29
1 MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA WENYEVITI WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BARAZA LA WAWAKILISHI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016 Mheshimiwa Spika, Kwanza naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutukutanisha tena hapa tukiwa wazima wenye afya njema, katika kipindi hiki muhimu cha kujadili Bajeti kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Bajet hii itakua na Umuhimu mkubwa kwani itakuwa ni Bajeti ya mwisho katika uhai wa Baraza hili la Nane ambalo wewe Mheshimiwa Spika kwa kushirikiana na wasaidizi wako mmeliongoza kwa ufanisi mkubwa tokea lilipozinduliwa mnamo mwezi Novemba 2010. Mheshimiwa Spika, Makadirio haya ya Bajeti yaliyowasilishwa na Mhe Waziri wa Mipango na Waziri wa Fedha juzi siku ya Jumatano ya tarehe 13/05/2015, hivi sasa wananchi kwa hamu kubwa wanataka kujuwa yanawagusa kwa kiasi gani, kwa kuwa bajeti siku zote huwa ni suala la wananchi na maisha yao moja kwa moja yanaguswa na mipango inayohusu mahitaji ya jamii kama vile kilimo, afya, elimu, miundombinu n.k wananchi watataka pia kujuwa bajeti yao hii imezingatia kiasi gani vipaumbele katika maendeleo ya nchi.

MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

1

MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA WENYEVITI WA

KAMATI ZA KUDUMU ZA BARAZA LA WAWAKILISHI KUHUSU MAKADIRIO YA

MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA

2015/2016

Mheshimiwa Spika,

Kwanza naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutukutanisha tena

hapa tukiwa wazima wenye afya njema, katika kipindi hiki muhimu cha kujadili Bajeti

kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Bajet hii

itakua na Umuhimu mkubwa kwani itakuwa ni Bajeti ya mwisho katika uhai wa Baraza

hili la Nane ambalo wewe Mheshimiwa Spika kwa kushirikiana na wasaidizi wako

mmeliongoza kwa ufanisi mkubwa tokea lilipozinduliwa mnamo mwezi Novemba 2010.

Mheshimiwa Spika,

Makadirio haya ya Bajeti yaliyowasilishwa na Mhe Waziri wa Mipango na Waziri wa

Fedha juzi siku ya Jumatano ya tarehe 13/05/2015, hivi sasa wananchi kwa hamu kubwa

wanataka kujuwa yanawagusa kwa kiasi gani, kwa kuwa bajeti siku zote huwa ni suala la

wananchi na maisha yao moja kwa moja yanaguswa na mipango inayohusu mahitaji ya

jamii kama vile kilimo, afya, elimu, miundombinu n.k wananchi watataka pia kujuwa

bajeti yao hii imezingatia kiasi gani vipaumbele katika maendeleo ya nchi.

Page 2: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

2

Mheshimiwa Spika,

Serikali yoyote duniani lazima iwe na malengo yake na mipango yake sisi kama wajumbe

kuanzia leo hii tutapata nafasi ya kuyachambua malengo na mipango ya Serikali yetu ili

kuweza kuishauri vizuri Serikali yetu kwa faida ya Nchi yetu na Wananchi wetu. Katiba

yetu ya Mwaka 1984 imeweka msingi huo wa lengo kuu la Serikali kama zilivyo serikali

nyengine, ambalo katika Kifungu cha 9 (2) (b) cha Katiba ya Zanzibar imeelezwa kuwa

usalama na hali nzuri kwa wananchi itakuwa ndiyo lengo kubwa la Serikali. Hivyo ni

sawa na kusema kuwa mipango yetu, dira za maendeleo, ilani za vyama vyetu kadiri

zitakavyokuwa na mipango mizuri na mikakati mbali mbali lazima zifuate msingi huu wa

kikatiba wa kuwapa wananchi usalama wao na hali nzuri katika maisha yao.

Mheshimiwa Spika,

Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa

mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele vyake. Tutakumbuka kuwa katika

bajeti ya mwaka wa fedha unaomalizika mwezi Juni, 2015 Serikali imejiwekea malengo

makuu ya kujenga jamii iliyoelimika kwa elimu bora na inayotoa wataalamu wenye

hadhi ya Kimataifa, yenye siha, iliyoimarika kiuchumi na inayojali umoja wa kitaifa na

kufuata misingi ya utawala bora.

Mheshimiwa Spika,

Mambo hayo yote kwa pamoja yanajenga falsafa iliyomo katika Dira ya Maendeleo ya

2020 ambayo utekelezaji wake umo katika MKUZA II na Mpango wake wa utekelezaji.

Ukitazama katika bejeti za miaka minne iliyopita ya 2011/2012, bajeti ya mwaka

2012/2013, bajeti ya mwaka 2013/2014, 2014/2015 na hatimaye bajeti ya mwaka

2015/2016 ambapo malengo na vipaombele vyake vinafanana au ni sawa na kusema ni

vile vile.

Page 3: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

3

Mheshimiwa Spika,

Kamati yangu inaona kuwa si vibaya kuwa na malengo yanaofanana wakati tumekusudia

kuwa na muelekeo wa kustawisha jamii yetu kupitia malengo hayo lakini ni vyema basi

katika bajeti zetu tueleze ni kwa kiasi gani tumeweza kutekeleza lengo moja na jengine,

na wapi tumekwama na lengo gani tumeshafikia hatua nzuri ya kulitimiza. Kwa kufanya

hivyo tungelijuwa na wananchi wakaelewa kuwa katika bajeti ya mwaka huu

tumebakisha lengo gani kulitimiza ili tuangalie na mambo mengine.

MWELEKEO WA HALI YA UCHUMI MWAKA 2015 NA MPANGO WA MAENDELEO

MWAKA 2015/2016.

Mheshimiwa Spika,

Baada ya utangulizi huo mfupi naomba sasa nielekee katika maoni ya Kamati kuhusu

Mapitio ya Hali ya Uchumi mwaka 2014 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka

2014/15 pamoja na Mwelekeo wa Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2015 na Mpango wa

Maendeleo mwaka 2015/2016.

Mheshimiwa Spika,

Katika Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2015/16 uliowasilishwa na AR Ikulu na

Utawala Bora, imeripotiwa kukuwa kwa uchumi ambako kumeenda sambamba na

kuimarika kwa ustawi wa wananchi. Kamati yangu katika kuchambua hali ya ukuaji wa

uchumi kwa kuzingatia Mpango wa Utekelezaji wa Mkuza II imeona kuwa taarifa hizi ni

nzuri lakini hazijitoshelezi kuleta tafsiri halisi ya hali za wananchi kuimarika kiuchumi.

Mheshimiwa Spika,

Miongoni mwa mambo yaliyoelezwa ni kuongezeka idadi ya wananchi waliounganishwa

na huduma ya umeme katika gridi ya taifa kutoka watu 8,126 mwaka 2013 hadi kufikia

watu 10,410 mwaka 2014 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 28. Kwa tafsiri ya

kawaida utaona kweli kuwa nambari zimeongezeka lakini tafsiri halisi ya nambari hizo

Page 4: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

4

haisemi ni kwa namna gani hali ya uchumi ya mwananchi imekuwa baada ya ongezeko

hilo.

Mheshimiwa Spika,

Kamati yangu imeona kuwa kwa kuwa lengo la Mkuza II ni kustawisha hali za wananchi

na kuimarisha uchumi, tafsiri ya ongezeko hilo halionekani hapa kwa mfano bado

mwananchi wa kawaida aliyeunganishwa na gridi ya taifa, kama ilivyoelezwa hapo juu

analipa kodi ile ile ya 16% ya VAT anayolipa mfanyabiashara ingawa matumizi

yanatofautiana, hali kama hii bado inaonyesha mwananchi huyu analipa gharama kubwa

za maisha na kurejesha nyuma ustawi wa maendeleo yake ambapo siyo lengo la Mkuza

II. Mhe Spika, kamati yangu inaiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwapunguzia

wananchi malipo ya V.A.T ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wetu wengi

ambao hutumia huduma ya umeme kwa matumizi ya kawaida ambayo sio ya biashara,

na kuongeza udhibiti kwa waekezaji wakubwa hasa wenye Viwanda na Mahoteli ambao

Kamati yangu inahisi huko ndiko umeme mwingi unatumika bila ya kulipiwa bili

inayostahili jambo ambalo tunahisi mapato mengi ya Shirika la Umeme yanapotea,

ambapo mzigo huo hubebeshwa wananchi bila ya kujua. Kwa hiyo tunalitaka Shirika la

Umeme kuhakikisha Mahoteli yote ya Kitalii yanaekewa mita za Tukuza ambazo

tunaimani zinasaidia kudhibiti upotevu wa malipo ya Umeme.

