Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    1/14

    SIMULIZI ZA MKASA WA AJALI YA KILIMANJARO; MPAKA LINI WAHUSIKA WATAENDELEA KUKINGIWA

    KIFUA? MPAKA LINI MCHEZO HUU WAKUENDELEA KUUWANA UTAKOMA !!!

    Ajali hii ya Kilimanjaro II ya tarehe 5/1/2014 ni ya tatu kubwa katika kipindi kisichozidi miaka miwili iliopita, ajali ambazo

    kwa ujumla wake zimesababisha vifo vya watu na kubakisha mayatima, wajane na upweke usiomithilika katika nyoyo za

    wananchi wa Unguja na Pemba. Ilikuwa majira ya saa 5: 42 nilipopata taarifa ya Ajali ya Kilimanjaro ii kutoka Kwa

    mfanyakazi mwenzangu wa Shirika la Bima la Zanzibar kwamba meli hiyo imezama ikitokea Pemba.

    Nilipewa taarifa hii kwa sababu miaka miwili iliyopita Aon Tanzania Limited kwa kushirikiana na Shirika la Bima la

    Zanzibar na mashirika mengine tulikuwa tukizikatia baadhi ya Bima za Meli za Kampuni ya Azam Marine.

    Kama kawaida niliifanyia kazi taarifa hii kwa kumuuliza mdogo wangu amabae naye ni mmoja wa nahodha mzoefu wa

    meli. Nilikuwa na uhakika atakuwa ameshapata taarifa hizo. Naam, alinijibu kuwa amepata taarifa hizo ila meli haikuwa

    imezama, ilipata hitilafu katika moja ya injin zake na imefika salama katika bandari ya Unguja. Taarifa hizi yeye alizipata

    baada ya kuongea na Nahodha mwenzake Bwana Nassor Aboubakar ambae ndie aliekuwa Nahodha wa safari hiyo.

    Sikuridhika moja kwa moja na jibu hili kwa hivyo nilimpigia mtu mwengine ili anipe taarifa zaidi. Nilimpigia Bwana Abdallah

    Hamad(Magarawa), mkaazi wa mjini Zanzibar.

    Abdallah wakati huo alikuwa tayari bandarini kwani ndugu zake wanne walikuwa wanatarajiwa kurudi kutoka Pemba na

    meli hiyo na alishapata habari za meli hiyo tangu saa nne ya asubuhi. Majibu ya Abdallah ni kuwa meli ilipata msukosoko

    na ilimwaga baadhi ya abiria ambao walikuwa wamekaa sehemu ya mbele. Mtoto mmoja kati ya wanne alishapatikana

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    2/14

    akiwa hai ila alieleza kwamba wenzake aliwaona wakichukuliwa na maji. Baba wa watoto hao Bw Khamis Issa kwa wakati

    huo alikuwa ndani ya meli akijaribu kuwasaka ili kupata uhakika wa kilichotokea.

    Dakika tatu baadae nilipigiwa simu nyengine kutoka Pemba na Bwana Seif Alawi akinipa taarifa ya mkasa huo. Yeye bila

    ya kigugumizi aliniambia kuwa watoto watatu kati ya wanne waliokuwa sehemu ya mbele ya abiria , wamezama na

    hakuna dalili za kuokolewa. Nadhani alikuwa anaelewa fika udhaifu wa taasisi zetu katika kupambana na maafa. Huwa

    tuko reactive badala ya kuwa proactive. (Kwa aina hii ya kupambana na majanga tutegemea vilio na maafa makubwa

    zaidi ya haya siku chache zijazo).

    Baada ya baba ya watoto hao kufanya ukaguzi wa abiria hakuweza kuwaona watoto wake watatu kati ya wanne na

    hakukuwa na maelezo wako wapi kutoka kwa wafanyakazi wa kwenye meli wala ofisi ya mmiliki wa meli.

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    3/14

    BANDARINI ZANZIBAR:

    ABIRIA:

    Mara baada ya meli kutia nanga abiria waliruhusiwa kushuka kama vile hakuna kitu chochote kilichotokea. Abiria waliofika

    salama waliruhusiwa kwenda makwao kama utaratibu wa kawaida. Kuna baadhi ya abiria wachache ambao walipata

    majeraha waliachwa wakigaragara kwenye ukumbi wa kupumzikia abiria bila ya huduma ya kwanza.

