20
1 Wafanyakazi Bora TPA wahamasika na utalii wa ndani Uk. 5 Dar yakabidhiwa Vifaa vya Kisasa Kutunza Mazingira Baharini Uk. 12 Wadau Bandari ya Mtwara Wakutana Uk. 2 TANZANIA PORTS AUTHORITY www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 12 Julai 9 - 15 Julai, 2012 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri V ifo vya waliokuwa viongozi waandamizi wa DOWUTA, Hayati Abdallah Kibunda, Hayati Edward I. Wakuruwasi na Hayati Deodatus C. Milinga ambao walifariki katika vipindi tofauti mwaka huu 2012 vimepokewa kwa mstuko na majozi makubwa na wanachama wa DOWUTA, wafanyakazi na wadau wengine kutokana na viongozi hao kuwa mahiri katika kutetea maslahi ya wafanyakazi pamoja na majukumu yao mbalimbali katika kipindi cha uhai wao. Tunasikitika mno kuondokewa na wafanyakazi na viongozi hao huku Chama kikiwa bado kinawahitaji ukizingatia kwamba walikuwa wachapakazi mahiri wenye ueledi mkubwa katika shughuli za vyama vya wafanyakazi na majukumu yao ya kila siku. Kwa wanaowafahamu vizuri Hayati Kibunda, Hayati Wakuruwasi na Hayati Milinga ‘DC’ watakuwa mashahidi wa hili tunalosema. WASIFU: KATIBU MKUU DOWUTA (TAIFA) Alisoma shule ya msingi na kumaliza mwaka 1965 ambapo baadae mwaka 1966 alijiunga na kozi ya vyama vya ushirika kabla ya kujiunga na mafunzo Na Mwandishi Wetu zake za kujiendeleza ambapo mwaka 1979 alifanya mafunzo ya utunzaji stoo ngazi ya cheti. Kibunda aliendelea na jitihada zake za kujiendeleza kielimu katika uhai wake ambapo pia aliiudhuria kozi zifuatazo, mwaka 1982 Diploma ya Biashara huko Manchesta Uingereza na mwaka 1986 mafunzo kuhusu maslahi ya wafanyakazi. Hayati Kibunda pia alipata fursa ya kuudhuria mafunzo ya sayansi ya jamii mwaka 1988 huko USSR, mwaka 1989 alifanya diploma ya sayansi ya jamii huko Ujerumani na mafunzo kuhusu namna bora ya kuboresha mifuko ya jamii ya kimataifa huko Brazili. ya jeshi la kujenga taifa mwaka 1969. Mwaka 1974 alifanya kozi ya mauzo na utunzaji vitabu vya hesabu na aliendelea na jitihada Inaendelea Uk. 2 Hayati Abdallah Kibunda

na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

1

Wafanyakazi Bora TPA wahamasika na utalii wa ndani Uk. 5

Dar yakabidhiwa Vifaa vya Kisasa Kutunza Mazingira Baharini Uk. 12

Wadau Bandari yaMtwara Wakutana Uk. 2

TANZANIA PORTS AUTHORITY

Wadau Bandari yaWadau Bandari ya

www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 12 Julai 9 - 15 Julai, 2012

DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri

Vifo vya waliokuwa viongozi waandamizi wa DOWUTA, Hayati Abdallah Kibunda, Hayati Edward I. Wakuruwasi na Hayati Deodatus C. Milinga ambao walifariki katika vipindi tofauti mwaka huu 2012 vimepokewa

kwa mstuko na majozi makubwa na wanachama wa DOWUTA, wafanyakazi na wadau wengine kutokana na viongozi hao kuwa mahiri katika kutetea maslahi ya wafanyakazi pamoja na majukumu yao mbalimbali katika kipindi cha uhai wao.

Tunasikitika mno kuondokewa na wafanyakazi na viongozi hao huku Chama kikiwa bado kinawahitaji ukizingatia kwamba walikuwa wachapakazi mahiri wenye ueledi mkubwa katika shughuli za vyama vya wafanyakazi na majukumu yao ya kila siku. Kwa wanaowafahamu vizuri Hayati Kibunda, Hayati Wakuruwasi na Hayati Milinga ‘DC’ watakuwa mashahidi wa hili tunalosema.

WASIFU: KATIBU MKUU DOWUTA (TAIFA)

Alisoma shule ya msingi na kumaliza mwaka 1965 ambapo baadae mwaka 1966 alijiunga na kozi ya vyama vya ushirika kabla ya kujiunga na mafunzo

Na Mwandishi Wetu

zake za kujiendeleza ambapo mwaka 1979 alifanya mafunzo ya utunzaji stoo ngazi ya cheti.

Kibunda aliendelea na jitihada zake za kujiendeleza kielimu katika uhai wake ambapo pia aliiudhuria kozi zifuatazo, mwaka 1982 Diploma ya Biashara huko Manchesta Uingereza na mwaka 1986 mafunzo kuhusu maslahi ya wafanyakazi.

Hayati Kibunda pia alipata fursa ya kuudhuria mafunzo ya sayansi ya jamii mwaka 1988 huko USSR, mwaka 1989 alifanya diploma ya sayansi ya jamii huko Ujerumani na mafunzo kuhusu namna bora ya kuboresha mifuko ya jamii ya kimataifa huko Brazili.

ya jeshi la kujenga taifa mwaka 1969.

Mwaka 1974 alifanya kozi ya mauzo na utunzaji vitabu vya hesabu na aliendelea na jitihada

Inaendelea Uk. 2

Hayati Abdallah Kibunda

Page 2: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

22

Tanzia

Inatoka Uk. 1

Mwaka 1967 alifanya kazi na vyama vya ushirika na baadae mwaka 1975 alikuwa meneja wa klabu ya EAHC kabla ya mwaka 1976 kuingia katika ajira kwa vitendo katika idara ya zima moto na baadae kuwa afi sa zimamoto.

Alimaliza mafunzo yake ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kinondoni mwaka 1986 ambapo mwaka 1988 alifanya mafunzo ya ngazi ya cheti kwenye eneo la utunzaji wa vitabu vya fedha katika Bodi ya Uhasibu na Wahasibu ya Taifa (NBAA).

Mwaka 1989 alifanya mafunzo ya uendeshaji ngazi ya karani daraja B katika chuo cha Bandari na baadae mwaka 2000 alifanya mafunzo hayo katika ngazi ya karani daraja A chuoni hapo.

msimamizi wa rasilimali watu daraja la kwanza.

