6
NGANU ZA UTUMWA NA GHALA ZA MADAWA KWA KIMOTO - Turudi kwenye Mapango ya Madawa na Mkataba wa Ujirani Mwema. Na Aretas Ghassany Nilishtuka nilipoisoma makala ”Racial Violence, Universal History, and Echoes of Abolition in Twentieth-Century Zanzibar” ya mtafiti mahiri wa Kimarekani, Profesa Jonathon Glassman wa Northwestern University. Makala hiyo imechapishwa katika kitabu kiitwacho Abolitionism and Imperialism in Britain, Africa, and the Atlantic, ambacho kimehaririwa na Derek R. Peterson na kuchapishwa na Ohio University Press, mwaka 2010. Kwenye makala yake, Glassman ameandika yafuatayo ambayo nayafasiri hapa kwa lugha ya Kiswahili: “Mzunguko wa soko la watumwa [la Zanzibar] haukamiliki bila ya kuyatembelea “mapango ya watumwa” yenye sifa mbovu kabisa, ambayo ni vyumba viwili vyenye masafa mafupi baina ya dari na ardhi chini ya jengo la Bweni la Mtakatifu Monica, ambalo ni jumba kubwa pembezoni mwa kanisa. Hapa ndipo mahala penye kuzidhihirisha hadithi za waongoza misafara ya watalii zilizojaa jazba na hasira. Watumwa mia au zaidi, wanasema waongozaji watalii, wakikusanywa usiku ndani ya mapango hayo na walifanywa walale juu ya mabaraza yaliokuwa karibu na kuta. (Mabaraza hayo yamepambwa kwa pingu na minyororo). Watalii wanaambiwa kuwa wengi kati ya watumwa walikufa kwa kukosa pumzi kutokana na msongamano, na hao kidogo walioweza kuishi, kama wale walioweza kuishi baada ya kupigwa mikwaju ya kila siku pale kwenye sehemu ya ndani ya kanisa penye meza panapotolewa kafara, hudhihirisha uzima wao na kuuzwa kwa wateja.” “Hadithi hizi na nyenginezo zisizoonekana kuwa ni za kweli kuhusu soko la watumwa la Zanzibar huwa zinarudiwa mara kwa mara na kuiarifu dunia bila ya kuhojiwa, wakiwemo wasomi ambao wanapaswa kuwa wameilimika zaidi, na ambao walishiriki vizuri tu katika sherehe rasmi za Kanisa la Angilikani za miaka mia mbili za Kitendo cha Kuusimamisha Utumwa. Hizo hadithi pia zinasisitiza ukatili uliokuwa ukifanyika katika soko la watumwa; zenye kunoga zaidi zinasema vipi watoto wa watumwa walivokuwa wakiuliwa ovyoovyo, koo zao zikichinjwa pale penye kanisa la leo penye kuwekwa birika la kubatizia. Pia wanasisitiza juu ya ukongwe wa hilo soko [la watumwa]. Inasemwa kuwa watumwa wakiuzwa hapo kwa makarne na inafika hata miaka elfu moja. Juu ya yote, hadithi zinasisitiza ukabila wa maonevu, wenye kununua na kuuza watumwa wanaitwa ni Waarabu na wenye kuonewa ni watu weusi au Waafrika” “Kwa uhahika hakuna hata hadithi moja kati ya hizi ambayo ni ya kweli. Zile zenye kuchukiza zaidi ni wazi kuwa haziingii akilini: ni kinyume na mantiki kufikiria wafanya biashara kuzivuruga mali zao kwa namna hii. (Kwanini watalii kutoka nchi za Magharibi wako tayari kuamini hadithi za kusadikika za aina hii ni suala ambalo nitalizungumzia sehemu nyengine).

Mapango Ya Uongo Na Sumu Ya Ukoloni

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Makala ya mwanazuoni mwenye asili ya Zanzibar kuhusu Muungano na kirusi kinachoutatiza Muungano huo wa Tanganyika na Zanzibar, uliozaa Tanzania

Citation preview

Page 1: Mapango Ya Uongo Na Sumu Ya Ukoloni

NGANU ZA UTUMWA NA GHALA ZA MADAWA KWA KIMOTO - Turudi kwenye Mapango ya Madawa na Mkataba wa Ujirani Mwema.