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    4/14

    Wananchi ambao wengi wao walipata taarifa hizi kupitia simu zao za mikononi walikusanyika bandarin bila ya kujua wapi

    watapata taarifa za jamaa zao waliofika salama na wale waliopotea. Ilikuwa ni hamkani. Kulikuwa na zaidi ya familia 17

    ndani ya bandari na wengi zaidi walikuwa nje wakisubiri kupata taarifa za ajali na jamaa zao.

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    5/14

    KIKAO KIDOGO BANDARINI

    Bahati nzuri Bwana Abdallah Magarawa, Mr Masoud wa Mellenium, Beka Magarawa na Khamis Issa (baba wa watoto

    wanne waliokuwa wakisafiri) na baadhi ya watu kwa idadi kama watano ambao nao walikuwa miongoni mwa

    waliopotelewa walibahatika kuwa baadhi ya wananchi walioingia ndani ya bandari na kutoa taarifa ya kupotelewa na

    ndugu zao. Kikao hicho hakuruhusiwa mwandishi wa habari wala mpiga picha yoyote kuingia. Hizi zilikuwa ni dalili tosha

    kuwa hakukuwa na uwazi katika kutoa taarifa na mambo yalikuwa yakifunikwa funikwa tu , hatujui kwa niaba ya nini,

    serikali, mmiliki wa meli au wananchi.

    Ni fedheha kubwa kuelezea kilichotokea ndani ya kikao hicho. Watu wengine waliokuwa ndani ya Kikao ukiachlilia mbali

    tuliowataja hapo juu ni pamoja na Mheshimiwa Aboubakar Khamis, Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi

    ya Zanzibar akiwa na Bwana mmoja mwenye asili ya Tanzania bara ambae jina lake hatukulitambuwa ndio waliokitawala

    kikao hicho. Alikuwepo Nahodha, Chief Engineer, Mwakilishi wa mwenye meli Bwana Abdulrazak, Mkurugenzi wa

    Bandari bwana Abdi, Mwakilishi waJeshi la Polisi , Jeshi la Wananchi na watendaji wengine washirika la bandari.

    Kikao kiligubikwa na dharau, kebehi, bezo na inda kwa wamiliki wa chombo, Nahodha na Mheshimiwa Aboubakar wote

    wakiwa na msimamo mmoja tu kuwa meli haikumwaga abiria hata mmoja, ni mizigo tu ndio iliyoanguka baharini. Jawabu

    lao wakati watu wakilalamika lilikuwa moja tu, bado hamjaturidhisha, hamjatushawishi na hatujaawamini, huku Nahodha

    akizidi kushikilia msimamo wake kuwa mizigo tu ndio iliomwagika. Jazba ilitawala kwa upande wa waliopotelewa na

    ndugu zao wakitaka wapewe maelezo ya ziada ya walipo wapendwa wao ikiwa meli haikumwaga abiria. Waliwaona

    wenzao wakilichukulia hili jambo kama mzaha. Ni kweli halikupewa nafasi yake iliyostahili

    Ni dhahir Nahodha alikuwa ametoa taarifa ya uongo Huku akiwa chini ya mwevuli wa Mheshimiwa Aboubabakar. Ndipo

    baadae tulipogunduwa kuwa Nahodha ni mtoto wa Aboubakar na alikuwa pale mahsusi kuja kumuhami mwanawe na sio

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    6/14

    kuwafanyia uadilifu wananchi. Kulikuwa na mgongano wa kimaslahi na mezani iliangukia upande wa pili. Damu nzito

    kuliko maji. Hii ilikuwa changamoto kubwa kwani kulikuwa na maelezo ya abiria kuwa watu wamezama ila abiria waliofika

    salama waliharakishwa waondoke sehemu ya bandari. (kuna clip ya abiria aliepona , shuhuda ya dakika 4:27)

    Baada ya mabishano ya takriban saa moja waathiriwa waliomba wenye meli basi angalau wawasaidie majeruhi

    kuwapeleka hospital na kama bado msimamo wao ni kuwa abiria hawakuzama waelekee Mkokotoni kujiridhisha. Nasema

    kwa shingo upande Mheshimiwa Aboubakar, Nahodha, Kampuni ya Azam marine na serekali walikubali wazo hili na kila

    mmoja aliyekuwepo na kwa nafasi yake walielekea Mkokotoni.

    TAFSIRI YA WAATHIRIKA NA JAMII ZAO

    Serikali kwa upande wake haikufanya juhudi zozote za uokozi au kuzifanyia kazi taarifa hizi hata punje. Waziri wa

    Mawasiliano kwa kauli yake mwenyewe alipokuja kuwahani wafiwa siku ya Jumanne tarehe 7/1/2014 alikiri kuwa walipata

    taarifa juu ya ajali hii kabla ya saa nne (3:30 4:00), jee tumuulize baina ya saa nne hadi saa 9 jioni walipookolewa abiria

    watatu na maiti mbili zilipookolewa :

    Serikali ilikuwa wapi na ilifanya nini katika juhudi za uokozi na uopoaje wa maiti?

