Upload
others
View
44
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Haki na Wajibu Wa Mtumiaji
Katika Sekta ya Usafirishaji
Oscar Kikoyo
Katibu Mtendaji,
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazothibitiwa na
SUMATRA
NSSF Waterfront Building, 7th Floor,
P.O BOX 14154, Dar es Salaam
Simu +255 22 2127410, Fax +255 22 2127410
Barua Pepe: [email protected]
Tofuti: www.sumatraccc.go.tz
Nukuu ya Mada hii.
“Haki isiyodaiwa ni Haki iliyopotea
kwenye upeo lakini Wajibu usiotimizwa ni
adui wa Haki iliyo usoni”.
James Earl “Jimmy” Carter Jr. (Sources of
Strength)
Wajumbe wa Baraza –Kituo cha DART Ferry
Utangulizi
Chimbuko la dhana ya haki za Mtumiaji ni
mfumo wa uchumi wa soko
Sekta binafsi huendesha uzalishaji mali na
usambazaji kwa ajili ya kutengeneza faida.
Watumiaji hubaki waangaliaji kwa kukosa mbinu
za kukabiliana na watoa huduma.
Soko kukosa uwiano baina ya ubora wa huduma
zitolewazo na gharama za huduma hizo
Utangulizi unae.
Wadau wakuu katika uchumi wa soko ni Watoa
Huduma, Watumiaji na Serikali
Kila kundi lina maslahi binafsi yanayokinzana
kimtazamo.
Mtoa huduma – HUDUMA HAFIFU, FAIDA
KUBWA.
Mtumiaji – HUDUMA BORA, GHARAMA NAFUU.
Serikali - KODI
Utangulizi unae.
Maslahi ya Mtoa huduma yanarandana na
maslahi ya Serikali katika Uchumi wa
soko.
Faida kubwa kwa mtoa huduma - huzaa
Kodi Kubwa kwa Serikali.
Dira ya sera ya Uchukuzi
Dira ya uchukuzi ni kuwa na huduma
bora, nafuu, za uhakika, zenye kukidhi
mahitaji ya kila nyanja ya jamii kiuchumi,
na zinazozingatia usalama na pia
kuhifadhi mazingira
Dhamira ya Sera ya Taifa
Kuendeleza miundombinu na huduma za
uchukuzi zenye kuzingatia usalama,
uhakika wa upatikanaji, kukidhi mahitaji
ya uchukuzi kwa gharama nafuu
kulingana na mikakati ya Serikali kwa
maendeleo ya jamii kiuchumi na
mazingira endelevu
Taswira ya Sekta ya Uchukuzi
Gharama za juu (Value for Money
Concept)
Huduma zisizokidhi mahitaji
(Demand/Supply ratio)
Uchakavu wa vyombo vya
usafiri/miundombinu
Ukiukwaji wa haki za watumiaji
HAKI ZA MTUMIAJI
Watumiaji wote bila kujali hali zao za
kimaumbile wana haki sawa.
Kanuni za John F. Kennedy
Maendeleo ya utetezi wa haki za watumiaji
yalianza katika miaka ya 1960 huko
marekani. Aliyekuwa Rais wa Marekani
kwa wakati huo bwana John F. Kennedy
ndiye aliyekuwa chachu ya vuguvugu la
kutetea maslahi ya Watumiaji katika soko.
Kanuni za John F. Kennedy
Watoa huduma na wazalishaji walionekana
kuwa na nguvu na hila nyingi katika
kuhakikisha kuwa wanachokiuza
kinakubalika kwa watumiaji bila kujali
ubora wa huduma au bidhaa hiyo.
Kanuni za John F. Kennedy
Kutokana na hali hiyo, J.F.Kennedy alikuja
na Haki nne za mtumiaji katika suala zima
la kumkomboa mtumiaji kutokana na hila
za soko. Haki hizo zilikuwa haki ya
usalama, haki ya kupewa taarifa, haki ya
kuchagua na haki ya kusikilizwa. Haki hizi
nne zilijulikana kama Kanuni za Kennedy.
Mwaka 1970 raisi Gerald Ford aliongeza
haki ya kuelimishwa
Kanuni za CI
Tarehe 23/03/1978 Consumer
International, katika mkutano wake mkuu
uliofanyika Kyoto, Japan, uliongeza haki
nyingine tatu ambazo ni haki ya kupata
mahitaji muhimu, haki ya kulipwa fidia na
haki ya mazingira salama.
Tarehe 09/04/1985 Umoja wa Mataifa
uliridhia na kuzipitisha rasmi kama Haki
nane za kimataifa za Mtumiaji.
