21
QURAN NI YA AJABU Gary Miller Imetafsiriwa na: Ibrahim H. Kabuga Islamic Centre for Research (ICR) Dar es Salaam - Tanzania

Quran Ni Ya Ajabu

  • Upload
    x-paster

  • View
    1.797

  • Download
    23

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Qur'an kuipa jina la „Kitabu cha Ajabu‟ sio jambo lililofanywa na Waislamu pekee, ambao wanaitambua na kuifurahia; bali pia imepewa jina hilo na Wasio Waislamu. Kwa kweli, hata wale wanaouchukia Uislamu kupita kiasi wameendelea kuipa sifa hiyo ya kuwa Qur'an ni ya Ajabu.Kitu kinachowashangaza wasio Waislamu wanaokichunguza kitabu hiki kwa ukaribu sana ni kwamba, Qur'an inajitokeza mbele ya macho yao kuwa katika hali ambayo hawakuitarajia. Wanachofikiri ni kwamba wana kitabu cha kale kilichotokea karne kumi na nne zilizopita kutoka katika jangwa la Arabia; na walitarajia kitabu hicho kionekane kama kitabu cha kale kutoka jangwani. Na kisha wanagundua kwamba hakifanani hata kidogo na vile walivyotegemea. Aidha, miongoni mwa vitu vya awali ambavyo baadhi ya watu wanavifikiria ni kwamba, kwa kuwa ni kitabu cha kale kilichokuja kutoka jangwani, kilipaswa kuzungumzia mambo ya jangwani. Ndiyo, Qur‟an imezungumzia kuhusu jangwa – baadhi ya tamathali zake zinaelezea jangwa; lakini pia inazungumzia bahari -- kuhusu kuwa kwenye bahari yenye dhoruba...

Citation preview

QUR‟AN NI YA AJABU

Gary Miller

Imetafsiriwa na:

Ibrahim H. Kabuga

Islamic Centre for Research (ICR)

Dar es Salaam - Tanzania

2

Qur'an kuipa jina la „Kitabu cha Ajabu‟ sio jambo lililofanywa na Waislamu pekee,

ambao wanaitambua na kuifurahia; bali pia imepewa jina hilo na Wasio Waislamu. Kwa

kweli, hata wale wanaouchukia Uislamu kupita kiasi wameendelea kuipa sifa hiyo ya kuwa

Qur'an ni ya Ajabu.

Kitu kinachowashangaza wasio Waislamu wanaokichunguza kitabu hiki kwa ukaribu sana ni

kwamba, Qur'an inajitokeza mbele ya macho yao kuwa katika hali ambayo hawakuitarajia.

Wanachofikiri ni kwamba wana kitabu cha kale kilichotokea karne kumi na nne zilizopita

kutoka katika jangwa la Arabia; na walitarajia kitabu hicho kionekane kama kitabu cha kale

kutoka jangwani. Na kisha wanagundua kwamba hakifanani hata kidogo na vile

walivyotegemea. Aidha, miongoni mwa vitu vya awali ambavyo baadhi ya watu

wanavifikiria ni kwamba, kwa kuwa ni kitabu cha kale kilichokuja kutoka jangwani,

kilipaswa kuzungumzia mambo ya jangwani. Ndiyo, Qur‟an imezungumzia kuhusu jangwa

– baadhi ya tamathali zake zinaelezea jangwa; lakini pia inazungumzia bahari -- kuhusu

kuwa kwenye bahari yenye dhoruba.

Miaka kadhaa iliyopita, kuna kisa kilitufikia kutoka Toronto kikimhusu mmoja aliyekuwa

akisafiri ndani ya meli ya biashara na kukaa muda mrefu baharini na kuwa na uzoefu

mkubwa wa mambo ya bahari. Mwislamu mmoja alimpatia Qur‟an yenye tafsiri ili apate

kuisoma. Mfanyabiashara huyo hakuwa akijua chochote kuhusu historia ya Uislamu lakini

alivutika kuisoma Qur‟an. Alipomaliza kuisoma alimrejeshea Mwislamu kitabu hicho na

kumuuliza: “Je, Muhammad alikuwa baharia?” alikuwa amevutiwa na jinsi Qur‟an

ilivyoielezea bahari yenye dhoruba kwa umakini mkubwa (hali ya dhoruba kwenye bahari).

Alipoambiwa kuwa “Hakika Muhammad aliishi jangwani”, jawabu hilo lilimtosheleza

kabisa. Alisilimu hapo hapo. Alivutiwa na maelezo hayo ya Qur‟an kwa sababu amekuwa

katika bahari yenye dhoruba, na alijua kwamba yeyote yule aliyekuwa ameandika maelezo

hayo naye angekuwa ameishi kwenye bahari nyenye dhoruba. Maelezo yasemayo “mawimbi

juu ya mawimbi, na juu yake yakiwepo mawingu” sio maelezo ya mtu asiyejua jinsi dhoruba

ya bahari inavyokuwa, bali ni maelezeo ya mtu aijuaye vema hali halisi ya dhoruba

inavyokuwa. Huu ni mfano mmoja tu wa jinsi ambavyo Qur‟an haikujifunga kwenye sehemu

moja na muda mmoja tu. Kwa hakika, mawazo na nadharia za kisayansi zilizoelezwa ndani

ya Qur‟an Tukufu hayaonekani kuwa yalitoka jangwani karne kumi na nne zilizopita.

Kwa karne nyingi kabla ya utume wa Muhammad, palikuwepo na nadharia maarufu ya kitu

kiitwacho „atom‟ (kitu kidogo mno au chembe) iliyoendelezwa na mwanafalsafa wa

Kigiriki, Democritus. Mwanafalsafa huyo pamoja na wale waliokuja baada yake walikuwa

na fikra kwamba maada („matter‟) ni muungano wa chembe chembe ndogo mno, zisizoweza

kuharibiwa, zisizochanguka au kugawanyika ziitwazo atomu. Waarabu nao pia walikuwa na

fikra hiyo hiyo, ambapo neno la Kiarabu liitwalo „dharrah‟ kwa kawaida lilitumika

kumaanisha kitu kidogo zaidi kuliko kitu chochote kile. Leo hii, sayansi mpya imegundua

3

kuwa maada hii ndogo kuliko maada zote (yaani, „atom‟ yenye sifa sawa na „element‟ yake)

inaweza kugawanywa katika vipande vidogo vidogo zaidi. Hili ni wazo au nadharia mpya

iliyoibuliwa karne iliyopita, lakini kitu kinachovutia ni kwamba, ilikuwa imeshathibitishwa

na Qur‟an Tukufu inayoeleza: “Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata

wa chembe (dharrah) katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho ….” Bila shaka, lau kama maelezo hayo yangetolewa katika zama hizo za karne kumi na nne

zilizopita, yangeonekana kuwa ya ajabu hata kwa Mwarabu mwenyewe. Kwani kwake yeye,

„dharrah‟ ndicho kilichokuwa kitu kidogo zaidi kuliko vitu vyote. Kwa hakika, huu ni

uthibitisho kuwa Qur‟an Tukufu haijapitwa na wakati.

Mfano mwingine wa kitu ambacho mtu angetegemea kukikuta katika “kitabu cha zamani”

kinachozungumzia maudhui ya afya na tiba ni dawa na tiba zilizopitwa na wakati.

Wanahistoria mbalimbali wanaeleza kuwa Mtume (s.a.w.) alitoa ushauri kadhaa kuhusu afya

na usafi, lakini ushauri huu haukujumuishwa ndani ya Qur‟an Tukufu. Kwa mara ya kwanza,

wale wasiokuwa Waislamu wanaweza kuona suala hili la kutojumuisha ushauri huo wa

Mtume ndani ya Qur‟an kuwa ni uzembe mkubwa. Hawawezi kujua kwa nini Mwenyezi

Mungu “hakujumuisha” taarifa hizo, muhimu na zenye manufaa, ndani ya Qur‟an Tukufu.

Baadhi ya Waislamu wanajaribu kufafanua jambo hili kwa hoja ifuatayo: “Ingawa ushauri na

maelekezo ya Mtume vilikuwa sahihi na vyenye manufaa kwa zama alizoishi, Mwenyezi

Mungu kwa Hekima Yake isiyo na kikomo, alijua kwamba baadaye yangekuja maendeleo ya

tiba na sayansi ambayo yangeufanya ushauri wa Mtume uonekane kuwa uliopitwa na wakati.

Pindi ambapo ugunduzi mbalimbali ungetokea, watu wangesema kwamba taarifa za

ugunduzi huo zinapingana na zile zilizotolewa na Mtume. Hivyo basi, kwa kuwa Mwenyezi

Mungu asingeruhusu kuwepo na mwanya wowote kwa wasiokuwa Waislamu kudai kwamba

Qur‟an inajipinga yenyewe au ni mafundisho ya Mtume, ndio maana ndani ya Qur‟an

akaweka taarifa na mifano ambayo ingeweza kufaulu mitihani na majaribio ya kila aina ya

wakati au zama”.

Hata hivyo, tukichunguza ukweli hasa wa Qur‟an katika namna ya kwamba ni ufunuo wa

Mwenyezi Mungu, suala zima laweza kupata kuchambuliwa haraka na kwa njia sahihi, na

makosa yaliyopo katika hoja hiyo hubainika na kueleweka. Lazima ieleweke kuwa Qur‟an ni

ufunuo wa Mwenyezi Mungu, na kwa hiyo, habari zote zilizomo ndani yake zinatoka kwa

Mwenyezi Mungu. Allah aliiteremsha Qur‟an kutoka kwake Mwenyewe. Quir‟an ni neno la

Mwenyezi Mungu lililokuwepo kabla ya kuumbwa kwa kitu chochote, na kwa maana hiyo

hakuna kinachoweza kuongezwa, kupunguzwa au kuondolewa. Kimsingi, Qur‟an ilikuwepo

na ilikuwa kamili kabla ya kuumbwa kwa Mtume Muhammad, na hivyo isingewezekana

kuwa na neno au ushauri wowote wa Mtume mwenyewe. Ujumuishaji wa habari hizo

ungepingana, kwa uwazi kabisa, na malengo ya kuwepo kwa Qur‟an, kuhatarisha mamlaka

yake na kuitoa katika usahihi wake kama ufunuo wa Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo, ndani ya Qur'an hakuna "tiba za ndani/nyumbani" (home remedies) ambazo mtu

angeweza kudai kuwa zimepitwa na wakati; wala ndani yake hakuna maoni ya mwanadamu

kuhusu kitu chenye manufaa kwa afya, chakula kinachopaswa kuliwa, au dawa inayoweza

4

kuponya ugonjwa huu au ule. Qur'an Tukufu inataja kitu kimoja tu kinachohusika na

matibabu, na kitu hicho hakipingwi na yeyote. Inaeleza kuwa kuna ponyo ndani ya asali. Na

bila shaka, sidhani kuwa kuna mtu atakayebisha ukweli huo!

