11
Kenya RANCHI YA IL NGWESI Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii Empowered lives. Resilient nations.

RANCHI YA IL NGWESI - Equator Initiative · kupelekwa kwa kikundi cha kamati ya ranchi. Kikundi hiki cha kamati ya ranchi kimeundwa na wanachama ambao hutoka katika koo zote za kimaasai

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

KenyaRANCHI YA IL NGWESI Miradi ya EquatorWanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

Empowered lives. Resilient nations.

MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

WahaririMhariri Mkuu : Joseph CorcoranMuhariri Meneja : Oliver HughesWahariri Waliochangia : Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes, Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma, Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, Amy Korngiebel, John Mulqueen, Lorena de la Parra, Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

ShukraniEquator ingependa kuwashukuru wanachama wa Ranchi ya Il Ngwesi, haswa mwongozo na mchango wa James Kasoo na Caroline Karimi. Picha zote ni za Ranchi ya Il Ngwesi, ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia. Masimulizi juu ya mradi huu yalitafsiriwa kwa Kiswahili na Dr. Ken Ramani.

Nukuu ziadaUnited Nations Development Programme. 2012. Il Ngwesi Group Ranch, Kenya. Equator Initiative Case Study Series. New York, NY.

MUHTASARI KUHUSU MRADIHiki ni kikundi cha kimaasai kinachojishughulisha na ufugaji na makao yao ni sehemu ya Laikipia kasikazini mwa Kenya. Kikundi hiki kina miliki hekari 8.645 ambamo wanafanyia ufugaji wa mifugo huku wakitunza wanyama pori. Kikundi kinanuia kujenga hoteli ya kifahari katika eneo hili. Shughuli za II Ngwesi za kuhimiza utalii zimepigiwa mfano na kuigwa kote nchini. Kikundi kimehifadhi eneo hili vyema na kuwafanya wanyama pori kuzunguka bila shida.

Isitoshe, kipato kinachopatikana kutokana na utalii, kimetumika kuinua huduma za kijamii kama; elimu, maji safi na matibabu. Kikundi hiki kiko mstari wa mbele kuhamasisha raia kuhusu magonjwa kama; ukimwi, malaria na kifua kikuu. Watu zaidi ya 40,000 wamenufaika kutokana na shughuli za hiki kikundi.

MUHTASARIULISHINDA TUZO YA EQUATOR: Mwaka 2002

ULIANZISHWA: Mwaka 1995

ENEO: Wilaya ya Laikipia, Kenya

WANAOFAIDI: Wachungaji 7,000 wa Kimaasai wa Laikipia

MAZINGIRA: Hifadhi ya wanyama ya Lewa

3

RANCHI YA IL NGWESIKenya

YALIYOMOHistoria na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 6

Matokeo ya Kimazingira 7

Matokeo ya Kijamii 7

Matokeo ya Kisera 8

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 9

Maono 10

Wahisani 10

4

Kikundi cha Ngwesi kina hekari takribani 8.645 katika kata ya Mukogodo Wilayani Laikipia Kaskazini mwa mlima Kenya. Shamba hili liko karibu na Mto Ngare Ndare na ubavuni mwa milima ya Mukogodo - sehemu yenyewe ikikaliwa na takribani wamaasai 7,000 ambao ni wafugaji. Baadhi ya wanyama wa pori ambao hupatikana hapa ni kama kifaru mweupe (ceratotherium simum), ndovu ya kiafrika (loxondonta Africana),mbwa koko (lycaon pintus) na punda-milia (equus grevyi). Sehemu hii vile vile ni makao ya kifaru mweusi wanaotishiwa kuangamizwa na wawindaji haramu. Kikundi hiki kimeweza kuhifadhi ranchi hii na kujipatia riziki huku wakipunguza utegemeaji kwa mifugo, na kuhimiza utalii pamoja na kuchunga mazingira.

