56

Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

  • Upload
    others

  • View
    4

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa
Page 2: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Padre Massimiliano Taroni ni wa Shirika la Ndugu

Wadogo Wafransiskani. Alipewa Daraja ya Upadre

mwaka 1992 na kuanza kuwa Mwandishi mwaka

1993. Kwa miaka kumi na miwili amekuwa Paroko

Msaidizi katika parokia iliyo nje ya jiji la Milano

na Mkurugenzi wa Malezi ya Vijana.

Kwa miaka kumi na miwili amekuwa akifanya kazi

kama mhamasishaji wa kimisionari na kiongozi wa

misioni za kifransiskani katika nchi mbalimbali

ulimwenguni kote. Kwa miaka mitano amesimamia

gazeti la kimisionari na kuweza kuchapisha mamia

ya kazi: majarida 65 yanayohusu maisha ya

watakatifu na mashahidi wa imani, na vitabu

kadhaa vinavyohusu ibada ya Moyo Mtakatifu na

vitu vingine vya msaada kwa ajili ya Katekesi ya

kuingizwa katika Ukristo.

Watu wengi wamepokea neema kwa njia ya maombeziya Mtukuka Sista Tarsilla Osti.

Tuendelee kumwomba ili atupatie mema ya kiroho naya kimwili kutoka kwa Bwana.

SALA

Ee Mungu, ambaye ndani ya Moyo waMtumishi wako Mwenye Heri Tarsilla Osti,uliwasha moto wa upendo mkuu ambaoaliuonyesha kwa wagonjwa, maskini nawaliodharauliwa na hivyo kuiga mfano waMwanao Msulibiwa, tunakuomba upendekudhirisha utukufu wake pia hapa dunianina kwa maombezi yake utujalie neematunazoomba...

Baba Yetu, Salamu Maria, Atukuzwe.

Mwenye Heri Sista Tarsilla Osti, utuombee!

Kwa idhini ya Mamlaka ya Kanisa

Kwa taarifa, maombi ya machapisho ya wasifu na picha, kwataarifa za neema zilizopokelewa, wasiliana na:

Casa GeneraliziaVia del Trullo 372

00148 – RomaTel. +39 06.6530612

Email: [email protected]@istitutosacricuori.it

Sito: www.istitutosacricuori.it

Page 3: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Massimiliano Taroni

MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Moyo wa kiekaristi

Page 4: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Hitimisho la uchapishaji ni mwezi wa juni 2018

Page 5: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

• Utangulizi •

Mtukuka Sista Tarsilla Osti ambaye ni mhusika wasimulizi hili anastaajabisha kwa upendo wake

mkubwa kwa Yesu Msulibiwa na kwa Ekaristi; upendouliojidhihirisha katika hali halisi ya maisha ya kila siku,hasa katika kuhudumia wagonjwa.

Yeye hakufanya mambo makubwa, lakini alifanya kuwamakubwa matendo madogo ya kila siku kwa vile alifanyayote akisukumwa na upendo na nguvu ya ndani iliyomfanyakustahimili kwa furaha kila aina ya sadaka na matatizo.

Alikuwa mtawa mnyenyekevu aliyekuwa tayari kabisakupokea neema ya Mungu ambayo ilimfanya daima akuekiroho kwa undani zaidi na daima kujitahidi kutimizamapenzi ya Mungu na imani isiyo na ukomo katika sala.

Baada ya kuchapisha kijitabu hiki, ninawatakia wasomaji,kwa msaada wa neema ya Mungu, waweze kufahamu utajiriwa maisha ya ndani ya Mtukuka na kuwa lishe kwa wenyehamu ya kuiga fadhila zake.

Sista Maria Lidia RosmarinoMama Mkuu

Page 6: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa
Page 7: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

5 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

• Utoto na ujana •

Familia ya Osti iliishi Pola katika nchiya Istria wakati ambao maeneo hayo

yalikuwa chini ya Pola ya Austro-Hungari.Mhusika wetu, Anna Osti, alizaliwapalepale Pola tarehe 6 Desemba 1895,baba yake akiwa Pietro Osti (Hast-Ivessic)na mama yake Maria Maraspin. Wanandoahawa walikuwa na watoto saba, lakiniwatoto watatu tu walikua na kufikia utuuzima. Taaluma ya familia hii ilikuwaushonaji wa mavazi.Anna alikua katika upendo wa familiayake na tangu akiwa mtoto alianzakuonyesha baadhi ya sifa zake nzuri, kamavile utayari wa kutoa sadaka ndogo-ndogona daima kuwa tayari kujitoa kwa ajili yafamilia yake. Alikuwa mtoto kama walivyowatoto wote, lakini katika malumbano yakila siku na ndugu zake, alikuwa tayarikuomba msamaha mara moja.Alipoanza shule, alijaribu kuwasaidia walewaliokuwa na ugumu zaidi katika kujifunza,na hasa alivutwa kuwasaidia masikini. Alisoma shule hadi akawa na umri wamiaka kumi na miwili, naalipokaribia kuhitimumasomo yake aliachishwashule. Na hilililimsikitisha sana kamaalivyoandika baadayekatika shajara yake:“Nilitamani sanakuendelea na masomo,

Mama na babawa Sista Tarsilla

Mwonekano waPola

Page 8: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

6MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Kanisa Kuu laPola - ndani

Kanisa Kuu laPola - nje

lakini mama yangu hakuniruhusu kwasababu alimhitaji dada yangu kwa ajili yaushonaji wa nguo (yeye dada yanguhakutaka kwenda shuleni kusoma). Kwahiyo, mama hakutaka hata mimi niendeleena masomo kwani lilionekana kuwa jambolisilo pendeza. Kwa mtazamo wa mama:tulitakiwa kuwa sawa. Nilikuwa nikiumiasana wakati shule zilipokuwazikifunguliwa! Badala ya kuangalia madukaya nguo za mitindo nilikuwa nikisimamambele ya makabati ya vioo yaliyo na vitabu,madaftari, nk. Na mwaka wa masomoulipokuwa ukiisha na kuona wenzanguwakipandishwa madaraja, hata waleniliowafahamu kuwa na uwezo mdogokuliko mimi, niliona kwamba hata mimi

Page 9: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

7 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

ningeweza kufaulu. Kwa miaka niliendeleakuumia lakini nyumbani sikusema kitu kwayeyote. Kwa uchungu nilitunza vitabuvyangu na madaftari yangu ya mwaka wamwisho hadi siku moja vilipoondolewa (sijuina nani, labda na mama); nikakuta drootupu. Mungu ni mwema sana, kwa hakikaatakuwa aliruhusu haya kufanyika kwa faidayangu mwenyewe. Alitaka niwemnyenyekevu, nijitawale na kushindamatamanio yangu. Baadaye mwaka 1909 ukaanza; na kwakeAnna ulikuwa ni mwaka muhimu kwasababu katika mwaka huo alipokeaKipaimara na Komunyo ya Kwanza.Alipokea Kipaimara tarehe 10 Mei naKomunyo ya Kwanza tarehe 29 Juni baadaya kuwa tayari ameandaliwa kwa umakinikatika mafundisho ya Katekisimuyaliyofanyika katika Kanisa Kuu laPola.“Siku moja baadaye wakatinikizungumza na mama, nilimsimuliakuhusu tukio hili. Nilimweleza kwamba

