38
1 MASHARTI YA CHAMA JEDWALI LA YALIYOMO SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI Kifungu cha 1: Jina Kifungu cha 2: Tafsiri SEHEMU YA PILI: MASHARTI, JINA LA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO, MAKAO MAKUU NA ANUANI, ENEO LA MFUNGAMANO WA UANACHAMA. Kifungu cha 3: Masharti Kifungu cha 4: Jina la Chama Kifungu cha 5: Usajili Kifungu cha 6: Makao Makuu na anuani Kifungu cha 7: Eneo la shughuli Kifungu cha 8: Mfungamano wa pamoja na uanachama Kifungu cha 9: Maadili ya uanachama Kifungu cha 10: Misingi ya Ushirika Kifungu cha 11: Uanachama wa Chama na ukwasi SEHEMU YA TATU: MAONO, UJUMBE, MALENGO NA MADHUMUNI YA CHAMA. Kifungu cha 12: Maono, Ujumbe na Malengo Kifungu cha 13: Madhumuni Kifungu cha 14: Makosa na adhabu kwa ukiukaji wa Sheria, Kanuni na Masharti ya Chama SEHEMU YA NNE: UANACHAMA Kifungu cha 15: Sifa za kujiunga na Chama. Kifungu cha 16: Utaratibu wa kujiunga na Chama Kifungu cha 17: Huduma zinazotolewa kwa Wanachama Kifungu cha 18: Malipo ya huduma Kifungu cha 19: Kupoteza hadhi ya uanachama Kifungu cha 20: Kujiuzulu uanachama Kifungu cha 21: Ishia ya uanachama Kifungu cha 22: Misingi ya kusimamishwa uanachama Kifungu cha 23: Utaratibu wa kumsimamisha mwanachama Kifungu cha 24: Utekelezaji wa kusimamishwa na/au kuondolewa uanachama Kifungu cha 25: Athari za kusimamishwa na kuondolewa uanachama Kifungu cha 26: Utaratibu wa malipo kwa mwanachama aliyejitoa na/au aliyeishia. Kifungu cha 27: Kudaiwa mwanachama Kifungu cha 28: Kuteua mrithi wa mali za mwanachama Kifungu cha 29: Haki za mwanachama Kifungu cha 30: Wajibu wa mwanachama Kifungu cha 31: Wajibu wa Chama SEHEMU YA TANO: MTAJI WA CHAMA Kifungu cha 32: Mjengeko na sura ya hisa na mtaji wa Chama Kifungu cha 33: Kuongezeka au kupungua mtaji

MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

  • Upload
    others

  • View
    8

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

1

MASHARTI YA CHAMA JEDWALI LA YALIYOMO SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI Kifungu cha 1: Jina Kifungu cha 2: Tafsiri SEHEMU YA PILI: MASHARTI, JINA LA USHIRIKA WA AKIBA

NA MIKOPO, MAKAO MAKUU NA ANUANI, ENEO LA MFUNGAMANO WA UANACHAMA.

Kifungu cha 3: Masharti Kifungu cha 4: Jina la Chama Kifungu cha 5: Usajili Kifungu cha 6: Makao Makuu na anuani Kifungu cha 7: Eneo la shughuli Kifungu cha 8: Mfungamano wa pamoja na uanachama Kifungu cha 9: Maadili ya uanachama Kifungu cha 10: Misingi ya Ushirika Kifungu cha 11: Uanachama wa Chama na ukwasi SEHEMU YA TATU: MAONO, UJUMBE, MALENGO NA MADHUMUNI YA

CHAMA. Kifungu cha 12: Maono, Ujumbe na Malengo Kifungu cha 13: Madhumuni Kifungu cha 14: Makosa na adhabu kwa ukiukaji wa Sheria, Kanuni na Masharti ya

Chama SEHEMU YA NNE: UANACHAMA Kifungu cha 15: Sifa za kujiunga na Chama. Kifungu cha 16: Utaratibu wa kujiunga na Chama Kifungu cha 17: Huduma zinazotolewa kwa Wanachama Kifungu cha 18: Malipo ya huduma Kifungu cha 19: Kupoteza hadhi ya uanachama Kifungu cha 20: Kujiuzulu uanachama Kifungu cha 21: Ishia ya uanachama Kifungu cha 22: Misingi ya kusimamishwa uanachama Kifungu cha 23: Utaratibu wa kumsimamisha mwanachama Kifungu cha 24: Utekelezaji wa kusimamishwa na/au kuondolewa uanachama Kifungu cha 25: Athari za kusimamishwa na kuondolewa uanachama Kifungu cha 26: Utaratibu wa malipo kwa mwanachama aliyejitoa na/au aliyeishia. Kifungu cha 27: Kudaiwa mwanachama Kifungu cha 28: Kuteua mrithi wa mali za mwanachama Kifungu cha 29: Haki za mwanachama Kifungu cha 30: Wajibu wa mwanachama Kifungu cha 31: Wajibu wa Chama SEHEMU YA TANO: MTAJI WA CHAMA Kifungu cha 32: Mjengeko na sura ya hisa na mtaji wa Chama Kifungu cha 33: Kuongezeka au kupungua mtaji

Page 2: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

2

Kifungu cha 34: Utaratibu wa marejesho ya hisa SEHEMU YA SITA: MAPATO YA CHAMA Kifungu cha 35: Mapato ya Chama SEHEMU YA SABA: MENEJIMENTI YA CHAMA Kifungu cha 36 Uwakilishi na Mkutano Mkuu Kifungu cha 37: Mkutano Mkuu wa mwaka Kifungu cha 38: Mkutano Mkuu wa kawaida Kifungu cha 39: Mkutano Mkuu maalum Kifungu cha 40: Mkutano Mkuu maalum ulioitishwa na Mrajis Kifungu cha 41: Uwezo maalum wa Mkutano Mkuu wa Chama Kifungu cha 42: Uwezo maalum wa Mkutano Mkuu wa Tawi Kifungu cha 43: Kukasimu madaraka Kifungu cha 44: Kuitisha Mkutano Mkuu Kifungu cha 45: Akidi Kifungu cha 46: Uwakilishi Kifungu cha 47: Upigaji kura: Kifungu cha 48: Uongozi, maamuzi na maazimio ya mikutano Kifungu cha 49: Mwenyekiti wa Chama Kifungu cha 50: Makamu Mwenyekiti wa Chama SEHEMU YA NANE: MUUNDO WA UONGOZI WA CHAMA Kifungu cha 52: Muundo wa Bodi na Kamati Kifungu cha 53: Sifa za Mjumbe wa Bodi na Kamati Kifungu cha 54: Wajibu wa Wajumbe wa Bodi Kifungu cha 55: Mihtasari, nyaraka na hati Kifungu cha 56: Chaguzi za Wajumbe wa Bodi/Kamati Kifungu cha 57: Kujiuzulu na kusimamishwa Kifungu cha 58: Stahili za malipo kwa Wajumbe wa Bodi Kifungu cha 59: Akidi ya vikao Kifungu cha 60: Maamuzi na maazimio ya vikao SEHEMU YA KUMI: UWEZO MAALUM WA BODI Kifungu cha 69: Kazi na madaraka ya Bodi Kifungu cha 70: Mikutano ya Bodi Kifungu cha 71: Mjumbe wa Bodi Kifungu cha 73: Muundo, kazi na madaraka ya Kamati ya Mikopo Kifungu cha 74: Utaratibu wa kukata na kusikiliza rufaa dhidi ya Kamati ya Mikopo Kifungu cha 75: Rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Mikopo Kifungu cha 76: Muundo, kazi na madaraka ya Kamati ya Usimamizi Kifungu cha 77: Malalamiko ya Wanachama na maadili Kifungu cha 78: Madaraka ya Kamati ya Usimamizi Kifungu cha 79: Wajibu wa Kamati ya Usimamizi Kifungu cha 80: Utoaji wa taarifa ya Kamati ya Usimamizi

SEHEMU YA KUMI NA MOJA: MUUNDO NA KAZI ZA TAWI Kifungu cha 81: Muundo, kazi na madaraka ya Kamati ya Tawi Kifungu cha 82: Mwenyekiti wa Kamati ngazi ya Tawi. Kifungu cha 83: Katibu wa Kamati ya Tawi Kifungu cha 84: Mjumbe wa Kamati ya Tawi Kifungu cha 85: Kikao cha Kamati ya Tawi

Page 3: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

3

Kifungu cha 86: Uwasilishaji wa taarifa kwenye Mkutano Mkuu wa Tawi

SEHEMU YA KUMI NA MBILI: UENDESHAJI NA UONGOZI Kifungu cha 87: Uongozi Kifungu cha 88: Madaraka na Kazi za Meneja Kifungu cha 89: Viongozi Kifungu cha 90: Utunzaji wa Siri wa Hali ya Juu Kifungu cha 91: Migongano ya Kimaslahi Kifungu cha 92: Tamko Kuhusu Mali Binafsi ya Afisa

SEHEMU YA KUMI NA TATU: UHASIBU Kifungu cha 93: Mwaka wa Fedha Kifungu cha 94: Utunzaji wa Hesabu Kifungu cha 95: Utoaji Taarifa ya Mwaka Kifungu cha 96: Ukaguzi wa Hesabu na Udhibiti Kifungu cha 97: Uthibiti na Uhakiki Kifungu cha 98: Taarifa Kuhusu Hitilafu na Mashaka Kifungu cha 99: Rasilimali Kifungu cha 100: Mtaji wa Unaokidhi na Dhima Kifungu cha 101: Mgao wa Ziada na/au Motisha Kifungu cha 102: Kufanya Shughuli Tofauti na Akiba na Mikopo Kifungu cha 103: Ukomo wa Madeni Kifungu cha 104: Uwezo wa Mali Kulipa Dhima Kifungu cha 105: Kiwango cha juu cha Utoaji Mkopo kwa Mwanachama Kifungu cha 106: Utoaji Mikopo kwa Wajumbe wa Bodi, Kamati ya Usimamizi na

Watendaji Wakuu. Kifungu cha 107: Ukwasi Kifungu cha 108: Ubora wa Mali na Uangalizi wa Mikopo na Kinga Dhidi ya Mikopo

Kifungu cha 109: Muundo wa Uendeshaji Kifungu cha 110: Mapato na Kujiendesha kwa Faida Kifungu cha 111: Taarifa ya Hesabu na Uwasilishaji wake kwa Mrajis na Benki Kuu ya

Tanzania. SEHEMU YA KUMI NA NNE: MENGINEYO Kifungu cha 112: Hatua za Kushughulikia Migogoro Kifungu cha 113: Muda Unaotakiwa kutoa Uamuzi juu ya Malalamiko Kifungu cha 114: Ufilisi Kifungu cha 115: Mgao wa Ziada baada ya Ufilisi Kifungu cha 116: Vitabu na daftari Kifungu cha 117: Maudhui ya daftari la wanachama Kifungu cha 118: Utunzaji wa vitabu na kumbukumbu nyinginezo Kifungu cha 119: Wanachama Kutazama Vitabu na kupata Taarifa Kifungu cha 120: Sera za Ndani na Taratibu Kifungu cha 121: Kuidhinisha Masharti Kifungu cha 122: Usajili na Marekebisho ya Masharti Kifungu cha 123: Utekelezaji wa Masharti Kifungu cha 124: Kuvunjwa kwa CHAMA SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI Kifungu cha 1: Jina Masharti haya ni kwa ajili ya Posta na Simu Savings and Credit Cooperative Society Limited na yataanza kutumika kwa mujibu wa kifungu cha 122.

Page 4: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

4

Kifungu cha 2: Tafsiri Katika Masharti haya, isipokuwa kama itakavyohitajika vinginevyo-

"Afisa” maana yake ni Mwanachama au mwajiriwa yoyote wa Chama wakiwemo Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Wajumbe wa Bodi, Meneja au mtu mwingine yeyote aliyepewa uwezo kwa mujibu wa Kanuni au Masharti kufanya shughuli kwa niaba ya Wanachama.

“Afisa Usimamizi wa Uchaguzi” maana yake Afisa Ushirika au Afisa mwingine yeyote aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 23 Jedwali la Sheria la Kanuni za Maadili na kifungu cha 57 cha Kanuni.

“Afisa Ushirika” maana yake afisa wa umma aliyekabidhiwa mambo yanayohusiana na maendeleo ya ushirika.

“Asasi ya fedha ya Ushirika” maana yake Chama kilichosajiliwa kutoa huduma za fedha.

“Bahashishi/Motisha” maana yake ni sehemu ya akiba nyinginezo iliyotengwa kwa ajili ya kuwarejeshea Wanachama kwa msingi wa uwiano wa kushiriki katika shughuli za Chama au kushiriki katika aina ya shughuli za Chama,kwa mfano, kuweka akiba na kukopa.

“Baki halisi ya ziada ya mwaka” (annual net balance) maana yake ni sehemu ya ziada halisi kwa mwaka wowote baada ya makato ya mfuko wa akiba, mfuko wa kukombolea/ kuhamisha hisa pamoja na ikiwa lazima au kwa manufaa ya Chama na baada ya kulipa mgao wa ziada juu ya hisa.yao kuwa katika hali nzuri.

“Benki” maana yake Benki Kuu ya Tanzania iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Benki ya Tanzania “benki” maana yake benki ya ushirika iliyosajiliwa katika ngazi ya Chama kikuu au ngazi ya tatu.

“Bodi” maana yake chombo cha uongozi na usimamizi wa Chama kilichosajiliwa na kilichokabidhiwa dhamana ya menejimenti ya Chama.

“Bonasi” maana yake kiasi kile cha baki ya ziada halisi ya mwaka ambacho kinaweza kugawanywa kwa Wanachama kwa kuzingatia uteja wao kwenye biashara ya Chama au ushiriki wao katika biashara hiyo.

“Chama” maana yake Chama cha Ushirika kilichosajiliwa chini ya Sheria na ni pamoja na Chama cha msingi, Chama kikuu, cha kilele na shirikisho.

“Chama cha kilele” maana yake ni Chama kilichoundwa na vyama vikuu kwa madhumuni ya kutoa huduma kwa vyama vikuu na vya msingi.

“Chama cha kilimo” maana yake Chama ambacho dhumuni lake kuu ni biashara ya ugavi wa pembejeo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, ununuzi, usindikaji, uuzaji na usaambazaji wa mazao ya kilimo.

“Chama cha msingi” maana yake ni Chama kilichosajiliwa ambacho Wanachama wake ni watu binafsi au muungano wa watu, chombo, shirika lolote lenye uhalali wa kisheria isipokuwa chombo au shirika lililosajiliwa chini ya Sheria ya makampuni na ni pamoja na ubia ambao Wanachama wake ni vyama vya msingi.

“Chama cha Ushirika” maana yake ni muungano wa watu kwa hiari yao wenyewe wameamua kujiunga pamoja kwa madhumuni ya kupata huduma ya pamoja iliyokusudiwa kwa kuanzisha chombo kinachoendeshwa kidemokrasia, kuchangia hisa inayokidhi uanzilishi na kukubali kuchukua tahadhari dhidi ya hatari na majanga pamoja na manufaa ya shughuli watakayoshiriki kuanzisha na kuiendesha.

“Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo” maana yake Chama kilichosajiliwa ambacho dhumuni lake kuu ni kuhimiza wekevu miongoni mwa Wanachama wake na kuanzisha chanzo cha mikopo kwa Wanachama wake kwa viwango vya kiasi na riba nafuu, kwa jumla na, hasa, Chama cha Akiba na Mikopo cha Posta na Simu.

“Chama kilichosajiliwa” maana yake ni Chama cha Ushirika kilichosajiliwa au kuchukuliwa kuwa kimesajiliwa chini ya Sheria na ni pamoja na vyama vya majaribio.

Page 5: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

5

"Éneo la shughuli” maana yake mahali ambapo Chama kinatarajia kupata Wanachama na kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa kifungu cha 45 (2) (b) na kifungu cha 75 (b) cha Sheria.

"Honararia" maana yake ni malipo kwa wajumbe wa Bodi au Watumishi kuwatuza kwa utumishi uliotukuka kwa mujibu wa kifungu cha 21cha Jedwali la Sheria na kifungu cha 48 cha Kanuni.

“Kamati” maana yake ni kundi la Wanachama walioteuliwa au kuchaguliwa na Bodi au Mkutano Mkuu au Afisa Usimamizi wa Uchaguzi kwa kazi maalum ya Chama cha Ushirika kama inavyoweza kuagiziwa na Sheria, Kanuni na Masharti.

“Kamati ya ufundi” maana yake ni kundi linaloundwa na Meneja, wataalamu wengine na mjumbe aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu.

“Kanuni” maana yake ni Kanuni za Vyama vya Ushirika za mwaka wa 2004 zilizotungwa chini ya kifungu cha 131 cha Sheria.

“Kanuni za Maadili” maana yake Kanuni za maadili ya Menejimenti ya Vyama vya Ushirika katika Jedwali zilizotengenezwa chini ya kifungu cha 125 cha Sheria.

“Masharti” maana yake Masharti yaliyoundwa na Chama cha Posta na Simu Savings and Credit Cooperative Society kwa mujibu wa kifungu cha 45 cha Sheria na kifungu cha 9 cha Kanuni.

“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli za Chama ambako wanachaguliwa wawakilishi wa Mkutano Mkuu kwa mujibu wa maelekezo ya kifungu cha 61 (6) cha Sheria.

“Mfungamano wa pamoja” maana yake mahitaji ya huduma na bidhaa za fedha ama yanayotakiwa au yanawatungamanisha Wanachama kwa mujibu wa kifungu cha 75 cha Kanuni.

“Mgao wa ziada” maana yake mgao wa fedha zinazolipwa dhidi ya hisa zilizochangwa na Wanachama.

“Mrajis” maana yake Mrajis wa vyama vya Ushirika aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 10 cha Sheria na ni pamoja, pale panapohitajika, na Naibu Mrajis au Warajis Wasaidizi.

