Upload
wanachuoni
View
277
Download
19
Embed Size (px)
DESCRIPTION
Kauli Za Ma´ulamaa Kuhusu Maulidi
Citation preview
1
Mfasiri:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
2
Yaliomo:
1. Maulidi Hayana Kheri Yoyote
2. al-Faakihaaniy Kuhusu Sherehe Ya Maulidi
3. Mgawanyiko Wa Imaam ash-Shaafi'iy Wa Bid´ah Hauyasapoti Maadhimisho
Ya Maulidi
4. Maadhimisho Ya Maulidi Yanapingana Na Qur-aan, Sunnah Na Matendo Ya
Salaf
5. Ibn Hajar Kuhusu Bid´ah Nzuri Ya Maadhimisho Ya Maulidi
6. Maadhimisho Ya Maulidi Ni Kujifananisha Na Manaswara
7. as-Suyuutwiy Asemae Maadhimisho Ya Maulidi Ni Bid´ah Nzuri
8. Shaytwaan Anapenda Sherehe Ya Maulidi
9. Imaam al-Albaaniy Kuhusu Maadhimisho Ya Maulidi
10. Je, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Anahudhuria Katika Sherehe
Ya Maulidi?
11. Hukumu Ya Kusherehekea Maulidi Msikitini
12. Shaykh Ibn ´Uthaymiyn Akiwaombea Du´aa Waliopotea Katika Bid´ah Ya
Maulidi
13. Inajuzu Kusherehekea Maulidi Kama Ada Tu Na Si ´Ibaadah?
14. Maulidi Hayakufanywa Na Mtume Wala Maswahabah
15. Tofauti Kati Ya Sherehe Ya Maulidi Na Siku Ya Taifa
16. Maulidi Yana Bid´ah Na Shirki
17. Kupeana Hongera Siku Ya Maulidi
18. Kufanya Maulidi Ni Bid´ah
19. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Madu´aat Wanaohudhuria Katika Maulidi
20. Kufunga Siku Ya Maulidi Ya Mtume (´alayhis-Salaam)
21. Je, Kusherehekea Maulidi Ni Katika Kumpenda Mtume (´alayhis-Salaam)?
3
22. Sikukuu Za Makafiri Kama Krismasi Na Za Waislamu Kama Maulidi
23. Wajinga Wanaodanganywa Kwamba Kusherehekea Maulidi Ni Kumpenda
Mtume
Ma´ulamaa waliomo:
1. Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
2. Imaam Abu Hafs Taadj-ud-Diyn al-Faakihaaniy
3. Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
4. Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
5. Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
6. 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy
7. ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
8. ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
9. ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
10. ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
11. Shaykh Swaalih bin Sa´iyd as-Suhaymiy
4
Dibaji Ya Mfasiri:
Alhamdulillaah. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad.
Amma ba´ad:
Nimekusanya baadhi ya kauli za ma´ulamaa waliotangulia (Rahimahumu
Allaah) na wa sasa (Hafidhwahumu Allaah) kuhusiana na Bid´ah sugu hii ya
Maulidi ambayo Shaytwaan amewapambia baadhi ya Waislamu. Natumai hoja
zilizotajwa humu zitawaondolea shubuha kwa wale waliokuwa wakifuata
kichwa mchunga na kibubusa walinganiaji wapotofu ambao wamekuwa kwa
siku nyingi wakiwadanganya ndugu zetu Waislamu wasiokuwa na elimu ya
kwamba kusherehekea Maulidi ni kumpenda Mtume. Allaah Atukinge.
Ama kuhusiana maimamu wakubwa wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah
waliotangulia ambao wameonelea ya kwamba yanajuzu, hoja zao zimerudishwa
na kuradiwa (kupigwa Radd) na ma´ulamaa wakubwa wa Ahl-us-Sunnah wal-
Jamaa´ah. Kama alivyosema Imaam Maalik “Sote kauli zetu zinachukuliwa – yaani
pale ambapo zimeafiki Kitabu na Sunnah, na kurudishwa – pale ambapo zimekhalifu
Kitabu na Sunnah.” Na huu ndio msimamo sahihi wa Salaf na waliowafuata kwa
wema.
Kauli za ma´aulamaa tumezigawa sehemu mbili; wanachuoni wa Salaf – yaani
tukimaanisha wale wambao wameshatangulia makaburini (Allaah Awarehemu)
na wanachuoni wa Khalaf – wale ambao bado wako hai kwa sasa (Allaah
Awahifadhi).
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Atuoneshe haki na Atuwafikishe
tuwe ni wenye kuifuata, na Atuoneshe batili na Atuwafikishe tuwe ni wenye
kuifuata. Aamiyn.
5
Wanachuoni Wa Salaf
1. Maulidi Hayana Kheri Yoyote
Hali kadhalika na kwa yale waliozua baadhi ya watu ima ili kuiga manaswara
au kwa ajili ya mapenzi na kumuadhimisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam). Huenda Allaah Akawalipa kwa mapenzi na shughuli hii, lakini si kwa
Bid´ah hii ya kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam). Isitoshe, kuna tofauti kuhusiana na tarehe sahihi [za kuzaliwa kwake].
Jambo hili halikufanywa na Salaf, ingawa walikuwa na uwezo juu ya hilo
wakati vikwazo vyake kulikuwa hakuna. Lau jambo hili lingekuwa na kheri
ndani yake, au lau lingekuwa na faida nyingi kuliko khasara, basi Salaf
(Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa na haki zaidi juu yake kuliko sisi.
Walikuwa wakimpenda Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) zaidi kuliko
sisi vile vile kama ambavyo walikuwa wakimuadhimisha (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) zaidi kuliko sisi. Walikuwa na hima ya kufanya matendo mema
kuliko sisi.
Lakini mapenzi kamilifu na uadhimisho unapatikana katika kumfuata na kumtii,
kufuata amri zake, kuhuisha Sunnah zake sawa za ndani na za dhahiri, kueneza
mafunzo yake na kupigana kwa hilo kwa moyo, mkono na ulimi. Hii ndio njia
ya wale Makhalifah wa kwanza katika Muhaajiruun na Answaar, na wale
waliowafuata kwa wema.
