VVU ikiwa wewe ni mama mjamzito unayeishi na VVU ili kupunguza
hatari ya kumwambukiza mtoto wako wakati wa ujauzito, kuzaa na kunyonyesha.
Hakikisha kwamba mazao ya damu unayopokea yamefanyiwa uchunguzi wa VVU.
Vaa vifaa vya kujikinga (Kama glavu na miwani ya kuzuilia vumbi) na safisha mikono
baada ya kushika damu na maji maji mengine (hasa kwa wataalamu wa huduma za afya
au watoa huduma).
Tumia dawa za kurefusha maisha au kinga ili kujikinga na uwepo wa maambukizi (ikiwa
inapatikana) ikiwa upo katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.
Jitolee mwenyewe, katahiriwe hospitalini
Punguza idadi ya watu unaofanya nao mapenzi. Unapokuwa na idadi kubwa ya wapenzi
unajiongezea nafasi ya kupata mpenzi mwenye VVU au ugonjwa mwingine uenezwao
kwa njia ya ngono.
Hatua 5: Elezea
Elezea “mapenzi salama” kwenye magereza
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
12
Zoezi 4: Uhusiano baina ya VVU na jinsi
Dakika 10
Hatua 1: Eleza
Kijamii jinsi imefafanuliwa, kwa kuzingatia zaidi majukumu ambayo wanaume na wanawake
huyafanya katika jamii.Jinsi inaweza kufanya jambo kubwa katika kupandikiza ufuasi. Kwa
pamoja jinsia na jinsi hutoa uzoefu wa kipekee kwa wanaume na wanawake waishio na VVU.
Kwa hiyo kuelewa desturi za jinsi na ukosefu wa usawa wa jinsi ni muhimu katika kupunguza
hatari ya VVU miongoni mwa wanaume na wanawake, wavulana na wasichana. Ijapokuwa
kuwa mambo yanayofanana baina ya vihatarishi vya VVU na tabia katika jinsi mbalimbali,
tofauti zipo na baadhi ya watu huambukizwa zaidi kuliko wengine.
Hatua 2: Maswali na majibu
Swali: Kuna mtu anayeweza kutupa mfano wa namna ambavyo majukumu ya kijinsi
yanavyoweza kuathiri uwezo wa mwanamke kutumia dawa.
Jibu: Wanawake wanaweza kukumbana na changamoto nyingi na vikwazo inapokuja suala la
afya zao wenyewe na ustawi wao. Wengi wanaishi kwenye mazingira ya uonevu,
wanakumbana na unyanyapaa na ubaguzi katika jamii, ukosefu wa amana za kiuchumi na
huduma za kiafya na mara kwa mara wao ndio watoa huduma wa kwanza katika familia.
Changamoto hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa uwezo wao wa kumwona daktari, kufuata
dawa, kunywa dawa, kupumzika na kushusha kiwango cha msongo wa mawazo.
Hatua 3: Hitimisho
Swali: Hivyo, nini kifanyike kuhusu jambo hili?
Jibu: Tukumbuke kwamba jinsia zetu, umri, hadhi katika jamii zetu, nakadhalika ni mambo
yanayobadilika ambayo yanaweza kumfanya kila mmoja wetu kuwa na kiwango tofauti cha
hatari, uzoefu na uwezo wa kupata huduma na fursa.
Kipindi 1.2 Ufahamu juu ya Kifua Kikuu
Dakika 110
Kipindi 1.2: Mazoezi
Utangulizi juu ya kifua kikuu na ugonjwa
Ueneaji wa kifua kikuu
Kifua kikuu kisichoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu
Jinsi ya kuchunguza kifua kikuu
Mambo ya uhakika na upotoshaji kuhusu kifua kikuu
Maambukizi ya kifua kikuu na changamoto za ugonjwa magerezani.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
13
Madhumuni ya kipindi
Mwisho wa kipindi hiki, washiriki wataweza:
Kuelezea aina mbili za kifua kikuu
Kuainisha kifua kikuu kulingana na sehemu ya mwili iliyoathiriwa
Kufuta dhana ya upotoshaji kuhusu kifua kikuu
Kuelezea namna ambavyo kifua kikuu kinaenezwa
Kuorodhesha viashiria na dalili za kifua kikuu
Kuelezea tofauti baina ya maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa kifua
kikuu.
Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na maambukizi ya VVU.
Zoezi 1. Utangulizi kuhusu maambukizi ya kifua kikuu na ugonjwa
Dakika 10
Hatua 1: Eleza—kifua kikuu na vvu
VVU na kifua kikuu ni muunganiko hatari mno. Kila ugonjwa huufanya ugonjwa mwingine
uenee haraka zaidi. VVU huufanya mfumo wa kinga wa mwili kuwa dhaifu na mtu mwenye
VVU halafu akaambukizwa kifua kikuu huwa katika nafasi kubwa kuugua ugonjwa wa kifua
kikuu kuliko yule mwenye kifua kikuu asiye na VVU.
Hatua 2: Elezakifua kikuu nchini tanzania
Shirika la afya ulimwenguni limeitaja Tanzania kama nchi yenye mzigo mkubwa wa kifua
kikuu (TB), na moja kati ya nchi zenye mzigo mzito wa kifua kikuu na VVU. Mnamo mwaka
2013, wagonjwa 64,000 wa kifua kikuu waliripotiwa na asilimia 83 (53,120) ya wagonjwa hawa
walikuwa wamepatiwa ushauri nasaha na kupimwa VVU. Katika kundi hili, asilimia 39 (20,717)
walikutwa wakiwa na maambukizi ya VVU. Mwezi Aprili 2016 kulikuwa na takribani wagonjwa
295 wa kifua kikuu mapafuni katika kila watu wazima 100,000 katika Tanzania (International
Organization for Migration in Tanzania 2016).
Serikali imeweka kipaumbele kutolewa kwa pamoja kwa huduma za kifua kikuu na VVU ili
kupunguza mzigo wa magonjwa haya. Kwa hiyo, watu waishio na VVU wanaotumia vidonge
vya kupunguza makali wana nafasi nzuri ya kupambana na maambukizi ya kifua kikuu. Utoaji
wa huduma hizi pamoja utahakikisha pia upatikanaji wa matibabu ya kifua kikuu na VVU kwa
kiwango kikubwa zaidi.
Hatua 3: Jadili
Kifupisho “TB” kinamaanisha nini?
Unadhani ni jambo gani husababisha kifua kikuu?
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
14
Hatua 5: Elezavipi na kwa nini
Kifua kikuu kinasababishwa na bakiteria wanaoitwa Mycobacterium tuberculosis. Kwa kawaida
bakiteria hawa hushambulia mapafu, lakini bakiteria wa kifua kikuu wanaweza kushambulia
sehemu yoyote ya mwili ikiwemo figo, uti wa mgongo na ubongo. Si kila aliyeambukizwa na
bakiteria wa kifua kikuu huugua. Hivyo basi, kuna namna mbili zenye uhusiano na kifua
kikuu: maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu. Ikiwa
hautatibiwa vizuri, ugonjwa wa kifua kikuu unaweza kuwa ugonjwa wa kifo. Wote wenye hali
fulani kiafya inayodhoofisha mfumo wa kinga vile vile huwa hatarini kupata kifua kikuu.
Maziringira yanayowafanya watu kuwa katika hatari kubwa ya kuathiriwa haraka na ugonjwa
wa kifua kikuu ni pamoja na:
Maambukizi ya VVU
Matumizi mabaya ya madawa
Silikosisi/asbestosi: ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na kuvuta hewa iliyo na madini
ya silika ambayo ni sehemu ya mchanga, miamba na mawe yenye madini kama vile
kwazi. Baada ya muda, kuwepo katika mazingira yenye chembechembe za silika
husababisha makovu kwenye mapafu, ambayo yanaweza kuathiri uwezo wa mtu
kupumua.
Ugonjwa wa kisukari (aina ya 2): ugonjwa sugu wenye kiwango cha juu cha sukari
(glukosi) isivyo kawaida kwenye damu.
Ugonjwa mkali wa figo
Uzito mdogo wa mwili
Saratani
Matibabu kama vile corticosteroids au upandikizaji wa viungo.
Zoezi 2: Ueneaji wa kifua kikuu cha mapafu
Dakika 20
Hatua 1: Eleza: kifua kikuu cha mapafuni nchini Tanzania
Idadi ya waathirika wa kifua kikuu cha mapafuni katika Tanzania iliripotiwa kuwa watu 295
kati ya watu 100,000, kulingana na hotuba ya bajeti ya mwaka 2014/2015 ya waziri wa afya.
Kifua kikuu cha mapafuni ni moja kati ya maambukizi nyemelezi kwa wengi miongoni mwa
watu waishio na VVU. Karibu asilimia 39 ya wagonjwa wa kifua kikuu nchini Tanzania
wameambukizwa VVU (WHO 2012).
Hatua 2: Chemsha bongo
Wagawe washiriki katika makundi ya watu 3 au 4 na acha wajadili njia ambazo kifua kikuu
kinaenezwa kwa dakika 5. Yaombe makundi yawasilishe majibu yao.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
15
Kuvuta hewa yenye
matone madogo sana
ya erosoli ambayo
hutolewa pale mtu
mwenye PTB ambukizi
anapokohoa, piga
chafya, tema mate,
zungumza au kuimba.
Namna kifua kikuu cha
mapafu kinavyoweza
enezwa
Hatua 3: ElezaNamna kifua kikuu cha mapafu kinavyoweza
enezwa
Mtu anapovuta hewa iliyou na bakiteria wanaosababisha kifua
kikuu cha kwenye mapafu, bakiteria wanaweza kukaa kwenye
mapafu na kuanza kuzaliana. Kifua kikuu cha mapafu
kinaambukizwa, maana yake bacteria wanaweza kuenezwa kwa
watu wengine. Kifua kikuu kwenye sehemu nyingine za mwili,
kama vile, figo au uti wa mgongo hakiambukizi. Eleza zaidi
kwamba kuna aina mbili za kifua kikuu: (1) kifua kikuu ndani ya
mapafu, ambacho kinaambukiza, na (2) kifua kikuu nje ya
mapafu, ambacho hakiambukizi.
Hatua 4: Maswali na majibu: kwa nini kifua kikuu cha mapafu ni ambukizi
Swali: Kwa nini wanadhani kifua kikuu cha mapafu ni ambukizi?
Jibu: Kifua kikuu ndani ya mapafu kimo mapafuni. Kinaenea pale mtu mwenye kifua kikuu
ambukizi anapotoa hewa nje iliyo na bacteria wa kifua kikuu halafu mtu mwingine anawavuta
ndani bakiteria waliopo kwenye hewa hiyo. Mtu mwenye maabukizi ya kifua kikuu cha
mapafu hutoa bakiteria zaidi pale anapofanya vitendo kama kukohoa au kucheka. Kifua kikuu
nje ya mapafu hakiambukizwi kwa watu wengine kwani kipo katika sehemu nyingine za mwili
na sio kwenye mapafu. Watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu cha mapafu wana uwezekano
mkubwa wa kuueneza kwa watu wanaokuwa nao kwa karibu kila siku, ikiwemo wanafamilia,
rafiki, wafanya kazi wenzao na wafungwa.
Hatua 5: Fuatilia
Angalia kama washiriki wana maswali
Hatua 6: Fafanua zaidi
Kuna aina nyingine ya kifua kikuu inayoitwa bovine TB ambayo ipo zaidi Tanzania. Bovine TB,
au Kifua kikuu cha mifugo, kinaweza kuambukiza zaidi kwa wanyama, wakiwemo binadamu.
Bovine TB husababishwa na bacteria wajulikanao kitaalamu kama Mycobacterium bovis (M.
bovis) ambao ni sehemu ya aina ya wadudu wanaoambukiza kifua kikuu wajulikanao kama
Mycobacterium tuberculosis complex.
Hatua 7: Uliza
Mnadhani zipi ni dalili na viashiria vya kifua kikuu?
Pitia majibu yaliyoorodheshwa kwenye boksi.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
16
Viashiria na dalili za kifua kikuu
Kujisikia kuumwa au dhaifu
Kupungua uzito
Homa za jioni na kutoka jasho jingi usiku.
Kukohoa kwa zaidi ya wiki mbili
Maumivu ya kifua na kukohoa damu.
Zoezi 3: Maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana na ugonjwa wa kifua
kikuu
Dakika 10
Hatua 1: Eleza
Bakteria wa kifua kikuu wanaweza kuishi mwilini bila ya wewe kuugua. Hii hujulikana kama
maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana. Kwa watu wengi ambao wanawavuta bacteria wa
kifua kikuu na kuambukizwa, mwili huwa na uwezo wa kupambana na bacteria ili kuwazuia
wasikue. Watu wenye maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana:
Hawana dalili
Hawajisikii kuumwa
Hawawezi kueneza bacteria wa kifua kikuu kwa wengine
Mara nyingi huonekana kuwa na maambukizi ya kifua kikuu kwa kipimo cha kuchunguza
athari kwenye ngozi au kipimo cha damu.
Wengi huugua ugonjwa wa kifua kikuu ikiwa hawatapatiwa matibabu kwa ajili ya
maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana.
Hatua 2: Taja
Watu wengi wenye maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana hawataugua ugonjwa wa kifua
kikuu. Kwa watu hawa, bacteria wa kifua kikuu hubaki mwilini bila kuwa na madhara kwa
kipindi chote cha maisha bila kusababisha ugonjwa. Lakini kwa watu wengine, hasa wale
wenye mifumo dhaifu ya kinga kutokana na maambukizi ya VVU, bakteria huweza kuleta
athari, kuzaliana, na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.
Bakteria wa kifua kikuu huwa na athari ikiwa mfumo wa kinga hautakuwa na uwezo wa
kuwazuia kukua. Bakteria wa kifua kikuu wanapokuwa na athari (wanapoongezeka mwilini
mwako), hii huitwa ugonjwa wa kifua kikuu. Watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu ni
wagonjwa. Wanaweza vili vile kueneza bacteria kwa watu wanaokuwa nao kila siku, hasa kwa
kifua kikuu cha kwenye mapafu. Baadhi ya watu hufikia kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu
mapema mara baada ya kuambukizwa (ndani ya wiki kadhaa) kabla hata ya mifumo yao ya
kinga kupambana na bakteria. Watu wengine wanaweza kuanza kuugua baada ya miaka
kadhaa pale ambapo mifumo yao ya kinga inapokuwa dhaifu kwa sababu nyingine.
Uwezekano wa kuugua ugonjwa wa kifua kikuu ni mkubwa kwa watu wenye VVU
ukilinganisha na wale ambao hawana maambukizi. Watu wenye mifumo dhaifu ya kinga,
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
17
hasa wale wenye maambukizi ya VVU, wana hatari kubwa ya kupatwa na ugonjwa wa kifua
kikuu kuliko watu wenye mfumo wa kinga usio na maambukizi.
Zoezi 4: Tofauti kati ya kifua kikuu kisichoonekana na kifua kikuu cha
kwenye mapafu
Dakika10
Hatua 1: Maswali na majibu
Swali: Ni nini tofauti kati ya kifua kikuu kisichoonekana na kifua kikuu cha kwenye mapafu?
Jadili na pitia majibu yaliyopo kwenye jedwali hapa chini.
MTU MWENYE MAAMBUKIZI YA KIFUA KIKUU
KISICHOONEKANA
MTU MWENYE KIFUA KIKUU NDANI YA
MAPAFU
Hana dalili Dalili zaweza kuwa:
Kikohozi kibaya kinachochukua wiki 3
au zaidi
Maumivu kifuani
Kukohoa damu au makohozi
Udhaifu au uchovu
Kupoteza uzito
Kukosa hamu ya kula
Homa za baridi
Homa
Kutoka jasho usiku (kupita kiasi)
Hajisikii kuumwa Kwa kawaida hujisikia kuumwa
Hawezi kueneza bacteria wa kifua kikuu kwa
wengine
Anaweza kueneza kifua kikuu kwa
wengine
Kwa kawaida matokeo ya kipimo cha TB kwenye
ngozi ama damu huonesha kuwa ana
maambukizi ya TB
Kwa kawaida matokeo ya kipimo cha
ngozi ama damu huonesha kuwa ana
maambukizi ya kifua kikuu.
Kipimo cha x-ray ya kifua hakina shida na
makohozi hayana maambukizi.
Anaweza kuwa na kipimo cha x-ray ya
kifua kikionesha tatizo, au makohozi
yakaonesha maambukizi.
Anahitaji matibabu ili kuzuia kifua kikuu ndani
ya mapafu
Anahitaji matibabu kwa ajili ya kifua kikuu
ndani ya mapafu
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
18
Zoezi 5: Uchunguzi wa kifua kikuu
Dakika 20
Hatua 1: Maswali na majibu
Swali: Nani anapaswa kupimwa kifua kikuu?
Jibu: Wale ambao wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa na bakiteria wa kifua
kikuu ikiwemo:
Watu wanaoishi kwa karibu na mtu mwenye ugonjwa wa kifua kikuu (kama, wanafamilia,
wafungwa)
Watu kutoka kwenye nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha kifua kikuu
Watu wanaoishi au kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi (kwa mfano: magerezani,
vituo vya kutolea matibabu ya kifua kikuu)
Watoa huduma za afya wanaowahudumia wagonjwa walio katika hatari zaidi ya ugonjwa
wa kifua kikuu.
Watoto wachanga, watoto, vijana walio pamoja na watu wa zima walio kwenye hatari
zaidi ya maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana au ugonjwa wa kifua kikuu.
Wenye VVU au wagonjwa wa UKIMWI.
Watu walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu
Wajawazito wenye VVU
Watu wenye maambukizi ya VVU
Watu waliopata maambukizi ya bakteria wa
kifua kikuu miaka miwili iliyopita
Watu ambao hawakupata matibabu ya kifua
kikuu vizuri hapo zamani
Watoto wachanga na watoto wadogo
Watu wanaojidunga madawa ya kulevya
Watu wanaoumwa magonjwa mengine
yanayodhoofisha mfumo wa kinga
Watu wenye umri mkubwa
Swali: Ni nani aliye katika hatari zaidi ya kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu?
Jibu: Eleza kwamba vipimo ya kifua kikuu kwa ujumla huwa havihitajiki kwa watu waliopo
kwenye hatari ndogo ya maambukizi ya bacteria wa kifua kikuu.
Hatua 2: Maswali na majibuUpimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu
Swali: Je mnafahamu jinsi ugonjwa wa kifua kikuu unavyopimwa?
Jibu: Elezea aina mbalimbali za vipimo kwa maambukizi ya kifua kikuu:
Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya ngozi (kipimo cha uchunguzi cha mantoux)
Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya damu
Makohozi (mchanganyiko wa mate na uteute uliokoholewa kutoka kwenye njia ya
upumuaji, hasa kama matokeo ya maambukizi au magonjwa mengine na mara nyingi
huchunguzwa kwa kutumia darubini ili kusaidia uchunguzi wa kitabibu.
Hatua 3: Eleza
Mtoa huduma za afya anapaswa kuchagua ni kipimo gani cha kifua kikuu anapaswa kutumia.
Vigezo katika kuchagua kipimo gani kitumike ni pamoja na sababu ya kufanya vipimo,
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
19
uwepo wa vipimo, na gharama. Kwa ujumla, haishauriwi kumpima mtu kwa vipimo vyote
viwili yaani kipimo cha kifua kikuu kwenye ngozi na kile cha damu.
Zoezi 6: Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua kikuu cha kwenye mapafu
Dakika 15
Hatua 1: Eleza
Waambie washiriki kwamba utasoma maelezo na kama wanadhani maelezo ni UKWELI
wahamie upande wa kulia, na kama wanadhani ni UPOTOSHAJI wahamie kushoto. Kama
hawajui, wasihame. Hakikisha washiriki wameelewa maelekezo.Muulize mshiriki mmoja
ama wawili kutoa maelezo kwa nini wanadhani maelezo ni ukweli au uongo. Tumia
ufunguo wa majibu (chini) kwani una maelezo ya kina ambayo unaweza kuhitaji
kuwashirikisha washiriki ikibidi.
Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua kikuu cha kwenye mapafu
MAELEZO MAJIBU
Kifua kikuu cha kwenye mapafu hutokea
kwenye jamii masikini tu. UPOTOSHAJI Kifua kikuu cha kwenye mapafu
unaweza kumpata mtu yeyote. Ingawa, watu
fulani wapo katika hatari kubwa Zaidi ya
kupata kifua kikuu cha mapafu kushinda
wengine. Kama mtu anatambua vihatarishi,
inaweza kupunguza uwezekano wa mtu
kupata kifua kikuu cha mapafu.
Kwa kawaida matibabu ya kifua kikuu cha
kwenye mapafu huchukua miezi 6–8.
KWELI: Matibabu ya kifua kikuu cha kwenye
mapafu kwa kawaida huchukua miezi 6–8 na
yanaweza kufikia hadi miezi 12 kwa kesi
maalumu.
