Tamko La Tajoc

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Tamko La Tajoc

Citation preview

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu Waandishi wa Habari, Leo ni siku ya mtoto wa Afrika.

Siku hii ina umuhimu wa kipekee kwa mtoto wa Afrika.

Ni siku ambayo watoto wote barani Afrika wanakumbuka mauaji ya kinyama yaliyotekelezwa na utawala wa makaburu dhidi ya watoto wa mji wa SOWETO, tarehe 16, Juni 1976.

Ikiwa ni miaka 39 toka kutokea kwa mauaji hayo dhidi ya damu isiyokuwa na hatia, Chama Cha Waandishi wa Habari za Watoto Tanzania (TAJOC), kinalaani vikali kila aina ya dhuluma zinazoendelea kutekelezwa dhidi ya watoto hapa nchini Tanzania, na pia tunaiomba serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahusika wa matukio hayo.

Mfano wa matukio hayo ni lile la mkoani Kilimanjaro ambapo watoto kadhaa walikutwa wamefichwa kwenye nyumba ya mkazi mmoja.

Chama cha TAJOC, kinaitaka serikali kuchukua hatua za haraka dhidi ya watu wa aina hiyo, kwani huko ni kuwadhulumu watoto haki zao.

Lakini pia watoto nchini bado wanakabiliwa na tatizo la lishe ambapo takwimu zinaonyesha kwamba, asilimia 42 ya watoto chini ya miaka mitano nchini wana utapiamlo.TAJOC kinawaasa wananchi kuwa, ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa wanapambana na tatizo hili la utapiamlo kwa watoto, na kutoa kipaumbele kwa siku 1,000 za mwanzo za mtoto, kwa maana ya kuwa toka mimba inapotungwa hadi kipindi cha miaka miwili toka kuzaliwa, kwani ndicho kipindi kinachotoa picha kamili ya maendeleo ya mtoto.

Tunaiomba serikali kuwa na bajeti maalumu kwenye eneo la lishe, lakini na wadau wengine kuliangalia suala la lishe ya watoto ili tatizo la utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano liweze kuisha.

Watoto, Kwanza!

Edward Qorro

Mwenyekiti

TAJOC