32
ISSN: 0856-8995 Jipange ujifungue salama Haliuzwi

Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

  • Upload
    others

  • View
    33

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

ISSN

: 08

56-8

995 Jipange

ujifungue salama

Haliuzwi

Page 2: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

2 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Si Mchezo! Huzalishwa na kusambazwa.

Si Mchezo! husambazwa.

Lilikozalishwa toleo hili.

Uhai wa mama na mtoto ni changamoto

kubwa hapa nchini lakini imezidi kushika chati

vijijini. Najua ni jukumu letu sote kukabiliana

na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora

upewe kipaumbele!

Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa

unapojitambua kuwa umepata ujauzito. Anza kuandaa vitu kama vile nguo, chakula, pesa n.k

ambazo zitakusaidia wakati utakapojifungua.

Page 3: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

3

TAHARIRIKigooooomaaaa eeee Kigoma yeeee…. Naaam tumefika Kigoma! Mji maarufu kwa dagaa na migebuka! Mafuta ya mawese ndiyo mwake. Lakini zaidi ya yote tunaufagilia ukarimu wa wana Kigoma. Tumefarijika sana kuwa na ninyi katika uandaaji wa toleo hili. Shirika na Vijana la KIVIDEA tunawapa ‘big up’ kwani mmetupa ushirikiano wa hali ya juu. Sasa ni zamu yako msomaji kuperuzi yaliyomo humu tuliyokukusanyia huko mwisho wa reli. Kitu kinahusu uzazi salama. Twende sawa.

Majuka

YALIYOMO4 Stori Yangu: Jipange ujifungue salama

6 Mambo Mapya

8 Hadithi ya Picha: Uchungu wa mwana

12 Je, Wajua: Tumkomboe mama na mtoto

14 Sauti yangu

16 Burudani: Leka dutigite

18 Ruka Juu: Washiriki wa Ruka Juu II

20 Nguvu za mwanaume: Nenda naye bega kwa bega

21 Nguvu za mwanamke: Usimdharau mkunga

22 Chezasalama: Malaria ni adui wa mjamzito

24 Katuni: Lawama

27 Ukweli wa mambo: Huduma rafiki huleta maendeleo

28 Sema Tenda: Haki za mjamzito

30 Marie Stopes: Utoaji mimba kwa njia zisizo salama ni hatari

31 Ushauri

Mkurugenzi MtendajiDr. Minou Fuglesang

Mkurugenzi wa Habari Amabilis Batamula

Meneja MachapishoJiang Alipo

Mhariri Majuka Ololkeri

WaandishiRaphael NyoniRebeca GyumiBetty Liduke

WashauriTimu ya Femina HIP

Meneja UhusianoLilian Nsemwa

Katuni na UsanifuBabaTau, Inc.

Mpiga Chapa Jamana Printers Ltd

Usambazaji EAM Logistic LtdFemina HIP na Washirika

Si Mchezo! limefanyika kwa hisani kubwa ya Serikali za Sweden (Sida), Denmark (DANIDA), HIVOS, RFSU, Mama Misitu , TWAWEZA na JHU-CCP/TCCP

Yaliyomo humu ndani ni jukumu la Femina HIP na hayawakilishi maoni au mitazamo ya wafadhili.

Wasiliana nasi kwa:S.L.P. 2065, Dar es SalaamSimu: (22) 212 8265, 2126851/2 Fax: (22) 2110842email: [email protected] Mchezo! huchapishwa na Femina HIP.Sms: 15665

Hapa ndiyo mwisho wa

reli...

Karibuni Kigoma

Page 4: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

4 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Umbali kutoka ninakoishi hadi mahali unapoweza kupata huduma za kituo

cha afya ni zaidi ya saa tatu kwa usafiri wa baiskeli. Pata picha umbali huo natembea kwa miguu kwenda kliniki huku nikiwa mjamzito!

Naitwa Hadija Malik (18), naishi Kijiji cha Kajeje, Kigoma Vijijini. Niliacha shule nilipokuwa darasa la nne kutokana na wazazi kutotilia maanani masomo yangu na pia mazingira magumu ya kujifunzia huko shuleni. Nilikaa nyumbani nikijishughulisha na kilimo. Mwaka 2007, nilikutana na mvulana ambaye tumependana hadi tukaanza kupanga kuoana. Mipango hiyo iliingia dosari niliposhika ujauzito. Nilipomueleza kuwa nimeshika ujauzito akanibadilikia hata akahama kijiji na sikujua alikoelekea.

Wakati wa ujauzito sikupata shida zaidi ya uchovu wa kawaida na kichefuchefu kwa muda mrefu. Kutokana na umbali wa kituo cha afya, nilihudhuria kliniki kwa mara mbili tu, nikiwa na ujauzito wa miezi mitano na minane. Nilishauriwa kliniki niwe nahudhuria kila mwezi lakini

Jipange ujifungue salama

Hadija Malik akiwa kwenye shughuli zake za kilimo huko Kigoma.

STORI YANGU

Page 5: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

5MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Jipange ujifungue salama

Hadija akiwa na mtoto wake wa kwanza katika Kijiji cha Ilagala, Kigoma.

nilishindwa. Ukiachilia changamoto ya umbali kutoka Kajeje hadi Ilagala, kuna gharama za usafiri na pia njiani humuoni mtu labda siku ya soko la Ilagala. Siku mimba ikiwa na miezi tisa, nilisikia kuumwa. Kwa kuwa sikujua ni jinsi gani mtu

atasikia uchungu wa kujifungua, sikufahamu kuwa ndiyo uchungu wenyewe umeshaanza. Bibi yangu aliponiona nahangaika akajua tayari, kwa hiyo akamwita mkunga wa jadi. Uchungu ulinianza kwenye saa tisa usiku nikajifungua saa tatu asubuhi kwa msaada wa mkunga. Lakini damu zilinitoka nyingi sana hadi nikazimia. Nilipewa dawa za kienyeji za kuongeza damu lakini hazikusaidia, niliendelea kudhoofu.

