12
Toleo Namba 19 Julai 2011 Je, wanawake watatimiza kanuni zote za kijinsia zilizomo katiba mpya? H uku utekelezaji wa katiba mpya ukianza kwa dhati ku- fuatia kuteuliwa kwa Jaji Mkuu mpya na majaji wa Mahakama Kuu, hali ya wasiwasi imetanda kuhusi- ana na utekelezaji kikamilifu wa katiba hiyo mpya. Kama serikali haitajitokeza na mbinu za kuhakikisha kupatikana kwa kanuni ya kila upande wa kijinsia usiwe na chini ya thuluthi moja kwenye afisi za umma, nchi hii huenda isitekeleze kwa ukamilifu maagizo ya katiba ya kuhakiki- sha kwamba hakuna upande wowote wa kijinsia ambao utawakilishwa na chini ya thuluthi moja ya waakilishi katika mas- wala ya uwakilishi na utoaji maamuzi. Kama ilivyo sasa watu wengi wakiwemo Wakenya hawawezi kufafanua kanuni ya thuluthi moja na kama wanawake wanad- hamiria kufikia kiwango cha viti 116 katika bunge la taifa, basi kuna haja ya kuzindua kampeini ya nchi nzima kuwaelimisha umma kuhusu ni kwa nini safari hii Wak- enya ni lazima waheshimu kanuni ya thu- luthi moja kama inavyotaka katiba mpya. Nchi hii haiwezi kujikita katika ma- hali pake sahihi katika Umoja wa Mataifa kama nafasi ya zaidi ya asilimia 50 ya idadi ya raia wake ambao ni wanawake haz- itashirikishwa katika mamlaka ya uongozi na uwakilishi, na kushughulikiwa kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2012. Ni wazi na hata uchunguzi umefany- wa na benki ya Ulimwengu na kuonyesha kwamba ukiwapa wanawake na wanaume nafasi sawa , hata uchumi utaelekea ka- tika mwelekeo bora. Kwa mfano Rwanda imeongoza na kuwa kielelezo chema na imeutangulia ulimwengu kuhusiana na uongozi wa wanawake na sasa uchumi wake unastawi kwa kasi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote barani Afrika. Kwa hivi sasa katika kanda hii Kenya ndiyo inayoshika mkia katika masuala ya uwakilishi wa wanawake na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Kenya ina nafasi ya kurekebbisha jambo hilo. Kwa hivyo kilichofanyika kuhisiana na uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu ambapo kanuni ya thuluthi moja ya waak- ilishi haikufanikishwa ni dalili mbaya kwamba utekelezaji wa katiba mpya un- afanyywa kama kwamba shughuli zinaen- deshwa kama kawaida. Vibaya zaidi ni kwamba jambo hili li- metokea katika jaribio la kwanza wakati wa uteuzi wa Jaji Mkuu, Mkuu wa Sheria, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, na Msimamizi wa Bajeti ambapo wanawake waliachwa nje ya nyadhifa hizo. Wanawake lazima wana hofu kuhusi- ana na ukiukaji na uivunjaji huowa haki za kikatiba za wanawake juu ya usawa na kuto- baguliwa katika misingi ya kijinsia. Hali hii kama itaachwa kuendelea itazidi kupanua pengo la utovu wa usawa kati ya wanawake na wanaume katika nyadhifa za uongozi. Tunashikilia msimamo kwamba ka- nuni yoyote ya kikatiba, ambayo inai- dhinisha utekelezaji wa hatua yoyote ni lazima ifanyiwe ufafanuzi unaostahili am- bao utatokana na katiba yenyewe, historia ya kikatiba na hali halisi ilivyo. Kanuni ya wingi wa thuluthi mbili ya jinsia moja katika kifungu cha 27 (7)haki- paswi kueleweka visivyo. Maswala ya wanawake kuhusu bajeti ya 2011 Na Joyce Chimbi B ajeti ya kitaifa iliyosomwa mwaka huu na Waziri wa Fedha ambaye pia ni Maka- mu Waziri Mkuu Mheshimi- wa Uhuru Kenyatta, mnamo tarehe 8 mwezi Juni ina mtazamo tofauti ka- bisa na bajeti zilizotangulia kwa kuwa ilijitahidi kushughulikia maswala ya wanawake. Kwa muda mrefu, umaskini mi- ongoni mwa mwanawake umechu- kuliwa kama chombo cha kuelezea kima ambacho umaskini umewaathiri wanawake. Lakini bajeti ya mwaka huu ambayo ilihusisha kiasi cha shi- lingi trilioni 1.16 iliweka mambo wazi kwa vile ilijaribu kushughulikia swala la haki za binadamu ambalo lina- kokotezwa katika katiba mpya. Chuo Kikuu Wanawake walifurahia hasa sekta za kilimo na huduma muhimu na bidhaa muhimu. . Akizungumzia kuhusu bajeti hiyo na kuisifu kuwa inayomtilia maanani masikini, Ed- win Omondi ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu alisema, “Kuon- dolewa kwa ushuru wa mafuta ya taa ni muhimu sana kwa sababu bid- haa hiyo ni muhimu katika maboma mengi hapa nchini na hasa katika sehemu za mashambani ambako asil- imia 70 ya Wakenya huishi.” Matamshi hayo kadhalika yanaweza kuzungumziwa kuhusiana na mafuta ya dizeli ambayo bei yake ilishuka kufuatia kupunguzwa kwa ushuru wa uagizaji mafuta hayo. Mafuta hayo ni muhimu pia kwa sababu yanategemewa sana katika upande wa usafiri ambapo vyombo vingi vya kusafiria hutegemea mafuta hayo. Kupungua kwa ushuru wa bidhaa hiyo kuna maana ya kughuka kwa gharama za usafiri. Hali ya umaskini wa wanawake haimaanishi kwamba ni sawa kwa wa- naume kuwa maskini ina maanisha kwamba kuna haja ya kutafuta mbinu za kukabiliana na kuongezeka kwa viwango vya umas- kini. Kwamba harakati za kupambana na umaskini ni lazima zitambue hali za kijinsia , anael- ezea James Kahara ambaye ni mshauri wa mambo ya pesa. Kihara anaendelea kueleza kwamba haja ya kuwa na bajeti in- ayotambua haki za kijinsia ni jambo la kimsingi ambalo linapasa kutiliwa maanani kwa sababu wanawake na wanaume hujikuta katika umaskini katika hali mbali mbali. Matamshi yake yanatiliwa nguvu na taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la Habitat ambapo wanawake na wanaume waliombwa kutayarisha mambo ambayo yanafaa kupewa kip- aumbele katika kuishi maisha bora. Wanaume katika taarifa hiyo io- likuwa ni nadra kutaja maji na vifaa vya kujinadhifisha, ilhali wanawake waliotoa maoni yao walitaja vitu hivyo kuwa maswala muhimu. Mam- bo ambayo wanawake na wanaume wanayapa nafasi ya kwanza katika maswala ya ghharama ya maisha huongozwa zaidi na majukumu ya kijinsia ya wahusika hao . Ni kwa sababu hiyo ndipo bajeti im- eonekana kushughulikia tofauti hizo za kijinsia , na kwa kufanya hivyo kushu- ghulikia mahitaji ya wote wanawake na wanaume jambo ambalo ni muhimu katika kuangamiza umasikini. Inatia moyo sana kuona kwamba serikali imetenga kima kikubwa cha pesa , yaamni shiklingi milioni mia tatu kuagiza vifaa vya usafi wa akina mama, yaani pamba ya kusitiri hali zao. Tumnafahamu kwamba wana- funzi wengi wanaohitaji usaidizi hukosa masomo kwa wiki nzima kila mwezi kwa sababu ya kukosa pamba hiyo ya kujistiri wakati wa hedhi, ael- eza Anita Njoki mkazi wa mtaa wa Makadara. Athari zake pia zitaifikia sekta ya usafiri ambako wengi wa Wakenya hutegemea usafiri wa umma ambako Akina mama wakiuza vyakula aina mbali mbali katika soko moja la mjini. Wanawake ni miongoni mwa wale watakaonufaika kutokana na bajeti kuu ya kitaifa iliyosomwa na Waziri wa Fedha, Bw Uhuru Kenyatta (picha kulia) ambaye alitenga kiasi cha Sh 100 bilioni kwa mambo ya kilimo. “Ni jambo la kutia moyo kuona kwamba serikali ilitenga kiasi cha Sh 300 milioni kwa taulo za kujikimu” — Anita Njoki, mkazi wa mtaa wa Madaraka TAHARIRI Angalia Uk.4

Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

  • Upload
    others

  • View
    35

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

1 Toleo Namba 19 • Julai 2011 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Je, wanawake watatimiza kanuni

zote za kijinsia zilizomo katiba mpya?

Huku utekelezaji wa katiba mpya ukianza kwa dhati ku-fuatia kuteuliwa kwa Jaji Mkuu mpya na majaji wa Mahakama

Kuu, hali ya wasiwasi imetanda kuhusi-ana na utekelezaji kikamilifu wa katiba hiyo mpya. Kama serikali haitajitokeza na mbinu za kuhakikisha kupatikana kwa kanuni ya kila upande wa kijinsia usiwe na chini ya thuluthi moja kwenye afisi za umma, nchi hii huenda isitekeleze kwa ukamilifu maagizo ya katiba ya kuhakiki-sha kwamba hakuna upande wowote wa kijinsia ambao utawakilishwa na chini ya thuluthi moja ya waakilishi katika mas-wala ya uwakilishi na utoaji maamuzi.

Kama ilivyo sasa watu wengi wakiwemo Wakenya hawawezi kufafanua kanuni ya thuluthi moja na kama wanawake wanad-hamiria kufikia kiwango cha viti 116 katika bunge la taifa, basi kuna haja ya kuzindua kampeini ya nchi nzima kuwaelimisha umma kuhusu ni kwa nini safari hii Wak-enya ni lazima waheshimu kanuni ya thu-luthi moja kama inavyotaka katiba mpya.

Nchi hii haiwezi kujikita katika ma-hali pake sahihi katika Umoja wa Mataifa kama nafasi ya zaidi ya asilimia 50 ya idadi ya raia wake ambao ni wanawake haz-itashirikishwa katika mamlaka ya uongozi na uwakilishi, na kushughulikiwa kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2012.

Ni wazi na hata uchunguzi umefany-wa na benki ya Ulimwengu na kuonyesha kwamba ukiwapa wanawake na wanaume nafasi sawa , hata uchumi utaelekea ka-tika mwelekeo bora. Kwa mfano Rwanda imeongoza na kuwa kielelezo chema na imeutangulia ulimwengu kuhusiana na uongozi wa wanawake na sasa uchumi wake unastawi kwa kasi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote barani Afrika.

Kwa hivi sasa katika kanda hii Kenya ndiyo inayoshika mkia katika masuala ya uwakilishi wa wanawake na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Kenya ina nafasi ya kurekebbisha jambo hilo.

Kwa hivyo kilichofanyika kuhisiana na uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu ambapo kanuni ya thuluthi moja ya waak-ilishi haikufanikishwa ni dalili mbaya kwamba utekelezaji wa katiba mpya un-afanyywa kama kwamba shughuli zinaen-deshwa kama kawaida.

Vibaya zaidi ni kwamba jambo hili li-metokea katika jaribio la kwanza wakati wa uteuzi wa Jaji Mkuu, Mkuu wa Sheria, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, na Msimamizi wa Bajeti ambapo wanawake waliachwa nje ya nyadhifa hizo.

Wanawake lazima wana hofu kuhusi-ana na ukiukaji na uivunjaji huowa haki za kikatiba za wanawake juu ya usawa na kuto-baguliwa katika misingi ya kijinsia. Hali hii kama itaachwa kuendelea itazidi kupanua pengo la utovu wa usawa kati ya wanawake na wanaume katika nyadhifa za uongozi.

Tunashikilia msimamo kwamba ka-nuni yoyote ya kikatiba, ambayo inai-dhinisha utekelezaji wa hatua yoyote ni lazima ifanyiwe ufafanuzi unaostahili am-bao utatokana na katiba yenyewe, historia ya kikatiba na hali halisi ilivyo.

Kanuni ya wingi wa thuluthi mbili ya jinsia moja katika kifungu cha 27 (7)haki-paswi kueleweka visivyo.

Maswala ya wanawake kuhusu bajeti ya 2011

Na Joyce Chimbi…

Bajeti ya kitaifa iliyosomwa mwaka huu na Waziri wa Fedha ambaye pia ni Maka-mu Waziri Mkuu Mheshimi-

wa Uhuru Kenyatta, mnamo tarehe 8 mwezi Juni ina mtazamo tofauti ka-bisa na bajeti zilizotangulia kwa kuwa ilijitahidi kushughulikia maswala ya wanawake.

Kwa muda mrefu, umaskini mi-ongoni mwa mwanawake umechu-kuliwa kama chombo cha kuelezea kima ambacho umaskini umewaathiri wanawake. Lakini bajeti ya mwaka huu ambayo ilihusisha kiasi cha shi-lingi trilioni 1.16 iliweka mambo wazi kwa vile ilijaribu kushughulikia swala la haki za binadamu ambalo lina-kokotezwa katika katiba mpya.

Chuo KikuuWanawake walifurahia hasa sekta

za kilimo na huduma muhimu na bidhaa muhimu. . Akizungumzia kuhusu bajeti hiyo na kuisifu kuwa inayomtilia maanani masikini, Ed-win Omondi ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu alisema, “Kuon-dolewa kwa ushuru wa mafuta ya taa ni muhimu sana kwa sababu bid-haa hiyo ni muhimu katika maboma mengi hapa nchini na hasa katika sehemu za mashambani ambako asil-imia 70 ya Wakenya huishi.”

Matamshi hayo kadhalika yanaweza kuzungumziwa kuhusiana na mafuta ya dizeli ambayo bei yake ilishuka kufuatia

kupunguzwa kwa ushuru wa uagizaji mafuta hayo. Mafuta hayo ni muhimu pia kwa sababu yanategemewa sana katika upande wa usafiri ambapo vyombo vingi vya kusafiria hutegemea mafuta hayo. Kupungua kwa ushuru wa bidhaa hiyo kuna maana ya kughuka kwa gharama za usafiri.

Hali ya umaskini wa wanawake haimaanishi kwamba ni sawa kwa wa-naume kuwa maskini ina maanisha kwamba kuna haja ya kutafuta mbinu za kukabiliana na kuongezeka kwa viwango vya umas-kini. Kwamba harakati za kupambana na umaskini ni lazima zitambue hali za kijinsia , anael-ezea James Kahara ambaye ni mshauri wa mambo ya pesa.

Kihara anaendelea kueleza kwamba haja ya kuwa na bajeti in-ayotambua haki za kijinsia ni jambo la kimsingi ambalo linapasa kutiliwa maanani kwa sababu wanawake na wanaume hujikuta katika umaskini katika hali mbali mbali.

Matamshi yake yanatiliwa nguvu na taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la Habitat ambapo wanawake

na wanaume waliombwa kutayarisha mambo ambayo yanafaa kupewa kip-aumbele katika kuishi maisha bora.

Wanaume katika taarifa hiyo io-likuwa ni nadra kutaja maji na vifaa vya kujinadhifisha, ilhali wanawake waliotoa maoni yao walitaja vitu hivyo kuwa maswala muhimu. Mam-bo ambayo wanawake na wanaume wanayapa nafasi ya kwanza katika maswala ya ghharama ya maisha huongozwa zaidi na majukumu ya kijinsia ya wahusika hao .

Ni kwa sababu hiyo ndipo bajeti im-eonekana kushughulikia tofauti hizo za

kijinsia , na kwa kufanya hivyo kushu-ghulikia mahitaji ya wote wanawake na wanaume jambo ambalo ni muhimu katika kuangamiza umasikini.

Inatia moyo sana kuona kwamba serikali imetenga kima kikubwa cha pesa , yaamni shiklingi milioni mia tatu kuagiza vifaa vya usafi wa akina mama, yaani pamba ya kusitiri hali zao. Tumnafahamu kwamba wana-funzi wengi wanaohitaji usaidizi hukosa masomo kwa wiki nzima kila mwezi kwa sababu ya kukosa pamba hiyo ya kujistiri wakati wa hedhi, ael-eza Anita Njoki mkazi wa mtaa wa Makadara.

Athari zake pia zitaifikia sekta ya usafiri ambako wengi wa Wakenya hutegemea usafiri wa umma ambako

Akina mama wakiuza vyakula aina mbali

mbali katika soko moja la mjini. Wanawake ni miongoni mwa

wale watakaonufaika kutokana na bajeti kuu ya kitaifa iliyosomwa na Waziri wa Fedha, Bw Uhuru Kenyatta (picha kulia) ambaye alitenga kiasi cha Sh

100 bilioni kwa mambo ya kilimo.

“Ni jambo la kutia moyo kuona kwamba serikali ilitenga kiasi cha Sh 300 milioni kwa taulo za kujikimu”

— Anita Njoki, mkazi wa mtaa wa Madaraka

TAHARIRI

Angalia Uk.4

Page 2: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

2 Toleo Namba 19 • Julai 2011

India huenda ikawadhamini wagombezi wanawake kwa uwazi

Na Nita Balla…

Wizara ya sheria ya India inaitaka serikali ya nchi hiyo kuwad-hamini wagombeaji wanawake wa viti vya kisiasa kwenye uchaguzi . Wizara hiyo inasema kufanya hivyo kutasaidia kudhibiti gharama za uchaguzi na kutoa vihimizo kwa wan-

awake kujiunga na siasa, limesema gazeti la Hindustan Times.Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi

wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi wengine kutoka makundi yanay-ogandamizwa kama ya kikabila na makabila ya daraja ya chini ambao wako katika vyama vya kisiasa vinavyotambuliwa wanapaswa kupata udhamini wa pesa kutoka serikalini ili kuendesha kampeini zao, lilisema gazeti hilo. Hata hivyo halikutaja kiasi cha pesa ambacho kinapaswa kutolewa.

“Pendekezo hilo linafaa kutekelezwa kwa vyama vinavyotambuliwa ki-taifa na hivyo basi kuleta uwazi na uwajibikaji ili kuthibiti kuingizwa kwa pesa zisizoweza kukadiriwa kima chake kwenye uchaguzi,” gazeti hilo la Hindustani Times likinakili arafa kutoka kwa wizara ya sheria. Ugharamiaji wa kampeini za uchaguzi ni swala lenye mgogoro m,kubwa nchini India.

Licha ya kuwepo kwa sheria ambayo inaweka kiwango cha pesa ambacho chama cha siasa kinaweza kutumia katika kampeini, sheria huwa zinavunjwa pakubwa huku vyama vikitumia pesa nyingi zaidi ya kiwango kilichowekwa.

Gazeti hilo linasema wizara ya sheria ilipendekeza serikali iwadhamini wagombea uchaguzi ambao wana pato la mwaka la chini ya rupia laki tano(500,000) au dola 11,1128.

Mapato hayo na mali yatajumuisha pia yale ya waume wa wagombeaji na kukabiliana na hatua ya jinsi wanasiasa wanaume wanavyowadhamini wake zao kwenye uchaguzi , na kutumia maelfu ya rupia kwewnye kampeini zao bila ya kutangaza kima hicho cha pesa kwenye akaunti zao za mwaka.