Mwaka 2009 alipanda tena ngazi na kuwa afi sa msaidizi rasilimali watu ambapo Januari 2012 alipata mkataba wa miaka miwili makao makuu na kuwa Afi sa Utawala bandari ya Dar es Salaam.

Baadae mwaka 1982 Kibunda alipanda daraja na kuwa karani daraja la kwanza na baadae mwaka 1987 afi sa msaidizi mkuu. Hayati Kibunda aliendelea kupanda ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989 alikuwa afi sa rasilimali watu na mwaka 1995

Baadae mwaka 2010 aliihudhuria warsha ya huduma kwa wateja ambayo iliandaliwa na taasisi ya elimu ya jamii mkoani Morogoro. Milinga aliteuliwa na THA kuwa karani uendeshaji ngazi ‘B.’ Mnamo mwaka 2006 alipanda ngazi na kuwa karani uendeshaji ngazi ‘A’ na baadae mwaka 2009 alipanda ngazi na kufi kia cheo cha afi sa uendeshaji msaidizi kabla ya mauti hayajamkuta. Mpaka anafariki Milinga alikuwa ni mtumishi wa Mamlaka katika Bandari ya Kyela.

Mwaka 1989 alijiunga na THA akiwa dereva wa idara ya zimamoto na baadae mwaka 1989 alipanda ngazi na kuwa mtaalamu wa mashine ya zimamoto. Alifanikiwa kuaminika na kutokana na uwezo wake kazini alipanda daraja mwaka 2009 na kuwa afi sa zimamoto kiongozi.

Alihitimu shule ya sekondari ya usagara mwaka 2007 huko Tanga, ambapo kabla ya hapo mwaka 1991 alipitia mafunzo maalumu (VIP) ya udereva katika Chuo cha Taifa cha Usafi rishaji (NIT).

Mwaka 1986 Wakuruwasi alipata mafunzo ya utunzaji vifaa kutoka Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo pia alifanya mafunzo ya zimamoto mwaka 1997 na 1998 katika Chuo Cha Bandari. Baadae mwaka 2005 Wakuruwasi alifanya Mafunzo ya Ubaharia katika Chuo cha DMI Tanga. Mpaka anafariki Wakuruwasi alikuwa ni mtumishi wa Mamlaka katika Bandari ya Tanga.

WASIFU: MWENYEKITI WA DOWUTA (TANGA)

Edward I. Wakuruwasi

Deodatus C. Milinga ‘DC’

WASIFU: MWENYEKITI WA DOWUTA (KYELA)

Page 3: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

3

Uwekezaji

Wadau Bandari yaMtwara Wakutana

Wadau wa Bandari Mkoani Mtwara w a m e k u t a n a

hivi karibuni kujadili pamoja na mambo mengine taarifa ya Mshauri Mwelekezi juu ya namna bora ya kuendeleza Bandari ya Mtwara na Ukanda wake wa kiuchumi.

Katika Kikao hicho ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia wajumbe walitoa maoni mbalimbali yatakayosaidia kuboresha

Na Focus Mauki

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Joseph Simbakalia (watatu kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Bw. Raphael Mollel (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Ephraim Mgawe (kushoto) pamoja na wajumbe wengine wa Mkutano wa Wadau wa Bandari ya Mtwara.

Wajumbe na Wadau wa Mkutano wa Bandari ya Mtwara wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Veta Mtwara.

Page 4: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

4

Wajumbe na Wadau wa Mkutano wa Bandari ya Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano.

Uwekezaji

Mtwara ambazo zinatoa fursa kwa Bandari kupanuka kama vile viwanda vya saruji, gypsum, chuma, makaa ya mawe na methanol. Aina nyingine mpya ya biashara inayokuwa kwa kasi katika eneo hilo ni pamoja na biashara ya mbolea, na ammonia.

Kampuni ya URS inashirikiana na Kampuni ya Inter-Consult ya hapa nchini katika kutathimini na kafanikisha kandarasi za miradi mbalimbali ya maendeleo na Usafi rishaji wa mizigo kwa ajili ya miradi mbalimbali. Bandari ya Mtwara pia inatajwa kuwa na nafasi nzuri kibiashara kwa kuwa na miundombinu inayofi kika kiurahisi, ikiwemo huduma mbalimbali za kijamii, hali nzuri ya kijografi a kwa kuwa ni bandari ya asili (natural harbor) pamoja na upatikanaji wa ardhi nzuri ya kuwekeza.

Mkoa wa Mtwara, Kampuni za Kutafi ti na Kuchimba Gesi na Mafuta pamoja na Wawekezaji wengine walipata fursa ya kuijadili taarifa hiyo ambayo imewasilishwa kwa mara ya pili na timu ya URS kwa lengo la kukusanya maoni zaidi kutoka kwa Wadau.

Mtaalamu Mwelekezi huyo alipewa kazi ya kufanya Upembuzi Yakinifu ‘Feasibility Study’ ya namna ya kuendeleza Bandari ya Mtwara pamoja na Ukanda Huru wa Biashara katika Bandari hiyo (Feasibility Study for Development of Port and Economic Zone at Mtwara Port) kwa lengo la kuiwezesha Bandari hiyo kuendana na kasi ya kukuwa kwa biashara mbalimbali katika eneo hilo.

Ripoti ya uchambuzi ya URS inaonesha kukua kwa biashara mpya mbalimbali mkoani

upembuzi yakinifu huo uliofanywa na Kampuni ya URS kutoka nchini Marekani ambayo inajihusisha na shughuli za ukandarasi na ujenzi ambapo Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa URS kujumuisha maoni yaliyotolewa na Wadau mbalimbali ili kuifanya taarifa hiyo kupata uzito na usahihi unaostahili kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa TPA kwa utekelezaji zaidi.

“Ni vizuri mkazingatia maoni yaliyotolewa hapa na wadau mbalimbali na pia mkazingatia na maoni yetu kutoka Mkoani ili kuweka uwiano na kuwa na taarifa iliyozingatia maoni ya Wadau wote,” alifafanua Simbakalia.

Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na wajumbe kutoka Taasisi za Kifedha,

Serikali Kuu, Uongozi wa

Page 5: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

5

Jumla ya Wafanyakazi Bora 33 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) wameunga mkono utalii wa ndani kwa kufanya ziara katika mbuga za wanyama za Ziwa Manyara, Serengeti na Bonde la Ngorongoro.