Watu wengi katika watu hawa ambao wako na bidii ya kujishughulisha na
Bid´ah hii - angalau kwa nia njema na shughuli ambayo tunatarajia watapewa
ujira kwa ajili yake - ni madhaifu katika kufuata amri za Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam). Utawapata wao ni kama yule mwenye kuipamba Qur-aan
bila ya kuisoma au anaisoma lakini bila ya kuifuata. Mtu kama huyo ni kama
yule anaeupamba Msikiti bila ya kuswali au anafanya hivyo mara chache.
Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
6
Iqtidhwaa´ as-Swiraat al-Mustaqiym (2/123-124)
Daar-ul-'Asimah, 1419
2. al-Faakihaaniy Kuhusu Sherehe Ya Maulidi
Watu wema wameuliza mara nyingi swali kuhusu ukusanyanyikaji unaofanyika
na baadhi ya watu katika Rabiy´ al-Awwal, ambayo wanaiita "Maulidi". Je, yana
msingi katika Dini? Wanataka jibu la ufafanuuzi. Nikajibu na kwa Allaah ndio
kwenye mafanikio:
Sijui kuwa Maulidi haya yana msingi katika Qur-aan au Sunnah. Na haijathibiti
kutoka kwa mwanachuoni yeyote wa Ummah ambaye ni ruwaza njema katika
Dini na ambaye anashikamana na wa kale. Ukweli ni kwamba jambo hili ni
Bid´ah. Yalizushwa na wavivu na watu waroho. Dalili ya hilo ni kwamba, ikiwa
tutayakutanisha na zile hukumu tano, tungelisema kuwa jambo hili ima ni
wajibu, limependekezwa, linaruhusiwa, linachukiza au haramu pia.
Ni jambo waislamu wamekubaliana ya kwamba si wajibu au kupendekezwa.
Jambo lililopendekezwa ni jambo ambalo Shari´ah imeliamrisha bila ya
kumhukumu yule ambaye hakulifanya. Jambo hili Shari'ah haikuliruhusu.
Maswahabah na waliokuja baada yao hawakulifanya. Na wala sijui ya kwamba
wanachuoni wa Dini walilifanya. Hili ndio jibu langu mbele ya Allaah (Ta´ala)
ikiwa nitaulizwa kuhusu hilo.
Hayawezi pia kuwa yanaruhusiwa kwa sababu jamhuri imekubaliana ya
kwamba ni haramu kuzusha katika Dini.
Hivyo, jambo hili linaweza kuwa ima lenye kuchukiza au haramu pia. Katika
hali hii mtu anaweza kuyaongelea katika njia mbili tofauti:
Jambo la kwanza: Mtu kufanya hilo na mke wake, rafiki zake na familia yake,
kuyasimamia kwa pesa zake mwenyewe na kula tu wakati wa mkusanyiko bila
ya kushiriki dhambi yoyote. Ni mkusanyiko huu ndio tunauelezea kuwa ni
Bid´ah yenye kuchukiza na kitendo cha machukizo. Kwa maana hakuna mtu
yeyote katika karne za kale, ambaye ni mwanachuoni wa Uislamu na watu
aliyeyafanya.
7
Jambo la pili: Kwamba dhambi imeshiriki [katika Maulidi hayo] na mtu
anaomba wengine pesa kwa ajili yake. Roho imejisalimisha kwa hilo wakati
moyo unateseka kwa mateso ya dhuluma. Baadhi ya wanachuoni wamesema:
"Kuchukua pesa kwa kustahi ni kama kuzichukua kwa upanga."
Na hili ni hususan pale ambapo mkusanyiko unafuatana na nyimbo na vyombo
kama matari na vijana wanawake na wanaume ambao wanakaa pamoja na
vijana wasiokuwa na ndevu na waimbaji. Hili linaweza kufanyika kwa
mchanganyiko wa moja kwa moja au kwamba wanawake kuwahudumia
wanaume na kucheza kwa kuamsha hisia. Aidha, mkusanyiko unakuwa na
burudani zisizohitajika ambapo husahau Siku ya Qiyaamah.
Hali kadhalika wanawake wanapokusanyika wao wenyewe, kupandisha sauti
zao, kuimba na kushindwa kusoma na kumkumbuka Allaah kwa njia ya kidini
na ya kawaida. Wanapuuza Maneno ya Allaah (Ta´ala):
إن ربك لبالمرصاد
“Hakika Mola wako bila shaka Yuko katika Kuchunga (na kuwavizia).” (89:14)
Hakuna yeyote anayeonelea hili linajuzu. Si mwenye heshima, busara na
wanaume shujaa kuona hili ni zuri. Watu ambao wanaruhusu jambo hili ni wale
wenye mioyo ya maradhi ambao hawaachi dhambi. Na hawakutosheka na hilo.
Wanafikia mpaka kusema hata ya kwamba jambo hili ni aina ya ´Ibaadah na
halikukatazwa. Inna liLlaahi wa inna Ilayhi raaji´uun. Uislamu ulianza kitu
kigeni na utarudi kuwa kama ulivyoanza.
Imaam Abu 'Amr bin al-' Alaa' kapatia aliposema:
"Watu watakuwa katika hali nzuri maadamu wanastaajabu katika ajabu."
Isitoshe mwezi huu - Rabiy' al-Awwal – ambao Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) alizaliwa katika mwezi huo, ni mwezi huo huo alifariki. Hakuna haki
zaidi ya kufurahia katika mwezi huo kuliko kusikitika.
Hili ndio limelazimika kwangu kulisema. Ninamuomba Allaah Ataqabali ´amali
hii.
Mwandishi: Imaam Abu Hafs Taadj-ud-Diyn al-Faakihaaniy (d. 734)
al-Mawrid fiy 'Amal-il-Mawlid, uk. 20-27
8
3. Mgawanyiko Wa Imaam ash-Shaafi'iy Wa Bid´ah
Hauyasapoti Maadhimisho Ya Maulidi
ar-Rifaa'iy kasema:
"Kinachothibitisha ya kwamba tendo hili ni Bid´ah nzuri, ni maneno ya ash-
Shaafi'iy yaliyopokelewa na al-Bayhaqiy: "Kuna aina mbili ya Bid´ah. Ya kwanza
ni ile inayopingana na Qur-aan, Sunnah, mapokezi au Ijmaa´1. Bid´ah hii ni
upotofu. Bid´ah ya pili si ni ile inayopingana na moja katika hayo tuliyotaja.
