22
i KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO TANZANIA PERSONAL SECRETARIES ASSOCIATION (TAPSEA) Februari, 2016

KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

  • Upload
    others

  • View
    28

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

i

KATIBA YA

CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA

ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO

TANZANIA PERSONAL SECRETARIES ASSOCIATION

(TAPSEA)

Februari, 2016

Page 2: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

ii

YALIYOMO UKURASA

UTANGULIZI.................................................................................................... iii

SEHEMU YA KWANZA ..................................................................................... 1

1.0 FASIRI/UFAFANUZI .................................................................................... 1

SEHEMU YA PILI ............................................................................................ 3

2.0 JINA LA CHAMA ......................................................................................... 3

3.0 ANUANI YA CHAMA ................................................................................... 3

4.0 MOTTO WA CHAMA ................................................................................... 3

5.0 NEMBO YA CHAMA .................................................................................... 3

6.0 MADHUMUNI YA CHAMA ......................................................................... 4

SEHEMU YA TATU .......................................................................................... 6

7.0 UANACHAMA .......................................................................................... 6

7.1 AINA YA UANACHAMA .......................................................................... 6

7.2 SIFA ZA KUWA MWANACHAMA ............................................................ 6

7.3 WANACHAMA WA HESHIMA ................................................................. 7

8.0 HAKI NA WAJIBU WA WANACHAMA .................................................... 7

(a) HAKI ZA MWANACHAMA KAMILI ........................................................ 7

(b) WAJIBU WA MWANACHAMA ............................................................... 7

9.0 UKOMO WA UANACHAMA....................................................................... 8

SEHEMU YA NNE ............................................................................................ 9

10. UONGOZI ................................................................................................... 9

(i) SIFA ZA KUWA KIONGOZI ................................................................... 9

(ii) MIIKO YA UONGOZI ............................................................................. 9

11. KAZI NA MADARAKA YA VIONGOZI WA CHAMA ............................... 10

(a) MWENYEKITI ...................................................................................... 10

(b) MAKAMU WA MWENYEKITI .............................................................. 10

(c) KATIBU MKUU .................................................................................... 10

(d) NAIBU KATIBU MKUU ........................................................................ 11

(e) MWEKA HAZINA ................................................................................. 11

Page 3: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

iii

12. KAMATI TENDAJI .................................................................................... 12

(a) MUUNDO WA KAMATI TENDAJI........................................................ 12

(b) KAZI ZA KAMATI TENDAJI ................................................................. 12

(c) BARAZA KUU ...................................................................................... 12

(d) KAZI ZA BARAZA KUU ....................................................................... 12

13. BODI YA WADHAMINI ............................................................................. 13

UKOMO WA KUWA MDHAMINI WA CHAMA ........................................... 13

14. MUDA WA VIONGOZI KUKAA MADARAKANI ......................................... 14

15. MUDA WA KUKAIMU UONGOZI NDANI YA CHAMA .............................. 14

SEHEMU YA TANO ....................................................................................... 15

16. MKUTANO MKUU ..................................................................................... 15

17. WAWAKILISHI KATIKA MIKOA ................................................................ 16

18. WAJIBU WA WAWAKILISHI WA CHAMA ................................................. 16

SEHEMU YA SITA ......................................................................................... 17

19. UCHAGUZI MKUU .................................................................................... 17

20. UTARATIBU WA UTATUZI WA MIGOGORO NDANI YA CHAMA ........... 17

21. MABADILIKO YA KATIBA: ....................................................................... 18

22. KUVUNJIKA KWA CHAMA: ...................................................................... 18

Page 4: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

iv

UTANGULIZI

I. KWA KUWA lengo letu ni kukuza na kudumisha taaluma, uwajibikaji na hadhi ya

taaluma ya UHAZILI kwa kuhamasisha na kuwasaidia wanachama kuendeleza

fani yao ndani na nje ya mipaka ya taaluma ya UHAZILI; na

II. KWA KUWA lengo letu ni kuwakilisha Makatibu Mahsusi, kimataifa kwa

kudumisha na kuimarisha mawasiliano na mahusiano mazuri miongoni mwa

wanataaluma wa fani ya Ukatibu Mahsusi; na

III. KWA KUWA Katibu Mahsusi kama raia mwingine yeyote nchini ana haki ya

kupata huduma bora za kijamii, kiuchumi na kimaslahi kama vile afya, chakula,

usafiri na huduma nyingine za kijamii;

IV. KWA HIYO BASI, Sisi Makatibu Mahsusi wote kwa pamoja tunaazimia

kuungana na kuunda Chama chetu kitakachohakikisha kuwa tunatekeleza wajibu

wetu kwa kutoa huduma bora za uhazili kwa waajiri wetu, kukuza taaluma ya

Makatibu Mahsusi Nchini, kuboresha na kuendeleza maslahi ya Makatibu

Mahsusi Wanachama bila kujali tofauti za sekta au maeneo Mwanachama

anakotoka.

