45
1 HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA RASIMU YA MPANGO WA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MSITU WA HIFADHI WA KAMPESE - KIJIJI CHA KAGUNGA HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA S. L. P. 1 MPANDA

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

  • Upload
    others

  • View
    12

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

1

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA

KAGUNGA

RASIMU YA MPANGO WA USIMAMIZI

SHIRIKISHI WA MSITU WA HIFADHI WA

KAMPESE - KIJIJI CHA KAGUNGA

HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA

S. L. P. 1

MPANDA

Page 2: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

i

MAELEZO YA JUMLA YA MPANGO........................................................................................................... 1

MAELEZO.................................................................................................................................................. 2

Msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Kagunga .................................................................................................... 2

MATUMIZI YA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA KAGUNGA .................................................................. 3

KIJIJI CHA KAGUNGA ................................................................................................................................ 4

Sehemu ya tatu: ....................................................................................................................................... 5

Madhumuni ya mpango wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga.................................................. 5

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MABA. .................................................................................................... 7

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MAJINDO ............................................................................................... 8

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KATUNU ................................................................................................. 8

SEHEMU YA PILI ....................................................................................................................................... 9

MPANGO WA UTEKELEZAJI...................................................................................................................... 9

Meneja Mteule ........................................................................................................................................ 9

Uwezo na Majukumu ya Kamati ya Mazingira ......................................................................................10

Majukumu ya Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili ya Kjiji .....................................................................11

Majukumu ya Katibu wa kamati ya mazingira: ......................................................................................12

Majukumu ya Mtunza hazina: ...............................................................................................................13

Msimamizi wa Doria: .............................................................................................................................13

Majukumu ya Wahusika Wengine .........................................................................................................13

Halmashauri ya Kijiji:..............................................................................................................................13

Wanakijiji ...............................................................................................................................................14

Wataalamu wa Misitu katika ngazi mbalimbali .....................................................................................14

Viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, na Taifa (Mtendaji kata, Diwani, Katibu Tarafa, Mkuu wa

Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji (W), Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri).............................................14

UTENDAJI KAZI WA KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI. .............................................................................15

MAELEZO MENGINEYO ..........................................................................................................................15

UTOAJI TAARIFA .....................................................................................................................................15

UWEKAJI WA KUMBUKUMBU ...............................................................................................................15

MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAMATI YA MALIASILI ..............................................................16

MATARAJIO YA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USIMAMIZI WA MSITU.........................16

UTUNZAJI KUMBUKUMBU .....................................................................................................................17

VITABU VYA KUMBUKUMBU .................................................................................................................17

KITABU CHA MAKOSA NA FAINI ............................................................................................................17

Page 3: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

ii

KITABU CHA STAKABADHI......................................................................................................................17

VITABU VYA VIBALI ................................................................................................................................17

KITABU CHA DORIA ................................................................................................................................18

KITABU CHA AKAUNTI ............................................................................................................................18

KITABU CHA MAPATO NA MATUMIZI....................................................................................................19

USIMAMIZI WA FEDHA ..........................................................................................................................19

WAHUSIKA WAKUU; ..............................................................................................................................19

AFISA MUWAJIBIKAJI WA MASUALA YA FEDHA ....................................................................................19

MATUMIZI YANAYOIDHINISHWA; .........................................................................................................20

Mipaka ya Msitu wa hifadhi wa kijiji cha Kagunga ................................................................................21

MAELEKEZO MAALUM ...........................................................................................................................21

ULINZI NA UKAGUZI WA ENEO LA MSITU WA KIJIJI CHA KAGUNGA .....................................................21

Sifa za Walinzi wa Msitu. .......................................................................................................................22

Wajibu, Majukumu na Mafao ya Walinzi wa Msitu wa Hifadhi ya Kijiji ................................................22

OPERESHENI ...........................................................................................................................................23

ZAWADI YA PONGEZI KWA MWANA DORIA ........................................................................................23

Kanuni za Kutumia Msitu wa Hifadhi ya kijiji .........................................................................................23

Kanuni za matumizi ya msitu: ................................................................................................................24

Matumizi ya Msitu yanayohusu Ukataji wa Miti ...................................................................................24

TARATIBU NA SHERIA NYINGINEZO .......................................................................................................24

Adhabu ...................................................................................................................................................24

MCHAKATO WA KUMSHUGHULIKIA MKOSAJI NA KOSA .......................................................................24

FAINI NA ADHABU KWA KILA KOSA .......................................................................................................25

FAINI ZA KUTOWAJIBIKA ........................................................................................................................26

KUUENDELEZA MSITU ............................................................................................................................26

UTANGULIZI: ..........................................................................................................................................27

UVUNAJI WA MITI ..................................................................................................................................27

HATUA ZA HARAKA ................................................................................................................................28

UFUATILIAJI ............................................................................................................................................28

Vigezo vya Mafanikio: ............................................................................................................................28

Wafuatiliaji .............................................................................................................................................29

Taarifa ya Ufuatiliaji Itatolewa kwa: ......................................................................................................29

Muda wa Kufanya Ufuatiliaji..................................................................................................................29

RATIBA YA UTEKELEZAJI .........................................................................................................................30

Hatua za Awali za Utekelezaji: ...............................................................................................................30

Page 4: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

iii

Hatua Zitakazofuata ...............................................................................................................................30

MUDA WA MPANGO, MAREKEBISHO NA MAPITIO YAKE: ....................................................................30

VIAMBATA ..............................................................................................................................................32

Page 5: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

1

MPANGO WA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA

KAGUNGA

SEHEMU YA KWANZA - UTANGULIZI

MAELEZO YA JUMLA YA MPANGO Mpango huu wa usimamizi umeandaliwa na timu ya Tathimini Shirikishi ya Rasilimali

za Msitu kwa kushiriana na wataalamu wa misitu wa Halmashauri ya wilaya ya

Mpanda.

Maandalizi ya mpango huu wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga umefanyika

kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Kagunga ambao ndio wamiliki wa msitu huu.

Mpango huu umepitishwa na Halmashauri ya kijiji na Mkutano Mkuu wa kijiji cha

Kagunga na kuidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya Mpanda.

Uamuzi wa kutenga na kuuhifadhi msitu huu wa kijiji cha Kagunga kuwa msitu wa

Hifadhi wa kijiji umetokana na wanakijiji wenyewe kuona umuhimu wa uhifadhi. Pia

kuweka taratibu za kisheria ili kuwezesha kijiji kupata manufaa yatokanayo na mazao

na huduma za msitu na kuepusha vizazi vijavyo kukosa kabisa rasilimali za msitu huu.

Malengo makuu ya mpango huu wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga ni

kuhifadhi, Kuuendeleza na Kutumia kwa namna endelevu kwa manufaa ya kizazi cha

sasa na kijacho cha Tanzania na dunia kwa ujumla

Page 6: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

2

MAELEZO Msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Kagunga Msitu wa Hifadhi ya kijiji cha Kagunga unamilikiwa kuhifadhiwa na Halmashauri ya

Kijiji cha Kagunga kwa niaba ya wananchi wote wa kagunga. Madhumuni ya msingi

ya kuhifadhi msitu huu ni kutunza na kuhifadhi uoto wa asili uliopo kwa wingi kwenye

msitu huu, kutoa mazao ya msitu na huduma ya/za misitu kwa kuzingatia misingi ya

matumizi endelevu na kuhifadhi bioanuai muhimu zinazopatikana ndani yake kwa

manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo vya Tanzania na ulimwengu kwa jumla.

Msitu huu wa hifadhi ya kijiji ni matokeo ya zoezi la Mpango wa Matumizi Bora ya

Ardhi ya kijiji cha Kagunga lililofanyika mwezi November mwaka 2016 na kuridhiwa na

wananchi wote wa Kagunga.

Msitu huu umeenea eneo la Milima Maba na kuanzia hadi mlima Mbamba Msitu huu

una eneo la ukubwa wa hekta 5465.

Msitu huu una uoto wa miti mchanganyiko sehemu kubwa una umri mkubwa na

sehemu nyingi vilevile ambazo zina uoto mchanga. Kwa juu msitu umefunga kwa

viwango tofauti tofauti toka sehemu moja hadi nyingine. Kuna sehemu ambazo msitu

umefunga sana kwa juu hasa kando kando ya mito na makorongo marefu, sehemu

zilizofunga wastani, na sehemu zilizo wazi hasa kutokana na uvamizi wa msitu kwa

ajili ya kilimo na zile sehemu za mabonde na mbuga ambazo ni vyanzo vya maji. Ndani

ya msitu huu kuna njia za miguu zinazounganisha kijiji cha Kagunga na baadhi ya

vitongoji vyake vya Mantena na kagunga B (kalaba). Pia kuna njia nyingi zisizo halali

za miguu ambazo hutumiwa na wavamizi wa msitu kwa ajili ya kilimo, wapasua mbao

na wategaji wa wanyamapori. Mipaka ya msitu huu imewekwa alama za kudumu za

maboya ya zege (beacons).

MSITU WA HIFADHI WA KIJIJI CHA KAGUNGA;

Msitu huu umeenea Magharibi na kaskazini mwa Kijiji cha Kagunga. Msitu huu una

ukubwa wa hekta 5465 wenye bioanuai nyingi muhimu kwa kijiji na taifa kwa ujumla.

Msitu huu umeathiriwa kwa kiasi na shughuli za kibinadamu kama vile uchungiaji wa

mifugo, uchomaji moto, uvunaji holela, Kilimo na makazi holela msituni.

Page 7: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

3

Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na

uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje ya kijiji cha kagunga.

Moto ni tishio la msitu wote wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga. Madhara ya moto ndani

ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga ni kuwa umeathiri ustawi wa uoto wa msitu

huu. Vyanzo vya moto ndani msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga ni wawindaji wa

wanyamapori, wakulima na warinaji wa asali kwa kutumia moto.