Bid´ah hii sio yenye kulaumiwa. 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kasema kuhusu
Swalah ya usiku katika Ramadhaan: "Bid´ah nzuri ilioje hii!"
Jambo la kwanza, sio maoni ya wanachuoni ndio yenye kuamua
yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa, kizuri, haramu na kibaya. Dalili ni Qur-
aan, Sunnah, Ijmaa´ au kauli ya Swahabah rafiki maadumu haijulikani ya
kwamba kuna Swahabah mwingine ana maoni tofauti. Alichosema ash-Shaafi'iy
(Rahimahu Allaah) hakitolei dalili uzushi wa Maulidi, au Bid´ah nyingine kwa
jambo hilo, kuwa ni nzuri. Kutokana na maneno yake, mtu anapata kuelewa ya
kwamba maadhimisho ya Maulidi yamekatazwa kwa vile yanakwenda kinyume
na Qur-aan, Sunnah, mapokezi na matendo ya Salaf taarifa na maimamu.
Aidha, maneno ya ash-Shaafi'iy yamepokelewa kwa taarifa nyingine. Abu
Nu'aym kapokea katika "al-Hilyah" yake kutoka kwa Ibraahiym bin al-Junayd
ambaye kasema: Harmalah bin Yahyaa katueleza ambaye kasema kwamba
alimsikia Muhammad bin Idriys ash-Shaafi'iy akisema:
"Kuna aina mbili ya Bid´ah. Bid´ah inayosifiwa na Bid´ah ya kulaumiwa.
Inayokwenda sambamba na Sunnah inasifiwa na inayokwenda kinyume na
Sunnah inalaumiwa. "
Kisha akatumia hoja kwa maneno ya 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) kuhusu
Swalah ya usiku katika Ramadhan:
"Bid´ah nzuri ilioje hii!"
1 Makubaliano ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)
9
Ibn Rajab kasema katika 'Jaami'-ul-'Uluum wal-Hikam":
"ash-Shaafi'iy anamaanisha ya kwamba msingi wa Bid´ah ya kulaumiwa ni
kuwa ni ile inayokosa msingi katika Shari'ah ambao mtu anaweza kuurejea.
Ndio maana ya Bid´ah kwa mujibu wa Shari'ah. Ama kuhusiana na Bid´ah
yakusifiwa, hiyo inayokwenda sambamba na Sunnah. Inamaana ina msingi
ambao mtu anaweza kuurejea. Kwa njia hii, hii ni Bid´ah tu ya kilugha2, na sio ya
Dini, hivyo inakwenda sambamba na Sunnah."
Jambo la pili, uzushi wa Maulidi hauna msingi katika Shari'ah. Jambo hili
linapingana na uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) na Sunnah. Hivyo ni kitendo cha Bid´ah ya kulaumiwa.
Jambo la tatu uzushi wa Maulidi unapingana na Qur-aan, Sunnah, mapokezi na
matendo ya Salaf na maimamu.
Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 44-45
4. Maadhimisho Ya Maulidi Yanapingana Na Qur-aan,
Sunnah Na Matendo Ya Salaf
ar-Rifaa'iy kasema kuwa maadhimisho ya Maulidi hayapingani na Qur-aan,
Sunnah na Ijmaa´ ya Waislamu, hata kama yamekuja baada ya Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) na kufa kwa Maswahabah wake. Kwa hiyo, mtu
hawezi kusema ya kwamba tendo hili ni la kulaumiwa kwa seuze tusiseme ya
kuwa ni dhambi na kuwa ni Bid´ah ovu.
2 Anasema Shaykh ´Allaamah al-Fawzaan: ”Bid´ah ya kilugha ni kwa mfano wa hii gari yako. Gari yako hii ni Bid´ah lakini ni Bid´ah ya kilugha. Kwa kuwa ni kitu kipya ambacho hakikuwepo, mwanzoni watu walikuwa wakipanda punda na mipando mingine. Kukaja badala yavyo gari n.k. Hii ndio Bid´ah ya kilugha.” (Sharh Sunnah lil-Barbahaariy).
10
Maadhimisho ya Maulidi ni Bid´ah katika Uislamu na maadhimisho yake
yanapingana na Qur-aan, Sunnah na matendo ya Waislamu tangu wakati wa
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wakati wa sallam) hadi karne ya 600.
Yanapingana na Qur-aan pale ambapo Allaah Anamuamrisha mja Wake kufuata
yale Aliyoteremsha na hapana mwingine badala Yake. Allaah (Ta´ala) Anasema:
ن ربكم ول ت تبعوا من دونه أولياء رون اتبعوا ما أنزل إليكم م ا تذك قليلا م
”Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu (Qur-aan na Sunnah) na wala msifuate badala Yake (Allaah), awliyaa (marafiki wapenzi, walinzi wanaokuamrisheni kufru, shirki). Ni machache mnayoyakumbuka.” (07:03)
Maadhimisho ya Maulidi yanaingia katika makatazo haya ya jumla yaliyotajwa
katika Aayah hii tukufu. Si Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) hakuamrisha kitendo hichi. Yule ambaye kaamrisha hili, ni yule ambaye
kalizusha, yaani ni mfalme wa Arbil3. Wale ambao wanasherehekea Maulidi
wanamfuata mfalme wa Arbil na wanafanya yale Aliyokataza Allaah pale
wanapofuata wengine badala Yake.
ين ما ل يأذن به الل ه ن الد أم لم شركاء شرعوا لم م
“Je, wanao washirika waliowaamuru (Shari’ah ya) Dini ambayo Allaah
Hakuitolea idhini?” (42:21)
Sherehe ya Maulidi inaingia katika makatazo haya ya jumla yaliyokatazwa
katika Aayah hii tukufu. Allaah (Ta´ala) Hakuweka kitendo hichi katika
Shari´ah. Ni mfalme Arbil ndio kaiweka. Wale wenye kusherehekea Maulidi
wanafuata sheria ambayo Allaah Hakuitolea idhini. Isitoshe, maadhimisho ya
Maulidi yanapingana pia na Sunnah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi
wa sallam) kasema:
“Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifah wangu waongofu
baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Na tahadharini na mambo mepya ya
kuzusha, kwa hakika kila jambo lenye kuzushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni
upotofu.”
Maadhimisho ya Maulidi sio katika Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) na Makhalifah wake. Kitendo hichi ni katika mambo
3 http://en.wikipedia.org/wiki/Erbil
11
yaliyozushwa na hivyo yanaingia katika yale ambayo Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) aliyokataza.