“Mwanachama” maana yake- kwa Chama cha msingi ambacho Mkutano Mkuu wa Wanachama unahudhuriwa na wawakilishi, mwakilishi wa idadi maalum ya Wanachama anayechaguliwa au kuteuliwa kuhudhuria na kupiga kura katika mkutano wa Wawakilishi; kwa Chama ambacho ni Mwanachama wa Chama kingine, mwakilishi wa Chama chake aliyechaguliwa au kuteuliwa kuhudhuria na kupiga kura katika mkutano wa Chama kile; mtu aliyejiunga na Chama au aliyeomba na kukubalika kuwa Mwanachama baada ya usajili kupatikana kwa mujibu wa Masharti na Kanuni.

“Sheria” maana yake Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.20 ya mwaka 2003.

“Shirika” maana yake Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika lilioanzishwa chini ya Sheria ya Ushirika, Ukaguzi na Usimamizi ya mwaka wa 1982. “Shirikisho” maana yake Chama cha ushirika ambacho Wanachama wake ni vyama vya kilele.

“Ubia” maana yake muungano wa vyama viwili au zaidi ambavyo vinajiunga pamoja kwa madhumuni ya kuendesha shughuli ya kiuchumi. “Ujuzi maalum” maana yake stadi anayoweza kuwa nao mtu katika fani maalum kama inavyoweza kutajwa katika Kanuni.

“Upekuzi” maana yake kufanya uchunguzi kwa nia ya kuangalia kwa makini mwombaji nafasi kwenye menejimenti ya Vyama vya Ushirika kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (3) cha Jedwali la Kanuni za maadili na kifungu cha 53 cha Kanuni. “Ushirika wa Kifedha” maana yake asasi ya kifedha isiyokuwa ya kibenki ambayo kazi yake ya msingi ni kutoa mikopo yenye dhamana na isiyokuwa na dhamana kwa kaya, wazalishaji wadogo pamoja na biashara ndogo na za mijini na vijijini.

“Uwezo wa kiuchumi” maana yake uwezo wa Chama kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa Kanuni na

Page 6: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

6

kutotegemea sana misaada na kupigwa jeki na asasi, mamlaka au watu wa nje.

“Waziri” maana yake Waziri mwenye dhamana ya Ushirika kwa wakati huo.

“Watumishi watendaji” maana yake watumishi wa Chama walioteuliwa na Bodi na wamekabidhiwa uwezo kuendesha na kusimamia shughuli za kila siku za Chama na watakuwa ni pamoja na meneja/katibu, mhasibu au mtunza hazina, wakuu wa idara na keshia.

“Ziada halisi ya mwaka” (annual net surplus) maana yake ni sehemu ya mapato yaliyopatikana kwa malipo au madai/bado kulipwa katika kipindi chochote cha mwaka baada ya makato yatokanayo na gharama za uendeshaji kwa mwaka huo, baada ya kutenga kinga dhidi ya madeni mabaya, uchakavu, kodi na hasara. Kwa mujibu wa tafsiri hii, ruzuku siyo mapato na inatakiwa kuondolewa katika hesabu ya mapato.

“Huduma ndogo za fedha” maana yake ni huduma ndogo za kifedha zinazotolewa na Taasisi mbalimbali (Micro Finance) SEHEMU YA PILI: MASHARTI, JINA LA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO, MAKAO MAKUU NA ANUANI, ENEO LA SHUGHULI NA MFUNGAMANO WA UANACHAMA. Kifungu cha 3: Masharti

Waanzilishi wa Chama ambao, majina yao yamo katika muhtasari wa mkutano wa kiSheria na wengine watakaofuata baadaye, wameunda Chama chenye mtaji unaobadilika kwa mujibu wa mwongozo wa Sheria ya Ushirika ya mwaka 2003, Kanuni ya Vyama vya Ushirika za mwaka 2004 na Masharti haya.

Kifungu cha 4: Jina la Chama

Jina la CHAMA ni Posta na Simu Savings and Credit Cooperative Society Limited Kifungu cha 5: Usajili

CHAMA hiki kimesajiliwa tarehe 26 Oktoba, 1976 chenye hati ya usajili Na.DSR118. Kifungu cha 6: Makao Makuu na Anuani

Makao makuu ya CHAMA yatakuwa katika Nyumba Na.18 kiwanja Na.76 Mtaa wa Sophia Kawawa Manispaa ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam Anuani ya CHAMA itakuwa S.L.P 3948 Dar es Salaam.

Bodi ya Chama inaweza kuyahamisha makao makuu hayo na kwenda eneo lolote lililo ndani ya shughuli za uendeshaji wa Chama endapo italazimika, na uamuzi huo lazima uthibitishwe katika Mkutano Mkuu unaofuata. Kifungu cha 7: Eneo la Shughuli

Eneo la Uendeshaji wa shughuli za Chama litakuwa nchini Tanzania

Kifungu cha 8: Mfungamano wa Pamoja wa Uanachama

(a) Kwa mujibu wa kifungu cha 75 (3) cha Kanuni, msingi wa kiungo na mfungamano wa uanachama ni kufanya kazi pamoja, kuishi sehemu moja, kuwa katika jumuia na kusaidiana.

(b) Kwa madhumuni ya ushirika wa akiba na mikopo wa Posta na Simu, mfungamano wa pamoja unajumuisha tungamanisha ya mahitaji ya huduma za fedha ya waajiriwa wa Shirika la Posta, Benki ya Posta, Kampuni ya Simu, Tume ya Mawasiliano, Watumishi wa ushirika huu na Jamii za Wanachama nchini Tanzania. Waajiriwa watakaostaafu lakini watakaopenda kuendelea na uanachama wao pia wanajumuishwa kuwa na mfungamano wa pamoja.

Kifungu cha 9: Maadili ya Uanachama

(a) Chama kimejengwa katika misingi ya maadili ya kujitolea, kujituma, uwajibikaji binafsi, demokrasia, usawa, haki na mshikamano.

(b) Kwa kufuata nyayo za mila na utamaduni wa waasisi wa ushirika, Wanachama wanakiri Kanuni za

Page 7: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

7

maadili ya uaminifu, uwazi, uwajibikaji kijamii, uadilifu na kujali utu wa wengine. Kifungu cha 10: Misingi ya Ushirika

(a) Chama kitaongozwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Misingi ya Ushirika. Misingi hii ni mwongozo ambao vyama vya ushirika hutekeleza kwa vitendo.

(b) kinawajibika kuheshimu misingi ya kuendeleza ushirika, hasa ifuatayo-

Uanachama Uliowazi na wa Hiari Uanachama katika Chama ni wa uwazi na wa hiari bila vipingamizi vyovyote. Watu wote ambao wako tayari kutumia huduma za ushirika na wako tayari kutimiza wajibu wa uanachama wanaruhusiwa kujiunga bila kujali hali yao ya kijinsia, kijamii, mbari (racial), kisiasa, au dini yao.

Udhibiti na Utawala wa Wanachama Kidemokrasia Ushirika ni vyombo vya kidemokrasia vinavyoongozwa na Wanachama ambao wanashiriki kikamilifu katika kuunda sera na maamuzi. Wake kwa waume, waliochaguliwa na Wanachama wenzao, wanaendesha shughuli kwa niaba ya wenzao na kuwajibika kwa Wanachama. Katika vyama vya ushirika vya msingi, Wanachama wana haki sawa ya kupiga kura (kila mtu kura moja) na katika ngazi zingine za ushirika uendeshaji unaongozwa kidemokrasia.

Wanachama Kushiriki Kiuchumi Wanachama wana haki ya kuchangia kidemokrasia mtaji wa ushirika wao. Angalao sehemu ya mtaji, kwa kawaida, inakuwa mali ya ushirika. Wanachama wanatenga ziada kwa madhumuni yoyote au makusudio yafuatayo: maaendeleo ya ushirika, kwa kutenga akiba ambayo sehemu yake itagawanywa kwa Wanachama kwa uwiano wa jinsi alivyoshiriki katika biashara, na shughuli nyinginezo zilizoidhinishwa na Wanachama.

Uhuru na Kujitawala Ushirika ni asasi huru zenye kujitegemea na kudhibitiwa na Wanachama wake. Kama zitaingia katika makubaliano na asasi nyingine ikiwa ni pamoja na serikali au kupata mtaji kutoka vyanzo vya nje, zitafanya hivyo kwa Masharti ambayo yatahakikisha uongozi wa kidemokrasia wa Wanachama wake na kudumisha uhuru wao.

Elimu, Mafunzo na Taarifa Ushirika hutoa Elimu na Mafunzo kwa Wanachama, viongozi, mameneja na watumishi wa vyama vya ushirika na kutumia Elimu na Mafunzo hayo kwa manufaa ya kuendeleza ushirika wao. Vile vile, wataifahamisha jamii hasa vijana na viongozi kuhusu faida za ushirika.

Ushirikiano Miongoni mwa Vyama vya Ushirika Vyama vyote vya ushirika vinawatumikia Wanachama na jumuia zao katika njia zilizo bora zaidi na kuimarisha shughuli za ushirika kuanzia ngazi ya Msingi, Mkoa, Taifa na Kimataifa.

Kujali na Kujihusisha na Jamii Ushirika hufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya uhakika kwa jamii na kuzingatia sera zilizoidhinishwa na Wanachama wake.

Kifungu cha 11: Uanachama wa Chama na Ukwasi

(a) Chama kinaweza kujiunga na/au kushiriki kuunda Chama chochote katika ngazi ya Chama Kikuu, Chama cha Kilele na Shirikisho; ama ushirika wa kifedha; au ubia kwa mujibu wa kifungu cha 16 na 21 cha Sheria na kifungu cha 108 cha Kanuni kama itakavyoonelewa kuwa ni kwa manufaa ya kufanikisha madhumuni na malengo ya Chama.

(b) Chama kinakubali kushiriki katika uhamasishaji wa maendeleo ya mtandao wenye nguvu wa asasi

za kifedha za ushirika utakaowezesha usimamizi wa fedha wa pamoja kuimarisha umoja, usalama na nguvu ya pamoja miongoni mwa vyama.

Page 8: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

8

SEHEMU YA TATU: MAONO, UJUMBE, MALENGO NA MADHUMUNI YA CHAMA

Kifungu cha 12: Maono, Ujumbe na Malengo Maono

Kuwezesha kukuza ushirika wa akiba na mikopo unaotoa huduma ndogo za fedha ambazo ni bora, nafuu, rahisi, zinazokidhi na za kuridhisha kwa Wanachama.

Ujumbe Kukuza na kuendeleza huduma za kifedha endelevu kiushirika za aina yake kwa kuhamasisha na kuhimiza uwekaji wa akiba na amana; utunzaji salama na wa uhakika wa akiba, amana na hisa; kutoa bidhaa mbalimbali za mikopo zinazofaa; kutoa elimu kwa Wanachama; na kujiendesha kwa faida ili kujiimarisha na, hatimaye, kujitegemea kifedha na kujitosheleza kiuchumi.

Malengo Kukuza Chama chenye uwezo wa kujiendesha kwa kulipia gharama zake, kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha ya Wanachama bila kutegemea asasi/mamlaka/watu wengine na kutoa msukumo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuwa sehemu ya mtandao wa huduma za kifedha katika misingi, njia na taratibu za ushirikiano.

Kifungu cha 13: Madhumuni.

(a) Madhumuni ya Chama ni kuendelea kuinua, kustawisha na kuboresha hali na ustawi wa kiuchumi na kijamii ya Wanachama wake kiushirika kwa kufuata taratibu za kidemokrasia, Misingi ya Ushirika, Sheria ya Vyama vya Ushirika, Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti haya na misingi ya mwenendo bora wa huduma ndogo za fedha.

(b) Ili kuweza kufikia madhumuni haya, Chama kitajitahidi, kulingana na Misingi ya Ushirika, kufanya yafuatayo- (i) Kutoa huduma ya kupokea na kuweka akiba na amana pamoja na kutoa mikopo (ii) Kuhamasisha, kuhimiza na kushauri wasiokuwa Wanachama kuwa Wanachama (iii) Kukuza mapato ya Chama kwa kuhimiza Wanachama kuongeza akiba na amana zao mara

kwa mara; kuwekeza ziada katika asasi za fedha kwa mujibu wa kifungu cha 73 cha Sheria (iv) Kuanzisha na kuendeleza shughuli zo zote za kiuchumi zenye manufaa na maslahi kwa

Wanachama kama itakavyoidhinishwa na Mkutano Mkuu na Mrajis (v) Kusaidia shughuli za Wanachama binafsi (vi) Kuendeleza elimu ya ushirika miongoni mwa Wanachama

(c) Kupambana na umasikini, ujinga, maradhi na ubaguzi, hasa wa kijinsia. Kifungu cha 14: Makosa na adhabu kwa Ukiukaji wa Sheria, Kanuni na Masharti

(a) Karatasi (Hati), kumbukumbu na mihuri yote ya Chama havitaondolewa katika ofisi za Chama isipokuwa kwa maelekezo ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 29 cha Sheria

(b) Afisa au mwajiriwa atayekwenda kinyume cha maelekezo ya Sehemu ya Kumi na Tano ya Sheria, maelekezo ya Kanuni na Masharti haya atakuwa ametenda kosa na, akipatikana na hatia, atastahili adhabu iliyoanishwa katika kifungu husika cha Sheria, Kanuni na Masharti.

SEHEMU YA NNE: UANACHAMA

Kifungu cha 15: Sifa za kujiunga na Chama.

(a) Kikundi/Asasi au mtu yeyote aliye na akili timamu anaweza kuwa Mwanachama wa Chama ikiwa ametimiza Masharti yafuatayo - (i) Awe Raia wa Tanzania. (ii) Ana mfungamano wa uanachama kwa mujibu wa kifungu cha 8 (iii) Ana umri usiopungua miaka kumi na nane. (iv) Ana uwezo wa kulipa viingilio

Page 9: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

9

(v) Atakuwa tayari kuheshimu Masharti, mwenendo wa ndani, taratibu na sera za Chama (vi) Awe wa kuaminika na kufahamika na Wanachama.

(b) Kwa mujibu wa kifungu hiki, mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na nane (18) lakini umri wake si chini ya miaka kumi na tano (15) lakini anakubaliana na madhumuni ya Chama, anaweza kuwa Mwanachama. Hata hivyo, hataruhusiwa kuwa mjumbe wa Bodi au Kamati yoyote pamoja na kuomba na kupewa mikopo hadi atakapotimiza umri wa miaka kumi na nane (18).

Kifungu cha 16: Utaratibu wa Kujiunga na Chama

(a) Isipokuwa Wanachama Waanzilishi waliojiandikisha wakati wa kuomba usajili, ili kukubaliwa kuwa Mwanachama, itabidi mwombaji awasilishe maombi ya uanachama kwa maandishi kwa Bodi ya Chama au mhusika yeyote aliyeidhinishwa. Maombi haya lazima yaambatane na angalao malipo ya hisa tano za shilingi tano elfu (5,000), yaani shilingi elfu ishirini na tano (25,000) kati ya hisa 20 zenye thamani ya shilingi mia moja elfu (100,000) na alipe kiingilio cha shillingi elfu ishirini (20,000). Salio la thamani za hisa lililobaki linapaswa kulipwa katika muda wa kipindi kisichozidi miezi sita (6) tangu kujiunga kwake.

(b) Mwanachama atatakiwa kukabidhi picha zake mbili ndogo za utambulisho. (c) Viingilio vinalipwa kwa mara moja tu wakati wa kuingia Chama. Kiingilio hakirudishwi tena kwa

Mwanachama. (d) Mwanachama anatambuliwa, kwanza, kwa uthibitisho wa kusajiliwa katika Daftari ya Wanachama

linalowekwa makao makuu ya Chama. Pili, kwa kufungua akaunti/hesabu za Mwanachama na, tatu, kwa kupewa kitambulisho cha akaunti hiyo.

(e) Viwango vya kiingilio, hisa, michango, vinaweza kubadilishwa na /au kuongezeka kwa mujibu wa maamuzi ya Mkutano Mkuu

(f) Yeyote aliyeishia uanachama au aliyejiuzulu anaweza kujiunga upya katika Chama iwapo atakubaliana na kifungu cha 15 cha Masharti haya.

(g) Hakuna Mwanachama atakayeruhusiwa kuwa na hisa zaidi ya moja ya tano (1/5) ya thamani ya hisa zilizowekwa na Wanachama

Kifungu cha 17: Huduma Zinazotolewa kwa Wanachama

(a) Huduma zitakazotolewa na Chama zitakuwa ni kwa ajili ya Mwanachama peke yake na zitatolewa katika muda wa saa za kazi uliopangwa na Bodi ya Chama.

(b) Wanachama watapewa huduma zifuatazo baada ya kuomba kwa mujibu wa taratibu na Kanuni katika muda wa saa za kazi- (i) Mwanachama anaweza kuweka akiba yake katika akaunti/akiba kiwango cha chini

kitapangwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la Wawakilishi. Akiba ya Mwanachama inaweza kutolewa na Mwanachama husika siku ye yote wakati wa saa za kazi. Kiwango cha juu kinachoweza kutolewa kutoka katika hesabu ya akiba mara moja bila taarifa ni Tshs.300,000/=. Taarifa ya maandishi ya siku saba inapaswa kutolewa na Mwanachama anayetaka kuchukua zaidi ya kiasi hicho

(ii) Mwanachama anaweza pia, kwa mapatano na Chama, kuweka kiasi maalum cha fedha katika muda maalum wa makubaliano mahsusi yaliyowekwa na Chama. Chama kinaweza kulipa riba juu ya akiba hiyo. Kiwango cha riba kitapangwa na Mkutano Mkuu

(iii) Mwanachama anaweza kuomba mkopo. Mikopo itatolewa kwa kutumia misingi na vigezo vya sera na taratibu zilizotolewa na CHAMA (angalia vifungu 73, 106 na 108). Mikopo itakayotolewa na CHAMA itakuwa kwa ajili ya uzalishaji na huduma muhimu.

Kifungu cha 18: Malipo ya Huduma

(a) Viwango vya malipo kwa huduma zinazotolewa na Chama hupangwa na Bodi na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu. Viwango hivyo vinawekwa kwa mujibu wa kifungu cha 110. Viwango hivyo vitakuwa vikitangazwa na kusajiliwa katika Daftari ya Chama.