Hakuna tofauti kati ya ugonjwa wa kifua
kikuu cha mapafu na maambukizi ya kifua
kikuu.
UPOTOSHAJI: Mtu mwenye maambukizi ya
kifua kikuu haambukizi kwa kuwa wadudu
hawana athari ama hawaonekani. Mtu
hatambui kama ameambukizwa kwa kuwa
hakuna viashiria wala dalili zinazoonekana.
Mtu mwenye kifua kikuu cha mapafu
ameathirika kwa namna ya tofauti kabisa. Mtu
mwenye kifua kikuu cha mapafu anaweza
kuambukiza na ana viashiria na dalili.
Kama mtu anakohoa naweza kupata kifua
kikuu cha mapafu.
UPOTOSHAJI: Kifua kikuu cha mapafu
hakikoholeki kwa urahisi. Unalazimika kuwa
karibu kabisa na mtu mwenye kifua kikuu cha
mapafu kwa muda mrefu (kwa kawaida masaa
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
20
MAELEZO MAJIBU
mengi au siku nyingi, kama vile gerezani).
Unapaswa kutambua dalili za ugonjwa ili
uweze kutafuta matibabu mapema
iwezekanavyo.
Kifua kikuu cha kwenye mapafu ni ugonjwa
unaoambukiza na unaweza kuenezwa kwa
njia ya hewa.
KWELI: Kifua kikuu cha kwenye mapafu ni
ugonjwa ambao unaenezwa kutoka kwa mtu
mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya
hewa wakati wa kukohoa, kupiga chafya,
kucheka, kuimba, kupiga makelele na hata
kuzungumza. Ikiwa mtu mwenye maambukizi
anakohoa ama kupiga chafya, vijidudu
husambaa hewani ambapo vinaweza kuvutwa
na wale waliopo katika eneo hilo.
Kama mgonjwa anakamilisha matibabu, kwa
kawaida huwa amepona.
KWELI: Kama hakuna usumbufu kwenye
matibabu na yamefuatwa kama ilivyoelekezwa
kwa kipindi husika, kwa kawaida unakuwa
umepona kifua kikuu cha mapafu.
Kumbuka: Kukamilisha matibabu maana yake
ni kumaliza kozi ya matibabu ya kifua kikuu
ndani ya mapafu na kufanyiwa uchunguzi wa
kifua kikuu na madaktari ili kuthibitisha
uponyaji.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
21
Zoezi 7: Kifua Kikuu Magerezani
Dakika 10
Hatua 1: Eleza
Kuzuia ueneaji wa kifua kikuu ni moja ya changamoto kubwa kwenye maeneo ya magereza
hasa pale kunapokuwa na msongomano wa watu.
Hatua 2: Jadili
Ni changamoto zipi zinazojitokeza wakati wa kukabiliana na maambukizi ya kifua kikuu
katika magereza?
Hatua 3: Eleza
Kuna changamoto nyingi: binafsi, kijamii na kiutamaduni, sera, na mazingira, ikiwemo
zifuatazo:
Upungufu wa mbinu za kuthibiti maambukizi na uwepo wa kiwango kidogo cha huduma
za afya kutokana na ufinyu wa rasilimali.
Wafungwa mara nyingi hutenganishwa kwenye vizimba ama sehemu ya wagonjwa bila ya
kufanyiwa vipimo vya kiafya (Wagonjwa wa kifua kikuu hutengwa).
Mlundikano, lishe hafifu, na ukosefu wa hewa ya kutosha.
Idadi ndogo ya wafanyakazi wa afya.
Upungufu wa rasilimali kuendesha uchunguzi wa kiafya na kununua madawa.
Kutofuata masharti ya matibabu miongoni mwa wakazi wenza.
Hatari kubwa miongoni mwa wafungwa kupata usugu wa kifua kikuu (kwa mfano,
wadudu wa TB kupata usugu kutoka kwenye dawa mbalimbali za TB) kutokana na
kutofuata masharti, ingawa utumiaji wa dawa chini ya uangalizi wa mtoa huduma ukiwa
umezingatiwa kila siku.
Zoezi 8: Uhusiano kati ya VVU na kifua kikuu
Dakika 15
Hatua 1: Mapitio
Waambie washiriki kuwa tumezungumzia VVU, kifua kikuu, na madhara ya VVU kwenye
mfumo wa kinga wa mwili wa binadamu.
Hatua 2: Jadili
Jinsi gani maambukizi ya VVU yanaweza kumwathiri mtu mwenye maambukizi ya kifua kikuu.
Pokea maoni machache.
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
22
Hatua 3: Eleza
VVU huongeza kasi ya maambukizi ya kifua kikuu kuwa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa
VVU hudhoofisha mfumo wa kinga. Ukiwa una maambukizi ya VVU una nafasi kubwa ya
kupata kifua kikuu kuliko mtu asiye na maambukizi ya VVU. Bakteria wa kifua kikuu wana
nafasi kubwa ya kuwa na madhara na kushambulia mapafu na sehemu nyingine za mwili.
Hatua 4: Maswali na majibu
Swali: Watu wafanyeje ikiwa wana VVU na kifua kikuu ndani ya mapafu?
Jibu: Wanalazimika kupata matibabu moja kwa moja pasipo kuchelewa ili kupunguza kuugua
zaidi. Kila mmoja anapaswa kutumia dawa zake kwa usahihi kabisa kama daktari au mtoa
huduma za afya alivyowaelekeza.
Hatua 5: Fafanua zaidi
Vidonge vya kifua kikuu ni vikali sana. Vinaweza kutibu kifua kikuu, hata kwa watu wenye
VVU kwa baadhi ya watu. Kumbuka, Vidonge vya kifua kikuu hufanya kazi vizuri pale tu
ambapo hutumiwa kulingana na maelekezo ya mtoa huduma za afya.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
23
SOMO 2: VIWANGO VYA HATARI YA
MAAMBUKIZI YA VVU KWENYE
MAGEREZA
Lengo
Kukuza elimu juu ya vihatarishi vya VVU katika maeneo ya magereza
Dhamira
Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:
Kutambua na kuelezea viwango tofauti vya vihatarishi vinavyochochea hatari ya
maambukizi ya VVU katika magereza.
Kuainisha jinsia na kuchunguza namna gani desturi za kijinsia zinauhusiano na
maambukizi ya VVU.
Kueleza tofauti kati ya kuchukua tahadhari ya VVU na kukabiliana na hatari za VVU
Kutambua viwango vya hatari ya VVU kutokana na tabia mbalimbali za kimapenzi
Kutambua majukumu ya kijinsia yaliyopangwa na jamii kwa ajili ya wanaume na
wanawake.
Kulinganisha njia mbalimbali zilizopo za kujikinga na VVU
Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya maambukizi ya VVU
Masaa 2, dakika 15
Kipindi 2.1: Mazoezi
Utangulizi juu ya ngazi tatu za hatari za VVU
Jinsi na jinsia
Jinsi, jinsia na VVU: Kuchukua tahadhari na kukubaliana na hatari
Kiwango cha hatari
Igiza kama mwanaume, igiza kama mwanamke
Kufanya maamuzi kuhusu jambo linalofaa na lisilofaa
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
24
Zoezi 1: Ngazi tatu za Viwango vya hatari vya VVU
Dakika 10
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi kubwa za kuandikia, ubao wa chaki
Hatua 1: ElezaViwango vya hatari
Wafahamishe washiriki kwamba kuna ngazi tatu za hatari za VVU:
Ngazi ya mtu binafsi
Ngazi ya familia
Ngazi ya jamii
Elezea zaidi kuhusu vihatarishi vya VVU:
Viwango vina uhusiano na mambo ambayo huwaweka watu kwenye hatari ya
maambukizi ya VVU.
Vihatarishi vya VVU katika viwango vya mtu binafsi, familia, na jamii na mifano ifuatayo
kwenye jedwali hapa chini:
NGAZI YA MTU BINAFSI NGAZI YA
FAMILIA NGAZI YA JAMII
Elimu (kwa mfano, Kutokuwa kabisa au
kuwepo na kiwango kidogo cha elimu)
Mtazamo (kwa mafano., dhana ya uwanaume
miongoni mwa wanaume ambayo inapelekea
tabia hatarishi, dhana ya uwanawake
miongoni mwa wanawake inayozuia
majadiliano kuhusu mapenzi salama)
Umri (kwa mfano, wakazi wenza vijana mara
nyingi huwa katika hatari kubwa kimwili,
kiakili, na ukatili wa kijinsia kutoka kwa
wakazi wenza wakubwa)
Matendo ya kimapenzi yasiyo salama
Kuchangia vitu vyenye ncha kali (kama,
nyembe)
Ukosefu wa elimu (kwa mfano, ukosefu wa
elimu kuhusu namna ambavyo VVU
huenezwa)
Matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na
pombe.
Mila za
kitamaduni na
imani
Miiko.
Mila za kijamii
(kwa mafano,
wajibu na
majukumu ya
wanaume na
wanawake)
Sera za serikali
Siasa/uimara wa
kisiasa
Rasilimali (kwa
mfano; ukosefu wa
vifaaa vya
kujifungulia kwa
wafungwa
wajawazito).
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
25
Mazingira ya kizuizi na msongamano
ambayo mara nyingi hupelekea msongo,
wasiwasi, fadhaa, na unyanyasaji, ikiwemo
unyanyasaji wa kimapenzi.
Baadhi ya wafungwa wa kiume wanaweza
kukumbana na unyanyasaji wa kimapenzi
na kushiriki shughuli za mapenzi yasiyo
salama na wanaume wengine kwa
kubadilishana vitu ama huduma, kitu
kinachoongeza hatari kwao kuambukizwa
VVU.
Magonjwa ya ngono, kama herpes,
chlamydia, kaswende, au gono yapo
miongoni mwa wakazi wenza, huongeza
hatari yao kwa VVU.
(Serekali ya Muungano ya Tanzania 2010)
Mazingira hatarishi kwa VVU ndani ya
magereza Hatua 2: ElezaGerezani
Nchini Tanzania, tafiti zinaonesha uwepo wa
kiwango cha juu cha VVU (asilimia 6.7) ndani
ya magereza ukilinganisha na watu wazima
kwingineko (asilimia 5.1)(Das and Horton,
2016) kutokana na mazingira hatarishi
ambayo ni pamoja na: (tazama boksi la bluu).
Tanzania imetia sahihi na kuridhia hati zote
rasmi za haki za binadamu, sheria na sera za
kimataifa (umoja wa kimataifa) na kikanda
kuhusu uzuiaji wa VVU, zinazotoa idhini ya
kuwapima watu VVU kwa hiari, wakiwemo
wafungwa walio katika magereza.
Hatua 3
Kwa kina, jadili nini kifanyike ili kupunguza
mazingira haya hatarishi kwenye magereza.
Zoezi 2: Jinsi na Jinsia
Dakika 20
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi kubwa ya kuandikia na ubao
Maandalizi ya awali:
Andaa alama mbili moja iandikwe “jinsia” na nyingine iandikwe “jinsi” kwa ajili ya zoezi
hili.
Hatua 1: Eleza
Ingawa wafungwa hukaa kwenye vyumba vidogo kulingana na jinsia zao, ni muhimu
kwao kuwa na taarifa kuhusu usawa wa kijinsi, vurugu zenye misingi ya kijinsi, na ukatili
wa kijinsia. Elimu hiyo inaweza kuwasaidia wafungwa baada ya kutumikia vifungo vyao
kuendeleza mila sahihi za kijinsi na usawa wa kijinsi, ikiwa ni pamoja na kupambana na
ukatili wenye misingi ya kijinsi.
Hatua 2: Uliza na jadili maswali yafuatayo:
Jinsi maana yake ni nini?
Jinsi humaanisha sifa za kibaiolojia na kimaumbile za wanaume na wanawake ambazo
hazibadiliki isipokuwa kwa upasuaji. Mifano ya sifa za jinsia ni:
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
26
Viungo vya mwili: uume, uke, matiti, korodani
Maumbile: mzunguko wa hedhi, uzalishaji manii
Muundo wa kijenetiki: kromosomu XX na XY.
1. Jinsia maana yake ni nini?
Jinsia humaanisha kazi, haki, majukumu, fursa, heshima, mipaka, matarajio na wajibu wa mtu
uliopangwa na jamii.
Sifa za jinsi ni:
Hutofautiana miongoni na ndani ya tamaduni
Hubadilika baada ya muda
Kazi na matarajio hupangwa kulingana na jinsia, umri, ukabila, dini, na sababu nyingine
za kitamaduni
Huwahusu wanaume, wavulana, wanawake, na wasichana; si wanawake pekee.
Hatua 3: Eleza
Baadhi ya mila za jinsi na ukosefu wa usawa wa kijinsi huwaweka wanaume, wavulana,
wanawake, na wasichana katika hatari mbalimbali za kupata maambukizi ya VVU:
Wanaume na wavulana wameathiriwa na matarajio ya jinsi ambayo yanaweza
kuhamasisha tabia za kujihatarisha, kupinga upatikanaji wa huduma za afya na kwa kiasi
kidogo kujipangia kazi zao kama wenza na wanafamilia. Kwa wasitani, kiwango cha
upimaji VVU na kupata matibabu ni mdogo miongoni mwa wanaume ukilinganisha na
wanawake. Kote mashariki na kusini mwa Afrika, kuna tofauti kubwa ya utumiaji na
unufaikaji wa huduma kati ya wanaume, wavulana, wanawake, na wasichana. Wanaume
na wavulana hupata huduma za afya kwa kiwango cha chini sana ukilinganisha na
wanawake na wasichana.
Asilimia 54 ya vifo vya watu wazima vyenye uhusiano na UKIMWI vilitokea miongoni mwa
wanaume mashariki na kusini mwa ukanda wa Afrika (makadirio ya UNAIDS 2016).
Huduma za afya haziwafikii wanaume wengi kusini mwa jangwa la Sahara, na hii
huchangia sana wanaume kuhitaji na kutumia kwa kiasi kidogo huduma za VVU katika
kanda hizi. Matarajio ya wanaume kuanza matibabu ni madogo sana, na mara nyingi
hutegemewa kuwa na kiwango cha chini cha CD4 wanapoanza na kukatiza matibabu na
kupoteza ufuatiliaji, hivyo kufikiwa kwa kiasi kidogo kupungua kwa virusi vya ukimwi (
Sonke Gender Justice and Men Engage, 2017).
Ukosefu wa usawa wa kijinsi na usiri wa ukatili wa wenza zinaweza kuwazuia wanawake
na wasichana, hasa wanawake vijana kujikinga wenyewe dhidi ya VVU. Nchini Tanzania,
wanawake wameathirika mno na VVU, Tanzania ina wanawake 690,000 wenye miaka 15
na zaidi waishio na VVU. Kulingana na Utafiti wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria
Tanzania Mwaka 2011–12, (TACAIDS et al. 2011) maambukizi ya VVU kwa wanawake
yalikuwa asilimia 6.2, ukilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume. Wanawake wenye umri
wa miaka 23–24 walikuwa na uwezekano wa kuishi na VVU mara mbili zaidi ya wanaume
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
27
wa umri huo. Wanawake huathiriwa mapema, kwa kuwa wana wapenzi wakubwa na
huolewa mapema. Lakini pia wanakumbana na wakati mgumu kujadiliana kuhusu
mapenzi salama kwa sababu ya ukosefu wa usawa wa kijinsi. Nchini Tanzania asilimia 35
ya wanawake inaaminika wamekumbana na ukatili wa siri kwa wapenzi. Utafiti kutoka
Tanzania unaonesha kuwa huku wanawake wakitegemewa kuwa watiifu kwa wapenzi
wao hata kama wapo kwenye mahusiano mabaya, wanaume wanashawishiwa kujihusisha
na mapenzi ya ziada yasiyosalama.
Hatua 3: Zoezi la jinsi na jinsia
Eleza kwamba sasa tutashiriki katika shuughuli ya pamoja ili kujifunza zaidi maneno jinsi
na jinsia.
Onesha alama mbili ambazo zimetengwa kwa umbali wa fiti kadhaa. Moja ina
neno“jinsia” lililoandikwa juu yake, na nyingine ina neno “jinsi.”
Soma sentensi moja moja na uwaombe washiriki kuhamia kwenye alama ambapo
wanadhani sentensi inaegemea yaani jinsia au jinsi. Baada ya kila mmoja kuhama,
endelea kwa kumwomba mtu mmoja aliyesimama upande mmoja wa chumba aeleze kwa
nini waliamua kusimama upande huo. Uliza ikiwa wengine wangependa kuchangia
sababu zao. Waulize kundi jingine kwa nini wameamua kusimama chini ya alama
waliyopo. Baada ya kufanya hivyo kwa muda soma sentensi inayofuata.
MAELEZO YA JINSIA AU JINSI MAJIBU
Wanawake huzaa watoto Jinsi
Wasichana ni wapole na wakimya Jinsia
Wavulana ni werevu na thabiti Jinsia
Wanawake hunyonyesha watoto Jinsi
Wanaume ni vichwa vya familia zao Jinsia
Wanaume huanzisha mapenzi kwa wenza wao Jinsia
Wanaume wana akili kuliko wanawake Jinsia
Zoezi 3: Jinsi, jinsia, na VVU: Kuchukua tahadhari, kukabiliana na hatari
Dakika 20
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi kubwa za kuandikia au ubao wa chaki
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
28
Hatua 1. Utangulizi
Andika neno “hatari” kwenye karatasi ya ubaoni au kwenye ubao wa chaki. Andika
maelezo yao ya ufafanuzi kwenye karatasi ya ubaoni/ubao wa chaki. Fikieni muafaka
kuhusu maana ya neno hatari (tazama kisanduku)
Hatua 2: Uliza
Waombe washiriki watoe mifano ya mazingira ambayo wanaweza au mtu wanayemjua,
au watu wengine huchukua tahadhari au hukabiliana na hatari za VVU
Hatua 3: Maswali ya kujadiliana:
Kuhusiana na VVU, ni nani anayechukua tahadhari zaidi, mwanaume au mwanamke? Kwa
nini?
Kuhusiana na VVU, ni nani
anayekabiliana na hatari zaidi,
mwanaume au mwanamke? Kwa nini?
Nini faida na hasara za kuchukua
tahadhari na kukabiliana na hatari hizi kwa wanaume na wanawake?
Ni mambo gani mengine yanayoathiri tahadhari za VVU ambazo watu huchukua na
ambazo watu hukabiliana nazo?
Hatari hizi zinaweza kupunguzwa vipi?
Hatua 4: Eleza
Wanawake hukumbana na hatari zaidi za maambukizi ya VVU ukilinganisha na wanaume kwa
sababu ya mila za kijamii na kiutamaduni (jinsia) na sababu za kibaiolojia (jinsi) (tazama
sanduku chini):
MILA ZA KIJAMII NA KIUTAMADUNI
(JINSIA)
SABABU ZA KIBAIOLOJIA (JINSI)
Wanawake mara nyingi hawana nguvu na
maamuzi katika maisha yao ya kimapenzi.
Wanawake hawatarajiwi kujadili au
kuamua kuhusu mapenzi; jambo hili
huchukuliwa kama ni kazi ya mwanaume.
Wanawake wanaweza kuhisi kwamba
hawawezi kuuliza au kusisitiza kutumia
kondomu au njia yoyote ya kujikinga.
Wanawake wanaweza kujisikia, ingawa
hawawezi kukataa kufanya mapenzi hata
kama wanajua wanajiweka katika hatari
ya kupata mimba au kuambukizwa
magonjwa ya ngono au VVU.
Wanawake wana uwezekano mkubwa wa
kupata VVU kutokana na kitendo
chochote kimoja cha kufanya mapenzi
kwa sababu shahawa hubaki ndani ya uke
kwa muda mrefu baada ya kujamiiana, na
hivyo kuongeza uwezekano wa
kuambukizwa. Pia kuna virusi vingi
kwenye shahawa kuliko kwenye majimaji
ya ukeni. Kuta za uke ni laini sana na
zinaruhusu vitu kupenya, na kuruhusu
VVU kupenya, na ngozi laini ya ukeni ni
rahisi zaidi kupata michubuko au
kuchanika kuliko ngozi ya kawaida.
Maana ya hatari:
Hatari ni uwezekano au tishio la kupata
maambukizi (VVU, TB, n.k.), uharibifu, jeraha,
deni, upotevu, au matukio yoyote
yanayoweza kuzuiwa kwa kuchukua hatua
stahiki.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
29
MILA ZA KIJAMII NA KIUTAMADUNI
(JINSIA)
SABABU ZA KIBAIOLOJIA (JINSI)
Baadhi ya wanawake hujihusisha kwenye
mahusiano ya kimapenzi kupata, pesa,
simu, chakula, au namna nyingine za
hadhi na ulinzi.
Wanawake wanaweza kukumbana na
namna nyingi za mizozo kutokana na
unyonge wao katika jamii, na kuongeza
hatari za maambukizi ya VVU.