Kama mtu atakuwa na fikra ya kwamba Qu'an ni zao la akili ya mwanadamu, basi mtu huyo

atategemea kitabu kiakisi baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiendelea katika akili ya

mwanadamu huyo "aliyeitunga" (composed). Baadhi ya ensaiklopidia na vitabu kadhaa

vinadai kwamba Qur'an ni zao la "maradhi ya kuona kisichokuwepo/ kusikia sauti

zisizokuwepo" (hallucinations) yaliyokuwa yamemkumba Muhammad. Kama madai haya

ni ya kweli --– iwapo kweli ilitokana na matatizo ya kisaikolojia katika akili ya Muhammad -

-- basi ushahidi wa madai hayo ungeonekana wazi ndani ya Qur'an. Lakini je, ushahidi huo

upo? Ili kuchunguza kama yapo au hayapo, yatakiwa kwanza kuainisha kile ambacho

kingekuwa kikiendelea katika akili yake wakati huo na kisha kuzichunguza fikra na mawazo

hayo ndani ya Qur'an.

Inafahamika na kila mtu kwamba Muhammad aliishi maisha ya shida sana. Mabinti zake

walifariki kabla yake isipokuwa mmoja tu, na alikuwa na mke mwenye umri mkubwa

aliyekuwa mpendwa wake na muhimu kwake, na ambaye alimtangulia kufariki dunia wakati

Muhammad akiwa katika kipindi muhimu sana cha maisha yake. Kusema kweli alikuwa

mwanamke wa kipekee, kwa sababu ufunuo wa mwanzo ulipomfikia Mtume alikimbilia kwa

mkewe huyo akiwa ni mwenye hofu kubwa. Bila shaka, hata leo hii utakuwa na wakati

mgumu ukijaribu kumtafuta Mwarabu atakayekwambia, “Nilikuwa na hofu kubwa

nikakimbilia nyumbani kwa mke wangu”. Hawako hivyo. Lakini Muhammad alijisikia

mwenye utulivu na kuliwazika kwa mke wake kwa kiasi cha kuweza kufanya hivyo. Hivyo

ndivyo mwanamke huyo alivyokuwa mhimili na nguzo imara kwake. Ingawa mifano hiyo ni

michache kuhusu maudhui ya mambo ambayo yangekuwa katika akili ya Muhammad,

inatosha sana kuthibitisha hoja yangu. Pamoja na umuhimu wa mambo hayo kwa

Muhammad Qur‟an haitaji hata jambo moja katika hayo --- haitaji kifo cha wanawe, wala

kifo cha mkewe mpendwa, wala hofu aliyokuwa nayo mwanzoni mwa kupewa ufunuo,

ambayo alimshirikisha mkewe --- haikutaja chochote; kama vitu hivyo vitakuwa

vimemuumiza, kumchukiza, na kumsababishia maumivu na msongo wakati wa matatizo ya

wasiwasi wa kisaikolojia, basi vitu hivyo vingeonekana wazi au angalau hata kutajwa kila

mahali ndani ya Qur‟an.

Mtazamo halisi wa kisayansi juu ya Qur‟an unawezekana, kwa sababu Qur‟an imekuja na

kitu ambacho hakijapokelewa katika maandiko mengine ya kidini, na hakijaletwa pia na dini

nyingine kwa ujumla. Ni kitu kinachohitajiwa na wanasayansi. Leo hii kuna watu wengi

wenye mawazo na nadharia kuhusu ulimwengu unavyofanya kazi. Watu hawa wapo kila

mahali, lakini jamii ya wanasayansi haisumbuki hata kuwasikiliza. Hii inatokana na sababu

kwamba katika kipindi cha karne iliyopita jamii ya wanasayansi (scientific community)

iliweka kipimo cha kupima/kuthibitisha ukweli au uwongo wa nadharia fulani (test of

falsification). Wakasema, “kama una nadharia, usitusumbue nayo mpaka utapotuletea

5

nadharia hiyo na njia ya kutuwezesha kuipima kama inamakosa au la (------ unless you

bring with that theory a way for us to prove whether you are wrong or not)”.

Kipimo kama hicho ndio hasa kiliifanya jamii hiyo ya wanasayansi imsikilize Einstein

kuelekea mwanzoni mwa karne hiyo. Yeye alikuja na nadharia mpya na kusema, “Ninaamini

kuwa ulimwengu (universe) unafanya kazi hivi; na hapa kuna njia tatu za kuthibitisha

kama mimi sipo sahihi!” Hivyo, jamii hiyo ya wanasayansi waliipima nadharia hiyo kwa

kutumia vipimo (tests), na ndani ya miaka sita jamii hiyo ilizipitisha njia zote tatu. Hata

hivyo, hii haina maana kuwa alikuwa mtu mkubwa, bali yathibitisha kuwa alistahiki

kusikilizwa kwa sababu alisema, “Hii ni nadharia yangu; na kama mnataka kujaribu

kuthibitisha kama mimi ni muongo, fanyeni hivi au jaribuni vile”. Hili ndilo hasa lililoletwa

na Qur‟an --- vipimo vya kuthibitisha uwongo au ukweli wa kitu. Baadhi yake ni za kitambo

(na hivyo zimeshathibitishwa kuwa ni za kweli), na baadhi bado zipo hadi leo. Kimsingi

inasema, “Iwapo kitabu hiki ni kinyume na kinavyodai kuwa, basi mnachotakiwa

kufanya ni hiki au hiki au hiki ili kuthibitisha kuwa ni uwongo”. Na sasa, katika kipindi

cha miaka 1400 hakuna aliyeweza kufanya “Hili au hili au hili,” na hivyo mawazo hayo ya

Qur‟an yameendelea kuwa kweli na sahihi. Ninakushauri kwamba ikitokea kubishana na mtu

kuhusu Uislamu na akadai kuwa anao ukweli na kwamba wewe uko gizani, achana na hoja

zote kwanza na mpe wazo hili. Muulize: “Je, katika dini yako kuna kipimo chochote cha

kuthibitisha uwongo au ukweli wa jambo fulani? Je, katika dini yako kuna chochote

kinachoweza kuthibitisha kama upo kwenye makosa na iwapo nitaweza kuthibitisha uwepo

wa makosa hayo? Nakuahidi kuwa watu hao hawatokuwa nauthibitisho wowote --–

hawatokuwa na kipimo, kithibitisho wala chochote! Kwa sababu hawana mawazo kwamba

hawatakiwi tu kuwasilisha kile wanachokiamini bali pia wanatakiwa kuwapa wengine nafasi

ya kuthibitisha kama wako sahihi katika wanacho kiamini au la. Hata hivyo, Uislamu unatoa

nafasi hiyo kwa watu kuthibitisha usahihi wa imani au uwongo wake. Mfano kamili wa

namna Uislamu unavyompa mtu nafasi ya kuthibitisha usahihi au “kuthibitisha kuwa hauko

sahihi”, mfano huo unapatikana katika Sura ya 4. Kwa kweli kabisa, nilishikwa na mshangao

nilipoigundua changamoto hii kwa mara ya kwanza. Sura inasema:

"Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kama ingekuwa imetoka kwa asiye kuwa

Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi."

Hii ni changamoto ya wazi kwa asiyekuwa-Mwislamu. Kimsingi inamuita kutafuta kosa hata

moja. Kiukweli, uzito na ugumu wa changamoto hii kwa upande mmoja, uwasilishaji hasa

wa changamoto hiyo katika sehemu ya kwanza haipo hata katika maumbile ya mwanadamu

na hailingani na jinsi mwanadamu alivyo. Mtu hafanyi mtihani shuleni baada ya kumaliza

mtihani husika, mwisho akamuandikia mwalimu husika maelezo na kumtaarifu akisema:

“Huu mtihani ni mkamilifu. Hakuna makosa hata kidogo. Tafuta kosa hata moja kama

unaweza!”. Hakuna afanyaye hivyo. Akifanya hivyo mwalimu hatolala mpaka alione kosa!

Na sasa hivi ndivyo Qur‟an inavyowaambia watu. Msimamo mwingine wa Qur‟an unaovutia

sana na unaojirudia rudia sana unahusu namna Qur‟an inavyomshauri yule anayeisoma.

Qur‟an inamweleza msomaji kuhusu mambo tofauti tofauti kisha inampa ushauri: “Kama

6

unataka kujua zaidi kuhusu kitu hiki au kile, au kama una shaka na kinachosemwa,

basi waulize wenye elimu na maarifa”. Huu ni msimamo unaoshangaza sana. Sio jambo la

kawaida kabisa kuona kitabu kutoka kwa mtu ambaye hakusoma jiografia, botania, baiolojia,

n.k., anayezungumzia masomo haya kisha akamshauri msomaji kuwauliza watu wenye elimu

na maarifa kama atakuwa na shaka juu ya chochote.

Katika kila zama wamekuwepo Waislamu ambao wamefuata ushauri wa Qur‟an na

wakafanya ugunduzi wa hali ya juu. Ukizitazama kazi au vitabu vya wanasayansi wa

Kiisalmu wa karne kadhaa zilizopita, utavikuta vitabu hivyo vikiwa vimejaa nukuu kutoka

ndani ya Qur‟an Tukufu. Vitabu hivi vinatoa maelezo kuwa watu hao walifanya utafiti katika

mahali fulani, wakitafuta kitu fulani. Na vinathibitisha kuwa sababu iliyowafanya watazame

sehemu fulani na sehemu fulani ni kwa kuwa Qur‟an iliwaonyesha kwenda upande fulani au

uelekeo huo. Kwa mfano, Qur‟an yaelezea asili ya mwanadamu na kumwambia msomaji,

“Ifanyie utafiti!” Inampa msomaji dokezo au mahali pa kutazama na kisha inamueleza mtu

huyo kwamba atafute zaidi kuhusu kitu hicho. Hiki ni kitu ambacho kwa kiasi kikubwa

Waislamu wa leo hawakitilii maanani- ingawa sio wote, kama inavyoonesha katika mfano

ufuatao. Miaka michache iliyopita, kundi la watu mjini Riyadh, Saudi Arabia walizikusanya

aya zote za Qur‟an zinazozungumzia embrolojia -–- maendeleo ya mwanadamu katika

tumbo la uzazi. Wakasema: “Hivi ndivyo isemavyo Qur‟an. Je, ni kweli?” Wakachukua

ushauri wa Qur‟an: “Waulizeni wanaojua”. Kama ilivyotokea, wakamteua Profesa

asiyekuwa Mwislamu kutoka Chuo Kikuu cha Toronto (Kanada). Jina la Profesa huyo ni

Keith Moore, naye ni mtunzi wa vitabu mbalimbali vinavyozungumzia embrolojia – ni

mtaalamu mashuhuri ulimwenguni katika somo hilo. Walimualika mjini Riadh na

kumwambia, “Hivi ndivyo isemavyo Qur‟an kuhusu somo lako. Je, ni kweli? Wasemaje?”