Msitu huu pia una vivutio vingine vya utalii kama vile safu za Milima na maeneo mengi

yanayopendelewa na Sokwe kwa ajili ya malazi na chakula na maporomoko ya maji.

Mmiliki mkuu wa msitu huu ni Halmashauri ya Kijiji Cha Kagunga, kutokana na

muundo wa serikali za mitaa, itaiteua kamati ya Maliasili ya Kijiji kusimamia msitu huu

kwa niaba ya wananchi wote wa kijiji cha Kagunga kwa kuwa hii ndiyo kamati

inayohusika na usimamizi wa masuala ya mazingira ya kijiji kwa ujumla.

MATUMIZI YA MSITU WA HIFADHI YA KIJIJI CHA KAGUNGA Kabla ya kuanza kwa utaratibu huu wa usimamizi shirikishi hapa kijijini, msitu huu

haukuwa na utaratibu wowote wa jinsi ya kutumia au kuvuna rasilimali zake, na kila

mtu aliingia kwa wakati wake na kuvuna chochote alichohitaji kwa manufaa yake na

kutoka bila ya kuhojiwa na mtu. Hali kadhalika, ndani ya msitu huu kuna wafugaji na

wakulima ambao huchangia miti midogo kupotea kabisa kama itakavyo onyeshwa

kwenye viambatanisho vya mpango huu wa usimamizi wa misitu.

Ukataji wa miti usiofuata mpango wa Uvunaji kulingana na uwezo wa msitu hupelekea

kutoweka kwa miti muhimmu kama Mninga, Mpilipili, Mkora na Msawala katika msitu

huu. Hali kadhalika uchomaji moto unaofanywa na wafugaji ili kupata nyasi mpya na

wawindaji ili kurahisisha kazi yao ya kuwinda. Vitendo hivi huua kabisa makuzi ya

machipukizi na hivyo msitu hubaki na kizazi cha miti mikubwa tu ambayo ndiyo ilikuwa

ikivunwa.

Kwa upande wa matumizi ya rasilimali za msitu huu zipo rasilimali zipatikanazo katika

msitu huu ambazo zina manufaa kwa uchumi wa kila mwananchi na kijiji kwa ujumla,

hizi ni pamoja na; -

▪ Msitu huu ni makazi ya wanyamapori ambao ni faida kwa kijiji na taifa kwa

ujumla.

Page 8: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

4

▪ Ipo miti yenye manufaa kiuchumi kwa wananchi mfano miti ya mbao kama

Milembela, Mitundu, Mininga, Mibanga, Mikurungu, Mpilipili, ambayo ina

umuhimu kiuchumi na kwamba itakinufaisha kijiji endapo utaratibu wa uvunaji

utasimamiwa ipasavyo na kwa uaminifu,

▪ Ndani ya msitu huu kuna makorongo ambayo ni mito ya misimu na mengine

hutiririsha maji mwaka mzima, hivyo kama yakitumiwa vizurini fursa ya utalii

asilia utakao ingizia kijiji kipato.

▪ Kuni ni moja wapo ya matumizi muhimu kiuchumi toka katika msitu huu.

▪ Aidha, watumiaji wakuu wa rasilimali za msitu huu wa kijiji cha Kagunga, ni

wanakijiji wenyewe wa Kagunga, pili ni wananchi toka vijiji jirani kama

Kasekese. Watumiaji wengine ni wale wakutoka nje ya kijiji na kata hii ya

Kasekese. Pamoja na taratibu za kulipia zatakazowekwa lakini yapo mahitaji

mengine ambayo wanakijiji wa Kagunga pekee wataruhusiwa kuingia na

kuvuna bila malipo bali kwa utaratibu maalum.

KIJIJI CHA KAGUNGA Kijiji cha Kagunga ni miongoni mwa vijiji hamsini na tano (55) vya wilaya ya Mpanda.

Kipo katika Kata ya Kasekese, Tarafa ya Mwese, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.

Vijiji vingine vilivyomo kwenye kata hii ni pamoja na Kasekese na Kaseganyama. Kijiji

hiki kilianzishwa mwaka 2014, kabla ya hapo eneo hili lilikuwa chini ya kijiji cha

Sibwesa na mwaka 2009 Sibwesa ilizaa kijiji cha Kasekese na eneo la Kagunga kuwa

miongoni mwa vitongoji vya kijiji cha Kasekese. Jina Kagunga lilitokana na mtu

aliyetoka kigoma aliyejulikana kwa jina la Mtabala. Eneo ambalo kijiji hiki kinapatika

kulikua na miti mingi sana aina ya Migunga na hapo ndipo jina Kagunga lilipotokea.

Kijiji hiki kina vitongoji vinne (4) ambavyo ni Kagunga A, Kagunga B, Mantena na

Kamkola Katika upande wa Kaskazini, kijiji kinapakana na kijiji cha Katuma, upande

wa Kusini kinapakana na kijiji cha Kasekese, upande wa Mashariki kinapakana na kijiji

cha Sibwesa, Magharibi kinapakana na kijiji cha Kaseganyama.

Kijiji hiki kina mchanganyiko wa makabila kadhaa. Makabila yanayotawala katika kijiji

hiki ni Watongwe, Wabende, Wafipa Wasukuma, na waha.

Page 9: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

5

Shughuli za kiuchumi za wakazi wa kijiji cha Kagunga zinategemea sana kilimo na

ufugaji. Kwa upande wa kilimo wananchi wa kijiji hiki hulima sana zao la Mahindi,

Maharage Mihogo, Ufuta, Tumbaku, Mpunga, Ufuta na Mtama. Mazao haya huuzwa

hapa kijijini na na mengine kwa wingi huuzwa kwa wafanyabiashara toka Kasekese

na kwingineko.

Aidha, shughuli ya ufugaji hufanywa na kabila la wasukuma, wanyamwezi na wafipa

kwa kiasi kikubwa pia mifugo midogo midogo kama mbuzi, kondoo bata na kuku

hufugwa hapa kijijini.

Sehemu ya tatu: Madhumuni ya mpango wa usimamizi wa msitu wa kijiji cha Kagunga Msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga ni msitu wa kijiji unaohifadhiwa kwa lengo la

kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji pamoja na kuwezesha upatikanaji wa mazao na

huduma za msitu kwa njia endelevu. Kutokana na uharibifu wa msitu unaoendelea

kufanyika madhumuni hayo ya msingi yanaendelea kuathiriwa. Hivyo dhumuni kuu la

mpango huu ni kuimarisha ulinzi, uendelezaji na utumiaji wa eneo hilo la msitu kwa

kushirikisha wananchi ili kurejesha hali nzuri ya msitu iliyokuwepo. Hii itafanikiwa kwa

kufanya yafuatayo:

▪ Kuweka taratibu / kanuni za kutumia, kulinda, na kuendeleza msitu kwa njia

endelevu.

▪ Kuboresha ushiriki wa wadau wote katika usimamizi wa msitu.

▪ Kuongeza ushirikiano kati ya wananchi, Halmashauri ya Kijiji, Halmashauri ya

Wilaya na wakala wa huduma za misitu Tanzania.

▪ Kuwaelimisha wanakijiji wa Kagunga juu ya umuhimu wa msitu kwao, Taifa na

Ulimwengu na jukumu lao la kufuata taratibu za utunzaji na matumizi

zilizowekwa na kukubalika.

▪ Kuuweka msitu wetu katika udhibiti madhubuti unaokubalika na wanakijiji wote

ili kwamba kusiwe na uvunaji holela, uvamizi wa mifugo, na ujenzi wa makazi

holela au kupanua mashamba kuingia katika msitu huu. Kwa kufanya hivi,

tutasaidia msitu huu kuwa chini ya umiliki wa kijiji chote kwa manufaa yetu na

kwamba rasilimali zilizopo zitumike katika misingi endelevu kwa faida ya kizazi

hiki na kijacho.

Msitu huu umegawanyika katika maeneo makuu Matatu ya usimamizi (3) yaitwayo

“maeneo madogo ya usimamizi” (EDU) kama ifuatavyo; -

Page 10: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

6

▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MABA (2479 ha)

▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KATUNU (1498 ha)

▪ ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MAJINDO (1408ha)

Page 11: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

7

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MABA. Eneo hili dogo la usimamizi (EDU) la Maba (milima ya Igombe) lina ukubwa wa hekta

2479 ambalo linaanzia kusini magharibi mwa msitu wa kijiji cha Kagunga, bonde la

mama bahati, pembezoni mwa mlima Maba Usawa wa bikoni namba VF35, VF36 na

VF37 kuelekea kaskazini mashariki mwa kitongoji cha Mantena na kuvuka barabara

ya mkoloni milima ya maraha kulekea kaskazini na kuishia kwenye bikoni namba VF49

na VF50 kwenye safu ya milima ya Mngengebe. Kwa upande wa kaskazini inapakana

na EDU ya Majindo Lengo kuu la EDU hii ni “MATUMIZI” na “UHIFADHI”. Kutokana

na hali halisi ya EDU hii na uwiano wa ukubwa wa miti, uvunaji unaweza kufanyika,

pamoja na kuipa nafasi ya ukuaji wa miti muhimu ifikie kwenye kiwango cha kuweza

kuvunwa miaka ijayo. EDU hii ina jumla ya miti 493,500 wakati jumla ya miti 784 ni

miti inayofaa kuvunwa kwa ajili ya mbao, ambayo ni sawa na miti 157 kwa mwaka.