Na Aretas Ghassany Nilishtuka nilipoisoma makala ”Racial Violence, Universal History, and Echoes of Abolition in Twentieth-Century Zanzibar” ya mtafiti mahiri wa Kimarekani, Profesa Jonathon Glassman wa Northwestern University. Makala hiyo imechapishwa katika kitabu kiitwacho Abolitionism and Imperialism in Britain, Africa, and the Atlantic, ambacho kimehaririwa na Derek R. Peterson na kuchapishwa na Ohio University Press, mwaka 2010. Kwenye makala yake, Glassman ameandika yafuatayo ambayo nayafasiri hapa kwa lugha ya Kiswahili: “Mzunguko wa soko la watumwa [la Zanzibar] haukamiliki bila ya kuyatembelea “mapango ya watumwa” yenye sifa mbovu kabisa, ambayo ni vyumba viwili vyenye masafa mafupi baina ya dari na ardhi chini ya jengo la Bweni la Mtakatifu Monica, ambalo ni jumba kubwa pembezoni mwa kanisa. Hapa ndipo mahala penye kuzidhihirisha hadithi za waongoza misafara ya watalii zilizojaa jazba na hasira. Watumwa mia au zaidi, wanasema waongozaji watalii, wakikusanywa usiku ndani ya mapango hayo na walifanywa walale juu ya mabaraza yaliokuwa karibu na kuta. (Mabaraza hayo yamepambwa kwa pingu na minyororo). Watalii wanaambiwa kuwa wengi kati ya watumwa walikufa kwa kukosa pumzi kutokana na msongamano, na hao kidogo walioweza kuishi, kama wale walioweza kuishi baada ya kupigwa mikwaju ya kila siku pale kwenye sehemu ya ndani ya kanisa penye meza panapotolewa kafara, hudhihirisha uzima wao na kuuzwa kwa wateja.” “Hadithi hizi na nyenginezo zisizoonekana kuwa ni za kweli kuhusu soko la watumwa la Zanzibar huwa zinarudiwa mara kwa mara na kuiarifu dunia bila ya kuhojiwa, wakiwemo wasomi ambao wanapaswa kuwa wameilimika zaidi, na ambao walishiriki vizuri tu katika sherehe rasmi za Kanisa la Angilikani za miaka mia mbili za Kitendo cha Kuusimamisha Utumwa. Hizo hadithi pia zinasisitiza ukatili uliokuwa ukifanyika katika soko la watumwa; zenye kunoga zaidi zinasema vipi watoto wa watumwa walivokuwa wakiuliwa ovyoovyo, koo zao zikichinjwa pale penye kanisa la leo penye kuwekwa birika la kubatizia. Pia wanasisitiza juu ya ukongwe wa hilo soko [la watumwa]. Inasemwa kuwa watumwa wakiuzwa hapo kwa makarne na inafika hata miaka elfu moja. Juu ya yote, hadithi zinasisitiza ukabila wa maonevu, wenye kununua na kuuza watumwa wanaitwa ni Waarabu na wenye kuonewa ni watu weusi au Waafrika” “Kwa uhahika hakuna hata hadithi moja kati ya hizi ambayo ni ya kweli. Zile zenye kuchukiza zaidi ni wazi kuwa haziingii akilini: ni kinyume na mantiki kufikiria wafanya biashara kuzivuruga mali zao kwa namna hii. (Kwanini watalii kutoka nchi za Magharibi wako tayari kuamini hadithi za kusadikika za aina hii ni suala ambalo nitalizungumzia sehemu nyengine).