Hali yangu iliendelea kuwa mbaya kutokana na kupoteza damu nyingi na sikuweza kupelekwa hospitali kwani hatukuwa na uwezo kifedha na hata hivyo, hapakuwa na usafiri. Ilibidi kaka yangu atoke Kajeje kwenda kunitafutia dawa katika Zahanati ya Ilagala ambazo zilinisaidia.

Sasa hivi nina ujauzito wa pili. Kutokana na taabu nilizokutana nazo katika ujauzito wa kwanza, nimejifunza mengi. Nimeanza kuhudhuria kliniki ingawa bado siwezi kwenda kila mwezi. Ila sasa nimejipanga, nikifika mwezi wa mwisho naenda kukaa kwa bibi yangu mwingine anayeishi Ilagala ili niwe karibu na kituo cha afya kwa ajili ya kujifungua.

Nawashauri wasichana ambao wamepata ujauzito kuwa ni vizuri kujipanga ili uweze kujifungua salama. Hiyo ni pamoja na kuhudhuria kliniki, kujitahidi kujiwekea akiba angalau uwe na fedha au chakula kusaidia pindi utakapojifungua, kuwa karibu na kituo cha afya pale unapokaribia kujifungua. Kumbuka kuwa ni jukumu lako kufanikisha hayo ili muwe salama, wewe na mtoto wako.

Page 6: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

6 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

MAMBO MAPYA

Kikundi cha Polisi jamii wakiwa katika picha ya pamoja huko Kigoma. Kikundi hiki kimeanzishwa na wananchi wa Kata ya Katubuka. Baada ya kuona kuna haja ya kuchukua hatua wao we-nyewe kuweka ulinzi katika eneo lao, vijana hao waliwashirikisha viongozi wa ngazi ya Kata yao. Walisaidiwa na Halmashauri kuwapatia askari polisi wa kuwapa mafunzo ya mbinu za kupam-bana na wahalifu kama vile kufanya upelelezi, kugundua ishara za kihalifu na kugundua sehemu zenye vigenge visivyo salama kwa raia

Kupata mafuta ya mawese ni shughuli pevu

Mwandishi wa habari wa Femina HIP, Raphael Nyoni (wa pili kushoto) akipewa maelezo namna mafuta ya mawese yanavyotengenezwa na mmiliki wa kiwanda cha kukamua mafuta hayo, Hamisi Shabani Maganda kwenye Kivuko cha Lusesa Mto Malagarasi katika Kijiji cha Ilagala, Kigoma. Wengine ni Mtangazaji wa Fema Radio, Rebeca Gyumi (kulia) na Mkuu wa Idara ya Vijana katika Shirika la Kigoma Vijana Development Asso-ciation (KIVIDEA), Babu Paschal

Dagaa bwerere Kigoma

Moja ya shughuli kuu za wakazi wa Kigoma ni uvuvi na uuzaji wa dagaa. Unaweza ukawapata wakiwa wabichi au wal-iokaushwa. (Hapa ni Kijiji cha Muyobozi ambako baadhi ya vijana walitutambua tu-liposhuka tu kwenye gari kwani wamewahi kutuona baadhi yetu kwenye vipindi vyetu vya luninga, Fema TV talk show.)

Usisubiri ajira ikufuate, chakarika!

Hiki ni kikundi cha vijana watano, walioshauri-ana kufanya biashara ya kutengeneza na kuuza majiko, mabanio ya kushikia moto, masanduku ya wanafunzi, makopoya kubania mikate n.k. Wako Kigoma Mjini. Licha ya kusafisha mji kwa kufanya vyuma chakavu kutumika tena, wame-saidia jamii kupata vifaa mbalimbali vya jikoni na wamewezesha wajasiriamali wadogo kupata vifaa kwa bei nafuu na wao kujipatia kipato kinachoendesha maisha yao.

Vijana wakianika dagaa baada ya kuvua kwenye Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Muyobozi, Kigoma.

Hii ni nguvu ya pamoja

Page 7: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

7MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Page 8: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

8 Si Mchezo! MACHI-APRILI 20138 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013 9MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Page 9: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

9MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo! 9MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Page 10: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

10 Si Mchezo! MACHI-APRILI 201310 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Page 11: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

11MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo! 11MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Page 12: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

12 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

JE, WAJUA?

Tumkomboe mama na mtoto…Yaliyomkuta Ilakoze ni uwasilishi wa

mazingira halisi yaliyoko maeneo mengi hasa kwa wananchi waishio vijijini. Mara nyingi tu utasikia vifo vya mama na mtoto vimetokea kutokana na sababu mbalimbali.

Ni wajibu wetu sote…

Wanaopewa huduma wana wajibu:• Kufahamu haki zao za huduma za afya kama

kusikilizwa na daktari, kutotolewa kwa mtu yeyote siri za ugonjwa wake, kudai huduma bora

• Kuwatetea watoa huduma pale watawala wa-naposhindwa kuweka mazingira rafiki ya kutoa huduma n.k

Wanaotoa huduma wana wajibu:• Kutoa huduma kulingana na uwezo wao wote• Kutimiza kiapo chao cha kazi kwa kutoa hu-

duma muda wote wanapohitajika• Kutoa huduma bila kulalamika • Kutunza siri za wapewa huduma.

Hata hivyo, watoa huduma pia wanahitaji kuwekewa mazingira stahiki kama vile zahanati au hospitali kuwezeshwa vifaa, kupewa maslahi kulingana na kazi zao, kupewa motisha na kuishi katika mazingira yanayostahili.

Nani alaumiwe?

Katika mazungumzo yetu, vijana huko Kigoma, im-eonekana kwamba kila mmoja ana jukumu la kuyat-afutia ufumbuzi matatizo yaliyotajwa hapo juu. Suluhu la matatizo hayo isiachiwe Serikali peke yake, bali ni ju-kumu la jamii nzima. Mama mjamzito ni jukumu lake pia kuchukua hatua za haraka kuhakikisha anakuwa katika mazingira salama wakati akielekea kipindi cha kujifungua.

