142

Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

Embed Size (px)

Citation preview

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 1/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 2/142

MIONGOZO MIWILI

KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA

 AZIMIO LA ARUSHA 

 Yamekusanywa na kuhaririwa na:

Bashiru Ally Saida Yahya-Othman

Issa Shivji

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAMKigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika Umajumui wa Afrika

S. L. P. 35091, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2410 763Barua pepe: [email protected] Tovuti: nyererechair.udsm.ac.tz

Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili wa Shirika la HakiElimu katika maadhimisho ya Tamasha la Tano la Kitaaluma la Julius Nyerere, Aprili 10-12, 2013, lililoandaliwa

na Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika Umajumui wa Afrika,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

      I      G      O     D      A

     C    H     A 

 

    T   A   A    L  U M

 A  CH  A  M  W   

 A   L   

I     M   U     

 N      Y  E   R  E   R

      K

   E

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 3/142

      I      G      O     D      A

     C    H     A 

 

    T   A   A    L  U

 M A  

CH  A  

M  W    A   

L   I     M   

U      N      Y  E   R  E   R

      K   E

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAMKigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika Umajumui wa Afrika

S. L. P. 35091, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2410 763Barua pepe: [email protected] Tovuti: nyererechair.udsm.ac.tz

Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili wa Shirika la HakiElimu katika maadhimisho ya Tamasha la Tano la Kitaaluma la Julius Nyerere, Aprili 10-12, 2013, lililoandaliwa

na Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika Umajumui wa Afrika,

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

ISBN 978-9987-9418-2-7

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 4/142

MIONGOZO MIWILI 3

YALIYOMO

Dibaji 4

Utangulizi: Ujio na uzito wa Miongozo Miwili 11Kingunge Ngombale Mwiru

Sura ya Kwanza 23  Azimio la Arusha la 1967

Sura ya Pili 43  Mwongozo wa TANU wa 1971

Sura ya Tatu 55  Mwongozo wa CCM wa 1981

Sura ya Nne 116  Maamuzi ya Zanzibar ya 1991

Sura ya Tano 132Miongozo Miwili ya Chama na tabaka lililopindua UjamaaIssa Shivji

 

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 5/142

MIONGOZO MIWILI4

DIBAJI

Kitabu hiki kimeandaliwa na Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere

kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya matukio muhimu katika historiaya nchi yetu tangu Uhuru. Kuna nyaraka nne katika kitabu hiki:  Azimio

la Arusha la 1967 , Mwongozo wa 1971, Mwongozo wa 1981 na Maamuzi

 ya Zanzibar ya 1991, ambayo ni hotuba ya Mzee Ali Hassan Mwinyi. Kwa

nini tumechagua nyaraka hizo na sio nyengine? Kwa sababu kila nyaraka

ina muhula wa kihistoria wa kuhadithia. Muongo mmoja kati ya 1971

na 1981 ni kipindi cha uzalendo wa hali ya juu, uzalendo wa mrengo wa

kushoto, uliozaliwa na itikadi ya Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism).

Kipindi hiki kilipewa jina rasmi la kipindi cha ‘Ujamaa na Kujitegemea’.

Mwongozo wa 1981 ni waraka wa kipekee ambayo inafanya uchambuzi

wa miaka 14 ya Azimio kwa mtazamo wa kitabaka, ambao, lazima tukiri,

haukuwa mtazamo wa Chama wala Mwalimu.

Muongo wa 1981 mpaka 1991 ni kipindi cha mpito kutoka muhula

wa kizalendo na kuingia muhula wa uliberali mambo-leo. Maamuzi ya

 Zanzibar ya 1991 (kwa msamiati wa kisiasa huitwa ‘Azimio la Zanzibar’),

ni hotuba ya Rais wa Awamu ya Pili, inayoelezea na kuhalalisha mtazamo,

mwelekeo, itikadi na sera za uliberali mambo-leo.

Baada ya kuchagua nyaraka hizi, tukamuomba Mzee Kingunge Ngombale

Mwiru, kutuandikia Utangulizi wa Miongozo Miwili. Mzee Ngombale

anajulikana kwa sifa yake – ambayo anaistahili - ya kuzungumzia itikadi

na nadharia ya Chama kwa ufasaha, na kwa undani; ni kingunge hasa

wa itikadi ya Chama. Yeye amekuwa mwanaitikadi (ideologue) wa Chama

kwa miongo kama minne hivi. Umahiri wake wa kiitikadi unadhihirishwa

vema na ukweli usiopingika kwamba amekuwa msemaji mkuu wa itikadi

ya Chama katika awamu zote za utawala wa kisiasa nchini – kuanzia

awamu ya Mwalimu, ambayo ilikuwa awamu ya kizalendo; kupitia awamu

ya Mzee Ali Hassan Mwinyi ambayo ilikuwa awamu ya mpito kuelekea

kwenye uliberali mambo-leo; ikifuatiwa na awamu ya Mheshemiwa

Benjamin William Mkapa, ambayo ilikuwa awamu ya kuiimarisha bila

vikwazo misingi mikuu ya uliberali mambo-leo, au kwa msamiati wake

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 6/142

MIONGOZO MIWILI 5

mwenyewe, utandawazi; kuikia kipindi cha kwanza cha Mheshemiwa

Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amefuata nyayo za Mzee Mkapa na kwa

mara ya kwanza utawala wake umeanza kuonja joto kali la uchumi wa

ubepari wa kimataifa.

Ili tuweze kuelewa kwa ufasaha na kwa kina, hasa chimbuko la

Miongozo Miwili na umuhimi wake wa kihistoria, tumeweka makala

ya mwanazuoni Issa Shivji, iliyoandikwa kwa mara ya kwanza mnamo

2009, inayochambua Miongozo hii kwa mtazamo wa kitabaka.

 Azimio la Arusha, 1967

Miaka sita tu baada ya Uhuru wetu mnamo 1961, chama tawala,TANU, ambacho kwa asili na hulka yake tunaweza tukakiita chama

cha ukombozi, kilitangaza  Azimio la Arusha (ang. Sura ya Kwanza).

Azimio lilikuwa ni dalili ya kutambua kwamba uhuru wa nchi na watu

wake haukamiliki kutokana na kupata wimbo na bendera ya kitaifa au

mawaziri na viongozi wazawa.

Uhuru wa kinchi kilichotawaliwa na wakoloni ni hatua ya kwanza, ya

awali kabisa, katika mchakato wa ukombozi. Ukombozi katika jamii kamayetu una pembe tatu. Kwanza kuna uhuru wa nchi, kwa maana kwamba,

huwezi ukawa huru katika nchi ambayo inatawaliwa kimabavu na nchi

ya nje. Pili, kuna uhuru wa watu au jamii katika nchi. Unaweza ukawa na

nchi huru bila ya watu kuwa huru, kwa maana kwamba hawana uwezo

wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Ingawa nchi yao ni huru, lakini bado

wanajikuta kwamba kuna kundi au tabaka dogo la watu wanaowatawala

na kufanya maamuzi kwa niaba yao au kwa ajili ya waliowengi. Katika

hali yetu halisi, tabaka-tawala la ndani linakuwa bado chini ya himaya ya

ubeberu na kwa hiyo watawala hao wanakuwa vibaraka wa matabaka-

tawala ya kibeberu. Na hali hii inasababisha, sio tu tabaka-tawala la ndani

kuwa tegemezi, lakini hata nchi yenyewe inakuwa tegemezi kwa sababu

inakosa uongozi unaojitegemea na kufanya maamuzi kwa manufaa na

maslahi ya watu wake.

Pembe ya tatu ya ukombozi ni ukombozi wa wavujajasho kutoka makucha

ya unyonyaji na ukandamizaji. Na ukombozi wa kijamii-tabaka (social

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 7/142

MIONGOZO MIWILI6

emancipation) hauwezi kupatikana bila kufanya mapinduzi ya mfumo

wenyewe wa uzalishaji na utawala; kwa sababu unyonyaji na ukandamizaji

havitokani na nia, dhamira au lengo la mtu binafsi. Hakuna mtu anayezaliwa

akiwa mnyonyaji. Tabaka la wanyonyaji linatokana na nafasi yao katikamfumo wa uzalishaji. Ukiwa bepari, bila kujali usamaria mwema wako,

lazima utakuwa mnyonyaji. Ndivyo ulivyo mfumo wa kibepari.

 Azimio la Arusha  lilizungumzia pembe zote tatu za ukombozi. Mosi,

lilitambua kwamba uhuru wa nchi hautakuwa na maana wala hautakuwa

salama kama tukiendelea kuwa tegemezi, yaani, kutegemea misaada,

mikopo na uwekezaji kutoka nje. Kwa sababu mikopo haitapatikana

ya kutosha na hiyo kidogo itakayopatikana itaambatana na mashartiyatakayoididimiza nchi zaidi. Isitoshe, hata kama tungepata misaada,

mikopo na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo, vitahatarisha uhuru

wetu. ‘Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli hakuwezekani

ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya Taifa jingine kwa

maendeleo yake.’ (ang. Sura ya kwanza, uk) Ukweli huu unajidhihirisha

wazi tukiangalia mwenendo wetu wa kama miongo miwili iliyopita.

Tumekuwa tegemezi sana kiasi kwamba leo hii hatuna uhakika kwamba

tunajitawala au tunatawaliwa na wawekezaji na ‘wafadhili’ wa nje, yaani,

nchi za kibeberu.

Pili,  Azimio  liliainisha matabaka-nyonyaji na matabaka-nyonywaji -

mabepari na makabaila kwa upande mmoja na wakulima na wafanyakazi

kwa upande mwingine. ‘Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi:

haina ubepari wala ukabaila.’ (ang. Sura ya kwanza, uk.25)

Hata hivyo, mkakati wa Azimio wa kujikomboa kutokana na unyonyajiulikuwa ni kutaiisha njia kuu za uchumi kwa maana ya serikali kumiliki

na kudhibiti viwanda vikubwa, migodi, mabenki, taasisi nyingine za

fedha, na biashara za nje na ndani. Ni ukweli usiopingika kwamba Azimio

lilitambua kwa dhati kuwa haitoshi serikali kumiliki njia za uchumi

kama serikali yenyewe sio ya kidemokrasia, kwa maana ya kudhibitiwa

na kuwajibika kwa wananchi. Hata hivyo, kama tutakavyobainisha hivi

punde, katika suala la demokrasia Azimio halikufanikiwa, pamoja na

kuwa na nia njema ya kukomboa wanyonge. Wanyonge hujikomboa wao

wenyewe kupitia vyombo vyao na huendeleza mapambano ya kitabaka

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 8/142

MIONGOZO MIWILI 7

kwa ustadi na kwa kutumia mikakati yao wenyewe. Mapinduzi kamwe

sio fadhila ya wakubwa au wasamaria wema.

Mwongozo wa 1971Baada ya miaka minne tu ya  Azimio, TANU ikapitisha nyaraka nyingine

ya kihistoria, Mwongozo wa TANU (ang. Sura ya Pili). Msimamo wa

Mwongozo  ulikuwa wa kimapinduzi zaidi kuliko ule wa  Azimio. Mzee

Ngombale, katika Utangulizi wake wa kitabu hiki anaeleza kwa ufasaha

chimbuko la Mwongozo wa 1971 na maudhui yake. Aidha anasisitiza

ibara muhimu za Mwongozo kuhusu ulinzi wa Taifa dhidi ya ukoloni wa

Kireno na Kikaburu ambao waliendelea kukalia nchi za Afrika ya kusini.Kwa msimamo thabiti wa Mwalimu, vita vya ukombozi katika nchi za

Msumbiji, Angola na Afrika ya kusini, viliungwa mkono na Tanzania

kwa hali na mali. Kwa hivyo, Tanzania yenyewe ilikuwa katika hatari ya

kuvamiwa au kushambuliwa. Ili kujilinda dhidi ya uwezekano huo, ndipo 

Mwongozo  wa 1971 ukaweka sera ya kuwa na Jeshi la Wananchi, kwa

maana ya mgambo.

Kama anavyoeleza Mzee Ngombale, wananchi, hasa wafanyakazi

viwandani, walishawishika sana na wakajitolea kujiunga na mgambo. Ni

sahihi kabisa kwa Mzee Ngombale kusisitiza kwamba sera hii ilifanikiwa

kiasi kwamba wakati nchi yetu ilipovamiwa na nduli Iddi Amin Dada,

dikteta wa Uganda, askari wa mgambo walipigana kwa ustadi na ujasiri.

Mchango wao kamwe hauwezi kusahaulika.

Lakini, kwa mtazamo wa kitabaka, nafasi mahsusi na ya kihistoria ya

Mwongozo  inatokana na ibara yake ya 15. Ibara hii ambayo ilishutumu

tabaka chipukizi wakati huo la warasimu viwandani na serikalini ilikuja

kuwa panga na ngao ya tabaka la wafanyakazi kuibua na kuendeleza

mapambano yao dhidi ya tabaka la vibwenyeye wa kirasimu. Katika

historia ya mapambano ya tabaka la wafanyakazi nchini mwetu, hakuna

kipindi kilichokuwa na msisimko mkubwa kama hiki (1971-1975). Kwa

sababu ambazo haziko wazi, Mzee Ngombale, ingawa anagusia ibara

ya 15 katika  Utangulizi  wake, hakuchambua kwa undani umuhimu

wa kipekee wa ibara hii katika mapambano ya kitabaka. Hata hivyo,

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 9/142

MIONGOZO MIWILI8

wasomaji wanaweza wakaangalia makala ya uchambuzi ya Shivji (ang.

Sura ya Tano) kuhusu mapambano hayo. Mapambano hayo, hatimaye,

yalidhooishwa na kukosa nguvu na uhalali kwa tamko la Mwenyekiti wa

Chama, naye sio mwingine isipokuwa Mwalimu. Katika hotuba yake yaMei Mosi mwaka 1974 Mwalimu alihoji: Mnapogoma mnamgomea nani?

akiwa na maana kwamba kwa kuwa viwanda na mashirika yalikuwa

mali ya ‘umma’, wakiwemo wafanyakazi wenyewe, basi walikuwa

wanajigomea wenyewe!

Jibu la swali la Mwalimu kwamba wafanyakazi walikuwa wanamgomea

nani lilipatikana katika uchambuzi wa Mwongozo wa 1981.

Mwongozo wa 1981Mchakato wa kuandaa Mwongozo wa 1981, kama ulivyoelezwa na Mzee

Ngombale, ni wa kipekee na ni tofauti na taratibu za Chama zilizozoeleka.

Kwanza, tuuelewe muktadha wa mchakato wenyewe. Kipindi cha

mwisho cha utawala wa Mwalimu, 1980-85, kilikuwa kigumu kupita

kiasi kutokana na sababu mbalimbali. Hapa sio mahali pake kuangalia

kwa undani sababu hizo isipokuwa kusisitiza tu kwamba ilikuwa katika

hali hii ndipo Mzee Ngombale mwenyewe alipoonyesha dhamira yake

ya kupendekeza kwamba Chama hakina budi kuzungumzia hali hii. Kwa

hivyo, mchakato wa Mwongozo haukuanzia katika sekretariati ya Chama

wala Kamati Kuu. Badala yake, ulianza kutokana na pendekezo lililotolewa

na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama (NEC), yaani Mzee Ngombale

mwenyewe. Pili katika kikao hikihiki cha NEC, kamati ya kuandaa

Programu, ikiwa ni pamoja na kufanya uchambuzi kosoa, ilichaguliwa.

Na kinyume na taratibu zilizozoeleka za Chama, aliyewasilisha Programukatika Mkutano Mkuu alikuwa Mzee Ngombale na sio Mwenyekiti,

yaani Mwalimu mwenyewe. Kwa mujibu wa Mzee Ngombale, Mwalimu

alipendekeza kwamba nyaraka iitwe Mwongozo badala ya programu

kwa sababu wanachama walikuwa hawajazoea msamiati wa Programu.

Katika Utangulizi  wake, mwandishi anaweka mkazo katika ibara za

Mwongozo wa 1981 zinazozungumzia suala la demokrasia katika

Chama na muundo wa Chama. Pia anatuarifu kwamba vyombo vyaChama vilizungumzia Mwongozo. Kwa kadri ninavyokumbuka mimi,

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 10/142

MIONGOZO MIWILI 9

Mwongozo wa 1981 haukuwa gumzo la wananchi katika ujumla wao

kama ulivyokuwa ule wa 1971. Kwa kiasi kikubwa, Mwongozo wa 1981

ama ulisahaulika au ulisahaulishwa. Hakuna kumbukumbu zozote

zinazoonyesha kwamba Mwongozo wa 1981 ulipigiwa debe au kufanyiwakampeni au kuzungumziwa mitaani na matawini. Wazee wengi wa

chama waliokuwepo wakati ule, ukiwauliza juu ya Mwongozo wa 1981,

wanakuwa ama wanachanganya mambo au wanajifanya hawaukumbuki.

Hatuna ushahidi wa moja kwa moja, lakini ushahidi wa mazingira na

hali halisi unatulazimisha kujenga hoja kwamba Mwongozo wa 1981

haukuwa utashi wa viongozi wakuu wa CCM. Mwongozo wa 1981

unatahadharisha kwamba tayari kulikuwa na watu/wanachama ambaowalikuwa wananung’unika na kusema kichinichini kwamba Ujamaa

ulishindwa na kulikuwa na haja ya kubadili mtazamo na mwelekeo wa

nchi. Mwongozo ulisema kwa ufasaha kwamba chini ya mwavuli wa

 Azimio na sekta ya umma lilijengeka tabaka la vibwanyenye wa kirasimu

(bureaucratic bourgeoisie) ambalo lilikuwa linahujumu Ujamaa. Kwa

mara ya kwanza katika nyaraka ya Chama, mapambano ya kitabaka

yalizungumziwa waziwazi bila kutafuna maneno.

Makala ya Shivji (ang. Sura ya Tano) inajaribu kufanya uchambuzi

wa ibara muhimu za Mwongozo wa 1981. Hitimisho la makala hiyo

ni kwamba tabaka linaloshutumiwa katika Mwongozo kuhusiana na

hujuma dhidi ya Ujamaa ndilo likawa kinara wa kubeba mtazamo, itikadi

na sera za uliberali mambo-leo. Bila shaka, kama kawaida ya nchi zetu

ambamo matabaka-tawala ya ndani ni dhaifu, tabaka hili liliungwa

mkono na taasisi za kifedha za kimataifa na nchi za kibeberu wakiwemo

eti ‘wafadhili’. Kinadharia na kiitikadi, wasomi wa Chuo Kikuu, hususan

wachumi waliosoma Marekani, ndio wakawa wasemaji wakuu wa sera

za uliberali.

Hatimaye, Mwalimu akang’atuka kwa hiari yake, na labda pia kwa

kutambua kwamba sera zake hazingefua dafu tena, na viongozi wa

awamu ya pili ndio wakakumbatia, hatua kwa hatua, sera za ulegezaji wa

masharti ya biashara, uwekezaji na ubinafsishaji.

Sura ya Nne inaashiria kuzikwa kwa Azimio na mambo yote yalosimamiwa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 11/142

MIONGOZO MIWILI10

na Azimio. Bila shaka, Mzee Ruksa bado anajitangaza kuwa muumini wa

 Azimio. Kwake yeye, maamuzi ya Zanzibar yalipitishwa ili kupanua tafsiri

ya Azimio na sio kulizika. Kila zama ina Mwongozo wake, anasema Mzee

Mwinyi katika hotuba yake, na mwongozo wa zama ya uliberali mambo-leo ni ‘Azimio la Zanzibar’! Naam.

HitimishoSio nia yangu kuendelea kuchambua historia yetu ya miongo miwili

tangu Maamuzi ya Zanzibar. Ni juu ya vijana-wanazuoni wetu kuchambua

hali halisi na hasa zama zetu hizi za misukosuko na zahma za kisiasa

na kiuchumi. Jukumu mojawapo la Kigoda ni kuibua mijadala juu yamasuala muhimu na magumu ambayo watawala hupenda kuyakwepa

au kuyazika. Nia yetu ya kuchapisha upya toleo hili la nyaraka muhimu

katika historia yetu ni kuwakumbusha vijana-wanazuoni kwamba

huwezi ukaelewa kwa undani na ufasaha hali iliyopo bila kuelewa na

kuchambua hali iliyotangulia na iliyozaa hali ya leo.

ShukraniKwa mara nyingine tena ningependa kuishukuru taasisi ya HakiElimu na

hasa Mkurugenzi Mtendaji wake Bi. Elizabeth Missokia kwa kuwezesha

uchapishaji wa kitabu hiki. Ninapenda pia kumshukuru Mzee Ngombale

kwa kutuandikia Utangulizi. Namshukuru kwa namna ya kipekee

mchoraji mashuhuri wa katuni , Masudi ‘Kipanya’ kwa kutuchorea katuni

murua.

Mwisho, bila ya ushupavu, ukereketwa na uchapakazi wa wanakigoda,

hasa Mwalimu Bashiru Ally, Profesa Saida Yahya-Othman na Walter

Rodney Luanda, tusingeweza kukamilisha kitabu hiki. Asanteni sana na

kila la heri.

Issa Shivji

Profesa wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Aprili 2013

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 12/142

MIONGOZO MIWILI 11

UTANGULIZI

 UJIO NA UZITO WA

MIONGOZO MIWILI

Kingunge Ngombale Mwiru

Mwongozo wa TANU wa 1971

Mwongozo wa TANU wa 1971 ni mwendelezo wa moyo wa Azimio la

Arusha. Waandazi wa Mwongozo huu ni watu waliojazwa hisia kali za

uzalendo zilizotamka: “tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa

kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio

uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka kufanya

mapinduzi, ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena!’’

Katika moyo ule ule wa Azimio la Arusha, Mwongozo wa TANU wa 1971

unapalilia ari ya mapambano ya Waafrika dhidi ya Ukoloni, Ukoloni-

Mamboleo na Ubeberu na dhidi ya Waafrika wanaotumia madaraka

kuiisha Uhuru na kudhalilisha utu wa wananchi.

Ujio wa MwongozoMwongozo wa TANU wa 1971 ulitolewa na kutangazwa na Halmashauri

Kuu ya Taifa ya TANU ya dharura mwanzoni mwa mwezi wa Februari,

Dar es Salaam. Mwezi wa Januari mwaka 1971 Jeshi la Uganda chini

ya Iddi Amin Dada, liliangusha serikali ya Rais Milton Obote na kutwaa

madaraka. Kuika Agosti kitendo cha uchokozi kisicho cha kawaida kikosi

cha Jeshi la Iddi Amin kilikivamia kikosi cha doria cha polisi wa Tanzania

mpakani Mutukula na kumteka nyara Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC)

na kumtoroshea Uganda.

Kitendo hiki cha uhasama kutoka kwa nchi jirani kilihitaji kupatiwa

jibu la haraka na la kimkakati. Ndipo nilipoitwa Oisini kwa Makamu

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 13/142

MIONGOZO MIWILI12

wa Pili wa Rais, Ndugu Rashid Mfaume Kawawa, ambaye nilimkuta na

Meja Hashim Mbita (wakati ule Katibu Mtendaji Mkuu wa TANU). Ndugu

Kawawa alinieleza kwa kifupi kuwa Mwalimu alimwagiza aniarifu

kuwa ameamua mimi niongoze timu ya viongozi wa vijana kadhaa waTYL kwenda Mkoa wa Ziwa Magharibi kufanya kazi ya kuhamasisha

wananchi kisiasa na kiulinzi na usalama ili waweze kukabiliana ipasavyo

na chokochoko zozote zile kutoka nchi jirani.

Pamoja na kukubali jukumu nililopewa na kuahidi kuanza maandalizi

mara moja, nilitoa rai kwa Makamu wa Pili wa Rais kwamba kwa kuwa

tishio kwa usalama wa nchi kutoka Uganda ni sehemu tu ya tishio

kwa taifa maana kuna tishio kubwa zaidi kwenye Ukanda wa Kusini

la majeshi ya Wareno na uhasama wa Wareno na uhasama wa dola za

Afrika ya Kusini na Rhodesia, ingekuwa busara kuitisha kikao cha NEC

kutafakari juu ya ulinzi na usalama wa Taifa. Ndugu Kawawa alikubaliana

na pendekezo langu na palepale aliondoka akifuatana na Ndugu Hashim

Mbita, kwenda kuonana na Mwalimu Ikulu. Walirejea baada ya nusu saa

na kunitaarifu kuwa Mwalimu amekubali pendekezo nililolitoa na tayari

ameagiza NEC iitishwe kwa dharura.

Kikao cha NEC kilipoketi wiki moja baadaye mimi nilipata fursa ya

kufungua dimba la mjadala baada ya hotuba fupi ya ufunguzi ya

Mwenyekiti. Pamoja na kuchangia mawazo kuhusu mapambano ya

ukombozi wa Afrika na suala muhimu wakati ule la kuunga mkono vyama

halisi vya ukombozi wa nchi za Afrika, nilitumia muda kujenga hoja ili

NEC iikubali dhana ya msingi ya ulinzi na usalama wa Umma ambapo

wananchi wenyewe ndio wanaokabidhiwa jukumu la ulinzi na usalamawao. Wananchi wote wanahusika na ulinzi na usalama wao kwa njia ya

ulinzi wa mgambo na majeshi ni sehemu ya mstari wa mbele wa ulinzi na

usalama huo wa Umma.

Utekelezaji wa Mwongozo wa TANU na mafanikio yakeKupitishwa na kutangazwa kwa Mwongozo wa TANU wa 1971 kulipokewa

kwa shangwe kubwa sana hasa Dar es Salaam. Matawi mengi ya chama

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 14/142

MIONGOZO MIWILI 13

wakati huo jijini Dar es Salaam yalianzisha utaratibu wa wanachama wote

kukutana baada ya kazi ili kuzijadili ibara moja moja za Mwongozo. Matawi

mengine yalianzisha madarasa ya itikadi ili kujadili Mwongozo. Maelfu ya

wafanyakazi wa jijini Dar es Salaam walijiunga na mafunzo ya ulinzi wamgambo kuitikia wito wa Mwongozo wa TANU. Wakati wa mafunzo ya

mgambo muda kidogo ulitengwa kujadili ibara za Mwongozo.

Makada waliohamasisha wakazi kujiunga na ulinzi wa mgambo walijenga

hoja za uzalendo. Basi msimamo na lugha iliyotawala miongoni mwa

wanamgambo ilikuwa ya kizalendo na kuihami nchi. Wanazuoni wa

historia watakuja kufanya tathmini na kutoa kauli lakini sisi wenye

busara za kawaida tu tunaweza kutamka bila kukosea kwamba uamuzi

wa NEC ya TANU ya Februari 1971 kukubali sera ya ulinzi wa mgambo

na kuagiza itekelezwe ulikuwa mwafaka na ulisaidia sana kuyafanya

matokea ya vita ya Kagera kuwa yalivyokuwa.

Hali ilivyo hivi sasa ni kwamba tunahitaji kuifanyia uchambuzi na tafakuri

ya kina hali ya sasa ya ulinzi wa mgambo tukizingatia hoja za ibara za 21,

22 na 23 za Mwongozo wa 1971 zilizotuikisha kwenye uamuzi wa kuwana sera ya ulinzi wa mgambo nchini.

Katika kuhitimisha sehemu hii napenda kusisistiza kuwa suala la sera

ya ulinzi na usalama wa Umma ambalo ndilo linaloibeba sera ndogo

sahihi ya ulinzi wa mgambo ndio uamuzi mkuu wa Mwongozo wa

TANU wa 1971. Dhana na nadharia ya ukombozi wa Mwafrika na hasa

kama ilivyochambuliwa katika ibara ya 28 ya Mwongozo wa 1971 ina

umuhimu wa kipekee hasa kwa viongozi na watafutao madaraka yakisiasa nchini kwetu. Ibara ya 28 inatuambia kuwa kwa watu waliotokana

na mifumo kandamizi kama Utumwa, Ukoloni, Ukabaila au/na Ubepari,

maendeleo ni ‘ukombozi’. Na ‘ukombozi’ unaainishwa kama kitendo

kinachowaongezea watu uhuru wa kuamua mambo yao wenyewe na

kutawala maisha yao wenyewe.

Mwongozo katika ibara hii ya 28 unaendelea kusema ‘kwetu sisi

maendeleo yenye maana ni yale yanayotuondolea kuonewa, kunyonywa,

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 15/142

MIONGOZO MIWILI14

kunyanyaswa na mawazo ya kufungwa, na kutuongezea uhuru na utu

wetu’.

Mwongozo unalileta suala la maendeleo ya watu kwa kutamka: ‘Kwa hiyokatika kuikiria maendeleo ya Taifa letu na katika kupanga mipango ya

maendeleo wakati wote mkazo mkubwa uwekwe kwenye maendeleo ya

WATU na sio ya vitu. … [W]atu wenyewe lazima washiriki katika kuikiria,

kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo yao.’

Mwongozo wa 1981

Mwongozo wa CCM wa 1981, kama ulivyokuwa mwongozo wa TANUwa 1971, ulikuwa ni mwendelezo wa ikra na matarajio ya Ujamaa na

Kujitegemea uliotangazwa na Azimio la Arusha. Mwongozo huu ni

matokeo ya mila iliyokuwa imejengwa ndani ya Chama ya kutumia

vikao vikuu vyake, hususan NEC, kujadili na kuchambua masuala mazito

ya nchi, ya siasa, uchumi na jamii, na kuyatolea maelekezo ya kisera,

kiufafanuzi na kiutekelezaji.

Wakati Mwongozo wa TANU wa 1971 ulijielekeza kwenye mapambanodhidi ya Ukoloni, Ukoloni-Mamboleo na Ubeberu ili kufanikisha

Ukombozi wa Afrika na wa Mwafrika na kuweka mkakati wa ulinzi na

usalama wa umma ili nchi iwe na uwezo wa kukabiliana na uvamizi

wowote kutoka kwa ubeberu au na vibaraka vyake, Mwongozo wa CCM

wa 1981 umejikita katika kufanya uchambuzi kosoa wa kina na mpana

juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi iliyokuwepo nchini, hali ya maendeleo

ya demokrasia nchini na ndani ya chama, n.k., na kutoa mapendekezo yakuimarisha na kupanua demokrasia katika Chama na nchi.

Ujio wa MwongozoMambo matatu yaliwezesha kikao kiamue kujadili yaliyomo katika

Mwongozo huu. La kwanza ni kuwa hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii

ilikuwa ngumu wakati ule na hivyo kuhitaji kuzungumzwa. Pili ni ujasiri na

umahiri wa mmoja wa wajumbe wa NEC ambaye kwa unyenyekevu kabisa

alitoa ombi la kusema jambo kabla shughuli kuanza. Aliporuhusiwa na kiti

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 16/142

MIONGOZO MIWILI 15

alisema kama hivi: ‘Ndugu mwenyekiti na ndugu wajumbe naamini wote

mnafahamu hali yetu ya sasa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hali ni ngumu.

Ingefaa tutumie muda wa kikao hiki kutafakari na kufanya uchambuzi wa

kina juu ya hali ya sasa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ili tupate mikakati yakukipa chama chetu na serikali zake nguvu na msukumo mpya na uwezo

zaidi wa kuwahudumia wananchi. Naomba kikao chetu kijadili hali ya

nchi na ya chama chetu’. Sababu ya tatu ni usikivu aliokuwa nao Mwalimu

Nyerere kwa mambo yaliyohusu watu na yanayoihusu nchi. Na katika

hili, mara mjumbe alipomaliza kusema na kukaa Mwalimu alinena ‘naona

hili ni jambo jema, wakati umeika wa kuzungumzia hali yetu. Mnaonaje

wajumbe?’ Wajumbe wote wakaunga mkono.

Mjadala ulianza mara baada ya kikao kupitisha kumbukumbu za

mkutano uliotangulia pamoja na yatokanayo yake. Mimi niliyetoa hoja

ya kuomba mjadala huo maalum ufanyike nilipewa nafasi ya kuanzisha

mazungumzo. Wajumbe wengi wa kikao hicho walishiriki kwa kuchangia

mawazo katika mjadala ulioendelea kwa siku mbili.

Jioni ya siku ya pili, Mwenyekiti alipendekeza majina ya wajumbewa Kamati. Kutokana na pendekezo la msemaji wa kwanza kwamba

NEC iunde Kamati itakayoandaa Programu ya Chama yenye kuainisha

majukumu makuu (Central Tasks) katika kipindi ambacho kingeamuliwa

pamoja na mpangilio wa vipaumbele katika maeneo mbali mbali ya

kiuchumi na kijamii bila kusahau maendeleo ya chama chenywe, kamati

ikaitwa kamati ya Programu ya Chama.

Wajumbe wa kamati walikubaliana kumchagua Ndugu Peter Siyovelwa(marehemu) kuwa Mwenyekiti wake na Kingunge Ngombale Mwiru

kuwa Katibu/Rapporteur. Wajumbe wengine walikuwa Ndugu Peter

Kisumo, Moses Nnauye (Marehemu), Getrude Mongella, Maalim Seif

Shariff Hamad, Isaac Sepetu, Pius Msekwa na Joseph Sinde Warioba

(hawa wawili wa mwisho walichaguliwa baadae).

Wajumbe wa Kamati ya Programu ya Chama walipiga kambi mjini Dodoma

ili kufanya kazi waliyopewa. Kwanza wajumbe walijadili mapendekezo ya

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 17/142

MIONGOZO MIWILI16

sura ya Programu na dondoo za kila SEHEMU yake na kukubaliana nayo.

