32
JANUARI 2013 TOLEO II ISSN 1821-8245 Mkulima ULIMWENGU WA FARMER’S WORLD WAKULIMA WADOGO WAKUTANA NA RAIS Sauda Ntakiteye na Hadithi yake... MINYORORO YA THAMANI UBORA WA MIPANGO YA MAENDELEO - (DADP) WAJIBU WA WANAWAKE KATIKA KILIMO Mkulima na Mfanyabiashara aliyefanikiwa

MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

  • Upload
    others

  • View
    15

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

JANUARI 2013 TOLEO IIISSN 1821-8245

MkulimaUliMwengU wa

farMer’s world

WAKULIMA WADOGO WAKUTANA

NA RAIS

Sauda Ntakiteye na Hadithi yake...MINYORORO YA THAMANI

UBORA WA MIPANGO YA MAENDELEO - (DADP)

WAJIBU WAWANAWAKEKATIKA KILIMO

Mkulima na Mfanyabiashara aliyefanikiwa

Page 2: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

kama mtangazaji wa kituo cha redio, East Africa. Msubirie Michael, sasa ana-mix kwa mtindo wa Fema.

Pia utakutana na vijana wengi wakulima na wataalam kutoka pande mbalimbali za Tanzania wanaoishi na na kufurahia zawadi ya ardhi. Kwa timu hiyo machachari hiyo usikose kufuatilia Ruka Juu II, itakupagawisha.

kwa nini kilimo?

• kilimo ni maisha: chakula kinajenga miili yetu, kinatupa nguvu. Kwa kutumia chakula tunakuwa, tunakidhi njaa zetu, tunaponya magonjwa mbalimbali. Tupo tulivyo kwa sababu ya chakula.

• kilimo ni utajiri: Kila mtu ni lazima ale ili aishi kwa hiyo soko la kilimo haliishi na hivyo basi hakuna kazi nyingine yenye umuhimu kuliko kilimo. Lima kwa usahihi na ubora, kuna pesa ya uhakika kwenye kilimo.

• ardhi kubwa yenye rutuba: Nchi yetu imebarikiwa ardhi yenye fursa kibao za kuendeleza kilimo. Wakulima wajanja wanaofahamu nini cha kufanya kubadilisha ardhi hii kuwa pesa.

• kilimo ni uti wa mgongo: Unafahamu kuwa asilimia 85 ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea ardhi. Nchi hii inategemea kilimo. Sasa ni muda muafaka wote tuweke msisitizo kwenye kilimo na kukifanya kiwe na faida zaidi.

• kilimo Bomba! Unaweza kuita kilimo bomba au kilimo kwanza, kama kampeni inayoendeshwa na serikali. Tuungane wote na kukipa kilimo kipa umbele. Tulishe kizazi kijacho, tujenge maisha yetu.

TUmETEmBEa, TUkaJiFUnZa, TUkaFURaHi!

‘Tembea uone’ ni msemo wa Kiswahili wenye maana, ukitembea unajifunza mambo mengi. Na ndivyo ilivyotokea kwa timu ya msimu wa pili wa Ruka Juu wakati wakitafuta washiriki katika mikoa ya Arusha, Morogoro na Rukwa.

Kutoka kwenye barabara korofi ya Rukwa mpaka zenye vumbi ya Karatu timu ya msimu wa pili wa Ruka Juu ilikutana na vijana wengi wakulima (miaka 18 – 30), wakiendesha maisha yao na wale wawapendao kwa kutumia kilimo. Timu imechagua wakulima sita kutoka Monduli, Karatu, Kilosa, Mvomero, Sumbawanga na Nkasi ambao watashiriki katika shindano la luninga. Tutakutana na wengi zaidi kupitia kipindi cha radio.

SHinDano la TV!

Washiriki ambao kwa sasa wanalima mazao mbalimbali ya chakula kwa ajili ya kujiingizia kipato, wataweka stadi zao za kilimo na ujasiriamali kwenye majaribio watakapokuwa wanapewa changamoto za shamba. Vipindi vimerekodiwa katika mazingira ya kawaida ya washiriki. Utakutana na familia zao, marafiki, kuangalia uwezo wao wa ushiriki na pia utashiriki katika kuchagua mshindi. Utaona jinsi shamba, inamtoa ushamba, mtu wa shamba! Na zaidi ya yote utapata mawazo mapya kuhusu kilimo.

USikoSE

Ungana nasi kwenye msimu wa pili wa Ruka Juu! Angalia, piga kura, na jifunze kwa kiasi gani kilimo bora kinabadilisha maisha ya vijana nchini Tanzania. Kilimo ni bomba, na tunasikia harufu ya pesa kwenye kilimo.

nakumbuka shindano la ujasiriamali la Ruka Juu kwenye luninga mwaka 2011 lilikutanisha vijana machachari sita walioshindania nafasi ya kubadili maisha yao? Yap, lile ambalo kinyozi kutoka Kibaha, Idrissa Mannah aliibuka kidedea?

Sasa sikia, habari ya mjini ndio hii, shindano la Ruka Juu limerudi tenaa… na sasa ni kuhusu vijana wanaofanya kilimo kibiashara zaidi.

Kilimo ni bomba! Tumetembelea vijana makini wajasiriamali nchi nzima wanaotumia kilimo kujenga maisha yao. Kila mtu anahitaji ajira itakayomletea kipato, ila fursa za ajira zinaweza kuwa ngumu kupatikana. Wakati fursa za ajira katika sekta nyingine zinaweza kuwa chache, kilimo kina fursa kibao kwa vijana. Kilimo cha kisasa ni muhimu, kama kijana mmoja anavyosema “ udongo unanukia pesa, sema watu hawaoni tu”. Femina tunataka kukusaidia kugundua fursa iliyojificha kwenye kilimo, usije ukapitwa kwa kilimo kinaweza badili maisha yako.

Shindano la kwenye luninga Ruka Juu limerudi, na msimu huu pia tuna kipindi cha radio, Fema Redio, ambavyo vitakwenda sambamba. Kwa hiyo usikose kuangalia TV na kusikiliza radio yako, upate maujanja ya kilimo.

TimU ya RUka JUU

amabalis aka aBC: Ulimpenda mtangazaji wetu mchangamfu kwenye msimu wa kwanza, utampenda zaidi katika msimu huu wa pili, muda huu anakuja amekamilika na maujanja ya shamba. ABC atatuonesha njia, na kututhibitishia kuwa kilimo ni bomba.

Bwana ishi: hautamani kujua Bwana Ishi anatafuta nini shambani? Haswaa, mchekeshaji Bwana Ishi anaingia kwenye kilimo, atakutana na siri na changamoto za kilimo, usikose kuangalia.

Dada Bahati: Washiriki na watazamaji wa msimu wa pili wa Ruka Juu wote wana nafasi ya kushinda. Wasiliana na Bahati, ubahatike. Tuna majaji katika kila kipindi cha Ruka Juu cha kwenye luninga, lakini wewe pia uliyeko nyumbani unaweza kupiga kura na kura yako ni muhimu.

Rebeca: Ulimuona Rebeca akitangaza kipindi cha Fema TV Talk show, akiwa na ABC. Sasa utamsikia kwenye radio, ambapo atakua mtangazaji mwenza wa Fema Radio.

michael Baruti: Unaweza ukakumbuka sauti yake maridhawa, nzito kidogo wakati akifanya kazi

Ruka Juu IMERuDI

TENana Rebeca Gyumi

U

Kilimo ni bomba! Tumetembelea vijana makini wajasiriamali nchi nzima wanaotumia kilimo kujenga maisha yao. Kila mtu anahitaji ajira itakayomletea kipato, ila fursa za ajira zinaweza kuwa ngumu kupatikana.

RUka JUU ni nini? Ruka Juu ni moja ya zao la Femina lenye lengo la kuhamasisha upatikanaji wa ajira na kipato. Kwenye luninga, Ruka Juu ni shindano la ujasirimali linatumia maisha halisi. Msimu wa kwanza ulioneshwa 2011, na kutokana na maoni yenu ulifurahisha sana.

Wengi wenu mlituomba tuendelee na vipindi na kuongelea vijana na kilimo cha biashara. Kwahiyo 2013 Machi tutazindua msimu mpya, weka macho na masikio yako wazi.

Page 3: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

Neno kutoka kwa Mkurugenzi

Kutoka Meza ya Mhariri

Malalamiko kuhusu kilimo yaliyotiwa saini na zaidi ya Waafrika 16,000

Wakulima wadogo wawasilisha matatizo kwa Mheshimiwa Jakaya

Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mradi wa Umwagiliaji – MINEPA

Mipango bora ya programu za maendeleo ya sekta ya kilimo ya wilaya

na kutolewa kwa fedha kwa wakati

Wafugaji wa Kigorogoro - Mkasa wa Bwana

Uporaji wa ardhi

Kuvaa ‘miwani ya jinsia’ kwenye minyororo yetu ya thamani

VVU/UKIMWI na Wanawake katika Minyororo ya thamani

Sauda Ntakiteye: Mkulima na mfanyabiashara

Programu Endelevu ya Uhakika wa Chakula katika Wilaya ya Chunya

Visa Mkasa vya Jinsia kutoka Mkuranga

Mkulima mwenye mafanikio katika Wilaya ya Simanjiro

Kukuza nafasi ya Wanawake katika Kilimo

Kikundi cha Wanawake cha Maua Rombo

Uwezeshaji jinsia, minyororo ya thamani na mabadiliko ya tabia nchi

Maendeleo ya Ufugaji Samaki Kijamii kisiwani Zanzibar

Chololo Kijiji Asilia

Mradi wa Kuendeleza Masoko ya Vijijini (RMDI)

25

13

5

345

68

1011121314151617181920222527

2

4

yaliyomo

Page 4: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

Neno kutoka kwa MkurugenziMpendwa MSOMAJI

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu la Ulimwengu wa Mkulima. Lilipozinduliwa mwaka 2011, Jarida lilishirikisha mawazo na kusambazwa kwa wadau, wengi wao wakiwa wakulima kupitia mashirika yao, vyombo vya habari, wabia wa maendeleo ya kilimo, viongozi wa kuchaguliwa na

watumishi wa umma katika ngazi za vijiji na taifa. Kwa mara nyingine tena kupitia Jarida hili, Jukwaa la Watendaji wa Kilimo Wasiokuwa wa Kiserikali (ANSAF) linalenga kushirikishana na kukuza kujifunza kuhusu utendaji uliothibitishwa na ulio bunifu miongoni mwa watendaji wa sekta ya kilimo kama njia ya kuendeleza uelewa wa pamoja wa changamoto, hatari na fursa ndani ya sekta hii, tukiweka msisitizo mkubwa kwa wakulima wadogo. Naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru wanachama wa ANSAF, hasa kwa utayari wao wa kushirikishana uzoefu wao kupitia Jarida la Ulimwengu wa Mkulima. Kwa kweli, ni kutokana na kujituma huku ndipo ANSAF imeweza kuzifikia jamii zilizoko maeneo mbalimbali (Bara na Visiwani) nchini Tanzania. Aidha, ningependa kuwashukuru wabia wetu, hasa mashirika ya: Ushirikiano wa Maendeleo la Uswisi (SDC), Irish Aid (IA) na Programu ya Uwajibikaji Tanzania (AcT) kwa msaada wao katika shughuli za ANSAF. Ni wazi kwamba bila ya misaada ya wanachama na wabia, toleo hili lisingeweza kupatikana kwa wasomaji wetu watukufu, ambao nina uhakika wana hamu kubwa ya kulisoma.

Kuna lipi jipya anSaF?Jarida la Ulimwengu wa Mkulima linatoka wakati ANSAF imemaliza kuandaa mpango mkakati wa mwaka 2013 – 2017. Hivyo Jarida hili linashamirisha mafanikio ya mpango mkakati. Tunalenga katika kuwawezesha wakulima wadogo kupata fursa na uwezo wa kujibu fursa hizo. Hii inamaanisha nini? Tutafanya kazi ili tuweze kuchangia katika kufanya mageuzi ya maisha na mifumo ya kilimo ambayo inafanya kazi kuhudumia watu masikini. Tutafanya kazi ili tuone mabadiliko chanya ya tabia miongoni mwa majirani tunaopakana nao. Kulingana na mpango mkakati mpya, wasomaji wa matoleo yajayo ya Jarida wategemee kupata makala mengi zaidi yanayohusu ahadi zilizotolewa na nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika huko Maputo mwaka 2003. Suala zima la kutengwa kwa rasilimali na usawa kuhusiana na jamii za vijijini, vyombo vya habari na wajibu wake katika kukuza kilimo na uchumi nchini Tanzania vitajadiliwa. Kama njia ya kuhimiza vyombo vya habari na waandishi wa habari binafsi kuandika makala mengi zaidi kuhusu kilimo, ANSAF kwa kushirikiana na Shirika la BEST AC/ BEST (Kuimarisha Mazingira ya Biashara Tanzania) – Kitengo cha Utetezi, na kufanya kazi na wabia wa Tuzo Bora ya Waandishi wa Habari Tanzania (EJAT), wameanzisha kundi jipya katika Tuzo ya Kilimo na Biashara za Kilimo. Katika miezi sita iliyopita, ANSAF kwa kushirikiana na BEST AC/ BEST na Chuo Kikuu cha Mt. Agustino wamekuwa wakisaidia waandishi wa habari vijana katika Uandishi wa Habari za Biashara za Uchunguzi – wakiweka msisitizo katika kilimo na mazingira ya biashara vijijini.

Toleo hili lina mambo gani?Kwa kutumia maoni na mapendekezo yaliyopokelewa kutoka kwa wasomaji wa toleo letu lililopita, Jarida la sasa linajenga msingi wa taarifa katika baadhi ya mada. Unaweza kuwa unafahamu kuhusu vurugu katika masoko ya mazao yetu mengi ya kilimo. Toleo hili lina majadiliano mafupi kuhusu sekta ndogo ya korosho. Tunaweka msisitizo maalumu katika minyororo ya thamani kupitia jicho la jinsia na Siku ya Kimataifa ya Wanawake kama ilivyosherehekewa na Muungano wa Jinsia wa Asasi za Kiraia nchini Tanzania. Utafurahia kusoma visa mkasa mahususi kutoka pembe ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania Bara hadi pembe ya Zanzibar Mashariki. Wakati unaanza kusoma makala katika Jarida hili, tafadhali jitayarishe kutupatia mrejesho, ama kupitia tovuti yetu, fesibuku, barua pepe au kwa kutupigia simu. Tutafurahi kuyafanyia kazi maoni na mapendekezo yako ili kuboresha Jarida letu.

Karibuni sana

Audax RukongeKatibu MtendajiANSAF

TuTafaNya kazI IlI TuwEzE kuchaNgIa

kaTIka kufaNya MagEuzI ya MaIsha

Na MIfuMo ya kIlIMo aMbayo INafaNya kazI

kuhuDuMIa waTu MasIkINI. TuTafaNya

kazI IlI TuoNE MabaDIlIko chaNya ya TabIa MIoNgoNI

Mwa MaJIRaNI TuNaopakaNa Nao.