Ziara hiyo ni sehemu ya kuthamini utendaji wao uliowafanya kuwa Wafanyakazi bora mwaka 2012 miongoni mwa waajiriwa wengine na pia motisha kwao kuwafanya wafanye kazi kwa bidii na kwa ufanisi mwaka ujao wa fedha ili kuongeza ufanisi na tija kwa Mamlaka.

Wafanyakazi bora 17 wa kutoka Makao Makuu waliungana na wenzao 16 wa Bandari ya Dar es Salaam kutembelea mbuga hizo maarufu si nchini tu bali kote ulimwenguni.

Akizungumza katika tafrija ya kuwapongeza wafanyakazi hao jijini Arusha, Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Apolonia Mosha, amewapongeza wafanyakazi hao na kuwapa changamoto ya kuendeleza uchapaji kazi wao wa bidii na maarifa na kujiwekea malengo ya kuibuka tena mfanyakazi bora.

“Mafanikio haya mliyofi kia yasiwe mwisho bali iwe ni chachu kwa kila mmoja wenu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kumbukeni kwamba inawezekana kabisa kuchaguliwa tena kuwa mfanyakazi bora katika awamu nyingine, sasa ni juu yenu kufanya kazi kwa bidii kufi kia

malengo haya,” amewaasa Mosha.

Wafanyakazi Bora TPA wahamasika na utalii wa ndani

Kwa upande wake Bi. Melody Lema ambaye aliibuka mfanyakazi bora kutoka Idara ya Utawala, Mawasiliano, Takwimu na Mipango amesema kwa ujumla ziara katika mbuga za wanyama ilikuwa ya mafanikio makubwa na ilipangwa katika msimu mzuri ambapo waliweza kuona wanyama wa aina mbalimbali katika mbuga zote walizotembelea.

“Nimefarijika sana kupata nafasi hii ya kuwa mfanyakazi bora na ninawashukuru wenzangu wote ambao wameona nafaa kuwa mfanyakazi bora, katika ziara tuliyofanya mbugani nimefurahi pia kuona wanyama hasa lile kundi la ‘Big Five’ Simba, Tembo, Nyati, Chui na Faru,” anasema Lema.

Lema ameongeza kuwa, wakiwa katika hifadhi ya Ngorongoro walipata fursa ya kutembelea

bonde la Oldupai Gorge (chimbuko la mwanadamu) ambapo pamoja na mambo mengine walipata fursa ya kusikiliza historia ya bonde hilo na ufumbuzi wa nyayo za mtu wa kale zenye zaidi ya umri wa miaka milioni 3.

Bonde la Oldupai linalotokana na jina la mmea unaoota katika eneo hilo ambalo lipo kaskazini

Na: Focus Mauki

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Apolonia Mosha

Bibi Hawa Kapiteni Rasilimali Watu

Juma Salum Ngwele Uhandisi

Isaak GodsonPMU

Wafanyakazi Bora

Page 6: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

66

mwa Tanzania takribani kilometa 180 kutoka jiji la Arusha likiwa karibu na bonde la Ngorongoro pembeni mwa barabara ya kutoka mbuga ya wanyama ya Manyara kuelekea mbuga maarufu ulimwenguni ya Serengeti inayohifadhi wanyama wa kila aina huku pia ikiwa ndio mbuga kubwa kuliko zote nchini.

Naye Bw. Seleman Mketo wa idara ya Ugavi ametoa pongezi kwa uongozi wa Mamlaka kwa kudhamini na kugharamia ziara yao ya kutalii katika mbuga maarufu za wanyama na kusema kwamba imekuwa ni zawadi nzuri kwa wafanyakazi bila kusahau umuhimu wa kila Mtanzania kuunga mkono jitihada za Serikali kuhamasisha utalii wa ndani.

“Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vya kila aina lakini bado utalii wa ndani ni changamoto kubwa kwa sisi Watanzania, kwa kupata fursa kama hii ya kutembelea mbuga tatu maarufu kwa wakati mmoja ni fursa pekee kwetu sisi kuunga mkono utalii wa ndani, kwa kuzingatia hilo natoa pongeza uongozi wa TPA kwa kutupatia fursa hii,” ameongeza Mketo.

Wafanyakazi bora wanne (4) wa Mamlaka waling’ara kimkoa kutoka Bandari ya Dar es Salaam na idara wanazotoka ni pamoja na Bw. Ephraim Malewo (Rasilimali Watu), Bw. Wilson Marwa (Ukaguzi wa Ndani), Mhandisi Sifuel Feliz (Uhandisi Dock Yard) na Bi. Valeria Othman (Ulinzi). Wafanyakazi

hao walikabidhiwa kitita cha shilingi 800,000 kila mmoja wakati wale wengine wa Bandari walijinyakulia shilingi 400,000 kila mmoja.

Kwa upande wa Makao Makuu Wafanyakazi waliong’ara na idara wanazotoka ni pamoja na Bi. Hawa Kapiteni (Rasilimali Watu), Bw. Prosper Kimaro (Fedha), Bw. J. Ngwere (Uhandisi), Bw. Issack Godson (PMU), Bw. Ayubu Msangi (TEHAMA), Bw. Abdallah Nassoro (Mipango na Uwezeshaji), Bw. Kezzy Raphael (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri (Zimamoto), Bi. Marcelina Mhando (TEHAMA) na Bw. Ramadhan Zikatimu (Menejimenti).

Wakiwa katika Ziwa Manyara lenye ukubwa wa kilometa za mraba 3,200 walipata fursa ya kujionea baadhi ya ndege wanaosafi ri kutoka Tanzania mpaka bara Ulaya. Hifadhi ya Ziwa Manyara ina zaidi ya aina 4,00 za ndege na inasifi ka kwa kupokea aina ya ndege wanaohama kutoka Bara la Ulaya katika majira ya baridi ambao hutaga na kuishi katika mbuga hiyo ya Ziwa Manyara.

Prosper Kimaro Fedha

Mwenyekiti wa DOWUTA Makao Makuu Bw. Samuli Chalaakiwa na Bw. Isaak Godson wa PMU wakiwa kwenye picha pamoja na sanamu ya Hayati Mwl. Nyerere na mwanzilishi wa mbuga ya Taifa ya Serengeti.

