9
Hukumu za Najisi https://www.al-feqh.com/sw https://www.al-feqh.com/sw

sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

Hukumu za Kiislamu zilizowepesishwa

Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

HijjaZakat Funga Swala Tohara

Tarjama Dr Abdalla Khatib Sheikh Salim Barhayan

Ustadh Said AbduUstadh Ahmed Yasin MustafaSheikh Said Bawazir

Marejeo

Hukumu za Najisi

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 2: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

16

Mlango wa Tohara

Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

2

Najisi kilughaUchafu

Hukumu za Najisi

Sampuli ya vitu Najisi1. Mkojo wa binadamu na choo chake Kwa Hadithi ya Mbedui aliyekojoa msikitini, Mtume صلى الله عليه وسلم akamwambia (Hii misikiti haifai ikojolewe au ichafuliwe. Linalopasa ni kutajwa Mwenyezi Mungu, kuswaliwa na kusomwa Qur’ani) (1).

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim

Y a l i y o m oKuieleza najisi

Aina za najisi

1- Mkojo wa mwanadamu na choo chake

2- Damu ya hedhi

3- Mkojo wa mnyama asiyeliwa na choo chake

4- Mfu

5- Nyama ya nguruwe

6- Ute wa mbwa

7- Madhii

8- Wadii

Njia za kutwahirisha najisi

Najisi kisheriaUchafu ambao Sheria imeamuru uondolewe

2. Damu ya Hedhi Kwa ilivyothubutu kuwa Khaulah binti Yasaar alimjia Mtume صلى الله عليه وسلم akasema: « Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sina isipokuwa nguo moja, na ninaingia hedhini nikiwa nimeivaa. Mtume صلى الله عليه وسلم akasema: (Ukitwahirika osha pale mahali pa damu kisha uswali ukiwa na hiyo nguo). Na damu isiyokuwa ya hedhi ni twahara, iwe ni damu inayotiririka au isiyotiririka, kwa hadithi iliyothubutu kuwa mmoja wa washirikina alimfuma mmoja wa Waislamu kwa mshale naye yuwaswali ukampata, akaushopoa na akaendelea kwenye Swala yake na damu ikimtiririka.

3. Mkojo na choo cha wanyama wasio liwa Kwa hadithi iliyosimuliwa na Ibn Mas›uud kwamba Mtume SAW alienda chooni akaniamuru nimletee mawe matatu. Nikapata mawe mawili, nikatafuta la tatu nisipate, nikachukua choo kikavu cha mnyama nikamletea. Akachukua mawe mawili na kile choo akakitupa na akasema “Hiki ni najisi (2) ” (3).

(2) Riks: najisi.(3) Imepokewa na Bukhari.

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 3: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

17Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

4. Mfu Naye ni aliyekufa mwenyewe bila kuchinjwa kisheria, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Alisema: {Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho haramishwa kwa mja kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayo mwagika au nyama ya nguruwe kwani hiyo ni uchafu} [6: 145]. Na kinaingia katika maana ya mfu kile kilichokatwa kutoka kwa mnyama aliye hai kabla hajachinjwa.

Na vinavyovuliwa katika mfu ni:

1. Mfu wa Samaki na Parare Kwa neno lake Mtume (s.a.w.): (Tumehalalishiwa mfu aina mbili, na damu aina mbili. Ama aina mbili za mfu, ni samaki na parare, na ama aina mbili za damu, ni ini na wengo) (1)

2.Mfu asiye na Damu inayotiririka kama vile Nzi: Kwa kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم alisema: (Anapoingia nzi kwenye chombo cha mmoja wenu, basi na amzamishe kisha amtoe na kumtupa, kwani kwenye mojawapo ya mabawa yake kuna ponyesho na katika lingine kuna ugonjwa) (2).(1) Imepokewa na Ahmad(2) Imepokewa na Bukhari.

Ni hukmu gani ya Mkojo na choo cha wanyama wanaoliwa ? Mkojo wa mnyama anayeliwa na choo chake ni twahara, kwa kuwa ilithubutu kutoka kwa Anas bin Malik kwamba kuna watu walikuja Madina, na hewa yake isiwafae - yaani walishikwa na ugonjwa huko -. Mtume صلى الله عليه وسلم akawapeleka kwenye ngamia wa Zaka wapate kunywa mikojo na maziwa ya hao ngamia(1).

(1) Imepokewa na Bukhari.

Mfu

Samaki

Nzi

Parare

Hukumu za Najisi

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 4: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

18

Mlango wa Tohara

Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

5. Nyama ya Nguruwe Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesema: {Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho haramishwa kwa mja kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayo mwagika au nyama ya nguruwe kwani hiyo ni uchmfu } [6: 145].

Ute wa mbwa

Nguruwe

6. Ute wa Mbwa Mbwa ni najisi yeye mzima. Na unajisi wa ute wake umefanywa mzito, kwa kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم alisema: (Kutwahirika kwa chombo cha mmoja wenu iwapo mbwa amekiramba ni kukiosha mara saba, mara mojawapo kwa mchanga) (1). Na kuramba ni atiapo mbwa ulimi wake ndani ya chombo na kuutikisa, anywe au asinywe.

