11
 MUHTAHSARI WA MIAKA 53 YA MAFANIKIO YA KUJIVUNIA

Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

Citation preview

Page 1: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 1/11

 

MUHTAHSARI WA MIAKA 53 YA

MAFANIKIO YA KUJIVUNIA

Page 2: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 2/11

AWAMU YA KWANZA

Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMwalimu Julius Nyerere

Page 3: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 3/11

 

Mafanikio ya Kijamii:

  Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitatu ya Kwanza ulianzisha

shule za msingi, sekondari na ufundi ili kuandaa wataalam wa kusimamia

masuala ya utawala wa Tanganyika mpya.   Uanzishwaji wa Elimu ya Watu Wazima mwaka 1972. 

Mafanikio ya Kisiasa:

  Kuunda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania mwaka 1964. 

  Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano 1964 - 1969. 

  Azimio la Arusha 1967 lililojenga misingi ya usawa na maadili ya uongozi

katika nchi inayoamini katika siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. 

  Mpango wa Maendeleo wa miaka 15 (1964 - 1980) na Mpango wa Pili wa

Maendeleo (1969 - 1974) na Mpango wa Tatu wa Maendeleo (1975 - 1980).   Azimio la Arusha lilipelekea nchi yetu kupata nchi marafiki kama vile China,

Urusi na Cuba, na matokeo ya uhusiano huo ni misaada, kwa mfano Reli ya

 TAZARA. 

  Mwongozo wa TANU mwaka 1971 ulirekebisha maadili ya uongozi. 

  Uanzishaji Kikosi cha Kuzuwia Rushwa mwaka 1975 

  Muungano wa kipekee barani Afrika kati ya TANU na ASP kuunda CCM

mwaka 1977. Muungano huu wa vyama hivi viwili ulisaidia kuwaweka

karibu zaidi watu wa Bara na Visiwani ambao awali waliunganishwa na

Muungano wa mwaka 1964. 

  Mwaka huohuo 1977 Katiba ya Jamhuri ya Muungano iliandikwa na

kutangaza Tanzania kuwa nchi inayofuata siasa ya Ujamaa na yenye chama

Kimoja CCM. Katiba hiyo iliainisha mihimili mitatu ya Dola: Utawala, Bunge

na Mahakama. 

  Kushiriki mapambano ya ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika. 

  Kulinda mipaka kikamilifu kwa kushinda Vita ya Kagera mwaka 1979. 

  Sheria ya Uhujumu Uchumi ilitungwa mwaka 1984 kuwabana wanyonyaji

na wahujumu wa uchumi wa Taifa, na baadaye kubadilisha kuwa Sheria ya

Makosa ya Uhujumu Uchumi. 

  Marekebisho ya Katiba ya mwaka 1977 yaliyofanyika mwaka 1984. 

  Mwalimu Nyerere ang'atuka kwa hiari yake mwenyewe. 

 

Kuanzisha utaratibu wa rais kuongoza kipindi kisichozidi miaka 10 katikawamu mbili za miaka mitano mitano. 

   Tanzania kama kiongozi wa mapambano dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa

rangi barani Afrika na ilikuwa kiongozi wa Kamati ya Ukombozi Kunisi mwa

Bara la Afrika na ilisaidia harakati za uhuru nchini Msumbiji, Angola,

Namibia, Botswana, Zimbabwe na Afrika Kusini. 

Mafaniko ya Kiuchumi:

  Mipango mbalimbali ya Maendeleo kama ilivyobainishwa hapo juu. 

 

Uwekezaji katika elimu ili kuandaa wataalamu wa kutumikia taifa. 

Page 4: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 4/11

  Uanzishwaji Vijiji vya Ujamaa mwaka 1975vilivyowezesha kuwakusanya

wananchi kushi na kufanya kazi pamoja na kuharakisha upatikanaji wa

huduma na kuongez uzalishaji mali.

  Matamko mbalimbali kama vile Kilimo cha Kufa na Kupona na Siasa ni

Kilimo kuhamasisha ushiriki na usimizi wa kilimo. 

 

Uanzishwaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea kusaidia na kujenga uwezowa familia masikini. 

Siasa za Kimataifa:

  Msimamo imara uliopelekea Tanzania kuwa miongoni mwa vinara wa Nchi

Zisizofungamana na Upande Wowote. 

  Uenyekiti wa South-South Commission. 

  Kushiriki na kuchangia ripoti muhimu ya Challenge to the South mwaka

1980. Matokeo ya ripoti hiyo yalipelekea nchi zilizoendelea kukubali

kuundwa kwa Kituo cha Kudumu cha Ushirikiano kwa Nchi za Kusini

(South South Centre) mwaka 1995.   Ziara mbalimbali za viongozi wa kimataifa. 

  Mwalimu Nyerere kama mwanasiasa anayeheshimika kimataifa, suala

lililoifanya Tanzania pia kuheshimika kimataifa. 

