112
Shirika la Kazi Duniani International Labour Organization MWONGOZO WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI By Talib Mbwana Mohammed Mwamadzingo Z A N Z I B A R T R A D E U N I O N C O N G R E S S S O L I D A R I T Y F O R E V E R Z A T U C

MWONGOZO WA VYAMA VYA · MWONGOZO WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI iii KUHUSU ACTRAV ACTRAV (The Bureau for Workers’ Activities) ni kitengo cha Shirika la Kazi Duniani kina-chounganisha

  • Upload
    others

  • View
    56

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Shirika la Kazi Duniani

International Labour Organization

MWONGOZO WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

By Talib Mbwana

Mohammed Mwamadzingo

ZANZ

IBA

R TRADE UNION CONGRESS

SOLIDARIT Y FOREVER

Z A T U C

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

i

MWONGOZO WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

ii

Copyright page: ILO/ACTRAV and ZATUC

Copyright © International Labour Organization 2016First published 2016

Publications of the International Labour Office enjoy copyright under Protocol 2 of the Universal Copy-right Convention. Nevertheless, short excerpts from them may be reproduced without authorization, on condition that the source is indicated. For rights of reproduction or translation, application should be made to ILO Publications (Rights and Permissions), International Labour Office, CH-1211 Geneva 22, Switzerland, or by email: [email protected]. The International Labour Office welcomes such applica-tions.

Libraries, institutions and other users registered with reproduction rights organizations may make copies in accordance with the licences issued to them for this purpose. Visit www.ifrro.org to find the reproduction rights organization in your country.

MWONGOZO WA VYAMA VYA WAFANYAKAZIInternational Labour Organization, Bureau for Workers’ Activities, 2016

ISBN: 978-92-2-931054-1 (print)ISBN: 978-92-2-931055-8 (web pdf)

ILO Cataloguing in Publication Data

The designations employed in ILO publications, which are in conformity with United Nations practice, and the presentation of material therein do not imply the expression of any opinion whatsoever on the part of the International Labour Office concerning the legal status of any country, area or territory or of its authorities, or concerning the delimitation of its frontiers.

The responsibility for opinions expressed in signed articles, studies and other contributions rests sole-ly with their authors, and publication does not constitute an endorsement by the International Labour Office of the opinions expressed in them.

Reference to names of firms and commercial products and processes does not imply their endorse-ment by the International Labour Office, and any failure to mention a particular firm, commercial product or process is not a sign of disapproval.

ILO publications can be obtained through major booksellers or ILO local offices in many countries, or direct from ILO Publications, International Labour Office, CH-1211 Geneva 22, Switzerland. Catalogues or lists of new publications are available free of charge from the above address, or by email: [email protected]

Visit our website: www.ilo.org/publns

Printed in Kenya

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

iii

KUHUSU ACTRAVACTRAV (The Bureau for Workers’ Activities) ni kitengo cha Shirika la Kazi Duniani kina-chounganisha Ofisi Kuu ya Shirika hilo na wafanyakazi wote duniani. Jukumu kubwa la kiten-go hicho ni kuendesha na kuratibu shughuli zote za Ofisi Kuu zinazohusiana na wafanyakazi na Jumuiya zao zinazofanyika Makao Makuu au katika sehemu nyingine.

Shirika la Kazi Duniani ambalo Ofisi yake Kuu ndio chombo cha utendaji la Shirika hilo ndilo Shirika pekee la Umoja wa Mataifa ambalo utendaji wake unashirikisha kwa uzito sawa ma-husiano ya Utatu (tripartite) kati ya Serikali za Nchi wanachama, Jumuiya za Waajiri na Ju-muiya au Vyama vya Wafanyakazi.

Kwa mujibu wa utaratibu wa Shirika la Kazi Duniani wadau hao wote wanashiriki katika shu-ghuli za Shirika la Kazi na kufaidika na huduma zinazotolewa na Shirika hilo zikiwemo ushau-ri wa kitaalamu, msaada wa kifedha na utekelezaji miongozo inayotolewa

Dhamira Kuu ya ACTRAV ni kuhakikisha mahusiano ya karibu na Vyama vya Wafanyakazi Du-niani kote na kuvisaidia vyama hivyo ili viwe na uwezo wa kufanya shughuli zitakazo shawishi kuwepo kwa mifumo bora ya kudai, kulinda na kutetea haki za wafanyakazi

KUHUSU ZATUCShirikisho la Vyama vya wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) lilianzishwa na kusajiliwa kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya wafanyakazi Zanzibar Nambari 4 ya mwaka 2001 (iliyofutwa na She-ria ya Mahusiano Kazini Nambari 1 ya Mwaka 2005) iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ambalo ndilo Bunge la Zanzibar kwa mujibu wa Katiba

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) ndio Shirikisho pekee la Vyama vya Wafanyakazi kwa upande wa Zanzibar. Malengo makuu ya shirikisho hilo ni kuwaunganisha wafanyakazi kupitia vyama vyao katika kudai, kulinda na kutetea haki zao kitaifa na kimataifa, kuwakilisha wafanyakazi kupitia vyama shiriki katika vyombo vya kitaifa na kimataifa vina-vyoshughulikia mambo yanayowahusu, kushirikiana na watunga sera na sheria katika ku-hakikisha sera na sheria zinazotungwa, zinakuwa na maslahi na wafanyakazi na wananchi, kuwaelimisha wafanyakazi juu ya mambo yanayohusu ajira katika kujenga mahusiano bora sehemu za kazi na kuchukua hatua yoyote inayofaa kwa mujibu wa Sheria endapo haki na maslahi ya wafanyakazi yamevunjwa au kukiukwa na mtu binafsi, Muajiri au Serikali

Hadi sasa ZATUC inaundwa na vyama Tisa vya kisekta ambavyo ni Chama cha Wafanyakazi ya Viwanda na Biashara (Zanzibar Union of Industrial and Commercial Workers -TUICO-Z); Chama cha Walimu (Zanzibar Teachers’ Union - ZATU); Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Umma (Zanzibar Public Sector Workers’ Union -ZAPSWU); Chama cha wafanyakazi wa Hifadhi, Utalii, Hoteli na wafanyakazi wa Majumbani (Zanzibar Tourism, Hotel, Conservation, Domestic and Allied Workers’ Union CHODAWU-Z); Chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Zan-zibar Union for Public and Health employees -ZUPHE); Chama cha wa Mawasiliano na Usa-firishaji (Communication and Transport Workers’ Union of Zanzibar - COTWU-ZNZ); Chama cha Mawasiliano ya Simu (Telecommunication Worker’s Union of Tanzania Zanzibar TEWUTA-Z); Chama cha wafanyakazi wa Fedha na Biashara (Zanzibar Financial and Commercial Workers’ Union (ZAFICOWU); na Chama cha Mabaharia (Zanzibar Seamen’s Union -ZASU).

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

iv

DIBAJIVyama vya Wafanyakazi ni vyombo vikongwe katika historia ya ulimwengu wa kazi. Lakini shughuli zake zimekuwa zikichukuliwa juu juu na hata wafanyakazi wenyewe. Aidha masuala ya vyama vya wafanyakazi hasa katika ukanda wa Afrika ya Mashariki hayajapata bahati ya kufanyiwa utafiti wa kutosha kuandikwa na kuwekwa wazi ili yapate kujulikana na wote. Kwa sababu hizo basi, waandishi wa kitabu hiki wamejaribu kuonesha njia kwa wengine kuendeleza pale walipopaachia. Vyama vya wafanyakazi ni asasi muhimu katika ulimwengu wa kazi. Vyama vya wafanyakazi ni daraja baina ya tabaka la wafanyakazi, waajiri na serikali. Kwa sababu malengo ya wafanyakazi na waajiri hayakubaliani, migogoro baina ya tabaka mbili hizi ni vitu vinavyotarajiwa. Vyama vya wafanyakazi hutumiwa na wafanyakazi wenyewe kama chombo chao cha utetezi. Waandishi wa kitabu hiki wamejaribu kukielezea chombo hiki muhimu kwa wafanyakazi na hata wadau wengine wa maendeleo, Katika jitihada hizo waandishi wamejitahidi kuzungumzia masuala mengine yahusuyo kazi, utawala bora na masuala mtambuka ya kazi.

Waandishi wa kitabu hiki wamejaribu kuzungumzia masuala mengi kuhusu kazi, kiasi kwamba msomaji hatakuwa na haja ya kusoma vitabu vingine ili kupata fununu za masuala karibu yote muhimu yahusuyo vyama vya wafanyakazi na ulimwengu wa kazi kwa ujumla wake. Kitabu hiki kwa hakika ni Kiongozi cha vyama vya wafanyakazi kilichogusia mambo muhimu yahusuyo ulimwengu wa kazi. Tunachukua fursa hii kuwapongeza waandishi wa kitabu hiki kwa jitihada zao za kuelimisha watu wote wanaohitaji elimu kuhusu vyama vya wafanyakazi. Tunapendekeza wale wote wanaohitaji elimu ya msingi ya vyama vya wafanyakazi wafanye juu chini wakipate kitabu hiki ili kiwasaidie kuelewa masuala ya msingi ya vyama vya wafanyakazi.

Maria Helena André,Mkurugenzi,Kitengo cha Wafanyakazi,Shirika la Kazi Duniani,Geneva, Uswizi.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

v

YALIYOMOKUHUSU ACTRAV ...................................................................................................................... iiiKUHUSU ZATUC ........................................................................................................................ iiiDIBAJI ........................................................................................................................................ iv

Sura 1: HISTORIA NA CHIMBUKO LA SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) ............................... 1Udidimiaji na Vita ........................................................................................................................3Kipindi baada ya vita ..................................................................................................................3Mfumo wa Shirika la Kazi Duniani .............................................................................................5Kongamano.................................................................................................................................5Bodi Simamizi .............................................................................................................................5Afisi ya Shirika la Kazi Duniani .................................................................................................5Chimbuko La Kuundwa kwa Shirika la Kazi Duniani ................................................................5Mikataba ya Kazi Kimataifa ........................................................................................................7Jinsi Mikataba ya Kazi ya Kimataifa Inavyotayarishwa .............................................................8Hali hadi sasa ya Viwango vya Kimataifa vya Kazi ...................................................................10Idadi ya mikataba ......................................................................................................................10

Sura 2: VYAMA VYA WAFANYAKAZI ................................................................................... 13Maana ya Chama cha Wafanyakazi ..........................................................................................13Misingi ya Vyama Vya Wafanyakazi ..........................................................................................14Sababu za Kuunda Vyama vya Wafanyakazi ............................................................................15Umoja ni nguvu .........................................................................................................................16Aina ya Vyama Vya Wafanyakazi- Manufaa na Kasoro zake ....................................................16Haki za Vyama vya wafanyakazi na Haki Nyinginezo za Binadamu ........................................21Majadiliano ...............................................................................................................................23Umuhimu wa Majadiliano ........................................................................................................23Njia za Kujadiliana ....................................................................................................................24Haja ya Kuwa na Chombo cha Majadiliano .............................................................................24Mambo Muhimu Yanayosaidia Kufikiwa kwa Majadiliano Yenye Tija......................................24Mikataba Ya Hali Bora Ya Kazi ..................................................................................................26Fedha za Chama cha Wafanyakazi ...........................................................................................27Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ..................................................................................29Mambo ya Kujifunza kutokana na Historia ya Mei Dei ............................................................31Wasia kwa Wafanyakazi ............................................................................................................32

Sura 3: UONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ............................................................. 34Upatikanaji wa Viongozi katika Vyama Vya Wafanyakazi .........................................................34Sifa za Kiongozi wa Chama Cha Wafanyakazi .........................................................................34Wajibu/Majukumu ya Kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi ..................................................35Umuhimu wa Tawi katika Muundo wa Chama cha Wafanyakazi ...........................................35Uundaji wa Tawi la Chama cha Wafanyakazi ...........................................................................36Jinsi mwanachama anavyohitaji kutumia Tawi lake la chama ...............................................36Vikao vya Chama cha Wafanyakazi ..........................................................................................36Jinsi ya kuandaa vikao vya Chama cha Wafanyakazi ..............................................................37Vyama Vya Wafanyakazi na Demokrasia ..................................................................................37Mbinu za Uhamasishaji na Uingizaji Wanachama ..................................................................39Uimarishaji wa chama na Utetezi wa Wanachama .................................................................40Hatua za Utetezi .......................................................................................................................41

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

vi

Sura 4: KATIBA YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI ................................................................ 43Maana ya Katiba .......................................................................................................................43Umuhimu wa Katiba .................................................................................................................43Katiba ya chama cha Wafanyakazi ...........................................................................................43Utungaji wa Katiba ...................................................................................................................43Usajili wa Katiba .......................................................................................................................44Kupitisha Katiba na Kuifanyia Marekebisho ............................................................................44Kubadilika kwa Katiba ..............................................................................................................44Maudhui ya Katiba ya Chama cha Wafanyakazi .....................................................................45Ukiukaji wa Katiba ....................................................................................................................45Njia za Kuepuka Kuvunja Katiba ya Chama ............................................................................47

Sura 5: UTAWALA BORA KATIKA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ........................................... 49Elimu ya Wafanyakazi ...............................................................................................................49Ushirikishwaji wa Wafanyakazi ................................................................................................49Migomo katika vyama vya wafanyakazi ...................................................................................50Aina za Migomo .......................................................................................................................50Chanzo cha Migomo .................................................................................................................51Jinsi ya Kuandaa Mgomo .........................................................................................................52Faida na Hasara za Migomo.....................................................................................................53Jinsi ya kuepuka Migomo .........................................................................................................53Vyama vya Wafanyakazi na Wafanyakazi Vijana .......................................................................54Hadhi ya Wafanyakazi Vijana katika Ulimwengu wa Kazi .......................................................54Matatizo ya Vijana Sehemu za Kazi..........................................................................................55Wito kwa Vyama vya Wafanyakazi Kuhusu Vijana....................................................................55Athari za Utumikishaji kwa Watoto ..........................................................................................58Hatua za Kuchukuliwa katika Kukinga Utumikishaji wa Watoto ............................................59Hatua za Kitaifa na Kimataifa za Kushughulikia Utumikishaji wa Mtoto ...............................59Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi katika Kuzuia Utumikishaji wa Watoto ...........................59Mwisho ......................................................................................................................................60

Sura 6: AFYA NA USALAMA KATIKA SEHEMU YA KAZI ..................................................... 63Afya na Usalama Kazini ............................................................................................................63Kiwango cha Madhara ya Afya na Usalama Kazini .................................................................63Waathirika Wakubwa ................................................................................................................64Umuhimu wa Afya na Usalama sehemu za kazi .....................................................................64Athari zisizo za moja kwa moja ................................................................................................65Aina za Madhara Sehemu za Kazi ...........................................................................................66Jinsi ya Kudhibiti Madhara katika sehemu za Kazi .................................................................69Alama za Tahadhari ..................................................................................................................70VVU/UKIMWI NA WAFANYAKAZI ..............................................................................................71Hatua za Kitaifa na Kimataifa za kupambana na Ukimwi sehemu za kazi ............................72

Sura 7: UMOJA WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI AFRIKA (OATUU) ..................................... 75Chimbuko ..................................................................................................................................75Madhumuni ya OATUU .............................................................................................................76Vyombo vya OATUU ...................................................................................................................76Mafanikio OATUU ......................................................................................................................78Changamoto za OATUU ...........................................................................................................78

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

vii

Sura 8: MASUALA MTAMBUKA YA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ......................................... 81Hifadhi ya Jamii ........................................................................................................................81Aina za Hifadhi ya Jamii Duniani ..............................................................................................81Kustaafu Kazi ............................................................................................................................82Aina za kustaafu .......................................................................................................................82Matayarisho ya Kustaafu ..........................................................................................................82Hatua za Matayarisho ya Kustaafu ..........................................................................................82Maandalizi ya Kustaafu Hasa ..................................................................................................84Taathira za Utandawazi kwa Wafanyakazi na Vyama vya Wafanyakazi ...................................85Kupambana na Utandawazi .....................................................................................................86Changamoto Za Vyama vya Wafanyakazi Katika Kupambana na Utandawazi .......................86Kukabiliana na Changamoto ....................................................................................................86Mpango Mkakati .......................................................................................................................87Vyama vya Wafanyakazi na Uchumi Usio Rasmi .....................................................................88Matatizo ya Uchumi Usio Rasmi ..............................................................................................89Mikakati ya Kuunganisha Vyama Vya Wafanyakazi .................................................................90Haja ya Vyama vya Wafanyakazi Kuungana .............................................................................91Kwa Nini Vyama Viungane ........................................................................................................92Kurahisisha Mkakati wa Kuunganisha Vyama Vya Wafanyakazi ............................................92Hatua za Matayarisho ya Kuunganisha Vyama .......................................................................94Hatua Muhimu za Kufikia Muunganiko wa Vyama ..................................................................95

REJEA ................................................................................................................................ 97MFANYAKAZI THAMANI WAAJIRI TAMBUENI ................................................................... 98WIMBO WA MSHIKAMANO ................................................................................................ 99

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

viii

HISTORIA NA CHIMBUKO LA

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO)

Sura1111A COMMITTEE AT WORK …A COMMITTEE AT WORK …

14

Kongamano la Kimataifa

HIS

TORI

A N

A CH

IMBU

KO L

A IL

O

1

“Amani ya kudumu kote itaafikiwa kama imekuzwa juu ya misingi ya haki za jamii”

Itafahamika kuwa mchakato wa kubuni shirika litakalo shugulikia masuala ya wafanya kazi,ulianzishwa karne 19 ukion-gozwa na wamiliki viwanda Robert Owen (1771-1853) kutoka Wales na Daniel Le Grand (1783-1859) kutoka ufaransa .

Msukumo wa kubuni shirika la kazi duniani ulitokana na masuala ya ki-usalama, ubin-adamu, siasa na uchumi na kwa muhtasari utangulizi wa katiba ya shirika la kazi duni-ani (ILO) unasema makundi yaliyoko kwe-nye kandarasi yaliongozwa na hisia za haki, ubinadamu pamoja na matamanio ya ku-pata amani ya kudumu duniani.

Kulikuwa na kukubalika kwa umuhimu wa haki ya jamii katika upatikanaji wa amani dhidi ya dhuluma kwa wafanyakazi katika mataifa yaliyoendelea wakati huo. Kuto-kana na kuzidi kwa maelewano ya kujisi-mamia kiuchumi ulimwenguni na kuwepo kwa ushirikiano wa kupatikana kwa usawa wa hali za kufanya kazi katika nchi zilizos-hindania soko duniani na kwa mujibu wa fikra hizi, utangulizi umeshikilia kuwa am-ani ya kudumu inaweza kuafikiwa tu pale palipo misingi ya haki ya jamii na kwamba

Shirika la kazi duniani (ILO) liliasisiwa mnamo mwaka wa 1919, kama sehemu ya mkataba wa Versailles uliohitimisha vita vya kwanza vya dunia kama kielelezo cha imani kuwa, amani ya kudumu duniani in-aweza kuafikiwa ikiwa imejengwa kwa mis-ingi ya haki za msingi za binadamu.

Katiba hii iliundwa kati ya Januari na Aprili 1919 na Tume inayoshughulikia masuala ya kazi iliyobuniwa kwa kikao kilichohusu amani kilichokutana kwa mara ya kwanza Paris na kisha Vesailles chini ya mwenyekiti Samuel Gompers kiongozi wa shirikisho la wafanyakazi Marekani (AFL) na kujumui-sha wawakilishi kutoka nchi tisa: Ubelgiji, Cuba, Czechoslovakia, Ufaransa,Italia, Uja-pani, Poland na Uingereza.

Kikao hiki kilijitokeza na mfumo wa utendaji wa UTATU na ndio wa kipekee unaoshiriki-sha kwa uzito sawa mahusiano ya utatu katika chombo cha utawala na afisi yaani: serikali, waajiri na wafanyakazi.

Katiba hii ilibuni mawazo yaliyokwisha tath-miniwa na shirika la kimataifa la uundaji sera kuhusu kazi lililoundwa Basel mnamo 1901.

1919

HISTORIA NA CHIMBUKO LA SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO)

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

2

kuwepo kwa mazingira magumu ya kazi yanayozua vurugu na kuhatarisha amani duniani kuna umuhimu wa kuboresha kwa haraka mazingira hayo.

Kutokana na kutoshughulikiwa kwa maz-ingira ya kazi kwa taifa lolote kunakua kiz-ingiti kikubwa kwa mataifa yanayotamani kuboresha hali hizo nchini mwao.

Sehemu zinazohitaji kuboreshwa zilizo-orodheshwa kwenye utangulizi hivi leo zin-gali na umuhimu kwa mfano:

• Masaa ya kufanya kazi kwa siku na juma nzima

• Kuzuia kutokuwepo kwa ajira na kutoa ujira unaotosheleza mahitaji.

• Kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ma-gonjwa na majeraha wakiwa kazini.

• Kuwakinga watoto, vijana na wanawake.

• Huduma za uzeeni na majeraha, utunzaji masilahi ya wafanyakazi wanapoajiriwa katika nchi zingine mbali na kwao.

• Utiliaji maanani wa usawa wa malipo kulingana na thamani ya kazi.

• Utiliaji maanani wa haki ya utangamano.

• Mpangilio wa elimu anuai na ya kiufundi na mengineyo.

Shirika la kazi duniani (ILO) lilichangia pa-kubwa katika nyanja ya utendakazi kutoka awali. Kongamano la utendakazi la kwanza la kimataifa lililofanyika Washington DC Oktoba 1919 lilikubalia mikataba sita ya kimataifa kuhusu utendakazi ambayo il-ishughulikia saa za kutenda kazi kwenye viwanda, ukosefu wa ajira, kinga ya uzazi, kufanya kazi usiku kwa wanawake, umri wa chini wa kuajiriwa, na kufanya kazi usiku kwa vijana katika viwanda.

Shirika la kazi duniani (ILO) lilikuwa na makao yake Geneva mwaka 1920 na Albert Thomas wa Ufaransa akiwa mkurugenzi wa afisi kuu ya Shirika la kazi ,ambayo ndiyo afisi kuu ya kudumu. Chini ya uongozi wake mikataba 16 ya kimataifa kuhusu kazi duni-ani na mapendekezo 18 yaliafikiwa chini ya miaka miwili.

Azma hii ya mwanzo ilidhibitiwa kwa saba-bu baadhi ya serikali zilihisi kwamba kuli-kuwa na mikataba mingi zaidi, bajeti kub-wa na ripoti zenye utata mwingi. Isitoshe, mahakama ya haki ya kimataifa ilitangaza kwamba utawala wa shirika la kazi duniani uliendeleza mfumo wake hadi kusawazisha

Utatu wa Shirika la Kazi Duniani

ILO

Serikali

Wafanyakazi

Waajiri

HIS

TORI

A N

A CH

IMBU

KO L

A IL

O

3

kanuni za kimataifa za mazingira ya kazi katika sekta ya kilimo.

Jopo la wataalamu liliundwa mwaka 1926 kama njia ya usimamizi katika kuhakikisha taratibu za (ILO) zimefuatwa. Jopo hilo, am-balo lipo hadi sasa limejumuisha wanashe-ria wasioegemea upande wowote na ambao hutathmini ripoti za serikali na kuwasilisha mtazamo wake kila mwaka kwenye konga-mano kuu.

Udidimiaji na Vita

Udidimiaji mkubwa na matokeo ya ukosefu mkubwa wa ajira ulimkabili Harold But-tler aliyechukua hatamu kutoka kwa Albert Thomas mwaka 1932. Baada ya kugundua kuwa kuangazia masuala ya kazi ulimwen-guni kunahitaji ushirikiano wa kimataifa, Marekani ilijiunga na Shirika la kazi duniani(ILO) mwaka 1934, japo iliendelea kutojihusisha na uhusiano wa kimataifa.

Mmarekani John Winnant alichukua hata-mu za uongozi mwaka 1939, wakati vita vya pili vya dunia vilipochacha. Alihamisha

makao makuu ya Shirika la Kazi Duniani hadi Montreal, Canada Mei 1940 kwa saba-bu za ki-usalama, lakini aliondoka mnamo mwaka 1941 alipoteuliwa kama Balozi wa Marekani kwenda Uingereza.

Mrithi wake Edward Phelan wa Ireland, ali-yechukua uongozi, alikuwa amesaidia uan-dishi wa katiba ya 1919 na kuchukua nafasi kubwa katika kongamano la Philadelphia la Mkutano wa kimataifa kuhusu utend-akazi duniani, katikati ya vita vya pili vya dunia. Mkutano huo ulihudhuriwa na seri-kali, waajiri, na wafanyakazi kutoka nchi 41. Wajumbe waliratibisha maazimio ya Philadelphia ambayo yalizingatia malengo ya ILO.

Mnamo mwaka wa 1946 shirika la kazi dun-iani (ILO) likawa chombo maalum cha shiri-ka la umoja wa mataifa na mnamo Mwaka 1948 bado wakati wa kipindi cha utawala wa Phelan, kongamano la kimataifa la kazi liliratibisha mkataba nam. 87 kuhusu uhu-ru wa kutangamana na haki ya maandalizi.

Kipindi baada ya vita

Kipindi cha Mmarekani David Morse kama mkurugenzi mkuu kutoka mwaka (1948-1970), idadi ya wanachama iliongezeka maradufu na kulifanya shirika kuchukua majukumu yake na kufanya mataifa yali-yoendelea kupungua idadi miongoni mwa yale yanayoendelea. Makadirio yaka-ongezeka mara tano na idadi ya maafisa kuongezeka.

Shirika la kazi duniani likazindua Taasisi ya masomo ya wafanyakazi mwaka 1960 na kituo cha mafunzo ya wafanyakazi cha kimataifa Turin mnamo mwaka wa 1965. Shirika hili lilishinda tuzo la Nobel wakati wa maadhimisho ya miaka 50 mwaka wa 1969.

Chini ya Wilfred Jenks kutoka Uingereza kama Mkurugenzi Mkuu (1970–1973), Shiri-ka la Kazi Duniani liliimarisha viwango vya maendeleo na mbinu za usimamizi katika kushughulikia kuinua viwango vya uhuru wa kutangamana na haki za maandalizi.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

4

Aliyechukua hatamu baada yake, Francis Blanchard wa Ufaransa, alipanua uhusiano wa ki-uhandisi na mataifa yanayoendelea na kuepusha madhara kwa shirikisho li-cha ya kupotea kwa robo ya mtaji kwenye bajeti kutokana na kujiondoa kwa Mare-kani (1977–1980). Shirika la Kazi duniani pia lilichangia pakubwa uhuru wa Poland kutokana na udikteta kwa kuunga mkono kuwepo kwa muungano wa ‘Solidernose’ kwa kuheshimu mkataba nam. 87 kuhusu uhuru wa kutangamana ambao Poland ili-ratibisha mwaka 1957.

Michel Hernsene kutoka Ubelgiji alichukua hatamu za uongozi mnamo mwaka 1989 na kuongoza Shirika la Kazi Duniani kipindi cha baada ya vita na kusisitiza umuhimu wa kutilia mkazo haki za jamii kama msingi wa kulinda sera za kimataifa kuhusu uchumi na jamii. Zaidi ya hayo, alianzisha mchaka-

to wa kugatua shughuli na rasilmali kutoka makao makuu Geneva.

Mnamo Machi 4, 1999, Juan Somavia ku-toka Chile alichukua hatamu kama Mkuru-gezi Mkuu na kutilia mkazo umuhimu wa ajira ya kuheshimika kama azimio maalum katika uimarishaji wa utandawazi. Alitilia mkazo kazi kama chombo cha kukabiliana na umaskini na jukumu la Shirika la Kazi Duniani katika kusaidia kuafi kia malengo ya Milenia ya maendeleo pamoja na kupun-guza viwango vya umaskini duniani kufi kia 2015.

Mnamo Mei 2012, Guy Ryder kutoka Uin-gereza alichaguliwa kama Mkurugenzi Mkuu wa kumi wa Shirika la Kazi Duniani na kuanza hatamu yake ya miaka mitano Oktoba 2012.

Viwango vya Kimataifa vya Kazi

Viwango vya Kimataifa vya Kazi

Mikataba

• Ikiratibiwa huwa sheria

• Pasipo kuratibiwa husalia kuwa malengo na huathiri sheria za nchi

Mapendekezo

• Maelekezo ya kijumla au ya kitaalamu

• Yasiyowezwa kuratibiwa

HIS

TORI

A N

A CH

IMBU

KO L

A IL

O

5

Mfumo wa Shirika la Kazi Duniani

Shirika la Kazi duniani (ILO) linajumuisha Baraza Kuu – kongamano la kazi la ki-mataifa ambalo hukutana kila mwaka; Bodi ya Utawala na afisi ya kudumu – Shirika la Kazi Duniani. Shirika hili pia hutenda kazi kupitia kwa makongamano ya maeneo mbalimbali kama kamati za viwanda na majopo ya wataalam.

Kongamano

Kongamano la kimataifa la kazi huteua Bodi simamizi ili kuratibisha mipangilio ya shiri-ka na kupigia kura bajeti (inayofadhiliwa na Mataifa wanachama). Kongamano pia hui-dhinisha viwango vya kazi vya kimataifa na kusimamia utekelezaji wake (kulingana na utaratibu uliofafanuliwa hapa chini): hupiti-sha maazimio yanayotoa mwelekeo wa sera za shirika la kazi duniani na utendakazi, huamua usajili wa wanachama wapya na kutoa nafasi ya mdahalo kuhusu masuala ya jamii na maswali ya utendakazi.

Kila kongamano huhusisha wajumbe wawili wa serikali, mmoja wa waajiri na mmoja mwajiriwa akiambatana inapobidi na washauri maalum. Wajumbe kutoka ju-muia ya waajiri na waajiriwa huwa na uhuru wa kupiga kura.

Bodi Simamizi

Bodi simamizi ambayo huwa na wanacha-ma waliochaguliwa kila baada ya miaka mi-tatu, kwa kawaida hukutana mara tatu kwa mwaka. Hutayarisha ajenda ya kongamano na mikutano mingine ya shirika la kazi duniani; hunukuu maamuzi na kuamua utekelezaji wake. Humteua mkurugenzi mkuu, na kuelekeza shughuli za afisi ya ki-mataifa ya wafanyakazi.

Sawa na kongamano, Bodi simamizi ina mfumo wa utatu, na kwa sasa hujumuisha wanachama kamili 56 (10 ni wa kudumu sababu ya umuhimu wao), 28 kuwakilisha serikali, 14 wafanyakazi na 14 waajiri. Kati

ya viti 28 vya serikali, 10 vinashikiliwa na nchi zenye umuhimu mkubwa viwandani. Mataifa hayo mengine 18 huchaguliwa na wajumbe wa serikali kwenye kongamano (isipokuwa nchi zenye mvuto mkubwa vi-wandani). Wawakilishi wa waajiri na waajiri-wa huchaguliwa na wajumbe wa waajiri na waajiriwa katika kongamano. Wao huch-aguliwa kwa njia ya kipekee na wahusika wanaowawakilisha binafsi.

Bodi simamizi pia hutekeleza majukumu maalum katika kusimamia utekelezaji wa kazi katika viwango vya kimataifa; kwa sababu hiyo hulinda haki za muungano wa wafanyakazi, kupitia kwa Bodi zingine tatu ambazo ni: Jopo la wataalam kuhusu utekelezaji mikataba na mapendekezo, Halmashauri ya maridhiano kuhusu uhuru wa kutangamana na Kamati ya uhuru wa kutangamana.

Afisi ya Shirika la Kazi Duniani

Afisi ya Shirika la Kazi Duniani huko Ge-neva ni afisi ya kudumu ya shirika hili na inahusisha idara mabalimbali: hutayarisha miswada na ripoti ambazo hutumika ka-tika makongamano na mikutano ya shirika pamoja na kuendesha mipangilio ya kip-ekee ili kuwezesha usawazishaji wa kazi ya shirika hilo.

Chimbuko La Kuundwa kwa Shirika la Kazi Duniani

Shirika la Kazi Duniani ni miongoni mwa vyombo vya Umoja wa Mataifa (UN) am-balo hushughulika na masuala ya kazi na wafanyakazi kwa kushirikiana na serikali. Azimio la kuunda Umoja wa Mataifa lilitiwa saini na nchi 50 huko mjini San Fransisco Marekani mwaka 1945. Katika utangulizi wa Azimio Shirika la Kazi Duniani, nchi wa-nachama zilidhamiria kuokoa vizazi vijavyo kutokana na madhara ya vita ambayo mara mbili yalileta huzuni kubwa kwa binadamu.

Chimbuko la shughuli za Shirika la Kazi Duniani linatokana na Tamko la Haki za Bi-nadamu Duniani lililotolewa na Umoja wa

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

6

Mataifa mwaka 1948. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilizitaka nchi zote wanachama kulitangaza na kulisambaza tamko la Shiri-ka la Kazi Duniani ili lisomwe mashuleni na katika asasi nyingine zote za kielimu. Watu wote, mataifa yote na kila mtu ajitahidi kwa njia ya uelimishaji kukuza haki hizi na kwa hatua endelevu kitaifa na kimataifa kuwez-esha haki hizi kukubalika kote duniani na kufuatwa na wananchi wote katika nchi wa-nachama. Kifungu cha 23 cha Tamko Shiri-ka la Kazi Duniani kinasema:

• Kila mmoja ana haki ya kufanya kazi, uhuru wa kuchagua ajira aitakayo, maz-ingira na hali bora za kazi, na kuzuia ukosefu wa ajira.

• Kila mfanyakazi anastahiki malipo ya haki ya kazi aifanyayo ili kumwezesha yeye na familia yake kuishi maisha ya heshima, na kupatiwa hifadhi nyingine za jamii.

• Kila mmoja ana haki ya kuunda na kuji-unga na vyama vya wafanyakazi kwa ajili ya kulinda maslahi yake

Tamko hili linakwenda sambamba na Kati-ba ya Umoja wa Mataifa ambapo nchi wana-chama zimesisitiza imani zao kwa haki hizi za msingi za binadamu, heshima, na utu wa

Shirika la Kazi Duniani hufanya kazi kwa mfumo wa Utatu- Serikali, Jumuiya za Waajiri na Jumuiya za Wafanyakazi, na mara zote husisitiza umuhimu wa mashirikiano ya vyombo hivi na husisitiza pia mazungumzo ya pamoja baina ya vyombo hivi.

What is the relationship betweenWhat is the relationship between

Productivity Innovation Competition Flexibility

Labour rights

Ni uhusiano upi ulioko kati ya

Uzalishaji Uvumbuzi

Haki za Wafanyakazi

Ushindani Uwazi

binadamu na haki sawa kwa wanawake na wanaume na zimedhamiria kukuza maen-deleo ya kijamii na kuinua hali ya maisha ya watu.

HIS

TORI

A N

A CH

IMBU

KO L

A IL

O

7

Shirika la Kazi Duniani ni chombo pekee cha Umoja wa Mataifa ambapo serikali, vyama vya wafanyakazi na waajiri wanawakilishwa kwa uzito

sawa. Hii ndio maana Shirika la Kazi Duniani linafahamika kama chombo cha utatu. Wawakilishi wa pande hizo tatu hukutana Geneva, Uswizi kila

mwaka katika mwezi wa Juni katika Kongamano la Kimataifa la Kazi. Katikati ya makongamano haya, kuna mikutano ya pande hizi tatu ambayo

hushughulikia mambo maalumu yahusuyo kazi

Shirika la Kazi Duniani ni chombo pekee cha Umoja wa Mataifa ambapo

Wahalalishaji

Shirika la Kazi la Duniani hufanya kazi kwa mfumo wa Utatu- Serikali, Jumuiya za Waajiri na Jumuiya za Wafanyakazi, na mara zote husisitiza umuhimu wa ma-shirikiano ya vyombo hivi na husisitiza pia mazungumzo ya pamoja baina ya vyombo hivi. Mfumo wa Shirika la Kazi Duniani una-tilia mkazo mazungumzo ya pamoja mion-goni mwa vyombo vya utatu vilivyo sawa. Mfumo huo unahakikisha kuwa mawazo/mapendekezo yatokanayo na wadau hao yanaingizwa katika viwango vya kimataifa vya kazi, sera, na mipango mingine.

Shirika la Kazi Duniani hukamilisha shu-ghuli zake kwa kupitia vyombo vyake vikuu vitatu – Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Kazi, Chombo cha Utawala, na Ofi si, am-bavyo huundwa na wawakilishi wa serikali, wawakilishi wa waajiri, na wawakilishi wa wafanyakazi. Kazi za Chombo cha Utawala na Ofi si zinasaidiwa na kamati za utatu za sehemu kuu za kazi, na kamati za mabing-wa katika mambo kama vile mafunzo ya ufundi, maendeleo ya uendeshaji, afya na usalama kazini, mahusiano kazini, elimu ya wafanyakazi, na matatizo mahususi ya

wafanyakazi vijana na wanawake. Mikutano ya Shirika la Kazi Duniani hufanyika kila baada ya muda fulani kuzingatia masuala ya kazi na wafanyakazi.

Mikataba ya Kazi Kimataifa

Shirikisho la Kazi Duniani katika kujaribu kuhakikisha haki za msingi za wafanyakazi duniani hupitisha mikataba yenye viwango vya chini vya kazi.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa-natakiwa kutekeleza mikataba hiyo. Shirika la Kazi Duniani limepitisha na linaendelea kupitisha mikataba kadha pamoja na map-endekezo ya utekelezaji wa mikataba hiyo kwa nia ya kuimarisha mazingira ya kazi na haki za wafanyakazi. Mikataba muhimu ya Kazi ya Kimataifa ni hii ifuatayo:

• Kazi za Shuruti wa mwaka 1930, – nam. 29: Mkataba huu unakataza watu kula-zimishwa kufanya kazi wasioichagua wenyewe.

• Uhuru wa Kujiunga na Kinga ya Haki ya Kuunda Chama wa mwaka 1948, nam.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

8

87: Mkataba huu unatoa uhuru wa ku-jiunga pamoja na unatoa haki kwa wa-fanyakazi kuunda vyama vyao.

• Haki ya Kuunda Chama na Haki ya Ku-fanya Majadiliano ya Pamoja wa mwaka 1949 nam. 98: Mkataba huu unatoa haki kwa wafanyakazi kuunda vyama vyao na haki ya kufanya majadiliano ya pamoja kuhusu hali bora za kazi katika sehemu za kazi.

• Malipo Sawa kwa Kazi Sawa wa mwaka 1951,nam. 100: Mkataba huu unatoa maelekezo kwa waajiri kutoa malipo sawa kwa wafanyakazi wenye ujuzi sawa na wanaofanya kazi za aina moja.

• Marufuku ya Kazi za Shuruti wa mwaka 1957,nam. 105: Mkataba huu unapiga marufuku kazi za shuruti.

• Ubaguzi katika Ajira wa mwaka 1958,nam 111: Mkataba huu unawakin-ga wafanyakazi katika masuala ya ajira.

• Umri wa Kufanya Kazi wa mwaka 1973, nam. 138: Mkataba huu unaweka umri wa chini wa mtu kuajiriwa. Lengo la mkataba huu ni kuzuia ajira ya watoto.

• Kuondoa Ajira Mbaya ya Watoto wa mwaka 1999, nam. 182: Mkataba huu unakusudia kuondoa kabisa ajira mbaya ya watoto kama vile kutumia watoto kufanya sinema za utupu, na mambo ya aina hiyo.

Jinsi Mikataba ya Kazi ya Kimataifa Inavyotayarishwa

Shirika la Kazi Duniani, ni chombo maal-umu cha Umoja wa Mataifa (UN). Vyombo vingine ni UNESCO kinachoshughulikia elimu, UNICEF kinachoshughulikia masu-ala ya watoto, FAO kinachoshughulikia chakula, UNHCR kinashughulikia wakim-bizi, na UNDP kinachoshughulikia maen-deleo.