Pola: Uwanja wamichezo

Page 10: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

8MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

sikujua kuwa watu hujisikia furaha hivikutokana na Bwana kukaa ndani mwetu.Mama alinisikiliza lakini hakusema kitu.Aa! Nilitamani kama ningekwisha pokeaKomunyo Takatifu mara nyingi zaidi. Lakinihakuna mtu aliyekuwa ameniambia juu yauzuri wa kupokea Komunyo Takatifu; nahivyo sikujua. Halafu kwa kuwa familia yetuhaikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hatana ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waaminiwakatoliki, lakini hawakuwa washika dini;lakini Anna alivutiwa kwa namna ya pekeena mambo ya Mungu. Mara nyingi mamayake alimwelekeza kusali hata wakati wamichezo. Baadaye kidogo Anna alikutana namateso na machungu katika familia yake

Lango la kambiya wakimbizi ya

Pottendorf-Landegg

(Hungari)

Wakimbiziwanaingia

kambini(Hungari)

Page 11: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

9 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

ambayo ilibidi ayazoee kwani katika kipindicha miaka michache walifariki kaka zakewatatu. Kutokana na kuzuka kwa Vita Vikuuvya Kwanza vya Dunia, mwaka wa 1915familia ya Osti ililazimika kukimbilia katikakambi ya wakimbizi huko Pontendorff-Landegg katika nchi ya Hungariambako ilikaa kwa miezi michache.Baba yake Anna akawa msimamiziwa kitengo cha ushonaji wa nguokatika kambi hiyo akisaidiwa namke wake.Misiba miwili iliifika tena familia yaOsti. Anna alipokuwa akikuaalisikia daima sauti yenye nguvuzaidi ya Mungu iliyokuwa ikimwita;lakini lini na wapi? Katika kipindicha mwanzo cha usichana wake nabaadaye katika ujana wake, Annaalizidi kuwa mzuri na mwenyenguvu, na baadhi ya vijana wakiume wakawa na nia ya kutakakumchumbia: “Nilikuwa mzuri, vijanawengi walinitafuta uchumba, nilikuwa nafuraha na nilipenda kutazamwa na wao.Lakini kamwe sikuwa na imani yoyote namtu yeyote. Jibu langu lilikuwa ndiyo nahapana mara baada ya salamu. Mara nyinginilihisi kufuatiliwa, kwa hiyo niliogopa nakutetemeka na niliongeza mwendo. Labdahili halikusababishwa na chochote chenyeuzito kwangu isipokuwa lilitokana na wogatu. Hao vijana walijisikia vibaya nahawakunitazama tena. Kwa kufanya hivyowalitoa nafasi kwa Yesu ambaye alitakaniwe wake kabisa.”

Anna Osti, kablaya kuingiaShirikani

Page 12: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Mwonekano waPola

• Wito •

Anna daima alijisikia kuwa na hamukubwa ya kumtolea Mungu maisha

yake, lakini hakupata mazingira ya kufaakatika familia yake. Alipanga kwendakanisani, lakini wakati huo huo hakutakakuvunja mahusiano na wanafamilia yake;kwa hivyo kwa uvumilivu aliacha muda

upite akisubiri ishara zamuda sahihi utakapofika.Wakati mmoja, kijanaaliyekuwa ameajiriwakatika posta ya mji wakewa Pola alimwomba Annaawe mchumba wake.Wakati huo Familia ya Ostiilikuwa imerudi Pola baadaya kukaa kwa muda nchini

Hungaria. Kinyume na matamanio yakeAnna aliwatii wazazi wake na kukubalikuchumbiwa; lakini katika moyo wakealimwomba Mungu amnasue kutoka katikamazingira yale mbayo hakuyapenda! Salayake ilisikika ... Kwa kweli, baada ya muda,

Shirika la MoyoMtakatifu hukoPola na Kanisa

la MoyoMtakatifu

Page 13: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

11 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Anna wakati akisomabaadhi ya barua zamchumba wake alikutanana taarifa juu ya ugonjwaaliokuwa nao mchumbawake. Jambo hili likawamsaada kwake; nalikawapa ujasiri yeye namama yake wa kukataakila kitu licha ya kujiteteakwingi kwa kijana huyo.Pia, asubuhi moja,alipokuwa Kanisani,aliandika hivi katikashajara yake huku akiwaamepiga magoti katikabenchi: “Kutoka altareni,kutoka sehemu ya Injili, kana kwambaalikuwa amesimama kwa miguu, lakini bilakumwona, aliniambia kwa sauti laini nayenye upole akasema, ‘unakumbuka wazolako la kutaka kuwa mtawa?” Hii ilikuwaalama kuwa maisha ya Anna yalikuwayakibadilika... Katika shajara yakealiandika: “Nakumbuka vizuri, ilikuwabaada ya chakula cha mchana na nilikuwa

Altare Kuu yaKanisa la MoyoMtakatifu hukoPola

Kanisa la MoyoMtakatifulililojengwa naMama RosaD’Ovidio - Pola

Page 14: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

12MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

nazuuza vyombo na kuviwekamoja kwa moja kwenye drooya meza. Wakati nikiwabado nawaza juu yamatamanio yangu yakuingia utawani ... nilisikiandani yangu sauti ikisema:“Utaweza kuwa mtawa marabaada ya kufariki dadayako.” Muda mfupi baadayealifariki Zaira dada yake.Siku moja, akiwa kanisani,alimwona bibi mzee akisalirozari; Anna akamsogelea

akamwuliza, “Bibi, nataka kuwa mtawa;tafadhali, ninaweza kumwona nani kuhususuala hili? Mwanamke yule akasema,“Nenda kwa Masista wa MoyoMtakatifu.”Ilikuwa mwezi Novemba mwaka1924 ... na mwanzo wa mwaka mpya AnnaOsti alianza kwenda kwenye Misa kila siku;lakini baadaye kidogo aliamua kuchukuahatua ya maamuzi. Kwa kweli tarehe 15Januari 1925 aliingia katika nyumba ya Polaya Masista wa Moyo Mtakatifu. Miezimichache baadaye, yaani tarehe 15 Agosti1925 alivishwa mavazi rasmi ya kitawa nakubadilisha jina; akaitwa Sista Tarsilla waMsulibiwa. Jina hili lisilo la kawaida lilitokawapi? Historia inaonyesha kwambaMtakatifu Tarsilla ambaye hukumbukwakatika kalenda tarehe 24 Desemba, alikuwashangazi ya Mtakatifu Gregori Mkuu. Maishayake yalitawaliwa na roho ya toba na sala, hiiikiwa ni alama ya maisha ambayo atakujakuyaishi Sista huyu kijana: Tarsilla!

