23
SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2011 MPANGILIO WA VIFUNGU Kifungu Maelezo SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Jina na kuanza kutumika 2. Matumizi 3. Tafsiri SEHEMU YA PILI MADHUMUNI 4. Madhumuni SEHEMU YA TATU UUNDAJI WA TUME 5. Uundaji wa Tume 6. Uteuzi wa wajumbe wa Tume 7. Muundo wa Tume 8. Hadidu za Rejea 9. Kazi za Tume 10. Uhuru wa Tume 11. Kiapo cha wajumbe na Katibu. 12. Ukomo wa ujumbe 13. Sekretarieti. 14. Gharama za Tume 15. Kinga kwa wajumbe wa Tume na Sekretarieti SEHEMU YA NNE UTARATIBU WA UTENDAJI KAZI WA TUME 16. Utaratibu wa utendaji kazi. 17. Ripoti ya Tume.

Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Huu ni Muswada kwa ajili ya kutunga sheria itakayosimamia mchakato wa kuundwa kwa Katiba Mpya nchini Tanzania.

Citation preview

Page 1: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2011

MPANGILIO WA VIFUNGU

Kifungu Maelezo

SEHEMU YA KWANZA

MASHARTI YA UTANGULIZI

1. Jina na kuanza kutumika

2. Matumizi

3. Tafsiri

SEHEMU YA PILI

MADHUMUNI

4. Madhumuni

SEHEMU YA TATU

UUNDAJI WA TUME

5. Uundaji wa Tume

6. Uteuzi wa wajumbe wa Tume

7. Muundo wa Tume

8. Hadidu za Rejea

9. Kazi za Tume

10. Uhuru wa Tume

11. Kiapo cha wajumbe na Katibu.

12. Ukomo wa ujumbe

13. Sekretarieti.

14. Gharama za Tume

15. Kinga kwa wajumbe wa Tume na Sekretarieti

SEHEMU YA NNE

UTARATIBU WA UTENDAJI KAZI WA TUME

16. Utaratibu wa utendaji kazi.

17. Ripoti ya Tume.

Page 2: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

18. Uwasilishaji wa ripoti ya Tume.

19. Makosa na adhabu.

SEHEMU YA TANO

KUUNDWA BUNGE LA KATIBA

20. Kuundwa Bunge la katiba.

21. Spika na Naibu Spika wa Bunge la katiba.

22. Katibu na watumishi wa Bunge la katiba.

23. Mamlaka ya Bunge la katiba.

24. Masharti kuhusu Bunge la katiba.

25. Sheria za Bunge la katiba.

26. Ukomo wa mamlaka ya Bunge la katiba.

SEHEMU YA SITA

UHALALISHAJI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

27. Utendeshaji wa kura ya maoni.

28. Swali la Kura ya maoni.

29. Taarifa ya uendeshaji wa kura katika kura ya maoni.

30. Haki ya kupiga kura katika kura ya maoni

31. Utaratibu wa kuendesha kura ya maoni

32. Matokeo ya Kura ya maoni.

33. Kuvunjwa kwa Tume.

34. Kuanza kutumia kwa katiba.

_____

MAJEDWALI

_____

Page 3: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

____

TAARIFA

____

Muswada huu, utakaowasilishwa Bungeni ulichapishwa katika Toleo Maalum la

Muswada Na.1 wa tarehe 11 March, 2011 na kusomwa mara ya kwanza Bungeni

tarehe 5 Aprili, 2011. Muswada huu sasa unachapishwa tena kwa lugha ya

Kiswahili na kiingereza kwa madhumuni ya kusomwa mara ya pili na kusomwa

mara ya tatu.

Dar es Salaam, PHILLEMON L.LUHANJO,

9 Juni, 2011 Katibu wa Braza la Mawaziri

MUSWADA

wa

Sheria kwa ajili ya kuunda Tume ya Mabadiliko ya katiba kwa madhumuni

ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba; kuainisha na

kuchambua maoni ya wananchi;kuainisha masharti kuhusu mabaraza ya

kuhalalisha masharti yaliyomo kwenye Rasimu ya katiba; kuweka masharti juu ya

utayarishaji na uwasilishaji wa ripoti kuhusu maoni ya wananchi;kuweka utaratibu

wa kuunda Bunge la katiba, uendeshaji wa kura ya maoni na kuweka Bunge la

katiba, uendeshaji wa kura ya maoni na kuweka masharti yanayohusiana na

mambo hayo.

IMETUNGWA Na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

SEHEMU YA KWANZA

MASHARTI YA UTANGULIZI

Jina na 1.-(1) Sheria hii itaitwa Sheria ya Mabadiliko ya katiba ya

mwaka 2011.

Sheria

Kuanza

Kutumia

Page 4: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

(2) Sheria hii itaanza kutumika tarehe 1 Desemba, 2011.