Shirika la Kazi Duniani linajihusisha na masuala ya haki za wafanyakazi na za vy-ama vya wafanyakazi kama njia za kuleta mahusiano mazuri sehemu za kazi na hivyo kusaidia kuongeza uzalishaji na kuleta maendeleo ya wafanyakazi na jamii kwa ujumla. Kwamba hili ni lengo la pamoja la vyama vya wafanyakazi, mashirikisho ya waajiri, na serikali, ni jambo linalokuba-lika na nchi nyingi duniani na limewezesha

Utumikishwaji wa mtoto

HIS

TORI

A N

A CH

IMBU

KO L

A IL

O

9

pande hizi tatu- serikali, waajiri, na wafan-yakazi kuunda Shirika la Kazi Duniani muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa Umoja wa Mataifa (UN). Shirika la Kazi Duniani lilia-sisiwa katika kipindi cha katikati ya vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Shirika la Kazi Duniani ni chombo pekee cha Umoja wa Mataifa ambapo serikali, vyama vya wafan-yakazi na waajiri wanawakilishwa kwa uzito sawa. Hii ndio maana Shirika la Kazi Duni-ani linafahamika kama chombo cha utatu. Wawakilishi wa pande hizo tatu hukutana Geneva, Uswizi kila mwaka katika mwezi wa Juni katika Kongamano la Kimataifa la Kazi. Katikati ya makongamano haya, kuna mikutano ya pande hizi tatu ambayo hushu-ghulikia mambo maalumu yahusuyo kazi.

Makongamano haya ya Shirika la Kazi Dun-iani, pamoja na mambo mengine hupitisha Mikataba na Mapendekezo ya Mikataba hiyo. Haya yanaamuliwa na idadi kubwa ya washiriki wa makongamano hayo. Inat-egemewa kuwa mikataba na mapendekezo haya ya Shirika la Kazi Duniani, yatathibit-ishwa kwa kuridhiwa na nchi wanachama.

Shirika la Kazi Duniani hupitisha Mkataba kama sheria ya mfano na nchi ambayo itaridhia mkataba huo, inapaswa kurekebi-sha sheria yake ya nchi yenye mnasaba na mkataba husika ili ilingane na mkataba huo. Iwapo nchi hiyo haina sheria hiyo, itapaswa kupitisha sheria yenye lengo la kutekeleza mkataba huo. Mapendekezo yanaelekeza jinsi ya kutekeleza mkataba husika.

Kati ya mikataba karibu ya mia mbili (200) iliyokwishapitishwa na Shirika la Kazi Du-niani, mikataba minane (08) huunda kanuni za msingi za Shirika la Kazi Duniani za haki za binadamu na hujulikana kwa jina la Mi-kataba mikuu.

Mikataba yenyewe ni:

• Uhuru wa kukusanyika na kufanya ma-jadiliano ya pamoja – Mikataba nam 87 nam. 98.

• Malipo sawa Kwa Kazi zenye Uzito sawa- Mkataba nam. 111.

• Ubaguzi katika Ajira na Sehemu za Kazi – Mkatba nam. 100 ambao pia unahu-sisha wafanyakazi wa kuhamahama na masuala ya kijinsia.

• Umri wa chini wa kuanza Ajira na ajira kwa Watoto – Mkataba nam. 138.

• Utokomezaji wa Ajira ya Kulazimisha (kutumia nguvu) – Mikataba nam. 29 nam. 105.

• Utokomezaji wa utumikishwaji mbaya zaidi wa mtoto – Mkataba nam. 182.

Mikataba yenye umuhimu mkubwa katika mapambano ya kutetea haki za vyama vya wafanyakazi ni:

1. Mkataba nam. 87 Kuhusu Uhuru wa kukusanyika na Kinga ya Kujiunga (1948).Umeridhiwa na zaidi ya nchi 120 na unaeleza:

• Kwamba wafanyakazi wanaweza kuanzisha na kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi wap-

Chama cha wafanyakazi ni

umoja wa hiari na wa kidemokrasia

ulioanzishwa na wafanyakazi

wenyewe kutokana na mahitaji yao bila ya kushawishiwa na

bila ya kuingiliwa na chombo cho chote,

kiwe cha serikali au kinginecho

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

10

Jedwali la idadi ya mikataba iliyoratibishwa

7400

2006

2007

2008

2009

2010

2011

2012

2013

2014

2015

2016

7500

7600

7700

7800

7900

8000

8100

8200

Jumla 8059

endacho bila ya kwanza kutafuta kukubaliwa na serikali.

• Kwamba vyama vya wafanyakazi viko huru kuanzisha mashirikisho ambayo pia yanaweza kuungana katika ngazi ya kimataifa.

• Kwamba vyama vya wafanyakazi haviwezi kufutwa au kusimam-ishwa na serikali.

2. Mkataba nam. 98 kuhusiana na Haki ya Kujiunga na Majadiliano ya pamoja (1949).

Mkataba huu umeridhiwa na zaidi ya nchi 135 lakini hauhusiani na wafanyakazi wa mashirika ya umma. Wao wanaelezewa ka-tika mkataba nam. 151 (1978).

Mkataba nam. 98:

• Unaongeza nguvu ya wafanyakazi katika kuondoa vitendo vya kup-inga vyama vya wafanyakazi.

• Unaimarisha na kulinda hatua za majadiliano ya hiari kati ya vy-ama vya wafanyakazi na vyama vya waajiri ili kusimamia kanuni

na masharti ya kazi kwa njia ya makubalino ya pamoja.

Nchi nyingi zimesharidhia mikataba ya Shirika la Kazi Duniani nam. 87 na 98 lakini kutoridhia mkataba wowote hakuzui nchi yoyote kutekeleza mikataba iliyokwisha pit-ishwa na Shirika la Kazi Duniani. Kila mwa-ka serikali za nchi zinalazimika kupeleka taarifa kwa Shirika la Kazi Duniani kueleza uwezekano wa ukiukwaji wa mikataba na migongano mingine inayohusisha haki za wafanyakazi. Vyama vya wafanyakazi vina haki ya kupitia na kutoa maoni kuhusu taarifa hii na hata kusahihisha makosa yo yote kama yapo. Hii ni muhimu ifanyike ka-tika mpangilio mzuri ili uvunjwaji wa haki za wafanyakazi kama upo taarifa zake zi-weze kutumwa haraka mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Hali hadi sasa ya Viwango vya Kimataifa vya Kazi

Idadi ya mikataba

Hadi sasa nchi wanachama 187 wamerati-bisha jumla ya mikataba 8059 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO).

HIS

TORI

A N

A CH

IMBU

KO L

A IL

O

11

Jedwali la mikataba hususi ya usimamizi

144

40 60 80 100 120 140 160 180 200

13953

111

144

180

169173

172175

178

164

153

129

122

081182138111

100

105

029098

087

Uratibishaji wa mikataba muhimu kulingana na maeneo

Nchi Uhuru wa kutangamana

Ajira za kushurutishwa

Ubaguzi Ajira ya watoto

087 098 029 105 100 111 138 182

Jumla 187 153 164 178 175 172 173 168 180

Afrika (54) 49 54 54 54 52 54 52 53

Amerika (35) 33 32 34 35 33 33 31 35

Uarabuni (11) 3 6 11 11 7 10 11 11

Bara hindi (35) 18 21 28 24 29 25 23 30

Uropa (51) 50 51 51 51 51 51 51 51

Uratibishaji wa mikataba ya usimamizi kulingana na maeneo

Nchi 081 122 129 144

Jumla 187 145 111 53 139

Afrika (54) 46 22 10 40

Amerika (35) 28 23 9 30

Uarabuni (11) 10 4 1 5

Bara hindi (35) 14 15 1 19

Uropa (51) 47 47 32 45

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

12

Labour Rights abour Rights

VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Sura2222222Sura2Sura2Sura2Sura

Haki za Wafanyakazi

Ujira unaotosheleza Wafanyakazi

Mfanyakazi aweze kumudu yafuatayo:

Chakula Malazi Afya bora Elimu

Mavazi Usafi ri Akiba

Ujira unaotosheleza ni haki ya kila mtu duniani kote

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

13

VYAMA VYA WAFANYAKAZIMaana ya Chama cha Wafanyakazi

Chama cha wafanyakazi ni umoja wa hiari na wa kidemokrasia unaoanzishwa na wa-fanyakazi wenyewe kutokana na mahitaji yao bila ya kushawishiwa na bila ya kuin-giliwa na chombo chochote, kiwe cha seri-kali au kinginecho. Malengo makuu ya cha-ma cha wafanyakazi ni kulinda na kupeleka mbele mahitaji na matakwa ya pamoja ya wafanyakazi yawe ya kiuchumi, kijamii, au kisiasa. Mahitaji haya yanajumuisha uhaki-ka wa ajira, malipo maridhawa ya ujira na marupurupu mengine, masharti bora ya kazi, na uboreshaji wa maisha ya mfan-yakazi na wananchi kwa ujumla. Mambo yenyewe yanahusisha vile vile masuala ya demokrasia, kimataifa, sera mbadala za uchumi wa nchi, na masuala ya kijumla ya maendeleo ya wananchi. Hivyo wafanyakazi nao ni wadau wakubwa wa mambo yote yahusuyo nchi yao na wanahitaji kushirik-ishwa kikamilifu.

Mapinduzi ya viwanda yalitokea Ulaya karne ya kumi na tisa. Msingi wa mapinduzi haya ulikuwa ni mtaji, na hali hiyo ilipelekea kukua kwa miji midogo na mikubwa na ma-tokeo yake ni kuwa watu wengi walihamia mijini kwa lengo la kutafuta kazi za kua-jiriwa katika miji iliyokua kwa kasi. Watu wengi walipata ajira katika viwanda. Wenye viwanda walilenga zaidi kupata faida kubwa kutokana na mitaji yao na hivyo kulazimika kuwalipa wafanyakazi wao ujira mdogo usi-olingana na jasho lao. Mishahara ilikuwa midogo na mazingira ya kufanyia kazi ya-likuwa mabaya. Hakukuwa na utaratibu wa wafanyakazi kupatiwa nyumba za kuishi na wala hapakuwa na mfumo wowote wa hifa-dhi ya jamii ulioimarisha maisha ya jumla ya wafanyakazi. Kwa hiyo mambo makubwa yaliyowakwaza wafanyakazi hao na kujiona wananyanyasika ni:

• Kufanyishwa kazi kwa muda mrefu/saa nyingi bila ya kupumzika.

• Kufanyishwa kazi katika mazingira magumu kiafya na ustawi wao.

• Kufanyishwa kazi kwa malipo yasiyoki-dhi mahitaji yao ya lazima.

• Kutosikilizwa wanapoeleza matatizo yao katika kazi.

Hali hii iliwalazimisha wafanyakazi hao ku-ungana pamoja ili kulinda na kutetea ma-slahi yao. Hiki ndicho chanzo na mwanzo wa kuundwa kwa vyama vya wafanyakazi.

Kuna sababu kubwa mbili zinazomsukuma mfanyakazi kujiunga na chama cha wafan-yakazi:

• Vyama vya Wafanyakazi vina shabaha ya kuboresha hali bora ya mahala pa kazi, kuboresha maisha ya wanachama wake, na vinajihusisha na haki za jamii.

• Wafanyakazi wanapoeleza matakwa yao ya pamoja kwa waajiri wao, huwa wa-naimarisha msimamo wa pamoja wa wafanyakazi. Hakika waajiri wanakuwa waangalifu zaidi wanapokabiliana na wafanyakazi waliojiunga katika chama chao, kuliko mfanyakazi mmoja mmoja. Hivyo, nguvu za chama cha wafanyakazi chochote zinategemea juu ya ukubwa wake na wingi wa wanachama wake, na jinsi chama hicho kilivyojiunda na kujiimarisha. Chama kikiungwa mkono na wafanyakazi wengi ndio kinakuwa na nguvu na uwezo wa kufikia malengo yake. Wingi wa wanachama wa chama cha wafanyakazi una maana ya kuwa na nguvu zaidi za kujadiliana na waajiri ikiwa ni pamoja na serikali na pia kuwa na ushawishi mkubwa katika jamii.

Tafiti nyingi zimefanywa na wanasayansi jamii zinazotaka kujua mambo muhimu

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

14

yanayowavutia wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi. Karibu tafiti zote zimebaini kuwa kuna sababu kuu mbili; moja ikiwa inamuhusu mfanyakazi mmoja mmoja, na nyingine inahusu kikundi kizima cha wafanyakazi.

Ile sababu ya mfanyakazi mmoja mmoja inatokana na jinsi mfanyakazi anavyowak-ilishwa na kiongozi wake katika sehemu yake ya kazi na faida za wazi wanazopata wafanyakazi wanachama. Hii ina maana kwamba kazi nzuri na za uwakilishi za chama zinawavutia sana wafanyakazi ku-jiunga na chama cha wafanyakazi. Aidha faida zaidi za wazi wanazopata kutoka kwe-nye chama chao, ni sababu ya kutosha ya kuwavutia wafanyakazi kujiunga na chama cha wafanyakazi.

Ama sababu za pamoja ni kuhusu:

• Uwezo mkubwa wa chama wa kufikia mazungumzo na mwajiri yahusuyo malipo bora na hali bora za kazi.

• Uwezo mkubwa wa viongozi wa kush-awishi wafanyakazi kujiunga na chama.

• Uwezo mkubwa wa chama kuhami ajira za wanachama.

• Wafanyakazi/wanachama kuwa na uw-ezo wa kumiliki mazingira ya kazi, na wafanyakazi/wanachama kuweza ku-pata uungwaji mkono wa kijumla. Kazi za viongozi mbali mbali wa chama zimefafanuliwa kwa ufasaha katika vi-fungu vya Katiba za chama husika.

Misingi ya Vyama Vya Wafanyakazi

Tumeona kuwa zipo sababu za msingi ziliz-opelekea kuundwa kwa vyama vya wafan-yakazi. Vyama hivyo vinaundwa kutokana na misingi muhimu ifuatayo:

(i) Umoja

Msingi wa kwanza wa kuundwa kwa vyama vya wafanyakazi ni Umoja. Nguvu za chama chochote cha wafanyakazi zinatokana na umoja, mshikamano, kujituma na kujitolea

kwa wanachama wake. Chama kinamudu kutekeleza majukumu yake na matarajio ya wanachama wake chini ya msingi muhimu wa umoja na mshikamano wa wanachama wake. Katika hali hii wanachama wote wa-naamini kabisa kuwa kinachomgusa mwa-nachama mmoja huwagusa wote. Katika hali hiyohiyo kinachowagusa wanachama wote humgusa mwanachama mmoja mmoja. Nguvu na msukumo wa chama cha wafanyakazi dhidi ya waajiri hutegemea kwa kiasi kikubwa jinsi wafanyakazi katika sehemu ya kazi inayohusika walivyounga-na. Kama idadi ya wanachama ni kubwa na wanazungumza kwa sauti moja, basi nguvu yao inakuwa kubwa zaidi.

(ii) Uhuru

Chama cha wafanyakazi kitaweza kukidhi mahitaji ya wanachama wake na kufikia malengo yaliyoundiwa na kuungwa mkono na wafanyakazi kama kitaongozwa na wa-nachama wenyewe. Ni wanachama pekee wanaojua mambo yanayowasibu katika se-hemu zao za kazi na hivyo kuyaainisha na kuyalinda malengo yao. Vyama vya wafan-yakazi vinapaswa kuwa huru na kwa vyo-vyote vile visitawaliwe na serikali, waajiri, taasisi za dini au vyama vya siasa. Chama cha wafanyakazi ni umoja wa wafanyakazi unaoundwa na wafanyakazi wenyewe na wenye:

• Kuongozwa na wanachama wenyewe.

• Kuendeshwa kwa niaba ya wanachama.

• Kugharimiwa na wanachama wenyewe.

(iii) Demokrasia

Demokrasia ya vyama vya wafanyakazi ni nafasi ya wanachama kuendesha umoja wao kwa uhuru na kwa uwazi kwa lengo la kuleta maendeleo ya wanachama wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote. Demokrasia ni nguzo muhimu ya chama cha wafanyakazi. Chama cha wafanyakazi kinachoendeshwa kidemokrasia kinatoa nafasi kwa wanacha-ma wake kutawala shughuli za chama chao na kutoa maamuzi mbali mbali ya kuende-leza chama chao.

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

15

Njia za kidemokrasia za kuendesha vyama vya wafanyakazi ni pamoja na:

• Viongozi wa vyama vya wafanyakazi huchaguliwa kidemokrasia na wana-chama wenyewe kila baada ya muda maalumu kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu za chama.

• Wanachama kuwa na haki ya kuelim-ishwa kuhusu masuala ya vyama vya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kupewa elimu kuhusu katiba na kanuni za cha-ma ili kuwawezesha kuwa na upeo wa kuweza kushiriki kikamilifu katika shu-ghuli zote za chama pamoja na taratibu za chama za kutoa maamuzi.

• Wanachama wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote kupewa haki na majukumu sawa.

• Wanachama katika ngazi zote kuwakil-ishwa katika vikao vyote vyenye kutoa/kufanya maamuzi.

• Wanachama kuwakilishwa katika vyom-bo vya wafanyakazi, kitaifa, kikanda, na kimataifa.

Sababu za Kuunda Vyama vya Wafanyakazi

Wafanyakazi wanakuwa na matatizo kadhaa katika sehemu zao za kazi. Matatizo hayo hayatokani na amri ya Mungu. Hivyo wafan-yakazi hawana budi kuyatatua ili kuondoa vikwazo katika shughuli zao za kazi na kuin-ua hali zao za maisha wakiwa wafanyakazi. Kwa mfano, katika kiwanda kuna mtaji, utawala/uongozi na nguvukazi. Kila kimoja kinajitegemea ingawa katika uendeshaji/utendaji wa kazi vinategemeana na malen-go yao pia yanatafautiana. Mabepari ambao ndio wenye kuwekeza mtaji, malengo yao ni kupata faida kubwa kadri inavyowezekana ambapo utawala/uongozi upo pale kulinda na kukuza maslahi ya mabepari (wenye mtaji) na wafanyakazi huuza nguvu zao. Katika mazingira hayo, wafanyakazi huishia kunyonywa. Wafanyakazi kwa hivyo wanas-tahiki malipo ya haki na usawa kwa ngu-vukazi wanayoitoa .Uwezo wa mfanyakazi mmoja mmoja kupigania haki yake ni mdogo. Hakuna mafanikio ya maana anay-oweza kupata mfanyakazi peke yake katika kupigania haki yake. Ni kwa kupitia chama cha wafanyakazi pekee kinachounganisha pamoja nguvu za wafanyakazi wote kina-

Dhuluma kazini

Malipo duni

MafutaMaziwa Mkate

Wewe! Mshahara, mbona hukui? Marafiki zako wote wamekua.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

16

choweza kuinua heshima ya wafanyakazi mbele ya waajiri, na kupigania ujira utaka-omwezesha mfanyakazi kuishi, kupata hali bora ya maisha, na kupata marupurupu mengine. Hayo hasa ndiyo yaliyoleta haja ya wafanyakazi kujiunga pamoja na kuibuka na vyama vya wafanyakazi. Kuunda vyama vya wafanyakazi ni haki ya msingi ya wafan-yakazi wenyewe.

Aina ya Vyama Vya Wafanyakazi- Manufaa na Kasoro zake

Kimsingi, kuna aina tatu za Vyama vya Wa-fanyakazi, nazo ni:

i) Vyama vya Fani za kazi.ii) Vyama vya Fani za kazi tafauti. iii) Vyama vya Kisekta.

Vyama vya Fani za kazi

Hivi ndivyo vyama vya mwanzo kabisa vya wafanyakazi. Vyama hivi hujumuisha wa-fanyakazi wa fani maalumu kama, waashi, madereva, mafundi umeme, na wengine. Kwa mantiki hiyo, madereva pekee wa-naruhusiwa kujiunga na chama cha wa-

fanyakazi madereva, bila ya kujali eneo wa-nakofanyia kazi au mwajiri wao. Kwa hiyo wafanyakazi huungana kutokana na fani yao ya kazi.

Vyama vya aina hii hudhibiti upatikanaji wa nguvu kazi kwa mtindo wa utoaji mafunzo kwa wafanyakazi wapya wanaopenda fani hiyo.

Vile vile vyama vya aina hii vinaweza kuwe-ka viwango vya malipo ya mfanyakazi kwa saa, siku, wiki au mwezi.

Vyama hivi haviwezi kufanya kazi katika vi-wanda vikubwa (na hasa vya siku hizi) vy-enye shughuli nyingi.

Vyama vya Wafanyakazi wa Fani Tafauti

Vyama hivi huundwa na wafanyakazi wote katika sehemu ya kazi bila ya kujali mwa-jiri wao, fani/stadi au kiwanda watokacho. Historia inaonesha kuwa vyama hivi viliun-ganisha wafanyakazi wasio na stadi yoyote ya kazi ambao hawakubaliki kujiunga na vy-ama vya wafanyakazi wenye fani maalumu.

Umoja ni nguvu

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

17

vile sekta ya viwanda vya kemikali, mbao, uchapaji, na nyinginezo. Katika hali hii, wafanyakazi wote wenye stadi na wasio na stadi, wa maofi sini, na wasio maofi sini, wanaweza kuunda chama kimoja, mradi tu wanafanya kazi katika sekta moja.

Katika chama cha aina hii ni rahisi wana-chama kuchukua hatua za pamoja au kuwa na msimamo wa pamoja pale inapobidi.In-awawia rahisi wanachama kushughulikia matatizo ya pamoja yanayowakabili wana-chama/wafanyakazi wote katika sekta in-ayohusika.

Kama ilivyokuwa katika vyama vya wafan-yakazi wa fani za kazi tofauti, ni vigumu kutengeneza sera itakayokidhi matakwa na mahitaji ya vikundi mbali mbali vya wafan-yakazi katika sekta husika.

Wajibu wa Vyama Vya Wafanyakazi na Uhusiano wake na Umma

Vyama vya wafanyakazi vinaundwa na wa-fanyakazi wenyewe kwa dhamira ya ku-tumia chombo hicho kutatulia matatizo yao yanayohusu kazi na ustawi wao kama

Vyama vya jumla vya wafanyakazi wenye fani za kazi mbali mbali vinafaa sana katika nchi ambayo haina kundi moja la wafan-yakazi linalotosheleza kuunda chama cha wafanyakazi chenye nguvu.Vyama hivi vin-aunganisha wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika kampuni moja au sehemu moja ya kazi ili kuwakabili waajiri ambao hush-irikiana na kufanya kazi kama timu, Katika maeneo yenye chama cha aina hii, ni ra-hisi kuchukua hatua/msimamo wa pamoja, Baadhi ya huduma (kama utafi ti) zinaweza kutolewa kwa pamoja na hivyo kuokoa muda na kupunguza gharama.

Kasoro ya vyama hivi ni kuwa vinaweza ku-leta ushindani na kugombea wanachama pale penye chama zaidi ya kimoja. Hali hii inaweza kudhoofi sha nguvu za chama/vy-ama.Aidha katika maeneo ya chama cha aina hii ni vigumu kutengeneza sera itakay-oweza kukidhi matakwa ya vikundi vyote vya wafanyakazi vinavyohusika.

Vyama vya Kisekta

Vyama vya kisekta huunganisha wafan-yakazi wote wa sekta inayohusika kama

MapatoUtoaji Mafunzo

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

18

wafanyakazi. Vyama vya wafanyakazi kwa hivyo vitakuwa na wajibu ufuatao:

• Kuunganisha nguvu za wafanyakazi.

• Kuimarisha umoja na mshikamano wa wafanyakazi.

• Kutoa huduma maridhawa kwa wana-chama.

• Kuwashirikisha wanachama katika masuala yote ya chama.

• Kujihusisha katika kukuza uchumi wa nchi.

• Kusimamia utekelezaji wa kazi kwa ufanisi na kwa tija.

Uhusiano wake na Umma

Chama cha wafanyakazi kilicho makini hakiwezi kufanya kazi zake kwa mafanikio bila ya kushirikiana na umma unaozunguka mazingira ya kufanyia kazi ya chama hicho. Hii ina maana kuwa umma lazima utam-bue kuwepo kwa chama hicho na pia uunge mkono juhudi na shughuli zinazotendwa na chama hicho. Hali hii inakilazimisha cha-ma cha wafanyakazi kujitahidi kujitangaza

kwa umma pamoja na majukumu yake ya kawaida na kuweka wazi malengo na ma-jukumu yake ambavyo vitahitaji kuungwa mkono na umma na wafanyakazi wenyewe. Chama cha wafanyakazi kinachofanya kazi nje ya ufahamu wa umma mara nyingi huwa vigumu kufanikisha majukumu yake, na pia hutoa nafasi kwa umma kukishuku. Chama cha wafanyakazi hushughulikia waajiriwa ambao ni sehemu ya umma. Ndio maana inasisitizwa kuwa chama cha wafanyakazi kisijitenge kando na umma.

Majukumu ya Vyama Vya Wafanyakazi

Shughuli za Vyama vya Wafanyakazi zi-naambatana na historia ya kuundwa kwao. Kihistoria wafanyakazi walilazimika kujiku-sanya na kuunda umoja wao kutokana na madhila waliyokuwa wakifanyiwa na waajiri wao enzi za Mapinduzi ya Viwanda huko Ul-aya katika karne ya kumi na tisa. Hivyo shu-ghuli za mwanzo za umoja wa wafanyakazi zikawa kupaza sauti zao kupinga madhila waliyokuwa wakitendewa na waajiri wao. Wakipinga kufanyishwa kazi kwa muda mrefu/saa nyingi bila ya mapumziko na bila ya kupatiwa malipo yaliyolingana na nguvu walizozitumia. Wakipinga kufanyishwa kazi

Kuhamasisha

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

19

katika mazingira hatarishi kiafya na usala-ma wao bila ya kuchukuliwa hatua za ta-hadhari za kutosha.Walipinga kutosikilizwa na waajiri wao wanapohitaji kuwaeleza ma-tatizo yanayowafika wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kazi. Hivyo majukumu ya msingi ya vyama vya wafanyakazi ni kupiga-nia haki na maslahi ya wanachama wake na wafanyakazi kwa ujumla. Shughuli nyingine za vyama vya wafanyakazi ni:

• kuhamasisha na kushawishi wafan-yakazi kujiunga pamoja.

• kuwatetea wanachama na wafanyakazi kwa ujumla maendeleo ya uchumi, usta-wi wa jamii, na elimu.

• Kutatua matatizo ya wanachama mmoja mmoja na matatizo ya jumla ya wafan-yakazi; kwa mfano masuala ya likizo, vi-faa vya kutendea kazi, vifaa kwa ajili ya kinga ya mfanyakazi, nyongeza ya msha-hara.

• Kujihusisha na shughuli za siasa na maendeleo ya nchi.

Majukumu mengine ya msingi ya vyama vya wafanyakazi ni:

Kulinda haki za wafanyakazi

Kuwa mwanachama kunamfanya mfan-yakazi alindwe na chama chake katika ajira yake na kulinda usalama wa ajira yake.

Chama chake cha wafanyakazi kinahakiki-sha kuwa haonewi wala hanyanyaswi au kufukuzwa kazi bila ya sababu za msingi na bila ya kuzingatiwa taratibu na sheria za kazi katika nchi.

Kushughulikia Mashauri ya Kikazi

Chama cha wafanyakazi humuakili-sha mwanachama wake aliyeonewa kwa kutafuta suluhu ya haki.

Kusuluhisha Migogoro

Chama cha wafanyakazi kina uwezo, mbi-nu, na hata nyenzo za kushauriana na ku-

suluhisha migogoro ya kikazi kwa niaba ya mwanachama wake.

Kuimarisha masharti ya kazi

Chama cha wafanyakazi kina wajibu wa kupigania ujira bora, usalama kazini, masharti bora ya kazi, na maisha bora kwa mwanachama pamoja na familia yake.

Kuhamasisha na Kuingiza Wanachama Wapya

Nguvu kuu ya chama cha wafanyakazi in-atokana na wingi wa wanachama wake. Hivyo uongozi wa chama cha wafanyakazi hauna budi kutilia mkazo suala la kuingiza wanachama wapya wakati wote. Uzoefu unaonesha kuwa idadi ya wanachama wa chama cha wafanyakazi haibaki ilivyo kwa muda mrefu kwa vile wanachama baadhi ya wakati hubadili sehemu za kazi na hivyo kulazimika kuhamishia uanachama wake kwa chama kingine. Wanachama wengine hufikia muda wa kustaafu na hivyo kupoteza sifa za kuwa wanachama wa chama cha wafanyakazi. Na wengine hupunguza idadi ya wanachama kwa kufariki dunia. Hali hii inalazimisha uongozi wa chama cha wafan-yakazi wakati wote kufanya maandalizi ya kuingiza wanachama wapya katika chama. Juhudi hizo ni zile za kuwahamasisha kuji-unga na chama.

Kufanya Majadiliano kwa Ajili ya Kufunga Mikataba ya Hali Bora ya Kazi

Moja kati ya majukumu makuu ya chama cha wafanyakazi ni kufanya majadiliano yenye lengo la kufunga mkataba wa hali bora ya kazi kwa niaba ya wanachama. Mi-kataba hii inatarajiwa kuwanufaisha wa-nachama wa chama cha wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla. Mikataba hii kwa kawaida huimarisha ujira wa wanachama, huweka masharti bora ya kazi pamoja na maisha bora kwa wanachama na familia zao.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

20

Kuelimisha Wanachama

Elimu ni nguzo muhimu ya vyama vya wa-fanyakazi. Vyama vya wafanyakazi vina wa-jibu wa kuwaelimisha viongozi wake na wanachama kwa ujumla kuhusu masuala mbali mbali ya vyama vya wafanyakazi ili kuwapa uwezo wa kushiriki kikamilifu kati-ka shughuli zote za chama cha wafanyaka-zi. Elimu hii pia itawasaidia wanachama wa kawaida kutekeleza majukumu yao ya kazi katika sehemu zao za kazi kwa ueledi. Aid-ha ni jukumu la chama kuelimisha wana-chama kwa kutoa habari na mafunzo kwa njia ya machapisho; mfano vipeperushi, makala, vijarida, magazeti, na machapisho mengine.

Kuweka Shindikizo na Kuhamasisha

Kuhamasisha na wakati mwingine kushindikiza serikali ili itunge sheria bora za kazi kwa manufaa ya wanachama na wafanyakazi kwa ujumla, ni jukumu am-balo husaidia kuimarisha chama cha wa-fanyakazi.

Kukusanya Michango ya Chama

Chama cha wafanyakazi ni cha wafanyakazi kwa ajili ya wafanyakazi. Chama cha wa-fanyakazi kina majukumu mengi ambayo utekelezaji wake unahitaji rasilimaliwatu na fedha. Mahitaji hayo lazima yatokane na wanachama wenyewe. Vyama rafiki vinaweza kusaidia juhudi za wanachama wenyewe. Hivyo wanachama wana wajibu wa kulipa ada na kutoa michango min-gine , kwa ajili ya kuendeshea chama chao. Michango hii huwezesha chama kufanya shughuli zake pamoja na kutoa huduma kwa wanachama wake.

Kuendesha/Kuongoza Migomo

Kugoma ni haki ya wafanyakazi. Mgomo ni silaha muhimu sana ya wafanyakazi. Lakini silaha hii hutumika kwa nadra. Silaha hii hutumika pale mwafaka unapokosekana baada ya kupitia na kumaliza hatua zote zilizopo za kusuluhisha mgogoro. Katika hatua hii chama cha wafanyakazi huchukua

jukumu la kuendesha na kuongoza mgomo kwa mujibu wa maelekezo ya katiba ya cha-ma na sheria za kazi za nchi

Kushirikiana na Vyama na Mashirikisho ya Taifa na Kimataifa

Chama cha wafanyakazi hakipaswi kufanya shughuli zake peke yake. Lazima kishiriki-ane na vyama vingine na mashirikisho, nchini na kimataifa. Mashirika muhimu na maarufu katika ulimwengu wa kazi ni Shiri-ka la Kazi la Duniani, Lo-Norway na taasisi nyingine.

Majukumu Mapya ya Chama cha Wafan-yakazi;

• Kujadili mikataba ya afya na usalama kazini.

• Kuunda ushirikiano na taasisi nyingine za kijamii, vikundi vya mazingira ili kue-ndesha kampeni kuhusu uhifadhi wa mazingira.

• Elimisha wanachama kuhusu ukimwi kwa wanachama.

• Kuelimisha juu ya masuala ya jinsia na jinsi ya kuyahusisha na maswala ya vy-ama vya wafanyakazi.

• Kushawishi na kuingiza wanachama ku-toka sekta isiyo rasmi.

• Kuvinadi vyama vya wafanyakazi.

• Kuelimisha wanachama kuhusu athari za utandawazi hasa katika masuala ya kazi.

• Kutoa mafunzo kwa wanachama walio-punguzwa kazi ili waweze kuingia katika ajira mbadala.

• Kuwatayarisha wanachama wanaokar-ibia kustaafu kazi kwa kuwapa mafunzo ya kukabili hali ya kustaafu.

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

21

Haki za Vyama vya wafanyakazi na Haki Nyinginezo za Binadamu

Baadhi ya Haki za Msingi za Binadamu am-bazo zinapaswa kutiliwa maanani kama haki za mfanyakazi ni:

• Binadamu wote wamezaliwa huru na wako sawa katika heshima na haki. Seri-kali na vyombo vingine havitoi haki kwa watu. Haki hizi tunazo kama binadamu tangu kuzaliwa.

• Kila mtu anastahiki haki zote na uhuru wa kila namna bila kujali kabila, rangi, jinsia, lugha, dini, siasa, au mawazo tafauti, utaifa, au chanzo cha ujamii, mali, kuzaliwa au hali nyingine.

• Watu wote wako sawa mbele ya sheria na wanastahili, bila ya ubaguzi wowote, kupata ulinzi sawa wa sheria.

• Kila mtu ana haki ya kuishi kwa uhuru na kuwa na usalama wake mwenyewe.

• Hakuna atakayefanywa mtumwa au ku-fanyishwa kazi za kinyama.

• Hakuna atakayehamishwa, kuteswa, ku-fanyiwa ukatili, kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu, matendo au adhabu zi-nazodhalilisha.

• Hakuna atakayekamatwa bila ya kosa la wazi, au kuwekwa kizuizini au kuham-ishwa na kuwa mkimbizi.

• Kila mtu anastahiki, kupata usawa ka-mili, kusikilizwa kwa haki na uwazi na vyombo huru, visivyofungamana na upande wowote.

Haki hizi ni za dunia nzima na zinatumika kwa watu wote popote pale, wakiwemo wafanyakazi. Haziwezi kugawanywa, zi-kawekwa mbadala au zikapewa vipaum-bele tafauti. Kwenye haki hizi za msingi, haki nyingine zinajitokeza:-

i) Haki ya kuishi: inaleta haki ya kufanya kazi na

• Haki ya malipo ya kutosha kulin-gana na kazi iliyofanyika.

• Haki ya usalama sehemu za kazi pasipo na hatari kama vile ajali, kemikali zinazoathiri au kitu cho chote kinachotishia afya ya mfan-yakazi kimwili, kiakili, au kisai-kolojia.

ii) Haki ya kuishi: inaruhusu pia haki ya mtu kutafuta njia zozote za kisheria kumwezesha kumudu maisha yake.

Njia hizi zinajumuisha:

• Haki ya kujiunga pamoja.

• Haki ya majadiliano ya pamoja, hivyo kumpa mfanyakazi haki ya kujishirikisha na kuunda vyama vya wafanyakazi.

Haki za Vyama vya Wafanyakazi:

Vyama vya wafanyakazi ni taasisi huru zi-nazoundwa na wafanyakazi wenyewe kwa hiari zao, ili kwa pamoja, watetee, walinde, na waendeleze haki na maslahi yao sehe-mu za kazi.

Hii inamaanisha kwamba wafanyakazi wana uhuru wa kuunda na kujiunga katika umo-ja kwa ridhaa yao na kuruhusika kufanya majadiliano ya pamoja.Ili kuweza kujiunga na kufanya majadiliano ya pamoja, haki za chama cha wafanyakazi za kiraia, na haki nyingine za binadamu zilizoanzishwa hapo juu, lazima zitolewe. Haki hizi zinatambua heshima, uhuru, na usalama wa mtu.

Haki za vyama na haki nyingine za binadamu mara nyingi haziheshimiwi kwa hivyo ni nadra kutekelezwa

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

22

Haki za vyama vya wafanyakazi ni sehemu ya haki za binadamu. Haki ya kuunda na kujiunga na chama cha wafanyakazi ni haki ya msingi katika haki hizi. Haki hii inawapa wafanyakazi haki ya kutetea, kulinda, na kuendeleza haki binafsi na haki za pamoja za wafanyakazi, ambazo ni pamoja na :-

• Haki ya kufanya kazi katika mazingira yaliyohuru/tulivu, na yasiyokuwa na vu-rugu na unyanyasaji.

• Haki ya kulindwa dhidi ya ukosefu wa ajira.

• Haki ya hifadhi ya jamii pamoja na haki ya kuburudika, mapumziko, saa muwa-faka za kufanya kazi, na haki ya kupata likizo na malipo.

Haki za vyama na haki nyingine za binad-amu mara nyingi haziheshimiwi kwa hivyo ni nadra kutekelezwa. Serikali nyingine zinafi kia hatua ya kudai kwamba haki za kiuchumi lazima zipewe kipaumbele zaidi ya haki za kisiasa, na kwamba watu lazima wale kwanza kabla ya kuanza kufurahia haki za kidemokrasia. Huu ni msimamo potofu! Wanaharakati wa vyama vya wafan-yakazi wanakataa kuunga mkono msima-mo huu. Wanashikilia kwamba kuwepo kwa

demokrasia ya kweli tu ndipo kunaweza kuwepo maendeleo ya uchumi pamoja na haki za kijamii kwa wananchi wote.

Msimamo wa chama cha wafanyakazi kwamba maendeleo ya kiuchumi na haki ya jamii kwa raia wote, vinaweza kupatikana kweli kweli kama demokrasia kamili itaku-wepo, inaungwa mkono wazi na kuima-rishwa na maazimio/mikataba mbali mbali ya kitaifa na kimataifa ambayo inaelezea nafasi ya haki za vyama vya wafanyakazi na haki nyingine za binadamu.

Haki za vyama vya wafanyakazi ni sehemu ya haki za binadamu. Haki hizi hazitolewi moja kwa moja na kwa urahisi na waajiri wetu au wanasiasa. Haki za wafanyakazi huvunjwa kwa urahisi mara kwa mara ingawa mara nyingi haki hizo hutolewa angalau kwenye mikataba – katika sheria na katika mikata-ba ya kimataifa, na kuheshimiwa kwa haki hizi mara nyingi husikika katika hotuba za wanasiasa. Ni wazi kwamba wanasiasa na wakuu wa serikali huzisifu juhudi za seri-kali zao kuhusu utoaji haki. Lakini haki hizi, kwa kweli haziheshimiwi ipasavyo.

Katika ulimwengu wa sasa, unaoshuhu-dia ubinafsishaji, utandawazi wa kiuchumi na masharti yanayotolewa kwa serikali,

Umuhimu wa majadiliano

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

23

hasa katika ulimwengu wa tatu, na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, ma-badiliko ya biashara duniani, husababisha kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za wa-fanyakazi. Wengine, hasa waajiri, husema kuwa haki za binadamu ni starehe ambayo lazima isubiri mpaka maendeleo ya kiu-chumi yafikie kiwango cha juu.

Vyama vya wafanyakazi vinaamini kwam-ba demokrasia haiwezi kumea na kukua endapo haki za msingi za binadamu hazi-heshimiwi. Suala hili ni dhahiri kwa vyama vya wafanyakazi kwani haviwezi kufanya kazi ipasavyo au kuwakilisha wafanyakazi katika majadiliano na waajiri kuhusu haki zao. Maendeleo ya kiuchumi na kijamii hukwamishwa na ukosefu wa haki za bin-adamu.