Wizara ya sheria ilisema pendekezo hilo likikubaliwa litakuwa kihimizo kwa vyama vya siasa kuwatoa wagombea uchaguzi ambao ni wanawake na makundi mengine ya watu wanaokandamizwa , ambao wote hawawakil-ishwi vyema katika ulingo wa kisiasa katika nchi hiyo ambayo ndiyo kubwa zaidi yenye kuzingatia mfumo wa demokrasia.

nauli zake hazina usimamizi wa ser-ikali, na hupanda mara tu bei ya ma-futa inapoongezwa.

Huku kilimo kikichukua sehemu kubwa ya bajeti ya kiasi cha sjhilingi bilioni mia moja, inatarajiwa kwamba wakulima wanaweza kupata manufaa makubwa kufuatia usaidizi wa serikali katika kugharamia pembejeo za kili-mo kama vile mbegu, na mboleaam-bavyo zinaweza kugharamiwa kwa pesa hizo.

Kilimo ndicho uti wa mgongio wa uchumi wan chi. Kulingana na ruwaza ya mwaka 2030maboma milioni tano kati ya maboma milioni nane hapa nchini hutegemea kilimo moja kwa moja. Sekta hii inapewa umuhimu mkubwa zaidi kuliko sekta ya viwanda na huzalisha kima cha asilimia 24 ya pato la kitaifa.

KLutokana na shughuli za kilimo kuwa chini ya uangalizi wa wanawake ambapo wanawake wengi hufanya kazi katika sekta hii, lakini kama vibarua , in-atarajiwa kwamba wanawake wana na-fasi ya kunufaika kama bajeti hii itash-inikiza mbinu za kijinsia na utekelezaji wa mipango ya sekta ya kilimo.

Kwa kuwa asilimia 70 ya wafan-yakazi wa sekta hii ni wanawake, ni muhimu kwamba sekta hii ifanye marekebisho makubwa ambayo

yatawawezesha wanawake kunufaika na ardhi, akasema Kihara.

Mgawo mwingine wa kiasi cha sho-lingi bilioni 109 zilizotengewa miradi ya ujenzi wa barabara unafungamana moja kwa moja na sekta ya kilimo. Wakati barabara zinapopitia kwa urahi-si na gharama ya mafuta ni ya wastani, bidhaa za kilimo zinaweza kusafirishwa kwa urahisi kutoka eneo moja hadi lingine kwa gharama ndogo.

Wanawake kadhalika wana nafasi ya kunufaika na shilingi biolioni 9.8 zilizo-tengwa kuwapa makao watu walioham-ishwa makwao na kadhalika wale walio-fukuzwa kutoka msitu wa Mau.

Mzigo wa sarataniNi jambo lililo wazi kwamba wengi

wa watu waliotoroka makwao wakati wa ghasia za kisiasa ni wanawake na watoto wao ambao wanavumilia mashaka makubwa ya mabadilikop ya hali ya hewahuku wakitumai kwamba siku moja maisha yao yatarejea katika hali ya kawaida.

Kiasi kingine cha shilingi bilioni 64 kimetengewa sekta ya afya kushughu-likia tiba na kinga dhidi ya magonjwa. La maana zaidi ni kutengwa kwa shi-lingi milioni 903hususan kwa madawa ya kupambana na athari za ukimwi jambo ambalo litawapa wakenya wa-naoishi na ukimwi na virusi vya ukim-

wi kuendelea kuwa na maisha mazuri.Kulingana na uchunguzi wa shirika la

utafiti wa mambo ya ukimwi wa mwaka 2007 ambao hufanywa kila baada ya mi-aka mitano, Ukimwi na virusi vya ukim-wi bado ni swala la wanawake kwani wanawake watatu kati ya watu watano wanaishi na virusi vya ukimwi. Hali ni mbaya zaidi kwa wanawake chipukizi wa kuanzia umri wa miaka kumi na mitabno hadi ishirini na minne ambao wamo ka-tika hatari mara nne zaidi ya kuambukiz-wa virusi vya ukimwi , ikilinganishwa na wenzao wanaume.

“Saratani ya mfuko wa uzazi bado inaendelea kuua wanawake hata in-gawa inaweza kuzuiwa na kutibiwa . Wanawake wanahimizwa kutembelea hospitali mara kwa mara ili kufanyiwa uchunguzi , na kwa wale ambao bado hawajapata kufanya mapenzi kabisa wanaweza kuchanjwa dhidi ya ugon-jwa huo,” aeleza Dkt. Brigid Monda, mtaalam wa magonjwa ya wanawake ambaye pia ni mhadhiri wa chuo ki-kuu . Dkt. Monda alikuwa akizung-umza kwenye mjadala uliobandikwa jina la Siosta to Siosta.

Tarakimu kutoka hospitali kuu ya Ke-nyatta (KNH) zinaonyesha kwamba kiasi cha visa elfu mbili vya mardhi ya saratani hugunduliwa kwenye uchunguizi kila mwaka , huku idadi sawa yna hiyo ya watu hufa kwa kansa kila mwaka.

Bajeti ya 2011inavyogusia maswala ya wanawakeKutoka Uk1

Na Wilson Rotich…

Wakati Kenya ilipojin-yakulia uhuru kuoka kwa wakoloni, kwa ba-hati mbaya wanawane

walilazimika kusubiri kwa miaka kumi na minne ili kutambuliwa kuwa na haki sawa za kiuraia.

Wengi wa wanawake na watoto waliendelea kuishi ama kuangamia bila ya hesabi yao kujulikana kwa sa-babu hata hati ya kuzaliwa zilikuwa hazijafahamika kuwepo kwake hasa kwa wale waliozaliwa mbali ay nje ya vituo vya afya. Serikali haikutenga bajeti kwa ajili ya wanawake na wa-toto. Hali hiyo ilichangia kuwepo kwa huduma mbaya za afya , elimu duni na huduma nyingine za kijamii zisi-zofaa hadi hadi miaka kumi na minne baadaye kuanzia mwaka 1963.

WametimizaWakikwamia kwenye desturi za ki-

tamaduni za kikabila, wanaume wali-chukua nyadhifa dhidi ya wanawake na watoto tangu mwaka 1963 wakati nchi hii ilipopata madaraka ya kuji-tawala . Haki ya kuwa na kitambulisho cha kitaifa ilikuwa ni ya wanaume kati-ka kila jamii, ambao wametimiza umri wa miaka kumi na minane.

Vitambulisho vilitolewa kwa vion-gozi wa jamii au familia ambaye ilid-aiwa ndiye mlipa kodi huku wanajamii au wanafamilia hiyo wengi wao waki-wa wanawake na watoto, wakiwekwa katika kundi la raia wa daraja ya pili.

Mnamo mwaka 1977 serikali ya Jomo Kenyatta ilisukumwa hadi ukutani katika harakati za kuilazi-misha kuchunguza upya na kufanyia marekebisho sheria ili kushirikisha haki za watoto na wanawake.

“Hiyo ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa wanawake wa Kenya kupe-wa vitambulisho vya kitaifa,” akasema Bi Rachel Yegon ambaye alikuwa afisa wa usajili wa watu wa wilaya ya Keicho.

Yegon ni shahidi wa masuala haya

kwa sababu katika kipindi hicho ali-kuwa msichana aliyeishi katika kijiji ki-dogo cha Roret, wilaya ya Buret ambayo sasa ni sehemu ya wilaya ya Kericho.

Akiwa motto mdogo katika jamii ya Kikristo huko Roret, Yegon hakush-indwa kujua kuwepo kwa idadi ndogo ya wasichana katika shule ya msingi ya Roret ambako yeye mwenyewe alikuwa akisoma . Wasichana wengi walikosa masomo kwa kotukuwa na vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi.

Katika kipindi hicho cha masomo Yegon alihanganishwa na wingi wa wanafunzi wa kiume katika jitihada zake za kuleta tofauti kwa kupata elimu ili aweze kupigania haki na ku-tambuliwa kwa wanawake waliokuwa hawatiliwi maanani na badala yake kushurutishwa kuolewa mapema.

Katika ujana huo Yegon alikuwa mweledi wa kutosha katika masomo na kupata nafasi ya kuendelea na masomo yake katika shule ya Alliance Girls High School , na Kipsigis Girls kwa elimu ya kidato cha tano na sita.

Kando na ndoa za mapema na ukeketaji wa wanawake, Yegon ali-kuwa na ndoto ya kupigania wan-

awake kupata vitambulisho kama wanaume na kuelelkea katika miji mikubwa kama vile Nairobi na Mom-basa ambayo ndiyo iliyokuwa ikizun-gumziwa sana na watu wakati huo.

Psi na kujua kama Mungu anam-sikiza, mnamo mwaka 1980 aliajiriwa kazi ya ofisa wa uhamiaji. Akiwa ka-zini daima alitaka kuthibitisha ya kwamba wanawake pia wanaweza huduma bora kwa umma.

Juhudi zake zilitunukuwa tunu kubwa wakati alipopandishwa cheo na kuwa afisa wa usajili wa watu ka-tika wilaya kubwa ya Kericho ambayo kwa sasa inajumuisha kaunti za Ker-icho, Bomet, na Transmara.

Kwa miaka minane aliyokuwa ka-

tika mamlaka hayo, Yegon alipata um-aarufu mkubwa miongoni mwa maelfu ya watu ambao aliwasaidia kazini kwake kupata vitambulisho vya kitaifa.

Yegon ambaye alimaliza masomo yake katika chuo kikuu cha DALC alijitupa katika ulingo wa kisiasa ka-tika mwaka 2007, na ingawa haku-fanyikiwa kukinyakua kiti cha Bureti alichopigania, kwa sasa ameelekeza macho yake kwa kiti cha mwakilishi mwanamke katika kaunti ya Kericho.

Ahsante kwa katiba mpya ambayo imeleta ugavi mkubwa wa mamlaka na kuwapa wakenya nafasi ya kugombea nyadhifa mbali mbali, wanawake wa Ker-icho hawatataka kukosa nafasi ya uakilishi katika viti vya serikali ya kaunti.

“Ninafuraha kwamba katiba ya

sasa imetoa nafasi ya usawa kwa jin-sia zote katika siasa,” anasema Yegon huku akiongeza kwamba wapiga kura sasa wanafahamu kwamba wanahita-jika kuwachagua viongozi wao bila ya ubaguzi wowote wa kijinsia.

Hata hivyo Yegon anakabiliwa na upinzani wa wagombezi wengine ku-toka kaunti hiyo ambayo inashiriki-sha wilaya nne, Kericho , Kipkelion, Buret na Belgut.

Yegon ambaye ni mzaliwa wa Bu-ret anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Mwenyeiti wa Baraza la Leiten Bi. Hellen Chepkwony ambaye ametan-gaza nia ya kugombea wadhifa huo. Chepkwony ndiye m,wanamke wa pili kuwakilisha kaunti katika eneo la Kericho ambayo inaanzia Kuresoi hadi Transmara.

KutogombeaWagombezi wengine ambao wana

umaarufu mkubwa ni Bi. Keter am-baye ni mke wa Mbunge wa Belgut Charles Keter ambaye amepende-kezwa na baadhi ya watu kugombea wadhifa huo.

Bi Keter hajajitokeza kukanusha au kuthibitisha kwamba atagombeama ku-togombea wadhifa huo naye mumewe anapohojiwa kuhusiana na swala hilo hucheka bila kutoa jawabu.

Anafahamika kwa kuwatayarisha wanawake katika eneo la Belgut katika maelfu yao na kunufaika na hazina za vijana na wanawake, huduma ambayo imesaidia kuimarisha hali za maisha ya wengi wa wakazi wa kaunti hiyo.

Kupitia umaarufu wa mumewe na Mbunge wa Eldoret Kaskazini ambao ni wendani wa Rais Kibaki huko Rift Valley Kusini, Bi. Keter atamtoa jasho Yegon huko Belgut ambako anaung-wa mkono sana.

Katika wilaya ya Kericho ambayo iko katika eneo bunge la Ainamoi na wilaya au eneo bunge la Kipkelion, Ye-gon atapambana na Bi. Lucy Kirui ku-toka Londiani na Diw. Florance Koskei ambaye anatoka sehemu ya Kabianga.

Miaka 48 baada ya uhuru wa Kenya wanawake wangali waking’ang’ania vyeo

Bi Rachel Yegon zamani afisa mwandikishaji watu wilayani

Kericho akiwa pamoja na Waziri wa Usalama, Prof

George Saitoti (kulia). Picha ya ndani kulia ni Bi Yegon ambaye anawania cheo cha

mwakilishi wa wanawake kwa kwenye uchaguzi ujao Picha na:

Wilson Rotich

Page 3: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

3 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Naibu Jaji Mkuu Barasa

Na Omwa Ombara…

“Kama uchaguzi utaitishwa leo Je sisi kama wanawake tuko tayari kushiriki kwe-nye uchaguzi huo?” Hili

ndilo swala kuu muhimu linalopiga kwenye fikra za Nancy Baraza. “Kazi ni nyingi la-kini wanawake ni wachache. Jitafutie jambo wewe mwenyewe . Je unataka kuwa nini au nani.” Huo ndio wito wake wa ushindi kwa wanawake kuhusiana na katiba mpya am-bayo inawapa wanawake nafasi za kiasi cha asilimia 30 za kiutawala. Hiyo ndiyo hamu yake kubwa kuhusu haki za wanawake katika maelezo yake kwenye mahojiano na Tume ya uajiri wa mahakimu juu ya harakati zake za kupigania haki za wanawake.

Lakini katika dhati hiyo ya kupigania haki hizo Nancy ni mtu mpole anayependa urafiki na mwenye kupenda ushirikiano na ambaye anapenda mahojiano na waandishi habari bila ya masharti.

Uteuzi wa kihistoriaNancy Makokha Baraza ndiye mwa-

namke wa kwanza hapa nchini kuhudumu kama Kaimu Jaji Mkuu. Huu ni uteuzi wa kihistoria na heshima kubwa kwa wanawake na shughuli za utawala nchini. Haijatokea katika historia ya nchi hii kwamba wadhifa kama huo kufikiriwa wala kudhaniwa kupe-wa mwanamke. Tangu kupatikana kwa uhu-ru Kenya imekuwa ni chama cha wanaume katika kila sekta.

Aliyekuwa waziri wa sheria Martha KLarua anaitaja serikali kuwa chama cha wanaume cha akiba na mikopo ambako wanaume wanachukiwa na kudharauliwa. Lakini kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa katiba mpya, kupewa aslimia 30 ya nafasi za kazi kwa wanawake serikalini kunatoa na-fasi kubwa kwa wanawake kushiriki kwenye harakati za utawala za nchi hii nafasi ambayo hatimaye itakuwa haina upeo.

Baadhi ya wachunguzi wamelalamika kwamba mahojiano ya kuwaajiri wafanyikazi hao katika Idara ya Mahakama yaliendeshwa ka-tika misingi ya chuki na kuwadharau wahojiwa , lakini wengine waliunga mkono kufanywa had-harani kwa mahojiano hayo wakisema utaratibu huo ulikuwa wa haki na usawa.

Safari ya Nancy Baraza katika idara ya ma-hakama haikuwa rahisi akilazimika kupitia harakati kubwa ya kuchunguzwa . Lakini pamo-ja na hayo aliwashangaza wengi kwa ukakamavu wake na ufahamu wa maswala yaliyomkabili.

Raila OdingaKati ya washiriki 18 ambao walikuwa wam-

eratibiwa kwa mahojiano ya kung’ang’ania wa-dhifa wa Kaimu Jaji Mkuu, Nancy alifanikiwa kishikilia nafasi ya pili. Tume ya kuwaajiri ma-jaji iliandaa mahojiano hayo kati ya tarehe tatu mwezi Mei na tarehe 12 mwezi Mei mwaka huu na kupeleka jina kwa Rais Mwai Kibaki na Wa-ziri mkuu Raila Odinga. Ili kuidhinishwa. Vion-gozi hao wawili waliidhinisha jina la Baraza na kuiachia tume ya usimamizi wa autekelezaji kat-iba ambayo ilipiga kura kwa kauli moja kumwi-dhinisha Baraza kuchukua wadhifa huo.

Zamani akiwa kamishna wa Tume ya uc-hunguzi wa marekebisho ya katiba CKRC na ambaye kwa sasa ni mhadhiri wa sheria katika chuo kikuu cha Kenyatta , Baraza aliendesha mambo yake kwa heshima kubwa na makini wakati wa mahojiano hayo akiwa mtulivu huku maswali yakimjia kama mvua ya mawe. Baraza alisukumiwa maswali makali makali hasa ka-tika nyanja mbili historia yake kuhusiana na harakati zake za upiganaji haki na hali yake ya sasa hasa katika masomo yake ya Phd ambapo alisomea ngono ya jinsia moja na sheria.

Taarifa hiyo ya masomo ya Phd ilizusha hamu kubwa ya tume ya mahojiano kutaka ku-

jua iwapo ilikusudiwa kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja . Lakini Baraza alisema uamzi wake wa kufuatilia swala hilo kimasomo ilitokana na kutaka kujua zaidi swala hilo baada ya kupata hamasa ya kufanya hivyo wakati alipoongoza kamati ya CKRC kuhusu haki za binadamu ili-yokuwa na jukumu la kukusanya maoni kutoka kwa wakenya ili kutayarisha sura kuhusiana na mjadala huo.

Taarifa hiyo ya kimasomo ilisababisha masuala mengi kutoka kwa baadhi ya wana-siasa waliopinga uteuzi wake kwa sababu hiyo. Lakini katika matukio ya hivi karibuni walimu wakuuu wa shule walilalamika kwamba usagaji miongoni mwa wanafunzi wa kike umeongeze-ka katika shule za boda na hatua za haraka zi-napasa kuchukuliwa kwani mambo yanazidi kuwa mabaya. Katika nchi jirani ya Uganda ma-jadiliano bungeni yalikuwa makali hivyo ma-jadiliano kuhusu mswada huo yakaahirishwa. Mswada huo ulidhamiria kuwanyonga mashoga na wasagaji.

Kuhusu upiganaji wake wa kuleta mareke-bisho katika idara ya mahakama Bi. Baraza alisema harakati hizo zinakufanya ubadilishe mambo katika idara husika na kuleta hali bora. Alisema nchini India kwa mfano kupitia haraka-ti za kupigania mageuzi, walifanikiwa kuleta mageuzi na kuleta maarifa ya kisheria ambayo Nancy anayaita matengenezo ya mahakama. Al-ipendekeza uanaharakati wa kima fulani amba-cho alisema hakipo katika idara ya mahakama.

Nancy ambaye anaelekea kumaliza masomo yake ya Phd katika sheria, amesema kuwa kume-kuwa na upinzani mkali katika idara ya ma-

hakama dhidi ya mageuzi, na akalalamika vikali kwa idara hiyo kwa kupinga marekebisho, licha ya Wakenya kutaka mabadiliko kama hayo.

Baraza anakumbuka kwamba wakati ali-pokuwa katika tume ya CKRC, maafisa wawili wakuu wa idara ya mahakama kupitia kwa wakili wao waliwasilisha mashtaka kupinga ku-pachikwa kwa sura nzima kuhusu idara ya ma-hakama kwenye mapendekezo ya katiba mbali na kukataa kuzungumzia swala la marekebisho katika idara hiyo.

Alipoulizwa na kamishna Abdulahi Ahmed-nassir juu ya hatua inayopasa kuchukuliwa dhi-di ya maafisa hao wawili waliopinga uchunguzi wa marekebisho ya katiba, Baraza alisema ni jukumu la Tume ya uajiri wa majaji kuamua ni hatua gain ambayo wanapasa kuchukuliwa maafisa hao.