Page 5: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

JANUARI 2013 TOLEO IIISSN 1821-8245

MkulimaUliMwengU wa

farMer’s world

WAKULIMA WADOGO WAKU-

TANA NA RAIS

Sauda Ntakiteye na Hadithi yake...MINYORORO YA THAMANI

UBORA WA MIPANGO YA MAENDELEO - (DADP)

WAJIBU WAWANAWAKEKATIKA KILIMO

Mkulima na Mfanyabiashara aliyefanikiwa

boDi ya uhaRiRi

mKuRugenZi mTenDaji

Audax Rukonge

mhaRiRi mKuu

Alawiya Mohammed

mhaRiRi mShauRi

Mbarwa Kivuyo

WaChangiaji

Audax RukongeMary Githinji

Michelle FroatsRegina Mongi

Alawiya MohammedMbarwa Kivuyo

Mwanzo MillingaIsla Gilmore

uSambaZaji, mauZo na maSoKo

Alawiya Mohammed

mChapiShaji:

Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF) S.L.P 33562, Plot 566, Senga Road,

Mikocheni A. Dar es Salaam,Simu: + 255 22 2771566 / 2775970

Nukushi: + 255 22 2773217Barua Pepe: [email protected]

Tovuti: www.ansaf.or.tz

mSaniFu na mpiga Chapa iprint (T) ltd

S.L.P 10009, Dar es SalaamSimu: (+255 22) 286 5810

Barua pepe: [email protected]

Kutoka Meza ya MhaririM

iezi imepita tangu kuzinduliwa kwa toleo la kwanza la jarida la Ulimwengu wa Mkulima. Katika toleo lile, tuliwakaribisha wasomaji wetu watutumie “kadi za siku ya kuzaliwa” ili kusherehekea kuzaliwa kwa jarida letu. Kwa makusudi kabisa tuliwaomba watoe maoni yao

kuhusu njia bora zaidi ya kumfanya “mtoto akue” akiwa na nguvu zaidi. Shukrani kwa wale waliotutumia maoni yao. Michango ya mawazo kutoka kwa wanachama na wabia wa ANSAF kwa kweli yametuwezesha kujenga fikra zetu na hatua za jinsi ya kuendeleza jarida letu. Hivyo basi inatubidi tuchambue maoni tofauti yaliyowasilishwa na wasomaji wetu waliotukuka na kupanga hatua zinazofuata. Mapendekezo mengi yamejumuishwa katika toleo hili la pili. Baadhi ya mapendekezo ni pamoja na haja ya kuongeza idadi ya nakala ili ziwafikie wasomaji wengi zaidi. Tumeamua kuongeza idadi ya nakala kutoka 1000 hadi 1,500 kwa toleo la Kiingereza, na kutoka nakala 2,000 hadi 3,500 kwa toleo la Kiswahili kuanzia toleo hili. Tumedhamiria kupanua mtandao wa ugawaji kuvuka mipaka yetu. Suala la kushughulikia mada moja kwa wakati mmoja pia liliwasilishwa na wasomaji wetu. Tumeanza sasa kuchukua mwelekeo huo, ambao ni kuwasilisha masuala yanayohusu mada mahususi yatakayofanya majadiliano yalenge katika mada husika na si vinginevyo. Lazima tukubali kwamba hatuwezi kushughulikia maoni yote kwa mara moja, lakini tutaendelea kuwa makini zaidi ili kuboresha maudhui ya matoleo yajayo. Kwa hiyo toleo hili linaweka msisitizo katika kuendeleza mnyororo wa thamani wenye mtazamo wa kijinsia. Ukichukulia maendeleo ya kiuchumi duniani kwa sasa, haja ya kujenga na kuendeleza muunganisho imara wa masoko ni jambo muhimu sana. Wakulima wadogo, wanaume kwa wanawake lazima wawe sehemu ya maendeleo ya kiuchumi duniani. Wakati huo huo, wakulima wanahitaji kuwa na sauti ya kushawishi sera za masoko. Wanahitaji kujenga ushirikiano na taasisi ambazo zinaunga mkono wakulima. Wanahitaji kuwa na msemaji wa kutetea haki zao. ANSAF inaliona jarida la Ulimwengu wa Mkulima kama msemaji wa wakulima wadogo. Hebu tuliunge mkono jarida letu na kulitumia kuleta mageuzi ya jamii yetu.

Alawiya Mohammed & Mbarwa Kivuyo

Page 6: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

4 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

Shughuli hii ya maandamano ilianzia katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha majira ya saa 4.30 na kuelekea Ikulu kwenda kutoa

malalamiko ya wadau wa sekta ya kilimo kwa Rais. Walalamikaji walijipanga vyema kiasi ya kwamba Rais Kikwete aliwapokea kwa heshima. Malalamiko yalisisitiza masaibu wanayokabiliana nayo wakulima wadogo nchini Tanzania. Hotuba ya Dk. Simpho Moyo, Mkurugenzi wa Afrika wa Shirika la ONE.org ilieleza kwa muhtasari wasiwasi wa wadau hao. Dk. Simpho alielezea sababu iliyopelekea malalamiko haya ambayo yaliwasilishwa kwa niaba ya Waafrika 16,000 kutoka kote katika barani Afrika. Njaa iliyotokea hivi karibuni katika Pembe ya Afrika ambapo watoto 30,000 walikufa ndani ya kipindi cha miezi mitatu iligusa mioyo ya watu wengi. Yakiwa yamewekwa saini na wadau wa kilimo takriban 16,000 kutoka kote barani Afrika. Malalamiko haya yanawataka viongozi wa Kiafrika kufanya njaa hii iwe ya mwisho katika bara la Afrika na kukubali kuinua maendeleo ya kilimo ya Afrika. Mashirika ya ANSAF, ONE na wadau wengine walimuomba Mheshimiwa Raisi awasilishe ujumbe huo huo kwa viongozi wengine wa Afrika kama uthibitisho wa dhamira yake ya kuleta usalama wa chakula na lishe, kwa kuchukua hatua zifuatazo: • Kusaidia utoaji wamisaada ya dharura

iliyoahidiwa kwa Somalia; • Kuwekaahadiyamudamrefuyakutenga

Malalamiko kuhusu kilimo yaliyotiwa saini na zaidi ya waafrika 16000Mnamo Machi 1, 2012, wakiwa wamelowa na kuchoka, mchanganyiko wa wadau wa kilimo waliokuwa wanaongozwa na ANSAF na Shirika la ONE International, walifanya shughuli isiyo ya kawaida katika jiji la Dar es Salaam, Tanzania.

baJETI Na sERa

Na Alawiya Mohammed

asilimia 10 ya bajeti ya taifa katika kilimo na usalama wa chakula;

• Kuwasaidia wakulima wadogo kwaniwao ndio wanaolisha Afrika

• Kuleta uwazi katika bajeti ili wananchiwajue fedha inatumikaje.

Mheshimiwa Jakaya Kikwete aliheshimu malalamiko yaliyotolewa na kuwashukuru waandaaji wakuu ANSAF na ONE, kwa kuhamasisha “wito wa mwamko” katika mfumo wa malalamiko juu ya masuala ya haraka katika sekta ya kilimo. Sekta ya Kilimo imekuwa ni kiungo kinachofanya kazi taratibu, licha ya kuongezeka kwa bajeti kutoka TZS 233 bilioni mwaka wa fedha 2005/2006 hadi TZS 926 mwaka wa fedha 2011/2012. Rais Kikwete alikiri kwamba serikali inafahamu kwamba imeshindwa kukidhi matakwa ya Azimio la Maputo linalotaka kiwango cha bajeti ya kilimo ifikie asilimia 10 ya bajeti ya taifa. Rais Kikwete alivitaja vipengele muhimu ili kilimo kikue kama ilivyofafanuliwa katika Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP). Lakini ni bahati mbaya kwamba vipengele sita vilivyoainishwa ndio vimekuwa kero kuu zilizoibuliwa na mkurugenzi mtendaji wa ANSAF, Audax Rukonge, mkurugenzi wa One.org, Dk. Simpho Moyo na mwakilishi wa wakulima wadogo, Bw. Yosia Mahava. Wote watatu walizungumzia kuhusu zana bora za kilimo, kilimo cha umwagiliaji, pembejeo za kilimo, uboreshaji wa miundombinu na kuendeleza stadi kama matatizo makuu ya sekta. Kuhusu zana bora za kilimo, wanaharakati walitaka serikali ifanye tathmini ya hatua yake ya kufanya mageuzi kutoka jembe la mkono hadi trekta za “pawa tila”. Wanasema mageuzi haya hayajaleta mabadiliko yoyote katika kilimo na pia imesababisha kushuka kwa uzalishaji. Rais alisema kwamba matumizi ya “pawa tilla” yalikuwa ni lazima kwa kila mkulima. Alipendekeza pawepo na utaratibu mzuri wa kukodisha “pawa tilla” ili kuepuka mlundikano katika sehemu moja. Inatarajiwa kwamba kampeni ya Kilimo Kwanza itaweza kusimamia mageuzi vizuri na kuleta matokeo yanayotakiwa.

Kuhusu kilimo cha umwagiliaji; wanaharakati walisema kwamba hii ni mojawapo ya fursa ambazo zinazotumika kwa kiwango cha chini sana. Wakulima wengi wa Kitanzania bado wanategemea kilimo cha mvua. Rais alisisitiza matumizi sahihi ya mabwawa, mito na vyanzo vingine vya umwagiliaji. Rais pia alizungumzia kuhusu pembejeo za kilimo. Alisema pembejeo za kilimo ndizo zinazotoa sura ya “mapinduzi ya kijani”. Wanaharakati walisema pamekuwepo na ucheleweshaji mkubwa katika utoaji wa pembejeo na ruzuku za kilimo. Kuendeleza stadi za kilimo ni eneo ambalo limepuuzwa kwa hali ya juu. Rais alieleza kwamba wakulima wanahitaji kupata stadi za kisasa za kilimo ili waweze kuendesha vyema mashine ambazo zitapunguza mzigo wa kazi za shamba. Aidha Mheshimiwa Rais alitoa muhtasari wa mipango ya serikali ya kuboresha mifumo ya Masoko na kukuza muunganisho wa masoko. Alisema dhana ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Binafsi inalenga katika kuhakikisha ukuaji wa kilimo. Maboresho ya miundombinu kama vile barabara, umeme na vituo vya kuhifadhia mazao yana wajibu mkubwa katika ukuaji wa sekta ya kilimo. Wakulima wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa maandishi ili uweze kuwasaidia katika taasisi zote za fedha. Pia wakulima wanataka serikali kupitisha au kubatilisha sheria na sera ili ziweze kuwapatia wakulia usalama wa kutosha. Walimweleza Rais kwamba ni muhimu kwa serikali kuweka vigezo vya kuwatambua wakulima wadogo ili waweze kupewa upendeleo unaostahili kwao.Wanaharakati walimuomba Rais aiagize serikali kujenga mazingira yatakayowawezesha wakulima wadogo kujihusisha katika kupanga na kutekeleza miradi ya kilimo. Rais Kikwete aliahidi “kwa uaminifu na wajibu kutuma ujumbe,” kwa viongozi wengine wa Afrika wakati wa Mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia, hapo Juni 2012. Rais aliwaagiza ANSAF na One.org kutoa ujumbe huo huo katika majukwaa yao ya kitaifa na kimataifa.

Wakulima wakitembea kuelekea Ikulu

Phot

o : I

sla

Gilm

ore

Page 7: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 5

hiSToRia Fupi

Kama hatua inayofuatia ya matumizi bora ya rasilimali, serikali pia ilisaini Ubia wa Serikali Inayoendesha Shughuli

kwa Uwazi (OGP) kama ishara ya kuzingatia uwazi bila kificho katika matumizi ya umma. Bajeti ya sekta ya kilimo imekuwa ikiongezeka, kutoka asilimia 2.9 (Mwaka wa Fedha 2001/02) hadi asilimia 6.9% ilipofika 2011/12. Licha ya mafanikio haya makubwa, utendaji wa sekta bado uko chini, asilimia 4 ukilinganisha na asilimia 6 za ukuaji kwa mwaka kitaifa. Ni kwa kuelewa hivyo, ndipo ANSAF kwa kushirikiana na ONE (shirika la kimataifa la utetezi) waliamua kukusanya saini (kupitia njia za kawaida na mtandao) kutoka ndani na nje ya Tanzania, kama malalamiko yanayolenga kuwakumbusha viongozi wa nchi za Afrika, hasa Tanzania kwamba muda umewadia wa kufikia lengo la asilimia 10 na kushughulikia masuala ya uwazi katika matumizi ya rasilimali za umma. Zaidi ya saini 16,000 zilikusanywa kupitia mtandao na 800 kwa njia za kawaida kutoka vijiji nchini Tanzania. ANSAF iliwaalika wanachama na wadau wengine kushiriki katika zoezi hili. Wasilisho la malalamiko lilifanywa na zaidi ya washiriki 100 waliopokelewa na Mheshimiwa Kikwete huko Ikulu. Zaidi ya Rais Kikwete, katika viwanja vya Ikulu walikuwepo maafisa waandamizi wa serikali (mawaziri na makatibu wakuu), mabalozi kutoka nchi mbali mbali za Afrika, wakulima wadogo, wabia wa maendeleo, Asasi za Kiraia za Kimataifa na za ndani.

KuWaSiliSha malalamiKo Wakati wa kuwasilisha malalamiko kwa Mheshimiwa Jakaya Kikwete mnamo Machi 1, 2012, Fatma Mohammed, mwanachama wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) alipata nafasi ya kuzungumza na Rais kuhusu mpango uliopangwa wa kuwafukuza mamia ya wakulima wadogo kutoka kwenye ardhi yao. Jumla ya kaya 270 za wakulima

Wakulima wadogo wawasilisha matatizo yao kwa Mheshimiwa Jakaya kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaTanzania, nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika, mwaka 2003 iliahidi kutenga asilimia 10 ya bajeti yake ya taifa kwa ajili ya sekta ya kilimo.

Wanawake wa Kijiji cha Mbigiri, Morogoro, wakidai haki zao mbele ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mnamo Novemba 2012

Na Alawiya Mohammed

baJETI Na sERa

Pich

a : S

usum

a Su

sum

a

wadogo zilikuwa zinatishiwa kufukuzwa kutoka ardhi yao ya asili huko Mateteni, Wilaya ya Kilosa. Fatma Mohammed ni miongoni mwa waathirika 50 za zoezi hili kutoka Mateteni ambao nyumba zao zilibomolewa na Polisi wa Dakawa kutoka Mvomero, wilaya ya jirani. Polisi walidai walikuwa na barua iliyo na amri halali ya kuwafukuza kutoka kwenye mamlaka nyingine na walikuwa katika mchakato wa kubomoa nyumba na kuharibu mashamba ya wanavijiji ili kuhakikisha mwekezaji anapata ardhi. Fatma Mohammed pamoja na wahanga wengine Fransisca William na Eddy Ally (mwenyekiti wa kata) waliojitokeza katika harakati za malamiko waliambiwa warudi Ikulu na kuonana na Naibu Katibu wa Ofisi ya Rais, Bw. Muhidi Mbaito wakiwa na barua inayoelezea mkasa wao. Bw. Mbaito mara moja alichukua hatua kwa kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya wa Kilosa ambako msaada ulitolewa kwa kuwapatia mahema na chakula hadi hapo michakato mingine itakapofanywa. Kufuatia mkasa huu, wakulima hao waliahidiwa kuhamishiwa katika mradi wa nyumba uliofadhiliwa na serikali ya Marekani katika kijiji cha Mateteni; ijapokuwa hili halijafanyika hadi sasa. Mwanachama wa ANSAF–MVIWATA

kupitia maafisa wake wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na wakulima kwa kuwahamasisha kutambua haki zao kwa kuratibu kikamilifu hatua za kuwawajibisha viongozi wao katika kile ambacho ni haki yao. Katika mwezi wa Agosti, Mkuu wa Wilaya wa sasa alikubali kukutana na wakulima na kuahidi kuwalinda hadi hapo hatua za ziada zitakapochukuliwa na serikali. Mwekezaji wa eneo hilo alikubali kuachia nusu ya eneo ili itumike kwa wakulima na yeye aendelee na kilimo katika nusu nyingine. Wakulima walikataa suluhisho hili na kusisitiza waachiwe eneo lote kwa ajili ya watoto wao na wajukuu waendelee kuishi.

TuliyojiFunZa:1. Sauti za wakulima wadogo zinaweza

kufanyiwa kazi iwapo zitasikilizwa na mtu sahihi kwa muda sahihi na watu sahihi

2. Uratibu wa michakato katika ngazi za kijiji na taifa (ANSAF & MVIWATA) ni muhimu sana ili kuongezea nguvu mabadiliko

3. Kiwango cha uelewa miongoni mwa jamii masikini, na hasa wakulima wadogo ni muhimu sana kama wanataka kuendelea na kusukuma haki zao wenyewe.

Page 8: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

6 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

Wakitumia nyaraka husika kutoka kwa halmashauri ya wilaya ya Ulanga, wajumbe wa kamati ya SAM walichagua miradi ya mfano ya kutembelea. Mmoja kati ya miradi iliyochaguliwa ulikuwa Mradi wa Umwagiliaji wa Minepa.

AhiSToRia FupiNSAF inafanya kazi na wanachama kukuza uwajibikaji kwa jamii katika ngazi za chini. Ni

kupitia mpango wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) ndipo hatua muhimu hujadiliwa. ANSAF na mwanachama wa eneo husika – CEMDO waliandaa mafunzo kuhusu SAM, yaliyowahusisha washiriki kutoka asasi za kiraia, wakulima na mamlaka za serikali za mitaa. Mafunzo yalilenga katika:• Utambuzi wa rasilimali, kuweka

vipaumbele na kupanga mipango – rasilimali na huduma zinazopatikana, mpango mkakati na mpango wa biashara .

• Usimamizi wa matumizi ya fedha – jinsigani fedha za umma zinavyotumika kuleta mabadiliko, mgawo wa bajeti na ripoti za matumizi.

• Tathminiyautendaji–Uborawahudumazinazotolewa hufanyiwa tathmini

• Uadilifu kwa umma – taratibu zilizopo zakuchukua hatua stahiki

• Kazi ya kuchunguza makosa – maafisa

baadaye mfereji wa umwagiliaji

ulipanuliwa ili uweze kumwagilia eneo

la takribani eka za mraba 400 au kilomita 2, ukiwa na urefu wa kilomita 11 na upana

wa kilomita 1.5.

wanawajibishwa. Hii inahusisha mapitio ya ripoti za mkaguzi mkuu.