Baada ya hapo, kwenye kila hatua, wajumbe walipokea na kujadili kwa

kina rasimu ya maudhui ambayo Katibu wa Kamati aliwasilisha. Rasimu

mpya juu ya sehemu iliyojadiliwa iliandaliwa kwa msingi wa mwelekeo wamichango ya wajumbe na uzito wa hoja.

Rasimu za kwanza ya Programu ya Chama iliwasilishwa kwenye NEC ya

Mwezi Septemba 1981. Mjadala wa NEC ulikuwa wa kusisimua kulingana

na mawazo chanya na changamfu yaliyobebwa na Programu hiyo.

Ilibainika waziwazi kuwa maudhui ya Programu yatahitaji marekebisho

makubwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na baadhi ya sheria. Kwa

hivyo, NEC iliona vyema kuwateua wajumbe wapya wawili wa Kamati ya

Programu, Ndugu Pius Msekwa na Ndugu Joseph Sinde Warioba.

Kamati iliagizwa kwenda kuandaa rasimu ya mwisho kwa ajili ya NEC

ya Desemba 1981. NEC ilikutana Mwezi Desemba 1981 ili kupitisha

Programu hiyo. Mambo mawili yalitokea. Kwanza Mwalimu alishauri

kuwa Programu ya chama tuiite Mwongozo wa chama wa 1981; neno

Programu ni jipya lingeweza kuwatatanisha watu bure. Na pili kutokanana pendekezo la Mwenyekiti iliamuliwa kuwa Mwongozo wa CCM wa

1981 upitishwe na kutangazwa na Mkutano Mkuu wa dharura ambao

ungefanyika Tarehe 19 Januari, 1982, Dar es Salaam.

Mkutano Mkuu ulifanyika kama ilivyopangwa. Baada ya kuufungua

mkutano na kuwakaribisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa

Mwenyekiti, Mwalimu Nyerere, alimwomba Katibu wa Kamati, Ndugu

Kingunge Ngombale Mwiru, awasilishe Mwongozo wa CCM wa Mwaka1981 kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mkutano Mkuu ulipokea Mwongozo wa 1981.

Mwongozo wa 1981: maudhui na utekelezaji

MWONGOZO wa CCM wa 1981 uliandaliwa ili kukiwezesha Chama cha

Mapinduzi kuikabili hali ngumu ya kiuchumi na kijamii ya wakati ule.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 18/142

MIONGOZO MIWILI 17

Lakini ni muhimu ikumbukwe kuwa matarajio ya wananchi yaliyoibuliwa

na kutangazwa kwa Azimio la Arusha na Siasa ya TANU ya Ujamaa na

Kujitegemea yalichangia katika kuwasukuma Wajumbe wa NEC watoe

mawazo yaliyomo katika MWONGOZO huo. Ndiyo maana sehemu kubwaya maudhui ya MWONGOZO wa 1981 ni uchambuzi kosoa wa utekelezaji

wa Azimio la Arusha.

Waandazi wa MWONGOZO walikuwa na hisia kwamba sera za Chama na

hasa Azimio la Arusha, lilikuwa sahihi lakini mafanikio katika utekelezaji

wake ili yakidhi matarajio ya wananchi, yangehitaji Chama kiwe

madhubuti zaidi katika ikra, muundo na utekelezaji na serikali sawia.

Ili kuikia lengo hilo, walitumia methodolojia ya kufanya uchambuzi wakujikosoa kama Chama.

Sehemu hii ya pili ya MWONGOZO ina umuhimu mkubwa sana. Kwa

upande mmoja inaonyesha upungufu wa Chama katika maeneo

mbalimbali na hatua za kurekebisha ili kukiimarisha na kwa upande

mwingine inatoa mchango wa mawazo ambao ni mwongozo katika

nadharia ya ujenzi wa Chama. Katika kila kipengele kilichoorodheshwa

kwenye sehemu hii ya pili kuna mchango mahsusi wa kukifanya Chama

kiwe madhubuti na chenye ufanisi.

Tuchukue kipengele cha pili (2) katika Sehemu ya Pili ya MWONGOZO

inayosema ‘Wana-CCM ndio askari wa mstari wa mbele wa mapambano…’

Historia yetu inatuonyesha jinsi wanaTANU waliopigania uhuru wetu

walivyokuwa na hamasa za kuupinga ukoloni na kukataa kutawaliwa.

Wito wa TANU na ASP uliwafanya washikamane kwa kauli na vitendo.

Tanzania Bara haikuchelewa kunyakuwa uhuru wake.

Tangu tupate Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar hadi sasa pumzi ya

wanachama wetu ya kusukuma mapambano na kujenga jamii mpya

imepungua hasa kwa kuachia ubinafsi uwe na nafasi kubwa katika siasa

na jamii kwa ujumla. Kwa wana CCM sasa kuwa askari wa mstari wa

mbele wa mapambano yetu kutahitajika mageuzi ya msingi. Lakini hili

bado linawezekana.

Wasomi wa falsafa wanasema nadharia ni mwanga muhimu kwawanaohusika na kutekeleza mambo, kutenda. Nadharia ni mwanga

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 19/142

MIONGOZO MIWILI18

unaoangaza ili wanaohusika na kutenda waangaziwe. Ndiyo maana kuna

vipengele juu ya umuhimu wa nadharia sahihi ya Chama na ‘Mshikamano wa

nadharia na vitendo’. Uchambuzi huu umefanywa kwanza ili kuwaonyesha

wanaodharau nadharia kuwa wanakosea na pili kusisitiza kuwa viongozi/makada wasioandaliwa vizuri katika nadharia wana hatari ya kufanya

kazi ya Chama kwa kubahatisha. Viongozi na makada wanatakiwa wawe

watu wanaojiamini, wenye uhakika na wanayoyaeleza, wenye uwezo wa

kujenga hoja na kutumia nguvu ya hoja siyo hoja ya nguvu, kuwaelimisha,

kuwashauri na kuwavuta watu upande wa Chama.

Suala la chombo na maudhui yakeMwaka 1981 ulikuwa mwaka wa kumi na nne (14) tangu Azimio la

Arusha. Utekelezaji wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ya TANU ulikuwa

umeikia kiwango kikubwa nchini. Sekta ya Umma iliyoundwa katika

kipindi hicho ilikuwa kubwa na anuai. Viwanda vya Umma na Mashirika

mbalimbali ya Umma ndiyo yaliyokuwa yakiongoza. Sekta hii ya Umma

ya uchumi ilikuwa inaajiri wafanyakazi wengi na kutarajiwa kuzalisha

mali na kutoa huduma kwa ufanisi.

Mwongozo pamoja na mambo mengine unajadili upungufu uliojitokeza

ndani ya sekta ya umma na kuhoji kama hali hiyo haianzishi mgongano

na makusudio ya kuundwa kwa sekta ya umma ambayo ndiyo ya ujamaa.

Itakumbukwa pia kuwa katika MWONGOZO wa TANU wa 1971 kuna

Ibara ya 15 ambayo inahoji viongozi wa kazi wenye tabia ya unyapara,

wasioheshimu watu, wakaripiaji n.k. katika sehemu za kazi.

Hapa pana suala kubwa kwa watu wanaoamini katika ujamaa na

wale wanaoamini katika uhuru na utu, na kuwa maendeleo yenye

maana ni maendeleo ya watu. Haitoshi katika nchi kuunda vyombo

vya ujamaa kama viwanda, mabenki, mashirika ya umma ya huduma n.k.;

lazima ndani ya vyombo hivyo kujenga uhusiano wa kijamaa yaani ule

unaoheshimu misingi ya usawa, haki, ushirikiano, mshikamano, kuchapa

kazi na uaminifu. Je, demokrasia ina nafasi ipi? Na nidhamu nayo?

MWONGOZO wa CCM wa 1981 katika kufanya uchambuzi kosoa

ulilenga kubainisha mapungufu katika maeneo ya uchumi, siasa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 20/142

MIONGOZO MIWILI 19

na jamii ili kutoa mapendekezo chanya ya kukijenga Chama

na dola.

Watu wenye ikra za kimaendeleo tayari wakati ule walikuwa wanaona

haja ya kuleta mabadiliko makubwa ndani ya Chama ili kupanua

demokrasia na kuimarisha uongozi na utendaji. Kwa hiyo, MWONGOZO

ulisisitiza umuhimu wa kuwapata viongozi wa Chama kwa njia ya

uchaguzi badala ya uteuzi kwa lengo la kuunganisha uongozi wa chama

(Halmashauri Kuu za kila ngazi) na utendaji katika Chama. MWONGOZO

ulielekeza kuanzishwa kwa Sekretarieti za Halmashauri Kuu za kila ngazi

ambazo zingeongozwa na makatibu wa Halmashauri Kuu hizo.

Sekretarieti za Halmashauri Kuu ya Chama katika kila ngazi zilikusudiwa

ziwe timu za uongozi wa pamoja katika ngazi husika na chemchem za

ikra za chama, wakati kila mmoja ni kiongozi na msimamizi mahiri wa

shughuli za Chama katika idara yake.

MWONGOZO katika kusisitiza umuhimu wa kupanua demokrasia ndani

ya Chama umetilia mkazo uwakilishi wa wanawake na vijana kutokana

na uzito wa makundi haya katika jamii.

Waandazi wa MWONGOZO wa CCM wa 1981 hawakusita kujielekeza

kwenye suala la demokrasia katika dola. Ndiyo maana MWONGOZO

uliona umuhimu wa kuimarisha uwakilishi wa wafanyakazi, wakulima,

vijana na wanawake Bungeni. Aidha, ulisisitiza umuhimu wa uchaguzi

kama kigezo cha msingi cha demokrasia ya kijamaa na hivyo uchaguzi

uwe ndiyo njia kuu ya kuwapata wabunge na wawakilishi wengine

katika dola. MWONGOZO vile vile ulihimiza haja ya kupanua demokrasia

kwa kusisitiza umuhimu wa kuimarisha madaraka ya umma hadikwenye ngazi ya vijiji na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za

maendeleo yao.

Mapokezi na utekelezaji

MWONGOZO wa CCM wa 1981 ulipata mapokezi makubwa ndani ya

Chama na katika jamii nzima nchini. Kitendo cha kuitishwa Mkutano

Mkuu wa Taifa wa CCM wa dharura ili kuupokea na kuupitisha

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 21/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 22/142

MIONGOZO MIWILI 21

ya kuwa sehemu ya Dibaji tu ya Katiba hiyo. Pili ni hatua ya kuimarisha

na kupanua demokrasia nchini kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki

wa uwakilishi wa wananchi katika ngazi za Ubunge na Serikali za Mitaa.

Jambo la tatu linahusu madaraka ya umma. Mwongozo ulisisitiza juu yamadaraka ya umma kuanzia vijijini hadi wilayani na mijini. Kutokana na

mwelekeo huo wa MWONGOZO marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya

Muungano yaliyofanywa mwaka 1984 yalipanua dhana inyu ya Serikali za

Mitaa katika mtazamo nyumbufu wa madaraka ya umma na kusisitiza juu

ya haki ya wananchi kwa serikali zao katika maeneo yao.

Changamoto zinazohitaji tafakuri• Unapoisoma miongozo hii miwili, wa TANU wa 1971 na wa

CCM wa 1981, huwezi kukosa kubaini kuwa ikra, nadharia na

tafakuri kubwa zilitumika katika utunzi wake. Haya ni matokeo

ya viongozi wa chama wanapokaa pamoja na kuikiri pamoja.

Hii ni aina mojawapo ya uhai wa chama iliyo muhimu sana kwa

uhai wa jumla wa chama cha siasa.

• Je, mila hii iliyokuwa imejengeka huko nyuma CCM yetu ya

sasa inaiendeleza? Je Vyama vingine vya siasa nchini vinajaribukujenga tabia ya viongozi wake kuketi pamoja na kuikiri

pamoja na kuchambua pamoja hali ya nchi yetu na namna

vitakavyozikabili changamoto mbalimbali?

• Huu umaskini wetu wa sasa wa falsafa unaotuathiri vibaya

unatokana na nini?

• Mwongozo wa TANU wa 1971, katika ibara zake za 21, 22 na

23 ulijenga msingi wa sera ya ulinzi na usalama wa umma, serailiyozaa ulinzi wa mgambo. Maandalizi sahihi ya wanamgambo,

yaani kuhamasishwa kwa mbinu ya uzalendo, uandikishaji na

mafunzo makini ya kijeshi chini ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi

wa Tanzania ndiyo yaliyowezesha wanamgambo kushiriki

bega kwa bega na wapiganaji wengine katika Jeshi la Tanzania

lilolishinda na kulitokomeza Jeshi la Nduli Iddi Amin wa Uganda.

• Miaka 33 imekwishapita tangu vita vya Kagera viishe. Vita hivyo

vya kujihami dhidi ya uvamizi uliofanywa na majeshi ya Iddi

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 23/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 24/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 25/142

MIONGOZO MIWILI24

(i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,

kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili

kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya

mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine nakuzuia limbikizo la utajiri kuikia kiasi ambacho hakipatani na

siasa ya watu wote kuwa sawa.

MADHUMUNI YA TANUKwa hiyo basi, makusudi na madhumuni ya TANU yatakuwa kama hiviyafuatavyo:

(a) Kuudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake;(b) Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara kanuni

za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu;

(c) Kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na Serikali ya watu

ya kidemokrasia na ya kisoshalist;

(d) Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika

vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika;

(e) Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa

kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi;

(f) Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na

kudumisha vyama vya ushirika;

(g) Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa katika

maendeleo ya uchumi wa nchi yetu;

(h) Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote,

wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;

(i) Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma,

vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;

(j) Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara njia

kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo itarahisisha njia

ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu;

(k) Kuona kwamba Serikali inashirikiana na dola nyingine katika

Afrika katika kuleta Umoja wa Afrika.

(l) Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salamaulimwenguni kwa njia ya Chama cha Umoja wa Mataifa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 26/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 27/142

MIONGOZO MIWILI26

makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima katika viwanda

vikubwa.

Baadhi ya njia hizi na nyingine zisizotajwa hapa hivi sasa zinamilikiwa au

kutawaliwa na Serikali ya Wananchi.

(c) Kuna Demokrasi

Nchi haiwi ya Ujamaa kwa sababu tu njia zake kuu au zote za uchumi

hutawaliwa na humilikiwa na Serikali. Sharti Serikali iwe inachaguliwa na

kuongozwa na Wakulima na Wafanyakazi wenyewe. Serikali ya Makaburu

wa Rhodesia au Afrika ya Kusini ikitawala au kumiliki njia zote za uchumi,

hiyo itakuwa ni njia ya kukomaza Udhalimu siyo njia ya kuleta Ujamaa.Hakuna Ujamaa wa kweli pasipo na Demokrasi ya kweli.

(d) Ujamaa ni Imani

Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani Ujamaa ni imani.

Hauna budi kujengwa na watu wanaoamini na kufuata kanuni zake.

Mwana-TANU wa kweli ni Mjamaa, na Wajamaa wenzie, yaani waamini

wenzie katika imani hii ya kisiasa na uchumi ni wote wale wanaopigania

haki za wakulima na wafanyakazi katika Afrika na popote duniani. Wajibu

wa kwanza wa mwana-TANU na hasa kiongozi wa TANU, ni kutii kanuni

hizi za ujamaa hasa katika maisha yake mwenyewe. Na hasa mwana-

TANU kiongozi hataishi kwa jasho la mtu mwingine au kufanya jambo

lolote ambalo ni la kibepari au kikabaila.

Utimizaji wa shabaha hizo na nyinginezo zinazofuatana na siasa ya ujamaa

unategemea sana viongozi kwa sababu ujamaa ni imani na ni vigumu kwa

viongozi kujenga siasa ya ujamaa ikiwa hawaikubali imani hiyo.

SEHEMU YA TATU

SIASA YA KUJITEGEMEA 

Tunapigana Vita

TANU ina vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na kulitia

katika hali ya nguvu; vita vya kuwafanya wananchi wa Tanzania (na

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 28/142

MIONGOZO MIWILI 27

wananchi wa Afrika) watoke katika hali ya dhiki na kuwa katika hali ya

neema.

Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, na

tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe,

tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa

unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na wala tusipuuzwe tena.

Mnyonge Hapigani kwa Fedha

Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua silaha;

kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa unyonge wetu

kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo sisi wenyewe hatuna.Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na vitendo vyetu ni kama

tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi yetu hayawezekani. Ni

kama tumesema, ‘Fedha ndiyo msingi wa maendeleo. Bila fedha hakuna

maendeleo’!

Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni kwenye

fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi, mawazo yao na

matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa wananchi na wananchiwenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT, Vyama vya Ushirika, TAPA

na makundi mengine ya wananchi, mawazo yao na maombi yao na

matumaini yao ni FEDHA. Ni kama wote tumekubaliana na tunasema

kwa sauti moja, ‘Tukipata fedha tutaendelea, bila fedha hatutaendelea’!

Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake kwa kifupi ni

shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yetu tuliyotilia mkazo sana

ni fedha. Ni kama tumesema, ‘Katika miaka mitano ifuatayo tunakusudiakujiongezea shibe, elimu na afya, na ili kutimiza shabaha hizo tunatumia

£ 250,000,000’. Kama tumetaja na tunapotaja vyombo vingine vya

kututimizia shabaha hizo tunavitaja kama nyongeza tu; lakini chombo

kikubwa katika akili zetu, silaha kubwa katika mawazo yetu, ni FEDHA.

Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu yake wana

shida ya maji, je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa shida hiyo? Jibu

analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa kuwapa maji wananchi

wa sehemu hiyo – KWA FEDHA.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 29/142

MIONGOZO MIWILI28

Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina barabara au

shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani? Naye pia jibu

ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao mpango sai kabisa

wa kutengeneza barabara au kujenga shule au hospitali au vyote kwawananchi wa sehemu ya Mbunge Mheshimiwa huyo – kwa FEDHA.

Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya chini

kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba wanazolala

si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo kusikia ni kuwa

Serikali inao mpango maalum wa kuongeza mishahara na kujenga

majumba bora – KWA FEDHA.

Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana ambazo

hazipati msaada wa Serikali, je, Serikali ina mpango gani wa kuzisaidia

shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko tayari kabisa

kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa – wa FEDHA!

Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yoyote ya mkulima jibu

apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za mkulima – kwa

FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili Taifa letu wananchi tunawaza

Fedha, Fedha, Fedha!

Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya makadirio yake ya

matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo kwa kazi za kawaida na

mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na Wizara moja tu hushughulika

pia kufanya makadirio ya mapato. Ni Waziri wa Fedha. Kila Wizara ina

mipango mizuri sana ya maendeleo. Wizara zinapoleta makadirio yao ya

matumizi huwa zinaamini kwamba fedha zipo ila mkoroi ni Waziri wa

Fedha na Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizarayake awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna

fedha. Na kila mwaka Wizara zote huinung’unikia Wizara ya Fedha kwa

kupunguza Makadirio yao ya matumizi.

Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali itimize

mipango mbalimbali huwa nao wakiamini kwamba fedha zipo ila mkoroi

ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge na Viongozi

wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba Serikali haina fedha.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 30/142

MIONGOZO MIWILI 29

Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini? Maana yake ni

kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi walichonacho hutozwa

kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha shughuli za Serikali hivi sasa na

maendeleo mengine ya nchi. Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidiza maendeleo kwa fedha tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama

Serikali haina fedha zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.

Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya kuzipata

ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi zaidi bila kukubali kodi zaidi

ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi bila

kutaka ng’ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri kwamba

tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka Serikaliiongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa kuongeza kodi.

Tunatambua kuwa ng’ombe hana maziwa zaidi; kwamba hata kama

ng’ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo au yanywewe na

ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa yake; utashi huo hauwezi

kuondoa ukweli kwamba hana maziwa zaidi.

Fedha kutoka Nje ya Tanzania, je?

Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri kodi

zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za kutoka nje

ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-

(a)  Zawadi : Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure tu

kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo. Wakati

mwingine shirika lolote la nje liipe Serikali yetu au Shirika

jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya maendeleo.

(b) Mkopo:  Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata kutokanchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo. Serikali ya nje au

Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha Serikali yetu fedha fulani

kwa ajili ya kazi zetu za maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti

yake ya kulipa, kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.

(c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa kuliko

ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni yanayotaka

kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbalimbali za uchumi

kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti kubwa walitakalo jamaa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 31/142

MIONGOZO MIWILI30

hawa wenye fedha zao ni kwamba shughuli yenyewe iwe ni ya

faida – kwao – na pia kwamba Serikali iwaruhusu kuondoa faida

hiyo Tanzania na kuipeleka kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali

iwe na siasa wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishiuchumi wao.

Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya nchi yetu. Kuna

mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili la kupata fedha kutoka nchi za

kigeni. Serikali yetu na viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi

kuikiria njia za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata

ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na viongozi

wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa neema imekuja au ikonjiani inakuja! Tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza;

tukipata kiwanda kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au

kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au

shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara hutangaza japo

hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha

wananchi kwamba, tunaanza mazungumzo ya neema!

TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO

Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu kikubwa cha

maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini. Ni ujinga vilevile,

kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya

unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu

wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.

Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo zaweza

na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani ambayo iko

tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga viwanda katika nchi

yetu kwa kiasi cha kuiwezesha nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za

maendeleo. Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi

zote zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa

msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata katika

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 32/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 33/142

MIONGOZO MIWILI32

fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama tulivyokwishasema

Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu maskini mikopo ambayo

inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni kuwaumiza. Na hasa inapokuwa,

mikopo hiyo ambayo wanatakiwa walipe, haikuwafaidia wao, bali ilifaidiawatu wachache tu.

Na Viwanda vya wenye raslimali zao je?  Ni kweli tunavitaka. Hata tumepitisha

katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni wanaoanzisha mipango

mbalimbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia yetu na matumaini yetu ni

kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi inayofaa kuingiza raslimali zao.

Kwani raslimali yao itakuwa salama italeta faida. Na faida hiyo wenyewe

wataweza kuiondoa bila vipingamizi. Tunayo matumaini ya kupatafedha za maendeleo mbalimbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za

kutosha. Lakini hata kama tungeweza kuwaridhisha kabisa Wageni hao

na Makampuni hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi

tunayohitaji katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli?

Kama tungeweza kushawishi wenye raslimali wa kutosha kutoka Amerika,

na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na mipango mingine

yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi kweli tungekubali bilakujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha uchumi wetu wote uwe

mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata faida na kuipeleka katika nchi

zao? Hata kama wasingedai kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali

faida yote watakayopata wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo

zaidi. Hivi kweli tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa

letu? Huu Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje?

Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa misaada namikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha uhuru wetu?

Waingereza wana methali isemayo ‘Amlipaye mwimbaji ndiye huchagua

wimbo’. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na Makampuni ya kigeni kwa

sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila kuzipa nchi hizo na makampuni

hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu wa kutenda tupendavyo? Ukweli

wenyewe ni kwamba hatuwezi.

Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu ambacho hatuna,

kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya maendeleo. Tunafanya

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 34/142

MIONGOZO MIWILI 33

makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka nchi za kigeni. Kwanza, kwa

sababu kwa kweli hatuwezi kupata fedha za kutosha kwa maendeleo yetu.

Na pili, hata kama tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha

uhuru wetu na siasa nyingine za nchi yetu.

TUMEKAZANIA MNO VIWANDA 

Kwa sababu ya kutilia mkazo fedha tumefanya kosa kubwa la pili.

Tumekazania mno viwanda. Kama vile tulivyosema ‘Bila Fedha hakuna

maendeleo’, ni kama twasema pia ‘Viwanda ndiyo maendeleo. Bila

viwanda hakuna maendeleo’. Hii ni kweli siku tutakapokuwa na fedha

nyingi, tutaweza kusema kwamba tumeendelea. Tutaweza kusema,‘Tulipoanza mipango yetu tulikuwa hatuna fedha za kutosha na upungufu

huu wa fedha ulitupunguzia nguvu za kuendesha maendeleo yetu haraka

zaidi. Lakini leo tumeendelea na tunazo fedha za kutosha’. Na hivyo

ndivyo itakavyotupasa kusema, ‘Tumeendelea, kwa hiyo, tunazo fedha za

kutosha’. Yaani fedha zetu zitakuwa zimeletwa na maendeleo.

Kadhalika siku tutakapokuwa na viwanda tuna haki ya kusema kuwa

tumeendelea. Maendeleo yatakuwa yametuwezesha kupata viwanda.Kosa tunalofanya ni kudhani kwamba maendeleo yetu yataanza kwa

viwanda. Ni kosa maana hatuna uwezo wa kuanzisha viwanda vingi

vya kisasa katika nchi yetu. Hatuna fedha zinazohitajiwa na hatuna

ufundi unaohitajiwa. Haitoshi kusema kuwa tutakopa fedha na kuazima

mafundi kutoka nje kuja kuanzisha viwanda hivyo. Kosa hili jibu lake ni

lilelile kwamba hatuwezi kupata fedha za kutosha na kuazima mafundi

wa kutosha kutuanzishia viwanda hivyo tunavyotaka. Na pia kwamba

hata kama tungeweza kupata msaada huo kuutegemea huko kunaweza

kukapotosha siasa yetu ya Ujamaa. Siasa ya kualika msululu wa mabepari

kuja kuhodhi viwanda katika nchi yetu ingefanikiwa kutupatia viwanda

vyote tunavyotaka, basi ingefanikiwa pia kuzuia maendeleo ya Ujamaa.

Ila labda tuwe tunaamini kwamba bila kujenga ubepari kwanza hatuwezi

kujenga Ujamaa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 35/142

MIONGOZO MIWILI34

TUMJALI ZAIDI MKULIMA VIJIJINI

Vilevile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie zaidi

maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha za

kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo yatamfaa kila

mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwanda katika kila

kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na viwanda katika kila kijiji;

jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili hiyo, basi, fedha zetu

huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia hujengwa katika miji.

Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule, hospitali,

majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima zilipwe.

Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha zinazotokanana maendeleo ya mijini au maendeleo ya viwanda. Hazina budi zilipwe

kwa fedha tunazopata kutokana na vitu tunavyouza katika nchi za nje.

Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi na kwa muda mrefu sana hatutauza

vitu vingi katika nchi za nje. Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia

kupata vitu hapa hapa ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za

nje. Itapita miaka mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za nje vitu

vinavyotokana na viwanda vyetu.Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa madeni haya

ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda mijini hazitatoka mijini

na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi, basi? Zitatoka vijijini

na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu ni nini? Ni kwamba

wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na fedha tunazokopa sio kwa

kweli watakaozilipa. Fedha zitatumika zaidi katika miji lakini walipaji

watakuwa zaidi ni wakulima.

Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi za

kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa mijini

wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini.

Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo

sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha za

mkopo walipaji wa mkopo ni wakulima, yaani wale ambao hawafaidiwi

sana na hospitali hizo. Mabarabara ya lami yako katika miji, kwa faida

ya wakaaji wa mijini na hasa wenye magari. Kama mabarabaraba hayo

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 36/142

MIONGOZO MIWILI 35

tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni wakulima; na fedha

zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao ya wakulima. Taa

za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na maendeleo mengine yote

ya kisasa yako zaidi katika miji. Karibu yote yametokana na fedhaza mikopo na karibu yote hayana faida kubwa kwa mkulima, lakini

yatalipwa kwa fedha zitakazotokana na jasho la mkulima. Tusisahau

jambo hili.

Japo tunapotaja unyonyaji huikiria mabepari, tusisahau kuwa bahari

ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa hutafuna mdogo na

mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi yetu twaweza kugawa

wananchi kwa njia mbili. Mabepari na Makabaila upande mmoja; nawafanyakazi na wakulima upande mwingine. Pia twaweza tukawagawa

wakaaji wa mijini upande mmoja, na wakulima wa vijijini upande

mwingine. Tusipoangalia tutakuja kugundua kuwa wakaaji wa mijini nao

ni wanyonyaji wa wakulima.

 WANANCHI NA KILIMO

Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha. Fedha ni

matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji vitu vinne: (i)

Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa sai na (iv) Uongozi bora. Nchi yetu ina zaidi

ya watu milioni kumi1* na eneo la eka 362,000.

MAENDELEO YATALETWA NA KILIMO

Sehemu kubwa ya eneo hili ni yenye rutuba na mvua ya kutosha. Nchiyetu inaweza kutoa mazao ya aina mbalimbali ambayo tunayahitaji kwa

chakula na kwa fedha. Mazao ya chakula (na fedha kama tukiyatoa kwa

wingi) ni kama vile mahindi, mchele, ngano, maharage, karanga n.k.

Mazao ya fedha ni kama vile mkonge, pamba, kahawa, tumbaku, pareto,

chai n.k.

1 *Hesabu ya watu ya mwaka 1967 ilionesha kuwa watanzania ni zaidi ya milioni

kumi na mbili.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 37/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 38/142

MIONGOZO MIWILI 37

Yafaa kujiuliza wananchi wakulima hasa wanaume, hufanya kazi kwa

saa ngapi kwa juma na miezi mingapi kwa mwaka. Ni wengi mno ambao

hawatimizi hata nusu ya wastani wa mfanyakazi wa mshahara.

Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana kazi.

Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na hawana livu.

Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote

katika Tanzania. Lakini kina baba wa vijijini (na baadhi ya kina mama wa

mijini) nusu ya maisha yao ni livu. Nguvu hizi za mamilioni ya kina baba

vijijini na maelfu ya kina mama wa mijini ambazo hivi sasa hazifanyi

kazi yoyote ila kupiga soga, kucheza ngoma na kunywa pombe, ni hazina

kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeeo ya nchi yetu kuliko hazina zamataifa matajiri.

Tutafanya jambo la faida kubwa kwa nchi yetu kama tukienda vijijini na

kuwaambia wananchi kwamba wanayo hazina hii na kwamba ni wajibu

wao kuitumia kwa faida yao wenyewe na faida ya Taifa letu.

(b) Maarifa

Sharti la pili la maendeleo ni MAARIFA. Juhudi bila maarifa haiwezi kutoamatunda bora kama juhudi na maarifa. Kutumia jembe kubwa badala ya

jembe dogo, kutumia jembe la kuvutwa na ng’ombe badala ya jembe la

mkono, kutumia mbolea badala ya ardhi tupu, kunyunyizia dawa ili kuua

wadudu, kujua ni zao gani lifaalo kupandwa na zao gani lisilofaa, kuchagua

mbegu vizuri kabla ya kuzipanda, kujua wakati mzuri wa kupanda, wakati

wa kupalilia n.k., ni maarifa yanayowezesha juhudi kutoa mazao mengi zaidi.

Fedha na wakati tunaotumia kuwapa wakulima maarifa haya ni fedha nawakati uletao faida kubwa zaidi kwa nchi yetu kuliko fedha na wakati

mwingi tunaotumia katika mambo mengi tunayoyaita maendeleo.

Jambo hili kwa kweli tunalifahamu. Katika mpango wetu wa miaka

mitano, mipango inayoendelea vizuri na hata kuzidi makisio ni ile

inayotegemea juhudi ya wananchi wenyewe. Pamba, kahawa, korosho,

tumbaku, pareto ni mazao yaliyoongezeka kwa haraka sana katika muda

wa miaka mitatu iliyopita. Lakini ni mazao ambayo yameongezeka kwasababu ya juhudi na uongozi wa wananchi, siyo kwa sababu ya fedha.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 39/142

MIONGOZO MIWILI38

Kadhalika wananchi kwa juhudi zao wenyewe na maelekezo au msaada

kidogo wametimiza mipango mingi sana ya maendeleo huko vijijini.

Wamejenga shule, dispensari, majumba ya maendeleo, wamechimba

visima, mifereji ya maji, mabwawa, mabarabara, wamejenga mabirika yakukoshea mifugo na kujiletea wenyewe maendeleo ya aina mbalimbali.

Kama wangengoja fedha wasingeyapata maendeleo hayo.

 JUHUDI NI SHINA LA MAENDELEOMipango inayotegemea fedha inakwenda vizuri lakini kuna mingi ambayo

imesimama na yumkini mingine haitatimizwa kwa sababu ya upungufu

wa fedha. Lakini kelele zetu bado ni kelele za fedha. Juhudi yetu ya

kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio kwamba tuipunguze, bali, badala

ya safari nyingi, ndefu na zenye gharama kubwa za kwenda katika miji

mikuu ya mataifa ya kigeni kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu,

itafaa kufunga safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza

wananchi katika kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo

njia ya kweli ya kuleta maendeleo kwa kila mtu.

Hii maana yake si kwamba tangu sasa hatutajali fedha, wala hatutajengaviwanda au kufanya mipango yoyote ya maendeleo inayohitaji fedha.

Wala siyo kusema kuwa tangu sasa hatutapokea wala kutafuta fedha

kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo yetu. LA, SIVYO. Tutaendelea

kutumia fedha; na mwaka hata mwaka tutatumia fedha nyingi zaidi kwa

maendeleo yetu ya aina mbalimbali kuzidi mwaka uliopita. Kwani hiyo

itakuwa ni dalili moja ya maendeleo yetu.

Lakini hii ni kusema kwamba tangu sasa tutajua nini ni shina na nini nitunda la maendeleo yetu. Katika vitu viwili hivyo FEDHA na WATU, ni

dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina la maendeleo, fedha ni

moja ya matunda ya juhudi hiyo.

Tangu sasa tutasimama wima na kutembea kwa miguu yetu badala ya

kupinduka na kuwa miguu juu vichwa chini. Viwanda vitakuja, na fedha

zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI yao na hasa katika

KILIMO. Hii ndiyo maana ya kujitegemea. Kwa hiyo basi, mkazo wetuna uwe:

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 40/142

MIONGOZO MIWILI 39

(a) Ardhi na Kilimo.