(b) Viwango vya malipo ya mgawo wa ziada dhidi ya hisa zilizochangwa na Wanachama na riba kwa

Page 10: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

10

ajili ya hesabu ya akiba pia vitatangazwa kwa mujibu wa maamuzi ya Mkutano Mkuu. Kifungu cha 19: Kupoteza Hadhi ya Uanachama

(a) Uanachama utaishia ikiwa Mwanachama (i) Amefariki (ii) Amejiuzulu (iii) Amethibitika na daktari kuwa hana akili timamu (iv) Amepoteza sifa za mfungamano wa pamoja kwa mujibu wa kifungu cha 8 (v) Amethibitika kupatikana na makosa kwa mujibu wa kifungu cha 23 (a).

(b) Amefukuzwa uanachama na theluthi mbili (2/3) ya Wanachama waliohudhuria Mkutano Mkuu. Kifungu cha 20: Kujiuzulu Uanachama

(a) Mwanachama anaweza kujiuzulu wakati wo wote anaotaka kwa kutoa taarifa rasmi ya maandishi ya siku tisini (90) kwa Bodi ya Chama

(b) Kujiuzulu kutaanza tangu tarehe ya kupokelewa barua ya taarifa ya kujiuzulu (c) Chama kitarejesha hisa katika muda wa siku 90 baada ya kutolewa taarifa na kufuata taratibu

zilizowekwa katika kifungu cha 34 cha Masharti haya. Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) na kifungu cha 75 cha Kanuni, ombi la kurejeshewa hisa linapaswa kuwasilishwa kwa maandishi na taarifa ya angalao siku sitini (60)

(d) Mwanachama mwenye deni anayejiuzulu hatarejeshewa hisa zake hadi atakapokamilisha marejesho ya kulipa deni lake.

(e) Endapo Mwanachama amepewa mkopo, hisa na akiba yake vitachukuliwa kama dhamana dhidi ya mkopo.

(f) Mwanachama aliyedhamini mkopo ambaye anataka kujiuzulu hatarejeshewa hisa na akiba zake hadi deni litakapokamilika kulipwa na mdaiwa.

Kifungu cha 21: Ishia ya Uanachama

(a) Uanachama utaishia iwapo- (i) Atachukua hisa zote katika Chama (ii) Atapoteza sifa za mfungamano na Chama (iii) Atatiwa hatiani kwa kosa la jinai na au kufungwa jela (iv) Atabainika kutokuwa mwaminifu (v) Atathibitika na daktari kuwa hana akili timamu (vi) Atatoa au kuwa tayari kutoa hongo (rushwa) au kamisheni kwa mtumishi yeyote wa Chama (vii) Atafukuzwa uanachama na theluthi mbili (2/3) ya Wanachama waliohudhuria Mkutano Mkuu (viii) Atatenda kitendo chochote ambacho Bodi itaridhika kuwa ni cha kutokuwa mwaminifu, kinyume na maadili au madhumuni ya Chama ama cha kukipaka matope, kukidhalilisha, kukashifu na kuharibu jina zuri na sifa njema za Chama (ix) Atashindwa kulipa mkopo katika muda na Masharti yaliyowekwa bila sababu maalum (x) Atakuwa na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na vitendo vinavyohatarisha kukiangusha Chama.

(b) Tarehe ya mwisho ya kusimamishwa uanachama ni ile iliyotolewa uamuzi wa mwisho wa Mkutano Mkuu.

Kifungu cha 22: Misingi ya Kusimamishwa Uanachama

(a) Bodi ina madaraka ya kusimamisha uanachama.

Page 11: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

11

(b) Uamuzi huo sherti uwe na sababu za msingi. (c) Uamuzi huu unaweza kuchukuliwa katika mazingira yafuatayo- (i) Kutoheshimu Masharti na mwenendo wa ndani wa Chama

(ii) Kutoheshimu na kutotekeleza ahadi hasa kutowajibika na urejeshwaji wa mikopo (iii) Kukosa kiungo cha mfungamano na kusaidiana kwa mujibu wa kifungu cha 8

(iv) Kuwa na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na vitendo vinavyohatarisha kukiangusha Chama

(v) Sababu nyingine kama zilivyoelezwa katika Masharti. Kifungu cha 23: Utaratibu wa Kumsimamisha Mwanachama

(a) Bodi itamsimamisha Mwanachama yeyote anayekabiliwa na tuhuma za kwenda kinyume au amethibitika kukiuka maelekezo ya kifungu cha 21.

(b) Muhtasari wa kikao cha Bodi kilichomsimamisha lazima ubainishe jambo analotuhumiwa na kusababisha kufikiwa uamuzi huo.

(c) Chama kitampa Mwanachama taarifa ya maandishi ya kusimamishwa kwake katika kipindi cha muda wa siku kumi na tano (15) tokea tarehe ya uamuzi pamoja na sababu za kusimamishwa.

Kifungu cha 24: Utekelezaji wa Kusimamishwa na/au Kuondolewa Uanachama

(a) Utekelezaji wa kusimamishwa na/au kuondolewa Uanachama kuanzia tarehe ulipopitishwa uamuzi na Bodi

(b) Kusimamishwa kwa Mwanachama hakusababishi kupoteza hadhi yake ya uanachama Kifungu cha 25: Athari za Kusimamishwa na Kuondolewa Uanachama

(a) Chini ya utaratibu wa kinga/ tahadhari dhidi ya rufaa kwa mujibu wa kifungu cha 112, Mwanachama aliyesimamishwa na/au kuondolewa anapoteza haki ya kuendesha, kuhudhuria, kupiga kura katika mkutano, vile vile kushiriki shughuli za uendeshaji ndani ya Kamati za Chama

(b) Mwanachama aliyesimamishwa atapoteza haki za uanachama kwa kipindi kisichozidi miezi sita tu. Kifungu cha 26: Utaratibu wa Malipo kwa Mwanachama Aliyejitoa na/au Kuishia.

(a) Kupoteza hadhi ya uanachama kwa mujibu wa kifungu cha 20 na 21 kunatoa nafasi ya kufanya mahesabu ya mwisho ya aliyekuwa Mwanachama ya madeni yake pamoja na mikopo ambayo bado kulipwa, malimbikizo ya faida juu ya mikopo, adhabu; hesabu yake ya madai kama akiba, malimbikizo ya riba ambayo bado hajalipwa

(b) Mwanachama aliyeishia hawezi kulipwa hisa na akiba zake hadi hapo Wanachama aliowadhamini kupata mikopo wamelipa kwa ukamilifu.

(c) Wanachama waliokoma hawawezi kurejeshewa viingilio. Kifungu cha 27: Kudaiwa Mwanachama

(a) Dhima ya Mwanachama kwa madeni ya Chama haitazidi thamani ya hisa zake. (b) Kwa mujibu wa kifungu cha 41 cha Sheria kudaiwa kwa Mwanachama wa zamani kwa deni la

Chama kilichosajiliwa, kwa madeni ya Chama yaliyokuwa wakati alipoacha uanachama, bila kujali maelekezo ya Sheria yo yote iliyoandikwa inayopingana, kutaendelea kwa kipindi cha muda ambao Masharti ya Chama yataelekeza kuanzia tarehe alipoacha uanachama.

(c) Mwanachama anayejiuzulu au kuachishwa/kufukuzwa uanachama bado anawajibika kwa Wanachama pamoja na washiriki wengine kutekeleza majukumu na mihadi iliyokuwapo wakati anajiuzulu au kuachishwa/kufukuzwa hadi shughuli za ufilisi zimekamilika.

Kifungu cha 28: Kuteua Mrithi wa Mali za Mwanachama

(a) Kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha Kanuni, kila Mwanachama ana haki ya kuteua mrithi kwa

Page 12: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

12

maandishi na ushuhuda wa mashahidi wawili ambaye atakuwa na haki za kurithi hisa na maslahi mengine katika Chama kutokana na kifo au Mwanachama kutokuwa na akili timamu. Usia wake utawekwa katika Daftari ya Usajili.

(b) Mwanachama atakuwa na haki ya kubadilisha jina la mrithi wake wakati wowote bila Masharti yoyote.

(c) Mrithi anaweza kuomba kuwa Mwanachama. Kifungu cha 29: Haki za Mwanachama

(a) Kila Mwanachama ana haki; (b) Mwanachama yeyote wa Chama kilichosajiliwa atakuwa na haki za uanachama zifuatazo-

(i) Kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli za Chama baada ya kulipia ada ya kiingilio, hisa na ada nyinginezo

(ii) Kushiriki katika Mkutano Mkuu na kupiga kura (iii) Kupendekezwa kuwa mjumbe wa Bodi na Kamati mbalimbali za Chama (iv) Kupata taarifa kutoka Bodi ya Chama na watendaji wakuu wa Chama kuhusu mahesabu na

hali halisi ya Chama. (v) Kuchaguliwa katika Bodi na Kamati za Chama (vi) Kupitia kumbukumbu na hati za Chama kwa mujibu wa kifungu cha 117 (vii) Kuitisha Mkutano Mkuu Maalum kwa mujibu wa kifungu cha 39 (viii) Kufaidika na shughuli za Chama kwa mujibu wa kifungu cha 13 na 17. (ix) Kukagua orodha ya mikopo iliyocheleweshwa kurejeshwa kwa mujibu wa kifungu kidogo

cha (1) cha 102 cha Kanuni (x) Kuteua mrithi kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha Kanuni (xi) Kukopa alimradi ameweka akiba au amana ya kutosha (xii) Kupata cheti cha hisa baada ya kukamilisha malipo ya hisa (xiii) Kusikilizwa (xiv) Kukagua nyaraka za Chama (xv) Kuanzisha uchunguzi katika shughuli za Chama (xvi) Kukata rufaa

(c) Huduma za Chama ni kwa ajili ya Wanachama wake kwa mujibu wa kifungu cha 17 na kwa mujibu wa Kanuni za ndani za Chama.

Kifungu cha 30: Wajibu wa Mwanachama

(a) Kila Mwanachama wa Chama ana wajibu. (b) Wajibu wa Wanachama ni pamoja na -

(i) Kuheshimu, kufuata na kutii Masharti, Kanuni za maadili, mwenendo, sera na taratibu za ndani

(ii) Kukubali maamuzi ya Mkutano Mkuu, Bodi na Kamati nyinginezo za Chama (iii) Kuweka akiba, amana na/ au kushiriki katika shughuli za fedha za Chama (iv) Kuheshimu ahadi na makubaliano na Chama kwa mujibu wa kiwango, Masharti na muda (v) Kulinda na kutetea mali na dhima za Chama (vi) Kuhifadhi na kulinda mwongozo na hadhi ya Chama (vii) Kuendeleza mahusiano mazuri, majadiliano na kuheshimiana miongoni mwa Wanachama (viii) Kuwa mwaminifu na kufanya juhudi za kukisaidia Chama kiweze kufikia malengo yake (ix) Kulipa ada na michango iliyowekwa na Chama (x) Kuhudhuria na kushiriki katika Mkutano Mkuu (xi) Kukifadhili Chama (xii) Kuteua mrithi (xiii) Kulipa madeni ya Chama (xiv) Kufuata maamuzi ya Mkutano Mkuu (xv) Kudumisha na kutetea taswira na sifa ya Chama

Page 13: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

13

Kifungu cha 31: Wajibu wa Chama

(a) Kila Chama kilichosajiliwa kina wajibu (b) Wajibu wa Chama kilichosajiliwa ni pamoja na-

(i) Kutunza Daftari ya Wanachama inayoonyesha jina, anwani, kazi ya kila Mwanachama; idadi ya hisa zake; tarehe ambayo aliingizwa katika daftari; tarehe ambayo aliacha kuwa Mwanachama; na mrithi, kama yupo.

(ii) Kuwahudumia Wanachama wake wote bila upendeleo; (iii) Kuandaa sera nzuri kwa ajili ya uwekezaji wa fedha za Wanachama pamoja na utaratibu wa

utoaji mikopo (iv) Kuhakikisha kwamba mahitaji ya mikopo ya Wanachama yanatekelezwa kwa wakati (v) Kuboresha huduma na kuweka utaratibu unaofaa kwa Wanachama kutunza fedha zao

Chamani. (vi) Kulinda maslahi ya Wanachama (vii) Kutunza nakala ya Sheria, Kanuni na Masharti wazi kwa ukaguzi muda unaofaa na bila

malipo kwenye ofisi ya Chama iliyosajiliwa (viii) Kuwa na anwani kwa mujibu wa Kanuni ambayo mawasiliano yote yatapitia (ix) Kuandaa na kurekebisha Masharti (x) Kuonyesha mizania ya mwaka mnamo muda wa saa za kazi kwa watu wanaoweza kuwa na

shauku kuhusu mapato ya Chama kama Wanachama au wadai. SEHEMU YA TANO: MTAJI WA CHAMA

Kifungu cha 32: Mjengeko na Sura ya Hisa na Mtaji wa Chama

(a) Kila hisa itakuwa na thamani ya shilingi elfu tano (5,000/=). (b) Hakuna Mwanachama atakayeruhusiwa kuwa na zaidi ya moja ya tano (1/5) au asilimia ishirini ya

jumla ya hisa zote za Chama (c) Mtaji ulioidhinishwa na Chama utatokana na hisa zilizolipwa. Hisa zinaainishwa kwa majina na

zinamhusu mtu binafsi na haziuzwi, kubadilishwa na wala haziwezi kuchukuliwa na mtu mwingine. (d) Hisa zinaweza kurejeshwa kwa Mwanachama au mrithi wake ambaye uanachama wake umeishia,

baada ya kusawazisha mahesabu kwa mujibu wa kifungu cha 26 na baada ya muda na kwa mujibu wa mpangilio wa utaratibu uliowekwa katika kifungu cha 34. Hisa zinahamishika baada ya kupata idhini ya Bodi.

(e) Mgao wa ziada juu ya hisa unaweza kulipwa kulingana na viwango vilivyowekwa na Mkutano Mkuu

(f) Mwanachama yeyote anayetaka kupunguza hisa bila kuathiri hadhi ya uanachama wake anaruhusiwa alimradi atoe taarifa ya siku thelathini kwa Bodi.

Kifungu cha 33: Kuongezeka au Kupungua Mtaji (a) Mtaji wa Chama unaweza kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Wanachama,

kuongeza kiwango cha hisa na kuongeza thamani ya kila hisa. (b) Mtaji wa Chama unaweza kupungua kutokana na kufukuzwa, vifo au kuachishwa Wanachama. Kifungu cha 34: Utaratibu wa Marejesho ya Hisa

(a) Isipokuwa kama Chama kinafilisiwa, hakina uwezo au kimeishia vinginevyo, hisa zinarejesheka katika utaratibu na mpangilio maalum wa mahitaji na katika kipindi kisichozidi siku tisini (90) tangu siku ya tukio husika.

(b) Fedha zilizoingizwa katika hesabu ya hisa zinaweza kutolewa kutokana na Maombi ya maandishi yaliyotumwa kwenye Chama kwa siku yoyote katika saa za kazi

SEHEMU YA SITA: MAPATO YA CHAMA

Page 14: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

14

Kifungu cha 35: Mapato ya Chama

(a) Fedha za Chama zitatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato. (b) Kifungu cha 69 (1) cha Sheria kimeainisha vyanzo mbalimbali vya mapato baadhi yake ni:-

(i) Viingilio, ada na michango mbalimbali kwa mujibu wa Masharti (ii) Hisa (iii) Mapato yatokanayo na riba ya mikopo na akiba (iv) Fedha inayotokana na ongezeko kutokana na akiba ya Wanachama (v) Mauzo ya mali na/au huduma zitolewazo na Chama (vi) Vitega uchumi

(c) Mikopo kutoka asasi za fedha kwa kufuata Masharti yatumikayo-

(i) Lazima ithibitishwe na Bodi (ii) Mikopo hiyo isizidi asilimia ishirini na tano (25%) ya hisa na akiba katika Chama wakati wa

kuwekeana mkataba (iii) Mikopo yote ambayo thamani yake ni zaidi ya asilimia ishirini na tano (25%) lakini haizidi

asilimia hamsini (50%) ya mtaji, akiba pamoja na hisa lazima iidhinishwe na Mkutano Mkuu baada ya kupendekezwa na Bodi.

(d) Ruzuku, misaada n.k. SEHEMU YA SABA: MENEJIMENTI YA CHAMA Kifungu cha 36: Uwakilishi na Mkutano Mkuu

(a) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) cha kifungu cha 61 cha Sheria, Mkutano Mkuu ulioitishwa kwa mujibu wa Masharti ya Chama ndio mamlaka ya juu kabisa katika Chama iliyokabidhiwa madaraka ya udhibiti na usimamizi wa shughuli za Chama. Ni mkusanyiko wa wawakilishi wa Wanachama kutoka kila Tawi walioitwa kwa makusudi hayo.

(b) Wanachama katika ngazi ya Tawi, hufanya Tawi la Chama. Kwa mujibu wa maelekezo ya kifungu kidogo cha 6 cha kifungu cha 61 cha Sheria na kifungu kidogo cha (2)cha kifungu cha 35 cha Kanuni, Wanachama katika ngazi ya Tawi watawachagua wawakilishi ambao watahudhuria mikutano mikuu kwa ajili na kwa niaba yao

(c) Kwa kila Wanachama arobaini (40) katika ngazi ya Tawi, atachaguliwa mwakilishi mmoja. Katika hali yoyote ile, kutakuwa na angalao mwakilishi mmoja katika ngazi ya Tawi kwenye mikutano mikuu. Endapo Tawi husika litakuwa na Wawakilishi zaidi ya mmoja uwiano wa taasisi utazingatiwa katika uchaguzi.

(d) Mkutano Mkuu utaitishwa katika kipindi kisichozidi miezi sita baada ya kumalizika kwa mwaka wa fedha wa Chama

(e) Mkutano Mkuu wa mwaka utaitishwa wakati wo wote alimradi mkutano mmoja ufanyike miezi

miwili kabla ya kufunga mwaka wa fedha kwa ajili kupitisha makisio ya mapato na matumizi ya Chama

(f) Mkutano Maalumu utaitishwa muda unaohitajika Kifungu cha 37: Mkutano Mkuu wa Mwaka

(a) Utafanyika katika kipindi cha miezi sita baada ya kufunga mahesabu ya Chama (b) Mambo yafuatayo yatakayojadiliwa katika Mkutano Mkuu wa mwaka-

(i) Kuthibitisha akidi ya mkutano (ii) Kusoma na kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita kupokea na kufikiria mahesabu ya

fedha ya mwaka yaliyokaguliwa na mizania ya Chama, muhtasari wa taarifa ya menejimenti ya ukaguzi na taarifa nyingine.

