Upload
irene-john
View
164
Download
1
Embed Size (px)
Citation preview
DIBAJI
Ndugu wanajumuiya,
Assalam alaikum
Naomba nianze kwanza kwa kumshukuru ALLAH (SW) mwingi wa rehema kwa kutujalia afya
kwa mwaka 2012, kuweza kutekeleza kazi mbalimbali za Jumuiya.
Pili napenda kuwapa pole wanajumuiya mbalimbali ambao kwa mwaka 2012, walifiwa na
wawapendao, kama wazazi, waume, wake au watoto
Pia nichukue fursa hii kuwapongeza wale wote waliofanikiwa kufunga ndoa, na wale
waliojaliwa kupata watoto. Mwenyezi Mungu awape Baraka tele na afya.
Ndugu Wanajumuiya kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 10: 7;3 na 13, Jumuiya inapaswa
kuandaa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mwaka mmoja na kufanya mkutano mkuu wa
mwaka kati ya Januari/ Februari. Mkutano mkuu utapokea taarifa za Jumuiya kwa kipindi cha
mwaka mmoja na kujadili, kutoa maoni na mapendekezo.
Nichukue pia fursa hii kuwashukuru nyinyi wanajumuiya kwa ushiriki wenu mzuri kwa mwaka
2012, pia niwashukuru viongozi wote wa ngazi mbalimbali kwa kufanikisha utendaji wa kazi
mbalimbali za Jumuiya kwa mwaka 2012.
Baada ya utangulizi huo naomba sasa nihudhurishe mbele yenu taarifa ya Jumuiya ya mwaka
2012, nanyi muijadili ,mtoe maoni au mapendekezo
Wenu
Abdallah Bihoga
Amir
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
Jumuiya ya waislam KCMC (KMA) ni jumuiya huru ya Kiislamu iliyopo Moshi- Kilimanjaro.
Jumuiya hii wanachama wake ni wanafunzi wanaosoma vyuo mbalimbali vya KCMC,
Wataalamu wa afya mafunzoni( Interns) na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za KCMC.
Pia Jumuiya hii hutoa nafasi ya Uanachama wa heshima kwa Muislamu yeyote mwenye mapenzi
na jumuiya na kwa wale waliowahi kuwa wanachama wa Jumuiya (wale waliomaliza mafunzo
au kuacha/ kustaafu kazi KCMC).
Madhumuni ya Jumuiya hii ni kuwaunganisha na kuwaweka pamoja waislamu wote waliopo
kwenye jamii ya KCMC ili kukuza moyo wa kidugu wa kiislamu na ushirikiano baina yao; pia
kuhakikisha wanajumuiya wanaishi kwa kufuata miongozo, mila na hulka za dini ya kiislamu.
2
SURA YA PILI
UONGOZI
Kwa mwaka 2012, Jumuiya ya Kislamu ya KCMC (KMA) imekuwa na viongozi kwa awamu
mbili (2) kutokana na kufanya uchaguzi katikati ya mwaka.
Kwa mwaka 2012, Viongozi wakuu wa Jumuiya walikuwa ni:_
Awamu ya kwanza Awamu ya pili
Abdallah Bihoga- Amir Abdallah Bihoga- Amir
Amour Shaaban- Naibu Amir Mwalimu Khalid- Naibu Amir
Fani Musa- Katibu Mkuu Fani Musa- Katibu Mkuu
Pia katika kuhakikisha kuwa kuna kuwa na ufanisi katika utendaji wa kazi za Jumuiya. Jumuiya
ina kamati tano (5) za utendaji na katika mwaka 2012, wafuatao ndio walikuwa viongozi wa
kamati
KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII
Awamu ya kwanza Awamu ya pili
Othman Wamala- Amir Shamiru Ismail- Amir
Shamiru Ismail- Katibu Abubakar Sudi- Katibu
Nyanza Simba- Mjumbe Heri Nyamvi- Mjumbe
Mary Kawiche- Mjumbe Shaban Yusuf- Mjumbe
Maimuna Mohamed- Mjumbe Husna Muna- Mjumbe
Nazmin Nazir- Mjumbe Hamisi Matula- Mjumbe
Warda Baltazar- Mjumbe Juma B.Juma- Mjumbe