(b) Wananchi.

(c) Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na

(d) Uongozi bora.

(a) Ardhi

Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea na utaendelea kutegemea

kilimo na mifugo, Watanzania wanaweza kuyaendesha maisha yao

barabara bila ya kutegemea misaada kutoka nje kwa matumizi bora

ya ardhi hiyo. Ardhi ni ufunguo wa maisha ya binadamu kwa hiyo

Watanzania wote waitumie ardhi kama ni raslimali yao kwa maendeleo

ya baadaye. Kwa kuwa Ardhi ni mali ya Taifa, Serikali ni lazima iangaliekuwa ardhi inatumiwa kwa faida ya Taifa zima na wala isitumiwe kwa

faida ya mtu binafsi au kwa watu wachache tu.

Ni wajibu wa TANU kuona kuwa nchi yetu inalima chakula cha kutosha

na kutoa mazao ambayo yataleta fedha nchini kwa kuuzwa katika nchi

za ng’ambo. Ni wajibu wa Serikali na Vyama vya Ushirika kuona kuwa

wananchi wanapatiwa vyombo, mafunzo ya uongozi unaohitajika katika

kilimo na ufugaji wa kisasa.

(b) Watu

Kuiwezesha siasa ya kujitegemea itekelezwe vizuri, wananchi ni budi

wajengwe moyo na shauku ya kujitegemea. Wajitegemee katika kuwa na

chakula cha kutosha, mavazi ya kufaa na mahali pazuri pa malazi.

Katika nchi yetu kazi iwe ni kitu cha kujivunia. Bali uvivu, ulevi na

uzururaji uwe ni jambo la aibu kwa kila mwananchi. Katika upandewa ulinzi wa Taifa, wananchi wawe macho na vibaraka waliomo nchini

ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nje wenye nia mbaya ya

kuliangamiza Taifa hili na wawe tayari kulilinda Taifa inapolazimika

kufanya hivyo.

(c) Siasa Saf

Msingi wa siasa ya kujitegemea lazima uambatane na siasa ya Ujamaa

ya TANU. Ili kuzuia unyonyaji ni lazima kila mtu afanye kazi na aishi kwa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 41/142

MIONGOZO MIWILI40

jasho lake yeye mwenyewe. Na ili kuleta usawa wa kugawana mapato ya

nchi ni lazima kila mtu atimize wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii

zake zote. Asiweko mtu wa kwenda kwa ndugu yake na kukaa kwa muda

mrefu bila kufanya kazi kwa sababu atakuwa anamnyonya yule nduguyake. Vilevile mtu yeyote asiruhusiwe kuzurura zurura hovyo mijini au

vijijini bila kufanya kazi ya kumwezesha kujitegemea mwenyewe bila

kuwanyonya ndugu zake.

TANU inaamini kuwa kila anayelipenda Taifa lake ni budi aweze

kulitumikia kwa kujitolea nafsi yake na kushirikiana na wananchi

wenzake kwa kuijenga nchi kwa manufaa ya watu wote. Ili kudumisha

Uhuru wa nchi yetu na raia zake barabara ni budi kujitegemea kwa kilahali bila kwenda kuomba misaada nchi zingine.

Kujitegemea kwa mtu mmoja ni kujitegemea kwa nyumba kumi.

Kujitegemea kwa nyumba zote kumi za balozi ni kujitegemea kwa tawi

zima. Kujitegemea kwa matawi ni kujitegemea kwa Wilaya ambayo ni

kujitegemea kwa Mkoa. Kujitegemea kwa Mikoa yote ni kujitegemea kwa

Taifa lote ambalo ndilo lengo letu.

(d) Uongozi Bora

TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo lililopo

ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi na kwa

hiyo Oisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze utaratibu maalum kuhusu

mafundisho ya Viongozi tangu wa Taifa zima hadi Mabalozi ili waielewe

siasa yetu na mipango ya uchumi. Viongozi ni lazima wawe mfano mzuri

kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia.

SEHEMU YA NNE

UANACHAMA 

Tangu Chama kilipoanzishwa, tumethamini sana kuwa na wanachama

wengi iwezekanavyo. Hii ilifaa wakati wa kupigania vita vya kumng’oa

mkoloni. Hivyo ndivyo ilivyobidi TANU kufanya kwa wakati huo. Lakini

sasa Halmashauri Kuu inaona kuwa wakati umeika wa kutilia mkazo

kwenye imani ya Chama chetu na siasa yake ya Ujamaa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 42/142

MIONGOZO MIWILI 41

Kifungu cha Katiba ya TANU kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye

Chama kifuatwe na ikiwa inaonekana kuwa mtu haelekei kuwa anakubali

imani, madhumuni na sheria na amri za Chama, basi asikubaliwe kuingia.

Na hasa isisahauliwe kuwa TANU ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.

SEHEMU YA TANO

 AZIMIO LA ARUSHA 

Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community

Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka 29/1/67, inaazimia

ifuatavyo:

A. Viongozi

1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au

mfanyakazi na asishiriki katika jambo lolote la kibepari au

kikabaila.

2. Asiwe na hisa katika makampuni yoyote.

3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.

4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi

5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.

6. Viongozi tunaoikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya

Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa

na TANU, Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali, Viongozi kutokana

na kifungu chochote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na

Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa

mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au

mke na mumewe).

B. Serikali na Vyombo Vingine

1. Inaipongeza Serikali kwa hatua zote ilizokwishachukua mpaka

hivi sasa katika kutimiza siasa ya Ujamaa.

2. Inaihimiza Serikali, bila kungojea Tume ya Ujamaa, ichukue

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 43/142

MIONGOZO MIWILI42

hatua zaidi za kutimiza siasa yetu ya Ujamaa kama ilivyoelezwa

katika Tamko la TANU juu ya Ujamaa.

3. Inahimiza Serikali kutengeneza mipango yake kwa kutegemea

uwezo wa nchi hii kuiendesha mipango hiyo na wala isitegemee

mno mikopo na misaada ya nchi za ng’ambo kama ilivyofanya

katika mpango wa maendeleo ya miaka mitano. Halmashauri

Kuu ya Taifa inaazimia mpango huo urekebishwe ili ulingane na

siasa ya kujitegemea.

4. Serikali ione kuwa mapato ya wafanyakazi nje ya Serikali

hayapitani mno na yale ya wafanyakazi Serikalini.

5. Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.

6. Inahimiza NUTA, Vyama vya Ushirika, TAPA, UWT, TYL, mashirika

yote ya Serikali, kuchukua hatua ili kutekeleza siasa ya Ujamaa

na Kujitegemea.

C. Uanachama

Wanachama wafundishwe kwa ukamilifu imani ya TANU ili waielewe, na

wakumbushwe wakati wote umuhimu wa kuishika imani hiyo.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 44/142

MIONGOZO MIWILI 43

SURA YA PILI

MWONGOZO WA TANU WA 1971

  TUMECHOKA KUCHEZEWA

1. Mabeberu wathubutu  Kujifanya mbwa-mwitu,  Au kujifanya mwewe,  Kwa kuachia wenyewe  Tudhaniwe tu makoo  Ya kuku au kondoo.

2. Lakini watu ni watu,Watu si mang’ondi katu:Beberu angajigamba,Angaruka, angatamba,Ni mtu, hana mabawa:Naye hufa, hana dawa.

3. Sasa linalia tena

La mgambo, linanena:Beberu, leo ni leo!Tulipozima koleo,Mlidhani ndiyo mwisho,Mkazidisha vitisho!

4. Linalia la mgambo,  Lisikike hadi ng’ambo:  Tumechoka kuonewa!

  Tumechoka kuchezewa!  Tunasema: sasa basi  Ubeberu na uasi!

5. Kwani sasa kimeika,Kizazi cha Afrika;Kizazi kipya thabiti,Sumu yao wasaliti;Mabeberu watajuta

Hapo kitapowakuta.

6. Si kizazi cha vivuli,Na wala sio cha nduliSi kizazi cha watwana:Ni kizazi cha vijanaMadhubuti, Wajamaa,Waso ila, waso waa.

7. Kimeika pasi shaka  Kiyashike madaraka;  Wanaojidai ubwana  Watalia kama wana;  Watatetema kwa homa,  Na kutubu: Tumekoma!

8. Vijana wa Afrika,

Siku yenu imeika!Siku yenu ndiyo leo,Siku ya kufunga teo:Tumechoka kuonewa!Tumechoka kuchezewa!

9. Shime, Onyesheni njia,Vijana wa Tanzania:Wapigeni wanyonyao,

Pamwe na vijibwa vyao;Mabeberu makaburu,Wapigeni kwa uhuru.

 10. Wamezidi kutughasiKwa kudhani ndiyo basi:Semeni: leo ni leo,Twali tukisuka teo!Kimbieni, tumeika:

Iacheni Afrika!

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 45/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 46/142

MIONGOZO MIWILI 45

na mbinu zitakazotuwezesha kulinda, kuimarisha na kuendeleza

mapinduzi yetu.

2. Mapinduzi ni mabadiliko ya haraka katika jamii, mabadiliko

ambayo yanawanyang’anya wachache madaraka ambayo walikuwa

wakiyatumia kwa manufaa yao (na ya wanyonyaji wa nje), na

kuyaweka madaraka hayo mikononi mwa wengi ili kuendeleza

maslahi yao. Kinyume cha mapinduzi ni kupinga mapinduzi, yaani

mabadiliko ya haraka yanayo wanyang’anya madaraka wananchi

walio wengi, na kuwapa wachache, kwa madhumuni ya kuzuia

maendeleo ya Umma.

3. Shabaha kuu ya mapinduzi ya Afrika ni kumkomboa Mwafrika.

Ukombozi huu haudondoki kama mvua, bali hupatikana kwa

kupambana na unyonyaji, ukoloni, na ubeberu. Wala ukombozi

huu hauletwi na wataalam maalum. Wataalam wa ukombozi huu

ni sisi wenyewe tunaonyanyaswa, tunaonyonywa, na tunaoonewa.

Hakuna taifa lolote ulimwenguni lenye utaalam wa kufundisha

Waafrika jinsi ya kujikomboa. Wajibu wa kujikomboa ni wetu, na

utaalam wa mbinu za mapambano ya kujikomboa tutaupata katikamapambano yenyewe.

4. Kadhalika, hali ilivyo hivi sasa katika Afrika ni kwanba hakujawa

na wananchi wa nchi yoyote ya Afrika ambao wamekwisha ikia

kiwango cha ukombozi halisi. Afrika bado ni Bara la watu waliomo

katika unyonge wa kuonewa na kunyanyaswa, ndiyo kusema

kwamba Vyama vya Siasa vya kimapinduzi katika nchi nyingi za

Afrika zinazojitawala, kama vile TANU, bado vingali ni Vyama vyaUkombozi.

5. Mapinduzi ya Afrika ambayo lengo lake ni ukombozi kamili wa

Mwafrika yanapingana na siasa za unyonyaji za Ukoloni-Mamboleo

na Ubeberu na kuhakikisha kwamba utajiri wa Afrika unatumika

kwa maslahi ya nchi za kibepari za Ulaya na Marekani, badala

ya kuwanufaisha Waafrika wenyewe. Kwa hiyo kushiriki katika

mapinduzi ya Afrika ni kushiriki katika mapambano ya kupinga

Ukoloni na Ubeberu.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 47/142

MIONGOZO MIWILI46

6. Nchi za kibeberu ambazo zimekuwa zikinyonya na kukandamiza

Afrika kwa karne nyingi ni nchi za Ulaya Magharibi, hasa Uingereza,

Ufaransa, Ureno, Ubelgiji na Hispania. Nichi za kibeberu ndiyo hasa

zinazokabiliana na wananchi wa Afrika katika suala la ukomboziwa Mwafrika. Majaribio mbali mbali yanayofanywa kuvuruga

maendeleo ya mapinduzi ya Afrika hasa kutokana na hila za

mabeberu wa Ulaya kutaka kuhifadhi na kuendeleza mirija yao ya

zamani.

7. Kwa Tanzania lazima ieleweke kwamba maadui tunaokabiliana

nao ana kwa ana ni ubeberu wa Kiingereza, ukoloni wa Kireno, na

ubaguzi wa rangi wa makaburu wa Afrika ya Kusini na Rhodesia.Kwa sababu za historia, za jiograia na za siasa, mabeberu hawa

watakuwa tayari kutushambulia pindi wapatapo nafasi.

8. Mashambulio yaliyofanywa na mabeberu wa Kireno kuivamia

Jamhuri ya Guinea ni funzo kubwa sana kwetu. Sababu ya kwanza

ya Guinea kuvamiwa na mabeberu wa Kireno ni siasa yake ya usawa

na kupinga unyonyaji; na sababu ya pili ni msimamo wake thabiti

wa kuunga mkono wapigania ukombozi wa Guinea Bissau na waAfrika. Kwa sababu hizo hizo mabeberu hawa wanaweza siku moja

wakathubutu kuishambulia Tanzania. Lakini Guinea inatufundisha

vile vile kuwa wananchi na majeshi yao wakisimama imara pamoja,

hakuna mtu atakayeweza kuwanayang’anya uhuru wao.

9. Funzo tulilojifunza Uganda ni la usaliti na la kupinga mapinduzi.

Yaani, badala ya kuivamia nchi ili kuiangusha Serikali ya

kimapinduzi, mabeberu hupendelea sana kuwatumia vibarakawananchi kuiangusha Serikali halali, ili kuunda Serikali ya

wanyapara, itakayowaruhusu mabeberu hao, wakishirikiana

na vibwanyenye vienyeji, kunyonya mali ya Taifa. Wananchi

inawapasa kuelewa, kutokana na tukio la Uganda na hata la

Guinea kwamba ingawa ubeberu bado una nguvu, uwezo wake wa

kuangusha Serikali ya Kimapinduzi unategemea sana uwezekano

wa kuwapata wapinga mapinduzi wa ndani wa kuwasaidia

kuyasaliti mapinduzi.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 48/142

MIONGOZO MIWILI 47

10. Watanzania tunathamini sana uhuru wa Taifa letu, maana hapo

ndipo unapoanzia ukombozi wetu, na mategemeo ya mapambano

ya ukombozi wa wananchi wengi wa Afrika. Kwa sabau hii

tunawajibu wa kuchukua hatua zote muhimu zitakazotuwezeshakuulinda uhuru wetu, ili tuweze kuendeleza mapinduzi yetu, na

kuifanya nchi yetu kuwa mfano imara wa mapinduzi ya Afrika.

SIASA 

Chama

11. Wajibu wa kuongoza Umma na vyombo vyake mbali mbali katika

juhudi ya kulinda uhuru, ili mapinduzi ya ukombozi wa Mwafrika

yaendelee, ni wa Chama. Wajibu wa Chama cha Kijamaa ni kuongoza

shughuli zote za Umma. Serikali, Mashirika, Vyama vya Umma, n.k,

ni vyombo vya kutekelezea siasa ya Chama. Historia yetu fupi ya

uhuru inaonyesha matatizo yanayoweza kutokea wakati Chama

hakiongozi vyombo vyake. Sasa wakati umeika wa chama kushika

barabara hatamu na kuongoza shughuli zote za Umma.

12. Kuongoza kwanza maana yake ni kutoa lengo la Taifa. Hili

linaeleweka, na Chama kimekwisha timiza wajibu huo. Lengo letu

ni kujenga Ujamaa Tanzania. Chama kimekwisha toa miongozo juu

ya Ujamaa vijijini, Elimu ya Kujitegemea¸n.k. Lakini, ili lengo la Taifa

liweze kuikiwa, lazima chama kitoe siasa na miongozo kuhusu

mipango mbali mbali ya shughuli za umma. Uko umuhimu wa

kufafanua siasa ya Chama juu ya nyumba, afya, kazi, siasa ya fedha,mikopo n.k.

13. Lakini kutoa lengo la siasa hakutoshi kudhihirisha uongozi

madhubuti wa Chama. Maana nyingine ya kuongoza ni kuwaandaa

watu. Ndiyo kusema Chama ndicho kinachoamua umbile la

Serikali, mashirika mbali mbali, majeshi, n.k. Pamoja na umbile

la Serikali, Chama kitoe mwongozo juu ya utaratibu wa kutenda

kazi, na namna ya kuikia uamuzi. Ukweli ni kwamba siyo tu kuwatumerithi muundo wa Serikali ya kikoloni, bali hata tabia za kikoloni

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 49/142

MIONGOZO MIWILI48

za utaratibu wa uongozi tumezifanya zetu. Kwa mfano, Serikalini,

viwandani, na katika Mashirika ya Umma, tumerithi tabia ya utawala

wa mtu mmoja, na wengine ni watu wa kupokea amri. Matokeo ya

watu kutokushirikishwa katika mipango ya kazi ni kuwafanya watuwakione chombo cha Umma kana kwamba si chombo chao, na

wafanya kazi kuwa na tabia ya wakodiwa. Chama kina wajibu wa

kuchukua hatua za kudhihirisha uongozi wake katika jambo hili.

14. Pamoja na kuwaandaa watu, kuongoza ni kusimamia utekelezaji

wa siasa ya chama. Lazima zitafutwe njia za kuhakikisha kwamba

Chama kinasimamia, kwa vitendo shughuli na mwendo wa vyombo

vyake vya utekelezaji. Kadhalika, kuongoza ni kuweza kupimamatokeo ya utekelezaji. Ni wajibu wa Chama kuhakikisha kwamba

kinapima matokeo ya utekelizaji wa siasa unaofanywa na vyombo

vyake. Hii ndiyo njia ya pekee ya kuweza kuwa na hakika kwamba

maoisini, viwandani, katika majeshi, vijijini, n.k. wananchi wenyewe

wanashiriki katika kutafuta njia za kutatua matatizo yao.

15. Pamoja na suala la watu kushiriki katika kutatua matatizo yao

kuna swala la tabia ya viongozi kazini na katika maisha yao ya kilasiku. Lazima iwepo jitihada ya kujenga usawa kati ya viongozi na

waongozwa. Iwe ni mwiko kwa kiongozi wa Tanzania kuwa mwenye

majivuno, ubadhirifu, dharau au uonevu. Kiongozi wa Tanzania awe

mtu anayeheshimu watu, asiwe mpenda makuu; siyo mnyapara,

mkaripiaji na mwamrishaji watu. Kiongozi awe mfano wa ushujaa,

upiganiaji haki na usawa. Kadhalika Chama kina wajibu wa kukomesha

maonevu yanayofanywa na baadhi ya vyombo vyake kwa wananchi,

maana vitendo hivi haviendelezi Siasa ya Ujamaa. Hivyo ni vitendo

vinavyokifanya Chama na Serikali vifarakane na watu.

 16. Kuna tabia hivi sasa ya baadhi ya viongozi kutotimiza masharti hayo,

na kupuuza na kukwepa kiujanja masharti na nia ya masharti ya

Uongozi. Wakati umeika wa Chama kuwa na utaratibu wa kusimamia

mwenendo na tabia za viongozi.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 50/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 51/142

MIONGOZO MIWILI50

wa nchi za Afrika Mashariki huenda ukawa wa shida sana na dhaifu.

Chama kinaunga mkono msimamo wa Serikali ya Tanzania juu ya

Uganda na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ingawa swala la ukombozi

wa Uganda ni la wananchi wa Uganda, ni wajibu wa wananchi waTanzania kuunga mkono ndugu zetu wa Uganda katika juhudi zao

za kujikomboa.

ULINZI NA USALAMA 

“Katika upande wa ulinzi wa Taifa, wananchi wawe macho

na vibaraka waliomo nchini ambao wanaweza kutumiwa

na maadui wa nje wenye nia mbaya ya kuliangamiza Taifa

inapolazimika kufanya hivyo.” 

  (Azimio la Arusha)

21. Msingi wa Maendeleo yote ya Watanzania ni Watanzania wenyewe:

kila Mtanzania; na hasa kila mzalendo, na kila mjamaa. Msingi

wa Maendeleo ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania ni Watanzania

wenyewe: kila Mtanzania; na hasa kila mzalendo, na kila mjamaa.

22. Kama Chama chetu kingalilazimika kupigana Vita vya Ukombozi,

kila mwana-TANU angalilazimika kuwa askari, ama ndani ya

jeshi, au popote alipo: Mwana-TANU angalikuwa ni Mwanajeshi,

na Mwanajeshi angalikuwa ni Mwana-TANU. Siyo Chama chetu tu

ambacho kingalikuwa ni Chama cha Ukombozi; bali Jeshi letu pia

lingalikuwa ni jeshi la Ukombozi-ngumi na ngao ya Chama cha

Ukombozi.

23. Chama chetu hakikulazimika kupigana Vita ya Ukombozi. Kilikuwa

Chama cha Ukombozi bila Jeshi la Ukombozi. Likini tangu mwaka

1964 tumekuwa tukiunda Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Kama vile

Chama cha TANU kilivyo bado ni Chama cha Ukombozi; basi Jeshi

la Wananchi wa Tanzania pia ni Jeshi la Ukombozi wa Wananchi wa

Tanzania. Uhusiano wa TANU na Jeshi la Wananchi ni lazima uwe

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 52/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 53/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 54/142

MIONGOZO MIWILI 53

si haki kwa viongozi na wataalam kujinyakulia wajibu wa kuamua

kila jambo badala ya wananchi wenyewe, ati kwa sababu wao ndio

wenye ujuzi.

 29. Ili wananchi wawe na ari ya kulinda nchi yao, lazima Serikali ya

TANU kwanza itilie nguvu sana hali ya Uchumi wa wananchi.

Mtindo wa Uchumi tuliorithi kwa wakoloni, ambao umewatupa

wananchi wengi nje ya uchumi, lazima ubadilishwe bila kukawia,

na kuanzisha mipango ya kuongeza matumizi na kutumbukiza

rasilimali katika Wilaya zote. Kwa mfano, Mpango wa Fedha za

Maendeleo Mikoani umeonyesha kusaidia kuamsha shughuli za

kiuchumi na kuleta manufaa ya wazi wazi kwa wananchi, na itafaampango huo utiliwe mkazo kwa kuongeza fedha hizo na kufanya

matumizi hayo yawe ya mwanzo katika makisio ya fedha za Serikali.

Chama kitilie mkazo kushirikisha watu katika kazi mbali mbali za

kujenga Taifa.

 Akiba

30. Pia ni wajibu wa Chama kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa

kujiwekea Akiba katika vyombo vya Umma, kama vile Benki ya

Akiba na Benki ya Biashara badala ya kuweka ovyo ovyo tu.

Uchumi wa Kitaifa

31. Katika kuimarisha Maendeleo ya watu, hivi sasa ipo haja kubwa ya

kujenga na kustawisha uchumi wa ndani ya Taifa letu. Ingawa jambo

hili limegusiwa katika Mpango wa Pili wa Miaka Mitano, halikutiliwa

mkazo katika utekelezaji, na matokeo yake hayajaonekana. Kadhalika,

vitu ambavyo vinatengenezwa nchini mwetu lazima vilindwe na

mashindano yasiyo ya lazima kutoka nchi za nje.

Biashara ya Nje

32. Juu ya Biashara yetu na nchi za nje ni lazima kuepuka utumiaji

wa akiba yetu ya fedha za Kigeni kwa kununua vitu visivyosaidia

Uchumi wetu. Serikali na Mashirika yake vionyeshe mfano katika

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 55/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 56/142

MIONGOZO MIWILI 55

SURA YA TATU

MWONGOZO WA CCM WA 1981

YALIYOMO

DIBAJI 

SEHEMUYA KWANZA

UTANGULIZI

 SEHEMUYA PILI

UCHAMBUZIWA KUJIKOSOA KAMA CHAMA

SEHEMUYA TATU

KUJENGAMSINGI WA UCHUMI WA KIJAMAA WA TAIFA

LINALOJITEGEMEA

SEHEMUYA NNE

CHAMANA MAPINDUZI YETU

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 57/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 58/142

MIONGOZO MIWILI 57

SEHEMU YA KWANZA 

Utangulizi

1. Historia ya Watanzania kwa vile ni sehemu tu ya historia kubwazaidi ya Waafrika kwa jumla lazima wakati wote ichambuliwe na

kueleweka katika mazingira ya umoja wa Afrika na watu wake.

Waafrika wamepitia vipindi na karne za fanaka na maendeleo ya

jamii na pia vipindi na karne za misukosuko mikubwa na hata

unyonge kitaifa.

2. Historia ya Waafrika ina mifano ya dola zilizoikia hatua kubwa

ya maendeleo, ustaarabu na fanaka katika sehemu mbalimbali zabara hili na kwa nyakati mbalimbali. Maandishi, magofu, zana na

mabaki ya vifaa vya aina mbalimbali vinavyogunduliwa sasa na

wataalamu katika sehemu mbalimbali za Afrika vinathibitisha

ustaarabu wa wakati huo katika fani za kilimo, ujenzi, vita,

biashara na siasa.

3. Historia ya bara hili pia ina kumbukumbu za vipindi vya misukosuko

ya kuingia kwa mataifa ya kigeni. Kuna kipindi Waasia walipoingiaAfrika kwa madhumuni ya kujinufaisha na biashara walizoendesha

humu Afrika. Mojawapo ya biashara haramu walizoanzisha ni

biashara ya watumwa ambayo ilienea hata hapa Tanzania. Biashara

ya Watumwa katika Afrika iliendeshwa pia na mataifa ya Ulaya.

Inakisiwa kuwa Waafrika wapatao milioni mia moja walihusika

na biashara hii ya utumwa. Kumbukumbu za kipindi hiki ambacho

watu walisakwa, walikamatwa na kuuzwa bado zingali hai miongoni

mwa Watanzania.

4. Kipindi kilichofuatia ni cha wakoloni wa mataifa ya Ulaya

waliowanyang’anya Waafrika ardhi yao, kuigawa na halafu

wakawatawala. Wakati huu Watanzania walitumikishwa na

wakoloni. Mazao na matunda ya jasho lao yalichukuliwa kupelekwa

nchi za wakoloni kujenga uchumi wao.

5. Watanzania, kama ilivyokuwa kwa Waafrika wengine kote

barani Afrika, hawakukiri uvamizi, utumwa wala kutawaliwa bali

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 59/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 60/142

MIONGOZO MIWILI 59

walilazimishwa kushirikiana na wakoloni wa Kijerumani au wa

Kiingereza kutetea ukoloni na kwa mara nyingine tena wengi

walipoteza maisha yao katika vita visivyokuwa vyao.

10. Lakini, pamoja na hayo vuguvugu la kisiasa liliongezeka. Haikupita

miaka mingi baada ya Vita Vikuu vya Kwanza ishara za kwanza

zilijitokeza Bara na Visiwani. Mwaka 1929 Waafrika walianzisha

African Association kwa Bara ambayo mwaka 1948 ikajiita

Tanganyika African Association na 1934 walianzisha African

Association Visiwani, vyote vikiwa vyama vilivyojishughulisha

na ustawi wa jamii pamoja na utetezi wa maslahi fulani fulani ya

Waafrika.

11. Mwisho wa Vita Vikuu vya Pili ulifuatiwa na vuguvugu la mwamko

wa kisiasa ulioongezeka kutokana na hali ya ukoloni nchini

kuwakera na kuwabana mno wananchi pamoja na vuguvugu la

askari waliorudi toka mpakani.

12. Wakati huo huo, kuongezeka kwa idadi ya wafanyakazi bandarini

na Serikalini na siasa ya ubaguzi wa rangi na ya mishahara

iliyoendeshwa na watawala wa Kiingereza kuliwatia wafanyakazi

dukuduku la kutaka kuungana na kupigania haki zao. Mgomo

mkubwa wa kwanza wa makuli wa Dar es Salaam na pia Zanzibar

uliowatikisa wakoloni ulitokea kunako mwaka 1948. Hali ilikuwa

inajiandaa kwa uwezekano wa kuanzishwa vyama halisi vya kisiasa

nchini.

 A. KUZALIWA KWA TANU NA ASP

13. Historia ya sasa ya mapambano ya ukombozi katika Tanzania

ni historia ya vyama vya kisiasa vya TANU na ASP. Tanganyika

African Association na African Association na Shirazi Association

kwa Zanzibar vilianzisha vuguvugu la siasa na kuandaa mazingira

ya kuviwezesha vyama kamili vya kisiasa kujitokeza. Vuguvugu la

vyama vya wafanyakazi nalo liliongezea joto joto la kisiasa nchini.

Wakati huo huo nchi nyingine kama Ghana ya Kwame Nkrumah

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 61/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 62/142

MIONGOZO MIWILI 61

kimapinduzi cha kuunganisha nchi mbili hizi katika Muungano wa

Tanganyika na Zanzibar ambao sasa unaitwa Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania.

B. MAPAMBANO YA KULINDA UHURU NAKUJENGA JAMII MPYA 

18. Serikali ya Mapinduzi ya ASP haikuchelewa kuchukua hatua za

kuimarisha ushindi iliyoupata dhidi ya usultani. Hatua muhimu

katika fani za siasa, uchumi na ustawi wa jamii zilichukuliwa kama

msingi wa kwanza katika kazi ngumu ya kuijenga jamii mpya ya

haki na usawa. Ardhi ilitaiishwa na hodhi kubwa za makabaila

wa kiarabu waligawiwa umma wa wananchi wasiokuwa na ardhi.

Wakati huo huo mabenki na biashara ya nje zilitaiishwa na vyombo

vya umma kuundwa.

19. Serikali ya TANU haikuchelewa kuchukua hatua za dhati za

kujiimarisha ili kuikabili kazi kubwa ya kulinda uhuru na kuanza

ujenzi wa uchumi na wa jamii mpya inayojitawala katika hali ya

matazamio makubwa ya wananchi kwamba uhuru utawaleteamabadiliko ya haraka katika hali ya maisha yao. Miaka mitano ya

kwanza iliyofuatia uhuru ilikuwa kipindi kigumu kwa TANU na

Serikali yake changa. TANU yenyewe ilibidi iondokane na hali ya

kuwa Chama cha kupigania uhuru na kuwa Chama cha kulinda

uhuru na kujenga Taifa linalojitawala. Wakati huo huo Chama

kiliwajibika kuiongoza Serikali na wananchi kwa jumla katika

jitihada ya kutafuta falsafa ya jamii itakayolingana na matazamio yawananchi na inayoweza kuwaletea maendeleo halisi nchini.

20. Ilidhihirika katika miaka hiyo ya mwanzo ya uhuru wa Tanganyika

kuwa mgongano ulianza kujengeka kati ya matazamio ya wananchi

kwa jumla kwamba uhuru ungaliwaletea mabadiliko katika

hali ya maisha yao na kwa haraka, na uwezo mdogo wa Serikali

wa kukidhi haja za wananchi kulingana na matazamio yao.

Mabadiliko makubwa ya mapato na hali ya maisha yaliyoonekanakwa wachache, viongozi na maaisa wa Chama na serikali

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 63/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 64/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 65/142

MIONGOZO MIWILI64

kupoteza maisha yao na pia ushindi wetu dhidi ya majeshi ya uvamizi

ya Iddi Amin ambao umepatikana kutokana na mshikamano sahihi

wa Chama, Serikali, wananchi na wapiganaji, yote haya ni mafanikio

ya ujamaa.

26. Tungeweza kuendelea kukariri mafanikio yaliyopatikana

nchini kutokana na utekelezaji wa siaisa ya Chama ya Ujamaa

na Kujitegemea. Lakini jambo la kuzingatia ni kuwa hatua

tulizozichukua katika kutekeleza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea

ni za awali tu na kwamba kubwa zaidi tulilofanikiwa ni kujichorea

barabara tunayodhamiria kufuata katika kulijenga Taifa letu la

watu sawa na huru ambalo lengo lake ni maendeleo kwa wote.

SEHEMU YA PILI

UCHAMBUZI WA KUJIKOSOA KAMA CHAMA 

(1) Upungufu katika kusimamia uchumi

27. Halmashari Kuu ya Chama ya Taifa katika kikao chake cha tarehe 15

hadi 17 Mei, 1981 ilizingatia hali ya uchumi na jamii inayolikabiliTaifa na kufanya uchambuzi ili kubainisha kiini cha matatizo haya.

Uchambuzi uliofanywa ulidhihirisha mambo makubwa matatu.

Kwanza, ni kwamba matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi yetu

si ya kipekee kwa Tanzania bali ni matatizo yaliyozikumba nchi

zote, zisizoendelea na hata zile zilizoendelea, zilizoamua kujenga

ujamaa na zile zilizoamua kujenga ubebari.

28. Jambo la pili lililodhihirika ni kuwa baadhi ya sababu za matatizoyetu ya kiuchumi ziko nje ya uwezo wetu. Mfumo wa biashara ya

kimataifa ulivyo unazikandamiza na kuzinyonya nchi changa kama

Tanzania. Kwa mujibu wa mfumo huu wa biashara ya kimataifa nchi

za viwanda zinajipangia bei za bidhaa za viwanda vyao na kutuuzia

sisi na wakati huo huo nchi hizo hupanga wao bei za mazao ya

kilimo tunayozalisha sisi na kuwauzia. Vile vile Tanzania haina

kauli na bei za mafuta tunayoyaagiza toka ng’ambo.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 66/142

MIONGOZO MIWILI 65

29. Sasa, bei za mafuta na bei za bidhaa za viwanda vya nchi zilizoendelea

zimepanda sana katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Tanzania

sasa inawajibika kutumia asilimia sitini ya mapato yake yote ya

fedha za kigeni kununulia mafuta ambapo mwaka 1972 ilitumiaasilimia kumi ya fedha za kigeni kununua kiasi hicho hicho cha

mafuta. Wakati huo huo, kwa kutumia mbinu za kupandisha

bei za bidhaa zao za viwanda na kushusha bei za mazao ya nchi

changa, nchi zilizoendelea zimefaulu kuupunguza kabisa uwezo

wetu wa kununua bidhaa za viwanda vyao zinazohitajika sana na

nchi changa. Kwa mfano, miaka kumi iliyopita Tanzania iliweza

kununua trekta moja toka ng’ambo kwa thamani ya tani tano za

chai iliyouzwa ng’ambo. Leo Tanzania inahitaji tani kumi na saba za

chai ili kununua trekta la aina ile ile. Hali hii lazima iwe na matokeo

mabaya kwa uchumi wa Taifa letu.

