9
Bulletin News HABARI ZA MAFUTA NA GESI Toleo NO: O07 Desemba, 2018 Tovuti: www. tpdc-tz.com TPDC NAIBU WAZIRI WA NISHATI , Mhe. Subira Mgalu (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba wakati Naibu Waziri alipofanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa kusambaza gesi asilia viwandani na kwa matumizi ya nyumbani jijini Dar es Salaam. Shughuli za utafiti zashika kasi TPDC UK 4 TPDC yajipanga kusambaza gesi zaidi Habari zaidi Uk 2

MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETINMAFUTA NA GESI MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

TPDC

BulletinNewsHABARI ZA MAFUTA NA GESI

Toleo NO: O07 Desemba, 2018 Tovuti: www. tpdc-tz.com

TPDC

N A I B U WA Z I R I WA N I S H AT I , Mhe. Subira Mgalu (kushoto) ak ipata maelezo kutok a k wa K aimu Mkurugenzi Mtendaj i wa TPDC, Mha. K apuulya Musomba wak at i Naibu Wazir i a l ipofanya z iara ya uk aguzi wa mradi wa kusambaza gesi as i l ia v iwandani na k wa matumizi ya nyumbani j i j in i Dar

es Salaam.

Shughuli za utafiti zashika kasi TPDC Uk 4

TPDC yajipanga kusambaza gesi zaidi

Habari zaidi Uk 2

Page 2: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETIN MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

2 DECEMBER 2018

Na Theopista Nsanzugwako

Kaya zaidi ya 500, magari 100 na viwanda katika maeneo ya viwanda Mikocheni, ikiwemo Coca-Cola, wataan-za kutumia gesi hiyo mwishoni mwa mwaka 2018.

Awamu ya pili itaunganisha magari 800ya mwendo kasi. Hatua hiyo ni baada ya kazi ya uunganishaji mabomba na mitambo mbalimbali inayoendelea kufanyika kuka-milika. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limebainisha mikakati ya kuongeza matumizi ya gesi asilia katika magari kwa kuweka mikakati mbalimbali.

Mpaka sasa magari 100 yanatumia gesi hiyo na awamu ya pili itahusu magari yaendayo haraka magari 800 kutumia gesi hiyo. Hayo yamebainika wakati wa zi-ara ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipo-kagua ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia viwandani, majumbani na kwenye magari.

Katika ziara hiyo, alijionea kazi ya ukamilishaji wa miun-dombinu katika kiwanda cha Coca-Cola, ambacho kitaanan-za kutumia gesi asilia mapema mwishoni mwa mwaka huu.

Baadaye aliangalia sehemu ya kuunganisha mitam-bo na mabomba katika eneo la Ubungo Kibo na Ubungo Maziwa. Mgalu aliridhishwa na kasi ya ukamilishaji kuunganisha miundombinu hiyo.

Amewahakikishia wananchi wa maeneo ya Sinza, Mlalakuwa, Mikocheni na Chuo Ki-kuu kuwa zaidi ya kaya 500 na viwanda viwi-li vitaungwa katika mtandao wa gesi asilia.

Amesema kwa sasa TPDC inafanya kazi kib-iashara katika kuhakikisha viwanda vinap-ata nishati hiyo na kupunguza gharama za uendeshaji, jambo litakalosaidia kuandaa mazingira ya mapato ya uhakika na kudumu.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Coca-Cola, Gary Pay alisema wamejenga miundombinu ya ku-ingiza gesi asilia katika kiwanda hicho kwa Sh milioni 160 na ujenzi huo ulianza mwaka 2013. Alisema tayari wamekamilisha ujenzi na wanachosubiri ni kufikishiwa gesi tu. Amese-ma baada ya kuanza kutumia gesi asilia, wata-okoa asilimia 30 ya gharama wanazotumia sasa, ambayo ni lita 2,200 za mafuta hayo kwa siku.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba amesema, kwa sasa kazi ndiyo inaanza. Alisema watasambaza gesi maeneo mbalimbali na wanaendelea na kuweka mabomba ambapo kazi hiyo itakamilika Oktoba.