Alipokuwa Riyadh, walimpatia kila aina ya msaada aliouhitaji katika kutafsiri na kumpa

ushirikiano wote aliouomba. Alishangazwa sana na kile alichokigundua kwa kiasi kwamba

alivifanyia mabadiliko vitabu vyake. Katika toleo la pili la mojawapo ya vitabu vyake

kiitwacho “Before we are born”, katika toleo la pili kuhusu historia ya emrolojia, aliongeza

baadhi ya mambo ambayo hayakuwepo katika toleo la kwanza, kutokana na kile

alichokigundua ndani ya Qur‟an Tukufu. Kwa hakika jambo hili laonyesha kwamba Qur‟an

imeutangulia wakati na kwamba wale wanaoiamini Qur‟an wanajua mambo ambayo watu

wengine hawayajui.

Nilipata bahati ya kufanya mahojiano kwa ajili ya kipindi cha televisheni na Dr. Keith

Moore, na tulizungumzia sana kuhusu suala hili. Alitaja baadhi ya vitu vinavyoelezewa na

Qur‟an kuhusu ukuaji wa binadamu katika tumbo la uzazi ambavyo vimekuja kujulikana

miaka thelani tu iliyopita. Alisema kuwa kitu kimoja –-- maelezo ya Qur‟an juu ya

mwanadamu kuwa “donge lenye muonekano wa luba” (leech-like clot = „alaqah‟) katika

hatua moja ---- lilikuwa ni jambo jipya kwake; lakini alipolitazama kwa utafiti alikuta

kwamba ni kweli, na hivyo akakiongeza katika kitabu chake. Alisema, “Hapo kabla sikuwa

na fikra kama hiyo”, akaenda kwenye idara ya zuolojia akaomba picha ya luba. Alipokuta

kwamba ilifanana na kiinitete cha binadamu, aliamua kuzijumuisha picha zote mbili kwenye

mojawapo ya vitabu vyake. Dr. Moore pia aliandika kitabu kuhusu uhalisia wa embrolojia

7

(clinical embryology), na pindi alipowasilisha habari hizi mjini Toronto, zilisababisha

msukosuko ndani ya Kanada nzima. Iliandikwa katika kurasa za mbele za magazeti nchini

kote Kanada, na baadhi ya vichwa vya habari vilikuwa ni vyenye kuchekesha. Kwa mfano

kichwa kimoja cha habari kilisomeka: "SURPRISING THING FOUND IN ANCIENT

BOOK!" (KITU CHA AJABU CHAGUNDULIWA NDANI YA KITABU CHA KALE!).

Kutokana na mfano huu inaonekana wazi kuwa watu hawajui hasa kitu hicho ni kitu gani.

Mwandishi wa gazeti moja alimuuliza Profesa Moore, "Hufikiri kuwa huenda Waarabu

watakuwa wamevijua vitu hivi –-- maelezo kuhusu kiinitete, muonekano wake

kinavyobadilika na kukua? Huenda hapakuwepo na wanasayansi, lakini huenda watu hao

walifanya uchunguzi wao kwa kupasua sehemu za mwili na kuzichunguza na kisha

kugundua vitu hivi”.

Bila kuchelewa Profesa akamfahamisha kuwa yeye (yaani huyo mwandishi wa habari)

alikuwa amekosa pointi ya msingi sana- picha zote za kiinitete (embryo) ambazo zimekuwa

zikiioneshwa zimetengenezwa kwa mkanda wa filamu kutoka kwenye picha zilizochukuliwa

kupitia hadubini (microscope). Akaendelea kusema: “Sio tatizo kama mtu alikuwa

amejaribu kugundua embrolojia karne kumi na nne zilizopita, wasingeweza kuiona!”

Maelezo yote yaliyomo ndani ya Qur‟an kuhusu muonekano wa kiinitete yanahusu kitu

kinapokuwa bado kidogo sana kwa kiasi cha kutoonekana kwa macho; hivyo inahitajika

hadubini (microscope) kukiona. Kwa kuwa kifaa hicho hakina muda wa zaidi ya miaka mia

mbili tangu kuwepo kwake, Dr. Moore akasema kwa dhihaka: “Labda karne kumi na nne

zilizopita kuna mtu alikuwa na hadubini kwa njia ya siri na akafanya utafiti huu, bila

kukosea mahali popote. Kisha kwa namna fulani akamfundisha Muhammad na kumshawishi

aziweke habari hizi ndani ya kitabu chake. Kisha mtu huyo akakiharibu kifaa chake hicho

(hadubini) na kukifanya kuwa siri daima. Je, kweli waamini hivyo? Kwa hakika hupaswi

kuamini hivyo ila kama utaleta uthibitisho kwa sababu hiyo ni nadharia inayochekesha”.

Alipoulizwa kuwa: “Unaielezeaje habari hii iliyomo ndani ya Qur‟an?” Dr. Moore alijibu:

“Habari hii itakuwa tu iliteremshwa na Mwenyezi Mungu”.

Ingawa mfano uliotajwa hapo juu wa mtu kutafuta taarifa zilizomo ndani ya Qur‟an Tukufu

imefanywa na kuhusishwa na asiyekuwa mwislamu, bado ni sahihi kwa sababu mtu huyo

alikuwa miongoni mwa wale wenye maarifa katika mada na maudhui husika. Kama mtu

asiye mtaalamu angedai kuwa kinachosemwa na Qur‟an kuhusu embrolojia ni kweli, basi

bila shaka hakuna mtu ambaye angetakiwa kuyakubali maneno yake. Hata hivyo, kwa

sababu ya daraja, heshima na hadhi kubwa wanayopewa wasomi, basi kwa asili, mtu

hukubali kwamba kama wanachuoni hao wamefanya utafiti na kufikia hitimisho la utafiti

huo, hitimisho hilo litakuwa sahihi. Miongoni mwa walimu wenzi wa Profesa Moore, Bwana

Marshall Johnson, anajishughulisha sana na masuala ya jiolojia katika Chuo Kikuu cha

Toronto (Kanada).

Alivutiwa na ukweli kwamba maelezo ya Qur‟an kuhusu embrolojia ni sahihi, na hivyo

akawaomba Waislamu wakusanye maandiko yote ya Qur‟an yanayozungumzia na

kushughulikia utaalamu wake huo (wa Jiolojia). Kwa mara nyingine watu walishangazwa na

8

matokeo ya utafiti huo. Kwa kuwa kuna idadi kubwa ya maudhui zilizozungumziwa ndani ya

Qur‟an, kitahitajika kiwango kikubwa cha muda kuizungumzia sana kila maudhui. Kwa

malengo ya mada hii inatosha kueleza kwamba Qur‟an inayaweka wazi sana na kwa

mukhtasari maelezo mbalimbali kuhusu mada mbalimbali huku ikimshauri msomaji kwa

msisitizo kuthibitisha usahihi na ukweli wa maelezo hayo kwa kutumia utafiti uliofanywa na

wasomi mbalimbali kuhusu mada husika. Na kama ilivyoonyeshwa na Qur‟an, maelezo yake

yamedhihirika kuwa sahihi na kweli bila shaka yoyote.

Ndani ya Qur‟an kuna msimamo na maelezo ambayo hayapatikani mahali popote pengine.

Inavutia sana pale Qur‟an inapotoa taarifa fulani, ambapo mara zote humwambia msomaji,

“Hapo awali hukuwa ukilijua hili”. Kwa kweli, hakuna maandiko yoyote mengine ya

kidini yaliyopo sasa yanayotoa madai kama hayo. Vitabu na Maandiko mengine yote ya

zamani ambayo watu wanayo, yanatoa taarifa nyingi tu, lakini mara zote hueleza mahali

taarifa hizo zilipotoka.

Kwa mfano, Biblia inazungumzia historia ya mambo ya kale, inaeleza kuwa mfalme huyu

aliishi hapa, huyu alipigana vita fulani, mwingine alikuwa na watoto wengi, n.k. Lakini mara

zote inasema kwamba kama unataka taarifa zaidi, basi watakiwa kusoma kitabu kile na kile

kwa sababu hapo ndipo taarifa hizo zilipotoka. Kinyume na fikra hii, Qur‟an Tukufu humpa

msomaji habari fulani na kumweleza kuwa habari hii ni mpya. Hata hivyo, Qur‟an imekuwa

ikitoa ushauri wa kuifanyia utafiti habari iliyotolewa na kuthibitisha usahihi wake. Inavutia

sana kwamba fikra hiyo kamwe haikuhojiwa na wasio Waislamu karne kumi na nne

zilizopita. Kwa kweli, makafiri wa Makka walikuwa wakiwachukia sana Waislamu, lakini

mara zote waliposikia ufunuo kama huo unaodai kuleta habari mpya; hawakufungua vinywa

vyao na kusema, “Habari hii sio mpya. Tunajua Muhammad alipoitoa habari hii. Habari hii

tuliisoma shuleni, n.k.”

Hawakuhoji usahihi wake kwa sababu ni kweli kuwa habari hizo kwao zilikuwa ni mpya!

Katika kwenda sambamba na ushauri wa Qur‟an unaotaka watu waitafiti habari fulani (hata

kama ni mpya), pindi Omar alipokuwa Khalifa, aliteua kikundi cha watu na kuwatuma

kwenda kutafuta ukuta wa Dhul-Qarnayn. Kabla ya kuteremka kwa Qur‟an, Waarabu

hawakuwa na taarifa yoyote ya ukuta huo, lakini kwa sababu Qur‟an iliuelezea, waliweza

kuugundua. Ukuta huo upo katika eneo liitwalo Durbend katika Umoja wa nchi za Kisovieti

(Soviet Union). Hapa ni lazima kusisitiza kuwa Qur‟an ni sahihi kuhusu mambo yote

iliyoyazungumzia, lakini usahihi haumaanishi kwamba kitabu fulani kimeteremshwa na

Mwenyezi Mungu. Bali usahihi ni miongoni mwa vigezo vya ufunuo wa Mwenyezi Mungu.

Kwa mfano, kitabu cha simu ni sahihi, lakini haina maana kuwa kimeteremshwa na

Mwenyezi Mungu. Suala la msingi hapa ni kwamba mtu anatakiwa kuweka uthibitisho wa

chanzo cha taarifa za Qur‟an. Msisitizo umewekwa kwa msomaji.Mtu hawezi tu kukanusha

usahihi na ukweli wa Qur‟an bila ushahidi na uthibitisho wa kutosha. Kama kweli akikuta

kosa, ana haki ya kuiondolea sifa ya usahihi. Hili ndilo linalohamasishwa hasa na Qur‟an.