Page 5: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

1

SEHEMU YA KWANZA

1.0 FASIRI/UFAFANUZI

Kila neno ambalo limetamkwa katika Katiba hii litakuwa na maana kama fasiri ya

Katiba hii inavyoelekeza na si vinginevyo:-

(i) “Baraza Kuu”, ni chombo kitakachoundwa na Kamati Tendaji na Wanachama tisa (9) watakaoteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama watakaosaidia Uongozi wa Chama kutekeleza majukumu yake na ndicho chombo kitakuwa muhimili mkuu wa shughuli za Chama, kwa masuala yote yatakayohitaji Kamati mbalimbali za Chama;

(ii) “Bodi ya Wadhamini”, ni chombo ndani ya Chama kinachosimamia mali za

Chama, zile zinazohamishika na zisizohamishika kwa niaba ya Wanachama; (iii) “Chama”, maana yake ni Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (Tanzania

Personal Secretaries Association – (TAPSEA); (iv) “Katiba” – Mwongozo wa msingi wenye kuainisha haki, wajibu na uwajibikaji

wa Wanachama unaosaidia Chama kuendesha shughuli zake; (v) “Katibu Mahsusi” ni mtu yeyote aliyepata mafunzo ya Ukatibu Mahsusi

(UHAZILI) katika Taasisi yeyote inayotambuliwa na Serikali;

(vi) “Mwenyekiti”, maana yake ni Mwanachama hai wa TAPSEA aliyechaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Chama kuwa Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Katiba hii;

(vii) “Makamu Mwenyekiti” ni Mwanachama hai wa Chama aliyechaguliwa

kwenye Uchaguzi Mkuu wa Chama kushika wadhifa wa Makamu Mwenyekiti;

(viii) “Katibu Mkuu” ni Mwanachama hai wa Chama aliyechaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Chama kushika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama kwa mujibu wa Katiba hii;

(ix) “Naibu Katibu Mkuu” ni mwanachama wa Chama hai aliyechaguliwa

kwenye uchaguzi mkuu wa Chama kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama kwa mujibu wa Katiba hii;

Page 6: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

2

(x) “Kamati Tendaji” ni Chombo kitakachoshughulika na kazi za kila siku za Chama na ndicho Chombo kitakachowajibika moja kwa moja katika Mkutano Mkuu juu ya masuala yote yanayokihusu Chama na itaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mweka Hazina wa Chama;

(xi) “Kanuni” – Taratibu zinazoitafasiri Katiba na kutoa mwongozo wa

kutekeleza Katiba ya chama; (xii) “Kamati ya Uchaguzi” maana yake ni Kamati mahsusi iliyoteuliwa na

Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu;

(xiii) “Mfanyakazi” – Mtu aliyeingia katika makubaliano au mkataba wa maandishi na mwajiri yeyote yule kwa kutenda kazi kwa kupewa fidia/malipo ya ajira au mshahara kwa kila juma, majuma au mwezi na mwajiri wake;

(ix) “Mgombea” maana yake ni Mwanachama yeyote hai wa TAPSEA

anayegombea wadhifa wowote katika Chama kwa mujibu wa Katiba hii; (x) “Mkutano Mkuu” maana yake ni Mkutano wa Wanachama kulingana na

akidi iliyokubaliwa katika Katiba hii; (xi) “Mwanachama” kwa tafasiri ya Katiba hii kutakuwa na aina tatu ya

wanachama wa chama hiki kama ilivyoelekezwa katika Ibara ndani ya Katiba hii;

(xii) “Tawi” – ngazi ya Mkoa/Wilaya katika Muundo wa Chama na (xiii) “Uchaguzi”, maana yake ni Uchaguzi Mkuu au Uchaguzi wa dharura wa

Chama utakaoitishwa na Baraza la Chama ili kuchagua nafasi yoyote ile ya Uongozi ndani ya Chama iliyoachwa wazi au kuchagua Uongozi mpya baada ya Uongozi uliokuwepo hapo awali kumaliza muda wake.