Baraza aliiambia tume hiyo ya mahojiano kwamba licha ya matengenezo ya mwaka 2003 katika idara ya mahakama, ufisasi umekuwa mbaya zaidi. Mahitaji ya ofisi ya Jaji Mkuu yana-mtaka mwenye kuchukua wadhifa huo awe ni mtu anayeweza kutoa mwelekeo mwema wa uongozi kwa idara hiyo ya mahakama kisheria na kiusimamizi. Mtu huyo ni lazima awe na uw-ezo wakufanyia marekebisho idara hiyo.

Mbali na hayo wenye kupigania wadhifa huo ni lazima wawe na historia safi na kisomo bora na ambaye uthabiti wake ni thabiti.

“Tunatafuta viongozi wenye vipawa ambao watatoa mwongozo na mwelekeo kwa idara ya mahakama na kwa nchi nzima ,” akasisitiza mwenyekiti wa Tume ya uajiri wa mahakimu Christine Mango.

Kuthibitisha jinsi idara ya mahakama ilivyooza, mmoja wa wagombea nyadhifa Justice Mary Ang’awa alikiti kwa tume hiyo kwamba mirungula ni maisha ya kawaida ka-tika mahakama na iko katika sampuli nyingi hivi kwamba hata kilo ya nyama hupelekewa hakimu katika mlango wake wa mahakama mapema saa kumi na mbili asubuhi. Ang’awa aliutaja ufisadi kuwa ni jambo ambalo lina-fanyika katika kila mahakama hapa nchini. Aliongeza kwamba baadhi ya mawakili huchelewesha kesi kwa hata miaka 17 huku waliowekwa rumande wakiteseka jela.

Akitoa wasifa wake kwa Baraza mwandi-shi mmoja alimtaja kuwa mpiganaji wa mas-kini na demokrasia asiyechoka ambaye ana utaalam unaohitajika na ufahamu wa kiufundi wa kushughulikia marekebisho na kuhakiki-sha kwamba idara ya mahakama iko huru.

KutayarishaKila mgombeaji wadhifa aliulizwa ni ipi

ajjenda yao katika idara ya mahakama katika seku 100 za kwanza ofisini. Baraza anasema atatafuta kuushirikisha umma , kutayarisha mipango ya mafunzo kuhusu thamani za kitamaduni na kuanzisha utaratibu wa ku-kabiliana na mawakili ambao anawalaumu kwa kuendeleza ufisadi mahakamani.

Ni mawakili ndio wanaohimiza ufisadi mahakamani . Hatupaswi kuwalaumu maafisa wa mahakama peke yao kwa sababu ni lazima kuwe na pande mbili ndipo ufisadi ufanyike.

Wagombezi wengine wa wadhifa wa kazi ya Jaji Mkuu walikuwa ni majaji Joseph Nya-mu, Riaga Omollo, Samuel Bosire, KAPLANA Rawal, Paul Kihara, Msagha Mbogholi, na Mary Ang”awa na Jaji Lee Muthoga wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu Rwanda.

Baraza ni mmoja wa waanzilishi wa Shirikisho la kimataifa la wanawake mawak-ili (FIDA). Amefanya kazi ya uwakili kwa miaka 30. Mapema mwaka huu alichaguliwa mwenyekiti wa Tume ya vyombo vya habari nchini kuhusu kanuni za utenda kazi.

Alihudumu katika Tume ya uchunguzi wa marekebisho ya katiba iliyokuwa ikiongozwa na Profesa Yash Pal Ghai, (CKRC) ambayo ilitoa mapendekezo ya katika ya Bomas, am-bayo ilitumiwa kutayarishia katiba mpya.

Wanachama wa tume ya kuwaajiri ma-hakama ni pamoja na Christine Mango, Amos Wako, Ahnednassir Abdulahi, Jaji Isaac Lenaola,

Mwenyekiti wa tuyme ya kuwaajiri watumishi wa serikali Titus Gateere, Kaimu msajili wa mahaka-ma Emily Ominde na mwakilishi wa Chama cha mawakili nchini Florance Mwangangi.

Kwa maneno yake“Ninataka kuchukua fursa hii kuishukuru

haki ya kike , kumsifu mwanamke wa Kenya . Mimi ni matokeo ya uwezo wa wanawake . Kama mfanyikazi wa shughuli za kisheria nimekum-bana na matatizo, ugandamizaji na hali ngumu zinazowakabili wanawake.

Kwa jinsi hiyo ndivyo tulivyokuja pamoja na kuanza kupigania haki za wanawake. Ninajivunia kuwa kuwa mwanamke wa Kenya. Thamani zote hizi zinazozungumziwa na kila mtu.

“Iwapo uchaguzi mkuu ungeitishwa leo, je, tuko tayari kama wanawake kupambana kwenye kinyang’iro hicho?”

— Nancy Barasa, Naibu Jaji Mkuu wa Kenya

Bi Nancy Makokha Barasa ambaye sasa ndiye Naibu Jaji Mkuu wa Kenya.

Ajenda ya jinsia yazalisha matunda kwa Nancy Barasa kuchaguliwa

kama Naibu Jaji Mkuu wa kwanza wa Kenya

Yanayomhusu Bi Nancy Makokha Baraza alizaliwa eneo

la mlima Elgon nchini Kenya. .Alianza maso-mo yake katika Shule ya Msingi ya Chesikaki, na baadaye akajiunga na shule ya sekondari ya wasichana ya Lugulu, kasha Highlands Girls Eldoret ambayo sasa inajulikana kama Moi Girls Eldoret, na Kipsigis Girls. Baada ya masomo yake ya kidato cha tano na sita alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi kwa di-grii yake ya kwanza, kisha Masters digrii na PhD katka masomo ya sheria.

Nancy ana watoto wawili wa kiume, Michael na Yuri Baraza. Kwenye mahojiano na Kenyan Woman kwenye mkutano wa mashauri katika ofisi ya waziri mkuu kuhusu usawa, alitaja uteuzi wake kwenye wadhifa wa makamu jaji mkuu kuwa tukio kubwa la heshima. Bi Baraza ameshikilia nyadhifa muhimu mbalimbali hapo awali kama vile ya kuwa Kamishna wa Tume ya zamani ya uchunguzi wa marekebisho ya katiba.

Page 4: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

4 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Wabunge wanawake waazimia kuanzisha harakati za kupata viti zaidi mnamo 2012

Na Faith Muiruri…

Harakati mpya za kuongeza uwaklilishi wa wanawake bungeni zimeanza kush-amiri. Mapambano yame-

pangwa huku wabunge wanawake wakijiandaa kupambana kutetea viti vyao wakati huu ambapo tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

“Tuna mipango ya kutetea viti vyetu kwenye uchaguzi mkuu ujao. Hatuna mipango ya kugombea viti maalumu vilivyowekwa na katiba” athibitisha Profesa Margaret Kamar kwenye mkutano wa kifungua kinywa ambao uliwaleta pamoja wanachama wa chama cha wabunge wanawake nchini (KEWOPA).

Profesa KamarWakati wa mkutano huo ulioan-

daliwa na wanawake wa Umoja wa Mataifa kupitia ubalozi wa Sweden, wanachama wa KEWOPA walipata fursa ya kubadilishana tajriba zao baada ya kupitia mafunzo mahsusi kuhusu uongozi kwa wanawake katika siasa yaliyofanywa mjini Stockholm.

Profesa Kamar alisema kwamba wabunge wanawake wanadhamira kubwa ya kuhifadhi viti vyao na endapo watataka kugombea nyadhifa za ugavana na useneta basi watafan-ya kampeini kubwa za kuhakikisha kwamba wanahifadhi viti hivyo.

Waliohutubu kwenye mkutano huo walikuwa ni pamoja na Sally Kos-gei na Mawaziri wasaidizi Linah Jebii Kilimo, Askofu Margaret Wanjiru na Cecilia Mbarire. Viongozi hao walise-ma wana lengo la kufanya kwa pamo-ja kampeini ambayo itawahakikishia kuhifadhi viti hivyo wanavyoshikilia huku wakipigania wanawake wen-gine kuchukua viti vya bunge na viti maalum vilivyotengwa na katiba kwa ajili ya wanawake.

“Tunadhamiria kupata viti 116 kwenye uchaguzi mkuu ujao kama sehemu ya mipango yetu thabiti ya kuimarisha manufaa ya wanawake yaliyopatikana kwenye katiba,” aka-ongeza Profesa Kamar.

Wabunge hao wanawake wame-panga mbinu za kampeini ambazo zitawawezesha kuongeza idadi ya wabunge kutoka 47 kwa sasa hadi ku-fikia wabunge 116 katika bunge lijalo.

Ngazi za kijinsiaProfesa Kamar ambaye ni mbunge

wa Eldoret Mashariki amesema kwamba wabunge wanawake chini ya ubawa wa chama chao cha KEWOPA, watafanya mikutano katika kaunti zote arobaini na saba ili kutafuta kuwatambua wanawake wanaofaa kugombea na kujaza viti hivyo 116 vya bunge.

Dkt. Kosgey alisema kwamba wa-nawake ambao ni wabunge maalum wanapaswa kuelezea jinsi wanavyota-ka kuchaguliwa kwenda bunge kwe-nye uchaguzi mkuu ujao ili wapate kuungwa mkono.

Mwenyekiti wa chama hicho cha wabunge wanawake Linah Kilimo alisisitiza haja ya wanawake zaidi kutayarishwa kuchukua mamlaka ya uongozi ili kuwawezesha kunufaika na utekelezwaji wa katiba mpya.

Aliwahimiza watayarishaji wa mafunzo ya uongozi kuwashirikisha wanawake zaidi katika siku zijazo ili waweze kuwa na uwezo mkubwa ki-siasa.

Alisema kwamba chama cha KE-WOPA daima kitakuwa na shukurani kwa maarifa ya hali ya juu walityoji-funza kutoka kwa DR Barboro Hall

kwani wametumia maarfa hayo kue-lewe hali zao.

Alisema wakati wanawake wa-napoingia katika nyadhifa za kisiasa, watu hufikiria, kutarajia na kudhani kuwa wana majibu ya kila kitu, wana-jua kila mtu na matarajio ni mema.

“Hayo hayajalishi ni changamoto gain zinazowakabili katika ulingo ambao umetawaliwa na wanaume.

Mbunge maalum Millie Odhia-mbo alitilia mkazo haja ya kuanzisha mradi wa kutoa nasaha kwa wana-onuia kujitupa katika ulingo wa ki-siasa.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Balozi wa Sweden hapa nchini Bi. Ann Dismor alithibitisha dhamira ya serikali ya nchi yake ya kuimarisha ushiriki wa kisiasa wa wanawake na kukabiliana na vizingiti vya kitama-duni.

Alisema katiba mpya ya Kenya in-atoa muundo msingi wa kusuluhisha vitendo vya kiubaguzi ambavyo vi-mekuwapo kwa muda mrefu dhidi ya wanawake iwe ni katika nyanja za kisiasa, kijamii au kitamaduni.

“Huku utekelezaji wa vifungu vya katiba kuhusu masuala ya usa-wa wa kijinsia unapoendelea katika

katiba, tutashughudia haki za kibi-nadamu za wanawake nchini Kenya zikiimarika,”akasema.

Alizungumzia haswa mswada wa haki za binadamu ambao alisema unahakikisha usawa na uhuru dhidi ya kubaguliwa na unaitwika serikali jukumu la kuchukua hatua kukabili-ana na madhara yanayowakabili watu kibinafsi au makundi ya watu kwa sababu ya ubaguzi wa awali.

“Katiba kadhalika inaunga mkono harakati za upiganaji haki kuimarisha uwakilishi wa wanawake katika sekta ya umma na inaharamisha ubaguzi wa kijinsia kisheria, kitamaduni , umilikaji wa mali, mirathi ikiwa ni pamoja na ukeketaji wa sehemu za siri za wasichana.

Peris SimamBalozi huyo amesema kanuni

zinazotiliwa mkazo na katiba zina-paswa kuhimiza mabadiliko nchini na akawashauri wabunge hao wan-awake kuwa chombo cha kunasihi na kudhibiti msokumo wa kuhakikisha kufikiwa kwa marekebisho ya ki-demokrasia.

Alitilia mkazo haja ya sauti za wa-nawake wa sehemu za mashambani kusikika katika ngazi za kitaifa.

“Kuhimiza sauti za wanawake wa sehemu za mashambani na wanao-gandamizwa kusikika, kunanuiwa kuleta ufahamu matatizo yanayowak-abili wanawake hao jambo ambalo Sweden inaliunga mkono. Alisema kwamba vifungu vya katiba vinavyo-himiza usawa vinapatikana katika kila nchi ya dunia na zinawahusu wa-nawake wote wa Kenya bila ya kuba-gua asili zao,” akasema.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Waheshimiwa Peris Simam na Joyce Laboso.

Akina mama kunufaika zaidi kutokana na katiba mpya

Na Joyce Chimbi na Rosemary Okello…

Baada ya miaka mingi ya kupigania mabadiliko na hatimaye kuzindu-liwa kwa katiba mpya,Wakenya sasa wameanza kufurahia matunda ya kuwa na katiba ambayo inaenda sambamba na matakwa yao na hasa wale wa kima cha Wanjiku.

Matukio ya hivi karibuni hapa nchini ni ishara kubwa kwamba ingawa mambo yanaenda polepole, nchi hii sasa imeanza kubadiklika kuwa taifa lime lililokuwa katika ndoto na fikra za mababu zetu. Mz\ozo uliokumba kusiomwa kwa bajeti ni moja ya dalili kwamba hakika Wakenya wanaelewa kanuni zili-zomo ndani ya katiba na wana hamu kubwa ya kuona kutekelezwa kwake.

Tatizo lilikuwa ni kwamba Waziri wa Fedha alinuia kuisoma bajeti ya kiasi cha shilingi 1.155 trilioni ya kipindi cha mwaka 2011na 2012 katika bunge mwendo wa saa tisia unusu mnamo tarehe nane mwezi Machibila ya kwanza kuyawasilisha makadirio hayo miezi miwili kabla ya mwisho wa kipindi kili-chotangulia cha makadirio ya mapato na matumizi ya serikali, kama katiba mpya inavyoagiza.

Hilo ni tukio muhimu sana kama lile la kuwahojiwakenya wanaopiga-nia kuchukua nyadhifa za ofisi kubwa za kitaifa. La muhimu zaidi ni athari za matukio hayo kuhusu jinsi zitakavyomhusu mwanamke wa Kenya ambaye ameendelea kugandamizwa na kutengwa kwenye taratibu za utekelezaji maen-deleo muhimu.

Utekelezwaji wa katibaNi jambo lililozua hamasa kubwa kwamba maelfu ya wakenya walifuatilia

mahojiano ya Nancy Baraza na kamati ya usimamizi wa utekelezaji katiba mnamo tarehe saba mwezi Juni mwaka huu. Wazo tu kwamba kwa mara ya kwanza Kenya itapata Kaimu jaji mkuu wa kwanza mwanamke ni ishara tosha kuhusu jinsi katiba mpya ni katika ya maendeleo na jinsi inavyoweza kubadil-isha maisha ya mwanamke kutoka historia ya utumishi hadi kufikia hali ya mwanamke kuwa sehemu moja ya harakati za ustawi wa maendeleo.

Kwa miaka mingi sura ya umaskini ni sura ya mwanamke, sura ya ukimwi ndiyo sura tya mwanamke na kadhalika sura ya ukulima. Ni jambo la kusikit-isha kwamba ingawa wanawake wapatao asilimia 75 ndiowanaofanyakazi ka-tika sekta ya kilimo na ndio uti wa mgongo wa uchumi wan chi, ni asilimia ndogo tu ya wanawake ndio wanaoshikilia hati za kumiliki mashamba. Ni asili-mia tatu pekee ya wanawake ndio walio na hati za kumiliki mashamba, lakini kutokana na jinsi marekebisho yanavyoendelea hali hiyo itabadilika.

Wanawake zaidi sasa wataanza kushiriki katika taratibu za utoaji maamuzi muhimu , na kushiriki katika kila sekta ya maendeleo , kupata nafasi za kusi-mamia nyadhifa tofauti ambazo hapo awali ilikuwa vigumu, licha ya kuzison-gelea hata kuzifikiria pia. Kutokana na dalili za utekelezwaji wa katiba hiyo maslahi yao yataimarika na watu wote kupata manufaa.

Hakika katika hali ya ukosefu mkubwa wa usawa , na ili serikali kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha usawa kama unavyoagiza mswada wa haki katika katiba, kiwango cha wingi wa thuluthi mbili hakipasi kuwa kigezo cha kuwa-tengea nyadhifa wanawake.

Mawaziri kutoka kushoto, Bi Elizabeth Ongoro, Bw Otieno Kajwang’, Prof Anyang’ Nyong’o wakiwa kwenye dhifa iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Raila Odinga kuzungumzia usawa wa kijinsia. Picha na: Omwa Ombara

“Tunaazimia kunyakua viti visivyo chini ya 116 kwenye uchaguzi mkuu

ujao, hiyo ikiwa ni mojawapo wa mbinu za wanawake kujiimarisha

kutokana na katiba mpya.” — Prof Margaret Kamar

Page 5: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

5 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Na Rosemary Okello…

Huku wanasiasa wakianza kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao nchini ambao utafanywa chini ya katiba mpya, moja ya maswala ambayo

yamepewa heshima zaidi katika shughuli nzima ya mapambano ya kuipigania katiba mpya ni mahali pa mwanamke.

Swala la uwakilishi wa wanawake katika nyadhifa zozote za kiuchuguzi ndilo mwamuzi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Bi Elizabeth Muli ambaye ni makamu mwe-nyekiti wa tume ya utekelezaji wa katiba mpya, anatambua na kukubali kwamba manufaa ya wanawake katika katiba yanaweza kupatikana kupitia sehemu ya 259 ya katiba ambayo inahi-taji kwamba katiba ifafanuliwe katika misingi ya usawa na haki.

Ni katika msingi huu ndipo wanawake Wabunge chini ya uongozi wa chama cha Kenya cha Wanawake Wabunge (KEWOPA) kimean-zisha kampeini ya kunyakua viti 116 vya Bunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2012.

KampeiniKulingana na Prof Margaret Kamar ambaye

ni Waziri Msaidizi wa Mazingira na Maliasil, iwanawake wanatarajia kunyakua viti 116 vya Bunge kwenye uchaguzi mkuu huo.

Akizungumza kwenye mkutano wa ufaha-mishaji mambo baada ya kuhudhuria mkutano wa Barbro Dahlbom-Hall wa mafunzo ya uon-gozi nchini Sweden, Prof Kamar alieleza hakika yake kwamba kwa kutumia maarifa waliyopata kwenye mafunzo hayo, wanawake wa Kenya wataweza kufanikiwa kunyakua viti hivyo 116.

“Sisi viongozi wa wanawake tumeazimia ya kwamba kwanza tutachukua viti saba ambavyo kwa sasa vinashikiliwa na Wabunge wanawake, na kuimarisha harakati za kunyakua viti 116.

Wakifahamu kuwa kutakuwa na pingamizina changamoto nyingi, wanachama wa chama cha KEWOPA wamekubaliana kujitokeza na mbinu kuwashirikisha wote kwenye harakati hizo za kupambana kunyakua vit ihivyo 116. Mbinu hizo ni pamoja na kuwasilisha mswada bungeni ambao utalihimiza Bunge kutunga sheria, na kadhalika utaratibu wa kampeini wa kuleta ufa-hamu miongoni mwa wanawake na umma kwa jumla kuhusu haja ya kunyakua viti hivyo 116.