Page 2: Mapango Ya Uongo Na Sumu Ya Ukoloni

Jengo ambalo lina mapango ya watumwa lilijengwa na mamishionari wenyewe kama ni hospitali, miaka ishirini baada ya soko la utumwa kufungwa. Mabaraza ya saruji yalioko chini ya jengo ni wazi yalikuwa ni sehemu ya kuwekea vitu ili visipate maji, na hapana shaka yalikuwa ni kwa ajili ya kuwekea dawa. Hata maelezo ambayo yanaweza kuaminika hayawezi kuhakikiwa. Ukongwe wa soko la watumwa limetiwa chumvi kupita kiasi: biashara ya utumwa yenye upana mkubwa ilikuwa sehemu ya uchumi wa Zanzibar kwa vizazi viwili au vitatu tu, na wala si kwa makarne, na ukweli ni soko la utumwa la Mkunazini lilikuwepo kwa muda wa miongo michache tu kabla ya kufungwa.” “Sehemu kubwa ya upotoshaji wa hizo hadithi na makusudio ni maumbile ya utumwa uliofanyika Zanzibar, na khasa, kama tutakavoona hapa chini, ukabila wa huo utumwa: ni upotoshaji mkubwa kudai kuwa wenye kumiliki na wafanyabiashara wakubwa wa utumwa walikuwa ni Waarabu.” Mshituko wangu baada ya kumsoma Jonathan Glassman ukanitia hima ya kwenda kuzitafuta rejea za Central Africa: A Monthly Record of the Work of the Universities’ Mission to Central Africa ili nijionee mwenyewe kilichoandikwa badala ya kuitegemea tafsiri sahihi ya mwandishi/mtafiti Glassman. Nilikwenda Library of Congress ya Washington DC kuzitafuta hizo rejea lakini kwa bahati mbaya walikuwa hawanazo. Nikawasiliana na mwanafunzi mmoja ambaye anafanya shahada ya PhD Chuo Kikuu cha Georgetown. Baada ya kama wiki moja tu akanipatia rejea kutoka Chuo Kikuu cha Yale, kutoka maktaba ya Yale Divinity School. Mshituko mwengine! Wakristo walioijenga hospitali mpya ya pale Mkunazini Unguja karibu na Kanisa la Kianglikani walikuwa ni wakweli na hawa walioko hivi sasa pamoja na Waislam wanaowatembeza watalii ya ima hawaifahamu fitina wanayoieneza ndani na nje ya Zanzibar, au ni wapotoshaji wa makusudi ambao wanapaswa kuonywa kwa mujibu wa Sheria za Zanzibar. Na iwapo hawakujitengeza ni wa kufunguliwa mashtaka ya kuifitinisha jamii na kujenga chuki baina ya Wazanzibari Waislam wenyewe kwa wenyewe, na baina ya Wazanzibari Waislam na Wakristo popote pale walipo, na kuliharibu jina la Zanzibar duniani. Hii hapa tafsiri ya haraka kwa lugha ya Kiswahili ya yale walioyaandika mamishionari wenyewe juu ya hospitali mpya iliokaribu na Kanisa la Anglikan, Mkunazini, Unguja, ambayo hivi sasa inatangazwa ndani na nje ya Zanzibar kuwa ni “mapango ya watumwa”: Dondoo zifuatazo zinatoka kwenye makala “The New Hospital in Zanzibar,” Central Africa: A Monthly Record of the Work of the Universities’ Mission to Central Africa, Edited by the Reverend R. M. Heanley, Vol. IX, 1891, London: “Jiwe la msingi liliwekwa na Bishop kabla ya kuondoka kwenda Nyasa, na kwa vile hospitali ilikusudiwa kwa ajili ya matumizi ya Wazungu wenye kuishi mjini pamoja na wenyeji, Wazungu ndio walioalikwa khasa wahudhurie na kuwa sehemu ya hiyo hafla. Kwa hiyo waliombwa wakutane kanisani mnano saa kumi za jioni, na baada ya ibada, kwenda kwenye Nyumba ya Mkunazini kwa ajili ya kunywa chai.