(iii) Kugawa faida iliyokuwapo kwa ajili ya mgawano

Page 15: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

15

(iv) Kuboresha au kufanyia mabadiliko ya Masharti ya Chama (v) Kupanga viwango vya riba kwa ajili ya mikopo na akiba, (vi) Kuridhia ununuzi au uuzaji wa mali ya Chama inayozidi Tshs.1,500,000/= (vii) Kuweka thamani na kiasi cha hisa (viii) Kutoa maelekezo kwa Kamati za Chama (ix) Kuamua kiasi cha honararia, kama ipo, kwa watumishi wasiolipwa mishahara na wajumbe

wa Bodi (x) Kufikiria na kuidhinisha mpango wa kimkakati wa Chama, mpango wa biashara na

programu ya utekelezaji (xi) Kufikiria shughuli yo yote ambayo Bodi inaona inafaa

Kifungu cha 38 Mkutano Mkuu wa Kawaida

(a) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa kawaida angalao mara moja kila mwaka ndani ya miezi miwili (2) kabla ya kufunga mwaka wa fedha wa Chama.

(b) Mambo yanayoweza kujadiliwa na Mkutano Mkuu wa kawaida ni kama yafuatayo- (i) Kuthibitisha akidi ya mkutano (ii) Kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita (iii) Kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya utekelezaji kutoka kwenye Bodi (iv) Kupokea Wanachama wapya na kuwafukuza Wanachama wakorofi (v) Kujadili makisio ya mapato na matumizi ya Chama kwa kipindi cha mwaka unaofuata. (vi) Kuweka ukomo wa madeni (vii) Kuchagua, kufukuza na kusimamisha wajumbe wa Bodi na Kamati (viii) Kuteua Wanachama watakaowawakilisha Chama katika vyama na asasi nyingine

zinazohusika na maendeleo ya Chama (ix) Kufikiria na kukubali tafsiri na utekelezaji wa Sera ya Mendeleo ya Ushirika (x) Kuidhinisha mikataba na mapatano (xi) Shughuli nyinginezo kama itakavyoelekezwa na Bodi.

Kifungu cha 39: Mkutano Mkuu Maalum

(a) Mkutano unaweza kuitishwa kwa maombi ya zaidi ya theluthi moja ya Wanachama wote wa Chama angalao kutoka katika Matawi yasiyopungua sita. Lazima kuwe na sababu ya maombi ya mkutano yaliyotiwa saini na Wanachama wahusika katika taarifa, na kupeleka nakala kwa Mwenyekiti wa Chama. Endapo Mkutano Mkuu utakataa ajenda za mkutano, itabidi theluthi moja ya Wanachama walioitisha mkutano wawajibike kulipa gharama za mkutano huo.

(b) Mkutano Mkuu maalum unaweza kuitishwa kwa matakwa ya idadi kubwa ya wajumbe wa Bodi au Kamati ya Usimamizi.

(c) Bodi pia inaweza kuitisha Mkutano Mkuu maalum baada ya kugundua kuwa kuna nafasi mbili zilizowazi katika Kamati ya Usimamizi.

(d) Mkutano Mkuu maalum unaweza kuitishwa na Mrajis wa vyama vya ushirika. (e) Ni hoja tu zilizokuwa katika taarifa ya kuitisha Mkutano Mkuu maalum zitakazojadiliwa. Kifungu cha 40: Mkutano Mkuu Maalum Ulioitishwa na Mrajis

(a) Mrajis au mtu yeyote aliyepewa madaraka anaweza kuitisha Mkutano Mkuu maalum wa Chama kwa muda na mahali pa kufanyia mkutano. Vile vile, ataelekeza mambo ya kuzungumzia katika mkutano huo. Mkutano huo utakuwa na madaraka kamili na kwa mujibu wa Kanuni zilizotumika kuuitisha kwa mujibu wa Masharti ya Chama.

(b) Katika mkutano ulioitishwa na Mrajis wa vyama vya ushirika, idadi yo yote ya Wanachama waliohudhuria wataendesha mkutano na mambo yote yatakayojadiliwa na kuazimiwa yatakuwa halali

(c) Ni hoja tu zilizopo katika taarifa ya kuitisha mkutano maalum zitakazojadiliwa.

Page 16: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

16

Kifungu cha 41: Uwezo Maalum wa Mkutano Mkuu wa Chama

(a) Kwa mujibu wa kifungu kidogo (2) cha kifungu cha 61 cha Sheria, Mkutano Mkuu amekabidhiwa dhamana ya kisimamia utekelezaji wa majukumu kadhaa ya jumla.

(b) Mambo yafuatayo au zaidi yanapaswa kujadiliwa katika Mkutano Mkuu - (i) Kuthibitisha muhutasari wa Mkutano Mkuu uliopita na mkutano wo wote maalum (ii) Kupokea na kuthibitisha taarifa za Kamati za uongozi wa Chama (iii) Kuhakikisha kuwepo kwa uongozi imara pamoja na uendeshaji bora wa Chama (iv) Kusoma na kurekebisha na/au kuboresha Masharti pamoja na Kanuni na mwenendo wa

ndani (v) Kuchagua, kusimamisha na kuondoa madarakani wajumbe wa Bodi na Kamati waliokiuka

taratibu (vi) Kuanzisha akiba au mfuko maalum, hasa ulio na kinga na mfuko wa maendeleo. (vii) Kuthibitisha mahesabu na kutoa maamuzi kuhusu ziada halisi ya mwaka iliyopatikana (viii) Kutoa uamuzi wa kulipa mgao na motisha kwa ziada iliyopatikana. (ix) Kusoma na kupitisha makisio ya miradi ya Chama (x) Kusoma na kupitisha sera na taratibu za mikopo za Chama (xi) Kutengeneza muundo wo wote wa uongozi unaofaa (xii) Kuazimia kufanyika kwa uchunguzi juu ya mambo ya Chama (xiii) Kushughulikia jambo lolote la kiutawala na utekelezaji la Chama.

Kifungu cha 42. Uwezo maalum wa Mkutano Mkuu wa Tawi

(a) Katika ngazi ya Tawi, Mkutano Mkuu umepewa uwezo wa kusimamia utekelezaji wa majukumu kadhaa.

(b) Mkutano Mkuu ngazi ya Tawi una uwezo wa kufanya yafuatayo au zaidi- (i) Kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita (ii) Kupokea na kupitia taarifa za Bodi na maaumzi ya mikutano mikuu (iii) Kuchagua Mwenyekiti, Katibu, na mjumbe wa Kamati ya Tawi. (iv) Kuchagua Wawakilishi wa Tawi kulingana na Kifungu cha 36 ambao watahudhuria

mikutano mikuu ya Chama miongoni mwa Wanachama waajiriwa kutoka Shirika la Posta, Kampuni ya Simu, Benki ya Posta na Tume ya Mawasiliano.

(v) Kutoa maoni na mapendekezo yanayohusu Chama katika Tawi na kuyapeleka kwenye Bodi ili yajadiliwe kwenye Mkutano Mkuu

Kifungu cha 43: Kukasimu Madaraka

(a) Mkutano Mkuu unaweza kukasimu baadhi ya madaraka yake kwa Bodi na Kamati yoyote ya Chama.

(b) Hata hivyo, Mkutano Mkuu hauna uwezo wa kukabidhi baadhi ya madaraka yake kama kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita; kuthibitisha na/au kurekebisha na/au kuboresha Masharti; uchaguzi wa wajumbe wa Bodi; kuidhinisha mahesabu na makisio; kutoa uamuzi kuhusu ziada halisi ya mwaka.

Kifungu cha 44: Kuitisha Mkutano Mkuu

(a) Bodi ndiyo inayoitisha Mkutano Mkuu na pia inawajibika kuitisha Mkutano Mkuu kwenye ngazi ya Tawi.

(b) Kwenye ngazi ya Tawi, Mkutano Mkuu utafanyika si chini ya mwezi mmoja kabla ya ule Mkutano Mkuu wa Chama. Ajenda za kuzungumzia kwenye ngazi ya Tawi ni kama zilivyoainishwa katika kifungu cha 42 (b) cha masharti haya.

(c) Taarifa ya kuitisha (i) Mkutano Mkuu wa mwaka ni siku ishirini na moja (21) (ii) Mkutano Mkuu wa kawaida ni siku kumi na nne (14)

Page 17: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

17

(iii) Mkutano Mkuu maalum ni siku saba (7) (d) Taarifa hiyo itatangazwa kwenye mbao za matangazo ya Chama, matawi, kutuma barua au kutumia

taratibu nyinginezo zitakazofanikisha kuwafikia Wanachama. (e) Tangazo la mkutano litaonyesha nia, madhumuni na ajenda za mkutano na zinaweza kugawiwa kwa

kila Mwanachama kabla ya kuanza Mkutano Mkuu. (f) Taarifa ya mkutano lazima ionyeshe mahali, saa pamoja na ajenda za mkutano, ikiwa lazima itabidi

taarifa iambatane na muhtasari wa mwenendo wa uendeshaji wa ajenda. (g) Kukosa taarifa kwa Mwanachama yeyote kuhusu tarehe, muda na mahali pa kufanyia Mkutano

Mkuu si kigezo cha kutohalalisha kwa mkutano huo kuendelea au jambo lolote lililoletwa katika mkutano

Kifungu cha 45: Akidi (Korum)

(a) Akidi ya Mkutano Mkuu wa Chama ni Wanachama wawakilishi mia moja (100) au [theluthi mbili (2/3) ya Wanachama (wawakilishi wote waliopo waliochaguliwa kwenye ngazi ya Tawi) la sivyo idadi yoyote iliyo ndogo.

(b) Mkutano Mkuu wo wote wa Chama ngazi ya Tawi utakuwa mkutano halali pale tu Wanachama mia moja (100) au asilimia hamsini ya Wanachama wote wa Chama ngazi ya Tawi wamehudhuria, la sivyo idadi yoyote iliyo ndogo.

(c) Kwa mikutano mikuu ya mwaka na kawaida, ikiwa mahudhurio hayatoshi baada ya saa moja na nusu (dakika 90) ya muda uliopangwa, mkutano utaahirishwa kwa siku saba (7) na mambo yatakayozungumzwa ni yale yale ya mkutano ulioahirishwa. Katika Mkutano Mkuu huu, Wanachama waliohudhuria [(ngazi ya Tawi) au wawakilishi (ngazi ya Chama)] hawafikii akidi` na iwapo mahudhurio hayatoshi tena basi mkutano huo utahalalishwa kuendelea na maamuzi yake yatakuwa halali

Kifungu cha 46: Uwakilishi

Mwanachama haruhusiwi kuwakilishwa na mtu yeyote kwa niaba yake kwa mujibu wa kifungu cha 22 cha Kanuni Kifungu cha 47: Upigaji Kura

(a) Kila Mwanachama ana haki ya kupiga kura moja kwa mtu mmoja bila kujali ukubwa wa idadi ya hisa alizolipia.

(b) Upigaji kura utaendeshwa na Mwenyekiti wa Chama au Mwanachama aliyechaguliwa na mkutano husika. Upigaji kura utakuwa wa siri

(c) Maazimio hupitishwa na idadi iliyokubwa ya Wanachama waliohudhuria katika mkutano. Iwapo kutakuwepo na usawa wa matokeo ya kura kuhusu ajenda, basi itaahirishwa, kurudiwa au kufutwa

Kifungu cha 48: Uongozi , Maamuzi na Maazimio ya Mikutano

(a) Mwenyekiti wa Bodi ndiye huwa mwenyekiti wa mikutano mikuu yote ya Chama (b) Isipokuwa mikutano itakayoitishwa na Mrajisi, Mwenyekiti wa Bodi atakapokuwa hayupo,

Makamu Mwenyekiti ndiye atakayekuwa mwenyekiti wa mkutano na, kama wote hawapo, Mwanachama yeyote atakayechaguliwa na Mkutano Mkuu anaweza kuwa mwenyekiti wa mkutano.

(c) Kila uamuzi na azimio uliopitishwa na Mkutano Mkuu na/au mkutano maalum lazima uwe kwa maandishi na kuwekwa katika kitabu cha kumbukumbu katika makao makuu ya Chama

Kifungu cha 49: Mwenyekiti wa Chama

(a) Mwenyekiti wa Chama ni kiongozi kinara wa Chama aliyechaguliwa katika Mkutano Mkuu. Madaraka yake yanatokana na Mkutano Mkuu na hutoa taarifa kwa Mkutano Mkuu.

(b) Kazi za Mwenyekiti wa Chama ni –

Page 18: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

18

(i) Msemaji mkuu wa Chama (ii) Kiongozi wa Mkutano Mkuu na vikao vya Bodi. (iii) Mwajibikaji katika kuyafanyia kazi maamuzi yote ya Mkutano Mkuu na kuhakikisha

wanafikia malengo ya Chama. (iv) Kutekeleza kazi nyingine kwa mujibu wa madaraka au zile kazi maalum alizopewa na

Bodi. (v) Atakuwa mwakilishi wa vyombo na miundo mbalimbali iliyoundwa na Mkutano Mkuu

kwa kuteuliwa na Bodi. Kifungu cha 50: Makamu Mwenyekiti wa Chama

(a) Makamu Mwenyekiti wa Chama ni kiongozi msaidizi wa Chama aliyechaguliwa katika Mkutano Mkuu. Madaraka yake yanatokana na Mkutano Mkuu.

(b) Kazi za Makamu Mwenyekiti wa Chama ni – (i) Kuendesha mikutano na vikao vya Bodi. (ii) Atakuwa mwakilishi wa vyombo na miundo mbalimbali iliyoundwa na Mkutano Mkuu kwa

kuteuliwa na Bodi. (iii) Kutekeleza kazi nyingine na kazi maalum kama itakavyoamuliwa na Bodi.

Kifungu cha 51: Katibu wa Chama / Meneja

(a) Katibu atahakikisha kuwa kazi zote za sekretarieti kwa Mkutano Mkuu, Bodi na Kamati zinafanywa na kuhifadhi mihtasari yote.

(b) Kazi za katibu zitakuwa –

(i) Kupokea maombi ya kujiunga na uanachama. (ii) Kuandaa na kuhifadhi mihtasari ya Bodi na Kamati

(iii) Kutia saini kwenye hundi, hati za malipo, kumbukumbu za mikutano na nyaraka nyingine za Chama

(iv) Kutunza kumbukumbu na nyaraka za Chama (v) Kushiriki kikamilifu katika utawala wa shughuli za Chama

SEHEMU YA NANE: MUUNDO WA UONGOZI WA CHAMA

Kifungu cha 52: Muundo wa Bodi na Kamati

(a) Kwa mujibu wa kifungu cha 62 cha Sheria, Chama kilichosajiliwa kinapaswa kuunda Bodi kuongoza na kusimamia shughuli zake za kila siku.

(b) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) cha kifungu cha 63 cha Sheria kila Bodi ya Chama kilichosajiliwa itakuwa na wajumbe wasiopungua watano na wasiozidi tisa ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Kamati ya Mikopo kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bodi au kukasimu kazi hiyo kwa Bodi.

(c) Kwa kuzingatia kifungu cha 36 (c) cha Masharti haya nafasi za uongozi katika Bodi utakuwa katika muundo ufuatao: 4, 3 na 2.

(d) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) cha kifungu cha 78 cha Kanuni, Mkutano Mkuu pia utachagua Kamati ya Usimamizi ya wajumbe hadi watatu, ambao sio wajumbe wa Bodi.

(e) Kwa mujibu wa kifungu cha 32 (3) cha Kanuni, Mkutano Mkuu huchagua miongoni mwa Wajumbe Bodi na Kamati nyingine.

(f) Ili kuboresha mawasiliano kati na baina ya Wanachama, hasa ngazi ya matawi, kutakuwa na Kamati ya Tawi. Wajumbe wa Bodi moja kwa moja ni wawakilishi wa Tawi katika eneo lao

(g) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) na (3) cha 63 muda wa Bodi kuwa katika madaraka ni miaka hadi tisa isipokuwa kwamba, kwa wajumbe waliochaguliwa na mkutano wa kwanza wa Chama, theluthi moja itajiuzulu baada ya miaka mitatu tangu tarehe ya kuchaguliwa na nusu ya wajumbe waliobaki itajiuzulu mwaka wa sita na waliobakia mwaka wa tisa. Hivyo basi, Mkutano Mkuu utachagua theluthi ya wajumbe wa Bodi wapya mwisho wa miaka ya 3, 6 na 9.

(h) Sehemu ya tisa ya Masharti ya Chama inafafanua taratibu za uchaguzi wa viongozi wa Chama.

Page 19: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

19

Hata hivyo Mkutano Mkuu una uwezo wa kupunguza kipindi cha uongozi. Bodi itamfukuza mjumbe wa Bodi ya Chama kwa kushindwa kuhudhuria vikao vitatu (3) mfululizo bila sababu za msingi.

(i) Kwa mujibu wa kifungu 63(6) cha Sheria, hakuna mjumbe wa Bodi atakayekuwa madarakani kwa zaidi ya vipindi vitatu mfululizo lakini anaweza kustahili kuchaguliwa tena baada ya kupita kipindi kimoja cha miaka mitatu ambapo hakuwa madarakani

(j) Kwa ajili ya usimamizi mzuri, kuongeza ufanisi na kupunguza gharama wajumbe wa Bodi watachaguliwa kutoka miongoni mwa wawakilishi waliokuwa karibu na makao makuu ya Chama

Kifungu cha 53: Sifa za Mjumbe wa Bodi na Kamati

(a) Kila Mwanachama ana haki ya kupendekezwa na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi na Kamati za Chama alimradi awe na sifa zinazofaa.