Siku moja mtu mmoja alinijia baada ya hotuba niliyoitoa Afrika ya Kusini. Alikuwa

9

amekasirishwa na kile nilichokisema, na hivyo akasema: “Nitakwenda nyumbani usiku huu

na kutafuta makosa ndani ya Qur‟an”. Bila kusita nikamwambia: “Hongera! Hilo ulilosema

ni jambo la akili sana”. Kwa hakika, hivi ndivyo Waislamu wanavyotakiwa kushughulika na

wale wenye shaka ya usahihi wa Qur‟an, kwa sababu Qur‟an yenyewe yatoa changamoto

kama hiyo. Baada ya wao kuikubali changamoto hii na kugundua kwamba ni kweli, lazima

wataiamini kwa sababu hawakuweza kuthibitisha uwongo wa yale iliyoyaeleza. Kwa msingi

huo, watapata kuiheshimu Qur‟an kwa sababu wao wenyewe ndio waliolazimika kuthibitisha

usahihi wake. Jambo la msingi ambalo haliwezi kurudiwa kusemwa kuhusu usahihi na

ukweli wa Qur‟an ni kwamba hali ya mtu mwenyewe kutoweza kufafanua tukio fulani

haihitaji yeye kukubali uwepo wa tukio hilo au ufafanuzi wa mtu mwengine kuhusu tukio

husika.

Kwa maana kwamba, sababu tu ya mtu kutoweza kufafanua kitu fulani haimaanishi kwamba

lazima akubali maelezo ya mtu mwengine. Hata hivyo, hatua ya mtu kuyakataa maelezo na

ufafanuzi wa watu wengine humuongezea mzigo wa kutafuta jibu stahili. Nadharia hii ya

jumla inahusika katika fikra na mambo mengi katika maisha, lakini inaendana kwa namna ya

ajabu na changamoto zinazotolewa na Qur‟an, kwani inatengeneza ugumu na uzito kwa yule

asemaye, “Siiamini”. Pale tu anapokataa, bila ya kuchelewa huwa ana wajibu wa kutafuta

ufafanuzi yeye mwenyewe kama atahisi kwamba majibu ya watu wengine hayajitoshelezi.

Katika mojawapo ya aya za Qur‟an, ambayo mara nyingi nimeona ikitafsiriwa vibaya katika

lugha ya Kiingereza, Mwenyezi Mungu anamtaja mtu aliyeusikia ukweli aliofafanuliwa.

Inaeleza kwamba itabakia ni dhima yake mtu iwapo baada ya kusikia taarifa hiyo aliikubali

bila kuichunguza usahihi wa kile alichokisikia. Kwa maneno mengine, mtu anakuwa ni

mwenye hatia kama atakisikia kitu na akakifuata wakati hajakitafiti na kukichunguza kama

kina usahihi au la. Anatakiwa kuchambua taarifa zote na kuamua ni zipi ambazo ni takataka

zitupwe na zipi yenye faida zihifadhiwe na kutumika katika siku za baadaye. Mtu hatakiwi

kuzizunguusha tu taarifa kichwani bila kujihakikishia ukweli wake. Inatakiwa kuwekwa

katika orodha sahihi na kushughulika nayo kwa mtazamo sahihi. Kwa mfano, kama taarifa

husika bado ipo katika mazingira ya makisio, basi atatakiwa kutambua iwapo ipo karibu na

ukweli au ipo jirani na uwongo. Lakini iwapo mambo yote husika yamewasilishwa mbele

yake, basi anatakiwa kuamua hasa kati ya machaguo haya mawili. Na kama hatokuwa

chanya kuhusu ukweli na usahihi wa taarifa hiyo, bado analazimika kuchambua taarifa zote

na kukiri kwamba hajui kwa uhakika. Ingawa nukta hii ya mwisho yaonekana kutokuwa na

maana, kiukweli, inakuwa na faida pindi ufikapo katika hitimisho zuri hapo baadaye, jambo

ambalo humlazimu mtu angalau kutambua, kufanya utafiti na kugundua ukweli. Hali hii ya

kuwa na mazoea na taarifa hiyo humpa mtu huyo “kinga” pindi ugunduzi unapofanyika hapo

baadaye na taarifa za ziada zikawasilishwa. Kitu cha msingi ni kwamba mtu huyakabili

mambo na hawezi kuyakimbia kwa kutokuwa na uwezo na kuhisi kutofaidika.

Uhakika halisi wa ukweli wa Qur‟an unaonekana wazi katika hali ya kujiamini sana iliyomo

kwa wingi ndani yake; na kujiamini huku kunatoka katika maeneo mbalimbali ----"kwa

kutumia vibadala (alternatives)." Kimsingi, Qur‟an inasema, “Kitabu hiki kimeteremshwa

na Mwenyezi Mungu; kama huliamini hilo, basi ukweli ni upi?” Kwa maneno mengine,

10

msomaji anapewa changamoto ya kuja na maelezo mengine. Hapa kuna kitabu

kilichotengenezwa kwa karatasi na wino. Kilitoka wapi? Kinasema kwamba kiliteremshwa

na Mwneyezi Mungu; kama sio, sasa nini chanzo chake? Jambo la kuvutia ni kwamba

hakuna mwenye maelezo yanayokubalika.

Kwa kweli, vibadala (alternatives) vyote hivyo vimezungumziwa. Kama inavyokubalika pia

na wasio-Waislamu, vibadala hivi kimsingi vimepunguzwa na kuwa mambo mawili

yanayojumuisha pande mbili za kifikra, msisitizo ukiwekwa kwenye kukubali jambo

mojawapo. Kwa upande mmoja, lilijitokeza kundi kubwa la watu lililofanya utafiti kuhusu

Qur‟an kwa kipindi cha mamia ya miaka na ambalo linadai, “Kitu kimoja tunakijua kwa

uhakika –-- kwamba mtu huyo, Muhammad, alikuwa na fikra kwamba yeye ni mtume. Yeye

ni mwendawazimu!” Wanashawishika kwamba Muhammad alilaghaiwa kwa namna fulani.

Kisha kwa upande mwengine, kuna kundi jingine linalotoa madai kuwa, “Kwa sababu ya

ushahidi huu, kitu kimoja tunakijua kwa uhakika kwamba, mtu huyo, Muhammad, alikuwa

mwongo!” Kwa kejeli, makundi haya mawili kamwe hayaonekani kuwa pamoja bila

migongano na kupingana. Kwa kweli, rejea nyingi zinazozungumzia Uislamu kwa kawaida

hutoa madai ya nadharia zote mbili. Huanza kwa kudai kwamba Muhammad (s.a.w.) alikuwa

mwendawazimu na kisha kuishia kudai kuwa alikuwa mwongo. Kamwe hawaonekani

kutambua kuwa asingeweza kuwa na sifa zote hizo mbili (yaani awe muongo na wakati

huohuo awe mwendawazimu)!

Kwa mfano, kama mtu amehadaiwa na akadhani kweli kuwa yeye ni mtume, basi hawezi

tena kukaa usiku kucha akipanga, “Kesho nitawadanganyaje watu ili wafikiri kuwa mimi ni

mtume?” Anaamini kweli kwamba yeye ni mtume, na anategemea kuwa atapewa jibu kwa

njia ya ufunuo. Kiukweli, sehemu kubwa ya Qur‟an ilikuja kujibu maswali mbalimbali. Mtu

alikuwa akimuuliza Muhammad (s.a.w.), na jibu lililetwa na ufunuo. Kwa hakika, kama mtu

ni mwendawazimu na akaamini kuwa malaika humnong‟oneza neno sikioni mwake, na kisha

mtu atapomuuliza swali fulani, yeye hufikiri kuwa malaika atampa jibu. Kwa sababu yeye ni

mwendawazimu, kweli atafikiri hivyo. Hatomwambia mtu aliyemuuliza swali asubiri kidogo

na kisha akakimbilia kwa rafiki zake na kuwauliza, “Je, kuna yeyote mwenye jibu la swali

aliloulizwa?” Tabia hii ni sifa ya mtu asiyeamini kuwa yeye ni mtume. Kitu ambacho

Wasiokuwa Waislamu wanakikataa kukikubali ni kwamba huwezi kuwa na sifa zote mbili.

Mtu anaweza kuhadaiwa, au anaweza kuwa muongo. Ima anaweza akawa na sifa moja na

asiwe na nyingine, lakini kwa hakika hawezi kuwa na sifa zote mbili! Msisitizo ulipo hapa ni

kwamba, sifa hizo mbili haziwezi kupatikana kwa mtu kwa pamoja (yaani awe

„mwendawazimu‟ na „muongo‟ kwa wakati mmoja).

Mukhtasari ufuatao ni mfano mzuri wa aina ya duara ambalo siku zote wasio Waislamu

huzunguka humo. Ukimuuliza mmoja wao: “Chanzo cha Qur‟an ni kipi?” Atakwambia

kwamba Qur‟an ilitoka katika akili ya mtu aliyekuwa mwendawazimu. Ukimuuliza tena:

“Kama ilitoka katika kichwa chake, taarifa zilizomo ndani ya kitabu hicho alizipata wapi?

Kwa hakika Qur‟an inaeleza vitu vingi ambavyo havikuwa vikijulikana kwa Waarabu”. Ili

kuukabili ukweli ambao umempa, atabadilisha msimamo wake na kusema: “Sawa, huenda

11

hakuwa mwendawazimu. Huenda kuna mtu fulani mgeni alimpa taarifa hizo. Hivyo, alificha

jambo hilo na kusema uwongo kwa kuwaambia watu kuwa ati yeye alikuwa mtume”. Hapo

utatakiwa kumuuliza: “Kama Muhammad alikuwa mwongo, alipata wapi hali ya kujiamini

(confidence)? Kwa nini alikuwa na tabia ya kana kwamba yeye ni mtume?” Mwishowe

akiwa amefika kwenye kona, kama paka, utamuona haraka sana akitupilia mbali jawabu lake

la mwanzo alilolitoa akilini mwake. Utamuona akidai, “Vyema, huenda hakuwa muongo.

Labda alikuwa mwendawazimu na akaamini kuwa yeye ni mtume”. Na hapo ataanza kurejea

mzunguuko wake kwenye duara lake kwa mara nyingine.

Kama ilivyokwishaelezwa hapo awali, ndani ya Qur‟an kuna taarifa na habari nyingi ambazo

chanzo chake hakiwezi kuwa kingine zaidi ya Allah. Kwa mfano, nani aliyemwambia

Muhammad kuhusu ukuta wa Dhul-Qarnayn --– ulioko umbali wa mamia ya maili huko

kaskazini? Nani aliyemwambia kuhusu embrolojia? Watu wanapokusanya mambo na ukweli

kama huu, iwapo hawataki kuuhusisha na Mwenyezi Mungu, utawaona wanakimbilia

kufikiri na kudhani kuwa kuna mtu aliyempa Muhammad taarifa hizi na kwamba alizitumia

kuwahadaa watu. Hata hivyo, fikra hiyo yenye chuki na inda inaweza kubatilishwa kwa

urahisi kwa swali moja jepesi: “Kama Muhammad alikuwa muongo, aliipata wapi hali ya

kujiamini (confidence)? Kwanini aliwaambia watu papo kwa papo yale ambayo watu

wengine hawakuweza kuyasema?” Hali kama hiyo ya kujiamini, moja kwa moja, inategemea

uwe na uhakika usiokuwa na shaka kwamba kweli unapewa ufunuo na Mwenyezi Mungu.