Matumizi 2. Sheria hii itatumikaTanzania Bara na Tanzania Zanzibar

Tafsiri 3. Katiba Sheria hii, isipokua kama muktadha utahitaji vinginevyo:

“Katiba” maana yake ni sheria ya msingi, iliyoandikwa au

isiyoandikwa, ambayo inaweka mfumo wa Taifa kwa kuanisha

misingi ya taifa ambayo jamii italazimika kuifuata, mgawanyo wa

madaraka na majukumu ya mihimili mikuu ya dola, kwa kuanisha

muundo wa serikali, bunge na mahakama, usimamizi wake

mgawanyo na ukomo wa mamlaka ya vyombo mbalimbali vya dola,

na kwa kuanisha namna na taratibu za utekelezaji wa mamlaka yao;

Sura ya 2 ‘Katiba “maana yake ni Katiba ya Jamuhuri ya muungno wa

Tanzania ya mwaka 1977;

“Katiba inayopendekezwa” maana yake ni Risimu ya katiba

iliyopitishwa na Bunge la katiba kwa ajili ya kupigiwa kura ya

maoni;

“Katibu” maana yake ni katibu aliyetanjwa chini ya kifungu cha 13;

“Kura ya maoni” maana yake ni kura iliyopingwa na wananchi

kwa mujibu wa masharti ya sheria hii kwa madhumuni ya kuridhia

katiba inayopendekezwa;

“Mapitio ya Katiba “maana ni mchakato wa kukusanya maoni ya

wananchi juu ya kutunga upya katiba ya jamuhuri ya Muungano wa

Tanzania;

“Mabaraza” maana yake ni mikutano, mikusanyiko, hadhara au

majadiliano huru na ya wazi yaliyotayarishwa au kuandaliwa na

Tume kwa madhumuni ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya

Rasimu ya Muswada wa katiba;

“Maoni ya wananchi” maana yake ni mawazo, maoni, fikra,

taarifa au mapendekezo yaliyokusanywa kotoka kwa wananchi kwa

madhumuni ya mchakato wa mabadiliko ya katiba;

Sura ya 2 “Rais” maana yake ni Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania;

Page 5: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

“Tume” maana yake ni Tume iliyoanzishwa kwa madhumuni ya

kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mchakato wa

mabadiliko ya katiba;

“Waziri” maana yake ni Waziri wa serikali ya jamuhuri ya

Muungano mwenye dhamana ya mambo ya katiba.

SEHEMU YA PILI

MADHUMUNI

Madhumuni 4. Madhumuni ya Sheria hii yatakuwa ni;

a) Kuweka utaratibu wa kuunda Tume itakayokusanya na

kuratibu maoni ya wananchi;

b) Kuanisha viapo au yamini na kuweka taratibu kuhusu

namna ya wajumbe wa Tume na Sekretarieti

watakavyoapa au kula yamini;

c) Kuweka masharti kuhusu Hadidu za Rejea za Tume;

d) Kuweka masharti ya kuundwa kwa Sekretarieti ya Tume

itakayoongozwa na katibu;

e) Kuweka utaratibu ambao utaruhusu wananchi kushiriki

kwa mapema katika kutoa na kuwasilisha maoni yao

kuhusu katiba;

f) Kuweka utaratibu ambao Tume itatumia katika

kutayarisha na kuwasilisha ripoti;

g) Kuainisha majukumu na mamlaka ya Tume;

h) Kuweka utaratibu kuhusu namna ambayo Tume

itakusanya maoni kutoka katika taasisi za umma na

binafsi, vyama vya hiari na mashirika ya kidini;

i) Kuweka utaratibu utakaowezesha Tume kupata taarifa za

kitaalam kutoka kwa wataalam elekezi;

j) Kwa ujumla, kuweka utaratibu utakaowezesha kujenga

muafaka wa kitaifa katika masuala yenye maslahi kwa

taifa wakati wa mchakato kukhusu katiba;

k) Kuweka utaratibu utakaoweza kuchambua Rasimu ya

Muswada wa katiba;

Page 6: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

l) Kuanzisha mfumo wa kisheria utakaomwezesha Rais

kuunda Bunge La katiba;

m) Kuweka mfumo utakaowezesha uchaguzi wa spika na

Naibu wa Bunge la katiba na kupatikana kwa katibu na

watendaji wengine;

n) Kuweka mfumo wa sheria utakaowezesha kupiga kura ya

maoni;na

o) Kuweka utaratibu wa namna katiba Mpya

itakavyozinduliwa;

SEHEMU YA TATU

UUNDAJI WA TUME

Uundaji wa Tume 5. Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais

wa Zanzibar, na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu

wa serikali wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na

Mwanasheria mkuu wa Zanzibar na kwa kuzingatia

hali ya jamii, kisiasa na kiuchumi iliyopo katika

jamuhuri ya muungano katika nyakati zote na kwa

amri itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali

ataunda Tume.

Uteuzi wa 6.-(1) Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na

Rais wa Zanzibar atateua wajumbe wa Tume

Wajumbe

Wa Tume

(2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (3)

muundo wa Tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa

uwakilishi ulio sawa kwa kila upande wa jamuhuri ya

muungano.

(3) Katika kufanya uteuzi wa wajumbe wa Tume, Rais

atazingatia masuala yafuatayo;

Page 7: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

a) Uzoefu katika kufanya mapitio ya katiba na sifa

za kitaalam za wajumbe kwenye mambo ya

katiba, sheria , utawala , uchumi, fedha na

sayansi ya jamii;

b) Jiohrafia na mtawanyiko wa watu katika

jamuhuri ya muungano wa Tanzania;

c) Maslahi ya Umma;

d) Umri , jinsia na uwakilishi wa makundi

mbalimbali ya kijamii; na

e) Vigezo vingine ambavyo Rais ataona vinafaa.