(b) Sifa za mjumbe wa Bodi na Kamati ni zifuatazo- (i) Awe Mwanachama hai (ii) Awe ni kielelezo sahihi cha maadili mema kwa mujibu wa kifungu cha 9 ikiwa ni pamoja na

uadilifu, uaminifu, uwajibikaji, uwezo na kuwa na moyo wa kujituma na kujali wengine. (iii) Awe mjumbe wa Baraza la Wawakilishi. (iv) Awe na historia nzuri ya kutokuwa na sifa mbaya ya kushitakiwa au kuthibitika kutenda

kosa la jinai (v) Asiwe amewahi kuhukumiwa na kuwekwa kizuizini kutokana na makosa ya ubadhirifu

na/au matumizi mabaya ya fedha na/au kutiwa hatiana kulingana na Kanuni ya adhabu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

(vi) Asiwe amesimamishwa uanachama (vii) Asiwe amewahi kufukuzwa ujumbe wa Bodi ya Chama (viii) Asiwe mwajiriwa katika Chama (ix) Asiwe kiongozi au kuwa na wadhifa wa kuchaguliwa katika Chama cha kisiasa cha kitaifa (x) Iwapo Mwanachama ana mkopo kutoka kwenye Chama, asiwe na ucheleweshwaji wa

marejesho na/au sifa ya kuchelewesha malipo. Kifungu cha 54: Wajibu wa Wajumbe wa Bodi

(a) Kuendesha na kusimamia shughuli za Chama kidemokrasia chini ya misingi, njia na taratibu za ushirikiano kama ilivyoelekezwa katika kifungu cha 4 cha Sheria.

(b) Kujitahidi kukidhi mahitaji ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ya Wanachama na kuinua uelewa wao wa kisiasa

(c) Kuboresha hali ya maisha na ustawi wa Wanachama wake (d) Kuendeleza na kukuza elimu ya ushirika miongoni mwa Wanachama wake (e) Mjumbe wa Bodi/Kamati anawajibika kwa kosa lolote lililojitokeza wakati wa uendeshaji wa

majukumu ya Chama ama akiwa peke yake, au kwa pamoja (f) Hata kama muda wa madaraka umekwisha, mjumbe atawajibika mpaka hapo atakapochaguliwa

mjumbe mwingine au yeye kuchaguliwa tena (g) Kupungua kwa idadi ya wajumbe hakufuti uwezo na madaraka ya wajumbe waliobaki. (h) Kila Kamati itafanya kazi yake kwa mujibu wa Masharti na kujiepusha na kuingiliana madaraka na

kazi ya Kamati nyingine (i) Kamati zitahakikisha zinatumia madaraka yake ipasavyo katika utawala bora wa Chama kwa

mujibu wa Masharti, Sheria, Kanuni na maazimio yoyote yaliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Kifungu cha 55: Mihtasari, Nyaraka na Hati

(a) Kwa mujibu wa kifungu cha 119, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu wanaruhusiwa kutoa nyaraka au nakala zilizoidhinishwa za mwenendo wa ndani, Masharti, au mihtasari ya Mikutano Mikuu na vikao vya Bodi.

(b) Mwenyekiti na katibu wa Kamati nyingine zilizoteuliwa na Bodi wanaweza kutoa nyaraka au

Page 20: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

20

nakala za mikutano yao. (c) Watu wote hao wanapaswa kuwa na tabia ya kutunza siri za Chama. Kifungu cha 56: Chaguzi za Wajumbe wa Bodi/Kamati

(a) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi huchaguliwa na Mkutano Mkuu (b) Baada ya wajumbe wa Kamati kuchaguliwa, Kamati hufanya vikao kuchagua Mwenyekiti na

Katibu (c) Mkutano Mkuu una madaraka ya kupunguza au kusitisha muda wa viongozi hao (d) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, na katibu wa Bodi ya Chama pia ni Mwenyekiti, Makamu

Mwenyekiti na Katibu wa Chama K

ifungu cha 57: Kujiuzulu na Kusimamishwa

(a) Mjumbe yeyote anaweza kujiuzulu kutoka katika madaraka yake, hata hivyo taarifa ya maandishi ya kujiuzulu lazima ifikishwe kwenye Kamati yake

(b) Kujiuzulu kwake kunaanza mara moja tokea tarehe ya kukubaliwa kujiuzulu (c) Bodi ndiyo yenye mamlaka ya kusimamisha mjumbe kwa sababu zifuatazo –

(i) Kufuja rasilimali za Chama na/au kukosa uaminifu (ii) Kujihusisha na maamuzi ya kutoa mikopo bila kufuata sera au taratibu zilizokuwapo (iii) Kutoheshimu maamuzi ya Kamati yake husika, Bodi au Mkutano Mkuu (iv) Kuingilia madaraka ya Kamati nyingine (v) Kuwa na tabia ya kupotosha mwelekeo na hadhi ya Chama (vi) Kutokuheshimu Kanuni za maadili ya uongozi ya Chama (vii) Kutoa hati bandia kwa Chama au kwa niaba ya Chama (viii) Kuwa na malimbikizo ya ucheleweshaji wa mikopo kwa zaidi ya siku tisini (ix) Kutohudhuria kwa zaidi ya vikao vitatu vya Bodi, Kamati husika, Kamati ya Usimamizi,

Kamati ya Mikopo, Mkutano Mkuu wa mwaka, wa kawaida na maalum bila sababu za msingi

(x) Kukosekana kwa zaidi ya vipindi vitatu vya mafunzo aliyoalikwa (xi) Ikiwa yuko katika mgogoro wa maslahi baina yake na Chama.

(d) Baada ya kufanya uamuzi wake, Bodi itapeleka taarifa yake kwenye Mkutano Mkuu iliyoambatishwa na hoja pamoja na sababu zilizosababisha kufikia uamuzi ule

(e) Mjumbe aliyesimamishwa ana haki ya kupinga uamuzi huo kwa kukata rufaa kwa maandishi kwa Mwenyekiti wa mkutano akitoa hoja na sababu za utetezi wake. Mjumbe anaweza kujieleza mbele ya Mkutano Mkuu

(f) Mjumbe anaweza kuachishwa/kufukuzwa na Mkutano Mkuu maalum ikiwa tu aliarifiwa, kwa maandishi, sababu zilizofanya taarifa kuhusu suala hilo kuchelewa, hoja na sababu za kumwachisha/kumfukuza pamoja na mahali tarehe na muda wa kikao hicho

(g) Muhtasari wa kikao kilichomwachisha/kumfukuza lazima ueleze ukweli wa sababu zilizosababisha kufanyika uamuzi ule.

(h) Wiki mbili baada ya uamuzi wa kumwachisha/kumfukuza, Chama kitamwaarifu, kwa maandishi, mjumbe sababu za kuachishwa/kufukuzwa kwake.

(i) Kuachishwa/kufukuzwa kunasababisha kupoteza haki ya kufanya shughuli zo zote za Chama katika kipindi cha miaka mitano.

(j) Kusimamishwa kwa mjumbe kunasababisha kupoteza haki hizo wakati wa kipindi alichosimamishwa ambacho hakiwezi kuzidi miezi sita (6).

Kifungu cha 58: Stahili za Malipo kwa Wajumbe wa Bodi

(a) Shughuli zozote zinazofanywa na wajumbe wa Bodi hazina malipo ya mshahara au ujira. (b) Hata hivyo gharama zilizotumika katika uendeshaji wa Bodi, Kamati ya Mikopo au Kamati ya

Usimamizi zinaweza kulipwa kwa Masharti yaliyowekwa katika maamuzi ya Mkutano Mkuu. (c) Kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha Kanuni na kutegemea maelekezo ya ibara ya 21 ya Jedwali la

Page 21: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

21

Sheria, wajumbe wa Bodi wanaweza kulipwa honararia itakayoamuliwa na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu alimradi hali ya ukwasi inaruhusu.

Kifungu cha 59: Akidi ya Vikao

Akidi ya vikao vya Bodi, Kamati ya Mikopo, Kamati ya Usimamizi na (Kamati ya Tawi) ni zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya wajumbe wote. Kifungu cha 60: Maamuzi na Maazimio ya Vikao

(a) Maamuzi ya Bodi, Kamati ya Usimamizi na Kamati ya Tawi yatatokana na uwingi wa kura za wajumbe waliounga au kukataa. Kwa upande wa Bodi, kura zikilingana, Mwenyekiti ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho.

(b) Uamuzi wa Kamati ya Mikopo utokane na makubaliano ya Wajumbe wote. (c) Maazimio yaliyoandikwa na kutiwa saini na Wajumbe wote wa Kamati, yana hadhi sawa na

maazimio yale ya mikutano. (d) Maazimio hayo yanawekwa pamoja na mihtasari ya mikutano. SEHEMU YA TISA: UTARATIBU WA UCHAGUZI

Kifungu cha 61: Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi

(a) Kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Kanuni chaguzi zote zitafanyika chini ya Afisa Msimamizi wa uchaguzi ambaye atakuwa Mwenyekiti mwangalizi wa uchaguzi kama Mrajis atakavyo agiza.

(b) Uchaguzi utafanyika kwa njia ya kura ya siri, utakuwa wa kidemokrasia na hakuna atakayechaguliwa kwa hila au njia isiyokuwa ya halali.

Kifungu cha 62: Uteuzi wa Wagombea

(a) Kila Mwanachama anayetaka kugombea kuwa mjumbe wa Bodi atajaza fomu husika ambazo hutoa taarifa zifuatazo-

(i) Maelezo binafsi ya kina au historia binafsi na uzoefu katika uongozi wa ushirika (ii) Kumbukumbu ya uanachama wa ushirika ikionyesha sifa ya utendaji mzuri katika kutimiza

wajibu wa uanachama ilivyoagiziwa katika Sheria, Kanuni na Masharti (iii) Mchango anaotarajia kuutoa katika maendeleo ya Chama cha ushirika baada ya kuwa

kiongozi wa ushirika (iv) Kiwango cha elimu (v) Elimu ya ushirika aliyoipata, ikiwa ipo (vi) Aina ya biashara au shughuli zinazofanywa na Mwanachama (vii) Taarifa yo yote inayofikiriwa inafaa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi.

(b) Fomu zote zitapatikana katika ofisi ya Chama wakati wa saa za kazi siku ishirini na moja kabla ya Mkutano Mkuu wa kawaida au Mkutano Mkuu wa mwaka ambapo uchaguzi utafanyika.

(c) Fomu zote zilizojazwa ipasavyo zitarudishwa kwa Afisa Msimamizi wa Uchaguzi siku kumi na nne kabla ya mkutano wa kawaida au Mkutano Mkuu wa mwaka ambapo uchaguzi utafanyika

(d) Afisa Msimamizi wa Uchaguzi ataunda Kamati ya angalao watu wanne wenye uadilifu unaotambulika kuangalia kwa makini fomu na kutoa alama kwa kila mgombea, na Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Afisa Msimamizi wa Uchaguzi itapendekeza mbele ya mkutano wagombea wa kupigiwa kura kwa kufuata utaratibu ulioelekezwa na Mrajis;

(e) Kufuatia mapendekezo ya Kamati, Mkutano Mkuu utaamua orodha ya mwisho ya majina na kupiga kura

(f) Isipokuwa kwa wajumbe watakaochaguliwa katika uchaguzi wa kwanza wa Bodi, hakuna Mwanachama ambaye atastahili kuchaguliwa kwenye Bodi mpaka awe amehudhuria angalao mikutano mikuu miwili ya mwaka

Kifungu cha 63: Uchaguzi Mdogo

Page 22: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

22

Kwa kutumia kifungu cha 52 cha Masharti ya Chama, utaratibu wa uchaguzi mdogo utafanyika baada ya Mwanachama- (a) Kujiuzulu (b) Kufa (c) Kuishia madaraka ya Bodi (d) Kufukuzwa Kifungu cha 64: Upigaji wa Kura

(a) Upigaji kura katika chaguzi zote utakuwa kwa kura ya siri na kila Mwanachama atakuwa na kura moja.

(b) Kabla ya kupiga kura wakati wa uchaguzi wa wajumbe wa Bodi, kila mgombea atachagua wenzie wawili wenye haki ya kupiga kura lakini si wagombea kuwa wachambuaji kura.

(c) Mambo mengine ya kupigiwa kura wakati wa Mkutano Mkuu yataamuliwa kwa kunyoosha mikono isipokuwa kama Wanachama au wawakilishi walioudhuria wanataka uamuzi ufanyike kwa kura ya siri.

Kifungu cha 65: Kura za Uwakilishi

Kwa mujibu wa kifungu cha 22 cha Kanuni za vyama vya Ushirika, hakuna kura za uwakilishi au uwakilishi wa Mwanachama zitakazoruhusiwa. Kifungu cha 66: Kuhesabu Kura

(a) Mwenyekiti mwangalizi wa uchaguzi akisaidiwa na wachambuzi wa kura ndio watakaofanya zoezi la kuhesabu kura za kila mgombea.

(b) Matokeo ya uchaguzi yatawasilishwa kwa Mwenyekiti mwangalizi wa uchaguzi. Ikiwa kuna kura baina ya wagombea zilizolingana basi Mwenyekiti wa uchaguzi ataamuru uchaguzi urudiwe.

Kifungu cha 67: Uhakiki wa Kura

(a) Kwa kila Kamati Mwenyekiti mwangalizi wa uchaguzi atatangaza matokeo ya uchaguzi kwa kuanza na wagombea waliopata kura kidogo na kuendelea kutangaza hadi wagombea wote kwisha

(b) Baada ya hapo wasimamizi wataendelea na zoezi la kuhesabu kura kwa Kamati nyingine Kifungu cha 68: Kutangaza Rasmi Matokeo ya Uchaguzi

(a) Mwenyekiti mwangalizi wa uchaguzi ndiye anayetangaza matokeo rasmi ya kura. (b) Matokeo hayo lazima yaandikwe katika muhtasari wa mkutano. SEHEMU YA KUMI: UWEZO MAALUM WA BODI

Kifungu cha 69: Kazi na Madaraka ya Bodi

(a) Bodi ndiyo yenye dhamana ya uangalizi na usimamizi wa shughuli za kila siku (b) Kazi, majukumu na wajibu wa Bodi ni-

(i) Kufuata maelekezo Sheria, Kanuni na taratibu zilizomo, Nyaraka za Mrajis, Kanuni za Maadili na Masharti ya Chama.

(ii) Kuandaa mwenendo na taratibu za fedha zinazofaa ambazo ni lazima kutunza kumbukumbu sahihi na za kweli za shughuli za Chama

(iii) Kuhakikisha kwamba hesabu za Chama zinaandaliwa na kukaguliwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Masharti

(iv) Kutunza daftari ya orodha na saini za Wanachama (v) Kuwasilisha mbele ya Mkutano Mkuu wa mwaka taarifa ya hesabu za mapato na matumizi

zilizokaguliwa zikionyesha mapato na matumizi, mizania na vianzio na matumizi ya fedha (vi) Kuwezesha ukaguzi wa vitabu na ofisa aliyeidhinishwa kuvikagua

Page 23: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

23

(vii) Kuhakikisha kuwa mikopo inatumika kama ilivyoombwa na kuwa ina dhamana ya kutosha imetolewa kwa kila mkopo unaotolewa kwa mujibu wa Masharti ya Chama

(viii) Kuandaa mikataba ya muda maalum, mpango/taratibu za kazi za kuongoza na kutawala watumishi na waajiriwa

(ix) Kutafuta na kuandaa ajira ya Meneja na maafisa wengine wa Chama kwa mujibu wa Kanuni za utumishi;

(x) Kupitisha sera mbali mbali za kulinda mali za Chama na kutoa taarifa mara kwa mara kwa Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Masharti haya

(xi) Kusimamisha mjumbe wa Bodi ambaye hafuati maelekezo ya Sheria, Kanuni na Masharti kungojea uamuzi wa Mkutano Mkuu

(xii) Kutunza daftari ya mahudhurio ya Wajumbe wa Bodi (xiii) Kutunza vitabu vya mihtasari wa mikutano yote (xiv) Kutafsiri na kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Ushirika (xv) Kuandaa Mpango wa Kimkakati wa Shirika wa Chama, Mpango wa Biashara na programu

ya utekelezaji ya mwaka (xvi) Kuhakikisha kuwa riba zinazotozwa/kulipwa ziko ndani ya viwango vilivyowekwa kisheria (xvii) Kuandaa makisio na kuyawasilisha kwenye Mkutano Mkuu (xviii) Kuweka malengo maalum ya kifedha (xix) Kutoa mapendekezo juu ya mgao wa faida katika mwaka (xx) Kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu (xxi) Kutoa madaraka kwa meneja ya kusimamia bajeti. (xxii) Kutoa kwa Mkutano Mkuu taarifa ya shuguli za Chama. Taarifa hiyo ijumuishe taarifa za

Kamati (xxiii) Kutoa maamuzi ya rufaa za mikopo (xxiv) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu marekebisho ya Masharti. (xxv) Kuhakikisha kuwa mikopo inalipwa kulingana na taratibu zilizowekwa, kuchukuwa hatua za

kisheria kwa wakopaji wasiolipa (xxvi) kupanga saa za kazi katika Chama (xxvii) Kumaliza migogoro ya Chama kwa njia za maelewano (xxviii)Kudumisha na kulinda jina, sifa na taswira ya Chama (xxix) Kutekeleza lolote zuri kwa Chama. (xxx) Kujiepusha kuingilia moja kwa moja katika shughuli za kila siku za Meneja na watumishi. (xxxi) Kuteua mwakilishi wa Chama kwenye Taasisi mbalimbali

(c) Hivyo basi, maamuzi na maazimio yote yanayofanywa na Bodi yalenge kulinda na kuhifadhi maadili na hali bora ya kifedha ya Chama.

Kifungu cha 70: Mikutano ya Bodi

(a) Wajumbe wa Bodi wanakutana katika vikao baada ya kuitishwa na Mwenyekiti au idadi kubwa ya Wajumbe.