Page 5: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 5/11

 

AWAMU YA PILI

Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi

Page 6: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 6/11

 

Mafaniko ya Kijamii:

  Kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa katika Awamu ya Kwanza. 

  Kumudu vuguvugu kubwa la mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi duaniani. 

 

Uboreshwaji wa sekta za afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara,

umeme, nk ili kukabiliana na changamoto zilizokuwepo muda huo. 

  Kuboresha na kudumisha ushirikiano na nchi za SADC, Afrika, Ulaya, Asia

na Amerika. 

  Ziara ya Mandela na Baba Mtakatifu Yohana Paulo wa Pili, kama uthibitisho

wa uhusiano mzuri na nchi za nje. 

  Ukurasa mpya wa mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Malawi kufuatia

Rais Bakili Mulizi kuingia madarakani. 

Mafanikio ya Kisiasa:

 

Mabadiliko makubwa ya Kikatiba mwaka 1992 kuruhusu mfumo wa siasaza vyama vingi vya siasa. 

  Kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi,

mwaka 1995. 

  Kutungwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Namba 13, mwaka

1995 ambapo Sekretari ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa. 

Mafanikio ya Kiuchumi:

  Kuendeleza kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wa nchi. 

 

Mageuzi ya kiuchumi mwaka 1986 yaliyobadilisha mifumo na mipango yakiuchumi kujielekeza kwenye mfumo wa soko huria. 

  Kufungua milango ya biashara na kukaribisha wawekezaji wa ndani na nje. 

  Kutungwa sera ya Ubinafsidhaji wa Mashirika ya Umma mwaka 1992. 

  Ujenzi wa miundombinu ya barabara kuu na vijijini, chini ya mradi

kabambe wa barabara, Integrated Road Project

  .Kuanzisha mchakato wa kufufa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Page 7: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 7/11

 

AWAMU YA TATU

Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa

Page 8: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 8/11

Mafanikio ya Kijamii:

  Kuendeleza falsafa za Awamu ya Kwanza na mageuzi ya kisiasa na uchumi

 yaliyoanzishwa na Awamu ya Pili. 

  Uanzishwaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na

Mapngo wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) ili kuboresha elimu ya msingi na sekondari. Mpinago hiyo ilipelekea ongezeko la idadi ya shule

na wahitimu. 

  Utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kama vile Mradi wa Maji

Kahama-Shinyanga kutoka chanzo cha maji cha Ziwa Victoria, na Mradi wa

Maji wa Chalinze. 

  Ujenzi wa mtandao mkubwa wa barabara kwa kiwango cha lami. 

  Ujenzi wa daraja katika Mto Rufiji (Daraja la Mkapa). 

  Uanzishwaji wa Mamlaka ya Barabara (TANROADS). 

  Ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo (Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es

Salaam). 

 

Kuendeleza mahusiano mazuri na nchi nyingine duniani, mafanikio ni

pamoja na ziara ya Rais wa 42 wa Marekani Bill Clinton mwaka 2000,

ambapo pamoja na masuala mengine, Mkataba wa Masuala ya Anga kati ya

 Tanzania na Marekani ulisainiwa. 

Mafanikio ya Kisiasa:

  Kuendelea kujenga taifa kwa misngi ya utawala bora na uadilifu. 

  Kuundwa Tume ya Rais ya kuchunguza Kero za Rushwa mwaka 1996,

ambayo ripoti yake ilipelekea Serikali kuandaa Makakati wa Kitaifa Dhidi ya

Rushwa na Mapngo wa Utekelezaji kwa lengo la kuziba mianya ya rushwa. 

 

Kuandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Utawala Bora mwana 1999.   Kutunga Sheria ya Kuanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

mwaka 2001. 

  Mchango mkubwa katika jitihada za usuluhishi wa migogoro kimataifa, kwa

mfano DRC, Burundi na Rwanda 

Mafanikio ya Kiuchumi:

  Kuendeleza na kuboresha uchumi. 

  Ubinafsishaji wa mashirika ya umma, hususan yaliyokuwa yakiendeshwa

kwa hasara. 

 

Kuimarisha miundombinu kulingana na mageuzi ya kiuchumi.   Maandalizi na zunduzi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 iliyotoa

mwelekeo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyozinduliwa mwaka 1999. 

  Kutungwa Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma mwaka 2001 

  Kutungwa Sheria ya Manuniz ya Umma mwaka 2001 iliyopelekea kuundwa

kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma mwaka 2004. 

  Uanzishwaji wa programu mbalimbali za maboresho kwa ajili ya kuimarisha

utawala bora. 

  Kuanzisha miradi na mipango mbalimbali ya kuendeleza uchumi wa taifa,

kwa mfano MKURABITA na TASAF. 

Page 9: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 9/11

AWAMU YA NNE:

Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete

Page 10: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 10/11

Mafanikio ya Kijamii:

  Kupanua na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa na uhuru wa

kutoa maoni. 

  Upanuzi wa sekta ya elimu kuanzia ya msingi, sekondari kila kata, vyuo na

vyo vikuu.   Ongezeko kubwa la shule la sekondari za serikali na za binafsi. 

  Ongezeko la vyuo na vyuo vikuu, kwa mfano Chuo Kikuu cha Dodoma,

kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na Kati. 

  Ongezeko la zahanati, vituo vya afya na upanuzi wa hospitali za rufaa na

mikoa, sambamba na mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya afya.  

  Maendeleo katika sekta ya maji, kwa mfano kukamilisha mradi wa maji wa

Kahama-Shinyanga ulioanza kutekelezwa katika Awamu ya Tatu. 

  Uhusiano mzuri na nchi za nje, uliopelekea ziara za viongozi wa mataifa

makubwa duniani, Rais Obama wa Marekani, na mtangulizi wake Rais

George W. Bush na Rais Hu Jintao wa China. 

 

Kupitisha Sheria ya Kuzuwia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya

mwaka 2007 iliyoipa TAKUKURU Mamlaka zaidi ya kushughulikia makosa

 ya rushwa. Taasisi hiyo sasa ina Ofisi kila wilaya. 

  Sheria ya Kuanzisha Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa ilipitisha mwaka

2008. 

  Kuweka kipaumbele katika kuendeleza na kuimarisha michezo. 

  Kutoa uhuru mpana zaidi kwa vyombo vya habari. 

Mafanikio ya Kisiasa:

 

Kufungua milango ya uhuru zaidi kwa lengo la kupanua demokrasia.   Kuridhia na kuingia katika utaratibu uliowekwa na Umoja wa Afika, wa

kujitathmini katika nyanja za Utawala Bora, Kupambana na Rushwa na

Utawala Bora, mwaka 2009. 

  Kuongeza idadi ya wanawake kwenye nafasi za juu za uongozi, na

kuwezesha wanawake wengi kuteuliwa akiwemo Dkt Asha-Rose Migiro

aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2006. 

  Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 uliokuwa wa huru na haki. 

  Kupitisha Sheria ya Gharama za Uchaguzi Namba 6, mwaka 2010. 

  Kupanua muundo wa Mahakama na kuongeza idadi ya majaji, kuwajengea

uwezo na kuwapatia vitendea kazi. 

  Kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kati ya CCM na CUF huko Zanzibar

baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, na kumaliza mgogoro wa kisiasa

Visiwani humo uliodumu kwa muda mrefu. 

  Kuweka historia kwa kumteua mwanasiasa wa chama cha upinzani, James

Mbatia, kutoka NCCR- Mageuzi, kuwa mmoja wa wabunge 10 wanaoteuliwa

na Rais. 

Mafanikio ya Kiuchumi:

   Jitihada za kuendeleza programu za maboresho katika nyanja za uchumi. 

  Vipaumbele katika kuendeleza sekta za kilimo na ujenzi wa miundombinu

 ya barabara kuu na za mikoa, mambo yaliyobainishwa katika Mkakati waKupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi Tanzania (MKUKUTA II). 

Page 11: Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

7/17/2019 Muhtasari Wa Miaka 53 Ya Mafanikio Ya Kujivunia

http://slidepdf.com/reader/full/muhtasari-wa-miaka-53-ya-mafanikio-ya-kujivunia 11/11

  Kufanya mapitio ya Dira ya Maendeleo ya Taifa mwaka 2025. 

  Kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano, mwaka 2011, ili

kuimarisha na kuendeleza shughuli zinazochangia kukuza uchumi na

kuwezesha taifa kufikia hadhi ya nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka

2025. 

 

Kupitia Sera ya madini ili kuliongezea taifa mapato kutoka katika sekta yamadini. 

  Dhana ya Kilimo Kwanza ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na

biashara. 

  Kuwapatia wakulima pembejeo na kuwapeleka wataalam wa ugani kwa

wakulima ili kusaidia maendeleo ya kilimo. 

  Kuweka msisitizo katika utunzaji na matumizi ya maliasili za kitaifa. 

  Kuweka umuhimu katika utunzaji mazingira, sambamba na kuimarisha

utunzaji na usimamizi wa vyanzo vya maji. 

  Kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, wa kikanda na wa kimataifa. 

 

Rais Jakaya Kikwete alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrikamwaka 2008. Akiwa Mwenyekiti wa Umoja huo, Rais Kikwete alishughulikia

matatizo makubwa ya kisiasa, kama vile mgogoro wa uchaguzi nchin

Kenya, matatizo ya kisiasa nchini Somali, Sudan, Chad, Comoro na Jamhuri

 ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo. 

  Rais Kikwete alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Tume Maalum ya

Afrika. 

  Mchango mkubwa wa Rais Kikwete katika mijadala mbalimbali ya kimataifa. 

  Kufuta Sheria ya Kuzuwia Rushwa, Namba 16, ya mwaka 1971 na k

utungwa Sheria ya Kuzuwia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya

mwaka 2007, iliyoongoza makosa ya rushwa kutoka manne hadi 24.