Ziad Abdul- Mjumbe Salama Omar Mahawi- Mjumbe
Heri Nyamvi- Mjumbe
3
KAMATI YA DA’AWA
Awamu ya kwanza Awamu ya pili
Mwalimu Khalid- Amir Abdallah Mwinyihaji- Amir
Yahaya Ali- Katibu Ramadhani Y.Ramadhani- Katibu
Athumani Mwedi- Mjumbe Musa Makame- Mjumbe
Fatma Msemo- Mjumbe Ramadhani Hamis- Mjumbe
Hussein Mwangi’mba- Mjumbe Salum Ally- Mjumbe
Masoud Rashid- Mjumbe Salma Jafari- Mjumbe
Abdallah Mwinyihaji- Mjumbe Fatma Miraji- Mjumbe
Arafat S.Suleiman- Mjumbe Uwesu Muki-Mjumbe
KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI
Awamu ya kwanza Awamu ya pili
Hamisi Mvugalo- Amir Shabani Massawe- Amir
Asha Kumpuni- Katibu Lulu Mushi- Katibu
Mwanaid Mwinjuma- Mjumbe Faudhia Hadith- Mjumbe
Shabani Massawe-Mjumbe Arafat Massawe- Mjumbe
Daudi Katwana- Mjumbe Ismail A.Chuwa- Mjumbe
Samiha A. Juma- Mjumbe Hamisi Sembe- Mjumbe
Mohamed Mbalazi- Mjumbe Amri Kyaruzi- Mjumbe
Mwanaid Mwinjuma- Mjumbe
4
KAMATI YA HABARI, MAWASILIANO NA TAKWIMU
Awamu ya kwanza Awamu ya pili
Hassan Kabange- Amir Othman Wamala- Amir
Daudi A. Joho- Katibu Daudi A. Joho- Katibu
Mubashir Jusabani- Mjumbe Ibrahim Sassilo- Mjumbe
Nuru Mwaluwinga- Mjumbe Maulid Abdallah- Mjumbe
Ashraf Hamza- Mjumbe Yusuf Abdulrahman- Mjumbe
Ibrahim Sassilo- Mjumbe Dawani Ngomelo- Mjumbe
Maulid Abdallah- Mjumbe Thabit K- Ramadhani- Mjumbe
Asha Mswahili- Mjumbe
KAMATI YA WANAWAKE
Awamu ya kwanza Awamu ya pili
Zubeda Amir- Amira Ashura Kazema- Amira
Salma Sued- Naibu Amira Samiha Abdallah- Naibu Amira
Salma Mwamba- Katibu Nuru Mwaluwinga- Katibu
Orpar E Msuya- Mjumbe Aisha Abubakar-Mjumbe
Mwema Ndekio- Mjumbe Rabia Mmanga-Mjumbe
Sabra Yahya- Mjumbe Asha Kumpuni-Mjumbe
Dr. Hudaa Akabi-Mjumbe Nabila F. Ally-Mjumbe
Dr. Fatma Makuka-Mjumbe Maimuna Ally-Mjumbe
Samiha Abdallah-Mjumbe
Salha M. Sheikh-Mjumbe
5
Pia kulingana na mahitaji ya jumuiya iliunda kamati ndogo, ya nusra na viongozi wake walikuwa
ni:-
Othman Wamala - Amir
Mwalimu Khalid - Naibu Amir
Mussa Makame - Katibu
Salha Ally Omari - Mjumbe
Rashida Ismail - Mjumbe
Zuwena Gwotta - Mjumbe
6
SURA YA TATU
UTEKELEZAJI WA KAZI MBALIMBALI ZA JUMUIYA
A: MAFANIKIO;
Mafanikio ya jumla
(i) Umoja
jumuiya ya kiislamu, inajivunia kwa kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa
wanajumuiya, bila kujali tofauti baina yetu. kwa kipindi chote cha 2012, tumekuwa wamoja,
na tumekuwa na mshikamano thabiti.
(ii) Ushirikishwaji wanajumuiya
Wanajumuiya wote , wamekuwa wakishirikishwa na kushiriki kikamilifu katika kazi za
utendaji za kila siku, na pia katika majukumu ya uongozi katika ngazi zote. Na maamuzi
yote yamekuwa yakitolewa na wote na wala sio watu au kikundi mahususi
(iii) Katiba
Mwaka 2012, wanajumuiya walifanikiwa kutoa maoni yao na hatimaye tumekamilisha
uandishi wa katiba ya jumuiya yetu na tunategemea mwaka 2013 kusajiliwa rasmi
(iv) Kufungua sanduku la barua
Mwaka 2012, jumuiya imefanikiwa kufungua sanduku la barua rasmi S.L.P 287 Moshi,
kwa jili ya mawasiliano, kupokea barua na vifurushi
(v) Seminaelekezi
Jumuiya ilifanikisha kuendesha semina elekezi mbili (2) kwa mwaka 2012.