(b) Taarifa ya vikao lazima iwe kwa maandishi na kupelekewa wajumbe angalao siku tatu (3) kabla ya kufanyika kwa kikao hicho

(c) Taarifa hiyo lazima ionyeshe mahali, tarehe, saa na mambo yatakayozungumziwa katika ajenda. (d) Bodi ya Chama itakutana kila mwezi, lakini inaweza kufanya vikao vya dharura wakati wowote Kifungu cha 71: Mjumbe wa Bodi

(a) Mjumbe wa Bodi ni sehemu ya uongozi wa Chama uliokabidhiwa dhamana ya usimamizi wa shughuli za kila siku za Chama kwa mujibu wa Sheria na Kanuni

(b) Kwa sababu hiyo, anatakiwa kushiriki kwa ukamilifu kusaidia kufanikisha utekelezaji wa shughuli za Chama, hasa- (i) Kuhudhuria vikao vyote vya Bodi (ii) Kushiriki katika kuchanganua masuala mbalimbali yanayowasilishwa kwa ajili ya

Page 24: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

24

kuzingatiwa au kufanyiwa uamuzi.

Kifungu cha 73: Muundo, Kazi na Madaraka ya Kamati ya Mikopo

(a) Muundo na utaratibu wa Kamati ya mikopo utakuwa kama ifuatavyo- (i) Wajumbe wanne waliochaguliwa na Mkutano Mkuu. Wajumbe wa Kamati ya Mikopo

watamchagua Mwenyekiti wao na Katibu. (ii) Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo atakuwa anatoa taarifa za mara kwa mara kwenye

Kamati ya Mikopo kwa mikopo iliyotolewa, marejesho n.k. kulingana na maagizo na utaratibu uliowekwa na Chama

(iii) Kamati itafanya mikutano yake mara moja kwa mwezi na inaweza kukutana zaidi ya hapo kama itaonekana ni lazima. Utaratibu wa kuitisha vikao utaamuliwa na Bodi

(iv) Akidi ya vikao ni nusu ya wajumbe (v) Kamati itakasimu madaraka ya kutathmini maombi ya mikopo na kutoa mikopo ya dharura

kwenye Kamati ya Ufundi. Hata hivyo, mikopo hiyo lazima itolewe taarifa kwenye Kamati kwa ajili ya kuthibitishwa

(b) Kamati ya mikopo chini ya Bodi inatekeleza jukumu la kusimamia mikopo kwa mujibu wa sera na taratibu zilizopo za Chama. Hakuna mkopo utakaotolewa bila kufuata sera na taratibu zilizopo wala kuzingatia vigezo vitano (5) vilivyopo katika kifungu cha 108 (i).

(c) Kazi, majukumu na wajibu wa Kamati ya mikopo- (i) Kujadili maombi ya mikopo kama ilivyoletwa na Kamati ya Ufundi na kuhakikisha kuna

dhamana inayozidi mkopo na wadhamini wawili wenye jumla ya akiba inayozidi mikopo hiyo. Mikopo itatolewa baada ya wajumbe wote wa Kamati kukubaliana

(ii) Kuchambua na kuchunguza kwa uangalifu mwenendo na tabia ya kila mwombaji wa mkopo, hali ya kifedha dhamana na wadhamini alionao ili kujua uwezo wa kulipa na kuangalia ikiwa mkopo ni wa huduma au uzalishaji na jinsi gani atafaidika na mkopo huo.

(iii) Kufuatilia mikopo yote, na kuangalia kwamba mikopo hiyo inatumika kwa madhumuni yaliyoombewa na marejesho ya mikopo yanafuata utaratibu uliowekwa.

(iv) Iwapo kutakuwa na maombi mengi ya mikopo kuliko inavyoweza kulipwa na Chama kutokana na akiba iliyopo, kipaumbele/upendeleo utatolewa na Kamati ya Mikopo kwa waombaji wenye mikopo midogo kama maombi yalivyopokelewa na kama mahitaji ya mkopo pamoja na dhamana iliyotolewa inalingana na maombi ya mikopo mikubwa.

(v) Kuarifu Bodi bila kuchelewa wakati mkopo haujarejeshwa kwa mujibu wa mapatano na unapokuwapo ucheleweshwaji wa marejesho wa zaidi ya siku thelathini (30). Kamati inatoa mapendekezo kwenye Bodi juu ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi ya wakopaji wasiowajibika.

(vi) Hakuna mkopo utakaotolewa kwa Mwanachama kwa muda unaozidi miaka minne (4). (vii) Hakuna mtu atakayekopeshwa mkopo mpaka ameweka ushahidi wa kutosha kwamba

ataulipa mkopo huo. (viii) Wajumbe wa Kamati ya mikopo wanawajibika, mmoja mmoja na katika ujumla wao,

kifedha kwa makosa watakayoyafanya katika utekelezaji wa kazi zao. Ukiukaji wa sera utasababisha kufukuzwa mara moja kwa wajumbe wa Bodi waliohusika na uamuzi huo.

Kifungu cha 74: Utaratibu wa Kukata na Kusikiliza Rufaa Dhidi ya Kamati ya Mikopo

(a) Mwanachama asiyeridhika na uamuzi wa Kamati ya Mikopo anaweza kupinga uamuzi huo kwa maandishi na kupeleka rufaa yake kwa Bodi.

(b) Rufaa hiyo itasikilizwa kwenye kikao cha Bodi ambacho kitahudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo pamoja na mlalamikaji mahali na tarehe itakayopangwa. Kulingana na hali mjumbe anaweza kumwakilisha mwenyekiti wa Kamati ya mikopo.

(c) Bodi itafanya uamuzi wake kwa mujibu wa sera ya mikopo na taratibu za Chama.

Page 25: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

25

Kifungu cha 75: Rufaa Dhidi ya Uamuzi wa Kamati ya Mikopo

(a) Mwanachama ambaye ombi lake la mkopo limekataliwa anaweza kupinga uamuzi huo kwa kukata rufaa kwenye Bodi

(b) Baada ya kusikiliza rufaa, Bodi itafanya uamuzi wake kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa chini ya kifungu cha 74 cha Masharti haya.

(c) Endapo mwanachama hataridhika na maamuzi ya Bodi, atatakiwa kuwasilisha malalamiko yake katika Bodi.

Kifungu cha 76: Muundo, Kazi na Madaraka ya Kamati ya Usimamizi

(a) Muundo na utaratibu wa Kamati utakuwa kama ifuatavyo- (i) Wajumbe hadi watatu (3) waliochaguliwa na Mkutano Mkuu miongoni mwa wawakilishi na

itashirikisha wataalam pale inapohitajika, lakini bila haki ya kupiga kura. (ii) Wajumbe wa Kamati ya usimamizi hawatakuwa wajumbe wa Bodi: (iii) Kamati itakutana mara moja kila miezi mitatu (3)’ lakini itaweza kufanya vikao vya dharura

endapo italazimu. (b) Kamati ya Usimamizi itahakikisha kuwa -

(i) Inapitia malinganisho na uhakiki wa fedha taslimu na vigezo vingine vya mali. (ii) Bodi, Kamati na waajiriwa wanazingatia Sheria zinazotumika, taratibu, Masharti na sera

zilizokuwapo. (iii) Kumbukumbu za uhasibu na nyinginezo, pamoja na leja kadi za Wanachama na daftari ya

mikopo vinasimamiwa kwa uangalifu na usahihi upasao; (iv) Utawala na uongozi unahakikiwa mara kwa mara; (v) Kuna kuwa na ufuatiliaji juu ya mapendekezo yaliyomo katika taarifa ya usimamizi; (vi) Chama kinatoa mawasilisho yake ya utekelezaji wa maelekezo ya kifungu cha 125 cha

Sheria, ibara ya 10, 11 na 17(3) ya Jedwali la Sheria na kifungu cha 55 cha Kanuni. (vii) Kuhakikisha kwamba Chama kinafuata taratibu zilizowekwa katika utekelezaji wa shughuli

zake; (viii) Kuhakikisha kwamba vitabu vya hesabu vinatunzwa kwa usahihi na vinaandikwa mara kwa

mara; (ix) Kukagua kazi zote zilizokamilika katika Chama zikiwemo zile za uwekezaji na uwekaji

akiba za Wanachama (x) Kushauri Bodi na watendaji juu ya uendeshajii bora wa shughuli za Chama, kutoa maoni juu

ya hali ya fedha katika Chama na kutoa taarifa moja kwa moja kwa Wanachama katika Mkutano Mkuu

(xi) Kusimamia na kupokea taarifa ya Mkaguzi wa ndani atakapochaguliwa; (xii) Kuagiza kusimamisha utoaji wa mikopo wakati orodha ya mikopo iliyocheleweshwa

kurejeshwa haijatolewa kwa Wanachama mnamo wiki ya kwanza mwezi unaohusika kwa mujibu wa kifungu 102 (3) cha Kanuni.

(xiii) Kuridhia/kutoridhia mikataba na sababu zilizotolewa juu ya mikataba ya mikopo ambayo hailingani na Sheria, Kanuni na Masharti ama Sera za Chama.

(xiv) Kupitia upya sifa na uzoefu wa wafanyakazi kwa madhumuni ya kulinganisha na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa na Chama

(xv) Kuhakikisha kwamba maamuzi yaliyopitishwa na Mkutano Mkuu yanatekelezwa. (xvi) Kubuni mbinu ambayo itasaidia kupata malalamiko ama maoni ya Wanachama bila ya

kikwazo (xvii) Kuwaarifu Wanachama juu ya ubadhilifu uliofanywa na Bodi kwa kuitisha Mkutano Mkuu. (xviii) Kupendekeza kusimamishwa wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao, wanaoonyesha

kupotosha utaratibu wa Sheria, Masharti ya Chama au maamuzi ya Mkutano Mkuu. (xix) kuhakikisha mahesabu ya Chama yanakaguliwa kila mwaka (xx) Kupokea malalamiko kutoka kwa Wanachama.

Page 26: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

26

(c) Wakati wote mkaguzi huyo atakuwa na fursa ya kuona na kupitia vitabu na kumbukumbu za fedha na mahesabu pamoja na ushahidi mwingine na atakuwa na haki ya kutaka Bodi na waajiriwa wa Chama kumpatia kumbukumbu na taarifa yo yote ambayo anafikiri itakuwa ni ya msaada kumwezesha kutekeleza kazi zake

(d) Mkaguzi wa Mahesabu wa nje ana uwezo wa kutaka kikao cha Kamati yo yote ya Chama kuitishwa ili kuwasilisha au kuelezea taarifa

Kifungu cha 77: Malalamiko ya Wanachama na Maadili

Kamati ya Usimamizi pamoja na kazi zingine, hupokea malalamiko kutoka kwa Wanachama na kuyawakilisha katika Kamati husika ya Chama kwa kuyapatia majibu. Kifungu cha 78: Madaraka ya Kamati ya Usimamizi

(a) Kuhakiki na/au kukagua vitabu vya mahesabu, vitabu vya kumbukumbu na uendeshaji wa Chama. (b) Kuwa na haki ya kupata misingi ya kinga ya madeni na mali za Chama. (c) Kushirikisha wataalam na pia haki ya kupata ushahidi, vielelezo na taarifa nyingine muhimu. (d) Kusimamisha utoaji wa mikopo wakati-

(i) Mikopo iliyocheleweshwa kurejeshwa inazidi asilimia tano (5%) ya mikopo yote iliyotolewa;

(ii) Bodi inashindwa kutoa taarifa ya fedha katika muda uliowekwa; Kifungu cha 79: Wajibu wa Kamati ya Usimamizi

(a) Kuandika taarifa kwenye Bodi ya Chama iwapo itagundua uzembe wowote uliopo katika uongozi wa Chama

(b) Kuitisha Mkutano Mkuu maalum ikiwa itakadiria kuwa Bodi itachelewa kuchukua hatua zinazostahili.

(c) Kupeleka taarifa kwa Mrajis mapema iwezekanavyo ikiwa, katika Mkutano Mkuu maalum, suala ambalo ililolipeleka halikupatiwa ufumbuzi

Kifungu cha 80: Utoaji wa Taarifa ya Kamati ya Usimamizi

Ikifika mwisho wa mwaka wa fedha, Kamati itatayarisha taarifa ya utekelezaji na kuwasilisha mbele ya Mkutano Mkuu. SEHEMU YA KUMI NA MOJA: MUUNDO NA KAZI ZA TAWI

Kifungu cha 81: Muundo, Kazi na Madaraka ya Kamati ya Tawi

(a) Mkutano Mkuu utakuwa na uwezo wa kuamua juu ya uundaji wa matawi na utaratibu utakaotumika kuyafungua.

(b) Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Tawi ambao utahudhuriwa na Wanachama wote (c) Kutakuwa na Kamati ya Tawi yenye wajumbe watatu (3) waliochaguliwa na Mkutano Mkuu na

itakutana angalao mara nne kwa mwaka na kuweka kumbukumbu za vikao hivyo. (d) Wajumbe waliochaguliwa wataliwakilisha Tawi kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na wanaweza

kuchaguliwa tena. (e) Endapo kutatokea na upungufu wa mjumbe mmoja katika Tawi kutokana na uhamisho, kifo au

kutoka Chama nafasi hiyo itajazwa na mwanachama aliyefuatia kwa wingi wa kura katika ngazi husika.

(f) Kazi, Majukumu na Wajibu wa Kamati ya Tawi. (i) Kupokea nakala na orodha ya mikopo iliyoidhinishwa na Kamati ya Mikopo

(ii) Kuandaa mafunzo ya Wanachama kwa kushirikiana na Bodi (iii) Kupokea ushauri na kujadili malalamiko kutoka kwa Wanachama

(iv) Kuwa kiungo kati ya Bodi na Wanachama

Page 27: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

27

(v) Kutoa taarifa juu ya Chama. (vi) Kuwaarifu viongozi wa Chama juu ya mahitaji na maoni ya Wanachama. (vii) Kutoa elimu kwa Wanachama juu ya huduma mbali mbali za Chama na Masharti yake, sera

na taratibu za Chama. (viii) Kuhakikisha uaminifu, uadilifu, uwezo na tabia ya Mwanachama wa Tawi anayeomba

mkopo (ix) Kutafuta na kuhamasisha Wanachama wapya. (x) Kusaidia Bodi kushawishi Wanachama kutunza fedha zao kwenye Chama na kushawishi

urejeshwaji wa mikopo. (xi) Kuweka msisitizo maalum juu ya mwenendo/utendaji mzuri wa Chama ngazi ya Tawi ili

Kuhakikisha huduma zitakiwazo zinatolewa kwa Wanachama.. (xii) Kuhakikisha kwamba maamuzi ya Mkutano Mkuu yanafuatwa na kutekelezwa ipasavyo (xiii) Kufanya shughuli nyingine ambazo zina manufaa kwa Chama na Wanachama.

Kifungu cha 82: Mwenyekiti wa Kamati Ngazi ya Tawi.

(a) Mwenyekiti wa ngazi ya Tawi ni mmojawapo wa viongozi aliyechaguliwa katika uongozi wa Chama na ni kiongozi mwakilishi wa kwanza wa Chama kwenye ngazi hiyo

(b) Kwa ujumla Mwenyekiti atafanya yafuatayo- (i) Kuwa mwakilishi wa tawi kwenye Mkutano Mkuu. (ii) Kuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu ngazi ya Tawi na vikao vya Kamati ya Tawi (iii) Kuwajibika kusimamia maamuzi yote ya Bodi na kuhakikisha malengo ya Chama

yanafikiwa; (iv) Kufanya kazi nyingine kutokana na wajibu wake au alioagizwa na Tawi au Bodi

Kifungu cha 83: Katibu wa Kamati ya Tawi

(a) Katibu hufanya kazi za ukatibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi na Kamati ya Tawi na anawajibika kutunza mihtasari ya Kamati ya Tawi na Mkutano Mkuu wa Tawi.

(b) Kazi za Katibu zitakuwa- (i) Kupokea maombi ya uanachama (ii) Kutunza mihtasari ya Chama ya Mikutano Mikuu ya Tawi na Kamati (iii) Kushiriki katika shughuli za utawala za Chama ngazi ya Tawi (iv) Kuwa Mwakilishi wa tawi kwenye Mkutano Mkuu endapo Tawi litatakiwa kuwa na

mwakilishi zaidi ya mmoja. Kifungu cha 84: Mjumbe wa Kamati ya Tawi

Anawajibika kushiriki katika vikao vyote ya Kamati ya Tawi, kuchangia katika kuchambua maswala yote yaliyowasilishwa kwenye Kamati ya Tawi na kushiriki katika majukumu ya Kamati ya Tawi.

Kifungu cha 85: Kikao cha Kamati ya Tawi

(a) Kamati ya Tawi itakutana baada ya kikao kuitishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Tawi au kutokana na uwingi wa wajumbe waliohitaji kikao

(b) Taarifa ya kuitisha kikao itakuwa ya maandishi na kupelekwa kwa wajumbe angalao siku tatu (3) kabla ya tarehe ya kikao

(c) Taarifa ya kuitisha kikao lazima ionyeshe mahali pa kufanyia kikao, tarehe na muda wa kuanza kikao pamoja na ajenda za kujadiliwa

(d) Kamati ya Tawi itafanya kikao angalao mara moja kila baada ya miezi mitatu Kifungu cha 86: Uwasilishaji wa Taarifa kwenye Mkutano Mkuu wa Tawi

Kamati ya Tawi inawajibika kuwasilisha taarifa ya mwaka ya Chama kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka ngazi ya Tawi.

Page 28: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

28

SEHEMU YA KUMI NA MBILI: UENDESHAJI NA UONGOZI

Kifungu cha 87: Uongozi

(a) Bodi ya Chama itaajiri Meneja na Watumishi wengine wa Chama wenye taaluma kwa mujibu wa taratibu na Kanuni za utumishi (Scheme of Service).