Maadhimisho ya Maulidi yanapingana hata na matendo ya Waislamu kwa
miaka 600. Ni jambo linalojulikana ya kwamba ilikuwa ni mfalme wa Arbil ndio
mtu wa kwanza kuyasherehekea Maulidi. Aliyafanya Maulidi kuwa sherehe ya
kuadhimishwa kila mwaka. Yalizushwa mwisho wa karne ya sita au mwanzo
wa karne ya saba. Kabla ya hili ilikuwa ni kitendo kisichojulikana kwa
Waislamu. Lau kama kungekuwepo mazuri yoyote katika kitendo hichi basi
Maswahabah wangeliyafanya. Hakuna watu waliokuwa na hima katika
matendo mazuri kama Maswahabah. Hakuna mtu yeyote katika Ummah huu
ampendae Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kama Maswahabah.
Hakuna mtu yeyote ashikamanae na kufuata Sunnah zake kama Maswahabah.
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema kuwa kundi
lililookoka ni lile linalofuata yale ambayo yeye na Maswahabah wake
wanayofuata.
Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 122-123
5. Ibn Hajar Kuhusu Bid´ah Nzuri Ya Maadhimisho Ya
Maulidi
Vilevile kama alivyonukuu as-Suyuutwiy, anasema Ibn Hajar kwanza kuwa
sherehe ya Maulidi ni Bid´ah ambayo haikuthibiti kutoka kwa Salaf yoyote.
Sentensi hii ya Ibn Hajar inatosha kuyahukumu Maulidi. Yangelikuwa mazuri,
Maswahabah, waliokuja baada yao, na maimamu baada yao
wangeliyasherehekea. Kisha Ibn Hajar akasema:
"Lakini ikiwa jambo hili lina mazuri na mabaya, hivyo ni Bid´ah nzuri ikiwa mtu
atafanya hayo mambo mazuri na kuepuka hayo mabaya na vinginevyo hapana."
Kasema pia:
12
"Naamini ya kwamba jambo hili lina msingi imara. al-Bukhaariy na Muslim
wamepokea ya kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)
alipoenda al-Madiynah, alikuta Mayahudi wanafunga siku ya Aashuura´.
Akawauliza kuhusu hilo na wao wakasema wanafunga siku hiyo kumshukuru
Allaah kwa kumuokoa Muusa na kumuangamiza Fir´awn siku hiyo. Kutokana
na hili, tunapata kujua ya kwamba ni sahihi kumshukuru Allaah kwa siku fulani
Kaneemesha au Kuondosha mabaya na kwamba inaweza kufanywa siku hiyo
hiyo mwaka baada ya mwaka. "
Ambayo anasema Ibn Hajar yanaradiwa na maneno yake ya kwanza, nayo ni
kwamba sherehe ya Maulidi ni Bid´ah ambayo haikuthibiti kutoka kwa Salaf
yoyote. Nimekwishataja Aayah na Hadiyth zinazokataza na kutahadharisha
Bid´ah na kubainisha kwamba hayakubaliwi. Kuna Radd ya kutosha kwa
maneno ya mwisho ya Ibn Hajar.
Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 30-31
6. Maadhimisho Ya Maulidi Ni Kujifananisha Na
Manaswara
Kuhusu nukuu ya ar-Rifaa'iy ya as-Sakhaawiy ambaye amesema:
"Ikiwa wakristo wamefanya Krismasi kuwa sikukuu, Waislamu wana haki zaidi
juu yake kwa Mtume wao."
hakuna shaka kwamba maadhimisho ya Maulidi yamejengeka juu ya
kujifananisha na manaswara ambao wamechukua kuzaliwa kwa Masiyh kuwa
ni sikukuu. Hili linathibitisha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam):
"Mtafuata desturi (mwenendo) za waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na
pima kwa pima hata wakiingia katika shimo la mburukenge (yaani ndani ya
shimo lenye mnyama anayeweza kukudhuru) mutaingia nao.” Tukasema: “Je,
13
unakusudia mayahudi na manasara?” Akasema: “Ni nani wengine ikiwa si
wao?"
Imepokelewa na Imaam Ahmad, al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Abu
Sa'iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu 'anhu).
Wakati mtu anajua kuwa maadhimisho ya Maulidi ya wajinga msingi wake
umejengeka juu ya kujifananisha na manaswara, basi mtu anapaswa pia kujua
kwamba imekatazwa vikali kujifananisha na manaswara na washirikina. Mtume
(Salla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:
“Yule anayejifananisha na watu basi [mtu huyo] ni katika wao.”
Imepokelewa na Imaam Ahmad na Abu Daawuud kutoka kwa 'Abdullaah bin
'Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa).
Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 25-26
7. as-Suyuutwiy Asemae Maadhimisho Ya Maulidi
Ni Bid´ah Nzuri
Kuhusiana na nukuu ya ar-Rifaa'iy ya as-Suyuutwiy ambaye kasema:
"Maulidi ni katika Bid´ah nzuri ambayo mtu hupewa thawabu juu yake."
maneno ya as-Suyuutwiy yanaradiwa na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa sallam):
"Na shari ya mambo ni [mambo] ya kuzua."
na:
"Kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni."
na:
14
"Yule ambaye atafanya ´amali isiyokuwa humo na mri yetu atarudishiwa
mwenyewe."
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kaeleza Bid´ah kuwa ovu na upotofu.
Sifa hizi ni mbaya na zimekatazwa. Yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)
kaeleza pia kwamba matendo yao yanatupiliwa mbali na kwamba yanaingia
Motoni. Hii ni dalili ioneshayo ya kwamba mtu wa Bid´ah hapewi ujira kwa
Bid´ah yake. Badala yake, kuna khatari ya kupata mtihani na adhabu chungu.
Allaah (Ta´ala) Kasema:
نة أو يصيب هم عذاب أليم ف ليحذر الذين يالفون عن أمره أن تصيب هم فت
“Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au
ikawasibu adhabu iumizayo.” (24:63)
Aidha, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:
"Kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni."
Mtu anapewa ujira tu wakati anamfuata Mjumbe (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) na kuipa kipaumbele uongofu wake kabla ya kila kitu kingine. Allaah
(Ta´ala) Kasema:
بون الل ه فاتبعون يببكم الل ه وي غفر لكم ذنوبكم والل ه غفور رحيم قل إن كنتم ت
”Sema (ee Muhammad صلى هللا عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi
nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na
Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufiria - Mwenye kurehemu).”