Page 7: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

3

SEHEMU YA PILI

2.0 JINA LA CHAMA

Jina la Chama hiki litakuwa:

CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA kwa lugha ya Kiswahili na

kwa lugha ya Kiingereza TANZANIA PERSONAL SECRETARIES

ASSOCIATION na kwa kifupi (TAPSEA).

3.0 Anuani ya Chama

Anuani na mahali Ofisi za Chama zilipo: Makao Makuu ya Chama yatakuwa

katika Nyumba ya Maarifa, Ghorofa ya kwanza, Barabara ya Ohio Dar es

Salaam.

Anuani ya Chama ni:-

Katibu Mkuu,

Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania,

S.L.P 11461

Dar es Salaam.

E-mail: [email protected], Website: www.tapsea.or.tz

4.0 MOTTO WA CHAMA

“Kukuza na Kudumisha Taaluma ya Uhazili”.

5.0 NEMBO YA CHAMA

Page 8: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

4

6.0 MADHUMUNI YA CHAMA

(i) Kuendeleza na kulinda hadhi ya kazi ya Ukatibu Mahsusi pamoja na kusimamia viwango vya juu vya maadili, ufahamu, maarifa na ujuzi.

(ii) Kusimamia, kuendeleza na kulinda maslahi ya Makatibu Mahsusi katika

Taasisi mbalimbali na kuhakikisha kuwa kuna vivutio vya kutosha na mazingira mazuri ya kuwafanya waipende na kuizingatia kazi yao ipasavyo.

(iii) Kuhakikisha kuwa Waajiri wanaohusika wanatambua umuhimu wa Chama

cha Makatibu Mahsusi nchini na kuwaelimisha kuwa Makatibu Mahsusi wana uhuru wa kujiunga na chama hicho.

(iv) Kuhakikisha kuwa waajiri na Makatibu Mahsusi wanazingatia na

kutekeleza vyema sheria na kanuni za nchi zinazohusu kazi, pamoja na mikataba iliyopo kati ya waajiri hao na Makatibu Mahsusi au chama cha Makatibu Mahsusi ili mradi Sheria hizo zinazingatia HAKI.

(v) Kuwaelimisha wanachama juu ya masuala yote yanayohusiana na ajira

zao ikiwa ni pamoja na kuwapa ushauri wa kisheria unapohitajika. (vi) Kuwakutanisha Makatibu Mahsusi kwa lengo la kubadilishana mawazo,

maarifa na uzoefu kati ya wanachama, vyama shirikishi, na watu mbalimbali juu ya nafasi ya wanataaluma ya Ukatibu Mahsusi na maslahi ya wanachama kupitia; a) uchapishaji na usambazaji wa majarida na magazeti; b) usimamizi na uendeshaji wa makongamano, semina midahalo na

majadiliano kuhusu masuala ya taaluma ya Uhazili, na c) Tovuti ya Chama.

(vii) Kukuza na kudumisha taaluma na hadhi ya taaluma ya Ukatibu Muhsusi kwa kuhamasisha na kuwasaidia wanachama kuendeleza taaluma zao.

(viii) Kuwawakilisha wanataaluma wa fani ya Ukatibu mahsusi kitaifa na kimataifa kwa:-

a) Kuwasilisha maoni na mitazamo ya wanachama serikalini na kwa wanajamii kwa ujumla.

b) Kuendeleza mawasiliano na mahusiano kati ya taaluma ya Ukatibu mahsusi na taaluma nyingine.

Page 9: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

5

(ix) Kutoa elimu kwa wanachama kwa njia ya mafunzo, makongamano na midahalo ya wazi kuhusu mabadiliko ya kiteknolojia,

(x) Kuwekeza katika vitega uchumi vitakavyoboresha ustawi wa wanachama

ingawa TAPSEA si Chama cha kibiashara. (xi) Kutafuta misaada kwa watu binafsi, Taasisi, Vyama, Makampuni na

serilkalini kwa lengo la kufikia malengo ya Chama, na (xii) Kuhakikisha kwamba hakuna ubaguzi wa rangi, kabila, dini, hali au jinsia

baina ya Wanachama na baina ya watu wengine.

Page 10: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

6

SEHEMU YA TATU

7.0 UANACHAMA

7.1 AINA YA UANACHAMA

Chama kitakuwa na Uanachama wa aina tatu:

(i) Wanachama Waanzilishi;

(ii) Wanachama wakujiunga, na

(iii) Wanachama wa Heshima.

HATA HIVYO; Mwanachama kamili wa chama hiki ni yule tu

atakayekuwa amewajibika kutimiza wajibu na masharti ya uanachama na

si vinginevyo.