Miti hiyo ni; -

▪ Mpilipili

▪ Mlembela

▪ Mbanga

▪ Mninga

▪ Mkurungu

Pamoja na kuruhusiwa uvunaji yapo matumizi mengine yanayoruhusiwa nayo ni kama

yafuatayo; -

• Ufugaji nyuki

• Uchimbaji wa dawa za asili (miti shamba)

• Kusenya kuni kavu (si miti mibichi)

• Ukataji wa nyasi za kuezekea nyumba

• Uvunaji wa miti ya boriti (pau), fito na nguzo

Page 12: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

8

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA MAJINDO Linaanzia mashariki mwa kijiji cha Kagunga, mpakani mwa kijiji cha Sibwesa na

katuma kwa upande wa kaskazini kwenye milima Masoso A na Masoso B, kwenye

bikoni namba VF9, VF10 hadi VF15 na VF17, kuelekea kaskazini kuvuka mlima

kampese na barabara ya mkoloni na kuishia mpakani mwa ushoroba na milima ya

Mngengebe. Kwa upande wa mashariki linapakana na Katuma na upande wa kusini

inapakana na kijiji cha Sibwesa. Ndani ya msitu huu kuna milima na maporomoko

marefu na vyanzo vya maji. Eneo hili dogo la usimamizi la Majindo lina ukubwa wa

hekta 1408. kutokana na hali ya eneo hili lilivyo, litakua la “UHIFADHI na MATUMIZI”.

Matumizi yatakayoruhusiwa katika EDU hii ni pamoja na:

▪ Ufugaji nyuki na Urinaji wa asali

▪ Uchimbaji wa dawa za asili [miti shamba]

▪ Kusenya kuni zilizokauka.

▪ Ukataji wa nyasi za kuezekea nyumba

▪ Shughuli za Utalii.

▪ Matambiko

▪ Vyanzo vya maji

▪ Utafiti

ENEO DOGO LA USIMAMIZI LA KATUNU Eneo hili linaanzia njia panda ya Kansalu na barabara ya mkoloni kuvuka mlima bunga

kuzunguka maeneo ya ushoroba. Eneo hili lina ukubwa wa hekta 1498. Lengo la

kutenga eneo hili ni “UHIFADHI” wa vyanzo vya maji kwa ajili ya kulisha maji eneo la

ufugaji a mbalo linapakana nalo, Uhifadhi wa wanyamapori wanaoishi humo ndani ya

msitu.

Page 13: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

9

SEHEMU YA PILI MPANGO WA UTEKELEZAJI Meneja Mteule Katika mpango huu wa usimamizi wa msitu wa hifadhi wa Kijiji cha Kagunga, meneja

atakuwa ni Halmashauri ya kijiji cha Kagunga. Halmashauri ya kijiji cha Kagunga

itaiteua KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI ili kusimamia msitu huu kwa niaba yake na

wanakijiji wote kwa ujumla. Kamati hii ni ile inayoelekezwa katika muundo wa uongozi

wa vijiji. Kamati hii itakuwa na wajumbe 14 kwa mchanganuo ufuatao;

▪ Wawakilisha toka kila kitongoji cha kijiji.

▪ Skauti wa kijiji wasiopungua wawili kama hawapo basi hata askari mgambo

wanaweza kutumika badala ya Skauti wa kijiji.

▪ Mtu / watu maarufu katika kijiji wanaoweza kuchangia katika suala zima la

uhifadhi. mfano wazee maarufu na wakongwe wa kijiji n.k.

▪ Wanawake (Theluthi moja au 30% ya wajumbe wote) maalumu kwa nafasi ya

upendeleo kwa wanawake

Kamati hii itapatikana kwa kufuata utaratibu ufuatao; -

▪ Wajumbe hawa watapendekezwa na halmashauri ya kijiji

Page 14: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

10

▪ Baada ya majina hayo kupatikana mkutano mkuu wa Kijiji huketi na

kuyathibitisha majina ya wajumbe wa kamati hii.

▪ Kamati hii itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu (3) baada ya hapo

uchaguzi unafanyika tena. mjumbe anaweza kuchaguliwa tena kulingana na

imani ya wananchi kwake.

▪ Mwenyekiti, katibu na mweka hazina watachaguliwa miongoni mwa wajumbe

waliochaguliwa na mkutano mkuu na kuthibitishwa na Halmashauri ya kijiji.

▪ Kamati hii itapewa nguvu ya kisheria ya kusimamia sheria ya kijiji na

itawajibika kwa Halmashauri kuu ya Kijiji.

▪ Itaandika taarifa ya utekelezaji kwa Halmashauri ya kijiji mara moja kila mwezi,

yenye nakala kwa Afisa Misitu (W).

▪ Itafanya vikao vyake mara moja kila mwezi na vya dharura pale inapobidi.

▪ Itapokea, kujadili na kufuatilia taarifa za walinzi wa msitu (Kamati ya doria) na

vikundi vingine vitakavyo undwa kuisaidia Kamati ya Mazingira katika

kutekeleza majukumu yake.

Uwezo na Majukumu ya Kamati ya Mazingira ▪ Kuhakikisha kuwa mipaka yote ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga

inaeleweka waziwazi kwa wanakijiji wote wa Kagunga.

▪ Kusimamia utekelezaji wa mipango yote inayohusu utumiaji, ulinzi na

uendelezaji wa msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.

▪ Kutunza kumbukumbu zote zinazohusu shughuli za utumiaji, ulinzi, na

uendelezaji wa msitu wa hifadhi ya kijiji. Kumbukumbu hizo ni: -

• Mihtasari ya mikutano

• Doria

• Uhalifu na faini

• Vibali vilivyotolewa

• Mapato na matumizi ya fedha za msitu

▪ Uoteshaji na upandaji miti, pia shughuli zote za uhifadhi mazingira ndani ya

maeneo ya kijiji

▪ Kuhakikisha kuwa walinzi wa msitu (timu ya doria) wanatekeleza kazi yao

kikamilifu na kuchukua hatua zinazopasa kuondoa dosari zinazojitokeza katika

kazi ya ulinzi.

Page 15: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

11

▪ Kufanya ukaguzi wa msitu wa hifadhi ya kijiji angalau mara mbili kwa mwezi.

▪ Kuhakikisha matumizi endelevu ya msitu yanazingatiwa kulingana na kanuni za

matumizi zilizowekwa na kukubaliwa.

▪ Kuwashughulikia wahalifu wa msitu kwa mujibu wa kanuni za adhabu

zilizowekwa na kukubalika kwa ushirikiano na Halmasahauri ya kijiji.

▪ Kwa ushirikiano na Halmashauri ya kijiji, kuwahamasisha wanakiiji kushiriki

katika suala zima la uhifadhi wa msitu na mazingira ya kijiji kwa ujumla.

▪ Kutumia na kutunza vitabu vya stakabadhi vilivyoidhinishwa na Halmashauri ya

Wilaya ya Mpanda.

▪ Kufungua Akaunti Benki ya Kamati ya Mazingira ya kijiji kwa ajili ya kuweka fedha

za mapato ya msitu (ushuru na faini).

▪ Kuhakikisha kuwa fedha za Akaunti ya Kamati ya Mazingira zinatumika kama

zilivyokusudiwa na kuidhinishwa na Halmashauri ya kijiji cha Kagunga.

▪ Kuweka utaratibu wa utoaji wa vibali ili kuhakikisha kuwa vibali vinavyotolewa ni

vile vilivyoko katika mamlaka ya Kamati ya Mazingira na kwamba utoaji wa vibali

unakwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na sio vinginevyo.

Majukumu ya Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili ya Kjiji ▪ Kuhakikisha kuwa mikutano ya Kamati ya Mazingira inafanyika ipasavyo kwa

kufuata ratiba iliyopangwa. (angalau mara moja kila mwezi)

▪ Kuhakikisha kuwa Mhasibu na Katibu wa Kamati ya Mazingira wanafanya kazi

zao ipasavyo kwa kuweka kumbukumbu zote za vibali, doria, faini, idadi ya

wahalifu, fedha zilizopo, matumizi n.k.

▪ Kuhakikisha kuwa Kamati ya doria ya msitu wa hifadhi ya kijiji wanafanya kazi

yao ipasavyo na wanapewa haki zao kama zilizoainishwa kwenye Mpango huu.

▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa

kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa

ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.

▪ Atawajibika kuhudhuria vikao vyote vya Halmashauri kuu ya kijiji na kutoa taarifa

ya utendaji kazi wa kamati.

Page 16: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

12

Majukumu ya Katibu wa kamati ya mazingira: ▪ Atawajibika Kuweka na kutunza kumbukumbu zifuatazo: -

• Kumbukumbu za mikutano yote (Kitabu cha kumbukumbu za mikutano)

• Doria zilizofanyika, uhalifu/uharibifu ulioonekana kwenye kitabu cha

Doria.

• Uhalifu ulioonekana, wahalifu waliohusika, faini zilizotozwa, tarehe ya

uhalifu na faini zilizolipwa kwenye kitabu cha “Uhalifu na faini”

• Vibali ilivyotolewa, kwa nani, kwa ajili gani, fedha zilizolipwa, tarehe,

namba ya risiti, n.k kwenye kitabu cha Vibali

• Fedha zilizotolewa, tarehe, kwa ajili gani, namba ya risiti kwenye kitabu

cha Risiti na fedha.

▪ Atahakikisha kuwa Akaunti ya Mazingira inafunguliwa na mara kwa mara baada

ya kupokea fedha na kuziingiza kwenye vitabu vinavyohusika zinapelekwa

Benki na Mweka Hazina.

▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa

kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa

ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.

▪ Atawajibika kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Kijiji na

Halmashauri kuu ya kijiji

▪ Atawajibika kuandaa taarifa ya utendaji kazi wa kamati na maendeleo ya msitu

kila mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka na kuwasilisha katika

mkutano mkuu wa kijiji wa robo mwaka baada ya kupitiwa na Halmashauri kuu

ya kijiji.

▪ Ataidhinisha doria kufanyika kwa maandishi maalumu ambayo mwenyekiti wa

kijiji pia atapaswa kujulishwa kwa wakati utakaoonekana unafaa kulingana na

mazingira.

▪ Atapokea taarifa ya doria mara baada ya kumalizika na kukagua daftari la doria.

▪ Atatunza kumbukumbu za kesi zote za wavunaji haramu wa mazao ya msitu

wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.

▪ Atawajibika kutunza orodha ya wavunaji wote wa rasilimali za msitu wa hifadhi

ya kijiji cha Kagunga pamoja na kiasi walichovuna na kuwasilisha kwa

DFO/DED kila mwezi.