Haki za Watumiaji katika sekta
ya usafirishaji Haki ya kupata mahitaji muhimu
Haki ya Usalama
Haki ya kupewa taarifa
Haki ya kuchagua
Haki ya kusikilizwa
Haki ya kulipwa fidia
Haki ya kuelimishwa
Haki ya mazingira salama
Haki ya kupata mahitaji muhimu
Mwananchi yeyote kwa ujumla anayo haki ya
kupata mahitaji muhimu katika maisha ya
kila siku.
Miundombinu ya usafiri na uchukuzi ni moja
ya mahitaji muhimu kwa watumiaji katika
sekta hiyo. Bara bara nzuri, vyombo vya
uchukuzi vilivyo bora, viwanja vya ndege,
njia za reli, bandari, vivuko vya majini, meli
nk ni mfano wa mahitaji muhimu.
Haki ya kupata mahitaji muhimu
Ibara ya 11 ya Katiba ya nchi yetu ya 1977
pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya
hali bora na maendeleo kwa wananchi.
Sheria mbali mbali zimetungwa ili kukidhi
haja ya ibara hii.
Mifano ya sheria hizi katika sekta ya
usafirishaji ni ile inayoanzisha Tanroads,
Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mamlaka ya
viwanja vya ndege (TAA) na RAHCO.
Haki ya Watu wenye ulemavu
kupata Usafiri Watu wenye ulemavu wanalindwa na Sheria ya Watu
wenye ulemavu ya Mwaka 2010 na Kanuni za SUMATRA.
Kifungu cha 50(b) inatamka bayana kuwa ni kosa la jinai kumkatalia mtu kupata usafiri kwa kisingizio cha ulemavu wake.
Kanuni za SUMATRA za (usalama na viwango vya ubora wa huduma) kwa magari ya abiria, 2008 kupitia kanuni 5 (1) (g) inatamka bayana kwamba kila gari la abiri mjini liwe na sehemu yenye upana wa sentimita 90 x 140 kwa ajili ya “wheel chair”
Haki ya Watu wenye ulemavu
kupata Usafiri
Kanuni ya 5(1)(h) inamtaka kila mtoa
huduma kuweka vifaa vya kumsaidia
mtu mwenye ulemavu.
Ibara ya 44(1)(c) ya Rasimu ya Katiba
Mpya inaweka wazi zaidi haki ya watu
wenye ulemavu kupata usafiri.
Haki ya Watu wenye ulemavu
kupata Usafiri
Ibara ya 44(1)(c) ya Rasimu ya Katiba
inasomeka hivi:-
Mtu mwenye ulemavu anastahiki
kuwekewa miundombinu na mazingira
yatakayowezesha kwenda anapotaka,
kutumia vyombo vya usafiri na kupata
habari
Haki ya Usalama
Mtumiaji wa bidhaa na huduma anayo haki ya kupata bidhaa au huduma iliyo salama isiyokuwa hatarishi kwa maisha yake.
Ibara ya 14 ya katiba inamhakikishia kila raia haki ya kuishi. Sheria mbali mbali zimetungwa ili kukidhi haja ya ibara hii. Mifano ya sheria hizi katika sekta ya usafirishaji ni :
Sheria ya SUMATRA, 2001
Sheria ya leseni za usafirishaji Cap 317
Sheria ya Reli, 2002
Sheria ya meli za biashara, 2003
Sheria ya Usafiri wa anga Cap 80
Sheria ya ushindani, 2003
Factory ordinance cap 297
Haki ya usalama
Kwa mfano Kanuni za SUMATRA za (usalama na viwango vya ubora wa huduma) kwa magari ya abiria, 2008 kupitia kanuni 5 (1) (a) inatamka kuwa ujenzi wa bodi ya basi ni lazima uendane na viwango maalumu vilivyowekwa na TBS (TZS 598:1999).
Haki ya usalama
Kanuni 5 (1) b inatamka kuwa ubora au
uimara wa basi ni lazima uwe umekidhi
viwango vya TBS (TZS 608:2003)
Kanuni 5 (1) c inatamka matairi ni lazima
yakidhi matakwa ya TBS (TZS 617:1999)
Kanuni 5 (2) inataka vitu vifuatavyo visiwe na
nyufa
Chasis frame, leaf spring, axles na rim za
matairi
Haki ya usalama
Kanuni 6 (1) inataka “modifikesheni” ya gari isifanywe ispokuwa kwa kufuata maelekezo ya mtengenezaji.
Mwenye gari anayetaka kufanya modifikesheni nje ya maelekezo ya mtengenezaji ni lazima apate kibali kutoka TBS (Kanuni 6 (2))
Sehemu ya IV ya sheria ya Reli kwa ujumla wake inazungumzia usalama.