Amesema wateja wataanza kutumia gesi hiyo mwis-honi mwa mwaka huu. Alisema watu wengi wame-onesha nia ya kuunganishiwa kwa mabomba hayo.

Kwamba katika bajeti ya mwaka huu, watafikisha kwa wakazi wa Sinza na Chuo Kikuu, ambapo migahawa yote ya chuo hicho itaunganishwa. Wakazi wa Mlalakuwa na Mikocheni na viwanda maeneo hayo, pia wataunganishwa.

“Gesi tuliyonayo inatosha katika kuunganisha viwanda vilivyopo na wananchi. Mwaka ujao wa fedha tunatarajia kuwafikia wakazi wa maeneo ya Ubungo na kwingineko, lakini hawa walio karibu na eneo hili na miundombinu, wana changamoto ya nyumba hazijakaa katika mistari, hivyo inahitajika umakini katika kufikisha gesi hii,” alisema.

Akizungumzia matumizi ya gesi kwenye magari, alisema mpaka sasa yapo zaidi ya 100. Lakini, alisema changamoto ni kuwepo kituo kimoja cha kujaza gesi katika magari, am-bacho kinajaza magari ya kawaida 10 kwa siku. Amesema kazi ya kufunga mifumo ya gesi asilia katika gari, inafanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Teknolojia Dar es Salam (DIT) kwa gharama ya milioni 1.6 mpaka milioni mbi-li. Alibainisha gesi inapunguza gharama za matumizi fedha, ambapo ndani ya miezi sita fedha hizo, zinakuwa zimerudi.

Amebainisha kuwa TPDC imekubaliana na Wakala wa Usafiri Dar es Salaam (DART) kuweka gesi asilia katika awamu ya pili, itakayohusisha magari 800. Pia kutaku-wa na vituo vya kujaza gesi Kariakoo, Ubungo sehemu yenye kituo cha mabasi, Gongo la Mboto na Mbagala.

Akiwa katika kituo cha kujaza gesi cha Ubungo Maziwa, Mgalu alitaka TPDC ku-harakisha ujenzi wa vituo zaidi ili wananchi wengi waunganishwe kwenye matumi-zi ya gesi asilia kwenye magari, hivyo ku-punguza matumizi ya nishati ya mafuta.

Mmoja wa wananchi waliokutwa akijaza gesi kwenye gari yake aina ya Toyota IST, Beni Kasisiwe alisema ameunganisha mfu-mo huo kwa Sh. milioni 1.6 na ametumia kwa miezi nane kwa kujaza gesi ya kilo tisa kwa Sh 12,000 na anatumia katika kilometa 200.

Alisema katika muda huo, amepunguza gharama kubwa ya matumizi ya mafuta, kwani alipokuwa anatumia Sh 30,000 kwa sasa ana-tumia Sh 10,000. Aliomba TPDC kuangalia uwezekano wa kituo hicho, kufanya kazi saa 24; na siyo sasa ambapo wanafunga saa 12 jioni.

Akizungumzia usambazaji wa gesi hiyo majumba-ni, Meneja Biashara wa TPDC, Dora Ernest alibainisha kuwa katika kuhakikisha gesi inasambazwa kwa wate-ja wa majumbani na viwandani kutoka Ubungo Kibo mpaka Ubungo Maziwa, kuna matoleo manne, kati yake moja ni kubwa na manne madogo. Kutoka Ubun-go Maziwa mpaka Mikocheni, kukiwa na matoleo sita.

TPDC yajipanga kusambaza gesi zaidi Inatoka Uk 1

kwa gesi ya shilingi 12,000 am-bayo hujaa mtungi wa kilo tisa huni-wezesha kutembea umbali wa kilometa 200

Page 3: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETINMAFUTA NA GESI MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

3

TahaririNi mara nyingine tena napenda kutumia

fursa hii kuwakaribisha wasomaji katika Jarida letu. Jarida hili linalenga kutoa taa-rifa za shughuli mbalimbali zilizofanywa na TPDC katika kipindi cha robo ya kwan-

za ya mwaka wa fedha 2018/19. Katika toleo hili tume-gusia masuala ya mkondo wa juu kwa kuangazia kazi zilizotekelezwa na Shirika katika vitalu vilivyotengwa kwa ajili ya Shirika la Taifa la Mafuta (NOC) ikiwa ni jiti-hada za makusudi za Serikali kuliwezesha Shirika hili. Kadhalika toleo hili limeangazia kazi za mkondo wa chini ambazo zinahusisha miradi ya kusambaza gesi asilia katika taasisi, viwandani na matumizi ya nyum-bani ambapo tayari kazi mbalimbali zimeshaanza katika kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali ya gesi asilia moja kwa moja, na tunawezesha kuinua uchumi na kufanya Tanzania ya viwanda kuwa halisia.

Katika kuchangia dhana ya Tanzania ya viwanda, TPDC imeendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha upati-kanaji wa nishati ya gesi asilia unawezekana. Mchango wa TPDC katika Tanzania ya viwanda una sura mbili, moja ni ile ya kusambaza gesi kwa kampuni ya kuzali-sha umeme (TANESCO) na pili ni kwa kusambaza gesi kwa viwanda moja kwa moja ambapo gesi hutumika kama chanzo cha nishati. Hivyo TPDC inasaidia katika upatakanaji wa umeme wa uhakika hapa nchini jam-bo ambalo linaongeza mvuto wa nchi kama kituo cha uwekezaji Afrika Mashariki na pia inatoa mbadala wa nishati kwa wawekezaji wa viwanda ambapo kupitia TPDC wanaweza kuchagua kutumia gesi asilia badala ya aina nyingine za nishati kama mafuta mazito na dizeli ambazo ni ghali na si rafiki wa mazingira.

Ni matumani yetu kwamba jarida hili litatoa mwan-gaza wa yale tunayoyafanya kama Shirika na hivyo kutuweka wote katika nafasi sawa ya uelewa wa shu-ghuli tuzifanyazo. Tunaendelea kutoa msisitizo kwa wale wote wenye taarifa au jambo ambalo wanataka kuwajuza wadau na wasomaji wa jarida hili wafanye mawasiliano na kitengo cha mawasiliano cha Shirika ili kuhakikisha habari au taarifa hiyo inapata nafasi katika jarida letu.

Nawatakia usomaji mwema wa jarida la Mafuta na Gesi.

Marie Msellemu,

Meneja Mawasiliano

BODI YA UHARIRIMhariri:Marie Msellemu

Wajumbe:Francis LupokelaEugene IsayaOscar MwakasegeMalik Munisi

LIMETOLEWA NA: Kitengo cha MawasilianoShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)Benjamin W. Mkapa Pensions Towers, Azikiwe/Jamuhuri StreetS.L.P. 2774,Dar Es Salaam, TanzaniaSimu:+255 22 2200103/4, 2200112.Nukushi: +255 22 22 2200113Barua pepe: [email protected]: www.tpdc.co.tz

@TPDCTZ

TPDC Tanzania

DECEMBER 2018

Page 4: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETIN MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

4

Mkondo wa juu wa sek-ta ya mafuta na gesi ndio lan-

go kuu la ugunduzi wa mafuta na gesi.

Wengi hufurahia kuona ugunduzi umefanyika na ama kwa hakika hapo ndipo furaha na matu-maini ya wengi huibuka. Lakini jambo ambalo wengi husahau ni kwamba kabla ya mafanikio ni lazima akili, kujituma na ubunifu vitumike ku-weza kufikia mafanikio hayo. Moja ya majuku-mu makuu ya TPDC kama Shirika la Mafuta la Taifa ni kufanya utafiti wa mafuta na gesi nchini.