Wanawake ambao huwaambia wenza
wao kwamba wana ugonjwa wa
ngono/VVU wanaweza kukumbana na
ukatili wa kimwili, kiakili, au hisia au
kuachwa.
Wanawake wanaweza kudai matakwa ya
kimapenzi kwa wenza wao kuzuia,
kuzomewa, kuachwa, kupigwa, au
kuuawa.
Wanawake pia wanategemewa kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na au kuolewa
na wazee, ambao wana uwezekano
mkubwa kuwa na VVU.
Wanaume wanahimizwa kufanya mapenzi
kadri iwezekanavyo, bila kufundishwa
jinsi ya kujilinda wenyewe, na hivyo
kuongeza hatari kwao kuambukizwa VVU.
Kiashiria kikuu cha uanaume na
mafanikio ni kuwa na wapenzi wengi wa
kike kadri iwezekanavyo. Kwa wanaume
waliooa na wale ambao hawajaoa,
wapenzi wengi ni jambo linalokubalika
kiutamaduni.
Wanaume wanaweza kudharauliwa na
kutaniwa kama hawataonesha kwamba
watachangamkia fursa zozote ama zote
za kimapenzi.
Ushindani husisitizwa kwa wanaume
kuonesha ni nani aliye mkuu na bora.
Kiashiria kingine cha uanaume ni kuwa na
uthubutu kwenye mapenzi, ikiwemo
Wanawake wapo katika hatari zaidi ya
kupata VVU wakati wa kujamiiana kuliko
wanaume kwani shahawa zinaweza
kusalia ndani ya uke kwa siku kadhaaa
baada ya kujamiiana, wakati wanaume
hujihatarisha na majimaji yenye
maambukizi ya VVU tu wakati wa
kujamiiana.
Wanaume ambao hawajatahiriwa wana
uwezekano mkubwa wa kuambukizwa
VVU ukilinganisha na wale waliotahiriwa.
Uume haupo kwenye hatari kubwa ya
kusababisha maambukizi kwa sababu
inakingwa na ngozi ngumu ukilinganisha
na uke ambao una sehemu kubwa
inayoweza kuruhusu maambukizi ya VVU
toka kwenye shahawa. Unapokuwa na
magonjwa ya ngono ambayo
hayajatibiwa kunaongeza uwezekano wa
mtu kupata VVU.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
30
MILA ZA KIJAMII NA KIUTAMADUNI
(JINSIA)
SABABU ZA KIBAIOLOJIA (JINSI)
kutotumia kondomu (matumizi ya
kondomu huchukuliwa kama ni ishara ya
udhuru na ni udhaifu).
Wanaume wengi wanaamini kuwa
kondomu hupunguza raha ya mapenzi au
ni kiashiria cha ukafiri na uzinzi.
Matumizi ya kondomu vile vile
yanakinzana na kile kinachoonekana
kama kiashiria muhimu cha uanaume—
kuwa na watoto wengi iwezekanavyo.
Zoezi 4: Viwango vya hatari mchezo wa kadi
Dakika 25
Vifaa vinavyohitajika:
Kadi zilizoandikwa “vielelezo” Andika yafuatayo kwenye kila kadi: Kuacha kabisa, kupiga
punyeto,mapenzi kwenye uke-bila kondomu, kumkumbatia mtu mwenye VVU, Kupiga busu,
mapenzi makavu-bila kondomu, Kuchua, Mwanaume aliyetahiriwa akijamiiana na
mwanamke, Kumnyonya mwanaume uume kwa kutumia kondomu, Kumnyonya mwanamke
ukeni bila kondomu, watoto wachanga kunyonya kwa mama mwenye maambukizi ya VVU,
Mapenzi kinyume na maumbile—bila kondomu
Kadi zilizoandikwa “kadi za hisa”: Andika viwango kwenye kadi za hisa kwa mfano. Hatari
kubwa zaidi, Hatari kidogo, Hatari kiasi, Hakuna hatari yenye uhusiano na ueneaji wa
VVU.
Hatua 1: Fahamisha
Wafahamishe washiriki kuwa wanakwenda kukamilisha zoezi linaloangazia tabia
zilizobeba hatari za kuambukiza VVU.
Weka kadi zenye tabia za kimapenzi kuelekea chini kwenye kitita (tazama orodha chini)
halafu waombe washiriki kuchukua kadi na kuiweka ukutani/sakafuni kwenye kipengele
sahihi, “Hatari kubwa” “Hatari kidogo” “Hatari kiasi” na “ Hakuna hatari” kuhusiana na
ueneaji wa VVU
Kuachana na mapenzi kabisa
Kupiga punyeto
Mapenzi ukeni-bila kondomu
Kumkumbatia mtu mwenye VVU
Kupiga busu
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
31
Mapenzi makavu—bila kondomu
Kuchua
Mwanaume aliyetahiriwa akifanya mapenzi na mwanamke
Kumnyonya uume mwanaume kwa kutumia kondomu
Kumnyonya mwanamke ukeni bila kutumia kondomu
Watoto wachanga kunyonya kwa mama mwenye maambukizi ya VVU.
Mapenzi kinyume cha maumbile-bila kondomu.
Baada ya kadi zote kuwa ukutani/sakafuni, waombe washiriki wapitie mahali ambapo
kadi zimewekwa. Halafu waombe wajitolee kusema kama:
Hawakubaliani na mahali kadi zote zilipowekwa
Hawaelewi uwepo wa kadi zote mahali zilipo
Walipata wakati mgumu kuweka kadi zote.
Hatua 2: Jadili
Jadili uwepo wa baadhi ya kadi, hasa zile zenye utata kuhusu hatari, au kadi ambazo
zimewekwa dhahiri mahali pasipo sahihi. Anza kwa kuwauliza washiriki kwa nini
wanadhani kadi iliwekwa kwenye kipengele fulani. Pitia vipengele hapa chini kama huna
uhakika mahali ambapo tabia fulani inapaswa kuwapo.
Hatari za ueneaji wa VVU kutokana na shughuli za mapenzi
HAKUNA HATARI HATARI KIDOGO HATARI KIASI HATARI KUBWA
Kuachana na
mapenzi
Kupiga punyeto
Kumkumbatia mtu
mwenye VVU
Kupiga busu
Kuwaza tendo la
kimapenzi
Kuchua
Kufanya mapenzi
kwenye uke kwa
kondomu
Kumnyonya mboo
mwanaume
mwenye VVU-
kwa kutumia
kondomu
Kufanya mapenzi
mdomoni na
mwanamke
mwenye VVU
Kutumia
vidole/mikono/vit
u vilivyosafishwa
kabla ya
kuchangia
Watoto wachanga
kunyonya kutoka
kwa Mwanamke
mwenye VVU
Mapenzi kinyume
cha maumbile kwa
kutumia kondumu
na vilainishi
Mapenzi ukeni—
bila kondomu
Mapenzi kinyume
cha maumbile-
bila kondomu
Mapenzi
makavu-bila
kondomu
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
32
Hatua 3: Uliza
Waombe washiriki watazame tabia zilizopo kwenye vipengele vya “Hatari kidogo” na
“Hakuna hatari”. Weka msisitizo kwenye dhana ya kwamba baadhi ya tabia za kimapenzi
zenye kufurahisha zina hatari kidogo au hazina hatari kabisa.
Hatua 4: Hitimisha
Hitimisha na sisitiza kwamba hatari hutegemea mazingira ya tabia au sababu zingine. Hizi
ni pamoja na mila za jinsio, ikiwa kama mwenza ameambukizwa au la, ikiwa kama mtu
ni/si mtoaji au mpokeaji wa tabia za kimapenzi, na ugumu wa kufahamu ikiwa kama
mwenza wa mtu ame/hajaambukizwa VVU.
Kiwango cha hatari kwa kiasi kikubwa kwa tabia hizi kitatofautiana kulingana na sababu
kadhaa. Hizi ni pamoja na mila na ukosefu wa usawa wa kijinsia, ikiwa kama mwenza ni/si
mwathirika wa VVU, ikiwa kama mtu ni/si mtoaji au mpokeaji wa tabia za kimapenzi, historia
ya kimapenzi na hali ya VVU kwa kila mwenza, na matumizi sahihi ya kondomu. Kwa mapenzi
ya mdomoni, uwepo wa vidonda, au fizi zinazotoa damu kunaweza kuongeza hatari ya
kuambukizwa VVU kwa mtoaji.
Zoezi 5: Igiza kama mwanaume, igiza kama mwanamke
Dakika 40
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki
Hatua 1: Uliza
Waulize washiriki kama wamewahi kuambiwa “kuigiza kama mwanaume” au “kuigiza
kama mwanamke.” Wape nafasi ya kuchangia baadhi ya uzoefu ambao mmoja wao
ameusema au kitu kinachofanana kwao. Kwa nini mtu kasema hili? Jambo hili linamfanya
mshiriki ajisikie vipi?
Hatua 2: Sema
Tutatazama kwa kina zaidi aya hizi mbili. Kwa kuzichunguza, tunaweza kuanza kuona namna
ambavyo jamii inatambua maana ya kuwa mwanaume au mwanamke.
Hatua 3: Chunguza “kama mwanaume”
Kwa herufi kubwa, chapa kwenye kipande cha karatasi ya ubaoni maneno, “Igiza kama
mwanaume.”
Waombe washiriki kuchangia mawazo yao kuhusu maana ya maneno haya. Andika
mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
33
“IGIZA KAMA MWANAUME”
Kuwa shupavu
Usilie
Wakoromee watu Usioneshe hisia
Walinde watu wengine (wanawake na
watoto)
Pambana na utakayokabiliana nayo
maishani , usionyeshe uwoga
Kuwa bosi
Ingiza kipato
Miliki wapenzi/wake zaidi ya mmoja
Safiri kutafuta ajira
Hatua 5: Jadili—“kama mwanaume”
Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya
matarajio ya kijamii?
Kunaweza kuwako na mipaka kwa mwanaume kutazamiwa kutenda namna hii? Kwa nini?
Ni hisia zipi wanaume hawapaswi kuzionesha?
Ni kwa namna gani “kujifanya mwanaume” kunaathiri mahusiano ya mwanaume na
mwenza na watoto wake?
Ni kwa namna gani mila za kijamii na matarajio ya “kuigiza kama mwanaume” yana
matokeo hasi kwenye afya ya uzazi na mapenzi kwa mwanaume?
Je inawezekana wanaume kutoa changamoto na kubadili majukumu yaliyopo kulingana
na jinsi?
Hatua 5: Chunguza “kama mwanamke”
Sasa kwa herufi kubwa, chapa kwenye kipande cha karatasi ya ubaoni maneno, “Igiza
kama mwanamke.”
Waombe washiriki kuchangia mawazo yao kuhusu maana ya maneno haya. Andika
mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki.
“IGIZA KAMA MWANAMKE”
Usioneshe hisia
Kuwa mwangalizi
Kuwa mrembo, ila usiwe mrembo sana
Kuwa nadhifu, ila usiwe nadhifu sana
Kuwa mkimya
Kuwa mke mwema
Kuwa mwaminifu
Kuwa mnyenyekevu
Hatua 6: Jadili
Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya
matarajio ya kijamii?
Kunaweza kuwako na mipaka kwa wanawake kutarajiwa kujimudu kwa namna hii? Kwa
nini?
Ni kwa namna gani “kuigiza kama mwanamke” kunaathiri mahusiano ya mwanamke na
mwenza na watoto wake?
Ni kwa jinsi gani mila za kijamiii na matarajio ya “kujifanya mwanamke” yana matokeo
hasi kwenye afya ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke?
Je wanawake wanaweza kuishi kinyume cha mambo haya?
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
34
Je inawezekana wanawake kutoa changamoto na kubadilisha majukumu yaliyopo
kulingana na jinsia?
Hatua 7: Hitimisha
Hitimisha zoezi hili kwa kueleza kwa ufupi baadhi ya majadiliano na kuchangia mawazo
yoyote ya mwisho. Swali la mwisho laweza kuwa kama ifuatavyo:
Shughuli hii ni njia nzuri ya kuelewa maana ya mila za jinsi. Lakini kumbuka kuwa hizi mila za
jinsi zinaweza pia kuathiriwa na matabaka, utamaduni, kikundi fulani, na tofauti nyingine.
Ujumbe ambao wanaume wanaupata kutokana na “kuigiza kama mwanaume” ni pamoja
na:
• Kuwa shupavu na usilie
• Kuwa mwingizaji wa kipato
• Jisimamie na usirudi nyuma
• Fanya mapenzi unapohitaji
• Wanawake ni vitu fulani kuwa navyo—mali
Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi kufuatia “kuigiza kama mwanaume” zina
matokeo (madhara) yafuatayo kwenye mitazamo ya wanaume na uume:
Wanaume wanathaminiwa zaidi kuliko wanawake.
Wanaume wanaogopa kudhuriwa na kuonesha hisia zao.
Wanaume wanahitaji uthibitisho mara zote kwamba wao ni wanaume kweli.
Wanaume hutumia mapenzi kuthibitisha kuwa wao ni wanaume kweli.
Wanaume hutumia nguvu kuthibitisha kuwa wao ni wanaume kweli.
Ujumbe ambao wanawake wanapata kutokana na “kuigiza kama mwanamke” ni pamoja
na:
Kutoonesha hisia na kukaa kimya
Kuwa waangalizi na wajenzi wa nyumba
Jifanye mrembo, ila usiwe mrembo sana
Kuwa nadhifu, ila usiwe nadhifu sana
Fuata miongozo ya wanaume
Mtunze mmeo—mpe starehe ya mapenzi
Usilalamike
Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi kufuatia “kuigiza kama mwanamke” vile vile
yana matokeo (madhara) yafuatayo kwenye mitazamo ya wanawake na uke:
Mara nyingi wanawake hawajiamini
Wanawake huthaminiwa kwanza kama mama na si kama watu
Wanawake huwategemea wenza wao
Wanawake wana maamuzi kidogo kuliko wanaume kuhusu maisha yao kimapenzi
Wanawake wameathirika zaidi na VVU na UKIMWI na ukatili
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
35
Mila za jinsia zisizo na manufaa huongeza hatari ya magonjwa ya ngono na VVU na
mimba zisizotarajiwa, na hutengeneza vikwazo vikubwa kwa maendeleo ya wanawake
kijamii, kiuchumi, na kisiasa.
Zoezi 6: Kufanya maamuzi kuhusu jambo linalofaa na lisilofaa
Dakika 30
Hatua 1: Eleza
Tutatazama mchakato wa kufanya maamuzi sahihi kwa kujitambua ili kujikinga na VVU.
Eleza kwamba watapewa orodha iliyo katika namna tofauti na wanapaswa kuonesha kwa
matamshi au kwenye karatasi kama hatua iliyochukuliwa ilikuwa “sahihi” au “si sahihi”
Hatua 2: Fafanua
Toa maana ya maneno haya: “kufaa” na “kutofaa.”
KUFAA KUTOFAA
“Kufaa inamaanisha kitendo au mwitikio
unaostahili, sahihi, au unaoendana na
mazingira ya uzuiaji VVU na mila za jinsia na
usawa kama ilivyojadiliwa katika shughuli
zilizotangulia.
Kutofaa inamaanisha kitendo au mwitikio
usiostahili, usio sahihi, na usioendana na
mazingira ya uzuiaji wa VVU na mila za jinsi
na usawa kama ilivyojadiliwa katika shughuli
zilizotangulia.
Hatua 3: Soma
Kariri hadithi ya kwanza (ukurasa unaofuata) halafu washiriki waseme wapi panafaa na
wapi hapafai na kwa nini.
Hatua 4: Jadili
Kufungua mjadala wa ukweli kuhusu mapenzi inaweza kuwa jambo gumu lakini ni
mhimu.
Watu wenye madaraka wasitumie vibaya nafasi zao kuwalazimisha wengine kutenda
kinyume na matakwa yao.
Watu wanapaswa kuheshimu haki za wengine kuchagua kama wanataka kufanya
mapenzi na kufanya mapenzi salama kwa kutumia kondomu za kike au kiume.
Ili mradi tabia za kimapenzi ni jambo la maridhiano pasipo kuumiza au kujeruhi, wengine
hawapaswi kuingilia.
Wapange washiriki wawili wawili halafu wape eneo la kujadili na kuamua kama linafaa au
halifai. Wape dakika 10 kufanya hivyo na elezea kwa kifupi kila eneo.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
36
Simulizi za Matukio
Tukio 1: Kumtembelea daktari
Afisa magereza ameambiwa na daktari kuwa ana kifua
kikuu, ambayo ni maambukizi nyemelezi ya kawaida
kwa wale waishio na VVU. Daktari akashauri kwamba
wote wawili afisa magaereza na mwenzi wake wapate
ushauri nasaha na kupima VVU. Afisa magereza
akamweleza mpenzi wake kuwa kikohozi chake
kisichoisha kinasababishwa na hali mbaya ya ubaridi
baada ya muda kitaisha.
Haifai: Afisa magereza ana wajibu wa kumfahamisha mwenza wake ukweli kuhusu mkutano
wake na daktari na kumpa nafasi mwenza wake kujilinda na kushughulika na uwezekano wa
kuwa mwathirika wa VVU.
Tukio 2 : Fadhaa za magonjwa ya ngono
Mfungwa ambaye hivi karibuni ameachiliwa kutoka gerezani amekutana na binti/kijana
mtaani na kuanza mahusiano naye kimapenzi. Siku moja wakati akioga, binti/kijana aliona
kidonda chekundu kwenye sehemu zake za siri. Anaona soni sana kuzungumza na mwenzi
wake lakini alimpeleka hospitali ili kupata vipimo na kumweleza dakitari kuhusu kidonda.
Haifai: Ni muhimu kabisa kumfahamisha mpenzi wako kuhusiana na ugonjwa wowote wa
ngono (VVU au vinginevyo) unaoutambua ili aweze kuchunguzwa. Hii si kwa ajili ya afya zao
tuu, lakini pia kwa ajili ya afya ya jamii nzima kwa sababu ugonjwa ukitibiwa mapema, ndivyo
unavyoweza kudhibitiwa mapema na kupunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine.
Tukio 3: Hakuna zawadi ya bure
Afisa magereza amekuwa akimchumbia msichana anayeuza machungwa na mayai sokoni.
Alinunua vitafunwa vyake kila mara alipomwona, pamoja na kumpa zawadi ndogo ndogo.
Alikuwa na usongo wa kufanya mapenzi nae. Jioni moja walipigana busu na alimtomasa
matiti yake. Mzuka ulimpanda sana lakini binti alisema hayuko tayari. Alimsukuma binti chini,
akamkandamiza mikono yake chini na akajilazimisha hadi akazama ndani yake.
Haifai: Afisa magereza huwenda alifikiri binti “alipaswa kumpa”mapenzi kwa kuchukua
chakula na zawadi lakini hakuwa na haki ya kumbaka. Ubakaji huongeza hatari ya
maambukizi ya VVU kwa kuwa wabakaji mara chache sana hutumia kondomu na kitendo cha
kutumia nguvu kufanya ubakaji hupelekea kuchanika kwa kuta za uke au njia ya haja kubwa.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani
37
Tukio 4: Matumizi mabaya ya cheo
Siku moja, mwalimu mkuu katika chuo cha mafunzo alimwomba mmoja wa wanafunzi wake
wa kike kubaki baada ya vipindi kwisha na kumwambia kwamba alitaka kujadiliana naye
kuhusu maendeleo yake kitaaluma. Baada ya vipindi msichana alibaki na mkuu wa chuo
alimsifia sana kuhusu uzuri wake. Kitendo hicho cha kumsifia kilimchukiza sana msichana,
lakini hakusema chochote kwa kuwa alikuwa mwalimu wake. Mwalimu alipoona kwamba
msichana hajafurahi, alimwambia awe makini sana, kwani matokeo ya maendeleo yake
kitaaluma yalikuwa mikononi mwake, na alimwomba msichana kwenda nyumbani kwake jioni
ile, kitu ambacho msichana alitii kwani aliogopeshwa kuwa hatafaulu mitihani yake.
Haifai: Mwalimu hakupaswa kutumia cheo chake au nafasi yake kumtisha msichana mdogo.
Ingawa msichana alikwenda nyumbani kwa mwalimu, ilikuwa ni kwa sababu ya vitisho
kwamba uhalali wa matokeo yake kitaaluma ungeharibiwa kama asingefuata alichoambiwa
na mwalimu kufanya.
Tukio 5: Tabia za kutowajibika
Afisa magereza alihamishwa kwenda gereza la wilaya ambapo alidhani angepaswa kwenda
bila ya mke wake na watoto ili kuepusha usumbufu kwao kuhusiana na mambo ya shule na
familia. Afisa alikaa peke yake katika makazi yake mapya. Siku moja, alipokuwa baa, alikutana
na mwanamke na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi ulioendelea kwa kipindi fulani. Pamoja
na kuwa Afisa alikuwa ameoa na akijua kuwa mwanamke huyu alikuwa na mpenzi mwingine,
hakuona hili kama ni tatizo. Mwanamke alisisitiza kutumia kondomu, lakini Afisa hakuona
umuhimu wa kondomu, na baadaye baaada ya muda mwanamke aliacha kusisitizia.