Mwanaidi AmiriZimamoto

Kezzy Raphael Menejimenti

Ayub MsangiTEHAMA

Inaendelea Uk. 6

Wafanyakazi Bora

Page 7: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

7

Abdallah NassoroMipango na Uwekezaji

Nuru KisalaChuo cha Bandari

Ramadhani ZikatimuMenejimenti

Nassibu Kasita Mawasiliano

Wafanyakazi hao pia walitembelea mbuga ya Serengeti inayofahamika kama urithi wa dunia na ambayo hivi karibuni iliwekwa katika kumbukumbu ya mojawapo ya maajabu saba ya dunia. Zaidi ya nyumbu milioni 7 katika hifadhi ya Serengeti kila mwaka wanahama kutafuta malisho mapya jambo linalofanya uhamaji huo kuwa kivutio cha aina yake.

Mbuga ya Serengeti ipo kilometa 335 kutoka katika jiji la Arusha na ina ukubwa wa kilometa za mraba 14,763, ambapo eneo la mbuga hiyo linafi ka mpaka kaskazini mwa Kenya na kupakana na ziwa Victoria kwa upande wa Mashariki.

Mbali na mbuga ya Serengeti Wafanyakazi hao pia walitembelea Hifadhi ya Bonde

la Ngorongoro ambayo ipo chini ya usimamizi

wa Mamlaka ya Ngorongoro (NCA) na kujionea faru ambaye anaelekea kutoweka ulimwenguni.

Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ipo kilometa 180 kutoka Arusha mjini ni kivutio cha aina yake kwa kuwa pembeni ya bonde la ufa ndani ya bonde la volcano. Hifadhi hii mwaka 1979 ilitangazwa rasmi kuwa ni urithi wa dunia (World Heritage Site).

Inatoka Uk. 5

Wafanyakazi Bora

Watalii na wafanyakazi wa Bandari wakiwa katika Hifadhi ya Serengeti.

Inaendelea Uk. 6

Page 8: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

8

Mafunzo ya Zimamoto ni kiwango

Na: Focus Mauki

Wahitimu wa mafunzo ya Msingi ya Zimamoto na Usalama sehemu za kazi ‘Basic Firemenship Course’ wameonyesha ari na ukakamavu wa hali ya juu , hali iliyowafurahisha wageni waalikwa walioshuhudia

gwaride maalumu la kuhitimisha mafunzo hayo ya miezi mitatu.

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 20 Februari na kukamilika tarehe 18 Mei mwaka huu yaliwahusisha wanafunzi hamsini na tano (55) wa kujitegemea, miongoni mwao wakiwa waajiriwa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA).

Idara ya Zimamoto ya Mamlaka ndio inayoratibu mafunzo hayo yaliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi tisa (9) kutoka Bandari ya Dar es Salaa, na Bandari za Tanga na Mtwara kutoa wanafunzi wanne (4)

kila moja huku wanafunzi wengine thelathini na tano (35) wa kujitegemea.

Tumeiva Kitaaluma Gwaride ‘Drill’ latia Fora

Wazimamoto wakifanya mazoezi ya kukabiliana na moto.

Inaendelea Uk. 8

Mafunzo

Wazimamoto wakionesha namna ya kutoa huduma ya kwanza.

Page 9: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

9

Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Cassian Ng’amilo katika hafl a fupi ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu Meneja wa Maghala ya nafaka katika Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Daniel Kissa aliwapongeza wahitimu hao na kuwataka kuwa imara ili kukabiliana na majanga ya moto na usalama sehemu za kazi.

“…napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa wanafunzi wote kuhitimu mafunzo haya ambayo naamini yamewafundisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuzima moto, usalama mahali pa kazi, kutoa huduma ya kwanza pamoja na utunzaji wa mazingira,” alisema Bw. Kissa.

Aliwashauri wahitimu hao kutumia mbinu za kisasa za kuweza kuzuia na kuzima moto utakaotokea katika maeneo mbalimbali ya kazi ikiwa ni pamoja na maeneo wanayoishi.

Mbali na mafunzo nadharia pia wahitimu walifundishwa mazoezi

ya viungo ili kuwawezesha kufanya kazi katika mazingira mbalimbali.

Katika hali ya kawaida Afi sa wa zimamoto anapaswa kuwa na afya nzuri, kufanya mazoezi na kujiweka tayari kukabiliana na moto au janga lolote mahali pa kazi.

Kuhusiana na changamoto zilizojitokeza wakati wa mafunzo, uongozi wa Bandari kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.

“Natambua changamoto zilizojitokeza wakati wa mafunzo, zilikuwa nje ya uwezo wetu lakini tutazitafutia ufumbuzi wa kudumu,” amefafanua Kissa.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi, wahitimu walibainisha changamoto mbalimbali na kuomba uongozi kuzitatua haraka ili kufanikisha na kuboresha mafunzo.

Wahitimu wameipongeza Mamlaka kwa kujifunza kwa uhuru zaidi na kuruhusu kutumiwa kwa vitendea kazi vilivyopo katika Kituo Kikuu cha Zimamoto, Dar es Salaam.

Wahitimu pia wamepongeza mbinu shirikishi iliyotumiwa na walimu wao kufundisha darasani kuwa iliwapa hali ya kujifunza na kuinua viwango vyao vya uelewa, hali iliyowafanya kuiva kitaaluma.

Hali hiyo ilijiidhirisha pale wahitimu walipoonyesha uwezo na viwango vya hali ya juu katika gwaride ‘drill’ maalumu ambalo liliandaliwa kwa heshima ya wageni waalikwa.

Wahitimu wa Shirika la Bandari waliahidi kupunguza ajali, kukinga majanga ya moto kutokea ikiwa ni pamoja na kuweka mipango mizuri ya usalama itakayopunguza gharama kwa shirika.

Bw. Daniel Kissa Baadhi ya Wazimamoto wakifanya mazoezi na kujiweka tayari kukabiliana na moto au janga lolote mahali pa kazi.

Inatoka Uk. 7

Mafunzo

Page 10: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

10

Mwakilishi wa Tume ya IOC-Indian Ocean Commission, Bw. Raj Prayang (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo (katikati) Hati ya Makabidhiano ya Vifaa vya Kisasa vya Kudhibiti Umwagikaji Mafuta Baharini kwa ajili ya matumizi ya Bandari Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanyika Kurasini Oil Jet (KOJ) hivi karibuni.

Waziri wa Uchukuzi wa Serikali ya Zambia, Mh. Panji Kaunda (wapili kushoto) na Maafi sa wengine wakifurahia jambo na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Cassian Ng’amilo (kulia) wakati wa ziara yake Bandarini hapo hivi karibuni.

Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Modest Kakusa akuwahutubia Wafanyakazi katika hafl a maalumu ya kuwapongza Wafanyakazi Bora wa Bandari ya Mtwara kwa mwaka 2012.

Wafanyakazi bora wa Makao Makuu, Dar Port naKigoma walipotembelea bonde la Ngorongoro.

Page 11: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

11

Mwakilishi wa Tume ya IOC-Indian Ocean Commission, Bw. Raj Prayang (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo (katikati) Hati ya Makabidhiano ya Vifaa vya Kisasa vya Kudhibiti Umwagikaji Mafuta Baharini kwa ajili ya matumizi ya Bandari Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanyika Kurasini Oil Jet (KOJ) hivi karibuni.

Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Modest Kakusa akuwahutubia Wafanyakazi katika hafl a maalumu ya kuwapongza Wafanyakazi Bora wa Bandari ya Mtwara kwa mwaka 2012.

Wafanyakazi bora wa Makao Makuu, Dar Port naKigoma walipotembelea bonde la Ngorongoro.

Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Cassian Ng’amilo (watatu kushoto) akiwa na baadhi ya Maafi sa wa Jeshi kutoka Uganda wakati walipofanya ziara Bandarini hapo hivi karibuni.

Wafanyakazi Bora wa Bandari ya Mtwara mwaka 2012 wakiwa katika Bonde la Ngorongoro.

Page 12: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

1212

Bandari Dar yakabidhiwa Vifaa vya Kisasa Kutunza Mazingira Baharini

Mamlaka ya U s i m a m i z i wa Bandari

Tanzania (TPA) kupitia Serikali imekabidhiwa Vifaa ya Kisasa vya Kudhibiti Umwagikaji wa Mafuta Baharini na kutunza Mazingira kutoka Tume ya IOC (Indian Ocean Commission) vitakavyotumiwa na kitengo cha Kurasini Oil Jet (KOJ).

Shughuli ya makabidhiano hayo iliandaliwa na TPA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafi ri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

Na: Innocent Mhando TPA iliwakilishwa na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Cassian Ng’amilo ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Bw. Ephraim Mgawe huku SUMATRA ikiwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wake, Bw. Ahmad Kilima na Tume ya IOC iliwakilishwa na Bw. Raj Prayang.

Vifaa hivyo hivyo ambavyo viliwasili Mei 2012 na kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania kupitia kwa mwakilishi wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. John Mngondo vinategemewa kuwa msaada mkubwa katika kudhibiti uchafuzi wa mazingira baharini na kudhihirisha juhudi za pamoja kati ya Serikali

na Mamlaka katika kutunza mazingira nchini.

“Naishukuru Jumuiya ya IOC kwa kutupatia vifaa hivi na nina imani kwamba vifaa hivi vitasaidia kwa kiwango kikubwa katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira baharini,” alifafanua Bw. Mngondo mara baada ya makabadhiano hayo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa IOC Bw. Raj amesema vifaa hivyo ni vipya na vya kisasa na vitasaidia kukabiliana na umwagikaji wa mafuta baharini na akatoa wito kwa idara inayohusika na mazingira kuwapa Wafanyakazi wake mazoezi ya mara kwa mara ili kuzoea matumizi ya vifaa hivyo.

Mwakilishi wa Tume ya IOC-Indian Ocean Commission, Bw. Raj Prayang akifafanua jambo wakati wa kukabidhi Vifaa vya Kisasa vya Kudhibiti Umwagikaji Mafuta Baharini. Kulia kwa Prayang ni Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Cassian Ng’amilo.

Mazingira

Page 13: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

13

Harbour Master wa Bandari ya Mtwara, Capt.

Hussein Kasugulu ameibuka Mfanyakazi Bora wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Mkoa wa Mtwara na kukabidhiwa Cheti Maalumu pamoja na kitita cha Shilingi Milioni Moja.

Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Modest Kakusa alikuwa miongoni mwa Wafanyakazi walioshuhudia Capt. Hussein akikabidhiwa zawadi zake na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh. Joseph Simbakalia wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika hivi karibuni Wilayani Newala.

Maafi sa wengine wa Bandari ya Mtwara ambao walihudhuria shamrashamra hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa DOWUTA (Tawi) Bw. Oliver Maeda, Katibu wa DOWUTA (Tawi) Bw. Hamimu Mawazo, Afi sa Ununuzi na Ugavi wa Bandari Bw. Abdilah Salim, Afi sa Rasilimali Watu Bi. Sharifa Nuhu na Afi sa Utawala na Mawasiliano Bw. Paul

Mirwato.

Mara baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo ya Kitaifa kulifanyika tafrija ya kupongezana katika ukumbi wa ‘Bandari Social and Sports Club’ iliyohudhuriwa na Wafanyakazi wote. Katika tafrija hiyo Bw. Kakusa alitoa zawadi za cheti pamoja na hundi zenye thamani ya Shilingi Lakini Sita kwa Wafanyakazi Hodari wengine kutoka Idara mbalimbali.

Wafanyakazi waliotunukiwa zawadi hizo na Idara wanazotoka katika mabano ni pamoja na Bw. Muharami Manyara (Utekelezaji), Bw. David Ndege (Utekelezaji), Bw. Mohamed Mataka (Ulinzi na Usalama), Bw. Abdallah Kassita (Uhandisi) na Bi. Stella Ngonyani (Ugavi na Tiba).

Wengine ni Bw. Ludovick Kihuru (Utawala), Bibi Sanura Kulagha (Rasilimali Watu), Bw. Humphrey Kachamila (Fedha), Bi. Rose Mganga (Zimamoto na Usalama) na Bw. Said Abbasi (Marine).

Bw. Kakusa aliwapongeza Wafanyakazi waliochaguliwa mwaka huu na kuwaasa kuongeza bidii ili kuleta ufanisi katika Bandari ya Mtwara. Mkuu huyo wa Bandari pia alitumia fursa hiyo kuwataarifu

Wafanyakazi kwamba pamoja na msimu wa korosho kusuasua mwaka huu kutokana na ununuzi kutofanyika kwa wakati bado kazi inaendelea na kufanya pato la Bandari linalotokana na mzigo wa zao la Korosho kubaki kama kawaida.

Ameongeza pia kwa kupitia fursa za biashara kwenye shughuli zinazoendelea za utafi ti wa mafuta na gesi baharini, hivi sasa Bandari ya Mtwara imeweza kuongeza mapato yanayoiwezesha kumudu gharama zake za uendeshaji na kubaki na faida jambo ambalo ni la kujivunia. ”Kinachotakiwa sasa ni kuongeza bidii katika kuhudumia mzigo unaoingia na kutoka Bandarini,” aliwaasa Wafanyakazi.