30. Nchi yetu pia imepatwa na matatizo ya ndani ambayo pia

tusingekuwa na uwezo wa kuyazuia na yote yameathiri hali

yetu ya uchumi. Matatizo hayo ni pamoja na vita vya kujihami

tulivyolazimika kupigana dhidi ya majeshi ya uvamizi wa Iddi Amin,

mafuriko makubwa ya 1978/79 na hali ya ukame katika baadhi ya

mikoa.

31. Jambo la tatu lililodhihirika vile vile ni kwamba sisi wenyewe

kama taifa hatukutumia kwa kiasi cha kutosha nguvu za Chama,

Serikali na za wananchi katika kutatua matatizo ya uchumi ambayo

ufumbuzi wake tuna uwezo nao.

32. Jambo la kwanza linahusu kilimo kwa jumla. Pamoja na kuwa bei zamazao yetu tuyauzayo ng’ambo imekuwa ikishuka, mapato ya fedha

za kigeni kwa Taifa kutokana na mazao yanategemea pia kiasi taifa

linachozalisha na kuuza. Taifa linalozalisha kidogo litauza kidogo

na kupata fedha chache za kigeni. Likizalisha mazao kwa wingi na

kuuza litapata fedha za kigeni zaidi. Lakini, utoaji wa karibu mazao

yetu yote ya biashara umepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Ni dhahiri kuwa hata kama tumekuwa na matatizo ya mafuriko

na ya ukame hapa na pale, kushindwa kwetu kuongeza utoaji

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 67/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 68/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 69/142

MIONGOZO MIWILI68

la kujenga ujamaa haliwezi kuikiwa. Kikosi hicho cha wapiganiaji

ujamaa wa mstari wa mbele ni wanachama wa Chama Cha

Mapinduzi.

39. Vyama vyetu asilia, ASP na TANU, vilifaulu kuwawezesha

wanachama wake kuwa kikosi thabiti cha mstari wa mbele cha

kupigania uhuru. Wanachama hao kwa jumla walijitolea mhanga

kwa ajili ya mapambano ya uhuru wa nchi yao, mapambano yao

waliyaweka kabla ya maslahi yao binafsi na mengine yoyote.

Tutakuwa tunajidanganya tukisema kuwa wanachama wote wa

Chama cha Mapinduzi na pia wanachama wote wa TANU na ASP

katika miaka kadhaa kabla ya kuundwa kwa CCM, walikuwa kikosikinachotimiza sifa hizo kwa upande wa lengo la kujenga Ujamaa.

Mapambano ya uhuru yalikuwa ya wenyewe, wanaTANU na wana

ASP wa enzi hizo, na kuwa wananchi waliobaki walielimishwa,

walihamasishwa na walishirikishwa katika mapambano ambayo

chimbuko la vuguvugu lake lilikuwa msimamo na vitendo vya

wanachama. Katika maana hiyo, mapambano ya kujenga Ujamaa

Tanzania lazima yawe na wenyewe.

40. Hali hii haikuzuka siku moja bali ni matokeo ya msimamo na

vitendo vya miaka mingi. Ilianza tangu baada ya uhuru, wakati

viongozi wa ngazi ya taifa, Mkoa na Wilaya hawakuipa uzito kwa

vitendo nafasi ya mwanachama katika mapambano yetu. Karibu

viongozi wote tulishughulika na mikutano ya hadhara, mikutano

ya wananchi kwa jumla bila ya kujali kukutana na wanachama.

Viongozi wengine wa Chama tulilemazwa na umangi meza na

wengine hata kuikiri wangeimarisha utekelezaji wa shughuli

za Chama kwa njia ya vyombo vya habari tu. Ingewezekana kwa

viongozi kuhakikisha kuwa kila baada ya mikutano ya hadhara ya

wananchi wote, ambayo pia ina umuhimu wake, wanakutana na

wanachama wenzi wao ili kuulizia juu ya hali ya Chama mahali

hapo na pia kuonyesha kuwa uanachama ulikuwa na maana na

uzito maalum ambao viongozi wanautambua. Lakini hatukufanya

hivyo na matokeo yake ni kwamba ikra zilijengeka kuwa uananchiulikuwa unatosha kabisa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 70/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 71/142

MIONGOZO MIWILI70

upeo wao wa kuielewa siasa ya ujamaa, mafunzo ya mbinu za

kushiriki na kuongoza umma mahali walipo katika harakati za

kujenga ujamaa na mafunzo ya kuwapa uwezo wa kueneza na

kutetea siasa ya Chama. Mafunzo haya hutolewa na vyuo vya Chamakwa utaratibu na malengo yaliyo wazi.

(3) Umuhimu wa nadharia sahihi ya Ujamaa

44. Pamoja na upungufu wetu kama Chama kuhusu nafasi ya uanachama

na wanachama katika mapambano yetu ya kujenga ujamaa kuna

suala linalohusu umuhimu wa nadharia sahihi ya Chama. Chama

ni muungano wa watu wanaokubaliana juu ya lengo katika jamii na

namna ya kuliikia. Kinachowaunganisha ni ikra zao, itikadi yao,

inayohusu jinsi gani shughuli za jamii nchini ziendeshwe na kwa

maslahi ya nani. Ni muhimu kusisitiza kuwa kinachowaunganisha

wanachama ni itikadi, ikra na falsafa yao ya siasa.

45. Lakini masuala ya falsafa, itikadi na ikra ni masuala ya nadharia.

Hivyo suala la nadharia ya Chama ni suala la msingi kabisa kwa uhai

wa Chama, kwa maendeleo ya mapambano ya Chama, kwa malengo

na mbinu za mapambano hayo na kwa umoja, nguvu na usahihi wa

vitendo vya Chama na vya wanachama.

46. Chama chetu ni miongoni mwa vyama vichache katika Afrika

ambavyo vimefaulu kubuni nadharia ya ujamaa iliyo sahihi, wazi

na ya kiwango cha juu. Nadharia hiyo ya Chama inajidhihirisha

yenyewe katika Katiba, Azimio la Arusha, Mwongozo na maandishi

mengine muhimu ya Chama. Nadharia hii ya siasa yetu ya Ujamaa

na Kujitegemea imetujengea msingi wa uelewano, umoja na

ushirikiano wa aina mpya katika ujenzi wa taifa na kutufanya

tueleweke na wengi kimataifa, jambo ambalo limetupa sifa na

heshima duniani kote.

47. Tumetamka hapo awali katika kujikosoa kuwa siku za nyuma

tumeonyesha upungufu kwa kutokuwa na mipango thabiti ya

kuwaandaa wanachama na hasa viongozi. Upungufu huu umekuwa

na matokeo kwa upande wa nadharia. Pamoja na nadharia fasaha

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 72/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 73/142

MIONGOZO MIWILI72

Kuielewa vema jamii ya Tanzania ya leo kunataka uchambuzi wa hali

ya juu pia. Uchambuzi huu ukiwezeshe Chama kuielewa migongano

ya maslahi ya tabaka ambayo imejitokeza nchini. M i g o n g a n o

hii ina mizizi yake katika mgongano wa msingi kati ya ujamaa naubepari, kati ya maslahi ya wakulima na wafanyakazi kwa upande

mmoja, na ya ubinafsi ubwanyenye na ubepari ambao umekuwa

ukijengeka tangu Azimio la Arusha kwa upande mwingine. Kwa

hiyo, ili Chama kiweze kuendelea kuongoza mapambano ya kujenga

ujamaa ni muhimu kuwa na uwezo wa kufanya uchambuzi sahihi

wa hali ya jamii yetu.

51. Jambo linalosisitizwa hapa ni kuwa kwa Chama Cha Mapinduzikuongoza ipasavyo siasa ya ndani na ya nje ya nchi yetu ni muhimu

kwa viongozi wa ngazi zote na pia wanachama kuwa na uwezo

wa hali inayoridhisha ya nadharia kama silaha katika kutekeleza

jukumu hilo. Hivyo, ni jambo la umuhimu wa kwanza kwa viongozi

na wanachama kujiendeleza katika nadharia ya siasa ya Chama.

Kwa kiongozi au mwanachama wa CCM kupuuza, kudharau au

kukataa kujiendeleza katika nadharia kwa visingizio vyovyote ni

msimamo wa uhasama dhidi ya maendeleo ya Chama.

52. Ujenzi wa ujamaa si lelemama bali ni mapambano, mapambano ya

kudumu dhidi ya ubepari na unyonyaji, dhidi ya wapinga maendeleo

na wababaishaji wa kisiasa, dhidi ya wahujumu uchumi, majambazi,

wezi, wazururaji na wazembe. Msimamo sahihi wa mapambano

unaotokana na nadharia sahihi ya ujamaa ungelituepusha na maamuzi

na vitendo ambavyo vimerahisisha kuoteshwa kwa mizizi ya ubepari,

kinyume cha msimao wa mapambano dhidi ya ubepari. Leo ubepari

una vishawishi vingi zaidi nchini kuliko ulivyokuwa kabla ya Azimio

la Arusha kwa sababu pamoja na kwamba sasa tuna sekta kubwa

ya umma lakini kutokana na udhaifu wa kutopambana nao, ubepari

umefaulu kujipanua na kujipenyeza hata ndani ya sekta yenyewe

ya Umma. Na ndiyo maana ubepari sasa unathubutu kujitokeza

hadharani kuukashifu ujamaa, kubabaisha baadhi ya viongozi na

kututaka tubadilishe siasa yetu.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 74/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 75/142

MIONGOZO MIWILI74

nyuma ni kuwa hatukutilia mkazo umuhimu wa kujenga ujamaa

ndani ya vyombo vya umma na hii imerahisisha ikra na tamaa za

kibepari kuzagaa katika vyombo hivi na mwisho kutekwa nyara ili

vihudumie ubepari na ubinafsi.

56. Upungufu wa kuuelewa vilivyo uhusiano wa nadharia na vitendo katika

harakati za ujamaa unaweza kusababisha pia msimamo usio sahihi wa

kutenganisha jukumu la uongozi na utendaji au kazi. Uongozi si kazi

ingawa zipo kazi za uongozi. Hivyo, wajumbe wa vikao vya Chama ni

lazima wawe au na kazi zao za kawaida kama za ajira au kilimo ama

wawe na kazi za uongozi katika Chama, Serikali au Mashirika ya Umma.

Vinginevyo kutakuwa na watu katika Chama ambao si wakulima walasi wafanyakazi na huu ndio mwanzo wa kujenga kundi la wababaishaji

wa kisiasa, jambo ambalo ni hatari sana kwa harakati za ujamaa. Tabia

ya kutenganisha uongozi na utendaji imeathiri maendeleo ya Chama

kwa msukumo, usimamizi na utekelezaji maana kati ya uamuzi na

utendaji kumekuwa hakuna kiungo.

57. Tatizo hili la kutenganisha uongozi na utendaji linaweza pia

kukizorotesha Chama kwa kukifanya kisahau kuwa chenyewevile vile ni mtendaji na kwamba kitapimwa kwa vitendo vyake

kama Chama. Katika maana hiyo Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi

ipimwe na vikao vya juu kwa utekelezaji wake wa Siasa ya Chama;

kama wanachama wake wako mstari wa mbele kwa ujamaa, kama

wanashiriki katika shughuli za kujitolea, kama ni wafanyakazi hodari,

kama kijiji chao kina maendeleo ya kijamaa na kadhalika. Vivyo hivyo

kwa kamati ya utendaji ya Wilaya, Mkoa na Taifa. Kwa hiyo, pamoja

na kushughulikia uongozi wa serikali, Jumuiya na vyombo vingine,

Chama kina kazi ya kujijenga chenyewe ili kujipa uwezo wa kutosha

wa kuongoza Umma na vyombo vyake, ili kutekeleza majukumu yake

ambayo ndiyo sababu ya kuwepo kwake.

(5) Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi

58. Kuna mambo mawili tuliyojifunza ambayo ni muhimu pia

kuyazingatia. La kwanza linahusu suala la kukosoa, kujikosoa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 76/142

MIONGOZO MIWILI 75

na kukosoana kama njia ya kukijenga na kukiimarisha Chama

na wanachama. Ni kweli kuwa katika TUJISAHIHISHE Mwalimu

anasisitiza jambo hili na kwamba Katiba ya CCM inatamka waziwazi

juu ya umuhimu wake. Lakini ni kweli pia kuwa hatujaijenga tabiahii ipasavyo. Mara nyingi tumependelea kuteteana, kuichiana

makosa na hata kutafuta visingizio visivyo na msingi. Neno kuleana,

kwetu sisi (ingawa kuna malezi mema na mabaya) limechukua

nafasi ya kukosoana. Wanachama wenye upungufu husaidiwa

kama wanakosolewa ili wajirekebishe. Lakini hatua za nidhamu

wakati mwingine zimechukuliwa bila ya mhusika kuelezwa wazi

wazi upungufu wake ili ajirekebishe na pia wananchi wameachiwa

wabuni wenyewe sababu.

59. Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana lina sura kadhaa.

Kwanza linataka wanachama na viongozi kuwa tayari kusema

kweli katika vitendo vyao na kukubali kuambizana ukweli. Pili,

linataka wanachama na hasa viongozi wawe tayari kukosolewa

bila kuhamaki na inapobidi kukubali kujirekebisha. Tatu ni kuwa

Chama chenyewe katika vikao vyake vya ngazi mbalimbali kuwa na

utaratibu wa kujikosoa.

60. Sura hii ya tatu ni muhimu sana kwa mafanikio ya utekelezaji

wa siasa ya Chama. Kuongoza ni kutoa maamuzi yanayohusu

utekelezaji wa siasa. Kujikosoa kama Chama ni kuwa na utaratibu

wa kuyarudia maamuzi ya nyuma, kuona jinsi yalivyotekelezwa na

kupima matokeo ya utekelezaji huo kwa kuzingatia nia ya Chama

katika kutoa uamuzi huo. Kama makosa yamefanyika katika

utekelezaji basi ni muhimu kutafuta sababu za makosa hayo na

kuchukua hatua za haraka za kuyarekebisha. Makosa pia yanaweza

kutokana na uamuzi wenyewe kutokuwa sahihi. Katika hali hiyo,

itabidi uchambuzi ufanywe ili kubainisha kiini cha upungufu wa

uamuzi huo na kuchukua hatua za kurekebisha mambo. Kama kuna

mafanikio basi ni nafasi kwa Chama kuzingatia mbinu zilizotumika

kwa manufaa ya utekelezaji wa baadaye. Hivyo utaratibu wa

kujikosoa kwa Chama ukitekelezwa kwa dhati ni shule kubwa yaujenzi wa Ujamaa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 77/142

MIONGOZO MIWILI76

61. Ni dhahiri kuwa mapinduzi yetu yangekuwa yamepiga hatua

kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa kama tungezingatia utaratibu huu

wa harakati za kujenga Ujamaa. Mfano mmoja unatosha kuelezea

ukweli wa mambo. Msimamo wa Chama juu ya UJAMAA VIJIJINIuliopitishwa na Mkutano Mkuu wa Chama, Mwanza, mwezi Oktoba,

1967. Tangu wakati huo wananchi wameitikia mwito huo kwa njia

na mafanikio mbalimbali. Lakini hadi sasa, miaka kumi na minne

baadaye, hakuna kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichokaa

na kupima maendeleo ya Ujamaa vijijini, kubainisha kilichofanya

kuwa mpaka sasa sekta ya ujamaa vijijini ikawa bado inyu na

kutafuta malengo na mbinu mpya za kuleta msukumo wa ujenzi

wa ujamaa vijijni. Ni dhahiri kuwa Chama kingalifanya hivyo kila

mwaka na baada ya kila miaka mitano, kiwango cha ujamaa vijijini

na nchini kingelikuwa cha juu kuliko kilivyo sasa na kwamba Chama

kingalikuwa na hazina kubwa zaidi ya mbinu za kuongoza harakati za

ujamaa. Na kwa kuwa ujamaa vijijini kwanza kabisa ni utengenezaji

mali, basi maendeleo ya vijijini hii leo yangekuwa yamepiga hatua

kubwa na kwamba huenda matatizo ya sasa ya upungufu wa ziada ya

mazao nchini yangelikuwa yamepatiwa ufumbuzi wake.

62. Msimamo wa kujikosoa ni msimamo wa kimapinduzi. Unazingatia

upungufu wa binadamu na papo hapo kutambua uwezo wa

binadamu wa kufanya vizuri na zaidi mradi tu anajipa nafasi ya

kujifunza, kujirekebisha na kujaribu tena na tena. Kwa Chama

cha kijamaa kama Chama cha Mapinduzi hakuna kinachoweza

kuchukua nafasi ya kujikosoa.

(6) Umuhimu wa kuzungumzia jinsi ya kutekeleza

63. Jambo la pili tulilojifunza katika kujikosoa na ambalo linahitaji

kuzingatiwa linahusu methodolojia ya kuunganisha uamuzi wetu

na utekelezaji. Tumekuwa na tabia ya kuzungumzia suala na

kufanya uamuzi. Baada ya hapo tunaachia utekelezaji ufanyike kwa

kutegemea hisia, uwezo na msimamo wa wanaohusika. Kwa kawaida,

suala la kuzungumzia namna ya kutekeleza, kuzungumzia mipango

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 78/142

MIONGOZO MIWILI 77

na mbinu za utekelezaji, hatukuwa na tabia ya kulishughulikia hasa

kitaifa. Huu ni upungufu katika Chama maana namna ya kutekeleza

uamuzi, mipango na mbinu za utekelezaji ni sehemu muhimu ya

harakati za kutafsiri ikra (uamuzi) katika vitendo na ndiyo njiailiyo wazi ya kuhakikisha mafanikio ya utekelezaji.

64. Tabia ya kutozungumzia namna ya kutekeleza mipango na mbinu

za utekelezaji husababisha matatizo katika Chama. Tatizo lililo

dhahiri ni kuwa viongozi mmoja mmoja au vikao vya mikoa, wilaya

na vijiji vinaachiwa vibuni njia za utekelezaji kwa kutegemea

aonavyo kiongozi mhusika au kikao kihusika. Pale ambapo kiongozi

mhusika ana msimamo thabiti wa chama au wajumbe wa kikaoni watu makini na wenye uwezo na busara, utekelezaji unaweza

kufanyika vizuri. Lakini kuna pia sehemu nyingine katika nchi

yetu na kwa vipindi mbalimbali ambako viongozi wamelazimisha

utekelezaji kinyume cha matazamio ya Chama na wananchi na

mara nyingine hata kusababisha usumbufu usio wa lazima kwa

wananchi. Ufafanuzi wa namna ya kutenda na mbinu za utekelezaji

unajenga nidhamu katika utekelezaji, unarahisisha usimamizi wa

shughuli za Chama katika ngazi zote na unajenga na unawezesha

kutumika kwa utaratibu wa kujikosoa na kukosoana. Zaidi ya hayo,

unaimarisha umoja na nguvu za Chama kama chombo cha kutenda,

yaani kuongoza mapinduzi ya kujenga Ujamaa Tanzania.

65. Mwongozo mpaka hapa umegusia historia ya mapambano ya taifa

letu katika vipindi mbalimbali, umechambua mafanikio makubwa

tuliyoyapata katika kutekeleza siasa ya Chama ya Ujamaa na

Kujitegemea na kumalizia kwa kufanya uchambuzi wa kujikosoa

katika Chama ili kwa kuzielewa nguvu na upungufu wa Chama

chetu tuweze kujizatiti kwa kuikabili kazi kubwa iliyo mbele yetu.

66. Historia ya nchi yetu tangu kuzaliwa kwa TANU na ASP ni historia ya

mapambano makali dhidi ya ukoloni na ubeberu na tumefanikiwa

kupata ushindi mwaka hadi mwaka. Hali yetu ya uchumi na ya jamii

ni ngumu kuliko ambavyo imewahi kuwa tangu tupate uhuru. Huko

nyuma tulishinda katika mapambano yetu kutokana na umoja wetu

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 79/142

MIONGOZO MIWILI78

wa kitaifa, usahihi wa siasa yetu na uongozi bora wa Chama. Leo

na katika siku za usoni tutahitaji umoja imara zaidi, siasa sahihi na

uongozi bora wa chama. Lakini katika kipindi hiki ambapo ubepari

na ubeberu wa dunia umejitokeza hadharani kwa kampeni na njamaza kuhujumu ujamaa na kutaka kulibana Taifa, wakati ambapo

vibepari na vibwanyenye vya humu nchini vimeonyesha dhahiri

uhasama wao dhidi ya maslahi ya wakulima na wafanyakazi, umoja

wa sasa lazima usimame juu ya misingi iliyo wazi na sahihi, misingi

ya ujamaa; kwa hiyo ni umoja wa wakulima na wafanyakazi na wale

wote wanaounga mkono kwa vitendao ujenzi wa ujamaa nchini.

SEHEMU YA TATU

KUJENGA MSINGI WA UCHUMI WA UJAMAA WA TAIFA LINALOJITEGEMEA 

67. Lengo kuu la mapinduzi ya Tanzania ni kujenga nchi ya ujamaa

ambamo unyonyaji wa mtu na mtu utakuwa umetokomezwa,

ambamo uchumi wa taifa utakuwa unamilikiwa na kudhibitiwa naumma wa wakulima na wafanyakazi washirika na ambamo uhusiano

wa watu katika jamii utakuwa ni wa udugu na kushirikiana kwa

maendeleo ya wote na ambamo kazi imepewa hadhi ya kuwa wajibu

wa kila mtu.

68. Uamuzi wa kujenga ujamaa Tanzania ni uamuzi wa kimsingi na

kihistoria na haubadiliki. Chama kilijua tangu mwanzo kuwa kujenga

ujamaa hakungekuwa mteremko bali ni mapambano magumu dhidiya ubepari na unyonge wa humu humu ndani na dhidi ya njama za

ubeberu wa dunia. Na isitoshe, Chama kilijua tangu mwanzo kuwa

kujenga ujamaa ni pia mapambano dhidi yetu wenyewe katika

ubinafsi na upungufu wetu wa aina mbalimbali. Harakati za miaka

kumi na minne tangu Azimio la Arusha zimetuthibitishia ukweli huu.

69. Mapambano ya kutekeleza siasa ya Ujamaa ya Chama katika miaka

kumi na minne tangu Azimio la Arusha yametuwezesha kufanyamabadiliko ya kimsingi katika uchumi wa nchi yetu. Kabla ya Azimio

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 80/142

MIONGOZO MIWILI 79

la Arusha uchumi wetu ulikuwa na mfumo wa kikoloni mamboleo

kwani benki, bima, biashara ya nje yote yalikuwa matawi tu ya

makampuni ya kibepari ya ulaya na marekani wakati mazao ya

kilimo cha biashara yaliwekewa lengo la kutumikia viwanda vyakibepari vya nchi za ng’ambo.

70. Kutaiishwa kwa benki, bima na kampuni za biashara za nje za

kibepari na kuanzishwa kwa mashirika ya biashara ya ndani na ya

nje katika kutekeleza Azimio la Arusha kumeleta marekebisho ya

kimapinduzi ya mfumo wa uchumi. Hatua thabiti zimechukuliwa pia

za kuanzisha na kupanua viwanda vinavyotumia bidhaa asili za kilimo

chetu kama ngozi, pamba, katani, korosho, tumbaku, pareto, miwa nakadhalika. Kwa upande wa kilimo hatua za mwanzo zimechukuliwa

kukielekeza kwenye mfumo wa kijamaa: sehemu kubwa ya

mashamba ya kibepari, hasa ya mkonge ilitaiishwa, mashamba

makubwa kadhaa ya Taifa ya kilimo na ya ufugaji yameanzishwa

wakati sekta ya ujamaa katika baadhi ya vijiji imeanza kushamiri.

Tanzania Visiwani, Serikali ya Mapinduzi ilitaiisha ardhi, benki,

nyumba na kuanzisha mashirika ya biashara ya nje na ya ndani na

kuanzisha viwanda vinavyotumia miwa na mbata. Hatua zote hizi

zilizochukuliwa zimetujengea msingi wa uchumi wenye mwelekeo

wa nchi ya ujamaa. Mafanikio haya yamewezekana kutokana na

kazi, ujasiri na kujitolea mhanga kwa wakulima na wafanyakazi

chini ya uongozi wa Chama.

71. Lakini, pamoja na mafanikio haya, nchi yetu hivi sasa imekumbwa

na hali mbaya ya uchumi kama vile hali hiyo ilivyozikumba nchi

zote duniani, zilizoendelea na zisizoendelea, nchi kubwa na ndogo,

za kibepari na za kijamaa. Hali hii lazima tuikabili kwa kujipa kazi

mbili ambazo zitakwenda sambamba. Kazi moja ni kutekeleza

malengo ya muda mrefu ya kujenga msingi wa uchumi wa kijamaa

wa Taifa linalojitegemea. Na kazi ya pili ni kuchukua hatua thabiti

kuanzia sasa za kujihami kiuchumi ili kuhakikisha kuwa hali

ya uchumi wetu haiendelei kudidimia na kuathiri hata msingi

tuliokwisha ujenga.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 81/142

MIONGOZO MIWILI80

72. Ni muhimu kutamka hapa kuwa siasa ya uchumi ya Chama cha

Mapinduzi ina lengo la kutosheleza mahitaji ya wananchi ya

chakula na kulipa Taifa uwezo wa kujitegemea katika mahitaji ya

maendeleo ya sasa na ya baadaye.

MWELEKEO WA MAENDELEO YA UCHUMI NA

 JAMII YA MUDA MREFU

73. Chama Cha Mapinduzi kiimekwishatoa mwelekeo wa maendeleo ya

uchumi na jamii kwa miaka ishirini ijayo. MWONGOZO wa Chama

unayazingatia na kuyafanya maelekezo hayo ndiyo msingi wa

mwelekeo wake wa uchumi na wa jamii kwa kipindi hicho.

74. Kwa hiyo, Mwongozo wa Chama hautayakariri yaliyomo katika

mwelekeo wa miaka ishirini isipokuwa kusisitiza juu ya masuala

yanayohitaji mkazo maalum pia ni kutoa mwelekeo mpya pale

ambapo pana umuhimu wa kutazamwa upya na hapakushughulikiwa

na mwelekeo wa maendeleo ya miaka ishirini.

75. Mambo makubwa mawili yanastahili kutajwa katika kiwango

hiki. La kwanza linahusu kilimo. Kwa kuwa kilimo ndio msingi wa

maendeleo yetu ya sasa na ya miaka mingi ijayo, ni muhimu kwa

Chama kulitilia mkazo suala hili kwa kufanya ufafanuzi wa nafasi ya

kilimo katika maendeleo ya uchumi wa taifa na njia inayohitajika

kuhudumia maendeleo hayo. Hivyo, suala la kilimo na hasa kilimo

cha kijamaa linapewa nafasi kubwa katika mwongozo huu.

76. Jambo la pili linahusu mfumo wa upangaji wetu wa maendeleo.

Kwa kuzingatia kwamba maendeleo ya kijamaa ni maendeleo

yaliyopangwa, Chama katika kipindi kinachoanza sasa kitalitazama

kwa undani zaidi suala la upangaji wetu wa mipango ya maendeleo

kwa madhumuni ya kuimarisha na kukaza usimamizi wa utekelezaji.

Chama kitaona kama Tume ya Mipango katika sura yake ya sasa

kinatimiza makusudio ya Chama. Wakati huo huo Tume ya Bei

itafanyiwa uchambuzi ili ipatiwe nafasi yake ya kuwa chombo cha

upangaji wa uchumi badala ya kuwa chombo cha biashara kama

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 82/142

MIONGOZO MIWILI 81

ilivyo sasa. Sifa moja kubwa ya uchumi wa kijamaa ni kuwa ni

uchumi wa mpango tofauti na uchumi wa kibepari ambao ni uchumi

wa soko. Uchumi wetu kwa sasa ni mchanganyiko: kwa sehemu

fulani unapangwa na kwa sehemu kubwa unategemea mvutano wasoko. Chama kitalitazama suala hili kwa undani zaidi ili kuelekeza

zaidi uchumi wetu kwenye mfumo wa uchumi wa mpango kuliko

ilivyo sasa. Nafasi ya Tume ya Mipango na Bunge katika kupanga

na kusimamia utekelezaji wa mipango itatazamwa upya. Aidha,

matumizi ya fedha za kigeni yataingizwa katika mfumo wa upangaji

mipango.

77. Kwa kuwa uchumi wa kijamaa ni uchumi wa mipango, basitutahitaji watu wenye taaluma ya kupanga katika taifa. Mikoa,

Wilaya na Vijiji na kwa viwango mbalimbali vya utaalamu. Hivyo

Serikali itawajibika kuwaandaa mapema iwezekanavyo wataalam

wa mipango kwa wingi. Wakati huo huo ihakikishwe kuwa upangaji

wa kinchi unapewa uzito sawa na upangaji wa kimradi ambao ndio

unaoeleweka zaidi na wataalam wetu.

 A. MAPINDUZI KATIKA KILIMO NDIYO KAZI YAUMUHIMU WA KWANZA 

78. Msingi wa uchumi wa nchi yetu ni kilimo. Asilimia themanini na

tano ya Watanzania wanaishi kwa kilimo; biashara yetu na nchi za

kigeni inategemea zaidi mazao tunayoyatoa katika kilimo; viwanda

vichache tulivyonavyo nchini vinategemea mazao ya kilimo;

uwezekano wa kutoa ziada itakayowezesha nchi kugharimiamapinduzi ya viwanda (kugharimia viwanda vya madawa) upo

katika sekta ya Kilimo.

79. Katika hali hii, uongozi na usimamizi thabiti na makini wa Chama

cha Mapinduzi uelekezwe zaidi katika sekta hii ya uchumi wa Taifa.

Kazi iliyo mbele yetu ni kuleta mapinduzi katika kilimo. Kwa kuwa

asilimia themanini na tano ya Watanzania ni wakulima wa vijijini,

basi mkazo wa mapinduzi katika kilimo lazima uwe kilimo chavijijini wakati mashamba ya Taifa pia yanashughulikiwa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 83/142

MIONGOZO MIWILI82

80. Mapinduzi ya kilimo vijijini katika nchi yetu ni kilimo cha kijamaa

na cha kisasa ambacho kina sifa zifuatazo: Kwanza ni kilimo cha

mashamba makubwa ya kijamaa ya vijiji, pili ni kilimo kinachotumia

pembejeo, zana za utaalamu na tatu ni kilimo kinachotekelezwakwa utaratibu bora wa kazi unaoleta ufanisi.

81. Sifa moja ya kilimo cha kisasa duniani kote ni kuwa ni kilimo cha

mashamba makubwa. Tofauti iliyopo ya mashamba hayo ni katika

umilikaji. Katika nchi za kibepari mashamba hayo makubwa ni

mali ya mabepari, wakati katika nchi za kijamaa mashamba hayo

makubwa ni mali ya Taifa au ni mali ya ushirika wa wanavijiji.

Hali hiyo imeanza kujitokeza pia katika kilimo cha kisasa nchiniTanzania.

82. Mantiki iliyokisukuma kilimo cha kibepari cha kisasa kiwe cha

mashamba makubwa ni ile ile iliyokisukuma kilimo cha kijamaa cha

kisasa kiwe cha mashamba makubwa. Kilimo cha kisasa ni kilimo

cha zana, na ukishavuka kilimo cha plau za maksai na kuingia

katika matrekta na mashine nyingine za kupandia na kuvunia,

basi ni hasara kubwa kuzitumia zana hizo katika vishamba vidogovidogo vya ekari kadhaa tu. Ufanisi wa hali ya juu unapatikana

wakati zana hizo zinatumika katika maeneo makubwa. Wakati huo

huo ni kuwa zana hizi za kisasa ni aghali na haiwezekani kwa kila

mkulima mwenye ekari chache kupata uwezo wa kuzinunua hata

katika nchi za kibepari. Hivyo, katika nchi za kibepari ni wakulima

wakubwa tu ndio wenye uwezo wa kumiliki zana hizi na katika

mashindano hayo, wakulima wadogo wamelazimika kutoa nafasi

kwa wakulima wakubwa. Katika nchi za kijamaa uwezekano wa

kumiliki zana hizi ni kwa kupitia Serikali (Mashamba ya Taifa) na

ushirika wa wakulima vijijini.

83. Uwezekano wa kuanzishwa kwa mashamba makubwa ya ujamaa

vijijini ni mkubwa katika Tanzania maana mafanikio yaliyopatikana

mpaka sasa katika vijiji vilivyotekeleza ujamaa vijijini yameufungua

macho umma wa Wakulima vijijini. Wakati huo huo maeneo ya

kuanzisha na kupanua mashamba ya ujamaa hayana matatizo katika

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 84/142

MIONGOZO MIWILI 83

sehemu kubwa ya vijiji vyetu nchini mradi tu kuna nia, mipango na

uongozi thabiti.