Akielezea ni kwa nini viti 116, Prof Kamar alisema kwamba kwa katiba mpya, idadi ya Wabunge itakuwa ni 290 na kama katiba hiyo itatekelezwa itakikanavyo, wanawake wana-paswa kuchukua viti 162 ama ifuatavyo, Bunge linapaswa kuwa na Wabunge 96 waliochagu-liwa. Kisha kunapaswa kuwa na Wabunge 47 wanawake kutoka kutoka kila kaunti ambao watakuwa wamechaguliwa na wapiga kura, kisha

Wabunge 12 ambao wanatarajiwa kuteuliwa na vyama vya kisiasa kulingana na kiwango kili-chetengwa kwa mujibu wa idadi ya Wabunge ambao vyama hivyo vitakuwa vimepata kwenye uchaguzi. Hayo ni kwa muhimu wa kifungu cha 90 cha katiba ambacho kinasema thuluthi moja ya wabunge hao watakuwa wanawake. Hatua hiyo itaongeza fungu la wanawake kwa viti vinne vya Bunge. Kisha kuna viti 47 vya baraza la Sen-ate ambako kutakuwa na viti 15 vya wanawake.

“Kupatikana kwa viti 116 kutatokana na Bunge la kawaida na bunge lille la Senate”, akael-eza Prof Kamar.

Lakini ili hayo yafanikishwe,” wanawake ni lazima wajiunge na vyama vya siasa kwa wingi. Hata ingawa kuna vyama viwili vinavyoongoz-wa na wanawake, Narc-Kenya kinachoongozwa naBi Martha Karua na chama cha NARC kina-

choongozwa na Bi Charity Ngilu ambaye pia ni WazirI wa Ustawi wa Mipango ya Maji na Un-yunyizaji Maji Mashambani. Kuna wanawake wachache sana ambao wanashikilia nyadhifa za mamlaka kwenye vyama vya siasa na wachache wengine hawana uanachama wowote na chama cha siasa chochote.

“Twaweza tu kuona kikombe kikiwa nusu tele badala ya kuwa nusu shoinda kama tutaji-unga na vyama vya siasa ili kupata viti hivyo,” asema Mheshimiwa Millie Odhiambo.

WanachamaMswada wa vyama vya siasa uliopo uko wazi

kuhusiana na jinsi uteuzi huo unavyopaswa kutekelezwa na jinsi watu wanavyoweza kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa.

Kulingana na Bi Winnie Gichu wa Tume Huru ya Muda ya Uchaguzi (IIEC), mswada wa vyama vya siasa una masharti magumu kuhusu uteuzi wa watu ambao watateuliwa kugombea wadhifa wowote wa kiasia.

Alieleza kwamba, “Chama kitahitajika kutoa majina ya wagombezi wote walioteuliwa ambao ni lazima wawe wanachama wa chama husika miezi mitatu kabla ya uteuzi kufanywa, na hati

za kuwa mwanachama ambapo kila mwana-chama ni sharti kuwasilishwa kwa msajili wa vyama vya siasa.

Alieleza wasiwasi wake kulingana na jinsi mambo yanavyokwenda, orodha ya chama ya majina ya wateuliwa kwa upande wa Bunge la ki-taifa, huenda likazusha hali ya wasiwasi hasa kwa wanawake. Alisema kwamba wakati utakapofika wa uteuzi wa vyama, je, tutapata idadi ya wan-awake hasa katika kaunti kugombea viti hivyo?

Aliwahimiza wanawake wawe sehemu ta muundo wa kisiasa ili kutayarisha nbinu za jinsi orodha ya majina katika vyama itakavy-otayarishwa ili kuhakikisha kwamba kanuni ya harakati za kupigania maslahi ya wanawake ina-tiliwa maanani wakati wa uteuzi huo wa wago-mbea uchaguzi wa bunge la kitaifa, maseneta, magavana na madiwani.

Akiyataka mashirika ya wanawake kuhakik-isha kwamba wanatumia vilivyo moyo wa kati-ba kupitia utaratibu wa utekelezaji, Bw Stephen Etemesi alikiambia chama hicho cha wanawake kwamba ni jukumu la mashirika ya wanawake kama vile G10 kuomba azimio kutoka kwa Ser-ikali kuhusu jinsi utezi na uchaguzi sampuli mbali mbali na kadhalika katika nyadhifa za umma utakavyofanywa katika katiba mpya.

Swala la idadi ya viti kwa wanawake kwa uchaguzi mkuu ujao limekuwa sasa ni donda sugu

Mwanamuziki aanzisha kampeni ya taulo ya kujisetiri kwa wasichana Na Faith Muiruri…

Akijulikana kwa jina maarufu la Size 8 katika ulimwen-gu wa tafrija za starehe, Linet Munyali ameanza kupata umaarufu kila mahali. Amezindua mpango ambao unadhamiriwa kutoa vifaa vya usafi kwa wanafunzi wa

shule za sekondari kutoka jamii masikini.Kupitia harakati hiyo ambayo imebandikwa jina la kasichana

Kanghe Munyali ambaye ana umri wa miaka 23 amekuwa aki-zuru shule moja hadi nyingine katika mitaa ya mabanda mjini Nairobi akitoa michango ya pamba za kujistiri wasichana wakati wa hedhi ya kila mwezi.

Anasema kwamba tajriba yake wakati alipokuwa akikua, imeifanya kampeini hiyo kuimarika. “Nilikulia katika mtaa wa Eastlegh mjini Nairobi ambako pamba ya kujisitiri kwa hedhi zilikuwa ni vigumu kupatikana kwa ajili ya gharama. Kupatikana kwa pamba hizo kulikuwa ni vigumu na hilo ni fedheha kubwa. Sitaki wasichana wadogo wapitie katika hangaiko hilo,” akasema.

Munyali ambaye wimbo wake uitwao Fire ama moto, umem-fanya kuwa maarufu nchini, anasema amekuwa akitumia mapato yanayotokana na mauzo ya wimbo huo kuwasaidia wasichana wanaoishi katika mitaa hiyo ya mabanda.

Anasema kwamba katika safari zake kwenye shule hizo mjini Nairobi amesikitishwa sana na matatizo yanayowakumba wasi-

chana ambao humwambia kuwa hawajatumia pamba za kujisitiri wakati wa siku zao za hedhi.

“Nimekumbana na mateso ya wasichana wadogo ambao ha-wawezi kupata pamba za kujisitiri . Kwa kweli wao huniambia kwamba tangu walipoanza kuona hedhi, hawajawahi kutumia pamba ya kujisitiri,” akaongeza. Munyali alisema hayo wakati wa mahojiano na gazeti hili la Mwanamke wa Kenya muda mfupi baada ya kuhudhuria tamasha la majadiliano la Sista Sista katika hoteli moja ya Nairobi.

Alitoa mwito kwa wanawake waliohudhuria kongamano hilo waache kupoteza pesa na badala yake wawasaidie wasichana hao kupata pamba ya kujisitiri. Anasema kwamba baadhi ya wasichana wamemwambia kwamba wanalazimika kufanya mapenzi wakiwa wangali wadogo ili kupata pesa za kununulia pamba hizo.

Changamoto za manufaaNi hali ya kusikitisha na tunahitajika kuhimiza njia za ku-

wawezesha kupata pamba hizo kwa urahisi ili ili kuwatayarishia hali zao za baadaye kuwa nzuri, akaongeza.

Munyali anasema ingawa kuzifikia shule hizo limekuwa jambo gumu kwa sababu ni lazima kuwepo na ushawishi kwa wasimamizi wa shule kwamba jambo la manufaa kwa wasichana hao. Kwa sasa ana furaha kwamba kampeini yake itaendelea na kusambaa katika kila sehemu nchini.

“Nilianzisha kampeini hii mnamo mwaka mwa 2005 na hadi sasa nimefanikiwa kuingiza pesa nyingine zaidi kutokana na muziki wangu.

Anasema kwamba kwa wakati huu amebanwa kidogo na rasli-mali na anafanya kila jitihada kuungana na Serikali kwenye mi-pango iliyotangazwa hivi karibuni na Waziri Mkuu Raila Odinga kwamba wasichana wa shule za msingi na za sekondari wagawiwe pamba za kujisitiri wanapokuwa shuleni.

Munyali anasema kwamba, habari kwamba Waziri Mkuu al-isikitishwa na mahangaiko ya wasichana ambao wanatoka jamii masikini wanaoendelea kukosa masomo kwa sababu ya kukosa pamba hizo ni wito mkubwa wa kumhimiza kila mtu kuanza ku-zungumzia swala la pamba za kuwastiri wasichana ambao jamaa zao hawawezi kugharamia vifaa hivyo.

“Kwa sasa tuna puto za kufanyia mapenzi ambazo zinauzwa kwa bei ya shilingi kumi, ni kwa nini hatuwezi kupunguza ghara-ma za pamba ili kila msichana kutoka jamii masikini aweze kuz-igharamia?” akauliza mwimbaji huyo.

kujua ni kiasi gain kinachohitajika na ni kiasi gain ambacho mashirika hayo ya misaada watakachotoa.

Habari kutoka shirika la UNICEF zasema wanafunzi wa kike kutoka jamii maskini hukosa kuhudhuria shule kwa hadi siku ar-obaini kwa mwaka kwa sababu ya hedhi kwa kuwa wengi wao hawana uwezo wa kupata pamba za kujistiri wakati wa hedhi.

Wabunge kutoka kushoto, Dkt Sally Kosgei, Bi Millie Odhiambo na Dkt Joyce Laboso wakishauriani juu ya jambo fulani wakati wa mkutano uliokuwa umetayarishwa na shirika la KEWOPA kuzungumzia juu ya maswala ya mambo ya kijinsia.

“Tunaweza tu kuona kama glasi iko nusu badala ya kuwa nusu

tupu iwapo tutajiunga na vyama vya kisiasa kupata viti hivyo.”

— Mheshimiwa Millie Odhiambo

Page 6: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

6 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Na Omondi Gwengi …

Miaka mitatu baada ya ghasia za kisiasa kui-kumba nchi hii na baada ya kuundwa kwa

seriikali ya mseto sifa ambayo nchi hii ilikuwa ikifurahia kama kisiwa cha uthabiti wa kiasiasa na demokrasia imefifia zaidi.

Licha ya kuwa na ukwasi wa mali asili na wa kibinadamu na nafasi bora zaidi Kenya haijafikia kilele cha ustawi wa maendeleo kwa sababu haijapata uongozi usio na mwelekeo wa kikabi-la, uongozi ambao una maono chungu nzima katika masuala ya kiuchumi, kidemokrasia na kijamii, uonmgozi ambao una dhamira kubwa ya kufikia maendeleo ya kitaifa wala sio uongozi ambao uko klatika misingi ya majisifu ya kibinafsi au ule wa kluwa na wafua-si wa ndani katika misingi ya kikabila.

Maisha ya kijamiiKulingana na taarifa ya hivi punde

ya shirika la Jadili Coalition, kuhusu uamuzi wa watu juu ya utendaji kazi wa serikali, wengi wa waliotoa maoni yao kwenye mahojiano hayo walitaja ukosefu wa kazi kama tatizo kubwa la kiuchumi ambalo linawakabili wak-enya kwa wakati huu. Kadhalika wali-taja ukabila upendeleo na ukosefu wa usalama kama mambo yanayo-tishia vikubwa maisha yao ya kijamii. . Utawala mbaya na ufisadi vilitajwa kuwa matatizo makubwa ya kisiasa yanayowakumba Wakenya.

Huku kaunti mbali mbali ziki-toa maoni yao kuhusu matatizo ya kiuchumi katika kanda hizo, ambayo yanahitaji kushughulikiwa kwa dhar-

ura, kaunti za Kisumu na Siaya zili-taja tataizo la vifaa vya huduma kuwa changamoto kubwa inayozikabili.

Huku utekelezajki wa katiba mpya ukiendelezwa, wakenya wengi wanat-arajia kwamba katiba hiyo itashughu-likia swala la utawala mbaya, ugavi usio sawa wa aslimi mali na ukosefu wa kazi. Lakini wataalam wana ma-oni tofauti wakisema kwamba uko-sefu wa elimu bado ni swala ambalo linapaswa kushughulikiwa ili raia waweze kuwa na uwezo wa kupigania huduma bora na kuepuka kutumiwa vibaya na viongozi.

Serikali ya NarcAkiwahutubia washiriki wakati

wa kongamano hilo juu ya uitendaji kazi wa serikali na utekelezaji wa kat-iba, Mkurugenzi mkuu wa shirika la Com,munity Aid International Joseph Kwaka alisema kwamba mashauriano pekee hayawezi kuletamaendeleo isi-pokuwa kuwe na uongozi mwema.

Akikumbuka uongozi wa ser-ikali ya Narc, Kwaka alisema tumaini la wakenya la kumchagua kiongozi mtaalam wa kiuchumi ambaye wali-fikiria atasimamia vyema uchumi wan chi hii, sasa umebadilika kuwa tamau-ko kubwa kwa kuwa wanakabiliwa na wakati mgumu wa kiuchumi

“Kama uchumi hautawekwa mikononi mwa watu wanaofaa, haku-na litakalokuwa,”akasema Kwaka.

Kulingana na Profesa Emilly Akuna wa Chuo Kikuu cha Maseno, alisema kwamba vi0ngozi wanapas-wa kuwapa raia uwezo.

Kwa Elphas Omino mwenye umri wa miaka 69, hamu yake kubwa ni kuona Kenya imepata viongozi wema

kabla hajaaga dunia. Anasema kwam-ba wengi wa waliohitimu shahada za chuo kikuu wamekaa majumbani na hati zao kwa sababu viongozi ha-washughulikii maslahi yao. “Nyanza inahitaji harakati za kuwaelimisha watu kuhusu uongozi na utawala,” akasema Omino.

Omino anazidi kulaumu utawala mbaya kwa maafa wanayopata wa-siojiweza kifedha hasa kuhusiana na misaada ya masomo. Ugavi wa mis-aada ya masomo uko katika misingi ya ninayemjua sio ni yupi anayestahili misaada hiyo, akasema. Alisema pia kwamba si sawa kwa kamati ya mis-aada ya masomo ya CDF kupeleka pesa kwa mwanafunzi aliyeko Ugan-da huku kukiwa na wanafunzi wengi ambao hawawezi kupata misaada hiyo hapa Kenya.

Anapendekeza kwamba wadhifa wa Gavana wa kaunti upewe mtaala lakini sio mwanasiasa.

Akihutubia mkutano huo, Wilkis-ter Olule kutoka Kisumu Magharibi alisema viongozi wanapaswa ku-tuhimiza kutumia asilimali zilizopo katika harakati za kustawisha mae-neo yetu. “Wananchi wanawewza kuleta mabadiliko katika uongozi lakini mpaka wawe na ufahamu wa kutosha,”akaongeza Olule.

Kwa kutazama mahojiano ya hivi majuzi kwa wale awaliokuwa wakipigania nyadhifa za idara ya m,ahakama, Kenya imechukua nafasi ya uongozi wa nchi nyingine kuhusi-ana na uchunguzi wazi wazi wa vion-gozi kupitia matangazo ya moja kwa moja ya mahojiano ya wapigania nya-dhifa hizo.

Umma yaikosoa serikali kuhusu vipengee kadhaa

vilivyoko katiba mpya

“Ila tu kama katiba imo mikononi mwa watu wadilifu, hayo yote hayatafanikiwa.”

— Joseph Kwaka Mkurugenzi Mkuu wa Community Aid International

(CAI)

Uteuzi wa Rais wazua kasheshe Mahakama Kuu Na Duncan Mboyah…

Mnamo mwisho wa mwezi Januar, mwaka huu, i Rais Mwai Kibaki alimteua Jaji Al-Nashir

Visram kuwa Jaji Mkuu, Prof Githu Muigai kuwa Mkuu wa Sheria na Bw Kioko Kilukumi kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

Uteuzi huo ulipokelewa kwa msh-tuko na mshangao mkubwa na wana-siasa na mashirika ya upiganaji haki za jamii kwa kuwa ulivunja katiba.

UtumiajiMashirika ya wanawake chini ya

mwavuli wa shirika la G-10 yalika-sirishwa na uteuzi huo na kwenda kutafuta mwongozo mahakamani kuhusu inavyosema sheria kuhusiana na uwakilishi wa kijinsia . Makundi mengine pia yalihoji utaratibu ulio-tumiwa na Rais katika uteuzi wa maafisa hao.

Waliotuma maombi ya kupinga uteuzi huo ni pamoja na Centre for Rights Education Awareness(Creaw), Kundi la Upiganaji wa Wanawake Uongozini, Tomorrow Child Initia-tive, (TCI), Wanawake katika Sheria na Maendeleo, na Shirika la Maendeleo Kupitia Vyombo vya Habari (DTM).

Mengine ni Muungano wa Wa-nawake dhidi ya dhuluma kwa wa-nawake, (COVAW),Young Women Leadership Initiative(YWLI) na Mu-ungano wa Wanawake wa Kenya Wa-piga Kura.

Aliyekuwa Jaji Mkuu wakati huo,

Bw Evans Gicheru aliteua jopo la ma-jaji watatu kuchunguza swala hilo na wakaamua kwamba nyadhifa hizo zi-tangazwe na wanaotaka kutuma mao-mbi ya kujaza nafasi hizo wafanyiwe mahojiano na Tume ya Uajiri wa-Maafisa wa Idara ya Mahakama, JSC.

Shughuli hiyo imeshafanywa na sasa tuna Jaji Mkuu mpya na naibu wake na mkurugenzi wa mashtaka ya umma ambao wote waliteuliwa baada ya kufanyiwa mahojiano makali am-bayo yalitangazwa moja kwa moja na vituo vya humu nchini vya televisheni.

Lakini leo tume hiyo ambayo mapema ilijipatia sifa kwa kufanya kazi njema kutoka kwa Wakenya mbali mbali, imetumbukia kwenye mtego ule ule aliotumbukia Rais Kibaki mapema mwaka huu.

MakundiBaada ya kutangazwa kwa nya-

dhifa za majaji wa mahakama kuu , walioteuliwa walikuwa majaji wa-tano wanaume wanne na mwanamke mmoja na hivyo basi kulilazimisha shirika la mawakili wanawake, FIDA, na makundi mengine matano ya kupi-gania maslahi ya wanawake, walik-wenda mahakamani kupinga uteuzi huo kabla ya walioteuliwa kuapishwa.

Shirika la FIDA na mashirika sawa na hilo kutoka Tanzania, Ugan-da yameichukulia hatua tume ya JSC kwa kupuuza katiba wakati wa kuwa-teua majaji wa mahakama kuu.

Mkurugenzxi Mkuu wa shirika la FIDA, Bi Grace Maingi anasema kwamba kwa kumteua mwanamke

mmoja kuhudumu katika mahakama hiyo tume hiyo imepuuza katiba ya Kenya na sheria inayosimamia hudu-ma ya Idara ya mahakama ya mwaka 2011 ambayo inataka kanuni ya thu-luthi moja ya majaji wawe wanawake.

“Kwa kumteua mwanamke mmo-ja pekee tume ya JSC imeunda Ma-hakama Kuu kinyume cha katiba kwa vile wamevunja kifungu cha katiba cha 28(8) na zaidi ya hayo kushindwa kudumisha usawa wa kijinsia katika kifungu nambari 172(2) (b) cha kat-iba akasema Bi Maingi.