(4) Bila ya Kujali kifungu kidogo cha (3) , mtu

hatakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa

Tume endapo mtu huyo;

a) Ni mbunge , mjumbe wa Baraza la

wawakilishi la Zanzibar, Diwani au

Kiongozi wa chama cha siasa wa ngazi ya

Taifa , Mkoa au Wilaya;

b) Ni mtumishi katika vyombo vya usalama;

c) Ni mtu aliyewahi kuhukumiwa kwa kutenda

kosa au ni mtuhumiwa katika shauri lililopo

mahakamani. linalohusu shitaka la kukosa

uaminifu au maadili;au

d) Si raia wa Tanzania

Muundo wa Tume 7,-(1) Tume itakuwa na wajumbe kama ifuatayo:

a) Mwenyekiti;

b) Makamu Mwenyekiti; na

c) Makamishna wengine wasiozidi thelathini.

(2) Uteuzi wa Mwenyekiti na makamu mwenyekiti

utafanyika kwa msingi kwamba iwapo mwenyekiti

atatoka upande mmoja wa jamuhuri ya Muungano,

basi Makamu mwenyekiti atakuwa mtu anayetoka

upande mwingine wa jamuhuri ya Muungano.

Page 8: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

(3) Wajumbe wa Tume watateuliwa kupitia amri

itakayotangazwa kwenye Gazeti la serikali.

Hadidu za Rejea 8,-(1) Hadidu za rejea za Tume zitatolewa na Rais kwa

makubaliano na Rais wa Zanzibar katika amri ile ile

ambayo uteuzi wa wajumbe wa Tume utafanyika na

kuanisha muda ambao Tume inatakiwa kukamilisha na

kuwasilisha na kuwasilisha ripoti.

(2) Rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar anaweza, kama hali itahitaji

kufanya hivyo, kuongeza muda usiozidi miezi mitatu

ili kuwezesha Tume, kukamilisha na kuwasilisha

ripoti.

(3) Hazidu za rejea zitakuwa ni hati ya kisheria ambayo Tume itaizingatia katika

utekelezaji wa majukumu na utumiaji wa mamlaka

yake kwa mujibu wa sheria hii.

Kazi za Tume 9,-(1) Majukumu ya Tume yatakuwa ni-

a) Kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi;

b) Kupitia na kutafiti usahihi na ulinganifu wa

masharti ya kikatiba yanayohusu mamlaka ya

watu, mifumo ya kisiasa, demokrasia, utawala

wa sheria na utawala bora;

c) Kutoa mapendekezo kwa kila hadidu ya

rejea;na

d) Kuandaa na kuwasilisha ripoti

(2) Katika kutekeleza masharti ya kifungu kidogo

cha (1), Tume itazingatia misingi mikuu ya

kitaifa na maadili ya jamii na kwa mantiki hiyo,

kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo:

a) Kuwepo kwa jamuhuri ya Muungano ;

b) Uwepo wa serikali, Bunge na Mahakama;

c) Mfumo wa kiutawala wa kijamuhuri;

d) Uwepo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar;

e) Umoja wakitaifa,amani na utulivu;

Page 9: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

f) Uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara

katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya

watu wote kupiga kura;

g) Ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu;

h) Utu, usawa mbele ya Sheria na mwenendo wa

sheria; na

i) Uhuru wa kuabudu na uvumilivu wa dini

nyingine.

(3) Kwa madhumuni ya vifungu vya (1), (2) na

kwa jambo lolote jingine muhimu kwa taifa,

Tume itatoa fursa kwa watu kutoa maoni yao

kwa uhuru kwa lengo la kuendeleza na

kuboresha masuala hayo.

Mamlaka ya Tume 10. Tume itakuwa na mamlaka na uhuru kwa kadri

itakavyokuwa muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa

majukumu na matumizi ya mamlaka yak echini ya

sheria hii na haitaingiliwa na mtu au mamlaka yoyote

Kiapo cha wajumbe na katibu 11. Kabla ya kuanza kutekeleza majukumu

yake, kila mjumbe wa Tume na katibu ataapa au kula

yamini mbele ya Rais kwa namna ilivyoainishwa

katika jedwali la kwanza la sheria hii.

Ukomo wa wajumbe 12. –(1) Mtu atakoma kuwa mjumbe wa Tume endapo

litatokea tukio lolote kati ya matukio yafuatayo:

a) Kifo;

b) Kujiuzulu;

c) Kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu

yake kwa sababu za kiafya;

d) Kuondolewa kwa makosa ya kukiuka kanuni za

maadili;

e) Kutiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni

kifungo gerezani kwa muda usiopungua mwezi

mmoja;au

Page 10: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

f) Kupoteza sifa ambazo kwazo aliteuliwa

(2) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu

ya Tume, kutakuwa na kanuni za maadili kama

zilivyoainishwa katika jedwali la pili la sheria hii.

(3) Mjumbe wa Tume au sekretarieti ambaye atakiuka

masharti ya kanuni za maadili atapoteza sifa za

kuendelea kuwa mjumbe.

Sekretarieti 13.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Tume itakayoongozwa

na katibu.

(2) Katibu atateuliwa na Rais baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibar.

(3) Mtu atakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa katibu endapo mtu huyo ni mtumishi

wa serikali na ana taaluma ya sheria na amefanya kazi hiyo

kwa muda usiopungua miaka kumi na ana mwenendo na tabia

nzuri.

(4) Katibu atawajibika kwa Tume na atafanya kazi na kutekeleza majukumu ya

Sekretarieti.

(5) Watendaji wengine wa Sekretarieti watateuliwa na waziri kwa makubaliano na

waziri mwenye dhamana ya mambo ya katiba wa Serikali ya

Mapinduzi Zanzibar.

(6) Sekretarieti itakuwa na idadi ya watumishi wa umma kwa kadri

itakavyohitajika kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa

majukumu na matumizi ya mamlaka ya Tume.