84. Wakulima vijijini wamepiga hatua za mwanzo katika kutekeleza

maagizo ya Siasa ni Kilimo kwa upande wa masharti ya kilimo bora

cha mazao ya chakula na mazao ya biashara. Pembejeo za viwanda

na samadi zimeanza kutumika pia. Katika siku za usoni Chama

kitawajibika kufanya mambo mawili kuendelea kuwaelimisha

wakulima juu ya umuhimu wa kutimiza masharti ya kilimo bora

na kuhakikisha kuwa serikali inakuwa na mipango thabiti ya

upatikanaji wa pembejeo na kwa bei nafuu kwa wakulima. Matumizi

ya samadi lazima yahimizwe kwa mkazo zaidi.

85. Suala la zana za kisasa ni gumu zaidi. Hivi sasa sehemu kubwa ya

kilimo vijijini inalimwa kwa jembe la mkono. Kuna maeneo yenye

mifugo mingi ambako kazi ya kilimo inaendeshwa pia na plau za

kuvutwa na maksai. Yapo pia matrekta katika baadhi ya vijiji. Lengo

la Chama katika miaka ijayo ni kumtoa mkulima kutoka kwenye hali

yake ya sasa ya kutegemea jembe la mkono na kumikisha kwenye

kutumia zana za kisasa. Kazi hiyo, pamoja na ya kuhakikisha kuwamatumizi ya mikokoteni yanaenea vijijini kote lazima itekelezwe

kwa nguvu zote.

86. Wakati huo huo Chama kihakikishe kuwa serikali inaagiza matrekta

toka ng’ambo kwa kuzingatia uwezo na uzito unaolingana na umuhimu

wa kilimo kwa maendeleo ya Taifa letu. Kupanga ni kuchagua. Hivyo,

kama kwa mfano, ni kuchagua kati ya magari madogo na matrekta,

basi uzito uwe kwenye matrekta. Lakini, kwa kuzingatia hali halisiya uchumi wetu (upungufu wa fedha za kigeni na kwamba hatuna

viwanda vyetu vya chuma na vya matrekta), itachukua muda wa

miaka mingi kabla ya kilimo cha trekta kuwa ndicho kilimo cha vijiji

vyetu. Kwa sasa mbinu ya kutuikisha huko siyo kungoja matrekta

bali ni kutumia majembe ya mkono na plau za maksai katika kilimo

cha kijamaa na cha binafsi vijijini ili kuongeza ziada ya mazao kitaifa

ambayo ndiyo ufunguo wa kulipatia Taifa uwezo wa matrekta zaidi

na kukuza uwezo wetu wa kuanzisha viwanda mama na vinginevyo.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 85/142

MIONGOZO MIWILI84

87. Sifa ya tatu ya mapinduzi ya kijamaa katika kilimo vijijini ni utaratibu

wa kazi wenye ufanisi. Shughuli za kijamaa vijijini huko nyuma

zimezoroteshwa pia kutokana na vijiji kutokuwa na utaratibu

mzuri wa kazi. Mara nyingi kazi za ujamaa zimefanywa holela, bilakujali ufanisi wa kuridhisha. Chama kitawajibika kuhakikisha kuwa

unabuniwa utaratibu wa kupanga na kugawa kazi kwa mfumo

ambao utajenga nidhamu, kurahisisha utekelezaji wa majukumu,

kubainisha mchango wa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi

kuendeleza hisia za ushirikiano na kuongeza ufanisi.

88. Lakini mapinduzi katika kilimo nchini lazima pia yaambatane

na mapinduzi ya msimamo wa serikali na vyombo vyake kuhusunafasi ya kilimo katika mapambano ya ujenzi wa taifa. Katika siku

za usoni, Chama kitahakikisha kuwa serikali na vyombo vyake, kwa

vitendo, vinautekeleza wajibu wake wa kuhudumia na kusukuma

maendeleo ya kilimo, kilimo cha kijamaa kikipewa nafasi ya kwanza.

89. Mapinduzi katika msimamo ni pamoja na kuupiga vita umangi meza

na mila na tabia zinazopingana na mahitaji ya kilimo cha kisasa na

pia kubuni njia bora zaidi za kuandaa wataalamu watakaohitajikasana vijijini kama zile zilizotuwezesha kutekeleza Azimio la

Musoma kuhusu Elimu ya msingi kwa wote. Kwa kuwa kilimo

cha kijamaa ni kilimo cha mashamba makubwa, basi ihakikishwe

kuwa mafunzo ya kilimo yanazingatia pia suala la menejimenti ya

mashamba makubwa.

B. HATUA NYINGINE ZA UMUHIMU WA KWANZA

KATIKA UCHUMI

90. Pamoja na maelekezo ya maendeleo ya miaka ishirini

yaliyokwishapitishwa na Chama, masuala yafuatayo yanahitaji

kusisitizwa:

(1) Kilimo cha umwagiliaji maji

Kilimo hiki kimepewa umuhimu wake katika mwelekeo wa muda

mrefu. Kwa kuelewa kuwa pamoja na miradi mikubwa ya kitaifa ya

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 86/142

MIONGOZO MIWILI 85

umwagiliaji, miradi midogo midogo ya vijijini ndiyo ambayo inaweza

kutoa matunda ya haraka, hatua za dhati zichukuliwe za kuandaa

wataalam wa fani hiyo kwa wingi nchini na ng’ambo na pia kutafuta

uwezekano wa kuanzisha kiwanda cha zana za umwagiliaji maji. Wakatihuo huo Chama kijizatiti barabara ili kuimudu kazi ya kuwashirikisha

wananchi, maana utekelezji wa miradi ya umwagiliaji vijijini utategemea

zaidi jasho la wananchi wenyewe kuliko matumizi ya zana za kisasa.

(2) Kilimo cha matunda na mboga

Kilimo hiki hadi sasa hakijatiliwa mkazo nchini. Licha ya mahitaji ya

chakula bora yanavyozidi kuongezeka, matunda na mboga yanaweza

kuwa mazao muhimu ya biashara ya nje kwa nchi yetu. Nchi nyingi

za Afrika ambazo hazina mazingira bora zaidi ya haya ya nchi yetu

hujipatia fedha nyingi za kigeni kutokana na matunda na mboga. Chama

kihakikishe kuwa m i r a d i ya Taifa na ya vijiji ya kilimo cha matunda na

mboga inaanzishwa kwa madhumuni ya kuwapatia wananchi matunda

na mboga za kutosha nchini kote na ziada ya kuuza ng’ambo. Katika

lengo maalum la kuwapatia wafanyakazi wa mijini matunda na mboga

kwa wingi, vijiji vilivyo karibu na miji mikubwa visaidiwe kuanzishamiradi mikubwa ya vijiji ya mazao haya.

(3) Uendelezaji wa mifugo na ufugaji

Tanzania ina utajiri mkubwa wa mifugo hasa ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Inakisiwa kuwa idadi ya ng’ombe peke yake waliomo nchini ni zaidi ya

milioni kumi. Lakini hali ya mifugo yenyewe ni duni maana wafugaji

walio wengi bado wanathamini zaidi wingi wa mifugo badala yaubora wa mifugo. Misingi ya ufugaji wa kisasa haijaikishwa ipasavyo

kwa wananchi na aina bora za mifugo kwa ajili ya maziwa na nyama

hazijaenezwa nchini.

Katika hali hii kazi kubwa ya Chama katika fani ya mifugo itakuwa

kuhakikisha kuwa Serikali inaandaa sera ya kuendeleza mifugo nchini

na kuhakikisha kuwa wafugaji wanaelimishwa na wanatekeleza misingi

ya ufugaji wa kisasa na kuchukua hatua za dhati za kueneza mbegubora za ng’ombe wa maziwa na wa nyama.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 87/142

MIONGOZO MIWILI86

Chama kitaongoza jitihada za kuanzisha na kupanua ufugaji wa

kijamaa vijijini kwa njia ya ranchi za ng’ombe bora wa maziwa na ranchi

za vijijini za kunenepesha mifugo. Katika hali hiyo, suala la mipango ya

matumizi bora ya ardhi vijijini linakuwa la umuhimu wa kwanza.

Jingine la kulikabili ni suala la uhaba wa nyama, maziwa na mayai na

bei za juu mno za mazao hayo nchini. Ili kulipatia ufumbuzi tatizo hili,

Chama kitawajibika kuhakikisha kuwa serikali inaingiza katika mipango

yake miradi mikubwa ya ufugaji wa kuku, nguruwe na ng’ombe karibu na

miji mikubwa. Aidha, Chama na Serikali visaidie vijiji vinavyozunguka

miji kuanzisha miradi ya ufugaji hasa wa kuku, nguruwe, sungura na

ng’ombe wa maziwa.

Wakati huo huo, jitihada za kueneza mifugo katika maeneo yasiyo nayo

ya kutosha itabidi isimamiwe na Taifa. Pamoja na kwamba wafugaji

wengi wa Tanzania wana mifugo mingi, bado wengi wao hawaitumii

wala kuiona mifugo kama chombo cha kuwaletea maendeleo na

maisha bora zaidi. Hivyo, suala la kutumia mifugo ili kuinua hali halisi

ya maisha ya wafugaji na ya vijiji vyao lazima liwe mkabala maalum wa

Chama kuanzia sasa.

(4) Viwanda

Jambo la kusisitiza linahusu hali ya utengenezaji mali katika viwanda

vilivyopo nchini hivi sasa ambapo vilivyo vingi havitengenezi mali kwa

kadiri ya uwezo vilivyo nao. Chama itabidi kijihusishe na matatizo

ya viwanda hivi na kuhakikisha kuwa vinapata misaada yote ili viweze

kutengneza mali kwa kadiri ya uwezo wake. Licha ya matatizo ya vipuri

na utaalam, viwanda hivi vinakabiliwa pia na matatizo ya kisiasa kama

vile upungufu wa mwamko wa siasa na utovu wa nidhamu.

Viwanda vingi tulivyonavyo nchini hutoa makapi ambayo yangeweza

kutumika kwa utengenezaji wa bidhaa nyingine, lakini jitihada hiyo

haijafanywa. Viwanda kama vya sukari, mafuta, mbolea, nyama na vya nguo

ni miongoni mwa viwanda vya aina hiyo. Kuanzia sasa Serikali itawajibika

kuandaa mipango ya kuyatumia makapi yatokanayo na viwanda vya aina

hiyo ili kutengeneza bidhaa zinazoweza kutengenezwa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 88/142

MIONGOZO MIWILI 87

Chama pia kitatilia mkazo utekelezaji wa Agizo la Viwanda Vidogo

Vidogo mijini na vijijini. Chama kitahakikisha kuwa kila Mkoa unaandaa

mpango wa muda mrefu wa utekelezaji wa Agizo hili la viwanda vidogo.

(5) Mwamko wa Siasa wa wafanyakazi

Mwamko wa siasa una uwezo mkubwa wa kuongeza ufanisi wa kazi

kwa kuwatia wafanyakazi ari na makini zaidi katika kazi. Hali ya sasa

viwandani na oisini inaonyesha upungufu wa mwamko wa siasa.

Hisia za kimapinduzi za kuthamini kazi na wajibu, moyo wa uaminifu

na wa kujitolea muhanga, tabia ya kuthamini mali ya umma, yote haya

yamepoteza nguvu zake.

Ni jukumu la Chama kutia pumzi mpya wakati wote katika viwanda,

Serikalini na katika Mashirika ya Umma itakayoleta vuguvugu la

kimapinduzi miongoni mwa wafanyakazi kwa kuuinua mwamko wao wa

siasa, mwamko wa uvumbuzi, ili waongeze juhudi ya kazi wakitambua

kuwa sehemu zao za kazi ndio uwanja wao wa mapambano ya kujenga

ujamaa na hivyo washiriki kwa dhati katika harakati hizo.

(6) Wizi wa mali ya umma, hujuma katka uchumi, magendo na ujambazi

Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu wa aina mbalimbali nchini

tangu tupate uhuru. Uhalifu wenye kutia wasiwasi maalum ni uhalifu

katika uchumi. Wizi wa mali ya umma umeanza kuwa jambo la kawaida.

Kumekuwa na matukio ya baadhi ya maaisa kuhusika na kuidhinisha

mikataba na kampuni za nchi za nje bila kujali maslahi ya Taifa. Wakati

huo huo vipusa, dhahabu na mali mbalimbali za taifa zinatoroshwa nje

ya nchi kwa magendo na kusabisha hasara kubwa kwa Taifa. Ujambaziwa kutumia silaha nao umetumika ili kunyang’anya mali na kutisha

wananchi.

Chama kitahakikisha kuwa serikali inachukua hatua kali za kupambana

na vitendo hivi vinavyodhooisha uchumi wa Taifa. Iko haja pia kwa

sasa ya kubuni sheria maalum zitakazoelekezwa kwenye vita dhidi

ya uhalifu katika uchumi unaozidi kuongezeka.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 89/142

MIONGOZO MIWILI88

(7) Uharibifu wa vyombo vya kazi na wa mali ya umma

Imezuka tabia ya aibu nchini ambayo imekuwa ikiongezeka ya vitendo

vya kuharibu na kuvitumia vibaya vyombo muhimu vya kazi na mali ya

umma kwa jumla. Magari, matrekta zana nyingine muhimu za Chama,Serikali na Mashirika ya Umma mara nyingi hayadumu muda mrefu

kama ambavyo ingetazamiwa kutokana na matumizi mabaya. Nchi

inapatishwa hasara kubwa ya fedha za kigeni itokanayo na ajali za

malori, mabasi, magari madogo n.k. zinazosababishwa na uzembe na

ulevi. Kuna tabia ya baadhi ya abiria kuharibu mabehewa ya treni

ambayo kesho watahitaji kuyatumia mabehewa hayo hayo tena. Tunalo

tatizo vile vile la tabia ya kuchafua na kuharibu nyumba za serikali na

za mashirika za kuishi inayofanywa na baadhi ya wapangaji wenyewe.

Wakati mwingine majengo ya oisi za Chama, Serikali na Mashirika ya

Umma hayahifadhiwi na kuhudumiwa ipasavyo.

Tabia ambayo baadhi ya mifano yake imetolewa hapo juu ni ishara

kuwa kuna mushkeli wa msimamo katika jamii. Chama kuanzia

sasa kitalifanyia uchunguzi suala hili ili kukielewa chanzo chake na

kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

C . MAENDELEO YA JAMII

91. Katika kipindi kinachoanzia sasa Chama kitatilia mkazo suala la

ujenzi wa tabia na maadili ya kijamaa nchini. Pamoja na jitihada

iliyofanywa ya kutoa elimu na kuunda vyombo vya umma, jamii

yetu bado inazo mila, tabia na maadili yaliyo kinyume na maadili

ambayo yanafanana na misingi ya siasa ya ujamaa tunayosukudia

kuijenga.

92. Watu wameanza kuthamini zaidi vitu kuliko utu na tamaa ya

kujipatia mali bila ya kuitokea jasho inaenea, matukio ya wizi

wa mali ya umma yameongezeka. Lakini lililo baya zaidi ni kuwa

mwizi wa aina hiyo anapogunduliwa, baadhi ya wananchi badala

ya kumichua au kulaani kitendo chake, humsifu na kumhusudu.

Wakati mwingine mvivu na mtegaji kazini hutetewa hata na vyombo

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 90/142

MIONGOZO MIWILI 89

vya Chama vyenyewe. Wakati huo huo, bado kuna mabaki ya tabia

ya kupuuza elimu ya shule kwa watoto na badala yake kuna wazazi

wanaopendelea watoto wao wachunge mifugo au hata kuolewa

badala ya kuendelea na shule.

93. Jitihada ya Chama za kujenga tabia na maadili ya kijamaa

itaelekezwa kwenye taasisi muhimu za nchi kama shule na vyuo,

majeshi na sehemu za kazi. Lakini Chama kitahakikisha pia kuwa

maisha ya hadhara ya jamii yetu yanasaidia kujenga misingi ya

tabia na maadili ya Taifa linalojenga ujamaa na la kimaendeleo kwa

ujumla. Hivyo, Chama kitapiga vita tabia ya baadhi ya wananchi

na hasa wakiwa viongozi inayokwaza na kupotosha umma. Jamiilazima iwe shule ya kwanza ya maadili ya kijamaa.

(1) Maendeleo ya jamii

(a) Uchumi wa fedha ni mpya katika nchi yetu na ndiyo maana tabia

ya kutumia fedha kwa mipango haijaenea. Chama kitaendelea

kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutumia fedha kwa

mipango, kuweka akiba benki na kupiga vita tabia ya ufujaji mali na

matumizi ya fahari.

(b) Uzururaji wa aina mbalimbali umeongezeka nchini. Kwa kuzingatia

kushindwa kwa hatua za pupa zilizotumika katika siku za nyuma,

Chama kitalitafakari kwa undani zaidi suala la mipango na mbinu

za kupambana na uzururaji kwa kutia maanani kuwa ufumbuzi wa

kudumu utategemea maendeleo ya ujenzi wa ujamaa vijijini pamoja

na mipango thabiti ya kuwashirikisha wakazi wa mijini katika

ushirika wa viwanda vidogo. Vijiji ambavyo vimepiga hatua za

ujamaa vimekwishaanza kulitatua tatizo la uzururaji na vimeanza

kuwa na mipango ya kuwatunza vikongwe na walemavu.

(c) Utaratibu wa bima na pensheni hauwezi kuwa wa wafanyakazi

pekee. Katika siku za usoni Chama kitahakikisha kuwa unaanzishwa

utaratibu wa bima na pensheni kwa wakulima washirika kwa

kutegemea maendeleo yao.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 91/142

MIONGOZO MIWILI90

(d) Hali ya vijiji vingi ingali duni kwa ustawi wa jamii na utamaduni.

Chama kitalishughulikia suala la kuleta mapinduzi ya mazingira

vijijini katika fani hiyo.

(e) Kuhusu walemavu, Chama kitahimiza serikali kuchukua hatua

za kuimarisha na kuvipanua vifaa muhimu kwa walemavu kama

baiskeli, viatu, magongo, na kadhalika.

(2) Elimu

Chama kuanzia sasa kitajihusisha zaidi na shughuli za elimu nchini

hasa kwa upande wa maandalizi ya waalimu na maendeleo yao na ya

shule na vyuo maana waalimu wana mchango mkubwa wa kutoa katikakumjenga Mtanzania mpya. Katika lengo hilo, Chama kitafanya tathmini

ya mafanikio tuliyoyapata katika kuielewa na kuitekeleza falsafa ya

Chama ya Elimu ya Kujitegemea.

Aidha, Chama kitalitazama upya Agizo la Musoma katika vipengele vyake

vyote. Kwa sasa imedhihirika kuwa utekelezaji wa Azimio hilo kuhusu

utaratibu wa kuingia Chuo Kikuu unahitaji mabadiliko ya msingi.

Pamoja na mafanikio tuliyoyapata katika Elimu ya Watu Wazima

Chama kitaendelea kuhimiza wananchi na hasa wanaCCM na viongozi

kujiendeleza kwa elimu kwa kadiri ya uwezo wao na kujenga tabia ya

kusoma kama sehemu ya maisha yao.

(3) Afya

Kazi moja muhimu ambayo ni ya Chama katika miaka ijayo ni kuhimiza

kuenezwa kwa elimu ya kinga ya maradhi pamoja na kuongozamapambano dhidi ya tabia na mila zisizo nadhifu. Hali ya afya ya

wananchi wengi vijijini inaathiriwa na tabia na mila ambazo zinapingana

na maendeleo ya jamii kama vile tabia ya kutotumia vitanda, tabia ya

kuishi katika nyumba moja na mifugo, tabia ya kutotumia vyoo, tabia ya

kunywa maji yasiyochemshwa, miiko mbalimbali, na kadhalika. Wakati

huo huo Chama kitatilia mkazo suala la usai wa mazingira mijini na

vijijini pamoja na umuhimu wa kuwepo kwa vyoo vya umma mijini.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 92/142

MIONGOZO MIWILI 91

(4) Ujenzi wa nyumba

Mahitaji ya ujenzi wa nyumba za kuishi mijini na wa majengo ya oisi

na viwanda nchini yanazidi kuwa makubwa. Kazi moja ya Chama ni

kuona kama kuna umuhimu wa kuingiza teknolojia mpya ya ujenzinchini itakayosaidia kutoa msukumo wa shughuli za ujenzi wa nyumba

za kuishi na za kazi. Kuna ukweli kuwa upungufu wa vifaa vya ujenzi

umechelewesha maendeleo ya ujenzi nchini. Lakini huenda ikadhirika pia

kuwa mashirika ya Msajili wa Majumba na Shirika la Nyumba yatahitaji

pia teknolojia bora zaidi ili kuweza kutatua matatizo ya nyumba za

wafanyakazi mijini. Sera ya nyumba itashughulikiwa pia katika kipindi

kinachoanza sasa.

(5) Nishat

Suala la nishati ni la msingi kwa maendeleo ya Taifa letu. Pamoja na

kuendelea kutafuta mafuta, Chama kitahakikisha kuwa serikali inazidisha

mipango thabiti itakayoliwezesha Taifa kuanza kutumia nguvu za maji,

makaa, upepo na jua. Pamoja na miradi mikubwa ya nguvu za maji

kuna haja ya kutia maanani miradi midogo midogo ya nguvu za maji.

Suala la kuni itabidi lipewe umuhimu mkubwa kwa kuwa na mipangokamambe ya kupanda miti vijijini na miradi ya Mikoa na Taifa. Chama

kiihimize Serikali kuendelea na kutafuta mbinu za kutumia makaa ya

mawe tuliyonayo kusukuma uchumi wetu. Umuhimu wa suala la nishati

utahitaji sera maalum.

(6) Msimamo juu ya kuendeleza sayansi na teknolojia

Mpango wa miaka Ishirini unatoa mwelekeo wa maendeleo ya sayansi nateknolojia, kwani sayansi na teknolojia ni msingi muhimu kwa maendeleo

ya kisasa. Chama kijihusishe zaidi na mipango ya kuwapata wanasayansi

na wanateknolojia wenye uwezo wa viwango mbalimbali vya utaalamu na

msimamo sahihi wa siasa. Wakati huo huo, Chama kishughulikie ustawi

wa wataalamu na mabingwa tulionao hivi sasa nchini ili kuhakikisha

kuwa wanaishi katika mazingira yanayowawezesha kutoa mchango wao

kwa ukamilifu katika ujenzi wa Taifa letu. Kutokana na kukosa msimamo

sahihi wa kuwashughulikia wataalamu wetu kumewafanya baadhi ya

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 93/142

MIONGOZO MIWILI92

wataalam kubabaika na Serikali kupoteza mabingwa katika fani za

uganga, uhandisi, urubani wa ndege na kadhalika.

Maendeleo ya uchumi wetu hasa kwa upande wa viwanda na nishati

utahitaji mafundi wa viwango mbalimbali kwa wingi sana. Chama

kihakikishe kuwa serikali inakuwa na mipango thabiti ya namna ya

kuwapata mafundi hawa na kwamba inatumia nafasi zinazoweza

kupatikana kuwaandaa hapa nchini na ng’ambo.

94. Chama kitakuwa na utaratibu wa kuandaa mikutano na wataalamu

wa fani mbalimbali ili kubadilishana mawazo juu ya mbinu za

kusukuma mbele mapinduzi katika sayansi na teknolojia nchini.

D. ULINZI NA USALAMA 

“Msingi wa maendeleo ya Ulinzi na Usalama wa

Tanzania ni Watanzania wenyewe, kila Mtanzania,

na hasa kila mzalendo na kila mjamaa”.

(Mwongozo wa TANU, 1971)

95. Kazi kubwa ya Chama ni kuhakikisha kuwa uhuru wa taifa, mipaka ya

nchi na matunda ya uhuru na ya ujamaa ya wakulima na wafanyakazi

yanalindwa na kuhifadhiwa. Majeshi yetu yote kwa pamoja ndicho

chombo kikuu cha kutekeleza siasa ya Chama ya ulinzi na usalama.

Lakini chimbuko la majeshi ni Umma wa wakulima na wafanyakazi

ambao pia wanashiriki katika ulinzi na usalama wa nchi yao kwa

kupitia ulinzi wa mgambo na kwa kuwa macho katika sehemu zao

za kazi na za kuishi viwandani na maoisini, vijijini na mijini.

96. Chama kitaendelea kuimarisha kazi ya kuyaelimisha majeshi na

wananchi kwa jumla juu ya maumbile ya mapambano yetu na

kufanya uchambuzi wa kutambulisha maadui wa taifa na wa siasa

ya Ujamaa na Kujitegemea ambao ni ubepari na ubeberu wa dunia

na vibaraka wao wa humu nchini.

97. Kazi ya Chama ni kuhakikisha kuwa majeshi yetu yanakuwa

tayari kwa mapigano wakati wote. Ili kuikia lengo hilo, Chama

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 94/142

MIONGOZO MIWILI 93

kitahakikisha kuwa wanajeshi wanakuwa na mwamko wa hali ya

juu wa kizalendo na wa kijamaa na wanajengeka katika misingi ya

nidhamu ya kujituma ya jeshi la kijamaa. Chama kitahakikisha pia

kuwa maendeleo ya teknolojia na uimarishaji wa michepuo jeshiniyanapewa umuhimu wa kwanza. Ni muhimu kwa Chama kuyasaidia

majeshi yetu katika jitihada zao za kupambana na tabia iliyoanza

kujitokeza hapa na pale majeshini ya kutothamini mali ya jeshi,

ubadhirifu na tabia ya kutojali kwa jumla. Vitendo hivi ni kinyume

cha mila za kijeshi na maadili ya jeshi lolote na hasa jeshi la kijamaa

amayo majeshi yetu, chini ya uongozi wa Chama, yatatilia mkazo

wakati wote.

98. Ushindi wetu wa vita dhidi ya majeshi ya uvamizi ya fashist Idd

Amin umetudhihirishia usahihi wa siasa ya Chama ya Ulinzi na

Usalama, kutuonyesha ushujaa na uzalendo wa wanajeshi wetu

na uwezo mkubwa walionao makamanda wetu wa kuongoza

mapigano. Kazi ya Chama sasa ni kufanya majumuisho ya ujuzi

mkubwa tulioupata kwa manufaa ya harakati za ulinzi na usalama

wa Taifa kwa siku za usoni. Miongoni mwa mambo yanayohitaji

uchambuzi na ufafanuzi wa Chama ni uhusiano wa majeshi, nafasi

ya ulinzi wa mgambo katika mfumo wa ulinzi na usalama wa

Taifa wakati wa amani na vita, muundo wa ulinzi na usalama kwa

uongozi na utendaji yaani uhusiano wa wizara na majeshi, nafasi ya

wanawake katika majeshi yetu na kazi za Chama katika majeshi.

99. Chama kitahakikisha kuwa jeshi la Polisi linapata misaada yote

toka Serikalini ili kuliimarisha. Jeshi la Polisi linahitaji kupewa

uwezo zaidi wa mafunzo ya hali ya juu ya mbinu za kupambana na

majambazi na wahalifu wenye ujuzi mkubwa pamoja na kupewa

uwezo wa zana muhimu za kazi.

100. Chama pia kina kazi ya kuchambua tena na kwa makini nafasi ya

Jeshi la Kujenga Taifa katika kusukuma mapinduzi ya ulinzi na ya

uchumi wa Taifa. Pamoja na kwamba madhumuni ya awali ya J.K.T.

bado hayajakiukwa na wakati, Chama kitazame namna ya kulipa

J.K.T. na J.K.U. uwezo wa kuwa chombo cha kukabili kazi za ujenzi

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 95/142

MIONGOZO MIWILI94

wa barabara, majengo, mabwawa n.k. kwa hali ya juu zaidi, kuukuza

uwezo wao wa kutoa chakula na mifugo kwa ajili ya Taifa na pia

kuwezesha J.K.T. na J.K.U. kuwa mahali pa kutoa mafunzo ya muda

mfupi ya wataalamu wengi wa kada ya chini ya ufugaji, kilimo naufundi toka Vijijini.

101. Jambo moja tulilojifunza kutokana na vita dhidi ya uvamizi ni

umuhimu wa viwanda vinavyohudumia majeshi. Chama kitahimiza

Serikali kulipa uzito maalum suala la kukuza na kupanua viwanda

vya majeshi kwa madhumuni ya kuyapatia majeshi na ulinzi wa

mgambo vifaa muhimu wanavyohitaji.

E. MSUKUMO WA UJENZI WA UJAMAA 

102. Imedhihirika katika kipindi cha miaka kumi na minne tangu

Azimio la Arusha kuwa serikali na vyombo vyake na hata baadhi

ya viongozi wamehusika katika kuupa nguvu na kuukuza ubepari

nchini. Katika kipindi kinachoanzia sasa, Chama kitakuwa macho

na kitahakikisha kuwa uwezo wa Serikali na vyombo vyake, uwezo

wa Chama, unatumika kuimarisha na kuendeleza Ujamaa.

103. Katika lengo hili, dhamira ya Chama ya kujenga ujamaa ijidhihirishe

kwa kuhakikisha kuwa:

(a) Benki zinaelekeza nguvu za fedha za Taifa kwenye kujenga

ujamaa kwa kuvipa umuhimu wa kwanza vijiji, vyama halisi

vya ushirika na mashirika ya umma.

(b) Kampuni za umma za ujenzi zilizopo zinapewa uwezo wa kumudukazi zaidi na kwamba kampuni mpya za umma za ujenzi zinaundwa

ili kuikabili kazi ya ujenzi nchini inayoongezeka mwaka hadi

mwaka. Ihakikishwe pia kuwa Serikali na mashirika ya umma

hayawapi kazi za ujenzi makontrakta wa kibepari isipokuwa

wakati hakuna uwezekano mwingine. Fedha za Serikali na

mashirika ya umma zimesaidia sana kuupa nguvu ubepari katika

sekta hii.

(c) Utaratibu wa sasa wa serikali na vyombo vyake kutumia

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 96/142

MIONGOZO MIWILI 95

mawakala wa biashara za nje na biashara za ndani ya nchi

ukomeshwe. Utaratibu huu pia umesaidia kujenga ubepari

nchini.

(d) Kamati za kugawa matrekta na magari nchini zinatoa umuhimu

wa kwanza kwa mashirika na makampuni ya umma, vijiji na

vikundi vya ushirika halisi.

(e) Mipango thabiti inafanywa na serikali ya kuhakikisha

kuwa mtindo wa sasa wa watu binafsi kupewa zabuni za

kulisha makundi ya umma kama majeshi, shule na vyuo

unakomeshwa hatua kwa hatua. Kwa hatua ya kwanza, vyakula

vinavyoshughulikiwa na mashirika ya umma kama sembe,

mchele, maharage na sukari vipatikane moja kwa moja toka

huko.

(f) Usairishaji unaofanywa na vyombo vya umma uimarishwe na

kupanuliwa na kwamba ugawaji wa malori na mabasi ufanywe

kwa lengo la kukuza ujamaa katika sekta hii.

(g) Kila Mkoa unaandaa mpango wa muda mrefu unaoonyeshamalengo ya ukuaji wa sekta ya ujamaa katika kilimo, ufugaji,

viwanda na viwanda vidogo, biashara na usairishaji. Mpango

huo uhakikishe kuwa kila kijiji kinakuwa na malengo

yanayoonyesha ukuaji wa shughuli za kijamaa, mkazo ukiwa

katika kukuza uzalishaji mali. Kutokana na mipango yake,

Serikali iandae mpango unaoonyesha mwelekeo wa ukuaji wa

sekta ya ujamaa nchini.

(h) Utekelezaji wa Siasa ya ujamaa unatilia mkazo suala la

Kujitegemea maana Ujamaa unaojengwa kwa misingi ya

kutegemea ni ujamaa batili. Chama kitaichambua falsafa

inayoongoza upangaji wetu wa mipango ili kuhakikisha kuwa

mipango ijayo ya maendeleo inaonyesha waziwazi mwelekeo

wa kujitegemea katika mpango. Serikali ihakikishe pia kuwa

uwezo wetu wa kujitegemea katika vipuri mbalimbali unakuzwa

kwa kutumia uwezo uliopo nchini.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 97/142

MIONGOZO MIWILI96

SEHEMU YA NNE

CHAMA NA MAPINDUZI YETU

“Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo madhubuti

katika muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo

vyake vya kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote

 za unyonyaji nchini, na kupambana na jaribio lolote lile

la mtu kumwonea mtu, au shirika au chombo cha nchi

kuonea au kudhalilisha wananchi, kudhoo fisha uchumi au

kuzorotesha maendeleo ya Taifa”.

(Katba ya CCM)

104. Chama chetu, Chama cha Mapinduzi, ni Chama chenye historia

ya kipekee katika Afrika. Historia yake ni ya mafanikio na ushindi

katika fani mbalimbali za utekelezaji wa malengo ya siasa yake.

Wanazuoni watakapokuja andika historia ya Chama chetu wataweza

kuyachambua kwa kina na mapana mafanikio hayo yasiyo na kifani.

105. Chama cha Mapinduzi ni Chama cha kijamaa. Kazi kubwa ya CCM

ya sasa ni kuziunganisha nguvu zote za kijamaa na za kimaendeleo

nchini na kuziongoza katika mapambano ya kujenga ujamaa

Tanzania na kujenga ushirikiano wa kimapinduzi wa wajamaa

na wapenda maendeleo wote katika Afrika na Dunia katika

mapambano dhidi ya ukoloni, ukoloni mambo leo, ubepari na

ubeberu.