7.2 Sifa za kuwa Mwanachama:-

Sifa hizi zitawahusu wanachama Waanzilishi na wanachama wa

kujiunga tu na hivyo basi hazitawagusa wanachama wa heshima.

(i) Lazima awe ni Katibu Mahsusi mwenye cheti cha taaluma hiyo

kinachotambuliwa na Serikali aliyeajiriwa na Taasisi ya Umma au

binafsi au aliyejiajiri mwenyewe anayeishi ndani na nje ya Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania;

(ii) Awe Mtanzania;

(iii) Awe ametimiza umri wa miaka 18;

(iv) Awe tayari kutimiza masharti na maadili ya Chama;

(v) Awe mtu anayejiheshimu na kulinda maadili ya Taaluma ya Ukatibu

Mahsusi kwa kiapo na chama kwa ujumla na

(vi) Akubali kwa hiari yake kuwa Mwanachama.

Page 11: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

7

7.3 Wanachama wa Heshima

Uanachama wa Heshima utatolewa na Mkutano Mkuu wa Chama cha

Makatibu Mahsusi Tanzania kwa watu mashuhuri ambao wametoa

mchango maalum kwenye Chama au katika Taaluma ya UHAZILI.

8.0 HAKI NA WAJIBU WA WANACHAMA

(a) Haki za Mwanachama Kamili;

(i) Haki ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wowote wa Chama;

(ii) Haki ya kupiga kura;

(iii) Haki ya kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi katika Chama kulingana na masharti ya Katiba hii;

(iv) Haki ya kusikilizwa na kuhoji jambo lolote linalomtatiza katika

uendeshaji wa chama na kupata majibu kutoka kwa viongozi;

(v) Haki ya kupata uteteze kutoka katika chama pale maslahi yake yanayohusu kazi yanapokuwa yanavunjwa/yamevunjwa au yanakaribia kuvunjwa;

(vi) Haki ya kujitetea na kupewa nafasi ya kusikilizwa pale anapoitwa na kamati yoyote ya chama kujieleza juu ya tuhuma zozote zinazomkabili;

(vii) Haki ya kukata rufaa juu ya maamuzi yoyote juu yake kwa

mamlaka zilizowekwa na Katiba hii au Mamlaka za Nchi kulingana na Sheria na

(viii) Haki ya kushiriki na kufaidi matunda yote yatokanayo na shughuli

za kitaaluma, ushirika na ustawi wa jamii zinazoendeshwa na Chama kwa mujibu wa Sheria au Kanuni na taratibu zilizowekwa.

(b) Wajibu wa Mwanachama:

(i) Kulipa ada ambayo inalipwa kila mwaka kwa viwango vilivyopangwa;

(ii) Kuhudhuria vikao vya Chama vinavyohusika; (iii) Kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama ikiwemo Mkutano

Mkuu wa Chama;

Page 12: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

8

(iv) Kutekeleza maamuzi halali ya chama; (v) Kujiendeleza kielimu na kitaaluma kwa uwezo wake wote

walau mara 1 kila mwaka na (vi) Kulinda, kukitangaza na kukitetea Chama wakati wote na kwa

nguvu zote.

9.0 UKOMO WA UANACHAMA

9.1 Mwanachama atakoma uanachama iwapo:-

(i) Atapoteza sifa ya Uanachama au kufukuzwa Uanachama; Hata hivyo Mwanachama aliyefukuzwa hataruhusiwa kuwa Mwanachama mpaka pale muda wa kipindi cha miaka mitatu utakapokwisha tangu kufukuzwa kwake, Mwanachama huyo atahitajika kuwasilisha maombi ya kurejeshewa Uanachama kwenye Mkutano Mkuu wa Chama na si vinginevyo.

(ii) Mwanachama hakutoa ada yake kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu mfululizo;

(iii) Hatakuwa mfanyakazi wa kuajiriwa kwa kuacha kuachishwa kazi au

kufukuzwa kazi na chama kuridhika kuwa kufukuzwa kwake ni halali;

(iv) Atajiuzulu uanachama;

(v) Atashindwa kutimiza masharti ya katiba hii na maadili ya taaluma ya Ukatibu Mahsusi;

(vi) Atafukuzwa uanachama;

(vii) Atafariki dunia na

(viii) Ataugua ukichaa usioponyeka.