Haifai: Pamoja na kwamba wote wawili walikuwa wawazi kuwa wana wapenzi wengi lakini
hawakuwajibika kwa kufanya mapenzi yasiyo salama, jambo ambalo haliwaweki wao tu katika
hatari lakini pia linawaweka wenzi wao wengine katika hatari ya maambukizi ya VVU, ambao
huenda hawafahamu kuwa wenzi wao walikuwa wakifanya mapenzi na watu wengine, na
mapenzi yasiyo salama.)
Tukio 6: Woga usiotakiwa
Mfungwa ajulikanaye kama Victor alihamishiwa kwenye chumba kimoja kidogo kutokana na
umri wake mdogo ukilinganisha na wengine ambao walionekana mabingwa na wenye
kupenda kutaniana. Victor alikuwa mpole na mwenye aibu na mara nyingi alipendelea kukaa
peke yake. Kwa tabia hiyo wenzake walimtania kwa kumwita mwanamke nakadhalika. Siku
moja wenzake walimzunguka, wakamsukuma, na kumvua suruali yake ili kuthibitisha kama
kweli alikuwa mwanaume au la. Mmoja wao alimshika kwa nguvu na kumtisha.
Haifai: Ingawa walikuwa ni wakazi wenza wa kiume, ukandamizaji na matendo mabaya
yanaweza kutokea kutokana na tofauti ya nguvu za mamlaka. Waelimisha rika wanapaswa
kujadiliana na wafungwa nini kinapaswa kufanyika kwenye tukio kama hili na taratibu
zinazopaswa kufuatwa katika kuripoti tukio kama hili.)
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
38
SOMO 3: KIFUA KIKUU NA VVU:
MATIBABU, HUDUMA NA MSAADA
Lengo
Kupata maelezo ya msingi kuhusu kinga, matibabu, huduma, na msaada wa Kifua kikuu
na VVU.
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:
Kueleza umuhimu wa kujua hali yako ya kifua kikuu na VVU.
Kueleza maana ya upimaji VVU wa hiari na ule unaoasisiwa na mtoa huduma.
Kuelezea umuhimu wa huduma za upimaji VVU.
Kujadili dawa za kupunguza makali na mahali pa kupata huduma na msaada.
Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia kondomu za kike na kiume.
Kueleza kwa kifupi upatikanaji wa matibabu mengine kwa matatizo mtambuka ya kiafya
kama vile, magonjwa ya ngono, maambukizi kwenye njia ya uzazi, na maambukizi
nyemelezi.
Kueleza maana ya maneno kinga ya maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto na kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza mama mwenye VVU na mtoto.
Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU
Dakika 145
Kipindi 3.1: Mazoezi
Kuelezea maana ya maneno
Ufunguzi kuhusu upimaji wa VVU
Kweli/Uongo kuhusu upimaji VVU
Upimaji wa VVU kwa ujumla
Upimaji wa VVU gerezani
Matumizi ya kondomu za kike na kiume
Dhamira
Mwisho wa kipindi hiki washiriki wataweza:
Kufafanua upimaji wa hiari na ulioasisiwa na mtoa huduma
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
39
Kueleza umuhimu wa kujua hali ya VVU
Kujadili umuhimu wa huduma za kupima VVU
Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia kondomu za kike na kiume
Zoezi 1: Kueleza maana ya maneno muhimu
Dakika 30
Shirika la afya duniani lilibadilisha maneno yao mwezi wa saba 2015 kutoka “ Ushauri nasaha
na upimaji wa VVU” kuwa “Huduma za upimaji wa VVU,” na nchi zinafuata inavyostahili
zinapokuwa zinahuisha miongozo yao. Maneno huduma za upimaji wa VVU yanatumika
kujumuisha huduma zote zinazopaswa kutolewa pamoja na upimaji wa VVU: ushauri nasaha
(maelezo ya ushauri nasaha kabla na baada ya kupima); zilizounganishwa na huduma stahiki
za kinga, matibabu na usimamizi na huduma zingine za kliniki na msaada; na kushirikiana na
huduma za maabara ili kusaidia uthibiti wa ubora na utolewaji wa majibu sahihi.
Hatua 1
Waambie washiriki kuwa watatumia dakika takribani 30 au chini yake wakitazama baadhi
ya maneno muhimu ambayo watakuwa wakiyatumia katika kipindi hiki na kwa muda
mrefu baada ya kozi.
Chaguo 1
Kwa kutumia karatasi ya ubaoni iliyoandaliwa yenye vifupisho vyote, ligawe kundi katika
timu mbili. Waambie washiriki kwamba watacheza mchezo wa vifupisho. Wafahamishe
kuwa vifupisho hivi vimeandikwa kwenye karatasi ya ubaoni ambayo mtaifungua mchezo
utapoanza. Taja kuwa kila kikundi kitachagua mwakilishi ambaye atachagua kifupisho
kimoja na kuwaambia wanakikundi maana yake. Atakapopatia kundi litapata alama 2
lakini akikosea kundi litapoteza alama 2. Waambie kuwa watapeana zamu mpaka
vifupisho vyote vitakapokwisha.
Chaguo 2
Waalike washiriki kukaa wawili wawili na kuchukua kipande cha karatasi. Wafahamishe
kwamba utatamka kifupisho ili wao waandike kwa kirefu kama pea. Kwa ufafanuzi zaidi
ziunganishe pea mbili ili ziweze kusahihishiana pale unapokuwa ukitoa majibu sahihi
kama yalivyotolewa kwenye kisanduku cha maneno kulia kwako
Hatua 2: Pongezi
Pongeza kundi zilizopata majibu kwa usahihi zaidi.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
40
Zoezi 2: Utangulizi kuhusu upimaji wa VVU
Dakika 20
Hatua 1: Eleza
Katika kipindi hiki tutatazama/zungumza mambo
kadhaa ya huduma za uchunguzi, uangalizi, matibabu,
na msaada, ikiwemo upimaji VVU wa hiari, upimaji
VVU ulioasisiwa na mtoa huduma na kuzuia
maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa
mtoto.
Hatua 2: Tamka
Shabaha mpya duniani 90–90–90 zinatoa wito
kwamba asilimia 90 ya watu waishio na VVU
kufanyiwa uchunguzi, asilimia 90 ya watu wenye VVU
waliofanyiwa vipimo kupatiwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, na asilimia 90
ya wale wanaotumia dawa za kupunguza makali wanalazimika kuwa na kiwango kidogo cha
virusi ifikapo 2020. Asilimia 90 ya kwanza (upimaji wa VVU), ni muhimu kwenye asilimia 90 ya
pili (kuanzishiwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa watu
waishio na VVU), na matokeo ya msingi ya asilimia 90 ya tatu (kupungua kwa virusi miongoni
mwa watu wanaotumia dawa za kupunguza makali virusi vya ukimwi), ambayo huboresha
matokeo ya wateja na kuzuia ueneaji wa VVU. Huku ikiwa ni jambo muhimu kupata watu
wengi zaidi kufanyiwa vipimo na kufanikiwa kuwafikisha kwenye huduma za matibabu na
uangalizi, ni muhimu kwamba kiwango cha ongezeko kisididimize ubora wa huduma.
Hatua 3: Zoezi la kikundi
Zoezi hili linazingatia faida na hasara kwa mtu kujua hali yake ya VVU.
Kabla ya kuanza zoezi, waulize washiriki kama wanafikiri ni lazima kujua hali zao za VVU.
Wapange washiriki katika makundi ya watu 4 ili waweze kujadili na kuorodhesha faida na
hasara za mtu kujua hali yake ya VVU.
Wape washiriki dakika 10 kufanya hivyo.
FAIDA MAELEZO
Ishi kwa muda mrefu Mpaka sasa dawa za kupunguza makali zimeweza kuimarisha afya
za watu waishio na VVU, na kwa kiasi kikubwa zimesaidia
kurefusha maisha kuanzia miaka 5–20. Inawezekana pia kuongeza
kipindi ambacho mfungwa mwenye maambukizi anaweza kuishi
kwa kubadili mfumo wa maisha na kupata matibabu ya
maambukizi nyemelezi. Kwa mfano, kujiepusha na hatari zaidi,
kupunguza unywaji wa pombe, na kula vizuri kunasaidia
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
41
FAIDA MAELEZO
kurefusha maisha.
Kunamaliza wasiwasi
kuhusu hali yako
Kupima VVU kunaondoa wasiwasi kwamba umeambukizwa au la.
Wale wenye wasiwasi kuhusu tabia zao za zamani wanaweza
kupata nguvu mpya ya maisha kwa kutambua hali zao.
Kuanza kujikinga upya Kutambua kuwa hujaambukizwa VVU kunakupa wewe mwanzo
mpya ulio safi ambao kwao kunaweza kujengwa utamaduni wa
kufanya mapenzi salama. Kumbuka kwamba robo tatu ya watu
waliopima hawajaambukizwa.
Kuweka mipango ya
maisha yako yaliyobaki
Kwa wapenzi wachanga, kupima pamoja kabla ya kuoana
kunawawezesha kutambua ya kuwa wanaweza kupata watoto
ambao hawajaambukizwa ikiwa wataendelea kujikinga na
maambukizi. Wale watakaogundua kuwa wameambukizwa VVU
wanaweza sasa kupanga maisha yao yaliyobaki. Inaweza kuwa ni
miaka mingi ijayo kabla hawajaanza kuugua na hatimaye kufariki.
Wakati huo huo, wanaweza kuwakinga wenza wao na maambukizi
na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto. Wanaweza pia kupanga dhamana za hapo baadaye kwa
familia zao kwa kuandaa usia na kuweka mipango ya kifedha.
Hatua 4: Wahakikishie
Washukuru washiriki kwa ushiriki wao na eleza kuwa mara tutapoelewa ukweli kuhusu
VVU tutaweza kupunguza ueneaji wake na kuishi kwa muda mrefu, maisha yenye afya.
Pia tunaweza kujilinda na kuwalinda wengine kutokana na maambukizi ya VVU kwa kwa
kupunguza vihatarishi tunazokumbana nazo gerezanni na mara baada ya kutoka. Kama
mwelimisha rika, unaweza kuwahakikishia kuwa kama mwongozo wa kitaifa kuhusu VVU
utafuatwa na wafungwa na wafanyakazi wa magereza tunaweza kupunguza hatari nyingi za
maambukizi ya VVU magerezani na kusaidia upimaji wa VVU.
Zoezi 3: Kueleza maana ya ushauri nasaha na upimaji wa hiari na ushauri
nasaha na upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa huduma
Dakika 20
Hatua 1: Dadisi
Waulize washiriki wanafikiri nini tofauti kati ya upimaji VVU kwa hiari na ulioasisiwa na
mtoa huduma?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
42
Hatua 2: Elezea jedwali lifuatalo
USHAURI NASAHA NA UPIMAJI WA
HIARI
USHAURI NASAHA NA UPIMAJI WA VVU
ULIOASISIWA NA MTOA HUDUMA
Mtu huchagua kutafuta vipimo. Mtu anatafuta huduma za matibabu, halafu
upimaji unapendekezwa na kufanywa na daktari
kama sehemu ya mashauriano.
Huduma pasipokuweka jina au huduma
za siri zinaweza kutolewa.
Huduma zitolewazo ni za siri na hutunzwa
kwenye kumbukumbu za hospitali ili kuhakikisha
mwendelezo wa huduma.
Lengo la msingi limejikita katika kuzuia
ueneaji wa VVU kwa kutathimini hatari,
kupunguza hatari, na upimaji.
Lengo la msingi ni kuwatambua watu
walioambukizwa VVU na kuwaunganisha na
huduma za kinga, uangalizi na matibabu.
Maridhiano kwenye maandishi au alama
za vidole kwa wasiojua kuandika na
kusoma huhitajika.
Maridhiano ya mdomo huhitajika na yanapaswa
kutunzwa kwenye kumbukumbu za mgonjwa.
Mtumiaji wa kwanza wa matokeo ya
vipimo ni mteja, anayetumia taarifa
kufanya maamuzi binafsi ya maisha
yake.
Mtumiaji wa kwanza wa matokeo ya vipimo ni
mtoa huduma za afya kufanya uchunguzi sahihi
na kutoa matibabu sahihi.
Hatua 3: Faida za upimaji wa vvu ulioasisiwa na mtoa huduma
Waulize washiriki wanafikiri ni zipi faida za upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa huduma?
Elezea yafuatayo:
Huwasaidia wataalamu wa afya kuwatibu wateja wao kwa usahihi kwa kuwatambua wale
wanaohitaji matibabu/au program za uzima mapema.
Huwasaidia watoa huduma za afya kuboresha huduma za matibabu zitolewazo kwa
wateja wao na kupunguza ugonjwa na vifo.
Inasaidia kupunguza unyanyapaa katika jumuiya kama magerezani kwa kufanya upimaji
wa VVU kuwa ni jambo la kawaida.
Hatua 4: Sisitiza
Sisitiza kwamba bila kujali ni njia gani ya upimaji imetumika, kanuni tano za upimaji wa
VVU zinapaswa kufuatwa. Waulize washiriki “kanuni za upimaji wa VVU” ni nini. Washiriki
wanaweza kujibu au unaweza kueleza kanuni hizi tano kama ifuatavyo:
KANUNI ZA
UPIMAJI WA
VVU
MAELEZO
Ushauri Ushauri nasaha ni majadiliano baina ya mshauri wa VVU aliyepata mafunzo
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
43
KANUNI ZA
UPIMAJI WA
VVU
MAELEZO
nasaha na mteja anayetafuta kupunguza kupata na kueneza VVU kupitia:
- Maelezo: Mteja hupokea maelezo kuhusu ueneaji na namna ya kujikinga na
VVU na maana ya matokeo ya vipimo vya VVU. Watu ambao hupima na
kuonekana hawana maambukizi ya VVU wanapaswa kupata maelezo ya
afya kwa kifupi juu ya matokeo ya vipimo vyao.
- Ushauri nasaha na kinga ya VVU: Wateja hupokea msaada ili kutambua
tabia hatarishi mahususi zinazopelekea kupata au kueneza VVU na kupiga
hatua ya kupunguza hatari hii.
Mpaka leo tafiti hazijaonesha kwamba kutoa ushauri nasaha kwa muda
mrefu kunahitajika au kunamanufaa zaidi. Isitoshe, utoaji ushauri nasaha kwa
muda mrefu baada ya vipimo kwa watu ambao hawakukutwa na maambukizi
unaweza kuelekezwa kwingine rasilimali zilizotengwa kwa ushauri nasaha
ambazo zinahitajika na wale wanaokutwa na VVU, wale ambao majibu yao
bado hayana hitimisho, na wale waliokutwa katika mahusiano ambayo
mmoja wao ana VVU na mwingine hana VVU
Kuridhia Mtoa vipimo amekupatia maelezo ya kina ili uweze kufanya maamuzi sahihi
kwa kujitambua kuhusu ikiwa kama unataka kupima au la, ikiwa ni pamoja na
uhuru wa kukataa kupima. Maelezo yanapaswa kugusia, vipimo vinahusisha
nini, majibu tarajiwa, na uwezekano wa matokeo yatokanayo. Upimaji wa
lazima haufai.
Usiri Kile unachokijadili na mshauri kitabaki kuwa siri yenu wawili. Mshauri
hataweza kumwambia mtu mwingine yeyote mlichokijadili au nini matokeo
ya vipimo vyako.
Usahihi Watu wote ambao vipimo vyao vinaonesha wana VVU wanapaswa kupimwa
tena ili kuthibitisha vipimo vyao kabla ya kuanzisha huduma na matibabu ya
VVU.
Mshikamano Kutoa huduma za upimaji VVU mahali ambapo hakuna upatikanaji wa
huduma, au uunganishwaji dhaifu kwenye huduma, ikiwepo dawa za
kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, una manufaa kidogo kwa wale wenye
VVU.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
44
Zoezi 4: Upimaji VVU: Zoezi Kweli/Uongo
Dakika 15
Hatua 1: Zoezi
Waelezee washiriki kuwa utataja orodha ya maelezo. Ungependa wao wasimame ikiwa
maelezo ni KWELI, au wakae ikiwa wanadhani maelezo ni UONGO. Waambie kuwa
utawauliza waeleze sababu za majibu yao.
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
Upimaji pasipo kutumia
jina maana yake unapewa
namba na hakuna anayejua
jina lako unapopimwa.
KWELI: Kutuliza hofu na kupunguza unyanyapaa baadhi ya
huduma za upimaji haziwahitaji wale walifanyiwa vipimo kutoa
majina yao. Sampuli ya damu zao hutambuliwa kwa kutumia
namba pekee. Huduma za upimaji wa VVU zinapaswa kuwa siri,
maana yake kile ambacho mtoa huduma na mteja wanajadili
hakitatolewa kwa mtu yeyote bila ya ridhaa ya mtu
anayepimwa. Usiri unapaswa kuheshimiwa, lakini usiruhusiwe
kutilia mkazo siri, unyanyapaa, au fedheha.
Mtu akigundulika kuwa na
VVU baada ya kufanya
vipimo ya lazima basi moja
kwa moja hufukuzwa kazi.
UONGO: Upimaji wa hiari unathaminiwa na watu wenye VVU
hawapaswi kufukuzwa kazi. Ingawa, baadhi ya waajiri huhitaji
wafanyakazi kupima kabla ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi.
Mtu anayekutwa na maambukizi ya VVU kwa kawaida
huruhusiwa kuendelea kufanya kazi lakini haruhusiwi kusafiri
nje ya nchi.
“Kipindi cha mficho” ni
kipindi ambacho kinga
dhidi ya VVU huenda
isionekane kwenye damu
ya mtu aliyeambukizwa.
KWELI: Huchukua hadi kati ya miezi mitatu hadi sita kwa kinga
ya VVU kuonekana kwenye damu. Ushauri siku zote kwa kila
anayepima VVU na kujikuta hana maambukizi ni kupima tena
baada ya “kipindi cha miezi mitatu” si sahihi. Marudio ya
upimaji yanahitajika kwa wale tu ambao matokeo ya vipimo
vyao yanaonesha hawajaambukizwa ambao wameripoti hivi
karibuni (miezi mitatu iliyopita) au uwepo katika hatari
enderevu. Kwa watu wengi ambao hawana maambukizi ya VVU
baada ya kupima, upimaji kwa mara nyingine kufanya uamuzi
wakati wa kipindi cha mficho si lazima na inaweza kupoteza
rasilimali.
Wale wanaokutwa bila
maambukizi ya VVU baada
ya kupima hawapaswi
kujizuia na tabia hatarishi
hapo baadaye
UONGO: Mtu anaweza kujiingiza katika mahusiano hatari ya
kimapenzi pasipo kuambukizwa. Lakini hii haimaanishi kuwa
hawataambukizwa kwenye shughuli zao za kufanya mapenzi
yasiyo salama zinazofuata
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
45
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
Kila mmoja anapaswa
kupimwa.
KWELI: Upimaji wa VVU ni njia ya kujikinga, kupata matibabu,
uangalizi, na huduma zingine za msaada dhidi ya VVU. Uelewa
wa watu juu ya hali zao za VVU kupitia huduma za upimaji ni
muhimu kwenye mafanikio ya kupambana na VVU. Wigo wa
upimaji VVU miongoni mwa watoto ni mdogo. Mbinu
zinahitajika kuongeza uchunguzi wa mapema kwa watoto
wachanga na kuwaunganisha kwa wakati watoto wachanga
watakaogundulika kuwa na VVU kwenye matibabu na huduma.
Mbinu za ziada zinahitajika kuongeza utumiaji wa huduma za
upimaji VVU miongoni mwa wanaume, ikiwemo utolewaji wa
huduma za upimaji VVU katika maeneo ambayo yanafaa zaid
na kukubalika na wanaume, na kubadili njia za kuwahimiza
upimaji wa wenza wa wanaume katika maeneo ambapo kuna
uwepo mkubwa na kwa wapenzi na wenzi wa wanaume na
wanawake wenye VVU kwenye maeneo yote. Kuyafikia
makundi maalumu ya watu, kama vile wakazi wenza, ni jambo
la kupewa kipaumbele.
Kama mtu atagundulika
kuwa na VVU mtu huyu
anapaswa kuwaeleza wenzi
wake wote kuhusu majibu
ya vipimo.
KWELI: Ingawa kuweka wazi kwa wapenzi, wanafamilia wenye
msaada, na wafanyakazi wa afya, mara nyingi kuna manufaa,
hii inapaswa kufanywa na au kwa ridhaa ya mtu aliyepimwa.
Ushauri nasaha kwa wateja wenye VVU inapaswa kujadili
majibu yanayowezekana kuwekwa wazi, na hatari na manufaa
ya kuweka wazi, hasa miongoni mwa wanandoa na wapenzi.