Kwa mfano: Mtume (s.a.w.) alikuwa na Ami yake aliyeitwa Abu Lahab. Mtu huyu alikuwa

akiuchukia sana Uislamu kwa kiasi kwamba alikuwa akimfuata Muhammad popote

alipokwenda kwa lengo la kuwafanya watu wasimuamini. Anapomuona Mtume (s.a.w.)

akizungumza na mtu mgeni, husubiri mpaka wanapoagana na kisha yeye (Abu Lahab)

huenda kwa mtu huyo na kumuuliza, “Alikwambia nini? Je, alikwambia „rangi Nyeusi‟?

Basi sio kweli, bali ni Nyeupe. Je, alisema „Asubuhi‟? Sio hivyo, ni usiku”. Alikuwa

akisema kinyume kabisa na kile alichomsikia Muhammad (s.a.w.) na Waislamu wakikisema.

Hata hivyo, miaka kumi kabla ya Abu Lahab kufariki dunia, Muhammad aliteremshiwa Sura

moja ndogo. Sura hiyo ilisema wazi kuwa Abu Lahab ataenda Motoni (Jahannam). Kwa

maneno mengine, ilithibitisha kwamba kamwe asingekuwa Mwislamu na hivyo angelaaniwa

milele. Kwa kipindi chote hicho cha miaka kumi, Abu Lahab angetakiwa kusema,

“Nimesikia kwamba Muhammad amefunuliwa ya kwamba kamwe sintobadilika --- kwamba

sintosilimu na nitaingia Jahannam. Sasa nataka kuwa Mwislamu. Mwasemaje? Sasa

mnaufikiriaje ufunuo wenu uliotoka kwa Mungu?” Lakini abadan hakufanya hivyo. Kwa

kuwa alikuwa akifanya juhudi za kuupinga Uislamu ilitarajiwa kwamba angefanya hivyo

(yaani angesilimu) ili afanikishe lengo lake la kuonyesha watu kuwa Uislamu hausemi

ukweli. Kimsingi, Muhammad (s.a.w.) alimwambia: “Je, wanichukia na wataka kunimaliza?

Sema haya maneno (kwamba umeukubali Uislamu), utakuwa umenimaliza. Tamka maneno

hayo!” Lakini Abu Lahab kamwe hakuyatamka. Miaka kumi! Na katika kipindi hicho chote

hakuukubali Uislamu au hata kuwa na huruma juu ya dini ya Kiislamu. Kama kweli

Muhammad hakuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwezaje kujua kwa uhakika kwamba

Abu Lahab angeyafanya maneno ya Qur‟an yathibitike kuwa ya kweli? Aliwezaje kujiamini

sana kwa kiasi cha kumpa mtu miaka kumi ya kuyaadhiri madai yake ya utume? Jibu pekee

12

ni kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu; kwani ili kuwasilisha changamoto

kama hiyo mbele ya watu, mtu huyo anatakiwa awe na uhakika wa moja kwa moja,

usiokuwa na shaka kwamba anapewa ufunuo na Mwenyezi Mungu.

Mfano mwingine wa hali ya kujiamini aliyokuwa nayo Muhammad (s.a.w.) katika

utume wake na kwa hiyo imani aliyokuwa nayo ya yeye na ujumbe wake kulindwa na

Mwenyezi Mungu ni wakati wa kuhamia Madina pale alipoikimbia Makkah na kujificha

pangoni pamoja na Abu Bakr. Kama kweli Muhammad (s.a.w.) angekuwa mrongo,

mdanganyifu na mtu aliyejaribu kuwalaghai watu waamini kwamba ni mtume, katika

mazingira hayo ya pangoni angetarajiwa kumwambia rafiki yake, “Eeh! Abu Bakr, tafuta

sehemu ya kujificha humu pangoni”. Au “Chuchumaa katika ile kona na ukae kimya”.

Lakini, hakika alichomwambia Abu Bakr kinaonesha wazi hali ya kujiamini aliyokuwa nayo.

Alimwambia: “Tulia! Allah yu pamoja nasi, na Allah atatuokoa!”

Sasa basi, kama mtu anajua kwamba anawalaghai watu, aina hii ya msimamo anaitoa wapi?

Kwa kweli, aina ya hali hii ya akili sio sifa ya mtu muongo au mdanganyifu hata kidogo.

Hivyo, kama ilivyoelezwa hapo awali, wasio Waislamu wanazunguukazunguuka katika

duara, wakitafuta njia ya kutokea ---- njia ya kufafanua matokeo ya utafiti wa mambo

yaliyomo ndani ya Qur‟an bila kuyahusisha na chanzo chake halisi. Kwa upande mmoja,

siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa watakwambia: “Mtu huyu alikuwa muongo”, na kwa

upande mwingine, siku ya Jumanne, Alhamisi na Jumamosi watakwambia: “Alikuwa

mwendawazimu”. Wanachokataa kukubali ni kwamba mtu hawezi kuwa na hali zote mbili

wakati mmoja; lakini wanapenda tu kutumia hoja ya visingizio hivyo viwili kuelezea habari

zilizomo ndani ya Qur‟an.

Kiasi cha miaka saba iliyopita, nilitembelewa na mchungaji mmoja nyumbani kwangu.

Katika chumba tulichokuwemo ilikuwepo Qur‟an juu ya meza ikiwa imeelekea upande wa

sakafuni, na hivyo mchungaji huyo hakuwa akijua kuwa kitabu hicho ni kitabu gani. Katikati

ya maongezi yetu niliunyosha mkono wangu upande wa Qur‟an na kusema: “Sina shaka na

kitabu kile”. Akiiangalia Qur‟an bila kujua kuwa ni kitabu gani, alijibu: “Ninakwambia,

kama kitabu hicho sio Biblia, basi kiliandikwa na mwanadamu!” Katika kuyajibu maelezo

yake hayo nikasema: “acha nikuelezee baadhi ya mambo yaliyomo ndani ya kitabu hiki”. Na

ndani ya dakika tatu au nne nilimhadithia vitu vichache vilivyomo ndani ya Qur‟an. Baada

ya dakika hizo tatu au nne, alibadilisha kabisa msimamo wake na kusema: “Uko sahihi.

Kitabu hiki hakikuandikwa na mwanadamu. Shetani ndiye aliyekiandika!” Kwa kweli,

kushikilia msimamo kama huo ni kitu cha bahati mbaya sana –-- kutokana na sababu nyingi.

Kwanza, ni kisingizio cha harakaharaka na dhaifu sana. Ni mlango mwepesi wa kutokea

kwenye hali isiyofurahisha. Kuna kisa mashuhuri katika Biblia kinachoelezea jinsi siku moja

Wayahudi walishuhudia namna Yesu alivyomfufua mfu. Mtu huyo alikuwa amekufa siku

nne kabla, na Yesu alipofika alisema: “Amka!” na mtu huyo akainuka na kutembea. Baadhi

ya Wayahudi walioshuhudia tukio hilo walisema wakiwa hawaamini kilichotokea, “Huyu ni

shetani. Shetani ndiye aliyemsaidia!” Leo hii kisa hicho hukaririwa mara nyingi

makanisani ulimwenguni kote, na watu hulia kwa uchungu wakisema: “Oh, lau ningekuwepo

13

hapo, nisingekuwa mpumbavu kama Wayahudi!” Watu hawa wanastaajabisha, kwani

hufanya kile kile kilichofanywa na Wayahudi. Pale unapowaonyesha sehemu ndogo tu ya

Qur‟an husema: “Oh, Shetani ndiye aliyetunga. Shetani ndiye aliyekiandika kitabu hicho!”

Kwa kuwa wamebanwa kwenye kona na hawana jibu jingine lenye kujitosheleza, hukimbilia

kwenye kisingizio cha harakaharaka na cha rahisi. Mfano mwingine wa watu wanaotumia

msimamo huu dhaifu, unaweza kuonekana katika maelezo ya washirikina wa Makka kuhusu

chanzo cha ujumbe wa Muhammad. Walikuwa wakisema: “Mashetani ndio wanaomletea

Muhammad hiyo Qur‟an!” Lakini kila yalipotolewa madai mapya, Qur‟an hutoa jibu. Aya

mojawapo yasema:

"Na wanasema: Hakika yeye ni mtu aliyevamiwa (na shetani). Na hayakuwa haya

(yaani Qur‟an, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote" (Qur‟an 68: 51-52).

Kwa hivyo, Qur‟an inatoa hoja katika kujibu fikra na madai hayo. Kwa kweli, kuna hoja

nyingi ndani ya Qur‟an katika kujibu madai na tuhuma kwamba mashetani ndio waliomletea

Muhammad (s.a.w.) ujumbe wake. Kwa mfano, katika Sura ya 26, Allah anasisitiza:

"Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo, Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi,

Hakika hao wametengwa na kusikia" (Qur‟an 26: 210-212).

Na sehemu nyingine ya Qur‟an, Allah anatuelekeza:

"Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni".

(Qur‟an: 16 : 98)

Sasa je, hivi ndivyo Shetani anavyoandika kitabu? Anamwambia mtu kwamba: “Kabla ya

kusoma kitabu changu, mwombe Mwenyezi Mungu akulinde dhidi yangu”? Hili ni gumu

sana, tena sana. Mtu angeweza kuandika kitu kama hiki, lakini je sheteni angeweza kufanya

hivi? Watu wengi wanaonesha wazi kuwa hawawezi kuafikiana katika mada hii. Kwa

upande mmoja, wanadai kwamba Shetani asingeweza kufanya kitu kama hicho na hata kama

angeweza, Mwenyezi Mungu asingemruhusu; lakini kwa upande mwengine, wanaamini pia

kwamba Shetani ana uwezo kidogo ulio chini ya uwezo wa Mungu. Kimsingi wanadai

kwamba yumkini Shetani akaweza kufanya kile kinachoweza kufanywa na Mungu. Na

kutokana na msimamo wao huo, wanapoitazama Qur‟an, hata wanaposhangazwa na jinsi

ilivyo ya ajabu, huendelea kusisitiza, “Shetani ndiye aliyetengeneza!” Alhamdulillah,

Waislamu hawana msimamo kama huo. Ingawa Shetani anaweza kuwa na uwezo fulani,

lakini uwezo huo ni mdogo mno kuulinganisha na uwezo wa Mungu. Na hakuna Mwislamu

awezaye kuwa Mwislamu kama hatoamini kwamba Shetani hana uwezo wowote kwa

Mwenyezi Mungu. Inafafahamika kwa kila mtu hata kwa wasio Waislamu kwamba Shetani

anaweza kufanya makosa kiurahisi kabisa, na ingetarajiwa kwamba angetoa taarifa

zinazopingana na kuhitilafiana kama angeandika kitabu. Kwani Qur‟an yasema:

“Je, hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi

Mungu bila ya shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi” (Qur‟an 4: 82).