Kimsingi ni kweli katika bara la Afrika, Zanzibar ni Nchi pekee iliyoweza kuwafikishia

wananchi huduma muhimu ya umeme kwa asilimia kubwa zaidi hadi vijijini na ni kweli

imeweza kuwasaidia kuinua kipato chao na pia kuibua ajira mpya kupitia matumizi ya

umeme, lakini pia tunalipongeza Shirika la Umeme “ZECO” kwa kukubali ushauri wetu

wa kuwaungia Umeme wananchi kwa njia ya mkopo jambo ambalo limewasaidia

wananchi wengi kuweza kuunga umeme ambao baadhi yao wameanza kwa kuutumia

kwa shughuli mbalimbali za biashara. Kwa hiyo tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya

Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kufika vijijini na kuwaelezea wananchi matumizi bora ya

Page 5: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

5

huduma ya Umeme kwa ajili ya uzalishaji ili kuwaongezea kipato na isiwe kuwashia taa

tu peke yake.

Mhe Spika, lakini pia kwa Program mpya za Serikali hivi sasa katika PBB je tujiulize katika

Program ya usambazaji wa Umeme mijini na vijini kumepatikana mafanikio

“OUTCOME” gani hadi hivi sasa, kimsingi Kamati yangu imekubali kuwa mafanikio ya

upatikanaji wa huduma ya Umeme imefanikiwa kwa asilimia 80. Kwa hiyo tunaiomba

Serikali kupitia Shirika la Umeme basi kuhakikisha hiyo asilimia 20 ya usambazaji wa

huduma ya umeme iliyobaki ikamilishwe katika Bajet hii inayofuata. Lakini pia

Mtakwimu Mkuu wa Serikali afanye tathmini baada ya wananchi wote kufikiwa na

Umeme katika maeneo yao je umasikini umepungua kwa kiasi gani katika maeneo

mapya yaliyofikiwa na huduma ya umeme.

Mheshimiwa Spika,

Kwenye Sekta ya Elimu, Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2015/16, pia kumeelezwa

wastani wa uwiano wa walimu kwa wanafunzi walioorodheshwa katika shule za msingi

za Serikali na binafsi kuwa umeendelea kuwa 1:26 sawa na mwaka 2013. Ukiangalia

wastani huu unaridhisha kwa kuwa hatua hii inasaidia mwalimu mmoja kufanyakazi yake

kwa ufanisi na kuweza kutoa elimu bora.

Lakini kama nilivyotangulia kusema kuwa uwiano huu ni nyenzo ya kufikia kwenye

elimu bora, bado mpango wa maendeleo haujatafsiri kwa uhalisia uwiano huo umeleta

matokeo gani tokea mwaka 2013 hadi mwaka huu wa bajeti, ili tuweze kuona ni kwa

kiasi gani tumepiga hatua katika elimu bora ya msingi. Ninachokusudia kusisitiza hapa ni

kuwa tunapoeleza Mipango yetu tuonyeshe na matokeo yake ambayo yatasaidia

kujitathmini katika kupanga mipango mengine. Lakini pia kamati yangu imeona katika

uwiano wa waalim na wanafunzi umeelezwa kwa ujumla lakini bado kuna baadhi ya

Skuli walimu wanazidiwa sana na idadi ya wanafunzi jambo ambalo huwatwika mzigo

mkubwa walimu lakini pia na kuwanyima fursa nzuri wanafunzi kupata usimamizi mzuri

kutoka kwa walimu wao, tofauti na wanavyopata wanafunzi wenzao.

Page 6: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

6

Mheshimiwa Spika,

Sambamba na hilo, Mpango wa Maendeleo pia, umeeleza kuhusu kuongezeka idadi ya

Skuli za Msingi na Sekondari kutoka 392 mwaka 2013 hadi 407 mwaka 2014 kwa Skuli

za Serikali na Skuli 94 mwaka 2013 hadi skuli 99 mwaka 2014 kwa Skuli binafsi. Kamati

yangu ingetaka kujuwa katika ongezeko hilo tumefikiaje malengo ya Dira ya Maendeleo

2020 na Mkuza II, tarakimu za ongezeko hilo hazielezi tulivyofikia malengo kwenye

elimu ya msingi na Sekondari ya kiasi gani elimu yetu imekuwa bora kuanzia ngazi ya

msingi. Hakuna matokeo yaliyoelezwa, kwa mfano, ongezeko hilo limesaidiaje

kuwezesha kila mwanafunzi aliyefikia umri wa kuanza skuli amepata fursa hiyo na

maeneo gani hayajafikia malengo hayo. Kwa hiyo tunaitaka Wizara ya Elimu wakati

watakapokuja kusoma Bajet yao watutolee ufafanuzi kuhusiana na suala hili.

Pia kamati yangu inaishauri Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu

kutokuridhika na idadi ya Skuli na idadi ya wanafunzi walioweza kupata Elimu ya msingi

tu bali kujielekeza sasa na kuandaa mitaala ya kutoa Elimu ya Amali kwa Vyuo vya

Serikali kwa kuvipatia vifaa vya kutosha vya kufundishia kwa kuviimarisha vyuo hivyo

pamoja na Skuli za taaluma ya Ufundi, Afya, Utalii, Kilimo, ili kutoa Elimu bora na

baadae kutoa wahitimu bora katika fani tofati hapo ndio tutakapoona faida ya vijana

wetu wasomi, ambao watakua ndio wataalamu katika mashirika na Makampuni yote

yatakayoamua kufanyakazi Zanzibar. Pia kuimarisha Karakana zetu ili kutoa huduma

bora inayostahiki jambo ambalo litaipunguzia sana mzigo Serikali katika matengenezo ya

magari na zana nyingine za Serikali.

Samba na kuanzisha mitaala ya Elimu ya Kujitegemea katika shule zote za Zanzibar ili kila

mwanafunzi anaemaliza Elimu ya awali basi aweze kua na elimu ya kazi ya mkono

ambapo akiamua kuanzisha shughuli yeyote ya kujiajiri yeye mwenyewe basi dhima yake

kubwa iwe ni kutafuta mtaji wa kuanzisha biashara jambo ambalo vijana wengi watakua

wajasiria mali na kupunguza wimbi la vijana wasiokua na ajira mitaani, na huo umasikini

ndipo tutakapoweza kuupiga vita au kuumaliza kabisa.

Page 7: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

7

Mheshimiwa Spika,

Hali ni kama hiyo katika elimu ya juu, ambapo Mpango wa Maendeleo umeeleza idadi

ya wanafunzi waliopata mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kutoka wanafaunzi 881

iliyogharimu Tsh. 5.22 bilioni mwaka 2012/13 hadi wanafunzi 1,467 iliyogharimu Tsh.

6.42 bilioni mwaka 2013/14.

Mheshimiwa Spika,

Tarakimu hizo ni nzuri lakini haziotowi picha halisi ya malengo tunayotaka kufikia ya

kusomesha vijana wetu wengi katika elimu ya juu na kuwa na wataalamu wenye uwezo

katika sekta mbali mbali. Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2015/16 haujaeleza wazi

ni idadi ya wanafunzi wangapi wameomba mikopo katika kila kipindi na kati ya hao ni

idadi gani ya wanafunzi wamepata mikopo hiyo, na wangapi walikosa na ni asilimia

ngapi? vile vile kwa kuwa katika kipaumbele chetu cha elimu tunajielekeza kuwa na jamii

iliyoelimika na inayotoa wataalamu wenye hadhi ya kitaifa na kimataifa kama Dira ya

Maendeleo ya 2020 na Mkuza II zinavyoeleza, bado katika mipango yetu hailezi wazi

idadi ya wanafunzi tuliowakopesha miaka ya nyuma ni wangapi wamehitimu na katika

fani zipi, na fani za aina gani bado tuna mapungufu na tunahitaji kuwekeza zaidi, kama

Program mpya ya PBB inavyotaka kuwa tuangalie ( INPUT, ACTIVITIES, OUTPUT na

OUTCOME ). Sasa hapa tunahitaji kuona Outcome ya wasomi wtu katika malengo yetu

ya Milenia.

Lakini isitoshe ni vyema tunahitaji tuone Serikali imeandaa mipango gani ili kuhakikisha

vijana wetu wote wanaohitaji mikopo ya Elimu ya juu wanafanikiwa kupata mikopo

hiyo, kwani lengo la kuboresha huduma za Elimu ni kupata wataalam wanaotosha na

wengine kutoa nje kusaidia wenzetu waliokua na upungufu.

Mhe Spika, tunajua lengo la Serikali la kutoa Mikopo ya Elimu ya juu ni kuhakikisha kila

mwenye uwezo wa kusoma asome bila ya vikwazo, sasa Serikali imejipanga vipi

kushirikisha taasisi binafsi ikiwemo kuzishirikisha Sekta binafsi kushiriki katika kutoa

mikopo hiyo ikiwemo mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Mabenki, na taasisi nyingine za fedha.

Page 8: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

8

Mhe Spika, Serikali kila mwaka inatoa fedha kwa ajili ya mfuko wa Elimu ya Juu basi pia

tunaitaka Wizara ya Elimu itueleze mipango yake ni hadi mwaka gani mfuko huu

utaweza kujitegemea kama ulivyokusudiwa kwani Kamati yangu inaamini mfuko huu

umetakiwa kuwa ni ( REVOLVING FUND) sio kila siku kuingizwa fedha bila ya kikomo,

kwa hiyo iko haja ya Bodi ya Miokopo ya Elimu ya juu kuweka utaratibu maalumu wa

usimamizi na ufuatiliaji wa urejeshaji wa mikopo hiyo kwa kuweka (DATABASE) ya

wanafunzi waliopata mikopo ili kufuatilia urejeshaji wake. Mhe Spika kamati yangu

inaamini Bodi ikiweza kuusimamia vizuri mfuko huu basi hapo baadae mfuko huu utakua

na pesa za kutosha na pia kuweza kuziekeza katika mifuko mingine au kuziekeza katika

kununua hisa kwa ajili ya kuzizalisha.

