Upload
cathbert-angelo
View
338
Download
10
Embed Size (px)
DESCRIPTION
TATHMINI KUHUSU UFINYU WA BAJETI INAYOTENGWA KWA AJILI YA DAWA MUHIMU, VIFAA TIBA NA VITENDANISHI
Citation preview
1
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
01 – 06 -‐ 2014
TATHMINI KUHUSU UFINYU WA BAJETI INAYOTENGWA KWA AJILI YA
DAWA MUHIMU, VIFAA TIBA NA VITENDANISHI
Ukosefu wa mara kwa mara wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo vya
huduma za afya vya umma bado ni tatizo Tanzania. Tatizo hili linachangia
kutolewa kwa huduma duni za afya zinazopelekea athari kwa afya za wananchi.
Tathmini mbalimbali zimeonesha kuwa upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa
tiba ni mdogo katika vituo vya huduma za afya vya umma. Kwa mfano, utafiti
uliofanywa na Sikika mwaka 2012 umeonesha kuwa asilimia 52 ya hospitali
[N=52] hazikuwa na dawa muhimu na vifaa tiba kwa zaidi ya wiki nne.1
Moja ya sababu kuu za kukosekana kwa dawa muhimu na vifaa tiba ni bajeti ndogo inayotengwa na serikali.
Mwenendo wa mgao wa fedha za dawa muhimu na vifaa tiba kutoka Bajeti
ya WAUJ kutoka 2008/09 hadi 2014/15
1 Sikika: Report on Availability of Essential Medicines, Medical Supplies and Bed Capacity in Hospitals in Tanzania mainland, March 2013
Mwaka Bajeti ya WAUJ (Tsh Bilioni)
Bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba (Tsh Bilioni)
Mabadiliko ya asilimia ya bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba
2008/09 440.2 53.4 2009/10 478.9 49.6 -‐7.1 2010/11 676.3 61.4 23.8 2011/12 584.2 78.7 28.2 2012/13 576.1 80.5 2.3 2013/14 753.9 64 -‐20.5 2014/15 622.9 45.8 -‐28.4
2
Chanzo: Sikika 2010/2011 Health Sector Budget Analysis, Sikika Budget Analysis of the MoHSW for
fiscal year 2013/14.
Mahitaji ya dawa muhimu na vifaa tiba Ingawa mojawapo ya vipaumbele vya Wizara ya Afya ni kuboresha upatikanaji
wa dawa muhimu, mgao wa fedha kwa dawa muhimu na vifaa tiba umekuwa
hauendani na mahitaji yake. Kwa mfano kwa mujibu wa makadirio ya Wizara ya
Afya zitahitajika kiasi cha Tsh 250 bilioni kukidhi mahitaji ya dawa muhimu kwa
mwaka wa fedha 2014/15. Hata hivyo, mgao unaotarajiwa kupangwa ni shilingi
bilioni 45 tu. Mgao huu ni sawa na asilimia 7.7 ya mahitaji.
Pamoja na hivyo, ingawa kipaumbele cha Wizara ya Afya ni kupungunguza vifo
vya kina mama vitokanavyo na kujifungua, bajeti ya vifaa vya kujifungulia
(delivery kits) inapungua mwaka hadi mwaka. Mfano, kwa mwaka wa fedha
2012/13 zilitengwa jumla ya Tsh bilioni nne kwa ajili ya vifaa vya kujifungulia.
Bajeti hii ilipungua kufikia bilioni tatu mwaka 2013/14, na kama hakutakuwepo
mabadiliko itapungua hadi kufikia shilingi bilioni moja na nusu mwaka ujao wa
fedha 2014/15
Pia, pamoja na serikali kuahidi bunge mwaka jana kulipa deni ambalo MSD
inaidai serikali, deni hilo limeongezeka toka shilingi bilioni 76 mwaka 2013 hadi
bilioni 89 mwaka 2014
Mjadala wa Bunge juu ya Bajeti ya WAUJ Mapitio ya hansards (2008/09 – 2012/13) yamebaini kuwa takribani asilimia 35
ya wabunge ambao huchangia katika mjadala wa bajeti ya Afya hulalamika
kuhusu uhaba wa dawa vituoni na huitaka serikali, pamoja na mambo mengine
kuongeza bajeti. Tunawapongeza Wabunge kwa kazi hii nzuri. Lakini kama
ilivyoainishwa hapo juu, bajeti ya dawa imekuwa ikipungua na uhaba wa dawa
muhimu umeendelea kuwepo. Pia akina mama wanaojifungua wameendelea
kulalamika ukosefu wa vifaa vya kujifungulia
Mapendekezo
3
1. Serikali itafute fedha za ziada kutoka katika sekta nyingine (kuhamisha) ili
kuongeza bajeti ya dawa muhimu inayotarajiwa kutengwa kwa mwaka wa
fedha 2014/15 kutoka bilioni 45 hadi bilioni 250 (kwa mujibu wa makadirio
ya Wizara ya Afya)
2. Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii ihamishe fedha kutoka kwenye idara
nyingine kwenda kwenye dawa muhimu na vifaa tiba ili kuweza kuwa na
bajeti inayolingana na mahitaji.
3. Serikali ijadiliane na wafadhili ili waweze kuongeza fedha katika bajeti hii ya
mwaka 2014/15 (kama suluhisho la muda mfupi) wakati ikiendelea
kubainisha suluhisho la kudumu kama kuboresha na kusimamia ukusanyaji
wa kodi, kupunguza au kuondoa misamaha ya kodi pia kuboresha
makusanyo yannayokana na mifuko ya afya kama Mfuko wa Afya wa
jamii(CHF) na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa.(NHIF). Serikali inapaswa
kuwa Mchangiaji mkuu wa dawa muhimu na vifaa tiba na sio kuwaachia
jukumu hili wafadhili.
4. Mipango na mgao wa bajeti unapaswa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa
na bunge kupitia kamati ya kudumu ya huduma za jamii.
Mr. Irenei Kiria Executive Director of Sikika, P.O. Box 12183 Dar es Salaam,
Tel: +255 222 666355/57, Fax: 2668015, Email: [email protected], Website: www.sikika.or.tz