Semina ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kuItambulisha jumuiya na semina ya pili ilikuwa
ni kuwapa mafunzo viongozi wa kamati mbalimbali juu ya utekelezaji wa kazi zao za kila
siku.
(vi) Ujenzi wa sehemu ya kuchukua udhu
Jumuiya na kupitia wahisani tumefanikiwa kutengeneza sehemu nzuri ya kuchukulia udhu
katika msikiti wetu na hivyo kuupa msikiti mandhari ya kupendeza
7
(vii) Ununuzi wa vitabu mbalimbali
Jumuiya yetu imefanikiwa kununua vitabu mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha maktaba
yetu pia tulipokea msaada wa vitabu kutoka taasisi ya African Muslims Agency
(viii) Kuchapisha vitabu vya stakabadhi
Jumuiya ilichapisha vitabu vya stakabadhi, ambavyo vimetumika kuweka kumbukumbu
sahihi za mapato ya jumuiya
(ix) Ununuzi wa viandiko na muhuri,
Jumuiya imenunua viandiko (stationaries) mbalimbali na pia ilichonga mihuri ya jumuiya
ili kufanikisha kazi za kiofisi za jumuiya
(x) Vikao vya jumuiya
Jumuiya imekuwa ikifanya kazi kwa vikao vyake rasmi, kama vikao vya ngazi za
mashina na Shura ili kuleta ufanisi zaidi
(xi) Uchaguzi mkuu
Jumuiya ilifanya uchaguzi wake mkuu juni 2012 na kuchagua viongozi wa kuendesha
jumuiya mpaka Februari 2013
(xii) Kusimamia utendaji wa kazi za jumuiya na uelekezi
Jumuiya imekuwa ikifanya kazi za usimamiaji wa utendaji wa kamati ( supervision) na
mashina na kutoa uelekezi ili kuboresha utendaji kazi
8
Mafanikio mahsusi:-
Masuala ya huduma ya jamii;
i. Kusimamia matukio ya msiba
kamati ilifanya kazi ya kuarifu wanajumuiya juu ya misiba iliyowafika wanajumuiya
wenzetu na kuwashirikisha wanajumuiya katika kuwafariji wenzetu.Mwaka 2012 Dr. Mtagi
Kibatala, Neema Massawe na Fatma Ahmed na Mwanaidi Mwinjuma walifikwa na misiba
ya wapendwa wao.
ii. Kusimamia masuala ya maradhi
Kamati pia imekuwa ikiwaarifu wanajumuiya juu ya wanaofikwa na maradhi na
kuhamasisha kuwahudumia.Wanajumuiya mbalimbali walifikwa na maradhi na mwenzetu
mmoja,Amani Kapinga (MD4) alipatwa na ajali ya kupigwa na risasi.
iii. Kusimamia masuala ya harusi
Kamati pia imekua ikitoa taarifa za wanajumuiya wanaofunga ndoa na kuhamasisha ushiriki
wa wanajumuiya katika harusi hizo kwa hali na mali.Mwaka 2012 wanajumuiya wafuatao
walifunga ndoa Dr. Adnan Juma na Dr. Rehema, Asma Bakari
iv. Michezo
Kamati iliandaa tamasha la michezo la ndani kwa ajili ya wanajumuiya pia tulishiriki katika
tamasha la michezo nje ya jumuiya kwa madhumuni ya kuimarisha udugu na umoja wetu wa
kiislamu
v. Kuratibu mfungo wa mwezi wa Ramadhani
Kamati iliandaa utaratibu mzuri wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani,kwa kuhakikisha
wanajumuiya tunafuturu pamoja na pia kuandaa daku kwa wote
vi. Kutoa msaada na kutembelea watoto yatima
Kamati iliandaa siku maalum ya kutembelea watoto yatima kuwafariji na kuwapa msaada
vii. Kutoa elimu ya Afya
Kamati kwa kushirikia na kamati ya Da’awa walitoa elimu ya Afya ya magonjwa ya zinaa
kwa vijana wa sekondari
viii. Kuandaa sherehe mbalimbali
Mwaka 2012, kamati iliratibu na kuandaa sherehe za Idd El fitri & Eid El Haji, sherehe ya
kuwakaribisha mwaka wa kwanza na mahafali.
