2
7/21/2019 Risala Ya Kdt -2015 http://slidepdf.com/reader/full/risala-ya-kdt-2015 1/2  1 RISALA YA WAHITIMU KIDATO CHA NNE KWA MGENI RASMI NOVEMBA - 2015 Ndugu Mgeni Rasmi, wageni waalikwa, wazazi, walimu, wanafunzi wanaobaki shule nyote mliohudhuria hafla hii, kwanza kabisa tunamshukuru Allah (s.w) kutujaalia afya njema na kuifikia siku ya leo. Pia tunatoa shukrani za dhati kwa kuacha shughuli zenu na kuja kujumuika nasi katika hafla hii ya kuhitimu kidato cha nne. Ndugu Mgeni Rasmi Walioko mbele yako ni wahitimu wa kidato cha nne ambao tulianza masomo mwaka 2012 tukiwa jumla ya wanafunzi 180 ambao kati ya hao wavulana walikuwa 75 na wasichana walikuwa 105. Leo tunahitimu tukiwa wanafunzi 47 ambao wavulana ni 26 na wasichana ni 21, baadhi yao walishindwa kufika hapa tulipo kwa sababu mbali mbali kama vile ukosefu wa ada, kuhama shule, kushindwa kufikia wastani wa shule na utovu wa nidhamu. Ndugu mgeni rasmi Katika kipindi tulichoishi tulipokuwa hapa shuleni yafuatayo ni mafanikio tuliyoyapa; 1.  Ufaulu mzuri kwa mitihani ya ndani na nje ya shule, hili linadhihirishwa kwa kutazama takwimu ya mtihani wa mock kidato cha pili ambapo shule ilishika nafasi ya nne kati ya shule zilizo shiriki ,na katika mtihani wa kidato cha pili tulifanya mtihani jumla ya wanafunzi 86 na wote tulifaulu kuingia kidato cha tatu. 2.  Kusoma masomo ya sayansi kwa njia ya vitendo (Practical) na pia tumekua wanafunzi wa kwanza kufanya mitihani yote ya sayansi kwa vitendo hapa shuleni, hii ni kutokana na shule kujenga maabara na kununua vifaa mbali mbali kama kemikali za kufanyia majaribio na viumbe vya kufanyia majaribio. 3.  Kupatikana makazi (hostels) ya furaha kwa wanafunzi baada ya kuanzishwa kwa  bweni la wavulana na kuongezwa chumba cha bweni la wasichana ,hii imetusaidia kujipatia muda wa kutosha wa kujisomea, kufanya majadiliano ya sisi kwa sisi na kuwa karibu na waalimu kwa msaada zaidi. 4.  Kujipatia elimu ya kujitegemea kwa kushiriki kikamilifu katika ufyatuaji wa tofari katika eneo la Mtumba na tofari hizo kutumika katika maendeleo ya dini yetu kwa kujengea misikiti na vituo vya elimu ikiwemo shule yetu.

Risala Ya Kdt -2015

Embed Size (px)

DESCRIPTION

w

Citation preview

Page 1: Risala Ya Kdt -2015

7/21/2019 Risala Ya Kdt -2015

http://slidepdf.com/reader/full/risala-ya-kdt-2015 1/2

 

1

RISALA YA WAHITIMU KIDATO CHA NNE KWA MGENI

RASMI NOVEMBA - 2015

Ndugu Mgeni Rasmi, wageni waalikwa, wazazi, walimu, wanafunzi wanaobaki shulenyote mliohudhuria hafla hii, kwanza kabisa tunamshukuru Allah (s.w) kutujaalia afyanjema na kuifikia siku ya leo. Pia tunatoa shukrani za dhati kwa kuacha shughuli zenu

na kuja kujumuika nasi katika hafla hii ya kuhitimu kidato cha nne.

Ndugu Mgeni RasmiWalioko mbele yako ni wahitimu wa kidato cha nne ambao tulianza masomo mwaka

2012 tukiwa jumla ya wanafunzi 180 ambao kati ya hao wavulana walikuwa 75 nawasichana walikuwa 105. Leo tunahitimu tukiwa wanafunzi 47 ambao wavulana ni 26

na wasichana ni 21, baadhi yao walishindwa kufika hapa tulipo kwa sababu mbali mbalikama vile ukosefu wa ada, kuhama shule, kushindwa kufikia wastani wa shule na utovu

wa nidhamu.