(03:31)
ي الذي ي ؤمن بالل ه وكلماته واتبعوه لعلكم ت هتدو ن فآمنوا بالل ه ورسوله النب الم
”Basi mwaminini Allaah na Mtume Wake, an-Nabiyyi al-Ummiyy (Mtume
Muhammad صلى اهلل عليه وآله وسلم asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye
anamwamini Allaah na Maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuongoka.” (07:158)
Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Kafanya watu kupata sehemu ya mapenzi Yake,
uongofu wake na msamaha wake ikiwa tu watamchukua Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) kama mfano mzuri wa kuigwa. Maadhimisho ya
Maulidi sio katika uongofu wala Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam). Ni katika uongofu na Sunnah ya mtawala Irbil na aliishi takriban miaka
600 baada ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam).
15
Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 29
8. Shaytwaan Anapenda Sherehe Ya Maulidi
Shaytwaan hufurahia maadhimisho ya Maulidi wakati Bid´ah zote ni katika
matendo na upambiaji wa Shaytwaan. Hakuna shaka ya kwamba Shaytwaan
hufurahia Waislamu kufanya Bid´ah anazowachochea. Ibn-ul-Jawziy kapokea ya
kwamba Sufyaan ath-Thawriy kasema:
"Ibliys anapenda Bid´ah zaidi kuliko dhambi. Mtu hutubia kwa dhambi tofauti
na Bid´ah."
Dalili ya kuwa Bid´ah zote katika Dini ni katika matendo ya Shaytwaan ni
kwamba Allaah (Ta´ala) Katueleza ya kuwa Shaytwaan kasema:
هم ولضلن
”Na hakika nitawapoteza.” (04:119)
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:
"Na shari ya mambo ni [mambo] ya kuzua, na kila Bid´ah ni upotofu."
Aayah na Hadiyth Swahiyh zinatoa dalili kwamba Bid´ah za Dini ni katika
upotofu wa Shaytwaan.
Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 24-25
16
9. Imaam al-Albaaniy Kuhusu Maadhimisho Ya Maulidi
Imaam al-Albaaniy:
Maulidi yanayofanywa Iraaq, Oman au Syria, kwa hakika ni katika mambo
yaliyozuliwa. Kule kutenga siku maalum, na kuiita “Sherehe ya Maulidi ya
Mtume”, hili bila ya shaka ni katika mambo yaliyozuliwa.
Isitoshe, kuna mukhaalafah4 mwingi katika yanayofanywa katika sherehe hii. Kwa
mfano kunatokea mukhaalafah wa Kishari´ah mwingine, mukhaalafah unazidi.
Ama kwa mfano kunafanywa mihadhara, katika mihadhara hii
wakakumbushana kitu katika Siyrah na Sunnah ya Mtume, hili bila ya shaka
ingekuwa ni kheri kubwa kuliko kutenga siku ya Maulidi [kuzaliwa kwake].
Lakini pamoja na hivyo, haijuzu kutenga mwezi maalum au siku maalum
kusherehekea Maulidi hata kama itakuwa sherehe hii haina ndani yake
mukhaalafah unaokwenda kinyume na Shari´ah.
Muulizaji:
Katika sherehe hii huletwa vyakula Shaykh.
Imaam al-Albaaniy:
Kila kinachofanywa katika mwezi huu, ni katika mambo yaliyozuliwa.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=7wdda0LQDRo
10. Je Mtume (´alayhis-Salaam) Anahudhuria Katika
Sherehe Ya Maulidi?
4 Mambo yanayofanywa yanayokwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah.
17
Baadhi ya watu wanaamini ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
sallam) anahudhuria wakati wa sherehe ya Maulidi. Hii ndio sababu ya wao
kumkaribisha huko. Jambo hili ni katika uongo mkubwa sana na ujinga wa
kuchukiza. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) hatotoka nje ya kaburi
lake mpaka Siku ya Qiyaamah. Hana mawasiliano na mtu yoyote. Hahudhurii
katika mkusanyiko wowote. Bado yuko katika kaburi lake mpaka Siku ya
Qiyaamah. Nafsi yake iko kwa Mola katika jamii ya juu, katika makazi ya
maisha ya kupendeza. Allaah (Ta´ala) Kasema katika Suurat "al-Mu'minuun":
ثم إنكم بعد ذلك لميتون ثم إنكم يوم القيامة تبعثون
“Kisha nyinyi baada ya hayo, ni wenye kufa. Kisha hakika nyinyi Siku ya
Qiyaamah mtafufuliwa.”(23:15-16)
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:
"Mimi ndo mtu wa kwanza atakayetoka ndani ya kaburi siku ya Qiyaamah.
Mimi ndo muombezi wa kwanza. Mimi ndo wa kwanza ambaye shafaa´ah
uombezi wake utakubaliwa. "
Ninaomba baraka na salaam za Mola Wake ziwe pamoja naye.
Aayah na Hadiyth hii tukufu - na Aayah na Hadiyth zingine – zinatoa dalili ya
kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na wengine wote wamekufa
au watakufa. Watatoka katika makaburi yao siku ya Qiyaamah. Suala hili
wamekubaliana juu yake wanachuoni wa Waislamu. Kwa hivyo, Waislamu wote
wanatakiwa kuzingatia masuala haya. Aidha, ni lazima watahadhari na Bid´ah
na ukhurafi wa watu wajinga na mfano wao waliozusha. Allaah Hakuteremsha
dalili yoyote kuhusiana na masuala haya.
Mwandishi: Imaam 'Abdul-' Aziyz bin 'Abdillaah bin Baaz
Fataawaa Arkan-ul-Islam, uk. 109-110
Daar-ud-Daa'iy, 1420
11. Hukumu Ya Kusherehekea Maulidi Msikitini
18
Swali:
Inajuzu kwa Waislamu kusherehekea sikukuu katika Misikiti kumbukumbu ya
usiku wa Maulidi [kuzaliwa] kwa Mtume katika tarehe ya kumi na mbili Rabiy'
al-Awwal bila ya kuzembea katika siku hii kama mtu alivyo siku ya 'Iyd?