Vitisho vya kimazingira, kijamii na kibiashara

Idadi ya ndovu ilipungua sana katika sehemu hii baada ya uwindaji wa kiholela uliofanywa kwa kutumia bunduki haramu kutoka Somalia. Shamba hili la II Ngwesi ambalo huwa mkondo wa uhamaji wa wanyama pori linaangamizwa na vitendo vya kibinadamu kama upasuaji mbao, ukulima na kuni. Licha ya kuharibu misitu, vitendo hivi aidha vimeongezea uhasama kati ya jamii za wafugaji na wakulima. Eneo hili limeachwa nyuma kimaendeleo huku kukiwa na shule chache mno na hivyo watoto wengi kutopata elimu. Aidha, eneo hili lina hospitali moja ya kiserikali ambamo daktari mmoja

hutibu takribani wagonjwa 44,000. Jamii ya Wamaasai inayotegemea mifugo imejipata katika hali mbaya baada ya malisho yao kuvamiwa na wanyama pori. Jambo ambalo limeongezea viwango vya umasikini na hivyo kuhatarisha Lewa Downs - mbuga ya kibinafsi iliyoko chini ya II Ngwesi. Ili kuepukana na uvamiaji wa Lewa Downs, shirika la kiserikali la uhifadhi wa wanyama pori (KWS) likishirikiana na uongozi wa Lewa Downs limehimiza uanzishaji wa mbuga inayoendeshwa na jamii ya mashinani ndiposa kujipatia pato. KWS lilihusisha wazee wa kimaasai na viongozi wengine katika juhudi za kuwafunza wenyeji wawalinde wanyama pori ndiposa kuondoa wasiwasi kuhusu shughuli za kikundi cha II Ngwesi kilichoanzishwa mnanmo 1995.

Uhifadhi wa kijamii

Uhifadhi wa Lewa Downs umesaidia sana kikundi cha II Ngwesi katika shughuli za uhifadhi tangia mwaka 1995. Mbinu muhimu ya kulifikia lengo hili ilikua kupitia ujenzi wa hoteli ya kifahari itakayowaletea pato la kudumu na hivyo watu kuwa na motisha wa kuhifadhi manzingira, wanyama pori na shamba lao. Hoteli ya II Ngwesi ilifunguliwa mnamo 1996 ili kuwahudumia watalii. Hoteli hiyo iliendeshwa na kampuni ya II Ngwesi . Hoteli hiyo huwa na vitega uchumi vingine kama vile; uuzaji wa vinyago, nyumba za kitamaduni (bomas) na kambi za kupumzika kadhaa. Mapato yanayopatikana

Historia na Mandhari

“Sera zote lazima zitathmini matokeo mazuri na mabaya kwa jamii: Jamii kwa jumla lazima izielewe sera na kuhamasishwa kuhusu matokeo yazo. Serikali pamoja na wafadhili wa nchi za nje lazima wafahamu kuwa jamii huwa haifaidiki kutoka kwa misaada vile wanavyodhani

-uchunguzi wa kina kuhusu matokeo ya misaada hiyo ni muhimu sana” James Kasoo, Ranchi ya Il Ngwesi

55

kutoka hoteli hiyo hutumika katika ujenzi na uendelezaji wa shule, hospitali pamoja na miundo msingi nyinginezo.

Kikundi hiki kinanuia kutumia mbinu ya umiliki wa kijamii wa shamba ili kupata maendeleo na uhifadhi wa wanyama pori. Ranchi hli la II Ngwesi imegawanywa mara mbili: sehemu ya makao ya binadamu na ya wanyama pori. Jambo hili limesaidia katika usimamizi wa ranchi. Wafugaji huruhusiwa kulisha sehemu ya wanyama ili kuepuka makali ya ukame. Miradi nyingine hufanywa katika shamba hili kama; huzuiaji wa mmonyoko wa udongo, ukarabati wa njia na uhifadhi wa sehemu za chemichemi za maji. Wanachama wa kikundi cha Maasai ndio wanao usemi wa mwisho kuhusu matumizi yote ya ranchi.

Ngazi ya uongozi wa kikundi

Kamati ya II Ngwesi inajumuisha wawakilishi 14 kutoka jamii 7 za kimaasai. Kamati hii hukutana mara 3 kwa mwaka ili kujadili kuhusu mapendekezo yaliyozuliwa na waakilishi kadha. Aidha, hujadili kuhusu maswala ya matumizi ya ardhi. Kamati hii huwa na wakili ambaye hutathmini mapendekezo yote yaliyoafikiwa na kisha kupelekwa kwa kikundi cha kamati ya ranchi.

Kikundi hiki cha kamati ya ranchi kimeundwa na wanachama ambao hutoka katika koo zote za kimaasai na ndicho kina usemi mkubwa katika uongozi wa ranchi hili. Kabla hawajafikia uamuzi wowote lazima kamati hii ipate mawaidha kutoka kwa serikali na washirika wengine. Kamati hii kuu uongozwa na madairekta sita wakuu wa bodi ambao huchaguliwa kutoka jamii ya mashinani na watatu ambao ni wa kigeni. Maamuzi yote makuu hupigiwa kura katika kamati hii kuu kabla ya kuidhinishwa na watu wote mwishoni mwa mwaka. Uchaguzi hufanywa katika mkutano mkuu wa mwaka. Aidha, vitabu vyote na hesabu za matumizi zote zilizokaghuliwa huwasilishwa siku hiyo. Isitoshe, kamati hii kuu ina katiba ambayo huelezea majukumu ya kila mwanachama, namna ya kutumia fedha, kusuluhisha matatizo, mikutano, malisho na uhifadhi kwa jumla.

Kamati kuu ina wafanyakazi walipwao mishahara yaani meneja wa miradi anayesimamia ranchi pamoja na wafanyakazi wengine. Asilimia 50 ya wanakamati hung’atuka afisini baada ya kila miaka mitano ambapo uchaguzi hufanyika kupata viongozi wa ranchi na baada ya miaka miwili kwa viongozi wa kamati ya wakfu wa ranchi. Hoteli hii ya kifahari huendeshwa na kampuni huku wanachama wakiruhusiwa kumiliki kwa kununua sheha. Aidha, kuna bodi ya watu wanne ambayo huwakilisha wahifadhi wa Lewa na Borana pamoja na mbunge wa eneo hilo ambaye huchangia katika uongozi wa hoteli hii. Mradi huu umeajiri wafanyakazi 32; wa kudumu wakiwa ni 24, ambao 15 hufanya kazi katika hoteli na walinzi wakiwa ni 9 ilihali vibarua huajiriwa mara kwa mara wanapohitajika.

“Kikundi cha II Ngwesi kinafuatilia kwa makini mabadiliko ya hewa. Mapapato yake yamepungua kutokana na sababu za kiangazi kiletwacho na mifuno ya mvua isiyotabirika.

Kikundi cha II Ngwesi kimeadhirika mara kwa mara kutokana na kiangazi cha mwaka wa 2008 -9 (ambapo asilimia 75 wa nyati walikufa) na hili limesababisha mpango wa kugeuza asilimia

100 ya eneo lote zima kuwa hifadhi. Vijana nao wanelengwa ili wakomeshwe kutumia kuni na wapewe mitambo ya sola watakayotumia kama nguvu za umeme – ili kuzuia uharibifu wa

misitu” James Kasoo, Ranchi ya Il Ngwesi

6

Majukumu Makuu na Ubunifu

Lengo kuu la kikundi hiki ni uhifadhi wa kimazingira wa eneo hili, huku wakiinua viwango vya maisha ya wamaasai kiuchumi na kijamii. Mkakati mmoja wa uhifadhi ni kuajiri walinzi wenye silaha ili kushika doria kwenye sehemu hii ya uhifadhi. Vitega uchumi mbadala vimeanzishwa ili kuletea wamaasai hela za kusukuma maisha kuliko kutegemea mifugo. Huduma muhimu za elimu na afya zimeanzishwa ili kusaidia wenyeji.