HATA HIVYO: Kwa Mwanachama aliyefukuzwa uanachama wake kwa

sababu za kimadili, kujiuzulu au kushindwa kulipa ada hatarudishiwa ada

zake za uanachama lakini kwa wale wenye matatizo ya kiafya, kifo au

kustaafu basi wategemezi wao au wao wenyewe watapewa kiasi cha fedha

za ada ya mwanachama kama mkono wa kwaheri, kulingana na kanuni ya

ukokotoaji wa fedha iliyopitishwa na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu,

itakayojali usawa wa Wanachama wote.

Page 13: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

9

SEHEMU YA NNE

10. UONGOZI

(i) Sifa za kuwa Kiongozi

(a) Awe mwanachama hai;

(b) Awe na Taaluma ya UHAZILI kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;

(c) Sifa ya Stashahada ya UHAZILI itaongeza sifa ya ziada;

(d) Awe muadilifu;

(e) Awe mchapa kazi;

(f) Asiwe mchelewaji;

(g) Awe mtenda haki kwa Wanachama wote/mwenye hekima;

(h) Asiwe mwenye upendeleo wala makundi na awe na uvumilivu;

(i) Awe anajua kusoma na kuandika na

(j) Awe Mwanachama anayeijua Katiba na kuitetea.

(ii) Miiko ya Uongozi

(a) Ni marufuku Kiongozi kutumia madaraka aliyopewa kuonea na kukandamiza wengine ndani ya Chama kinyume na Utaratibu;

(b) Ni mwiko kwa Kiongozi kutoa nje siri za Chama au za Mwanachama;

(c) Ni marufuku Kiongozi aliyesimamishwa Uongozi kutokana na

kashfa au makosa mbali mbali ya utekelezaji wa taratibu za Chama au utovu wa nidhamu kutaka kugombea tena Uongozi, hata kama atatubu na kuomba msamaha, mpaka miaka mitatu ya Mkutano Mkuu wa Chama ipite tangu pale aliposimamishwa Uongozi;

Page 14: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

10

(d) Ni marufuku Kiongozi kutumia lugha chafu za matusi na dharau kwa Wanachama au viongozi wenzake wakati wa vikao au wakati wa shughuli yoyote ya Chama au shughuli ya Mwanachama na

(e) Ni marufuku Kiongozi kujiamuria kutumia pesa au mali ya Chama kwa faida yake binafsi kinyume na utaratibu uliowekwa.

NB:- Endapo Kiongozi atapatikana na na makosa hayo yaliyoainishwa katika ibara ndogo a, b, d, na e hapo juu atasimamishwa uongozi mara moja.

11. KAZI NA MADARAKA YA VIONGOZI WA CHAMA

(a) Mwenyekiti

(i) Kiongozi Mkuu wa Chama; (ii) Kuwa Mwenyekiti wa Mikutano chama ; (iii) Kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya Mikutano na Vikao vya Chama; (iv) Kuwa mweka saini katika Hundi za Chama; (v) Mdhibiti Mkuu wa fedha na mali za chama; (vi) Kuwa Msemaji na mtetezi Mkuu wa Chama na (vii) Kutoa msimamo na sera za chama kama itakavyoamuriwa na

vikao vya chama.

(b) Makamu wa Mwenyekiti

(i) Naibu Kiongozi Mkuu wa Chama;

(ii) Kuongoza vikao Chama kama Mwenyekiti hayupo;

(iii) Kuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama na

(iv) Kukaimu nafasi ya Mwenyekiti kama hayupo.

(c) Katibu Mkuu

(i) Kuitisha vikao vya Chama kwa kushauriana na Mwenyekiti;

(ii) Kusimamia shughuli za uendeshaji za kila siku za Chama;

(iii) Kuwa Katibu wa Vikao vyote vya Chama;

(iv) Kuweka kumbukumbu za shughuli zote za Chama;

Page 15: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

11

(v) Kuhusika na utoaji wa vitambulisho kwa wanachama;

(vi) Mkuu wa Watumishi wote wa Chama;

(vii) Kuandaa taarifa ya shughuli za Chama katika kipindi husika;

(viii) Kutunza Muhuri wa Chama;

Hata hivyo, Muhuri wa Chama utatumiwa kwa shughuli rasmi

za Chama zilizoidhinishwa na Kamati Tendaji ya Chama na

(ix) Kujenga na kudumisha uhusiano bora kati ya Chama na

Taasisi nyingine.

(d) Naibu Katibu Mkuu

(i) Naibu Katibu Mkuu atamsaidia Katibu Mkuu katika utekelezaji wa shughuli zote zilivyoanishwa katika Katiba hii.