Picha yaMtakatifuTarsilla -

shangazi waMtakatifu

Gregori MkuuPapa

Page 15: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

13 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Pola - Sanamu kutoka kanisa la Moyo Mtakatifu ambayo kwa sasa imokatika Parokia ya Mtakatifu Antonio huko Lanciano (Chieti)

Page 16: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

14MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

• Kati ya Masista wa MoyoMtakatifu •

Shirika la Masista wa Moyo Mtakatifulilianzishwa huko Roma na Sista Rosa

Rosato na Sista Rosa D’Ovidio. Baada yakupitia magumu mengi ya kihistoria,masista hawa walifungua nyumba ya pilihuko Pola. Hii ni kutokana na kazi nzuriiliyofanywa na Sista Rosa D’Ovidio. WakatiSista Tarsila anakwenda kukaa Pola, kazinyingine mbili zilikwisha fanyika huko,

yaani ufunguzi wa hospitali ya Jeshi laWanamaji, shule ya chekechea na shule yabweni ambapo Sista Tarsilla alikuwa akikaa.Kwa jumla kulikuwa na masista thelathinihivi. Mara baada ya kufika, Sista Tarsillaalionesha kupapenda mahali pale kamaanavyoshuhudia katka ukurasa wa shajarayake: “Nilikuwa na furaha siku zote zakukaa kwangu pale, kila kitu kilikuwakizuri, kila kitu kilikuwa sahihi, kila kitu

Waanzilishi nanembo ya

Masista wa MoyoMtakatifu - Rosa

Rosato na RosaD’Ovidio

(Nyumba Mama- Roma)

Page 17: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

15 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

kilinifaa, mambo mengi yalikuwa kamanilivyotarajia; sikuwahi kunyanyaswa.Kutokana na tabia yangu ya kujishusha,nilihisi kuwa ningeishi kwa amani na kilammoja. Kwa kweli, kwa upande wanguilionekana mbingu imefunguka nainagusika kwa vidole.”Wakati huo huo, alipewa kazi za ndani,kama vile kuweka vizuri mazingira yanyumba na kusaidia katika kitengo chaushonaji cha hapo nyumbani. Mwaka wa kwanza wa unovisi wa SistaTarsilla ulikuwa unaelekea kwisha na hivyokulikuwa na matarajio kwamba angepewamajukumu mapya na pengine angepelekwasehemu nyingine mpya. Katika Hospitali yaWanamaji kulikuwa na Sista ambayealitamani sana kurudi Roma, lakini mamamkubwa hakujua jinsi ya kupata Sistambadala wake. SistaTarsilla, akijua matamanioya Sista huyo, siku mojaalimwambia kwa unyoofukabisa, “Uwe na uvumilivu,utaona kuwa hivi karibunimimi nitakuja hospitalini.”Na kweli muda kidogobaadaye ikawa hivyo...

Pola - Hospitali yaJeshi la Wanamaji

Bustani yawatoto ya Jeshila Wanamajihuko Pola

Page 18: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

16MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

• Akiwa hospitalini •

Mwanzoni maisha katika hospitalihayakuwa marahisi kwa hakika kwa

sababu ilikuwa lazima kujifunza kwavitendo masuala mbalimbali kwenyemaeneo mengi na kukabiliana na matukioya kuumiza ambayo wakati mwingine

yalikuwa mabaya sana. Sista Tarsillaalijulikana mapema sana kutokana namajitoleo yake ya kuwahudumia wagonjwa.Kuhusu kipindi hicho Sista Tarsillaalibainisha katika shajara yake: “Mbele yawagonjwa mahututi, moyo wanguuliongezeka; kwa upande wangu mgonjwaalinifariji kana kwamba nilikuwa mbele yatabernakulo takatifu. Mara nyingi ilinitokea(kwa wagonjwa mahututi) kumwitamgonjwa ‘Yesu’. Wakati mwingine nilikoseahata katika maungamo: nilifikiri

Kanisa lamasista ndani yahospitali ya Jeshi

la Wanamaji

Page 19: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

ninaungama kwa Yesu mwenyewe.Nilipokuwa njiani ndani ya majengonilikuwa nikisema: “Yesu nitakuja hima,Yesu nitakuletea hiki au kile... halafunitarudi tena, unajua?”Mbali na uuguzi, Sista Tarsilla alikuwa nakazi ya kuandaa wagonjwa ili wapokeeSakramenti. Alipokuwa akifanya hivyo,alikuwa akiwafikiria wazazi wake ambaokwa muda mrefu hawakuwa wakipokeaEkaristi Takatifu... lakini mwaka 1928mama yake alikwenda kumtembelea;ilikuwa mara baada ya sikukuu ya Krismasina alimjulisha kwamba alikuwa amepokeaKomunyo! Sista Tarsilla alikuwa amesalisala nyingi sana; alikuwa amefanya malipizina majitoleo madogo-madogo kwa lengo hili...Miezi michache kabla yahapo alikuwa amewekanadhiri zake za kwanza zakujiweka wakfu kwaMungu tarehe 5 Agosti1927.Sista Tarsilla mara nyingialitumia muda wakekuabudu mbele ya Yesu

17 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Hospitali ya Jeshila Wanamaji -Pola - Mwonekanokutoka juu

Hospitali yaWanajeshiWanamaji - Pola,katika picha yasasa

Page 20: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

18MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Shule yaChekechea ya

Jeshi la Wanamaji- Pola

Ekaristi na aliishi utume wake kati yawagonjwa kama mwendelezo wa ibada yakuabudu aliyokuwa akiifanya. Alikuwaakimwacha Yesu katika tabernakulo nakwenda kuonana na Yesu katika nyuso zawagonjwa. Ilitokea siku moja Sista Tarsillaalikuta vyumba viwili ambavyo hutumiwa nawagonjwa kusubiri matibabu vikiwa vimejaawagonjwa wa homa ya mapafu; Sistaakaandika katika shajara yake ujumbe huu:“Tazama, Bwana anatupatia uzima ilituweze kuwasaidia watu hawa maskini ...ninafika, ninafungua chumba naninamkuta Yesu amesimama wima, chini yamiguu yake yupo kijana mdogo, naminikajisemea: Oo! Ndiyo, Bwana ameahidikwamba atakuwa pamoja na walewanaoteseka na anatutaka tumwendee Yeye.

Hivyo, ni hakika kwamba lazima tuwekaribu na wagonjwa, hasa wale

walio mahututi.”

Page 21: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

19 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Siri ya upendo wa Sista Tarsilla kwawagonjwa ilikuwa ni hii hasa: kuuona usowa Kristo katika mgonjwa na kwa hiyokumtumikia kwa uangalifu na umakinimkubwa sana. Baadaye Sista Tarsilla alianza kusoma iliapate stashahada ya uuguzi; na hivyo tarehe13 Februari 1929 alifanya mtihani nakufaulu kwa kiwango cha juu kabisa naakawa wa kwanza katika kozi hiyo! Katikashajara yake aliandika hivi: “Pia kwa hili,nimekuwa na upendo zaidi kwa wagonjwa.Niliona kwamba Bwana alitaka niwepamoja nao, na kwa sababu hiyoaliniwezesha kufaulu vizuri mtihani.”Jambo lingine la kustaajabisha kuhusu SistaTarsilla ni ukweli kwamba licha ya kutoahuduma na kupendwa na wagonjwa wote,alikuwa daima tayari kuchukua nafasi yamasista wengine, hasa katika kukesha usikuakiwa karibu na wagonjwa mahututi.

Masistawaliokuwawakitoa hudumaya afya katikahospitali (SistaTarsilla wa pilikutoka kushotokatika mstari wapili)

Page 22: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

20MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

• Sala na upendo •

Kwa karibu miaka 20 maisha ya SistaTarsilla yatajipambanua kwa njia ya

mihimili miwili yenye mvuto: Tabernakulona wodi ya wagonjwa! Baada ya kushirikimaisha ya jumuiya pamoja na masistawenzake, Sista Tarsilla alitumia muda mfupiwa mapumziko kukaa mbele ya SakramentiTakatifu na kusali kwa moyo.