Gharama za Tume 14.-(1) Gharama za shughuli za Tume wakati wa mchakato

wa mapitio ya katiba kwa mujibu wa sheria hii zitalipwa

kutoka mfuko mkuu wa Hazina.

(2) Wajumbe wa Tume na Sekretarieti watalipwa kwa kadri waziri atakavyoamua

kulingana na sheria na kanuni za nchi.

Kinga kwa wajumbe wa Tume na Sekretarieti 15. Mjumbe wa Tume au Sekretarieti

hatashitakiwa yeye binafsi kwa ushauri la madai au jinai

kutokana na jambo lolote au kitu chochote atakachofanya au

kutofanya kwa nia njema kama mjumbe wa Tume au

Sekretarieti katika utekelezaji wa majukumu na utumiaji wa

mamlaka yak echini ya sheria hii.

Page 11: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

SEHMU YA NNE

UTARATIBU WA UTENDAJI KAZI WA TUME

Utratibu wa utendaji kazi 16.-(1) Tume itatekeleza majukumu yake kwa mujibu

wa sheria hii na hadidu za rejea.

(2) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa kifungu kidogo cha (1), Tume itafanya kazi

zifuatazo:

a) Kuandaa na kuendesha programu za kuelimisha juu ya madhumuni na

majukumu ya Tume;

b) Kuitisha na kusamamia mikutano au mabaraza katika sehemu na nyakati

mbakimbali kama ambavyo itakavyoamua;

c) Kutathmini na kuchambua kwa kutofautiana maoni ya wananchi

yanayokubaliana na yale yasiyokubaliana; na

d) Kutayarisha na kuwasilisha ripoti kwa kuzingatia hadidu za rejea.

(3) Tume yaweza kumtaka mtu yeyote atakaye hiari kufanya hivyo kwenda mbele

ya Tume kufanya majadiliano, kwa mazungumzo au

kuwasilisha nyaraka, kuhusu jambo lolote la kikatiba ambalo

Tume inaona ni muhimu na linahusiana na mchakato wa

mapitio ya katiba.

(4) Katika kutekeleza majukumu yak echini ya sheria hii, Tume itapitia au

kuchambua michango, mawazo, maoni, taarifa na

mapendekezo yaliyokusanywa na kufanyiwa tathmini siku za

nyuma ikiwemo:

a) Muhtasari wa maoni ya wananchi

wanayokubaliana na wasiyo kubaliana kwa pande zote

mbili za jamhuri ya Muungano;

b) Nyaraka zote zinazowakilisha mawazo, maoni ya wananchi kwa ujumla katika

waraka wa serikali Na.1 wa mwaka 1962 kuhusu kuanzishwa

kwa jamhuri ya Tanganyika, Tume ya Rais kuhusu

kuanzishwa kwa mfumo wa kidemokrasia wa chama kimoja,

Mapendekezo ya Halmashauri kuu ya CCM ya jamhuri

mwaka 1983 kuhusu mabadiliko ya katiba ya jamhuri ya

Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya

Zanzibar ya mwaka 1979, Tume ya Rais ya mfumo wa chama

Page 12: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

kimoja au vyama vingi vya siasa Tanzania ya mwaka 1991 na

kamati ya kukusanya maoni kuhusu katiba (Waraka wa

serikali Na.1 wa mwaka 1998);

c) Katiba ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961;

d) Katiba ya jamhuri ya Tanganyika ya mwaka 1962

e) Hati za Muungano wa Jamhuri YA Tanganyika na Jamhuri ya watu wa

Zanzibar;

f) Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1965;

g) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977;

h) Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1979;

j) Ripoti ya pamoja ya Tume ya Fedha na Ripoti ya Shellukindo juu ya

Changamoto za muungano;

k) Ripoti ya Wangwe juu uharakishaji wa shirikisho la Afrika Mashariki;

i) Tafiti za kiuchambuzi na kitaalam zitakazofanywa na Tume; na

m) Nyaraka nyingine zozote ambazo Tume itaona ni muhimu.

5. Tume yaweza.

a) Kwa Tanzania Bara, kumtaka Mkuu wa wilaya, Afisa mtendaji wa kata au mtaa

au Afisa mtendaji wa kijijij kuitisha mkutano wa wakazi wa

mji, kata, mtaa au kijijij, kwa vyovyote itakavyo kuwa;na

b) Kwa Tanzania Zanzibar, kumtaka Mkuu Wa wilaya au sheha kuitisha mkutano

wa wakazi wa mji au shehia mbalimbali.Kwa madhumuni ya

kukusanya maoni ya wananchi kuhusu masuala ya katiba

kama yalivyoainishwa kwenye hadidu za rejea.

(6) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, kutakuwa na mabaraza ya maapitio ya

katiba.

(7) Mabaraza ya katiba yataundwa na Tume kwa muda maalum kwa kuzingatia

mgawanyiko wa kijiografia wa jamhuri ya muungano na

yatashirikisha na kuwakutanisha wawakilishi toka makundi

mbalimbali ya watu katika jamii.

(8) Mabaraza ya katiba yatatoa ushauri juu ya Rasimu ya Muswada wa katiba

kupitia mikutano maalum itakayoandaliwa na Tume.

(9) Mabaraza yanayorejewa katika kifungu kidogo cha (6) na katika vifungu

vingine vya sheria hii yatakuwa maalum kwa ajili ya, na

yatahudhuriwa na raia wa Tanzania pekee.

Page 13: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

(10) Ili kutekeleza majukumu yake Kwa ufanisi, Tume inaweza kuunda kamati na

inaweza kuipatia kamati yoyote iliyoiunda kazi za jumla au

kazi maalum za kufanya.