Mhe Spika, kamati yangu inashauri kua lengo kuu la kutoa mikopo ya Elimu ya juu iwe

ni kupata wataalamu wa kutosha lakini pia iwe na lengo jingine la kuwadhibiti wataalam

(KUMAINTAIN) ili wabakie nchini kuwatumikia wananchi, lakini kuwe na utaratibu

maalum wa kuwalipa maslahi mazuri na kuwapatia vitendea kazi vya kutosha ili waweze

kuzitumia vizuri elimu zao na kuleta tija iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika,

Katika sekta ya afya nako, Mpango wa Maendeleo haujaeleza matokeo ya ustawi kama

yanavyojieleza katika Mpango wa Utekelezaji wa Mkuza II, katika taarifa yake

Mheshimiwa Waziri ameeleza kuimarika kwa utoaji huduma katika sekta ya afya kwa

kuongezeka madaktari kutoka 40 mwaka 2013 hadi 90 mwaka 2014, na wataalamu wa

Maabara kutoka 212 mwaka 2013 hadi 235 mwaka 2014, vile vile katika Mpango huo

kumeelezwa kuongezeka kwa watabibu kutoka 185 mwaka 2013 hadi 194 mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika,

Katika maelezo hayo yote yanayokusudia kutekeleza hatua za ukuaji uchumi ambao

unakwenda sambamba na ukuaji wa ustawi wa jamii katika eneo hili la afya, ambalo

hakuna atakaebisha kuwa ongezeko hilo lina faida kubwa kiuchumi, lakini Mpango

haujaleza ni kwa kiasi gani ongezeko hilo limesaidia kupunguza vifo vya mama

Page 9: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

9

wajawazito, vifo vya watoto wachanga, na watoto wadogo wa chini ya umri wa miaka

mitano ambavyo kama ilivyoelezwa kwenye Mkuza tushuke kutoka vifo 48 vya watoto

wanaozaliwa kati ya 1000 wanaozaliwa. Aidha, ongezeko hilo la madaktari, watabibu

na wataalamu wa maabara halijaeleza ni kwa kiasi gani limeweza kukabiliana na maradhi

na kuweza kuwasaidia wananchi kujua mapema matatizo ya afya yanayowakabili.

Mhe Spika, kamati yangu inaipongeza Serikali kwa kuweka miongoni mwa vipau mbele

vyake kuwa ni suala huduma za Afya na ni kweli tumeona jitihada kubwa zikifanyika,

lakini bado kuna changamoto nyingi katika sekta hii ili kufikia yale malengo ya

Mapinduzi yetu matukufu ya Afro-Shirazi ambayo yamerithiwa na CCM ya kuwapatia

huduma za Afya wananchi wote bila ya malipo, kwa hiyo kamati yangu inaishauri

Serikali kupitia Wizara ya Afya, kuhakikisha lile lengo la kuifanya Hospitali ya Mnazi

Mmoja kuwa Hospitali ya rufaa likamilike ,kwani hivi sasa bado kuna huduma nyingi

hazipatikani ipasavyo hapo Hospitalini, kwa mfano huduma ya X-RAY haiko sawa kwani

ni machine moja tu ndio inayofanya kazi na uwezo wake ni mdogo na wahitaji wako

wengi, kwa hiyo tunaitaka Wizara katika Program ya mwaka huu kuhakikisha ile

Machine kubwa ya X-RAY iliyoharibika itengenezwe kwani inayo uwezo mkubwa mara

mbili ya ili ilikuwepo hivi sasa , na kamati yangu inayo taarifa kua katika nchi za Afrika

machine za aina ile ziko mbili tu Zanzibar na Misri kwa hiyo tunaamini ikitengenezwa

itasaidia kutimiza lengo la kuifanya ni Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa Rufaa kweli, pia

bado katika kitengo cha (EMERGENCY) hakuna madawa va vifaa vya kutosha inabidi

wagonjwa waende wakanunue dawa kwenye Pharmacy sasa tujiulize ikiwa imetokezea

mgonjwa hana jamaa je hizo dawa atanunuliwa na nani? wakati Hospitalini hapo

hazipatikani, kutokana na muda hayo ni baadhi tu ya mambo tu ya kuyashughulikia

miongoni mwa mengi ambayo yanahitaji kuyashughulikia ili kuifanya iwe kweli ni

Hospitali ya Rufaa. Kwa hiyo kamati yangu inataka kwa mipango ya mwaka huu wa

2015/16 tunataka kuona (OUT-COME ) ya Hospitali ya Mnazi Mmoja je tumeweza

kufikia kuiwezesha kuwa ya Rufaa? vinginevyo Manager wa Mradi itambidi aje

kuwajibika pamoja na Waziri muhusika. kwenye mwisho wa mwaka wa bajet ijayo.

Pamoja na hayo lakini tunapongeza kwa jitihada zinazochukuliwa kuongeza na

Page 10: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

10

kuboresha huduma za Afya hapa Zanzibar, pia sambamba na hilo kuzingatia maslahi ya

Madaktari wetu pamoja na wauguzi ili wawezekufanya kazi zao kwa utulivu na ufanisi

mkubwa.

Mhe Spika, pamoja na changamoto zilizopo tunaipongeza Serikali kuendelea kuthibiti

ongezeko la maradhi ya Malaria jambo ambalo limewafanya wananchi wengi kuimarika

afya zao, kwa hiyo tunatoa wito kwa wananchi kuimarisha usafi katika makaazi yao ili

kuondoa mazalio ya mbu wanaosababisha homa ya Malaria.

Mhe Spika, pamoja na mafanikio hayo kumejitokeza tatizo jingine la kuongezeka kwa

kasi kubwa kwa Maradhi ya KISUKARI na PREASURE hapa Zanzibar na kupelekea

kusababisha vifo vingi na kuwaacha baadhi ya wananchi na ulemavu wa viungo kwa

kukatwa baadhi ya viungo vyao kutokana na maradhi ya KISUKARI. Kwa hiyo

tunaiomba Serikali kama ilvyochukua jitihada katika kutokomeza maradhi ya Malaria na

tukawatunatolewa mfano Duniani basi sasa nguvu kubwa zaidi ipelekwe katika kudhibiti

maradhi haya ya KISUKARI na PREASURE.

Mheshimiwa Spika,

Mipango yetu ya Maendeleo siku zote inalenga kustawisha hali za wananchi kama

nilivyotangulia kusema. Katika huduma za kijamii bado mwananchi anakwazwa na

gharama kubwa za kupata huduma za lazima kama chakula, maji, afya, umeme,

mawasiliano n.k. Mpango wa Maendeleo umeonesha kuwa Mchango wa sekta ya

huduma katika pato la taifa umeongezeka kutoka asilimia 41.5 mwaka 2013 hadi kufikia

asilimia 44.7 mwaka 2014 kutokana mchango wa sekta za kifedha, uwekezaji katika

majengo, taaluma, ufundi, habari na mawasiliano. Hata hivyo ukuaji huo bado haujaleta

athari ya moja kwa moja katika pato la mwananchi wa kawaida.

Page 11: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

11

Mheshimiwa Spika,

Hilo linakwenda sambamba na mfumko wa bei kwa bidhaa na huduma ambao

umepanda kutoka asilimia 5.0 mwaka 2013 kufikia asilimia 5.6 mwaka 2014 hasa katika

bei za chakula. Hali hiyo bado haijadhibitiwa, kamati yangu inashauri kuwa Serikali

lazima iweke udhibiti wa ukuaji huu kwa kutowaachia wafanyabiashara kuendesha soko

huria wanavyotaka. Tumeona katika sekta ya nishati, bei ya mafuta na upatikanaji wake

imekuwa shida mara kwa mara katika siku za hivi karibuni suala hili nalo pia lipatiwe

ufumbuzi wa kudumu. .hivi sasa kumekua na kupanda na kushuka kwa bei ya matuta

ndani ya kipindi cha miezi miwili tu hili jambo la hatari sana kwa uchumi wa nchi yoyote

haya yanaleta usumbufu katika upatikanaji wa huduma za lazima kwa mwananchi wa

kawaida, na suala hili linaweza pia kuivuruga bajet ya Serikali kwani tunapitisha pesa

nyingi kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya magari na viwanda pia.

Mhe Spika, suala la bidhaa na huduma muhimu ikiwa Serikali haikujitahidi kudhibiti

upandaji wa bei zake basi hata Serikali ikiongeza kiwango cha Mshahara basi itakua ni

bure kwani purchasing power ya fedha hizo zitakua haziendani ya bei za huduma na

bidhaa katika soko kwa hiyo Serikali iangalie uwezekano wa kuboresha, kudhibiti na

kupunguza bei za huduma na bidhaa muhimu kwa maisha ya kila siku, ili kuongeza

perchessing power kwa kipato cha wananchi.

Mhe Spika, pamoja na hayo kwa kulinganisha maisha ya kawaida ya wananchi katika

bara la Afrika Zanzibar wananchi wanaishi maisha mazuri hadi vijijini kuliko nchi nyingi

za Afrika kwani huduma muhimu ikiwemo barabara, Shule za msingi na Sekondari,

umeme, maji, vituo vya Afya, huduma za fedha, ikiwemo Mabenki Tigo pesa, Easypesa,

M-pesa. Airtel Money n.k. hizi zote ni huduma ambazo katika nchi nyingi za Kiafrika

hazipatikani kwa karibu vijijini, ila ni mijini tu, Mhe Spika, tatizo ambalo wananchi wengi

wanafikiria kuwa ukuaji wa uchumi kua haulingani na kipato cha mwananchi wa

kawaida, ni kwa sababu wanapenda kulinganisha maisha baina yao kwa kipato na

jingine ni kwamba pesa haikai mifukoni kwani kila kitu au bidhaa unayoihitaji

inapatikana katika soko, na kwa kuwa watu wengi hupenda kuboresha maisha yao basi

Page 12: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

12

akipata pesa huimarisha aidha makaazi yao, kununua usafiri wao binafsi, kununua mavazi

mazuri, haya ndiyo yanayosababisha kuona pesa haitoshi lakini wanashindwa

kulinganisha maisha walioshi wazee wao huko miaka ya nyuma kulingana na wanayoishi

wao hivi sasa, ukiangalia kiasi miaka kumi nyuma vijijini katika kijiji unaweza kumkuta

mtu mmoja tu ndie anaemiliki simu ya mkononi, lakini leo hii karibu kila nyumba tatu

basi lazima utawakuta watu wanaomiliki simu za mkononi, pia vijiji vingi hapa Zanzibar

kulikuwa hakuna watu wanaomiliki Gari za kwao wenyewe labda Gari za Ushirika

walizopewa na Serikali, lakini leo hii vijiji zaidi ya asilimia 80 wamo watu wanaomiliki

Gari zao wenyewe, hiyo ni baadhi ya mifano kuwa Pato la Taifa linapokua basi

linachangia kukua kipato cha wananchi wa kawaida na kuimarika kwa maisha yao.

Mheshimiwa Spika,

Umefika wakati Serikali iwezeshe Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (ZURA), ambao sheria

yake imepitishwa hivi karibuni na Baraza hili tukufu, kufanyakazi yake kudhibiti mtindo

huu wa wafanyabiashara wa mafuta kuhodhi soko la mafuta kwa kuwa wao peke yao

ndiyo waagizaji, wasambazaji na wauzaji reja reja, kamati inashauri mtindo huu

ukiachwa kama ulivyo tatizo la upatikanaji wa nishati ya mafuta litaendelea na kuathiri

upatikanaji wa huduma za jamii kwa wananchi. Aidha, kamati inaishauri Serikali kuwa na

miundombinu yake ya akiba ya mafuta (GOVERNMENT DEPORT) pindi inapotekea

upungufu kwa namna yoyote ile basi iweze kuingiza mafuta kwenye soko ili kusaidia na

kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika,

Jambo jengine muhimu kamati yangu inataka kulisema kwa msisitizo ni bajeti yetu katika

kuhudumia mahitaji ya lazima kama ilivyoelezwa na Mheshimiwa Waziri. Katika hili

kamati yangu imetambuwa kuwa Malengo ya Mkuza II yameweka wazi namna Serikali

Page 13: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

13

inavyoweza kujitoa katika kufanya kila jambo na kuziacha Serikali za Mitaa kufanya

majukumu hayo.

Mheshimiwa Spika,

Mpango mzuri uliowekwa katika Mkuza II wa kukasimisha (ugatuzi) madaraka katika

Serikali za Mitaa, kama ungefanyika mapema, ungesaidia sana kuipunguzia Serikali mzigo

mzito wa kupanga bajeti kwa kila jambo katika ngazi ya Serikali kuu.

Mheshimiwa Spika,

Katika Mpango wa Utekelezaji wa Maendeleo wa Mkuza II imewekwa vizuri dhana

kukasimu (ugatuzi) madaraka kwa serikali za mitaa (D by D) yaani (Decentralization by

Devolution). Mpango huu umo kwenye Mkuza lakini utekelezaji wake unahitaji

kusimamiwa na hivi sasa sheria zimeshatungwa kwa ajili ya kushurutisha utekeleza wa

Sera na malengo hayo.

Kamati yangu inaomba Serikali kuzingatia kwa makini na kuziwezesha Serikali za mitaa

zikafanyakazi kwa uhuru lakini kwa mujibu wa Sheria kwa lengo la kuisaidia Serikali kuu

katika kuteleza vipaumbele vyake vya afya, elimu, maji, miundombinu, biashara na

uwekezaji wenye tija.

Mhe Spika, suala la utawala wa Serikali la Mitaa ni jipya ingawa sehemu kubwa ya

watendaji ni walewale kwa hiyo yatahitajika mafunzo ya kutosha katika kuibua,

kutekeleza na kusimamia mipango na miradi yote iliyopangwa na itakayoibuliwa na

wadau mbali mbali katika kila halmashauri na Mabaraza ya Miji. Kwa hiyo kwa kua

Serikali kwa makusudi imeamua kukasimu madaraka kwa Serikali za mitaa basi itoe uhuru

wa kutosha kwa wakurugenzi wa Halmashauri na mabaraza ya miji kuonyesha uwezo

wao katika kuibua na kuisimamia miradi hiyo kikamilifu bila ya usumbufu kwa mujibu

wa Sheria na Kanuni kama zitakavyoeleza, kamati yangu inawataka viongozi wote wa

Halmashauri na Mabaraza ya Miji kuwa waadilifu na fedha watakazotengewa pamoja na

kua na uadilifu katika kuingia mikataba kwa miradi yote mikubwa na midogo

Page 14: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

14

watakayoiibua kwatika maeneo yao, hili likifanyika tunaamini litaharakisha maendeleo

kwa haraka hapa Zanzibar na kuongeza kipato kwa wananchi wetu na kupata huduma

bora kwa unafuu na kwa urahisi.

Mhe Spika, kamati yangu inaiomba Tume ya Mipango kusimamia kikamilifu miradi yote

itakayoibuliwa na Halmashauri na Mabaraza ya Miji hasa katika matumizi bora ya ardhi

kwa kuzigatia ardhi ya Zanzibar ni ndogo kwa hiyo kuhakikisha hakutotokea migongano

kwa matumizi ya ardhi na mipango ya maendeleo ya kitaifa na ile ya Halmashauri, kwa

hiyo ni vyema kuyatangaza maeneo yote ya hifadhi ya Taifa, maeneo ya vianzio vya

maji, lakini pia maeneo ya Kilimo ili shughuli za maendeleo zisijekutuletea changamoto

nyingine katika matumizi ya ardhi.

MAONI YA KAMATI KUHUSU MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMZI YA SERIKALI

KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

Mheshimiwa Spika,

Naomba sasa nielekeze maoni ya Kamati yangu katika Makadirio ya Mapato na

Matumizi ya Serikali katika mwaka wa fedha 2015/2016, bajeti ambayo imewasilishwa

mbele ya Baraza lako na Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

Mheshimiwa Spika,

Bajeti ya mwaka huu ni tofauti sana na bajeti zilizotanguliwa kujadiliwa nakupitishwa na

Baraza hili. Bajeti hii imekuja katika Mtindo mpya kwa kuwa ni bajeti inayozingatia

Programu za Maendeleo. Itakumbukwa kuwa kuanzia mwaka 2011/12 Serikali ilianza

matayarisho ya maandalizi ya mfumo wa mageuzi ya bajeti yenye lengo la kuimarisha

uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa bajeti, ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa bajeti.

Lengo kubwa ambalo kamati yetu tunakubaliana nalo katika mpango huu mpya ni

kuhakikisha kuwa kila shilingi inayoidhinishwa na Baraza na kutumiwa na Serikali iwe

inaleta manufaa kwa walengwa na wananchi kwa ujumla. Tena kwa kuzingatia Program

iliyokubaliwa na Baraza la Wawakilishi.

Page 15: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

15

Mheshimiwa Spika,

Pamoja na kuwa na mfumo mpya wa bajeti ambayo inazingatia programu, lakini bado

bajeti yetu inaendelea kuwa ya makusanyo kwanza na kutumia baadaye (cash budget).

Katika mtindo huu wa bajeti inailazimu Serikali kuwa na vyanzo vya uhakika vya

kukusanya kodi na mpango madhubuti wa kudhibiti uvujaji wa makusanyo hayo. Mara

nyingi katika bajeti zetu kinachokadiriwa kukusanywa sicho kinachopatikana, aidha,

kinachotumika huwa ni kikubwa zaidi kutoka na sababu mbali mbali.

Mhe Spika, kama alivyotoa ufafanuzi Waziri wa Fedha kuhusu hali ya Uchumi wetu

katika kipindi kinachoishia june 2015, kwamba uchumi wetu kwa mwaka 2014

umeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 7.0 kulinganisha asilimia 7.2 ya mwaka 2013,

ambapo pato la Taifa la kila mtu limeongezeka kufikia wastan wa 1,552,000 sawa na

USD 939, 2014 kulingana na 1,384,000 sawa na 866 mwaka 2013.

Mhe Spika, kwa kuangalia kijumla kwa miaka 5 ya Serikali hii ya awamu ya saba

inayoongozwa na D.k A.M. Shein uchumi wetu umeendelea kukua kwa wastan wa

asilimia 6.3 kwa mwaka ambapo pato la Taifa limekua kwa wastan kutoka 848.2 Bil.

hadi kufikia 1,115.4 Bil. Sawa ma kasi ya 31.5 kwa mwaka, ambapo pato la mtu

mmojammoja, pia limekua kutoka 856,000 mwaka 2010 hadi kufikia 1,552 (939) kwa

mwaka 2014 .

Mhe Spika, kutoka mwaka 2010/11 hadi 2014/15 mapato ya ndani yamongezeka kutoka

181.4 Bil. Kufikia 360.4,Bil mwaka 2014/15 sawa na ukaji wa asilimia 98.7 kwa miaka 5

ambapo ni sawa 19,7 kwa kila mwaka, Mhe ongezeko hili ni kubwa na linatia moyo na

mafanikio haya yasingeliweza kufikiwa bila ya kelele na makaripio mbali mbali kutoka

kwa wajumbe wako wazito wa Baraza la Wawakilishi walipoamua kikamilifu bila ya

kujali tofauti zao za kisiasa na KUISIMAMIA Serikali kikamilifu katika kuonyesha maeneo

yaliyokua pesa za Serikali zilimokua zikivuja, ingawa kuna baadhi ya watu wakiwemo

baadhi ya viongozi wasiojua nini wajibu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walikua

wakinuna na kutuona wabaya lakini faida yake leo hii ndio tunaiona kuwa mapato

Page 16: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

16

yameongezeka maradufu na udokozi umepungua kwa asilimia kubwa, Mhe Spika, katika

kipindi chote hicho tunamshukuru sana Rais wetu alitulia kimya na wala hakutuingilia

wakati tulipokua tukipiga kelele kuisema ,tukiikosoa na tukiisimamia Serikali yake katika

kupiga vita ubadhirifu wa mali na fedha za umma usatahamilivu wake kwetu leo yeye

mwenyewe anaweza kupanda majukwaani akijinasibu kuwa Serikali yake ndani ya

kipindi alichokabidhiwa kuiongoza Zanzibar Serikali yake imeweza kuongeza ukusanyaji

wa mapato kwa karibu asilimia 98 lutoka kiasi cha Bilioni 181. hadi Bilioni 360 ,hii ni

hatua kubwa ya mafanikio kwa uongozi wake na uadilifu wake kwa Taifa letu kwa hiyo

hatunabudi sote wananchi wa Zanzibar tumpongeze kwa kazi kubwa aliyoifanya na

inafaa tuendelee kumuunga mkono ili atuletee matunda mengi zaidi katika miaka ijayo.

Mhe Spika, mafanikio hayo lazima tujiulize yametokana na nini? Hili ni suala kila mmoja

wetu anapaswa ajiulize na tutafute jawabu ya pamoja ili tuendelee na ukuaji wa mapato

na Uchumi wa Nchi yetu, Mhe Spika, bila shaka mafanikio hayo yametokana hali ya

Amani na utulivu uliopo hapa nchini kwetu, Mhe Spika, lakini mimi nimeanza kua na

wasiwasi kua hali hiyo ya Amani imeanza kuingia mashaka hasa katika kipindi hiki

tunachoelekea kwenye uchaguzi mkuu kwani tumeanza kuona viashiria vya uvunjifu wa

Amani kuanzia humu ndani ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi ikiwa ndio kioo cha

jamii kwani kulianza kujitokeza vurugu wakati Serikali ilipoleta hoja ya taarifa ya sheria

ya kura ya maoni iliyopitishwa na Bunge ifanyekazi na hapa Zanzibar tulianza kuona

mpasuko mkubwa wa Serikali yetu kwani kulitokea zomea zomea kutoka baadhi ya

Mawaziri na Wajumbe kutoka kambi ya Upinzani kuonyesha kua hawaiungi mkono, sasa

suala la kujiuliza kwani mawaziri hawana vikao vyao vya BLM ambapo kama

wanatofautiana kimawazo watofautiane hukohuko lakini cha kushangaza walikuja

kupingana ndani ya ukumbi wa Baraza ambapo ni kinyume na Katiba ya Zanzibar ibara

ya 43(5) inawataka Mawaziri wote kuwajibika kwa pamoja ndani ya Baraza la

Wawakilishi, laikni isitoshe na katika kikao hicho hicho cha Mwezi wa April tulishuhudia

kwa mara nyingine tena Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikatika pande mbili ndani ya

Baraza la Wawakilishi pale ilipowasilishwa hoja ya Mhe Hamaad Masoud kuhusu

vitambulisho vya Uzanzibari pamoja na Kauli ya Serikali iliyotolewa na Mnadhim wa

Page 17: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

17

Serikali Mhe Waziri katika afisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kua hoja ile

haina msingi na wananchi wanatakiwa wafuate taratibu za kisheria katika kutafuta haki

zao bila ya kutumia shindikizo la Baraza la Wawakilishi tuliona tena Mawaziri wa pande

zote walitofautiana tena ndani ya Baraza la Wawakilishi ambapo kifungu kilekile cha

43(5) cha Katiba ya Zanzibar kilikiukwa tena hii ni ishara mbaya kwa Serikali hii ya

Umoja wa kitaifa na inaweza kuashiria kua viongozi ambao wao ndio walitunga Katiba

hii ndio hao hao wanaanza kuikiuka Katiba hiyo hiyo.

Mhe Spika, kwa maana hiyo kama anavyotuasa Rais wetu pamoja na Makamo wa Pili

wa Rais kuendelea kuwa wamoja tueke mbali tofauti zetu hasa katika mambo ya msingi

lakini kubwa ni kufuata Katiba na Sheria za Nchi katika kutekeleza majukumu yetu kwani

ikiwa Serikali wenyewe hawaonyeshi Umoja ndaNI YA Baraza kama Katiba inavyoeleza

basi tusitegemee na waliobaki kuwa wataweza kuvumiliana, sasa naomba sisi wenyewe

tuwe mfano kwani isijekua anachelewa Ng’ombe wa mbele akapata bakora Ng’ombe

wa nyuma ambao ni Wawananchi.

Mhe Spika, kama Waziri wa Fedha alivyotuomba mwaka uliopita tumruhusu Serikali

itumie kiasi cha 707.8 Bil.kwa ajili ya kuendeshea Serikali kwa mwaka 2014/15 ambapo

kwa kazi za kawaida T/sh 376.5 na kazi za Maendeleo 331.3 hapa ametuelezea hadi

kufikia March makusanyo halisi yamefikia karibu Bil 275 sawa na asilimia 92.1 kati ya

298.7 Bil zilizotarajiwa matarajio hadi kufikia june yatafikia 375.4 ambapo itafikia kiasi

cha asilimia 93.1 ya makadirio ya mwaka huu.

Mhe Spika, kama alivyoelezea Waziri wa Fedha kuwa matumizi halisi hadi kufikia March,

mwaka huu karibu 369,Bil zimetumika sawa na 52 asilimia ya malengo ya mwaka

ambapo kati ya hizo kiasi 261.2 zimetumika kwa kazi wa kawaida sawa na 96 ya

matarajio. Mhe Spika kama mchanganuo kwenye hotuba ya Waziri inavyoonesha kuwa

Mishahara 74% ,OC 61%, Mfuko Mkuu 69.3% na Ruzuku 65%.

Mhe Spika, kamati yangu haijaridhika kwa kuona kua kwa upande wa OC 61% tu ndizo

zilizoingizwa wakati pesa hizo ndio pesa za kuendeshea shughuli muhimu za mawizara

Page 18: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

18

wakati katika mfuko mkuu wa Serikali zimetumika karibu 69.3% hali hii hairidhishi hata

kidogo kwa hiyo kamati yangu inaitaka Serikali kupunguza matumizi yasiyokua ya lazima

na pesa zaidi zielekezwe kwenye OC ili malengo ya mawizara yaweze kufanikiwa kama

wanavyotuomba kila mwaka hapa Barazani, kwa hiyo safari za viongozi zisizokua za

lazima zipungue ili pesa nyingi ziende kuendeshea Serikali. Mhe Spika, kamati yangu

inaitaka Serikali katika Bajeti hii asilimia ya OC iwe ya pili kiasilimia baada ya mishahara

ambayo haiwezi kuepukika.

Mhe Spika, kwa upande wa shughuli za Maendeleo, kwa miezi tisa ni Bil. 108.5 tu ndizo

zilizotumika ikiwa ni 32.7 tu ya lengo hii imetokana na kuendelea kusua sua kwa miradi

ya TERMINAL BUILDING Karume Air-port Zanzibar, BARABARA ZA KATI na Mradi wa

ZUSP, na uzembe huu umesababisha hata kupungua kwa mchango wa Washirika wa

Maendeleo kuchangia miradi hiyo.

Mhe Spika, kwakweli kamati yangu haijaridhika kabisa na kusua sua kwa miradi hii

wakati tunaambiwa ilifanyiwa uchambuzi yakinifu kabla lakini hadi leo miradi

imombioni na haijulikani itakamilika lini ingawa kila mwaka tunaambiwa itamaliza kabla

ya mwaka husika na tunaridhia kwa hiyo tunaitaka Serikali.

Mhe Spika, hali hii ya uzorotaji wa baadhi ya miradi mikubwa hapa Zanzibar

inazorotesha uchumi wa Zanzibar, lakini kuna kila dalili ya kua kuna baadhi ya watu

aidha kwa tama au kwa kutokujua kile wanachokifanya, basi hutafuta Wakandarasi

wabovu au wasiokua na uwezo wa kufanya miradi mikubwa makampuni ya mifukoni

ambayo hushindwa kazi njiani au kujenga chini ya kiwango, na kwa kutahadharisha

Serikali kwa mambo kama haya, kunafunu kua katika mradi wa ZANZIBAR GROUND-

HANDLING katika Uwanja wa ndege wa ABEID AMAAN KARUME kuna taarifa ya kua

tayari makosa kama hayo yameanza kwa kazi hiyo kupewa Kampuni FEKI ambayo kwa

taarifa inasemekana haikushinda Tender, haina uwezo , haina uzoefu, haijawahi

kufanyakazi hata pahala popote Duniani haina kigezo chochote,baya zaidi pia

inavyosemekana hata usajili wake kwa msajili wa Makampuni unautata, baya zaidi

inasemekana kua hata zana walizoleta hapa nchini kwa ajili ya kufanyia ni mitumba

Page 19: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

19

ambayo imeshafanyiwa kazi na kampuni nyingine huko falme za Kiarabu, eti kampuni

hiyo ndio inakuja kuanzia kazi kwenye Uwanja wa Ndege mpya wac Kimataifa wa

ABEID AMAAN KARUME ZANZIBAR, kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana wakati

kuna makampuni mengi ambayo yaliomba kazi hiyo ambayo yanasifa, uzoefu , ubora na

tungelitarajia zingeliweza kuleta zana mpya zinazolingana na hadhi ya Uwanja wetu

mpya wa kimataifa wa Zanzibar hii ni aibu kwetu Uwanja mpya zana za kufanyia kazi

mitumba, Mhe Spika, tunaitaka Serikali kutupatia maelezo kamili ya mradi huu na uhalali

wa Kapuni hii na kwa hivi sasa kuna tatizo gani katika usajili wa Kampuni hii, Nadhani

wakati umefika kwa Serikali yetu iwaonee huruma wananchi wetu kwa kuwafanyia

mambo mazuri kwani pesa haitoshi hata tukipata ngapi basi tutaona hazitoshi kwani

tunapenda kujitajirisha japo wananchi wakiumia.

Mhe Spika, kamati yanguinaitaka Serikali kuhakikisha katika kipindi kijacho kuifanyia

tathmini miradi yote na kutafuta makampuni yenye ubora na uwezo , pia kuweza

kusimamia na kujua ni kwa muda gani itakamilika, kwani kuchelewa kumalizika kwa

miradi hiyo au kukosa ubora kwa miradi hiyo kunaibebesha Serikali gharama za ziada ili

kukamilisha miradi hiyo na kuubebesha mzigo wa madeni wananchi.

Mhe Spika, kamati imeridhika na hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya

Fedha, za kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa upande wa TRA na ZRB ya usimamizi

wa kimaeneo ( BLOCK MANAGEMENT SYSTEM) kwa kutumia Technologia ya GPS,

uimarishaji wa Uthamini katika maeneo ya Forodha, (VALUATION) ili kujua thamani

halisi ya bidhaa zinazoingizwa nchini. ingawa hapa bado kuna bandari bubu nyingi

ambazo huingiza bidhaa bila ya kulipiwa kodi. Hasa katika kisiwa cha Pemba. Hatua

nyingine Marekebisho ya ada za Bandari ambayo imesaidi kutatua tatizo la madawati

hapa Zanzibar ingawa kamati yangu haijaridhika na usimamizi wa matumizi wa fedha

hizi tunaitaka kamati husika kufuatilia hilo. Na katika hili tunaungana mkono na

mapendekezo mapya ya Waziri kutoza ada hii kuanzia mwaka huu kwa wasafiri

wanaoenda Pemba kwani matunda yake tumeanza kuyaona. Pia hatua kupunguza

misamaha ya kodi ambapo kamati yangu inaitaka Serikali kupitia Wizara ya Fedha,

Page 20: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

20

kuangalia misamaha ile tu ambayo itazalisha ajira au kutoa huduma za nafuu kwa jamii.

Mhe Spika, kamati yangu pia inaitaka Serikali kutokuridhika tu na kutoa misamaha ya

kodi lakini ifuatilie matumizi ya misamaha hiyo je inatumika kwa asilimia 100% kama

ilivyokusudiwa? Kwani tunawasiwasi kua kuna baadhi ya bidhaa zinazosamehewa kodi

kwa ajili ya miradi ya uekezaji sehemu Fulani huingia mitaani kwa kuingizwa kwenye

soko kwa kuuzwa jambo ambalo huikosesha Serikali mapato.

Mhe Spika, ili kuweza kuitekeleza kwa ufanisi Bajet inayotumia Program, tunaiomba

Serikali kupitia Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kuanza kuweka

utaratibu wa kufungua Account Maalum na kuweka fedha, ili kuweka akiba ya kuanzia

Bajeti ya mwaka unaofuata, ili kufikia lengo la kuwa na akiba ya fedha ya mwaka mzima

wakati wa kupitisha Bajet ya Serikali, na mapato yanayopatikana kwa mwaka ule iwe

kujazia tu bajet hiyo ya mwaka husika hapo ndipo tutakapoweza kuitekeleza vizuri

BAJET INAYOTUMIA PROGRAM.

Mheshimiwa Spika,

Katika Makadirio ya bajeti ya mwaka 2015/16, Serikali inakusudia kuifanya iwe bajeti

inayotegemea vyanzo vya ndani zaidi kwa vile vyanzo vyengine vya mapato kama vile

misaada ya kibajeti havina uhakika kupatikana kwake na kunaleta athari katika

utekelezaji wa bajeti. Kamati yangu imeliona hili na ingawa Serikali itaweka namna ya

kuzipokea fedha za misaada ya kibajeti zitakapopatikana, lakini utaratibu huu uwe wa

wazi ambao utawezesha ufuatiliaji na kujua kiasi gani kimepatikana na kimetumika katika

mipango ipi. Mhe Spika, katika utaratibu huu kamati yangu inamuomba waziri wa

Mipango pamoja na Fedha, kuweka utaratibu maalum wa kila robo ya Mwaka kukutana

na Kamati ya Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi ili kutoa taarifa ya upatikanaji wa hizo

fedha za GBS au kutokupatikanwa, na kuweza kupatiwa taarifa ya mgawanyo wa fedha

Page 21: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

21

hizo katika miradi mbali mbali, kwani tumepitisha Bajeti ambayo inaruhusu mapato

ambayo hayakulengwa MOJA MOJA.

Mheshimiwa Spika,

Changamoto kubwa ya bajeti yetu ni namna ya kudhibiti ukusanyaji wa mapato ya

ndani na kudhibiti matumizi yasiyozingatia sheria. Kamati yangu imeona kuwa kuna

udhibiti hafifu wa makusanyo sambamba na njia za ukusanyaji wa mapato hayo

zilizopitwa na wakati ambazo makusanyo hufanyika mkono kwa mkono.

Mheshimiwa Sipika,

Makadario ya Bajeti ya mwaka 2014/15 yalilenga katika ukusanyaji mapato katika

vyanzo ambavyo vimezoeleka, ingawa kila bajeti vyanzo hivyo huwa havifikii makadirio

halisi, mfano mapato yasiyokuwa ya kodi, yalikadiriwa kuwa jumla ya Tsh.16.4 bilioni

ambapo hadi mwezi Machi 2015 ni Shilingi Bilioni 12.8 zimekusanywa. Mara nyingi

kamati yangu imeshauri kuwa uwezekano wa kufikia na kuvuka lengo la ukusanyaji wa

mapato hayo upo endapo tutaachana na mtindo wa kukuanya kwa njia za mikoba na

vikapu (CASH COLLECTION) badala yake kutumia mfumo wa kibenki (E-CARD), bado

Kamati yangu inasisitiza kuwa malipo ya ada zote katika huduma zinazotolewa na

Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali, yalipwe kupitia benki ili kudhibiti uvujaji wa

mapato hayo na kuongeza mapato ya Serikali.

Mhe Spika, suala hili linawezekana kwani kuna baadhi ya maeneo kwa mfano, hivi sasa

Air-port kwenye malipo ya VISA na Uhamiaji kupitia malipo ya huduma za Pas-port , pia

baadhi ya malipo kupitia ZRB. Kwa mifano hiyo hili linawezekana.

Mhe Spika, Sasa kwa mifano hiyo tunaishauri Serikali, kuanzisha ada mpya ya malipo ya

ada ya Utalii kwa kutoza ada moja tu ya USD 100 kwa kila mtalii anaeingia Nchini na

baadae igawanywe katika yale maeneo ambayo watakayo amua kutembelea. Hii pia

itasaidia kukusanya mapato katika ada ya vivutio vya utalii kwa mfano kwenye Spice

Tour’s Farms, Baet-El –Jaib, Kanisa la Mkunazini, Minara miwili, kwenye magofu ya

Page 22: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

22

Serikali, na maeneo mengine, lakini ada hii pia itasaidia kujua wale watalii waliongia

Nchini wametembelea maeneo gani na pia kujua ni maeneo gani hutembelewa na

wageni wengi zaidi kuliko pengine, ili kuweza kuboresha miundombinu kwa maeneo

hayo.

Mhe Spika, eneo jingine tunaloshauri Serikali kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya

Serikali ni katika malipo ya wageni kwenye Mahoteli ya kitalii, eneo hili kamati yangu

imegundua Mahoteli mengi ya Kitalii yamekua na utamaduni wa wageni wao kulipia

vyumba nje ya Nchi (malazi) wakati walipaswa malipo hayo kulipiwa hapa Zanzibar,

jambo hili linasababisha udanganyifu mkubwa wa kujua ni wageni wangapi wamelala

katika Mahoteli hayo , ili kuweza kupata kodi ya Serikali, kwa hiyo pia eneo hili Serikali

kuanzisha utaratibu wa kuanzisha kadi maalum ya Utalii ambayo atapewa pale uwanja

wa ndege baada ya kulipia ada ya VISA na mtalii atai-(SWAAP) hiyo card wakati wa

kuingia Nchini na atai-(SWAAP TENA) wakati wa kuondoka Nchini ili kujua alipoingia

nchini alikaa kwa muda gani hapa Zanzibar. Tukiweza kutumia utaratibu huu basi

utaweza kusaidia kukusanya pesa nyingi na mapato hayo yataweza kuziba lile pengo la

Serikali kutaka kukopa karibu 30 Bil. ili kufidia pengo la Bajeti yetu.

Mheshimiwa Spika,

Katika mapato yasiyokuwa ya kodi, zipo fedha za gawio kutoka Mashirika

yanayomilikiwa na Serikali. Katika gawio hilo Serikali iliongeza kutoka asilimia 10 kwa

mwaka wa fedha 2014/2015 hadi asilimia 20 ambapo jumla ya Tsh. 727 milioni

zimekusanywa. Kamati yangu ingependa kujuwa ni Mashirika yepi yameweza kumudu

kulipa gawio kwa asilimia hiyo 20 iliyoongezwa na Mashirika yepi hayajaweza kumudu

kulipa na kwa sababu gani. Nasema hivyo, kwasababu Mashirika haya huwa

hatuidhinishi fedha zao za makusanyo na matumizi, isipokuwa ruzuku tu kwa yale

yanayopata ruzuku, na ingawa Sheria ya Mitaji ya Umma namba 4 ya mwaka 2002,

inataka taarifa za mwaka na fedha za mashirika ya Umma ziwasilishwe katika Baraza la

Wawakilishi na Waziri husika.

Page 23: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

23

Mheshimiwa Spika,

Katika mwaka huu wa bajeti 2015/2016, Mapato ya ndani yaliyokadiriwa kukusanywa ni

Tsh.450.5 bilioni, ambayo ni ongezeko la asilimia 25 ya matarajio ya mapato ya mwaka

2014/15 ya Tsh. 360.4 bilioni. Katika matarajio ya mwaka huu ambayo Serikali

imeshaeleza kuwa itategemea zaidi makusanyo ya ndani kuendesha bajeti, bado Kamati

yangu ina wasiwasi wa kufikia malengo ya ukusanyaji kwa vile vyanzo vya mapato ni

vile vile na mfumo wa ukusanyaji wa mapato hayo una mianya mingi na kuvuja.

Mheshimiwa Spika,

Katika eneo la Uwanja wa ndege ambapo malipo ya viza za watalii yanafanyika

kumekuwa na changamoto kubwa ya ukusanyaji. Utaratibu uliokuwapo awali

umeonesha kuwa mapato yamekuwa yakivuja kwa kiwango kikubwa kutoka na mapato

hayo kukusanywa kwa njia ya mkono (cash). Imedhihirika kuwa baada ya mpango wa

majaribio wa kukusanya mapato hayo kwa njiaya kieletroniki kupitia benki ya CRDB

mapato hayo yameongezeka mara tatu zaidi ya yale yaliyokuwa yakikusanywa kwa

mkono. Mfumo huu wa ukusanyaji wa fedha kwa njia za kibenki umeonesha ni kwa kiasi

gani tunaweza kuongeza makusanyo na kudhibiti uvujaji wa mapato hayo.

Mheshimiwa Spika,

Kama nilivyoelezea hapo awali Katika maeneo mengi ambayo watalii wanatembelea

Serikali imekua haipati fedha inayotokana na utalii huo, maana yake ni kusema kwamba

mtalii anapokuja nchini kile kitendo cha yeye kuja hakiongezi fedha yoyote katika mfuko

wa Serikali, mtalii huyo akishalipa malazi hakuna na pahala anapotembea hakuna

sehemu ya malipo hayo yanayoingia Serikalini. Kamati yangu inaona kuwa ili utalii uwe

na faida maeneo yote yanayotembelewa na watalii lazima yawe na mfumo wa malipo

ambao kasma fulani ya kodi itakwenda Serikalini, kamati yangu imepata taarifa na kujua

Page 24: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

24

kuwa maeno ya Msikiti wa Kizimkazi, kanisa la Mkunazini na Minara Miwili, Mashamba

ya Viungo (spice farms) na Fukwe za Bahari nyingi watalii wanakwenda kwenye maeneo

hayo wanalipa na hakuna fedha inayoingia Serikalini.

Mheshimiwa Spika,

Kamati yangu tumependekeza kuwa ili Serikali iweze kupata fedha zinazotokana na utalii

lazima iweke miundombinu ya kisasa ya ya mashine za kieletroniki za ukusanyaji

mapato, ambayo ipo, na wataalamu wake wapo na imeshafanyiwa majaribio pale

uwanja wa ndege na kuleta matokeo mazuri. Miundombinu hiyo iwekwe kwenye

maeneo yote ambayo watalii wanatembelea na kila senti itakayolipwa Serikali itapata

kodi yake.

Mheshimiwa Spika,

Utalii imekuwa ni miongoni mwa sekta kiongozi katika kuchangia mapato ya Serikali,

tukiacha iendeshwe tu na Wawekezaji, kama tunavyoacha sekta ya nishati ya mafuta,

basi wananchi hawataona umuhimu wake, na ile sera ya utalii kwa wote itaonekana

kama imeshindwa kufanya kazi, hivyo basi, Kamati yangu inaitaka Serikali kuwatambuwa

waendesha biashara ya utalii wote (tour operators) kwa kuwaweka chini ya mwamvuli

mmoja kama nilivyoseama awali na kuwatoza kodi kwa mujibu wa sheria. Kamati yangu

imepata taarifa kuwa kuna waendesha biashara ya utalii wengi ambao hawalipi kodi na

wanaendelea kufanya shughuli hizo kinyume na sheria na kuikosesha mapato Serikali.

Endapo watawekwa kwenye mwamvuli mmoja kupitia taasisi za waendesha biashara ya

utalii mfano ZATI au ZATO na kila anayefanya biashara hii akalazimika kutambuliwa na

taasisi hizi, italeta urahisi kuwatambua na kupata kodi ya Serikali.

Mheshimiwa Spika,

Imefika wakati sasa Serikali itoe tamko rasmi kwa waendesha biashara ya utalii

kuhakikisha kuwa malipo yote ya fedha za viza kwa wageni, yanalipwa kwa njia ya kadi

(e-card) badala ya njia ya mkono (cash). Kamati imepata taarifa kuwa wapo baadhi ya

Page 25: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

25

waendesha biashara ya utalii wanaowashawishi watalii kulipa fedha za viza kwa njia ya

mkono (cash) ingawa watalii wenyewe wapo tayari kufanya malipo hayo kwa njia ya

kadi. Sambamba na tamko hilo, Serikali isisite kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria

wale wote watakaokiuka tamko hilo.

Mheshimiwa Spika,

Kamati yangu inasisitia kuwa katika sekta ya utalii, Serikali imekuwa ikipoteza mapato ya

malazi ya wageni katika hoteli, moja ya sababu kubwa ya kukosekana kwa mapato hayo

ni kukosekana kwa takwimu sahihi za malazi ya wageni pamoja na wenye mahoteli

kupokea malipo hayo kupitia akaunti za benki za nje ya nchi. Utaratibu huu unaifanya

ZRB kushindwa kujuwa ni kiasi gani kimelipwa na kinachostahiki kukatwa kodi kwa vile

hawana uwezo wa kufikia akaunti za benki za nje za mahoteli hayo.

Kamati imeona kuwa huu ni ujanja unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya wenye

mahoteli kukwepa kulipa kodi. Kisingizio kinachotumika ni kuwa hakuna mfumo wa

kulipa fedha wa kielekroniki ambao wageni wakiwa nje wanalipa, jambo ambalo kamati

imebaini siyo la kweli, Kamati imekaa na wataalamu wa fedha na kutambua kuwa

mifumo ya malipo ya fedha ya aina yoyote ipo nchini kwetu, ikiwemo mfumo wa

malipo kwa njia za kieletroniki.

Mheshimiwa Spika,

Kamati inapendekeza kuwepo na mfumo huu wa ukusanyaji kwa vile kwanza kama

nilivyoeleza hauna gharama kwa Serikali, wataalamu wapo, teknolojia ipo, mfumo huu

unarahisisha huduma, unaongeza mapato ya Serikali na kupunguza kuvuja kwa mapato

hayo, lakni la muhimu zaidi hata utitiri wa kodi unaepukwa na kuondoa urasimu, kwani

kama kodi italipwa kwa njia ya mashine kila eneo ambalo huduma inatolewa litapata

fedha yake Serikalini ambayo itakuwa imeshalipwa kwa njia ya pamoja (Centralized

system).

Page 26: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

26

Mheshimiwa Spika,

Eneo jengine ambalo Kamati inapendekeza kwa Serikali kulifanyia kazi ili iongeze

mapato yake ni fedha za Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora), bado Serikali

haijalifanyiakazi ipasavyo eneo hili, Kamati imefanya utafiti na kuona kuwa Wafanyakazi

wa kigeni waliopo hapa nchini wanalipa fedha zao za hifadhi ya jamii kupitia kwenye

mifuko ya hifadhi ya nchi zao huku wao wakiwa hapa hapa, matokeo yake ni kuwa

fedha hizo zinafaidisha nchi zao. Kamati inaona kuwa na sisi tungeweka utaratibu

mwepesi kuwezesha wananchi wetu wanaofanyakazi nchi za nje waweze kuleta fedha

zao za hifadhi ya jamii kwa ZSSF, ambazo zingesaidia kujenga nchi yao na kuongeza

mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, eneo jingine mapato ya Serikali yanapotea kwa wingi ni magendo ya

mafuta, kumekua na ujanja mwingi unaofanywa na waingizaji mafuta kwa kushirikiana

na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu katika kupima kiwango halisi cha

mafuta yanayoingizwa Nchini, lakini pia mashirikiano ya baadhi ya wafanyabiashara ya

Magendo ya Mafuta wanaotumia meli ndogo kupakua mafuta Baharini

(TRANSHIPMENT) kabla ya kuletwa kwenye (DEPORT) Maeneo haya mawili ndio hasa

njia kuu za uvujaji wa mapato ya Magendo ya mafuta hapa Nchini, kwa hiyo kamati

yangu ili kupunguza wizi huu basi tunaitaka Serikali kuleta Sheria itakayozuia Makampuni

yanayoingiza Mafuta Nchini kumiliki vituo vyao vya Mafuta na kuuza rejareja kwani

hapo nyuma miaka ya 90 ulikuwepo utaratibu huu na ulisaidia sana udhibiti wa mapato

ya serikali na magendo ya mafuta.

Mheshimiwa Spika,

Kamati kwa kirefu imejeribu kushauri njia mbali mbali za kusaidia Serikali kuongeza

makusanyo ya bajeti yake, bila shaka kama ushauri wa kamati utafanyiwa kazi huenda

tukaondokana na utegemezi wa bajeti kwa kiasi kikubwa pamoja na kupungua nakisi ya

bajeti ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2015/16, Serikali imepanga kukopa Tsh. bilioni

Page 27: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

27

30 kufidia upungufu huo wa bajeti. Pamoja na hivyo, bado tunaamini kuwa vyanzo

vyetu vya mapato tukivisimamia na kuviendesha kitaalamu tunaweza kupanuwa wigo

wa makusanyo kutoka hapa tulipo.

Mheshimiwa Spika,

Katika kuimarisha mapato lazima na kwenye matumizi kuwe na udhibiti, tumeona katika

Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuna mapungufu mengi ya udhibiti

wa matumizi yasiyozingatia taratibu za fedha katika taasisi mbali mbali za Serikali. Ripoti

za Mdhibiti zilizowasilishwa katika Baraza hili zimebainisha mapungufu hayo kwa kirefu.

Kamati yangu inaamini kuwa endapo tutaendelea na kufumbiana macho katika kudhibiti

matumizi yasiyozingatia sheria basi hata tuimarishe vipi vyanzo vya mapato bado

tutakuwa na tatizo la kufikia malengo ya utekelezaji wa bajeti zetu.

Mheshimiwa Spika.

Kamati yangu inaipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa mikikati yake katika

hatua zake za kuimarisha mapato ya ndani kwa mashirikiani ya TRA,ZRB na Ofisi ya

Mtakwimu Mkuu kwa kuanzisha mfumo wa walipa kodi kwa maeneo maalum (BLOCK

MANAGEMENT SYSTEM) kwa kutumia System ya Technologia ya (GPS) ,kuimarisha

UTHAMINI wa Forodha, kupunguza misamaha ya kodi ,n.k kamati yangu iaitaka Serikali

kwa upande wa Forodha bidhaa zote zinazoingia N chini basi zilipiwe kupitia mfumo wa

kibenki kwav kufungwa machine za kukusanya fedha kama ilivyofanyika katika Uwanja

wa Ndege wa A.A.Karume Zanzibar ambao umeonyesha mafanikio makubwa.,

Pia kwa upande wa misamaha ya kodi kamati yangu inaitaka Serikali kutokuridhika na

utoaji wa misamaha tu bali kufuatilia hizo bidhaa zinazosamehewa ushuru je zinatumika

katika maeneo yaliyokusudiwa? Kwani kunataarifa kua baadhi ya vifaa hivyo huingizwa

madukani na kuuzwa na kuikosesha pesa Serikali yetu, lakini pia kufuatilia je ni kweli

Page 28: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

28

bidhaa zinazosamehewa ushuru je zinatumika kwa kutoa unafuu wa huduma kwa

wananchi wetu? Ili msamaha huo uwe na tija kwa jamii yetu.

Mhe Spika, katika kuimarisha mapato kwa mwaka huu unaonzia July 2015/16 kamati

yangu imeridhika na hatua zinazotaka kuchukuliwa katika kuongeza mapato ikiwemo

kuanzisha matumizi ya Machuine za Electrical Fiscal Devices FEDs kamati yangu inaomba

kabla ya kuanza kutumika Machine hizi basi ni vyema kukatolewa semina maalum kwa

wafanya biashara wetu wa Zanziba ili kuepuka matatizo yaliyojitokeza kwa upande wa

TZ,bara ambapo ulileta usumbufu mkubwa kwa wananchi watumiaji wa bidhaa.

Mhe Spika, pia kamati yangu inaomba kutoa angalizo kwa Serikali katika mapitio hayo

ya ada yafanywe kwa uangalifu mkubwa vinginevyo mzigo huo utarudi kwa wananchi

na kupunguza uwezo wao matumizi sambamba na mfumko wa bei.

Mhe Spika, katika marekebisho ya kodi ambapo mswaada wake utakuja baadae

ningelitaka kujua hiyo tozo ya asilimia 2 ya ununuzi wa Umeme imekusudiwa nini kwani

hofu yangu itakua ni kumuongezea mwananchi bei ya Umeme jambo ambalo kamati

yangu haikubaliani nalo kwani litamuongezea mwnanchi ugumu wa maisha, kwani

umeme kwa sasa sio anasa bali ni sehemu ya maisha yetu.

Mhe Spika, kamati yangu inapongeza hatua ya Serikali kuanzisha mifuko mbali mbali ili

kukidhi baadhi ya mahitaji ya lazima kwa wakati muafaka kwani mifuko hiyo tayari

itakua na fedha za kuanzia.

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia naomba kutoa pongezi kwa wajumbe wenzangu wote

wa Kamati ya Wenyeviti kwa mashirikiano makubwa walionipa kwa kipindi chote cha

miaka mitano nikiiongoza kamati hii kwa ruksa yako naomba niwatambue wajumbe hao

kama hivi ifuatavyo.

1) Mhe. Hamza Hassan Juma ====Mwenyekiti,

2) Mhe. Mgeni Hassan Juma === Mjumbe,

Page 29: MUHUTASARI WA HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI YA … · Kwa maana hiyo sasa, Kamati yangu imezingatia vizuri Bajeti iliyoletwa na Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 pamoja na vipaombele

29

3) Mhe. Mahmood Mohd Mussa ==== Mjumbe,

4) Mhe. Mlinde Nassor Juma === Mjumbe,

5) Mhe. Omar Ali Shehe ==== Mjumbe,

6) Mhe. Hija Hassan Hija === Mjumbe,

7) Mhe. Ussi Jecha Simai == Mjumbe,

8) Ndg. Nasra Awadh Salmin === Katibu

9) Ndg. Khamis Hamad Haji ===Katibu

Mhe Spika baada ya hayo naomba kuwasilisha.

Ahsante,

……………………………….

Hamza Hassan Juma,

Mwenyekiti,

Kamati ya Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi,

Zanzibar.