Ni vigumu kuelezea jinsi alivyojisikiakatika muda huo wa muunganiko na Bwana.Hata hivyo, kitu fulani kinaonekana katikamaandishi yake. Siku moja aliandikakwenye shajara yake simulizi kuhusumang’amuzi ya sala yake ya taamuli:“Nilikusudia kupambana na maisha kwanguvu bila kujiumiza, na kuichukua ndani

Sista Tarsilla (wa6 kutoka

kushoto) Pola,akiwa na

jumuiya yahospitali

Page 23: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

21 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

mwangu tabernakulotakatifu kwani ilikuwa namonstransi yenye hostia...yote ilikuwa imejaa Bwana.Nakumbuka nilifanya ah!ah! ah! Kama mang’amuzihaya yangelidumu kwamuda mrefu zaidi,ningelipitiliza na kuingiakatika uzima mwingine.Haiwezekani kupenda kwajinsi hii mpaka nafsiinaungana na mwili. Baadaya kurudi katika hali yakawaida nikiwa na rohonilijisikia kuruka kutokanana nguvu nilizokuwa nazo nanililazimika kutulia nakujishikilia na mikono yotemiwili na kushikilia pumzi yangu ilinisisikike. Nilikuwa pia makini kamamasista walitambua hilo... lakini kulikuwana ukimya kamili mahali hapo.” Baada yasala ya kuabudu, Sista Tarsilla aliwaendeawagonjwa wake kama Msamaria mwema.Masista wengi vijana walisimulia baadayekwamba walikuwa na furaha ya kukaakaribu naye kanisani wakati wa ibada yakuabudu Ekaristi... kwa baadhi yaoilionekana kuwa Sista Tarsilla alikuwa naburudiko la roho daima!Shirika ambalo Sista Tarsilla alikuwamwanachama wake lilianzisha na badolinaishi mwelekeo wake wa kiroho juu yaupendo na ibada kwa Moyo Mtakatifu waYesu na Moyo wa Maria.

Kanisa dogo lakitengo chaUangalizimaalum chahospitali ya Jeshila Wanamaji -Pola

Page 24: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

22MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

• Mhanga wa upendo •

SIkiwa tabernakulo ndiyo iliyomvuta SistaTarsilla kwenye sala, ikumbukwe

kwamba katika kanisa dogo la hospitalikulikuwa na sanamu nzuri ya MoyoMtakatifu wa Yesu . Mara moja kilitokeakile ambacho Sista Tarsilla aliandika katikashajara yake: “Jioni moja, nikiwa naitazamasanamu ya Moyo Mtakatifu, nilionakwamba macho ya Bwana yalikuwayamejaa machozi. Niliwaza: niko peke yangu

na lazima nihakikishe ... niliwasha zile taatatu zilizokuwa chini ya sanamu, halafunikachukua meza ndogo na kupanda juuyake. Hata hivyo bado haikutosha; nilitwaakiti na kukiweka juu ya meza hiyo ndogo nakupanda juu yake kiasi kwamba uso wanguukafikia usawa wa urefu wake. Sikuwezatena kufanya jambo lingine. Nilijikutanikiwa na uwepo hai wa Bwana mbele

Jumuiya yahospitali ya Jeshi

la wanamaji(Sista Tarsilla

yuko mstari wapili, nafasi ya 3kutoka kushoto)

Page 25: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

23 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

yangu na kwa harakanikajilaza chini mbeleyake; na usiku huosikuutazama tena uso waBwana. Nilianza kusalikama kawaida mbele yatabernakulo takatifu.”Sanamu hiyo ilionyeshakwa ufupi sehemumuhimu ya Karamaambayo Sista Tarsillaaliishi. Kuwa na ibada nakujiweka wakfu kwaMoyo Mtakatifu wa Yesuna Moyo wa Maria kunamaana ya kuweka maishajuu ya upendo wa Yesuulio na upole na hurumaambao kilele chake ni uwepo Wake katikasakramenti ya Ekaristi; kuna maana yakutazama fumbo la upendo na la matesolinalotimizwa juu ya msalaba wa Yesu; kunamaana ya kujitoa na kutoa maisha yetukaribu na Yesu kwa roho ya majitoleo namateso, roho ya kujitoa mhanga na kufanyamalipizi.

Sanamu ya MoyoMtakatifu katikaparokia ya Mt.Rafaelihuko Trullo -Roma, siyo mbalina NyumbaMama yaMasista

Parokia ya Mt.Rafaeli hukoTrullo -Roma, ambakoinapatikanaNyumbaMama

Page 26: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

24MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Kati ya mwaka1929 na 1930,Sista Tarsillaaliandikakatika shajara

yake kuhusu MsalabaMtakatifu na Majeraha yaBwana Wetu Msulibiwa:“Daima nilibusu Majeraha

Matakatifu ya Bwana.Wakati mwingine nilikuwanikichoka; kitendo hicho chakubusu kilinifanya nikosepumzi, na niliwaza kuwa

labda haikuwa lazimakufanya ibada hii. Usiku

mmoja wakati nikiendelea naibada hii, nikimwangalia Yesu

juu ya msalaba ndani yatabernakulo, kulitoka ndani yatabernakulo kitu kama fundo lamiali ambayo ilipenya ndani yakifua changu na kuugusa moyowangu, na mimi niliujua vizurimoyo wangu kama ulivyokuwa

na jinsi ulivyokuwa umeguswa sasa. Wakatihuo huo Bwana aliniambia: Kila wakatiunaponibusu, mimi ninakubusu ndani yamoyo wako.”Sista Tarsilla alifanya Njia ya Msalaba kilasiku na aliishi maisha yake kwa kujitoamhanga na kwa roho ya malipizi. Hii inamaana gani? Ina maana kwamba alijitoamwenyewe kama mhanga wa upendoakichukua kwa upole mateso na majitoleoya kila siku kama sadaka ya upendo karibu

Msalaba kutokanyumba ya

masista wa Pola,kwa sasa

umetunzwa katikasakristia ya

Nyumba Mama,Roma

Page 27: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

25 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

na Yesu ambaye alikataliwa na kutukanwa;aliishi kwa moyo wa malipizi akionyeshakatika uhalisia matendo ya upendo kwawagonjwa. Hivyo, alifanya malipizi kwamakosa ya watu ya kutokujali na kukosashukrani kwa upendo wa Kristo na uwepowake katika Ekaristi. Kadiri watu wengiwalivyokuwa baridi na wenye chuki kwaEkaristi Takatifu, ndivyo Sista Tarsillaalivyozidi kumwabudu Yesu ili kujazaombwe hili!