Page 3: Mapango Ya Uongo Na Sumu Ya Ukoloni

Takriban wote walioalikwa walihudhuria, pamoja na mabalozi wa nchi za nje. Ni wachache tu ambao hawakuhudhuria kutokana na ama kuumwa au jambo jengine la dharura. Sehemu zote vilipambwa vitambaa vya rangi, na bendera zilitolewa na Captain Henderson wa meli iitwayo Conquest, ambaye kwa wema wake aliwaachia mabaharia wake wazitundike na kusaidia katika kupamba. Siku nyingi kabla kulikuwa na mvua kali na kulikuwa na shaka ya kupatikana hali ya hewa nzuri katika tukio kama hili. Hata hivyo, wakati ulipofika mvua ilisita na kila kitu kilikwenda vizuri. Ibada ziligawiwa sehemu mbili, ya kwanza ilifanyika kwenye kanisa liliopo karibu. Kwaya zote mbili, ya Kiengereza na ya kienyeji, zilikuwa tayari, na muziki wa maandalizi ulikuwa mzuri sana. Ulifanywa mstari wa watu kutoka kwenye kanisa mpaka kwenye kipande cha ardhi kitakachojengewa Hospitali, ambacho kipo nyuma tu ya nyumba ya kutowa dawa ya hivi sasa ambayo madirisha take yanatazamana na soko la zamani la watumwa. Kila upande wa pembe nne...Zina majengo maalumu; kaskazini lipo kanisa, kusini ipo Nyumba, magharibi ipo nyumba ya kutoa dawa, na mashariki ipo Nyumba ya Ufundi ya Watoto Wanaume. ”Alipofika kwenye sehemu itakayojengwa Hospital, Bishop aliomba dua: ”Ewe Mungu mwenye nguvu na mwenye kudumu milele, kwa rehema zako libariki jiwe hili, ambalo tuko tayari kuliweka kwa ajili ya msingi kwa Jina la Yule Ambaye ni Jiwe lililojaribiwa na lenye thamani; na utupe wale ambao wataiendeleza hii kazi, ambao watajitolea nafsi zao Kwako, na daima wahifadhike kimwili na kiroho. Kupitia Yesu Kristo Bwana wetu. Amin.” ”Na baadae, kwa kufanya alama ya msaraba, akalibariki jiwe kwa maneno haya: ”Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amin. Na tuombe. ”Ewe Mola, Libariki hili jiwe, na jaalia kwa ombi la Jina Lako Tukufu, yoyote atakayesaidia kiuchaji Mungu katika kuisimamisha nyumba hii, apate afya ya kiwiliwili na ya kiroho. Kupitia Yesu Kristo Bwana wetu. Amin. ”Dongo lilipokuwa tayari kwaya ikaimba aya kutoka Zaburi, ”Ni Mola tu alieijenga nyumba,” na kwa kumalizia Bishop aliliweka jiwe mahala pake, na kusema: ”Kwa Yesu Kristo tunaliweka jiwe hili ndani ya msingi, kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, kuwa imani ya kweli, khofu ya Mungu, na mapenzi ya kidugu yaishi, na pahala hapa patengwe kwa ajili ya kuwapa shifaa wenye kuumwa na kwa kuwaliwaza wenye kusibika, na kwa sharaf ya Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Ambaye aliishi na kutawala pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, na ulimwengu usiokuwa na mwisho. Amin.... ”Katika hotuba yake Bishop alisema maneno yafuatao ambayo tunayatoa kwa kutarajia yatawaamsha watakaoyasoma ili waisaidie kazi hii. Ni jambo lililo wazi kuwa hii ni kazi ya kimishionari, na kwa hakika tutatafuta msaada wa lazima kutoka kwa marafiki zetu wa Ulaya ili kuikamilisha.