    Mmiliki wa meli wajibu wake ni nini baada ya ajali?

    SAFARI YA KUELEKEA MKOKOTONI

    Mara baada ya mkutano ambao haukuzaa jambo lolote la maana baada ya kutofautiana kimsimamo baina ya Wamiliki wa

    chombo na Serikali kwa upande mmoja na waathirika kwa upande mwengine, wamiliki kwa upande wao walishikilia kuwa

    hakuna abiria waliozama na waathirika kwa upande wao msimamo wao ulikuwa meli ilimwaga abiria safari ya kuelekea

    Mkokotoni ilianza.

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    7/14

    Kwenye majira ya saa 10 jioni tulipata taarifa kuwa kuna abiria watatu wameokolewa na maiti mbili za watoto

    zimepatikana. Abiria watatu waliokololewa wanaitwa Bwana Nahir Ali Issa, Ali Maulid Haji na Ally Salum Alli . Hawa wote

    watatu walikuwa na ujuzi mkubwa wa kuogelewa na Allah aliamua kuwahifadhi waje wawe mashahidi kwa kilichotokea

    kwa wale tu waliopenda kusikia ukweli wa kisa hichi na wale waliokuwa wakiikadhibisha kweli kwa maslahi binafsi.

    Wanasimulia jinsi walivyojiokoa na walivyojitahidi kuwasaidia abiria wengine. Simulizi za kusikitisha baharini na visa

    ndani ya meli nitaviacha kwa sasa.

    KUTAMBUA MAITI HOSPITALI YA KIVUNGE

    Tulipata taarifa moja ya maiti iliyoopolewa ilikuwa ni ile ya mtoto mkubwa wa kiume wa Bwana Khamis Issa, wa umri wa

    miaka 11, Akram Khamis Issa. Yeye alitambuliwa na kaka yake. Tukiwa tunaelekea Kivunge tulipata taarifa ya kuwa kuna

    maiti nyengine ya mtoto wa Bwana Khamis Issa imepatikana , hii ilikuwa ni ile ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka

    10, Nashirah Khamis Issa.

    Hospitali ya kivunge kulikuwa na maiti tano, nne kati ya hizo zilitambuliwa na moja haikuweza kutambuliwa. Tulichukua

    maiti zetu mbili ila wenzetu wengine walipatwa na fadhaa nyengine, hawakuwa na usafiri wala uwezo wakuchukua maiti

    zao kwa wakati huo. Chakusikitisha zaidi hakukuwa na mtu wa serikali au mmiliki wa chombo wa kuweza kuokoa jahazi.

    Kazi ikaachwa kwa uongozi wa Hospital kufanya maarifa ya kuwasaidia wafiwa. Lazima niupongeze uongozi wa

    Hospital ya Kivunge kwa umahiri wao mkubwa katika kuwahudumia maiti na wale waliokuja kuchukua maiti zao. Pamoja

    na kuwa hawakuwa na rasilimali (resources) ila juhudi zao zilificha udhaifu wao. Wakati serikali ikishindwa kuwasaidia

    wananchi angalau kuchukua maiti zao , kulikuwa na watu wakipita wakikataza taarifa za maafa zisitoke / zisisambae,

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    8/14

    kwanini juhudi hizi za kuchuja taarifa zisitumike kwa mambo mazuri (resources should have been used in good course

    instead) kama za uokozi na kusaidia wafiwa angalau kuchukua maiti zao kwenda kuzihifadhi?

    MAZISHI BILA YA MWAKILISHI WA SERIKALI AU MMILIKI WA CHOMBO

    Kwa bahati mbaya sana nilihamia Tanzania Bara zaidi ya miaka 25 iliyopita ila niliamini kwenye misiba ya namna hii

    serikali na mmiliki wa chombo siku zote huwa wako mbele katika kuwafariji wafiwa alau kwa kuja kutoa pole kama si

    kushiriki mazishi kabisa. Huu ndio ustaarabu wa Zanzibar niliouzoea. Hakukuwa na hata mmoja wapo kwa siku hiyo na

    siku iliyofuata. Maiti zile mbili zilizikwa siku hiyo yatukio usiku saa nne na nusu. Siku ya pili tulihamia tena Nungwi kwa ajili

    ya kutambua maiti iliyobaki endapo zitapatikana.