MtukukaMtumishi waMungu SistaTarsilla Ostikatika picharasmi

Page 28: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

26MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Kutokana na upendo wake kwa EkaristiTakatifu na ibada yake kwa Mateso na kwaMoyo Mtakatifu, alifanya pia malipizi yakuutesa mwili wake ili kusahihisha maovu

kwa njia ya wema na sadaka ya maishayake (moja ya malipizi haya ilikuwa nikuvaa vazi zito lenye vifundovilivyochongoka ambalo lilimfanyaateseke sana). Hivyo, alitolea matesohaya karibu na Yesu aliyeteseka hukoGetsemane na katika njia ya kuelekeaKalvario.Wakati wa Sista Tarsilla kulikuwa nakitabu cha sala kilichokuwa kimeeneasana. Kitabu hicho kilichoitwa “Roho

Zilizojitoa Muhanga” kilikuwa moja yavitabu vyake vya sala alivyovipenda na

kuvitumia sana kwa sababu roho iliyotokakatika maandishi hayo ilikuwa ya kujitoakwa Mungu kila siku, yaani kujitoa sadakakiroho karibu na mateso ya Kristo.

Nembo ya Jeshi laWanamaji ambayo

masistawaliibandika

katika mavazi

Picha ya kumbukumbu ya Nadhiri za Daima za Sista Tarsilla

Page 29: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

• Katika njia ya upendo •

Sista Tarsilla alikuwa ni mtu wa Mungu,aliyezamishwa katika fumbo lake la

upendo na moyo wake ulijaa wema wenyekuwaelekea wagonjwa nawenye kuteseka; uso wakeuliojaa unyenyekevu nawenye kung’aa ulikuwa nauwezo wa kuvuta kila mtu.Kama malaika alitembeakwenye barabara zahospitali ya Jeshi laWanamaji akihudumiakama msamaria mwemakila aina ya mhitaji wakiwemo walewaliokuwa vitandani wamelazwa. Hatahivyo, matatizo na majaribu ya shetanihayakukosekana. Yote hayo aliyakabili kwaroho ya imani na kujikabidhi kwa Mungu!Hata kama wakati mwingine moyo wakeulikuwa katika mfadhaiko,tabasamu halikukosekana kamwekatika midomo yake. Aliandikakatika shajara yake: “Mbele yaBwana aliyewekwa altareni,sikuacha kumwomba msamahakwa makosa yangu na makosa yawenzangu, sikuacha kuwatakiamema mengi wenzangu nakuwashukuru sana kwa mabayawaliyonitendea. NilimwombaBwana anifanye nitambue kwaharaka pale nilipokosa upendokwa mawazo... niliogopa sana

27 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Masista nawatoto, katikamatembezibaharini, Pola

Sista Tarsilla,wakati akikaaPola

Page 30: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

28MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

kufanya makosa, lakinisikumlalamikia mtu yeyote...sikumbuki kama niliwahikumshutumu mtu yeyote.Asubuhi moja moyo wanguulikuwa na mahangaiko;nilikuwa nimesimamanyuma ya altare na nilikuwanikipanga nguo za ibada,wakati huo nilikuwa nahasira dhidi ya ... Kwa hiyo,Bwana akanikaripia kwasauti kubwa kutoka kwenyetabernakulo akinitaka niachehasira. Na pamoja na hayoyote kwa wakati huonakumbuka sikuwezakujirekebisha na kuachanana hasira yangu. Bwanaalisema nini juu ya hilo?Sasa, ndani ya huyu... sioniubaya wowote.”Wakati fulani palitokea Sistammoja kijana aliyekuwa natabia ngumu sana kiasikwamba hata Sista Tarsillaaliyekuwa mpole namnyenyekevu alipata ugumukumvumilia. Lakini SistaTarsilla aliona kwamba kamavile Bwana asivyomtenga

mtu yeyote na karamu yake, hivyo hivyo nayeye alipaswa kuacha kupalilia uadui dhidiya Sista yule; na aliandika katika shajarayake: “Baada ya Misa takatifu nilirudikanisani, nikamwomba Bwana msamaha na

Mioyo Mitakatifuya Yesu na Mariachanzo cha uhai

wa Shirika

Page 31: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

29 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

kumwomba anisaidie ili niondokane namawazo ya chuki. Kisha niliondoka nauchungu mkubwa kwani nikiwa katikati yamabenchi Bwana aliniambia: Nitakupaishara juu yake. Kisha nikiwa ninairudiaaltare, nilimwambia: Oh! Hapana Bwana.Sihitaji mambo haya. Neema yakoyanitosha. Jioni ya sikuhiyohiyo tulikuwa kanisanitukifanya mazoezi ya nyimbo;Mama Mkuu alikuwa akipigakinanda na Sista huyu alikuwakwenye benchi huko nyuma.Mama alimwita ili aje kuimba.Nilimwonea huruma kwasababu nilijua alikuwa akiumwatumbo, lakini sikukumbuka yaleyaliyokuwa yametokea asubuhi.Yule Sista alisimama ukutani na karibu nasanamu ya Moyo Mtakatifu. Wakatitukiiimba niliona miali ya dhahabuikishuka kutoka kwenye sanamu na kutuajuu ya kichwa cha Sista huyu. Kwa tukio hiliBwana alitaka kutuonyesha yule ambayetulikuwa tukimchukia.”Wongofu unaendelea, katika njia ya upendo!Ndiyo, kila siku Sista Tarsilla aliishi maishahaya kama fursa ya kumpenda nakumtumikia Bwana wetu aliyeonekanakatika sura ya jirani na wagonjwa. Kulikuwapia na matukio ya kustaajabisha nayasiyoelezeka. Baada ya Sista Tarsilla kutoahuduma za kitabibu na kusali baadhi yawagonjwa walikuwa wakipona kwa muujiza!“Mgonjwa katika kitengo cha upasuajialiniomba nimwombee ili apone. Nilisali

MjeledialioutumiaMtukukakujipiga, kamanjia ya kufanyatoba

Page 32: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

akapata nafuu. Sijui shida aliyokuwa nayona alinisihi kwa mara ya pili nisali tena kwaajili yake. Kwa hiyo niliomba ili Bwana ampeneema, ili imani yake iweze kuongezeka naupendo wake wote umwelekee Bwana, nafamilia yake yote iweze kuwa familia yaKikristo kweli. Nilijua kwamba Bwanaalikuwa amesikia sala yangu na kunitimizia,na bila kufikiria chochote nilikwenda kwamgonjwa na mbele ya watu wenginenilimwambia kuwa kila kitu kilikuwa tayarikimefanyika ... kwamba nilikuwa nimesali ...Jumatatu usiku bila kukumbuka chochotekuhusu tukio, nilimwuliza juu ya hali yake.Na yeye akiwa amenitazama kwa mshangaoalinijibu: Uliniambia nini jana jioni? ...Nimepona kabisa. Kisha nikakumbuka ... na

jinsi nilivyofanya ... NadhaniBwana aliruhusu hili kufanyikaili kumwimarisha mtu huyukatika imani kama nilivyokuwanimeomba. Halafu niligunduakuwa mtu huyu alikwishawaambia watu juu ya tukio hilina labda hata daktariwalikwisha pata habari zake...”Watu wote ambao walimwomba

Sista Tarsilla awaombee waliombewa. SistaTarsilla aliwachukua kiroho watu hao nakuwaleta mbele ya tabernakulo nakuwakabidhi kwa Yesu mwenye huruma. Mwelekeo mmojawapo wa ibada yake yaKikristo ulikuwa ni kuwaombea marehemuna wale wanaokaribia kifo; alitolea sala nasadaka kwa ajili yao ili wawe tayarikukutana na Bwana baada ya kuwa

30MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Kitabu chaKatiba

kilichotumiwa naMtukuka Sista

Tarsilla

Page 33: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Vazi zitoalilolitumia SistaTarsilla, kama njiaya kufanya toba