▪ Atawajibika kusimamia mapato na matumizi kwa umakini na kutoa taarifa kwa

Halmashauri ya kijiji kila inapoonekana inafaa.

Page 17: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

13

Majukumu ya Mtunza hazina: ▪ Atawajibika kutunza kumbukumbu zote za mapato yatokanayo na leseni za

uvunaji wa mazao ya misitu na vibali mbalimbali.

▪ Atawajibika kutunza kumbukumbu za matumizi yote ya fedha zitokanazo na

maduhuli ya mazao ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga kama

ilivyoidhinishwa na vikao husika vya kijiji cha Kagunga na siyo vinginevyo.

▪ Ataandaa taarifa ya Mapato na Matumizi ya fedha ya Kamati ya Mazingira na

kuiwasilisha kwenye vikao vya Kamati ya Mazingira.

▪ Atakuwa mmoja wa watia sahihi wa Akaunti ya Kamati ya Mazingira wakati wa

kutoa fedha Benki kwa matumizi yaliyoidhinishwa na Halmashauri ya kijiji kwa

ajili ya uendelezaji wa msitu na shughuli zingine za maendeleo kijijini.

Msimamizi wa Doria: ▪ Atatakiwa kusimamia doria zote na kuziongoza

▪ Atatunza daftari la kila mtu atakayekamatwa katika msitu wa kijiji akivuna

mazao ya misitu bila idhini (kibali) cha kijiji.

▪ Atawajibika kumuweka chini ya ulinzi mtu yeyote pamoja na maliasili

aliyokamatwa nayo (kama ipo) na kumkabidhisha kwa mtendaji wa Kijiji kwa

hatua zaidi za kisheria.

▪ Atawajibika kuhakikisha ulinzi wa mipaka ya msitu unadumu na kuwa imara ili

msitu usivamiwe kwa kilimo, makazi au kuchungia.

Majukumu ya Wahusika Wengine Halmashauri ya Kijiji: Itakuwa mhusika mkuu katika utekelezaji wa mpango huu kwa upande wa kijiji na

itakuwa na wajibu na majukumu yafuatayo: -

▪ Kusimamia utekelezaji wa mpango

▪ Kutunga na kusimamia Sheria ndogo

▪ Kuhakikisha kuwa Kamati ya Mazingira inafanya kazi yake ipasavyo.

▪ Kushirikiana na wataalamu wa Misitu wa ngazi zote katika kuandaa mikakati

mipya ya uhifadhi misitu na mazingira kwa jumla.

▪ Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mpango huu, kwa kuwa na

agenda ya kudumu katika vikao vyake vya kila mwezi pia kutembelea msitu wa

hifadhi angalau mara moja kila mwezi.

Page 18: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

14

Wanakijiji Watashiriki katika shughuli za utumiaji, ulinzi na uendelezaji wa msitu wa hifadhi

kama ifuatavyo: -

▪ Kuzuia na kuzima moto katika maeneo yao ya makazi, mashamba na misitu

inayowazunguka.

▪ Kusafisha mipaka ya nje ya msitu wa hifadhi ya kijiji na kuhakikisha kuwa iko

wazi wakati wote wa mwaka.

▪ Kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

▪ Kuotesha na kupanda miti kwa lengo la kupunguza utegemezi wa misitu ya asili

kwa kila zao au huduma ya msitu.

▪ Kushiriki katika mikutano na kuchangia katika kuandaa mikakati mipya ya

kutumia, kulinda na kuendeleza msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.

▪ Kubuni na kutekeleza shughuli mbadala za kuongeza kipato ili kupunguza

umaskini kwa kutumia rasilimali zilizo ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji, zilizo

katika maeneo ya makazi. Baadhi ya mbinu hizo ni ufugaji wa nyuki kwa njia

za kisasa, usukaji wa mikeka kwa kutumia ukindu kwa ajili ya soko, Kuzingatia

matumizi ya majiko banifu, nishati mbadala na matumizi sahihi ya mazao ya

misitu.

Wataalamu wa Misitu katika ngazi mbalimbali ▪ Kutoa msaada wa kitaalam katika kubuni mikakati mipya ya kuhifadhi msitu wa

hifadhi ya kijiji cha Kagunga

▪ Kusaidia shughuli za uoteshaji na upandaji miti.

▪ Kusimamia Sera ya Misitu na Sheria ya Misitu 14, 2002.

▪ Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mpango huu wa usimamizi.

▪ Kusaidia utekelezaji wa mpango.

Viongozi wa Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, na Taifa (Mtendaji kata, Diwani, Katibu Tarafa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji (W), Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri).

▪ Kutoa msukumo katika utekelezaji wa mpango

▪ Kuhakikisha kuwa Polisi na Mahakama zinatekeleza wajibu wao ipasavyo

katika utekelezaji wa Sheria ya Misitu No. 14, 2002 na Sheria zinazosimamia

rasilimali za misitu.

▪ Kushirikiana na Idara ya Misitu na Nyuki.

▪ Kutoa msukumo katika utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za kutunza na

kulinda misitu.

Page 19: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

15

▪ Kusaidia utatuzi wa migogoro inapotokea.

UTENDAJI KAZI WA KAMATI YA MALIASILI YA KIJIJI. ▪ Itafanya kazi zile zile zilizoainishwa katika majukumu ya kamati ya kudumu ya

maliasili ya kijiji

▪ Itakutana mara moja kila mwezi

▪ Itatunza mihutasari ya mikutano yake

▪ Mkutano utafanyika iwapo tu idadi ya wajumbe imefika nusu.

▪ Katika kila mkutano watapaswa kupokea taarifa ya doria na mwenendo wa

uvunaji wa mazao ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga kutoka kwa kiongozi

wa doria.

▪ Watatakiwa kujua idadi ya leseni zilizotolewa katika mwezi husika, kiasi cha

maliasili kilichovunwa na mapato yaliyopatikana.

▪ Watapokea na kujadili maombi ya leseni za kuvuna mbao na kuwasilisha kwa

Serikali ya Kijiji.

MAELEZO MENGINEYO UTOAJI TAARIFA

▪ Kamati ya Maliasili ya kijiji itatoa taarifa ya utekelezaji kwa Halmashauri ya kijiji

mara moja kwa mwezi yenye nakala kwa Afisa Misitu wa Wilaya Mpanda.

▪ Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) atatoa taarifa ya maendeleo ya shughuli za msitu

wa hifadhi ya kijiji na kwa Mkutano Mkuu mara nne (4) kwa mwaka yenye

nakala kwa Afisa Mtendaji Kata (WEO) na Afisa Misitu (W).

UWEKAJI WA KUMBUKUMBU Kumbukumbu zifuatazo zitawekwa na kuhifadhiwa na Kamati ya Mazingira ya Kijiji:

▪ Mihutasari ya vikao vya kamati

▪ Uhalifu na faini zilizotozwa

▪ Doria zilizofanyika

▪ Stakabadhi ya fedha na Hati ya malipo.

Page 20: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

16

▪ Vibali vilivyotolewa

▪ Akaunti ya Kamati ya Mazingira

▪ Mapato na matumizi ya fedha za msitu.

MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAMATI YA MALIASILI Mapato ya Kamati ya Mazingira yatatokana na:

▪ Faini zitakazotozwa wahalifu wa msitu wa hifadhi ya kijiji.

▪ Malipo ya mazao na huduma ya msitu yaliyoruhusiwa kwa kulipia katika

Mpango huu.

▪ Mauzo ya mazao ya msitu yaliyokamatwa na zana zilizokamatwa katika ulinzi.

▪ Wafadhili na wasamaria wema watakaotoa fedha/ msaada kwa ajili ya

Usimamizi wa msitu wa hifadhi ya kijiji.

Mapato yatokanayo na mazao na huduma za msitu wa kijiji cha Kagunga yatakua ni

mali ya kijiji cha Kagunga kwa asilimia 100% na hayatagawanywa kati yake na

Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.

MATARAJIO YA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USIMAMIZI WA MSITU Katika matembezi ya kukatiza msitu vikwazo Matatizo yafuatavyo vilibainika msituni;

▪ Moto kichaa

▪ Uvunaji haramu wa mbao

▪ Uchungiaji wa mifugo

▪ Kilimo msituni

▪ Ukataji wa miti

Mpango wa usimamizi ukitekelezwa vilivyo kwa msitu huu hifadhi wa kijiji cha Kagunga

kwa kuzingatia vikwazo vilivyobainika katika matembezi ya kukatiza msitu kama

yalivyofupishwa hapo juu yafuatayo yanatarajiwa kuonekana;

▪ Kupungua au kutoweka kabisa kwa matukio ya moto

▪ Kushughulikiwa kwa watuhumiwa wa kesi za uchomaji moto hovyo msituni kwa

utaratibu wa kukubalika/kwa kufuata taratibu za nchi.

Page 21: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

17

UTUNZAJI KUMBUKUMBU Mpango huu wa usimamizi unaainisha bayana ni kumbukumbu zipi zitatunzwa,

zitatunzwa katika vitabu gani na vitabu hivyo vitatunzwa na nani kwa utaratibu gani.

Ufuatao ni ufafanuzi; -

VITABU VYA KUMBUKUMBU Hiki ni kitabu kitakachohusika na kutunza kumbukumbu zifuatazo,

▪ Kumbukumbu za mihutasari ya vikao vya kamati

▪ Kumbukumbu za maamuzi mbalimbali ya kamati

▪ Tukio lolote linalofanywa na kamati au watu wachache waliotumwa na kamati.

▪ Matokeo ya shughuli yoyote iliyofanywa na kamati au watu wachache

walioteuliwa na kamati

▪ Kumbukumbu za ukaguzi wowote uliofanywa na kamati au baadhi ya

wanakamati waliotumwa na kamati

KITABU CHA MAKOSA NA FAINI Kumbukumbu za makosa yoyote yaliyofanywa na mhalifu dhidi ya sheria ndogo za

Kijiji cha Kagunga ya Kuhifadhi Msitu wa Kijiji.