Page 4: Mapango Ya Uongo Na Sumu Ya Ukoloni

Tayari kuta za jengo zinaanza kusimama na kabla ya mwaka mmoja kumalizika tunatarajia kupata habari za sherehe za ufunguzi. Matukio ya karibuni yanaonyesha umuhimu wa dharura wa kuwa na hospitali ya kawaida Zanzibar, yenye uwezo wa kupokea wagonjwa thalathini mpaka arubaini, na tunaamini msaada mkubwa utakuja kama ni utambulisho wa juhudi zinazofanywa kukamilisha si mahitajio ya wenyeji tu bali idadi yenye kuongezeka ya jamii ya Kizungu yenye kuishi Zanzibar.... ”Sehemu ya hotuba ya Bishop alipoliweka jiwe la msingi la Hospitali ya Zanzibar, May 12, 1891.... ”Kwa muda mrefu tulifikiria kujenga hospitali, lakini nilihisi itakuwa ni dhamana kubwa kuweka kundi la manasi kutoka nchi yetu. Lakini hivi sasa wanawake wenye umahiri na uzowefu wa muda mrefu wamejitolea kufanya kazi katika Misheni yetu, na wamenihakikishia kwa ushawishi walionao Uingereza tutaweza kuwapata wafanyakazi tunaowahitajia, na wana tamaa pia sehemu kubwa ya fedha zinazohitajika zitaweza kukusanywa.... ”Tunapendekeza ziwepo wodi mbili ghorofa ya usawa na ardhi, na juu viwepo vyumba kadhaa vyenye kitanda kimoja kwa ajili ya Wazungu.” Jarida la Central Africa: A Monthly Record of the Work of the Universities’ Mission to Central Africa, Edited by the Reverend R. M. Heanley, Vol. Xi la mwaka 1893 linatoa taarifa ya kufunguliwa hospitali. “…Jumapili iliopita…palifanyika Ibada maalumu ya Kuomba Kheri kanisani kwa mnasaba wa kufunguliwa hospitali ya Mkunazini ambayo imechukuwa miezi kumi na nane kujengwa.” Msomaji inakupasa uzingatie kuwa dondoo zote za hapo juu zinaonyesha wazi kuwa jengo liliopo Zanzibar hii leo pale Mkunazini karibu ya kanisa la Anglikan ambalo linajulikana na Wazanzibari na walimwengu kwa ujumla, ni jengo ambalo lilijengwa na Mamishionari waliofanya “mstari wa watu kutoka kwenye kanisa mpaka kwenye kipande cha ardhi kitakachojengewa Hospitali.” Madhumuni ya hii makala ni kuwaamsha Waislam na Wakristo wafahamu kuwa Wakristo walioijenga hospitali yenye vyumba vya kuwekea madawa hawajapatapo kusema kwamba vyumba hivyo vilikuwepo kwenye kipande cha ardhi kilichojengewa hospitali kwa ajili ya kuwekewa watumwa. Wazanzibari tunauliwa duniani kwa uwongo na tumefanywa mahabusi tunaoshindwa kujitetea kila Zanzibar inapotajwa kuwa ilikuwa ni kituo kikubwa cha utumwa Afrika Mashariki na ushahidi mkubwa wa hilo ni “mapango ya kuwekea watumwa” pale Mkunazini kunako Kanisa la Anglikan. Tunataka viongozi watakaotutoa kwenye “mapango ya kuekea watumwa” na kuturudisha kwenye vyumba vya kuwekea madawa! Tunataka uongozi na viongozi watakaotutoa kutoka kwenye Muungano usiokuwa na nchi na kuturudishia Jamhuri ya Watu wa Zanzibar itakayoongozwa na Katiba ya Zanzibar na Mkataba baina yake na Tanzania Bara/Tanganyika.

Page 5: Mapango Ya Uongo Na Sumu Ya Ukoloni

Waislamu, Wakristo, na Mayahudi, wote wanaamini kuwepo kwa Masih Dajjal (Antichrist) ambaye atakuja kuwadanganya waumini kuwa yeye ndie Nabii Issa mtoto wa Bibi Maryam (rehema za Allah ziwe juu yao). Kwa hiyo si ajabu kuwaona wafuasi wa Dajjal wakieneza uwongo pale kwa Kimoto kwa kulitumia jina la Nabii Issa!

Fitina zinaenezwa kwa njia ya kuuficha ukweli/ushahidi wa mamishionari wa Kizungu, na baadae wa Profesa Glassman, kuwa yale yenye kuitwa “mapango ya watumwa” vilikuwa ni vyumba vya chini ya ardhi ambavyo vilikuwa ni sehemu ya hospitali.

Fitina kubwa ZAIDI ya upotoshaji wa yenye kuitwa “mapango ya watumwa” ni pale unapounganishwa upotoshaji huo na Uislam ambayo ilikuwa dini ya hao Waarabu na Ukristo wa Wazungu ambao unasemwa na kuonyeshwa hapo kwa Kimoto kuwa ndio uliokuja kumkomboa Muafrika kutokana na utumwa wa Mwarabu Muislam!

Hapo ndipo palipojengwa uwongo uliozaa watoto wa chuki dhidi ya watu wa dini fulani na kuwafanya watu wa dini fulani (Wazungu Wakristo) kuwa ndio watu wema na Waarabu/Waislam na waliokaribu nao ambao ni Waafrika Waislam ni watu waovu kabisa duniani.

Uislamu usingeliimarika ingelikuwa Mtume Muhammad (sala na salamu za Allah zimshukie) asingeliwapeleka wale Waislam wachache Ethiopia na kupokelewa na Mfalme (Al-Najashi) wa Kikristo, Ashama ibn Abjar.

Upotoshaji wa historia ya mapango ya madawa kuna siku utaondolewa na Wazanzibari wenyewe, lakini kabla ya hapo utaoendelea kutetewa kwa sababu ya pato la pesa wanalolipata Kanisa kutokana na biashara haramu wanayowauzia watalii ya “mapango ya kuwekea watumwa!”