Kulingana na kifungu cha 172 (2) (b), “Tume ya JSC itaimarisha na kuhakiki-sha uwajibikaji wa Idara ya Mahakama na kusimamia kwa ustadi, uthabiti na uwajibikaji wa haki na itadumisha na kuendeleza usawa wa kijinsia.“

Alisema kwamba ni makosa kum-teua mwanamke mmoja pekee ilhali mahakama kuu haina hata mwanam-ke mmoja ambaye ni jaji licha ya hitaji hilo la katiba.

“Tunatoa mwito kwa JSC kuondoa orodha hiyo ya wateuliwa na kutayar-isha nyingine ambayo itahakikisha usawa wa kijinsia kwa vitendo na kwa dhati ya moyo ambapo kinyume ya hivyo tutakwenda mahakamani ku-dai utekelezwaji wa kanuni hiyo ya katiba,”akasema Bi Maingi.

Alieleza kwamba uteuzi huo un-athibitisha kuwepo kwa ugandamizaji wa wanawake kwenye nyadhifa za juu za katika idara ya mahakama na katika jamii tunayoishi na kupuuzwa kimakusudi kwa usawa wa kijinsia.

Dkt. Maria Nassali ambaye ni

mkurugenzi mkuu wa shirikisho la mawakili wanawake nchini Uganda anasema kwamba tume ya JSC ili-paswa kuiga mfano wa Uganda am-bapo wanawake wawili na wanaume wanne ndio wanaosimamia katika Mahakama Kuu, huku wanawake watatu na wanaume wanne wanasi-mamia Mahakama ya Rufani.

Anasema kwamba ni jambo la kusikitisha kwamba tume hiyo ilivun-ja sheria ilhali uteuzi huo unaelezwa kinaga ubaga kwenye katiba.

Bi Annemarie Nkelame wa Tan-zania aliiambia tume hiyo ya JSC kwamba ilitekeleza jambo hilo bila ya kufikiria akisema kwamba kwa kuwa ndugu mkubwa katika kanda hii,Kenya inapaswa kufanya mambo yake kwa taratibu zinazostahili ili kuwa mfano mwema.

Alifichua kwamba Kenya ina wa-nawake wengi waliosoma kuliko nchi nyingine yoyote katika kanda hii, am-bao wanaweza kuhudumu katika ma-hakama kuu.

Katika uteuzi tume hiyo iliwateua Bi Njoki Ndung’ú kama mmoja wa wanawake wa pekee katika orodha ya mahakimu wa mahakama kuu ambaye anatarajiwa kuidhinishwa na Rais Kibaki. Rais alichapisha majina kwenye gazeti rasmi la Serikali na an-gelikuwa amewaapisha kama si kwa kesi iliyowasilishwa mahakamani.

Akiwatangaza walioteuliwa, mwe-nyekiti wa tume hiyo, Prof Christine Mango alisema wamewateua watu wanaofaa kabisa kufanyia marekebi-sho idara ya mahakama.

“Kwa kuteua mwanamke mmoja

tu kwa vyeo vilivyoko kwenye mahakama kuu zaidi nchini,

JSC, ilienda kinyume cha kifungu 28 (8) cha katiba mpya kuhusu usawa

wa kijinsia kama inavyoorodheshwa na

katiba mpya.” — Grace Maingi, Mkurugenzi

Mkuu wa FIDA K.

Bw Elphas Omino akitoa mchango wake akisema ugawaji mbaya wa fedha za misaada ya masomo hutokana na uongozi hafifu.

Page 7: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

7 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Na Joyce Chimbi…

Julia Nabasa alikuwa amekwisha tamaukwa kwenye jitihada zake za kupata njia muafakla ya upangaji uzazi ambayo itakuwa shwari kwa mwili wake, huku mpango huo wa uzazi

na ustadi mkubwa wa utendaji kazi.”Kuletwa kwa ‘shanga za mwezi’ kama njia

ya upangaji uzazi ni faraja kubwa kwangu, na kuniduwaza kwamba ni njia ya kimaumbile isi-yokuwa na madhara yoyote,” anasema Julia Na-basa mwenye umri wa miaka 29.

Mwanamke huyo mwenye watoto watatu anasema kwamba mbinu hiiya “Shanga za mwezi’ ni tukio lililomletea afueni yeye na wanawake wengine wengi ambao miili yao imezikataa njia nyingine za upangaji uzazi .

“Nimekuwa nikitumia sindano kwa miaka mitatu na madhara yaliyotokana na utumiaji wa sindano yalikuwa makubwa, nilio geza uzani mno huku nikiwa sina hamu ya chakula,” akaeleza Na-basa huku akiongeza kwamba “hiyo haimaanishi kwamba wanawake wengine hawawezi kutumia mbinu hiyo ya kupanga uzazi.”

Shirika la misaadaJulia ni mmoja tu miongoni mwa wanawake wa

Ugandaambao wamepata suluhu kwa matatizo yao ya upangaji uzazi kwa kutumia shanga hizo.

Mbinu hii ambayo ilianzishwa nchini Uganda yapata miaka mine iliyopita imepata fursa kubwa ya kutangazwa na Mama Janet Museveni mke wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Njia hii ya upangaji uzazi ilianzishwa na shirika la AFFORD kwa lengoo la kuwasaidia wanawake kutambua taratibu zao za siku za hedhi kwa urahisi.

Kampeini ya huduma za afya za AFFORD hud-haminiwa na shirika la USAID kukiwa na shabaha ya kuima5risha hauduma za upangaji uzazi.

Lucy Kabatebe ambaye ni muuguzi msajiliwa anayeshughulika na afya ya uzazi nchini Uganda anasema kwamba shanga hizo zinautenbdaji kazi bora wa asilimia 95wakati masharti yanaypozin-gatiwa kikamilifu.

“Shanga hizo za mwezi zimepangwa katika misingi ya siku salama, ni njia ya kimaumbile ya upangaji uzazi,” aeleza Kabatebe.

Siku salama ni zile ambazo mwanamke huwa hayuko katika hatari ya kupata mimba.

Shanga za mwezi ni ushamnga unaofanana na ushanga unaovaliwa shingoni wenye shanga za rangi tofauti. Ushanga huo una shanga thelathini na mbioli za rangi tofauti na kila moja inawakil-isha utaratibu wa hedhi wa mwanamke.

“Kila tembe ni siku katika utaratibu wa hedhi. Kuna ki0pete cha mpira na kimviringo chenye mshale . Kishale hicho kinaonyesha upande am-bao kipete hicho kitasongezwa. Tembe nyekundu ya ushanga inaashiria siku ya kwanza ya hedhi,” akaeleza Lucy.

Shanga nyeupe inaashiria siku ambayo mwa-namke anaweza kupata mimba. Shanga zote zxa hudhurungi ni za siku ambapo mwanamke anaweza kushika mimba na shanga za hudhurun-gi nzito zaidi hukusaidia kufahamu idadi ya siku katika utaratibu mzima wa hedhi.

Shanga za mwezi ni utaratibu wa hesabu ya siku za hedhi uliotayarishwa na kituo cha mati-babu cha Chuo Kikuu cha Georgetown ambacho miongoni mwa mengine hutoa usaidizi wa kima-ongozi katika huduma za upangaji uzazi. Shanga hizo ambazo zinajulikana kiwa kimombo kama Moonbeads zimewahi kusambawa katika sehemu nyingine za dunia kama Cyclebeads.

Licha ya uzuri wa mbinu hii ya upangaji uzazi, utekelezaji wake unahitaji dhamira kubwa..

“Utaratibu wa hedhi wa mwanamke huchukua kati ya siku 26 na siku 32, hivyo tyunawashauri wanawake wasitumie mbinu nyingine za upangaji uzazi kwa karibu miezi mine ili kukadiria taratibu zao,” aelezea Kabatebe.

“Mwanam,ke anaweza kukadiria hali yake kwa kuweka alama siku ambazo ataanza siku zake za hedhi na kuona ni vipi zitakavyotokea katika maiezi itakayofuata.,”

Kama mwanamke anatumia njia fu-lani ya upangaji uzazi huenda asiweze kupata

makadirio sahihikwa sababu chembechembe zake za mwili zitakuwa zimevurugwa na njia hiyo ya upangaji uzazi anayotumia.

“Nilijifanyia uchunguzi mwenyewe kwa kipin-di cha miezi mine na nimekuwa nikitumia mbinu hii kwa miaka miwili ,´asema Esther Nsali.

Nsali mwenye umri wa miaka ishirini na mi-tano na mama wa watoto wawili anasema anai-pata mbinu hii ya upangaji uzazi kuwa na ustadi wa utendaji kazi.

Shanga hizo pia hazina gharama kubwa, na mwanamke anaweza kutumia ushanga huo mmo-ja kwa miaka mingi.

Katika shirika la Uganda la afya ya uzazi, am-balo ni shirika lisilo la serikali lenye dfdhamira ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya ya uzazi, ush-anga mmoja wa mwezi unagharimu shirklingi elfu tatu za Uganda, sawa na shilingi 125 za Kenya.

Hata hivyo ushanga huo unauzwa ghali zaidi katika maduka ya madawa , maduka ya kawaida na maduka ya supermarket ambako mtu anaweza kuununua kwa shilingi elfu sita za Uganda sawa na shilingi 250 za Kenya.

Licha ya umaarufu wake miongoni mwa wan-awake, wanawake wengine wamezikatalia mbali.

Hii ni kwa sababu utumiaji wake ni mgumu. Mwanamke anayeamua kutumia shanga nizo kama njia ya upangaji uzazi ni lazima awe na ushirikiano mwema na mumewe.

“Ushirikishaji wa mwanaume ni lazima kwa njia hii ya upangaji uzazi kufanya kazi. Wapenzi ni lazima wakubaliane kutoshiriki ngono au kutumia puto kwa siku 12 ambapo mwanamke anaweza kupata mimba,” asema Kabatebe. Hili ndilo tatizo kubwa kwenye ufanisi wa ushanga huu wa upangaji uzazi.

“Wakati mwanamke anapotumia mbinu fulani ya upangaji uzazi huwa anajisikia kutaka kufanya mapenzi wakati wowote anapotaka bila ya kufikiria wakati ambapo mbinu hiyo ya upangaji uzazi itaka-pomlinda, “anasema Margaret Oyundo.

“Kumwambia mwanaume asifanye mapenzi au atumie puto, huku ukiwa unatumia aina fu-lani ya upangaji uzazi kunaweza kusababisha mzozo mkubwa.”

Utumiaji wa puto na kuacha kufanya mapenzi kumewafanya wanaume wengi kuacha kautumia njia za kinga bila kufanyiwa uchunguzi. Hii ina-onyesha kwamba watui wengi katika jamii hawana imani sana na njia hizo m,bili za upangaji uzazi.

“Ni wanaume wangapi watakaoweza kutumia mipira ama kuacha kufanya mapenzi kwa siku kumi na mbili wakati mwanamke anazo njia ny-ingine za kuzuia mimba,” auliza Job Ogwang.

Shanga za mwezi kutangulia kujinusuru

Uamuzi wa kutenga 150 milioni lilikuwa

wazo la manufaaNa Joyce Chimbi…

Hazina kuu ya serikali im-etenga Shilingi 150-milioni za kununulia vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa magon-

jwa ya saratani au kansa, ikiwa ni pamoja na kansa ya mfuko wa uzazi na kansa ya matiti, magonjwa ambayo yanaongoza katika kusababisha vifo vya wanawake hapa nchini hasa wanawake ambao wako katika umri wa kupata watoto..

Saratani ya matiti imefanyiwa kam-peini kubwa kwa miaka mingi iliyopita ambapo mwezi wa ufahamu wa kansa ya matiti ukiimarisha idadi ya wanawake wenye ufahamu wanaokwenda kufanyiwa uchunguzi wa kansa ya matiti.

Ni jambo la kawaida kuona mabango makubwa kwenye barabara zenye shu-ghuli nyingi yakiwahimiza wanawake kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kansa ya matiti.

“Mnamo mwaka wa 2008, mimi na marafiki zangu tulikuwa tunavinjari mjini na tukaamua kuingia katika kliniki ili tufanyiwe uchunguzi wa matiti tuone kama tunaweza kuwa tuna ugonjwa huo wa kansa. Uchunguzi huo uligundua kivi-mbe kwenye titi langu la kulia,” akasema Ann Nduta mwenye umri wa miaka 29.

Aliongeza, “Nilishangaa mno hata si-kuwa na la kufanya wakati huo, lakini kwa bahati nzuri nikafanyiwa upasuaji duni na uvimbe huo ukaondolewa na sasa mimi ni mama wa watoto wawili na matiti yangu yako sawa kama ilivyothibitishwa na uc-hunguzi niliofanyiwa hivi majuzi.

Katika hali kama hiyo kansa ya kizazi inaendelea kusababisha vifo vya maelfu ya wanawake hapa nchini kwa kuwa ufa-hamu kwamba ugonjwa huo unaweza ku-zuiwa na kutibiwa ni haba mno.

Dhana potofuDhana potofu kwamba saratani hu-

wapata wanawake waliozeeka, inaende-lea kuangamia polepole na wanawake chipukizi sasa wanakwenda kliniki am-bako wengi wanagunduliwa kuwa na kansa hiyo.

Hakuna anayefahamu vyema mad-hara hayo bali ni Anna Ogwel mwenye umri wa miaka 26 ambaye kwenda kwake hospitali mnamo mwezi Juni mwaka mmoja uliopita, ulimfanya akagundua kuwa alikuwa na kansa ya kizazi.

Wakati nilipopewa matokeo ya uchun-guzi nilikuwa na hakika kwamba kulikuwa na makosa yaliyofanyika, lakinin uchun-guzi mmoja baada ya mwingine ukath-ibitisha wasiwasi mkubwa niliokuwa nao,” akasema mama huyo akiwa na hasira.

“Niliolewa miaka miwili iliyopita na nimekuwa nikitarajia kupata watoto, la-kini ndoto hiyo imebaki kuwa ndoto am-bayo sijui kama itatimia.”

Wataalamu sasa wanasema kwamba kisa hicho ni moja ya visa vingi ambavyo wanakumbana navyo kila wakati.

Moja ya dhana potofu kuhusu ugon-jwa wa kansa ni kwamba ugonjwa huo ni wa kurithi. Lakini kile ambacho watu hawajui ni kwamba kansa ya aina hii huambazwa na wanaume kwa wanawake kupitia tendo la ngono.

Wanaume ndio wachukuzi wa virusi vinavyojulikana kama Human Papiloma-virus (HPV) ambavyo husababisha kansa ya kizazi.

Virusi hivyo ni kundi la viini ambavyo vinaweza kuingia kwenye kizazi na kusa-babisha mabadiliko ya chembechembe za kimaumbile na kusababisha magonjwa ya sugu katika sehemu za siri za mwanamke saratani na magonjwa mengineyo.

Uchunguzi umeonyesha ya kwamba mambo mengine yambayo yanamfanya mwanamke kuwa katika hatari ya kuam-bukizwa saratani ya kizazi ni kufanya mapenzi mapema na kupata mimba mara kwa mara.

“Shanga za mwezi kwa kweli huwa na matumizi

kama kinga ya kujinisuru wakati wa hedhi na ni kama njia mojawapo ya upangaji

uzazi. Kipindi cha hedhi ya mwezi kwa mwanamke ni sharti kuwa kati ya siku 26-32 ili uchunguzi zaidi uweze kufanywa wakati

huo.” — Lucy Kabatebe, Mkunga kutoka

Reproductive Health Uganda

Hi ni mfano wa shanga iliyoundwa na kituo kimoja cha utabibu cha Georgetown University Medical Centre cha huko Marekani. Picha na: Joyce Chimbi

Page 8: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

8 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Kubuniwa kwa benki ya maslahi ya akina mama kumewapatia motisha

Na Florence Sipilla…

Historia ya biashara ya mashirika madogo ma-dogo ya fedha hapa nchi-ni imefungamana mno ya

ile ya shirika la pesa wanawake la Ke-nya Women Finance Trust (KWFT) shirika ambalo ndilo kongwe zaidi la fedha ambalo huhudumia sekta ya ki-pekee ya wanawake.

Shirika hilo ndilo lenye mtandao mpana zaidi ambao umezagaa ka-tika sehemu za mijini na sehemu za mashambani. Shirika hilo ni tawi la sekta ya pesa la shirika linalojulikana kama Kenya Women Group(KWG) ambalo husimamiwa na Benki Kuu ya Kenya, shirika hilo sasa linajulikana kama KWFT DTM, shirika ambalo linachukua dhamana.

Shirika hilo dogo la pesa linazin-gatia utaratibu wa kipekee wa shu-ghuli za benkI, ambapo hutoa miko-po chini ya kanuni maalum. Hii ni kusema kwamba mtu binafsi au kundi la kina mama linamdhamini mtu ku-chukua mkopo. Utaratibu wa kusima-mia mikopo ya aina hiyo ni mrefu na wenye kuhakikisha uhusiano wa kari-bu kwa vile afisa wa mikopo ni lazima awe amemfahamu mwenye kuchukua mkopo kwa muda mrefu. Hali hiyo inahitaji kuanzisha na kudumisha uhusiano mwema kati ya shirika la pesa na wateja wake.

MadharaYaelekea kuna madhara makub-

wa ndio, lakini dhara hilo limeleta manufaa makubwa tangu shirika hilo lilipoanzishwa mnamo mwaka 1981 ambapo shirika hilo limestawi na ku-panuka na sasa linajivunia ofisi 215 kote nchini.

Shirika hilo haliwapi wanawake uwezo wa kifedha tu bali pia linawa-saidia kupanua mahusiano yao ya ki-jamii. Shirika la KWFT linawahimiza wanawake kuunda vyama vya kuch-angizana pesa ambako huendesha utaratibu wa uwekaji pesa, lakini hilo halishughuliki na mikopo, asisitiza Dkt Jennifer Riria ambaye ni afisa mkuu wa kundi hilo.

Wanawake hao kupitia vyama vyao,wameweza kuimarisha hali zao za maisha . Wamenunua matangi ya kuhifadhia maji miongoni mwa manu-faa mengine mengi ambayo kundi hilo linaamini ni muhimu. Kadhalika wan-awake hao husaidia wakati wa sherehe kama vile harusi na wakati wa misiba kama vile kifo kinapotokea.

Usaidizi huo wa kijamii umekuwa kama mazowea makubwa kwa baa-dhi ya wanawake. Huku biashara zao zikistawi, wana chaguo la kujiondoa kwenye makundi hayo na kujichuku-lia mikopo kibinafsi ya kati ya shilingi laki mbili na laki tano. Hata hivyo, wa-nawake hawa wamedumisha uhusiano wao na vyama hivyo kwa kuwa wana-thamini mtandao huo wa kijamii.

“Baadhi yao hukataa kuondoka kwa vile wanapoondoka hukosa ule usaidizi wa kijamii, äsema Dkt Riria. Shirika hilo linajulikana sana kwa huduma hiyo ya pesa kidogo kidogo lakini ni machache yanayojulikana kuhusiana na maslahi yao mengine katika mambo ya nishati, afya ya uzazi, kukabiliana na ugandamizaji wa kijin-sia, utoaji mafunzo na udhamini.