Wakitumia nyaraka husika kutoka kwa halmashauri ya wilaya ya Ulanga, wajumbe wa kamati ya SAM walichagua miradi ya mfano ya kutembelea. Mmoja kati ya miradi iliyochaguliwa ulikuwa Mradi wa Umwagiliaji wa Minepa.

mapiTio ya mRaDi Wa umWagiliaji Wa minepaBw. Eliwedi Ngomoi ni mkulima anayeishi katika kijiji cha Minepa, wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro. Mwaka 1999, mkulima huyu mbunifu alianzisha mradi wa umwagiliaji kwa kuchimba mfereji wa umwagiliaji wenye urefu wa mita 100, ambao unaleta maji shambani kwake kwa sababu mvua zilikuwa haziaminiki. Baadaye aliomba msaada wa vifaa kama vile darubini kutoka Idara ya Kilimo, wilaya ya Ulanga ili aendeleze zaidi mradi wake. Lakini ili serikali itoe msaada kwa mradi kama huu, Ngomoi aliombwa

kukabidhi mradi kwa serikali ya kijiji ili, utakapopanuliwa, watu wengi wanufaike. Mwaka 1999 taarifa ilitolewa kwa umma wote wa wananchi wa Minepa na wanakijiji wakaunda chama chao kilichoitwa kikundi cha Makangaga ili kusimamia mradi. Wanachama wa kikundi walikuwa wakulima 13 (wanaume 12 na mwanamke 1). Baada ya idhini ya serikali ya mtaa, kikundi kilibadili jina na kuitwa Wakulima wa Mpunga wa Umwagiliaji Makangaga (MAKAIR). Baadaye mfereji wa umwagiliaji ulipanuliwa ili uweze kumwagilia eneo la takribani eka za mraba 400 au kilomita 2, ukiwa na urefu wa kilomita 11 na upana wa kilomita 1.5km. Kwa sababu Ngomoi ndiye yeye mwenyewe aliyeanzisha mradi, chama

Mradi wa Umwagiliaji MINEpaMradi wa Umwagiliaji MINEPA - Mfereji ambako maji hutawanyika kuelekea sehemu mbali mbali za mashamba

Na Alawiya Mohammed

baJETI Na sERa

Page 9: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 7

wakulima

wanaotumia huduma

ya maji walichangia

asilimia 20 ya jumla

ya gharama za

mradi hadi hatua ya

kukamilika.

cha MAKAIR walikubali kumlipa fidia kwa kazi ya awali iliyofanyika katika mita 100 za mwanzo wa mfereji. Baadaye MAKAIR walikubali kuendeleza zaidi mradi. Moja ya mikakati iliyotumika ilikuwa ni kukusanya michango kutoka kwa kila mwanachama kwa wastani wa TZS 35,000 kwa ajili ya ununuzi wa mifuko na vifaa vingine hadi hapo serikali itakapoidhinisha kutengewa fedha. Mwaka 2002, chama kilipokea rasmi barua inayoeleza ahadi ya serikali ya kujenga ukuta wa kudumu wa kuzuia maji, lakini thamani yake haikuelezwa katika barua. Ijapokuwa halmashauri ya wilaya ilithibitisha ahadi hiyo, ni kupitia TASAF ndipo ilipojulikana kwamba pesa iliyotengwa ni TZS 32 milioni. Kila mkulima aliyejihusisha na kilimo ndani ya mradi alitakiwa kulipa TZS 2,000 kwa eka, ambapo, ada ya mtumiaji wa maji ilikuwa inapangwa bila ya kushauriana na watumiaji wa huduma za maji katika kijiji cha Minepa. Kulingana na kanuni za mtumiaji wa maji, vikundi vya watumiaji wa maji wanatakiwa kulipa ankra zao za maji kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji, kupitia kwa afisa umwagiliaji wa Mto Rufiji. MAKAIR imesajili kikundi chao na wamekuwa wakilipa ankra zao, ijapokuwa malipo yanayofanywa na vikundi vingine hayawekwi hadharani hadi sasa. Watumiaji wa maji wa Minepa walihoji mchakato wa kupata mkandarasi wa kujenga ukuta wa kuzuia maji. Wakati wa ziara ya timu ya SAM, wakulima walionyesha kwamba vifaa vilivyotumika vilikuwa na ubora wa chini na mkandarasi hakuwa na uzoefu wa kufanya kazi hiyo. Ilipofika 2010, ukuta pamoja na mfereji vilikwishabomoka na vilikuwa havifanyi kazi. Mwaka huo huo, serikali ya Tanzania kupitia Programu Shirikishi ya Maendeleo ya Kilimo (PADEP) ilitoa fedha (TZS 40 milioni) kwa ajili ya ukarabati wa ukuta na mfereji uliobomoka.

Wakulima wanaotumia huduma ya maji walichangia asilimia 20 ya jumla ya gharama za mradi hadi hatua ya kukamilika. Hata hivyo, wakulima waligundua kwamba ni mkandarasi yule yule ndiye aliyepewa mkataba wa kukarabati mfereji na ukuta. Utaratibu unaamuru mashauriano sahihi na ridhaa kutoka kwa jamii kabla mtu hajapewa mkataba. Pia palikuwepo na wasiwasi kwamba kampuni iliyoshinda zabuni ilikuwa haijakamilisha kazi yake iliyopita kwa kiwango cha kuridhisha, iliyosababisha kazi kusombwa na maji. Mamlaka ya Kurekebu Manunuzi ya Umma na Sheria zinazoendana nayo, zinamtaka mtu kuhakikisha umakini wa kazi (katika masuala ya kisheria na uwezo wa kufanya kazi) kabla kampuni haijapewa mkataba wowote. Tathmini haikufanyika ili kuhakiki umakini wa kazi, iliyosababisha mradi kutokukamilika.

mWiTiKio na maenDeleo mapya Ni kwa kuelewa hivyo na matokeo ya mkutano wa mrejesho uliofanyika Februari 2012, kwamba mamlaka za wilaya zilikubali kuufanyia kazi upya mradi kupitia msaada wa Serikali ya Japan. Serikali ya Japan ilikubali kujenga mifereji na ukuta uliobomoka kwenye mradi wa umwagiliaji wa Minepa. Huu ni mradi wa ushirikiano ambapo Halmashauri itatoa vifaa vyenye thamani ya TZS 3.4 milioni, jamii itachangia nguvu kazi na vifaa vinavyopatikana kijijini kwa thamani ya TZS 1.2 milioni. Halmashauri ya wilaya imeahidi kusimamia mradi wakati wa ukarabati na baada ya hapo. Kwa sasa, makandarasi wa Kijapani wanatelekeza mradi. Afisa umwagiliaji alimtambulisha mkandarasi kwa wanakijiji na kuwaeleza kwamba watajenga ili kutatua matatizo yao. Wanakijiji wanashukuru kwamba matatizo yao sasa yamemalizika.

maSuala maKuu: • Madiwani walikubali kwamba

hapakuwepo na utaratibu rasmi wa Mamlaka ya Kuratibu Manunuzi ya Umma katika kuteua wajenzi wa Mradi wa Umwagiliaji. Hata hivyo, madiwani walieleza kwamba kuna wajenzi wazuri wachache na ugumu wa kuwapata kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji.

• Wakati Sheria ya Manunuzi ya Ummaya mwaka 2011, kifungu 64 kuhusu Uchaguzi wa njia za manunuzi inatamka: “…mzabuni aliyeshinda atakuwa Yule mzabuni mwenye uwezo na nyenzo za ugavi wa bidhaa, kutoa huduma au kufanya kazi au ahadi iliyotathminiwa katika kiwango cha juu zaidi kuhusiana na huduma za kukusanya mapato au uuzaji wa mali za umma katika mazingira ambapo:

1. Wagavi wa bidhaa, makandarasi au washauri tayari wameshateuliwa kwa mujibu wa kifungu 52.

2. Kuna haja ya kufikia malengo ya kijamii ya aina fulani kwa kuomba ushiriki wa jamii za maeneo husika”• Kifungu 52 kuhusu sifa za mzabuni:

“Vigezo vinavyohitaji vikidhiwe vitawekwa katika nyaraka za zabuni na iwapo mzabuni hakidhi kigezo chochote kati ya hivyo, zabuni itakataliwa”.

• Wanakijiji wanahisiwananyamazishwa ili sauti zao zisisikike kuhusu pesa (ya PADEP na TASAF) ilikokwenda? Bado wanauliza kama fedha hizi zimeongezwa ili kuchangia katika mradi wa Wajapani unaoendelea au zimerudishwa serikalini? Wanakijiji bado hawajapata jibu la swali walilouliza.

Bw Eliwedi Ngomoi (kushoto) na wakulima katika eneo la Mradi wa Umwagiliaji Minepa, mbele yao ni banio lilovunjika

baJETI Na sERa

Page 10: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

8 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

wabia wa maendeleo na serikali wamekuwa

wakisaidia miradi ya kilimo kupitia

utaratibu wa fedha inayopitia kwenye

kapu, licha ya kuwepo kwa taratibu nyingine

kupitia miradi inayojitegemea na

msaada wa jumla wa bajeti.

hiSToRia Fupi:

Serikali ya Tanzania inasaidia utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDS) kupitia Programu ya Maendeleo ya

Sekta ya Kilimo (ASDP). Kulingana na muundo wa utekelezaji, Mkakati wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo hutekelezwa kwa kiwango kikubwa katika ngazi za chini kupitia Mipango ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo ya Wilaya (DADPs). Wabia wa maendeleo na serikali wamekuwa wakisaidia miradi ya kilimo kupitia utaratibu wa fedha inayopitia kwenye kapu, licha ya kuwepo kwa taratibu nyingine kupitia miradi inayojitegemea na msaada wa jumla wa bajeti. Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo ya Wilaya unategemea zaidi katika upatikanaji wa fedha za nje, kutoka hazina na wafadhili, na fedha kidogo kutokana na vyanzo vetu wenyewe zinazowekezwa upya katika sekta. Mipango ya miradi ya kijiji na jamii (VADPs) hukusanywa na kuingizwa kwenye Mipango ya DADPs ambayo ni sehemu ya Mipango Jumuishi ya Halmashauri (CCP), kwa kawaida huwasilishwa katika mipango ya mwaka chini ya mpango wa utekelezaji wa miaka mitatu – Muundo wa Matumizi ya Muda wa Kati (MTEF).

mipango KaTiKa ngaZi ya Kijiji/mTaa Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita

2007-2011, sekretarieti ya ANSAF imekuwa ikifanya kazi na wanachama wake katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mbalimbali. Masuala makuu matatu yalijitokeza kutokana na ushirikiano huu katika ngazi ya kijiji/mtaa:-1. Kukosa mkakati katika utekelezaji wa

miradi. Ijapokuwa DADPs zinaonekana kuwa zana za kuleta mageuzi katika sekta katika ngazi za chini, mipango mingi ya DADP ilikosa msisitizo. Mamlaka za Serikali za Mitaa nyingi zilijaribu kuelekeza nguvu kwenye miradi mingi midogo ambayo italeta mabadiliko katika eneo husika. Miradi midogo ilipatiwa msaada, kuanzia vitunguu, mpunga, kuku na kujenga uwezo. Kwa wastani, baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zilitenga takribani TZS 1.5 milioni kwa ajili ya mradi. Ni wazi kwamba mgawo huu mdogo hauwezi kuonyesha matokeo yoyote ya maana. Ilifahamika kwamba licha ya ahadi zinazojirudia kutoka kwa wafadhili na serikali kusaidia sekta ya kilimo (kama inavyoonyeshwa katika ongezeko kwenye bajeti), sio rahisi kwa mtu kuona mabadiliko yanayotokana na uwekezaji huo. Rasilimali za mradi zilitawanywa katika maeneo mengi kwa namna ambayo mtu hawezi kuona mabadiliko kwa urahisi.

Kuleta mageuzi katika kilimo cha mkulima mdogo inamaanisha kuwaunganisha kwenye minyororo ya thamani, pamoja na mambo mengine. Ijapokuwa msisitizo

ulikuwa katika uzalishaji, juhudi chache zilifanyika kuwaunganisha wazalishaji na wasindikaji na mtandao wa masoko. Hii inajidhihirisha kwa kuwepo upotevu mkubwa baada ya kuvuna ambao hauwekewi mkazo wakati wa kukuza uzalishaji.

2. Ucheleweshaji katika kutoa fedha kutoka hazina. Kutolewa kwa fedha kutoka hazina kunatarajiwa kufanyika katika kila robo. Katika kipindi hicho, ilifahamika kwamba, ijapokuwa robo ya kwanza huanza Julai 1 kila mwaka, baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hazitapokea fedha mpaka mwezi wa mwisho wa robo ya tatu, ambao ni mwezi Machi. Ucheleweshaji wa kutoa fedha kwa sekta ambayo inategemea zaidi misimu kama kilimo huwa na athari kubwa zaidi katika utendaji wa sekta. Kinachotokea kutokana na mazoea haya ni kwamba maafisa wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hujenga tabia ya kuogopa tarehe 30 Juni. Watajaribu kadri iwezekanavyo kutumia mafungu ya fedha ili kuhakikisha kwamba ifikapo Juni 31 fedha yote imetumika au imeshalipia shughuli/mkataba. Katika hali hii kuna uwezekano mkubwa kwa ubora wa mradi kudidimizwa.

3. Utaratibu mbovu wa wadau katika ngazi ya kijiji/mtaa. Ilikuwa dhahiri kwamba ijapokuwa katika ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kunaweza kuwepo taasisi

Pich

a : S

usum

a Su

sum

a

Na Audax Rukonge

Mkutano wa Kijiji, Mateteni - Morogoro.

Mipango bora ya programu za maendeleo ya sekta ya kilimo ya wilaya na kutolewa fedha kwa wakati

baJETI Na sERa

Page 11: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 9

mbalimbali zinazofanya kazi katika sekta ya kilimo, lakini hakuna majukwaa (taratibu) ambayo yana mamlaka ya kuwaleta pamoja angalau mara mbili kwa mwaka. Hili ni jambo muhimu sana ili kupunguza kurudufu kwa juhudi za watendaji, kuinua kwa kiwango cha juu upeanaji wa maarifa miongoni mwa watendaji na kukuza uwazi miongoni mwao. Katika baadhi ya wilaya (kama vile Kasulu, Kibondo, Iringa na Kilolo), asasi za kiraia na sekta binafsi zilikuwa na bajeti kubwa zaidi (fedha nyingi zaidi) ukilinganisha na fedha ambazo Mamlaka za Serikali za Mitaa zilikuwa zikipokea kutoka hazina. Kwa bahati mbaya watendaji wa sekta walikuwa hawakutani, ili kuweka mikakati ya jinsi ya kusaidia sekta.

Kwa mara ya kwanza, mwaka 2008 ANSAF wakati wa shughuli za kila mwaka za kubadilishana uzoefu, iliibua masuala haya. Katika mikutano iliyofuatia na maafisa waandamizi wa serikali na mijadala na wafadhili na watendaji wengine, masuala yaliyoorodheshwa hapo juu yalijadiliwa. Hadi sasa pamekuwepo na mwitikio chanya. 1. Ilipofika Desemba 2010, serikali ilitoa

mwongozo mpya wa DADP. Kifungu kinachohusu ruzuku ya uwekezaji (Kifungu 4.1(i) cha mwongozo mpya) kinachojulikana vizuri zaidi kama Ruzuku ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADG) iliweka kikomo cha kiasi cha chini ambacho kinaweza kutengwa kwa ajili ya kijiji fulani, TZS 56 milioni ziliwekwa kama kiasi cha chini ambacho kijiji kinaweza kupewa kama ruzuku. Mwongozo mpya pia unasisitiza kuhusu umuhimu wa kuhamisha fedha moja kwa moja kwenye akaunti za jamii/kijiji.

2. Pia ilikubaliwa kwamba ili kupunguza ucheleweshaji na kupunguza matokeo

hasi, fedha kwa ajili ya robo ya kwanza lazima zitolewe ifikapo wiki ya kwanza ya robo ya pili . Hazina iliahidi kufanya hivyo, kwa matarajio kwamba mipango kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa itakuwa yenye ubora na kutakuwa na hoja chache za ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Tangu mwaka wa fedha wa 2010/11, hazina imekuwa ikijaribu kuhamisha fedha kama ilivyokubaliwa, licha ya kuwepo kwa changamoto . Ni kweli ilipofika Oktoba 2010/11 Mamlaka nyingi za Serikali za Mitaa zilipata mgawo wao kwa muda muafaka, na robo mbili zilihamishwa ukilinganisha na uhamishaji wa kawaida wa robo moja moja!

3. Uratibu dhaifu wa wadau. Uratibu wa wadau wa sekta ni muhimu sana. Ijapokuwa wakuu wa idara za kilimo ndio wanaotarajiwa kuitisha mikuatano hiyo, hufanya hivyo kwa nadra sana. Tangu 2011, idara imejaribu kukuza ushirikiano na wadau kupitia majukwaa ya watoa huduma. Ijapokuwa juhudi hizi zinatarajiwa kuanza na mikoa kumi ya majaribio, haijafahamika vyema jinsi itakavyopokelewa katika ngazi ya wilaya. Hata hivyo, serikali imeamua kukabiliana na changamoto hii ya kuanzisha majukwaa kama hayo ambayo huwaleta pamoja watendaji katika ngazi ya mkoa ili wajadili kwa kina masuala ya kilimo. Sekretarieti ya ANSAF na wanachama katika kanda mbalimbali wamekaribishwa kutoa mawasilisho kuhusu jinsi gani majukwaa haya yanaweza kutekeleza kwa ukamilifu programu za ASDP, na hasa DADPs.