Kwa upande wa burudani Kama ilivyo ada Wafanyakazi walikula na kunywa na kusakata dansi la Bendi ‘BOKA BOMA’ na baadae walipata fursa ya kutembelea Mbuga za Wanyama za Ziwa Manyara na Bonde la Ngorongoro mkoani Arusha.

Wafanyakazi Hodari walisikika wakisema hakika mwaka huu mambo “YALINOGA” Kweli.

Kepteni Kasugulu Ang’ara Mtwara

Na Paul Mirwato

Wafanyakazi Bora

Page 14: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

1414

Serikali ya Uswidi imepongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari na kufurahishwa na jitihada zinazoendelea katika Bandari ya Dar es Salaam za kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kutoa huduma bora

kwa wateja wake.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Uchumi wa nchi ya Swideni, Anders Borg wakati alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kupata taarifa ufanisi na changamoto zilizopo katika Bandari ya Dar es Salaam iliyowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Ephraim Mgawe.

“…napenda niwapongeze kwa taarifa nzuri na yenye kujitosheleza lakini kubwa zaidi ni namna mnavyokabiliana na changamoto zilizopo na pia namna mlivyojiwekea mkakati wa kukabiliana na changamoto hizo, pia ni vyema mkaongeza bidii na kuifanya Bandari hii kuwa na huduma bora na za kisasa katika siku za usoni,” alisema Waziri Borg.

Mgawe alimshukuru Waziri kwa niaba ya Serikali yake

kwa misaada mingi yenye thamani kubwa kutoka kwenye shirika la misaada la Swideni (SIDA) ambayo inalenga katika kuboresha maeneo ya kimkakati ndani ya Bandari kama vile kuboresha Kitengo cha Mizigo, Kitengo cha Utoaji Mizigo Mikubwa, Uhandisi, Kuendeleza Rasilimani Watu, pamoja na Kitengo cha Uendeshaji.

Pamoja na Serikali ya Uswidi kutoa mchango mkubwa katika kuisadia Mamlaka kupitia Serikali ya Tanzania Bw. Mgawe alisema Mamlaka ingependa kuona SIDA inaifadhili TPA kiuchumi katika miradi muhimu kama vile kuboresha Gati namba 1 na 2 pamoja na ujenzi wa kituo cha kisasa cha abiria.

Mgawe aidha alisema wadau mbalimbali wanaoiunga mkono TPA ikiwemo SIDA wana malengo ya kupunguza

mtizamo hasi wa changamoto zilizopo zinazoikumba Bandari ya Dar es Salaam ili kufi kia malengo ya kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa na hadhi yake inayostahili ya kutoa huduma bora na kuwezesha usafi rishaji ndani ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

Mbali na SIDA, Bandari ya Dar es Salaam pia inashirikiana na Shirika la ‘Trade Mark East Africa’ (TMEA).

Akijibu swali la Waziri Borg juu ya muda wa muda wa kuhudumia makasha bandarini, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Cassian Ng’amilo alisema muda wa kuhudumia makasha umepungua kwa kiasi kikubwa na kwa kiwango cha kuridhisha kufuatia matumizi ya Tehama na kufungua kituo kimoja cha wadau wote cha kuhudumia wateja (One Stop Center).

Serikali ya Uswidiyapongeza

ufanisi wa TPANa: Focus Mauki

Pongezi

Page 15: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

15

Afya

Huduma za X-Ray zina-patikana zahanati yetu • Mchakato wa Kupata Mashine ya Ultra-Sound upo mbioni

Huduma ya vipimo vya X-Ray sasa imeanza kutolewa

tena katika zahanati ya Bandari iliyopo katika Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya huduma hiyo kusimama kwa muda kufuatia mashine iliyokuwa inatumika mwanzoni kupata hitilafu.

Na Cartace Ngajiro

Kutokana na kuwa na watalaam waliobobea na dawa za kutosha, Dkt. Senkoro amesema zahanati ya Mamlaka imejizatiti kutoa huduma kwa wagonjwa na kukabiliana na hali yoyote.

Dkt. Senkoro pia ametoa wito kwa Wafanyakazi kuondokana na imani potofu kwamba maabara ya Zahanati ya Bandari haitoi majibu sahihi ya vipimo kwa magonjwa kama malaria.

Mtaalamu wa Chumba cha X-Ray, Ndg. Silvester Msafi ri amesema kwamba mashine hiyo ya kisasa (Fixed Machine) ina uwezo wa kupima vipimo vingi tofauti na machine ya mwanzo (Mobile Machine)

Akiongea kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Dkt. Hawa Senkoro alibainisha kuwa sasa huduma ya X-Ray inapatikana katika zahanati hiyo baada ya mashine hiyo kuharibika na hivyo kufanya huduma hiyo kusitishwa kwa muda mrefu.

“Kwa sasa mashine mpya imeshapatikana na imeanza kutumika kutoa huduma kama awali na hivyo natoa wito kwa wafanyakazi wagonjwa na familia zao ambao wanahitaji huduma hii wasisite kufi ka katika zahanati yetu na waache kutumia huduma ya namna hii kutoka hospitali za nje,” alifafanua Dkt. Senkoro.

Dkt. Hawa Senkoro

JUU: Mashine mpya ya X-ray

CHINI: Mashine ya zamani ya X-ray

Inaendelea Uk. 16

Page 16: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

1616

DOWUTA yakanusha kuhusishwa na habari ya uchochezi

Na Focus Mauki

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa

Bandari Tanzania (TPA) kupitia Chama chao cha Wafanyakazi (DOWUTA) wamekanusha vikali habari iliyoandikwa na gazeti moja la Kiswahili (Dira ya Mtanzania) iliyodai kuwa wafanyakazi wa Bandari wamewakataa wakurugenzi wao.

Tamko hilo la wafanyakazi lilitolewa katika kikao cha dharura baina ya wafanyakazi na Viongozi wa DOWUTA kilichofanyika Jumanne, Mei 29 katika ukumbi wa ghala la nafaka uliopo Bandari ya Dar es Salaam.

Katika kikao hicho ilibainika wazi kuwa taarifa zilizokaririwa

na chombo hicho cha habari hazikupata baraka za uongozi wa DOWUTA na ni za kutunga zisizokuwa na ukweli wowote.