Baada ya kupata mafanikio makubwa katika sekta ya huduma ya pesa, shirika hilo sasa linaelekeza jiti-hada zake katika kusisimua ufahamu

wa harakati zake nyengine. Shirika la KWG kwa sasa linakusanya pesa kwa ajili ya miradi ambayo haiendeshwi kwa ajili ya kupata faida.

Kadhalika tunatafuta pesa kutoka kwa wafadhili asilia, anasema Bi Riria na kuongeza kwamba watayafuata mashirika yasiyo ya ufadhili asilia ili kudhamini miradi ya aina hiyo. Ali-poulizwa ni kwa nini kuzingatia mira-di ambayo iko kinyume na mwelekeo wao wa kimsingi wa kibiashara, ki-nara huyo alisema kwamba mama mwenye afya hakika ni kufanya taifa kuwa na afya.

Wanawake“Mwanamke mwenye afya atafan-

ya kazi yenye afya,” na matokeo yake ni mapato thabiti kwa familia jambo ambalo linaleta mfano bora utakaoi-gwa na umma katika mazingira yake.

Wanawake barani Afrika daima wamekuwa wakifanya kazi katika makundi, huu si utaratibu mpya, wan-awake wamekuwa wakishirikiana ka-tika kazi. Asilimia tisini ya wanawake wanaoomba mikopo kutoka shirika la KWFT ni wanachama wa vikundi, asilimia kumi iliyobaki ambayo ni ya wateja wenye uwezo mkubwa wana uwezo wa kujitegemea katika kuchu-kua mikopo.

Moja ya miradi ambayo Dkt Riria anaishabihikia zaidi ni ule wa “Nishike mkono na utwae hali ya maisha ya baadaye,” ambao unakusudiwa kutoa udhamini kwa vijana. “Madhumuni ya mradi huuni ni kuanza kutayarisha viongozi na watu wenye mwelekeo kutoka shuleni,” akasema.

Afisa mkuu huyo anakutaja kusam-baratika kwa taratibu za kitamaduni ambazo zilihakikisha utayarishaji wa vijana na kupewa mwongozo kuhusu masuala muhimu kama vile elimu

ya mambo ya ngono, kuwa jambo la kusikitisha. Kundi hilo tayari limean-zisha miradi na wasichana wa Macha-kos Academy ambako wanawahimiza wanafunzi hao kujuitahidi kupata mafanikio makubwa katika masomo. Je, ninataka kuwa nini? Nitafanyaje mpaka nifikie kilele hicho?

Hayo ndiyo maswali waliyoulizwa wasichana hao ili kuwapa changa-moto ya kuanza kufikiri jinsi wat-akavyojitayarisha kusomea kazi fulani mapema. Shirika hilo lina hamu ya kushikamana na mashirika mengine yenye mawazo sawa ambayo yana uwezo wa kufanikisha malengo hayo.

Katika kazi ya kuimarisha shughuli za wanawake, Dkt Riria anasema hilo haliwezi kutendeka bila ya wanaume kushirikishwa. Hii ndiyo sababu shiri-ka hilo lina ushirikiano na shirika la wanaume la kuwapa uwezo wanawake (MEW). “Tunatambua wajibu un-aoweza kutekelezwa na wanaume kwa vile wanaume nao mara nyingine hu-wafikiria sana wanawake,” akasema.

ManufaaTunafanya kazi na na wanawake

600,000 jambo ambalo linamaanisha ya kwamba kutawapa maishilio watu milioni tatu,äkaeleza, huku akifafa-nua manufaa ya hazina hiyo kwa wa-nawake na nyumba zao.

Alielezea sababu za shirika hilo kujishughulisha na masuala yasiyo ya pesa. Alisema shirika la KWG si la mambo ya pesa pekee. Shabaha ya shirika hilo ni kuungana na wanawake ili kujenga taifa thabiti na bora.

Hayo ni pamoja na kuimarisha kampeini ya kudumisha afya bora, kupambana na dhuluma za kijinsia mbali na kutoa huduma kuwaweze-sha wanawake kifedha.

“Mahitaji ya mwanamke si ya pesa

pekee,” anasema na kuongeza kwam-ba shirika lake lina lengo la kumpa uwezo mwanamke na kumweka ma-hali ambapo patakuwa ni kwa manu-faa yake bora.

Kulingana na Meneja Mkurugen-zi wa shirika la KWFT, Bw Mwangi Githaiga, shirika hilo limetoa mchango mkubwa katika kuzuia mmiminiko wa watu kutoka sehemu za mashambani kuingia mijini, kwa kuanzisha shughuli zenye kuleta ajira katika sehemu hizo. Kwa kuleta ajira katika sehemu hizo za mashambani, wamezuia uhamaji wa watu kutoka sehemu za mashambani kwenda mijini kutafuta kazi. Wafanyika-zi wa benki hiyo wametumkia pikipiki kuzifikia sehemu ambazo hazifikiki kwa usafiri wa kawaida kuhakikisha kwamba watu wa sehemu za mashambani wa-napata huduma hiyo ya benki.

“Kufuatia hatua ya benki hiyo ya kuanzisha huduma ya kuweka akiba, benki hiyo imeanzisha mpango wa wanawake kukutana kwenye ukumbi wa kuweka akiba wa benki hiyo kwa njia ya kirafiki. Benki hiyo haiendeshi shughuli za kibiashara lakini huwapa wateja wake ujumbe wa uwezo wakati wanapoendessha shughuli zao,” äka-fafanua Bw Githaiga.

Katika ushirikiano wake na John-son and Johnson shirika hilo linatoa habari juu ya maswala ya afya ya uzazi na kuna sehemuj maalum am-bapo wanawake walio na watoto hu-enda kuwabadilisha vibinda au nappi. Hii ni sehemuj ya kazi za manufaa za shirika hilo za kuwaongezea thamani wateja hao na kuwaleta pamoja katika kila sekta ya maisha yao.

Dkt Riria anajivunia mafanikio ya shirika hilo ambalo harakati zake zimeya-fanya mabenki ya biashara kutambua kwamba wanawake wana umuhimu mkubwa kama wateja wa mabenki.

“Sisi hufanya kazi na wanawake 600,000 hii hesabu

ni kumaanisha chakula kinachopitia

midomoni ya watu milioni

tatu. Mahitaji ya mwanamke sio tu

pesa hivyo pia KWG sio tu mambo ya

fedha ila kujihusisha kama kitengo cha kuinua maisha ya

jamii.” — Dkt Jennifer Riria Kinara

wa Kenya Women Group

Hawa ni baadhi ya wanachama wa KWFT wakisherekea ustawi waliowahi kuupata dhidi ya ufanisi ya fedha zilizotoka kwenye benki hiyo kwa shughuli zao za kibiashara.

Page 9: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

9 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Uwezo utawala upandishwe zaidi ya cheo cha kinara wa pili mkuu

Na Karani Kelvin…

Kuanzishwa kwa katiba ya sasa kulionekana kuwa mwangaza wa kijani uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kufikisha kituoni sa-

fari kuu ya kuwapa uwezo wanawake.Kwa hakika ilikuwa ni ishara ya kila kitu ni shwari kwa usawa wa kijinsia katika seh-emu za kazi, shule bunge na nyumbani.

Katika katiba iliyopita, imedaiwa kwamba swala la kijinsia halikutiliwa maanani. Kwa sababu hiyo basi, sheria mahsusi ziloizotayarishwa kwa ajili ya kumchomoa kibwengo wa utovu wa usa-wa wa kijinsia zikatayarishwa.

Wakati ukuta wal.isema wahenga, na kwa kweli wakati uliweka wazi dhuluma zote za kijuamii kote ulimwenguni na Ke-nya ikasimama kucheza ngoma ya usawa iliyopigwa na mashairika maalum ya aki-na mama. Katiba yetu ikawa na kuendelea kuwa chombo cha kusimamisha ngoma ya ustawi ambayo bila shaka itazidi kunoga.

Haki zisizo na shakaKutokana na haki zilizotyiliwa mka-

zo ndani ya katiba, shirika la AFRICAN wOMAN And Child Features limeratibu manufaa kumi ya kimsingi kwa wanawake. Manufaqa hayo ni pamoja na haki sawa katika ndoa, kugawana kwa usawa majukumu ya kiu-zazi, umiliki wa ardhi, haki za kiafya ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi na thuluthi moja katika uakilishi miongoni mwa mengine.

Huku katiba ikihakikisha haki za wanawake, inabainika wazi mwendo wa kobe kwenye shu-ghuli za kuleta mabadiliko miongoni mwa wa-nawake wenyewe.Tukichukuamfano wa ute8uzi wa Jaji Mkuu na naibu wake, bila shaka tuna sa-babu ya kuwa na wasiwasi.

Kulikuwa na barua nyingi za maombi ya kazi kutoka kwa wanawake za kuomba kazi ya naibu Jaji Mkuu lakini maombi ya kazi ya Jaji Mkuu maombi yalikuwa haba. Kati ya maombi kumi na matatu ya wadhifa wa naibu wa Jaji mkuu,

maombi manane yalifanikiwa kufikia hatua ya mahojiano. Kwa upande mwingine ni wan-awake wawili pekee ndio waliotuma maombi9 ya kutaka wadhifa wa Jaji Mkuu.

Tarakimu hizo hafifu zinatuambia kuwa in-gawa wanawake wa Kenya wanasherehekea ush-indi wao kwenye mapambano ya kupigania usa-wa katika katiba, msimamo wao katika kulinda manufaa hayo ni wa kusikitisha. Inasikitisha kwamba idadi ya wanawake waliotuma maombi kuhusiana na nyadhifa za idara ya mahakama na ni kwa nini wakatuma maombi mengi ya naibu jaji mkuu na kutotruma maombi ya kutoka ka-tika wadhifa wa Jaji mkuu.

Ni kuogopa huko kuchukua wadhifa mkuu na kutosheka na wadhifa mdogo wa naibu jaji mkuu ndipo tunapoonekana kuwa tumehit-

imu tu kwa ajili ya wadhifa mdogo wa naibu wa mkuu fulani. Ikifahamika kwamba wanawake hawakushurutishwa kuchagua kiutuma mao-mbi katika wadhifa wa naibu wa jaji mkuu na kutotumia maombi ya kupigania wadhifa wa jaji mkuu ila maombi machache, vitendo vyao kwa njia nyingine vinatoa wazi dhana kwamba mwa-namke hawezi kuwa katika ngazi ya juu kabisa.

Kwa mfano kama walikuwa wametuma maombi ya kutaka kazi hiyo kubwa kabisa la Jaji Mkuu, wangekuwa wameanzisha barabara mpya kwa nwanawake chipukizi. Wangekuwa kama jeshi la utangulizi ;a ukombozi wa wan-awake. Wangekuwa jeshi la utangulizi la wan-awake katika utekelezaji wa katiba mpya.

Kwa kutokutuma maombi ya kupigsnis es-fhifsa mkuu es jsji mkuu kwa wingi, wanawake

hao walishindwa kukomesha dhana ya kidesturi inayomfanya mwanaume kuwa mkuu zaidi. Huku tukiheshimu haki yao ya kuchagua wadhifa wowote wanaotaka, mtu anashangaa ni nini kilichoifioka nurui ya kijani . Je nuru hiyo ilizima lini?

Ipo haja kwa wanawake kuvunja viz-ingiti vya kifikra ambavyo vimekitwa na dhana za kumdhalilisha mwanamke na kupanda ngazi kufikia ngazi za juu zaidi katika umma. Ufanisi wao majumbani, ka-zini na katika sekta za kibinafsi udhihirike pia katika sekta ya huduma za serikali. Tu-nachohitaji ni wanawake ambao wanawe-za kwenda zaidi ya wazo finyu la “wewe ni shingo,”na kuanza kupeleka mawazo kupita fikra zisizo na maana zinazozuia maendeleo ya mwanamke kazini.

Matokeo ya uteuzi wa nyadhifa za Jaji Mkuu na naibu wake na mamlaka makuu, yanatuambia kwamba mamlaka makuu ni ya mwanaume na msaidizi wake kuwa mwanamke. Tarakimu hizo ndivyo zina-vyotufahamisha.

Mtu anaweza kusema kwamba hili ni tukio moja ambalo halikukusudiwa, la-kini hatuwezi kuliacha likapita na upepo kwa kuwa linahalalisha uteuzi wa wan-awake ili wawe wasaidizi katika taaqsisi mbali mbali. Wakati mtu anapotazama hapa na pale iwe ni katika siasa (mawa-

ziri na tume), elimu (wakuu wa vyuo kwa mfano) na katika sekta ya kibinafsi(maafisa wakuu wa makampuni) hali ni hiyo moja. Tu-nawaona wanawake wakishikilia mamlaka ya kuwa wasaidizi huku wanaume wakishikilia nyadhifa za juu uongozini ni sehemu chache tu ambako wanawake ndio wanaoshikilia ny-adhifa za juu zaidi.

Kama wanawake wengi zaidi wangetuma maombi ya kupigania wadhifa wa Jaji mkuu, ingemaanisha kwamba kwa wingi wao peke yake wangekuwa wametuma ujumbe mkubwa. Wangekuwa wamesema wanahitaji zaidi ya kuwa wasaidizi wa wanaume, kwamba wana haki ya kuwa katika mamlaka makuu na haifai kuogopa nyadhifa hizo.

Na Henry Kahara…

Kuanzishwa kwa soko la pamoja la kanda ya Af-rika Mashariki katikati ya mwaka jana kumeyafanya

makampuni kuanzisha biashara kote katika nchi tano za kanda hii ka-tika jitihada za kutumia manufaa ya upanuzi wa nafasi za kibiashara.

Wauzaji bidhaa katika nchi za nje, mabenki, kampuni za bima, na men-gineyo yamejizatiti kufanya biashara katika nchi hizo za kanda. Lakini to-fauti na biashara hizo, mwanamke mmoja katika sekta ya unadhigfishaji kadhalika anatafuta kupata pande lake la keki katika sehemu hii.

TangamanoMercy Wangari, mdhamini wa

Uzuri Institute of Technology, ame-jizatiti kuanzisha huduma za ukwatuzi katika nchi hizi tano, akisema kwam-ba itahakikisha kwamba vijana katika kanda hii wananufaika na tangamano hili la kiuchumi.

“Taasisi hii ambayo ni maarufu sana hapa nchini kwa kutoa wa-fanyikazi bora katika biashara ya una-dhifishaji, imepokelewa kwa taadhima na makampuni mengine huko Sudan Kusini, Rwanda, Uganda na Tanzania,” anasema Wangari.

Mipango hiyo ya upanuzi anase-ma imetokana na kuimarisha kwa mahitaji ya huduma zake bora katika sekta hiyo pamoja na hamu ya watu

kuonekana kuwa nadhifu.Kazi ya kumnadhifisha mwa-

naume kwa mfano kwa sasa inakisiwa kuwa ya thamani ya shilingi trilioni moja nukta nane na inakadiriwa ku-fikia trillion mbili nukta mbili katika muda wa miaka mine ijayo. Afrika Mashariki haijaachwa nyuma pia.

Kwa kutumia teknolojia ya kisasa klatika sekta hiyo ya unadhifishaji, Uzuri inasema imeanza kupata ma-fanikio katika upande wa mapato licha ya kuweko na mashindano makali..

Tuna nafasi bora zaidi kwa sa-babu tunatoa mafunzo bora zaidi kwa kushirikisha teknolojia, akasema mkurugenzi huyo wa Uzuri.

Kadhalika anaelezea kwamba upanuzi huo wa kanda umehimizwa na utendakazi bora wa wanafunzi wa taasisi hiyo.

“Tumewaona wanafunzi wetu wa-liohitimu wakijianzishia kazi zao kote katika kanda hii. Kampala kwa mfano imejaa wanafunzi waliohitimu kutoka Uruzi,” akaongeza.

Miongoni mwa mafunzo ambayo yamevutia kanda hii ni ukwatuzi wa nywele na urembo. Muhimu zaidi ni kwamba taasisi hiyo ina mafunzo ya

juu zaidi katika urembo jambo am-balo limeifanya biashara ya unadh-ifishaji kuimarika sana nchini Kenya.

“Hadi kufikia sasa hiki ndicho chuo cha pekee nchini ambacho kina mechanical na electrical therapy am-bavyo havina madhara,” akasema Wangare.

Anaongeza pia kwamba kuna mafunzo mengine ya kitaalam zaidi ambayo ni bora zaidi yenye kutumia teknolojia za kisasa zaidi katika una-dhifishaji wa mwili. Hii ndiyo sababu wanaofuzu katika chuo cha Uzuri huwa walimu wa walimu wa unadh-ifishaji katika kanda hii.

Uzuri kadhalika inatoa mafunzo ya aina nyingine mbali nay ale ya ure-mbo na unadhifishaji. Mafunzo hayo ni mapishi na utoaji wa huduma za chakula na somo jingine lililoanzish-wa majuzi la uandishi habari.

“Wangari anasema,”Vijana wa ki-zazi hiki ambao wanavipaji vya hali ya juu wanapaswa kusaidiwa kujitege-mea kiuchumi. Hi ndiyo sababu Chuo cha Uzuri kina mipango mikubwa ya kuanzisha mafunzoya kiteknolojia ambayo yatawawezesha vijana kupata kazi kwa urahisi.

Ni kupitia jitihada hizo ndipo Uzuri ikashinda kandarasi ya Kenya Wildlife Services mwaka 2009 ya kuta-yarisha vazi la huduma kwa wateja.

Mkurugenzi huyo ambaye pia hutoa huduma za kiroho na kuendesha miradi ya uongozi, ameandika kitabu kinachojulikana kama Extra Ordinary Life, [maisha yasiyo ya kawaida] am-bacho kitatolewa hivi karibuni.

Lakini licha ya miradi hiyo am-bayo inadhamiriwa kuwapa vijana uwezo, Wangari anasema serikali inapaswa kuzisaidia tasisi ambazo zi-nanuia kuwasaidia vijana kupata na-fasi za kazi na za kujianzishia miradi yao wenyewe. Alisema ni hatua haba

zinazofanywa kuimarisha sekta hiyo.Huku serikali ikiwa imepeleka

mabilioni ya pesa katika taasisi za kati, wadhamini wa miradi hiyo wanasema pesa hizo zimetwaliwa na kupelekwa katika vyuo vikuu. Wakati umefika ambapo Halmashauri ya mikopo ya elimu ya juu (HELB) inapaswa ku-wadhamini wanafunzi wanaosomea katika vyuo hivyo vya kati.

Wangari ambaye hutoa huduma za ushauri kuhusiana na mambo ya uongozi anasema wakati umefika ambapo mikopo inapaswa kutolewa kuimarisha vyuo vya kati ambavyo hutekeleza wajibu mkubwa katika ku-wapa vijana maarifa ya kujistawishia.

Asambaza soko la pamoja kandani

Wabunge Mheshimiwa Millie Odhiambo (kushoto) na mwenzake Bi Sophia Abdi wakijumuika kufurahia sherehe za miaka kumi za mwanamke Mwafrika zilizoandaliwa kwenye ukumbi wa KICC.

Huyu ndiye Bi Mercy Wangari, mlezi wa kituo cha Uzuri Institute of Technology akiwa na baadhi ya vifaa vya mafunzo vilivyoko hapo.

“Vijana wenye vipawa mbali mbali ni sharti wasaidiwe kiuchumi ili waweze kujiendeleza na kujisimamia. Hiyo

ndiyo kwa sababu kituo cha Uzuri kina mipango ya kuanzisha mafunzo ya kiteknolojia inayokubalika.”