Wape ushauri ili kusaidia kuweka wazi kwa pamoja. Wanandoa
na wenzi wanapaswa kupewa ushauri nasaha na upimaji wa
hiari pamoja na msaada wa kuweka wazi kwa pamoja. Mshauri
anapaswa kutazama hatari za vurugu za ndani za wapenzi na
kujadili hatua zinazowezekana ili kuhakikisha usalama wa
kimwili wa mteja hasa wanawake ambao wamegundulika kuwa
na VVU.
Mtu wa kwanza kwa
wanandoa kugundulika na
VVU ndiye aliyeleta virusi
kwenye familia.
UONGO: Wakati ambapo mtu anajua kuwa ana maambukizi ya
VVU hauna uhusiano na muda alioambukizwa. Baada ya
kipimo kuonesha uwepo wa VVU, unapaswa kuhimiza na
kuwapima wenzi, watoto, na wanafamilia wengine wa mteja.
Jambo hili linaweza kuwa mmoja mmoja, vipimo kwa wapenzi,
kupima kwa pamoja, au kumfahamisha mwenza kwa ridhaa.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
46
Zoezi 5: Upimaji wa VVU uraiani na magerezani
Dakika 30
Hatua 1: ElezaUpimaji wa VVU
Kupima VVU ni njia pekee na muhimu kujua kama una VVU. Ikiwa una VVU, ni jambo
muhimu kutambua ugonjwa. Jambo hili litakupa nafasi nzuri ya kupata matibabu na
huduma unazohitaji ili kuishi kwa afya. Unapokwenda kupima VVU, utakuwa na nafasi
kuzungumza na mtu aliyepata mafunzo, hivyo unaweza kuuliza swali lolote amabalo
unaweza kuwa nalo. Mtu anayekupima atakupatia maelezo jinsi ambavyo vipimo
vinafanyika na jinsi utavyopata majibu.
Kutegemeana na aina ya kipimo, utachukuliwa sampuli ndogo ya damu kutoka mkononi
mwako, au tone la damu kutoka kwenye kidole chako. Kuna baadhi ya vipimo hufanyika
kwa kutumia maji maji yanayopatikana kuzunguka fizi.
Kuna aina mbalimbali za vipimo vya VVU. Baadhi ya vipimo vya VVU huonesha uwepo wa
virusi halisi kwenye damu (kipimo cha antijeni) na vipimo vingine huonesha kinga za VVU
zinzofanya kazi ya kupambana na VVU. (kipimo cha kinga).
Ikiwa vipimo vitaonesha kuwa una VVU, inamaanisha una maambukizi ya VVU. Ikiwa
vipimo vitaonesha kuwa huna VVU, maana yake huna maambukizi ya VVU. Kwa baadhi ya
vipimo utahitaji kufanyiwa vipimo vya ufuatiliaji ikiwa majibu ya yataonesha kuwa una
maambukizi ya VVU.
Hatua 2: Maswali na majibu kipindi cha mficho
Swali: Kipindi cha mficho maana yake nini?
Jibu: Kipindi kuanzia ulipoambukizwa VVU mpaka pale ambapo mwili utatoa kinga ya
kutosha kwa VVU itakayoweza kuonekana kwa kutumia kipimo cha kinga ya VVU hujulikana
kama kipindi cha mficho. Watu wengi huweza kutengeneza kinga ya VVU ndani ya miezi
mitatu mara baada ya kupata maambukizi ya VVU. Lakini kipindi cha mficho kinaweza
kutofautiana kulingana na kipimo cha VVU kilichotumika. Kwa ujumla, mtu yeyote mwenye
matokeo hasi kupitia kipimo cha kinga ya VVU ndani ya miezi mitatu ya uwezekano wa kuwa
na VVU, anapaswa kupima tena baada ya miezi mitatu.
Hatua 3: Maswali na majibuupimaji wa VVU
Swali: Kipimo cha antijeni ni nini?
Jibu: Kipimo cha antijeni hugundua antijeni za VVU (sehemu ya virusi) kwenye damu. Kipimo
cha antijeni kinaweza kugundua maambukizi ya VVU kabla ya kinga ya kutosha ya VVU
haijatolewa ili kuweza kugunduliwa kwa kipimo cha kinga ya VVU.
Swali: Inachukua muda gani kupata majibu ya vipimo vya VVU?
Jibu: Matokeo ya haraka ya kipimo cha kinga ya VVU yanaweza kutolewa ndani ya dakika
15–30. Ingawa, inaweza kuchukua siku kadhaa au wiki kadhaa, kutegemeana na aina ya
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
47
kipimo kilichotumika. Katika Tanzania matokeo chanya ya kipimo cha VVU ni lazima
yathibitishwe kwa kipimo cha uthibitishaji.
Swali: Watu waliopo nje ya gereza wanaweza kwenda kupima wapi?
Jibu: Watoa huduma za afya wanaweza kukufanyia vipimo vya VVU. Vipimo vya VVU vile vile
vinapatikana katika hospitali nyingi, kliniki za matibabu, vituo vya afya vya jamiii, vituo vya
ushauri nasaha na upimaji kwa hiari, na mashirika ya huduma za UKIMWI.
Hatua 4: Maswali na majibu—vipimo vya VVU gerezani
Swali: Ukiwa gerezani vipimo vya VVU hufanyika vipi?
Jibu: Vipimo vya VVU hutolewa katika vituo vya afya vya magereza ikiwemo huduma za
kliniki za ushauri nasaha na upimaji kwa hiari zinazotembea ambazo hutembelea maeneo ya
magereza. Ingawa, upimaji wa lazima kwa wafungwa ni kinyume cha maadili na hauna
ufanisi, upimaji unapaswa kuwa wa hiari ukiambatana na ushauri nasaha kabla na baada ya
kupima. Matokeo yanapaswa kutolewa kwa wafungwa na mfanyakazi wa afya ambaye
anapaswa kuhakikisha kutunza siri za kihospitali.
Hatua 5: Maswali na majibu—bada ya kugundua ugonjwa
Swali: Je unapaswa kufanya nini ikigundulika una VVU au hauna maambukizi ya VVU?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
48
UFANYE NINI IKIWA HUNA VVU
Kuachana kabisa na shuguli za
mapenzi ni njia bora zaidi kuzuia
kupata VVU. Kuepuka maambukizi
huja pale unapokuwa mwaminifu
kabisa kwa mpenzi mmoja, inayohitaji
wewe na mpenzi wako anagalau
kupima VVU kila mmoja, kwa
anagalau miezi mitatu tofauti; na
mkiamua kufanya mambo ya mapenzi
ya ndani ya(uke, mdomo, na njia ya
haja kubwa) kwamba mtumie kwa
usahihi kondomu ya kike au kiume.
UFANYE NINI IKIWA UNA VVU.
Kitu cha kwanza ambacho kliniki itakifanya ni
kupima kiwango cha CD4. Watachukua damu kutoka
kwako itakayopelekwa maambara ili kupima idadi ya
seli za CD4 kwenye ujazo wa mililita moja ya damu.
Hii itakusaidia kujua mfumo wako wa kinga una afya
kiasi gani. Inapendekezwa kuwa watu wenye VVU
wapime viwango vya CD4 zao kila baada ya miezi
sita. Pia unaweza kuhitaji kipimo cha kutaza wingi wa
virusi utapoanza kutumia ARVs na mara nyingine
baadaye kupima upunguaji wa virusi kwa kutumia
dawa za ARVs (ufanisi).Unapokuwa tayari na salama
kufanya hivyo, ni muhimu kuweka wazi kwa mwenzi
wako kuwa una VVU
Zoezi 6: Matumizi ya kondomu za kike na kiume
Kuzuia ueneaji wa VVU
Dakika 30
Hatua 1: Eleza
Eleza kwamba hii ni fursa kwa ajili yao kujifunza au kuchangia taarifa kuhusu jinsi ya
kutumia kondomu ya kiume na kike kwa ufasaha kama njia ya kujikinga na VVU.
Kuzungungumzia kuhusu kondomu kwenye maeneo ya gerezani inaweza kuwa ni jambo
gumu. Ingawa, ni muhimu kuweka wazi kuwa kondumu hazitagawiwa magerezani.
Hairuhusiwa na sheria za Tanzania. Kwa hiyo ni muhimu kupata taarifa hizi kuhusu kondomu
kwani zitawanufaisha mara baada ya kumaliza kifungo au kuachiliwa kutoka gerezani kwa
mfano, mahabusu.
Eleza kuwa kondomu hutoa kinga madhubuti dhidi ya VVU ikiwa itatumika kwa usahihi
na wakati wote. Ingawa kondomu zimezuiliwa gerezani, wafungwa wanaweza kutumia
kondomu mara baada ya kutoka gerezani.
Hatua 2: Uliza
Kwa kunyosha mikono wangapi wamewahi kutumia kondomu? Nani anaweza kueleza hatua
za namna ya kutumia kondomu ya kiume kuanzia mwanzo hadi mwisho?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
49
Hatua 3: Hatua jinsi ya kutumia kondomu ya kiume
Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kiume
Kata pakiti ya kondomu kwa kufuata alama pembeni mwa
pakiti. Unapofungua pakiti ya kondomu usitumie kucha wala
meno.
Iweke kondomu kwenye ncha ya uume halafu ikunjue kuelekea
chini ya urefu wa uboo kwa kuisukuma chini kwenye mzingo
wa duara wa kondomu.Valisha kondomu kwenye uboo ukiwa
bado umesimama. Minya chuchu ya kondomu katikati ya
kidole na kidole gumba cha mkono mmjoja (Ukiacha nafasi
nchani ili kukusanya shahawa au manii).
Baada ya kufanya mapenzi na kukojoa, shikilia mzingo wa
kondomu halafu toa uume nje kabla haujalala. Ifunge
kondomu katika kifundo kwenye manii au shahawa.
Itupe kondomu iliyotumika mahali salama. Kama vile kondomu
ya kike, kamwe usiidumbukize chooni kondomu ya kiume.
Inaweza kuziba choo chako na haiozi. Ifunike kwenye tishi
halafu itupe kwenye pipa la takataka au kwenye choo cha
shimo.
Hatua 4: Orodhesha
Jadili mambo magumu zaidi tunayokabiliana nayo wakati wa kutumia kondomu.
Waombe washiriki kupendekeza ni namna gani changamoto hizi zinaweza kutatuliwa.
Baadhi ya matatizo ya kawaida mara zote ni pamoja na:
Kujaribu kuiviringisha kondomu kuelekea chini wakati ikiwa “nje—ndani.”
Kondomu haikunjuki kuelekea kote chini.
Kondomu haijawekwa sawa kwenye kielelezo
Mtumiaji hana utulivu wakati akifungua pakiti au hutumia meno kuifungua.
Hewa kwenye chuchu haijatolewa
Kamwe usitumie mafuta ya mgando kama Vaseline® au mafuta ya taa kama kilainishi
wanapotumia kondomu.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
50
Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kike
Fungua pakiti ya kondomu. Chana moja ya mapengo mwishoni na
usitumie mkasi wala kisu. Kwani hutakiwi kuiharibu kondomu.
Shikilia sehemu ya juu ya kondomu na wakati huo huo sukumiza
sehemu ya ndani ya duara, huku sehemu ya wazi ikining’inia.
Utagundua kwamba kuna duara mbili kwenye kondomu ya kike,
tofauti na kondomu ya kiume. Duara ya nje, ambayo ipo wazi,
huenda nje ya kondomu. Duara ya ndani huenda ndani na husaidia
kushikilia kondomu juu wakati wa tendo la ndoa. Sukumiza
sehemu ya ndani, duara iliyofungwa.Mara baada ya duara
kuonekana ndefu na nyembamba, sasa ipo tayari kuingizwa ndani
ya uke.
Tafuta sehemu ya faragha na iingize sehemu ya ndani, sukumiza
duara ndani ya uke wako. Kama ni mara ya kwanza kuingiza kisodo
au kufanya mapenzi, itakuchukua muda kabla hujawa mzoefu wa
kuisokomeza hapo. Kiasi kidogo cha kilainishi kinaweza kusaidia
mambo kwenda shwari. Unaweza kutumia kidole cha kati
kuisukuma ila hakikisha haijageuzwa. Duara ya nje inapaswa kubaki
nje ya uke. Uko tayari kwenda! Ukiwa tayari, hakikisha
unamwongoza mpenzi wako kuingiza uume kwenye kondomu.
Hakikisha haingizi pembeni au kwa bahati mbaya kuikosa kabisa
kwa namna yoyote
Safisha. Ukishamaliza, geuza duara ya nje mara kadhaa ili kuifunga halafu ivute nje taratibu. Kama
ilivyo kwa kondomu ya kiume, kamwe usitupe kondomu ya kike kwenye choo cha maji. Inaweza
kuziba choo chako na haiozi. Ikunje kwenye tishu na uitupe kwenye pipa la takataka au choo cha
shimo.
Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU: matibabu, huduma, na msaada
Dakika 40
Kipindi 3.2: Mazoezi
Matibabu ya vvu na maambukizi nyemelezi
Matibabu ya mgonjwa mwenye maambukizi ya vvu
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
51
Dhamira
Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:
Kueleza kwa kifupi uwepo wa matibabu kwa matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo,
magonjwa ya ngono, maambukizi ya njia ya uzazi, na maambukizi nyemelezi.
Zoezi 1: Matibabu ya VVU na maambukizi nyemelezi
Dakika 40
Hatua 1: Eleza
Waambie washiriki kwamba sasa watajadili matibabu ya maambukizi tuliyokwisha kujadili
kama VVU, kifua kikuu, magonjwa mengine ya ngono, na maambukizi ya njia ya uzazi.
Hatua 2: Maswali na majibu—maambukizi
Swali: Tunajikinga vipi na magonjwa ya ngono?
Chukua mawazo machache
Jibu: Njia bora ya kujikinga na magonjwa ya ngono ni kuzuia kuupata. Katika hatua hii ya
kwanza ya kujikinga, uwezekano wa kupata magonjwa ya ngono unaweza kupunguzwa kwa:
Usianze kufanya mapenzi mapema (kwa vijana wadogo)
Kupunguza idadi ya wapenzi
Kutumia kondomu kwa usahihi na wakati wote
Utambuzi wa haraka na kupata matibabu sahihi ya ugonjwa wa ngono
Swali: Maambukizi njia ya uzazi inamaanisha nini?
Jibu: Maambukizi kwenye njia ya uzazi ni maambukizi yaliyopo kwenye mkondo wa sehemu
za siri. Huwaathiri wanaume na wanawake. Baadhi ya magonjwa katika njia ya uzazi (kama
vile kaswende na gono) huambukizwa kwa njia ya kujamiiana lakini mengi yao
hayaambukizwi kwa njia hiyo (kama maambukizi ya fangasi). Njia bora ya kushughulikia
ugonjwa wa ngono ni kutafuta matibabu mara moja.
Hatua 3: Maswali na majibu—matibabu ya VVU
Swali: VVU hutibiwa vipi?
Unaweza usiwe na muda wa kupitia maswali yote yafuatayo. Pitia maelezo kwa ufupi
kuhusu dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI kwenye ukurasa ufuatao.
Jibu: Maambukizi ya VVU hutibiwa kwa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya
UKIMWI
Swali: Nini maana ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
52
Jibu: Ni dawa zinazotumika kutibu mambukizi ya VVU. Watu wanaotumia dawa za
kupunguza makali hutumia muunganiko wa madawa (yaitwayo ARV regimen) kila siku. Kuna
muunganiko mbalimbali wa madawa. Dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI
zinapendekezwa kwa kila mtu mwenye maambukizi ya VVU. Dawa za kupunguza makali ya
ukimwi haziwezi kuponyesha kabisa VVU, bali huwasaidia watu kuishi kwa muda mrefu,
maisha yenye afya. Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi pia hupunguza hatari ya
kueneza VVU kwa mtu mwingine. Nchini Tanzania, kwa watu wazima na vijana wadogo,
hatua ya mwanzo (ya kwanza) madawa ya ARV regimen ni miongoni mwa miunganiko
ifuatayo ya dawa tatu: (1) (tenofovir (TDF) + lamivudine (3TC) + efavirenz (EFV); (2)
zidovudine (AZT) + lamivudine (3TC) + lopinavir/ritonavir (LPV/r); or (3) abacavir (ABC) +
lamivudine (3TC) + nevirapine (NVP).
Dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI kwa kifupi
Dawa za kupunguza makali ya virusi vya
UKIMWI ni utumiaji wa dawa za VVU
kutibu maambukizi ya VVU.
Inapendekezwa kwa kila aliyeambukizwa
na VVU, na husaidia watu wenye VVU
kuishi kwa muda mrefu, maisha yenye
afya.
Watu wenye VVU wanapaswa kuanza
kutumia dawa kulingana na mwongozo wa
kitaifa wa usimamizi wa VVU/UKIMWI. Kwa
watu wenye VVU wenye hali zifuatazo. Ni
muhimu sana kuanza matumizi ya mara
moja mwanamke akiwa na mimba
Magonjwa fulani yenye uhusiano na
maambukizi ya VVU kama vile utando
mdomoni, herpes simplex, mkanda wa
jeshi, dalili kiunoni, kansa ya mlango wa
kizazi, na kifua kikuu.
Toleo jipya la miongozo ya kimataifa
linapendekeza kutumia dawa mara baada
ya kugundulika na VVU (“Pima na Tibu”)
kwa kuanza matibabu mapema
yatapunguza hatari ya VVU na matatizo ya
kiafya yasiyo na uhusiano na VVU
miongoni mwa watu wenye VVU na
UKIMWI Na itapunguza wingi wa virusi
kwa kiwango kisichogundulika na hivyo
kupunguza hatari ya kuenea kwa VVU.
Ufanisi wa dawa hutegemea ufuasi mzuri
wa dawa—kutumia dawa kila siku kama
ulivyoelekezwa na mtoa huduma wa afya.
Kabla ya kuanza kutumia dawa, ni muhimu
kukabiliana na maswala yoyote
yatakayoathiri makali ya dawa.
Swali: Tiba ya virusi vya UKIMWI hufanya kazi vipi?
Jibu: VVU hushambulia na kuharibu seli za CD4 kwenye mfumo wa kinga ambazo
hupambana na maambukizi. Seli zikiwa chache, ni vigumu kwa mwili kupambana na
maambukizi na aina fulani za saratani. Dawa huzuia VVU kuongezeka (kuzaliana wenyewe),
kitu ambacho hupunguza kiwango cha VVU mwilini ingawa haiondoi VVU vyote mwilini.
Uwepo wa VVU wachache mwilini huupatia mfumo wa kinga nafasi ya kuponyesha na
kuzalisha seli za CD4 zaidi. Hata kama bado mna kiasi fulani cha VVU mwilini, mfumo wa
kinga una nguvu za kutosha kupambana na maambukizi na magonjwa yajulikanayo kama
maambukizi nyemelezi kama vile kifua kikuu, homa ya mapafu, na kansa ya mlango wa kizazi.
Maambukizi nyemelezi ni maambukizi ambayo hutokea mara kwa mara na huwa makubwa
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
53
zaidi kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kinga, kama vile watu waishio na VVU. Kwa
kupunguza kiwango cha VVU mwilini, dawa za VVU zinaweza pia kupunguza hatari ya
kueneza VVU kwa mtu mwingine.
Swali: Ni wakati gani muafaka kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya
ukimwi?
Jibu: Watu wenye maambukizi ya VVU wanaostahili wanapaswa kuanza dawa mapema
iwezekanavyo. Watoa huduma za afya watashirikiana na wagonjwa ili kuona nani anastahili
kulingana na mwongozo wa kitaifa. Kwa watu wenye hali zifuatazo, ni muhimu sana kuanza
kutumia dawa mara moja: Ujauzito na magonjwa fulani yenye uhisiano na maambukizi ya
VVU kama utando mdomoni, mkanda wa jeshi, au kansa ya malango wa kizazi.
Kulingana na Mwongozo Wa Kitaifa Wa Kusimamia VVU Na UKIMWI Toleo 5 (Wizara ya Afya
na Maendeleo ya Jamii, Tanzania [MOHSW] 2015), dawa zinapaswa kuanzishwa kwa watu
wote wenye kifua kikuu na maambukizi ya uhusiano na VVU, bila kujali hatua za kliniki za
WHO au kiwango cha seli za CD4. Matibabu ya kifua kikuu yanapaswa kuanza kwanza,
yakifuatiwa na matibabu mapema iwezekanavyo, ndani ya wiki mbili za awali baada ya
kuanza matibabu ya kifua kikuu.Watu wenye VVU wasio na ishara wala dalili za uwepo wa
kifua kikuu wanastahili kupata dawa za kujikinga za isoniazid. Jitihada zote zinapaswa
kufanyika kupambana na maambukizi nyemelezi. Msisitizo unapaswa kuwekwa katika
utambuzi wa mapema, matibabu, na rufaa, pakiwa na ulazima.