31 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

wamepokea sakramenti za mwisho.Sista Tarsilla, ambaye alijaliwavipaji vya pekee, mara nyingialikuwa na uwezo wa kuonamambo yatakayo tokea baadayekwani aliweza kujua watuambao wangekufa pale mudamfupi baadaye. Mwaka 1940kaka yake Ettore alisimulia tukiohili ambalo linasimuliwa kwamaneno yake mwenyewe: “Ilikuwaalasiri siku ya Jumapili: masistawalikuwa wamemaliza kula na walikuwawakifanya matembezi ya kawaida katikabustani, ambapo ghafla dada yangualisema, ‘Masista, leo hatuwezikwenda kutembea, ila tutakwendakanisani kusali kwa ajili ya MamaMkuu wetu ambaye amefariki hukoRoma. - Unasemaje? Waliuliza kwamshangao masista; hili linawezekanaje kuwani kweli ikiwa leo asubuhi tumepokeatelegramu yake akitujulisha kwamba alifikasalama na alikuwa mwenye afyanjema na kututakia heri? Lakinidada yangu alijibu kuwa kwabahati mbaya Mama Mkuualikuwa amefariki ghafla mudahuohuo. Ingawa masistahawakuamini maneno yake lakiniwalikwenda kanisani kusali nakuachana na matembezi, nabaada ya masaa machachetelegramu nyingine ya Mama Mkuu ilifikakutoka Roma ikithibitisha kutokea kwa kifocha Mama Mkuu wao.”

Monstransiiliyotumiwa naMtukuka SistaTarsilla hukoPiedimonted’Alife

Page 34: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

• Karibu na familia yake ya asili •

Sista Tarsilla Ostialilipenda sana Shirika

lake, aliwapendawagonjwa wake, alikuwana uhusiano wa pekee waupendo kwa familia yake.Aliteseka sana alipoonawanafamilia yakewakishiriki kidogo sanamaisha ya sala nashughuli za Kanisa. Kwasababu hii aliweka nia yakujitoa sadaka kwa Bwanakwa ajili ya wokovu wawanafamilia yake. Kwanyakati tofauti aliwezakufurahi sana baada yakujua kuwa baba yake namama yake walikuwawameanza kushiriki

katika Misa Takatifu na kupokea KomunyoTakatifu. Shajara inatuonyesha salamaalum ya Sista Tarsilla kwa mama yake

Mwonekano waPola

Pola, kaburi lamama wa Sista

Tarsilla

Page 35: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

wakati wa Juma Takatifu lamwaka 1929: “NilimwombaBwana kwa ajili ya mamayangu na hasa baada ya kifochake... Niliwakumbukamjomba wangu, bibi yangu,nk. Nilielewa kuwa Bwanaalikuwa amewachukua wotena kuwaweka chini ya ulinziwake, na hakika ni jambojema, kwamba kutokana nahali hiyo ilibidi nitulie nakusherehekea vizuri sikukuuya Pasaka.” Mama yake alifariki tarehe 20Aprili 1929 akisaidiwa kwa karibu na SistaTarsilla, binti yake. Baba yake akiwa mganealiweza kushiriki kwa furaha sherehe yabinti yake kuweka nadhiri za daima tarehe14 Agosti 1932, na akapokeaKomunyo Takatifu baada yamiaka 40! Labda hiyoilikuwa ndiyo zawadi borazaidi kwa Sista Tarsilla! Sikuzote alibaki kuwa nauhusiano imara na nduguzake waliobaki.Wakati wa Vita Kuu ya Piliya Dunia, familia ya Ostiilikuwa imetawanyika nakuishi katika maeneombalimbali: Sista Tarsilladaima alikaa Pola wakatibaba yake alikuwa amelazwa katika taasisimoja ya afya huko Genova na kaka yakeEttore alikuwa jeshini. Baadaye baba yakealifariki tarehe 18 Februari 1944.

33 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Gino - kaka yaSista Tarsilla

Ettore - kaka yaSista Tarsilla

Page 36: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

• Maisha ya kiekaristikwelikweli, wakati wa vita •

Sista Tarsilla aliipenda mno EkaristiTakatifu. Kama ilivyoelezwa mara kwa

mara, mambo makuuyaliyomvutia yalikuwa niTabernakulo na wagonjwa. Maranyingi alitumia nyakati za usikuakitembelea kwa zamu kanisa lahospitalini na wagonjwa.Siku moja aliandika katikashajara yake: “Bwana, najuakwamba kesho Sista Eleonoraatakesha na wagonjwa, lakiniikiwa hawezi kufanya hivyo namimi siwezi kulala walakusimama, ningependa kwa ajiliya upendo wako nitambaesakafuni, lakini yote kwa ajiliyako, na hakika kwa ajili yakotu... tazama Bwana, hakuna mtu

yeyote anayejua chochote kuhusu uchovuwangu. Baada ya kufika kanisani nilipiga

Mwonekano wakanisa na altarekatika kambi ya

Jeshi laWanamaji huko

Pola

Kitambaa kilichofumwa kwa mkono na Sista Tarsilla

Page 37: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

35 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

magoti mbele ya altare kama kawaida nakubusu sanamu ya Moyo Mtakatifu... nikiwanimeyafumba nusu-nusu macho yangu kwasababu ya usingizi. Mara alionekanamalaika akiwa amesimama juu ya ngazi yakwanza, nami wakati huo nilikuwanimepiga magoti; malaika alikuwa na kimokinachofikia kimo changu au kunizidikidogo. Alikuwa na bakora mkononi mwakena kwa kutumia bakora hiyo aliipitishakiunoni na mikononi mwangu, akanigusakichwa changu na kadiri alivyokuwaakinigusa uchovu wote na usingizivilikwisha. Kwa hivyo niliweza kuendeleabila mateso hadi saa 3 asubuhi wakati

Sanamu ya MoyoMtakatifu, katikaKanisa laNyumba Mamaya Masistakatika mtaa waTrullo, Roma

Page 38: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

36MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

nilipokwenda kupumzika kwa utulivu nafuraha katika Bwana.”Mwezi juni ulipoadhimishwa kwa heshimaya pekee na utukufu Moyo Mtakatifu wa

Yesu, Sista Tarsillaalijishughulishakupamba kwa mauamengi altare na sanamuya Moyo Mtakatifu waYesu; lakini haya yoteyalikuwa ishara ya nje yaimani na upendo mkubwakwa Yesu; upendo ambaouliujaa moyo

mnyenyekevu wa Sista Tarsila. Katikati ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, SistaTarsilla alielekea kutimiza miaka ishirini yakutoa huduma katika hospitali ya Pola;sehemu za Istria na Pola zilipitia kipindichenye huzuni kubwa sana kilichojaamateso makubwa kutokana na sehmu hizikupigwa mabomu. Hata hivyo, sehemukubwa ya hospitali ya Pola ilisalimika nakazi ya madaktari na masista iliendelea.Katika wakati huo mgumu, Waitaliawaliokuwa wakikaa Istria iliwapasakuondoka huko kutokana na ujio waWakomunisti wa Jemedari Tito waYugoslavia. Hata masista wa hospitaliniwalipaswa kujiandaa kuondoka mahali hapona kuacha kazi ya kuwahudumia wagonjwa.Hali ilikuwa hiyo hiyo katika nyumbanyingine za shirika katika nchi hiyo; kwahiyo wakati ulikuwa umefika kwa SistaTarsilla kuondoka moja kwa moja Pola nakwenda Italia.