Sheria za uhifadhi

Sheria zilitungwa ili kusaidia katika uhifadhi wa eneo hili lenye hekari takribani 6,500. Sheria hizo zimepiga marufuku ukataji wa miti, uchomaji makaa, uwindaji wa wanyama pori na uanzishaji ovyo wa moto katika eneo hili. Eneo hili la II Ngwesi halijazungushwa ua na hivyo walinzi 9 waliojihami vilivyo wamepewa jukumu la kushika doria. Walinzi hawa huwazuia watu kuingia kwenye eneo hilo wakiwa na panga, mbwa au viberiti.

Kutoka ufugaji hadi ukulima

Juhudi za uhifadhi zilipigwa jeki kwa kununua shamba la hekari 200 linalotumiwa kukuza ngano. Ununuzi huu ulidhaminiwa na UNDP Equator Prize mnamo 2002. Wenyeji aidha, wamehimizwa kuanza kufanya ukulima wa mimea kuliko kutegemea mifugo pekee. Wenyeji wengi wameanza ukulima na unyunyuzaji maji viungani mwa mlima Kenya.

Mbinu hii ya kikundi cha II Ngwesi ya kuhamisha vifaru mara kwa mara na uzuiaji wa ulishaji wa kiholela umesaidia sana katika kuifanya nyasi na miti kufufuka na kumea upya. Juhudi zimefanywa ili kupanda nyasi ya aina Rhodesia sehemu ambazo zimetumiwa sana na watu wamehimizwa kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa kuchimba mitaro kwenye milima na miinuko.Wenyeji wamepata huduma ya maji ya mifereji kutoka mtoni.

Juhudi za kuinua haliya maisha ya jamii

Mbinu inayotumiwa na kikundi hiki ya utumizi bora wa ranchi imechangia upanuzi wa huduma za elimu na za afya katika eneo hili. Sehemu ya kipato kinachotokana na utalii hutumiwa kujenga madarasa mapya mashuleni, kuwalipa waalimu mishahara na kuwapa wanafunzi misaada ya masomo. Katika mwaka wa 2006 II Ngwesi ilipata ufadhili kutoka nchi ya Canada ambao ulitumika kuwahamasisha wenyeji kuhusu ugonjwa wa ukimwi. Kufikia mwaka wa 2010 wenyeji zaidi ya 4,000 walikuwa wamepimwa na kujua hali zao. II Ngwesi na Lewa walishirikiana kujenga vituo vya matibabu katika eneo hilo.

Tuzo za kitaifa na za kimataifa

II Ngwesi imepata sifa kama hifadhi muhimu nchini Kenya na katika Afrika mashariki kwa jumla. Hili limetokana na mikakati ambayo imefanya eneo hili kuwa kivutio kikubwa cha utalii na uhifadhi bora wa mazingira na wanyama pori. Hoteli ya kikundi hiki ilitangazwa kupitia mtandao na hili likaifanya kupewe tuzo na Shirika la Ndege la Uingereza (British Airways) kama kivutio bora zaidi cha kitalii - 1997). Aidha, kilishinda tuzo la hoteli ndogo bora mnamo 2006.

Hifadhi ya vifaru imeongezea kikundi hiki sifa zaidi. Mnamo 2002 eneo la II Ngwesi lilipokea kifaru mweusi mmoja kupitia usaidizi wa shirika la uhifadhi la Lewa na lile la KWS. Uhifadhi wa vifaru hawa watatu ni ushahidi tosha kuwa kuna usalama wa kutosha katika eneo la kikundi hiki. Walinzi 9 waliojihami na wenye redio za mawasiliano wameimarisha usalama eneo hili.