Kwa kawaida taarifa zote za wafanyakazi hutolewa na DOWUTA, chombo ambacho ndiye msemaji rasmi wa mambo ya wafanyakazi bandarini.

Hata hivyo, katika toleo la gazeti la DIRA ya Mtanzania Na. ISSN 1821 - 641 Toleo namba 182 lilidai wafanyakazi wa Bandari hawawataki baadhi ya wakurugenzi wao bila kuhusisha taarifa hizo na DOWUTA.

Katika kikao cha viongozi kilichohudhuriwa na viongozi wote wa matawi na baaadae kufuatiwa na mkutano wa wafanyakazi ilikubaliwa kwa kauli moja kuwa habari hiyo ni ya kichochezi na inalenga

kuvuruga amani iliyopo ndani ya Mamlaka (kiwandani).

Kikao hicho cha DOWUTA na Wafanyakazi kilihudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka Bandari za Kyela, Mwanza, Mtwara na Tanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa DOWUTA Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Athumani Mkangara amewakumbusha Wafanyakazi kuwa DOWUTA itaendelea kuwa msemaji na chombo sahihi cha kusimamia maslahi yao.

“Ni vyema tukakumbuka kwamba tuna haki ya kuzungumza kwa uhuru na kujadili mambo yetu mbalimbali, tofauti na hivyo tutakuwa tunakiuka taratibu zetu za kiutendaji ndani ya chama chetu,” amefafanua Mkangara.

Inatoka Uk. 15

ambayo ilikuwa ndogo na ilikuwa inachukua vipimo vichache.

Mbali na hayo pia Msafi ri aliwataka wagonjwa wanaoandikiwa kwenda nje kupima kipimo cha Utra-Sound ambacho kwa sasa hakipatikani katika Zahanati hiyo ya Bandari kuwa wavumilivu kwani zoezi la

upatikanaji wa mashine hiyo linaendelea.

BANDARI BILAUKIMWI

INAWEZEKANA

DOWUTA

Page 17: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

17

Vitambulisho kutumika badala ya Stika za Magari Dar Port

Wa f a n y a k a z i wa Mamlaka ya Usimamizi

wa Bandari Tanzania wamekumbushwa kuvaa vitambulisho mara tu wanapoingia katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam na wakati wote wawapo Bandarini kwani kibali cha kuingia Bandarini sasa kitakuwa ni kitambulisho cha kazi cha mfanyakazi na si vinginevyo.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Afi sa Mlinzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Lazaro Twange kwa wakuu wa idara Bandarini na wafanyakazi walioko chini yao na wadau wote wa Mamlaka.

“…awali Bandari ilikuwa na utaratibu wa kutoa stika kwa wafanyakazi na wateja kama kibali rasmi cha kuingia bandarini lakini sasa utaratibu huo tumeusitisha mara baada ofi si yetu kugundua ukiukwaji mkubwa wa matumizi yake.

Tulibaini baadhi ya watu wasio husika na shughuli zetu Bandarini wanafanya Bandari kama njia ya mkato ya kuepuka foleni ya magari” alifafanua Bw. Twange.

Na: Innocent Mhando Pia, alisema ni lazima wafanyakazi wa wakala wa mizigo, wakala wa meli, TICTS na TRA walio na stika kwenye magari yao wawe na vitambulisho vyao vya kazi ili waweze kuruhusiwa kuingia bandarini.

Kuhusiana na wageni Bw. Twange alisema yeyote anayeingia bandarini na kuthibitishwa na mwenyeji wake atapewa kitambulisho cha wageni (Visitor’s Pass)

na atatakiwa kutokea geti aliloingilia ili kupata uhakika kwamba ametoka Bandarini salama.

Aidha Twange alisema ni marufuku kwa biashara yoyote ya taxi au taxi bubu kuingia bandarini.

Wafanyakazi wa Mamlaka wenye magari yaliyo na stika wameshauriwa kutumia magari hayo wao wenyewe na pindi wanapoyauza waondoe stika za Bandari ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.

Kwa upande mwingine Idara ya Ulinzi imetoa ombi kwa Wafanyakazi wote wa Mamlaka

na wanaomiliki magari kutoa ushirikiano katika kudhibiti uingiaji Bandarini ili kuleta ufanisi na usalama wa bandari ya Dar es Salaam.

Baadhi ya walinzi walio vaa vitambulisho vinavyotakiwa mahala pa kazi wakiwa katika mlango wa kuingilia namba 3.

Vitambulisho

Page 18: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

18

Micheco

Matalena Mhagama: Nyota ya Bandari Queens iliyopeperusha Bendera ya Taifa

Kwanza nikiri kwamba nilipata sifa zake nyingi kabla ya kukutana na Mwanamichezo machachari ‘the best goal shooter’. Mara tu nilipoanza mahojiano haya kuhusu nafasi yake na mchango wake katika kukuza

mchezo wa netiboli ndipo nilipogundua kumbe licha ya sifa zilizopo kwamba ana kipaji cha hali ya juu lakini kumbe alikuwa anaupenda mchezo wa netiboli tangu akiwa shule ya msingi.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja nilikuwa nangoja fursa ya kufanya mahojiano na Matalena Mhagama mtumishi wa Mamlaka ambaye kwa kuonyesha juhudi na kipaji katika mchezo wa netiboli alibahatika kuchaguliwa kwenye kikosi cha Timu ya Netiboli ya Taifa al-maarufu kama Taifa Queens ambayo wakati huo ilikuwa kambini kujiandaa na michuano ya Afrika iliyofanyika hapa nchini mwezi Mei mwaka huu.

Katika michuano hiyo iliyomalizika mwezi Mei mwaka huu Matalena alikuwa katika kikosi kazi cha Taifa Queens ambacho kilicheza na timu ya Botswana na kuifumua kwa goli 32-23. Timu ya Malawi ambayo inashika nafasi ya tano duniani na ya kwanza Afrika kwa ubora walitwaa ubingwa huo baada ya kushinda mechi zake zote huku Tanzania ambayo ni ya nne Afrika na ya 20 duniani ikiibuka na nafasi

ya pili. Tanzania ilipoteza mchezo wake pekee dhidi

ya Malawi na kushinda mechi nyingine zote.