Kanuni ya 5 (1) ya Kanuni za usalama wa reli, 2006 inawataka watoa huduma kuandaa mpango wa usalama (safety plan) kama sharti la kupewa leseni.
Haki ya kupewa taarifa Mtumiaji wa huduma na bidhaa anayo haki ya
kupewa taarifa muhimu zinazo husu bidhaa au huduma inayotarajiwa kuuzwa kwake.
Ibara ya 18 ya katiba inazungumzia juu ya haki ya kupata taarifa na uhuru wa kujieleza. Sheria mbali mbali zimetungwa zinazokidhi haja ya ibara hii. Katika sekta ya usafirishaji kuna Kanuni za SUMATRA za (usalama na viwango vya ubora wa huduma) kwa magari ya abiria, 2008, sheria ya meli za biashara ya 2003, sheria ya reli ya 2002, sheria ya usafiri wa anga cap 80, Sheria ya ushindani, 2003 nk.
Tiketi ya abiria
Kanuni ya 14 (2) ya Kanuni za SUMATRA za
(usalama na viwango vya ubora wa huduma)
kwa magari ya abiria, 2008, imeweka mambo
yafuatayo juu ya tiketi ya abiria:
Jina la abiria na namba ya seat
Muda wa kuripoti na kuondoka
Mahali chombo kinapoondoka na mwisho wa safari
Nauli ya safari
Anuani, namba za simu za mtoa huduma
Namba ya chombo
Jina la njia
Haki ya kuchagua
Mtumiaji wa huduma na bidhaa anayo haki ya kuchagua bidhaa au huduma aitakayo kulingana na viwango vinavyoweza kukidhi mahitaji yake. Mzalishaji haruhusiwi kumlaghai mtumiaji ili achague bidhaa au huduma inayokusudiwa kutolewa.
Sheria ya ushindani ya mwaka 2003, sheria ya SUMATRA 2003, TCAA 2003 nk zimemhakikishia mtumiaji juu ya haki hii.
Haki ya kuchagua
Kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Ushindani,
2003 kinakataza kabisa tabia zozote zile za
ufanyaji biashara ambazo zinamuelekeo wa
kudangaya au kupotosha.
Kifungu 16 (a) mpaka (k) cha Sheria hiyo hiyo
kinakataza kabisa tabia au vitendo vyovyote vile
ambavyo vinaweza kumfanya mtumiaji achague
bidhaa au huduma kutokana na hila au
udanganyifu. Ubora wa bidhaa/huduma ndio
kigezo cha kuchagua.
Haki ya kusikilizwa(Kuwakilishwa)
Mtumiaji wa huduma na bidhaa anayo haki ya kusikilizwa katika masuala yote yanayogusa maslahi yake katika soko kupitia njia ya uwakilishi.
Sheria zinazoanzisha mabaraza ya watumiaji za mamlaka za udhibiti zinakidhi haja ya haki hii.
Kazi kuu ya mabaraza haya ni kuwasilisha maoni ya watumiaji kwa Serikali na mamlaka za udhibiti.
Haki ya kulipwa fidia
Mtumiaji wa huduma na bidhaa anayo haki ya kulipwa fidia kutokana na madhara atakayoyapata yanayotokana na huduma au bidhaa aliyoitumia.
Sheria ya leseni za usafirishaji (Transport Licensing Act cap 317) imeweka sharti la kila muombaji wa leseni hiyo kuwa na bima ambayo itawawezesha kuwalipa fidia abiria wao zinapotokea ajali. Sheria nyingine ni kama Sheria ya meli za biashara (merchant shipping Act, 2003), Sheria ya Reli 2002 na Sheria ya uchukuzi wa anga 2006.
Haki ya kulipwa fidia
Sheria za kimataifa ni kama Sheria ya Athens
ya usafirishaji wa abiria na mizigo yao kwa njia
ya majini ya 1974(Athens Convention relating
to the carriage of Passengers and their
Luggage by Sea), Sheria ya Montreal ya
usafirishaji wa anga ya 1999.
Haki ya kulipwa fidia
Kulingana na Sheria za kimataifa na safari za kimataifa Mtoa huduma anawajibika kuwalipa fidia abiria wanapopata madhara yafuatayo:
Kuchelewa kuanza safari, Kuchelewa kwa mizigo au shehena, kuharibika kwa mizigo au shehena, kuumia au kupoteza maisha kunakotokana na ajali.
Haki ya kulipwa fidia
Kulingana na sheria ya Athens fidia kwa majeruhi
na vifo safari za majini ni kiwango kisichozidi
700,000 francs kwa kila abiria, mizigo ya ndani ni
kiwango kisichozidi 12,500 francs kwa kila abiria.