9
Masuala ya kamati ya Da’awa
i. Uendeshaji wa madarasa ya Ijumaa , Jumamosi na Jumapili
Kamati iliandaa madarasa ya Ijumaa, kwa ufanisi mkubwa
Pia iliendesha kwa wastani madarasa ya Jumamosi na Jumapili
Kamati pia ilitafuta watoa mada katika madarasa na sherehe mbalimbali za jumuiya
ii. Uangalizi wa Msikiti
Kamati ilihakikisha usafi wa msikiti wa kila wiki mwisho wa mwezi unafanyika, pia
kuuweka msikiti katika mandhari nzuri.Kamati pia ilisimamia ibada mbali kama sala
tano(5), tarawehe, hadithi ya siku vinasimamishwa katika msikiti
iii. Jaula
Kamati ilifanya ziara za kuwatembelea wanajumuiya katika hosteli na pia wanafunzi wa
sekondari nje ya jumuiya kwa lengo la kubadilishana mawazo,kuamrishana mema na
kukatazana mabaya
Masuala ya Kamati ya fedha na uchumi
i. Kukusanya michango na kuendesha miradi
Kamati ilikusanya michango mbalimbali kama ada za wanajumuiya,zaka/ sadaka na
michango ya ngazi ya kifamilia. Pia iliweza kukusanya fedha kutoka katika miradi ya
jumuiya.Kamati lifanikiwa kukusanya jumla ya Tsh 2, 948,985/=
ii. Kuandaa bajeti na taarifa za fedha
Kamati ilikuwa ikiandaa taarifa za fedha (mapato na matumizi) za mwezi, miezi 3,6, na
ya mwaka na pia kuandaa bajeti ya mwaka ya jumuiya.
iii. Kuweka Akiba
Kamati pia imeendeleza kuweka akiba, kuhakikisha hazina ya jumuiya haitetereki.Kwa
mwaka 2012, Kamati iliweka akiba ya Tsh. 627,123.91 na mpaka mwisho wa mwaka
2012, Jumuiya imebaki na salio la Tsh 1, 267, 591.51 benki.
10
Masuala ya Kamati ya habari, takwimu na mawasiliano
i. Kusimamia vyombo vya habari vya jumuiya
Kamati ilisimamia sanduku la barua, blogu, barua pepe na mitandao ya kijamii ya
facebook ili kurahisisha mawasiliano na uenezaji wa habari.
ii. Utunzaji wa kumbukumbu takwimu na uchambuzi wa taarifa za usajili za uanachama
Kamati imekuwa ikikusanya taarifa za wanajumuiya katika faili la usajili, pia imekuwa
ikitunza taarifa za uanachama na takwimu za mahudhurio katika semina na sherehe
mbalimbali.
iii. Kusaidia mitambo ya kompyuta katika sherehe na madarasa mbalimbali.
Kamati imekuwa ikisimamia mitambo ya kompyuta au projekta kwenye madarasa au
sherehe mbalimbali za jumuiya na pia kuandaa waendeshaji wa sherehe (MCs)
iv. Kuendesha mradi wa kuuza DVD za mahafali
Kamati ilizalisha na kuuza DVD za mahafali ya jumuiya yetu, ambazo zilisaidia kuingiza
mapato katika jumuiya.
Masuala ya kamati ya wanawake
i. Kuendesha darasa la wanawake la kila jumapili na kutafuta wahadhiri
Kamati iliendesha darasa la wanawake la kila jumapili ili kuwainua kiimani wanawake na
pia ilitafuta wahadhiri kutoka nje, kufanikisha uendeshaji wa darasa hilo.
ii. Kushiriki kongamano la wanawake
Kamati ilishirikiana na kamati ya wanawake wa Mkoa, katika kuandaa na kushiriki
katika kongamano la wanawake la mkoa lililofanyika January 2012
iii. Siku ya Hijabu
Kwa mara ya kwanza, kamati yetu iliweka historia kuasisi siku ya Hijabu kwa wanawake
wa KCMC. Siku hiyo ilifana na wanawake waliweza kubadilishana
mawazo,kuelimishana na kupeana mawaidha yenye manufaa
iv. Kuimarisha Umoja wa wanawake
Kamati umefanya juhudi kubwa katika kuhimiza na kufanikisha umoja wa wanawake
waliopo KCMC na nje ya Jumuiya.
11
B: CHANGAMOTO / MATATIZO
1. Simu ya Jumuiya
Jumuiya licha ya kufanikiwa kufungua sanduku la barua,bado haijafanikiwa kuwa na
simu ya jumuiya kwa kuwa usajili wa jumuiya haujakamilika.Ni matazamio yetu kwa
mwaka 2013 huenda tukafanikiwa kuwa na simu ya jumuiya.
2. Mahudhurio hafifu ya vikao
Vikao vya ngazi zote vimekuwa na mahudhurio ya wastani kwa wajumbe, hivyo
kumekuwa na ukosefu wa ufanisi katika baadhi ya maamuzi
3. Ukosefu wa mfuko maalum wa harusi, msiba na majanga
- Jumuiya bado haina mfuko maalum wa harusi, misiba na majanga
- Jumuiya iko mbioni kuandaa mfuko huo na kupendekeza kiwango maalum cha
mfuko huo.