Matalena Mhagama ni muajiriwa katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa zaidi ya miaka kumi na sasa anatumikia idara ya tiba. Nilipata fursa hasa ya kufahamu habari zake wakati nilipoodhuria hafl a ya kugawa zawadi kwa washindi wa jumla michezo ya Bandari, ambayo ni Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Wafanyakazi wengi hasa wapenda michezo wananifahamu lakini sijawahi kuhojiwa na Gazeti la Mamlaka hii ni mara yangu ya kwanza na ninayo furaha,” anakiri Matalena. Namfafanulia kwamba lengo mahojiano haya ni kuwaeleza Waajiriwa undani wa kipaji chake na historia ya maisha yake ya michezo ili pia kuwapa chachu waajiiriwa ya kupenda michezo.

“Ningekuwa nacheza katika mashindano yale hakika

kikombe cha Afrika kingebaki hapa nchini lakini kwa bahati mbaya sana nilipata majeraha,” anasema Matalena. Lakini pamoja na kuumia kwake bado Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) waliona umuhimu wake na kuhakikisha anakuwa kambini muda wote pamoja na timu hadi mwisho wa mashindano.

Na Focus Mauki

Mchezaji wa kutumaniwa Taifa Queens Anamudu vyema Nafasi za GS na GA

Matalena Mhagama

Page 19: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

19

“Nimesoma Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na Shule ya Sekondari Hekima pale Buguruni lakini pia nimeeudhuria mafunzo mbalimbali kama vile mafunzo ya Clerk C ambayo nimefanya katika Chuo cha Bandari hapa jijini Dar es Salaam,” anafafanua zaidi Matelana.

Kipaji cha Matalena kilikuja kugundilika wakati akicheza mashindano ya mtaani au ukipenda mchangani na anakumbuka kushiriki vilivyo katika michezo ya UMISHUMTA na muhimu zaidi anamkumbuka Mwalimu wake anayemtaja kwa jina moja la Juma kuwa ndiye alikuwa wa kwanza kuona kipaji chake na kumshauri kujiunga na timu ya Bohari Kuu.

Matalena Mhagama amezaliwa mwaka 1972 katika hospitali ya Ocean Road na anatoka katika Familia ya watoto nane (8) katika eneo la Manda Mbamba Bay Mkoani Ruvuma, “Kwa bahati mbaya sana Dada yetu wa kwanza ameshafariki lakini ndugu zangu wengine wote wapo,” anasema Matalena, ambaye ameolewa na ana watoto wawili (2) na wajukuu wawili (2) wote wakiwa jijini Dar es Salaam. Mmoja wa watoto wake ambaye yupo kidato cha tatu Shabani Athman tayari ameonyesha kufuata nyayo za Mama yake kwa kucheza mpira wa soka. Matalena amesoma elimu yake ya msingi na sekondari hapa Dar es Salaam na kuudhuria kozi mbalimbali zinazohusiana na kazi yake.

Sio Bohari pekee aliyochezea Matalena lakini pia amemudu kuchezea timu nyingine mbalimbali kama vile Benki Kuu (BOT), JUWATA, NASACO na hata Bandari yenyewe kabla ya kuajiriwa. Matalena anaweka wazi kuwa ni michezo hasa iliyompatia ajira na anajivunia ukweli kwamba wakati ule taasisi zote hizo zilimwania kumuajiri lakini moyo wake ulikuwa kwa Bandari.

“Nikupe siri moja taasisi zote nilizokutajia walitaka sana kuniajiri na hiyo ni kutokana na kuwa na kipaji cha hali ya juu katika mchezo huu wa netiboli lakini mwishowe Bandari waliibuka kidedea na sasa nipo hapa na nina jivunia kuwa Mfanyakazi wa Bandari,” anafafanua zaidi Matalena.

Matalena (wa sita nyuma) akiwa na imu ya Mpira wa pete ya bandari ya Dar es Salaam.

Michezo

Page 20: na utalii wa ndani Uk. 5 DOWUTA yapoteza Viongozi mahiri · 2015-10-28 · (Menejimenti), Bi. Nuru Kisala (Chuo Cha Bandari), Bw. Nassibu Kasita (Mawasiliano), Bi. Mwanaidi Amiri

20

mbalimbali kama vile soka, mpira wa pete (netball) mpira wa kikapu (basketball), kuvuta kamba na mingineyo.

Michezo pia imempa Matalena fursa ya kutembelea nchi mbalimbali za Afrika kama vile Zimbabwe, Malawi, Kenya, Afrika ya Kusini na Botswana ambapo anakumbuka kote walisafi ri wakiwa na kikosi cha Mamlaka.

Akijibu swali la namna alivyopata fursa ya kuchezea timu ya Taifa, anasema CHANETA ndio wenye jukumu la kuchagua vipaji vya kuchezea timu ya taifa na mara nyingi sana wanatafuta vipaji kwa kuangalia wachezaji kwenye michuano ya daraja la kwanza au la pili.

Anakumbuka kuitwa kwenye timu ya Taifa wakati akichezea

Matalena anakiri kuwa tofauti na miaka ya nyuma kwa sasa ari ya kupenda michezo ipo chini na amewausia Wafanyakazi kupenda michezo kwani inajenga afya. “Michezo kwa sasa ipo nyuma sana tofauti na zamani, nakumbuka wakati huo Bandari tuliwahi kushiriki michuano mikubwa na kuimudu kama vile michuano ya Bara, Muungano na ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuvunjika,” anafafanua zaidi.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ni miongoni mwa Taasisi kubwa nchini ambazo zinaunga mkono michezo na kuhimiza Wafanyakazi wake kujishughulisha na michezo. Kwa kutambua hili Mamlaka inadhamini michezo ya Inter-

Ports ambapo Wanabandari hushindana katika michezo

daraja la pili na ndipo viongozi wa CHANETA walipomuona na haraka sana kumuita kwenye timu ya Taifa Queens. Matalena anabainisha kuwa hii si mara yake ya kwanza kuchezea Timu ya Taifa kwani mwaka 1999 aliitwa kuchezea timu hiyo akiwa na wachezaji wengine wawili.

Kwa sasa kambi ya Taifa Queens imevunjwa na itaundwa tena na CHANETA wakati wa mashindano ya Africa Games ambayo Matalena anasema yanategemewa kufanyika katika jiji la Uingereza. Anamalizia kwa kusema ana matarajio makubwa kocha atamwita katika kikosi hicho na kukwea pipa mpaka kwa malkia ikiwa mambo yataenda sawa, na sisi tunamtakia kila la heri.

Matalena Mhagama wakati wa mashindano ya Interport yaliyofanyika Bandari ya Tanga 2011.