Majadiliano

Majadiliano ni utaratibu wa mawasiliano baina ya watu au kikundi cha watu amba-cho kina lengo la kufikia makubaliano kwa pande zote zinazohusika. Majadiliano ni mazungumzo baina ya watu au pande to-fauti zenye malengo ya kuelewesha mam-bo, kuondoa matatizo, kuondoa tafauti, kuleta makubaliano, na kuleta muwafaka. Kuna mambo mengi yanayoangaliwa katika majadiliano ili kila upande unufaike kuto-kana na majadiliano hayo.

Mawasiliano yanaweza kufanyika kwa njia tafauti zikiwemo:

• Uso kwa uso.• Kwa simu.• Kwa maandishi.• Kwa mikutano.

Majadiliano ndio kazi kubwa na muhimu na kwa hakika ndio sababu ya msingi ya ku-undwa vyama vya wafanyakazi ili kuanzisha na kufanya majadiliano ya mapatano na waajiri yenye lengo la kufanya kazi katika mazingira tulivu na salama na kuwapatia hali bora ya maisha ya wanachama wake na wafanyakazi kwa ujumla. Hivyo nchi yoyote inapokubaliana na mikataba ya uhuru wa kuanzishwa vyama vya wafanyakazi, ni lazi-ma ikubaliane na uhuru wa wafanyakazi wa

kujadiliana na waajiri wao kuhusu hali bora za kazi katika sehemu zao za kazi. Kazi hii ya utetezi ina gharama, ngumu na yenye kuhitaji weledi, ujuzi , mbinu za kitaalamu, umakini hasa katika ufuatiliaji, ukakamavu, kujiamini, hoja maridhawa, uvumilivu, na ujasiri. Lengo kuu la majadiliano ni kuleta mabadiliko ya maisha ya wafanyakazi na mwenendo mzima wa ajira katika sehemu za kazi. Matokeo mema ya kazi hii muhimu ndio inayowapa heshima viongozi wa vyama vya wafanyakazi, serikali na waajiri. Ikum-bukwe kuwa majadiliano katika sehemu za kazi ni miongoni mwa haki za binadamu.

Umuhimu wa Majadiliano

Majadiliano ni muhimu sana katika mai-sha yetu ya kila siku tukiwa majumbani mwetu, sehemu zetu za kazi, katika sa-fari zetu, katika kutafuta mahitaji yetu, na hata katika kuishi na jamii zinazotuzun-guka. Tunashuhudia jamii zikizozana, wa-fanyakazi na waajiri kutoelewana, majirani kupapurana, na hata mataifa kupigana, kwa sababu tu ya ukosefu wa kujadiliana itokeapo tafauti ya aina yoyote baina yao. Majadiliano ni haki ya msingi ya mfanyakazi na nguzo miongoni mwa nguzo za ajira ze-nye staha. Nguzo nyingine ni:

• Haki ya wafanyakazi kujiunga pamoja.• Haki ya kufanya kazi.

• Haki ya Hifadhi ya Jamii ya wafanyakazi na familia zao.

Majadiliano, pamoja na ukweli kwamba hutoa fursa kwa wafanyakazi kueleza ma-tatizo yao katika sehemu zao za kazi, hu-saidia pia kuleta mambo yafuatayo:-

• Kuimarisha ufanisi na kuleta tija.

• Kutoa fursa ya kueleweshana kuhusu haki, wajibu, na mipaka ya majukumu ya kila upande.

• Kujenga uhusiano bora sehemu za kazi na katika jamii.

• Wadau wa sehemu za kazi kwa sababu wanajisikia kuwa wana umiliki wa se-

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

24

hemu zao za kazi, kuongeza ari ya uzal-ishaji kwa tija.

• Kupunguza na kutatua migogoro sehe-mu za kazi na hivyo kudumisha utulivu kazini.

• Yanaongeza mambo yasiyojumuishwa na kulindwa na sheria za kazi.

• Kukuza umoja miongoni mwa wafan-yakazi.

Njia za Kujadiliana

Tumeona haja kwa jamii kujadiliana ka-tika masuala mbali mbali yanayohusu maisha yao. Jamii ama asasi hujadiliana mambo yao kwa kutumia njia mbali mbali kutegemeana na hali halisi inayotawala kwa wakati husika. Miongoni mwa njia maarufu za majadiliano ni:

• Kuandikiana barua.• Kupigiana simu.• Kutumiana ujumbe.• Kukutana uso kwa uso.• Kukutana kwenye vyombo vya kisheria.• Kukutana kwenye mikutano ya hadhara.

Vyama vya wafanyakazi vinaamini na vinakubaliana na rai ya kukutana na ku-fanya majadiliano katika vyombo rasmi vili-vyowekwa kisheria. Mijadala katika hali hii itakuwa yenye tija na manufaa kwa pande zote zinazohusika. Wafanyakazi wanaami-ni hivyo kutokana na ukweli kwamba ku-fanya majadiliano ya hali bora ya kazi za wafanyakazi ni shughuli rasmi na muhimu ya vyama vya wafanyakazi. Kwa hivyo ma-jadiliano yanayoendeshwa baina ya vyama vya wafanyakazi na waajiri lazima yafanywe kwenye chombo maalumu kilichowekwa rasmi kisheria. Kinyume chake kutakuwa na majadiliano yaliyotayarishwa bila ya mpangilio kisheria, na matokeo yake ma-jadiliano hayo hayatakuwa na mashiko.

Kwa hivyo ili majadiliano yawe na maana na manufaa kwa mwajiri na mwajiriwa, lazima kuweko na chombo mahususi cha ma-jadiliano. Chombo hicho lazima kiundwe kisheria ili maamuzi yatokanayo na ma-

jadiliano hayo yawafunge wahusika wote. Aidha iwapo chombo hicho cha majadil-iano kitaundwa kisheria, uendeshaji wake utabainishwa ndani ya sheria na suala la chombo gani kinahusika na nini, wapi, vipi, lini, na masuala mengine, kama vile ya gharama za kuendesha chombo hicho yat-awekwa wazi na sheria .

Haja ya Kuwa na Chombo cha Majadiliano

Majadiliano ni shughuli ya mawasiliano baina ya wadau yanayokusudiwa kuleta maendeleo yanayohusu mambo ya kazi na wafanyakazi. Majadiliano hayo yanahusu uhusiano wa moja kwa moja baina ya wa-dau au uhusiano baina ya serikali na wadau. Majadiliano ni kubadilishana mawazo baina ya waajiri, wafanyakazi, na serikali. Wakati mwingine yanahusisha uhusiano baina ya wafanyakazi na uongozi bila ya hata kuhu-sisha serikali.Majadiliano ni njia inayowez-esha serikali, waajiri na wafanyakazi kuleta mabadiliko na kufikia malengo ya uchumi na maendeleo ya jamii. Ukweli kuhusu majadiliano ni kuwa kila mmoja miongoni mwa wanaojadiliana anabaki na nafasi yake na wajibu wa kila mmoja utawekwa wazi na haki ya kila mmoja itapatikana kwa wepesi na bila ya vikwazo.

Mambo Muhimu Yanayosaidia Kufikiwa kwa Majadiliano Yenye Tija

Maendeleo katika sehemu ya kazi na usta-wi wa wafanyakazi hayawezi kufikiwa bila ya ushiriki kikamalifu wa wafanyakazi, waajiri, na serikali. Majadiliano ya pamoja yanasaidia serikali, vyama vya waajiri na wafanyakazi kuwa na uhusiano madhubuti wa kikazi, kuona haja ya kutunga sheria bora za kazi zinazoweza kukabiliana sawa sawa na mabadiliko ya uchumi, na mahitaji ya jamii na pia kusaidia kuimarisha utawala wa shughuli za kazi nchini. Majadiliano yal-iyofanikiwa yana sifa ya kusaidia kuleta ma-jibu bora ya matatizo ya uchumi na jamii, yanasaidia kufikia utawala bora, yanasaidia kuleta amani sehemu za kazi na katika

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

25

jamii na pia yanasaidia katika kuendeleza uchumi. Ili majadiliano yenye tija kufi kiwa mambo yafuatayo yanahitaji kuzingatiwa:

i) kuimarisha na kutekeleza haki za msin-gi za uhuru wa kuunda vyama, kujiunga, na kufanya majadiliano ya pamoja.

ii) pawepo vyama imara vya wafanyakazi na waajiri vyenye uwezo na weledi wa ku-fanya majadiliano.

iii) pawepo dhamira ya kisiasa ya kufanya majadiliano miongoni mwa husika

iv) kuwepo chombo madhubuti cha kusaid-ia katika mchakato mzima wa majadil-iano.

Utaratibu wa Majadiliano:

Majadiliano ni utaratibu unaotumiwa na pande mbili au zaidi kufi kia makubaliano kuhusu matakwa ya pande zote. Majadil-iano yanaruhusu ufumbuzi huku mahu-siano mazuri yakiendelea. Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu yanayohitajika katika mchakato wa majadiliano:

• Kuwepo na pande mbili au zaidi zitaka-zojadiliana.

• Kuwepo na Matakwa/Matarajio tofauti ya pande hizo.

• Kuwe na nguvu sawa katika majadiliano.

• Kuwe na hali ya kutoa na kupokea hoja ili kuweka uhusiano bora katika ma-jadiliano.

• Kuwepo muendelezo wa uhusiano mwe-ma baada ya majadiliano.

• Kuwepo kwa nidhamu katika majadil-iano.

Hatua Tano Muhimu Katika Majadiliano:

Katika hali ya kawaida kuna hatua muhimu tano katika majadiliano:

(a)Hatua ya Kwanza

• Kupanga Mahitaji.

• Kutayarisha mambo ya kujadiliwa.

• Kuweka sababu/hoja – kutafuta taarifa na takwimu ili kuzipa uzito hoja za wa-naojadiliana.

Njia za Kujadiliana

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

26

• Kuweka mapendekezo kwa utaratibu wa viwango.

• Kuweka malengo yatakayotoa nafasi ya kufanikiwa.

• kutayarisha ujumbe – mzungumzaji, mwandishi wa muhtasari, na atakaye-fanya tathmini.

• kushughulikia suala moja baada ya jen-gine.

• kuhakikisha matumizi bora ya wakati.

(b)Hatua ya Pili• kutoa fursa kwa upande wa pili kutoa

msimamo wao.• kuanza kwa kujadili masuala rahisi kwa

kukubaliana. • kuangalia dalili (viashiria) kwa mfano

kuangalia ishara za mapema zinazo-onyesha ufanisi/matatizo ya majadiliano ili kutafuta mbinu bora zaidi za majadil-iano.

(c )Hatua ya Tatu: Mapendekezo• kuuliza maswali ili ipatikane taarifa zai-

di.• kuangalia vipengele mbali mbali.• Kutoa muhtsari wa makubaliano.• Kuepusha majadiliano kukwama kwa

kauli na vitendo. • Kutokuwa na hofu na kutosababisha

wengine kuwa na hofu.• kuangalia mwelekeo ili ujue yame-

pokewaje mapendekezo.• kuomba kuahirishwa majadiliano ili

upatikane muda wa mashauriano zaidi na kutoa taarifa.

(d)Hatua ya Nne:

• kuangalia faida kwa pande zote zinazo-husika.

• mtindo wa nipe nikupe huzingatiwa.

(e) Hatua ya Tano:

• Kuhakikisha yote yaliyotakiwa kujadiliwa yamejadiliwa.

• Kuhakikisha majadiliano yanawekwa katika maandishi/mkataba.

• Kuhakikisha kutokubaliana na kitu nje ya mamlaka ya wanaofanya majadiliano.

Sifa za Mkataba wa Bora Uliofikiwa kwa Majadiliano:

(i) Kila iwezekanavyo mkataba ufikie ma-takwa ya pande zote.

(ii) Juhudi zilizotumika ni ndogo kuliko mafanikio.

(iii) Mkataba unasifa za kuimarisha mahu-siano ya pande zilizofanya majadiliano.

(iv) Mkataba huzingatiwa na pande zote kwa kipindi kilichokubaliwa.

Mikataba Ya Hali Bora Ya Kazi

Majadiliano ya pamoja kwa kawaida huhu-sisha wafanyakazi, waajiri, na wakati mwingine serikali kutegemeana na aina ya mikataba wahusika waliyodhamiria kuifun-ga. Katika shughuli hii wahusika huunda timu yenye wajuzi wa fani mbali mbali zina-zohitajika katika utekelezaji wa majadiliano kwa ufanisi hadi kufikia tamati. Majadiliano haya kwa kiwango kikubwa huhusisha hali za ajira na wakati mwingine masuala yoy-ote yanayohusu matakwa ya wafanyakazi au waajiri.

Aina za Mikataba ya Hali Bora za Kazi

Kuna aina kuu mbili za mikataba ya hali bora za kazi:

i) Mikataba ya Utatu: Hii ni mikataba ya hali bora za kazi ya ngazi ya kitaifa.

Kabla ya kufikia kwenye kutia saini mika-taba, majadiliano yanaandaliwa ambayo yanahusisha vyama vya waajiri, vyama vya wafanyakazi na serikali. Majadiliano haya hufanyika kwa kupitia vyombo vya utatu ambavyo vimetajwa katika sheria za kazi za nchi inayohusika.

Katika nchi zinazoendelea, vyama vya wa-fanyakazi mara nyingi huwa dhaifu katika

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

27

kushiriki kwenye majadiliano ya pamo-ja. Katika hali hii maelekezo ya kisheria yanawekwa ili kusaidia majadiliano yawe ya manufaa kwa wahusika wote na hasa wa-fanyakazi. Katika nchi zilizoendelea tatizo la aina hii si kubwa kwani huko majadiliano ya pamoja ni jambo la kawaida na ni mad-hubuti.

ii) Mikataba ya Hali Bora za Kazi Inayohusisha Pande Mbili:

Mikataba ya aina hii hufikiwa baada ya kuhu-sisha pande mbili- vyama vya wafanyakazi kwa upande mmoja na waajiri kwa upande wa pili. Mikataba inaweza kuwa ya kitaifa au wakati mwingine inaweza kuwa ya se-hemu tu ya kazi inayohusika kutegemeana na maudhui ya mambo yanayojadiliwa ka-tika mikataba hiyo.

Mambo Yanayofaa Kuingizwa Katika Mika-taba Ya Hali Bora za Kazi:

1. Kuna mambo mengi yanayofaa kujadil-iwa katika majadiliano ya pamoja na kuingizwa katika mikataba ya hali bora za kazi.

2. Yafuatayo ni baadhi tu ya mambo yanay-oweza kujadiliwa na baadaye kuingizwa katika mikataba ya hali bora za kazi:-

• Malipo.• Bonasi /nyongeza ya mishahara.• Posho.• Saa za Kazi/saa za ziada za kazi.• Malipo ya saa za ziada za kazi.• Likizo.• Siku za Mapumziko/Sikukuu.• Afya na Usalama sehemu za Kazi.• Huduma za Kijamii.• Mafao ya Uzeeni.• Notisi.• Kupunguzwa Kazi.• Kanuni za Utumishi.• Mwongozo/Masharti ya Kazi.• Ajira na Mafunzo ya Kazi.

• Suala la uzazi na Wajibu Katika familia.

• Usawa wa kijinsia, Unyanyasaji, na Ubaguzi, na masuala mengine ya kikazi.

Inawezakana masuala haya yote yakawa yameshughulikiwa katika sheria ya kazi inayohusika, lakini kupelekwa kwenye ma-jadiliano ya pamoja yanaweza kupewa uzito zaidi, na kupata maboresho na hata baadhi ya wakati kuondosha baadhi ya vikwazo vili-vyotokana na sheria

Fedha za Chama cha Wafanyakazi

Chama cha wafanyakazi kama asasi kina-hitaji kuendeshwa na kuendelezwa ili iweze kufanikisha majukumu yake. Moja kati ya nyenzo muhimu ya kuendeshea chama ni rasimali fedha. Vyanzo vikuu vya mapato ya chama cha wafanyakazi ni – michango ya wanachama, michango maalumu, misaada na mikopo na mapato kutoka miradi inay-otekelezwa na chama.

• Michango ya wanachama – wanachama wa chama cha wafanyakazi ndio wenye wajibu wa kuendesha chama chao. Hivyo wanachama wana wajibu wa kukichang-ia chama chao. Mara nyingi michango hii hutokana na mikato kutoka katika mishahara yao ya mwezi kwa kiwango ambacho hutamkwa kwenye katiba za chama kinachohusika. Mkato huo huta-yarishwa na waajiri katika sehemu ya kazi ambayo mwanachama yupo, na kuituma moja kwa moja kwenye chama chake.

• Michango Maalumu – Katika njia ya ku-jinasua kiuchumi na wakati mwingine utekelezaji wa mradi fulani maalumu, chama huandaa shughuli ya muda ya kuingiza fedha. Walengwa wa uchangi-aji katika shughuli hii huwa wanachama wenyewe, viongozi maarufu wa chama, serikali, na hata waajiri. Shughuli maal-umu zenyewe zinaweza kuwa kama sherehe za kutunuku zawadi kwa wa-nachama na viongozi bora, na kukabili matukio mengine yasiyotarajiwa.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

28

• Misaada na Mikopo – Chama kwa kuongezea mapato yake kutoka michan-go ya wanachama na vyanzo vingine vya mapato, hupata misaada ya fedha ku-toka vyama rafi ki ndani na nje ya nchi. Wakati mwingine chama hulazimika ku-kopa fedha kutoka vyombo vya fedha au vyanzo vinginevyo kwa ajili ya kutekeleza shughuli maalumu za chama. Fedha hizi zilizokopwa hatimaye hurudishwa. Fedha hizi husaidia chama kutoa hudu-ma bora kwa wanachama wake. Aidha hutumika kutekeleza miradi maalumu ya chama wanachama waliyokubaliana kutekeleza.

• Miradi ya Uchumi – Chama cha wafan-yakazi kilichojipanga na kilichoimara, hutunisha mfuko wa mapato yake kwa kuanzisha miradi ya uchumi. Suala hili linahitaji kushughulikiwa kwa tahad-hari kubwa kwani kuendesha miradi ya uchumi kwa ufanisi kunahitaji ujuzi wa masuala ya uchumi. Uzoefu unatuone-sha kuwa si vyama vingi vya wafanyakazi vilivyofanikiwa katika nyanja hii.

Matumizi na Uhifadhi wa Fedha na Mali za Chama

Fedha na mali za chama mara nyingi vime-sababisha migogoro katika vyama vya wa-fanyakazi hadi wakati mwingine kufi kia

kusambaratika kwa chama. Chanzo cha migogoro ni matumizi yasiyoeleweka ya fedha za chama. Vyama vya wafanyakazi huendesha shughuli zake za kila siku kwa kutegemea pamoja na mambo mengine, hali ya fedha ya chama. Ili kuwa na hali nzuri kifedha, vyama hujiwekea taratibu ze-nye misingi bora na imara juu ya ukusanyaji, upokeaji, utunzaji, na utoaji wa fedha zake pamoja na kanuni zenye kuwaelekeza wote walioteuliwa ama kuajiriwa kusimamia au kushughulikia fedha za chama cha wafan-yakazi ipasavyo. Hivo basi, kanuni za fedha za vyama vya wafanyakazi ni kanuni zina-zoelekeza taratibu zinazotakiwa kufuatwa katika kushughulikia masuala ya fedha ya vyama yanayohusu mapato na matumizi ya fedha za chama. Baada ya chama kupata mapato yake kwa njia mbali mbali, hatua inayofuata ni chama kupanga namna fedha hizo zitakavyotumika.

Shughuli kubwa za chama cha wafanyakazi ambazo utekelezaji wake unahitaji fedha ni mishahara na ujira kwa ajili ya watumi-shi wa chama, shughuli za elimu ya wa-fanyakazi, huduma ya wanachama, kama vile ya utetezi katika mahakama ya kazi, msaada kwa mwanachama anapofi kwa na matatizo yasiyotarajiwa, matumizi kwa ajili ya vikao vya kikatiba vya chama, malipo ya huduma inayopatiwa chama na matumizi mengine yatakayoidhinishwa na vyombo vya chama.

Ili kuhifadhi na kutunza vyema fedha na mali za chama, vyombo vinavyohusika na chama huandaa kanuni za fedha kwa ajili hiyo. Kanuni hizo kwa kawaida huelekeza jinsi ya kufanya matumizi, vyombo vina-vyohusika na usimamizi wa fedha na mali za chama na maelekezo ya maeneo ya matumizi na jinsi ya kutunza mali za cha-ma. Vyombo maalumu vya chama cha wa-fanyakazi vya usimamizi wa fedha na mali za chama ni Kamati ya Fedha na Baraza la Wadhamini. Ili kuhakikisha fedha na mali za wanachama zinatunzwa na kutumika vizuri, Kamati ya Fedha hukagua fedha na mali na kutayarisha taarifa ambayo ina-wasilishwa katika Kamati ya Utendaji ya Rasilmali fedha

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

29

chama ambayo nayo hutayarisha taarifa ya fedha ya kila mwaka na kuiwasilisha kwa Baraza Kuu. Vitabu vya fedha vinakaguliwa na mkaguzi wa nje kila mwaka. Taarifa hii ya fedha iliyokaguliwa na mkaguzi wa nje kila mwaka inatakiwa itumwe kwa msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini, baada ya kupitishwa katika Baraza Kuu la Chama. Hizi zote ni jitihada za kuhakikisha matunzo na matumizi bora ya fedha na mali nyingine za wanachama.

Kiongozi wa vyama vya wafanyakazi ana-paswa kutilia maanani kipengele hicho. Ni kipengele ambacho kikitekelezwa vi-zuri hukijengea chama pamoja na viongozi wake haiba na uaminifu; sifa ambazo zina-hitajika sana kwa maendeleo ya chama cha wafanyakazi.

Viongozi ambao huvifanya vyama kama mali yao binafsi kwa kufanya watakavyo na kutumia mali na fedha bila ya utaratibu na kwa ubadhirifu, huwa wanajiaibisha we-nyewe mbele ya wanachama na hivyo ku-poteza sifa za kuwa viongozi bora wa vyama vya wafanyakazi. Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa ngazi zote za chama wa-napaswa kuepukana na tabia ya kuvifanya vyama vya wafanyakazi kama vitega uchumi (kuwanufaisha binafsi.)

Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi)

Chimbuko la siku ya Wafanyakazi Duniani

Siku ya tarehe 01 Mei ya kila mwaka ni siku maalumu ya wafanyakazi ulimwen-guni kote. Siku hii hujulikana kwa majina tofauti na husherehekewa kwa njia tofauti kutegemeana na mazingira, na uamuzi wa wafanyakazi wenyewe wa nchi inayohusika. Siku hii tukufu kwa tabaka la wafanyakazi hujulikana kwa majina kama vile “Labour Day” International Workers’ Day’ ‘ May Day’, na majina mengine. Lakini nini chimbuko la maadhimisho la siku hii ya wafanyakazi? Mei Dei ni kumbukumbu ya kihistoria kwa tabaka la wafanyakazi ulimwenguni kote ambayo chimbuko lake lilikuwa huko Chi-cago, Marekani mnamo mwaka 1886. Kili-chotokea huko ni kwamba wafanyakazi wa viwanda waliamua kufanya maandamano ya amani kuonesha kutoridhika kwao kuto-kana na madhila waliyokuwa wakitendewa na waajiri katika sehemu zao za kazi am-bapo kwa muda mrefu wafanyakazi mmoja mmoja walilalamikia hali hiyo bila ya ku-pata mafanikio yoyote ya mabadiliko. Hivyo kwa pamoja wakaamua kuingia barabarani

Migomo Kazini

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

30

kwa maandamano kuelezea masaibu yao katika kazi. Mikusanyiko hii ya wafanyakazi ilidhihirisha umoja na nguvu zao kama wa-fanyakazi. Malalamiko ya wafanyakazi hawa yalikuwa katika mambo makuu yafuatayo:

• Hali ngumu za kazi viwandani – wafan-yakazi walikuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu bila ya mapumziko ya ku-tosha. Matokeo yake walikuwa na umri mfupi wa kuishi.

• Kutokuwepo kwa sheria za kazi, na hasa sheria za kulinda usalama wa kazi na wafanyakazi.

• Kutokuwepo ushirikishwaji na uhuru wa kutoa mawazo.

• Kufanyishwa kazi zisizolingana na umri wao; watoto wenye umri kati ya miaka 6 – 18.

• Kutokuwepo kwa demokrasia hasa wa-fanyakazi kuzuiwa kuanzisha vyama vya wafanyakazi na kufanya majadiliano na mwajiri yaliyohusu hali bora ya kazi.

Kwa hivyo, wafanyakazi wa Chicago Mare-kani, siku ya tarehe 01 Mei katika mwaka 1886 walijiponza pale walipofanya maanda-mano ya amani kuelezea malalamiko yao na kutoridhika kwao katika mambo ya msingi kabisa yaliyotajwa hapo juu. Hawakuwa na njia nyingine isipokuwa hiyo kwa vile juhudi za mfanyakazi mmoja mmoja za kueleza kutoridhika kwao na hali hiyo hazikufua dafu. Wafanyakazi hao ambao ndio chanzo cha wenye viwanda kupata faida, badala ya malalamiko yao kusikilizwa na kujibiwa kwa amani, na kwa makini, walitawanywa kwa mtutu wa bunduki na baadhi yao kuje-ruhiwa na wengine kupoteza maisha.

Picha hii inadhihirisha jinsi mabepari wa-sivyo thamini utu wa mtu, hasa mfanyakazi. Siku hiyo waliuwawa makumi elfu ya wa-fanyakazi lakini damu yao haikupotea bure. Damu yao iliyomwagika ikawa chachu na vuguvugu kwa wafanyakazi kuweka msi-mamo wa kukataa kukandamizwa, kunyan-yaswa, na kunyonywa. Tukio hili la kihisto-ria liliamsha hisia mpya ya mapambano ya wafanyakazi dhidi ya dhuluma ulimwenguni kote. Kila palipokuwa na madhila na mate-so, mapambano ya wafanyakazi yalishami-ri. Wafanyakazi waliungana kudai haki zao, heshima na utu wao. Mshikamano wa wa-fanyakazi ulijidhihirisha ulimwenguni kote. Kwa mfano wafanyakazi wa kiwanda cha chuma walipogoma nchini Marekani, wali-ungwa mkono na wafanyakazi wa kiwanda cha magari cha huko Marekani, kwa nia ya kuonesha mshikamano na wafanyakazi wenzao.

Hali kama hii ilisambaa ulimwenguni kote kama moto wa kichaka. Kwa mfano wafan-yakazi wa kiwanda kimoja nchini Ufaransa wakigoma, basi huungwa mkono na wen-zao wa Ujerumani na kwengineko kote. Hali hii ilikuwa ni chanzo cha mshikamano wa kweli wa wafanyakazi wakati huo. Miaka mitatu baada ya maandamano ya Mei Mosi, yaani mwaka 1889, huko Mjini Paris nchini Ufaransa, kulifanyika Mkutano Mkuu wa Chama cha Kisoshalisti cha Dunia (Social-ist International). Mijadala ya Mkutano huo ilitawaliwa na maelezo ya hali mbaya ya

Wafanyakazi wana dhima kubwa katika

nchi zao ya kuendeleza amani na utulivu kwa manufaa ya nchi zao

na vizazi vijavyo. Kazi kubwa ya wafanyakazi

ni kulinda heshima ya kazi na kusaidia

kukuwa kwa uchumi wa nchi zao

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

31

maisha ya wafanyakazi ulimwenguni kote. Hatimaye Mkutano huo uliibuka na maazi-mio mazito na mambo yafuatayo yaliweke-wa mkakati maalumu:

1) wafanyakazi wafanyishwe kazi kwa saa zisizozidi nane kwa siku ili kwenda sam-bamba na uwezo wa binadamu wa ku-fanya kazi (Hapo awali wafanyakazi wa-likuwa wakifanyishwa kazi kwa zaidi ya saa 16 kwa siku).

2) Tarehe Mosi Mei ya kila mwaka iwe ikia-dhimishwa na kukumbukwa na wafan-yakazi ulimwenguni kote na waungane kwa maadhimisho ya kusherehekea siku ya kuanzishwa Umoja wa Wafanyakazi wa Ulimwengu mzima na kama ukum-busho wa mafanikio makubwa ya kuele-kea kwenye demokrasia na kujikomboa kwa tabaka la wafanyakazi.

Mambo ya Kujifunza kutokana na Historia ya Mei Dei

Mambo ya kujifunza kutokana na historia ya maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ni kwamba wafanyakazi popote pale walipo wana nguvu thabiti za

kuporomoa hata mlima Kilimanjaro iwapo watatumia nguvu zao hizo ipasavyo kwa ku-tumia umoja na mshikamano. Kwa hivyo-tunajifunza kwamba ‘Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu’. Siku ya tarehe 01 Mei kila mwaka wafanyakazi wanatakiwa kui-tumia kutathmini nguvu zao kama wafan-yakazi pamoja na kutathmini mafanikio na matatizo ya umoja wao wa wafanyakazi. Ni siku ya kutafakari jinsi viongozi wa wafan-yakazi walivyowaongoza wafanyakazi katika kujiletea maendeleo yao na ya mataifa kwa ujumla. Aidha historia ya maadhimisho haya imetufunza kwamba dhuluma haisimami mbele ya haki. Pamoja na uwezo, nguvu za mabavu, na za uchumi walizokuwanazo ma-bepari, ilibidi wasalimu amri na wayakubali matakwa ya wavujajasho, kwa kiasi fulani, kwa kuanzia. Wafanyakazi kwa hivyo, wana kila sababu ya kuendeleza mapambano ya kweli ya kudai haki na maslahi yao. Lakini wanapaswa kutumia nguvu na umoja wao katika kuandaa mikakati ya kuinua uchumi wa nchi zao. Wafanyakazi katika nchi zao huru hawapaswi kuwa watazamaji katika nyanja ya uchumi na maendeleo kwa ujum-la, bali wanapaswa kuwa washiriki wakuu. Hali na kazi na wafanyakazi katika karne ya

Hali ngumu kazini

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

32

kumi na tisa ni tofauti na hali ilivyo leo. Wa-fanyakazi waendelee kujifunza kuwa ‘Kazi ni Uhai ‘ Bila ya Kazi hakuna maisha na ni Kazi tu ndiyo inayoweza kubadili maisha ya watu na uchumi wa nchi kwa ujumla. Aidha kazi ndio inayompa heshima binadamu. Kufanya kazi kwa ufanisi na tija ndio liwe lengo la wafanyakazi popote walipo.

Wasia kwa Wafanyakazi

Wafanyakazi wana dhima kubwa katika nchi zao ya kuendeleza amani na utulivu kwa manufaa ya nchi zao na vizazi vijavyo. Kazi kubwa ya wafanyakazi ni kulinda heshima ya kazi na kusaidia kukuwa kwa uchumi wa nchi zao. Adui mkubwa wa wafanyakazi ni mwajiri anayewakandamiza, na anayewad-halilisha wafanyakazi. Wafanyakazi pop-ote walipo, kwa pamoja waungane na kwa sauti moja wakatae hali hiyo. Katika kua-dhimisha siku hii muhimu ya wafanyakazi duniani, wafanyakazi popote walipo wana-paswa kutafakari na kupima juhudi zao ka-zini na kuona iwapo zinaridhisha na kama kuna uwezekano wa kufanya jitihada zaidi za kuongeza faida/tija kwa manufaa yao na vizazi vyao vijavyo. Siku hii wafanyakazi wana wajibu wa kujiuliza iwapo malengo ya kazi waliyojipangia mwaka uliotangulia ya-mefi kiwa au hapana. Kama ‘hapana’, tatizo lilikuwa nini? Ikiwa jibu ni ‘ndiyo’, walifan-yakazi kwa tija?

Siku hii ni ya wafanyakazi kujivunia ma-fanikio yao na kutafakari matatizo yao na baadaye kuyapatia ufumbuzi au majibu. Siku hii ni ya kuandaa mipango mipya ya kazi kwa ajili ya mwaka unaofuata, na kujadiliana juu ya mbinu na mikakati ya kutekeleza mipango hiyo. Siku hii pia in-awapa wafanyakazi nafasi ya kujiuliza iwapo walifanya shughuli zao za kazi kwa ushirikiano na viongozi wa kazi ili kuende-leza amani katika sehemu za kazi na hivyo kupata nafasi ya kufanya shughuli zao kwa utulivu na kwa tija.

Wafanyakazi ndio wazalishaji wakubwa na pia ndio watoa huduma. Siku ya Mei Mosi ni siku muhimu kwao wakizingatia historia ya siku hiyo. Wanapaswa kufanya kazi kwa mashirikiano na kwa amani ili waweze ku-zalisha kwa tija na kutoa huduma bora kwa wananchi wao. Aidha wafanyakazi hawa-paswi kujiingiza katika mtindo mbaya wa kutoa na kupokea rushwa licha ya matatizo ya kiuchumi yanayowakabili. Wasisahau kuwa ‘Rushwa ni Adui wa Haki’, namba moja. Vyama vya wafanyakazi vinatakiwa kuunga mkono hatua zo zote za serikali zao zinazochukuliwa dhidi ya watoa/wapokea rushwa, wazembe, na wabadhirifu wa mali za umma. Wafanyakazi waendelee kuhubiri na kulinda amani ya nchi zao na kamwe wasikubali kurubuniwa na kuvunja amani ya nchi zao.

UONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Sura3333333

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

34

na vitendo vyake kwa chama, wanachama na wafanyakazi kwa ujumla. Zifuatazo ni baadhi tu ya sifa za kiongozi wa chama cha wafanyakazi:

• Awe na uwezo wa kugundua tatizo lin-alowasibu anaowaongoza.

• Awe na uwezo wa kushawishi wafan-yakazi ili wajiunge pamoja.

• Awe na uwezo wa kupanga malen-go ya shughuli za chama, kusimamia utekelezaji wake, na kupima matokeo ya utekelezaji.

• Awe na uwezo wa kuweka kanuni na vy-ombo vya utekelezaji.

• Awe na uwezo wa kupanga na kuwapatia wanachama shughuli za kufanya ndani ya chama.

• Awe na uwezo wa kupanga na kutayari-sha mafunzo kwa ajili ya wanachama.

• Awe na utaratibu wa kuwatembelea na kuwakusanya wanachama na kueleza maendeleo ya chama chao.

Chama cha wafanyakazi kilicho makini ki-nahitaji uongozi ulio makini, ili kuwaonesha njia wanachama wake.

Upatikanaji wa Viongozi katika Vyama Vya Wafanyakazi

Chama cha wafanyakazi kinaundwa kwa mujibu wa sheria ya nchi. Hivyo shughuli zake ni rasmi kwa mujibu wa sheria za nchi. Kwa sababu shughuli za vyama vya wafan-yakazi ni rasmi, hivyo uongozi wake lazi-ma uwe rasmi baada ya kupitia mchakato rasmi ulioandikwa katika katiba na kanu-ni za vyama. Uongozi halali wa vyama vya wafanyakazi unapatikana kwa uchaguzi ulioandaliwa kwa mujibu wa taratibu za kidemokrasia na zilizoelekezwa na katiba na kanuni za vyama.

Sifa za Kiongozi wa Chama Cha Wafanyakazi

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi ni kioo cha chama. Hivyo kiongozi wa chama cha wafanyakazi lazima awe ni mfano kwa kauli

UONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Kiongozi ni kioo

UON

GOZI

WA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

35

Kutokana na maelezo yahusuyo sababu zi-nazo wasukuma wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi, ni dhahiri kuwa chombo chenyewe kinahitaji kuwa imara na chenye sifa za kuweza kuvutia wafan-yakazi ili wajiunge navyo. Lakini vyombo hivi vinaongozwa na watu/binadamu ambao la-zima wawe na sifa zilizotajwa hapo juu

Wajibu/Majukumu ya Kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi

Kama vile kiongozi wa chama cha wafan-yakazi alivyo na haki zake, pia kwa upande wa pili ana wajibu/majukumu yanayokwen-da sambamba na haki hizo.

Yafuatayo ni baadhi ya majukumu yake:

- Kutoa huduma kwa wanachama:

• Kutetea mwanachama anapofikwa na matatizo ya kikazi.

• Kumwakilisha mwanachama katika vy-ombo mbali mbali.

• Kushiriki katika shughuli zote za cha-ma na mikutano kwa mujibu wa katiba ya chama.

• Kuwa tayari kutoa majibu ya masuala yoyote yenye utata kwa wanachama ya-husuyo chama.

• Kufanya maandalizi ya shughuli za cha-ma.

• Kuunga mkono na kusaidia kwa vitendo maendeleo ya chama.

• Kuzingatia katiba na kanuni za chama na kuheshimu na kutekeleza kwa viten-do maamuzi yatokanayo na vikao halali vya chama.

• Kulinda, kutetea, na kutekeleza katiba ya chama, Kutoa elimu ya wafanyakazi kwa wanachama.

Umuhimu wa Tawi katika Muundo wa Chama cha Wafanyakazi

Msingi wa chama cha wafanyakazi una-tokana na tawi . Shughuli na harakati za vyama vya wafanyakazi zinaanzia kwenye tawi. Wanachama wa vyama vya wafanyaka-zi chimbuko lao linatokana na tawi. Hivyo umuhimu wa tawi hauhitaji msisitizo. Tawi

Ukwepaji wa majukumu

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

36

ni sehemu muhimu na ya msingi ya chama chochote cha wafanyakazi, lakini ni wana-chama wachache sana wanaojua umuhimu wa tawi. Kwao ngazi ya taifa ndio wanayoio-na kuwa yenye nguvu na uwezo wa kutatua matatizo yao na kukidhi mahitaji yao.

Uundaji wa Tawi la Chama cha Wafanyakazi

Wafanyakazi katika sehemu yao ya kazi wanahitaji kusimamisha chombo chao cha chama kitakachokuwa na wajibu wa kusi-mamia mambo yao kama wafanyakazi na pia kitakachokuwa msemaji mkuu kwa niaba ya wanachama wake. Chombo hicho cha chama cha wafanyakazi katika ngazi ya sehemu ya kazi ni tawi.

Wanachama wa chama cha wafanyakazi wanaofikia idadi iliyotajwa katika katiba ya chama kinachohusika wanaweza ku-unda tawi la chama. Tawi lililoundwa, ili liweze kutekeleza majukumu yake lazima liwe na uongozi. Uongozi wa tawi unasi-mamishwa kwa mujibu wa maelekezo ya katiba ya chama kupitia kwenye uchaguzi wa kidemokrasia. Uongozi wa tawi baada ya kusimamishwa huanza kutekeleza ma-jukumu yake kwa kushirikiana na uongozi wa mwajiri kwa mujibu wa maelekezo ya katiba ya chama kinachohusika.

Uimara wa tawi la chama cha wafanyakazi unategemea uimara wa uongozi wa tawi. Uongozi wa tawi unatarajiwa kuongoza kwa misingi ya utawala wa pamoja, ush-irikishwaji na demokrasia. Uongozi wa tawi ulio imara siku zote utatafuta shughuli za kufanya ili tawi lionekane liko hai na kila mwanachama anaelimishwa kujua wajibu wake kama mwanachama na kama mfan-yakazi. Uhai wa tawi unapimwa kwa jinsi gani wanachama wake wanavyokutanishwa kwa mujibu wa katiba ya chama na kujadili maendeleo ya chama chao.

Jinsi mwanachama anavyohitaji kutumia Tawi lake la chama

Wanachama wa vyama vya wafanyakazi wanapatikana katika matawi yao ya chama. Matawini ndiko kwenye shughuli za kazi ambako wanachama wanapaswa kuwa ndio kimbilio lao wakati wa matatizo katika maisha yao ya kazi. Kwa hivyo mwanacha-ma ndiye muhimili mkuu wa tawi na katika hali zote anatarajiwa aanzie harakati zake kama mwanachama kwenye tawi lake kwa kuzingatia kwamba:

• Ana wajibu wa kuhimiza maendeleo ya tawi lake.

• Anapofikwa na tatizo la kikazi anatara-jiwa alifikishe tatizo Shirika la Kazi Du-niani kwenye tawi lake kwanza na kwa haraka iwezekanavyo.

• Uongozi wa tawi lake una wajibu wa kushughulikia matatizo ya wanachama wake bila ya kuchelewa.