▪ Jina la mkosaji na kosa alilokosa, Kiasi alichotozwa, tarehe aliyotozwa na

namba ya stakabadhi aliyopewa kwa faini aliyotozwa.

▪ Ionyeshwe ni katika akaunti gani pesa hiyo imeingizwa.

▪ kama idhini ya kutumika nimetolewa na mamlaka husika, onyesha hapa

imetumika kufanyia nini?

KITABU CHA STAKABADHI Hivi ni vitabu ambavyo Mtunza hazina wa Halmashauri ya Wilaya atatoa kwa kijiji,

lakini ionyeshwe nani kapewa vitabu vingapi kuvitumia ndani ya kamati.

VITABU VYA VIBALI Kazi ya kitabu hiki ni kutunza kumbukumbu za vibali vyote vilivyoidhinishwa na kamati

ya Maliasili ya Kijiji, Kitabu hiki kionyeshe mambo yafuatayo; -

▪ Kuainisha lengo la kibali, jina la aliyepewa kibali hicho,

Page 22: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

18

▪ kiasi cha malipo aliyolipa,

▪ Namba ya stakabadhi iliyotolewa kwa mteja

▪ tarehe ya kutolewa kibali na ya kuisha kutumika kibali hicho.

▪ Pia kitabu kionyeshe jina la mjumbe atakayekagua kibali hicho na la mjumbe

atakayesimamia matumizi ya kibali hicho.

Kimsingi, leseni na vibali vitasainiwa na katibu/ Mhasibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji

kugongwa muhuri wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji.

KITABU CHA DORIA Hiki ni kitabu kitakachokuwa kinatunzwa na msimamizi wa doria. kinapaswa

kuandikwa mambo yafuatayo;

▪ Tarehe ya doria,

▪ Majiina ya wanaofanya doria siku hiyo,

▪ eneo ambalo watu hao watafanya doria,

▪ ni uharibifu gani umefanyika katika eneo hilo la msitu ambalo watu hao

wamepangiwa kufanya doria.

▪ Pia katika taarifa ya hao waliopangiwa kufanya doria katika eneo husika

wakiona kitu mfano, wanyamapori. wanapaswa kutoa taarifa kwa kamati ya

maliasili ya Kijiji.

KITABU CHA AKAUNTI Baada ya muda kijiji kitakuwa na fedha nyingi kutokana na mapato ya msitu, hivyo

kutakuwa na kitabu cha benki kwa ajili ya kumbukumbu za kibenki. Katika kitabu hiki

kutakuwa na majina ya watia saini. watia saini watakuwa kama ifuatavyo;

▪ mtia saini kundi ‘A’ – toka Serikali ya Kijiji,

▪ Mtia saini kundi ‘A’ – toka Kamati ya Maliasili ya Kijiji,

▪ Mtia saini kundi ‘B’ – toka Serikali ya Kijiji

▪ Mtia saini kundi ‘B’ – toka Kamati ya Maliasili ya Kijiji.

Page 23: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

19

Izingatiwe kuwa hakuna fedha itakayo chukuliwa benki bila ya kuwa na saini za watia

saini wawili toka makundi mawili tofauti pamoja na muhtasari wa kikao cha mkutano

mkuu wa kijiji ulioidhinisha matumizi ya fedha hizo.

KITABU CHA MAPATO NA MATUMIZI Hiki ni kitabu kitakachukuwa kinatunza kumbukumbu za fedha zote zinazoingia kutoka

katika faini na ada za vibali au leseni mbalimbali. Pia kitakuwa na kumbukumbu za

matumizi yote ya fedha zinazotumika ikionyesha saini ya aliyechukuwa na

viambatanisho vya uthibitisho kuwa malipo hayo yameidhinishwa na mamlaka husika.

Mfano wa malipo ni pamoja na zawadi ya pongezi kwa wafanya doria kwa kazi nzuri

itakayokuwa imethibitishwa na kuidhinishwa kuwa wapewe kiasi kadhaa kwa

maandishi. Hapa ni lazima mpokeaji athibitishe kuwa amepokea pesa hiyo.

USIMAMIZI WA FEDHA Katika kifungu hiki sisi wanakijiji cha Kagunga tunaainisha mfumo utakaotumika

kusimamia fedha hususani katika matumizi yake.

WAHUSIKA WAKUU; Mtu atakaye husika kushika vitabu vya risiti na kupokea fedha toka kwa mlipaji

atakuwa ni mtunza fedha. Fedha hizo zitahifadhiwa kwa muda na kisha kupelekwa

benki kwenye akaunti ambayo imefunguliwa kwaajili ya fedha zitokanazo na msitu wa

hifadhi ya kijiji cha Kagunga.

AFISA MUWAJIBIKAJI WA MASUALA YA FEDHA Afisa muwajibikaji wa fedha za Msitu wa Kijiji atakuwa AFISA MTENDAJI WA KIJIJI

kwakuwa huyu ndiye anayewajibika kwa masuala yote yahusuyo fedha hapa kijijini.

Anaweza kumhoji mtunza fedha na kukagua vitabu vya fedha wakati wowote

atakapoona inafaa. Hata hivyo mtunza hazina anapaswa kutoa taarifa ya mwenendo

wa makusanyo ya fedha kila wiki.

Hata hivyo, kwa kuzingatia misingi ya uhuru wa habari na taratibu za utawala bora

mwananchi yeyote anaweza kuomba kukagua kitabu cha makusanyo. pamoja na

taratibu hizi za pekee, Mamlaka inayowajibika ya juu kabisa katika kijiji ni Mkutano

mkuu, hivyo, taarifa ya mapato na matumizi yatasomwa kila baada ya miezi mitatu

katika mikutano mkuu wa kijiji kama ilivyo desturi ya mikutano hiyo hapa kijijini.

Kwa upande wa ukiukwaji wa taratibu au tuhuma dhidi ya mtunza hazina taratibu

zifuatazo zitatumika;

Page 24: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

20

Endapo mtunza hazina /fedha atahisiwa kuwa katumia fedha tofauti na utaratibu au

ridhaa ya wananchi hatua zifuatazo zitumike; -

▪ Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji ataitisha kikao cha kamati yake

na kumhoji juu ya tuhuma husika

▪ Ikiwa ameshindwa kutoa maelezo ya kujitosheleza na kushindwa kuondoa

mashaka hayo, Taarifa hiyo itapelekwa kwa mwenyekiti wa kijiji ambaye

anapaswa kuitisha kikao cha Serikali ya Kijiji kumhoji juu ya tuhuma husika,

kama maelezo yake hayajajitosheleza kiasi cha kuuongezea uongozi wa

kijiji mashaka, Atapewa barua ya kujieleza ikiwa ni nafasi ya kujieleza

kufuatia tuhuma au mashaka dhidi ya matumizi mbaya ya fedha ya kijiji.

▪ Endapo maelezo yake katika barua hayataondoa utata, mwenyekiti

ataitisha Halmashauri ya kijiji iliyomchagua na kuwasilisha hoja ya

kumsimamisha kazi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake. Hoja

ikipitishwa VEO ataandika barua ya kumsimamisha kazi hadi hapo

mahakama/baraza la kata itakapo amua kuwa ana hatia ama la,

▪ Baada ya kusimamishwa kazi VEO atamfikisha mtuhumiwa

polisi/mahakamani/baraza la kata. moja ya vyombo hivyo ndicho

kitakachotoa tamko la mwisho.

▪ Akipatikana na hatia atafukuzwa kazi hiyo na kutekeleza adhabu

zilizoamriwa, na mara moja Mwenyekiti wa kijiji kufanya taratibu za kuziba

pengo la mtunza hazina aliyepita.

MATUMIZI YANAYOIDHINISHWA; Kwanza ifahamike kuwa matumizi makuu ya fedha itokanayo na uhifadhi wa msitu

wetu yatagawanyika katika makundi makuu matatu kama ifuatavyo; -

▪ 50% itatumika katika shughuli za maendeleo ya kijiji kwaajili ya wananchi wote

▪ 25% pesa hii itatumika kwaajili ya kuboresha kamati ya maliasili ya Kijiji.

▪ 25% itatumika kwaajili ya kufanya shughuli za uhifadhi wa msitu wa kijiji cha

Kagunga kuwa endelevu kama vile:

• Ununuzi wa vitabu vya kumbukumbu kama vilivyoainishwa katika

“Kugharamia marekebisho ya mipaka".

Page 25: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

21

• Kugharamia tathimini ya Rasilimali na kuboresha Mpango huu wa

Usimamizi

• Kugharamia uendeshaji wa kesi.

• Kutoa motisha kwa kikosi cha doria na Kamati ya Maliasili ya Kijiji katika

kutekeleza majukumu yao.

• Kununua zana za doria mfano sare, mahema, tochi, makoti ya mvua n.k.

• Kugharamia mahitaji wakati wa doria kama chakula n.k.

Mipaka ya Msitu wa hifadhi wa kijiji cha Kagunga Msitu huu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga una bikoni zinazozunguka mipaka ya nje

ya msitu huu.

MAELEKEZO MAALUM Katika maelekezo haya inasisitizwa kwamba maamuzi yote kuhusu usimamizi wa

msitu wetu turejee vipengele vilivyoelekezwa na kukubaliwa na sisi wenyewe katika

mpango huu. Hatutegemei tena wataalamu toka wilayani kuja kufanya maamuzi kwa

ajili yetu bali kuwaomba ushauri katika kupambanua mkwamo fulani ili baadaye sisi

tufanye maamuzi.

ULINZI NA UKAGUZI WA ENEO LA MSITU WA KIJIJI CHA KAGUNGA Kila mwanakijiji wa Kagunga ana jukumu la kulinda na kutunza hifadhi ya msitu wa

kijiji. Hili jukumu litafanyika kwa kutekeleza yafuatayo:

▪ Kutoa taarifa za uhalifu

▪ Kutambua na kutoa taarifa za wahalifu wa msitu wa hifadhi ya kijiji na zana za

uvunaji haramu ndani na hifadhi ya msitu wa kijiji.