ChangamoTo • Kuendeleza mabadiliko. Ijapokuwa

serikali kuu na wafadhili wamedhamiria kuhamisha fedha kwa wakati kwa ajili ya sekta ya kilimo; mipango mibovu na hoja

za ukaguzi zinaendelea kuchelewesha kasi ya kushughulikia maombi ya fedha

• Kuendelezauratibundani yaMamlaka zaSerikali za Mitaa. Ijapokuwa kuna mwitikio chanya kuhusu haja ya kuwa wazi na kuratibu juhudi miongoni mwa watendaji, Mamlaka za Serikali za Mitaa hazina uwezo wa kuendeleza kufanya morali kuwa juu miongoni mwa wadau.

• Upatikanaji wa habari. Ijapokuwamwongozo na sera ni masuala katika ngazi ya taifa, watekelezaji wake wana ufahamu mdogo wa masuala haya. Hii huchangia watu kufanya kazi kwa mazoea, ambapo hata kama nyaraka zimebadilika lakini uelewa miongoni mwa watendaji bado mdogo, hivyo kuchangia matokeo mabovu.

• Kuadhibu jamii badala ya watumishi waumma. Hati za mashaka na hati chafu za ukaguzi zina athari hasi kwenye utoaji wa mafungu ya fedha kwa muda unaotakiwa kwa ajili ya programu za DADPs. Aidha, uwezo wa kutumia fedha (uwezo wa kufyonza) huchukuliwa kama kipengele muhimu katika kutoa fedha kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kwa bahati mbaya katika mikasa yote miwili, watu wanaoadhibiwa ni walengwa wa huduma (wanawake na wanaume masikini katika maeneo ya vijijini) ambao wanaweza kuwa hawana habari kuhusu ni nani anayechelewesha mchakato huu na kwa sababu zipi.

uwezo wa kutumia fedha huchukuliwa

kama kipengele muhimu katika

kutoa fedha kwa Mamlaka za

serikali za Mitaa.

Pich

a : N

asho

n Ke

nned

y

baJETI Na sERa

Page 12: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

10 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

hiSToRia FupiMchakato wa kupanga mipango wa serikali za mitaa hutoa fursa kwa jamii kuweka vipaumbele vya mahitaji yao kutegemea rasilimali na fursa. Fursa na vikwazo vya maendeleo (O&OD) ni mojawapo ya mbinu shirikishi, ambayo mipango ya maendeleo ya sekta – kama vile mipango ya maendeleo ya kilimo ya kijiji hutayarishwa. Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, katika michakato yake ya kupanga mipango na uidhinishaji kwa mwaka 2009 iliainisha ujenzi wa bwawa kwa ajili ya jamii ya Kigorogoro. Bwawa hilo lilikuwa litumike kama chanzo cha maji kwa ajili ya mifugo. Ufugaji ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya kipato kwa wakazi wa wilaya ya Karagwe. Ijapokuwa bwawa lilikuwa lijengwe katika vitongoji vya Kajumilo na Kibanda katika kijiji cha Kigorogoro, kuna vijiji vingine jirani ambavyo vingeweza kunufaika na mradi huo. Jumla ya gharama za bwawa ilikuwa TZS 33.5 milioni. Hata hivyo, licha ya mradi kuidhinishwa, ujenzi haukufanyika. Cha kushangaza zaidi, ripoti za utendaji zinaeleza kwamba ‘mradi unaendelea’, lakini hali halisi kulikuwa hakuna kitu kama hicho. Ukweli ni kwamba mradi haukutekelezwa mpaka baada ya miaka miwili baadaye (mwaka 2011). ANSAF, kwa ushirikiano na mwanachama wake, KADERES katika ngazi ya kijiji wamekuwa wakitekeleza programu ya SAM (Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii) katika wilaya ya Karagwe tangu Julai 2011. Wakati wa mafunzo ya, wajumbe wa timu walipata nyaraka mbalimbali za Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuzipitia kabla ya kutembelea maeneo ya miradi

Wafugaji wa Kigorogoro kisa cha bwawa la Mkaa

waliyochagua. Ilipangwa kwamba mradi wa bwawa wa Kigorogoro utatembelewa, kwa ajili kufanya tathmini ya maendeleo na utendaji.

jamii ya ChigoRogoRo Kijiji cha Chigorogoro kipo takribani kilomita 80 kutoka mji wa Kayanga – makao makuu ya wilaya. Kijiji hiki pamoja na vijiji vinavyokizunguka (Kijumbura/Nyakatera na Kibare) vina jumla ya wakazi 13,088 na wanatarajiwa kunufaika na mradi wa bwawa. Zaidi ya asilimia 80 ya kaya katika eneo hili ni wafugaji na walitarajiwa kunufaika. Mradi wa bwawa chini ya mipango ya wilaya ya maendeleo ya kilimo (DADPs) ulichaguliwa wakati wa mchakato uliotumia mbinu ya O&OD na jamii zilipata shauku kubwa kwamba mifugo yao sasa itakuwa na maji ya kunywa ya kutosha, hususani wakati wa kiangazi. Kwa kawaida vijana (wakati mwingine watoto wa umri wa kwenda shule) huswaga mifugo kwenda maeneo ya maji wakati wazee wakipumzika wakati wa mchana. Hata hivyo, kutokana na mipango mibovu na utaratibu mbovu wa kutenga rasilimali, zaidi ya asilimia 45 ya makadirio ya gharama zote (TZS 15 milioni kati ya TZS 33.5 milioni) zilitumika katika shughuli za awali za ujenzi wa bwawa (kupima udongo). Ijapokuwa mradi ulitakiwa uanze mwaka wa fedha 2008/09, hadi 2010 ripoti za utekelezaji kutoka Mpango wa Wilaya wa Maendeleo ya Kilimo ulionyesha kwamba mradi unaendelea. Lakini hali halisi hakuna kilichokuwa kinaendelea.

Timu ya Sam KaTiKa Kijiji Cha KigoRogoRoTimu ya SAM ilitembelea jamii ya Kigorogoro, ambako walifanya mahojiano na: viongozi wa jamii, wanakijiji, wafugaji, pia na diwani wa kata husika. Rasimu ya ripoti ilitayarishwa na mkutano wa kufuatilia pamoja na maafisa wa serikali ulifanyika mnamo Oktoba 2011. Kulingana na majibu kutoka kwa maafisa wa serikali, mradi haukutekelezwa kwa sababu makadirio ya bajeti yalikuwa chini sana hadi kufikia hatua ya kukamilisha mradi. Ni kutokana na sababu hii, kwamba serikali ilikuwa ikitekeleza mradi mwingine kilomita kadhaa kutoka Kigorogoro) wa ujenzi wa barabara ndogo za vijijini. Utekelezaji halisi (ukarabati wa barabara ndogo za vijijini) ulifanyika kati ya Novemba 2011 na Januari 2012 – miezi mingi baada ya timu ya SAM kumaliza mafunzo na ziara za maeneo husika.

maSuala muhimu Ijapokuwa jamii ya Kigorogoro haikunufaika na mpango wa awali, ni wazi kwamba ripoti zilikuwa hazimfikii kila. Kama ripoti za Mpango wa Wilaya wa Maendeleo ya Kilimo zingekuwa zinashirikishana na wadau wote, madiwani wangekuwa katika nafasi ya kuweza kuwauliza maafisa wa serikali. Pia ilijionyesha wazi kwamba katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, maafisa waliweza kwa urahisi kubadili vipaumbele kutoka mradi mmoja kwenda mwingine bila ya mashauriano ya awali na jamii. Hapakuwepo na nyaraka za maandishi ambazo zingeweza kuelezea jinsi mabadiliko ya mradi yalivyofanyika. Aidha, haikuwekwa wazi, jinsi gani kupima udongo kuliweza kugharimu asilimia 45 ya gharama za mradi. Watu watakuwa na dhana kwamba ukaguzi wa umakini ulifanyika kabla mipango haijawasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa. Kama isingekuwa timu ya SAM, jamii hii ingeendelea kusubiri mradi utekelezwe, wakati ukweli ni kwamba mradi umebadilishwa na kuwa kitu kingine.

TuTaKavyoSonga mbele Kwa sababu jamii bado inasisitiza umuhimu wa kuwa na bwawa, imewasilisha upya mapendekezo yake kwa mwaka wa fedha 2013/14. Mamlaka ya Halmashauri imekubali kuufikiria upya mradi, ijapokuwa ahadi si ya uhakika hadi mradi utakapoidhinishwa. Mwanachama wa ANSAF – aliyeko ngazi ya kijiji (KADERES) ameonyesha wasiwasi kuhusu jambo hili na amepanga kuwaona mamlaka ya wilaya na chama cha hisani cha Rotary International ili waweze kutekeleza mradi huu kwa pamoja.

Na Audax Rukonge

baJETI Na sERa

Page 13: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 11

Uporaji wa ardhiMoja ya rasilimali zinazohitajika kwa maisha na maendeleo ya kiuchumi ya wakulima wadogo ni ardhi.

Na Mbarwa Kivuyo Hata hivyo, changamoto inayozikabili jamii za vijijini nchini Tanzania leo, ni uhaba wa ardhi yenye rutuba kutokana na sababu nyingi ikiwemo

kuvamiwa na makundi ya watu wenye uwezo. Hivi karibuni, pamekuwepo na wimbi la kutisha la uporaji wa ardhi unaotokea katika maeneo mengi ya Tanzania. Uporaji wa ardhi nchini Tanzania unasemekana unawezeshwa na sheria zilizowekwa na wakoloni kabla ya miaka ya 1960. Washiriki wa warsha ya siku mbili kuhusu “uporaji wa ardhi nchini Tanzania na athari zake kwa wakulima wadogo” iliyoandaliwa na Shirika la INADES Formation Tanzania (IFTz), waliangalia sheria tofauti na sera za ardhi zinazoamuru upatikanaji na umiliki wa ardhi. Washiriki hao walisema kwamba sheria na sera za ardhi za Tanzania zimepitwa na wakati na zinakuza uporaji wa ardhi. Sera za Tanzania ni za kipekee kwa namna ambayo zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji katika kupata ardhi tofauti na wenyeji ambao wanahangaika kupata ardhi. Matukio ya jamii kufukuzwa maeneo yao yameripotiwa sehemu nyingi ikiwemo kata ya Mwanambaya katika wilaya ya Mkuranga na Idete katika wilaya ya Kilombero. Hebu tuiachie katiba mpya ishughulikie masuala muhimu sana ya ardhi. Katiba irudishe ardhi iliyochukuliwa na serikali kwa wamiliki halali,” mmoja wa washiriki alitamka. Si kitendo cha haki kwa wakulima wadogo kwamba serikali inaweza kuingia mapatano na wawekezaji wa nje yanayohusu ardhi yao.” Serikali inatumia hoja ya kile inachokiita “ardhi isiyotumika” kuwaondoa wakulima masikini kutoka kwenye ardhi yao ya asili. Baadhi ya tabia hizi za kupora ardhi zina athari kubwa katika kuendeleza umasikini kwa wakazi wa vijijini nchini. Sheria za ardhi za Tanzania zinaruhusu umiliki wa ardhi katika maeneo ya vijijini na mijini hadi miaka 99. Mmoja wa wawekezaji wa kigeni katika shirika la viwanda-kilimo, Agrisol Energy, alichukua ekari 800,000 (hekta 325,000) za ardhi na kuwafukuza watu 162,000. Elimu ya kutosha kuhusu umiliki wa ardhi inahitajika itolewe kwa wana kijiji ili waweze kufanya maamuzi ya busara kuhusu nini wanachotaka kufanya na ardhi yao ya asili.

Washiriki wa warsha ya Shirika la IFTz kuhusu “uporaji wa ardhi” wanaitaka serikali ya Tanzania kufanya mapitio ya sheria ambazo zainaongeza uporaji wa ardhi unaofanywa na makampuni makubwa ya kimataifa. Walisema kwamba Watanzania wanaweza kuishauri tume ya mabadiliko ya katiba kuweka umiliki na upatikanaji wa ardhi kama ajenda ya juu. Mwenyekiti wa Bodi ya IFTz, Oziniel Kibwana alisema kwamba asasi za kiraia lazima zikutane pamoja kubadili sheria ambazo zinakuza uporaji wa ardhi. “Kwa kweli wajibu wa asasi za kiraia ni kufichua sheria mbaya na kuishinikiza serikali kuzibatilisha,” alisema.

sheria na sera za ardhi za Tanzania zimepitwa na wakati na zinakuza uporaji wa ardhi

baJETI Na sERa

Page 14: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

12 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

oXFamVibarua vya msimu vinaweza kuwa chanzo cha kipato cha ziada kwa wanawake ambao pia hulima mashamba yao au ardhi ya kaya. Kwao ajira inakuwa sehemu ya mikakati mingi ya kumudu maisha katika kaya.

KipaTo Cha WanaWeKe na KaZi Za Kiba RuaKa KaTiKa minyoRoRo ya ThamaniKipato cha wanawake ndio injini ya kuendesha maisha ya kila siku ya familia katika nchi nyingi za Kiafrika. Wanawake katika maeneo ya vijinini huchukulia kazi za vibarua kama chanzo cha pili cha kuingiza kipato. Kazi za vibarua huwasaidia wanawake kupata pesa za kulipia baadhi ya gharama za mahitaji ya

minyororo yetu ya thamaniKwa mamilioni ya wanawake wasio na ardhi au wenye ardhi kidogo na ambao wana fursa chache za kuingiza kipato kwa njia nyingine, ajira katika biashara ya kilimo ni chanzo mbadala cha kuingiza kipato ili kuhakikisha uhakika wa chakula na uwezo wa kujikimu kiuchumi.

Na Naomi MakotaMshauriwaProgramu –Uongozi wa Kiuchumi wa Wanawake Oxfam

Kuvaa ‘miwani za jinsia’ kwenyeWanawake wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kazi za vibarua.

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Pich

a : N

aom

i Mak

ota

kila siku kama vile chakula, sabuni na pia huwaruhusu kuweka akiba kwa ajili ya majukumu mengine ya kijamii. Wanawake wengi hawamiliki ardhi. Wanaruhusiwa tukuitumia na hivyo wana haki ya kuitumia. Kwa sehemu kubwa maamuzi yanayohusu ardhi ni wajibu wa wanaume. Ndio maana inawabidi wanawake kutafuta vyanzo vya kipato vya ziada. Mbali na uwezo wa kumiliki ardhi, wanaume pia wanaweza kupata mikopo na mafunzo ya kitaalamu kwani wanachukuliwa kuwa ndio viongozi wa kaya. Wanaume pia wanaweza kadri wanyotaka, kufanya kazi kwa masaa machache ukilinganisha na wanawake. Ushahidi uliopo unaonyesha kwamba fursa za kazi katika mnyororo wa thamani hutoa faida za kujikimu kimaisha kwa

watu masikini vijijini hasa kwa wale wenye uwezekano finyu wa kupata ardhi. Wanawake wanaochangaya kilimo na ajira wana uwezekano mkubwa wa kuingiza kipato cha ziada kusaidia familia zao.

WanaWaKe WanaoFanya KaZi Za vibaRua na KuKoSeKana uSaWa KaTiKa minyoRoRoRo ya ThamaniBado kuna tofauti kubwa ya usawa wa kijinsia miongoni mwa watendaji mbali mbali katika minyororo tofauti ya thamani. Kwa mfano, katika Mnyororo wa Thamani kwenye Mboga mkoani Tanga, wanawake wengi wanaojihusisha wanalipwa fedha kidogo kuliko wanaume kwa kufanya kazi ile ile. Mfano mzuri ni katika upakiaji wa mizigo kwenye malori. Wanaume wanaopakiza kabichi kwenye malori wanalipwa vizuri zaidi. Wanawake wanovuna na kuleta kabichi kutoka mashambani hadi sehemu ya kupakiza kwenye lori wanalipwa pesa kidogo, kwa kawaida mara nne chini ya kile wanacholipwa wanaume. Mnyororo wa thamani unaofanya kazi vizuri lazima uendeshwe na watendaji wanaovaa “miwani za jinisia” ili kuwasaidia kuona tofauti hizi za kijinisia na hivyo kuzirekebisha mara moja.

Page 15: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 13

Na Naomi MakotaMshauriwa Programu –Uongozi wa Kiuchumi wa Wanawake Oxfam

katika Minyororo ya ThamaniVVU/UKIMWI na Wanawake

Wanawake wanakabiliwa na hatari mbalimbali wanapokuwa wanatafuta kazi za kibarua. Hatari zinazoweza kujitokeza zinajumuisha jinsi watakavyoepuka kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI.

Wanawake wakiwa wamepumzika baada ya kazi za vibarua.