Mwonekano waPola

Page 39: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

• Sista Tarsilla aenda Italia •

Sista Tarsilla alikuwa kati yawatu wa kwanza kuondoka

Istria kwenda Roma ambapoalifika tarehe 22 Agosti 1945katika nyumba mama ambayowakati huo ilikuwa katika mtaa waPettinari, na. 64. Alikaa Roma kwawiki chache tu kwa sababu alikuwaamepangwa kwenda katikanyumba ya shirika ya Lancianohuko Abruzzo ambapo masistawalikuwa na nyumba ya kuleleawanovisi, shule ya chekechea,kituo cha kulelea watoto yatima,karakana ya kina mama, piawalitoa msaada wa kichungaji katikaparokia, gereza la wanawake na seminari.Sista Tarsilla, akiwa muuguzi mwenye ujuzina uzoefu alipewa jukumu la kuwahudumiawagonjwa kwenye nyumba zao na kufanya

kazi na Mabibi wa Upendo (Ladies ofCharity) na kushika ofisi nyingi

ambazo zilikuwa za lazima kwa ajiliNyumba yaShirika hukoLanciano

Kanisa laShirika katikaNyumba Mama,mtaa waPettinari hukoRoma

Page 40: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

38MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

ya usimamizi wa nyumba ile kubwa. Kwa miaka miwili hivi alitoa huduma hizihuko Lanciano na mara moja akajulikana nawenyeji kwa tabia yake ya kuhudumia kwaharaka na kwa upendo wagonjwa kwenyenyumba zao. Katika uzoefu huo, piakutokana na ushauri wa Mwungamishi wakena ushauri wa Sista Raffaella Casna, MamaMkuu wake, Sista Tarsilla alianza kuandika“Shajara yake ya Kiroho”.

Lanciano - ndaniya Kanisa,

katika picha zawakati ule

Kanisa Kuu laLanciano

Page 41: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Mnamo Januari 1948, Sista TarsillaOsti alichaguliwa kuwa mamamkubwa wa jumuiya ya masistaambao walikuwa wakitoa hudumakatika hospitali ya serikali yaPiedimonte d’Alife katika provinsiya Caserta.Masista walikuwa karibu na hospitalina pia walikuwa karibu na shule yakilimo, hivyo walikuwa pia na hostelikwa ajili ya wanafunzi. Ilikuwa nimara ya kwanza kwa Sista Tarsillakuwa mama mkubwa...

39 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Ndani ya kanisa la Moyo Mtakatifu hukoLanciano kwa sasa

Lanciano -Muujiza waEkaristi

Mwonekano wanje wa nyumbaya Shirika hukoLanciano

Page 42: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Hospitali yaPiedimonte

d’Alife (Caserta)

Jumuiya yaPiedimonte

d’Alife (sistaTarsilla ni huyo

aliyekaa)

• Sista Tarsilla MamaMkubwa na maradhi •

Huko Piedimonte d’AlifeSista Tarsilla alikaa kwa

muda wa miaka kumi hiviakiwaonyesha pia masista uleupendo na wema wa moyo;mambo ambayo yalikuwayametambulisha maisha yakewakati huo. Miaka hiyo haikuwaya utulivu sana kwake kwasababu aliteseka kutokana namajaribu mengi ya nafsinimwake na mahangaikoyaliyosababishwa na shetanialiyemtesa.

Yote haya aliyavumilia kwa ujasiri mkubwana kwa roho yake ya kawaida ya sala na

Page 43: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

sadaka. Hata hapo Piedimonte, watuwaliomfahamu walimwona kuwa nimtakatifu wa kweli na halisi! Pamoja namateso ya ndani, alianza pia kuwa namatatizo ya afya; la kwanza likiwa ni tatizola tumbo ambalo lilipelekea kufanyiwaupasuaji. Halafu alipatwa na maumivumakali yatokanayo na ugonjwa wa baridiyabisi na ugonjwawa mshipa wanyonga. AlimtoleaMungu mateso hayokwa ajili yawanafamilia yakewaliobaki iliwaweze kurudiKanisani. Miaka kumi ilikuwaimepita tangualipofikaPiedimonte d’Alife.Mnamo tarehe 17

41 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Sista Tarsilla (wa3 kutokakushoto) katikaMisa ya ufunguziwa NyumbaMama ya sasahuko Roma

Mwonekano waPiedimonted’Alife (Provinsiya Caserta)

Page 44: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Kanisa laNyumba Mamakatika mtaa wa

Trullo, Roma

Picha yaukumbusho wa

kutimiza miaka25 Nadhiri za

Kitawa

Agosti 1958, wakati wa Misa Takatifualitolea nafsini mwake mateso yake kwamanufaa ya kiroho ya ndugu zake. Sikumoja alipokuwa akirudi nyumbani kutokahospitalini, kwenye hatua za ngazi

Page 45: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

43 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

alisimama na hakuweza tena kupiga hatua,na hivyo ilibidi apelekwe nyumbani akiwaameshikiliwa. Alikwenda moja kwa moja kulala nahakuweza kuamka tena isipokuwa kwamsaada wa kiti cha mikono kilichowekwapembeni mwa kitanda. Watu wengi walikujakumwona hasa wafanyakazi wa hospitali.Ndugu zake, baada ya kujua jambo hilo,walitaka kumhamishia Napoli kwa matibabuzaidi; hivyo tarehe 28 Septemba 1958aliondoka kuelekea Napoli na kupelekwakwenye kliniki iliyoitwa “Villa dei Gerani,”lakini matibabu aliyoyapata yalimsaidiakidogo sana! Ugonjwa wa baridi yabisiulienea kwa haraka mwilini hivyo tarehe 1Novemba wakuu wake wa shirika waliamuakumpeleka Roma kwenye nyumba mama yashirika iliyopo Mtaa wa Trullo. Maumivuyalizidi kuwa makali sana kiasi kwambahata kukaa kitandani kwake ikawa nimateso!

Sehemu ya ndaniya Kanisa,Nyumba Mama,Roma

Page 46: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

44MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Huduma kutoka kwa dada zake zilikuwanzuri sana na mahali alipokaa palikuwapazuri, lakini maumivu yake yalikuwa yakutisha. Mara nyingi alisema: “Miminimeungana na Yesu.” Kila siku alipokeaKomunyo chumbani kwake na hii peke yakeilikuwa ndiyo nguvu yake ya ndani yakumsaidia kukabiliana na maumivu yamuda mrefu ya kila siku. Wakati huo huosikuu ya Krismasi ilifika na afya ya SistaTarsilla ilizidi kudorora zaidi. Dada zakewalipomtazama walimwona akiwa na usowenye tabasamu tulivu zaidi kulikokawaida. Hali hii ilionesha kwamba safariyake ya kuingia katika ufalme wa mbinguniilikuwa karibu! Siku ya Mtakatifu Stefanoalipokea Komunyo-pamba na kila kitu sasakilikuwa kinakaribia mwisho wake. Ndugu

Barua ya mwishoiliyoandikwa na

Mtukuka SistaTarsilla

Page 47: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

45 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

zake walikuja pia kutoka Napoli.Sista Tarsilla alikuwa ameketi katika kitichake cha mikono na kama taa alizimikapolepole. Hiyo ilikuwa tarehe 26 Desemba1958 saa 2:50 usiku baada ya kutembelewana padre Celso Serri, paroko wa Trullo.