    Tulikutana karibu familia tano hospital ya Kivunge lakini hakuna maiti iliyopatikana siku hiyo na hakukuwa na mtu yeyote

    wa serikalini aliyekuja kutoa maelekezo nini kinachofuata kwa wale waliokuwa hawakuona jamaa zao. Mambo yaliishia

    hivyo hivyo kimya kimya.

    Hatukufanikiwa kupata maiti ya mtoto mmoja wa kiume wa miaka 5.

    KUTEMBELEWA NA WAZIRI WA MAWASILIANO NA MAKAMO WA PILI WA RAIS

    Tunashukuru siku ya tatu tulipata nafasi ya kutembelewa na Waziri wa Mawasiliano ambae alitoa udhuru kuwa alikuwa

    mgonjwa ila nayeye alitamani ashiriki kwenye mazishi. Udhuru wake ulikubaliwa. Makamo wa Rais , Mh Seif Sharif

    Hamad yeye alikuja kuwapa pole wafiwa siku ya Jumamosi.

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    9/14

    AJALI IMEACHA MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU

    1. Tulitegemea serikali ichukue hatua muafaka na za haraka (response time) mara baada ya kupata taarifa za ajali.

    Taarifa zilipatikana mapema , kabla ya saa nne, hatua zilianza kuchukuliwa baada ya saa saba na baada ya

    waathirika kuangusha zogo bandarini, hiyo dharura iko wapi hapo? Tunakubali Nahodha alitoa taarifa za uongo ila

    serikali iliwajibika vipi? Kwa maoni yangu binafsi na mtu yeyote mwenye busara za kawaida tu hivi sivyo serikali

    iliyo makini inavyoshughulikia majanga.

    2. Nadhani moja ya kazi ya orodha ya abiria wanaopanda meli ni kulinganisha na abiria wanaoshuka hasa meli

    inapokuwa imekumbwa na mikasa ya namna hii. Kwa sababu kulikuwa na muda wa kutosha kati ya Nungwi na

    bandari ya Unguja tulitegemea mara meli baada kufunga nanga maofisa wa meli , bandari na idara zinazohusika

    wachukue orodha ya abiria wote walioshuka. Hii kwa kulinganisha na orodha ya abiria waliopanda tungejua

    mambo yafuatayo:

    Abiria waliofika salama

    Abiria waliopanda meli ambao hawamo kwenye orodha, ikiwa fursa nzuri ya kuwauliza walipandaje kwenye

    meli (ama walitumia majina ya watu wengine au walipandishwa na mabaharia kinyemela/ kienyeji)

    Abiria ambao hawakufika salama

    Abiria ambao wasingehesabika ni wale tu ambao hawamo kwenye orodha na hawakupanda meli kisheria. Nadhani hawa

    idadi yao itakuwa ni ndogo.

    Hili naamini lingefanyika lingetoa mwanga wa kutosha jinsi ya kuweka takwimu za abiria. Hili halikufanyika. Swali

    linakuja orodha ya wasafiri kazi yake ni nini?

    3. Tulitegemea kuona angalau watu wa huduma ya kwanza pale bandarini kuwasaidia waliopata mshituko na

    walioumia. Kilichotokea hakukuwa na hata mtu mmoja wa huduma ya kwanza. Mheshimiwa Aboubakar na

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    10/14

    wanzake waliekwa ukumbi wa watu mashuhuri (VIP Lounge) wakinywa kahawa na tende wakati waathirika

    wakihangaika jinsi ya kupata maiti zao na taarifa za ndugu zao.

    4. Mimi nilitegemea serikali ingeratibu utaratibu wa wale wasiojiweza kuchukua au kushughulikia kutafuta maiti zao

    angalau kwa kuwapatia usafiri badala ya kuwatelekeza kila mtu atoke kivyake vyake. Waathirika walisononeka

    sana. Mtu hukuwa na haja ya kuwa na PHD kujua walisoneneka kwa kiasi gani , ukiangalia tu nyuso zao zilitosha

    kuona wanafadhaa ya kiwango gani

    5. Mimi siamini kama ule ustaarabu wa chini ya miaka ya mpaka 1980s wa kufarijiana umekwisha na Unguja

    imekuwa kubwa kiasi ambacho kwamba mwenye meli hadi leo hajapata taarifa kuwa meli yake imeua. Nilitegemea

    kumona siku ya pili ya msiba (sio lazima yeye, najua anawawakilishi wake). Nimeshangaa kupewa jibu eti hana

    taarifa, anategemea taarifa zitoke mbinguni?