(11) Tume inaweza kumshirikisha mtu yoyote au kumtumia mtaalam mwelwkwzi

yeyote kama itakavyokuwa lazima kwa ajili ya utekalazaji

bora wa majukumu yake.

(12) Isipikuwa kama mazingira yatahitaji vinginevyo, katika utekelezaji wa

majukumu yake Tume itabuni utaratibu unaofanana ambao

utakao tumika katika kila upande wa Jamuhuri ya Muungano

katika ukusanyaji na uchambuzi wa maoni ya wananchi,

uendeshaji wa mabaraza na uandaaji wa ripoti.Ripoti ya tume

7-(1) Kwa msingi wa mahojiano wa uchambuzi uliofanywa na kuzingatia kifungu

cha 16, Tume itatayarisha ripoti itakayokuwa na:

a) muhutasari wa maoni ya wananchi kwa

kila hadithi ya rejea;

b) mapendekezo ya Tume kwa kila hadithi ya

rejea;

c)ripoti za wataalam welekezi ambao Tume

iliwatumia;

d)Rasimu ya Maswada wa Katiba; na

e)Taarifa nyingine yeyote muhimu.

(2) Rasimu ya Muswada wa katiba itakuwa ni

kiambatisho kwenye ripoti ya Tume.Uwasilishaji wa ripoti ya tume

18-(1) Baada ya Tume kumaliza kazi yake, itawasilisha ripoti kwa Rais na Rais wa

Zanzibar.

(2) Baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar na baada ya

kukamilisha majadiliano kuhusu masuala ya kisera na taratibu za kiutendaji, Rais

atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba.

19-(1) Mtu atakayemkwamisha, kumkwaza aua kumzuia mjumbe wa. Tume au

sekretarieti kutekeleza mujukumu au kutekeleka mamlaka ya Tume au sekretarieti

atakuwa ametenda kosa.

Page 14: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

(2) Mtu atakaepatikana na hatia kwa kosa la kuvunja masharti ya kifungu kidogo

cha (1) atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi milioni tano au kutumikia

kifungo cha kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili.

SEHEMU YA TANO

KUUNDWA BUNGE LA KATIBA

Tamko la Bunge la Katiba. 20-(1) Rias, baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibarna kwa

ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kwa kupitia Tangazo la Serikali, ataunda Bunge

la Katiba.

(2)Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1), Bunge la Katiba litakuwa

na wajumbe wa aina zifuatazo, yaani:

(a) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;

(b) Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar;

(c) Mawaziri wenye dhamana ya mambo ya katiba wa Serikali ya Jamhuri ya

Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;

(d) Mwanasheria Mkuu wa Serikaliya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria

Mkuu wa Zanzibar; na

(e) Wajumbe mia moja na kumi na sita watakao teuliwa kutoka:

i. Asai zisizokuwa za kiserikali;

ii. Asasi za kidini;

iii. Vyama vya siasa vilivyo na usajili wa kudumu;

iv. Taasisi za elimu ya juu; na

v. Makundi yenye mahitaji maalumkatika jamii.

(3) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (2), idadi wa wajumbe wa Bunge la

katiba ya kutika Tanzania Zanzibar wataopatikana kwa mujibu wa aya ya (a) hadi

(e) haitapungua theluthi moja ya Wajumbe wote wa Bunge la katiba.

(4) Rais atachapisha majina ya watu atakaowateuwa kuwa wajumbe wa Bunge la

katiba pamoja na wajumbe waliotajwa katika kifungu kidogo cha (2) katika

Tangazo la Serikali litakalochapishwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu kidogo

cha (1).

21-(1) Siku ya kwanza ya kikao cha Bunge la Katiba, watawachagua

Spika na Naibu Spika wa Bunge la Katiba.

(2) Spika na Naibu Spika wa Bunge la katiba watachaguliwa

kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba kwa msingi Kwamba endap

Page 15: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Naibu Spika atatoka

upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano.

(3) Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika ataendeshwa kwa kura ya siri na mshindi

atachaguliwa kutokana na wingi wa kura.

(4) Kabla ya kushika madaraka, Spika na Naibu Spika wa Bunge la Katiba

wataapa au kula yamini, vyovyote itakavyokuwa, mbele ya Bunge la Katiba kama

ilivyoainishwa kwenye kanuni za kudumu za Bunge.

22-(1) Mara baada ya Rais kulitangaza Bunge laKatiba na kwa kizingatia masharti

ya kifungu kidogocha (2), Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu

wa Baraza la Wawakilishi, kwa mujibu wa sheria hii, watakuwa katibu na Naibu

Katibu wa Bunge la Katiba au kinyume chake.

(2) Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, watashika nyadhifa zao

kwa msingi kwamba, endapo Spika atachaguliwa kutoka upande mmoja wa

Jamhuri ya Muungano basi Katibu wa Bunge la Katiba atatoka upande wa piliwa

Jamhuri ya Muungano.

(3) Katibu ` wa Bunge la Katiba na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba

watatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa maelekezo wa Spika au Naibu Spika

kadri itakavyokuwa.

(4) Katibu wa Bunge la katiba baada ya kushauriana na Naibu Katibu wa Bunge la

katiba watateuwa watumishi kutoka kwenye Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa

idadi watayoona inafaa kwa ajili ya kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya Bunge la

katiba.

(5) Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la katiba, kabla ya kushika madaraka yao

wataapa au kula yamini mbele ya Rais kwa namna ilivyoainishwa mbele ya

Jadweli la Taifa la Sheria hii.