▪ Kuzuia moto usitokee na kuzima unapotokea.

▪ Kushiriki katika shughuli za uoteshaji miche ya miti na upandaji wa miti katika

maeneo ya makazi na mashambani.

▪ Ni wajibu wa wakazi wote wa kijiji cha Kagunga kushirikiana katika ulinzi wa

msitu wa hifadhi ya kijiji.

▪ Doria za ukaguzi katika msitu wa hifadhi ya kijiji zitafanywa na kamati ya doria

angalau mara mbili kwa mwezi.

Page 26: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

22

▪ Walinzi wa msitu na hifadhi watachaguliwa na Halmashauri ya kijiji na

kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji kutoka katika vitongoji vyote vya kijiji

kwa uwakilishi wa Vitongoji vya Kagunga A, Kagunga B, Mantena na Kamkola.

Sifa za Walinzi wa Msitu. Zifuatazo ni miongni mwa sifa ambazo inabidi mlinzi wa msitu sharti awe nazo:

▪ Awe na tabia na mwenendo mzuri.

▪ Wenye kujituma na mwaminifu.

▪ Mkakamavu na mwenye afya nzuri.

▪ Asiwe mlevi

▪ Awe mkazi wa kijiji cha Kagunga na raia wa Tanzania.

▪ Awe na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

▪ Ajue kusoma na kuandika.

Wajibu, Majukumu na Mafao ya Walinzi wa Msitu wa Hifadhi ya Kijiji

▪ Walinzi watachagua kiongizi wao (Kamanda) kutoka miongoni mwao ambaye

atawajibika kupanga utaratibu kwa kushirikiana na walinzi wenzake wa doria

na utoaji taarifa kwa Kamati ya Mazingira.

▪ Walinzi wa msitu hawatalipwa mishahara lakini watapata motisha kama

itakavyoamuliwa na Serikali ya kijiji. Aidha walinzi husika wanaweza kupewa

25% ya faini anayotozwa mhalifu.

▪ Walinzi wa msitu wanaweza kusamehewa kazi nyingine za maendeleo kijijini.

▪ Walinzi watakaokwenda kinyume na maadili yao ya kazi wataadhibiwa kwa

kuonywa, kutozwa faini na kufukuzwa au kushitakiwa Mahakamani kutokana

na ukubwa wa kosa lililotendeka.

▪ Walinzi watatoa taarifa yao ya doria kila wanapofanya doria kwa Kamanda wao

ambaye atapaswa kutoa taarifa kwa Kamati ya Mazingira haraka iwezekanavyo

(isizidi siku moja).

▪ Walinzi waliofanya kazi nzuri watazawadiwa kila mwisho wa mwaka na

Halmashaurii ya Kijiji. Walinzi hao watapendekezwa na Kamati ya Mazingira na

kuthibitishwa na Halmashauri ya kijiji. Zawadi/ motisha kwa walinzi waliofanya

vizuri itakuwa kama ilivyopendekezwa hapo juu.

Page 27: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

23

OPERESHENI Yapo mazingira ya pekee ambapo kikosi pekee hakitoweza kukabiliana na uhalifu

fulani wa mpito, hivyo operesheni maalumu itaandaliwa kwa idhini ya mwenyekiti wa

kijiji kupitia kamati yake ya serikali ya kijiji kwa ushauri wa kamati kuu mbili; -

▪ Kamati ya Ulinzi ya Kijiji na

▪ Kamati ya Maliasili ya Kijiji.

N.B: Maandalizi haya lazima yawe ya siri sana.

ZAWADI YA PONGEZI KWA MWANA DORIA Kutakuwa na utaratibu wa kutoa zawadi ya pongezi au motisha kwa mwana kikosi cha

doria ambaye atafanya kazi kwa ujasiri, ushujaa na uadilifu mkubwa utakao thibitishwa

na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri kuu ya Kijiji na Kuungwa mkono na Mkutano

Mkuu wa Kijiji. Kiasi cha pongezi au motisha kitapangwa na Halmashauri kuu ya kijiji.

zawadi hii itatolewa hadharani na kuwekwa katika kumbukumbu za vitabu husika.

Kifungu Cha Kumi Taratibu

Kanuni za Kutumia Msitu wa Hifadhi ya kijiji ▪ Mkazi yeyote wa kijiji cha Kagunga, Afisa Misitu au mtu yeyote aliyeruhusiwa

wanaweza kuingia ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji kwa idhini ya Kamati ya

Mazingira.

▪ Afisa Misitu yeyote wa Idara ya Misitu na Nyuki wakati wowote anaweza kuingia

ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji aidha akiwa peke yake au kwa kushirikiana

na Kamati ya Mazingira ya kijiji kwa lengo la kufanya ukaguzi na kutoa ushauri

kwa Kamati ya Mazingira ambao unapaswa kupokelewa na kufanyiwa kazi kwa

lengo la kuboresha uendelezaji wa eneo hilo la msitu.

▪ Sio ruksa kwa mtu yeyote kuingia msitu wa hifadhi ya kijiji bila kibali kutoka kwa

Kamati ya Mazingira isipokuwa Walinzi wa msitu, Halmashauri ya kijiji, Kamati

ya Mazingira na Afisa Misitu wanaweza kufanya hivyo bila kibali.

▪ Wageni wote wenye vibali toka Wizarani, Wilayani au wafadhili ni sharti wapite

kijijini na kuonyesha vibali vyao kwa Kamati ya Mazingira ya kijiji kabla ya

kuanza kufanya kazi yoyote ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji.

Page 28: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

24

Kanuni za matumizi ya msitu: Mahitaji yaliyoruhusiwa yatapaswa kupatikana kutoka maeneo ya matumizi ndani ya

msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga. Maeneo yaliyohifadhiwa hayataruhusiwa

kupata mahitaji ya mbao, miti ya nguzo/miamba ya nyumba na mengineyo

yasiyoruhusiwa.

Matumizi ya Msitu yanayohusu Ukataji wa Miti Mahitaji yote yanayohusu ukataji miti aina fulani kwa ajili ya mbao, nguzo na miamba

ya nyumba ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga yanaruhusiwa katika EDU

ya Maba kwa kibali kitakachotolewa na Kamati ya Maliasili na kuwekwa alama kwa

kutumia nyundo maalum ya Idara ya Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Miti

husika itavunwa kwa kiwango ambacho hakitaathiri lengo la msingi la kuhifadhi msitu

ambalo ni kuhifadhi vyanzo vya maji na upatikanaji endelevu wa rasilimali na huduma

ya msitu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

TARATIBU NA SHERIA NYINGINEZO Adhabu Uwezo wa Kamati ya Mazingira ya kijiji cha Kagunga kutoza faini umetolewa kwake

na Halmashauri ya kijiji cha Kagunga kulingana na Sheria za Serikali za Mitaa (Serikali

za Vijiji) 1982 No. 7 zilizoundwa chini ya kifungu cha 120 (i) na 167.

Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya matumizi ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha

Kagunga yaliyowekwa na kukubaliwa atatozwa faini kwa mujibu wa Sheria Ndogo ya

kijiji cha Kagunga ya kulinda na kutunza msitu wa hifadhi ya kijiji.

Kifungu Cha Kumi na Moja Adhabu

MCHAKATO WA KUMSHUGHULIKIA MKOSAJI NA KOSA ▪ Hairuhusiwi kwa mwanakijiji, mwanakamati, mlinzi au kiongozi yeyote kumtoza

faini mhalifu akiwa peke yake.

▪ Mazao ya misitu yaliyovunwa kinyume cha utaratibu pamoja na zana

zilizotumika katika uhalifu huo yakikamatwa ni lazima yafikishwe kwenye ofisi

ya kijiji ambapo hatua zaidi itachuliwa na Kamati ya Mazingira ya kijiji.

▪ Iwapo itabainika kuwa mtu au watu wamekiuka taratibu za matumizi ya msitu

wa hifadhi ya kijiji, mtu huyo au watu hao watafikishwa mbele ya Kamati ya

Page 29: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

25

Mazingira ya kijiji na suala lao litashughulikiwa kwa utaratuibu ufuatao hapa

chini:

• Mhalifu/wahalifu watafikishwa katika ofisi ya kijiji ambapo Afisa Mtendaji

wa Kijiji atamuweka/atawaweka chini ya ulinzi. Afisa Mtendaji wa Kijiji

atawaarifu viongozi wa kamati/wajumbe wa Kamati ya Mazingira

angalau wawili ili kuwatoza faini wahalifu iwapo watakiri/atakiri kosa kwa

kuweka sahihi katika daftari la “makosa na faini”

• Iwapo mhalifu/mtuhumiwa atakataa kukiri kutenda kosa kwa kukataa

kuweka sahihi katika daftari, mtu huyo atatakiwa kupelekwa

mahakamani.

• Endapo mhalifu/wahalifu watakiri kutenda kosa, faini yote lazima iwe

imelipwa katika muda wa siku tatu (3) toka siku ya kukiri kutenda kosa

hilo. Hata hivyo mhalifu atalazimika kuwekewa dhamana na mtu

anayekubalika katika kijiji cha Kagunga.

▪ Katibu atapokea malipo ya faini iliyolipwa kwa kuandika stakabadhi ambayo

atampatia mhalifu. Namba ya stakabadhi iliyotolewa itaandikwa kwenye daftari

la “Makosa na Faini” na kumkabidhi Mweka Hazina azipeleke kwenye akaunti

ya Kamati ya Mazingira ya kijiji.

▪ Iwapo mtu anayetuhumiwa kutenda kosa atakataa kukiri kosa mbele ya Kamati

ya Mazingira na mbele ya Mwenyekiti wa Kijiji au Afisa Mtendji wa Kijiji basi

itabidi vyombo hivyo vya utendaji vifikishe shauri hili mahakamani kwa uamuzi

zaidi.