7

Matokeo

MATOKEO YA KIMAZINGIRATangu jadi eneo la II Ngwesi limekuwa makao ya idadi kubwa ya wanyama kabla ya uwindaji haramu wa miaka 1970 na 1980. Mnyama aliyeathirika zaidi na uwindaji huo ni kifaru mweusi. Ndovu nao waliangamizwa na wawindaji haramu kutoka Kenya na Somalia. Mfumo wa matumizi ya ardhi ulioanzishwa na kikundi cha II Ngwesi umefufua matumaini ya uhifadhi na utunzi wa ndovu na vifaru ambao wametishiwa kuangamizwa. Uhifadhi wa II Ngwesi umepigwa jeki na jamii nzima ya wilaya ya Laikipia na washirika wengine kama Lewa Downs. Kufaulu kwa juhudi za kikundi hiki zimetokana na kuwa na

vitega uchumi vingi miongoni mwa wafugaji na ulinzi wa kutosha uliopewa sehemu ya uhifadhi ya II Ngwesi.

Uhifadhi wa wanyama pori wanaotishiwa kuangamia

Mnamo mwaka wa 2002, tukio la kihstoria lilitendeka wakati kifaru mweusi alihamishwa kutoka eneo la uhifadhi la Lewa hadi II Ngwesi. Jambo hili la kuhifadhi vifaru katika eneo hili limetimiza lengo kuu la KWS. Kuhifadhi wanyama wanaotishiwa kuangamia. Hadi sasa vifaru weupe walioletwa eneo la II Ngwesi wangalipo. Lakini bado ni jambo lisiloeleweka wazi ikiwa KWS liko tayari kuwaongeza vifaru wengine hata baada ya kikundi cha II Ngwesi kuhakikisha kuwa kuna usalama wa kutosha kwa wanyama hao katika eneo hilo.

Juhudi za II Ngwesi zimeimarisha na kusaidia uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya karibu. Kikundi hiki kimesaidia wanyama kama punda-milia ambao hutembea baina ya hifadhi ya lewa na mbuga za Samburu, Buffalo Springs na ile ya Shaba.

Uhifadhi huo umeongezea idadi ya wanyama kama vile ndovu, twiga, punda-milia, ngiri nakhadhalika. Idadi ya miti nayo imeongezeka ndani ya eneo la uhifadhi la II Ngwesi. Aidha, idadi ya ndege imeongezeka yaani zaidi ya aina 300 za ndege wanapatikana katika eneo la II Ngwesi. Eneo hili la II Ngwesi vilevile linatumika kwa utafiti unaofanywa na mashirika mbalimbali.

MATOKEO YA KIJAMIIMiradi mingi ya II Ngwesi hugharamia kipato kitokacho kwenye utalii na hela hizo zinanuia kuimarisha kiwango cha maisha ya wanachama wa kikundi hicho. Kipato cha utalii kinatumika kama ifuatavyo: Asilimia 40 ya faida kutokana na hoteli hutumiwa katika maendeleo ya jamii, asilimia 60 hutumika katika kuendeleza hoteli yenyewe, hoteli ya kikundi hiki huleta kitita cha Shilingi milioni tisa (USD 86,500) kwa mwaka. Faida nayo ni shilingi milioni mbili.

i.Nafasi za kazi: Kikundi kimeweza kuunda nafasi za kazi kwenye hoteli yao ya kitalii. Hoteli ina wafanyakazi 15 na walinzi wa msitu 9. Aidha, vibarua hupata kazi katika miradi ya ujenzi katika ranchi.

ii. Vitega uchumi vingine: Katika kujipatia riziki, wanawake wa eneo hili huwauzia watalii vinyago wanavyovitengeneza. Aidha II Ngwesi kinanuia kununua na kuwauzia asali watalii ili kupata riziki. Vilevile II Ngwesi ikishirikiana na shirika la ngambo la kujitolea kutoa huduma (VSO) wameanzisha mradi wa miaka 4 unaonuia kuwapa mafunzo ya kuunda bidhaa kadhaa vya shanga ili kuwauzia watalii na kujipatia riziki. Wanawake hao vilevile husaidiwa kupata mikopo midogo midogo ili waweze kununua malighafi watakayotumia katika mradi huo wao. Aidha, wanawake hao watapata mafunzo kuhusu uongozi na utawala kukuza biashara na mafunzo kuhusu kutafuta masoko ya bidhaa zao. Kikundi kinalenga kuanzisha benki ya kijamii kwa usaidizi wa benki ya K-Rep.