• Uongozi wa tawi ukishindwa kushughu-likia matatizo ya wanachama kwa ufani-si, unalazimika kuyapeleka mbele ma-tatizo hayo ili yapatiwe ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

• Uongozi una wajibu wa kushughulikia tatizo la kijumla linalowagusa wanacha-ma wote katika tawi. Uongozi wa tawi la-zima ulishughulikie tatizo Shirika la Kazi Duniani kwa haraka na jibu lirejeshwe kwa mwanachama haraka sana.

Vikao vya Chama cha Wafanyakazi

Chama cha wafanyakazi kinatakiwa kiendeshwe kidemokrasia. Vikao ni se-hemu ya utekelezaji wa shughuli za chama kidemokrasia. Vikao vya chama vimo katika ngazi mbili mbali za chama kutegemeana na maelekezo ya katiba za chama kinacho-husika. Chama cha wafanyakazi kina vikao vilivyoagizwa katika katiba ya chama ikiwa ni pamoja na vikao vya dharura.

UON

GOZI

WA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

37

Jinsi ya kuandaa vikao vya Chama cha Wafanyakazi

Katika mwendelezo wa demokrasia na kuhusisha wanachama katika kuendesha chama chao, chama lazima kiandae vikao kama ilivyoelekezwa katika katiba ya cha-ma cha wafanyakazi husika. Zifuatazo ni hatua za kuandaa vikao vya chama:

• Uongozi wa chama (Mwenyekiti na Ka-tibu ) katika ngazi husika lazima, kwa kushirikiana, wafanye matayarisho ya kikao kabla ya kuitishwa, na waweke bayana malengo yanayotarajiwa kufiki-wa katika kikao hicho.

• Uongozi uwapatie wajumbe wa kikao hizo ajenda za kikao mapema kadiri itakavyowezekana.

• Uongozi uandae ratiba ya kikao na kutoa ratiba hiyo kwa wajumbe.

Kwenye ukumbi wa mkutano yafuatayo ya-natarajiwa kujitokeza:

1. Mwenyekiti wa chama ndiye mwenye wajibu wa kuongoza kikao.

2. Katibu wa chama ndiye mwenye wa-jibu wa kutoa maelekezo ya kikao na mwekaji na mtunzaji wa kumbukumbu za kikao.

3. Kabla ya kuanza kikao katibu atathibit-isha idadi ya wajumbe (akidi) wa kikao.

4. Mwenyekiti atasoma ajenda na ratiba ya kikao, na wajumbe kuvipitisha na ikibidi kuvifanyia marekebisho.

5. Mwenyekiti atafungua kikao kisha atamruhusu Katibu kusoma kumbu-kumbu za kikao kilichopita.

6. Baada ya mjadala wa kumbukumbu za kikao kilichopita Katibu atawasili-sha yatokanayo na kumbukumbu za kikao hicho na Mwenyekiti ataruhusu mjadala wa yatokanayo na kumbu-kumbu hizo.

7. Mwenyekiti atawajibika kuendesha kikao kwa utaratibu unaoeleweka, ataongoza mjadala wa ajenda moja moja na baadaye kufikia hatima na makubaliano.

8. Mwenyekiti atawapa wajumbe nafasi ya kutosha ya kujadili ajenda zilizo-letwa mbele yao (asiachilie kuletwa mazungumzo/maneno nje ya ajenda zilizoandaliwa).

9. Mwisho wa mjadala wa kila ajenda, mwenyekiti atalazimika kuweka wazi azimio/maazimio yaliyofikiwa kuhusi-ana na ajenda inayohusika.

10. Mwenyekiti hatimaye atafunga kikao kwa tamko.

Vyama Vya Wafanyakazi na Demokrasia

Maana ya Demokrasia

Demokrasia ni neno kongwe ambalo husiki-ka katika maeneo kama ya kaya, sokoni, vilabuni na katika vyombo vya habari vya kitaifa na vya kimataifa. Lakini demokrasia hasa maana yake nini?

Wasomi, wataalamu na wanasiasa kadhaa, wa kale na hata wa sasa, wametoa tafsiri mbali mbali za demokrasia. Karibu taf-siri zao zote zimekubaliana kimsingi kuwa demokrasia ni uhuru wa watu wa kujiam-ulia mambo wenyewe kwa manufaa yao.

Demokrasia katika vyama vya wafanyakazi

Kihistoria, chimbuko la matabaka ya wafan-yakazi na wafanyiwa kazi ni pale binadamu alipoweza kuzalisha ziada. Hii iliwezekana baada ya kuvumbua zana na njia bora za kutendea kazi. Ilipoibuka mifumo ya uka-baila na baadaye ubepari, wale waliomiliki ardhi na kuifanyia kazi waliwaajiri na ku-wanyonya wale wasiomiliki kitu isipokuwa uwezo wao wa kufanya kazi.

Lengo la kabaila na bepari ni kutumikisha watu kwa lengo la kupata faida bila ya kujali

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

38

mafao yake, yaani ustawi wa mfanyakazi, haki na maslahi yake, hali bora za kazi na mazingira bora ya kazi kiafya na kiusalama. Hali hii ya wafanyakazi kupuuzwa na mwa-jiri wao, kunyanyaswa, kukandamizwa, ku-nyonywa na kudhalilishwa ndio iliyowafanya wafanyakazi kuungana.

Lengo kuu la kwanza la wafanyakazi la ku-ungana ni kudai haki na maslahi yao. Lengo kuu la pili lilikuwa ni kudai hali bora za kazi ikiwemo, kupunguza saa za kufanyakazi, mapumziko baada ya saa za kazi na maz-ingira bora ya kazi kwa afya na usalama wa mfanyakazi. Hivyo vyama vya wafanyakazi vya aina ya fani vilianzishwa. Baada ya muda vyama hivi vilihamasisha na kuunganisha wafanyakazi wote waliokuwa wakifanya kazi za aina moja hasa katika viwanda.

Vyama hivi vilichukua sura tofauti kwa mu-jibu wa haja, matakwa na mazingira ya wakati. Aidha vyama hivi viliundwa kwa malengo maalumu. Kwa hivyo ilibidi vijihu-sishe na mambo ambayo kwayo viliundwa; yaani mambo yaliyowahusu wafanyakazi wenyewe. Vilipaswa kubaini matatizo yao na kuamua iwapo matatizo hayo yangetatu-liwa kwa kujiunga pamoja. Kwa ufupi ilibidi mashauri muhimu ya chama yashughu-likiwe kwa uhuru bila vitisho au ushawi-shi kutoka kwa mwajiri binafsi, serikali au shirika.

Sifa za chama cha wafanyakazi chenye demokrasia

Chama cha wafanyakazi chenye demokra-sia kina sifa zifuatazo:

Kwanza chama hicho lazima kihusishe wa-nachama wake katika kutoa maamuzi ya-nayohusu uongozi, kazi za chama na mam-bo yote yanayohusu wanachama wake. Pili chama hicho lazima kiwape nafasi wa-nachama kuchagua viongozi wao ambao watafanya kazi kwa ridhaa yao kwa kipindi kinachojulikana na kinachokubalika kwa mujibu wa katiba, kanuni, na taratibu za chama . Ni ukiukaji wa demokrasia kuwa na viongozi wanaojiweka wenyewe au wa-naowekana ili kupata mwanya wa kufanya

mambo wapendayo. Sifa hizi lazima ziji-tokeze katika katiba, kanuni na taratibu za chama. Tatu, viongozi wa chama cha wa-fanyakazi kilicho na demokrasia huwapatia nafasi wanachama kuzungumzia mambo yanayohusu chama chao na hatima yao kwa uwazi na kwa uhuru. Chama cha aina hii huwa na upeo wa kutosha na misingi bora ya kutoa maamuzi.

Hivyo, demokrasia ya vyama vya wafan-yakazi sio tu utawala wa walio wengi, bali ni utawala unaohakikisha kuwa kila fikra ya mfanyakazi, na hasa mwanachama, inapa-tiwa nafasi katika kukidhi mahitaji ya wa-fanyakazi na umoja wao; kuimarisha umoja wao wa wafanyakazi, na pia katika kuimari-sha demokrasia yenyewe. Tabia ya viongozi wa chama cha wafanyakazi kuongoza kwa ujanja na kutowasikiliza wanachama wake inadumaza demokrasia pamoja na vyama vyenyewe.

Elimu kama Nyenzo ya Kuimarisha Demokrasia

Chama cha wafanyakazi chenye nguvu na heshima, na kinachostahiki kuungwa mko-no, lazima kiwe na viongozi wenye uwezo wa kuongoza. Viongozi wa aina hiyo hupa-tikana kutokana na wanachama wenyewe. Uwezo wa kuongoza hupatikana kutokana na elimu, maarifa, uzoefu na weledi. Ni muhimu kwa wanachama na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuwa na nyenzo hii muhimu ya elimu hasa wakati wa sasa. Hii ni kwa sababu miongoni mwa shu-ghuli muhimu za vyama vya wafanyakazi ni kutetea au kuboresha maslahi ya wafan-yakazi na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi. Baadhi ya shughuli mahususi zinazotakiwa kufanywa na vion-gozi hao ni:

• Kudai haki na maslahi au marupurupu bora ya kazi kwa ajili ya wanachama.

• Kudai mazingira bora ya kazi kwa afya na usalama wa wanachama na wafan-yakazi kwa jumla.

UON

GOZI

WA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

39

• Kushiriki katika vyombo vya utetezi wa mfanyakazi kama vile Baraza la Wafan-yakazi, Mahakama ya Kazi na Vyombo vingine.

• Kushiriki katika vikao vya kitaifa na ki-mataifa vinavyojadili masuala ya wafan-yakazi na vyama vya wafanyakazi.

• Kushiriki katika mijadala na waajiri kuhusu hali bora za kazi.

• Kuchambua sheria za kazi za nchi na kuhakikisha kuwa sheria hizo zinam-saidia na kumlinda mfanyakazi.

• Kutafakari mwelekeo wa utawala na siasa za nchi ili kuhakikisha kuwa haki za wafanyakazi zinalindwa.

• Kuhakikisha kuwa upo uongozi bora, umoja na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi.

• Kufanya utafiti wa hali ya uchumi wa nchi na hata wa kimataifa ili kupata taarifa na uwezo wa kutosha wa kujen-ga hoja na kuishauri serikali au taasisi nyinginezo kuhusu masuala ya kazi na ya wafanyakazi.

Ili kutenda mambo hayo yote, inabidi wa-husika wawe na elimu ya kutosha. Wa-fanyakazi na viongozi wao hupambana na waajiri, serikali, na taasisi nyingine zenye watu wenye ujuzi mkubwa sana na upeo wa ufahamu wa masuala ya uchumi na kazi. Ili kufanikiwa, ni lazima nao wawe na uwezo unaolingana na wapinzani wao au washiriki wao. Mtaalamu mmoja wa falsafa wa kale alisema:

“Wakati wa matatizo, elimu ni silaha ya mapambano na wakati wa amani elimu ni vazi la heshima.”

Mbinu za Uhamasishaji na Uingizaji Wanachama

Vyama vya wafanyakazi ni asasi kongwe ambazo hadi leo hutumia mbinu kongwe za uendeshaji pamoja na ukweli kwamba vyama hivi vinafanya kazi katika mazingira

mapya tofauti kabisa na ya zamani. Kwa sababu hiyo kuna haja viongozi wa vyama vya wafanyakazi kubuni mbinu mpya za uendeshaji wa vyama vyao ikiwemo hata kubadilisha mfumo wa vyama vyenyewe ikiwemo uongozi.

Kihistoria vyama vya wafanyakazi vilian-zishwa wakati wa vugu vugu la kisiasa. Leo vyama vya wafanyakazi viko huru na havi-ambatani na vyama vya siasa. Lakini vyama hivi ili visikilizwe, lazima viwe na wanacha-ma. Wingi wa wanachama ndio unaokipa chama nguvu na sauti ya kusikilizwa. Hivyo chama cha wafanyakazi, ili kitambulike la-zima kiwe na wanachama wa kutosha. Wa-nachama lazima watafutwe miongoni mwa wafanyakazi. Viongozi wa vyama wanapas-wa kujifunza mbinu mpya za kushawishi wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafan-yakazi. Mbinu kongwe za kuhamasisha wa-fanyakazi kisiasa hazifai tena leo. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu za uhamasishaji na uin-gizaji wa wanachama wapya:

i) Mradi wa kuingiza wanachama wapya

• viongozi waandae mpango maalumu unaotekelezwa wakati wote.

• viongozi wanatakiwa kufanya utafiti wa maeneo yenye wanachama watarajiwa.

• viongozi watafiti matatizo sugu waliyo-nayo wafanyakazi katika maeneo yenye wanachama watarajiwa.

“Wakati wa matatizo, elimu ni silaha ya mapambano na wakati wa amani elimu ni vazi la heshima.”

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

40

ii) Elimu ya Wafanyakazi

Chama kitayarishe vipindi vya elimu kwa wafanyakazi. Katika masomo hayo wafan-yakazi waelimishwe yafuatayo:

• Masuala ya chama cha wafanyakazi – umuhimu na majukumu yake.

• Jinsi chama kilivyofaidisha wanachama wake; ioneshe vielelezo vya misaada ya chama kwa wanachama; utetezi wa wanachama.

• Ufafanuzi wa malengo na majukumu ya chama.

iii) Tathmini ya Chama

Kufanyike tathmini ya chama ya mara kwa mara ili kubaini utekelezaji wa malengo ya chama; kukubalika na kuaminika kwa cha-ma na viongozi wake

iv) Kujenga uwezo wa viongozi

Viongozi lazima wawe na uwezo kielimu na uelewa kuliko wanachama wenyewe. Hali hii itafikiwa iwapo viongozi watapa-tiwa mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa uhakika na kwa weledi, hasa ya utetezi na uwakilishi wa wanachama katika vyombo mbali mbali.

v) Kutumia umaarufu wa wanachama

Wanachama maarufu, hasa wanawake, wana sifa na uwezo wa kuwavutia wenziwao waliokuwa bado si wanachama, kuingia kwenye chama. Nguvu hii ya wanachama inahitaji kutumiwa vizuri ili kuingiza wana-chama wapya. Chama hakiwezi kuimarika bila ya kuongezeka wanachama

Uimarishaji wa chama na Utetezi wa Wanachama

Moja kati ya malengo makuu ya kuundwa kwa chama cha wafanyakazi ni kusaidia kuleta maendeleo ya uchumi na ya kijamii kwa wanachama wake. Maendeleo hayo huja kwa viongozi wa chama kujipanga vi-zuri katika kuimarisha chama ili kiweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia

haki na maslahi na pia utetezi wa wanacha-ma wake. Chama legelege na kisichokuwa imara hakiwezi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi unaotarajiwa. Chama imara ni kile chenye uongozi imara unaojua wajibu wake na wenye kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya chama, kanuni, na taratibu nyingine za chama chenye kuung-wa mkono na wafanyakazi wengi. Uima-rishaji wa chama na utetezi wa wanachama wake ni shughuli za siku zote na za kudumu za chama cha wafanyakazi. Lakini shughuli hizi hazitekelezwi kwa kubahatisha bali kwa uhakika. Hivyo viongozi wa wafanyaka-zi ambao ndio wanaotarajiwa kuwa wa-tekelezaji wa majukumu haya lazima wawe watu waliotayarishwa kielimu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa ufanisi unaotarajiwa. Ubabaishaji ka-tika suala hili hudhoofisha chama.

Umuhimu wa Uimarishaji wa Chama

Kazi kubwa ya kuimarisha chama cha wa-fanyakazi ni kuwapatia wanachama chom-bo kitakachowasaidia watu hao kufikia malengo yao ya kiuchumi na kijamii. Mbali na vyama hivyo kutekeleza majukumu yao ya kuwatetea wanachama wao, vyama hivyo vitakuwa na wajibu wa kuwaweka pamoja wafanyakazi na pia kushughulikia matatizo yao ya kikazi bila ya kuchelewa na kutafuta ufumbuzi wa mambo yanayowaathiri katika sehemu zao za kazi bila ya kuchelewesha shauri.

Hivyo kazi kubwa na muhimu katika uima-rishaji wa chama cha wafanyakazi ni:

• Kukipa uwezo wa hali na mali chama ili kiweze kutekeleza majukumu yake kwa kujitegemea bila ya kutetereka.

• Kuinua hali ya uchumi ya chama na ku-hakikisha kina uwezo wa kujiendesha.

• Kuendeleza ari ya chama na kuhakiki-sha mshikamano miongoni mwa wana-chama.

UON

GOZI

WA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

41

• Kuchukua hatua thabiti za kukitangaza chama na kuingiza wanachama wapya katika chama.

• Kuongoza mchakato wa kupanga na kuingia katika mikataba ya hali bora za kazi. Yote haya hayawezi kutekelezwa kwa ufanisi unaofaa bila ya viongozi wa chama kuwa makini na kuwa karibu sana na wanachama.

Umuhimu wa Utetezi wa Wanachama

Chama cha wafanyakazi kina wajibu mkub-wa wa kumtetea mwanachama wake afik-wapo na matatizo yahusuyo kazi yake kati-ka sehemu ya kazi. Chama cha wafanyakazi kilicho imara huwa na utaratibu unaoe-leweka wa kutetea wanachama wake.

Sifa muhimu ya utetezi wa mwanachama ni kuchukuliwa hatua za haraka za utetezi mara tu tatizo linapojitokeza. Si vyema na wala si sahihi kuendeleza shauri kwa muda mrefu kabla ya kufikia ufumbuzi. Hali hii ambayo inaweza kumkatisha tamaa mwa-nachama aliyeathirika na kufikia hatua ya kuathirika kisaikolojia na kutoona umuhimu wa chama. Mafanikio katika utetezi yanaki-patia chama sifa na umaarufu, na hivyo ku-vutia wafanyakazi kujiunga na chama hicho bila ya hofu na wasiwasi.

Hatua za Utetezi

Zifuatazo ni baadhi tu ya hatua za ku-chukuliwa katika uchambuzi/upembuzi wa mchakato wa utetezi wa mwanachama:

• Mwanachama mwenye kadhia awasili-ane na uongozi wa tawi lake la chama katika sehemu yake ya kazi, na kueleza tatizo lake kwa ukweli bila ya kudang-anya.

• Viongozi wa tawi wajiridhishe na ukweli wa kadhia ya mwanachama.

• Uongozi wa tawi ushughulikie kadhia hiyo ya mwanachama bila ya kuchelewa.

• Uongozi wa tawi ukiona haupati ushiriki-ano kutoka kwa viongozi wa sehemu ya

kazi, haraka utayarishe taarifa kuhusu kadhia hiyo pamoja na vielelezo vyote vi-navyohusika na kuvipeleka katika ngazi ya juu yake ili ipate kushughulikiwa.

• Uongozi unaohusika unapaswa ku-chukuwa hatua zenye lengo la utatuzi wa kadhia ya mwanachama anayehusi-ka.

• Ni muhimu kupatikana taarifa sahihi za kadhia ya mwanachama, kushughuliki-wa kwa haraka kama itakavyowezekana, na kila hatua, inayopigwa lazima mwa-nachama anayehusika ajulishwe.

Kwa ujumla chama cha wafanyakazi kina wajibu wa kupekuwa na kutafiti matatizo ya jumla ya wafanyakazi na kuyatatua.

Moja kati ya malengo makuu

ya kuundwa kwa chama cha wafanyakazi ni kusaidia kuleta

maendeleo ya uchumi na ya

kijamii kwa wanachama

wake

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

42

KATIBA YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI

Sura

Kuchangiana mawazo

Kama mshirika

Usawa

Mawasiliano kikazi na usimamizi kirasilimali

KUAMINIANA

4444

KATI

BA Y

A CH

AMA

CHA

WAF

ANYA

KAZI

43

Maana ya Katiba

Katiba ni sheria mama ya asasi yoyote ya kidemokrasia. Kwa nchi, katiba ndiyo she-ria mama, mwongozo wa jinsi nchi inavyo-takiwa kuendeshwa. Kwa upande wa vy-ama vya wafanyakazi katiba vile vile ndiyo sheria mama inayotoa mwongozo wa jinsi chama kinachohusika kinavyotarajiwa kue-ndeshwa. Katiba ya chama cha wafanyakazi ni jumuisho la kanuni na taratibu za kue-ndeshea chama. Hivyo katiba ya chama cha wafanyakazi inatayarishwa na wanachama wenyewe kupitia vikao vyao, ikielekeza jinsi ya kuendesha chama hicho.

Umuhimu wa Katiba

Katiba tumeona kuwa ndiyo dira/mwongo-zo wa jinsi ya kuendesha asasi inayohusika;

Kwa Nchi

Kwa nchi, katiba ndicho chombo chenye mamlaka kuliko vyombo vingine vyote. Kat-iba ndiyo:

• Huweka kanuni za msingi za siasa na uendeshaji wa serikali.

• Huweka mfumo mzima wa uendeshaji wa serikali.

• Huainisha mamlaka ya serikali.

• Hujumuisha misingi ya haki, ikiorodhe-sha haki za kila mwananchi.

• Huweka viwango na ukomo wa ma-daraka ya serikali.

• Huweka vipengele vya kuidhibiti serikali isitumie vibaya madaraka yake.

• Kuweka nidhamu na utaratibu wa kue-ndesha nchi.

Nchi yoyote ina sheria nyingi ambazo kwa kawaida hutungwa na chombo cha ku-tunga sheria kama vile Bunge. Sheria hizi

KATIBA YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI

ni lazima zikidhi matakwa ya katiba. Vivyo hivyo kanuni na taratibu ni lazima zitokane na sheria na ni lazima zikidhi matakwa ya sheria inayohusika. Kwa hiyo basi, mihimili ya sheria, kanuni na taratibu zote za kue-ndesha nchi na asasi ni katiba.

Katiba ya chama cha Wafanyakazi

Katiba ya chama cha wafanyakazi ni lazima iweke wazi majukumu ya vyombo mbali mbali vya chama pamoja na haki na wajibu wa wanachama. Aidha katiba ya chama cha wafanyakazi kama vile katiba ya nchi ina-vyofanya kwa wananchi wake wote inaweka wazi mambo yafuatayo:

• Kanuni za msingi za utaratibu wa uendeshaji wa chama.

• Mifumo, kanuni na taratibu za uende-shaji wa chama.

• Mfumo mzima wa uendeshaji wa cha-ma.

• Haki na wajibu wa kila mwanachama.

• Viwango na ukomo wa madaraka kwa viongozi na watendaji wa chama.

• Vipengele vya kudhibiti viongozi na wa-tendaji ili wasiweze kutumia vibaya ma-daraka yao.

Kama ilivyo kwa katiba ya nchi, katiba ya chama cha wafanyakazi, kanuni, taratibu, na mifumo ya uendeshaji lazima vikidhi matakwa ya katiba ya chama cha wafan-yakazi kinacho husika.

Utungaji wa Katiba

Katiba ni dira ama mwongozo wa kuende-sha nchi au asasi. Kuna njia kadhaa zinazo-fuatwa katika kutunga katiba. Zifuatazo ni njia maarufu za kutunga katiba kwa njia ya kidemokrasia:

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

44

i) Kupitia Uwakilishi

Uongozi wa muda wa chama cha wafan-yakazi kinachotarajiwa kusajiliwa, kwa ushirikiano na wawakilishi wa wanachama unakaa kuandaa rasimu ya chama. Rasimu hii ya chama ambayo inaweka wazi masua-la muhimu kama vile malengo, uongozi, vy-ombo, chaguzi za chama ndiyo inayokuwa msingi wa usajili wa chama. Hivyo chama baada ya kupewa usajili wa muda kinaanda ratiba ya shughuli zake kama vile suala la kuwafikia wanachama na kuwaingiza kwe-nye chama, kuunda matawi, kusimamisha uongozi katika ngazi mbali mbali, na hati-maye kuitisha Mkutano Mkuu na kufanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa. Rasimu ya katiba ya chama inapitishwa katika vyombo mbali mbali vya chama ambapo wanacha-ma wanapata fursa ya kuichangia. Mwisho rasimu hiyo ya katiba inapelekwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Katiba ambako huwa kuna wawakilishi waliochaguliwa na wanachama wenyewe ambao wanapata na-fasi ya kutosha kuijadili na kuichangia na hatimaye kuipitisha rasimu hiyo kwa kuipi-gia kura tayari kwa kutumika kama chom-bo cha kuendeshea chama. Hii ndiyo njia halisi ya kidemokrasia iliyozoweleka katika kutunga katiba ya chama cha wafanyakazi.

ii) Ushiriki wa Moja kwa Moja

Katika njia hii wanachama wote wa chama cha siasa au wafanyakazi hukutana na ku-jadiliana hadi kupitisha katiba yao. Mfumo huu unawezekana pale ambapo chama kin-achohusika kina wanachama wachache na kinafanya kazi katika maeneo madogo tu.

Kwa kawaida, katiba ni lazima iandikwe in-gawa kuna baadhi ya nchi kama vile Uin-gereza ambako katiba ya nchi haimo vi-tabuni na nyingine imeandikwa kwa kiasi fulani tu.

Katika nchi yenye mfumo wa utawala wa kidemokrasia katiba hutungwa na wazal-endo wenyewe kwa kupitiwa na kuulizwa mawazo yao kuhusu katiba waitakayo. Aid-ha katika chama

chochote, kama vile chama cha wafanyaka-zi, ni wanachama pekee wa chama ndio wenye haki, jukumu na wajibu wa kutun-ga katiba itakayokidhi matakwa, mahitaji, shabaha, na malengo waliyojiwekea.

Usajili wa Katiba

Kwa kawaida na kwa mujibu wa sheria ya nchi, kabla ya katiba ya chama kutumika lazima katiba hio isajiliwe sambamba na usajili wa chama chenyewe, kwa msajili anayehusika kwa mujibu wa sheria na tara-tibu za nchi inayohusika.

Kupitisha Katiba na Kuifanyia Marekebisho

Katiba ya chama cha wafanyakazi ik-ishaandikwa, hupitishwa kwa njia ya ku-pigiwa kura katika kikao cha kikatiba che-nye uwakilishi wa wanachama wenyewe. Katiba ya chama lazima ipitishwe kwa wingi wa kura za ‘ndio’ katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama. Wingi wa kura wa kupiti-sha katiba unapendekezwa usiwe chini ya nusu ya wajumbe wote, wa Mkutano Mkuu bali afadhali zaidi iwe theluthi mbili (2∕3) au hata robo tatu (3/4) ya wajumbe wote waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama.

Kubadilika kwa KatibaKwa sababu taifa ama asasi hukua kutoka-na na mazingira na haja za wakati, chom-bo cha kuendeshea taifa na asasi hizo pia hukua. Katiba hukua na kubadilika ili kuki-dhi matakwa na mahitaji ya wakati uliopo. Kwa hivyo, ni wazi kwamba mabadiliko ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi yatokeapo, hulazimisha katiba nayo kubadilika. Jambo hili hufanywa kwa kuandika kitu kinachoit-wa ‘marekebisho ya katiba’.

Katiba inaweza kurekebishwa au kufutwa kabisa:

(i) Kwa njia ya marekebisho: Katiba in-aweza kurekebishwa baadhi ya vifungu vyake ili iendane na mahitaji ya wakati. Hii ndiyo njia halisi na inayotumika ka-tika hali ya kawaida.

KATI

BA Y

A CH

AMA

CHA

WAF

ANYA

KAZI

45

(ii) Kuifuta iliyopo na kuandika katiba mpya: Njia hii hutumika kwa nadra, inat-egemea mabadiliko ya hali ya juu katika nchi ambayo si kitu cha kawaida.

Maudhui ya Katiba ya Chama cha Wafanyakazi

Katika kila nchi kuna asasi kadha na kila moja ina katiba yake. Kila asasi ina madhu-muni, malengo na makusudio yake tofauti na asasi nyingine. Aidha vyama vya wafan-yakazi ambavyo ni asasi muhimu sana za kidemokrasia, katiba zake kwa uchache zi-natakiwa ziwe na mambo yafuatayo:

• Nembo ya Chama.

• Jina na Anwani ya Chama.

• Haki za Kisheria.

• Malengo ya Chama.

• Imani ya Chama.

• Kujishirikisha – kitaifa na kimataifa.

• Uanachama na Michango.

• Maeneo ya kufanyia shughuli /mipaka majukumu ya wanachama.

• Watendaji/Maafisa na Majukumu yao.

• Mifumo ya Chama: Majukumu, Haki na Wajibu.

• Chaguzi na taratibu zake.

• Akidi ya vikao na Upigaji wa Kura.

• Vikao.

• Elimu na Mafunzo.

• Jinsi ya Kurekebisha katiba.

• Uundaji wa Kamati mbali mbali.

• Mamlaka na wajibu wa kutunga kanuni na taratibu mbali mbali.

• Wadhamini.

• Muda wa Uongozi.

• Masuala ya Fedha: Wakaguzi wa Ndani na Nje.

• Hatma ya chama endapo kitafikia hatua ya:

i. Kuunganishwa na kingine/vingine.

ii. Kusambaratika.

iii. Kufilisika.

iv. Kufutwa kwa mujibu wa sheria.

• Jinsi ya kutunza fedha na mali za cha-ma.

• Mwelekeo/itikadi za kisiasa.

Ukiukaji wa Katiba

Vyama vingi vya wafanyakazi huendeshwa kwa utulivu hasa vikipata uongozi bora na ulio imara. Vyama vya aina hii huwa vina-timiza malengo, madhumuni, na matara-jio ya wanachama wake. Hata hivyo baadhi ya vyama vinaweza kuwa na hali ambayo si shuwari. Vyama vya aina hii huwa na uongozi mbovu na wenye kujali zaidi ma-slahi binafsi. Matokeo yake ni kuwepo kwa migongano na mizozo isiyomalizika. Kwa kiasi kikubwa migongano hii huwa inatoka-na na ukiukwaji wa katiba ya chama. Mam-bo yafuatayo huchangia kukiukwa katiba:

i) Tafauti za Matarajio

Kimsingi, wanachama ndio watungaji na wamiliki wa katiba ya chama chao. Kuna baadhi ya wanachama kimakosa hujiunga na chama kabla ya kuyafahamu kikamilifu matakwa ya katiba yao. Hatimaye hujikuta wakiwa na malengo na matarajio tafauti na yale yaliyomo kwenye katiba. Baadhi ya wakati wafanyakazi hufuata mkumbo kuji-unga na chama kabla ya kujifunza malengo na madhumuni ya chama hicho. Wana-chama wasioijua katiba ya chama chao huchangia kwa kiasi kikubwa kwa wao we-nyewe kunyimwa haki zao hasa wanapopa-mbana na mwajiri mkorofi au kiongozi wa chama chake asiye mwadilifu na asiyefuata misingi ya demokrasia.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

46

ii) Uwezo mdogo wa Uongozi

Baadhi ya viongozi wa vyama vya wafan-yakazi kuanzia ngazi ya taifa hadi tawi wa-naweza kuwa na uelewa mdogo wa uongozi na katiba ambapo:

• Wanashindwa kutafuta au kutoa ushauri unaofaa kwa tatizo linalohusika.

• Wanashindwa kutimiza majukumu kama yalivyoelekezwa na katiba. Kwa mfano Mwenyekiti wa chama kutenda kazi za kila siku za chama sambamba na Katibu wake badala ya kuendesha vikao vya chama na kutoa ushauri.

iii) Ubadhirifu wa Fedha za Chama

Kwa sababu ya kuendeleza ubinafsi na ku-zoea kujinufaisha wenyewe, baadhi ya vion-gozi wa vyama vya wafanyakazi mara nyingi huweka kando katiba, kanuni na taratibu za chama na kuanza kutumia fedha za chama bila ya kuzingatia taratibu za fedha, natija ya chama na mara nyingi kwa ubadhirifu. Baadhi ya viongozi huongoza kwa kiburi ki-asi kwamba hutumia vibaya madaraka yao, na mamlaka zinazohusika za chama au wa-nachama wanapowauliza juu ya mwenendo

wao huo mbaya, huja juu na kuwa wakali katika chama. Baadhi ya viongozi kwa ku-tokujua na wakati mwingine kwa makusudi hutafsiri visivyo baadhi ya vifungu vya katiba zao na za vyama vingine ili wajinufaishe na tafsiri hiyo hasa katika suala la mipaka ya maeneo ya kufanyia kazi vyama vyao. Hali hii mara nyingi husababisha mizozo baina ya chama na chama.

vi) Ukosefu wa Demokrasia

Vyama vya wafanyakazi vinatarajiwa kuwa vya kidemokrasia– kwa kushirikisha wa-nachama katika maamuzi na kuendesha chama kwa ujumla. Maamuzi katika vy-ama vya kidemokrasia hufi kiwa kwa njia ya makubaliano yatokanayo na majadil-iano au kwa njia ya kupiga kura. Baadhi ya wakati viongozi wengine hujitia hamnazo na kwa makusudi hukiuka kanuni na hu-fanya maamuzi makubwa ambayo bila hata ya kupokea ushauri kutoka vikao vinavyo-husika jambo ambalo ni kinyume na mis-ingi ya demokrasia na hivyo kuathiri utulivu wa chama .

TafakariTafakari

KATI

BA Y

A CH

AMA

CHA

WAF

ANYA

KAZI

47

v) Kutoitishwa vikao vya kikatiba

Uhai wa chama cha wafanyakazi unadhi-hirishwa na jinsi chama hicho kinavyowa-husisha wanachama katika uendeshaji wa shughuli za chama hasa kwa kupitia vikao katika ngazi mbali mbali. Katiba za vyama vya wafanyakazi zina vifungu vinavyoainisha jinsi inavyotakiwa vikao vya chama vikae; kwa mara ngapi na kwa kipindi gani. Ni ba-hati mbaya kwamba baadhi ya vyama havi-itishi vikao kikawaida kama inavyoelekezwa na katiba ya vyama hivyo. Matokeo ya hali hii ni kufikia wanachama hatua ya kucho-ka kwa kutokujua kinachoendelea katika chama chao. Hali hii ya kutoitishwa vikao vya kikatiba bila ya sababu za msingi, hu-changia kuwepo kwa mizozo katika chama kwa vile katiba huwa imepuuzwa.

vi) Ukosefu wa uwazi katika kuendesha Chama

Chama cha wafanyakazi mara zote huwa ni wajuzi wa mambo, hivyo kuwaongoza kuna-hitaji ujuzi na mbinu za hali ya juu na hasa wanahitaji kuongozwa kwa weledi na uwazi. Kutokuwepo kwa uwazi katika utendaji na hasa katika matumizi ya fedha za chama kunaweza kusababisha migogoro na kutok-uelewana baina ya viongozi na wanachama

ndani ya chama. Hizi ni baadhi tu ya sababu za ukiukwaji wa katiba ambazo huchangia kudhoofika kwa chama kinachohusika.

Njia za Kuepuka Kuvunja Katiba ya Chama

Kwa sababu ya kutokujua na wakati mwing-ine kwa makusudi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, na kwa kuendeleza utashi wao, huongoza vyama vyao huku wakiweka kando katiba za vyama, kwa muda mrefu. Hii inachangiwa pia na wanachama ambao hawajali kujifunza katiba za vyama vyao. Hivyo njia bora ya kuepukana na mizozo na migogoro itokanayo na ukiukwaji wa katiba ni:

• Kufikia maamuzi kwa njia ya vikao.

• Kuendesha mambo ya chama kwa uwazi na demokrasia.

• Kutoa elimu ya vyama vya wafanyakazi na elimu ya katiba kwa wanachama, viongozi wa chama, na watendaji wa chama.

• Kuwawajibisha viongozi wanaokiuka katiba, kanuni na taratibu nyingine za chama.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

48

UTAWALA BORA KATIKA VYAMA VYA

WAFANYAKAZI

Sura5555

UTA

WAL

A BO

RA K

ATIK

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

49

UTAWALA BORA KATIKA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Chama cha wafanyakazi kilicho makini wakati wote hufanya shughuli zake kwa uwazi na kwa demokrasia. Chama cha wafanyakazi kina wajibu wa kusimamia na kuhakikisha kuwa haki ya kufanya kazi nchini inadumishwa na pia hakuna mwa-nanchi anayefanyishwa kazi kwa kushur-tishwa bali awe huru kuchagua kazi aipen-dayo yenye kuendeleza heshima, uhuru, na utu wake, kwa malipo yanayokidhi mahitaji yake ya maisha ya kila siku, kama binad-amu. Wapatiwe ajira zenye staha na wa-hakikishiwe usalama wa ajira zao. Aidha misingi ya utawala bora ya vyama vya wa-fanyakazi inasisitiza uhuru wa wafanyakazi kutoa mawazo/maoni yao, na kuruhusiwa kujikusanya pamoja na kuunda jumuiya zao bila ya maamuzi yao kuingiliwa . Pale mfanyakazi anapopoteza uwezo wa kufanya kazi na kujipatia kipato, aidha kwa sababu ya uzee au ugonjwa, serikali iwajibike kum-tunza kwa kumpatia matibabu na hifadhi ya jamii. Wafanyakazi wapatiwe haki ya kush-iriki katika kuendesha nchi, wapate fursa ya kuchagua na kuchaguliwa, na waelim-ishwe hasa juu ya masuala ya kazi zao. Vyama vya wafanyakazi vihakikishe kuwa masuala yote ya kazi nchini yanawiana na walau viwango vya chini vya kazi duniani.

Elimu ya Wafanyakazi

Vyama vya wafanyakazi vilivyo makini hu-sisitiza sana umuhimu wa kuwapatia vion-gozi wake na wanachama wake elimu, hasa elimu ya wafanyakazi. Viongozi na wana-chama wa vyama vya wafanyakazi walioe-limika wanarahisisha shughuli za uende-shaji wa vyama vya wafanyakazi. Uongozi ulioelimika huendesha chama kwa weledi na kwa mafanikio yaliyotarajiwa na wana-chama wake. Wanachama walioelimika hu-saidia sana katika kuchangia maendeleo ya chama chao.

Elimu ya wafanyakazi husaidia chama kue-ndeshwa kidemokrasia hasa pale elimu hiyo inapotumika kubadili mitazamo ya wa-nachama na viongozi.

Ushirikishwaji wa Wafanyakazi

Moja kati ya misingi ya demokrasia ya vy-ama vya wafanyakazi ni kuwashirikisha wafanyakazi katika masuala yanayohusu mambo yao ili wajisikie kuwa ni sehemu ya mambo hayo na pia.

• wahusishwe katika kujadili na kuchang-ia masuala yanayohusu maendeleo ya chama chao.

• Wawe ni sehemu ya kukata shauri juu ya masuala mbali mbali ya chama chao.

Utekelezaji wa ushirikishwaji wa wafan-yakazi umo katika viwango na sura zi-fuatazo:

Katika tawi

Wafanyakazi katika sehemu yao ya kazi wana mambo mengi ya kushirikishwa nayo ili wajione kuwa ni sehemu hiyo ya kazi.

Kwanza katika masuala ya tawi lao la cha-ma wafanyakazi wanahitaji kushirikishwa na kushiriki katika uendeshaji wa tawi lao la chama. Wanahitaji kuchagua miongoni mwao uongozi wa tawi, na kushiriki na ku-changia katika mijadala inayoletwa katika vikao vya chama. Katika kiwango cha mfan-yakazi, wafanyakazi wanatarajiwa kushiriki katika kuweka malengo ya kazi, utekelezaji na upimaji wa matokeo ya utekelezaji wa malengo hayo.

Katika sehemu pana zaidi ya kazi: Wafan-yakazi wanahitaji kushirikishwa katika vy-ombo kama Kamati za Uongozi, Mabaraza ya Kazi ambapo wafanyakazi hukutana

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

50

baada ya muda fulani, kutegemeana na maelekezo na taratibu za chama chao, ku-jadili masuala ya kazi na wafanyakazi.

Katika kiwango cha taifa: Wafanyakazi wa-natakiwa kushiriki katika chombo cha ki-taifa kuwakilisha wafanyakazi wenziwao katika mijadala inayohusu kazi na wafan-yakazi .