Kwa nini vifo hivi vinatokea?

Zipo sababu za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja;

Moja kwa moja ni hizi:• Kifafachamimba• Kuvujadamunyingikabla,wakati

na baada ya kujifungua nk.

Zisizo za moja kwa moja ni hizi:

• Kushindwakulipiagharamazausafiri na za kujifungua

• Ushawishiwawakungawajadi• Ufahamumdogokuhusuafyaya

uzazi• Milanadesturimbayazinazozuia

wajawazito kujifungua chini ya usimamizi wa mtaalamu wa afya kwenye vituo vya afya.

• Miundombinumibovuyabarabara

• Kukithirikwarushwakwenyevituo vya afya

• Idadindogoyawatoahudumayaafya

• Umbaliwavituovyaafya• Kutokuwanavituovyakutosha

vyenye huduma za dharura• Uongozimbaya

SwaliPamoja na juhudi nyingi za serikali kuweza kufaniki-sha uzazi salama, unadhani una nafasi gani kuweza kuchangia juhudi hizo kufanikiwa zaidi? Tujadili.

Page 13: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

13MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

MAMAMISITUAD

Page 14: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

14 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Wewe pia unaweza kulonga na vijana wenzako. Tuandike maoni, ushauri, vichekesho,maswali nk,

weka anuani yako na tuma ukiambatanisha na picha

yako kwa Mhariri, Jarida la Si Mchezo!,

S.L.P 2065, Dar es [email protected]

Au tumbukiza katika boksi la Si Mchezo! kama lipo katika

eneo unaloishi.

SAUTI YANGU Kama una chochote unachotaka kusema tuandikie ili upate fursa ya kuwaelimisha wengine

Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu ni ya wasomaji, si lazima yalingane na msimamo wa Femina.

Si Mchezo!Femina HIPSLP 2065,

DSM

Tuzingatie haki za watoto

Kero yangu mimi ni kwa watu wan-aohujumu haki za watoto yatima na kuwafanya vijakazi wa ndani na ku-wanyima haki zao za msingi, kama kusoma, kushiriki michezo na kutoa mchango wao wa mawazo katika jamii. Ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha tunalidhibiti hili na ku-wapatia watoto haki zao za msingi ili wakue katika mazingira bora.

Seif H. Shabani Majengo, Kigoma

Naifagilia ManispaaNaishukuru Manispaa ya Kigoma kwa kutoa vifaa vya msaada kwa watoto wasio-jiweza na wanaoishi katika mazingira magumu na wale wasiojiweza kiuchumi ili kuweza kutimiza malengo yao ya baadaye na kujenga Taifa la wasomi.

Kinley Stanley,Kibondo, Kigoma

Tahadhari kabla ya hatari

Kero yangu ni kuhusu madampo ya uchafu yaliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji ambayo ya-mewekwa katikati ya mitaa na yanaweza kukaa hata miezi mitatu bila kuzolewa. Hii ni hatari kwa wakazi wanaoishi maeneo hayo kwani ma-gonjwa ya mlipuko yanaweza kutokea. Jamani tuwajibike kusafisha mazingira yetu.

Hemed Moshi Ujiji, Kigoma

Tufikirieni kuhusu hii michango

Sielewi kuhusu wanavyosema shuleni tutoe michango ya chaku-la na wakati sisi wengine hatuna uwezo wa kutoa kiwango cha fedha walichokiweka. Naomba Serikali itusaidie kuhusu suala la mchango wa hizo fedha ili na sisi ambao wazazi wetu hawajiwezi kiuchumi tuweze kupata chakula shuleni.

Asha Hamisi Kigoma

Page 15: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

15MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Page 16: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

16 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Kigoma aeeee, Kigoma weaaah (Tu-nayo furaha) Leka Dutigite

Tunayo furaha kuwa wazawa wa KigomaaLeka dutigite wishava mineke x3

(Ommy Dimpoz)K k k K-town Kasulu ndio baba alipo-zaliwa ooh japo niko Dar,Naupenda mkoa wangu k k Kigoma,Kama vipaji tumejaliwa,Kaseja na Lunya, fahari mkoa wangu,Amabhese ni vhilibwa ni vhi kulabha ukalumba (dimpozi kwa pozi)Kigoma mkoa wangu, ndio fahari yangu

Abdul KibaArdhi yenye rutuba, ya kustawisha chelewa,Gombe na Mahale, zenye sokwe wasi-olewa,Kigoma inapendeza sanaaa, Twaishukuru hivi ndivyo ninavyosema,Mina furaha mbuga zetu, mina furaha makumbusho yetu, Mi nafurahii hey! Mina furaha

KiitikioKigoma aeeee, kigoma mama wee aaahhh (Kigomaaaaa)Leka Dutigite wishava mineke x4

ChegeKigoma ndipo nlipotoka aaah, nime-kuja Dar kutafutaSiku zote nitawakumbuka, najivunia na sitojuta (Nakumbuka)Nakumbuka mama alisema (Nakum-buka)Mkataa kwao mtumwa, (Lakujijweee),

RechoKigoma inatamba, Tanganyika ina-

bamba,Tufurahi, tusherehekee pamoja,

MwasitiTwajivunia Kigomaaa,Tunamshukuru Maulana,

Baba LevoKigoma lango la Tanzania,Bandari kwa kahawa, shaba kwa matania,Amani kwa wazawa, Kasulu Kibondo uvinza,

LinexAvhantu bhakundi vikobwaa

Baba LevoZiwa refu tunalo (aunhaaa), na madini tunayo (Aunhaa),Tuna mbuga za wanyama kama Gombe na Mahale,Ardhi safi tunayo (aunhaa), na vipaji tunavyo (Aunhaa),Sauti safi tena tamu, tamu, tamu,tamu

Vigelegele na mashamushamu, sha-mushamu, Kigoma yetu mambo bambam, bam-bam

Banana ZoroMeli ya Liemba, wanasiasa mashujaa, watetezi wa taifa Kigoma tunatoka wote mastaa yeeah,Miss Tanzania K Lynn yeeah, Kaseba Champion yeah