Tulipata maoni tofauti katika suala hili na baadhi ya wengine wakasema kuwa ni
Bid'ah nzuri wakati baadhi wakasema sio Bid'ah nzuri.
´Allaamah Ibn Baaz:
Haijuzu kwa Waislamu kusherehekea siku ya Maulidi ya Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam), sawa ikiwa yatafanyika tarehe kumi na mbili Rabiy'
al-Awwal au siku nyingine yoyote, kama jinsi haijuzu kusherehekea kuzaliwa
kwa mtu mwengine yeyote. Kusherehekea kuzaliwa ni Bid'ah katika Dini.
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) hakusherehekea kuzaliwa kwake
katika maisha yake na yeye ni mjuzi zaidi wa Mola katika Dini na Shari´ah.
Hakuamrisha hilo na wala halikufanywa hilo na Makhalifah wake waongofu,
Maswahabah wengine au mtu mwingine katika wao ambaye kawafuata kwa
wema miongoni mwa karne tatu bora. Kutokana na hili mtu anapata kujua ya
kwamba jambo hili ni Bid'ah. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:
"Yule mwenye kuzusha kitu kisichokuwa humo na amri yetu kitarudishwa." (al-
Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).)
Katika mapokezi mengine ya Swahiyh Muslim kumesemwa:
"Yule ambaye atafanya ´amali isiyokuwa humo na amri yetu atarudishiwa
mwenyewe."
Imaam 'Abdul-'Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Fataawaaa al-´Ulamaa´ Balad al-Haraam, uk. 467
19
12. Shaykh Ibn ´Uthaymiyn Akiwaombea Du´aa Waliopotea
Katika Bid´ah Ya Maulidi
Swali:
Wanadai watu hawa ya kwamba wanampenda Mtume, wakaleta sherehe ya
Maulidi. Ipi hukumu ya kusherehekea Maulidi kwa vile wao wanadai ya
kwamba ni kumpenda Mtume?
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Hili swali limeshaulizwa sana nikalijibu. Mwenye kumpenda Mtume, basi afuate
Sunnah zake. Mwenye kumpenda Mtume, basi asizue katika Dini ya
Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na wala haifai juu yetu wala
kwa mwengine [... sauti haiko wazi... ] kwa Mtume na ubainisho.
Tunachowaombea kwa Allaah (Ta´ala) Awaongoze ndugu zetu katika Njia
iliyonyooka.
Yaa Subhaana Allaah! Yuko wapi Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy,
Maswahabah katika jambo hili au hawakuyajua au waliyapuuza? Ni moja katika
mambo haya; ima hawakujua haki ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
kwa kutofanya kwao Maulidi au walipuuza. Karne tatu [bora] zote zinapita
hawakufanya Bid´ah hii halafu tunasema kuwa yanajuzu na kwamba
yanapendwa na Allaah na Mtume Wake na wanayoyafanya? Haiwezekani.
Isitoshe, Maulidini kunatokea maovu makubwa na kuchupa mipaka kwa Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna mambo mengi.
Tunamuomba Allaah (Ta´ala) Aturuzuku sote kumfuata Mtume, Imani
isiyokuwa ndani yake na mapungufu, yakini isiyokuwa ndani yake na shaka,
Ikhlaasw isiyokuwa ndani yake Shirki, kufuata kusiokuwa ndani yake na kuzua.
Chanzo: http://youtu.be/EBbhs_vJOdE
20
Wanachuoni Wa Khalaf
13. Inajuzu Kusherehekea Maulidi Kama Ada Tu Na
Si ´Ibaadah?
Swali:
Sisi tunasherehekea siku ya Maulidi kama ada na hapana ´Ibaadah?
Shaykh as-Suhaymiy:
Bali kwa watu wengine ni ´Ibaadah; wanasoma, wanamdhukuru, wanasoma
mashairi na Anashiyd. Yote haya wanayafanya... Hata ikiwa mnayafanya kama
ada, je Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walifanya kuwa ada?
ابقون سان والس بعوهم بإحأ نصار والذين ات مهاجرين والأ لون من الأ و الأ
"Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn
(waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (waliowasaida na kuwanusuru
Muhaajiriyn katika wakaazi wa Madiynah), na wale waliowafuata kwa ihsaan."
(09:100)
Kuwa katika wale waliowafuata kwa wema.
Chanzo: http://youtu.be/r2ZckS6aH6c
14. Maulidi Hayakufanywa Na Mtume Wala Maswahabah
Swali:
21
Ipi hukumu ya kusherehekea Maulidi ya Mtume?
´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh:
Sisi tunasema, kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni msingi
katika mambo ya msingi ya Dini na ni katika mambo yanakamilisha Dini.
“Hatoamini mmoja wenu mpaka mimi niwe napendwa kwake zaidi kuliko
watoto wake, wazazi wake na watu wote.”
Waislamu wanajua hilo. Sherehe ya Maulidi tukiangalia asli yake haikupatikana
isipokuwa baada ya karne tatu bora. Imekuja kupatikana katika karne ya tano au
baada yake. Na wala hayakuwa hata yakitajwa katika karne ya kwanza, ya pili
wala ya tatu. Na wala Maswahabah na waliokuwa baada yao hawakuwa
wakiyajali: Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy walikuwa wakijua usiku wa
Maulidi [kuzaliwa] na kufa kwa Mtume lakini hawakuyajali. Na wala hakufanya
siku ya kumi na mbili [Rabiy´ al-Awwal] Khutbah, kusoma, ukumbusho na
Qaswiydah. Hawakufanya haya. Haina maana walipunguza katika haki za
Mtume, lakini hawakuwa na msingi wanaoutegemea.
Msiba ni kwamba, kuna baadhi ya Suufiyyah wanafanya makosa makubwa. Na
kama mlisikia mkanda kuhusu Maulidi, ni mambo maovu sana kukiwemo
taarabu na nyimbo yanayofanywa ambayo Mtume yuko mbali nayo.
Kisha usiku wa mwisho, wanaamini ya kwamba roho ya Mtume inawahudhuria
na kwamba wanaona roho yake na kadhalika katika mambo ya ukhurafi na
uongo na batili. Kunaimbwa Qaswiydah za Shirki kumsifu Mtume na
kumuomba shafaa´ah uombezi kutoka kwake n.k. Mtume yuko mbali kabisa na
yote haya.
Enyi ndugu zangu! Kumpenda Mtume wa Allaah ni kufuata Sunnah zake.