106. Chama cha Mapinduzi ni chombo kikuu na cha pekee cha uongozi

wa taifa letu. Kuongoza ni kuonyesha njia. Kwa hiyo, Chama chetu

ni mwanga unaotumulikia njia katika hali ngumu ya mapambano

ya wakulima na wafanyakazi kuelekea kwenye ujamaa. Uhalali wa

uongozi wa Chama chetu una misingi ya kihistoria ingawa historia

peke yake haitoshi kuelezea uhalali wa Chama cha Mapinduzi kwa

sasa kuongoza Taifa. TANU na ASP vilijijengea uhalali machoni

mwa wananchi kwa kuwadhihirishia kuwa vinastahili kuongoza

kutokana na usahihi wa siasa na mbinu zao katika mapambano

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 98/142

MIONGOZO MIWILI 97

dhidi ya ukoloni, kwa vitendo vya kujitoa mhanga vya wanachama

na viongozi wa vyama hivyo na kwa kudhihirisha kwa vitendo kuwa

ndio watetezi halisi wa maslahi ya wananchi. Hatua za kimapinduzi

zilizochukuliwa Zanzibar baada ya Mapinduzi Januari 12, 1964,na hatua za kimapinduzi zilizofuatia kutangazwa kwa Azimio la

Arusha Februari 5, 1967 zilijenga uhalali mpya wa ASP na TANU

katika misingi ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

107. Pamoja na uhalali wa kihistoria, ambao ni uhalali wa kurithi, Chama

cha Mapinduzi chenyewe lazima kijijengee uhalali wake katika hali

ya mapambano ya sasa kwa kudhihirisha kwa vitendo kuwa ndicho

mtetezi wa kuaminika wa maslahi ya wakulima na wafanyakazinchini. Kwa kuwa kukubalika na kuaminika kwa ASP na TANU

kulijengwa kwa vitendo vya kimapinduzi vya uamininifu na ukweli

kwa umma na kwa kujitolea mhanga kwa wanachama na viongozi

wa TANU na ASP wakati huo, vivyo hivyo, uhalali wa uongozi wa

CCM na kukubalika na kuaminiwa kwake na umma kutategemea

vitendo vya kimapinduzi vya uaminifu na ukweli kwa umma vya

wanachama na hasa viongozi wa CCM katika harakati za kila siku za

kujenga ujamaa viwandani, oisini, vijijini na mijini. Hii ndiyo njia ya

pekee ya kukifanya Chama kiwe ndani ya umma na kiwe mwakilishi

wa kweli na halali wa matumaini yao ya haki.

 A. CHAMA NA SERIKALI

108. Serikali ndicho chombo kikuu cha utekelezaji wa siasa ya Chama.

Chama kinaiongoza Serikali na vyombo vyake kwanza kabisa

kwa kutoa shabaha na malengo, siasa (sera), maelekezo na

maagizo ya mara kwa mara ambayo Serikali huyatafsiri katika

mipango ya utekelezaji na sheria. Hii ina maana kuwa Chama

ndicho kinachowajibika kuzungumzia na kuamua juu ya masuala

mazito na makubwa ya nchi kabla hayajaelekezwa Serikalini kwa

uchambuzi na utekelezaji.

109. Serikali kwa maumbile yake ni chombo cha madaraka ya mabavu.

Serikali ni sheria, ni majeshi, ni mahakama na ni jela. Kwa hiyo,

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 99/142

MIONGOZO MIWILI98

hata katika hali yetu ya demokrasia na ujamaa, wakati wote ni

muhimu kwa Chama na umma kuwa na hakika na anayekabidhiwa

madaraka haya ya Serikali maana yakiangukia mikononi mwa

mpinga mapinduzi madaraka hayo yanaweza kutumiwa dhidiya maslahi ya umma wenyewe. Hivyo, Chama kuongoza maana

yake ni kuhakikisha pia kuwa madaraka muhimu ya Serikali na

ya mashirika ya umma wanakabidhiwa watu ambao pamoja

na uwezo wao wa kitaalamu ni wenye msimamo wa kizalendo

na waaminifu kwa Chama na kwa wakulima na wafanyakazi wa

Tanzania.

110. Kuhusu suala hili, Chama cha Mapinduzi kina kazi mbele yake yakujumlisha tuliyojifunza tangu tupate uhuru na hasa baada ya

Azimio la Arusha juu ya hatari zinazoweza kutokea kwa siasa ya

Chama na kwa taifa wakati madaraka muhimu ya Chama, Serikali

au Mashirika ya Umma wanakabidhiwa watu ambao kisiasa ni

chui katika ngozi ya kondoo.

111. Serikali na Mashirika ya Umma vile vile ni vyombo vya kutoa

huduma kwa wananchi. Katika nafasi yake ya uongozi, Chamakina wajibu wa kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma kwa umma

hausababishi manung’uniko. Kuongoza katika hali hii maana yake

ni kuwaelimisha na kuwasaidia watendaji katika siasa ili kuinua

na kuimarisha ari na uwezo wao wa kutoa huduma. Wakati

huo huo kuongoza ni kuwaelimisha na kuwaelekeza wananchi

juu ya maamuzi halali ya serikali na umuhimu wa kuyatekeleza

kwa maendeleo yao na ya taifa na pia wakati wote kuhakikisha

kuwa wananchi hawaichwi au kudanganywa juu ya hali halisi na

matatizo ya kweli ya nchi yao.

112. Aidha katika nafasi yake ya kiongozi wa serikali na vyombo vyake,

Chama kina wajibu wa kuhakikisha kuwa muundo, taratibu na

utendaji kazi wa serikali na wa mashirika ni wenye kutekeleza

siasa ya Chama kama ilivyokusudiwa na kuleta ufanisi. Hapa ni

muhimu kusisitiza kuwa Chama kiongoze mapambano dhidi ya

umangi meza na tabia zozote zionazozorotesha kazi na utoaji wa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 100/142

MIONGOZO MIWILI 99

huduma bora kwa umma. Chama kione pia kuwa mifumo iliyopo

Serikalini na katika Mashirika ya Umma inamwezesha mfanyakazi

kushiriki katika uongozi wa kazi mahali alipo na kwamba kwa

kushirikiana na wenzake anapata nafasi anayostahili ya kulijengana kulitumikia Taifa lake.

Chama na mfumo wa siasa na jamii

113. Chama cha Mapinduzi ni muungano wa Wakulima na Wafanyakazi

wa mstari wa mbele kaika mapambano ya kujenga Ujamaa

Tanzania. Mfumo wetu wa kisiasa na kijamii unajengwa kwa

mujibu wa msingi na mahitaji ya nchi inayojenga ujamaa. Lengoni kujenga mfumo wa demokrasia ya kijamaa ambamo wakulima,

wafanyakazi, washirika na watu wote wanaoishi kwa jasho lao sio

tu kuwa watashirikiana na kuwa na kauli ya mwisho katika mambo

ya siasa na ya jamii ya nchi yao bali wakati huo huo watamiliki

na kudhibiti uchumi wa Taifa kwa kupitia Serikali, Mashirika ya

umma, Vijiji vya ujamaa na vyama vya ushirika. Demokrasi ya

Chama kimoja ya sasa ni hatua inayotuelekeza kwenye lengo hilo.

114. Hivyo ni muhimu kwa Chama katika kipindi kinachoanza sasa

kuonyesha njia itakayolielekeza Taifa kwenye kiwango cha juu

zaidi cha demokrasi ya wakulima na wafanyakazi washiriki kila

hali inapohitaji ifanyike hivyo. Katika maana hiyo, ni muhimu

kwa Chama kuutazama tena mfumo wa demokrasi yetu ya Chama

kimoja kwa lengo la kuuimarisha.

115. Kwanza kuna suala la mgawanyo wa madaraka ya nchi kati ya Chama,Rais wa Jamhuri ya Muungano na Bunge na kati ya Chama, Rais wa

Zanzibar na Baraza la Wawakilishi. Sasa ni miaka ishirini tangu

Tanzania bara ipate uhuru na miaka 18 tangu Mapinduzi ya Zanzibar.

Huu ni wakati unaofaa kutazama upya mfumo wa madaraka wa nchi

yetu ili kuchukua hatua za kuimarisha uongozi wa pamoja kwa kutoa

madaraka zaidi kwa Bunge ambalo pamoja na Rais ndio wawakilishi

wa taifa. Kulipa Bunge madaraka zaidi ya kusimamia utekelezaji wa

Serikali ni kuimarisha madaraka ya Umma.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 101/142

MIONGOZO MIWILI100

116. Jambo la pili ni kuwa Bunge lenyewe linahitaji kufanyiwa uchambuzi

kwa madhumuni ya kuimarisha uwakilishaji wa maslahi ya

wakulima na wafanyakazi. Chama kitatumia kipindi kinachoanza

sasa kutafakari juu ya njia bora zaidi zitakazohakikisha kuwawakulima, wafanyakazi, washirika, vijana na wanawake wote

wanawakilishwa kulingana na nia ya Chama ya kuendeleza

mapinduzi yetu ambayo yanahitaji Bunge linalowakilisha maslahi

halisi ya Wakulima na Wafanyakazi na kwa kutia maanani nafasi

ya wanawake na vijana katika Taifa letu.

117. Jambo la tatu linahusu wabunge wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa.

Bunge letu katika sura yake ya sasa lina asilimia kubwa yawateuliwa. Chama kitalitafakari suala hili ili kuona kuwa ubunge

wa kuchaguliwa unapata nafasi kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa

ikieleweka kuwa uchaguzi wa wawakilishi ni sehemu muhimu ya

demokrasi ya kijamaa.

118. Wakati huo huo, Chama kitafanya uchambuzi ili kupata njia za

kuimarisha madaraka ya umma tangu vijijini hadi Taifa kwa

jumla. Chama kitayarudia maamuzi yake ya nyuma kuhusu sualahili tangu tupate uhuru hadi sasa ili kujipa msingi wa kubuni

utaratibu wa kujenga madaraka ya umma yatakayotuelekeza

kwenye demokrasia ya kijamaa, katika jitihada hii, Chama

kitaepuka jaribio la kurudisha mifumo ya tawala za kizamani,

badala yake Chama kitajifunza toka mifumo ya zamani na hata ya

nchi nyingine ili kubuni mfumo mpya utakaolingana na mahitaji

ya maendeleo ya kidemokrasi na ya ujamaa ya Tanzania ya leo na

ya kesho. Hivyo, Chama kitayashughulikia masuala ya madaraka

ya miji, wilaya na vijiji pamoja na suala la vyama vya ushirika

katika msimamo huo.

119. Kwa hiyo, Chama pia kina wajibu wa kuhakikisha kuwa wananchi

katika fani zote za maisha wanashiriki kwa ukamilifu katika ujenzi

wa taifa lao. Katika nchi yetu wakulima na wafanyakazi ndio

msingi wa mfumo wa jamii yetu na siasa ya ujamaa ya Chama ni

siasa ya tabaka hili. Hivyo harakati za kujenga ujamaa ni harakati

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 102/142

MIONGOZO MIWILI 101

za kuwaendeleza wakulima na wafanyakazi. Pamoja na hayo,

Chama kinatambua nafasi maalum ya wanawake na vijana katika

mapambano yetu. Lengo hili linaweza kuikiwa kwa kupitia Jumuia

ya wafanyakazi, Jumuia ya vijana, Jumuia ya wanawake na Jumuiaya Washirika. Suala la Jumuiya ni suala ambalo Chama kinahitaji

kulifanyia uchambuzi zaidi ili kufafanua waziwazi uhusiano wake

na Chama na nafasi yao halisi katika harakati za ujenzi wa Taifa.

120. Pamoja na suala la Jumuia za Wananchi kuna umuhimu kwa Chama

kuunda mazingira nchini yatakayowawezesha wakulima na

wafanyakazi kushiriki kwa ukamilifu zaidi katika mapambano ya

kisiasa na ya kiitikadi. Miaka iliyofuata Azimio la Arusha na baadayemwongozo wa TANU ilikuwa kipindi cha vuguvugu la kimapinduzi

lililowawezesha vijana, wakulima na wafanyakazi nchini kushiriki

katika kuijadili siasa ya Chama na kujiendeleza kinadharia na

kiitikadi. Utekelezaji wa Mwongozo wa Chama cha mapinduzi

unahitaji vuguvugu la namna yake. Hakuna msukumo wa kweli wa

ujenzi wa ujamaa unaowezekana bila ya msukumo unaolingana

na mijadala juu ya nadharia na itikadi ya ujamaa. Chama kitaunda

mazingira nchini yatakayouwezesha umma kushiriki kwa nadharia

na kwa vitendo katika utekelezaji wa maelekezo ya mwongozo

wa Chama.

121. Tabia moja ya mapinduzi iliyoanza kujengeka wakati wa vuguvugu

la Azimio la Arusha na Mwongozo wa TANU na imeiia sasa ni ile

ya wafanyakazi na vijana wa vyuoni na shule za Sekondari kujenga

uhusiano wa kidugu na ushirikiano na vijiji vilivyo karibu nao.

Maelfu ya wafanyakazi na vijana walifanya kazi za kujitolea wakati

wa mwisho wa juma kudhihirisha mshikamano wa wakulima na

wafanyakazi, na vijana katika kujenga ujamaa.

122. Utaratibu wa kazi za kujitolea kwa wanachama wa Chama Cha

Kijamaa, kwa wafanyakazi na vijana wana mapinduzi, ni jambo

muhimu kwa maendeleo yao ya kisiasa na kiitikadi na kwa

maendeleo ya Ujamaa. Katika jitihada zake za kushirikisha umma

katika ujenzi wa Taifa, Chama cha mapinduzi kitawajibika kufufua

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 103/142

MIONGOZO MIWILI102

na kuendeleza tabia itakayowawezesha wana CCM, wafanyakazi

na vijana kujitokeza kwa wingi katika kazi za kujitolea na kujenga

ushirikiano kwa vitendo kwa vijana, wanajeshi, wakulima na

wafanyakazi vijijini.

Chama na siasa ya nchi za nje

123. Siasa ya nchi za nje ya Chama cha Mapinduzi inaongozwa na misingi

ya Uhuru wa Taifa wa kujiamulia mambo yake bila kuingiliwa na

yeyote; kushirikiana na vyama na nchi za kimaendeleo na za kijamaa

katika kuimarisha mapambano dhidi ya nguvu za ukoloni, ukoloni

mamboleo, ubepari, ubeberu na ubaguzi wa rangi katika Afrika na

kote duniani; kuunga mkono ukombozi wa Afrika na Umoja wa

Afrika; na kushirikiana na mataifa mengine katika umoja wa nchi

huru za Afrika, katika nchi zisizofungamana na upande wowote na

katika Umoja wa Mataifa katika jitihada za kulinda na kudumisha

amani na usalama duniani.

124. Kwa kuwa chimbuko la siasa yetu ya nje ni ya ndani ya ujamaa

na kujitegemea tunayoijenga, basi kazi moja kubwa ya Chama na

Serikali katika suala hili ni kuielezea siasa yetu na kutetea misingi

ya haki, usawa na uhuru katika mikutano ya kimataifa na kulijengea

Taifa uhusiano wa kidugu na ushirikiano na mataifa ya kimaendeleo

na ya kimapinduzi na yale yote ambayo yanataka ushirikiano nasi

katika misingi ya kuheshimiana, kutoingiliana katika mambo ya

ndani na ya kuzingatia maslahi ya pande zote mbili.

125. Chama chetu, tangu wakati wa ASP na TANU kiliwajenga wanachama

wake na wananchi kwa jumla katika hisia za kimapinduzi za

kujishirikisha na mapambano ya ukombozi wa nchi nyingine za

Afrika na za dunia. Lakini pamoja na historia hiyo ya Chama na

wananchi kushiriki kwa vitendo katika kuongoza siasa yetu ya nchi

za nje, kumekuwa na vipindi ambapo shughuli za nchi za nje Chama

kiliachia Serikali pekee.

126. Kuanzia sasa Chama kitahakikisha kuwa uhusiano wetu

na nchi za kigeni unakuwa sehemu muhimu ya shughuli zake.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 104/142

MIONGOZO MIWILI 103

Katika lengo hilo Chama kitaendeleza na kujenga uhusiano

maalum na vyama halisi vya ukombozi, vya kijamaa na vya

kimaendeleo vya Afrika na kote duniani ili kubadilishana

uzoefu na kuimarisha mapambano dhidi ya ubeberuwa dunia.

B. CHAMA KUJIZATITI ILI KUONGOZA MAPINDUZI

“Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani

Ujamaa ni Imani. Hauna budi kujengwa na watu

wanaoamini na kufuata kanuni zake. Mwana-

TANU wa kweli ni mjamaa, na wajamaa wenziwe yaani waamini wenziwe katika imani hii ya kisiasa

na kiuchumi ni wote wale wanaopigania haki za

wakulima na wafanyakazi katika Afrika na popote

duniani.”

Azimio la Arusha

127. Kazi kubwa ya Chama Cha Mapinduzi kwa mujibu wa Mwongozo

huu ni kuchukua hatua za kujizatiti, kujijenga na kujiimarisha ilikujipa uwezo unaolingana na uzito wa mapambano yaliyo mbele

yetu ya kujenga ujamaa katika kipindi ambapo ubepari na ubeberu

wa dunia na vibwanyenye na wapinga Ujamaa wa humuhumu

nchini wanazidisha kujenga vitimbi vya uhasama dhidi ya siasa

yetu ya Ujamaa na Kujitegemea.

128. Kujizatiti kwa mapambano ya kujenga ujamaa kwanza kabisa ni

kuwa na hakika na wapiganaji wa mstari wa mbele wa mapambanohayo ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Kwa

hiyo, hatua ya kwanza ya Chama kujizatiti kwa mapambano ni

kuwawezesha wanachama wa CCM kiikra na vitendo, mmoja

mmoja na katika umoja wao, kutimiza wajibu wao wa kimapinduzi.

(1) Kazi ya kuwajengea na kuwaimarisha wanachama:

(a) Maandalizi: Vuguvugu la mijadala ya kichama katika Mashina,Matawi na Nchini kote.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 105/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 106/142

MIONGOZO MIWILI 105

133. Mijadala hii ya wanachama na ya wananchi kwa jumla itasaidia

kuinua mwamko wa kisiasa wa wananchi, kuwaelimisha zaidi juu ya

matatizo ya nchi yetu na kuwaongezea ari ya kudhamiria kushiriki

kwa ukamilifu zaidi katika harakati za kujihami kiuchumi nakisiasa. Mijadala hii katika Matawi, ikiendeshwa kwa makini na kwa

utaratibu mzuri, itawezesha wanachama wa kweli kufahamiana

na wanachama wa bandia kuichuliwa. Hii itahusu pia viongozi

kueleweka katika msimamo.

134. Katika hali hii, hatua inayofuata ni kwa kila Tawi la Chama

kuchukua hatua ya kuwajadili wanachama wake mmoja mmoja ili

kuamua kama bado wanastahili kuendelea na uanachama au la.Kwa kuwa wazembe, wazururaji, wezi na majambazi watakuwa

wameichuliwa katika vikao hivi, kwa kuwa wapinga ujamaa

kiitikadi na kwa vitendo watakuwa pia wameichuliwa, basi hii

ndiyo nafasi ya kukitakasa Chama. Matawi yapendekeze kwenye

vikao vya juu hatua za kuwachukulia wanachama watakaodhihirika

kuwa hawatimizi masharti na wajibu wa wanachama. Azimio la

Arusha linasisitiza juu ya ubora wa wanachama badala ya wingi wa

wanachama. Vuvuvugu hili la mijadala ya wanachama wenyewe tu

litasaidia kuunda hali itakayowezesha kupiga hatua za mwanzo za

kuelekea kwenye lengo hilo la Azimio la Arusha.

135. Kazi hii ya Chama ya kuongoza mijadala ya kujikosoa na kukosoana

iendelee hadi itakapoikia kipindi cha mikutano mikuu ya mwaka

wa tano tangu CCM kuzaliwa. Kipindi hiki ni kirefu cha kutosha

kwa mashina na matawi ya Chama kufanya vikao kadhaa vya

wanachama wote ili kuwezesha kuelewana na kupimana kwa

makini. Kipindi hiki ni kizuri pia kupimana kwa sababu ni kipindi

ambapo Chama kitaongoza mapambano ya utekelezaji wa hatua za

kujihami kiuchumi nchini kote. Na wakati huo huo hiki ni kipindi

cha kuanzisha msukumo mpya wa ujenzi wa ujamaa nchini.

136. Ni dhahiri kuwa katika hali hii ya vuguvugu la mapinduzi la

utekelezji wa siasa ya Chama, wanachama matawini watapata

nafasi nzuri ya kufahamiana na kuelewana kwa vitendo. Wana

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 107/142

MIONGOZO MIWILI106

CCM halisi watajitokeza kwa vitendo katika utendaji wao wa kila

siku kazini na wanakoishi. Wana CCM wa vijijini watadhihirisha

uanachama wao kwa kuwa katika mstari wa mbele katika

kutekeleza majukumu ya Ujamaa ya kijiji na katika kushiriki kwadhati katika kazi za kujitolea kwa jumla kama ujenzi wa shule,

zahanati, barabara za kijiji, shamba la kijiji, kushiriki katika elimu

ya watu wazima, ulinzi wa kijiji na kadhalika.

137. Wana CCM wafanyakazi, watadhihirisha uanachama wao kwa

vitendo kwa kufanya kazi kwa makini na kwa nidhamu, kwa

kushirikiana na wafanyakazi wenzao kuhakikisha kuwa malengo

ya kazi yaliyowekwa yanatimizwa, kwa kupambana bila woga navitendo vyo vyote vile vya uvivu na uzembe kazini, vya kuzorotesha

kazi au vya kuhujumu uchumi.

(b) Mafunzo ya Siasa ya Chama

138. Chama kinapanga na kuendesha mafunzo ya siasa yake ikiwa

na malengo makubwa matatu: Mafunzo ya Siasa ya Chama

yanatolewa kwa wananchi kwa jumla kwa lengo la kuieneza

siasa hiyo ili ieleweke na kukubalika na wakati huo ili kupiga

vita upotoshaji na uzushi juu ya siasa ya ujamaa unaoenezwa na

maadui wa ujamaa kwa nia ya kukifanya Chama kifarakane na

Umma. Nia wakati wote ni kuelimisha umma na kuufanya uwe

karibu zaidi na Chama ili ushiriki katika kutekeleza maelekezo

na mwito wake kwa ari na hiari.

139. Lengo la pili la mafunzo ya siasa ya Chama ni kuhakikisha

kuwa wananchi katika taasisi maalum za wananchi: wanafunzi,

wanajeshi, wafanyakazi, vijana, wanawake, wanautamaduni,

viongozi wa kazi, waandishi wa habari n.k. wanahamasishwa ili

kuinua mwamko wao wa kisiasa, na kuwapa wahusika mwelekeo

wa siasa kulingana na jinsi Chama kinavyoiona nafasi yao katika

ujenzi wa taifa kwa sasa na kwa baadaye.

140. Lengo la tatu la mafunzo ya siasa ya Chama ni kuhakikisha kuwa

wanachama na viongozi wanaimarika katika itikadi ya ujamaa na

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 108/142

MIONGOZO MIWILI 107

kujitegemea; kuwapanua wanachama na viongozi upeo wao wa

kuyaelewa masuala mbalimbali; kuwapa methodolojia na mantiki

ya kutafakari na kufanya uchambuzi wa msuala; kuwazatiti kwa

hoja na mbinu zitakazowasaidia katika harakati za kuongozautekelezaji wa siasa ya ujamaa pia kueneza na kutetea siasa

ya Chama.

141. Mafunzo ya aina zote tatu ni muhimu kwa maendeleo ya mapinduzi

yetu. Mafunzo ya aina ya tatu, yaani mafunzo ya wanachama na

viongozi, ndiyo yatakayowezesha kufanikiwa kwa mafunzo ya aina

ya kwanza na ya pili. Katika miaka ya usoni, Chama kitaendelea

kuendesha mafunzo ya siasa ya Chama kwa mipango na msukumomkubwa zaidi kwa kuzingatia kuwa mapambano ya kisiasa na

kiitikadi ni sehemu muhimu ya mapambano ya kujenga ujamaa na

kuziichua na kuzishinda mbinu za adui.

142. Hivyo, Chama kitachukua hatua za kuimarisha na kupanua

mipango ya mafunzo ya wanachama na viongozi. Wanachama

walio wengi itabidi wapate mafunzo yao ya nadharia matawini

kwao. Mafunzo hayo yatakayoendeshwa kwa msingi wa seminayatasimamiwa na mikoa na wilaya zenyewe. Wanachama

watakaojitokeza, kwa msimamo na uwezo, yaani wanachama

wenye sifa za kada, pamoja na viongozi wa matawi, wilaya, mikoa

na Taifa wataingia katika mpango maalum wa kupata mafunzo

katika vyuo vya Chama vya ngazi zinazolingana na mahitji yao.

Utaratibu katika vyuo vya Chama wa mafunzo ya kada na viongozi

wa Chama utahitaji maandalizi ya makini na ya hali ya juu.

143. Chuo cha Chama ni mahala anapopelekwa mwanachama

aliyejitokeza katika Chama, yaani kada wa Chama au kiongozi wa

Chama, kwa madhumuni ya kumwandaa kwa kazi kubwa zaidi za

Chama. Chama ndicho kinachomwandaa mwanachama mwenye

msimamo wa sifa za kada wa Chama au kinaamua kumpeleka

chuoni apate upeo mkubwa zaidi wa kukitumikia Chama.

Mwanachama huyu anaweza akawa aisa wa serikali, mfanyakazi

wa chama au mkulima. La msingi ni kuwa anateuliwa na Chama

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 109/142

MIONGOZO MIWILI108

kutokana na sifa zake katika Chama na kwa madhumuni ya Chama

ya kuendeleza kazi zake za kuongoza Taifa kama Chama.

144. Wakati huo huo Chama kitaimarisha mafunzo ya siasa ya Chama

ya aina ya pili kwa ajili ya taasisi kama majeshi, shule na vyuo,

wafanyakazi, vijana pamoja na wataalamu na Wakuu wa kazi wa

viwango na taasisi mbalimbali. Kwa utaratibu, mafunzo ya aina hii

huendeshwa kwenye taasisi zenyewe na kusimamiwa na Chama.

145. Mafunzo haya ya siasa ya Chama yatatumika pia kuwatambua wale

wenye sifa za kada wa Chama. Wale watakaobainika kuwa wana

mwelekeo huo basi wataingizwa katika utaratibu wa kupatiwa

mafunzo zaidi katika vyuo vya Chama. Hii ina maana kuwa maaisa

wa serikali na mashirika yake hata wafanyakazi katika sekta ya

kibepari walio wana CCM wakijitokeza katika mafunzo ya Chama

ya taasisi zao kwa kuwa wana sifa za kada wa Chama watafanyiwa

mpango ili inapotokea nafasi wajiunge na vyuo vya Chama.

(2) Kuimarisha muundo, demokrasi na utendaji wa Chama

146. Vyama hujipa muundo unaowesesha shughuli zake kutekelezwakwa nidhamu na ufanisi. Kwa madhumuni hayo vyama hujipa

vikao vya aina tatu hivi katika kila kiwango: Kikao cha aina ya

Mkutano Mkuu ambacho ni cha wajumbe wengi na ndicho kikao

kinachotoa mwelekeo na kupanga siasa na mambo makubwa ya

kutekelezwa katika kipindi kirefu kifuatacho. Vikao vya aina hii

hukutana baada ya kipindi kirefu kupita. Kikao cha aina ya pili

ni kipana na kina wajumbe wengi na ndicho kinachoongoza nakusimamia utekelezaji na maamuzi ya mkutano mkuu. Mwisho

huwa kuna chombo kidogo cha wajumbe wachache ambao huunda

Kamati ya Utendaji ya kikao kikubwa cha aina ya pili.

147. Sasa, utaratibu wa zamani wa TANU na wa ASP ulikuwa na

mfumo wa aina hii. Na uzoefu tulioupata hadi sasa unadhihirisha

ubora wa mfumo wa aina hii maana unaunganisha mahitaji ya

demokrasi pana ya vikao vya aina ya kwanza na ya pili na wakati

huo huo unarahisisha utendaji kwa kuwa na kamati ya utendaji

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 110/142

MIONGOZO MIWILI 109

ya Wajumbe wachache watakaokabidhiwa majukumu ya utendaji

siasa wa kila siku. Chama kitachukua hatua za kurekebisha

muundo wake wa sasa ili kuliikia lengo hili katika ngazi zote za

Chama.

148. Imedhihirika pia kuwa kuna umuhimu kwa sasa wa kuimarisha

demokrasi ya Chama katika kiwango cha Taifa na baadaye katika

viwango vya chini yake. Hali ilivyo kikatiba hivi sasa ni kuwa

wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ni mchanganyiko wa

wanaochaguliwa na wanaoteuliwa. Wakati umeika wa kuimarisha

demokrasi ya Chama kwa kurekebisha Katiba ili wajumbe wote

wa Halmashauri Kuu ya Taifa watokane na uchaguzi wa Chama.

149. Hatua nyingine inayohitaji kuchukuliwa ili kuimarisha Chama

inahusu kuunganisha uongozi wa Chama yaani wa Halmashauri

Kuu ya Taifa na utendaji kazi wa Oisi yake yaani Makao Makuu ya

Chama. Mfumo wa hivi sasa una hitilafu inayoathiri kazi za Chama.

Kwa mujibu wa mfumo huu viongozi kazi yao ni kuamua katika vikao

na halafu kuna watendaji ambao ni maaisa waajiriwa wa Chama

wa kutekeleza maamuzi hayo. Chama kitaurekebisha utaratibu huu(pamoja na mfumo wa sasa wa Kamati za Kamati Kuu) kwa kuweka

utendaji kazi za Halmashauri Kuu ya Taifa chini ya makatibu wa

Halmashauri Kuu ya Taifa yenyewe. Kazi muhimu za Halmashauri

Kuu ya Taifa ni pamoja na Elimu, Uenezi na Itikadi ya Siasa, Uchumi

na Mipango, Organaizesheni, Ulinzi na Usalama, Uhusiano na Nchi za

Nje na Nidhamu na Udhibiti. Utaratibu huu utahusu Mikoa, Wilaya na

Matawi kwa hatua zitakazoamuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

(3) Kuimarisha uongozi wa Chama katika sehemu za kazi

150. Kuanzia sasa Chama kitahakikisha kuwa serikali inachukua hatua

za kuuwezesha utaratibu wa malengo ya utoaji mali kutumika

katika viwanda na mashirika yake na kuinua uwezo wa utoaji

huduma wa vyombo vyake. Wakati huo huo Chama kitahakikisha

kuwa wakuu wa kazi wanasaidia kisiasa ili wawe na msimamo wa

kizalendo utakaoimarisha uwezo wao wa kitaalamu.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 111/142

MIONGOZO MIWILI110

151. Hata hivyo, kazi kubwa ya Chama katika sehemu ya kazi itafanywa

na tawi la Chama la mahali pa kazi panapohusika. Kazi ya Chama

katika Taifa, Mkoa na Wilaya ni kuunda hali itakayoliwezesha Tawi

la Chama kutekeleza wajibu wake wa uongozi. Ili kuhakikishakuwa Chama katika sehemu ya kazi kinashika nafasi yake ya

uongozi kuna masuala kadhaa ya kutia maanani.

152. La kwanza ni kuwa suala la umuhimu wa kwanza kwa Chama katika

mahali pa kazi katika mazingira ya nchi inayojenga ujamaa ni kuleta

mafanikio ya utekelezaji wa kazi. Hivyo, jitihada ya Chama katika

sehemu ya kazi ni kuhakikisha kuwa wanachama na viongozi wa

chama wanakuwa katika msitari wa mbele katika kutimiza wajibuwao wa kazi na kuona kuwa malengo yaliyowekwa yanaikiwa. Ni

mwiko kwa mwanachama wa CCM au kiongozi kuwa miongoni

mwa wategaji, wavivu na wazoroteshaji kazi.

153. Jambo la pili ni kuwa vyama vya kijamaa halisi haviongozi kwa

mabavu bali kwa kuelimisha, kushawishi, kuelekeza na kwa

chama chenyewe kuonyesha njia kwa vitendo. Kwa hiyo, kazi ya

Chama katika sehemu za kazi itakuwa kuwajenga wana CCM kujuanamna ya kuwashirikisha wafanyakazi wenzao katika kutekeleza

malengo na wajibu wa kazi kutokana na mfano wao wenyewe

wa kutekeleza wajibu kwa makini na kwa ari na uwezo wao wa

kushawishi, kushauri na kuwashirikisha wafanyakazi.

154. Jambo la tatu la kuzingatia kuhusu suala la uongozi wa Chama

katika sehemu za kazi ni kuwa “ujuzi ni madaraka.” Watu wana

tabia ya kumsikiliza anayejua zaidi kuliko wao juu ya suala fulani.Sasa, mahali pa kazi ni mahali penye ujuzi wa aina mbalimbali.

Atakayejitokeza kuwa anajua zaidi katika fani fulani wenzake

humheshimu, humtegemea na kumsikiliza. Chama kitahakikisha

kuwa katika siku za usoni wanachama wa CCM wanajiendeleza

katika fani zao za kazi ili kuwa miongoni mwa wanaotegemewa na

kusikilizwa na wafanyakazi wenzao katika fani zao za kazi.