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Pich

a : N

aom

i Mak

ota

Kwa sababu wanawake wanajikuta ikiwalazimu kufanya kazi ya kibarua wanalazimishwa kujihusisha katika vitendo vya

ngono ili walipwe pesa inayofanana na pesa ambayo wangeipata kama wangeajiriwa shambani. Wanaume wanatumia udhaifu wa wanawake kama njia ya kuwalazimisha wanawake kufanya ngono bila ya ridhaa yao. Kulingana na mahojiano mbalimbali, wanawake wanafahamu kuhusu VVU/

UKIMWI lakini wanasema hawana njia nyingine. Wanalazimishwa kuuza miili yao ili wapate pesa ya kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Suluhisho la tishio hili inaweza kuwa kwa serikali na wadau kujenga uwezo wa wanawake kujihusisha katika minyororo ya soko. Mafunzo yatakuwa ndio suluhisho la muda mrefu lakini kupatikana kwa mtaji kunaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya wanawake.

kulingana na mahojiano mbalimbali,

wanawake wanafahamu kuhusu VVu/ukIMwI lakini wanasema hawana

njia nyingine. wanalazimishwa kuuza miili yao ili wapate pesa ya

kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Page 16: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

Mara moja nikaanza kujisikia vizuri, na

dawa zangu zikafanya kazi. Niliendelea kuwa na nguvu na baada ya kipindi kifupi nikaanza kulima tena – mahindi, muhogo, na maharage.

Sauda Ntakiteye, mwenye umri wa miaka 44, aligundulika baada ya kupima kwamba ana Virusi Vya Ukimwi (VVU) miaka tisa iliyopita

baada ya mume wake kufariki. Tangu wakati huo ameshapoteza watoto sita – wote walikuwa wameambukizwa. Sasa hivi anaishi karibu na watoto wake wawili waliobaki na wajukuu wawili. Miaka michache iliyopita, Sauda alikuwa karibu na kufa. Dawa zake za kupunguza makali ya virusi zilikataa kufanya kazi kwa sababu hakuwa na virutubisho vinavyohitajika ili ameze dawa. Alipiga picha ili jirani zake waweze kumkumbuka. Lakini kufika 2011, alikuwa bado yuko hai. Na kulingana na maelezo ya Sauda, anajisikia vizuri kuliko wakati mwingine wowote. Mwaka 2007, Sauda alianza kufanya kazi na Shirika la REDESO, mbia wa Shirika la Concern Tanzania katika wilaya ya Kibondo magharibi ya Tanzania. “REDESO waliniambia ninahitaji kuanza kula mboga mboga, kwa hiyo walinifundisha jinsi ya kupanda mboga kwa kutumia mifuko mikubwa ya mbolea ya mboji. Mara moja nikaanza kujisikia vizuri, na dawa zangu zikafanya kazi. Niliendelea kuwa na nguvu na baada ya kipindi kifupi nikaanza kulima tena – mahindi, muhogo, na maharage. Nilikuwa sijaenda shambani kwangu kwa miaka mingi.” Toka wakati huo Sauda amekuwa akifanya

kazi kwa bidii shambani kwake na ana chakula cha kutosha, pia anaingiza kipato kutokana na kuuza mboga na mazao ya ziada. Anaona kuna mabadiliko makubwa katika maisha yake. “Nilikuwa nalala katika nguo hizo hizo nilizoshinda nazo mchana. Nilikuwa na gauni moja tu. Sasa hivi nina nguo za kutosha, baiskeli, redio na simu – sikuwa na vitu hivi huko nyuma,” anaelezea Sauda. “Nimekarabati nyumba yangu; sasa hivi naishi kwa raha na sina njaa tena.” Kwa Sauda, mabadiliko makubwa yalikuja katika hisia zake kwamba anajiona ana thamani na anaamini kwamba anaweza kufanya kitu chochote. Kwa sababu ya dhamira yake ya kipekee, ni mmoja wapo wa wakulima bora katika jamii yake. “Nilipogundulika nina VVU hata ndugu zangu hawakuniruhusu kuwa karibu na watoto wao. Kanisa katika eneo letu lilisaidia kuwafanya watu waelewe kwamba nilichohitaji ilikuwa

ni kusaidiwa na wala sio unyanyapaa wao, kwa hiyo walisaidia kubadili mambo kwangu katika jamii. Sasa mimi ni mtu muhimu hapa. Wakulima 19 kutoka vijiji vingine wamekuja nyumbani kwangu kujifunza kuhusu kilimo cha mboga, na nimeweza kupata mkopo kupitia REDESO kwa kuwapa mafunzo watu wengine. Sasa hivi mimi ni mtaalamu msaidizi katika kijiji hiki; watu wanakuja kujifunza kuhusu kilimo, na ninajaribisha kilimo-hifadhi. Ninafanya kazi kwa bidii, na ninaweza kufanya chochote.” Sauda haogopi kuelezea hali yake ya VVU. Anafanya kazi na timu ya madaktari kutoa elimu na msaada kwa watu wa Kibondo waliopimwa na kukutwa na VVU na ambao wanaanza kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU. Sasa, anasema Sauda, watu wengine nao wanaeleza hali zao za VVU katika jamii. “Hii inatufanya tujiamini na kuonekana tuna thamani, na tunatumai itasaidia kuzuia maambukizi mapya hapo baadaye. Watu wanapoficha hali zao za VVU inafanya iwe vigumu kwao kupata huduma ambazo zingeweza kuwasaidia.” Kwenye mlango wa mbele wa nyumba ya Sauda, kuna maneno yameandikwa vizuri kabisa “Achana na mimi, wewe si Mungu” (Leave me alone, you are not God). Ni wazi hapa Sauda anahoji wale wanaotaka kumnyanyapaa. Sauda anasema, “Nimeandika maneno haya kwa sababu mimi sitakufa sasa hivi, na sitakufa hivi karibuni.”

Sauda Ntakiteye: Mkulima na Mfanyabiashara

Phot

o : M

wan

zo M

illin

gi

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 17: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 15

Programu Endelevu ya Uhakika wa chakula katika wilaya ya chunyaShirika la VECO Tanzania linatekeleza Programu Endelevu ya Uhakika wa Chakula katika Wilaya ya Chunya inayoendana na mbinu ya Maendeleo Endelevu ya Kilimo ya Mnyororo wa Thamani.

Bi. Fibe Sanga mwanachama wa Kikundi cha Upendo akiwa kwenye shamba la alizeti

Wanachama wa Kikundi cha Upendo wakiwa katika shamba lao la alizeti

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

VECO inawezesha programu ya Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani kwa Zao la Alizeti katika kata za Chalangwa, Sangambi, Ifumbo, Tete, Matundasi, Makongorosi na Mtanila. Wakulima hushiriki katika maendeleo ya mnyororo wa thamani kupitia uanachama wa kikundi chao. Vikundi vya wakulima hukutana pamoja kuunda Asasi ya Kifamilia ya Wakulima wa Mazao ya Biashara katika kata (CFFO). Kikundi cha Wanawake cha Upendo katika kijiji cha Matundasi ni mojawapo ya mifano ya CFFO zinazofanya kazi katika wilaya.

KiSa mKaSa na. 5: KiKunDi Cha WanaWaKe Cha upenDoKikundi cha Wanawake cha Upendo kina wanachama wanawake 30 wenye shauku ya kuboresha hali zao za kijamii na kiuchumi. Kikundi kilianzishwa mwaka 2009 kikiwa na mtaji wa msingi wa TZS 6 milioni. Pesa hii inatumika kama fungu linalozunguka. Ili waweze kuongea mtaji riba ndogo hutozwa kwa wateja, na wanachama hulipa ada ya mwezi ya TZS 2000. Ili uweze kuwa mwanachama wa Asasi ya CFFO,

Shirika la VECO ambalo ndio mwezeshaji, limeweka kuundwa kwa kikundi kama kigezo cha ushiriki. Kwa hiyo, Kikundi cha Upendo kiliwapatia wanawake hao uwezo wa kuingia katika familia ya Asasi ya CFFO ya Matundasi. VECO huhimiza wanawake kushiriki katika minyororo ya thamani kwa vile takribani asilimia 80 ya vibarua katika shughuli za vijijini ni wanawake. Ushiriki wa wanawake katika mnyororo wa thamani wa zao la alizeti ni mbinu za makusudi zinazotumiwa na VECO ili kuwawezesha wanawake kuunda na kuendesha afua zao wenyewe za minyororo ya thamani. Kikundi kilianzisha uzalishaji wa alizeti kwa ushirika katika eka nane za ardhi. Wakati huo huo, kila mwanachama alimiliki eka moja. Mbali na faida ya kiuchumi, wanawake pia walipata mafunzo kuhusu mahusiano ya kikundi, kilimo kama biashara, stadi za ujasiriamali, stadi za usimamizi wa biashara, stadi za usuluhishi na stadi za masoko. Pia walijifunza jinsi ya kutengeneza vyakula vya mifugo na jinsi ya kufanya utafiti wa masoko. Maarifa waliyoyapata yaliwasaidia katika kusimamia maeneo mengine nje ya

mnyororo wa thamani wa zao la alizeti. Kikundi kina mipango ya baadaye ya kununua trekta aina ya “pawa tilla” na kupanua eneo la shamba kutoka eka 8 hadi 20. Bi. Fibe ambaye ni mwanachama wa kikundi anasema “tunataka kupanua shamba kwa sababu tumeona faida zake zinazoweza kupatikana kutokana na uzalishaji wa alizeti.”

ushiriki wa wanawake katika mnyororo wa

thamani wa zao la alizeti ni mbinu za makusudi

zinazotumiwa na VEco ili kuwawezesha wanawake kuunda na kuendesha afua zao

wenyewe za minyororo ya thamani.

Page 18: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

16 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

Visa Mkasa vya Jinsia kutoka MkurangaKiSa mKaSa #1

Juma Nyamgunda ni mkulima kutoka wilaya ya Mkuranga katika kata ya Kizapala. Ni baba wa watoto nane na wake zake wawili. Nyamgunda ni mwanachama na Katibu wa Asasi ya Kifamilia ya Wakulima wa Mazao ya Biashara (CFFO), katika kijiji cha Kizapala, asasi ambayo inajihusisha na uzalishaji na usindikaji wa muhogo. Wanachama 38 wa Asasi ya CFFO wanawezeshwa na Shirika la VECO –Tanzania ili kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa zao la muhogo na mifumo ya masoko. Alipoulizwa kuhusu usawa wa kijinsia katika ngazi ya kaya, Nyamgunda alisema yeye na wake zake wawili wote ni wanachama wa CFFO. Asasi ya CFFO ina wanachama wanaume 12 na wanawake 26, asasi ikiongozwa na mwanamke. Bodi ta utawala ina jumla ya wajumbe nane, watano kati yao ni wanawake na wanaume watatu. Nyamgunda anasema wanawake wanatekeleza wajibu muhimu katika kufanya shughuli za CFFO. Ijapokuwa wanaume katika kata wanahimizwa kujiunga na CFFO, kwa ujumla mwitikio umekuwa mdogo. Jambo la kufurahisha kuhusu sifa za asasi hii ya CFFO ni kwamba wanachama walio wengi ni wanandoa, mke na mume. “Wanaume wote 12 kwenye asasi wanashirki kikamilifu na wake zao,” anasema Nyamgunda. Wanawake wanawazidi wanaume kwa idadi, kwa sababu baadhi ya wanawake wanaishi na waume wenye wake wengi kama ilivyo kwa wake wa Nyamgunda, wakati wengine hawana waume au ni wajane. Katika kisa hiki, idadi kweli inaweza kuleta mabadiIiko? Si kweli kwani wanaume wachache waliopo bado wanatawala majadiliano mengi yanayohusu kufanya maamuzi. Wanawake wengi hawazungumzi katika mikutano. Lakini tofauti na wale ambao sio wanachama wa CFFO, wanawake hawa wanatoka majumbani kwao kuja kushiriki katika shughuli za kikundi.

KiSa mKaSa #2

Tungi ni Asasi ya Kifamilia ya Wakulima wa Mazao ya Biashara (CFFO) katika wilaya ya Mkuranga. Mmoja wa wanachama wa Asasi hii ya CFFO ni Bi. Mosi Uwange Mohamed. Mosi na Mohamed ni wazazi wa watoto watatu. Anaelezea uzoefu wake kupitia ushiriki wake katika maendeleo ya mnyororo wa thamani katika zao la muhogo. Alipojiunga na kuwa mwanachama haikuwa rahisi kwake kwa sababu mume wake alikuwa anapinga karibu vitu vyote vinavyohusiana na uwezeshaji kiuchumi wa wanawake. Mke kupigwa lilikuwa jambo la kawaida katika nyumba ya Mohamed na Mosi. Chanzo cha ugomvi ilikuwa ni kwa sababu tu Mosi amejiunga na Asasi hiyo ya Wakulima. Mosi alivumilia na hakukata tamaa mpaka akachaguliwa kuwa kiongozi wa kikundi. Aliendelea kupanda chati ya uongozi hata kufikia nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Muhogo kwenye Wilaya. Juhudi nyingi za kuamsha ufahamu ziliwafanya wanaume kuanza kubadilika. “Wanaume sasa wanaruhusu wake zao kushiriki katika miradi ya kijamii na kiuchumi kama vile maendeleo ya mnyororo wa thamani kwa zao la muhogo,” anasema Mosi. Faida alizopata kutokana na kushiriki katika Asasi ya Wakulima ndio ilikuwa sababu kubwa iliyomshawishi mume wake kumruhusu kushiriki. “Habari njema,” anaeleza Bi. Mosi, “Mohamed pia anafikiria kujiunga na Asasi ya Wakulima.”

KiSa mKaSa # 3

Bi. Chiku Raha Mgoto anaishi katika kijiji cha Lupondo. Ni mhamasishaji jamii na mwanachama wa Asasi ya Kifamilia ya Wakulima wa Mazao ya Biashara katika kijiji cha Lupondo. Bi. Chiku ni mjane mwenye watoto watano. Zaidi ya kuwa mwana jamii anayejituma, pia anaendesha miradi midogo kadhaa anayoimiliki ambayo inamsaidia kujikimu kimaisha. Alipoulizwa kuhusu usawa wa kijinsia na mageuzi katika wilaya, Bi. Chiku alisema wanawake wengi katika kata wanakosa ufahamu wa masuala ya jinsia ukilinganisha na wanaume. Wajibu wake kama mhamasishaji jamii unaambatana na changamoto nyingi, ikiwemo ugumu wa kushawishi wanawake wajihusishe katika shughuli za kijamii na kiuchumi. ”Wanawake wanajihisi ni watu wa chini. Sio kweli kwamba wanaume wanawazuia wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi,” anatamka Chiku. Anaongeza kwa kusema: programu kadhaa za maendeleo kama vile MVIWATA, Mamlaka za Serikali za Mitaa na VECO zinajaribu kuleta usawa wa kijinsia lakini wanawake wa Lupondo wanasita kujihusisha kikamilifu, tofauti na wenzao katika kata ya Kizapala.

Bw. Juma Omary Nyamgunda

Bi. Chiku Mgoto

Bi. Mosi Mohamed Uwange na watoto wake watatu

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 19: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 17

Mkulima mwenye mafanikio Wilaya ya SimanjiroKiSa mKaSa # 4

Theresia Kipondo ni miongoni mwa wanachama wanzilishi wa Kikundi cha Kifamilia cha Wakulima kinachoitwa Ereto. Kikundi hiki kilianzishwa mwaka 2008 kupitia kuwezeshwa na Shirika la VECO, Asasi ya Kibelgiji Isiyokuwa ya Kiserikali inayoendesha programu ya uwezeshaji wa uchumi endelevu katika wilaya za Simanjiro na Same (SiSa). Kikundi kina wanachama wapatao 27, wengi wao wakiwa wanawake ambao wanajihusisha katika uzalishaji wa vitunguu katika bonde la Mto Pangani katika kijiji cha Remit, Wilaya ya Simanjiro. Theresia na wanachama wengine wa kikundi walihamasishwa na mafunzo mbalimbali kuhusu uzalishaji wa vitunguu kibiashara na afua nyingine za programu. Aliweza kulima eka moja ya vitunguu mwaka 2009 kwa kutumia mkopo mdogo alioupata kutoka kwenye Benki ya Jamii ya Kijiji (VICOBA). Kuanzia hapo Theresia amekuwa akipanua shamba lake kila mwaka kwa kuwekeza kutokana na mapato yanayotokana na biashara. Kwa mfano, mwaka 2011alilima eka mbili za vitunguu na akafanikiwa kupata gunia 89. Alitakiwa kuvuna gunia 140 kama mvua zingekuwa nzuri. Vitunguu viliuzwa kwa TZS 57,000 kwa gunia, hivyo aliweza kupata TZS 5,073,000. Theresia ni mjane mwenye watoto saba, wasichana wawili na wavulana watano. Kuhusiana na kilimo cha vitunguu, Theresia anasema: “Kilimo cha vitunguu kimekuwa kikisaidia familia yangu kiuchumi. Nimeweza kununua mabati ya ya nyumba yenye thamani ya TZS 768,000. Nilitumia TZS 150,000 kujenga stoo kwa ajili ya vitunguu na pia nimeweza kuwapeleka watoto wangu shule,” anasema. Theresa anaongezea kusema kwamba awekeza salio la pesa katika biashara nyingine ndogo ndogo. “Ninalipa TZS 1,360,000 kwa ajili ya karo ya shule ya mtoto wangu anayesoma sekondari nchini Uganda.”

Theresia akikagua sehemu ya kuhifadhi vitunguu karibu na shamba lake

Bi. Theresia shambani kwake.