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim

7. Madhii Nayo ni maji meupe mapesi yenye kunata, yanayotoka wakati wa kucheza na mke au kufikiria kuundama, si kwa matamanio ya nguvu wala hayatoki kwa kasi, na hayafuatiwi na hali ya kulegea, na wakati mwingine mtu hahisi kamwe kuwa yametoka. Hii ni kwa kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi iliyopokelewa na Ali bin Abi Twalib alipomuuliza mtume s.a.w kuhusu madhii, alisema: (Tawadha na uoshe dhakari yako) (2).

8. Wadii Nayo ni maji meupe mazito yanayotoka baada ya kukojoa.

(2) Imepokewa na Bukhari na Muslim

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 5: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

19Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

Pombe Pombe ni twahara kinje ingawa kimaana ni najisi na kuwa kulinywa ni miongoni mwa dhambi kubwa, isipokuwa ya kwamba hakuna dalili kuwa ni najisi.

Ama neno lake Mwenyezi Mungu {Enyi mlio amin!bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani basi jiepusheni navyo } [5: 90] Lililokusudiwa ni uchafu wa kimaana na sio uchafu wa kidhahiri, kama ilivyo kamari na masanamu. Hukumu inayochukuliwa hapa ni kuwa utumiaji wa mafuta mazuri yenye alkoholi unafaa, kwa kuwa alkoholi inatolewa kwenye pombe.

Kuyaosha yakiwa majimaji

Kuyakangura yakiwa makavu

Pombe

Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana harufu inayofanana na yai lililoharibika.

Nayo ni twahara, kwani lau yangekuwa najisi Mtume صلى الله عليه وسلم angeamrisha yaoshwe.

Na inatosheleza, katika kuondoa manii, kuyaosha yakiwa majimaji, na kuyakangura yakiwa makavu, kwa hadithi ya Aishah kuwa alisema: (Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وسلم akiosha manii kisha akitoka kwenda kuswali kwa nguo hiyo na mimi nikiona athari yamuosho katika ile nguo) (1). Na katika riwaya ya Muslim: (Nilikuwa nikiyakangura manii kwenye nguo ya Mtume صلى الله عليه وسلم kisha akiswalia) (2).

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim.(2) Imepokewa na Muslim.

Hukumu za Najisi

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 6: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

20

Mlango wa Tohara

Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

2. Kuyatwahirisha Maji Yaliyonajisika Yanatwahirika kwa kuongeza maji mengi ndani yake mapaka athari ya najisi iondoke. Pia yanatwahirika kwa kuyasafisha kwa njia za kiteknolojia za kisasa.

3.Kuitwahirisha Nguo Iliyonajisika Huoshwa kwa maji, ikangurwe ikamuliwe mpaka Najisi Iondoke

Njia za Kutwahirisha Najisi1. Kutwahirisha Ardhi Iliyonajisika Ardhi ikinajisika, najisi hiyo huondolewa iwe ni kwa maji au kinginecho. Katika hadithi ya mbedui aliyekojoa msikitini, Mtume صلى الله عليه وسلم: (Muwacheni na mwageni kwenye mkojo wake ndoo ya maji) (1). Na iwapo najisi ni majimaji ya kutiririka kisha ikakauka basi kwa hivyo huwa ishatwahirika kulingana na hadithi ya Abuu Qilaabah kuwa alisema: “Ardhi ikikauka huwa imetwahirika” (2).

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim.(2) Imepokewa na Bukhari na Muslim.

Kutwahirisha Ardhi Iliyonajisika

Najisi majimaji kinachomiminika ardhini

Kukauka kwa najisi majimaji

Kutwahirisha kwa vitu vya kisasa

Kutwahirisha kwa kuongeza maji

Kutwahirisha nguo iliyonajisika

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 7: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

21Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

4.Kuyatwahirisha matandiko Huoshwa kwa maji au kwa visafishaji vya kisasa, Na hukangurwa mpaka najisi iondoke.

5. Kuitwahirisha Ngozi ya Mfu1. Ngozi ya mfu wa mnyama anaeliwa Hutwahirishwa kwa kuitia rangi kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم: (Ngozi ikitiwa rangi huwa imetwahirika)(1). Na dibaagh ni kutengeneza ngozi kwa baadhi ya madawa mpaka zilainike na uvundo wake uondoke. Ama mnyama anayeliwa awapo si mfu na akawa amechinjwa kwa njia ya kisheria, basi ngozi yake ni twahara

(1) Imepokewa na Muslim.

2. Ngozi ya Mfu wa Mnyama Asieliwa Kwa Yule mnyama ambae haiwi halali kuchinjwa kwake ngozi yake haitotwahirika kwa kukaushwa hata kama katika uhai wake alikuwa twahara

6. Kutwahirisha mkojo wa mtoto wa kike na mkojo wa mtoto wa kiume ambaye hajala chakula Mkojo wa mtoto wa kike huoshwa. Ama mkojo wa mtoto wa kiume, inatosha kunyunyiza maji juu yake, kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم: (Mkojo wa mtoto wa kike huoshwa, na mkojo wa mtoto wa kiume hunyunyizwa maji) (2)

(2) Imepokewa na Abu Daud.