Kumsifu Mtume wetu si katika siku maalum, hapana! Bali ni katika kila siku;
katika kula kwetu, kunywa kwetu, Swalah yetu, Wudhuu wetu, kutembea
kwetu na katika harakati zetu zote. Usitenge siku maalum. Bali ni jambo la
daima na milele. Swalah na salaam zimwendee.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=55y01uXEDv4
22
15. Tofauti Kati Ya Sherehe Ya Maulidi Na Siku Ya Taifa
Swali:
Baadhi ya watu wanaona kujuzu kusherehekea Maulidi, licha ya kwamba
yamezushwa, wanasema ni sawa na sherehe zingine zinazoadhimishwa kama
vile Siku ya Taifa.
´Allaamah al-Fawzaan:
Sherehe ya Maulidi ni jambo la kidini na huchukuliwa ni Bid´ah. Ama kuhusiana
na Siku ya Taifa, huku ni kujifananisha na makafiri ambao wanaadhimisha siku
zao za kitaifa na sherehe. Ina maana ni kujifananisha nao. Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:
"Yule mwenye kujifananisha na watu basi [mtu huyo] ni katika wao."
'Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzan
Mhadhara: al-Fitan wa Mawqif-ul-Muslim Minhaa
Chanzo: http://alfawzan.ws/allmohadrat?page=2
16. Maulidi Yana Bid´ah Na Shirki
Swali:
Je, Bid´ah ya kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) ni Bid´ah khafifu inayotujuzushia kukaa na wanayoifanya au hapana?
23
´Allaamah al-Fawzaan:
Kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Bid´ah
bila ya shaka. Kwa kuwa ni kitendo ambacho hakikufanya Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam), Makhalifah wake waongofu wala karne bora. Wala
hayakuzushwa isipokuwa baada ya karne ya nne, wakati utawala wa
Faatwimiyyuun, ambao ni Mashia wanaotoka magharibi. Wao ndio walikuja na
Bid´ah ya Maulidi. Hivyo ni Bid´ah bila ya shaka.
Isitoshe, yanaingia kitu katika Shirki, nayo ni kumuomba msaada Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuomba atatue haja na kumshtakia kwa
mambo yaliowasibu Waislamu. Wanamshtakia Mtume na wala hawamshtakii
Allaah (Jalla wa ´Alaa). Na wala hawamuombi msaada Allaah, wanamuomba
msaada Mtume katika mnasaba huu. Na wao wanajua ya kwamba hutokea kitu
katika haya. Hivyo yamejumuisha baina ya Bid´ah na baina ya Shirki.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=164 &
http://www.youtube.com/watch?v=zC27-UOohPY
17. Kupeana Hongera Siku Ya Maulidi
Swali:
Je, inajuzu kupeana hongera siku ya Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kila Bid´ah haijuzu kuifanya na wala haijuzu kupeana hongera kwayo, kwa
kuwa kupeana hongera ni kuiridhia na kuishaji´isha5. Na wajibu ni kinyume
chake, kukataza na si kupeana hongera.
5 Kuipa nguvu
24
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=240 &
http://www.youtube.com/watch?v=clh2iXpO-hE
18. Kufanya Maulidi Ni Bid´ah
´Allaamah al-Luhaydaan:
Bila ya shaka, kufanya Maulidi ni Bid´ah. Kwa hakika haya Maulidi hayajulikani
kuwepo kwake katika uhai wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam), wala katika uhai wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), wala
katika uhai wa Taabi´iyn6, wala katika uhai wa maimamu wanne, wala uhai wa
wanafunzi wao. Hayakujulikana katika ulimwengu wa Uislamu kitu
kinachoitwa Maulidi kabisa. Sehemu ya kwanza yalipopatikana ni Misri,
yalizusha na Faatwimiyyuun, dola iliyokuwa chafu ya maovu; al-Baatwiniyyah.
Na yalipoanza kusambaa, katika watu wa Ahl-us-Sunnah mtu wa kwanza
aliyeanza kuyasambaza ni mfalme aitwae Irbil Iraaq kutokana na ujinga wake
wa kuwaiga manaswara ambao na wao wanaadhimisha siku ya ´Iysa (´alayhis-
Salaam). Wakakataza wanachuoni hilo. Yakaendelea kukua mpaka yakaenea leo
katika ulimwengu wa Uislamu. Maulidi yanaingia katika maneno ya Mtume:
“Na tahadharini na mambo ya kuzua, kwa hakika kila kitakachozushwa ni
Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu."
Na yanaingia katika maneno ya Mtume:
"Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo amri yetu, atarudishiwa."
Mtu asijikurubishe kwa kitu anachokizingatia kuwa ni utiifu na kujikurubisha
kwa Allaah isipokuwa kwa dalili. La sivyo atarudishiwa mwenyewe. Na
kuichukulia siku hii kama ´Iyd, na pengine kukafanywa makubwa zaidi ya
yanayofanywa katika ´Iyd. Mtume alipoenda Madiynah na walikuwa Answaar
na siku ambazo wanasherehekea, akawaambia:
"Allaah Amewapa badala ya sikukuu za Kijaahiliyyah, Amewapa Idi al-Fitwr na
Id-ul-Adhhaa."
6 Waliokuja baada ya Maswahabah
25
Chanzo:
http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarsubject&schid=30981
& http://www.youtube.com/watch?v=etf2lUZSpZA
19. ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Madu´aat Wanaohudhuria
Katika Maulidi
Swali:
Baadhi ya watu wa Bid´ah Suufiyyah na khasa Tijaaniyyah katika mji wetu wana
harakati mbali mbali kwa mnasaba wa kusherehekea Maulidi. Kunakuja baadhi
ya Madu´aat na wanahudhuria nao na wanawaombea mwishoni siha na afya na
Du´aa nyinginezo katika Mashaykh wa Suufiyyah walioandaa mambo haya. Ipi
hukumu ya mambo kama haya na kuhudhuria Madu´aat hao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu anaafikiana nao na kuwasifu. Halijuzu hili, halijuzu hili. Isipokuwa tu
wakati tu pale unapohudhuria unawakataza na kuwabainishia kuwa hili
halijuzu na wasifanye mambo haya na si sawa. Walinganie kwa Allaah kabla na
la sivyo jendee zako waache. Usikae nao, unaafikiana, ukala nao chakula
ukapiga nao vijicheko. Ukadai ni kuwalingania [Da´wah]! Hapana katu hii si
Da´wah.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=252 &
http://www.youtube.com/watch?v=VK1EA5bDcio
20. Kufunga Siku Ya Maulidi Ya Mtume (´alayhis-Salaam)
26
Swali:
Inajuzu kufunga siku ya kuzaliwa kwa Mtume?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, ni Swawm ambayo Haikuweka Allaah wala Mtume Wake na wala
haikuwekwa kwetu kufunga. Naam, siku ya Juma tatu unafunga, hapana ya
tarehe 12 Rabiy´ al-Awwal - unafunga Juma tatu kwa kila wiki, hii ni Sunnah.