— Mercy Wangari, Mlezi wa Uzuri institute of Technology.

Page 10: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

10 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Na Florence Sipalla…

Hitaji la kuwepo kwa wa-fanyikazi wa huduma za afya wenye ujuzi halina haja ya kutiliwa mkazo

kutokana na umuhimu wake. Hivi leo ulimwengu unahitaji wakunga wenye ujuzi wa kupambana na vifo vinavyo-sababishwa na uzazi na maafa men-gine yanayosababishwa na uzazi.

Huu ni ujumbe ulioko katika taarifa ya shirika la UNFPA kuhusu hali ya ukunga duniani.

“Wakunga wenye ujuzi waliopata motisha na vihimizo ni muhimu kwa ufanisi wa kushughulikia matatizo makubwa na kupunguza vifo na ule-mavu,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inakariri kwamba idadi ya wakunga hudhihirisha hali halisi ya huduma za afya ya uzazi. Ka-tika nchi zaidi ya hamsini na nane zili-zofanyiwa uchunguzi, kuna upungufu wa wakunga 112,000 katika nchi 38. Upungufu huo unamaanisha kwamba hata kule ambako kuna wakunga wal-iopata mafunzo ya ukunga kuwashu-ghulikia akina mama na watoto wao, huduma zinazotolewa ni duni.

Hakuna usawa katika ugavi wa wafanyikazi katika sehemu za mashambani ikilinganishwa na seh-emu za mijini. Hali hiyo inazidi kuongeza matatizo ya wanawake waja wazito katika sehemu ambazo haz-itiliwi maanani kimaendeleo ambako wanahitaji huduma za wakunga.

Idadi ya wakungaUpungufu wa wakunga umewa-

fanya wanawake wengi wa sehemu za mashambani kuwategemea wakunga wa kienyeji. Hali hiyo huwasukuma katika hatari kubwa wakati wanapo-hitaji huduma za dharura.

Kuna ukosefu mkubwa wa usawa katika taratibu za huduma za afya ambazo zinapaswa kushughulikiwa kwa dharura. Taarifa hiyo inasema kuwa chini ya asilimia 17 ya wakunga wenye ujuzi kote duniani hupatikana kuwahudumia wanawake wanaohitaji huduma hizo.

Kenya haikuachwa nyuma katika janga hilo la tarakimu kuhusu upun-gufu wa wakunga wenye maarifa. Hata hivyo, jambo la kutatiza ni kwamba wakunga waliohitimu na wauguzi bado wanang’ang’ana kutafuta kazi. Kulin-gana na taarifa hiyo, katika jitihada za kuimartisha huduma za afya, serikali ya Kenya imeazimia kuwaajiri na kuwa-tuma wahudumu elfu ishirini wa afya.

“Kiwango kinachofaa cha wakun-ga na wanawake wanaohitaji huduma hizo ni mkunga mmoja kwa wan-awake wanne wanaohitaji huduma hizo, lakini katika hali ilivyo nchini Kenya kila mkunga mmoja anasu-biriwa na wanawake kumi na watano, anasema Donald Epalat ambaye ni muuguzi na mwanachama wa Shirik-isho la Wauguzi wa Mataifa ya Com-monwealth, lionalowakilisha kanda ya Afrika Mashariki na Kati na Kusini mwa Afrika. Anaongeza kwamba, “Matokeo ni mzigo mkubwa wa kazi kwa wakunga hao.”

Labda mzigo huo mkubwa wa kikazi huwafanya baadhi ya wau-guzi kuwatendea vibaya wanawake wanaotembelea vituo vyao vya afya kutafuta huduma za uzazi.

“Kuheshimu haki za wanawake wanaotafuta huduma za afya ya uzazi ni haki muhimu ya kibinadamu na muhimu katika kuhakikisha kwamba serikali inatekeleza shabaha zake za huduma za afya kwa umma,” anaeleza

Elisa Slattery ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha haki za uzazi wa kanda ya Afrika.

Mrundo huo wa kazi za kuwad-hoofisha wakunga hao husababishwa pia na vifaa vya kutolea huduma za uzazi ambavyo havitoshi. Baadhi ya vituo vya afya havina maji na umeme hasa vile vilivyoko katika sehemu za mashambani.

“Jambo hili husababisha huduma duni kwa wagonjwa,” asema Epalat. Hali hiyo inazidi kufanywa mbaya na wauguzi wanaohama ambao hufanya kazi nyingi za ukunga nchini hadi katika

nchi nyingine. Mishahara duni na masharti magumu ya kazi pamoja na kazi nyingi na ukusefu wa mipango ya kuendeleza elimu ya kazi, ni baadhi ya mambo ambayo yanachangia kuhama kwa wauguzi wakiwemo wakunga.

“Kinachowahimiza kuhamia ka-tika nchi hizo ni mishahara minono zaidi, na nafasi ya kujiongezea maso-mo ya kazi,” akaeleza Epalat.

Hata hivyo, shabaha ya Maende-leo ya Milenia inaelekeza malengo yake katika kupunguza vifo kwa akina mama waja wazito na vifo vya watoto.

Kulingana na Dkt. Pape Amadou Gaye ambaye ni kinara na afisa mkuu wa |Shirika la Intra Health International swala la wafanyikazi wenye ujuzi ku-hama kwenda kutafuta kazi za manufaa zaidi ni tatizo la dunia nzima.

“Kwa hakika kuna upungufu wa wafanyikazi wa afya duniani kote, iki-wa na Amerika,” akasema Gaye. Alion-geza, Afrika ina asilimia 24 ya mzigo wa magonjwa lakini wafanyikazi we-nye ujuzi ni kati ya 1.2 hadi 1.5 pekee. Alisema upungufu wa wafanyikazi uko kila mahali katika nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na upun-gufu huo unatatiza huduma na kupati-kana kwa huduma hizo.

“Hakuna nchi yoyote katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara am-bayo imefikia viwango vilivyowekwa na Shirika la Afya la Ulimwengu. Hali hiyo imetatiza sana huduma za afya ya uzazi,”akasema Gaye.

Ili kufanikisha malengo ya ki-maendeleo ya Milenia awamu za nne na tano kuhusu kupunguzwa kwa idadi ya vifo vya watoto wachanga na vifo vya akina mama wakati wa kujifungua, asilimia 95 ya watoto wa-naozaliwa, wanapasa kuwa chini ya uangalizi wa wakunga wenye elimu, maarifa na ujuzi.

Kwa sasa mafunzo ya ukunga hu-tolewa katika viwango vya diploma na digrii lakini matayarisho yanafanywa ya kutoa mafunzo ya elimu ya juu zai-di baada ya digrii ya kwanza.

Hii ni changamoto kubwa kwa sababu hakuna pembejeo zinazo-faa za kutolea elimu hiyo kama vile elimu na utafiti kuhusiana na ukunga nchini Kenya.”Wauguzi na wakunga kwa kawaida hawaruhusiwi kushiriki kwenye kazi za ziada,” asema Epalat.

Amehimiza kuimarishwa kwa ka-nuni za usimamizi wa sekta hiyo ili kuwanufaisha wakunga na wanawake wanaohitaji huduma zao.

Hata hivyo Gaye anasema katika kipindi cha miaka kati ya minne na mitano, kumekuwa na kiwango cha kulifurahisha cha ongezeko la ufaha-mu kuhusiana na wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta ya afya.

Habari njema ni kwamba kila mtu anapigania kuimarishwa kwa afya bora ya uzazi. Lakini kulingana na Gaye habari mbaya ni kwamba maendeleo katika sekta hiyo ni finyu mno katika kukomesha uhamaji wa wafanyikazi hao wenye ujuzi. Hata hivyo, anaendelea kutoa habari njema kwamba nchi zimestawisha nguvu kazi za kibinadamu au zimo katika harakati za uandalizi wa mipango ya ustawishaji nguvu kazi.

“Hata ingawa ustawi huo unaen-delea bado hatujaona athari njema za ustawi wa nguvu kazi katika miradi ya sekta ya afya,” asema Gaye.

Alikariri kwamba nchi nyingi zimeanza kubadilisha majukumu. “Baadhi ya wauguzi wamepelekwa ku-fanya kazi za nyadhifa za chini . Jam-bo hilo limepata mafanikio makubwa nchini Msumbiji, lakini pia limeanza kudhihirika katika nchi za Burkina Faso na Senegal,” Gaye akasema.

“Harakati sasa zinaelekezwa kwa wahudumu wa afya wa kijamii na hilo limesaidia sana hasa katika sehemu za mashambani.”

Gaye alikuwa akizungumza na kundi la waandishi habari kutoka Shirika la African Woman and Child Features Serv ices katika kituo cha shirika la Communications Consor-tium Media Centre mjini Washington.

Hatua kabambe zafaa kuchukuliwa ili kuzuia wajuzi wa afya kuhama

“Kimataifa kuna upungufu mkubwa mno wa watumishi kwenye vituo vya afya ikiwa ni pamoja na Marekani.

Bara la Afrika lina mzigo wa asilimia 24 wa magonjwa ambapo 1.2

hadi 1.5 kuna wafanyikazi wajuzi kwenye sekta ya

utabibu.”— Dkt Pape Amadou Gaye,

Kinara wa IntraHealth International

Muuguzi akimshugulikia mtoto mchanga katika mojawapo ya hospitali za kitaifa ambapo kiwango ni muuguzi mmoja kwa wagonjwa 15 na hivyo huwa na kazi nyingi kuweza kufikia lengo la

muuguzi mmoja kwa wagonjwa 4. Picha na: Florence Sipalla

Vifo vya mapema vitokeavyo nchiniNa Joyce Chimbi…

Ingawa vifo vinavyotokana na uzazi vinaweza kuzuiwa, shabaha ya mil-lennia ya maendeleo kifungu cha tano, kuimarisha afya ya uzazi,

kimekuwa kigumu kutekeleza huku maelfu ya wanawake wakiendelea kufa nchini kutokana na sababu zinazohusi-ana na uja uzito. Hii ni kwa sababu wan-awake hao hawawezi kupata huduma za dharura ambazo zinapatikana kwenye vituo vya afya na wakati mwingine hata hawapatui upinzani wowote wa kutumia huduma za upangaji uzazi za kuwasaidia kuepuka kuhimili, au kupata mimba. Ukosefu wa huduma za upangaji uzazi zimefikia kiwamngo cha asilimia 24 (KDSH2008/2009).

TarakimuUchunguzi uliofanywa na Shirika la

Afya la Ulimwengu (WHO), UNICEF-na Benki ya Ulimwenguumeonyesha kwamba Kenya ni miongoni mwa matai-fa manane ulimwenguni yaliyoshindwa kupunguza idadi ya vifo miongoni mwa wanawake waja wazito kati ya mwaka 1990 na 2008, Kwa hakika vifo vya aki-na mama walja wazitoni kiashirio cha msingi kinachodhihirisha kudhoofika kwa huduma za afya ya uzazi.

Kulingana na taarifa ya KDHS ya mwaka 2003, viwango vya vifo vilivyo-tokana na uja uzito wanawake 414 kati ya wanawake laki moja na kulingana na taarifa ya KDHS ya mwaka 2008 hadi 2009 kiwango hicho kiliongezeka hadi wanawake 488 kati ya wanawake laki moja waja wazito.

Taarifa ya kila mwaka kuhusu hali ya watoto, ilieleza kwamba hapa nchini mwanamke mmoja kati ya kila wan-awake 38 waja wazito hupata matatizo ya uja uzito.

Page 11: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

11 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Hatua thabiti kulinda wale

wako kwa ndoaNa Patrick Mwanzia…

Kwa wanawake wengi ndoa ndiyo nguzo ya nguvu zao. Kwa hivyo watafanya kila wawezalo kuhakikisha kudu-

mu kwa uthabiti wa ndoa yao.Hii ndiyo hali halisi ya mambo hasa

kwa wanawake ambao wanaishi na ukim-wi.Wanawake hao mara nyingi huwa wamo katika hatari ya kubaki makiwani.

Wakihofia kuvunjika kwa ndoa zao, qwengi wa wanawake walio na virusi vya ukimwi huenda kinyume cha ush-auri wa daktarina kupata mimba hata ingawa hesabu ya chembechembe zina-zojulikana kama CD4 ndani ya miili yao iko chini. Haya ndiyo yaliyomkumba Ruth Mwikali ambaye ni mfano mmoja tu wa wanawake wengi ambao wamepi-tia janga hilo.

“Niliolewa na mume wangu alihitaji watoto. Sikuweza kubaki katika ndoa bila ya kupata watoto zaidi na alitaka nimzalie watoto wengine.. Hakujali juu ya hali yan-gu ya afya,” akasema Mwikali.

Mwikali mwenye umri wa miaka thelathini na mitano ana virusi vya ukimwi na ana watoto watano. Amekuwa aking’ang’ana kwa kila njia kudumisha ndoa yake baada ya kupimwa na kupati-kana kuwa na virusi vya ukimwi wakati alipokuwa na watoto wawili pekee. Hali yake ya afya ilikuwa mbaya huku hesabu ya chembechembe za CD4 zikiwa chini ya 200 lakini hilo halikumzuia mumewe kudai kuzaliwa watoto zaidi.

UambukizajiKulingana na mwongozo uliotolewa

na Shirika la Afya la Ulimwengu, WHO, mtu yeyote ambaye chembechembe zake za CD4 ziko chini ya kiwango cha 350 anapaswa kutumia madawa ya kupam-bana na virusi vya ukimwi. Hapa nchini Kenya kutokana na kuwepo idadi kub-wa ya watu walio na virusi vya ukimwi, kiwango hicho cha CD4 kimepunguzwa hadi kiasi cha CD4 200. Hii ni kwa kuwa idadi ya watu wenye virusi vya ukimwi imefikia milioni moja na laki nne.

Kati ya waathiriwa hao milioni moja na laki nne, ni laki nne pekee ndio am-bao wanatumia madawa ya kupunguza nguvu za virusi vya ukimwi.

Kulingana na mtaalam wa mbinu za kupunguza uambukizaji wa virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mja mzito hadi kwa mtoto aliye ndani ya mim-ba, uja uzito huongeza uwezekano wa kuongeza uambukizaji wa magonjwa kwa wanawake ambao tayari wameam-bukizwa virusi hivyo. Hali hiyo hu-punguzakinga ya mwili wa mhusika na kuufanya kuwa dhaifuna kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa hatari.

Mtaalam huyo amafafanua kwamba ni muhimu kwa wanawke walioam-bukizwa vurusi vya ukimwi kutafuta ushauri wa daktari kama ni vyema ku-shika mimba au la, na kadhalika njia za tahadhari zinazopaswa kuzingatiwa endapo mhusika atapata mimba.. Ku-fanya hivyo kutawawezesha wanawake hao kudumisha hali zao za afya ili kuk-abiliana na magonjwa yanayotumia ud-haifu wa kinga kuushambulia mwili.

Baada ya kupatikana na virusi vya ukimwi akiwa na mimba ya mtoto wa tatu, Mwikali anasema hakutahadhar-ishwa lolote kuhusu madhara ya kupata motto mwingine, wala si baada ya ku-pata motto wake wan ne wala wa tano.

“Daktari alibaki kimya kuhusiana na swala hilo ingawa alikuwa akinichunguza mara kwa mara zaidi ya kawaida wakati wa mimba zote, akaeleza Mwikali.

Aliongeza: “Daktari hakuniambia kama uja uzito unaweza kudhoofsha hali yangu ya afya. Nafikiri daktari ali-hofia kunitia wasiwasi zaidi baada ya kumfahamisha hali yangu ya ndoa.”

Changamoto kwa akina mama mashinaniNa Ben Oroko…

Ijapokuwa ni haki ya kila mwanamke kujifany-ia uamuzi kuhusiana na maswala ya kimap-enzi na afya ya uzazi, kama inavyotambuliwa na kuti iliwa mkazo na mikataba mbali mbali

ya haki za binadamu, wanawake walioambukizwa ukimwi wanaendelea kutaabika kutokana na fed-heaha na kubaguliwa na wahudumu wa afya.

Huko Kisii pekee hali inainadhihirisha wingu jeusi kuhusiana na wanavyochukuliwa na ku-tendewa wale am,bao wanatafuta matibabu ya ku-punguza makali ya ukimwi, hasa katika vituo vya afya vya umma.

Wanawake kadha wanaotafuta huduma hiyo wanaendelea kutaabika kimya kimya huku baadhi yao wakiteseka kutokana na habari 0otofu zina-zosambazwa kuhusiana na ugonjwa huo na hivyo basi kuwalazimisha kutafuta matibabu kutoka kwa waganga wa kienyeji na waganga wa miti shamba kama hatua ya mwisho ya kupambana na athari zi-nazosababishwa na ukimwi.

ZitatangazwaUchunguzi uliofanywa unaonyesha kwam,ba

wanawake waja wazito ambao wana virusi vya ukimwi yasemekana hawaendi kliniki kupimwa kwenye vituo vya afya vya umma kwa kuhofia kwamba hali zao za ugonjwa huo zitatangazwa na wafanyikazi wa vituo hivyo vya afya wasiojali ka-nuni za kimatibabu.

Ingawa Milka Moraa mkazi wa kijiji kikubwa cha Daraja mbili ambacho ni kitongoji cha mji wa Kisii, anasema hajakumbwa na tatizo la kutendewa vibaya na maafisa wa matibabu anapokwenda kutafuta madawa ya kupunguza athari za virusi vya ukimwi katika hospitali ya Kisii Level Five. Anase-ma kwamba wale wanaokwenda kutafuta huduma hizo katika hospitali za sehemu za mashambani hukabiliwa na fedheha na kubaguliwa.

“Dhana mbaya kuhusu wanawake walioam-bukizwa virusi vya ukimwi ni tataizo kubwa na sewrikali ina mengi ya kufanya katika kuwafanya wahudumu wa afya kubadili fikra zao kwa wan-awake wanaotafuta matibabu ya kupambana na makali ya virusi vya ukimwi,” akasema Moraa.

Moraa alielezea wasiwasi wake juu ya hofu in-ayozidi kuongezeka miongoni mwa wakazi, hasa wale wa sehemu za mashambani kwa kutoweza kupata huduma za madawa ya kupambana na ukimwi kwa urahisi. Wanawake hao wana haki ya kulindwa kwa habari zao kuhusu maradhi wanay-ougua wakati wanapotafuta huduma za uchunguzi wa virusi vya ukimwi na wakati wanapotafuta mat-ibabu katika vituo vya afya vya umma.

Ingawa kupatikana kwa madawa ya kuzuia athari za virusi vya ukimwi kwaweza kusaidia ku-walinda wanawake kiafya na kuzuia usambazaji wa viiini vya ugonjwa huo kutoka kwa mama hadi kwa mtoto anayezaliwa, wanawake wengi wenye virusi vya ukimwi hawapati matibabu dhidi ya makali ya virusi vya ukimwi.

Moraa anaeleza kwamba licha ya kujua hali yake ya ukimwi kwamba ana virusi alitafuta ushauri wa

kimatibabu kuhusiana na kupata mtoto mwingine. Madaktari katika hospitali ya Kisii Level Five wal-imfanyia Moraa vikao kadha vya ushauri, ikiwa ni pamoja na kumfahamisha mbinu tofauti za upangaji uzazi endapo atachagua kutopata tena uja uzito..