Kumbuka: Mwongozo mpya unapendekeza kuanzisha dawa kwa wagonjwa wote mapema
mara maambukizi ya VVU yanapothibitishwa kuwepo. (“Pima na Tibu”). Serikali inaweza
kutengeneza miongozo mipya kulingana na kiwango cha utayari wao (usambazaji wa
madawa, uwezo wa maabara, rasilimali watu, fedha, nakadhalika).
Swali: Nini faida za kutumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi?
Jibu: Baadhi ya faida za dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
Watu wenye VVU wanaotumia dawa wanaweza kuishi kwa muda mrefu ukilinganisha na
wale wasiotumia dawa.
Watu wanaotumia dawa wana magonjwa machache yenye uhusiano na VVU
ukilinganisha na wale wasiotumia dawa.
Kwa kuwa watu wanaotumia dawa kama ilivyoelekezwa wana afya bora, huenda hospitali
mara chache na huepuka gharama nyingine za kiafya.
Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia dawa wana muda zaidi kukamilisha malengo na
dira za maisha yao.
Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia dawa wanaweza kuzitunza familia zao vizuri
zaidi.
Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia dawa wanaweza kuishi kama kawaida.
Kwa kuwa watu wanaotumia dawa wana kiasi kidogo cha VVU ndani ya miili yao, wana
nafasi ndogo ya kueneza VVU kwa watu wengine.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
54
Hatua 4: Maswali na majibukuishi kwa kutumia dawa za kupunguza makali
Swali: Sababu kubwa ya dawa kuota usugu na matibabu kutofanya kazi ni nini?
Jibu: Ufuasi hafifu wa dawa huongeza hatari ya dawa kuota usugu na matibabu kutofanya
kazi. Kutumia dawa kila siku kama ilivyoelekezwa, ijulikanavyo kama “ufuasi,” ni muhimu sana
kwa dawa kuweza kufanya kazi. Baadhi ya watu huacha kutumia dawa kama ilivyoelekezwa
kwa kuwa hupatwa na madhara ya pembeni, au kwa kuwa wanajisikia kuwa na nguvu na
wenye afya na kudhani hawahitaji dawa tena. Baada ya muda, japo, bila ya dawa, VVU
huongezeka tena mwilini na watu huanza kuugua. Isitoshe, kuna uwezekano kwamba dawa
hizo hizo za kupunguza makali zisimsaidie tena huyu mtu mara atakapotaka kuanza
matibabu tena kwa kuwa VVU mwilini watakuwa wameshatengeneza usugu kwa dawa hizo.
Wanaweza wakaanza kutumia aina nyingine ya dawa, lakini inaweza kuwa ni vigumu sana
kuzipata na /au kukumbwa na madhara ya pembeni kuliko ulipokuwa ukitumia dawa za
mwanzo. Uenezaji wa kirusi kinachopelekea usugu wa dawa za VVU kwa njia ya mapenzi ni
jambo linalowezekana pia. Usugu ni sababu ya msingi kwa nini matibabu yanaweza yasifanye
kazi.
Swali: Ni kwa muda gani dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI humwezesha mtu
mwenye maambukizi kuishi?
Jibu: Watu wengi wanaotumia dawa kama ilivyoelekezwa huishi maisha ya kawaida na
huugua kwa vipindi sawa na watu wasio na maambukizi ya VVU.
Swali: Changamoto za dawa za kupunguza makali ya UKIMWI ni zipi?
Jibu: Uwezekano wa hatari za dawa ni pamoja na madhara ya pembeni (madhara yoyote ya
dawa, kemikali, au dawa nyingine ambazo ni za nyongeza kwa ajili ya madhara mahususi,
hasa madhara ambayo ni ya kudhuru au yenye maudhi) yanayosababishwa na dawa za
kupunguza makali au dawa nyingine ambazo mtu mwenye VVU anazitumia. Asili ya madhara
ya pembeni inategemeana na sehemu ya mwili ambako dawa imekusudiwa kutibu au namna
ambayo mwili unashughulika na dawa.
Dawa za kupunguza makali ni matibabu ya muda mrefu—mtu analazimika kutumia dawa
kila siku kama ilivyoelekezwa na mtoa huduma za afya. Ufuasi hafifu—kutotumia dawa
kila siku na kama ilivyoelekezwa—huongeza hatari ya dawa kuota usugu na matibabu
kutofanya kazi.
Dawa nyingi za kupunguza makali humezwa mara moja kwa siku, pamoja na au bila ya
chakula. Baadhi humezwa mara mbili kwa siku au zinapaswa kumezwa pamoja na
chakula.
Baadhi ya aina za dawa za kupunguza makali zinaweza kuwa na madhara ikiwa
zitamezwa pamoja na vidonge vingine au wakati wa mimba. Ni muhimu kuzungumza na
mtoa huduma za afya kuhusu dawa zingine unazotumia na mfahamishe kama una
mimba.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
55
Dawa za kupunguza makali zinaweza kusababisha matatizo mengine. Baadhi ya matatizo
yanaweza kutatuliwa baada ya wiki kadhaa za utumiaji, matatizo mengine yanahitaji
ushauri wa daktari au wataalamu wa afya.
Ikiwa dawa hazimezwi kila siku kama ilivyoelekezwa, dawa hazitafanya kazi vizuri na mtu
anaweza kuugua. Watu ambao dawa hazifanyi kazi kabisa wanalazimika kubadilisha na
kupata aina nyingine ya dawa, lakini machaguzi yao ya dawa hapo baadaye yatakuwa
yamepungua.
Ikiwa unapata matibabu kutibu matatizo mengine ya kiafya au kinzamimba (uzazi wa
mpango), ni muhimu kumfahamisha daktari wako. Baadhi ya dawa za kupunguza makali
(kama, efavirenz, nevirapine) huingiliana na baadhi ya madawa ya uzazi wa mpango.
Kutumia madawa ya kulevya (kama bangi, cocaine, ecstasy, na kadhalika) pia kunaweza
kusababisha dawa kuacha kufanya kazi vizuri.
Swali: Madhara ya pembeni ya kawaida ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI
ni yapi?
Jibu: Madhara ya pembeni ya dawa yanaweza kutofautiana kulingana na dawa na mtu
anayetumia dawa hizo. Watu wanaotumia aina moja ya dawa wanaweza kuwa na madhara ya
pembeni tofauti kabisa. Madhara ya pembeni ya kawaida ni pamoja na:
Maumivu ya kichwa, kizunguzungu cha mara kwa mara, ambayo huenda yasiwe
makubwa sana.
Kuvimba kwa mdomo na ulimi au kuharibiwa kwa ini, ambayo inaweza kutishia maisha
Ukurutu mwilini kote
Ganzi miguuni
Matatizo ya figo (hasa kwa matumizi ya tenofovir)
Ndoto za ajabu (hasa kwa matumizi ya efavirenz)
Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto
Dakika 30
Kipindi 3.1: Mazoezi
Utangulizi kuhusu kuzuia na kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:
Kueleza maana ya maneno kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto na kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza mama mwenye VVU na mtoto
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
56
Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuzuia maambukizi kwenda kwa mtoto
Dakika 30
Hatua 1: Anza
Waulize washiriki wanaelewa nini kuhusu kuzuia na kukomesha maambukizi.
Hatua 2: Eleza
Eleza kuwa kuzuia inamaanisha kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto na kukomesha inamaanisha kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto.
Hatua 3: Maswali na majibumaambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Swali: Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto maana yake ni nini?
Jibu: Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ya VVU hutoka kwa mama aliye na
VVU kwenda kwa mtoto wake wakati wa ujauzito, kuzaa, (hujulikana pia kama uchungu wa
uzazi na kujifungua), au wakati wa kunyonyesha (kwa njia ya maziwa ya mama). Maambukizi
ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto vile vile huitwa maambukizi ya perinatal ya
VVU. Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni njia ambayo mara nyingi watoto
wachanga huambukizwa VVU.
Swali: Unadhani maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanaweza
kukingwa?
Jibu: Ndiyo
Hatari za maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni ndogo pale ambapo
Wanawake wenye VVU wanapopata dawa
wakati wa ujauzito na kujifungua na katika
mazingira fulani, kuzaa kwa upasuaji
uliopangwa (mara nyingine hujulikana
kama C-section).
Watoto waliozaliwa na wanawake wenye
VVU hupokea dawa za VVU kwa kipindi
cha wiki sita baada ya kuzaliwa na
kunyonya maziwa ya mama kwa miezi sita
halafu anaachishwa
Hatua 4: Eleza
Wizara ya afya na ustawi wa jamii imeridhia njia bora kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto
wachanga na watoto wadogo ili kufikia lengo la kutokomeza maambukizi toka kwa mama
kwenda kwa mtoto. Mbinu ni pamoja na hizi zifuatazo:
Kinga za awali za maambukizi ya VVU kwa wanawake wenye umri wa kuzaa na wenza
wao.
Kuzuia mimba zisizotarajiwa kwa wanawake wenye VVU
Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa wanawake waathirika kwenda kwa watoto
wachanga
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
57
Kutoa matibabu, huduma, na msada kwa wanawake wenye maambukizi ya VVU, watoto
wao wachanga na familia zao.
Hatua 5: Maswali na majibu—wanaume na nafasi yao katika kuzuia maambukizi ya vvu
toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Swali: kuna faida gani za kuwashirikisha wanaume kwenye kuzuia
maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto?
Jibu: Ushahidi unaonesha kwamba wanaume wanapounga
mkono huduma za afya kwa wanawake:
Utumiaji wa huduma za kuzuia na kupata matibabu ya VVU
kwa wanawake na watoto huongezeka.
Matokeo kiafya huboreka.
Kuna ongezeko na ufuasi wa matumizi ya dawa.
Kuna ongezeko la upimaji na matibabu miongoni mwa wanaume.
Unyanyapaa hupungua.
Hatua 6: Maswali na majibu—lengo
Swali: Nini lengo la kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto nchini
Tanzania?
Jibu: Lengo ni kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kutoa
matibabu kwa wajawazito wote wenye maambukizi ya VVU na watoto wao wenye VVU
wanaohudhuria afya ya mtoto na uzazi na huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa
mama kwenda kwa mtoto katika vituo vya afya gerezani. Hili linaweza kufikiwa kwa kutoa
huduma za upimaji wa VVU kwa wanawake wajawazito ikifuatiwa na kuwapa mbinu kwa
wanawake wenye VVU kuzuia maambukizi wima ya VVU kwa watoto wao wachanga.
Hatua 7: Fupisha
Kutokomeza maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto nchini Tanzania
kunahitajika:Jitihada endelevu ili kuzuia maambukizi mapya miongoni mwa wanawake, na
kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango miongoni mwa wanawake
waishio na VVUKuboresha upatikanaji wa huduma kabla ya kujifungua na wahudumu
wenye ujuzi wakati wa kuzaa kwa wanawake wote, bila kujali mali, hali, na makazi.
Uharakisha upanuzi wa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda
kwa mtoto zenye ubora wa juu kwenye huduma zote kabla ya uzazi na vituo vya
kujifungulia na kuimarisha uwepo wa huduma kwa kuzishirikisha jamii na vituo vya afya.
Ubora na mwendelezo wa huduma kwa wakati muafaka kwa mama na mtoto.
Ushirikishwaji wa wanaume kwenye jitihada za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa
mama kwenda kwa mtoto ni hatua muhimu ya kuweza kuwapima VVU wanaume.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
58
SOMO 4: KUVUNJA UKIMYA KUHUSU
KIFUA KIKUU NA VVU.
Lengo
Kukuza elimu na ujuzi wa mawasiliano kwa mfungwa ili aweze kuripoti shutuma zenye
uhusiano na kifua kikuu na VVU miongoni mwa wafungwa wenzake.
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa mafunzo, wafungwa na wafanyakazi wa magereza wataweza:
Kuelezea na kutambua aina za shutuma kwenye magereza.
Kuzungumzia shutuma za kimwili au kimapenzi kwa uwazi zaidi.
Kueleza maana na manufaa ya mawasiliano kwa wenza.
Kutambua njia za asili na zenye ufanisi za mawasiliano kwa mwenza miongoni mwa
wakazi wenza na wafanyakazi wa magereza.
Kuelezea njia za kutoa taarifa na kutafuta huduma miongoni mwa wakazi wenza.
Kutambua changamoto kuu na njia za kuzitatua.
Kipindi 4.1: Kutambua aina za shutuma katika magereza
Saa 2, Dakika 5.
Kipindi 4.1: Mazoezi
Aina za shutuma katika magereza
Kuzungumzia shutuma za kimwili na kimapenzi
Jinsi ya kuvunja mazoea ya ukimya
Zoezi 1: Aina za shutuma katika magereza
Dakika 20
Vifaa vinavyohitajika
Ubao wa chaki au karatasi za kuandikia ubaoni
Maandalizi ya awali
Ikiwezekana washirikishe baraza la magereza katika mjadala huu.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
59
Hatua 1: Fafanua
Wafahamishe washiriki kuwa wafungwa wanaweza kukumbana na uonevu wa kimwili au
kimapenzi na aina nyingine za vurugu na kuonewa na wafungwa wenzao na wafanyakazi wa
magereza na kushindwa kutoa taarifa ya uonevu kwa kuhofia ulipizaji kisasi.
Endelea kueleza kwamba wafungwa vile vile wanaweza kukumbana na mambo ya kutendewa
vibaya, kudhihakiwa, lugha zisizi na adabu, na uongo wa kupindukia kutoka kwa wafungwa
wenzao. Wafanya kazi wa magereza wanaweza kutumia kauli za vitisho kama njia ya
kuwaogopesha au kuwavunja moyo wafungwa wenzao ili kuwafanya watii kanuni na taratibu
za magereza
Hatua 2: Jadili
Eleza kwamba majadiliano haya yatatoa mwanga juu ya haya mambo hivyo wafungwa
pamoja na wafanyakazi wa magereza wanaweza kutatua mambo haya.
Matukio ya unyanyasaji kwa kiasi kikubwa husababishwa na sababu za kimazingira na mahali
kama vile umati mkubwa/msongamano, usimamizi hafifu, nguvu ya madaraka ambayo
inaweza kutengeneza fursa kwa aina mbalimbali za unyanyasaji. Madhara ya unyanyasaji wa
kimwili na kimapenzi yanaweza kuwa pamoja na majeraha, ugonjwa, kujiumiza mwenyewe,
msongo wa mawazo, na ugonjwa wa akili. Sababu hizi zinaweza kutatuliwa na kuzuiwa kwa
kuongeza usimamizi thabiti na kwa wafanyakazi wa magereza kuzungukia vizimba na
program za elimu rika na uhamasishaji. Usimamizi usio thabiti kutoka kwa maafisa wa
magereza huleta mianya kwa wafungwa kujiingiza kwenye vurugu na kuwatendea vibaya
wengine. Si rahisi kufuatilia shutuma za unyanyasaji au uonevu miongoni mwa wafungwa
wenye maelezo yasiyijitosheleza hasa kuhusu shutuma za unyanyasaji wa kimapenzi
miongoni mwa wafungwa wenzao. Hali hii imekuzwa na mazoea ya ukimya na ukosefu wa,
au upungufu wa, njia za ufuatiliaji na uwekaji kumbukumbu za shutuma hizo katika vizimba
vya magereza. Uwekaji wa kamera na vibonyezo hisishi kwenye vizimba kunaweza kusaidia
kufuatilia unyanyasaji na tabia za vurugu miongoni mwa wafungwa.
Hatua 3: Chemsha Bongo
Wapange washiriki wawili wawili kwa ajili ya chemsha bongo halafu waombe wajadili na
kuandika aina gani za unyanyasaji wa—kimwili, hisia na kimapenzi—ambao hutokea
katika magereza. Wape takiribani dakika 10.
Hatua 4: Maoni
Waombe washiriki kuchangia aina za unyanyasaji walizoziainisha.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
60
Hatua 5: Mapitio
Eleza maneno kwenye jedwali hapa chini:
NENO MAANA
Ukatili: Shirika la afya duniani (WHO) linaeleza ukatili kuwa ni “matumizi ya nguvu
za kimwili au madaraka kwa kukusudia, kutishwa au kwa uhalisia, dhidi ya
mtu mwenyewe, mtu mwingine, au dhidi ya kikundi au jumuiya ambayo
huenda yakasababisha au yakawa na uwezekano mkubwa sana wa
kusababisha majeraha, kifo, madhara ya kisaikolojia, maendeleo mabaya au
unyimaji” (Krug et al. 2002). maneno “Matumizi kwa kukusudia” ni ya
msingi mno ambayo yanatofautisha vurugu na madhara na majeraha ya
kutokukusudia.
Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani pamoja na kusimamia na kuwashawishi
watu wengine na matendo yao. Madaraka yanaweza kutumiwa kwa njia
chanya na hasi pia. Unyanyasaji unaweza kutokea iwapo madaraka
yatatumika kwa nia ya kudhulumu au kupata fadhila kutoka kwa mtu asiye
na nguvu kwa kubadilishana faida au ahadi. Ukosefu wa usawa wa
madaraka kati ya watu unaweza kufanywa kwa mabavu au kwa vitisho.
Miundo ya madaraka yaweza kuwa halisi au ya kutambua. Miundo ya
madaraka yaweza kuwa; kuwa na madaraka, uwezo wa kufanya maamuzi,
au umiliki wa chakula, pesa, au silaha.
Ridhaa: Maana yake ni kufanya uchaguzi sahihi wa kufanya jambo fulani kwa uhuru
na kwa hiari. Hakuna ridhaa pale ambapo makubaliano hufikiwa kwa njia
ya vitisho, nguvu, au njia nyingine za lazima, utekaji nyara, ulaghai,
udanganyifu, uwakilishi mbaya. Kutishia au kuzuilia au kuahidi kutoa
fadhila ili kupata ridhaa ya mtu ni matumizi mabaya ya madaraka. Matendo
yote ya ukatili na unyanyasaji wa kimapenzi hutokea bila ya ridhaa stahiki.
Hata kama mtu atasema ndiyo wakati wa moja ya matendo haya, si ridhaa
ikiwa alisema kwa kushinikizwa—yaani mkosaji alitumia nguvu fulani au
vishawishi ili kumshawishi mhanga kusema ndiyo.
Ukatili wa
kimwili:
Inamaanisha matumizi ya nguvu kwa kukusudia yenye nia ya kusababisha
kifo, ulemavu, majeraha, au madhara mengine. Matendo ya ukatili ni
pamoja na kukwaruza, kusukuma, kutupa, kukwida, kung’ata, kukaba,
kutikisa, kupiga kofi, kupiga ngumi, kuunguza, na matumizi ya silaha,
vizuizi, au ukubwa wa mwili wa mtu au nguvu dhidi ya mtu mwingine.
Ukatili wa
kimapenzi:
Inamaanisha matumizi ya nguvu kumlazimisha mtu kushiriki mapenzi
kinyume cha ridhaa yake, jaribio au kukamilisha kitendo bila ya ruhusa
yake au kuelewa, au mwingiliano wa ukatili wa kimapenzi. Vitendo vya
ukatili wa kimapenzi ni pamoja na, usumbufu wa kimapenzi, ubakaji, jaribio
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
61
NENO MAANA
la ubakaji, ubakaji kwenye ndoa, unyonyaji, ukatili wa watoto
kimapenzi/uzinzi wa maharimu, vitendo vya kimapenzi (bila-kuingiliana
kimapenzi), ukahaba wa kulazimishwa, ukahaba kwa watoto, na biashara
za mapenzi. Unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili huambatana na tabia
hatarishi.Hatari ya ueneaji wa VVU huongezeka wakati wa ukatili wa
kimapenzi kwa kuwa nguvu nyingi hutumika, au kitendo cha kulazimisha
ambacho kinaweza kusababisha kuchanika kwa ngozi au ngozi
nyembamba na hivyo majimaji kuweza kupenya.
Hatua 6: Uliza
Waombe washiriki wataje baadhi ya njia za kuzungumzia ukatili wa kimapenzi kwa
ujumla.
Hatua 7: Tafakari
Jadili na washiriki kwa nini ni vigumu kuzungumzia ukatili kwenye mazingira ya magereza
na uandike kwenye karatasi ya kuandikia ubaoni au kwenye ubao wa chaki.
Mazoea ya kukaa kimya yaweza kuwa ni moja ya sababu zinazopelekea ugumu wa
kuzungumzia ukatili katika magereza.
Zoezi 2: Kuzungumzia ukatili wa kijinsia na kimwili: Kuvunja mazoea ya
ukimya
Dakika 45
Hatua 1: Eleza
Sema kwamba uongozi wa magereza nchini Tanzania umejipanga kuhakikisha uwepo wa
usalama kwa wafungwa. Ingawa, kama ilivyo kwenye magereza mengi ulimwenguni
(Dennehy na Nantel, 2006), Magereza ya Tanzania yanakumbana na changamoto nyingi za
uongozi mbaya, matumizi mabaya ya madaraka, na ukatili ambazo menejimenti ya magereza
inajaribu kuzishughulikia. Kama ilivyojadiliwa kwenye shughuli zilizotangulia, eleza kwamba,
wafungwa wanaweza kukumbana na ukatili wa kimapenzi, kimwili na namna nyinginezo za
ukatili ndani ya magereza kutoka kwenye mikono ya wafungwa wengine ama wafanyakazi wa
magereza wasio waaminifu.