▪ Iwapo mhalifu atashindwa kulipa faini katika kipindi kilichokubaliwa basi Kamati

ya Mazingira au Afisa Mtendaji wa Kijiji atafikisha suala hilo mahakamani.

FAINI NA ADHABU KWA KILA KOSA Mtu yoyote atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa lolote lililoidhinishwa katika

kifungu cha 10 cha sheria ndogo hizi ataadhibiwa kama ifuatavyo:

▪ Kosa la kuingiza na kuchunga mifugo atatozwa Tshs 5000/= kwa kila

mbwa, nguruwe, ng’ombe na Punda na Tsh 2500/= kwa mbuzi na

kondoo. Atakayeshindwa kulipa mifugo yake itaifishwe kulingana na gharama

ya faini.

Page 30: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

26

▪ Kosa la kuingia msituni bila kibali adhabu yake itakuwa ni faini isiyopungua

Tsh 10,000/= na isiyozidi Tsh 50,000/=

▪ Kosa la Kuchoma mkaa faini shilingi Tsh 50,000/= na kutaifisha mkaa huo.

▪ Kosa la Kukata miti bila kibali adhabu itatolewa kulingana na thamani ya mti

uliokatwa na faini isiyopungua Tsh 10,000/= na isizidi Tsh 50,000/= pamoja na

kutaifisha miti hiyo.

▪ Kosa la Kufanya shughuli za kilimo faini shilingi elfu hamsini (50,000/=) kwa

hekari moja, kutaifisha mazao na kupelekwa mahakamani.

▪ Kosa la Kuchoma moto faini ya isiyopungua Tsh 20,000/= na isiyozidi Tsh

50,000/= na atashitakiwa kwa mujibu wa sheria ya kosa husika.

▪ Kosa la Kufanya shughuli nyingine yoyote isiyohusika katika msitu huo

atatozwa faini Tsh 30,000/=

FAINI ZA KUTOWAJIBIKA Iwapo mjumbe yeyote katika Halmashauri ya Kijiji, Kamati ya Mazingira au walinzi wa

msitu atakiuka taratibu za kiutendaji kuhusiana na uhifadhi wa msitu wa hifadhi ya kijiji

cha Kagunga, atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii na atatozwa faini

itakayojulikana kama faini ya wenye dhamana/madaraka. Faini hiyo itakuwa mara

mbili ya faini zitakazotozwa kwa watu wasiokuwa na madaraka kijijini/ zilizoainishwa

hapo juu.

• Pamoja na faini hizo, makosa ya viongozi hao lazima yajadiliwe kwenye vikao

vya juu katika kijiji na kuwachukulia hatua kali kama vile barua za onyo la

maandishi, kusimamishwa na kuwaondoa kwenye nafasi zao baada ya

kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.

• Kwa wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Afisa Mtendaji Kata ataitisha Kikao

kujadili hatima ya kiongozi aliyefanya uhalifu huo.

Kifungu Cha Kumi na Mbili Kuboresha msitu na Ukarabati wake

KUUENDELEZA MSITU Kwa bahati nzuri utengaji wa msitu ulizingatia maeneo ya kulima kuchungia mifugo,

makazi n.k. hivyo hakuna mvutano wa mgogoro wa hitaji la shughuli hizi katika eneo

la msitu huu. Shughuli kama hizi zitafanyika nje ya msitu kwa kujitosheleza. Hapa

Page 31: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

27

Mpango huu wa Usimamizi wa Msitu unapiga marufuku kufanyika shughuli za aina hii

ndani ya msitu.

Aidha, ni marufuku mtu au kikundi cha watu kupanda mti wowote wa kigeni ndani ya

msitu huu.

Aina pekee za miti zinazoruhusiwa kuvunwa na kiasi chake zimeorodheshwa katika

majedwali yaliyoambatanishwa na mpango huu. Hairuhusiwi kutumia msumeno wa

mnyororo katika msitu huu.

Kifungu Cha Kumi na Tatu Matumizi

UTANGULIZI: Msitu huu ni msitu wa matumizi na Uhifadhi hivyo uvunaji wa miti ya mbao

unaruhusiwa kwa kiwango kilicho ainishwa katika mpango huu, uvunaji wa rasilimali

za msitu unaruhusiwa katika EDU ya MABA. Lakini jambo la kuzingatia ni kiasi, wakati

na utaratibu wa uvunaji kama ilivyo ainishwa katika mpango huu. EDU ya Uhifadhi ya

KATUNU na MAJINDO haitaruhusiwa kufanyika shughuli zozote za uvunaji kwani ni

kwa ajili ya Uhifadhi na matumizi mengine yasiyokuwa ya uvunaji wa miti na kutokana

na kuwa maeneo yanayopendelewa na wanyamapori aina ya sokwe pia makorongo

marefu, vyanzo vya maji na bioanuai mbalimbali muhimu. Hivyo basi, Mahitaji

yaliyoruhusiwa yatapaswa kupatikana kutoka maeneo ya matumizi ndani ya msitu wa

hifadhi ya kijiji cha Kagunga. Maeneo yaliyozuiliwa/hifadhiwa hayataruhusiwa kupata

mahitaji ya mbao, miti ya nguzo/miamba ya nyumba na mengineyo yasiyoruhusiwa.

UVUNAJI WA MITI Uvunaji wa miti unaoruhusiwa ni kwa miti ya aina zilizoorodheshwa katika Jedwali Na

1. EDU hii ina jumla ya miti kama inavyoonyeshwa katika Jedwali (tazama katika

viambata) ikiwa ni pamoja na matumizi mengineyo ya EDU hii.

Kiasi kamili cha miti ya kuvunwa kwa kila aina ya mti vimeonyeshwa katika jedwali

namba 5 na 7. Katika majedwali haya imeonyeshwa bayana kiasi gani cha kuvunwa

kwa kila mwaka na ni aina gani ya miti. Inapaswa kuzingatiwa bila kuongeza hata

kidogo.

Page 32: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

28

Kifungu Cha Kumi na Nne Ratiba

HATUA ZA HARAKA ▪ KAMATI YA MALIASILI KIJIJI na Timu ya Doria zinapaswa kuchaguliwa

katika mkutano mkuu wa kijiji

▪ Kamati ya Maliasili ya Kijiji inapaswa kufanya mkutano wake wa kwanza

▪ Taratibu za ununuzi wa vitabu vya kumbukumbu zinatakiwa zifanyike ili

Kamati ikutane na Mtunza Hazina wa Wilaya. zoezi hili litakamilishwa na

Hafla au mkutano utakaohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kwa

uzinduzi rasmi.

▪ Mwezi June 2017 ni mwezi wa kuanza kazi rasmi kwa utekelezaji wa Mpango

wa Usimamizi wa Msitu huu wa hifadhi ya kijiji cha Kagunga.

UFUATILIAJI Vigezo vya Mafanikio: Vifuatavyo ni Vigezo vya mafanikio vitatumika katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa

Mpango huu wa Usimamizi wa msitu wa hifadhi ya kijiji:

▪ Wanakijiji kuunga mkono juhudi za uhifadhi kwa:

• Kutoa ushirikiano kwa Kamati ya Mazingira na walinzi wa msitu na

hifadhi.

• Kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

• Kuotesha na kupanda miti katika maeneo ya kaya na mashamba.

• Kuheshimu na kutekeleza taratibu za ulinzi na utunzaji Misitu.

▪ Kupungua kwa matukio ya upasuaji mbao, moto, uwindaji wa wanyama pori,

uvamizi wa msitu kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

▪ Kupungua na kufunga kwa njia zisizoruhusiwa msituni.

▪ Kuongezeka kwa uoto wa asili na hivyo msitu kufunga hasa katika maeneo

yaliyoharibiwa.

▪ Kurejea au kuongezeka kwa wanyama pori, ndege na viumbe vingine hai katika

msitu wa kijiji.

▪ Kuongezeka kwa kiwango cha maji kwenye mito, chemchem au kufufuka kwa

chemechem zilizokufa kutokana na uharibifu.

▪ Kuongezeka kwa makundi ya nyuki ndani ya msitu wa hifadhi ya kijiji.

Page 33: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

29

▪ Mipaka ya nje ya msitu wa hifadhi kuwa wazi, safi na kuonekana bila ugumu

wowote.

Wafuatiliaji Wafuatao watahusika kufanya ufuatiliaji kwa kukusanya taarifa kuhusu vigezo vya

mafanikio:

▪ Wataalamu wa Misitu wa ngazi zote.

▪ Halmashauri ya kijiji

▪ Kamati ya Mazingira ya kijiji.

Taarifa ya Ufuatiliaji Itatolewa kwa: ▪ Afisa Misitu (W)/ Afisa Misitu (M)

▪ Mkutano Mkuu wa kijiji.

▪ Mkuu wa Wilaya/Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.

▪ Halmashauri ya kijiji.

Muda wa Kufanya Ufuatiliaji Kamati ya Mazingira: Itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mpango huu mara mbili

(2) kila mwezi na kuandaa taarifa kwa Halmashauri ya kijiji mara moja kwa mwezi

yenye nakala kwa Afisa Misitu (W).

Halmasahauri ya kijiji: Itafuatilia mpango huu mara moja (1) kila mwezi

▪ kwa kutembelea msitu wa hifadhi ya kijiji angalau mara moja kila mwezi

▪ kuwa na agenda ya kudumu katika vikao vyake

▪ Kwa kutumia taarifa ya Kamati ya Mazingira.

Wataalam wa Misitu & ngazi za Eneo, (W)/ (M):

▪ Wataalam wa ngazi ya Eneo (Kata/Tarafa) watafanya ufuatiliaji wa mpango huu

mara moja kila mwezi.

▪ Wataalam wa ngazi ya Wilaya & Mkoa watafuatilia utekelezaji wa mpango huu

mara moja kila baada ya miezi mitatu (3) yaani robo mwaka.