Katika robo ya kwanza ya mwaka, TPDC kupitia idara ya mkondo wa juu imefanikiwa kutekeleza

shughuli mbalimbali za utafiti wa awali katika vi-talu ambavyo vinamilikiwa na Shirika. Akiongea na mwandishi wa habari hii, Mkurugenzi wa Idara ya Mkondo wa Juu, Bi. Venosa Ngowi anasema “tu-meweka nguvu kubwa katika kufanya shughuli za utafiti kwa kuzingatia mahitaji makubwa ya gesi asilia nchini kuwezesha dhamira ya Tanzania ya vi-wanda kufanikiwa”.

Ngowi anaeleza kuwa TPDC ilipanga kufanya kazi za kuchakata na kutafsiri takwimu za mitetemo ya mfumo wa 3D na kuandaa mpango wa kuchimba kisima cha utafiti kwa kitalu cha Mnazi Bay Kas-kazini. Kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/19 tumefanikiwa kumpata mkandarasi am-baye ni kampuni ya Schlumberger, kwa kushiriki-ana na wataalam wa ndani, kazi imeanza, anaeleza zaidi Ngowi.

Katika kitalu 4/1b na 4/1c ambavyo viko katika kina kirefu cha bahari mshauri mwelekezi amepa-tikana kwa ajili ya kuboresha cheti cha tathmini ya mazingira ili kuruhusu kazi za kukusanya tak-wimu za mitetemo za 3D kufanyika katika vitalu hivi, pamoja na tathimini ya mazingira kwa vitalu vya Songosongo Magaharibi, Eyasi Wembere na Mnazi Bay Kaskazini anafafanua Bi. Venosa Ngowi.

Wakati huo huo, kazi ya kuandaa hadidu za rejea im-ekamilika na mchakato wa kupata kampuni ya kiji-ofizikia itakayo kusanya takwimu za mitetemo za 3D, kuzichakata na kuzitafsiri kwa vitalu vya Songo Son-go Magharibi, Mnazi Bay Kaskazini na 4/1b na 4/1c umeanza, anaongeza Bi. Ngowi katika taarifa yake.

Zoezi la kuongeza thamani katika vitalu hivi ni pamoja na kuchukua takwimu za mitete-mo za 2D na 3D, kuchakata na kutafsiri tak-wimu hizo ili kuvielewa kwa kina vitalu jam-bo ambalo litaipa TPDC uwezo wa kujadiliana na mshirika wa kimkakati ikiwa kifua mbele.

tumewe-ka ngu-vu kubwa katika ku-fanya shu-ghuli za utafiti kwa kuzingatia mahitaji makubwa ya gesi asi-lia nchini kuwezesha dhamira ya Tanzania ya viwanda kufanikiwa

Shughuli za Utafiti zashika Kasi TPDC

VIFAA maalumu vya kuchukua takwimu za mitetemo (Geophone)vikiwa vimesimikwa ardhini kwa ajili ya kuwezesha zoezi lakukusanya takwimu za mitetemo.

Faustine Kayombo, Mjiofizikia kutoka TPDC akichukua tak-wimu za mitetemo katika kitalu cha Ruvu. Hii ni hatua ya awali ya utafiti wa mafuta na gesi ambapo takwimu za mite-temo husaidia kutoa taswira ya miamba tabaka chini ya ardhi.

DECEMBER 2018

Zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mitetemo likiendelea ka-tika kitalu cha Ruvu kinachomilikiwa na kampuni ya Dodsal. Kitalu hiki tayari kina ugunduzi wa gesi asilia takribani futi za ujazo trilioni 2.17 (2.17TCF).

Page 5: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETINMAFUTA NA GESI MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

5 DECEMBER 2018

Kuelekea Tanzania ya viwanda, jambo moja kubwa liko wazi kwamba Tanzania inahitaji nishati ya kutosha kuwezesha ujenzi wa viwanda vingi na kuipeleka Tanzania kufikia uchumi wa kati. Moja ya nishati ambayo

Tanzania imebarikiwa kwa wingi ni gesi asilia ambapo tayari ugunduzi wa futi za ujazo trilioni 57.54 umefanyika katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani. Ugunduzi huu umefanyika katika maeneo ya nchi kavu pamoja na maeneo ya bahari ya kina kirefu.