(ii) Atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu kama Katibu Mkuu hayupo

(e) Mweka Hazina

(i) Kusimamia Mapato na Matumizi ya fedha za Chama; (ii) Kwa Mweka Hazina, ni lazima awe na taaluma yeyote ya

fedha;

(iii) Kuweka kumbukumbu sahihi ya mapato na matumizi ya chama; kwa kushirikiana na Katibu Mkuu;

(iv) Kuandaa na kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwenye Kamati Utendaji na Mkutano Mkuu;

(v) Kubuni mbinu za kuongeza mapato ya chama;

(vi) Kutunza mali za Chama kwa kushirikiana na Mwenyekiti na

(vii) Kuwa mweka saini katika Hundi.

Page 16: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

12

12. KAMATI TENDAJI

(a) Muundo wa Kamati Tendaji

Kamati Tendaji ya Chama itakuwa na Wajumbe wafuatao:-

(i) Mwenyekiti;

(ii) Makamu Mwenyekiti;

(iii) Katibu Mkuu;

(iv) Naibu Katibu Mkuu na

(v) Mweka Hazina.

(b) Kazi za Kamati Tendaji

(i) Kusimamia shughuli zote za Chama za kila siku;

(ii) Kuandaa Mpango wa kazi wa Chama;

(iii) Kupokea na kupitia maombi mapya ya Wanachama;

(iv) Itaanda taarifa za Mikutano yote ya Chama;

(v) Itatoa taarifa ya fedha, Mali za Chama katika Mkutano Mkuu zilizokaguliwa na kuthibitishwa na Mkaguzi wa Hesabu anayetambuliwa Kisheria na

(vi) Kupendekeza majina ya Bodi ya Wadhamini.

(c) Baraza Kuu

Baraza Kuu litaundwa na Kamati Tendaji na Wajumbe 9 (tisa)

watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu.

(d) Kazi za Baraza Kuu

(i) Kuendesha na kusimamia shughuli za Chama;

(ii) Kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa na

Mkutano Mkuu;

Page 17: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

13

(iii) Kudhibiti Mapato na Matumizi ya fedha za Chama na kutoa taarifa kwenye Mkutano Mkuu;

(vii) Kuchagua Mjumbe mmoja kuwa mweka sahihi katika Hundi

za Chama wakati wa kutoa fedha benki; (viii) Kusimamia miradi ya kiuchumi na kijamii ya Chama;

(ix) Kumteua na kumpendekeza Mkaguzi wa Nje wa Mahesabu

ya Chama kila mwaka;

(x) Kushughulikia maendeleo ya Makatibu Mahsusi kuhusu elimu na mafunzo, Ushirika wa Akiba na Mikopo na ushirikishwaji, Uchumi, Utafiti na mipango, Mambo ya Nje, Fedha, Utawala, Sheria, Uhusiano kazini, Uimarishwaji wa Chama, Usafi wa Mazingira na mengineyo katika kuinua hadhi ya taaluma ya Katibu Mahsusi;

(xi) Kuajiri Watumishi/ Wafanyakazi wa Chama ;

(xii) Kupendekeza kwenye Mkutano Mkuu Majina ya Wanachama

wa Heshima na

(xiii) Kusikiliza mashauri ya kinidhamu ya Wanachama na

kuchukua hatua.

13. BODI YA WADHAMINI

(a) Bodi hii itaundwa na watu waliojitolea kukisaidia Chama kwa hali na mali, katika kuhakikisha malengo ya Chama yanafikiwa kwa kujitolea kwao kwa fedha, ushauri na mali;

(b) Bodi ya Wadhamini itapendekezwa na Kamati Tendaji na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Chama;

(c) Ukomo wa kuwa Mdhamini wa Chama:-

(i) Endapo itaamuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama;

(ii) Endapo atapata maradhi ambayo kwa ushahidi wa kitabibu

itaonekana hataweza kuyatekeleza majukumu yake;

(iii) Endapo Atafariki;

(iv) Endapo atahukumiwa na Mahakama kwa kosa la jinai adhabu

ya kifungo au adhabu inayofanana na kifungo;

(v) Endapo atawasilisha ombi la kujiuzulu kwa maandishi;

Page 18: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

14

14. MUDA WA VIONGOZI KUKAA MADARAKANI

Muda wa Viongozi kukaa madarakani ni miaka mitatu (3) tu isipokuwa

wanaweza kugombea tena kuongoza kwa kipindi kingine kwa muda

usiozidi mika sita. Baada ya hapo kiongozi yeyote hatakuwa na haki ya

kugombea tena uongozi.