14

Sambamba na visingizio vinavyotolewa na wasio Waislamu katika majaribio yao ya kipuuzi

ya kuhalalisha maelezo ambayo hayapo ndani ya Qur‟an, kuna shambulio jingine litolewalo

mara kwa mara linaloonekana kuwa ni muunganiko wa fikra za kwamba Muhammad (s.a.w.)

alikuwa mwendawazimu na muongo. Kimsingi, watu hawa wanadai kwamba Muhammad

alikuwa na wazimu, na kutokana na maono yake ya uwongo, aliwadanganya na kuwapotosha

watu. Kuna jina la kitu hiki katika saikolojia. Kinajulikana kama maithomania

(mythomania). Humaanisha kwamba mtu aseme uwongo na kisha yeye mwenyewe

akauamini huo uwongo kuwa ni kweli. Hili ndilo wasemalo wasiokuwa Waislamu kuwa

ndio lililokuwa likimsumbua Muhammad (s.a.w.). Lakini tatizo pekee la wazo hili ni

kwamba mtu anayesumbuliwa na mythomonia hawezi kabisa kushughulika na mambo ya

hakika na kweli, na lakini Qur‟an yote --– mwanzo mpaka mwisho ---- imesimama kwenye

misingi ya ukweli. Kila kilichomo ndani yake kinaweza kufanyiwa utafiti na kugunduliwa

kuwa ni kweli. Kwa kuwa mambo ya kweli ni tatizo kwa mtu mwenye mythomania, basi

mwanasaikolojia anapojaribu kumtibu mtu anayesumbuliwa na hali hiyo, huendelea

kumkabili kwa mambo ya ukweli. Kwa mfano, kama mtu ni mgonjwa wa akili na akadai

kuwa: “Mimi ndiye mfalme wa Uingereza”, mwanasaikolojia hamwambii “hapana, wewe

siye. Wewe ni mwendawazimu!”. Hafanyi hivyo. Badala yake, humkabili kwa mambo ya

hakika na kweli na kumwambia, “Sawa, wasema wewe ni mfalme wa Uingereza. Sasa

niambie malkia yu wapi sasa. Na yu wapi waziri wako mkuu? Na walinzi wako wapo

wapi?”. Sasa, mtu huyo anapokuwa na taabu ya kujaribu kujibu maswali haya, hujaribu

kutoa visingizio mbalimbali, akisema, “Ah… malkia…amekwenda kwa mama yake. Ah…

waziri mkuu …oh..amekufa”. Na hapo hapo huwa anapona kwa sababu hawezi kupambana

na mambo ya uhakika na ukweli. Iwapo mwanasaikolojia huyo ataendelea kumkabili kwa

mambo mengi ya hakika na ukweli, mwishowe huukubali ukweli na kusema, “Nahisi mimi

sio mfalme wa Uingereza”. Qur‟an Tukufu humkabili kila anayeisoma kwa katika njia sawa

na ile ya mwanasaikolojia anayemtibu mgonjwa wa maradhi ya mythomania. Kuna aya moja

ndani ya Qur‟an isemayo:

"Enyi watu! Yamekujieni mawaidha (yaani Qur‟an) kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na

poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini.”

(Qur‟an 10: 57).

Kwa mara ya kwanza, maelezo haya huonekana kuwa yasiyo wazi, lakini maana ya aya hii

huwa wazi pale inapotazamwa kwa kutumia mfano uliotajwa hapo juu. Kimsingi, mtu

huponywa dhidi ya maono yake ya uwongo kwa kuisoma Qur‟an. Kimsingi, Qur‟an ni tiba.

Huwaponya kabisa watu wenye maono ya uwongo (waliohadaiwa) kwa kuwakabili kwa

ukweli na mambo ya uhakika. Msimamo ulio mashuhuri ndani ya Qur‟an ni ule usemao,

“Enyi watu, mwasema hiki na kile kuhusu jambo hili; lakini vipi kuhusu hiki na hiki?

Mwawezaje kusema hiki wakati mwajua kile?” na kuendelea. Qur‟an humlazimisha mtu

kutafakari jambo husika na wakati huohuo ikimtibu na kumponya dhidi ya maono ya

uwongo aliyonayo kwamba mambo ya kweli yaliyoletwa na Mwenyezi Mungu kwa

wanadamu yanaweza kutolewa visingizio kiurahisi kwa fikra, mawazo na visingizio hafifu.

15

Ni aina hii ya msimamo --– kuwakabili watu kwa ukweli ---- ambayo kwamba imeziteka

fikra na macho ya watu wengi wasio Waislamu. Kwa hakika, kuna marejeo yanayovutia sana

kuhusu mada hii ndani ya Ensaiklopidia Mpya ya Kanisa Katoliki.

Katika makala moja chini ya mada ya Qur‟an, Kanisa Katoliki lasema: “Kwa muda wa

karne nyingi, zimetolewa fikra nyingi kuhusu chanzo cha Qur‟an… Leo hii hakuna

mtu mwenye akili anayekubaliana na fikra yoyote katika fikra hizo”!!. Sasa hili ni

Kanisa kongwe la Kikatoliki, ambalo limekuwepo kwa karne nyingi, likikanusha majaribio

haya ya kipuuzi yanayofanywa katika kuitolea visingizio Qur‟an Tukufu. Kwa kweli Qur‟an

ni fumbo kwa Kanisa Katoliki. Linasema kwamba ni kitabu cha Mungu (ufunuo), hivyo

wanaidurusu. Hakika wangependa kupata uthibitisho ambao sio, lakini haiwezekani.

Hawawezi kupata kisingizio kinachojitosheleza. Lakini angalau wamekuwa waaminifu

katika utafiti wao na hawayakubali maelezo ya mwanzo ambayo hayakuthibitishwa. Kanisa

hilo linasema kuwa kwa kipindi cha karne kumi na nne hayajawasilishwa maelezo ya

ufafanuzi wenye kukubalika kiakili. Angalau kanisa hilo linakiri kwamba Qur‟an sio suala

linaloweza kuachwa kiurahisi. Kwa kweli watu wengine hawaaminiki sana. Hudai kwa

namna ya harakaharaka, “Oh, Qur‟an ilitokea hapa. Qur‟an ilitokea pale”. Na hawapimi hata

uaminifu wa yale wayaelezayo muda wote. Hata hivyo, maelezo hayo ya Kanisa Katoliki

humuacha Mkristo wa kawaida katika taabu. Huenda akawa na mawazo binafsi kuhusu

chanzo cha Qur‟an, lakini akiwa kama mfuasi mmoja wa Kanisa, hawezi kabisa

kuifanyia kazi fikra yake binafsi. Kwani kwa kufanya hivyo aweza kwenda kinyume na

utiifu, uaminifu na utii kwa kanisa. Kwa sababu ya kuwa mwanakanisa, anatakiwa kukubali

kile kilichotangazwa na Kanisa Katoliki bila kuhoji na atekeleze mafundisho yake kama

sehemu ya maisha yake ya kila siku. Hivyo, kimsingi, Kanisa katoliki kwa ujumla wake

linasema: “Msizisikilize taarifa hizo zisizothibitishwa dhidi ya Qur‟an”, sasa kipi

kinachoweza kusemwa kuhusu mtazamo wa Kiislamu? Hata wasio Waislamu wanakiri

kwamba kuna kitu kwenye Qur‟an ---- kinachotakiwa kutambuliwa ---- sasa kwanini watu

wanakereheka, kuchukia na kuudhika sana pindi Waislamu wanapotoa mtazamo kama huo?

Kwa hakika hiki ni kitu ambacho watu wenye akili wanatakiwa kukitaamali ---– kitu

ambacho watu wenye ufahamu na uelewa wanatakiwa kukitafakari.

Hivi karibuni, msomi mkubwa wa Kanisa Katoliki ---–aitwaye Hans ---- aliisoma Qur‟an na

kutoa maoni yake kuhusu alichosoma. Mtu huyu amekuwepo kwa muda fulani, na

anaheshimika sana katika Kanisa, na baada ya kufanya uchunguzi kwa umakini, aliripoti

matokeo ya utafiti wake, akihitimisha kwa kusema : “Mungu ameongea na mwanadamu

kupitia kwa mtu, Muhammad”. Haya ni matokeo mengine ya utafiti uliofanywa na chanzo

kisichokuwa cha Kiisalmu ---– msomi mkubwa anayeheshimiwa na Kanisa Katoliki! Sidhani

kuwa Papa anakubaliana naye, lakini hata hivyo, maoni ya mtu huyo mashuhuri,

anayeheshimiwa na umma wa watu lazima yatakuwa yamebeba uzito mkubwa katika kutetea

msimamo wa Waislamu. Anatakiwa kuungwa mkono kwa kuukubali ukweli kwamba Qur‟an

sio kitu kinachoweza kutupiliwa mbali kiurahisi, bali kwa hakika Mungu ndiye chanzo cha

Maneno haya (yaani Qur‟an). Kama inavyoonekana katika taarifa iliyopita, kila uwezekano

umezungumzwa kwa undani, hivyo nafasi ya kutafuta uwezekano mwingine wa kuipuuza

16

Qur‟an haipo kabisa. Kwani kama kitabu hiki sio ufunuo wa Mungu, basi itakuwa ni

udanganyifu; na kama ni udanganyifu, mtu lazima aulize, “Ni kipi chanzo chake?” na ni

wapi Qur‟an inapotudanganya?” Kwa kweli, majibu ya kweli ya maswali haya yatatoa

mwanga juu ya usahihi na ukweli wa Qur‟an na kuyanyamazisha madai yasiyothitishwa ya

makafiri. Kiukweli, kama watu wataendelea kusisitiza kwamba Qur‟an ni udanganyifu, basi

watatakiwa kuleta ushahidi unaounga mkono madai yao. Mzigo wa kuthibitisha ni wa kwao,

sio wetu! Kwani mtu hatakiwi kutoa fikra na nadharia fulani bila ushahidi wenye uthibitisho;

hivyo ninawaambia hao watu: “Nionyesheni udanganyifu hata mmoja! Nionyesheni sehemu

ambayo Qur‟an inanidanganya! Nionyesheni, la sivyo, msiseme kwamba Qur‟an ni

udanganyifu!”. Sifa ya kuvutia iliyonayo Qur‟an Tukufu ni namna inavyoshughulikia

matukio ya kushangaza ambayo sio tu kwamba yanahusiana na zama za kale bali pia

yanahusiana na wakati wa sasa. Kimsingi, Qur‟an sio fumbo la zamani. Limeendelea kuwa

fumbo hata sasa ---- ni fumbo kwa wasio Waislamu. Kwani kila siku, kila wiki, kila mwaka

huleta ushahidi kwamba Qur‟an ni nguvu ambayo watu wanapaswa kuitambua ---- yaani

usahihi na ukweli wake hauhitaji tena kuhojiwa au kushindaniwa! Kwa mfano, aya moja

ndani ya Qur‟an Tukufu yasema:

“Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana,

kisha Sisi tukazibandua? Na tukajaalia kutokana na maji kila kilicho hai? Basi je,

hawaamini?" (Qur‟an 21: 30).

Inashangaza kuona kuwa, taarifa hii ndiyo hasa iliyowafanya watoe tuzo ya Nobel kuwapa

makafiri ---- mtu na mkewe ---- mwaka 1973. Qur‟an inaeleza chanzo cha ulimwengu –

namna ilivyoanza kutoka kwenye kipande kimoja – na mwanadamu ameendelea kuthibitisha

ukweli wa ufunuo huu mpaka leo. Aidha, ukweli ni kwamba kusema uhai wote asili yake ni

maji isingekuwa jambo rahisi kuwafanya watu wa karne kumi na nne zilizopita waliamini.

Kwa kweli, kama miaka 1400 iliyopita ungesimama jangwani na kumwambia mtu kuwa ,

“Yote hii, unaona (ukijiashiria mwenyewe), kwa kiasi kikubwa inatokana na maji”, hakuna

mtu ambaye angekuamini. Uthibitisho wa jambo hilo haukuwepo mpaka pale

ilipovumbuliwa hadubini (microscope). Walilazimika kusubiri ili kuugundua huo uteseli

(cytoplasm), sehemu ya kiini cha seli (cell), inayotengenezwa na 80% ya maji. Hata hivyo,

ushahidi ulikuja, na kwa mara nyingine Qur‟an ikafaulu majaribio na mitihani ya wakati huu.

Tukirudi kwenye vipimo vya kuthibitisha usahihi wa kitu (falsification tests) vilivyotajwa

hapo awali, inavutia kufahamu kuwa, vipimo hivyo pia vinahusika na mambo ya zamani na

ya wakati wa sasa. Baadhi yake yalitumika kuonyesha kudura (omnipotence) na Elimu ya

Mwenyezi Mungu, wakati mengine yakiendelea kusimama kama changamoto mpaka leo.

Mfano wa hilo la kwanza ni maelezo yaliyotolewa na Qur‟an kuhusu Abu Lahab. Maelezo

hayo yanaonyesha wazi wazi kwamba Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa mambo ya siri, alijua

kwamba Abu Lahab asingebadili msimamo wake na kuukubali Uislamu. Hivyo, Mwenyezi

Mungu akatangaza kwamba (Abu Lahab) angelaaniwa milele mpaka atakapoingia katika

moto wa Jahannam. Sura hiyo inaonyesha mambo yote mawili yaliyoelezwa hapo juu , yaani

hekima ya Mwenyezi Mungu na kuwaonya wale waliokuwa kama Abu Lahab.

17

Mfano unaovutia wa aina ya pili ya kipimo cha kuthibitisha yaliyomo ndani ya Qur‟an ni aya

inayoelezea mahusiano baina ya Waislamu na Wayahudi. Aya hiyo imekuwa makini

kutopunguza eneo lake kwa mahusiano tu ya mtu mmoja mmoja katika watu wa dini hizi

mbili, badala yake inatoa mukhtasari wa mahusiano kati ya makundi hayo mawili ya watu

kwa ujumla wao. Kimsingi, Qur‟an Tukufu inaeleza kuwa siku zote Wakristo wataamiliana

vizuri na Waislamu kuliko Wayahudi wanavyoamiliana na Waislamu. Kwa kweli, athari ya

maelezo hayo inaweza kuonekana baada tu ya kutafakari kwa makini maana halisi ya aya

hiyo. Ni kweli kwamba kuna Wakristo wengi na wayahudi wengi ambao wamekuwa

Waislamu, lakini Jamii ya Kiyahudi kwa ujumla wake itaendelea kutazamwa na kuonekana

kama adui mkubwa wa Uislamu. Aidha, ni watu wachache ndio wanaotambua kile

kinachonadiwa na tangazo hilo la wazi la Qur‟an. Kimsingi, ni fursa nyepesi kwa Wayahudi

kuthibitisha kwamba Qur‟an ni uwongo ---– kwamba sio ufunuo wa Mungu. Wanachotakiwa

kufanya ni wao kujikusanya, waamiliane vizuri na Waislamu na kisha waseme: “Sasa kitabu

chenu kitukufu kinasemaje kuhusu yule ambaye ni rafiki yenu wa kweli ulimwenguni --– je,

ni Wayahudi au Wakristo? Angalieni kile ambacho sisi Wayahudi tumekufanyieni!” Hayo tu

ndiyo wanayotakiwa kuyafanya ili kukanusha usahihi na ukweli wa Qur‟an, lakini

hawajafanya hivyo kwa kipindi cha mika 1400. Na zaidi ya hapo, siku zote, changamoto

hiyo bado ipo na nafasi ya wao kuthibitisha uwongo wa Qur‟an bado ipo wazi!

Mifano yote iliyokwishatolewa kuhusu mitazamo mbalimbali ambayo mtu anaweza

kuidurusu Qur‟an bila shaka imekuwa mifano ya ndani (subjective) kwa asili; hata hivyo

kuna mtazamo mwingine, miongoni mwa mifamo mingi, ambao ni wa nje (objective) na

wenye msingi wa kimahesabu. Inashangaza sana jinsi Qur‟an inavyokuwa ya ajabu na ya

kweli pindi mtu anapolinganisha vitu vinavyoweza kutumika kama orodha ya makisio

mazuri. Kimahesabu, inaweza kufafanuliwa kwa kutumia mifano ya kukisia (kubahatisha) na

kutabiri. Kwa mfano, kama mtu ana machaguo mawili (yaani, chaguo moja sahihi na jingine

lisilokuwa sahihi), na kwakuyafunga macho yake na akachagua, hivyo nusu ya

atakavyochagua (yaani mara moja kati ya mara mbili) atapatia. Nafasi moja kati ya mbili

angepatia katika kuchagua na angeweza kukosea katika kuchagua. Sasa, kama mtu huyo

huyo ana nafasi mbili kama hiyo (yaani aweze kupatia au kukosea kuhusu hali namba moja,

na akapatia au kukosea kuhusu hali namba pili), na akayafunga macho yake na kubahatisha,

atakuwa sahihi katika moja ya nne ya muda husika (yaani mara moja katika mara nne). Sasa

ana nafasi moja katika nne kwa sababu sasa kuna namna tatu za yeye kukosea na moja tu ya

yeye kupatia. Kwa lugha nyepesi, anaweza kukosea katika hali namba moja na kisha

anaweza kukosea tena katika hali namba mbili; AU anaweza kukosea kuchagua katika hali

namba moja na kupatia kuchagua katika hali namba mbili; AU anaweza kupatia katika hali

namba moja na kisha akakosea katika hali namba mbili; AU anaweza kupatia katika hali

namba moja na kupatia kuchagua katika hali namba mbili. Bila shaka, mfano pekee ambapo

anaweza kupatia moja kwa moja ni katika eneo la mwisho ambapo anaweza kukisia

kiusahihi katika hali zote mbili. Mategemeo ya makisio yake sahihi moja kwa moja

yamekuwa makubwa kwa sababu idadi ya hali ya yeye kuweza kukisia imeongezeka; na

mlinganyo wa kimahesabu unaowakilisha mpangilio huo ni 1/2x 1/2 (yaani, nafasi moja

18

katika nafasi mbili kwa hali ya kwanza ikizidishwa kwa nafasi moja katika mbili za hali ya

pili).

Tukiendelea na mfano huo, kama mtu huyo huyo atakuwa na hali tatu ambazo anatakiwa

kubahatisha kabisa (blind guess), uwezo wake wa kupatia ni moja ya nane kwa muda wote

(yaani mara moja katika nane au 1/2 x 1/2 x 1/2). Kwa mara nyingine mategemeo ya kufanya

chaguo sahihi katika hali zote tatu yameongeza nafasi yake ya kupatia moja kwa moja na

kuwa mara moja tu katika nane. Ieleweke kwamba idadi ya kubahatisha inapoongezeka,

nafasi za kupatia hupungua, kwani matukio hayo mawili yana uwiano unaoenda kinyume.

Sasa tukiuhusisha mfano huu na hali za ndani ya Qur‟an, kama mtu akitengeneza orodha ya

mada zote ambazo Qur‟an imetolea maelezo yaliyothibitishwa kuwa sahihi, itabainika wazi

kuwa haielekei kabisa kwamba yote yalikuwa ya kubahatisha tu (blind guesses). Kwa kweli,

maudhui zilizozungumziwa ndani ya Qur‟an Tukufu ni nyingi, na hivyo kama mategemeo

(odds) ya mtu ni kupatia katika kuyabahatisha yote kwa kweli kimatendo huwa ni sifuri.

Kama kuna njia milioni moja za Qur‟an kutokuwa sahihi, lakini Qur‟an ikawa sahihi, basi

haielekei kwamba kuna mtu aliyekuwa akibahatisha. Mifano mitatu ifuatayo ya mada

ambazo kwamba Qur‟an imetoa maelezo yaliyo sahihi yote kwa pamoja inaonyesha jinsi

Qur‟an inavyoendelea kuyashinda makisio (odds).

Katika Sura ya 16 Qur‟an yasema kwamba nyuki jike huyaacha makazi yao kwenda

kukusanya chakula. Sasa, mtu aweza kubahatisha juu ya hilo, akisema, “Nyuki mnayemuona

akirukaruka mahali mbalimbali ---– anaweza kuwa nyuki dume, au inawezekana akawa

nyuki jike. Nafikiri nitabahatisha kuwa ni jike”. Kwa hakika ana nafasi moja katika mbili ya

kuwa sahihi. Hivyo, hutokea kwamba Qur‟an ikawa sahihi. Lakini pia yaweza kutokea

kwamba hicho sicho kilichokuwa kikiaminiwa na watu wakati Qur‟an ilipoteremshwa.

Waweza kueleza tofauti kati ya nyuki jike na nyuki dume? Sawa, inahitaji mtaalamu kufanya

hivyo, lakini imegunduliwa kwamba nyuki dume kamwe hayaachi makazi yake kwenda

kukusanya chakula. Hata hivyo, katika mchezo wa Shakespeare, Henry the Fourth, baadhi

ya wahusika wanazungumzia nyuki na kutaja kwamba nyuki ni askari na wana mfalme.

Hivyo ndivyo walivyofikiria watu katika zama za Shakespeare ---– kwamba nyuki

wanaoonekana kurukaruka mahali mbali mbali ni nyuki dume na kwamba wao hurudi

nyumbani na kuwajibika kwa mfalme. Lakini, hiyo sio sahihi hata kidogo. Ukweli ni

kwamba nyuki hao ni nyuki jike, na wanawajibika kwa malkia. Lakini ni katika kipindi cha

miaka 300 tu iliyopita ambapo kwamba utafiti wa kisasa wa sayansi uliweza kugundua kuwa

hii ndio hali halisi.

Hivyo, tukirudi kwenye orodha ya kubahatisha kwa usahihi (good guesses), kuhusu mada ya

nyuki, Qur‟an ilikuwa na nafasi ya 50/50 ya kuwa sahihi, na makisio (odds) yalikuwa moja

kwa mbili.

Pamoja na maudhui ya nyuki, Qur‟an pia yazungumzia jua na namna linavyosafiri katika

anga (space). Kwa mara nyingine, mtu anaweza kubahatisha kwenye maudhui hiyo. Pindi

jua linapotembea katika anga, kuna mambo mawili: linaweza kutembea kama jiwe

19

litembeavyo pale linapotupwa, au linaweza kutembea kwa hiari yake. Qur‟an Tukufu inataja

hiyo hali ya pili ---– kwamba linatembea kutokana na mwendo wake lenyewe. Katika

kufanya hivyo, Qur‟an imetumia neno maalumu “sabaha” kuelezea mwendo wa jua katika

anga. Ili kumwelewesha vizuri msomaji kuhusu matumizi ya kitenzi hiki cha Kiarabu,

tunatoa mfano ufuatao. Mtu awapo ndani ya maji na kitenzi hiki “sabaha” kikatumika katika

kuelezea mwendo wake, hufahamika kuwa anaogelea, akisogea kwa hiari yake na sio

kutokana na nguvu ya moja kwa moja inayotumika kwake. Hivyo kitenzi hiki kinapotumika

kuelezea mwendo wa jua katika anga, hakimaanishi hata kidogo kwamba jua linaelea angani

bila mpangilio kutokana na kutupwa au kitu kama hicho. Bali humaanisha tu kwamba jua

linajigeuza na kuzunguka (turning and rotating) wakati likisafiri. Sasa, hili ndilo

linalothibitishwa na Qur‟an. Lakini je, kilikuwa kitu rahisi kugunduliwa? Je, mtu wa

kawaida aweza kueleza kuwa jua linazunguka? Ni hivi karibuni tu ambapo kilitengenezwa

kifaa cha kutoa na kudhihirisha picha ya jua ili mtu aweze kulitazama bila kuwa amefumba

macho. Na kupitia mchakato huu iligunduliwa kuwa sio tu kwamba kuna vituo vitatu

kwenye jua lakini vituo hivi husogea mara moja kila baada ya siku 25. Mwendo huu

hujulikana kama mzunguko wa jua kwenye mhimili wake na kwa ujumla huthibitisha

kwamba, kama Qur‟an ilivyoeleza miaka 1400 iliyopita, kweli jua hujizungusha wakati wa

kusafiri katika anga.

Na tukirudi kwa mara nyingine kwenye mada ya kubahatisha vizuri (good guesses),

mategemeo (odds) ya kupatia kuhusu mada zote mbili –--- mada ya jinsia ya nyuki na

mwendo wa jua---- ni moja katika nne!

Tukitazama nyuma karne kumi na nne zilizopita yumkini watu hawakuwa wakijua sana

kuhusu kanda zinazogawa masaa (time zones), maelezo ya Qur‟an kuhusu maudhui hii ni ya

kushangaza sana. Fikra ya kwamba familia moja inakula kifungua kinywa wakati jua

linapoinuka wakati familia nyingine inafurahia hali ya hewa ya usiku mwanana (brisk night

air) kwa hakika ni kitu cha maajabu, hata katika zama za sasa. Kwa kweli, karne kumi na

nne zilizopita, mtu asingeweza kusafiri zaidi ya maili thelathini kwa siku moja, na hivyo

ilimchukua miezi mingi kutoka India mpaka Morocco, kwa mfano. Na yumkini, wakati akila

chakula cha jioni Morocco, alikuwa akijifikiria, “Wakati huu huko nyumbani India wanakula

chakula cha jioni pia”. Hii inatokana na kwamba hakutambua kwamba, katika harakati za

safari yake, alipitia kwenye ukanda unaogawa masaa (time zone). Lakini, kwa kuwa ni

maneno ya Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa yote, Qur‟an Tukufu inalijua na kulitambua tukio

hilo. Katika aya moja inayovutia sana inaeleza kwamba historia itakapofikia kikomo na

ikawadia Siku ya Hukumu, yote yatatokea mara moja; na tukio hili la mara moja litawakuta

baadhi ya watu wakiwa katika wakati wa mchana na wengine wakiwa katika wakati wa

usiku. Hii inaonyesha waziwazi Hekima na Elimu ya Mwenyezi Mungu isiyokuwa na

mwanzo wala mwisho juu ya uwepo wa kanda za masaa (time zones), japokuwa uvumbuzi

huu haukuwepo kabla ya karne kumi na nne zilizopita. Kwa hakika, kitu hiki sio kitu

kinachoweza kuonekana na macho ya mtu au kwa uzoefu wa mtu, na jambo hili la hakika, ni

ushahidi na uthibitisho tosha wa ukweli na usahihi wa Qur‟an.

20

Tukirudi kwa mara ya mwisho kwenye mada ya bahati nzuri (kupatia katika kuchagua) kwa

ajili ya mfano uliopo, mategemeo (odds) kwamba mtu alipatia katika kubahatisha kwenye

mada zote tatu zilizotangulia –--- jinsia ya nyuki, kutembea kwa jua na uwepo wa ukanda wa

masaa ---- mategemeo hayo ya kubahatisha kwa usahihi ni moja katika nane!

Kwa kweli, mtu anaweza kuendelea zaidi na mfano huu, akiorodhesha orodha ndefu na

kubwa ya mambo ya bahati nzuri; na bila shaka, mategemeo ya kukosa (odds) yatakuwa

makubwa zaidi na zaidi kwa kila ongezeko la mada ambayo anaweza kuibahatisha. Lakini

hakuna awezaye kukanusha yafuatayo; mategemeo kwamba Muhammad ambaye hakuwahi

kusoma wala kuandika, alipatia katika kubahatisha na kukisia kuhusu maelfu na maelfu ya

maudhui na mada, bila kufanya hata kosa moja, ni jambo gumu sana. Na kwamba mawazo

ya kusema yeye ndiye aliyeandika Qur‟an ni ya kutupiliwa mbali kabisa ---– yatupiliwe

mbali hata na maadui wakubwa wa Uislamu!

Kwa hakika, Qur‟an inatarajia aina hii ya changamoto. Bila shaka, iwapo mtu anapoingia

katika ardhi ya kigeni akamwambia mtu fulani kwamba, “Ninamjua baba yako. Nimekutana

naye”, bila shaka huyo mwenyeji atatilia shaka maneno ya mgeni na kusema, “Umefika hapa

sasa hivi. Ulimjuaje baba yangu”. Na hivyo atamuuliza, “Niambie, je baba yangu ni mrefu,

mfupi, mweusi, mweupe? Ni upi muonekano wake?” Na hapo kama mgeni ataendelea

kuyajibu maswali yote kwa usahihi, mtu yule mwenye shaka hatokuwa na chaguo jingine

zaidi ya kusema, “Ninahisi wamfahamu baba yangu. Sijui umemfahamu vipi, lakini naamini

unamfahamu!”. Hali ni hiyo hiyo kwa Qur‟an. Inaeleza kwamba inatoka kwa Yule

aliyeumba kila kitu. Hivyo kila mtu ana haki ya kusema, “Nithibitishie! Kama kweli

mwenye kitabu hiki ndiye aliyeumba uhai na kila kitu katika mbingu na ardhi, basi atakuwa

anajua kuhusu hiki, kuhusu kile, na kadhalika”. Na kwa hali hiyo, baada ya kuidurusu na

kuitafiti Qur‟an, kila mtu atapata kugundua ukweli kama huo. Aidha, sote tunafahamu kwa

uhakika kwamba: Hatuwajibiki sisi wote kuwa wataalamu ili kuthibitisha yale

yanayothibitishwa na Qur‟an Tukufu. Imani ya mtu hustawi pale anapoendelea kuchunguza

na kuuthibitisha ukweli uliomo ndani ya Qur‟an. Na mtu anatakiwa kuendelea kufanya hivyo

katika maisha yake yote.

Mwenyezi Mungu amuongoze kila anayeukurubia ukweli.

NYONGEZA

Mhandisi mmoja katika Chuo Kikuu cha Toronto (Canada) aliyekuwa akishughulika na

masuala ya Saikolojia na ambaye alikuwa amesoma mambo mengi kuhusu mada hiyo na

kuifanyia utafiti aliandika kitabu juu ya Ufanisi wa Kujadiliana katika Makundi. Lengo la

utafiti wake ilikuwa kutafuta namna watu wanavyoweza kufanikiwa zaidi wanapojikusanya

21

na kujadiliana katika makundi ya watu wawili wawili, watatu, kumi, n.k. Matokeo ya utafiti

wake yalionesha kuwa: Watu hufanikiwa zaidi wanapozungumza katika makundi ya watu

wawili wawili. Ugunduzi huu wote ulikuwa kinyume na matarajio yake, bali ni ushauri

uliotolewa na Qur‟an tangu zamani.

Aidha, Sura ya 89 ya Qur‟an inautaja mji fulani uitwao „Iram (mji wa maguzo), ambao

haukuwa ukijulikana katika historia ya zamani na haukuwepo kwa kiasi cha

kuwashughulisha wanahistoria. Hata hivyo, katika mwezi wa Desemba 1978 idara ya Taifa

ya Mambo ya Kijiografia ilitoa taarifa za kuvutia zilizoeleza kwamba mwaka 1973, mji wa

Elba ulikuwa umegunduliwa nchini Syria. Mji huo uligundulika kuwa na umri wa karne 43,

lakini hili sio lilokuwa la kushangaza zaidi. Watafiti walikuta katika maktaba ya mji wa Elba

orodha ya miji yote iliyokuwa ikifanya biashara na mji wa Elba. Amini usiamini, katika

orodha hiyo lilikuwepo jina la mji wa „Iram. Watu wa Elba walikuwa wakifanya biashara na

watu wa „Iram!

"Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu ---- ya kwamba msimame kwa ajili ya

Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri.....”

Katika kuhitimisha ninawaomba mtafakari kwa umakini haya yafuatayo:

"Na walisema: Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema:

Ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye

kubainisha tu. Je! Kwani hayakuwatosha ya kwamba tumekuteremshia Kitabu hiki

wanacho somewa? Hakika katika hayo zipo rehema na mawaidha kwa watu wanao

amini"