23-(1) Bunge la katiba litakuwa na mamlaka na litatumia mamlaka hayo kutunga

upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutunga masharti

yatokanayo, masharti ya mpito na vile vile kutunga na kuweka masharti mengine

kama Bunge la katiba litakavyoona linafaa.

(2) Mamlaka ya Bunge la Katiba kutunga masharti ya katiba Musawda

utakaowasilishwa na Waziri na kupitishwa na Bunge la Katiba.

24-(1) Bunge la katiba linaweza kuandaa kanuni kwa ajili ya kuendesha shughuli

katika Bunge la Katiba.

Page 16: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

(2) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha (1) na kwa kuzingatia marekebisho

yatayolazimu, Bunge la Katiba linaweza kutumia kanunia za kudumu za Bunge na

masharti yote yanayohusu upitishaji wa Miswada ya Sheria yanayotumiwa na

Bunge.

(3) Ili masharti ya Mswada wa Katiba yapate kupitishwa katika Bunge la Katiba,

yatahitaji kuungwa mkono kwa wingi theluthi mbili ya idadi ya Wajumbe wote wa

Bunge la Katiba kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya idadi ya Wajumbe

wote wa Bunge la Katiba kutoka Tanzania Zanzibar.

25-(1) Kwa kuzingatia masharti ya nsheria yoyote ya Bunge la Katiba, Sheria ya

Tafsiri za sheria itatumika katika kutoa tafsiri kwa sheria ya Bunge la Katiba na

kwamba rejea kwenye Sheria hiyo au Sheria nyingine yoyote, isipokuwa kama

maktadha utahitaji vinginevyo, itajumuisha rejea kwenye sheria ya Bunge la

Katiba.

(2) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge la

Katiba, na kwa madhumuni hayo, masharti ya ibara 100 ya katiba na Sheria ya

kinga, Madaraka na Haki ya Bunge, kwa kuzingatia marekebisho yatayolazimu,

yatatumika katika Bunge la Katiba.

26-(1) Baada ya kutunga katiba, masharti yatokanayo, na masharti ya mpito

yatakoma.

(2) Kuvunjwa na kukoma kwa mamlaka ya Bunge la Katiba hakutachukuliwa

kuwa kunaondoa mamlaka ya Raia kuliitisha tene Bunge la Katiba lenye wajumbe

wale wale siku zijazo kwa ajili ya kutunga masharti ya katiba kabla ya kuizindua

katiba inavyopelekezwa kwa lengo la kurekebisha masharti yaliyomo katiba

iliyopendekezwa.

SEHEMU YA SITA

UHALALISHAJI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

27-(1) Kwa madhumuni ya kuyapatia uhalali masharti yaliyomo kwenye katiba,

kutakuwa na kura ya maoni itakayoandaliwa, kuendeshwa na kusimamiwana

Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirirkiana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

(2) Katika utekelezaji wa kifungu kidogo cha (1), Tume ya Uchaguzi Zanzibar

itandaa, kuendesha na kusimamia upigaji wa kura ya maoni, kasha itawasilisha

kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi matokeo ya kura zilizopigwa Tanzania

Zanzibar kwa ajili ya kutangazwa.

Page 17: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

28-(1) Ndani ya siki saba baada ya kuchapishwa kwa Katiba, Tume ya Taifa ya

Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar itatayarisha na

kuchapisha kwenye Gazeti la Serikali swali litakaloamuliwa kwa kura ya maoni.

(2) Swali linalorejewa katika kifungu cha kidogo cha (1) litatayariswa baada ya

mashauriano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano

akishirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

(3) Swali litakaloulizwa katika kura ya maonilitamtaka mpiga kura kuonyesha

kuwa anaridhia au kutoridhia katiba hiyo na litatayarishwa kwa namna ambayo

litamtaka mpiga kura kujibu ‘Ndio’ au ‘Hapana’.

(4) Upigaji kura ya maoniutakuwa wa siri.

29-(1) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kuchapishwa kwa swali katika Gazeti

la Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi

Zanzibar itaainisha:

(a) Siku ambayo kura ya maoni itafanyika;

(b) Muda wa upigaji kura ya maoni; na

(d) Muda wa kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu kuipigia kura ya maoni

katiba inayopendekezwa, Tume italazimika, na vyama vya siasa na vyama vya

kijamii vinaweza kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha upigaji wa kura ya maoni.

(3)Ndani ya siku ishirini na moja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza

taarifa, msimamizi wa uchaguzi wa kila jimbo la uchaguzi atatoa taarifa kwa

wananchi kuhusu utaratibu wa uendeshaji wa kura za maoni.

30.Mtu ambaye jina lake limeingizwa katika Daftari la kudumu la wapiga

kuralililoanziswa chini ya sheria ya Taifa ya Uchaguzi na Daftari la Wakazi wa

Zanzibar lililoanziswa chini ya sheria ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 1984,

atakuwa na haki ya kupiga kura isipokuwa kama mtu huyo atakuwa amezuiwa

kupiga kura na sheria nyingine yoyopte.

31. Utaratibu wa uendeshaji wa Uchaguzi Mkuu chini ya sheria ya Taifa ya

Uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibarya mwaka 1984 na sheria ya Uchaguzi

wa Serikali ya Mitaa na kwa kufanya marekebisho yatakayolazimu, utatumika

katika kuendesha kura ya maoni kwa mujibu wa sheria hii.