Katika kanda na katika ngazi za kimataifa: Kuna vyombo vya masuala ya kazi na wa-fanyakazi ambapo vyama vya wafanyakazi hushiriki kwa niaba ya wafanyakazi. Vy-ama vya wafanyakazi hufanya mashirikiano na vyombo vya kikanda na kimataifa kwa lengo la kusaidiana, kubadilishana uzoefu na kuendeleza mshikamano wa kimataifa wa wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi. Chombo muhimu na maarufu cha kimataifa ambacho vyama vya wafanyakazi hushiriki-ana nacho katika nyanja zilizotajwa hapo juu ni Shirika la Kazi Duniani.

Migomo katika vyama vya wafanyakazi

Mgomo ni kitendo cha wafanyakazi kusu-sia kufanya kazi kwa lengo la kushindiki-za waajiri ili kufi kia muafaka wa madai

yao. Mambo yanayosababisha migomo ni pamoja na hali duni za afya na usalama kazini, mishahara duni, marupurupu yasi-yoridhisha, unyanyasaji, ubaguzi na kupuu-zwa kwa ustawi wa wafanyakazi. Wagomaji hutarajia kwamba matakwa yao yote au se-hemu yao yatatekelezwa.

Aina za Migomo

Kuna aina mbali mbali za migomo ambazo zote zinalenga kuonyesha kuwa wafan-yakazi hawakubaliani na hali fulani katika kazi. Baadhi ya aina hizo za migomo ni:

Mgomo wa wazi

Ni kitendo cha wafanyakazi kuweka zana za kazi chini na kuacha kufanya kazi ka-bisa. Katika mgomo wa aina hii, watu wote wanaweza kuelewa kuwa katika sehemu fulani ya kazi, wafanyakazi wamegoma. Itaonekana wazi wazi, kuwa wafanyakazi hawako sehemu yao ya kazi. Mgomo wa aina hii unakuwa na nafuu kwa mwajiri kwa vile anaelewa wazi kuwa mgomo upo na athari zake anaweza kuzipima haraka, na anaweza kuchukua hatua za haraka za kuuzuia kabla haujatekelezwa kikamilifu au kabla haujaleta madhara makubwa.

Kustaafu

UTA

WAL

A BO

RA K

ATIK

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

51

Mgomo baridi

Katika mgomo huu kazi huonekana zi-nafanyika lakini sio katika kiwango cha kawaida. Wakati mwingine wafanyakazi wa-naweza kuamua kuhudhuria sehemu zao za kazi lakini wakaamua kuweka zana chi-ni, au kusimamisha mitambo ya uzalishaji hususani katika viwanda. Wafanyakazi hua-mua kufanya mgomo baridi kwa sababu ya kuogopa hatua kali ambazo zinaweza ku-chukuliwa dhidi yao.

Mgomo baridi hutia hasara sehemu za kazi, hasa katika viwanda kwani hakuna kinachozalishwa, au kama kipo, basi hu-zalishwa kwa hasara kubwa sana. Kuna wakati wafanyakazi, hasa katika viwanda, wanaweza kuamua kuharibu mitambo ya uzalishaji kwa makusudi ikiwa ni njia ya kuelezea malalamiko yao. Mgomo wa aina hii ni hatari zaidi kwa vile muajiri anaweza kuchelewa kuugundua na matokeo yake kumsababishia muajiri hasara kubwa.

Mgomo wa Mshikamano

Aina hii ya mgomo hutokana na umoja na mshikamano kati ya wafanyakazi popote pale walipo. Wafanyakazi wa kiwanda fulani wanapogoma, wafanyakazi wengine nchini na hata nje ya nchi, wanaweza kugoma ku-fanya kazi zao ikiwa ni ishara ya kuwaunga mkono wafanyakazi wenzao.

Tumeshaona kuwa madhumuni ya mgomo ni kuyapa nguvu madai ya wafanyakazi pale njia za amani zinaposhindwa. Lengo kuu la migomo sio kuleta vurugu ili patokee uharibifu katika sehemu za kazi. Aidha wafanyakazi wanapogoma matarajio yao ni kuwa mgomo utafanikiwa na matakwa yao kutekelezwa. Wakati wa mgomo, wa-fanyakazi huhitaji pia kuungwa mkono na umma. Wananchi hawawezi kuunga mkono mgomo iwapo wanahisi kuwa utaathiri au utahatarisha maisha yao. Kwa kuzingatia ukweli huu, baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanapoandaa migomo huiwekea mipaka katika utekelezaji wake. Yaweza kuamuliwa kwamba sehemu nyeti za kazi wakati wa mgomo ziendelee na kazi

ili kuepusha matatizo na wakati mwingine maafa kwa wananchi.

Lakini viongozi wengine wanadhani kuwa haifai kutoa mwanya wa aina hii. Msimamo wao ni kwamba kila sehemu ya kazi ni ny-eti, na kwa hiyo kugawa wafanyakazi katika makundi kunaweza kudhoofisha mgomo.

Chanzo cha Migomo

Mtu asiyeelewa masuala yanayowakabili wafanyakazi hutafsiri kugoma kama ki-tendo kisichokuwa na maana yoyote. La-kini kwa ajuaye maana, kitendo hicho ni cha kishujaa na chenye kustahili. Suala muhimu la kujiuliza hapo ni kwa nini wa-fanyakazi huamua kugoma?

Mfanyakazi ana haki zake za msingi. An-apoanza kazi huingia mkataba na mwa-jiri wake ambaye huweka bayana mambo anayowajibika kuyafanya na yale asiyotak-iwa kufanya. Aidha, mkataba hueleza tunzo kwa mfanyakazi pamoja na haki na masla-hi yake baada ya kutekeleza wajibu wake. Baadhi ya haki za wafanyakazi ni kama zi-fuatazo:

• Kushirikishwa katika shughuli zina-zowahusu katika sehemu za kazi.

• Kupatiwa hifadhi ya jamii ikiwemo ma-fao ya kutopatiwa ajira.

• Kupatiwa elimu ya kuendeleza kazi yake.

• Kupatiwa ujira wa haki kwa kazi aifan-yayo.

• Kupatiwa siku za mapumziko zenye malipo katika mwaka.

• Kupumzika mwisho wa juma.

• Kupatiwa muda wa mapumziko na bu-rudani baada ya saa za kazi.

Haki kama hizo zisipotekelezwa, na baada ya majadiliano mezani kushindwa kutoa ufumbuzi, ndipo wafanyakazi huchukua hatua ya mwisho ya kugoma. Vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wenyewe wana

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

52

thamini majadiliano, ndio maana wakati wote vyama vya wafanyakazi kwa niaba ya wanachama wao vimekuwa vikisisitiza umuhimu wa mazungumzo na serikali na waajiri, katika vyombo vya utatu na katika vyombo vya usuluhishi. Wafanyakazi hula-zimika kuchukua hatua za kugoma ikiwa madai yao hayakufanikiwa kwa njia ya majadiliano. Hali hii hufi kiwa kwa sababu ya kuwepo waajiri wasiokuwa na ushiriki-ano, wasiopenda kuweka mambo wazi, na wenye kiburi. Wafanyakazi, kwa sababu ya kuzielewa vyema athari za mgomo kiuchu-mi, na kijamii, hujitahidi kuepusha migomo kila inapowezekana. Katika majadiliano hakuna mshindi bali muafaka wa aina fu-lani hufi kiwa lakini katika mgomo ushindi hupatikana pale matakwa ya wafanyakazi yanapotekelezwa.

Jinsi ya Kuandaa Mgomo

Chama cha wafanyakazi katika ngazi zake mbali mbali ndicho kinachotakiwa kuitisha mgomo na sio kikundi cha wafanyakazi ki-sichokuwa cha kisheria. Aidha mtu binafsi au chama cha siasa, havipaswi kuitisha

mgomo wa wafanyakazi. Chama cha wa-fanyakazi kabla ya kuitisha mgomo kina-paswa kufanya mambo yafuatayo:

• Kwanza, ni lazima kuwaelimisha wa-nachama wake pamoja na wafanyakazi kwa ujumla juu ya hatua mbali mbali zilizochukuliwa na uongozi wa chama chao kuhusiana na madai yao mbali mbali. Aidha waelezwe jinsi mazun-gumzo yao yalivyofi kia hatua ya kuk-wama.

• Pili, chama kijadiliane na wanachama wake kutoka ngazi ya tawi na kupata uamuzi kuhusu ugumu wa kuendelea na mazungumzo au ugumu wa kufi kia mapatano na waajiri wao. Uamuzi wa mgomo lazima uchukuliwe na wana-chama wenyewe kutoka ngazi ya tawi, wilaya, mkoa/kanda hadi taifa. Kwa hivyo inabidi kila mwanachama aelim-ishwe kwa nini wafanyakazi wanatak-iwa kugoma, manufaa ya kugoma na hasara za kugoma. Kwa njia hii chama kitajihakikishia kwamba mgomo un-aopangwa unafahamika na unaungwa

Muajiri Muajiriwa

Mvutano

UTA

WAL

A BO

RA K

ATIK

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

53

mkono na wafanyakazi wote wanao-husika. Ni makosa kupandikiza mgomo kwa wanachama. Wanachama we-nyewe ndiyo wanaopaswa kuwa chim-buko la mgomo na utekelezaji wake.

• Tatu, wakati wa mgomo lazima wafan-yakazi wanaohusika wapatiwe maelezo ya kutosha mara kwa mara juu ya hatua mbali mbali zinazochukuliwa na vion-gozi wao katika kufanikisha mgomo huo. Kwa sababu hiyo ni muhimu kuwa na uwezo wa kufi kia na kutumia vy-ombo vya mawasiliano kama vile redio, magazeti, televisheni, simu na vyombo vya usafi ri kama magari. Mawasiliano yawe katika lugha nyepesi na yenye kueleweka kwa wafanyakazi wote.

• Wanachama katika ngazi za chama wa-pige kura ya siri kuunga mkono au kut-ounga mkono mgomo unaoandaliwa.

• Mwisho wahusika waeleweshwe wajibu wao katika kufanikisha mgomo huo.

Faida na Hasara za Migomo

Mgomo katika kazi unaathari kwa pande tatu- mgomaji, mwajiri na hata taifa kwa ujumla. Faida za mgomo kwa mgomaji, ni pale anapotekelezewa madai yake na mwa-jiri kutokana na shindikizo la mgomo. Ka-

tika hali hii inabainika wazi wazi kuwa mgo-mo wake umekuwa na mafanikio. Lakini wakati mwingine mambo hayaendi kama yalivyotarajiwa na mgomaji. Mwajiri katili asiyejali mashauriano anaweza kumfukuza kazi kabisa mgomaji kwa visingizio mbali mbali vikiwemo vya kuhatarisha utulivu na usalama katika sehemu ya kazi. Aidha wakati mwingine mwajiri au serikali hu-tumia vyombo vya dola kuzima migomo. Hii ikitokea baadhi ya wafanyakazi huumizwa, hufungwa au hupoteza maisha.

Hizi ni baadhi tu ya hasara za migomo kwa muajiriwa. Kwa muajiri, mgomo wa aina yoyote haumnufaishi zaidi ya kumtia hasara. Wakati wa mgomo kazi husita, mitambo inakuwa hatarini kuhujumiwa na wagomaji wenye hasira, na hatimaye uchumi wa ki-wanda au sehemu ya kazi huanguka. Kwa taifa migomo husababisha kuathirika kwa uchumi na matokeo yake taifa hushindwa kuwahudumia wananchi wake kwa uka-milifu.

Jinsi ya kuepuka Migomo

Migomo husababishwa na waajiri kwa kukiuka mikataba ya hali bora za kazi kwa wafanyakazi wao. Wakati mwingine waajiri hukataa kuzungumza na wawakilishi wa wafanyakazi au hukataa matakwa yao bila

UKOSEFU WA MAWASILIANO

Hakuna Usawa

Uhasama

Migogoro

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

54

kuwa na sababu za msingi. Hakuna saba-bu ya wafanyakazi kuitisha migomo iwapo kutakuwepo utaratibu wenye nguvu za kisheria wa kulinda au kuimarisha haki na maslahi yao. Panapotokea tofauti baina ya wafanyakazi na waajiri, kuweko chombo cha usuluhishi chenye nguvu na chenye kufanya kazi kitakachosuluhisha mzozo huo. Kubwa zaidi, ni vizuri chama cha wa-fanyakazi kikatambuliwa kuwa ni chom-bo chenye uwezo na kishiriki hasa katika mashauriano ya utatu. Vile vile, serikali na waajiri wanaweza kuepusha migogoro ya kazi pindi wakichukua hatua za makusudi za kuwashirikisha wafanyakazi katika mas-uala yanayowahusu kazini pao au hata kati-ka masuala ya sera mbali mbali za uchumi na jamii.

Vyama vya Wafanyakazi na Wafanyakazi Vijana

Kwa miaka mingi vijana na makundi men-gine maalumu katika jamii hasa katika nchi zinazoendelea yamekuwa na shauku ya kutaka usawa wa haki za binadamu. Mkazo umekuwa ukiwekwa katika shughuli ya ushajiishaji wa masuala ya haki na wa-jibu katika jamii zinazowazunguka baina ya vijana, wanawake, watoto, wazee, waathiri-ka, walemavu, na makundi mengine maal-umu. Katika ulimwengu wa kazi, makundi yote hayo ya jamii yana jukumu na wajibu wa kushiriki katika mapambano ya kudai, kulinda, na kutetea haki za wafanyakazi na ni muhimu kuweka mkazo maalumu ka-tika muhtasari, mikutano, makongamano, mafunzo, na semina za kitaifa na kimataifa juu ya ushiriki wa vikundi hivyo.

Kutokana na umuhimu wa suala Shirika la Kazi Duniani, hivi karibuni kumekuweko na jitihada za makusudi za jumuiya za kitaifa na kimataifa kuchukua hatua kadhaa kwa nia ya kupunguza ubaguzi na kushajiisha usawa na kuhimiza ushiriki wa makundi yote ya jamii. Juhudi maalumu zinafanywa zikiwemo kupunguza aina zote za ubaguzi wa makundi maalumu hasa watoto, wa-nawake, walemavu na vijana.

Hadhi ya Wafanyakazi Vijana katika Ulimwengu wa Kazi

Wafanyakazi vijana hukabiliana na mambo kadha katika sehemu za kazi yakiwemo:

• Ubaguzi na kutengwa kwa vijana (kwa dhahiri au vinginevyo) katika ajira, ku-pandishwa vyeo, kupatiwa nafasi ya masomo zaidi, na kushirikishwa katika maamuzi.

Mgawanyo wa nafasi za kazi na vyeo kutegemea kujulikana/usuhuba na vyombo vya uteuzi

• Mara nyingi vijana hufanya kazi saa nyingi katika jamii hasa katika ajira za mashambani, maofisini, viwandani, ku-tunza wazee, kutoa misaada kwa jamii, na katika ujenzi wa taifa kwa ujumla.

• Upungufu wa kazi za kuajiriwa unawa-fanya vijana kujiingiza katika ajira zisizo rasmi, ambazo huwapatia kipato kido-go. Ajira hizi zina ushindani mkubwa wa soko na ni zenye kuhatarisha maisha yao kwa vile mara nyingi huwa ni ajira zisizo na kinga kwa afya, usalama, na ustawi wa wafanyakazi.

• Umuhimu wa Vyama vya Wafanyakazi Kushirikisha Vijana.

• Vijana wako mstari wa mbele katika ui-marishaji nguvukazi, kwa hivyo vyama vya wafanyakazi vibainishe wazi suala la kulinda na kutetea haki za wafan-yakazi vijana.

• Vyama vya wafanyakazi vina wajibu wa kuhakikisha kutokuwepo kwa ubaguzi katika upatikanaji wa ajira, kutoa vyeo, kulipa mishahara inayolingana na haki za msingi.

• Vyama vya wafanyakazi viweke wazi majukumu na sera zao zinazopelekea vijana kushawishika kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

• Vyama vya wafanyakazi vioneshe kwa vitendo kwamba vinakwenda sambam-

UTA

WAL

A BO

RA K

ATIK

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

55

ba na wakati kwa kusawazisha malen-go na mipango yao katika majukumu ya kijamii na yaendane na mabadiliko na matakwa ya wafanyakazi vijana.

• Vyombo mbali mbali vya vyama vya wa-fanyakazi vioneshe wazi nafasi ya vijana katika ushirikishwaji na uongozi wa vy-ama.

• Wafanyakazi vijana ni hazina ya muda mrefu ya wanachama na hata uongozi wa chama.

Matatizo ya Vijana Sehemu za Kazi

Vijana hukumbana na matatizo kadhaa ka-tika sehemu za kazi yakiwemo:

• Hali ya sehemu za kazi kutojali vijana kwa kutokuwa na mikakati inayozinga-tia masuala ya wafanyakazi vijana.

• Hali ya utoaji hafifu wa habari kuhusu masuala ya kazi na ushiriki wao katika masuala ya vyama vya wafanyakazi.

• Uhafifu wa utoaji habari wa tafiti zina-zofanywa zihusuzo vijana.

• Kutokuwepo kwa kumbukumbu na taratibu nzuri za wafanyakazi vijana zi-husuzo hali zao, matatizo na maende-leo yao.

• Hali ya kubaguliwa kwa wafanyakazi vi-jana katika sehemu za kazi kwa kuone-kana ni hatari kwa ustawi wa wafan-yakazi waliotangulia.

• Umuhimu wa Vijana Katika Vyama vya Wafanyakazi.

Kwa sababu ya umri wao mdogo, vijana watashiriki katika shughuli za vyama vya wafanyakazi kwa muda mrefu zaidi, hivyo watapata nafasi ya:

• Kuendeleza uhai wa vyama vya wafan-yakazi.

• Kutokana na mvuto wao kwa vijana wenziwao, watasaidia katika mchakato wa kampeni za kuongeza idadi ya wa-

nachama vijana katika vyama vya wa-fanyakazi.

• Watatumika kuingiza mitazamo na fikra mpya katika vyama.

• Watapata fursa ya kutoa mchango wao katika kudai, kulinda, na kutetea haki zao na za wafanyakazi wengine.

• Wataelewa kwa wepesi wajibu wao ka-tika maendeleo ya wafanyakazi.

• Watajipatia ujuzi wa uongozi kwa vile ni rahisi kwa wao kujifunza.

Changamoto za Vijana katika Vyama vya Wafanyakazi

Wafanyakazi vijana ambao hujiunga na vyama vya wafanyakazi hukumbana na changamoto kadhaa ambazo lazima zishu-ghulikiwe mara moja iwapo vyama vina-hitaji nguvukazi mpya. Changamoto hizo ni pamoja na:

• Kubadili mitizamo: wafanyakazi vijana watakuwa ndio kwanza wanatoka vyuoni na mitazamo yao kuhusu masuala mbali mbali ya kifikra, kijamii, na mengineyo, tofauti na hali halisi watayoikuta. Ili kue-pusha migongano ya mitazamo, vyama vya wafanyakazi lazima vifanye kazi ya ziada kubadili hali hii.

• Nyenzo za Elimu: Vyama vijitayarishe kuandaa mipango maalumu ya elimu kwa ajili ya vijana kwa nia ya kugeuza mitazamo yao, kuwaelimisha kuhusu kutambua hali zao, ushirikiano na jamii, uwiano wao na makundi mengine ya jamii, haki zao, na wajibu wao kama wa-fanyakazi vijana, na masuala mengine ya aina hiyo.

Wito kwa Vyama vya Wafanyakazi Kuhusu Vijana

Uhai wa vyama vya wafanyakazi kwa kiasi kikubwa unategemea ushiriki wa wafan-yakazi vijana kwa vile wao ni wengi na ku-tokana na umri wao mdogo, wanatarajiwa kuchukua muda mrefu katika harakati za

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

56

vyama vya wafanyakazi na pia ushiriki wao kama wafanyakazi. Hivyo kuna haja kwa vyama vya wafanyakazi kuchukua hatua za maksudi na thabiti za kuwashirikisha wa-fanyakazi vijana. Vijana nao kwa upande wao wanahitaji kuchukua nafasi zao katika kuimarisha misingi ya utetezi wa haki na maslahi ya wafanyakazi. Hatua zifuatazo zinaweza kusaidia kufikia:

• Vyama vya wafanyakazi vifuatilie kwa karibu na kwa makini matatizo ya wa-fanyakazi makazini na kusaidia kuyapa-tia ufumbuzi.

• Vyama vya wafanyakazi viwafikie wafan-yakazi vijana mara kwa mara kwa nia ya kuwaelimisha juu ya umuhimu wa umoja wa wafanyakazi.

• Vyama vya wafanyakazi viwashajiishe wafanyakazi vijana kujiunga na vyama vya wafanyakazi, na kuchukua nafasi za juu za uongozi wa vyama kwa kuwaone-sha kwa vitendo manufaa ya kuwa wa-nachama.

• Katiba za vyama vya wafanyakazi zitoe nafasi kwa vijana na makundi mengine kushiriki kikamilifu katika shughuli za vyama na katika uongozi wa vyama.

Utumikishaji wa Watoto

Moja kati ya mambo muhimu anayojifunza binadamu mara tu azaliwapo, kwa ajili ya kuendelea kuishi, ni tendo la kufanya kazi. Kazi ni shughuli moja takatifu ambayo wa-zazi huwafunza na kuwazoesha kufanya kazi watoto wao tangu wanapokuwa wado-go. Hivyo ulimwenguni kote watoto hufanya kazi majumbani mwao na tendo hili hu-saidia familia kuiweka pamoja katika mai-sha. Lakini baadhi yetu kwa sababu mbali mbali ambazo hazikubaliki huwapa kazi kuzidi watoto uwezo wao kiafya na kiumri kiasi kwamba hatimaye huhatarisha afya ya mtoto anayehusika na hata mustakabali wake kijamii.

Ukubwa wa Tatizo

Inakadiriwa kwamba watoto wafanyao kazi ulimwenguni kote ni kiasi cha millioni 100 hadi 200 ambayo ni sawa na asilimia 4 hadi asilimia 8 ya watu wote wenye uwezo wa kufanya kazi wapatao 2.4 bilioni. Ajira ya watoto imezungushwa ukuta imara barani Afrika kuliko kokote duniani. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kazi Duniani, Bara la Afrika limetia fora kwa kunyonya nguvukazi ya watoto wadogo chini ya umri wa miaka kumi na nne ambao ni asilimia 17 ya wafanyakazi wote. Mtoto mmoja kati ya watoto watatu wa Kiafrika hufanya kazi. Watoto chini ya umri wa miaka 14 wame-onekana katika viwanda vya nguo nchini Lesotho, wameonekana wakikata mkonge nchini Tanzania, wanafanya kazi za sulubu katika machimbo nchini Zimbabwe na Ivory Coast, na hata wameonekana wakifuma mazulia nchini Misri na Morocco. Ajira ya watoto pia ilitia fora nchini Afrika ya Kusini wakati wa utawala wa kibaguzi.

Tatizo kubwa tunalo katika nchi zinazoen-delea ni ukosefu wa takwimu sahihi zihu-suzo mambo ya jamii na hata ya uchumi. Si ajabu kwa hivyo mipango yetu yote kushindwa kutekelezwa vyema kutokana na mipango hiyo kupangwa kutokana na takwimu zisizo sahihiika. Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Zambia kuhusu ajira ya watoto unabaini kuwa asilimia 35 ya watoto wa Zambia wenye umri baina ya miaka 12 na 14 wanafanya kazi na kwamba si na-dra kukuta watoto wakianza kufanya kazi wafikiapo umri wa miaka 7. Tarakimu hii inawiana na tarakimu nyingine zilizotolewa na watafiti mbali mbali. Kwa vyovyote vile kuweko na takwimu au kukosekana kwa takwimu hakuondoi ukweli kwamba tatizo la ajira ya watoto lipo ingawa hatuelewi kwa yakini kima cha tatizo lenyewe. Nchini Tanzania, mfano, taarifa dhaifu tulizona-zo zinatueleza kuwepo kwa tatizo ambalo limesambaa hasa katika viwanda na katika mashamba makubwa ya chai, buni, tum-baku na katani, katika sekta isiyo rasmi na katika shughuli za majumbani. Hali mbaya ya ajira ya watoto inaonekana viwandani na

UTA

WAL

A BO

RA K

ATIK

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

57

mashambani ambako watoto wadogo hu-kumbana na mashine zenye hatari, kemi-kali za hatari, na kazi ngumu inayofanywa kwa muda mrefu. Watoto pia huonekana wakifanya kazi zenye hatari katika machim-bo, mashambani na katika majumba ya kuishi na ya starehe. Kwa mujibu wa utafiti uliogharimiwa na Shirika la Kazi Duniani uliofanywa katika mwaka 1990 katika miji ya Arusha, Dar-es- Salaam na Shinyanga, imebainika kuwa watoto wengi wanaofanya shughuli ndogo ndogo za uchumi katika sekta isiyo rasmi, umri wao ni kati ya miaka 5 na 14. La muhimu hapa ni kwamba iwe watoto wanafanya kazi za sulubu viwanda-ni, mashambani au katika sekta isiyo ras-mi, ukweli ni kwamba watoto hawa wana-jusurisha maisha yao kwa mashine hatari, kemikali zenye sumu kali katika mazingira yao ya kazi, na pia wanalazimika kufanya kazi kwa muda mrefu bila ya mapumziko. Watoto wadogo wa Tanzania chini ya umri wa miaka 14 wameripotiwa kufanya kazi zenye kuwaletea madhara makubwa kiafya katika sehemu mbali mbali za masham-bani na viwandani. Vile vile watoto hawa wamekuwa wakifanyishwa kazi majumbani kwa muda mrefu bila ya mapumziko na wa-toto wa kike wamekuwa wakikerwa kijinsia na waajiri wao wanaume katika majumba, na wengine wamefikia hatua ya kubakwa.

Sababu za Utumikishaji wa Watoto

Utumikishaji wa watoto ni tatizo karibu la ulimwengu mzima. Tatizo lenyewe lina mitazamo na sura mbali mbali katika hali halisi na pia katika aina za athari za ajira hiyo kwa watoto kiafya, kiusalama, na ki-maendeleo. Mazingira na historia ya nchi inayohusika vinatoa mwanga wa kwa nini tatizo hili linaendelea katika nchi hiyo, la-kini sababu kubwa ni kama zifuatazo:

Umaskini uliokithiri katika nchi

Historia inatueleza kuwa hali hii ilikuwa maarufu wakati wa Mapinduzi ya Viwanda huko Ulaya kwenye karne ya 19 ambapo kulikuwa na matatizo ya ukosefu wa ngu-vukazi ya kutosha ya kuendesha viwanda

vilivyokuwa vinaibuka na kwa sababu ya umasikini, watoto wakipewa ajira kwenye viwanda hivyo. Zamani wazee wetu wali-penda kuzaa watoto wengi ili watumie ngu-vukazi yao katika kujitajirisha. Leo, kwa sababu ya sera mbovu za nchi zetu, watu wanabakia masikini na kwa hivyo kulazimi-sha kuibuka kwa uchumi usiyo rasmi am-bao huhitaji waajiriwa wengi wasio na uju-zi. Sera hizi mbovu za uchumi katika nchi zetu huwapa uwezo watu wachache binafsi kuhodhi uchumi wa nchi na kwa hivyo ku-watumia watu wengi kama waajiriwa.

Tatizo la Jamii

Katika familia zetu mara nyingi patokeapo matatizo ya familia anayepata shida wa kwanza ni mtoto. Wazazi wanapofaraka-na watoto mara nyingi hutelekezwa kwa mama wa kambo na mara nyingine hupele-kwa kwa bibi zao ambao ni maskini kiasi kwamba hawamudu kupata mahitaji yao ya maisha, hivyo kuwasababisha kutafuta njia ya kupata mahitaji yao kwa kufanya kazi ingawa kwa ujira wa chini. Watoto hawa hulazimika kuishi maisha magumu ya ku-nyonywa kwa hali zote.

Kiwango cha Elimu

Pengine kiwango cha chini cha elimu ya dunia kwa watu wetu nacho kinachangia katika kuwa na mwamko wa chini kuhu-su umuhimu wa mtoto na kutambuliwa na kutekelezwa kwa haki za mtoto katika jamii. Hii inatokana na kupotea kwa maadili katika jamii zetu.

Sheria za Nchi

Maeneo mengine yanayochangia katika kuenea na kuendelea kuweko kwa ajira ya watoto katika nchi zetu kunatokana na ukweli kwamba sheria za nchi hazisai-dii kukataza utumikishaji wa watoto. Katika nchi nyingine sheria kali zinakuwepo zenye kukataza utumikishwaji wa watoto lakini tatizo linakuwepo kwenye utekelezaji wa sheria hizo. Kwa ujumla kunakuwa na ul-egevu katika utekelezaji na usimamizi wa sheria hizo.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

58

Tatizo la Mila na Desturi za Jamii

Kuna baadhi ya jamii kutokana na mila zao wanaume wanaweza kuoa wake zaidi ya mmoja na matokeo yake wanapata watoto wengi kiasi kwamba wanashindwa kuwa-tunza ipasavyo watoto hao. Matokeo ni kwamba watoto hao hujishughulikia we-nyewe kwa mahitaji ya lazima kutokana na ajira wazipatazo wakiwa watoto wadogo. Wazazi wengine hutumia nguvukazi ya wa-toto wao kwa kujinufaisha wao wenyewe. Watu wengine hujisikia wenye furaha wa-napopewa sifa kwamba wamezaa watoto wengi ingawa pengine wameshindwa ku-washughulikia vyema kwa mahitaji yao ya lazima na kwa malezi yao ya jumla.

Athari za Utumikishaji kwa Watoto

Utumikishaji wa watoto unaathari za muda mfupi na zile za muda mrefu. Mtoto mwe-nyewe kwa sababu ya umri wake mdogo akili yake bado haijakomaa na kwa hivyo hawezi kuelewa matokeo ya kufanya kazi katika umri mdogo, atafurahia kipato kido-go atakacholipwa. Wazazi ingawa wanaele-wa athari za kumtaka mtoto wao afanye kazi mapema, hawawezi kuizuia hali hiyo kutokana na hali halisi ya umasikini wao, watafurahia msaada wa kimaisha unaolet-wa na watoto wao.

Kutokana na hali hiyo ya watoto kutumik-ishwa , watoto hukosa fursa ya elimu ka-

bisa kwa kutopelekwa skuli. Wale walioba-hatika kupelekwa skuli hawapati muda wa kutosha wa kushughulikia masomo yao kwa sababu ya kushughulishwa na maju-kumu yao. Kuna baadhi ya watoto ambao hukatisha masomo yao na hatimaye kuko-sa muda wa kujiendeleza kielimu. Baadhi ya watoto waliojikuta katika ajira wanako-sa nafasi ya kupata malezi bora kifamilia kwa vile muda mrefu wanautumia katika sehemu zao za kazi. Hili ni tatizo ambalo baadaye litakuwa na athari mbaya sio kwa mtoto muhusika pekee bali hata kwa jamii nzima.

Utumikishaji wa watoto una athari pia za baadaye. Kwa mfano, katika tatizo la wa-toto kukosa elimu, taifa linapata hasara kubwa kwa vile itabidi taifa Shirika la Kazi Duniani likuze kundi kubwa la wajinga na wababaishaji kimaisha, na kwa hivyo kuk-wama kwa jitihada za kuleta maendeleo katika nchi kwa sababu misingi ya kuleta maendeleo (sayansi na teknolojia) itakose-kana. Taifa litabidi kuendelea kulea vijana wasio na uwezo wa kuleta maendeleo na pia kujiletea wenyewe maendeleo. Kuhusu suala la afya na usalama, kwa kuwa watoto wanafanya kazi hawakuwi kikawaida kuto-kana na kazi ngumu zinazozidi uwezo wao kiumri, na zinazofanywa katika mazingira magumu ya viwanda na mashambani, afya na usalama wa watoto hawa vimo katika hatari wakati wote, na pia kuwafanya wa-toto hao wawe masugu na kukomaa siku si zao na baadaye tatizo kwa jamii; kwani watoto hawa ndio wanaokuwa wavunjaji wakubwa wa sheria za nchi hali ambayo imesababishwa na mazingira magumu ya kazi wazifanyazo. Pia kwa sababu miili ya watoto hawa haijakomaa vilivyo, kutokana na mazingira haya magumu ya kazi, wa-toto hawa wanaishia kudumaa na wakati mwingine magonjwa yatokanayo na kazi na hata kuwa walemavu. Matokeo ya hali hii ni kama ifuatavyo:-

• Kuwa na taifa lisilo na uwezo wa kutosha wa vijana wake kujitegemea na hivyo ku-jenga tabia ya utegemezi.

Kutokana na hali hiyo ya watoto kutumikishwa , watoto hukosa fursa ya elimu

kabisa kwa kutopelekwa skuli

UTA

WAL

A BO

RA K

ATIK

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

59

• Kwa Vyama vya Wafanyakazi, kuwa na wafanyakazi wasio na elimu na wale-mavu ni sawa na kupunguza kasi ya harakati za wafanyakazi. Hapa naitoshe kusema kwamba utumikishwaji wa wa-toto una faida ya muda mfupi kwa wa-toto wenyewe na familia zao lakini pia ina athari mbaya za baadaye kwa wa-toto wenyewe, wazazi na hata jamii kwa ujumla.

Hatua za Kuchukuliwa katika Kukinga Utumikishaji wa Watoto

Si jambo jema kueleza bayana juu ya uovu wa kitu na hapa utumikishaji wa watoto, bila ya kusaidia katika kutafuta mbinu na mikakati ya kupiga vita uovu huo moja kwa moja kwa nia ya kulinda mataifa yetu na majanga ya jamii ya hapo baadaye kuto-kana na athari zitokanazo na utumikishaji wa watoto. Kwa mintarafu hiyo yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ambayo yana lengo la kupunguza ikiwa si kutokomeza kabisa utumikishaji wa watoto katika nchini zetu:

i) Tuangalie sheria za nchi zenye kuhu-siana na mambo, haya ya utumikishaji wa watoto kama zinakidhi haja ya kuzu-wia hali hii au hapana. Tushauri mkazo uwekwe kwenye utekelezaji wake iwapo tunahisi sheria hizo zinakidhi haja, au tupendekeze mabadiliko ya sheria hizo iwapo tunaamini kuwa kama zilivyo hazitusaidii.

ii) Tushauri serikali zetu juu ya sera za uchumi za nchi zetu zitakazoleta uta-jiri kwa watu wake, badala ya zile zina-zowafukarisha siku hadi siku.

iii) Wafanyakazi na wananchi chini ya vyama vyao wapinge kwa nguvu zao zote sera zozote za uchumi wa nchi au zile zina-zoshindikizwa kutoka nje zitakazoen-delea kuweka watu kwenye umasikini badala ya kuwakwamua.

iv) Juhudi ziendelezwe za kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuwatunza na kuwaelimisha watoto wao, na pia ku-jua, kutetea na kutekeleza haki za mtoto

katika jamii; hili linaweza kusaidia ku-wazuwia wazazi kuwatumia watoto wao kuwa ni kama kitega uchumi cha famil-ia.

v) Tuendelee kushindikiza sheria (kama hapana) inayomtaka kila mtoto aliye na umri wa kwenda skuli apatiwe nafasi ya masomo (kuwa na elimu ya msingi ya lazima).

vi) Vyombo vya serikali na visivyokuwa vya serikali vishirikiane katika kazi hii muhimu ya kutokomeza utumikishaji wa watoto katika nchini zetu.

Hatua za Kitaifa na Kimataifa za Kushughulikia Utumikishaji wa Mtoto

Katiba nyingi za nchi zinatoa ulinzi kwa haki za watoto, ikiwa ni pamoja na haki ya elimu, afya, na nyumba. Kuna vyombo vya kitaifa na kimataifa ambavyo navyo vinalinda haki za watoto kwa zile nchi zilizoridhia mika-taba inayohusika

Pamoja na vyombo hivyo vya kitaifa na kimataifa kulinda haki za mtoto, kuna mambo kadhaa yanayozuia maendeleo ya utekelezaji wa sheria hizo. Hasa sheria zi-nazotungwa huwa hazitoshelezi kushughu-likia tatizo linalohusika na utekelezaji wake huwa legelege. Hivyo kuna haja ya ku-chukuliwa hatua mahususi ikiwa ni pamoja na kuunda vyombo maalumu ili kushughu-likia tatizo la utumikishaji wa watoto.

Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi katika Kuzuia Utumikishaji wa Watoto

Vyama vya wafanyakazi ni sehemu ya wa-shirika wakuu wa maendeleo katika nchi. Vyama vina wajibu wa kutoa mchango wake katika maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii. Watoto ambao ndio wajenzi wa taifa la baadaye wanahitaji kuwekewa misingi ya maisha yao kuanzia kipindi cha mape-ma katika maisha yao. Watoto wanahi-taji kujengwa kiafya na kielimu ili waweze

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

60

kuchukua nafasi yao ya ujenzi wa taifa lao watakapokuwa wakubwa. Bila ya kujengwa kiafya na kielimu watoto hawa hawataweza kutimiza wajibu wao wa kiraia kwa ufanisi unaofaa.

Watoto wanapotumikishwa hawapati nafasi ya kujipatia elimu ya darasani, na wanap-opewa kazi za sulubu huwadumaza kimwili, kiakili, na kisaikolojia. Hivyo mtoto kama huyu anayekuwa katika mazingira kama haya hajakuwa na manufaa katika jamii. Vyama vya wafanyakazi kwa hiyo vitakuwa na wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa vizuri na wanapatiwa elimu bora ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya ujenzi wa taifa lao. Vyama vya wafanyakazi vina wajibu huo kwanza kwa sababu ni wadau wakubwa wa maen-deleo ya nchi na pili vinaengaenga watoto kwa sababu vinatarajia kupata wanachama miongoni mwao hapo baadaye. Vyama vya wafanyakazi katika kusaidia kuzuwia utu-mikishaji wa watoto, vitawajibika kuchukua hatua zifuatazo:

i) Kuandaa kampeni za mara kwa mara zenye lengo la kuzuia utumikishwaji wa watoto.

ii) Kufanya utafiti kila baada ya muda wa kupima ukubwa wa tatizo la utumikish-waji wa watoto.

iii) Kuelimisha viongozi wa wafanyakazi, wafanyakazi, na wananchi kwa ujumla kuhusu ubaya wa utumikishaji wa wa-toto popote watakapogundua, na ku-pendekeza hatua za kuchukuliwa.

iv) Vyama vya wafanyakazi vipendekeze sheria ya kuzuia utumikishaji wa wa-toto, na viwe mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa sheria hiyo inatekele-zwa.

Mwisho

Utumikishaji wa watoto kutokana na saba-bu zozote zinazoelezwa na jamii ni uovu katika mataifa yetu yaliohuru ambao una-hitaji kuondolewa mara moja kwa ajili ya afya njema ya mataifa yetu. Lakini kupun-gua, au kuondoka kabisa kwa tatizo hili, kutategemea juhudi za makusudi na za pamoja za mtu mmoja mmoja, familia, vy-ombo vya serikali, vyombo visivyokuwa vya serikali, vyama vya wafanyakazi, waajiri na

Kongamano

UTA

WAL

A BO

RA K

ATIK

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

61

wale wote wanaokerwa na kitendo hiki kio-vu cha kumnyonya na kumdhalilisha mtoto, malaika wa Mungu, ambaye katika hali yake hiyo ya utoto alikuwa na haki zake kadhaa atekelezewe na familia yake na jamii, mo-jawapo ikiwa ni hifadhi ya maisha yake. Ili tuweze kunusuru maisha ya watoto wetu , lazima sisi sote tuchukuwe hatua sasa hivi.

Lakini lazima tukiri kuwa, kwa sababu utu-mikishwaji wa watoto umekithiri na kuota mizizi nchini mwetu, haiwezekani kuondoa tatizo kufumba na kufumbua. Tumeona kuwa sababu kubwa iliyotufikisha kwenye hali hili na mengine yanayohusiana nayo ni umasikini wa wananchi wetu. Juhudi la-

zima zifanyike za kukuza uchumi wa nchi na mapato ya wananchi.