Ama tarehe 12 ya Rabiy´ al-Awwal ikikutana na siku ya Juma tatu
unasherehekea [na kufunga] kwa kuwa imeangukia siku ya Maulidi, hapana
haijuzu hili.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=AZNuq_-Nm7w
21. Je, Kusherehekea Maulidi Ni Katika Kumpenda Mtume
(´alayhis-Salaam)?
Swali:
Je, kusherehekea Maulidi ni katika kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Hili ni katika Bid´ah. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
hapendi Bid´ah.
Kasema:
27
”Na tahadharini na mambo ya kuzuliwa...”
Mtume hapendi Bid´ah na anaikataza. Vipi utadai ya kwamba unampenda na
hali ya kuwa unamuasi? Unapenda maadui wa mpenzi [Mtume] kisha unadai
unampeda? Mapenzi yako yako wapi?
Na wakasema wengine [washairi]:
”Lau mapenzi yako yangekuwa ya kweli basi ungelimtii, hakika mwenye kupenda kwa
yule ampendae humtii.”
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa
22. Sikukuu Za Makafiri Kama Krismasi Na Za Waislamu
Kama Maulidi
Swali:
Ipi hukumu ya kusherehekea sikukuu, iitwayo "Sikukuu ya manaswara", au
"Krismasi". Ipi nasaza yako kwa Waislamu ambao wanashiriki katika hili na
wanapeana zawadi na kuwapa pongezi n.k.?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kwa Muislamu kushiriki sikukuu za manaswara - hata sikukuu za
Waislamu ambazo zimezushwa. Kama Maulidi na kadhalika, sherehe ya Maulidi
- haijuzu kwa kuwa ni sherehe za Bid´ah.
Na sikukuu za manaswara ni sikukuu za Bid´ah na Shirki, kwa kuwa wao
hufanya kwa kuitakidi kama ´Ibaadah kwa ´Iysa (´alayhis-Salaam).
Haijuzu kuwashaji´isha kwa hili wala kuwapongeza. Kule kuwapa tu pongezi ni
jambo lisilojuzu. Vipi kwa yule ambaye anahudhuria kwao? Hata kuwauzia,
asiwauzie mtu vifaa ambavyo vitawasaidia kufanya hayo Maulidi. Wala mtu
asiwape pongezi kwayo, wala asiwauzie kwa haya Maulidi na wala asile katika
kichinjo chao. Muislamu anatakiwa awasuse kabisa kwa haya Maulidi.
28
Kama alivyosema hilo al-´Allaamah Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na
mwanafunzi wake Ibn-ul-Qayyim katika kitabu "Ahkaam Ahl-idh-Dhimmah."
Ni wajibu kujiweka mbali kuwashiriki katika mambo haya, kwa kuwa haya ni
katika Dini yao. Na sisi tumekatazwa kuwashaji´isha au kuwasaidia katika
Kufuru zao na Shirki zao.
Chanzo: http://youtu.be/-wHD0HfeV18
23. Wajinga Wanaodanganywa Kwamba Kusherehekea
Maulidi Ni Kumpenda Mtume
Swali:
Ipi hukumu ya kusherehekea Maulidi ya Mtume katika Shari´ah ya Kiislamu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hukumu ya kusherehekea Maulidi ya Mtume ni katika Bid´ah kwa Ahl-us-
Sunnah wal-Jamaa´ah na hayakufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) na ni kuzaliwa kwake, maisha yake yote. Na hayakufanywa na
Makhalifah wanne waongofu ambao ni wenye ufahamu zaidi wa Ummah na
wenye kumpenda zaidi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Na hayakufanywa na Swahabah yoyote katika Maswahabah kamwe, na wala
waliokuja baada yao katika wanachuoni mpaka siku ya Qiyaamah.
Hivyo ni katika Bid´ah ambayo inakuwa na shari ambayo watu hawawezi kuwa
wajinga kwayo, kama mchanganyiko, mashari – burdaa ya al-Buswiyriy7
7 ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu at-Tijaaniyyun Na Burda Swali: Katika mji wetu Tijaniyyuun [kipote cha Mashia na Masufi] wanamrehemu Buswiyriy [Gogo la Suufiy aliyetunga Qaswiydah ya Burdaa, kaburi lake liko ndani ya Msikiti Misri] na wanamtakasa.
29
ambayo iko na Shirki na uongo. Wanasema Mtume anadhudhuria pamoja na
wao katika usiku ambao kutakuwa sherehe ya Maulidi wanadai ya kwamba
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anahudhuria usiku ule pamoja nao.
Na huu ni katika uongo kwa Allaah na Mtume Wake (´alayhis-Swalaat was-
Salaam).
Hawa watu wajinga katika Suufiyyah wapotofu na katika watu wajinga ambao
hawana elimu na ambao huwadanganya na kusema ”nyinyi mnampenda
Mtume wa Allaah” kwa kusherehekea kuzaliwa kwake.
Watu watahadhari kutokana na Bid´ah hii ambayo imebainishwa upotofu wake
na wanachuoni wa zamani na wa sasa.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=4e3oXfa-vjk
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na
Maswahabah ajmaa´iyn.
´Allaamah al-Fawzaan: Si katika mji wenu tu, ni kila mahala. Baadhi yao wanasema Burdaa ni bora kuliko hata Qur-aan. Hivyo ndo maana hawaipi umuhimu Qur-aan. Wanaipa umuhimu Burdaa, wanaihifadhi, wanaiimba kila wakati. Huu ni upotevu - A´udhubi Allaah. Huu ni mtihani khasa ukizingatia Burdaa ina baadhi ya maneno maalumu, ya kupambia, kuimbika vizuri. Hii ni fitina - Allaah Atukinge. Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=252