Kwenye baadhi ya matukio wafungwa na wafanyakazi wanaamini ya kwamba kinachoendelea
nyuma ya ukuta wa gereza, hasa, ukatili wa kimapenzi, haupaswi kuwekwa wazi kwa umma.
Mitazamo kama hii hutambulika kama “Mazoea ya ukimya,” ambayo, isiposhughulikiwa,
inaweza kupelekea kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kimapenzi, kimwili, na ukatili
mwingine ndani ya magereza. Kutoshughulikia mazoea ya ukimya kunadumisha na
kuendeleza tabia za ukatili ambazo zinaongeza hatari ya kifua kikuu,, VVU, na magonjwa ya
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
62
ngono, na hivyo kuwadhuru wafungwa na maofisa wa magereza (Dannehy na Nantel, 2006
uk. 177)
Hatua 2: Maswali na majibu—mazoea ya kukaa kimya
Swali: Mazoea ya kukaa kimya maana yake nini?”
Wape nafasi washiriki wakupe maoni yao wenyewe kabla hujawaelezea.
Jibu: ”Mazoea ya ukimya” (Martin 2002) maana yake ni hali ya wafungwa, wafanyakazi, au
uongozi kutokuwa tayari kuzungumzia kwa uwazi matukio ya uvunjifu wa sheria, ukiukaji wa
miiko, au yenye utata, kama vile ukatili wa kimapenzi. Mazoea ya ukimya yamejengwa katika
kanuni zisizozungumzika.
Wafungwa wengi hushabihia mazoea ya ukimya kwa sababu ya woga wa kulipiza kisasi na
kwamba wengine huenda wasiwalinde mara baada ya kuvunja ukimya. Wangeweza
kuhatarisha nidhamu kuliko kukiuka mazoea ya ukimya ndani ya gereza. Lakini ukimya huu si
sahihi kwani unawalinda wakosaji, hasa kwa kuwa lengo la magereza ni kuhakikisha usalama
na mazingira salama kwa watu kupitia usimamizi unaofaa na maofisa wanaowasimamia.
Uwepo wa tabia zinazokiuka maadili, matumizi mabaya ya madaraka, kufunika mambo
kunaweza kupelekea magereza kuwa mahali hatari kuishi na kufanya kazi kwa kuruhusu
makundi ya watu kutumia kanuni wanavyopenda wao pasipo kuwajibishwa. Jambo hili
hupelekea hasira, kuvunjika moyo, na mara nyingine huzuni na ugonjwa wa akili
Hatua 3: Eleza
Ili kushughulikia mazingira yasiyo salama yaliyosababishwa na ukatili wa kimapenzi na
namna nyingine za ukatili, mazoea ya ukimya yanapaswa kushughulikiwa kwa kuhakikisha
wafungwa wanaelewa tofauti kati ya kuaminiana, na kutii adhabu kwa ujumla. Kwa kutambua
kuwa, uaminifu ndani ya kikundi ni muhimu katika kuimarisha umoja, kukuza usalama, na
kujenga uaminifu, kutii dhamira za magereza za kuhakikisha usalama, ulinzi, na mazingira
wezeshi ni muhimu zaidi.
Hatua 4: Ufupisho
Fupisha kwa kusema kwamba ni muhimu kwa wafungwa kuvunja mazoea ya ukimya kwa
kuzungumzia ukatili gerezani, ikiwemo ukatili wa kimapenzi. Serikali ya Tanzania ina vyombo,
program na miradi kadhaa, ambayo inadhibiti unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili. Ikiwemo
“toleo maalumu la Sheria ya makosa ya kimapenzi ya mwaka1998 ambayo inaweka wazi aina
mbalimbali za makosa ya jinai yenye uhusiano wa ukatili wa kijinsi, ikiwemo ubakaji,
mashambulizi na maudhi kimapenzi, ukahaba, ukeketaji, na biashara ya mapenzi.
Hatua 5: Funga somo
Wape nakala (ikiwa zipo). Kama hakuna, soma nakala zifuatazo kwa washiriki:
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
63
Toleo maalumu la Sheria ya makosa ya kimapenzi Tanzania (SOSPA)
Mnamo mwaka 1998 bunge la Tanzania lilipitisha Toleo Maalumu la Sheria ya Makosa ya
Kimapenzi (SOSPA)(Serikali ya Muungano wa Tanzania 1998) ili kulinda “heshima na uadilifu
wa wanawake na watoto,” iliyotambulisha makosa mapya kama vile maudhi kimapenzi,
unyanyasaji kimapenzi, na usafirishaji wa binadamu.
SOSPA Ni chombo kikuuu cha kitaifa kinachotoa idhini kupambana na ukatili wa kijinsi na
namna nyingine za unyanyasaji wa kimapenzi. Inatoa adhabu kali na haki ya kupata fidia kwa
wahanga wa ukatili.
SOSPA imerasimisha ubakaji kuwa ni kosa la jinai na inatoa adhabu kali kwa mbakaji.
SOSPA imeingizwa kwenye sheria za adhabu za Tanzania. Sheria za adhabu sura 16, Toleo
jipya, imeweka wazi yafuatayo:
Kifungu 130, sura 16, kinaeleza kuwa, ni kosa kwa mwanaume kumbaka msichana au
mwanamke. Mwanaume atakuwa ametenda kosa la ubakaji ikiwa atashirikiana mapenzi
na msichana au mwanamke ambaye si mke wake, au kuwa mkewe ambaye ameachana
naye; au bila ya ridhaa yake kufanya jambo hili wakati wa kufanya mapenzi; au kwa ridhaa
yake, pale ambapo ridhaa imepatikana kwa mabavu, vitisho, au kumweka katika hofu ya
kifo au majeraha
Mtu yeyote anayejaribu kubaka anatenda kosa la kujaribu kubaka na, isipokuwa kwa
mambo yaliyoainishwa kwenye kifungu kidogo cha 3, anastahili kifungo cha maisha
gerezani ikiwa kosa lake litathibitishwa, na kwa namna yoyote ile anastahili kifungo jela
kwa si chini ya miaka 30 pamoja na au bila ya adhabu ya viboko.
Mtu yeyote ambaye, anakusudia kusababisha maudhi kimapenzi kwa mtu yeyote kwa
kutamka neno lolote au sauti, kufanya ishara ya mwili, au kuonesha neno lolote au kitu
kwa nia kwamba neno hilo au sauti isikike, au ishara ya mwili au kitendo ionekane na mtu
mwingine, mtu huyu anatenda kosa la shambulizi kimapenzi. Ikithibitika, anastahili
adhabu ya kifungo gerezani kwa kipindi kisichozidi miaka mitano, faini isiyozidi shilingi
300, 000, au vyote viwili faini na kifungo.
Mtu yeyote ambaye, kwa kujifurahisha kimapenzi, anafanya kitendo chochote, kwa
kutumia sehemu zake za siri au kutumia vibaya sehemu nyingine yeyote ya mwili wa
binadamu au kitu chochote katika tundu lolote au sehemu ya mwili ya mtu mwingine
yeyote, iwe kitendo ambacho hakijumuishi ubakaji chini ya kifungu 130, ametenda kosa
kubwa la unyanyasaji wa kimapenzi.
Zoezi 3: Mazoezi ya jinsi ya kuvunja ukimya
Dakika 60
Vifaa vinavyohitajika
Ubao wa chaki au karatasi ya kuandikia ubaoni
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
64
Maandalizi ya awali
Soma na elewa kipengele hiki.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
65
Hatua 1: Jadili
Fungua kwa kusema kwamba kwa namna nyingi gereza ni kama mji mdogo.
Katika mji huu wafungwa ndio raia. Na kama ilivyo katika mji wako na mji wangu, raia wa
gerezani wanapaswa kuwekwa mahali salama na pa uhakika. Hili hufanyika kwa kuwapa
makazi ambayo yanakidhi viwango vya afya ya jamii, huduma za afya kitabibu na kiakili
ambazo zinakidhi viwango vya kitaifa, vyakula ambavyo vina mahitaji ya msingi ya lishe, na
misaada mingine ili kusaidia urejeaji wenye mafanikio kwenye jamii zao.
Ingawa, kama ilivyo kwa miji midogo, magereza hayawezi kwa ufanisi huku kukiwa na
mazoea ya ukimya. Tunahitaji kuvunja mazoea ya ukimya kwa sababu inadidimiza lengo la
uwepo wa magereza: “Kutoa huduma rekebishi kwa kutengeneza maisha ya kirafiki na thabiti
na mazingira ya kazi kwa ajili ya wafungwa na wafanyakazi wasimamizi wa magereza.” (Smith
na Yarussi 2007)
Hatua 2: Eleza
Ukali wa aina yoyote ile, hasa ukatili wa kijinsia, ni aina kubwa zaidi ya ukiukwaji wa haki za
binadamu katika mazingira rekebishi. Ukatili wa kijinsia miongoni mwa wafungwa na au kati
ya wafanya kazi wa magereza pia ni jambo la kiusalama na ulinzi kwa:
Kuhatarisha usalama, ulinzi na afya za wafungwa na wafanya kazi
Kuongeza hatari ya kupata na kueneza VVU, magonjwa ya ngono, na maambukizi
yanayohusiana.
Kupunguza uaminifu na motisha miongoni mwa wafungwa na wafanyakazi gerezani.
Kupunguza heshima miongoni na baina ya wafungwa na wafanya kazi.
Kutishia usalama na ulinzi wa vituo vya magereza.
Kudhuru mahusiano ya kifamilia
Kujenga mtazamo hasi kwa umma juu ya magereza.
Kudumisha tabia za ukatili ndani na nje ya magereza.
Hatua 3: Maswali na majibu—wakati tunpovunja mazoea ya ukimya
Swali: Ni wakati gani tungeweza kusema mazoea ya ukimya yamevunjwa?
Chukua maoni machache
Jibu: ”Wafungwa huhakikishiwa usiri mara baada ya kuripoti matukio ya ukatili wa kimapenzi
kuwaepusha na maudhi au kisasi kutoka kwa wakosaji. Pasipo na kamera zinazotazama,
walalamikaji wanapaswa kuruhusiwa kuonesha ushahidi wa kimwili kuhusu kesi za
unyanyasaji wa kimwili na kimapenzi. Tekinolojia inaweza kusaidia kuvunja mazoea ya
ukimya kwa kuwa wafungwa na wafanyakazi wanajua kuwa kamera zinatazama matendo na
tabia zao.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani
66
Hatua 4: Maelezo
Mfumo wa mawasiliano unaathiri sana namna ambavyo wafungwa wanavunja mazoea ya
ukimya. Kwa mfano wafungwa wa kiume na kike wanaweza kutofautiana tabia zao na mfumo
wa mawasiliano, hata kama hawajawahi kukumbana na ukatili katika mazingira ya magereza.
Ingawa, ni mhimu kwa wafungwa kujua kwamba endapowamewahi kunyanyaswa kimapenzi,
kushambuliwa, au kuudhiwa na wafungwa wenzao au wafanya kazi, wana haki ya kuripoti
kosa kwa usalama, kwa siri, na bila ya kutaja jina. Mfungwa anaweza kutoa taarifa zote au
kuminya kiwango cha taarifa anazozitoa kadri anavyoona yafaa. Ingawa, kadri taarifa nyingi
zinapotolewa, ndivyo itavyopelekea mfanyakazi wa magereza kuchukua hatua dhidi ya
mkosaji na kumweka mhanga na wafungwa wengine salama.
Hatua 5: Shauri
Mfungwa yeyote akikumbana na unyanyasaji wa kimapenzi, uonevu au kupigwa bila
sababu halali anatakiwa atoe taarifa kwa uongozi wa gereza mara moja.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
67
SOMO 5: KUISHI KWA MATUMAINI
UKIWA NA VVU NA KIFUA KIKUU
Lengo
Kuwajenga washiriki kiakili, kwa hisia, kiroho, na kimwili jinsi ya kukubaliana na kuishi na kifua
kikuu na VVU.
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa somo hili washiriki wataweza:
Kusema umuhimu wa ufuasi mzuri na kuishi maisha yenye afya.
Kueleza madhara ya kifua kikuu na VVU, kimwili, kisaikolojia, kijamii, kitabia, na kiuchumi
miongoni mwa wafungwa na familia zao.
Kubainisha njia za kupunguza unyanyapaa, na ubaguzi dhidi ya watu wenye VVU.
Kueleza jinsi ya kuwasaidia watu waishio na VVU na magonjwa nyemelezi.
Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya kuwa na VVU
Dakika 60
Kipindi 5.1: Mazoezi
Utangulizi kuhusu kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na TB.
Kupunguza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU
Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na TB
Dakika 30
Vifaa vinavyohitajika
Jadili maswali yaliyopo kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki
Vipeperushi vinavyoelezea kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU gerezani (ikiwezekana)
Maandalizi ya awali
Andika maswali ya kujadili (tazama hatua ya 3 chini) kwenye karatasi ya ubaoni au ubao
wa chaki
Hatua 1: Eleza
Kutambua ya kuwa una maambukizi ya VVU kutabadili maisha yako ghafla. Unaweza
kukumbana na wigo mpana wa hisia—wasiwasi, kupoteza, majonzi, huzuni, kukanwa, hasira,
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
68
mashaka. Haijalishi ni kwa kiasi gani daktari na marafiki wanakuhakikishia, namna ambavyo
vidonge vina ufanisi mkubwa sasa na zitakavyokuwa hapo baadaye, udogo wa madhara
kimwili yatokanayo na kiwango kidogo cha maambukizi yaliyopo mwilini mwako kwa sasa,
au ni jinsi gani unapaswa kujiandaa kiakili na kimawazo, uhitaji wako wa msaada itakuwa
jambo bora. Maswala kisaikolijia yanayowakumba watu wengi wenye VVU hutofautiana.
Matumaini na matarajio ya maisha yako ya baadaye, mahusiano yako, na mwenendo wa
maisha yako yote yatahitaji mabadiliko fulani ili kukufanya uweze kukabiliana na hali ya kuwa
na VVU na kuishi maisha mazuri yenye afya.
Majadiliano haya yanalenga kujadili na kuibua mbinu na njia za namna ambavyo mtu
anaweza kukabiliana na hali ya kuthibitika kuwa na maambukizi ya Kifua Kikuuau VVU
gerezani mahali ambapo rasilimali zinaweza kuwa chache na kuna hatari ya ukatili,
unyanyapaa na ubaguzi.
Hatua 2: Jadili
Yapatie makundi ya watu wanne wanne maswali yafuatayo kwa ajili ya majadiliano:
Nini maana ya kuishi kwa matumaini ukiwa na Kifua Kikuu na VVU gerezani?
Mfungwa au mfanyakazi wa magereza anaweza kufanya nini ili kuishi kwa matumaini
akiwa na maambukizi?
Ni jinsi gani mafanyakazi wa magereza au mfungwa anaweza kumjali mtu aishie na VVU
gerezani?
Wafanye au wasifanye nini ili kuonesha kujali?
Hatua 3: Maelezo
Eleza kwa kifupi majibu kwa maswali haya pamoja na washiriki.
Gawa vipeperushi vifuatavyo (ikiwa vipo). Kama havipo, soma baadhi ya njia muhimu
kuonesha kuwajali watu wenye VVU magerezani.
Wafungwa waishio na VVU wanapaswa wajitahidi kuiweka miili yao kuwa na nguvu, kwa
kuhusisha yafuatayo:
Kula mlo uliokamilika au kuongeza kiwango, kila inapowezekana, ikiwemo vyakula vyenye
virutubisho ambavyo vina protini, vitamini, na wanga. Ukosefu wa virutubisho utachangia
sana kuharibiwa kwa mfumo wa kinga wa mwili. Mlo kamili huupatia mwili nguvu za
kuweza kupambana na magonjwa. Vyakula vya asili vinafaa zaini kuliko vile vya kwenye
makopo na vyakula vilivyosindikwa. Mboga mboga zina madini na vitamin mahususi kwa
ajili ya mwili kustawi .Chakula kinapaswa kusafishwa na kupikwa vizuri kabla ya kuliwa ili
kuulinda mwili kutokana na magonjwa yatokanayo na vyakula.
Kuwa mkakamavu kwa kufanya mazoezi na kupata muda wa kutosha kulala. Mazoezi ya
viungo yatapunguza msongo na uvunjikaji moyo na kuchangia kupata afya njema na
uvumilivu.
Kujiunga au kuunda vikundi saidizi na wafungwa wenzio ambao wana VVU
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
69
Kuzungumza na wafungwa wengine kuhusu upimaji wa ugonjwa.
Kutafuta ushauri wa kidaktari pale mtu anapojisikia kuumwa, au kuwa na msongo, na
kufuata ushauri, ikiwemo kutafuta ushauri wa kidaktari, nasaha, na kijamii.
Ukiwa kwenye matumizi ya vidonge fuata maelekezo ya dawa uliyoandikiwa. Kuwa na
rafiki wa matibabu ambaye utakumbushana naye muda wa kunywa vidonge.
Usivute sigara na usitumie dawa bila ya maelekezo ya daktari.
Kuzungumza na mtu unayemwamini kuhusu hisia zako.
Kumwambia mtu fulani unayemwamini kwamba una VVU.
Njia za kuwahudumia watu waishio na VVU gerezani
Usijitenge na wafungwa wenzio au wafanyakazi wa magereza. Jenga urafiki. Ishi kama
ambavyo mmekuwa mkiishi kabla. Usibadilike kwa sababu tu unajua mtu fulani ana
maambukizi ya VVU.
Tambua hisia zao. Usiwafanye wafadhaike kutokana na hisia zao. Ni sawa kulia wanapolia
na kucheka wanapocheka. Ni jambo zuri kiafya kutoa hisia kuliko kuziweka moyoni.
Kuweka hisia mbaya moyoni husababisha msongo na msongo husababisha madhara
kwenye mfumo wa kinga.
Ikiwezekana waalike kwenye matembezi unapopata nafasi ya kufanya mazoezi. Kuwa
mwangalifu na nguvu za miili yao. Usiwaruhusu kufanya vitu ambavyo hawana nguvu za
kutosha kuvifanya.
Wasaidie kuweka mambo yao sawa. Watu wengi waishio na VVU hawapendi kufanya vitu
vigumu kama kuandika wosia au kuziambia familia zao kuhusu ugonjwa wao.
Washirikishe kwenye sikukuu za kidini au za asili au sherehe ikiwa inawezekana.
Jitolee kuwahudumia watu wenye VVU ili daktari wa magereza aweze kupumzika. Ikiwa ni
mfanya kazi wa magereza, wasaidie baadhi ya majukumu ili kurahisisha maisha.
Ni sawa kuzungumzia ugonjwa wao, lakini kuwa mwepesi wa kuhisi. Wafungwa wenzako
au wafanyakazi wa magereza wanaweza kuchagua siku ya kuzungumza. Itategemea na
namna ambavyo anajisikia siku hiyo.
Kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote, watu wenye VVU wana siku nzuri na mbaya.
Katika siku nzuri watendee kama ilivyo kawaida. Katika siku mbaya watendee kwa
kuwajali zaidi na huruma.
Kujali kunaweza kuoneshwa pasipo maneno. Huhitaji kuzungumza muda wote.
Wahimize kufanya maamuzi kwa muda mrefu iwezekanavyo kwa ajili yao. Mtu
anapoumwa, maamuzi mengi hutolewa kwao, hivyo basi waruhusu wafanye maamuzi
mengi iwezekanavyo.
Zingatia ahadi zako ikiwa utawaahidi watu waishio na VVU. Usiwaambie utawaona kesho
huku ukijua kuwa kesho hutaweza kuonana nao.
Kuwa tayari kuona watu waishio na VVU wakikasirika pasipo na sababu.
Hawajakukasirikia wewe. Wamekasirishwa na kile kinachoendelea kwao na kutokuwa na
uwezo wa kukishughulikia.
Usiwafanyie kile ambacho bado wana uwezo wa kukifanya.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
70
Jaribu kuwa na mtazamo chanya.
Kwa kujenga urafiki unaleta mwanga kwenye mazingira yenye giza nene.
Zoezi 2: Punguza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU
Dakika 30
Vifaa vinavyohitajika
Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki
Maandalizi ya awali:
Andika maswali(tazama hatua 3 chini) kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki.
Hatua 1: Eleza
Uliza washiriki nini maana ya unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU.
Chukua maoni machache.
Hatua 2: Eleza
UNYANYAPAA UBAGUZI
Unyanyapaa maana yake ni tabia isiyopendeza au
isiyoya heshima ambayo mtu au kikundi kinakuwa
nayo ambayo hupelekea kushuka kwa hadhi ya
mtu au kikundi hicho katika macho ya jamii.