Fidia kwa uchelewaji wa safari za ndege ni
kiwango kisichozidi dola za kimarekani 5000 kwa
kila abiria, madhara kwa mizigo ni kiwango
kisichozidi dola za kimarekani 1200 kwa kila
abiria, na majeraha au vifo vya ajali ni kiwango
kisichozidi dola za kimarekani 120,000 kwa kila
abiria
Haki ya Kulipwa fidia
Kwa usafiri wa majini ndani ya Tanzania,
sheria ya meli za biashara, 2003, imeweka
kiwango cha hesabu cha 333,000 kwa meli
zisizozidi tani 500. tani 501 mpaka 3000
kiwango cha hesabu 500. Tani 3001 mpaka
30,000 kiwango cha hesabu 333.Tani 30,001
mpaka 70,000 kiwango cha hesabu 250. Meli
zinazozidi tani 70,000 ni kiwango cha hesabu
167.
Haki ya kulipwa Fidia
Kurudishiwa nauli pindi safari iliyopangwa inapovunjika.
Kanuni ya 11 (1) a ya Kanuni za SUMATRA za (usalama na viwango vya ubora wa huduma) kwa magari ya abiria, 2008, inasema kuwa endapo Basi litaharibika kwa safari za mijini, mtoa huduma anatakiwa atoe usafiri mbadala ndani ya dakika 15 au arudishe nauli kwa abiria inayofanana na nauli ya sehemu iliyobakia ya safari.
Haki ya kulipwa Fidia
Kanuni ya 11 (1) b ya kanuni hizo hizo, Kwa
safari za kutoka mkoa hadi mkoa, basi
likiharibika njiani litengenezwe ndani ya
masaa mawili au mtoa huduma atoe usafiri
mbadala ndani ya masaa hayo.
Abiria akiamua arudishiwe nauli, basi mtoa
huduma atarudisha nauli kwa abiria ya
sehemu iliyobaki ya safari yake ndani ya siku
saba. Kanuni ya 11 (2) a
Haki ya kuelimishwa
Mtumiaji wa huduma na bidhaa anayo haki ya
kupewa elimu juu ya huduma au bidhaa anayo
tarajiwa kuitumia.
Hii ni haki ya Elimu kwa ujumla wake. Kazi ya
kuwaelimisha watumiaji wa huduma za usafiri
inafanywa na mabaraza ya watumiaji ya
Mamlaka za Udhibiti. SUMATRA CCC, TCAA
CCC, SUMATRA na TCAA.
Haki ya mazingira salama
Mtumiaji ana haki ya kusafiri na kutumia huduma au bidhaa za usafiri katika mazingira yaliyo salama.
Sheria mbali mbali zimemhakikishia mtumiaji juu ya haki hii. Sheria hizo ni kama Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, Sheria ya leseni za usafirishaji cap 317, Kanuni za SUMATRA za (usalama na viwango vya ubora wa huduma) kwa magari ya abiria, 2008, sheria ya mamlaka ya usafiri wa anga cap 80, Kanuni ya 18 juu ya mazingira katika usafirishaji wa anga nk
Haki ya mazingira salama
Kwa mfano Kanuni za SUMATRA za
(usalama na viwango vya ubora wa
huduma) kwa magari ya abiria, 2008,
watoa huduma wanatakiwa kuhakikisha
kuwa kuna huduma ya vyoo vilivyo safi
katika vituo vya kungojelea abiria (Kanuni
18 (1) a. Kanuni 18 (2) inawataka watoa
huduma kuwa na huduma hiyo katika
vituo vyote vya njiani.
Wajibu wa Mtumiaji
Wajibu wa kudai mahitaji muhimu
Wajibu wa kusoma na kufuata maelekezo ya
usalama
Wajibu wa kutafuta taarifa muhimu
Wajibu wa kuchagua na kufanya maamuzi sahihi
Wajibu wa kuwasilisha maoni na kero
Wajibu wa kudai fidia
Wajibu wa kujielimisha
Wajibu wa kutetea mazingira salama na
kuyatunza
Hitimisho
Katika uchumi wa soko, watumiaji wanaulazima mkubwa sana wa kujua haki zao na masuala mengine yanayo husu soko. Serikali iliamua kuunda mabaraza ya watumiaji katika sekta mbali mbali ili kukidhi haja hiyo. Watumiaji wanapaswa kuyatumia mabaraza haya ili kupata ufahamu wa haki zao na uwezo wa kusimama imara katika soko.
Mabaraza kupitia kamati zake za mikoa na kanda yana wajubu mkubwa wa kuwafikishia elimu hiyo watumiaji wote waishio vijijini, wilayani na mijini ili kumkomboa mtumiaji.
Asanteni sana
Timiza wajibu wako,
utapata haki yako.