Theresia akifanya kazi katika shamba lake la vitunguu kijijini Remit

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 20: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

18 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

“...kuongezeka kwa mzunguko wa

fedha ndani ya jamii yetu, mchango wetu

katika programu ya unywaji wa

Maziwa shuleni, na kuanzishwa kwa

majiko yanayotumia kuni chache katika nyumba za vijijini.”

Wananchi wa vijijini walio wengi ni wakulima wadogo wanaomiliki vipande vidogo vya ardhi

kati ya hekta 0.5 hadi hekta 5. Kwa sehemu kubwa, shughuli za shamba hufanywa na familia, lakini wanawake ndio wanaobeba jukumu kubwa zaidi. Wanawake hutumia muda wao mwingi katika kulima shamba, kupanda, kupalilia, kuvuna na kuhifadhi mazao yaliyovunwa. Maendeleo endelevu ya uchumi nchini Tanzania hutegemea kwa sehemu kubwa katika msaada wanaopatiwa watu wanaosimamia ardhi. Nguvu kazi iiliyo kubwa zaidi katika kilimo nchini ni “kundi la wanawake”. Hawa huzalisha takribani asilimia 75 ya chakula tunachozalisha shambani na tunachokula. Iwapo kundi hili litapatiwa msaada kamilifu, lina uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha kuondoa njaa na kupunguza utapiamlo nchini. Wakulima wanawake ndio ambao hupanda na kusindika mazao ya chakula ili kuongeza thamani. Licha ya wajibu huu,

Idadi ya watu wa Tanzania inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 44, kati ya hao takribani asilimia 70 wanaishi maeneo ya vijijini ambako wanajishughulisha na kilimo ili kuendesha maisha yao.

Na Cleophas RwechunguraBaraza la Kilimo Tanzania

katika kilimoKukuza wajibu wa Wanawake

mara nyingi hawathaminiwi na tamaduni au taasisi zinazotunga sera na kufanya maamuzi ambayo yanagusa maisha yao na ustawi. Kulingana na matokeo ya utafiti wa Shirika la Kilimo na Chakula (FAO) la Umoja wa Mataifa, wanawake wengi katika nchi zinazoendelea hukabiliwa na matatizo katika kupata ardhi, mifugo, mtaji, teknolojia mpya na programu za misaada ya kilimo. Ripoti hii inasisitiza haja ya mabadiliko ya sera ambayo itawapatia wanawake fursa kubwa zaidi ya kuongeza mavuno ya mazao.

WajaSiRiamali WanaWaKe Wa Kijiji Cha nRonga Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Wanawake wa Nronga (maarufu kama Chama cha Maziwa cha Wanawake wa Nronga) kilianzishwa Machi 1988 na kikundi cha wanawake waliokuwa na dira ya pamoja. Chama hiki kina wanachama zaidi ya 400 ambao kazi yao kubwa ni kukusanya maziwa kutoka kwa wanachama na wasiokuwa wanachama na kuzalisha

bidhaa mbalimbali katika kiwanda chao cha kisasa kabisa cha usindikaji. Makusanyo ya kila siku yanakaribia lita 1,000. Sehemu ya maziwa huuzwa kama yalivyo, iliyobaki husindikwa na kuwa siagi na mtindi. Zaidi ya watu 650 wa kijijini wamejiajiri katika biashara zinazohusiana na maziwa na kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha yao kwa vigezo vya: Fursa za ajira, kuongezeka kwa unywaji wa maziwa kwa kila mtu, na kuongezeka kwa ulaji wa chakula chenye lishe. Aidha, jamii ya Nronga imeanzisha taasisi mbili muhimu za kifedha katika kijiji chao, ambazo ni Chama cha Kuweka na Kukopa – SACCOS, na Benki ya Jamii ya Kijiji – VICOBA. Bi. Helen Ussiri ambaye ni msimamizi wa Chama, ana haya ya kusema: “Ninajivunia mafanikio tuliyopata hadi sasa. Hii inajumuisha uhakika wa soko wa bidhaa zetu, kuongezeka kwa mzunguko wa fedha ndani ya jamii yetu, mchango wetu katika Programu ya Unywaji wa Maziwa Shuleni, na kuanzishwa kwa majiko yanayotumia kuni chache katika nyumba za vijijini.”

Watoto wa shule wakipokea paketi za maziwa zilizotolewa na Chama cha Ushirika wa Ng’ombe wa Maziwa cha Wanawake wa Nronga

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 21: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 19

Kikundi cha Wanawake cha MauaKikundi cha Wanawake cha Maua kinaundwa na wanawake wajane ambao waliamua kukusanya pamoja rasilimali zao kidogo walizokuwa nazo ili kujiletea maendeleo.

Kikundi hiki ambacho makao yake ni katika kata ya Maua, Wilaya ya Rombo, kiliundwa na wanachama 30 waliodhamiria. Baadaye kikundi kilisajiliwa kama Chama mwaka 1995. Miaka michache baadaye, kwa sababu moja au nyingine, baadhi ya wanachama wanzilishi waliamua kujitoa. Wanachama waliopo sasa

wanafika 24. “Kuna mtu alipendekeza wazo la kuungana ili tutokomeze umasikini miongoni mwetu. Tulilikubali wazo hilo na tukakubaliana jinsi tutakavyosonga mbele,” alisema Bi. Agnes Kavishe, Katibu Mtendaji wa sasa wa kikundi. Kikundi kilianza na nguruwe watano, wawili walinunuliwa na watatu walitolewa kama msaada na Enviro-Care. Baadaye, Shirika la CARITAS (Catholic Relief Agency) lilitupatia nguruwe wengine watatu. Huu ulikuwa mwanzo mzuri ambao ulituwezesha kujaza nguruwe kwenye mabanda. “Soko la nyama ya nguruwe halina kikomo,” anasema Bi. Kavishe. Zaidi ya ufugaji wa nguruwe, kikundi hiki pia kinamiliki mashine ya kusaga nafaka na mashine za kukamua mafuta ya kula, ambazo zote zilitolewa kama msaada na Shirika la Equal Opportunity Fund linaloongozwa na Mama Anna Mkapa. Kikundi sasa kinaingiza mapato ya ziada kutokana na usindikaji wa vyakula vya nafaka inayoletwa na wakulima wenzao. Sehemu ya kipato kilichozalishwa kutoka kwenye miradi hugawanywa miongoni mwao kama gawio. Kwa sasa kikundi kimewezeshwa kiuchumi na kijamii.

kuna mtu alipendekeza

wazo la kuungana ili

tutokomeze umasikini

miongoni mwetu.

Tulilikubali wazo hilo

na tukakubaliana jinsi

tutakavyosonga mbele

Pich

a : M

illy

Sang

a

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 22: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

20 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

Kijiji Asilia Chololo ni mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya ili kujenga mfano wa utendaji mzuri katika kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo kame ya Afrika.

Na Michael Farrelly, Mratibu wa Programu, Mtandao wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM)

na mabadiliko ya tabia nchiUwezeshaji jinsia, minyororo ya thamani

Wabia sita wanashirikiana kusaidia jamii ya Wagogo katika kijiji hiki kilicho karibu ya mji wa Dodoma, kufanya

majaribio, kutathmini na hatimaye kukubali kutumia mbinu endelevu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika sekta za kilimo, mifugo, maji, nishati na maliasili. Mradi umedhamiria kuhakikisha kwamba wanawake wanawezeshwa kufanya kazi wakiwa mstari wa mbele wa mageuzi. Kwa kutumia mbinu ya mnyororo wa thamani uliobuniwa na Shirika la OXFAM na kushirkisha wadau wengine katika Hafla ya Kujifunza ya ANSAF ya mwaka 2010, mbia wa Chololo Kijiji Asilia, Mtandao wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM) hivi karibuni alifanya utafiti ili kutayarisha hatua za kuendeleza masoko zinazoweza kutumika na zilizo bunifu katika sekta ndogo / minyororo ya masoko ambayo itawanufaisha zaidi wanawake. Kazi

ya kwanza ilikuwa ni kutambua na kuchagua sekta ndogo zitakazowanufaisha zaidi wanawake.

muhtasari wa mbinu ya mnyororo wa thamani

1 Uchaguzi wa mnyororo wa thamani

2 Uchambuzi wa modeli ya soko

3 Utambuzi wa fursa

4 Kubuni na kutekeleza mkakati

5 Tathmini, jifunza, na buni upya

KuChagua SeKTa nDogo Timu iliendesha warsha nne katika kipindi cha siku tatu na kushirikisha wajumbe 192 wa jamii ya kijiji (wakiwemo wanawake 105). Warsha ya kwanza ilitayarisha orodha ya sekta ndogo za shughuli za uzalishaji mali. Hii ilionyesha mahali pa kuanzia katika uchaguzi

wa sekta ndogo. Katika kila warsha orodha hii ilihakikiwa, iliongezewa, na kupunguzwa hadi kufikia kama sekta ndogo 10 zilizo na maslahi mahususi na faida kwa wanawake. Sekta zilizoingizwa katika orodha fupi baada ya hapo zilipewa alama dhidi ya 10 na washiriki kwa kutumia vigezo vitano, viwili vikipima soko, na vitatu vikipima ushiriki wa wanawake.

KigeZo 1: uhiTaji Wa SoKo • Uhitajiuliothibitishwakwabidhaa;• Uhitajiunazidiupatikanaji;

KigeZo 2: uShiRiKi Wa WanaWaKe • Mabadiliko na matumizi yenye wigo

mpana kwa wanawake;• Wanawakewanakubalibilataabukufanya

shughuli hiyo;• Wanawake wanaweza kudhibiti mapato

kutokana na mauzo ya bidhaa.

Warsha zilitawaliwa na kazi ngumu, majadiliano makali na ucheshi mwingi. Wakati mwingine washiriki waliombwa ‘kupiga kura’ kwa kutamka kwa nguvu ‘NDIYO’ kuonyesha kukubaliana na shughuli iliyotajwa, na sauti zilizotoka zilitoa kiashiria kizuri cha alama ya shughuli hiyo. Mambo yaliyojificha yaliibuka. Ilionekana kwamba ijapokuwa ufugaji wa mbuzi

Mradi umedhamiria kuhakikisha

kwamba wanawake

wanawezeshwa kuwa mstari wa

mbele katika mageuzi ya mbinu

ya mnyororo wa thamani

uliotayarishwa na oXfaM.

Pich

a : M

icha

el F

arre

lly

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 23: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 21

na nguruwe ulikuwa ni shughuli nzuri ya biashara, kutokana na kiasi cha fedha kinachopatikana wakati wa mauzo kuwa kikubwa, mwanaume ndani ya nyumba ndiye kwa kawaida anayeshika fedha hiyo. Wakati katika suala la biashara ya kuku, kiasi kidogo cha fedha kinachopatikana hushikwa na kutumiwa na wanawake. Alama zilizopatikana zilijumlishwa na washiriki kupewa mrejesho. Katika kila kikundi cha warsha ilionekana dhahiri kwamba ufugaji wa kuku wa kienyeji ndio sekta iliyokuwa na manufaa zaidi kwa wanawake. Sekta ndogo nyingine zilizopata alama za juu pia zilihusisha mifugo, wakiwemo ng’ombe wa maziwa, mbuzi na nguruwe, wakati alizeti, karanga na ufuta zikifuatatia kama mazao ya shambani yanayoongoza. Ushonaji uliibuka kuwa sekta iliyopata alama nyingi zaidi ambayo haihusiani na kilimo.

SeKTa nDogo / uChambuZi Wa mnyoRoRo Wa Thamani Baada ya hapo timu ilifanya uchambuzi wa sekta ndogo ya kuku wa kienyeji kupitia mlolongo wa mikutano na wadau wa sekta ya kuku wakiwemo Idara ya Kilimo na Mifugo ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Kampuni ya Maendeleo Vijijini, INADES Formation Tanzania, wanunuzi katika migahawa, Chuo cha Mipango na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mpwapwa. Katika kila mkutano majadiliano yalilenga kwenye uelewa wa mfumo wa uzalishaji wa kuku na mnyororo wa thamani, na kuaianisha vikwazo na fursa.

viKWaZo vilijumuiSha:• Magonjwa:Kideri,Gumbolo,NduiyaKuku• Hasara katika kutotoa kutokananamayai

kutorutubishwa • Vifo vya vifaranga zaidi ya asilimia 50

kutokana na kuliwa na wanyama /ajali

 

• Muda mrefu wa kupevuka (miezi sita –saba)

• Kukosekana kwa mabanda kunazuiakuongeza idadi ya kuku

• Uhabawachakulahuzuiakuongeza idadiya kuku

• Beiyasokokubadilika-badilika(TZS3000-8000)

FuRSa ZiliZoainiShWa:• Wachanjajikatikajamiiwaliopatamafunzo• Mbeguborazamajogoo• Chakulakinapatikanakijijini• Afisauganianapatikana• Wanajamiiwanashauku• Chakulanighalisanalakiniviambatovingi

tayari vinapatikana • Mayai ya kukuwa kienyeji yana bei nzuri

mjini Dodoma• Mauzo ya moja kwa moja kwenye

migahawa ni TZS 8,000 kwa kila kuku

muunDo Wa pRogRamuWarsha ilifanyika na watoa huduma wakuu ili kuwapa mrejesho wa matokeo na kutayarisha programu madhubuti ya afua zinazohitajika ili kutumia fursa zilizoainishwa. Warsha pia ilishughulikia vikwazo katika sekta ndogo ya kuku wa kienyeji. Hii inajumuisha afua zinazolenga katika:• Kusaidiawakulimawaelekeekatikambinu

mchanganyiko za ufugaji wenye uwekezaji mdogo

• Maboresho katika uzalishaji kupunguzamuda wa kupevuka kwa kuku kutoka miezi sita hadi mitatu au minne

• Udhibitiwamagonjwakupitiakuboreshwakwa upatikanaji wa chanjo

• Mabandaborayakukunaulinzi• Chakulabora• Sokolapamojailikupatabeinzurizaidi

Wabia wa mradi na watoa huduma kwa sasa wanaandaa mipango ya kutekeleza afua hizi ili kusaidia kuwawezesha wanawake wa Chololo Kijiji Asilia kuendeleza ufugaji wa kuku kama njia ya kuinua kipato vijijini na kushika uongozi katika kuimarisha jamii kupitia maendeleo ya ujasiriamali. Mradi wa Chololo Kijiji Asilia unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na kutekelezwa na ubia wa mashirika yafuatayo: • ChuochaMipango• HalmashauriyaManispaayaDodoma• TaasisiyaUtafitiwaKilimoHombolo• MajinaMaendeleoDodoma(MAMADO)• MtandaowaKilimoHaiTanzania(TOAM)• MtandaowaMazingiraDodoma(DONET)

Angalizo: Alama za juu kabisa = 50 (Alama za juu za uhitaji wa soko = 20, Alama za juu za

ushiriki wa wanawake = 30)

Pich

a : M

icha

el F

arre

lly

Alama ya Wastani ya Ushiriki wa Wanawake

Alama ya Wastani ya Uhitaji wa Soko

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 24: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

22 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

Shirika la VSO (Volunteers Services Overseas) tayari lilikwishaona uwezekano huu, hivyo kuamua kujiingiza katika mradi wa ufugaji

samaki ambao unashughulikia uboreshaji wa uwezo wa kitaalamu wa vikundi vya kijamii na upatikanaji wa masoko bora. Shirika la VSO-Tanzania ni Asasi Isiyokuwa ya Kiserikali (AZISE) ambayo hubuni na kutekeleza mikakati ya kuongeza uzalishaji kipato kwa jamii masikini na zilizotengwa katika mikoa minne ya Tanzania bara na visiwa vya Zanzibar. Shirika hili linashirikiana na wabia mbalimbali nchini

na Vso na zaffIDEKisiwa cha Zanzibar kina maliasili na mazingira ya Bahari ya Hindi ambayo yanakifanya kuwa mahali ambako ufugaji samaki unawezekana. Shughuli hii, kama itafanyika vyema, itajenga fursa nyingi za kujikimu kimaisha kwa jamii zenye kipato cha chini zinazoishi pwani.