15. MUDA WA KUKAIMU UONGOZI NDANI YA CHAMA

(a) Muda wa kukaimu nafasi ya uongozi ndani ya Chama utakuwa muda usiozidi miezi kumi na mbili (12),

(b) Pale nafasi ya uongozi itakapokuwa wazi, kutokana na:-

i. Kiongozi kukosa sifa ya kuongoza;

ii. Kiongozi kufariki dunia;

iii. Kiongozi kujiuzulu;

iv. Kiongozi kupata ugonjwa wa akili usioponyeka na

v. Kiongozi kufukuzwa uanachama/Uongozi

(c) Basi, nafasi iliyoachwa wazi na kiongozi huyo itajazwa na Makamu

wake. Na kama nafasi iliyoachwa wazi ni Makamu, Baraza Kuu litamteua Mjumbe yeyote mwenye sifa kati ya Wajumbe tisa (9) kukaimu nafasi hiyo hadi pale Uchaguzi Mkuu utakapoitishwa.

(d) Pale ambapo nafasi itakuwa wazi kwa sababu Kiongozi atakuwa

masomoni au kwenye kazi yeyote itakayokubaliwa na Chama, nafasi hiyo itaendelea kukaimiwa kwa kipindi cha miezi Kumi na mbili (12).

Page 19: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

15

SEHEMU YA TANO

16. MKUTANO MKUU

Mkutano Mkuu utaitishwa mara moja kwa mwaka. Ili Mwanachama ashiriki

lazima alipe ada ya ushiriki wa Mkutano Mkuu;

(i) Mwanachama halali atakayeruhusiwa kuingia kwenye Mkutano Mkuu

ni yule ambaye atakuwa amelipa ada ya mwaka; (ii) Kiwango cha gharama za ushiriki wa Mkutano Mkuu kitapangwa na

Baraza Kuu na kuthibitishwa na Mkutano Mkuu;

(iii) Katibu Mkuu ataitisha Mkutano Mkuu wa Chama baaada ya kupata maelekezo kutoka Kamati Tendaji;

(iv) Akidi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka itakuwa zaidi ya asilimia hamsini

(50%) ya Wanachama; (v) Iwapo kuna sababu ya kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura, wakati wowote

ule Wanachama wasiopungua asilimia 25% ya Wanachama wote wanaweza kutoa taarifa kwa Mwenyekiti kuitisha Mkutano wa dharura. Hata hivyo, Wanachama hao wanapaswa kutoa Waraka unaoonyesha malengo ya Mkutano huo, na sababu hasa ya kumfanya Mwenyekiti kuitisha Mkutano wa dharura. Baada ya Mwenyekiti kujiridhisha atamuamuru Katibu Mkuu kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura;

(vi) Kama Katibu Mkuu atashindwa kuitisha mkutano huo ndani ya siku ishirini

na moja (21) baada ya kupokea taarifa ya kuitisha; Mkutano Mkuu wa dharura, basi Wanachama wanaweza kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura kwa kipindi kisichopungua miezi minne tangu siku taarifa ilipotolewa.

(vii) Katika kila Mkutano Mkuu wa Chama Mwenyekiti wa Chama atakuwa

ndiye Mwenyekiti wa Mkutano, ikiwa itatokea kuwa hayupo Makamu Mwenyekiti ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano, ikiwa wote wawili hawapo basi wajumbe wa Mkutano watamchagua mjumbe mmoja kati yao kuwa Mwenyekiti wa Kikao;

Page 20: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

16

(viii) Katika kila Mkutano Mkuu Mwenyekiti ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano, ikitokea hayupo Makamu Mwenyekiti atakuwa ndiye Mwenyekiti wa mkutano huo. Na kama wote wawili hawapo basi

Wajumbe watamchaguwa mmoja kati yao kuwa Mwenyekiti wa Mkutano; (ix) Kila Mwanachama, katika Mkutano Mkuu atakuwa na haki ya kupiga kura

moja. Na ikitokea kura zimefungana, Mwenyekiti atakuwa na kura ya veto na

(iv) Maamuzi yote ndani ya vikao vya Chama, na Mikutano yatapitishwa na

kura za wengi.

17. WAWAKILISHI KATIKA MIKOA

(a) Kutakuwa na Mwakilishi wa Chama kila Mkoa ambaye atawawakilisha Wanachama walioko katika Ofisi mbali mbali za Mkoa ambaye atawakilishwa Wanachama walioko katika Mkoa husika;

(b) Mwakilishi huyu ataongozwa na Katiba na Kanuni za Chama katika

kutekeleza malengo ya Chama na (c) Wawakilishi wote wa Mikoa watachaguliwa miongoni mwa Wanachama

wa Chama, wa Mkoa husika.