Ndugu mgeni rasmiKatika kipindi tulichoishi tulipokuwa hapa shuleni yafuatayo ni mafanikio tuliyoyapa;

1. 

Ufaulu mzuri kwa mitihani ya ndani na nje ya shule, hili linadhihirishwa kwakutazama takwimu ya mtihani wa mock kidato cha pili ambapo shule ilishika

nafasi ya nne kati ya shule zilizo shiriki ,na katika mtihani wa kidato cha pilitulifanya mtihani jumla ya wanafunzi 86 na wote tulifaulu kuingia kidato cha

tatu.

2. 

Kusoma masomo ya sayansi kwa njia ya vitendo (Practical) na pia tumekuawanafunzi wa kwanza kufanya mitihani yote ya sayansi kwa vitendo hapa

shuleni, hii ni kutokana na shule kujenga maabara na kununua vifaa mbali mbalikama kemikali za kufanyia majaribio na viumbe vya kufanyia majaribio.

3. 

Kupatikana makazi (hostels) ya furaha kwa wanafunzi baada ya kuanzishwa kwa

 bweni la wavulana na kuongezwa chumba cha bweni la wasichana ,hii

imetusaidia kujipatia muda wa kutosha wa kujisomea, kufanya majadiliano yasisi kwa sisi na kuwa karibu na waalimu kwa msaada zaidi.

4. 

Kujipatia elimu ya kujitegemea kwa kushiriki kikamilifu katika ufyatuaji wa

tofari katika eneo la Mtumba na tofari hizo kutumika katika maendeleo ya diniyetu kwa kujengea misikiti na vituo vya elimu ikiwemo shule yetu.

Page 2: Risala Ya Kdt -2015

7/21/2019 Risala Ya Kdt -2015

http://slidepdf.com/reader/full/risala-ya-kdt-2015 2/2

 

2

Ndugu mgeni rasmiPalipo na mafanikio hapakosi changamoto. Zifuatazo ni changamoto zilizo tukumba

katika maisha ya uanafunzi hapa shuleni;-

1. 

Upungufu wa vifaa na madawa ya kufanyia majaribio kwa vitendo,haliiliyosababisha kutofanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya maandalizi ya mtihani

wa kidato cha nne.

2. 

Ukosefu wa wataalamu wa maabara (Laboratory technician) wa kusimamiamasomo ya sayansi kwa vitendo hali iliyosababisha kutumia wataalamu kutokanje ya shule.

3. 

Kutokamilika kwa jengo la maabara na kupelekea masomo yote ya sayansi kwavitendo kufanyikia katika chumba kimoja tu.

4. 

Ukosefu wa bwalo la kulia chakula kwa wanafunzi wa bweni haliinayosababisha wanafunzi kulia chakula sehemu ya wazi. Hali hiyo husababishausumbufu wakati wa chakula hususani wakati wa mvua.

5. 

Kutokamilika kwa jengo la msikiti hali inayosababisha ugumu wa kutekelezaibada ya swala hasa wakati wa mvua na jua kali kwani swala hufanyikia eneo la

wazi.

6. 

Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada kwa wanafunzi kujipatia maarifambalimbali hali hii inapelekea kitabu kimoja kutumiwa na mwanafunzi zaidi ya

mmoja hivyo kusababisha wanafunzi kutegemea maarifa kutoka kwa walimu badala ya kujisomea vitabu wenyewe.

Ndugu mgeni rasmi.

 Ni matumaini yetu kuwa wewe na wote mliohudhuria hafla hii mtakua chachu yakuzitatua changamoto hizo ili kuchochea ufanisi zaidi. Tunawaombea kwa Allah [s.w]

kheri na baraka mrudipo nyumbani mfike salama.

Risala hii imeandaliwa na wahitimu wa kidato cha nne na kuwasilishwa na;

1. 

Hussein Hamisi Noboka.2.

 

Hassan Saidi Jumanne.

Wabillah tawfiq.