155. Jambo la nne linahusu matatizo ya kila siku ya wafanyakazi.Kiongozi, pamoja na sifa nyingine, ni mtu mwenye kuyaelewa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 112/142

MIONGOZO MIWILI 111

matatizo ya watu na anayejua vile vile kuyaelezea na kuyajengea

hoja. Chama kitahakikisha kuwa wanachama wa CCM wanaaminiwa

na wafanyakazi wenzao kwa kuwa wanayaelewa matatizo yao

na wana uwezo wa kuyaelezea kwa ufasaha na kushirikiana naokatika kutafuta jawabu. Ili kuikia hapo Wana CCM watawajibika

kujiendeleza katika nadharia ya Chama na elimu kwa jumla.

156. Suala linarudia pale pale tulipoanzia. Kwa Chama cha Mapinduzi

kuongoza mapinduzi katika sehemu za kazi, kazi ya msingi ni

kuwaandaa wanachama na viongozi wa matawini kwa mafunzo

thabiti ya siasa ya Chama; ni kwa Chama kuhakikisha kuwa katika

kila sehemu ya kazi viongozi wa Chama waliopo na wanachamakwa jumla wanapata miongoni mwao kada wa Chama wenye

uwezo wa juu wa uchambuzi na mbinu watakaosaidiana nao

katika mawimbi ya harakati. Hii ndiyo kazi kubwa ya Chama

katika siku zijazo.

K.m. katika jitihada za kuimarisha uongozi wa chama katika

majeshi, miradi muhimu ya Taifa na taasisi, Chama kinaweza

kuteua kamisaa wa siasa na kumpeleka katika sehemu hiyo. Kaziyake ni kusaidiana na uongozi uliopo kuimarisha utekelezaji wa

majukumu, kuendeleza nidhamu na kwa kusaidiana na Chama

katika sehemu hizi, kuuinua mwamko wa siasa na wa uzalendo wa

wapiganaji, wafanyakazi au wanafunzi na kuwaongezea ari katika

utekelezaji wao.

Matawi na Mashina ya kazini na mijinikuimarishwa

157. Ili Chama kitimize wajibu wake wa kuongoza katika sehemu za

kazi tegemeo lake kubwa ni wanachama. Lakini wanachama pia

wanategemea muundo wa mashina na matawi uliopo. Hivi sasa

kuna matawi ambayo wanachama wao ni wengi mno kwamba

uwezekano wao wa kufahamiana na kushirikiana ni minyu mno.

Katika siku zijazo Chama kitahakikisha kuwa katika sehemu za

kazi suala la kuwaunganisha wanachama katika mashina linatiliwa

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 113/142

MIONGOZO MIWILI112

mkazo zaidi. Wakati huo huo utatazamwa uwezekano wa kuunda

matawi zaidi ya moja katika sehemu za kazi zenye wanachama wa

CCM wengi mno.

158. Aidha, Chama kitalishughulikia suala la matawi ya Chama ya Kata

za Mijini. Katika hali ya sasa matawi mengi ya kata za mjini ni

makubwa kiasi kwamba wanachama hawawezi kujihusisha kwa

ukamilifu katika matawi yao.

(4) Kuimarisha Chama kwa kuimarisha uongozi

159. Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi kwanza kabisa lazima awe na

msimamo wa kijamaa. Itikadi yake ya ujamaa, vitendo na tabia yake

vijidhihirishe kwa wanaowaongoza, wanachama na wananchi,

kuwa ni vya kijamaa. Imani ya kiongozi inaambukiza na kuimarisha

imani ya anaowaongoza. Lakini kiongozi anayegunduliwa na

anaowaongoza kuwa ni mnaiki kwa msimamo ni adui mkubwa

kwa Chama maana anawavunja moyo wanachama, anawavuruga

wananchi na kuunda hali itakayowafanya wananchi wasiwe na

imani na viongozi wengine na Chama. Hivyo suala la viongozi wa

Chama kuwa na msimamo sahihi kwa itikadi na katika maisha

ya kila siku ni jambo lenye umuhimu wa kwanza kwa Chama cha

Mapinduzi.

160. Lakini pia msimamo thabiti wa ujamaa wa kiongozi uambatane

na uwezo wa kuongoza. Tumetamka hapo juu katika Mwongozo

huu kuwa Chama cha Mapinduzi hakiongozi kwa mabavu bali kwa

kuelimisha, kuelekeza, kushauri, kushawishi na kushirikiasha.

Hii ina maana kuwa kiongozi wa Chama hana budi awe na uwezo

wa kushauri na kuelimisha, kushawishi na kushirikisha, kwa

jumla awe na uwezo wa kuieneza na kuitetea siasa ya Chama

na kuwaunganisha wanachama na wananchi katika harakati za

kujenga ujamaa nchini na kwa kiwango cha uongozi wake.

161. Kutokana na hayo, Chama kuanzia sasa kitalipa uzito suala lamsimamo na uwezo wa viongozi wake. Ndiyo kusema kwamba

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 114/142

MIONGOZO MIWILI 113

katika siku za usoni uchambuzi wa viongozi waliopo na waombao

nafasi za uongozi utasisitiza juu ya msimamo wao kwa itikadi na

kwa vitendo pamoja na uwezo wao wa kumudu uongozi huo.

162. Chama kitatumia njia mbali mbali za mafunzo ili kuwasaidia

viongozi wenye nia njema kuimarisha msimamo wao kiitikadi.

Chama pia kitakuwa na utaratibu wa kuwasaidia viongozi wenye

msimamo sahihi lakini uwezo mdogo wa kuongoza kupata nafasi ya

kuendeleza uwezo wao. Lakini Chama kitahakikisha kuwa viongozi

ambao msimamo wao kwa itikadi na kwa vitendo ni kinyume cha

misingi ya ujamaa hawapewi nafasi ya kukihujumu Chama kutoka

ndani ya Chama. Wakati huohuo Chama kitahakikisha pia kuwa

suala la uwezo linakuwa sehemu muhimu ya uchaguzi au uteuzi

wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi.

(5) Maandalizi ya waombaji unachama

163. Chama kitaendelea kupokea wanachama wapya isipokuwa

kwamba kuanzia sasa suala la wanachama litekeleze kwa vitendo

agizo la Azimio la Arusha kuhusu ubora wa wanachama badala

ya wingi wao. Wakati huo huo, jitihada zitafanywa ili kuhakikisha

kuwa idadi ya wanachama wanawake, wakulima, wafanyakazi na

vijana inafanana na nafasi yao halisi katika jamii yetu.

Mafunzo kwa waombaji uanachama

164. Mwelekeo na mkazo wa mafunzo ya wanachama wapya

yatafanyiwa mabadiliko ya kimsingi. Mwanachama wa CCM kwamujibu wa Mwongozo huu atapimwa kwa vitendo vyake vya

kutekeleza siasa ya Chama katika maisha yake ya kila siku. Vivyo

hivyo, mtu anayeomba kuwa mwanachama wa CCM itabidi apewe

kipindi cha majaribio ambapo atapimwa kuhusu kufaa kwake

kuingia katka Chama kwanza kabisa kwa vitendo vyake vya

kutekeleza siasa ya Chama. Aidha, atawajibika kuhusika na shina

na tawi ambalo ndilo litakalompangia majukumu ya kichama yakuyatekeleza na ndiko atakakokuwa akijadiliwa hatua kwa hatua

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 115/142

MIONGOZO MIWILI114

na uamuzi kufanywa kuhusu kuingizwa au kutoingizwa katika

Chama wakati utakapoika.

(6) Kuimarisha Chama kifedha

165. Pamoja na kuimarisha usimamizi wa Fedha za Chama, Chama

kitachukua hatua thabiti za kujiimarisha kwa kujiongezea mapato.

Mambo matatu yanakusudiwa kufanywa: -

Jambo la kwanza ni kuwa Chama kitaimarisha udhibiti wa fedha

zake. Jambo la pili ni kuwa kitawataka wanachama na viongozi wa

CCM kutoa mchango wa hiari wa kuimarisha Chama kwa kiwango

cha asilimia itakayoamuliwa ya mshahara wa kila mwezi kwa kila

kiongozi na mwanachama. Utaratibu wa aina hiyo utabuniwa kwa

ajili ya wanachama wakulima na wanaojiajiri wenyewe. Hatua ya

tatu ni Chama kutafuta njia nyingine za kudumu za kukiwezesha

kuongeza mapato yake.

(7) Kuimarisha Jumuia za Wananchi

166. Jumuia za wananchi zina umuhimu mkubwa sana kwa Chama

katika malengo na mbinu zake za mapambano. Pamoja na kuwa

vyombo vinavyowaunganisha wananchi wenye hali inayofanana

katika shughuli zao za kazi za kila siku au wananchi wanaofanana

kwa maumbile ili kuendeleza maslahi yao, Jumuia za wananchi pia

ni mikondo inayokiwezesha Chama kuuikia umma wa wananchi

kwa ikra, msimamo, maelekezo na miito mbalimbali.

167. Katika hali hii Jumuia za wananchi zinaweza kuwa vyombo muhimu

vya mapambano ya Chama na kuwa nguvu zake za akiba. Katika

kipindi kinachoanzia sasa, Chama kitajitahidi kuzijenga jumuia

kwa kushirikiana nazo ili ziweze kuwa nguvu thabiti za mapinduzi

ya kujenga ujamaa. Papo hapo, Chama kitahakikisha kuwa Jumuia

za wananchi zinapata msaada utakaoziwezesha kushirikiana na

Chama bila ya kupoteza uwezo wao wa kuziendesha shughuli zao

wenyewe bila ya kuingiliwa.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 116/142

MIONGOZO MIWILI 115

168. Kwa sasa, wakati Chama kinaanzisha vuguvugu la mapinduzi la

mijadala ya kujikosoa na kukosoana kwenye Chama katika matawi

yake, Jumuiya zichukue nafasi hii kushiriki kwa ukamilifu katika

harakati hizi. Chama kitawataka wana CCM wote kuwa katikamstari wa mbele katika vuguvugu la kuleta mwamko wa siasa

katika Jumuia zao. Ni wajibu wa kila mwanachama wa jumuiya

hizo kujiunga na Jumuiya zinazomhusu kueneza siasa ya Chama

miongoni mwa wanachama wa Jumuiya hizo na kuwashawishi

wananchi wengine kujiunga na Jumuiya.

MWISHO

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 117/142

MIONGOZO MIWILI116

SURA YA NNE

MAAMUZI YA ZANZIBAR, 1991 

(Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Ali Hassan Mwinyi wakati

akizungumza na wazee wa chama, viongozi wa taifa, mashirika ya umma

na watu binafsi juu ya ufafanuzi wa maamuzi ya Halmashauri Kuu ya

Taifa katika kikao chake cha Zanzibar: Diamond Jubilee Dar es Salaam,

tarehe 25/2/1991)

Ndugu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam,Ndugu Katibu Mkuu,

Ndugu Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam,

Ndugu Viongozi wa Chama na Serikali na

Ndugu zetu waalikwa,

Kabla ya yote, labda niseme kwamba kwa kuwa tumo katika mwezi wa

pili tokea kuanza kwa mwaka mpya, nami sijapata nafasi ya kukutana

nanyi wazee, ni vyema nitumie nafasi hii kwanza kukutakieni heri ya

mwaka mpya, na baraka zote za mwaka 1991. (Makoi). Ninakuombeeni

uzima, nguvu, baraka na mafanikio.

Pili, tuna kawaida katika nchi yetu, kwamba kila linapotokea jambo

muhimu katika Taifa, tunatafuta nafasi ya kukutana nanyi na kukuelezeni.

Hivyo, leo napenda kuzungumza nanyi wazee wa Dar es Salaam na, kupitia

kwenu, iwe ninazungumza na Wazee wenzenu wa Tanzania nzima. Kwa

hiyo, hayo nitakayokuambieni nyinyi, ninawaambia pia Wazee wa Taifaletu wote kwa jumla.

Hivi karibuni Halmashauri Kuu ya Taifa ilifanya kikao chake cha

kawaida Zanzibar, ambacho kilijadili mambo mbalimbali. Kikao hicho

kilimalizika kwa kutoa maamuzi maalum. Maamuzi hayo yana uzito

mkubwa. Inaelekea baadhi yetu, pamoja na Vyombo vyetu vya Habari,

hatukuyaelewa vizuri maamuzi hayo. Kwanza, nataka nivivue lawama

Vyombo vyetu vya Habari. Maana hatukuwa nao huko. Kwa hivyo

walitangaza vile walivyoelewa. Kwa sababu hiyo nimeona ni vyema

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 118/142

MIONGOZO MIWILI 117

kuzungumza nanyi ili kusahihisha matangazo ya vyombo vyetu. Nimeona

ni vyema kutumia nafasi hii kutoa ufafanuzi.

LAZIMA TWENDE NA WAKATIInaelekea kuna hofu kwamba Azimio la Arusha linageuzwa. Kwa hiyo,

tokea mwanzo, kabla ya kusema lolote, nataka tuelewane kwamba siasa

yetu bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea. (Makofi). Haikugeuka wala

hatutazamii kuigeuza. Kwa hali yoyote sisi Wanachama wa Chama Cha

Mapinduzi hatutaigeuza Siasa hii. (Makofi). Kule Zanzibar tulizungumza

mambo mengi, miongoni mwao, ni kutoa tafsiri ya baadhi ya vipengele

vya Azimio ili vifanane na wakati tulionao.

Azimio la Arusha, kama tunavyojua, limetangazwa mwaka 1967. Hii

leo tuko katika mwaka 1991. Imepita miaka mingi, zaidi ya 20 tokea

kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Na katika kipindi cha miaka 20

yametokea mabadiliko mengi duniani na pia katika hali ya maisha

yetu. Hali yetu ya sasa, hasa ya kiuchumi, siyo ile ile ya mwaka 1967.

Ndio maana mishahara ya wafanyakazi ingawa imeongezeka sana

lakini bado haikidhi mahitaji yao - haiwatoshi hata wale wanaopokea

mishahara mikubwa miongoni mwetu. Isitoshe, wakati wa Azimio idadi

ya Watanzania ilikuwa ndogo. Sasa hivi idadi yetu imeongezeka zaidi ya

mara mbili. Kwa sababu ya wingi wetu mahitaji yetu nayo yemeongezeka

sana, wakati mapato yetu yamekuwa yakipungua wakati wote.

Kwa hivyo ni dhahiri kwamba jamii ya Tanzania lazima itie maanani

mabadiliko haya na ijiandae kwenda na wakati. Kama hatukwenda na

wakati, kazi yetu itakuwa ni kufukuzia wakati - jambo ambalo hatulimudu.

Tabia ya wakati ni kama ile ya bahari. Bahari inakupwa na kujaa mpaka

ukingoni mwa maji. Baadaye maji huopwa polepole, mpaka kuika

wakati ikawa maji yote yamekwishaondoka ufukoni. Samaki werevu

huondoka nayo hayo maji, yaani yakijaa huja nayo, yakitoka hutoka nayo,

vinginevyo hupwelewa. Samaki watakaozembea kufuata maji watajikuta

wamechelewa wanatapatapa juu ya mchanga wakati maji hayo hayapo.

Hiyo ndiyo maana ya kupwelewa (Makofi).

Hapa Afrika, kwa mfano, imeanzishwa mipango mbalimbali ya

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 119/142

MIONGOZO MIWILI118

ushirikiano wa uchumi. Mipango hiyo ni pamoja na Ushirikiano wa

Nchi za Kusini mwa Afrika (SADCC) na Eneo la Soko Nafuu (PTA). Afrika

pia imeazimia kuunda Jumuiya ya Uchumi. Nchi zinazoendelea nazo

zimedhamiria kuzidisha ushirikiano miongoni mwao. Nchi yetu lazimaifanye mabadiliko ili iweze kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli zote

hizo zinazosaidia maendeleo yetu.

KILA ZAMA NA MWONGOZO WAKE

Ndugu Wazee, Msahafu wa Waislam unasema “LIKULLI AJALIN KITABU”

Mwingereza mmoja kaitafsiri aya hiyo hivi: ‘”TO EVERY AGE ITS BOOK”

yaani “Kila zama ina Kitabu (Mwongozo) chake”. Na sisi Wana-CCMtunakubali kuwa “kila Zama zinahitaji kuwa na Mwongozo wake”. Azimio

la Arusha ni Mwongozo wetu wa msingi. Ni dira inayoongoza mwelekeo

wa jamii yetu. Lakini tafsiri zake zinabidi zirekebishwe kila inapohitajika

ili zisipitwe na wakati. Miongozo ina tabia moja: inakuja ili kufafanua,

kuelekeza au kukemea hali mbaya inayojitokeza.

Mojawapo ya malengo ya maamuzi ya Zanzibar ni kutoa tafsiri sahihi

ili kupunguza kebehi inayofanywa dhidi ya siasa yetu ya Ujamaa naKujitegemea na pia kwenda na wakati.

Mwaka 1967 lilitangazwa Azimio la Arusha. Mwaka 1971 ulifuatiwa

na tamko la Iringa la “Siasa ni Kilimo”. Tamko hili lilikuwa ni mbinu na

msisitizo wa Siasa yetu ya Kujitegemea. Lilipanua tafsiri ya Azimio la

Arusha. Katika mwaka 1981 ilionekana kuna haja ya kutolewa mwongozo

mwingine kulingana na wakati ule ambao nao ni upanuzi wa tafsiri ya

Azimio. Ulitangazwa ili kukidhi haja ya wakati ule.Aidha, kabla ya hapo, katika mwaka 1974, Chama kilipitisha Agizo

la Musoma kuhusu Elimu ya Kujitegemea ambalo madhumuni yake

yalikuwa kutazama upya suala la uingizaji wanafunzi Chuo Kikuu na

kupanua Elimu ya Msingi ili kutoa fursa kwa watoto wote wenye umri

wa kwenda shule kufanya hivyo.

Maandiko yote hayo hayakupingana na Azimio la Arusha ila yakiongeza

mwangaza kwa mambo ambayo yalihitaji yafanane na wakati wake. Nalazima iwe hivyo, kwani bila ya kwenda na wakati tungechekesha.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 120/142

MIONGOZO MIWILI 119

Kwa mfano wakati wa Azimio la Arusha, mtakumbuka kuwa tafsiri

ya neno Kiongozi ni pamoja na yule mwenye mshahra ulioikia

shilingi 1,066/= kwa mwezi. Tungeng’ang’ania tafsiri hii tu, basi leo

pasingekuwapo wafuasi. Wafanyakazi wote wangetafsirika kuwa niviongozi wa CCM. Kwani ukiacha wakulima, wafanyakazi wote sasa kwa

tafasiri ya 1967 ni viongozi tena maradufu. Maana kima cha chini sasa ni

Sh.2,500/=, ambazo ni zaidi ya mara mbili ya Sh.1,066/=. Ndiyo maana

tukasema jamii yetu italazimika kufanya marekebisho kila inapokuwa

lazima kufuatana na wakati. Tutafanya hivyo bila ya kuachana na misingi

ya siasa yetu.

Kwa hivyo, tulichokifanya kule Zanzibar ni kupanua tafsiri za Azimioili ilingane na wakati tulionao. Kufanya hivyo si kuua Azimio bali ni

kuliimarisha.

CHIMBUKO LA AZIMIO LA ARUSHA 

Historia ya Azimio la Arusha tunaijua sote. TANU ilipigania kwa

maneno mpaka nchi ikapata UHURU wake. Tanganyika ilipopata Uhuru

na tukaanza kujitawala ishara potofu zilianza kuchomoza. Baadhi ya

viongozi walianza kuutumia uongozi wao kama mradi wa kujineemesha.

Kwa kutumia nyadhifa zao, wakikopa fedha benki na kuanza kujijengea

mashamba - si ya miti - bali ya majumba; si nyumba za kuishi tu bali

majumba mengi ya kupangisha.

Tabia hiyo ilizusha manung’uniko ya watu. Jamii ilianza kugawanyika

makundi mawili; manaizi na makabwela. Kitendo hicho ndio chimbuko

la kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Azimio lilikuja kutoa mwongozo wa

maadili ya wanachama na viongozi wa TANU. Kwa hivyo nia ya Azimio la

Arusha, miongoni mwa mambo mengine, ilikuwa ni kuwazuia viongozi

kutumia uongozi wao kujitajirisha. Hilo ndilo lililokuwa tatizo la hatari

miongoni mwa matatizo wakati ule. Azimio lilikuja kuokoa jahazi -

kukemea tabia potofu.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 121/142

MIONGOZO MIWILI120

TATIZO LA SASA NI UCHUMI TEGEMEZI

Mtu anaweza kuuliza je sasa kuna tatizo gani? Tatizo letu katika miaka ya

tisini na kuendelea ni lile la uchumi tegemezi. Tatizo letu sasa ni kwamba

uchumi wetu ni duni mno. Wakati idadi yetu inaongezeka, mapato yaTaifa, hasa ya fedha za kigeni, hayaongezeki. Wakati wa Uhuru idadi

yetu ilikuwa ni watu milioni tisa. Lakini leo, tuko milioni tisa na tisa tena

na nusu ya tisa. Lakini mapato yetu ya pesa za kigeni yapo pale pale, $

milioni 400. Wakati Azimio la Arusha lilitutaka tujitegemee, hali halisi ni

kuwa tumekuwa wategemezi wakubwa. Maana Taifa letu hivi sasa, kwa

pato lake lenyewe la fedha za ndani, linaweza kujitegemea kwa kipindi

cha miezi saba tu katika mwaka. Tunategemea watu wengine, kwa njia yaruzuku na mikopo, kumalizia miezi mitano inayosalia katika mwaka. Hii

ni hatari. Lazima tuendelee kubuni mbinu za kuondokana na hali hiyo.

MBINU ZA KUJITEGEMEA 

Ilani ya Uchaguzi inasema hivi:

Makusudi ya Chama katika kipindi cha miaka

mitano ijayo ni kwa Taifa kukusanya nguvu zote zawananchi kwa kusaidiana na Serikali zao (Mbili), nakuzitumia katika kila eneo la maendeleo ili kutoamsukumo mpya wa utekelezaji wa siasa ya Ujamaa

na Kujitegmea.

Hivyo, Chama na Serikali zake zinawajibika kuwarahisishia wananchi

wao kujitegemea kwa chakula, kujitegemea kwa mavazi na kujitegemea

kwa malazi. Ili kutimiza lengo hilo Taifa lazima liwawezeshe wananchiwake kuzalisha mazao ya biashara na chakula kwa wingi. Pia ni wajibu

wa Chama na Serikali kuandaa mbinu za kuwasaidia wananchi kujijengea

nyumba zao za kuishi ili ziwasitiri wanapostaafu au kuwa wazee.

Je wananchi wakituuliza: hivi ni mbinu gani mlizofanya kumshirikisha

kila mmoja wetu kutumia nguvu zake zote katika kuzalisha kama Ilani

inavyosema? Tungejibu nini? Lakini sasa kila mwananchi, pamoja na

mwana CCM, hataweza kutoa kisingizio kwa kusema:-

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 122/142

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 123/142

MIONGOZO MIWILI122

nimekuwa nikiutetea tangu zamani. Utaratibu

huu unawasaidia sana watu wenye mapato madogo,

wanafunzi, au wafanyakazi ambao bado hawajaoa

au kuolewa kupata vyumba vya kupanga kwa kodinafuu.

Ni kweli kwamba huko nyuma tumekuwa wakali

mno katika kutafsiri msharti haya.

Azimio la Arusha linachokataa ni unyonyaji. Hivyo maskini ya Mungu

mwenye kijumba chake cha mbavu za mbwa akimwona maskini

mwenziwe anapata taabu, hana pakukaa, asimpangishe? Je akimpangishaatakuwa anamnyonya? Au anamstiri? Kwa hiyo tangu zamani kustiriana

ni ruhusa (Makofi).

Hatukuishia hapo kule Zanzibar, tulikwenda zaidi, tulisema pia kwamba

wapo viongozi miongoni mwetu ambao baadhi yao wamefanya kazi za

Chama au za Serikali kwa miaka 30 au zaidi. Lakini hawana nyumba;

ukiika wakati wao wa kustaafu viongozi hao huwa wanababaika kwa

kutojua wataishi wapi. Ndipo wanapoanza kutafuta mbinu - ndiyo maanasiku hizi utakuta misururu mirefu katika Oisi ya Vyeti vya kuzaliwa.

Watu wanakwenda kubadilisha tarehe zao za kuzaliwa, kujifanya bado

wangali vijana ili wachelewe kustaafu. (Makofi).

Sisi tunaamini kwamba baada ya kipindi kirefu cha utumishi, mtu aweze

kuwa na nyumba ili, hata akiwa kipofu angalau aweze kupapasa kuta

zake na kusema: Hii ni nyumba yangu niliyoipata kwa jasho langu la kazi

ya miaka 30. Tunataka awe na kitu. Lakini, Ndugu Wazee, bahati nzuriwanachama wa CCM, kama wananchi wengine, wanaruhusiwa kukopa.

Wanaweza kukopa kwenye benki zetu wakajenga nyumba za kukaa. Sasa

jamani tukisema kwamba hata mtu aliyekopa asiipangishe nyumba hiyo

atalipia nini huo mkopo?

Vinginevyo tutakuwa tunamfanyia mzaha mtu huyo. Maana

atachukua mkopo, ajenge nyumba, kisha ashindwe kulipa huo mkopo.

Waliomkopesha wataikamata hiyo nyumba na kuiuza ili kurudisha

fedha yao. Katika hali hiyo mwana-CCM gani atakayekuwa na nyumba

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 124/142

MIONGOZO MIWILI 123

iwapo mwisho wake ni kuchukuliwa na kile chombo kilichomkopesha?

Kwa hivyo nasema mtu kama huyu ana dharura; ana dharura ya deni.

Amejenga nyumba kwa nia ya kukaa mwenyewe lakini ana deni la

mkopo. Kama anaweza kukaa nyumbani mwake, akae. Lakini pia awe naruhusa ya kupangisha nyumba yake, akitaka, ili imsaidie kulipa mkopo.

Anapostaafu awe anayo nyumba ya kumstiri uzeeni. Kitendo hicho

kisimpotezee uanachama wake wa CCM.

Kwa hivyo Ndugu Wanachama, huko ndiko kwenda na wakati, vinginevyo

tutapwelewa. Mtu kama huyu aruhusiwe kupangisha nyumba yake, iwe

nusu ya nyumba, ama robo ya nyumba au yote (makofi).

BIASHARA YA KUPANGISHA MAJUMBA BADONI MWIKO

Lakini kikao cha Zanzibar hakikutengua miiko ya kiongozi wala ya

mwanachama wa CCM. Bado ni mwiko kwao kuwa na biashara ya

kupangisha majumba. Kwa mfano, kama kuna mwanachama anayeomba

mkopo, akipata anajenga nyumba, halafu anaikodisha, akipata fedha za

kodi anajenga nyingine mpya, ambayo nayo anaikodisha na kuendeleakujenga nyingine. Huyo ni mfanyabiashara. Kazi yake ni kujenga na

kupangisha majumba. Kikao cha Zanzibar hakikusudii mwanachama wa

aina hii. Huyu siye (Makofi).

Vile vile, Mwanachama wa CCM, hata akiwa kiongozi katika mazingira

maalum, aruhusiwe kukodisha nyumba yake, ikiwa haihitaji kuikaa

wakati ule. Inawezekana haihitaji kuishi katika nyumba yake kwa kuwa

kapata uhamisho. Mfano, mtu kahamishiwa Iringa kwa kazi wakatinyumba yake iko Dar es Salaam. Je ikae bure watu waitumie bure tu

kweli? (Makofi).

Ni mwanachama wa aina hii ndiyo tulisema huko Zanzibar kuwa

aruhusiwe kupangisha nusu ya nyumba ama robo ya nyumba au yote,

maadam mtu huyo anapo pengine pa kukaa. Lakini tunasisitiza kuwa

bado si ruhusa kwa mwana CCM wala kiongozi wa CCM kuendesha

biashara ya kupangisha majumba.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 125/142

MIONGOZO MIWILI124

HISA KATIKA MAKAMPUNI YA UMMA,KUPUNGUZA UKWASI!

La pili lililoamuliwa huko Zanzibar ni kuwaruhusu wanachama wa CCM,

kwa kufuatana na hali ya wakati ulivyo, sasa aruhusiwe kuwa na hisakatika kampuni ya Umma. Hii leo tunayo Mashirika ya Umma zaidi ya

400, lakini mengine yao hayana fedha za kuendeshea kazi zao.

Mfano kuna mwananchi mmoja alikwenda kwenye kiwanda cha

Umma kutaka huduma ya kusaishiwa ngozi zake. Alipoika hapo

alikuta “pamelala paka”; yaani palikuwa kimya, hapakuwa na kazi

yoyote inayofanyika. Kumbe kile kiwanda kilikuwa kimefungwa kwa

kukosekana fedha za kukiendeshea ... umeme ulikatwa na wafanyakaziwalipewa likizo.

Meneja alimfahamisha huyo mteja kuwa kiwanda kimefungwa kwa

sababu ya deni la maji na umeme pamoja na pesa za mishahara ya

wafanyakazi. Huyo mteja alikubali kulipa arubuni (advance) ya milioni

saba ili kukikwamua kiwanda. Wiki ya pili yake kiwanda kilianza kufanya

kazi zake za kuzalisha kama kawaida.

Kisa cha kiwanda hicho kusimama kazi ni kukosa fedha za kuendeshea.

Kiswahili cha siku hizi huitwa ukwasi. Kwa hiyo kazi ilisimama.

Katika hali kama hii, tumeona ni vyema kuwaruhusu wananchi wote

pamoja na wakulima, na wafanyakazi wa shirika lenyewe wakiwemo

wanachama wa CCM kununua hisa chache kwa kila atakaetaka.

UBIA WA UMMA NA DOLA KATIKA SHIRIKA 

Narudia, watakaoruhusiwa kununua hisa ni wananchi wowote

watakaopenda pamoja na wakulima wa pamba, korosho, kahawa,

tumbaku na wafanyakazi wa hilo shirika lenyewe. Kwa njia hiyo,

Shirika hilo sasa litapata sura mpya, litakuwa ni la ubia kati ya Serikali,

wafanyakazi na wananchi. Fedha tunazozizungumzia hivi sasa, za kulipia

taa na mahitaji mengine zingetokana na ununuzi wa hisa ili uzalishaji

uendelee. Katika hali kama hiyo kiwanda kitakuwa ni mali ya umma

kweli. Maana kuna tofauti ya Shirika la Dola na Shirika la Umma kwamaana ya wananchi wenyewe.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 126/142

MIONGOZO MIWILI 125

Endapo shirika la umma litataka kuwashirikisha wananchi na

wafanyakazi wake kwa kulichangia ili kuondoa tatizo la Ukwasi, jambo

hilo liwe ni halali, na Mwana CCM naye aruhusiwe kuwa miongoni mwao.

(Makofi)..Kilichofanywa na maamuzi ya Zanzibar ni kumruhusumwanachama wa CCM naye kushiriki kikamilifu katika sera ya Taifa

ya uwekezaji wa rasilimali nchini.

Katika sera ya uwekezaji rasilimali tunaruhusu ubia katika uchumi wetu.

Ubia huo unaweza kuwa baina ya watu wa ndani ya nchi peke yao, au

kati ya wawekezaji wa nje na wa ndani. Baada ya kuikubali misingi hiyo

hatuoni kwa nini tusianzie kwa kuwaruhusu wananchi, wakulima na

wafanyakazi kuwa na hisa katika Mashirika wanayofanyia kazi (Makoi).

 WAFANYAKAZI KUSIMAMIA UWAJIBIKAJI

Nia nyingine ya kufanya hivyo inatokana na kutambua kuwa wafanyakazi

wenye hisa katika kiwanda watakuwa wasimamizi wakereketwa wa

uwajibikaji katika viwanda hivyo. Watakereketwa zaidi pakiwa na

ubadhirifu au kutowajibika.

Hivi leo baadhi ya mashirika ya Umma ni mashirika ya umma kwa jinatu. Watu wanayaibia wakidai wanachukua chao. Pengine wanashindana

kufanya hivyo ili wasipunjwe. Baadhi ya mashirika ya Umma

yanahujumiwa kana kwamba hayana wenyewe. Baada ya maamuzi ya

Zanzibar kuanza kutekelezwa, Mashirika hayo yatakuwa na wenyewe.

MWONGOZO WA 1981 KUHUSU UWAJIBIKAJI

Maamuzi ya Zanzibar si mapya. Mwongozo wa chama wa 1981 umetoailani juu ya kupungua kwa uwajibikaji katika Mashirika ya Umma, jambo

ambalo hivi sasa tunalitafutia ufumbuzi. Mwongozo wa 1981 unasema

hivi:

Imezuka tabia ya aibu nchini ambayo imekuwa

ikiongezeka ya vitendo vya kuharibu na kuvitumia

vibaya vyombo muhimu vya kazi na mali ya umma

kwa jumla. Magari, matrekta, zana nyinginemuhimu za chama, serikali, mashirika ya umma

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 127/142

MIONGOZO MIWILI126

mara nyingi hayadumu muda mrefu kama ambavyo

ingetazamiwa kutokana na matumzi mabaya.

Lakini ikiwa watu pale pale wenyewe wana hisa katika kampuni au

shirika - mfano – TANESCO – [au] kuwa Mkurugenzi katika kampuni ya

Kibepari. Napenda suala hili lieleweke vizuri ili kujibu ikra zilizojengeka

kuwa uamuzi huo umevunja Azimio la Arusha.

Kwanza inafaa tufafanue maana ya Mkurugenzi. Tafsiri ya Mkurugenzi

inayojulikana sana ni ile ya mjumbe wa bodi ya wenye hisa katika

Kampuni fulani. Kwa hiyo wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi katika

Kampuni ya Kibepari huwa ni miongoni mwa wale wenye hisa zao

katika kampuni inayohusika. Watu hao huchaguliwa na wenzao wenye

hisa kama wa kuongoza shughuli za Kampuni yao kwa faida ya pamoja.