“Baada ya kupitia shughuli za ushauri zinazo-hitajika, niliamua kupata mimba. Nilihudhuria kliniki za kabla ya kujifungua kama nilivyoshau-riwa na madaktari wangu na hatimaye nikampata motto wangu wa mwisho wa kike ambaye sasa ana miaka mitatu,” akaeleza Moraa.

Wakunga katika hospitali hiyo walitumia mbinu za kimatibabu zilizozuia usambazaji wa virusi vya ukimwi kutoka kwa mama hadi kwa motto.

Binti yake Moraa alifanyiwa uchunguzi wa vi-rusi vya ukimwi mara tatu ambao uliodhihirisha kwamba hana virusi vya ukimwi kabla ya mad-aktari katika hospitali hiyo kufunga faili yake ya uchunguzi na kumtangaza binti hiuyo kuwa hana virusi vya ukimwi.

“Kutokana na tajriba yangu, nina hakika kwamba inawezekana kwa mama mwenye virusi vya ukimwi kupata mtoto ambaye hana virusi vya ukimwi.”

Kuna umuhimu kuhamasisha uana dhidi ya miradi ya HIV Na Joyce Chimbi…

Watu wanaokadiriwa ku-fikia milioni moja na laki nne hapa nchini wanaishi na Ukimwi

na virusi vya Ukimwi huku wanawake watatu kati ya watano wakiwa wameam-bukizwa virusi vya Ukimwi nchini.

Kulingana na shirika la uchunguzi wa hali ya Ukimwi Kenya Aids Indi-cator Survey (KAIS), wa mwaka 2007, miongoni mwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 nhadi 24, wan-awake wamo katika hatarti ya kauwa wameambukizwa viini vya Ukimwi mara nne zaidi ya wanaume.

Shirika la KAQIS ndilo linaloam-inika zaidi katika uchunguzi wa hali ya Ukimwi na uchunguzi huo hu-fanywa kila baada ya miaka mitano na uchunguzi wa mwaka 2007 ndio wa hivi punde zaidi.

Katika mwaka 2006, shirika la UNAIDS la Umoja wa Mataifa lilitoa taarifa ambayo ilionyesha kwamba uambukizaji wa virusi vya Ukimwi umefikia kiwango cha kati ya wa-nawake wawili hadi wanne huam-bukizwa virusi hivyo na wanaume.

Matokeo ya uchunguzi huo yanazidi kuonyesha kwamba mwana-mke mmoja kati ya wanawake kumi waja wazito ana virusi vya Ukimwi.

Tarakimu hizi zinaomnyesha

kwamba mzigo wa kuambukizwa virusi vya Ukimwi uko juu zaidi kwa upande wa wanawake kuliko kwa wanaume.

Tangu mwaka 2003 wanawake 121,600 wamekuwa wakipokea madawa ya kauvunjua makali ya vi-rusi vya Ukimwi chini ya mpango wa kuzuia uambukizaji wa virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa.

KushirikishaHuku mzigo wa ugonjwa huu am-

bao umekuwa changa moto kubwa katika historia ya mwanadamu uk-iendelea kuwalemea zaidi wanawake, mipango ya kuweka raslimali kwenye miradi ya kijinsia hapa nchini hivi majuzi ilipata pigo kubwa.

Wakati hazina ya uliomwengu ili-pokataa kufadhili awamu ya nane ya kupambana na Ukimwi na virusi vya Ukimwi katika mwaka 2008, harakati ya kiushirikisha mkono wa kijin-sia kwenye vita vya kupambana na Ukimwi ziliendelea kuwa ndoto isiyo na mwelekeo.

Hazina hiyo ya uloimwengu ya kufadhili miradi ya kupambana na Ukimwi, kifua kikuu na Malaria, ilidhamiriwa kuongeza kwa kima kikubwa aslimali za kupambana na magonjwa hayo matatu hatarti duni-ani kwa kuelekeza pesa na aslimali nyinginezo katika sehemu zenye uhi-

taji mkubwa.KusambaaInakadiriwa kwamba

watu laki moja wanaambukizwa vi-rusi vya Ukimwi kila mwaka huku ugonjwa wa Malaria ukiwaua watu elfu thelathimni na nne . Pia ugonjwa wa kifua kikuu umekita mizizi mi-ongoni mwa watu wenye virusi vya Ukimwi na wagonjwa wa Ukimwi kwa jumla.

Awamu ya nane ya ufadhili huo ilikuwa muhimu mno kwa wan-awake. Hakuna awamu ambayo ilikuwa imeshirikisha wanawake kama hiyo ya nane. Awamu za awali zilishughulikia maswala kama vile kukadiria athari za kifua kikuu na Ukimwi na maambukizi mengine na upunguzaji wa athari za Ukimwi na virusi vya Ukimwi .

Hivyo basi uwezo wa Kenya wa ku-pata raslimali kwa ajili ya kugharamia mipango ya kuzuia maambukizi ya vi-rusi vya Ukimwi, matibabu, na utunzaji wa wagonjwa katika mtazamo wa kijin-sia bado uko mbali na kutekelezwa.

Katika awamu ya saba Kenya ilidhamiria kuimarisha sekta ya afya lakini awamu ya nane ilikuwa bora zaidi kwa sababu ilizungumza na mwanamke wa Kenya kwa sababu ilizungumzia juu ya mwanamke wa Kenya ambaye bado sura yake ni sura ya Ukimwi.

“Awamu ya nane ilikusudiwa

kushughulikia maswala muhimu ya mwanamke hapa nchini. Hazina hiyo ilikuwa itaingilia kati maswala ya ki-jinsia, ya kijamii na kuimarisha sekta ya afya.”

Mzigo wa ugonjwa huu bado hau-jabadiloika na uko vile vile kama hapo awali kwa mwanamke. Upungufu wowote uwe wa kisiasa, kitaalamu, kifedha unaelekea kumhangaisha mwanamke.”amesema Dkt. Nduku Ki-lonzo, ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa kituo cha uchunguzi wa virusi vya Ukimwi cha Liverpool VCT kilichoko Hurlingham, Nairobi.

Kenya ilianza kupokea ufadhili kutoka hazina hiyo ya ulimwengum-namo mwakia 2003 ambapo tangu hapo masuala ya kijinsia hayakutajwa kuwa na miradi yoyote kwenye mao-mbi yake.

Kusahaulika huko kumetenga kando miradi inayoshirikisha ma-hitaji muhimu ya wanawake. Uwe unazungumzia uambukizaji, mati-babu au utunzaji, hakuna ambaye ana uwajibikaji mkubwa kuliko mwana-mke, katika maswala yanayohusiana na Ukimwi, asisitiza Dkt Nduku.

Mbali na hayo anasema wajibu wa kumtunza na kumsaidia mume, jamaa au rafiki ambaye ana virusi vya Ukim-wi, nio changamoto kubwa ambayo wanawake wengi hukabiliana nayo.

Mnamo mwaka 2007 watu 452,800

Bi Milkah Moraa mkazi wa Daraja Mbili mjini Kisii akielezea habari za wanawake wengi wanaoishi na virusi vya HIV. Yeye ni mmoja Wakenya milioni 1.4 wanaoishi na virusi vya HIV

na ambaye uhamasisha wengi na habari zinazomhusu. Picha na: Ben Oroko

“Habari za dhana zinazotolewa dhidi ya wanawake walio na

virusi vya HIV ni changamoto kuu na serikali inawajibu

mkubwa kuhakikisha kwamba hali ya afya ya wananchi

inadumishwa.” — Milkah Moraa

Page 12: Maswala ya wanawake TAHARIRI kuhusu bajeti ya 2011 Woman 019... · 2016-04-05 · Waziri wa Sheria Veerappa Moily amependekeza kwamba wagombezi wanawake wa viti vya kisiasa na wagombezi

12 Toleo Namba 19 • Julai 2011

Mwanamke Mkenya ni toleo la African Woman and Child Feature Service

Email: [email protected]

Jarida hili limechapishwa kutokana na usaidizi wa Hazina la Kidemokrasia la Umoja wa Mataifa (UNDEF)

Mkurugenzi Mkuu: Rosemary Okello-Orlale

Mhariri Mkurugenzi: Arthur Okwemba

Mhariri Msimamizi: Jane Godia

Wahariri Wasaidizi: Bob Okoth, Gunga Chea

Waandishi: Joyce Chimbi, Wilson Rotich, Nita Bhalla, Faith Muiruri, Omondi Gwengi, Duncan Mboya, Omwa Ombara, Florence Sipalla, Karani Kelvin, Henry Kahara, Ben Oroko, Patrick Mwanzia, Kata Fustos

Wapambe: Bernadette Muliru na Noel Lumbama, (Noel Creative

Media Ltd)

Dhuluma zinaongeza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa

Na Kata Fustos…

Kiwango cha watu walio-athiriwa na virusi vya ukim-wi katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kimefikia

asilimia 68, na wengi wa waathiriwa wa janga hili ni wanawake.

Ghasia za kijinsia ndizo zina-zochochea zaidi maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanawke katika kanda hii. Kwa sababu hiyo basi mashirika mengi ya ulimwengu yameimarisha jitihada za kupambana na ghasia dhidi ya wanawake kama chombo muhimu cha kukabiliana na kuzaghaa kwa janga la ukimwi.

Mbinu za kuzuia kuenea kwa virusi hivyo zinatakikana kushughu-likia utovu wa usawa kati ya wanaume na wanawake, na kawaida na desturi ambazo zina3wafanya wanawake kusukumwa karibu zaidi na kuam-bukizwa virusi hivyo.

Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, wanawake wame-kuwa ndio sura ya ukimwi katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara kwani asilimia 61 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika kanda hii ni wanawake. Viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya virusi vya ukimwi kati ya wanawake wa kuanzia umri wa kuanzia miaka 15 hadi 49 vina-patikana katika eneo la kusini mwa Afrika, hasa Botswana, Lesoth, Swa-ziland na Afrika Kusini.

WanaoambukizwaNchini Afrika Kusini, kuzagaa

kwa virusi vya ukimwi miongoni mwa wanawake chipukizi wa kuanzia umri wa miaka 20 hadi 24 ni vya juu mara tatu zaidi. Asilimia 21 ikilinm-ganishwa na asilimia 7 ikilinganishwa na wanaume wa umri sawa na huo wa wanawake. Huko Lesothokaribu asilimia nane ya wanawake cfhipukizi wa kuanzia umri wa miaka 15 hadi 19 wameambukizwa virusi vya ukimwi ilhali kwa upoande wa wanaume , walioambukizwa ni asilimia tatu pe-kee katika umri huo. Viwango hivyo vinaashiria kwamba kuna mambo ambayo yanawasukuma wanawake kuambukizwa virusi vya ukimwi.

Kulingana na shirika la UNAIDS wanawake ambao wamepitia katika mikono ya ghasia wamo katika hatari ya kuambukizwa virusi vya ukimwi mara tatu zaidi ya wale ambao hawa-ko katika maeneo yenye ghasia.

Tarakimu za nchi zilizotayarishwa na Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba wanawake chipukizi barani Afrika wamo katika hatari kubwa zaidi ya kukabiliwa na ghasia za ki-mapenzi na za kimabavu kuliko wa-nawake watu wazima, kwa kawaida kutoka kwa mpenzi.

Ingawa ghasia dhidi ya wanawake zinategemea nchi na eneo, uchunguzi unaonyesha kwamba ghasia hizo hu-wapata wamawake chipukizi wakati wanapofikia umri wa miaka kati ya 20 na 30 na kasha huanza kupungua.

. Kusambaa kwa virusi vya ukim-wi kadhalika hufikia kilele ka-tika umri wa miaka 25 miongoni mwa wanawake. Kwa upande mwingine, uambukizaji wa virusi vya ukimwi miopngoni mwa wa-naume hifikia kilele miaka kati ya mitano hadi kumi baadaye na kwa viwango vya chini.

Ghasia huongeza uwezekano wa kuambukizwa virusi vya ukim-wi miongoni mwa wanawake ku-tokana na sababu za kifikra.

Wanawake ambao hawa-jaambukizwa virusi vya ukiwmi wamo katika hatari mara mbili zaidi ya kuambukizwa virusi hivyo na wanaume walionavyo, kuliko mwanamke kumwam-bukiza mwanaume ambaye hana virusi hivyo.

Kibiolojia wanawake wamo katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa virusi hivyo, na kulazimishwa kufanya ngono kadhalika huongeza uwezekano wa wanawake kuambukizwa virusi hivyo. Hasa kutokana na michubuko hasa miongoni mwa wasichana wadogo. Hata hivyo tishio la ghasia linaweza kusababisha athari mbaya . Wa-nawake wanaoagopa ghasia huwa hawawezi kujilinda dhidi ya maambukizo hya virusi vya ugonjwa huo. Hawana uwezo wa ku-fanya makubaliano ya kufanya map-enzi kwa njia ya usalama au kukataa kufanya mapenzi ambayo hawayata-ki. Wanawake hao hawaendi kuchun-guzwa virusi vya ukimwi na huwa hawendi kutafuta matibabu baada ya kuambukizwa.

Uchunguzi uliofanywa mwaka 2005 ulipata kwamba asilimia 60 ya wanawake waliokuwa na virusi vya ukimwi walikataa kwenda kutafuta matibnabu kwenye kliniki moja ya Zambia kwa sababu walihofia kufanyi-wa ghasia na kutengwa na jamaa zao.

Wanawake wanafahamika kuho-fia kubaguliwa, ghasia na kutengwa na jamaa zao watakaposema kuwa wana virusi vya ukimwi. Kwenye uchunguzi kuhusu ghasia za ngono huko Afrika Kusini, asilimia 16 ya wanaume na asilimia 14 ya wanawake wa umri wa kuanzia miaka 15 hadi 19 hawangeweza kuelezea jamaa zao kuwa wana virusi vya ukimwi baada ya kupatikana na virusi hivyo. Vijana ambao walikuwa wamelazimishwa kufanya mapenzi katika kipindi cha mwaka mmoja uliotangulia hawaku-weza kufichua hali zao kuhusu ugon-jwa wa ukimwi.

Kukubalika kijamii kwa desturi ya kuwa mwanaume ana nguvu dhidi ya

mwanamke , na kutumiwa kwa uwezo wa mwanamume dhidi ya mwanam-ke kunahimiza ukosefu wa usawa wa kijinsia jambo ambalo husababisha ghasia hizo za kijinsia. Aina nyingi za ubabe wa kiume dhidi ya wanawake ambao huungwa mkono na idadi kubwa ya wanaume hukubaliwa kwa kiwango kikubwa na wanawake. Kwa mfano Uchunguzi wa hali ya ukimwi na mienendo ya kimapenzi nchini Afrioka Kusini ulionyesha kwamba miongoni mwa vijana wa umri kati ya miaka 15 na 19, yaani asilimia 28 ya wavulana na asilimia 27 ya wasichana wanaamini kwamba msichana hana haki ya kukataa vishawishi vya kufan-ya mapenzi kutoka kwa rafiki yake wa kiume. Na asilimia 55 ya wanaume na asilimia 54 ya wanawake wana dhana kwamba “ghasia za kimapenzi haz-ishairikishi kuwalazimisha wanawake kufanya mapenzi na mtu unayemjua.

Zaidi ya hayo ni kwamba asilimia 15 ya wanawake wa umri wa miaka 19 na asilimia 12 ya wavulana kwenye uchunguzi huo walisema walilazi-mishwa kufanya mapenzi katika kip-indi cha mwaka uliotangulia kabla ya uchunguzi huo kufanywa.

Pamoja na hayo ukosefu wa usawa wa uwezo kati ya wanawake na wa-naume unazidi kuvurugwa na tofauti kubwa ya kiumri kwenye mahusiano.

Ni kawaida kwa wanawake wa kusini mwa jangwa la Sahara kuolewa waki-wa na umri mdogo au kuwa na waume wazee kuwashinda wenye tajriba kubwa ya kimapenzi. Wanaume watu wazima kadhalika huenda wameam-bukizwa virusi vya ukimwi na kuweza kuwaambukiza wapenzi wao wadogo, hasa wanawake hao wanapojipata kwamba hawawezi kushaurana na wapenzi wao kuhusu kutumia njia za kiusalama za kufanya mapenzi kwa sa-babu ya ukosefu wa usawa wa uwezo kwenye uhusiano wao.

KushughulikiaUchunguzi uliofanywa huko

Zambia ulipata kwamba ni asilimia 11 tu ya wanawake walioolewa ndio wanaoamini kwamba wana haki ya kuwaomba waume zao kutumia puto au mipira ya kufanyia mapenz, hata kama wanajua ya kwamba mume huyo aliambukizwa virusi vya ukim-wi. Chini ya asilimia 25 wanaamini ya kwamba wana haki ya kukataa kufan-ya mapenzi na mume huyo . Huko Le-sotho karibu asilimia 37 ya wanawake walioolewa wanaamimi kwamba wa-naume ana haki ya kumpiga mkewe kama mke huyo atabishana naye. Asilimia ishirini na tatu wanakubali kwamba kupigwa ni sawa kama mwa-namke huyo atakataa kufanya map-enzi na mumewe.

Kushughulikia masuala ya ghasia dhidi ya wanawake na wasichana kwe-nye vita vya kupambana na ukimwi ni suala gumu kwa kuwa mbinu zote za kuingilia kati zinachukua mkono wa desturi za kitamaduni katika kuko-mesha janga hili.

Umuhimu wa kuhamasisha

Hawa ni wajane na mayatima ambao ni sehemu kubwa ya wale walioathirika na Ukimwi. Picha na: Paul Olale

Kulingana na ripoti ya UNAIDS, akina mama ambao wamewahi kuathirika na visa vya dhuluma za ngono kwa kawaida ni mara tatu ya wale wanaoambukizwa

na virusi vya HIV kwenye ndoa.UNAIDS Report

wenye virusi vya Ukimwi ambao kadha-lika waliugua ugonjwa wa kifua kikuu, walikuwa wakipata huduma ya mati-babu na kutunzwa chini ya mpango9 wa rais wa hudhuma za dharura kwa wag-onjwa hao wwenye Ukimwi.

Matibabu na utunzaji wa wagonjwa wa Ukimwi pamoja na mipango ya kuwa-tunza wagonjwa majumbani ambayo ina-tambua mambo ya kijinsia ingesaidia sana katika kuwaondolea wanawake, mizigo ambayo wanawake wanaendelea kuibeba.

Uwekaji raslimali katika harakati zinazoshirikisha mipango ya kijinsia zimekuwa muhimu mno kuzingatiwa, alisistiza Dkt Nduku.

Vita vya kupambana na Ukimwi vi-nahitaji kwamba miradi ya Ukimwi ya kitaifa inashaughulikia utovu wa usawa wa kijinsia. Hayo yanaweza kufanikish-wa kwa kufungamanisha masuala ya ki-jinsia kwenye miradi ya Ukimwi katika sekta ya afya, ili kukabiliana na desturi zinazovuruga uthabiti wa kijinsia.

Hapa nchini wanawake walioolewa wanaokadiriwa kuwa asiloimia 43 wa-nakabiliwa na ghasia za ngono na kupig-wa na waume zao jambo ambalo linawa-fanya kusogelea hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi.

Kwa wanawake wengi haloi zaom za afya zinategemea unyoofu wa kimaadili wa waume zao.

Lakusikitisha ni kwamba hilo si swa-la linaloikabili Kenya pekee, kulingana na matokeo ya uchunguzi yaliyofanywa na shirika la UNAIDS katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Kutoka Uk11