Pia juhudi zifanywe za kuelimisha umma juu ya umuhimu wa mtoto ambaye atafanya taifa la kesho. Hapana budi watu waelim-ishwe jinsi ya kutekeleza haki za mtoto ili baadaye tatizo la kutumikisha watoto ki-dogo kidogo lipate kutokomezwa. Jamii zetu lazima zijifunze kwamba kipindi cha utoto katika maisha ya binadamu ni kipindi cha kujifunza, kukuwa, na kujiendeleza. Ni jamii ndio inayokuwa na wajibu wa kuandaa mazingira ya kufikia lengo Shirika la Kazi Duniani lilotajwa hapo juu.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

62

AFYA NA USALAMA KATIKA SEHEMU YA

KAZI

Sura6666

AFYA

NA

USA

LAM

A KA

TIKA

SEH

EMU

YA

KAZI

63

AFYA NA USALAMA KATIKA SEHEMU YA KAZIKuna haja gani kwa mfanyakazi kupata mshahara mnono na marupurupu mazuri lakini akaishia kulazwa spitali, au kupata madhara yanayomsababishia ulemavu wa maisha, au kifo muda mfupi tu kabla ya kustaafu kutokana na maradhi au maumivu yatokanayo na kazi katika sehemu za kazi? Utajiri utakuwa na haja gani bila ya kuwa na afya njema?

Ni bahati mbaya sana kuona mamilioni ya wafanyakazi ulimwenguni kote wakip-atwa na maafa ya aina kadhaa yakiwemo kutokulipwa vizuri, afya na usalama wao wakati wote kuwa hatarini kutokana na ha-tari mbaya katika sehemu za kazi. Taarifa zinazotokana na hatari katika sehemu za kazi, maumivu, na upotevu wa mali zina-zohusiana na kazi zinaandikwa sana ka-tika magazeti na kusikika katika vyombo vya habari. Takwimu za kazi za kimataifa kuhusu majanga, maumivu, na upotevu wa mali vitokanavyo na hatari katika sehemu za kazi zinatisha na siku zote zinazidi kuwa kubwa.

Nani wa kulaumiwa? Tumlaumu mfanyaka-zi ambaye kwa makosa hulaumiwa kwa uzembe na uvivu wa kujifunza na kufuata maelekezo ya nini la kufanya kuepuka ma-janga katika sehemu za kazi? Tumlaumu mwajiri ambaye ana wajibu wa kuhakikisha kuwa sehemu ya kazi ziko salama, zenye afya na zisizokuwa na hatari? Tuilaumu serikali kama mwajiri na pia kama mam-laka yenye dhamana ya kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata haki zao ikiwa ni pamoja na afya na usalama katika sehemu zao za kazi, na pia kutoa nafasi kwa wa-shirika wa maendeleo wote kutekeleza ma-jukumu yao? Tuilaumu serikali yenye dha-mana ya kuziweka vizuri sheria na kanuni za afya na usalama kazini na kuhakikisha zinatekelezwa?

Kama waathirika wakuu, wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi vina wajibu gani ka-tika kuhakikisha kuwa afya na usalama ka-zini vinatekelezwa na kudumishwa?. Ni vipi wafanyakazi na vyama vyao vinahusishwa kidemokrasia katika kupanga, kutekeleza, na kufuatilia/kutathmini sera za usalama na afya katika sehemu za kazi na programu zake? Wafanyakazi wana wajibu gani katika kutambua hatari, kukinga na kuzuwia ajali na mapambano dhidi ya HIV/AIDS, na dhi-di ya unyanyapaa? Kama hayo ni sawa, ni vipi basi washiriki wote wa maendeleo wa-naweza kuchukua nafasi zao katika kukuza na kuhakikisha viwango bora vya afya na usalama kazini katika ngazi zote?

Kwa pamoja tulete mabadiliko kwa mambo yasiyokubalika ya hali ya afya na usalama kazini na mengineyo katika sehemu za kazi.

Afya na Usalama Kazini

Afya na Usalama kazini ni tawi la sayansi linalohusisha mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya kulinda na kuendeleza afya ya mfanyakazi kimwili, kiakili, na kijamii wakati wote awapo katika ajira na hata nje ya ajira ikihusisha pia utunzaji wa mazin-gira hasa ya kazi.

Kiwango cha Madhara ya Afya na Usalama Kazini

Katika hali ya kawaida madhara yatokanayo na shughuli za kazi yamegawanyika katika mafungu mawili yafuatayo:

• Katika sehemu za kazi na hasa viwan-dani hutokea ajali wakati wa shughuli za kazi. Ajali huathiri wafanyakazi kim-wili na wakati mwingine kisaikolojia.

• Magonjwa- Kutokana na matumizi ya vifaa mbali mbali hasa vya kemikali, wakati wa kufanya kazi, wafanyakazi

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

64

hatimaye huambulia magonjwa yatoka-nayo na kazi wanazozifanya., Mamilioni ya wafanyakazi wanawake,wanaume, na watoto dunani kote hufanya kazi ka-tika mazingira mabaya na yenye mad-hara kwa afya na usalama wao kama wafanyakazi. Taarifa za Shirika la Kazi Duniani kuhusu afya na usalama katika sehemu za kazi ni za kutisha, kusikiti-sha na kushtusha.

• Zaidi ya wafanyakazi milioni 160 huu-gua kila mwaka kutokana na madhara yatokanayo na kazi. Hii ni sawa na wa-fanyakazi nusu milioni wanaougua kila siku.

Wafanyakazi milioni 1.2 hufa kila mwaka kutokana na ajali sehemu za kazi na ma-gonjwa yatokanayo na kazi. Hii ni sawa na wafanyakazi wawili wanaofariki kila dakika moja.

• Mabilioni ya saa za kazi hupotea kila mwaka kutokana na ajali kazini na ma-gonjwa yanayotokana/ yanayosababish-wa na kazi.

• Mali zinazogharimu mabilioni ya fed-ha hupotea au huharibika kila mwaka kutokana na ajali kazini na magonjwa yatokanayo na kazi. Takwimu hizi ni kiashiria kidogo cha tatizo kubwa lin-alozidi kukua siku hadi siku kutokana na maendeleo ya teknolojia na mabadi-liko mengine.

Waathirika Wakubwa

Wafuatao ni waathirika wakubwa kutokana na taathira za hali ya afya na usalama ka-tika sehemu za kazi. Wafanyakazi masikini na mafukara na hasa wanawake na watoto na wahamiaji:

• Viwanda vidogo vidogo huchangia kwa zaidi ya asilimia 90 ya ajali katika se-hemu za kazi ambazo mazingira yake ni yenye madhara na wafanyakazi wali-omo kwenye viwanda hivyo mara nyingi hawapati kinga.

• Uchafuzi wa mazingira, hasa katika maeneo ya viwanda.

• Athari za kiafya kwa watu waishio ka-ribu na maeneo ya viwanda.

• Kutokana na utaalamu mpya, maende-leo ya teknolojia na juhudi zifanywazo na vyama vya wafanyakazi, madhara yatokanayo na kazi yamechambuliwa zaidi, katika nchi zilizoendelea ku-liko katika nchi zinazoendelea ambako hakuna utamaduni wa kuweka kumbu-kumbu kwa usahihi na utaratibu na kwa usahihi unaofaa. Nyingi ya takwimu zi-lizoainishwa hapo juu ni za kutoka nchi zilizoendelea ambapo wana utamaduni wa kutoa taarifa na kuweka kumbu-kumbu kwa utaratibu unaokubalika. Hali ni mbaya zaidi kwa nchi zinazoen-delea ambapo utoaji wa taarifa, uweka-ji, na utunzaji wa kumbukumbu ni duni. Kwa mfano, makadirio ya Shirika la Kazi Duniani kuhusu viwango vya vifo vitokanavyo na madhara yatokanayo na kazi katika nchi zinazoendelea ni kati ya mara nne hadi sita ikilinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea katika nchi zi-lizoendelea.

Umuhimu wa Afya na Usalama sehemu za kazi

Ajali na magonjwa yatokanayo na kazi tuzi-fanyazo huchangia kwa kiasi kikubwa ki-wango kikubwa kuteseka kwa wafanyakazi pamoja na familia zao. Vitu hivi pia husaba-bisha upotevu wa mali na hata maisha ya watu. Kwa bahati mbaya magonjwa yatoka-nayo na kazi tunazofanya wakati mwingine huchukua muda mrefu kugunduliwa huku kidogo kidogo yakiathiri afya za wafanyaka-zi wanaohusika; matokeo yake utendaji wa wafanyakazi hao huwa hafifu na kushuka kwa ufanisi na tija katika sehemu ya kazi. Kufanya kazi katika mazingira yasiyozin-gatia afya na usalama wa wafanyakazi hu-changia, kwa kiasi kikubwa kutokea ajali na magonjwa yatokanayo na kazi tuzifanyazo katika sehemu za kazi. Ajali na magonjwa hupunguza kipato cha mfanyakazi na cha

AFYA

NA

USA

LAM

A KA

TIKA

SEH

EMU

YA

KAZI

65

familia yake na kusababisha mtafaruku na fadhaa kwa familia nzima. Kwa upande wa sehemu ya kazi kama vile kiwandani, ajali na maradhi huathiri wingi na ubora wa bid-haa zinazozalishwa. Ni dhahiri kuwa athari ziletwazo na mazingira mabaya ya kazi kwa jamii yote ni kubwa. Athari hizo huchangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la umasi-kini katika jamii na katika taifa kwa ujumla.

Matatizo ya afya na usalama kazini katika nchi zinazoendelea huzidishwa na mambo yafuatayo:

• Matumizi ya teknolojia dhaifu na zilizo-pitwa na wakati.

• Kutoeleweka kwa wakati viwango vya tatizo na makali ya tatizo lenyewe.

• Wafanyakazi kutokuwa na elimu ya afya na usalama kazini.

• Waajiri kutokuwa na elimu ya masuala ya afya na usalama.

• Udhaifu wa sheria na utekelezaji wa sheria zinazohusu afya na usalama ka-tika sehemu za kazi.

• Udhaifu wa mtandao wa habari na teknolojia.

• Uhaba wa ajira- jambo hili hupelekea aliyeajiriwa kukubali kufanya kazi hata kama za hatari kwa afya yake.

Gharama na athari za Ajali na Magonjwa yanayotokana na kazi

Ajali na magonjwa yatokanayo na kazi yana-gharama kubwa .Vile vile yana athari nyingi na kubwa za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja kwa wote; waajiri kwa upande mmoja na wafanyakazi na familia zao kwa upande mwingine.

Athari za moja kwa moja kwa wafanyakazi

• Fadhaa, maumivu, na mateso yatoka-nayo na kuumia na/au kuugua.

• Kudidimia kwa uchumi wa wafanyakazi wanaohusika.

• Kutokea hali ya uwezekano wa ku-poteza ajira.

• Kulazimika kukabili gharama za tiba na dawa.

Athari zisizo za moja kwa moja

Athari zisizokuwa za moja kwa moja ni ny-ingi na wala si rahisi kuzipima kwa usahihi. Shirika la Kazi la Duniani linakisia kwamba athari hizo zisizokuwa za moja kwa moja zi-tokanazo na magonjwa yatokanayo na kazi ni mara nne zaidi ya zile athari za moja kwa moja. Moja ya athari za wazi wazi ni ile fad-haa inayopata familia ya mfanyakazi, athari ambayo haiwezi kufidiwa hata kwa fedha.

Athari za moja kwa moja kwa Mwajiri

• Kulipa mishahara bila ya kufanyiwa kazi.

• Kulipia tiba na fidia kwa mujibu wa she-ria.

• Kukarabati na wakati mwingine kubadilisha mitambo na vifaa vilivyo-haribika.

• Kupungua na/au kusimama kwa uzal-ishaji.

• Kushuka kwa ubora wa vifaa vinavyo zalishwa.

• Kuathirika na kupungua ari ya kufanya kazi.

Athari zisizokuwa za moja kwa moja kwa Mwajiri

• Kutafuta mfanyakazi mbadala wa aliye-jeruhiwa/anayeugua.

• Mfanyakazi mpya, itabidi kupewa mafunzo na muda wa kuizoea kazi, na hivyo kuchukua muda kabla ya kuzali-sha kwa kiwango bora na hasa kile cha mfanyakazi aliyekuweko.

• Ajali itokeapo mara nyingi huathiri wa-fanyakazi kisaikolojia na hivyo kuathiri mahusiano mahali pa kazi.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

66

• Mazingira ya kazi yasiyo salama huathiri mahusiano kati ya kiwanda na jamii.

Athari za moja kwa moja kwa jamii na taifa

• Kudhoofika kwa ustawi wa jamii.

• Kuwepo kwa gharama za tiba kwa wal-ioathirika na ajali na maradhi yatoka-nayo na kazi.

• Kutokana na ajali baadhi ya wafanyaka-zi wenye taaluma na uzowefu huathiri-ka na hivyo kulazimisha waajiri kuingia gharama za ziada za kuwapatia elimu na ujuzi waajiriwa wapya wanaochukua nafasi ya walioathirika.

• Sehemu ya kazi huingia gharama za matibabu na kuuguza kutokana na athari za ajali katika sehemu za kazi. Ni dhahiri kwamba gharama zinazohu-siana na ajali na magonjwa ni kubwa kwa waajiri, wafanyakazi pamoja na familia zao – kupoteza maisha, kupata maumivu, kupata ulemavu wa maisha, na hata waajiri kutumia fedha nyingi kwa mambo mbali mbali kukabili ma-tokeo ya ajali katika sehemu za kazi.

Aina za Madhara Sehemu za Kazi

Madhara yaliyopo na yanayolingana sehemu za kazi ni mengi. Mojawapo ya madhara in-aweza ikawa ni chanzo cha madhara men-gine anuwai. Aidha madhara kadhaa huwa na athari na/au dalili zinazofanana. Kila aina ya madhara huwa na viwango tofauti ya taathira, na viwango tofauti vya muda unavyopita kabla ya kujitokeza. Baadhi ya magonjwa yanayotokana na kazi huchukua muda mfupi tu kujitokeza, lakini mengine huchukua muda mrefu kati ya miaka kumi hadi thelathini kabla ya kujitokeza. Mad-hara yanayotokana na kazi yanaweza kuga-wanywa katika mafungu makuu sita:

i) Madhara ya Kimazingira:

Madhara haya mara kwa mara huhusishwa na maumbile na mazingira ya kazi yalivyo, kama vile:

• Viwango vya joto kuwa ni vya juu au chini.

• Kelele za mashine, hasa kiwandani.

• Kiwango cha mwangaza au mavumbi.

• Madhara ya umeme.

• Miale mikali kama vile ya X- ray.

• Mitikisiko.

• Viwango vya hali ya unyevunyevu katika hewa.

ii) Madhara ya Kiufundi

Madhara ya aina hii huibuka kutokana na matatizo ya kimitambo, njia za kupitia kama vile ngazi, mahali pa kufanyia kazi,vitu kuanguka, na vitu kuwa katika mwendo wenye hatari.

iii) Madhara ya kibayolojia

Madhara haya kwa kawaida hutokana na viumbe hai kama:

• Wanyama.• Mimea.• Vimelea.• Virusi.

Kwa mfano daktari wa mifugo kuugua ugonjwa wa kimeta ambao kimsingi ni ugonjwa wa mifugo. Ni dhahiri kuwa dak-tari huyu wa mifugo atakuwa ameambuki-zwa kutokana na kazi anayoifanya ya kutibu mifugo.

iv) Madhara ya Kimaumbile/Kimwili:

Madhara haya hutokana na vitu vifuatavyo:

• Mkao wakati wa kufanya kazi.

• Uzito wa kazi.

• Aina za vitendea kazi vinavyotumika kufanyia kazi.

• Mpango na mfumo (mpangilio) wa kazi.

Licha ya madhara haya kusababisha athari za kimaumbile, husababisha pia msongo wa mawazo na usumbufu mkubwa wa ki-

AFYA

NA

USA

LAM

A KA

TIKA

SEH

EMU

YA

KAZI

67

akili na kimwili. Kwa kawaida mfanyakazi atapata athari za kimaumbile akifanya kazi zinazohusiana na:

• Kusimama wakati wa kufanya kazi kwa kipindi kirefu.

• Kufanya kazi wakati amekaa mkao mbaya utakaothiri maumbile yake; kwa mfano kuinama, kujipinda, kujilazimisha kufi kia kitu cha mbali.

• Kuinua, kubeba vibaya mizigo mizito.

• Kufanya kazi katika urefu usiofaa un-aolazimisha kujinyoosha, kujipinda.

• Kufanya kazi yenye kurudiarudia.

v) Madhara ya Kemikali

Madhara haya huonekana pale mfanyakazi anapotumia kemikali katika shughuli zake za kazi. Kemikali hizo humuingia mwilini mfanyakazi kwa kupitia:

• Kwenye ngozi.• Kinywani, kwa kumeza.

• Puani, kwa kupumua.

Kemikali huwa katika mifumo kama:

• Mavumbi.

• Vimiminika.

• Gesi na mvuke, kama vile corbonmonox-ide –(gesi ukaa). .

Kemikali ziingiapo mwilini husababisha madhara ya papo kwa papo au ya muda mfupi wa kati ya siku moja au mbili , au muda mrefu. Madhara ya sumu huwa ya wastani au makali yenye kudumu kwa muda mfupi au mrefu. Madhara mengine huchukua muda mrefu sana kabla ya kuji-tokeza. Kwa mfano madhara yanayotokana na madini ya ‘asbestos’ huchukua muda mrefu wa kati ya miaka 20 hadi 40 kabla ya kujitokeza. Hali hii inalazimisha haja ya wafanyakazi kukaguliwa afya zao baada ya kila kipindi maalumu.

Mfano hai wa madhara na magonjwa ya-nayotokana na kazi kuchukua muda mrefu

Athari za kemikali

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

68

kabla ya kujitokeza uliotokea katika Gazeti moja liitwalo Workers’ Health International News letter (WHIN) Nam 43 la 1995 liliarifu kuwa katika kijiji kimoja kiitwacho Andhra Pradesh nchini India, ilikuwepo kampuni moja iliyojihusisha na uchimbaji wa madini ya aina ya ‘quartz’ ambayo ikijulikana kwa jina la Andhra Pradesh Mineral Develop-ment Cooperation.

Kampuni hii ilianza kazi mwaka 1965 ikiwa na jumla ya wafanyakazi 450. Katika mwa-ka 1974, miaka tisa baadaye, mfanyakazi mmoja aliugua ugonjwa ambao kwa wakati huo haukuweza kutambulikana. Mgonjwa huyo alifariki licha ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu ya hali ya juu hospi-talini. Muda mfupi tu baadaye, mfanyakazi mwingine aliugua ugonjwa wenye dalili na usugu wa kusikia dawa kama wa yule mfanyakazi aliyetangulia.

Jambo hili liliushtua uongozi wa Kampuni ambapo ulichukua jukumu la kuwapeleka wafanyakazi wote hospitali kwa uchunguzi zaidi na wa kina wa afya zao. Hata hivyo, wafanyakazi wenyewe hawakupewa taarifa za uchunguzi huo. Badala yake wafanyakazi wote waliachishwa kazi, kwa visingizio to-fauti ikiwemo kwamba kampuni ilikuwa in-apata hasara kwa vile uzalishaji wa kiwan-da ulikuwa dhaifu. Miaka 30 baadaye, yaani kwenye mwaka 1995, wafanyakazi 300 kati ya wafanyakazi 450 waliokuwa kampuni hiyo, tayari walikwisha fariki kwa kuugua ugonjwa wenye dalili na sifa kama wale wawili wa mwanzo. Katika kijiji hiki cha Andhra Pradesh, kuna kitongoji kilicho ka-ribu sana na mahali penye mgodi huu, kin-achoitwa Mundarella Thana; tafsiri yake ni ‘Kitongoji cha Wajane’. Wanaume wote we-nye umri zaidi ya miaka 35 katika kitongoji hiki walikuwa wamefariki; na ndiyo sababu kikaitwa ‘Kitongoji cha Wajane’. Tukio hili ni la kushtusha na kusikitisha; lakini ndio hali halisi! Mkasa huu uliowakumba waliokuwa wafanyakazi wa Andhra Pradesh Mineral Development Cooperation na wakaazi wen-gine wa kitongoji cha Mundarella Thanda yawezekana kabisa unaendelea kuwakum-

ba wengine pahali pengine duniani hasa katika ulimwengu wa tatu.

Huduma za afya na Usalama Kazini

Huduma za afya na usalama katika sehemu za kazi endapo zitatolewa ipasavyo na kwa wakati muwafaka, hupunguza viwango vya madhara. Hizi ni aina ya huduma zinazo-lenga kupunguza ukubwa na ukali wa mad-hara yanayohusika. Mojawapo ya huduma hizi ni ile ya utoaji wa huduma ya kwanza mahali pa kazi kwa mfanyakazi aliyepata ajali na kuumia katika sehemu ya kazi.

Huduma ya Kwanza

Huduma ya kwanza ni msaada unaotolewa kwa mfanyakazi aliyeumia kwa ajali ka-zini ili kumpunguzia mhusika maumivu na kuokoa maisha yake. Ajali hizo ni kama vile kuungua moto, kuanguka, kuangukiwa na kitu kizito, kuumizwa na mitambo, kushitu-liwa na umeme. Ili kutoa Huduma ya Kwan-za kwa ukamilifu, waajiri hasa katika viwan-da wanalazimika kuajiri watoaji huduma ya kwanza ambao watakuwepo mahali pa kazi wakati wote wa kazi. Aidha mwajiri yampa-sa kuhakikisha kuwa kila mfanyakazi wake amepatiwa elimu na mafunzo ya msingi ya utoaji wa huduma ya kwanza.

Upatikanaji wa huduma ya kwanza una umuhimu wa aina ya pekee hasa panapo-tokea ajali ambayo inasababisha upotezaji wa damu mwilini, kuvunjika kwa mifupa, kuungua moto, kuumia jicho, kupata ma-jeraha madogo madogo, kunaswa na umeme.

Huduma ya Kwanza ni, msaada unaotolewa kwa mfanyakazi aliyeumia kwa ajali ka-zini; iwe ya kuungua kwa moto, kuanguka, kuangukiwa na kitu kizito, kuumizwa na mitambo, kushituliwa na umeme, n.k, kwa nia ya kumpunguzia muhusika maumivu na kuokoa maisha yake.

Kisanduku cha huduma ya kwanza

Kisanduku cha huduma ya kwanza kinatak-iwa kiwe na vifaa na vyombo vyote vinavyo-hitajika katika utoaji wa huduma yenyewe.

AFYA

NA

USA

LAM

A KA

TIKA

SEH

EMU

YA

KAZI

69

Kisanduku cha huduma ya kwanza ni la-zima kihusishwe na huduma za dharura. Sehemu za kazi hasa kwenye kiwanda, la-zima pawe na kisanduku cha huduma ya kwanza chenye vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kushughulikia matokeo ya dharura ya ajali. Kisanduku hicho lazima kiwekwe mahala ambapo ni rahisi kukifikia na katika maeneo ambayo yana uwezekano mkubwa kutokea kwa ajili na kuhitaji huduma ya kwanza. Mara kwa mara kikaguliwe kwa kuhakikisha ni kisafi na kina vifaa vyote muhimu vinavyohitajika kwa matokeo ya dharura ya ajali.

Jinsi ya Kudhibiti Madhara katika sehemu za Kazi

Hakika wafanyakazi wanawajibu mkub-wa wa kudhibiti madhara katika sehemu za kazi kutokana na ukweli kwamba wao ndio wahusika wakuu. Kwa mfano katika sehemu za huduma, wafanyakazi ndio wa mwanzo kubaini madhara yaliyopo na hata yanayoweza kutokea. Katika kiwanda, wa-fanyakazi ndio waendeshaji mashine, hivyo wao ndio watu wa kwanza kuweza kubaini madhara katika mashine hizo kabla ya mwajiri. Lakini mwajiri ndiye muhusika mkuu ambaye ana wajibu wa kudhibiti madhara katika sehemu za kazi kwa vile yeye ndiye mmiliki wa sehemu ya kazi na mwenye uwezo kifedha wa kuyakinga, kuyapunguza, ama kuyaondoa kabisa.

Zipo mbinu kuu tatu za kudhibiti madhara sehemu za kazi:

a) Mbinu za Kiufundi.

b) Mbinu za kiutawala.

c) Mbinu ya Kutumia vifaa vya Kujikinga.

a) Mbinu za Kiufundi

Hii ni mbinu ya kudhibiti madhara kuan-zia pale kwa mfano mitambo na mashine vinapokuwa katika hali ya kuundwa ki-wandani. Mbinu hii huhakikisha kwamba mitambo imefanyiwa marekebisho tangu inapotengenezwa kiwandani. Mfumo wa

mitambo na mashine hutengenezwa kwa namna ambayo madhara yanakingwa au yanaondolewa, au kemikali hatari na zenye sumu kali zinakuwa na mbadala ambazo zina unafuu.

Kukinga ajali au madhara yanayotokea, kuanzia kwenye chanzo ni mbinu mad-hubuti kabisa ingawa kwa haraka haraka mbinu hii huonekana kuwa ni yenye ghara-ma. Lakini kwa uchambuzi wa kina, mbinu hii ina faida kubwa kwani:

• huwalinda watu wote – wafanyakazi, waajiri wenyewe, jamii, pamoja na kutoa ulinzi na uhifadhi wa mazingira.

• hupunguza gharama – hazihitajiki mbi-nu za kiutawala wala za kutumia vifaa vya kujikinga.

• hutoa huduma ya muda mrefu kabla hajahitaji marekebisho. Hakika hii ni mbinu madhubuti ambayo wataalamu wa masuala ya afya na usalama kazini huwashauri waajiri kuitumia, na wafan-yakazi kwa upande wao huipigania.

b) Mbinu za Kiutawala

Hii ni mbinu inayotumiwa ili kupunguza mfululizo wa muda anaoutumia mfanyakazi katika eneo lenye madhara, ingawa mbinu hii haiondoi kabisa madhara yaliyopo, bali husaidia kupunguza muda wa kuathirika mfululizo.

Ifuatayo ni mifano ya mbinu za kiutawala:

• Kubadilisha mfumo mpango wa Kazi. Kwa mfano badala ya mfanyakazi mmo-ja kufanya kazi hiyo hiyo kwa saa nane mfululizo, wafanyakazi hupangwa kui-fanya kwa saa nne nne.

• Kuwapa wafanyakazi muda wa kutosha wa kupumzika.

c) Mbinu ya Kutumia Vifaa vya Kinga

Hii ni mbinu ya mfanyakazi kujilinda binafsi kwa kutumia vifaa vya kujikinga. Ufanisi wa mbinu hii, ni wa kiwango cha chini kabisa kwa sababu vifaa vya kinga:

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

70

• Haviondoi madhara yenyewe.

• Humkinga mtumiaji binafsi tena pale tu anapokuwa kavaa kama kinga kwa usa-hihi na ipasavyo.

• Humkosesha mfanyakazi raha an-apovaa kifaa cha kinga wakati ana-potekeleza shughuli zake za kazi.

• Vinaweza kuchangia kupunguza usa-hihi na uharaka wa utendaji wa kazi.

• Vinaweza kuwa chanzo cha madhara mapya; kwa mfano kinga za masikio zinaweza kumzuia mvaaji kusikia mbiu ya tahadhari.

• Vichuja-hewa vinaweza kumkwaza mvaaji kuvuta hewa vizuri.

• Vizibia masikio, vinaweza kusababi-sha magonjwa ya uambukizo kwenye masikio.

• Mipira ya kuvaa liyochakaa na kuto-boka inaweza kuruhusu kemikali za sumu kupenya hadi kugusana na ngozi ya mwili na papo hapo kuzihifadhi kwa muda mrefu zaidi na hivyo kufyonzwa mwilini kwa wingi zaidi.

Mara nyingi vifaa vya kujikinga havimkai sawa sawa mvaaji. Wakati mwingine uvaaji wa vifaa vya kujikinga huchangia katika ku-sababisha ajali. Endapo mwajiri ataweka kumbukumbu sawa sawa za gharama za kununulia vifaa vya kujikinga, itadhihirika wazi kuwa matumizi ya vifaa vya kujikinga ni ghali zaidi kwani vinahitajika kununuliwa vipya kuchukua nafasi ya vilivyochakaa kila baada ya muda fulani. Baadhi ya vifaa vya kujikinga ni kama vifuatavyo:

• Kioo cha kukinga macho na uso.• Kinga za masikio.• Vichuja hewa.• Vichuja vumbi.• Mipira ya kuvaa mikononi.• Vazi maalumu la kukinga mwili.• Kofia ya chuma.

Alama za Tahadhari

Inashauriwa kuwa kila kwenye sehemu ya kazi ni vyema kukawekwa alama za tahad-hari ili wafanyakazi wazielewe, kuzifuata, na kuzitekeleza. Madhara na matatizo ya-nayotokana na kutozingatiwa kwa tahad-hari juu ya afya na usalama kazini ni mengi na yenye kutisha.

• Vyombo vya Kusimamia Afya na Usala-ma katika sehemu za Kazi.

• Kazi za aina zote zina kiwango fulani cha madhara. Miongoni mwa maju-kumu ya vyama vya wafanyakazi ni ku-hakikisha wanachama na wafanyakazi kwa ujumla wanafanya kazi katika maz-ingira tulivu safi na salama. Hapo awali vyama vya wafanyakazi vilijikita katika kazi ya kuhakikisha kuwa wanapiga-nia zaidi haki za kawaida za kazi kama vile mishahara bora, kushughulikia migogoro ya kikazi, na masuala men-gine ya kuimarisha mahusiano mahali pa kazi. Masuala muhimu kama vile ya afya na usalama wa wafanyakazi kazini, hayakupewa kipaumbele. Madhara na matatizo yanayotokana na kutozingati-wa kwa tahadhari kwa afya na usalama kazini ni mengi na yenye kutisha. Kwa upande wake, vyama vya wafanyakazi vina wajibu wa kujenga msingi imara na mifumo thabiti ya kusimamia afya na usalama kazini kuanzia matawini hadi ngazi ya chama kitaifa, na hati-maye ngazi ya shirikisho. Kwa kuanzia ili chama kiweze kuhakikisha usalama wa wanachama wake na wafanyakazi kwa ujumla, ni lazima kianzishe chom-bo ambacho kitaundwa na wanachama wenyewe. Chombo hiki kitakuwa na wa-jibu wa kusimamia usalama wa wafan-yakazi katika sehemu ya kazi. Chombo hiki kinaweza kuitwa ‘Kamati ya Afya na Usalama’.

• Muundo wa Kamati ya Afya na Usalama mahali pa Kazi

Hakuna utaratibu maalumu wa kuunda Kamati ya Afya na Usalama katika sehemu

AFYA

NA

USA

LAM

A KA

TIKA

SEH

EMU

YA

KAZI

71

za kazi. La muhimu ni kuwa, kamati inatak-iwa iundwe na wawakilishi wa wafanyakazi na waajiri. Mahala pa kazi penye tawi la chama cha wafanyakazi inashauriwa kuwa viongozi wa tawi wahusishwe katika kama-ti. Kamati yaweza kuwaalika wataalamu wa masuala ya afya na usalama kwa ajili ya kuelimisha na kutoa ushauri wenye lengo la kufanikisha shughuli za kamati.

• Majukumu ya Kamati za Afya na Usala-ma Kazini

Kila mahali pa kazi ni vizuri pakawekwa chombo cha kusimamia afya na usalama wa wafanyakazi. Majukumu na matakwa ya mahali fulani pa kazi yanaweza kutafauti-ana na ya mahali pengine. Lakini tukiach-ilia mbali mahitaji/matakwa maalumu ya mahali fulani pa kazi, majukumu makuu ya kamati yatakuwa yafuatayo:

• Kutengeneza, kuratibu na kusimamia mpango wa mahali pa kazi wa masuala ya afya na usalama kazini, na kujumui-sha katika mipango mingine ya mwajiri.

• Kushiriki katika ukaguzi wa uzingatiaji wa masuala ya afya na usalama mahala pa kazi.

• Kutathmini taarifa za ukaguzi na uchun-guzi wa ajali sehemu za kazi.

• Kuratibu na kusimamia uendeshaji wa mafunzo ya afya na usalama kazini.

• Kutathmini athari za shughuli zote zi-fanywazo mahali pa kazi ikiwa ni pamo-ja na kuainisha kipaumbele, utatuzi, mpango wa kazi na ufuatiliaji.

• Kujadili jinsi ya kufanya marekebisho kwa lengo la kuimarisha utendaji wa kazi katika mazingira yenye hatari.

• Kutumika kama daraja la mawasiliano kwa mambo yanayohusu afya na us-alama kazini kati ya wafanyakazi na mwajiri.

• Kumzindua mwajiri ili ahakikishe kuwa mazingira ya kazi yanazingatia matak-wa ya afya na usalama mahala pa kazi.

• Katika kiwanda, kuushindikiza utawala kuiwekea kinga mitambo ili kudhibiti madhara.

• Kuhakikisha kuwa viwango na maelezo ya matumizi salama ya kemikali kutoka kwa watengenezaji na wasambazaji ya-natafsiriwa na kuandikwa katika lugha rahisi na inayoeleweka kwa wafanyaka-zi wote wa kawaida.

• Kusimamia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya wafanyakazi na mwajiri kuhusu masuala ya afya na us-alama kazini.

• Kusimamisha na kuzuia ufanyaji kazi yenye hatari na yenye kusababisha madhara.

• Kujadiliana na utawala kuhusu mika-taba ya hiari ya afya na usalama kazini.

• Majukumu ya Mwakilishi wa Afya na Usalama Kazini.

Mwakilishi wa Afya na Usalama Kazini licha ya kuwa ni mfanyakazi aliyechaguliwa na wenzake kuwawakilisha, pia ni mwanaha-rakati kama mwanachama wa chama cha wafanyakazi.

Miongoni mwa majukumu yake ni:

o Kuwashawishi wafanyakazi wenzake ku-tumia vifaa vya kinga pale inapobidi, na kufanya kazi kwa usalama.

o Kutoa taarifa na kushiriki katika uchun-guzi wa madhara na ajali mahali pa kazi.

o Kujiimarisha kwa kuwa na habari sahihi na za kutosha kuhusu kazi na maeneo yenye kutishia afya za wafanyakazi.

VVU/UKIMWI NA WAFANYAKAZI

Karibu zaidi ya miaka 30 sasa tangu ul-ipokugundulika ugonjwa wa Ukimwi duni-ani. Bara la Afrika hasa kusini mwa Jangwa la Sahara ndio sehemu iliyoathirika zaidi na janga la Ukimwi kuliko sehemu nyingine ulimwenguni. Kiasi cha watu milioni 45 du-niani wameambukizwa virusi vya ukimwi.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

72

Kati ya hao inakadiriwa kuwa milioni 28 ni wafanyakazi. Na inakadiriwa kuwa kiasi cha watu 15,000 huambukizwa kila siku. Pamo-ja na ukweli kwamba ugonjwa wa ukimwi ni janga la ulimwengu mzima, wafanyakazi wameathirika zaidi na hivyo kutaka kutam-buliwa kwa VVU/UKUMWI kama tatizo la sehemu ya kazi.

Athari za jumla za Ukimwi

Ukimwi unaathiri mpango mzima wa mai-sha, ustawi wa jamii, na uchumi wa familia na taifa. Pia huathiri kila kitu kuanzia ny-umbani katika familia, katika jamii, kazini, na taifa kwa jumla.

• Uzalishaji hupungua kutokana na wa-fanyakazi kutafuta matibabu mara kwa mara , kupata mapumziko, kufanya kazi kwa kiwango cha chini cha ufanisi, na hata kushindwa kufanya kazi kabisa.

• Faida ya taasisi na uwekezaji pia hu-pungua kutokana na uzalishaji kupor-omoka.

• Matumizi ya taasisi huongezeka ku-tokana na kuhudumia wafanyakazi waathirika na pia kuongeza ajira ili kuz-iba mapengo yaliyoachwa na waathiri-ka.

• Nguvu kazi ya kiwanda, taasisi, na sek-ta ya kazi hupungua na wakati mwing-ine husambaratika.

• Mfanyakazi muathirika hupoteza pato na haki zake.

• Unyanyapaa na ubaguzi kwa waathirika hujitokeza.

• Kukosa wafanyakazi wataalamu walio-bobea ambao huathirika.

Hatua za Kitaifa na Kimataifa za kupambana na Ukimwi sehemu za kazi

Katika kulipa umuhimu mkubwa tatizo la ukimwi sehemu ya kazi Shirika la Kazi Du-

niani, mwaka 2001 lilitoa maelekezo ya ku-kabiliana na tatizo, malengo yakiwa:

• Kuzuia ueneaji wa virusi na ukimwi.

• Kupambana na unyanyapaa na ubaguzi.

• Kutoa huduma za kupunguza makali ya waathirika kwa wenye virusi na wag-onjwa wa ukimwi.

• Kutoa huduma kwa waathirika.

Ili kufikia na kutekeleza malengo haya, ni vyema kwa taasisi kuweka suala la ukimwi katika sera yake kwa uwazi kabisa. Sera hiyo ni vizuri ikazingatia mambo ya msingi hasa suala la haki na usawa wa kijinsia se-hemu ya kazi, kuzuia ubaguzi na vikwazo kutokana na suala hili zito kwa waathirika. Pia inapendekezwa kuwa taasisi itayarishe na kutekeleza mpango wa kupambana na ukimwi kazini. Sera na mpango wa kupam-bana na Ukimwi sehemu za kazi ni muhimu sana na vitu hivyo vizingatie:

o Kusisitiza ukweli kwamba ukimwi ni su-ala muhimu la kushughulikiwa kazini na linahitaji kupewa kipaumbele.

o Kusisitiza kuwa ubaguzi ni mwiko katika uajiri, fursa ya mafunzo na kupandishwa vyeo.

o Kuzingatia usawa wa jinsia.

o Kusisitiza uwazi katika mazungumzo ya utekelezaji wa sera ya ukimwi.

o Kupima virusi si suala la lazima katika uajiri na katika hatua za kuomba kazi.

o Kusisitiza kutunza siri kuhusu masuala ya waathirika wa ukimwi.

Mpango wa Masuala ya Ukimwi Kazini

Kila taasisi inashauriwa iwe na mpango wa kupambana na ukimwi sehemu ya kazi. Mpango huo lazima ukubaliwe na utawala/uongozi na wafanyakazi wenyewe. Kufikia muwafaka, inapendekezwa kuchukuliwa hatua za pamoja zifuatazo baina ya utawa-la/uongozi na wafanyakazi:

AFYA

NA

USA

LAM

A KA

TIKA

SEH

EMU

YA

KAZI

73

• Paundwe kamati ya ukimwi sehemu za kazi yenye wajumbe kutoka upande wa utawala/uongozi na wafanyakazi.

• Kupitia na kusaidia kutekeleza sera ya ukimwi kwa manufaa ya taasisi na wa-fanyakazi.

• Kutathmini hali ya ukimwi sehemu ya kazi.

• Kutayarisha mpango wa mapambano dhidi ya ukimwi sehemu ya kazi.

• Kutayarisha mpango wa elimu ya VVU/UKIMWI na kuitekeleza sehemu ya kazi.

Suala la Kinga

Hili ni eneo muhimu sana tukizingatia uk-weli kwamba hadi sasa ukimwi hauna tiba wala chanjo. Ni vyema wafanyakazi waka-jihadhari na kuchukua hatua za kujikinga kwa maambukizo kwa kila hali.

Wafanyakazi wanashauriwa waepukane na mazingira ya hatari ya aina zote yanay-opelekea kupata VVU/UKIMWI.

Shirika la Kazi Duniani linasisitiza mahala pa kazi kuwepo na utaratibu wa kutoa:

• Taarifa na ufahamu wa kutosha kwa wa-fanyakazi kuhusu suala la ukimwi kwa kutumia njia mbali mbali.

• Mafunzo kuhusu ukimwi kwa wafan-yakazi wote.