Unyanyapaa unaweza kuletwa na mwonekano
mwilini, kama vile, dalili za ugonjwa
zinazoonekana, au mtazamo hasi kwa kundi fulani
la watu au mtu
Ubaguzi unaweza kuelezewa kwa kujumuisha
mtazamo hasi au tabia fulani au vitendo. Mara
nyingi huelezewa kama ni utofauti unaojengwa
kuhusiana na mtu unaopelekea kutendewa bila
haki na bila kuthibitisha kwa misingi ya uhusika
wao, au kuchukuliwa kama wanahusika katika
kundi fulani. Kwa mfano unyanyapaa unaweza
kusababisha madhara na ubaguzi unaoelekezwa
kwa watu ambao kweli, au wanahisiwa tu kuwa na
VVU, na vikundi vya kijamii na watu wanaoishi
nao
Hatua 3: Zoezi
Wagawe washiriki kwenye makundi matano na wape kila kundi hadithi moja. Waeleze
washiriki kuwa watajadili maswali yafuatayo:
Kwa maoni yako, unadhani kwa nini katika hadithi hii watu wameonesha tabia hizo?
Unadhani nini kifanyike ili kupunguza unyanyapaa na ubaguzi?
Unadhani ni nani anaweza kuwasaidia watu wanaonyanyapaliwa au kubaguliwa?
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
71
Hadithi 1
Siku moja afisa Mapendo aliporudi nyumbani kutoka
kwenye majukumu alikuta mke wake akilia. Baada ya
kumwuliza kwa nini analia, mkewe alisema ametoka
kliniki ya uzazi na ameambiwa kuwa ana VVU. Baada
ya kusikia haya, afisa Mapendo alighadhabika sana na
kuanza kumfokea mke wake, akisema kuwa amepata
maambukizi ya VVU kutoka kwa mwanaume
mwingine nje ya ndoa, na hivyo hastahili kuendelea
kuishi nae. Kwa hiyo, alimtolea vitu vyake ndani ya nyumba na kumfukuza nyumbani.
Hadithi 2
Jane ni muuguzi katika gereza mkoani mwanza.
Amefanya kazi pale kwa zaidi ya miaka 10. Anafanya
kazi kwa bidii anapotoa huduma kwa wagonjwa wake.
Mara zote anapogundua kuwa mgonjwa ana
maambukizi ya VVU, huhakikisha kuwa
anapomhudumia anavaa glavu na barakoa ili kuikinga
pua yake, hata kama mgonjwa hana vidonda
ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi.Mara
nyingi mgonjwa anapogundua jambo hili huchukizwa.
Hadithi 3
Mariam ni mke wa mfungwa aliyefunguliwa gerezani
hivi karibuni. Ana shiriki katika vikundi vya ushirika
wa kukopa na kuweka katika mji wake. Anashirikiana
vizuri na wenzake kwenye shughuli zao za kila siku.
Miezi miwili iliyopita yeye na mmewe walikwenda
kliniki kupima VVU, na wote waligundulika kuwa na
maambukizi ya VVU. Tokea wakati huo wanachama
wenzake kwenye kikundi wamemtenga na
hawashirikiani naye tena kwenye shughuli zao za kikundi kwa kuhofia kuwa nao wangeweza
kuambukizwa VVU. Hali hii inamsikitisha Mariam na inatishia hali ya uchumi wa familia yake.
Hadithi 4
Salum ni mfungwa anayetumikia kifungo cha miaka mitano gerezani. Anaishi na VVU na
amekuwa akitumia vidonge vya ARV kwa miaka miwili. Kwa kipindi chote hicho amejitahidi
kuficha vidonge vyake ndani ya vitu vyake, lakini siku moja mfungwa mwenzake alivikuta na
alianza kumzungumzia na kufikia hatua ya kumtenga wakati wa chakula. Baada ya muda
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
72
Salum aligundua kuwa wenzake walikuwa wakijiweka kando na yeye, hivyo aliamua kueleza
hali halisi lakini waliendelea kumcheka na kumtenga.
Hadithi 5
Shida alifunguliwa kutoka gerezani. Alikuwa na furaha kubwa kurudi nyumbani kuungana
tena na familia, mke, na watoto wake. Alipokuwa gerezani Shida alipima VVU na aligundulika
kuwa navyo. Aliudhika sana kuhusu namna ambavyo atakwenda kumweleza mke wake kwa
kuwa hakutaka kuharibu siku yake ya furaha, hivyo aliendelea kuficha na usiku huo alifanya
mapenzi na mkewe bila ya kutumia kondomu.
Hatua 4: Eleza kwa kifupi
Toa fursa kwa kila kundi kujadili hadithi yao kwa kina.
Hatua 5: Jadili
Swali: Tunawezaje kupunguza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU?
Jibu: Kuendeleza mbinu/njia zinazoshughulikia sababu kuu za unyanyapaa na makundi
maalumu ya waathirika, ikiwemo wafungwa. Zifuatazo ni baadhi ya njia tunazoweza kujaribu
na kupunguza unyanyapaa katika ngazi ya kisera na kijumuiya.
Kuzishirikisha jamii kuthibitisha kutoa msaada kwa watu waishio na VVU (kwa mfano.
biashara katika jamii, mashirika ya kijamii, mashule, na viongozi wa jumuiya).
Kukuza uongozi katika jamii kwa watu waishio na VVU.
Kukuza mbinu za kiafya kwa jamii kuhusu kinga na huduma ya Kifua Kikuu na VVU.
Kuendelea kutoa elimu kuhusu mambo yenye kuhusiana na Kifua Kikuu na VVU.
73
ORODHA YA MANENO
CD4: Aina ya chembechembe –T ambazo huukinga mwili dhidi ya maambukizi na kuutunza
mfumo wa kinga. VVU hushambulia chembechembe za CD4 moja kwa moja, na kuhatarisha
mfumo wa kinga.
Daraja: Kikundi cha watu waliowekwa pamoja kulingana na viwango vyao vya mali na/au
kazi wanazofanya katika uchumi.
Dhuluma: Kujenga maoni thabiti mara nyingi maoni hasi kuhusu kitu fulani au mtu fulani
(kitengo cha kikundi cha watu) bila ya kuwa na elimu ya kutosha au uchunguzi wa mambo
kwa kina.
Haki za binadamu: Haki za binadamu ni za watu wote na hazitofautishwi. Kanuni ya
kiulimwengu ya haki za binadamu ndio msingi wa sheria za kimataifa za haki za binadamu
zilizotiliwa mkazo katika azimio la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948, na
zimeelezewa katika mikutano, maazimio na maamuzi mbalimbali ya haki za binadamu za
kimataifa. Haki za binadamu zinarithiwa kwa wanadamu wote, bila kujali utaifa, makazi, jinsia,
taifa au asili ya kabila, dini, lugha, au hali nyingine.
Imani: Maoni thabiti na mara nyingi hutokana na misingi ya kidini na au kanuni za
kiutamaduni.
Jinsia: Kazi, haki, majukumu, fursa, mipaka, matarajio, stahili, na majukumu yanayotambuliwa
kijamii. Jinsi hutofautiana miongoni na ndani ya tamaduni na inaweza kubadilika baada ya
muda fulani.Majukumu ya jinsia huzingatia, jinsia, umri, kabila, dini, na sababu zingine za
kiutamaduni.
Jinsi: Sifa za kibaiolojia na kimaumbile za mwanaume na mwanamke ambazo hazibadiliki
bila ya kufanya upasuaji. Mfano wa viashiria vya jinsi: viungo: uume, uke, matiti, korodani;
maumbile: mzunguko wa hedhi, utengenezwaji wa shahawa; muundo wa kijenetiki:
kromosomu XX na XY.
Kujamiiana: Tabia zote za maisha ya watu kimapenzi, ikiwemo fikra, na hisia, shauku, tabia,
na sura.
Maambukizi yanayoenezwa kwa ngono: Kundi la maambukizi ambalo mara nyingi
huenezwa kwa njia ya mwingiliano wa mapenzi yasiyo salama na mtu mwenye maambukizi.
Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani pamoja na kusimamia na kuwashawishi watu
wengine na matendo yao. Madaraka yanaweza kutumiwa kwa njia chanya na hasi pia.
Makundi maalumu: Watu wanaotumia madawa, malaya, wasenge, watu wa jinsia mbili,
madereva wa masafa marefu, wachimbaji madini, wafungwa, na watoto wa mitaani ni
makundi maalumu. Makundi maalumu yana uwezo mdogo sana wa kupata huduma
zinazostahili, pia yana kiwango kikubwa cha hatari ya kupata na kueneza VVU, na viwango
74
vikubwa vya kukumbwa na mauti na /au ugonjwa kwenye maeneo yenye magonjwa ya
mlipuko/kuambukiza ukilinganisha na makundi mengine katika jamii.
Mapenzi kinyume na maumbile: Mapenzi katika njia ya haja kubwa, bila kujali jinsi za
washiriki. Neno hili hutumiwa vibaya kwa kuchanganywa na ubakaji, ambayo hushindwa
kutofautisha mapenzi ya lazima bila ya ridhaa. Mapenzi kinyume na maumbile ni jinai pale tu
inapokuwa imelazimishwa.
Mapenzi salama: Hujulikana pia kama “mapenzi yenye kinga,” humaanisha kupunguza
hatari za maabmbukizi au mimba, mara nyingi kwa kufanya mapenzi kwa kutumia kondomu
ya kike au kiume au kwa kutafuta njia mbadala za ushirikiano wa mapenzi.
Mateso: Adhabu kali za kimwili au mateso kiakili yaliyofanywa chini ya mamlaka ya sheria.
Haijumuishi maumivu au mateso yanayotokana na, asili, au matukio ya vizuizi
kisheria.Ubakaji wa wafungwa umetambuliwa kama mfumo wa mateso na kitengo maalumu
cha umoja wa mataifa kinachoshughulikia mateso. Hii ni kesi bila kujali kitendo kimefanywa
na mfungwa au mfanyakazi wa magereza. Matendo mepesi ya unyanyasaji wa kijinsi
yanaweza kujumuisha, ukatili, unyama, au kuwatendea vibaya. Kamati ya umoja wa mataifa
inayoshughulikia mateso wakati wote imekuwa ikipambana na ukatili wa kijinsi dhidi ya
wafungwa na imetoa wito kwa serikali kuchukua hatua thabiti kushughulikia jambo hili.
Mila: Mfumo au mpangilio wa tabia unaokubalika na kuchukuliwa kuwa ni “jambo la
kawaida” katika jamii au ndani ya kikundi kwenye jamii.
Mitazamo: Maoni, mawazo na hisia za mtu kuhusu kitu au jambo fulani.
Sera: Mpango, au mfumo wa utendaji wa serikali, chama cha siasa, au biashara uliokusudiwa
kushawishi na kufikia maamuzi, matendo, na mambo mengine, kama vile sera za serikali
kwenye elimu, afya (ikiwemo VVU), au usawa wa jinsi, sera ya kampuni kuhusu ajira na
mafunzo au rasilimali watu/wafanyakazi.
Ridhaa: Mmakubaliano ya hiari bila ya matumizi ya nguvu. Hakuna ridha pale ambapo
mkosaji anatumia vibaya nafasi ya madaraka kumfanya mhanga “kukubali” kitendo cha
mapenzi. Hakuna ridhaa huru ikiwa kulihusisha, ulaghai, udanganyifu na ujanja. Sera zina
malengo ya jumla na malengo maalumu na taratibu zinazoweka mfumo au njia za utendaji
zilizochaguliwa miongoni mwa njia nyingine kwa kuzingatia mazingira fulani ili kutoa
mwongozo na kutambua maamuzi ya sasa na ya baadaye.
Sheria: Mifumo ya usimamizi, na mbinu za kurekebisha maovu zinaweza kutungwa na
chombo chenye mamlaka; sheria hujenga muundo wa siasa, uchumi na historia ya nchi kwa
ujumla kwa kufanya kazi kama msuluhishi wa mahusiano kati ya watu. Zinatungwa na
husimamiwa na katiba za nchi na zina mfumo au seti ya kanuni zilizotungwa na serikali za
miji, taifa, au nchi ambazo husimamiwa na taasisi za kijamii kuongoza mienendo. Sheria
zilizotungwa na serikali hutumika kutoa mwongozo wa namna ambavyo jamii zinapaswa
kuwa, kama vile, sheria zinazokataza kuendesha huku ukiwa umelewa, wizi, kuua, kutumia
madawa, au kumiliki bunduki.
75
Ubaguzi: Huelezewa kuwa huenda ikajumuisha yote mawili mtazamo hasi au tabia fulani au
kitendo. Mara nyingi huelezewa kama tofauti inayotengenezwa kuhusu mtu inayosabaisha
mtu huyu kutendewa isivyofaa pasipo na haki kwa misingi ya uhusika wake ama kuhisiwa
kuhusika katika kundi fulani. Kwa mfano, unyanyapaa unaweza kusababisha madhara na
ubaguzi moja kwa moja kwa mtu ambaye kweli, au anahisiwa tu kuwa na maambukizi ya
VVU, na makundi katika jamii na watu wanaoshirikiana nao katika jamii.
Ubakaji: Kitendo chochote cha upenyezaji bila ya ridhaa kwenye uke, njia ya haja kubwa, au
mdomoni. Neno hili halibagui jinsi, wote mwanamke na mwanaume wanaweza kubakwa.
Uenevu: Kwa kawaida hutolewa kama asilimia, kama vile, uenevu wa VVU ni jamii yenye
maambukizi ya VVU katika kipindi fulani.
Ukatili: Shirika la afya duniani linaelezea ukatili kama ni “matumizi ya nguvu au madaraka
kwa makusudi, kutishia au kufanya kweli, dhidi ya mtu mwenyewe, mtu mwingine, au dhidi
ya kikundi au jamii ambapo kunaweza kupelekea uwezekano mkubwa wa majeraha, kifo,
madhara kisaikolojia, maendeleo mabaya, au unyimaji.” Neno” matumizi ya kukusudia” ni
kiungo muhimu ambacho kinatofautisha ukatili na majeraha au madhara ambayo
hayakukusudiwa.
Ukatili kimwili: Matumizi ya nguvu kwa kukusudia wenye nia ya kusababisha kifo, ulemavu,
mejeraha, au madhara mengine. Vitendo vya ukatili wa kimwili ni pamoja na kukwaruza,
kusukuma, kutupa, kukwida, kupiga, kukaba, kutikisa, kupiga kofi, kupiga ngumi, kuchoma,
na matumizi ya silaha, vizuizi, au kutumia ukubwa wa mwili wa mtu au nguvu dhidi ya
mwingine.
Ukatili wa kijinsia: Kudhuru kimwili, kimapenzi, au kisaikolojia kwa mwanaume au
mwanamke inayomlenga mtu kwa misingi ya jinsi yake. Ukosefu wa usawa wa kimamlaka
kati ya wanaume na wanawake unachangia kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia.Ukatili wa
kijinsia unalenga kudumisha ukosefu wa usawa wa kijinsia na/au kusisitiza wajibu wa kimila
wa jinsia kwa wanaume na wanawake.
Ukatili wa kimapenzi: Matumizi ya nguvu kumlazimisha mtu kushiriki tendo la kujamiiana
kinyume cha ridhaa yake, jaribio au kukamilisha kitendo bila ya ridhaa au uelewa wake, au
mwingiliano mbaya wa kimapenzi. Vitendo vya ukatili wa kimapenzi ni pamoja na usumbufu
kimapenzi, ubakaji, jaribio la ubakaji, ubakaji ndani ya ndoa, unyonyaji, unyanyasaji wa
watoto kimapenzi/ngono, vitendo vya mapenzi (bila upenyezaji) umalaya wa kulazimishwa,
umalaya kwa watoto, na biashara ya mapenzi.
Unyanyapaa: Mtazamo wa kijamii kuwa mtu au kikundi hakifai au ni cha hali ya chini.
Unyanyapaa unaweza kutokana na sifa za kimwili, kama vile, dalili za ugonjwa
zinazoonekana, au kutokana na mtazamo hasi unaoelekezwa kwenye kikundi fulani cha watu
au mtu.
Unyanyasaji: Matumizi ya kitu au kumtendea mtu isivyostahili, kwa kumdhuru, au kinyume
cha sheria.
76
Unyanyasaji wa kijinsi: Aina yoyote ya mwingiliano wa kimapenzi isiyotakiwa kama vile,
kulazimisha busu, kulazimisha, ulawiti, umalaya, au upekuzi mbaya. Unyanyasaji wa kijinsia
huendekezwa na shauku ya kutumia mabavu, amri, na utawala-si mapenzi au tamaa. Mkosaji
anaweza kutumia nguvu au vitisho.
Usiri: Makubaliano au uwakilishi unaoweka wazi kwamba taarifa hazitatolewa. Kuwa na
uwezo wa kuzungumza kwa usiri ni muhimu kwa wahanga wengi wa unyanyasaji wa kijinsia,
na mara nyingi panakuwa hakuna usiri kwa waathirika.
Utamaduni: Imani, desturi, na mzoea ya jamii au kikundi ndani ya jamii (kama vile
utamaduni wa vijana) na tabia za jamii zilizopatwa.
Wakala wa mabadiliko: Tukio, shirika, vifaa, au, mara nyingi, mtu anayetenda kama
kichocheo cha mabadiliko.
77
MIREJEO
AVERT. 2017. “HIV and AIDS in Tanzania.” http://www.avert.org/professionals/hiv-around-
world/sub-saharan-africa/tanzania.
Das, Pamela, and Richard Horton. 2016. “On Both Sides of the Prison Walls—Prisoners and
HIV.” The Lancet 388 (10049): 1032–33. doi:10.1016/S0140-6736(16)30892-3.
Dennehy, Kathleen M., and Kelly A. Nantel. 2006. “Improving Prison Safety: Breaking the
Code of Silence.” Washington University Journal of Law & Policy 22: 175–185.
http://openscholarship.wustl.edu/law_journal_law_policy/vol22/iss1/14.
International Organization for Migration (IOM). 2016. “Fighting Tuberculosis in Tanzania,”
April 15, 2016, Tanzania: Migration for the Benefit of All [website].
https://tanzania.iom.int/press-releases/fighting-tuberculosis-tanzania.
Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS). 2014a. The Gap Report.
http://www.unaids.org/sites/default/files/media_asset/UNAIDS_Gap_report_en.pdf
Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS). 2014b. On the Fast Track to End
AIDS: UNAIDS 2016–2021. Geneva, Switzerland: UNAIDS.
http://www.unaids.org/sites/default/files/media_asset/20151027_UNAIDS_PCB37_15_18_EN_rev1.
pdf.
Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS). 2016. Global AIDS Update 2016.
Geneva, Switzerland: UNAIDS. http://www.unaids.org/sites/default/files/media_asset/global-
AIDS-update-2016_en.pdf.
Krug, Etienne G., Linda L. Dahlberg, James A. Mercy, Anthony B. Zwi, and Rafael Lozano.
World Report on Violence and Health. Geneva, Switzerland: World Health Organization, 2002.
http://www.who.int/violence_injury_prevention/violence/world_report/en.
Martin, Keith L. “Cracking the Code of Silence.” Prisonerlife.com. July 6, 2002.
https://www.prearesourcecenter.org/sites/default/files/library/crackingthecodeofsilence7-6-
2002.pdf.
Mills Edward J., Nathan Ford, and Peter Mugyenyi. 2009. “Expanding HIV Care in Africa:
Making Men Matter.” The Lancet 374 (9686): 275–276. doi:10.1016/S0140-6736(09)61348-9.
Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights (OHCHR). 2005. Human
Rights and Prisons: A Compilation of International Human Rights Instruments Concerning the
Administration of Justice. Professional Training Series No. 11 Add.1.
https://www.un.org/ruleoflaw/files/training11Add1en.pdf.
Smith, Brenda V., and Jaime M. Yarussi. 2007. Breaking the Code of Silence: Correction
Officers' Handbook on Identifying and Addressing Sexual Misconduct. Washington, DC:
NIC/WCL Project on Addressing Prison Rape and National Institute of Corrections.
https://s3.amazonaws.com/static.nicic.gov/Library/022473.pdf.
Sonke Gender Justice Network and MenEngage. 2012. Addressing HIV and Sexual Violence in
Correctional Services Facilities: A Guide for Working with Members of the Correctional
78
Department of Correctional Services. http://detentionjusticeforum.org.za/wp-
content/uploads/2013/09/Sonke-and-Just-Detention-International-Addressing-HIV-and-Sexual-
Violence-in-Correctional-Facilities-Guide-for-Correctional-Staff.pdf.
Sonke Gender Justice and MenEngage. 2017. “Men and HIV in the ESA Region.” Sonke
Gender Justice. Accessed January 25. http://www.genderjustice.org.za/publication/men-hiv-esa-
region/.
79