18. WAJIBU WA WAWAKILISHI WA CHAMA

(i) Atakuwa ni kiungo kati ya Wanachama na Chama Makao Makuu;

(ii) Atakuwa ni Kiungo muhimu cha kuwaunganisha Makatibu Mahsusi katika Mkoa husika;

(iii) Kusimami masuala ya uingizaji Wanachama na kuhakikisha kuwa wanadumu katika Chama na kufanya shughuli nyingine za Chama kama zitakavyojitokeza;

(iv) Kutoa na kupokea taarifa mbalimbali kwa ajili ya Wanachama wa eneo hilo;

(v) Kuhimiza na kuelimisha Wanachama juu ya masuala ya Chama, wajibu na haki zao na

(vi) Kuhamasisha wanachama kikamilifu katika masuala ya Vyama vya Wafanyakazi na taaluma ili kuleta maisha na hali bora kwa Wanachama.

Page 21: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

17

SEHEMU YA SITA

19. UCHAGUZI MKUU

(i) Mkutano wa Uchaguzi Mkuu wa kumchagua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Mweka Hazina, Naibu Katibu Mkuu pamoja na Wajumbe 9 utaitishwa kila baada ya miaka mitatu;

(ii) Uchaguzi wa Viongozi ndani ya Chama, utasimamiwa na ofisi ya Msajili wa

Vyama vya Kijamii kwa kushirikiana na Kamati ya Uchaguzi itakayochaguliwa na Mkutano Mkuu siku ya Uchaguzi;

(iii) Uendeshaji wa shughuli za uchaguzi utakuwa chini ya maelekezo ya Kanuni

za Uchaguzi na (iv) Katika uchaguzi, mgombea atakayepata kura nyingi ndiye atakayetangazwa

mshindi.

20. UTARATIBU WA UTATUZI WA MIGOGORO NDANI YA CHAMA

Migogoro yote ndani ya Chama itatatatuliwa kwa njia ya usuluhishi. Kabla ya

mgogoro wowote haujapelekwa kwa msuluhishi, ni lazima upelekwe na kujadiliwa

katika Kamati ya Maadili na Nidhamu itakayoanzishwa kulingana na Kanuni za

Chama. Maamuzi ya Kamati ya Maadili na Nidhamu ya Chama, yatapingwa katika

Mkutano Mkuu. Hata hivyo, maamuzi ya Mkutano Mkuu yanaweza kuwasilishwa

mbele ya Msajili wa Vyama vya Kijamii kwa ajili ya usuluhishi. Maamuzi

yatakayotolewa na Msajili, ikiwa kuna upande katika mgogoro hautaridhika na

maamuzi ya Msajili basi, maamuzi hayo yaweza kukatiwa rufaa kwa Waziri wa

Mambo ya Ndani ya Nchi au kupinga Mahakamani.

Page 22: KATIBA YA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA …tapsea.or.tz/wp-content/uploads/2017/05/tapsea_katiba.pdf · Mkutano Mkuu wa Chama kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu; (xiii) “Mfanyakazi”

18

21. MABADILIKO YA KATIBA:

(i) Katiba hii inaweza kubadilishwa na Mkutano Mkuu baada ya theluthi mbili (2/3) ya Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kukubali mabadiliko hayo na

(ii) Taarifa za mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba lazima zifike kwenye

Kamati Kuu ya Utendaji siku sitini (60) kabla ya kuitishwa Mkutano Mkuu.

22. KUVUNJIKA KWA CHAMA:

(i) Chama chaweza kuvunjika endapo tu idadi ya wanachama (2/3) wataamua kivunjike au kutokana na amri ya Msajili, amri ya Mahakama au amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania;

(ii) Mali zote zinazohamishika na zisizohamishika baada ya amri ya

kuvunjika kwa Chama kutolewa, zitawekwa chini ya Bodi ya Wadhamini; (iii) Bodi ya Wadhamini, itawajibika kukusanya mali zote na kubaini Wadeni

na Wadaiwa wote na kuhakikisha kupitia mali zilizopo madeni yanalipwa, na wadaiwa wanalipa madeni yao na

(v) Mali zote zitakazokuwa zimebaki baada ya kulipwa wadeni na

makusanyo yote ya wadaiwa, zitagawanywa kwa Wanachama kulingana na michango na muda wa kila mwanachama aliokaa ndani ya Chama.