(b) Bodi ya Chama itapanga mshahara na marupurupu ya Meneja. Kifungu cha 88: Madaraka na Kazi za Meneja

(a) Meneja wa Chama atafanya shughuli chini ya usimamizi wa Bodi (b) Meneja atakuwa na wajibu kama ilivyoainishwa katika Kanuni za utumishi Kifungu cha 89: Viongozi

(a) Viongozi ni watu waliokabidhiwa dhamana ya uongozi, usimamizi na udhibiti katika Chama (b) Hawa ndio wanakuwa wawakilishi wa Wanachama. (c) Huwa macho, masikio, walinzi na pua za Wanachama. Kifungu cha 90: Utunzaji wa siri wa Hali ya Juu Viongozi wanawajibika kutunza siri. Wanaweza kuwasiliana kuhusu habari za Chama juu ya shughuli au Wanachama tu katika mipaka iliyomo katika Kanuni za Maadili ya uongozi. Kifungu cha 91: Migongano ya Kimaslahi (a) Ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka na ionekane inatendeka, panahitajika uangalifu mkubwa na

jitihada za makusudi kustawisha mazingira yanayohakikisha kuwa shughuli zote zinaendeshwa kwa haki, ukweli na uwazi.

(b) Ili kupunguza uwezekano wa kufanya kazi kwa upendeleo wakati wa kufanya maamuzi, kusikiliza rufaa au kutoa adhabu, kiongozi hawezi kuwa na kauli ya uamuzi katika masuala ya mikopo ama yanayomhusu mwenyewe binafsi au mtu mwenye uhusiano naye. Aidha kiongozi hawezi kuhudhuria mkutano/kikao au kushiriki katika kikao/mkutano wenye uwezo kutoa maamuzi yanayomhusu.

(c) Kipengele hiki pia kinamuhusu kiongozi ambaye ni mdau mwenye maslahi binafsi katika kampuni iliyokuwa na uhusiano wa kibiashara na Chama hali ambayo inasababisha mgongano wa kimaslahi na Chama kwa mujibu wa ibara ya 12 ya Jedwali la Sheria. Kiongozi huyo anawajibika kutangaza mali yake katika kampuni hiyo kwa mujibu wa ibara ya 11 ya Jedwali la Sheria na kifungu kidogo (2) cha kifungu cha 55 cha Kanuni.

Kifungu cha 92: Tamko Kuhusu Mali Binafsi ya Afisa

Katika kipindi cha miezi mitatu (3) baada ya kuchaguliwa na baada ya kila Mkutano Mkuu, mjumbe wa Bodi analazimika kutoa Tamko kuhusu Mali zake kwa mujibu wa maelekezo yaliyotajwa katika kifungu cha 91.Tamko na orodha vitawakilishwa kwenye Kamati ya Usimamizi SEHEMU YA KUMI NA TATU: UHASIBU

Kifungu cha 93: Mwaka wa Fedha

Mwaka wa fedha wa CHAMA utakuwa Januari Mosi hadi Desemba 31 kila mwaka. Kifungu cha 94: Utunzaji wa Hesabu

(a) Chama kina wajibu wa kutunza na kutoa mara kwa mara mahesabu ya shughuli zake na Wanachama, pamoja na miamala mbalimbali na taarifa ya mtiririko wa fedha

(b) Kila tukio la mahesabu ya shughuli linapofanywa linatakiwa liingizwe katika vitabu vya mahesabu ndani ya siku moja (1) za kazi kutoka siku ya tukio

(c) Chama kinapaswa kufuata utaratibu uliokubalika na ‘Tanzania Financial Accounting Standards (TFAS)’

Page 29: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

29

(d) Taarifa za fedha na ripoti za takwimu zinatakiwa kuandaliwa kila mwisho wa mwezi na kuwa tayari katika siku kumi (10) za kalenda baada ya mwisho wa mwezi huo

Kifungu cha 95: Utoaji Taarifa ya Mwaka

(a) Baada ya kumalizika mwaka wa fedha, Chama kinatakiwa kutoa taarifa yake ya mwaka kuhusu utekelezaji wa kazi zake

(b) Mbali na taarifa inayohusu shughuli nyingine za Chama, taarifa ya mwaka ya Chama itakuwa ni pamoja na taarifa ya mahesabu iliyothibitishwa na Mkutano Mkuu na yaliyotolewa kwa mujibu wa viwango maalum

(c) Taarifa na Mahesabu ya fedha vitawasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Chama ndani ya kipindi cha miezi sita (6) tokea kuisha mwaka wa fedha

(d) Iwapo Chama kinashindwa kutayarisha taarifa za mahesabu katika kipindi cha miezi mitatu (3) tokea kwisha kwa mwaka wa fedha wa shughuli zake, wajumbe wa Bodi husika moja kwa moja watapoteza haki yao ya ujumbe. Aidha, hawatastahili kuchaguliwa tena kuwa wajumbe kwa kipindi cha miaka sita (6) ijayo kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (7) cha kifungu cha 48 cha Sheria

Kifungu cha 96: Ukaguzi wa Hesabu na Udhibiti

(a) Uendeshaji pamoja na shughuli zote za Chama vinategemewa kukaguliwa na Mkaguzi wa Mahesabu wa nje anayejitegemea angalao mara moja kila mwaka.

(b) Ukaguzi wa mwaka au ukaguzi wa mahesabu wa shughuli za Chama kama inavyotakiwa na Sheria utajumuisha mkaguo na tathmini ya uanachama, muundo wa uongozi, hisa na amana, faida ilivyotozwa, malinganisho ya fedha, benki, hisa, mikopo na amana, mikopo iliyochukuliwa na malipo.

(c) Ukaguzi wa mwaka na ukaguzi wa mahesabu wa shughuli za Chama utajumuisha ukaguzi na tathmini ya kila mkopo ulioonyeshwa vitabuni ili kuweka matazamio ya malipo na iwapo dhamana inatosha na ni nzuri na ni hatua gani ya ziada itakuwa lazima kuhakikisha malipo ya mwisho.

Kifungu cha 97: Udhibiti na Uhakiki

(a) Kazi na shughuli za Chama zinategemewa kufanyiwa udhibiti na uhakiki wa kushitukiza na wa bila kutazamiwa wala taarifa ya awali angalao mara moja kila mwaka ili kuwezesha na kuhakikisha uhakiki wa kutegemea ushahidi wa papo kwa papo

(b) Udhibiti huu unagusa vipengele vyote vinavyohusu muundo na uendeshaji wa Chama kama vile vipengele vya Sheria, Masharti na taratibu za ndani zinazokiongoza

(c) Udhibiti na uhakiki utajielekeza katika mambo yafuatayo- (i) Faida ya kifedha, viwango, sera na taratibu (ii) Kuaminika kwa shughuli za mahesabu (iii) Ufanisi wa udhibiti wa ndani (iv) Utekelezaji wa matakwa ya kawaida ya utawala na uendeshaji, viwango, sera na taratibu

zilizopo (v) Sera na taratibu za ushirika.

Kifungu cha 98: Taarifa Kuhusu Hitilafu na Mashaka

(a) Hitilafu na mashaka yaliyogundulika wakati wa ukaguzi na uhakiki vinapaswa kutolewa taarifa itakayoambatanisha mapendekezo na kupelekwa kwenye Bodi na au Kamati ya Usimamizi ya Chama.

(b) Katika muda wa kipindi cha siku thelathini (30) baada ya hitilafu hizo kugundulika, nakala ya taarifa hiyo ipelekwe katika Chama

Kifungu cha 99: Rasilimali (a) Chama kitajijengea raslimali yake na kujenga raslimali hiyo ni wajibu wa Chama.

Page 30: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

30

(b) Kwa mujibu wa kifungu 67 cha Kanuni- (i) Sio chini ya asilimia ishirini (20%) ya ziada yote iliyowekwa katika mwaka wowote

itatengwa katika fedha taslimu na kuwekwa katika Mfuko wa akiba ya lazima (ii) Asilimia kumi na tano (15%) itaingizwa katika hesabu ya tengo la madeni mabaya na

madeni yenye mashaka kurejeshwa ilimradi hesabu hiyo haizidi asilimia kumi na tano (15%) ya madeni yote.

(iii) Asilimia isiyozidi kumi na tano (15%) ya ziada ya mwaka itatengwa katika fedha taslimu kudumisha Mfuko wa Kuhamishia Hisa ilimradi Mfuko huo hautazidi asilimia kumi na tano (15%) ya mtaji wa msingi/kiasasi kwa ajili ya kukombolea hisa za Wanachama wanaojitoa au uanachama wao umeishia

(iv) Asilimia kumi (10%) kwa ajili ya Mfuko wa Elimu

(c) Baada ya kufikia kiwango, kutenga fedha kwa jili ya Mfuko wa Akiba ya Lazima, Mfuko wa Kuhamishia Hisa na tengo kwa ajili ya Madeni Mabaya na Madeni yenye Mashaka ya kurejeshwa, Bodi itapendekeza mbele ya Mkutano Mkuu ikiwa faida ni nzuri kugawanya kiasi kilichobaki-

(i) Malipo ya gawio au mapato ya hisa kwa Wanachama (ii) Kugeuza hisa za Wanachama kuwa mtaji (iii) Mchango kwenye mfuko wa maendeleo (iv) Mchango kwa ajili ya hisani, afya au kusudi lingine kwa mujibu wa kifungu cha 79 cha

Sheria (v) Malipo ya honararia kwa wajumbe wa Bodi.

(vi) Malipo kwa njia nyingine iliyoidhinishwa na Mkutano Mkuu Kifungu cha 100: Mtaji Unaokidhi na Dhima (a) Chama lazima kijenge mtaji usiopungua asilimia ishirini (20%) ya mali zote (b) Mtaji huo utajengwa kutokana na-

(i) Hisa (ii) Hisa za kudumu (iii) Akiba ya lazima (iv) Akiba nyingine zilizowekwa na Mkutano Mkuu (v) Ruzuku (vi) Malimbikizo ya Ziada (vii) Mfuko wa Dhamana (viii) Mfuko wa Mshikamano (ix) Mfuko wa Maendeleo (x) Mfuko wa Elimu

Kifungu cha 101: Mgao wa Ziada na/au Motisha (a) Hakuna mgao wa ziada na/au motisha utakaotangazwa na kulipwa ikiwa utasababisha kupungua

kwa kiwango cha mtaji unaokubalika kwa mujibu wa kifungu cha 100 cha Masharti haya. (b) Chama kitatangaza na kulipa motisha na/au mgao wa ziada ikiwa faida ipo ya kutosha. Hakuna

mgao wa ziada na/au motisha utakaotangazwa na/au kulipwa iwapo kiwango cha mtaji hakijafikiwa kwa mujibu wa kifungu cha 67 cha Kanuni.

Kifungu cha 102: Kufanya Shughuli Tofauti na za Akiba na Mikopo (a) Isipokuwa kama Mkutano Mkuu utatoa azimio maalum, Chama hakiruhusiwi kutumia fedha yoyote

kuanzisha au kuendesha shughuli yoyote isipokuwa za Akiba na Mikopo ambazo ni za manufaa kwa Wanachama au laa, matumizi hayo yasizidi asilimia tano (5%) ya mtaji wa Chama

(b) Kimsingi tahadhari inaeleweka kuwa ni madeni (mikopo, akiba, wadai na kadhalika) pamoja na mihadi iliyothibitishwa kwa saini ya Chama.

Kifungu cha 103: Ukomo wa Madeni Ukomo wa madeni wa CHAMA hautazidi mara mbili ya Akiba zilizowekwa na Wanachama.

Page 31: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

31

Kifungu cha 104: Uwezo wa Mali kulipa Dhima Kutokana na mtaji wa Chama, sherti Chama kiwe na uwezo wakati wowote kinapotumia rasilimali ya muda mrefu na mfupi kwa kulipa madeni. Kifungu cha 105: Kiwango cha juu cha Utoaji Mkopo kwa Mwanachama Chama hakiwezi kutoa mkopo kwa Mwanachama binafsi zaidi ya - (a) Asilimia nane (8%) ya mtaji uliolipwa, ziada na akiba ya Chama (b) Asilimia kumi (10%) ya jumla ya akiba ya Wanachama. Kifungu cha 106: Utoaji Mikopo kwa Wajumbe wa Bodi, kamati ya Usimamizi na Watendaji

Wakuu. (a) Mikopo yoyote itakayotolewa na Chama kwa wajumbe wa Bodi, watendaji wakuu na watu wote

ambao wana uwezo wa kuingilia maamuzi ya utoaji mikopo, lazima mikopo hiyo iidhinishwe na Kamati ya mikopo kwa uamuzi wa pamoja wa wajumbe wote wa Kamati hiyo.

(b) Mikopo hiyo kwa mujibu wa kifungu hiki haitazidi asilimia ishirini (20%) ya akiba ya Wanachama. (c) Mikopo yoyote ya Chama inayotolewa kwa wajumbe wa Bodi, Kamati ya Usimamizi na Watendaji

wakuu wa Chama, walioomba mikopo inayozidi thamani ya hisa yao na akiba kwa ajili ya dhamana, itabidi ipate idhini kwa kura zote zitakazopigwa, wakati yeye mwombaji hayupo kutoka kwa hawa wafuatao - (i) Kwa idadi kubwa ya wajumbe wa Kamati ya Mikopo (ii) Wajumbe wawili au zaidi wa Bodi.

Kifungu cha 107: Ukwasi (a) Vitega uchumi na uwezo wa kupata pesa wa muda mfupi wa Chama lazima wakati wote

viwakilishe angalao asilimia kumi (10%) ya mali zote na isipungue asilimia kumi na tano (15%) ya akiba na hisa za Wanachama.

(b) Chama lazima kiimarishe na kuongeza uwezo wa urejeshwaji wa mali ya muda mfupi sana hadi kufikia kiwango cha upeo wake.

(c) Chama kinaweza tu kuhifadhi fedha taslimu kulingana na hali halisi ya mazingira ya nyenzo ya hifadhi salama ya fedha inavyoruhusu. Fedha zitahifadhiwa katika kasiki inayofaa hadi zitakapohitajika chini ya uangalizi wa meneja

(d) Chama lazima kiwe na sera ya ukwasi ili kujihakikishia mapato kwa kadiri inavyowezekana na kupunguza kabisa hatari mbali mbali. Ni aina ya kwanza tu ya vitega uchumi kama vile hati ya mawekezo na amana za SACCOS ndizo ziruhusiwe

(e) Mali ya Chama ya muda mfupi hairuhusiwi kutumika katika mambo yasiyokuwa na uhakika, ya kubahatisha na ya kilanguzi kama vitega uchumi.

Kifungu cha 108: Ubora wa Mali na Uangalizi wa Mikopo na Kinga Dhidi ya Mikopo (a) Chama lazima kitenge fungu la akiba kwa ajili ya madeni mabaya kwa mujibu wa kifungu cha 99 (b) Uwiano wa kiwango cha tahadhari unategemea aina ya mikopo ya kila mwezi. Chama kitaweka

taarifa sahihi, yakinifu na zinazokwenda na wakati kuhusu vitega uchumi, dhamana ya mikopo na zinazonyesha mwenendo wa malimbikizo ya mikopo

(c) Chama kitaweka na kutekeleza sera ya ufutaji madeni mabaya, kitashughulikia mara moja kutowajibika kwa Wanachama wanaoshindwa kurejesha mikopo yao na haraka kitachukua hatua za makusudi kufuatilia Wanachama wasiowajibika kwa kutorejesha mikopo yao mapema.

(d) Mikopo iliyocheleweshwa kurejeshwa kwa zaidi ya siku tisini (90) inatakiwa iwe kwa kiwango kilichokuwa chini ya asilimia tano (5%) ya kiwango cha mikopo iliyotolewa.

(e) Taarifa ya kila mwezi ya Chama itaonyesha orodha ya mikopo iliyocheleshwa kurejeshwa na malimbikizo ya mikopo kwa kila mkopo kama ifuatavyo- (i) Thamani ya mikopo ya jumla iliyotolewa ambayo bado kurejeshwa (ii) Masharti ya urejeshwaji na kiwango cha riba kama ilivyokubaliwa na mkopaji (iii) Thamani ya mkopo na awamu/mikupuo ya malimbikizo iliyochelewesha (iv) Tarehe ya mwisho ya malipo ya malimbikizo yalipofanyika

Page 32: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

32

(v) Thamani ya hisa na akiba ya mwenye malimbikizo katika Chama (vi) Maelezo kuhusu dhamana, kama ipo (vii) Makisio ya thamani ya dhamana kwa ajili ya mkopo ambao marejesho yake

yamelimbikizwa (viii) Thamani halisi ya mkopo wenye marejesho yaliyolimbikizwa baada ya kupunguza thamani

ya hisa na akiba yake aliyopangia na mkopo wenye malimbikizo ya marejesho (f) Orodha iliyotajwa hapo juu itatayarishwa katika kipindi cha muda wa siku thelathini (30) baada ya

muda unaohusika na orodha hiyo itatiwa saini na meneja kwa uthibitisho kuwa ni saini na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bodi na nakala itapelekwa kwa Mrajis mara moja.

(g) Kila mwaka Chama lazima kiweke uangalifu mkubwa juu ya mikopo ili kuhakikisha uendeshaji na usimamizi angalifu na wa busara. Hapa ni sera ya kinga ya madeni kwa SACCOs- (i) Ucheleweshi wa siku 1 – 30 = 10% ya thamani halisi ya mikopo bado kulipwa. (ii) Ucheleweshi wa siku 31 – 90 = 25% ya thamani halisi ya mikopo bado kulipwa. (iii) Ucheleweshi wa siku 91 – 180 = 50% ya thamani halisi ya mikopo bado kulipwa. (iv) Zaidi ya siku 181 = 100% ya thamani halisi ya mikopo bado kulipwa. (v) Mikopo mingineyo = 1% ya thamani halisi ya mikopo bado kulipwa. (vi) Mikopo bado kulipwa ambayo iko katika mashaka (hatari), kukokotolewa kwa kupunguza

mikopo isiyocheleweshwa jumla ya hisa na mawekezo ya lazima ya Mwanachama katika SACCOS.

(h) Ucheleweshwaji wa urejeshwaji wa mikopo unaozidi siku tisini (90) unapofikia kiwango cha kuwa asilimia tano (5%) ya mikopo iliyotolewa, Chama lazima kichukue hatua za haraka kudhibiti ubora wa madeni hayo. Ucheleweshaji huo unapofikia asilimia kumi (10%) ya mikopo iliyotolewa, Menejimenti ya Chama inalazimika kusimamisha utoaji wa mikopo ya aina yote.