• Kufanya kampeni ya kutosha na en-delevu dhidi ya ukimwi kazini na kutoa ushauri nasaha pale inapohitajika.

Matibabu na Huduma

• Kuwepo utaratibu wa wagonjwa/waathirika kupatiwa dawa za kudumaza VVU kwa ajili ya kupunguza makali ya ukimwi.

• Waathirika pamoja na familia zao wa-patiwe msaada wa fedha kukidhi haja muhimu na za huduma za dharura.

• Waathirika kutayarishiwa mpango wa kupunguziwa saa za kazi, au kubadil-ishwa kazi kwa mujibu wa hali zao.

• Mpango wa tiba uhusishwe na hadhari muhimu za utunzaji afya pamoja na mpango wa chakula bora.

Ukimwi ni maradhi ambayo hayana tiba wala dawa. Hivyo ni wajibu wetu kuelimis-hana na kukumbushana juu ya mapamba-no dhidi ya ukimwi katika jamii kwa ujumla, na kwamba kila mfanyakazi aoneshe kujali kwake maisha yake na ya wenzake kwa ku-fuata maadili mema na kupiga vita vitendo vyote yenye kupalilia kuenea kwa virusi vya ukimwi katika sehemu za kazi na jamii yetu kwa ujumla. Hatua madhubuti za kuaini-sha na kuendeleza sera na mpango wa kinga dhidi ya Ukimwi kazini zinapaswa kuimarishwa zaidi ili kupunguza taathira ya ukimwi kwa wafanyakazi wetu na sehemu za kazi.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

74

UMOJA WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

AFRIKA (OATUU)

Sura

Muunganiko

7777

UM

OJA

WA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI A

FRIK

A (O

ATU

U)

75

UMOJA WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI AFRIKA (OATUU)

Chimbuko

Vyama huru vya wafanyakazi Afrika vin-aungana kupitia Umoja wa vyama vya wa-fanyakazi barani Afrika. Umoja huu huitwa “ The Organization of African Trade Union Unity (OATUU)” Hivi sasa OATUU ina vyama shiriki sabini na tatu kutoka nchi huru za Afrika hamsini na mbili. OATUU ina wana-chama wapatao millioni thelathini.

Umoja huu uliundwa kutokana na Azimio la Mkutano Mkuu wa vyama huru vya wa-fanyakazi vya nchi za Afrika. Mkutano huo ulisimamiwa na Umoja wa Nchi Huru za Afrika. Mkutano huo ulifanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, mwezi April, 1973. Ku-undwa kwa OATUU kuliashiria mwisho wa tofauti za vikundi mbali mbali vya vyama vya wafanyakazi barani Afrika ambavyo viliku-wepo wakati huo.

Kabla ya mkutano mkuu uliozaa OATUU, mkutano wa matayarisho uliandaliwa na kufanyika Novemba, 1972 katika Makao Makuu ya OAU, Addis Ababa. Mkutano huo wa matayarisho ulijumuisha vyama vya wafanyakazi vyenye mitazamo tofauti. Ijapokuwa vyama vingi kati ya hivyo vili-unga mkono wazo la kuunda OATUU, kuna baadhi ambavyo vilipinga wazo Shirika la Kazi Duniani. Tatizo hili lilimalizika mwe-zi Machi, 1975 wakati wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa OATUU uliofanyika Accra, Ghana. Katika mkutano huo vyama vyote vya kitaifa vya wafanyakazi barani Afrika hatimaye vilikubali kwa kauli moja kuwa wanachama wa OATUU. Tangu kuundwa kwake OATUU imekuwa ikifanya mikutano yenye lengo la kuimarisha umoja wa vyama vya wafanyakazi wa Afrika. Mkutano wake mkuu wa pili ulifanyika Tripoli, Libya, April, 1978. Mkutano Mkuu wa Tatu wa OATUU ulifanyika Mogadishu, Somalia, mwezi wa Oktoba, 1980. Mkutano Mkuu wa Nne wa kawaida ulifanyika Januari, 1985, mjini La-gos, Nigeria. Katika mkutano huu kulitokea mfarakano ambao ulidhoofisha shughuli za OATUU kutoka Januari,1985 hadi Oktoba, 1986. Kiini cha mfarakano huo kilikuwa ni baadhi ya wanachama kutokuwa na imani na Sekretariati iliyokuwepo wakati huo.

Ili kutatua mgogoro huu Mkutano Mkuu wa dharura uliitishwa mjini Accra, Ghana, Feb-ruari,1986, lakini mkutano huu ulishindwa kutoa ufumbuzi na badala yake OATUU iligawanyika katika vikundi viwili vilivyopin-gana.

OATUU ina uhusiano na ushirikiano na vy-ama kadhaa vya wafanyakazi ulimwenguni kote. Mahusiano haya yapo katika misingi ya udugu na mshikamano wa tabaka la wafanyakazi ulimwenguni. Umoja huu pia unatambuliwa na OAU, sasa AU na una uw-ezo wa kushauriana na vyombo vyake. Aid-

Umoja huu huitwa The Organization of African Trade Union

Unity (OATUU)” Hivi sasa OATUU

ina vyama shiriki sabini na tatu

kutoka nchi huru za Afrika hamsini na mbili. OATUU ina

wanachama wapatao milioni thelathini

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

76

ha OATUU ina uwezo wa mashauriano na vyombo vya Umoja wa Mataifa vya Uchumi, Shirika la Kazi Duniani, UNESCO, FAO na vinginevyo.

Madhumuni ya OATUU

Yafuatayo ni madhumuni muhimu ya OATUU:

o Kujenga umoja miongoni mwa vyama vya wafanyakazi katika Bara la Afrika.

o Kuunganisha na kuongoza shughuli za vyama vya wafanyakazi vya mataifa ya Afrika.

o Kulinda uhuru wa vyama vya wafanyaka-zi dhidi ya matakwa potofu ya serikali na vyama tawala vya siasa.

o Kulinda matakwa ya tabaka la wafan-yakazi wa Afrika na kushawishi seri-kali za bara la Afrika kuhakikisha kuwa nafasi za kazi kwa wananchi wake zin-alindwa na wanapatiwa mgawanyo ulio sawa wa pato la taifa.

o Kuhakikisha kuwa kuna sheria za kazi zinazomsaidia mfanyakazi hasa zile za kuvipa vyama vya wafanyakazi haki ya kuwa na mazungumzo ya pamoja na waajiri kuhusu haki na maslahi ya wa-fanyakazi.

o Wakati wa harakati za kupigania uhuru, OATUU, ilishirikiana na vyama vya wa-fanyakazi katika makoloni na Afrika ya Kusini kuweka shindikizo ili nchi hizo zijikomboe haraka iwezekanavyo. Hivyo OATUU unapiga vita unyonyaji, ukoloni na hali zote za ukandamizaji barani Af-rika na ulimwenguni kote.

o Kuendeleza urafiki, udugu na mshika-mano miongoni mwa wafanyakazi pop-ote walipo.

o Kupigania uhuru wa uchumi na ushiriki-ano wa kiuchumi miongoni mwa mataifa ya Kiafrika.

o Kulinda amani ulimwenguni kote. Ili amani ya kweli na ya kudumu ipatikane

barani Afrika, OATUU huhimiza utawala wa sheria, haki na demokrasia. Aidha OATUU hutilia mkazo suala la ushirik-ishwaji wa wafanyakazi.

o Kutetea haki za msingi za binadamu za kuishi, kufanya kazi na kupata malipo ya haki.

o Kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na ajira ya watoto.

o Kushauri juu ya masuala ya uchumi wa bara la Afrika na kupinga sera zozote za uchumi zinazomkandamiza au zi-sizomnufaisha mfanyakazi. Mifano ya sera hizo ni zile za kurekebisha uchumi za mataifa ya Afrika zinazosimamiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Dun-iani. Sera hizo tayari zimeshathibitishwa kuwa haziwasaidii bali huwakandamiza wafanyakazi.

o Kushirikiana na vyama vya wafanyakazi vya mataifa ya Afrika katika kutatua tati-zo la mazingira yanayohatarisha afya na usalama wa wafanyakazi barani Afrika.

o Kuhimiza ukombozi wa mwanamke na usawa wa jinsia mahali pa kazi.

o Kusaidia kuwapa uwezo kielimu, viongo-zi wa wafanyakazi na vyama vyake shiriki ili vitoe huduma bora zaidi kwa vyama na wanachama wao.

Vyombo vya OATUU

Kwa mujibu wa Katiba OATUU ina vyombo vifuatavyo:

(a) Mkutano Mkuu

Hiki ndicho chombo cha juu cha uamuzi cha OATUU. Chombo hiki kinaundwa na wajumbe wanne kutoka kila chama cha wafanyakazi cha kitaifa kilichojishirikisha na OATUU. Mkutano Mkuu hukutana mara moja kila baada ya miaka minne kujadili, kutoa maamuzi na kupitisha mipango ya utekelezaji wa kazi za OATUU. Mkutano Mkuu pia huchagua wajumbe wa kuunda Kamati ya Utendaji wa OATUU. Mkutano

UM

OJA

WA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI A

FRIK

A (O

ATU

U)

77

Mkuu unaweza kukutana katika mkutano wa dharura iwapo utaombwa na vyama shiriki, visivyopungua idadi ya theluthi mbili.

(b) Baraza Kuu

Baraza Kuu linaundwa na mwakilishi mmo-ja mmoja kutoka vyama shiriki. Baraza hili hukutana mara moja kwa mwaka katika mkutano wa kawaida. Hukutana pia wakati wowote baada ya maombi ya theluthi mbili ya vyama shiriki vya OATUU. Jukumu kub-wa la Baraza Kuu ni kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka.

(c) Kamati ya Utendaji

Kamati hii inaundwa na wajumbe kumi na tatu (13). Wawili kati yao huwa ni wanawake

wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu kuto-kana na wanachama wanaolipa michango.

Wajumbe wenyewe ni kama wafuatavyo:

• Rais (1).• Makamu wa Rais. Watakaochaguliwa

kutoka Zoni tano za OATUU (5).• Katibu Mkuu (1).• Wasaidizi wa Katibu Mkuu (2).• Mtunza Hazina Mkuu (1).

Kamati ya Utendaji hufanya shughuli zake kwa kipindi cha miaka minne. Wajumbe wa Kamati wanaweza kuchaguliwa tena baada ya kipindi chao cha kwanza kumalizika. Kamati ya Utendaji ndio chombo cha utend-aji wa shughuli za OATUU za kila siku. Shu-ghuli mahususi za Kamati ya Utendaji ni:

• Kutekeleza maamuzi ya Baraza Kuu.

Kamati ya Utendaji

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

78

• Kusimamia shughuli za sekretariati za kutayarisha na kuwasilisha taarifa ya shughuli za kazi za OATUU mbele ya Baraza Kuu.

(d) Sekretariati ya OATUU

Makao Makuu ya OATUU yako mjini Accra, Ghana, chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa Umoja huo. Katibu Mkuu ana wasaid-izi wakuu wawili na mtunza hazina mkuu mmoja. Maafisa hawa huchaguliwa na Mkutano Mkuu na hufanya shughuli zao kwa kipindi cha miaka minne. Wanaweza wakachaguliwa tena baada ya kumalizika kwa kipidi hicho. Watendaji wengine katika Sektretariati wanaajiriwa na Katibu Mkuu baada ya maelekezo ya Kamati ya Utendaji.

Sektretariati ina vyombo kumi na moja (11) vinavyoshughulikia maeneo maalumu ya kazi. Kwa sasa Sekretariati inasaidiwa na vyama vinne vya wafanyakazi vya kanda katika majukumu ya kuratibu shughuli za vyama vya wafanyakazi, kuelezea sera na malengo ya OATUU, kuhakikisha kuwa wa-fanyakazi wanashirikishwa katika maende-leo ya sehemu zao. Vyama hivyo vya wafan-yakazi vya Kanda ni kama vifuatavyo:

• Umoja wa vyama vya wafanyakazi vya Af-rika ya Magharibi (OTUWA). Makao yake Cotonou, Benin.

• Umoja wa vyama vya wafanyakazi vya Af-rika ya Kati (OTUCA) Makao Makuu yake yako Kinshasa, Zaire.

• Umoja wa vyama vya wafanyakazi vya Kusini mwa Afrika (SATUCC) Makao yake Makuu ya Lilongwe Malawi na.

• Umoja wa vyama vya wafanyakazi katika sehemu ya Uarabuni Magharibi (OTUAM) Makao yake Makuu yako Tunis, Tunisia.

Mafanikio OATUUOATUU hushughulikia karibu vyama vyote vya wafanyakazi barani Afrika. Ijapokuwa tangu kuundwa kwake umoja huu ume-fanya kazi kwa mafanikio makubwa lakini pamekuwapo na matatizo pia. Miongoni

mwa mafanikio ambayo hayawezi kusahau-lika ni:

• Kitendo cha kuunganisha vyama vyote vya kitaifa vya wafanyakazi barani Af-rika.

• Kuanzishwa kwa Baraza Kuu ambapo viongozi wa vyama shiriki hukutana kuongelea matatizo na mafanikio ya vyama vya wafanyakazi barani Afrika. Baraza hili huandaa pia mikakati ya kutatua matatizo ya wafanyakazi. Aidha washiriki hupata fursa ya kubadilisha uzoefu na mawazo jinsi ya kuendesha vyama vya wafanyakazi.

• Kuwa mstari wa mbele katika harakati za kupinga unyonyaji, unyanyaswaji wa mfanyakazi, na dhuluma nyinginezo za kijamii na za kiuchumi. Kwa mfano OATUU ilikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya sera za kibaguzi za Afrika ya Kusini hadi kufikia utawala wa walio wengi.

• Kutoa shindikizo kwa serikali za mataifa mbali mbali ili ziweke mipango na sera zinazowanufaisha wafanyakazi.

Changamoto za OATUU

Pamoja na mafanikio ya OATUU, umoja huu unakabiliwa na changamoto za msingi zi-fuatazo:

• Upungufu wa fedha za kuendeshea kazi unaoukabili umoja huu kwa kipindi kirefu sasa. Kwa kawaida OATUU hupa-ta fedha za kuendeshea shughuli zake kutokana na michango ya wanachama wake au kutoka kwa wafadhili. Kwa kip-indi kirefu, michango haiwasilishwi kwa wakati na vyanzo vingine vya mapato navyo vimekauka. Hivyo OATUU inai-shi kama kuku anayekula leo na kesho yake hajui iwapo atapata riziki. Wakati mwingine hukosa hata uwezo wa kuiti-sha vikao vya kikatiba.

• Kuna dalili zinazoashiria mgawanyiko miongoni mwa wanachama wa OATUU; hali ile iliyojitokeza huko nyuma katika

UM

OJA

WA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI A

FRIK

A (O

ATU

U)

79

mwaka 1986. Hali hii ikiachiwa itasa-babisha janga kubwa lisilotabirika kwa OATUU na hata kwa umoja wenyewe wa nchi huru za Afrika. Hali hii siyo ya kujivunia. Ieleweke kwamba OATUU ni

chombo cha Afrika kwa ajili ya Afrika na kwa manufaa ya Afrika. Kwa hivyo ni wajibu wa viongozi wa vyama vya wafan-yakazi barani Afrika kuhakikisha kuwa OATUU inadumu na kuimarika.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

80

MASUALA MTAMBUKA YA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Sura8888

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

81

MASUALA MTAMBUKA YA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Hifadhi ya Jamii

Hifadhi ya Jamii ni dhana kongwe inay-owakilisha ufumbuzi wa matatizo ya kiu-chumi yanayoipata jamii.

Hifadhi ya Jamii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mpango wa kujipatia na kuendeleza ki-pato kwa mtu punde tu ajira yake inapoko-ma, kutokana na ukosefu wa kazi, ugonjwa, ajali, uzee, au kutoa msaada kwa warithi wa mfanyakazi aliyefariki. Kwa hivyo, hifadhi ya jamii ni mpango maalumu wa kugharimia majanga maalumu yaliyoainishwa hapo juu yanayoweza kumpata mfanyakazi wakati wa uhai wake au hata anapofariki.

Hifadhi ya Jamii ni haki ya msingi ya kila mwananchi popote katika ulimwengu huu kwa mujibu wa tangazo la Haki za Binad-amu la Umoja wa Mataifa la mwaka 1948. Utekelezaji wa tangazo hili, ulifuatiwa na Azimio la Shirika la Kazi Duniani Nam. 102 linalohusu Hifadhi ya Jamii la mwaka 1952.

Hapo kale jamii zilikuwa zikisaidiana kwa namna mbali mbali wakati wa majanga. Watoto mayatima wakilelewa na kutunzwa na watu wao wa karibu. Kwa njia za ujima, jamii zilisaidiana katika kilimo na hata ka-tika kuvuna mazao yakiwa mengi.Wazee-wakishughulikiwa na wakitunzwa na wato-to wao au jamaa zao. Mwanajamii alipopata msiba alichangiwa ili agharimie mazishi ya mtu wake. Hivyo jamii nzima ilikuwa na wajibu wa kuhakikisha hakuna anayekosa huduma ya lazima katika jamii hata kama hana tena uwezo wa kukimu maisha yake kwa sababu ya uzee, ugonjwa, au ukosefu wa ajira. Leo wajibu huu wa kutunza jamii umekuwa wa serikali. Serikali huunda chombo maalumu kwa ajili ya kushughu-likia Hifadhi ya Jamii. Hili yumkini lime-onekana kuwa la lazima kwa sasa kwa vile desturi za jamii kusaidiana zimeanza ku-pungua na watu kutelekeza jamaa zao hata wakaribu.

Aina za Hifadhi ya Jamii Duniani

Kuna aina tatu za Hifadhi ya Jamii duniani:

• Hifadhi ya Jamii katika mfumo wa mis-aada kwa jamii.

• Hifadhi ya Jamii katika mfumo wa ku-changia kupitia mifuko ya akiba au mi-fuko ya pensheni.

• Hifadhi ya Jamii katika mfumo wa hiari.

Hifadhi ya Jamii ni haki ya msingi ya kila

mwananchi popote katika ulimwengu

huu kwa mujibu wa tangazo la Haki za

Binadamu la Umoja wa Mataifa la mwaka

1948. Utekelezaji wa tangazo hili,

ulifuatiwa na Azimio la Shirika la Kazi

Duniani (Shirika la Kazi Duniani) Nam 102

linalohusu Hifadhi ya Jamii la mwaka 1952

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

82

Kustaafu Kazi

Kila mtu katika jamii ana wajibu wa kufanya kazi ili kujikimu yeye na familia yake. La-kini kufanya kazi kuna ukomo kwani inafika wakati binadamu anapoteza uwezo wa ku-fanya kazi kutokana na umri au maradhi. Katika kazi ya kuajiriwa, mfanyakazi ana-takiwa akifikia umri fulani, astaafu kufanya kazi kwa mujibu wa sheria iliopo. Kustaafu kazi kwa mwajiriwa ni hatua isiyoepukika, inayoambatana na kufikia umri fulani kwa mujibu wa sheria na taratibu za kazi za nchi zinazohusika, kitendo kinachoashiria kufikia ukomo wa muda wa utumishi.Wa-fanyakazi wengi hushituka wanapotajiwa kustaafu kazi. Hali hii husababishwa na uzowefu walioupata kutoka kwa wastaafu waliotangulia ambao walikabiliwa na mai-sha magumu kwa sababu hawakujiandaa na wala hawakuandaliwa kustaafu.

Aina za kustaafu

• Kustaafu kwa hiyari; yaani kustaafu kabla ya kufikia umri wa kustaafu kwa lazima kwa mujibu wa sheria ya nchi in-ayohusika.

• Kustaafu kwa lazima; kustaafu wakati muhusika anapofikia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ya nchi inayohusi-ka.

• Kustaafishwa kwa maradhi; mfanyakazi hustaafu kwa sababu ni mgonjwa kiasi kwamba hali ya afya yake haimruhusu kutekeleza majukumu yake kama mfan-yakazi. Hali hii haitabiriki; inaweza kum-tokea mfanyakazi wakati wowote. Kwa hivyo mfanyakazi hulazimika kustaafu kazi afikiapo umri wa kustaafu uliotajwa katika kifungu cha sheria inayohusika. Aidha mfanyakazi anaweza kuchagua kustaafu pale anapofikia umri unaom-ruhusu kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria inayohusika. Lakini pia mfan-yakazi hustaafishwa kazi na mamlaka inayohusika pale inapothibitishwa na Bodi ya Madaktari, iliyotayarishwa kwa ajili hiyo, kwamba hali ya afya ya mfan-

yakazi mhusika haimruhusu kuendelea na kazi.

Matayarisho ya KustaafuKila muajiriwa afikapo umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria analazimika kustaa-fu hata kama bado anamudu kutekeleza majukumu yake. Ili kuingia katika hali hii ya ustaafu ambayo mara nyingi huwa haipendezi, mfanyakazi anahitaji kufanya maandalizi ya kutosha. Wafanyakazi wengi huwa hawafanyi maandalizi ya kustaafu ndio maana huwa hawaikubali hali hiyo na hufanya juu chini ili waendelee kubaki ka-zini. Mfanyakazi mstaafu ambaye kabla ya kustaafu akipata ujira uliomsaidia kuende-leza maisha yake na ya jamii yake anaingia katika maisha ya ustaafu ambapo huwa hana uhakika wa maisha yake ya baadaye. Lakini wafanyakazi lazima wajitayarishe kisaikolojia ili waikubali hali hii mpya ya maisha. Lazima wafanyakazi wawapo ka-zini wakubali kuwa kustaafu ni hatua isi-yoepukika ambayo huambatana na umri wa mfanyakazi na hatimaye hulazimika kuondoka kazini kwa mujibu wa sheria na taratibu za kazi husika. Hivyo, katika hali hii haja ya mfanyakazi kujitayarisha ku-ingia katika maisha ya ustaafu inachukua umuhimu wake.

Hatua za Matayarisho ya Kustaafu

Chama cha wafanyakazi kina wajibu wa kumsaidia mwanachama wake katika matayarisho ya kustaafu kazi. Msaada mkubwa wa chama cha wafanyakazi kwa mwanachama wake ni wakati wote kumta-yarisha kisaikolojia na hasa kumkumbusha kuwa kuna siku itabidi akome kuwa mtumi-shi na hivyo atapaswa kujiandaa kustaafu. Sehemu kubwa ya maandalizi ya kustaafu inabidi ifanywe na mfanyakazi mwenyewe. Uchumi wa dunia siku zote huwa unabadi-lika kiasi kwamba huathiri maisha ya kila siku ya wafanyakazi. Kwa hivyo ni muhimu kila mfanyakazi kufanya matayarisho bi-nafsi kwa ajili ya kustaafu. Maandalizi ya mpango maalumu unaoweza kutekelezeka

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

83

ni moja kati ya hatua muhimu ya kufikia lengo la kustaafu.

Ni vyema mstaafu mtarajiwa akaanza kwa kujifanyia tathmini kuhusu uwezo alionao-aangalie rasilmali aliyonayo na jinsi atavy-oitumia kabla na baada ya kustaafu. Aidha mstaafu mtarajiwa abaini rasilmali anay-oihitaji lakini hanayo na jinsi atakavyoipata kwa ajili ya mipango yake ya kustaafu. Tath-mini hiyo itaweza kumsaidia kumpa fununu ya mafanikio na hata changamoto wakati wa kutekeleza mpango wake wa kustaafu.

Hatua ya Kwanza: Malengo ya Kustaafu

Kupanga malengo kwa ajili ya kustaafu ni jambo muhimu kwani hatua hii itamwez-esha muhusika kuelewa mahitaji yake hasa ya rasilimali katika utekelezaji wa mpango wake. Hatua hii itamwezesha muhusika kuweka vipaumbele kwa ile mipango ili-yomuhimu sana. Mipango ya kustaafu yaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu. La-kini mipango ya muda mrefu inapendelewa zaidi kutekelezwa kwa vile muda muwafaka utapatikana kupima matokeo ya utekelezaji wa mipango hiyo. Kwa bahati mbaya katika kipindi hicho mstaafu mtarajiwa anaweza kupata uhamisho wa kikazi, hali inay-oweza kusababisha; ukosefu wa muda wa kutekeleza mipango yake na kupungukiwa na rasilimali. Ili kukabiliana na hali hiyo, maswali yafuatayo yanahitaji kujibiwa na mstaafu mtarajiwa:

• Mfanyakazi anapendelea kustaafu wakati gani (mwaka gani, ukiwa na umri gani?).

• Anataka kufanikisha lengo gani kabla na hata baada ya kustaafu (lengo la kijamii, kisiasa, kielimu, kiuchumi).

• Iwapo nafasi au elimu aliyonayo inaweza kumsaidia kufikia lengo.

• Iwapo anahitaji kufanya kazi muda wa ziada ili kufanikisha lengo lake la kustaafu.

• Anaelewa mahitaji muhimu ya familia yake kama afya na elimu ya vijana wake.

• Iwapo nyaraka zote zinazohusu masu-ala ya ajira yake na pensheni zipo tayari na zipo katika hali nzuri.

Nyaraka muhimu ni: barua ya kuingizwa kazini, barua ya kuthibitishwa kazi, fomu ya ukaguzi wa afya, mkataba wa kazi.

Hatua ya Pili: Matumizi/Rasilimali zako

Baada ya kupanga malengo ya kustaafu mfanyakazi itamlazimu kuangalia rasilima-li alizonazo ili aweze kutekeleza malengo hayo. Rasilimali zinaweza kuwa:

• Wakati.• Fedha.• Mikopo.• Elimu.• Harakati/Nguvu.• Rasilimaliwatu.• Rasilimalivitu.

Hatua ya Tatu: Maandalizi ya Bajeti

Ni vizuri kupata mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kustaafu kwani ujuzi huu utam-wezesha mstaafu mtarajiwa kuweza kutaf-siri malengo ya kustaafu na rasilimali alizonazo katika fedha halisi, na kiasi cha fedha kitakachohitajika kwa kazi inayohusi-ka.

Hatua ya Nne: Utekelezaji wa Mpango

Ni vizuri mpango ukatekelezwa waka-ti mfanyakazi angali kazini, kwa sababu mwanzo wowote una ugumu wake. Mwan-zo unahitaji kujituma na uwajibikaji wa hali ya juu. Lazima kuwepo na ufuatiliaji na tathmini ya mara kwa mara ili kubaini ma-badiliko na marekebisho yanayohitajika. Ni muhimu kukumbuka kuwa uwekezaji wow-ote unaambatana na majanga. Kwa hivyo, upembuzi yakinifu ni hatua muhimu sana kumwezesha mstaafu kujua ni nini, wakati gani, kwa kima gani, na kiasi gani cha ku-wekeza hasa kwa vile hakuna njia maal-umu katika suala hili. Mstaafu akifanya uwekezaji kwa makosa, anaweza kukum-bana na hali ngumu ya maisha na kuchukia maisha ya kustaafu mapema.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

84

Maandalizi ya Kustaafu Hasa

Kabla ya kustaafu ni vizuri wafanyakazi wakafanya matayarisho ya kustaafu katika mambo yafuatayo:

i) Akiba na Kuwekeza

Jambo la msingi la kuangalia wakati mfan-yakazi anajitayarisha kustaafu ni kuhakiki-sha kuwa ana kipato cha kujitosheleza mara tu atakapoanza kuishi bila ya msha-hara wa kila mwisho wa mwezi. Akiba hii ni vizuri kududulizwa wakati mfanyakazi yupo kazini.

ii) Nyumba

Makaazi ni kitu cha lazima katika maisha ya binadamu. Ni jambo muhimu kwa mfan-yakazi kuhakisha ana nyumba yake ya kui-shi mwenyewe ikiwa na gharama ya chini ya matunzo, kabla ya kustaafu. Ni hatari mstaafu kujenga makaazi kwa fedha za kinua mgongo au mafao ya kinua mgongo na pensheni.

iii) Matibabu

Suala la matibabu ya mstaafu pamoja na familia yake ni muhimu. Hivyo mfanyakazi kujipanga vizuri ili ahakikishe suala la mat-ibabu yake na familia yake hayampi shida wakati wa kustaafu. Hapa ndipo matumizi ya fedha za mafao ya mstaafu yanapohita-jika.

iv) Elimu

Kustaafu hakumvui mstaafu majukumu muhimu kama vile elimu, chakula na nguo kwa ajili ya familia yake. Hivyo mfanyakazi kabla ya kustaafu atalazimika kuhakikisha mahitaji haya muhimu kwa maisha ya bin-adamu yanapatikana bila ya shida. Kustaa-fu ni pigo kwa maisha ya mtu aliyekuwa mfanyakazi na ambaye kwa bahati mbaya hakujitayarisha kwa maisha ya ustaafu. Maisha ya kustaafu husababisha mabadi-liko makubwa katika maisha, husababisha kupungukiwa na hadhi/heshima ambayo mfanyakazi alikuwa nayo. Hupungukiwa na

UHAMASISHAJI

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

85

kipato cha kawaida alichokuwa nacho na baadhi ya wakati mwingine hata uhusiano wake na jamii kuathirika . Hali hii huathiri mfumo mzima wa maisha ya mstaafu na wakati mwingine humuacha akiwa mkiwa na mnyonge.

Kutokana na hali hiyo, ni muhimu kabisa kwa wafanyakazi kujiandaa kustaafu kabla ya hata kufikia umri wa kustaafu. Maandal-izi mazuri ya kustaafu humwezesha mstaa-fu kuanza maisha ya kustaafu bila ya khofu kwa vile tayari alikwisha kujipanga kuingia katika maisha mapya ya kustaafu.

Tafiti nyingi duniani hasa katika ulimwengu wa tatu zinaonesha kuwa wastaafu wengi huishi maisha magumu na hata kufikia kuchanganyikiwa kwa vile hawakuwa na maandalizi ya kustaafu kazi. Ni asilimia ndogo sana ya wastaafu wamegundulika kuishi maisha ya kawaida na kufurahia mai-sha yao ya kustaafu. Bado swali linabaki ‘ni lini mfanyakazi anawajibika kufanya maan-dalizi ya kustaafu’? Baadhi ya wataalamu wanaelekeza kuwa siku ya mwanzo ya ajira kwa mfanyakazi, ndio iwe siku ya mwanzo ya kufanya maandalizi ya kustaafu. Wafan-yakazi wote wazingatie kwa dhati kwamba ‘ Ustaafu si janga au adhabu bali ni faraja.’

Utandawazi

Utandawazi ni mchakato unayohusiana na muongezeko wa muingiliano wa kimataifa hasa katika shughuli za kiuchumi. Baadhi ya wasomi wanaamini kuwa chanzo cha utandawazi kimeanzia wakati tulionao in-gawa wengine wanafikiria kuwa mchakato wa utandawazi umeanzia hata kabla ya sa-fari za uvumbuzi za watu wa Ulaya. Kwa vy-ovyote vile dhana hii ya utandawazi imeanza kusikika na kutumika kwa wingi zaidi kwe-nye miaka ya themanini na tisini, wakati hatua za kuunganisha shughuli za kiuchu-mi ulimwenguni, hasa masuala ya biashara za kimataifa, zilipozidi kushika kasi na kuu-fanya ulimwengu kuwa kijiji.

Taathira za Utandawazi kwa Wafanyakazi na Vyama vya Wafanyakazi

Utandawazi unasababisha mashinda-no ya biashara katika soko la dunia. Ni mashindano ya nchi zenye uwezo mkubwa kiuchumi na nchi zisizo na uwezo. Katika hali hii nchi zinazoendelea huathirika zai-di na hivyo kushindwa kushindana katika soko la biashara la dunia. Nchi tajiri hu-tumia teknolojia za kisasa katika uzalishaji wa bidhaa. Matokeo yake bidhaa zinazozal-ishwa zinakuwa na ubora zaidi na kwa hivyo kuweza kudhibiti soko, na wakati huo huo ni wafanyakazi wachache ndio wanaohita-jika katika uzalishaji kwa sababu sehemu kubwa ya uzalishaji hufanyika kwa kutumia mashine. Aidha katika hali hii mkazo hu-wekwa kwenye biashara huria na ushiriki wa mashirika binafsi katika kukuza uchu-mi. Kwa ujumla utandawazi umeathiri ul-imwengu wa kazi na hasa wafanyakazi kwa sababu:

• Wafanyakazi wamelazimika kuishi ka-tika dimbwi la umasikini.

• Wafanyakazi wamepoteza ajira.

• Kazi za heshima zimekuwa ngumu ku-patikana.

Tafiti nyingi duniani hasa katika ulimwengu wa tatu

zinaonesha kuwa wastaafu wengi kuishi

maisha magumu na hata kufikia

kuchanganyikiwa kwa vile hawakuwa

na maandalizi ya kustaafu kazi

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

86

• Vyama vya wafanyakazi vimeendelea kupoteza wanachama.

• Vyama vya wafanyakazi vimekosa mbi-nu bora za kushawishi wafanyakazi ku-jiunga na vyama.

• Vyama vya wafanyakazi vimeshawishika kwenda kwenye sekta isiyo rasmi, la-kini Shirika la Kazi Duniani halijawapa jawabu muafaka.

Kupambana na Utandawazi

Utandawazi ni mchakato wa dunia na hivyo si rahisi kuukwepa lakini la muhimu kwa vyama vya wafanyakazi ni kutafuta njia ya kukabiliana nao. Kwa hivyo vyama vya wa-fanyakazi vitakuwa na wajibu wa:

• Kuhakikisha kuwa serikali za nchi zao zinaingiza kifungu cha haki za wafan-yakazi katika katiba za nchi zao.

• Kuhakikisha kuwa serikali za nchi zao zinaridhia Mikataba Muhimu ya Kazi ya Kimataifa.

• Kuhakikisha kuwa vyama vya wafan-yakazi vinafanya shughuli zake za kuhu-dumia wanachama wake kwa umakini na weledi wa hali ya juu.

• Kuhakikisha kuwa vyama vya wafan-yakazi vinabuni mbinu bora za kush-awishi wafanyakazi kujiunga navyo.

• Kuhakikisha kuwa vyama vya wafan-yakazi vinaungwa mkono kwa wingi na wafanyakazi wenyewe na jamii kwa ujumla.

Changamoto Za Vyama vya Wafanyakazi Katika Kupambana na Utandawazi

Vyama vya wafanyakazi vimelazimika ku-fanya kazi katika mazingira yaliyobadilika kutokana na utandawazi na biashara huria duniani. Pamoja na mabadiliko hayo wajibu wa vyama vya wafanyakazi uko pale pale. Bado vinadhima ya kusaidia kuleta maen-deleo ya uchumi na jamii na kwa hivyo

kuhimiza uzalishaji wa tija katika sehemu za kazi. Vyama vya wafanyakazi kwa hivyo, lazima vielewe kuwa kutokana na mabadi-liko ya sasa ya uchumi, jamii, na siasa vinal-azimika kufanya kazi na sekta binafsi kwa kiasi kikubwa ambayo wakati wote inaan-galia faida na kufanya kazi kwa ufanisi na tija. Hali hii ya utandawazi na biashara hu-ria, imesababisha soko la ajira kupanuka na kusababisha mashindano katika kuwania soko na matokeo yake mfanyakazi mwenye sifa ndiye anayepata ajira na wakati mwing-ine waajiri huamua kuajiri watu wa familia ili kupunguza gharama za uendeshaji. Hali hii, pamoja na ile ya kuanzisha kazi za shu-ruti, kunazorotesha shughuli za vyama vya wafanyakazi na pia kusababisha kupoteza wanachama na hatimaye kupoteza nguvu za umoja, siasa, na uchumi. Hali hii vile vile inatoa fursa kwa waajiri kupata mwanya wa kuvunja haki za wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi.

Kukabiliana na Changamoto

Ili kuepukana na changamoto hizi vyama vya wafanyakazi vijitahidi kutekeleza yafuatayo:

• Vyama vya wafanyakazi vishawishi kwa vitendo serikali na waajiri kwamba vina wajibu mkubwa katika kuleta maende-leo.

• kushindikiza serikali na waajiri kutekeleza sheria za kazi na kuhakiki-sha utekelezaji wa ustawi wa jamii.

• Kusisitiza ushirikishwaji wa wafanyaka-zi.

• Kushughulikiwa suala la virusi vya ukimwi na ukimwi ambalo hupoteza maisha ya wafanyakazi wengi.

• Kuwapatia viongozi, wanachama na vi-jana wa vyama vya wafanyakazi mafun-zo ya maarifa na ujuzi wa kazi.

• Vyama vya wafanyakazi kwa kushiriki-ana vifanye kazi na vyama vingine vya kijamii.

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

87

Utamaduni na mambo yaliyozoeleka ni tabu kubadilika kwa haraka. Lakini kubadilika ni lazima. Hivyo elimu mpya ya vyama vya wa-fanyakazi lazima izingatie mada zifuatazo:

• Demokrasia na Utawala Bora.

• Elimu ya Ujasiriamali.

• Teknolojia ya Habari na mafunzo ya Teknolojia.

• Vyama vya wafanyakazi na Biashara ya Kimataifa.

• Vyama vya wafanyakazi na Siasa.

• Mikataba ya Shirika la Kazi la Kimataifa.

• Utunzaji wa Mazingira.

• Vyama vya wafanyakazi na Wafanyakazi Vijana.

Wajibu wa asili wa vyama vya wafanyaka-zi wa kudai mishahara bora na hali bora za kazi, kulinda haki za wafanyakazi, na kutekeleza matakwa ya wafanyakazi, lazi-ma uendelee kutekelezwa kwa nguvu zote, lakini uzito wa changamoto mpya za vyama vya wafanyakazi unalazimisha vyama vya wafanyakazi kujikita kwenye shughuli mpya tofauti na zile za asili. Miongoni mwa shu-ghuli hizo ni:

• Kuasisi na kuendesha vyama vya kuwe-ka na kukopa kwa ajili ya wanachama waliopo, wale walioondolewa na wale waliopunguzwa kazi kutokana na mab-adiliko ya teknolojia.

• Kuchunguza uwezekano wa kuanzisha benki ya wafanyakazi ambayo itawahu-dumia wafanyakazi wakiwa kazini na hata watakapo staafu.

• Kuunga mkono mipango ya kuanzisha bima kwa ajili ya wafanyakazi itayoshu-ghulikia pamoja na mambo mengine bima ya afya, elimu na shughuli ny-ingine za kijamii.

• Hizi ni changamoto mpya za vyama vya wafanyakazi, ambazo zinasababisha vyama kubadilika kutoka kutekeleza

shughuli za asili na kupanua maeneo mapya ya kufanyia kazi. Bila ya vyama kujibadili havitaweza kufanya kazi kati-ka mazingira haya mapya ya utandawa-zi.

Mpango Mkakati

Tunaishi katika ulimwengu wenye rasili-mali ndogo ambapo mahitaji ya binadamu hayana kikomo. Pamoja na rasilimali ndo-go, watu wangependa kujua jinsi rasilimali hizo za nchi au taasisi zinavyotumika. Hivyo hoja ya kuwa na Mpango Mkakati kwa ajili ya taasisi inajitokeza ili kujua rasilimali hizo zinatumikaje;na hatimaye iweze kujulikana nani ana dhamana gani ili iwe rahisi ku-weza kuwaajibisha wale wote walioshindwa kutimiza wajibu wao katika matumizi bora ya rasilimali hizo. Mpango Mkakati kwa hivyo, ni ramani au njia inayoonesha taasisi jinsi inavyofikia maendeleo yake. Ni ramani inayoonesha mwenendo wa ukataji shauri na mpango mzima wa maendeleo ya taasisi inayohusika. Mpango Mkakati unahakiki-sha uhai, ukuaji, na maendeleo ya taasisi. Ili Mpango Mkakati wa taasisi uweze kuan-daliwa matayarisho yafuatayo yanahitajika yafanywe kwanza:

1. Uchambuzi wa Taasisi

Uchambuzi kisayansi wa taasisi unahita-jika wenye kuonesha/kukadiria uwezo wa taasisi (inayoweza kufanya na isichoweza kufanya). Uchambuzi huu utaweka mis-ingi ya ukataji shauri kuhusu vipaumbele vya taasisi vya kuwekwa katika Mpango Mkakati. Katika uchambuzi huu, udhaifu wa taasisi, nguvu, fursa, na tahadhari vina-bainishwa wazi baada ya kufanyiwa ucham-buzi. Taarifa hizi zilizofanyiwa uchambuzi wa kina zitasaidia kuweka dira ya kufikia maendeleo ya taasisi.