4. Ushiriki wa michezo
- Kumekuwa na ushiriki hafifu wa michezo katika matamasha mbalimbali
yaliyofanyika mwaka 2012.
5. Usafi wa msikiti na utunzaji wa mazingira yake.
- Wanajumuiya wachache hushiriki katika usafi wa kila wiki na mwezi wa msikiti na
pia baadhi ya wanajumuiya wanaharibu mandhari ya msikiti mathalani kugeuza
sehemu ya malazi, kuweka mizigo yao pasipo na utaratibu au kugeuza sehemu ya
kutilia udhu kuwa sehemu kufulia nguo.
6. Kutokutoa michango kwa wakati au kutokutoa kabisa.
- Wanajumuiya wengi hawatoi ada ya uanachana kwa wakati na wengine hawatoi
kabisa. Mathalani kwa mwaka 2012, ni wanajumuiya 123 tu kati ya 269 ndio walitoa
ada ya uanachama.Michango hafifu au kutokutoa michango kunaathiri
kutokutimizwa au kutokidhi bajeti ya jumuiya.
7. Ukosefu wa miradi ya kutosha
- Jumuiya kwa mwaka 2012 ilikuwa na miradi miwili (2 )tu ya kuuza vocha na kuuza
DVD za mahafali miradi hiyo bado inaingiza kiasi kidogo cha mapato na pia
kuibiwa kwa simu moja kuliathiri kushuka kwa mapato
12
8. Ukosefu wa kompyuta na tovuti
Jumuiya inakosa kompyuta kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi, pia bado haina tovuti
ya kuweza kujitangaza na kutoa habari zake
9. Tatizo la usajili wa wanajumuiya
- Jumuiya kwa sasa haina daftari la kudumu la wanachama, pia kumekuwa na udhaifu
katika kuwaingiza wanajumuiya katika parua pepe za jumuiya.
Jumuiya ipo mbioni kuakikisha tunaanzisha daftari la kudumu la wanachama na pia
kuhakikisha wanajumuiya wanaingiza taarifa zao katika barua pepe yetu na pia
tutakapokuwa na tovuti yetu, itakuwa ni rahisi kwa wanajumuiya kuweka taarifa zao.
10. Uvaaji wa hijabu na darasa la wanawake
- Kumekuwa na mahudhurio hafifu ya darasa la wanawake na pia wanawake wengi
hawajitokezi kuwa wahadhiri sambamba na hilo bado uvaaji wa hijabu haukidhi
matarajio na pia baadhi ya hijabu hazikidhi viwango vilivyoanishwa katika Quran na
Hadith za Mtume(SAW).
C: MAPENDEKEZO/ MIPANGO YA BAADAYE
1. Jumuiya ina malengo/ mipango ya kuhakikisha
(i) Tunakuwa na simu ya jumuiya na tovuti ili kurahisisha mawasiliano
(ii) Kununua kompyuta ya jumuiya
(iii) Kuongeza na kubuni miradi ili kuiongezea jumuiya mapato, tunafikiri kuanzisha
mradi ya kuuza T-shirt, kalenda na mitandio na majuba
(iv) Kukuhakisha tunaweka akiba zaidi katika akaunti yetu ili kutunisha hazina yetu.
13
SURA YA NNE
4.0 SHUKRANI
Jumuiya inapenda kutoa shukrani kwa wanajumuiya na wadau mbalimbali kwa kufanikisha
utekelezaji wa shughuli za jumuiya.
Jumuiya inawashukuru Afrika Muslims Agency kwa msaada wa vitabu, pia inawashukuru
Friends of KMA kwa kusaidia baadhi ya shughuli za jumuiya
Jumuiya inawashukuru wanajumuiya waliokuwa na nafasi za uongozi, katika ngazi mbalimbali
kwa michango yao ambayo imesaidia jumuiya kupiga hatua.
Na mwisho tunawashukuru tena wanajumuiya wote kwa ushiriki wao wa hali na mali katika
kuhakikisha jumuiya inadumu na kusonga mbele.
4.1 MWISHO
Taarifa hii imeandikwa na viongozi wa kamati zote za jumuiya na kukusanywa katika taarifa
moja na Katibu Mkuu wa jumuiya kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa
4.2 MAWASILIANO
KCMC Muslims Association
P.O.Box 287 Moshi
Blogu: kcmcmuslimsassociation.blogspot.com
Facebook group: kcmc muslims association
Email: [email protected]
14