Page 34: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

30

IKUMBUKWE: Taarifa ya matokeo ya ufuatailiaji itajadiliwa mara baada ya kazi ya

ufuatiliaji kukamilika.

Mpango huu unaweza kufanyiwa marekekebisho baada ya miaka mitano (5) ya

utekelezaji kwa kuzingatia taarifa za ufuatiliaji na uamuzi uliofikiwa wakati wa kujadili

taarifa hiyo.

RATIBA YA UTEKELEZAJI Hatua za Awali za Utekelezaji:

▪ Kuchagua Kamati ya Mazingira na walinzi wa msitu (Kamati ya doria) itafanyika

mara baada ya mpango wa utekelezaji kupitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji.

▪ Kikao cha kwanza cha Kamati ya Mazingira na walinzi kitafanyika siku moja

baada ya uchaguzi wao kufanyika.

▪ Kununua vitabu vya kumbukumbu itafanyika baada ya Kamati ya Mazingira

kufanya kikao chake cha kwanza.

Hatua Zitakazofuata ▪ Kuweka mabango ya matangazo.

MUDA WA MPANGO, MAREKEBISHO NA MAPITIO YAKE: Mpango huu wa utekelezaji utatumika kwa miaka mitano (5) kuanzia mwaka 2017 –

2021. Marekebisho ya mpango yatafanyika kwa kuzingatia mahitaji yatakayojitokeza

kwa lengo la kuuboresha na Kamati ya Mazingira ya kijiji itahusika kwa ushirikiano na

Afisa Misitu (W) Mpanda.

Page 35: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

31

Page 36: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

32

VIAMBATA

MPANGO WA UVUNAJI KWA AINA MBALIMBALI ZA MITI KATIKA EDU ZA

MABA

JEDWALI Na 1: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA

MABA.

MITI MUHIMU MITI MINGINEYO MATUMIZI MENGINEYO

Mkoma Mkalya Ukataji wa milala

Mbanga Mhongolo Urinaji wa asali

Mlembela Mbombo Uvunaji wa miti ya mbao

Mninga Miyenze Kukata nyasi

Mkurungu Mitonga Kukusanya kuni

Mpilipili Msongati Ukatajiwa boriti, nguzo na fito

Mtundu Msongati Matambiko

Page 37: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

33

JEDWALI Na. 2: MAJUMUISHO YA TAKWIMU KUTOKA KATIKA PLOTI ZA SAMPULI

Forest assessment form C Kijiji Kagunga Jina la msitu Kampese Idadi ya ploti sampuli (N) 62 Jina la EDU Maba

Eneo la EDU (ha) (A) 2479 Eneo la ploti sampuli (ha) (P) 0.04

Madaraja ya vipimo (DBH)

<4 4 - 7 8 - 14 15 - 29 30 - 49 50+

Jum

la

iliyo

piu

mw

a

(T)

Jum

la

kwen

ye E

DU

(F

)

Jum

la

iliyo

pim

wa

(T)

Jum

la

kwen

ye

ED

U (

F)

Jum

la

iliyo

pim

wa

(T

)

Jum

la

kwen

ye

ED

U (

F)

Jum

la

iliyo

pim

wa

(T

)

Jum

la

kwen

ye

ED

U (

F)

Jum

la

iliyo

pim

wa

(T)

Jum

la

kwen

ye

ED

U (

F)

Jum

la

iliyo

pim

wa

(T)

Jum

la

kwen

ye

ED

U (

F)

Miti muhimu

Mninga 0 0 0 0 1 1,000 4 3,998 0 0 2 1,999

Mkurungu 5 4,998 6 5,998 12 11,995 15 14,994 5 4,998 1 1,000

Mbanga 0 0 0 0 6 5,998 3 2,999 3 2,999 1 1,000

mpilipili 0 0 0 0 1 1,000 0 0 1 1,000 0 0

Mtundu 15 14,994 2 1,999 1 1,000 4 3,998 3 2,999 2 1,999

Msawala 1 1,000 0 0 1 1,000 0 0 0 0 0

Mkola 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0 0 0 0 0

Mlembela 0 0 0 0 3 2,999 2 1,999 2 1,999 2 1,999

Mfulu 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0

Jumla kwenye EDU Miti muhimu 21,991 8,996 24,990 27,989 13,994 7,997

Wastani wa miti / ha 9 4 10 11 6 3

Miti mingineyo

mkoma 7 6,997 8 7,997 13 12,995 15 14,994 8 7,997 9 8,996

Msongati 0 0 1 1,000 6 5,998 4 3,998 4 3,998 0 0

Mlama 6 5,998 3 2,999 3 2,999 4 3,998 2 1,999 0 0

Mtonga 5 4,998 17 16,993 43 42,983 40 39,984 19 18,992 3 2,999

Page 38: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

34

Mtopetope 0 1 1,000 3 2,999 4 3,998 1 1,000 1 1,000

Kibhula 4 3,998 15 14,994 19 18,992 26 25,990 2 1,999 3 2,999

Mkuni 0 2 1,999 1 1,000 4 3,998 7 6,997 13 12,995

Mketya 0 2 1,999 0 0 1 1,000 0

Miyenze 0 4 3,998 5 4,998 1 1,000 3 2,999 4 3,998

Mlunguji 0 4 3,998 3 2,999 0 2 1,999 0

Kaselenge 1 1,000 4 3,998 3 2,999 0 0 0 0 0

Mgando 1 1,000 1 1,000 2 1,999 2 1,999 0 0 2 1,999

Mbarebare 0 0 1 1,000 1 1,000 3 2,999 0 0 0 0

Mgunga 0 0 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0 0

Mtiti 0 0 2 1,999 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0

Mputika 0 0 1 1,000 2 1,999 0 0 1 1,000 1 1,000

Mbeko 0 0 1 1,000 2 1,999 0 0 1 1,000 0 0

Chinga 0 0 1 1,000 3 2,999 4 3,998 0 0 0 0

Mwembepori 0 0 2 1,999 0 0 0 0 0 0 0 0

Mfundambogo 0 0 0 0 2 1,999 0 0 3 2,999 0 0

Mponda 0 0 0 0 0 0 0 0 4 3,998 5 4,998

Msantu 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0 1 1,000

Mgumbu 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0 0 0

Kafumla 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0 0 0

Nyengo 2 1,999 0 0 1 1,000 2 1,999 2 1,999 0 0

Mbuguso 0 0 0 0 1 1,000 0 0 0 0 0

Mkalya 0 0 0 0 0 0 0 0 1 1,000 0 0

Mnyoso 0 0 0 0 1 1,000 1 1,000 0 0 0 0

Mpapa 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 1 1,000

Mjuguji 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0

Msulula 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0

27,989 13,994 7,997

Jumla miningeyo 25,990 70,971 115,953 113,954 60,975 42,983

Page 39: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

35

Wastani wa miti/ha 10 29 47 46 25 17

Page 40: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

36

JEDWALI Na 3 FOMU ‘C’ YA TATHIMINI

Form C ya Tathmini ya msitu Kijiji Jina la Msitu Idadi ya ploti za sampuli (N)

Jina la EDU Eneo la EDU (ha) (A) Plot area (ha) (P)

Madaraja ya vipenyo

<4 4 - 7 8 - 14 15 - 29 30 – 49 50+

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Ju

mla

ili

yo

pim

wa

(T

)

Ju

mla

kw

en

ye

E

DU

(F

)

Miti muhimu

Miti Mingineyo

Page 41: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

37

Jumla (F) = A/P * T/N : A = eneo la EDU (ha),P = ukubwa wa ploti ya sampuli (ha), T = idadi ya miti iliyopimwa (kwenye ploti zote za sampuli), N = idadi ya ploti za sampuli

JEDWALI Na 4: MIHIMILI YA MSINGI KUONYESHA WINGI WA MITI KATIKA EDU YA MABA.

Page 42: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

38

JEDWALI Na. 5:

9

4

10

11

6

3

0

2

4

6

8

10

12

<4 4 - 7 8 - 14 15 - 29 30 - 49 50+

Idad

i ya

mit

i/h

a

DBH (cm)

Miti muhimu

Page 43: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

39

0

2000

4000

6000

8000

10000

12000

14000

16000

<4 4-7 8-14 15-29 30-49 50+

Idad

i ya

mit

i

DBH (cm)

Mihimili ya ukubwa wa miti aina ya Mkurungu - EDU ya Maba

Page 44: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

40

JEDWALI Na 6. UFUPISHO WA MPANGO WA UVUNAJI KATIKA EDU YA MABA KWA MWAKA 2017/2018 HADI 2021/2022

DBH Idadi katika

EDU Idadi halisi Pungufu / Ziada

Iliyopo kuvunwa (50% ya ziada)

Uvunaji 5 yrs Maoni

< 4 21,991

1,127,945

(1,105,954)

(552,977) -110595

4 -7 8,996 872608

(863,612)

(431,806) -86361

8-14 24990 391682

(366,692)

(183,346) -36669

15- 29 27989 24790

3,199

1,600 320

30- 49 13994 12395

1,599

800 160

50+ 7997 4958

3,039

1,520 304

JEDWALI Na 7: ORODHA YA MITI YA INAYORUHUSIWA KUVUNWA - EDU YA MABA

MITI MUHIMU MITI MINGINEYO MATUMIZI MENGINEYO

Msawala Mbarebare Urinaji wa asali

Kabamba Msongati Uyoga na matunda pori

Mpilipili Mvinje Uvunaji wa miti ya mbao

Mkola Mhongolo Uchimbaji wa dawa za kienyeji

Mninga Mkoma Kukata nyasi

Mkurungu Mhunsa Kukusanya kuni

Mlembela Mubha Kamba za miti

Mbombo Ukataji wa boriti, nguzo na fito

Page 45: HALMASHAURI YA KIJIJI CHA KAGUNGA · 3 Hali ya msitu huu sio nzuri sana kutokana na uharibifu unaoendelea hasa kilimo na uchungiaji mifugo. Wapasuaji mbao walio wengi wanatoka nje

41

Maji

Matambiko