Kiitikio

DiamondKigoma kwa Migebuka Wese na ugali wa muhogo, aghaa wa muhogo,Ndivyo vimenifanya nikawa Diamond, kwa vitenge na mashuka mise na chumvi kidogo, aghaa kidogoTena na muda nikawa mfalme, Tena Kigoma ya sasa sio kama ya zamani,

BURUDANI

Wimbo: Leka dutigite Wasanii: Kigoma All Stars

Page 17: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

17MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Vigelegele na mashamushamu, sha-mushamu, Kigoma yetu mambo bambam, bam-bam

Banana ZoroMeli ya Liemba, wanasiasa mashujaa, watetezi wa taifa Kigoma tunatoka wote mastaa yeeah,Miss Tanzania K Lynn yeeah, Kaseba Champion yeah

Kiitikio

DiamondKigoma kwa Migebuka Wese na ugali wa muhogo, aghaa wa muhogo,Ndivyo vimenifanya nikawa Diamond, kwa vitenge na mashuka mise na chumvi kidogo, aghaa kidogoTena na muda nikawa mfalme, Tena Kigoma ya sasa sio kama ya zamani,

Kigoma ya sasa imesonga mbele Buzebazeba ya sasa sio kama ya zamani, Kasulu ya leo iiiiiiiii yeeeeeeiiii

Peter MsechuAmani na upendo ndio lugha ya Kigoma,Kigoma haijagoma, Kigoma yaenda mbele,Rangi yako ya kijani, upepo wako ni mwanana,Kigoma nakupenda, Kigoma una-nipenda,

Queen DarleenUmwami mtahe (Kigoma)Umwami bhusindi (Kigoma)Umwami Ruhinda (kigoma)Shukrani Kigoma x2

Kigoma shukrani kigoma,Kigoma nyumbani kigoma,

Kiitikio

Wimbo: Leka dutigite Wasanii: Kigoma All Stars !!! !

Dogo janja...BABA: Kati ya mimi na mama yako unampenda nani zaidi?DOGO: Nawapenda woteBABA: Mimi ningeenda Mwanza halafu mamako akaenda Arusha, wewe ungeenda wapi?DOGO: Ningeenda ArushaBABA: Kwa nini?DOGO: Arusha nakupendaBABA: Je, mi ningeenda Arusha mama yako akaenda Mwanza wewe ungeenda wapi?DOGO: Ningeenda MwanzaBABA: Hee, unanikwepa unam-fuata mama yako!DOGO: Hapana, Arusha si ningekuwa nilishakwenda?

Mke huyu kiboko!Mume na mke walikuwa safarini, mume akawa anaendesha gari. Alisimamishwa na trafiki ikawa hivi:TRAFIKI: Mzee unajua kuwa ulikuwa spidi sana?MUME: Hapana.MKE: Nilimuambia apunguze spidi akawa mbishi.Mume akamjibu mke: Kelele, hayakuhusu nitakunasa vibao sasa hivi.MKE: Na leseni pia nimeimba wee hajachukua.MUME: Nitakung’oa huo mdo-mo!Trafiki akamuuliza mke, “eti mama anakujibu hivi siku zote?”MKE: Hapana, mpaka akiwa amelewa.

Huyu naye zuzu!Kuna jamaa mmoja alikwenda nyumbani kwa rafiki yake kupiga stori, mara mvua kubwa ikanyesha, mwenyeji akamwambia jamaa usijali utalala hapa sebuleni. Jamaa akasema hamna shida, mwenyeji akaenda bafuni kuoga, alipotoka akachungulia sebuleni akamuona jamaa amelowa tepe tepe, akamuuliza kulikoni rafiki? Jamaa akasema nilienda nyumbani kuchukua shuka.

Page 18: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

18 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

RUKA JUU

Mustapha Mohamed Mwingu (27)

Mkulima kijana kutoka kijiiji cha Mkindo Wilaya ya Mvomero, Morogoro. Baada ya kumaliza darasa la saba mwaka 1999, alielekea jijini Dar es Salaam na kujaribu biashara kadhaa bila ya mafanikio. Mustapha aliamua kurudi nyumbani mwaka 2004 ili kujihusisha rasmi na kilimo katika kipande cha ardhi alichopewa na wazazi wake mwaka 1998. Alijihusisha katika kilimo cha umwagiliaji cha mpunga. Mustapha anashirikiana na mkewe katika shughuli zake za kilimo.Anaweza kuihudumia familia yake, kulipa ada na kununua eneo zaidi kwa ajili ya kilimo. Kilimo ni moja ya sababu ambazo hazitamtoa tena kijijini.

Aziza Juma Saki (28)

Mkulima kutoka Wilaya ya Monduli, Arusha. Alianza shughuli hii akiwa mdogo kwa kufanya vibarua mashambaniMwaka 2009 alirithishwa ekari moja ya ardhi baada ya wazazi wake kufariki. Ndipo aliamua kukaza buti katika kilimo cha mpunga kwa ajili ya biashara ili aweze kumudu familia yake na ndugu wengine watatu waliokuwa wakilelewa na wazazi kabla ya kufariki. Japo Aziza hakufanikiwa kupata elimu ya sekondari, anatamani kuona ndugu zake wanafika mbali zaidi kielimu.

Yusta Mwilinga Mwanalinze (21)

Alianza kilimo tangu akiwa darasa la kwanza akiwa kule kijiji cha Mkunda, Wilaya ya Sumbawanga, Rukwa. Amekulia katika familia ya wakulima na kwenda shamba siyo jambo la kulifikiria. Anajishughulisha na kilimo cha mahindi.Wakati alipokuwa akiendelea na masomo yake ya sekondari, ekari mbili za shamba zilikuwa tayari ni zake. Kilimo kimempa pesa za kujikimu bila kuwahusisha wazazi. Ukiachilia mbali kilimo, Yusta huchoma maandazi ili kujiongezea kipato ambacho hutumia kuwalipa vibarua wake shambani.