Na Elgin M. Arriesgado

Maendeleo ya Ufugaji Samaki Kijamii kisiwani Zanzibar: Kisa Mkasa kuhusu Miradi ya Ufugaji Samaki inayotekelezwa

kupitia Programu ya Maisha Salama inayokuza upatikanaji wa masoko ya bidhaa zinazoweza kuinua kipato cha Watanzania wenye uwezo mdogo kiuchumi. VSO ilianzisha mikakati kwa ubia na Shirika la Accenture kwa kuchukua hatua za kusaidia kuunganisha kilimo cha mboga na uvuvi, ufugaji samaki na masoko ya sekta ya utalii kupitia mradi unaojulikana kama ZEST (Ujasiriamali na Utalii Endelevu Zanzibar). Kwa kuanzia kabla ya kujishughulisha katika miradi hii, VSO ilifanya utafiti wa tathmini ya soko ili kupata uelewa wa kina wa minyororo ya thamani kwa sekta

ndogo za matunda, mboga, uvuvi na utalii unaozingatia mazingira. VSO ilitoa msaada wa kitaalamu kujenga uwezo wa mashirika na vikundi vya kijamii ili shughuli za uzalishaji na mabadiliko katika kipato yaweze kuongezeka kwa kiwango cha juu. Mwaka 2007, VSO Tanzania kwa kutumia mbinu ijulikanayo kama “Kufanya Masoko Yahudumie Masikini” iliyo chini ya Mradi wa ZEST, ilianzisha mradi wa kunenepesha kaa kwa kutumia mbinu zinazotokana na kazi ya shirika dada la Programu ya VSO Kenya. Jumuiya ya Maendeleo ya Wavuvi na Wakulima Zanzibar (ZAFFIDE) ndio ilikuwa mbia mkuu kisiwani Zanzibar. Mwaka 2009, VSO ilituma mtaalamu wa kujitolea katika asasi ya ZAFFIDE ili atoe ushauri wa shughuli za ufugaji samaki kwa kipindi cha miaka miwili. Lengo la kumuweka mtaalamu huyo ni kuboresha teknolojia za kitamaduni zilizopo kwa sasa pia kuendeleza teknolojia za ufugaji samaki za gharama nafuu ambazo zitaongeza fursa za kipato na kuleta mabadiliko katika maisha ya jamii za pwani zilizo pembezoni. Katika kipindi hiki, VSO ilipanua miradi yake ya ufugaji samaki na kuongeza mbinu za kuongeza thamani ya mazao ya samaki. Mradi pia ulifanya utafiti kushughulikia uendelevu wa mradi wa ufugaji samaki. Walengwa wa mradi huo vilikuwa ni vikundi saba vya kijamii kikiwemo kikundi kimoja kisiwani Pemba, jumla ya wavuvi wadogo 150 na wavuvi wanaume na wanawake wanaotumia ndoano. Mradi ulichagua bidhaa zitokanazo na ufugaji samaki ambazo zinakidhi vigezo vifuatavyo: thamani ya juu, kutoharibika haraka, inakua haraka na uhitaji mkubwa wa soko na zilizo na kutumia teknolojia zinazppatikana kwa urahisi. Bidhaa za ufugaji samaki zilijumuisha kaa wa ufukweni, kamba na samaki. Vikundi vya kijamii vilitumia mifumo miwili ya ufugaji samaki; bwawa kwa ajili ya samaki wanaokua, na vizimba kwa ajili ya kufugia na kunenepeshea kaa. Mradi pia ulifanya utafiti kuhusu tathmini ya idadi

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 25: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 23

ya kaa na kitalu ili kushughulikia suala la uendelevu na matatizo la kupata mbegu za kaa wadogo wa kutosha kuendeleza mradi.Mradi ulitoa mafunzo kwa vikundi vya jamii kuhusu mbinu za msingi za uendeshaji wa mabwawa ya samaki na ufugaji wa kaa, ikiwemo kuchagua eneo, kubuni michoro na kujenga mifumo ya ufugaji, matayarisho ya bwawa/kizimba, ukusanyaji wa mbegu za samaki/kaa wadogo na kuongeza idadi, kusimamia ufugaji.

bWaWa la SamaKiVikundi vitatu vya jamii vilikubali kuanza kutumia teknolojia ya bwawa la samaki, ambavyo ni Kikundi cha Wavuvi wa Makoba, Kikundi cha Wanawake wa Makoba katika kisiwa cha Unguja na Kikundi cha Mwisho Ngumu kisiwani Pemba. Mradi ulishirikiana na Taasisi ya ACRA katika kisiwa cha Zanzibar kwa ajili ya vikundi vya jamii kisiwani Unguja. Mabwawa mawili yalijengwa Unguja na ukarabati wa mabwawa madogo na ujenzi wa bwawa moja kubwa na mfereji wa kuingiza maji ulijengwa Pemba. Kwa ujumla, ukubwa wa mabwawa ulianzia mita za mraba 324 hadi mita za mraba 2500, ikiwa ni jumla ya mita za mraba 8,648 za eneo la uzalishaji. Mradi ulitoa vifaa vya kujengea kama majembe, sululu, mabomba, n.k. kwa vikundi vyote vitatu vya jamii.

uFugaji Wa Kaa Vikundi vinne vya jamii vinajihusisha na unenepeshaji wa kaa, ambavyo ni: Kikundi cha Kaunda Kazi cha Kisakasaka, Kikundi cha Nyamanzi, Kikundi cha Wanawake cha Mwanda SACCOS na Kikundi cha Ushirika wa Tuwesafi cha Mwonguni; vyote vikiwa kisiwani Unguja. Mfanyakazi wa kujitolea wa VSO aliyepita alivichukua vikundi katika ziara ya mafunzo katika Wilaya

ya Tanga kwenda kuona na kujifunza kuhusu unenepeshaji wa kaa. Vikundi vilitumia vizimba 700 vilivyopo kwa ajili ya unenepeshaji wa kaa. Ama walinunua au walikusanya vitoto vya kaa kwa kutumia mitego ya kaa, mishipi yenye chambo, nyavu na fimbo. Vikundi hulisha kaa wao mabaki ya samaki, mabaki ya chakula na vyakula maalumu vilivyotengenezwa na kuwanenepesha kwa kipindi cha siku 15 hadi 45. Kwa kawaida vikundi huuza kaa wao baada ya kufikisha gramu 700 au zaidi. Mradi uliwezesha kuunganisha vikundi vya jamii na hoteli kisiwani Zanzibar kwa ajili ya kupata soko zuri na kipato kizuri kwa bidhaa zao.

uTaFiTiMradi ulifanya utafiti wa kutatua tatizo la kupata kaa wadogo wa kuanzia unenepeshaji kwa ajili ya kuanzishia unenepeshaji. Shughuli mbili kuu za utafiti ambazo mradi ulitekeleza ni pamoja na mbinu za kuanzisha vitalu vya uzalishaji wa kaa kwenye mabwawa uliofanyika Makoba, na utafiti wa idadi ya kaa katika eneo lote la Unguja. Kikundi cha Wavuvi wa Makoba kilishiriki katika utafiti wa miezi mitano kuhusu kitalu cha kaa. Mradi ulifuga kaa wa saizi ndogo kati ya gramu 100 hadi 150 katika mabwawa kwa kipindi cha miezi mitano na kufuatilia ukuaji wao na uhai. Mbinu za Kuongeza Thamani ya Bidhaa Mradi ulitoa mafunzo kwa Kikundi cha Wavuvi wa Makoba kuhusu jinsi ya kutayarisha samaki kwa kuondoa miba ili kujenga ujuzi wao katika usindikaji wa samaki baada ya kuvunwa. Uvunaji wa samaki ulifanyika katika sehemu ya bwawa la zamani na samaki kutayarishwa kwa kuondoa miba. Kuondoa miba kwenye samaki ni mojawapo ya mbinu inayojulikana zaidi ya kuongeza thamani na kuzalisha mnofu wa samaki usio na miba nchini Ufilipino; mbinu hii inaweza kutumika katika mazingira ya Kitanzania.

maToKeoMradi ulitatua tatizo la upatikanaji wa maji katika kikundi cha Pemba baada ya kujengwa kwa mfereji wa kuleta maji na ukarabati wa mabwawa yao. Vikundi vyote vya jamii vilijisikia vimehamasishwa kumiliki mabwawa makubwa yaliyojengwa vizuri na vilipanga kujenga mabwawa mengine zaidi. Lakini uvunaji haukufanyika katika mabwawa yaliyojengwa hivi karibuni kutokana na ucheleweshaji kwenye ujenzi wa mabwawa uliojitokeza wakati wa mvua kubwa na shughuli nyingine za kawaida

Mradi ulichagua bidhaa zitokanazo na ufugaji samaki ambazo zinakidhi vigezo vifuatavyo:

thamani ya juu, kutoharibika haraka,

inakua haraka na uhitaji mkubwa wa

soko na zilizo na kutumia teknolojia

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 26: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

24 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

zilizopewa kipaumbele, pia na upatikanaji wa samaki wachanga kwa wakati huo. Kwa wakati huu, isipokuwa kwa bwawa kubwa lililopo Makoba, mabwawa yote mengine yana samaki wa saizi inayoweza kuvunwa, ambayo ni samaki 3 hadi 4 kwa kilo. Kiwango hiki cha ukuaji wa samaki kinamaanisha kwamba uzalishaji wa samaki katika mabwawa unaweza kumpatia mvuvi kipato cha TZS 1,000 kwa kila mita mraba ya eneo la bwawa. Kikundi kinaweza kuvuna mabwawa yao wakati wowote na uzalishaji halisi utafuatiliwa. Kikundi cha Wavuvi wa Makoba kinakuwa mahali pa mafunzo kisiwani Unguja. Idara ya Rasilimali za Baharini kisiwani Zanzibar ilishukuru kuwepo kwa mradi na kutambua utendaji na mchango wa Kikundi cha Wavuvi wa Makoba. Idara ilielekeza takribani vikundi 35 vya jamii kisiwani Unguja kujifunza mbinu za uendeshaji wa mabwawa ya samaki kutoka kwa Kikundi cha Makoba. Wageni kutoka idara za serikali, wanafunzi na wengineo hutembelea eneo hili. Upatikanaji wa samaki na kaa wachanga ndio kikwazo kikubwa katika uzalishaji wa kaa kwa vile vikundi hivi hutumia saizi moja ya kaa wanaovunwa kwa ajili ya soko. Kikundi cha Mwonguni kinauza kati ya kilo 10 na 40 za kaa kila wiki. Kutokana na faida yao ya mwaka mmoja wameweza kuwekeza katika ununuzi wa mashua na nyavu kwa thamani ya TZS 691,500; na kugawana kati yao TZS 1,210,500; na kuweka akiba benki ya karibu Shilingi 150,000. Wana mpango wa kupanua uzalishaji na kufanya unenepeshaji wa kaa kuwa ndio shughuli yao kuu ya kuwaingizia kipato. Unenepeshaji wa kaa katika Kikundi cha Kisakasaka kinachotumia vizimba 142 kinaweza kukipatia kikundi kipato cha ziada kila mwaka cha TZS 3,000,000, lakini kutokana na uhaba wa kaa wachanga,

Kikundi kilipata faida ya TZS 825,000 tu. Kwa vikundi vya Mwanda na Nyamanzi, uzalishaji wa kaa unapungua kutokana na kutopatikana kwa kaa wachanga ndani ya maeneo yao. Utafiti wa vitalu katika Kikundi cha Makoba umeonyesha kwamba katika kipindi cha miezi mitano, baadhi ya kaa walifikisha uzito wa gramu 500. Matokeo haya yanaonyesha uwezekano wa kufuga kaa wengi wadogo wanaopatikana kwa urahisi katika mabwawa au vizimba na kuwezesha upatikanaji wa kaa wachanga kwa ajili ya shughuli ya unenepeshaji. Matokeo ya utafiti wa idadi ya kaa yanaonyesha kuwepo kwa kaa wa kutosha ambao wana uzito chini ya gramu 200 kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji mdogo wa kibiashara wa vitalu. Kuanza kutumika kwa mbinu za uzalishaji kwenye vitalu kutatatua uhaba wa kaa wachanga unaokabili vikundi vya jamii na kutaongeza uwezo wao wa uzalishaji na kipato katika unenepeshaji wa kaa. Kikundi cha Wavuvi wa Makoba kinaamini kwamba wanaweza kuvipatia vikundi vingine vya jamii ujuzi wao wa kutengeneza mnofu wa samaki usio na miba pale itakapohitajika. Kutegemea uwezo wao wa uzalishaji na mahitaji ya wateja, Kikundi cha Makoba kinaweza wakati wote kutengeneza minofu ya samaki isiyo na miba baada ya mavuno. Mradi ulianzisha utayarishaji wa minofu ya samaki isiyo na miba ili kusaidia vikundi kupata bei nzuri za bidhaa za samaki katika mahoteli, maduka ya bidhaa za nyumbani na waendesha migahawa. Aidha, mbinu za kutengeneza minofu ya samaki isiyo na miba ina uwezekano wa kuhimili misukosuko ya soko inayotarajiwa kutokea wakati uzalishaji wa samaki kwenye mabwawa utakapoongezeka hapo baadaye.

Licha ya kuonyesha matumaini makubwa katika uendelezaji wa ufugaji samaki na fursa nzuri zaidi za kuongeza kipato kwa ufugaji samaki wa jamii kisiwani Zanzibar, uhakika wa uzalishaji bado haujajitokeza. Katika kipindi ambapo mradi ulivipatia vikundi vya jamii msaada wa kitaalamu, inaonekana kwamba sababu zifuatazo zinadumaza uhakika wa uzalishaji:

• Ucheleweshaji wa ujenzi wamabwawa na kuweka samaki/kaa

• Uhabawasamakiwachanga• Gharamakubwazapembejeona

ukarabati hasa kwa jamii ambazo hazina uwezo mkubwa wa kifedha ambapo shilingi mia kadhaa ni pesa nyingi, na zinaweza kutumika katika mahitaji mengine ya msingi

• Kiwango kidogo cha kujitumamiongoni mwa wanachama wa kikundi cha jamii wanaotoa kipaumbele kwa shughuli zinazoingiza kipato cha haraka

• Uwezo finyu wa kitaalamu namatumizi madogo ya teknolojia katika vikundi

• Kutokuwepo kwa maafisa uganiwa kusaidia vikundi

Kwa kuhitimisha, ufugaji samaki wa kijamii kisiwani Zanzibar ulivyo sasa ni kwamba umeenea sehemu nyingi, ni rahisi na ni rafiki wa mazingira. Soko la bidhaa zake kwa sasa sio tatizo. Ongezeko kubwa la uzalishaji na kuongezeka kwa mabwawa kupitia uzalishaji wa kibiashara bado ni mustakabali usiotabirika. Jambo la msingi kabisa katika mafanikio ya uzalishaji na kuzalisha kipato ni dhamira ya jamii kusimamia kwa dhati na kutumia mradi wao uliopo kama ilivyoonyeshwa katika dhamira zao, utendaji, hali ya kijamii na kiuchumi na utamaduni.

JINsIa Na MNyoRoRowa ThaMaNI

Page 27: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 25

Tangu mradi ulipoanza mwezi Oktoba 2011, zaidi ya nusu ya kaya zote zilishiriki katika shughuli za kuamsha ufahamu

kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Wakati shughuli nyingi zikifanyika katika shule ya msingi Chololo zilizohusisha wanafunzi 800, watoto wanajifunza kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Hadi sasa mbinu kumi na nne za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi zimeshafanyiwa majaribio, na tathmini yake itafuata hivi karibuni. Watoto pia wanajifunza jinsi ya kuvuna maji ya mvua na kuanzisha vitalu vya miti. Mavuno mazuri ya mazao, hasa mtama, uwele na alizeti zinazokomaa mapema yanachangia katika uhakika wa chakula kwa mamia ya kaya za wakulima na kuongeza kipato cha kaya kwa zaidi ya wakulima 100, wakati wafugaji wa kuku 123, wengi wao wanawake, wanaanza kuona matunda ya kutumia mbegu bora za kuku na ufugaji bora. Ulipozinduliwa Oktoba 2011, mradi wa Chololo Kijiji Endelevu ulibidi ufanye kazi haraka kuwatayarisha wakulima kwa msimu wa kupanda mazao, ambao kwa kawaida huanza Desemba. Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, mvua sasa hazitabiriki kama ilivyokuwa huko nyuma. Msimu wa mvua wa mwaka 2011/12 ulikuwa na siku 42 za ukame ambao uliharibu baadhi ya mazao, hasa mahindi. Kwa sababu hii, mradi uliweka msisitizo katika ubunifu wa kilimo ambao ulitumia kikamilifu mvua iliyopo. Baadhi ya hatua zilizochukuliwa zilijumuisha kujenga uwezo wa wakulima 400 kupitia mafunzo ya kina kuhusu kilimo

Mtandao wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM) ni sehemu ya timu ya mashirika sita yanayofanya kazi kuleta mageuzi ya kijiji cha Chololo, kilichopo karibu na Dodoma, na kukifanya kuwa Kijiji Endelevu. Mradi unasaidia na kuwezesha jamii kujaribu, kufanya tathmini na kutumia mbinu mpya bunifu katika sekta za kilimo, mifugo, maji, nishati, na misitu.