Makaburi yaVerano (Roma)mahalialipozikwa SistaTarsilla, kablaya kuhamishwa

Page 48: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

46MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Sista Tarsillakatika picha ya

kumbukumbu

• Safari kuelekea kwenyeutakatifu •

Mtu aliyemjua Sista Tarsilla hawezikuwa na shaka kuutambua utakatifu

ndani ya maisha yake. Miaka mitatu baadaya kifo chake kiliandikwa kitabu chakwanza kinachoelezea maisha yakekilichoitwa “Upendo na Usafi,” kwa sababu

Page 49: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

47 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Masalia ya Mtukuka yanahamishiwa kwenyeKanisa la Nyumba Mama, Roma

Page 50: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

48MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Hati ya Utukuka,15 machi 2008

watu wengi walitaka kujua zaidi juu yamaisha yake ya unyenyekevu lakini piayaliyojaa ushujaa. Sifa ya utakatifu wakeilienea kila mahali hata nje ya mipaka yasehemu alizowahi kuishi na kufanya kazi.

Miaka michache baada ya kifo chake, hasamwaka 1977 kulitokea tukio kubwa sana nalisiloelezeka ambalo lilikuwa ni matokeo yamaombezi yake. Paulo Nepa, mvulana wamiaka 11 tarehe 2 Aprili alilazwa katikahospitali ya watoto huko Chieti. Matokeo yauchunguzi yalikuwa ya kutisha: mtotoalikuwa na homa kali ya uti wa mgongo nakulikuwa na matumaini kidogo ya kupona.

Page 51: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

49 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Mvulana huyo alishuhudia hivi: “Licha yajitihada zote za madaktari, hali yanguiliendelea kuwa mbaya. Usiku wa siku yakwanza, mama mkuu wa MasistaWamisionari wa Moyo Mtakatifu, alileta

Misa Takatifu yashukrani kwa ajiliya Hati yaUtukuka wa sistaTarsilla, NyumbaMama, Roma

Page 52: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

50MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

kwenye kitanda changu picha ya SistaTarsilla na mara moja ndugu zanguwakaanza kusali wakielekeza maombi yaokwake. Mimi pia nilipozinduka nilipatanguvu ya kumwomba Bwana na SistaTarsilla. Ninashukuru kutokana na msaadawa Bwana, Sista Tarsilla na kazi ya

maprofesa na wasaidizi wao, nimeponakabisa.” Na madaktari walitambua kutokeakwa jambo lisilo la kawaida katika uponajiwa haraka wa mvulana huyo. Daktari mkuu,Profesa Mario Midulla, aliacha ripotikuhusu tukio hili. Ripoti hiyo iliandikwatarehe 17 Mei 1977.Mnamo tarehe 23 Februari 1987ulianzishwa mchakato wa kijimbo wenyelengo la kumtangaza Sista Tarsilla kuwaMwenyeheri. Papa Benedikti XVIaliutambua ushujaa katika fadhila waMtumishi wa Mungu, na akamtangaza kuwa

Misa Takatifu yashukrani kwa

ajili ya Hati yaUtukuka wa sistaTarsilla, Nyumba

Mama, Roma

Page 53: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

51 MTUKUKA SISTA TARSILLA OSTI

Kaburi la sasakatika NyumbaMama yamasista katikamtaa wa Trullo,Roma

Mtukuka tarehe 15 Machi 2008.Kwa sasa masalia ya mwili wa Sista Tarsillayamehifadhiwa katika kanisa la MoyoMtakatifu katika Nyumba Mama iliyokoMtaa wa Trullo, na. 372 huko Roma.Sifa ya utakatifu wa Sista Tarsilla Ostiilienea kwa haraka katika mabara manne,hasa katika nchi ambazo Wamisionari waMoyo Mtakatifu wanakaa na kufanya kazi,yaani Italia, Brazili, Korea, Tanzania,Guatemala na Vietnam. Waamini wengiwakiwemo walei, mapadre na Waseminariwamekuwa wakiomba sala, maandishi juuya maisha yake, picha na masalia yake.

Page 54: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

YalioyomoUtangulizi 3

Utoto na ujana 5

Wito 10

Kati ya masista wa Moyo Mtakatifu 14

Akiwa hospitalini 16

Sala na upendo 20

Mhanga wa upendo 22

Katika njia ya upendo 27

Karibu na familia yake ya asili 32

Maisha ya kiekaristi kwelikweli,

wakati wa vita 34

Sista Tarsilla aenda Italia 37

Sista Tarsilla Mama Mkubwa na maradhi 40

Safari kuelekea kwenye utakatifu 46

Page 55: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa

Padre Massimiliano Taroni ni wa Shirika la Ndugu

Wadogo Wafransiskani. Alipewa Daraja ya Upadre

mwaka 1992 na kuanza kuwa Mwandishi mwaka

1993. Kwa miaka kumi na miwili amekuwa Paroko

Msaidizi katika parokia iliyo nje ya jiji la Milano

na Mkurugenzi wa Malezi ya Vijana.

Kwa miaka kumi na miwili amekuwa akifanya kazi

kama mhamasishaji wa kimisionari na kiongozi wa

misioni za kifransiskani katika nchi mbalimbali

ulimwenguni kote. Kwa miaka mitano amesimamia

gazeti la kimisionari na kuweza kuchapisha mamia

ya kazi: majarida 65 yanayohusu maisha ya

watakatifu na mashahidi wa imani, na vitabu

kadhaa vinavyohusu ibada ya Moyo Mtakatifu na

vitu vingine vya msaada kwa ajili ya Katekesi ya

kuingizwa katika Ukristo.

Watu wengi wamepokea neema kwa njia ya maombeziya Mtukuka Sista Tarsilla Osti.

Tuendelee kumwomba ili atupatie mema ya kiroho naya kimwili kutoka kwa Bwana.

SALA

Ee Mungu, ambaye ndani ya Moyo waMtumishi wako Mwenye Heri Tarsilla Osti,uliwasha moto wa upendo mkuu ambaoaliuonyesha kwa wagonjwa, maskini nawaliodharauliwa na hivyo kuiga mfano waMwanao Msulibiwa, tunakuomba upendekudhirisha utukufu wake pia hapa dunianina kwa maombezi yake utujalie neematunazoomba...

Baba Yetu, Salamu Maria, Atukuzwe.

Mwenye Heri Sista Tarsilla Osti, utuombee!

Kwa idhini ya Mamlaka ya Kanisa

Kwa taarifa, maombi ya machapisho ya wasifu na picha, kwataarifa za neema zilizopokelewa, wasiliana na:

Casa GeneraliziaVia del Trullo 372

00148 – RomaTel. +39 06.6530612

Email: [email protected]@istitutosacricuori.it

Sito: www.istitutosacricuori.it

Page 56: Impaginato tarsilla swahili:Layout 1 · haikuwa na mazoea ya kusali, sikuwa hata na ujasiri wa kuzungumzia hilo.” Wanafamilia ya Osti walikuwa waamini wakatoliki, lakini hawakuwa