iii. Faida za kijamii: Kikundi kimemarisha pato la wenyeji kupitia biashara vya kijijini. Utumizi bora wa ardhi umepiga jeki kilimo na ufugaji. Mnamo mwaka wa 2008-9 wakati wa kiangazi mifugo waliruhusiwa maeneo ya wanyama pori na hivyo kuokoa maisha yao kutokana na makali ya ukame.

iv. Uwekezaji katika elimu: Elimu imepata ufanisi mwingi kutokana na mradi huu ambapo takribani shilling nusu million hutumika kila mwaka ili kuwafadhili wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu. Wasichana hupewa misaada ili waepuke kuolewa mapema. II Ngwesi imesaidia kujenga nyumba za walimu katika shule ya msingi ya Sang’a. Aidha kikundi kilichimba kisima katika shule ya msingi ya Enakishoni. Misaada ya kigeni imetumika kulipa walimu mishahara yao.

v. Mifumo ya usambazaji maji: Mnamo mwaka wa 2008 mifereji itoayo maji Mtoni Ngare Ndare iliyokuwa imeharibika ilikarabatiwa kutokana na ufadhili wa Kansas Zoo na Reid Park Zoo (zote ya Marekani) na Northern Rangeland Trust. Maji haya yamesaidia sana mifugo pamoja na kutumiwa hotelini. Mifereji imepanuliwa ili kunufaisha wanajamii wengi pamoja na kutumiwa na shule nyingi. Wanajamii vilievile wamefaidika na miradi ya maji iliyokarabatiwa na ufadhili wa kushughulikia elimu wa kikundi cha Lewa Downs. Kwa ufupi mifumo saba ya mifereji imewekwa ili kutoa maji mitoni hadi vijijini.

vi. Huduma za afya: Kikundi cha II Ngwesi kimeekeza kwa huduma za afya kwa kujenga zahanati ya Nadungoro na wanatafuta kibali cha serikali ili kuanza shughuli zake rasmi. Aidha, wanashirikiana na kikundi cha uhifadhi cha Lewa ili kuwapelekea wanakijiji huduma za kimatibabu angaa mara moja kwa wiki.

Isitoshe wenyeji wamefaidika mno na mradi wa kikundi cha II Ngwesi huitwao, Mradi wa Afya II. Mradi huu ulipigwa jeki na ufadhili wa shirika la kutoa misaada la Marekani la USAID ambalo linafanya kazi Mkoani Bonde la Ufa. Aidha, mnamo mwaka wa 2006 II Ngwesi likishirikiana na Taasisi ya Maswala ya Kitamadumi la Canada (ICA), wamefanya utafiti ili kupata taswira kamili ya wamaasai kuhusu ugonjwa wa ukimwi. Kutokana na matokeo ya utafiti huo, wenyeji walipewa mafunzo kuhusu magonjwa ya Ukimwi, malaria na kifua

kikuu. Mafunzo na uhamasisho huu ulifikia takriban watu 40,000 nje ya eneo la II Ngwesi. Mwanzoni, makundi ya ranchi mbi za IINgwesi na Makurian ambapo watu 5000 walikusudiwa kupewa ushauri na kupimwa na zaidi ya 20,000 walikusudiwa katika kipindi cha miaka ya 2007/8 kuhamasishwa ili kujiathari kutokana na Ukimwi. Katilka kipindi cha miaka ya 2009 na 2010, zaidi ya watu 3000 walipimwa na kushauriwa. Utafiti uliofanywa mwaka wa 2009 na Chuo Kikuu cha Toronto, Canada, ulionyesha kwamba watu 8,000 walikuwa wamepimwa na idadi ya waliopatikana na virusi ilikuwa chini ya asilimia 5 na walikuwa wanapokea huduma za matibabu. Asilimia 70 ya waliohojiwa walikuwa wamehudhuria mkutano wa uhamasisho juu ya Ukimwi, asilimia 56 walikuwa wamepimwa huko II Ngwesi, asilimia 80 walikuwa wametembelewa nyumbani.

