LUAMBANO-BRN

  • Upload
    ilala

  • View
    466

  • Download
    0

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Tangazo la ukusanyaji takwimu

Citation preview

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

TANGAZO LA UKUSANYAJI WA TAKWIMUMkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala anawatangazia Wananchi, Wafanyabiashara na wamiliki wa nyumba na majengo katika Manispaa ya Ilala kwamba, Manispaa inaendelea na zoezi la kukusanya takwimu za Wakazi pamoja na walipa kodi wa Manispaa kwa lengo la kupata taarifa na takwimu sahihi za wakazi, wamiliki wa majengo na Wafanyabiashara ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ili kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi wetu. Zoezi la ukusanyaji wa takwimu na taarifa linafanywa na Watumishi wa Manispaa pamoja na wasaidizi wao kwa kupita katika maeneo yote kukagua na kuuliza maswali kuhusu taarifa zinazohusu:1. Jina kamili la mmiliki wa jengo2. Stakabadhi za malipo ya Kodi ya Majengo yaliyofanyika kwa mara ya mwisho kama zipo3. Makadirio ya malipo yaliyofanywa na Manispaa kama yapo. Pamoja na zoezi hili shughuli zote za kukusanya mapato, ulipaji wa tozo mbalimbali na ukataji wa leseni za biashara zitaendelea kama kawaida.Ifahamike kwamba kumzuia Afisa yoyote wa Serikali kutekeleza wajibu wake ni kosa kisheria na Halmashauri haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria Mtu yoyote au kikundi cha Watu wakatao kwamisha kwa namna moja ua nyingine zoezi hii la ukusanyaji wa takwimu na taarifa.Limetolewa na;Isaya M. MngurumiMKURUGENZI WA MANISPAAHALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA