Upload
vankhue
View
959
Download
25
Embed Size (px)
Citation preview
Draft 03
i
MWENGE
KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO
MWENGE
MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA
MAENDELEO YA KANISA 2013-2017
Draft 03
ii
YALIYOMO
1. UTANGULIZI ....................................................................................................................... 1
1.1 Lengo kuu .................................................................................................................... 1
1.2 Historia kwa ufupi ....................................................................................................... 1
1.3 Malengo ya mkakati .................................................................................................... 2
Rasilimali za Kiroho ........................................................................................................... 4
1.3.2 Rasilimali Watu ................................................................................................... 5
1.3.3 Rasilimali Fedha .................................................................................................. 6
1.3.4 Rasilimali Miongozo ............................................................................................ 6
1.3.5 Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu ................................................. 7
1.3.6 Miradi mikuu ya ujenzi ........................................................................................ 7
2. DHIMA, DIRA, NA KAULI MBIU ................................................................................ 8
2.1 Dhima (Mission) ......................................................................................................... 8
2.2 Dira (Vision) ............................................................................................................... 8
2.3 Kauli mbiu (Mission Statement) ................................................................................. 8
3. MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO KUANZIA 2013-2017 .......................... 8
3.1 Mfumo wa uongozi ..................................................................................................... 8
3.2 Idadi ya washiriki na Makisio ya ukuaji wa kanisa kuanzia 2005-2020 ..................... 9
3.3 Mambo muhimu (Key issues) ................................................................................... 10
3.4 Mikakati ya kukabili changamoto zilizoainishwa ..................................................... 11
4. MAENEO YA UTEKELEZAJI KIMKAKATI .............................................................. 11
4.1 Uwakili ........................................................................................................................... 11
4.2 Huduma za Kanisa ......................................................................................................... 12
4.3 Elimu .............................................................................................................................. 12
4.4 Vijana ............................................................................................................................. 12
4.5 Shule ya Sabato .............................................................................................................. 12
4.6 Huduma za watoto .......................................................................................................... 13
4.7 Afya ................................................................................................................................ 13
4.8 Kwaya za Kanisa na vikundi vya uimbaji ................................................................. 13
4.9 Ofisi ya Karani wa Kanisa ............................................................................................ 13
4.10 Mawasiliano ................................................................................................................. 14
4.11 MIUNDO MBINU (Majengo ya kanisa, vyoo, viwanja).......................................... 14
4.11.1 Hali ilivyo sasa ................................................................................................... 14
Draft 03
iii
4.11.2 Maboresho ya Miundombinu (Majengo, Viwanja) ........................................... 14
4.11.3 Uboreshaji wa mandhari ya eneo na Jengo la Kanisa (Mwenge) ..................... 14
................................................................................................................................... 15
4.11.3.1 Faida na Hasara za mapendekezo ya upanuzi wajengo la kanisa la sasa.... 15
4.11.4 Ujenzi wa Jengo la matumizi anuai ................................................................... 16
4.11.5 Majengo Kanisa Makundini ............................................................................... 16
4.11.6 Ukarabati wa nyumba ya mchungaji .................................................................... 17
4.11.7 Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi makao mapya ya ETC ................................... 17
5. MIKAKATI YA KUPATA FEDHA KWAAJILI YA MIRADI YA MAJENGO .......... 17
5.1. Kuanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa ................................................. 17
5.2 Kikosi kazi cha watu 100-200 .................................................................................. 18
5.3 Washiriki wote wa kanisa kuhusishwa...................................................................... 18
5.4 Changizo kutoka watu wa nje ya kanisa kwa njia ya harambee ............................... 18
6. RAMANI YA UTEKELEZAJI ........................................................................................ 19
6.1 Ramani yaa kila mwaka ya utekelezaji wa mpango mkakati ......................................... 19
6.2 Ramani ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi kwa mwaka 2013 ................................. 21
7. BAJETI YA UTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI ..................................................... 23
8. VIELELEZO NA VIAMBATANISHI ........................................................................... 26
8.1 Ramani ya upanuzi wa Kanisa (Sehemu za office .................................................... 26
8.2 Picha au mtazamo wa kisanifu katika picha za pande tatu (3D Views photos) ........ 28
Draft 03
1
1. UTANGULIZI
Mpango ni mfumo wa kimaandishi unaoonesha kazi zinazotakiwa kufanywa na hatua
mbalimbali za kufikia malengo yaliyowekwa kwa muda maalumu. Mpango mkakati husaidia
ufanisi katika utekelezaji na kuweka mpangilio mzuri wa matumizi ya rasilimali. Pia husaidia
kuratibu kazi zote ili kufikia malengo kwa kuweka vipaumbele. Ni muhimu sana kuwa na
mpango mkakati kwa kuwa utatupatia mwelekeo wa ni wapi tunataka kwenda na tutafika
kwa namna gani. Shughuli mbalimbali na maeneo ya kimkakati huwekwa bayana, hii
inasaidia kufahamu nyenzo na raslimali zinazohitajika na namna ya kuzipata. Ugawaji wa
majukumu na dhamana miongoni mwa viongozi au washiriki ni moja ya faida za kuwa na
mpango kazi. Mipango mkakati huwezesha kufanya tathmini kuona kama malengo na
mipango tuliyojiwekea imefanikiwa au haikufanikiwa kama ilivyopangwa.
Kanisa la Mwenge limekuwa na mipango ya muda mfupi mfupi hususani kila mwaka, hali
ambayo haiwezi kutoa dira endelevu kwa kanisa. Hivyo mpango huu ni hatua muhimu katika
kulipatia kanisa dira ya kuliongoza katika mipango mbalimbali bila kujali mabadiliko ya
uongozi yanayofanyika kila mwaka. Hii italiwezesha kanisa kuwa na mipango endelevu
itakayokuwa ikitekelezwa na kila uongozi unapoingia madarakani wakati wa uhai wa
mpango husika.
1.1 Lengo kuu
Lengo kuu la mpango mkakati huu ni kuliongoza katika uendeshaji wa majukumu yake
makubwa ambayo ni: malezi ya washiriki kiroho, uinjilisti, uwakili na majengo kwa kuweka
malengo mahususi na namna ya kufikia malengo hayo ifikapo mwaka 2017.
1.2 Historia kwa ufupi
Kanisa la Waadventista wa Sabato Mwenge ni miongoni mwa makanisa mengi ya
waadventista wa Sabato Tanzania ambalo liko katika eneo la Mwenge, kando kidogo mwa
barabara mpya ya Bagamoyo, likipapakana na zahanati ya Mwenge kijijini wilaya ya
Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.
Kanisa lilianza mwaka 1967 likiwa ni tawi la Shule ya Sabato Lugalo Sergeant Mess. Tawi
liliendelea hadi mwaka 1980 lilipopewa hadhi ya kuwa Kundi la Shule ya Sabato. Kutokana na
matatizo yaliyojitokeza ya kutokuwa na uhuru wa kuingia eneo la jeshi kufanya ibada, mwaka 1981
likawa ni kundi la Kanisa la Magomeni na kuendelea kukua hadi Juni mwaka 1985
lilipotengwa rasmi kwa kupewa hadhi ya kuwa Kanisa kamili na hivyo kutambuliwa rasmi
kuwa miongoni mwa makanisa mahalia ya Waadventista wa Sabato ulimwenguni. Kanisa
liliendelea kukua kwa kuanzisha makundi ambayo nayo yalitengwa kuwa makanisa.
Makanisa ambayo ni zao la Mwenge ni pamoja na Ushindi, Bagamoyo, Lugalo, Tegeta,
Mbezi Beach, Mbezi juu, Kerege na Bunju. Kwa sasa Kanisa lina makundi 7 ambayo ni:
Bumafa, Chivilikiti, Mabwepande, Zinga, Amani, Kimele na Vikawe; pia kuna tawi moja la
shule ya Sabato katika shule ya sekondari ya Lord Barden. Hadi kutengwa kuwa Kanisa,
Kanisa halikuwa na nyumba ya kuabudia, hivyo juhudi zilifanyika za kutafuta kiwanja na
Draft 03
2
hatimaye kiwanja kilipatikana eneo la Mwenge na ujenzi kuanza rasmi mwaka 1989; jengo la
Kanisa kwa wakati huo lilisanifiwa kuwa na uwezo wa kuchukua waumini 900 wakiwa
wamekaa, ujenzi uliendelea hadi mwaka 2000 ulipokamilika.
Baada ya shughuli za ujenzi kukamilika, utaratibu wa kuliweka wakfu ulifanyika. Tarehe 22-
12-2002 jengo la kanisa liliwekwa wakfu rasmi; huduma hiyo ilifanywa na Mchungaji Dr.
Herry Mhando.
Idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka licha ya washiriki wengine
kuhamia makanisa mengine, idadi ya washiriki hadi kufikia Juni mwaka 2012 ilikuwa ni
2,330.
1.3 Malengo ya mkakati Kwa kipindi cha kuanzia 2013 – 2017 kanisa linaazimia kuwa na maeneo makuu ya
kimkakati yafuatayo:
A: Rasilimali za kiroho
Lengo #1: Kuongeza washiriki kwa 100% ifikapo 2017
Lengo #2: Makundi yaliyopo sasa kuwa makanisa ifikapo 2017 (Zinga,
Mabwepande, Kimele, na Bumafa)
Lengo #3: Kuimarisha na kuyawezesha makundi kujitegemea ifikapo
mwaka 2017 au baadaya 2017
Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo
2017
Lengo #5: Kuhakikisha kuwa 70% ya washiriki wana ufahamu mpana
kuhusiana na mtindo na mwenendo wa maisha ya ki-adventista
katika nyanja za afya, elimu, vyakula na vinywaji, na
maburudisho.
B: Rasilimali watu
Lengo #1: Kuelimisha Wainjilisti Walei 15 wanaoweza kutumwa kama
wainjilisti ifikapo mwaka 2017.
Lengo #2: Kusomesha wanafunzi wawili elimu ya uchungaji ifikapo
mwaka 2017
Lengo #3: Kuhakikisha kuwa asilimia tisini (90%) ya wahubiri
wawe na elimu ya homilia ifikapo mwaka 2017
C: Rasilimali fedha
Lengo #1: Kuhakikisha idadi ya washiriki wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango
inaongezeka mara tatu zaidi ya miaka ya nyuma ifikapo 2017
Lengo #2: Kuwezesha asilimia sabini (70% ) ya washiriki wasio na ajira na wale wenye
kupenda kujianjiri na kuanzisha biashara wawe na elimu ya ujasiriamali ya
ujasiliamali ifikapo 2017.
Draft 03
3
D: Rasilimali miongozo
Lengo: Kuhakikisha kuwa 100% ya washiriki wanafundishwa na kuelewa misingi 28 ya
kanisa; waumini na viongozi wawe wamefundishwa kufuata sera na taratibu za
kanisa, na washiriki wawe ameelimishwa kuhusu utumiaji wa maandishi ya Roho
ya unabii ifikapo 2017.
E: Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu
Lengo: Kuhakikisha vitabu 20,000 vinanunuliwa na kusambazwa.
F: Miradi mikuu ya ujenzi
Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa
majengo ya ibada makundini.
Lengo #2: Kukarabati nyumba ya mchungaji
Lengo #3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao mapya ya ETC.
Lengo #4: Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa Jamii
Kwa kila eneo la kimkakati malengo mahsusi yameainishwa katika jedwali hapa chini.
Draft 03
4
Rasilimali za Kiroho
MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA
Lengo 1: Kuongeza washiriki kwa 100%
ifikapo 2017
Washiriki wa makundini wote
wamejumlishwa
Semina za uinjilisti kwa washiriki –kanisani na makundini
mara moja kila robo
Unijilisti kwa njia ya machapisho ikihusisha masomo kwa njia
ya sauti ya unabii, vitabu, vijizuu na magazeti.
Mikutano ya injili ya hadhara mitatu kwa mwaka, mmoja
ukifanyika kupitia radio ya Morning Star 105.3 FM.
Uinjilisti kupitia shule ya sabato: o Vikosi vya shule ya sabato
o Sabato za wageni
o Kuanzisha matawi ya kujifunza biblia kwa kaya zilizo karibu na
kuhusisha wasio washiriki pia.
Elimu ya dini shuleni-vipindi vya dini (uinjilisti na malezi)
o kufikia kila shule iliyopo katika eneo letu la kiutawala
kuimarisha utaandaaji {kila idara/ chama knsn kuweka mkakati wa kuongoa roho}
- Mzee wa kanisa
-Mkuu wa
huduma za kanisa
-Mkurugenzi
VOP
-Mkurugenzi wa
S/Sabato
-Kiongozi wa
uchapishaji
-Mkurugenzi wa
Elimu
-Kiongozi wa
Champlensia
-Sabato ya kwanza ya
kila mwezi
-Mwezi Aprili/Juni
na Septemba/Okt.
-Sabato ya 2 ya
robo
-kila Sabato
-Mei/Oktoba
Lengo 2: Kutenga makundi yaliyopo sasa
kuwa makanisa ifikapo 2017
(Zinga - 2013, Mabwepande -
2014, Kimele- 2015 , Bumafa-
2016, na Vikawe – 2017)
kuwaandaa washirki wa makundini kujitegemea kiroho,
kiuchumi na kijamii.
-Kiongozi wa
Kundi/mzee wa
kanisa
-Sabato ya
kwanza ya kila
mwezi.
Lengo 3:
Kuimarisha na kuyawezesha
makundi kujitegemea
ifikapo mwaka 2017 au baada
ya hapo.
Kuyajengea uwezo wa wa kuimarika, makundi mapya yaanzishwe
pale tu inapobidi. Hii itatupati fursa ya kuyahudumia vyema
makundi yaliyopo sasa kwa kuyawezesha kuwa na nyumba za
ibada zilizokamilika na zenye kuleta utukufu kwa Mungu.
Wazee wa
kanisa/Mchungaji
Mara moja kila
robo
Draft 03
5
Lengo 4: Kuwa na 60% ya washiriki
wanaosoma Biblia na Lesoni
ifikapo 2017
kuwatembelea washiriki nyumbani. kila mshiriki atembelewe
angalau mara moja kwa mwaka.
kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa lesoni kwa njia
tofauti,,,mpesa kwa fue
[[kila idara/chama itengeneze mkakati itakavyohusika na
mpango]]
Wazee wa kanisa
/mashemasi/... /…
/SS, utandaaji/
huduma
Kila sabato
kupitia vipindi
vya mchana
Lengo 5: Kuhakikisha kuwa 70% ya
washiriki wana ufahamu mpana
kuhusiana na mtindo na
mwenendo wa maisha ya ki-
adventista katika nyanja za afya,
elimu, vyakula na vinywaji, na,
maburudisho.
Semina, mafundisho, na mahubiri
- semina mara moja kwa mwezi muda wa mchana
Wazee wa kanisa
/Mchungaji/
Kila sabato
kupitia vipindi
vya mchana
1.3.2 Rasilimali Watu
MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA
Lengo 1:
Kuelimisha wainjilisti walei 15
wanaoweza kutumwa kama
wainjilisti ifikapo 2017.
Kuimarisha mfuko wa uinjilisti hasa kwenye eneo linalohusu
udhamini wa mafunzo ya uinjilisti.
Mchungaji wa
Mtaa
N/A
Lengo 2:
Kusomesha mwanafunzi wawili
elimu ya uchungaji ifikapo 17.
Kutenga sehemu kidogo kutoka katika bajeti ya kanisa
Kutumia washiriki wa kanisa kuchangisha pesa
Mchungaji wa
Mtaa
Mratibu wa
mpango
atakayechaguliwa
na uongozi wa
kanisa
N/A
Lengo 3:
90% ya wahubiri wawe na elimu
ya homilia ifikapo 2017
Semina ifanyike mara moja kwa mwaka
Mchungaji wa
Mtaa
Mara moja au
mbili kwa mwaka
Draft 03
6
1.3.3 Rasilimali Fedha
MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA
Lengo 1
Kuhakikisha idadi ya washiriki
wanaorudisha zaka na wanaotoa
kwa mpango inaongezeka kwa
asilimia hamsini (50%) ya
washiriki.
Mafundisho/mahubiri/Semina za zaka na sadaka kila mwezi (wiki
ya mwisho)
Kiongozi/Katibu
wa Uwakili na
Maendeleo
kanisani
Mchungaji
Wazee wa
kanisa
Mara moja kila
mwezi. Wiki ya
mwisho ya kila
mwezi
Lengo 2
Kuwezesha 70% ya washiriki
wasio na ajira wawe na elimu ya
ujasiliamali na wale wanaopenda
kuanzisha na kuendeleza biashara
wawe na elimu ya ujasiriamali.
Washiriki wa ndani watumike kufundisha mara moja kwa kila robo
na utaratibu maalumu uwekwe kuratibu semina hizo.
ATAP wahusishwe katika kufanikisha azima hii
Kiongozi/Katibu
wa Uwakili na
Maendeleo
kanisani
Kiongozi wa
ATAP
Mara mbili kwa
kila mwaka
1.3.4 Rasilimali Miongozo
MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA
Lengo: 1
Kuhakikisha kuwa 100% ya
washiriki wanafundishwa na
kuelewa masomo muhimu
yafuatayo :
misingi 28 ya kanisa
kufuata sera na taratibu za
kanisa
utumiaji wa vitabu vya Roho
ya Unabii.
Mahubiri/mafundisho na semina zifanyike mara mbili kwa robo
Washiriki waelezwe kuhususiana na vitabu bora na vya uhakika
ambavyo havikuchakachuliwa.
Mchungaji
Wazee wa
kanisa
Kiongozi wa
Roho ya unabii
Kila sabato
kupitia vipindi
vya mchana na
pia kupitia
mahubiri ya
ibada kuu.
Draft 03
7
1.3.5 Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu
MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA
Lengo: 1
Kuhakikisha vitabu 20,000
vitanunuliwa na kusambazwa.
Uhamasishaji na kila mshiriki ahakikishe amechangia angalau
vitabu 5 kila mwaka kwa miaka mitano hadi 2017.
Mkurugenzi wa
Uchapishaji
kanisani
Mara moja kila
robo ya mwaka.
1.3.6 Miradi mikuu ya ujenzi
MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA
Lengo: 1
Kufanya ukarabati mkubwa wa
jengo la kanisa na kukamilisha
ujenzi wa majengo ya ibada
makundini.
Kukusanya michango kutoka kwa washiriki au familia hadi 200
watakao kuwa tayari kuchangia shilingi 1,000, 000 kila mmoja kwa
mwaka.
Kwa kutumia michango kutoka kwa washiriki wote
Changizo kutoka kwa watu mbalimbali ndani na nje ya kanisa
Kiongozi /
kamati ya
majengo
Mzee wa
kanisa
Kamati ya
uwakili-
(Maendeleo)
Endelevu hadi
lengo lifikiwe
kwa kuanzia na
mwaka 2013
Lengo: 2
Kukarabati nyumba ya mchungaji
Kutumia sehemu ya bajeti ya kanisa kadri itakavyoamuliwa na
baraza la kanisa na, au mashauri ya kanisa kulingana na mgawanyo
wa mtaa
Michango ya washiriki
Kamati ya
majengo
Mzee wa
kanisa
Wakati wowote
itakapohitajika
Lengo: 3
Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi
makao makuu mapya ya ETC.
Kutumia sehemu ya bajeti ya kanisa kadri itakavyoamuliwa na
baraza la kanisa na au mashauri ya kanisa
Michango ya washiriki
Kamati ya majengo
Mzee wa kanisa
Wakati wowote
itakapohitajika
Lengo: 4
Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa
Jamii
Kukusanya michango kutoka kwa washiriki au familia hadi 200
watakao kuwa tayari kuchangia shilingi 1,000, 000 kila mmoja kwa
mwaka.
Ramani ya jengo na michoro yote iwe tayari ifikapo Septemba
2013 (Architectural drawing, Structural drawing, Plumbing
drawings, Electrical drawings)
Kiongozi /
kamati ya
majengo
kanisa la
Mwenge
Mzee wa
kanisa
Endelevu hadi
lengo lifikiwe
Draft 03
8
2. DHIMA, DIRA, NA KAULI MBIU
2.1 Dhima (Mission)
Dhima yetu ni kutekeleza agizo kuu la utume wa Yesu la Mathayo 28:19,20 na kushuhudia
ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12 kwa watu wa mataifa yote ili wampokee Yesu
kuwa Bwana na mwokozi wao na waweze kujiunga na kanisa la Mungu la masalio
kuhudumia jamii na kujiweka tayari kwa marejeo yake mara ya pili.
2.2 Dira (Vision)
Kuwa kanisa la mfano nchini Tanzania na duniani lenye kumpenda Mungu na kushuhudia
upendo wake kwa ajili ya wokovu wa kila mmoja kabla ya marejeo yake mara ya pili
kuwachukuwa wateule wake mbinguni (Mathayo 22:37-39).
2.3 Kauli mbiu (Mission Statement)
Kutangaza injili ya milele kwa watu wote katika muktadha wa ujumbe wa malaika wa tatu
wa Ufunuo 14:6-12.
3. MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO KUANZIA 2013-2017
3.1 Mfumo wa uongozi
Kanisa la Mwenge linaongozwa na Mchungaji anayesaidiana kwa karibu na wazee wa
kanisa ambao wanawajibika kwa baraza la kanisa katika kuongoza shughuli za kila siku za
kanisa. Kikao kikubwa cha maamuzi ya mwisho ni mashauri ya kanisa ambayo ndiyo kikao
kikubwa chenye kufanya maamuzi muhimu kwa ajili ya kanisa. Muundo wa uongozi uko
kama ulivyoonyeshwa kwenye mchoro hapa chini.
Draft 03
9
3.2 Idadi ya washiriki na Makisio ya ukuaji wa kanisa kuanzia 2005-2020
Kwa mujibu wa taarifa ya mwezi June 2012 kanisa la Mwenge lina washiriki wapatao
…………… Katika kipindi cha miaka mktano iliyopita idadi ya washiriki ilikuwa kama
ifuatavyo:
Mwaka Idadi ya washiriki
2007
2008
2009
2010
2011
June 2012
Kwa kuzingatia ukuaji wa kanisa kwa ongezeko la watani wa washiriki ………….. kwa
mwaka. Matarajio ya ongezeko la washiriki ifikapo mwaka 2020 ni washiriki wapatao
………
Hii inaleta changamoto ya miundo mbinu hasa jengo la ibada kukabiliana na ongezeko hili.
Baraza la Mashauri ya Kanisa
Baraza la Kanisa
Wazee wa Kanisa
Maofisa wasimamizi
(Karani mkuu, Mhazini, Shemasi mkuu
Maofisa watendaji
(Wakuu wa Idara za Kanisa)
Mchungaji
Draft 03
10
3.3 Mambo muhimu (Key issues)
Ili kujiweka katika mazingira ya kujitambu na kuweka malengo na mbinu za kusonga mbele ,
mambo muhimu yameainishwa hapa chini kuonyesha uwezo wetu, udhaifu na fursa tulizo
nazo. Hii itatuwezesha kupanga na kutekeleza maeneo ya vipaumbele.
Uwezo tulionao
Washiriki
Kanisa lina idadi kubwa ya washiriki wa jinsi zote za na rika zote
Kanisa lina washiriki wengi wenye taaluma na ujuzi mbalimbali
Kanisa lina washiriki wenye uchumi mzuri kwa maana ni waajiriwa na
wafanya biashara
Kanisa lina washiriki wenye mwitikio wa kujitoa kufanya kazi ya Mungu
na kuchangia maendeleo ya kanisa katika nyanja mbalimbali
Mali za kanisa
Kanisa lina mali kadha ikiwemo viti, meza, vyombo vya meza ya Bwana, na
vyombo vya mawasiliano. Pia lina Majengo ya kanisa japo yanahitaji
kukarabatiwa na viwanja vya kanisa
Uzoefu (kuanzia mwaka 1981)
Kanisa linauzoefu wa muda mrefu wa kuanzia mwaka 1981, hii ni takribani miaka 31
Tuko mjini kijiografia
Kanisa liko sehemu nzuri kijiografia na linafikika kwa urahisi kutoka pande zote za
jiji la Dar es Salaam.
Udhaifu na changamoto
Kanisa halina mipango endelevu
Utunzaji hafifu wa kumbukumbu mbalimbali za kanisa
Mawasiliano hafifu kunasababisha muingiliano wa majukumu
Mahudhurio hafifu sana katika vipindi vya mchana
Udhaifu katika utunzaji wa wakati kwenye ibada
Udhaifu katika makabidhiano ya kazi mwisho wa mwaka,
Udhaifu katika kutayarisha na kuwasilisha taarifa kwa wakati hasa za kila robo
Mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi kwa mujibu wa taratibu zilizoainishwa na
kanuni ya kanisa.
Kushindwa kufahamu washiriki walipo, wanapoishi na uwezo wao kiuchumi
Kufuatilia michango mbalimbali itolewayo na washiriki hususani ahadi
Mahudhurio hafifu ya washiriki katika vikao vya mashauri ya kanisa
Draft 03
11
Fursa zilizopo
Kuweka miradi ya kanisa kwenye maeneo tuliyonayo
Kuweza kutumia rasilimali watu tulionao na rasilimali walizo nazo washiriki
Tunao marafiki wetu wengi wanaoweza kutuchangia na kutusaidia
Changamoto
Kukusanya rasilimali fedha kutoka ndani na nje ya kanisa (zaka, sadaka, na
michango mingine)
Kuwafikia washiriki wote na kuwetambelea
Urasimu uliopo - tukitaka kufanya mambo yetu kwa wakati tunahitaji kupitia
utaratibu wa kirasimu kiuongozi
Mfumo wa uchaguzi – inaonekana kuwa washiriki wanachaguliwa katika nafasi
mbalimbali za uongozi ni walewale karibu kila mwaka.
3.4 Mikakati ya kukabili changamoto zilizoainishwa
Ili kukabiliana na changamoto zilizoainishwa, mambo yafuatayo yanapendekezwa:
Kutumia madarasa ya shule ya sabato kuwafikia washiriki kwa njia ya kutembeleana
Kuboresha mfumo wa uwekaji kumbukumbu wa kanisa (Database)
Kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa fesha za kanisa hasa katika maeneo ya majengo
na uinjilisti.
Semina zitolewe kuhusiana na uchaguzi wa maofisa wa kanisa
Tuweke sehemu ya kutunza vitu na tuwaelemishe watu jinsi ya kutunza kumbukumbu
Kutoa mafunzo ya utawala kwa maofisa wa kanisa
Ili kuongeza na kuhamasisha utoaji wa zaka, sadaka na michango mingine, tangazo
kuhusiu utoaji liwekwe kwenye jalida la matangazo (Bulletin) muda wote wa mwaka
Washiriki watembelewe kuhimizwa kutoa zaka na sadaka na kufundishwa somo la
uaminifu.
Washiriki wote kuanzia kwa wachungaji, wazee wa kanisa na maofisa wote
kuhimizwa kuzingatia uwakili wa muda katika utendaji.
4. MAENEO YA UTEKELEZAJI KIMKAKATI
Kanisa litatekeleza mpango wa maendeleao unaohusisha idara zake zote za kanisa, na pia
kuweka kipaumbele maeneo maalumu ya kimkakati.
4.1 Uwakili
Uwakili ni eneo muhimu sana kwa ukuaji wa kanisa kiroho na kiuchumi kwa kuwa
unahusisha kila kitu katika maisha ya mkristo. Baadhi ya mambo muhimu katika uwakili
ambayo kanisa linapaswa kuboresha na kuongeza juhudi ni pamoja na:
Uwakili wa wakati
Kuwahi katika ibada za siku ya Sabato
Kufuata muda katika ratiba za siku ya ibada
Uwakili wa mali za bwana
Draft 03
12
Majengo ya kanisa, viti, mazingira
Zaka na sadaka
Uwakili wa uwezo alionao mtu/mshiriki mmoja mmoja.
4.2 Huduma za Kanisa
Hudama za kanisa zinahusisha mipango inayolenga ukuaji wa kanisa kiroho na kuunganisha
baadhi ya idara katika majukumu na utendaji, hii ni pamoja na kupanga:
Mipango ya uinjilisti hususani mikutano ya hadhara
Semina za malezi ya kanisa (kiroho)
Uelimishaji kuhusiana na mambo mbalimbli ya uhai wa washiriki na kanisa kwa
ujumla.
4.3 Elimu
Katika kukabiliana na changamoto za elimu kwa watoto na vijana wetu, kanisa halina budi
kuwa na mipango madhubuti kwa ajili ya kuanzisha shule za awali hadi za sekondary. Hivyo
basi, kanisa azimia kuweka mipango ya elimu kama ifuatavyo:
Kuanzisha shule ya chekechea
Kuanzisha mfuko wa maendeleo ya elimu
Kutoa huduma za elimu ya dini mashuleni
4.4 Vijana
Vijana ni nguzo kubwa ya kanisa katika nyanja zote, hivyo wanapaswa kuandaliwa
kulitumikia na kuliwezesha kanisa kupitia raslimali watu na fedha. Kwa hiyo, kanisa
linakusudia kuwaimarisha vijana katika maeneo yafuatayo
i. Kutoa mafunzo ya ujasiriamali
ii. Kuongeza mafundisho ya kiimani ili kutengeza/kuandaa kanisa la kesho
iii. Kuhamasisha vijana wengi zaidi washiriki kwenye vyama na shughuli zinazowahusu
iv. Kuimarisha vyama vya vijana
v. Kutumia vyama vya vijana kuwapa mafundisho ya ujuzi ili kukabiliana na
changamoto za maisha
4.5 Shule ya Sabato
Shule ya Sabato ni moyo na uhai wa kanisa. Kanisa linakusudia kuendelea kuboresha shule
ya sabato kama ifuatavyo:
i. Kuimarisha vikosi vya madarasa ya shule sabato
ii. Kutembeleana na kufanya uinjilisti kule mitaani kwetu na uhamasishaji wa kusoma
lesoni na biblia
iii. Ualikaji wa wageni-liwe jambo la kudumu
Draft 03
13
4.6 Huduma za watoto
Huduma za watoto ni jambo muhimu kwa kanisa na kwa jamii nzima. Huduma kwa watoto
zinalenga kukuza imani ya watoto wakiwa hawajazaliwa hadi wafikishapo umri wa miaka 14
wakiongozwa na kukua katika maadili ya Kikristo na kutambua mfumo wa kanisa. Hivyo,
kanisa litaendelea kuwapa umuhimu unaostahili watoto kwa kuwapa huduma za kiroho na
kijamii ili wakue ndani ya kanisa wakiwa na madili yanayofaa wakionyesha mfano mzuri
wakiwa watoto wakristo wa adventista. Hii ni kwa kuwa watoto wana upeo mwepesi wa
kushika mafundisho ya injili na wana uwezo wa kuyaweka katika vitendo maishani mwao.
4.7 Afya
Kanisa lina amini katika wajibu wa kumfanya Kristo ajulikane ulimwenguni ni pamoja na
wajibu wa kiroho wa kutunza utu wa binadamu kwa kuhakikisha usalama wa afya yake
kimwili, kiakili na na kiroho. Kanisa linakusudia kuendelea kutoa huduma za elimu ya afya
kwa uana wake wote kwa nia ya kuzuia magonjwa na kutoa elimu ya afya itakayowawezesha
washiriki kuwa na afya njema katika maisha yao hasa kuhusiana na vyakula, vinyaji na
maburudisho.
4.8 Kwaya za Kanisa na vikundi vya uimbaji
Huduma ya kwaya au nyimbo ni muhimu katika ibada kwa kuongoa roho kupitia ujumbe wa
injili unaoimbwa katika nyimbo. Kanisa litadumisha huduma za kwaya na uimbaji kupitia
vikundi vilivyojiambatanisha na huduma za uimbaji ili kuhakikisha kuwa nyimbo, na aina ya
muziki wa dini unaimbwa na kupigwa kanisani unafuata misingi ya kiadventista. Kwa
kuzingatia mafunuo na mafundisho kuhusu muziki, kanisa litasimamia weledi katika muziki
wa kidini unaoimbwa na kwaya na vikundi vyote kanisani, na kuhakikisha kuwa uimbaji na
upigaji wa ala za muziki usiofaa au usioendana na Biblia unaachwa mara moja, mfano
midundo ya ngoma na mchanganyiko wa manyanga kwenye nyimbo unaachwa mara moja.
Mkazo utawekwa katika kufundisha elimu ya muziki kwa waimbaji wote pamoja na
mafunzo ya vinanda ili waimbaji waimbe nyimbo zilizochezwa kwa weledi mkubwa kwa
kinanda pasipo kutumia midundo kuongoza muziki, bali muziki uongoze nyimbo.
4.9 Ofisi ya Karani wa Kanisa
Hii ni ofisi muhimu sana katika uendeshaji wa shughuli za kanisa na utunzaji wa
kumbukumbu.. Ofisi hii inatakiwa iwezeshwe kwa kupatiwa vifaa vya kisasa vya kufanyia
kazi. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo ofisi hi itawezeshwa kwa kupatiwa nyenzo
zifuatazo:
1. Kompyuta mpya
2. Printer yenye kasi (high speed printer)
3. Machine ya kudurufia (photocopier machine)
Draft 03
14
4.10 Mawasiliano
Mawasiliano ni nyenzo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa walengwa. Ili kuwepo
mawasiliano mazuri kanisani, hatuna budi kujizatiti kuwa na vifaa bora nyenye kiwango cha
juu cha ufanisi. Hivyo, kanisa linakusudia kuboresha mfumo wa mawasiliano kanisani kwa
kununua vifaa vya kisasa vya mawasialino vifuatayo:
i. Mfumo mzima wa vipaza sauti na nyenzo zake (Complete PA system and
accessories)
ii. Kununua kinanda kikubwa kwa ajili ya ibada (Church Piano/Organ)
iii. Kununua LCD screen 4 za dijitali
iv. Kununua vifaa vya ukalimani (Translation equipments)
4.11 MIUNDO MBINU (Majengo ya kanisa, vyoo, viwanja)
Kanisa linakusudia kuweka msisitizo mkubwa katika kuimarisha miundo mbinu ya kanisa
hasa majengo, viwanja na huduma msingi kwa kanisa na makundi yake yote, ili kuweka
mazingira mazuri ya ibada na utendaji mzuri wa kazi ya Mungu.
4.11.1 Hali ilivyo sasa
Kwa sasa jengo la kanisa linachakaa na kuhitaji kufanyiwa ukarabati na marekebisha
makubwa ya sakafu, kuondoa paa la Asbestos, kurekebisha madirisha na kuangalia
uwezekano wa kuweka vipoza hewa (air conditioning) kwa ajili ya kukabiliana na hali ya joto
la Dar es salaam. Pia kiwanja cha kanisa hakijafanyiwa landscaping na kupanga vizuri
maeneo kwa ajili ya kuegesha magari.
Kanisa lina choo cha kisasa ambacho kipo katika hali nzuri na kinahudumiwa vizuri kwa
usafi muda wote wa wiki. Kanisa pia lina kisima cha ubatizo ambacho hakiko katika hali
nzuri kiafya. Hii inaleta changamoto ya kufanya maboresho katika kisima hiki.
4.11.2 Maboresho ya Miundombinu (Majengo, Viwanja)
Kwa kuzingatia mahitaji ya baadaye ya kanisa, na hali ya sasa ya uchakavu wa kanisa; ni
njozi yetu kuwa na mpango mkakati wa kuwezesha kanisa kuwa na nyumba nzuri ya ibada.
Njozi hii ni pamoja na kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la ibada la sasa kwa kuliongeza
(kulipanua) au kwa kwenda juu (vertical extension) au kwa kulipanua kiusambamba
(horizontal extension). Hii itaendana na uandaaji wa eneo la kanisa kwa ajili ya kutengeza
mandhari ya eneo la kanisa na maegesho ya magari (landscaping and car parking lots).
Kwa upande wa makundi, ni kusudi letu kukamilisha ujenzi wa nyumba za ibada katika
makundio yote na kuweka vifaa muhimu kwa ajili ya ibada.
4.11.3 Uboreshaji wa mandhari ya eneo na Jengo la Kanisa (Mwenge)
Kanisa lina azimia kuweka jitihada ya kuboresha mazingira ya eneo la kanisa. Maboresho
hayo yatahusisha mabadiliko makubwa kwenye jengo la kanisa na mandhari yote ya eneo la
kanisa. Kanisa linakusudia kufanya ukarabati mkubwa na maboresho kwenye jengo la sasa
Draft 03
15
ili kukidhi ongezeko la washiriki, na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kinda na mafundi
mitambo. Katika kutekeleza nia hii, yafuatayo yapaswa yatekelezwe:
Kufanya upanuzi na maboresho ya eneo la kanisa utakaohusisha mambo
yafuatayo:
o Kuongeza nafasi kwa ajili ya office ya karani, mchungaji, mashemasi,
wazee, na wahazini kwa kuongeza kwa mita tatu sehemu ya jengo la
kanisa zilipo ofisi za sasa;
o Kujenga ndani kisima cha ubatizo;
o Kupanua kanisa ili kuongeza nafasi kwa ajili ya kuwezesha kuchukua watu
wengi zaidi. upanuzi waweza kufanyika kwa kwenda juu (vertical
extension) au kwa upanda upande (horizontal extension). Faida na hasara
za kila kila chaguzi zimeainishwa katika kipengele 4.12.3.1 na 4.12.3.2
o Kuboresha sakafu kwa kuweka sakafu mpya ya kisasa na yenye kudumu
muda mrefu;
o Kurekebisha paa la kanisa na kuondoa asbestos;
o Kutengeneza mandhari ya eneo la kanisa (landscaping);
o Kujenga mfumo wa kutolea maji ya mvua;
o Kuweka vipoza hewa kwenye ofisi zote za kanisa.
Kufanya matengenezo ya uzio kwa kupaka rangi na kuweka bango elekezi la
mawasiliano;
Kutengeneza au kuboresha barabara ya kuingilia kanisani kwa kuweka moram na
kushindilia;
Kuweka uzio katika nyumba ya mchungaji.
Kuweka uzio katika nyumba ya mlinzi
(a) Sehemu ya kanisa ilivyo kwa sasa (b) Kisima cha ubatizo kinavyoonekana kwa
sasa
4.11.3.1 Faida na Hasara za mapendekezo ya upanuzi wajengo la kanisa la sasa
Upanuzi kwenda juu (Vertical extension)
Faida zake
Matumizi mazuri ya nafasi ya juu (good use of sky space) na eneo la kanisa
halitapungua
Jengo la kanisa litakuwa na mwonekano mzuri (aesthetics)
Draft 03
16
Changamoto zake
Zinahitaji fedha nyingi kwa wakati mmoja ili kutekeleza
Kanisa halitakuwa likitumika kwa ibada wakati wa ujenzi, hii itasababisha kanisa
kuingia gharama kukodisha mahema ili kufanyia ibada nje wakati ujenzi ukiendelea
kwa kipindi chote.
Ujenzi lazima ufanyike wote kwa mara moja
Upanuzi kwenda upende upande (Horizontal l extension)
Faida zake
Ibada wakati wa ujenzi zitaendelea ndani ya kanisa
Haihitaji uwekezaji mkubwa sana na ujenzi unaweza kufanywa kwa awamu
Changamoto zake
Nafasi ya eneo la kanisa itapunguka
Mwonekana wa kanisa hautakuwa mzuri (aesthetics)
4.11.4 Ujenzi wa Jengo la matumizi anuai
Ujenzi wa jengo kubwa la kisasa kwa matumizi mbalimbali ya kanisa ikiwa ni pamoja na
sehemu ya ibada kwa watoto unapaswa kutekelezwa ili kukabiliana na baadhi ya changamoto
zilizoanishwa hapo juu. Kwa mfano, jengo hilo litakapokamilika litakuwa limepatia
ufumbuzi tatizo la ufinyu wa ofisi za idara za uangalizi (Ofisi ya wazee, karani wa kanisa,
mhazini) na store kwa ajili ya utunzaji wa vifaa vya kanisa. Hivyo, basi michoro na mipango
ambayo ilikwishaanza miaka ya nyuma inapaswa iendelezwe. Gharama isiwe ni kikwazo cha
kutokuanza kwa mradi huu. Kwa kuwa tayari kanisa lilishaingia gharama kubwa kusanifu
michoro ya jengo husika, inapendekezwa kwamba michoro ya usanifu ujenzi wa jengo
upitishwe rasmi na kanisa ili taratibu zingine za kutafuta vibali vya ujenzi kutoka mamlaka za
manispaa ziweze kuendelea.
Ni vyema mradi huu usikwamishwe kwa sababu za matumizi ya jengo kwani matumizi
yanaweza kubadilishwa pasipo kukwamisha mradi husika.
4.11.5 Majengo Kanisa Makundini
Ni kusudi la Kanisa kuhakikisha kuwa ujwnzi wa majengo ya ibada makundini unakamilika
kwa ukamilifu ili ibada zifanyike katika nzuri na yenye utukufu. Hivyo, majengo ya kanisa
katika makundi yaliyoainishwa katika vipengle hapa chini yatakamilishwa kwa kuwekewa
sakafu, madirisha na viti ili yafae kwa ibada. Gharama za kukamisha ujenzi wa majengo haya
zimeainishwa katika jedwali la gharama za utekelezaji mpango mkakati.
Draft 03
17
Bumafa
Chivilikiti
Mabwepande
Zinga
Amani
Kimele
Mnyambe
Mpekeso
4.11.6 Ukarabati wa nyumba ya mchungaji
Kulingana na sera za kanisa, mtaa unapaswa kumjengea na ama kukarabati nyumba ya
mchungaji. Hivyo, Kanisa la Mwenge litachangia sehemu yake kwenye ukarabati wa
nyumba ya mchungaji pale itakapohitajika kulingana na mgawanyo wa uchangiaji katika
mtaa wa Mwenge.
4.11.7 Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi makao mapya ya ETC
Kanisa litachukua jukumu la kuchangia sehemu yake kwenye mchango wa mtaa pale
gharama halisi za ujenzi huo zitakapokuwa zimeainishwa na kugawanywa kwenye makanisa
ya mtaa wa. Mchungaji wa mtaa anapaswa kuulizia gharama hizi kutoka ofisi ya Konferensi.
5. MIKAKATI YA KUPATA FEDHA KWAAJILI YA MIRADI YA MAJENGO
Ili kutekeleza mipango yote iliyoainishwa katika mpango huu, kiasi kikubwa cha fedha
kinahitajika. Fedha hizi zinapaswa kutafutwa kutoka vyanzo mbalimbali, wahusika wakuu
wakiwa ni washiriki wenyewe. Pia kunahitajika mikakati mahususi kuhakikisha yote
yaliyopangwa na kukubaliwa na washiriki yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
Mapendekezo ya kupata fedha ni yafuatayo:
1. Kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kanisa utakao
hamasishwa na idara ya uwakili kwa kushirikiana na idara ya majengo
2. Kuwa na kikosi kazi cha washiriki wachache watakaoongoza changizo za
ujenzi.
3. Kuwashirikisha washiriki wote katika kuchangia shughuli za maendeleo ya
kanisa.
4. Kuendesha harambee za kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi
5.1. Kuanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa
Inapendekezwa kuanzishwa kwa mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa. Mfuko huu
utakuwa maalumu kwa ajili ya miradi mikubwa ya ujenzi wa makanisa na jengo la huduma
kwa matumizi anuai. Washiriki wataombwa kuchangia katika mfuko huu kila wiki kwa kadri
wanavyobarikiwa, na pia kuwe na changizo maalumu kwa ajili hiyo.
Draft 03
18
5.2 Kikosi kazi cha watu 100-200
Ili kuwezesha kazi ya ujenzi wa jengo la matumizi mbalimbali unafanyika, kuwe na kikosi
ongozi cha watu au familia 100 hadi 200 zitakazoombwa kuchangia kila mtu/familia kuanzia
kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa mwaka; lengo ni kukusanya kiasi cha Shilingi 100,000,000
hadi 200,000,000 kwa mwaka kinachohitajika kwa kuanzia ili kutekeleza miradi mikubwa ya
ujenzi ambayo itatekelezwa kwa kufuata kipaumbele kwa kuanzia na: 1. Maboresho na
upanuzi wa jengo la kanisa, na 2. ujenzi wa jengo la matumizi mbalimbali.
5.3 Washiriki wote wa kanisa kuhusishwa
Kwa kuwa ushiriki wa washiriki wote ni muhimu kwa kila kazi ya kanisa, washiriki wote
watakuwa sehemu ya kuchangia kwa kutumia njia mbalimbali zifuatazo:
○ Fomu za kuchangisha watu mbalimbali kwa kila mshiriki (wasio washiriki wa
mwenge, na pia kwa watu wengine wa madhehebu mengine na kwa marafiki)
kwa kuomba vibali vya kitaifa na kanisa.
○ Uchangiaji kwa njia ya simu i.e. tuma neno Mwenge kwenda 15555 kwa
kutumia mitandao ya simu iliyopo kama vodacom, airtel n.k.
○ Uuzaji wa bidhaa za kanisa kwa bei ya juu kidogo kwa washiriki na watu
wengine i.e Tshirts, Kalenda n.k.
○ Washiriki wa mwenge wa zamani kuhusishwa (ndani na nje ya nchi).
○ Kuweka Magoli kwa kila mshiriki/familia
○ Kila mshiriki apeleke kadi maalumu zilizochapwa majina kwa watu watano
wa karibu (wasiwe washiriki wa mwenge na au wawe ni marafiki,
wafanyakazi wenzetu katika sehemu za kazi n.k)
○ Kutoa matangazo ya changizo kupitia Morning Star radio
5.4 Changizo kutoka watu wa nje ya kanisa kwa njia ya harambee
Kanisa halijatumia ipasavyo fursa ya kufanya harambee za uchangiaji zenye kuwahusisha
watu wasio washiriki wa kanisa la waadventista wasabato katika kuchangia shughuli za
maendeleo. Hivyo, inapendekezwa kwamba njia hii itumike pia kama sehemu ya mkakati wa
kukusanya pesa. Harambee iliyotayarishwa vizuri kwa kuwaalika watu wenye nafasi kubwa
serikalini na katika taasisi za umma na watu binafsi ifanyike, hii itakuwa katika mfumo
ufuatao:
Ifanyike nje ya eneo la kanisa
Iwe ni katika mfumo wa chakula cha jioni (dinner)
Michoro ya kanisa na model zake iwe tayari wakati wa harambee
Kamati maalumu iundwe kuandaa harambee hii ili kuangalia sehemu ya kufanyia harambee,
watu wa kualikwa, utaratibu utakaotumika unaozingatia misingi ya kanisa n.k
Draft 03
19
6. RAMANI YA UTEKELEZAJI
6.1 Ramani ya kila mwaka ya utekelezaji wa mpango mkakati
2013 2014 2015 2016 2017 IDARA HUSIKA
A: RASILIMALI ZA KIROHO
Lengo 1: Kuongeza washiriki kwa 100% ifikapo 2017 20% 20% 20% 20% 20% Wazee wa Kanisa
Mchungaji
Huduma
Shule ya Sabato
Lengo 2: Kutenga makundi yaliyopo sasa kuwa makanisa ifikapo 2017 Zinga M'Pande Kimele Bumafa Vikawe
Lengo 3: Kuimarisha na kuyawezesha makundi kujitegemea ifikapo mwaka 2017 au baada ya
hapo. Zinga M'Pande Kimele Bumafa Vikawe
Lengo 4:
i). Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia na Lesoni ifikapo 2017 10% 15% 15%
15%
15%
Wazee wa Kanisa
Huduma
Shule ya Sabato
ii). Kuhakikisha kuwa 70% ya washiriki wana ufahamu mpana kuhusiana na mtindo na mwenendo wa
maisha ya ki-adventista katika nyanja za afya, elimu, vyakula na vinywaji, na, maburudisho.
10% 15% 15% 15% 15% Afya na Kiasi
Elimu
Uwakili
B: RASILIMALI WATU
Lengo 1: Kuelimisha wainjilisti walei 15 wanaoweza kutumwa kama wainjilisti ifikapo 2017. 3 3 3 3 3 Wazee wa Kanisa
Mchungaji
Huduma
Lengo 2: Kusomesha mwanafunzi wawili elimu ya uchungaji ifikapo 17 Hezron Mgwenya & Nathaniel
Wazee wa Kanisa
Mchungaji
Huduma
Lengo 3: 90% ya wahubiri wawe na elimu ya homilia ifikapo 2017 15% 15% 20% 20% 20% Mchungaji
Draft 03
20
2013 2014 2015 2016 2017 IDARA HUSIKA
C: RASILIMALI FEDHA
Lengo 1: Kuhakikisha idadi ya washiriki wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango
inaongezeka kwa asilimia hamsini (50%) ya washiriki.
10% 10% 10% 10% 10% Mchungaji
Wazee wa Kanisa
Uwakili
Lengo 2: Kuwezesha 70% ya washiriki wasio na ajira wawe na elimu ya ujasiliamali na
wale wanaopenda kuanzisha na kuendeleza biashara wawe na elimu ya ujasiriamali.
10% 15% 15% 15% 15% ATAP
Uwakili
Huduma za wanawake
D: RASILIMALI MIONGOZO
Lengo1: Kuhakikisha kuwa 100% ya washiriki wanafundishwa na kuelewa masomo
muhimu yafuatayo :
20% 20% 20% 20% 20%
Mchungaji
Wazee wa Kanisa
Roho ya Unabii
Idara ya huduma · misingi 28 ya kanisa
· kufuata sera na taratibu za kanisa
· utumiaji wa vitabu vya Roho ya Unabii.
E: MRADI WA KUSAMBAZA KITABU CHA PAMBANO KUU
Lengo 1: Kuhakikisha vitabu 20,000 vitanunuliwa na kusambazwa 4000 4000 4000 4000 4000 Wazee wa Kanisa
Roho ya Unabii
F: MIRADI MIKUU YA UJENZI
Lengo 1: Kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa
majengo ya ibada makundini.
Mwenge
kukusanya
200,000,000
na kuanza
upanuzi wa
ofisi za kanisa
Kuendelea
kukusanya
fedha za
ujenzi
Kuanza
upanuzi na
maboresho
ya kanisa
Kuendelea
na ujenzi
Kukamilish
a maboresho
na upanuzi
wote
Wazee wa Kanisa
Majengo
Uwakili
Lengo 2: Kukarabati nyumba ya mchungaji Kwa kadri ya mahitaji kwa mwaka husika Wazee wa Kanisa
Majengo
Lengo 3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao makuu mapya ya ETC. Kadri ya bajeti itakayoletwa na conference kwa kuzingatia mgawanyo
wa uchangiaji kimtaa
Wazee wa Kanisa
Mchungaji
Lengo 4: Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa Jamii
Kuandaa na
kukamilisha
michoro yote
ya usanifu
Draft 03
21
6.2 Ramani ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi kwa mwaka 2013
F: MIRADI MIKUU YA
UJENZI JANUARI FEBRUARI MACHI APRILI MEI JUNI
Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 W1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4
Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa na
upanuzi wa jengo la kanisa na
kukamilisha ujenzi wa majengo ya
kuabudia makundini
Kutengeneza 3D model ya kanisa
litakapokamilika (3D Physical Model)
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya familia 100-200, na michango ya
washiriki
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya kuchangisha kutumia kadi kutoka
kwa watu wa nje ya kanisa.
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa
njia ya "majengo day" ndani ya kanisa
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa
njia ya "majengo day" ndani ya kanisa na nje
ya kanisa.
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa
njia SMS namba maalum.
Ukusanyaji wa fedha za kutekeleza mradi
Kuanza ujenzi wa upanuzi wa ofisi za kanisa
Lengo #2 : Kukarabati nyumba ya
mchungaji
Pale itakapohitajika
Lengo # 3: Ujenzi wa nyumba ya
mkurugenzi makao makuu mapya ya
ETC
Pale itakapohitajika
Lengo # 4: Ujenzi wa Jengo la ustawi wa
jamii
i). Kupitia upya michoro iliyopo kuona kama
inakidhi haja za sasa na wakati ujao ili
kufanya marekebisho pale inapobidi.
ii). Kuandaa michoro mipya (kama kutakuwa na mabadiliko)
iii). Kuandaa michoro ya kihandisi
(structural engineering drawings).
iv). Kuandaa michoro ya mfumo wa maji
v). Kuandaa michoro ya mfumo wa umeme
Draft 03
22
F: MIRADI MIKUU YA
UJENZI
JULAI AGOSTI SEPTEMBA OCTOBA NOVEMBA DESEMBA
Wk
1
Wk2 Wk3 Wk4 Wk
1
Wk
2
Wk
3
Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4
Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa na
upanuzi wa jengo la kanisa na
kukamilisha ujenzi wa majengo ya
kuabudia makundini
Kutengeneza 3D model ya kanisa
litakapokamilika
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa
njia ya familia 100-200, na michango ya
washiriki
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa
njia ya kuchangisha kutumia kadi kutoka kwa watu wa nje ya kanisa
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa na nje
ya kanisa
Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa
njia SMS namba maalum
Ukusanyaji wa fedha za kutekeleza mradi
Kuanza ujenzi wa upanuzi wa ofisi za kanisa
Lengo #2 : Kukarabati nyumba ya
mchungaji
Pale itakapohitajika
Lengo # 3: Ujenzi wa nyumba ya
mkurugenzi makao makuu mapya ya
ETC
Pale itakapohitajika
Lengo # 4: Ujenzi wa Jengo la ustawi wa
jamii
i). Kupitia upya michoro iliyopo kuona kama inakidhi haja za sasa na wakati ujao ili
kufanya marekebisho pale inapobidi.
ii). Kuandaa michoro mipya (kama kutakuwa na mabadiliko)
iii). Kuandaa michoro ya kihandisi
(structural engineering drawings).
iv). Kuandaa michoro ya mfumo wa maji
v). Kuandaa michoro ya mfumo wa umeme
Draft 03
23
7. BAJETI YA UTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI
7.1 MAJENGO YA IBADA MAKUNDINI
KUNDI LA BUMAFA
Maelezo SHS.
1. Kuweka sakafu
2. Kupiga lipu (plaster) ndani na nje ya jengo
3. Kuweka grill kwenye madirisha
4. Kuweka milango
5. Kujenga choo
Jumla ya gharama inayohitajika 11,403,700.00
KUNDI LA CHIVILIKITI
1. Kuweka lipu ndani na nje
2. Kuweka madirisha
3. Kuweka milango
Jumla ya gharama inayohitajika 5,170,000.00
KUNDI LA MABWEPANDE
1. Kupiga lipu na kuziba nyufa
2. Kuweka umeme
3. Kufanya marekebisho ya mimbari
Jumla ya gharama inayohitajika 1,300,000.00
KUNDI LA ZINGA
Kufuatilia fidia kwa kuwa sehemu ya Kanisa iko
katika hifadhi ya barabara. Hivyo kwa sasa hakuna
shughuli za ujenzi zinazohitajika
Jumla ya gharama inayohitajika 0.00
KUNDI LA AMANI
1. Kuweka sakafu
2. Kuweka lipu ya ndani na nje
3. Kufanya ukarafati wa choo kwa kuziba nyufa
4. Kubadilisha mlango mmoja wa choo
5. Kuweka milango
Jumla ya gharama inayohitajika 4,361,500.00
Draft 03
24
KUNDI LA KIMELE
1 Kuweka lipu ndani na nje ya jengo
2 Kweka milango (frame na milango)
3 Kuweka madirisha
4 Kuta za ndani za kutenganisha
5 Kukarabati nyufa kwenye choo
Jumla ya gharama inayohitajika 7,290,000.00
KANISA LA MNYAMBE
1
Ujenzi wa kanisa lenye uwezo wa kuchukua
waumini 200 waliokaa vitini
Jumla ya gharama inayohitajika 29,524,375.00
JUMLA KUU KWA MAKUNDI YOTE 59,049,575.00
NB: Mchanganuo wa gharama kwa kila kipengele utatolewa na idara ya majengo
(Sehemu hii ni kwa ajili ya kuweka bajeti nzima ya kutekeleza mpango huu)
Draft 03
25
7.2 GHARAMA ZA MABORESHO YA MAZINGIRA YA KANISA LA MWENGE
Draft 03
26
8. VIELELEZO NA VIAMBATANISHI
8.1 Ramani ya upanuzi wa Kanisa (Sehemu za office)
Picha 1: Sehemu ya chini (Ground floor) ikionyesha offisi ofisi za kanisa na kisima cha ubatizo
Draft 03
27
Picha 2: Sehemu ya juu (First floor) ikionyesha ofisi za mbalimbali za kanisa
Draft 03
28
8.2 Picha au mtazamo wa kisanifu katika picha za pande tatu (3D Views photos)
Picha 3: Mwonekano wa Kanisa upande wa kuingilia kwenye ofisi mpya
Picha 4: Mwonekano wa Kanisa upande wa mbele
Draft 03
29
Picha 5: Mwonekano wa Kanisa upande wa kushoto
Picha 6: Mwonekano wa Kanisa kwa ndani