Kutwahirisha matandiko

Mnyama anayeliwa

Kupaka rangi ngozi

Mnyama asiyeliwa

Kunyunyiza Maji mkojo wa Mtoto wa Kiume

Kuuosha Mkojo wa Mtoto wa Kike

Hukumu za Najisi

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 8: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

22

Mlango wa Tohara

Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa

10. Kuvitwahirisha Viatu Husuguliwa chini mpaka iondoke athari ya najisi, kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم: (Mmoja wenu anapokanyaga uchafu kwa kiatu chake, basi mchanga unakitwahirisha)(5).

11. Kuitwahirisha Nguo ndefu ya Mwanamke Najisi ikipakana na ukingo wa nguo ya mwanamke, basi inamtosheleza yeye atembee mahali twahara na ardhi itaitwahirisha, kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم (Kitaitwahirisha kilicho baada yake) (6).

12. Kuvitwahirisha Vyakula Vikavu Vinatwahirika kwa kuiondoa najisi na zile sehemu zilizo pambizoni mwa hivyo vyakula, na kinachosalia kitakuwa twahara, kwa ilivyothubutu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وسلم aliulizwa kuhusu panya aliyeingia ndani ya samli, akasema: (Vitupeni! Na vile vilivyo pambizoni mwakeviondoeni namule samli yenu).(7)

(5) Imepokewa na Abu Daud.(6) Imepokewa na Abu Daud.(7) Imepokewa na Bukhari.

7. Kukitwahirisha kilichorambwa na Mbwa Huoshwa mara saba, mara ya kwanza yake ni kwa mchanga, kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم: (Utwahara wa chombo cha mmoja wenu iwapo mbwa amekiramba ni kukiosha mara saba, mara ya kwanza yake ni kwa mchanga) (1).

8. Kuyatwahirisha Madhii na Wadii Ataosha dhakari yake na atatawadha, kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi ya Ali bin Abii Twalib: (Tawadha na uoshe dhakari yako) (2).

Ama kuitwahirisha nguo, inatosha kunyunyiza maji mahali palipo na madhii au wadii, kwa hadithi ya Sahl bin Hanif kuwa yeye alimuuliza mtume !Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu“ :صلى الله عليه وسلمNguo yangu ikiiingiwa na chochote katika vitu hivyo itakuwaje?” Akasema: (Inakutosheleza utie maji kwenye kitanga cha mkono uyamimine nguoni mwako mpaka uone kwamba yameviondoa) (3).

9. Kutwahirisha Damu ya Hedhi Ni kuiosha kwa maji. Na haidhuru ikisalia athari yake, kwa kauli yake Mtume صلى الله عليه وسلم: (Yanakutosheleza maji, na athari yake haikudhuru) (4)

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim(2) Imepokewa na Bukhari na Muslim.(3) Imepokewa na Abu Daud.(4) Imepokewa na Abu Daud.

Kuitwahirisha Ardhi nguo ya mwanamke

Kisha

Mara sitaMara moja

Kutwahirisha kwa kuoshaKutwahirisha kwa Mchanga

Kutwahirisha viatu kwa kuvisugua kwenye Ardhi

Samli iliyoingia Panya Aliyekufa

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w

Page 9: sw - فقه العبادات المصور | علم · Utwahara wa Manii Manii: ni maji meupe, mazito, yanayotoka kwa matamanio ya nguvu kwa kasi, na yanafuatiwa na ulegevu, na yana

23Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa 23232332FiFiFiFiqhqhqhqhhhq iiiiii yayayayayayayayyyyayayayaay ‘‘‘‘‘‘IbIbIbIbIbIbIbadadadaddda a a aa yeyeyeyeyeenynynynynynnnyn e eee pipippip chchchaa ziziziziililililizozoozooz chchhchorororrrrrrrrorrrorrrrwawawawawawawawwawwwwwwwwwwwww 23

Maelezo kuhusu Najisi1- Asili ya vitu ni twahara isipokuwa vile ambavyo kuna dalili ya unajisi wake.

2- Najisi ikiingia kwenye kitu na isijulikane ilipo, basi chote kitaoshwa.

3- Najisi ikigeuka ikawa kitu kingine, kama vile kikichomwa choo cha punda kikawa jivu, basi itakuwa twahara.

Kugeuka choo kuwa jivu kunakukifanya kitwahirike

13- Kutwahirisha Vitu Vigumu kama Viyoo na Gilasi Itapanguswa mpaka athari ya najisi iondoke.`

IllustratedIslamicJurisprudencefortheActsofWorshipIllustratedIslamicJurisprudencefortheActsofWorship

Kutwahirisha Ukoa kwa Kuupangusa

Hukumu za Najisi

https://www.al-feqh.com/swht

tps:

//ww

w.a

l-feq

h.co

m/s

w