(i) Tathmini ya mikopo lazima izingatie vigezo vifuatavyo- (i) Tabia, (ii) Uwezo, (iii) Dhamana/Mtaji,

(iv) Mtiririko wa Fedha (v) Hali Halisi ya Uchumi.

(j) Uwezo wa Chama wa kukopesha hauwezi kuwa zaidi ya asilimia themanini na tano (85%) ya mali zote.

Kifungu cha 109: Muundo wa Uendeshaji (a) Chama lazima kifuatilie mara kwa mara, na sio chini ya mara moja katika kipindi cha robo mwaka,

mambo yafuatayo- (i) Faida halisi juu ya mikopo (mapato dhidi ya matumizi) (ii) Kinga dhidi ya hasara inayoweza kutokea (iii) Uongozi mzito ambao ni mzigo na hauna ufanisi [mapato yasiyo ya fedha dhidi ya

matumizi] (iv) Uwezo wa kumudu fedha

(v) Usimamizi wa mtaji wa msingi (vi) Usimamizi wa masuala ya kodi

(b) Menejimenti ya Chama lazima ifuatilie mara kwa mara na sio chini ya mara moja katika kipindi cha robo mwaka viashirio vya hali ya utendaji wa kiasasi na kifedha.

(c) Chama lazima kiweke mfumo wa utoaji taarifa unaowezesha kupatikana habari sahihi na za uhakika kuhusu- (i) Utengenezaji wa faida (ii) Ufanisi (iii) Ubora wa vitega uchumi na mali (iv) Ukuaji (v) Kupanuka na kuenea ili kuwafikia walengwa wengi

(d) Mizania ya Chama inatakiwa kuwa katika muundo ufuatao- (i) Kwa upande wa mali-

Page 33: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

33

Fedha taslimu na katika benki: zisiwe chini ya asilimia kumi (10%) ya mali na asilimia kumi na tano (15%) ya akiba za Wanachama

Vitega uchumi: visiwe zaidi ya asilimia kumi na tano (15%) ya mali Mikopo kwa Wanachama: isiwe zaidi ya asilimia themanini na tano (85%) ya mali Mali ya kudumu na mali nyingine zisizotumika katika uzalishaji: zisiwe zaidi ya asilimia

kumi (10%) ya mali zote. (ii) Kwa upande wa madeni na mtaji:

Akiba za Wanachama: zisiwe zaidi ya asilimia thamanini (80%) ya mali. Mikopo kutoka benki na/au deni katika akaunti ya benki na madai mengine: isiwe zaidi

ya asilimia kumi na tao (15%) ya mali Mtaji wa msingi usiwe zaidi ya asilimia kumi na tano (15%) ya mali.

Kifungu cha 110: Mapato na Kujiendesha kwa Faida (a) Chama lazima kiendeshwe kwa faida. Kiwango cha kujiendesha kwa faida kinapatikana baada ya

kutoa uchakavu, tengo kwa ajili ya mahitaji ya siku za baadaye, matukio yasiyotarajiwa, hasara na kodi.

(b) Hesabu ya faida lazima ionyeshe bayana mchango wa ruzuku kusudi uwezekano wa kuondoa ruzuku uweze kukadiriwa.

(c) Kila huduma inayotolewa na Chama lazima ithamanishwe ili kufidia gharama na kuleta ziada ya kutosha. Katika kukadiria thamani hiyo, Menejimenti ya Chama lazima izingatie yafuatayo- (i) Kiwango cha gharama za uendeshaji (ii) Kiwango cha juu cha hasara ya mikopo inayotarajiwa (iii) Gharama za fedha (iv) Kima cha kuweka mtaji kinachopendelewa

(d) Endapo shughuli za Chama haziendeshwi kwa faida na/au kima cha bei zilizotumika hakiruhusu kupatikana faida inayoridhisha ili kufikia kiwango cha mtaji unaotakiwa na kuhakikisha maendeleo bora ya kiasasi na kifedha, Chama lazima kichukue hatua za haraka kudhibiti na kurekebisha hali hiyo. Kutokana na (d) hatua hizo zinaweza kuwa- (i) Kuimarisha na kuboresha udhibiti wa gharama za uendeshaji na utawala (ii) Kuongeza viwango vya bei ya huduma zinazotolewa ili kupata faida. (iii) Mchanganyiko wa njia zote mbili.

Kifungu cha 111: Taarifa za Hesabu na Uwasilishaji wake kwa Mrajis na Benki Kuu ya Tanzania.

(a) Kwa mujibu wa kifungu cha 101 cha Kanuni, Bodi za kila Chama kilichosajiliwa cha Ushirika cha akiba na mikopo zinatakiwa kuandaa taarifa za Hesabu na kuziwasilisha kwa Mrajis na Benki Kuu ya Tanzania.

(b) Taarifa hizo ni mizania ya mwaka na taarifa ya mapato ya mwaka mpaka siku ya mwisho ya mwaka wa fedha kama ifuatavyo:- (i) Kama mali ya Chama haizidi shilingi 100,000,000/= (shilingi milioni mia moja), Chama

hicho kitaandaa taarifa ya kifedha na kitakwimu ya kila mwezi na kuziwasilisha kwa Mrajis; (ii) Kama mali inazidi shilingi 100,000,000/= (shilingi milioni mia moja), zaidi ya taarifa ya

kifedha na kitakwimu ya kila mwezi, Chama hicho pia kitaandaa seti nzima ya taarifa za kifedha mpaka siku ya mwisho ya mwaka wa fedha kama ilivyoagiziwa katika Viwango vya Utunzaji Mahesabu vilivyotolewa na Bodi ya Wahasibu na

Wakaguzi; (iii) Kama mali inazidi shilingi 200,000,000/= (shilingi milioni mia mbili), zaidi ya kukidhi

Masharti yaliyotajwa katika ibara ya (i) na ya (ii) kila Chama pia kitakamilisha seti nzima ya taarifa za kifedha kila miezi sita katika mwaka wa fedha;

(iv) Kama mali inazidi shilingi 500,000,000/= (shilingi milioni tano), zaidi ya kukidhi Masharti katika ibara ya (i) na (ii) kila Chama pia kitakamilisha seti nzima ya taarifa za kifedha kila

Page 34: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

34

miezi minne katika mwaka wa fedha; (v) Vyama vyote vya ushirika vya akiba na mikopo chini ya maelekezo ya (iii) na (iv) vitatuma

taarifa za kifedha kwa Mrajis zilizotiwa saini na idadi kubwa ya wajumbe wa Bodi na Kamati ya usimamizi sio zaidi ya siku thelathini ya tarehe zilizotajwa katika ibara ya (i) hadi ya (iv);

(vi) Vyama vya ushirika chini ya ibara za (iii) na (iv) vinatakiwa kupeleka taarifa ya hesabu zake kwenye Kurugenzi ya Huduma Ndogo za Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania.

(c) Kwa mujibu wa ibara ya (c) ya kifungu cha 82 cha Kanuni, Chama cha ushirika cha akiba na mikopo kitaweka amana katika benki, au asasi ya kifedha inayosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania au dhamana zilizotolewa na Serikali au Benki Kuu ya Tanzania kiasi ambacho sio chini ya asilimia ishirini (20 %) ya akiba na amana zote.

SEHEMU YA KUMI NA NNE: MENGINEYO Kifungu cha 112: Hatua za Kushughulikia Migogoro (a) Isipokuwa kama kutakuwa na mgogoro wa mahitaji ya mikopo, migogoro yoyote inayohusu kati ya

Mwanachama na Chama itapelekwa kwa Bodi kwa njia ya hati ya maandishi ya malalamiko yaliyoainishwa habari zake kwa ufupi

(b) Bodi itatathimini uhalali wa malalamiko kwa mujibu wa sera za Chama na taratibu, madhumuni, malengo, kabla ya kuitaarifu Bodi ya Chama.

(c) Mwanachama kama hataridhika na maamuzi ya Bodi ataruhusiwa kukata rufaa kwenye Bodi na taarifa ya maandishi.. Kiongozi yeyote au mtumishi aliyehusishwa na malalamiko hayo anaweza kuitwa.

(d) Bodi itatoa uamuzi juu ya mgogoro huo kwa mujibu wa maamuzi yanayoongozwa na sera na taratibu za Chama.

(e) Ikiwa Mwanachama hataridhishwa na uamuzi wa Bodi ya Chama basi anaweza kulifikisha suala lake mbele ya Mkutano Mkuu wa Chama.

(f) Mgogoro wowote unaohusu Masharti au huduma za Chama hiki ambao unashindikana kuamuliwa utafikishwa kwa Mrajis kwa maamuzi. (g) Zaidi ya hapo itabidi apeleke malalamiko yake kwa Waziri wa Ushirika ambaye uamuzi wake

utakuwa wa mwisho.

Kifungu cha 113: Muda unaotakiwa kutoa Uamuzi juu ya Malalamiko (a) Malalamiko yoyote yaliyowasilishwa mbele ya mamlaka ya Chama isipokuwa kwa Mkutano Mkuu,

ufumbuzi wake unatakiwa upatikane katika kipindi cha miezi miwili tokea siku ya kupokea malamiko. Mwanachama aliyelalamika lazima apewe majibu yake kwa maandishi.

(b) Malalamiko yoyote yaliyowasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu lazima yapatiwe majibu katika Mkutano Mkuu unaofuata ikiwa malalamiko hayo yaliwasilishwa miezi miwili kabla ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu huo.

Kifungu cha 114: Ufilisi (a) Uamuzi wa juu wa kuvunja Chama ndio utakaosababisha kufilisi Chama. (b) Kitakachofuata ni uteuzi wa mfilisi kwa mujibu wa Sheria inayotawala. (c) Ufilisi utafanyika kufuatana na Sheria Sehemu ya XIV na Kanuni Sehemu ya X. Kifungu cha 115: Mgao wa Ziada baada ya Ufilisi (a) Baada ya kumaliza zoezi la ufilisi, ikiwa kuna ziada iliyobaki, basi Mkutano Mkuu unaweza

kuamua kutenga katika fungu la kuwarejeshea Wanachama hisa. (b) Mgao wa ziada, baada ya ufilisi, unaweza kulipwa kwa Wanachama. (c) Ikiwa kuna baki yoyote ya fedha baada ya hisa kurejeshwa, msaada unaweza kutolewa kwa jumuia

yoyote inayotambuliwa ya kujitolea.

Page 35: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

35

Kifungu cha 116: Vitabu na Daftari (a) Chama, kwa mujibu wa maelekezo chini ya kifungu cha 117, 118 na 119 ya Masharti ya Chama,

kinatakiwa kuonyesha aina ya vitabu na kumbukumbu na yaliyomo vinavyotakiwa vitunzwe katika makao makuu ya Chama

(b) Hata hivyo, Wanachama wataruhusiwa kuangalia, kupitia vitabu na kumbukumbu hizo. Kifungu cha 117: Maudhui ya Daftari la Wanachama (a) Chama kitaweka katika makao makuu yake Kitabu cha Kumbukumbu (b) Kitabu hiki kitaonyesha kumbukumbu zifuatazo -

(i) Masharti na uamuzi wa Usajili na Msajili. (ii) Kanuni za ndani (Masharti). (iii) Muhutasari na maazimio ya Mkutano Mkuu. (iv) Mihtasari ya vikao na maazimio ya Bodi, Kamati ya Mikopo na Kamati ya Usimamizi. (v) Orodha ya viongozi inayoonyesha Jina, Anuani, makazi ya mjumbe na taarifa

zinazoonyesha tarehe ya kuingia na kutoka madarakani. (vi) Orodha inayoonyesha, majina na anuani ya mwisho inayojulikana kwa Wanachama wote wa

Chama. (vii) Maelezo ya kununua kila hisa pamoja na tarehe iliyolipwa, iliyorejeshwa au kuhamishwa. (viii) Orodha ya viwango vya bei ya Chama kwa huduma mbalimbali zinazotolewa. (ix) Mpango wa utekelezaji wa kifedha, kiutawala n.k wa Chama

(x) Makubaliano ya uongozi na jumuia zingine kama yapo. (xi) Hati ya utambulisho na/au mawasiliano ya kibiashara na jumuia nyingine kama yapo. (xii) Sheria na Kanuni za Ushirika na Nyaraka za Mrajis (xii) Na nyaraka muhimu nyinginezo

Kifungu cha 118: Utunzaji wa Vitabu na Kumbukumbu Nyinginezo (a) Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Posta na Simu kitatunza katika makao makuu yake

vitabu na kumbukumbu nyinginezo (b) Vitabu na Kumbukumbu hizo ni-

(i) Vitabu, vya kumbukumbu na kumbukumbu za miamala ya hesabu za mwisho kwa ajili ya kutengeneza mizania.

(ii) Taarifa za mahesabu zinazoonyesha hesabu za kila siku za Mwanachama kwa shughuli au tukio lolote na Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Posta na Simu pamoja na/au baki ya hesabu ya madeni au madai.

Kifungu cha 119: Wanachama Kutazama Vitabu na kupata Taarifa (a) Mwanachama anayo haki ya kupitia vitabu vya kumbukumbu kwa mujibu wa aya ya i, ii, iii. v na

viii za kifungu cha 117 ya Masharti haya. (b) Mwanachama kupata taarifa au nakala za kumbukumbu zilizoainishwa katika aya i. ii. iii. v. viii za

kifungu cha 117 ya Masharti haya. (c) Kwa matumizi ya kifungu cha 39 cha Masharti ya Chama, Wanachama wanaotaka kuitisha

Mkutano Mkuu usio wa kawaida wanaweza kupata nakala ya orodha ya Wanachama kama ilivyoainishwa katika aya ya (vi) ya kifungu cha 117.

(d) Chama kitatoza ada ya gharama za kuchapisha na usambazaji wa kumbukumbu hizo. Kifungu cha 120: Sera za ndani na Taratibu (a) Mfumo wa madaraka na uongozi wa Chama upo kwa mujibu wa sera za ndani na taratibu

zilizowekwa na Chama. (b) Baadhi ya sera hizo ni -

(i) Sera ya Utawala (ii) Sera ya Fedha (iii) Sera ya Mikopo (iv) Sera ya Utumishi

Page 36: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

36

(v) Sera yaVifaa na Vitendea kazi (vi) Sera ya Hifadhi ya Muda Mfupi sana ya Mali na Vitega Uchumi. (vii) Sera za Usalama (Dhamana) (viii) Sera za Uangalizi wa Ndani (ix) Sera za Kuimarisha Mtaji (x) Sera za Utengenezaji wa Faida (xi) Sera za Uangalizi wa Mikopo na Kinga Dhidi ya Mikopo Mibaya (xii) Sera za Muundo wa Mizania na Matumizi ya Mali (xiii) Sera za Uongozi (xiv) Na kadhalika

Kifungu cha 121: Kuidhinisha Masharti Masharti haya ya sasa yalipitishwa na angalao theluthi mbili (2/3) ya waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika ______________________________________________ tarehe Kifungu cha 122: Usajili na Marekebisho ya Masharti (a) Masharti haya yametengenezwa katika nakala nne, nakala moja kwa ajili ya ofisi ya Mrajis wa

Vyama vya Ushirika, nyingine kwa ajili ya ofisi ya Afisa Ushirika ya wilaya na nakala mbili ni kwa ajili ya Chama ambazo zitatunzwa makao makuu ya Chama.

(b) Yataambatishwa na orodha ya viongozi na watumishi ikionyesha sifa zao binafsi na makazi yao. (c) Kama kuna kuboresha na/au kufanya marekebisho ya Masharti lazima yapitishwe na Mkutano

Mkuu kwa maamuzi ya idadi ya theluthi mbili (2/3) ya Wanachama waliohudhuria na kupiga kura. (d) Baada ya kuboresha na kurekebisha Masharti yakiambatana na orodha ya viongozi na watumishi

lazima yawasilishwe mbele ya ofisi ya Mrajis katika muda wa mwezi mmoja tokea tarehe ya Mkutano Mkuu uliopitisha marekebisho hayo.

Kifungu cha 123: Utekelezaji wa Masharti Utekelezaji wa Masharti haya ya sasa unaanza tangu tarehe yalipopitishwa na kuchukua nafasi ya yale ya zamani. Kifungu cha 124: Kuvunjwa kwa Chama (a) Chama kitavunjwa kutokana na maamuzi ya idadi ya juu ya theluthi mbili (2/3) ya Wanachama

wote waliohudhuria katika Mkutano Mkuu usio wa kawaida. (b) Sababu za kuvunjwa ni -

(i) Amri ya Mrajisi wa vyama vya ushirika chini ya Sehemu ya XIV ya Sheria (ii) Ikiwa idadi ya Wanachama itapungua chini ya kiwango kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha

Sheria. (iii) Ikiwa Chama kimesimama kufanya kazi/shughuli zake katika kipindi cha mwaka wa fedha. (iv) Ikiwa Chama kimeshindwa kufanya mikutano mikuu ya Wanachama na kutoa taarifa zake

za mwaka katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo. (v) Ikiwa angalao robo tatu (3/4) ya Wanachama wote wameomba kukivunja.

(c) Kuvunjwa huko lazima kuheshimu Sheria ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2003.

Page 37: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

37

HATI

Sisi tuliojiorodhesha na kutia saini

Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Jina________________________________Umri_________ saini_________________________ Wanachama wanathibitisha kuwa Masharti haya yalipitishwa kwa mujibu wa kifungu cha 123 cha Masharti kinachoonyesha kuwa angalao theluthi mbili (2/3) ya Wanachama waliokuwapo katika Mkutano Mkuu walipiga kura ya kuunga mkono, uliofanyika siku ya________________________ Tarehe_________________________________ Mahali.________________________________ . Katibu wa Chama______________________ Mwenyekiti wa Chama_________________

Page 38: MASHARTI YA CHAMA - POSTA NA SIMU SACCOSpostanasimusaccos.co.tz/Documents/kk_pdf/katiba.pdf“Matawi” maana yake sehemu ambazo ni maeneo ya ngazi ya awali na ya msingi ya shughuli

38

Tarehe_______________________________ Tarehe______________________________

Masharti ya Posta na Simu Savings and Credit Cooperative Society Limited