Na Michael Farrelly, Mratibu wa Programu, TOAM

Kijiji Endelevu Chololo: mfano wa utendaji mzuri katika kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi

bora. Walijifunza utifuaji na utayarishaji wa shamba, kupanda kwa nafasi, kilimo mseto, hifadhi ya unyevunyevu wa udongo na uzalishaji wa mbegu bora zilizothibitishwa. Mradi pia ulianzisha na kuwapatia wakulima zana 24 za utifuaji zinazokokotwa na maksai, ambazo ni chimbuo aina ya Magoye, jembe la kupalilia, jembe la matuta na plau. Wakulima 80 walipata mafunzo ya jinsi ya kutumia zana hizi. Jembe la Kuchimbua aina ya Magoye huvunjavunja ardhi iliyokuwa ngumu, na kuruhusu maji ya mvua kupenya ardhini. Mradi pia ulianzisha na kuwapatia wakulima mbegu bora zinazohimili ukame, zinazotoa mavuno mengi na kupevuka mapema. Wakulima 100 walipata mbegu za mtama, 190 (mbegu za uwele), 122 (mbegu bora za kunde), 8 (karanga) na 112 (mbegu bora za alizeti). Uchaguzi na uchambuzi wa kisekta ulifanyika kwa lengo la kuainisha shughuli za uzalishaji mali ambazo

zitawanufaisha wanawake zaidi. Zaidi ya wakulima 190 walihusika. Matumizi ya mbinu bora za kilimo yamesababisha matokeo yanayoleta matumaini hasa katika uhakika wa chakula. Mbegu bora za mtama, uwele, kunde na alizeti zimefanya vizuri na uhakika wa chakula kwa familia umeongezeka. Kwa upande mwingine, ufugaji bora kabla ya mradi haukuwa rahisi. Uharibifu

Kilimo bora ni pamoja na kupanda kwa nafasi sahihi, kilimo mseto, hifadhi ya maji ardhini na uzalishaji wa mbegu

Jembe la kukokotwa na maksai aina ya Magoye ikitifua arshi ngumu, kuruhusu mvua kurutubisha udongo

MabaDIlIko ya TabIa NchINI

Pich

a : K

erry

Far

relly

Pich

a : M

icha

el F

arre

lly

Page 28: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

26 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

wa ardhi ya malisho na uharibifu wa mazao ulihusishwa na ufugaji. Baada ya kuanzishwa kwa mradi, ufugaji uliboreshwa na sasa kuna mwingiliano chanya baina ya mifugo na kilimo. Maksai hutumika kwa ajili ya utayarishaji wa shamba na kupanda. Mifugo huzalisha mbolea ya shambani ambayo ni rahisi kutumia. Miongoni mwa vitu vingine ambavyo mradi unataka kuvishughulikia ni pamoja na kuanzisha mbegu bora za ng’ombe, mbuzi na kuku. Wakulima 118 miongoni mwao wanawake 54 walipata mafunzo ya ufugaji bora. Mradi ulitoa madume bora 30 aina ya Mpwapwa, beberu 60 na majogoo bora 123. Mradi pia ulitoa dawa za kuogeshea kwa ajili ya kudhibiti kupe na madawa mengine ya mifugo. Mradi pia ulianzisha eka tano za malisho bora na eka tano kwa ajili ya mbuzi na kondoo. Ufugaji samaki ulianzishwa Chololo Kijiji Endelevu. Mradi ulianzisha mabwawa mawili madogo ya perege. Hata hivyo, mradi unakabiliwa na uhaba wa maji. Mradi ulipoanza Oktoba 2011, kulikuwa hakuna chanzo cha maji safi ya kunywa kijijini. Iliwabidi wanawake kutembea kwa masaa mawili kila siku kuchota maji kutoka kijiji jirani. Mvua haikusaidia katika upatikanaji wa maji, badala yake ilitengeneza makorongo na kusababisha mmomonyoko wa udongo. Mradi ulianza kuvuna maji ya mvua kwa kuweka vikingio katika paa za shule ya msingi ya kijiji. Zaidi ya lita 60,000 za maji huvunwa na kuhifadhiwa katika matangi chini ya ardhi. Mbinu nyingine ni pamoja na ujenzi wa lambo litakalokusanya maelfu ya lita za maji kutoka mto jirani. Juhudi hizi zimewapatia wananchi maji kwa matumizi

mfano, hutembea masaa matano kutafuta kuni kutoka msituni. Mradi unalenga katika kukuza upandaji miti na kuwezesha mipango na usimamizi wa matumizi ya ardhi kwa jamii. Pia utahimiza matumizi ya vyanzo mbadala vya nishati. Kwa kuzingatia uboreshaji wa usimamizi wa maliasili, mradi umetoa mafunzo kwa wanajamii pamoja na viongozi 133 kuhusu kupandikiza misitu, usimamizi wa vitalu na upandaji miti. Kutokana na mafunzo haya, miche ya miti 14,668 ilipandwa ikiwemo leusina, migunga, miarobaini, miembe na mipera. Miti mingine 3,000 ilipandwa katika eka tatu za hifadhi ya msitu wa kijiji. Wakazi wanasaidia kuchukua, kujaribisha, kutathmini teknolojia mbalimbali za nishati jadidifu, ikiwemo majiko yanayookoa nishati na mitambo ya bei nafuu ya gesi itokanayo na kinyesi cha ng’ombe (bio-gesi). Matumizi ya majiko yanayookoa nishati yatapunguza kiasi cha kuni kinachohitajika na kupunguza ukataji miti, wakati huo ikipunguza muda na nguvu wanazotumia wanawake. Mitambo ya Bio-gesi hubadili kinyesi na kuwa gesi inayoweza kutumika kuwasha jiko na taa. Baadhi ya mafanikio ya mradi katika eneo la nishati asilia yanajumuisha kuanzishwa kwa mitambo 10 ya bio-gesi inayotoa nishati kwa kupikia na kuwashia taa, na kufungwa kwa majiko 60 ya kupikia yanayookoa nishati katika kaya 60. Mradi wa Chololo Kijiji Endelevu unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na hutekelezwa kwa ubia unaohusisha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Hombolo (ARIH), Mtandao wa Mazingira Dodoma (DONET), Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma (DMC), Maji na Maendeleo Dodoma (MAMADO) na Mtandao wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM).

Mradi unalenga katika kukuza upandaji

miti na kuwezesha mipango na usimamizi

wa matumizi ya ardhi kwa jamii. pia

utahimiza matumizi ya vyanzo mbadala vya

nishati.

Mwanamke akipika kwa kutumia jiko bora linalotumia kuni kidogo

ya nyumbani na mifugo kwa kipindi chote cha kiangazi. Mradi wa Chololo Kijiji Endelevu pia kinafanya kazi katika uendelezaji wa maliasili na nishati kutatua mahitaji ya jinsia. Wanawake kwa

Pich

a : M

icha

el F

arre

lly

Pich

a : M

icha

el F

arre

lly

MabaDIlIko ya TabIa NchINI

Page 29: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013 27

ufugaji wa kuku unatoa mchango muhimu katika

kuboresha kipato cha kaya na lishe. ufugaji wa kuku wa kienyeji unaanza kuangaliwa

kwa karibu zaidi na mashirika ya maendeleo na

wafanya biashara.

Mradi wa Kuendeleza Masoko ya Vijijini (RMDI) unaliona suala la kukosekana kwa uwiano mzuri katika ubora na wingi

wa uzalishaji na mahitaji kuwa ndio sababu kuu ya kuwepo kwa pengo la habari na kutoaminiana baina ya wazalishaji wa kijijini kwa upande mmoja, na wafanyabiashara kwa upande mwingine. Kwa hiyo mradi wa RMDI unatarajia kutoa mchango mkubwa katika kupunguza umasikini kwenye maeneo ya vijijini kwa kuendeleza mifumo ya masoko ili kuongeza kipato na ajira. Kufuatia kuamini hivyo, Mradi wa Kuendeleza Masoko ya Vijijini kwa kuingia ubia na Kampuni ya Kuendeleza Kipato ya Vijijini, imesaidia uboreshaji wa uzalishaji na masoko ya kuku wa kienyeji Kondoa, na kuwafikia wafugaji na wafanyabiashara 900 ambao walijengewa uwezo mwaka 2011. Ijapokuwa shughuli kuu ya kiuchumi katika maeneo ya vijijini Tanzania ni kilimo, na ukichukulia ukame mkubwa unaotokea mara kwa mara na kuathiri uzalishaji wa mazao, ufugaji wa kuku vijijini umekuwa sehemu muhimu ya uchumi wa vijijini kwa Tanzania. Ufugaji wa kuku unatoa mchango muhimu katika kuboresha kipato cha kaya na lishe. Ufugaji wa kuku wa kienyeji unaanza kuangaliwa kwa karibu zaidi na mashirika ya maendeleo na wafanya biashara.

Mradi wa Kuendeleza Masoko

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo imekadiria kwa mwaka 2002/2003 kwamba kuna kuku takribani 34,827,675 nchini. Katika idadi hii, takribani 32,559,208 ni kuku wanaofugwa kienyeji ambao kwa sehemu kubwa hufugwa maeneo ya vijijini. Kuku wa kisasa ni pamoja na kuku wa nyama 589,563 na wa mayai 1,222,267 ambao hugugwa na wakulima wadogo; na jumla ya kuku 456,638 (wa nyama na mayai) wanaofugwa katika

mashamba makubwa. Mradi wa Kuendeleza Masoko ya Vijijini ulipewa jukumu la kuboresha uzalishaji na masoko ya kuku wa kienyeji katika wilaya ya Kondoa, na hivyo ulifanya utafiti wa awali wa takwimu muhimu ambao ulionyesha kwamba licha ya kuku wa kienyeji kuwepo katika karibu kila kaya katika maeneo yaliyochunguzwa, mchango wao katika uboreshaji wa kaya na chumi za vijijini ni mdogo sana kutokana na

Bi Khadija Madina akilisha kuku wake.

Pich

a : I

brah

im K

isun

gwe

Vijijini (RMDI) - Mradi wa kukuNa Ibrahim Kisungwe na Cliff Malemi

bIashaRaya kIlIMo

Idad

i ya

wah

ojiw

a

Mifugo inayofugwa na kaya nyingi

Ng’ombe naMbuzi

Ng’ombe Kuku Mbuzi Kondoo Wasiofuga kitu

30

20

10

0

Page 30: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

28 ULIMWENGU WA MKULIMA januarI 2013

tija ndogo na mifumo duni ya usimamizi. Utagaji mbovu, kiwango duni cha ukuaji, magonjwa, wanyama wakali na kukosekana na Masoko yaliyoandaliwa vyema ni baadhi ya vikwazo vikuu katika uzalishaji wa kuku kwa wakulima wadogo. Kielelezo hapa chini kinaonyesha wastani wa mifugo inayofugwa katika wilaya ya Kondoa. KiliChoFanyiKa KuboReSha uZaliShaji Wa KuKu Wa Kienyeji Kuanzia Agosti 2011 hadi Januari 2012, mradi wa RMDI ulitekeleza kwa mafanikio makubwa mradi wa kugeuza uzalishaji na masoko ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kuwa wa kibiashara katika wilaya ya Kondoa, mkoa wa Dodoma kwa kufuata modeli ya Bangladesh. Njia bora zaidi ya kushughulikia masuala ya tija duni na mifumo mibovu ya usimamizi ilionekana kuwa ni kuboresha uzalishaji wa kuku wa kienyeji kwa kuanzisha mfumo wa usimamizi ulio mzuri zaidi kwa kuku wa kienyeji. Mafunzo ya kujenga uwezo yalitolewa ili kubadili mfumo wa kuku kujiokotea wenyewe hadi mfumo ambao aina fulani ya matunzo yanatolewa kwa kuku. Modeli hii ilihusisha ujenzi wa mabanda ya kuku, kuanzisha chakula cha ziada, uchanjaji na kutumia madawa ili kuzuia na kutibu magonjwa. Modeli pia ilijumuisha ukuzaji wa vifaranga ili kuongeza idadi ya kuku haraka na kujenga mtandao na wafaya biashara ili kufungua fursa za masoko mapya. Wafugaji wa kuku wa kienyeji pia walisaidiwa kuendesha vyama vya kuweka na kukopa ili kuongeza uwezo wa

mitaji yao kwa mzunguko. maFunZo ya uFugaji boRa Wa KuKu Wa Kienyeji KWa WaKulima Wa Kijiji Cha jenjeluSe KaTiKa Wilaya ya KonDoaBaada ya kukamilika kwa programu ya kujenga uwezo, vikundi vilianza kutumia maarifa mapya vizuri sana. Tabia ya wanachama wa vikundi ilibadilika sana. Wastani wa watu 60 walijiunga katika vijiji 15 vilivyochaguliwa awali walijiunga na vikundi vya ufugaji wa kuku. Kupitia vikundi hivi, ilikuwa rahisi kwa mradi wa RMDI kusambaza maarifa na ujuzi. Vikundi viliundwa kulingana na aina ya kuku watu binafsi wanaotaka kufuga. Kulikuwa na vikundi vya wazalishaji wa kuku mama/baba, wachanganya chakula, watoa huduma za afya kwa kuku, wafanya biashara pia na vyama vya kuweka na kukopa. Kila kikundi kilipata mafunzo maalumu ambayo yanalingana na shughuli zao na jinsi ya kusaidia wanachama wengine wa vikundi waliobaki. Mbinu hii ilichangia kuongezeka kwa idadi ya kuku kutoka wastani wa kuku 5-20 wastani wa kuku 50-200 kwa kaya. Kupitia vikundi vya wafanya biashara ya kuku, maeneo ya mauzo ya kuku yalianzishwa na masoko ya mjini yalifikika kwa urahisi.

haDiThi ya maFaniKio ya bi. KhaDija maDinaMwisho wa mradi uliacha matokeo mengi chanya katika maeneo mbalimbali. Bi. Khadija Madina wa kijiji cha Gwandi alihadithia

kwamba kabla ya mradi wa RMDI kwenda kwenye kijiji chake hakufikiria kwamba kuku wanaweza kuwa biashara yenye faida. Magonjwa yalikuwa yanaua kuku wote kwa vile hawakuwa na maarifa ya kudhibiti magonjwa. “Sikudhania kwamba siku moja kuku wangeweza kuwa shughuli yangu kuu ya kiuchumi.” Khadija alikuwa na zaidi ya kuku 200. Aprili 2012 alipata TZS 630,000 kutokana na kuku 90 aliowauza. Kipato hiki kilizidi mapato yote aliyopata kutokana na alizeti katika msimu wa 2010-2011. Kwa sababu kuku wa kienyeji wanafugwa na kaya nyingi za vijijini, kupunguza umasikini kupitia uboreshaji wa uzalishaji na masoko kunaweza kufanikiwa kwa urahisi zaidi. Uhitaji wa “kuku asilia” unaongezeka katika miji, ambako kunahitaji uzalishaji uongezeke.

Mbinu hii ilichangia kuongezeka kwa

idadi ya kuku kutoka wastani wa kuku 5-20 wastani

wa kuku 50-200 kwa kaya.

Mafunzo ya ufugaji bora wa kuku wa kienyeji katika Kijiji cha Jenjeluse, Kondoa.

Pich

a : I

brah

im K

isun

gwe

bIashaRaya kIlIMo

Page 31: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

foMu ya MaoNI

je unapenDa KupaTa habaRi ZaiDi au una maoni unayoTaKa KuShiRiKiana na Wengine?

TaFaDhali jaZa Fomu hapa Chini

Ningependa kufahamu kuhusu maeneo yafuatayo, tafadhali nitumie habari zaidi zinazohusu maeneo haya:

Bajeti na Sera Mabadiliko ya tabia nchini

Jinsia na Mnyororo wa thamani Biashara ya Kilimo

Ningependa kupata nakala nyingi zaidi za jarida. Tafadhali nitumie nakala____________.

Ni somo/mada zipi nyingine ambazo ungependa ANSAF itayarishe katika matoleo yajayo na Jarida?

1 _______________________________________________________________________________________________________

2 _______________________________________________________________________________________________________

3 _______________________________________________________________________________________________________

Jina na Anuani: ___________________________________________________________________________________________

________________________________________________________________________________________________________

Namba ya Simu: _____________________________________________ Nukushi:_____________________________________

Maoni: __________________________________________________________________________________________________

________________________________________________________________________________________________________

________________________________________________________________________________________________________

________________________________________________________________________________________________________

je, ungepenDa KupaTa habaRi KuhuSu anSaF?

Ndiyo, ningependa kupata habari kuhusu ANSAF.

Ningependa kuwa mwanachama wa ANSAF.

Ningependa kuingizwa katika orodha ya wanaotumiwa jarida na habari.

Mawasiliano na anuani yangu ni:

Jina na Anuani: S.L.P: ______________________________________________________________________________________

Mji/Jiji: _________________________________________________________________________________________________

Namba ya Simu: ___________________________________________ Barua pepe: ____________________________________

Tafadhali tembelea tovuti yetu: www.facebook.com ili uweze kupata fomu hii, au tembelea mtandao wa jamii wa facebook: www.facebook.com/ANSAFForum ili kututumia maoni yako.

Ahsante kwa kutumia muda wako kutoa mrejesho.

Tafadhali tuma kwa posta katika anuani ifuatayo:

agRiCulTuRal non STaTe aCToRS FoRum,S.l.p 33562,barabara ya Senga, Kiwanja 566, mikocheni bDar es Salaam, Tanzania

Page 32: MINYORORO YA THAMANI - ansaf.or.tzansaf.or.tz/dev/wp-content/uploads/2015/05/Farmers-Magazine-KISWAHILI... · wa moyo mkunjufu tunakukaribisha katika toleo la pili la Jarida letu

AGRIcULTURAL NON STATe AcTORS FORUM (ANSAF) S.L.P 33562, Kiwanja 566, Barabara ya Senga, Mikocheni A. Dar es Salaam,

Simu: + 255 22 2771566 / 2775970 Nukushi: + 255 22 2773217Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.ansaf.or.tz

Tangaza biashara na huduma mbali mbali za kilimo kupitia kwetu!

Tumedhamiria kukuza mifumo ya kilimo yenye tija kwa maskini