Washiriki wa shindano la Ruka Juu II hawa hapaNi shindano kabambe ambalo linawashindanisha wakulima vijana wadogo sita wakionyesha mbinu wanazotumia kufanikiwa katika kilimo kama biashara. Baada ya ‘chuja nikuchuje’, hawa sita ndiyo waliobahatika kufika fainali. Utapata kuwajua kwa kifupi juu shughuli zao.

Page 19: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

19MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Lawrian Batlomeo Joseph (26)

Kijana mkuli-ma kutoka Wilaya ya Kara-tu, Arusha. Ali-pomaliza elimu yake ya msingi, wazazi wake hawakuweza kumsomesha kwa kiwango cha elimu ya sekondari hivyo akaamua kujihusisha na kilimo.

Alipewa ekari tano na mama yake, akaanza kilimo cha biashara ya mahindi na mbaazi. Taratibu akaendelea kuongeza mazao kama vile maharage na alizeti.Ameweza kununua mifugo, plau na ameweka nishati ya umeme wa jua nyumbani kwa wazazi wake. Jembe la plau anakodisha kwa wakulima wengine ili kuongeza kipato.

Joseph Obalidi Kizito (27)

Akiwa ni baba wa watoto wanne, anajihusisha na kilimo cha nyanya katika Wilaya ya Nkasi, Rukwa. Anatumia kilimo

cha umwagiliaji. Umwagiliaji huo unafanyika kwa kutumia visima ambavyo alitumia nguvu zake kuvichimba. Mwaka 2009, alirithishwa ekari nne na robo tatu na babu yake.Amenunua mashine ya kusukuma maji pamoja na jenereta kwa ajili ya umwagiliaji na amefungua akaunti ya benki. Mbali na hayo, amenunua ng’ombe; wawili kwa ajili ya kilimo na mmoja anafuga kama chanzo cha mapato iwapo itatokea dharura na familia kuyumba.

Tatu Rashid Kilolo (22)

Anatoka Wilaya ya Kilosa, Morogoro ni mkulima wa nyanyachungu kwa ajili ya biashara, na mahindi kwa ajii ya chakula kwenye shamba la robo tatu ya ekari alilopewa na mzazi.Kutokana na kulelewa na mama ambaye ni mkulima, Tatu alimuomba mzazi wake huyo kumpa kipande cha ardhi ili aweze kujihusisha na kilimo yeye mwenyewe. Hivi sasa akiwa na watoto wawili, anaweza kuwapatia mahitaji muhimu. Anafurahia kilimo na hajawahi kujuta kwa nini aliingia katika kilimo.

Washiriki wa shindano la Ruka Juu II hawa hapa

Page 20: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

20 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

NGUVU ZA MWANAMUME

Nenda naye bega kwa bega!

Tetesi zilizozagaa

• Ukiongozananamkeo kliniki, basi umeshalishwa limb-wata.

• Niaibukuongozanana mke mjamzito.

• Niwanawaketundiowanaostahili kwenda kliniki.

Ni muhimu

• Kupataelimuyauzazisalama

• Kutosikilizauzushiwawatu.

• Kuijalinakuilindafamilia yako kwa kuwa na taarifa muhimu.

Muhimu kuzingatia

Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa kina mama wanajifungua katika mazingira salama na wanapata msaada ambao unawezekana kutoka kwa wanaume ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Ni wanaume wachache wanaofahamu umuhimu wa

kuongozana na mjamzito kwenda kliniki. Mara nyingi wanaume hawapatikani kutoa msaada wa hali zaidi ya mali (pesa ya kwenda na kurudi kliniki). Wengi huchukulia kuwa ni suala la kina mama peke yao. Je, unafahamu ni kwa kiasi gani mama mjamzito anakuwa kwenye hatari ya kupata matatizo wakati wa kujifungua? Na ni kwa kiasi gani unahitajika kuhudhuria kliniki?

Hali halisi ni kwamba

Ukiongozana na mkeo kwenda kliniki utasaidia: • Kuboreshwakwahuduma

kutoka kwa watoa huduma • Utapataelimustahili• Kuokoamaishayamama

na mtoto wakati wa kuji-fungua.

• Kuboreshahusianowakona mtoto atakayezaliwa

J K u m b u k a

Ushiriki wako katika huduma za afya hasa kipindi cha ujauzito wa mama, utachangia kwa kiasi kikubwa kujenga familia yenye furaha

Page 21: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

21MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

NGUVU ZA MWANAMKE

Mhariri wa Jarida la Si Mchezo!, Majuka Ololkeri akifanya mahojiano na Wakunga Ashura Moha-medi (kulia) na Ashura Athumani walipotem-belewa na timu ya Si Mchezo katika Kijiji cha Ilagala, Kigoma.

Usidharau mkunga…

Wamefurahia mabadiliko

Ashura Mohamedi na Ashura Athumani ni wakunga wa jadi waliofanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 30. Mwanzoni walikuwa wakifanya shughuli hiyo kienyeji lakini kwa sasa wamepewa mafunzo na wataalamu wa afya ili waweze kushirikiana na vituo vya afya vilivyoko maeneo yao.

Wamejifunza mambo ya msingi…

Pamoja na kwamba wana utaalamu wa kijadi, wakunga hao wameelezea kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kwani wamegundua kuwa walikuwa wakifanya kazi hiyo katika mazingira hatarishi kwa afya zao na wazazi. Mafunzo yalijikita katika:• Jinsiyakutumiavifaavyakisasakama

glovu n.k ili kujikinga na magonjwa ya maambukizi kama vile VVU

• Namnayakumsaidiamamanamtotokablana baada ya kujifungua.

• Namnayakutumiakadiyaklinikikutoahuduma rafiki kwa wajawazito.

J K u m b u k aKutokana na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya haiwezekani kwa wajawazito wote kufika hospitali hivyo basi kuna umuhimu mkubwa wa uwepo wa wakunga wa jadi waliowezeshwa kwa kuongezewa ujuzi ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto

Unapozungumzia masuala ya uzazi, hutoacha

kuwagusia wakunga wa jadi kwani wamekuwa wakitoa huduma ya kuwazalisha kinamama tangu enzi na enzi. Kutokana na maendeleo ya miundombinu, watoto wengi huzaliwa hospitalini, lakini hiyo haijapunguza uhitaji wa wakunga hasa maeneo ya vijijini. Tulipata fursa ya kuwatembelea baadhi ya wakunga wa jadi na kuteta nao.

Page 22: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

22 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Malaria ni adui wa mjamzito

Unaweza ukaona ni ugonjwa mdogo sana, mara nyingi utasikia, ‘Aah,

malaria inanisumbua kidogo,’ na watu wanaichukulia ‘poa’. Ila malaria ni moja ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi sana hapa nchini. Malaria huchangia zaidi ya asilimia 20 ya vifo vya wajawazito Tanzania.

Si kwamba malaria inayowapata wajawazito ni tofauti na hii ya kawaida, wadudu ni walewale, ila wajawazito wana uwezekan0 mkubwa zaidi wa kushambuliwa na vijidudu vya malaria na kuathirika zaidi kuliko mtu asiye mjamzito.

Hiyo inatokana na kwamba kinga ya mwili huwa inapungua mtu anapokuwa mjamzito, hivyo kumfanya awe hatarini zaidi kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria.

Athari za malaria kwa mjamzito

Mjamzito anapokuwa na malaria na isipotibiwa haraka na kwa uhakika inaweza ikamsababishia matatizo mbalimbali yeye na mtoto aliye tumboni. Malaria inaweza kusababisha:• Matatizo ya ukuaji kwa mtoto aliye

tumboni ambayo husababisha ulemavu• Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati ‘njiti’• Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo• Mimba kuharibika• Mama kupungukiwa na damu kiasi

cha kuhatarisha maisha yake wakati wa kujifungua

CHEZASALAMA

Page 23: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

23MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

J K u m b u k a

Malaria inaua, mjamzito hakikisha unalinda afya yako na ya mwanao kwa kuzingatia kunywa dozi mbili za SP wakati wa ujauzito. Malaria Haikubaliki!

Tahadhari kabla ya hatari

Ndiyo, usisubiri kupata malaria na athari zake ili uanze kuitibu, kwani malaria inaua. Mjamzito akipata inaweza kuwa ameshachelewa kwa kuwa inaweza ikawa tayari imeshaanza kumuathiri mtoto aliye tumboni. Kwa hiyo chukua tahadhari kabla ya hatari kwa kujikinga dhidi ya ugonjwa huu hatari. Yaani mjamzito kujikinga dhidi ya malaria ni rahisi kama kuhesabu moja, mbili, tatu!

• Mjamzitoahakikisheanalalakwenyechandarua kilichowekwa dawa kila siku. Vyandarua hivi vinapatikana kwa bei ya punguzo kwa wajawazito wote kwa kutumia hati punguzo inayotolewa kwenye vituo vya afya.

• Mjamzitoahakikisheanapatadozimbiliza‘SP’ katika kipindi cha ujauzito ili kujikinga na malaria yeye na mtoto.

• Mjamzitoakihisitudalilizamalariaawahikwenye kituo cha afya kwa vipimo na matibabu ya haraka!

Page 24: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

24 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Mich

oro:

bab

atau

car

toon

s 201

3

Kimbembe cha kupata huduma

katika baadhi ya vituo vya afya huumiza kichwa. Kwa wajawazito huwa ni kuumiza kichwa na matumbo! Fuatilia hadithi hii kuona kilichomtokea Aisha.

Lawama

Page 25: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

25MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Page 26: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

26 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

Kuna sehemu matukio kama haya yameshazoeleka hadi wenyeji hawaoni kama ni tatizo. Si jambo la kufumbia macho hili tukemee kwa nguvu zote!

Page 27: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

27MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

UKWELI WA MAMBO

Huduma rafiki huleta maendeleo

Ni kawaida kwenda duka la karibu na mahali unapoishi na kutarajia huduma rafiki na hata kuwa na urafiki na muuza duka kwa kuwa tu umefurahishwa na huduma uliyopewa. Vivyo hivyo,

ingetakiwa kuwa katika vituo vya afya lakini mara nyingi mambo yanakuwa tofauti katika eneo hili.

Kuna mitazamo tofauti kuhusu sababu…

Vijana wa Kigoma walitoa maoni yao juu ya suala hili la hu-duma zisizo rafiki katika vituo vya afya na hivi ndivyo wana-vyotiririka;

• Hospitalinyingiauvituovyaafyavimekuwavikitoahuduma za afya bila kuzingatia rika za wateja wao hali ambayo inachangia jamii kutokuwa wawazi kuelezea hali zao kwa watoa huduma”, Kimori John, Mwanga, Kigoma.

• Uelewamdogowawatoahudumakutojuamajukumuyao ya kazi kinawafanya waonekane kama huduma wa-nayotoa ni ya hiari yao”, alisema Ester Patric, Kigoma.

• Mitazamoyawenginikuhusutofautikatiyawaliosomana wasiosoma. Hili limesemwa kwa wingi kuwa ni kik-wazo kikubwa hasa maeneo ya vijijini.

• Mishaharamidogowanayolipwawatoahudumawaafyani kitendo kinachowafanya watoa huduma za afya kuji-husisha na rushwa.

• Idadiyawatoahudumanindogoikilinganishwanama-hitaji.

Tulijadili: Nini ki-fanyike…

• Serikaliitoeelimukwawananchi na watoa huduma ili watambue umuhimu wa huduma rafiki.

• Watoahudumawaonge-zwe hasa katika maeneo ya vijijini ambako vituo ni vichache.

• Watoahudumawa-jengewe mazingira mazuri ya utendaji wao wa kazi vijijini ili kuwavutia wengi kufanya kazi katika mazingira hayo. Mfano kujengewa nyumba za kuishi na kuongezewa mishahara kutokana na mazingira hayo.

J K u m b u k a

Kuboreshwa kwa sekta ya afya vijijini kutasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto. Kila mtu achukue hatua kufanikisha hili.

Page 28: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

28 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

SEMA, TENDA

Tukiwa tumejikita katika uzazi salama na mazingira tofauti tofauti yaliyozunguka wajawazito, ni muhimu tukatupia jicho haki za

mwanamke mjamzito ili kuzuia matatizo mbalimbali yanayoweza kutokea kama hazitafuatwa. Tumeshawahi kusikia wajawazito wakitukanwa, kusimangwa au hata kuachwa wakitaabika kwa sababu ya umri wao, hali zao kiuchumi na hali ya uhusiano. Kimsingi huu ni unyanyapaa.

Haijalishi umri wako, hali yako ya uhusiano (yaani kama umeolewa au la), dini wala kabila au uwezo wa kiuchumi, unastahili huduma nzuri, zenye kulinda na kujali utu wako na ambazo zinakupa haki zako zote.

Haki za mwanamke mjamzito

Zifuatazo ni baadhi tu ya haki za msingi ambazo kila mjamzito anatakiwa apewe kwenye kituo cha afya:

• Hakiyakutokuumizwanakutokutendewavibaya. Mjamzito hatakiwi kupigwa wala kupata shurba, vitendo vyovy-

ote vya unyanyasaji kwani vinaweza kumfanya akapata matatizo ikiwamo kutoka kwa mimba.

• Hakiyakupatataarifa,kutoaaukutokutoaridhaanauamuziwake unapaswa kuheshimiwa.

Kila mwanamke ana haki ya kuamua nani amsindikize anapokwen-da kupata huduma zinazohusiana na ujauzito.

• Hakiyafaraghanausiri. Anapokwenda kupata huduma au kuomba ushauri kutokana na

hali yake, ana haki ya kuheshimiwa na siri yake kutunzwa. • Hakiyakuheshimiwanakuthaminiwautuwake. Haijalishi umri au hali yake ya uhusiano, mjamzito hapaswi kukan-

damizwa wala kunyanyaswa kwa maneno au kwa vyovyote vile. Kila mwanamke mjamzito ana haki ya kupata huduma na kujaliwa

bila ubaguzi wa namna yoyote. • Hakiyakupatahudumazaafyanakiwangochajuukadri

inavyowezekana. • Hakiyakuwahuru,kujiamuliamamboyakemwenyewebila

kulazimishwa wala vitisho. Hakuna mwenye haki ya kukuweka kizuizini wewe wala mtoto

wako bila mamlaka ya kisheria. Kumdharau na kumdhalilisha mtu wakati wa kutoa huduma za

uzazi ni ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu.

Matibabu bure:

Ndiyo. Mjamzito anatakiwa apate bure huduma za ujauz-ito wakati anapohudhuria kliniki. Pamoja na hayo, hu-duma ya kujifungua inatakiwa iwe bure kwenye hospitali za Serikali.

Page 29: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

29MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Haki zikikiukwa inakuwaje?

Kwanza, jielimishe kuhusu haki zako. Uzijue ili zikikiukwa uweze kujua kuwa zimekiukwa. Pia hakikisha unapata haki hizo. Kama mhudumu wa afya anakiuka haki hizo, toa ripoti kwa mkuu wake wa kazi juu ya tabia yake kwani hazikubaliki, wala usidhani kila mhudumu wa afya anafurahia. Kama mwenzenu ananyanyaswa, wagonjwa wenzake mna haki ya kumtetea, kwani mkiacha anyan-yaswe mnaendeleza tabia hizo. Kama tabia hizo zimekidhiri kwe-nye kitu cha afya katika eneo lako ni vizuri zaidi ukaripoti kwenye serikali ya kijiji. Wanawake wote wajawazito mkishirikiana na kue-teta haki zenu mtakomesha tabia mbaya ya baadhi ya wahudumu wa afya na kuboresha huduma za afya kwa ujumla.

SwaliUnadhani haki za mama mjamzito zinaz-ingatiwa na kutekelezwa katika kituo cha afya kilicho katika eneo lako? Tuambie kwa kutumia mawasiliano hapa chini;Barua pepe: [email protected]: Andika SM acha nafasi, andika maoni

yako kisha tuma kwenda namba 15665S.L.P. 2065, Dar es Salaam.

J K u m b u k a

Haki hizi ni muhimu kuzingatiwa wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua. Usikubali zikiukwe. Sema. Tetea haki za mjamzito.

Page 30: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

30 Si Mchezo! MACHI-APRILI 2013

MARIE STOPES

Mara kibao utasikia mtoto wa fulani amefariki kutokana na utoaji mimba, au amenusurika kufa. Masuala haya yanafanyika

kila mahali na wananchi wanajua! Samia Abdallah (15) mkazi wa Kilimani, Zanzibar anatushirikisha stori yake jinsi alivyonusurika kifo baada ya kutoa mimba. Hivi ndiyo anavyotusimulia; “Nikiwa na miaka 13 nilikuwa nasoma darasa la sita katika shule fulani hapa Wilaya ya Mjini Zanzibar. Jumamosi moja nilikwenda kujisomea kwa rafiki yangu ambapo siku zote tunakutana wasichana wengi kujisomea. Ilipofika jioni wote tukawa tumechoka mmoja wetu akashauri twende Forodhani kupunga upepo na alikuwa na pesa ya kutununulia msosi. Sikutegemea kuwa pale Forodhani walikuwepo wavulana wanaotusubiri na kila msichana alipangiwa mvulana wake. Nilitamani nirudi nyumbani lakini sikuwa na nauli na kijana aliyekuwa ananifuatilia alikuwa na gari ya nyumbani kwao hivyo kila wakati alisema tutarudi nyumbani mapema. Alipokuwa ananirudisha nilishangaa ananiambia tunapita kwa rafiki yake. Huko kwa rafiki yake alinishawishi hadi tukafanya ngono. Nilishika mimba”.