MATOKEO YA KISERAKikundi cha II Ngwesi kikishirikiana na kikundi cha uhifadhi cha Lewa pamoja na Wakifu wa Northern Rangeland wameathiri sana sera za shirika la uhifadhi wa KWS ambapo shirika hili limekipa kikundi cha II Ngwesi kifaru mweusi baada ya kuhakikisha kuwa hii ranchi ilikuwa salama kwa uhifadhi wa wanyama pori.

Hata hivyo, uhusiano wa kikundi na KWS umedorora baada ya kudinda kuongeza kifaru mwingine likilalamikia usalama wa wanyama hao. Licha ya misukosuko hii II Ngwesi bado ni eneo la kupigiwa mfano kama mradi uliofaulu wa kuwahifadhi wanyama pori. Kutokana na kufaulu kwa mradi huu, watu wengi nchini Kenya na Tanzania wamefaidika kutokana na mbinu hizi.

8

9

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu

JINSI YA KUDUMISHA MRADI HUUKikundi hiki kinajitosheleza kifedha hususan kipato kinachopatikana kutoka kwa hoteli yao ya kitalii – kwa mwaka mzima hoteli huleta Dolla za kimarekani 86,500 (Ksh millioni 7). Asilimia 40 ya fedha hizi huekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo ya kijamii na zilizobakia huendeza hoteli. Hoteli hii imejiendeleza na kujisimamia bila ufadhili wowote tangia mwaka wa 2004. Isitoshe, kipato hupatikana kutoka kwa kiingilio ambapo kila mtu hulipa Dolla za kimarekani 40 na wanaoishi kambini hulipa Dolla 300 (KSh 25000) kila usiku. Uuzaji vinyago na vitega uchumi vingine pia huwa pato la kikundi. Watalii wanapoingia kwa boma za Kimaasai huwapa pato wenyeji na wala si kikundi.Watalii wanapokodisha magari ya ranchi pia huleta mapato zaidi kwa kikundi cha II Ngwesi huku wanawake wakinufaika kutokana na mauzo ya vinyago wanavyojitengenezea.

Uwekezaji

Ufadhili wa kigeni huhitajika tu wakati kipato cha kikundi hakitoshi. Wafadhili wa kigeni wamechangia sana katika miradi ya huduma za afya na ile ya kutoa mafunzo ya kibiashara kwa wenyeji “Mradi wa Afya II” humefadhiliwa na mashirika ya FHI na ICA na mafunzo ya kibiashara yalifadhiliwa na shirika la VSO. Mishahara ya walimu hulipwa na kikundi cha II Ngwesi, serikali na wafadhili mahsusi. Kwa upande mwingine, ukarabati wa mifereji ya maji na ulipaji walinzi hufanywa na kikundi ili kujitosheleza. Kikundi kinanuia kununua shamba mjini Timau na kujenga nyumba za upangaji. Pesa za kulipa mpango huu zitatolewa kutoka kwa marupurupu ambayo wangepewa wanachama wa kikundi. Kamati imeuundwa ili kufanya hesabu kamili ya mpango huu ili kuomba ufadhili.