Uendelezaji wa biashara ya fitina haunistaajabishi hata kidogo kwani ni dhahiri kuwa kuna upungufu wa fedha na ndio maana unatangazwa mchango kupitia tovuti ifuatayo:

http://www.zanzibarfriends.org/

Jua kuwa yale ya Waislam wa mwanzo na Mfalme Mkristo wa Ethiopia aliyewapokea kwa mikono miwili ndiyo yatakayokuja kuwaunganisha Waafrika Waislam na Waafrika Wakristo.

Nabii Issa na Nabii Muhammad (sala na salamu za Allah ziwashukie wote wawili) ni ndugu na ni wa dini moja.

Wafuasi wao wenye kuongozwa na ukweli kamwe hawatotumbukizwa ndani ya mapango ya uwongo bali wataishi ndani ya majumba ya ukweli yaliosimama juu ya majabali ni si juu ya madongo poromoka ya fitina na uzushi.

“Na mtaujuwa ukweli na ukweli utawaweka huru.” Biblia Yohane 8:32.

Mara ngapi tumeshasikia kuwa “ukweli ukidhihiri uwongo hujitenga” lakini fikiria nafsi ngapi za Wazanzibari na wasiokuwa Wazanzibari, Waislam kwa Wakristo, waliojazwa chuki kutokana na uwongo huu. Mamishionari wenyewe waliolijenga jengo la hospitali lenye vyumba vya kuwekea madawa hawakupata kueneza uwongo wa namna hii. Suala ni ilikuwaje uzushi wa fitna kali ya namna hii ukaweza kuenezwa Zanzibar na nje Zanzibar kabla na baada ya Muungano wa 1964 wakati ukweli wa mamishionari uko wazi kama jua la mchana? Nani wa kulaumiwa?

Page 6: Mapango Ya Uongo Na Sumu Ya Ukoloni

Wazanzibari wenyewe walio Waislam na Wakristo kwa kuzembea uwongo wa namna hii au uvivu wa wasomi na walimu wa Kizanzibari kuuwachia uendelee bila ya kuuhoji? Hayo yalifanywa nusu karne iliopita na yamewakosesha vijana ilimu iliosimama juu ya ukweli, imewafutia historia yao, na kwa baadhi yao, hata kuwaulia utu wao. Vyumba vya kuhifadhia madawa vimegeuzwa kuwa mapango ya watumwa. Hivi juzi tu nimesikia kuwa Mzee Abuu wa Shauri Moyo amemuuliza Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar: "Tanganyika haipo, na Zanzibar si nchi, sasa tukiwa tunajadiliana rasimu ya katiba huwa tunajadiliana na nani?" Masih Dajjal (Antichrist) na wasaidizi wake wamevibadilisha vyumba vya madawa na kuvifanya mapango ya kuwekea watumwa. Nchi mbili huru zilizoungana na ambazo hazipo wanazitengenezea Katiba ya nyumba ya buibui na wasaidizi wake wanakwenda mbio kuujenga msingi juu ya kilima cha mchanga.

Wazanzibari hivi sasa wameamka na hawataki tena porojo la kudanganywa na wanasiasa, wanasheria au wasomi. Wanataka viongozi wa kuwafikisha pale wanapotaka wao kwenda sio wanapotaka wajenzi wa nyumba ya buibui.

Mwanzo wanasiasa walielewa kwamba vijana walikuwa hawajui nini wanataka kwa hiyo wakawatumilia vile wanavyotaka wao lakini sasa hakuna wa kumdanganya tena Zanzibar. Kila Mzanzibari anajua nini anataka kwa hiyo tunachohitaji ni viongozi madhubuti wenye uzalendo wa kweli watufikishe kwenye Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo itajulikana ndani na nje ya Afrika Mashariki, na si vyenginevyo.

Harith Ghassany

Makala hii nimeileta kwa Hisani ya Muandishi ili vizazi visome viujue ukweli na viwache kupotoshwa na kutiwa sumu na kuja kuingia katika ile kauli ya Mabepari na Mabeberu :" Tenga utawale " . Wazanzibari na Watanganyika , Waislamu na Wakristo wakae wasome na waujue ukweli wa Historia ya nchi yao na kutokomeza fitina na sumu zinazopachikwa za kidini na makabila na kutoa mwanya wa Mataifa ya Kibwanyenye kuzidi kututawala ikiwa ni Ukoloni Mamboleo tuliokuwa nao hivi sasa.

Ndugu yenu : Abdulaziz El Shuwehdy