Utoaji mimba kwa njia zisizo salama ni hatari

Utoaji mimba

“Baada ya miezi mitatu nilishangaa najisikia homa na siku zangu zimesimama. Nilikwenda hospitali na dada yangu kupima nikakutwa nina malaria nikapewa dawa lakini sikumwambia kuwa sioni siku zangu. Nilipomwambia rafiki yangu, alinipeleka hospitali moja ya binafsi walinipima na kuniambia nina mimba ya miezi minne. Tukampigia yule kijana akaja na kushauri turudi kwa huyo daktari. Alimuomba kuitoa ili nyumbani wasijue. Baada ya muda daktari aliniingiza dawa ukeni na kunipa nyingine nimeze. Niliambiwa nirudi kesho yake. Usiku wa manane tumbo liliuma sana nikaanza kutokwa mabonge ya damu ikabidi mama anipeleke hospitali ya Marie Stopes kesho yake iliyoko Kilimani Mnara wa Mbao. Nilifika hali yangu ikiwa mbaya kwa maumivu na kuishiwa pumzi.”

Huduma ya kusafishwa

“Kwa maumivu niliyokuwa nayo sikutaka kuguswa kabisa! Nilipigwa ganzi. Nilipewa ushauri na nesi akaniambia ni hatari kutoa mimba na kunifundisha jinsi ya kujikinga na mimba zisizotarajiwa. Nilirudishwa nyumbani. Nilihojiwa na mama na dada zangu. Yule kijana alipoulizwa alikataa kabisa. Tokea siku hiyo nawachukia wanaume hata sijui kama nitaolewa”.

Samia anatoa ushauri

“Naomba wazazi wasiwalaumu wasichana yakiwatokea kama yaliyonitokea kwani sikutarajia kufanya mapenzi na wala kushika mimba. Wasichana wengi tunadanganywa kwa sababu hatuna elimu ya kutosha. Vijana wapate ushauri kwa wataalamu ili kujikinga kabla majanga kama haya hayajawakuta. Tujifunze jinsi ya kutumia kinga kama vile kondom na kupambana na wanaume wahuni hata ikibidi kuwapeleka katika vyombo vya sheria”.

Kwa huduma za kuokoa maisha kwa walioharibu mimba, fika Kituo cha Marie stopes Kilimani Mnara wa Mbao au kliniki yoyote ya Serikali. Kwa mawasiliano piga 0767160038 au tuma ujumbe au kwa njia ya baruapepe [email protected]

Page 31: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata

31MACHI-APRILI 2013 Si Mchezo!

Betty Liduke ni rafiki mkubwa wa vijana, hata wewe unaweza kulonga naye. Ni msambazaji mkubwa wa Jarida la Si Mchezo! Mkoani Njombe. Ni mshauri nasaha na ni Mratibu wa Kitengo cha Udhibiti Ukimwi katika Kampuni ya TANWAT, Njombe.Mwandikie kupitia Jarida la Si Mchezo!Si Mchezo! S. L. P. 2065 Dar es SalaamSMs; Andika SM acha nafasi, andika maoni yako kisha tuma kwenda namba 15665na utuambie kama ungependa uchapishwe.

USHAURI

Swali

Umri wako bado mdogo, jaribu kuwa makini na mambo yako maana mapenzi kwa umri wako ni hatari. Jaribu kujipanga kimaisha kwanza na mambo mengine yanafuata.Fidelis Francis Kigoma

Napenda kukushauri ndugu rafiki kuwa mkweli kwa yule unayempenda ili atambue hisia zako, kwani usipomwambia utajikuta akipita na mtu mwingine na wewe unaumia moyo kwa kuwa unampenda.Mazindo Juma Kigoma

Nina miaka 21, nina rafiki wa kike ambaye tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja hadi sasa. Nampenda ila naogopa kumueleza kwani nitavunja urafiki wetu. Pia kuna

mwanamke anayenipenda sana ila mie simpendi na yupo jirani sana na mimi kuliko yule nimpen-dae ambaye ni rafiki yangu, vijana wenzangu naomba mnishauri nifanye nini katika suala hili.Hantish Jozack, Njombe.

Kwa kuwa una mazoea na huyo binti ni vyema umweleze ukweli kuwa unampenda. Hatashindwa kukuelewa kutokana na ukaribu mlionao tangu mwanzo. Isitoshe naamini kuwa huyo binti atakuwa anakupenda lakini anashindwa kukuambia ukweli kulingana na desturi ya Watanzania. Kuhusu huyo mwanamke mwingine ni kumpotezea tu.Angelina Nyalinga.

Nimekaa saluni, mume wangu anajadiliwa na wasichana waliopo hapo saluni. Hawajui kama mimi ndiye mkewe. Msichana anayetem-bea naye anaongea na mume wangu kwenye simu. Namsikia mume wangu anajiachia tu. Hajui kama kawekwa ‘loud speaker’. Wanakata simu wanacheka sana! Mbaya zaidi, wanasema jamaa ananiponda ile mbaya, wanataja na mapungufu yangu ambayo kwa asilimia kubwa ni ya kweli. Je, nifanyeje?Msomaji Geita

Nashukuru kwa swali lako zuri na pole kwa kuwa katika njia panda. Moyo unapopenda kitu hasa katika hali ya uhusiano hutakiwa hekima na kutafakari ili kuweza kuupendezesha au kuusononesha. Kabla hujachukua uamuzi wowote tafakari jiulize je jambo hili litakuwa na athari gani? Je, athari yake ni kubwa kwa kiasi gani? Je, huyu ninayempenda naye ananipenda vivyo hivyo? Je, akisikia nina uhusiano na mtu mwingine itakuwaje? Ukipata jibu unaweza kuusemea moyo wako na kufikisha ujumbe wako kwa huyo unayefikiri unampenda zaidi. Huyu mwingine usiye mpenda mwambie ukweli.

SWALI LA TOLEO LIJALO

Page 32: Haliuzwi - Femina HIP€¦ · letu sote kukabiliana na janga hili, lakini zaidi nahimiza utawala bora upewe kipaumbele! Wito wangu ni huu, kumbuka kujiandaa unapojitambua kuwa umepata