Manufaa kwa jamii na na mazingira

Kufaulu kwa kikundi hiki kumetokana na uhusishaji wa jamii kwa jumla katika uongozi wao. Wanachama vilevile wana usemi mkuu katika kikundi hiki jambo ambalo limeongezea uunguaji mkono na

jamii za mashinani. Licha ya uunguaji mkono huu kutoka kwa jamii ya mashinani, kumekuwa na mitafaruku ya kung’ang’ania malisho na shamba kati ya kikundi cha II Ngwesi na wanakijiji. Misukosuko hii imeongezewa na ukuaji wa idadi ya watu na mabadiliko ya hewa. Hali hii imesababisha kung’anga’nia nyasi kati ya wanyama pori na mifugo. Wanachama wa kikundi wamependekeza wanakijiji wahamishe ili kubuni nafasi za kazi za kutosha kwa shughuli za utalii ingawa wanachama wanahofia kuwa jambo hili laweza kusababisha sehemu hii ya uhifadhi kutwaliwa na KWS.

Kikundi hiki kimechangia sana uhifadhi wa mazingira na wanyama pori katika wilaya hii ya Laikipia wakishirikiana na wakfu wa Northern Rangeland. Ikiwa jamii ya Wamaasai watahamishwa na kupata makao mbadala katika kipindi cha miaka mitano ijayo, eneo lote litatumiwa kikamilifu kwa uhifadhi wa wanyama pori. Wanyama watahamishwa kutoka hifadhi ya Lewa, Lekurruki na ranchi ya Borana ili kuunda hifadhi moja kubwa inayojumuisha ranchi nne. Aidha, kikundi kinadhamiria kuongezea idadi ya vifaru weusi na kuongeza vikundi vingine ili kuungana na kupanua shughuli hizi za uhifadhi.

Changamoto

Ushindani kutoka vikundi vingine: Kikundi kinadhana kuimarisha miundo msingi kama barabara maana kufika eneo la II Ngwesi ni tatizo kubwa kwa sasa.

Mabadiliko ya hali ya hewa: Hali ya hewa hubadilika badilika na kutatiza wafugaji jambo linalowafanya kupeleka mifugo wao katika hifadhi za wanyama pori.

Umuliki wa shamba lililonunuliwa: Kuna maswali ambayo bado kupata majibu kuhusu namna shamba litakalonunuliwa na kujengwa kwa nyumba za kuishi na nani atakayesimamia mradi huo.

Usalama: II Ngwesi inadhamiria kuongezea usalama zaidi katika eneo la uhifadhi ndiposa wapate kupewa vifaru weusi zaidi na wanyama wengine waliotishiwa kuangamia.

“Mazingira huhusu kila mtu. Ni jukumu la kila mtu kulinda mazingira. Kila mtu lazima achangie”

James Kasoo, Ranchi ya Il Ngwesi

1010

MAONOII Ngwesi imetumiwa kama kielelezo kwa vikundi vingine vya uhifadhi wa wanyama pori vya humu nchini Kenya, Tanzania, Uganda na Sudan ya kusini. Wageni wengi wamekaribishwa na kikundi cha II Ngwesi ili kujionea na kupata maarifa na ujuzi zaidi. Aidha wazee wa eneo hili wamewahi kuitwa na KWS ili kuhimizwa na kupongezwa kwa uhifadhi wa wanyama pori. Vikundi vilivyofanikiwa kuiga juhudi hizi ni pamoja na Naibunga ambayo imehifadhi wanyama katika takriban hekari 1,700 na wakfu wa kijamii wa Shompole kutoka Magadi kusini mwa Kenya.

WAHISANI• Lewa Wildlife Conservancy• Northern Rangelands Trust• Laikipia Wildlife Forum• Africa Wildlife Foundation• Kenya Wildlife Service • University of Nairobi• Kenya Forestry Research Institute• Voluntary Service Overseas • Borana Ranch• Family Health International

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa:

MAREJELEO YA ZIADA

• Ranchi ya Il Ngwesi Group website: ilngwesi.com • Ranchi ya Il Ngwesi PhotoStory (Vimeo) vimeo.com/27016070 (English) vimeo.com/15750010 (Swahili)

Equator InitiativeEnvironment and Energy GroupUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781-4023 www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator