43
KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI Y AKE Hebu tuendelee kusimama sasa tunapoomba. Na tuinamishe vichwa vyetu. 1 Bwana, tuna furaha asubuhi hii kurudi nyumbani kwa Mungu kwenye ibada nyingine. Na tunaomba Mungu kwamba utatusahihisha asubuhi hii makosa yetu yote. Tuonyeshe njia zile ulizochagua zitupasazo kupitia, na tupe Neema Yako na upendo, ili tupate kufuata njia zile na maagizo kwa moyo wetu wote, ili tuonekane siku ile katika Kristo, bila lawama, kwani tunaamini, Bwana, kwamba kufunuliwa Kwake ku karibu. 2 Tunaona ishara zote alizonena zitatokea kabla tu ya kuja Kwake sasa zikitimia. Na kwa furaha tunatazamia muda huo. Kama Ibrahimu wa kale alivyomtazamia yule mwana wa ahadi, na kuona zile ishara za mwisho za Mungu zikishuka ulimwenguni, hapo alijua kwamba haitachukua muda mrefu hadi huyo mwana atokeapo. Na sasa twaliona hilo likirudia tena. Yesu alituambia kwamba wakati mambo haya yaanzapo kutokea tuinue vichwa vyetu, kwamba ukombozi—ukombozi wetu unakaribia: mshangao wa wakati huo, dhiki kati ya mataifa, matetemeko ya nchi mahali mahali, bahari ikivuma, na moyo wa mwanadamu ukikoma kwa hofu. 3 Nasi twatambua kwamba tuko katika saa hiyo wakati ambapo mataifa hayajui la kufanya. Inaonekana vita vingine vinakuja. Hicho kingekuwa kitu kibaya jinsi gani. Dunia ikivunjika-vunjika, wanasayansi walisema kwamba kitu cha kutisha kiko karibu. Tunaona Biblia ikinena juu ya jambo hili. Basi, Bwana, tusaidie leo kusimama katika hii nyumba ya kusahihishwa, na kutii amri kutoka kwa Mungu wetu kusonga mbele katika saa hii ya giza kuangaza Nuru, kwani huenda ikawa nafasi yetu ya mwisho kufanya hivyo. Kwani twaomba hili katika Jina la Yesu na kwa ajili Yake. Amina. (Ketini.) 4 Hakika naona hii kuwa ni heshima kuu kuwepo hapa katika maskani asubuhi hii. Na samahani kwamba hatuna nafasi yenu ya kuketi hapa. Na mahali hapa pamejaa watu, na wamesimama kila mahali kule nje…Ninyi watu mliopo nje sasa, mwaweza kusikia hili katika redio zenu, nasahau… [Ndugu Neville anamwambia Ndugu Branham ni katika mita bendi ngapi yaweza kusikika—Mh.]…55 hadi 57. Ninyi watu mliopo nje na katika sehemu za kupaki magari na barabarani, mwaweza kusikia hili katika redio zenu kati ya 55 na 57 katika bamba la redio zenu.

SWA65-0718M Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake …download.branham.org/pdf/SWA/SWA65-0718M Trying To Do God A Se… · Tunaona Biblia ikinena juu ya jambo hili.Basi,Bwana,tusaidieleokusimamakatikahiinyumbaya

  • Upload
    vukhanh

  • View
    577

  • Download
    19

Embed Size (px)

Citation preview

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA

MAPENZIYAKE

Hebu tuendelee kusimama sasa tunapoomba. Natuinamishe vichwa vyetu.

1 Bwana, tuna furaha asubuhi hii kurudi nyumbani kwaMungu kwenye ibada nyingine. Na tunaomba Mungu kwambautatusahihisha asubuhi hii makosa yetu yote. Tuonyeshe njia zileulizochagua zitupasazo kupitia, na tupe Neema Yako na upendo,ili tupate kufuata njia zile na maagizo kwa moyo wetu wote, ilituonekane siku ile katika Kristo, bila lawama, kwani tunaamini,Bwana, kwamba kufunuliwaKwake ku karibu.2 Tunaona ishara zote alizonena zitatokea kabla tu ya kujaKwake sasa zikitimia. Na kwa furaha tunatazamia muda huo.Kama Ibrahimu wa kale alivyomtazamia yule mwana waahadi, na kuona zile ishara za mwisho za Mungu zikishukaulimwenguni, hapo alijua kwamba haitachukua muda mrefuhadi huyo mwana atokeapo. Na sasa twaliona hilo likirudiatena. Yesu alituambia kwamba wakati mambo haya yaanzapokutokea tuinue vichwa vyetu, kwamba ukombozi—ukomboziwetu unakaribia: mshangao wa wakati huo, dhiki kati yamataifa, matetemeko ya nchi mahali mahali, bahari ikivuma, namoyo wamwanadamu ukikoma kwa hofu.3 Nasi twatambua kwamba tuko katika saa hiyo wakatiambapo mataifa hayajui la kufanya. Inaonekana vita vinginevinakuja. Hicho kingekuwa kitu kibaya jinsi gani. Duniaikivunjika-vunjika, wanasayansi walisema kwamba kitu chakutisha kiko karibu. Tunaona Biblia ikinena juu ya jambohili. Basi, Bwana, tusaidie leo kusimama katika hii nyumba yakusahihishwa, na kutii amri kutoka kwa Mungu wetu kusongambele katika saa hii ya giza kuangaza Nuru, kwani huendaikawa nafasi yetu yamwisho kufanya hivyo. Kwani twaomba hilikatika Jina la Yesu na kwa ajili Yake. Amina. (Ketini.)4 Hakika naona hii kuwa ni heshima kuu kuwepo hapakatika maskani asubuhi hii. Na samahani kwamba hatunanafasi yenu ya kuketi hapa. Na mahali hapa pamejaa watu,na wamesimama kila mahali kule nje…Ninyi watu mlioponje sasa, mwaweza kusikia hili katika redio zenu, nasahau…[Ndugu Neville anamwambia Ndugu Branham ni katika mitabendi ngapi yaweza kusikika—Mh.]…55 hadi 57. Ninyi watumliopo nje na katika sehemu za kupaki magari na barabarani,mwaweza kusikia hili katika redio zenu kati ya 55 na 57 katikabamba la redio zenu.

2 LILE NENO LILILONENWA

5 Kwa hiyo tumejaribu…Nalikuwa nikirudi, hasa, kwa—hapa kujaribu kufanya mkutano wa kama siku kumikuzungumzia juu ya somo la vile Vitasa Saba vyaMwisho; kwanikati ya Vitasa vile ni zile Baragumu. Na nilikuwa nikiwaambiakatika ule—wakati nilipokuwa ninakwenda kuhubiri juu yazile Baragumu Saba, kwamba nitavileta pamoja vile Vitasa nayale Mapigo. Na nalifikiri ingekuwa wakati mzuri, nilikuwanimerudi tu kutoka Afrika; na—na watoto hawakuwa wamepatalikizo yao. Mtoto wangu mdogo wa kiume, Joseph, amekuwa—amekuwa akiendelea—anahitaji wiki chache za kujifunza juu yakusoma kwake. Alifuzu haidhuru, lakini hakufikia wastani, kwahiyo tulimwacha Tucson hivyo—wakati nilipokuwa Afrika, naaliendelea na kusoma kwake na kufaulu kwa kisomo cha shuleya mchana. Kisha tulirudi. Basi nalifikiri, huku watoto wakiwalikizoni nitafanya mkutano mdogo hapa na watu na kuhubirimasomo haya. Lakini basi tulipofika hapa, tuliona kwambahatungeweza kupata ukumbi wa shule.6 Na nalijua maskani hayatakuwa yanatosha kuwaketishawatu na kuwafanya wastarehe inavyowapasa wakati wao—ninapokuwa na ujumbe huu; kwa hivyo, ilitupasa ku—kufanyampango tofauti. Na badala ya kuwa na zile—zile siku kumiambazo tulikuwa tukipanga kuwa nazo; vema, nilifanyaibada mbili tu kwa kila Jumapili—Jumapili hii, Jumapiliijayo, na Jumapili ifuatayo, ibada mbili, ili kwamba…Nasihatukuitangaza. Na kisha, kama ye yote alisikia kwa njia yoyote ya kwamba mikutano itaanza tarehe ishirini na nanekwenye ukumbi wa shule, kama Mungu angeruhusu, vema,kama mna rafiki wo wote na mmekodisha vyumba vyo vyotekwenye vyumba vya kulala, ni—ningefutilia hilo mbali (waona?),kwa sababu ina—kwamba wao—hatuwezi kuupata kwa urahisi;hawawezi kupata ule—ule ukumbi wa shule.7 Na sasa, nataka kuzungumza juu ya—ibada tu za kiinjilistiJumapili asubuhi. Na Jumapili usiku nataka niwe na maombikwa wagonjwa. Na tunatumaini kwamba Mungu atakutanana ninyi watu mlio wagonjwa. Sijui Billy atawashughulikiajinsi gani, nafikiri, kutoa kadi za maombi, au namna zo zotekulisimamia kusanyiko. Lakini tutafanya yo yote tuwezayokufanya kumuombea kila mtu katika hizi wiki tatu zijazoambazo tunakusudia kuwa na ibada, kama ni mapenzi yaBwana.8 Na kisha, mara nyingi kuna mahojiano ya kibinafsi, mtufulani anataka kukuona kwa dakika moja juu ya jambo fulaniau jambo kama hilo. Nasi tuta…Ni wangapi hapa wanatakamahojiano ya kibinafsi, hebu tuone mikono yenu. Ala! Naniasiyependa?9 Kwa hiyo basi, tuna…Yaonekana itakuwa vigumukuyapata, kwa hiyo andikeni matakwa yenu na muyatume—pelekeni kwa Billy, kisha nitayapata kutoka huko. Na sasa,

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 3

atatangaza kuhusu—nakisia, kadi za maombi, kila zinapopaswakutolewa.10 Ni wangapi wa ndugu zetu wanaohudumu walio hapaasubuhi hii. Hatukuwa na nafasi ku…sidhani…mmemtambuaye yote wao? Kuna wahudumu wangapi hapa asubuhi hii?Tafadhalini inueni mikono yenu juu tu, au msimame. Hebutuone ni wahudumu wangapi walio katika kusanyiko asubuhihii. Vema, vizuri! Bwana ashukuriwe kwa watu hawa. Laititungelikuwa na muda wa kufahamiana na kila mmoja wao,lakini nina hakika mnawaona nasi—Mungu anawajua katikahuduma yao; na tunaomba kwambaMungu awabariki sana. Bilashaka wengi wao wamefunga ibada zao kuwepo hapa.—NduguJunior Jackson, na nadhani, Ndugu Don Ruddell. Na matangazohaya yanakuja katika makanisa yao. Na katika—pia kule NewYork namahali pengine katika taifa hili ni kwa simu za kibinafsikatika kila kanisa asubuhi hii.11 Ninafurahi kumuona Ndugu Richard Blair akiketi hapa.Nilisoma hivi karibuni tu barua kuhusu jambo kuu ambaloMungu alilitenda miongoni mwa watu kule. Hivi majunzi, kamaninavyoelewa (Naweza nikosee, Ndugu Blair; kama nimekosea,nisahihishe), alikuwa akifanya kazi, akimsaidia mtu kuwekeagari waya au kitu fulani, naamini ilikuwa hivyo. (Nalisomabarua ile.) Na waligeuza kitu fulani; na hata hivyo, ilichukuaumeme hadi kwenye maji ambapo m—mtoto mdogo wa kiumealikuwa (mmojawapo wa—mtu yule aliyekuwa mwenye gari lile,mtoto wake mdogo wa kiume, kijana tu mdogo, na lilimuuayule mvulana mdogo. Na tumbo lake lilivimba na…Twajuamshtusho wa umeme, hicho ndicho—wanapokufa hicho ndichokinachotokea. Akakondoa macho yale madogo; meno yakeyakaumana.12 Liliwatisha wandugu vibaya sana. Ndugu Blair alisemaaliwazia angeweza kunipata mahali fulani kumuombea, lakinialikumbuka kwamba ilikuwa kwamba “Walipo wawili watatuwamekusanyika kwa ajili ya Jina Langu, nami nipo papohapo katikati yao.” Na yule baba alichuna vidole vyakeakijaribu kuingiza vidole vyake katika kinywa cha mvulanayule akifungue. Kisha walipiga magoti wakaanza kumuombeamvulana yule mdogo, naye akapata uhai wake tena.13 Hilo lilikuwa kweli, Ndugu Blair? Mmoja wa ndugu zetuwaaminifu hapa. Lo, huyo kijana mwanamume yuko hapa.Vema, Bwana ashukuriwe! Hilo ni zuri. Tungependa usimame,mvulana Sonny. Sasa, tunashukuru Bwana wetu mpenzi kwahili. Huyo ni baba wa mvulana yule mdogo? Wewe ndiwe baba?Hilo ni sawa. Na hapo yupo Ndugu Richard Blair. Munguwetu aweza kufanya kitu cho chote. Ndiyo, bwana. Aliliahidi.Tunaishi katika UwepowaMungu yule mkuu, wa utukufu, Babawambinguni. Namambo yote ambayo sisi—yanawezekana kamatwaweza tu kuliamini.

4 LILE NENO LILILONENWA

14 Mnaona kile hilo hufanya, ilivyofaidi maisha ya mtu yulekuamini hilo? Liliokoa mvulana wake mdogo. Sasa, Mungualikuwa na watumishi Wake waaminifu hapo ku—Ndugu Blairna wao—kuombea mvulana yule mdogo alipokuwa katika haliile. Ndiyo, kitu cho chote kinapotokea, kumbuka, ninyi ni watotowa Mungu aliye Hai. “Walipo wawili au zaidi wamekusanyikakatika Jina Langu, nipo hapo.” Na tena imeandikwa: “Yeyeni msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.” Na kamapamewahi kuwa na matatizo, mvulana yule mdogo akiwaamelala pale amekufa ardhini kutokana na mshtusho wa umemeuliompitia…Kwa hiyo, tunamshukuru Mungu asubuhi hii kwamioyo yetu yote kwa hizi—kwa mambo haya ambayo ametendakwa ajili yetu.15 Mungu awabariki watu hawa waaminifu pia. Katikawakati wa dharura huo ndio muda wa kumtafuta Mungu; nakumtazamia Yeye na muwe rafiki Zake kabla ya dharura kuja.Twajua hili: Kama tunampendeza Mungu, twaweza kumuombakitu cho chote, kama ambavyo ungemuomba rafiki mwingine yeyote; na Yeye nimsaada utakaonekana telewakati wamateso.16 Nilikutana hivi jana tu huko barabarani na dada wa NduguJohn Martin. Nilikuwa…Mtu mmoja alikuwa amenisimamishahuko barabarani na mtu mwingine alipita karibu naakanipungiamkonowake.Wakati wa kurudi nyumbani, mnajua,unawaona watu kila mahali wakisimama na kupeana mikonona kadhalika. Na bibi huyu, nakumbuka waliniita hivi majuziambapo mtu fulani alimgonga nyuma katika gari dogo naakapasua uti wake wa mgongo na kadhalika juu chini. Ilikuwaapooze maishani mwake mwote. Anaketi mkutanoni asubuhihii akifurahia Uwepo wa Mungu. Nalikuwa tu nikizungumzanaye chumbani mle; nataka kuomba pamoja naye tena, nayealikuwa…Yupo hapa mahali fulani. Nakisia hakuweza kurudindani. Lakini hapa! Hakika, yupo hapa akiketi papa hapa nasi.Hilo ni sawa. Hebu simama kidogo tu, Dada, ili watu waweze…Yupo hapa bibi huyo ambaye daktari alisema siku chachezilizopita hatatembea kamwe, aliyepasukiwa na uti wa mgongona kila kitu kutokana na mgongano—mgongano; na hapoanasimama, mzima. Unajua Biblia ilisema, “Nao hawakuwana neno la kujibu, sababu yule mtu alikuwa akisimama katiyao.” Hilo ni sawa. Hapa yupo kijana mdogo aliyefufuliwa,na hapa pana mwanamke mwenye uti wa mgongo uliopasukawakisimama kati yetu. Imeisha fanyika tu. Kwa hivyo Yeye niyule jana, leo, na hata milele. Na libarikiwe Jina la Bwana! Jinsiitupasavyo kufurahi kwamba tunaishi sasa katika uwepo Wakena kujua kwamba Yeye ni huu msaada upatikanao wakati wamateso.

Nina furaha kumuona Ndugu Vayle, Ndugu Martin, wengisana wakiwepo asubuhi hii. Na Bwana awabariki sana ninyindugu.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 5

17 Sasa, ni…najua si baridi humu kwa umati huu wote, hatahivyo, nilipoondoka Tucson hivi majuzi, joto lilikuwa kama miamoja na nne au tano; na yapata usiku wa manane ilikuwa tisinina tatu, na basi naona hili ni zuri sana kwangu. Kisha hukoParker walisema lilikuwa mia moja na arobaini Ijumaa kablahatujaondoka. Na waweza kufikiri jinsi ilivyokuwa joto. Bilashaka hiyo ni jangwani.18 Na sasa, hizi Jumapili tatu zijazo…Leo, tarehe kumi natano, naamini, hilo ni sahihi, au kumi na sita? Kumi na tano,siyo? [Mtu fulani anajibu, “Kumi na nane”—Mh.] Kumi na nane.Na ishirini na nane na A—Agosti moja. Ni sawa? [Mtu fulanianajibu, akitoa tarehe sahihi—Mh.] Ishirini na tano—kumi nanane, ishirini na tano—na tarehe ya kwanza kutakuwa na ibadakwenye maskani. Msialike, mnajua, msialike wengi kupita kiasisababu, mnaona, hatuwezi kuwaweka walio ndani—walio njehapa ndani sasa, mwajua, na inazidi kuwa baya. Rudini tumkiweza.19 Na—na kisha nipo hapa kuwakusanya wadhamini pamoja.Yaonekana ninavunjwa na huku kukatazwa kwote kwa mahalipa kufanyia mkutano wakati ninajisikia kuongozwa kuufanya.Kwa hiyo nitakwenda kuwaomba kama hatuwezi kuchukuahema letu na—na kulisimamisha na kukaa pale tu, na,mwajua. Kuenda hapa katika uwanja wa mpira au njekatika shamba na kulichukua mahali hadi mahali kama tuBwana atakavyoongoza. Na naona kwamba hivyo ndivyo Yeyeatakavyotenda. Mnajua kuna ono kuhusu hilo. Na nafikirikwamba labda hiyo ndiyo sababu haya yanatokea…Sasamwajua, mara nyingi tunafikiria ni vibaya sana kwa sababumambo fulani hutokea, lakini mwajua, huyo huenda ikawa niMungu (mwaona?) akikusukuma katika mambo haya. WakatiYeye alinenapo, atalitenda.20 Siku chache zilizopita wengi wenu—yapata mwezi mmojakabla ya kwenda Afrika…Wengi wenu labda wana kanda(ninyi watu mnaopata kanda) juu ya Kuchagua Bibi Arusi.Ulihubiriwa California. Dakika chache za mwisho za kandaile, sikumbuki kamwe kuhusu kuwepo huko. Lakini Roho waBwana alikuja kwa nguvu sana. Nalikuwa nikiwalaumia jinsiwalivyokuwawakiishi na kufanya, na baada ya Injili kuhubiriwana kutangazwa mbele yao. Mara Roho Mtakatifu akanena naakasema, “Kapernaumu (mwaona?), mji ule unaojiita wenyewekwa jina la malaika (huo ni Los Angeles), wewe umejikuzampaka Mbinguni, lakini utashushwa mpaka kuzimu!” Mnaona?Na kisha baada ya hayo ukaisha, naam, nilikuwa nje. NaNduguMosley na Billy walikuwa pamoja nami, naowalisema…Walirudi wakaangalia, na sakafu yote ilikuwa imejaa watu,wahudumu wakilia kwa huzuni.21 Nami nalikwenda na kuchukua Andiko; nikasema, “Kunakitu kuhusu hilo katika Biblia.” Na ilikuwa Yesu akikemea

6 LILE NENO LILILONENWA

Kapernaumu, miji yote ile ya pwani ambayo alikuwa ameizuru.Kwa nini alisema, “Nawe Kapernaumu, umetukuzwa mpakambinguni, utashushwa mpaka kuzimu.” Alisema, “Kwa kuwakama kazi zilizofanyika kwako zingefanyika katika Sodomana Gomora, ingalikuweko hata leo.” Na wakati ule Sodomana Gomora ilikuwa chini ya Bahari. Na baada tu ya hilo,labda miaka mia moja au yo yote ile baada ya unabii waYesu, Kapernaumu, mji pekee wa pwani ambao yeye aliuzuru,tetemeko la nchi liliuzamisha baharini. Wajua, hilo lilikuwa jibulamoja kwamoja kwa California, kwa Los Angeles.22 Na kisha huko Tucson hivi majuzi, niliporudi tu, tetemekokubwa la nchi lilitokea kule. Na wanasayansi walikuwa katikatelevisheni wakilichora. Ilikuwa katika magazeti, kwambadunia hivi majuzi ilipasuliwa toka visiwa vya Aleusia—au tokaAlaska kuzunguka Visiwa vya Aleutia, kama maili mia mbilikupenyeza baharini, ikurudi hadi San Diego, ikazunguka LosAngeles, na kutokea San Diego. Na iliachana inchi kadhaa.Nyumba zimebomolewa. Nyumba za kulala zimezama. Namwanasayansi katika tume hii ati—aliulizwa, akasema, “Vema,hiyo yaweza kuanguka siku moja.”23 Yeye alisema, “Ati yaweza? Itaanguka!” Naye alitumiamajina ya kisayansi jinsi yale mawe ya volkeno yame…Hilondilo lililosababisha haya matetemeko ya ardhi kuzunguka SanDiego na chini ndani kule; imekuwa sehemu ile tupu. Na sasayote imeanza kuporomoka kama changarawe inayobonyea. Nasasa ni ganda tu na imeachana inchi nyingi. Wangechukua radana kadhalika na kufuatilia ufa ule, na kutia alama, kuonailipokuwa. Na iliachana inchi nyingi zaidi, labda inchi mbili autatu hivimajuzi, tena,mara tu baada ya kutolewa unabii ule.

Na wale waliokuwa wakimhoji mwana sayansi yulewalisema, “Vema, labda jambo hilo halitatukia katika wakatiwetu.”24 Alisema, “Lingetukia katika dakika tano au miaka mitano,lakini patazama.”25 Bibi Simpson—sidhani yuko nasi leo; au…ninamuonaNdugu Fred akiketi hapa, lakini sijui alipo Bibi Simpson.Alikwenda akapata unabii ambao niliutoa mnamo 1935 au kitukama hicho, na kusema: “Wakati waja (imeandikwa katikakitabu mahali fulani) bahari itatiririka mpaka jangwani.”Angalia litakalotokea. Kama hayo maelfu ya maili mrabayatakayotumbukia katika mawe ya volkano yanayoyeyuka yadunia na kudidimia ndani, patakuwa namamilioni watakaokufakwa wakati mmoja. Na hilo litasababisha wimbi kubwa sana labahari…Kumbuka, hadi kufikia Bahari ya Salten ni futi miamoja au mia mbili chini ya usawa wa bahari. Maji hayo labdayatakaribia sana Tucson na hilo wimbi kubwa la bahari likijahuko. Na bahari itatiririka hadi jangwani.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 7

Mataifa yanavunjika;Israeli inaamka,Ishara walizotabiri manabii;Siku za mataifa zimehesabiwa,Zimekubwa na hofu,Rudini, Enyi mliotawanyika, makwenu.

26 Tuko wakati wa mwisho. Sasa, Bwana awabariki sana.Ninaanza hayo na kusahau saa. Tutafifia hivi karibuni katikaumilele kwa vyo vyote.27 Na sasa, katikaMarkoMt. sura ya 7 na aya ya 7, kuleta fungulamaneno kwenye somo hili ambalo ndiomara tu lisomwe katika1Mambo yaNyakati 13. Ili kufanya somo kwa ajili ya hili natakaMarko 7:7:

…Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundishoyaliyo maagizo ya wanadamu.

28 Sasa, sijui neno ila ule Ujumbe alionipa Bwana, na huo tundio niwezao kuzungumzia. Na sasa, nitazungumza juu ya somoasubuhi hii ambalo nilidhania lingefaa. Na usiku wa leo natakakuzungumza juu ya, chakula kwa Wakati Wake, kama Bwanaakipenda—Chakula cha Kiroho kwa Wakati Wake, na Jinsi yaKukipokea. Sasa na asubuhi hii: Kujaribu Kumtendea MunguKazi Bila ya KuwaMapenzi ya Mungu.29 Mungu yu mwenye enzi. Na tunaona hapa Daudi alilofanyakatika Maandiko yaliyosomwa ya 1 Mambo ya Nyakati 13.Naye alikuwa—makusudio yake yalikuwa mema. Lakini Munguhatupi thawabu kwa ajili ya makusudio mema. Kuna njia mojapekee ya kumtumikia Mungu, nayo ni kwa kutenda mapenziYake kwa amri Yake. Naye Mungu, akiwa mwenye enzi, hakunamtu wa kumwambia la kufanya au jinsi ya kulifanya; Yeyehutenda hilo namna…Anajua njia sahihi ya kulitenda. Na hilohunifanya mimi nijisikie vizuri. Na lapaswa kutufanya sisi sotekujisikia vizuri. Na nina hakika hutenda hivyo. Kwani mmojaatakuwa nalo likija namna hii, na mmoja atakuwa nalo likiendanamna ile, na mmoja njia nyingine…30 Lakini kitu kimoja kikubwa tena kuhusu Mungu, Yeyehakutuacha, sasa, bila kujua ukweli ni nini na jinsi yakuutekeleza. Hangelikuwa wa haki kutuadhibu kwa kutendakitu ambacho hatukujua jinsi ya kukitenda, na kisha kutuachiliatujikwae katika kitu fulani. Si Mungu wa aina hiyo. Yeyeni Mungu ambaye hunena neno na anawatazamia wanawekuliamini. Na kwa hiyo, Yeye ajua kilicho bora sana, na wakatiwa kukifanya, na jinsi ya kukifanya. Sisi tunayo mawazo yetujuu yake, lakini Yeye anajua.31 Na kisha, kama Yeye angaliweka taratibu ya yaleatakayotenda na hakutuambia yale yatakayotokea na jinsiyatakavyotokea, basi sisi tukijikwaa kwa hayo ingekuwa—tungehesabiwa haki katika—katika kujikwaa kwetu au kujaribu

8 LILE NENO LILILONENWA

kufanya kitu, kila mmoja angalihesabiwa haki. Lakini kuna njiamoja pekee tu, nayo ni Neno lake.32 Na jambo lingine, Daudi hapa, twaona kwamba katika moyowake alitaka kutenda jambo lililokuwa jema. Hakuwa na niambaya au hakuwa na kusudi baya, lakini nyumba—au sandukula Bwana lilikuwa mbali na hao watu; naye alitaka kulirudishasanduku la Mungumahali pake, ili watu wamtakeMungu shaurikuhusu mambo waliyohitaji.33 Badala ya—ya kuliachilia tu, sisi…Vipi kama NduguBlair na baba wa mvulana huyu mdogo angesema, “Vema, nivibaya mno kijana ameumia tu, ameuawa. Nadhani, kitu tukilichotukia”? Lakini walimwendeaMungu haraka.34 Vipi kama maskini bibi yule, na mumewe ni mhudumuwa Injili, siku chache zilizopita usiku au siku, wakati bibiyule alipovunjikiwa na uti wa mgongo ambaye ndio maraasimame…Daktari alisema, “Atapooza maisha yake yote.” Vipikama mumewe—bibi huyo alisema, “Vema, mpenzi, tutajifarijitu kwa hilo.” Lakini haraka walifanya kitu kuhusu jambo hilo;walimwendea Mungu. Ni vitu vingapi katika Biblia tungewezakuvitaja jinsi ambavyo watu wanapopata shida, humwendeaMungu.35 Vema basi, katika siku hizo walikuwa na mahali pamoja tuambapo waliweza kukutana na Mungu, na hapo ni penye lilesanduku chini ya damu. Bado ndipo mahali pa kukutanikia,chini ya Damu. Kiti cha rehema kilinyunyiziwa kutoa neemakwa anayeabudu au anayeomba wakati alipomuomba Munguhaja yake. Naye Mungu alikuwa na utaratibu maalumu, njiailiyokupasa kuendea—kuhusu hilo, na Yeye asingalikubali kitukingine cho chote. Asingekubali njia nyingine iliyotolewa, nijinsi tu alivyoitengeneza.36 Hivi majuzi nimehubiri tu juu ya ujumbe (wengi wenumwajua hilo) kwamba mna mahali pamoja tu palipoandaliwaambapo Mungu hukutana na mwabudu, mahali pale ambapoalisema, “Nitaliweka Jina langu.” Kama twaweza kupata kanisaambamo aliweka Jina Lake, basi tumepapata mahali hapo.Alisema, “Sitawabariki katika malango yote, ni yale malangotu ambomo naliweka Jina Langu. Nitaliweka mahali pamojananyi yawapasa mkutane nami hapo; na hapo ndipo mahalipekee nitakapokutana nanyi.”Nasi tuliona kupitia hapo ambapoaliweka Jina Lake. Na hapo ndipo mahali pekee ambapohukutana na mwabudu; na Jina Lake lilikuwa Yesu Kristo. Jinala Mungu ni Yesu Kristo.37 Yesu alisema, “Mimi nimekuja kwa Jina la Baba Yangu.”Kila mwana huja katika Jina la baba yake. Naye alikujakatika Jina la Baba. Na hakuna Jina jingine chini ya Mbingulililotolewa miongoni mwa watu, au linaitwa MethodistiPresbiteria, Church of Christ, hata ifanyweje, kuna mahali

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 9

pamoja tu pa kukutania ambapo Mungu hukutana namwanadamu, na hapo ni wakati awapo ndani ya Yesu Kristo,mahali pekee. Na mambo yote haya ya kale nyuma kule chini yaAgano la Kale ni kivuli cha hilo. Nawatakeni muelewe waziwazihilo. Sasa, ni somo la shule ya Jumapili. Na nina baadhi yaMaandiko na maandishi yaliyoandikwa hapa. Nami niliwazakwamba hili litasaidia muelewa, kwani mambo yote ya zamaniyalitokea kama mifano kwetu sisi.38 Sasa, twaona kwamba Mungu alikuwa na njia ya kufanyamambo, lakini Daudi, akibarikiwa tu na Mungu kwa kuwaangekuwa mfalme, alifikiri tu kwamba angemtendea Mungukitu kwa vyo vyote. Naye kamwe hakuliendea hilo kwa njiailiyokuwa sawa.39 Tunaona, Mungu hulifunua Neno Lake katika majiraYake Mwenyewe aliyoyachagua tangu awali. Sasa, MartinLuther angewezaje kujua kuhusu Ujumbe wa leo? AngewezajeMpresbaiteria…Martin angewezaje—au kanisaKatoliki kuujuaujumbe wa Martin Luther? John Wesley angewezaje kujuaujumbe wa Luther? Wesley angejuaje ujumbe wa Wapentekoste?Au Wapentekoste wangejuaje Ujumbe huu? Unaona? Yeyehuufunua katika majira Yake, kwa sababu ni Mbegu; na kadiriikuavyo na kukomaa hujifunuaMwenyewe.40 Kama joto la jua kuifungua. Inapokuwa nyororo na changa,kuichipusha toka ardhini, hiyo mbegu, kisha katika hatuanyingine ya jua kuipa majani yake. Jua kali litaiva kamani mbegu ya kukomaa au wakati wa kukomaa. Kwa hiyohulirekebisha jua na huyarekebisha maumbile kuafikiana naNeno Lake. Hulirekebisha Kanisa, waliochaguliwa tangu awali,Bibi-arusi, kukabiliana namajira wanayoishi.41 Hata maumbile yenyewe hutuambia leo, tunapoona mataifayakivunjika, dunia ikididimia, maandiko kwenye ukuta.Tunaona kanisa na hali lilimo. Twamuona Bibi-arusi na halialiyomo. Nasi twajua kwa mambo ya asili kwamba Kanisalinajiweka tayari kuondoka. Ni wakati wenye fahari vipi. Niwakati ambaomanabii wotewalitamani kuuona, saa hii.42 Sasa, hulifunua Neno Lake katika majira Yake tu. MartinLuther alisoma Biblia ile ile tuliyosoma. Wesley alisoma Bibliaile ile Martin Luther aliyosoma. Wapentekoste walisoma Bibliaile ile tunayosoma. Yesu alisoma Biblia ile ile Mafarisayowaliyosoma, lakini walikuwa…Wakijaribu kuiweka nganokatika hatua ya mapema ambapo ilikuwa inaiva, walishindwakuiona saa yao.43 Sasa Daudi amefanya jambo lile lile hapa. Mungu hulifunuaNeno hili katika majira yake na kwa yule amchaguaye kulifunuakwake. Mungu huchagua wa kulifunua kwake. Alichagua hilokabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Matendo Yakeyote yalijulikana Kwake, yakiwa yamefichwa wanadamu; Yeye

10 LILE NENO LILILONENWA

huyafunua tu apendavyo. Ni majira Yake aliyochagua, mtuWakealiyemchagua. Na kamwe hajachagua kundi au dhehebu; ni mtualiyechaguliwa. Jinsi atendavyo hilo.44 Ni nani yule atakayethubutu kumsahihisha na kusema,“Sasa, Bwana, ulifanya kosa kwa kumweka mtu huyukatika huduma. Mtu huyu haamini kama tuaminivyo.” Naniatakayekwenda kumwambia Mungu amekosea katika jambohilo? Itahitaji mtu ambaye ana hatia zaidi kidogo kuliko mimikumwambia hilo. Yeye anajua atendalo. Anajua amchaguenani na asimchague nani, la kufanya na wakati wa kulifanya.Haidhuru tunavyofikiri mtu fulani anastahili kufanya kazifulani, Mungu anajua ni yupi anayestahili kwa wakati huo namajira hayo, aumajira hayo nawakati unaofaawa kuitenda.45 NayeMkristo halisi nawa kweli, mwamini halisi nawa kwelikatika Mungu, humngojea Bwana kwa mambo haya. Ngojea juuhuduma yako. Kama ukijisikia kuitwa, hakikisha kwamba niMungu. Hakikisha kwamba ni sahihi. Hakikisha kwamba yaleusemayo yako katika wakati. Biblia ilisema, “Wao wamngojeaoBwana watapata nguvumpya. Watapanda juu kwambawa kamatai. Watapiga mbio, wala hawatachoka. Wakienda kwa miguu,hawatazimia.”46 Angalia Daudi, mfalme wa Israeli; akiwa ndio tuapakwe mafuta. Samueli alimmiminia mafuta, naye alikuwaamechaguliwa na Mungu awe mfalme wa Israeli. Naye Daudialipata ufunuo huu kulileta sanduku la Bwana hadi mjiwa Daudi. Sasa, hakuna kosa lo lote, lakini unaona, Daudialiliendea isivyo sahihi.47 Sasa, yaonekana kana kwamba mtu kama huyo angepataufunuo, mtu mkuu kama mfalme aliyechaguliwa na Mungu(mfalme mkuu kuliko wote aliyewahi kuishi duniani nje yaKristo, nadhani, alikuwa Daudi, kwa sababu Kristo ni Mwanawa Daudi)…Sasa, mtu mkuu zaidi ya wote, aliyekuwa ndio tuapakwe mafuta, akitoka kwenye Uwepo waMungu hasa, alipataufunuo kumfanyia Mungu kitu na alitaka kukifanya kwa ajili yaMungu, lakini ule ufunuo ulikuwa sio sahihi. Sasa, hilo ni jambokuu. Litahusu somo letu: Kujaribu Kumfanyia Mungu Kazi Bilaya Kuitwa Kuifanya.48 Angalia, Daudi alipata ufunuo. Na angalia, haikuwanabii Nathanieli ambaye alipata ufunuo; ilikuwa mfalmeDaudi ambaye alipata ufunuo. Wala Nathanieli hakutakwashauri juu ya hilo. Hakumuuliza Nathanieli kamwe. Lakiniuliona hapa katika 1 Mambo ya Nyakati, alifanya shauri namaakida wa maelfu na maakida wa mamia. Hakumtaka shauriNathanieli kamwe. Aliwataka shauri watu, na aliwataka shauripia makuhani na wanatheologia wa siku ile, waandishi nawanatheologia. Daudi kwanza alitaka shauri, kasema, “Hilo—kama hili ni la…Mungu, hebu basi tushuke twende huko

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 11

tukalete sanduku la agano la Mungu wetu mjini, na tumtakeMungu shauri kabla ya kufanya mambo.”49 Walisema katika siku za Sauli waliacha kumtaka shauriMungu kwa lile—lile—lile sanduku, ile Urimu—Urimu Thumimu;waliacha kufanya hivyo. Kisha Daudi akasema, “Sasa, hebuna tumrudie Mungu, sisi sote. Hebu na turudie mambo yaliyosahihi. Hebu tushuke twende huko tukachukue lile sandukutulilete hapa (tuulete Uwepo wa Mungu, kwa maneno mengine,mjini). Hebu tufanye ufufuo. Natuwarejeshe watu.” Lakinialipata ufunuo, ambao ilionekana kuwa mzuri, lakini hayakuwamapenzi ya Mungu.50 Badala ya kuuliza chanzo ambacho alipaswa kuuliza,aliwataka shauri maakida wake, kwa sababu ndio mara tu awemfalme, naye alifuatia mawazo kama hayo ambayo maakidawake na watu wake wakuu…51 Kisha akaenda katika kanisa la kawaida akauliza kamawangeweza kuwa na ufufuo: wale makuhani, waandishi,maakida wa maelfu, maakida wa mamia, naye akawatakashauri, “Je, hili lilikuwa mapenzi ya Bwana?” Nao wakasemandivyo. Lakini, unaona, alishindwa kuuliza chanzo muhimuambacho siku zote Mungu hutenda kazi kwake (unaona?);akashindwa kukipata.52 Sasa makusudio yake yalikuwa mema. Nia yake ilikuwanjema. Makusudio yake yalikuwa mema, na—kuleta ufufuomjini, kuwarudisha watu kwa Mungu. Lakini kamwe hakutakashauri jinsi Mungu alimwambia atende. Unaona?53 Hata watu wote walikubali na wale makuhani na—kwambamfalme alikuwa sahihi. Walihitaji sanduku lirudi mjini. Sasa,walihitaji Uwepo wa Mungu. Walihitaji ufufuo. Lakini Munguhakuwa ameahidi kufunua Neno Lake katika majira yakekwa watu. Hakuahidi kamwe kulifunua kwa mfalme katikamajira. Naye Mungu habadiliki hata kidogo. Yeye hakuahidikufanya hilo.54 Hata lifanywe kwa uaminifu vipi, na kwa nia nzuri vipi,na makusudi mazuri vipi, na hata watu wapende mambohayo vipi, na kuona haja yake, kuna mapenzi ya Munguyanayopaswa kutekelezwa katika mambo haya. Hilo ndiloninalotaka kusisitiza sana usiku wa leo. Nataka kulifanya hiliili kwamba huna budi kuliona kama—kama Roho wa Munguanakaa ndani yako. Na hiyo ndiyo sababu ninakawia sana hapa.Si kuchukua wakati wenu ninyi watu mnaosikiza kwa simu nakwenye redio za motokaa, lakini na—nawataka mulione hilo.Kama wakati wenu ukimalizika, chukueni kanda yake. Kwambakuna…55 Haidhuru inahitajika vipi. Kila mmoja anakubali kwambajambo hilo lahitajika, hata hilo liwe kweli vipi, bado kungalikuna kitu kimoja cha kutafuta: Je, hilo nimapenzi yaMungu?

12 LILE NENO LILILONENWA

Sasa, Mungu hakuahidi kamwe kwamba angefunua siriZake kwawafalmewake, angefunua siri zake kwawatuWake.56 Kitu kama wakati wa Mikaya, mwana wa Imla. Kamatunapoliacha, si fungu, lakini wakati mwingine, kuliingiza hilina kulifanya kweli kwenu, dhahiri kwenu, ili msilikose.57 Kulikuwako katika siku zaMikaya…Alikuwamtumaskini,na pia alitoka kwenye familia maskini. Lakini Ahabu, mfalmewa Israeli, kama taifa likiwa chini ya Mungu, alitengakando shule moja na alikuwa ameleta manabii walioteuliwa,waliochaguliwa kwa uangalifu sana, naye alikuwa na mia nnewao chuoni. Nao walikuwa watu wakuu. Hawakuwa tu manabiiwa uongo. Walikuwa manabii wa Kiebrania, watu halisi. Nawalimtaka Bwana shauri kwawatu hawa. Naowalitabiri. Lakiniunaona, wakati lile shindano halisi la kuamua lilipofika, kilammoja alikuwa nje yaNeno laMungu namapenzi Yake.58 Kwani Yehoshafati alishuka toka Yerusalemu kumlakim—mfalme Ahabu, nao wakavaa mavazi yao, wakaketi la—langoni, na akawaleta manabii mbele yao. Kwanza Ahabualisema, “Tunapo mahali hapa Ramothi iliyo Gileadi ambaponi petu kweli.” Sasa, hiyo ni BWANA ASEMA HIVI: Yoshuaaliwagawia watu na akawapa hapo, lakini Wafilisti walikuwawamepachukua. Kisha kasema, “Hapa watoto wetu wanahitajichakula, na hatuna ardhi ya kutosha kukuza chakula; na aduiyetu, Mfilisti, huwalisha watoto wao, hao makafiri, katika ardhiile ile ambayo Yehova Mungu alitupa sisi.” Hilo ni dhahirisana. Kisha kasema, “Hapa sisi, watu wa Mungu, tumeketina watoto wetu wahitaji; na adui yetu analisha watoto waokatika ardhi ambayoMungu alituitia tokaMisri na akatupa sisi.”Hilo lingemuinua Mthiologia, ama sivyo? Alisema, “Tutaendatuchukuemashamba yetu ambayoMungu alitupa?”59 Yehoshafati alisema, “Ndio, nitawasaidia. Sisi ni ndugu.Ninyi mko Yuda, na mimi niko katika—nimo Yerusalemu” (au—au ilikuwa vinginevyo? Naamini…La, hilo ni sahihi, nafikirikwamba Yehoshafati…) Hata hivyo, Yehoshafati alikuwamtu mzuri, mfalme, mtu wa haki ambaye alimpenda Bwana.Ahabu alikuwa mwamini vuguvugu. Kwa hiyo waliwaleta,na Yehoshafati alisema, “Sikilizeni, na tumtake Bwanashauri kwanza. Yatupasa kujua hili.” (Unaona, kama Daudiangalitenda kile Yehoshafati alitenda…) Alisema, “Tusitendehili?”

Na haraka, akiwa Mwisraeli, Ahabu alisema, “Bila shaka.Ninao mia nne, Waebrania kama tulivyo sisi, manabii waKiebrania wa dhehebu letu. Na nitawataka shauri. Wao nimanabii.”60 Sasa, waona, hili…Unasema, “Hilo hunikwanza, NduguBranham. Nabii?” Lo, ndiyo! Palikuwepo na mmoja katikawakati wa Yeremia ambaye alisema watakuweko huko miaka

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 13

miwili tu. Bwana alimwambia Yeremia, sabini. Akaweka nirakatika shingo Lake, naye yule nabii Hanania akaivunja. LakiniMnajua lililompata. Lo, ndio! Yakubidi ukae naNeno.

Kwa hiyo manabii hawa walipanda, na wakatabiri,wakasema, “Kweeni, Bwana yu pamoja nanyi.”61 Na mmoja wao, naamini ni—nasahau jina lake sasa, mkuuwao, Zedekia, naamini, alisema—aliweka pembe mbili za chumaakasema “Bwana asema hivi, kwa hili (sasa, mtu yule alikuwamwaminifu) utawasukuma maadui zako warudi nyuma katikanchi zao na kuchukua kilicho cha Mungu; umepewa hiyo.”Siamini alikuwa mnafiki. Naamini alikuwa mtu mzuri. Naaminihao manabii wote walikuwa watu wazuri.62 Unasema, “Manabii?” Ndio! Kumbuka, mtu yule yuleambaye alikubali kumuua Yesu Kristo alitabiri, kwa sababuilikuwa ni zamu yake. Alikuwa kuhani mkuu mwaka huo,na kwa kuwa hicho kilikuwa cheo chake naye alikishikiliahicho cheo, Roho wa Bwana alimjia. Na hilo halikumaanishaameokolewa au cho chote kile. Na alitabiri (Kayafa) kwa sababukilikuwa cheo chake kilichotenda hilo.63 Na hawa manabii, wakiwa manabii wa cheo cha manabii,walitabiri, na Roho wa Mungu aliwajia, watu walio na karamaza Roho.64 Natambua ninazungumzia asilimia tisini na tisa yaWapentekoste, lakini mtu…Mara nyingi mtu, Mungu anawezakutenda kazi pamoja nao, awape kipawa, na watu watawabanawatu hao. Kama hawakuwa wameitwa sawasawa na kutumwana Mungu, atamfanya mwanamume huyo au mwanamkekusema kitu ambacho si mapenzi Yake, kwa sababu watuwanawashurutisha kulitenda.65 Jinsi ilivyonibidi kumshika maskini mchungaji wetu hapajuu ya jambo hilo. Nje huku mwituni asubuhi moja, mnamo saa9 usiku, kasema “Nenda kamwambia Ndugu Neville!” Nilikujakwako, sivyo, Ndugu Neville?66 Kila mtu, “Ndugu Neville, nitabirie. Niambie hili au lile.”Unaona? Mtamfanya aseme mambo basi ambayo hayatatimia.Wao ambao hungojea kujua ambalo Bwana ataka kutenda.Waona?67 Kwa hiyo watu hawa waliliangalia katika hisi ya maumbile,“Ni yetu.” Lakini waona, hawakutafuta Neno na mapenzi yaMungu.68 Kisha Mikaya akashuka akaja, naye alikuwa na ono. Naakaangalia kwanza. Unatambua? Alisema “Ngoja. Nipeni usikuhuu. Ngoja nitafute na kesho labda naweza kuwajibu.” Hakuwana haraka, “BWANA ASEMA HIVI,” kama katika kupatana namanabii wengine; alisema, “Nitasema tu asemayo Mungu.” Nasiku iliyofuata twaona Mungu alimwabia yatakayotendeka. Na

14 LILE NENO LILILONENWA

lilikuwa kinyume kabisa cha wale wengine. Chuo chote kilikuwakinyume. Na hata mmoja wao aliondoka akaenda akampigakofi la uso kwa ajili ya hilo. Lakini unaona, alingojea. Kishaalipofanya hilo alilinganisha unabii wake, ono lake, na Nenolililoandikwa, na ulikuwa unapatana na Neno.69 Mtu asemapo wana ufunuo kubatiza watu katika Jina LaBaba, Mwana na Roho Mtakatifu, hilo ni kinyume cha Neno.Hamna mmoja kati ya hao wengine aliyewahi kutenda hivyo.Wakati wasemapo kwamba, “Lo, tutasimama…” na hili, lilena lile lingine, na kadhalika, hayo ni kinyume cha Neno.Wanaposema hawaamini katika uzao wa nyoka, hilo ni kinyumecha Neno. Na Mambo haya mengine yote, hilo ni kinyume chaNeno. Lazima ipatane naNeno na iwe katikamajira yake.70 Sasa, laiti Daudi angefanya hilo. Sanduku lilikuwa lije,lakini si wakati ule. Hakukuweko namahali pake.71 Angalia sasa, waliposhuka wakaenda kuchukua lilesanduku, hao mabwana wote walisema, “Hivyo ndivyoinapaswa kufanywa, Daudi, Mungu atukuzwe! Twahitajiufufuo.” Na hiyo ilikuwa Pentekoste halisi leo—Wabatisti,Presbaiteria. “Daudi, wewe ni mfalme wetu. Ninyi nyote…Akida fulani na Meya fulani na Jemadari fulani atakuwepokwenye mkutano wako. Naam, wanasema hivyo ndivyounapaswa kufanya, Daudi. Nchi yote iko pamoja nawe.” Hiyondiyo shida leo hii! Sitaki nchi. Nataka Mungu, kama hakunamtu mwingine anayesimama.72 Daudi alikuwa na maakida wote. Alikuwa na ushirikianona jeshi. Alikuwa na ushirikiano na madhehebu yote, nawathiologia wote, na wote—kila mtu akikubaliana naye. Hivyondivyo alivyofanya Ahabu, na wengine katika Maandiko; lakinihakuwa na Mungu, kwa sababu alikuwa nje ya mapenzi yaMungu. Natumaini tunaelewa hili!73 Angalia! Walifanya kila kitu cha kidini walichoweza.Lazima labda waliweka matangazo na kila kitu: “Ufufuo mkuu,sanduku litarudishwa. Tutakuwa na ufufuo! Tutafanya hili.”74 Angalia, aliwatuma waimbaji. Aliwatuma watu wenyevinubi, walio na tarumbeta, na walitenda kila kitu cha kidiniwalichojua; na bado Mungu hakuwa katika hilo! Kwa namnafulani twaliona likijirudia tena, sivyo?75 Waliwachukua waimbaji wote. Walichukua wapiga vinubiwote, wapiga tarumbeta, wanawake wanaume, ye yotealiyeimba; wote waliwachukua chini huko, na walipitiakila kitendo cha kidini, sitaki kusema hili, lakini sina budikulisema: Vivyo hivyo madhehebu haya leo hii, Wapentekostena kadhalika, wanapitia kila kitendo cha kidini cha kuimba nakupaza sauti kwa nguvu.76 Angalia, Daudi alipaza sauti kwa nguvu zake zote, akapigavigelegele akaruka, na akapitia kila tendo la kidini liwezalo

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 15

kuwepo; na badoMungu hakuwa katika jambo hilo. Na nia yake,na makusudi yake, na kila kitu kilikuwa sahihi; lakini akapitianalo njia isiyo sahihi. Unaona? Alifanya matendo yote ya kidini:alipaza sauti, aliimba, alikuwa na waimbaji maalumu, wapigakelele maalumu, kila kitu. Walicheza katika roho.Walifanya kilakitu ambacho kilikuwa cha kidini.

77 Ni kitu kama mikutano yetu mikuu ya wakati wetu.Walitaka kuushinda ulimwengu kwa ajili ya Kristo. Hakunakitu kama hicho! Ufufuo mkuu wa halaiki ya watu,mambo makuu yakitokea, laiti wangalitambua, siku hizozimepita. Limeangamia! Lakini wanafanyiza mikutano mikuu,madhehebu na kila kitu; bali matokeo ni kama tu ilivyokuwakatika wakati wa Daudi; hayakufaa kitu.

78 Twaenda na kuwa na ufufuo. Wajilisti—baadhi ya wainjilistiwetu wakuu leo, wanasema wana waongofu elfu thelathinikatika muda wa majuma sita; na mwaka mmoja tokea hapowakirudi, hawawezi kupata thelathini. Kuna kasoro fulani.Jambo ni kwamba, ni kitu kile kile tu alichofanya Daudi. Watumashuhuri, mabwana, wahubiri wakuu, shule kuu, mamlakamakuu, lakini badowangali wanataka shauri dhehebu la zamanibadala ya kuangalia katika uso wa Neno la Mungu na kuonamajira yataanza lini. Huwezi kukuza vyakula fulani ila nyakatifulani za mwaka.

79 Sasa, na tuone nini kilichotokea. Ingawa—ingawa hangaikolao la kidini na kadhalika lilikuwa kuu, makusudio yaoyalikuwa makuu, mikutano ilikuwa mikuu, kuimba kwaokulikuwa kuzuri sana, kucheza kwao kulikuwa kuzuri sana,kupaza sauti kwao kulikuwa kukuu, mziki wao ulikuwa murua;na walikuwa na lile sanduku. Sanduku lina faida gani bilaMungu? Ni sanduku tu la mbao, meza mbili za mawe. Hivyo nikama kufanya Ushirika, kubatizwa. Kuna faida gani kubatizwakama kwanza hukutubu? Ina faida gani kupokea Ushirika nakuwa mnafiki, kama huishi maisha yale na kuamini Neno lilelingine la Mungu? Kuchukua Sehemu Yake na si lile lingineyaonyesha kuna kasoro.

80 Sasa, wakati hili lote litokeapo…Na tuone sasa ninikinatokea wakati Mungu na kizazi chake, na wakati Wake,hafifikiriwi, ila tu mawazo ya watu.

81 Watu wengi waniambia, “Kwa nini huji huku na kufanyamkutano? Vema, tunakuita. Tia sahihi hili, lile au lingine.”Ngojea! Mwaweza kutaka hilo, lakini je, Mungu anasema ninikuhusu jambo hilo? Watu wengi wameniambia…Nimekuwana mwaliko, nimekuwa na mahojiano—mahojiano ya kibinafsina kadhalika—nikangojea mwaka mzima. Ngojea! Nitajuaje lakusema mpaka Mungu aniambie la kusema? Mnaona? Yabidikungoja. Hiyo ndiyo sababu nilisema, “Andika hilo, na hebu

16 LILE NENO LILILONENWA

nione alichosema.” Unaona? Ngoja. “Wao wamngojeao Bwanawatapata nguvu mpya.” Sivyo?82 Angalia, walimtaka tu shauri kuhani wa siku ile, nawatheologia, madhehebu. Na tazama, kwa kufanya hilo,kumtaka shauri kuhani na kulitaka shauri kusanyiko, kuwatakashauri watu, walilitenda vibaya.83 Angalia! Sanduku lile lilikuwa Neno. Twajua hilo nisahihi, kwa sababu sanduku lile ni Kristo, na Kristo niNeno. Waona? Sanduku lile au Neno halikuwekwa kwanzakatika mahali palipoamriwa, mahali pa asili palipoamriwa. Lo,msikose kuliona hili, Kanisa! Kila kitu kilikuwa kikamilifu,na kila kitu kilionekana kizuri, kama kwamba ufufuo mkuuulikuwa ukija; lakini kwa sababu walishindwa kumtakashauri mtu yule aliyefaa kuhusu hilo…Waliwataka shaurikuhani, waliwataka shauri watu mashuhuri, waliwataka shauriwatheologia, waliwataka shauri waimbaji na waliweka kila kitumahali pamoja katika nia moja, na utaratibu mkuu wa jeshi, napia ma—ma—majeshi ya taifa, kila kitu kilikuwa kikichukuanana kingine kwa ajili ya mkutano mkuu; lakini walishindwakumtaka shauri Mungu. Vivyo hivyo, Ahabu, hali kadhalika nawengine. Wakati wa jinsi gani.84 Sasa, usikose hili! Walishindwa kuipata, kwa sababuhawakutaka shauri. Na kwa kufanya hilo (angalia!), kwakumwendea kuhani, kwa kuwaendea wale wanatheologia, nakwa kuyaendea majeshi, na kutokumfikiria hata mjumbe waowaliyepelekewa na Mungu wa saa ile, Nathani, walilifanyavibaya. Walikwenda na kulichukua lile sanduku na kuliwekajuu ya gari jipya, wakaliweka juu ya gari jipya (au dhehebujipya litaanzishwa) na si katika njia iliyotolewa na Mungu, njiailiyochaguliwa kulichukua. Lilipaswa kubebwa kwa mabega yaWalawi. Lakini unaona, ukianza vibaya, utaendelea kukosea.85 Kama risasi inatakiwa ielekezwe kwenye shabaha, naweusogeze ghafula mtutu vibaya hapa kiasi cha moja juu ya elfumoja kwanza, kwenye yadi mia moja umeenda kombo inchi nneau tano. Ulianza vibaya. Ee, Mungu tusaidie kujua kitu hikikimeanza vibaya, mikutano hii mikuu ya wakati huu, kamainavyoitwa.86 Mungu hukutakwa shauri kuhusu hiyo.Makuhani namtuwakidini wanatakiwa shauri, madhehebu yalitakwa shauri. “Vema,mtakuwa na hili na lile? Naamini kama tungeweza kukusanyakila mtu pamoja…” Usiwakusanye watu pamoja! Chukua tuNeno la Mungu kuhusu hilo.87 Basi tunaona kwamba watendapo hilo, wanatenda nini?Huendelea mbele moja kwa moja na mipango yao ile ile ya kaleya kidini ambayo iko nje ya Neno la Mungu na mapenzi yaMungu. Kitu hicho kilikufa miaka mingi iliyopita, hayo mamboya kale yaliyokauka yamiakamingi iliyopita.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 17

88 Ilikwisha kauka katika siku zaBwanaYesu.Hawakujua hilo.Alisema, “Kama mngalimjua Musa, mngenijua Mimi, kwaniMusa alisema nitakuja.”

Walisema, “Baba zetuwalikulamana jangwani.”89 Alisema, “Wote wamekufa. Vipofu!” Aliwaita, Mafarisayo,viongozi wa dini. “Msiposadiki ya kuwa Mimi Ndiye, mtakufakatika dhambi zenu.” Lakini hawakufanya hivyo. Walikuwawameshika njia zao sana. Ilibidi wafanyewatakavyo.90 Hivyo ndivyo Daudi alivyotenda hilo. Alilitenda alivyotaka,kwa hiyo alisema tu, “Unajua nitafanya nini? Tunaendelea.”Alikuwa na ufunuo. “Tunaendelea sasa, kwa hiyo tutalifanyakatika njia mpya. Siku za miujiza zimepita, kwa hiyotutajitengenezea dhehebu jingine. Tutaunda gari jipya, nakuwaonyesha kitu kipya kilichoanzishwa.” Unabii wa uongojinsi gani. Yakulazimukurudia njiaMungu alivyosema litendwe.91 Waliliweka juu ya mabega ya Mlawi, na hiyo ilikuwa juu yamoyo. Sanduku lile, Neno, halipaswi libebwe juu ya dhehebujipya, juu ya nadharia za mtu fulani, lakini moyoni. Neno laMungu si la kushikwa-shikwa na madhehebu; lapaswa lishikwena moyo wa mtu ambapo Mungu aweza kuingia mle ndanina kujifunua Mwenyewe. Na kama akilifunua kulingana naNeno, ni Mungu. Kama siyo, si Mungu. Halafu basi, Neno lamajira hayo.

Hakika, Mfarisayo angesema, “Nani alituambia kwambahatuwezi kufanya hili na kufanya lile? Musa alitupa amri hizi.”Lakini Musa pia alisema…

Shetani alisema, “Naam, imeandikwa, atakuagiza…”92 “Na pia imeandikwa,” alisema Yesu.

Majira yale, wakati ule. “Kama mngelimjua Musa…Mnammoja awahukumuye, kama mngelimjua Musa, mngenijuaMimi,” alisema, “kwani Musa aliandika habari Zangu: ‘BwanaMungu wako atakuondokeshea Nabii miongoni mwa nduguzako; msikilizeni yeye.” Kama wangalimjua Musa wangalimjuaYeye.93 Sasa sikiliza. Usikose hili sasa. Unaona, kitu cha kwanzawalipomtaka shauri kuhani, walipowataka shauri watumashuhuri, wakawataka shauri wanajeshi, wakawatakashauri kusanyiko lote, majirani kukusanyika pamoja kwaajili ya mkutano huu mkuu ujao, walishindwa kufanya sahihi.Hawakumtaka shauriMungu, na kwakufanya hivyo, kutokurudinyuma na kuona ilikuwa ni wakati gani…94 Ee ndugu, sikiliza! Twaishi wakati gani? Ni wakatigani? Tunaishi katika saa ipi? Si wakati wa mambo hayaambayo wanazungumzia. Hilo limepita. Hukumu inakaribiasasa. Unaweza kuiona ikianza. Unakumbuka mwamba uleuliokuwa juu ya mlima ule? Saa ya hukumu! Unakumbuka ule

18 LILE NENO LILILONENWA

ufunuo au ono la Bibi-arusi? Hebu aendelee kupiga hatua sahihi.Usimwache apige hatua baya.95 Angalia, katika mabega ya kuhani. Na Daudi na makuhaniwote ambao hasa iliwapasa kujua vema zaidi, lakini ilikuwanini? Makuhani walipaswa kujua vema zaidi. Waandishi,wanatheologia iliwabidi wajue vema zaidi, kwa sababu Nenolilisema wasifanye hivyo.96 Na leo wanapotaka kusema, “Loo, Yesu Kristo si yeye yulejana, leo, na hata milele; hilo ni kuwasiliana kwa mawazo;hilo ni hili, lile au lile lingine,” wanashindwa kuona lile Nenolililoahidiwa. “Loo, Hilo lilikuwa la siku iliyopita.”

Daudi alisema, “Loo, vema, sasa ngoja kidogo. Juu yamabega ya—yamakuhani, hilo lilikuwa kule nyumawakatiMusaalipojitokeza. Hakika, sisi, tutaliweka juu ya gari jipya leo. Ninaufunuo wa hilo.”

Kuhani alisema, “Amina, Daudi.”Waona?97 Huku wameshawishiwa na halmashauri mpya ya ekumeniakwamba iliwapasa waunganike na kufanya hili hivi na vile,hilo ndilo lililosababisha makuhani kujikwaa. Hawakumtakashauri mtu anayefaa. Hawakulifanya sawa; kwa hivyo, waliingiamatatani! Ndio!98 Nasikitika katika mambo mengi leo…Wakati mwalimumkuu, mmoja wa Wapentekoste mashuhuri sana aliposimamambele ya kundi la dini hivi majuzi usiku huko Chicago…Nalitarajiwa kuwa namkutano ule pamoja naWafanyi Biashara,lakini niliwaza nitakuwa Afrika wakati ule; lakini nilirudi tusiku moja kabla haujaanza. Nao walimchagua Mpentekostemaarufu aliyejaa bongo, naye alisimama akawaambia kwambahuu mwenendo wa ekumenia ulikuwa kitu cha Mungu. Naalisema wote wanarudi; hata kanisa Katoliki litarudia haliyake ya awali, wote wakinena kwa lugha kwa udhihirisho nakadhalika. Na bila kujua kwamba huo nimtegowa ibilisi.99 Na mtu ambaye sikumjua…Wakati mwingine unapandambegu. Haujui litakalotendeka. Lakini rais wa WafanyiBiashara wa Injili Yote, mara tu msemaji yule mashuhurialipoketi; akasema, “Kwa kawaida sisemi mambo dhidi yawasemaji wetu, lakini hivyo sivyo Ndugu Branham alisemaingetendeka. Lakini alisema hilo litawaelekeza kwenye alamaya mnyama.”

Alisema, “Lakini Ndugu Branham hajui asemayo.” Akasema“Tuna—tunaamini anajua.”100 Na huko Chicago walisema ni wangapi hapa wangependamimi kuja kutoa maoni yangu juu ya hilo. Walianza kuliakwa furaha na kupaza sauti. Unaona, unapanda mbegu. Hujuilitakalotokea. Endelea tu kupanda Mbegu. Saa ile itakapowadiabaadhi yake…

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 19

101 Kama vile Thomas, alikuwa karibu mtu wa mwishokumuona Bwana, lakini ilikuwa lazima amuone ili amuamini.Waona? Walipoliona likitokea, loo, Thomas akaingia, lakinialikuwa amechelewa kidogo.102 Sasa, watakapoona mambo haya ambayo yametabiriwa nakusemwa BWANA ASEMA HIVI yakitokea, basi watasema,“Tupeni mafuta yenu kidogo.” Waona?103 Lakini sasa, angalia ushawishi. Wakati mwingine watumashuhuri hukutanika pamoja. Unawasikia wakisema bwanamkubwa Fulani na bwana mkubwa Fulani, bwana wetumkubwa…Usifanye hivyo kamwe. Hakuna watu wakubwamiongoni mwetu. Kuna mkubwa Mmoja tu, na huyo ni Mungu.Sisi ni ndugu na dada. Sijui kama umchungaji wa kanisa ambalolinawatuwatano, hilo halikufanyimdogo; hilo hukufanya ndugu(unaona?), kama unalitii Neno la Mungu. Sijali nini, jinsi gani,huwi mdogo. Mungu hana watoto wadogo na watoto wakubwa.Ana watoto tu, na wote ni hali moja.104 Angalia, MunguMwenyewe alishuka akaja kutokamajumbaya kifalme yenye Utukufu ya pembe za ndovu kuwammoja wetu.Basi ni nani aliye mkuu? Alichukua…Hakushuka kuja hapakuchukua namna ya kuhani, lakini mtumishi na kuosha udongoule ulewamfinyazi aliouumba,miguu yawanafunziWake katikaile…Sasa ni nani aliye mkuu?105 Lakini walishawishiwa, watu hawa walishawishiwa.Hawakuelewa.Walifikiri kitu kipya kitatokea (la), kitu ambachoMungu hakusema kingetokea. Walikiendea kwa njia baya.Ndivyo ilivyo shauku yote hii wakati ile—ilipoanza nyumakule miaka mingi iliyopita, kila dhehebu lilipaswa liwe namponyaji wa Kiungu; kila dhehebu lilipaswa liwe na hili, lileau lile lingine. Kila dhehebu lilipaswa liwe na Daudi mdogo.Kila moja lilipaswa liwe na hili, lile au lile lingine. Unaonalililotokea? Ilifanya kitu kile kile ilifanya hapa. Kitu kile kile.Ushawishi…106 Neno kwa majira yake, waliupuuza wakati walimokuwawakiishi.107 Angalia, mabega ya Walawi ndiyo njia ya awali ya Mungualiyoiandaa ya kufanya mambo haya. Beba sanduku hilo katikamabega ya Walawi. Kitu cho chote nje ya hilo kilikuwakinyume. Alichosema, hicho ndicho alichomaanisha. Munguhawezi kubadilika. Hiyo ndiyo sababu ya kukaa naNenoLake.108 Nina 1 Mambo ya Nyakati 15:15, kama unataka kuandikahilo. Angalia, sasa angalia, hapo katika kumfuata Mungu…Sasa, nataka wewe u—upate kuandika hili bongoni mwako.Kushika amri za Mungu, kufanya kitu cho chote sawa sawakwaMungu, kufanya—kumfanyia kazi kwa usahihi, kuna lazimatano, kumfanyia Mungu kazi kwa usahihi.

20 LILE NENO LILILONENWA

109 Sasa, Daudi alikuwa akimfanyia Mungu kazi. Alikuwaakifanya kila kitu alichojua kufanya, isipokuwa kumuachaMungu. Unaona? Alikuwa akifanya kitu ambacho kilikuwasahihi, kitu kizuri kwawatu, kitu kizuri kwa kanisa.110 Lakini kuna lazima tano; nawatakeni mkumbuke haya.Haidhuru mtu ni mwaminifu jinsi gani katika kufanya jambo,kumtendeaMungu kazi, hili—hizi tano lazima ziwepo:

Kwanza, lazima iwe ni wakatiWakewa kuitenda.111 Vipi kama—kama Musa angekuja kasema, “Tutakujakujenga safina na kuieleza juu ya Nile kamaNuhu alivyofanya?”Wakati wa Nuhu ulikuwa sawa kwa safina, lakini si wakatiwake.112 Vipi kama Yesu angekuja, kasema, “Sasa nitawaambiatutafanya nini. Tutapanda juu mlimani kama Musa alivyofanyana kupata tangazo jipya la sheria? Unaona? A, a! Yeye alikuwasheria ile. Unaona? Lazima wewe uwe katika wakati Wake.Lazima iwe katikamajira Yake. Umelipata hilo sasa?113 Sharti iwe katika wakati Wake Yeye. Lazima iwe katikamajira Yake, wakati na majira, na lazima iwe kulingana na NenoLake ambalo limenenwa. Lazima…114 Sijali unasema vema jinsi gani hili lapaswa kutokea, ama hililapaswa kutokea, au hili lapaswa kutokea, lazima liwe lalinganana Neno Lake, kulingana na wakati Wake na majira yake; na nilazima litolewe kulingana namtu yule aliyemchagua kulitenda.115 Sijali watu ni wakuu vipi. Hapo pana mfalme Daudi mkuukama ye yote wao. Alikuwa mfalme juu ya taifa lile. LakiniYeye alikuwa na njia ya kulifanya, naye alikwisha waambia jinsiambavyo angalitenda. Lakini walishindwa kulifanya.116 Lazima iwe ni kulingana naNeno Lake, kulingana nawakatiWake, kulingana na—mpango Wake; na sharti ifanywe na mtuyule aliyemchagua kulitoa na kulifanya.117 Musa alijaribu kuikimbia. “Chukua mtu mwingine!”Lakini Mungu alimchagua Musa kuifanya. Wengi wao…Pauloalijaribu kuiepa, wengine wengi. Lakini lazima ifanywe namtu yule amchaguaye kulitenda. Na lazima lije kwanza kwamanabii Wake. Neno la Mungu, halina budi kuwajilia manabiiWake, Amosi 3:7. “Bwana Mungu hatafanya neno lo lote mpakakwanza alifunue kwamtumishi wake nabii.” Nne.118 Naye nabii lazima athibitishwe naNeno laMungu.119 Lazima zako tano ndizo hizo. Lazima iwe hivyo; wakatiWake; majira Yake (wakati aliposema itakuwa); na mtu yulealiyemchagua, na lazima ije kwa nabii; na nabii yule lazimaawe nabii aliyethibitishwa. Tunaona wengi wao katika Bibliailiwajilia manabii nao hawakuthibitishwa. Nabii wetu ni YesuKristo.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 21

120 Kwa hiyo sasa angalia. Unaona, Mungu hakuwa amefunuakitu kile kwao kwa njia Yake aliyoiandaa ya kukifanya.Walikubali njia ya Daudi. Walikuwawamekubali njia ya kuhani.Walikuwa wamekubali njia ya waandishi, ya wanatheologia,lakini si njia ya Mungu. Nathanieli alikuwa—alikuwa nabii wasiku ile. Baadaye Nathanieli aliwaambia jinsi ya kulifanya.Lakini waona walilitenda bila ya kumtaka shauri Nathanieli.Hakuna neno lisemalo kwamba Nathanieli alitakwa shauri.Ushawishi wote ule, jambo lile kuu likiendelea…Na, jamani,naufikiria wimbo ule;

Hebu—niweke, nisaidie Bwana mioyoinapowaka moto,

Niache niyadhilishe majivuno (niende pamojana wengine wao) na kuliita tu Jina Lako;

Nifundishe kutotegemea yale wafanyayowengine,

Lakini ningojee tu katika maombi jibu tokaKwako.

Hivyo ndivyo ilivyo. Hebu nione likitokea katika njia sahihi,kisha linaaminiwa.121 Sasa, Mungu alifunua jambo lile kwao kwa Daudi, na kwawahudumu, na kwa watu, na kwa maakida wa maelfu, namaakida wa mamia, lakini sio kwa Nathanieli ambaye alikuwana BWANA ASEMA HIVI. Na Bwana alisema asingefanya lolote mpaka amuonyeshe kwanza nabii yule wa wakati ule lakufanya. Unaona walilotenda? Walitoka moja kwa moja katikaNeno la Mungu, walikwenda wakaliweka sanduku katika garijipya. Unaona? Kwa hivyo walikwenda kulitenda mbali na amriya njia ya Mungu aliyoiandaa…Na hilo ndilo limetokea leo,marafiki. Hiyo ndiyo sababu tumekuwa na mikutano mikubwasana na kadhalika na bila matokeo. Kumkana Mungu zaidi,dhambi zaidi, zaidi…Nakuambia, taifa hili limekwisha, si taifahili tu, lakini mataifa mengine. Taifa hili kama Uingereza yawakatimwingine limekuwa kahabawamataifamengine yote.122 Kule mbali katika Mozambiki, maili mia nne na themaninitoka kwenye ustaarabu, msituni, watoto walioharibikiwa naakili wanamsikiliza Elvis Presley, wakitikisa vichwa vyao nakurukaruka juu na chini hivyo wakikaa usiku kucha na kukaa—na redio dogo kama hivyo wanazilinganisha maelfu ya mailimpaka Rhodesia kupata Elvis Presley. Na bado wanasema, “Nimtu wa kidini sana, yeye, na Pat Boone na wengine.” Naam, niYudawawakati huu, na hawajui hilo. Na hiyo ndio sehemu baya.Wanaamini wako—wako sahihi. Yesu hakusema kwaWakati huuwa Kanisa la Laodikia, “Wewe u uchi, na mwenye mashaka, namnyonge, na kipofu, nawe hujui?” Hujui hilo!123 Vema, watoto wa Kipentekoste huko Afrika na mahalipengine wanasema, “Vema, Elvis Presley, hujawahi kusikia

22 LILE NENO LILILONENWA

kuimba kuzuri kamaKwake.” Hakuna shakaDaudi alifanya hilopia; hakuna shaka waimbaji walifanya hilo, lakini lilisababishakifo kuipiga kambi.Mnaonawalipo—tulipo leomarafiki?124 Mabega ya Walawi ilikuwa njia ya asili ya Mungu kufanyahilo, na walikuwa wameliweka juu ya gari jipya. Sasa,haitafanya kazi. Hawakutaka shauri ipasavyo. Unaona? Kwahiyo walitoka kwa ajili yake na kuliendea kwa njia iliyo makosa,na hivyo ndivyo imetendeka leo.125 Wakati watu, haidhuru u mwaminifu jinsi gani,wanapojaribu kumfanyia kazi Yeye nje ya njia yake aliyoiandaaya kufunua, siku zote wanaivuruga. Mungu huliweka katika njiaYake. Mwanadamu, haidhuru u mwaminifu jinsi gani kujaribukulifanya nje ya hiyo, u—utalivuruga.126 Kitu kama Baalamu alivyokuwa katika siku za Baalamu.Mungu alimwambia Baalamu, nabii yule…Alikuwa nabii,nabii Baalamu. Alikuwa nabii, na lile Neno lilimjia sawa kabisa,kasema, “Usiende huko. Hao ni wateule Wangu; hao ni chaguoLangu.”

Kisha Baalamu aliambatana na watu mashuhuri, nawanajeshi, wahubiri, watu walioshawishiwa, na akasema,“Vema, na—nawaambieni, mfalme ata…” Unaona, inafanananaDaudi, inafanana na siku hizi, chukua kila kitu tu kwamfano,na utaliona. Ukiliona sema, “Amina!” [Kusanyika linasema,“Amina!”—Mh.] Unaona, unaona? Kama tu ilivyo sasa.127 Lakini wale—wale—wale makasisi walisema, wale—wale—wale—wale—wale makuhani walisema, waandishi walisema,wanatheologia walisema, “Hivi ndivyo inavyopaswa kutendwa.”Lakini haikuwa hivyo! Na ilidhihirisha haikuwa hivyo.128 Kisha Mungu akamwambia Baalamu—kwa maana alikuwanabii kwanza—alimwambia, “Usiende huko!”129 Lakini ushawishi wa hawa watu wengine ulimfanyakulifanya kinyume cha vile Mungu alisema lifanywe, halafuilikuwa laana badala ya ufufuo. Loo, hakika, alishukaakaenda kule akawafundisha watu, akisema, “Sasa tazama!Ngoja! Mwajua nini?” Kasema; “Sisi ni—sisi ni Wamoabu.Mnakumbuka, binti wa Lutu ni malkia wetu. Ndiye chanzochetu. Wote tu wa damu moja. Wote tu…Sisi madhehebu yoteni kitu kile kile.” Usichanganyikane na kitu hicho. Usikikaribie.Unaona? Kwa hiyo alisema, “Sote tu kitu kile kile. Naam, watuwenu ni kama watu wangu. Twaweza kuoana miongoni mwetu,tupate kuwa na halmashauri ya ekumeni hasa. Unaona? Sisi sotetwaweza kukusanyika na kurudia kile kitu cha asili tena.” NaMungu akalaani kitu kile. Dhambi ile kamwe haikusamehewaIsraeli. Ilikaa nao siku zao zilizobakia. Na haikusamehewakamwe. Waliangamia jangwani nayo (hiyo ni kweli!), kwa kuwahawakuchukua njia iliyoandaliwa na Mungu kwa njia Yakeiliyodhihirishwa ya kulifanya.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 23

130 Angalia, kitu hiki ambacho walifanya kilisababisha Israelikufa kifo huko jangwani, na Yesu alisema, “Kila mmoja waoameangamia na kutoweka.” Angalia ni nani aliyesimama naMusa nyuma kule Yoshua naKalebu na ule—na ulempango.

131 Angalia tena, hapa pana Daudi, alichotenda. Na alipofanyahivyo, nini ilitendeka? Ilisababisha kifo kimpige mtumwaminifu. Na nadhani bado tumeunganishwa kwa radio,nami nawatakeni ninyi msikie nchini kote. Kitu hiki Daudialichofanya bila ya kumtaka shauri Nathanieli na kupataNeno la Bwana kwa ajili ya hilo, kilisababisha kifo kiwapigewatu waaminifu. Naam, hapo aliunyosha mkono wake, ambaoulikuwa ukikaa kwenye uwepo wa lile sanduku, ulitokakwenye—kwenye nyumba yake. Na maksai akakunguwaa, nasanduku lilikuwa likianguka.

132 Walikuwa wamekwisha tenda kitu kimoja kisicho sahihi,mambo mawili yasiyo sahihi. Kwanza, hawakumtaka shauriNathanieli. Jambo jingine walilofanya walikwenda huko bilakuliangalia Neno la Mungu ambalo lile—Samuel alikuwa Nenokatika siku ile. Nao kamwe hawakuliangalia Neno la Bwana,basi walipotenda, walikwenda kinyume na Neno la Mungu. Nahapa mtu huyu mzuri, ambaye alikuwa muangalizi—alikuwaaskofu—alifikiria, “Vema hapa, sitaki Mungu aaibishwe.” Kwahiyo akaweka mkono wake juu ya sanduku, ambapo yeyehakuwaMlawi, naye akafa—mambomatatu.

133 Sasa fikiria sana na tazama ambacho madhehebuwamefanya leo. Unaona? Wamelikataa, wameliita mafundishoya uongo. Unaona? Angalia walipo. Watakuwa na halmashauriyao ya ekumeni haidhuru. Wameliita uwezo wa kupitishianamawazo kiakili. Wakati Mungu Mwenyewe analithibitishakuwa Ukweli na kuhakikisha ni Kweli. “Loo, wao ni kikundikidogo tu cha watu wasio na akili kule,” wao husema; “hawajuiwanachonena.” Hilo ni sahihi; hatujui. Lakini twanena manenoYake tu, naye anajua analosema. Unaona? Siwezi kuelezea hilo,hakuna anayeweza, lakini Yeye—Yeye—Yeye hulidhibitisha.

134 Sasa angalia. Mara nyingi mwaminio wa kweli ajaye kwaKristo, anataka kuja kwa moyo wake wote, huuawa kirohonamna ile ile. Watu wengi waaminifu huenda kwenye kanisaKatoliki wakitaka wawe Wakristo, huenda kwa Wamethodisti,Wabatisti, Church of Christ, na hata Wapentekoste (unaona),na wanataka kuwa Wakristo, anaweka mkono wake juu yake,anajiunga nao.

135 Naye Daudi alipoona jambo hili likitokea, lilimwamsha.Usiamke huku umechelewa sana huko, ndugu. Aliona kwambamauti yamewapiga. Nionyeshe matokeo. Kwa nini huu uitwaoufufuo kuwarudisha makanisani umefanya katika taifa kwawale—kwa kundi la waamini? Si kitu ila umetengeneza taratibu

24 LILE NENO LILILONENWA

mpya na madhehehebu wakati huu wote, wanachama zaidi nakadhalika. Taifa limekuwa na hali nzuri zaidi?

136 Walisema walikuwa wakienda…Marekani—“Munguaibariki Marekani, ni—ni taifa, ni nchi ya Kikristo.” Iko umbaliwa maili milioni moja kutoka kwa nchi ya Kikristo! Walahata siiombei. Nawezaje kuiombea, nayo haitatubu chini yanguvu kuu za Mungu zilizoonyeshwa mbele yake, na kukana,na kufungia milango na kuzipa kisogo? Naikabidhi kwaMungu. Na linaenda mbali zaidi, na sasa litazama. Tazamatu yatakayotendeka.

137 Watu wengi waaminifu huenda kujiunga na dhehebu aukundi fulani au kikundi kilichojitenga cha namna fulani, nahapo hufa kiroho. Huwezi kuwaambia kitu. Wanashindiliwatakataka hizo: “Naam, maaskofu hawa walisema hili, na huyualisema hili; huyu alisema hili.”Unawaonyesha papa hapa katikaNeno la Mungu ambapo ni BWANA ASEMA HIVI, “Lakinimchungaji wetu…” Sijali mchungaji wenu anasema nini, sijalinisemalo, aumtumwingine asemalo. Kama ni kinyume chaNenola Mungu lililothibitishwa, la saa hiyo, wakati huo, Ujumbe ule,na kadhalika, lisahau! Kaa mbali nalo. Na yanipasa nisimamembele ya kila mmoja wenu katika siku ya hukumu, nanyimwajua hilo. Na singethubutu kusema hilo, nikijuamimi nimzeesasa. Nita…Si kwamba najua kitu, lakini Yeye anajua. Nafuatatu yale aliyosema.

138 Angalia leo ile mikutano mikubwa tumekuwa nayo nchinimwote, imethibitisha kwamba imekuwa bure. Na je, Yesuhakusema hapa sasa, Luka 7:7, “Nao waniabudu bure. (Daudialilipandisha sanduku bure, Ahabu aliwafunza hao manabiibure. Baalamu alichukua fedha ile bure!) wakifundishamafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu”? Maagizo ya Mungundiyo jambomuhimu. Haidhuru jinsi gani…

139 “Hao watu ni waaminifu kwelikweli.” Unasikia hilo sana.“Ni waaminifu sana.” Vema, hilo halimaanishi kitu. Shahidiwa Yehova, Seventh Day Adventist, na vikundi hivyo vyotevilivyojitenga wanakuja barabarani hapa na kutenda mamboambayo mmoja wetu asingalitenda. Wakatoliki wanasimamapembeni na kuomba na kadhalika, na vyama hivyo vyake,vyenye mabilioni mara bilioni mara bilioni ya dola, badowanaziomba. Waaminifu, bila shaka. Makanisa yanakwendana—na kuhubiri na kadhalika, na wahudumu wanasimamamimbarani na kufanya kila kitu wanachoweza kufanya kuingizawanachama wapya katika kanisa lao; lakini ni sanduku jipya.Kuna Sanduku moja tu la kufuata; hilo ni Neno la Mungu. Kitucho chote dhidi ya Sanduku hiyo, kaa mbali nacho; kiko juu yagari jipya na si katika mabega ya Mungu. Hilo ni sawa. Kaambali na kitu kile. Usijishughulishe nacho kamwe.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 25

140 Mikutano yetu mikubwa, mabilioni na mamilioniwameungama. Nami nashangaa kama kutakuwepo mia mojawao toka kwa hiyo yote. Unaona? Haimaanishi kitu. Kishaangalia ahadi ya Neno.141 Utafikiria kwamba hiyo imeshindwa, na tunajuaimeshindwa. Baadhi ya wa—wanaufufuo wetu mashuhuri sananchini leo husema kwamba hiyo imeshindwa kabisa. Kanisalinajua imeshindwa. Kila mtu anajua imeshindwa. Vema, nikwa nini? Kwa nini ikashindwa? Ni kwa ajili ya kusudi jema;ilikuwa ilete watu kwenye uwepo wa Mungu, mikutano mikuu.Na mamilioni ya watu wametumia fedha zao na kuziwekakatika mikutano mikuu, na makanisa yote yakaungana pamoja,majumba makubwa ya mikutano, na mambo makuu, na mambomakuu yaliyofanyika; Kwa nini imeshindwa? Ilikuwa kwasababu hawakujua kamwe saa ile waliyokuwa wanaishi. Siajabu Yesu alisimama, na katika moyo Wake akalia; machoziyakimtiririkia mashavuni Mwake, naye alisema, “Yerusalemu,Ee Yerusalemu, mara ngapi nimetaka kuwakusanya kama vilekuku avikusanyavyo vifaranga vyake. Umempiga mawe kilanabii niliyempeleka kwako. Lakini hukutaka. Lakini sasa saayako imefika.”142 Je, huwezi kuhisi Roho Mtakatifu akilia akitoka ndani yako?“Ee, Marekani na ulimwengu, mara ngapi ningewakusanya,lakini hamkutaka. Sasa, saa yako imekuja. Mungu wenu waanasa, Mungu wenu wa uchafu, mungu wako wa Sodoma naGomora, ambaye amekuja miongoni mwenu…” Hata watotowetu, wadogo, walio na nywele zilizonyolewa kama za beatlena kukatwa kukingama nyuso zao, mambo madogomadogoya kupotosha yakianza. Wanawake wetu wamekwisha!Hawakomboleki. Wanaume wetu wamekuwa majike wakubwa,wakienda wamevaa kaptura wakijifanya kama msichana, nanywele zikining’inia shingoni, na…Tumekuwa Walawiti, namoto na hasira ya Mungu watungojea.143 Unajua jinsi atakavyoua, jinsi atakavyouharibu? Jinsiafanyavyo siku zote. Kahaba alipotenda kitu cho chotekisicho sahihi, aliuwawa kwa kupigwa mawe. Waliokotamawe kumuuwa mwanamke aliyekuwa kahaba. Hivyo ndivyoatakavyoliuwa kanisa. Biblia ilisema atanyesha mvua ya mawetoka mbinguni, yatakuwa na uzito wa ratili mia moja kilamoja, naye atawapiga kwa mawe. Nani atamzuia? Sayansi ganiitakayosema haiwezekani? Atalifanya vile vile alivyotengenezasafina na akamweleza Nuhu kwenye usalama; atafanya hilotena kwa Kanisa Lake. Na kwa sheria Zake, na kwa njia Yake,atampiga kwa mawe kahaba yule ambaye ametenda uzinzina wafalme na maakida wa mamia na maelfu. Atamuua kwakumpiga mawe kwa sheria Zake mwenyewe ambazo amewekakatika utaratibu. Nani atamwambia Yeye hawezi kutengenezamvua ya mawe?

26 LILE NENO LILILONENWA

144 Uliza mtu ajuaye jinsi tone la mvua linavyoanza, na duarana kurudi katika…?…na kukusanya zaidi na zaidi na zaidihadi linafikia uzito fulani, kisha linaanguka. Yeye, ni Munguambaye nguvu za uvutano hata hazikuweza kumshikilia dunianina akainuliwaMbinguni, Mungu, ambaye alitengeneza nguvu yauvutano, pia anaweza kutengeneza…?…kubwa vya kutoshakuning’iniza jiwe mpaka liwe na uzito wa ratili mia. Alisemaatafanya hivyo, na atalifanya. Nani atamwambia asilifanye?Atalifanya kwa sababu alisema angelitenda.145 Tuko katika siku za mwisho. Tunasimama karibu nahukumu. Kwa sababu gani? Wanajaribu kula mana ya kaleambayo ilianguka nyuma kule miaka hamsini iliyopita, kanisa laKipentekoste. Kanisa la Holiness linajaribu ku—zaidi ya miakamia mbili iliyopita, Waluteri kama miaka mia tatu au zaidiiliyopita, mamia ya miaka iliyopita. Wanajaribu kula mana yakale, Ee, ndugu, kitu hicho kimeharibika. Kimechafuka. Kita…Kina—Kina—siku zote nimesema —wadudu ndani yake, mabuu.Kitakuuwa ukila.146 Chunguza kama Daudi au kama ye yote wa wale wenginelaiti angetaka shauri toka kwa Mkate wa saa hiyo. Laitimakuhani, na manabii, na wahubiri, na wanatheologia, na vyuo,na madhehebu wangeangalia ule wakati, lakini sasa haitawafaakitu. Umekwisha sogea. Haitasaidia hata, chembe. Limekwishasasa. Limevuka mstari huo kama miaka mitano iliyopita, kati yatoba, hukumu, na rehema.147 Angalia, kuna nini sasa? Ifanyweje? Tutafanya nini? Hebutumtake shauri nabii, Biblia, ambapo hatuwezi kuongeza aukupunguza. Kama tukifanya hivyo, Mungu atatuondoa katikaKitabu cha Uzima. Biblia ilisema katika Malaki 4 jambo ganilingeteneka leo, Ufunuo 10, jinsi zileMuhuri Saba zingefunuliwana kufunua siri hizi zote ambazo zilikuwa zimefichwa katikahawa watengenezaji. Alisema jinsi litakavyotendeka. Limokatika Biblia, BWANA ASEMA HIVI. Mungu amethibitishahilo kabisa na kwa ukamilifu na kulihakikisha kuwa Kwelikwa ishara, maajabu mbinguni na angani, na kila kitu kinginekwa miaka thelathini na mitatu. Unafikiri watalisikiliza? La,wamekufa.Wameuwekamkonowao juu ya jambo ambalo limeuakitu hicho chote. La, haiwezekani—haiwezekani, kamwe tena.148 Ilikuwa wakati kitu hiki kilipotokea ndipo Daudiakaona. Ee, Mungu, tupelekee Daudi ambaye anaweza kuonaanaposimama, ambaye aweza kuangalia na kuona Mungualifanya ahadi ambayo—jinsi angetenda leo. Mungu amelinenapapa hapa katika Neno Lake jinsi angelitenda.149 Mungu alimwambia Mikaya; Mikaya alichunguza ono lakembele ya manabii mia nne mashuhuri. Alichunguza ono lake,kuona kama kwamba ni sahihi. Aliangalia kule nyuma kwa yalenabii aliyemtangulia alisema kuona kilichotokea. Alitazama

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 27

nyuma, naye akaona kwamba Eliya aliposimama pale, alisema,“Ahabu, mbwa wataramba damu yako pia.” Sasa, aliona basikwamba ono lile lililingana kabisa na Neno la Mungu, kwahivyo akalitamka; naye alikuwa sahihi. Hilo ni sawa. Haidhuruwengine waowalisema nini, alidumu naNeno lile.150 Sasa, hebu na tuangalie lile ono tulilo nalo leo hii. Je, nikujenga makanisa? Ni kujenga vitu vipya? Ni mambo makubwayatakayotendeka, au ni hukumu? Tazama nyuma uone ahadi yaleo. Ona majira tunayoishi.151 Wasema, “Mungu na abarikiwe, ndugu, mimi ni mwaminifu.Najiunga na kanisa. Nina shahada yangu ya sanaa. Nimefanyahili.” Hivyo ni sawa. Hivyo ni vyema; silipingi kamwe.Daudi alikuwa nayo pia; na makuhani wa siku zile pia, nawanatheologia pia; lakini ilikuwa dhidi ya Neno.152 Mungu alisema jinsi atalitenda leo, jinsi angerudishamambo yote, lile ambalo angetenda tena. Aliahidi kurudisha.Hilo ni kweli kabisa. Katika Yoeli 2:28 aliahidi kurudisha:“Nitawarudishieni, asema Bwana, hiyo miaka iliyoliwa naparare.” Wana…Waona, huyo ni mdudu yule yule. Yukokatika hatua tofauti ya uhai. Na Ukatoliki ulipoanza kula,kisha Ulutheri, Wamethodisti na Wapentekoste na wote, chini,alisema, “Nitarudisha kila kitu Kanisani vile vile hasa lilelilivyokuwa hapo awali.”153 Tazama ono lile hivi majuzi. Bibi-arusi yule yule hasaaliyekuja upande huu ndiye aliyekuja upande huu. Baadaya kahaba yule kupita wamevaa majoho yao, vitu vyaovidogovidogo vya kale vikiwa tu upande huu, na wakichezarumba na wakijiita kanisa. Wasema, “Vema, sisi hatufanyi hilo.”Hivyo ndivyo Mungu anavyowaona. Si vile unavyojiona wewemwenyewe; ni vile Mungu akuonavyo. Hakuna mtu anayejionamwenyewe anakosea. Ni wakati unapotazama katika kioo chaNeno laMungu, linakuambia kama unakosea au la. KamaDaudiangalitenda hilo, angaliona alikuwa amekosea. Kama Ahabuangelitenda hilo, au hao manabii wangetenda hilo, wangejionawako makosani.154 Nabii aliyethibitishwa alisema Ahabu atakufa na mbwawatairamba damu yake. Na unabii wake ulipatana nalo. Basialijua yuko sahihi. Hata Jehoshafati ilimpasa alione hilo nakulijua.Mikaya alipoona ono lile, hakuwa sana pamoja nawale—na haowatu katika siku hizo, lakini alikuwa naBWANAASEMAHIVI. Ilikuwa sahihi.155 Angalia, twaleta jambo hili sasa katika siku hii tunapoonasaa ile kuu ambayo tunaijia. Angalia ambalo Daudi alikuwaakijaribu kufanya pia. Nalikuwa na maadishi madogo hapa juuya hilo. Alikuwa akijaribu kuleta lile sanduku kwenye mji waDaudi; dhehebu lake mwenyewe.

28 LILE NENO LILILONENWA

156 Angalia nyuma kule wakati Bwana kwanza alinena kulemtoni: “Kama Yohana Mbatizaji alivyopelekwa kutangulia kujakwa kwanza…”Ndugu,Waasembly hawangevumilia hilo, walaWa-United, hao wote. Iliwalazimu wawe na mtu mahali fulani.Lo, iliwapasa wote kulitenda. Unaona? Vivyo hivyo hasa. Woteiliwalazimu walilete nyumbani kwao.157 Walitaka kulileta kwenye mji wa Daudi. Kwa sababu gani?Hapakuwepo na mahali palipokuwa tayari kwa ajili yake.Na hiyo ndiyo sababu huwezi kuuleta Ujumbe kwa dhehebu.Neno; Sanduku; Kristo, yeye yule jana, leo, na hata milele;na kufahamika Kwake kwote; huwezi kulileta kwenye dhehebulako. Hawataliamini kamwe, kwa sababu hakuna nafasi kwaajili Yake. Si Biblia husema kwamba alikuwa nje ya kanisala wakati wa Laodekia akijaribu kuingia ndani? Hapakuwana nafasi katika mji wa Daudi, haidhuru ulikuwa mwaminifujinsi gani, na jinsi ulivyokuwa mkuu, na—na kadhalika.Bado hapakuwa na nafasi; ilikuwa iwe Yerusalemu. Hukondiko ambako lilikwenda baadaye wakati nabii alipowaambiawafanye nini na hilo sanduku. Unaona? Kwa hiyo ilimbidiDaudi kulilete katika mji wake mwenyewe. Halikuwa na mahalipalipokuwa tayari.158 Kristo ndiye Sanduku letu, nao hawatampokea. Kristondiye Neno. Hawatalipokea. Wanapenda kanuni zao za imani,dhehebu lao, sanduku jipya, au—au—au gari jipya. Wanatakadhehebu lilibebe, sanduku jipya. Kumbuka Kristo ndiyeSanduku letu. Unaamini Kristo ni Neno? Hilo ndilo lile Sandukubasi. Sivyo? Sawa. Kristo hawezi kubebwa kupelekwa mahaliPake panapofaa na gari lo lote la kidhehebu. Yeye hushughulikiamtu mmoja na si kundi. Hajawahi kushughulika na kundikamwe; mtu mmoja. Wakati Yeye…?…Kama angefanya hivyo,Yu kinyume cha Neno Lake, Amos 3:7. Nawe huwezi kulifanyaliseme uongo. La, bwana! Ni—ni kweli.159 Lakini waona, walijaribu…Sanduku haliwezi kubebwana dhehebu; kuna viongozi wengi sana ndani yake. Unaona?Haiwezekani. Aliahidi hatatenda hilo, naye hatatenda. Yeye—Yeye alisema, wakati alipoahidi—wakati aliahidi kulitenda kwanjia nyingine, hiyo ndiyo sababu aliahidi hatalifanya. (Msiwaziehayo mawazo. Naweza kuyahisi. Mnaona?)160 Kwa hiyo Yeye—Yeye aliahidi angelitenda kwa njia fulanina kila kitu kinyume cha hiyo hatakifanya. Unaona? Lakinikwa njia Yake ya awali kulingana na alilosema katika Amos3:7, hivyo ndivyo atalitenda. Na hilo lazima lithibitishwena kuhakikishwa kuwa sahihi. Sasa, unajua nini alichoahidileo, basi anakifanya hicho leo. Hicho ndicho tu alichosemaatatenda: angefungua zile Muhuri Saba na yote ambayoangefanya; kufunua siri nyuma kule, jinsi ambavyo ubatizohuu na kadhalika ulivyokuwa umevurugwa. Na ndiyo hayahapa katika uwepo Wake hasa. Sayansi imelihakikisha. Mbingu

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 29

zimelitangaza. Binadamu amesimama, akiliangalia vizuri nakuona likitendeka. Na hamna hata jambo moja limenenwaasilolifanya kweli. Naambasi. Ili tu upate kuona tulipo leo.161 Sasa, mtu ye yote aliye na roho zake anajua—ana Roho waMungu juu yake, anajua huu ni Ukweli; kwa sababu Roho waMungu hatanena kinyume cha Neno. Loo la, itapatana kabisana Neno. Unasema, “Ninaye Roho Mtakatifu. Nilipaza sauti;nilinena kwa lugha. Nilicheza katika Roho.” Hilo halimaanishikitu kwa Mungu. Unaona? Daudi alifanya kitu hicho hicho—kwa kweli jambo lilo hilo nyuma kule. Waliimba kwa nguvuzake zote, naye akapaza sauti kwa nguvu zake zote; wotewaliosalia walifanya hivyo, nao wanatembea moja kwa mojakuelekea mautini: Hilo ni kweli! Hilo halihusiani nalo; Nenondilo jambo muhimu, Neno la Bwana. Wale wamngojeao Bwana.Ndiyo, bwana.162 Unaona, wao ambao wana Roho wa Mungu ndani yaohuitazama ahadi ya siku ya leo, na kukesha, na kungojea mpakawaione, kishawanasema, “Ndiyo hiyo.”Mungu huwafunulia.163 Kama Nathanieli. Filipo alikwenda akampata Nathanieli,naye Nathanieli akasema, “Sasa, ngoja kidogo najua hilolimeahidiwa, lakini hebu nilione.” Naye alipoliona, akasema,“Ndilo hilo.”

Yule mwanamke alisema, “Sasa, najua, nimewasikizawanatheologia wa kila namna, nimetenda hili na lile. Nanimesoma Biblia mimi mwenyewe, na najua kwamba tuna—kuna Masihi ajaye ambaye atafanya mambo haya, kwa hiyohuna budi kuwa nabii Wake.”

Akasema, “Mimi ndiye.”164 Alisema “Njoni, mmwone Mtu, hili ndilo.” Alingojea mpakaalipomwona Masihi huyo akitambulishwa na Neno la Mungu.Kisha akasema, “Huyo ndiye tumemngoja miaka mia nne.Hatujawa na nabii au cho chote. Yuko hapa, na Yeye Mwenyeweanasema kwamba Yeye ndiye. Sasa…[Sehemu tupu katikaukanda—Mh.] Njoni mmwone Mtu ambaye ameniambia mamboyale niliyotenda.” Lakini makuhani walitaka kumuua, namwishowe walilitenda. Unaona? Lakini hawawezi kuua RohoWake leo. Hiyo ni kweli! La, hawawezi kumuua. Alikuwepo hapakutuleta Kwake, kwa hiyo tunashukuru.165 Angalia jinsi Mungu alivyo mkuu, jinsi kazi Zake zilivyokuu. Jinsi asivyoweza kushindwa kamwe. Sasa, Mungu ana njiailiyoandaliwa na ya asili ya kufanya mambo, naye hatatendakinyume cha hiyo.166 Sasa, aliahidi katika siku za mwisho kile ambachoangetenda. Na aliwapelekea—sisi Ujumbe, na Ujumbe huuungekuwa na utambulisho ule ule aliokuwa nao kama uliokuwana Eliya, kama uliokuwa na Elisha, kama ulivyokuwa na YohanaMbatizaji. Na utageuza mioyo ya watu, si kuelekea dhehebu,

30 LILE NENO LILILONENWA

lakini kuelekea kwa wale baba wa asili na wa kimitume,kurudi kwenye Neno. Jinsi mambo haya yalivyothibitishwa.Jinsi katika kutolewa kwa sauti ya malaika wa mwisho,Ufunuo 10: Katika siku za malaika wa saba siri hizi zoteambazo…Kwa nini Wamethodisti walifanya hili, na Wabatisti,na Church of Christ, na Mashahidi wa Yehova, wote hufanyahilo? Hizo siri zitafunuliwa katika siku za mwisho wakatiwale malaika saba—Ujumbe wa malaika wa saba, wakatiyeye, si wakati atakapoanza kufanya hili, lakini atakapoanzakutangaza Ujumbe wake. Unaona? Si miaka ile ya maandalizi,lakini ule—wakati atakapoanza kutangaza Ujumbe, siri hizibasi zitafunuliwa. Na ndizo hizi hapa, bila kuzijua, naninyi watu ni shahidi wa hilo. Na kisha katika kituo kilecha kuchunguzia anga—ili ulimwengu usitilie shaka—badowanashangaa kumetokea nini.167 Huko Tucson hivyo vituo vikubwa vya kuchunguzia angawalichukua picha yake kule juu, bado wangali wakishangaa niniilitendeka. Ni nini? Bado wangali wanayaandika magazetini,“Kuna mtu ye yote anayejua cho chote kuihusu? Nini, jinsiilivyotendeka?” Hakuna ukungu huko juu; hakuna hewa,hakuna unyevu, maili thelathini juu angani. Loo, jamani!“Kutakuwa na ishara katika mbingu juu. Na mambo hayayatakapotendeka, matetemeko ya nchi mahali mahali, ndipoitakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni.”Siku hiyo (Luka) Mwana wa Adamu atajifunua tena, na aweamefunuliwa Mwenyewe. Na ulimwengu utaonekana kamaSodoma na Gomora. Loo, jamani, ndugu, msiwe wajinga wamambo ya kiroho. Mnaona? Yachunguzeni Maandiko kwanikatika hayo mnafikiri—mna uzima wa Milele, na hayo ndiyoyanayoshuhudia Neno. Hayo ndiyo yanayoishuhudia ile Kweli,mambo ambayoMungu anatenda katika saa hii.168 Na sasa, angalia! Hao walio na Roho wa Mungu hungojeamambo haya. Na wanapoona mambo hayo, huamini mambohayo. Yesu alisema, “Hakuna mtu awezaye kuja kwanguasipovutwa na Baba Yangu, na wote alionipa Baba (Yeye niNeno), watakuja Kwangu—watakuja Kwangu.”169 Nimekuwa mkali sana asubuhi hii. Unoana? WanamngojeaBwana, kungojea; na wangojeapo, huona ahadi ile ya siku yaleo ikithibitishwa, huifanya upya imani yao katika Neno Lake,sababu aliahidi kulifanya, na yuko hapa akilitekeleza. Basihakuna shaka.Mungu hunena; NenoLake kwanza hunena, kishaRoho yule anayelileta anatenda kitu kile ambacho Neno lilisemaangetenda. Loo, tuna maigizo mengi sana. Bado tutakuwa nayomengi, mtu mwenye moyo mwaminifu akijaribu kufanya jambonjia hii na njia ile, lakini angalia kilichotokea. Watu watawekamikono yao, na kisha—kisha wafe. Unaona?170 Angalia, hakuna mipango ya binadamu ya kidhehebuitakayotenda kazi. Wakijitengenezea wanachama kwa sanduku

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 31

lao la madhehebu walilojitengenezea…Mungu kamwe hajawana dhehebu. Kamwe hatakuwa na dhehebu. Na ni kitukilichotengenezwa na binadamu.171 Nami leo nashangaa kama katika kuwavuta kwetu kote namikutano mikubwa na ufufuo mwingi, kama hatukuwa tukijazasanduku la Kimethodisti, sanduku la Kibatisti, sandukuKipresbeiteria. Vipi Sanduku la Kristo Neno? Na kama Bibi-arusi anapaswa kuwa Neno, basi yampasa—na kuwa wa Kristo,sehemu ya Bwana Arusi, yampasa awe Neno, Neno si kwasiku Yake, Neno la siku hii ambalo aliahidi litatimia siku hii.Alisema amepeleka Neno Lake kumfinyanga Bibi-arusi Wakena kumtengeneza. Natumaini tunaliona. Usiweke mawazo yakomwenyewe sasa, na usichukue wazo la mtu mwingine. ChukuaNeno lililothibitishwa hapa, Biblia. Linasema…172 Mungu ameahidi katika Neno Lake jinsi ambavyoangechagua Bibi-arusi Wake katika siku ya mwisho. Ulijuahilo? Aliliahidi, jinsi ambavyo angelifanya, na hilo kwa mpangoWake wa awali wa kumchagua Kristo, wa kuchagua wakati,kuchagua majira jinsi yeye…Hawezi kulikosa katika Bibi-arusi Wake, kwa sababu Yeye ni sehemu ya Neno lile. Hawezikulichagua kwa dhehebu na huku hakumchagua Kristo kwadhehebu. Kristo alikuja kupitia dhehebu? Alilijilia dhehebu?La! Walimkataa. Vema, hicho ndicho madhehebu yalifanyabasi; ndipo amchaguapo Bibi-arusi, anaweza kuja kwa njianyingine? Alimletaje Kristo hapa? Kwa Neno la manabii. Sivyo?Angeleta Bibi-arusi Wake hapa jinsi gani? KwaNeno la manabii.Alimtambulishaje alipokuja? Kwa mtu aliyekuwa na roho yaEliya juu yake akitokea jangwani. Atamtambulishaje Bibi-arusiWake? Aliahidi katika Malaki 4 kitu kile kile kabla ya kuiharibudunia kama ilivyokuwa katika siku za Sodoma.173 Kumbuka, Sodoma iliteketazwa. Hili ni kweli? Vema, duniahii itateketezwa. Yesu alisema hivyo. Na itakuwa wakatiambao—kama Luka sura ya 17 na mstari wa 30 ilivyosema:Katika siku zile itakuwa kama Sodoma na Gomora, kishaMwana wa Adamu atafunuliwa. Na basi nini kingetokea?Kulingana na Malaki, ataiteketeza dunia tena, nao wenye hakikatika ule Utawala wa miaka Elfu watatembea katika majivu yawaovu. Sivyo? Unaona? Kwa hiyo tuko katika wakati wamwishokabisa. Tumeketi hapamlangoni sasa tukimngojea aje.174 Angalia, Mungu aliahidi katika Neno Lake kwambaatachaguaBibi-arusiWake kwa njia yake ya awali aliyomchaguaBwa—Bwana Arusi Wake. Alilitabiri kwamanabii na akamtumanabii kumtambulisha. Nabii alisema akiketi katika kingo zaYordani, “Tazama!”

Walisema, “Wewe ni Masihi, sivyo?”Alisema, “La, mimi siye Masihi.”“Hunabudi kuwaMasihi yule.”

32 LILE NENO LILILONENWA

175 “Lakini Mimi siye, lakini anasimama kati yenu. Naviatu Vyake, sistahili kuvifungua. Ajapo, hujitambulishaMwenyewe…” Na leo anasimama kati yenu katika Umbola Roho Mtakatifu, akijidhihirisha Mwenyewe zaidi na zaidi,akija katika Kanisa Lake, akijijulisha Mwenyewe; kwa sababuYeye na Bibi-arusi, na Bwana Arusi, watakuwa kitu Kimoja,akijijulisha Mwenyewe: Na siku moja utaona ya kwamba yuleambaye ulimhisi moyoni mwako na kuona utambulisho Wake,atafanyika mwili mbele yako. Kisha wewe na Yeye ni Mmoja.Na mmeunganishwa na Neno, kisha Neno lililokuwako hapomwanzo litarudi mwanzo ambaye ni Mungu. “Na siku ile ninyimtatmbua ya kuwa Mimi ni ndani ya Baba, Baba ndani Yangu,Mimi ndani yenu, nanyi ndani Yangu.” Haleluya! Tumewasili!Haleluya! Ninafurahi sana kumuona yeye akijifanya mwili katiyetu na kuona kile alichoahidi kwa Neno, si misisimko ya mtufulani, kuimba na kuruka, na kucheza, lakini kwa Neno Lake(amina!) Anajifanya ajulikane.176 Angalia walipoleta—na kujenga hekalu na kuliingiza lilesanduku ndani yake, Mungu aliingia humo na Nguzo ya Moto.Amina! Ilikuwa Daudi akiruka na kupiga kelele za furaha.Ilikuwa waimbaji wote na makuhani wakisherehekea hukuwakiwa nje ya mapenzi ya Mungu. Lakini Mungu alipoliona lilesanduku katika mahali na sehemu Yake, kabla hawajaliingizalile sanduku mle ndani, hapa ikaja Nguzo ya Moto ikiongozanjia, moja kwa moja juu ya mbawa za makerubi na mojakwa moja nyuma ya patakatifu pa patakatifu, mahali pake pakupumzikia, Nguzo ya Moto. Na utukufu wa Mungu ulikuwepondani mle hadi…?…hawakuona jinsi ya kuhudumu. Amina!Itafunga macho ya kila mtheologia atakapokuja kumchukuaBibi-arusi Wake. Atachukuliwa juu u—usiku wa manane, kamailivyokuwa, kwao. Hata hawatamuona akienda. Lo, sifa ziwekwa Mungu!177 Angalia. Mungu aliahidi kwamba angemwondoa Bibi-arusiWake, lile angetenda: Patakuwa na mbegu; kutakuweko Nuruwakati wa jioni, ambavyo angetenda haya mambo yote, sawakabisa, na kwa njia ambayo alipanga awali katika Agano laKale naAgano Jipya—na si kupitia katikamadhehebu. Si kupitiamipango yetu tunayotumia leo. Tunasababisha mauti. Weka…watu wana—wanaliwekea mikono yao nao hufa kwa sababuhiyo. Unaona?178 Neno, Ujumbe wa jioni lazima uwe na matokeo ya jioni.Ujumbe wa jioni lazima upande mbegu za jioni, si za asubuhi,mbegu ya jioni. Sivyo? Tukio la saa sita— mbegu zake nyumakule zilikuwa dhehebu. Likafa, likaangamia. Lakini Ujumbewa wakati wa jioni utaonyesha Nuru ya wakati wa jioni,utaonyesha matokeo ya jioni. Ujumbe wa wakati wa jioni…wakati wa Yesu, ule ujumbe wa adhuhuri ulionyesha matokeoya adhuhuri. Ujumbe wa mwanzo ulionyesha matokeo ya

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 33

mwanzoni: ulifanya maumbile. Alimfanya Mwanawe katikaSura Yake adhuhuri. Wakati wa jioni anatengeneza Bibi-arusi kwake. Unaona? Kwa nini? Neno Lake. Alitengenezajedunia? Aliitamkaje ikatokea? Kwa Neno Lake! Mwanawealikuwa nani? Neno! “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, nayeNeno alikuwako kwa Mungu…Naye Neno alifanyika mwiliakakaa…” Atachukuaje Bibi-arusi Wake? Kwa Neno, sio kwagari jipya, si kwa wazo la mwanatheologia, lakini kulingana naNeno Lake atamtambulisha. Usiweke kitu kimoja katika hilo aukuondoa kitu kimoja toka hilo sasa. Liache jinsi lilivyo.Unaona?179 Wakati wa jioni, aliahidi atafunua—atafunua hizi MuhuriSaba na kuonyesha yale ambayo makanisa yalikuwa yamekosanyuma kule. Ufunuo 10, na Malaki 4, Luka 17:30, alisemaatalifanya, kwa hivyo tusilichanganye. Hebu tuliweke moja kwamoja hivyo.180 Hebu katika kufunga…Ni kama, karibu kabisa saa sitakasorobo; hebu nifunge katika kusema hili. Rafiki zangu,sikilizeni katika Jina la Bwana Yesu, mambo haya ni wazisana kwenu kutokuyaamini. Ni wazi sana kwenu kutokuyaona.Hakika mnaweza kuona hayo. Hakika ulimwengu unawezakuyaona. Lakini…Sasa, usishawishiwe na huu umaridadi waupuzi na mambo waliyo nayo leo. Sijali ni watu wazuri namnagani, jinsi walivyo waaminifu, ikiwa hawasemi sawa sawa nasheria na manabii, Biblia ilisema hawana Uzima ndani yao.Unaona?181 Daudi alifikiria alikuwa sahihi; alikuwa mwaminifu. Haomakuhani walifikiria walikuwa sahihi; walikuwa waaminifu.Lakini walishindwa tu kumtaka shauri Bwana kuhusu hilo.Nao wangalilifanyaje hilo? Labda walisema, “Tuliomba sana.”Lakini hiyo haikuwa njia ya Mungu ya kulifanya. Aliahidikwamba hatafanya neno mpaka kwanza awafunulie watumishiWake manabii. Na hapo alikuwa amesimama Nathanieli katiyao, na kamwe hawakumtaka shauri.182 Sasa soma sura chache zinazofuata za Mambo ya Nyakatihapo, nawe utaona wakati Daudi alipoketi katika nyumba ilena kusema, “Ni sawa (Nathanieli alikuwa ameketi pamoja naye)kwamba nikae katika nyumba ya mierezi na—na sanduku laMungu linakaa chini ya hema huko nje. NayeNathanieli akapatakutoka kwa Bwana jambo la kumwambia afanye.183 Naye alikuwa amekosea, kwa hiyo Mungu alisema,“Mwambie mtumishi wangu Daudi, ninampenda. Nilimfanyiajina kama watu wakuu duniani, lakini siwezi kumruhusualitende (Waona?); alinikosea. (Waona?) Sitamruhusu alitende.Nitamleta mtu: mwanawe atainua nyumba ya milele ya Mungu.”Na huyo alikuwa Daudi bila shaka. Ambaye Sulemani alikuwamfano wake, lakini basi alishindwa. Kila mtu lazima hana budikushindwa. Kila mwanadamu hana budi kushindwa. Mungu

34 LILE NENO LILILONENWA

ndiye pekee ambaye hawezi kushindwa.Hawezi kushindwa.Hiloni jambo moja ambalo Mungu hawezi kufanya, ni kushindwa.NaMungu ni Neno. Na Neno…Haidhuru ionekaneje lazima lijenjia hii nyingine, litakuja jinsi hasaNeno lilivyosema.184 Sasa kumbuka, yakupasa ufuate majira, muda. Unaona?Na majira unayoishi, wakati gani, na kuthibitisha hilo kuonakwamba ni Kweli kabisa.185 Sasa chukua lazima hizi zote, Neno lote, mifano yote, namambo yale, kisha angalia unapokaa. Fikiria juu ya wakatitunaoishi. Angalia kule ng’ambo ya kwamba karibu moja asilikumi ya dunia iko tayari kuzama. Sayansi inasema hivyo.Wanaangalia saa. Miaka michache iliyopita walisema, “Ni usikuwa manane kasoro dakika tatu tu.” Huenda ikawa ni dakikamoja; huenda ikawa ni nusu dakika sasa.

Walisema, “Halitatendeka katika kizazi chetu.”186 “Yaweza kutendeka mnamo dakika tano.” Na angalia,jambo jingine alilosema, “Miaka mitano” Sikusema hilo sasa,Yeye alisema hilo, yule mwanasayansi. Wanasongamana kutokaCalifornia kama inzi. Unaona? Vema, siku ile Lutu aliyotokaSodoma, siku ile ile ilinyesha mvua ya moto juu ya nchi.Mojawapo ya siku hizi Mungu atachukua Ujumbe wetu, nasitutaondoka hapa. Kitu fulani kitatokea bila shaka, Kanisalitakapoondoka, Mwili Wake, Bibi-arusi Wake.187 Sasa, nataka kuwasomea Andiko, na nawataka mlisomepamoja nami. Nataka mfungue katika kumbukumbu la Torati 4katika kufunga. Nafikiri ya kutosha labda yamekwisha nenwampate kuelewa. Kumbukumbu la Torati 4. Nitasoma mahalipawili humu ndani. Na kwa kanisa hili, na kwenye kanda—watuwanaosikiza kanda, na watu katika sehemu zilizounganishwakwa redio wanaosikiza nchini kote, nawatakeni msikilize hilikwa makini na msikose. Hili ni jambo ambalo mimi…Kumbukumbu la Torati sura ya 4, sasa, nitaanzia mstari wakwanza. Nataka kusoma msitari wa kwanza, kisha nitasomamstari wa 25 na 26. Mwaweza kusoma yote mtakapofikanyumbani, lakini kuokoa tu muda ili tupate kuondoka katikawakati, sababu sina budi kurudi tena usiku wa leo, Bwanaakipenda. Sikilizeni akinena nabii huyu. Alikuwa katika uwepowaMungu. Alijua ambalo alikuwa anazungumzia. Sikilizeni:

Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumuniwafundishazo, ili mzitende; mpate kuishi na kuingiana kumiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wa babazenu. (Hilo ni mfano wa ule Utawala wetu wa MiakaElfu.)

Msiliongeze neno niwaamurulo, walamsilipunguze,…(Msiongeze kitu kimoja kwenye hilonamsipunguze kitu kimoja toka kwa hilo, kaeni, semeni

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 35

tu lisemavyo.)…mpate kuzishika amri za BWANA,Mungu wenu, niwaamuruzo.Macho yenu yameona aliyoyatenda BWANA…kwa

sababu ya Baal-peori; maana watu wote waliomfuataBaal-peori, BWANA, Mungu wako, amewaangamizakutoka kati yako. (Sasa, ninyi ni wateule kutoka katikamadhehebu hayo. Mnaona, mnaona?)Bali ninyi mlioambatana na BWANA Mungu wenu,

mnaishi kila mmoja wenu hata leo. (Hamkufa pamojana madhehebu yenu; mnaishi sasa na katika uwepo waMungu. Kwa kufunga usilikose.)Msitari wa ishirini na tano sasawanapoingia nchinimle, sasa

angalia kitakachotendeka.Utakapozaa wana, wana wa wana, na mki…mkisha

kuwa katika nchi siku nyingi, mkajaribu wenyewe,…(Hilo ndilo lilitendeka.) na kujifanyia…sanamu zakuchonga…(kitu kingine)…au kwa umbo la kitu chochote, mkafanya ambayo ni maovumachoni pa BWANA,Mungu wako, na kumtia hasira: (Sikilizeni!)Nawashuhudizia mbingu na nchi hivi leo,…

(Mnaona?)…kwamba karibu mtaangamia kabisa juuya nchi…au mahali…ambapo mwivukiayo Yordanikuimiliki; hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake,ila mtaangamizwa kabisa.

188 Huyu alikuwa Musa akinena na Israeli baada ya yeyekuthibitishwa na Mungu kwa Nguzo ya Moto na kujuaalithibitishwa kuwa mtumishi wa Mungu kuwaongoza watoke.Na kabla hawajakwenda katika nchi ile, kabla hawajaingia,Musa alisema, “Sasa maneno niliyonena kwenu, naita mbinguna nchi kushuhudia dhidi yenu. Mkiongeza kitu kimoja kwakeau kuondoa neno moja toka kwake, hamtadumu katika nchiawapayo Bwana Mungu.” Nasema vivyo hivyo katika Jinala Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazoyako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tendasawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda.Usiongezee Kwake.189 Yeye kama kawaida, hutimiza ahadi Yake kwetu. Kilaahadi aliyotoa ameitimiza. Aliwaambieni yatakayotendeka,na je, yalitendeka? Nazileta mbingu na nchi mbele yenuleo kuwahimiza, Mungu aliwahi kusema cho chote ambachohakutimiza na kutenda sawasawa na alivyosema angetutendea?Ametenda sawasawa hasa na alivyosema angetenda? Hilo nisawa hasa! Ataendelea kufanya vivyo hivyo. Usiliongezee.Usilipunguzie. Liamini tu nawe utembee kwa unyenyekevumbele ya Bwana Mungu wako, kwani tunakaribia kuingiakatika nchi ile. Ndipo hutarudi. Hutarudia maisha kamahaya tena. Utarudi kama kiumbe kisichokufa. Utarudi dhambi

36 LILE NENO LILILONENWA

itakapokuwa imeondolewa, Shetani atakapofungwa. Na kwamiaka elfu moja utaishi juu ya nchi hii ambayo Bwana Munguwako amekupa. “Maana wapole watairithi nchi. Heri yeyeazitendaye amri Zake zote, ili aweze kuwa na haki ya kuingiakatika Mji ule, kwani huko nje wako wachawi, waongo, wazinzi,na mbwa; hawataingia humo.” Ni kwa waliokombolewa tu nakwa wale waendao katika amri Zake.190 Usichukue kitu kipya. Vinaruka kila mahali, na kutakuwana zaidi ya hayo yatakayokuja. Lakini usichukue mambohaya mapya. Bwana Mungu wako amekutangazia yaliyo Kweli.BwanaMunguWako amethibitisha Kweli ni nini kwaNeno Lakena kwa Roho Wake. “Si kwa uweza, wala si kwa nguvu, bali nikwa Roho Yangu.” Na Roho…Mungu anawatafuta wale ambaowanamwabudu katika Roho na Kweli. “Neno Lake ni Kweli.” Naamethibitisha vizuri kabisa kwamba Yesu Kristo ni yeye yulejana, leo, na hata milele. Amewaonyesha ninyi mbegu za jioni.Ameifunua kwenu katika Neno. Amethibitisha hilo kwenu kwaRoho Wake.191 Msianzishe au kujaribu kuunda dhehebu kamwe. Msijaribukujenga juu ya kitu cho chote kingine, lakini dumuniwanyenyekevu mbele za Bwana Mungu wenu, kwani yaonekanakama malango huenda yakafunguliwa ya kuingia katika nchi yaahadi hivi karibuni. Basi natuingie kwa kuimba kwa kweli nashangwe, wakati Bibi na Bwana Arusi wanapochukua mahalipao kwenye kiti cha enzi.192 Ishini wanyenyekevu; ishini wenye kupendana. Pendaneni.Msiingize kamwe kitu kati yenu. Ukiona kitu kinakuja moyonimwako dhidi ya mtu fulani, kitoe papo hapo. Usimuachie…NaShetani atafanya awezavyo kuingia kati yenu. Mnaona? Msiachehilo litokee. Mtu fulani mwenye ulimi laini huenda akajaakakutoa katika hilo. Unafikiri waliweza kumshawishi Musaatoke katika uwepo wa Mungu ambapo alikuwa amesimamapale na kuliona? La, bwana! La, hatulipunguzi au kuliongeza!Liwekeni tu vile ambavyo Bwana alisema. Hatutaki dhehebu;hatutaki vyama. Hatutaki uovu; hatutaki fitina; twamtakaMungu; naye ni Neno. Sasa na tuinamishe vichwa vyetu.193 Ee Mungu, naangalia huku na huko na jicho la kiroho;najaribu kuona kinachotendeka. Naona Neno Lako, namnalilivyothibitishwa, namna lilivyohakikishwa. Siku zote tokamiaka thelathini na mitatu, hapa mtoni, ulivyosema, nalipo hapa miaka thelathini na mitatu baadaye, na unatendaulilosema tu. Na umetenda ulilonena tu. Bwana, jambo hili naliwe mbali nasi kujaribu kulifanya dogo au kujaribu kulifanyakubwa. Niliweke tu vile ulivyolitengeneza. Nitembee kwaunyenyekevu na kukufuata Wewe.194 Hawa ndio wao, Bwana, ambao umewatoa kwa hudumambali na wale wanalala nchini, pande zote za dunia. Makaburini

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 37

hapa yanashikilia wengi wa wale wanaongoja, watakatifuwaliobarikiwa. Lakini ni kama ilivyosema; sisi tulio hai,tuliosalia, hatutawatangulia wao waliolala. Parapanda italia,nao waliokufa watafufuliwa kwanza, kisha tutanyakuliwapamoja nao. Utukufu wa Mungu utakapokuwa duniani,utalificha Kanisa toka kwa ulimwengu. Hata hautalionaliendapo.195 Baba Mungu, waweke hawa mikononi Mwako. Niwako. Naomba, Mungu, kwamba siku zote tutatembea kwaunyenyekevu mbele Zako. Hatujui ni muda gani; Hatunahamu ya kujua ni muda gani; Si kazi yetu. Ni kazi Yako. Simapenzi yetu kujua utakuja lini; ni mapenzi yetu, Bwana, kuwawanyenyekevu hata utakapokuja, na kutembea pamoja Nawe.Tunataka sana Wewe kujithihirisha mara kwa mara, Baba, katiyetu, tupate kuona kwamba bado twatembea pamoja nawe.196 Tusamehe dhambi zetu zilizopita. Tuongoze na utulindena kila mtego wa ibilisi kwa ajili ya siku zijazo. Tuongozena utulinde, ee Mungu, Baba yetu. Tusamehe dhambi zetu nautusaidie kuwa watoto Wako. Tu watu wa tabaka maskini.Tu waliokataliwa na watu wa dunia hii, na madhehebu yamakanisa. Tunaona mwisho, na tunakushukuru kwa kuona kwajicho la kiroho katika Neno Lako kuona wakati wa mwisho.Kwani mambo yote haya lazima yafikie kule kupigwa kwamawe kukuu toka Mbinguni. Tusaidie, Bwana, tusiwe hapa sikuile, lakini tuwe tumekwenda katika uwepo Wako, kuruka hadikifuani Mwako.197 Ponya wagonjwa na wanaoteseka Bwana. Twaomba yakwamba usiku huu utatupa ibada kuu. Twaomba kusiwe na mtumnyonge miongoni mwetu kwa sababu ya Uwepo Wako, Bwana.Mioyo yetu na ikuelekee Wewe daima. Na twajua, Bwana,kwamba fedha, mali, mambo ya ulimwengu hayanamaana, ni yamuda tu. Yote lazima yatoweke. Kazi zetu, mahali petu, rafikizetu, kila kitu hakina budi kuondolewa. Haidhuru tu matajiri,tu maskini, tunapendwa au hatupendwi jinsi gani, yote hayanabudi kuondolewa. Lakini kuna kitu kimoja tu hapa ambachondio kiini cha kuwepo kwetu humu, na hicho ni YesuKristo. Kwahivyo, Mungu, hebu na tuweke kando kila kitu ambacho si chamaana na kushikilia Yeye, naye ni Neno. (Tujalie, Bwana) Nenolililothibitishwa la saa hii.198 Neno lililothibitishwa la siku za Musa lilikuwa Yesu. Nenolililothibitishwa la siku za Isaya, Eliya, Yohana, wote, lilikuwaYesu. Na Neno lililothibitishwa leo ni Yesu, yeye yule jana, leona hata milele. Tusaidie, Bwana, kuamini hilo, kuona hilo, nakutembea ndani yake. Tu—tunaomba katika Jina la Yesu.199 Na huku vichwa vyetu vimeinamishwa, nataka kujua kamakuna wengine ndani hapa ambao kamwe hawajafikia ile hatuakuu inayotosheleza…Unaliamini hilo, lakini kuliamini tu

38 LILE NENO LILILONENWA

hakutoshi. Naamini kwamba mke wangu alikuwa msichanamzuri. Nilimjua baba yake, mama yake. Nilimjua kwa miakana miaka. Aliishi maisha yaliyonyoka. Ninaamini alikuwamwanamke mzuri, lakini hilo halikumfanya wangu. Hakuwawangu mpaka yeye—nilipomkubali, aliponikubali. Sasa Yesuanataka kukubali. Hutamkubali na kuwa sehemu ya Neno Lake?Kama hujafanya hilo, huku vichwa vyenu vimeinamishwa namioyo yenu imeinamishwa, natumaini…200 Hakuna nafasi kwa mwito wa madhabahuni hapa. Siaminisana hiyo kwa vyo vyote. Naamini Mungu hukuzuru papohapo ulipo. Nyosheni mikono yenu, mseme, “Ndugu Branham,nikumbuke katika maombi. Nataka kufanya hilo.” Munguakubariki. Mimi…Mungu akubariki. Jamani, mikono kilamahali. Nataka kuwa hivyo. Mungu akubariki, Ndugu, Munguakubirika Ndugu wote mlio hapa. “Nataka kuwa hivyo.” Munguabariki…“Kwa kweli nataka kuwa hilo.” Na—naliona…Vemasasa, tazama, rafiki, huenda kukawa na kitu kidogo…kama tuhilo, basi, kuna kitu fulani kimekuwa kiini chako mbali na hilo.Uko karibu sana nacho, unakiangalia. Unakiona. Umekionakwa miaka kadhaa kikisogea. Unakiona kikikomaa sasa. Kamahilo linamaanisha kila kitu kwetu na hakuna kitu kinginekitakachodumu isipokuwa Hicho, kwa nini usikipe kisogo kituhicho ulichokuwa ukiangalia na kuweka moyo wako Kwake,ambaye ni Kiini cha maisha yote ya hapa baadaye ni Yeye.Mbona usifanye hilo wakati tunaomba pamoja?201 Mungu mpenzi, hapo pana mikono ya wanaume, wanawake,wavulana, wasichana, hata wahudumu, wameinua mikono yaojuu. Wao—walitaka ku—kusema kwamba walitaka kiini chaokiwe ni Bwana Yesu, na bado inaonekana kama hawawezikulitenda; kuna kitu kinawavuta hivi na vile: Huenda ikawani dhehebu; huenda ikawa ni mtu, huenda ikawa ni dhambi;huenda ikawa ni kitu wanachofichamoyoni mwao. Sijui, Bwana;Wewe unajua. Hata iwe ni nini, na iwe hivi, Bwana, unapoitawengine…Umekwisha waita; Ni wako. Na wakati unawaita,na waachilie hiyo—hiyo dhambi inayowasumbua, kama Bibliailivyosema “Na tuweke kando kila mzigo mzito na dhambiile ituzingayo kwa upesi, ili tupige mbio kwa saburi katikayale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.” Tukimtazama nani?Kazi yetu? Dhehebu? Jamii yetu? Halmashauri? Kristo, Mwenyekuazisha na Mwenye Kutimiza imani tuliyo nayo katika Yeye.Tenda hilo, Baba, kwa ajili yetu leo. Kwani tunaomba hilo katikaJina Lake na kwa utukufu Wake.202 Sasa, niWako, Bwana; tenda nao kamauonavyo yafaa. Tendanasi kama uonavyo yafaa; tuWako.Katika Jina la Yesu. Amina.

Ni nampenda, ninampenda,Kwa kunipenda kwanza,Kaninunulia wokovuKalvari.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 39

203 Mmesahau chakula cha jioni? Mmesahau kama watoto woteni salama kule nje katika gari au la? Mmesahau yote kuhusuwakati uliopita na kutambua hicho unachokisikia ni nini sasa?Kinafanyika mwili mbele yako siku kwa siku. Unaona? Achahilo liwe kiini cha lo lote…Acha mambo yaliyosalia yaondoke;yataangamizwa kwa vyo vyote. Lo, endelea tu kumfuata. KamaElisha alivyomfuata Eliya, na tumfuate. Kwani nasi lazimatutwaliwe juu pia siku moja. Tumeona gari la moto ambalolilimtoa kaburini. Tunalihisi kati yetu sasa. Siku moja ataendakufungulia farasi vijitini. Tunaenda juu.Mtampenda?

Kaninunulia wokovuKalvari.

Loo, huwezi karibu kabisa tu—kufumba macho yako naumwone Yeye akining’inia kule?

Ninampenda, (Nimpende mwingine yupi?)Ninampenda,Kwa kunipenda kwanza,Kaninunulia wokovuKalvari.

204 Kila wakati ninaporudi nyumbani, mtu fulani amekwishakuaga dunia. Nitaondoka miezi michache, nirudipo, mtu fulaniameaga dunia. Ninapatwa na huzuni kila wakati nijapo.Hivi majuzi mvulana tulisoma shuleni naye, alipokuwa akijabarabarani alisema, “Hujambo, Billy.”205 Nilimtazama; alikuwa ni kijana mdogo mwenye sura nzuri,nywele nyeusi zinazometameta zimechanwa kuelekea nyuma.Sasa, ni nyeupe kama theluji. Alikuwa amenyoka sana; naana kitambi hivi. Nilisema, “Hujambo, Jim.” Nilimuangalia;nikamsikitikia; nilifikiri, “Mungu, mimi na mvulana huyo,mimi na mtu yule tuna umri mmoja.” Basi najua siku zanguzimehesabiwa. Najua si muda mrefu sana uliosalia. Ninaangaliapande zote, nafikiri, “Nifanyeje, Bwana? Nisaidie. Sitakikukutangulia. Nataka nidumu moja kwa moja—moja kwa mojanyuma Yako. Wewe ongoza njia. Nami naangalia, nafikiri,“Miaka hamsini na sita, loo, jamani, haujasalia muda mrefusana.” Nami naangalia chini, namuona rafiki yangu mzuri BillDauch akikaa pale, miaka sabini namiwili sabini namitatu.206 Naangalia pande zote; nawaona watoto hawa wakifikiria,“vema, nitangojea mpaka niwe mzee kama Ndugu Branham,nitawazia hayo…” Mpenzi, inawezekana usilione hilo; naonashaka sana kwako kuliona hilo. Unaona? Lakini hebu fikiriatu, kama Ndugu Bill Dauch akimaliza siku hii, ataishi zaidiya mamia ya watu wenye umri wa miaka kumi na mitano,kumi na sita. Wanakufa kila saa. Kwa hivyo kuna tofautigani una umri gani? Unafanya nini kuhusu saa unayoishi.Unamfanyia nini Yesu wakati huu? Unaona? Loo, natakakumwona Yeye. Nataka kuona saa ile nitakapoiona miili hii

40 LILE NENO LILILONENWA

yote hii mizee imebadilishwa, kuwaona wamebadilika katikamuda wa kufumba na kufumbua. Kama hilo sivyo, basisisi ni watu wapumbuvu kuliko wote; kuleni, kunyweni namfurahi kwani kesho mnakufa. Mnaona? U kama mnyamatu; unakufa na kuingia katika takataka na hayo ni mwisho.Lakini kuna isiyokufa—nafsi isiyokufa inayoishi ndani yako,ndugu. Tumekwisha sikia toka Mbinguni. Tumekwisha lionalikithibitishwa. Tunajua Yeye yuko, na kwamba huwapathawabu wale wamtafutao kwa bidii.207 Sasa, enyi washiriki wa Mwili wa Kristo, tunapoliimba hilotena nawatakeni mketi katika viti vyenu na kupeana mikonotunapoimba hilo tena.

Ninampenda, (Msalimie tu ndugu yako, dada)ninampenda,

Kwa kunipenda kwanza, (Richard!)Kaninunulia wokovu.Kalvari.

208 Mnampenda, semeni, “Amina!” [Kusanyiko linajibu“Amina! “—Mh.] Mnalipenda Neno Lake, semeni “Amina”![Kusanyiko linajibu, “Amina “—Mh.] Mnapenda ushirikaWake, semeni, “Amina! [Kusanyiko linajibu, “Amina! “—Mh.]Mnapenda mwili Wake, semeni, “Amina! “] [Kusanyiko linajibu,“Amina! “—Mh.] Basi pendaneni! Amina. Hilo ni kweli. “Hivyowatu wote watatambua ya kuwa ninyi ni wanafunzi Wangu,mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”209 Sasa, nimeweka mikono yangu juu ya vitambaa hivi kamaitawalazimu kuwa navyo kabla ya usiku…Nitamuomba NduguRichard Blair, Mungu alijibu sala yake, yeye na ndugu yulemwingine, hapo akiomba hivi majuzi kumrudisha huyumvulanamdogo ambaye anaketi kati yetu leo, ambaye anaishi kwasababu ya imani yao katika Mungu…Na sasa, nitamuombaaturuhusu tuondoke katika neno la maombi katika mudamchache tu ujao, ili tuweze kuja tena usiku huu. Ni kamasaa sita na dakika tano kwa saa ile. Nami nawatakeni mrudiusiku huu, kama mkiweza, kama mpo. Kama huna budikwenda nyumbani, Mungu na akupe safari njema barabarani,na akusaidie, na akulinde. Kama waweza kubaki na unatakakubaki, unakaribishwa kubaki hapa. Mungu awe pamojananyi sasa.

Hata twonane huko juu,Hata (Hebu tuinue mikono yetu kwa…)twonane Kwake kwema,

Hata twonane huko juu,Mungu awe nanyi daima.[Ndugu Branham anaanza kuugugumizawimbo uo huo—Mh.] (Hiyo ndiyo njia yakuondoka katika nyumba ya Mungu, kwa

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZI YAKE 41

maombi, kwa unyenyekevu, tukitumainitutakutana tena usiku huu. Kamahatukutani, Mungu awe nanyi) hatatutakapoonana tena…

Na tuinamishe vichwa vyetu sasa. Ndugu Blair.

KUMTENDEA MUNGU KAZI BILA MAPENZIYAKE SWA65-0718M(Trying To Do God A Service Without Being The Will Of God)

Ujumbe huu uliohubiriwa na Ndugu William Marrion Branham, uliotolewahapo awali katika Kiingereza mnamo Jumapili jioni, Julai 18, 1965, katikaMaskani ya Branham kule Jeffersonville, Indiana, Marekani, umetolewa kwenyekanda ya sumaku iliyorekodiwa na kuchapishwa bila kufupishwa katikaKiingereza. Tafsiri hii ya Kiswahili ilichapishwa na kusambazwa na Voice OfGod Recordings.

SWAHILI

©2015 VGR, ALL RIGHTS RESERVED

VOICE OF GOD RECORDINGS

P.O. BOX 950, JEFFERSONVILLE, INDIANA 47131 U.S.A.www.branham.org

Ilani ya haki ya kunakili

Haki zote zimehifadhiwa. Kitabu hiki kinaweza kuchapishwa kwa matbaa ya nyumbani kwa matumizi ya kibinafsi ama kusambaza, bila malipo, kama chombo cha kuitangazia Injili ya Yesu Kristo. Kitabu hiki hakiwezi kikauzwa, kunakiliwa kwa wingi, kuwekwa kwenye mtandao, kuhifadhiwa kikatolewe tena, kufasiriwa katika lugha zingine ama kutumiwa kuomba fedha bila idhini halisi iliyoandikwa moja kwa moja kutoka Voice Of God Recordings®.

Kwa habari zaidi ama kwa vifaa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Voice of God RecoRdinGsP.o. Box 950, JeffeRsonVille, indiana 47131 U.s.a.

www.branham.org