    6. Kwa muundo wa meli zote sehemu ya dereva (bridge) huwa juu ili kuona mbele. Suala linakuja ikiwa abiria

    waliomwagika walikuwa mbele je nahodha alikuwa anaangalia wapi?. Na je Kilimanjaro 2 haina ukubwa wa

    TITANIC wala OASIS ni meli ndogo Je inaingia akilini kuwa Nahodha asione mbele ya boti Kinachotokea? Hivi

    inawezekana dereva wa gari asione kinacho mwagika Juu ya kioo au Bonet ya gari yake?. Kwa waliowahi kusafiri

    kwa boti hizi naomba tuaangalie muundo kisha Tuyajibu masuala hayo. Naambiwa kwenye chumba cha

    Nahodha kwa kawaida hukaa watu wanne kwa kupokezana, ama Nahodha, Chief Enginee, AB (Able Seaman) ,

    Engine Room Outlook, Afisa wa zamu nakadhalika. Hebu tuambiwe wakati meli inachota maji hadi inamwaga

    abiria nani na nani walikuwa kwenye hicho chumba? Hapo naweza nikakubali kuwa hawakuona watu wakimwaga

    kwa sababu hakukuwa na mtu!

    7. Suala kubwa linakuja hapa. Je Mh Abuubakar kwanini alifika mapema sana mara baada ya tukio? Alipata wapi taarifa

    za tukio? Je alikuja pale kwa maslahi ya nani? Au ndio ule msemo wa funika kombe mwanaharamu apite?.

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    11/14

    MWISHO:

    Ningependa kumalizia kwa mambo mawili yafuatayo:

    Tumeshaona ajali tatu kubwa katika kipindi cha miaka miwili na tutaendelea kuona nyengine nyingi katika kipindi

    kifupi kijacho, jee tumejifunza nini kutokana na ajali hizi? Au tutaishia kuunda tume tu na kuziweka taarifa kwenye

    makabrasha zikiota mwani na shigiwashi?

    Bado nashindwa kuamini hizi aina za meli zinazotoa huduma za kwenda Pemba kama zina uwezo wa kuhimili

    pilikapilika za mkondo wa Nungwi. Kumbukumbu zangu za MV Afrika na Jamhuri, baadae MV Mapindizi na

    Maendeleo sikupata kusikia au kuona dhahma za namna hii pamoja na meli hizo kuwa zimechakaa sana. Naamini

    hizi meli za kisasa ziko kwa ajili ya kipato zaidi au maslahi kwa wamiliki na serikali kuliko usalama na huduma kwa

    wananchi. Pia nina wasiwasi na Nahodha , mabaharia na masarahange kama huwa wana ujuzi na uzoefu wa

    kutosha wa bahari. Haiyumkiniki mara baada ya ajali mabaharia wawe wa kwanza kuvaa vifaa vya uokozi

    wakiwaacha abiria wakihangaika. Na hata meli ilipofika lile tishio la Nahodha la kuwa eti hata tia nanga hadi abiria

    wavue vifaa vya uokozi ni tukio la kuhudhunisha zaidi. Sawa hii ilikuwa ni kwa ajili ya kujihami. Hivi lipo kwenye

    muhtasari somo la maadili ya kazi za ubaharia? Sidhani! Hili sina utaalamu nalo hata kidogo. Tuwaachie

    wataalamu walichambue.

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    12/14

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    13/14

    Kwa kumalizia nisingependa kuwa mwizi wa fadhila kwa serikali yangu ya Mapinduzi, naipongeza kwa kutimiza Miaka

    Hamsini, sawa na Umri wangu. Naamini baada ya sherehe serikali sasa itakuwa imeshika nafasi yake na kuanza

    kushughulikia matatizo na kero za wananchi nikiamini na hili lipo katika dondoo zake

  • 8/13/2019 Simulizi Za Mkasa Wa Ajali Ya Kilimanjaro_ii

    14/14

    MAPINDUZI DAIMA

    Khamis Suleiman

    Msaidizi wa Kiongozi wa wafiwa (Khamis Issa & Sharifa Abdallah)

    Mwandishi ni mzaliwa wa Zanzibar na alipata elimu yake ya msingi na upili Zanzibar kabla ya kuhamia Tanzania bara

    baada ya kumaliza elimu yake ya juu. Ana uzoefu wa Bima za mali za ajali wa takriban miaka 30 na amejikita zaidi

    kwenye Bima za Meli na Mizigo