Juhudi nyingi zinafanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kutimiza adhma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati. Moja ya juhudi hizo ni maonesho mbalimbali yanayolenga kuisambaza nadharia ya Tanzania ya viwanda na kuchochea uwekezaji zaidi katika sekta viwanda. Juma hili tumeshuhudia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akifungua rasmi maonesho ya viwanda mkoa wa Pwani. Katika ufunguzi huo Makamu wa Rais aliliasa Shirika la Maendeleo ya Petroli

Tanzania (TPDC) kusambaza gesi zaidi viwandani ambapo alisema “TPDC tunataka gesi zaidi viwandani, tuleteeni”. Kauli hii ya Makamu wa Rais ni chachu zaidi kwa TPDC kuendelea na jukumu lake la kutafuta, kuendeleza na kusambaza gesi asilia hapa nchini, anasema Afisa Uhusiano wa TPDC, Malik Munisi. Hadi sasa kuna viwanda vipatavyo 40 vinavyotumia gesi asilia katika uzalishaji wake, na TPDC inaendelea na mazungumzo na viwanda takribani saba maeneo ya Mkuranga ambavyo vina mahitaji ya gesi asilia, anaongeza Malik Munisi. Nae

Mhandisi Limi Lagu kutoka Idara ya Mkondo wa Juu aliongeza kwamba katika kuchochea uchumi wa viwanda, TPDC imetekeleza mradi wa kutoboa bomba kubwa la gesi maeneo ya Mwanambaya, Mkuranga ili kuwezesha wateja zaidi wa viwandani kuunganishiwa gesi asilia. Mhandisi Limi aliendelea kwa kusema kuwa “mradi huu umehusisha kutoboa bomba kitaalamu bila kuzuia gesi kwa kutumia teknolojia ya hot tapping na kisha kutandaza bomba la kilometa 3. kuelekea kiwanda cha Lodhia Steel”. Kwa mujibu wa Mhandisi Lagu, bomba hilo lina uwezo wa kuunganisha viwanda vingi zaidi na hivyo wawekezaji wanahimizwa kuja kuwekeza zaidi maeneo hayo na kutumia nishati ya gesi asilia.

Gesi asilia viwandani inaweza kutumika kwa namna tofauti, kwanza inaweza kutumika kama chanzo cha nishati ambapo inaweza kuzalisha umeme wa kutumia kiwandani, pili inaweza kutumika kwa ajili ya kupashia moto “heating” kama mbadala wa nishati nyingine kama mafuta mazito, kuni au umeme katika uzalishaji wa bidhaa viwandani au majumbani mfano inavyotumika katika viwanda vya saruji. Vile vile gesi asilia inaweza kutumika viwandani kama malighafi katika viwanda vya kemikali za petroli ambavyo huzalisha mbolea, plastiki, methanol

na kadhalika. Kuna faida nyingi katika kutumia gesi asilia ambapo kwanza ni nishati rafiki kwa mazingira hivyo kwa kutumia gesi asilia unaokoa mazingira, pili gesi asilia ni nafuu ukilinganisha na vyanzo vingine vya nishati kama mafuta mazito na umeme lakini pia gesi asilia inaokoa matumizi ya fedha za kigeni kuagiza mafuta mazito nje ya nchi. Tanzania ya viwanda inawezekana na TPDC iko mstari wa mbele kuchochea Tanzania ya Viwanda.

Makamu wa Rais ahimiza TPDC kusambaza gesi viwandani

Bi Neema Maganza, Mjiolojia kutoka TPDC (mwenye suti ya bluu) akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi

waliotembelea banda la TPDC katika maonesho

ya viwanda Pwani.

Page 6: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETIN MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

6 DECEMBER 2018

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kiwanda cha saruji cha Dangote wamefikia makubaliano na kutia saini mkataba wa kuuz-iana gesi asilia kwa matumizi ya uzalishaji wa

megawati 45 za umeme kwa matumizi ya kiwanda hicho.

Akiongea wakati wa utiaji saini wa mkataba huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Mu-somba alisema “mkataba huu unafungua ukurasa mpya wa kibiashara baina ya TPDC na kiwanda cha saruji cha Dan-gote na utadumu kwa mia-ka 20”. Mhandisi Musomba alieleza pia usambazaji wa gesi asilia kwa kiwanda cha Dangote unaongeza matumizi ya gesi asilia katika viwanda hapa nchini kufikia futi za ujazo milioni 23 kwa siku (23mmsfd). “Kama shirika la mafuta na Taifa, pia tuna jukumu la kuchochea ukuaji wa uchumi na tunafanya hivyo kwa kuzalisha na kusambaza nisha-ti nafuu ya gesi asilia” aliongeza Mhandisi Musomba.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha saruji cha Dangote, Jagat Rathee alisema “tunatarajia kuanza uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia ndani

ya miezi miwili ijayo na ni mategemeo yetu kuwa matumizi ya gesi asilia yatapunguza gharama za uzalishaji kwa kiwango kikubwa”. Ndugu Rathee pia aliishukuru Serikali kupitia TPDC kwa kufikia makubaliano hayo na kueleza kwamba upatikanaji wa gesi asilia unafungua fursa kwa uzalishaji zaidi ku-fanyika na pia kuvutia wawekezaji wengi zaidi nchini.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuru-genzi Mtendaji wa TPDC Mhan-disi Kapuulya Musomba mi-kakati ya shirika ni kusambaza gesi asilia kwa wateja wengi zai-di wa viwandani na majumbani.

Mhandisi Musomba anasema katika mwaka wa fedha 2018/19 wanatarajia kuunganisha wate-

ja takribani saba wa viwandani ambapo majadiliano ya mauziano ya gesi yamekwishaanza. Mhandisi Mu-somba alitoa hamasa kwa wawekezaji wa viwandani kuchangamkia fursa ya uwepo wa miundombinu ya gesi asilia katika eneo la Kilometa 550 kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo bomba linapita na ku-ruhusu kutoa gesi kwa yeyote mwenye uhitaji.

“katika eneo la kilometa 550 kutoka Mtwara hadi DSM ambapo miundombinu ya gesi

asilia inapita, uwekezaji wa kiwanda unawe-za kufanyika na sisi tuko tayari kumuungan-

ishia mteja gesi haraka iwezekanavyo”

Mhandisi Kapuulya MusombaKaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba (katikati) na Ofi-sa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha saruji cha Dangote, Ndg. Jagat Rathee (kulia) wakitia saini mkataba wa mauziano ya gesi asilia baina ya TPDC na kiwanda hicho. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TPDC, Wakili Msomi Raymond Baravuga .

TPDC na Dangote watia saini mkataba wa kuuziana gesi asilia

Page 7: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETINMAFUTA NA GESI MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

7

Hayawi hayawi sasa yame-kuwa, kiwanda cha saru-ji cha Dangote chaanza

kutumia gesi asilia kuzalisha umeme wake wenyewe. Suala la kiwanda cha Dangote kutumia gesi asilia limekuwa ni suala lilijodaliwa na wengi na hata wengine kudhani gesi ya kukipatia kiwanda haipo. Hata hivyo wasiwa-si na sintofahamu hiyo ilifikia kikomo mwezi agosti 2018 baada ya TPDC na kiwanda cha saruji cha Dangote kutia saini mkataba wa kuuziana gesi asilia.

Baada ya kusaini mkataba wa mau-ziano ya gesi asilia, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alizindua ras-mi matumizi ya gesi asilia kuzalisha umeme katika kiwanda cha saruji cha Dangote mwezi Septemba. Akion-gea wakati wa uzinduzi huo, Wazi-ri Kalemani alisema”kwa mujibu wa mpango kabambe wa matumizi sahi-hi ya gesi asilia nchini, kati ya futi za ujazo trilioni 57.54 serikali imepan-ga kutumia futi za ujazo trilioni 8.8 kwa ajili ya matumizi ya viwandani ambapo hadi sasa viwanda 40 vina-tumia gesi asilia katika uzalishaji wake”.

Waziri Kalemani aliongeza kuwa matumizi ya gesi asilia kwa kiwanda cha Dangote yatasaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kukiweze-sha kiwanda kuzalisha katika kiwan-go cha juu jambo ambalo litakuwa na atahari chanya kwa kufungua fursa za ajira na kuhakikisha upati-kanaji wa uhakika wa saruji sokoni.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha saruji cha Dangote Jagat Rath-ee alisema “kwa sasa kiwanda kinazalisha umeme kwa kutumia dizeli ambapo kwa siku tunatumia lita 160,000 ambazo zinagharimu takribani shilingi milioni 315 kwa siku, kwa kutumia gesi asilia tutaokoa asilimia 40 ya gharama tunazotumia sasa”. Jagat alieleza ku-furahishwa na jitihada za serikali kuweka maz-ingira wezeshi ya uwekezaji nchini ambayo yanafungua fursa zaidi kwa serikali kuongeza pato lake, ajira kwa wananchi na unafuu wa bidhaa sokoni. “Kwa kupunguza gharama za uendeshaji tunaamini sasa tutaweza ku-zalisha zaidi na pia hapo mbeleni tutaweza hata kuongeza ajira zaidi” alisema Rathee.

Akielezea mradi wa kukipatia kiwanda cha saruji cha Dangote gesi asilia, Mkurugen-zi wa Shughuli za Mkondo wa Chini, Mhan-disi Emmanuel Simon alisema “mradi huu umegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza ni ya kukipatia kiwanda gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme na awamu ya pili ni kukipatia kiwanda gesi kwa ajili ya ku-chomea klinka”. TPDC ilimaliza kazi za ujen-zi wa miundombinu ya kusambaza gesi kwa ajili ya umeme mwezi Septemba 2017 na kazi ikabaki kwa muwekezaji kuleta mashine za kuzalisha umeme wa gesi asilia, anaeleza Mhandisi Simon. Mhandisi Simon anaongeza kwamba, TPDC itasambaza kiasi cha gesi asi-lia futi za ujazo milioni 8 kwa siku kwa ajili ya kuzalisha umeme na baada ya kukamilika kwa awamu ya pili mahitaji ya gesi yatapan-da na kufikia futi za ujazo milioni 30 kwa siku.

Mradi huu unatarajiwa kukamilika Disem-ba 2018 ambapo utapelekea pato la serikali kukua kwani inakadiriwa mapato yatafikia dola za marekani 36,485,400 kwa mwaka. Kiwanda cha saruji cha Dangote kinatarajia kutumia gesi asilia kuzalisha umeme hadi kufikia megawati 45 katika kipindi cha mi-aka miwili ya mwanzo na baadae uzalishaji utaongezeka hadi kufikia megawati 75 mwa-ka 2019. Sehemu ya mradi inahusisha utan-dazaji wa bomba la gesi lenye kipenyo cha 12” na urefu wa kilometa 2.7 kutoka toleo namba moja (BVS 1) hadi kiwandani. Pia mradi un-ahusisha usimikaji wa mtambo wa kupun-guza mgandamizo na kupima kiasi cha gesi (Pressure Reduction and Metering Station).

Usambazaji wa gesi asilia kwa kiwan-da cha saruji cha Dangote ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Shirika la TPDC kusambaza gesi asilia kwa viwanda vin-gi zaidi kuwezesha Tanzania ya viwanda.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) akiwa katika ukaguzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa gesi asilia kwa matumizi ya kiwanda cha saruji cha Dan-gote. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Evod Mmanda, Meneja mradi wa kiwanda cha saruji cha Dangote, Ndg. Aravind Naik, Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Jaji Mstaafu Josephat Mackanja na Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO, Mha. Baltazar Mrosso.

Umeme wa gesi wawaka Dangote

DECEMBER 2018

matumizi ya gesi asilia yatasaidia ku-punguza gharama za uendeshaji kwa asilimia 40%Jagath RatheeAfisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha Saruji cha Dangote

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati jeupe) akijadiliana jambo na Mhandisi Mwa-naidi Saidi ambaye ni mtumishi wa GASCO ambayo kampuni tanzu ya TPDC. Hii ni baada ya Waziri kuzindua rasmi matumizi ya gesi asilia kuzalisha umeme katika kiwanda cha saruji cha Dangote.

Page 8: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETIN MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

Mafundi wakiwa kazini kuunganisha bomba la gesi litaka-lopeleka gesi asilia kutoka kituo cha kutolea gesi cha BVS1 kuelekea kiwanda cha saruji cha Dangote kwa matumizi ya kiwanda.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu ( kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mha. Victoria Munisi (wa pili kulia) alipoku-wa akikagua mradi wa kutoboa bomba la gesi kwa ajili ya ku-unganisha wateja wapya maeneo ya Mwanambaya, Mkuranga. Wengine pichani ni Meneja bomba la gesi, Mha. Joseph Kavishe (wa pili kushoto) na Mhandisi Dominic Ngunyali (wa kwanza kulia).

Naibu Waziri wa Nishati,Mhe.Subira Mgalu akijadiliana jambo na Mmiliki wa moja ya gari linalotumia gesi asilia al-ipokuwa akikagua maendeleo ya Mradi wa kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani.

MHANDISI Ismail Naleja (Mwenye vest ya njano )akifafanua ku-husu ujenzi wa mtandao wa usambazaji gesi asilia kwa matumizi ya Nyumbani,wengine kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe : Evody Manda,Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe:Gelasius Byakanwa,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TPDC ,Mha:Kapuulya Musomba,Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO,Mha:Baltazar Mroso na Kaimu Mkurugenzi wa Shughuli za Mkondo wa Chini Mha.GilbertEmmanuel

Meneja Mawasiliano wa TPDC, Bi. Marie Msellemu akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 16 kwa Ndg. Ramadhani Hatibu, Afisa Mifugo wa Wilaya ya Kilwa Masoko ambaye alipokea hundi hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Masoko. Mchango huo umelenga kuchangia ujenzi wa jengo la choo kwa ajili ya shule ya msingi Kivinje.

Matukio mbalimbali katika picha

8 DECEMBER 2018

Page 9: MAUTA NA ESI MAUTA NA ESI - tpdc.co.tz

TPDC NEWS BULLETINMAFUTA NA GESI MAFUTA NA GESI AGOSTI 2018

Wananchi Mkoani Mtwara wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa ndugu Francis Lupokela Afisa uhusiano na Mhandisi Tumaini Daniel afisa Utafiti walipokuwa wakitoa elimu ya Uhamasishaji kuhusu matumizi ya gesi silia kwa matumizi.

Wananchi Mkoani Mtwara wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu kutoka TPDC (hawapo pichani) kuhusu mradi wa us-ambazaji gesi asilia kwa matumizi ya Nyumbani

MKUU wa mkoa wa pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo(Kulia)akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba alipotembelea maonesho ya viwanda Mkoani Pwani.

Wananchi Mkoani Mtwara wakisikiliza kwa mak-ini maelezo kutoka kwa wataalamu kutoka TPDC (hawapo pichani) kuhusu mradi wa usambazaji gesi asilia kwa matumizi ya Nyumbani

9 DECEMBER 2018

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akishu-hudia moja ya gari linalotumia gesi asilia likiwa katika kituo cha kujazia gesi hiyo tayari kwa kujaza gesi.