32-(1) Matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kutokana na wingi wa kura zote

zilizopigwa kwa swali litakalopigiwa kura ya maoni na matokeo

yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yataheshimiwa na Serikali ya

Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Page 18: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

(2) Matokeo ya kura ya maoni yataanuliwa kwa msingi mkono kwa asilimia

inayozidi hamsini ya jumla ya kura zote zilizopigwa kutoka Tanzania Bara na

asilimia inayozidi hamsini ya jumla ya kura zote zilizopigwa kutoka Tanzania

Zanzibar.

(3) Endapo patakuwa na kulingana kwa kura za ‘DNIYO’ na ‘HAPANA’ katika

swali linalopigiwa kura ya maoni, basi, kwa kupitia taarifa itakayochapishwa

katika Gazeti la Serikali na ndani ya siku thelathini baada ya kutangaza matokeo,

Tume ya Taifa ya Uchaguzi itateuwa siku nyingine ya kurudiwa kwa upigaji kura

ya maoni na utaratibu wa kura ya maoni utaanza upya.

(4) Endapo wingi wa kura ya maoni utakuwa ni ‘HAPANA’, Katika Jamhuri ya

Muunganoya mwaka 1977, itaendelea kutumika.

33-(1) Matokeo ya kura ya maoni kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,

Rais kwa kupitiwa amri iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali, ataivunja

Tume.

(2) Kuvunjwa kwa Tume kwa amri ya Rais kutakuwa na maana ya ukomo wa

mamlaka ya Tume na Sekretarieti.

34-(1) Masharti ya Katiba Mpya yataanza kutumika tarehe itakayotajwa kwenye

Katiba hiyo.

(2) Rais atazindua kwa namna atakayoona inafaa kuanza kutumika kwa Katiba

Mpya.

(3) Baada ya kuzinduliwa kwa Katiba Mpya, sheria hii itakuwa imemaliza

matumizi yake na itapoteza nguvu ya kisheria.

(4) Katika matumizi ya sheria hii, toleo la lugha ya Kiswahili na toleo la lugha ya

kiingereza yote ni sahihi.

_____

JADWELI LA KWANZA

_____

(Chini ya kifungu 11)

________

Page 19: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

SEHEMU YA 1

KIAPO/YAMINIYA MJUMBE WA TUME

Mimi……………………………………………..nilikuwa nimeteuliwa na Rais

kuwa………………………………………tarehe………………………….siku ya

……………………………………………..2011kufanya kazi mjumbe wa

Tume,naapa/nathibitisha kwamba nitakuwa mtiifu na bila na bila kuwa

naupendeleo na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu

na kufanya kazi zinazonihusu kama Mjumbe wa Tume.

Ewe Mungu nisaidie.

…………………….

Mjumbe wa Tume

SEHEMU YA 11

KIAPO/ YAMINI YA KATIBU/ NAIBU KATIBU.

Mimi…………………………………nilikuwa nimeteuliwa na Rais

kuwa………………………………….tarehe……………………….siku ya

…………………….20………………..kufanya kazi ya kutibu, naapa/ nathibitisha

kwamba nitakuwa mtiifu na bila ya upendeleo na kadri ya uwezo naufahamu

wangu, nitatimiza wajibu wangu kufanyakazi zinazonihusu kama katibu,.

Ewe Mungu nisaidie.

……………………..

Katibu

______________

JADWELI LA PILI

_______________

(Chini ya kifungu 12(2))

KANUNI ZA MAADILI YA WAJUMBE WA TUME NA SEKRETARIETI

1. Kila mjumbe wa Tume / sekretarieti atapaswa kufanya kazi zake kwa uadilifu

bila ya upendeleo na bila kuingiliwa na atafanya kazi za ofisi yake kwa nia njema

na bila woga, upendekeo au chuki.

2. Mjumbe wa Tume / sekretarieti katika kipindi cha kutumikia yake, hatakuwa

na sifa ya kuteuliwa au kuchaguliwa kwenye nafsi yoyote ya kisiasa.

3. Mjumbe wa Tume / sekretarieti.

Page 20: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

(a) Kupitia ujumbe wake, hatoshiriki, hatatoa kauli, kufanya matendo au kwa

namna yoyote ile kuhatarisha uhuru wa mjumbe au kuathiri hadhi, uadilifu, uhuru

au hadhi ya Tume;au

(b) Kutumia kwa manufaa yake au kufaidika na taarifa yoyote ya siri akiwa kama

mjumbe wa Tume.

_________________

JADWELI LA TATU

___________________

(Chini ya kifungu 22(4))

________________

KIAPO / YAMINI YA KATIBU WA BUNGE LA KATIBA

Mimi……………………………………….nilikuwa nimeteuliwa siku

ya………….............20…….kwa mujibu wa sheria kufanya kazi za katibu wa

Bunge la katiba, naapa / nathibitisha kwamba nitakuwa mtiifu na bila upendeleo

na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu wa kufanya

kazi zinazonihusu kama katibu wa Bunge la Katiba.

Ewe Mungu nisaidie.

……………………..

Katibu wa Bunge la Katiba

___________________

MADHUMUNI NA SABABU

_____________________

Muswada huu ambao umegawanyika katika sehemu sita unapendekezwa

kutungwa kwa sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Nchi ya mwaka 2011. Mchakato

wa mabadiliko ya Katiba pamoja na masuala mengine utaangalia chimbuko na

mahusiano ya Katiba iliyopo kwa kuzingatia uhuru wa wananchi, mfumo wa siasa,

demokrasia na utawala bora. Utaratibu wa kisheria unaopendekezwa utawahusisha

na kuwashirikisha wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika

mchakato wa mabadiliko ya katiba ya nchi. Endapo Muswada huu utapitishwa na

kuwa sheria, kutakuwa na utaratibu wa kisheria utakaomwezesha Rais kuunda

Tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba na kuunda Bunge la Katiba kwa

madhumuni ya kutunga katiba mpya.

