Upload
duongnhan
View
216
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Januari 2016
Kitabu hiki cha Kiswahili kimetayarishwa na kuchapishwa chini ya mradi
wa TUSOME. Kimeandikwa kufuatia mwongozo wa mawanda na mfuatano
uliofanyiwa utafiti wa hali ya juu kwa miaka mitatu katika mradi wa kuboresha
ujuzi wa hisabati na usomaji nchini. Utafiti huu uliegemea kubuni njia mwafaka za
kufunza usomaji na ufahamu.
Vipengele muhimu na vya kipekee kuhusu hiki kitabu ni:
• Kitabu hiki kinafuata mtaala wa taifa la Kenya.
• Mazoezi ya somo yamefuata mpangilio wa mantiki kutokana na utafiti wa njia
bora za kufunza Kiswahili katika darasa la kwanza na la pili.
• Kitabu hiki kina michoro ya kupendeza ambayo hufanya somo la Kiswahili liwe
la kuvutia.
• Masomo katika kitabu hiki hujumuisha vijenzi vyote vya lugha ambavyo ni;
kusikiza, kuongea, kusoma na kuandika.
• Mpangilio wa kitabu hiki umekusudia kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa
uzoefu kwa sababu kinawapatia nafasi ya kukumbana na vijenzi vyote vya
kusoma.
Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili
kutoka kwa Shirika la maendeleo ya
kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)
na Idara ya maendeleo ya kimataifa ya
Uingereza (DFID/Kenya) kupitia mradi wa
Tusome Early Grade Reading Activity.