2. Vipaumbele vya Taasisi

Katika Mpango Mkakati wa taasisi, lazima vipaumbele vioneshwe ikiwa ni pamoja na matarajio, dira ya njia za kufikia matarajio hayo.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

88

3. Ufuatiliaji na Tathmini

Ili kupima mafanikio yatokanayo na shu-ghuli zilizopangwa katika Mpango Mkakati, lazima utaratibu uwekwe wa ufuatiliaji na hatimaye tathmini ifanywe. Ili shughuli ya ufuatiliaji ifanywe kwa ufanisi, lazima vy-ombo vya ufuatiliaji viandaliwe. Tathmini nayo hufanywa baada ya kuwekwa mpango mahsusi wa tathmini. Tathmini hufanywa katika kila hatua ya utekelezaji wa Mpango Mkakati.

4. Utayarishaji wa Bangokitita

Kwa urahisi wa ufuatiliaji na utekelezaji wa Mpango Mkakati, inashauriwa kwamba bangokitita liandaliwe linaloonesha Mpan-go Mkakati pamoja na utekelezaji wake na bajeti yake. Aidha bangokitita litabainisha wazi muda wa utekelezaji wa shughuli, walengwa, na pia wahusika wakuu wa usimamizi na utekelezaji wa shughuli zi-lizoainishwa.

5. Maandalizi ya Bajeti

Ili Mpango Mkakati utekelezeke kuna haja ya kutayarisha bajeti inayoonesha gharama za shughuli zote zinazotarajiwa kutekele-zwa katika kipindi kizima cha Mpango Mkakati. Gharama hizo zinaweza kuonesh-wa katika bangokitita kwa urahisi wa kufa-hamu na ufuatiliaji.

Vyama vya Wafanyakazi na Uchumi Usio Rasmi

Maana ya Uchumi Usio Rasmi

Uchumi usio rasmi ni shughuli za uzalishaji mali ama utoaji huduma nje ya utaratibu wa kawaida wa serikali, makampuni na vi-wanda. Ni uchumi uliosahaulika kwa muda mrefu hadi katika miaka ya 1970, ambapo mchango wake katika pato la taifa ulitam-bulika na serikali za nchi mbali mbali hasa katika ulimwengu wa tatu.

Uchumi usio rasmi ni muhimu sana. Ukip-ewa misaada unaweza ukatoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa wananchi wengi. Inakadiriwa

kuwa kati ya asilimia 50 na 60 ya nguvuka-zi mijini imeajiriwa katika sekta hii. Aidha inakadiriwa kuwa shughuli za sekta hii zin-achangia asilimia 25 hadi 35 ya mapato ya watu duniani. Kuanzia miaka ya 1980 sekta hii imepanuka sana. Hii imetokana na ma-tatizo ya uchumi ulimwenguni ambayo ya-melazimisha nchi nyingi kubadili mifumo yao ya uchumi wao.

Shughuli na Umuhimu wa Uchumi usio Rasmi

Sekta hii ina shughuli nyingi za uzalishaji mali na utoaji wa huduma hasa katika ul-imwengu wa tatu. Inajumuisha uzalishaji viwandani, uchimbaji wa mawe, ujenzi wa nyumba na majengo mengine, biashara ndogo ndogo na usafirishaji. Utafiti katika sekta hii umeonesha kwamba duniani ka-ribu asilimia 57 ya ajira yote katika sekta hii inatokana na shughuli za viwanda, asi-liamia 33 ya ajira inatokana na shughuli za kibishara na mikahawa, asilimia 10 ni shu-ghuli za utoaji wa huduma na utengenezaji wa vifaa.

Umuhimu wa sekta hii umezidi kuonekana wakati uchumi wa nchi maskini ulipoanza kuzorota. Wakati huo nchi hizo zililazimi-ka kutekeleza masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa ili zipate mikopo na misaada kutoka vyombo hivyo. Masharti hayo yalisababisha wafanyakazi wengi kupunguzwa kazini. Hawa walilazi-mika kutafuta njia za kujiajiri wenyewe ili waweze kuendelea kuishi na kupata ma-hitaji ya lazima.

Aidha sekta hii hutoa bidhaa na huduma kwa walaji. Katika hali ya uchumi duni, uko-sefu wa kazi na ukosefu wa njia za uhakika za mapato, sekta hii huwa chanzo cha ku-ingiza mapato kwa watu wengi. Aidha sekta hii hutoa kazi za muda wakati wa majira yasiyokuwa na kazi nyingi. Hivyo sekta hii husaidia kuongeza mapato ya watu wasio na mapato ya uhakika. Zaidi ya hayo, uchu-mi usio rasmi huimarisha uchumi kwa ku-unganisha sekta mbali mbali za uchumi wa nchi inayohusika. Wakati wa kufanya kazi

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

89

katika sekta hii, raia wanapata uzoefu wa shughuli mbali mbali. Hivyo nchi zinazoen-delea hujipatia raia wenye ujuzi.

Baadhi ya watu, sekta hii wameipa jina la “Sekta ya Wanyonge, inayoongozwa na wanyonge, na kwa ajili ya wanyonge”. Im-esaidia sana kutoa bidhaa na hata huduma kwa watu wenye kipato cha chini. Hii ni kwa sababu gharama zake ni za chini ambazo watu wengi wanaweza kuzimudu. Sekta hii hutoa mchango muhimu katika mapato ya kaya. Hivyo imesaidia kwa kiasi kikub-wa kupunguza umasikini uliokithiri kwa kuongeza mapato ya kaya.

Matatizo ya Uchumi Usio Rasmi

Kwa bahati mbaya, baadhi ya taasisi za serikali na hata viongozi wa nchi kad-haa hawatambui umuhimu wa sekta hii. Hivyo wakati wote sekta hii imekumbana na vikwazo vinavyosababisha isiendelee. Vikwazo hivyo ni pamoja na sheria za nchi. Sheria za nchi nyingine hazitambui kuwepo kwa sekta hii na kwa hivyo hazielekezi jinsi sekta hii inavyoweza kufanya shughuli zake na jinsi inavyoweza kuendelezwa. Tatizo jengine ni kuwa na mitaji midogo. Hii ina-tokana na ukweli kwamba ni malimbikizo ya mtu binafsi, mikopo kutoka kwa jamaa na hata marafiki. Kwa kawaida vyombo vya fedha katika nchi nyingi havina mipa-ngo mahususi ya kurahisisha mikopo kwa ajili ya kuendeshea shughuli mbali mbali za sekta hii. Pale ambapo vyombo hivi vinaonesha nia kutaka kusaidia, hatua za kupata mikopo hiyo ni ndefu, zenye ku-chosha na zenye usumbufu mwingi. Mara nyingi mtu anayetaka mikopo hiyo hukata tamaa na kuacha kufuatilia hata kabla ya kufika nusu ya utaratibu mzima.

Tatizo jengine ni ukosefu wa sehemu rasmi za kudumu na uhakika kwa kuendeshea shughuli mbali mbali. Mara nyingi wakuu wa miji huwasumbua na hata kuwabomolea sehemu za majengo wanamoendeshea bi-ashara zao kwa visingizio mbali mbali kama vile kusafisha miji . Hivyo sekta hii imekuwa ni shabaha ya unyanyasaji au chanzo cha rushwa na hongo kwa viongozi wabovu.

Aidha soko la kuuzia bidhaa zitokanazo na uchumi usio rasmi halimilikiwi na wa-naoendesha shughuli za sekta hii. Hali hii husababisha ukosefu wa soko la uhakika. Mazao ya viwanda ya uchumi usio rasmi mara nyingi hayana ubora wa viwango vya kimataifa. Hii inatokana na waendeshaji wa sekta hii kukosa uwezo wa kupata zana bora, ufundi unaohitajika na malighafi sa-hihi.

Kikwazo kikubwa zaidi kwa uchumi usio rasmi ni kutokutambuliwa kisheria. Seri-kali nyingi haziwapi wahusika uwezo wa kisheria wa kufanya shughuli zao.

Tatizo jengine linahusu watu na taasisi bi-nafsi zinazotoa misaada mbali mbali kue-ndeleza uchumi usio rasmi. Imedhihirika kuwa misaada yao haina mpangilio mahu-susi. Mara kadhaa misaada hutolewa kwa miradi isiyo na mwelekeo. Hii ni kwa saba-bu wafadhili wengi hutoa misaada siyo kwa sababu ya kusaidia jamii bali kwa kutafuta sifa tu. Sababu hizi na nyingi nyinginezo zi-naonyesha umuhimu wa kuwa na chombo madhubuti cha kuongoza, kusaidia na ku-unganisha shughuli mbali mbali za sekta hii.

Kusaidia Uchumi Usio Rasmi

Umuhimu wa sekta isiyo rasmi utadumu kwa sababu uchumi ulio rasmi umeshind-wa kutoa kazi, bidhaa na huduma kwa watu wanaoongezeka siku hadi siku katika nchi zinazoendelea. Itachukua muda mrefu kwa serikali za nchi hizi kupata uwezo wa kiu-fundi na wa kifedha wa kuziwezesha kutoa mahitaji yake yote. Hivyo bado umuhimu upo wa serikali zetu kusaidia sekta hii kwa hali zote.

Serikali zina wajibu wa kuhakikisha kuwa uchumi usio rasmi unafanya shughuli zake bila ya vipingamizi. Ni muhimu kutunga sheria zinazotambua kuweko kwa sekta hii na kuilinda. Ni muhimu pia kuunda chom-bo maalumu kitakachokuwa na wajibu wa kubuni mipango maalumu ambayo itasaid-ia ukuaji wa sekta hii; kuitafutia mitaji ya fedha na vifaa kwa ajili ya kuendeshea shu-

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

90

ghuli mbali mbali. Aidha serikali zingeten-ga maeneo maalumu ambapo wanaofanya shughuli za sekta hii wanaweza kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa.

Vyama vya wafanyakazi vinapaswa kujihu-sisha na sekta hii muhimu.Vinawajibika kuhakikisha kwamba wanachama wake wanaokosa kazi katika uchumi ulio rasmi, wanaendelea kufanya kazi katika sekta ya uchumi usio rasmi. Kwa kufanya hivyo, vyama vya wafanyakazi vitaweza kuwahu-dumia wanachama wake na kuhakikisha kuwa wanaendelea kuishi. Katika hali halisi iliyopo hivi sasa sekta iliyo rasmi inasinyaa taratibu. Badala yake uchumi usio rasmi unazidi kukua. Hivyo, vyama vya wafan-yakazi havina budi kujiingiza katika uchu-mi usio rasmi ili kuusaidia na kushawishi wafanyakazi wa sekta hii kujiunga na vy-ama vya wafanyakazi. Katika nafasi hiyo, vitahakikisha kuwa wafanyakazi wa sekta hii wanafanyiwa haki na wanafanya kazi katika mazingira yanayokubalika kiafya na kiusalama kwa mujibu wa sheria za nchi.

Vyama vya wafanyakazi vina wajibu pia wa kushawishi serikali kutunga sheria zitaka-zosaidia kukua na kushamiri kwa uchumi usio rasmi. Vinapaswa kushirikiana na vy-ama visivyokuwa vya serikali kwa nia ya ku-saidia uchumi usio rasmi kupata mikopo, malighafi, na soko la kuuzia bidhaa zake. Mfano mzuri wa kuigwa ni ule wa chama cha wafanyakazi wa misitu na mbao cha Ghana. Chama hicho kimefanikiwa ku-waunganisha watengenezaji wa samani na wachomaji wa mkaa kwa nia ya kukuza uchumi usio rasmi. Aidha kimewasaidia wafanyakazi wa sekta hizi kuwa na chama madhubuti.

Wafanyakazi wa uchumi usio rasmi wa-napaswa kuelimishwa kuhusu umuhimu wa umoja. Wahenga walisema, “ Umoja ni nguvu, Utengano ni Udhaifu.” Hivyo wana-paswa kufahamu faida za kujiunga pamoja kama vile kujiendeleza na kutatua matatizo yao ya kikazi.

Ukinzani kati ya uchumi usio rasmi na uchu-mi ulio rasmi upo kwa muda mrefu. Msingi wake ni mishahara na hali bora za kazi. Wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi mara nyingi wamekubali kupokea mishahara mi-dogo na kufanya kazi katika mazingira duni . Hali hii imedhoofisha juhudi za wafan-yakazi wenzao katika uchumi ulio rasmi ya kuboresha mishahara na mazingira ya kazi. Kwa hiyo vyama vya wafanyakazi vinawajibi-ka kuwasaidia wafanyakazi katika uchumi usio rasmi ili waanzishe umoja wao. Kwa kutumia umoja wao na kwa kushirikiana na vyama vya wafanayakazi, mishahara na mazingira ya kazi yatahuishwa kote nchini.

Mwisho, waendeshaji wa uchumi usio ras-mi wanawajibika kuhakikisha kuwa sekta hii inakuwa ya manufaa kwao na kwa nchi zao. Wale wanaoajiri watu wengine, hata kama ni jamaa zao, wanapaswa kuwa-tendea haki kwa kuwalipa malipo halali na marupurupu mengine. Wahakikishe pia kuwa waajiriwa wao wanafanya kazi katika mazingira yanayofaa kwa afya na usalama wao. Upo umuhimu wa waendeshaji wa sekta hii kujiunga pamoja na kuanzisha chama chao. Hii ingesaidia kuboresha na kuendeleza uchumi usio rasmi.

Mikakati ya Kuunganisha Vyama Vya Wafanyakazi

Kwa ujumla kuunganisha vyama kunaweza kutekelezwa kwa njia mbili kutegemeana na makubaliano ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi husika. Vyama vya wafanyaka-zi viwili au zaidi vinaweza kuungana kuwa chama kimoja cha wafanyakazi. Katika hali hii wanachama kutoka vyama vyote vilivy-oungana wanakuwa kitu kimoja pamoja na kuchanganya mali na fedha za vyama vyote vilivyounganishwa. Matokeo ya muungan-iko huu ni kuwa na chama kimoja kinacho-tawaliwa na kanuni na taratibu mpya to-fauti kabisa na zile za vyama vilivyoungana. Baada ya utekelezaji wa muunganisho huu wa vyama viwili au zaidi, vyama vilivyoun-ganishwa vinasita kufanya shughuli zake zilizopangwa kabla.

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

91

Aidha vyama vya wafanyakazi viwili vilivy-okubaliana kutekeleza muungano vinaweza kufanya hivyo kwa chama kimoja kuhamshia wanachama wake, mali zake, na fedha zake kwa chama kingine, kama viongozi wa vy-ama hivo walivyokubaliana katika mkataba wao wa makubaliano. Baada ya utekelezaji wa muungano huo, chama kilichohamishia mambo yake kwa chama kingine kinakufa na chama kilichopokea kinabaki kuende-lea na shughuli zake na kinabaki kuwa na nguvu za kisheria kama awali.

Wakati muunganiko huu wa pili wa vyama vya wafanyakazi hautoi fursa ya kujibadili kwa chama kikuu kilichounganishwa kwa kupokea kutoka chama kingine, muungan-iko wa kwanza unatoa nafasi ya kutosha ya mabadiliko kwa vile kinaanza upya pamoja na ukweli kwamba nafasi hiyo ya mabadi-liko si rahisi kutekelezeka kutokana na hali halisi inayojikuta. Mara nyingi vyama vilivyoungana kwa kutekeleza muungano kwa namna ya kwanza hapo juu hujikuta vinaingia katika matatizo ya muda mrefu ya kiutendaji na fedha mara tu vinapotekeleza muungano wao.

Haja ya Vyama vya Wafanyakazi Kuungana

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mida-halo kuhusu umuhimu wa vyama vya wafan-yakazi katika hali ya sasa hivi ya utandawazi ambayo imeleta changamoto kwa ulim-wengu wa kazi na vyama vya wafanyakazi. Midahalo hiyo imehusisha pia mikakati ya kuhusisha vyama vya wafanyakazi. Hali hii imesababishwa na ukweli kwamba vyama vya wafanyakazi vinakabiliwa na changa-moto kadhaa ambazo zinaviza maendeleo yao. Changamoto zenyewe ni pamoja na zile zinazohusiana na:

• Mageuzi ya kiuchumi ulimwenguni.

• Maendeleo ya sayansi na teknolojia.

• Mabadiliko ya ghafla na yasiyotegeme-wa ya mazingira.

• Mabadiliko ya mwenendo wa soko la ajira.

Matatizo haya yanafanya mambo yawe magumu zaidi hasa katika ulimwengu wa kazi pale uchumi wa ulimwengu unap-opata misukosuko bila ya kupata majibu ya haraka ya kutokana na hali hiyo. Katika hali hii kunaonekana shida kubwa ya ajira miongoni mwa vijana, watu kukimbia nchi zao na kujitafutia mahala penye ajira yenye tija zaidi, mizozo ya kijamii, maambukizi ya ukimwi miongoni mwa wananchi, na hata ukiukwaji wa hali ya juu wa haki za binad-amu.

Wakati huo huo vyama vya wafanyakazi vinajikuta vinapambana na changamoto kadha zikiwemo kuporomoka kwa idadi ya wanachama, kupungua kwa uwanja na uwezo wa kufanya majadiliano ya pamoja. Katika nchi nyingi wafanyakazi wamejikuta bila ya mtetezi na sheria za kuwatetea pia zimedhoofishwa. Tatizo lingine linalosaidia kudhoofisha vyama vya wafanyakazi ni ku-fanya kazi bila ya mashirikiano kutokana na udhaifu wa viongozi wake, ukosefu wa fedha za kutosha za kuendeshea vyama, udhaifu wa muundo wa vyama vyenyewe, ukosefu wa demokrasia katika vyama, baa-dhi ya viongozi kuhubiri kuvigawa vyama kutokana na sababu zisizo za msingi na wengine kuendesha vyama kibinafsi na ku-vifanya vitega uchumi vyao.

Ni kutokana na hali hii ya kupoteza wana-chama na nguvu za umoja wa wafanyakazi ndio umoja wa wafanyakazi ulimwengu umeanzisha mjadala kuhusu jinsi gani vy-ama vya wafanyakazi vinaweza kusimama na kuwa na nguvu za kuweza kutekeleza majukumu yake kwa weledi. Vyama vya wafanyakazi vimeona iko haja ya kujipanga upya, kutafuta mbinu mpya, mikakati mi-pya, na kuanzisha mipango mipya itakayo-saidia vyama kuonekana bado vinahitajika. Matokeo ya juhudi zote hizi zimalizie kwe-nye kuonekana kwamba umoja ni nguzo muhimu katika ulimwengu wa kazi na ndio utakaosaidia katika kuendeleza shughuli za umma kitaifa na kimataifa. Katika hali

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

92

hii vyama vya wafanyakazi ili kwenda sam-bamba na mabadiliko ya ulimwengu ya uchumi na siasa vimeamua kukubaliana na fikra ya kuunganisha nguvu zao kwa kuun-ganisha vyama yao.

Kwa Nini Vyama Viungane

Vyama vya wafanyakazi vinakumbana na changamoto za ndani na nje zinazolazi-misha vyama kuanzisha miundo mipya ya kujiendesha ikiwemo kuunganisha nguvu zao kwa kuungana. Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwa nini vyama vinaungana:-

i) Kupanua Upeo wa Kupata Wanachama

Mifano mingi ya muunganiko wa vyama ina-tokana na kuporomoka kwa idadi ya wana-chama wa walau chama kimoja kinachoun-gana na kingine au vingine. Muunganiko wa vyama viwili au zaidi unaweza kusababisha ongezeko la thamani ya wanachama ku-liko vyama vile vingefanya kazi mbali mbali bila ya kuungana. Kwa kuungana vyama vinaweza kupata uwanja mpana zaidi wa kupata wanachama, viongozi bora, elimu na uwezo zaidi. Kuporomoka kwa idadi ya wanachama katika chama kumelazimisha kutumika kwa mbinu ya kuunganisha vy-ama ili kuendeleza idadi ya wanachama na ukubwa wa chama.

ii) Kupunguza Gharama za Uendeshaji

Vyama vingi vimepoteza wanachama kuto-kana na mabadiliko ya ajira. Hivyo vyama vinakosa uwezo wa kuendeleza mazun-gumzo ya pamoja na mwajiri. Hali hii im-esababisha vyama kuungana ili viweze ku-punguza gharama za uendeshaji wa vyama na kupata nafasi ya kugharimia kwa pamo-ja mazungumzo ya pamoja. Aidha vyama vinaungana ili vipate uwezo wa kutoa hu-duma bora kwa wanachama wake na kwa gharama nafuu.

iii) Kubadilisha Eneo la Sekta

Vyama vya wafanyakazi vinavyoungana ku-toka sekta tofauti vinasaidia kutuliza hali na kupunguza hali mbaya ya mapato. Iwapo mapato ya vyama kutoka sekta tofauti,

yanawekwa pamoja yatakuwa na usalama zaidi kuliko kuwa katika mifuko tofauti.

iv) Kuhakikisha Nguvu ya Kisiasa

Vyama vya wafanyakazi huungana kwa lengo la kuongeza nguvu ya kisiasa, uwezo wa kusema na kusikika, na kushiriki katika masuala ya kitaifa na kimataifa. Kuongeze-ka kwa wanachama kunategemea vile vile na chama kuwa na nguvu kisiasa.

v) Kuunganisha Vyama Kama Mkakati

Vyama vinaungana kwa kuwa na hoja ya kutawanya gharama za:-

• Kuanzisha huduma mpya kwa wanacha-ma.

• Kufanya utafiti katika maeneo mapya ya sera.

• Kupata nafasi ya kuingia katika maeneo mapya ya chanzo cha kupata wanacha-ma.

Mkakati huu unasaidia vyama vilivyounga-na kuweza kuhimili mabadiliko ya nje hasa katika masuala ya kanuni na taratibu za mazungumzo ya pamoja.

vi) Kupunguza Hali ya Mashindano na Uhasama baina ya Vyama

Kuunganisha vyama kunaweza kusaidia kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa vyama na wanachama hali itakayo-saidia kuwafikia wanachama katika mae-neo ya aina moja. Kuchukua wanachama waliokwisha andaliwa ni rahisi zaidi kuliko kuandaa wanachama wapya. Vyama maha-la pamoja vinaunganisha nguvu za pamoja hali inayosaidia kupunguza gharama, kuon-doa hali ya kufanya vitu vya aina moja, hali itakayosaidia kuongeza mapato ya chama.

Kurahisisha Mkakati wa Kuunganisha Vyama Vya Wafanyakazi

Kuna njia kadhaa za kufikia mkakati wa kuunganisha vyama vya wafanyakazi

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

93

kutegemeana na sababu za muungano huo. Mara nyingi muungano wa vyama hu-fikiwa hata bila ya mpangilio wa awali; am-bapo vyama husika huchukua njia tofauti za kufikia kwenye uamuzi wa kuunganisha vyama. Wanachama wa vyama husika wa-naweza kuwa na matumaini tofauti ya muungano wao lakini la muhimu ni kuwa wahusika wote lazima wakubaliane katika mambo muhimu yahusuyo muungano wao. Kila chama kinachohusika katika muun-gano wa vyama lazima kiandae ratiba na mkakati unaonesha wazi jinsi chama hicho kitakavyotoka na kuingia katika muungano wa vyama ulioandaliwa. Jinsi vyama husika katika muungano vilivyotumia wakati wa kutosha katika maandalizi ndivyo kunavy-okuwa na hakikisho la mafanikio ya muun-gano huo.

Mkakati wa kufikia muunganisho wa vyama viwili au zaidi wenye mafanikio unaweza kuchukua hatua zifuatazo:

A: Kufikia Uamuzi wa Kuunganisha Vyama

1. Kuelewa vyema malengo ya kuungani-sha vyama.

2. Kujenga misingi ya matokeo bora ya ku-unganisha vyama.

3. kuweka mpangilio bora.

4. kuhakikisha matokeo ya jamii, uchumi, na kuangalia masuala ya kisheria kuhu-su suala la kuunganisha vyama.

B: Kusafisha Chama

1. Kutayarisha timu itakayoshauri kuhusu kuunganisha vyama.

2. Kuhakikisha masuala ya sheria na kusafisha njia.

3. kufanya tathmini ya msingi.

4. kutayarisha misingi ya makubaliano ya kuunganisha vyama.

5. kutayarisha mpango wa kuingia kwenye mchakato wa kuunganisha vyama.

C: Kuandaa Mkakati

1. kutafuta wataalamu wa masuala ya ku-unganisha vyama.

2. kutumia mtu wa tatu kwa ajili ya mashauriano.

D: Kuchagua Chama/Vyama vya Kuungana navyo

1. Kuchagua chama/vyama bora vyenye eneo kubwa zaidi kutegemea malengo ya kutaka kuunganisha vyama.

2. kutayarisha mapatano ya awali.

3. Kutayarisha makubaliano ya siri.

E: Majadiliano1. Utekelezaji wa Makubaliano.

2. Kufanya majadiliano ya kina na kufanya marekebisho ya msingi.

3. Kuyaweka vizuri Makubaliano.

F: Kujitayarisha kwa Kuunganisha Vyama1. Kutayarisha nyaraka za sheria zihusuzo

masuala ya kuunganisha vyama.

2. Utekelezaji wa matakwa yote ya kuun-ganisha vyama.

3. kupata ridhaa ya mtu wa tatu.

G: Kuunganisha Vyama

1. Kuvunja vyama vinavyohitaji kuungana.

2. Kuitisha Mkutano Mkuu utakaozingatia kuunganisha vyama.

3. Hatua za kusajili chama kipya.

H: Mambo yanayojitokeza baada ya Kuun-ganisha Vyama

1. Kutayarisha mahitaji ya fidia (kama yapo) baada ya kuunganisha vyama.

2. Kutekeleza mpango wa kuunganisha shughuli za vyama vilivyoungana.

3. Kushughulikia masuala mengine yanay-ojitokeza baada ya kuunganishwa vy-ama.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

94

Hatua za Matayarisho ya Kuunganisha Vyama

Jambo muhimu linalohitajika katika kufan-ikisha mchakato wa kuunganisha vyama ni matayarisho kabambe. Chama kinachoun-ganishwa na kingine kitatarajia masuala kadhaa kutoka chama/vyama vinavyoun-gana nacho, hivyo kitalazimika kujitayari-sha kutoa taarifa/majibu ya kweli kuhusu masuala hayo. Matayarisho ya mchakato wa kuunganisha vyama lazima yaanzie na mkutano wa kuweka mikakati wa wana-chama wote wa vyama vyote vyenye nia ya kuunganisha vyama vyao. Itakuwa ni kazi ya timu hii kufanya mambo yafuatayo:

• Kuonesha malengo ya kiuchumi na ya kimfumo ya kuunganisha vyama.

• Kutayarisha Mpango wa Utekelezaji pamoja na Ratiba ya Utekelezaji wa ku-unganisha vyama.

• Kujielimisha kuhusu hali halisi ya vy-ama na hali ya uchumi.

• Kuangalia wahusika wengine wa suala la kuunganisha vyama.

• Kutambua vipingamizi vya kisheria na fedha kwendea kwenye kuunganisha vyama.

• Kutayarisha Hati ya Makubaliano.

• Mambo ya Kuonesha Katika Matayar-isho ya Kuunganisha Vyama.

A: Taarifa za Vyama:

1. Nyaraka za Kisheria.

• Chama/ vyama husika vipo kisheria?

Orodha ya viongozi wa chama/vyama husi-ka waliochaguliwa na vyombo husika vya vyama kwa mujibu wa katiba za vyama na sheria za nchi

Utekelezaji wa sheria

2. Kumbukumbu za vikao vya vyama.

• Kumbukumbu hizo zinaelezea chochote kuhusu uamuzi wa kuunganishwa vy-ama?

HATUA 7

HATUA 6

HATUA 5

HATUA 4

HATUA 3

HATUA 2

HATUA 1

MUUNGANIKO

MAS

UAL

A M

TAM

BUKA

YA

VYAM

A VY

A W

AFAN

YAKA

ZI

95

3. Orodha ya Nyaraka zinazobainisha shu-ghuli vyama inafanywa na taasisi ny-ingine ikiwa ni pamoja na mali, biashara na uwekezaji.

4. Orodha ya vyama vilivyojishirikisha na-vyo pamoja na wanachama.

B: Nyaraka za Vyama

1. Mipango Mkakati.

2. Taarifa za vyama za mwaka, miezi sita.

3. Matoleo ya vyama.

4. Taarifa za Tathmini zilizowahi kutekele-zwa.

C: Masuala ya Fedha na Kumbukumbu

1. Taarifa ya Mahesabu yaliyokaguliwa.

2. Mpango wa shughuli za Kazi.

3. Taarifa, tafiti zihusuzo msimamo wa fed-ha za chama/vyama.

4. Taarifa ya Mkaguzi wa Nje kwa Uongozi wa chama.

5. Maelezo ya karibuni yanayohusu fedha.

6. Marejesho yanayohusu malipo ya kodi pamoja na mawasiliano ya chama na chombo cha kodi.

7. Mikataba ya Mikopo na mambo mengine yahusianayo.

D: Mikataba, Makubaliano na Sera

1. Makubaliano ya chama, na maafisa wa chama na watumishi wa chama (ikiwa ni pamoja na taarifa isiyoandikwa kuhusu makubaliano yo yote).

2. Mikataba na makubaliano baina ya cha-ma na watoa huduma na wauzaji wa vi-faa.

3. Nyaraka kuhusu uwekezaji wa chama na mali za chama.

4. Maelezo kuhusu uwekezaji wa pamoja wa chama na taasisi nyingine.

E: Masuala ya Watumishi

1. Makubaliano ya Uajiri.

2. Mpango wa Mafao ya Watumishi na makubaliano.

3. Mikopo ya Watumishi.

4. Sera za Utumishi na miongozo ya Wa-tumishi.

5. Makubaliano na washirika pamoja na Makubaliano ya Pamoja.

Hatua Muhimu za Kufikia Muunganiko wa Vyama

Hakuna utaratibu wala kanuni mahususi za kufikia muunganiko wa vyama. Nchi nyingi hazina hata sheria mahsusi zinazoelekeza utaratibu wa kuunganisha vyama kisheria.

Hatua zifuatazo ni muhimu kufuatwa ili ku-fikia muungano wa vyama ulio na mafani-kio:

1. Utayarishaji wa makubaliano baina ya vyama vinavyoungana

Makubaliano haya lazima yatekelezwe mara tu baada ya Azimio la kupitisha muungano huo kupitishwa na wanachama wa vyama vinavyohusika na muungano huo. Makubaliano hayo lazima yasajiliwe. Kuha-lalisha wanachama, mali za chama, na wa-tumishi kutategemea maelekezo yaliyomo kwenye makubaliano hayo.

Hivyo ni muhimu kusisitiza juu ya matayar-isho bora na ya kitaalamu ya makubaliano hayo.

2. Taarifa kwa Wanachama

Wanachama lazima waarifiwe kuhusu makubaliano hayo na wapewe nafasi ya kutoa dukuduku lao kuhusu matokeo ya muunganiko huo wa vyama. Vyama pia vi-tawajibika kubadili baadhi ya mambo hasa kanuni mbali mbali ili viendane na hali mpya.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

96

3. Kuteua Msimamizi Huru

Huyu atakuwa na wajibu wa kusimamia mchakato mzima wa kuunganisha vyama. Atatakiwa kufanya shughuli hii kwa ujuzi na weledi wa hali ya juu. Hali hii itategemea hali halisi itakayolazimisha kuteua msi-mamizi huru.

4. Kuweka Sahihi kwenye Waraka wa Makubaliano

Ili makubaliano yawafunge wahusika wote lazima watie sahihi kwenye waraka wa makubaliano.

5. Kusajili Chama Kipya

Chama kipya hatimaye lazima kisajiliwe ili kiweze kutekeleza majukumu yake kishe-ria. Taarifa zote za fedha, mali nyingine za chama na watumishi lazima iwasilishwe ili hatua za kufaa za kuviweka katika mfuko mmoja ziweze kuchukuliwa tayari kwa chama kipya kuanza kutekeleza majukumu yake.

Hatua zifaazo

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

97

REJEA

1. Haki za Vyama vya Wafanyakazi na Haki nyinginezo za Binadamu katika Afrika-Toleo la ICFTU- AFRO, 1999

2. A Guide on Trade Union Merger Processes – Lessons from Africa and Norway – A Publica-tion of Lo-Norway, 2012

3. Kitabu cha Mafunzo kwa Vikundi – DANIDA/TUCTA Publication, 2002

4. Historia ya Kuundwa kwa Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar - A Seminar Paper presented at the ZATUC Seminar, 2000

5. Conflict Prevention, Management, and Resolution- Role of African Trade Unions – Inter-national Tripartite conference Paper, 2010

6. International Labour Organisation; International Labour Conventions and Recommenda-tions 1919 -1995

7. ILO/SLAREA: A guide to Fundamental Standards and Principles of Freedom of Association ILO Office, Dar- es-Salaam

8. ICFTU AFRO: Training Manual for Trade Union Organizers

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

98

MFANYAKAZI THAMANI WAAJIRI TAMBUENI

1. Kwa jina lake Manani Muumbaji wa dunia Yupweke hako wa thani Na wala hatotokea Shairi nalibaini Anipe nguvu Jalia Mfanyakazi thamani Waajiri nawambia

2. Katika historia Mfanyakazi juweni Chanzo cha kutajirika Kwa waajiri jamani Ila thamani hakika Haipati asilani Mfanyakazi thamani Waajiri tambueni

3. Kwa kweli hutarajiwa Kuuza uwezo wake Afanya kazi imara Atoe ujuzi wake Bei na wake ujira Atoe mwajiri wake Mfanyakazi thamani Waajiri muiweke

4. Anauza nguvu zake Mfanyakazi hakika Hutoa uwezo wake Kukuza kinotajika Ila si fursa kwake Bei ilo muafaka Mfanyakazi thamani Waajiri natamka

5. Muajiri mnunuzi Wa nguvu za mfanyakazi Pia na wake ujuzi Huhitaji uwe wazi Sasa kujipa mapenzi Kutoa bei maudhi Mfanyakazi thamani Waajiri kubarizi

6. Kawekwa mfanyakazi Kama mkwezi sikia Siku zote yake moja Hakuna cha kuzidia Hata akwee mia moja Minazi na kupitia Mfanyakazi thamani Waajiri kusikia

7. Chama cha wafanyakazi Ni la kwake tumaini Anahitajia wazi Aipate ahueni Kimtetee kwa radhi Kumkomboa yakini Thamani ya mfanyakazi Iwe juu duniani

8. Madhila aliyonayo Mfanyakazi jamani Na Ubaguzi ambao Ni hatari duniani Chama kiwe na upeo Kimkomboe yakini Mfanyakazi thamani Awe juu duniani

9. Pia sheria za kazi mfanyakazi Ajuwe Ailinde yake hadhi Nje na ndani mwenyewe Achague kwa mapenzi Kazi atakayo yeye Mfanyakazi thamani Awe juu duniani

10. Bado mapambano bado mfanyakazi nchini Ukombozi wake bado Kuipata afueni Twahitajia matendo Ya chama kumuauni Mfanyakazi thamani Awe juu duniani.

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

99

WIMBO WA MSHIKAMANOWafanyakazi wote tujiunge pamoja,Wafanyakazi wote tujiunge pamoja,Wafanyakazi wote tujiunge pamoja, kujitenga hatari.Haya shime tujiunge, haya shime tujiunge,Haya shime tujiunge, kujitenga hatari.Mshikamano, daima ndio ukombozi wetu.

Kauli za mshikamano(i) Kiongozi: Mshikamano(ii) Wote: Tujiunge pamoja(iii) Kiongozi: Shime(iv) Wote: Nguvu moja, sauti umoja.(v) Kiongozi: Umoja wetu(vi) Wote: Nguvu za mabadiliko ya jamii

MW

ONGO

ZO W

A VY

AMA

VYA

WAF

ANYA

KAZI

102 9 789229 310541 00001

ISBN 978-92-2-931054-1

Kuhusu WaandishiMOHAMMED MWAMADZINGO

Mohammed Mwamadzingo anafanya kazi na kitengo cha Shirika la Kazi Duniani kinachounganisha ofi si kuu ya shirika hilo na wafanyakazi wote duniani (ILO/ACTRAV) kuanzia Oktoba mwaka 1997 hadi sasa. Amefanya kazi katika vituo kadhaa Afrika (Abidjan, Addis Ababa, Harare na Pretoria) kama mtaalam wa maeneo kuhusu elimu ya wafanyakazi; kabla ya kuteuliwa kama Mchumi Mwandamizi katika afi si kuu ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) Geneva, mnamo Machi 2008. Alichukua wadhifa wa Afi sa Msimamizi kanda ya Afrika mnamo Mei 2013.

Kabla ya kujiunga na Shirika la Kazi Duniani, alikuwa mhadhiri wa somo la Uchumi Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya, kwa miaka tisa, kati ya Agosti 1988 na Septemba 1997. Wakati wa kipindi hiki alichukua majukumu mengi kama Mshauri wa mashirika mbalimbali kama Benki ya Dunia, Halmashauri ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, Chuo cha Umoja wa Mataifa, katika Chombo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia elimu (UNESCO), Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo na Utafi ti, DANIDA, kampuni mbali mbali nchini Kenya, Serikali ya Kenya na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Mwamadzingo ni Msomi wa masuala ya Uchumi, baada ya kuhitimu shahada ya Digrii, Uzamili (Masters) kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 1986 na 1988 mtawalia. Isitoshe, alisomea Sera kuhusu Sayansi na Teknolojia katika Chuo cha Sussex, Uingereza, ambapo alihitimu shahada ya Uzamivu (PhD) katika falsafa mwaka 1995.

Alizaliwa Mombasa, Kenya, mwaka wa 1962.

TALIB OMAR MBWANA

Talib Omar Mbwana ni mkongwe katika mambo ya vyama vya wafanyakazi na amehudumu katika nyadhifa kuu mbalimbali kwenye vitengo vya wafanyakazi vya Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania (JUWATA), kuanzia mwaka wa 1979. JUWATA ndiyo jumuiya tangulizi ya muungano wa sasa wa Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania (TUCTA).

Mbwana alihudumu kama mwanakamati katika kamati kuu za Kituo cha Muungano wa Kitaifa wa vyama vya wafanyakazi ambacho kilibadili jina kutoka JUWATA, Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (OTTU), hadi Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TFTU). Kati ya kipindi cha mwaka 1986 hadi 1992, Mbwana alihudumu kama Naibu wa Katibu Mkuu wa TFTU huko Zanzibar. Kufuatia uamuzi wa Bunge la Tanzania (Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi 1998) iliyodhibiti ndoa kati ya wafanyakazi wa Tanzania na wale wa Zanzibar kwa kusingizia kuwa masuala ya wafanyakazi hayakujumuishwa kwenye masuala ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Mbwana alikuwa mstari wa mbele katika kuanzisha Muungano wa Wafanyakazi wa Serikali za mitaa ambapo alichaguliwa kama Katibu Mkuu. Alihudumu ZALGWU kuanzia mwaka wa 2000 hadi 2012 na kisha kustaafu.

Kabla ya kujiunga na Vyama vya Wafanyakazi, Mbwana alikuwa kwenye taaluma ya Ualimu na alifundisha katika shule kadhaa huko Pemba kuanzia 1969. Mnamo mwaka wa 1985 aliajiriwa na Serikali ya Mapinduzi kama afi sa mwendeshaji wa eneo na kuteuliwa kama Mkurugenzi Mwendeshaji wa Eneo mwaka wa 1990. Mbwana alitunukiwa shahada ya Digrii katika Maendeleo ya Jamii na Uendeshaji na Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam baada ya kujiunga nacho mwaka 1982.

Talib Omar Mbwana alizaliwa Pemba, Zanzibar mwaka 1947.