Mkurugenzi wa aina hii hawezi kuwa mwanachama wa CCM.

Lakini kuna Mkurugenzi wa aina nyingine ambaye ni tofauti kabisa na

Mkurugenzi mwenye mali. Mkurugenzi huyu ni yule ambaye ameajiriwa

tu na wenye mali yao, kutokana na sifa zake za utaalam, kuendesha

kampuni. Mtu huyu huwa ni mwajiri tu, anayefanya kazi. Huyu ni mtumishi

tu kama watumishi wengine, hana chake katika kampuni inayohusika.Anachotegemea ni mshahara wake na marupurupu mengine kama yapo.

Huyu ndiye Mkurugenzi anayeruhusiwa kuwa mwanachama wa CCM.

Azimio la Arusha bado liko pale pale kwa wale wakurugenzi wa aina ya

kwanza. Wao Azimio linawabana, hawawezi kuwa wanachama wa CCM.

Lakini huyu wa aina ya pili aliyeajiriwa tu, akija kuomba uwanachama

tunamkubali.  Azimio la Arusha kamwe halijamkataa mfanyakazi

mwenziwao kwa “koa” la kutumikia Kampuni ya Kibepari, hivyondivyo tulivyoamua Zanzibar.

  MWANA-CCM KUWA NA HISA KATIKAKAMPUNI YA KIBEPARI

Jambo jingine ambalo halikueleweka vizuri na linahitaji ufafanuzi ni lile

la kumruhusu mwanachama wa CCM kuwa na hisa katika kampuni ya

Kibepari. Hili nalo tumeliruhusu huko Zanzibar, lakini sharti iwe katikamazingira maalum.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 128/142

MIONGOZO MIWILI 127

Ni vyema kukumbushana kuwa yapo makampuni ya kibepari ambayo

tumekuwa nayo hata kabla ya Azimio la Arusha. Kampuni hizo zimekuwa

zikikidhi kiasi fulani cha ajira ya Watanzania, pamoja na Wanachama

wa CCM.

Ili jambo hili lieleweke vizuri, nitatoa mfano tu wa Kampuni ya mtu

binafsi. Mwenye Kampuni ya binafsi anaweza kabisa akaamua kwa hiari

yake kuuza baadhi ya hisa kwa wafanyakazi wake ili kuwapa motisha ya

kazi. Tajiri yeyote akiamua kufanya hivyo, Chama na Serikali vitamwona

kuwa amechukua hatua ya kimaendeleo. Kitendo chake hicho ni halali.

Kwa sababu itakuwa ameuzimua ubepari kwa kuifanya kampuni yake

ni ya ubia kati yake na wananchi aliowaajiri. Kwa kweli kampuni hiyoitakuwa kama chama cha ushirika.

Katika hali hiyo, hata Mwanachama wa CCM anaruhusiwa kupokea/

kununua hisa alingane na wafanyakazi wenzie. Ni mazingira maalum

ya namna hii tu ndiyo yanayoruhusu Mwanachama wa CCM, kama

mfanyakazi mwingine, kuchukua hisa katika Kampuni anayofanyia kazi.

Atakapostaafu ataweza kuendelea kupokea faida ya hisa yake au kuiuza.

MISHAHARA MIWILI KWA MWANA-CCM

Kuhusu mishahara miwili, Azimio la Arusha linasema hivi:

Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya

haki kutokana na kazi yake.

Kufuatana na ukweli huo, anayefanya kazi mbili za halali anastahiki

kupata malipo ya kazi ya pili. Tuchukue mfano wa Profesa ambayemchana kutwa anasomesha Chuo Kikuu. Baada ya saa za kazi anaweza

kuamua kufanya kazi ya akili, kwa mfano kutoa ushauri au kuandika

mradi kwa aliyemwomba huduma hiyo.

Mwanachama huyo atastahiki kupata malipo ya kazi hiyo. Hili si geni,

katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Azimio la Arusha, baba wa

taifa alisema hivi:

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 129/142

MIONGOZO MIWILI128

Lile sharti la kutopokea mishahara miwili kwa kweli

ni sharti la tahadhari tu. Ni vigumu sana kufanya kazi

mbili za kuajiriwa na zote mbili ukazifanya vizuri.

Huwezi kuwatumikia mabwana wawili! Lakini shartihili halimkatazi kiongozi wetu kujiongezea pato kwa

kutumia muda wake wa kupumzika kwa kufanya

shughuli nyingine: kama kulima au kufuga, ikiwa

yeye si mkulima au mfugaji, kuandika, kufanya kazi

ya useremala, au kufanya shughuli nyingine yoyote

kwa mikono yake au kwa ajili zake.

Jambo la msingi ni kwamba lazima twende na wakati. Mwaka 1967lilipotungwa Azimio la Arusha ilikuwa hakuna haja ya kuwa na mishahra

au malipo ya kazi zaidi ya moja kwa sababu wakati ule mshahara mmoja

ulikuwa unatosha kukidhi mahitaji yote muhimu. Kwa mfano, mimi,

mwenyewe, mshahara wangu wakati ule ulikuwa shilingi 2,200/= kwa

mwezi. Mshahara huo, hasa kwa Zanzibar, ulikuwa ukinitosha kukidhi

mahitaji yangu yote ya lazima.

Wazee wangu watakumbuka kwamba wakati ule kule kitunguu, pilipili nabizari - vyote hivyo kwa senti tano tu. Ilikuwa inawezekana pia kununua

samaki mkubwa kiasi kwa senti ishirini mpaka 50 tu; au kununua kuni

za kuweza kupikia mlo mzima kwa senti kumi tu. Siku hizo iliwezekana

mnunuzi kujaziwa mafuta ya kupikia au samli kikombe kizima kwa

senti ishirini au sitini tu. Halikadhalika kwa senti ishirini tu mtu aliweza

kununua matunda, kama vile fungu la ndizi mbivu au machungwa au

papai. Kwa ufupi, kwa mahitaji ya siku nzima, tangu asubuhi hadi jioni,

iliwezekana mtu kutumia pesa kidogo sana.

Katika hali hiyo, kulikuwa hakuna ulazima wa kufanya kazi ya pili. Afanyae

kazi zaidi ya moja huonekana ni mlai au ana tamaa. Kwa mshahara huo

huo niliweza kudunduliza pesa na mwishowe kununua gari mpya kabisa.

Gari hilo lilinigharimu pesa nyingi kwa wakati huo - shilingi 13,000/=!!

Wakati huo bei ya mafuta nayo ilikuwa shilingi tatu tu kwa galoni zima.

Katika mazingira ya aina hii mshahara mmoja ulimudu kukidhi mahitaji

ya wafanyakazi wengi ukiacha walevi.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 130/142

MIONGOZO MIWILI 129

HALI IMEBADILIKA 

Lakini leo mambo yamebadilika. Gharama ya maisha imepanda sana.

Serikali yenyewe imeungama waziwazi kuwa haina uwezo wa kumlipa

mfanyakazi wake mshahara unaomwezesha kumudu gharama zamaisha. Kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wengi, wanashindwa kukidhi

mahitaji yao muhimu. Ndio maana Chama na Serikali yake vimekuwa

vikiwahimiza wafanyakazi kufanya shughuli nyingine za halali, baada

ya saa za kazi, ili kujiongezea mapato. Mfano wa kazi hizo ni kama vile:

kutibu, kuandika vitabu, kuandika mradi, kutoa ushauri wa kitaalamu,

kufundisha, ‘overtime’, useremala, ufundi bomba, ufundi umeme, ufundi

cherahani, kilimo, ufugaji, kuziba mipira ya magari, kuteka maji ya kuuza,kupiga matofali, kutengeneza baiskeli na kadhalika.

KOFIA MBILI MSHAHARA MMOJA 

Lakini lazima tuelewane kuwa hii mishahara miwili tunayozungumzia

haimhusu kiongozi mwenye koia mbili. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa

na Mkuu wa Wilaya, ambao vile vile ni Katibu wa Chama wa Mkoa au

Wilaya, hawaruhusiwi kupokea mishahara miwili. Hawa watalipwamshahara mmoja tu, maana hii kazi ya pili ni sehemu tu ya ile ya kwanza.

Lakini wanaruhusiwa kufanya kazi za ziada kama vile kilimo, ufugaji

na kadhalika, baada ya saa za kazi, kama walivyoruhusiwa wafanyakazi

wengine. Hapa nitapenda kusisitiza kuwa wale watu wanaoeneza maneno

ya kejeli kuwa ati Maamuzi ya Zanzibar ni mbinu tu za “wakubwa”

kujinufaisha wenyewe, ijulikane kuwa si kweli. Kazi zilizoorodheshwa

hapa si za wakubwa bali ni kazi zinazoweza kufanywa na kila mtu

kufuatana na ujuzi alionao na mazingira ya mahali anapofanyika kazi.

MWANA-CCM MKULIMA NA MFUGAJI

Watanzania wengi ni wakulima, wakulima ndio wengi zaidi. Mkulima

kwa maana pana ni pamoja na mfugaji. Katika siku za nyuma, baadhi

ya wanachama waliwahi kutiwa msukosuko kwa kuwa na mashamba

makubwa au kufuga kuku 500. Lakini baadaye Chama kilijisahihisha

kama inavyosema Programu ya Chama:

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 131/142

MIONGOZO MIWILI130

Chama Cha Mapinduzi ni Chama kinachokua

(haikudumaa). Kinakaa katika nadharia na falsafa 

yake, (ili kwenda na wakati).

Hii ndio ilivyokifanya Chama kijisahihishe kila kinapokosea.

Kwa hiyo kama siku moja tulimtia mwenzetu msukosuko kwa kuwa

na shamba kubwa, mbuzi 18 au kuku 500, sasa Chama kimekua katika

falsafa yake. Falsafa ya sasa inatia maanani hali halisi ya wakati wa sasa.

Ndio maana kule Zanzibar tukaruhusu kiongozi awe na shamba lisilozidi

hekta 20, hasa kama shamba hilo limo katika eneo la kijiji.

Kuhusu ufugaji, kuna baadhi ya wenzetu katika makabila ya Tanzania

ambao kwao ni utamaduni wao kuwa na ng’ombe wengi. Mfano mzuri

ni wenzetu wa makabila ya Wamasai, Wasukuma na Wagogo. Je, mwenye

utamaduni wa kumiliki ng’ombe wengi akataliwe katika Chama kwa

sababu ya kumiliki ng’ombe wengi? Tunasema hapana. Akiomba

uanachama wa CCM akubaliwe. Chama Cha Mapinduzi hakimkatai tajiri

aliyepata utajiri wake kwa njia ya halali na kulipa kodi ya Serikali analipa.

Anayekataliwa na CCM ni yule aliyepata utajiri kwa wizi, kwa rushwa,dhuluma na kwa njia nyingine za haramu.

Huko Zanzibar tuliikiria labda tuweke kiwango maalum cha mifugo,

kama vile iwe mwisho ng’ombe 200 peke yake. Lakini tulijiuliza kama

ng’ombe mmoja akizaa na jumla kuikai 201, je huyo ndama amnyonge

shingo?

Hiyo ndio hali halisi iliyotufanya tukubaliane kuwa mfugaji yeyote

anaetaka kuwa mwanachama bila ya kujali idadi ya mifugo yake. Mwenyemshahara mkubwa, vile vile hata wa malaki, maadam ni mshahara wa

kazi halali, naye pia aruhusiwe kuwa mwanachama wa CCM.

MAFUNZO YA MIEZI MITATU

Ili kukiimarisha zaidi Chama, tumewaruhusu wananchi kuwa wanachama

wa CCM bila ya kuhudhuria yale mafunzo ya miezi mitatu.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 132/142

MIONGOZO MIWILI 131

BIASHARA NDOGO NDOGO

Huko Unguja hatukuishia hapo. Tuliamua kuwa Mwanachama wa CCM

wa kawaida naye pia aruhusiwe kuwa na biashara ndogo ndogo ili

kumwongezea kipato. Biashara hizo, ambazo sharti zifanywe baada ya saa

za kazi, ni pamoja na uvuvi, kuwa na gari ndogo au pick-up ya kukodisha

kwa kuchukulia abiria au mizigo, kushona, kusindika matunda, mafuta

na mashine ya kukoboa au kusaga unga.

Mwanachama mwenye mashine ya kusaga unga hanyonyi bali anatoa

huduma kwa jirani zake kijijini. Chama na Serikali vimo mbioni kuhimiza

na kutafuta teknolojia ya kumrahisishia kazi Mtanzania, hasa wanawake.

Ni vyema kukaribisha teknolojia ya kuwasaidia wanawake waondokane

na kufanya kazi ngumu ngumu zinazoweza kuwapotezea wakati na

kuathiri afya zao, kama vile kutwanga au kusaga nafaka, kubeba mizigo

ya kuni, maji na mtoto mgongoni. Si vyema kwa jamii yetu kuingia katika

karne ya ishirini na moja katika hali hiyo. Ndio maana kule Zanzibar

tuliamua kuruhusu biashara ndogo ndogo kuendeshwa na mwanachama

wa CCM kwa manufaa yao na ya jamii.

Ndugu Wazee, haya kwa muhtasari ndio yaliyoamuliwa Zanzibar. Haya

kamwe hayabomoi Azimio la Arusha, badala yake yanaliimarisha. Azimio

la Arusha ni msingi wa siasa yatu ya Ujamaa na Kujitegemea. Ili tuweze

kujitegemea lazima tuandae mbinu na mikakati ya kuzalisha mali,

huduma na chakula. Hili ndio lengo la maamuzi ya Zanzibar.

Mshairi mmoja amesema:-

Kutaraji uongofu bila kupitia njia zake ni kama kulitaka

jahazi kutembea nchi kavu.Ndugu Wazee Ahsanteni sana. (Makofi)

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 133/142

MIONGOZO MIWILI132

SURA YA TANO

MIONGOZO MIWILI YA CHAMA NA

TABAKA LILILOPINDUA UJAMAA*Issa Shivji

Mwongozo wa TANU, 1971

Chama cha TANU kilichopigania uhuru wa Tanganyika chini ya uongozi

wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndicho kilichoasisi Azimio la

Arusha mwaka wa 1967. Azimio liliweka mtazamo na sera za Ujamaa na

Kujitegemea. Wakati ule nyaraka mbalimbali ziliandaliwa na kuandikwa

ili kutoa miongozo katika kutekeleza Azimio la Arusha. Waraka muhimu

mmojawapo ni Mwongozo wa TANU wa 1971. Mwongozo huo una

umuhimu wa kipekee katika historia ya siasa za Tanzania. Mambo

muhimu matatu yamezungumziwa katika Mwongozo huo. Mosi ni

kutambua kwamba ubeberu unaendelea kunyanyasa na kunyonya

Waafrika hata baada ya ukoloni kupitia sura yake mpya ya ukoloni-

mamboleo. Kutokana na ukweli huo, “Vyama vya Siasa vya kimapinduzikatika nchi nyingi za Afrika zinazojitawala, kama vile TANU, bado vingali

ni Vyama vya Ukombozi.”

Pili ni umuhimu na ulazima wa kuunda jeshi la mgambo ambalo litalinda

uhuru wa nchi dhidi ya maadui. Chimbuko la uamuzi huo linajulikana.

Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kusaidia ukombozi wa nchi za

Afrika ambazo bado zilikuwa chini ya ukoloni. Wapigania uhuru ambao

walikuwa wanasaidiwa na Tanzania moja kwa moja walikuwa wale waAfrika ya Kusini, Namibia, wakati ule ikiitwa ‘South West Afrika’, na

Msumbiji ambayo ilikuwa chini ya ukoloni katili wa Wareno.

Huko Afrika ya Magharibi, nchi mojawapo ambayo ilifanana sana na

Tanzania katika sera zake na hasa katika kusaidia wapigania uhuru

ilikuwa Guinea-Conakry chini ya uongozi wa Sekou Toure. Wapigania

* Makala hii yalichapishwa mara ya kwanza katika jarida la Chemchemi, toleo na. 2, Oktoba,2009. Imesahishishwa kwa ajili ya kitabu hiki.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 134/142

MIONGOZO MIWILI 133

uhuru wa Guinea-Bissau na Cape Verde, ambazo zilikuwa nchi moja

wakati huo, chini ya uongozi shupavu wa Amilcar Cabral, walisaidiwa

na Sekou Toure. Kutokana na nafasi ya Guinea-Conakry katika vita vya

ukombozi, majeshi ya Wareno yalivamia Guinea-Conakry. Hata hivyohawakufanikiwa kwa sababu Guinea-Conakry iliweza kuwashinda, hasa

kutokana na jinsi wanamgambo walivyopigana kwa ujasiri na ushupavu.

Isitoshe, karibu na nyumbani, Rais Obote wa Uganda alipinduliwa na jeshi

lake chini ya Idi Amin Dada akisaidiwa na Uingereza na Israeli. Hii ilitokea

baada ya Obote kutangaza kasiasa ka kijamaa na pia kuunga mkono nchi

zilizokuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika

ambazo bado zilikuwa zinatawaliwa na wakoloni na makaburu.

Mambo haya yote mawili ni wazi yalikuwa tishio kwa Tanzania. Tanzania

pia ilikuwa na wasiwasi wa kuvamiwa na jeshi la Wareno. Ndio maana

chama na serikali waliamua kuwa na jeshi la wanamgambo. Jambo hili

ni la kwanza linalozungumziwa katika Mwongozo wa TANU wa 1971.

Pia, Tanzania ilikuwa haipendwi na mabeberu kutokana na siasa zake

za kijamaa.

Pamoja na mambo haya, sifa moja ya Mwongozo ni uchambuzi wake wa

radikali wa hali halisi ambao unaufanya Mwongozo kuwa nyaraka ya

kimapinduzi zaidi kuliko zote zingine zilizoandikwa wakati wa enzi za

Azimio la Arusha. Mfano mmoja tu unatosha kudhihirisha hili.

Mapinduzi ni mabadiliko ya haraka katika jamii,

mabadiliko ambayo yanawanyang’anya wachache

madaraka ambayo walikuwa wakiyatumia kwa manufaayao (na ya wanyonyaji wa nje), na kuyaweka madaraka

hayo mikononi mwa wengi ili kuendeleza maslahi yao.

Katika hili, Chama chini ya uongozi wa Mwalimu, kwa mara ya kwanza,

umeweka wazi maadui wa Mapinduzi ya kijamaa, wakiwa vibaraka wa

ndani wakiungwa mkono na wanyonyaji wa nje kwa maana ya mabepari

wa kimataifa kutoka nchi za kibeberu.

***

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 135/142

MIONGOZO MIWILI134

Lakini zaidi ya yote jambo ambalo lilifanya Mwongozo uwe na historia ya

kipekee ni ibara ya 15 ya Mwongozo. Ibara hii inasema:

Lazima iwepo jitihada ya kujenga hali ya usawa

kati ya viongozi na wanaowaongoza. Iwe ni mwiko

kwa kiongozi wa Tanzania kuwa mwenye majivuno,

ubadhirifu, dharau na uonevu. Kiongozi wa Tanzania

awe ni mtu anayeheshimu watu, asiwe ni mpenda

makuu, sio mnyapara, mkaripiaji na muamrishaji

watu.

Ibara hii ikawa kauli mbiu na itikadi ya tabaka la wafanyakazi dhidi yamenejimenti yao viwandani. Takribani miaka minne kufuatia kutangazwa

kwa Mwongozo, kuliibuka vuguvugu la wafanyakazi ambalo lilikuwa

halijawahi kutokea katika historia ya nchi. Katika kipindi kifupi cha

miaka mitatu tu (1971-1974), kulikuwa na migomo zaidi ya 30, ambayo

ilihusisha wafanyakazi takriban 23,000 na siku za kazi zilizopotea ni

takriban 64,000. Kwa kasi kubwa sana wafanyakazi walijifunza mikakati

na mbinu za mapambano ya kitabaka. Walianza na migomo ya kawaida

kwa maana ya kuweka chini zana za kazi. Kutokana na kulaumiwakwamba wafanyakazi walikuwa hawajali maslahi ya taifa, wafanyakazi

wakabadili mbinu zao katika awamu ya pili. Badala ya kugoma, wakaanza

kuwafungia nje wanyapara na wamiliki wa viwanda wakati wakiendelea

na uzalishaji.

Lakini kama unaweza kuzalisha bila menejimenti, kwa nini ukubali

menejimenti? Kwa hivyo, mapambano yakakoma na wafanyakazi

wakaanza kutwaa viwanda. Hapo ndipo, watawala wa kisiasa na kiuchumi

wakashtuka. Viongozi wa chama na serikali wakaanza kuwashutumu

wafanyakazi wazi wazi kwa kusema kwamba ingawa chama kilikuwa na

sera ya kutaiisha viwanda hii haikuwa na maana kwamba wafanyakazi

wenyewe waanze mtindo huo. Utaiishaji lazima ufuate taratibu na

ustaarabu!

Katika hotuba ya Mei Mosi (ya mwaka wa 1974) yenye kichwa cha habari

Ukigoma unamgomea nani?  Mwalimu aliwashutumu wafanyakazi, jambo

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 136/142

MIONGOZO MIWILI 135

ambalo mara moja lilivunja nguvu za wafanyakazi. Hotuba ya Mei Mosi

ikawa mwongozo wa menejimenti au warasimu, nao walifurahia sana.

Kwa kweli, vuguvugu la wafanyakazi lilikuwa mapambano ya kitabaka

dhidi ya tabaka la warasimu. Katika makala yangu (“The Silent Class

Struggle”  au Mapambano Baridi ya Kitabaka) iliyochapishwa na jarida

la kimapinduzi la wanafunzi wanamapinduzi wa Chuo Kikuu cha Dar

es Salaam, Cheche, nilifanya uchambuzi na nikaliita tabaka hili jipya

mabepari wa kirasimu  (bureaucratic bourgeoisie). Baada ya mwaka

mmoja nikaandika makala ya pili ambayo hatimaye ilichapishwa kama

kitabu, kwa jina la Class Struggles in Tanzania (Mapambano ya Kitabaka

Nchini Tanzania). Wakati ule watu wachache sana waliweza kukubalianana uchambuzi wangu na viongozi walibeza kwamba Tanzania ni nchi

ya wakulima na wafanyakazi na hakuna matabaka. Kwa kiasi fulani,

kulikuwa na ukweli humu kwa sababu matabaka bado yalikuwa katika

uchanga wake, yalikuwa hayajakomaa hasa kutokana na sera mbalimbali

za Mwalimu za kuzuia viongozi na warasimu wasijilimbikizie mali (kwa

mfano kwa kupitia katika Miiko ya Uongozi).

Kwa hivyo, nguvu ya tabaka la wafanyakazi ikavunjika na hatimaye kwasheria ya 1975, wafanyakazi wakawekwa chini ya chama cha NUTA

(National Union of Tanganyika Workers) ambacho kwa vyovyote vile

kilikuwa chini ya himaya ya chama tawala.

Kwa upande mwingine, sera ya Chama juu ya vijiji vya ujamaa pia

ikatekwa na wenye jazba na wapiga debe katika Chama. Mtazamo

wa Ujamaa Vijijini ambao ulisisitiza kwamba vijiji vya ujamaa viwe

chaguo la hiari la wakulima wenyewe ukageuzwa. Sera ukawa ‘vijiji vya

maendeleo’ na wanakijiji wakalazimshwa, mara nyingine chini ya ulinzi

na mabavu ya FFU (Field Force Unit) kuhamia katika vijiji vya maendeleo.

Jambo hili lilifanya wakulima waanze kupoteza imani na Chama. Kwa

ufupi basi, matabaka ya wafanyakazi na wakulima wakafarakanishwa na

kutenganishwa na Chama, na kwa kiasi fulani Mwalimu mwenyewe. Kwa

upande mwinigine, kuvunjika kwa nguvu za wavujajasho, kukasaisha

njia kwa warasimu na wamangimeza wa Chama na Serikali, kuendeleakujilimbikizia madaraka (na hata mali angalau kwa kiicho) na kujijenga

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 137/142

MIONGOZO MIWILI136

kama tabaka jipya la vibepari chini ya himaya ya ubeberu. Hawa ndio

hatimaye wakaja kuainishwa kwa ufasaha kama wapingamapinduzi

katika Mwongozo wa 1981.

Mwongozo wa CCM, 1981

Kipindi cha mwisho cha Mwalimu Nyerere (1980-85) kilikuwa kigumu

kuliko vyote katika utawala wake. Hali ya uchumi ilidorora kutokana na

sababu mbalimbali za ndani na nje, pamoja na vita vya Uganda, ambavyo

viliigharimu nchi sana; kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na

kupanda kwa bei za petroli. Mnamo 1981, Chama tawala, wakati huo CCM,

kilifanya tathmini ya miaka 14 ya Azimio la Arusha na kiliainisha hali halisiya siasa, jamii na uchumi. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Chama kufanya

uchambuzi wa kina bila ya kujali maslahi yake ya muda mfupi.

Kwa maoni yangu, hoja ambayo ni nzito katika uchambuzi huo ni kwamba

chini ya mwavuli wa Azimio la Arusha na sekta ya umma, hususan

mashirika ya “umma”, lilijengeka tabaka jipya la mabepari. Mwongozo 

unasema:

Kwani ukweli unaojitokeza wazi wazi ni kuwa baadhi

ya matatizo yetu ya uchumi yanatokana na kutotekeleza

kwa dhati siasa ya Ujamaa na Kujitegemea vijijini na

katika sekta ya umma tuliyoianzisha. Zaidi ya hivyo,

wakati mwingine katika miaka kumi na minne tangu

Azimio la Arusha, Chama, Serikali, na vyombo vyake

vilitumika kukuza sekta ya kibepari nchini katika

viwanda, biashara, usairishaji, ujenzi na kadhalika na

ubepari huo uliopanuka katika kipindi hiki umeimarisha

vitendo vya kuivuruga na kuidhooisha sekta yetu ya

Umaa (ib. 35).

Sehemu nyingine, Mwongozo unaendelea kueleza kwa ufasaha mkubwa

kwamba:

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 138/142

MIONGOZO MIWILI 137

Leo ubepari una vishawishi vingi zaidi nchini kuliko

ulivyokuwa kabla ya Azimio la Arusha kwa sababu

pamoja na kwamba sasa tuna sekta kubwa ya umma

lakini kutokana na udhaifu wa kutopambana nao,ubepari umefaulu kujipanua na kujipenyeza hata ndani

ya sekta yenyewe ya umma. Na ndio maana ubepari sasa

unathubutu kujitokeza hadharani kuukashifu Ujamaa,

kubabaisha baadhi ya viongozi na kututaka tubadilishe

siasa yetu (ib. 52).

Kwa hakika matamko haya yalikuwa ni kukiri wazi wazi kwamba sera

za Ujamaa zilikuwa zimehujumiwa na viongozi wenyewe waliopewajukumu la kuongoza ujenzi wa Ujamaa kutokana na maslahi yao ya

kitabaka ya kibepari.

Hapa tunashuhudia kwa mara ya kwanza, Chama kikikiri kwamba kuna

mapambano au harakati za kitabaka dhana ambayo kila mara Chama, na

hasa Mwalimu mwenyewe, alikuwa anaikanusha. Kinadharia na kiitikadi

Mwalimu hakukubaliana kabisa na dhana ya mapambano ya kitabaka.

Hata hivyo ibara ya 50 ya Mwongozo  inaenda mbali zaidi kwa kuelezakwamba:

Kuielewa vema jamii ya Tanzania ya leo kunataka

uchambuzi wa hali ya juu pia. Uchambuzi huu

ukiwezeshe Chama kuielewa migongano ya maslahi ya

tabaka ambayo imejitokeza nchini. Migongano hii ina

mizizi katika mgongano wa msingi kati ya Ujamaa na

ubepari, kati ya maslahi ya wakulima na wafanyakazi

kwa upande mmoja, na ya ubinafsi, ubwanyenye na

ubepari ambao umekuwa ukijengeka tangu Azimio la

Arusha kwa upande mwingine.

Uchambuzi huo ni wazi na umefanywa kwa ufasaha na kisayansi. Swali

muhimu kwa wasomi, wanazuoni na wakereketwa wa Usoshalisti ni:

Je, Chama kilifanikiwa katika mapambano haya na kurudisha nchi

kwenye Ujamaa? Au tabaka hili liliojengeka lilishinda mapambano na

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 139/142

MIONGOZO MIWILI138

ndilo injini inayosukuma gurudumu la mageuzi ya kisiasa na kiuchumi

kuelekea kwenye uliberali mamboleo, ambao ni mfumo wa kibepari?

Je, tabaka hilo la mabepari warasimu ndilo hasa chimbuko la mfumo

huo wa ubepari uchwara, ukiungwa mkono na ubeberu, na ambao ndiounatutawala leo? Je, si kweli kwamba, katika awamu hasa ya tatu tabaka

hili la mabepari warasimu ndilo lililokuwa mstari wa mbele kutetea

ubepari wakimnukuu kwa furaha Deng Tsio-Ping, kiongozi wa China,

aliyepindua ujamaa nchini China?

Katika mahojiano yake na mwandishi wa habari Jonathan Power wa

jarida la Prospect   (na. 112, Julai 2005), Rais mstaafu Benjamin Mkapa

alikiri kwamba yeye alikuwa anamheshimu Deng Tsio-Ping. Alipoulizwana Jonathan Power kwamba je, Nyerere akifufuka angesemaje, Mkapa

akamjibu: ‘Angesema kwamba mimi nimegawia mengi yaliyokuwa

katika sekta ya umma. Na angefadhaishwa na ukweli kwamba mimi

nimefanikiwa kujenga tabaka la mabepari matajiri.’

Sina hakika kama Rais Mkapa alifanikiwa kujenga tabaka la mabepari

matajiri au alijenga tabaka la vibepari uchwara tu. Ni suala la kutaiti.

Haikuwa nia yangu kuangalia suala hili kwa undani bali ni kudokeza tukwamba kama tunataka kuelewa vema na kisayansi hali halisi ya nchi

na jamii yetu ya leo hatuna budi kufanya uchambuzi wa kitabaka katika

mfumo wa ubepari uchwara chini ya utawala wa kibeberu, hususan,

tabaka lililoongoza mageuzi. Na hoja yangu ni kwamba Mwongozo wa

CCM wa 1981 unatuweka mahali pazuri pa kuanzia. Kazi kwetu!

Ni jukumu la wasomi na wanazuoni kuchambua jamii yao, kuonyesha

jamii sura yake halisi na kuainisha mielekeo ya maendeleo na mielekeo

ya wapingamendeleo. Kama Mwongozo wa 1981 unasema : mapinduzi

sio lelemama. Mapinduzi yanahitaji wakereketwa wa kijamii ambao

msimamo wao kwa upande wa wavujajasho hautetereki:

Ujenzi wa ujamaa si lelemama bali ni mapambano,

mapambano ya kudumu dhidi ya ubepari na unyonyaji,

dhidi ya wapinga maendeleo na wababaishaji wa

kisiasa, dhidi ya wahujumu uchumi, majambazi,

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 140/142

MIONGOZO MIWILI 139

wezi, wazururaji na wazembe. Msimamo sahihi wa

mapambano unaotokana na nadharia sahihi ya ujamaa

ungelituepusha na maamuzi na vitendo ambavyo

vimerahisisha kuoteshwa kwa mizizi ya ubepari,kinyume cha msimamo wa mapambano dhidi ya

ubepari. Leo ubepari, una vishawishi vingi zaidi nchini

kuliko ulivyokuwa kabla ya Azimio la Arusha kwa

sababu pamoja na kwamba sasa tuna sekta kubwa ya

umma lakini kutokana na udhaifu wa kutopambana nao,

ubepari umefaulu kujipanua na kujipenyeza hata ndani

ya sekta yenyewe ya Umma. Na ndiyo maana ubepari sasa

unathubutu kujitokeza hadharani kuukashifu ujamaa,

kubabaisha baadhi ya viongozi na kututaka tubadilishe

siasa yetu. (ibara ya 52)

Ukweli uliojitokeza tangu uchambuzi huo wa Mwongozo wa 1981, ni

kwamba ubepari ukisimamiwa na vibepari uchwara wa ndani na nchi

za kibeberu (ambao siku hizi wanaitwa eti wabia wetu wa maedeleo)

ukashinda katika mapambano. Chini ya visingizio mbalimbali, pamoja

na ikra haifu ya “kwenda na wakati”, Azimio likapinduliwa na uliberali

mambo-leo ukashinda.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 141/142

MIONGOZO MIWILI140

Marejeo

Mapolu, Henry. (mh.), (1976), Workers and Management, Dar es Salaam,

Tanzania Publishing House.

Mapolu, Henry na Issa Shivji. (1984), Vuguvugu la Wafanyakazi Nchini

Tanzania, Kampala, Urban Rural Mission.

Mihyo, P. (1975), ‘The Struggle for Workers Control in Tanzania’, Review

of African Political Economy, No.4.

Shivji, Issa G. (1976), Class Struggles in Tanzania, Dar es Salaam, London

& New York, Tanzania Publishing House, Heinemaan and

Monthly Review.

Shivji, Issa G., (1970), Tanzania : The Silent Class Struggle (Cheche 1970)

na kuchapishwa tena katika Issa G. Shivji (mh.) na wengine : The

Silent Class Struggle, ( 1972), Tanzania Publishing House.

7/26/2019 Kupaa Na Kutunguliwa Kwa Azimio La Arusha

http://slidepdf.com/reader/full/kupaa-na-kutunguliwa-kwa-azimio-la-arusha 142/142