Page 21: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

Awali, Muswada huu uliwasiliswa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na

kusomwa kwa Mara ya kwanza tarehe 5 mwezi Aprili 2011. Muswada

uliwasilishwa kwenye kikao cha wadau kilichoandaliwa na Bunge la Jamhuri ya

Muungano na uliendeshwa kwa wakati mmoja katika miji ya Dododma, Dar-es-

salaam na Zanzibar kuanzia tarehe 7 Aprili 2011 hadi tarehe 9 Aprili 2011.

Muswada huu sasa umetangazwa kwa mara nyingine kwa kuchapiswa kwenye

Gazeti la Serikali kwa lugha za Kiingereza na lugha ya Kiswahili kwa madhumuni

ya kusomwa kwa Mara ya pili na kusomwa kwa mara ya tatu.

Sehemu ya kwanza inaweka masharti ya utangulizi ambayo inajumuisha

jina la sheria inayopendekezwa, tarehe ya kuanza kutumika na matumizi ya sheria

inayopendekezwa. Inaendelea kutoa tafsiri ya baadhi ya misamiati na maneno

yoliyotumika na mamlaka zilizotajwa katika Muswada.

Sehemu ya pili inaweka masharti yanayohusu madhumuni ya

Muswada. Sehemu hii inaainisha kwa undani madhumuni ya chimbuko la mcakato

wa mabadiliko ya Katiba, ikijumuisha viapo vya yamini za Wajumbe wa Tume na

Sekretarieti na utaratibu wa kuendesha mchakato wa mabadiliko ya katiba

utakavyofanywa.

Sehemu ya tatu inaweka masharti kuanzishwa kwa Tume na kuainisha

utaratibu na kukusanya maoni. Tume hii itaundwa na Rais wa Mwanasheria

Mkuu wa Serikali ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Masharti

mengine yaliyomo katika sehemu hii ni kuteuliwa kwa wajumbe wa Tume ambao

watatoka katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano kwa idadi sawa na

majina yaokutangazwa kwenye Gazeti la Serikali. Aidha sehemu hii pia inaweka

masharti kuhusu mambo ambayo yanapaswa kuzingatia na kilindwa katika

mchakato wa kukusanya maoni kutokana na umuhimu na uzito wake katika Taifa

letu na inaweka masharti na inaweka masharti ya utaratibu wa Tume kuwasilisha

taarifa na kinga kwa wajumbe wa Tume na Sekretarieti.

Sehemu ya nne inaweka masharti kuhusu utaratibu wa wa utendaji kazi

wa Tume pamoja na kuanisha kazi, wajibu wa mamlaka ya Tume.

Sehemu hii pia inaitaka Tume kutayarisha ripoti ambayo itaambatisha rasimu ya

Muswada wa katiba na kiwasilisha kwa Rais na Rais wa Zanzibar.

Sehemu ya tano inaweka masharti ya kuundwa kwa Bunge la Katiba

ambapo Rais atashauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar baada ya kupata

ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Muungano na Mwanasheria Mkuu

Page 22: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

wa Zanzibar wataunda Bunge la Katiba. Utaratibu wa kuwapata Wajumbe wa

Bunge la Katiba, utaratibu wa kuwapata spika Naibu Spika, katibu na Naibu

Katibu wa Bunge la katiba na jinsi watakavyoapishwa umeaminishwa. Aidha,

mamlaka ya Bunge la katiba na masharti kuhusu Bunge la Katkba pia yameelezwa

kwa lina.

Masharti mengine yaliyomo ni namna ya kuwapata makatibu

Wasaidizi wa Bunge la Katiba, masharti yatokanayo na masharti ya mpito, sheria

na kanuni zitakazotumika katika kuongoza Bunge la Katiba na kuvunjwa kwa

Bunge la katiba.

Sehemu ya sita inahusu uhalalishaji wa katiba inayopendekezwa

kwa utaratibu wa kura ya maoni, utaratibu wa uendeshaji wa kura ya maoni

itakavyotolewa, ikiwa ni pamoja na haki ya wananchi kupiga kura ya maoni kama

inavyoelekezwa na sheria ya Taifa ya Uchaguzi na sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar

ya mwaka 1984.

Wakati wa mchakato wa kura ya maoni, wananchi

watahamasishwa kupitia vipindi maalum vitakavyoendeshwa na vyama vya kiraia,

vyama vya siasa na Tume. Kura ya maoni itaendeshwa na Tume ya Taifa ya

Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kutumia

Daftari la kudumu la Wapiga kura, kwa upande wa Tanzania Bara na Daftari la

Wakazi, kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

Katiba Mpya itabainisha tarehe ya kuanza kutumika na namna Rais

atakavyoizindua na kuanza kutumika. Sheria hii inayopandekezwa , ambayo

kimsingi sasa itakoma kutumika na masharti yake yatapoteza nguvu ya kisheria

mara tu

Baada ya kuzinduliwa kwa Katiba Mpya.

Dar es salaam, CELINA O. KOMBANI,

8 Machi,2011 Waziri wa katiba na sheria

Page 23: Sheria Ya Mabadiliko Ya Katiba Ya Mwaka 2011

.